SEHEMU 420.
Wazee wale wa kichina hali zao za kiafya zilikuja kutengemaa muda wa usiku baada ya kupumzika kwa muda mrefu.
Upande wa Roma na Magdalena walitumia nafasi ya mchana wote kutembelea maeneo mengi ambayo alikuwa akifanyia mafunzo, Magdalena alionekana kuwa na furaha kweli kuliko siku zote ,kitendo cha kuwa karibu na Roma siku nzima wakiongea na kucheka pamoja kwake ilikuwa ni kama ndoto ambayo hakutaka iishe.
Tokea siku ambayo Roma aliweza kumuokoa Magdalena kutoka kukatwa na panga la Lilith wakati wa kugombania kwa Holygrail ndio mapenzi yake kwa mwanaume huyo yalipoanzia.
Familia yake ilikuwa ikijaribu kumfanyia mchakato wa kuoelewa na Jumbe lakini hakuwa akimpenda kabisa , ijapokuwa Jumbe hakuwa na kasoro kama mwanaume lakini hisia zake kwake zilikuwa mbali na hakuwa akihitaji mwanaume wa aina ya Jumbe , alihitaji mwanaume mwenye nguvu na uwezo kama Roma Ramoni.
Lakini hata hivyo mrembo huyu alikuwa vyema zaidi katika kuficha hisia zake , ni kweli kwamba alikuwa akimpenda Roma lakini kutokana na kwamba Roma alikuwa mume wa rafiki yake wa utotoni , lakini pia mpenzi wa pacha mwenzake aliishia kutotaka kuchukua hatua ya ziada juu ya hisia zake , alijiambia ni kheri kubakia na hisia zake ndani ya moyo wake kuliko kuziweka hadharani kwani isingekuwa na maana yoyote.
Upande wa Roma kwakua alikuwa na uzoefu mkubwa sana na maswala yanayohusiana na wanawake , aliweza kugundua Magdalena kuonekana kuwa na hisia nae za kimapenzi lakini hakutaka kabisa kugusia habari hizo , aliamini zingemletea matatizo makubwa mno sio kwa Mage tu lakini pia kwa mke wake Edna.
Muda wa usiku wakiwa wameketi kwenye miti ya Mianzi waliweza kufuatwa na Tang Luyi ambaye ni Master wake Magdalena.
“Naona wenyewe mmekaa ki wapenzi wapenzi”Aliongea Tang Luyi huku akiwa na sura isioelezeka kama alikuwa na furaha au na huzun huku kauli yake ikimfanya Magdalena kuwa na aibu.
“Mbona unaonekana kukasirika kwani tukiwa wapenzi ni jambo baya?”Aliongea Roma bila ya kumzingatia sana lakini kauli yake ilionekana kuwa kejeli kwa Tang Luyi ukizingatia pia siku zote alikuwa ni mwenye kujiamini na uwezo wake.
“Kwasababu umeweza kutuokoa leo , ninakukaribisha kwenye jamii yetu kwa ukalimu”
“Magdalena naona Master wako akili zake zimekaa sawa mara baada ya akili yake kuachiwa huru”Aliongea Roma kwa namna ya kumkejeli Tang Luyi.
“Nyamaza..!”Aliongea huku akionekana kukasirika , hakutaka hata kusikia kama siku zote za kujiona yupo juu kimapigano kuweza kutawaliwa akili yake kizembe na alichoongea Roma ilikuwa ni kama kutonesha kidonda.
“Roma usimtanie hivyo , ni Master wangu na namheshimu sana lakini pia ni mkubwa kwetu’Aliongea Magdalena a kisha akamgeukia Master wake.
“Master naamini kuna jambo limekuleta mpaka kuja kututafuta huku”Aliongea lakini Tang Luyi alimwangalia Magdalena kwa kumchunguza.
“Vipi maendeleao yako huko Tanzania tokea urudi?”Aliongea na kumfanya Magdalena hisia kumjaa hakuamini Master wake angemjali na kumuuliza swali hilo.
“Asante sana kwa kuuliza Master, Maisha yangu yanaendelea vyema nilikumiss sana”Aliongea kwa sauti ndogo.
