Simulizi : Safari Ndefu Kuelekea Kaburini

Simulizi : Safari Ndefu Kuelekea Kaburini

SEHEMU YA 29

upande kuhakikisha usalama ndani ya nyumba hiyo.
Patricia akabaki akiwa ameduwaa tu, hakuamini kama hapa duniani kulikuwa na nyumba kubwa na nzuri kama ile. Bwawa kubwa la kuogelea, sehemu ya kupaki magari, sehemu iliyokuwa na mbuga ya wanyama, sehemu iliyokuwa na kiwanja cha mpira wa kikapu vilikuwa baadhi ya vitu vilivyokuwa vikionekana katika eneo la nyumba ile.
Hapo ndipo ambapo maisha ya Patricia yalitakiwa kuanzia. Moyoni mwake alitamani kumuita Martin na kisha kuishi nae ndani ya jumba hio la kifahari lakini kitu kama hicho kilionekana kuwa kama ndoto maishani mwake.
“I missed you my only daughter (Nilikukumbuka binti yangu pekee)” Bwana Thomson alimwambia Patricia huku akionekana kuwa na furaha.
Muda wote Bwana Thomson alikuwa akionekana kuwa na furaha. Patricia ndiye alikuwa binti yake pekee ambaye alikuwa akimpenda katika maisha yake, yeye ndiye alikuwa binti na mtoto pekee katika maisha yake. Alimthamini Patricia, alikuwa tayari kupoteza kitu chochote lakini si kumpoteza Patricia.
Baada ya wiki moja Patricia alitakiwa kuanza chuo. Bwana Thomson hakutaka mwanae akae hostel, alikuwa akitamani muda wote amuone. Alichokifanya ni kumpeleka katika chuo cha St’ Mariana ambacho kilikuwa kinachukua watoto wa watu wenye fedha tu na watu ambao walikuwa maarufu nchini Marekani.
Patricia akaanza katika chuo hicho huku akisoma na kurudi nyumbani kwao. Masomo ya Biashara ambayo alikuwa akiyachukua hayakuonekana kuwa magumu kwake kitu ambacho kilimfanya kuyafurahia kupita kiasi.
Mambo yakaanza kuonekana kubadilika. Uzuri ambao alikuwa nao Patricia ukaanza kumvutia kila mwanaume ambaye alikuwa akimwangalia chuoni hapo. Kila mvulana akatamani kuwa pamoja nae, uso wake na mchanganyiko wake wa rangi vilikuwa vitu ambavyo vilimvutia kila mtu.
Wavulana wakaanza kuanzisha ukaribu na Patricia, Patricia akazoeleka lakini kila alipokuwa akitongozwa na wavulana mbalimbali wala hakuwa radhi kuwakubalia. Bado kichwani mwake kulikuwa na mwanaume mmoja, moyo wake haukutaka kumsahau mvulana huyu. Alimpenda na alitamani aje kuishi nae hapo baadae lakini aliona kitu hicho kutokuwezekana kwa kuwa hakuwa
 
SEHEMU YA 30

na ndoto zozote za kurudi nchini Tanzania.
Uzuri wa Patricia ukaanza kuwa gumzo, wanachuo ambao walikuwa wakisoma chuoni hapo wakaanza kupeleka taarifa kwa wanachuo wa vyuo vingine jambo ambalo liliwafanya watu wengi kufika chuoni hapo. Uzuri wa Patricia ulionekana kumshinda hata Sandra Manucho, msichana aiyekuwa akivuma ambaye alikuwa na asili ya Mexico.
Katika kipindi hiho gumzo kubwa lilikuwa ni Patricia. Wavulana mbalimbali wakaanza kupiga nae picha na kuziweka kwenye kompyuta zao na simu zao. Patricia hakukubalika na wavulana tu, bali hata wasichana walikuwa wakiukubali uzuri wake. Kwa mara ya kwanza msichana Sandra akaonekana kushtuka mara tu alipouona uzuri wa Patricia, hakuamini kama kweli kulikuwa na msichana mzuri namna ile.
Ndani ya miezi miwili, sifa za uzuri wa Patricia zikaanza kuenea taratibu mpaka kufika katika jengo la kampuni ya kutengeneza majarida ya Cow Boy. Meneja wa kampuni hiyo akaanza kufanya jitihada za haraka haraka za kumpata Patricia kwa ajili ya kuandikisha nae mkataba kwa ajili ya kuzitoa picha zake katika kava la mbele katika majarida yake kwa kuona kwamba angeingiza kiasi kikubwa cha fedha kutokana na uzuri aliokuwa nao.
Bwana Smith hakutulia garini, muda wote macho yake yalikuwa yakiiangalia picha ya Patricia ambayo alikuwa ametumiwa kwenye simu yake. Katika kipindi hicho alikuwa katika mwendo wa kasi kuelekea katika chuo cha St’ Mariana kwa ajili ya kuonana na Patricia na kisha kuweka nae mkataba. Japokuwa kazi ya kuandikishiana mikataba halikuwa jukumu lake lakini uzuri wa Patricia ukamfanya kujipa jukumu hilo.
Gari likaanza kuingia katika eneo la chuo hicho, ni picha za Patricia ndizo ambazo zilikuwa zikionekana mbele yake huku zikiwa zimebandikwa katika sehemu mbalimbali huku maneno yaliyosomeka ‘MISS ST’ MARIANA’ yakisomeka katika kila picha aliyoiona.
“I have to see her (Inanibidi nimuone)” Bwana Smith alisema huku akianza kupiga hatua kuelekea katika ofisi za chuo hicho huku mawazo yake yakimfikiria Patricia na namna ambavyo angetengeneza fedha kupitia
 
SEHEMU YA 31

msichana huyo kutokana na uzuri aliokuwa nao.

Bwana Smith akafika katika ofisi ile na kuanza kuanza kuongea na professa Mickey. Akalielezea lengo la yeye kuwa mahali hapo. Professa Mickey akaonekana kushtuka, macho yake yakaonyesha msangao ambao ukamfanya Bwana Smith kushindwa kuelewa sababu ambayo ilisababisha hali ile usoni mwa Profesa.
“Kuna nini?” Bwana Smith aliuliza.
“Mnanishangaza sana”
“Kwa nini?”
“Wewe ni mkurugenzi wa jarida la kumi kuja kumuulizia. Naomba uende kwenye darasa lile kule utakutana nae pamoja na wenzako” Profesa alimwambia.
Bwana Smith hakutaka kubaki ndani ya ofisi ile, kwa haraka haraka huku akionekana kuwa na haraka akaanza kupiga hatua kuelekea katika darasa ambalo alikuwa ameelekezwa. Mpaka kufika kipindi hicho tayari akaona kwamba kulikuwa an upinzani mkubwa ambao ulikuwa ukimkabili kutoka kwa majarida mengine ambayo yalikuwa yakitaka kufanya kazi na Patricia.
Akaingia darasani, watu zaidi ya ishirini walikuwa wamemzunguka Paticia ambaye alikuwa amekaa katika kati yao. Bwana Smith akawasogelea na kukivuta kiti kukaa pamoja nae. Bado watu wale ambao walikuwa wametoka katika majarida mbalimbali walikuwa wakimlazimisha Patricia kuingia nao mkataba wa kufanya nae kazi.
Tayari sura na umbo la Patricia likaonekana kuwa faida, fedha zilionekana waziwazi kwa mtu yeyote ambaye angeshinda kumsainisha mkataba Patricia ambaye alikuwa akionekana kuhitaji kiasi kikubwa cha fedha.
“150000000$ per year(Dola milioni kumi na tano kwa mwaka)” Mkurugenzi wa jarida la Mississippi alimwambia Patricia.
“I will pay you 20000000$ Per year (Nitakulipa dola milioni ishirni kwa mwaka)” Mkurugenzi wa kampuni ya jarida la Washington Daily alimambia Patricia.
Ubishi ulikuwa mkubwa mahali hapo, kila mtu alikuwa akizidisha madau makubwa kama njia mojawapo ya kuweza kumsainisha mkataba Patricia. Wenyewe ka wenyewe walikuwa wakiendelea kubishana. Malipo ya dola milioni moja yakafika lakini hakukuwa na mtu ambaye alionekana kushinda. Madau yakaongezwa zaidi na zaidi mpaka kufika dola milioni tano, na hapo ndipo Bwana Smith akashinda huku akiwa amewaacha vibaya wenzake.
Patricia hakuwa na jinsi, kiasi ambacho alikuwa ameahidiwa kukipata kwa
 
