Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Mbona al Majiid aliniambia mpka kesho ili nifanye kama leo kutuma episode 3 kwa pamoja au hayakuwa makubaliano? 😅
Hapana tusimamie kanuni #4 hakuna mpango juu ya mpango tumalize kwanza kazi moja ya ahadi ya leo 2 alafu kesho ndo mpango mpya utaanza😅. Au unataka kwenda tofauti na kanuni zako binafsi za kazi?
 
Kuna ile "Asali haitiwi kidole" nilikuwa sijaisoma ni moto aisee,, nikija hapa nikakuta Abou Shaymaa hajaweka muendelezo wa hii "Nyuma ya mlango wa adui" najichimbia kule,, sijui ikiisha ile alosto yangu nitaimudu vipi,,
 
Kuna ile "Asali haitiwi kidole" nilikuwa sijaisoma ni moto aisee,, nikija hapa nikakuta Abou Shaymaa hajaweka muendelezo wa hii "Nyuma ya mlango wa adui" najichimbia kule,, sijui ikiisha ile alosto yangu nitaimudu vipi,,
Huku tunaendelea na sheria zetu utatukuta 😅
 
Haya sasa kaeni mkao wa kula naanza kuzimwaga,
Sema tatizo kila ninaposema niishie naona ndio patamu zaidi hadi now sijui niishie wapi au nilete tu episode moja yaan we acha tu.
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA TISINI NA TATU
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA MBILI : kwamba kijana huyo ni dereva msafirishaji “hata jina simfahamu, yeye nilimuagiza tu” alisema Emmy, ambae alikuwa anaachia kilio cha uongo na ukweli, “sasa hapa umekuja kufanya nini?” aliuliza Eze huku anazungusha macho mule chumbani, “mimi mara nyingi tu huwa nakuja kulala hapa mwenyewe, hasa nikitaka kubadilisha mawazo” alisema kwa kulalamika Emmy na kumfanya Eze atazame chini kwa aibu, “nifuateni” ilisikika sauti ya Side, akiwaeleza wale wenzake, huku anakimbia kutoka nje na kuelekea kwenye lift, ambayo ilionyesha ilikuwa inapanda juu na sasa ilikuwa ghorofa ya pili. …….ENDELEA…

Hapo Eze, ambae nikama alikuwa ameachiwa nafasi na vijana wake, sasa alikuwa amebakia peke yake na Emmy, “yani Eze leo umenidhalilisha sana, bora tuachane tu” alisema Emmy huku analia kilio cha kwikwi, “jamani Emmy, kwanini tufike hivyo, mimi bado nakupenda Emmy” alisema Ezze kwa sauti ya kubembeleza huku anapiga magoti sakafuni, “hapana kwa kweli, huwezi kuidhalilisha namna hii, yani nitembee na mtoto mdogo kama yule, naanzaje kumvulia nguo” alisema Emmy kwa sauti yake ile ile iliyoambatana na kilio cha kwikwi, “hapana mama yangu, usiseme hivyo siwezi kukuacha, basi nipe adhabu yoyote au niambie nikufanyie kitu kama fidia” alisema Eze kwa kuombeleza.

Hapo Emmy akaona amefanikiwa kumlaghai Eze na sasa ndio wakati wa kujipatia faida kwa kile kilichotokea, “una uhakika na unacho kisema Eze?” aliuliza Emmy kwa sauti iliyoanza kuchangamka, “ndiyo mama yangu, we sema chochote nitakufanyia” alisisitiza Eze na hapo kikapita kimya kifupi kilichodumu kwa sekunde chache, “sawa, nataka uingize million tano kwenye account ya Spesioza” alisema Emmy kwa sauti ya kudeka, “sawa… sawa nitaweka million saba” alisema Eze huku anasimama na kutoa simu yake mfukoni kisha akafanya utumaji wa fedha kwenye account aliyotajiwa namba zake na Emmy au mama P.******

Naam Chumba na nane cha ghorofa ya tatu kijana Deus, ambae alihakikisha watu hawa watano aliowakuta ndani ya chumba hiki, ambacho aliingia ikiwa njia ya kujiokoa toka kwenye shambalizi la risasi toka kwa watu, ambao aliamini kuwa wametumwa na mume wa Emmy, yaani yule mteja aliemletea bos chumba namba nane ghorofa la nne, tayari alikuwa ameshaweka bastola mezani, maana hakuihitaji tena, sasa alipiga hatua kuufuata mlango kwa lengo la kutoka nje.

Lakini kabla hajaufikia mlango akageuka haraka, kwa kuhisi kuwa kuna mtu mwingine mule ndani zaidi ya wale watano aliowashungulikia ni kweli alimuona mwanaume moja wa makamo akiinuka toka ubavuni mwa kochi haraka sana akajiandaa kumzibiti, lakini alipomtazama vyema hakuwa na silaha yeyote mkono mwake, “kijana tadhari naomba unisaidie kutoka humu ndani” alisema yule mzee kwa sauti yenye kutetemeka kwa uoga huku anachukuwa mkoba mweusi wa ngozi mezani, “kwanini nikusaidie?” aliuliza Deus, huku anamtazama mzee yule ambae sura yake sio ngeni usoni mwake, ni kama alishawahi kumuona mara kadhaa, “naitwa….” alisema yule mzee, lakini Deus akamuwahi, “hauna sababu ya kujitambulisha” alisema Deus kwa sauti tulivu kama ilivyo kawaida yake, na hapo mzee James akajua kuwa tayari kijana huyu alishamfahamu kutokana na umaarufu wake, maana alishawahi kuonekana kwenye vyombo vya habari, “sababu mimi sitojitambulisha mbele yako, hiyo ni sheria yangu namba moja” alisema Deus kwa sauti tulivu.

Hapo bwana James akatoa macho ya mshangao, maana hakujuwa sheria zake zinahusiana na nini, “ni vyema ukaokoa muda wangu kwa kunieleza sababu ya mimi kukutoa nje kabla sijalazimika kuumiza watu wengine ambao wapo njiani wananifuata” alisema Deus, japo sauti yake ilikuwa tulivu, lakini ilionyesha msisitizo, hata mzee huyu wa makamo akatambua kuwa kijana yule hakuwa anaigiza, alikuwa anahitaji sababu za msingi, “hawa jamaa walikuwa wanataka kuniuwa, wengine wapo nje sitoweza kutoka peke yangu” alisema mzee huyu ambae ni tajiri mkubwa sana hapa Africa, “wapo wangapi na wana silaha gani?” aliuliza Deus, kwa sauti ile ile tulivu, “wapo wawili, sijaona bunduki mikononi mwao ila wana mabegi makubwa” alisema tajiri James.