“Kama ulinimisi kwanini hukurudi hata kwa zaidi ya mwaka tokea uondoke?”Aliuliza na Magdalena alionekana kukosa jibu la kutoa lakini hata hivyo Tang Luyi alipotezea na kumwangalia Roma.
“Mr Roma najua sasa unao uwezo mkubwa kuliko mtu yoyote ndani ya jamii yetu lakini licha ya hivyo siwezi kukuacha ukamfanya Magdalena kitu kibaya , nilimlea mwenyewe tokea alivyoletwa hapa na sasa amekuwa mtu mzima kwangu nilikuwa namchukulia kama mtoto wangu, wakati alipokuwa hapa sikutaka kabisa ajihusishe na maswala ya mapenzi kutokana na kwamba sikutaka apitie maisha niliopitia mimi mwenyewe”Aliongea na kumfanya Roma kushangazwa na maneno ya Master wake Magdalena hakudhania kama angeweza kuongea hivyo.
“Hivi naonekana mimi na Magdalena ni wapenzi?”Aliuliza Roma na kumfanya Tang Luyi kutabasamu kwa kejeli.
“Nimemlea Magdalena mwenyewe kwa anavyokuangalia tu naona kabisa umemchanganya huyu mtoto ndio hofu yangu ilipo”Aliongea nakumfanya Magdalena atamani kujichimbia kwani siri zake zilikuwa zikifichuka.
“Master siohivyo…”
“Nadhani umekuja kwa ajili ya kutuita kwenye chakula nina njaa sana nadhani litakuwa jambo zuri tukiacha kuongea na kuelekea huko”Aliongea Roma akimkatiza Magdalena na Tang Luyi hakuongea zaidi ya kugeuka na wote kwa pamoja wakafuatishana mpaka kwenye nyumba nyingine kabisa ambayo ni ya Tang Dianshan.
Roma mara baada ya kuingia tu ndani aliweza kufurahishwa na harufu nzuri ya vyakula, wazee wote walionekana wapo ndani ya nyumba hio
Hakukua na viti hivyo mara baada ya Roma kuingia alijitafutia nafasi ya kukaa chini kwenye mkeka huku akiangalia mapande ya nyama ya kuku pamoja na ya kitimoto.
Wachina na Korea ndio moja ya mataifa ambayo wanaongoza kula nyama ya nguruwe ni mara chache sana ukawakuta wanakula nyama ya ng’ombe ni kheri kwao kula nyama ya mbwa kuliko ya ng’ombe.
Basi chakula pale kiliandaliwa na wote kwa pamoja walianza kula huku maongezi yakiendelea, Wazee hao walikuwa wakimhusudu Roma kweli kwani wao walikuwa wamejifunza mbinu za kijini kwa muda mrefu pasipo hata ya kufanikiwa kufikisha levo ya Nafsi , lakini ajabu kwa kijana mdogo kama Roma alikuwa amekwisha kufikisha levo za juu kabisa za mafunzo hayo , lilikuwa jambo ambalo sio la kawaida kabisa kwao na ndio maana walijaribu kumdadisi.
“Wapishi wenu ni wataalamu kweli, Wameweka na baadhi ya dawa za kimitshamba nini, nahisi harufu flani ya kuvutia ya miti kwenye hizi nyama”Aliongea Roma huku akilamba vidole..
“Ni vizuri sana kama umependa mapishi yetu , kwetu sisi ni utamadunni kila linapokuja swala la mapishi tunajali sana faida za chakula kwenye mwili tofauti na utamu wake , wapishi wetu kila siku wanafanya utafiti wa mimea ambayo inafaida mwilini na inayoweza kutumika kwenye vyakula mbalimbali”Aliongea Tang Dianshan na Roma alitingisha kichwa kwa namna ya kuelewa hata hivyo alikuwa akielewa tamaduni za China na baadhi ya maeneo yake ya karibu kuanzia Japani , Korea , Thailland , Ufilipino na China yenyewe, ni rahisi sana kukuta nchi za Ulaya watu kushindia vyakula vya supermarket lakini kwenye mataifa haya ya Asia wengi wanapenda kupika sana na vyakula vyao vinazingatia uwiano sawia wa mahitaji ya mwili na ndio maana vifo vingi ndani ya China kiasilia kabisa ni vya wazee kuanzia miaka themanini kuendelea , ni rahisi kusema kwamba China ni mojawapo ya taifa ambalo watu wake wanaishi miaka mingi sana na wana afya nzuri.
