Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Naona anajipanga aangushe vitu singanojr tumpe muda naamini atatushushia mzigo wa kutosha.

Nina imani nae tumpe muda tu.
 
NILIMDHANIA KAHANA KUMBE BIKRA

MTUNZI:SINGANO JR

SEASON 14



SEHEMU YA 391.



Baada ya Jeremy kutoka Kizwe alijikuta akilia kilio kisichokuwa cha kawaida , alikuwa akijitahidi tu kuwa jasiri mbele ya Raisi Jeremy lakini ukweli alikuwa akiogopa sana , hakuamini ndio hivyo anakwenda kufa , tena mtu ambaye anakwenda kumuua ni mume wake ambaye ameoana nae kwa miaka mingi.

“Kumbe mwenzangu ulikuwa mke wa raisi , ukashindwa kunipasha habari?”Aliongea Lekcha bila wasiwasi.

“Haijalishi kuwa mke wa raisi kwasasa kwani haina maana , mimi ni mwanamke ambaye nina laana ndio maana mume wangu mwenyewe ananiua”Aliongea huku akiwa ni mwenye huzuni.

“Kuna kitu nimeona katika maongezi yako, kauli yako ya mwisho inaonyesha haikuwa na ukweli wowote , si kweli ?”

“Unamaanisha nini?”

“Namaanisha kauli yako ya kumuua sijui nani , haina ukweli wowote na umeongea ili kumpandisha jazba”

“Umejuaje?”

“Kwa muonekano wako , unaweza kuwa mkatili lakini naamini pia ulikuwa ukiheshimu cheo chako , siamini kama wewe mwenyewe ndio ulitekeleza kifo cha huyo mwanamke , kuna uwezekano aliefanya hivyo ni mtu mwingine”Aliongea Lekcha na kumfanya Kizwe kupata nuru kidogo ya furaha.

“Inakuwaje mtu kama wewe ukanielewa sana kuliko hata mume wangu , ni kweli sijamuua , ijapokuwa nilikuwa na chuki sana zidi yake , lakini kuna watu pia waliokuwa wakimchukia kuliko mimi, nilichokifanya nikuongezea kachumbari tu, mtu kama wewe unaeonekana kunijali na kunielewa tunakutana nikiwa kwenye hatua za mwisho za kifo changu”

“Hehe haina haja tena ya kulalamika na kutoa hayo machozi , wote tunakwenda kufa .. ila sio mbaya ni kheri nakufa sasa nikiwa na mke wa raisi kuliko ningefia kule majalalani”Aliongea huku akiwa haeleweki ni hisia gani alizokuwa nazo kwenye moyo wake.

“Kuna namna ya wewe kuishi , nishaifikiria tokea tunaletwa hapa..”Aliongea Kizwe na kumshangaza Lekcha.

“Unasemaje , usiniambie kama kuna namna ya kumfanya mheshimiwa kubadili mawazo na kutuacha hai wote”

“Simaanishi mimi, namaanisha kuna namna ya wewe kuishi hawezi kuniacha hai kwani ananiona kama adui kwenye uongozi wake , kwa upande wako wewe huna thamani kwake akuue au asikuue ila kama utakuwa na kitu cha kumbadili mawazo atakuacha hai”

“Kwahio ni kipi naweza kufanya ili kumpa sababu ya kuniacha hai?”Aliuliza na Kizwe alimpa ishara ya kumsogelea na kisha akamnong’oneza.

“Una uhakika na jambo hilo , hiki kitu ni hatari kama kitafahamika?”

“Ndio, unachotakiwa ni kuongea kama nilivyokueleza na atakuamini , kadri utakavyokuwa msiri atakuwa hana sababu ya kukuua na atakuacha hai na huenda akakupa ulinzi pia”

“Kwanini unaniambia haya mimi , ungemwambia wewe huenda angekuacha hai?”

“Hawezi kuniacha hai hata nikimuambia , nilijua muda mrefu tokea tunakamatwa kule Tanzania na kutuleta kwa ndege ya jeshi , siku zote alikuwa akitafuta namna ya kuachana na mimi na amepata nafasi hivyo haawezi kuipoteza”

“Lakini utakuwa na sababu ya kuniambia hivi pia ili kuniokoa na kifo?”Aliuliza Lekcha akiwa kwenye kuchanganyikiwa.

“Ndio sitaki kukulipa mabaya kwa yale ulionitendea , kwenye Maisha yangu niliishi Maisha ambayo sikuwahi kukosa pesa , lakini kitu kikubwa nilichokosa ni mapenzi ya dhati , siku mbili tulizokuwa pamoja nimeguswa sana na uwepo wako kwenye maisha yangu , Nakufa kabla ya kujua historia ya Maisha yako , lakini kama utaishi naomba uniahidi kitu kimoja”

“Nipo tayari kukuahidi chochote?”Aliongea na kumfanya Kizwe atoe tabasamu la uchungu.

“Hakikisha unaishi Maisha yenye sababu kubwa , naamini kwa umri wako bado una nafasi ya kufanya makubwa , lakini jambo lingine nataka kukuona ukitimiza kitu ambacho ulisema ni tofauti na pesa”Aliongea na Lekcha kwa huzuni sana alitingisha kichwa chake kukubaliana nae.

Muda huo huo mlango wa chumba chao ulifunguliwa na watu wawili waliovalia makoti ya kimaabara wakiwa na vijitray vilivyojaa mabomba yenye vimiminika ndani yake kwa ajili ya kufanya kazi yao.

“Mwambieni mheshimiwa , huyu bwana hapa anasiri anataka kumweleza, toeni msisitizo kwamba siri hio itamfanya kumuacha hai na mtu atakaekufa siku ya leo atakuwa ni mimi pekee”Aliongea Kizwe na kisha alisimama haraka na kuchukua bomba lenye kimiminika na kisha akajichoma mwenyewe kwenye shingo akilenga mshipa mkubwa wa damu ,hata wale wataalamu wa maabara walishangazwa na kitendo chake , lakini walijikuta wakisimama wakimwangalia Kizwe akitapatapa na ndani ya dakika tano tu alikata moto na kunyoosha miguu huku macho akimkodolea Lekcha,

Lekcha alitolewa kwenye chumba mara baada ya taarifa kutolewa kwamba alikuwa na siri ya kumuelezea raisi Jeremy, baada ya kuburuzwa na mabodigadi alijikuta akigeuka nyuma na kumwangalia Kizwe aliekuwa chini hana uhai alijikuta moyo ukimuuma sana kwa mara ya kwanza kwenye Maisha yake , hakuamini kama kweli mwanamke huyo aliemuokoa kule jijini Dar Es salaam ndio huyo amekufa kifo cha aina hio , alijihisi mkosaji na kujiambia huenda angemuacha tu ajiue kule kule kuliko kuuliwa na mume wake.

Dakika chache mbele Lekcha alipelekwa mpaka ofisini kwa Raisi Jeremhy na kishwa kutupwa chini na mabodigadi.

*******

Taarrifa iliotolewa na Makedoni ilimchanganya sana Roma na kujiuliza ni mtu gani anajaribu kumchokoza.

“Mfalle Pluto huna haja ya kunificha , tumekuwa marafiki kwa muda mrefu, niambie kama kweli umehusika?”Aliongea Makedoni.

“Nieleze kwa kina nini kimetokea sijui chochote”

“Kwahio unasema sio wewe?”

“Sio mimi kwenye nini Makedoni hebu acha kuwa mwanasiasa”Aliongea Roma

“Mfalme hili swala mbona kama ni la ajabu, nusu saa iliopita meli ya Marekani iliokuwa ikirudi kutoka kusini mwa bahari ya China imeharibiwa , ni kati ya meli zilizokuwa na mzozo na taifa la uchina katika mgogoro unaoendelea na Taiwan , sasa kubwa yake yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita za Nimtz na wanajeshi elfu moja wanamaji ndio ilioharibiwa na mtu ambaye unafanana nae kwa asiliamia mia moja”Aliongea Makedoni.

“Mbaya Zaidi mfalme Pluto ni kwamba meli hio pamoja na wanajeshi na baadhi ya ndege zilizokuwemo vimeharibiwa ndani ya dakika moja tu na kuzama ndani ya bahari”Aliongea Makedoni..Roma alishanga

“Makedoni unamaanisha kwamba mtu aliehusika ana uwezo kama wangu ?”

“Ndio mfalme Pluto ,ijapokuwa ni mara chache sana nimeshuhuduia ukitumia uwezo wako wote , lakini mtu aliefanya hivyo naweza kusema kwamba anakukaribia na amefanya kama ilivyokuwa kawaida yako na tukikadiria , inaonekana ni kama unapofikia hatua ya macho yako kuwa mekundu”Aliongea Makedoni

“Hebu subiri , si umesema unayo Vidio?”

“Vidio tunayo , meli hio imerekodi tukio kwa dakika kadhaa na nimeweza kuiiba kutoka shirika la kijasusi la Marekani na kuangalia ndio maana nikakupigia”

“Nitumie hio video niangalie mwenyewe”Aliongea Roma na Mekedoni alikata simu na kisha akamtumia wakati huo huo video hio.

Roma aliweza kuangalia kila kitu kupitia tarakishi yake , ni kweli kabisa kilionekana kivuli ambacho kinafanana kabisa kama yeye , tena kikishuka kutoka angani na kilivyoshuka karibu na meli ile alifanya makusudi ya kuangalia Kamera na palepale ulitokea mlipuko mkubwa kama wa bomu ambao hata Kamera zilishindwa kuonyesha kilichoendelea, lakini kitu kikubwa ambacho Kamera hizo zilifanikuwa kurekodi sura yake halisi, kilichomtofautisha ni mavazi tu basi.

Baada ya kumaliza tu kuangalia palepale simu yake tena iliunganishwa na ya Makedoni.

“Your majest Pluto that wasn’t you?”

“Mfalme sio wewe si ndio?”

“No”

“Then”(Kwahio)

“That was spacetime manipulation but that man is definitely not me I can’t explain why he look like me though”Aliongea Roma

“Hio ni mbinu ya umanipulishaji wa muda wa Anga , lakini huyo mtu hakika sio mimi siwezi kuelezea kwanini anafanana na mimi lakini”Alijitetea Roma .

“Inaweza kuwa ‘Clone’ lakini hilo haliwezekani, kama kweli ni Clone inawezekana vipi mtu kuiba DNA zako bila ya wewe mwenyewe kufahamu? Lakini hata kama iwe ni Clone haileti maana kuweza kuwa na uwezo wa kucheza na Muda wa anga”

“Hakuna mtu anaeweza kunifanyia Clone kwasababu mwili wangu tayari ulishamulikwa na Devine light, hata mimi mwenyewe nishawahi kujiuliza kama mtu anaweza kuiba damu yangu na kutengeneza siraha ya kibailoia , lakini tafiti zilizofanywa zilibainisha hilo haliwezi kufanikiwa, kwasababu lazima waweze kupata damu yangu ikiwa ya moto kabisa na isigusane na hewa, lakini pia inawezekanaje mtu kuiba damu yangu nisijue?”

“Kweli kabisa mtu kuiba damu yako na wewe mwenyewe usifahamu , nadhani ni jambo ambalo haliwezekani kabisa”Alijibu Makedoni upande wa pili.

