Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,985
- 10,840
- Thread starter
- #161
SEHEMU YA 126
Alikuwa akicheka!
Nilimkodolea macho ya mshangao, pale kwenye kundi la watu walioketi nao wakisikiliza simulizi ambazo sina shaka zilisisimua sana, kwani kila mtu alikuwa akimsikiliza kwa makini huku baadhi wakicheka. Alikuwa akitoa kichekesho. “Baba akamwambia mwanaye, ‘Toto jinga sana wewe. Kwa umri wako huo Idd Amin alishakuwa mkuu wa majeshi ya Uganda.’
“Mtoto akamjibu, ‘Na kwa umri wako huo alishakuwa Rais wa Uganda. Wewe mbona bado tarishi?”
Mie pia niliangua kicheko. Mchekeshaji huyo akageuka kunitazama. Akanikazia macho. Mara nikamwona akiachia tabasamu pevu zaidi huku akiinuka kunifuata.
“Petro!”
Aliniita. Sikuelewa. Nikamtolea macho ya mshangao. “Petro, hunikumbuki?”.
Nilitikisa kichwa kukataa. “Humkumbuki Umsolopogaas?” “Umsolopogaas mwenyewe?”
“Naam, Mzulu halisi. Kiboko ya Wajivuni.” “Kwa jina halisi Matayo Butiku?”
“Naam. Mathew Butiku halisi.” “Mang’ana” nilimjibu.
“Mayia.” Alijibu akicheka.
Tukaletewa Safari ya Sindbad. Mara mathayo akawa ‘Baharia Sindbad.’ Muda si mrefu akasoma Alfu lela U lela, akawa ‘Mfalme Harun Radhid wa Baghdad.’ Aliposoma hadithi ya Allan Quatermain, akavutiwa na yule mzee wa Kizulu, akaachana na jina la umbopa alilolipata katika Mashimo ya Mfalme Suleiman na kuwa ‘Umsolopogaas,’ jina ambalo naona amedumu nalo hadi leo. Hata kabati lake la shule aliweka vitu ambavyo vilipigwa marufuku shuleni hapo; panga, kisu, rungu na shoka ambalo aliliita inkoskaaz.
Aliponifikia, Matayo alitaka kunikumbatia. Haikuwa rahisi. Mikono yake iliyokatika juu ya viwiko ilichoweza kufanya ni kunipapasa kidogo tu mgongoni. Ni mimi niliyeweza kumkumbatia kikamilifu.
Tukaachana na kutazamana kwa muda. “Nini kimetukia Matayo?”
Kwa mshangao wangu alicheka tena. “Ni hadithi ndefu,” alijibu na kuongeza. “Tutatafuta muda tukae mahala nikusimulie.” Akasita kumeza mate. “Na wewe kilikutokea nini?”
“Ni hadithi ndefu vilevile,” nilimjibu. “Au ndio ile hirizi?”
“Hirizi gani?”
“Yako. Ile iliyopotea. Unajua iliokotwa ikachomwa moto lakini ikakataa kuungua? Nasikia mapadre wameipeleka Ujerumani kuifanyia utafiti.”
Nikajisingizia kutabasamu. Kichwani niliwaza jambo moja tu: Babyabato hakusema uongo. Hirizi yangu iliokotwa tena!
Wafungwa waliotuzunguka walionyesha kuvutiwa na taarifa hizo. Wakaanza kusogea ili kutusikiliza vizuri zaidi.
