Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 426.

Watu wote walirudi ndani na kumuacha Rose na Roma pamoja na Mzee Bakari wakitaka kusikiliza sababu yake , Roma hakutaka kwenda kuongea nae ndani kwani alijiambia kama mzee huyo asingekuwa na sababu ya kuridhisha basi angemuua hapo hapo na kumtupa majini.

“Nipe sababu ya kuridhisha nikuache hai?”Aliongea Roma.

“Mr Roma ni kweli kwamba nimefanya nilichokifanya , lakini kuna watu nyuma yangu ambao napokea maagizo kutoka kwao lakini licha ya hivyo lazima tufahamu kwamba likija swala la biashara haramu , mwenye nguvu ndio anaetawala na sio sheria”

“Hio ndio sababu , naona unajielezea pasipo ya kutoa sababu”Aliuongea Rose.

“Mr Roma nadhani unakumbuka tukio la Mzee Chino kuchomwa na kisu na majambazi?”Aliongea Mzeee Bakari na kumfanya Roma kushangaa kidogo huku upande wa Rose akishindwa kufahamu juu ya swala hilo.

“Unataka kusema nini?”

“Kuchomwa kisu kwa Mzee Chino hakukua kwa bahati mbaya bali ulikuwa ni mpango maalumu wa kukuangamiza”Aliongea Mzee Bakari na kumfanya Roma kuvutiwa na maelezo hayo.huku akikumbuka siku ambayo alimuokoa Mzee Chino kutoka hali ya kifo.

“Elezea vizuri maelezo yanyooke la sivyo sitokuacha hai”Aliongea Roma huku hasira zikianza kumtawala.

“Mzee Longoli ndio alienipa maelekezo ya kuandaa vijana kumjeruhi Mzee Chino, baada ya kupewa kwa maagizo hayo nilitaka kujua ni kwasababu gani kumjeruhi yule mzee kutokana na uhusiano wa Mzee Chino na Neema Luwazo na kwenye udadisi wangu nilikuja kugundua ni mpango wa kupata damu yako”Aliongea Bakari na kumfanya Roma palepale kumshika Shingo Mzee Bakari na kumkaba kwa kumning’niza hewani na kumfanya aanze kutapa tapa miguu na kukohoa.

Kitendo ambacho hata Rose aliogopa ijapokuwa hakujua sana kuhusu Mzee Chino lakini baada ya kusikia kuhusu damu alishaelewa usiriasi wa swala lenyewe , alikuwa akijua uwezo mkubwa wa damu ya Roma kwani hata yeye ilishawahi kumponyesha tena kwa zaidi ya mara mbili.

Roma baada ya kumkaba kwa nguvu kiasi cha Mzee Bakari kutaka kupoteza fahamu alimtupa chini na Mzee alijikuta akitapika pombe na mauchafu palepale huku akihema kwa shida.

“Nataka kusikia ukweli wote sio nusu nusu, niambie w ambao wanahusika kwenye swala ambalo umeongea?”Aliongea Roma kwa kuamrisha na Mzee Bakari na kitambi chake alikaa vizuri na kuanza kuelezea waliohusika .

“Vijana wangu ndio niliwapa kazi ya kufuatilia, nilifanya hivyo kwa namna ya kijihami , kwenye maisha yangu sijawahi kuamini mtu kabisa na ndio maana kila inapotokea misheni ambayo sina maelezo nayo ya kutosha nitaitimiza lakini huku nikihakikisha nachimba ukweli wote na hicho ndio nilifanya , ijapokuwa mpango huo ulikuwa wa siri lakini niliweza kujua aghalabu kwa kile kilichokuwa kikiendelea hii yote ni kuniepushia na kutumika na mwisho wa siku kutolewa kafara, watu wanaohusika kwenye mpango wenyewe najua wawili tu ni Mzee Longoli pamoja na Mchina mmoja ambaye ni mkuu wa jeshi la China anafahaika kwa jina la Afande Yang Gongming”Aliongea Mzee Bakari na Roma mara baada ya kusikia kuhusu jina la Afande Yang hakumfahamu mara moja , ni kama watu wote waliotajwa hapo hakuwafahamu.

“Mzee Longoli ndio nani hapa Tanzania?”

“Ni Jenerali wa jeshi mstaafu kabla ya Afande Gambino Tozo , mtoto wake ni mwanasiasa maarufu , mbunge na waziri wa sayansi na teknolojia”Aliongea na kumfanya Roma kuwaza kidogo.

Mpaka hapo alishaelewa kitu kimoja kikubwa sana, tukio la damu yake kuchukuliwa kwa kumtumia Mzee Chino, alijikuta akitabasamu kifedhuli kama kawaida yake.

“Sababu yako imeniridhisha angalau”Aliongea Roma na kumfanya Mzee Bakari kutoa macho ya mshangao.

“Ila haimaanishi nitakuacha hai?”Aliongea Roma na kumfanya Mzee Bakari kupagawa.

“Mr Roma uliahidi utaniacha hai , nilichokuambia ni kitu kikubwa sana”Aliongea.

“Kwanini unaamini ulichoniambia ni kitu kikubwa na hata hivyo sikukuahidi kama sitokuua nilikuambia unielezee sababu ya kuniridhisha ndio nitakuacha hai”Aliongea Roma na Rose mwenyewe alishindwa kumuelewa mpenzi wake.

“Mr Roma nilichokuambia ni jambo kubwa sana”.

“Hio ndio sababu ambayo itanifanya nikuue sasa hivi”Aliongea huku akiweka usiriasi kwenye macho yake kwa mara nyingine na kuanza kuachia nguvu ya kijini ya kuogofya

“Nielezee sababu ya kukuridhisha, kama akili zako zitakuwa timamu utajua ninachomaanisha”Aliongea Roma kwa namna ya kuamrisha na kumfanya Mzee Bakari kufikiria kwa muda.

“Mr Roma nadhani unataka kujua kwanini nimejua kwasababu gani nimesema ni taarifa niliokuambia kuwa kubwa kwako?”Aliongea Mzee Bakari.

“Safi , hicho ndio ninachotaka kujua kutoka kwako ukiniridhisha nitakuacha hai”

“Licha ya kuwa na undungu wa mbali na mheshimiwa kigombola , lakini vile vile mimi ni mwanajeshi kitendo cha intelijensia na nawajibika moja kwa moja kwa Afande Maeda”Aliongea na kumfanya Rose mwenyewe kushangaa lakini Mzee Bakari aliendelea kuongea.

Ni kweli kabisa Mzee Bakari licha ya kwamba alikuwa mmiliki wakundi la kihalifu la Black Mamba alikuwa ni mwanajeshi ambaye aliomba kustaafu na alivyostaafu ndipo alipoweza kuja kuwa mkuu wa mkoa wa jiji la Dar es salam kipindi cha uongozi wa Raisi Kigombola , sasa haikueleweka ni lini alianza kuwa shushu ndani ya mzunguko wa Raisi Kigombola..

Lakini anasema jeshi lilikuwa likichunguza baadhi ya matukio yaliokuwa yakiendelea ndani ya Tanzania nje ya idara ya usalama wa taifa, moja ya sababu kubwa za kuanzishwa kwa uchunguzi ni juu ya kifo cha Profesa Shelukindo na Safari za mara kwa mara za jenerali wa jeshi la China nchini Tanzania kutokana na kwamba hakuwa akija kikazi bali alikutana moja kwa moja na Mzee Longoli pamoja na Raisi Mstaafu Kigombola.

“Kwahio unasema kwamba mpango wa kuchomwa kwa Mzee Chino ulikuwa ukiujua na hivyo hivyo Afande Maeda alikuwa akiujua?”

“Mr Roma kama nilivyosema mwanzo sijadanganya kitu , kazi niliopewa ni kukusanya taarifa ya kila kinachoendelea katika vikao vya mstaafu kigombola , kuhusu Mzee Chino niligundua baada ya kufanya uchunguzi wangu mwenyewe binafsi nje ya ushushu kwa kutumia vijana wangu na mwanzoni sikuchukulia swala hilo kwa uzito kwani niliriripoti moja kwa moja kwa Afande Maeda na hata nilipomuelezea hakuonyesha kama ilikuwa taarifa kubwa kwake”

“Kwahio ulijuaje ni taarifa kubwa kwangu?”Aliuliza Roma.na Mzee Bakari alikurupuka na kutoa simu yake janja na kisha aliingia upande wa watsapp.

Ilionekana baada ya mambo kubadilika Mzee Bakari alitafuta msaada kwa Afande Maeda kwa njia ya mtandao wa watsapp, aliweza kuwasiliana nae kutokana na Boti hio imeunganishwa na Wifi.

Roma alijikuta akitabasamu kwa uchungu , alijiambia inamaana huyu Afande Maeda alikuwa akifahamu hili jambo muda mrefu halafu akakaa kimya alijiambia asipokuwa na maelezo ya kutosha atamkomesha. Pasipo kujali nafasi yake jeshini.

Mpaka hapo hakuwa na sababu ya kumuua Mzee Bakari , alijiambia moja kwa moja atadili na Mzee Maeda moja kwa moja, lakini hata hivyo kuna mambo makubwa zaidi ambayo alipanga kuyajua a, maelezo ya Mzee Bakari hakuyaamini alijua tu kama kuna watu amewaficha.

Na ni kweli kabisa Mzee Bakari Juma alikuwa amemficha Mheshimiwa Kigombola kwa uhusikaji wake wa moja kwa moja , hata hivyo licha ya kuwa shushu wa serikali lakini kwa wakati mmoja alikuwa akimchukulia Mheshimiwa Kigombola kama ndugu yake na ndio maana alipima uzito ni nani anafaa kutolewa kafara na mtu sahihi ni Longoli pamoja na Afande Yang Kutoka China

Roma sasa alijua moja kwa moja huenda damu yake ilitumika kutengenezea kopi yake , lakini jambo hilo lilimshangaza mno kwani kwa maelezo ya Profesa Clark ni kwamba hakuna uwezekano wa damu yake kuweza kutengenezea Clone kutokana na kwamba ikiguswa na hewa tu inapitia mabadiliko kutokana na kumulikwa na Divine Light.

……….

Roma baada ya kurudi ndani na Rose ilibidi ampatie maelezo kidogo juu ya Mzee Chino, kuhusu kilichotokea , Rose alishangazwa na jambo hilo mno.

“Babe sasa haitokuwa hatari?”

“Usijali sana , wakati nayaokoa maisha ya Mzee Chino nilihisi kuna kitu ambacho haikuwa cha kawaida kinaendelea lakini niliendelea kumfanyia matibabu kwasababu nilikuwa nikiamini hakuna uwezekano wa damu yangu kutumika kama siraha , lakini kama jambo hili limetokea kweli nitahakikisha nadili nalo mbele kwa mbele, haitokea kiumbe feki kikanizidi ujanja mimi”Aliongea Roma kwa kumhakikishia Rose.

“Babe mwili wako unaonekana kuimarika mno nadhani ni sahihi ukaanza kabisa mafunzo”Aliongea Roma na kumkumbusha Rose juu ya swala la yeye kwenda China.

