Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 403

Licha ya kuanza kuhisi huenda Hades hajapoteza uwezo wake kama taarifa zilivyowafikia lakini bado hawakutaka kuamini kama wameshindwa , kitendo cha Gashadokuro kupotea kwa namna ya kuyeyuka kilifanya wote kuwa ni wenye kiwewe.

Nurarihyon alikuwa ni moja ya watu waliokuwa kwenye mshangao mkubwa alijiuliza inakuwaje mtu akawa na uwezo wa namna hio halafu asione nguvu alizokuwa nazo kwa namna yoyote ile,jambo hilo lilimshangaza mno.

“Inaonekana uwezo wako haukupotea kama tulivyopata taarifa , lakini haimainishi kama tutakimbia na kukubali kushindwa, tutapigana mpaka pumzi yetu ya mwisho”Aliongea Generali Nurarihyon na palepale aliwapa ishara vijana wake wote kushambulia , akiwemo Namera ambaye alikuwa na mpango wa kulipiza kisasi cha mrembo wake SnowGirl.

Ni kama Roma alikuwa akisubiria mashambulio ya pamoja , Namera na yeye hakuwa vibaya kwenye kutumia uwezo wake , kwani palepale alifanya tukio la ajabu, haikueleweka majani ya miti yalitokea wapi , lakini yalianza kudondoka kuelekea sehemu ambayo Roma amesimama na yalipomfikia karibu na kichwa yaligeuka kutoka kuwa majani na kuwa mawe ghafla yakimshukia Roma kwa namna ya kumjeruhi.

Roma alikuwa ashausoma mchezo kwani baada ya majani yale kugeuka na kuwa mawe aliyageuza tena na kuwa majani na kumfanya Namera kutoa macho baada ya kugeuka majani , tena yalishika moto halafu akayakusanya kwa macho na kuyatengeneza kama mpira na kwa kasi ya ajabu yaliwafuata na kuwalipukia.

Ni kitendo cha ajabu mno kwani Roma hajasogea hata hatua moja, lakini vilevile hakuwa akitumia mikono kutengeneza maajabu anayoyataka.

Baada ya kuona hali imekuwa mbaya Nurarihyon na jeshi lake walimchangia kwa pamoja kwa kasi kubwa kwa namna ya kupaa lakini walijikuta kila wakitaka kumsogelea Roma aliposimama hawamfikii , ni kama kuna nguvu isio kuwa ya kawaida iliokuwa ikiwasukuma nyuma na kushindwa kusogea.

“Pluto naomba kabla haujaniua uniambie umewezaje kutuzuia tusikufikie , umewazeaje kumyeyusha Gashakoduro?”

“Hahaha….hata mimi siwezi kuelewa ukishajua ushajua na kama hujui hujui tu , hisia zangu ndio zinaniambia fanya hivi na akili yangu ikikubali kila kitu kinatokea”Aliongea Roma kwa furaha na palepale Nurarihyon na maninja wake walipotea na kumfanya Seidel pamoja na Stark kushangaa.

“Puu!!!!”

Maninja wote walionekana kudondoka kutoka juu na kupoteza Maisha palepale akiwemo mkuu wao Nurarihyon.

Seidel baada ya kuona aliowategemea kufa kifo kibaya kama vile wamesukumwa kutoka kwenye jengo refu , aliwaamsrisha wanajeshi waliobaki kushambulia kwa risasi.

“Ratatatata….”

Milindimo ya risasi ilifunika eneo lote kwa muda wa dakika mbili huku wanajeshi wakishambulia sehemu moja ambayo Roma amesimama na kufanya eneo hilo kufuka moshi na kumfanya asionekane.

Ile wanakuja kuacha walijikuta wakipagawa na kutetemeka kwani risasi zote zilikuwa hewani ni kama zimegoma kumfikia Roma kwa kushikiliwa na kitu hewani.

Roma alitabasamu kifedhuli na risasi zile ziligeuka kama nyuki na kujigeuza kwa kasi kama vile zimetoka kwenye bunduki na kuwarudia wale wanajeshi na ndani ya dakika wanajeshi wote wako chini.

Seidel na Stark baada ya kuona wamebaki walikunja ngumi na kumsogelea Roma kwa kasi , lakini kabla hata hawajamfikia walijikuta wakielea hawani huku damu zikianza kuwatoka , walikuwa ni kama bendera juu ya mlingoti na Roma baada ya kuona ameridhika aliwaachia na ile wanakuja kudondoka hawakuwa hai tena.

Kazi ikawa imeisha lakini Roma alijiambia haijaisha kama anavyotaka alikumbuka katika watu ambao walikuwa wakijua juu ya yeye kupoteza uwezo wake ni Prandell ambaye ni Poseidon , pamoja na Christen lakini pia alikutana na Robert Mueller Kamishina wa FBI lakini pia mkuu wa kikosi cha Dhoruba nyekundu ndani ya taifa la Marekani.

Roma alishakuwa na kisasi cha muda mrefu na Robert Mueller tokea tukio lililotokea kule Japani na alijiambia haondoki Marekani mpaka aone mwisho wake.

Baada ya kazi yake kukamilika alipotea na alipokuja kutokea ni kwenye balcony ya jumba la Christen.

Sally alishangazwa na Roma kutokezea kwa juu kwani hakumuona akiingia wakati alikuwepo ndani ya eneo hilo la sebuleni muda wote.

“Mr Roma kuna kitu chochote unataka nikuhudumie?”Aliuliza baada ya kusimama na kumpa heshima yake.

“Nina njaa andaa chakula kitamu kuliko vyote”Aliongea na kumfanya Sally atabasamu , mwanzoni alijua Roma atarudi akiwa amekula , lakini imekuwa tofauti.

Baada ya Sally Kwenda kuandaa chakula Roma alisogelea simu ya ukutani iliokuwa hapo eneo la sebuleni na kuingiza namba anazozifahamu yeye.

“Mfalme Pluto tokea usiku ule nimeshindwa kukupata hewani, ulipotelea wapi?, kwanini namba yako inasoma upo Marekanni?”Ilisikika sauti inayotumia lugha ya Kiebrania upande wa pili, alikuwa ni Makedon jasusi wa Mossad.

“Huna haja ya kujua maelezo yote Makedon muda mchache , nimekupigia simu kwasababu kuna taarifa ninazozihitaji , itakuwa vyema sana kama utafanikisha kabla sijamaliza kula chakula cha usiku, mtu ninaetaka taarifa yake sio mgeni kwa Mossad hivyo naamini taarifa zake mtakuwa nazo”

“Who is it ?”

“Robert Mueller”

“The Commisioner , Mfalme Pluto unataka kuanzisha vita na Marekani , Kujiingiza kwenye maswala ya kisiasa si nje ya kanuni zako?”

“Sina haja na taifa la Marekani, ninachotaka ni huyu mpuuzi Robert Mueller anajaribu kunichokonoa na unajua sipendezwi na watu wa namna hio , Kazi yako ni kuelewa tu ninachotaka kwako na kunipa majibu, je tupo sawa?”

“Ni furaha kwangu kukusiidia Mfalme Pluto ,endelea na chakula chako nitakupatia taarifa muda si mrefu”Aliongea Makedon na simu ilikatwa.

Christen alikuwa bado hayupo nyumbani ikiashiria bado yupo kazini na Roma hakujali sana kuhusu hilo kwanza ilimpa uafadhali wa kuwa mwenyewe .

Dakika chache mbele Roma aliwekewa mezani chakula kitamu na Sally , chakula ambacho aliona ni kweli mrembo huyo alikuwa amefuzu sio tu kwenye maswala ya ukijakazi lakini pia katika maswala ya upishi na Roma aliona ndio maana Christen akamchangua.

Roma alikula mapande mawili ya nyama ya kuoka , akamalizia na kuku nusu na baada ya hapo akashushia na Champaigne kisha akaongezea juu na Soseji zinazotoka Urusi.

Sallly muda wote alikuwa pembeni akishangazwa na uwezo wa kula wa Roma , lakini Roma hakumjali muda huo alijali kwanza tumbo lake na baada ya kumaliza ndio akamwangalia.

“Sally unaniangalia kama mtu unaetegemea chochote kutoka kwangu?”

“Mr Roma nipo tayari kukuhudumia kwa kila utakachotaka?”

“Una uhakika!! je kama hatakupa hela tena?”

“Atanipa nina uhakika”Aliongea huku akitabasamu , ilionekana hela aliopoewa asubuhi ilishamnogea na sasa alikuwa tayari Kiiendelea Zaidi na Zaidi na Zaidi.

“Leo huna bahati naweza kusema , kwani kuna sehemu natakiwa Kwenda, labda siku nyingine “Aliongea huku akinyanyuka na kisha akapandisha Kwenda juu ghorofani.

Ukweli Roma hakutaka tena kumtumia Sally kutokana na kwamba alihisi utofauti mkubwa kati yake na mrembo Rufi , kila akikumbuka Ngozi laini ya Rufi hamu na Sally ilipotea .

Roma alikuwa akijihisi mwepesi sana kuliko isivyokuwa kawaida , ijapokuwa mwanzoni alikuwa akiogopa kusafiri kwa kuteleport , lakini muda huo hakuwa na woga , kila ambacho alikuwa akihofia kilishapita huku akijiambia kama kuna hatua ya Dhiki labda ni kwenye Maisha yake ya kawaida lakini sio kugongwa na Radi tena, baada ya kuwaza kidogo tu alipotea tena bila kueleweka anaelekea wapi.

********

Upande mwingine ndani ya Marekani katika jimbo la Washington D.C inaonekana jengo ambalo limesimama kama vile ni ngome , hilo ndio jengo ambalo linatumiwa kama makao makuu ya FBI linalofahamika kwa jina maarufu la Hoover Building.

Ni jengo ambalo lilisimamishwa tokea miaka ya 70 na ni moja ya sehemu ambayo ilikuwa ikiangaliwa na wananchi wengi kwa matamanio kutokana na ndoto za kupenda kufanya kazi katika jengo hilo.

Lakini licha hivyo wafanyakazi wanaofanya kazi ndani yake hawana utofauti sana na wafanyakazi wanaofanya kazi katika maeneo mengine , wote walikuwa wakifanya kazi muda wote na kulipwa mshahara wao na serikali kama ilivyo tu kwa wafanyakazi wengine wa serikali na hakuna mfanyakazi ambaye unaaweza ukasema ni Tajiri kuliko mwenzake kutokana na wote kuendesha magari ya kawaida ya bei rahisi kilichowatofautisha ni ile heshima kwenye jamii ni pale wanapojitambulisha kama FBI a. k.a ‘Law enforcers’.

Kamishina wa FBI ni Robert Mueller , ijapokuwa hakikuwa cheo kikubwa sana lakini vile vile hakikuwa cheo kidogo kama kiongozi wa FBI kwa maana kwamba kulikuwa na wakubwa wake Zaidi kicheo.

Ni saa nne sasa za usiku ndani ya jengo lakini jengo lilionekana kutoa mwanga ikionyesha wafanyakazi walikuwa wakiendelea na majukumu yao ya kuhakikisha Marekani inakuwa salama kwa raia na sheria inafuatwa kikamilifu.

Upande wa chini katika vyumba vya ardhi sauti ya Robert Mueller ilisikika kwenye korido yote ikiwa katika jazba kubwa sana.

“Nakuuliza wewe mpuuzi , unaniambiaje wanajeshi wote wamekufa halafu kusiwe na damu sehemu ya tukio?”Aliongea Robert Mueller huku akipiga kofi kwenye meza na kufanya makaratasi yalio juu yake kupeperushwa na upepo.

Mbele yake walionekana wanajeshi waliokuwa katika sare wakiwa wamesimama kwa wasiwasi mita moja kutoka kwenye meza yake.

Hasira ya Robert Mueller ilitokana na taarifa alioipokea juu ya wanajeshi aliowaagiza Kwenda kumkamata Hades mara baada ya kupata taarifa kwamba amepoteza uwezo wake.

Roberts Muellerr licha ya kwamba alikuwa kiongozi wa Dhoruba nyekundu tawi la Marekani lakini haikumaanisha alikuwa na nguvu Zaidi ya kujiamulia baadhi ya mambo kwasababu kulikuwa na wakuu wake ambao wanampa maagizo na kuyafuata.

Baada ya taarifa za Hades kupoteza uwezo wake ziliweza kufika katika makao makuu ya Dhoruba nyekundu na Robert alielekezwa kutofanya kitu chochote mpaka kutakapokuwa na taarifa za kutosha kutoka makao makuu ya Zeros organisation juu ya uwezo wa Ajent 13 kupotea.

Sasa Robert akadharau maagizo ya mabosi wake na kutoa kikosi Kwenda kumkamata Hades, ukweli ni kwamba Robert hakuwahi kabisa kumpenda Hades kutokana na Ngozi yake na hata wakubwa zake aliwashangaa kwa kumruhusu mwafrika kuwa na nguvu kubwa ambayo imekuwa tishio.

Hivyo baada ya kusikia kutoka kwa Prandell kama Hades amepoteza uwezo wake , aliona hio ndio nafasi yake , aliamini anchokifanya wakuu wake watakuja kumuelewa na kumshukuru baadae tu.

Mpango wake ulikuwa ni kumkamata Hades na kumuweka nyuma ya nondo na wakati ho huo akitafuta namna ya kumpunguza nguvu kwa kumshawishi kuachia baaadhi ya mali na nguvu ya kijeshi anayoimiliki ndani ya The Eagles.

Alifanya hivyo kwakuwa alikuwa akimwamini Zaidi Poseidon kuliko hata Zeros ambao wenyewe ndio waliohusika katika kumtegeneza , alijiambia miungu inatambuana , kama imesema Hades kapoteza uwezo wake basi hilo ndio jibu na sio la Zeros.

Yaani kwa lugha nyepesi hakutaka kutilia maanani wasiwasi wa Zeros , kwani kwa upande wao waliamini huenda Roma hajapoteza uwezo wake wote kutokana na kwamba hawakuwa na uelewa wa kisayansi juu ya mbinu za kijini anazojifunza.

Sasa baada ya kuletewa taarifa kwamba wanajeshi wake wamekufa na Hades pasipo kuonekana ndani ya eneo alipagawa mno na kupandwa na Jaza kali.

“Boss nadhani upunguze jazba , licha ya kwamba wanajeshi tuliotuma wamekufa haimaanishi misheni yetu imefeli , bado tunaamini yule mpuuzi kapoteza uwezo wake, kukimbia kwake hakuwezi pia kutuletea shida”Aliongea.

“Ubongo wako umekufa ?, unafikiri unachoongea sijakifikiria , ninachokifanya muda huu ni kuhakikisha namkamata wa kwanza , unafikiri kama atakamatwa na maadui zetu nini kitatokea? , jibu ni kwamba watamshawishi atoe hatimiliki za vile vyote vilivyopo chini yake na hilo litakuwa tatizo wewe mpuuzi uliejaza makamasi kichwani”Aliongea kwa hasira.

Lakini muda huo akiendelea kuwazodoa wanajeshi wake mtaalamu wa mitambo alitokezea kwenye mlango wa ofisi akiwa kwenye haraka huku akihema kama mbwa.

