Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THEMANINI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA TISA: Hapo kikapita kimya kifupi, “babu bado upo na mimi?” aliuliza Elvis baada ya kuona kimya, “najaribu kukumbuka, lakini…. lakiniii… nime msahau… yes anaitwa Frank, huyo ni kanal Frank, alisema maneno hayo kabla ya kutoroka nchi” alisema babu kwa sauti yenye kuvuta kumbu………….ENDELEA…

“kwanini alitoroka nchi?” aliuliza Elvis kwa sauti ile ile ya taratibu, “haaaa alikuwa ni muasi, ni kati ya askari waliokosa nidhamu, walikuwa wanaunda kikundi cha UMD, hivyo kabla hajakamatwa akafanikiwa kutoroka” alisema mfalme wa zamani Eugen.

Hapo Elvis akatulia kidogo, huku akirudia kuyasoma yale maandishi kwenye kipande cha karatasi, “hicho ndicho kinachofanywa na watu unao waamini” alinong’ona Elvis, akisoma kwenye karatasi, “babu kwani kuna watu ulikuwa unawaamini kipindi hicho ambao sasa sio wema kwako?” aliuliza Elvis, “lakini babu yake akakataa kwamba hakukuwa na mtu aliemgeuka, “hakuna muasi aliesalia serikalini kati yao ndio maana umeona mpaka leo hakuna hata dalili ya uasi” alisema Eugen, na hapo Elvis kengere ya tahadhari ikagonga kichwani mwake, “una uhakika babu..?” aliuliza Elvis, ambae kabla hajamaliza swali lake, akamuona mwanaume mmoja mwenye mwili wa kikamanda alievalia mavazi nadhifu ya kijeshi akiingia ndani ya ofisi yake na kutembea kwa mwendo wakikakamavu kuja usawa wa meza yake.

Kitu ambacho ni vyema ukifahamu juu ya chumba cha ofisi ya king Elvis, ukubwa wake ni sawa na nyumba kubwa ya vyumba sita vikubwa, yaani ni sawa na ukumbi mdogo wa mikutano, ambapo ndani yake kulikuwa na ukumbi mdogo wa mikutano wenye counter ya vinywaji na sehemu ya mgao wa chakula, pea kadhaa za makochi ya kisasa kwaajli ya watu kukaa wakati wa maongezi na mikutano, achana na meza yake ambayo ilikuwa upande wa mbele kabisa wa ukumbi ule, meza na kiti ambavyo nakshi zake kila mgeni alietembelea pale toka nje ya nchi awe raisi, mfalme au waziri toka nchi yoyote lazima afanye mambo yafuatayo.

Moja lazima angeuliza kama dhahabu na almasi zilizo nakshiwa kwenye meza na viti vile ni halisi au vitu vya mfano wake?, na hapo angejibiwa kuwa ni madini halisi na sio vya bandia, pili angeomba kuhakikisha uhalisia wake na baada ya kuthibitisha kuwa ni halisi basi angeomba kupiga picha na kiti pamoja na meza.

Tatu wangeenda kusimulia kwa familia zao na watu wao wakaribu wakisifia kile walichokiona kwa King Elvis, huku wakionyesha ushaidi wa picha na video walizochukuwa ndani ya ofisi hiyo, na hivyo ilifanywa na viongozi wengi wa nchi mbali mbali, tena mataifa makubwa sana duniani, vingozi ambao wengine wameshawishi watu wenye akili za panya wajaribu kuleta mapinduzi, ndani ya nchi ile, ili nchi ikichukuliwa na watu hao wenye kuyajali matumbo yao pekee, basi na wao wageuze #mbogo_Land, kuwa muembe wa njiani kujiokotea matunda wanavyo taka.

Yap! Elvis alimtazama askari yule wenye cheo cha major Gen aliekuwa amebeba mkoba mweusi mkono wake wakushoto, “babu nitakupigia baadae, “alisema Elvis na kukata simu, “mzee Sixmund, sijakuita ofisini kwangu na wala hujatoa taarifa ya kwamba utakuja, hivyo ni wazi kuwa kunajambo umekuja nalo, “alisema kingi Elvis huku akimtazama major General Sixmund, ambae ni mkuu wa kitengo cha uchunguzi wa siri jeshini.
Japo King Elvis, hupenda kukiuka taratibu za salamu, hasa anapokuwa pekee sehemu kama hii, lakini Sixmund hakufanya hivyo, maana kicheko cha simba sio cha kirafiki, pengine anacheka sababu amekuona wewe chakula chake, “salaam mtukufu mfalme” alisalimia Gen Sixmund, huku anavua kofia yake na kuiweka kifuani, huku anainamisha kichwa chini na mkono wa kushoto akiwa ameuweka mgongoni, “Salaaam general, unaweza kuketi na kuniambia kilicho kuleta, tena umekuja wakati muafaka” alisema King Elvis ambae sasa uso wake ulionyesha tabasamu, kwa sasa anaweza kupata jibu la swali lake.********

Wakati hayo yakiendelea #mbogo_land wakati huo nje ya jiji la Dar es salaam, kijana Deus, alikuwa sebuleni kwake, anatazama filamu ya za vichekesho zilizotengenezwa Uingeleza na marekani, hizo ndizo filamu zake anazo zipenda sana, huku mara kwa mara akiwa anatazama simu zake kama kuna ujumbe umeingia, na kuna wakati kwa mara ya kwanza alikuta ujumbe kwenye simu yake, “usisahau kuzingatia sheria yako ya muda, saa mbili na nusu, mama p saloon” ulikuwa ujumbe wa kusisitiza, ujumbe ambao kama sio kuwa haujatoka kwenye namba ya mzigo wa msumbiji, angejua kuwa ni yule yule aliempatia mzigo ule wa kwenda mpakani, tofauti ni namba, maana sehemu aliyoelekezwa ilikuwa ni ile ile aliochukulia mzigo sikuile, “kipaumbele changu ni kufuata sheria nilizo ziweka na nitakazo ziweka” alijibu Deus, kisha akaweka simu pembeni na kutupia macho yake kwenye TV kubwa.

Lakini kabla haja tazama hata kipande kimoja, mara akasikia ujumbe ukiingia kwenye simu yake ile ya mawasiliano ya kawaida, akachukuwa na kuitazama, ulikuwa ni ujumbe wa Whatsapp, akaitazama na kuona kuwa ilikuwa inatoka kwa Pacha wake, yani yule mwanamke anaewasilina nae siku zote bila kuonana nae, “mambo mchoraji wangu” ndivyo ulivyosema ujumbe huo, “poa Pacha niaje” alijibu Deus na kabla hajaweka simu pembeni ukaingia ujumbe mwingine, nao ulikuwa unatoka kwa Pacha, “poa lakini sio poa mchoraji wangu” ndivyo ilivyosema ile sms, ambayo ilimfanya Deus atabasamu kidogo.