Hapo mzee James, akamuona kijana yule mwenye sura ya upole, anainama na kupapasa kwenye mguu wake wa kulia usawa wa sox, ambapo aliibuka na kisu kimoja kikubwa, kilichong’aa kwamakali yake. “ok! nifuate na muda wote ukae mita mbili nyuma yangu” alisema Deus huku anapiga hatua mbili, kisha akakamata kitasa cha mlango na kukionyonga, mlango nao ukafunguka wakati huo tayari bwana James alikuwa amesha msogelea Deus kama alivyoelekezwa, “zima taa” alisema Deus kwa sauti yake tulivu.******

Naam saa tatu na nusu usiku huu, general Sixmund akiwa nyumbani kwake akisubiri taarifa toka Tanzania kwa askari wake waliotumwa kwenda kumsaka Frank Nyati ambae alihitajika kwa mfalme Elvis Mbogo wa kwanza wa nchi ya #mbogo_land aje atoe majibu ya maswali yaliyokuwa yana muumiza kichwa mfalme huyo,

Mida hii ndiyo mida ambayo Sixmund alipokea simu toka kwa captain Amos Makey, ambae baada ya kusalimina Amos akaanza kueleza jinsi maongezi yao na kanal luten kanal mtoro jeshi la MLA, yani bwana Frank Nyati, “kikubwa anachosema ni kwamba msako wa saliti ndani ya jeshi la serikali, licha ya kuwa na lengo zuri, lakini ndani yake walikuwepo UMD, ambao waligeuza operation kupunguza nguvu ya serikali kwa kuuwa watu ambao kwa namna moja au nyingine wangekuwa kikwazo kwao katika kutekeleza azma yao ya mapinduzi” alieleza Amos, na hapo kengele ya tahadhari ikagonga kichwani mwa general Sixmund, “hilo ndilo tatizo kubwa, naimani mpaka sasa watakuwepo ndani ya serikali” alisema Sixmund kwa sauti iliyojaa fadhaha, “tena bwana Frank amesisitiza kuwa mtu huyo atakuwa mwenye nafasi kubwa na mwenye kuaminika serikalini” alisisitiza captain Amos, huku akieleza kuwa, “frank amesema kuwa, kuna baadhi ya watu wamewaingiza kwenye hili kwa makusudi ilikuweka chuki kati yao na serikali kwa lengo la kuja kuwa tumia baadae, mmoja wao ni bwana James” alieleza Amos.

Naaam hapo bwana Six akaona kuwa kuna umuhimu wa mfalme kulijua hilo mapema ili hatua za haraka zichukuliwe, “subiri maelekezo, wacha niongee na mfalme” alisema Sixmund na kukata simu.******

Hotel Sisterfada, wanaonekana askari wawili wa UMD, wakiwa bado wamesimama nje ya chumba namba nane cha ghorofa namba tatu, mmja kushoto kwa mlango na mwingine kulia kwa mlango huku wamebeba silaha zao migongoni mwao zilizohifadhiwa ndani ya mabegi makubwa, kuhofia kuwashtua wateja wengine wa hotel ile kubwa, waliendelea kusubiri mkuu wao na wenzao walioko ndani wamalimalize kikao na bwana James, kikao ambacho mpaka dakika hiyo, waliamini hakikuenda vyema, kutokana na kwamba, walisha sikia milio mingi ya risasi, walitambua kuwa tayari bwana Jaes amesha pigwa risasi kama ilivyopangwa endapo atakataa mpango wao.

Naaam wakiwa wanasubiri wenzao watoke, mara wakasikia mlango ukifunguliwa, wote wakatazama mlango wakitarajia kuwaona wenzao wakitoka nje, japo haikuwa hivyo, baada yake wakamuona kijana mmoja akitoka mule ndani akiwa amemshika bwana James na kumvuta kwa nguvu kama vile mwizi, nao wakatoa macho kwa mshangao, “boss anawaita ndani” alisema yule kijana huku anatembea kuelekea upande iliko lift ambayo ilikuwa inasoma kuwa inapandisha juu, wale jamaa bila kujiuliza mara mbili wakakimbilia ndani ya chumba, ambako walikutana na giza nene.

Lilikuwa kosa kubwa sana kwa vijana wale, maana ile kutahamaki walishtuka mlango ukifungwa kwa nje, ile wanataka kuwahi kuufungua wakasikia kacha, maana funguo ilikuwa inafunga mlango.

Alikuwa ni Deus Nyati aliefunga mlango kwa nje, ilikuwa ni mara baada ya wale vijana wawili kuingia kwenye mtego wake, haya fanya haraka, kuna watu wanaweza kuingia hapa sasa hivi” alisema Deus, huku anatembea kuelekea upande wa lift ambako pia kulikuwa na ngazi, huku bwana James akimfuata kama alivyo elekezwa, “kijana nina gari langu kule maegesho utaweza kuendesha?” aliuliza mzee James huku wakiendelea kutembea, “mpango ni kukutoa humu chumbani na sio zaidi ya hapo, isitoshe na mimi nina gari langu ambayo ndiyo ofisi yangu” alisema Deus kwa sauti kavu na tulivu kama ilikuwa imesetiwa mdomoni mwake, “unamaanisha wewe ni dereva wa taxi?” aliuliza james, wakati huo wameshazifikia ngazi na kuanza kushuka.

“hapana, mimi ni msafirishaji nasafirisha kitu chochote katika hali yeyote, muhimu kufuata sheria zangu tu” alijibu Deus, huku wanaendelea kushuka ngazi, “sawa, ni kiasi gani kunifikisha nyumbani nikiwa salama?” aliuliza James huku wanaendelea kushuka ngazi pasipo kujua kuwa ile wanapotelea kwenye ngazi tayari lift ilikuwa imesimama na mlango ukafunguka kisha wakashuka watu wa tano wenye kuvalia makoti marefu meusi na bunduki zao mikononi, wakiongozwa na bwana Songoro, Hesabu milango, mlango wa nne kushoto” alisema Songoro huku anapiga hatua kutembea kutoka kwenye lift na kutembea kwenye korido huku anahesabu milango,

Wakati Songoro anahesabu milango, huku Deus na mzee James walikuwa wanashuka ngazi kwa haraka, “laki tatu keshi” alisema Deus, wakati huo wanamaliza kushuka ngazi na kuibukia eneo la mapokezi, ambapo palikuwa peupe kabisa, “sawa imekubarika, nitakulipa mara mbili ya hizo cha msingi nifikishe nyumbani haraka, familia yangu itakuwa katika hatari” alisema mzee James huku akimfuata Deus ambae alikuwa anaongoza kuelekea nje ya jengo, mpango umekubariwa, tutatumia BMW S7 muda ni huu, mwisho wa mpango ni saa tatu na dakika arobaini na tano” alisema Deus huku anaongoza kuelekea gari liliko.

Naam sekunde chache baadae tayari walikuwa ndani ya gari, yaani BMW S7, na gari liliondoka mara moja huku Deus akisisitiza James afunge mkanda wa usalama.*******

Naam picha za tajiri mkubwa Africa akiwa na watu wanne watatu wakiwa na bunduki mikononi mwao, zinaonekana kusambaa kwa kasi sana kwenye mitandao ya kijamii zikiambatana na kichwa cha habari, JAMES KERVIN MFADHIRI WA KUNDI LA UMD TOKA MBOGO LAND, picha hizo za kushtua zinazagaa dunia nzima na kuwashangaza watu wengi sana, ni kutokana na umaarufu wa bwana James ambae ni mfanya biashara tajiri barani Africa.

Picha hizo ambazo zilikuwa na maelezo mafupi, yaliyoeleza kuwa, “pichani ni tajiri mkubwa afrika, bwana James Kervin, akiwa na general Kadumya, kiongozi wa kundi la waasi wa UMD toka nchini Mbogo Land, wakipanga namna ya kuondoa uongozi dhalimu wa kifalme toka madarakani”

“ikumbukwe tajiri huyo aliwahi kuhusishwa kimakosa katika uasi wa nchi hiyo mwana 1992, na kumsababishia hasara kubwa katika biashara zake pale alipoamua kutoroka nchini na familia yake huku akiacha biashara na mali zake nchini humo na baadae kuamua kujiunga na kundi hilo kwaajili ya kutimiza mapinduzi”

Hakika taarifa hii iliumiza vichwa vya watu wengi sana, kuanzia uongozi wa Tanzania ambao ulimchukulia bwana James kama mtu wa karibu wa serikali anaechangia kipato kikubwa kutokana na kulipa kodi, pia kurahishisha upatikanaji wa mahitajio ya wanachi wake.

Maoni na baadhi ya post za watumiaji wa mitandao ya kijamii ziliikosoa serikali ya kifalme ya mbogo land wakiita ni serikali kandamizi, serikali ambayo haikufaa kuendelea kuwepo madarakani, wengine walisema ni vyema kama wangebadilisha mfumo wa utawala na kuwa katika mfumo wa kuongozwa na rais aliechaguliwa na wananchi.