“Sir pardon my interruption but our systems seemed to be attacked by unkown hacker, The entire server now is out of our control”

“Sir naomba unisamehe kwa kuwaingilia lakini mifumo yetu imeshambuliwa na mdukuaji asiefahamika na Seva zote zipo nje ya uwezo wetu wa udhibiti”

Aliongea Mzungu huyo wa makamo ambaye ni mtaalamu wa mitambo ya teknolojia ya jengo hilo aliekuwa akiaminika na mara nyingi akiongea kauli ya namna hio inamaanisha kwamba ni kweli kuna shida.

********

Upande mwingine muda huo huo kukiwa na tofauti ya lisaa tu yaani ikiwa ni saa tatu za usiku ndani ya jimbo la Illnois-Chicago , ni katika makazi ya raisi mstaafu wa Marekani bwana Barack Mabo , katika kizuizi cha kuingia katika eneo hilo la kifahari lililokuwa kando ya bahari , ilionekana gari aina ya Ford rangi nyeusi ikiruhusiwa kupita mara baada ya kufanyiwa ukaguzi na walinzi.

Dakika chache tu mara baada ya gari hio Kwenda kusimama katika maegeisho ya muda mfupi , alionekana mwanamama Dyana alievalia vazi la suti nyeusi akitoka kwenye gari mara baada ya mlango wa gari yake kufunguliwa.

“Miss Dyana! Welcome my friend”Ilisikika sauti upande wa kulia kwake kutokea kwenye bustani na alionekana Raisi Barack Mabo akiwa na mtoto mdogo wa kiafrika ambaye ni mjukuu akiwa ameshikilia mpira wa kuchezea basketi ball na ilionekana yeye na babu yake walikuwa wakicheza licha ya usiku kuwa mkubwa.

“Thanks Barrack”Alijibu Diana na kumsogelea mheshimiwa na kukumbatiana kishikaji na kisha kuachiana.

“Joe tangulia ndani , tunakuja kujumuika kwenye chukula cha usiku”Aliongea mheshimiwa mstaafu na Joe alitingisha kichwa na kukimbilia ndani.

“Mara ya mwisho namuona Joe alikuwa na mwaka mmoja, nadhani ilikuwa mara yetu ya mwisho ya sisi kuonana”Aliongea Diana.

“Upo sahihi kabisa , ni muda mrefu hatujaonana Zaidi ya kuwasiliana kwa njia ya simu”Aliongea huku akimpa ishara ya kutembea kuelekea upande wa kushoto kwenye bustani , sehemu ambayo imejengwa kama sehemu ya mapumziko na kukaa chini huku wakiongea kwa kucheka walionekana kuzoeana , hata hivyo ni jambo la kuzoeleka kwani raisi huyo alisifika kwa ucheshi wakati wa uongozi wake.

“Nipe ripoti Diana , naamini jambo ambalo limekuleta ni muhimu Zaidi , kwani ni mara chache unatoka makao makuu Kisiwani”Aliongea mheshimiwa na kumfanya Diana kuvuta pumzi kidogo.

“Tuna wasiwasi na ajenti 13 mheshimiwa, amepitia mabadiliko makubwa kuliko sisi wenyewe tulivyotegemea”

“Unamaanisha nini?”Aliuliza na kumfanya Diana kutoa simu na kupangusa kwa dakika kadhaa na kumpatia na kuanza kuangalia, ilikuwa ni Vidio ikionyesha Roma akipambana na watu waliotumwa na Robert.

“ Nadhani taarifa ya mwisho ilielezea amepoteza uwezo wake na yupo nyumbani kwa Christen , kwanini anaonekana kuwa kama mwanzo?”

“Hayupo kama mwanzo Mheshimiwa na hili ndio limenileta kwa dharula nyumbani kwako”

“Unamaanisha nini?”

“Amekuwa vile ambavyo hatukutaka, kama unavyoona hapo alikuwa akipambana lakini hakuna ishara yoyote kama anatumia uwezo tuliomtengenezea sisi , anatumia mbinu ambayo alifundishwa na yule mpuuzi Tang Chi”Aliongea na kumfanya Barack Mabo macho yake kuongezeka ukubwa kidogo , ni kama mtu ambaye hajaelewa vizuri na alituliza mawazo na baada ya dakika kadhaa alitabasamu na kumfanya Diana aliekuwa na wasiwasi kushangaa.

“Kwa maneno yako napaswa kuamini kwamba amekuwa Hades na sio Ajent 13 tena?”

“Naaweza kujibu ndio kwasababu mpaka sasa hatuna uwezo wa kumfuatilia kwa ukaribu kama ajenti 13 , amekuwa Hades ndio kwasababu hategemei tena kile tulichokiweka kwenye mwili wake”Aliongea.

“Diana this is good news?”Aliongea akimaanisha kwmaba hio ni Habari njema.

“Unamaanisha nini mheshimiwa?”

“Nilikuwa kwenye mazungumzo ya muda mrefu na The First Black miaka mitatu iliopita mara baada ya kupewa uongozi wa juu wa Zeros , Diana unajua kwanini nilifungua maabara ya teknolojia ya juu nchini Tanzania na yapi yalikuwa malengo yangu kwa taifa la Marekani na dunia kwa ujumla?”Aliuliza kwa sauti ya chini.

“Hatujawahi kupata nafasi ya kuzungumzia maswala yako ya kisiasa , licha najua wewe ni moja ya raisi uliepigania maslahi ya taifa na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa”Aliongea Diana na kumfanya Barak kutabasamu.

“Sijapigania tu maslahi ya taifa la Marekani , bali naendelea kupigania maslahai ya Marekani licha ya kwamba nimetoka madarakani , moja ya ndoto yangu kubwa ni kupunguza nguvu ya The Doni katika hii dunia”Aliongea na kumfanya Diana kutoa macho.

“Mheshimiwa unamaanisha..?”

“Exactlly..”

“Taifa letu kwa ujumla linamhitaji Zaidi Hades kuliko Agent 13, kama ulivyosema amekuwa Hades kwa maana anaendelea kuwa huru, Zeros licha ya kwamba ni ya kimuunganiko katika mataifa makubwa lakini nguvu yake imeshikiliwa na The Doni”

“Lakini mheshimiwa sera za kimsingi za serikali yetu zimeasisiwa na The Doni na wanasiasa tunaendelea kuzipigania kuhakikisha kufanikiwa”

“Unachoongea ni sahihi lakini Marekani ni taifa na haliweze kuendelea kutokana na maagizo ya mtu mmoja , kwa nje tunaonekana kama wanademokrasia wa kweli , lakini kwa ndani tunatawaliwa kwa mawazo ya mtu mmoja , tunahitaji mtu ambaye atampunguza nguvu na kuwa mshindani wake, hii ni dunia yetu kwanini tuendelee kutawaliwa na mawazo ya mtu kutoka sayari nyingine”Aliongea na kisha akatabasamu na kuendelea.

“Diana nataka muendelee kutimiza wajibu wenu ndani ya Zeros HQ, kazi pale ni kubwa na sio ya kumfuatilia Agent 13 peke yake ,Dunia haipo salama Zaidi kama inavyoonekana kwa sasa na Marekani siku zote italinda maslahi ya taifa letu pamoja na dunia kwa ujumla”

“Mheshimiwa kabla sijaondoka naomba kuuliza swali?”Aliongea na kisha Mheshimiwa akatingisha kichwa kumruhusu.

“Matokeo ya mashambulizi ya meli yetu ya kivita , je ni kile kinachoendelea ndani ya Even Lab?”Aliuliza na mheshimiwa alitingisha kichwa akikubali.

“Matokeo hayo, je ni sehemu ya faida uliotegemea?”

“Diana katika moja ya vitu ambavyo najilaumu mpaka leo hii ni ujenzi wa ile maabara , mwanzoni nilifahamu naijenga kwasababu ya kushindana na The Doni , nakiri nilikuwa na mawazo hayo mara baada ya kushawishiwa na The First Black kuijenga kwa ajili ya Profesa Shelukindo lakini mwisho wa siku nilikuja kugundua nilikuwa nikitumika”

“Unamaanisha ujenzi wa Even Lab yalikuwa maagizo ya The Doni pasipo ya wewe kufahamu?”

“Exactly na zipo maabara kama zile Zaidi ya tano ambazo zipo chini yake , tunajaribu kupambana lakini yule mwanamke mipango yake ni kama imeandikwa kwenye karatasi kwani hakosei , ana akili nyingi sana kutuzidi nategemea mabadiliko makubwa ya dunia ndani ya miaka ijayo kama dunia haitoshituka mapema , kinachotupa changamoto ni kutokana na kwamba wote hatuna taarifa zilizokamili , kwani mipango yake tumeikuta na tunakufa na kuiacha na anakuja kutafuta wengine wa kuendeleza huo ndio udhaifu mkubwa tuliokuwa nao, Wewe ni rafiki yangu ndio maana nahitaji uendelee na majukumu yako, tunatakiwa kushukuru mabadiliko ya Agent13”

“Lakini mheshimiwa hujawahi kuhisi kuna kitu hakipo sawa , wote tunafahamu The Doni ndio aliependekeza utekelezwaji wa Mpango LADO ambao ulikuja kufanikiwa , lakini baada ya kutimiza hatua ya pili ya mpango Ajent 13 akaenda tofauti na kile kilichokuwa kwenye ramani ya mpango na sasa matokeo yamekuwa haya , huoni kuna kitu ambacho hakija kaa sawa”.

“Diana hakika unaonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiria , ni kweli kabisa kwa nafasi yako kuna mambo ambayo hauyajui licha ya kuwa katika mstari wa kutekeleza majukumu yako , Zeros kwa maneno ya The First Black hawakupenda Ajent 13 kujifunza mbinu za kijini ambazo hazina maelezo kisayansi , lakini mwisho wa siku The Doni mwenyewe ndio alieruhusu kwa Ajent 13 kufanya anachotaka, bado kuna kitu kikubwa Zaidi nyuma ya pazia ambacho serikali yetu haikifahamu ndio maana nasema ndani ya miaka michache ijayo tutarajie mabadiliko makubwa ya dunia”

Waliendelea kuongea mpaka walipokuja kufuatwa kwa ajili ya chakula cha usiku , lakini Diana aligoma na kuondoka na Mheshimiwa Barrack hakumzuia.
 
SEHEMU YA 404.

Robert alijikuta akiwa kwenye mshangao na sio kwake tu na wafanyakazi aliokuwa akiwafokea pia walijikuta kuchanganyikiwa.

“Pumbavu kabisa , inaonekana tumapata tatizo lingine la kushughurikia kwanza, tunapaswa kuondoka”Aliongea akiwapa ishara wamfuate.

Walitoka na moja kwa moja walienda mpaka floor ya chini Zaidi , sehemu ambayo ndio kuna udhibiti wa mitambo yote ya idara hio.

Eneo hilo na la juu lilikuwa na utofauti mkubwa sana , chini yake pia kulikuwa na eneo kubwa sana ambalo limejengwa kwa teknolojia kubwa , huku Gajeti na skrini mbalimbali pamoja na taratikishi zikiwa zimezungukwa na wafanyakazi Zaidi ya mia moja wakifanya kazi yao , eneo hilo ndio moyo wa idara hio kwa taarifa zote.

Lakini licha ya mkusanyiko ya wabobevu wa komputa wakizicharanga batani , lakini kulionekana hakuna mafanikio ya aina yoyote kabisa na mbaya Zaidi sasa ni kwamba mdukuzi aliehusika alifanya skrini zote kuonyesha muvi moja maarufu kwenye skrini zote.

“What the hell do you think you are paid for ?How can the HQ be hacked by just anyone , Our national intel is at stake”Alianza kufokea wafanyakazi wake kwa hasira

Robert Mueller kilichomfanya kukalia kiti cha ukamishina kwa muda mrefu ni kutokana na umahili wake katika kuzuia mambo ya udukuzi lakini pia kuwa mkamilifu katika kila misheni inayoibuliwa na idara hio.

Lakini mambo yanayomtokea siku hio , yalikuwa ni kama yanahatarisha nafasi yake , kwanza kabisa alikiuka maagizo ya wakuu wake na Kwenda kumshambulia Hades na pili makao makuu yamedukuliwa ilikuwa ni kibao cha uso kwake kwa aliefanya hivyo.

“Sir kaa kwa kutulia kabisa , mtu ambae amedukua anaonyesha kutokuwa na shida na taarifa zetu , bali amedukua mfupo wa mawasiliano wa Frequency , inaonyesa kuna kitu anataka kuonyesha laivu”Aliongea mmoja wapo

“Tayari mdudu ashaingia kwenye mitambo yetu halafu unaniambia huo upuuzi , unajua inamaanisha nini kama kuna mtu ndani ya dunia anaweza kutudukua?”Aliuliza kwa hasira.

“Sir”Aliita msichana mmoja mwenye nywele nyeupe kichwahi na kumfanya Robert amuangalie.

“Nadhani nimefanikiwa kujua mdukuzi wetu ni nani?’’

“Nini ?Ni nani?”

“Inaonekana ni Mossad kutoka Israel “Aliongea na kumfanya Robert kuwa katika mshangao , alijiuliza kwanini Israel wachukue hatua ya kudukua taarifa zao.

Lakini kabla wote hawajafahamu ni ipi nia ya wayahudi kuwadukua , ghafla muvi ilibadilika kwenye skrini na kuwafanya wote kushangaa.

“Oooh!... Taratibu mpenzi unaniumiza wewe mtoto”

“Una genye la kufa mtu mbwa wewe kama vile Nguruwe”

“Ni kwasababu yako wewe mpuuzi mambo yako si haba .. Aissii”

Kwenye skrini hizo kilionekana chumba cha sebule kikiwa na mwanga mkali wa taa unaomulika , huku mwanamke mmoja anaekaribia kuuaga ujana akiwa amekunjwa vizuri na mvulana wa makadirio ya miaka ishirini.

Kitendo kilichokuwa kikifanyika kilikuwa ni cha aibu mno mbaya Zaidi wafanyaikazi wote waliokuwa wakiangalia muvi hio walikuwa wakiwafahamu watu wanaoonekana kwenye hizo skrini.

Na walijikuta wote kwa pamoja wakimwangalia Robert ambaye alikuwa kwenye mshituko wa kutoamini kile kinachoendelea .

Miaka mitatu nyuma mara baada ya Robert kutalikiana na mke wake alijikuja kupata mwanamke mrembo sana mwanamitindo na kumuoa , Wakati huo Robert alikuwa tayari anaishi na mtoto wake wa kiume wa miaka kumi na saba katika nyumba yake aliempata na mke wake wa kwanza.

Hivyo watu waliokuwa wakionekana ni mke wake pamoja na mtoto wake wa miaka ishirini wakifanya ufilauni , kwa haraka haraka mpaka kufika kwa video hio ndani ya makao makuu inaonyesha kwamba ni skendo kubwa sana kama ingetoka hadharani na ingemaanisha kumdidimiza kabisa Robert katika fani yake na kumuondolea vyeo vyote, ijapokuwa ni mwana na mama wa kambo haikumaanisha kwamba wanakosa uhusiano wa kindugu wa kuhalalisha matendo yao.

“Unaonaje umahiri wangu … vipi mimi na mzee yupi ni noma?”Aliongea lile toto lisilokuwa na aibu.