“Babe ushapata mbunu rahisi ya sisi kujifunza?”

“Ndio nimefanikiwa kupata taarifa nyingi , lakini hata hivyo naendelea kuirahisisha , ninataka kwanza kile nilichopata nione kama kitafanya kazi”Aliongea Roma.

“Nipo tayari mpenzi kuanza muda wowote, ninatamani sana kuwa na uwezo wa kupaa kama ulivyofanya pale”Aliongea Rose na kumfanya Roma kucheka.

“Ukiweza kufanikisha kufika hata levo ya Mzunguko kamili utaweza kufanya mambo mengi ya ajabu hata kutembea juu ya maji”.

“Kweli!!!”

“Umeanza lini kutokuniamini?”

“Hapana sio kwamba sikuamini mpenzi , lakini nashindwa kabisa kuamini kama nitakuja kua na uwezo wa kupaaa angani , ni jambo ambalo mtu yoyote atashindwa kuelewa”Aliongea na Roma aliona ni sahihi kwa mtu wa kawaida kutoamini juu ya jambo hilo.

Baada ya masaa matatu hatimae saa kumi na moja kamili za jioni ndio muda ambao Roma aliweza kurudi nyumbani akiwa pamoja na Rose

Kurudi kwa Roma kuliwafanya wote kupata ahueni ya amani kwani walikuwa na wasiwasi.

“Mmeyamaliza?”Aliuliza Blandina.

“Ndio halikuwa jambo kubwa sana hata hivyo , ilikuwa kasafari ka kwenda katikati ya bahari na kugeuza”Aliongea Roma.

“Katikati ya Bahari?”Walijikuta wakiuliza wote kwa pamoja na Roma ilibidi atoe maelezo ya mafupi ya kile kilichotokea huku akiacha kugusia swala la damu , alifanya hivyo kwasababu angechukua muda mrefu kuwaelewesha.

Wote walimsikitikia Zonga mpaka mwisho wa stori , hawakuamini angechukua maamuzi ya kijinga ya namna hio licha ya kwamba alikuwa na makosa makubwa.

Baada ya Roma kumaliza ni kama hali ilibadilika ghafla sasa, Nasra na Amina wangeweza kurudi nyumbani , lakini kwa upande wa Dorisi na Rose nyumba yao ndio hio ilikuwa imelipuliwa , hivyo ni rahisi kusema kwamba hawakuwa na pakuishi..

Moja ya watu ambao walikuwa na shauku ya kujua nini kinaendelea hapo ndani ni Qian Xi , alikuwa akifahamu wanawake wote hao ni wa Roma , sasa wote wwapo ndani ya nyumba moja kwa mara ya kwanza, Blandina aliekaa karibu na Roma alimshtua kwa bega lake la kushoto..

“Roma kwahio tunafanyaje?”Aliuliza Blandina maana kwa namna yoyote mwenyewe aliona ni hivyo tu kulikuwa kuna tishio la usalama , lakini Rose , Nasra , Amina Dorisi hawakuwa na sababu kabisa ya kukutana na Edna wala kukaa pamoja nyumba moja kwani walikuwa michepuko tu..

“Mimi mwenyewe hata sijui tunafanyaje nawasikiliza nyie”Aliongea Roma akijifanyisha hakuwa akijua nini kinaweza kufuatia na alimwangalia Edna alietulia muda wote pembeni akionyesha hali ya kumtaka aongee jambo..

Edna alijikuta aking’ata lipsi zake na kukusanya ujasiri ,mpaka hapo alikuwa akijua Dorisi na Rose walikuwa wakiishi pamoja na nyumba yao ndio hio imepatwa na majanga.

“Nadhani Dorisi na Rose wanaweza kukaa hapa kwa muda kuna vyumba vya nje ambavyo vina hali nzuri havitumiki”Aliongea Edna.

“Miss Edna hilo halitowezekana vile vyumba mara ya mwisho navikagua Gypsum yake imeharibika”Aliongea Bi Wema na kumfanya Edna kuona aibu kidogo ni kweli kulikuwa na vyumba ambavyo mara nyingi vilijengwa kwa ajili ya wageni pamoja na wafanyakazi lakini hakuwahi kwenda kukagua.

“Nina pendekezo kwasababu kilichotufanya hapa kukusanyika ni usalama wetu , kwanini tusimpunguzie Roma majukumu ya kuhakikisha usalam wetu kwa kukaa majirani?”Aliongea Rose na kuwafanya wote kushangaa wazo lake , hata Roma ambaye alijifanyisha kukosa maamuzi alishangazwa na pendekezo hilo lakini kwa upande mmoja kuliona kuwa zuri mno.

“Ninachomaanisha tunaweza kununua nyumba mbili ambazo zipo sehemu moja , sehemu ambayo tunaweza kuwa majirani ili iwe rahisi kwenye maswala ya kiusalama”Aliongea Rose lakini wazo lake lilishangaza watu.

Ukweli Rose alitoa pendekezo hilo kwasababu tu alitaka kuwa karibu na Roma , Dorisi mwenyewe alipenda wazo hilo lakini aliogopa kumpa sapoti Rose wazo lake mbele ya Edna.

Roma alifurahishwa sana na akili za Rose aliishia kutingisha kichwa tu kwa tabasamu murua, huku akikosa aibu kabisa lakini hata hivyo amezoeleka kama mtu ambaye hana aibu na hata mama yake alishangazwa na hilo.

Edna alimwangalia Rose moja kwa moja kwenye macho yake , alichohisi kwenye akili yake aliona ni kama Rose anamchokonoa.

Familia yote akiwemo Roma mwenyewe walisubiri kusikia maamuzi ya Edna kwani yeye ndio mwenye mamlaka ijapokuwa msemaji wa mwisho ni Roma hivyo Roma asingetoa wazo tu la kusema waende wakaishi karibu ili aweze kuwatembelea wote kwa wakati mmoja.

Unafikiria Edna atakubaliana na wazo la Rose.
 
SEHEMU YA 427

Edna alimwangalia Rose kwa namna ya kumsoma mawazo , alitaka kujua kama Rose alikuwa na nia ovu ya kutaka wao kuwa majirani , lakini kwa mwonekano wa Rose aliona hakuwa na nia mbaya na alijiambia kuna haja gani ya kugopa kuwa na ujirani na Rose na Dorisi.

“Okey kama tunaweza kupata nyumba ambazo zipo eneo moja na tukawa majirani sawa , kwani hela sio tatizo”Aliongea Edna na kufanya watu wote kupata ahueni.

“Lakini hili linawezekana , kupata nyumba ambazo zipo eneo moja?”Aliuliza Blandina.

“Inawezekana , kuna kampuni mbili za Real Estate hapa Tanzania wanafanya kazi ya kujenga majumba na kuyauza moja ni Paple Group nyingine ni BOSNIA Group, uzuri ni kwamba nyumba nyingi wanajenga kwenye eneo moja”Aliongea Rose.

“Kuna uwezekano wa kupata nyumba tatu kwa wakati mmoja?”Aliuliza Edna na kufanya watu wote kushangaa kwanini anauliza hivyo..

“Nilikuwa na mpango wa kununua nyumba moja chini ya jina la kampuni, nafikiria nyumba hio akae Nasra kama CEO msaidizi na mama yake watoke kwenye Apartment”Aliongea Edna na kumfanya Nasra kutoa macho na sio kwa Nasra tu kila mmoja alishangazwa na kauli ya Edna.

“Ednaa..!”Aliita Nasra kwa wasiwasi.

“Ni haki yako kutoka kwenye jengo la Apartment na kuwa na mahali pazuri pa kuishi ,ushakuwa CEO msaidizi cheo chako ni kikubwa lazima pia kampuni iwajibike na michangyo ya wafanyakazi wa kampuni”Aliongea Edna lakini licha ya maneno yake kuongea kama bosi wa kampuni lakini yalimgusa kila mmoja hata kwa Roma mwenyewe.

Edna licha ya kuwa kauzu na siriasi kwenye maswala ya kazi zake lakini kwenye maswala ya kujali wafanyakazi wake hakuingiza maswala binafsi ndio maana hata licha ya Nasra na Dorisi kujihusha na mume wake hakuwachukulia hatua kwani ni maswala ya maisha yake ya binafsi na hakutaka yaingilie utendaji wa kampuni.alikuwa na kipaumbele na hakuwa na roho mbaya na huenda ndio maana wafanyakazi walikuwa wakimpenda licha ya kwamba hakuwa na ukaribu nao sana.

Edna na yeye alkuwa akijihusisha na biashara ya mali zisizohamishika lakini miradi ilikuwa mbali na jiji , kwa mfano mradi wa Kibaha mji wa kisasa ulikuwa mbali sana na jijini hivyo wafanyakazi wake asingewapeleka kule kuishi.

“Ngoja nijaribu kuingia mtandaoni kuona kama kuna uwezekano wa kupata nyumba tatu ambazo zipo eneo moja|”

“Ngoja nikalete laptop itakuwa rahisi zaidi”Aliongea Edna na kuamka kupandisha juu na kufanya wanawake wote kumwangalia kwa macho ya kiulizo.

Dakika chache Edna alishuka na laptop mbili za brandi tofauti moja ya Mack Book na moja HP na kumkabidhi Rose kutafuta huku yeye pia akitafyuta.

“Nadhani nyumba iwe karibu na baharini ndio itafaa zaidi nitaangalia Bosnia Real Estate Kigamboni , Wewe angalia Maple”Aliongea Edna.

“Nasra , Dorisi na nyie changieni mawazo linawahusu pia hili”

“Mimi popote tu mtakapochagua nipo tayari , kwanza sina ubavu wa kununua nyumba zaidi ya bilioni moja”Aliongea Nasra .

“Unaweza”Alijibu Edna na kumfanya Nasra amwangalie.

“Mkataba wako na kampuni yangu utaisha miaka miwili ijayo na unao uwezo wa kuuvunja mwaka jana uliweza kupata ofa kutoka kampuni mbili tofauti tofauti , kampni ya Toyota ilikuhitaji kuwa mkurugenzi kwa tawi lao lililipo hapa Tanzania lakini ulikataa kama ungekubali ungekuwa na zaidi ya bilioni za hela , vile vile kampuni ya LV ilikuhitaji kwenda Kenya kusimamia tawi lao lakini ukatakataa”Aliongeda Edna na kuwafanya hata Blandina kushangaa.

“Edna ulijuaje , nadhani sikuwahi kukuelezea hilo?”Aliuliza Nasra kwa mshangao

Ni kweli Nasra alikuwa akipokea ofa nyingi kutoka kwa makampuni makubwa kwa ajili ya kufanya nayo kazi, CV ya Nasra ilikuwa ikiwavutia vibosile wengi sana ukizingatia pia na kusoma kwenye chuo kikubwa duniani cha Cambridge na kutoka na GPA ya daraja la kwanza.