SEHEMU YA 32

mwaka kilikuwa kiasi kikubwa sana ambacho kilikuwa ni zaidi ya Bilioni mia moja kwa mwaka. Mawazo yake yalikuwa kwa Martin tu. Yeye alikuwa amezaliwa katika familia iliyokuwa na fedha, hakuona umuhimu wa kuendelea kuhitaji fedha, kila fedha ambazo angekuwa akiingiza katika maisha yake, basi aliona fedha zile kuwa mali ya Martin ambaye alikuwa akiishi maisha ya dhiki nchini Tanzania.
Mkataba ukaandikishwa na moja kwa moja Patricia kuanza kazi. Mategemeo ambayo yalikuwa yametegemewa ndio ambayo yalitokea. Kwa mara ya kwanza picha za Patricia zilipoanza kutoewa kwenye majarida ya Cow Boy, majarida yakanunuliwa kupita kawaida.
Sura ya Patricia ikaonekana kumvutia kila mtu ambaye alikuwa akiiangalia, urembo wake ulionekana kuwa mkubwa machoni mwa watu. Watu wengi wakashindwa kuvumilia, hawakuamini kama duniani kulikuwa na msichana mrembo namna ile jambo ambalo liliwafanya kuanza kuelekea katika chuo cha St’ Marianna kwa ajili ya kumuona msichana huyo mrembo.
Kila siku wanaume walikuwa wakimiminika chuoni hapo kwa ajili ya kumuona msichana ambaye alikuwa akivutia sana. Kila mmoja alikuwa na kiu ya kumuona msichana huyo ambaye alionekana kuwa na uzuri wa ajabu. Walipofika chuoni hapo, walimuona Patricia ambaye alionekana kuwachanganya kupita kawaida.
Huo ndio ukawa mwanzo wa umaarufu wa Patricia, asilimia zaidi ya themanini nchini Marekani wakamfahamu Patricia ambaye uzuri wake ulikuwa ukizidi kuongezeka zaidi na zaidi. Wanaume hawakuisha kujigonga, kila siku walikuwa wakimtaka Patricia kwa ajili ya kuanzisha mahusiano pamoja nae.
Patricia hakuonekana kuwa mwepesi kuwakubali. Bado akili yake na moyo wake katika kipindi hicho alikuwa akimfikiria mwanaume ambaye alikuwa amemtoa bikira yake, Martin. Kitendo cha kumkubalia mvulana mwingine ilionyesha dhahiri kwamba alikuwa radhi kumsaiti Martin.
Miezi ikaendelea kukatika na hatimae mwaka mmoja kukatika. Uzuri wa Patricia ukaonekana kumteka kila mwanaume nchini Marekani. Majarida ya Cow Boy bado yalikuwa ykiuza sana kutokana na picha mbalimbali za Patricia ambazo zilikuwa zikionekana katika ukurasa wa mbele kabisa.
Patricia akafanikiwa kuingia mikataba na makampuni mbalimbali kama Pepsi,
 
SEHEMU YA 33

makampuni ya pafyumu pamoja na vinywaji vingine. Patricia aliendelea kulishika soko la Marekani na duniani kwa ujumla mpaka pale ambapo alifuatwa kwa ajili ya kushiriki katika filamu ya BLOWN JEANS. Akasaini mkataba mnono wa kushiriki katika filamu hiyo, mkataba ambao uligharimu zaidi ya dola milioni nane mara tu atakapomaliza kurekodi filamu hiyo.
Maisha ya Patricia yakawa yamebadilika kabisa, utajiri ambao alikuwa akiumiliki kwa wakati huo ulikuwa ni zaidi ya dola bilioni themanini. Akanunua nyumba kubwa ya kifahari, magari ya kifahari pamoja na kuanzisha biashara zake nyingi ambazo zilikuwa zikimuongezea kiasi kikubwa cha fedha.
Bado fedha zilikuwa zikiendelea kuingia katika akaunti yake kila siku. Ingawa katika kipindi hicho kichwa chake kilikuwa kimemsahau Martin lakini kamwe hakuweza kuzisahahu ahadi ambazo alikuwa amempa. Kila mwezi alikuwa akimtumia kiasi kile cha fedha huku mwaka ulipokwisha akiwa amemtumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kununulia nyumba nchini Tanzania.
Maisha yaliendelea zaidi na zaidi mpaka pale ambapo Patricia akaingia katika mahusiano na mchezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya Chicago Bulls, Banana Kelvin. Uhusiano huo ukatangazwa sana kuwa uhusiano ambao ulikuwa ukivutia kuliko uhusiano zote kwa wakati huo.
Patricia alikuwa akionekana kuwa na furaha, sehemu nyingi ambazo alikuwepo, alikuwa pamoja na Banana ambaye alikuwa akimpenda sana katika kipindi hicho. Walikuwa wakitembea sehemu nyingi duniani kwa ajili ya kuhudhuria matamasha mengi pamoja na sherehe mbalimbali. Kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Patricia, jina la Banana likakua zaidi na kuwa mwanamichezo ambaye alikuwa akijulikana sana.
Banana ndiye ambaye alikuwa akitumia kiasi kikubwa cha fedha. Hakutaka kabisa Patricia atumie fedha alizokuwa akiziingiza katika biashara mbalimbali alizokuwa akizifanya pamoja na mikataba mingi aliyokuwa akiingiza. Banana ndiye alikuwa kila kitu, alikuwa akimnunulia Patricia vitu mbalimbali vya thamani.
Mwaka wa pili ukakatika, Patricia akaendelea kung’aa zaidi na zaidi, akazidi kuingiza fedha nyingi kuliko wasichana wote duniani. Jina lake likazidi kukua
 
SEHEMU YA 34

huku uhusiano na Banana ukiwa umeendelea zaidi na zaidi mpaka kufikia hatua ambayo wakaamua kutangaza kwamba walikuwa mbioni kufunga ndoa jambo ambao liliwafurahisha watu wengi duniani.
********
Martin bado alikuwa akiendelea na maisha yake. Kiasi cha fedha ambacho alikuwa ameachiwa na Patricia kikamfanya kwenda kupanga vyumba viwili vilivyokuwa na hadhi na kisha fedha nyingine kuziingiza katika kazi yake ya muziki. Kila siku alikuwa mtu wa kuandika nyimbo mbalimbali na kisha kuanza kurekodi nyimbo moja baada ya nyingine.
Nyimbo zake zilikuwa zikivutia lakini si watu wote ambao walikuwa wakizisikia kutokana na ubaguzi ambao ulikuwa ukifanywa na madj mbalimbali waliokuwa katika vitu vya redio. Hapo ndipo Martin alipoanza kuhonga, hakuona kama kulikuwa na njia nyingine ambayo ingemfanya kusikika zaidi ya hiyo.
Nyimbo zake zikaanza kusikka zaidi na zaidi masikioni mwa Watanzania. Kutokana na nyimbo zake kuonekana kuwa nzuri, akaanza kujizolea mashabiki mbalimbali. Akaanza kuhalikwa kwenye matamasha mbalimbali. Jina lake likaanza kukua hatua kwa hatu.
Fedha ambazo alikuwa akiwahonga madj zikaonekana kuanza kurudi, akawa miongoni mwa wasanii chipukizi ambao walikuwa wametoka hivi karibuni. Martin hakutaka kuishia hapo, alichokifanya ni kuanza kutoa video ambazo zilikuwa kwenye ubora mkubwa ambazo zilimfanya kukubalika kupita kawaisa
Akazidi kualikwa zaidi na zaidi, akaanza kuitwa sehemu mbalimbali nje ya Tanzania, ingawa mara ya kwanza alikuwa akiimba jukwaani na kulipwa laki tano lakini baadae akaanza kulipwa mpaka kiasi cha shilingi milioni moja.
Martin hakumsahau mama yake, akampangishia nyumba nzima huku nae akiendelea na harakati zake za kufanya muziki. Maisha yakaonekana kubadilika kwa Martin, mafanikio yakaonekana kumfuata kwa haraka sana kiasi ambacho wengine wakawa na mashaka kwamba alikuwa amejiunga na dini imuabudio shetani ya Freemason.
Martin ambaye alikuwa akilitumia jina la MAPAC JNR akazidi kuwa maarufu zaidi na zaidi na kuwa miongoni mwa wasanii ambao walikuwa wakiingiza kiasi kikubwa cha fedha. Kila matamasha ambayo yalikuwa yakifanyika nchini Tanzania, Martin au Mapat Jnr alikuwa akiitwa na kuimba. Tayari
 