Lakini kabla hajajibu au kuuliza kulikoni, tayari ujumbe mwingine ukaingia kwenye simu yake, “naomba unisaidie kuhusu jambo moja” ndivyo ulivyosema ujumbe huo, safari hii Deus aliandika ujumbe kwa haraka, “jambo gani hilo?” aliuliza Deus, kisha akatuma kwenda kwa Pacha, jumbe zikapishana, huu unaenda huu unaingia, “hivi inawezekana kweli mwanaume akaridhika kimapenzi bila kuingiliana kimwili?” aliuliza Pacha na hapo Deus akacheka kidogo, “mh! kuna mtu anaingizwa mtegoni hapa” alijisemea Deus, huku anaandika ujumbe, “kiukweli nasikia hivyo lakini nakushaurikama ni mpenzi wako na una lmpenda, basi unapoenda huko jiandae kwa lolote, maana nasikia wengi hujaribu hivyo na kujikuta wakifanya kweli” alisema Deus akimaliza na vikaragosi vya kucheka, “ukweli siwezi kujaribu, maana mimi sijawahi kufanya na nimepanga kufanya mara baada ya kuingia kwenye ndoa” alisema Pacha, na hapo akaanza kueleza jinsi mwanaume wake anaeitwa John, alivyo muomba leo wakafanye romance ili kila mmoja aridhike.

“kwahiyo pacha wewe ni bikira?” aliuliza Deus, kwa maana ya kushangaa na kutokuamini, “kwan huamini!, sio mimi tu, hata mdogo wangu anaenifuatia pia hajawahi kufanya hivyo” alijibu Pacha, “dah! ningebahatika kukutana na mdogo wako awe mke wangu” aliandika Deus na kutuma kwenda kwa Pacha, ambae jibu lake lilipokuja lilitanguliwa na vikaragosi vya kicheko, “unamzungumzia huyo usiewahi kuwasilina nae baada ya kunizungumzia mimi au sababu ni mzee, lakini miaka 25 bado sijazeeka bwana” alisema Pacha, akimalizia na vikaragosi vingine vya kicheko, Deus alitabasamu kidogo huku anaandika ujumbe, “wewe ni mchumba wa mtu tayari” alimaliza kwa kikaragosi kimoja cha kicheko, kisha akaituma kwenda kwa Pacha.

Haikupita hata sekunde ukaja ujumbe wenye vikaragosi vya kicheko na sekunde chache baadae ukaja ujumbe wenye maandishi, “inaweza kuwa bahati yako, pengine leo ndio mwisho wa kuwa nae, maana sitoenda kufanya anachokitaka” ndivyo ulivyosema ujumbe wa Pacha na hapo Deus akatabasamu kidogo, “mpuuzi huyu, yani anaanza kutangaza uchumba hapa hapa, wanawake bwana” alijisemea Deus huku anaandika ujumbe “kweli ingekuwa bahati yangu, lakini kuna mambo nikiyaweka sawa bahati yangu nitaikuta tu” aliandika Deus akitumia busara kumjibu Pacha wake, ambapo Pacha nae akajibu haraka, “na mimi na kuahidi kama nitaachana na huyu, basi sitokubali mwanaume mwingine mpaka nikutane na wewe” alisema hivyo akimaliza na kicheko cha katuni zake, Deus nae akarudisha kicheko akimaliza na maneno, “tunza ahadi yako”

Waliongea mawili matatu, mwisho kila mmoja akaaga kwa mwenzie na kupeana ahadi ya kuchat baadae mida ya kulala, hawakujuwa kuwa baadae kuna mazito zaidi yanakuja, hatariii ila tuendelee

Ile anaweka simu pembeni, Deus akasikia simu inatetemesha kochi alilokalia, ilikuwa ni ile simu ya kazi, mwanzo alidhania ni yule mteja wake wa Saloon, lakini alipoitazama namba ilikuwa ni namba mpya kabisa, akaipokea na kuiweka simu sikioni, “Dereva hapa nakusikiliza” alisema Deus kwa sauti tulivu, “hoooo bwana Dereva, kuna jukumu usiku wa leo, utapigiwa simu kwa maelekezo zaidi” ilisikika sauti ya kiume upande wa pili wa simu, “sawa ni wewe na muda wako” alisema Deus na kukata simu, kisa akaiweka pembeni ya kochi lake, “itakuwa vyema kama muda hautoingiliana” alisema Deus, huku anatazama TV iliyoko mbele yake.*******

Turudi mbogo land ofisini kwa mfalme, ambako tuna mkuta General Sixmund, aliekuwa anatoa taarifa mbele ya mfalme, “mtukufu mfalme, tetesi za uwepo wa kikundi cha UMD zimethibitishwa, ni baada ya kubainika kwa jitihada za waasisi wa kikundi hicho, ambao wengi wao hawaja bainika wazi wazi zaidi ya wachache ambao hapo mwanzo walitoroka jeshi letu” alisema general Sixmund kwa sauti ya chini, hakutaka wale warembo wa mauwa wala walinzi wa mfalme waliopo mle ndani wasikie.

“askari hao wanao ongozwa na kanal Kadumya ni luten Enock Kafulu na private Zaid Tambwe, wote ni watoro jeshini” alizidi kuelekeza Sixmund huku taarifa zile za kutisha zikiendelea kumshtua Elvis, “mtukufu mfalme, taarifa toka kwa wakala wetu aliepo China amenasa habari kuwa kuna silaha zinasafirishwa kuja nchini, lakini kwa uchunguzi wangu ni kwamba jeshi halijaagiza silaha mpya hivi karibuni” alisema General Sixmund na kumshangaza zaidi mfalme wake.

“kwahiyo baada ya kuwauwa wale waasi wa zamani walijiunda upya?” aliuliza King Elisnkwa namna ya mshangao, “hivyo ndivyo tuavyoweza kuhisi, lakini ukweli ni kwamba, uchunguzi tulioufanya wengi waliuwawa kimakosa” alisema General na hapo mfalme akakumbuka shutuma alizozipata babu yake enzi za utawala wake kwamba anafanya mauwaji holela ya watu wanao hisiwa kuwa ni waasi, kwa hiyo unataka kusema king Eugen, alifanya makosa kuondoa waasi katika serikali” aliuliza Elvis, kwa sauti iliyoanza kuwa na hasira. (Kwa haraka haraka ndugu msomaji akitajwa six mundi inakujia taswira ya muigizaji gani wa ngumi? …. ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THEMANINI NA MOJA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI: “kwahiyo baada ya kuwauwa wale waasi wa zamani, walijiunda upya?” aliuliza King Elis kwa namna ya mshangao, “hivyo ndivyo tuavyoweza kuhisi, lakini ukweli ni kwamba, uchunguzi tulioufanya wengi waliuwawa kimakosa” alisema General, na hapo mfalme akakumbuka shutuma alizozipata babu yake enzi za utawala wake, kwamba anafanya mauwaji holela ya watu wanao hisiwa kuwa ni waasi, kwa hiyo unataka kusema king Eugen, alifanya makosa kuondoa waasi katika serikali” aliuliza Elvis, kwa sauti iliyoanza kuwa na hasira. ………….ENDELEA…

