SASHA MLINZI WA NAFSI
Sehemu ya............24
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
ILIPOISHIA...
Mafisa wapelelezi kutoka jeshi la polisi Inspekta Brandina na Inspekta Masoud wanapanga mikakati ya kuhakikisha wanamkamata Felix moja kati ya wahusika wa matukio ya utekaji. Upande wa pili katika bonde la Magnus, Dayana anamganda David akihitaji penzi kutoka kwake.
Je nini kitafuata?
SASA ENDELEA....
[emoji294][emoji294][emoji294]
Dayana alizidi kumsogelea David.
"Kasema anarudi baada ya dakika 10, Davii..zinatosha sana please nisaidie mwenzio nateseka" Alisema Dayana huku akianza kuushika shika mwili wa David. Ilikuwa ni rahisi kwa sababu pia wote walivaa nguo za ndani pekee
"Da...ya...naaa!!" David aliita kwa taabu kidogo lakini Dayana hakuacha, alidhamiria.
Punde Dayana alianza kummwagia David mvua ya mabusu shingoni kwa kasi na mwisho akahamia mdomoni huku taratibu akiupeleka mkono wake ndani ya boksa ya David. Hali hii ilizidi kumuweka David katika wakati mgumu, alijitahidi kumsukuma Dayana lakini tayari Dayana alishaingiza mkono hadi ndani kabisa ya boksa yake.
David akajikuta mwili wake unapata ganzi ya ghafula mithiri ya mtu aliyepigwa na shoti ya umeme. Wakati huo huo David alisikia vishindo vya miguu ya Zungu akirudi, lakini Dayana yeye hakuwa akisikia kitu aliyafumba macho yake huku akiwa amezama mazima na kuelea kwenye ulimwengu wa huba.
David hakutaka kuendelea kusubiri haraka alimsukuma Dayana kwa nguvu kubwa, Dayana alirudi nyuma na kuanguka chini.
"Oii! Twendeni basi kuposhwari hu....." Alisema Zungu lakini akashindwa kumalizia sentesi yake akabaki ameduwaa akishangazwa na mazingira aliyowakuta David na Dayana.
Dayana alikuwa amekaa chini huku David naye akizuga na kugeuka akawa anatazamana na ukuta wa bonde hilo.
"Nyie vipi kuna nini? Dayana mbona umekaa chini kwamba umeshachoka tayari?" Aliuliza Zungu akiwatazama David na Dayana kwa zamu.
Hakuna aliyejibu wote wakawa kimya.
"Aah! Dayana anasema anahisi kizunguzungu" Mwisho David alidanganya huku akiwa bado amegeukia kule ukutani. Hakuwa na jeuri ya kugeuka atazamane na Zungu kwani tayari hata yeye mwanajeshi wake alishasimama imara tayari kwa mapambano mara baada ya kushikwa na Dayana, mbaya zaidi alikuwa amevaa boksa pekee, ilikuwa ni rahisi mno kwa Zungu kumshtukia.
"Nilisema lakini usitufuate, si unaona sasa mambo ya kung'ang'ania mishe za kiume" Alisema Zungu huku akisogea hadi pale alipo Dayana.
"Vipi tukurudishe au?" Aliuliza Zungu.
"No! Nendeni nitarudi mwenyewe" Alijibu Dayana huku akisimama ghafula. Alionekana kuwa na hasira sana, Zungu akawa anashangaa mtu aliyeambiwa anahisi kizunguzungu kasimama kwa kasi bila tabu yoyote.
Mwisho walikubaliana hivyo, Dayana akawa anarudi, David na Zungu wao wakaendelea kusonga mbele. Lakini kabla hawajafika mbali mara walisikia kelele za Dayana akilia kwa nguvu.
"Mamaaa...nakufa!"
David na Zungu walisimama ghafula na kutazamana, wote walisikia kelele hizo kutoka kwa Dayana, wakawa wanasikilizia kwa mara ya pili lakini kukawa kimya.
"Oya turudi kuna shida mwanangu" Alisema Zungu na bila kujiuliza mara mbili mbili aligeuka haraka na kuanza kurudi, David naye akawa anamfuata nyuma kwa kasi.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Wakati huo upande wa pili Magnus alikuwa akiendelea kuongea na watu aliowaita wanafunzi wake kutoka ISRA, wale aliowateka kwa nyakati tofauti tofuauti akawaleta katika kisiwa hicho.
Sasa walikuwa darasani...
