SEHEMU YA 402.,
Roma aliekuwa juu ya mwili wa mrembo Rufi alijikuta akitoa macho baada ya kugundua kuna kitu hakipo sawa , tofauti na wanawake wengine ambao amefanya nao mapenzi ni Rufi peke yake ambaye alikuwa ni wa tofauti , mwanamke huyo alikuwa na sehemu za baridi mno, ijapokuwa ashawahi kufanya mapenzi na Lilith Vampire kule Ufaransa lakini sehemu za Rufi zilikuwa za baridi mno kuliko isivyokuwa kawaida mara baada ya mrembo huyo kuanza kutoa majimaji.
Roma alijiuliza kwamba je huyo mwanamke ana damu ya baridi, lakini hakupata jibu moja kwa moja.
Kitu kingine licha ya kumtoa mrembo huyo bikra lakini hakukuwa kabisa na tone la damu.
“Naona sumu ambazo zipo kwenye mwili wako zunafanya mwili wako kuwa wa baridi kama barafu”
“Inakuhusu nini, huna muda wa kuanza kufikiria kimantiki ,wewe ni wa Kwenda”Aliongea.
“Siamini kama naweza kufa”Aliongea Roma na kufanya kwa spidi kubwa na kumfanya Rufi kuzidi kutoa malalamishi ya maumivu huku Ngozi yae ikianza kupauka kama mgonjwa asie na maji mwilini.
“Yaani hapa ndio naanza , mpaka nihakikishe kisasi changu kishalipwa ndio nitakuacha”.Aliongea na kuendelea kufanya.
Show ilianza mchana lakini ilikuja kumalizika saa moja za usiku na Roma alifanikiwa kushusha mzigo mara mbili .
Upande wa Rufi hakuweza kumtafsiri mwanaume aliekuwa mbele yake , kwani alitegemea afe lakini alionekana kuzidi kupata nguvu Zaidi na Zaidi na kuendeleza kazi yake,, Baada ya kupumzika kama nusu saa alijikuta akimwangalia Roma.
“Bado hujisikii tu vibaya?”
“Kwanini nijisikie vibaya wakati umenipatia burudani”Aliongea Roma na kisha alimpiga bonge la kibao kwenye paja lake la mguu na kumfanya Rufi kufumba macho kwa maumivu , lakini palepale ni kama shoti za umeme zilikuwa zikitembea kwenye mwili wake kwa namna ya maajabu.
“Unajisikia vizuri?”Aliuliza Roma na kumfanya Rufi kufumbua macho yake taratibu , haikuwa akijisikia vibaya bali alikuwa akijisikia tofauti sana , hisia ambazo hakuwahi kuzisikia katika Maisha yake yote.
“Umefanyaje , mwili wangu nahisi umekuwa mwepesi , nahisi pia sumu zimeisha?”Aliongea huku akianza kutoa machozi.
“Ijapokuwa haujajielezea vya kutosha , lakini nilijua ni nini tatizo kwenye mwili wako , Una mwili wa tofauti sana , huenda tofauti kabisa na binadamu wa kawaida , ijapokuwa mwili wako una sumu nyingi lakini bado zilikufanya uendelee kuishi wakati huo huo ukiwa unapitia maumivu makali ya mara kwa mara”
“Mpango wangu mwanzo nikuachana na wewe na kutafuta mwanamke mwingine bila ya kukufanya kitu , lakini mara baada ya kuniwekea sumu niliona sitakiwi kukuachia kizembe hasa baada ya kugundua wewe ni bikra bado , hivyo kwa kutoa usichana wako nimekusaidia kwa kuponyesha sumu yako yote mwilini”
“Wewe ni nani haswa? , hata wazee ambao walishapewa kazi ya kunisaidia kupona walishindwa , kwanini imekuwa rahisi kwako?”
