SEHEMU YA 425.
Kati ya wafanyakazi wa kwanza kabisa ambao Rose alianza nazo mara baada ya kuanza biashara ni Zonga , kutokana na kudumu nae kwa muda mrefu lakini pia kumuamini ndio ilimpelekea kumpa cheo kikubwa ndani ya kundi lake na yote hio ni kutokana pia na Zonga kuwa na elimu kubwa tofauti ya wafanyakazi wake, lakini hakuamini mwisho wake na Zonga ungekuja kuwa mbaya kiasi hicho.
Kundi lote lilishangazwa na mabadiliko hayo kwani kati ya wasaliti wote hawakutegemea Zonga kuwa mmoja wapo , lakini hata hivyo ilikuwa ni ngumu kuamini kama Zonga angeweza kuwa na uwezo mpaka wa kukodi wapiganaji wa kundi la Lapland.
“Wewe mzee unastahili kuliwa na Papa , nimekupatia pesa zangu nyingi kukodi hao wanajeshi lakini hakuna kazi ya maana uliofanya”Aliongea huku akimwangalia Situ ambaye alionekana kupoteza damu nyingi sana kiasi kwamba macho yake yalikuwa yakianza kuona ukungu.
“Zonga unadhani unaweza kujiokoa kwa kumnyooshea hio siraha Rose?”Aliuliza Roma.
“Nilikuwa mjinga kuwaamini Situ na Mzee Bakari kujiingiza katika hili baada ya kuniaminisha wanajeshi wangefanya kazi ya kuaminiika , walivyoniambia unaweza kufa kwa bomu niliwaamini moja kwa moja , lakini ukaweza kupona”.
“Huna namna ya kujitetea ushajulikana kama msaliti”Aliongea mmoja ya watu waliokuwa nyuma.
“Nilijua fika kuna uwezekano wa kugundulika mara baada ya Roma kutoa maagizo ya safari baharini lakini bado nilitegemea hali isingebadilika na kuwa kama hivi”Aliongea Zonga kwa hasira
“Ni kosa kubwa sana ulilolifanya ,kwenye maisha yangu sijawahi kusamehe msaliti”.Aliongea Roma.
“Nishawasaliti sasa unaweza kunifanya nini , ukifanya ujinga wowote nampasua mpenzi wako”Aliongea na kufanya kundi lote kupatwa na wasiwasi.
Lakini upande wa Bakari alitamani kuzimia baada ya jina lake kutajwa na Zonga kungekuwa na uwezekano wa kutoroka eneo hilo alijiambia angefanya hivyo lakini walikuwa katikati ya maji angefanya nini.
“Zonga nimekufahamu kwa muda mrefu na nilikutoa kwenye umasikini na kukupa maisha mazuri lakini sio hivyo tu nikakupa nafasi kubwa ndani ya kundi , nataka kujua ni kwanini umeamua kubadilika na kula njama na kunisaliti?”Aliuliza Rose.
“Kwasababu wewe ndio ulieanza kunisaliti”Aliongea Zonga na kumfanya Rose kushangaa.
“Unamaanisha nini kukusaliti?”
“Sikufanya kazi chini yako kwasababu nilipenda , nilifanya kwasababu nakupenda sana , tulipokutana Mtwara kwa mara ya kwanza nilivutiwa na wewe sana na hata ulipopendekeza nikusaidie kwenye kazi zako nilifanya kwasababu nilitarajia mwisho wa siku ungekuwa mwanamke wangu”Aliongea Zonga kwa sauti na kufanya watu wote kushangazwa na maneno yake akiwemo Roma mwenyewe lakini zaidi sana Rose mwenyewe alishangaa..
“Nilijitoa kwako kwa kila nilichojaaliwa nacho ,nikafanya kazi kwa juhudi ili kukufurahisha lakini hukuwahi kuniona kama mwanaume bali uliamua kumchagua Roma mara tu baada ya kukutana nae licha ya kwamba hakuna cha maana alichokusaidia zaidi yangu”Aliongea kwa sauti bila kujali.
