Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Siku za mwamba hua zinasomeka kilatino hivyo jtano hua ni jumamosi nafikiri.
 
I died to save my president iweke namba moja we jamaa[emoji23][emoji23]
Haikuisha ile! Binadamu wa jf wenye vipaji vyao! Ila katika stor kali hii ikikamilika itaipiga gape peniela! Ila zitadroo na anga la washenji ooh! Washenzi ya mwamba ole moran steve mollel
 
hata mimi aisee; nikiona tu, jina la mwandishi ni ck, basi mudi inakata
Zote hizo kutoka kwa CK ziko vizuri sana
Screenshot_20230525-221424.jpg
 
SEHEMU YA 424.

Ilionekana kundi la Yamata walifanya kazi yao kwa weledi sana mara baada tu ya kupewa taarifa juu ya kuzuia meli ya kundi la Lapland kwani sio meli tu iliokuwa imewazingira lakini pia kulikuwa na Chopa za jeshi la Somalia juu yao zikiwapigia misele.

Wote kwa pamoja ilibidi wapande mpaka juu kabisa ya boti kuangalia mbele na kadri boti yao inavyosonga kwenda mbele ndio walivyoweza kuona ule mikonga ya kutolea mabomu na ilionekana ilikuwa kwenye utayari wa kurusha bomu kuelekea upande wao.

Meli hii ya Lapland ilikuwa katikati yaani mbele kabisa wakiwa Yamata na nyuma ndio walikuwepo boti ya Roma , ilionekana mara baada ya kupata tishio la Yamata kusimama waligeuza.

Juu kabisa kwenye deki wanaume waliovalia kombati za jeshi pamoja na siraha nzito walionekana huku wakiwa na sura ambazo hazikuwa na hasira kabisa , walionekana walikuwa tayari kuua au kuuliwa.

Roma na Rose walisimama mbele kabisa ya boti huku wale wahudhuriaji wakiwa nyuma , huku wakiwa kwenye mshituko kwani huenda wengi wao ilikuwa mara yao ya kwanza kuwa kwenye tukio la aina hio, lakini pia walikuwa katika mshangao baada ya kumuona Situ kuwa kwenye mavazi ya kijeshi tena akiwa na afya tele.

Rose alimwangalia baba yake kwa hali isiokuwa kawaida , alimpeleka Ujerumani kwa ajili ya kufia huko , lakini kwa hali ilivyokuwa inaonekana ni kama alimpeleka kujikusanya upya, alijiambia baba yake alikuwa na talanta ya aina yake kuweza kutoka kwenye kila hali inayokuwepo mbele yake.

Situ hakuwa muoga , kwanza kabisa alionyesha kujiamini na pili alionyesha dharau , alionekana kama General wa jeshi ambaye jeshi lake lipokaribu na ushindi.

“That is my daughter . Able to suvive anything anyone throws agaisnt her it would seem that I have lost once again”

“Yule ndio mtoto wangu wa kike , ambaye ana uwezo wa kuweza kuendelea kuishi hata kama mtu yoyote atamrushia mishale , inaonekana kama nimeweza kupoteza tena kwake”Aliongea Situ kwa Kingereza ili wanajeshi wake waweze kuelewa.

“Usingerudi tena Situ kunichokoza”Aliongea Rose kwa sauti.

“Unafikiri ningeendelea kuishi kwenye nchi kama ile yenye baridi kali na kufia kule na kusahaulika , Unanitania nini ninaweza kuwa dhaifu lakini mimi sio muoga wa kuogopa kifo bali siku zote ni mwenye kukikaribisha”Aliongea Situ.

“Kutokuogopa kwako kifo hakukufanyi kuwa jasiri”Aliongea Roma na palepale alifanya tukio lililoacha wote kuwa mdomo wazi , ilikuwa ni kama wanafunzi wa yesu wakimwangalia Yesu akipaa kwenda mbinguni mara baada ya kufufuka , kwani Roma alipaa palepale hewani na kwenda kutua kwenye deki ya meli ile bila ya woga kabisa na kufanya wale wanajeshi kurudi nyuma huku wakijawa na hofu na kukoki sirahao zao , huenda hili ndio tukio la kwanza kushuhudia kwenye maisha yao na walijiona ni kama wanaangalia Muvi za Kimarekani.

“Inaonekana nimekudharau , umekuwa na nguvu zaidi kuliko nilivyodhania”Aliongea Situ huku akijitahidi kuzuia mshituko wake , hata hivyo ashawahi kuona upande wa pili wa Roma hivyo haikuwa mara yake ya kwanza nna hata wanajeshi hao alisha watahadharisha.

“Niambie nani kakusaidia kukodi hawa wanajeshi na nitahakikisha nakusamehe kwa kukupa kifo kisichokuwa na maumivu mengi?”Aliongea Roma akiwa mita kadhaa kutoka waliposimama.

“Hakuna alienisaidia, unafikiri siwezi kuwakodi mwenyewe”Aliongea Situ.

“Kwasababu umekuwa muongo , basi nitakufanya uongee ukweli mwenyewe pasipo ya kupenda , nitawaua mmoja mmoja , hivyo anzeni kutubu na kufanya amani na pale mlipomkosea Mungu wenu”Aliongea Roma kwa Kisweeden ili kuwafanya wale wengine wapate kuelewa.