mfungwa asiye na mikono gerezani humo na kuanza kutumikia kifungo chake cha miaka thelathini. Gereza lilikuwa kubwa, lenye wafungwa tele, hivyo ilinichukua siku tatu nikisikia tu habari za mfungwa huyo bila kumwona kwa macho. Anakulaje? Anaogaje? Anavaaje na kuvua nguo zake? Nilijiuliza. Lakini swali kubwa zaidi lililonisumbua akili yangu ni pale nilipotaka kujua ni kitu gani kilimsibu mpaka akaipoteza mikono yake yote miwili. Kitu gani hasa kilimtokea? Gereza lilijaa simulizi tele juu yake. Mara anakula kwa kutumia miguu yake, mara hapana, anatumia kinywa chake pekee na kadhalika. Mara aliiba, akakatwa mikono, mara hapana, alizaliwa kama alivyo. Nilipokutana naye kwa mara ya kwanza nilishituka sana. Maumbile ya binadamu yana utaratibu wake. Akiwa na viungo vyake vyote binadamu anavutia macho. Akipoteza baadhi ya viungo vyake anatisha. Ndivyo nilivyomwona bwana huyu. Alionekana mrefu kupita kiasi, mwembamba kupita kiasi. Kwa ujumla, alionekana kama mnazi mrefu mweusi, unaotembea na kuzungumza. Uhai mkubwa zaidi katika umbo hili la kutisha ulikuwa katika sauti yake nzito na meno
yake meupe ambayo yaling’ara sana kila alipozungumza.Alikuwa akicheka!
Nilimkodolea macho ya mshangao, pale kwenye kundi la watu walioketi nao wakisikiliza simulizi ambazo sina shaka zilisisimua sana, kwani kila mtu alikuwa akimsikiliza kwa makini huku baadhi wakicheka. Alikuwa akitoa kichekesho. “Baba akamwambia mwanaye, ‘Toto jinga sana wewe. Kwa umri wako huo Idd Amin alishakuwa mkuu wa majeshi ya Uganda.’
“Mtoto akamjibu, ‘Na kwa umri wako huo alishakuwa Rais wa Uganda. Wewe mbona bado tarishi?”
Mie pia niliangua kicheko. Mchekeshaji huyo akageuka kunitazama. Akanikazia macho. Mara nikamwona akiachia tabasamu pevu zaidi huku akiinuka kunifuata.
“Petro!”
Aliniita. Sikuelewa. Nikamtolea macho ya mshangao. “Petro, hunikumbuki?”.
Nilitikisa kichwa kukataa. “Humkumbuki Umsolopogaas?” “Umsolopogaas mwenyewe?”
“Naam, Mzulu halisi. Kiboko ya Wajivuni.” “Kwa jina halisi Matayo Butiku?”
“Naam. Mathew Butiku halisi.” “Mang’ana” nilimjibu.
“Mayia.” Alijibu akicheka.
Sijapata kupigwa na mshangao kama ule. Tuliishi na Matayo katika bweni moja tukiwa katika darasa moja kwa takribani miaka minne. Siwezi kusema kuwa alikuwa rafiki yangu, lakini hakupata kuwa adui yangu. Kwa kweli, alikuwa rafiki wa kila mtu. Utundu wake, ucheshi wake na vituko vyake ndani na nje ya darasa vilifanya awe rafiki wa kila mtu, walimu na wanafunzi, jambo ambalo nadhani lilimsaidia sana kushinda mitihani yake, kwani kidogo kichwa chake kilikuwa kizito kuelewa, lakini akawa mwepesi wa kuibia. Hata uifiche vipi kazi yako Matayo atapenyeza jicho lake na kuchopoa jibu. Kipi kilimtokea? Nilijiuliza. Alikuwa kijana aliyekamilika,
kwa miguu na mikono ambayo haikupata kutulia. Nakumbuka alipenda sana vitabu vya riwaya, hasa zile za mashujaa. Na alipenda kudandia majina ya wahusika wa riwaya hizo. Kuna wakati tulipewa vitabu vya someni bila shida, mara mwenzetu akaanza kujiita ‘Bulicheka, kiboko ya Wagagagigikoko.’Tukaletewa Safari ya Sindbad. Mara mathayo akawa ‘Baharia Sindbad.’ Muda si mrefu akasoma Alfu lela U lela, akawa ‘Mfalme Harun Radhid wa Baghdad.’ Aliposoma hadithi ya Allan Quatermain, akavutiwa na yule mzee wa Kizulu, akaachana na jina la umbopa alilolipata katika Mashimo ya Mfalme Suleiman na kuwa ‘Umsolopogaas,’ jina ambalo naona amedumu nalo hadi leo. Hata kabati lake la shule aliweka vitu ambavyo vilipigwa marufuku shuleni hapo; panga, kisu, rungu na shoka ambalo aliliita inkoskaaz.