“Vipi kuhusu Pango la Scrolls?”Aliuliza Roma.
“Huh!”
“Mbona mnaonekana kama mnapango wa kunikatilia tena?”
“Hapana hatuwezi kukatalia ,ijapokuwa tunazo sheria lakini kwa ulivyoweza kutusaidia leo tutakuruhusu , hata hvyo unaonakana kutokuwa mtu mwenye tamaa sana”
“Kama ni hivyo mnielekeze lipo upande upi?”
“Ni chini ya mlima upande wa pili wa ngome hii , sio rahisi kufika kwani kuna mitego mingi lakini pia kuna watu ambao wanalinda eneo hilo kama mitego ikishindwa kufanya kazi, kama unataka kwenda huko siku ya kesho basi tutaweza kuondoa vizuizi ili uweze kuingia kwa urahisi”Alijibu Tang Luyi na Roma alionekana kuridhishwa na jibu hilo , mpaka hapo alishafanikiwa kile kilichomleta.
“Mr Roma tunaweza kujua yupo levo gani yule mtu alieweza kuingia hapa na kutawala akili zetu?”Aliuliza Tang Dianshan.
“Sina uhakika yupo kwenye levo ipi , ila ninaweza kukisia yupo mwishoni mwa levo ya Nafsi na inaonekana ameweza kufanya baadhi ya vitu kwa kutumia Dhana, ila kwasasa haina haja ya kuhofia naamini hawezi kurudi tena hapa kwani shida yake ilikuwa ni mimi na mbinu yangu ya Maandiko ya Urejesho”Aliongea Roma na kufanya wazee wote kuwa kimya huku wakiangaliana kwa kiulizo.
“Kimantiki ninaweza kusema kwamba licha ya kwamba siwajui sana Hongmeng lakini kwa uchache ninaofahamu wasingeweza kufanya kitu kama kile , kwani anaonekana njaa yake ni kutafuta mbinu ambayo itamuwezesha kupanda levo ya juu zaidi, nahisi ni jini kutoka jamii nyingine kabisa”Aliongea Roma.
“Haiwezekani”Alijibu Tang Luyi na kumfanya Roma kushangaa.
“Kwanini… kuna mtu mnamdhania?”
“Tumeamua kutokwenda moja kwa moja kwenye hitimisho kutokana na mkanganyiko, Mr Roma wewe una nguvu kubwa sana za mafunzo ya kijini na ni sahihi huko mbeleni kukutana na watu wengi maadui kutoka sehemu tofauti tofauti , labda kwa kukupatia taarifa tu ukiachana na Hongmeng kuna jamii nyingine kabisa ya Majini yenye nguvu”Aliongea Tang Luyi na kumfanya Roma kushangaa.
“Unamaanisha kuna jamii nyingine tofauti na Hongmeng ambayo inatumia mbinu za nishati ya Mbingu na Ardhi?”
“Ndio hio ni jamii ambayo haijulikani sana kutokana na kutokuwa na mwingiliano wowote na China, ijapokuwa hata sisi wenyewe hatujawahi kufika huko Hiongmeng na kujua namna wanavyoishi lakini habari za uwepo wa jamii nyingine yenye nguvu ipo na haina mfungamano wa aina yoyote na taifa hili”Aliongea Tang Luyi.
“Kama haina mfungamano na China inamaanisha kwamba ipo nje ya mipaka ya China au vipi?”