Moja ya mwanajeshi aliekuwa na mwili mkubwa alievalia sare za rangi nyeupe alilaani kwa lugha yake na kisha kusogela mbele.

“Wewe ni nani?” Aliongea huku kidogo akionyesha kuwa na wasiwasi kutokana na kuzingirwa na Helikopta za kijeshi ambazo zilikuwa zikiwapigia misele kwa juu na kuonekana na wanajeshi wa kiarabu , yote hio ilikuwa ni kazi ya Tanya.

Roma alianza kutembea kumsogelea yule mwanajeshi aliekuwa mbele ya Situ lakini alimpa onyo kutosogea hatua nyingine mbele .

“Don’t move , if you get any closer I’ll fire!, How dare you challenge the glory of the Lapland Rangers”Aliongea kwa lugha ya kingereza lakini Roma ni kama ameziba masikio yake kwani aliendelea kumsogelea .

Yule mwanajeshi aliacha kusita sita kutomlipua Roma na siraha yake , alijiambia ni kheri ije kutambulika amekufa akiwa anapigana kwani hio ndio heshima ya mwanajeshi.

BANG! , BANG , BANG , BANG!

Risasi zililindima kumpiga Roma , lakini wanajeshi wote walijikuta wakiwa kwenye mshangao kwani risasi zote hazikumgusa kabisa na kila zilipomkaribia ni kama ziligonga kwenye chuma kigumu na kudondoka chini.

Alijikuta akiacha kufyatua risasi na kumwangalia Roma akiwa ameachama kwa mshangao.

Lakini Roma hakujali mshangao wake , Roma alikuwa ni mrefu kumzidi mwanaume huyo wa kiswedish hivyo mara baada ya kumfikia tu alimshika shingo.

“Crack!”.

Ni sauti ya kuvunjika kwa baadhi ya misuli na mifupa ya shingo tu sauti iliosambaa kwenye masikio ya wanajeshi wote .

Roma hakusita tena bali alichokifanya ni kuutupia ule mwili kama uchafu kwenye maji ya baharini.

Situ alijikuta akihisi ubaridi usiokuwa wa kawaida na hata kule kujiamini kwake kulianza kumuishia , kwani kwa namna ambavyo Roma ameua ni kama si kitu kabisa kwake.

“Ninaweza kuua kila mmoja wenu hapa , fikirieni kuhusu ofa yangu mnieleze ukweli wote , nani yupo nyuma yenu mpaka kuja kunichokoza” Aliongea lakini wale wanajeshi walionekana kutokumuelewa kwani walinyanyua siraha zao na kuanza kumlenga na risasi.

Lakini ulikuwa mchezo wa kitoto sana kwa Roma kwani hakuna risasi iliompata na alichokifanya kila aliemkaribia alimvunja shingo na kumtupia majini.

Yaani kwa wale ambao walikuwa kwenye Boti walijikuta magoti yao kuwa malaini kwani alichokiona hakikuwa cha kawaida kabisa na akili zao ziliishia kusema Roma hakuwa mtu , kwani watu wale wanajeshi licha ya kurusha risasi walionekana hawakumdhuru kabisa zaidi ya kurushwa angani na kutupiwa majini, Bakari Juma ambaye alikuwa akihusika katika mipango hio mkojo ulianza kumnyemelea na alijiambia hapo kama ataweza kupona basi atakaeweza kumponyesha ni Situ , kwani kama bwana huyo atataja uhusika wao yeye pamoja na Raisi Kigombola , angeanzwa yeye na baada ya hapo angefuatia Mstaafu mwenyewe, alijikuta akianza kutoa simu yake kwa kificho na kutafuta namba ya mheshimiwa Kigombola kutaka kumuelezea kile kinachoendelea lakini bahati mbaya hakukuwa na aina yoyote ya mtandao, jasho lilimtoka hapo.

Upande wa Rose hakuathirika kabisa na matendo ya Roma ni kama alizidi kumpenda zaidi, tena alijikuta akipenda pale Roma aliponyofoa moyo wa moja ya mwanajeshi na kisha kuurushia baharini na kumfyatua na teke mwanajeshi kumtanguliza kuufuata moyo wake baharini .

Ndani ya dakika nne upeo wa bahari ulinuka damu , kila mmoja alifikiria mambo yanakwenda kuwa magumu kupambana na wanajeshi hao , lakini ilionekana kuwa tofauti kabisa na matarajio.

Ni Situ peke yake ambaye aliachwa akiwa hai , akiwa katika hali ya woga mno alikuwa ni kama mtu anaekiangalia kifo chake kwenye runinga.

“Vipi tunaweza sasa kuongea?”Aliuliza Roma ambaye alichafuka kama kichaa huku akifuta damu kwenye mikono yake kwenye nguo.

“Wewe.. wewe sio binadamu, wewe ni shetani”Aliongea kwa kubabaika

“Sitaki kusikia kauli ya aina hio kwa mtu kama wewe ambaye ulitaka kumuua mtoto wako mwenyewe”Aliongea Roma na Situ alijikuta akivuta pumzi nyingi za woga.

“Nimekwisha kukuambia mpango huu ni wangu mimi peke yangu , kama unataka kuniua fanya hivyo”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu.

