SEHEMU YA 431
Mpango wa Roma ulikuwa ni kwenda kumtoa Mzee Longoli huko huko kwenye kambi ya jeshi na kumuua mara tu baada ya kuona Yan Buwen kufanikiwa kutoroka ,aliamini huenda akimhoji mzee Longoli angeweza kujua ni wapi Yan Buwen kakimbilia.
Sasa Roma wakati alipokuwa akitoka katika makazi ya wanajeshi wake ndipo alipopata simu kutoka kwa Afande Kweka akihitajika kwenda kuonana nae bila kukosa na kutokana Afande Kweka kusisitiza ndio sababu iliomfanya Roma kufika nyumbani hapo ili kujua mzee huyo anataka kuongea nini.
Lakini kile ambacho Roma alitegemea mzee huyo kuongea ndio alichokutana nacho , lakini hata hivyo kulikuwa na kitu kingine ambacho aliweza kuelezewa na shukrani ziende kwa Zenzhei ndio aliweza kujua kitu kimoja muhimu sana.
Kwa maelezo ya Zenzhei hakukuwa na utofauti sana na maelezo ya Omari Tozo, Zenzhei anasema uhusikaji wa Afande Yang katika mipango ya Yan Buwen ni kutokana na mgogoro wa siri unaonendelea ndani ya serikali ya China ,mgogoro unaosababishwa na Hongmeng kuingilia mambo ya kisiasa na kijeshi.
Lakini kubwa zaidi ni kwamba miaka kadhaa iliopita kuna mwanasiasa mkubwa ndani ya taifa la China aliekuwa akiwania kiti cha uraisi alikufa kifo cha kutatanisha ambacho kwa uchuguzi wa chini ilifahamika kwa watu wachachekwamba aliuliwa na Hongmeng.
Mwanafamilia huyo alikuwa akitokea katika ukoo wa Afande Yang akiwa kama kaka wa bwana Yang Gongming , inasemekana mwanasiasa huyo hakupendwa na Hongmeng kuongoza nchi lakini wakati huo huo alikuwa akipendwa sana na raia na hio ndio sababu iliopelekea Hongmeng kumuua , sasa kitendo cha mwanafamilia kuuliwa kilitengeneza kisasi kati ya familia ya Afande Yang na Hongmeng.
Lakini licha ya kwamba ukoo wa Yang wanakisasi chao na Hongmeng hawakuwa na uwezo wa kuwafanya lolote , kwani walikuwa na nguvu kubwa hususani kwenye kuvuna nishati ya mbingu na ardhi yaani mbinu za kijini.
Sasa Afande Yang alitaka kulipiza kisasi cha kaka yake lakini nguvu hana na katika kuwaza namna ya kulipiza kisasi ndipo alipoigeukia sayansi , aliamini kwa sayansi tu ataweza kuiangamiza Hongmeng na katika jitihada zake ndipo alipoingia mwanasayansi nguli aliejizolea umaarufu afahamikae kwa jina la Yan Buwen kutoka ukoo wa Yan.
Sasa unachotakiwa kuelewa ukoo wa Yan pia haukuwa ukiwapenda Hongmeng yote hio ni kutokana na kwamba licha ya kuwa na nguvu kiuchumi lakini kwenye maswala ya siasa hawakuwa na nguvu kwasababu hawakuwa chaguo la Hongmeng, hivyo kuishia kuwa chini ya koo nyingine kama ukoo wa Ning ambao ni mahasimu wao wakubwa na walikuwa ni kama wakusubiria fursa tu ya siku itakapotokea kuondoa ushawishi wa Hongmeng..
Sasa baada ya Afande Yang kuleta pendekezo namna ya kuondoa utawala wa Hongmeng kupitia sayansi ndipo walipomshawishi mtoto wao Yan Buwen kuendeleza misheni kwa kugundua siraha ambazo zingekuwa na nguvu kubwa sana ili siku waweze kushinda vitisho vyote kutoka Hongmeng.
Sasa Afande Yang asichokijua ni kwamba wakati yeye mpango wake ukiwa ni kuiangamiza Hongmeng kwa kumtegemea Yan Buwen upande mwingine mtu anaemtegemea alikuwa na mipango yake.