“Hilo sio muhimu kwa sasa kama wataweza kutengeneza kopi ya mwili wangu haitakuwa na uwezo wa kuwa na nguvu za kuchezea kanuni za anga na kuwa tishio , kwa jinsi ninavyomuona kwenye hii Video anaonekana kuwa na uwezo wake binafsi”Aliongea Roma

“Mfalme Pluto lazima tufanye jambo , ni kweli kabisa mtu hiyo ana nguvu kama za kwako lakini jambo kubwa ni kwamba haheshimu kabisa The Gods Treaty , ameharibu meli yote ya kivita lakini pia anafanana na wewe , kama serikali ya kimarekani hawataweza kumtambua inamaanisha kwamba…”

“Makosa yake yote yatasukumiwa kwangu, kwasababu sitakuwa na ushahidi wa kutosha wa kujitetea , lakini pia huyu mtu sijui ni nani na kwanini kafanya hivyo”

“Ni kweli mfalme Pluto , serikali ya Marekani imeomba pia idara yetu kufanya uchunguzi , ni wenye hasira kwasasa kwani wanaamini umeanza kuvunja sheri za kimkataba ndani ya The Gods Treaty na kuegamia upande wa China, siku mbili zilizopita serikali ya Marekani na serikali ya kichina iliingia kwenye makubaliano ambayo Marekani ilibidi kuondoa meli na wanajeshi wake wote waliokaribu na mipaka ya China kutokana na mzozo unaondelea kati ya Taiwani na China , jambo ambalo Marekani ilitekeleza mara moja na meli ilioharibika ilikuwa kwenye safari ya kurudi Marekani na Zaidi ya wanajeshi wao elfu moja makomandoo wamekufa, Mpaka sasa wanaamini moja kwa mja unatumia uwezo wako kuiinua China kijeshi”

“Achana na maswala ya siasa Makedoni , kwasasa mtu huyu kavunja sheria za Gods Treaty mchana kweupe , ni lazima miungu mingine itachukua hatua zidi yangu , Makedoni nadhani mlifanye swala hili siri kwanza maana ninaweza kushambuliwa muda wowote , mbaya Zaidi ametumia mbunu zangu zote zilizo zoeleka hivyo hakuna namna ya kujitetea”

“Mfalme Pluto unamaanisha serikali ya kimarekani inao uwezo wa kuamrisha miungu mingine kukushambulia , je wanaifahamu?”

“Haina haja ya kuwaomba , unajua Christen yupo Marekani na wote wanazo koneksheni za kujua ni nini kinaendelea kwenye dunia , ni Dhahiri mpaka sasa watakuwa na taarifa”

“Sawa nitajaribu kuangalia namna ya kuituliza hali”

“Utakuwa umenisaidia , hili ni swala kubwa mno na mimi mwenyewe nitalifanyia kazi , nitaondoka Tanzania kuelekea bahari ya kusini sasa hivi” Aliongea Roma na palepale simu yake ilikatika ,hakuwa hat ana haja ya kuaga kwani alipotea mara moja.

Unachotakiwa kutambua likija swala la ‘Space Time Manipulation’ kuharibu kitu cha Zaidi ya tani elfu moja ni kama kukata kijiti tu na hicho ndio kilichofanyika kwa Meli ya kivita ya Kimarekani , mtu alieonekana akifanana na Hades alikuwa na ‘Spatial Powers’ ambazo anaweza kuchezea kanuni za anga kwa kutumia ‘Gravity’na kufanya anachotaka.

‘Quantam Mechanic’ na ‘General relativity’ inaelezea kwamba anga na muda ni vitu ambavyo havitofautiani katika utendaji wao na kama vitakusanywa pamoja ndio hutengeneza Muda wa anga, kwahio Eistein mwenyewe anahusisha maswala yote ya kani mvutano na mengineyo ya kifizikia yanabebwa ndani ya Space na muda, Taasisi ya utafiti wa mambo ya anga ya Kimarekani ya NASA kwa kutumia kifaa chao cha NASAs Gravity Probe B waliweza kuthibitisha nadharia ya Eistein kwamba ni kweli anga na muda ni vitu vilivyoungana na vipo vinafanya kazi.
 
SEHEMU YA 392.

SOUTH SEA -CHINA

Ni katikati ya bahari ya kusini ya China, upepo wa mchana ulionekana kuwa mwingi kwa siku hio tofauti kidogo na siku nyingine huku eneo lote likitawaliwa na makelele ya mawimbi ya maji ya wastani , kwa jinsi eneo lote lilivyoweza kuonekana ni kama hakuna ambacho kimetokea dakika kadhaa zilizopita.

Roma alievalia shati la mikono mirefu rangi nyeusi aliweza kutokezea katika eneo hilo , na aliweza kutokea pasipo kujulikana ni upande upi ametokea na kama kuna meli yoyote yenye watu kuona kwa namna alivyojitokeza hakika wangepatwa na kiwewe na kumuona kama kiumbe cha ajabu.

Kwa jinsi alivyosimama hewani ungedhania ni Malaika au kuna kifaa ambacho kimefungwa kwenye mwili wake ambao kinamsaidia kusimama hewani .

Licha kwamba ilikuwa ni mchana , lakini baridi ilikuwa ni kali vile vile kutokana na eneo hilo , Roma aliweza kufika eneo husika mara baada ya kupewa ‘Coordinates’ na Makedoni.

Roma hakuwa na haraka kwanza ya kushuka chini kwenye maji kwa ajili ya kukagua eneo hilo , bali alichokifanya ni kuangalia anga kuzunguka eneo hilo , huku akiwa na uhakika sehemu hio ndio meli ya kivita ilipolipuliwa.

Ukweli katika Maisha yake yote ya kujifunza mbinu za kijini hakuwahi kusafiri umbali mrefu , alikuwa akihofia kukumbana na janga lolote njiani ,lakini mpaka anafika mpaka kwenye hio bahari hakuna kitu chochote ambacho kilikuwa kimempata.

Jambo ambalo lilikuwa likimtia wasiwasi ni kwamba licha ya kwamba mbinu za kijini zilikuwa nzuri lakini pia zina athari zake kwani hazikuwa zikizingatia sana kanuni za anga , hivyo kama utasafairi kwa umbali mrefu unakuwa una kiuka kanuni hizo na unaweza kupatwa na malipizi kutoka angani.

Aliendelea kukagua huku moyo wake ukikosa utulivu kabisa , alikuwa kama mtu ambaye anahisi kuna kitu kibaya kitamtokea katika hilo eneo.

“Kwanini moyo wangu unahisi kuwa mzito sana , nimekosea sana ningetakiwa kwenda kwa Zenzhei na kumuuliza kama nitatumia uwezo wa kijini kusafiri umbali mrefu ni athari zipi zinaweza kunikumba”Aliwaza Roma huku akiwa na wasiwasi , kwenye Maisha yake hakuwahi kuwa na wasiwasi kama hivyo na lakini hata hivyo ilikuwa na ubinadamu, kwani hakuwahi kusafiri umbali mrefu kwa kutumia uwezo wa kijini.

Alikuwa ashapanda levo kutoka ya nusu mzunguko Kwenda mzunguko kamili na usiku ule alipokesha kufikiria juu ya kufikia levo ya Nafsi alihisi kama mtu ambaye ameifikia ila hakuwa na uhakika , hayo yote ni kutokana na kwamba hakuwa na mwalimu wa kumfundisha juu ya mbinu hizo, Zaidi ya kutegemea uwezo wake wa akili na ndio maana kuna mambo mengi ambayo hakuwa akiyajua, sasa alikuwa akijilaumu huenda kama angeenda kuongea na Zenzhei labda angepata mwanga kuhusu levo aliofikia , lakini kwa muda huo alijiona hayupo kwenye nafasi ya kujilaumu, hata hivyo tukio la kulipuliwa kwa meli hio ni tukio la ghafla sana ambalo hakuwa amejiandaa nalo.

Roma aliamua kupotezea hisia zake mbaya ambazo zinamsumbua na kuanza kuangalia chini kwenye maji ya bahari kutafuta namna yoyote ambayo itamuwezesha kupata ushahidi kwamba mtu aliehusika sio yeye.

Roma baada ya kusimama kwa muda akichunguza eneo hilo alibadilisha macho yake na kuwa ya kijani na palepale kama mshale aliingia ndani ya maji huku nia yake ni kuangalia vitu ambavyo vimezama chini kabisa.

Na ni kweli kwa kutumia macho yake aliweza kuona mapande ya mabaki ya chuma chini kabisa ya maji na kwa kuchunguza tu aliona hakuna namna ya mwanajeshi yoyote angeweza kupona kwa jinsi meli hiyo inavyoonekana kwa chini , lakini jambo moja ambalo aligundua huenda ndani ya meli hio kulikuwa na bomu la nyuklia ndio maana mlipuko ukawa mkubwa sana , kwani mwili wake ulikuwa ukihisi baadhi ya mionzi mikali inayotoka chini ya eneo hilo.

Kutokana na mwili wake kumulikuwa na ‘Divine light’ hakuna mionzi ambayo ilikuwa na uwezo wa kumdhuru na hilo ndio ilikuwa afadhali kwake , lakini kama ingekuwa binadamu wa kawaida basi angeathirika mara moja , baada ya kuona hakuna kitu cha maana chini ya hayo maji aliibukia na Kwenda kusimama tena juu kabisa ya hewa.

“Au niende mpaka kambini kwao nikawaelezee nilikuwa nyumbani nikiwa nimetulia zangu na sio mimi , lakini nani anaweza kuamini maneno yangu?”Aliwaza Roma mwenyewe huku akiwa kwenye sintofahamu ni kitu kipi kingine anaweza kufanya kwa wakati huo.

Lakini akiwa kwenye dilemma mara alihisi nguvu isiokuwa ya kawaida ikimsogelea kwa kasi kutoka nyuma yake na kumfanya kugeuka na palepale alionekana mwanamke ambaye ana nywele nyeupe na gauni la rangi nyeupe akiwa hajavaa kitu chochote miguuni , huku macho yake yakiwa ya bluu iliokolea , kwa jinsi nywele zake zilivyokuwa zinapeperushwa na upepo mtu yoyote angesema mwanamke huyo ni malaika bila ubishi.

“It wasn’t you , was it?”Aliuliza yule mwanamke huku sauti yake ikisafiri maili nyingi na kufanya kusikika kwa mbali kwa mtu yoyote aliekaribu.

Roma alimwangalia huyu mwanamke ambaye alikuwa akipendeza sana kwa jinsi alivyoonekana akielea hewani , na kwa jinsi alivyo alijua huenda hakutokea nyumbani bali alikuwa kwenye aina flani ya sherehe.

Roma alijikuta akiguswa kwa neno lake alilosema ‘ Sio wewe?’ ni aina ya swali ambalo kwake alitafsiri mwanamke huyu alikuwa akimwamini kama hajahusika , lakini kitu kikubwa kilichomfurahisha amekuja mwenyewe mpaka eneo hilo kwa haraka ikionyesha alikuwa na wasiwasi juu yake

“Christen unafikiri nina muda wa kufanya mambo ya ajabu kama haya , nina matatizo mengi yanaendelea kwenye Maisha yangu , kwanini nijihusishe na wachina ambao wanaamini wanalindwa na Hongmeng , kama kuna taifa ambalo ningetaka kuwasaidia basi ni watanzania wenzangu”Aliongea Roma.

“Nakuamini Hades , kama kweli ingekuwa wewe mwenyewe usingeruhusu Kamera zikapata sura yako, ungekuwa ni ujinga mkubwa ambao unakufanya usiwe wewe, Lakini umetaja kuhusu Hongmeng unawafahamu?”Aliuliza Christen kwa mshangao kidogo na kumfanya Roma kushangazwa.

Unajua licha ya kwamba alikuwa akijifunza mbinu za kijini , lakini katika Maisha yake hakuwahi kuongea na Christen kuhusu habari za Hongmeng licha ya kwamba amezisikia kwa Masterr Chi , ambaye ndio alikuwa mkufunzi wake.

Lakini pia Roma licha ya kuelezewa stori iliotokea miaka mingi iliopita baada ya Zeus na Athena Kwenda miliki ya kijini inayofahamika kwa jina la Hongmeng kwa ajili ya kupigana, hata kushindwa kwa Zeusi na kuwawa huku Athana akikimbia , hio habari Roma hakuwahi kusikia miungu wenzake wakiiongelea.

“Ndio nishawahi kusikia stori zilizotokea kati yenu na viumbe hivyo vya ajabu vilivyojificha katika eneo la nchi ya China miaka iliopita , hata namna ambavyo Zeus na Athena walivyoweza kudhibitiwa, naamni wote mna hasira na jamii hio?”

“Hades unafahamu nini wewe? , ushakuwa mmoja wetu sasa hivi na siku ukikutana na hawa viumbe unatakiwa kupambana nao na huruhisiwi kuwaacha hai, hawana lolote kazi yao ni kujificha ndani ya mipaka ya China na hawana ujasiri wa kutokea hadharani na kupambana na sisi”

“Lakini unachosema hakipo sawa , stori niliosikia ni kwamba hawa majini hawawaogopi kabisa na miaka hio Zeus na Athena walipigika vibaya?”Aliongea Roma na kumfanya Christen kushangaa

“Umesikiwa wapi huo upuuzi?, nani kakuambia walikuwa wakipigika?”Aliongea Christen lakini Roma alijikuta akishangaa mno aijiuliza inamaana Master chi alimdanganya kwamba Zeusi na Athena walipigika.