“Jamani mpenzi wangu , kuna haja gani ya kumtaja huyo mwanaume , tokea niolewe nae hajawahi kuwa kama mwanaume kwa Zaidi ya mwaka , nahisi kujuta hata kufunga nae ndoa”

“Huh.. sio mbaya lakini, huoni yote haya ni kama yamepangwa tuseme asingekuoa unafikiri tungekuwa na hii burudani”

Wafanyakazi wenzake walijikuta wakijitahidi kutumia nguvu zao zote kuzuia vicheko maana mazungumzo hayo hayakuwa ya kawaida hata kidogo.

“Natoa agizo ya kupasuliwa kwa Monitor zote , pasueni”Aliongea Robert kwa hasira

“Boss punguza hasira , hatuwezi kuruhusu adui yetu kuzidi kushinda tukipasua”

“Screw off”Aliongea kwa hasira na kusogelea kijisturi na kukinyanyua na kuanza kukipigiza kwenye skrini.

“Bang!”

“Mzuieni asiendelee, hasira zake hazina faida ni hasara”Aliongea mmoja wapo mwenye cheo na palepale wanajeshi walimsogelea na kumshika kwa nguvu kumzuia

“Niachieni nyie wapuuzi kama hamtaki niwafukuze kazi , mimi ni Robert Mueller Boss wenu”Aliongea lakini alishikiliwa vyema pasipo ya kuachiliwa.

“Sir hutakiwi kuwa hivi kwa muda huu , wote tunajua Mossad ndio wamemua kutushambulia , lazima tujue sababu ni nini?”Alishauri mmoja akijaribu kumtuliza Robert.

“Hapana sio kweli ninachokiona , nimemkuza mwenye yule mtoto kwanini kaamua kufanya vile”Aliongea kwa huzuni huku akitamani kulia , kwa hali alioina hakuna mwanaume ambaye anaweza kuvumilia , lakini sio hivyo ni bora mwanaume angekuwa ni wa nje lakini mtoto wake ,ilikuwa ni ibu kubwa sana kwake.

Wakati wakiendelea kumtuliza boss wao Alarm ilianza kutoa mlio kama vile jengo limeshika moto na mitambo kuanza kubipu kwa rangi nyekundu

“Nini kinaendeea?”

“Nadhani tupo chini ya mashambbulizi”Aliongea mmoja wao kwa wasiwasi na wanajeshi wote walijiandaa kwa ajili ya kujilinda , lakini kabla hata hawajazifikia siraha zao ulisikika kama mtikisiko.

“BANG”

Ukuta wa jengo wa juu ulionekana kubomoka na kuacha eneo lote kuwa vumbi na kushikwa na woga usiokuwa wa kawaida , lakni wakati bado wakijiuliza ni nini kinaendelea mwanaume mmoja mwenye Ngozi nyeusi alitokezea mara baada ya vumbi kutulia.

“Pluto!!”

Walijikuta wote wakiwa kwenye mshangao baada ya kugundua mtu aliebomoa ukuta na kufosi kuingia alikuwa ni Pluto mwenyewe , walijiuliza imekuwaje akawa hajaumia popote.

Walishangaa hivyo kutokana na kwamba kuna misheni iliokuwa ikiendelea , misheni ya kumkamata baada ya kusikia hana nguvu zozote baada ya kupigana na Poseidon.

Roma mara baada ya kuangalia skrini za humo ndani alijikuta akiridhishwa na alijiambia vijana wa Mekedoni chini ya Mossad hakika wanaijua kazi yao , hakutegemea wangeweza kufanya vizuri namna hio lakini hakujua pia Mossad watakuwa na aina hio ya Vidio kwenye mafaili yao.

Hata hivyo hakushangaa sana , kwani imekuwa tabia ya idara nyingi za kijasusi kuwashikia viongozi udhaifu wao, Kiongozi unaweza kujikuta unafanya mambo yanayochafua taswira yako ukajua hufuatiliwi , lakini kumbe watu muda wote wapo macho na sio kwa kiongozi tu mpaka kwa familia, hivyo ukishakuwa na madaraka ni kama upo gerezani kwni lazima uhakikishe familia yako inafanya mambo katika mstari wa maadili ndio uwasimamie wengine.

Sasa Roma siku zote alikuwa akichukia sana uchokozi , ijapokuwa siku zote alikuwa na visasi na kundi la Dhoruba Nyekundu lakini aliamua kupotezea , kitendo cha Robert kutuma watu kumchokoza aliamini ni uchokozi wa hali ya juu ambao adhabu yake ni kifo bila rufaa.

FBI walikuwa washirika wakubwa wa Dhoruba nyekundu , ijapokuwa mpaka sasa inashindwa kueleweka makao makuu ya Dhoruba nyekundu yako wapi , lakini inasemekeana kila nchi kubwa duniani wana ofisi zao za siri sana na mara nyingi hushirikiana na mamlaka husika kutekeleza mambo yao na hio ndio sababu ya kufanya mambo yao Kwenda rahisi , kwa mfano kwa Marekani walikuwa na kambi ambayo kiongozi wao mkuu ni moja ya viongozi wa FBI ambaye ni Robert Mueller.

Roma alilifahamu hilo muda mrefu tu ndio baada hata haikumpa shida kugundua mchawi wake ni Robert Mueller.

“Naomba mnisahemue kwa kuchelewa kwangu , najua wote mlikuwa mkinitafuta na kujiuliza nimetowekea wapi , nilikuwa nyumbani nikipata chakula kabla ya kuja hapa”Aliongea Roma bila ya wasiwasi utadhani kuna aliemuuliza.

“Wewe shetani , kwanini ukaamua kufanya kitendo cha namna hii cha kunidhalilisha?”

“Kamishina tuliza wenge ijapokuwa hatukubaliani mahusiano ya kimapenzi kati ya mtoto na mzazi , lakini hata hivyo una mke mzuri sana naweza kusema isingekuwa siku zangu chache za kukaa hapa Marekani , huenda ningeenda kumtembelea , siamini kama atanikataa”

“Kaa kimya mbwa wewe unaongea ujinga gani , mpigeni risasi”Aliamrisha lakini hakuna ambaye alikuwa na ujasiri wa kufanya kama alichoongea.

Mtu aingie ndani y makao makuu ya FBI bila wasiwsi tena kwa namna ya kuvunja ukuta ambao umejengwa kwa vyuma vizito na zege kisha kuingia kwenye vyumba vya ardhi kama ni kwake halafu siraha za risasi ziweze kumdhuru , ilikuwa kichekesho ndio maana walitulia.

Robert baada ya kuona hakuna mwajaeshi anae chukua hatua alijikuta akijituliza kidogo na kumwangalia Roma.

“Naona haukupoteza uwezo wako?’

“Imekuuma?”

“Kivipi .. kwanini iniume Generali Prandell najua hakuwa na sababu ya kutudanganya lakini nina uhakika kwa masikio yangu mawili nilimsikia akisema hauna nguvu zozote na umekuwa kama binadamu wa kawaida , lakini kwanini..”

“Unaniuliza mimi tena , hilo ni swali ambalo unatakiwa kujiuliza wewe mwenyewe , najua ni kweli kasema hivyo lakini je nilikuambia nimepoteza uwezo wangu?”Aliongea Roma.

“Kama ni hivyo naamni Seidel na Stark , pamoja na wanajeshi tuliotuma hakuna hata mfupa uliobakia dunani?”

“Mh sioni mwanajeshi yoyote wa Dhoruba nyekundu hapa , wewe ndio kiongozi wao kwa hapa nchni, unaonaje ukiwakusanya na wote mkawepo sina haraka , lakini itakuwa shangwe kwangu wakiwa wote baada nina hamu ya kuwamaliza wote niwe na amani”

“Nyie wengine mbona mpo mpo tu kizembe hammnichulii hatua wakati jengo lenu limeingiliwa?”Aliuliza Roma akiwangaangalia.

“Mtukufu mfalme Pluto tunaomba ukarimu wako kuliacha hili lipite , kwa mtu mwenye heshima yako na hadhi ya juu huruma na ukarimu ni vitu ulivyojaaliwa ,kwasababu watu walioagizwa kukuua wamekufa unaonaje ukituacha sisi hai”Aliongea Robert kinafiki mara baada ya kujituliza.

“Unaongea nini wewe , yaani umeagiza mimi niuliwe lakini nikajiokoa nakuja hapa kulipa kisasi unakata nisamehe , dunia haiendi hivyo unafiikiri nimekuja hapa kwa ajili ya kufanya utani au kujionyesha kwenu nina uwezo wangu”

“Mfalme Pluto nadhani unaelewa hapa ndio makao makuu ya usalama wa taifa na kama utafanya jambo lolote baya ni kama kutangaza vita na serikali yetu ya Marekani , naamni uwezo wa hisia zako ni mzuri na utafanya maamuzi yalioyabusara Zaidi”Aliongea mmoja wao lakini maneno yake hayakumfanya Roma kuona woga.

“BANG !BANG!”

Aliharibu takribani tarakishi kumi kwa kuzilipua na uchawi wake kama onyo la kutoletewa vitisho vya serikali ya Marekanni na upuuzi mwingine.Moto na cheche tu ndio zilijaza eneo lote na kuwafanya watu wote kunywea huku wadada wakiogopa Zaidi.

“Nikisikia tena mambo ya kidiplomasia kama majibu yenu nitahakikisha hakuna mtu atakaetoka hapa na uhai”Aliongea Roma na kuwafanya kunywea mno na Robert alielianzisha alijikuta akikosa cha kuongea na hasira zake juu ya Pluto ziliongezeka maradufu.

“Sir ilikuwa ni kosa letu kukuchokoza hivyo naamini swali la kukuuliza sio kukuomba utache hai bali ni kukuuliza unataka nini kutoka kwetu , Vipi tunaweza kusahihisha na kufanya hali itulie? , kama unataka kuwaua wanajeshi wote wa Dhoruba Nyekundu naogopa kusema kwamba ni swala ambalo lipo nje ya uwezo wetu na hata hivyo Dhoruba Nyekundu haishikiliwi na taifa la Kimarekani pekee, mpaka sasa tunajua Maisha yetu yapo mikononi mwako , lakini pia miungu mingine imekubaliana na serikali zote kuishi kwa kuheshimu sheria za binadamu bila kuleta machafuko , hivyo nikuombe usiendelee na hili na tutafanya kila linalowezekana kukufidia”Aliongea mwanajeshi mwingine wa Kiafrika na kumfanya Roma kuvutiwa nae.

“Unaitwa nani?”

“Mario Balotelli Sir”Alijibu

“Wewe ndio umezielewa hisia zangu ni kweli kabisa mpaka sasa mnaishi kwasababu nimemua , kama ningetaka ningebomoa jengo hili na mkafia ndani na hakuna mtu angeweza kunigusa “

“Ndio nafahamu hilo ndio maana nimechkua nafasi hii kuongea ile nisije kosa haki ya kuongea kabla kufa”

“Okey maneno yako yamenivutia , nitakupa nafasi ya kuwaokoa wenzako”

Aliongea Roma na kisha alisogelea siraha na kuikoki kisha akampatia Mario Baloteli.

“Kwasababu shida yangu ni boss wenu , nataka umpige risasi wewe mwenyewe na ukifanikisha hilo kila mtu hapa atatoka akiwa na uhai wake”Aliongea Roma na kuwafanya wengine wote kutoa macho ya mshangao.

“Mfalme Pluto unamaanisha nini juu ya hli?

“Namaanisha muue , jambo rahisi tu”Aliongea Roma na kumfanya Baloteli kumwangalia bosi wake na kuanza kusita sita kufanya kama alichoelekezwa.

“Narudia tena , una chaguzi mbili tu za kuachia risassi kumuua boss wako na kukoa kila mmoja hapa ndani , pili usimuue boss wako na mimi kwa niaba ya uaminifu wenu kwa boss wenu , nitahakikisha mnamsindikiza kuzimu” baada ya wote kuona Roma yupo siriasis waliangalina.

“Wewe mpuuzi kama haupo tayari kumuua nipe mimi hio siraha”Aliongea mmoja wapo na wote walianza kuunga mkono , hakuna ambaye alitaka kufa wakati nafasi ya kuwa hai ipo.

“Jiangalie ulivyomsaliti , unakwenda kweli kutotii maagizo ya wakuu wako na kuniua , je unajua ni kipi kitakukutana ukifanya hivyo, Baloteli hebu nisikilize , kwanini umuogope huyu mpuuzi na yupo kwenye makao yetu makuu na pia sio kwamba yeye ndio mungu pekee kati ya miungu yote, kama ataharibu na ktua ni hakika miungu mingine itaanza kumuwinda”

“BANG!”

Kabla hata hajamaliza sentensi yake Baloteli hakuta kuleta ujinga alivuta triga na palepale risasi ikampata Robert kwenye kifua , Robert alidondoka taratibu kama mtu ambaye hakuwa akiamini moja ya vijana wake aliokuwa akiwaongoza ameamua kumuua kifo kilimnyemelea kwa mafadhaiko.

“Sisi sio watumwa wako , bali tulikuwa wafanyakazi wenzako wewe mjinga”Aliongea Baloteli mara baada ya kuhakikisha Robert kadondoka chini na kuzungukwa na dimbwi la damu.

Roma alijikuta akipiga makofi kwa kuridhika , mpaka hapo alijiambia hana kesi kwani aliemuua sio yeye bali ni Baloteli.

“Hongera umefanikiwa kuwaokoa wenzako , kama itatokea siku ukaja kuwa Kamishina wa FBI usije ukafanya kosa kama hili tena”Aliongea a kumfanya Baloteli kuwa katika mshangao maana hata siku moja hakuwahi kufikiria kama anaweza kuwa Kamishina wa FBI, kwani siku zote waliopatiwa cheo hiko ni watu weupe.

Roma aliwapotezea kwa jinsi walivyokuwa wanashangaana , huku wengine wakimshukuru Baloteli kwa kuwaokoa , yeye alipita na kuiinamia mwili wa Robert na kuanza kumpapasa mfukoni na ndani ya dakika chache to aliweza kutoka na saa ya rangi ya Dhahabu na Copper.

Walimwangalia kwa mshangao na wachache walijiua saa alioshikilia Roma ni moja ya vitu ambavyo vilikuwa vikipendwa sana na Robert.

“Msiniangalie kwa macho yenu hayo , mnafikiri namuibia huyu mpuuzi, kasababisha nimepoteza gari ya watu mpaka sasa hivyo najaribu kujilipa fidia , ijapokuwa saa hii haiwezi kutosha kwa thaman ya ghari ila inaweza kupunguza hasara”Aliongea na akaendelea kumsachi na kukuta hakuwa na kitu kingine Zaidi ya pakiti ya sigara na kujikua akimpiga Teke na kujiambia kweli hakukuwa na mtu hapo na bora hajajitia mikosi kumuaa ,alijiuliza inakuwaje mkuu wa FBI kutokuwa na kitu cha thamani. ,

Roma mara baada ya kuridhika aliwageuka na kuwaangalia wafanyakazi wote waliojipanga msururu, mara nyingi idadi yao ni tofuati na nyakati za mchana kwani jengo hilo lingekuwa na wafanya kazi wengi .