Lakini wapo waliopinga swala hilo, kuanzia hoja ya kubadilika kwa mfumo wa utawala, na pia swala la kwamba bwana James ni mfadhili wa kundi la waasi, “kama mwananchi anapata kila anachotaka, anagharamiwa masomo hata makazi, matibabu, na huduma zote muhimu kama umeme na maji anapata bure, kwanini wabadili mfumo” hayo ni baadhi ya maoni ya wachangiaji, “hapo lazima kuna mkono wa mtu, lengo ni kumchafua bwana James wamshushe kibiashara, usikute hata hizo picha zimetengenezwa” mmoja alisema hivyo, huku mwingine akisema kuwa, “hapo kuna mabepari wamesha tamani mali za #mbogo_land,

Taarifa hizi zilimfia mfalme Elvis wa kwanza, akiwa kwenye ofisi ndogo ya chumbani kwake, anapitia makabrasha mbali mbali na kusoma record za watu mbali mbali, wengi wao ni viongozi na askari wa nchi yake, “mume wangu, ni vyema kama ukiacha unachokifanya na kutazama hii” ilisikika sauti ya malkia Vaselisa na kumfanya Elvis ageuke kumtazama, akamuona anawasha projector kubwa iliyomulika ukutani nae akakaza macho kutazama ukutani akiona projector inajifungua.

Naam Projector inamaliza kujifungua na kitu cha kwanza ambacho Elvis anakiona ni picha kubwa inayomuonyesha bwana James akiwa amezungukwa na watu watatu wenye bunduki za kisasa, pamoja na kiongozi wa kundi la UMD, alie jiita General Erasto Kadumya wamekaa kwa pamoja huku mezani kukiwa na chupa ya pombe kali, juu ya picha kulikuwa na maandishi makubwa, “TAJIRI MKUBWA AFRIKA BWANA JAMES AKIWA NA KIONGOZI WA KUNDI ANALO LIFADHIRI LA UMD GEN ERASTO KADUMYA” inamshtua sana Elvis, ambae wakati huo huo anaona simu yake inaita, anaitazama na kuona kuwa mpigaji ni General Sixmund, akaipokea kwa haraka. …….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA TISINI NA NNE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA TATU : Naam Projector inamaliza kujifungua na kitu cha kwanza ambacho Elvis anakiona ni picha kubwa inayomuonyesha bwana James akiwa amezungukwa na watu watatu wenye bunduki za kisasa pamoja na kiongozi wa kundi la UMD aliejiita General Erasto Kadumya, wamekaa kwa pamoja huku mezani kukiwa na chupa ya pombe kali, juu ya picha kulikuwa na maandishi makubwa, “TAJIRI MKUBWA AFRIKA BWANA JAMES AKIWA NA KIONGOZI WA KUNDI ANALO LIFADHIRI LA UMD GENERAL ESTO KADUMYA” inamshtua sana Elvis, ambae wakati huo huo anaona simu yake inaita, anaitazama na kuona kuwa mpigaji ni General Sixmund, akaipokea kwa haraka. …….ENDELEA…

Na hakumpa hata mafasi ya kutoa salmu ya heshima ya kifalme, “mzee six, nini hiki nacho kiona kwenye mitandao?” aliuliza king Elvis kwa sauti yenye kujawa mshangao na mshtuko mkubwa, “mtukufu mfalme sijaingia mtandaoni jioni hii” alijibu Sixmund toka upande wa pili wa simu, nadhani muda huo huo akaanza kuperuzi kwa kutumia kifaa cha karibu yake, “kuna habari zina thibitisha kuwa James Kervin ni mshirika na mfadhiri mkuu wa UMD” alisema mfalme kwa sauti ile ile ambayo sasa ilionyesha hasira za wazi kabisa, “naona hapa, lakini mtukufu ni kwanini waachie picha kama hii kipindi ambacho wanampango wa kuingiza silaha nchini, wakati ni miaka mingi imepita toka bwana James akimbie nchini?” aliuliza Sixmund, kwa maana ya kutilia shaka.

Hapo king Elvis ni kama alishawishika kuingiwa na mashaka juu ya jambo hilo, “kwahiyo Six unataka kusema hii ni habari ya uvumi?” aliuliza king Elvis kwa sauti iliyoanza kupoa kidogo, “yote yana wezekana mfalme, maana habari toka kwa ARTroop tuliyo iagiza Tanzania kumsaka bwana Frank zinasema kuwa, wameongea na Frank na amewaeleza hisia zake juu ya kupandikiza chuki kwa baadhi ya watu na serikali ya nchii tukufu, iliwaweze kuwatumia baadae na mmoja wapo ni bwana James, hivyo inaweza kuwa ni tamaa za kibinadamu akaamua kujiingiza kwenye kikundi hicho au akakataa kujiunga na wao kuamua kumchafua kwa kupost picha hizo mitandaoni” alisema Sixmund.

Hapo mfalme akakumbuka jambo, katika ujumbe wa bwana Frank, “na vipi kuhusu huyo Frank, amekubali kutoa majibu ya maswali yangu?” aliuliza kinga Elvis, “ukweli Frank ametoa ushirikiano mkubwa sana, tofauti na vile tulivyo tegemea, Frank ameeleza kila kilicho tokea mwaka 1992 na jinsi mfalme Eugen alivyo danganywa na MLSA waliokuwa wakiongoza zoezi lile la kusaka waasi ndani ya serikali, na kwamba kilichofanyika ilikuwa ni makusudi na sio bahati mbaya au taarifa zisizo thibitishwa” alieleza Sixmund.

“kwahiyo Six, unataka kusema ndani ya askari walioshiriki zoezi lile walikuwepo waasi?” aliuliza Elvis akiwa katika bumbuwazi, maana sasa alianza kuona kwanini mfalme wa wakati huo alilaumiwa na mashirika makubwa ya haki za binadamu, “ndiyo mfalme, kwa mujibu wa Frank Nyati ni kwamba, “kikundi cha MLASA, kilichotumwa kutekeleza mpango huo, kilikuwa na baadhi ya washirika wa UMD, inasemekana baadhi wapo serikalini mpaka sasa na wana nafasi kubwa tu katika serikali yako” alisema Sixmund akizidi kumduwaza Elvis, ambae sasa alikuwa anasikiliza simu ile pamoja na mke wake malkia Vaselisa.

“Six, kwa maana hiyo watu walio uwawa wakati ule wakihusishwa na UMD, hawakuwa wahusika?” aliuliza Elvis kwa sauti iliyodhihirisha mshangao wa fadhaha aliokuwa nao, “mtukufu ipo wazi kabisa, tena waliouwawa kipindi kile ni watu waliokuwa wanaaminiwa na serikali, ni watu wenye uwezo mkubwa wakimapigano na sanaa ya vita, ni wale ambao walijitolea kwa moyo mmoja, nguvu na maisha yao kuitumiakia serikali, ndio maana hata sasa tumechukua muda mrefu kugundua uwepo wa kundi hilo kwa mara nyingine, sababu tumepoteza watu kama hao muda mrefu sana” alisema Sixmund.

