Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THEMANINI NA SABA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA SITA: wanaume wawili wakiwa ndani ya jengo moja kubwa lisilomalizwa ujenzi, huku mwanaume mwingine anaonekana akiwa amelala chini huku nguo zake zikiwa zimechafuka damu chapa chapa, wasi wasi mkubwa unamshika Veroonica mapigo ya moyo yanamwenda mbio, “ni nani huyu? usiniambie kama ni John” alisema Verionica kwa sauti yenye kujawa na wasi wasi na mshtuko, “ni yeye wala hujakosea” alisema yule jamaa, wakati huo video inaonyesha kwa ukaribu zaidi tukio lile na kuivuta sura ya mtu alielala pale chini. ….ENDELEA…


Ni kweli huyu ni John Joseph, ambae ni mpenzi wake, hii inamshtua zaidi Veronica, “amefanya nini yupo wapi kwa sasa, basi tutoe taarifa polisi” alisema Varonica kwa sauti iliyokaribia kuangua kilio huku anatoa simu kwenye mkoba wake, lakini kabla hajaitoa simu yake anashtuka akiguswa na kitu kigumu mfano wa bomba dogo la maji kwenye mbavu zake, nae anaacha kutoa simu na kutazama alipoguswa.


Naam kwa macho yake Veronika anauona mtutu wa bunduki ukiwa umegusa mbavuni kwake huku simu yake ikichukuliwa toka mkononi mwake, “nadhani licha ya kuwa doctor lakini unafahamu hiki kifaa, hivyo tulia na unisikilize cha kufanya ili kumuokoa huyo fala wako, na pia kumbuka kuwa hauna chaguo jingine zaidi ya kukubaliana na mimi na kufanya kile ambacho nitakueleza” alisema yule jamaa na kuanza kutoa maelekezo,


Maelezo sio marefu sana, lakini ni mazito, hasa kwa mwanadada ambae hakuwahi kushiriki katika jambo kama hilo, maana yalikuwa ni maelezo ya mpango hatari, mpango ambao, ulipangwa ukapangika, “ukifanikisha hivyo, basi mtu wako ataachiwa” alisema yule jamaa ambae alikuwa anaongea kwa sauti ya chini, huku bado amemuelekezea bastora kwa siri eneo la ubavuni kwake, “nikikamatwa na polisi itakuwaje?” aliuliza Veronica kwa sauti iliyojawa na uoga, “hilo sahau, ni kama nilivyokueleza polisi ni kundi la tatu, kundi ambalo litafika wakati umeshaondoka na kuingia kwenye gari” alijibu yule jamaa na mwisho akasisitiza, “kumbuka kila unachofanya utakuwa una fuatiliwa kwa ukaribu sana, ukijaribu kufanya ujanja wowote, basi risasi itaenda sehemu yake” alisema yule jamaa, ambae hakuishia hapo, alichukuwa simu ya Veronica na kuizima kabisa kisha akaitia mfukoni mwake kwa miadi ya kwamba atampatia mara baada ya kumaliza kazi.


Naam baada ya maongezi yale ya kibabe ya dakika kadhaa, jamaa akamuambia Veronica, “haya sasa inuka na uongoze nje, kumbuka jambo lolote la kijinga utapoteza maisha yako na mpenzi wako” hapo kama vile mgonjwa, Veronica akainuka na kuanza kutembea kuongoza nje ya jengo lile la bar, akifuatiwa na huyu jamaa nyuma yake, walipofika nje wakaelekea kwenye maegesho ya magari, ambako walilipita gari la doctor Veronica na kwenda moja kwa moja kwenye gari aina ya land rover puma.


Walipolifikia gari hilo jipya la gharama wakaingia ndani yake wakipokelewa na watu wengine wanne wenye sare za jeshi la polisi, mikononi mwao wakiwa na bunduki aina ya SMG, mpaka hapo Veronica alihisi mikojo ina gonga hodi, maana licha ya kuwa na Elimu kubwa, kufahamiana na viongozi wengi na watu mashuhuri lakini hakuwahi kukaribiana na bunduki kwa ukaribu kama huu, hakika alishikwa na uoga wa hali ya juu, hasa wale jamaa walipo onekana wakimkodolea macho ya mshangao na matamanio, si unajua Veronica alivyo mzuri.


Hapo Veronica akajikuta anaanza kutetemeka, kwa uoga wa kuzidi uliomshika, maana alijuwa kuwa akifanya uzembe sio tu kuuwawa yeye na John, ila pia kuna hatari ya kubakwa kabla ya kuuwawa, “jamani naomba msinifanye chochote, nitafanya kamlivyosema” alisema Veronica kwa sauti yenye kuombeleza, sauti ambayo ilionyesha wazi kuwa alikuwa katika kiwango kukibwa cha uoga na wasi wasi, wale jamaa wakacheka kicheko cha dhihaka, “oya tuondoke zetu” alisema yule jamaa na hapo Dereva akawasha gari na kuweka gear namba moja, kisha akaondoa gari taratibu, “lakini Job, naona kama ni mapema sana kusogelea eneo la tukio, maana muda ni saa nne” alisema mmoja wao na hapo yule aliekuwa na Veronica akajibu, “twendeni eneo la tukio tukasome mchezo” hapo dereva akaongeza mwendo kuelekea mbezi stendi ya malamba mawili.********


