NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SABINI NA TISA
MTUNZI :
Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA NANE: Deus akiwa anatoka kigamboni, anapokea ujumbe wa whatsapp toka kwa Pacha wake, ukimtakia heli ya siku ya kuzaliwa, wakati huo huo anapokea simu toka kwa mteja wa kikike ambae anamueleza kuwa kesho saa mbili usiku, akachukue mzigo mwenge karibu na NMB, kisha aupeleke Sisterfada Hotel chumba namba nane, cha ghorofa ya nne……….ENDELEA…
Pia akiwa njiani anarudi kwenye maficho yake anakutana na vijana wanne wenye silaha waliotaka kumuibia gari, ambao hakuweza kuwavumilia na kuamua kuwaangamiza watatu, na kumuacha mmoja tu,, ambae aliona kuwa licha ya kuwa kijana mdogo lakini hakuwa na madhara kwake.
Na sasa kijana Deus, yupo chumbani kwake amesha jiweka safi, kisha akamaliza kula na kutulia kitandani anatazama kumbu kumbu zake za zamani alizozihifadhi kwenye simu yake hii aliyoiwasha leo.
Na siku hii yenye mambo mengi ndiyo siku ambayo tajiri mkubwa bwana James alieweza kukimbia nchini kwake #mbgo_land, na kuja kuishi Tanzania kama mkimbizi tajiri mkubwa sana barani Africa anapokea simu toka kwa waziri wa ulinzi wa nchi ya #mbogo_land, ambae anamueleza kuwa anahitaji washiriki biashara fulani lakini iwe siri yao, Kervin James anashangaa sana maana kiukweli kabisa, waziri wa ulinzi wa sasa wa #mbogo_land, ndie aliekuwa kiongozi mkuu wa operation kabambe ya kuwasaka waasi na kuwamalizia mbali, na ndio operation ambayo ilimkosa kosa yeye na kukimbilia nchi Tanzania akiwa na mtoto mmoja, na sasa ana watoto watatu, wakike wawili na wakiume mmoja, hivyo bwana James anaalikwa kwenye mkutano na wajumbe wa Chitopelah, ambao atakutana nao hiyo kesho chumba namba nane cha ghorofa ya pili cha hotel sisterfada, mida ni saa tatu.*******
Naaam usiku wa saa saba, kuna watu sita walikuwa wamekaa ndani ya nyumba moja ya kawaida kabisa iliyopo mitaa ya temeke kaburi moja wanapeana maelezo juu ya mpango wao wakujipatia fedha za kuweza kulipia silaha zilizopo njiani kwenda #mbogo_land, zikitokea nchini china, mipango ambayo ilikuwa ni lazima ifanyike kesho muda ukiwa ni kuanzia saa tatu usiku.
“kumbukeni tuna mipango miwili” alisema bwana Erasto Kadumya, kanal mtoro wa jeshi la MLA, ambae pia alikuwa ameingia masaa machache toka TTC yani Treanch Town City, huku akiwatazama wenzake ambao ni bwana Ramadhan Mbwambo na luten mtoro wa MLA, Enock Kafulu, pia alikuwepo private captain Zaid Tambwe na private Job, hao pia ni askari watoro wa jeshi hilo tiifu la #mbogo_land, huku kijana mmoja akiwa amesimama nje ya nyumba hiyo, kama vile anamsubiria mtu fulani, lakini pia alikuwa katika jukumu la ulinzi wa nyumba ile na kutazama usalama wa wenzake waliopo ndani.
“mpango wa kwanza ambao ukifanikiwa tutakuwa tumemaliza na kuachana na mpango pili, ambao ni kukuchukua fedha kwenye PTSB, yani Private Tresure Saving House” alieleza Kadumya huku anawatazama kwa zamu wale wenzake kuona kama kuna mtu anaonyesha dalili ya kupingana na mipango ile, lakini akaona wote wanamsikiliza, mpongo wa kwanza ni kumshawishi bwana James Kervin kufadhili kikundi chetu, tunaamini kwa kuwa yeye pia ni muathirika wa serikali ya #mbogo_land, lazima atakubaliana na sisi kwaajili ya kuhakikisha anawafanya wakina Mbogo kulipa kwa kile walichomfanyia na kumsababishia awe mkimbizi katika nchi yake” hapo Kadumya alitulia kidogo, kabla hajaendelea.
Mpango wa pili ambao ni wa huko PTSH, ambayo hufanya kazi masaa ishirini na nne, tume mlenga mfanyakazi wa tajiri mmoja wa usafiri wa anga ambae huleta fedha za kampuni kila siku za jumamosi mida ya saa nne usiku, ambapo huleta fedha isiopungua billion ishirini, ikiwa ni mauzo ya wiki nzima, tunaamini zitasaidia kwenye malipo ya silaha na posho za askari” alisema Kadumya, ambae ukimuona utakubaliana na bwana Chitopelah kwanini alimteua kusimia jeshi hilo la siri baada ya kumshawishi aachane na jeshi la serikali ya nchi ya kifalme ya #mbogo_land, kwa jinsi alivyo huyu mwamba.
