SEHEMU YA 395.
Roma mara baada ya kumpiga teke Poseidon ni kama alikuwa ametumia nafasi yake ya mwisho ya kutakiwa kujiokoa katika hilo eneo na angalau kukimbia, hivyo alipoteza nguvu nyingi mno , kiasi cha kuruhusu ugonjwa wake kuuongoza mwili wake.
Moja ya athari kubwa ambayo Roma aliipata kutokana na mpango LADO ni kupatwa na ukichaa wa ajabu na kushindwa kuzitawala fikra zake , na hiko ndio ambacho alichokuwa akikipitia mara baada ya kufunikwa na wingu.
Yeye mwenyewe sababu ya kumfukuza Poseidon kutoka alipokuwa amesimama karibu yake ni kutokana na kuhisi msuguano usiokuwa wa kawaida wa kukosekana kwa uwiano kati ya mbingu na ardhi na yeye kwakua ndio aliesababisha , basi alijihisi kama mtu mwenye homa , yaani ni hisia ambazo mwenyewe hakuwahi kuzitambua hapo kabla na hio yote ni kutokana na kwamba alikuwa akijifunza mbinu za kijini lakini hakuwa na mkufunzi wa kumuelekeza , hivyo alitumia akili yake mwenyewe kuweza kupanda levo bila ya kuwa na tahadhari.
Hisia hizo ndio sasa zinamjulisha kwamba , wakati alipokuwa anasafiri kuja eneo hilo , alikuwa akikiuka kanuni za anga na hata alipokuwa akiendelea kupigana na Poseidon alikuwa akikiuka kanuni za anga vilevile hivyo kupelekea kukasirika kwa anga.
Alijihisi ni kama yupo Jehanam kwa namna alivyokuwa akipitia maumivu mara baada ya kupigwa na radi ya awamu ya kwanza, anakumbuka baadhi ya kumbukumbu wakati akifanyiwa majaribu alikuwa akihisi maumivu makali ,lakini maumivu hayo aliokuwa akiyasikia yalikuwa ya aina yake .
Moja ya athari kubwa kwa kiumbe chochote kinapokumbwa na radi za aina hio , mara nyingi huaathiri mpaka Nafsi ya mtu sio mwili tu , Roma aliweza kuhimili Roho yake isimtoke kutokana na kwamba mwili wake ulishamulikwa na ‘Divine Light’ , lakini wakati huo huo alikuwa akipata msaada mkubwa wa nguvu ya Kimaandiko ya Urejesho isiokuwa na kikomo.
Na hio ndio faida kubwa sana , na akiwa katikati ya mateso alikuja kugundua kwamba mbinu yake ya Kimaandiko ya urejesho ilikuwa ikifanya kazi kwa spidi sana kwa namna ambavyo hakuwahi mwenyewe kutarajia na hio ndio ilimfanya kuvumilia maumivu ya awamu nne za Radi.
Lakini kupona kwake hakukuwa na spidi kama uharibifu uliokuwa ukifanywa na Radi kwenye mwili wake , hivyo kila alipokuwa akipitia pigo alihisi maumivu ambayo ni kama yamedumu kwa Karne moja licha ya kwamba radi ilikuwa ikipiga kwa sekunde kadhaa na kuacha.
Baada ya kupitia mapigo mawili ya Radi alikuja kugundua kitu kimoja kule kuchanganyikiwa kulikokuwa kunasababishwa na ‘Divine Light’ kumepotea ghafla, alikuwa ni kama mtu alieweza kuukomboa mwili wake na kuwa kiumbe kipya na hata uwezo wake wa kifikra ulimrudia .
Dhiki ni hatua iliokuwa ikiashiria maumivu makali sana ambayo mtu anaweza kuvumilia au kushindwa kuvumilia katika mbinu za mafunzo ya kijini katika kufanya maajabu ya kimapigano hilo Roma alielewa sana , lakini yeye ambacho hakuwa akifahamu ni kwamba katika hatua ya Dhiki mtu au Jini litapitia mpangilio wa awamu tisa za Radi malipizi.