“Hatuwezi kufahamu sana kwani jamii hio imekuwa ni ya siri sana na ni mara chache sana kujionyesha hadharani kama majini lakini jambo moja ambalo tunajua hawafungamani na tamaduni zozote za kichina na wanafanya mambo yao kwa kuzingatia tamaduni zote za ulimwengu , ni rahisi kwenye jamii hizo kukuta majini yenye mwonekano wa rangi ya ngozi nyeusi au kuwa na mwonekano wa kizungu kabisa , inasemekana ni jamii iliostaarabika zaidi kuliko hata Hiongmeng” Roma na Magdalena wote walijikuta wakishangaa kwani habari hio ilikuwa mpya kwao.
“Kuna habari nimeweza kusikia kuhusu jamii inayoitwa Pansas ambayo ndio chimbuko ya mbinu yangu hii ya Kimaandiko ya urejesho?”
“Kuhusu Pansas ni jamii ambayo mpaka sasa inasemekana ipo kwenye habari za kihistoria tu na ni kweli kabisa mbinu ya kimaandiko chimbuko lake ni Pansas hata hivyo hatuna taarifa ya kutosha juu ya hilo”Aliongea.
Katika maongezi hayo Roma alijikuta akikumbuka mwanamke aliekutana nae kule Marekani aliefahamika kwa jina la Rufi , alikummbuka mwanamke yule alitaja Hongmeng lakini wakati huo huo akataja wazee waliofahamika kwa jina la Luo ambapo alidai walikuwa wakimtafuta sasa alijiuliza mwenyewe je mwanamke yule alikuwa ni sehemu ya majini kutoka huko.
“Jina la jamii hio linaitwaje?”Aliuliza .
‘Wanajiita kwa lugha yao , lakini mara nyingi walisikika wakijiita kwa neno la Daiva”Aliongea Tang Dianshan na kumfanya Roma kutoa macho.
“Kwa ninavyojua Daiva ni sawa na kusema Daeva yaani viumbe wasiokuwa wa kawaida na neno hili limepatikana kwenye kitabu cha dini ya Zoloastrian kifahamikao kwa jina la Avestas , dini ya Persia ya kale ambapo mpaka leo kuna washirika wake duniani wanaoamini mungu wao ni Ahura Mazda”Aliongea Roma.
“Unaonekana upo na habari nyingi Mr Roma , unachosema ni kweli lakini hizo ni habari za miaka mingi iliopita , jamii hii kama nilivyosema haingiliani kabisa na maswala ya kidunia na kuna uwezekano hata kuibuka kwa Zoloastrian ilikuwa ni sababu yao”Aliongea Tang Luyi na Roma aliona asirefushe maelezo hayo , alijiambia atafuatilia zaidi na zaidi kwa watu wazoefu.
Lakini hisia mbaya juu ya yule mwanamke zilikuwa zikimtekenya ,kitendo cha kuwa na sumu mwilini iliokuwa imewekwa kijini kilimchanganya.
“Kwahio wenyewe mafunzo yao yanakuwaje?”
“Kwa tunavyojua mara nyingi wakifikisha levo ya kuweza kujitengenezea maumbo ,yaani levo ya Nafsi wanatoka kwenye ulimwengu wao na kuja katika ulimwengu wa kawaida huu wa kwetu kwa mafunzo ya levo nyingine ambayo wenyewe wanaiita kuhuisha miili yao na mapepo yanayowatawala akili zao na wakishafanikisha hilo ndio wanarudi tena kwenye miliki yao wakiwa wapya kiroho ,hawana habari kabisa na dunia kwani malengo yao makuu ni kufikia viwango vya juu kabisa ambavyo mababu zao walishawahi kufikia”Aliongea Tang Dianshan
“Kwahio kwa tamaa zao za kufikia levo za juu tunaweza kukisia kwamba wanaotafuta mbinu yangu ni wao?”
“Hilo haliwezekani huenda kuna kitu zaidi wanachokitafuta hata hivyo inawezekana kuna mtu binafsi ambaye anatafuta mbinu yako”Aliongea na wote walionekan kukubaliana na swala hilo na kuona huenda linawezekana.
Katika mazungumzo hayo Roma aliweza kunasa kitu kimoja , kama maneno yao yalikuwa sahihi basi aliamini huenda kuna watu ambao wapo levo kubwa kuliko yeye au wapo levo sawa na yeye alijikuta akipata tamaa ya kupanda levo zaidi na zaidi.