Inaonekana ni kweli kabisa Zonga alikuwa akimpenda Rose , ni kweli kwmaba alitoka mbali na Rose, lakini siku zote hakupenda kabisa mapenzi ya Roma na Rose lakini hakuweka hilo wazi.
Kuna kipindi Zonga mwenyewe alibuni mbinu ya kuweza kumkomesha Roma kwa kuungana na kiongozi wa kundi la Black Mamba ambaye pia alikuwa akimpenda Rose , kiongozi ambaye alikuja kuuliwa na Roma , kijana aliefahamika kwa jina la Karimu.
Zonga alifanya hivyo kwa kuamini Karimu angekuwa na uwezo wa kumdhibiti Roma kutokana na ukubwa wakundi la Black Mamba na baada ya hapo angemtonya Rose juu ya jambo hilo na kupelekea kuwa maadui na yeye kuchukua nafasi , lakini mwisho wa siku licha ya kumchoma Roma kwa Karimu matokeo yakaja kuwa tofauti, Karimu akaja kuuliwa na Roma mara baada ya kumteka Najma na kwanzia hapo Zonga alionekana kumuogopa mno Roma kutokana na uwezo wake , lakini hakuweza kukata tamaa , alikuwa akimtamani sana bosi wake , kila siku alipokuwa akiona uzuri wa Rose , namna mtoto alivyojaaliwa na kalio na umbo zuri udenda ulimtoka na kuzidi kuumia pale alipokumbuka Roma ndio ambaye alikuwa akimhondomora mrembo huyo , alichoweza kufanya ni kuficha hisia zake lakini ukweli alikuwa akiumia sana kwa wivu.
Sasa mara baada ya kupewa uongozi wa juu na Rose wa kundi hilo ndipo aliposhawishiwa na Mzee Bakari kufanya juu chini kumpindua Rose kwa kumtumia baba yake Situ , mwanzoni Bakari walijua lingekuwa jambo gumu kumshawishi Zonga kumsaliti Rose lakini baada ya kuweka mpango wake mezani Zonga alikubali kirahisi sana na hilo liliwashangaza lakini hawakutaka kuuliza zaidi .
Sasa Bakari ndio anajua Zonga alikubali kirahisi kutokana na kwamba alikuwa na kisasi na Roma , lakini pia alikuwa na kisasi na Rose kwa kuamua kumsaliti na mwanaume mwingine ilihali yeye alikuwa akiumia sirini hata hivyo alimuona Zonga kiumbe dhaifu sana kuwahi kutokea kwenye uso wa dunia , unapendaje mwanamke na usimwambie? , kwake alijiambia angekuwa na mtoto kama Zonga angemuua , alijiambia ni kheri kwa mtoto wake Karimu aliekufa akipigania penzi lake lakini sio kwa upuuzi wa Zonga..
Moja ya jambo ambalo lilimchukiza Zonga ni pale Rose alipohama anapoishi na kwenda kuishi na Dorisi Kimara , ilimchukiza kwani ni kama alihisi Rose alikuwa anaolewa na Roma.
Sasa wahenga wanasema mapenzi yanaweza kukufanya kichaa hata kuingia kwenye vita ambayo huwezi kushinda sasa ndicho alichokifanya Zonga , alijua kulikuwa na asilimia sabini za kutoweza kumdhibiti Roma lakini therathini zilizobaki ilikuwa zinamtosha sana kwake kulipigania penzi lake.
Kosa alilolifanya ni kwamba hata yule anaempigania hakuwahi kumwambia hisia zake , huenda angemuelewa lakini yeye akaamua kufanya vitu kimya kimya.