Roma akili yake ilikuwa ikimwambia mapigo ya Radi hayakuwa yameisha kutokana na kwamba ule msuguano wa hewa wa kukosekana kwa uwiano kati ya Mbingu na Ardhi ulikuwa ukiendelea , hivyo alijikuta akikata tamaa na kuona kwamba akipigwa upya anaweza asihimili kuizuia roho yake na kupoteza Maisha.
Aligopa kufa kwani kuna watu waliokuwa wakimpenda na kumtegemea na alitamani kutoka katika hio adha na kurudi nyumbani.
Wakati sasa akihisi kukata tamaa ndio muda ambao Poseidon Artemis na Apollo walijitokeza na kumsaidia kuweka kinga juu yake, ijapokuwa hakuwa ameweza kuwaona lakini alihisi uwepo wao na kile ambacho wanakifanya. , lakini baada ya radi iliokuwa kwenye rangi ya moto kushuka na kupita alijikuta akipoteza tumaini kabisa na hapo hapo alishindwa kuvumilia maumivu na kupoteza fahamu na kudondokea baharini .
Anga lenyewe ni kama tu limeona Roma hakuwa amekufa bado hivyo liliendelea kushuka mapigo kisawa sawa kutimiza hesabu ya awamu tisa , ijapokuwa alikuwa ndani ya maji , lakini Radi ilimfuata huko huko kumpatia mapigo yake ,ilikuwa ni kama kuna mtu ambaye anaiamrisha kufanya hivyo.
Pigo la nane lilibadili kabisa mwonekano wa Roma kumfanya kabisa kuwa kama kaa la moto na kilichoweza kuonekana ni mvuke tu ukitoka kwenye mwili wake huku Nguvu ya urejesho ikionekana kushindwa kuendelea kufanya kazi.
Aphrodite , Apollo , Poseidon na Artemis waliweza kushuhudia pigo la mwisho la Radi Nyekundu kama moto wa shetani, ambalo lilikuwa na nguvu kubwa kiasi kwamba waliamini hakuna namna ambavyo Roma anaweza kupona kwenye pigo hilo.
Unajua wenewe walikuwa na uelewa juu ya mbinu za kijini zinavyokuwa licha ya kwamba walikuwa wakizidharau , kuishi kwao miaka mingi kuliwafanya kujua mambo mengi yanayohusiana na ulimwengu , hivyo waliweza kujua kwamba mwendelezo wa Radi hizo za mipangilio tisa ni kutokana na kwamba Roma hakuwa amekufa bado.
Pigo la mwisho lilisababisha wimbi moja kubwa sana kiasi kwamba ni kama bahari ilikuwa imeinamishwa upande mmoja na baada ya radi ile ya awamu ya tisa kupita anga lilichanguka na kukatulia tuli.
“It has ended …”Poseidon dio aliekuwa wa kwanza kutoka kwenye mshituko, Christen alimwangalia Poseidon kwa hasira mno.
“Haya yote umeyasababisha wewe , kwanini ulishindwa kunisikiliza tokea mwanzo , hata kama haumtambui kama Hades inakufadisha nini kama akifa na kusubira kuzaliwa upya?”
“Aphrodite jichunge na maneno yako , nilichokifanya ni kumuonyesha Hades kwamba kanuni za anga haziwezi kushindwa kwa namna yoyote na nguvu zote za kijini za kuvuna nishati ya mbingu na ardhi , halafu nashangaa unanilaumu kwa Hades kupigwa na Radi , ilikuwa ni kwasababu yake sio mimi niliomsababishia”Aliongea kwa hasira huku akivua kijikofia chake cha upishi huku akikitupia kwenye bahari iliaoanza kutulia
“Wewe ndio umesababisha akapata malipizi kwasababu ulimshambulia”
“Unaongea ujinga , nilimpa nafasi ya kukubali kushindwa lakini alishupaza shingo , hata hivyo sikujua kama alifikia levo ya Nafsi”
“Jamani muache malumbano tumejuana kwa Zaidi ya miaka mingi sana , kwanini tugombane kwenye wakati kama huu , hebu tikaangalieni kama Roma bado yupo hai”Aliongea Alice.