“Nimeridhika sasa na kisasi changu sitaki swala hili lijirudie tena , kwasasa eneo hili sio salama kwa ninyi kuendelea na kazi , kwa niaba ya serikali yenu Marekani nawapa ruhusa ya Kwenda kupumzika majumbani kwenu, ambao mmeolewa mkatoe haki ya ndoa na ambao mmeoa mkatimize haki ya ndoa, ninyi warembo ambao hamjaolewa ni muhimu pia kupata usingizi wa kutosha sura zenu zisikunjamane na mkakosa soko , kwenu pia washikaji kulala mapema kunaongeza nguvu za kiume na mvuto”Aliwapa ushauri wa kiafya akijikuta ni mwenye kujali na kisha bila kujali mwonekano wao aliondoka na ile wanachungulia kwenye Korido , tayari alishapotea

Dakika chache mbele Roma alikuja kutua nje ya bustani ya jumba la Christen ndani ya Loss Angeles .

Christen alionekana tayari alisharudi na sasa alionekana juu ya balkoni akiwa ameshikilia mvinyo wake akiruhusu upepeo wa baharini kumpuliza , alimwona Roma alivyoibukia na kujikuta akitabasamu kwa kejeli.

Alikuwa na kila taarifa ya kile kilichotokea ndani ya jiji hilo, kitendo cha Roma kuwaangamiza wanajeshi wote pamoja na kundi la ninja kutokaTakamagahara.

Roma mara baada ya kugundua uwepo wa Christen juu ya Balkoni akiwa na kigauni chake kinachopeperushwa na upepo , mwili wake ulimsimka , kwani alikuwa akiona kila kitu ndani ya nguo za kigauni chepesi cha mrembo huyo na kugundua hana nguo ndani yake aliamini Christen alikuwa bado hajamkatia tamaa na alikuwa akiendelea na mitego yake.

“Siwezi kuendelea kukaa Hapana na huyu mwanamke , kesho narudi Bongo”Aliwaza Roma huku akianza kupiga hatua kuingia ndani ya jumba hilo.
 
SEHEMU YA 405.

BEIJING -CHINA.

Premier ni kiongozi wa baraza la kitaifa , ambalo ni chombo cha juu kabisa cha utendaji katika taifa la China ambaye ukifananisha na Serikali ya kitanzania basi tunaweza kumuita Waziri mkuu.

Moja ya kazi kubwa ya Premier ni kusimamia shughuli zote za kibaraza na idara zote lakini pia kutekeleza sera zote za uchumi , kijamii na kiutamaduni.

Hivyo kwa maneno marahisi Premier anahusika Zaidi na utamaduni akishirikiana na wizara husika.

Sasa katika ofisi ya Premier ndani ya jiji la Beijing bwana Ning alionekana akiendelea na majukumu yake kama kawaida kwa siku hio , huku Habari kubwa ambayo ilikuwa ikiwasumbua vichwa ni ile ya kulipuliwa kwa meli ya kivita ya taifa la Marekani.

Siku hio yote kwake ilikuwa ni ya msururu wa vikao na mpaka muda huo wa mchana, alionekana amechoka mno kuliko isivyokuwa kawaida , lakini kwasababu alikuwa na miadi na mtu muhimu siku hio hakutaka kuonddoka katika ofisi yake na Kwenda nyumbani kwake kupumzika.

Wakati akiendelea kupitia baadhi ya makabrasha yaliopangwa kwenye meza yake kutoka Masijala , mlango wa ofisi yake hio nzuri iliopambwa kitamaduni , aliingia bwana mmoja wa makamo alievalia suti.

“Premier mgeni amefika”Aliongea kwa lugha ya Mandarin na kumfanya Premier Ning kutabasamu na kuvuta pumzi na kisha alimpa ishara msaidizi wake kumruhusu mgeni wake kuingia.

Ning Guiyao ndio jina lake Waziri mkuu huyu , alikuwa ni mwanaume wa makadirio ya miaka sitini mwenye mwili mkubwa kidogo alieenda hewani huku akiwa na sura ya duara iliopambwa na macho madogo.

Alikuwa amehudumu katika ofisi hio kama Premier kwa Zaidi ya miaka mitatu chini ya chama cha kikomunist.

Ning Guiayao inasemekana sababu ya kupata cheo chake ni kutokana na familia yake kuwa na mzizi ndani ya taifa hilo katika maswala ya kitamaduni na ndio maana akapewa cheo kikubwa kwa kuchaguliwa na raisi halafu kuidhinishwa na bunge.

Sasa mara baada ya Premier Ning kutoa maagizo ya kuruhusiwa kwa mgeni aliefika , hatimae mlango ulifunguliwa na akaaingia mwanaume moja wa kichina ambaye amevalia mavazi ya kiutamaduni ya hariri , alikuwa ni kama anatokea kwenye tawala za kihistoria za miaka mingi iliopita.

“Premier Ning!”Aliita kwa bashasha mara baada ya mwanaume huyo kuingia katika ofisi hio na kumfanya Waziri mkuu kutoka kwenye meza yake na kupenda mkono na wote wakaketi, huku wakiongea kwa furaha wakibadilishana salamu kwa lugha ya Kimandarini au kichina.

“Sio kawaida kwa nyie wazee wetu kutokezea kwenye ulimwengu wetu huu wa kawaida , licha ya sehemu kubwa ya maendeleo ya taifa hili ni juhudi zenu kupitia misingi mliotuwekea na kufuata”Aliongea baada baada ya msichana mhudumu kuweka chai na kutoka.

“Umeongea kwa usahihi na mara zote Hongmeng wanapotuma mjumbe uraini ni hakika kuna jambo kubwa linaendelea”Aliongea na kumfanya Premier Ning kuinua kikombe cha chai na kunywa kidogo.

“Brother Luo nadhani ninaweza kuotea , ni juu ya kilichotokea siku ya jana, swala la kulipuliwa kwa meli ya kivita ya taifa la Marekani na moja ya miungu, swala hili serikali yetu bado inalifanyia kazi kubaini chanzo kwani serikali ya Kimarekani inadhania tunahusika kwa kushawishi moja ya miungu kuungana na upande wa jeshi letu , nje ya mkataba wa the gods treaty”

“Sijatumwa kuja kwa ajili ya kuzungumzia swala la uharibifu wa meli ya kivita bali nimekuja kuzungumzia juu ya tatizo la Kimbunga kilichotokea siku hio hio ya jana”Aliongea na kumfanya Ning kushangaa.

“Unataka kusema sio tatizo la kiasili Brother Luo?”

“Haliwezi kuwa janga la kiasili Ning, Hongmeng imekuchagua kama ‘main link’(kiunganishi) na ulimwengu wetu kwa maana kwamba tumeona unaweza kufanya kile ambacho tunaagiza kifanyike , yote hayo sio kwasababu tu ya historia ya familia yako katika tamaduni za Kichina zilizoanzishwa na mababu bali ni uwezo wako mkubwa wa kuchanganua mambo na kuyatolea majawabu”Aliongea na kumfanya Ning kuvuta pumzi.

“Brother Luo naomba unisamehe katika hili, lakini lazima uelewe kwamba nimekuwa moja ya watu wenye shauku wa kutambua ulimwengu wenu unaonekanaje na unavyofanya kazi”

“Huwezi kuingia kwenye ulimwengu wetu bila ya kuwa binadamu mwenye uwezo wa kijini katikaLevo ya Nafsi”Aliongea huku akitoa tabasamu la kejeli kidogo.

“Ning unatakiwa kuelewa historia yetu tokea mwanzo , kwanini tulizuia miungu kutumia kanuni za kuchezea anga , sababu kubwa ni kwamba wanasababisha machafuko ya uwiano sawia kati ya dunia na miliki zetu, lakini hata hivyo sijaja kuzungumzia hilo siku ya leo”

“Brother Luo kama hujajakuzungumzia hili naamni ni swala la Kimbunga , ni kweli kwamba kuna taarifa zinazoelezea Hades na Poseidon kupambana katika maji ya kimataifa katika uelekeo wa njia ya Kwenda visiwa vya Hawaii Marekani , hata mpaka sasa taarifa zilizofika ni Hades kupoteza uwezo wake”Aliongea na kumfanya Mchina huyo mwenye jina la Luo kushangaa.

“Hilo ndio sasa ambalo ninahitaji kuongea mpaka sasa , ambalo linafanya miliki yetu kuwa katika wasiwasi”

“Wasiwasi!!”Aliongea kwa mshangao.

“Ijapokuwa jambo hili unaweza usielewe , lakini kitu kimoja ambacho unatakiwa kufahamu ni kwamba tuliweza kuhisi Radi ya mipangilio tisa kutoka kwenye anga letu , tukio ambalo mara ya mwisho kutokea ni wakati wa utawala wa Jin Dynastry”Aliongea na kumfanya Mheshimiwa Ning kushangaa mno.

“Kwahio unamaanisha kwamba katika mapigano kati ya Hades na Poseidon kulitokea tukio la namna hio , kwanini hili tukio lifanye Hongmeng kuwa katika wasiwasi.?”Aliuliza na kumfanya Luo kutabasamu kifedhuli kidogo.

“Unaonekana kutokujua mambo mengi?”

“Siku zote mnataka sisi tufahamu kile mnachoruhusu , nadhani sipaswi kulaumiwa”

“Wasiwasi wetu upo kwenye uwiano ambao Hongmeng wameendelea kuudumisha miaka na miaka , nadhani ushasikia kwamba kila binadamu ambaye anafikia katika levo ya Nafsi sheria kubwa tulioiweka ni kutoendelea kuishi katika mazingira ya dunia ili kuendelea kudumisha uwiano?”Aliongea na Premier Ning alitingisha kichwa.

“Katika miungu yote kumi na mbili ni mrithi wa Hades pakee aliechagua kujifunza mbinu zetu katika kupambana na kutengeneza Maajabu ,hivyo Wazee wanaamini mipangilio tisa ya Radi imempata Hades mpya na hili ndio linaibua wasiwasi kusikia bado yupo hai”Aliongea na kumfanya Premier Ning kuwa katika hali ya mshangao mkubwa, ijapokuwa hakuwa akielewa sana kuhusu mbinu za kijini , lakini kwa akili zake za haraka haraka alielewa Brother Luo alichokuwa akitaka kumaanisha.

“Brother Luo naamini kuna maelezo mengi ya kunielezea , lakini pia naamini umekuja kwangu siku ya leo kwa ajili ya kuhitaji msaada?”

“Tunachohitaji kutoka kwako ni kutusaidia kuondoa wasiwasi wetu , kwa kuhakikisha Hades anarudi katika mipaka ya China , tunahitaji kumvua nguvu zote za kijini zilizopo kwenye mwili wake”Aliongea na kumfanya Premier Ning kushangaa ni kama hajaelewa vizuri.

Inasemekana kwamba Hongmeng ndio waasisi wakuu wa kiroho katika tamaduni zote za kichina na ni kwa uelewa wao ndio ulioifanya China kupata maendeleo kwa kasi sana, kwa mfano China haikuwahi kuwa Koloni rasmi la Waingereza bali kile kilichotokea ni vita ya kibiashara kati ya mataifa hayo mawili na Waingereza walikuja kushinda vita vyao kupata udhibiti wa kibiashara katika eneo lote la Hongkong na maeneo mengi ya pwani kwa kusainishana mikataba mingi ikiwemo ule maarufu wa Nanjing(!842).

Tokea enzi za kale China ilikuwa ni nchi ambayo ilikuwa ikijitegemea kwa kila kitu hata biashara walikuwa wakifanya wao kwa wao hawakuwa wakiingiza bidhaa za nje wala kuzitoa nje ya bara na staili yao hio ndio inalifanya taifa hili kuwa na utamaduni wa kipekee na hata ujio wa Waingereza uliathiri tu mfumo wa kibiashara lakini sio kuitawala kama kilichotokea kwa mataifa ya Afrika.

China , Misri, Mesopotamia India na Ugiriki ndio nchi za mwanzo kabisa ambazo zilikuwa na maendeleo makubwa ya kiroho , kiutamaduni na kisayansi kwa muda mrefu ni rahisi kusema ndio maeneo ya mwanzo katika dunia kustaarabika.

Huwezi kusikia sana kuhusu Hongmeng katika historia nyingi za kichina kutoka na kwamba neno lenyewe linasimama baadala ya usiri mkubwa, mkataba wa ‘the gods treaty’ haukuwabana miungu pekee bali ni makubaliano ambayo pia yaliwazuia majini yote kutoka miliki ya Hongmeng kutotoka nje ya mipaka ya China na ikiwemo itafanya hivyo miungu hio kumi na mbili ilikuwa na haki ya kupigana kwa kutumia kanuni za anga na kuangamiza.

Na sheria hio ilikuwa ikifanya kazi mpaka leo hii, kwa mfano Jinikutoka Hongmeng likata kuja Tanzania kumshambulia Roma , basi miungu mingine inayohaki ya kuja kupambana pia kumlinda mwenzao.

Lakini kama Roma atatokea kuwa ndani ya taifa la China na akashambuliwa na majini basi hana msaada tena kwani miungu hio hairuhusiwi kuingia huko na kufanya mashambulizi , unaweza ukajiuliza je sehemu nyingine hazina majini ,, jibu sehemu zingine zina majini lakini hayana nguvu kama ilivokuwa kwa miliki za Hongmeng na ndio wao walioweka sheria ya viumbe vyote visivyokuwa vya kawaida kuingilia Maisha ya kawaida ya binadamu , bali ushirikiano uwe ni ule wa kimaendeleo pekee na ili kudumisha uwiano kati ya ulimwengu wao na huu wa kawaida wakajiwekea sheria wao wenyewe ya kila binadamu yoyote aliefikisha hatua ya Nafsi katika mafunzo ya kijini kutoishi katika mazingira ya kawaida na Kwenda kuishi katika miliki hizo.

Sasa ndio maana bwana anaefahamika kwa jina la Luo anataka Hades kuingia katika mipaka ya China ili kumvua nguvu za kijini , inaonyesha kinachowafanya kuhofia ni kwamba Roma anaweza kuwa tishio kwao , kwani kama wameweza kuhisi kushuka kwa malipizi ya radi ya mipangilio tisa wakati wa mapambano kati ya Poseidon na Hades ni dhahiri kabisa Radi hio imempiga Hades ambaye walikuwa wakihamu alikuwa akijifunza mbinu za kijini.

“Brother Luo hakika naweza kufikiria mbinu ya kumfanya Hades kuja China, lakini tokea nikiwa mdogo baba ashawahi kusema haitotokea siku kiumbe ambacho kitakuwa tishio kwa ulimwengu wa kijijni”Aliongea Ning.

“Baba yako alichoongea ni sahihi , haitotokea kiumbe chochote kuwa na uwezo wa kijini kama wa wazee wetu kutokana na kwamba siku zote tumekuwa tukizuia binadamu wa kawaida kujifunza mbinu zetu na hata wale waliopata nafasi ya kujifunza walipofikisha hatua ya Nafsi , sheria ni kutoka katika dunia ya kawaida , wale wachache waliokuwepo katika mazingira ya kawaida ya dunia ni kutokana na maombi maalumu na faida zao kwetu na wale waliokaidi ni kuwavua mbinu zote”Aliongea na kumfanya Ning kuelewa.