SEHEMU YA 35

akaonekana kuwa kipenzi cha Watanzania, nyimbo zake zilikuwa zikisikika mara kwa mara katika vituo mbalimbali vya redio.
Ni ndani ya miezi saba tu, Martin akawa msanii mkubwa na kuongoza kwa malipo makubwa nchini Tanzania. Maisha yake yakabadilika kabisa, vituo mbalimbali vya redio vikaanza kumuita na kufanya nae mahojiao.
Watanzania wengi walikuwa wakihitaji kufahamu ni kwa namna gani ambavyo alikuwa amefanya mpaka kupata mafanikio makubwa namna ile tena kwa haraka kupita kawaida. Martin akaamua kwenda katika kituo cha Flavour Tv na kuanza kufanyiwa mahojiano.
Watanzania wengi walikuwa wamekusanyika katika televisheni zao tayari kwa kumuona Martin ambaye alionekana kuwa na mvuto kwa watu wengi katika kipindi hicho. Kule kuonekana moja kwa moja kwenye televisheni, kila mtu akaonekana kufarijika, kuonekana kwake kwenye televisheni kulionekana kumfurahisha kila mtu.
“Hebu tupe historia ya maisha yako Mapac” Mtangazaji ambaye alikuwa akimhoji Martin katika kipindi maalumu alimwambia Martin.
“Nilizaliwa miaka ishirini na mbili iliyopita na kusoma katika shule ya Salma Kikwete pale Kijitonyama. Maisha yangu katika kipindi hicho yalikuwa ni maisha ya shida sana, shuleni nilikuwa mwanafunzi ambaye nilikuwa mchafu kuliko wanafunzi wengine. Sidhani kama nilifikisha siku zaidi ya mia moja kuvaa viatu shuleni, yaani muda mwingi shuleni nilikuwa nikivaa kandambili tu” Martin alimwambia mtangazaji kauli ambayo iimshtua kila aliyekuwa akiangalia.
“Mmh! Ulimaliza shule mwaka gani?”
“Nilimaliza mwaka jana. Kwa hiyo haya maisha ambayo niliyapitia yalikuwa kama miaka mitatu iliyopita. Nilikuwa nikiuchukia sana umasikini na nilikuwa tayari kujitoa kwa ajili ya kupigana na umasikini huu kwa kuwa tu niliuchukia. Kiukweli watanzania msifikiri kwamba nilifaulu mitihani. Nilifeli sana na hata mtihani wa kidat cha nne nilifeli vibaya kwa kupata daraja la sifuri, yaani hapa hata cheti sina” Matin alimwambia mtangazaji.
“Pole sana”
“Asante”
“Sasa kwa nini uliamua kujiita Mapac Jnr?”
“Jina hili ni muunganiko mwa majina mawili. Ma ni kifupi cha jina langu Martin na Pac ni kifupi cha jina la msichana Patricia na Jnr ni neno ambalo
 
SEHEMU YA 36

linaonesha kwamba mimi ni kijana mdogo” Martin alimwambia mtangazaji.
“Kwa hiyo una msichana anayeitwa Patricia?”
“Hapana. Yeye ni rafiki yangu ambaye alinisaidi sana toka nilipokuwa shuleni. Nilikuwa kwenye maisha ya kimasikini sana lakini uzuri ulikuwa kwamba yeye alikuwa na uwezo wa kifedha jambo ambalo lilimfanya kunisaidi kwa kila kitu. Alininunulia nguo, viatu na kila kitu nilichokua nikikihitaji. Yaani aliyabadilisha maisha yangu mpaka ya mama yangu mpaka pale alipoondoka kuelekea nchini Marekani” Martin alijibu.
“Nimepata picha sasa. Huyu msichana likuwa akikupenda kama rafiki tu?”
“Ndio”
“Kwa hiyo hamkuwahi kuwa wapenzi?”
“Ndio”
“Sawa. Kwa hiyo huwa unawasiliana nae?”
“Hapana japokuwa huwa ananionyeshea upendo mkubwa wa kunitumia fedha. Yaani maisha yangu hayategemei muziki. Hata kama nisingekuwa mwanamuziki, bado maisha yangu yangekuwa hivi isipokuwa umaarufu tu. Nilijiingiza kwenye muziki kwa kuwa ulikuwa damuni tu” Martin alijibu.
“Kwa hiyo una ndoto za kuwa na msichana huyo baadae?”
“Bado nina kiu ya kuwa nae kwa kuwa ninampenda sana. Naamini kuna siku nitasafiri na kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya kumuona tu” Martin alijibu.
“Kwa hiyo wasichana ambao mara kwa mara wanatokea kwenye magazeti ya udaku kuwa wanakutaka waache kujitangaza kwa kuwa kuna msichana unampenda?”
“Yeah! Ikibidi waache tu. Ninampenda sana Patricia, ninampenda sana, tena sana tu” Martin alijibu.
Hayo ndio yalikuwa maisha yake, mara kwa mara alikuwa akiitwa katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni na kufanyiwa mahojiano, Bado alikuwa akisisitiza kwamba Patricia alikuwa msichana ambaye alikuwa akimpenda sana kuliko msichana yeyote yule katika maisha yake.
“Nitaendelea kumpenda na kumhitaji milele” Martin alisema huku tayari akiwa ametangazwa na kuwa msanii aliyekuwa na uwzo mkubwa kifedha kuliko mwanamuziki yeyote nchini Tanzania.

Je nini kitaendelea?
Je nini kitaendelea katika maisha ya Martin na Patricia?
Je Patricia ataweza kufunga ndoa na Banana kama walivyopanga?

