Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 538.

Ijapokuwa mwanzoni alisema hatomtambua Edna hadharani kama mtoto wake , lakini likija swala linalomuhusu mara nyingi huwa siriasi sana , hivyo mara baada ya Linda kumwmabia kwamba kuna kitu kinachoendelea katika jumuia ya siri ya Ant- illuminat kinachohusiana na Edna mapigo yake ya moyo yaliongezeka kasi.

“Edna anaetarajiwa kuwa kiongozi wa kundi la Ant – illuminat”Aliongea Linda na kumfanya raisi Jeremy kuwa kama mtu ambaye hajasikia vizuri.

“Linda unataka kumaanisha nini ?”

“Ni kama nilivyosema mheshimiwa , Edna ndio kiongozi mtarajiwa wa kundi la Ant- illuminat na mpaka sasa umoja upo katika hatua ya pili kuthibitisha hilo”Aliongea Linda na kumfanya Raisi Jeremy kuegamia kiti chake kwa muda kama mtu ambaye anajaribu kusharabu maneno ambayo amaeambiwa.

“Mheshimiwa nadhani upo kwenye mshutuko na taarifa hii , lakini ninachojaribu kukuambia ni kitu kilichotokea , Edna amepitia hatua ya kwanza kuthibitika kama kiongozi”

“Kama kauli yako ni sahihi, Linda unamaanisha nini swala la kuthibitisha , Edna hana uhusiano wowote na kundi la Ant- illuminat na sio mwanachama kwanini itokee tu awe kiongozi?”

“Hata hilo ni swali ambalo wengi walijiuliza na mpaka sasa hakuna jibu kamili”

“Unamaanisha nini hakuna jibu kamili?”Aliuliza na kumfanya Linda kufikiria na kisha akaamua kumwelezea kwa ufupi kile kilichotokea Tanzania mwezi uliopita Edna kutoa pete ambayo inamtambulisha kama kiongozi , mpaka anakuja kumaliza Raisi Jeremy alikuwa kwenye mshangao mno na hakuamini maneno ya Linda.

“Linda hiki ulichosema ni kweli?”

“Ni kweli mheshimiwa , lakini licha ya hivyo mpaka sasa Edna bado hajatambulika kama kiongozi , kilichofanyika ni hatua ya kwanza tu ya kuona kama kweli ni yeye”.Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy kuwaza, kama kweli kulikuwa na pete je pete hio Edna kaitoa wapi? Au Roma ndio kampatia , alijiuliza maswali ya aina hio.

“Okey tuseme maneno yako ni sahihi, vipi kuhusu hatua ya pili?”

“Mheshimiwa kuhusu hilo sijui chochote, lakini ninachofahamu upo mchoro wa unabii ambao ndio utathibitisha hilo”

“Mchoro wa unabii!!?”

Kila neno ambalo amesikia kutoka kwa Linda lilikuwa la kushangaza ambalo halikuaminika kabisa kwake.

“Mheshimiwa nilichojaribu kukuambia ni siri ya jumuia, nimejitoa muhanga kuvunja sheria kutokana na deni kubwa ambalo unanidai, hivo sina kingine cha kuelezea ila hiko ndio kinachoendelea na kinachomuhusu Edna”Aliongea na Raisi Jremy hakutoa jibu lolote zaidi ya kuonekana kuwaza kwa takribanni dakika mbili a kisha akamwangalia Linda.

“Jana nimepewa taarifa ya siri ambayo inahusiana na mpango TASAC na nilichosikia ni kwamba jamii hii ya Ant- illuminat ipo chini ya ushawishi wa ukamilishwaji wa mpango TASAC na mimi ndio kiongozi ambaye nilipatia jukumu la kuusimamia katika bara la Afrika”

“Najua hilo mheshimiwa wewe kuwa kiongozi wa mpango huo , lakini sina taarifa za mpango huu kuwa chini ya ushawishi wa umoja wetu”

“Ninachotaka kusema Linda kamnitaendelea kuendelea kuwa kiongozi basi nitahitaji majibu ninayoyataka”Aliongea Jeremy na kumfanya Linda kushangaa.