“Wewe unafikiria nini kimetokea ,kapigwa na Radi ya rangi nyekundu ni ngumu binadamu yoyote kuweza kupona hata kama awe na ngao kama wale majini wa zamani tuliokutana nao”Aliongea Poseidon bila ya kuwa hata na huzuni, lakini wote walimdharau na kusogea katika eneo ambalo Roma alikuwa akishambuliwa.
Christen ndio aliekuwa wa kwanza kufika na aliweza kuona mwili usiokuwa na mavazi ya aina yoyote ukiwa unaelea juu kabisa ya maji huku ukipigwa pigwa na mawimbi kulia na kushoto
“His body… is still intact?” Alishangaa Poseidon sana baada ya kuona Roma bado mwili wake haujaharibika kabisa , mwanzoni wote waliamini hakuna uwezekano wa kuona hata mwili wa Roma , kwani waliamini huenda umeyeyuka vipande vipande .
Miaka elfu mbili iliopita walikuwepo kwenye uso wa dunia na waliweza kushudia baadhi ya mapambano yaliopigwa kati ya majini na Zeus hivyo hata baadhi ya majini yalivyopitia hatua ya Dhiki wengi wao miili yao pamoja na Roho viliharibiwa kabisa., lakini jambo hilo likawa tofauti kwa Roma , bado angalau hata maiti yake ilionekana.
“That is odd Why do I sense like there isn’t any form of energy in this body”
“Hii inashangaza , kwanini siwezi kuhisi aina yoyote ya nishati kwenye mwili wake?”Aliongea Alice mara baada ya kutumia uwezo wake wa kiiuungu kuchunguza mwili wa Roma.
“You’re right , There is still life in him , he is not dead but he seemed to have lost all his ability”
“Uko sahihi , uhai anao na haakufa lakini anaonekana kupoteza uwezo wake wote wa kijini”Aliongea Poseidon
“Hio sio sawa kama mwili wake umepoteza uwezo wote , si inamaanisha kwamba inabidi aishi kama binadamu wa kawaida . Lakini pia naona mwili wake unajiponyesha wenyewe kwa haraka”Aliongea Alice tena huku akishangaa na kuwafanya wote kushuka usawa wa Roma na kumwangalia kwa ukaribu
Na ni kweli mwili wake ulikuwa ukipona kwa spidi na hata yale magamba magamba ya kuungua yalikuwa yakipukutika kwa kasi mno , kwa maana kwamaba ngozi yake ilikuwa ikijiunda upya
“Ni kweli anapona , lakini kwanini mwili wake umekuwa wa kibinadamu kabisa , hata nguvu inayotokana na Divine light hakuna?”Aliongea Stern na yeye akiwa kwenye mshangao.
Christen aliwapush wote na kisha aliingia kwenye maji na kuinua mwili wa Roma na kuukumbatia kwa mahaba mazito huku akitabasamu, hakujali wenzake waliokuwa wakishangazwa na Roma kupoteza uwezo wake wa kiuungu na kuwa binadamu wa kawaida , ila alichojali ni kwamba mwanaume huyo bado yupo hai.
“I knew you were too stubborn to die , Yo’ ve suffered so much”
“Nilijua tu wewe ni mbishi hata kwenye kufa , umeteseka sana”Aliongea huku machozi yakianza kumtoka.
Roma alikuwa bado hajarejewa na fahamu zake , akiwa amebebwa na mwanamke mrembo Christen, huku hata uso wake ulianza kumalizikia kupona kabisa , akiwa kama mtu aliekuwa usingizini.