Mkataba wa Nasra na kampuni ya Vexto ulikuwa ni wa miaka nane tu kumalizika na alikuwa ashahudumu kwa miaka sita ya mkataba wake , hivyo ingekuwa kwake rahisi kuvunja mkataba na kampuni ya Vexto na kwenda kwenye kampuni nyingine kubwa na kufanya nao kazi lakini alibakia ndani ya kampuni ya Vexto.

“Waliotaka kukuajili walinifuata pia na kuniomba nikushawishi lakini sikutaka kuingilia maamuzi yako kutokana a historia yako na familia yangu?”

“Ni kweli lakini hela si kitu sana kwangu, CEO aliepita alinisaidia sana kama ningetoka kwenye kampuni ya Vexto na kwenda kufanya kazi kwenye kampuni nyingine ningejihisi kuwa na hatia”Aliongea Nasra

“Ndio maana wewe na Dorisi nashukuru sana mchango wenu kwenye kampuni , nisingefikia hapa kama sio kwa msaada wenu”Aliongea Edna na kuwafanya Dorisi na Nasra kushangaa Edna leo akiwashukuru moja kwa moja.

Baada ya kutafuta hatimae Edna aliweza kupata nyumba ambayo aliona ingefaa sana kwa wao kuishi.

“Nadhani hizi zinaweza kufaa , zipo chini ya umiliki wa kampuni ya Bosnia nakumbuka hata upambaji wa samani za ndani ulifanywa na kampuni yetu , Nasra hebu angalia na toa maoni yako”Aliongea Edna na kumpatia Nasra laptop.

“Ni kweli Edna upambaji wa ndani pamoja na kuweka samani za nyumba hizi ni kampuni yetu iliohusika , ni nyumba nzuri lakini bei yake Mhmh.”Aliongea Nasra maana nyumba moja tu haikuwa chini ya bilioni moja na nusu.

“Kama zipo sehemu nzuri na mnazijua vizuri basi haina haja hata ya kwenda kukagua , bei sio shida sana, Dorisi unaonaje?”Aliuliza Rose.

“Ununio sio eneo baya lipo kando ya bahari na ni mazingira yenye nyumba nyingi nzuri na watu waliostaarabika , sio mbaya”Alichangia Dorisi.

“Naunga mkono hoja tutakuwa wote tunaishi njia moja”Aliongea Amina ambaye muda wote ni kama hakujali sana kile kilichokuwa kikizungumziwa kwani alikuwa bize na Lanlan.

“Zipo eneo moja?”Roma alivunja ukimya.

“Mbili zipo karibu sana lakini ya tatu ipo upande wa nyuma kabisa , lakini sio mbali sana”Aliongea Edna akimjibu Roma.

“Kama wote tumeridhika tumpigie wakala wao haraka , kama kuna uwezekano mimi na Dorisi tunaweza kuhamia muda huu”Aliongea Rose na kuwafanya washangae.

“Leo leo? Kwanini msisubiri siku ya kesho?”

“Hizi ni nyumba ambazo zipo na kila kitu tunaweza kufanya tu mazungumzo ya awali na tukahamia halafu kesho tukamalizia taratibu zingine , hatuna vitu vingi vya kuhama navyo kwani sehemu kubwa vimeungua”Aliongea Rose.

“Okey! kama mnataka kuhamia leo hakuna shida , sisi tutachukua hii, Rose nyie mnaweza kuchukua hii ya upande wa mbele na Nasra utachukua hii ya upande huu”Aliongea Edna na waliangaliana na kisha walikubali.

“Sisi tutahamia kesho baada ya taratibu kumalizika , kuhusu hii ya kwenu mnayotaka muda huu nitajaribu kuwasiliana na Mage tuone kama anaweza kuwasaidia kwenye taratibu zingine za vibali”..

Ni ndani ya nusu saa tu waliweza kumpata wakala wa nyumba hizo na uzuri waliweza kukubaliana kwamba wanaweza kwenda kukutana muda huo na kuanza kujadili utaratibu wa malipo na mazungumzo mengine.

“Nitawapeleka na kuwasaidia kwenye taratibu zingine”Aliongea Roma.

Amina alikuwa akiishi Mbezi hivyo waliongozana wote kuelekea huko , Amina akiendesha gari yake na Roma akiwa anaendesha ya kwake akiwa ameambatana na Rose pamoja na Dorisi.

Wakala aliwaambia waende moja kwa moja mpaka Ununio kwa ajili ya kuangalia kabisa na kuanza mazungumzo licha ya kwamba muda ulikuwa umeenda kwani ilikuwa ni saa kumi namoja kama dakika kumi na tano za jioni.

Baada ya kufika waliweza kukutana na wakala ambaye alikuwa ni mhindi ambaye alionekana kuwanyenyekea,dalali huyo mwanzoni alihisi huenda wateja wake ni wababaishi tu kwani tokea aanze kazi hio hakuwahi kupokea wateja wa nyumba tatu kwa wakati mmoja , lakini mara baada ya kuona gari waliokuja nayo mpaka hapo alionekana kuridhika.

Baada ya kukagua nyumba zote tatu walionekana kuridhika , nyumba hizo zilikuwa nzuri sana na za kisasa kuliko hata ya Edna ya Oysterbay na zilikuwa kubwa na mazingira yake yalikuwa safi zaidi , lakini pia kilichomfurahisha Roma mtaa ulikuwa msafi na umetulia.

Wakala aliwaambia muda huo hawezi kumaliza taratibu zote na kuwakabidhi kutokana na kwamba ilikuwa wikiend hivyo aliwashauri taratibu kufanyika siku inayofuata ndio waanze taratibu za malipo na kusainishana , kwani kulikuwa na tatatibu za serikali ya mtaa.

Roma aliwarudisha Dorisi na Rose mpaka hoteli ya Kunduchi na ile wanafika eneo la mapokezi tu , simu ya Roma ilianza kuita na alipoitoa na kuangalia jina la anaepiga ni Afande Maeda , alipokea na kuweka sikioni.

“Mr Roma habari za jioni?”

“Salama Afande, nadhani hatimae umeamua kunipigia simu mara baada ya shushu wako kukupasha habari ya kilichotokea?”Aliongea Roma na upande wa pili ulitulia kidogo.

“Ni kweli Mr Roma, nataka kujua kama tunaweza kuonana na kuongea kidogo muda huu”Roma alifikiria kidogo , ukweli alitaka akaendeleze alipoishia asubuhi yake na Dorisi kwani hakuwa amepata kitumbua kwa muda wa siku tano.

“Okey kwasababu nakudai maelezo nadhani sio mbaya kukutana nipo Kunduchi Maple hoteli nadhani sio mbaya kama mazungumzo yetu yatafayikia hapa”

“Nipo karibu na maeneo ya hapo nitafika muda si mrefu”Alionga Afande Maeda na simu ilikatwa.

“Kuna mtu napanga kuonana nae mnaaweza kutangulia kwenye vyumba vyenu”Aliongea Roma.

“Tumechukua chumba kimoja cha vitanda viwili , tutakukaribisha kama utakuja”Aliongea Dorisi huku akiweka tabasamu la kiuchokozi na kumfanya Roma kuanza kuvutiwa na mwaliko huo wa peponi , alikuwa akijua walichokuwa wakipanga warembo hao , jambo ambalo hata yeye lilikuwa likimfurahisha.

“Siwezi kupoteza hio nafasi , nikimaliza kuongea na mgeni wangu nitakuja moja kwa moja”Aliongea Roma huku akimkonyeza Rose ambaye akiishia kubetua mdomo.

“Hatutaki ugomvi na Edna ametukaribisha kwake kwa ukarimu leo”Aliongea Rose lakini Dorisi alimpotezea Rose na kumsogelea Roma sikioni na kumnong’neza.

“Chumba ni namba 105 achana na maneno ya kinafiki ya Rose”

“Una hoja, usikilizwe”Alijibu Roma bila aibu huku akitamani kumpiga Dorisi bao la makalioni lakini alijizuia kutokana na uwezo wa watu.

**********

Upande mwingine muda huo huo katika hoteli ya Eunice iliopo maneno ya Mbezi -Kimara katika eneo la maegeesho ya magari alionekana mrembo Suzzane alievalia suruali ya jeansi ya rangi nyeusi chini na viatu vya skuna rangi nyeupe , juu akiwa amevaa kikoti flani rangi ya ugoro aina ya Blazer pamoja na Pink Brallete ndani yake. Alikuwa amependeza mno na alionekana kabisa muda huo alikuwa na miadi na mtu ndani ya hoteli hio ya nyota tano.

Baada ya kuweka mkoba wake wa Hermes vizuri kwapani alijirekebisha na kisha kuingia ndani huku akipangusa simu yake na kisha akaweka sikioni na ilionekana akiongea kwa dakika kadhaa na baada ya kumaliza maongezi yake moja kwa moja alisogea eneo la mapokezi na kutoa maelezo na mdada mmoja wa mapokezi alievalia sare alitoa simu ya mkonga na kuweka sikioni na ndani ya dakika chache aliruhusiwa na kuendelea na safari.

Baada ya kuingia kwenye lift alikuja kutokezea juu kabisa kwenye floor namba saba na kuendelea mbele kwenye korido akihesabu vyumba na kusimama kwenye chumba kilichokuwa na namba 69 , alivuta pumzi na kujiweka sawa na kisha akagonga mlango na palepale ulifunguliwa.

“Karibu sana Miss Suzzane”Ilisikika sauti kwa kingereza ikimkaribisha na Suzzane alimwangalia mwanaume huyo kwa namna ya kumchunguza na kisha alitingisha kichwa na kuingia ndani , mwanaume huyo mzungu alitokezea sura yake kwa nje na kuangalia upande wa Korido kama vile anachunguza kuna mtu alikuwa nyuma ya Suzzane na baaada ya kuridhika aliingia ndani na kisha akafunga mlango.

Mzungu yule alikuwa amevalia taulo za hoteli hio na ilionekana alikuwa na makazi yake hapo.

“Jisikie huru Suzzane”Aliongea na Suzzane aliekaa kwenye sofa alitingisha kichwa kwa namna ya kupunguza wasiwasi wake.

“Do you mind..?”Aliongea yule mzungu baada kumiminina Mvinyo kwenye glass akimpatia lakini Suzzane alitingisha kichwa kwamba hatotumia kinywaji.

“Naona bado una wasiwasi Suzzane ila nitakuonyesha kitu ambacho kitakufanya angalau kukutoa wasiwasi na mazungumzo yetu kuanza”Aliongea kwa lugha ya kingereza na kisha alifunua kitabu mfano wa notebook na kuibuka na kikadi kisha akampatia Suzzane.

Suzzane mara baada ya kushika kile kikadi alijikuta akikigeuza geuza kwa kukiangalia kwa umamkini huku akionyesha mshangao kidogo.

“Unaonekana kushangaa , naamini umewahi kuona kikadi chenye nembo ya namna hio?”Aliongea na Suzzane alitingisha kichwa kukubali.

“Umejuaje ninaweza kufahamu kadi yenye nembo ya namna hii?”Aliuliza Suzzane na mwanaume yule alitabasamu.