“Sina uelewa sana lakini pia nashindwa kuamini kama stori nilioambiwa ni ya kweli , lakini kitu nilichosikia ni kwamba wanatumia nishati asili ya dunia inayoshikiliwa na mbingu na ardhi katika kufanya maajabu yao , na wengi wao levo yao ni ya Nafsi na ni wachache sana wanooweza kufanikiwa kuishinda Dhiki.”Aliongea Roma.

“Sio mbaya , ngoja nikuelezee baadhi ya vitu ambavyo huvijui , hizi Habari huwezi kuzipata kwani majini wengi yanakufa ndani ya miaka isiozidi mia tano ya uhai wao , hivyo kupelekea udhaifu na upendeleo kwenye utunzaji wa kumbukumbu zao”Aliongea Christen na akaaendelea,

“Ni kweli kabisa hawa viumbe wanaoishi katika milki inayoiitwa Hongmeng wapo na mimi mwenyewe nimewashuhudia , lakini haimaanishi kwamba viumbe hawa wapo ndani ya China tu , wapo sehemu nyingi ndani ya dunia na wana tabia zinazotofautiana, wengi wao wanaishi kama Roho kutokana na kwamba wanakosa miili , lakini wanapofikia levo ya Nafsi ndio huweza kupata miili kwa namna wanavyopenda kuwa , utofauti wa majini kutoka Hongmeng na wengine wanaoishi katika mazingira mengine ya dunia ni uwezo wao wa kuweza kuvuna nishati ya mbingu na ardhi na kuzibadilisha roho zao kuwa katika muundo wa kuonekana vyema”

“Nakumbuka wakati tunafika hapa duniani tuliweza kukuta hivi viumbe asilimia kubwa kati yao ni wachache sana ambao walikuwa wamefikia levo ya Kuipita Dhiki , walikuwa hawazidi hata kumi na hao ndio angalau waliweza kupambana na Zeus pamoja na Athena wengine wote walituchukulia kama tishio kwa Maisha yao hapa duniani”

“Unataka kumaanisha nini?”Aliongea Roma huku akionekana kama mtu aliechanganyikiwa , stori hii ilikuwa na utofauti kabisa na ile alioambiwa na Master Chi.

“Hades sikutaka kukuelezea sana kuhusu hivi viumbe , kwasababu sikutaka uchimbe sana mambo ya kikatili ambayo tulifanya wakati tulivyofika, lakini naona umedanganywa kwa kile kilichotokea”Aliongea Christen.

“Nadhani mtu alienielezea hii Habari alinidanganya kwa makusudi maalumu ya faida”

“Inawezekana kabisa na ninachokuambia ni ukweli , wakati tunafika kwenye huu uso wa dunia kulikuwa na nguvu ndogo sana za hawa viumbe wasioonekana tofauti na sasa , kilichowatofautisha wao na sisi ni namna tulivyokuwa na uwezo wa kutumia kanuni za anga na wao kukosa uelewa huo”

“Lakini mbona mara ya mwisho nilivyopambana na Ares niliweza kutumia aina flani ya mashambulizi nilioyatengeneza kwa mbinu za kijini na niliweza kumzuia kutumia kanuni za anga kwa kiasi kikubwa?, lakini pia kama ulivyooingea baadhi yao waliokuwa kwenye levo juu za kuipita Dhiki unataka kusema walikuwa na nguvu kidogo kuliko Zeus na Athena?”

“Hades unachoongea ni ujinga , tena ujinga mkubwa na sijui nani kakujaza , kama ulifanikiwa kumdhibiti Ares ulidhani ni kwasababu ya mbinu zako za kijini pekee , mbona unajidharau namna hio , labda nikuulize swali mbinu ya kijini ambayo ulijifunza, ni majini mangapi umesikia wameweza kuitumia”

“Kwa jinsi nilivyoambiwa mbinu hii ambayo niliipa jina la Maandiko ya urejesho yasio ya kikomo , nimeelezewa kwamba haikutokea katika miliki za kijini zilizopo China bali ni jamii nyingine kabisa inayofahamika kwa jina la PANASI na tokea kufahamika kwake ni watu wachache sana waliweza kufanikiwa kuitumia na sababu ya kushindwa ni kutokana na kukosa sifa zinazohitajika”Aliongea Roma.

“Upo sahihi kabisa , Hivi viumbe kutoka China vimekuwa na tabia ya majigambo lakini wanachoshindwa kuelewa wanakosa sifa kubwa ambayo upo nayo , umeweza kufanikiwa kujifunza hio mbinu kutokana na mwili wako ulivyo na naamini hata mtu aliekufundisha alijua ulikuwa na sifa za kujifunza hio mbinu , mbinu zao za kichawi kwanza kabisa zinatofautiana wao kwa wao , mnaweza wote kuwa katika levo ya Nafsi lakini mkawa na nguvu tofauti na hilo ndio linakutofautisha wewe na wao , wewe uwezo wako ni mkubwa Zaidi kuliko hata wa viumbe wote waliofikia levo ya Nafsi”Aliongea

Roma aliweza pia kukumbuka maneno ya Omari jicho moja , ni kweli unaweza kuwa katika levo sawa na mwingine lakini mkawa na nguvu zinazotofautiana , hivyo haijalishi mtu yupo kwenye levo ipi kikubwa ni namna ya uwezo wako ulivyo.

“Hades ngoja nikuambie kitu kimoja , majini wangekuwa na uwezo mkubwa sana kimbinu kama wangepata uwezo kama wetu wa kuweza kuzaliwa upya katika mwili wa mtu mwingine , lakini huo uwezo hawana na miili yao ikiezeeka basi hata uwezo wao pia huzeeka vilevile inawachukua miaka mingi sana kupanda levo moja Kwenda nyingine , hii ndio inasababisha wao kuwa dhaifu tofauti na sisi”

“Naomba nikuulize swali ni kwei nilipambana na Ares na nikafanikiwa kumzuia kutumia kanuni za anga kunishambulia mpaka nikamshinda je naweza pia kupambana na Athena na nikafanikiwa?”

“Kwasasa huna uwezo wa kumshinda Athena kwa uwezo wako ulio nao , ila kama utaweza kufikia levo ya juu ya Kuipita Dhiki huenda unaweza angalau kuleta ushindani , Hades kama ukifikia levo hio nakuomba usije ukatugeuka”Aliongea Christen.

“Mbona unanitisha , kwani huyu Athena na Zeus wana uwezo mkubwa sana?”

“Ndio labda nikuambie mpaka sasa Ares ndio dhaifu sana kuliko miungu yote na siku zote alikuwa ni mwenye tamaa ya kutafuta namna ya kuwa na nguvu kubwa lakini anashindwa kufanikiwa , kuhusu Athena sisi wote hapa hatuna uwezo wa kumshinda kwasababu ana viwango vya juu zaidi kwenye kuzielewa kanuni za Anga , sitaki kukuvunja moyo sana ila naamini hata Apollo na Artemis unaweza usiwafikie kwa uwezo wao mchache waliiobaki nao”

Roma alijikuta hata uso wake ukimshuka kabisa ,aliamua kuchagua mbinu za kijini kutokana na kwamba aliamini angeweza kuwa na nguvu kubwa Zaidi kuliko miungu mingine kutokana na stori alioambiwa na Master Chi kwamba majini yaliwapiga vibaya Zeus na Athena, lakini kitendo cha Christen kumwambia hata Apollo na Artemis anaweza asiwashinde katika mapambano ilizima kujiamini kwake..

“Siku zote niliamini mbinu za kijini zina nafasi yake kubwa kama ilivyo kwa mbinu za Anga na pia nilikuwa nikijua hakuna utofauti mkubwa uliopo , kwani zote zinategemea mbingu na ardhi , lakini je unafahamu ili kuweza kufikia levo ya Nafsi mtu anakuwa ameweza Kwenda mbali kimawazo mpaka kufikia mbingu ya tatu , lakini wakati huo huo kuwa na uwezo wa kukusanya anga na muda?”Aliuliza Roma lakini Christen alikodoa macho mara baada ya kuhisi kuongezeka kwa nguvu nyingine.

“Neptune!!!”Aliongea kwa sauti na kumchanganya na hapo hapo Roma alijua Christen alikuwa akimzungumzia Poseidon mungu wa bahari.

“Hades since you don’t seem to be fond of the laws of space , why don’t we have a duel , Let me show you what the laws of space truly are”

“Hades kwasababu hupendi mbinu za kikanuni za anga , kwanini tusipigane , nataka nikuonyeshe nini maana ya kanuni za anga”Ilisikika sauti tu pasipo Neptune kuonekana.
 
SEHEMU YA 393.

Muda huo huo Poseidon alionekana mbele yao , akiwa amevalia nguo za upishi na hata kile kikofia cha juu alikuwa nacho , ilionekana kabla ya kuanza safari alikuwa bize kukaangiza mahanjumati.

“Neptune there has been misunderstanding . Hades was not the one who broke the treat of gods”

“Neptune kuna makosa , Hades hajahusika na kuvunja mkataba wa kiuungu”Aliongea Christen lakini Poseidon aliyadharau maeneo yake na kisha kumwangalia Roma , lakini wakati huo huo Roma akimwangalia Poseidon au mfalme wa bahari.

Neptune ni jina sawa na Poseidon , wagiriki walikuw awakimtambua kama Poseidon ila Warumi walikuwa wakimtambua Poseidon kama Neptune.

Ukweli Roma licha ya kwamba wakati anamrithi Hades wa Zamani alipata baadhi ya nguvu zake, ukijumlisha na nguvu zinazotokana na mpango LADO , lakini pia nguvu za kijini ,hakuwahi kupigana na Poseidon , alikuwa akimfahamu tu kama moja ya miungu ambaye ana majigambo ya hali ya juu.

“Poseidon nishakuambia Hades hahusiki naomba unisikilize au huniamini”

“Aphrodite najua kile nilichoona kuhusu mambo ya ukweli nitayatafuta mimi mwenyewe na kuyathibitisha baada ya kumshikisha adabu huyu mpuuzi”Aliongea na ile Christen anataka kuongea tena palepale alijikuta akisukumwa mbali na upepo kama wa kimbunga

“Pumbavu kwanini unashindwa kusikiliza maneno yetu , Poseidon wewe ni mjeuri kama Ares tu”Aliongea Roma baada ya kusukumwa mbali .

Nguvu aliotumia Poseidon ilisababisha maji yote chini kuwa tafrani, ni hakika vyombo ambavyo vipo kilomita kadhaa kutoka walipo watakumbana na Dhoruba kubwa hata kusababisha kuzama.

Roma mwenyewe hakutegemea Poseidon kwa kuchezesha macho tu ameweza kuachia nguvu sio kuwa ya kawaida kama hio kwa kutumia kanuni za anga.

“Mhmh you are far weaker than the last the last one”

“Wewe ni dhaifu kuliko Hades aliepita”Aliongea Poseidon kwa dharau na palepale macho yake yalibadilika na kuwa kama nyota inayong’aa usiku , ni kama vile nafsi inaacha mwili wake.na chini yake kwenye bahari kulijitengeza kimbunga cha ajabu kikifanya maji kuzunguka kwa spidi sehemu moja huku mawimbi yale yakikusanya upepo wa juu na kusogelea aliposimama Roma.

Yaani kwa jinsi ilivyoonekana ni kama vile anga linacheza cheza kama vile linapeperushwa na upepo.

Roma alijua Poseidoni anatengeneza mtego wa kumkamata kwa mbinu za anga na jambo hilo hakuwa tayari kuruhusu litokee , alitumia uwezo wake wa kijini na kusukuma ukuta wa anga aliotengeneza Poseidon na aliweza kutengeneza ufa na ilionekana ni kama vile kitambaa kinavyochanwa katikati ndivyo ilivyoonekana , lakini jambo ambalo lilimshangaza Roma mara baada ya kuchana ukuta wa anga aliotengeneza Poseidon , ulitokea ukuta mwingine na hapo ndio akajua Poseiodon ametengeneza matabaka ya anga kwenye mtego wake , Roma baada ya kuangalia pande zote ,maji bahari yalikuwa yametengeneza mlima mkubwa kama vile Tsunami na kumfanya awe eneo la katikati.