“Mheshimiwa unamaanisha?”

“Linda nadhani unakumbuka makubaliano yangu na raisi wa Urusi yalikuwaje?”

“Ndio nakumbuka mheshimiwa”

“Nilikubali kuongoza mpango huu kutokana na kwamba nilihitaji majibu , kwa upande wangu nimefanya kazi kubwa lakini kwa upande wao hawajatimiza ahadi yao mpaka sasa , ni kweli kwamba nilipata baadhi ya taarifa lakini hawakutimiza kitu nilichokuwa nikitaka , kitu kinachohusiana na mtoto wangu Lorraine, kama kweli mpango TASAC upo chini ya ushawishi wa umoja huu basi nahitaji majibu zaidi”

“Lakini mheshimiwa ulishasema serikali ya Urusi imeacha kabisa kufatilia swala linahosiana na mpango LADO, unafikiri wanaweza kuwa na majibu unayoyataka?”

“Upo sahihi Linda kwasasa wanaweza wasinipe majibu kwasababu Rwanda ni nchi ndogo , ila kwa kushirikiana na PANAS nitapata majibu ya maswali yangu yote na isitoshe ushasema kuna mchoro wa unabii”

“Ndio mheshimiwa nimesema hilo lakini ni swala ambalo halijathibitishwa”

“Na siwezi kusubiri lisibitishwe ndio nichukue hatua , kwasasa Desmond hayupo nchini na haonekani mahali alipo na inabidi nianze harakati za kumrudisha Edna nchini Rwanda kwa namna yoyote ile na hatua ya kwanza lazima nimwambie kila kitu kuhusu pacha wake nadhani ana maswali juu ya hilo”Aliongea.

“Mheshimiwa kila kitu?, huoni kama mume wake kamficha kwasababu maalumu”

“Unafikiri kuna sababu gani ya kumficha mpaka sasa , Roma alipaswa amuambie kabla hata hawajaenda kufanya sherehe lakini akamficha , kama ameshindwa kumwambia yeye nitamwambia mimi kama mzazi”

**********

“Mkurugenzi , timu ambayo inasimamia filamu imetuma ripoti kwamba wanamalizia kipengele cha mwisho hapa nchini Tanzania kukamilisha muvi yote , hivyo mpango wao ni kuandaa sherehe ya kuwapongeza waigizaji na watu wote waliohusika?”Aliongea Daudi.

“Unamaanisha Muvi anayoongoza director Fabby Lassay?”

“Ndio mkurugenzi”.

Roma alijikuta kidogo akiwaza tokea muvi ianze ni kama hajahusika hata kidogo kufatilia maendeleo ya Sophia na isitoshe ni mara yake ya kwanza kuigiza filamu.

“Sindhani kama ni tatizo kampuni yetu inaweza kusaidia kuandaa kila kitu nadhani ndio maana wakakupatia taarifa”Aliongea Roma na Daudi alikubali.

“Sijamuona Wendy tokea asubuhi?”

“Ndio mkurugenzi Wendy yupo likizo ya uzazi?”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa lakini aliishia kutingisha kichwa.

Roma alijiuliza kama asingekuwa wa tofauti huenda muda huo angekuwa na watoto wengi tu , lakini vilevile aliona huenda maisha yake yasingekuwa ya aina hio, baada ya kupata wazo la watoto hapo hapo alimkumbuka Rose ambaye hakuw akijua maendeleo yake , kwani katika wanawake wake wote aliekuwa akipanda levo kwa spidi alikuwa ni Rose.