Naam saa tatu kasoro dakika nne, Inocent Matius akiwa amekaa kwenye eneo la mapokezi ya jengo kubwa la Sisterfada hotel, macho ameyaelekeza kwenye mlango mkubwa wa kioo wa kutokea nje ya hotel hii, mara anamuona kijana mmoja anaingia mule ndani akiwa na box mkononi mwake, kijana ambae anatembea kwa haraka, kuifuata lift na hata baada ya kufika usawa wa muhudumu wa mapokezi, anampungia mkono huku anaachia tabasamu.
Mwadada mrembo wa mapokezi, ambae anaonekana kuvutika na sura ya upole na umbo la mazoezi la kijana huyu mwenye urefu wa wastani, anapunga mkono huku ameachia tabasamu laini lenye kuonyesha kufurahiswa na salamu ile, ata hivyoo hapakuwa na mwendelezo, hasa baada ya kijana yule kuingia kwenye lift, innocent aliangalia mpaka lift ilipojifunga, “oya vipi umemuona huyo jamaa” alishtuka Inno, ambae hakujuwa kama mwenzie ameshafika pale alipo, “unamzungumzia huyo bishow aliepita sasa hivi?” aliuliza Innocent, akionyesha kwenye lift, “ndiyo, huyo jamaa amekuja na gari kama lile analolisaka yule rafiki wa boss, yule alievamiwa jana” alisema yule jamaa mwingine, “unasema kweli! Hebu twende tukalione” alisema yule inno, huku wanainuka na kuelekea nje, “tena ikiwezekana tupige picha halafu tumtumie boss, amuonyeshe rafiki yake kama ndio hilo” alishauri inno, wakati wanatoka nje.********


Naam, mida hii mzee Frank akiwa ametulia nyumbani kwake, anajiandaa kwenda kulala, mara akasikia ngurumo ya gari nje ya nyumba yake, “kwanza akakimbilia kwenye switch ya taa ya sebuleni na kuizima, halafu akakimbilia dirishani, akafunua panzia na kuchungulia nje kuona wageni hao, muda wote mke wake akiwa tayari kusikiliza mume wake anataka sema nini.


Bwana Frank Nyati, ambae ni baba mzazi wa kijana wetu Deus, akiwa pale dirishini anaweza kuliona gari aina ya Toyota V8 jeusi, likisimama nje ya nyumba yake, kisha wanashuka watu watatu wote wakiwa ni vijana wa kati umri wa miaka 25 mpaka 36, muonekano wao ulikuwa ni wa kawaida sana, awakuonyesha kama ni mawakala wa upelelezi toka MLSA wala MLA, lakini gari lao la kifahari na ujio wa usiku ndio uliomshtua sana bwana Nyati, ambae aliwaona watu wale wakiusogelea mlango wa mbele wa nyumba yake, nae akajitoa dirishani na kusogelea mlango, akasimama pembeni ya mlango ule.


Naam sekunde chache akasikia mlango unagongwa, “hodiiii” bwana Frank akapiga ukimya, mlango ukagongwa tena, “hodi hodi” ilisika sauti sambamba na kugonga mlango mara mbili mfululizo, “ni vyema kama mkajitambulisha wenyewe” alisema bwana Frank, kwa sauti yenye tahadhari kubwa, “sisi ni askari watatu, ambao ni Captain Amos David Makey, Sajent Girbat Ngasa na koplo Amadeus Peter toka MLA, tunaomba kuonana na wewe Afande” ilisikika sauti toka upande wa nyuma ya mlango.


Ilimshtua kidogo Bwana Frank Nyati, baada ya kusikia kuwa wageni wale walikuwa ni askari ambao wanatokea #mbogo_land, “mnahitaji nini usiku huu?” aliuliza bwana Frank Nyati, akiwa ametega pembeni ya mlango, “ni ujumbe toka kwa mfalme elvis wa kwanza, tunahitaji kuongea na wewe kwa njia ya amani afande, ” ilisikika ile sauti ya mwanzo, “mazungumzo yameshindwa kusubiri kesho mpaka mje usiku kama huu?” aliuliza mzee Frank kwa sauti ya mashaka, “ingeweza kusbiri, lakini kwa sababu za kiusalama tumeona tuje kwako kabla baadhi ya watu hawajafahamu uwepo wetu hapa nchini” ilisikika sauti ile ambayo ilikuwa semaji wakati wote, “sawa lakini msijaribu kufanya ujinga wowote” alisema mzee Frank, huku anawasha taa na kufungua mlango.


Bwana frank anakutana na sura ngeni za watu watatu waliovalia mavazi ya kiraia, karibun sana vijana” alisema mzee Frank huku anawatazama wale vijana watatu kuona kama anawafahamu au kuwakumbuka watu hawa, lakini hakuweza kuwatambua.*******


Yap! ndani ya jengo hilo hilo la sisterfada, ghorofa ya tatu, chumba namba nane, kama tulivyo acha, chumba bado kina harufu kari ya moshi wa bangi, ulikuwa umetawala ndani ya chumba, vijana wanne wenye silaha mikononi mwao, wakiwa wamesimama kama mwanzo, yani wawili wanatazama nje wawili wamewageukia wale wakina mzee James, waliokua wamekaa kwenye makochi mazuri ya kupendeza, “labda kwanza nijitambulishe kwako bwana James Kelvin” alisema yule aliekaa kwenye kochi huku anakung’uta jivu la sigara bwege kwenye kisonjo cha majivu kilichopo mezani huku bwana James Kelvin akiwa anamtazama.