“ My name is Chriss Alton as introduced myself over the phone ,former secret service agent”

“Jina langu naitwa Chriss Alton kama nilivyokwisha kujitambulisha kupitia simu , mimi ni ajenti wa kitengo cha Huduma ya siri”Alikunywa kidogo wine huku akikaa vizuri na kisha akaendelea.

“Although my name is Chriss Alton , I‘m also known as Daniel Smith as a member of the Ant -illuminat organization and the card you hold identifies me, However my membership is not something I Flaunt, as the true extent of my involvement is kept confidential within the organisation”

“Ijapokuwa jina langu ni Chriss Alton lakini pia nafahamika kwa jina la Daniel Smith kama mwanachama wa Ant- illuminat na kadi ulioshika ndio inanitambulisha hata hivyo uanachama wangu sio jambo la kujisifia kwani kiwango kamili cha ushiriki wangu kinabakia kuwa siri ndani ya shirika”Aliongea na kumfanya Service kushangaa hasa kwenye neno ‘Ant Illuminat’.

“Naomba nikuitwe Chriss”Aliongea Suzzane.

“You are welcome”

“Umeniambia unafahamiana na Dr Elvice Daniel , ndio sababu ilionifanya kukubali kuonana na wewe Mr Chriss, nadhani twende moja kwa moja kwenye dhumuni la mazungumzo”Aliongea Suzzane kwa lugha ya kingereza.
 
SEHEMU YA 428.

Mwanaume Chriss ambaye anaekutana na Suzzane alikuwa ndio moja ya vijana ambao walikuwa wakiaminiwa na Mheshimiwa Barack Mabo mpaka pale Chriss alipofanikisha kurekodi mazungumzo ya raisi na yeye mwenyewe lakini pia mazungumzo ya Raisi Kigombola na Raisi Barack Mabo.

Na baada ya Chriss kurekodi sauti hizo ndipo alipompatia mfanyakazi wa ikulu wa kitengo cha mawasiliano afahamikae kwa jina la Suphian Kangasi na ndio huyo Suphiani Kangasi alievujisha sauti hizo kwenda kwa Raisi Jeremy Paul lakini wakati huo huo akikabidhi sauti hizo kwa jasusi Dr Elvice Daniel kwa kumpa maagizo wa sauti hizo kupatiwa na Chriss.

Chriss anabanwa na serikali ya Marekani ili kusema nani alikuwa anashirikiana nae mpaka kufanikisha kurekodi sauti hizo pamoja na teknolojia aliotumia lakini Chriss anaonyesha hali ya kuchanganyikiwa kwani anashindwa kujibu maswali anayoulizwa na mwisho wa siku wanasaikolojia wanahitimisha Chriss kuugua ugonjwa wa Munchauson Syndrome.

Serikali ya Marekani ikiwa imemfungia gerezani wanajikuta kwenye sintofahamu mara baada ya Chriss kupotea kwa namna isioelezeka na utorokaji wake gerezani unakuwa kitendawili, FBI kushirikiana na vyombo vingine vya kiusalama wanamtafuta Chriss kwa kujaribu kufumbua fumbo la namna alivyotoroka lakini wanashindwa kuelewa.

Swala la kutoroka kwa Chriss akiwa kizuizini linamfikia mheshimiwa Barack Mabo na raisi huyo mara baada ya kufikiria sana anahitimisha huenda Chriss alitoroshwa na sehemu ya miungu , kwani kwa mazingira ya Chriss aliotorokea anaamini hakuna binadamu wa kawaida anaeweza kufanya hivyo na kufanikisha , lakini swali linabakia kama Chriss katoroshwa na miungu je ni kwasababu ipi na kwanini miungu hio ifanye hivyo anaendelea kufikiria na kufikia kwenye hitimisho kwamba huenda hata kitendo cha kufanikisha kurekodiwa kwa sauti yake ndani ya ikulu ya Tanzania kumefanikishwa na sehemu ya miungu.

Katika taifa ambalo linaongoza kwa kupitia mambo ya ajabu ni taifa la Marekani , huenda kila raisi aliehudumu ndani ya ikulu ya White hose amepitia mambo ambayo hayafikiriki kwa akili za kawaida na moja ya maajabu makubwa ni namna ambavyo watuhumiwa kupotea kwa namna isivyokuwa ya kawaida.

Huenda kwenye faili la watuhumiwa ambao wametoroka kwenye mazingira ya kutatanisha na kutafutwa mpaka leo ni wengi na katika majina hayo huwezi kukosa jina la Chriss Alton , Carlos , Phill Knight, Shekhe Assad , Afshar Bahman na wengine wengi.

Mambo haya yameishia kubakia kitendawili na sababu ni kwamba hata kama ndani ya ikulu kuwahisi miungu kwa kazi hizo waliishia kupotezea kuokana na sera ya utunzaji wa siri ya miungu hio chini ya kitengo cha Zeros.

Lakini sasa jambo ambalo limebakia kuwa kiza kwao ni kwamba kati ya watu wote waliopotea ndio asilimia kubwa huunda jamii ya siri ambayo inajiita Ant – Illuminat , jamii ambayo inatumia nembo ya visiwa vya wafu katika kujitambulisha , jamii ambayo mwanzilishi wake ni Hades.

Chriss sasa anarudi Tanzania kwa misheni maalumu baada ya kutokukamilisha kile alichokianzisha, haijulikani mara baada ya kutoka Marekani aliishi wapi na alifanya nini lakini kwa mara ya kwanza anaonekana ndani ya Taifa la Tanzania na mtu wa kwanza katika misheni yake anaonana na Suzzane.

“Kwanza nikupe pole kwa kumpoteza mpenzi wako , nilipata kusikia mlikuwa kwenye hatua za mwisho za kufunga ndoa mpaka umauti ulipomkuta”Aliongea Chriss na kumfanya Suzzane kuwa na huzuni kidogo.

“Nishapoa kwa sasa lakini Elvice ameshindwa kufutika kwenye akili yangu na ndio maana mtu yoyote anapotaja jina lake kwa namna ya kumfahamu naguswa sana”

“Miss Suzzane najua una kisasi ndani ya moyo wako kwa wale waliohusika na kifo cha mpenzi wako lakini nikueleze kwamba Chriss na Raheli walikuwa kwenye vita , hivyo naweza kusema wamekufa wakiwa mashujaa, hivyo pale mwanajeshi anapokufa kwenye vita sio kwamba vita inakwisha bali wanaobaki ndio wanaendeleza na ndio tunachokwenda kukifanya , siku ya leo nataka kukupa mwanga kwanini Elvice mpenzi wako alikufa na ni vita ya namna gani ambayo alikuwa akipigana ili tuone kama upo tayari kuendeleza pale alipoishia”Aliongea na kupozi.

“Vita aliokuwa akipigania Elvice na Boss wako Raheli ilikuwa ni ya kuiponya dunia na ugonjwa unaoanza kuonyesha dalili”

“Unamaanisha nini kusema ugonjwa unaoanza kuonyesha Dalili?”Aliuliza Suzzane huku akionyesha hali ya kuchanganyikiwa lakini bwana Chriss anaonekana kuwa kwenye utulivu wa hali ya juu.

“Miss Suzzane wewe ni dini gani?”Aliuliza.

“Mimi ni mkristo tu kwa jina kutokana na wazazi wangu kuwa wakatoliki”Aliongea.

“Unamaanisha wewe ni mkristo ambaye huzingatii sana maswala ya dini?”Aliuliza na Suzzane alitingisha kichwa.

“Kupitia dini yako unatafsiri vipi mwendendo wa dunia ya sasa kwa mtazamo wa kimaadili katika Dini?”Suzzane alishangazwa na swali hilo lakini aliishia kujibu kwa kifupu na kusema dunia kwa kupindi cha sasa kuna mmomonyoko wa maadili mkubwa tofauti na zamani , akagusia kidogo maswala ya ndoa za jinsia moja ambazo baadhi ya makanisa wanaanza kutambua na mambo mengine husianishi.

“Well! Ulichozungumza ni sahihi kabisa na sipaswi kuongezea zaidi ila ninachotaka kukufahamisha alichokuwa akipigania mpenzi wako ni kile kinachoendelea kwasasa, kitu ambacho napenda kuita dalili za ugonjwa ambapo umebainisha wewe mwenywe’Aliongea na kumfanya Suzzane kuonekana kuchanganyikiwa.

“Kama nilivyokwisha kujitambulisha mimi ni mwanachama wa jamii ya siri ya Ant -Illuminat basi jamii yetu inaenda kinyume na jamii ya siri ya Illuminat , labda kwa kukurahisishia mambo unayoyaona kwa sasa ambayo ni dalili ya ugonjwa ni kwamba yanasababishwa na jamii nyingi za siri ambazo zipo chini ya Illuminat”Aliongea , ijapokuwa Suzzane hakuwa mpenzi sana wa habari za kutunga kama vile uwepo wa Freemason na jamii nyingi za siri lakini alikuwa akisikia kuhusu hizo jamii na kwenye maisha yake hakuwahi kuamini kama zipo na kufanya kazi.

“Kwahio unachomaanisha ni kwamba Elvice alikuwa ndani ya jamii hii ya Ant illuminat?”

“Elvice alikuwa ni mwanachama anaeandaliwa lakini bahati mbaya umauti ulimkuta akiwa katika kutimiza wajibu na watu waliohusika na kifo chake ni hawa Illuminat , Miss Suzzane dhumuni la mazungumzo haya sio kukuchanganya ila kwanza ni kukubadilisha mtazamo wako pamoja na sumu iliopo ndani ya moyo wako , ninachojaribu kukuambia Elvice alikuwa kwenye mapambano kama mwanajeshi na amefia vitani na mapambano hayana budi kuendelea m hivyo kwa leo sitokuelezea zaidi kuhusu jamii yetu bali kile ninachotaka kutoka kwako”Aliongea

“Unataka nini kutoka kwangu?”

“Kabla sijakuelezea ninachotaka kutoka kwako haswa na kile ambacho unapaswa kufanya, nataka kuzungumza na Miss Edna na nitaweka wazi kile ambacho kimesababisha kifo cha Elvice haswa ni nini akiwa vitani”Aliongea na kumfanya Suzzane kushangaa.

“Kama ni swala la bosi wangu nadhani unao uwezo wa kuongea nae moja kwa moja sio kupitia mimi”

“Kuhusu kuongea na bosi wako moja kwa moja uwezekano huo upo lakini swala hili linakuhusu pia kama linavyomhusu Edna ,nataka upange namna ya mimi kukutana na Edna pasipo ya mume wake kufahamu na mengine muhimu zaidi utayajua hapo hapo”Aliongea na kumfanya Suzzane kufikiria.

“Nitajaribu lakini eneo nitachagua , pili lazima uniahidi utanielezea kila kitu kilichotokea na kumfanya Elvice kuingia kwenye vita na watu wasiofahamika”

“Naahidi kukuelezea kila kitu kama utakamilisha ombi langu , lakini swala la mwisho ninalotaka kujua kutoka kwako ni kwa kiasi gani Edna anajua kuhusu pacha wake?”Aliongea na kumfanya Suzzane kutoa mshangao.