Siku chache mbele , ikiwa ndio inaelekea mwishoni mwa mwezi wa sita Roma alitumia muda mwingi kufika kazini kama kawaida, ijapokuwa hakuwa na majukumu makubwa lakini aliweza kufanya baadhi ya vikao na kushiriki baadhi ya matukio ya kampuni na hakuboreka kwani aliona ratiba hizo ni kama kiungo tu kwenye maisha yake ya kiburudani, hakutaka kujichosha sana , kwani alichukulia kama vile yupo likizo ya maisha,

Aliona kazi kubwa alishafanya tokea alipokuwa mdogo na siku ambayo aliamua kujitoa katika maisha yake aliokuwa akifanya na kurejea Tanzania ilikuwa ni kama mapumziko au kustaafu , lakini licha ya hivyo historia ilikuwa ikimfuata kila mahali , hivyo hakutaka kushidana na kile kinachotokea mbele yake , kukiwa na tatizo aliona atashughulika nalo na akipata muda wa mapumziko anautumia vizuri.

Upande wa Tanya aliweza kukamilisha kazi ambayo aliagizwa na siku chache tu kifo cha Mzee Longoli kilitangazwa katika vyombo vya habari , huku chanzo cha kifo chake kikiwa ni mzee huyo kujipiga mwenyewe risasi , lakini ukweli ni kwamba Tanya aliweza kumchoma Mzee huyo na dawa maalumu ambayo ilimsababishia maumivu makali sana , maumivu ambayo alishindwa kuyavumilia na kuishia kukatisha uhai wake.

Staili hio ya kimauaji ilikuwa ikifanyika sana katika ulimwengu wa kihalifu lakini tatizo ni kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kutoa dawa hio na asigundulike.

Baada ya kifo cha Mzee Longoli moja kwa moja aliehusishwa kufanya jambo hilo ni ukoo wa Kweka , kwani kwa muda mrefu Raisi Senga na familia yake hawakuwa na mahusiano mazuri kutokana na mzee huyo kumsapoti sana marehemu raisi Kigombola, hivyo kifo chake kilitafsiriwa kama ukoo huo unajaribu kumaliza maadui zake na kuendeleza kujikita zaidi katika siasa ndani ya Tanzania.

Ilionekana kama babu yake Roma alikuwa akitarajia maamuzi ambayo angefanya kwani mara baada ya taarifa ya kifo cha Mzee Longoli kazi kubwa ilifanyika kutuliza familia nzima hususani mtoto wake mkubwa ambaye ni raisi.

Mheshimiwa Raisi Hassani Longoli kutoka Zanzibar alijua ni kipi kinaendelea lakini kwa wakati huo hakuwa na nguvu ya kisiaza zaidi kama ilivyo kuwa mwanzo wakati Raisi Kigombola akiwa hai, hivyo akafunika kombe mwanaharamu apite.

Jambo moja ambalo lilimshangaza Roma ni namna ambavyo Raisi Senga alihusika kwa kiasi kikubwa kuzima swala hilo na haikumshangaza yeye tu hata babu yake Afande Kweka aliliona hilo na moja kwa moja alichukulia kama ishara nzuri ya familia kurudi na kuwa kitu kimoja.

Tanya mara baada ya kazi hio , Roma hakuta aendeleee kubaki Tanzania , kwani alimleta kutokana na hofu ya Yan Buwen , hivyo alimpa likizo ya kurudi Japani ili kuendelea kusimamia maendeleo ya kundi la Yamata.

Roma alitumia muda mwingi kusimamia warembo wake kujifunza mbinu za kijini na wakati huo huo akiendelea kutengeneza vidonge na alijikuta akifarijika mara baada ya kuona karibia wote walikuwa na maendeleo makubwa zaidi.

Mtu ambaye alikuwa ndio anaanza ni Najma lakini alibahatika yeye kuanza na vidonge hivyo hakutumia nguvu nyingi kama ilivyokuwa kwa wenzake ambao walianza bila viodonge , lakini licha ya hivyo Roma aliamini atapanda levo taratibu.