“naitwa general Erasto Kadumya, toka #mbogo_land” alisema yule jamaa kwa sauti kavu, kisha akaweka kituo na kuvuta ile sigara yake isiyo na kishungi, kisha akaupuliza moshi hewani, japo bwana James ambae ni tajiri mkubwa sana, sio Tanzania peke yake, ni tajiri na mfanya biashara mkubwa nchi za afrika mashiriki ya kati na kuini, alikelwa na ule moshi wa sigara, lakini alifia kusema lolote, kutokana na mwonekano wa vijana wale wenye bunduki waliokuwa mle ndani.


Jina kadumya halikuwa geni masikioni mwa mzee James, haraka sana akaanza kuvuta kumbu kumbu aliwahi kulisikia wapi, ni kama Kadumya alisoma anachokiwaza bwana James, “nadhani unajiuliza umewahi kulisikia wapi jina langu?” aliongea Kadumya, huku anaachia tabasamu, kwenye midomo yake legevu iliyolewa bangi, “mimi ni mkuu wa jeshi la ukombozi linalosimamia harakati za mapinduzi kwa njia ya damu la nchini #mbogo_land” utambulisho huo wa Kadumya ulimshtua sana bwana James, ambae si kumkumbuka mtu aliewahi kusifika miaka ya 1992 kwa kitendo cha kukimbia jeshi na kujiunga na waasi, pia alianza kuona dalili ya muendelezo wa yale matatizo yaliyo mtokea mwaka 1992, na kumfanya akimbie nchi yake, wakati hakuwa anafahamu lolote juu ya UMD.


“bwana James kwa kifupi mimi ndie niliekupigia simu kukuokoa toka kwenye kifo wewe na familia yako, na hili swala niliagizwa na bwana Chitopelah ambae alipewa jukumu hilo, na nilifanya hivyo kwasababu nilikuwa najua kuwa, sio muhusika wa mapinduzi hayo” alisema bwana Kadumya, huku bwana James akiwa anamsikiliza kwa umakini mkubwa akingoja kwa hamu kusikia lengo la kikao kile, maana ni kama hakukuwa na dalili ya habari za kibiashara mahali pale, “nadhani unafahamu lengo la kundi langu, ni kutafuta uhuru wa wananchi kumchagua kiongozi wao wenyewe na sio kurithishana uongozi kama inavyofanyika sasa” hapo Kadumya akaweka kituo kidogo na kupuliza tena bangi yake ambayo sasa ilikuwa inakaribia kuunguza vidole vyake, maana ilishakwisha na kubakia usawa wa ukucha, wenyewe wanaita chaukucha.


Mapumziko hayo bwana James ambae hakujuwa kama binti yake pia yupo kwenye matatizo, akatumia kuuliza swali, “sasa mnataka nini kwangu, maana sidhani kama kuna linalo nihusu?” aliuliza James, huku akimtazama Kadumya ambae alikuwa anakisigina kile chaukucha kwenye sahani ya jivu…….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THEMANINI NA NANE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA SABA: Mapumziko hayo bwana James ambae hakujua kama binti yake pia yupo kwenye matatizo, akatumia kuuliza swali, “sasa mnataka nini kwangu, maana sidhani kama kuna linalonihusu?” aliuliza James, huku akimtazama Kadumya ambae alikuwa anakisigina kile chaukucha kwenye sahani ya jivu…….ENDELEA…

“bwana James lengo letu sisi utusaidie kulipia gharama za kuingiza silaha nchini #mbogo_ land, ambazo zitatusaidia kwenye mapinduzi” alisema Kadumya, huku anafungua chupa ya pombe kali pale mezani na kuimiminia kwenye grass, “eti! kwa nini niwe mimi?” aliuliza bwana James kwa mshangao na mshtuko mkubwa sana, “sikia bwana James, nadhani unapaswa unisikilize kwa umakini, huweze kuelewa, nina imani utaupenda mpango huu” hapo kilifuata kituo kingine cha bwana Kadumya kuweka grass mdomoni na kubwia funda moja kavu la pombe kali.

Na alipoishusha glass akaendelea, “kwa umakini mkubwa na kwa kutumia muda wetu mwingi jopo zima la UMD lilikaa na kukuchaguwa wewe, ni baada ya kuona kuwa wewe ni mwathirika wa uongozi wa kifalme, hasa kwa kitu kibaya ulicho fanyiwa na uongozi huo dhalimu na uonevu ambao tunapigania utoke madarakani, na kuweka serikali ya kidemokrasia, tumeona tukushirijishe wewe kuliko kumpa faida mtu mwingine” alisema Kadumya na kuweka tena kituo cha unywaji wa ile pombe yake safari hii akiwasha na sigara ya kawaida, “unazungumzia faida gani kwenye kuingiza silaha ambazo zitatumika kuleta machafuko kwenye nchi?” aliuliza bwana James kwa sauti yake ile ile yenye kushangaa na kushtushwa.*********

Wakati mazungumzo yanaendelea, chumba namba nane katika ghorofa ya tatu ya jengo hili la Sisterfada Hotel, hebu twendeni Nyumbani kwa Eze, ambae bado yupo sebuleni amepakata miguu mizito ya mke wake kibonge, hakika ungekuja ghafla ungeweza kumsimanga mke wa Ezekiel kwa kudhania kuwa amempakatisha mtoto miguu yake, ni kutokana na umbo dogo la bwana Eze, ambae ilibidi akomae tu ili mke wake aendelee kuwa na imani na penzi lao.