Yan Buwen yeye hakuwa na mpango kabisa na Hongmeng na hio ni mara tu baada ya kukutana na mrembo Athena , yeye nia yake ilikuwa ni kuwa na uwezo wa juu kumzidi Athena ili aje kumuweka chiini ya himaya yake na hatimae kupata kitumbua chake.
********
Umbali kutoka barabarani ni mbali kuliko umbali kutoka baharini , hapo ndipo ilipokuwa nyumba ya Tajiri Kanani ndani ya eneo la Mbezi Beach, tajiri anaesifika kwa kumiliki visima vingi vya mafuta na biashara zisizohamishika(Real estate).
Ndani ya jumba hilo kubwa anaishi Mzee Kanani na mtoto wake Amina tu hio yote ni kutokana tajiri huyu alikuwa na ngugu wachache sana , na ndugu hao wachache wengi wao walikuwa na maisha yao mbali na yeye , hivyo ni mara chache sana ndani ya nyumba hio kuwa na watu wengi ukiachana na wafanyakazi wa ndani.
Lakini siku mbili hizi hali ilikuwa tofauti kidogo , hili ni kutokana na kwamba Mzee Kanani alikuwa amesafiri kwenda nchini India hivyo nyumba yote alibakia Amina mtoto wake pekee pamoja na mfanyakazi wao mmoja.
Muda wa saa kumi na moja siku hio Mfanyakazi wao alikuwa ametoka kwenda kununua mahitaji ya maandalizi ya chakula cha usiku , hivyo nyumbani alibakia Amina pekee pamoja na mlinzi wa geti.
Wakati Amina akiwa ameketi kwenye masofa eneo la sebuleni akiwa ameshikilia kitabu cha riwaya kilichoandikwa kwa lugha ya kingereza akijisomea , mlango wa mbele wa nyumba yao ulifunguliwa taratibu na kisha ukafungwa kwa ndani.
Jumba hilo limejengwa kwa staili ya kipekee ,mtu anaeingia kutoka nje hawezi kuonekana moja kwa moja kutoka eneo la sebuleni , kwani ukiingia tu ndani kitu cha kwanza unachokutana nacho ni ngazi za kupandisha floor za juu.
Hivyo kwa Amina aliekuwa amekaa eneo la sebule akiwa ameangalia upande wa nje wa bustani k na madirisha kuwa makubwa , hakujihangaisha kuzungusha shingo kugeuka kuangalia anaeingia kwani alijua lazima atakuwa ni mfanyakazi wao wa ndani ambae aliaga anaenda Supermarket.
Lakini sasa kuna hisia zilisambaa kwenye mwili wake na kumfanya kugeuka haraka na hapo ndipo alipopigwa na mshangao mara baada ya kugundua mtu aliekuwa mbele yake hakuwa mfanyakazi wao , bali alikuwa ni mwanaume alievalia tishet nyeupe pamoja na Jeans huku akiwa amechomeka miwani ya jua eneo la kifuani , kilichomuacha hoi Amina ni kwamba mwanaume huyu alikuwa Roma mtupu.
Amina ambaye alikuwa amevaa mavazi ya kulalia ambayo mara nyingi hupendelea hata ikiwa mchana alijikuta akishindwa kuongea na kuishia kuachama na kurudi zaidi nyuma ya Sofa kwa wasiwasi.
Ijapokuwa mwanaume aliekuwa mbele yake alikuwa akifaana kwa vitu vingi kama Roma , lakini kilichomfanya kugundua haraka sio Roma ni kutokana na namna mwanaume huyo anavyomwangalia , alikuwa na macho makavu zaidi ambayo yamejaa usuriasi ndani yake , aina ya mwonekano ambao hakuwahi kumuona nao Roma, kwake mtu aliekuwa mbele yake ni kama nyoka ambaye anajiandaa kutema sumu, alijikuta akianza kutetemeka huku akishika simu yake na mkono wa kushoto.
“You… Are you clone?”Aliongea kwa sauti akiwa kwenye mshituko akiuliza ndio Roma feki yaani kopi yake.