Ilikuwa bado ni giza licha ya kwamba saa kumi na mbili asubuhi ilikuwa imetimia , pengine ni kutokana na dalili ya mvua ya siku hio.

Katika kitanda kikubwa cha tano kwa sita alionekana Amina ambaye alikuwa amelalia kifua cha Roma kama kifaranga cha kuku , mabega yake ya rangi nyeupe yalionekana wazi lakini muda huo alikuwa kwenye usingizi mzito na hio yote ni kutokana na kazi nzito ambayo imefanyika usiku kucha.

Roma tokea arudi Korea utaratibu wake ulikuwa ni uleule , kwasababu Lanlan alikazania kulala na mama yake, basi asingeendelea kulala peke yake na kukumbatia mto , hiyo ilimpa nafasi ya kwenda kutembelea wanawake zake usiku.

Mara nyingi Roma kila muda wa chai ukikaribia basi atakuwa chumbani kwake ndani ya muda akiwa ashajiandaa tayari ili kuonyesha kwamba alikuwa amelala ndani ya nyumba , lakini ukweli alikuwa akijua kabisa wanafamilia hao walikuwa wakijua kile kinachoendelea , lakini licha ya hivyo hakuna ambaye alikuwa na ujasiri wa kuongea neno lolote kuuliza.

Wakati Roma akiwa amefumba macho ghafla tu alishtuka kutoka usingizini na kufumbua macho na kitendo cha kutingishika kilimwamsha Amina.

Honey , unafanya nini , bado nina usingizi”Alilalamika mrembo Amina.

“Nimeweza hata kupata msisimko kwa hapa , Rose kafanikiwa kupata ufunuo na kukamilisha kuingia katika levo ya Nafsi”Aliongea Roma huku akionyesha furaha.







SEHEMU YA 539.

Kwa kipindi chote ambacho Roma alikuwa nje ya nchi Rose ndio ambaye pekee alionyesha jitihada kubwa za kujifunza mbinu hizo za kichawi , alikuwa ni mara chache sana kuonekana mtaani , kila alipoamka alikuwa akijifungia chumbani kwake na muda mwingine angetafuta mlima wowote na kutulia huko akiendelea kujifunza kuvuna nishati za mbingu na ardhi.

Roma tokea arudi alishindwa kumpata , kwani hakuwepo hata nyumbani na alijua atakuwa sehemu akiendelea kujifunza , hivyo hakutaka kumsumbua kumtafuta na kuacha yeye mwenyewe kuweza kufanikisha bila ya kumuingilia.

Sasa alikuwa na uwezo wa kuweza kupata hisia za uwepo wa mtu anaetumia nguvu za kijini hata kwa mbali kwasababu Tanzania ni nchi tulivu na ina nguvu kidogo sana za kiroho tofauti na nchi nyingine.

“Kweli , lakini umejuaje?”

“Tanzania inatembelewa na majini ndio , lakini hakuna jini lolote ambalo linajifunza kuvuna nishati za mbingu na ardhi na sio hivyo tu kwa binadamu pia , ukiachana na mtu ambaye najua yupo kwenye levo ya Nafsi , sidhani kama kuna mwingine ambaye anaweza kuwa katika levo hio akawa hapa Tanzania ,sasa kumeongezeka mtu mwingine ambaye yupo tayari kwenye levo ya Nafsi ambaye ashapata ufunuo wa siraha , unadhani atakuwa nani kama si Rose?”Aliongea Roma na palepale alitoka kitandani na kuvaa mavazi yake na kuondoka akimuaga kwamba anaenda kumtafuta Rose

Dakika chache mbele Roma aliweza kufuata upande ambao anapata msisimko na alikuja kutokezea kwenye kilele cha mlima wa msitu wa Pugu.