Naam bwana Eze akiwa anaendele kuvumilia, mara akasikia simu yake inaita, “nani huyu?” aliuliaza mke wa Eze, ambae ni wazi yeye ndie alieshika hatamu ya uongozi pale nyumbani, usingeamini kama bwana Eze alikuwa na uwezo wa kutoa Amri mbele ya kundi la vijana wenye miili iyojengeka kimazoezi kama wakina Inocent, na ikatekelezeka.

Eze anachukuwa simu na kuitazama kidogo huku wasi wasi ukimtanda moyoni akiomba asije kuwa hawara yake Emmy, lakini anapoliona jina la mpigaji anajikuta ametabasamu, “ni Ino huyu, nadhani anataka kunipa taarifa ya kazi” alisema Eze kwa sauti ya kujiamini huku anapokea “niambie Inno mmesha mpata huyo mjinga?” aliuliza Eze kwa namna ya kuto kufafanua ili mke wake asijue anamzungumzia nani, “boss bado tupo hapa hatujaona kitu ila kuna inshu nyingine hapa” ilisikika sauti ya Inocent Matius toka upande wa pili wa simu, “inshu gani tena ni muhimu zaidi ya hii?” aliuliza Eze kwa sauti ya ukali kidogo, “zote muhimu, ila ni vyema ukatazama whatsapp nimekutumia picha litazame hilo gari, kama ndiyo ambalo linatafutwa na Songoro” alisema Inocent kwa sauti ya upole kidogo, maana tayari Eze alikuwa ameshaanza kuwaka, “eti, unasema lile BMW jeusi mme liona hapo, hebu kwanza nilitazame” alisema Eze na kukata simu kisha akaingia upande wa whatsapp.*******

Naam kule songea mtaa wa making’inda nyumbani kwa mzee Frank, “ok! mfalme amekumbuka nini baada ya miaka ishirini kupita?” aliuliza bwana Frank, ikiwa ni baada ya kusalimia na wageni wale ambao bado wanamwita kwa heshima ya cheo chake, “afande kiukweli hivi karibu mfalme amebaini kuwa kindi cha UMD, kimerudi tena na sasa kina mipango mikubwa ya kupindua serikali” alisema captain Amos Makey, nakuweka kituo kidogo kuona kama mzee Frank anaweza kuweka neno lolote.

Lakini mzee huyu akapiga kimya, akionekana kutega sikio kusubiri kilele cha maelezo yale, kuona hivyo captain Amos Makey akaendelea, “na katika watu ambao kwa namna moja au nyingine, walihusishwa na kundi hilo ni wewe, japo kwa busara ya mfalme Elvis wa kwanza alitilia mashaka uhusika wako katika uasi huo na kuanza kufuatilia habari zako hata baadae alipouona ujumbe wako uliomuachia mfalme Eugen Mbogo wa 25, uliomuachia wakati unaondoka nchini” alisema Amos Makey, kisha akaweka kituo na kukagua mfuko wake akiibuka na kipande cha karatasi ambacho alikikunjua na kukisoma, “hicho ndicho kinachofanywa na watu unao waamini, lakini siwezi kuibadilisha akili yako kabla sija kamatwa na kuuwawa, wacha leo niikimbie nchi yangu ninayoipenda, lakini nakuahidi uwe wewe au kizazi chako, kitakumbuka maneno yangu, nikiweza nitaipigania nchi yangu mimi au kizazi changu”

Baada ya kusikia ujumbe ule Frank akajikuta anatabasamu, “kwahiyo mfalme anahitaji kujua nini toka kwangu” aliuliza mzee Frank, “afande sisi tumekuja na swali moja tu kwako” alisema Amos Makey, huku anamtazama mzee Frank, ambae alionyesha ishara ya kichwa, kwamba aulize swali hilo, “mfalme anataka kujua ulimaanisha nini katika jumbe huu” alisema Amos na hapo Frank akatulia kidogo kama anavuta kumbu kumbu.

Ilitumia sekunde kadhaa, kabla ya kuinua kichwa na kuwa tazama wageni wake kwa zamu, kama alikuwa anatazama uaminifu wao, “ok! kwa kifupi ni kwamba, nilicho mueleza mfalme ndicho ambacho mnakiona sasa” alisema mzee Frank, huku anawatazama wageni wake mmoja baada ya mwingine, “unamaanisha nini afande?” aliuliza captain Makey kwa sauti iliyojaa udadisi, “mutanielewa tu” alisema mzee Farank, huku anaachia tabasamu, “muasisi wa kundi la UMD ni kiongozi mkubwa sana serikali na alichukua imani ya wafalme wote waliopita, hata huyu wa sasa” alisema kwa kituo Frank huku wageni wake wakitega masikio kwa umakini kumsikiliza bwana Frank.

“kwanza alimshawishi bwana Kadumya kuacha jeshi ili kuandaa kikundi, ambacho kwa miaka ile ya 90, kilikuwa ni kanya boya, maana hakikuwa na mpango wowote endelevu, zaidi ni mpango wa viongozi wa kundi hilo kuandaa mpango mkakati wa kupunguza nguvu serikalini, na kuandaa mipango ya baadae, kitu ambacho walikiweza kwa asilimia hamsini” alisema Frank na hapo kidogo likapatika swali toka kwa sajent Ngasa, “walipunguza nguvu kivipi na walifanikiwaje?” swali hilo lilimfanya Frank atabasamu tena, “kwahiyo inaonyesha wazi kuwa bado hamja tambua njama za wale washenzi” alisema mzee Frank na hapo alianza kueleza ilivyokuwa.

