NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA TISINI NA TATU
MTUNZI :
Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA MBILI : kwamba kijana huyo ni dereva msafirishaji “hata jina simfahamu, yeye nilimuagiza tu” alisema Emmy, ambae alikuwa anaachia kilio cha uongo na ukweli, “sasa hapa umekuja kufanya nini?” aliuliza Eze huku anazungusha macho mule chumbani, “mimi mara nyingi tu huwa nakuja kulala hapa mwenyewe, hasa nikitaka kubadilisha mawazo” alisema kwa kulalamika Emmy na kumfanya Eze atazame chini kwa aibu, “nifuateni” ilisikika sauti ya Side, akiwaeleza wale wenzake, huku anakimbia kutoka nje na kuelekea kwenye lift, ambayo ilionyesha ilikuwa inapanda juu na sasa ilikuwa ghorofa ya pili. …….ENDELEA…
Hapo Eze, ambae nikama alikuwa ameachiwa nafasi na vijana wake, sasa alikuwa amebakia peke yake na Emmy, “yani Eze leo umenidhalilisha sana, bora tuachane tu” alisema Emmy huku analia kilio cha kwikwi, “jamani Emmy, kwanini tufike hivyo, mimi bado nakupenda Emmy” alisema Ezze kwa sauti ya kubembeleza huku anapiga magoti sakafuni, “hapana kwa kweli, huwezi kuidhalilisha namna hii, yani nitembee na mtoto mdogo kama yule, naanzaje kumvulia nguo” alisema Emmy kwa sauti yake ile ile iliyoambatana na kilio cha kwikwi, “hapana mama yangu, usiseme hivyo siwezi kukuacha, basi nipe adhabu yoyote au niambie nikufanyie kitu kama fidia” alisema Eze kwa kuombeleza.
Hapo Emmy akaona amefanikiwa kumlaghai Eze na sasa ndio wakati wa kujipatia faida kwa kile kilichotokea, “una uhakika na unacho kisema Eze?” aliuliza Emmy kwa sauti iliyoanza kuchangamka, “ndiyo mama yangu, we sema chochote nitakufanyia” alisisitiza Eze na hapo kikapita kimya kifupi kilichodumu kwa sekunde chache, “sawa, nataka uingize million tano kwenye account ya Spesioza” alisema Emmy kwa sauti ya kudeka, “sawa… sawa nitaweka million saba” alisema Eze huku anasimama na kutoa simu yake mfukoni kisha akafanya utumaji wa fedha kwenye account aliyotajiwa namba zake na Emmy au mama P.******
Naam Chumba na nane cha ghorofa ya tatu kijana Deus, ambae alihakikisha watu hawa watano aliowakuta ndani ya chumba hiki, ambacho aliingia ikiwa njia ya kujiokoa toka kwenye shambalizi la risasi toka kwa watu, ambao aliamini kuwa wametumwa na mume wa Emmy, yaani yule mteja aliemletea bos chumba namba nane ghorofa la nne, tayari alikuwa ameshaweka bastola mezani, maana hakuihitaji tena, sasa alipiga hatua kuufuata mlango kwa lengo la kutoka nje.
Lakini kabla hajaufikia mlango akageuka haraka, kwa kuhisi kuwa kuna mtu mwingine mule ndani zaidi ya wale watano aliowashungulikia ni kweli alimuona mwanaume moja wa makamo akiinuka toka ubavuni mwa kochi haraka sana akajiandaa kumzibiti, lakini alipomtazama vyema hakuwa na silaha yeyote mkono mwake, “kijana tadhari naomba unisaidie kutoka humu ndani” alisema yule mzee kwa sauti yenye kutetemeka kwa uoga huku anachukuwa mkoba mweusi wa ngozi mezani, “kwanini nikusaidie?” aliuliza Deus, huku anamtazama mzee yule ambae sura yake sio ngeni usoni mwake, ni kama alishawahi kumuona mara kadhaa, “naitwa….” alisema yule mzee, lakini Deus akamuwahi, “hauna sababu ya kujitambulisha” alisema Deus kwa sauti tulivu kama ilivyo kawaida yake, na hapo mzee James akajua kuwa tayari kijana huyu alishamfahamu kutokana na umaarufu wake, maana alishawahi kuonekana kwenye vyombo vya habari, “sababu mimi sitojitambulisha mbele yako, hiyo ni sheria yangu namba moja” alisema Deus kwa sauti tulivu.