General aliliona hilo, hivyo akaamua aliweke sawa kabisa, “hapana mtukufu mfalme, halikuwa kosa la Mfalme, ila ni baadhi ya watu walioshiriki operation hii” alisema Sixmund na hapo akili ya Elvis ikacheza kwa haraka sana, “hicho ndicho kinachofanywa na watu unao waamini” ukweli kuna mu aliliona ilo miaka mingi iliyopita, lakini kwa maelezo ya babu yake mtu huyo ni muasi na alishatoroka nchini kabla hajakamatwa, “Six, hujapata habari zozote za mmoja wa watoro alieitwa Frank ambae aliwahi kutoroka kabla ya kukamatwa wakati huo wa 1992?” aliuliza Elvis kwa sauti ya chini.

Na hapo Sixmund akaachia tabasamu ungesema alikua anasuburi swali lile kwa hamu kubwa, “hiyo ndiyo taarifa ambayo nilihitaji kukupatia mwishoni” alisema Sixmund na kumfanya Elvis, ajiweke vyema ili kusikiliza kwa umakini taarifa ya bwana Frank, “huyo anaitwa Frank Nyati, ambae alizuwa maswali mengi sana katika utoro wake” aliposikia jina Nyati, ndipo Elvis alipokumbuka jina hilo aliwahi kulisoma kwenye jarida la askari watoro, “yeye alikuwa ni askari aliejitolea sana kuliko askari wote kulinda uhai wa falme Eugen kipindi akiwa madarakani” alisema Six huku Elvis, akijaribu kukumbuka ni habari gani mpya aliipata inayo muhusu Nyati kwa siku za hivi karibuni.

Taarifa za uchunguzi, bwana Frank Nyati yupo Tanzania mkoa wa Ruvuma wilaya Songea, alisha achana na mambo ya kijeshi kabisa na hakuwahi kujihusisha na jambo lolote linalohusiana na nchi yetu, wala hajawahi kuonekana akiwa na muunganiko wowote na washirika wa UMD, yani wakina Kadumya na wenzake wakina Enock Kafulu” alieleza Sixmund, ambae hakuishia hapo, “ila sasa mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu, kumeibuka askari mmoja maarufu sana wa jeshi la ulinzi la Tanzania, anaesifika kwa uwezo wake mkubwa wakupambana kwa silaha na kwa mikon mitupu” alisema Sixmund huku anaweka na fungua mkoba wake na kutoa bahasha kubwa ya kaki, “huyo anaitwa Deus Frank Nyati, tumebaini kuwa ni mtoto wa bwana Nyati, ambae alikuwa na miaka miwili tu wakati wanaondoka nchini” alisema Six huku anatoa picha kwenye bahasha na kuiweka mezani mbele ya mfalme Elvis, ambae aliichukuwa na kuitazama.

Elvis alitumia dakika kadhaa kutazama ile picha ya Deus Frank Nyati, alieoneana akiwa amevalia mavazi ya kijeshi ya nchi ya Tanzania, akionyesha sura ya upole, “huyu amefukuzwa jeshi kutokana na nidhamu mbovu siyo?” aliuliza Elvis, huku macho yake yakiwa kwenye picha ya Deus, “ndiyo mtukufu mfalme, lakini habari zenye uhakika ni kwamba, hukumu ile ilikosolewana viongozi wote wa nchi na kufanya jeshi lianze kumtafuta Deus kwaajili ya kumrudisha jeshini, lakini ukweli inaonyesha kijana huyo hakuwa tayari kurudi jeshini, maana mpaka sasa hawajampata na hajulikani anafanya kazi gani” alisema major general Sixmund, huku king Elvis akiwa ametega sikio kusikiliza, huku kichwani mwake akiwa anatafakari juu ya taarifa hii nyeti ya kushtusha.

Naam hapo kikapita kimya kifupi, ni wazi wawili hawa kila mmoja alikuwa anajadili jambo hilo kichwani mwake na hoja kubwa ilikuwa ni nani ambae amesimama kati ya serikali na kikundi hicho cha waasi, “Six, kwa kauli ya Frank Nyati kwenda kwa King Eugen, ni wazi kuwa kuna jambo analifahamu kuhusu usalama wa nchi, ambalo sio vyombo vya usalama tu, mimi pia silifahamu, maana amesema ipo siku atathibitisha iwe yeye au kizazi chake” alisema King Elvis, kwa sauti yenye kuonyesha kuwa, alikuwa na uhakika na anachokisema, “ni kweli mfalme, maana hata kuondoka kwake nchini kulitia mashaka kwa kila mmoja” alisema Major General Sixmund.

Naam hapo ni kama mfalme akapata wazo fulani, “Six, nahitaji majibu toka kwa Frank Nyati, iwe kwa njia ya lazima au maelewano, cha msingi apatikane na atoemajibu” alisema Mfalme Elvis wa #mbogo_land, “mfalme nina wasi wasi juu Deus Nyati, mtoto wa Frank Nyati, ambae sasa yupo nje ya jeshi la tanzania, kwanini amekataa kurudi jeshini na hajulikani sehemu alipo mpaka sasa?” aliuliza major Sixmund na hapo akawa amemchokoza mfalme, ambae alimtolea jicho kama anampa onyo, sasa ukiangalia uso wa Elvis, ulivyokaa kiujana ujana na sura ya bwana Sixmundi, ambae ni mtu mzima, “kwahiyo unataka nikujibu kuwa atakuwa amechukuliwa na waasi? sasa mimi ndiyo unaanza kunihoji” hapo Sixmund aliinamisha kishwa na kuomba msamaha, “samahani mfalme nikama nilikuwa naeleza wasi wasi wangu, nilitaka nitoe ombi la pili la kuhakikisha tunafahamu kazi za sasa za Deus Frank Nyati na kumzuia asijiunge na kikundi hicho haramu” alisema Sixmund kwa sauti ya kuomboleza huku kichwani anawaza "ndio shida ya kuwapa madaraka makubwa vijana hayachelewi kuwalevya".