“kiongozi wao ambae yupo serikalini, ambae simfahamu, alieneza uvumi kuwa kuna wasiliti wengi ndani ya serikali, ambao ni wanachama wa UMD na ndipo mfalme Eugen alipotoa mamlaka kwa MLSA, kwamba wawasake waasi wote ndani ya serikali na kuwafykelea mbali, na hapo ndipo mfalme alipokuwa ametoa kibali cha washenzi hao kupunguza nguvu ya nchi katika ulinzi na usalama, maana waliuwawa watu wengi sana na familia zao, tena ni askari watiifu wenye uwezo mkubwa sana kijeshi na kiusalama na mimi nilikuwa mmoja katika orodha ya waliopaswa kuuwawa, niligundua hivyo dakika chache kabla hawajanifikia, niliweza kupambana na MLSA, kisha nikatoroka nchi” alisimulia Frank, ambae hakuishia hapo.

“Kama hilo halitoshi, pia walimuingiza katika hili, mfanya biashara mkubwa sana zamani na sasa, huyo ni bwana James Kelvin, ambae walimpigia simu mapema wakimjulisha kuwa atoroke nchi, nae akatorokea tanzania ambako anaishi mpaka sasa na kama mujuavyo ni tajiri mara dufu zaidi ya mwanzo, sasa basi lengo lao lilikuwa ni kuja kumtumia baadae, hivyo basi kama sasa wameanza harakati zao haramu, basi kuna watu wapo hatarini” alisema Frank, na hapo wale watatu wakatazamana, kila mmoja akiwa na hamu ya kusikia jina la mtu ambae yupo serikalini, ambae ni kiongozi wa UMD, na pia walitamani kuuliza juu ya Deus Nyati ikiwa ni moja ya jukumu lao.*******

Sasa turudi Sisterfada, safari hii tunaelekea ghorofa ya nne, ambako tuna muona kijana mmoja amesimama mwishoni kabisa mwa korido ya flow hii, akiwa anachezea simu yake, sisi tunaachana nae, tunatazama kwenye mlango wa lift ambao unafunguka na anatoka kijana wetu Deus Nyati alievalia suruali ya jinsi la blue, na tishet rangi ya kijivu lililomshika vyema mwili mwake na kuonyesha jinsi alivyouweka vizuri mwili wake kimazoezi, mkononi akiwa na box dogo jekundu.

Deus anatembea kwa haraka, huku anatazama namba za milango kushoto na kulia, mpaka anapoenda kusimama kwenye mlango wa chumba namba nane, anatoa simu yake na kutazama saa yake, ni saa tatu kamili, Deus anaiweka simu yake mfukoni na kugonga mlango, wa chumba namba nane, hapakusikika sauti ya mtu akikaribisha, baada yake mlango unafunguliwa, anacho kiona kijana wetu kina vutia, japo aliweza kuzuia hisia zake lakini moyoni alikoma kupokea ile kazi.

Maana anaonekana mwana dada mwenye shep yake akiwa amevaa taulo jeupe ambalo kwa namna moja au nyingine naweza kusema lilishindwa kuficha mapaja manene ya mwanamke huyo mwenye sura nzuri, huku kifuani kwake kama asinge saidia kushika kwa mkono, basi tauro lisinge funga, maana minyonyo yake mikubwa iliyojaa ilifanya taurlo lishindwe kukaa vizuri, “hakika unasimamia sheria zako, ni saa tatu kamili” alisema yule mwana dada kwa sauti tamu tulivu na ya taratibu huku anaachia tabasamu pana la furaha, tabasamu lililo legea kama music wa kulaza mtoto.

“Yah! lazima ni heshimu tulicho kubaliana” alisema Deus ambae bado alikuwa amesimama mlangoni anamtazama mteja wake, ambae alicheka kivivu, “ok! karibu ndani” alisema mwana dada huyu mwenye macho ya kusinzia, huku anageuka na kurudi ndani akimpa nafasi Deus ya kutazama uumbaji, maana mwanamke huyu alijaaliwa ukubwa wa sehemu za kukalia utadhani alichukuwa na makalio ya jirani yake, Deus alijikuta anashusha pumzi za uvumilivu, huku anapiga hatua kuingia ndani, kisha mlango ukafungwa, hawakujua kuwa kuna kijana alikuwa anatuma ujumbe kwa wenzake kuwajulisha kuwa, tayari mbuzi kaingia mtegoni.*******

Kigamboni dar es salaam, pale kwenye jumba ambalo linapulizwa na upepo wa bahari kila dakika, bwana Songoro akiwa ndani ya jumba lake anakunywa pombe kama ameweka dumu tumboni, anajisonya kila mara akimlaumu CP Ulenje kwa kukuto kupokea simu yake, mara anasikia simu yake inaita, “mshenzi sana wewe, nilijuwa tu huwezi kuacha kuwasiliana na mimi” alisema Songoro huku anachukuwa simu yake mezani na kutazama jina la mpigaji, “khaaaaaa! huyu shot chases anataka nini tena?” aling’aka Songoro kabla hajaipokea simu na kuweka sikioni, “unasemaje, wewe unapigwa na mke nije nikuamulie au?” aliuliza Songoro kwa sauti iliyoonyesha wazi kuwa ameona usumbufu, kuipokea simu ile, “acha ujinga wewe nina habari muhimu kwako kuhusu yule jamaa aliekunyea jana” alisikika Eze toka upande wapili wa simu. ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THEMANINI NA TISA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA NANE: “khaaaaaa! huyu shot chases anataka nini tena?” aling’aka Songoro, kabla hajaipokea simu na kuweka sikioni, “unasemaje wewe, unapigwa na mke nije nikuamulie au?” aliuliza Songoro kwa sauti iliyoonyesha wazi kuwa ameona usumbufu, kuipokea simu ile, “acha ujinga wewe, nina habari muhimu kwako kuhusu yule jamaa aliekunyea jana” alisikika Eze toka upande wapili wa simu. …….ENDELEA…