Hapo bwana James akatoa macho ya mshangao, maana hakujuwa sheria zake zinahusiana na nini, “ni vyema ukaokoa muda wangu kwa kunieleza sababu ya mimi kukutoa nje kabla sijalazimika kuumiza watu wengine ambao wapo njiani wananifuata” alisema Deus, japo sauti yake ilikuwa tulivu, lakini ilionyesha msisitizo, hata mzee huyu wa makamo akatambua kuwa kijana yule hakuwa anaigiza, alikuwa anahitaji sababu za msingi, “hawa jamaa walikuwa wanataka kuniuwa, wengine wapo nje sitoweza kutoka peke yangu” alisema mzee huyu ambae ni tajiri mkubwa sana hapa Africa, “wapo wangapi na wana silaha gani?” aliuliza Deus, kwa sauti ile ile tulivu, “wapo wawili, sijaona bunduki mikononi mwao ila wana mabegi makubwa” alisema tajiri James.
Hapo mzee James, akamuona kijana yule mwenye sura ya upole, anainama na kupapasa kwenye mguu wake wa kulia usawa wa sox, ambapo aliibuka na kisu kimoja kikubwa, kilichong’aa kwamakali yake. “ok! nifuate na muda wote ukae mita mbili nyuma yangu” alisema Deus huku anapiga hatua mbili, kisha akakamata kitasa cha mlango na kukionyonga, mlango nao ukafunguka wakati huo tayari bwana James alikuwa amesha msogelea Deus kama alivyoelekezwa, “zima taa” alisema Deus kwa sauti yake tulivu.******
Naam saa tatu na nusu usiku huu, general Sixmund akiwa nyumbani kwake akisubiri taarifa toka Tanzania kwa askari wake waliotumwa kwenda kumsaka Frank Nyati ambae alihitajika kwa mfalme Elvis Mbogo wa kwanza wa nchi ya #mbogo_land aje atoe majibu ya maswali yaliyokuwa yana muumiza kichwa mfalme huyo,
Mida hii ndiyo mida ambayo Sixmund alipokea simu toka kwa captain Amos Makey, ambae baada ya kusalimina Amos akaanza kueleza jinsi maongezi yao na kanal luten kanal mtoro jeshi la MLA, yani bwana Frank Nyati, “kikubwa anachosema ni kwamba msako wa saliti ndani ya jeshi la serikali, licha ya kuwa na lengo zuri, lakini ndani yake walikuwepo UMD, ambao waligeuza operation kupunguza nguvu ya serikali kwa kuuwa watu ambao kwa namna moja au nyingine wangekuwa kikwazo kwao katika kutekeleza azma yao ya mapinduzi” alieleza Amos, na hapo kengele ya tahadhari ikagonga kichwani mwa general Sixmund, “hilo ndilo tatizo kubwa, naimani mpaka sasa watakuwepo ndani ya serikali” alisema Sixmund kwa sauti iliyojaa fadhaha, “tena bwana Frank amesisitiza kuwa mtu huyo atakuwa mwenye nafasi kubwa na mwenye kuaminika serikalini” alisisitiza captain Amos, huku akieleza kuwa, “frank amesema kuwa, kuna baadhi ya watu wamewaingiza kwenye hili kwa makusudi ilikuweka chuki kati yao na serikali kwa lengo la kuja kuwa tumia baadae, mmoja wao ni bwana James” alieleza Amos.
Naaam hapo bwana Six akaona kuwa kuna umuhimu wa mfalme kulijua hilo mapema ili hatua za haraka zichukuliwe, “subiri maelekezo, wacha niongee na mfalme” alisema Sixmund na kukata simu.******
Hotel Sisterfada, wanaonekana askari wawili wa UMD, wakiwa bado wamesimama nje ya chumba namba nane cha ghorofa namba tatu, mmja kushoto kwa mlango na mwingine kulia kwa mlango huku wamebeba silaha zao migongoni mwao zilizohifadhiwa ndani ya mabegi makubwa, kuhofia kuwashtua wateja wengine wa hotel ile kubwa, waliendelea kusubiri mkuu wao na wenzao walioko ndani wamalimalize kikao na bwana James, kikao ambacho mpaka dakika hiyo, waliamini hakikuenda vyema, kutokana na kwamba, walisha sikia milio mingi ya risasi, walitambua kuwa tayari bwana Jaes amesha pigwa risasi kama ilivyopangwa endapo atakataa mpango wao.