“Unadhani kwanini napenda mapambano ya kwenye maji hususani ya bahari? Kwasababu kuna viumbe hai chini ya maji”Aliongea Roma na palepale alizungusha kiganja cha mkono wake bila kueleweka anafanya nini na alitulia kwa dakika kama tano hivi na palepale eneo lote lilionekana kuwa na mawimbi flani yakiongezeka na ile miili iliokuwa ikielea elea ilianza kupotea mmoja mmoja kwenda chini ya maji kwa haraka sana.

Roma palepale alitabasamu kifedhuli na kuingia ndani ya chumba cha meli kwa haraka sana kama muvi inayopelekewa mbele na alitoka na kamba , palepale alimfunga mfunga Situ pasipo ya Situ mwenyewe kujua namna ambavyo anafungwa fungwa.

Roma ilionekana hakujali tena Rose atamchukuliaje kwa kile anachopanga kumfanyia baba yake , kwani baada ya kumaliza kumfuga alimbutua na akamrusha juu na kutumbukia majini kwa sekunde kadhaa na kisha akamvuta juu, aliokota bunduki iliokuwa karibu yake na kwa kutumia mkono mmoja alimlenga kwenye paja na kisha kwenye mguu na kumfanya Situ kutoa ukulele usio kuwa wa kawaida huku damu nyingi zikimtoka.

“Niue acha kunitesa mbele ya mtoto wangu”Aliongea lakini damu yake pale ilipokuwa ikidondokea ilionekana kama bawa la samaki mkubwa likizunguka na hata wale waliokuwa mbali waliweza kuona kabisa na kugundua mara moja kwamba ni Papa wadogo wadogo na mpaka hapo walielewa kwanini miili iliokuwa ndani ya maji haikuwa ikielelea juu zaidi ya damu kuonekana tu.

Hakuna kiumbe cha baharini kinachoweza kunusa harufu ya damu kikiwa umbali mrefu kama Samaki aina ya Papa, ilikuwa ni nadra sana maeneo hayo kuonekana kwa aina samaki wa aina hio kwani aina ya samaki hao hupenda sana kukaa katikati ya bahari kwenye maji mengi.

“Daah ni Papa wale?”Aliongea mmoja kwa kushangaa sana kwani ni kama mara yake ya kwanza kuona

“Ndio ni wenyewe , wamefikaje kwenye hili eneo?”Aliuliza mwingine lakini ni kama alikumbuka kuna muda walipomuuliza Roma walikuwa wakielekea wapi aliwaambia wanaenda katikati ya maji kuvua.

Situ sasa alielewa Roma alichokuwa akijaribu kufanya , alikuwa akitaka kumlisha kwa Shark , alijikuta akianza kuogopa yeye mwenyewe mpaka kuhisi mkojo ukimtoka bila ya kupenda na kuanza kulaan kisasi na tamaa zake za kurudi Tanzania.

Roma aliekuwa kwenye msisimko alimwangalia Situ kama kituko huku akiwa ameshikilia kamba kwa mkono mmoja.

“Haya maeneo mara baada ya kufika tu niliweza kuhisi uwepo wa Papa kilomita kadhaa kutoka hapa , hao unaowaona wanafamika kama Sharks aina ya Tiger, ni hatari mno kwa binadamu ndio maana unaona hakuna mwili wa mwanajeshi yoyote unaozagaaa juu ya maji , hawa sio wakubwa sana kama binamu zao wanaofahamika kwa jina la White Shark ni rahisi kuwajua kwani wana madoa madoa kama ya Chui”Aliongea Roma huku akianza kucheka.

Huenda muda ule ule angekuwa asharukiwa na Papa hao , lakini kutokana na kwamba bado walikuwa kwenye sherehe ya kula wanajeshi walionekana kumpotezea kwa muda.

“Rose Rose mtoto wangu , sidhani kama unaweza kumuangalia baba yako nikifa mbele yako”Aliongea Situ kwa sauti kubwa akiomba msaada wa Rose.

“Kama sio kwa Roma ungeshaniua miaka miwili iliopita , sikumbuki hata siku moja ambayo ushawahi kunichukulia kama mtoto wako lakini licha ya yote nikakupatia nafasi ya mwisho ya kuishi lakini ukaichukulia poa , unaweza kuwa baba yangu lakini pia wewe ni adui yangu mkubwa , Roma ambae hakuwa hata akinifahamu aliniweza kuniokoa kwenye mikono yako na kunipa mapenzi tokea siku ya kwanza nakutana nae , mapenzi ambayo wewe kama baba umeshindwa kunipatia , amekuwa ndugu yangu wa pekee niliebakiwa nae , kwanini nimzuie kwa ajili yako?”Aliongea Rose kwa hisia na kufumba macho huku akijitahidi kuzuia machozi yake.

Roma ukweli alianza kuwaua wale wengine kwani aliamini huenda Rose angeomba baba yake asiuliwe na hata kama akimuua ampe kifo cha kistaarabu lakini kwa maneno ya Rose alijiambia mrembo wake huyo alikuwa imara zaidi kuliko alivyotarajia.

Labda hisia za huyu mwanaume kuwa baba yake zilipotea mara tu baada ya kupanga kumuua”Aliwaza.