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 37, 38 NA 39


Si kila mtu ambaye alikuwa akiufurahia uhusiano kati ya Patricia na Banana. Watu wazima, matajiri ambao walikuwa na fedha zao walionekana kuukasirikia uhusiano huo. Kila tajiri alikuwa akimtaka Patricia, urembo wake ulionekana kustahili kuwa na mwanaume ambaye alikuwa tajiri kama jinsi walivyokuwa wao.
Kila siku walikuwa wakifanya mishemishe za kumtongoza Patricia lakini msichana huyo alikuwa akionyesha uaminifu mkubwa kwa mchumba wake, Banana. Matajiri wale walijaribu kila siku mpaka kukata tamaa na kuamua kuachana nae.
Kila mmoja alikuwa akifanya mambo yake huku akiuacha uhusiano ule kuendelea kama kawaida huku wao wakitafuta wasichana wengine warembo wa kutembea nao lakini tajiri Jonathan hakutaka kukubaliana na hilo.
Moyoni mwa Bwana Jonathan bado alikuwa akimpenda sana Patricia na bado alikuwa akimhitaji sana katia maisha yake jambo ambalo lilimfanya kuukasirikia uhusiano ule kuliko mtu yeyote duniani. Moyoni mwake alikuwa akitamani kukaa na msichana huyo ambaye katika kipindi hicho alionekana kuwa msiachana mrembo kuliko wasichana wote ambao walikuwa maarufu duniani.
Alichokifanya mara baada ya kuona kwamba amekataliwa, akaamua kupanga mipango ya kuwamaliza wapenzi hao kwa kuandaa mpango kabambe. Alichokifanya ni kuwasiliana na watu wake ambao walikuwa wakiishi jijini New York kwa ajili ya kuwaua wapenzi hapo kwa kuwapiga risasi. Mipango ikapangwa na kukamilika, Patricia na Banana wakatakiwa kuuawa ndani ya ukumbi wa Stapple Centre katika siku za ugawaji wa tuzo za BET.
Vijana wakajipanga vilivyo, walichokifanya siku hiyo ni kufika katika ukumbi huo mapema sana na kuandaa bunduki zao zilizokuwa na lensi vizuri kabisa huku vyombo vya kuzuia milio ya risasi vikiwa mbele ya bunduki hizo. Walichokuwa wakikitaka ni kuwapiga risasi wapenzi hao kwa pamoja na kuwaua kwa pamoja.
Wakafika katika chuma kimoja ambacho kilikuwa na mavazi mengi, wakachukua mavazi ya wapishi na kisha kujifanya kama wapishi ambao walikuwa wakishughulikia chakula ndani ya ukumbi huo. Walijiona kutakiwa kufanya vitu kwa umakini mkubwa sana bila kugundulika na mtu yeyote ambaye angekua ndani ya ukumbi huo.
Walipoona kila kitu chao kipo tayari, wakaanza kwenda nyuma ya televisheni kubwa iliyokuwa mahali hapo na kutulia na bunduki zao. Muda ulizidi kwenda zaidi na zaidi mpaka kufika kipindi ambacho watu wakaanza kuingia ndani ya ukumbi huo.
Wasanii na masupastaa wengi walikuwa wakipita katika zuria moja jekundu na kupiga picha mbalimbali ambazo zilitakiwa kuwekwa kwenye majarida na magazeti ambayo yangetoka siku ifuatayo. Baada ya dakika kadhaa, gari zuri na la kifahari likasimama nje ya ukumbi ule, Patricia na Banana wakaanza kuteremka, wapiga picha mbalimbali wakaanza kuwasogelea na kuwapiga picha.
Nyuso zao zilikuwa zinaonyesha tabasamu pana, walikuwa wakipunga mikono hewani huku kelele za watu ambao walikuwa wakishangilia zikisikika mahali hapo. Wakaelekea katika zuria lile jekundu na kusimama na kisha picha kuanza kupigwa. Muda wote walikuwa wakionekana kuwa na furaha, hawakufahamu kitu chochote kwamba kwa wakati huo walitakiwa kubakiza dakika chache za kuishi duniani.
Walipoona zoezi la kupiga picha likiwa limekamilika, moja kwa moja wakaanza kuelekea ndani ya ukumbi ule na kukaa katika viti vya mbele kabisa. Huku ugawaji wa tuzo ukiendelea ukumbini pale. Tuzo ziligawiwa kwa washindi mbalimbali hasa wanamuziki.
“On my target....(Kwenye usawa wangu)” Mpiga risasi mmoja alisema kwenye chombo chake cha mawasiliano ambacho kilikuwa sikioni. Bunduki yake tayari ilikuwa imemuelekezea Patricia tayari kwa kuachia risasi nne mfululizo kifuani.
“On my target too...(Kwenye usawa wangu pia)” Mwanaume mwingine alisema na hapo hapo wote kujiandaa kupiga risasi. Bunduki yake pia ilikuwa imemuelekezea Banana kifuani tayari kwa kuachia risasi nne kifuani mwake.
“Three....twooo....oneee....” Walihesabu kwa pamoja.
*******
Umaarufu wa Martin ulikuwa mkubwa kupita kawaida, kila siku alikuwa akiingiza kiasi kikubwa cha fedha, alinunua magari ya kifahari huku asilimia kumi ya kila fedha ambazo alikuwa akiziingiza akizitumia katika kuwasaidia watoto yatima waliokuwa katika vituo mbalimbali. Martin akachaguliwa kuwa balozi wa Maralia na Vyakula, akaanza kuzunguka katika mikoa mbalimbali kwa kutumia ndege.
Muda wote alipokuwa akisafiri kwa kutumia ndege, alikuwa akilia. Maisha yake ya nyuma ambayo alikuwa ameishi yalionekana kumsumbua sana katika kichwa chake. Mpaka katika kipindi hicho bado alikuwa akiuchukia sana umasikini. Moyoni alikuwa na hamu ya kuwasaidia watu masikini kwani hali ile alikuwa akiijua vilivyo.
Hakupenda kumuona mtu akiwa katika hali ya umasikini kabisa na hiyo ndio ilikuwa sababu kubwa ya kuwasaidia watoto yatima na watu mbalimbali ambao walikuwa katika uhitaji mkubwa. Mara kwa mara alikuwa akisafiri mikoani kwa ajili ya kuwasaidia watu mbalimbali, alipiga picha na wanavijiji wengi ambao walikuwa wakitegemea maisha yao katika kazi ya ukulima waliyokuwa wakiifanya.
Maisha ya wanavijiji yalionekana kumuumiza hali ambayo ilimfanya kuwasaidia kwa kuwapa kiasi kikubwa cha fedha katika kila kijiji ambacho alikuwa akitembelea. Msaada wake ukaonekana kuwa mkubwa, magazeti na vyombo vingine vya habari vikazidi kumtangaza sana kiasi ambacho kikamfanya kuitwa bungeni na kushiriki katika kikao kimoja kama mgeni rasmi.
Hiyo ilikuwa ni heshima kubwa kwake, kwenda bungeni kama mgeni rasmi ilionekana kuwa kama bahati kwake. Bungeni, alikuwa akijisikia ufahari, kuwaona wabunge ambao walikuwa wakichagia mada mbalimbali hasa katika kipindi hicho cha kupanga bajeti ya mwaka ilionekana kumfurahisha moyoni.
Muda ambao alitakiwa kuongea ukafika, akakaribishwa na kusimama katika sehemu aliyokuwepo na kisha kuweka vizuri kipaza sauti chake. Bunge zima lilikuwa kimya, akaanza kuwaangalia wabunge kwa zamu. Hakuamini kuona kwamba watu waliokuwa na digrii, Elimu kubwa walikuwa wakimsikiliza yeye, mtu ambaye alifeli sana kidato cha nne.
Macho yake yakaanza kujaa machozi na baaada ya sekunde chache, machozi yakaanza kumtoka. Moyoni alikuwa na mambo mengi ya kuongea, yale ambayo alikuwa akitaka kuyaongea yakaanza kujipanga moyoni mwake.
“Namshukuru Mungu kwa kunifikisha mahali hapa siku ya leo na kusimama mbele yenu” Martin alisema na kisha kuendelea. Kila neno ambalo alikuwa akiliongea mahali hapo lilionekana kuwa la msingi sana.
Aliiongelea hali ambayo walikuwa wakiishi wakulima wengi vijijini, hali ya kimasikini ambayo haikutakiwa kuishi na watu kama wao kutokana na umuhimu mkubwa ambao walikuwa nao hapa nchini. Akaanza kuizungumzia Elimu ya Tanzania na matatizo kadhaa ambayo alikutana nayo kule vijijini, watoto kukosa madarasa, vitabu kutokuwepo madarasani.
 