Naaam wakiwa wanasubiri wenzao watoke, mara wakasikia mlango ukifunguliwa, wote wakatazama mlango wakitarajia kuwaona wenzao wakitoka nje, japo haikuwa hivyo, baada yake wakamuona kijana mmoja akitoka mule ndani akiwa amemshika bwana James na kumvuta kwa nguvu kama vile mwizi, nao wakatoa macho kwa mshangao, “boss anawaita ndani” alisema yule kijana huku anatembea kuelekea upande iliko lift ambayo ilikuwa inasoma kuwa inapandisha juu, wale jamaa bila kujiuliza mara mbili wakakimbilia ndani ya chumba, ambako walikutana na giza nene.
Lilikuwa kosa kubwa sana kwa vijana wale, maana ile kutahamaki walishtuka mlango ukifungwa kwa nje, ile wanataka kuwahi kuufungua wakasikia kacha, maana funguo ilikuwa inafunga mlango.
Alikuwa ni Deus Nyati aliefunga mlango kwa nje, ilikuwa ni mara baada ya wale vijana wawili kuingia kwenye mtego wake, haya fanya haraka, kuna watu wanaweza kuingia hapa sasa hivi” alisema Deus, huku anatembea kuelekea upande wa lift ambako pia kulikuwa na ngazi, huku bwana James akimfuata kama alivyo elekezwa, “kijana nina gari langu kule maegesho utaweza kuendesha?” aliuliza mzee James huku wakiendelea kutembea, “mpango ni kukutoa humu chumbani na sio zaidi ya hapo, isitoshe na mimi nina gari langu ambayo ndiyo ofisi yangu” alisema Deus kwa sauti kavu na tulivu kama ilikuwa imesetiwa mdomoni mwake, “unamaanisha wewe ni dereva wa taxi?” aliuliza james, wakati huo wameshazifikia ngazi na kuanza kushuka.
“hapana, mimi ni msafirishaji nasafirisha kitu chochote katika hali yeyote, muhimu kufuata sheria zangu tu” alijibu Deus, huku wanaendelea kushuka ngazi, “sawa, ni kiasi gani kunifikisha nyumbani nikiwa salama?” aliuliza James huku wanaendelea kushuka ngazi pasipo kujua kuwa ile wanapotelea kwenye ngazi tayari lift ilikuwa imesimama na mlango ukafunguka kisha wakashuka watu wa tano wenye kuvalia makoti marefu meusi na bunduki zao mikononi, wakiongozwa na bwana Songoro, Hesabu milango, mlango wa nne kushoto” alisema Songoro huku anapiga hatua kutembea kutoka kwenye lift na kutembea kwenye korido huku anahesabu milango,
Wakati Songoro anahesabu milango, huku Deus na mzee James walikuwa wanashuka ngazi kwa haraka, “laki tatu keshi” alisema Deus, wakati huo wanamaliza kushuka ngazi na kuibukia eneo la mapokezi, ambapo palikuwa peupe kabisa, “sawa imekubarika, nitakulipa mara mbili ya hizo cha msingi nifikishe nyumbani haraka, familia yangu itakuwa katika hatari” alisema mzee James huku akimfuata Deus ambae alikuwa anaongoza kuelekea nje ya jengo, mpango umekubariwa, tutatumia BMW S7 muda ni huu, mwisho wa mpango ni saa tatu na dakika arobaini na tano” alisema Deus huku anaongoza kuelekea gari liliko.
