Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SinganoJr. J4, Alhamis na Jimamosi... Jmos ndio leo sasa tupia mzigo.
 
Daaah nlivoona txt yko nkajua mambo tyari
Mkuu kuwa mpole! singanojr ni mtunzi/msanii mahiri! Elewa hlo! Ameingia kwanza kuangalia hadhira yake imekaaje! Ipo tayari au haipo tayari! Kwa mfano angeingia akakuta post ya mwisho ni yake! Angepost? Hapo mwamba katuona tupo na kiu kali anaweza akakasirika akatiririsha hata sasa hivi tu! Unamchezea alaa! Lkn pia tumejua yupo fit that was a kind of greeting
 
Kuna scene moja hivi amazing mwamba singanojr kairuka makusudi! Ile ya raisi senga na mwenzake njoroge wa kenya wakiliwa kiboga na mafirii masoni! Au labda mwamba kawawekea huko wasapu? Hapa yaliwekwa maandalizi tu!
Kwa makusudi kabisa Aliiheshimisha taasisi ya uRais sio😃😃
 
HAKUNA MWANDISHI ATAKAYEMFIKIA BEN MTOBWA DUUH. MWANZO TU NI MWAMBA!!!

KAMA maji ya bahari ya hindi yangekuwa na hisia, basi yangejisiskia fahari sana kwa kupata fursa nyingine ya kuiburudisha miili ya viumbe hawa wawili ambao walikuwa wakiogelea kandokando ya ufuko huku wakicheza na kucheka. Walifanya picha ya kuvutia sana, hasa sura zao nzuri zilipoibuka na kutoka majini na kumezwa na tabasamu lililosababishwa na mzaha waliokuwa wakifanyiana chini ya maji. Baada ya kuogelea kwa muda walirejea nchi kavu ambako walijibwaga juu ya mchanga ulioruhusu joto likaushe maji miilini mwao.



Ufuko pia ungekuwa na kila sababu ya kusherehekea johari ya kulaliwa na viumbe kama hawa kwani walioana kimaumbile kama pacha, ingawa hawakuwa mtu na dada yake. Walikuwa kama jozi ya kiatu cha kiume kwa cha kike. Mwanamume hakuwa mwingine zaidi ya yule kijana mwenye umbo refu, kakamavu, lililokaa kiriadhariadha na sura nzuri, yenye dalili zote za hekima, ushujaa na ucheshi. Kwa jina anaitwa Joram Kiango.
sasa tukusaidieje bwana ben mtobwa?
 
We have been waiting for it for too long singanojr drop it now.

Because we have a thirst with this story.
 
Huyu mwamba akibembelezwa sana sometimes anajiona kama vile yeye ndiye mfalme ni Bora kumpotezea TU atapost atakapojisikia.
Mbungi inapigwa saa 4 usk...kaka mbali na hapa watu wana majukumu mengi...enjoy, relax and cool down...atamwaga mzigo tu!!
 
SEHEMU YA 429.

Bwana yule hakuweza kupata ujasiri wa kukimbia kutokana na kwamba alishajua Roma sio saizi yake kwa namna ambavyo ametokea mbele yake , aliishia kumwangalia Roma na kujiuliza huyu mtu ni nani.

“Sauroni anafanya kazi gani , nilishamkataza Zero kufanya kazi ndani ya mataifa ya Afrika , Umeigiza kuwa mhudumu na kutia sumu kwenye chakula cha wateja kwa ajili ya kuwaua , umefanya kwa kuagizwa au umesaliti kundi la Zero?”Aliuliza Roma akiwa siriasi.

New Zero Asassin ni kundi la Roma analolomiliki , wakati alipokuwa ajent 13 alikuwa akipokea oda kwa nembo ya kundi hilo kabla kabisa ya kukutana na Hades na kupitia kundi hilo la Ninja aliweza kukutana na Malkia Catherine ndani ya jiji la Milan Itally ni kundi ambalo halifanani kabisa na Zeros Organisation kwani kazi ya kundi hilo ilikuwa ni kuua tu kwa kulipwa.

“Umetaja jina la kiongozi wetu , Sikujui wewe ni nani na chanzo cha taarifa yako kuhusu kundi letu ni kipi, lakini ni kweli Zero haijawahi kufanya misheni yoyote hapa Tanzania na hii ni ya kwanza baada ya kiongozi wetu kutangaza kundi linaweza kufanya misheni yoyote ndani ya dunia na nashindwa kwanini unaingilia hili swala huogopi Zero kuchukua hatua zidi yako?”Aliuliza yule bwana kwa lugha ya kingereza

“Nani katangaza kundi linaweza kufanya misheni dunnia nzima , hata kama ni kiongozi wenu hana mamlaka hio”Aliongea Roma kwa mshangao

“Ofcourse it wasn’t the leaders command , His Majestu Pluto was the one who gave the command! He permitted us to accept request in China and Africa”

“Hakika sio Sauroni alietoa magizo, Mfalme Pluto mwenyewe ndio alietoa maagizo ya kukubali maombi yote ya misheni kufanyika ndani ya China pamoja na Afrika”

Roma alishangaa ni kweli kabisa kundi lake liliacha kufanya misheni ndani ya bara la Afrika na taifa la China kwa ujumla wake lakini jambo linalomshangaza na kumchanganya ni kusikia kwamba yeye ndio katoa maagizo ya masharti kuvunjwa.

“Unamaanisha Pluto mwenywe ndio katoa maagizo?”Alimuuliza yule bwana.

“Inaonekana unaelewa operesheni zetu ndani ya Zero hivyo hivyo kumfahamu kiongozi wetu mkuu Mfalme Pluto , Sasa ushanifahamu mimi ni Ninja kutoka kundi la Zero linaloongozwa na mfalme Pluto bado unapanga kunizuia kuondoka na kukamilisha kazi yangu?”Aliongea na Roma aliona kabisa hakuna sababu ya ninja huyo kudanganya na pia hakuna uwezekano kabisa wa Sauroni kumsaliti hivyo jibu ni moja tu kwamba kuna mtu anajifanyisha ni yeye.

Pumbavu anapata wapi uthubutu wa kujifanyisha kuwa mimi na kutoa maagizo kwa makundi yangu lazima nifanyie kazi juu ya hili”Aliwaza.

“Nipe simu yako”Aliongea Roma akimpa maagizo yule bwana na kumfanya kushangaa lakini mwishowe alimpatia na kisha alitafuta namba ya Sauroni binafsi.

“Mfalme Pluto kwanini unanipigia tena , leo umenipigia zaidi ya mara tatu , jambo ambalo sio kawaida”Alilalamika Sauroni na kumfanya Roma kushangaa alimpigia saa ngapi kwa zaidi ya mara tatu.

“Sauroni unasema kweli nimekupigia zaidi ya mara tatu kabla ya hii ?”

“Mfalme Pluto matani yako hata nashindwa kuyelewa kwa siku hizi tatu , juzi ulinipigia na kunipa maagizo na tukaongea mambo mengi pia”Aliongea Sauoni

“You Bastard Sauroni Are you stupid ? I would never change my decision on something so impotant like this , Didn’t you think it to be suspicious when I would suddenly give you a command like this to kill peaple without reason?”

“Wewe mpumbavu Sauroni , wewe ni mjinga eti? , siwezi kubadilisha mawazo kwenye maamuzi muhimu , umeshindwa kufikiria sio kawaida kukupa maagizo ya ghafla ya namna hii ya kumuua mtu bila sababu?”Aliongea Roma kwa kingereza na kumfanya yule Ninja sasa kuelewa aliekuwa mbele yake ni nani.

“Mfalme Pluto najiona kama nimepotea na nashindwa kuelewa kwanini una hasira”Aliongea Sauroni na kumfanya Roma kuvuta pumzi na kuzishusha

“Sauroni adui yangu anaefanya mambo kificho anaonekana kuwa na nguvu kuliko nilivyotarajia...”Aliongea Roma huku hisia zikimwambia kazi yote hio ni ya Yan Buwen

“Adui!?”Sauroni alionekana kushangaa.

“Aliekupa maagizo sio mimi ila ni mtu tu anaefanana kama mimi “Aliongea Roma na kumfanya Sauron kushangaa na kuchanganyikiwa kwa wakati mmoja.

“Kama nisingekutana kwa bahati mbaya na ninja wako ambaye alikuwa tayari kumuua mtu kwa sumu ingeniingiza kwenye matatizo”Aliongea Roma.

“Nitatoa maagizo ya haraka waweze kurudi na kuachana na misheni ,mfalme Pluto najiona mjinga kutokukutambua”Aliongea.

“Amewezaje kuwasiliana na wewe na ni misheni gani ambayo ametoa?”

“Alinipigia kwa njia ya Vidio call kupitia internet niliona sio jambo la kawaida kwani alionekana ndani ya maabara lakini nilishindwa kutofautisha kwani najua hakuna mtu mwenye uwezo wa kukuigizia , Alitaka tuuze baadhi ya siraha kwa kundi la wapiganaji wa Afrika ya kati na Congo lakini pia kumuua waziri wa ulinzi wa jeshi la Tanzania kwa sumu”Aliongea na kumfanya sasa Roma kuelewa yule bwana kuwa ni waziri.

“Anajua mpaka namna ninavyowasiliana na wewe , mawasiliao yetu yalitengenezwa na Clark na kuwekewa kabisa ulinzi , inashangaza sana”

“Mfalme Pluto nadhani hili ni swala ambalo tunaweza kulifanya kuwa na faida kwetu”

“Kivipi?”

“Kwasababu ametumia mtandao wetu kuwasiliana na wewe na tunajua alieutengeneza ni Profesa Clark tutatumia njia hio hio kumkamata na kujua eneo alipo ,ngoja nimtumie profesa Clark kwenye hili”Aliongea

“Okey fanya hivyo na utanipa kinachoendelea , lakini pia nahitaji wanajeshi wengi zaidi wafike hapa nchini ndani ya siku mbili zijazo”

“Sawa mfalme Pluto nitawasiliana na Profesa Clark sasa hivi na pia nibatilishe maagizo yote ya misheni , kuhusu wanajeshi nitafanya utaratibu ndani ya siku ya kesho watakuwa wamefika”Aliongea na Roma alikubaliana nae na kukata simu.

“Rudi Ulaya sio kosa lako kuwa hapa Tanzania”Aliongea Roma mara baada ya kumaliza maongezi na Sauroni.

“Yes…. Yes your Majesty Pluto”Aliongea akiwa amepiga magoti huku akigonganisha kichwa chake chini ya bustani lakini Roma hakujali sana na kumpa ishara ya kuondoka.

Roma alijua yote hio ni kazi ya Yan Buwen , lakini kuna jambo bado linamtekenya na kumfanya asichukue maamuzi ya haraka ya kuvamia maabara ya Even lab , kinamfanya kusita sita kuchukua hatua ni juu ya mtu anaefanana nae kabisa na kuwa na uwezo wa kutumia kanuni za Anga, kwa maneno marahisi ni kwamba mwili wa mtu huyo feki ulikuwa umemulikwa na Devine light kama kilichofanyika kwake na kama jambo hilo ni kweli alijiuliza jiwe la kimungu Yan Buwen kalitoa wapi , kuna hisia zilimwambia huenda Yan Buwen alikuwa chambo tu na mpango unaendeshwa na mtu mwingine lakini swali liliibuka zaidi ni kwanini.