“Nahisi kuhusu wazee unaowazungumzia ambao siwajui hawajajaribu kukuponyesha , Sumu iliokuwa kwenye mwili wako haikutoka nje bali ilikuwa kwenye veini zako za mwili , hivyo niliitoa kwa kuzuia damu ya veini za upande moja na kuruhusu za upande mwingine”
“Kama tungekutana siku chache zilizopita nisingefanikiwa kukutibu , lakini sasa hivi ninaweza kukutibu , ijapokuwa haujapona kabisa lakini ndani ya miaka hamsini ijayo ndio unaweza kujisikia maumivu tena”
“Mika hamsini?”Aliongea kwa wasiwasi na mshangao juu
“Vipi ni michache , ushukuru tu umeewza kukutana na mimi , naweza kusema ni bahati kwako , hivyo kama hakuna kitu chochote mabacho kitaufanya mwili wako kupata tatizo utaweza kuishi bila tatizo kwa muda mrefu”
“Umeweza kweli kuponyesha Meridiani zangu?” Aliuliza kwa mshangao na Roma hakumjibu Zaidi ya kuingia bafuni na kuoga na ndani ya dakika kama tano tu alitoka na kuvaa nguo zake.
“Rufi nitachukua hii pete kuondoka nayo , ninapanga kumpatia mke wangu kama Zawadi , unaweza kuchukua Wine”Aliongea Roma mara baada ya kumaliza.
“Ndio unaondoka hivyo?”
“Ndio mimi na wewe hatuna deni, no string attached”
“Sijamaanisha hivyo, nataka kujua umefahamu vipi mpango wangu tokea mwanzo?”
“Kwahio unajaribu kutafuta wapi pamevuja mpaka mpango wako kuharibika ili usifanye makosa tena?, labda nikuambie tatizo ulilokosea ni kwenye kuchagua shabaha yako , wakati nafika karibu na jengo la mnada nilishagundua uwepo wako ukiwa katika mgahawa na ulikuwa ukichunguza kila anaefika na gari kali , sasa uliopona nimefika na gari la bei ndio ukaona nafaaa kwa mpango wako, naweza kusema mpango wako ulikuwa ni wa akili sana, kitu cha kwanza ulichofnaya ni kuchagua kitu cha bei rahisi kwenye mnada ambacho ni kinywaji , lakini kitu cha pili ukachagua ambacho ni cha bei ghali sana, yote ilikuwa ni kunijaribu”
“Yaani uliweza kunitamba licha ya kuwa mbali! , kama nitakuwa sahihi wewe ni Master kutoka Hongmeng?”
“Wow! ,sikudhania una ufahamu kuhusu Hongmeng , hata hivyo unakosea sina ukaribu wowote na wao , kama unavyoniona mimi sio mchina”Aliongea Roma na kisha akaondoka na kuacha chumba kuwa kimya.
Rufi mara baada ya kupumzika kwa dakika kadhaa akiwa ni mwenye kuandamwa na mawazo ya kutumiwa na kuachwa , lakini wakati huo huo kuponyeshwa ugonjwa wake wa miaka mingi , alijikuta fuaha yake ikirudi mara baada ya kuona Kamera ya siri alioitega kwenye chumba , alionekana kama mtu ambaye ameokota dodo kwenye muembe.
Roma akiwa anatembea alijikuta akimuwazia mrembo Rufi ,ukweli alijua sio binadamu wa kawaida , ni hisia ambazo hakuweza kuzielezea lakini kila kitu kilimwambia Rufi hatokei katika mazingira ya kawaida ya dunia na kama anatokea duniani basi kuna uwezekano mzazi wake upande wa baba sio binadamu wa kawaida ,lakini hakutaka sana kujihanganisha nae na ndio maana kaamua kuondoka , kwani aliamini kuadamana kwa muda mrefu na mwanamke huyo kungemletea matatizo Zaidi.
Roma mara baada ya kuingia kwenye gari lake na kuliwasha alijiikuta akitabasamu kwa kejeli mara baada ya kuona kitu nyuma yake na kuliondodisha taratibu kuingia barabara kuu.