Christen alionekana kuwa na mahaba mazito sana kwa Roma na hata haikueleweka ni hisia tu za kimapenzi au kuna kingine cha ziada.
“Una bahati sana Roma wangu , unaonekana Handsome hata baada ya kupigwa na Radi na kuungua”Aliongea na kuwafanya Stern na Alice kusogea na kumwangalia vizuri na kujikuta wote wakipumua kwa ahueni mara baada ya kuona hajafa.
“Aphrodite unaonekana kuwa na mahaba mazito kwa Hades , sikujua kama unapenda binadamu wa kawaida?”Aliongea kiutani akimaanisha kwamba kwasababu Roma kashapoteza uwezo wake hakuamini kama angeendelea kumpenda.
“I am not like you Siter Artemis , Not me”
“Mimi sipo kama wewe dada yangu Artemis “Aliongea Christen na Artemis alimpotezea huku akijikumbatisha kwenye mwili wa mpenzi wake Apollo kama vile ndege kwenye kiota.
“Mpaka sasa tupo sisi tu hapa, ukiachana na Ares wenzetu bado hawajaamka? Au wamepotezea hili swala”Aliongea Stern.
“Unajuaje ? Hapa ni mbali na inawezekana wapo mahali wanakula bata kama kawaida yao , lakini pia tunae mtu mwenye Roho mbaya kati yetu huenda waliamini kila kitu kitaenda sawa”Aliongea Christen huku akimwangalia Poseidon kwa chuki.
Poseidon alikuwa muda wote akimwangalia Roma aliekuwa kwenye mikono ya Christen akiwa ni mwenye maswali mengi mno , hakuamini kama Roma alikuwa hai kabisa na mwili wake haujaharibika
“Aphrodite vipi unapanga kumrudisha Roma Tanzania ? nadhani sio vyema kumpeleka akiwa hivyo kwa familia yake”Alishauri Stern.
“Nitaondoka nae kwenda Marekani ninapoishi , tutaongea nae Zaidi akisharejewa na fahamu”Alijibu Christen
“Kwahio alieharibu meli ya kimarekani ni..?”
“Sio yeye”
“Namna mtu huyo alivyotumia kanuni za anga nikiri kwamba kuna vitu vingi ambavyo anatofautiana na Hades na kama angekuwa Hades mwenyewe asingepigana na mimi kufa kupona , ilihali anajua sipo levo sawa na yake”Aliongea Poseidon.
“Kama sio yeye , kwahio atakuwa nani kama sio Hades , nadhani wote mnaelewa watu wanaojua mbinu za anga ni sisi wote kumi na mbili”Aliuliza Stern.
“Mwenyewe sijui ni nani?”Alijibu Poseidon kivivu.
“Kwahio ulikuwa ukijua muda wote sio Roma , lakini ukaamua kupambana nae mpaka kumsababishia haya matatizo”Aliongea Christen huku akin’gata meno kwa hasira , alitamani kuwa na uwezo mkubwa ampe kipondo Poseidon lakini hakuwa na uwezo huo, lakini Poseidon wala alionekana kutokuwa na hatia yoyote ni kama aliona Roma alikuwa akistahili.
“Aphrodite huna haja ya kuwa na hasira juu yake , sisi wote tunamjua tokea nyumbani hakuna siku ashawahi kusikiliza mtu , hata likija swala la Athena na Zeus, unatakiwa kumpeleka Roma akampumzika ili apone kwa haraka”Aliongea na kumfanya Christen kumwangalia Roma aliekuwa kwenye mikono yake kama mtoto.
“Ijapokuwa nataka apone haraka , lakini kuishi kama binadamu wa kawaida ni kheri kufa”Aliongea kwa huzuni na kisha alipotea na Roma wake na kuwaacha .