“Unazungumzia nni?”

“Oh kwa mshangao wako nadhani hautokuwa na ufahamu juu ya boss wako kuzaliwa na pacha wake, naamini huenda hata yeye mwenyewe hajui , kama ni hivyo naamini ushahidi wa sauti haujamfikia”Aliongea .

“Unamaanisha nini kuhusu ushahidi wa sauti?”Aliuliza Suzzane huku akianza kuchangamka na Chriss aliokota kile kikadi kwenye meza na kisha akamuonyesha ile nembo ya visiwa vya wafu iliokuwa kwenye kikadi hicho.

“Niambie umefahamu vipi kuhusu hii nembo?”

“Nilikuwa na kikadi mfano wa hiki ambacho kilikuwa na jina la Hades kama sikosei na nimempatia mume wake Edna”Aliongea Suzzane.

“Alright miss Suzzane fanya kama nilivyo kuelezea , hakikisha naonana na Miss Edna pasipo ya mume wake kufahamu na nitakuelezea kuhusu ushahidi wa sauti , ndio jibu la kwanini Elvice alikufa”Aliongea na kumfanya Suzzane kutingisha kichwa kukubali lakini bado akiwa kwenye hali ya kuchanganyikiwa , hususani sehemu ya pacha wa Edna pamoja na ushahidi wa sauti.

Suzzane mara baada ya kuingia kwenye gari yake alijikuta akivuta pumzi na kuanza kukumbuka moja ya kazi ambayo alipewa na Edna.

Edna mara baada ya kujua kwamba Suzzane alimficha kwa muda mrefu juu ya yale aliokuwa akiyajua juu ya kifo cha mama yake kusababishwa na watu kwa kufanyia mwili wake majaribio alijikuta akiwaza sana kwanini Suzzane alikuwa alimficha juu ya jambo hilo na aliweza kukutana na Suzzane na kumuhoji na ndipo Suzzane alipomwambia Edna kwamba maagizo aliopewa na mama yake ni kwamba nyaraka aliokuwa ameachiwa alipaswa kumpatia mume wake na sio yeye na ndio maana alikaa kimya.

Edna alishangazwa sana na jibu hilo , lakini kilichomchanganya zaidi ni kwanini mama yake kutoa maagizo hayo na zaidi ni pale Suzzane alipomtaja kabisa Hades kwa jina lake.

Yaani Suzzane alimwambia kwamba nyaraka alipaswa kupatiwa Hades na sio yeye , sasa kitendawili hiko kilimchanganya sana Edna kwani kauli ya mama yake ni kama aliona atakuja kuolewa na Roma ndio maana akatamka maneno hayo.

Swali alilokuwa nalo Edna tokea anaongea na Suzzane na kutaka kujua sababu ya kumficha ndio swali ambalo alikuwa nalo Roma , yaani wote walikuwa wakijiuliza kwanini Mama yake Edna akafahamu Roma na Edna kukutana na mwishoe kuwa mume na mke , kilikuwa ni kitendawili ambacho hata Suzzane pia hakuwa akijua jawabu lake , lakini kwa upande wa Roma kuna kitu ambacho alikuwa akihisi lakini hakuwa na uhakika sana lakini aliamini jibu hilo linahusiana na mtangulizi wake yaani Hades wa Zamani.

Sasa Suzzane aliekaa kwenye gari lake ndani ya eneo la maegesho alikuwa akijiuliza swali la namna moja , lakini kubwa zaidi alikumbuka wiki kadhaa nyumba bosi wake Edna alimpa kazi ya kutafuta taarifa za miaka mingi iliopita zinazohusiana na mama yake wakati alipokuwa mjamzito, taarifa ambazo ameshindwa kabisa kuzipata licha ya kufatilia sana ndani ya hospitali ya Muhimbili , lakin mara baada ya muda huo kumaliza maongezi yake na Chriss ni kama sasa anajua nini Edna anajaribu kutafuta , aliamini huenda bosi wake alikuwa alishafamu kuzaliwa na pacha wake.

Nitampelekea ripoti kesho na nitajua zaidi , huenda kuna kitu ambacho aliweza kupata ndani ya benki ya Swiss na hataki kuniambia , nadhani ndio ushahidi wa sauti anaozungumzia Chriss , nitaongea nae na kumshawishi kuonana na Chriss pia”Aliwaza Suzzane na kisha aliwasha gari lake na kuondoka eneo hilo

Upande wa Chriss mara baada ya Suzzane kuondoka alionekana kuongea na simu.

“Ndio nimemaliza kufanya nae mazungumzo na nimempa kazi ya kunikutanisha na Edna”.

“Kazi nzuri , unapanga kufanya nini baada ya kuonana nae?”

“Nadhani Hades kamficha mambo mengi kuhusu pacha wake , napanga kumwambia kila kitu kuhusu mpango LADO”

“Shekhe anasemaje?”

“Niumewapa maelezo kama ulivyonielezea na wametokea kuamini na wameniruhusu kuendelea na misheni yangu ila sijawaelezea inahusiana na nini moja kwa moja , niendelee kama ilivyopangwa?”

“No there are some changes of plan”

“Hapana , kuna mabadiliko ya mpango”Ilisikika sauti upande wa pili na kumfanya Chriss kushangaa.

“What..”

“Ambacho kilishindikikana kufanyika miaka nane iliopita awamu hii nataka ukitekeleze , ndio namna pekee ya kufanya mpango wetu kufanikiwa”

“Boss unamaanisha…?”

“Yes na ukifanikisha potea mara moja , nadhani umefunzwa kwa kazi hio , na unajua Alama ambayo inatakiwa kubakia eneo la tukio?”

“Ndio boss”.

“Then Good , I will call you myself as soon as I receive good news of success”

“Basi vizuri , nitakupigia mwenyewe mara tu baada ya kusikia taarifa nzuri ya mafanikio”Aliongea na kisha simu ikakatwa.

“F**ck kama sitokamilisha kwa ustadi wa hali ya juu naweza kupoteza maisha , natakiwa kuhakikisha swala hili linaenda vizuri”Aliwaza Chriss.

*********

Roma na Afande Maeda waliweza kukutana ndani ya hoteli hio katika eneo la mgahawa na kuanza mazungumzo yao mara moja.

“Okey Afande nadhani uanze kuzungumza , maana umenificha mambo mengi ambayo naamini unayajua na yananihusu mimi”Aliongea Roma mara baada ya kupatiwa vinywaji walivyoagiza.

“Nadhani unajua mengi zaidi kuliko mimi Mr Roma , lakini sio mbaya nitaeleza yale machache ambayo nayajua lakini pia kuweka lengo langu wazi la kutaka kufanya mazungumzo haya na wewe muda huu”Aliongea Afande na Roma alitingisha kichwa.

“Nadhani kama mwanajeshi unaelewa kwamba kuna mstari wa utenganisho kati ya jeshi na siasa licha ya kwamba wakuu wetu wa mwisho kimadaraka ni mwanasiasa”

“Ndio maana sipendi mwanasiasa ambae sio mwanajeshi na sipendezwi sana na demokrasia kwani ni chanzo cha matatizo mengi”Aliongea Rom na kumfanya Afande Maeda kucheka kidogo.

“Huo ndio mtazamo wako?”

“Nina mitazamo mingi”

“Ni wajibu wa jeshi kufatilia mambo yote ambayo yanagusa usalama wa nchi moja kwa moja ndio maana miezi michache iliopita jeshi lilianza kufatilia baadhi ya vikao vya siri ambavyo vilikuwa vikifanyika kwa siri kati ya Raisi mstaafu Kigombola na Jenerali wa jeshi la China bwana Yang Gongming , lakini licha ya hivyo pia serikali ina makubaliano na jeshi la china katika maswala ya utengenezwaji wa siraha za kivita”

“Ni jambo la kawaida kwa jeshi kama la Tanzania kuwa na makubaliano kwa nchi zilizoendelea katika maswala ya siraha , lakini siku zote makubaliano yanakuwa ‘Mutual’ , kwa maana kwamba pande zote lazima zinafaidika hivi ndio ambacho kinalifanya taifa letu kuendelea kuwa na ushirikano wa karibu na China kwa miaka mingi , lakini licha ya hivyo miaka ya hivi karibuni ushirikiano kati ya viongozi wa jeshi na Mheshimiwa mstaafu umeongozeka kwa kiasi kikubwa jambo ambalo sisi kama jeshi linatufanya kuona kama hatari na ndio llilipelekea kuanza kuweka watu wetu ndani ya ‘Circle’ ya mheshimiwa mstaafu ili kujua baadhi ya mambo muhimu ya kiusalama yanayoendelea , na katika kufatilia ndipo tulipokuja kugundua makubaliano ya mheshimiwa Kigombola na Afande Yang”Aliongea

“Makubaliano gani?”

“Makubaliano yaliopo ni kuhusu Yan Buwen kupewa ‘clearence’ ya kutumia maabara ya siri ya Even Lab, haya ni makubaliano ambayo kama jeshi yalitufikirisha , kwani ndani ya China kuna maabara bora zaidi kuliko Even Lab na hata kabla ya Yan Buwen kuhamia hapa nchini alikuwa akifanya kazi chini ya maabara ya kijeshi katika kitengo cha ugunduzi wa teknolojia za siraha”

“Unataka kusema kwamba kifo cha Profesa Shelukjindo kilisababishwa na Serikali ya China na ya Tanzania , kama ni kweli kwanini?”Aliuliza Roma ijapokuwa alikuwa na uhakika kiasi huenda Yan Buwen alikuwa akitengeneza siraha kwa kutumia kanuni na gunduzi zilizoachwa na Profesa Shelukindo.

“Kuhusu sababau halisi sijaipata moja kwa moja lakini kutoka na msururu wa matukio tunaamini kuna kitu kikubwa sana ambacho Yan Buwen anatengeneza ndani ya maabara na kinachofanya kupata hisia hizi ni mara baada ya ukamilishwaji wa mpango wa kupatikana kwa damu yako ,. Mwanzoni nilichulia swala hili kawaida sana , lakini mara baada ya wiki kadhaa kupokea taarifa ya wewe kushambulia meli ya kivita ya kimarekani moja kwa moja niliamini huenda kuna uhusiano mkubwa sana na kile kinachoendelea ndani ya maabara hio”

“Kuhusu damu yangu kuchukuliwa ni swala ambalo niliweza kufahamu lakini sikutaka sana kulipa kipaumbele sana , lakini nilishangazwa baada ya shushu wako kunielezea juu ya mpango wa upatikanaji wa damu yangu nilihisi kuna mchezo unajaribu kufanya”

“Hakuna mchezo ambao unafanyika kwa upande wa jeshi , lakini hata hivyo swala la damu nilikuwa bado tukilifanyia ufumbuzi na sasa kwa mbali nadhani tunapata majibu ambayo tunayategemea”

“Kwanini mnamruhusu mstaafu kuweza kuhatarisha usalama wa nchi kwa kufadhili mamluki?”