Shukrani ziwaendee wanajeshi wa The Eagles kwani kwa maagizo ya Roma waliweza kumpatia kila mwanamke ‘Bracelet’ za kuvaa mkononi ambazo urembo wake umetengenezwa kijasusi zaidi kama njia ya mawasiliano ya dharula , ili kuwa rahisi wakati wa hatari kupiga simu ya dharula iwapo simu itakuwa mbali.
Na hicho ndicho alichokifanya Amina , kwani mara baada ya kurudisha mkono nyuma aliweza kukandamiza ile Braceler na simu kwa nguvu mpaka alipohakikisha mawasiliano yametoka..
Hata kama asingepata muda wa kubonyeza kitufe, The Eagles tayari walikuwa washafahamu ujio wa kopi ya Roma ndani ya nyumba hio , lakini kwasababu walikuwa wamepewa maagizo na mfalme Pluto watoe taarifa tu pasipo ya kupambana ndicho walichofanya , lakini utofauti ni kwamba taarifa yao ilichelewa kuliko ile ya Amina.
“Mhmph” Roma feki alitoa tabasamu la kebehi kwa kuguna na kisha akaenda kuketi kwenye sofa huku akiuchunguza urembo wa Amina.
“Relax I have no interest in killing you , humiliting you infront of him would be much better , Wouldn’t it?”
“Kuwa mpole sina mpango wowote wa kukuua , kukudharirisha mbele yake ndio itakuwa jambo zuri zaidi , Si ndio?”Aliongea na kumfanya mrembo Amina uso wake kupauka kwa woga huku mwili ukitetema.
Lakini muda huo huo ghafla mtu aliingia kwa spidi isiokuwa ya kawaida na kumshika yule mwanaume shingo na kumuinua juu ka kumning’iniza.
“Kumdharirisha , labda kama unajisemea mwenyewe”
Alikuwa ni mtalamu Roma Ramoni ambaye tayari amefika hapo kwa namna ya kuteleport kutoka sehemu aliokuwepo mara baada ya kupata mawasiliano ya Amina.
Roma awamu hii alionekana kuwa kwenye hasira ya kiwango cha juu , huku macho yake yakiwa yashabadilika rangi na kuwa ya njano na kilichosambaa eneo lote ni nguvu za kijini ambazo zilikuwa zikiashilia mauaji na kufanya hata nywele za Amina kusimama.
Amina alijikuta akipoa kwa ahueni mara baada ya kugundua aliefika hapo ghafla alikuwa ni Roma halisi.
Roma feki alionekana kupaniki kidogo kutokana na kuvamiwa ghafla lakini hata hivyo alimwangalia Roma kwa dharau
“We will have to see about that , Pluto now die…”
“Tutaona kuhuu hilo , Pluto sasa kufaa”Aliongea Roma feki kwa sauti kubwa na palepale hali ya hewa ilibadilika na kilichoonekana ni kama anga likicheza huku likitengeza mawimbi kama yale ya baharini , lilikuwa jambo la kushangaza kwani kilichofanyika ni kama wakati Rroma alivyokuwa akipambana na Poseidon , Roma feki alionekana kutumia kanuni za anga.
Amina aliekuwa amesimama kando ya Sofa alivyoonekana ni kama vile mtu anavyoona kivuli cha sura yake kwenye maji yanayocheza cheza lakini utofauti hapo ni kwamba Amina hakuathirika kwani Roma alishamwekea ukuta wa kinga kwa kumzingira na nguvu ya Kijini ya Kimaandiko.
“Sikujui wewe ni aina gani ya miungu lakini inaonekana kabisa uwezo wako wa kudhibiti kanuni za anga ni mdogo mno , Yan Buwen kawa kichaa mpaka akaaamua kukutoa kafara?”Aliongea Roma kwa lugha ya kingereza huku macho yake yakiwa vile vile ya rangi ya njano huku mwili wake kutokuwa na aina yoyote ya mabadiliko.
