SIMULIZI RIWAYA
JF-Expert Member
- Feb 19, 2022
- 417
- 1,285
- Thread starter
- #181
Tukiamua tunaweza lkn [emoji16][emoji16]Hii ni script ya Hollywood kabisa yani sema ndio vile bongo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tukiamua tunaweza lkn [emoji16][emoji16]Hii ni script ya Hollywood kabisa yani sema ndio vile bongo
Hi Nini Sasa Kaka.SASHA MLINZI WA NAFSI
SEASON 3
Sehemu ya...........48
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
ILIPOISHIA…….
Upande wa pili wakati Felix na Tesha wakizidi kusogea, ghafula wote walishtushwa na milio ya pikipiki zikiwashwa kwa pamoja.
“Felix ….” Tesha aliita kwa hofu kubwa…
SASA ENDELEA…
Mara ghafula kufumba na kufumbua waliona pikipiki moja ikija kwa kasi kutokea mbele yao. Dereve alikuwa amenyoosha usukani kuwaelekea wao pale walipo. Walipokwepa kusogea kulia Dereva naye akakunja kona kulia waliporudi kushoto naye akanyonga usukani kuwafuata, ni wazi dereva wa pikipiki hiyo alikuwa amekusudia kuwagonga.
“Felix…..” Tesha aliita kwa hofu
“Kaa nyuma yangu Teshaaaa…..” Felix alipaza sauti, akamvuta Tesha nyuma yake kwa nguvu kisha yeye akasimama mbele, uso kwa uso akawa anatazamana na taili la mbele la pikipiki hiyo. Dereva akiwa amebakiza hatua kama mbili kumfikia Felix mara alikunja kona kwa kasi kwenda kushoto, badala ya kumgonga akaishia kumparaza Felix katika bega na mguu wake upande wa kulia, Felix akaanguka chini akiwa na maumivu makali.
“Felix….jamani msadaaaa….msaaaada” Tesha alipaza sauti huku akisogea kujaribu kumuinua Felix pale chini.
“Usijali Tesha niko salama…” Felix aliongea akijikaza kiume na kushika bega lake, alikuwa amejeruhiwa na taratibu damu yenye rangi ya ajabu ikawa inamtoka. Sasa akawa na mtihani mwingine wa kuficha jeraha lake ili Tesha asije gundua siri yake kubwa ambayo katu hakuwa akitamani mwanamke wake aijue.
Mara wakasikia tena muungurumo mkali wa pikipiki, ajabu yule dereva baada ya kwenda umbali wa kama hatua ishirini hivi, alikata kona kibabe sana huku taili la nyuma likiserereka kiasi cha kufanya vumbi jingi kutimka hewani, alionekana ni mtaalamu mno wa kucheza na pikipiki.
“Anakuja tena….” Alisema Tesha,hofu ikiwa imemjaa mara dufu, baada ya yule mtu mwenye pikipiki kugeuka kwa mara nyingine alianza kuwafuata Felix na Tesha pale walipo kwa kasi ileile kama mwanzo. Tofauti na walivyo tegemea, safari hii hakuwa peke yake bali waliongezeka wengine na kufanya idadi yao kuwa wanne, kila mmoja akiwa na pikipiki yake. Mmoja akawa anakuja kutokea mbele mwingine kutokea nyuma mwingine kushoto na mwingine wa mwisho anakuja kutokea kulia.
Hali hii ikampa ugumu hata Felix ambaye tayari alishasimama kiume kujaribu kukabiliana na yule anaekuja kutokea mbele yao lakini ghafula wanaongezeka na kuwa wanne. Sasa akawa hana la kufanya akaishia kumshikilia mpenzi wake Tesha huku akijaribu kumkinga kutoka pande zote asidhurike lakini haikuwa rahisi kihivyo. Mwisho wale watu walifika kwa kasi wakapita na kupishana kama upepo, kwa mara nyingine Felix akajikuta anapigwa vikali na pembe ya usukani katika ubavu wake wa kulia akaanguka chini akiwa na maumivu makali mno.
Felix alipokuja kutahamaki akawaona wale jamaa wenye pikipiki wakipotelea gizani na wala Tesha hakuwepo pembeni yake, tayari walishamchua na kuondoka naye kama vile ambavyo kifaranga hunyakuriwa na mwewe.
“Teshaa………” Felix aliita huku akijizoazoa na kusimama akajaribu kukimbia kuwafukuzia wale watu lakini hakufika mbali akaanguka, akasimama tena huku akiwa ameshikiria bega lake mahali alipojeruhiwa, baada ya hatua mbili akaanguka tena.
“Tesha…Tesha …Teshaaaaa….” Aliita Felix akiwa amelala chali na kutazama juu mawinguni. Kijana huyu alikuwa kwenye hali mbaya mno kwa sasa, moyo wake ulimuuma isivyo na mfano. Ni kwa mara ya kwanza anaufungua upya ukurasa wa mahusiano yake yeye na mrembo Tesha lakini hata nafasi ya kulala naye usiku mmoja hajapata tayari penzi lao linakutana na misukosuko mikali.