Baada ya kuendesha gari kwa madakika kadhaa akitafuta mgahawa mzuri kwa ajili ya kupata chakula cha usiku , kwani giza lishaingia alijikuta akisimamishwa na Polisi wa barabarani ambao aliwaona tokea akitoka hotelini na ilikuwa ni kama walikuwa wakimfuata kwa nyuma.
“Sir I’m going to have to see your ID”Aliongea Polisi mweusi baada ya kusogelea dirishani. Akiomba kitambulisho kutoka kwa Roma.
“Samahani sana ndugu polisi ,ila sijakibeba maana ndio ninakwenda kutafuta chakula cha usiku”Aliongea Roma akidanganya maana alijua hata kuletwa ndani ya Marekani sio kwa utaratibu , kwa maana kwamba ni mhamiaji haramu.
“Kama ni hivyo basi nina kila sababu ya kukusindikiza mpaka polisi , tunazo kila sababu za kuamini kwamba umeiba hili gari”Aliongea akiwa siriasis, ni kama walikuwa wakimwambia Roma hana uwezo wa kumiliki hio gari.
“Mr Polisi yanini yote hayo kuipenda sana kazi yako , muda huu ni usku unaonaje ukienda nyumbani kufanya mapenzi na mke wako”Aliongea Roma .
“Please watch your language , I can charge you for verbal assault against a police officer”
“Naomba chunga lugha yako ninaweza kukushitaki kwa kumtukana Polisi”aliongea na palepale alifungua mlango wa gari yake akimwamrisha kushuka.
Roma alijiuliza ni wapi amemtukana afande huyo mpaka akachukia , alijikuta akizima injini ya gari na kisha akashuka na kulifunga na polisi wale walimshika na kumuingiza kwenye gari yao ya kipolisi na dereva mwingine ambaye alikuwa polisi alitoa gari hio akiendelea mbele.
“Ofisa sijala chakula tokea mchana , unachochote hapo kunipatia ili nitulize njaa niliokuwa nayo?”Aliuliza Roma lakini hakuna majibu aliopewa na ndani ya madakika kadhaa tu waliweza kufika kwenye bandari ndogo na Roma alishangaa hakuna aina yoyote ya kituo cha polisi.
“Well , Well! , Who would have thought thet the magnificient Pluto would come to a point where he did not recognize his own enemies “
“Well, Well , nani anaweza kudhania Pluto mwamba ameshindwa hata kuwafahamu maadui zake””
“Ninyi sio polisi?”Aliongea Roma huku akiwa kwenye mshangao.
“All in good time”Aliongea na kisha gari ile ilisimama pembeni kwenye bandari
“Lala chini mpuuzi wewe , hatutaki kuchelewesha wageni wetu” Aliongea na kisha wote kwa pamoja walishuka na kuliacha gari.
Roma alijikuta akiinua uso wake mara baada ya kugundua wametoka nje ya gari,na kisha akaufungua mlango na kushuka na kujikuta akipulizwa na upepo mkali wa baharini na kufanya shati lake jepesi kugandiana mwilini.
Ijapokuwa kulikuwa na giza lakini mwanga wa taa zilizozunguka eneo hilo zlifanya eneo lote kuonekana vizuri.
Polisi wale baada ya kufika mbele kidogo walivua sare zao za kipolisi na kbakiwa na sare nyingine ambazo baada ya Roma kuzikodolea macho tu alizigundua.
“Dhoruba Nyekundu!!!”Aliongea Roma huku macho yake yakiongezeka ukubwa mara baada ya kugundua watu hao ni wanajeshi wa Dhorumba nyekundu.
“It’s an honor to be remembered by Pluto himself, Allow me to introduce myself I am Seidel and this is my partner Stark”
“Ni heshima kwetu kama unatutambua mfalme Pluto , naomba nijitambulishe mimi naitwa Seidel na huyu ni mwenzangu anaitwa Starrk”
“Kwahio mkaamua kunileta kwenye eneo hili pasipo ya kuwa na msaada?”