“Hatuwezi kumchukulia hatua Mheshimiwa mstaafu kwasababu jeshi letu sio kama la nchi nyingine , ndani ya jeshi kuna siasa nyingi hivyo unaweza kusema kupata wanajeshi wasioegemea upande mmoja ni bahati sana , tunafanya mambo kwa akili ili kuepusha migogoro, kuna wanajeshi wapo ‘ neurtral’ lakini kuna wale ambao wanam mtii mheshimiwa mstaafu, ni rahisi kusema kila raisi anaetoka madarakani ana wanajeshi wake wanaomtii na kusikiliza maagizo yake waachotofautiana ni ule ukubwa wake”Aliongea Afande Maeda na kumshangaza kidogo Roma , lakini hata hivyo maswala ya jeshi la Tanzania hayakuwa yakimhusu kabisa.

“Kama kazi mmeishidnwa nitawasaidia , nitaanza na huyu Mzee Longoli kumuua kwa kunichokoza na kisha atafuatia mheshimiwa mstaafu, huyu mpuuzi Yan Buwen chochote anachotengeneza huko ndani ya maabara hakiwezi kunipatia shida na siku akiingia kwenye kumi na nane zangu nitamuuua”Aliongea Roma.

“Mr Roma nikusihi usije ukamuua Mzee Longoli kwani ni moja ya watu wenye mizizi kwenye taifa hili”Aliongea na kumfanya Roma kukunja sura.

“Huyu Longoli anahuika hahusiki kuiba damu yangu?”

“Anahusika lakini ninachotaka kuongea ni kwamba mambo bado tunalifanyia kazi , nimetaka kukutana na wewe mapema ili kukusihi jambo hili utuachie sisi”

“Kazi hio unaifanyia kisiasa zaidi na mwanajeshi na siasa ni vitu viwili tofauti , nitamuua kwanza huyu Longoli na nitakusaidia kupata majibu ambayo wewe mwenyewe bado huyajui, ili kulinda usalama wa nchi hupaswi kuzunguka zunguka kuondoa tishio , unahitaji majibu ya haraka pasipo kujali jina la mtu ndani ya serikali”Aliongea Roma na kisha alisimama.

“Afande haya mazungumzo yashaisha , umeongea sana ila nilichotaka kutoka kwako ni kuthibitisha mambo mawili tu , kama kweli huyu anaejiita Longoli anahusika au Lah na jibu langu umenipatia anahusika , unaonekana kuwa na maswali mengi sana nitakusaidia kwenye maswala ya uchunguzi”Aliongea Roma na kisha hakutaka kusubiri jibu aliondoka akimuacha Afande Maeda akiwa mdomo wazi.

Roma baada ya kutoka tu ndani ya eneo hilo alitoa simu yake na kumpigia Diego na alionekana kuna maagizo ambayo alikuwa akimpatia na kisha akatabasamu na kuziendea lift, ndani ya dakika chache tu alikuwa kwenye chumba 104 na baada ya kugonga mlango ulifunguliwa na Rose aliekuwa amejifunga taulo Rangi nyeupe kuanzia kwenye kifua na likaishia kwenye magoti.

Rose alimwangalia Roma kwa tabasamu flani hivi la kihuni na kisha alimshika ukosi wa shati na kumvutia ndani ya chumba na Roma na yeye alijilegeza na kuingia kizembe.

“Leo ni kutekwa staili” Ilisikika sauti ya Roma.

Upande wa Afande Maeda mara baada ya Roma kumuacha alipangusa simu ya kwa sekunde kadhaa na kisha akaweka sikioni.

“Mmefikia wapi?”Aliuliza.

“Yupo tayari kwenye Safe House Afande”

“Okey kazi nzuri”Aliongea na kisha aling’ata meno kwa hasira na kutoka eneo hilo .

*****

Ilikuwa ni siku nyingine kabisa Edna alienda kazini kama kawaida huku kazi ya kufuatilia makazi mapya aliachiwa Roma.

Upande wa Edna asubuhi hio aliweza kupokea simu kutoka kwa Suzzane akimwambia kwamba anakuja kuonana nae ofisini kwani kuna ripoti anataka kumpatia na Edna alikubali huku akiwa na shauku ni kipi ambacho Suzzane anataka kumwambia kwani alimpa kazi muhimu sana.

Edna mara baada ya kufika kazini aliweza kupita kwenye idara baadhi na kuweza kutoa maagizo na mpaka anakuja kumaliza idara zote ilikuwa saa tano kamili na aliweza kuingia ofisini kwake na kisha akatulia kwenye kiti chake na haikupita muda mrefu Recho aliingia na kumpa taarifa ya kufika kwa Suzzane na Edna alimpa ruhusa ya kuingia.

“Enhe umefikia wapi?”Aliuliza Edna mara tu ya kusalimiana na Suzzane.

“Taarifa zimekuwa ngumu sana kupatikana , tumejaribu kutumia mpaka pesa lakini inaonekana hospitali haina taarifa”Aliongea Suzzane na kumfanya Edna kunyong’onyea.

“Vipi kuhusu manesi au madaktari wa kipindi hicho?”

“Tumejaribu kufuatilia na tumeweza kupata wawili ambao walikuwa wakihudumu kwa kipindi hicho lakini taarifa zao ni za kusikitisha , wote walishapoteza maisha”

“Nadhani kulikuwa na changamoto kweli kwa Taifa kama Tanzania kwenye utunzaji wa kumbukumbu hata hivyo ni miaka mingi iliopita na teknolojia haikuwa kubwa sana”Aliongea Edna kwa namna ya kukata tamaaa na Suzzane alimwangalia Edna na kisha akauvaa ujasiri.

“Edna unachotaka kujua ni kuhusu mama yako kujifungua mapacha si ndio?”Aliuliza Suzzane na kumfanya Edna amwangalie Suzzane kwa mshangao.

“Suzzane nadhani nilikuambia tu utafute taarifa na sijakuelezea kama zinahusiana na mimi kuzaliwa na pacha wangu?”Aliuliza Edna.

“Ni kweli kabisa hata mimi swala hili sikulifahamu mpaka siku ya jana”Aliongea na kumfanya Edna kumwangalia kwa kiulizo.

“Unamaanisha nini?”Aliuliza Edna na Suzzane ilibidi amuelezee kwa ufupi namna ambavo aliweza kupokea simu kwa mtu aliejitambulisha kwake kwa jina la Chriss na kumuelezea namna ambavyo anajua nini kilimuua Dr Elvice Daniel na kuomba kukutana nae ili aweze kuongea nae.

Aliendelea kumwambia namna ambavyo alaiweza kuonana na Chriss ndani ya hoteli ya Eunice na namna mazungumzo yao yalivyokuwa.

Mpaka Suzzane anamaliza kuongea Edna alishangazwa mno na taarifa hio na kujawa na shauku pia ya kumjua Chriss.

“Kwahio umesema amezungumzia mimi kuzaliwa na pacha wangu!!?”

“Ndio anasema ataongea zaidi mara baada ya kukutana”

“Lini anataka tukutane?”

“Kaniambia kwanza swala lenyewe linatakiwa kuwa siri , na kuhusu mahali na muda ni mimi ninapanga na kumtaarifu”

“Okey hili ni swala muhimu sana kwangu , tutakutana nae kesho unaweza kupanga eneo lolote ambalo unaona litafaa na utanitaarifu”

“Boss napanga iwe kule mji wa kisasa kwenye nyumba yangu , ni sehemu salama zaidi”Aliongea Suzzane na kumfanya Edna kufikiria kidogo.

“Okey sio mbaya hata pale ni mahali sahihi zaidi”Aliongea Edna na Suzzane alitingisha kichwa na kisha kuaga. Wakiwa kwenye makubaliano ya siku inayofuata waweze kukutana na Chriss mahali anapoishi Suzzane.

*******

Taratibu zote za kuhamia kwenye nyumba mpya zilikamilika kwa asilimia mia moja na kila kitu kilihamishwa kwa msaada wa kampuni.

Hivyo Dorisi , Rose , na Nasra wakawa majirani , mama yake Nasra alionekana kushangazwa sana na ukubwa jumba hilo kiasi kwamba alimshukuru mara kibao Edna kwa kuwezesha swala hilo , ijapokuwa hata kule kwenye Apartment walipokuwa wakiishi palikuwa pazuri lakini eneo la jumba hilo palikuwa pazuri zaidi ukilinganisha na ukubwa wake.

Saa moja za jioni ndio muda ambao waliweza kumaliza kupangilia kila kitu na hata Sophia aliweza kurudi kuona mahali familia yake ilipohamia na alipapenda mwenyewe kutokana na uzuri wa nyumba lakini pia kufurahishwa na eneo kuwa kubwa mno ndani ya uzio tofauti na Oysterbay.

Kwasababu kila mtu alichoka na kazi nzima ya kupanga ilibidi waende kula mgahawani chakula cha usiku wazo ambalo Roma alipendekeza na kuonekana bora.

Na familia nzima walitoka na kwenda katika moja ya mgahawa uliokuwa ndani ya eneo hilo ambalo ulikuwa wa hadhi ya juu, ulikuwa ni mgahawa wenye floor mbili yaani juu na chini na Edna ndio alipendekeza wakakae upande wa juu na hilo ni kutokana na uwepo wa Sophia ambaye ni maarufu , hawakutaka usumbufu.

Baada ya familia nzima kuingia ndani ya eneo hilo , huku wakipotezea baadhi ya macho yanayowaangalia walikaa kwenye meza mbili tofauti lakini zilizokuwa karibu karibu huku wakiongea na kucheka.

Edna yeye alikaa meza moja na Lanlan, Sophia pamoja na Roma huku Qiang Xi , Mama yake Roma na Bi Wema wakikaa meza moja.

Wakati Edna akiwa bize kuangalia Menu ya chakula kwa ajili ya kuagiza kuna jambo lilimvutia macho Roma na kumfanya agune kiasi cha kumfanya Edna kumwangalia kwa mshangao.

Alikuwa ni mhudumu wa kiume aliechanganya rangi , alionekana kushikilia sinia ya plastic kubwa yenye sahani nne juu yake za vyakula huku akieleka kwenye meza moja ambayo imekaliwa na familia ya watu wanne mmoja ni msichana mdogo miaka kama kumi na tano hivi na mwingine alikuwa ni mvulana mkubwa kuliko msichana huku wakiwa na wazazi wao , mmoja alikuwa ni mzee wa makamo miaka kama hamsini hivi na mwingine mwanamama mweupe ambaye pia alionekana kuwa na miaka kama arobaini.

Roma alimwangalia yule muhudumu anavyoendelea kuweka sinia kubwa liliojaa sahani nne jumla yake , ambapo ilikuwa ni oda kwa wanafamilia ,moja kwa moja alijua huenda ndio kwanza wanafika hapo ndani kama wao .