“Okey , sasa ushasikia kabisa hakuna wa kukusaidia mpaka sasa , ninaweza kukurahisishia kifo chako kama utanielezea ulioshirikiana nao wote kwanzia ndani ya kundi la Tembo mpaka nje, naamini kuna mtu mkubwa sana nyuma yako ndio maana umeweza kukodi wapiganaji wa Lapland ,sasa ni wakati wako kuwaweka wazi”Aluongea Roma huku akianza kumshusha chini akitanguliza miguu yake na kumfanya Situ kuanza kulia kwa woga

Kitendo kile kilifanya hata baadhi ya watu kutotaka kuangalia kile amabacho walitazamia kingeweza kutokea kwani walikosa ujasiri. Roma alimwingiza nusu mwili ndani ya maji.

“Argh”

Alijikuta akitoa ukulele mara baaada mguu wake kukamatwa na Papa ambaye ngozi yake ya kichui chui na nyeupe ilionekana kwa juu pamoja na masikio yake.

Pande la Nyama la mguu lilinyofolewa na kufanya eneo lote maji yake kubadilika rangi na Roma palepale alimpandisha juu kidogo.

“Vipi unaonaje hali?”

“Naomba uniue?”

“Sijamaliza bado , kama unataka kifo chako ni mpaka nipate jibu langu , nitahakikisha wanakushambulia kidogo kidogo mpaka pale utakapokuwa tayari kuongea”.

Kitendo kile kiliwaacha watu mdomo wazi na kumfanya bwana Baraka Juma Meya wa jiji la Dodoma kuhisi mchuruziko wa mkono aliona kabisa amejiingiza kwenye mdomo wa Papa yeye mwenyewe.

Mheshimiwa nadhani ulifahamu hili , umeamua kunitoa kafara na mimi siwezi kufanya unavyotaka”Aliwaza alijiambia kama Situ atamtaja basi kabla ya kifo chake atamwanga mchele wote nje na mipango yote ya Kigombola.

Muda ule ule upande wa Roma alimshusha kwa mara nyingine Situ kwenye maji ili kuruhusu paja linyofolewe tena.

“Usinishushe nitaongea kila kitu , kila watu waliohusika”Aliongea haraka haraka kwa kujitetea kwani aliweza kuona mgongo wa Jipapa chini yake.

“Nakusikiliza”Aliongea Roma huku akiacha kumshusha.

“Naomba unihidia nikikueleza uniache hai”

“Haupo kwenye nafasi ya kufanya mazungumzo na mimi hata usipo niambia nina mbinu nyingi za kuujua ukweli”Aliongea Roma na Situ alijikuta akifumba macho na kuangalia upande wa boti ile.

“Ni ni….”

“Paah!!!”Pale pale ilisikika bunduki ikikohoa upande wa boti.

“Usije kusogea hatua hata moja la sivyo nitakuchangua ubongo”Sauti ya Zonga ilisikika huku akiwa ameshika siraha akiwa amemuelekezea Rose kwenye kisogo.

Rose alijikuta akifumba macho kwa huzuni kubwa , hakuamini kati ya wasaliti wote mmojawapo atakuwa Zonga.
 
SEHEMU YA 425.

Kati ya wafanyakazi wa kwanza kabisa ambao Rose alianza nazo mara baada ya kuanza biashara ni Zonga , kutokana na kudumu nae kwa muda mrefu lakini pia kumuamini ndio ilimpelekea kumpa cheo kikubwa ndani ya kundi lake na yote hio ni kutokana pia na Zonga kuwa na elimu kubwa tofauti ya wafanyakazi wake, lakini hakuamini mwisho wake na Zonga ungekuja kuwa mbaya kiasi hicho.

Kundi lote lilishangazwa na mabadiliko hayo kwani kati ya wasaliti wote hawakutegemea Zonga kuwa mmoja wapo , lakini hata hivyo ilikuwa ni ngumu kuamini kama Zonga angeweza kuwa na uwezo mpaka wa kukodi wapiganaji wa kundi la Lapland.

“Wewe mzee unastahili kuliwa na Papa , nimekupatia pesa zangu nyingi kukodi hao wanajeshi lakini hakuna kazi ya maana uliofanya”Aliongea huku akimwangalia Situ ambaye alionekana kupoteza damu nyingi sana kiasi kwamba macho yake yalikuwa yakianza kuona ukungu.

“Zonga unadhani unaweza kujiokoa kwa kumnyooshea hio siraha Rose?”Aliuliza Roma.

“Nilikuwa mjinga kuwaamini Situ na Mzee Bakari kujiingiza katika hili baada ya kuniaminisha wanajeshi wangefanya kazi ya kuaminiika , walivyoniambia unaweza kufa kwa bomu niliwaamini moja kwa moja , lakini ukaweza kupona”.

“Huna namna ya kujitetea ushajulikana kama msaliti”Aliongea mmoja ya watu waliokuwa nyuma.

“Nilijua fika kuna uwezekano wa kugundulika mara baada ya Roma kutoa maagizo ya safari baharini lakini bado nilitegemea hali isingebadilika na kuwa kama hivi”Aliongea Zonga kwa hasira

“Ni kosa kubwa sana ulilolifanya ,kwenye maisha yangu sijawahi kusamehe msaliti”.Aliongea Roma.

“Nishawasaliti sasa unaweza kunifanya nini , ukifanya ujinga wowote nampasua mpenzi wako”Aliongea na kufanya kundi lote kupatwa na wasiwasi.