“Hahaha.. Hapana tulishawataarifu wenzetu kufika eneo hili , hata hivyo una kipi cha kugopesha , tushasikia Habari zako kwamba umebaki kama kuku tu”Aliongea Seidel kwa dharau na palepale Stark alipuliza kipenga na ghafla moja ya Contena lilifunguliwa na wakatoka wanajeshi kwa kujipanga mistari miwili wakimzunguka Roma.
“Mnapanga kuniua?”Aliuliza Roma mara baada kuona jeshi hilo.
“Mimi ndio nitapata heshima ya kukuua Mfalme Pluto”Ilisikika sauti ya mwanaume kutokea kwenye kivuli cha makontena upande wake wa kulia., mwenye nywele ndefu ambazo zilikuwa zikipepewa na upepo.
Alikuwa amevalia vazi la kijapani kama kanzu rangi nyeusi huku mkononi akiwa ameshikilia panga refu aina ya Samurai.
Lakini muda hio huo Roma alishangazwa pia na kuibukia kwa watu wengine kutoka kwenye maji kwa mfano wa kupaa ,wote wakiwa katika mavazi yanayofanana ya utamaduni wa Japani , Kimono.
“Takamagahara!, Nadhani taarifa zinasambaa kama kifuu cha nazi ,kwa hali hii naamini mshafahamu juu ya mimi kupoteza uwezo wangu , Vipi kuna mwakilishi kutoka Dhoruba nyekundu ambaye pia anahitaji kuniua?”
Roma aliweza kumgundua mwanaume aliekuwa mbele yake , alishawahi kukutana nae kule Ufaransa , kwenye mkutano wa siri uliondaliwa na serikali ya Ufaransa, alikuwa ni Nurarihyon ambaye ni generali wa kundi la Takamagahara.
“Inaonekana kweli umepoteza uwezo wako , mwanzoni sikuamini lakini kwa mwili wako ulivyo ni kweli hakuna kilichobakia , nasikia umepoteza uwezo wako mara baada ya kupigana na Poseidon?”Aliongea mwanaume mmoja aliekuwa kati ya maninja walioibuka kutoka kwenye maji halafu akaendelea.
“Nilitamani kuona jinsi ulivyodundwa na Poseidon lakini haima haja tena , naitwa Namera na nipo hapa kwa ajili ya kulipiza kifo cha mpenzi wangu SnowGirl”Aliongea yule ninja.
“Nilifikiria kutokana na kutokuwa na nguvu mngeniacha nikaendelea na Maisha yangu , kwanini nahisi kama mna katabia kakuchokoza watu wadhaifu”Aliongea Roma.
“Sio sisi tuliohusika kukufanya kuwa dhaifu na sio kosa letu wewe kupigwa na Poseidon ,hivyo kukuua leo hii ni jambo ambalo halikiuki kanuni zetu”
“Nurarihyon hatujakubaliana kwamba umuue huyu mtu , unatakiwa kuelewa kwamba anafaida kubwa kwetu akiwa hai kuliko mfu , kama utamuua hakika lazima tutakushugulikia”Aliongea Seidel wa Dhoruba nyekundu..
“Rest assured a powerless Pluto does not interest me , I cant leave empty-handed , however I don’t ask for much , All I want to do is to break every bone in his body”
“Kaa kwa kutulia sina haja ya kumuua Pluto asie na nguvu na siwezi pia kuondoka mikono mitupu , hata hivyo si ombi kitu kikubwa ninachotaka ni kuhakikisha navunja kila mfupa kwenye mwili wake”Aliongea Narurihyon.
“Naona mmechagua mbinu nzuri rafiki yangu , kwanini hamtaki akiniua?”Aliongea Roma akimwangalia Seidel
“Acha kuongea kilicho wazi”Alijibu Stark.
“Haupo imara kama mwanzo , hivyo sio ngumu kwetu kukudhibiti , ila usiwe na wasiwasi hii siri tunaifahamu sisi tu”Aliongea Seidel kisha akendelea.