Baada ya mhudumu yule kuweka oda ile kwa kila mmoja pamoja na vijiko na Umma alianza kupiga hatua na kuondoka lakini Roma palepale alinuia maneno flani hivi na Sahani zote nne ni kama zilipeperushwa na upepo chakula chote kumwagika.

Lakini ajabu ni kwamba licha ya tukio lile yule mwanaume shombe shombe mhudumu hakugeuka zaidi ya kuondoka na kushuka ngazi kuelekea chini huku wale wateja wakilalamika kwa kumuita na kufanya baadhi ya watu waliokuwa hapo ndani kushangazwa na kitendo hicho.

“Nakuja naenda kujisaidia”Aliongea Roma na kumfanya Edna kumwangalia kwa wasiwasi na kumtingishia kichwa aondoke , ni kama Edna alielewa kauli ya Roma ndio maana akawahi kuruhusu.

Roma alitembea taratibu mpaka chini na kisha akafuata mlango na kutoka nje na baada ya kutoka kwenye eneo la bustani karibu na maegesho aliangalia kulia na kushoto lakini hakuka sawa masikio yake yenye uwezo wa kusikia hata nzi alieoko mita kadhaa yalihisi mvumo wa kitu.

Swiiiii…!!” ulisikika mlio na palepale Roma alinyanyua mkono wake na kudaka kisu mfano wa Dagger kilichorushwa kumdhuru na alikiangalia mkononi nakukijuta akitoa macho ya mshangao.

“Zero assassin!!!” Kisu kile kilikuwa na nembo ya Zero Assasin na kujiuliza Zero wanafanya nini Tanzania

Roma aliangalia yule mwanaume na kuona akitokomea upande wa pili wa ukuta na Roma palepale alipotea na ile anaibuka alikuwa mbele ya yule mwanaume na kumshangaza.

“Who are you?”Aliuliza yule mwanaume kwa namna ya kushangaa

“Nikuulize wewe ni nani unaewekea watu sumu kwenye chakula huku ukitumia nembo ya kundi la New Zero Assassin”Aliongea Roma kwa kingereza na kumfanya bwana yule kushangaa kwa wasiwasi kutokana na kugundulika.

“Wewe ni nani?”Aliuliza kwa mara nyingine na Roma alimrushia kisu chake kwa namna ya kumrudishia na yule bwana shombe shombe alikidaka huku akishangaa shangaa akimwangalia Roma usoni..

Shughulli ya Yan Buwen inakuja

Mwendelezo ni jumapili au j4
Mkuje Watsapp kumenoga unalipia aftatu tu tupo sehemu ya 500 namba ya watsapp ni 0687151346
 
CK hamjamuelewa tu, fuatilieni story zake. Kuna Mathew Mulumbi huko ziko poa sana
Tatizo mathew hua ana mkoromea hadi mkuu wa nchi,kidizain inapoteza ladha ya story
 
SEHEMU YA 426.

Watu wote walirudi ndani na kumuacha Rose na Roma pamoja na Mzee Bakari wakitaka kusikiliza sababu yake , Roma hakutaka kwenda kuongea nae ndani kwani alijiambia kama mzee huyo asingekuwa na sababu ya kuridhisha basi angemuua hapo hapo na kumtupa majini.

“Nipe sababu ya kuridhisha nikuache hai?”Aliongea Roma.

“Mr Roma ni kweli kwamba nimefanya nilichokifanya , lakini kuna watu nyuma yangu ambao napokea maagizo kutoka kwao lakini licha ya hivyo lazima tufahamu kwamba likija swala la biashara haramu , mwenye nguvu ndio anaetawala na sio sheria”

“Hio ndio sababu , naona unajielezea pasipo ya kutoa sababu”Aliuongea Rose.

“Mr Roma nadhani unakumbuka tukio la Mzee Chino kuchomwa na kisu na majambazi?”Aliongea Mzeee Bakari na kumfanya Roma kushangaa kidogo huku upande wa Rose akishindwa kufahamu juu ya swala hilo.

“Unataka kusema nini?”

“Kuchomwa kisu kwa Mzee Chino hakukua kwa bahati mbaya bali ulikuwa ni mpango maalumu wa kukuangamiza”Aliongea Mzee Bakari na kumfanya Roma kuvutiwa na maelezo hayo.huku akikumbuka siku ambayo alimuokoa Mzee Chino kutoka hali ya kifo.

“Elezea vizuri maelezo yanyooke la sivyo sitokuacha hai”Aliongea Roma huku hasira zikianza kumtawala.

“Mzee Longoli ndio alienipa maelekezo ya kuandaa vijana kumjeruhi Mzee Chino, baada ya kupewa kwa maagizo hayo nilitaka kujua ni kwasababu gani kumjeruhi yule mzee kutokana na uhusiano wa Mzee Chino na Neema Luwazo na kwenye udadisi wangu nilikuja kugundua ni mpango wa kupata damu yako”Aliongea Bakari na kumfanya Roma palepale kumshika Shingo Mzee Bakari na kumkaba kwa kumning’niza hewani na kumfanya aanze kutapa tapa miguu na kukohoa.

Kitendo ambacho hata Rose aliogopa ijapokuwa hakujua sana kuhusu Mzee Chino lakini baada ya kusikia kuhusu damu alishaelewa usiriasi wa swala lenyewe , alikuwa akijua uwezo mkubwa wa damu ya Roma kwani hata yeye ilishawahi kumponyesha tena kwa zaidi ya mara mbili.

Roma baada ya kumkaba kwa nguvu kiasi cha Mzee Bakari kutaka kupoteza fahamu alimtupa chini na Mzee alijikuta akitapika pombe na mauchafu palepale huku akihema kwa shida.

“Nataka kusikia ukweli wote sio nusu nusu, niambie w ambao wanahusika kwenye swala ambalo umeongea?”Aliongea Roma kwa kuamrisha na Mzee Bakari na kitambi chake alikaa vizuri na kuanza kuelezea waliohusika .

“Vijana wangu ndio niliwapa kazi ya kufuatilia, nilifanya hivyo kwa namna ya kijihami , kwenye maisha yangu sijawahi kuamini mtu kabisa na ndio maana kila inapotokea misheni ambayo sina maelezo nayo ya kutosha nitaitimiza lakini huku nikihakikisha nachimba ukweli wote na hicho ndio nilifanya , ijapokuwa mpango huo ulikuwa wa siri lakini niliweza kujua aghalabu kwa kile kilichokuwa kikiendelea hii yote ni kuniepushia na kutumika na mwisho wa siku kutolewa kafara, watu wanaohusika kwenye mpango wenyewe najua wawili tu ni Mzee Longoli pamoja na Mchina mmoja ambaye ni mkuu wa jeshi la China anafahaika kwa jina la Afande Yang Gongming”Aliongea Mzee Bakari na Roma mara baada ya kusikia kuhusu jina la Afande Yang hakumfahamu mara moja , ni kama watu wote waliotajwa hapo hakuwafahamu.

“Mzee Longoli ndio nani hapa Tanzania?”

“Ni Jenerali wa jeshi mstaafu kabla ya Afande Gambino Tozo , mtoto wake ni mwanasiasa maarufu , mbunge na waziri wa sayansi na teknolojia”Aliongea na kumfanya Roma kuwaza kidogo.

Mpaka hapo alishaelewa kitu kimoja kikubwa sana, tukio la damu yake kuchukuliwa kwa kumtumia Mzee Chino, alijikuta akitabasamu kifedhuli kama kawaida yake.

“Sababu yako imeniridhisha angalau”Aliongea Roma na kumfanya Mzee Bakari kutoa macho ya mshangao.

“Ila haimaanishi nitakuacha hai?”Aliongea Roma na kumfanya Mzee Bakari kupagawa.

“Mr Roma uliahidi utaniacha hai , nilichokuambia ni kitu kikubwa sana”Aliongea.

“Kwanini unaamini ulichoniambia ni kitu kikubwa na hata hivyo sikukuahidi kama sitokuua nilikuambia unielezee sababu ya kuniridhisha ndio nitakuacha hai”Aliongea Roma na Rose mwenyewe alishindwa kumuelewa mpenzi wake.

“Mr Roma nilichokuambia ni jambo kubwa sana”.

“Hio ndio sababu ambayo itanifanya nikuue sasa hivi”Aliongea huku akiweka usiriasi kwenye macho yake kwa mara nyingine na kuanza kuachia nguvu ya kijini ya kuogofya

“Nielezee sababu ya kukuridhisha, kama akili zako zitakuwa timamu utajua ninachomaanisha”Aliongea Roma kwa namna ya kuamrisha na kumfanya Mzee Bakari kufikiria kwa muda.

“Mr Roma nadhani unataka kujua kwanini nimejua kwasababu gani nimesema ni taarifa niliokuambia kuwa kubwa kwako?”Aliongea Mzee Bakari.

“Safi , hicho ndio ninachotaka kujua kutoka kwako ukiniridhisha nitakuacha hai”

“Licha ya kuwa na undungu wa mbali na mheshimiwa kigombola , lakini vile vile mimi ni mwanajeshi kitendo cha intelijensia na nawajibika moja kwa moja kwa Afande Maeda”Aliongea na kumfanya Rose mwenyewe kushangaa lakini Mzee Bakari aliendelea kuongea.

Ni kweli kabisa Mzee Bakari licha ya kwamba alikuwa mmiliki wakundi la kihalifu la Black Mamba alikuwa ni mwanajeshi ambaye aliomba kustaafu na alivyostaafu ndipo alipoweza kuja kuwa mkuu wa mkoa wa jiji la Dar es salam kipindi cha uongozi wa Raisi Kigombola , sasa haikueleweka ni lini alianza kuwa shushu ndani ya mzunguko wa Raisi Kigombola..

Lakini anasema jeshi lilikuwa likichunguza baadhi ya matukio yaliokuwa yakiendelea ndani ya Tanzania nje ya idara ya usalama wa taifa, moja ya sababu kubwa za kuanzishwa kwa uchunguzi ni juu ya kifo cha Profesa Shelukindo na Safari za mara kwa mara za jenerali wa jeshi la China nchini Tanzania kutokana na kwamba hakuwa akija kikazi bali alikutana moja kwa moja na Mzee Longoli pamoja na Raisi Mstaafu Kigombola.

“Kwahio unasema kwamba mpango wa kuchomwa kwa Mzee Chino ulikuwa ukiujua na hivyo hivyo Afande Maeda alikuwa akiujua?”

“Mr Roma kama nilivyosema mwanzo sijadanganya kitu , kazi niliopewa ni kukusanya taarifa ya kila kinachoendelea katika vikao vya mstaafu kigombola , kuhusu Mzee Chino niligundua baada ya kufanya uchunguzi wangu mwenyewe binafsi nje ya ushushu kwa kutumia vijana wangu na mwanzoni sikuchukulia swala hilo kwa uzito kwani niliriripoti moja kwa moja kwa Afande Maeda na hata nilipomuelezea hakuonyesha kama ilikuwa taarifa kubwa kwake”

“Kwahio ulijuaje ni taarifa kubwa kwangu?”Aliuliza Roma.na Mzee Bakari alikurupuka na kutoa simu yake janja na kisha aliingia upande wa watsapp.