SEHEMU YA 43 & 44


Aliwaandaa vijana wake tayari kwa kutelekeza kile ambacho alikuwa akitaka kifanyike kwa wakati ule. Alitaka watu wale wapigwe risasi na wafe papo hapo. Mpango wake aliuona kufaa sana ila baada ya dakika kadhaa akaona kwamba mpango ule haukuwa na manufaa yoyote yale.
Kichwani alikuwa akifikiria vitu vingi, kitu cha kwanza alikuwa akiwafikiria wale vijana wake kama wangekamilisha kile alichotaka kifanyike harafu wakamatwe, je wangekuwa na moyo wa kutokumtaja? Kila alipofikiria hilo, wasiwasi ulikuwa ukimshika moyoni mwake.
Hapo ndipo alipoamua kupanga mpango mwingine. Alichokifanya ni kuwasiliana na vijana wake wengine na kisha kuwaeleza mpango kabambe ambao alikuwa ameufikiria mahali hapo. Alichokuwa akikitaka kwa wakati huo ni kuwaua kwa ajali ya gari, mauaji ambayo yangeonekana kuwa yalitokea kwa bahati mbaya.
Alichokifanya ni kumpigia simu kijana wake mwingine na kisha kumpa namba ya Patricia ambapo alitakiwa kutumia meseji. Hilo halikuonekana kuwa tatizo, muda ambao meseji ile ilitakiwa itumwe ikatumwa huku njiani akiwa ametegesha gari kubwa tayari kwa kusababisha ajali ambayo ingetokea katika barabara ya St’ Patrick.
Kila kilichokuwa kimepagwa kilikwenda kama alivyotaka kiwe, ukumbini taa zikazimwa na Patricia pamoja na Banana kutoka nje ya ukumbi na kuchukua gari lao huku wakielekea nyumbani kwao.
**********
Ulikuwa ni mlio mkubwa ambao uliskika katika maungano ya barabara ya St’ Patick na Kingstone. Gari dogo aina ya Aston Martin lilikuwa limerushwa mbali huku likiwa limebimbilika zaidi ya mara saba ardhini. Gari lile lilikuwa limebondeka vibaya, sehemu yote ya mbele ilikuwa haionekani kwa jinsi lilivyokuwa limebondeka.
Damu zilikuwa zinaonekana kutapakaa katika bati la gari lile, hakukuwa na vioo ambavyo vilikuwa vimesalia, vyote vilikuwa vimepasuka. Matairi ya gari lile yalikuwa yamepasuka yote. Kila mtu ambaye alikuwa ameishuhudia ajali ile alionekana kupigwa na mshangao.
Watu wakaanza kueleke kule ambako gari lile lilipokuwa limebimbilishwa na kuanza kuliangalia, hakukuwa an mtu ambye alidiriki kulisogelea, ajali ile ilionekana kuwa mbaya kuliko ajali zote ambazo ziliwahi kutokea mwaka huo. Wanawake ambao walikuwa wameiona ajali ile walikuwa wakilia kwa woga, walionekana kuogopa kupita kawaida.
Gari lile kubwa ambalo lilikuwa limeigonga gari ile bado lilikuwa mahali pale pale lakini dereva wake wala hakuonekana, alikuwa amekwishakimbia. Ndani ya dakika nne, gari la mapolisi likafika mahali pale na kisha kuweka kamba za rangi ya njano na kutotaka mtu yeyote kutokusogea sehemu ile. Wala hazikupita dakika nyingi baada ya hapo, gari la wagonjwa likafika mahali hapo.
Kazi kubwa ikawa ni kuwatoa watu ambao walikuwa ndani ya gari lile. Hakukuwa na dalili zozote kama watu ambao walikuwa ndani ya gari lile walikuwa wamesalimika kutokana na jinsi gari lilivyokuwa.. Mabati yakatanuliwa, picha ya miili ambayo ilikuwa ikionekana machoni mwa mapolisi ilikuwa imewashangaza kupita kawaida, ilikuwa imeharibika vibaya na wala haikuwa rahisi kugundua wale walikuwa wakina nani kwa jinsi damu zilivyokuwa zimetapakaa nyusoni mwao.

Gari la wagonjwa lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi kuelekea katika hospitali ya Metopolian iliyokuwa hapo jijini New York. King’ora kilikuwa kikisikika kikilia kitu ambacho kiliyafanya magari mengine kupaki pembeni kulipisha gari hilo la wagonjwa.
Ni ndani ya dakika mbili gari likafika katika eneo la hospitali hiyo na machela kuletwa na kisha miili ile kuakizwa na machela kuanza kuendeshwa ndani. Kila nesi ambaye alikuwa akiiangalia miili ile, alibaki akishangaa, miili ilionekana kutisha kupita kawaida.
Safari ile iliishia katika chumba cha wagonjwa mahututi na kisha kuanza kuisafisha. Hakukuwa na mtu ambaye aliyaamini macho yake mara baada ya kugundua kwamba watu wale walikuwa ni Patricia na Banana. Taarifa zikatolewa kwa mapolisi juu ya watu wale ambao walikuwa wamepata ajali na mapolisi kuvielezea vyombo vya habari.
Kwa haraka haraka taarifa zikaanza kutolewa. Ilikuwa ni taarifa ambayo ilijaa mshtuko sana kwa kila mtu ambaye alikuwa amezisikia habari zile. Kila mtu akataka kufahamu mengi kuhusiana na ajali ile ambayo ilionekana kuwa kama mchezo fulani wa maigizo. Watu wakaanza kujisogeza
 
SEHEMU YA 45 & 46

katika hospitali ile, watu ambao walikuwa wamepata ajali walionekana kuwa watu muhimu kwao.
Kila mtu ambaye alikuwa akifika katika hospitali ile alionekana kuhuzunika huku hata wengine wakilia kupita kawaida. Tukio la ajali ile lilionekana kuwagusa kupita kawaida, hawakuamini kama wale watu ambao walitakiwa kuoana siku chache zijazo walikuwa wamepata ajali na sasa hivi walikuwa mahututi hospitalini.
Mzee Thomson akaonekana kuchanganyikiwa, hakuamini kile ambacho alikuwa ameambiwa. Aliuhisi mwili wake ukipigwana ganzi, miguu ikilegea na kukaa kochini huku akiitupa simu yake chini. Alibaki pale kochini katika hali ya mshangao kwa muda wa dakika kadhaa na kisha kuinuka na kuanza kuelekea nje ya nyumba yake.
Alichokifanya ni kuingia garini na kisha kuondoka kuelekea hospitalini. Kwa jinsi ambavyo alikuwa amechanganyikiwa, alionekana kusahau kama alitakiwa kuendeshwa na dereva wake ambaye alikuwa akiishi nae ndani ya nyumba yake. Alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi kuelekea hospitalini.
Alichukua dakika tano akawa amefika katika hospitali hiyo. Waandishi wa habari pamoja na wananchi zaidi ya elfu mbili walikuwa katika eneo la hospitali ile huku wakitaka kusikia ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea
Waandishi wa habari walipomuona Bwana Thomson anatereka kutoka garini mwake wakaanza kumsogelea huku wakimuwekea maiki zao lakini Bwana Thomson hakuongea kitu chochote kile, alionekana kuchanganyikiwa kupita kawaida. Akaanza kupiga hatua kuelekea ndani ya hospitali ile, machoni alionekana akiwa ameumia kupita kawaida, machozi yalikuwa yamejazana machoni mwake.
Akaingia ndani ya hospitali ile na kisha kuanza kuelekea sehemu ya mapokezi ambako akachukuliwa mpaka nje ya chumba cha wagonjwa mahututi. Wachezaji kadhaa wa timu ya mpira wa kikapu ya Chicago Bulls walikuwa wametulia nje ya chumba kile huku nyuso zao zikiwa kwenye majonzi mazito juu ya rafiki yao kupatwa na ajali ya gari.
Bwana Thomson akaanza kulia, uwepo wake nje ya chumba kile ulionekana kumuhuzunisha kupita kawaida jambo ambalo lilimfanya kujiona kutokutakiwa kuwa nje ya chumba kile. Akatulia nje ya chumba kile pamoja na wachezaji wale na watu wengine kutoka katika makampuni mbalimbali ya urembo na majarida.
Walikaa nje ya chumba kile kwa muda wa masaa nane na ndipo miili ile kutolewa na kupelekwa katika chumba kingine kwa ajili ya mapumziko huku oparesheni kadhaa zikiwa zimekwishafanyika. Hawakutakiwa kuwaona wagonjwa wao katika kipindi hicho, bado walihitaji kupata muda wa mapumziko.
Hawakuwa wakijitambua, walikuwa wamepoteza fahamu tangu pale ambapo ajali ile ilikuwa imetokea. Kila mtu alikuwa akitamani kuwaona wakifumbua macho na kuwaangalia tena, ajali ile ilizidi kuwatia wasiwasi kwa kuona kwamba hali za wagonjwa wale zingeendelea kuwa mbaya zaidi.
**********
Martin alikuwa amekaa sebuleni huku akiandika mistari ya wimbo wake mpya aliyoupa jina la ‘Mapenzi yangu’. Kwake, wimbo ule ulionekana kuwa mzuri ambao ungewashika mashabiki wake wengi ambao walikuwa wakipenda kusikiliza nyimbo nyingi kutoka kwake.
Huku akiendelea kuandika wimbo ule, ghafla simu yake ikaanza kuita. Kwanza akaonekana kukereka, alijilaumu sababu iliyompelekea simu kuiacha wazi bla kuizoma. Mara ya kwanza akaidharau lakini alipoona mpigaji akati, akaamua kuichukua na moja kwa moja kuipeleka sikioni.
“Upo wapi Mapac?” Sauti ya upande wa pili ilisikika ikiuliza swali.
“Nipo nyumbani”
“Unaangalia televisheni?”
“Hapana. Kuna nini? Wanaonyesha konseti ile niliyoifanya Arusha?” Martin aliuliza huku tabasamu pana likiwa usoni mwake.
“Kuna ajali. Kuna ajali imetokea”
“Ajali? Ajali gani na imetokea wapi?”
“Marekani. Patricia amepata ajali. Fungua CNN” Sauti ya upande wa pili ilisikika.
Martin hakutaka kuendelea kuongea, alichokifanya huku akionekana kwenye mshtuo mkubwa akaiwasha televisheni na kuanza kuangalia habari ile. Maneno ambayo yalikuwa yameandikwa yakaonekana kumshtua kupita kawaida, hakuyaamini macho yake, hakuamini kama jina la mtu ambaye alikuwa miongoni mwa watu waliopata ajali alikuwa Patricia.
“Mungu wangu!” Martin alijikuta akijisemea huku akisogea karibu zaidi.
Bado hakuonekana kuamini kama kile alichokuwa akikiona kilikuwa kweli au si kweli, alishindwa kuamini kama kile kitu kilikuwa kimetokea kilikuwa kwenye ulimwengu halisi au alikuwa ndotoni na baada ya muda angeamka kutoka katika usingizi mzito na kujikuta yupo kitandani mwake.
Akamuita mama yake ambaye akafika mahali pale na macho yake kuyapeleka katika kioo cha televisheni ile. Yeye mwenyewe hakuonekana kuamini kabisa, akajisogeza karibu kana kwamba kwa mbali hakuwa akiona vizuri.
“Yesu wangu!” Bi Evadia alisema kwa mshtuo huku akiipeleka mikono usoni mwake na kuziba mdomo wake.
 