Dorisi mwenyewe alijikuta akijawa na huzuni baada ya kusikia sababu halisi iliomfanya Zonga kumsaliti, alijikuta akikumbuka maisha yake yalivyokuwa tokea siku ambayo alianza kumpenda Roma licha ya kwamba hakujua alikuwa wapi , alikumbuka hata safari yake ya kuanzisha club ndani ya jiji la Dar msukumo ulikuwa ni mapenzi alishindwa kujitofautisha na Zonga.
Ndio baada ya Rose kuweza kusaidiwa na mtu asiemjua , mtu ambaye alimuokoa kwa namna ya ajabu na kumuacha hotelini huku akiwa amemponyesha kwa namna ya ajabu , lakini wakati huo akimuachia na kiasi cha pesa aliguswa sana na msaada huo , alijiona ni kama alikuwa akisoma hadithi za SinganoJr ambazo zilikuwa za kufikirika , alijiambia inawezekanaje ikatokea mtu akakuokoa kwenye kifo akiwa hakujui na baada ya kukuokoa anakusafirisha umbali mrefu ndani ya muda mfupi kimaajabu lakini sio hivyo tu mtu huyo huyo anakuponyesha kwa namna ya kustaajabisha lakini baada ya hapo bado hakukatii tamaa anakuachia na pesa ya matumizi na kisha kupotea pasipo kusubiri hata shukrani.
Rose wakati ule alijiambia ni jambo ambalo haliwezekani kwa ulimwengu wa sasa ambao binadamu wengi walikuwa waovu , binadamu ambao wanaweza kupanga njama za kuwaua watoto wao wa kuwazaa bila huruma kama baba yake , hivyo alikuwa na kila sababu ya kumpenda mwanaume mwokozi wake licha ya kwamba hakumjua , licha ya kwamba kulikuwa na asilimia ndogo sana ya kuonana nae tena.
Sasa Rose baada ya kukumbwa na tukio la aina hio la ajabu kwa mtu wa kawaida kama yeye kumtokea alijiapiza kwa majina yote lazima atamtafuta mwanaume aliemsaidia kwa namna yoyote kwa ajili ya kurudisha deni.
Moja ya sababu kubwa ya Rose kuandamwa na baba yake ni kutokana na Situ kumtaka Rose amuelezee ni mahali gani mama yake marahemu aliweza kuficha pesa na dhahabu zake , Sehemu ambayo aliamini Rose alikuwa akiifahamu , lakini Rose licha ya kupewa mateso na baba yake ili kutaja eneo ambalo lina mali ambazo mama yake alificha hakuweza kufumbua mdomo , moja ya sababu ya kutofanya hivyo ni kutokana na kwamba Rose alikuwa akimchukia sana baba yake , kwani kwa macho yake yeye alimshuhudia baba yake akimpiga risasi mama yake kwa kosa dogo sana.
Sasa baada ya Roma kumuokoa kwenye mikono ya baba yake alichokifanya ni kutumia mali ambazo ziliachwa na mama yake na kuanzisha biashara , alikuwa na machaguo mengi sana , alikuwa na chaguo la kufanya biashara za halali za kujipatia kipato cha kawaida na kuendeleza maisha yake , kwani pesa alizoachiwa na mama yake zilikuwa nyingi lakini hakuchagua kufanya biashara halali kwasababu moja tu, moyoni mwake kwake pesa na maisha ya kawaida yasingekuwa na maana pasipo ya kumpata mwanaume anaempenda mwanaume ambaye alimuona kama malaika..
Hivyo Rose akafikiria mbinu rahisi ya kuweza kumpata mwanaume huyo ni kufanya biashara haramu akiamini siku zote mwanaume yule kwa mazingira yale aliomuokoa ni lazima angekuwa na uhusiano mkubwa sana na dunia ya ‘underwold’ , dunia ya wahalifu , hivyo aliamini kama atajikita huko asilimia za kukutana nae zingekuwa kubwa kuliko katika ulimwengu wa kawaida wa watu watii wa sheria.