“Poseidon ijapokuwa siku zote umekuwa mwenye kumkasirikia Roma kwa kujifunza mbinu za kijini , lakini nadhani uache Imani zako za kipumbavu na kuendelea kumfanya kama adui yako , Tuishi huku tukiendelea kuona binadamu wanavyozidi kuongezeka kila siku, tuliamua kufanya mahali hapa kama nyumbani mara baada ya kusaini the gods treaty haina haja ya kujali Roma anaishije Maisha yake hata kama unahisi anatukana urithi wetu”
“Apollo acha kuleta majingambo yako kama unafikiria labda nataka kufufua kile tulichokipoteza nisingefanya kazi za upishi , ninachokifanya ni kuulinda utu wetu uliobaki na kuhusu Hades haikuwa nia yangu kuharibu uwezo wake , kukiuka kanuni za anga halikuwa tatizo langu bali ni yeye mwenyewe aliejisababishia”Aliongea.
“Vyovyote unavyofikiria sisi tunaondoka”Aliongea Stern na akachukuana na mchumba wake na kisha wakapotea.
*******
Upande mwingine chini ya vyumba vya ardhi katika jengo la Bima ya Taifa ndani ya Tanzania , mwanga mweupe uliangaza eneo lote la maabara na kufanya kama vile ulikuwa ni wakati wa mchana.
Ukiachana na vyumba vya juu ambavyo vilitumika kama wodi za baadhi ya binadamu wanaofanyiwa utafiti na sayansi kwenye miili yao , lakini eneo hilo la chini kabisa lilikuwa tofauti , kwanza kabisa ni eneo pana sana ambalo limejazwa na vifaa vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu sana , kulia na kushoto , ni eneo ambalo kama utaambiwa lipo Tanzania basi ungekataa kabisa.
Naam hio ndio maabara ambayo siku zote ilikuwa chini ya Profesa Shelukindo , Maabara ambayo ilijengewa na Raisi wa Marekani na kufadiliwa na Tajiri mkubwa ambaye anapenda sana uwekezaji kwenye maswala ya sayansi na tiba, Tajiri Billie Tiege.
Yan Buwen aliekuwa amevalia mavazi ya kujikinga na maambukizi pamoja na mionzi , alionekana kusimama mbele ya Skrini kubwa ya nchi Zaidi ya 84 huku akiangalia data mbalimbali zilizokuwa zikionekana kupanda na kushuka ambazo yeye mwenyewe ndio alielewa zilikuwa zikimaanisha nini.
Wakati akiendelea kujiuliza maswali kadhaa kwenye kichwa chake , mara alihisi uwepo wa mtu ndani ya eneo hilo, alikuwa ni mwanamke mrembo ambaye haikueleweka ametokea kupitia mlango upi.
Yan Buwen alijikuta akihisi ubaridi usiokuwa na kifani , kwani mwanamke yule mrembo alionekana kuwa na hasira kiasi kwamba kusambaza mkandamizo wa hewa ambao ulifanya viungo vyake vya mwili kuwa kama vinapalalaizi.
Lakini hata hivyo Yan Buwen alikuwa akifikiria sana urembo wa mwanamke huyo , ijapokuwa kwamba alikuwa akionekana ni mwenye kukasirika , lakini kwake alionekana mrembo kupita maelezo , aliangalia nywele za mwanamke huyo zilizojiachia kwa nyuma , akaangalia gauni la rangi nyeusi alilovaa mwanamke huyo , gauni lililoweza kuacha miguu minono milani ya mwanamke huyo kuwa wazi.Akaangalia umbo lake , alijikuta akichanganyikiwa kabisa.
Baada ya kuona ile hali ya kukosa nguvu imemwishia alisimama wima huku akijiweka sawa.
“Unafanya nini hapa?” Aliuliza Yan Buwen , lakini mwanamke yule alitembea kimadaha kwa kujiamini huku akikagua eneo hilo akiangalia Skrini zilizokuwa zikionyesha upande wa pili.