Lakini upande wa Bakari alitamani kuzimia baada ya jina lake kutajwa na Zonga kungekuwa na uwezekano wa kutoroka eneo hilo alijiambia angefanya hivyo lakini walikuwa katikati ya maji angefanya nini.

“Zonga nimekufahamu kwa muda mrefu na nilikutoa kwenye umasikini na kukupa maisha mazuri lakini sio hivyo tu nikakupa nafasi kubwa ndani ya kundi , nataka kujua ni kwanini umeamua kubadilika na kula njama na kunisaliti?”Aliuliza Rose.

“Kwasababu wewe ndio ulieanza kunisaliti”Aliongea Zonga na kumfanya Rose kushangaa.

“Unamaanisha nini kukusaliti?”

“Sikufanya kazi chini yako kwasababu nilipenda , nilifanya kwasababu nakupenda sana , tulipokutana Mtwara kwa mara ya kwanza nilivutiwa na wewe sana na hata ulipopendekeza nikusaidie kwenye kazi zako nilifanya kwasababu nilitarajia mwisho wa siku ungekuwa mwanamke wangu”Aliongea Zonga kwa sauti na kufanya watu wote kushangazwa na maneno yake akiwemo Roma mwenyewe lakini zaidi sana Rose mwenyewe alishangaa..

“Nilijitoa kwako kwa kila nilichojaaliwa nacho ,nikafanya kazi kwa juhudi ili kukufurahisha lakini hukuwahi kuniona kama mwanaume bali uliamua kumchagua Roma mara tu baada ya kukutana nae licha ya kwamba hakuna cha maana alichokusaidia zaidi yangu”Aliongea kwa sauti bila kujali.

Inaonekana ni kweli kabisa Zonga alikuwa akimpenda Rose , ni kweli kwmaba alitoka mbali na Rose, lakini siku zote hakupenda kabisa mapenzi ya Roma na Rose lakini hakuweka hilo wazi.

Kuna kipindi Zonga mwenyewe alibuni mbinu ya kuweza kumkomesha Roma kwa kuungana na kiongozi wa kundi la Black Mamba ambaye pia alikuwa akimpenda Rose , kiongozi ambaye alikuja kuuliwa na Roma , kijana aliefahamika kwa jina la Karimu.

Zonga alifanya hivyo kwa kuamini Karimu angekuwa na uwezo wa kumdhibiti Roma kutokana na ukubwa wakundi la Black Mamba na baada ya hapo angemtonya Rose juu ya jambo hilo na kupelekea kuwa maadui na yeye kuchukua nafasi , lakini mwisho wa siku licha ya kumchoma Roma kwa Karimu matokeo yakaja kuwa tofauti, Karimu akaja kuuliwa na Roma mara baada ya kumteka Najma na kwanzia hapo Zonga alionekana kumuogopa mno Roma kutokana na uwezo wake , lakini hakuweza kukata tamaa , alikuwa akimtamani sana bosi wake , kila siku alipokuwa akiona uzuri wa Rose , namna mtoto alivyojaaliwa na kalio na umbo zuri udenda ulimtoka na kuzidi kuumia pale alipokumbuka Roma ndio ambaye alikuwa akimhondomora mrembo huyo , alichoweza kufanya ni kuficha hisia zake lakini ukweli alikuwa akiumia sana kwa wivu.

Sasa mara baada ya kupewa uongozi wa juu na Rose wa kundi hilo ndipo aliposhawishiwa na Mzee Bakari kufanya juu chini kumpindua Rose kwa kumtumia baba yake Situ , mwanzoni Bakari walijua lingekuwa jambo gumu kumshawishi Zonga kumsaliti Rose lakini baada ya kuweka mpango wake mezani Zonga alikubali kirahisi sana na hilo liliwashangaza lakini hawakutaka kuuliza zaidi .

Sasa Bakari ndio anajua Zonga alikubali kirahisi kutokana na kwamba alikuwa na kisasi na Roma , lakini pia alikuwa na kisasi na Rose kwa kuamua kumsaliti na mwanaume mwingine ilihali yeye alikuwa akiumia sirini hata hivyo alimuona Zonga kiumbe dhaifu sana kuwahi kutokea kwenye uso wa dunia , unapendaje mwanamke na usimwambie? , kwake alijiambia angekuwa na mtoto kama Zonga angemuua , alijiambia ni kheri kwa mtoto wake Karimu aliekufa akipigania penzi lake lakini sio kwa upuuzi wa Zonga..

Moja ya jambo ambalo lilimchukiza Zonga ni pale Rose alipohama anapoishi na kwenda kuishi na Dorisi Kimara , ilimchukiza kwani ni kama alihisi Rose alikuwa anaolewa na Roma.

Sasa wahenga wanasema mapenzi yanaweza kukufanya kichaa hata kuingia kwenye vita ambayo huwezi kushinda sasa ndicho alichokifanya Zonga , alijua kulikuwa na asilimia sabini za kutoweza kumdhibiti Roma lakini therathini zilizobaki ilikuwa zinamtosha sana kwake kulipigania penzi lake.

Kosa alilolifanya ni kwamba hata yule anaempigania hakuwahi kumwambia hisia zake , huenda angemuelewa lakini yeye akaamua kufanya vitu kimya kimya.