Naam, hapo mfalme mwenye usikivu na busara za kiuongozi, akashusha pumzi zake kwa nnguvu, akiashiria kupoa toka kwenye ghadhab, “nivyema kama ukimaliza maoni na ushauri wote kabla hujaondoka na kwenda kuanza kuandaa mpango kazi“ alisema Elivs akijitahidi kujionyesha kuwa alikuwa amechukia, lakini moyoni alikuwa anatabasamu kwa kuona mtendaji wake huyu, jinsi anavyo mchukulia kwa uzito wa kipekee, “mtukufu mfalme ushauri wangu ni kwamba kiundwe kikundi cha askari wa uchunguzi wa kimapigano wenye taaluma ya juu ya mapigano ya nchi kavu, waombewe kibali cha kufanya kazi Tanzania, kwaajili ya kuchunguza na kufanikisha kumpata Frank Nyati na kijana wake” alieleza Six.

Six alieleza sababu ya kutumia askari hao kwenda Tanzania ni kwamba, Frank na Deus taarifa zao zinaeleza ni askari wenye mafunzo ya hali ya juu, yani ni watu hatari sana, “hivyo tunahitaji kutumia nguvu kuwapata, endapo watashindwa kutoa ushirikiano kwa majibu tunayo yahitajaji”aliseme Sixmund na kuweka kituo kidogo kuona kama mfalme atakuwa na la kuongea.

Mfalme akampa ishara ya kuwa aendelee, kwa kukubaliana nae kwa kichwa, “maoni yangu mfalme kazi ambayo napendekeza ianze mara moja leo hii, sababu adui zetu wapo mbioni kuzipata silaha, iwe ya siri kubwa miongoni mwa viongizi na wafuasi wa ulinzi na usalama” alisema Six mund, akiwa amemaliza kutoa maoni yake.

Ukweli mfalme alikubaliana moja kwa moja na General Sixmund, “lakini sasa kikundi hicho mkabidhi kamanda ambae una muamini na una uhakika hawezi kuwa mmoja wao” alisema Elvis, ambae pia alisema kuwa yeye kwa wakati wake atajaribu kudodosa kwa watu mbali mbali waliowahi kushiriki operation ile yakuondoa waasi ndani ya serikali kuona kama atambaini kiongozi wa waasi, ambae adhabu yake ni kuchomwa kwenye chungu cha chuma, hiyo ni sheria ambayo iliwekwa miaka mia mbili hamsini iliyopita, zama za mfalme Elisha Mbogo wa kwanza wakati wa uvamizi wa majeshi ya wangoni kusini mwa Tanzania.

Baada ya maongezi kuisha, Sixmund akaondoka zake na kwenda kuandaa kikundi kitacho kwenda Tanzania, huku akimuacha king Elvis wa kwanza, anawasiliana na ubalozi wake nchini Tanzania kwaajili ya maombi ya kibali cha kuwapokea askari watakao teuliwa kwenda nchini humo kwa kazi maalumu ya kumnasa baba na mtoto wake.*******

Naam, saa nane mchana Deus akiwa bado yupo sebuleni kwake anaendelea kutazama filamu za vichekesho toka nchi za magharibi, aliendelea kupokea na kujibu ujumbe toka kwa mwanamke aliemuita Pacha, mwanamke ambae hakuwahi kumuona kwa macho yake wala kuomba picha yake, mwanamke ambae leo alikuwa anaeleza wasi wasi wake juu ya kile ambacho mpenzi wake JJ ameomba wakakifanye usiku wa leo.

“yaani mchoraji wangu, kama akijaribu kufanya kiukweli nitamuacha” alisema pacha wakati fulani, “kwani mnasubiri nini kuoana kama hamuwezi kufanya kabla ya ndoa?” aliuliza Deus, kwa ujumbe wa maandishi, “bado tupo kwenye mipango, tutafunga tu” alijibu Pacha na hapo Deus akatumavikaragosi vya kicheko, “unacheka nini sasa?” aliuliza Pacha akiweka kikaragosi cha kununa, “nimefurahia ubwabwa, najua lazima utanialika pacha” aliandika Deus, ambae wakati anatuma ujumbe huo kwenda kwa Pacha, mara akasikia smu yake ya kazi inaita, akaichukuwa na kutazama mpigaji, ambae alikuwa ni mteja namba mbili wa siku ile.

Deus akajiweka sawa na kupokea simu, “nakusikiliza” alisema Deus akiwa ameweka simu sikioni, “nadhani unanikumbuka, tuliwasiliana mapema leo asubuhi” ilisikika sauti nzito yenye mikwaruzo, “situnzi kumbu kumbu za mipango isiyo kamilika, ni vyema sasa ukija na mpango kamili”alisema Deus kwa sauti yake tulivu ya upole.

Hapo kikasikika kicheko kizito cha dharau, “napenda unavyo jiamini kijana, ila napenda uwe hivyo mpaka mwisho wa kazi yetu” alisema yule jamaa ambae alionyesha kuwa mwenye dharau kubwa, wakati huo Deus alikuwa ana tazama simu yake ambayo ilikuwa inapokea ujumbe, “usijari boss, sasa unaweza kueleza mpango” alisema Deus, huku anachukuwa simu yake nyingine na kuufungua ule ujumbe uliotoka kwa Pacha, uliosema, “mchoraji wangu utaweza kumuona mrembo wako anabebwa na mtu mwingine au ndiyo utaanzisha fujo” ujumbe ulimfanya Deus atabasamu kidogo huku moyoni akijisemea “mrembo unamjuwa wewe”

Wakati Deus anaandika ujumbe, masiko yake haya kuacha kumsikiliza mteja wake, “ni vyema ikiwa hivyo, sasa mpango ni kwamba, nne kamili usiku, eneo mbezi mwisho, barabara ya zamani ya morogoro, mita mia tatu toka PTSH, yani, Private Tresure Saving House, abiria mmoja mwenye begi” ilieleza ile sauti nzito yenye mikwaruzo, huku Deus aliekuwa anamsikiliza, huku anaandika ujumbe kwenda kwa pacha wake, “usijari Pacha, ila nina uhakika kuwa jamaa atashindwa tu, na wewe utakuja kwangu kama ulivyoahidi” aliandika Deus akimaliza na karagosi cha kicheko, “Dereva nakusikiliza gharama yako” ilisikika ile sauti nzito yenye mikwaruzo.

Hapo Deus ambae alishaiona dharau ya mteja wake huyo akatabasamu kidogo, “siwezi kutaja gharama sababu bado hujamaliza kueleza, sijasikia point B, sijasikia usalama ni juu ya nani” alisema Deus ambae wakati huo huo akaona ujumbe unaingia, ambao ulikuwa ni vikaragosi vya kicheko, ujumbe ambao Deus hakuhangaika nao, ndio kwanza akaweka simu pembeni na kubakia na ile moja.