“Inabidi kuwa makini na ulinzi wa watu wangu wa karibu”Aliwaza Roma huku akiwaza kazi aliowapa Diego wameifikisha wapi lakini alijiambia atawasiliana nao baada ya chakula cha usiku.

Roma wakati akirejea mgahawani kwa njia ya kawaida kuna gari ilipiga honi nyuma yake na kumfanya asimame na kuangalia nyuma na palepale kioo cha gari kilishushwa na alionekana Donyi akimpungia mkono akiwa kwenye gari aina ya Range Rover Sport na haraka haraka Roma alijua na Neema L?uwazo atakuwepo humo ndani lakini alishangazwa kuwaona hapo ndani.

Gari ile ilienda kuegesha katika huo mgahawa na kisha akashuka mwanamama Neema Luwazo alietangulizana na Donyi.

Neema usiku hio alikuwa amevalia suruali ya jeans na kuacha mshepu wake kuonekana wazi huku akiwa na tisheti kubwa ya punda milia lakini rangi ya kijani na nyeusi akiwa chini amevalia Raba huku kwapani akiwa mkoba wa rangi nyeusi.

Donyi ambaye alikuwa na urembo kama wa mama yake pia alikuwa amevalia vazi la jeans na tisheti ya formsix rangi nyekundu akiwa na earpod masikioni na kumfanya kupendeza zaidi na namna alivyofunga nywele zake nyuma kwa kibanio.

“Nasikia mmekuwa majirani zetu”Aliongea Neema Luwazo na kumfanya Roma kushangaa.

“Umejuaje tumekuwa majirani?”Aliuliza Roma.

“Anapokaa Nasra upande wa kushoto ndio ninapoishi , nilimuona leo akiingia pamoja na mama yake ndio akanipasha habari kwamba mnahamia mtaa huu , karibuni sana nitakuwa mwenyeji wako”Aliongea Neema na kumfanya Roma kuona hili jambo lishakuwa kubwa na kuona ni bahati ya namna gani wanawake wake karibia wote kuwa mtaa mmoja.

“Bro upo hapa na nani?”Aliuliza Donyi ambaye hakutaka kuingilia mazungumzo ya wakubwa.

“Nipo hapa na familia kupata chakula naamini hata nyie pia mmekuja kwa ajili ya chakula cha usiku?”

“Ndio leo huyu mtukutu kanisumbua kuja kura hapa baada ya kumsindikiza baba yake Airport”Aliongea.

“Baba yake anaenda wapi?”

“Anahamia Ujerumani kwa muda”Aliongea na kumfanya Roma kugundua kitu kwa haraka haraka aliamini Kigombola alikuwa akitoroka hii nchi , kwanini kusafiri leo kwenda Ujerumani ,lakini hata hivyo hakutaka sana kuzungumzia kuhusu baba yake Donyi mbele yake.

Waliongozana wote kuingia ndani ya mgahawa huo na Roma mara baada ya kufika Edna alishangazwa akirudi akiwa na Neema, ijapokuwa wote walikuwa wafanyabiashara lakini hawakuwa na mazoea na kubwa zaidi kati ya michepuko ya Roma hakuwa akimpenda Neema Luwazo kutokana na utu uzima wake lakini pia kuwa na mahusiano na Mheshimiwa Kigombola.

Neema Luwazo uanasiasa wake ulimfanya kujiongeza haraka haraka kujitambulisha yeye mwenyewe mbele ya famili ya Roima akianza kwa mama yake Roma huku Donyi pia akisalimia.

Jambo la kushangaza Neema hakuficha uhusiano wake kabisa na Roma bali alijitambulisha vizuri ili kufahamika na mama mkwe na kumfanya Blandina kumwangalia Roma kwa namna ya kiulizo lakini Roma alijifanyisha bize.

Ilibidi wawakaribishe kwenye meza yao kwani na wao pia walifika hapo kwa ajili ya chakula cha usiku.

Kwenye meza ya Edna aliongezeka Donyi ambaye alikuwa akiongea kama mashine mara aongee na Roma mara amchokoze Sophia lakini mara pia amchokoze Lanlan ambaye hakuwa na utani kabisa eneo hilo la kula kutokana na kuwa siriasi lakini mwisho wa siku chakula kilienda vizuri kutokana na uwepo wa watu wengi na stori za hapa na pale ziliwafanya kuwa na furaha kiasi cha kumfanya Roma kuona kuna haja ya haraka kudili na Yan Buwen na kujua ni mtu gani anashirikiana nae.

Roma aligundua ile familia iliotaka kuwekewa sumu imekwisha kuondoka na aliamini huenda hawakula kabisa lakini kwake hakujali sana.

“Kesho asubuhi kuna kitu nataka kuongea na nyie wote”Aliongea Roma na kumfanya Blandina kumwangalia Roma kwa wasiwasi.

“Roma una siri gani unataka kuongea?”

“Ni swala muhimu sana linalohusiana na usalama wetu ni bora nikiwafahamisha mapema ili kuwalinda”Aliongea Roma.

“Edna nitaomba kuchelewesha ratiba za kesho kidogo nahitaji masaa mawili tu ya mazungumzo”Aliongea Roma na Edna alitingisha kichwa kwani alimwelewa alichokuwa akijaribu kumaanisha ,alikuwa akiwaombea ruhusa Nasra na Dorisi.

Baada ya kumaliza kula chakula wote waliondoka kwenye mgahawa huo kama walivyokuja lakini Roma alikuwa ashamwambia Neema kwamba anahitaji kuonana nae usiku huo na Neema alirudisha jibu la kukubaliana kuonana nyumbani kwake atakuwa anamsubiri.

Roma alienda kulala kwenye chumba chake kutokana na Lanlan kung’ang’ania kulala na mama yake na Roma hakuona haja ya kulala na Edna kwanza washawekeana ahadi kwamba hatomgusa Edna mpaka siku watakayofunga ndoa , jambo ambalo lilimfanya Roma kukubali kwani alikuwa akimpenda Edna na aliona hana haja ya kumlizimisha, lakini pia aliona kulala peke yake ingekuwa rahisi kuchomoka usiku kijini na kutembelea wanawake wake kirahisi pasipo hata ya Edna kugundua.

Roma ilibidi awasiliane na warembo wake wote na kuwataarifu kufika nyumbani kwake asubuhi kwa ajili ya kikao muhimu na bahati nzuri aliwapata wote kasoro Mage ambaye alipanga kuongea nae kwa muda wake kwani alijua Edna hakuwa na ufahamu wa mahusiano yao ndio maana hakutaka kumshangaza Edna kwenye kikao.

Baada ya kumaliza kuwasiliana nao na kuhakikisha nyumba imetulia alivaa bukta na tisheni na kisha kwa kutumia balconi alipotea na ile anakwenda kuibuka ni upande wa pili wa mtaa huo sehemu ambayo nyumba ya Neema Luwazo ilikuwa ikipatikana.

Nyumba ya Neema Luwazo ilikuwa na ulinzi mkali mno na ndio iliokuwa kubwa kuliko nyumba zote ambazo zipo ndani ya eneo la Ununio na ilikuwa karibu kabisa na bahari.

Roma aliwasiliana na Neema na kuambiwa atamkuta kwenye Balconi , hivyo Roma aliweza kuibukia kwenye Balconi pasipo hata ya walinzi kuelewa kama kuna mtu kaongezeka.

“Sikuwahi kudhania nitakuja kukutana na mwanaume wa aina yako”Aliongea Neema huku akimwangalia Roma kwa tabasamu akiwa ameshikilia glasi ya mvinyo mwekundu.

“Unamaanisha nini?”

“Mara ya kwanza wakati tunakutana nilikuwa kama nipo kwenye kifungo cha muda mrefu , siku ile ulivyoniaproach kwa namna ya kujiamini ndio ilionifanya nivutike na wewe lakini nani angejua siku ile haukua binadamu wa kawaida haha..”Aliongea huku akicheka na Roma alimwangalia mrembo huyo ambaye awamu hii akiwa amebadili mavazi kutoka jeans mpaka gauni lililoacha mabega yake wazi na kuishia kwenye magoti , lilikuwa jepesi kiasi kwamba Roma aliona kila kitu alichovaa mwanamke huyu ndani na mwili wake ulimsisimka vilivyo.

“Ndio ujue mpenzi wako sio wa kawaida na anakwenda kukufanya usiwe wa kawaida pia”Aliongea Roma na kumfanya Neema Luwazo kuweka pembeni glasi yake ya mvinyo na kumsogelea Roma na kujidendesha kama kijana wa miaka ishirini na tano.

“Asante kwa kuja kwenye maisha yangu, umekamilisha ndoto yangu ya ujana kabla sijauaga, nakubali kubadilika na kutokuwa wa kawaida na kufanana na wewe”Aliongea Neema kimahaba na kumfanya Roma kubasamu na kumvutia tena kwake huku akipitisha mkono nyima ya kiuno na kufanya gauni liache mapaja yote wazi, lakini Roma hakujali alizidi kubadilishana mate na ndugu waziri kivuli kwa dakika kama kumi na tano na kadri walivyokuwa wakiendelea ndivyo mzuka ulivyozidi kumpanda Neema.

Ni uzuri tu kwamba Balconi ilikuwa gorofa ya tatu juu na imegeukia bahari la sivyo wa walinzi wangeweza kuona kinachoendelea.

Roma alimsogeza Neema Luwazo mpaka kwenye kijitanda kidogo cha nje cha kupumzikia na kuendeleza mashambulizi huku Neema akitoa ushirikiano wa kutosha kiasi cha kumfanya Roma na yeye kupagawa na kujiona ulimwengu mwingine na kujiambia alifanya chaguzi sahihi , aliona kufanya mapenzi na mtu mzima ni tofauti sana na vijana wa rika lake..

Neema alionekana kufurahia sana kwa kila kitu kinachofanywa kwenye mwili wake na hili ndio ambalo lilileta utofauti na wanawake wengine.

Purukushani ziliendelea kwa takribani masaa mawili ndipo Roma alipoweza kushusha mzigo na kumwachia Neema ambaye alikuwa akihema mno na kutoka jasho kwa wakati mmoja.

“Leo unaonekana kuwa na furaha kuliko siku zote , nini siri yako?”Aliuliza Roma mara baada ya Neema kumwangalia Roma na kutoa tabasamu.

“Nimemalizana kabisa na yule mwanaume leo hii na hatuna deni kati yetu tena zaidi ya kushirikiana katika malezi”Aliongea Neema huku wakijifunika viwiliviwili vyao vya chiini.

“Unamaanisha baba yake Donyi?”Aliuliza Roma na Neema aliitikia kwa kichwa na kumfanya Roma kutabasamu.

“Ni kheri umemalizana nae kwani huenda ninachokwenda kukuambia hakitokuumiza zaidi”Aliongea Roma na kumfanya Neema kumwangalia Roam kwa wasiwasi.

“Unataka kuongea nini?”Aliuliza Neema na Roma ilibidi amueleze swala lililomtokea Mzee Chino mpaka kujeruhiwa ulikuwa ni mpango wa Yan Buwen na Kigombola kwa kushirikiana na watu wengine wa serikali , mpaka Roma anamaliza Neema Luwazo alionekana kutoa machozi.

“Siamini kama Kigombola kaamua kunifanyia hivi, kwanini anihusishe kwenye mipango yake ovu”Aliongea huku akijihisi kusalitiwa hakumini kilichomtokea Mzee Chino alikisababisha Mheshimiwa Kigombola .