“Lakini serikali yetu kama itafanya mchakato wa Hades kuja katika mipaka ya China na mkamshambulia itaonyesha jambo hili ni la kupangwa na serikali , na kama itatokea mambo Kwenda vibaya ni lazima kutakuwa na uhasama nae , serikali yetu miaka yote imekuwa na ushirikiano na uwiano ulioimarishwa na jamii za siri kwa Zaidi ya millennium”Aliongea na kumfanya Luo kutabasamu.

“Uwiano unaouzungumzia ni Hongmeng ndio waliouweka , unafikiri kwanini mpaka sasa taifa letu linakuwa ni la kipekee katika uongozi wake dunia nzima , ni kwasababu sisi Hongmeng hatukuruhusu wale viumbe kuingiza sera zao mpaka leo hii , na ndio maana tamaduni zetu zimekuwa imara miaka na miaka pasipo ya kuathiriwa na jamii za nje, mpaka leo hii yule Shetani mwanamke akija katika mipaka yetu anaishi kwa unyenyekevu unahisi sababu ni nini , Ning yote ni kwasababu Wazee wetu walipambana na aina yote ya udhalimu”

“Mstari wa uzao wa familia yenu na familia ya Namba moja ndani ya nchi yetu hii ndio mmepata vibali vya kuelewa kuhusu jamii yetu na utaratibu huu utaendelea miaka na miaka na ndiomaana nipo hapa kwa ajili ya mazungumzo”

“Naamini kuna namna bora ya kuliweka hili sawa pasipo kuathiri uhusiano wetu tulionao na Serikali ya siri ya Mfalme Pluto, nitafikiri namna ya kumleta Hades ndani ya mipaka ya China hata hivyo mnachotaka kufanya naamini ni kwa maslahi ya taifa letu , hivyo ninayokila sababu ya kufanikisha hili ombi lakini wakati huo huo uwiano kuendelea kudumu”Aliongea. Na kumfanya bwana Luo kutabasamu alionyesha kufurahia sana kauli ya Ning.

Sasa hio ndio namna ambavyo Hongmen wamefanikisha kuitawala China kwa siri sana ni kwasababu wameamua kuhakikisha wanaojua uwepo wao ni watu wachache sana mathalani wale waliowachagua na ndio hao ambao hupewa nafasi kubwa katika uongozi wa taifa hilo, lakini swali la kujiuliza ni je ni watu wote ndani ya serikali hio wanafurahishwa na uingiliano wa kiutawala kati ya Hongmeng na binadamu wa kawaida.



********

Roma alimwangalia mrembo Christen kwa juu alieshikilia glasi ya mvinyo kwa mkono mmoja huku mwingine ukiwa umeshikilia nguzo , gauni lake la kulalia la kitambaa laini kilichopeperushwa kwa urahisi na upepo na kumuacha wazi lilifanya kuwa na uzuri ambao kwa mwanaume yoyote atakae muona kuwa na kumbukumbu ya mwanamke huyo kwa muda mrefu.

Roma alijihisi joto la ajabu kutoka sehemu zake za siri mara akimwangalia mrembo huyo ambaye alikuwa akimwangalia kwa macho malegevu yaliojaa madaha kutokea kwenye ghorofa ya juu.

Licha ya kwamba mchana wote wa siku hio alijirusha na mrembo Rufi , lakini mbele ya uzuri wa Christen alijihisi ni kama hakuwahi kukutana na mwanamke kwa Zaidi ya karne. Alijihisi njaa ya mwanamke isiokuwa ya kawaida , njaa ambayo aliamini haiwezi kutibiwa na mwanamke aliekuwa juu yake na jambo pekee la kujiepusha ni kurudi nyumbani , kwani kazi iliokuwa imemfanya kufika hapo Marekani imeisha na hata hivyo aliimisi familia yake huko nchini Tanzania.

“Nilivyopata taarifa juu ya vifo vya wanajeshi waDhoruba nyekundu na Takamagahara sikuweza kusadiki , lakini namna ulivyofika hapa nadhani kila kitu kipo wazi, Naomba nikusifu kwa kufanya kazi kubwa ya kutuweka kizani hata Poseidon na mimi pia tuliamini kabisa umepoteza uwezo wako, inaonyesha umefikia levo ambayo ni ngumu hata sisi wenyewe kuweza kuihisi katika mwili wako”Aliongea kwa mapozi na kumfanya Roma kumkwepa kumwangalia kwani upepo ulikuwa ukimwacha mtupu, licha ya kwamba Roma alikuwa chini kwenye bustani na Christen kuwa juu kabisa lakini haikuwafanya kuongea kwa sauti kubwa ni kama walikuwa wamekaribiana.

“Hakuna hata mmoja wenu alieniuliza swali la moja kwa moja kama ni kweli nimepoteza uwezo wangu , Zaidi ya kutegemea hisia zenu na mimi sikuona haja ya kujilazimisha kujielezea”Aliongea na kumfanya Christen kuweka sura ya kudharau maelezo yake.

“Nataka kujua kwanini tunashindwa kuangalia uwezo wako hata kwa hisia tu?”

“Mpaka sasa hata mimi mwenyewe nashindwa kujua kila kitu , lakini ninachoweza kusema najihisi kuwa binadamu wa kawaida kabisa tofauti na nilivyokuwa mwanzo na hisia ninazopata wakati wa kutumia nguvu zangu ni kitu ambacho nashindwa kukielezea labda kwa kukupa mwanga niseme hivi”

“Mwanzoni kabla ya kupigwa na Radi nilikuwa na uwezo wa kuiita uwezo wangu wa kijini na kuamua kipi kifanyike aidha kwa mikono yangu au kwa miguu yangu , lakini kwasasa hivi najihisi kama sina nguvu zozote zile hata mbinu ya Kimaandiko ya Urejesho isiokuwa na kikomo nashindwa pia kuelewa kama ipo katika hali gani kwenye mwili wangu”Aliongea na kumfanya Christen kionekana kuchanganyikiwa kidogo.

“Inashangaza , nishawahi kukutana na watu ambao wamepita katika hatua ya Dhiki lakini nguvu zao za kijini zinawazunguka na ni rahisi kuwatambua hata kwa umbali”Aliongea lakini kabla hata hajajibu hali ya hewa ya anga ilibadilika na nguumo kali ilioambatana na mwanga wa Radi ilipiga ni kama ishara ya mvua kunyesha sehemu nyingine na kumfanya Roma kufumba macho kwa woga

“Hahaha… Mfalme Pluto unaesifika kwa uwezo wako mwingi, leo hii unaogopa hata ngurumo za radi?”Alitania Christen.

“Kwanini wewe usijaribu kupigwa na radi kama mimi?”Aliongea Roma lakini Christen aliachia tabasamu na kisha akatupa glasi ya mvinyo na palepale aliruka kutoka kwenye ghorofa aliokuwepo mpaka chini na kufanya gauni lake kujifunua na kwenda kumvaa Roma kifuani.

“Mpenzi wangu Roma , kwa mwonekano wako umeguswa na staili yangu ya kuruka”Aliongea lakini Roma alojifanyisha kama hajasikia lakini Christen alimsogelea kwenye sikio lake kimadaha na kumpuliza.

“Isn’t gorgeous down there?”

“Sikuwa nikiangalia , Sijaona chochote”

“Mhmh hata sijataja ni kipi namaanisha lakini tayari ushajihami kwa kutokuangalia”Aliongea na kumfanya Roma ajitahidi kujitoa kwa mrembo huyo.

“Muda umeenda , bado hujachoka na siku nzima ya kurekodi nyimbo zako?”Aliongea Roma lakini Christen nikama hakumjali ,alianza kufanya manjonjo yake kuanzia kwenye shingo ya Roma na kushuka mpaka chini kama wale wanawake waliopo kwenye Macasino, aliendelea kushuka mpaka alipofika katikati kwenye kiuno.

Roma alijikuta akishindwa kufanya kitu kwani hisia alizokuwa akisikia hazikuwa za kawaida kabisa, Christen na yeye hakuishia katikati kwani aligusa dudu ya Roma na kisha akatabasamu baada ya kuhisi ugumu.

“Babe naona imetuma mno , naamini unavumilia sana kuniacha mwanamke kama mimi”Aliongea na kumfanya Roma atabasamu kwa uchungu , alijiambia ni mwanaume gani ambaye ataweza kushinda vitendo vya mwanamke huyu ni kweli kwamba alikuwa akivumilia sana.

“Aphrodite stop the ruckus”

“Aphrodite acha mambo yako”

“Kwanini unanifanyia ukatili hivyo”Aliongea kwa kulalamika na kutetemeka baada ya kusikia jina lake halisi.

“Unatakiwa kuelewa , kama ingekuwa wewe ni Christen halisi , Superstar na binadamu wa kawaida ningekuwa nishafanya mengi na wewe , nakiri mwili wako unavutia kiasi cha kunipa wakati mgumu , lakini Roho yako wewe ni Aphrodite na sio Christen, unajitahidi kunipa hisia zako mimi kwa kunifananisha na mtu mwingine , kama nitaamua kufanya mapenzi na wewe itakuwa ni kukuonea maana naamini hisia zako sio za kweli juu yangu bali za mwingine, na sitaki kufanya hivyo kwasababu wewe ni rafiki yangu ambaye nakuamini kwa kiasi kikubwa.”Aliongea na kumfanya Christen kutoa machozi.

“Wewe ni kama yeye tu hamna tofauti nadhani ndio maana akakuchagua kama mrithi wake , kwanini siku zote mnafikiria sana, Kwanini usijifanyishe kama mtu mbaya kwangu hata mara moja na kukidhi haja zangu , kwanini usinichukulie kama kichaa mwenye njaa , Kwanini kila mara unataka kuuweka uhalisia wangu wazi?”

“Ni kwasababu sitaki kukupoteza Christen , kama nitafanya mapenzi na wewe itaharibu uhusiano wetu”Aliongea na kumfanya kurudi nyuma.

“Ijapokuwa Ares , Apollo , Diana na Poseidon wanakuita Hades , lakini kwangu mimi wewe sio Hades wewe ni Roma binadamu wa kawaida Hades niliempenda aliondoka na kuniacha peke yangu”

“Hakika unaweza kusema hivyo na ndio maana aliniausia nihakikishe nakuwa karibu yako kwa kila jambo , aliamini kwamba nafasi yake kwenye moyo wako hakuna mtu wa kuiziba”

“Kama anajua nampenda sana , kwanini sasa hivi hayupo hapa?, Hades ni mwanaume mbinafsi sana ,Roma naomba unisamehe najua sipaswi kulalamikia kwasababu yalitokea sio kwasababu yako , Kwanini anataka wewe unijali mimi kwa kila kitu, labda Hongmeng waanzishe vita tena”

“Haha… usijali hata hivyo wanawake kuvutiwa na mimi ni jambo ambalo nimezoea kwenye Maisha yangu”Aliongea kwa utani na kumfanya Christen kutoa cheko.

“Ila kiukweli niliamini kabisa umepoteza uwezo wako , nimefarijika sana hujaupoteza, Ila Hades ni kweli huhisi chochote juu yangu?”.

“Kama ni kweli , hakuna ambacho kingenizuiwa kutokukupenda”Aliongea na Christen aliangalia juu na kuona kuna dalili ya mvua.

“Nataka Kwenda kulala , nadhani muda si mrefu itanyesha?”Aliongea huku akiondoka.

“Subiri kuna baadhi ya vitu nahitaji kukuuliza pia, kuhusu mchumba wako, kabla sijaanza safari yangu ya kurudi Tanzania”Aliongea. Roma , hakutaka kurudi Tanzania pasipo angalau kujua kidogo kuhusu Hades wa Zamani juu ya yale yote yalitokea ndani ya Tanzania tokea afike nchini humo.
 
SEHEMU YA 407.

MASAA MACHACHE NYUMA.

“Boss Edna!, Sikutegemea kama utafanya safari mwenyewe kuja mpaka huku?”Aliongea mmoja wapo wa wale mabwana wawili mara baada ya Edna na Roma kuingia ndani.

Edna aliwaangalia kwa zamu mabwana hao, lakini sura zao ni kama hakuwahi kuziona hapo kabla , Vexto ilikuwa na wafanyakazi wengi , hivyo ilikuwa ngumu kuwafahamu wote kwa sura kwani baadhi ya kazi nyingine ni Nasra aliekuwa akisimamia n ahata kiwanda hicho cha Ngozi hapo Chalinze alishawahi kukikagua mara moja tu na taratibu zote zilikuwa chini ya Meneja wa kampuni makao makuu.

“Nadhani umaendaa kila nilichoagiza?”Aliongea Edna huku akikwepa mkono wa mwanaume aliejitambulisha kama meneja wa kiwanda na Roma alitabasamu kwa kiburi alichokuwa nacho mke wake.

“Boss Edna tumejaribu kumfatilia muhasibu wa kampuni lakini inaonekana anachelewa kufika”Aliongea.

Wakati Edna anafanya safari ya kuja hapo alipiga simu na kuagiza mhasibu wa mahesabu ya kiwanda awepo ili akague hesabu , alishangazwa na kitendo cha wafanyakazi kugoma kwa kudai malimbikizi ya maslahi yao ilihali alikuwa akitoa pesa nyingi kuhakikisha kila mfanyakazi anakuwa analipwa ujira wake kwa kiasi ambacho anastahili kutokana na ugumu wa kazi yake.

Edna alijikuta akikunja sura mara baada ya kusikia mhasibu hakuwepo, Mabwana hao wote walikuwa na asili ya kihindi , ijapokuwa walikuwa wakijua kuzungumza lugha ya Kiswahili , lakini walionyesha wazazi wao walihamia nchini Tanzania, mmoja alikuwa mtu mzima wa miaka kama therathini na tano Kwenda arobaini hivi ambaye ndio meneja wa kiwanda anaefahamika kwa jina la Khalidi na mwingine alikuwa ni msaidizi wake ambaye anafahamika kwa jina la Baso.

“Kulikuwa na haja gani ya kutaka maongezi yafanyikie hapa hotelini wakati kuna ofisi ndani ya kiwanda?”Aliuliza Edna.

“Boss Edna kwanza niombe radhi kwa usumbufu uliojtokeza , ni kweli kabisa tunazo ofisi kwenye kiwanda lakini niliona hapa ni sehemu salama Zaidi kwa maongezi ukizingitia na hali inavyoendelea kwa sasa”Aliongea na Edna aliona maneno yake hayana mantiki.

“Boss Edna kabla ya maongezi hayajaanza , tumeandaa mvinyo ambao familia yetu imeutengeneza , tunajua kwa ukubwa wako utakuwa umejaribu aina nyingi ya mvinyo , tunaomba kwa heshima yako ujaribu hata nusu glasi na utoe mawazo yako”Aliongea Khalidi na kumfanya Edna kushangazwa na drama zao.

“Mimi kama msaidizi wa boss Edna , nitawasaidia kuonja”Aliongea Roma na kisha alipakua chupa kwenye mikono ya Baso na kujimiminia kwenye glasi na akapeleka wote tumboni na kisha akatabasamu , huku Khalidi na Baso wakimwangalia kwa mshangao , lakini Roma hakujali tena hakuweka chini chupa bali alipeleka mvinyo wote tumboni na alivyorudisha chupa chini ilikuwa haina kitu.