Kwanza yule jamaa aliachia kicheko fulani hafifu chenye uzani wa dharau, kisha akasema “hoooo! kumbe upo makini sana bwana mdogo” alisema yule jamaa kwa sauti ambayo ungesema jamaa anaongea na mtu ambae ni mdogo sana kwake, “ipo hivi dogo, usalama wa abiria ni juu yako usalama wa mzigo ni juu yako, cha msingi tunacho hitaji mzigo ufike salama, taja malipo yako” ilisikika sauti upande wa pili wa simu, hapo Deus akatulia sekunde chache akifikiria uzito wa kazi ile ambayo inafanyika mita chache toka nyumba ya uhifadhi hazina binafsi, abiria ni mwanamke mwenye begi na usalama ni juu yake yani kwa mwanamke na hilo begi, kwahiyo hivyo vyote ni muhimu kwake, “millioni mia mbili” alisema Deus, kwa sauti tulivu. ……….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THEMANINI NA MBILI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA MOJA: “ipo hivi dogo, usalama wa abiria ni juu yako usalama wa mzigo ni juu yako, cha msingi tunacho hitaji mzigo ufike salama, taja malipo yako” ilisikika sauti upande wapili wa simu, hapo Deus akatulia sekunde chache akifikiria uzito wa kazi ile, ambayo inafanyika mita chache toka nyumba ya uhifadhi hazina binafsi, abiria ni mwanamke mwenye begi na usalama ni juu yake yani kwa mwanamke na hilo begi, kwahiyo hivyo vyote ni muhimu kwake, “millioni mia mbili” alisema Deus, kwa sauti tulivu. ……….ENDELEA…


Sidhani kama kulikuwa na sababu ya huyu jamaa kucheka kicheko chake cha dharau, baada ya kusikia jibu la Deus, maana alicheka kidogo, kabla ya kujibu, “nitakulipa mara mbili, vipi kuna lolote jingine?” aliuliza huyu jamaa mwenye dharau, “jingine ni juu ya sheria zangu boss, kwanza sihitaji kujua jina la mtu yoyote, pili malipo ni fedha tasilimu sio benk wala mkopo, tatu sihitaji matumizi ya bunduki kwenye gari langu wala kati kati ya mpango, namba nne hakuna mpango ndani ya mpango, tunamaliza kazi kisha tuna anza kazi nyingine kama ipo, namba saba, nidhamu kwa kila mmoja na sheria namba nane, zingatia muda” alimaliza Deus, na hapo yule jamaa upande wapili akatoa sheria yake, mimi ninasheria moja bwana mdogo, nayo usije ukafungua mzigo” alisema yule jamaa kwa msisitizo.


Lakini hapo akakutana na jibu la haraka toka kwa Deus, “usijali hiyo ni sheria yangu ya kumi, hata kama ni asali sitotia hata ncha ya kidole, nahitaji uaminifu ndio maana ninakuwa muaminifu” alisema Deus, kabla hawajakati simu.


Hapo Deus akaweka simu pembeni na kuchukua simu yake ya kawaida, ambayo tayari ilikuwa na jumbe mbili, jumbe zote zikitoka kwa Veronica, “yaani natamani nikutane na wewe, unamambo makubwa sana mchoraji wangu” huo ulikuwa ujumbe wa kwanza, na ujumbe wapili ulikuwa ni “sasa mchoraji wangu, nitakuchek baadae, wacha mimi nijiande nielekee nyumbani, maana ndio mida ya kutoka chuo sasa” alisema Pacha, na Deus hakujibu kitu, baada yake akajisemea mweyewe, “nenda ukashangazwe huko, na kitacho kutokea sijui kama utaweza kusimulia” alijisemea Deus, ambae hakuishia hapo, “nani alikuambia kuna mapenzi ya kupapasana tu” *******


Naam saa kumi kasoro, King Elvis, akiwa ofisini kwake, anaendelea na kazi zake huku anapekuwa jarida lililofungwa la mwaka 1992/92, lililohusu operation ya kuondoa waasia akitazama majina ya washukiwa ambao kwa namna moja au nyingine waliweza kutoroka nchini, ndipo alipoliona jina la James Kervin, tajiri mkubwa aliepo Tanzania, “hivi huyu mzee hawezi kuwa ndie anaefadhiri hawa washenzi?” alijiuliza mfalme Elvis, huku kashika kofia yake ya kifalme iliyotengenezwa kwa dhahabu halisi na kunakshiwa kwa almas halisi.


“Hapana huyu nae ni lazima achunguzwe” alijisemea Elvis, huku ana chukuwa simu yake ya mezani yenye kutengenezwa kwa dhahabu, huku vile vitufe vya namba vikiwa ni almas pia, akaanza bonyeza namba kadhaa na kuweka mkonga sikioni kusikiliza simu ilivyokuwa inaita, bahati nzuri haikuchelewa kupokelewa, “salaam mtukufu mfalme wa Mbogo land” ilisikika salamu toka upande wa pili wa simu, “salaam General, nimekupigia ilinikueleze jambo” alisema mfalme Elvis na kwa sauti tulivu kabisa alisema king Elvis, “nipo tayari kusikiliza chochote utakachoeleza mtukufu” alijibu general Sixmund kwa sauti ya kinyenyekevu, “nahitaji mumfuatilie James Kervin, yule mfanyabiashara aliekimbia mwaka 92, pengine anafadhiri kikundi hiki cha waasi” alisema mfalme Elvis.


Na kabla ya kukata simu, General Sixmund akawahi, “mtukufu mfalme pia naomba nitumie muda huu, kuwakilisha taarifa ya maandalizi ya kikundi na safari ya Tanzania” alisema General kwa sauti ile ile yenye unyenyekevu, “hooo sawa, tena nimeshaongea na balozi ambae aliwakilisha ombi langu la siri na limekubalika” alisema King Elvis na hapo General, akaanza kueleza alipofikia kwenye mpango wake wa kuandaa askari wa kwenda Tanzania.


Ilikuwa hivi, General Sixmund alifanikiwa kuandaa askari kumi na sita, ikiwa ni troop moja ya askari wa uchunguzi wa kivita, AR kwa maana ya Amoured Recconices, wenye mafunzo mazuri ya hali ya juu ya kijeshi, katika mbinu za medani, miongoni mwao alikuwepo captain Amos Makey, na sajent Girbart Ngasa.


Pia kulikuwa na koplo wawili ambao ni Amadeus Peter na Side Nyenza, wote wanne kila mmoja akiwa na askari watatu, kwa maana ya timu, “sawa wataondoka nchini kwa jukumu bandia, nalo ni mafunzo ya dharura” alisema King Elvis, ambae pia alisema ataagiza wizara iandae mpango wa safari na watu waondoke usiku ule ule kuelekea Tanzania, ambapo watatuwa kwenye kiwanja cha ndege cha songea, lengo la kudanganya jukumu ni kuepuka usaliti katika jukumu lililopo mbele yao.********


Yap! saa kumi jioni, mwana dada Veronica, alikuwa nyumbani kwao kinyerezi amejifungia chumbani kwake yupo juu ya kitanda, simu yake mkononi anacharti na mpenzi wake JJ, yani John Joseph, huku amevalia kijigauni fulani chepesi sana, kijigauni ambacho ukaaji wake kwenye mwili huu wenye hips mchomozo, kifua mchongoma,makalio msuso, kingemfanya mtu kusahau majukumu yake, pengine hata risasi kukataa kutoka kwenye mtutu kwa kushindwa kuuwa mtoto mzuri kama huyu, “lakini John, itawezekana kweli, maana watu wanasema huwa haiwezekani” alinadika Vero na kutuma kwenda kwa JJ.