"Leo tunao wageni wawili ambao ni wenzetu kutoka ISRA, Zucc na Femi kule nyuma. Karibuni sana" Magnus aliongea kwa sauti nzito yenye kukoroma huku akinyoosha kidole chake kuwaelekea Zucc na Femi ambao walikaa nyuma kabisa ya darasa hilo.
Macho ya Magnus yalizidi kuwa mekundu kutokana na ule moshi uliokuwa ukitoka kwenye vile visahani mezani lakini yeye wala hakujali. Aliendelea kuifurahia harufu ya moshi huo, kwake ikiwa ni burudani kubwa.
Nywele zake ndefu, ndevu zake nyingi na nyeupe vilizidi kumfanya mzee huyo awe na muonekano wa kutisha mno. Aliendelea kuzungumza...
"Kule ISRA wananiita mimi muasi, lakini sio kweli. Mimi Magnus sio muasi bali ni mtu ambaye nilifanikiwa kuzijua siri nyingi za ISRA zilizofichwa kwa muda mrefu, siri ambazo zimefichwa kwa makusudi ili kuinyima uhuru ISRA na watu wake. Ni siri hizo ambazo zilinifanya mimi kutamani kufanya mabadiliko lakini watu wenye roho mbaya, watu wanaong'ang'ania madaraka wakaniita muasi, wakanishambulia wakaninyang'anya nguvu zangu na baadae wakanitupa nje ya ISRA" Magnus aliongea kwa masikitiko makubwa. Akatulia kwa muda kisha akaendelea...
"Hata baada ya kuwa nje ya ISRA sikuwahi kukata tamaa bado nimeendelea kupambana kuhakikisha haki ya ISRA inapatikana. Unaweza ukashangaa kwa nini na uzee wangu huu bado nataka sana kurudi ISRA, si kwa ajili yangu. Ni kwa ajili yenu ninyi na vizazi vyenu, ni lazima Mapinduzi yafanyike ili wajukuu zangu na watoto wenu wasije kuishi gizani kama sisi tulivyoishi. Nataka tutengeneze historia mpya ndani ya ISRA, mimi nikishirikiana na ninyi kwa pamoja tutamtoa Gu Gamilo na watu wake kwenye kiti kisha tutaweka watu watakaofuata haki na misingi ya ISRA iliyokuwepo tangu enzi za mababu zetu. Leo kwa mara ya kwanza nitaziweka wazi baadhi ya siri zilizofichwa ili na ninyi muone kama ni sahihi Magnus kuitwa muasi au alaa! MAPINDUZI YAFANYIKEEEE....."
"KWA AJILI YA MAISHA BORA YA ISRA NA WATU WAKE" Walijibu wanafunzi wa Magnus.
"Sisi leo tunaitwa WALINZI WA NAFSI tena nafsi za wanadamu, la hasha hilo sio jina letu tulipewa tu ili kutupotosha. Ukweli tunatofauti kubwa sana na Binadamu wala hatuhusiani kwa lolote ndio maana Mungu alituumba sisi akatupa nguvu na uwezo kuliko binadamu akatuweka ndani ya ISRA na binadamu akawaweka kwenye hii Dunia. Sisi kupewa nguvu zaidi yao ni kwamba tunaruhusiwa kuwatawala na si kulinda nafsi zao kama tunavyo danganywa siku zote. Sisi ni watawala na wao ni watawaliwa. Kama ni ulinzi wa nafsi zao kuna malaika ambao wanafanya kazi hiyo na sio sisi. Kuna malaika Gabriel, Michael, Israel na wengi wengi, sisi hatuhusiani na kazi zao KABISA, Ndugu zangu WAISRA tunahitaji kuungana na kwenda kuchukua kile kilichochetu kutoka kwa Gu Gamilo kule ISRA hatutaki tena kufanya mambo yasiyotuhusu Sijui kukusanya machozi, kuzuia ajali, kuua au kulinda binadamu zote hizo sio kazi zetu" Magnus aliongea kwa kumaanisha, sauti yake iliyojaa mamlaka na ushawishi mkubwa iliweza kuwaingia asilimia kubwa ya wanafunzi wake.
"Anaongea nini huyu?" Femi alimuuliza Zucc aliyekaa pembeni yake kwa sauti ya chini, wakawa wananong'ona.