Hapo ni kama akili ilimtulia Songoro, “nani huyo, unamaanisha yule kijana mshenzi?” aliuliza Songoro kwa sauti ya mshtuko na shauku, “huyo huyo, vijana wameliona gari lake pale Sisterfada hotel, mitaa ya shekilango, ngoja nikutumie picha ulione” alisema Eze na kabla hajakata simu Songoro akamuwahi, “sikia Eze nani yupo hapo SisterFada mida hii” aliuliza Songoro kwa shauku, “yupo kijana wangu Inno, kuna mtu anamfuatilia pale, unaweza kuchukuwa namba yake kwa side ukaongea nae akueleze zaidi” hapo songoro hakujibu, akakata simu mara moja, “side mpigie Inno haraka” alisema Songoro, huku yeye anapiga simu sehemu, simu ambayo ilipokelewa mapema zaidi, “Bakari kusanya vijana wote sasa hivi, waambie vijana wawe tayari kwa kazi, hakikisha mnabeba bunduki na risasi zote tulizo nazo kisha subiri maelekezo yangu” alisema Songoro kwa sauti iliyojaa amri, “ndiyo boss imetekelezwa hiyo”, ilisikika sauti upande wa pili wa simu, sauti ambayo Songoro hakusubiri imalize kutoa jibu akakata simu na kumtazama Side.

Naam said anaonekana akimsogelea Songoro, huku ameshika simu mkononi, “ameshapokea boss” alisema Said, huku anampatia simu Songoro, “Inno huyo mpuzi anae endesha hilo gari umefanikiwa kumuona?” aliuliza Songoro, ambae kulitambua gari ingekuwa inshu kidogo, lakini ageweza kumtambua dereva wa gari, “ndiyo mzee, yupo hapa Hotelini ameingia chumba namba nane ghorofa ya nne na sisi tunamfuata huyo huyo, alisikika innocent akionyesha kuwa alikuwa anatembea kwa haraka, unaweza kuniambia anaonekanaje” aliuliza Songoro huku yeye mwenye akianza kuvuta taswira ya kijana huyo ambae jana amemuonyesha kitu ambacho, hakutarajia kuonyeshwa na mtu mmoja, “ni dogo fulani hivi mrefu kiasi, ana sura ya mtoto wa mama, ila inaonekana huwa anaingia gym” kila innocent alivyotoa maelezo ndivyo Songoro alivyo ipata taswira ya kijana yule mwenye BMW jeusi, “ni huyo huyo mshenzi huyo, hakikisheni hatoki hapo, mpuuzi nataka nimuue kwa mkono wangu” alisema Songoro huku anasimama toka kwenye kochi, “tuondoke haraka tunaelekea sheklango” alisema Songoro huku anampatia Side simu yake.

Wote wakaanza kutembea kutoka nje ya jengo lile, wakimuacha yule mwanamke peke yake mle ndani, na walipofika nje ambako kulikuwana vjana wanne wanalinda jumba lile akawasemesha, “hakikisheni haingii mtu yoyote hapa, sisi tunaenda kumuadabisha mpuuzi mmoja, alisema Songoro, huku anatoa simu na kupiga kwa bakari, kumueleza wakutane wapi usiku ule kwaajili ya kumnasa Deus.*******

Ghorofa ya tatu chumba namba nane, Sisterfada Hotel, kikao kilikuwa kinaendelea huku bwana Kadumya akiendelea kunywa pombe na kuvuta sigara mfululizo na kujaza moshi chumba kile namba nane kiasi cha kumfanya bwana James ashikwe na chafya za mara kwa mara, “sidhani kama swala la umwagaji damu ni muhimu kwa faida utakayoipata bwana James, maana ukiachilia mbali kurudi #mbogo_land ukiwa mtu huru, pia utaendesha biashara zako pasipo kulipa kodi yoyote, wewe ndie utakuwa msimamizi wa mauzo yote ya madini na utapewa migodi kadhaa ya almas na dhahabu, hivyo ndivyo utavyoweza kurudisha fedha utakazo zitoa kwenye malipo ya usafirishaji wa silaha, na michango mingine ambayo tutahitaji kwa huduma za askari wetu” alimaliza kuongea Kadumya.

Naam wakati Kadumya anasubiri, James akubaliane na mpango wake mara ghafla akasikia kicheko toka kwa mzee huyo tajiri, ambae waliamini ndie kikamilishi cha mpango wao wa silaha, “sikuwahi kudhani kama mwisho wa haya yote itakuwa hivi, yani kumbe bwana Chitopelah, ndie mpangaji wa haya yote?” aliuliza James, ambae hakusubiri jibu, “kiukweli sitoweza kutumia jasho langu na juhudi zangu kuibomoa nchi yangu, japo kwa sasa naishi kama mkimbizi, lakini najua hii ilifanywa makusudi ili niingie mtegoni, hakika siwezi kufanya hivyo” alisema James kwa sauti ambayo haikuonyesha dalili yoyote ya utani.