Ujumbe haukukaa sana ukajibiwa, “achana na watu Vero, nisikilize mimi, ikishindikana si tunaacha tu” alisisitiza JJ, ila hata mimi naungana na Deus kwamba haiwezekani, Veronica ajiandae kutoa andazi, maana sio kwa muonekano huu, ambao nauona hapa kitandani, “Veronica James akaachia tabasamu kidogo na kuzidi kuwa mzuri, maana vile vijishimo vya mashavuni vikaonekana, wakati huo vidole vyake vizuri vinavyo weza hata kumaliza haja ya mfungwa, vikigusa gusa simu yake kuandika ujumbe, “sawa nitakuja, lakini tukubaliane kitu” ndivyo ujumbe ulivyo sema, ujumbe mbao mara baada ya kumaliza kuuandika akautuma kwenda kwa JJ, ambae pia hakuchelewa kujibu, “poa nakusikiliza” alijibu JJ.


Hapo haraka sana Veronica akaanza kutoa masharti yake, “kwanza kabisa hakuna kuvua nguo zote, pili hakuna kuingizana vidole, tatu mwisho kushikana kwenye maziwa tu, hakuna kushikana sehemu za siri” duh! sijuwi kama JJ, hakununa au kucheka, maana sijui ingekuwaje.


Lakini kwa wewe ambae umejitabiria jibu lako kama ungekuwa John, naamini umekosea, “wala usiwe na wasi wasi, nitafanya kile unachosema, sitaki kukukwaza” hilo ndilo jibu la kijana ambae tunamfahamu kama John Joseph Daud, mchumba wa mschana mrembo Veronica James, mtoto wa tajiri mmoja mkubwa sana mwenye asili ya nchi ya #mbogo_land, anaeishi Tanzania kama mkimbizi wa kisiasa, anaeshustumiwa kwa kufadhiri kikundi cha waasi wa UMD, wanao pambana na serikali ya nchi ya #mbogo_land.


Kwajibu hilo Verinoca aliachia tabasamu pana sana, huku anapiga picha zile sms alizotumiana na JJ mara ya mwisho na kutuma kwenda kwa mchoraji wake, akisindikiza na ujumbe, “umeona mchoraji, mume mwenzio amekubali masharti, wewe sijui kama ungeweza” akimalizia kwa vikaragosi vya kicheko cha furaha.


Hii ilichukuwa muda mrefu kidogo kujibiwa, kiasi kwamba Veronica akaanza kuhisi kuwa mchoraji wake amekosa amani kwa kitendo cha yeye kukubari kwenda kupapasana na mchumba wake JJ, “hata akikasirika shauri zake kwani yeye ni nani wangu” alijisemea Veronica huku anaweka simu pembeni na kuinuka toka kitandani.


Kaenda moja kwa moja kwenye kabati la nguo la ukutani, akafungua mlango na kutufanya tuweze kuona nguo nzuri za kisasa zilizopangwa ungesema ni dukani, hasa kwa uwingi wake na utofauti wa rangi, akachagua gauni moja zuri refu lenye rangi ya blue na mauwa ya samawati na nyekundu, akachukuwa viatu vyekundu na vyenye visigino virefu akajaribu kupatanisha rangi, akaona inafaa, kisha akarudisha kila kitu sehemu yake na kuelekea kitandani, ambako alikuta ujumbe umeingia kwenye simu.


Veronica akaufungua haraka na kuusoma, “mh! sina hakika kama unachokifikiria ni kitu cha kweli, nakushauri ujiandae kwa mabadiliko ya ratiba” ulikuwa ujumbe toka kwa mchoraji wake, ambao Veronica aliusoma huku akicheka kwa sauti ya chini, “anaona wivu hata bado hajaniona, sasa akiniona si atachanganyikiwa” alijisemea Veronika huku anaandika ujumbe, “usiwe na shaka juu ya hilo” akautuma kwa mchoraji, kisha akaandika nyingine, “wacha nijiandae nitakupa matokeo baadae” kisha akautuma kwa Mchoraji, na kuirushia simu kitandani, kisha akasaula nguo zote za mwilini mwake na kuingia bafuni.******


Naaaam saa kumi na mbili na robo za jioni, mbezi msakuzi ndani ya nyumba moja kubwa ambayo pengine ilijengwa kwa minajili ya ukumbi fulani au bar kubwa, lakini bado ilikuwa haijaanza kutumika, nje ya ukumbi huo tunaona magari sita, aina ya Land Rover pumer, mapya kabisa, yalikuwa yamejipanga huku kila moja lilikuwa na dereva ndani yake.


Tunapoingia ndani kabisa ya jengo lile kubwa, ambalo ndani yake lina viti vichache na mabaki ya vitu vilivyotumika kwenye ujenzi wa ukumbi ule, mkubwa ulioambatana na majengo mengine madogo madogo, tunawakuta wanaume kadhaa mle ndani wenye kufikia idadi ya watu thelathini pamoja na vingozi wao wanne waliokuwa wamesimama mbele yao.


Ukiachilia viongozi wao wanne, ambao tunapo watazama tuna muona Kadumya, Tambwe, Mbwambo, na Enock Kafulu, watu hawa waliogawana katika makundi manne ambayo ungeyatambua kwa utofauti wa mavazi yao.


Wakati kundi la kwanza, lenye watu kumi wakiwa wamevalia suruali nyeusi na zenye kufanana umbo na sare za majeshi ya ulinzi, chini walivalia viatu vyeusi vyenye shingo ndefu, yani buti za kijeshi na juu walivalia tishert nyeusi, kati yao walikuwa wenye muonekano wa watu waishio porini.