“Roma naomba unisamehe , kupitia mimi nimekuingiza matatizoni”.

“Huna haja ya kuomba msamaha , wakati namsadia Mzee Chino nilijua kabisa kuna mchezo unachezwa lakini nilitaka kupata uhakika kwanza”.Aliongea lakini licha ya hivyo Neema alihisi yote yanayoendelea ni kwasababu yake.

“Kigombola ni mshenzi sana , ni mtu wa tamaa ndio maana drama haziishi sijui atakuja kuzeeka lini na kuona mambo mengine kwake hayana maana zaidi ya kumvunjia heshima tu, Roma kwahio unapanga kufanya nini juu ya hili?”

“Kigombola kachangia kidogo sana juu ya hili kuna mtu anaehusika na mipango yote ndio ninaemtafuta nimeamua kutochukua maamuzi ya haraka kwani nisingetatua tatizo moja kwa moja , mimi ni mtu mwenye shauku na ndio maana napenda kudili na matokeo”Aliongea Roma na kumfanya Neema kumuelewa lakini hata hivyo alikuwa ashamchukia tayari Kiigombola kwa ubinafsi aliokuwa nao kwa kutojali kabisa watu wake wa karibu, kwani kumgusa Mzeee Chino ilikuwa kama kumgusa mzazi wake , jambo hilo alijiapia hawezi kulifumbia macho na kumsamehe kirahisi.

*********

Ni saa tatu kamili za asubuhi Dorisi na Rose ndio waliokuwa wa kwanza kufika ndani ya nyumba ya Roma na kupokelewa na Blandina kwa bashasha , akafuatia Nasra halafu Neema na baadae kidogo alimalizia kufika Amina ambaye alitoka mbali kidogo.

Mama yake Roma alijitahidi kuwafanya wote kujisikia huru ndani ya familia hio na alishukuru Edna kutoonekana kuonyesha utofauti wa kuchukia uwepo wa wanawake wenzake ndani ya eneo hilo.

Edna kwakua alikuwa na taarifa na ujio wa wageni asubuhi hio aliamka mapema na kuandaa kabisa mazingira ya kikao akisaidiana na Qiang Xi hakuwa na haja ya kufikiria sana , aliamua kumuelewa mume wake nia yake.

Upande wa Roma bado hakuwa ametoka kwenye chumba chake na alionekana kufanya baadhi ya mawasiliano , uwepo wa mtu anaefanana na yeye na mwenye uwezo wa kutumia kanuni za anga ulimfanya kidogo kuwa na wasiwasi hususani usalama wa watu wake wa karibu na asubuhi hio alifanya mawasiliano na Tanya ili kufika nchini na baadhi ya watu wake ndani ya Tanzania ili kuhakikisha ulinzi unakuwa mzuri , aliamini The Eagles wanaweza kuwa vizuri kwenye kupigana na binadamu wa kawaida lakini likija swala la kudili na watu wanaotumia nguvu za ziada inakuwa ni swal lingine.

Asubuhi hio alikuwa na mpango baada ya kumaliza kikao kwenda kuvamia maabara ambayo anahisi Yan Buwen ndipo anapofanyia kazi zake ili kujua ni nini kinaendelea na alijiambia angemkuta angemupoteza moja kwa moja ili kutatua tatizo.

Familia nzima mara baada ya kukusanyika ukweli walijihisi kuwa na shauku sana ya kile ambacho Roma alikuwa akipanga kuongea nao kiasi cha kuwakutananisha pamoja na hata pale Roma alipotokezea kutoka juu kuja sebuleni walizidi kuwa na wasiwasi.

Upande wa Roma mara baada ya kuona warembo wake wote wamefika ndani ya eneo hilo alijikuta akiwa na hisia za mchanganyiko , alijiona kama mfalme wa karne zilizopita maana ilikuwa sio jambo dogo kukusanya wanawake wote sehemu moja na kusiwe na tatizo.

Sophia mwenywe ambaye siku zote alikuwa akimtamani Roma kimapenzi alijikuta akijiambia Roma ameshindikana kabisa kutokana na uwepo wa warembo waliokusanyika hapo ndani , yeye siku kadhaa zilizopita wakati tukio la kulipuliwa kwa nyumba ya Rose linatokea hakuwepo hivyo uwepo wa wanawake hao wa Roma ni mara yake ya kwanza , lakini pia ndio kwanza alikuwa akiwajua kwani ukiachana na Amina ambaye alikuwa akimfahamu kama mchepuko wa Roma lakini wengine wote hakuwa kabisa na ukaribu nao na hakuwafahamu ,lakini hata hivyo jambo moja lililomfurahisha ni kwamba bado alijihisi ni mwenye kujiamini kutokana na kwamba katika sura zote za warembo wa Roma hakuna ambaye alikuwa akimfikia kwenye swala la uzuri ,ijapokuwa Amina alikuwa na sura flani ya kuvutia na kuwa na mwili uliokaa kimitego mitego lakini kwa Sophia alikuwa mzuri , huenda na Edna walipishana kidogo na si ajabu mtu akasema Edna na Sophia ni ndugu kutokaa na mwonekano wao na hata Edna mwenyewe alijua Sophia ni mzuri haswa na ndio maana kwenye moyo wake alishaweka nadhiri siku Roma atakayotoka kimapenzi na Sophia hajui nini atafanya lakini alijiambia huenda akaomba talaka.

Ni mwanaume mmoja tu ambaye alikuwa na uwezo wa kuwakusanya wanawake wengi namna hio ndani ya nyumba moja na bado akaonyesha kujiamini , huyu ndio Roma Ramoni aka mfalme Pluto, hakuonyesha kutokujiamini kabisa , kwake alifurahi zaidi kuona wanawake wake wakiwa eneo moja na kutamani wapatane na siku mmoja waweze kuishi pamoja.

Roma alishuka mpaka chini eneo la sebuleni na kukaa kwenye sofa ambalo liliachwa wazi sehemu ambayo ilimpa nafasi ya kuwaona wote.

“Nimewaita hapa kwasababu nina kitu muhimu sana cha kuzungumza ambacho kinahusiana na usalama wenu kwahio nataka mnisikilize kwa umakini na kama ni kuuliza maswali iwe ni baadae , ninachokwenda kuongea kinaweza kisiwe rahisi kuelezeka lakini nitajirahidi kuelezea kwa lugha nyepesi”Aliongea Roma.
 
SEHEMU YA 430.

Binadamu tokea enzi wamekuwa ni wenye kupenda simulizi nyingi za kufikirika na zile za kutunga ambazo katika mazingira ya kawaida haziwezi kutokea, watu walipenda dini pia ambayo misingi yake ni imani lakini mwisho wa siku imani ilipelekea binadamu akawa na shauku ya kuthibitisha kile ambacho hakuweza kukiamini na ndio maana ikaja kutokea ujenzi wa mlima wa Babeli yote hayo ilikuwa ni shauku ya stori za vitu ambavyo binadamu hawakuweza kuthibitisha , yote hayo ilikuwa ni shauku aliokuwa nayo binadamu aidha kupitia imani walizokuwa nazo ama hadhithi walizokwisha kusikia au kusoma.

Binadamu huvutiwa na mawazo pamoja na ahadi ambazo ni zaidi ya kilichopo kwenye mazingira ya kawaida ya kidunia yaani mambo yanayotukia mara baada ya mtu kufariki yote hayo ni kutokana na hofu ya kuogopa kifo , lakini hata hivyo katika wakati wa nadra sana inapotokea mstari mwembamba unaotenganisha upande wa uhalisia na ule usiokuwa wa uhalisia utakapoondoka na yale yakufikirika yatakapokuwa halisi ni ngumu sana kutabiri binadamu atakuwa kwenye hali gani katika namna ya kuonyesha mapokeo yake..

Ni kama moja ya hadithi ya mtu ambaye alipenda sana mnyama aina ya Dragoni lakini siku ambayo anakuja kukutana na Dragoni mwenyewe anajikuta anaogopa kiasi cha kujikojolea.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa wanawake waliokuwa wameijaza sebule, kila kitu Roma alichowaambia kilikuwa ni kama hadithi kwao, nani angeweza kuamini kama kuna uwezekano wa binadamu kutengeneza kopi ya mtu mwingine kwa namna kama anatoa karatasi photocopy , lilikuwa ni jambo ambalo haliwezekani kwa akili za kawaida na ndio maana liliwaacha wote mdomo wazi na kufanya hata wengine kuhisi presha kupanda na kushuka.

Roma aliwaelezea kila kitu kwanzia siku ambayo aliweza kwenda baharini ya South Sea China kwa ajili ya kutafuta namna ya kumfahamu adui anaetumia mwonekano wake kutaka kumchafua, lakini pia namna ya kile kilichotokea jana yake usiku ndani ya mgahawa waliotumia kupata chakula cha usiku.

Roma alijibu maswali yalioulizwa hususani ni mtu gani anajaribu kumchokoiza na Roma hakusita kujibu kwa kumtaja Yan Buwen , jambo ambalo pia lilimshangza Edna juu ya jina hilo kwani alishawahi kukutana na Yan Buwen, lakini alichanganyikiwa zaidi mara baada ya Roma kuelezea hata watu waliokuja kushambulia nyumbani kwake miezi kadhaa iliopita mpaka kusaidiwa na Christen watu wale walikuwa ni wafu waliofufuliwa na Yan Buwen kwa kutumia kimiminika cha Ressurection Fluid kauli ambayo ilimfanya Blandina kuanza kukumbuka biblia yake na kuona siku za mwisho zilizotabiriwa kwenye kitabu cha ufufuo wa Yohana zimekaribia.

Mpaka Roma anakuja kuhitimisha alizua zogo kati yao , kwani walianza kujadiliana kwa namna ya kushangaa lakini mwisho wa siku Roma alijitahidi kuwaelewesha.

Roma aliwaambia kuna namna ya kujilinda na maadui zake ambao anaamini wasingeisha leo wala kesho kwani siku zote ukiwa na nguvu ndio unavyotengeneza maadui , hivyo aliwaambia namna pekee ni kujifunza mbinu za kijini na kupanda levo ili angalau kuweza kujilinda wao wenyewe

Aliwaasa kwamba mbinu za kijini ni ngumu kujifuza na inahitaji uvumilivu na kutokata tamaa na kuahidi kwamba atawasaidia wote mmoja mmoja mpaka kufanikisha.

Baada ya kumaliza mazungumzo yake aliwaacha ili waendelee kuzungumza wao kwa wao , alitaka pia kuongea na Mage pamoja na Magdalena na kuwapa mbinu mpya ya namna ya kumtambua yeye na kumtofautisha na kopi yake.

Ndio Roma dhumuni lake la mazungumzo lilikuwa ni kuwapa mbinu ya kuweza kumtofautisha yeye na kopi yake kwa kutumia kodi maalumu na kama itatokea mmoja wapo kukutana na kopi yake kuweza kupiga namba maalumu ya dharuala ambayo pia aliwapatia na kuahidi kwamba atafika ndani ya muda na kuwasaidia

…………….

Roma pia aliweza kukutana na Mage pamoja na Magdalena nyumbani kwao na kuwaelezea kwa ufupi ya kile kinachoendelea , kwa Magdalena hakushangaaa sana kutokana na aina ya uanajeshi wake kujua mambo mengi lakini kwa Mage kila kitu kilikuwa cha kushangaza.