Kwanza ukiachana na ule muonekano wake wa kufuga ndevu nyingi usoni mwake zilizo zidi kuifanya sura yake ya kutisha kupendeza zaidi na kuwa katika muonekano wa kikamanda, pia mwamba alikuwa ameenda hewani, yani mrefu kiasi,mwenye mwili uliojaa na kujengeka kimazoezi, “lakini boss mimi naona kama tungeachana na mpango kwanza, ambao kama utashindikana lazima bwana James atafichua mipango yetu, na ukizingatia tutakuwa tumesha weka wazi mbele yake, hivyo itapelekea watu kuanza kutufuatilia kwa ukaribu zaidi” alisema kijana Enock Kafulu, ambae ni kijana mwenye umri wa miaka 28.
“Enock mpango wa pili ni hatari zaidi, ambao una mambo mengi sana kuliko mpango wa kwanza, nadhani hata wewe unalifahamu hilo, kuhusu bwana James yeye akikataa na kwa kuwa atakuwa amesha fahamu siri zetu basi tutamuua na kutengeneza uvumi kuwa ameuliwa na serikali ya mfalme Elvis ili kufanya raia waanze kumchukia na huku mataifa mengine yaki mlaumu kwa kufanya mauwaji hayo” alisema Kadumya pasipo kufafanua mpango wapili.
Lakini safari hii bwana Mbwambo alikumbuka kuhusu mpango wa pili, “na endapo tutalazimika kutumia mpango wa pili kuna lolote limeandaliwa ili kuepuka kufuatiliwa na vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania?” aliuliza bwana Hassan Mbwambo, “yah! yah! kuna watu wawili ambao wanahitaji kuwajibika juu ya hili, lakini bahati mbaya watapatikana wakiwa tayari wamesha kufa, hivyo hakuna atakae hoji marehemu zaidi ya kwenda kufukia miili yao” alisema Kadumya akiwa na uhakika na kile anachokisema, wote wakacheka kwa furaha.
Naa wakati wanaendelea na maongezi yao, mara mlango ukafunguliwa na akaingia yule kijana aliekuwa nje anatazama usalama wao, “afande, tayari mzigo umeingia” alisema yule kijana, aliekuwa amesimama mlangoni, “apite ndani” alisema Kadumya, na yule jamaa akatoka nje, akipishana na koplo Cheleji aliekuwa amebeba begi moja kubwa mkononi mwake, “karibu kijana, vipi mzigo umekamilika” aliuliza Kadumya, huku anasimama na kumsogelea Cheleji, “kila kitu kipo humu kaka” alisema Cheleji, huku anaweka begi chini.
Kadumya akashika zip na kufungua kisha akazamisha mkononi ndani ya begi na kuibuka na pea moja ya sare za jeshi la polisi” safi sana, mpango unaenda kama tulivyopanga” alisema Kadumya huku akiachia tabasamu la ushindi, wenzake pia wanasogea na kuanza kukagua vilivyo kwenye begi, ambapo walikuta mavazi mapya kabisa ya jeshi la polisi pamoja na kofia za patrol cap, pia viatu aina ya buti mpya kabisa, “ok! kamueleze Ulenje kuwa atazame salio kwenye account yake” alisema Kadumya, wakati wanarudisha vile vifaa kwenye begi na koplo Cheleji akaondoka zake.
Hapo hapo Kadumya akapiga simu kwa bwana Chitopelah ilikutoa taarifa za maandilizi yao.*******
Naaam siku ya pili ilikuwa ngumu sana kwa doctor Veronica, ambae sasa alikuwa ametulia kwenye kiti chake ofisini, huku uso wake mzuri wakupendeza ukionekana wazi kunyongeshwa na mawazo fulani mazito, “itawezekanaje mtu ajiridhishe bila kuniingilia kimwili?” alijiuliza Veronica, ambae leo alikuwa na miadi na mpenzi wake John Joseph Daud, yani kijana JJD kwamba waende sehemu wakafanye mapenzi ya bila kuingiliana, mapenzi ya romance, “ndiyo nimeshawahi kusikia hilo swala, lakini nasikia ni ngumu sana na vijana wengi huishia kuingiliana kimwili, “aliwaza Doctor Veronica huku anachukuwa simu yake na kuanza kupekuwa namba ya mdogo wake wa kike ili amuulize kuhusu jambo hili, “mh! huyu nae hawezi kujua chochote, maana hajawahi kuwa na mpenzi, labda nimuulize mama” aliwaza Doctor Veronica, ambae leo hakuwa na zamu ya kukutana na wagonjwa, zaidi alishamaliza zamu yake ya kuwazungukia wagonjwa waliopumzishwa hodini.