Mfano walikuwepo wenye ndevu nyingi, zilizokosa matunzo mazuri, pia walikuwepo wenye nywele ndefu zilizo jisokota hovyo hovyo, pia wapo walionyoa vipara tofauti na wenzao sita, wa kundi la pili, wao valia suit nyeusi na viatu kama vya wenzao, yani buti za kijeshi, hao walionekan kuwa smart kidogo, kundi la tatu, lilikuwa na watu wanne, tu, ambao walikuwa wamevalia nguo za kawaida, yani suruali ya jinsi na raba na tishert, huku kundi la nne likiwa ni kundi la vijana kumi nadhifu waliovalia sare za jeshi la polisi, hakika walikuwa polisi, maana ukiachilia uvaji wao, pia hata unadhifu wao katika unyoaji wa nywele za kichwani hata ndevu pia, iliwatambulisha kuwa ni askari wa jeshi la polisi. ……….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THEMANINI NA TATU
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA MBILI: tofauti na wenzao sita wa kundi la pili, walio walivalia suit nyeusi na viatu kama vya wenzao, yani buti za kijeshi, hao walionekan kuwa smart kidogo, kundi la tatu, lilikuwa na watu wanne, tu, ambao walikuwa wamevalia nguo za kawaida, yani suruali ya jinsi na raba na tishert huku kundi la nne likiwa ni kundi la vijana kumi nadhifu waliovalia sare za jeshi la polisi, hakika walikuwa polisi, maana ukiachilia uvaaji wao, pia hata unadhifu wao katika unyoaji wa nywele za kichwani hata ndevu pia, iliwatambulisha kuwa ni askari wa jeshi la polisi. ……….ENDELEA…


Viongozi wao pia, watatu kati yao walivalia suit, huku mmoja tu ambae ni Enock Kafulu alikuwa amevalia suruali ya kitambaa na shati nadhifu jeupe na viatu vyeusi, ungesema anatoka au anaenda kanisani, “nadhani kila mmoja wetu ameshaelewa nini anatakiwa kufanya” alisema Kadumya kwa sauti kavu nzkto yenye uzani mkubwa wa amri, “ndiyo mkuu” wale vijana walipaza sauti kubwa kwa pamoja, “hatutaki mchezo, hili ni tukio muhimu sana, tunajukumu ambalo litatuwezesha kuanza safari ya kuingia golden house” alisema Kadumya kwa sauti ile ile yenye msisitizo, “usiku wa leo hatukaki makosa zaidi, yeyote ambae atahusika au kusababisha kosa lolote ambalo litavuruga mipango hii mikubwa ya usiku wa leo atauwawa bila huruma yoyote” alisema Kadumya ambae usingewaza kama kuna wakati huwa anacheka au kutabasamu kwa jinsi alivyokunja sura yake, “cha msigi kila mmoja wetu azingatie anapambana kwaajili gani, kumbuka kuhusu maisha yako, kumbuka kuhusu familia yako, kuhusukila kitu utakachokipata baada ya kuwa mmoja kati ya watu wakubwa pale #mbogo_land” alisema Kadumya na wale vijana wote wakashangilia kwa furaha kubwa.


Baada ya hapo Kadumya akawatazama wenzake, yani wakina Enock kafulu, “jamani naona muda unasogea cha msingi, vijana wapatiwe bunduki, na tutawanyike, kila mmoja aende sehemu anayotakiwa kuwepo” alisema Kadumya, ambae pia alimtazama Enock Kafulu, “Enok mtasubiri simu yangu kukamilsha mpango wa pili endapo mpango wa kwanza utashindikana” alisema Kadumya na baada ya hapo vijana wawili wawili wakasogeza masanduku manne ya mbao na kuyafungua.


Naam yanafunguliwa mabox matatu kati ya yale manne, ndani tunaona silaha nyingi aina ya AK-47, pamoja na SMG, kikawaida bunduk hizi zinafanana kiasi, sababu zimeundwa kwa mfano mmoja, lakini tofauti ipo ndogo sana, wakati AK-47 iliyotengenezwa mwaka 1947, ilitengenezwa Urusi, miaka kumi kabla SMG haijatengenezwa burgaria china sehemu na nyingenezo duniani, watumiaji husema kuwa kuna utofauti kwenye bora wa ulengaji na upigaji wa malengo.


Hapo sasa, AK-47, walipatiwa wale vijana kumi, waliovalia suruali nyeusi na tishert nyeusi huku SMG wakipatiwa wale waliovalia sare za jeshi la polisi na wale waliovalia nguo za kawaida yani mavazi ya kiraia.


Box moja la mwisho lilikuwa na silaha aina ya HKGA, bunduki hatari yenye uwezo mkubwa tofauti na mzingo wa risasi yake, yenye mzingo wa mm 5.5, bunduki ambayo ilitumika na seal team kumkillr Osam Bin Laden mwaka 2011, hii ni HECKLER &KOCH G95 GERMANY ASSAULT RIFLE, ambazo idadi yake zilikuwa saba tu, ambazo walichukua wale vijana sita wenye kuvaa suit na moja akaichukuwa Kadumya, “mwanzo wakati wa msako wa dhahabu tulihisi kuwa Dereva alikuwa ni mwanamke, lakini nimeongea nae mara mbili ni mwanaume bwana” alisema Kadumya na Mbwambo akadakia, “huyu nadhani ndie aliepandia hapo kiluvya na mwanamke ndie aliekimbia na dhahabu” alisema bwana Ramadhani mbwambo, “lakini hiyo haimwondoi kwenye kifo, maana na yeye alihusika kwenye kutorosha dhahabu, pia na leo atakuwa ameona tukio zima” safari hii alikuwa ni Enock Kafulu ndie alieleza hayo.


“Ok! hakuna kitakacho badilika, sehemu ya kukutana ni hapa hapa kwa kila tukio na kwa kila matokeo” alisema Kadumya, huku anatoa ishara kwa kundi lake kwamba wamfuate, na hapo wale vijana Sita wakamfuata, “ok! mzee mbwambo, nadhani sasa ni wakati wa kukumbushana mpango, itakuwa vyema kila mmoja akasikia jukumu lake, kikubwa ni kuzingatia muda, maana dereva ameweka muda katika sheria zake” alisema Enock Kafulu, ambae kimadaraka katika kundi lililopo hapa dar es salaam yeye anafuatia toka kwa Kadumya.********


Naam, mida hii ya saa kumi na mbili na dakika arobaini na tano jioni, maeneo ya mbezi beach mtaa wa Isawerwa, jilani na Masana Hospital, anaonekana mwana dada Emmy akitoka nje ya nyumba yake kubwa ya kifahari. aliependeza kwa gauni lake ndefu jekundu lililomkaa vyema mwili mwake na kutoa luksa kwa macho ya watazamaji kuona jinsi umbo mwanana la mama P, lilivyojaa ndani ya gauni lile.


Emmy anatoka nje ya mlango, nyuma yake anafuatia mschana wake wakazi aliebeba begi dogo lenye kujaa vyema, Emmy anapiga hatua kadhaa za kuchagua kama vile anaogopa kukanyaga kitu fulani kwa viatu vyake vya mikanda vyenye visigino virefu na mkoba wake kwapani, kisha anasimama na kumtazama yule binti wa kazi, “usisahau, mtu yoyote akipiga simu kuuliza mwambie nimeenda morogoro nina dharura” aliongea Emmy kwa msisitizo, “sawa mama” aliitikia yule mschana, kisha akaendelea kutembea taratibu kwa mwendo ule ule, huku dada wakazi akimfuata nyuma, macho yake yakimtazama boss wake ambae kiukweli ukiachana na kupendeza kwa mavazi yake na lile umbo lake, lakini pia alikuwa amependeza kwa mtindo wa nywele zake na vipodose vya usoni mwake vilivyo zidisha uzuri wake mara dufu, “yani ningekuwa kama dada, mbona wangenikoma” alijisemea dada kimoyo moyo, huku anamtazama dada yake ambae alionekana wazi kuwa anaenda kwenye shughuli maalumu.