“Kama utashirikiana na sisi na kutupa Umiliki ya jeshi lako , Hifadhi ya mafuta .siraha na vitu vya thamani tunaweza kukaa chini na kuongea , huenda pia tukawa marafiki ,tunasikia huko Tanzania una warembo kibao , hivyo hatutaki wakapatwa na huzuni”Aliongea Seidel.
“Kwahio hicho ndio mnataka?, basi ngoja niwaulize swali”
“Uliza tu”Alijibu Seidel.
“Nani kawaelezea nimepoteza uwezo wangu?”
“Mfalme Pluto acha maigizo na kuonyesha bado una nguvu ,tusingekuwa na uhakika na taarifa tulionayo tusingekuja wachache hivi ,tumepata taarifa kutokaka chanzo cha kuaminika”Aliongea Seidel.
“Ooh! sasa hivi nadhani naelewa , ukiachana na Prandell pamoja na Christen mtu mweigine niliekutana nae ni mkuu wa kikosi cha Dhoruba nyekundu”
“Kwahio unataka kusema nini? , huna chaguo kwa sasa nashauri utupe ushirikianao na kutuachia vitu nilivyovitaja kabla hawa marafiki zetu kutoka Japani hawajachukua hatua , ukitaka pia tunaweza kuingia makubaliano tukuachie mguu au mkono , Ijapokuwa natamani sana kukuua kulipiuza kisasi cha Judy”Aliongea Stark.
Judy ni moja ya jasusi wa kundi la Dhoruba Nyekundu ambaye Roma alimuua , Judy alikuwa ni mrithi wa Christen ambaye alimchagua , lakini kutokana na tabia zake za kuingilia mambo ya Roma akaja kumuua, sasa hilo ni tukio ambalo Roma alifanya kabla hata hajarudi Tanzania.
Roma alijikuta mwili ukimsisimka maana mpaka hapo watu wote walionekna kuwa na visasi , kwa mfano Namera alionekana kutaka kulipiza kisasi cha mrembo wake Snowgril , lakini wakati huo huo Stark alitaka kulipiza kisasi cha mpenzi wake Judy.
Roma alijikuta akiwaangalia kila mmoja kama vile alikuwa akiwakagua na kisha kutabasamu kifedhuli.
“Mnauhakika ni nyie tu hapa?”Aliuliza.
“Ni sisi tu ndio na tunakushinda jiandae naachia mapigo muda si mrefu”Aliongea Nurarihyon.
Roma alionekana kama mtu ambaye hajaridhishwa na watu wachache namna hio alitembea huku akiwa amekunja mikono yake kwa nyuma huku akiwaangalia, ukweli Roma alitamani sana mtu ambaye alijifanyisha kuwa yeye ndio afike hapo kwenye hilo eneo lakini alikuwa mwingine.
“Nyie watu inaonekana mna muda wa kutosha mpaka kuja hapa , katika watu wote ambao nilitarajia ni yule aliejifanyisha kuwa mimi , lakini nyie mkajiingiza kwenye hili , kwanini hamkuja siku zote hizo mkaja siku ya leo?”Walijikuta wakiangaliana kwa kuchanganyikiwa kwani walishindwa kumuelewa.
“Siwezi kuhisi aina ya msisimko unaotokana na uwezo wako wa kimapigano sasa hivi , ngoja tuone kama utaendelea kubwabwaja mpaka saa ngapi ,nataka uonje joto la upanga wangu”Aliongea na kisha aliuchomoa
“NENEKIRIMARU””
Aliongea kwa sauti na pale pale upanga wake uling’aa kama mwezi na palepale akapotea na ile anakuja kutokea yupo mbele ya Roma akitokezea kwa juu na alishusha upanga wake akidhamria kumkata Roma vipande viwili kutoka kichwani.
Roma hakuondoka aliposimama na alikaa vile vile huku mikono yake akiwa ameikunja nyuma , mpaka wale wenzake kuona labda Roma alishindwa kumkwepa kutokana na kushitukizwa.