Kwa mazingira namna yalivyotulia , hakika ilionyesha Rose alikuwa ameamua haswa kutaka kujifunza mbinu hizo , maana ni ngumu sana kumkuta mtu ndani ya msitu huo bila ya kuwa na wasiwasi na baridi yote hio ya asubuhi , lakini licha ya hivyo Rose mwili wake haukua ukipata baridi kwani tayari alikuwa na nguvu za kijini zinazozunguka kwenye mwili wake , hivyo kuwa rahisi kuvumilia baridi kali.

Roma alimkuta Rose akiwa amesimama kwenye kilele hicho akionekana kushangaa mazingira , alikuwa amevalia sweta la rangi ya bluu na suruali ya jeans.

Katika macho ya Roma alimuona kama mrembo huyo amezaliwa upya , urembo wake uliongezeka maradufu mno na kwa mwanaume yoyote ambaye angemuona huenda angetokea kumpenda sana kwani alikuwa akisambaza Aura ya mvuto usiokuwa wa kawaida, hakika nguvu za kijini zilikuwa zinafaida.

Rose mara baada ya kuhisi mtu nyuma yake aligeuka na alijikuta akishangaa huku akimwangalia Roma , alijikuta akijawa na tabasamu kwani ni zaidi ya mwezi hawakuwa wameonana.

“Vipi unaonaje , kama vile umeingia kwenye ulimwengu mpya kabisa si ndio?”Aliuliza Roma

“Hapana”

“Kama sio hivyo unajisikiaje?”

“Ni ulimwengu huu huu, lakini kila kitu kinaonekana kuwa tofauti na zamani”Aliongea na kumfanya Roma kutingisha kichwa.

“Kila mtu ni tofauti hususani kwenye swala la utashi na hisia za kimazingira , hata kama kuwe kuna mfanano lakini ufunuo wa kiuelewa utakuwa tofauti , hivyo siwezi kuelewa ni kipi umefunuliwa mpaka kukamilisha levo ya nafsi na hivyo hivyo siwezi kujua wengine watapata ufunuo gani wa kimazingira”

Baada ya kuingia levo ya Nafsi moja kwa moja Rose ni kama amezaliwa upya kimwonekano , ijapokuwa alikuwa akionekana kwa nje ni yuleyule na ngozi yake ileile , lakini alikuwa akizingirwa na nguvu isiokuwa ya kawaida ambayo ilikuwa ikimlinda

Muda huo huo alihisi mkono waRoma ukipita ukipita juu ya uso wake na palepale wimbi la nguvu ya mbingu na ardhi liliweza kutikisa miti na kuinua upepo mkali.

“Ijapokuwa ni mwaka na nusu sasa tokea mara ya kwanza tulivyokutana lakini ni mara yangu ya kwanza kuhisi kuwa na ukaribu zaidi na wewe , ijapokuwa uwezo wangu bado ni wa chini lakini nimeanza kuelewa mawazo yako pamoja na hisia zako , kila kitu sasa ni uhalisia wenye kueleweka katika akili yangu , ninajihisi kuwa mwenye furaha sana”Aliongea Rose.

“Nadhani ni vizuri ukiachana na maswala ya furaha kwa sasa , ushaingia katika levo ya Nafsi lakini bado unapaswa kuendelea zaidi na zaidi , nimekuja na vidonge vya daraja la kati , unaweza sasa kutumia kwasababu ushapata ufunuo wako “Aliongea na kisha palepale alicheza na kauni za anga na palepale lilionekaa vijichupa vya platiki ambavyo huhifadhia vidonge kwenye mikono yake.

“Kuna vidonge vitano hapa vya mawingu na kimoja cha anga la bluu , unaweza kumeza kidongea cha mawingu ili kukusaidia kuweza kukusanya mvuke na kuugeuza mai na baada ya hapo kufanya maji kuwa siraha ya kiroho ya msisimko na baada ya hapo utatumia sasa kidonge cha anga la bluu na kitakusaidia sasa kuelewa zaidi mpangilio wa mbingu , kwa maelezo ya Rufi kidonge cha anga la bluu ni adimu sana katika miliki za kijini , kama sio bahati na uwezo wangu basi ingekuwa ni ngumu kwa binadamu wa kawaida kama wewe kuweza kupata kidonge cha aina hii”

Aliongea Roma na kisha akampatia Rose kijichupa ambacho kilikuwa na vidonge vya mawiangu na kimoja cha anga la bluu.alikwa anapenda sana kuendelea kuvuna nishati ya mbingu na ardhi hivyo hakutaka kukosa nafasi ya kupata kidonge.