Safari yao inaishia ubavuni mwa Toyota wishi jeusi, tayari mama P akiwa ameshafungua kifungo cha milango ya gari kwa kutumia kiongozea mbali, (remote control) “nitarudi kesho mapema sana” alisema tena mama P, huku anafungua mlango wa upande wa dereva na kuingia ndani ya gari, “sawa dada” aliitikia dada wa kazi huku na yeye akifungua mlango wa mbele wa upande wa abiria na kuweka begi, kisha akafunga mlango.


Naaam, Emmy anawasha gari ambalo linakubari kuwaka mara moja, kisha gari hilo lenye kunukia manukato mazuri, likiwa linaendelea kuunguruma, Emmy anatoa simu yake kwenye mkoba wake na kubofya namba 04472574, kisha akaweka sikioni, na kuisikia ikianza kuita, “hallow habari ya saa hizi” ilisikika sauti tulivu toka upande wa pili wa simu, “poa tu, mambo anko Dereva” alisalimia mama P kwa sauti moja laini yenye kuvutia na kuhamasisha, “safi tu, na kusikiliza boss” ilisema ile sauti tulivu, toka upande wa pili, “mi nilikuwa na kukumbusha, maana muda unakaribia” alisema Emmy kwa sauti fulani kama ya kaschana kadogo kanako kumbushia ahadi fulani, “usijari boss, muda ndio ni sheria yangu namba nane, huwasiendi tofauti na sheria zangu” ilisikika ile sauti tulivu, ambayo ilionyesha wazi kuwa muongeaji alikuwa sehemu tulivu.


Hapo mwana mama Emmy, ambae uzuri wake na umri wake havikuendana kabisa kwa kuonekana kama binti mdogo, akaachia tabasamu laini, “hooo kumbe unasheria zako, hebu nitajie nizijue|” alisema Emmy huku ana hamisha simu toka mkono wa kushoto na kupeleka mkono wa kulia na kubandika kwenye sikio la kulia, akiacha mkono wa kushoto ukamate kirungu cha gia huku akibonyeza kidude kwenye kirungu sambamba na kukanyaga brake kwa mguu wa kushoto na kuisokomeza gia ile kwenye sehemu ya D. “tutatumia sheria namba 1,2,3,4 na 8” ilisikika sauti ile tulivu.


Huku gari likiwa linatiririka taratibu kuelekea upande wa barabara kuu iendayo bagamoyo, “hoooo namba moja ni ipi?” aliuliza Emmy, huku anatembeza gari taratibu kulikwepa Toyota Sienta la silva lililokuwa limesimama mita kama hamsini toka nyumbani kwake na kutokana na giza lililokuwepo ndani ya gari lile lililokuwa limesimama pembeni ya barabara hii hakuweza kuwaona waliopo ndani yake, zaidi viming’ao vyekundu zaidi ya mmoja mfano wa mioto ya wavuta sigara, “namba moja ni hakuna majina, mbili malipo ni mkononi, hakuna mkopo, tatu hakunabunduki na nne hakuna mpango juu ya mpango, nane kama tulivyo ongea, kujali muda” ilisikika ile sauti tulivu ya dereva, “sawa bwana Dereva, chumba namba nane, ghorofa ya nne” alisema Emmy kwa sauti tamu sana, kisha akakata simu.


Wakati huu Emmy alikuwa amesimamisha gari kwenye maungio ya barabara ya bagamoyo, akisubiri magari ya pungue ili aweze kuingiza gari barabara kuu, lakini wakati huo huo Emmy akapiga tena simu kwenda kwa mtu mwingine, ambapo simu iliita kwa muda mfupi na kupokelewa, “Doris, hakikisha hutoki hapo saloon, kuna mtu anakuja kuchukuwa ule mzigo” alisema Emmy huku anatazama kwenye kioo cha upande, wake cha kutazamia nyuma, yani sight mirror, ambapo aliweza kuona lile gari moja lina kuja taratibu nyuma yake, lilikuwa ni lile Toyota Sienta alilolipita hapo nyuma, Lakini akulijari “sawa dada” ilisikika sauti ya kike upande wapili wa simu, Emmy akakata simu na kuondoa gari kuingia barabarani huku lile gari nalo likiingia barabarani na wote wakashika uelekeo wa upande wa Mwenge.********


Naaam saa moja na robo, huko #mbogo_land, ndani ya jiji la Treanch Town, ulionekana msafara wa magari matano ukiingia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Treanch Town, mawili yakiwa ni magari ya kijeshi, moja ni bus dogo lililo tanguliwa na land lover Puma nalo la kijeshi, na matatu nyuma yakiwa ni magari ya kiraia meusi, aina ya Toyota V8 moja katikati yao likiwa na bendera ya taifa na nembo ya serikali.


Msafara unaenda moja kwa moja na kusimama kwenye eneo la VIP, sehemu ambayo zinasimama ndege za viongozi wa serikali na koo za kifalme, na hapo milango ya magari inafunguliwa na watu wanashuka toka kwenye magari yale, gari la jeshi dogo anashuka general Sixmund, ambae alisogelea lile bus dogo ambalo lilishusha askari kumi na sita wenye mabegi makubwa migongoni mwao.


General Six mund alipowafikia askari wake, akasimama mbele ya captain Amos David Makey, akatazama upande wa kulia kwake, kule yalikokuwepo magari matatu ya kiraia, ambapo wakati huo tayari magari mawili yalishafunguliwa milango na wakashuka watu wawili toka kwenye kila gari, na wote wakasogelea gari la katikati na mmoja wao akafungua mlango wa abiria wa kati kati wa gari lile, “mtapokelewa na balozi mdogo katika ubalozi wa Songea, kuhusu maelekezo yote mtayapa huko, usiri ni kitu muhumu na ndio daraja la jukumu lenu, muda wote mutawasiliana na mimi” alisema general Sixmund, kwa sauti ya chini, huku kwa macho ya wizi anatazama lile gari la kati la kiraia, ambapo sasa alionekana waziri chitopelah akiwa anashuka toka kwenye gari. “bila shaka afande naamini kila kitu kitaenda sawa” alisema captain Makey kwa sauti ya chini, huku anatazama kule ambako waziri Chitopelah, alikuwa anatokea. ….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Back
Top Bottom