“This is just the appetizer, The main course is yet to be served …”
“Hiki ni kama kionjo tu , shughuli yenyewe bado..”Roma feki aliongea huku akitoa tabasamu la kebehi akimwangalia Roma halisi kama kituko..
Lakini palepale Roma alijikuta akihisi akili ya ubongo wake ikitoa mivumo ya sauti zisizoeleweka , ilikuwa ni kama mtu ambaye anachanganyikiwa ghafla na kitendo kile kilimfanya kushindwa kufanya maamuzi ya haraka , kwani palepale kulitokea mkandamizo wa hewa usio wa kawaida ambao ulifanya viungo vya mwili wake kuvutana, yaani ni kama kila kiungo kilikuwa kikiukataa mwili wake na kutaka kuchomoka na maumivu yalikuwa makali mno, alikuwa amesimama akishindwa kufanya chochote kwani alikuwa akijaribu kuifanya akili yake kuruhusu nguvu zake kudhibiti viungo vyake , lakini ni kama alikuwa akishindwa kwani akili yake ni kama ipo kwenye hali ya kuchanganyikiwa , kilichomshagaza ni kwamba mtu Roma feki alionekana kutofanya jitihada zozote na nguvu iliokuwa ikisambaa ni kama vile ni nguvu yake ile ya kimaandiko.
“Kufa…!!!”
Kopi ilibwatuka kwa sauti na palepale iliachia pigo kwa kunyumbulisha kanuni za anga na kutengeneza presha kubwa kama ya bomu na kisha akailekezea yote kwa Roma.
Lakini akili Roma ilionekana kurudi na palepale kwa haraka sana aliita nguvu zake za kijini kwa namna ya kunuia na palepale pigo la wimbi lililorushwa kwake likatawanyika na kufanya vioo vya nyumba kupasuka palepale na upepo mwingi ulitoka nje.
Ilikuwa ni kama vile bomu linapolipuka ndani ya nyumba, lakini utofauti ni kwamba hakukuwa na moshi wala moto, hapa ni upepeo tu ambao umepasua madirisha na kukusanya vitu vyote vyepesi na kuvirusha nje.
“Wewe ndio unakwenda kufa leo hii”
Aliongea Roma Roma na palepale alimsogelea Roma feki kwa spidi huku akitumia nguvu zote kuharibu ngao yake aliojitengenezea na kumpiga kwa ngvu eneo la kifuani.
“BAM…!”
Kopi ilikwenda kutua kwenye ukuta na kufanya nyumba yote kutetema, Ngumi ya Roma ilionekana kuwa nzito mno kwani ilikifumua kifua chote cha adui yake na kufanya damu kusambaa. mpaka ile tisheti aliokuwa amevalia ikichanika na kuacha eneo ngumi Sugunyo ya Roma ilipomoa kuonekana vyema.
Lakini ajabu ni kwamba licha ya Roma feki kupigwa na ngumi ile , hakuonyesha hali yoyote ya kuugulia maumivu , bali kitu cha kushanganya ni kwamba mwili wake ulikuwa ukipona kwa spidi ya haraka sana na kifua chake palepale kilifunga na kuonekana kama hajapigwa na kitu chochote jambo ambalo lilimfanya Roma kutoa macho, alichotegemea ni kutawanyisha mwili wa adui yake hapo hapo ili kumua , lakini cha ajabu ni kwamba alichofikiria ilikuwa tofauti kabisa.
“Hahaha… kidogo unaonyesha kuleta ushindani hakika una kila sifa ya kuwa adui yangu , inavutia , inavutia , inavutia , una nguvu kubwa kuliko nilivyokuwazia Hades”Aliongea Roma feki huku akijiweka sawa kwa kuzungusha kichwa kwa majigambo kama vile hakuna kilichomtokea.
“Yan Buwen ndio kawezesha kuwa na huo uwezo?”Aliuliza Roma kwa mshangao.
Hakika ilikuwa ni sahihi kusema Roma alikuwa akipigana na kopi yake , kwani alihisi kuna uwezekano asipokuwa makini anaweza kuzidiwa akili.
“That is right our master gave us ability to revive ourself , we are immortal hahaha..”