Siku iliofuata Roma aliweza kuingia kwenye pango la hifadhi ya kumbukumbu , lilikuwa ni pango lakini ndani yake lilionekana kama handaki ambalo lilikuwa limejengwa vyema na ilionekana ni sehemu ambayo ilikuwa ikitunzwa kwani haikuwa na uchafu mwingi.
Roma aliweza kupita kwa walinzi hao wa kichina bila ya tatizo lolote kwani taarifa zake zilikuwa zimekwisha kutolewa na sheria moja tu aliopewa asitoke na kitu chochote, yaani anaruhusiwa kusoma tu lakini sio kubeba hivyo alipewa muda wa siku tatu zote lakini ajabu Roma alitumia siku moja tu nzima kukaa ndani ya pango hilo kusoma na usiku akarudi akipokelewa na Magdalena ambaye alionekana kumsubiri.
“Umefanikiwa , nilidhani utachukua siku mbili”Aliongea Magdalena.
“Kama ulijua nitachukua siku mbili mbona unaonekana kama ulikuwa ukinisubiria?”Aliuliza Roma huku akiweka tabasamu.
“Hakuna ni wasiwasi tu , nimekuja ne wewe China chochote kibaya kikikupata unafikiri nitamwambia nini mkeo na Mage”Aliongea .
“Kwahio wasiwasi wako ni juu ya Mage na mke wangu na sio kwako mwenyewe?”
“Ndio , vipi lakini umefanikiwa?”
“Naweza kusema hivyo nimepata baadhi ya vitu muhimu”
“Una mpango wa kuanzisha mbinu yako mwenyewe tofauti na zilizopo za mafunzo ya kijini?”
“Unaweza kusema hivyo , najua hakuna ambaye ashawahi kuthubutu kuanzisha mbinu rahisi na hiki ndio ninachofanya”Waliongea huku wakitembea na walipofika sehemu ya mianzi sehemu ile ile ya jana yake walikaa chini.
Roma alipotoa simu yake aliweza kuona ‘Missed call’ kutoka Tanzania na alipangalia jina ni Omari , alishangaa na kujiuliza ni kipi ambacho anataka kumwambia mpaka kuchukua hatu ya kumpigia akiwa nje ya nchi.
Roma ilibidi yeye mwenyewe kwanza amtafute kwa kumpigia simu na shukrani kwa laini yake ya simu ilikuwa imewezeshwa kupata mtandao ndani ya nchi yoyote.
“Hades bora umenipigia”Ilisikika sauti upande wa pili ambayo ni ya Omari.
“Kuna shida gani?”
“Kuna uchunguzi nimekamilisha na taarifa niliona sio mbaya kama nitakupatia”Aliongea Omari na kumfanya Roma kuguna kidogo.
“Taarifa gani hizo?”
“Kabla sijaendelea nataka kujua kutoka kwako ni adhabu gani ambayo ulimpatia mke wa raisi wa Rwanda Madam Kizwe?”Aliongea na kumfanya Roma kufikiria kidogo.
“Unataka kusema nini?”Aliuliza Roma huku akijiambia huyu mpuuzi kajuaje alikuwa na bifu na Kizwe.
“Nadhani hata wewe unafahamu vyema juu ya kifo cha Mke wa raisi wa Rwanda , sasa habari ambayo nipo nayo mpaka sasa ni kwamba Madam Kizwe yupo hai”Aliongea Omari kwa sauti ya chini lakini iliosokika vyema kwenye sikio la Roma.
“Kizwe yupo hai , linawezekana vipi hilo?”
“Hapo hata mimi mwenyewe nilishangaa lakini taarifa nilionayo kwanza kabisa ni ya uhakika na mzee wangu pia kaithibirisha lakini jambo la kushangaza ni kwamba Kizwe alikufa kweli”
“Kama alikufa kwahio unamaannisha alifufuka au?”