Poseidon aliweza kuyafanya yote hayo kwa urahisi sana , yaani alikuwa akichezesha vidole tu huku akiwa ametulia na Roma ndio aliekuwa akipata shida , sasa kitu ambacho kilimpa ugumu Roma ni kwamba akitaka kurudi nyuma kuna tabaka la anga ambalo hawezi kupita na akitaka Kwenda mbele ivyo hivyo ametengenezewa tabaka ambalo hawezi kupita., aliishia kutumia uwezo wake kuchana matabaka lakini akichana hili linakuja lingine.

Ndani ya sekunde tu alikuwa amezingirwa katikati na alikuwa akizungushwa kama pia na kufanya damu zake kuchemka

“Hahahaha… Hades utanitambua leo , angalia hio”Aliongea Poseidon na palepale maji yaliokuwa chini yalipanda hewani , huku yakizunguka kwenye tabaka na kumfanya Roma kuwa katikati na kuonekana kwa mbaali.

Roma baada ya kuona anazidiwa , aliamini hawezi kuchomoka bila ya kutumia uwezo wake , alikuwa akijua kwa uchache sana kanuni za anga , hivyo aliamua kuanza kutumia hizo kwa kukusanya pamoja hewa

Christen alikuwa pembeni akiangalia kwa wasiwasi , aliona ni kama vile Dragoni limeamka kutoka chini ya kina cha majji kabisa na kupaa angani na kummeza Roma , kwani hakuwa akionekana kabisa na kumfanya kuwa na wasiwasi mno.

Unachotakiwa sasa kuelewa ni kwamba anga huundwa na matabaka, na uzio unaotenganisha matabaka ni mwembaba sana kama karatasi , lakini licha ya wembamba wake inahitajika nguvu kubwa sana kuchana tabaka moja Kwenda lingine na ndio maana unaona hata kama vitu vikitoka anga za mbali vikikaribia dunia vinaishia kwenye matabaka ya juu Zaidi , hio ni kutokana na kwmaba vinakosa nguvu ya kupita kwenye hizo kingo za anga.

Roma ambaye alizungukwa kati ya matabaka macho yake yalishabadilika muda tu na kuwa ya kijani tupu, ijapokuwa hakuwa na uelewa mkubwa sana wa kanuni za anga ila aliamini kutoka kwenye matabaka aliotengenezewa na Poseidoni lazima atumie kanuni za anga kwani mbinu zake zilikuwa zikimpa spidi ndogo ya kuchana hayo matabaka, alichokuwa akielewa ni kwamba kadri spidi yake inavyokuwa kubwa ndio nguvu yake inavyokuwa kubwa kuweza kuyachana hayo matabaka (f = Ma) , lakini kwasababu alikuwa kwenye levo za kawaida za kijini hivyo alikosa spidi ya juu sana kuweza kuchana matabaka na ndio maana alianza ku’ fold space’ ili kujitengenezea spidi.

Miungu ilikuwa na uwezo wa kusafiri kutoka sehemu moja Kwenda nyingine kwa kutumia kanuni moja inayofaamika kama ‘Space folding’ ilikuwa ni njia tofauti sana na ya Roma ku’telerport’ kutoka sehemu moja Kwenda nyingine , ijapokuwa miungu hii ilionekana kusafiri kama majini lakini ukweli ni kwamba ilikuwa ikitembea kwa spidi kubwa na ndio maana hata kuonekana kwenye macho ya kawaida inashindikana na wewe binadamu utaona mtu anapotea sehemu moja na kuibukia sehemu nyingine.

Roma alitengeneza nguvu kama wingu kwenye mkono wake na palepale alibadilisha wingu lile kuwa kama jiwe na kwa kutumia nguvu zake zote alirusha kuelekea kwenye tabaka alilotengenezewa na palepale likachanika, alijikuta akitabasamu.

“Hii mbinu inafanya kazi”Aliongea kwa kufurahi baada ya kuona ameweza kuchana tabaka la anga.

“Hades wewe ni mjinga sana .. ngoja nikufundishe Adabu mpumbavu wewe , nilikuwa nikiitafuta hii nafasi”Aliongea Poseidon mara baada ya kuona Roma kaweza kuchana tabaka moja alilolitengeneza kwa kukunja kunja anga.

Poseidon alitengeneza mkondo wa hewa palepale na kuubadilisha kuwa katika mfumo wa ‘mstari wa Ond’ na kuusukumizia ndani ya kimbunga cha hewa alichotengeneza kwa spidi kubwa na kitendo kile kilifanya dutu za hewa na za maji kusuguana kwa spiidi kubwa na kutengeneza umeme kama radi na kupita kwenye matabaka yale ya hewa kumsogelea Roma.

Roma baada ya kuona hivo alijitengenezea ngao ya kichawi ili kuzuia shoti zisimdhuru, alijikuta akikubali kuwa ni kweli kanuni za anga zilikuwa na athari kubwa mno na gepu lao sio dogo.

Roma aliona ilikuwa sahihi kwa Christen kumwambia kwamba alikuwa dhaifu hata kwa Apollo na Artemis maana kwa alivyokuwa akijua Artemis na Apollo hawakuwa wakimuweza Poseidon.

Roma alifikiria namna ya kujitoa kwenye gereza hilo la anga huku akijilinda kwa kutumia ngao ya kichawi alioitengeneza , hakuwa na mpango wa kujibadilisha kuwa mnyama , kwani siku zote kufanya hivyo ilikuwa ni kudhalilisha utu wake.

Kilichompa nafasi Poseidon kuweza kumdhibiti Roma kwenye mtego alioweka ni kutokana na kwamba alikuwa akitumia matabaka ya hewa mengi ambayo ameyaunganisha pamoja , hivyo Roma alishindwa kujinasua , kwani ilihitajika nguvu kubwa mno kujitoa.

Roma alijikuta akianza kufikiria maneno ya Master Chi, kuna hisia zilimwambia huenda Master Chi alikuwa akimdanganya , lakini wakati huo huo aliamini huenda kwenye ulimwengu wa kijini hali ya hewa ilikuwa tofauti na ulimwengu wa kawaida , ulimwengu wa kawaida umeundwa kwa Atomu mbalimbali na aliamini huenda huko kwenye ulimwengu wao hakuna atomu, na kama ni hivyo huenda ndio maana Zeus akashindwa kutumia kanuni za anga.

Roma alijikuta akikata tamaa , kwanza kabisa alianza kukosa pumzi , lakini pia nguvu zilimwishia , lakini pia hakutaka kujibadilisha mwili na kuwa mnyama , kwake jambo hilo lilimchukiza sana na alitafsiri kama vile ameshindwa na mara nyingi ataubadili mwili wake akiwa hana namna ya kuweza kupambana,

Christen aliekuwa mbali mwenyewe alishindwa kumsogelea Poseidoni kiutokana na nguvu ambayo ilikuwa ameitengeneza , huku akisababisha mvua ya Acid kunyesha katikati ya bahari na alijitahidi sana kujikinga asidhurike.

“Poseidon acha hasira zako , Roma hawezi kuwa kama hades wa zamani lakini hata hivyo ni mmoja wetu hatupaswi kumchukia na kupambana nae“

“Aphrodite wewe ni mpumbavu ,huyu ana nguvu chache sana za kiiungu ndani yake kuweza kuchukua nafasi ya Hades na nitamuonyesha leo”Aliongea Poseidon na kumfanya Christen kuzidi kuogopa.

“Hades nitaweza kukuachia kama utakubali nguvu zetu za kutumia kanuni za anga ni bora kuliko upumbavu wako wa kichawi unao Jifunza”Aliongea Poseidoni huku akimwangalia Roma ambaye ni kama alikuwa kwenye lijichupa kubwa la maji akiwa hana namna ya kujitoa.

Roma alishindwa kujibu, mvua na yenyewe ilikuwa kubwa mno ndani ya meneo hayo na bahari ilikuwa imechafuka kwa kiwango kikubwa mno na kwa spidi ya mawimbi ni Dhahiri nchi kavu wanatangaza Habari za dharula rais kujiondoka kwenye maeneo ya karibu kutoka na kimbuga kinachosogelea fukwe.

“Hades kama utafanikiwa kujitoa kwenye huo mtego leo hii nitatambua mbinu za kijini ni nzuri, usijifanyishe unao uwezo mkubwa kwasababu uliweza kumpiga Ares , kama utakubali kushindwa nitakuondolea maumivu , hata hivyo Hades wa zamani alikuchagua wewe lazima niheshimu maamuzi yake hata kama wewe ni dhaifu”Aliongea kwa kejeli.

Roma alikuwa akimsikia vyema Poseidon licha ya kuzungukwa na maji pande zoe pamoja na matabaka ya hewa na alikuwa akijikatia tamaa kabisa ya kuendeleza pambano , lakini baada ya kusikia maneno ya kejeli kutoka kwa Poseidon alijikuta akitoa tusi.

Pumbavu , sijawahi kuogopa kifo hata hivyo , nitapigana kufa kupona”Aliwaza Roma

Ukweli hakutaka kutumia uwezo wake wote kupambana kwani aliogopa jambo baya kumpata baada ya kufikiria nyumbani ameacha watu wanaomtegemea , alikuwa na mtoto na alikuwa pia na mke na wanawake wengine , ukijumlisha na mama yake na wengine.

“Naamini ninaweza kutumia uwezo wangu wote pasipo ya kubadilika mwili na kwa levo ya kijini niliofikia ninaweza kurudi kwenye hali yangu ya kawaida ndani ya dakika”Aliwaza Roma.

“Hahaha… Stupid Fake Hades , huna lolote, kubali kushindwa nikuachie , wewe kwangu ni kama yai kwenye kikaango muda huu”Aliongea kwa dharau Poseidon lakini kauli yake ilimfanya Roma kupandwa na jazba mno na palepale alikusanya nguvu zote za kichawi alizovuna kwa miaka , macho yake yalitoka kwenye ukijani na kuwa ya njano kwa dakika lakini palepale yalibadilika tena kuwa mekundu tii , huku mishipa ya damu ikibadilika rangi na kupanuka na kuwa kama mabomba la dripu ya maji huku ikitengeneza Weusi kwenye Ngozi wake, alijikuta akihisi maumivu yasiokuwa ya kawaida kuzuia mwili wake usipitie mabadiliko ila wakati huo huo aweze kutumia nguvu yake yote inayosababishwa na macho yake kuwa mekundu , alishindana kwa kutumia uwezo wake wote wa kijini na palepale macho yake yalibadilika kuwa mekudnu na kutoa mwanga kama wa dhahabu.

“Aaaaaargh…”Roma alijjikuta akitoa ukulele wa maumibu usiokuwa wa kawaida na kusikika pande zote kwa kurudia rudia na pale pale mishipa ya damu iliokuwa imevimba ilipasuka na kurusha damu nyeusi lakini kutokana na uwezo wake wa Kimaandiko wa kijini , mishipa ile ilifunga haraka sana.

“Poseidon aliekuwa amesimama hewani alijikuta nguvu isio kuwa ya kawaida ikimsukuma , ikitoka kwenye kimbunga cha hewa kilichomzunguka Roma na kuona hivyo alimuongeza matabaka ya anga ili asichoropoke

Lakini muda ule ule anga lilibadilika na kuwa kiza huku juu mawingu yakizunguka kwa spidi sana , jambo ambalo lilimfanya Poseidon kushangazwa na jambo hilo , mawingu yaliendelea kuzunguka kwa spidi huku ngutumo za radi zikisikika na baadhi ya cheche za radi zikionekana

Christen alijjikuta akisogea mbali Zaidi baada ya kuona tukio la namna hio na kujiuliza Roma anajaribu kufanya nini .

Ukumbuke Roma alikuwa ndani kwenye Kimbunga cha hewa kilichomzunguka na hakufanikiwa kuvunja matabaka aliotegenezewa na Poseidon.

“Hehe… nimefanikiwa” Roma alijikuta akipata tumaini mara baada ya kuweza kuziita nguvu zake zote bila mwili wake kugeuka wa mnyama .