Ilionekana baada ya mambo kubadilika Mzee Bakari alitafuta msaada kwa Afande Maeda kwa njia ya mtandao wa watsapp, aliweza kuwasiliana nae kutokana na Boti hio imeunganishwa na Wifi.

Roma alijikuta akitabasamu kwa uchungu , alijiambia inamaana huyu Afande Maeda alikuwa akifahamu hili jambo muda mrefu halafu akakaa kimya alijiambia asipokuwa na maelezo ya kutosha atamkomesha. Pasipo kujali nafasi yake jeshini.

Mpaka hapo hakuwa na sababu ya kumuua Mzee Bakari , alijiambia moja kwa moja atadili na Mzee Maeda moja kwa moja, lakini hata hivyo kuna mambo makubwa zaidi ambayo alipanga kuyajua a, maelezo ya Mzee Bakari hakuyaamini alijua tu kama kuna watu amewaficha.

Na ni kweli kabisa Mzee Bakari Juma alikuwa amemficha Mheshimiwa Kigombola kwa uhusikaji wake wa moja kwa moja , hata hivyo licha ya kuwa shushu wa serikali lakini kwa wakati mmoja alikuwa akimchukulia Mheshimiwa Kigombola kama ndugu yake na ndio maana alipima uzito ni nani anafaa kutolewa kafara na mtu sahihi ni Longoli pamoja na Afande Yang Kutoka China

Roma sasa alijua moja kwa moja huenda damu yake ilitumika kutengenezea kopi yake , lakini jambo hilo lilimshangaza mno kwani kwa maelezo ya Profesa Clark ni kwamba hakuna uwezekano wa damu yake kuweza kutengenezea Clone kutokana na kwamba ikiguswa na hewa tu inapitia mabadiliko kutokana na kumulikwa na Divine Light.

……….

Roma baada ya kurudi ndani na Rose ilibidi ampatie maelezo kidogo juu ya Mzee Chino, kuhusu kilichotokea , Rose alishangazwa na jambo hilo mno.

“Babe sasa haitokuwa hatari?”

“Usijali sana , wakati nayaokoa maisha ya Mzee Chino nilihisi kuna kitu ambacho haikuwa cha kawaida kinaendelea lakini niliendelea kumfanyia matibabu kwasababu nilikuwa nikiamini hakuna uwezekano wa damu yangu kutumika kama siraha , lakini kama jambo hili limetokea kweli nitahakikisha nadili nalo mbele kwa mbele, haitokea kiumbe feki kikanizidi ujanja mimi”Aliongea Roma kwa kumhakikishia Rose.

“Babe mwili wako unaonekana kuimarika mno nadhani ni sahihi ukaanza kabisa mafunzo”Aliongea Roma na kumkumbusha Rose juu ya swala la yeye kwenda China.

“Babe ushapata mbunu rahisi ya sisi kujifunza?”

“Ndio nimefanikiwa kupata taarifa nyingi , lakini hata hivyo naendelea kuirahisisha , ninataka kwanza kile nilichopata nione kama kitafanya kazi”Aliongea Roma.

“Nipo tayari mpenzi kuanza muda wowote, ninatamani sana kuwa na uwezo wa kupaa kama ulivyofanya pale”Aliongea Rose na kumfanya Roma kucheka.

“Ukiweza kufanikisha kufika hata levo ya Mzunguko kamili utaweza kufanya mambo mengi ya ajabu hata kutembea juu ya maji”.

“Kweli!!!”

“Umeanza lini kutokuniamini?”

“Hapana sio kwamba sikuamini mpenzi , lakini nashindwa kabisa kuamini kama nitakuja kua na uwezo wa kupaaa angani , ni jambo ambalo mtu yoyote atashindwa kuelewa”Aliongea na Roma aliona ni sahihi kwa mtu wa kawaida kutoamini juu ya jambo hilo.

Baada ya masaa matatu hatimae saa kumi na moja kamili za jioni ndio muda ambao Roma aliweza kurudi nyumbani akiwa pamoja na Rose

Kurudi kwa Roma kuliwafanya wote kupata ahueni ya amani kwani walikuwa na wasiwasi.

“Mmeyamaliza?”Aliuliza Blandina.

“Ndio halikuwa jambo kubwa sana hata hivyo , ilikuwa kasafari ka kwenda katikati ya bahari na kugeuza”Aliongea Roma.

“Katikati ya Bahari?”Walijikuta wakiuliza wote kwa pamoja na Roma ilibidi atoe maelezo ya mafupi ya kile kilichotokea huku akiacha kugusia swala la damu , alifanya hivyo kwasababu angechukua muda mrefu kuwaelewesha.

Wote walimsikitikia Zonga mpaka mwisho wa stori , hawakuamini angechukua maamuzi ya kijinga ya namna hio licha ya kwamba alikuwa na makosa makubwa.

Baada ya Roma kumaliza ni kama hali ilibadilika ghafla sasa, Nasra na Amina wangeweza kurudi nyumbani , lakini kwa upande wa Dorisi na Rose nyumba yao ndio hio ilikuwa imelipuliwa , hivyo ni rahisi kusema kwamba hawakuwa na pakuishi..

Moja ya watu ambao walikuwa na shauku ya kujua nini kinaendelea hapo ndani ni Qian Xi , alikuwa akifahamu wanawake wote hao ni wa Roma , sasa wote wwapo ndani ya nyumba moja kwa mara ya kwanza, Blandina aliekaa karibu na Roma alimshtua kwa bega lake la kushoto..

“Roma kwahio tunafanyaje?”Aliuliza Blandina maana kwa namna yoyote mwenyewe aliona ni hivyo tu kulikuwa kuna tishio la usalama , lakini Rose , Nasra , Amina Dorisi hawakuwa na sababu kabisa ya kukutana na Edna wala kukaa pamoja nyumba moja kwani walikuwa michepuko tu..

“Mimi mwenyewe hata sijui tunafanyaje nawasikiliza nyie”Aliongea Roma akijifanyisha hakuwa akijua nini kinaweza kufuatia na alimwangalia Edna alietulia muda wote pembeni akionyesha hali ya kumtaka aongee jambo..

Edna alijikuta aking’ata lipsi zake na kukusanya ujasiri ,mpaka hapo alikuwa akijua Dorisi na Rose walikuwa wakiishi pamoja na nyumba yao ndio hio imepatwa na majanga.

“Nadhani Dorisi na Rose wanaweza kukaa hapa kwa muda kuna vyumba vya nje ambavyo vina hali nzuri havitumiki”Aliongea Edna.

“Miss Edna hilo halitowezekana vile vyumba mara ya mwisho navikagua Gypsum yake imeharibika”Aliongea Bi Wema na kumfanya Edna kuona aibu kidogo ni kweli kulikuwa na vyumba ambavyo mara nyingi vilijengwa kwa ajili ya wageni pamoja na wafanyakazi lakini hakuwahi kwenda kukagua.

“Nina pendekezo kwasababu kilichotufanya hapa kukusanyika ni usalama wetu , kwanini tusimpunguzie Roma majukumu ya kuhakikisha usalam wetu kwa kukaa majirani?”Aliongea Rose na kuwafanya wote kushangaa wazo lake , hata Roma ambaye alijifanyisha kukosa maamuzi alishangazwa na pendekezo hilo lakini kwa upande mmoja kuliona kuwa zuri mno.

“Ninachomaanisha tunaweza kununua nyumba mbili ambazo zipo sehemu moja , sehemu ambayo tunaweza kuwa majirani ili iwe rahisi kwenye maswala ya kiusalama”Aliongea Rose lakini wazo lake lilishangaza watu.

Ukweli Rose alitoa pendekezo hilo kwasababu tu alitaka kuwa karibu na Roma , Dorisi mwenyewe alipenda wazo hilo lakini aliogopa kumpa sapoti Rose wazo lake mbele ya Edna.

Roma alifurahishwa sana na akili za Rose aliishia kutingisha kichwa tu kwa tabasamu murua, huku akikosa aibu kabisa lakini hata hivyo amezoeleka kama mtu ambaye hana aibu na hata mama yake alishangazwa na hilo.

Edna alimwangalia Rose moja kwa moja kwenye macho yake , alichohisi kwenye akili yake aliona ni kama Rose anamchokonoa.

Familia yote akiwemo Roma mwenyewe walisubiri kusikia maamuzi ya Edna kwani yeye ndio mwenye mamlaka ijapokuwa msemaji wa mwisho ni Roma hivyo Roma asingetoa wazo tu la kusema waende wakaishi karibu ili aweze kuwatembelea wote kwa wakati mmoja.

Unafikiria Edna atakubaliana na wazo la Rose.
Hatariiiii
 
Ila mkuu asikuambie mtu nakupa big up... ngoja nasisi tujiandae ili tupokee mafunzo haiwezekan demu(rose) atushnde sisi....
 
Ila mkuu asikuambie mtu nakupa big up... ngoja nasisi tujiandae ili tupokee mafunzo haiwezekan demu(rose) atushnde sisi....
 
wazee wakupredict! unahisi ni nani yupo nyuma ya chris? na kazi gani asipoikamilisha, atakufa?.... toa maoni yako
 
wazee wakupredict! unahisi ni nani yupo nyuma ya chris? na kazi gani asipoikamilisha, atakufa?.... toa maoni yako
KWA MAONI YANGU
mkuu #singanojr.. mwenyewe ndio yupo nyuma ya chriss coz yeye ndiye atakayeamua yupi afe na yupi abaki
 
HAKUNA MWANDISHI ATAKAYEMFIKIA BEN MTOBWA DUUH. MWANZO TU NI MWAMBA!!!

KAMA maji ya bahari ya hindi yangekuwa na hisia, basi yangejisiskia fahari sana kwa kupata fursa nyingine ya kuiburudisha miili ya viumbe hawa wawili ambao walikuwa wakiogelea kandokando ya ufuko huku wakicheza na kucheka. Walifanya picha ya kuvutia sana, hasa sura zao nzuri zilipoibuka na kutoka majini na kumezwa na tabasamu lililosababishwa na mzaha waliokuwa wakifanyiana chini ya maji. Baada ya kuogelea kwa muda walirejea nchi kavu ambako walijibwaga juu ya mchanga ulioruhusu joto likaushe maji miilini mwao.

Ufuko pia ungekuwa na kila sababu ya kusherehekea johari ya kulaliwa na viumbe kama hawa kwani walioana kimaumbile kama pacha, ingawa hawakuwa mtu na dada yake. Walikuwa kama jozi ya kiatu cha kiume kwa cha kike. Mwanamume hakuwa mwingine zaidi ya yule kijana mwenye umbo refu, kakamavu, lililokaa kiriadhariadha na sura nzuri, yenye dalili zote za hekima, ushujaa na ucheshi. Kwa jina anaitwa Joram Kiango.
 
Back
Top Bottom