“Ndio ninachotoka kukuuliza wewe je unaamini uwezekano huo upo maana mimi mwenyewe mpaka sasa nahisi akili yangu haifanyi kazi vizuri, kwasababu taarifa nyeti nliopata hapa aliehusika na kurudisha uhai wa Kizwe ni Yan Buwen na hilo liliwezekana mara baada ya mwili wake halisi kubadilishwa ndani ya ikulu na inaonekana moja kwa moja Raisi Kigombola anahusika katika hili”
“Kwaho unachotaka kusema ni kwamba mwili uliozikwa sio wa Kizwe bali mwili wake ulichukuliwa na Yan Buwen na kisha kurudishwa hai?”
“Hio ndio pointi yangu ya msingi”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu kifedhuli mpaka hapo kuna hisia zishaanza kumcheza alijiambia kama kweli maneno hayo yatakuwa sahihi basi hata tukio la Salah aliemuua yeye menyewe kwa mikono yake na kisha kufufuka na kwenda kushambulia kwenye familia yake kazi yote hio itakuwa imepangwa na Yan Buwen na kazi ya Ressurection fluid imetumika.
“Hades ninachokuambia ni sahihi kabisa , shushu alieko ndani ya ikulu ya Rwanda alituelezea kwamba mwanaume anaefahamika kwa jina maarufu la Lekcha alipelekwa Rwanda pamoja na Kizwe mara baada ya kutolewa Tanzania na siku ya jana katangazwa kama profesa mpya wa chuo kikuu cha Rwanda upande Fizikia”
Roma baada ya kusikia jina hilo akili yake ilimkubuka mwanaume ambaye alikutana nae Club B , kwa haraka haraka alijiambia huyo ndio atakuwa ndio anaezungumziwa lakini sasa alishangaaa kusikia kwamba amepewa nafasi ya kuwa Profesa.
“Kuna taarifa nyingine muhimu zaidi ambayo unahitaji niifahamu?”
“Ndio ukiachana na jibu ninalotaka kutoka kwako lakini pia nimegundua Yan Buwen ana ushirika wa karibu na Denisi Senga pamoja na Desmond Jeremy”Aliongea na kumfanya sasa Roma kuelewa kwanini siku ile aliweza kumuona Desmond akiwa Tanzania.
“Roma nahitaji huyu Yan Buwen kuondoka kwenye taifa la Tanzania mara moja lakini kuna nguvu kubwa ambayo inamlinda mpaka sasa nimejaribu kuongea na baba na ameniambia niachane na maswala yanayohusiana nae kabisa , jambo ambalo hata sijaliafiki na napanga kuendeleza”
“Mbona unaongea kama swala hili limekugusa sana?”Aliongea ni kweli Omari alionekana kuwa na hasira mno kwa namna anavyoongea.
“Huyu mpuuzi ameharibu maisha ya Queen mpaka sasa , kampa ujauzito na kaukataa na Queen ni kama kachanganyikiwa , halafu ndio mwanamke wa ndoto zangu unafikiri kwanin nisiwe na hasira nae”Aliongea na kumfanya Roma kuguna.
“Basi shukrani zimwendeee Yan Buwen kwa kumkataa Queen kwani na wewe utaweza kupata nafasi”Aliongea Roma huku akitamani kucheka maana alijua ni utani wa kuumiza.
“Hades najua mimi na wewe hatulingani na unapendwa sana na wanawake , lakini mimi ni tofauti sitaki wanawake namtaka Queen wangu mambo yaishe”
“Kwahio unachotaka nikusaidie ni nini?”
“Hili sio swala ambalo unapaswa kunisaidia ila ninachojua ni swala ambalo moja kwa moja linaweza kukuletea matatizo lazima tumchukulie siriasi Yan Buwen”
“Unaonekana kumuogopa sana huyu Yan Buwen , nikukumbushe tu yeye ni mwanasayansi tu na hawezi kunifanya chochote na siku akijichanganya ndio mwisho wake”
“Sidhani kama itakuwa rahisi kama unavyoongea jana niliweza kukutana na Denisi ambaye ni mdogo wako anaonekana kuwa wa tofauti sana”
“Unamaanisha nini kuwa wa tofauti?”