“Boom .. Booom”

Mvua iliongezeka ilioambatana na radi , ilikuwa ni kama kitendo alichokifanya Roma wakati anapigana na Ares kwenye mlima wa oldonyo lengai

Poseidon alifanikuwa kukwepa radi ilioshuka kutoka juu na kujikuta akishangaa na aliweza kukumbuka miaka mingi iliopita wakati akipambana na majini ya Hongmeng , ilikutana na kitu kinachofanana kabisa.

Poseidon uwezo wake wa kuongezea matabaka kumzunguka Roma ulikuwa umefikia kikomo na Hades alikuwa akiyachana kwa spidi kubwa mno , baada ya kuona hana namna ya kumzuia kutoboa , aliamua kumuachia kabisa kwenye kimbunga chake cha hawa na pale Roma alijihisi ahueni na kuvuta hewa safi , lakini pia hakutaka kuzubaa aliita nguvu zake zote kwenye mkono na kufunika ngumi yake na kuirusha hawani kuelekea aliposimama Poseidon na nguvu aliotumia ilikusanya na wimbi kubwa la maji.

Poseidon na yeye hakuchelewa aliita vile vile nguvu na kujaa kwenye mikono yake na kurusha ngumi upande wa Roma na kutengeneza ‘Zero Gravity’ na palepale ni kama anga lilipinda na nguvu yake ni kama ilikumbatiwa na hewa.

Yaani ilikuwa ni kama vile mpira upige golini , sasa vile unavyozuiwa na wavu wa goli ndio kilichofanyika,.

Kuna kitu hakipo sawa , hapana nimerumia nguvu nyingi sana kwanini pigo langu halijapita”Aliwaza Roma ambaye macho yake yalikuwa yakibadilika badilika rangi mara kijani, mara njano mara nyekundu , mara kama mwanga wa dhahabu inapopigwa tochi yalikuwa kama vile taa za gari za polisi zinazofungwa juu.

Jambo moja la uhakika ni kwamba Roma aliweza kuzuia mwili wake kupitia mabadiliko na wakati huo huo akawa na uwezo wa kutumia uwezo wake wote unaotokana na macho yake kuwa ya rangi nyekundu , hakuonekana kama mnyama tena , ilikuwa ni mafanikio ambayo yalimfanya Christen aliekuwa pembeni kupagawa mno na kushangaa kwa wakati mmoja na kujiuliza Roma amwezaje.

“Let me present to you our differences … spatial explosion”Aliongea Poseidon na palepale alisugua viganya vyake vya mikono kama vile anavipasha joto na kilichotokea baada ya hapo ni mlipuko usiokuwa wa kawaida uliomrusha Roma nyuma ,ni mlipuko ambao ulitengeneza ombwe katikati ya maji huku yakiruka Zaidi ya mita mia tano Kwenda juu.

Roma ilimshangaza, lakini alielewa kwamba alichokifanya Poseido ni kusuguanisha matabaka ya anga kwa kutumia madini yenye chaji yaliopo kwenye hewa na kutengeneza mlipuko kama wa bomu , aliona zote hizo ni kanuni za kikemia za organic na inorganic ambazo zikichanganya na kanuni za anga hufahamika kwa jina la ‘Spatial Manipulation’.

Spatila manipulation ni ule uwezo wa mtu kuweza kudhibiti anga , kulichezesha , kulizungusha na kulibadili atakavyo kwa kutumia ‘three point of dimension’ , sasa mtu anapofanya hivyo anaharibu tu uwiano wa chaji uliopo kwenye anga na uwiano huo ukikosekana ndio huleta madhara kama ya milipuko , ni kama radi inavyotokea tu , lakini hio tofauti kidogo.

Pigo la mlupuko ambalo aliachia Poseidon lilimpata vyema Roma na kumuunguza kwenye mkono kiasi kwamba kumsababisha maumivu makali sana lakini yaliokuwa yakiisha pia kwa kasi kutokana na nguvu ya kimaandiko.

“Mh! nimetupia nguvu kubwa sana kukupiga , lakini naomba mkono wako haujaharibika , naamini sio nguvu tu zinazotokana na Divine light , inaonyesha mbinu ya kijini uliojifunza ina faida, nimevutiwa kidogo”Aliongea Poseidon

“Bullshit”Alitoa ukulele Roma huku macho yake yakianza kubadilika kama taa inayokaribia kulipuka , alianza kupata hisia mbaya za mwili wake kupitia mabadiliko, Roma alijihisi alikuwa amepona tatizo lake , lakini aligundua aliweza kuzuia mabadiliko ya mwili kutokana na nguvu nyingi alizokuwa nazo , lakini muda huo sasa alikuwa na nguvu kidogo ya kuushinda mwili wake , damu kwenye mwili wake zilikuwa zikitembea kama vile ni maporomoko ya maji ya mto.

Alianza kutengeneza ‘Aura’ nzito sana ambayo ilitengeneza presha kubwa ya hawa na kumfanya hata Posieon kuhisi nguvu hio kutokuwa ya kawaida.

“Naona unatoa nguvu isiokuwa ya kawaida ,ndio maana Hades ahakuchagua kuwa mrithi wake”Aliongea Poseidon kwa mshangao.

“Omdokaa..”Aliongea Roma kwa sauti ya kuamrisha huku mwili wake ukimtetema na damu kuanza kumtoka kama mgonjwa mwenye Ebola , alionekana likuwa akiumia mno kwa maumivu.,

“Siwezi kuondoka , unafikiri nakuogopa”Aliongea Poseidona kwa kiburi.

“Nakuambia ondoka , kuna hatari kubwa , utakufa”Aliongea Roma kwa sauti kwa mara nyingine , huku ngurumo za radi hazikukoma juu angani na wingu lilikuwa likizunguka mno , yaani ilikuwa ni kama mtu unavyojaribu kuzunguka halafu ukaangalia hewani ndio wingu lilivyokuwa.

“Poseison ondoka , hakuna muda wa kutosha”Aliongea Roma .

Christen aliekuwa mbali alijikuta akipatwa na wasiwasi kwa kile kinachoendela na kuwalaumu wote , alimlaumu Poseidon kwa kuwa na kichwa kigumu kuelewa , lakini pia alimlaumu Roma kwa kutokubali kushindwa na kila kitu kumalizika kwa amani.

Muda huo huo walitokea watu wengine wawili kutoka mashariki , na waliweza kuonekana kutokana na macho yao kuwa na mwanga , ukizingatia na wingu lililotanda eneo lote na kiza walionekana vyema ming’ao yao , mmoja alikuwa na macho yaliokuwa yakitoa mwanga wa bluu na mwingine alikuwa na macho yaliokuwa yakitoa mwanga kama wa jua.

Mpaka wanakaribia ndio waliweza kuonekana sura zao , ni Stern pamoja na Alice na ilionekana walikuja eneo hilo baada na wao kupata taarifa kwamba kuna mtu kavunja The gods treaty’.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

SEHEMU YA 394.

Alice na Stern walijikuta wakishangazwa na kile kilichokuwa kikiendelea ndani ya hilo eneo , walionekana kama watu ambao hawajategemea Roma na Poseidon kupigana.

“Aphrodite what is going on, why is Poseidon attacking him?”

“Aphrodite nini kinaendelea , kwanini Poseidon anamshambulia?”Aliuliza Alice na kumfanya Christen angalau kupata ahueni mara baada ya kuwaona Apollo na Artemis.

“Apollo imekuwa vyema mmefika , fanyeni haraka kumzuia Poseidon asiendelee kumshambulia Hades, Roma anajaribu kumzuia Poseidon asiendelee kuwa karibu yake lakini inaonekana anakataa”Aliongea Christen huku akiangalia upande wa maili kadhaa sehemu wanayopambana Hades na Poseidon

“Unasemaje?”Aliuliza kwa mshangao kidogo.

“Hades kakataa kushindwa, hali ikiendelea hivi anaweza kupoteza Maisha”Aliongea Christen , akionekana kama mtu ambaye anakubali kabisa kwamba Roma hana uwezo wa kumshinda Poseidon.

“Hades ni mjinga sana , kwanini anakua na kichwa kigumu anafikiri Poseidon ni kama Ares’Aliongea Alice na pale alisogea mbele na alionekana kama mtu anaekinga hewa kwa mikono yake yote miwili na kisha akatamka kwa sauti kubwa maneno:

“Helios!!”Aliongea na pale pale ulitokea upinde wa dhahabu kwenye mikono yake

“Nitaangalia namna ya kufanya , kwa mkandamizo wa hewa pale walipo ni ngumu kupita na Kwenda kuwazuia”Aliongea na pale aliinua mkono kama mtu anaepokea na ukaonekana mshale wa shaba kwenye mikono yake na kisha aliuweka kwenye ule upinde huku akilenga muelekeo wa sehemu wanayopigana Hades na Poseidon na pale pale baada ya kuvuta tu ule mshale ni kama moto ukijikusanya kwenye ule mshale.

Wakati huo Roma alikuwa akiendelea kupambana na mwili wake, kila ulivyokuwa ukitaka kubadilika na kuwa kama mnyama ulirudi katika hali yake ya kawaida , huku akionekana kupitia maumivu makali sana kiasi kwamba kwenye kingo za macho yake zilianza kuvuja damu na ni kama yalitaka kumtoka.

“Nimekuambia ondoka.. ondoka”Aliongea huku akizidi kuvumilia maumivu makali mno , ni kama viungo vyake vya mwili vikinyofolewa kimoja kimoja, huku akijihisi kama vile yupo kwenye tanulu la moto nyama ya mwili wake ikikaangwa.

Poseidon aliona mabadiliko flani ya Roma na kuona kuna kitu hakipo sawa kwake , mwanzoni aliona labda Hades anatishia tu , lakini aliona kuna jambo linataka kutokea lakini yeye mwenyewe hakuwa akijua ni jambo gani

“Boom’.

Ngurumo kubwa ya Radi iliendelea kupiga kwa kasi haikuwa ngurumo ya kawaida ni kama vile wingu lote linataka kudondoka chini.

Roma nguvu zake za kijini ziliongezeka maradufu mno na ndio zilizoweza kumzuia kutokubadilika , licha ya macho yake kupitia mabadiliko ya haraka sana ya Rangi.

“Boom!”

Ile kinga ya anga ambayo alitengeneza Poseidon kwa kujikinga na ngumi ya Roma yenye nguvu kubwa za kichawi ilipasuka pasuka kama vile kioo kikipigwa na nyundo.

Ploseidon alijikuta akitoa macho kwa kile anachokishuhuduia , kwani alimuona Hades hajafanya chochote lakini ile nguvu tu iliokuwa ikimzunguka kwa kutengeneza mzingo , ndio ilivunja ngao yake ya anga aliotengeneza.

Roma baada ya kuona bado Poseidon hataki kuondoka kwenye eneo ambalo amesimama, alikusanya nguvu baadhi na kuzielekeza kwenye mguu wake wa kulia na kuachia teke uelekeo wa Poseidon na palepale Poseidon alijikuta akirushwa mbali na alishindwa kabisa kuzuia nguvu ile.

Sasa teke lile lilimfanya kugundua kitu kimoja, ni kwamba Hades alitaka akae nae mbali , sasa alijiuliza ni nini kinaendelea , muda huo huo na Artemis alishaachia mshale wake wa kiuungu akidhamiria kuvunja nguvu iliokuwa ikimzunguka Roma na mshale ule uliambaa ambaa kwa namna ya kutoboa baadhi ya matabaka ya hewa ambayo Poseidon alitengeneza kama kinga , mshale wake hakua umedhamiria kumdhuru yoyote bali alitaka kuwatishia Roma na Poseidon.

Lakini sasa kabla ya mshale ule kufika katika usawa wa Roma ghafla tu wingu zito lilimfunika na kumfanya asionekane kabisa, na palepale ilitokea Dhoruba kali mno ambayo iliwafanya wao wenyewe kusukumwa mbali presha ya upepo.

“Boom!, Boom!”

Iligonga ngurumo isiokuwa ya kawaida na palepale umeme wa radi endelevu ulishuka katika eneo ambalo Roma alifunikwa na wingu.

“Romaa..!!!!” Christen alishindwa kuzuia hisia zake kabisa mara baada ya kushuhudia sehemu aliosimama Roma ikipigwa na radi mfululizo.