“Mr Khalidi kama kweli mmehusika na utengeneaji wa huu mvinyo , basi nawapa alama zote”Aliongea kwa sauti ya chini , lakini mara baada ya dakika tatu tu kupita aliegamia meza na kupotelea usingizini na kumfanya Edna kushangaa.

“Boss Edna naona msaidizi wako ameshindwa kuvumilia ukali wa mvinyo wetu”Aliongea Baso na kumfanya Edna awaangalie.

“Nataka kujua kwanini wafanyakazi hawakupata stahiki zao kwa wakati uliopangwa , ilihali bajeti niliotoa kwa mwaka mzima ilikuwa ni ya kukidhi kila mahitaji ya kiwanda?”Aliuliza Edna huku akijawa na wasiwasi ni nini kinataka kuendelea.

“Boss Edna kama unavyojua mwaka huu wateja waliokuwa wanahitaji bidhaa tunazozalisha waliongezeka kwa asilimia hamsini , kiasi ambacho kilitupelekea kuomba mkopo benki , lakini licha ya kuomba mkopo kutokana na kuajili wafanyakazi wengi ilipelekea bajeti kutojitosheleza , hivyo tukaanza ulimbikizaji wa madeni ya baadhi ya wafanyakazi , lakini mwisho wa siku kwasababu benki ilikuwa ikitudai tulishindwa kutoa pesa kwa wakati kwa ajili ya wafanyakazi”Edna aliguna kivivu huki akionyesha kutoridhishwa na maelezo hayo.

“Nadhani hainihitaji hata kukagua vitabu vya mhasibu , naona uzembe mkubwa na ubadhirifu wa hela za kampuni , Mr Khalidi usinifanye mimi ni mjinga ijapokuwa ni kweli mahitaji ya biadhaa kutoka kwenye kiwanda hichi yaliongezeka lakini faida iliokuwa ikipatikana pamoja na kiasi cha uwekezaji hakikuwa na uhusiano wowote ambao tunaweza kusema biashara ilikuwa ikileta faida , kuna uwezekano pesa ambazo zilikuwa zikipaswa kulipwa wafanyakazi mliamua kuzitumia kwenye mambo yenu”Aliongea Edna.

“Boss Edna maelezo niliokuambia ni hayo , haijalishi unakubali kuyaelewa au hukubaliani nayo , hata hivyo msaidizi uliekuja nae amesinzia , unafikiri imetokea kwa bahati mbaya?”Aliongea na kisha akweka tabasamu la kifehduli na kumfanya Edna kumgusa Roma kumshitua , lakini hakukua na matokeo yoyote na Edna alimwangalia Khalidi kwa hasira.

“Unataka kufanya nini?”

“Huna haja ya kuuliza maswali kwa kile ninachotaka kukufanya , huu ni mpango tulioandaa muda mrefu , ijapokuwa hatukukutarajia wewe , lakini ujio wako umenifurahisha sana , nadhani mbingu zipo upande wangu, nani angejua huyu mpuuzi angekunywa kinywaji ambacho tulikuwa tumekuandalia”Aliongea.

“Boss hata kama hajakunywa , kama tutaamua kumfanyia hapa hapa hakuna mto yoyote atakaejua wala kuwa na nguvu za kutuzuia”Aliongea Baso.

“Upo sahihi Baso , leo ni siku ya kulupiza kisasi kwa huyu Malaya kwa kile alichoifanyia familia yangu”Aliongea huku akibadilika uso na kuwa wa siriasis.

“Mr Khalidi acha kucheza na moto , ukinigusa tu nitahakikisha unaozea jela”Aliongea Edna kwa kukaripiua.

“Hahaha.. wewe mwanamke unafikiri ninaweza kukuacha kwa vitisho vyako vya kipuuzi , unakumbuka ulichomfanyia baba yangu mpaka akafa kwa presha?”Aliongea na kumfanya Edna kushangaa maana hakuwa akielewa.

“Naona hata huelewi ulichokifanya, labda nikupe nafasi ya kuelewa ukatili wako wewe mwanamke, Unakumbuka mwaka jana ulipoamua kununua kiwanda chetu kwa pesa ya chini mara baada ya baba kukosa mkopo benki kwa ajili ya uendeshaji?”Aliongea na kumfanya Edna asijue ni kipi kilichotokea kwani kipindi hicho yeye alikuwa ni kutoa tu maagizo na wafanyakazi wake walikuwa wakitii , hivyo licha ya kumfahamu mmiliki wa kiwanda lakini hakuwahi kujua Watoto wake.

“Mr Khalidi pole kwa kufiwa na baba yako , lakini swala langu la kununua kiwanda chenu linahisiana nini?, kwani nilifuata sheria zote na sikununua kwa ulaghai”

“Wewe Malaya acha kujifanyisha , unakumbuka vyema ni wewe ambaye ulichonga na watu wa benki ili baba asipate mkopo na kiwanda kifilisike ili uweze kukinunua kwa bei ya chini , hivi unafikiria nilijisikiaje kumuona baba kapiga magoti benki kuomba mkopo kwa kujishusha lakini licha ya yote hayo akanyimwa? , hivi ulijua ni nguvu kiasi gani baba yangu aliwekeza kwenye kiwanda hiki mpaka kikasimama mpaka leo hii”

“Mr Khalidi unaongea mambo ambayo huna Ushahidi nayo , ni kweli nilinunua kiwanda chenu kwa pesa kidogo , lakini haikumaanisha niliwadhulumu , nilitoa hela kulingana na thamanni ya kiwanda na hayo unayosemea wewe ni uzushi , kiwanda chenu kama sio mimi kingekuwa kishakufa mpaka sasa hivi”Aliongea Edna kwa kujihami huku akihema kwa nguvu , alionekana alikuwa akijizuia kuongea.

“Hahahah… Unamjuona huyu Malaya sasa?”

“Boss Wanawake Malaya siku zote ndio walivyo kwenye kujitetea , anafikiri sisi wajinga tusifahamu kwamba alikula njama na wakubwa ili tu mzee wetu asipate mkopo?”

“Wewe Malaya huenda nisingeweka kisasi na wewe tokea mwanzo kwani ulichofanya ni kuokoa kiwanda chetu , lakini kubadilisha kiwanda chetu kutoka jina la TAJO Kwenda Vexto ilikuwa ni matusi kwa baba yangu na familia nzima , nani alikupa ruhusa ya kununua kiwanda chetu kwa njia zisizo za halali , unasifika kwa hela nyingi , kwanini usingeanzisha cha kwako?”

“Mr Khalidi naomba nikuheshimu kwasababu umenipita umri , lakini kauli zako zinakuonyesha hata uwezo wa kufikirria huna , unafikiri nilishindwa kuanzisha kiwanda?, kama ningeanzisha kiwanda ni hakika mngekosa ushindani wa kibiashara na biashara yenu ingeishia kufa , nilichokifanya ni mbinu za kiuwekezaji tu kununua cha kwenu na kukiendeleza ili kutoruhusu wafanyakazi kuishia mtaani bila ajira kwa uendeshaji wenu mbovu, kuhusu kubadilisha jina ilikuwa hiari yangu kwasababu nilishanunua na kikawa mali yangu lakini pia jina la kiwanda chenu liliingia doa kwa kashfa zenu za kunyanyasa wafanyakazi wa kike kingono , nilichofanya ni kushawishi watu kwa njia za kubadili jina ili waone mmiliki kubadilika”

“Boss haina haja ya kubishana na huyu mwanamke , leo ndio siku tuliopanga kupata haki yetu na maumivu aliosababishia familia yetu”

“Baso unaweza kuwaita vijana kuanza kazi , nataka kuona sura yake inavyokuwa akiwa anafanya mapenzi”Aliongea Khalidi mhindi akiwa siriasis kweli.

“Hahaha.. boss mwangalie anavyobana miguu naamini bado ni bikra huyu”Aliongea na kumfanya Edna kuwa na wasiwasi na kumwangalia Roma ambaye alionekana akikoroma.

“Khalidi acha maneno mengi , tunadakika chache za kukamilisha kisasi chetu na kupotea kwenye hii nchi iliolaaniwa”Aliongea.

“Nisikilizeni kama mnataka kuondoka hapa nchini na hela za kampuni mngefanya hivyo mapema, lakini sio kumgusa mke wangu”Aliongea Roma aliesimama ghalfa na kumfanya Edna amwangalie na kuvuta pumzi ya ahueni , ilionekana Roma tokea mwanzo hakuleweshwa bali alisinzia makudusi kabisa.

“Wewe.!!, . Baso .. si ulisema dawa inachukua muda mrefu kuisha?”Aliongea Khalidi huku akitoa mshangao.

“Boss ndio pia nilivoambiwa”

“Aliewaambia kawadanganya , dawa yenu haina nguvu yoyote “Aliongea Roma.

Khalidi baada ya kuona Roma hakusinzia tokea mwanzo alisimama na kuusogelea mlango kwa ajili ya kuondoka , lakini Roma hakutaka kumruhusu kuodoka alimpiga mtama uliompelekea kudondoka chini na kupigiza sura yake kwenye sakafu na kutoa ukulele kiasi cha kumfanya Edna kufumba mdomo.

Dakika zilizopita ni kama alisahau Roma alikuwa na uwezo wa ajabu na alikuwa ni mwenye wasiwasi ya kufanyiwa vitendo viovu , lakini mara baada ya Roma kuamka kutoka usingizni alijua tu Roma na yeye alimchezea kwa kujifanyisha ameleweshwa na kinywaji.

“Hakuna kuondoka wapuuzi nyie , na mtaozea jela”Aliongea Roma.

“Edna pigia simu polisi , sijisikii kuwaua hawa”Aliongea na Edna alishituka kwenye mshangao na kuwasha simu ambayo alishangaa ilikuwa imejizima na kumpiga simu polisi.

…………………

Baada ya masaa kadhaa hatimae Khalidi na mwenzake walikamatwa na polisi na kupelekwa kituoni , mpango wa Khalidi ulikuwa wa kitoto sana , hivyo hata polisi haikuwachukua muda mrefu kushugulika nao na hatimae kukutwa na hatia yeye na Baso, hata pesa ambazo walionekana kuzihamishia Kenya zilitolewa maelezo na benki ya Exim na kuzuiwa.

Siku nzima yote hio Edna na Roma walibakia Chalinze , Edna alichangua uongozi mpya mzima wa kiwanda na kwa kupigia wafanyakazi aliokuwa akiwajua kwenye viwanda vingine kulipoti Chalinze na hilo ndio liliwachukulia muda mrefu mpaka kumalizika na baada ya kumaliza kikao na kutoa maagizo ya wafanyakazi wote kulipwa stahiki yake ndipo aliporuhusu wote kuondoka na kazi ya kiwanda hio kuendelea siku ya kesho mara baada ya kuwapa wafanyakazi hao wadogo maelezo.

Saa kumi za jioni ndio safari ya kurudi ilianza , siku hio mvua na yenyewe ilinyesha sana kwa maeneo ya Dar es salaam na ya Pwani na kusababisha mafuriko baadhi ya sehemu.

Ijapkuwa mpango wa Khalidi ulikuwa wa kitoto sana , lakini Edna siku hio angekuwa peke yake huenda asingeweza kutoka kwenye hoteli ile salama.

Inabidi Roma aache gari yake na kupanda gari ya mke wake huku akiwapa maagizo vijana wake kuondoka nayo , kwani Roma alikuwa ashahisi uwepo wao muda mrefu wakimfuatilia Edna kutoka nyumbani kwa ajili ya ulinzi wao.

Kutokana na kujeruhusiwa kwa John kazi yake ilirithishwa kwa Molin na Adeline.

“Vipi bado tu unafikiria maneno waliokuambia wale wapuuzi?”Aliuliza Roma mara baada ya kugundua Edna hakuwa sawa kimawazo mara baada ya kungia kwenye gari..

“Ah..”Edna alitoa sauti pasipo kutoa jibu ni kama alikuwa akiitikiaa kwamba ndio alikuwa akiwazia maneno yao.

“Huna haja ya kuendelea kuwa na wasiwasi , unajua ni kwanini sikutaka kuamka mapema na kuwatia vibao licha ya kusikia wakikutukana?”

“Uliwaonea huruma?”

“Inaweza kuwa hivyo, unajua kuna tofauti kubwa sana kati ya Watanzania na wahindi, mara nyingi Wahindi ni wenye kuheshimu sana desturi zao , kwanzia kile ambacho familia inachokianzisha na vyote vinavyowazunguka , hivyo biashara hata iwe ndogo vipi kwao , wanafamilia wote watapambana kuhakikisha inasimama na hawataruhusu ,mtu mwingine wan je kuingiza mkono wa umiliki na ndio maana mara nyingi wanaonekana kama wabaguzi likija swala lakuajili watu , ijapokuwa wahindi wengu wanaohamia ndani ya mataifa ya Afrika wanaishi kwa sheria za nchi zetu lakini hamaanishi kwamba tabia zao na tamaduni wanazisahau, ndio maana baada ya kuchukua kiwanda chao na kukibadilisha jina ni kama tusi kwa ustaarabu wa familia , hivyo ilikuwa rahisi kwa wao kukuchukia na kuona kama adui”Aliongea Roma na kumfanya edna kufikiria na kuona kweli maneno yake yalikuwa na mantiki kwani wakati ananunua kiwanda hicho hakufikiria familia hio ya kihindi hapa Tanzania ilikuwa ikijisikiaje, yeye alichowaza wakati huo ni faida tu.

“Kwahio unachojarinbu kumaanisha ni nini?”

“Ninachomaanisha ni kwamba uliwakosea lakini wakati huo hu uliokoa kiwanda kutokufa na kusaidia familia nyigi ambazo zilikuwa zikitegemea kuendesha Maisha yao kwa kuendelea kuwapatia ajira , kama unaweza kufikiria kwa utashi utagundua wafanyakazi wengi wanaofanya maviwandani sio wale wenye elimu kubwa na wengi wao Maisha yao ni ya chini sana na kama itatokea kiwanda kikafungwa ghafla wengi wao ndio wanatateseka sana, hivyo mke wangu naweza kusema ulikosea familia ya watu wachache kuokoa watanzania wengi wa hali ya chini , faida ni kubwa kuliko hasara hivyo usijihisi mwenye huzuni”

Aliongea Roma na kumfanya Edna kutabasamu , maneno ya Roma yalionekana kumrudisha kwenye mudi yake ya mwanzo , alikuwa akijisikia vibaya kwa kumfanya Khalidi kupoteza familia yake na wakati huo huo Kwenda jela lakini mara baada ya kusikia ameokoa watanzania wengi ni kama alipata sababu ya kuona yu sahihi kwa maamuzi yake.

“Naona unajaribu kunipa maneno ya kunifurahisha”

“Babe wife hilo sio kweli nimetoa maelezo yangu kutokana na utashi wangu haimaanishi pia nipo sahihi”

“Unajua kila kitu kinafaida zake na hasara, na hakuna kitu ambacho kimekamilika , hivyo hata wewe kuchukua kiwanda chao kulikuwa na hasara lakini pia faida na kama utaangalia kwa jicho la kimahesabu utsona kuna faida kubwa”

Alichoongea Roma ni sahihi , kwani wakati Edna anaunua kiwanda hiko kilikuwa kina hali mbaya mno ya kiuchumi na wafanyakazi hawakuwa wakilipwa na wengi wao walikuwa wakinyanyasika hasa kwa wale wa kike , sio kwamba alishindwa kuanzisha cha kwake lakini aliamini kama angefanya hivyo angeua kile kilichokuwepo , hivyo njia ya kibiashara aliona inafaa ni kuendeleza kilichopo ili kuokoa na watu waliokuwa wamajiriwa kwenye kiwanda hiko .