Roma mara baada ya kumaliza mazungumzo yake aliondoka na kuelekea Kigamboni ambako aliweza kukutana na wanajeshi wake , kuna swala alililokuwa amewapatia walifanyie uchunguzi na alikuwa akitaka majibu.

“Vipi mmefikia wapi?”Aliuliza Roma mara baaada u ya kukaa.

“Mfalme Pluto tuliendelea kufuatilia majina ya watu uliotupatia na tumegundua kuna baadhi ya mambo hayapo sawa hususani kwa siku ya leo”Aliongea Diego na kumfanya Roma kumwangalia.

“Unamaanisha nini mambo ambayo hayapo sawa?”Aliuliza Roma kwa mshangao. Na Diego alimpa ishara Bram Carcia na palepale Tv iliwaka na kumfanya Roma aangalie kinachoonyeshwa na kujikuta akishangaa mno.

Ndio alichokuwa akiona Roma ni kwamba siku hio ya jumatatu raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa Senga Cammilius Kweka alikuwa akifanya ufunguzi wa maabara mpya ya kisasa ambayo ipo ndani ya jengo la bima ya taifa na muda huo ambao Roma alikuwa akiangalia ilikuwa ni hotuba yake huku akiongea kwa kusema kwamba umalizikaji wa maabara hio ndani ya Tanzania unakwenda kufanya mageuzi makubwa kwenye nyanja za utafiti wa maswala ya tiba na mwishoni kabisa mwa hotuba Mheshimiwa Raisi Senga anahitimisha kwa kusema kwamba maabara hio kwanzia sasa anaikabidhi kwa Chuo kikuu cha matibabu na utafiti Muhimbili.

Kauli iliomuacha hoi ni pale raisi Senga aliposema kwamba maabara hio haijawahi kutumika na ndio kwanza ujenzi wake wa kuweka vifaa vya kisasa umemalizika huku akienda mbali kabisa na kusema kwamba imegawanyika kwa viwango kwanzia mabara ambayo ipo chini kabisa ya vyumba vya ardhi ambayo ni ya BL-4 lakini pia kulikuwa na maabara za utafiti za kawaida ambazo zilikuwa kwenye levo za chini yaani kuanzia ya pili na ya tatu ambayo ipo kwenye floor za juu.

Raisi Senga alionekana kutumia nafasi hio vyema kwa kujigamba kisiasa kwamba kwenye uongozi wake ameweza kukamilisha ujenzi wa maabara hio ya viwango vya kimataifa ambapo ungechochea ukuaji wa sayansi ya utafiti ya maswala ya tiba jambo ambalo hakuna mtangulizi wake amelifanikisha na kumalizia kwamba jengo hilo kwanzia siku hio litatumiwa na Mkemia mkuu wa serikali pamoja na chuo cha Muhimbili.

Watu wengi walionekana kumpongeza Raisi Senga kwa maono yake makubwa ya ujenzi wa maabara hio jambo ambalo lilimchekesha Roma na kuona mwanasiasa siku zote ni mwanasiasa tu , maabara ambayo imejengwa miaka zaidi ya sita nyuma ndio inaitwa mpya.

“Mfalme Pluto hili nadhani linatuambia kwamba Yan Buwen hatumii tena maabara hii”Aliongea Diego.

“Nilimchukulia kawaida , ilionekana baada tu ya kuonyesha siraha yake wazi alioweza kuitengeneza alihamisha makazi yake kuchukua tahadhari”Aliwaza Roma na aliona ilikuwa mantiki aliamini huenda siku ile mtu aliefanana na yeye kwenda kuharibu meli ya kivita ya kimarekani ndio muda ambao Yan Buwen aliondoka , lakini alijiuliza kwanini serikali wakaamua kuiweka hadharani.

Wakati akiendelea kuwa kwenye takafakari simu yake iliita na alipoangalia jina la mpigaji ni Omari alijikuta akitabasamu kiuchungu na kupokea simu.

“Umepata taarifa gani?”Aliuliza Roma bila salamu.

“Yan Buwen kanipiga chenga”Aliongea Omari

‘”Nilijua upo vizuri kwenye ujasusi lakini udhaifu wako unaanza kujidhihirisha”

“Mbona unaongea kama unajua kilichonikuta”Ilisikika sauti ya Omari upande wa pili.

“Sijui kilichokukutana lakini kwa sauti yako nishajua ulichokutana nacho sio kidogo unaweza kuita Human instinct, Haya niambie kipi kimekukuta nikupe pole”Aliongea Roma huku akiweka tabasamu la kebehi.

“Siku ya jana nilipata ‘clearence’ ya kufanya uchunguzi ndani ya maabara ya Even lab na nilifanikiwa kupata kibali bila shida yoyote, nikiri kwamba nilichokiona ndani ya jengo hilo kilinishangaza mno”Aliongea Omari na kumfanya Roma kuvutiwa na maongezi.

“Unamaanisha nini kusema ulichokiona kimekushangaza”

“Acha tu kwenye maisha yangu sijawahi kudhania ndani ya hili taifa kuna sehemu ilioendelea kiteknolojia kama chini ya lile jengo , nilijjihisi labda nipo kwenye muvi za kufikirika”Roma alijikuta akishangazwa na kauli ya Omari na kujikuta akijikatia tamaa kwani alitegemea taarifa nzuri.

“Hicho ndio ulichofanikiwa kupata katika uchunguzi wako ndani ya maabara hio?”

“Ndio nilichogundua hakuna dalili zozote zinazoonyesha Yan Buwen kutumia maabara hio kwani kila kitu ni kipya na sehemu ni safii , kiasi kwamba hakuna dalili kama Yan Buwen alikuwepo jambo ambalo limenifikirisha usiku mzima”Aliongea.

“Hizo ni ‘side effect’ za kuishi sana ulimwengu wa majini naamini huko hakuna teknolojia kubwa kama ulioona ndani ya Even Lab?”

“Hongmeng hakuna teknolojjia yoyote kubwa, labda miliki zingine ambazo niliweza kusikia , ukienda Hongmeng ni kama unasafiri kwenda nyuma ya muda kwa ‘Time Travel Mashine’ ”Aliongea Omari na kumfanya Roma kutamani kucheka kwa kauli za Omari.

“Kwasasa nipo katikati ya kazi nitakutafuta endelea kutafakari uzuri wa Even Lab”Aliongea Roma na hakusubiri jibu la Omari na kukata simu , hata hivyo taarifa ya Omari haikuwa mbaya sana licha ya kwamba alichekeshwa na namna ambavyo Onari alionekana kuwa kwenye mshangao..Roma aliwaangalia Diego na wenzake na kisha akavuta pumzi.

“Diego nadhani Yan Buwen kashatoka ndani ya Tanzania na tafiti zote”Aliongea Roma na kumfanya Diego na wenzake kuangaliana.

“Mfalme kwa maana hio?”

“Tunarudi mwanzo kabisa wa kazi tulikuwa tukifahamu Yan Buwen yupo ndani ya maabara ya Even Lab lakini sasa hivi kashaondoka hivyo kazi ni kutafuta yupo upande upi wa Dunia”Aliongea na kuwafanya kuonenakana kunyong’onyea.

“Kuondoka kwa Yan Buwen ndani ya Tanzania naamini ndio kunaweka hali ya usalama kuwa katika harari zaidi, kwanzia sasa nataka umakini wenu wote muelekezee kwa familia yangu , lakini wakati huo huo mkiendelea kufuatilia majina ya watu niliowapatia”

“Sawa Mfalme Pluto”

“Sauroni atawaongezea nguvu ya jumla ya wanajeshi ishirini , nadhani leo usiku wataingia Tanzania nitawasiliana na mamlaka ili wapite bila bughuza uwanja wa ndege”Aliongea Roma na wote walipiga saluti.

“Vipi majina ya watu niliowaambia muwafatilie”Aliongea na Fannya alisogea mbele.

“Tumefanikiwa kupata kufahamu Desmond yupo nchini Rwanda, Mzee Longoli pia jeshi limemhamisha na kumpeleka morogoro kambi ndogo ya jeshi kwenye Safe House akiwa chini ya ulinzi wa jeshi , lakini pia kuhusu taarifa za Denisi Senga , kaondoka nchini wiki iliopita siku ya jummane kuelekea Uholanzi na baada ya hapo hakuna taarifa ya mahali alipoelekea”Aluongea Fanny na kumfanya Roma kukuna kichwa.

“Okey endeleeni kufuatilia , nitaanza kwanza na huyu Longoli”Aliongea Roma na kutoa maagizo mengine muhimu na kisha akaondoka hapo ndani.

******

Naam ilikuwa ni saa tisa kama na nusu za alasiri kuelekea kumi kamili ndio muda ambao Edna alipokea simu kutoka ka Suzzane kwamba wanapaswa kuonana na Chriss saa kumi na moja kamili ndani ya mji wakisasa kibaha.

Edna baada ya kupokea taarifa hio akiwa nyumbani aliaga kwa Mama Mkwe wake kuelekea huko huku Blandina akimsisitizia kuwa makini kutokana na uwepo wa Roma feki.

Dakika chache tu aliweza kuingia barabara ya kuelekea Madale ili akatokezee mbezi na kuelekea kibaha , akiwa njiani alimpigia simu Roma ambaye hakuwa amerudi nyumbani bado na kumuelezea alikuwa akielekea Kibaha kuna mtu anaenda kuonana nae.

“Uko wapi sasa hivi?” sauti ilisikika kupitia mfumo wa gari.

“Ndio nakaribia Mbezi”Aliongea Edna huku akikaza macho barabarani.

Wakati huo Roma akiwa anaongea na Roma alikuwa ndio anatokea Mapinga kwa Mzee Kweka kwani muda wa saa saba wakati akiwa njiani akipanga kwenda kuvamia kambi ya jeshi ya Morogoro kwenye safe house aliweza kupigiwa simu na Afande Kweka kwenda nyumbani kwake kwani kuna swala muhimu anapaswa wazungumze.

Roma hakupenda kwenda lakini Mzee Kweka alionekana jambo ambalo anataka kuongea nae kuwa muhimu na ndio maana alinyoosha moja kwa moja pasipo kuingia nyumbani, sasa alikuwa barabarani muda huo wa saa kumi kasoro akirejea nyumbani huku akifikiria baadhi ya maneno alioongea na babu yake.

Wakati ule Roma anaongea na Edna akimuuliza anaenda kukutana na nani huko kibaha simu yake ndogo ilitoa mlio kuashiria inaita kwa mwito wa dharula, ikimaanisha namba ambayo aliwapatia wanawake wake asubuhi kumpigia endapo wangekutana na Kopi yake ndio hio.

Roma alipunguza mwendo haraka na kisha akaitoa na kuangalia ambaye alikuwa akimpigia na aligundua simu inatoka kwa Amina.

“Sh****t”Roma aling’ata meno kwa hasira hakumini mambo yangekuwa mapema hivyo lakini aliona afadhari anakwenda kumshikisha adabu huyo mwanaharamu.

“Edna kama safari yako haina umuhimu kwanini usiende siku inayofuata?”

“Mh nini kinaendelea?”

“Amina anaonekana kukutana na kopi yangu kapiga namba ya dharula”Aliongea Roma.

“Okey nenda kamsaidie sasa, safari yangu haina shida nitaenda mwenyewe nitakuwa makini”Aliongea Edna.

“Okey kuwa makini , kukiwa na tatizo nitafute haraka nadhani pia Adeline yupo nyuma yako”Aliongea Roma na kisha akakata simu na kuegesha gari pembeni na palepale alipotea baada ya kuzima gari.