“Kaka Artemis unakumbuka ule mwaka tulipokutana na yale majini yaliokuwa yakizungumzia aina hii ya Radi”Aliongea Aliche huku akionekana kushangaa.

“Upo sahihi , alisema katika mbinu zao za kijini ili kufikia levo za juu lazima upitie mapigo ya AwamuTisa za Radi, Haya ni malipizi kwa kitendo cha kuvunja usawa wa nguvu za mbingu na Ardhi”Aliongea Apollo.

“Lakini kwanini anapata malipizi, ile siku tunakutana nae alionekana kutofikia hata levo ya mzunguko kamili? , ni wakati gani ameweza kuingia levo ya Nafsi na sasa kupitia hatua ya levo ya Dhiki?”Aliuliza Alice akiwa amechanganyikiwa.

Alichouliza ni sahihi kabisa kwa kanuni za namna majini wanavyo pata nguvu za ajabu , wakitoka levo ya Mzunguko kamili wanaingia levo ya Nafsi na hapo ndipo unaingia kwenye levo ya Dhiki,

Levo ya Dhiki mara nyingi haiwezi kudumu kwa muda mrefu sana , kwa mfano kama Jini litaingia levo ya Dhiki kuna majawabu matatu yanaweza kutokea , jawabu la kwanza linaweza kuwa kifo , Jawabu la pili ni kusalimika wakati huo huo jini likipoteza uwezo wake wote nguvu za kimaajabu jawabu la tatu ni kupona na wakati huo huo kupata uwezo wa viwango vya juu vya kufanya maajabu ya kimapigano , kwa lugha rahisi ni kwamba pale Jini linapokumbana na Radi awamu Tisa za Mbingu linaweza kupona au kutopona na kama litapona linaweza kuwa na nguvu Zaidi au lipoteze uwezo wake wote , kama litapona na kupata nguvu Zaidi ni kwamba limefanikiwa kuingia kwenye levo inayofahamika kwa jina la Kuipita Dhiki.

“Kwanini mnaongea bila wasiwasi , Roma hakuwa na mafunzo yoyote kuhusu hili na sasa anapitia hatua ya malipizi ya radi tisa , mnafikiri anaweza kupon?a , kwanini manashindwa kufikiria namna ya kumsaidia mnaanza kukumbushiana mambo yaliopita”Alionge aChristen huku akishindwa kuzia machozi.

“Hapana mimi naenda kumuokoa”Aliongea na palepale akaanza safari ya Kwenda upande ule wa wingu lakini Alice haraka haraka alimshika mkono.

“Aphrodite are you mad ? That is the most powerful punishment of the heavens , with your capability you would be seriously hurt , Evens Zeus and Athena wouldn’t try to defend against it , Rushing toward it would be suicide”

“Aphrodite una kichaa? , hio ndio adhabu kubwa ya mbingu na kwa uwezo wako utadhurika , hata Zeus na Athena hawawezi kupona kwenye radi ya namna hio , unachotaka kufanya ni kujiua”Aliongea Artemis.

‘Hapana siwezi kumuona Roma akifa”Aliongea huku machozi yakimtoka.

“Acha upuuzi Aphrodite hakuna uwezekano ukaweza hata kuokoa nafsi yako na kuingia kwenye mwili wa mtu mwingine”

“Lakini Diana wale majini ya karne iliopita walifikia levo ya kuipita Dhiki walikuwa na kinga ambazo ziliwawezesha kupona katika aina hii ya Dhiki , kwa Roma hana chochote cha kumkinga”Aliongea kwa wasiwasi mno huku machozi yakishindwa kujizuia kwenye mboni za macho yake , huku macho yake yakiangalia eneo ambalo limefunikwa na wingu zito , bila ya Roma kuonekana.

“Hades alikosea tokea mwanzo , kwanini asingejifunza tu mbinu za kanuni za anga , mbinu za kijini zinakiuka sheria za Anga , Kadri anaejifunza kuwa na nguvu kubwa ndio inavyokuwa rahisi kwa mbingu kumuadhibu , Sijui kama atakuwa hata na uwezo wa kuhamisha nafsi yake Kwenda kwenye mwili mwingine kama sisi”Aliongea Apollo huku akionyesha pia kuwa na wasiwasi.

Muda ule ule iligonga radi nyingine sehemu ile ile awamu hii ikiwa na rangi ya pink lakini muda huo huo kilionekana kivuli cha mtu juu ya wingu lile.

“Yule ni Poseidon , vipi anajaribu kumuokoa kwa kuzuia Radi?”

“Haiwezekani , Poseidon anaweza kuwa na uwezo mkuybwa kuliko sisi lakini hana uwezo wa kuzuia radi”

“Hapana huenda anao uwezo wa kuzuia hata awamu moja ya radi , lakini sidhani anaweza kuzuia awamu nyingine Zaidi”Aliongea Stern huku aking’ata meno yake kwa hasira mpaka macho yakawa mekundu na kisha akamgeukia dada yake.

“Alice unaonaje tukienda kuzunguka lile eneo na kuunganisha nguvu zetu na kuzuia hata awamu moja ya radi , Radi zinaendelea kushuka hivyo inamaanisha bado yupo hai na kama tutafanikiwa anaweza kupona”Aliongea na Alice alitingisha kichwa kukubaliana nae na wote kwa pamoja walikimbia kuelekea kwenye wingu ambao limemfunika Roma.

“Msiniongezee mzigo , kama mtapata matatizo sitowasaidia kuhamisha nafsi zenu”Aliongea Poseidon kwa kuwaamrisha.

“Hebu muone, sasa hivi ndio anajikuta kuwa na busara , nilifikiria ulitamani kweli kumuua Hades”Aliongea Stern

“Sijali hata akifa ila alinisukumia mbali kwa madhumuni ya kuniokoa nisipigwe na radi , sitaki kuwa na deni nae “Aliongea

“Nilijua tu unajifanyisha kuwa mgumu kwa nje , kumbe ndani umelegea , haya tuingieni wote kwa pamoja”Aliongea Stern huku akiwaamrisha wenzake kwamba waingie kwa pamoja kwenye maji ili wamuokoe kwa upande wa chini Kwenda juu ndio ingekuwa rahisi Zaidi bila wao kudhurika.

Hili lijinga ndio linatufanya kujiingiza matatizoni , kama angemsikiliza Christen angekufa , pumbavu zako Psoedion”Aliwaza Alice kwenye akili yake huku akimsuta.

Baada ya wote kwa pamoja kushuka chini usawa wa maji walianza kutengeneza matabaka ya hawa kwa kuchezea kanuni za anga na kwa kusimamisha juu ya kiwingu ili kumtengenezea Roma ngao.

Muda huo wingu bado lilikuwa vile vle huku ngurumo zikipiga makelele , ilikuwa ni kama linajiandaa kushusha pigo lingine ili kutimiza hesabu.

Artemis alikuwa akiweka tabaka kwa juu, Apollo na yeye alifanya umanipulishaji na kuweka anga lingine kwa juu , hivyo hivyo kwa Poseidon na walitumia nguvu zao zote kuyadhibiti ili kuzuia Radi inayotaka kushuka.

Muda ule ule Radi nyingine ilishuka , huku awamu hii ikiwa ni kama moto na kuwafanya wote kwa pamoja kufumba macho wakitegemea mbinu yao kufanya kazi.

“Vipi tumefanikiwa kuzuia?”

“Daah! , Hapana”

Aliongea Apollo na wote walijikuta wakitoa macho kwani Radi ilipita bila kipingamizi, walitumia nguvu zao nyingi kushikilia matabaka ya hewa kukinga radi hio lakini hakuna walichoambulia.

Radi za wamu tisa mara nyingi zinashuka kwa mpangilio wa sekunde kadhaa na hazipigi zote kwa pamoja na majini yenyewe yanazitofautisha ukali wake kupitia rangi , huwa mara nyingi zinapiga kwa mpangilio wa rangi zinazoonekana kwenye upinde wa mvua.

Hakuna namna yoyote ambayo majini yanakuwa na uwezo wa kuepuka hizi radi kama watavunja kanuni za anga ili kutaka kuingia levo ya Dhiki na hatimae kuipita Dhiki na ndio maana Majini mengi hayawezi hata kufikiria kuvuka levo ya Nafsi kwani walikuwa wakiogopa sana mateso hayo ya kifo na uhai.

Kwa mfano kama Jini litasafiri umbali mrefu kwa kuondoa uwiano ulipo kati ya nguvu ya ardhi na mbingu basi hupelekea hayo malipizi kwani ni kukiuka kanuni za ulimwengu , ni tofauti sana na mbinu za kanuni za anga kwani zinaenda kimahesabu hivyo kupunguza ile hatari ya kukumbana adhabu.

“Tuondokeni hapa , hakuna kingine tunachoweza kufanya”Aliongea Poseidon na kisha alitoweka eneo hilo na Apollo hivyo hivyo alimshika dada yake mkono na kumvuta.

Baada ya kufika umbali wa maili moja walisimama wote kwa pamoja , huku wakiwa si wenye kuamini kile walichokishuhudia.

“Inawezekanaje, nilisikia sana juu ya hizi radi lakini sikujua zina nguvu kiasi cha kuvunja matabaka tulioweka”

“Ndio, na nasikia hizi radi mara nyingi zinatofautiana makali yake mtu na mtu , kadri unavyovunja sheria za anga ndio inavyokupatia mapigo ya kina , Radi za mipangilio Tisa tuliweza kuzishuhudia miaka elfu moja iliopita, huenda tungeweza kufanikiwa kama Athena angekuwepo na kutumia ngao yake ya Aegis”Aliongea Poseidon na kumfanya Christen kuzidi kuwa na wasiwasi.

“Kwahio unamaanisha Roma..”Aliongea Alice kwa huzuni huku akimwegamia kaka yake.

“Hakuna namna , ngoja tusubirie awamu zote zipite tukaangalie kama atakuwa hai”Aliongea Apollo.

********

Upande mwingine ndani ya jiji la Dar ilikuwa ni usiku kama kawaida na wanafamilia ndani ya eneo la Osterbay walishangazwa na kutoweka kwa Roma kimazingara bila taarifa .

Wakati Roma anapandisha Kwenda juu kuongea na simu ilikuwa ni muda ambao chakula kinaandaliwa , hivyo hata baada ya matayarisho kukamilikaYezi ndio alieagizwa Kwenda kumuita Roma , lakini baada ya kurudisha majibu kwamba hayupo iliwashangaza kila mmoja.

Edna alijikuta akikunja sura mara baada ya kusikia jibu hilo na alitoka yeye mwenyewe kutoka sebuleni na Kwenda mpaka chumbani kwa Roma na kwake pia kumuangalia , lakini hakuweza kumuona na hapo hapo alikumbuka Sura ya Roma wakati anapigiwa simu.

Kapotea kichawi huyu, ila kaenda wapi?”Aliwaza Edna huku akifunga mlango wa chumba chake kivivu kushuka chini sebuleni.

“Edna hujamuona?”

“Mama itakuwa kuna sehemu kaenda , tuendeleeni kula”aliongea Edna na kumfanya Blandina aliekuwa na wasiwasi kuitikia kwa kutoridhika , alifanya hivyo kutokana na kwamba aliamini Edna alikuwa akimjua Zaidi Roma kuliko yeye.

Baada ya kula chakula cha usiku wote walikaa kwenye masofa kuangalia tamthilia za kikorea kwa kutumia chaneli moja ya TBS kutoka Korea kusini na ndani ya dakika arobaini na moja baadae chaneli ile ilizuia Tamthilia waliokuwa wakiangalia na ikatokea Habari kwa ufupi.