Hapo bwana Kadumya akatulia kama sekunde kadhaa akiwaza kitu fulani, kisha akatoa simu na kupiga kwa mtu fulani huku akiweka sauti ya wazi wote wakasikia ikianza kuita, hata ilipo pokelewa, “niambie Kadu, mpango umeendaje?” ili uliza sauti fulani ambayo ilijawa na mikwaluzo toka upande wa pili wa simu, “muheshimiwa tuna tatizo, bwana James amekataa” alisema Kadumya kwa sauti iliyopooza huku wote wakisikia, “ok! muuweni kufuta ushaidi, maana kiukweli kuna watu wamekuja huko Tanzania na hatujui wana mpango gani mpaka sasa, kisha anzeni mpango wa pili, mukikamilisha anzeni safari kwa magari kupitia kusini mwa Tanzania” ilisikika ile sauti ya mikwaluzo, ambayo niwazi ilikuwa katika ulevi, “ndiyo mheshimiwa” aliitikia Kadumya kabla mheshimiwa hajakata simu, tayari bwana James alikuwa anatetemeka kama vile amesimama mbele ya simba mla watu, kijasho kinamtoka kwenye paji la uso wake.*******

Yap! mara baada ya kukata simu ya bwana Songoro, bwana Eze ambae alikuwa ameipakata miguu na mapaja mazito ya mke wake kipande cha mtu, mara simu yake inaita tena, ana chukua na kuitazama haraka, alikuwa ni innocent Matius, kijana wake aliemtuma kumfuatilia hawara yake Emmy.

Eze akamtazama mke wake, ambae alikuwa anatazama TV, akaipokea simu, “niambie Inno” alisema Eze akitegemea taarifa zaidi, “boss tayari mtu kaingia mtegoni, kuna kijana kaingia chumba namba nane alichoingia shemeji” alisema Inocent, taarifa hiyo ilimuumiza moyo sana Eze, sio tu kwaajili ya gharama anazotumia kwa Emmy, lakini pia kwabjinsi alivyompenda mwanamke huyo na kumfanya kuwa ndiyo burudani yake na kipoozeo cha kero anazozipata kwa mke wake, “ok! mkamateni huyo mshenzi, na niwakute nae hapo ili nimfundishe kuheshimu mali za watu” alisema Eze, huku anaiinua miguu ya mke wake na kuibwaga pembeni kiasi cha mke wake kushangaa na kumtazama mume wake huyo ambae katika hali ya kawaida hawezi kuthubutu kufanya ujinga kama huo.

Mke wa Eze akamuona mume wake anatembea kueleka chumbani huku anakata simu na kuiweka mfukoni, “wewe hebu kuja hapa, umeifanyaje miguu yangu?” alisema mke wa Eze huku anamtazama mume wake aliekuwa anaingia chumbani bila kujibu kitu, ambako hakukaa sana kule chumbani akatoka akiwa na koti na bastora mkononi akatembea kueleka usawa wa meza na kuchukua funguo ya gari kisha akaanza kutembea kuelekea nje, muda wote akijisemesha mwenyewe, “Eze unatafuta kipigo, hebu rudi haraka na unieleze unaenda wapi” alisema mke wa Eze huku anainuka na kukimbilia nje, kule alikokuwa anaenda Eze, “we nisubiri bwana tutamalizana nikirudi” alisema Eze huku na yeye akianza kukimbia kulifuata gari lake lilipokuwa limeegeshwa,

Mke wa Eze ambae uzito wake unamfanya ashindwe kukimbia zaidi, anasimama huku anahema kwa nguvu na kubakia kumtazama mume wake aliekuwa anaingia kwenye gari na kuondoka zake, “we mshenzi leo nitakuuwa bora ulale huko huko” alisema mke wa Eze, lakini akasita kidogo, “mh! ulale huko huko, mbona nita kusaga saga vibaya sana” alisema mwana mama huyo kibonge cha mtu ambae ana uwezo wa kumpiga mumewe huku anatazama taa za gari la mumewe zikitokomea mbali.*******

Naam ndani ya chumba namba nane cha ghorofa ya tatu, Kadumya alimtazama bwana James aliekuwa amekaa kwenye kochi anatetemeka kwa uoga, “haya bwana James una muda mchache wa kufanya maamuzi, kufadhili UMD au kuuwawa?” alisema Kadumya huku anachukuwa sigara kwenye kasha lake na kuiweka domoni, kisha anaiwasha, “kwa kweli ndugu zangu siwezi kuisaliti nchi yangu” alisema mzee James, huku akionekana amejawa na uoga wa hali ya juu, “acha ujinga wewe, unawezaje kuikumbatia nchi ambayo ilikusaoiti?” aliuliza Kadumya kwa sauti ya dharau, hapana haikuwa serikali, huo ulikuwa ni mpango wenu, ili baadae munitumie kufanikisha lengo lenu huku lawama zikiendelea kunishukia mimi” alisema James kwa sauti ambayo licha ya kuonyesha kuwa na uoga wa hali ya juu, lakini ilikuwa na msisitizo.