Kile alichokuwa akikiona mwanamke huyo kama ni binadamu wa kawaida ambaye hujazoea, hakika ungepatwa na woga na kushangaa kwa wakati mmoja.
Kwenye skrini hio kulieonekana mfumo wa Tubes nyingi kubwa zilizozibwa pande zote zikiwa zimejazwa na maji mazito ambayo ndani yake kuna watu waliolala usingizi wakiwa uchi , jambo la kushangaza ni kwamba watu wote hao walionekana kufanana kabisa kimuonekano.
Zilikuwa ni Clones za binadamu mmoja , chini ya Skrini hizo kulionekana pia ishara za kidata ambazo zinaonyesha hali ya kiafya za watu hao kuwa nzuri sana.
“What do you think , I didn’t disappoint you? Did I”
“Unaonaje sijakuangusha , si ndio?”Aliongea Yan Biuwen mara baada ya kukusanya ujasili na kumfanya Yule mwanamke amgeukie na kumwangalia kwa sura yake ya kirembo isiokuwa na ukaribisho , hakika alikuwa mzuti kiasi kwamba kwa mwanaume yoyote ambaye angemuona angesema sio binadamu wa kawaida, lakini mawazo yake yakawa kwel.
“I told you not to touch Hades without my instructions , You Seem to be unable to follow the simplest of instructions”
“Nilikuambia haupaswi kumgusa Hades bila maagizo yangu , unaonekana kutoweza kufuata maagizo mepesi ninayokupatia”
“I am only trying to test some bodies , I ma trying to investigate the functions of space laws exhibit after the fusion…...”
“Nilikuwa najaribu tu baadhi ya miili , Najaribu kufanya uchunguzi wa kuona kazi za kanuni za anga nini kinatokea baada ya muunganisho wa…”
“Mh! Yan Buwen acha kujifanyisha kijogoo , unachokifanya sio kujaribisha kanuni za anga , una mipango yako mingine kichwani , kwanini ukaamua kuharibu meli ya Kimarekani ili kumtengenezea Hades lawama?”
“Nili..”
Kabla hajajibu alijikuta akitoa ukulele usiokuwa na kifani huku akidondoka chini kwa maumivu makali aliokuwa akipewa.
“Hii ni adhabu ndogo ana kwako , hata hivyo najua unao uwezo wa kujiponyesha, itakuwa kama kumbukumbu kwako ya onyo kutoka kwangu”
“Ndio naomba unisamehe , nimekosa”Aliongea huku akishindwa kuvumilia maumivu na mwanamke yule alimwachia.
“Yan Buwen unatakiwa kukumbuka kwamba mpaka sasa umetumia kiasi kikubwa cha nguvu kutoka kwa Jiwe la kimungu , sijakupatia ili utumie kwa matumizi yako binafsi , kama utaendelea na upuuzi wako hutoamini nitakacho kufanyia”Aliongea na kisha akageuka akiashria kwamba anataka kuondoka
“Let me tell you , this world is full of smart people , if you believe you are worth of my time it’s best you dispel those thought ! I can destroy you as easily as I breathed life into you , if you try to be sneaky again I will replace you as soon as I hear about it”
“Ngoja nikuambie , huu ulimwengu umejaa watu wengi wenye akili, kama unaamini una thamani ya muda wangu , ni vyema kama utaondoa hayo mawazo yako , ninaweza kukuharibu kama nilivyoweza kukupulizia pumzi ya uhai , Ukijifanyisha mjanja tena nitakuondoa haraka sana nitakapogundua”
Yan Buwen alijikuta akimwangukia yule mwanamke na kisha alianza kumsujudia kwenye miguu yake , huku akigonganisha kichwa chake kwenye sakafu kwa namna ya kujutia.
Naam mwanamke mwenyewe hakuwa mwingine bali ni Athena a,k, a The Doni