BREAKING NEWS -Severe Squali Hurricane warning for South China Sea Coastline and Nearby Islands:- A severe hurricane-storm is expected to hit the Souh Sea China Coastline and Nearby Islands , including Hainan , Taiwan , Phillipines , Malaysia .Indonesia and Brunei accompanied with Strong Winds ,Heavy Rain and Flooding , Residents are advised to take immediate precautions and follow the instruction’s of authorities

“TAARIFA KWA UFUPI: Tahadhari ya Kimbunga kikali kukumba ukanda wa pwani mwa Bahari kusini China na visiwa vya karibu:- Kimbunga Squali kinatarajiwa kukumba ukanda wote wa pwani mwa bahari ya Kusini ya China pamoja na visiwa vya karibu ikiwemo maeneo ya Hainan , Taiwan , Ufilipino , Malaysia , Indonesia na Brunei , ikiwa imeambatana na upepo mkali na mvua kubwa inayoweza kusababisha mafuriko , Wakazi wa maeneo hayo wote mnaaswa kuchukua hatua za haraka kutoka kwa maagizo ya mamlaka husika”

“Mh! jamani haya majanga ndio siku za mwisho hizi zilizotabiriwa , Mungu awasaidie waliopo katika hayo maeneo”Aliongea Blandina huku akijarubu kuvuta picha ya hofu watakazokuwa nazo watu waliopo kwenye hayo maeneo.

Edna alisindwa kuchangia chochote na wote walisikiliza taarifa hio huku tamthilia yao ikikatwa kabisa kutokana na dharula hio.

Wakati huo huo simu ya Mezani ya eneo la sebuleni ilitoa mlio na kumfanya Edna kusimama na Kwenda kuipokea kwani alifahamu itakuwa ni kutokea getini.

“Derick kuna nini?”

“Kuna mgeni Madam , amejitambulisha kwa jina la Omari Tozo”Ilisikika sauti na kumfanya Edna kufikiria kidogo maana hakumfahamu Omari Tozo ni nani.

“Amesema ana shida gani na anataka kuona na na nani?”

“Amesema yupo hapa kwa ajili ya kuonana na Mr Roma kwani kuna dharula ya kitaifa”Aliongea Derick na kumfanya Edna kuguna na kushangaa kwa wakati mmoja.

Unafikiri Roma tapona kwenye Radi Tisa? za malipizi ?”

Vipi huyu Omari nae na dharula za kitaifa?
 
SEHEMU YA 395.

Roma mara baada ya kumpiga teke Poseidon ni kama alikuwa ametumia nafasi yake ya mwisho ya kutakiwa kujiokoa katika hilo eneo na angalau kukimbia, hivyo alipoteza nguvu nyingi mno , kiasi cha kuruhusu ugonjwa wake kuuongoza mwili wake.

Moja ya athari kubwa ambayo Roma aliipata kutokana na mpango LADO ni kupatwa na ukichaa wa ajabu na kushindwa kuzitawala fikra zake , na hiko ndio ambacho alichokuwa akikipitia mara baada ya kufunikwa na wingu.

Yeye mwenyewe sababu ya kumfukuza Poseidon kutoka alipokuwa amesimama karibu yake ni kutokana na kuhisi msuguano usiokuwa wa kawaida wa kukosekana kwa uwiano kati ya mbingu na ardhi na yeye kwakua ndio aliesababisha , basi alijihisi kama mtu mwenye homa , yaani ni hisia ambazo mwenyewe hakuwahi kuzitambua hapo kabla na hio yote ni kutokana na kwamba alikuwa akijifunza mbinu za kijini lakini hakuwa na mkufunzi wa kumuelekeza , hivyo alitumia akili yake mwenyewe kuweza kupanda levo bila ya kuwa na tahadhari.

Hisia hizo ndio sasa zinamjulisha kwamba , wakati alipokuwa anasafiri kuja eneo hilo , alikuwa akikiuka kanuni za anga na hata alipokuwa akiendelea kupigana na Poseidon alikuwa akikiuka kanuni za anga vilevile hivyo kupelekea kukasirika kwa anga.

Alijihisi ni kama yupo Jehanam kwa namna alivyokuwa akipitia maumivu mara baada ya kupigwa na radi ya awamu ya kwanza, anakumbuka baadhi ya kumbukumbu wakati akifanyiwa majaribu alikuwa akihisi maumivu makali ,lakini maumivu hayo aliokuwa akiyasikia yalikuwa ya aina yake .

Moja ya athari kubwa kwa kiumbe chochote kinapokumbwa na radi za aina hio , mara nyingi huaathiri mpaka Nafsi ya mtu sio mwili tu , Roma aliweza kuhimili Roho yake isimtoke kutokana na kwamba mwili wake ulishamulikwa na ‘Divine Light’ , lakini wakati huo huo alikuwa akipata msaada mkubwa wa nguvu ya Kimaandiko ya Urejesho isiokuwa na kikomo.

Na hio ndio faida kubwa sana , na akiwa katikati ya mateso alikuja kugundua kwamba mbinu yake ya Kimaandiko ya urejesho ilikuwa ikifanya kazi kwa spidi sana kwa namna ambavyo hakuwahi mwenyewe kutarajia na hio ndio ilimfanya kuvumilia maumivu ya awamu nne za Radi.

Lakini kupona kwake hakukuwa na spidi kama uharibifu uliokuwa ukifanywa na Radi kwenye mwili wake , hivyo kila alipokuwa akipitia pigo alihisi maumivu ambayo ni kama yamedumu kwa Karne moja licha ya kwamba radi ilikuwa ikipiga kwa sekunde kadhaa na kuacha.

Baada ya kupitia mapigo mawili ya Radi alikuja kugundua kitu kimoja kule kuchanganyikiwa kulikokuwa kunasababishwa na ‘Divine Light’ kumepotea ghafla, alikuwa ni kama mtu alieweza kuukomboa mwili wake na kuwa kiumbe kipya na hata uwezo wake wa kifikra ulimrudia .

Dhiki ni hatua iliokuwa ikiashiria maumivu makali sana ambayo mtu anaweza kuvumilia au kushindwa kuvumilia katika mbinu za mafunzo ya kijini katika kufanya maajabu ya kimapigano hilo Roma alielewa sana , lakini yeye ambacho hakuwa akifahamu ni kwamba katika hatua ya Dhiki mtu au Jini litapitia mpangilio wa awamu tisa za Radi malipizi.

Roma akili yake ilikuwa ikimwambia mapigo ya Radi hayakuwa yameisha kutokana na kwamba ule msuguano wa hewa wa kukosekana kwa uwiano kati ya Mbingu na Ardhi ulikuwa ukiendelea , hivyo alijikuta akikata tamaa na kuona kwamba akipigwa upya anaweza asihimili kuizuia roho yake na kupoteza Maisha.

Aligopa kufa kwani kuna watu waliokuwa wakimpenda na kumtegemea na alitamani kutoka katika hio adha na kurudi nyumbani.

Wakati sasa akihisi kukata tamaa ndio muda ambao Poseidon Artemis na Apollo walijitokeza na kumsaidia kuweka kinga juu yake, ijapokuwa hakuwa ameweza kuwaona lakini alihisi uwepo wao na kile ambacho wanakifanya. , lakini baada ya radi iliokuwa kwenye rangi ya moto kushuka na kupita alijikuta akipoteza tumaini kabisa na hapo hapo alishindwa kuvumilia maumivu na kupoteza fahamu na kudondokea baharini .

Anga lenyewe ni kama tu limeona Roma hakuwa amekufa bado hivyo liliendelea kushuka mapigo kisawa sawa kutimiza hesabu ya awamu tisa , ijapokuwa alikuwa ndani ya maji , lakini Radi ilimfuata huko huko kumpatia mapigo yake ,ilikuwa ni kama kuna mtu ambaye anaiamrisha kufanya hivyo.

Pigo la nane lilibadili kabisa mwonekano wa Roma kumfanya kabisa kuwa kama kaa la moto na kilichoweza kuonekana ni mvuke tu ukitoka kwenye mwili wake huku Nguvu ya urejesho ikionekana kushindwa kuendelea kufanya kazi.

Aphrodite , Apollo , Poseidon na Artemis waliweza kushuhudia pigo la mwisho la Radi Nyekundu kama moto wa shetani, ambalo lilikuwa na nguvu kubwa kiasi kwamba waliamini hakuna namna ambavyo Roma anaweza kupona kwenye pigo hilo.

Unajua wenewe walikuwa na uelewa juu ya mbinu za kijini zinavyokuwa licha ya kwamba walikuwa wakizidharau , kuishi kwao miaka mingi kuliwafanya kujua mambo mengi yanayohusiana na ulimwengu , hivyo waliweza kujua kwamba mwendelezo wa Radi hizo za mipangilio tisa ni kutokana na kwamba Roma hakuwa amekufa bado.

Pigo la mwisho lilisababisha wimbi moja kubwa sana kiasi kwamba ni kama bahari ilikuwa imeinamishwa upande mmoja na baada ya radi ile ya awamu ya tisa kupita anga lilichanguka na kukatulia tuli.

“It has ended …”Poseidon dio aliekuwa wa kwanza kutoka kwenye mshituko, Christen alimwangalia Poseidon kwa hasira mno.

“Haya yote umeyasababisha wewe , kwanini ulishindwa kunisikiliza tokea mwanzo , hata kama haumtambui kama Hades inakufadisha nini kama akifa na kusubira kuzaliwa upya?”

“Aphrodite jichunge na maneno yako , nilichokifanya ni kumuonyesha Hades kwamba kanuni za anga haziwezi kushindwa kwa namna yoyote na nguvu zote za kijini za kuvuna nishati ya mbingu na ardhi , halafu nashangaa unanilaumu kwa Hades kupigwa na Radi , ilikuwa ni kwasababu yake sio mimi niliomsababishia”Aliongea kwa hasira huku akivua kijikofia chake cha upishi huku akikitupia kwenye bahari iliaoanza kutulia

“Wewe ndio umesababisha akapata malipizi kwasababu ulimshambulia”

“Unaongea ujinga , nilimpa nafasi ya kukubali kushindwa lakini alishupaza shingo , hata hivyo sikujua kama alifikia levo ya Nafsi”

“Jamani muache malumbano tumejuana kwa Zaidi ya miaka mingi sana , kwanini tugombane kwenye wakati kama huu , hebu tikaangalieni kama Roma bado yupo hai”Aliongea Alice.

“Wewe unafikiria nini kimetokea ,kapigwa na Radi ya rangi nyekundu ni ngumu binadamu yoyote kuweza kupona hata kama awe na ngao kama wale majini wa zamani tuliokutana nao”Aliongea Poseidon bila ya kuwa hata na huzuni, lakini wote walimdharau na kusogea katika eneo ambalo Roma alikuwa akishambuliwa.

Christen ndio aliekuwa wa kwanza kufika na aliweza kuona mwili usiokuwa na mavazi ya aina yoyote ukiwa unaelea juu kabisa ya maji huku ukipigwa pigwa na mawimbi kulia na kushoto

“His body… is still intact?” Alishangaa Poseidon sana baada ya kuona Roma bado mwili wake haujaharibika kabisa , mwanzoni wote waliamini hakuna uwezekano wa kuona hata mwili wa Roma , kwani waliamini huenda umeyeyuka vipande vipande .

Miaka elfu mbili iliopita walikuwepo kwenye uso wa dunia na waliweza kushudia baadhi ya mapambano yaliopigwa kati ya majini na Zeus hivyo hata baadhi ya majini yalivyopitia hatua ya Dhiki wengi wao miili yao pamoja na Roho viliharibiwa kabisa., lakini jambo hilo likawa tofauti kwa Roma , bado angalau hata maiti yake ilionekana.

“That is odd Why do I sense like there isn’t any form of energy in this body”

“Hii inashangaza , kwanini siwezi kuhisi aina yoyote ya nishati kwenye mwili wake?”Aliongea Alice mara baada ya kutumia uwezo wake wa kiiuungu kuchunguza mwili wa Roma.

“You’re right , There is still life in him , he is not dead but he seemed to have lost all his ability”

“Uko sahihi , uhai anao na haakufa lakini anaonekana kupoteza uwezo wake wote wa kijini”Aliongea Poseidon

“Hio sio sawa kama mwili wake umepoteza uwezo wote , si inamaanisha kwamba inabidi aishi kama binadamu wa kawaida . Lakini pia naona mwili wake unajiponyesha wenyewe kwa haraka”Aliongea Alice tena huku akishangaa na kuwafanya wote kushuka usawa wa Roma na kumwangalia kwa ukaribu

Na ni kweli mwili wake ulikuwa ukipona kwa spidi na hata yale magamba magamba ya kuungua yalikuwa yakipukutika kwa kasi mno , kwa maana kwamaba ngozi yake ilikuwa ikijiunda upya

“Ni kweli anapona , lakini kwanini mwili wake umekuwa wa kibinadamu kabisa , hata nguvu inayotokana na Divine light hakuna?”Aliongea Stern na yeye akiwa kwenye mshangao.