Dorisi mwenyewe alijikuta akijawa na huzuni baada ya kusikia sababu halisi iliomfanya Zonga kumsaliti, alijikuta akikumbuka maisha yake yalivyokuwa tokea siku ambayo alianza kumpenda Roma licha ya kwamba hakujua alikuwa wapi , alikumbuka hata safari yake ya kuanzisha club ndani ya jiji la Dar msukumo ulikuwa ni mapenzi alishindwa kujitofautisha na Zonga.

Ndio baada ya Rose kuweza kusaidiwa na mtu asiemjua , mtu ambaye alimuokoa kwa namna ya ajabu na kumuacha hotelini huku akiwa amemponyesha kwa namna ya ajabu , lakini wakati huo akimuachia na kiasi cha pesa aliguswa sana na msaada huo , alijiona ni kama alikuwa akisoma hadithi za SinganoJr ambazo zilikuwa za kufikirika , alijiambia inawezekanaje ikatokea mtu akakuokoa kwenye kifo akiwa hakujui na baada ya kukuokoa anakusafirisha umbali mrefu ndani ya muda mfupi kimaajabu lakini sio hivyo tu mtu huyo huyo anakuponyesha kwa namna ya kustaajabisha lakini baada ya hapo bado hakukatii tamaa anakuachia na pesa ya matumizi na kisha kupotea pasipo kusubiri hata shukrani.

Rose wakati ule alijiambia ni jambo ambalo haliwezekani kwa ulimwengu wa sasa ambao binadamu wengi walikuwa waovu , binadamu ambao wanaweza kupanga njama za kuwaua watoto wao wa kuwazaa bila huruma kama baba yake , hivyo alikuwa na kila sababu ya kumpenda mwanaume mwokozi wake licha ya kwamba hakumjua , licha ya kwamba kulikuwa na asilimia ndogo sana ya kuonana nae tena.

Sasa Rose baada ya kukumbwa na tukio la aina hio la ajabu kwa mtu wa kawaida kama yeye kumtokea alijiapiza kwa majina yote lazima atamtafuta mwanaume aliemsaidia kwa namna yoyote kwa ajili ya kurudisha deni.

Moja ya sababu kubwa ya Rose kuandamwa na baba yake ni kutokana na Situ kumtaka Rose amuelezee ni mahali gani mama yake marahemu aliweza kuficha pesa na dhahabu zake , Sehemu ambayo aliamini Rose alikuwa akiifahamu , lakini Rose licha ya kupewa mateso na baba yake ili kutaja eneo ambalo lina mali ambazo mama yake alificha hakuweza kufumbua mdomo , moja ya sababu ya kutofanya hivyo ni kutokana na kwamba Rose alikuwa akimchukia sana baba yake , kwani kwa macho yake yeye alimshuhudia baba yake akimpiga risasi mama yake kwa kosa dogo sana.

Sasa baada ya Roma kumuokoa kwenye mikono ya baba yake alichokifanya ni kutumia mali ambazo ziliachwa na mama yake na kuanzisha biashara , alikuwa na machaguo mengi sana , alikuwa na chaguo la kufanya biashara za halali za kujipatia kipato cha kawaida na kuendeleza maisha yake , kwani pesa alizoachiwa na mama yake zilikuwa nyingi lakini hakuchagua kufanya biashara halali kwasababu moja tu, moyoni mwake kwake pesa na maisha ya kawaida yasingekuwa na maana pasipo ya kumpata mwanaume anaempenda mwanaume ambaye alimuona kama malaika..

Hivyo Rose akafikiria mbinu rahisi ya kuweza kumpata mwanaume huyo ni kufanya biashara haramu akiamini siku zote mwanaume yule kwa mazingira yale aliomuokoa ni lazima angekuwa na uhusiano mkubwa sana na dunia ya ‘underwold’ , dunia ya wahalifu , hivyo aliamini kama atajikita huko asilimia za kukutana nae zingekuwa kubwa kuliko katika ulimwengu wa kawaida wa watu watii wa sheria.

Hivyo ndivyo Rose alivyojiingiza kwenye biashara ya uuzaji wa madawa ya kuleva , akatengeneza koneksheni ya kupata ‘supplier’ ndani ya mkoa wa Mtwara ambao ulikuwa na bandari na baada ya kufanikiwa kirahisi kutokana na kuwa na pesa ndipo alipofikiria hatua ya pili , aliamini ndani ya jiji la Dar es salaam ndio iwe sehemu ya uendeshaji wa biashara yake kutokana na uwingi wa watu , akiamini kwamba ndani ya jiji hilo lingempa asilimia kubwa ya kukutana na yule mwanaume kwa mara nyingine, basi ndipo ikazaliwa Club B ndani ya eneo la Mbagara Maji matitu.

Wanafalsafa wanaaamini ulimwengu upo kwa ajili ya kupigania nafsi zinazoendana kwa kukutana na hatimae kuwa pamoja , wanaendelea kusema baadhi ya vitu vinashangaza sana na vinanguvu kiasi kwamba tafsiri yake inakuwa sio bahati mbaya.