SEHEMU YA 47 & 48


Tayari Martin alikuwa akitokwa na machozi, alishindwa kuvumilia kabisa. Taarifa ile ya habari ikaonekana kumchanganya kupita kawaida. Alichokifanya ni kuinuka na kuanza kutoka nje. Mama yake akaonekana kumshangaa, hata kabla hajauliza swali lolote, Martin alikuwa amekwishatoka nje.
Akaanza kuifuata sehemu ya kupakia magari na kisha kufungua mlango wa gari lake aina ya Verosa na kisha kumwambia mlinzi afungue geti na yeye kuondoka. Njiani hakuwa na raha, bado machozi yalikuwa yakimtoka, taarifa ile ya habari kuhusiana na ajali ambayo ilikuwa imetokea ilikuwa imemchanganya.
Njiani alikuwa akiendesha gari kwa kasi, safari hiyo ilikuwa ni kuelekea Mikocheni B alipokuwa akiishi Bi Beatrice, mama yake Patricia. Kutokana na kasi ambayo alikuwa nayo wala hakuchukua muda mrefu akawa amekwishafika katika nyumba hiyo na mlinzi kufungua geti. Hata kabla ya salamu akaamua kuufuata mlango wa sebuleni na kuingia hata bila hodi.
Macho yake yakatua machoni mwa Bi Beatrice ambaye alikuwa akiangalia televisheni huku akiwa akisiliza simu iliyokuwa sikioni mwake. Uso wake ulionekana kuwa na huzuni, machozi yalikuwa yakimtoka huku mara kwa mara akiwa anayafuta kwa kitambaa alichokuwa nacho mkononi.
Alipoona Martin ameingia ndani ya nyumba ile, akaacha kuongea na simu ile na kisha kumfuata Martin na kisha kumkumbatia. Wote walikuwa wakilia, taarifa ile ya habari ikaonekana kuwaumiza.
“Oooh! Patricia!” Bi Beatrice alisema huku akiwa bado amemkumbatia Martin.
“Pole mama. Yote ni mambo ya Mungu!” Martin alimwambia.
Siku hiyo ilikuwa ni kama siku ya msiba, wote walikuwa wakitokwa na machozi, ajali ile ambayo ilikuwa imetokea ilikuwa imewagusa kupita kawaida. Wakaendelea kuangalia taarifa ile ili kujua hali ambayo alikuwa nayo Patricia pamoja na mpenzi wake, Banana.
Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele, hali ya Patricia na Banana hazikuonekana kuwa sawa kabisa. Kila mwandishi ambaye alikuwa akizungumza alikuwa akizungumza kwa majinzi mazito kwani hali za watu wale zilionekana kuwatisha kupita kawaida.
“Itanipasa kusafiri kuelekea Marekani” Bi Beatrice alimwambia Martin.
“Nami pia itanibidi kuongozana nawe” Martin alimwambia.
“Sawa. Ngoja niongee na Thomson ili atume tiketi za watu wawili na afanye mipango ya viza” Bi Beatrice alimwambia Martin ambaye akaonekana kuridhika kwani asingeweza kubaki nchini Tanzania na wakati msichana ambaye alikuwa akimpenda alikuwa amepata ajali mbaya.
**********
Wiki moja iliyofuata safari ya kuelekea nchini Marekani ikaanza. Ndani ya ndege kila mmoja akaonekana kuwa na majonzi, taarifa ya ajali ambayo ilikuwa ikisikika katika vyombo vingi vya habari duniani ilizidi kuwaumiza mioyo yao. Martin hakuonekana kuwa na furaha hata mara moja, muda mwingi alikuwa amekiinamisha kichwa chake chini.
Mawazo yake yalirudi mpaka katika kipindi cha nyuma, kipindi ambacho alikuwa amekutana kwa mara ya kwanza na msichana Patricia katika shule ya Salma Kikwete. Alikumbuka tangu siku ya kwanza alipoanza mahusiano ya kirafiki na msichana yule, katika kipindi kile ambacho alikuwa ameangukia katika mapenzi yake.
Mawazo yake wala hayakuishia hapo, alikumbuka siku ya kwanza alipomueleza Patricia juu ya moyo wake kwa jinsi ambavyo ulijisikia juu yake. Alikumbuka mambo mengi yaliyopita katika kipindi hicho mpaka siku ile ya kwanza walipofanya mapenzi hotelini bila kuwa na mahusiano ya kimapenzi.
Martin alibaki akiumia kupita kawaida, moyoni mwake, Patricia ndiye alikuwa msichana ambaye alimpenda kuliko msichana yeyote yule, alimthamini kupita maelezo na ndio maana hata aliposikia kwamba msichana huyo alitaka kufunga harusi na mcheza kikapu Banana, alibaki akiumia.
Maishani mwake alikuwa radhi kukosa kila kitu lakini si kumkosa Patricia ambaye alimuonyesha mwanga mkubwa sana katika maisha yake. Aliikumbuka barua ile ambayo alimwandikia dakika chache kabla ya kuondoka kuelekea nchini Marekani, aliyakumbuka maumivu makali ambayo aliyapata siku ile. Alilia kupita kawaida, mpaka kipindi hicho bado alikuwa akiendelea kulia.
Tangu Patricia aondoke kuelekea nchini Marekani, bado Martin hakuwahi kuwa na furaha. Alipata umaarufu mkubwa nchini Tanzania kutokana na muziki ambao alikuwa akiufanya, aliingiza kiasi kikubwa cha fedha na bado alikuwa akiendelea kuingiza kiasi kingi cha fedha lakini bado furaha yake wala haikukamilika hata kidogo.
 