Roma mara baada ya kumwangalia Rose aliekuwa na mwoneonako wa furaha na moyo wake ulipata joto la furaha pia.

“Nimekupa vidonge vya thamani kubwa , ni muda wako na wewe angalau kunipa hata zawadi”Aliongea Roma na Rose palepale alimkumbatia Roma na kuzungusha mikono shingoni na kumbusu

“Hubby kwahio mpaka sasa siwezi kuzeeka haraka ?”Aliuliza Rose na Roma alitingisha kichwa kukubali.

“Kwasasa huwezi kuzeeka haraka , lakini licha ya hivyo hupaswi kupumzika jitahidi angalau ufikie mwisho kabisa mwa levo ya Nafsi huenda ukafanikiwa kuingia katika levo ya Dhiki na kuipita kabisa lakini yote hayo yatatokea baaada ya kukusanya nguvu nyingi”

“Kwahio kama nitafika katika levo ya kupita dhiki nitakuwa na uwezo wa kuingia katika steji ya kudhibiti moto wa aina tatu , kubadilisha mvuke kuwa barafu na kudhibiti Radi si ndio?”Aliuliza Rose.

“Sijajua lakini naamini ni zaidi ya hivyo, mbinu yangu niliowapatia ni ya kipekee sana, sidhani kama ni kweli imeweza kutokea katika miliki ya kijini ya PANAS kama wengi walivyosema lakini kwa staili nilivyoirahisisha ni zaidi ya mbinu zote zinazotumiwa na majini”

PANAS ni jamii ya kijini pia kama ilivyo kwa Hongmeng , lakini inasemekana utofauti wa PANAS na Hongmeng ni kwamba miliki hio ipo nje ya bara la Asia na hata Hongmeng ambao walijaribu kusafiri kwenda PANAS ilibidi kwanza wasafiri kuja Afrika, ni jamii ambayo haina muunganiko wowote kabisa na jamii kibinadamu kwa miaka na miaka , lakini hivi karibuni jamii hio inaanza kuonyesha matamanio yao na binadamu wa kawaida.,

Rose sasa alikua sio wa kawaida, alikuwa binadamu ambaye amefanikiwa kupata ufunuo wa nguvu za kijini na hisia alizokuwa akipata akiangalia mazingira ni tofauti kabisa na binadamu wa kawaida na alijikuta hata kundi lake la Tembo kuona ni kitu ambacho hakina maisha marefu kabla ya serikali kuingilia.

Rose sasa alikuwa akipaa tu angani kama Roma na zoezi lake la kwanza kufanikiwa kupaa ni kurudi nyumbani kwa kumfuata Roma nyuma na alijikuta kufumba na kufumbua wapo maeneo ya Ununio na alijikuta mapigo ya moyo yakidunda kasi mno akiwa kama haamini , kwani kila kitu kinaonekana kuwa kipya kwake.

Baada ya kutembea wakipita nje ya nyumba ya Nasra waliweza kukukutana na mama yake Nasra ambaye alikuwa akitoka kwenda kukimbia kuchukua mazoezi.

Tokea mama yake Nasra kufika jijini alikuwa amebadilika mno , kwanza alinenepa na pia mwonekano wake ni wa kitajiri zaidi , hakuwa tofauti sana na Blandina au Bi Wema.