Hivyo ni rahisi kusema kwamba eneo , hali ya kimazingira na muda havina nafasi sana kwenye watu ambao wamepangiwa kuwa pamoja, hicho ndio kilichomtokea Rose kwani ndani ya miezi michache tu ya kutua ndani ya jiji la Dar es salaam na kuanzisha club yake ndio wakati ambao ameweza kukutana na mwanaume yule wa ajabu, ijapokuwa hakumjua vizuri kwa sura usiku ule, lakini baada ya kukutana nae moyo wake ulimtambua muda huo huo.

Roma mara yake ya kwanza kutua nchini Tanzania mtu wa kwanza kukutana nae ni Rose ambaye alikuwa kwenye mazingira ya kuhitaji msaada na hata yeye mwenyewe alishangazwa na tukio hilo na ndio maana baana ya kumsaidia alimtoroka, hakutaka kuchangamana nae tena kutokana na sababu zake.

Kwa upande wa Rose mara baada ya kupata nafasi ya kumlipizia baba yake kisasi hakufanya hivyo kutokana na kwamba aliamini huenda pasipo baba yake asingeweza kukutana na Roma ndio maana akamwacha hai na kumpa nafasi ya pili ya maisha licha ya chuki aliokuwa nayo zidi yake.

“Zonga asante sana kwa kuwepo na mimi kwa nyakati zote za mapambano yangu , lakini uliokuwa nayo sio mapenzi ya dhati juu yangu , kama kweli ulikuwa unanipenda ungekuwa na ujasiri wa kuweka wazi hisia zako na sio kupanga njama za kutaka kunidhuru , hisia zako juu yangu ni Lust(tamaa ya ngono) na Obsession(Wazimu wa mapenzi) ndio maana umeamua kunisaliti”Aliongea Rose.

“Unaweza kutafsiri hisia zangu utakavyo lakini leo hii siwezi kukuacha hai , tutakufa wote hapa na huenda kwasababu ushazielewa hisia zangu tukapendana huko kuzimu, hata hivyo wote tunadhambi kama yasemwayo ni kweli wote tutakuwa sehemu moja baada ya kufa nitafidia juhudi zangu zote nilizopoteza hapa duniani”Aliongea Zonga huku akikoki siraha yake vizuri lakini pasipo kuelewa alivyopigwa alijikuta siraha yake ikiwa kwenye mikono ya Rose kirahisi sana , kwani alipigwa pigo kwa spidi ambayo hakuweza kudhania Rose angeweza kuwa nayo.

Hata wale wahudhuriaji walijikuta wakishangazwa na umahili wa Rose kwani kitendo alichokifanya ni kama kwenye muvi.

Roma upande wake alishangazwa na Zonga sana na kujiambia kweli moyo wa mtu ni kichaka siku zoe Zonga alionyesha utiifu kwa Rose sio kwasababu alimchukulia kama bosi bali alikuwa na hisia za mapenzi.

“Zonga huenda hali yako ikafanana na yangu , lakini utofauti wako na wangu ni kwamba mimi nilikuwa na mapenzi ya dhati mapenzi ambayo sikuyaficha kwa yule niliempenda , huenda unadhani labda wewe ndio mtu wa kwanza kukutana na mimi lakini kwangu Roma ni mtu wa kwanza kukutana nae na kama sio yeye leo hii usingeweza hata kutambua kama naishi ndani ya uso huu wa dunia, Roma aliniokoa kutoka kwenye mikono ya baba yangu lakini licha ya hivyo hakuhitaji chochote kutoka kwangu , alinisaidia na kisha akatoweka na mimi ndio niliweka juhudi kumtafuta , leo hii nimefikia hapa nilipofika kwasababu tu nilikuwa na nguvu ilionisukuma kufanya hivyo, mapenzi hayapo kumtengenezea mtu uoga bali humpa ujasiri , ukijiona huna ujasiri hata wa kuweka hisia zako wazi tambua bado hujapenda”

“Nilikupenda kwasababu ulikuwa mtiifu kwangu na nilikuchukulia kama ndugu yangu ndio maana nikakupa nafasi yangu, ni kwasababu naheshimu juhudi zako , hili ni kosa lako la kwanza kunitendea nakupa nafasi ya mwisho kili mbele yangu umekosea na haupo tayari kurudia tena na kwanzia leo nitakuacha uendeleee na maisha yako”Aliongea Rose kwa sauti.

“Hahaha.. Hahaha… huenda ulichoongea ni sahihi lakini ninachotaka sio msamaha tena , ninachotaka ni penzi lako tu na kama hakuna uhakika wa kulipata siwezi kukuomba msahamaha na kukuachia , mafanikio ya biashara ya Kundi la Tembo yamesababishwa na mchango wangu mkubwa ila sio wewe nipo tayari kuomba msamaha kama nitakuwa na uhakika wa kuwa kiongozi wa Tembo lakini pia kama utazikubali hisia zangu”Aliongea kwa huzuni huku akicheka kama chizi na kumfanya Roma kushangazwa na maneno yake na watu walijiambia Zonga ni chizi kweli , hayo maneno alitakiwa ayatamke mapema na sio muda huo akiwa anachungulia kifo.

“Nakupa nafasi ya mwisho ya kukiri kosa lako na kuomba msahamaha”

“Haina hajaa..”Aliongea Zonga na katika tukio la kuchekesha na kuhuzunisha alijirusha majini na kufanya kila mtu kushangazwa na ukichaa wa Zonga na Rose alijikuta akivuta pumzi ya ahueni lakini iliochanganyika na majonzi , moyo wake ulikuwa mzito kumuadhibu Zonga kutokana na kuwa nae karibu kwa muda mrefu mpaka kumchukulia kama ndugu.