“Upo sahihi Master wetu katupa uwezo wa kujifufua wenyewe , Hatuwezi kufa milele”Aliongea huku akiuangalia mwili wake kwa namna ya kujisikia wa thamani sana na kisha akamwangalia Roma.
“Hata Zeus na Athena hawatokuwa na uwezo wa kushindana na Master, nimekuja kukuonyesha robo tu ya uwezo wake wote, Master anasema unamiliki uwezo wa kipekee sana ambao anahitaji kuutunza na kama utakubali kuwa chini yake anaahidi atakuacha uendelee kuishi”Roma feki aliongea huku akijitahidi kumsifia aliemtengeneza.
“Pumbavu kabisa , ninakwenda kukuharibu sasa hivi”
Roma alikasirishwa na majigambo yake na pale pale aliita nguvu za kichawi kwa kugonganisha nishati ya mbingu na Ardhi , mkono wa kushoto alitumia kudhibiti nishati zinazotokana na mbingu na mkono wa kulia alitumia kudhibiti nishati zinazotokana na Ardhi na palepale aling’ata meno kwa hasira na kukusanya vinganja vyake kwa pamoja.
Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana kiasi kwamba Roma feki alishindwa kuelewa kinachofanyika ni nini lakini mpaka anakuja kuelewa ni kama mwili wake unalazimishwa kuingia kwenye kijishimo kidogo kwa kusindiliwa.
Yaani hakuguswa popote lakini alikuwa akielea hewani kama tufe na Roma aling’ata meno kwa hasira zaidi na kwa nguvu zote alitoka nje kwa spidi na ile anatua aridhini aliviminya viganja vyake kwa nguvu kama mtu anaepasua yai na pale Roma feki alitawanyika kama bomu na kila kiungo kujitenganisha , ni nyama nyama zilizotawanyika na kutua na kusambaa kwenye eneo lote la bustani ndani ya eneo hilo.
Katika mafundisho ya kivita, kwenye kupambana na adui kuna kanuni nyingi lakini moja wapo ni mbili ambazo ni muhimu , kuna siraha ambayo unategemea kumkuta nayo adui yako hivyo utajiandaa kukabiliana nayo kwa kutafuta udhaifu wake lakini pia kuna ile siraha ambayo hutegemei kumkuta nayo adui yako hivyo utajipanga kukabiliana nayo katika uwanja wa vita , sasa ili ushinde akili yako ndio inatakiwa kufanya kazi kwa haraka sana kutafuta udhaifu wa kudhibiti siraha hio.
Roma kitendo cha kumpiga adui yake kwenye kifua kiasi cha kukitawanyisha kuna jambo aliweza kugundua palepale , ni kwamba Roma feki uwezo wake ulipungua kidogo na hili ndio lilimpa matumaini kwamba atashinda , aliamini kujigamba kote kuwa ‘immortal’ ni uongo , hivyo aliamini kama atauchangua mwili wake mara nyingi mwishowe atakufa.
Kanuni ya pili muhimu ya vita yoyote ile ni kujiamimisha kwamba una nguvu kuliko adui yako hata kama adui yako ataonyesha nguvu kubwa kuliko wewe wakati wa vita , ni mbimu ambayo hata kwenye maisha ya kawaida hutumika sana , ukiona changamoto iliokuwa mbele yako kuwa kubwa siku zote utashindwa lakini ukijichukulia wewe ni mkubwa zaidi kuliko changamoto inaashiria unauosogelea ushindi.
Wakati Roma akitafakari hayo , alijikuta akipatwa na mshangao mwingine , vipande vya nyama vilivyosambaratika viliaanza kujikusanya upya kwa spidi ya ajabu kama vile ni nyuki wanavyotua kwenye mzinga na hata matone yote ya damu pia yalivutwa sehemu moja.
Roma hakutaka kufanya ujinga palepale alituma wimbi lingine la nguvu ya kijini na kupasua mwili wa Clone na kuusambaratisha ili kutoruhusu Roma feki kujirudisha hai.
Roma alishindwa kuelewa ni jiwe la kimungu tu ambalo ndio limewezesha hayo yote lakini hakuwa na muda wa kufikiria .