Wakati akiwa amelala pale chini asijue cha kufanya mara simu yake ikaita tena. Felix alikurupuka akakaa chini mchangani kisha akaitoa simu yake mfukoni akatazama namba ya mpigaji alikuwa ni yule yule Madam Husnata.
“Fuc*** bila shaka ni wewe umefanya hivi…” Alisema Felix akiwa ameuma meno yake kwa hasira kisha akapokea simu na kuiweka sikioni.
“Najua uko hapa Night City Hotel Felix, kabla sijaharibu mambo njoo chumba namba 204 utanikuta…. una dakika 5 tu na ninaanza kuzihesabu kuanzia sasa” Sauti nyororo ya Madam Husnata ilisikika kutoka upande wa pili wa simu kisha ikakatwa. Mwanamke huyu kutoka MG Family alionekana akiwa amelala kitandani ndani ya chumba kimoja chenye kila aina ya fahari, Madam Husnata alilala kitandani hapo akiwa mtupu kama alivyozaliwa. Baada ya kukata simu alichukua glasi yenye kinywaji ndani yake, kisha akanywa fundo moja na kuirudisha. Sasa akawa anautazama mlango wa chumba chake huku uso wake ukionekana kujawa na tabasamu.
“Pumbavuu umenigusa pabaya Hustana, leo ndio utanijua mimi ni nani, haki ya Mungu naapa….” Alisema Felix kisha akainuka na kuanza kupiga hatua ndefu ndefu kuelekea lango la kuingilia ndani ya jengo kuu la hoteli hiyo. Njiani Felix anakutana na walinzi watatu wa hoteli hiyo wakija mkukumkuku.
“Bosi tumesikia makelele yakitokea upande huu vipi kwema? Haujaona chochote?” Aliuliza mlinzi mmoja lakini Felix hakujibu kitu, akapita katikati yao akaenda zake, akawaacha walinzi hao wakimsindikiza kwa macho na mwisho wakatazamana wenyewe kila mmoja akiwa na maswali yasiyo na majibu.
****
Ingawa ni kwa taabu sana lakini amini usiamini David alifanikiwa kushuka hadi chini, akakanyaga ardhi ya barabara ile inayokatiza chini ya mlima kutokea ufukweni hadi kule ilipo himaya ya Magnus. Barabara ambayo kwa kawaida huwa iko bize wakati wote, masaa 24.
“Oooh! Asante Mungu” Alisema Dayana akiwa kule juu pangoni na haraka akaanza kuivuta ile kamba ambayo David aliitumia kushuka. Baada ya kumaliza kuipandisha juu Dayana na David walipungiana mikono na ikiwa ni ishara ya kutakiana heri katika jukumu hilo zito la kujaribu kuitoroka himaya ya Magnus.
David alivuta pumzi ndefu na baada ya hapo akaanza kupiga hatua kusogea mbele hali akiwa na tahadhali kubwa. Miale ya moto iliyokuwa imetundikwa katika kuta za barabara hiyo ilimsaidia David kuona alikotoka na anapokwenda pia. Dayana aliendelea kumsindikiza kwa macho akiwa kule juu pangoni hadi pale David alipopotea kwenye upeo wa macho yake.
“Uuuhu!!….easy easy Dayana, everything will be fine….tutatoka hapa” Dayana alijisemea mwenyewe huku akijipiga piga kifuani akijaribu kuutuliza moyo wake uliokuwa ukidunda kwa kasi wakati huo.
Ni kama vile Dayana alijua kuna hatari inakwenda kutokea kwani ile anamaliza tu kuzungumza neno lake la mwisho mara anasikia muungurumo wa gari na alipotazama chini akaona msafara wa gari nne zikipita kwenye ile barabara kuelekea kule kule alikoelekea David muda mfupi uliopita.
“Shiiiit…” Alisema Dayana, tayari mambo yalikuwa karibu kuharibika kwa mara nyingine.
******
Upande wa pili ndani ya hoteli ya kifahari Night City Hotel katika ghorofa ya kumi na moja, mlango wa lifti ulionekana ukifunguka akatoka Felix akiwa anapiga hatua ndefu ndefu huku uso wake ukiwa umekunjamana kwa hasira, alitembea haraka na mwisho akasimama mbele ya mlango wa chumba kimoja, chumba namba 204. Ndani ya chumba hicho alikuwepo Madam Husnata ambaye tayari alishahisi kuna mtu mlangoni, tabasamu lake likazidi kuongezeka.
ITAENDELEA….
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
Simulizi hii ni Tsh 1000 tu lipia kwa mpesa namba 0756862047 jina Saul au Airtel money namba 0788967317 jina Saul
Kisha njoo WhatsApp namba hzo hzo
Dah haya leo nawarushia vipande 3 kw hasira[emoji16]Hi Nini Sasa Kaka.
Sentensi mbili tatu tu?
Kama hukuwa tayari ungeacha Hadi baadae
Sijapenda [emoji16]Kipande kizima kimeelezea Pikipiki tu ilivyomgonga Felix [emoji23][emoji23][emoji23]
WhatsApp 0756862047Vp imeisha au bado sipendi kusoma nusu nusu.