**??*

Upande wa Edna hakuwa na wasiwasi kwanza kabisa alishaona gari nyuma yake inamfuatilia ambayo ina watu waliowekwa na Roma , hivyo aliamini popotea pale angekuwa salama.

Masaa kadhaa tu ya kuendesha gari a hatimae aliweza kuingiza gari ndani ya mji mpya wa kisasa, alikuwa akijua anapoishi Suzzane hivyo hakukuwa na haja ya kupiga simu.

Alienda mpaka Floor husika ndani ya jengo hilo ambalo pia kulikuwa na kitengo chake cha Athena na kisha akabonyeza kengere na kufunguliwa, alikuwa ni Suzzane ambaye alikuwa amevalia kawaida tu, alikuwa amefika kabla ya muda wa kuonana na huyo Chriss hivyo alitarajia Suzzane kuwa peke yake.

Sasa Edna haikueleweka ni kutokana na kukosa uzoefu wa kunusa hatari , kwani Suzzane alionekana kuwa na wasiwasi kwenye macho yake lakini bado aliingia ndani.

“Miss Edna karibu sana”Ilisikika sauti ya mwanaume pembeni ya mlango na kumfanya Edna kugeuza macho yake na kuangalia sauti hio na alijikuta akibung’aa mara baada ya kuelewa alikuwa amejiingiza mtegoni.

Alikuwa ni mwanaume anaefahamika kwa jina la Chriss akiwa ameshikilia bastora na kumuonyesha ishara Edna ya kusonga mbele kuelekea kwenye masofa , upande wa Suzzane alijikuta chozi likimtoka kwa kumuingiza bosi wake kwenye mtego.

“Edna I am sorry”Aliongea Suzzane huku akiteteeka.

“Kimyaa..!!!”Aliamrisha Chriss , aliekuwa amebadilika haswa hakuwa yule Chriss wa jana aliekuwa akiongea kwa upole huyu alikuwa amebadilika na alionekana kuwa mkatili na muda wowote angeachhia risasi na kuua.

Edna alijikuta aking’ata lipsi zake na kujiambia huenda angemsikiliza Roma , nani angejua alikuwa akijiingiza kwenye mtego pasipo yeye mwenyewe kujua, alimwangalia Suzzane na kugundua hata yeye alionekana mwanaume huyo alimhadaa kwa kuweza kutimiza malengo yake.

“Miss Edna nimefurahi kukurata na wewe kwa mara ya kwanza”Aliongea Chriss kwa lugha ya Kingereza.

“Wewe ni nani…?”Aliuliza Edna na kumfanya Chriss kutabasamu huku akisogea na kukaa mbele yao.

“Mimi ni Chriss ninaekufahamu A to Z , umeshawishika kuja moja kwa moja hapa mara baada ya kupata habari zangu kutoka kwa Suzzane , ndio, leo kabla sijatekeleza kifo chako ambacho kilipangwa kufanikishwa miaka nane iliopita nitakuelezea kila kitu usicho kijua kilichotokea siku mbili baada ya kuzaliwa kwako”Aliongea na kuufanya moyo wa Edna kupiga kite kwa nguvu huku akiomba muujiza ufanyike alitamani kushika simu yake na kubonyeza namba ya dharula lakini hakuwa na nafasi hio.

“Naomba usimuue Boss tafadhari , unaweza kuniua mimi ila sio Bosi”Aliongea Suzzane kwa namna ya kuomba.

“Suzzane samahani sana, kila kitu nilichokuambia jana ni sahihi kabisa na sijakudanganya chochote , lakini kwa bahati mbaya kuna mabadiliko yaliotokea ambayo yananifanya nisiwe na jinsi ya kuwaacha hai, hakuna namna ,wote mnapaswa kufa la sivyo nitakufa mimi , lakini kabla ya kifo chako nitatimiza ahadi niliokuwekea nitakuambia kila kitu kilichosabababi….”Alitaka kumalizia tu sentensi yake ni kama taya la mdomo wake lilipata hitilafu kwani aliachama kwa namna ile ile na kuwafanya Edna na Suzzane kushangaa , lakini muda ule ule walijikuta wakitoa macho zaidi mara baada ya mwanamke mzuri sana kutokezea mbele yao kiasi cha kumfanya Edna na Suzzane kurudi nyuma kwa woga.
 
SEHEMU YA 431

Mpango wa Roma ulikuwa ni kwenda kumtoa Mzee Longoli huko huko kwenye kambi ya jeshi na kumuua mara tu baada ya kuona Yan Buwen kufanikiwa kutoroka ,aliamini huenda akimhoji mzee Longoli angeweza kujua ni wapi Yan Buwen kakimbilia.

Sasa Roma wakati alipokuwa akitoka katika makazi ya wanajeshi wake ndipo alipopata simu kutoka kwa Afande Kweka akihitajika kwenda kuonana nae bila kukosa na kutokana Afande Kweka kusisitiza ndio sababu iliomfanya Roma kufika nyumbani hapo ili kujua mzee huyo anataka kuongea nini.

Lakini kile ambacho Roma alitegemea mzee huyo kuongea ndio alichokutana nacho , lakini hata hivyo kulikuwa na kitu kingine ambacho aliweza kuelezewa na shukrani ziende kwa Zenzhei ndio aliweza kujua kitu kimoja muhimu sana.

Kwa maelezo ya Zenzhei hakukuwa na utofauti sana na maelezo ya Omari Tozo, Zenzhei anasema uhusikaji wa Afande Yang katika mipango ya Yan Buwen ni kutokana na mgogoro wa siri unaonendelea ndani ya serikali ya China ,mgogoro unaosababishwa na Hongmeng kuingilia mambo ya kisiasa na kijeshi.

Lakini kubwa zaidi ni kwamba miaka kadhaa iliopita kuna mwanasiasa mkubwa ndani ya taifa la China aliekuwa akiwania kiti cha uraisi alikufa kifo cha kutatanisha ambacho kwa uchuguzi wa chini ilifahamika kwa watu wachachekwamba aliuliwa na Hongmeng.

Mwanafamilia huyo alikuwa akitokea katika ukoo wa Afande Yang akiwa kama kaka wa bwana Yang Gongming , inasemekana mwanasiasa huyo hakupendwa na Hongmeng kuongoza nchi lakini wakati huo huo alikuwa akipendwa sana na raia na hio ndio sababu iliopelekea Hongmeng kumuua , sasa kitendo cha mwanafamilia kuuliwa kilitengeneza kisasi kati ya familia ya Afande Yang na Hongmeng.

Lakini licha ya kwamba ukoo wa Yang wanakisasi chao na Hongmeng hawakuwa na uwezo wa kuwafanya lolote , kwani walikuwa na nguvu kubwa hususani kwenye kuvuna nishati ya mbingu na ardhi yaani mbinu za kijini.

Sasa Afande Yang alitaka kulipiza kisasi cha kaka yake lakini nguvu hana na katika kuwaza namna ya kulipiza kisasi ndipo alipoigeukia sayansi , aliamini kwa sayansi tu ataweza kuiangamiza Hongmeng na katika jitihada zake ndipo alipoingia mwanasayansi nguli aliejizolea umaarufu afahamikae kwa jina la Yan Buwen kutoka ukoo wa Yan.

Sasa unachotakiwa kuelewa ukoo wa Yan pia haukuwa ukiwapenda Hongmeng yote hio ni kutokana na kwamba licha ya kuwa na nguvu kiuchumi lakini kwenye maswala ya siasa hawakuwa na nguvu kwasababu hawakuwa chaguo la Hongmeng, hivyo kuishia kuwa chini ya koo nyingine kama ukoo wa Ning ambao ni mahasimu wao wakubwa na walikuwa ni kama wakusubiria fursa tu ya siku itakapotokea kuondoa ushawishi wa Hongmeng..

Sasa baada ya Afande Yang kuleta pendekezo namna ya kuondoa utawala wa Hongmeng kupitia sayansi ndipo walipomshawishi mtoto wao Yan Buwen kuendeleza misheni kwa kugundua siraha ambazo zingekuwa na nguvu kubwa sana ili siku waweze kushinda vitisho vyote kutoka Hongmeng.

Sasa Afande Yang asichokijua ni kwamba wakati yeye mpango wake ukiwa ni kuiangamiza Hongmeng kwa kumtegemea Yan Buwen upande mwingine mtu anaemtegemea alikuwa na mipango yake.

Yan Buwen yeye hakuwa na mpango kabisa na Hongmeng na hio ni mara tu baada ya kukutana na mrembo Athena , yeye nia yake ilikuwa ni kuwa na uwezo wa juu kumzidi Athena ili aje kumuweka chiini ya himaya yake na hatimae kupata kitumbua chake.

********

Umbali kutoka barabarani ni mbali kuliko umbali kutoka baharini , hapo ndipo ilipokuwa nyumba ya Tajiri Kanani ndani ya eneo la Mbezi Beach, tajiri anaesifika kwa kumiliki visima vingi vya mafuta na biashara zisizohamishika(Real estate).

Ndani ya jumba hilo kubwa anaishi Mzee Kanani na mtoto wake Amina tu hio yote ni kutokana tajiri huyu alikuwa na ngugu wachache sana , na ndugu hao wachache wengi wao walikuwa na maisha yao mbali na yeye , hivyo ni mara chache sana ndani ya nyumba hio kuwa na watu wengi ukiachana na wafanyakazi wa ndani.

Lakini siku mbili hizi hali ilikuwa tofauti kidogo , hili ni kutokana na kwamba Mzee Kanani alikuwa amesafiri kwenda nchini India hivyo nyumba yote alibakia Amina mtoto wake pekee pamoja na mfanyakazi wao mmoja.

Muda wa saa kumi na moja siku hio Mfanyakazi wao alikuwa ametoka kwenda kununua mahitaji ya maandalizi ya chakula cha usiku , hivyo nyumbani alibakia Amina pekee pamoja na mlinzi wa geti.

Wakati Amina akiwa ameketi kwenye masofa eneo la sebuleni akiwa ameshikilia kitabu cha riwaya kilichoandikwa kwa lugha ya kingereza akijisomea , mlango wa mbele wa nyumba yao ulifunguliwa taratibu na kisha ukafungwa kwa ndani.

Jumba hilo limejengwa kwa staili ya kipekee ,mtu anaeingia kutoka nje hawezi kuonekana moja kwa moja kutoka eneo la sebuleni , kwani ukiingia tu ndani kitu cha kwanza unachokutana nacho ni ngazi za kupandisha floor za juu.

Hivyo kwa Amina aliekuwa amekaa eneo la sebule akiwa ameangalia upande wa nje wa bustani k na madirisha kuwa makubwa , hakujihangaisha kuzungusha shingo kugeuka kuangalia anaeingia kwani alijua lazima atakuwa ni mfanyakazi wao wa ndani ambae aliaga anaenda Supermarket.

Lakini sasa kuna hisia zilisambaa kwenye mwili wake na kumfanya kugeuka haraka na hapo ndipo alipopigwa na mshangao mara baada ya kugundua mtu aliekuwa mbele yake hakuwa mfanyakazi wao , bali alikuwa ni mwanaume alievalia tishet nyeupe pamoja na Jeans huku akiwa amechomeka miwani ya jua eneo la kifuani , kilichomuacha hoi Amina ni kwamba mwanaume huyu alikuwa Roma mtupu.