Kitu kingine palepale kilimfurahisha , alihisi miale flani ikisambaa eneo lote kama mfano wa sumaku na hapo hapo alielewa kila tone la damu , nyama na mifupa vimeunganishwa na nguvu inayovutana pamoja , na ndio chanzo cha kujifufua.
Roma alichokifanya ni kutengeneza moto mkali wa kichawi na kukausha matone ya damu na kuyesha kila kipande cha nyama ya Clone na palepale ile miale kama ya sumaku ilipotea na Clone kuyeyuka palapale na kupoteza uwezo wa kurudi hai upya hivyo ndio ukawa mwisho wa Roma feki.
Roma alijikuta akitabasamu kifedhuli na pale pale hakutaka kupoteza muda alirudi haraka sana ndani alikomuacha Amina
Amina alikuwa amekusanywa na nguvu ya kijini upande wa kona huku akiwa kwenye mshituko usio wa kawaida ni kama alikuwa ndotoni kwa kile ambacho ameshuhudia na alitamani make kutoka kwenye ndoto.
Roma alielewa mshituko aliokuwa nao Amina hivyo alimsogelea kwa haraka sana na kumkumbatia na pale pale aliachia nguvu ya kijini na kuutawala mwili wa Amina na mapigo yake ya moyo yalianza kurudi kawaida.
“Kila kitu kimekuwa sawa kwa sasa na hawezi kurudi tena, unaweza kupunguza wasiwasi sasa”Aliongea Roma kwa lugha ya kingereza akijitahidi kumpoza Amina aliekuwa kwenye mshituko.
*******
Upande mwingine ndani ya Apartment anayoishi Suzzane mwanaume alieitwa Chriss hakupewa hata nafasi ya kuongea tena , kwani mwanamke mrembo alietokeza kwa namna isieolezeka mbele ya Edna na Suzzane alimyonga palepale pasipo ya kutumia nguvu kabisa na ukawa mwisho wa Chriss.
“Persephone nimefurahi kukutana na wewe kwa mara ya kwanza , naitwa Clelia Allisanto”
“Wewe.. ni ni … Katibu mkuu wa umoja wa mataifa?”Aliuliza Edna huku akimkumbatia Suzzane na kurudi nyuma pasipo kupokea mkono wa mwanamke aliejitambulisha kwao kama Clelia Allisanto ilikuwa ngumu kuamini kama mwanamke huyo ndio yule ambaye ametambulishwa siku chache zilizopitakama mwanamke wa kwanza kuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa.
Yule mwanamke alitabasamu kwa namna ambavyo Edna na Suzzane walivyo kwenye mshituko na wala hakuonyesha kujali.
“Nadhani kwa hali yenu ya mshituko siwezi kuongea zaidi , lakini mimi sio Clelia Allisanto mnaemjua bali mimi ninaejitambulisha kwenu , hata hivyo siku yangu ya leo ni ya kipekee kwani nitakupa zawadi niliokuandalia kwa zaidi ya miaka elfu moja iliopita”Aliongea na palepale alizungusha mkono wake hewani kimaajabu na sehemu aliozungusha mkono anga lake lilionekana kama vile maji yanayoanza kuonyesha dalili ya kuchemka na palepale likatema boksi lililotengenezwa katika mfumo wa kioo lakini ndani yake kulikuwa na mmea mdogo uliochomoza ua la rangi ya bluu.
“Hii ni zawadi yangu kwako , ni ua adimu sana ambalo mpaka leo hii inaaminika mmea wake ushapotea kwenye uso wa dunia, linafahamika kwa jina la Blue Orchid, ni ishara yangu kwako kukutana na wewe leo , unaweza kufikisha salamu zangu kwa Hades kwa kile ulichoshuhudia leo hii”Aliongea Athena na kisha alitoa tabasamu murua sana na kuweka lile boksi kwenye meza ya kioo na kumwangalia Edna aliekuwa ameshikwa na mshangao na kutabasamu kwa namna ya pekee na kisha akapotea palepale.