Hapo Elvis akamtazama mke wake kama vile anamuuliza afanye nini, na mke wake akauliza kwa ishara ya midomo bila kutoa sauti, “muhusika mkuu ni nani?” hapo hapo Elvis akauliza, “huyo mhusuka mkuu aliepo serikalini ni nani?” aliuliza king Elvis, “mtukufu mfalme, kwa kweli mpaka sasa bado hatuja mfahamu, na kwa maelezo ya bwana Frank ni kwamba, tunahitaji ushahidi wenye nguvu kumtia nguvuni” alisema Sixmund, hapo nikama alipandisha hasira za king Elvis, nani kasema tunahitaji ushahidi, nadhani mume sahau kuwa hii nchi sio ya kisiasa, yani ni hivi nikibaini jina lake, huyo ataadhibiwa kutokana na sheria za mwaka 1894, atafungwa kamba kwenye nguzo, pembezoni mwa mji wa TT, na kushambuliwa kwa mawe mpaka afe” alisema Elvis alieonyesha kuwa mwenye hasira, “ndiyo mtukufu mfalme” alijibu Sixmund, na hapo mfalme akiwa mwenye hasira kali akatoa amri, “waambie vijana wako usiku huu wanaondoka kuelekea dar es salaam mpaka kuna kucha wawe tayari njiani wameshafika mbele yangu wakiwa na James kervin, sasa hivi nawasiliana na ubalozi watoe ndege itakayowapeleka dar es salaam” alisema king Elvis na kukata simu.

Ile kukata simu tu, akapiga simu kwenda ubalozi wa mdogo wa mbogoland uliopo mjini Songea, kichwani mwake akipanga kueleza itolewe ndege ya kuelekea dar, maana ubalozi wa hapa na ule wa dar es salaam ulikuwa na ndeg ndogo, pia king Elvis alipanga kuwa akisha malizana na balozi apige simu ikulu ya dar es salaam kuwasiliana na rais wa Tanzania kwaajili ya kupata kibali cha kumkamata bwana James Kervin ili aende mbogo land akaeleze juu ya habari zinazosambaa mtandaoni.*******

Naam mschana Caroline akiwa chumbani kwake amejilaza kitandani kwake, huku amevalia nguo nzuri za kulalia, nguo ambazo hata kama haukuwa na hamu ya kula, basi hamu ingekuja yenyewe, maana zilimkaa vyema, ungetamani ziwe nguo za kutembelea mtaani.

Mschana huyu ambae mpaka sasa sio dada yake, wala baba yake aliekuwa amerudi nyumbani, alikuwa ameshika simu yake anatazama picha ya kijana mmoja mwenye umbo la kivutia na sura ya upole, kijana ambae anahistoria kubwa sana katika maisha yake, “au niweke tangazo la kukutafuta mtandaoni” aliwaza Caroline, ambae sasa haikuwa tena kwaajili ya kumshukuru kijana huyu ila ni wazi alianza kuhisi kitu upendo moyoni mwake.

Wakati anaendelea kuitazama ile picha, ndipo ghafla ukaingia ujumbe dokezi kwenye simu yake, yani notifications, “tajiri mkubwa Afrika ni mdhamini wa kundi la waasi” ilimshtua kidogo Carlone, ambae aliamua kufungua ujumbe ule haraka kwa lengo la kusoma habari.

Ujumbe unafunguka na anachokiona kwenye ile ile habari, kinamfanya ajitoe kitandani haraka na kutoka chumban kwake, kisha akaelekea upande wa chumba cha mama yake, “mama!!!! mama!!!!!” aliita Caroline, na wakati huo akamuona mama yake anatokea chumbani kwake huku anaongea na simu, tena simu ambayo ilionyesha wazi haikuwa nzuri, “kuna nini baba Vero, mbona unanitisha” alisikika mama Vronica akiuliza hivyo, huku anatembea kuelekea sebuleni ambako alishika mango na kuona kama umefungwa vizuri.********

Yap! bwana Kadumya anazinduka toka gizani, anakutana na giza nene chumbani, huku sauti za miguno ya maumivu toka kwa vijana wake, ambao hawezi kuwaona kutokana na giza nene lilipo mle chumbani, “mzuieni huyo asiondoke” alipiga kelele Kadumya huku anapapasa pembeni yake kuona kama anaweza kuipata bastora yake aina ya Beretta 95, lakini kutokana na giza nene anaikosa, “boss wameshaondoka” isikikasauti.

Jibu lile lenye kushtua, hakulipenda kabisa bwana Kadumya, “wameondokaje nyie wapuuzi, halafu mbona mmezima taa, hebu washeni” alisema Kadumya huku anajiinua toka pale chini, wakati huo kwa haraka sana, mmoja kati ya wale vijana wawili walioingizwa mkenge na Deus akipapasa ukutani kutafuta switch ya kuwashia taa, ambapo sekunde chache taa ikawaka na kumfanya Kadumya aone vyema mle chumbani.

Kwanza kabisa bwana James hakuwepo, pili vijana wake wanne walikuwa wamelala chini mmoja amepoteza fahamu, mmoja amekufa kabisa na wawili wanaugulia maumivu ya risasi za miguu, pia kulikuwa na vijana wengine wawili, aliowaacha nje, nao wakiwa mle ndani na ndipo alipoiona bastora yake, “mnashangaa nini sasa, tuondoke tuwawai hao washenzi” alisema Kadumya kwa sauti ya juu yenye hasira na amri, huku anaiokota bastora yake mezani, “boss wametufungia mlango kwa nje, “alijibu mmoja kati ya wale vijana wawili, “khaaaaa!! mliingiaje ndani wakati mlikuwa nje?” aliuliza Kadumya huku ana usogelea mlango ila anashika kitasa tu, mlango nao ukafunguliwa toka nje, hapo uso kwa uso akakutana na kundi la watu wenye silaha mikononi mwao watu ambao aliwatambua kuwa ni watu waliokuwa wanamshambulia yule jamaa, aliewavamia chumbani.

“Mnamtafuta huyu mpuuzi alienivurugia mipango yangu, kwani hamjamuona huko mlikotoka?” aliuliza Kadumya kwa sauti ya ukali kidogo huku anawatazama wale jamaa, ambao walionyesha kushangaa kuwaona watu waliokuwa wanatoka nje huku nyuma yao wakiziona silaha zao za kisasa zikiwa zimezagaa sakafuni sambamba na watu wengine kadhaa walioonekana wamelala sakafuni huku damu zikiwa zimetapakaa sakafuni.

Niwazi kabisa kuwa, hapakuwa na hata mmoja kati ya wale watatu waliowaona pale mlangoni anaefanana au wangemshuku kuwa ndie mtu wanaemfuata, “inamaana ametoka humu ndani hai? wakati muna silaha nzito kama hizi?” aliuliza Songoro kwa sauti iliyojaa mshangao, “ni upuuzi, mbona wewe amekupita hapa hapa na haukumuona?” aliuliza Kadumya kwa namna ya kumshangaa au kudhaurau kundi la wakina Songoro, kuna njia nyingi za kutokea hapa, vipi kuhusu wewe umeshindwa kumzuia mtu asie na hata wembe kwa silaha hizi ulizo nazo” aliuliza Songoro.

Hapo Kadumya hakujibu swali hilo, baada yake aliwageukia vijana wake, “haraka sana kusanyeni hizo silaha kisha tuwasaidie hao kutoka hapa hotelini, nadhani polisi watakuwa njiani” alisema Kadumya ambae ni kama alimzindua Songoro, “haraka wahi chini asiondoke huyo mshenzi” alisema Songoro kwa sauti ya kupayuka.

Hapo vijana wake wakaondoka kwa haraka kuelekea kule walikotoka, safari hii wakipanga kutumia ngazi, hata walipo ikaribia ngazi ambayo ipo karibu na lift wakaona mlango wa lift unafunguka na wakina Said wakatoka kwenye lift, na wao bila kuuliza wakaungana wenzao kushuka chini kupitia kwenye lift, wakiwaacha wakina Kadumya wanachukua vitu vyao ikiwa pamoja na bunduki zao, kisha akawachukuwa watu wao, ambao wale watatu walijikongoja kwa kuchechemea, huku wale wawili wazima, wakiubeba mwili wa mwenzao na kutafuta mlango wa nyuma unaotokea moja kwa moja kwenye maegesho ya magari.********

Naaam saa tatuna dakika arobaini na nne, BMW S 7, linaonekana likikatiza mitaa ya segerea mwisho kueleka upande wa kinyerezi, dereva akiwa kimya anakanyaga mafuta kwa nguvu na kufanya gari litembee kwa speed kali sana huku mzee abiria wake akiongea na simu, “haikuwa biashara nzuri, jifungieni hakikisheni hamfungui mlango kwa mtu musiemfahamu, mimi nipo njiani nakuja” alimaliza kuongea na simu na kuikata, wakati huo huo simu yake ikaita.