Hapo Kadumya akawatazama vijana wake wawili, wale waliokuwa wamewageukia wao, ukiachilia wale ambao walikuwa wametazama dirishani, “ok! askari, tuna mfanyaje huyu, tunaondoka nae, tuka muuwe mbele ya safari au tumuuwa na kuuacha mzoga wake hapa hapa” aliuliza Kadumya, swali ambalo lilimuogopesha sana mzee James, ambae hakuwa tayari kuisaliti nchi yake, japo sasa aliishi kama mkimbizi, “boss nadhani itakuwa vyema tukimalizana nae hapa hapa, maana tukitoka nae tunaweza kushtukiwa” alisema mmoja kati ya wale askari wawili na mwingine akadakia, “mkuu, ni vyema ukatoa kibari kwa akina Kafulu kuanza kwa plan B” alisema yule mwingine.

Hapo Kadumya akamtazama James, “bwana James hauna bahati” alisema Kadumya huku anachukua simu yake na kuipiga kwenye namba, iliyoandikwa Dereva, akaipiga nayo ikaanza kuita, hakujua kama mtu anaempigia alikuwa ghorofa inayofuata juu.*******

Naam wakati huo mita kama mia tano magharibi na mashariki, mwa jengo la hotel ya SisterFada, vikundi vya Songoro vikiwa vinakuja kwa kasi kwa lengo la kukutana pale hotelini ili kumkamata kijana anae endesha BMW jeusi, pia Eze alikuwa anaendesha gari lake kwa speed na fujo ilikuwahi kumshughulikia kijana ambae anaamini anatembea na nyumba ndogo yake, makundi yote yalikuwa yana isogelea hotel kwa kasi sana.

Wakati huo huo vijana wa Eze walikuwa wanapanda ngazi kwa kasi kuelekea ghorofa ya nne, kule ambako kijana wetu Deus alikokuwepo, kumbukeni boss amesema anataka amkute huyo fala” alisema Inno akiwaeleza wenzake wawili aliokuwa nao.

Dakika mbili baadae, walikuwa tayari wamesha fika, ghorofa ya nne na ambako walimkuta yule mwenzao mmoja na kutimia wanne, “ok! wawili bakini hapa nje, kuangalia noma sisi wawili tunaingia kumdhibiti huyo mjinga” alisema Inno, huku anatoa bastora yake na kuikoki na wenzake wakafanya hivyo huku wanausogelea mlango wa chumba namba nane.*******

Wakati huo huo ndani ya chumba namba nane cha ghorofa ya nne, Deus akiwa amesimama na box mkononi ana tazama mazingira ya mule ndani ya chumba cha hotel, ambacho kilikuwa na taa zenye rangi hafifu, anaweza kuona wazi meza iliyojaa vyakula na vinywaji mbali mbali vyote vikiwa ni vilevi, Deus anaona kitanda kikubwa kilichotandikwa vizuri.

“Karibu dereva, jihisi uhuru” alisema yule mwanamke alie valia tauro jeupe huku anachukua box mkononi mwa Deus na kulifungua, “asante boss” aliitikia Deus na wakati huo huo akasikia simu yake inaanza kuita, ilikuwa ni simu ya maswala ya kazi, “samahani boss” alisema Deus kisha akapokea simu, “naaam nakusikiliza” alisema Deus, na kutulia kusikiliza upande wa pili, “mpango unaanza saa nne kamili, zingatia muda” ilisikika sauti toka upande wa pili wa simu, “sawa boss” alijibu Deus, na kukata simu, kisha akatazama muda, ilikuwa ni saa tatu na dakika kumi, “usiniite boss anko, niite Emmy na wewe unaitwa nani?” aliuliza yule mwanamke kwa sauti ya taratibu yenye mbwe mbwe za mbembelezo, “umevunja sheria namba moja, hakuna kujuana majina” aliisema Deus kwa sauti tulivu, huku anainua uso wake kumtazama mwanamke huyu.

Deus anacho kiona kwa Emmy, kinamfanya atoe macho kwa mshangao, maana anamwona mwanamke yule akiwa amepembua lile tauro na kubakia uchi wa mnyama, “jamani Dereva, sasa tutakaaje humu ndani bila kujuana majina?” aliuliza Emmy kwa sauti ya kujidekeza huku anainama kwa kubinua makalio yake, akiacha wazi sehemu hiyo aliyojaaliwa kuliko sehemu nyingine, mwana dada huyu mwenye umbo la kushawishi jambazi kurudisha kisu mfukoni, anachukuwa chupi aina bikini kwenye box, aliloleta Deus na kuitazama kama vile anaikagua, hatari jamani ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Visa vinanichanganya sana, labda nitaelewa baadae.
Mala veronika, mala Deus, mala Chitopela, mala Uze, mala Kadumya 🤣🤣🤣
Hakika ni hatari na nusu
 
Visa vinanichanganya sana, labda nitaelewa baadae.
Mala veronika, mala Deus, mala Chitopela, mala Uze, mala Kadumya 🤣🤣🤣
Hakika ni hatari na nusu
Kama hadi hapa hujaelewa anza tu mwanzo kwasababu story ishaisha had hapo ilipofika 😅
 
Kama hadi hapa hujaelewa anza tu mwanzo kwasababu story ishaisha had hapo ilipofika 😅
Hivi ukiacha hii hadithi na ile ya asali haitiwi kidole, ni hadithi gani umeisimulia.
Nataka nizifuatilie.
Pia nataka kujua kama utasimulia hadithi nyingine baada ya hii kuisha.
 
Back
Top Bottom