Hivyo ndivyo Rose alivyojiingiza kwenye biashara ya uuzaji wa madawa ya kuleva , akatengeneza koneksheni ya kupata ‘supplier’ ndani ya mkoa wa Mtwara ambao ulikuwa na bandari na baada ya kufanikiwa kirahisi kutokana na kuwa na pesa ndipo alipofikiria hatua ya pili , aliamini ndani ya jiji la Dar es salaam ndio iwe sehemu ya uendeshaji wa biashara yake kutokana na uwingi wa watu , akiamini kwamba ndani ya jiji hilo lingempa asilimia kubwa ya kukutana na yule mwanaume kwa mara nyingine, basi ndipo ikazaliwa Club B ndani ya eneo la Mbagara Maji matitu.
Wanafalsafa wanaaamini ulimwengu upo kwa ajili ya kupigania nafsi zinazoendana kwa kukutana na hatimae kuwa pamoja , wanaendelea kusema baadhi ya vitu vinashangaza sana na vinanguvu kiasi kwamba tafsiri yake inakuwa sio bahati mbaya.
Hivyo ni rahisi kusema kwamba eneo , hali ya kimazingira na muda havina nafasi sana kwenye watu ambao wamepangiwa kuwa pamoja, hicho ndio kilichomtokea Rose kwani ndani ya miezi michache tu ya kutua ndani ya jiji la Dar es salaam na kuanzisha club yake ndio wakati ambao ameweza kukutana na mwanaume yule wa ajabu, ijapokuwa hakumjua vizuri kwa sura usiku ule, lakini baada ya kukutana nae moyo wake ulimtambua muda huo huo.
Roma mara yake ya kwanza kutua nchini Tanzania mtu wa kwanza kukutana nae ni Rose ambaye alikuwa kwenye mazingira ya kuhitaji msaada na hata yeye mwenyewe alishangazwa na tukio hilo na ndio maana baana ya kumsaidia alimtoroka, hakutaka kuchangamana nae tena kutokana na sababu zake.
Kwa upande wa Rose mara baada ya kupata nafasi ya kumlipizia baba yake kisasi hakufanya hivyo kutokana na kwamba aliamini huenda pasipo baba yake asingeweza kukutana na Roma ndio maana akamwacha hai na kumpa nafasi ya pili ya maisha licha ya chuki aliokuwa nayo zidi yake.
“Zonga asante sana kwa kuwepo na mimi kwa nyakati zote za mapambano yangu , lakini uliokuwa nayo sio mapenzi ya dhati juu yangu , kama kweli ulikuwa unanipenda ungekuwa na ujasiri wa kuweka wazi hisia zako na sio kupanga njama za kutaka kunidhuru , hisia zako juu yangu ni Lust(tamaa ya ngono) na Obsession(Wazimu wa mapenzi) ndio maana umeamua kunisaliti”Aliongea Rose.
“Unaweza kutafsiri hisia zangu utakavyo lakini leo hii siwezi kukuacha hai , tutakufa wote hapa na huenda kwasababu ushazielewa hisia zangu tukapendana huko kuzimu, hata hivyo wote tunadhambi kama yasemwayo ni kweli wote tutakuwa sehemu moja baada ya kufa nitafidia juhudi zangu zote nilizopoteza hapa duniani”Aliongea Zonga huku akikoki siraha yake vizuri lakini pasipo kuelewa alivyopigwa alijikuta siraha yake ikiwa kwenye mikono ya Rose kirahisi sana , kwani alipigwa pigo kwa spidi ambayo hakuweza kudhania Rose angeweza kuwa nayo.
Hata wale wahudhuriaji walijikuta wakishangazwa na umahili wa Rose kwani kitendo alichokifanya ni kama kwenye muvi.
Roma upande wake alishangazwa na Zonga sana na kujiambia kweli moyo wa mtu ni kichaka siku zoe Zonga alionyesha utiifu kwa Rose sio kwasababu alimchukulia kama bosi bali alikuwa na hisia za mapenzi.