Mpigaji alikuwa ni bwana Selestine Kasanzu, yeye ni waziri wa viwanda na biashara wa serikali ya jamuhuri ya muungano, mtu ambae huwa anawasiliana nae mara kwa mara kutokana na wizara ya kiongozi huyo, akaipokea na kuiweka sikioni, “habari za jioni mheshimiwa” alisalimia James, “bwana James hili linaloendelea mtandaoni ni kweli? na kwanini ufanye hivyo? huoni kama unajiharibia heshima yako?” aliuliza waziri ambae sauti yake ilionyesha kusikitishwa na jambo fulani, “kuna nini kimetokea mheshimiwa?” aliuliza kwa mshtuko bwana James. …….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Naaam wakiwa wanasubiri wenzao watoke, mara wakasikia mlango ukifunguliwa, wote wakatazama mlango wakitarajia kuwaona wenzao wakitoka nje, japo haikuwa hivyo, baada yake wakamuona kijana mmoja akitoka mule ndani akiwa amemshika bwana James na kumvuta kwa nguvu kama vile mwizi, nao wakatoa macho kwa mshangao, “boss anawaita ndani” alisema yule kijana huku anatembea kuelekea upande iliko lift ambayo ilikuwa inasoma kuwa inapandisha juu, wale jamaa bila kujiuliza mara mbili wakakimbilia ndani ya chumba, ambako walikutana na giza nene.
Vijana wajinga sana mpka wanafungiwa kizembe 😅
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA TISINI NA TANO
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA NNE: Mpigaji alikuwa ni bwana Selestine Kasanzu, yeye ni waziri wa viwanda na biashara wa serikali ya jamuhuri ya muungano, mtu ambae huwa anawasiliana nae mara kwa mara, kutokana na wizara ya kiongozi huyo, akaipokea na kuiweka sikioni, “habari za jioni mheshimiwa” alisalimia James, “bwana James hili linaloendelea mtandaoni ni kweli, na kwanini ufanye hivyo, huoni kama unajiharibia heshima yako?” aliuliza waziri ambae sauti yake ilionyesha kusikitishwa na jambo fulani, “kuna nini kimetokea mheshimiwa?” aliuliza kwa mshtuko bwana James. …….ENDELEA…

Hapo waziri Kasanzu, akaanza kueleza jinsi habari za ufadhili wake wa kikundi cha uasi cha UMD zilivyo tapakaa mtandaoni, “hizo habari sio za kweli, tena umepiga wakati mzuri wazuri, naomba ulinzi wako” alisema bwana James, ambae alieleza kila kitu, toka alipopokea simu toka kwa waziri wa ulinzi wa #mbogo_land, na kualikwa kwenye kikao ambacho kilikusudiwa kuwa cha biashara na baadae akaja kufahamu kuwa ni kikao cha kupewa ombi la kukifadhiriy kikundi cha uasi,

Bwana James alieleza kila kitu kilivyokuwa mpaka kuokolewa na kijana alievamia chumba kwa bahati mbaya, “ok! wacha niwasiliane na ikulu kuomba wizara ya mambo ya ndani au ya Ulinzi walete ulinzi hapo kwako, kwa sasa hakikisha unakuwa sehemu salama” alisisitiza waziri Kasanzu, kabla hawajakata simu.

Wakati huo dereva wa gari hili , yani kijana Deus Frank Nyati, aliekuwa anawaza kuachana na kazi hii ya hatari ya usafirishaji mara baada ya kufanya kazi ya mwisho itakayoanza saa nne, lakini sasa kijana Deus alionekana kuvutiwa na maongezi ya simu ya abiria wake, ambae alionyesha kuwa ni mtu mwenye fedha nyingi na mwenye kufahamika na kutambuliwa na serikali ya Tanzania, “samahani mzee, una uhusiano wowote na kundi la UMD si lilisha toweka zamani sana huko nchini #Mbogo_land?” aliuliza Deus kwa sauti tulivu huku kichwani mwake ikimjia kumbu kumbu ya hadithi ambayo baba yake aliwahi kumsimulia, hadithi iliyowahi kutokea mwaka 1992.

“sina uhusiano nao, waliniletea madhara makubwa sana hapo zamani na leo wanajaribu kunishawishi, niwafadhili kuiharibu nchi yangu mwenyewe, tena kwa kudai nilipize kisasi wakati wao ndio walioidanganya serikali kuwa mimi ni muasi” alijibu mzee James, huku Deus akianza kupata picha ya mtu aliembeba na kitu kilicho tokea, kwamba huyu ni tajiri James Kervin, “kwanini mlifikia hatua ya kushikia bunduki wakati mlikuwa katika makubaliano?” aliuliza Deus, ambae kwa namna fulani aliona kama vile haya muhusu na upande mwingine alikuwa anataka kuthibitisha kile kilicho mtokea baba yake mwaka huo wa 1992, “walitaka kuniua kwasababu nimewakatalia kuwapa fedha ya kufanyia ujinga wao ambao ungesababisha mauwaji nchi #mbogo_land, ni bahati ulikuja kwa wakati kijana wangu” alijibu mzee James, ambae mpaka dakika hii hakuwa na wazo la kwamba kijan huyu, ndie yule ambae alimuokoa binti yake Caroline kwenye ajali ya tren,

Wakati huo tayari walikuwa wameshafika kinyerezi mwisho na kwa maelekezo ya james, Deus akakata kona kulia na kuifata njia inayo ingia mtaani, upande ambako nyumba ya bwana James iliko, “una mpango gani kwaajili ya usalama wako mzee?” aliuliza Deus kwa sauti tulivu, huku anatazama saa yake, ilikuwa ni saa tatu na dakika hamsini, alibakiza dakika kumi pekee, kuanza safari mpya “nimesha wasiliana na waziri Kasanzu, anafanya mpango nipate ulinzi haraka” alijibu James, wakati huo gari likiwa lina simama, mbele ya geti kubwa la nyumba ya tajiri huyo, “ok! nakutakia ulinzi mwema, ukihitaji usafiri nipo kwaajili hiyo, namba yangu ni hii hapa pamoja na sheria zangu zipo nyuma ya kadi hii” alisema Deus huku anampatia mzee James karatasi ndogo mfano wa card ya karata.

Mzee James akaipokea ile card, “umefanya vyema kijana, tena ukihitaji nitakuajiri kama mlinzi wangu binafsi, hasa katika kipindi hiki cha majanga, nitakulipa fedha nyingi sana” alisema mzee James huku anafungua mkoba wake na kuiweka ile card, kisha akatoa kijitabu cha kuandikia hundi, yaani check, pamoja na kalamu, “nakulipa millioni sit…” alisema mzee James huku anaanza kuandika, lakini kabla hajamaliza kuongea Deus akamuwahi “chukua hiyo card kisha soma sheria namba mbili” alisema Deus kwa sauti yake ile ile tulivu huku anaelekeza macho yake kwenye geti la uzio mkubwa wa jumba hili la kifahari, ambalo lilikuwa linafunguliwa taratibu, mzee James akaichukua ile card na kusoma maelezo.

Ni kweli sheria namba moja, ilikataza kujuana majina, na kweli mpaka sasa hakuna aliejua jina la mwenzie kwa kutajiana, japo Deus alisha mfahamu mtu aliembeba, hiyo laini, sheria namba mbili ndiyo ilikuwa tatizo kwa mzee James, HAKUNA MKOPO NA MALIPO NI CASH, kwa maana malipo ni mkononi.