Amina ambaye alikuwa amevaa mavazi ya kulalia ambayo mara nyingi hupendelea hata ikiwa mchana alijikuta akishindwa kuongea na kuishia kuachama na kurudi zaidi nyuma ya Sofa kwa wasiwasi.

Ijapokuwa mwanaume aliekuwa mbele yake alikuwa akifaana kwa vitu vingi kama Roma , lakini kilichomfanya kugundua haraka sio Roma ni kutokana na namna mwanaume huyo anavyomwangalia , alikuwa na macho makavu zaidi ambayo yamejaa usuriasi ndani yake , aina ya mwonekano ambao hakuwahi kumuona nao Roma, kwake mtu aliekuwa mbele yake ni kama nyoka ambaye anajiandaa kutema sumu, alijikuta akianza kutetemeka huku akishika simu yake na mkono wa kushoto.

“You… Are you clone?”Aliongea kwa sauti akiwa kwenye mshituko akiuliza ndio Roma feki yaani kopi yake.

Shukrani ziwaendee wanajeshi wa The Eagles kwani kwa maagizo ya Roma waliweza kumpatia kila mwanamke ‘Bracelet’ za kuvaa mkononi ambazo urembo wake umetengenezwa kijasusi zaidi kama njia ya mawasiliano ya dharula , ili kuwa rahisi wakati wa hatari kupiga simu ya dharula iwapo simu itakuwa mbali.

Na hicho ndicho alichokifanya Amina , kwani mara baada ya kurudisha mkono nyuma aliweza kukandamiza ile Braceler na simu kwa nguvu mpaka alipohakikisha mawasiliano yametoka..

Hata kama asingepata muda wa kubonyeza kitufe, The Eagles tayari walikuwa washafahamu ujio wa kopi ya Roma ndani ya nyumba hio , lakini kwasababu walikuwa wamepewa maagizo na mfalme Pluto watoe taarifa tu pasipo ya kupambana ndicho walichofanya , lakini utofauti ni kwamba taarifa yao ilichelewa kuliko ile ya Amina.

“Mhmph” Roma feki alitoa tabasamu la kebehi kwa kuguna na kisha akaenda kuketi kwenye sofa huku akiuchunguza urembo wa Amina.

“Relax I have no interest in killing you , humiliting you infront of him would be much better , Wouldn’t it?”

“Kuwa mpole sina mpango wowote wa kukuua , kukudharirisha mbele yake ndio itakuwa jambo zuri zaidi , Si ndio?”Aliongea na kumfanya mrembo Amina uso wake kupauka kwa woga huku mwili ukitetema.

Lakini muda huo huo ghafla mtu aliingia kwa spidi isiokuwa ya kawaida na kumshika yule mwanaume shingo na kumuinua juu ka kumning’iniza.

“Kumdharirisha , labda kama unajisemea mwenyewe”

Alikuwa ni mtalamu Roma Ramoni ambaye tayari amefika hapo kwa namna ya kuteleport kutoka sehemu aliokuwepo mara baada ya kupata mawasiliano ya Amina.

Roma awamu hii alionekana kuwa kwenye hasira ya kiwango cha juu , huku macho yake yakiwa yashabadilika rangi na kuwa ya njano na kilichosambaa eneo lote ni nguvu za kijini ambazo zilikuwa zikiashilia mauaji na kufanya hata nywele za Amina kusimama.

Amina alijikuta akipoa kwa ahueni mara baada ya kugundua aliefika hapo ghafla alikuwa ni Roma halisi.

Roma feki alionekana kupaniki kidogo kutokana na kuvamiwa ghafla lakini hata hivyo alimwangalia Roma kwa dharau

“We will have to see about that , Pluto now die…”

“Tutaona kuhuu hilo , Pluto sasa kufaa”Aliongea Roma feki kwa sauti kubwa na palepale hali ya hewa ilibadilika na kilichoonekana ni kama anga likicheza huku likitengeza mawimbi kama yale ya baharini , lilikuwa jambo la kushangaza kwani kilichofanyika ni kama wakati Rroma alivyokuwa akipambana na Poseidon , Roma feki alionekana kutumia kanuni za anga.

Amina aliekuwa amesimama kando ya Sofa alivyoonekana ni kama vile mtu anavyoona kivuli cha sura yake kwenye maji yanayocheza cheza lakini utofauti hapo ni kwamba Amina hakuathirika kwani Roma alishamwekea ukuta wa kinga kwa kumzingira na nguvu ya Kijini ya Kimaandiko.

“Sikujui wewe ni aina gani ya miungu lakini inaonekana kabisa uwezo wako wa kudhibiti kanuni za anga ni mdogo mno , Yan Buwen kawa kichaa mpaka akaaamua kukutoa kafara?”Aliongea Roma kwa lugha ya kingereza huku macho yake yakiwa vile vile ya rangi ya njano huku mwili wake kutokuwa na aina yoyote ya mabadiliko.

“This is just the appetizer, The main course is yet to be served …”

“Hiki ni kama kionjo tu , shughuli yenyewe bado..”Roma feki aliongea huku akitoa tabasamu la kebehi akimwangalia Roma halisi kama kituko..

Lakini palepale Roma alijikuta akihisi akili ya ubongo wake ikitoa mivumo ya sauti zisizoeleweka , ilikuwa ni kama mtu ambaye anachanganyikiwa ghafla na kitendo kile kilimfanya kushindwa kufanya maamuzi ya haraka , kwani palepale kulitokea mkandamizo wa hewa usio wa kawaida ambao ulifanya viungo vya mwili wake kuvutana, yaani ni kama kila kiungo kilikuwa kikiukataa mwili wake na kutaka kuchomoka na maumivu yalikuwa makali mno, alikuwa amesimama akishindwa kufanya chochote kwani alikuwa akijaribu kuifanya akili yake kuruhusu nguvu zake kudhibiti viungo vyake , lakini ni kama alikuwa akishindwa kwani akili yake ni kama ipo kwenye hali ya kuchanganyikiwa , kilichomshagaza ni kwamba mtu Roma feki alionekana kutofanya jitihada zozote na nguvu iliokuwa ikisambaa ni kama vile ni nguvu yake ile ya kimaandiko.

“Kufa…!!!”

Kopi ilibwatuka kwa sauti na palepale iliachia pigo kwa kunyumbulisha kanuni za anga na kutengeneza presha kubwa kama ya bomu na kisha akailekezea yote kwa Roma.

Lakini akili Roma ilionekana kurudi na palepale kwa haraka sana aliita nguvu zake za kijini kwa namna ya kunuia na palepale pigo la wimbi lililorushwa kwake likatawanyika na kufanya vioo vya nyumba kupasuka palepale na upepo mwingi ulitoka nje.

Ilikuwa ni kama vile bomu linapolipuka ndani ya nyumba, lakini utofauti ni kwamba hakukuwa na moshi wala moto, hapa ni upepeo tu ambao umepasua madirisha na kukusanya vitu vyote vyepesi na kuvirusha nje.

“Wewe ndio unakwenda kufa leo hii”

Aliongea Roma Roma na palepale alimsogelea Roma feki kwa spidi huku akitumia nguvu zote kuharibu ngao yake aliojitengenezea na kumpiga kwa ngvu eneo la kifuani.

“BAM…!”

Kopi ilikwenda kutua kwenye ukuta na kufanya nyumba yote kutetema, Ngumi ya Roma ilionekana kuwa nzito mno kwani ilikifumua kifua chote cha adui yake na kufanya damu kusambaa. mpaka ile tisheti aliokuwa amevalia ikichanika na kuacha eneo ngumi Sugunyo ya Roma ilipomoa kuonekana vyema.

Lakini ajabu ni kwamba licha ya Roma feki kupigwa na ngumi ile , hakuonyesha hali yoyote ya kuugulia maumivu , bali kitu cha kushanganya ni kwamba mwili wake ulikuwa ukipona kwa spidi ya haraka sana na kifua chake palepale kilifunga na kuonekana kama hajapigwa na kitu chochote jambo ambalo lilimfanya Roma kutoa macho, alichotegemea ni kutawanyisha mwili wa adui yake hapo hapo ili kumua , lakini cha ajabu ni kwamba alichofikiria ilikuwa tofauti kabisa.

“Hahaha… kidogo unaonyesha kuleta ushindani hakika una kila sifa ya kuwa adui yangu , inavutia , inavutia , inavutia , una nguvu kubwa kuliko nilivyokuwazia Hades”Aliongea Roma feki huku akijiweka sawa kwa kuzungusha kichwa kwa majigambo kama vile hakuna kilichomtokea.

“Yan Buwen ndio kawezesha kuwa na huo uwezo?”Aliuliza Roma kwa mshangao.

Hakika ilikuwa ni sahihi kusema Roma alikuwa akipigana na kopi yake , kwani alihisi kuna uwezekano asipokuwa makini anaweza kuzidiwa akili.

“That is right our master gave us ability to revive ourself , we are immortal hahaha..”

“Upo sahihi Master wetu katupa uwezo wa kujifufua wenyewe , Hatuwezi kufa milele”Aliongea huku akiuangalia mwili wake kwa namna ya kujisikia wa thamani sana na kisha akamwangalia Roma.

“Hata Zeus na Athena hawatokuwa na uwezo wa kushindana na Master, nimekuja kukuonyesha robo tu ya uwezo wake wote, Master anasema unamiliki uwezo wa kipekee sana ambao anahitaji kuutunza na kama utakubali kuwa chini yake anaahidi atakuacha uendelee kuishi”Roma feki aliongea huku akijitahidi kumsifia aliemtengeneza.

“Pumbavu kabisa , ninakwenda kukuharibu sasa hivi”

Roma alikasirishwa na majigambo yake na pale pale aliita nguvu za kichawi kwa kugonganisha nishati ya mbingu na Ardhi , mkono wa kushoto alitumia kudhibiti nishati zinazotokana na mbingu na mkono wa kulia alitumia kudhibiti nishati zinazotokana na Ardhi na palepale aling’ata meno kwa hasira na kukusanya vinganja vyake kwa pamoja.

Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana kiasi kwamba Roma feki alishindwa kuelewa kinachofanyika ni nini lakini mpaka anakuja kuelewa ni kama mwili wake unalazimishwa kuingia kwenye kijishimo kidogo kwa kusindiliwa.

Yaani hakuguswa popote lakini alikuwa akielea hewani kama tufe na Roma aling’ata meno kwa hasira zaidi na kwa nguvu zote alitoka nje kwa spidi na ile anatua aridhini aliviminya viganja vyake kwa nguvu kama mtu anaepasua yai na pale Roma feki alitawanyika kama bomu na kila kiungo kujitenganisha , ni nyama nyama zilizotawanyika na kutua na kusambaa kwenye eneo lote la bustani ndani ya eneo hilo.

Katika mafundisho ya kivita, kwenye kupambana na adui kuna kanuni nyingi lakini moja wapo ni mbili ambazo ni muhimu , kuna siraha ambayo unategemea kumkuta nayo adui yako hivyo utajiandaa kukabiliana nayo kwa kutafuta udhaifu wake lakini pia kuna ile siraha ambayo hutegemei kumkuta nayo adui yako hivyo utajipanga kukabiliana nayo katika uwanja wa vita , sasa ili ushinde akili yako ndio inatakiwa kufanya kazi kwa haraka sana kutafuta udhaifu wa kudhibiti siraha hio.