“Zonga huenda hali yako ikafanana na yangu , lakini utofauti wako na wangu ni kwamba mimi nilikuwa na mapenzi ya dhati mapenzi ambayo sikuyaficha kwa yule niliempenda , huenda unadhani labda wewe ndio mtu wa kwanza kukutana na mimi lakini kwangu Roma ni mtu wa kwanza kukutana nae na kama sio yeye leo hii usingeweza hata kutambua kama naishi ndani ya uso huu wa dunia, Roma aliniokoa kutoka kwenye mikono ya baba yangu lakini licha ya hivyo hakuhitaji chochote kutoka kwangu , alinisaidia na kisha akatoweka na mimi ndio niliweka juhudi kumtafuta , leo hii nimefikia hapa nilipofika kwasababu tu nilikuwa na nguvu ilionisukuma kufanya hivyo, mapenzi hayapo kumtengenezea mtu uoga bali humpa ujasiri , ukijiona huna ujasiri hata wa kuweka hisia zako wazi tambua bado hujapenda”
“Nilikupenda kwasababu ulikuwa mtiifu kwangu na nilikuchukulia kama ndugu yangu ndio maana nikakupa nafasi yangu, ni kwasababu naheshimu juhudi zako , hili ni kosa lako la kwanza kunitendea nakupa nafasi ya mwisho kili mbele yangu umekosea na haupo tayari kurudia tena na kwanzia leo nitakuacha uendeleee na maisha yako”Aliongea Rose kwa sauti.
“Hahaha.. Hahaha… huenda ulichoongea ni sahihi lakini ninachotaka sio msamaha tena , ninachotaka ni penzi lako tu na kama hakuna uhakika wa kulipata siwezi kukuomba msahamaha na kukuachia , mafanikio ya biashara ya Kundi la Tembo yamesababishwa na mchango wangu mkubwa ila sio wewe nipo tayari kuomba msamaha kama nitakuwa na uhakika wa kuwa kiongozi wa Tembo lakini pia kama utazikubali hisia zangu”Aliongea kwa huzuni huku akicheka kama chizi na kumfanya Roma kushangazwa na maneno yake na watu walijiambia Zonga ni chizi kweli , hayo maneno alitakiwa ayatamke mapema na sio muda huo akiwa anachungulia kifo.
“Nakupa nafasi ya mwisho ya kukiri kosa lako na kuomba msahamaha”
“Haina hajaa..”Aliongea Zonga na katika tukio la kuchekesha na kuhuzunisha alijirusha majini na kufanya kila mtu kushangazwa na ukichaa wa Zonga na Rose alijikuta akivuta pumzi ya ahueni lakini iliochanganyika na majonzi , moyo wake ulikuwa mzito kumuadhibu Zonga kutokana na kuwa nae karibu kwa muda mrefu mpaka kumchukulia kama ndugu.
Baada ya tukio hilo Rose alimgeukia Bakari ambaye baada ya Zonga kumtaja tu vijana wake waliokuwepo hapo walimuweka chini ya ulinzi.
“Mr Bakari nadhani uliamua kukiuka makubaliano yetu , kabla hujakutana na adhabu yako nakupa na wewe nafasi ya kujitetea lakini kama utajirusha majini na kuliwa na Papa ruhusa unayo”Aliongea Rose na Mzee Bakari aliekuwa kwenye hali ya wasiwasi palepale alimwangukia Rose miguuni.
“Naomba usiniue tafadhari , Usiniue tafadhari”
“Nina sababu ipi ya kukuacha hai mtu kama wewe, kama unakumbuka vizuri hili ni kosa lako la pili unarudia kufanya”Aliongea Rose na kumfanya Bakari kumeza mate mengi na kisha akamgeukia Roma aliekuwa kwenye meli nyingine.
“Nitakuambia kila kitu ila naomba uniache hai tafadhari”
“Unafikiri unachotaka kuongea kinaweza kunipa sababu ya kuweza kukuacha hai?”Aliuliza Rose.