Hapo mzee Jame akajua kuwa tayari ameshalikoroga, sababu kazi ya kijana huyu, aliishuhudia kwa macho yake mwenyewe wala hajasimuliwa na mtu yoyote, “samahani kijana, lakini mimi sitembei na fedha nyingi kiasi hicho, na fedha ya dharula niliyokuwa nayo nimeiacha kwenye gari kule hotelini” alisema mzee James kwa sauti ya kuomboleza iliyojaa uoga na wasi wasi huku moyoni mwake akiomba roho ya huruma imshukie kijana huyu.

Lakini licha ya maneno hayo, kijana huyu ambae hakupepesa macho ndio kwanza alitazama muda, “sheria yangu ya mwisho ni kuheshimu na kusimamia sheria zangu na zako, naomba cash haraka nina kazi saa nne kamili” alisisitiza Deus, huku anatazama saa yake kwenye dash board ya gari, ambayo ilionyesha kuwa ni saa tatu na dakika hamsini na mbili, alibakiza dakika nane tu.

Hapo mzee James akatazama kwenye gate, ambako aliweza kumuona mke wake na binti yake Caroline, wakiwa wamesimama mbali kwenye kibaraza cha nyumba ile huku wakilitazama lile gari kwa macho ya uoga na wasi wasi, huku mlinzi aliekuwa karibu akianza kulisogelea gari.

Kijana wangu nitakulipa million hamsini au mia ukikubali kulipwa kwa cheki naomba unisaidie si unaona mwenye sina kitu hapa” alisema mzee James kwa sauti ya kuomboleza huku anajipapasa mifukoni na kutoa wallet yake.

Hapo bila kusema kitu, Deus anageuka na kuichukuwa ile wallet kwa mtindo wakuipora, kisha anaifungua na kukutana na vitambulisho kibao na kadi za benki, zaidi ya hapo kulikuwa na shilingi 1000 ya mbogo land, ambayo kwa fedha ya Tanzania ni sawa na shilingi elfu kumi, Deus akaichukua na kuiweka mfukoni, kisha akamrudishia mzee James wallet yake, “siku nyingine tukikutana jitahidi kufuata sheria zilizotolewa, zinazotolewa, na zitakazotolewa” alisema Deus, huku anabofya kitufe fulani kwenye mlango wa gari lake, kisha akafunua kitu kama mkebe kati kati ya seat yake na ile ya abiria, na kikajitokeza kioo chenye kuwaka taa, mfanano wake ni kama kikokotozi (carculator) , au kilonga mbali (simu), maana kilikuwa namba akabofya juu ya zile namba mfano wa hizi simu za kisasa, simu tanashati au simu janja kisha ukasikika mlio “tii!! tii! tii!”

Muda wote mzee James alikuwa anamtazama kijana huyu kwa macho ya mshangao, maana hakuamini kama anamuacha kwa malipo ya elfu kumi, baada ya millioni za fedha, “unaweza kushuka” alisema Deus na hapo mzee James akafungua mlango wa gari na kutoka nje ya gari, “samahani sana kijana wangu, ni uzembe wangu wakuto kufuatilia sheria zako, ila naamini tutakutana tena kijana wangu na mambo yataenda sawa” alisema mzee James kisha akafunga mlango na gari likianza kuondoka kwa speed ndogo, kuifuata barabara na kila sekunde gari lile lilizidi kuongeza mwendo mpaka sekunde ya kumi tayari lilishatoweka macho pake.

Ile mzee James anageuka kutazama kwenye geti, ili aningie ndani tayari mke wake na binti yake walikuwa wameshamfikia pale alipokuwa amesimama analishangaa BMW S7, “mume wangu kuna usalama kweli?, hawajakudhuru hawa washenzi?” aliuliza mama Veronica, huku anamkagua mume wake wakati wanatembea kuingia ndani, “huyu kijana alienileta aliwanyoosha adabu, bila yeye sasa ningekuwa marehemu” alisema mzee James kwa sauti kama ya kutokuamini hivi na wakati huo huo akasikia simu yake inaanza kuita, alipoitazama mpigaji alikuwa ni waziri wa biashara bwana Kasanzu, “funga geti usimfulie mtu yoyote mpaka nikuambie, alisema mzee James kwa sauti ya msisitizo kumuambia mlinzi huku anapokea simu.

“naaam mheshimiwa” alisema mzee James huku anaendelea kutembea kuelekea ndani, akifuatiwa na mke wake na binti yake, “tayari serikali imekupatia ulinzi, askari wa jeshi la ulinzi wasiopungua thelathini toka kikosi cha karibu na hapo uwanja wa ndege muda wowote wataingia hapo kwako” alisema Kasanzu, na bwana James ambae sasa alikuwa ameshaingia ndani anafunga mlango akashukuru sana, “asante sana bwana Kasanzu, hakika wale watu wanaroho mbaya” alisema James, kabla hawajaagana na kukata simu, kisha bwana James kuanza kuwasimulia mke na binti yake juu ya kilichotokea, pasipo kujua kuwa mmoja hakuwepo pale nyumbani.*******

Yap sasa turudi mbezi mwisho, sasa tunafika maeneo ya jirani kabisa na stend ya malamba mawili, linaonekana gari aina ya Land Rover Puma, jipya kabisa lenye watu ndani yake, kulikuwa na watu tisa, baadhi yao walivalia nguo za kiraia na wengine walivalia mavazi ya jeshi la polisi.

Kati ya hao Tisa, mmoja wao alikuwa ni mschana mrembo Veronica, huyu ndio yule doctor au unaweza kumuita pacha, ambae kama angekuwa na mikojo ya karibu, tayari angekuwa amesha lowesha seat za gari la watu, “oya muda huu, ndio muda muafaka” alisema mmoja wao, ni yule ambae alimchukua Veronica pale bar, “ni sawa inabidi aende haraka, nadhani mumesikia mpango wa kwanza umeshindikana, huu inabidi ufanikiwe vizuri” alisema mwingine aliekaa seat ya mbele kabisa ya gari, ambae hakugeuka wala hakuonekana vyema sura yake kutokana na giza la mule ndani ya gari, ongeza na miwani ya giza aliyo ivaa.

Naam bwana Zaid Tambwe akamtazama Veronica, ambae kiukweli uoga wake ulikuwa unaonekana wazi wazi, “sikia mwanamke, ni vyema kama ukiacha uoga na kufanya tulicho kuelekeza, maana kazi yako ni ndogo na nyepesi sana” alisema Tambwe yani yule ambae alimchukuwa Veronica kule bar, na veronica akaitikia kwa kichwa kukubaliana na jambo hilo, lakini uoga ulionekana wazi usoni mwake, “ok! nenda” alisema Tambwe na hapo kwa roho shingo upande, Veronica akatoka kwenye gari na kuelekea ndani ya ukumbi wa ile bank ya hifadhi ya mali za wananchi ambako aliingia ndani moja kwa moja, wakati huo nyuma yake likaonekana gari aina ya Nissan Extral, oya kaeni tayari, mzigo huo unaingia” alisema yule aliekaa seat ya mbele, wote wakalitazama gari lililokuwa linaingia.

Lilikuwa ni mali ya bwana Lumend Endrew Manyonyi, mfanya biashara mkubwa sana hapa jijini dar es salaam, ambalo lilisimama karibu kabisa na mlango wa kuingilia ndani ya benk, kisha akashuka mmoja akiwa amebeba sanduku lenye ukubwa wa kipimo cha kati na kuingia nalo ndani ya benk ile, “hivi huyo dereva wa BMW mbona simuoni?” aliuliza Tambwe, huku anatazama saa yake kwenye simu, ilikuwa ni saa tatu na dakika hamsini na saba…. …….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao hapa hapa jamii forums
 
Vijana wajinga sana mpka wanafungiwa kizembe 😅.
Kadumya mwenye kamuogopa Deusi na vijana nao ni vinondo wasio fikiria

Eze ni kama Kisonge Kasongo yeye anaonewa na mke wake Bado pia mchepuko unamuonea afu anataka kuongoza genge la wahuni mahiri lazima wawe vinondo tu.
 