Upanga ulivyomfikia Roma karibu na kichwa aliinua mkono wake na kuukinga na ukashuka moja kwa moja kwenye mkono lakini sauti iliotoka hapo ni kama ya panga na kufanya wote kushangaa na kutafuta kilichotoa mlio.
Upanga Nenekirimaru ni kweli ulifika kwenye mkono wa Roma lakini makali yake yalishindwa kupita kwenye Ngozi yake na sio kupita tu hata tone la damu halikuonekana.
“Ndio ushamaliza?”Aliuliza Roma kwa dharau
“Inaonekana licha ya kupoteza uwezo wako lakini mwili wako una Ngozi ngumu kama zamani , pigo la kawaida naona limeshindikana kukumiza?”Aliongea Nurarihyon.
Roma alimwangalia huyu ninja aliekuwa mbele yake , huku akifikiria ni kipi cha kumfanya yaani hakuwa hata na wasiwasi wa aina yoyote kwenye macho yake licha ya kwamba alikuwa amezungukwa na watu wengi
“General kwasababu huyu mpuuzi mwili wake ni mgumu hata panga kushindwa kukata Ngozi yake , nipe nafasi nimuonyeshe uchawi wangu , naamini kuna mapigo akipatiwa ngozi yake haiwezi kuhimili”Aliongea moja ya vijana wa Nurarihyon.
“Gashadokuro fanya kistaarabu tusivute nzi”Aliongea akimwachia.
“Nyie msijali hapa hakuna ambaye anaweza kufika kwani Polisi wanazunguka hili eneo kulinda kinachofanyika hapa“Aliongea Seidel
“Hehe ,, Well then time to have fun”Aliongea Gashadokuro na palepale ulitokea mwanga kama wa radi hafifu kwenye mikono yake na hapo hapo lilionekana fupa , sasa haikueleweka ni mfupa wa mtu au wa mnyama ila ni mfupa uliochongwa kama mkuki kwa mbele huku katikati ukiwa na kinundu ambacho kina matobo ambayo yalionekana kama vile yanatoa moto.
Kitendo kile kiliwafanya wale wanajeshi waliozunguka kurudi nyuma kidogo kupisha mpambano.
Inasemekana enzi hizo wakati wa vita huko Japani , wale wanajeshi wanaokufa vitani mifupa yao haikuwa ikizikwa na wanachokifanya ni kuikusanya sehemu moja, inaaminika kwamba Roho ya mtu hukaa kwenye mifupa mara baada ya kufa hivyo kuamini kwamba kwasababu mwanajeshi amefia vitani basi Roho yake ya machukizo na visasi hufuata mifupa yake , hivyo zile roho za machukizo na visasi kutoka katika mfupa wa kile mwanajeshi ndio wanazikusanya kichawi , sasa wanasema muunganisho wa roho zenye machukizo zikiungana kwa wingi zinatengeneza Pepo.
Ndio maana jamii nyingi za bara la Asia wanaamini kuzika kwa namna ya kumchoma mtu moto mpaka kuwa majivu ili Roho isibakie duniani, wanamini chanzo cha mapepo katika dunia ni mifupa ya binadamu.
Sasa mambo hayo hayatokei kwa wanajeshi wa kawaida , ila ni kwa makundi ya kijapani yaliojikita katika tamaduni za kichawi kama Takamagahara na mengineyo , hivyo fupa la Gashadukuro limejaa pepo moja lililotokana na muuganisho wa Roho kwenye mifupa Zaidi ya elfu moja.
Fupa lake lililikuwa ni kama likiongezeka ukubwa ile sehemu ya nundu yake huku kukiwa na kama wingu linalozunguka pale katikati na ule mchongoko wa mbele ulirudi nyuma na kujaa kwenye ile nundu na kufanya iwe kubwa kama nyungo ya kupasulia miamba saizi ya kichwa cha mtoto.
“Pluto ngoja nikuadhibu na hii nyundo tuone ni ugumu gani unao?”Aliongea na palepale akamsogelea Roma kwa Spidi.
“BANG!”