SEHEMU YA 49 & 50


Hakujiona kama angetakiwa kufurahi na wakati Patricia hakuwa mikononi mwake, hakujiona kuwa na sababu ya kufurahi na wakati msichana ambaye alikuwa akimpenda sana alikuwa katika mapenzi na mwanaume mwingine. Kwake, kila siku ilionekana kuwa kama jehanamu, maumivu yalikuwa yakiendela kila siku.
Katika kipindi hiki alikuwa safarini akielekea nchini Marekani kumuona msichana ambaye alikuwa akimpenda kwa moyo wa dhati, Patricia. Ingawa alikuwa na uhakika wa kumuona lakini moyo wake wala haukuwa na furaha hata kidogo. Alikuwa akielekea nchini Marekani huku msichana huyo akiwa mahututi, akiwa amepoteza fahamu zake kabisa.
Martin aizidi kuumia, hakuamini kama siku ambayo angemuona Patricia basi ingekuwa siku ile ambayo asingeweza kuongea nae, angebaki kimya kitandani alipokuwa amelazwa. Wakati mwingine Martin alitamani kile ambacho kilikuwa kinaendelea kingekuwa ndoto na baada ya dakika kadhaa kuamka na kujikuta kitandani huku akiwa amechoka kutokana na tamasha ambalo alikuwa amelifanya Arusha.
Hiyo wala haikuwa ndoto, hiyo ilikuwa hali halisi ambayo ilikuwa ikiendelea katika ulimwengu halisi. Kila alipokuwa akimwangalia Bi Beatrice ambaye alikuwa pembeni yake, moyo wake ulikuwa ukimuuma sana, mwanamke yule alikuwa amefanana sana na Beatrice ambaye alikuwa akimfuata kwenda kumuangalia nchini Marekani.
Sala yake bado ilikuwa ikiendelea kimoyo moyo, hakutaka Patricia afariki na wakati wala hakuwa ameongea nae na wala kumshukuru kwa wema wote ambao alikuwa amemfanyia katika kipindi chote. Alihitaji aongee na msichana huyo na kumwambia ukweli kwamba alikuwa akiendelea kumpenda japokuwa alikuwa mahututi kitandani.
Ndege ilichukua masaa ishirini na mbili na ndipo ikaanza kukanyaga katika uwanja wa kimataifa wa John F Kennedy na kisha abiria wote kuteremka. Kutokana na wakati huo kutokuwa kipindi cha baridi kali, hali ya hewa ikaonekana kuzoeleka miilini mwao.
Bwana Thomson alikuwa akiwasubii nje. Alipomuona mpenzi wake, Bi Beatrice, akaanza kumfuata na kukumbatiana. Wote wakaanza kulia. Martin alikuwa pembeni huku akiangalia kila kitu ambacho kilikuwa kinaendelea mahali hapo mpaka pale ambapo Bi Beatrice alipoanza kumtambulisha kwa Bwana Thomson.
Hawakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, safari ya kuelekea katika hospitali ya Metopolian kuanza. Njiani kila mmoja alikuwa kimya, bado hali ya Patricia ilikuwa mbaya sana na wala hakuwa amerejewa na fahamu toka alipopata ajali wiki iliyopita. Walipofika katika hospitali ile, kama kawaida yao waandishi wa habari wakaanza kuwazunguka kwa lengo la kuwahoji lakini hawakutaka kuongea kitu chochote kile.
Wakafika mpaka katika chumba kile alicholazwa binti yao na kisha kumsogelea pale kitandani. Kila mmoja alibaki akimwangalia kwa majonzi. Wote wakajikuta wakianza kulia tena. Martin hakuweza kuvumilia kabisa, msichana ambaye alikuwa akimpenda kwa moyo wake wote kwa wakati huu alikuwa kitandani akipumua kwa msaada wa mashine ya oksijeni huku dripu tatu tofauti zikiwa zinaning’inia.
Martin akaanza kumsogelea Patricia. Patricia hakuwa akiongea, hakuwa amefumbua macho, yaani kwa kifupi alikuwa akionekana kama mtu ambaye tayari alikuwa amekwishakufa kitandani pale na alikuwa akisubiri kuagwa sura ya mwisho na kuzikwa.
“Fumbua macho Patricia....fumbua macho uniangalie. Nimekuja huku kwa ajili yako...naomba ufumbue macho uongee nami Patricia....fumbua macho Patricia....” Martin alijikuta akiongea kwa sauti ya chini huku akimwangalia Patricia na huku machozi yakimtoka. Maneno yake yale wala hayakuweza kubadilisha kitu chochote, bado Patricia alibaki kimya, alionekana kama tayari alikwishafariki pale kitandani.
Siku hiyo ilionekana kuwa siku ya huzuni zaidi kwao wote. Patricia ambaye walikuwa wamekuja kumuona alikuwa kimya kitandani, walitamani muujiza wowote ule utokee na kumuona Patricia akifumbua macho yake na kuwaangalia tena na kisha kuongea nao. Sala zao zilionekana kuwa si chochote kwani waliziona kutokuwa na majibu yoyote yale.
Wote kwa pamoja walimuona Mungu akiwa amewapa jaribu kubwa ambalo lilikuwa ni zaidi ya uwezo wao wote, wala hawakutaka kukata tamaa, bado walizidi kumuomba Mungu zaidi na zaidi.
Muda wa kuwaona wagonjwa ulipokwisha walitakiwa kuondoka chumbani hapo na kisha kuelekea katika nyumba ya Bwana Thomson. Kwa kuwa Martin alikuwa mgeni ambaye alitambulishwa kuwa kama mpenzi wa Patricia nchini Marekani, akapewa chumba cha Patricia kwa ajili ya kukitumia katika siku zote ambazo angekuwa nchini Marekani.
 
SEHEMU YA 51 & 52


Majonzi kwake bado yalikuwa makubwa, usiku hakulala, alikuwa akizidi kumkumbuka Patricia ambaye alikuwa kimya kitandani. Moyo wake ulizidi kumuomba Mungu afanye muujiza wowote wa kumuamsha Patricia kitandani lakini sala zake hazikuwa na majibu yoyote yale.
Alimuona Mungu akichelewa kujibu sala zake, alimuona Mungu akiwa haijali furaha yake ambayo ilikosekana kwa kipindi kirefu. Kitu ambacho alikuwa akikihitai katika kipindi hicho ni kumuona Patricia akifumbua macho na kuongea tena.
Usingizi ulikatika kwake, alishinda akimfikiria Patricia, asubuhi ikaingia huku akiwa hajalala hata dakika moja. Gari likafika katika nyumba hiyo na kuwachukua tena kuwapeleka hospitalini.
Kama ambavyo walimuacha Patricia na ndivyo ambavyo walimkuta, alikuwa kimya kitandani.
Mipira ambayo alikuwa amewekewa na madaktari ndio ambayo ilikuwa ikitumika kumpitishia chakula huku mingine akiitumia kama kujisaidia kila alipotaka kujisaidia.
Patricia alionekana kuwa kama mfu kitandani pale, alionekana kama tayari alikwishakufa ila madaktari hawakutaka kusema ukweli. Kila alipokuwa akimwangalia Patricia, Martin alibaki akitokwa na machozi mfululizo, bado alionekana kuumia kupita kawaida moyoni mwake.
Chakula hakula, hamu yote ya kula ilikuwa imemtoka, kuna kipindi alihitaji kutokuondoka hospitalini, alitamani aendelee kubaki na Patricia chumbani pale mpaka pale atakapoona mwisho wake ungekuwa nini. Alimpenda sana Patricia, hakutaka kumpoteza katika maisha yake, alimthamini na kumhitaji.
Alitamani kutumia kila kitu ambacho alikuwa nacho katika maisha yake lakini mwisho wa siku amuone Patricia akiyafumbua macho yake tena na kumwangalia huku akiachia tabasamu pana ambalo mara kwa mara lilikuwa likimchanganya sana shuleni. Kipindi hicho, ilionekana kuwa kama ndoto, tena ndoto mbaya ambayo wala hakutakiwa kuiota katika maisha yake yote.
"Au ninaota? Lakini kama ni ndoto mbona inatisha halafu ni ya muda mrefu hivi? Mmmh! Inatisha" Martin alijisemea huku akiswa amepiga magoti huku amekiegemea kitanda alicholazwa Patricia na mkono mmoja wa Patricia akiwa ameushika.