Kadumya mwenye kamuogopa Deusi na vijana nao ni vinondo wasio fikiria

Eze ni kama Kisonge Kasongo yeye anaonewa na mke wake Bado pia mchepuko unamuonea afu anataka kuongoza henge la wahuni mahiri lazima wawe vinondo tu.
Kwahy bwana eze moto ndani na nje 🤣
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA TISINI NA SITA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA TANO: Lilikuwa ni mali ya bwana Lumend Endrew Manyonyi, mfanya biashara mkubwa sana hapa jijini dar es salaam, ambalo lilisimama karibu kabisa na mlango wa kuingilia ndani ya benk, kisha akashuka mmoja akiwa amebeba sanduku lenye ukubwa wa kipomo cha kati na kuingia nalo ndani ya benk ile, “hivi huyo dereva na wa BMW mbona simuoni?” aliuliza Tambwe huku anatazama saa yake kwenye simu, ilikuwa ni saa tatu na dakika hamsini na saba…. …….ENDELEA…

“tutafanyaje kama asipo onekana kabisa” aliuliza mwingine, wote wakionekana kuwa na mashaka, “acheni uoga, hiyo ni kazi yake na anajali muda, hawezi kuchelewa, tena tuna dakika nne tu za kumaliza kazi, nendeni haraka, kumbukeni mpango huu unategemewa kufanikisha mapinduzi” alisema yule wa seat ya mbele, ambae toka mwanzo amekuwa akiongea bila kugeuza sura yake, akionyesha kusisitiza mafanikio “ndiyo mkuu, tutafanya kwa ufanisi wa hali ya juu” walijibu wote watatu kwa pamoja huku wanashusha sox zao walizo vaa kichwani yaani mizura na kuziba nyuso zao huku sox hizo zikiacha macho na midomo yao wazi, kisha wakashuka toka kwenye gari, wakiwa wamevalia makoti mazito ya baridi japo kulikuwa na joto kali, kisha wakaanza kutembea kuelekea kule jengo la hifadhi liliko, ambako bado watu walikuwa wanaingia na kutoka.

Naaam kabla hata hawajalifikia jengo lile, wakina Tambwe ambao walikuwa wanawasindikiza kwa macho vijana wale, mara wakaliona gari dogo aina ya BMW jeus likiwapita na kuelekea upande wa mjini likienda kusimama mita kama mia moja hamasini toka pale walipo, “huyooooo! nilidhania kakwepa mtego, kumbe amejiingiza mwenyewe” alisema yule aliekaa seat ya mbele huku anacheka kwa dharau.

Hapo Tambwe akatazama saa kwenye simu yake na kuacha mdomo wazi kwa mshangao, “mh! huyu jamaa sio wa mchezo” alisema Tambwe kwa sauti iliyojaa mshangao, “haijalishi, wacha picha ianze” alisema yule wa seat ya mbele huku anavua miwani na kugeuza sura yake kwa mara ya kwanza kutazama nyuma, “nyie shukeni musogee eneo la tukio, tunadakika mbili za kutoka na mzigo” alisema yule jamaa ambae sasa ndio tunafanikiwa kuiona sura yake kuwa ni bwana Ramadhan Mbwambo, ambae ni wazi kabisa alionekana kutotaka aonekane sura yake mbele Veronica.

Na hapo wanashuka wale vijana wa nne walio valia sale za jeshi la polisi huku wakiwa wameshika bunduki zao aina ya SMG mikononi mwao.*****

Shekilango bado mambo yalikuwa moto, ni dakika zaidi ya kumi na tano zilikuwa zimepita, toka kusikika kwa milipuko ya risasi, wakati Songoro anavuruga kila kona ya hotel kumtafuta dereva wa BMW, huku General Kadumya akifanikiwa kuingia kwenye gari na vijana wake pamoja na mwili wa kijana wake mmoja, kisha wakaondoka zao kuutafuta uelekeo wa segerea kinyerezi kwenda kumkamata bwana James ambae ni muhimu kumuua kabisa kabla haja ongea lolote kwa mtu yoyote, na hata walipofika maeneo ya njia panda kuingia barabara kuu ya morogoro, wakapishana na gari tatu za polisi, zikiingia hotel kwa fujo.

Na kwa kulijuwa hilo, bwana Songoro ambae alikuwa ndani ya hotel akatokea mlango wa nyuma kabisa, sio wa kwenye maegesho ni wa nyuma kabisa na kutokomea vichochoroni, huku akipiga simu kwa CP Ulenje, kwamba anahitaji magari yake ambayo yalikuwepo pale hotelini, “inamaana ni wewe ndie ulie fanya huo upumbavu?” aliuliza Ulenje kwa mshangao, “nilikupigia Ulenje, lakini hukutaka kupokea simu” alisema Songoro kwa sauti ya ukali yenye kupayuka, “tatizo Songoro ukisha panga maamuzi yako humsikilizi mtu, angalie usije kuvuruga mipango ya watu, na nilikuambia huyo mtu wako anaenda kukamatwa muda mfupi ujao” alisema Ulenje kwa sauti ya kumtuliza Songoro, ok! ongea na vijana wako, waambie wayaache magari yangu na sasa hivi watu wakachukuwe magari” alisema Songoro na kukata simu.

Baada ya hapo zilipita dakika chache wakiwa wamesimama kwenye chochoro za majengo ya wapangaji wa NHC, mara simu ya Songoro ikaita, alipoitazama alikuwa ni Ulenje, akaipokea mara moja, “waambie waende sasa hivi, kabla vikosi zaidi havijaongezeka pale hotelini” alisema Ulenje kwa msisitizo.*******

Yap! mida hii mbogo land, TTC, yani Trench Town City, Chotopela akiwa anakunywa wine yake taratibu huku anaperuzi mtandao akitazama maoni ya wananchi juu ya habari ya tajiri mkubwa Africa bwana James Kervin kukifadhili kikundi cha waasi cha UMD, “watashangaa watakapo okota mzoga wake, na lawama zote zikienda kwa king Elvis na erikali yake ya kilofa” alijisemea Chitopela huku ana tazama simu yake ndogo ambayo ilikuwa inaanza kuita.

Huyo alikuwa ni general Kadumya aliemfanya Chitopela atabasamu, huku anaichukua simu yake taratibu kisha akaipokea na kuiweka sikioni, “hallow General wangu mchapa kazi, mipango inaendaje” aliuliza Chotpela kwa sauti ya iliyojaa raha na furaha na raham “mheshimiwa James ametutoroka lakini tunaelekea nyumbani kwake, ni lazima tumkamate haraka kabla polisi hawajaenda kumpatia ulinzi, na kama hajaenda huko tutaondoka na mke wake na mtoto aliebakia, maana mmoja tayari tunae, kisha tuta mpigia simu ajisalimishe” alisema Kadumya na hapo Chitopelah, alicheka kidogo, “anajisumbua huyo mpuuzi, maana mpaka sasa amesha chafuka, watu wanamchukulia kama mtu mwenye mipango ya mapinduzi ya umwagaji damu, na wakati watu wanaendelea kumnyooshea vidole na kumsimanga tayari yeye atakuwa anachungulia kifo” alisema Chitopela kwa kujiamini, ila hakikisheni hyo mtu anakamtwa kabla ya jua kuchomoza” alisisitiza Chitopela.