********

Mara baada ya Nasra kupitwa na Roma bila salamu , kitendo kile kilimuumiza sana na kujiuliza ni kipi amemfanyia Roma mpaka kumuepuka , ndio alitafsiri kama kumuepuka kutokana na kwamba alipiga simu Zaidi ya mara therathini pasipo kupokelewa na mara baada ya Roma kurudi haonekani kujali kabisa, kitendo kile kwake alitafsiri ni kama Roma hakuwa akimtaka tena.

Nasra alijikuta akijifungia ofisini kwake huku machozi yakianza kumtoka , moyo wake ulikuwa ukimuuma kwani hakuwa tayari kuachana na Roma , hakuwa tayari kuukubali ukweli kama Roma alikuwa amemuacha kwasababu ya mama yake kutomkubali.

Alijiambia mwenyewe hata kama Roma hakuwa akimtaka tena kwasababu ya mama yake , kwanini amkimbie , kwanini asiwe na ujasiri wa kumwambia machoni kama hamtaki tena Zaidi ya kumkimbia, baada ya kuwaza kwa muda ndipo alipotaka Kwenda kumsikia Roma mwenyewe akimwambia hamtaki , alijiambia kama Roma alikuwa akimkimbia basi ataenda nyumbani kwake ili asikie kauli ya kuachwa na sio kuchanganywa kwa namna hio, hakujali Edna angemfikiriaje lakini wakati huo alijihisi kuonewa mno.

Baada ya kutoa maagizo kwa katibu wake alitoka na kuelekea nyumbani kwa Roma , alikuwa akipajua sana tu, kwasasabu ashawahi kufika mara kibao , hivyo haikumpa shida kufka nyumbani hapo , alichokuwa akitaka kwenye kichwa chake ni Roma kumtakia hamtaki ili apate ujasiri wa kuendelea na Maisha yake , hakupenda hisia za kuchanganyikiwa alizokuwa nazo.

Nasra mara baada ya kushushwa na Taksi nje ya geti la nyumba ya Roma hakuweza hata kupata ujasiri wa kugonga na kuruhusiwa kuingia ndani , bali alikaa kwenye kitaru cha maua pembeni na mlango wa geti hilo kubwa akisubiri, aliamini ni lazima Roma angemkuta hapo.

Nasra alikuwa kama mwanamke ambaye amechanganyikiwa na mapenzi na hata yeye mwenyewe hakujielewa kama itatokea siku kumuwinda mwanaume hivyo ,lakini licha ya hivyo hakujali uchizi wake kwa muda huo , alihitaji kukamilisha hitaji lake la Moyo.

Baada ya kukaa hapo muda wa asubuhi mpaka saa nne ndipo mlango wa geti ulipofunguliwa na Blandina mama yake Roma akionekana alikuwa akitoka kwa kutembea huku akiwa ameshikilia mfuko.

Baada ya kumuona Nasra aliemjua kutokana na kwamba alikuwa ashawahi kuonana nae akiwa anasoma kwenye kituo chake cha kulelea Yatima alijikuta akishangaa na kujiuliza maswali mengi.

Ijapokuwa Nasra alilelewa kwenye kituo hicho , lakini kwenye Maisha yake hakuwahi kumfahamu Blandina kwa sura yake halisi na hakuwahi pia kukutana na mama yake Roma licha ya kusikia walikuwa wakiishi pamoja.

Nasra alikuwa akimjua mwanzilishi wa vituo vya kulelea Watoto vya Son and Daughter Orphanage ni Marehemu Maina , aliekuwa mke wa raisi wa Kenya na hata siku ambayo alipata kufahamu juu ya kifo chake aliomumboleza pia , lakini pia alikuwa akimfahamu Blandina kama mwanzilishi mwenza kutokana na kwamba ndani ya ofisi ya Mama Issa picha ya Blandina ilikuwepo na hata siku moja alipouliza ndipo alipopewa maelezo na Mama Issa kwamba picha hio ni ya mwanzilishi mwenza.

Blandina alimsogelea Nasra kwa mshangao huku akijiuliza mrembo huyu wa hadhi alikuwa akifanya nini nje ya geti pasipo kugonga

“Nasra!”Aliita Blandina nna kumfanya Nasra amwangalie Blandina kwa namna ya kumshangaa na kwa upande wa Blandina alishasahau kwamba alikuwa akitumia sura yake halisi ndio maaana alipomwita Nasra alitegemea kutambuliwa , lakini ilikuwa tofauti na kukumbuka kwamba Nasra hakuwa akimfahamu kwa sura yake halisi.

Jumba la familia ya Roma lilikuwa mwisho wa barabara likitenganishwa na upande wa fukwe ya Cocco , hivyo ni mara chache sana kuona watu wakikatiza hayo maeneo na hata wale wanaoishi kama majirani mara nyingi wakitoka ni kwa kutumia magari na ni mara chache sana kuwaona wakijihangaisha na mtu ambaye yupo njiani.

Sasa kwa Nasra alivyokuwa mzuti ilikuwa ni jambo la kushangaza sana kumuona amekaa kwenye mitaa hio ya ushuani pasina sababu na hicho ndio kilimshangaza Blandina.

Nasra alimtambua mara moja Blandina alikuwa ni mama yake Roma , na alisimama na kumsalimia huku akishangaa mama huyo kumfahamu yeye kwani hawakuwahi kukutana nae.

Nasra alijielezea kwa ufupi kwanini yupo hapo na mpaka anamaliza Blandina alijikuta akiwa kwenye mshangao , hakuamini kama mwanamke wa Kariba ya Nasra anaweza kufanya maamuzi ya kuja kukaa nje ya geti kumsubiria mtoto wake Roma , ijapokuwa alijua mapenzi ni uchizi lakini kwa Nasra aliona uchizi umemzidia na kujiuliza ni kipi ambacho mwanae alikuwa akiwapa warembo hao mpaka kufikia hatua ya kumuwinda nyumbani.

Blandina alimwangalia Nasra mwenye sura ya kipole ya heshima na kujikuta akitabasamu , ijapokuwa ashawahi kukutana na Nasra mara chache alipokuwa akisoma kwenye shule yake , lakini mara baada ya Kwenda chuo hawakuhahi kuonana tena na alimuona kuwa mrembo Zaidi ya alivyokuwa mdogo.

Blandina mara baada ya kugundua makosa yalikuwa kwa Roma alimuonea huruma Nasra, lakini hata hivyo hakutaka kumtetea mwanae , aliacha Roma mwenyewe akirudi ndio ayamalize , hivyo alichokifanya ni kumtoa Nasra nje ya geti na kumwambia aingie akamsubirie ndani , lakini Nasra akagoma akisema atasubiria tu nje , lakini bado Blandina hakutaka Nasra kusubiria hapo nje kwani angejisikia vibaya hivyo akamwambia akasubiirie kwenye bustani ndani na hakuna haja ya kuingia ndani kabusa.

********

Kitendo cha Roma kuwa na wasiwasi kiasi cha kutomjali Sophia na yeye kilimuumiza sana Edna kwa wivu, ni kama hakupendezwana Roma kuwa na wasiwasi juu ya mwanamke mwingine.

Ijapokuwa Edna hakupata maelekezo ya kutosha juu ya kile kilichotokea nyumbani , lakini alijua tu ni maswala ya mapenzi ndio yaliomfikisha Nasra nyumbani kwake , jambo ambalo lilimuuzi sana kwa Nasra kufanya hivyo , aliona ni kama anamuwinda mume wake.

Sophia ambaye pia alirudi akiwa na mudi ya kumuona Roma kwa mara nyingine alijikuta akinywea mara baada ya kuona Roma hakuwa akimjali kama vile alivyotegemea na Zaidi alikuwa akiendesha gari kama mwehu kurudi nyumbani.

Roma mara baada ya kufikisha gari nyumbani ni kweli aliweza kumshuhudia Nasra aliekuwa ameketi na mama yake kwenye eneo la bustani na kujikuta akishangaa mno.

Ijapokuwa aneo la bustani lilikuwa limejengewa kwa kujikinga na mvua , lakini maji ya mvua yaliokuwa yakiruka yalitosha kumloanisha Nasra.

Roma aligundua Nasra alikuwa kwenye mavazi yake yale yale alioamkuta nayo asubuhi , upande wa Blandina na yeye alikuwa nje tokea asubuhi yote akiwa ni mwenye kumuonea huruma Nasra huku lawama zote akimbebesha mwanae Roma kwa kutotimiza majukumu yake kwa wanawake hao mpaka kuja kuleta sintofahamu nyumbani na aliishia kujiulaumu na kujiambia ni kutokana na Roma kukosa malezi stahiki..

Kitendo cha Roma kuoa lakini wakati huo huo kufuatwa na mwanamke mwingine nyumbani hakikuwa kizuti sana katika tamaduni za kitanzania na ndio maana alihuzunika mno.

Upande wa mama Nasra ukweli alijikuta akinyoosha mikono juu mara baada ya kitendo alichofanya Nasra ba kuona mpaka hapo hana cha kufanya tena.

Ni jana tu alichukua hatua ya kumweleza mtoto wake kile alichoambiwa na mganga , lakini licha ya kumweleza mtoto wake alionekana kutoamini kabisa mambo ya waganga na alisema kama hio ndio sababu iliokuwa ikimzuia kutompenda Roma , basi asiendelee kuwa na wasiwasi , kwani alikuwa tayari kumpenda Roma hata kama ilimaanisha yeye kudhurika.

Edna na Sophia mara baada ya kushuka kutoka kwenye gari wote walishangazwa na hali ilivyokuwepo , Nasra mara baada ya kukutanisha macho na bosi wake aliangalia pembeni na kukodolea maji ya bwawa la kuogelea.

Roma mara baaada ya kushuka kwenye gari na kuangalia mazingira alijikuta akijionea aibu yeye mwenyewe , maana wanafamilia wote walikuwepo kasoro tu Lanlan ambaye alikuwa kwa babu yake na hilo alishurkuru , Yezi alikuwepo, Bi Wema alikuwepo , mke wake , Sophia na mama yake wote walikuwa wakimwangalia ni hatua gani angeifanya.

Kwa lugha nyepesi ni kwamba kitendo cha Nasra kufika hapo nyumbani kwake akimsubiria kilileta hali isiokuwa ya kawaida.

Mama Nasra mara baada ya kuona Roma amerudi ilibidi asogee pembeni ili kutoingilia na Roma baada ya kuona mama mkwe kasogea alitembea mpaka aliposimama Nasra.

“Nasra nimerudi kwanin….?”

“Whack!!!”

Kabla hajamaliza kuongea , alijikuta akipewa kibao cha nguvu na Nasra , ijapokuwa Roma alikuwa na uwezo wa kukikwepa lakini alishindwa kufanya hivyo na kuacha kimchape kisawa sawa kwenye uso wake uliopigwa na radi siku chache zilizopita.
 
SEHEMU YA 408

Wanafamilia wote walishangazwa na kibao ambacho mfalme Pluto alipigwa , ni kama hawakutegemea Nasra angeamua kufanya vile , Edna ambaye ndio mwenye mume haikueleweka alikuwa akifikiria nini , Sophia na yeye haikueleweka alikuwa akifkiria nini , alieleweka tu ni Blandina kwani alionekana alikuwa na wasiwasi sana juu ya hali hio ingeishaje bila ya kutoathiri pande zote.

Aliamini hata Roma awe na uwezo wa kumpoza Nasra , lakini vpi kuhusu Edna, alijiambia hata kama ni yeye ambaye yupo kwenye nafasi ya Edna ni lazima angechukia.

“Unajisikia vizuri sasa ..?”

“Whack!!

Aliuliza Roma mara baada ya kulambwa kibao, lakini Hades au mfalme Pluto ukitaka kumuita kwa majina yake ya heshima aliongezewa kingine cha nguvu, ni hakika hata wanajeshi wake wangeshuhudia hali hio wangemdharau sana mfalme wao au huenda wangempiga Nasra risasi palepale kumlindia heshima mfalme wao.

Maumivu alioyasikia Roma sio kutokana na kibao hicho , lakini ni kile ambacho alikuwa akipitia Nasra, kwa mara ya kwanza ndio anashuhudia Nasra akiwa ni mwenye hasira namna hio na kuonekana kama mtu mwiingine kabisa.

“Naamini hivyo vinakutosha kwa maumivu ulionisababishia?”Aliongea Nasra huku machozi yakianza kumtoka.

“Maumivu gani niliokusabishia , kwanini umekuja nyumbani kwangu na kukaa nje kwenye mvua na kusababisha watu kujawa na wasiwasi?”Aliuiza Roma akiwa siriasi kidogo , ukweli hakuelewa ni kipi kilichomkuta mwanamke huyo mpaka kuchuku maamuzi magumu.

“Acha kujifanyisha hujui, Baada ya kuona mama yangu anakuwekea ngumu ukaamua kukata tamaa na mimi na sio kukata tamaa tu ukakosa ujasiri wa kunambia ana kwa ana kama hunitaki tena na kukimbia nchi , unajua nilichojisikia kwa siku zote nilizokuwa nikikutafuta , unajua nilijisikiaje nilivyotaka kuongea na wewe na ukanipita kama vile mtu back sana kwako?”

“Unamaanisha nini Nasra , nani kasema nimekuacha? Umekosea sijawahi kufikiria kukuacha kwenye Maisha yangu ”Aliongea Roma kwa mshangao mpaka hapo ni kama alikuwa sasa akipata picha, lakini kauli yake ya kwamba hawezi kumuacha Nasra kwenye Maisha yake ni kama ilikuwa ikijirudia tudia kwenye masikio ya Edna kwa sababu Roma aliongea kwa sauti ambayo ilimsababisha mpaka yeye kusikia.

“Roma acha kujitetea , nimekuja hapa nataka uniambie moja au mbili , kama hunitaki niendelee na masha yangu , mimi Nasra siwezi kumruhusu mwanaume kuchezea akili yangu na kunichanganya kiasi cha kufanya mambo yangu mengine kukwama”Aliongea kwa hasira

“Najua tokea mwanzo nakukubalia sikuwahi kufikiria kama utanioa na niliridhika na nafasi yangu , lakini kwanini unidharau , kwanini ushindwe hata kunipa taarifa , ni mara ngapi nilipiga? , lakini ukapotezea simu zangu na kuondoka Kwenda Marekani , yote hayo ni kwasabbau tu mama hakutaka tuendelee na mahusiano yetu, unajua ni ndoto ngapi nimezipotezea kwa sababu yako?”

