Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,985
- 10,840
- Thread starter
- #61
SEHEMU YA 45
Dereva akalipaki gari lake nje ya jengo la kanisa hilo, Bi Happy akateremka na kwenda kukitoa kibaiskeli katika boneti na kisha kuanza kumshusha mumewe na kumpakiza kwenye kibaiskeli kile na kisha kuanza kuelekea ndani ya kanisa lile.
Washirika wa kanisa hilo wakabaki wakiwa na mshangao, walikuwa wakimshangaa Bwana Wayne na mkewe. Kila mmoja alitambua kwamba Bwana Wayne alikuwa mtu maarufu sana kutokana na utajiri mkubwa ambao alikuwa nao.
Watu wengine wakachukua simu zao na kuanza kumpiga picha katika kipindi ambacho walikuwa wakiufuata mlango wa kuingia kanisani humo. Kwao ilionekana kuwa jambo gumu sana kukutana na mtu kama Bwana Wayne katika maisha yao, hivyo wakaichukua nafasi hiyo kuwa ya kipekee sana katika maisha yao.
Bwana Wayne na mkewe, Bi Happy wakaingia kanisani na kutulia. Ibada ilikuwa ikiendelea zaidi na mpaka mchungaji Gibson kusimama mbele ya kanisa na kuanza kuhubiri. Katika kila neno ambalo mchungaji Gibson alikuwa akiliongea, Bwana Wayne alikuwa akitikisa kichwa chake kutoka juu kwenda chini na chini kwenda juu.
Mwisho wa siku, Bwana Wayne akajikuta akilia, hakuamini kama kuna siku angesikia maneno matamu yaliyojaa faraja kama yale ambayo alikuwa akiyasikia kutoka kwa mchungaji Gibson. Mchungaji aliendelea kuhubiri mpaka katika kipindi ambacho aliwaita watu waliokuwa na magonjwa mbalimbali kwenda mbele ya kanisa hilo.
Bwana Wayne hakutaka kuchelewa, akaanza kukisukuma kibaiskeli kile na kuanza kuelekea mbele ya kanisa. Hakuwa peke yake mahali pale, zaidi ya watu mia tano walikuwa wamesimama. Mchungaji akawataka wagonjwa wale kushika sehemu ambazo zilikuwa na matatizo. Bwana Wayne akaupeleka mkono wake sehemu za siri.
Maombezi yakaanza hapo. Mchungaji Gibson akaanza kufanya maombezi, alichukua dakika tano, akawaruhusu wagonjwa wale kwenda kukaa katika sehemu zao huku akiwataka kuamini kwamba walikuwa wamepokea uponyaji.
Hiyo ndio ilikuwa siku ambayo ikayabadilisha maisha ya Bwana Wayne na mkewe, kila siku walikuwa watu wa kwenda kanisani huku mioyoni wakiamini kwamba Mungu alikuwa na mipango na maisha yao. Hali ya Bwana Wayne haikubadilika, iliendelea kuwa vile vile lakini moyoni alikuwa akiamini kwamba kuna siku agepokea uponyaji.
Bwana Wayne akaanza kujiingiza katika kumtumikia Mungu, alichokifanya ni kuanza kutoa kiasi kikubwa cha fedha kusaidia vituo mbalimbali vya uchungaji duniani. Kitu ambacho alikuwa amekipanga kwa wakati huo ni kumtumikia Mungu kwa njia tofauti tofauti kwani aliamini kwamba Mungu