Siku ziliendelea kukatika na hali ya Patricia iliendelea kuwa vile vile. Alikuwa amelala kitandani kama mtu ambaye alikwishakufa. Alipumua kwa kutumia mashine ya oksijeni huku mipira ya kumlisha ikiwa imewekwa mwilini mwake. Kila wakati Martin alipokuwa akimwangalia hakuweza kuamini kama maisha ya baadae ya patricia tangekuwa namna ile.
Kila siku alikuwa akifika pale hospitalini huku wakati mwingine akitamani kulala katika chumba kile ili mladi tu awe karibu na patricia. Kwake, kuugua kwa Patricia lilikuwa jaribu na pigo kubwa kwake kuliko pigo lolote ambalo alilipata kabla.
Mwezi wa kwanza ukakatika. Madaktari wakatoa taarifa ambayo ilikuwa imemshtua kila mtu, Banana alikuwa amekufa kitandani. Taarifa ile iliinua vilio kwa wapenzi wote wa mchezo wa kikapu nchini Marekani, hawakuamini kama mchezaji yule ambaye alikuwa ameanza kuvuma angeweza kuwatoka katika siku za karibuni.
Mazishi yakafanyika, wachezaji wengi wa mpira wa kikapu wakawa wamehudhuria mazishi hayo ambayo yalikuwa yamemgusa kila mtu. Macho na masikio ya watu yakawa yakisikilizia kuhusu hali ya Patricia ambaye alikuwa kitandani akiendelea kuugua. Kila siku hali yake ilikuwa vile vile.
Madaktari wakahangaika usiku na mchana, ripoti ya hali yake ikatolewa kwamba kamwe hasingeweza kuinuka kitandani, uti wake wa mgongo ulikuwa umevunjika vunjika jambo ambalo liliufanya mwili kupooza kuanzia shingoni kuja chini. Ile ilikuwa ni taarifa mbaya sana, kupooza kwa mwili wake kulimaanisha kwamba Patricia asingeweza kuinuka kitandani tena wala kukisogeza kiungo chochote cha mwili wake.
Taarifa ile ilikuwa mbaya zaidi kwa Martin, alibaki akilia chumbani mule huku akimwangalia Patricia ambaye bado aliendelea kuwa kimya. Kila siku alikuwa akitamani Patricia afumbue macho yake tena na aongee nae tena kama jinsi alivyozoea kufanya katika kipindi cha nyuma.
Mwezi wa pili ukakatika, wa tatu ukakatika na hata wa nne kukatika na ndipo Martin kuamua kurudi nchini Tanzania. Kila mtu ambaye alikuwa amemuona alimuonea huruma, mwili wake ulikuwa umekonda kupita kawaida. Nchini Tanzania hakutaka kufanya kitu kingine chochote zaidi ya kuendelea kuwasiliana na Bwana Thomson na kisha kurudi tena nchini Marekani.
Japokuwa Patricia alikuwa katika hali mbaya lakini wala hakutaka kuyaondoa mapenzi yake kwa msichana huyo. Bado alikuwa akimpenda kupita kawaida, japokuwa alikuwa katika hali mbaya lakini wala hakutaka kumuacha. Alikumbuka maneno ambayo alimwambia siku za nyuma kwamba
 
SEHEMU YA 53 & 54

angempenda katika hali zote, hayo ndiyo yaliyomfanya kuendelea kumpenda na kumhitaji Patricia.
Mwaka ukakatika na mwaka wa pili kuingia. Hali ya Patricia iliendelea kuwa vile vile, hakufumbua macho yake wala kinywa chake. Wakati mwingine taarifa zilikuwa zikiendelea kutangazwa kwamba Patricia alikuwa amekwishakufa kitandani jambo ambalo liliwataka watu kuuona mwili wake. Taarifa zile zilikanushwa vikali na Bwana Thomson ambaye bado alikuwa akiendelea kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya matibabu.
Miezi sita ikakatika. Mwaka mmoja na miezi sita, Patricia hakuwa amefumbua macho yake. Siku kadhaa zikasogea na ndipo pale Patricia alipoanza kuyafumbua macho yake. Manesi hawakuonekana kuamini, walichokifanya ni kuelekea katika ofisi ya dokta Simpson na kumwambia kuhusu hali ya mgonjwa.
Dokta Simpson hakutaka kuendelea kubaki ofisini mule, aichokifanya ni kuanza kukimbia kwa kasi kueleka katika chumba kile. Macho ya Patricia yalikuwa yakiangalia juu tu tena sehemu moja, hata pale alipokuwa akimchezeshea mkono karibu na macho yake, mboni nyeusi ya jicho haikucheza kabisa.
Dokta Simpson akachukua simu yake na kumpigia Bwana Thomson na kumpa taarifa ya maendeleo ya binti yake. Ni ndani ya dakika kumi tu Bwana Thomson akafika hospitalini hapo huku akiwa na Bi Beatrice pamoja na Martin.
Wote wakaonekana kuwa na furaha, tayari walikuwa wamesubiri kwa takribani mwaka mmoja na miezi sita kusubiri kwa maendeleo ya binti yao pale kitandani. Leo, Patricia alikuwa amefumbua macho yake.
Ingawa alikuwa ameyafumbua macho yake lakini wala Patricia hakuweza kuyapepesa., bado alikuwa akiangalia sehemu moja tu. Martin alikuwa akitabasamu tu, kitendo cha kuziona mbozi za Patricia kwa mara nyingine kilionekana kumpa furaha na matumaini kwamba kuna siku Patricia angeweza kuongea tena.
Ilipita miezi miwili mimgine na ndipo Patricia alipoanza kupepesa macho yake. Hiyo ilikuwa ni furaha ya kila mmoja, matumaini ya kuona kwamba Patricia angeweza kuongea kama zamani yalikuwa yameanza kuwarudia tena. Tatizo bado lilikuwepo, kuvunjika vunjika kwa uti wa mgongo na kumfanya kupooza pale kitandani.
Kila alipokuwa akipepesa macho yake huku na kule na kuyakutanisha na macho ya Martin na wazazi wake, alikuwa akitabasamu lakini wala hakuweza kufanya kitu ingine zaidi ya hicho. Bado hali yake haikuonekana kuwa nzuri hata mara moja.
Muda mwingi Patricia alikuwa akitokwa namachozi hasa kila wakati ambao alikuwa akimwangalia Martin. Moyoni alionekana kuwa na jambo ambalo lilikuwa likimliza lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alieleza sababu zilizompelekea Patricia kutokwa na machozi.
“Nitakupenda siku zote katika maisha yangu” Martin alimwambia Patricia maneno ambayo yalikuwa yakimuongzea tabasamu zaidi pale kitandani alipokuwa amelala huku asilimia kubwa ya mwili wake ukiwa umepooza.
********
Hali ya Patricia haikuendelea zaidi ya hapo. Kitendo chake cha kufumbua macho kilionekana kuwa hatua ya mwisho kabisa katika maisha yake pale kitandani. Alikuwa akiendelea kuwa kimya huku akimwangalia kila mtu ambaye alikuwa akiingia na kutoka ndani ya chumba kile.
Patricia alionekana kuwa kwenye mateso makali, kitendo cha kutokuongea wala kutokutikisa kiungo chochote mwilini mwake kilionekana kumpa wakati mgumu. Kamwe hakutaka kuwa hivyo, ajali ambayo alikuwa ameipata, ajali ambayo ilipangwa ndio ambayo ilikuwa imebadilisha maisha yake yote.
Uzuri wake wala haukupungua. Japokuwa mashine ya oksijeni ilikuwa imeziba mdomo na pua yake lakini uzuri wake ulikuwa vile vile. Watu wengi kutoka nje na ndani ya nchi ya Marekani walikuwa wakifika mara kwa mara katika hospitali hiyo na kumtakia afya njema.
Patricia alikuwa katika wakati mgumu sana, mwili wake ulikuwa umepungua kupita kawaida, kila mtu ambaye alikuwa akimwangalia alikuwa akimuonea huruma. Mwaka wa pili ukakatika, kidogo mafanikio mengine yakaanza kujionysha, mdomo wa Patricia ukaanza kufunguka na kuanza kuongea.
Hiyo ilionekana kuwa hatua kubwa na muhimu sana katika maisha yake. Aliweza kumuita mtu yeyote japokuwa kwa shida sana. Alikuwa akiongea vizuri kama kawaida japokuwa kwa sauti ya chini sana. Kila mmoja akaanza kumshukuru Mungu kwa ile hatua ambayo Patricia alikuwa ameifikia.
 
Back
Top Bottom