Baada ya tukio hilo Rose alimgeukia Bakari ambaye baada ya Zonga kumtaja tu vijana wake waliokuwepo hapo walimuweka chini ya ulinzi.

“Mr Bakari nadhani uliamua kukiuka makubaliano yetu , kabla hujakutana na adhabu yako nakupa na wewe nafasi ya kujitetea lakini kama utajirusha majini na kuliwa na Papa ruhusa unayo”Aliongea Rose na Mzee Bakari aliekuwa kwenye hali ya wasiwasi palepale alimwangukia Rose miguuni.

“Naomba usiniue tafadhari , Usiniue tafadhari”

“Nina sababu ipi ya kukuacha hai mtu kama wewe, kama unakumbuka vizuri hili ni kosa lako la pili unarudia kufanya”Aliongea Rose na kumfanya Bakari kumeza mate mengi na kisha akamgeukia Roma aliekuwa kwenye meli nyingine.

“Nitakuambia kila kitu ila naomba uniache hai tafadhari”

“Unafikiri unachotaka kuongea kinaweza kunipa sababu ya kuweza kukuacha hai?”Aliuliza Rose.

“Ndio kwasababu ninachokuambia kinamuhusu mwanaume unaempenda, kama utaahidi kuniacha hai nitakwambia , Mr Roma nakuhakikishia ninachokwenda kukuambia ni muhimu sana kwako kukifahamu”Aliongea kwa sauti na kumfanya Roma atamani kujua ni jambo gani ambalo Bakari anataka kumuambia.,Rose alimwangalia Roma kuomba mawazo yake .

“Mr Bakari unaweza kuongea na nitaamua mwenywe kukuacha hai kama utakuwa na sababu yenye uzito unaolingana na miasha yako”Aliongea Roma.

“Nipo tayari kuongea , lakini swala lenyewe siwezi kukuambia mbele ya watu hawa wote kwasababu ni siri kubwa”Aliongea na Roma alimwangalia na kuona Mzee Bakari alionekana kujiamini.

Roma alimwangalia Situ ambaye amemning’iniza na kugundua alishakufa tayari kutokana na kupoteza damu nyingi , alichokifanya ni kumuachia na kutumbukia majini.

“Mr Bakari nitakusikiliza sababu yako”Aliongea Roma na kumfanya Bakari kuvuta pumzi za ahueni , ijapokuwa hakujua sababu aliokuwa nayo ingekuwa kubwa kumfanya Roma asimuue lakini alijiambia ni kheri amepata dakika kadhaa za kuendelea kuishi.

“Tokea siku ambayo nilikuja kujitambua na kujua lipi jema na lipi baya , niligundua maisha yangu yote yameunganika moja kwa moja na ulimwengu wa uhalifu kutokana na kuzaliwa na wazazi ambao walikuwa wanajishusha na uhalifu , nilichoshwa na maisha ya aina hii lakini sikuwa na jinsi kukubaliana nayo , hivyo kwanzia sasa nataka kuwa huru na mambo yote hivyo najiondoa rasmi kwenye nafasi yangu kwa kujiuzuru na Jacob ndio atakuwa mrithi wangu na kuendesha operesheni zote zinazohusiana na kundi la Tembo”Aliongea Rose na kufanya watu wote kuwa kimya huku wakionyesha sura za kutokubaliana na jambo hilo , upande wa Jacob kibonge mwenyewe hakutarajia kauli hio kutoka kwa Rose.

“Babe hata mimi nakuunga mkono , naamini Kibonge anaiweza hio nafasi”Aliongea Roma lakini bado hakuna alieunga mkono.

“Najua wote hapa mna wasiwasi , lakini nawahakikishia Jacob anaiweza nafasi yangu na kama ndani ya miezi michache hatofanikisha kazi za kundi basi nipo tayari kumbadilisha na kuwapa nafasi ya kumchagua mnaemtaka, lakini niwatahadharishe tu kwamba kama kuna mmoja wenu ambaye atafanya njama za kufanya usaliti, niwakumbushe nina rekodi na kila mmoja wenu hapa juu ya machafu yake anayoyafanya na nitayaweka hadharani serikalini na sidhanni kama kuna mmoja wenu anaweza kutoka kwenye mkono wa sheria , pili hata kama ukapata nafasi hio maisha yako utakuwa huna , kitakupata kama kilichompaa Situ”Aliongea na kuwafanya wote kuogopa maana tukio la Roma kuvunja vunja watu shingo lilikuwa la kuogofya kweli na Watu wote walitingisha vichwa vyo kukubaliana na maneno ya Rose

“Jacob umepewa nafasi ya kuongoza kundi , lakini nikuhakikishie kwamba ukifanya jambo lolote la kijinga kama Zonga jihakikishie kuwa ni mfu , una mke na unatarajia mtoto hivyo nakushauri msingi wako wa kuongoza uwe ni wa amani”Aliongea Roma na Jacob alimwangalia Roma kwa woga mno na alijikuta akitingisha kichwa haraka haraka kutii maneno yake.
 
Back
Top Bottom