Christen aliwapush wote na kisha aliingia kwenye maji na kuinua mwili wa Roma na kuukumbatia kwa mahaba mazito huku akitabasamu, hakujali wenzake waliokuwa wakishangazwa na Roma kupoteza uwezo wake wa kiuungu na kuwa binadamu wa kawaida , ila alichojali ni kwamba mwanaume huyo bado yupo hai.

“I knew you were too stubborn to die , Yo’ ve suffered so much”

“Nilijua tu wewe ni mbishi hata kwenye kufa , umeteseka sana”Aliongea huku machozi yakianza kumtoka.

Roma alikuwa bado hajarejewa na fahamu zake , akiwa amebebwa na mwanamke mrembo Christen, huku hata uso wake ulianza kumalizikia kupona kabisa , akiwa kama mtu aliekuwa usingizini.

Christen alionekana kuwa na mahaba mazito sana kwa Roma na hata haikueleweka ni hisia tu za kimapenzi au kuna kingine cha ziada.

“Una bahati sana Roma wangu , unaonekana Handsome hata baada ya kupigwa na Radi na kuungua”Aliongea na kuwafanya Stern na Alice kusogea na kumwangalia vizuri na kujikuta wote wakipumua kwa ahueni mara baada ya kuona hajafa.

“Aphrodite unaonekana kuwa na mahaba mazito kwa Hades , sikujua kama unapenda binadamu wa kawaida?”Aliongea kiutani akimaanisha kwamba kwasababu Roma kashapoteza uwezo wake hakuamini kama angeendelea kumpenda.

“I am not like you Siter Artemis , Not me”

“Mimi sipo kama wewe dada yangu Artemis “Aliongea Christen na Artemis alimpotezea huku akijikumbatisha kwenye mwili wa mpenzi wake Apollo kama vile ndege kwenye kiota.

“Mpaka sasa tupo sisi tu hapa, ukiachana na Ares wenzetu bado hawajaamka? Au wamepotezea hili swala”Aliongea Stern.

“Unajuaje ? Hapa ni mbali na inawezekana wapo mahali wanakula bata kama kawaida yao , lakini pia tunae mtu mwenye Roho mbaya kati yetu huenda waliamini kila kitu kitaenda sawa”Aliongea Christen huku akimwangalia Poseidon kwa chuki.

Poseidon alikuwa muda wote akimwangalia Roma aliekuwa kwenye mikono ya Christen akiwa ni mwenye maswali mengi mno , hakuamini kama Roma alikuwa hai kabisa na mwili wake haujaharibika

“Aphrodite vipi unapanga kumrudisha Roma Tanzania ? nadhani sio vyema kumpeleka akiwa hivyo kwa familia yake”Alishauri Stern.

“Nitaondoka nae kwenda Marekani ninapoishi , tutaongea nae Zaidi akisharejewa na fahamu”Alijibu Christen

“Kwahio alieharibu meli ya kimarekani ni..?”

“Sio yeye”

“Namna mtu huyo alivyotumia kanuni za anga nikiri kwamba kuna vitu vingi ambavyo anatofautiana na Hades na kama angekuwa Hades mwenyewe asingepigana na mimi kufa kupona , ilihali anajua sipo levo sawa na yake”Aliongea Poseidon.

“Kama sio yeye , kwahio atakuwa nani kama sio Hades , nadhani wote mnaelewa watu wanaojua mbinu za anga ni sisi wote kumi na mbili”Aliuliza Stern.

“Mwenyewe sijui ni nani?”Alijibu Poseidon kivivu.

“Kwahio ulikuwa ukijua muda wote sio Roma , lakini ukaamua kupambana nae mpaka kumsababishia haya matatizo”Aliongea Christen huku akin’gata meno kwa hasira , alitamani kuwa na uwezo mkubwa ampe kipondo Poseidon lakini hakuwa na uwezo huo, lakini Poseidon wala alionekana kutokuwa na hatia yoyote ni kama aliona Roma alikuwa akistahili.

“Aphrodite huna haja ya kuwa na hasira juu yake , sisi wote tunamjua tokea nyumbani hakuna siku ashawahi kusikiliza mtu , hata likija swala la Athena na Zeus, unatakiwa kumpeleka Roma akampumzika ili apone kwa haraka”Aliongea na kumfanya Christen kumwangalia Roma aliekuwa kwenye mikono yake kama mtoto.

“Ijapokuwa nataka apone haraka , lakini kuishi kama binadamu wa kawaida ni kheri kufa”Aliongea kwa huzuni na kisha alipotea na Roma wake na kuwaacha .

“Poseidon ijapokuwa siku zote umekuwa mwenye kumkasirikia Roma kwa kujifunza mbinu za kijini , lakini nadhani uache Imani zako za kipumbavu na kuendelea kumfanya kama adui yako , Tuishi huku tukiendelea kuona binadamu wanavyozidi kuongezeka kila siku, tuliamua kufanya mahali hapa kama nyumbani mara baada ya kusaini the gods treaty haina haja ya kujali Roma anaishije Maisha yake hata kama unahisi anatukana urithi wetu”

“Apollo acha kuleta majingambo yako kama unafikiria labda nataka kufufua kile tulichokipoteza nisingefanya kazi za upishi , ninachokifanya ni kuulinda utu wetu uliobaki na kuhusu Hades haikuwa nia yangu kuharibu uwezo wake , kukiuka kanuni za anga halikuwa tatizo langu bali ni yeye mwenyewe aliejisababishia”Aliongea.

“Vyovyote unavyofikiria sisi tunaondoka”Aliongea Stern na akachukuana na mchumba wake na kisha wakapotea.

*******

Upande mwingine chini ya vyumba vya ardhi katika jengo la Bima ya Taifa ndani ya Tanzania , mwanga mweupe uliangaza eneo lote la maabara na kufanya kama vile ulikuwa ni wakati wa mchana.

Ukiachana na vyumba vya juu ambavyo vilitumika kama wodi za baadhi ya binadamu wanaofanyiwa utafiti na sayansi kwenye miili yao , lakini eneo hilo la chini kabisa lilikuwa tofauti , kwanza kabisa ni eneo pana sana ambalo limejazwa na vifaa vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu sana , kulia na kushoto , ni eneo ambalo kama utaambiwa lipo Tanzania basi ungekataa kabisa.

Naam hio ndio maabara ambayo siku zote ilikuwa chini ya Profesa Shelukindo , Maabara ambayo ilijengewa na Raisi wa Marekani na kufadiliwa na Tajiri mkubwa ambaye anapenda sana uwekezaji kwenye maswala ya sayansi na tiba, Tajiri Billie Tiege.

Yan Buwen aliekuwa amevalia mavazi ya kujikinga na maambukizi pamoja na mionzi , alionekana kusimama mbele ya Skrini kubwa ya nchi Zaidi ya 84 huku akiangalia data mbalimbali zilizokuwa zikionekana kupanda na kushuka ambazo yeye mwenyewe ndio alielewa zilikuwa zikimaanisha nini.

Wakati akiendelea kujiuliza maswali kadhaa kwenye kichwa chake , mara alihisi uwepo wa mtu ndani ya eneo hilo, alikuwa ni mwanamke mrembo ambaye haikueleweka ametokea kupitia mlango upi.

Yan Buwen alijikuta akihisi ubaridi usiokuwa na kifani , kwani mwanamke yule mrembo alionekana kuwa na hasira kiasi kwamba kusambaza mkandamizo wa hewa ambao ulifanya viungo vyake vya mwili kuwa kama vinapalalaizi.

Lakini hata hivyo Yan Buwen alikuwa akifikiria sana urembo wa mwanamke huyo , ijapokuwa kwamba alikuwa akionekana ni mwenye kukasirika , lakini kwake alionekana mrembo kupita maelezo , aliangalia nywele za mwanamke huyo zilizojiachia kwa nyuma , akaangalia gauni la rangi nyeusi alilovaa mwanamke huyo , gauni lililoweza kuacha miguu minono milani ya mwanamke huyo kuwa wazi.Akaangalia umbo lake , alijikuta akichanganyikiwa kabisa.

Baada ya kuona ile hali ya kukosa nguvu imemwishia alisimama wima huku akijiweka sawa.

“Unafanya nini hapa?” Aliuliza Yan Buwen , lakini mwanamke yule alitembea kimadaha kwa kujiamini huku akikagua eneo hilo akiangalia Skrini zilizokuwa zikionyesha upande wa pili.

Kile alichokuwa akikiona mwanamke huyo kama ni binadamu wa kawaida ambaye hujazoea, hakika ungepatwa na woga na kushangaa kwa wakati mmoja.

Kwenye skrini hio kulieonekana mfumo wa Tubes nyingi kubwa zilizozibwa pande zote zikiwa zimejazwa na maji mazito ambayo ndani yake kuna watu waliolala usingizi wakiwa uchi , jambo la kushangaza ni kwamba watu wote hao walionekana kufanana kabisa kimuonekano.

Zilikuwa ni Clones za binadamu mmoja , chini ya Skrini hizo kulionekana pia ishara za kidata ambazo zinaonyesha hali ya kiafya za watu hao kuwa nzuri sana.

“What do you think , I didn’t disappoint you? Did I”

“Unaonaje sijakuangusha , si ndio?”Aliongea Yan Biuwen mara baada ya kukusanya ujasili na kumfanya Yule mwanamke amgeukie na kumwangalia kwa sura yake ya kirembo isiokuwa na ukaribisho , hakika alikuwa mzuti kiasi kwamba kwa mwanaume yoyote ambaye angemuona angesema sio binadamu wa kawaida, lakini mawazo yake yakawa kwel.

“I told you not to touch Hades without my instructions , You Seem to be unable to follow the simplest of instructions”

“Nilikuambia haupaswi kumgusa Hades bila maagizo yangu , unaonekana kutoweza kufuata maagizo mepesi ninayokupatia”

“I am only trying to test some bodies , I ma trying to investigate the functions of space laws exhibit after the fusion…...”

“Nilikuwa najaribu tu baadhi ya miili , Najaribu kufanya uchunguzi wa kuona kazi za kanuni za anga nini kinatokea baada ya muunganisho wa…”

“Mh! Yan Buwen acha kujifanyisha kijogoo , unachokifanya sio kujaribisha kanuni za anga , una mipango yako mingine kichwani , kwanini ukaamua kuharibu meli ya Kimarekani ili kumtengenezea Hades lawama?”

“Nili..”

Kabla hajajibu alijikuta akitoa ukulele usiokuwa na kifani huku akidondoka chini kwa maumivu makali aliokuwa akipewa.

“Hii ni adhabu ndogo ana kwako , hata hivyo najua unao uwezo wa kujiponyesha, itakuwa kama kumbukumbu kwako ya onyo kutoka kwangu”

“Ndio naomba unisamehe , nimekosa”Aliongea huku akishindwa kuvumilia maumivu na mwanamke yule alimwachia.

“Yan Buwen unatakiwa kukumbuka kwamba mpaka sasa umetumia kiasi kikubwa cha nguvu kutoka kwa Jiwe la kimungu , sijakupatia ili utumie kwa matumizi yako binafsi , kama utaendelea na upuuzi wako hutoamini nitakacho kufanyia”Aliongea na kisha akageuka akiashria kwamba anataka kuondoka

“Let me tell you , this world is full of smart people , if you believe you are worth of my time it’s best you dispel those thought ! I can destroy you as easily as I breathed life into you , if you try to be sneaky again I will replace you as soon as I hear about it”

“Ngoja nikuambie , huu ulimwengu umejaa watu wengi wenye akili, kama unaamini una thamani ya muda wangu , ni vyema kama utaondoa hayo mawazo yako , ninaweza kukuharibu kama nilivyoweza kukupulizia pumzi ya uhai , Ukijifanyisha mjanja tena nitakuondoa haraka sana nitakapogundua”

Yan Buwen alijikuta akimwangukia yule mwanamke na kisha alianza kumsujudia kwenye miguu yake , huku akigonganisha kichwa chake kwenye sakafu kwa namna ya kujutia.

Naam mwanamke mwenyewe hakuwa mwingine bali ni Athena a,k, a The Doni
 
Back
Top Bottom