Nyundo lile lilikwenda kugonga ile sehemu ambayo Roma amesimama na kusababisha vumbi kubwa kama vile ni kimondo kutoka angani kimedondoka.
Walijikuta wote wakishangaa na hawakuelewa ni wakati gani Roma alipotea na kutokezea nyuma ya Gashadukuro akiwa hana maumivu ya aina yoyote, walishindwa kuelewa kwanini akaweza kupotoea na kutokezea.
“Damn it Si tumeambiwa amepoteza uwezo wake huyu?”Aliongea Stark huku akiwa ni mwenye mshangao mkubwa.
“Haiwezekani , Poseidon hawezi kufanya makosa , Kama nipo sahihi naamini licha ya kwamba amepoteza uwezo wake lakini mwili wake bado una baadhi ya vinguvu vinavyomsababishia kupinda pinda ndio maana akakwepa hana lolote huyo”Aliognea Seidel akijipa matumaini na kuwafanya wenzake wote kumuamini na presha ikapungua.
“Bastard”
Aliongea kwa hasira Gashadukuro baada ya pigo lake kugonga ardhi , palepale alirusha nyundo ya fupa la pepo kuelekea kwa Roma.
“Kwepa hio kama wewe ni mjanja”Aliongea na kumfanya Seidel kuwapa ishara baadhi ya wanajeshi wa kawaida kutoka upande wa Roma lakini ni kama wamechelewa kwani walimezwa na moshi mkubwa kwani ilitokea kama mlipuko wa bomu na kufanya nyama za miili yao kuruka hewani .
Upande wa Roma hakusogea kabisa na palepale aliziba pua zake baada ya kuhisii harufu mbaya.
“Nyama zao zinanuka”Aliongea .
Sasa ilionekana baada ya fupa lile Kwenda kwa Roma alilikwepa na likaenda kutua kwa wale wanajeshi na kusambaratishwa vibaya sana.
Gashadukuro mara baada ya Nundu ya fupa lake kuadhibu wanajeshi wale lilimrudia kwenye mikono yake.
“Nitakuwa makini muda huu na nitahakikisha hauna pakukimbbilia au kukwepa pigo langu”Aliongea kwa kijapani na palepale alileta nyundo lake la fupa lililojaa mapepo karibu na usawa wa Roma na ile linafikia nusu nchi kutoka kwenye mwili wa Roma lilisimama lenyewe pasipo ya kuendelea , ni kama limenasa hewani huku Gashadukuro akiwa amelishikilia.
Wenzake walijikuwa wakishangaa na kujiuliza kwanini kaishia njiani.
“Mbona umeishia njiani , mmalize haraka tuondoke?”Aliongea Siedel huku akimwangalia Gashadukuro bado akiwa ameshikilia fupa lake akijaribu kulivuta kurudi nyuma lakini mikono iliishia kumtetemeka.
“Siwezi “Aliongea kwa sauti ya kuchanganyikiwa na kufanya kila mmoja kushangaa .
“Nini kinatokea kwanini sioni ishara yoyote kama ana nguvu hata kidogo kwenye mwili wake?”
Inasemekeana Takamagahara ndio moja ya kundi ambalo linatumia mapepo katika mashambulizi , ndio kundi ambalo linaamini Zaidi katika nguvu zinazotokana na uchawi wa mapepo kuliko hata Yamata Sect , wanajiita The Demons kwa jina lingine na kama utafika kwenye kambi yao wanalo pango ambalo limejaa mifupa ya binadamu tupu kwa ajjili ya kuvuna roho zao na kuzigeuza mapepo , lakini hawachukui tu kila binadamu wanapendelea wale ambao wanakufa kwa visasi na chuki kwani mapepo yao yanakuwa makali Zaidi kuwa siraha.
“TAWANYIKA!!”
Roma aliongea kwa sauti akimwangalia Gashadukuro na palepale kilitokeza kitu cha kushangaza , mwili wa Gashadukuro pamoja na fupa lake vilianza kuyeyuka na kuwa kama unga unga ni kama vile alikuwa akiliwa na mchwa