“Ndio kwasababu ninachokuambia kinamuhusu mwanaume unaempenda, kama utaahidi kuniacha hai nitakwambia , Mr Roma nakuhakikishia ninachokwenda kukuambia ni muhimu sana kwako kukifahamu”Aliongea kwa sauti na kumfanya Roma atamani kujua ni jambo gani ambalo Bakari anataka kumuambia.,Rose alimwangalia Roma kuomba mawazo yake .
“Mr Bakari unaweza kuongea na nitaamua mwenywe kukuacha hai kama utakuwa na sababu yenye uzito unaolingana na miasha yako”Aliongea Roma.
“Nipo tayari kuongea , lakini swala lenyewe siwezi kukuambia mbele ya watu hawa wote kwasababu ni siri kubwa”Aliongea na Roma alimwangalia na kuona Mzee Bakari alionekana kujiamini.
Roma alimwangalia Situ ambaye amemning’iniza na kugundua alishakufa tayari kutokana na kupoteza damu nyingi , alichokifanya ni kumuachia na kutumbukia majini.
“Mr Bakari nitakusikiliza sababu yako”Aliongea Roma na kumfanya Bakari kuvuta pumzi za ahueni , ijapokuwa hakujua sababu aliokuwa nayo ingekuwa kubwa kumfanya Roma asimuue lakini alijiambia ni kheri amepata dakika kadhaa za kuendelea kuishi.
“Tokea siku ambayo nilikuja kujitambua na kujua lipi jema na lipi baya , niligundua maisha yangu yote yameunganika moja kwa moja na ulimwengu wa uhalifu kutokana na kuzaliwa na wazazi ambao walikuwa wanajishusha na uhalifu , nilichoshwa na maisha ya aina hii lakini sikuwa na jinsi kukubaliana nayo , hivyo kwanzia sasa nataka kuwa huru na mambo yote hivyo najiondoa rasmi kwenye nafasi yangu kwa kujiuzuru na Jacob ndio atakuwa mrithi wangu na kuendesha operesheni zote zinazohusiana na kundi la Tembo”Aliongea Rose na kufanya watu wote kuwa kimya huku wakionyesha sura za kutokubaliana na jambo hilo , upande wa Jacob kibonge mwenyewe hakutarajia kauli hio kutoka kwa Rose.
“Babe hata mimi nakuunga mkono , naamini Kibonge anaiweza hio nafasi”Aliongea Roma lakini bado hakuna alieunga mkono.
“Najua wote hapa mna wasiwasi , lakini nawahakikishia Jacob anaiweza nafasi yangu na kama ndani ya miezi michache hatofanikisha kazi za kundi basi nipo tayari kumbadilisha na kuwapa nafasi ya kumchagua mnaemtaka, lakini niwatahadharishe tu kwamba kama kuna mmoja wenu ambaye atafanya njama za kufanya usaliti, niwakumbushe nina rekodi na kila mmoja wenu hapa juu ya machafu yake anayoyafanya na nitayaweka hadharani serikalini na sidhanni kama kuna mmoja wenu anaweza kutoka kwenye mkono wa sheria , pili hata kama ukapata nafasi hio maisha yako utakuwa huna , kitakupata kama kilichompaa Situ”Aliongea na kuwafanya wote kuogopa maana tukio la Roma kuvunja vunja watu shingo lilikuwa la kuogofya kweli na Watu wote walitingisha vichwa vyo kukubaliana na maneno ya Rose
“Jacob umepewa nafasi ya kuongoza kundi , lakini nikuhakikishie kwamba ukifanya jambo lolote la kijinga kama Zonga jihakikishie kuwa ni mfu , una mke na unatarajia mtoto hivyo nakushauri msingi wako wa kuongoza uwe ni wa amani”Aliongea Roma na Jacob alimwangalia Roma kwa woga mno na alijikuta akitingisha kichwa haraka haraka kutii maneno yake.