“Najua mimi sio mrembo kama alivyo mkeo , sio Tajiri kama yeye ,najua mimi ni mfanyakazi wa kawaida tu ninaefanya kazi chini yake na familia yangu ni masikini , lakini hali yangu haimaanishi kwamba naweza kuzizuia hisia zangu kumpenda mtu, najua kila mtu ananiona mjinga na mbinafsi kwa kupenda mwanaume ambaye sikupaswa kupenda lakini nifanye nini Nasra mimi nishapenda tayari licha ya kujua siwezi kuwa mtu mwema tena machoni mwa Eda pamoja na familia yake kwa yale walionitendea , lakini yote nimepotezea kwasababu nimependa, unajua ni kiasi gani nilijisikia mara ya kwanza kuingia kwenye mahusiano na wewe?”Alihema huku akifuta machozi kwa mkono na akaendelea.

“Ndio siku niliokuwa na furaha kuliko siku zote , sikujali ulikuwa umeoa , sikujua mkeo ni Edna bosi wangu lakini niliamini nitacheza nafasi yangu hata kama sitopata kile wanawake wengi wanachotamani , sikujali kama nitakuja kuitwa kidudu mtu kwenye ndoa ya mke mwenzangu , lakini niliamua kujitoa muhanga kwasababu nilishakupenda”

“Lakini kwanini kikwazo kidogo tu hiki cha kushinda ukaamua kubadilika na kuniacha mwenyewe , kwanini ukaamua kunipotezea na kuanza kunipotezea ghafla bila sababu”Nasra aliongea kwa sauti na maneno yake yalisikika kwa kila mmoja.

Roma wenyewe alishindwa hata kujua aongee nini kumpoza , kuna muda alijilaumu kwa kujihusisha na wanawake wengi , lakini aifikiria labda ni tokea mwanzo kutokana na yeye asingeweza kuishi bila mwanamke wa kutuliza haja zake, lakini bado swali likaibuka aliwezaje kumjumlisha Neema Luwazo , vipi kuhusu Amina , Vipi kuhusu Rose na Dorisi na hatimae Nasra?

“Nasra sio kama unavyofikiria..”

“Naomba nimalize..”Aliongea huku akimwangalia Roma kwa macho makali

“Roma siku niliokubaliana kuanza mahusiano na wewe nilishaamua kupoteza kila kitu , thamani yangu na utu wangu , nilipoteza ndoto yangu ya siku zote kuwa na familia , lakini kama kwako unaona inafaa na kutaka kuniacha baada ya kujisikia kufanya hivyo kwa kuniona kama mzigo basi kwangu nisawa tu sina jinsi nitakubaliana na wewe kwa kila kitu , lakini mimi sipendi kuchanganywa ni bora ukaniweka wazi nijue kila kitu kuliko kuanza kuniepuka , kaa na mimi kiume na niambie hunipendi na niandelee na Maisha yangu ndio nitajua namna ya kupambana na hali yangu”

“Ushamaliza?”Aliuliza Roma mara baada ya Nasra kumaliza kuongea.

“Nishamaliza maneno yangu yote , sina kingine cha kuongea”Alijibu na Roma palepale alimvuta kwake pasipo kujali watu waliokuwa wakiangalia kinachoendelea na palepale aliingiza mkono kwenye mfuko wake wa sururali na kuibuka na pete ya Almasi alioninua kwa mapesa mengi huko Marekani.

Nasra mwenyewe mara baada ya kuona pete ile kutolewa kwenye kijimkebe chake alipagawa na sio kwake tu hata waliokuwa mbali waliweza kuina kutokana na mng’ao wake.

Wanasema wanawake wanavutiwa sana na vitu vnavyong’aa na hicho ndicho kilichoonekana kwenye macho ya kila mmoja . Edna aliekuwa mbali ijapokuwa alikuwa na vito vingi vya pesa , lakini hakuwa na uwezo wa kutopenda pete iliokuwa kwenye mikono ya Roma.

Nasra alijukta hata zile hasira zikiisha mara moja na macho yake yote yalikuwa kwenye pete iliokuwa kwenye mikono ya Roma.

“Hii ndio sababu sikuweza kupokea simu yako ”Aliongea Roma huku akiweka tabasamu .

Ijapokuwa alichoongea Roma hakikuwa na ukweli lakini hakuwa tayari kuelezea kila kitu , hata hivyo hata aelezee kwamba alipigwa na Radi hakuna ambaye angemuelewa na kitu pekee ambacho angefanya kwa wakati huo ni kumwambia uongo wenye nakshi nakshi ili kumaliza ile hali.

“Unataka kumaanisha nini?”Aliongea huku akimwangalia Roma kwa mshangao.

“Ninachomaanisha ni kwmaba hakuna siku ambayo nilipanga kukuacha , niliondoka Kwenda Marekani mara baada ya Christen kuniambia kuna mnada wa hii pete unafanyika na alivyonitumia picha na kuiona niliona inafaa sana kama zawadi ndio maana nikafanya safari ya dharula pasipo kuaga mtu”Aliongea Roma

“Unasema kweli? Ulienda Marekani kimya kimya kwasababu ulienda kushiriki mnada wa kupata hii pete?”

“Ndio kwanini huniamini , nilisahau simu yangu kwasababu ya haraka na hata nilipokuwa Marekani ni Christen aliepiga simu nyumbani kuwataarifu kama nipo Marekani, kilichotokea leo pale ofisini sio kukuepuka bali nilikuwa na wasiwasi juu ya Edna kuna kitu kibaya kinaweza kumkuta kwasababu alienda mwenyewe kutatua mgogoro wa wafanyakazi na bahati haikuwa kwetu kwani kuna mambo ambayo yalitokea mpaka tukachelewa kurudi “Aliongea Roma huku bado akiwa ameshikilia pete ile mkononi

“Naomba unisamehe , nilikuhisia vibaya , sikutakiwa kukuhukumu hata kwa sekunde , nisamehe”Aliongea huku akiona aibu zilizojaa furaha.

“Usijali ulikuwa na haki ya kuwa na wasiwasi lakini hata hivyo licha ya magumu yote ambayo yanaweza kututokea , hatupaswi kukata tamaa mapema”Aliongea Roma na kumfanya Nasra kutoa machozi ya furaha baada ya kujua sio kweli kwamba ameamuacha, ijapokuwa hakujua pete hio Roma alienda kuinunua kwa ajili ya nani , lakini alionekana kuridhika.

“Mbona huniulizi hii pete ni ya nani?”Aliongea Roma akimwangalia Nasra.

“Najua ni ya mkeo Edna”Alijibu huku akimgeukia Edna aliekuwa akiwaangalia kwa mbali akishindwa kuelewa kile anachosikia kwenye moyo wake , kulia alikuwa akitamani lakini hakuwa na ujasiri wa kutoa machozi kwa kitendo cha mume wake kuwa na mwanamke mwingine mbele ya familia yake.

Roma mara baada ya Nasra kujibu kama pete ile ni ya Edna alimshika mkono Nasra na kisha akaweka pete ile kwenye kiganja cha mkono wake.

“Ijapokuwa naweza nisiwe na haki ya kuingiza pete hii kwenye kidole chako cha pete ya ndoa , lakini sitaki unishuku kwa lolote kwani pete hii ni ya kwako”Aliongea Roma na kumshikisha Nasra pete ile.

Nasra kwenye Maisha yake ijapokuwa ahawahi kuota mara kibao kuolewa na kuwa na furaha , lakini hakuwahi kufikiria kama itatokea siku kupewa pete ya gharama kiasi hicho, ukizingatia na Maisha yake aliokulia , Maisha ya kimasikini alijihakikishia kwamba hakuwa akiota alikuwa na pete hio alikuwa amepewa yeye.

Upande wa Edna licha ya kwamba alitegemea kuona pete ile kupewa Nasra , lakini mara baada ya kuhakikisha mume wake akimpatia Nasra moyo wake ni kama ulichanwa chanwa na kujiona mwanamke sifuri kabisa, ijapokuwa kwake pete haikuwa kitu cha thamanni sana kwake kutokana na pesa alizokuwa nazo , lakini kuona mwanaume anaefahamika kuwa mume wake kumpa mwanamke mwingine pete tena mbele ya mama mkwe na wadogo zake ilimuuma hakika.

Upande wa Roma aliona asiitumbukize pete ile kidoleni ili kumheshimu mke wake ndio maana akamkabidhi Nasra kwenye mkono, lakini licha ya kufikiria hivyo ulikuwa ni sababu ya kimantiki tu ya kujifariji lakini kihisia ilitafsirika kivingine kabisa..

Hata kwa mama yake ijapokuwa alishukuru Nasra amerudi kwenye hali yake ya kawaida lakini kitendo cha Roma mwanae kumkabidhi pete mwanamke mbele ya mke wake ilimfanya moyo wake kuwa katika ubaridi usioelezeka , alijiambia imekuwaje Roma kufanya maamuzi kama yale ya kumpa mwanamke yoyote anaejisikia pete ya thamani mbele ya mke wake na yeye pia.

Sophia na Yezi pia ni kama hawakuamini kama Roma anaweza kufanya maamuzi ya aina ile na waliishia kumuonea huruma Edna na kujiaombia niheri kuwa mchepuko kuliko kuwa katika nafasi ya cheo cha kuitwa mke wa Roma asiejali nini maana ya ndoa.

Upande wa Mama yake Nasra ijapokuwa alikuwa mshamba lakini kitu kile kinachong’aa hakushindwa kutambua kama nni cha thamani.

Mama yake Nasra mara baada ya kumpigia sana simu Nasra ndipo ilipopokelewa na Blandina na kuelezwa kinachoendelea na ni Blandina alietoa funguo ya gari kwa Derick kwa ajili ya kufuatwa ili amsaidie kutuliza hio hali , lakini hata alivyofika hapo nyumbani hakuna ambacho aliweza kufanya kwani Nasra alibakia na msimambo wake uleule na kumfanya kunywea na kukaa nae vilevile kwa huzuni huku akimlaani Roma kwa kila laana , lakini kitendo cha Roma kurudi na kumpa mtoto wake pete mbele ya mke wake na mama yake ilionyesha kwamba Roma alikuwa na mapenzi na mwanae huenda Zaidi ya Edna mwenyewe , hicho ndio alichokifikiria.

“Miss Edna naomba unisamehe , najua familia yako ilifanya juu chini kuhakikisha Nasra anafanikiwa , lakini kama hiki ndio anachopenda na yupo tayari kujitoa kafara kwa ajili ya furaha yake , sipo kwenye nafasi ya kumzuia tena Zaidi ya kumsapoti kama mama”Aliwaza Mama Nasra huku akimwangalia mtoto wake aliekuwa kwenye hali ya furaha.

Nasra alikuwa na furaha kiasi kwamba alisahau kama alikuwa amezungukwa na watu, macho yake yote yalikuwa kwenye pete nzuri ya Dhahabu ilionunuliwa kwa mapesa mengi.

“Umeipenda?”Aliuliza Roma.

“Sana Roma , asante sana..”Aliongea huku akishindwa kuzuia machozi.

“Otea nimelipia kiasi gani kuinunua?”

“Nitajuaje sasa , kwani wewe ndio umelipia?”

“Nimeinunua bilioni ishirini na saba za Kitanzania sawa sawa na Dollar milioni kumi na tatu za kimarekani”Aliongea Roma na kumfanya Nasra kutetemeka kwa mshituko , ijapokuwa alijua pete hio inathamani kubwa lakini kitu cha mabilioni ya pesa kilikuwa cha thamani kubwa kwake mno .

“Unataka kunitoa uchizi , kwanini umenipa kitu cha thamani kiasi hiki?”

“Ukilinganisha na ninavyokupenda , kwangu hicho ni thamani ndogo sana”Aliongea Roma huku akiweka tabasamu lake la siku zote la mauaji kwa wanawake.

Mpaka hapo Roma alionekana kufanya kazi kubwa ya kumlainisha mrembo huyo lakini asichokijua ni kwamba alikuwa ameanzisha kitu kingine.

Edna mara baada ya kuona mlolongo huo wa matukio , alijikuta akijisemea kwamba inatosha sasa, aliondoka kwa kukimbia na kuingia ndani , huku kila mmoja akimwangalia na ndani ya dakika chache to alitoka akiwa na ufunguo wa gari nyingine na kukimbilia mpaka gereji na kutoka na gari ya Rolly Royce na kuondoka.

“Roma hata kama ulitaka kumtuliza Nasra , kwanini ufanye hivyo mbele ya mkeo”Aliongea kwa huzuni Blandina huku machozi akitamani yamtoke mara baada ya kumuona namna Edna alivyoondoka hapo ndani.

Nasra ambaye alikuwa kwenye mshituko baada ya Edna kuondoka , alijikuta akiona aibu kwa kilichotokea.

“Mama huna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu mimi , kuna baadhi ya vitu hata kama nisingevifanya sasa hivi ningevifanya baadae , lazima ieleweke siwezi kumaucha Nasra , Alichoweza kushuhudia Edna leo hii ilikuwa ni jambo la lazima ili kumuandaa”

“Mr Roma samahani , lakini unadhani baada ya kufanya hivi kila kitu kitakuwa sawa?”Aliuliza kwa upole Mama Nasra , ukweli hata yeye alikuwa na mawazo ya kibinafsi Kwenda kwa mwanae , lakini aliamini Edna aliumia kwa kitendo alichoafanya Roma.

“Najua Maisha yetu hayawezi kuwa mazuri muda wote lakini ninachoweza kukuahidi nitajitahidi kwa uwezo wangu wote kumfanya Nasra kuwa na furaha”Aliongea Roma , lakini palepale na Sophia aliekuwa amesimama muda wote akishindwa kujua afanyeje aliingia kwenye gari walilokuja nalo na kuondoka na kuacha macho yaliosindikiza gari hio ikipotelea nje kwenye geti.

“Unafikiri unachosema kinawezekana , najua naonekana kama mwanamke mshamba kuliko wote hapa , lakini ninachoamini huwezi kumfanya Nasra kuwa na furaha ilihali mke wako kaondoka hapa akiwa amekasirika , kadri utakavyofikria kumfurahisha Nasra ndio utakavyozidi kuibua matatizo sio kwa mkeo tu lakini kwa watu wanaokuzunguka”Aliongea mara baada ya gari ya Sophia kutokomea

“Mama kama nitamuacha Roma siwezi tena kuishi”Aliongea Nasra na palapale alilegea na kupoteza fahamu na bahati nzuri Roma aliweza kumdaka kabla hajatua chini.

Unahisi alichokifanya Roma ni sahihi, Edna achukue maamuzi gani toa maoni.

ITAENDELEA

MAWASILIANO WATSAPP 0687151346 KWA ANAEHITAJI MWENDELEZO
 
Daaaaah aiseee mkuu weee ni hatareee moyo wa kuotea mbali sijawahi kuona 🔥🔥🔥🔥huo burudani ni noma
 
Hii drama ya nasra inasisimua. Mwandishi kuna sehemu unatakiwa kuonyesha Roma akitaabika kwa huu upuuzi wake kwa wanawake. Seriously.
 
Umetisha sana mkuu singanojr

Sent from my Pixel 3 using JamiiForums mobile app
Huyu mwamba Singano pale WhatsApp anaishi kwa dharau ni bora nyie mnaisoma hii simulizi hapa jf.

Hana nidhamu na ahadi zake, mtu akikulipa mpe anachostahili, vingine negligence ndio inapodhirika na Kwa sabab wajuba wameamua kukaa kimya mwandish afanye anavyotaka, apost anavyopenda.
 
Pete
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…