"Hata sielewi lakini maneno yake ni kama yana ukweli Femi"
"Hapana, ni muongo anadanganya. Magnus ni mtu mwenye tamaa kama tulivyoambiwa, muangalie hata machoni, hafanani kabisa na mambo anayoongea. Anajaribu kutushawishi ili tuwe upande wake, anataka tufanye kazi badala yake kwa sababu hana nguvu tena za kuingia ISRA" Alisema Zucc.
"Lakini sisi tayari ni mateka wake, hatuwezi kutoka hapa kama tusipokuwa upande wake" Alijibu Zucc.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Upande wa pili Baada ya Zungu na David kusikia kelele za Dayana walirudi haraka na baada ya hatua kadhaa walimuona Dayana akiwa ametereza na kuangukia kwenye kichaka kilichokuwa na miiba.
"Dayana shida nini" Aliuliza Zungu huku akikimbia kumuwahi Dayana pale chini.
Dayana aliumia sana ukizingatia mwili wake ulikuwa wazi akajikuta anachomwa vibaya na miiba ile.
"Uko sawa Dayana" Aliuliza David huku naye akiwahiwa na kumshika mgongoni, akawa anasaidia kumuinua lakini Dayana akautoa mkono wake hakutaka kabisa David amguse.
Bado Dayana alikuwa amekasirishwa mno na kitendo alichokifanya David, kama mwanamke alikuwa amejizalilisha vya kutosha akiamini David angemsikiliza na kumtimizia haja yake lakini David hakufanya hivyo, badala yake alimsukuma.
David alijikuta anaumizwa pia na hali aliyokuwa nayo Dayana licha ya kutambua kwamba hana kosa lolote lakini bado alimuonea huruma mwanamke huyo.
Walisaidiana kumuinua Dayana kutoka pale chini kwenye miiba, wakati wanasimama mara ghafula mwanga mkali wa tochi ulipita mbele yao kwa kasi.
"Chuchumaeni chini" Alisema Zungu haraka wote wakafanya hivyo.
"Ni tochi za walinzi, bila sasha wamesikia kelele za Dayana" Alisema Zungu.
"Hapa mambo yameshaharibika, turudi tu hili zoezi tutalifanya kesho mshikaji wangu" Zungu alitoa wazo.
Mwisho Zungu, David na Dayana walirudi kule walipokaa mateka wengine, wakachagua sehemu nzuri pembeni ya kuta za bonde hilo wakawasha moto na kulala.
Ilikuwa ni ngumu sana kwa David kupata usingizi, hakuwa amezoea kuishi kwenye mazingira magumu kama hayo. Alikaa na kuegemea ukuta huku akitafakari hatima ya maisha yake itakuwa ni nini. Aliwaza pia kuhusu mdogo wake Tatu pamoja na mama yake ambaye kwa mara ya mwisho alimuacha akiwa ni mgonjwa amelazwa hospitali. Hadi inafika saa 11 alfajiri bado David hakuwa amepata usingizi.
[emoji294][emoji294][emoji294]
ASUBUHI SIKU INAYOFUATA.....ISRA.
Ilikuwa ni asubuhi na mapema siku inayofuata katika mji wa ISRA, tayari viongozi mbalimbali wa ISRA walishafika ndani ya jengo la Ikulu na moja kwa moja walielekea kwenye jengo ambalo hutumika kujadili na kutoa hukumu mbalimbali za kisheria ndani ya ISRA.
Sasha, Handan pamoja na wale wanawake wawili wakiongozwa na askari wa ulinzi waliletwa na kuingizwa ndani ya chumba hicho. Sasa alikuwa anasubiriwa mkuu wa ISRA Gu Gamilo ambaye pia ni baba yake Sasha.
Haukupita muda Gu Gamilo aliingia akiwa ameongoza na askari wawili nyuma yake. Sura yake ilionekana kujaa simanzi kubwa.
Gu Gamilo alikumbuka siku kama hiyo iliwahi kutokea miaka mingi iliyopita, siku ambayo alisimama mbele katika chumba hicho hicho akamuhukumu kaka yake Magnus na kumfukuza ISRA. Leo hii tukio kama lile lile linajirudia tena lakini safari hii si kaka yake bali ni mtoto wake SASHA.
Je, nini kitafuata?
Hii ni SASHA MLINZI WA NAFSI sehemu ya 24, tukutane sehemu ya 25.
Simulizi ni shillingi 1,000/= lipia kwa mpesa namba 0756862047 jina saul au Airtel money namba 0788967317 jina saul kisha njoo WhatsApp inbox namba hizo hizo
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047.