Roma kitendo cha kumpiga adui yake kwenye kifua kiasi cha kukitawanyisha kuna jambo aliweza kugundua palepale , ni kwamba Roma feki uwezo wake ulipungua kidogo na hili ndio lilimpa matumaini kwamba atashinda , aliamini kujigamba kote kuwa ‘immortal’ ni uongo , hivyo aliamini kama atauchangua mwili wake mara nyingi mwishowe atakufa.

Kanuni ya pili muhimu ya vita yoyote ile ni kujiamimisha kwamba una nguvu kuliko adui yako hata kama adui yako ataonyesha nguvu kubwa kuliko wewe wakati wa vita , ni mbimu ambayo hata kwenye maisha ya kawaida hutumika sana , ukiona changamoto iliokuwa mbele yako kuwa kubwa siku zote utashindwa lakini ukijichukulia wewe ni mkubwa zaidi kuliko changamoto inaashiria unauosogelea ushindi.

Wakati Roma akitafakari hayo , alijikuta akipatwa na mshangao mwingine , vipande vya nyama vilivyosambaratika viliaanza kujikusanya upya kwa spidi ya ajabu kama vile ni nyuki wanavyotua kwenye mzinga na hata matone yote ya damu pia yalivutwa sehemu moja.

Roma hakutaka kufanya ujinga palepale alituma wimbi lingine la nguvu ya kijini na kupasua mwili wa Clone na kuusambaratisha ili kutoruhusu Roma feki kujirudisha hai.

Roma alishindwa kuelewa ni jiwe la kimungu tu ambalo ndio limewezesha hayo yote lakini hakuwa na muda wa kufikiria .

Kitu kingine palepale kilimfurahisha , alihisi miale flani ikisambaa eneo lote kama mfano wa sumaku na hapo hapo alielewa kila tone la damu , nyama na mifupa vimeunganishwa na nguvu inayovutana pamoja , na ndio chanzo cha kujifufua.

Roma alichokifanya ni kutengeneza moto mkali wa kichawi na kukausha matone ya damu na kuyesha kila kipande cha nyama ya Clone na palepale ile miale kama ya sumaku ilipotea na Clone kuyeyuka palapale na kupoteza uwezo wa kurudi hai upya hivyo ndio ukawa mwisho wa Roma feki.

Roma alijikuta akitabasamu kifedhuli na pale pale hakutaka kupoteza muda alirudi haraka sana ndani alikomuacha Amina

Amina alikuwa amekusanywa na nguvu ya kijini upande wa kona huku akiwa kwenye mshituko usio wa kawaida ni kama alikuwa ndotoni kwa kile ambacho ameshuhudia na alitamani make kutoka kwenye ndoto.

Roma alielewa mshituko aliokuwa nao Amina hivyo alimsogelea kwa haraka sana na kumkumbatia na pale pale aliachia nguvu ya kijini na kuutawala mwili wa Amina na mapigo yake ya moyo yalianza kurudi kawaida.

“Kila kitu kimekuwa sawa kwa sasa na hawezi kurudi tena, unaweza kupunguza wasiwasi sasa”Aliongea Roma kwa lugha ya kingereza akijitahidi kumpoza Amina aliekuwa kwenye mshituko.

*******

Upande mwingine ndani ya Apartment anayoishi Suzzane mwanaume alieitwa Chriss hakupewa hata nafasi ya kuongea tena , kwani mwanamke mrembo alietokeza kwa namna isieolezeka mbele ya Edna na Suzzane alimyonga palepale pasipo ya kutumia nguvu kabisa na ukawa mwisho wa Chriss.

“Persephone nimefurahi kukutana na wewe kwa mara ya kwanza , naitwa Clelia Allisanto”

“Wewe.. ni ni … Katibu mkuu wa umoja wa mataifa?”Aliuliza Edna huku akimkumbatia Suzzane na kurudi nyuma pasipo kupokea mkono wa mwanamke aliejitambulisha kwao kama Clelia Allisanto ilikuwa ngumu kuamini kama mwanamke huyo ndio yule ambaye ametambulishwa siku chache zilizopitakama mwanamke wa kwanza kuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa.

Yule mwanamke alitabasamu kwa namna ambavyo Edna na Suzzane walivyo kwenye mshituko na wala hakuonyesha kujali.

“Nadhani kwa hali yenu ya mshituko siwezi kuongea zaidi , lakini mimi sio Clelia Allisanto mnaemjua bali mimi ninaejitambulisha kwenu , hata hivyo siku yangu ya leo ni ya kipekee kwani nitakupa zawadi niliokuandalia kwa zaidi ya miaka elfu moja iliopita”Aliongea na palepale alizungusha mkono wake hewani kimaajabu na sehemu aliozungusha mkono anga lake lilionekana kama vile maji yanayoanza kuonyesha dalili ya kuchemka na palepale likatema boksi lililotengenezwa katika mfumo wa kioo lakini ndani yake kulikuwa na mmea mdogo uliochomoza ua la rangi ya bluu.

“Hii ni zawadi yangu kwako , ni ua adimu sana ambalo mpaka leo hii inaaminika mmea wake ushapotea kwenye uso wa dunia, linafahamika kwa jina la Blue Orchid, ni ishara yangu kwako kukutana na wewe leo , unaweza kufikisha salamu zangu kwa Hades kwa kile ulichoshuhudia leo hii”Aliongea Athena na kisha alitoa tabasamu murua sana na kuweka lile boksi kwenye meza ya kioo na kumwangalia Edna aliekuwa ameshikwa na mshangao na kutabasamu kwa namna ya pekee na kisha akapotea palepale.

Suzzane alipoteza fahamu muda ule ule kwa kudondoka chini, lakini upande wa Edna macho yake yote yalikodolewa boksi la kioo lililoachwa kwenye meza , huku akishindwa kupiga hatua hata moja na alikuwa hana hata uelewa muda huo kama Suzzane amepoteza fahamu na hakuna neno hata moja ambalo ameelewa kutoka kwa yule mwanamke.

“Ngo.. ngo . ngo”Sauti ya kugongwa kwa nguvu kwa mlango pamoja na kengere ya Apartment hio ndivyo vilivyomshitua kutoka kwenye mshangao.

“Suzzane..!!!”Aliita Edna kwa nguvu na kuchuchumaa na kumshika Suzzane kwa kumtingisha na palepale ndipo alipojua mwenzake amepteza fahamu , alikimbilia mlangoni na kwenda kuangalia mtu anaegonga na alijikuta akipumua na kufungua mlango kwa haraka.

“Madam upo salama?”Ilikuwa ni sauti ya Adeline , lakini Edna alishindwa kumpa jibu na kumfanya Adeline kuangalia eneo la Sebuleni ndipo alipooana mwili wa Chriss uliopo chini kwenye sakafu ukiwa hauna uhai , lakini pia kushoto kwake aliona pia mwili wa suzzane ukiwa chini ,aliingia kwa haraka sana na mtu wa kwanza kwenda kumshika ni Suzzane na alimpima kwa kidole na kugundua hajafa , alimsogelea Chriss na kumshika na kugundua alishakufa m alijikuta akiangalia juu ya meza na macho yalimtoka na kumgeukia malkia Persephone na kumwangalia kwa mshangao.

“Yupo kwenye mshituko, afya yake ni kipaumbele”Aliongea Edna kwa sauti iliokuwa na wasiwasi akimnyooshea kidole Suzzane aliekuwa chini.

“Sawa Madam”Alijibu Suzzane na palepale alitoa simu ya upepo alioficha karibu na ilipo bastora yake na alionekana kuita msaada.

Dakika chache mbele waliingia wanajeshi wengine wazungu wa kundi la The Eagles jumla yao watatu na walishangazwa na hali iliokuwepo , lakini Adeline hakuwa na muda wa kuongea , aliwapa maelekezo kundoa mwili wa Chriss na pia kumtoa Suzzane hapo ndani kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya huduma ya kwanza na maagizo yalifanyiwa kazi kijeshi kwani ndani ya dakika chache tu Edna na Adeline walibakia.

“Madam nitakusindikiza kurudi nyumbani”Aliongea Adelina kwa lugha ya kingereza na kumfanya Edna kuitikia kwa kichwa na kuusogelea mkoba wake uliodondoka chini na kuubeba, lakini alipotaka kupiga hatua aligeukia boksi la ua na kulinyanyua juu na kuangalia ndani na aligundua licha ya kwamba ni mmea halisi , lakini lilikuwa limekaushwa kwa namna ya kuhifadhiwa.

Adeline kwakua alikuwa akimheshimu Edna kama malkia Persephone alishindwa kuuliza kitu chochote na kumwangalia Edna kwa wasiwasi.

“Edna hakupanda gari kuelekea nyumbani bali , alitaka kwenda kwenye kituo cha afya alikopelekwa Suzzane.

Ni ndani ya nusu saa mbele Roma aliweza kufika mji mpya akiwa na wasiwasi na hio ni mara baada ya kupewa taarifa na Adeline juu ya kile kinachoendelea.

“Edna nini kimetokea?”Aliuliza Roma mara baada tu ya kuingia kwenye wodi ambayo alimkuta Edna na Suzzane wakiwa wamekaa kitako wakiangaliana kwa namna ya kujadili.

Edna alishindwa kujibu swali la Roma moja kwa moja bali alimpa ishara ya kuangalia kiboksi cha zawadi aliopewa na Clelia Allisanto.

“Ghost Orchid”Alitamka Roma na kunyanyua kile kiboksi kwa namna ya kulichunguza huku na yeye akiwa kama haamini kuliona hapo ndani, hata hivyo sio mara yake ya kwanza kuliona ndio maana aliweza kulitambua haraka sana.
 
SEHEMU YA 432

Ni kama nusu saa au na zaidi , katika maabara iliopo ndani ya bara la barafu , yaani Antarctica alionekana Naira alievalia mavazi ya kitabibu huku akiwa ameshikilia kalamu mfano wa Marker pen , akiwa anaandika kwenye ubao kwa kasi ya ajabu mno kiasi kwamba kila baada ya sekunde sitini alikuwa akirekebisha miwani yake.

Aliandika kwenye ubao ule ambao haukuwa wa kawaida , ambao ni dhahiri ulikuwa ubao wa kieletroniki kwa zaidi ya dakika kumi na ukawa wote umejaa maandishi ya kimahesabu ambayo hayakueleweka kwani kulikuwa na miingiliano ya kanuni nyingi za kimahesabu , zikiwa ni zile ambazo huenda mwanafuzi wa kidato cha sita au wa chuo aliesomea hesabu kushindwa kuzitafutia ufumbuzi.

Baada ya kumaliza kuandika , ndani ya chumba hiko kilichojaa mwanga mweupe usionyesha chanzo chake , alijikuta akishika kiuno kwa namna ya kuyafanyia upembuzi maandishi yake huku akigonga kichwa kwa kutumia ile marker pen ya kisasa kabisa ambayo inafanana na zile za simu.

Wakati akiwa kwenye mawazo alijikuta akijikatia tamaa na palepale aliponyeza ile karamu kwa juu kwa namna ya kuminya na dole gumba na palepale yale maandishi yalipotea huku uso wake ukionyesha kutopata jawabu ambalo alikuwa akihitaji na alisogelea ubao akihitaji kuanza upya , lakini kabla tu ya kuanza mlango wa chumba hicho ulijifungua kwa namna isioelezeka kama vile umeyeyuika hewani na akaonekana mrembo Clelia Allisanto akiingia hapo ndani na kumfanya Naira kukakamaa kwa kumuangalia.