“Kwa taarifa nilizokuwa nazo sijawahi kusikia kwamba ashawahi kujifunza mafunzo yoyote ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi”
“Unachoongea ni sahihi mara ya mwisho nilimuona akiwa na nguvu za ziada lakini zinazosababishwa na kirusi cha Wolverine na niliweza kumponyesha lakini sio hivyo tu mwili wake niliuwekea mtego kiasi kwamba hakuna sayansi ambayo ingefanya kazi”
“Kama ni hivyo kwanini amebadilika na sasa hivi kuwa na levo ya juu ya mafunzo ya kijini?”
“Unamaanisha nini kuwa na mafunzo ya juu ya kijini?”
“Denisi nilikutana nae na anaonekana kuwa kwenye levo ya Nafsi ya mafunzo ya kijini”Aliongea Omari na kumfanya Roma kuona swala hilo haliwezekani hata kama Denisi anaweza kujifunza mbinu hizo si ndani ya muda mfupi huo.
“Una uhakika yupo kwenye levo ya Nafsi?”
“Kwanini nishindwe kujua mtu ambaye yupo kwenye levo sawa na yangu , akili yangu inanielezea huenda kuna kitu amefanyiwa kwenye mwili wake, na hisia zangu zinanielezea kabisa atakuwa Yan Buwen , nikijaribu kuunganisha matukio nahisi hata kilichotokea juu ya meli ya Marekani huenda Yan Buwen akawa mhusika , kama mtu ameweza kufufua mtu, na kuweza kumtengenezea Denisi nguvu za kijini ndani ya muda mfupi anashindwaje kutengeneza kopi yako?”Aliongea Omari na kumfanya Roma kufikiria.
Roma alijiambbia kama ni kweli labda Yan Buwen kuwa na umiliki wa Godstone ndio itakuwa mantiki ya kusema ni rahisi kuweza kufanikisha jambo la kutengeneza kopi yake, lakini akili yake bado haikuwa ikikubaliana na jambo moja , alichokuwa akijua jiwe la kimungu ni moja tu na mtu aliempokonya licha ya kutokuwa na uhakika alijua kabisa atakuwa ni Athena.
“Au kuna zaidi ya jiwe moja kama Christen alivyosema?”Alijiuliza Roma , ilikuwa ni ngumu kwake kuamini kama Athena anaweza kushirikiana na Yan Buwen halafu watengeneze kopi yake na kisha wapange njama ya kwenda kushambulia meli ya kivita na kisha kumsukumia makosa yeye , ilikuwa ni jambo gumu sana kwake kuamini kwani ilimaanisha Athena ndio amekiuka The Gods treaty na hata kama afanye hivyo ni kwa makusudi yapi?.
Sasa Roma asichokijua ni kwamba si kweli kwamba Omari alifanikisha kutafuta ukweli kwa shushu wala nini , na sio kweli kwamba alikuwa amekamilisha uchunguzi akiwa peke yake.
Lakini muda huo ambao alikuwa akiongea na simu alikuwa ndani ya hoteli moja ndani ya mji wa Bagamoyo akiwa kwenye chumba cha mikutano huku meza ikiwa imezungukwa na sura zaidi ya saba na maongezi simu yalikuwa yakisiikika kwa sauti , kwani simu ilikuwa kwenye mfumo wa Loudspeaker.
“Ni muda wa kumfanya kuchukulia hili kuwa siriasi”Ilisikika sauti mara baada ya Omari kukata simu.
“Shekhe unamaanisha nini?”Aliuliza Nadia Alfonso.
“Mpango wa pili wa kuongezeka umefanikiwa kwa asilimia zaidi ya sabini na mpaka sasa tuna wajumbe wengi kwa kila taifa, hilo ni la kwanza lakini ninayo habari mbaya na nzuri kwa wakati mmoja nikianza na habari mbaya ni kwamba Athena kafanikiwa kupiga hatua moja mbele kwa kuweza kudhibiti Umoja wa mataifa ya Dunnia(UN), habari nzuri kwetu ni kwamba moja ya mwanachama mkongwe mwenye nguvu ndani ya Illuminat ameamua kutuunga mkono”Aliongea Shekhe Idrissa na sura zote zilizokuwa kwenye meza hizo zilimwangalia kwa mshangao.