Maongezi yalichukuwa dakika tano nzima, huku Kadumya anatoa ahadi ya kuwa lazima watampata bwana James na kumfunga mdomo, “lazima wataikota miili ya James na binti yake, hawezi kutufanya sisi wapuuzi, yani mipango ya miaka yote hii yeye aje kuivuruga kwa nusu saa” alisema Kadumya, ambae kiukweli ungeweza kutambua jinsi alivyo vurugwa, “hivi huyo mpuuzi unasema aliingiaje ndani?” aliuliza Chitopelah, ambae ni wazi alishangazwa na uibukaji wa kijana huyu mvuruga mipango, “ni mshenzi mmoja alikuwa amefumaniwa na mke wa mtu, sasa katika kukimbia ndio akajikuta amevamia chumba chetu na kuvuruga kila kitu, na mbaya zaidi akasababisha James atoroke” alisema Kadumya, “ok! usiache kunipa taarifa, na kama kuna kitu munahitaji nijulisheni mapema, kumbuka tayari MLA wapo Tanzania, wamekutana na Nyati, hivyo kuweni makini” alisema Chitopelah kabla awajaagana na kukata simu.********

Naaam, akiwa nyumbani kwake Kinyerezi yeye na familia yake anawasimulia kilichotokea, mzee James na familia yake wanasikia sauti ya ngurumo za magari nje ya nyumba yao, hapo sasa kikazuka kizungu mkuti, hawakujua kama ni magari ya jeshi au wakina Kadumya, na wakati wana tazamana usoni wakiuliza maswali bila kutoa sauti, mara wakasikia mlinzi akigonga mlango, “boss boss kuna wanajeshi wamekuja, wanataka kukuona” hapo kidogo James akatuliza roho yake, “sawa sawa naa'nana kuja” alisema tajiri huyu mwenye jina kubwa Africa huku anainuka toka kwenye kochi na kuufuata mlango.

Na mara baada ya kutoka nje, anakutana na askari wanne mbele yake waliovalia mavazi ya vita, na silaha zao aina ya SMG mikononi, mikebe mitatu iliyofungwa kwa pamoja ikionekana kuning’inia kwenye silaha zao.

“Habari za jioni mzee James, sisi ni askari toka kambi ya jeshi ya jeshi ya mbawa za anga” alisalimia mmoja kati ya wale wanajeshi, aliekuwa na alama za nyota mbili mabegani mwake, “salama kabisa asanteni kwa kufika haraka hapa nyumbani, maana nilikuwa na wasi wasi kama wangenivamia hawa washenzi” alisema mzee James ambae licha ya kuona askari, lakini bado uso wake ulikuwa katika wasi wasi, “ondoa shaka mzee askari ni wengi wapo hapa, na wote wanasilaha, cha msingi hakikisha hakuna mtu kutoka nje, na kama kuna atakae ingia muda wowote, tujulishe mapema kabla hajafika, maana tumesha weka mafuruku ya kukatiza eneo hili mtu yeyote” alisema yule askari mwenye nyota mbili ambae alikuwa ameambatana na wenzake wenye vyeo mbali mbali, wawili wakiwa wanatepe mbili mfano wa V, na mwingine mmoja akiwa na tepe tatu mfano wa V.

“kwa sasa sitegemei mgeni yeyote na familia yangu yote ipo…” kabla hajamaliza kusema, akageuka nyuma kumtazama mke wake na binti yake, “hivi mama Carlo, mbona toka nimefika sijamuona Vero, yupo wapi?” aliuliza James kwa sauti yenye kutilia mashaka.

Hapo mama Vero na binti yake wakatazamana kwa macho ya kukosa jibu, “mnataka kuniambia kuwa Vero hayupo nyumbani?” aliuliz mzee James huku anatoa simu yake na kupiga namba ya Veronica ambayo ilileta jibu kuwa, namba haipatikani, wasi wasi ukatanda kati yao, “mzee punguza wasi wasi, naamini binti yako atakuwa salama, kama wangekuwa wameshamteka lazima wangekupigia simu na kukueleza ili wakupate wewe” alisema yule luteni, “sawa kijana, basi sisi wacha tupige simu kazini kwake, ili kujua kama ameenda huko pengine kulikuwa na mgonjwa wa dharula” alisema mzee James, ambae pia aliwaeleza wale wanajeshi kuwa kwa mahitaji ya vinywaji na vyakula, “nitatoa fedha kwaajili hiyo, cha msingi nyie mutajuwa namna ya kupata mahitajio hayo” alisema mzee James kabla ya kuingia ndani na kuanza kupiga simu sehemu zote ambazo, aliamini kuwa angempata binti yake.*********

Yap turudi tena Sisterfada hotel. ambako sasa tunaweza kuona wakina koplo Cheleji na askari wengine wengi wakiwa wamezagaa pale hotelini wanapekuwa kila kona kusaka waarifu, ambao wametoka kushambulia eneo hili kwa silaha, huku wakiwa hawaja jua chanzo cha kufyetuliana risasi, ndio wakati ambao vijana wa Songoro walipokuja kuchukua magari yao na kumkuta koplo Cheleji ambae aliwakabidhi magari nao wakaondoka haraka huku wakipishana na magari mawili meupe yenye namba za kiraia, yalioyokuwa yanaingia kwa mwendo wa kasi sana pale Sisterfada hotel.


Naam magari yale yalisimama mbele ya jengo kisha kila gari wakashuka watu wawili na kuelekea kwenye mlango mkubwa wa vioo, huku askari wakiwa wametapakaa eneo hilo na wawili wakiwa wamesimama mlangoni wakiwazuia wanaoingia na wanao toka, “”sisi ni maafisa usalama toka TSA, tunahitaji kuchunguza kwa undani eneo hili kutokana na tukio lililotoka kutokea muda mfupi uliopita, maana imebainika kuwa ni tukio linalo husisha nchi mbili” alisema mmoja kati ya wale watu wanne waliovalia nguo zao nzuri za kiraia, huku mmoja akiwa amebeba briefcase, yani sanduku dogo jeusi, “hooo karibuni” alisema yule polisi, huku akiwapisha nao wakaingia ndani, muda wote koplo Cheleji akiwa amesimama pembeni.

Ukweli leo kulikuwa na wakati mgumu kwa Cheleji, hasa kwenye kutumiwa katika ulinzi wa wavunja sheria, maana leo walikuwa ni vikundi vya askari toka sehemu mbali mbali, sio kama alivyozoea kuwa yeye na washirika wenzie wanao mfanyia kazi CP Ulenje, taratibu Cheleji akasogea pembeni na kupiga simu kwa CP Ulenje, “afande naona inshu imevamiwa na usalama wa taifa, kama vipi tutoe kwenye hili jukumu” alisema Cheleji, lakini ombi lake halikukubaliwa, “sikia Cheleji, ni muhimu wewe kuendelea kubakia hapo ili uweze kujua wamegundua nini hao jamaa, si unajua kuwa wakina Kadumya ni watu wetu, jambo lao ni jambo letu, isitoshe watatuwezesha fedha nyingi, cha kufanya uwe nao karibu hao jamaa kwa kila watachokuwa wanakifanya” alisikika Ulenje akiongea kwa namna ya kusisitiza na kushawishi, “sawa afande” alijibu Cheleji na kukata simu, kisha akaelekea ndani ya jengo lile la hotel.

Pale mapokezi hakuwaona kabisa wale jamaa wanne, wala jamaa wa mapokezi au meneja wa hotel, “wameenda wapi hawa jamaa” aliuliza Cheleji, akimuuliza mmoja wa askari aliekuwepo pale eneo la mapokezi, “wameelekea chumba cha kuongozea camera” alijibu yule askari huku akionyesha upande wenye chumba cha kuongozea camera za usalama wa jengo ilo…..….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Back
Top Bottom