Clelia alionekana kutabasamu pasipo kuongea lololote na kisha alimpa ishara Naira ya kumpatia ile Marker Pen au kalamu na kisha akampa ishara ya kurudi nyuma na Clelia alibonyeza ile karamu juu na kisha alisogelea ule ubao ulioshikilia ukuta wa chuma na kisha aliandika maneno kwa lugha ya kingereza makubwa kwa haraka na kisha akasogea pembeni na kumpa nafasi Naira kuyasoma.

Naira ambaye hakuwa akijua anachokusudia Athena , alisoma maandishi yale huku akionyesha mshangao kwenye uso wake akiwa kama mtu aliechanganyikia.

The Devil’s smile au tabasamu la shetani ndio neno ambalo lilisomeka kwenye ule ubao wa kieletroniki na kumfanya Clelia kumgeukia Athena na kumwangalia kwa namna ya kushangaa.

“The Devil’s smile kwanini ukaandika hivi?”Aliuliza na Athena ambaye hakujali mshangao wa Naira alitabasamu pasipo ya kumjibu na kisha alimpa ishara ya kuangalia tena ule ubao wa kieletroniki na pale pale yale maneno yalififia mpaka kupotea kabisa na ule ubao ulibadirika rangi na kutengeneza picha ya mwanamke mrembo , mwenye rangi ya kiafrika aliekaa kwenye kiti ambacho ni kama cha Enzi , yaani kiti cha kifalme huku kichwani akiwa na taji la kimalkia lakini ambalo lina urembo wa ncha yake juu uliotengenezwa na madini kama vigololi flani vya rangi ya kung’aa sana.

Ilikuwa ni picha ambayo hakika haikuwa ya kupigwa na kamera za kisasa na kama utaangalia kwa umakini ni kwamba picha hio ilikuwa kama mchoro lakini uliokuwa kwenye ukamilifu wa hali ya juu na kama itakuwa ni mchoraji ndio aliekamilisha kazi hio basi atakuwa ni kiwango cha juu.

Naira aliangalia picha ile kwa namna ya kushangaa sana kiasi cha kutoa macho , alisogea karibu zaidi kuichunguza ile picha na kuangalia watu waliokuwa pembeni ya mwanamke huyo aliechorwa amekaa kwenye kiti cha kifalme cha enzi alikuwa akionekana kutabasamu lakini tabasamu lake lilikaa vibaya mno, ni sahihi kusema ni tabasamu la kishetani maana haliashirii mzaha wa aina yoyote wala nia njema lakini kwa wakati mmoja likivutia kwa aina yake kutokana na urembo wa mwanamke.

Ukiachana na vazi ambalo lilionekana kuwa la gharama ambalo limevaliwa na mwanamke malkia aliekuwa kwenye picha , lakini pia mbele yake kuna wenye mavazi tofauti na rangi tofauti wakiwa wamezika vichwa vyao chini wakionyesha hali ya kusujudu , ni kama watu hao walikuwa wakiogopa kumwangalia mwanamke aliekuwa kwenye kiti cha enzi na yule mwanamke ambaye alionekana kuwa malkia aliwaangalia watu wake waliomsujudia kwa namna ya tabasamu ambalo sio la kawaida. The Devil’s smile au tabasamu la kishetani ndio uhalisia wa picha yenyewe , lakini hilo sicho kitu kilichomshangaza Naira , kilichomshangaza ni mwonekano wa utambuzi wa mtu mwenyewe.

“Siku zote umekuwa ukijiuliza kwanini mwili wa Seventeen nimeuhifadhi kwenye Cryosleep na nikakujibu nitautumia baadae , leo hii nataka kukufunulia ukweli , ili uweze kufikisha asilimia tano za kufahamu kila kitu kuhusu mimi, lakini kabla ya yote nataka unielezee mchoro unao uona , kwanzia sura ya mwanamke anaeonyesha tabasamu na watu waliokaa pembeni yake wanaashiria nini”Aliongea kwa lugha ya kingereza na kumfanya Naira kumeza mate.

Mrembo Naira licha ya kwamba amekuwa ni mwenye ukaribu na Athena lakini hakumjua kabisa kila siku aliweza kumuona mwanamke huyu kwa mwonekano na wasifu tofauti lakini sura ile ile na hili lilitengeneza ile hali ya muda wote kumuogopa , lakini kinachomtia wasiwasi zaidi na kumhofia ni kwamba tokea wawe na ukaribu na kuendeleza misheni zote kwa maagizo yake , alichojua kuhusu Athena kwa kila kitu ni asilimia nne tu , inamaana kuna zaidi ya asilimia tisini na sita hamjui Athena kiundani na mambo yake yote kuhusu ulimwengu na mipango yake.

“Namuona mwanamke mwenye mwonekano wa Seventeen akiwa zaidi ya malkia, naona utukufu uliokuwa juu yake , mbele yake na nyuma yake , naona mamlaka lakini naona tabasamu la ushindi unaoashiria utawala,lakini nashindwa kuelewa tabasamu lake kwani linaonyesha kuelezea mambo mengi”Aliongea kwa lugha ya kingereza.

“Hahaha…Hahaha..”Athena alicheka na kisha akasogela mbele.

“Unachokiona ndio maisha ya baadae, unachokiona ndio misheni yangu tokea siku nilioweza kumiliki huo mchoro, kadri huyu mwanamke atakavyoendelea kutabasamu , inamaanisha mipango yangu katika misheni zote inaendelea vizuri na ni asilimia kubwa ya matumaini nitayafikia mafanikio”Aliongea

“Unamaanisha nini kusema kadri mwanamke huyu kuendelea kutabasamu ndio mafanikio ya mipango yako?”

“Elewa kauli yangu ya mwanzo ni rahisi kugundua ninachomaanisha , kwa maneno marahisi ni sawa nikisema picha hii imepigwa miaka mingi mbeleni ambayo sijui wakati wake”Aliongea.

“Hii picha ni ya Seventeen , sura ya mwanamke kwenye Cryosleep , ina uhusiano gani na mipango yako?”

“Umekosea swali na sio kawaida yako Naira , swali lako linatakiwa kuwa hivi tokea mwanzo , kwanini kati ya sura za wanawake woote ndani ya dunia nikachagua mwili wa Seventeen? , jibu langu kwako ni hio picha ndio picha”

“Naira unajua ni kwanini kati ya vitu vyote ndani ya dunia ni ngumu sana kuelezea neno Muda kwa maneno marahisi , kuliko inavyoelezewa sasa?”

“Kwasababu kilichopangwa kutokea kulingana na muda ndio hutokea”Aliongea lakini Naira bado alikuwa njia panda.

“Hii picha ni wewe ukiwa kwenye mwili wa Seventeen na imepigwa miaka ya mbeleni hivyo naweza kusema unaichukulia kama unabiii ambao unaotarajiwa kutokea au naweza kusema kuna mtu aliefanikisha kwenda mbele ya muda na kupiga picha na kurudi nayo wakati wa sasa hivyo kukuwezesha kujua nini kitakajokucha kutokea nadhani ndio unachojaribu kuelezea”

“Upo sahihi kwa maneno yako , lakini hata hivyo maneno yako yanaweza kutokuwa sahihi vile vile, labda nikueleze picha hii iliweza kuwa chini ya umiliki wangu kwanzia karne ya kwanza na imekuwa kama tumaini pekee kwangu na maneno yako yanaweza kutokuwa sahihi kwasababu sura ya mwanamke unayoiona inaweza kuwa ya Seventeen au Persephone lakini pia inaawezekana nikawa mimi kwenye mwili wa Seventeen , lakini kwasababu Seventeen roho yake ishacha mwili makisio yanabakia kuwa mawili , inawezekana kuwa mimi au Persephone”Aliongea na kumfanya Naira kuelewa nusu.

Alichokuwa akimaanisha Athena ni kwamba picha anayoiona inaweza kuwa ya Seventeen au pia ikawa ya Edna yaani Persephone kutokana na sababu kwamba wanawake hao wanafanana kwa kila kitu kwani wote ni mapacha , lakini pia kwasababu alikuwa na mwili wa Seventeen ambao ana mpango wa kuutumia hapo baadae.

Mwanamke kwenye picha anaweza kuwa yeye akiwa ameuvaa mwili huo lakini pia anaweza asiwe yeye kwasababu yupo Edna ambaye ni pacha wake na Seventeen na hana namna ya kutofautisha ambaye yupo kwenye picha ni Seventeen au ni Edna.

Lakini pia picha hio anasema ilianza kuwa chini ya umiliki wake wakati wa karne ya kwanza na inaonyesha maisha ya miaka mingi mbeleni zaidi ya miaka ya sasa , miaka ambayo sasa mwanamke huyo inaonyesha kusujudiwa kwa kuashiria dunia yote ipo chini ya miguu yake na yeye ndio mtawala kwani kitendo cha watu kuzika vichwa vyao chini kwa namna ya kusujudu ni kuashiria kwamba mamlaka ya mwanamke huyo ni makubwa kuliko hata Mungu mwenyewe.

Ni rahisi kusema kwamba Athena alikuwa ni mwenye kuchanganyikiwa kwa kutojua picha hio ni yeye akiwa kwenye sura ya Seventeen au ni Edna.

Maelezo yale yalimshangaza Naira na kugundua sasa , kwanini Athena alikuwa akiumiliki mwili wa Seventeen, lakini hata hivyo anashangaa kwani ni swala kubwa mno kulifahamu siku hio.

“Kwahio ndio sababu unalinda maisha ya Edna , lakini pia wakati huo huo umehifadhi mwili wa Seventeen? Ni kwasababu huna jibu la moja kwa moja sura hio inamwakilisha nani kati yako na Edna?”Aliuliza na kumfanya Athena kutabasamu.

“Ni rahisi pia kufikiria hilo kwa haraka kwasababu lipo wazi , lakini swali hilo litakuwa ni sahihi kwasasa tu, kwenye maisha yangu yote mara baada ya kumiliki hii picha , nilijiuliza maswali mengi ni wakati gani wakati wa hio picha ungeweza kutimia niliweza kutaifsiri picha lakini nilishindwa kutafsiri muda”

“Picha hii kuimiliki inaelezea tafsiri nyingi , lakini tabasamu la huyu mwanamke ndio misheni yangu , je unafahamu ni changamoto gani nilipitia ilionitengenezea mawazo kwa muda mrefu?”Aliuliza Athena aliekuwa kwenye mwili wa Clelia Allisanto.

“Ni wakati gani huo?”

“Ni wakati mwanamke huyo akiwa anatoa machozi na watu wanaosujudu kuonekana kumkimbia”Aliongea Athena na kumfanya Naira kutoa macho.

“Unamaanisha picha hii ilishawahi kubadilika?”Aliuliza akiwa kama haamini.

“Ndio ilishawahi kubadilika kwa zaidi ya miaka ishirini mpaka pale lilipotokea tukio kubwa sana kwenye uso wa dunia ndio tabasamu la huyu mwanamke liliporudi vilevile future timeline imerudi kuwa vilevile”

“The choice we make today can shape the future timeline, However future is not determined by the present but rather shaped by a complex interplay of many different factors”Aliongea akimaanisha kwamba maamuzi ya sasa ndio yanatengeneza yanayokuja laini hata hivyo sio mambo ya wakati huu tu ambayo yanaamua yatakayokuja bali kuna mambo mengi yakuzingatiwa.
 
Back
Top Bottom