Naam sekunde chache baadae tayari walikuwa ndani ya gari, yaani BMW S7, na gari liliondoka mara moja huku Deus akisisitiza James afunge mkanda wa usalama.*******
Naam picha za tajiri mkubwa Africa akiwa na watu wanne watatu wakiwa na bunduki mikononi mwao, zinaonekana kusambaa kwa kasi sana kwenye mitandao ya kijamii zikiambatana na kichwa cha habari, JAMES KERVIN MFADHIRI WA KUNDI LA UMD TOKA MBOGO LAND, picha hizo za kushtua zinazagaa dunia nzima na kuwashangaza watu wengi sana, ni kutokana na umaarufu wa bwana James ambae ni mfanya biashara tajiri barani Africa.
Picha hizo ambazo zilikuwa na maelezo mafupi, yaliyoeleza kuwa, “pichani ni tajiri mkubwa afrika, bwana James Kervin, akiwa na general Kadumya, kiongozi wa kundi la waasi wa UMD toka nchini Mbogo Land, wakipanga namna ya kuondoa uongozi dhalimu wa kifalme toka madarakani”
“ikumbukwe tajiri huyo aliwahi kuhusishwa kimakosa katika uasi wa nchi hiyo mwana 1992, na kumsababishia hasara kubwa katika biashara zake pale alipoamua kutoroka nchini na familia yake huku akiacha biashara na mali zake nchini humo na baadae kuamua kujiunga na kundi hilo kwaajili ya kutimiza mapinduzi”
Hakika taarifa hii iliumiza vichwa vya watu wengi sana, kuanzia uongozi wa Tanzania ambao ulimchukulia bwana James kama mtu wa karibu wa serikali anaechangia kipato kikubwa kutokana na kulipa kodi, pia kurahishisha upatikanaji wa mahitajio ya wanachi wake.
Maoni na baadhi ya post za watumiaji wa mitandao ya kijamii ziliikosoa serikali ya kifalme ya mbogo land wakiita ni serikali kandamizi, serikali ambayo haikufaa kuendelea kuwepo madarakani, wengine walisema ni vyema kama wangebadilisha mfumo wa utawala na kuwa katika mfumo wa kuongozwa na rais aliechaguliwa na wananchi.
Lakini wapo waliopinga swala hilo, kuanzia hoja ya kubadilika kwa mfumo wa utawala, na pia swala la kwamba bwana James ni mfadhili wa kundi la waasi, “kama mwananchi anapata kila anachotaka, anagharamiwa masomo hata makazi, matibabu, na huduma zote muhimu kama umeme na maji anapata bure, kwanini wabadili mfumo” hayo ni baadhi ya maoni ya wachangiaji, “hapo lazima kuna mkono wa mtu, lengo ni kumchafua bwana James wamshushe kibiashara, usikute hata hizo picha zimetengenezwa” mmoja alisema hivyo, huku mwingine akisema kuwa, “hapo kuna mabepari wamesha tamani mali za #mbogo_land,
Taarifa hizi zilimfia mfalme Elvis wa kwanza, akiwa kwenye ofisi ndogo ya chumbani kwake, anapitia makabrasha mbali mbali na kusoma record za watu mbali mbali, wengi wao ni viongozi na askari wa nchi yake, “mume wangu, ni vyema kama ukiacha unachokifanya na kutazama hii” ilisikika sauti ya malkia Vaselisa na kumfanya Elvis ageuke kumtazama, akamuona anawasha projector kubwa iliyomulika ukutani nae akakaza macho kutazama ukutani akiona projector inajifungua.
Naam Projector inamaliza kujifungua na kitu cha kwanza ambacho Elvis anakiona ni picha kubwa inayomuonyesha bwana James akiwa amezungukwa na watu watatu wenye bunduki za kisasa, pamoja na kiongozi wa kundi la UMD, alie jiita General Erasto Kadumya wamekaa kwa pamoja huku mezani kukiwa na chupa ya pombe kali, juu ya picha kulikuwa na maandishi makubwa, “TAJIRI MKUBWA AFRIKA BWANA JAMES AKIWA NA KIONGOZI WA KUNDI ANALO LIFADHIRI LA UMD GEN ERASTO KADUMYA” inamshtua sana Elvis, ambae wakati huo huo anaona simu yake inaita, anaitazama na kuona kuwa mpigaji ni General Sixmund, akaipokea kwa haraka. …….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa
NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa
jamii forums