“Tunaweza kumfahamu”
“Kwasasa hatuwezi kumfahamu kwani sio kama ni mwanachama mtiifu kwetu bali yupo katikati , labda niwaambie tu licha ya kuwa mwenzetu lakini pia ni mwanachama mkubwa wa juu wa Freemason”
“Mheshimiwa huyo si atakuwa hatari kwetu?”
‘Hata mimi nilifikiria hivyo na wajumbe wengine walifikiria hivyo lakini yeye, hana mpango na kile tunachokifanya anachotaka ni uwiano wa nguvu katika dunia hii , najua anapigania maslahi ya taifa lake lakini ili tuweze kufanikiwa lazima tuweze kula nae sahani moja , kwasasa udhibiti wetu ndani ya bara la Ulaya ni nusu kwa nusu , Amerika ni asilimia ishirini tu , Mataifa ya kiarabu ndio tumepiga hatua na Afrika tunaendelea licha ya changamoto nyingi lakini hata hivyo kumtumia huyu bwana kuongeza nguvu yetu ni hatua nzuri”
“Shekhe kwahio mpango wa tatu ni upi?”
“Mpango unaofuatia ni kumfanya Hades kuchukulia haya maswala kwa uzito wake na Agent Omari hio ndio itakuwa kazi yako kwanzia sasa unahitajika kumfanya aone kile kinachoendelea huku sisi tukiendeleza wajibu wetu”Aliongea Shekhe na wajumbe walionekana kunyamaza.
“Shekhe nipo tayari kwa kazi hio , mpaka sasa nimeweza kumfanya Roma kuwa rafiki yangu na ndio kazi niliopewa mara baada ya kufanikiwa kutoka Hongmeng”
“Hilo halina shaka , lakini tunahitaji zaidi ya urafiki , tunahitaji aanze kuchukua hatua mapema na mtu wa kwanza kumpunguza nguvu ni huyu Yan Buwen”Aliongea na kumfanya Omari kutikisa kichwa na kuelewa.
“Linda umefanya kazi nzuri , kwasasa haina haja ya Jeremy kujua mke wake yupo hai , mtu wa kuwa nae makini zaidi ni mtoto wake Desmond hatutaki kuona anafanya jambo lolote kwa baba yake wala kushawishi serikali ya Rwanda kumuunga mkono , kwasasa wote tunajua ana kisasi na baba yake baada ya kufahamu Edna ni dada yake na hilo naamini kwa kuungana na mama yake ni lazima watalifanikisha”Aliongea na Linda alionekana kuelewa na aliitikia kwamba anajua ni kipi akifanye.
Naam watu waliokuwepo hapo ndani alikuwa ni Mellisa ,Phill, Nadia Alfonso , Omari , Shekhe Assad, Linda na mabwana wawili mmoja akiwa mzungu na mwingine alikuwa ni mhindi ni kundi lile ambalo wanajiita Ant Illuminat wato ambao waliokosekana ni Zenzhei , Afande Kweka na Paster Cohen.
“Chriss karibu sana Tanzania tunatumaini unaifahamu misheni yako”.Aliongea na Chriss aliitikia kwa kichwa.
Naam huyu Chriss hakuwa mwingine bali ni jasusi mstaafu wa kitengo cha Secret service ndio huyu ambaye alimpatia DR Elvice Daniel faili la sauti za maongezi ya raisi wa Marekani bwana Barrack Mabo sasa haikueleweka alikuwa nchini Tanzania kwa ajili ya misheni ipi , lakini jambo la uhakika ni kwamba alikuwa na misheni maalumu ya kufanya , lakini wakati huo huo akiwa ni mwanachama wa kikundi hiki cha Ant-Illuminat yaani wale watu ambao walikuwa na Chata la visiwa vya wafu.
Sasa je Omari ameingiaje pia kwenye kundi hili halafu wakati huo huo akawa na misheni ya kiuchunguzi kutoka Hongmeng?”
MWISHO SEASON 14.