Lakini wakati anataka kumpigia mama yake mara anasita kidogo, “mh! nikimuuliza mama lazima atajuwa ninachotaka kwenda kufanya, halafu atamuona J ni muhuni” aliwaza Veronica ambae hata yeye anafahamu fika kuwa kutokana na uzuri wa umbo na sura yake hakuna mwanaume anaweza kuvumilia muda wote huu bila hata kuchungulia chungu jikoni, “sasa hapa nafanyaje?” aliwaza sana Veronoca pasipo kupata majibu, alitafuta mtu wa kumpatia ushauri, lakini bado hakuweza kumpata mtu wa kumshirikisha jambo lake, hakika ilikuwa ngumu kwake na hakuwa na uwezo wa kuzungumzia kuhusu maswala ya ngono na mtu mwingine.
Lakini baada ya kuwaza kwa muda kidogo, akapata jibu, “ok…! ngoja ni mueleze mchoraji wangu” alisema Veronica huku anachukua simu yake mezani na kutafuta namba ya Mchoraji, katika upande wa whatsapp, namba ambayo hakuchelewa kuipata.*******
Yap saa nne na nusu kwa saa za afrika mashariki, king Elvis Mbogo, akiwa ofisini kwake amesha maliza baadhi ya kazi zake, sasa alikuwa anaptia baadhi ya nyaraka ambazo zilikuwa zinahitaji kuhakikiwa na kusainiwa kwaajili ya kufanyiwa utekelezaji, lakini wakati anapitia zile nyaraka ndipo akakumbuka jambo, “hebu subiri kwanza, alijisemea Elvis huku anachukuwa simu yake, ambayo huitumia kwa mawasiliano binafsi na kupiga kwa babu yake ambae ni mfalme wa zamani wa #mbogo_land.
Simu iliita kwa muda mfupi ikapokelewa, “Salam mfalme wa #mbogo_land, mimi ni mfalme pekee nilieona mjukuu wangu akiongoza” huyo alikuwa mfalme Eugen, ambae anapenda sana utani linapokuja swala kuongea na mjukuu wake, yeye ndie aliemruhusu Elvis kwenda Tanzania wakati huo kwaajili ya kutafuta mchumba wake, (ni hadithi nyingine ya Umekosea lakini tamu sehemu ya pili bado haijatoka) ambae kwa sasa alikuwa amefikisha miaka themanini na tisa, “salam king Eugen ni mjukuu wako kipenzi nimepiga kukusalimia” alisema Elvis, wakisindikiza salumu hizo kwa kicheko cha taratibu.
Ukweli ni kawaida yao kuwasiliana mara kwa mara, hasa Elvis anapohitaji ushaiuri wa kiuongozi, unaohusu taratibu za kimila na desturi, maana baba yake ambae alizaliwa na kupata makuzi nje ya himaya ya kifalme “haya niambie Elvis, unajuwa huishiwi maswali kila kukicha” alisema king Eugen, kwa sauti yake ya kizee na kumfanya Elvis ajitabasamulie kidogo, “babu kuna ujumbe uliuandika mwaka 1992, kwa mkono wako mwenyewe, nilitaka kujuwa ulikuwa umetoka kwa nani na ulikuwa na maana gani” alisema Elvis, kwa sauti tulivu, sauti ambayo babu yake katika uzee huu ndio anapenda sana kusikilizana nayo, “ujumbe gani huo Elvis, huishiwi maswali” alisema Eugen, huku anacheka ungesema wanazungumzia swala la utani.
Hapo Elvis akavuta kipande flani cha karatasi ambacho alinakilia maandishi yale ambayo hata jana usiku alikuwa anayakaguwa, kisha akaanza kuyasoma, “hicho ndicho kinachofanywa na watu unao waamini, lakini siwezi kuibadilisha akili yako kabla sijakamatwa na kuuwawa, wacha leo niikimbie nchi yangu ninayo ipenda, lakini nakuahidi, uwe wewe au kizazi chako, kitakumbuka maneno yangu, nikiweza nitaipigania nchi yangu, mimi au kizazi changu”alimaliza kusoma Elvis, “babu uliandika wewe hiyo unakumbuka alionge nani maneno hayo?” aliuliza Elvis, kwa sauti ile ile tulivu, lakini akijitahidi kurudisha kumbu kumbu za babu yake, ambae kwa umri huu, alikuwa amesahau mambo mengi sana na pia alikuwa mwepesi wa kusahau.
Hapo kikapita kimya kifupi, “babu bado upo na mimi?” aliuliza Elvis baada ya kuona kimya, “najaribu kukumbuka, lakini…. lakiniii… nime msahau… yes anaitwa Frank, huyo ni kanal Frank, alisema maneno hayo kabla ya kutoroka nchi” alisema babu kwa sauti yenye kuvuta kumbu kumbu ………….ENDELEA
Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa
jamii forums