Suzzane alipoteza fahamu muda ule ule kwa kudondoka chini, lakini upande wa Edna macho yake yote yalikodolewa boksi la kioo lililoachwa kwenye meza , huku akishindwa kupiga hatua hata moja na alikuwa hana hata uelewa muda huo kama Suzzane amepoteza fahamu na hakuna neno hata moja ambalo ameelewa kutoka kwa yule mwanamke.
“Ngo.. ngo . ngo”Sauti ya kugongwa kwa nguvu kwa mlango pamoja na kengere ya Apartment hio ndivyo vilivyomshitua kutoka kwenye mshangao.
“Suzzane..!!!”Aliita Edna kwa nguvu na kuchuchumaa na kumshika Suzzane kwa kumtingisha na palepale ndipo alipojua mwenzake amepteza fahamu , alikimbilia mlangoni na kwenda kuangalia mtu anaegonga na alijikuta akipumua na kufungua mlango kwa haraka.
“Madam upo salama?”Ilikuwa ni sauti ya Adeline , lakini Edna alishindwa kumpa jibu na kumfanya Adeline kuangalia eneo la Sebuleni ndipo alipooana mwili wa Chriss uliopo chini kwenye sakafu ukiwa hauna uhai , lakini pia kushoto kwake aliona pia mwili wa suzzane ukiwa chini ,aliingia kwa haraka sana na mtu wa kwanza kwenda kumshika ni Suzzane na alimpima kwa kidole na kugundua hajafa , alimsogelea Chriss na kumshika na kugundua alishakufa m alijikuta akiangalia juu ya meza na macho yalimtoka na kumgeukia malkia Persephone na kumwangalia kwa mshangao.
“Yupo kwenye mshituko, afya yake ni kipaumbele”Aliongea Edna kwa sauti iliokuwa na wasiwasi akimnyooshea kidole Suzzane aliekuwa chini.
“Sawa Madam”Alijibu Suzzane na palepale alitoa simu ya upepo alioficha karibu na ilipo bastora yake na alionekana kuita msaada.
Dakika chache mbele waliingia wanajeshi wengine wazungu wa kundi la The Eagles jumla yao watatu na walishangazwa na hali iliokuwepo , lakini Adeline hakuwa na muda wa kuongea , aliwapa maelekezo kundoa mwili wa Chriss na pia kumtoa Suzzane hapo ndani kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya huduma ya kwanza na maagizo yalifanyiwa kazi kijeshi kwani ndani ya dakika chache tu Edna na Adeline walibakia.
“Madam nitakusindikiza kurudi nyumbani”Aliongea Adelina kwa lugha ya kingereza na kumfanya Edna kuitikia kwa kichwa na kuusogelea mkoba wake uliodondoka chini na kuubeba, lakini alipotaka kupiga hatua aligeukia boksi la ua na kulinyanyua juu na kuangalia ndani na aligundua licha ya kwamba ni mmea halisi , lakini lilikuwa limekaushwa kwa namna ya kuhifadhiwa.
Adeline kwakua alikuwa akimheshimu Edna kama malkia Persephone alishindwa kuuliza kitu chochote na kumwangalia Edna kwa wasiwasi.
“Edna hakupanda gari kuelekea nyumbani bali , alitaka kwenda kwenye kituo cha afya alikopelekwa Suzzane.
Ni ndani ya nusu saa mbele Roma aliweza kufika mji mpya akiwa na wasiwasi na hio ni mara baada ya kupewa taarifa na Adeline juu ya kile kinachoendelea.
“Edna nini kimetokea?”Aliuliza Roma mara baada tu ya kuingia kwenye wodi ambayo alimkuta Edna na Suzzane wakiwa wamekaa kitako wakiangaliana kwa namna ya kujadili.
Edna alishindwa kujibu swali la Roma moja kwa moja bali alimpa ishara ya kuangalia kiboksi cha zawadi aliopewa na Clelia Allisanto.
“Ghost Orchid”Alitamka Roma na kunyanyua kile kiboksi kwa namna ya kulichunguza huku na yeye akiwa kama haamini kuliona hapo ndani, hata hivyo sio mara yake ya kwanza kuliona ndio maana aliweza kulitambua haraka sana.