Licha ya kumuona Roma na Rose wakiwa pamoja asubuhi hio hakushangaa sana kwani alikuwa akijua bwana huyo alikuwa na zaidi ya wanawake wengine nje na hata ile hatia aliokuwanayo juu ya Nasra kutoka na mume wa rafiki yake kupungua.

Roma mara baada ya kufika katika nyumba ya Rose waliweza kumkuta Dorisi akitokea jikoni , ilionekana ndio alikuwa akiandaa kifungua kinywa.

Dorisi uwezo wake wa kuvuna nishati za mbingu na Ardhi ulimtegemea zaidi Roma katika kufanya nae mapenzi, baada ya kusikia mwenzake kapasua , alijikuta akiona wivu na kuamini mtu ambaye ataweza kupata mtto wa Roma mapema basi ni Rose na sio yeye.

Roma hakujali sana mawazo ya Dorisi zaidi ya kumwambia ahimize kufungua kinywa kwani leo atapatia hapo hapo kabla ya kurudi nyumbani.

Roma mara baada ya kusema hivyo alimpigia simu mama yake na kumweleza kwamba asihesabiwe kwenye kifugua kinywa , lakini pia alimweleza juu ya mafanikio ya Rose na mara baada ya Blandina kusikia taarifa hio alijikuta akifurahi mno.

Alikuwa na wasiwasi kutokana na Roma kutokuwa wa kawaida hivyo kumpelekea kutokupata mtoto , lakini mara baada ya kusikia kuhusu Rose kupanda levo alijikuta akifurahi mno hakujali ni mwanamke gani wa kwanza kumzalia Roma mtoto , yeye shida yake ni mjukuu tu , alikuwa na mjukuu Lanlan lakini bado hakuridhika kwani bado alijua Lanlan ni wa kulelewa.

“Roma nadhani tusherehekee mafanikio ya Rose”

“Mama unataka tusherehekee vipi??”

“Leo si wikiend na hakuna mambo mengi ya kufanya , kwanini tusiwaalike wengine wakifika nyumbani na kupika chakula na kufurahi?”Aliongea Blandina na kumfanya Roma kuona sio jambo zuri kidogo kutokana na Edna lakini aliependekeza ni mama yake na ni kweli Rose kapata mafanikio makubwa na anapaswa kupongezwa.

“Kama ni hivyo basi tumshirikishe Edna kwanza na baada ya hapo nitawaambia”Aliongea Roma na kisha walikubaliana na kukata simu.

“Mbona unacheka Dorisi?”Aliuliza Roma mara baada ya kuwaambia pendekezo la mama yake.

“Najua mama anamtumia Rose kama kisingizio tu , ukweli ni kwamba ulivyokuwa Korea mara nyingi tulishinda nyumbai kwako tukicheza karata, nadhani anataka tukusanyike tuendelee na mchezo”

“Kucheza karata?”Roma alishangaa kwani ilikuwa ni habari mpya lakini wakati huo huo moyo wake ukiwa na wasiwasi , kwanni kama kitu kama hiko kikiendelea basi Edna lazima hatopendezwa na jambo hilo na kupelekea migogoro.

Roma mara baada ya kumaliza kifungua kinywa alipokea simu kutoka kwa Daudi akimkumbushia swala la tafrija ndogo inayohusiana na waigizaji wote walioshiriki katika filamu hivyo kumweleza eneo ambalo tafrija hio ingefanyika, baada ya kukata simu aliona itakuwa vizuri kumpigia simu Sophia kwa kufanikisha swala hilo.

Baada ya kukaa muda mfupi aliondoka na kurudi nyumbani na aliweza kumkuta Edna akicheza na Lanlan eneo la sebuleni na alimweleza juu ya Sophia na watu wa kampuni ya Penguin kuandaa tafrija lakini Edna alionyesha kujua kila kitu.

“Unaweza kwenda , mimi nitashiriki siku ya uzinduzi wa filamu “

“Lakini Sophia anaweza kuwa na huzuni kama hutoenda”

“Nishampigia tayari Sophia na kumpongeza na nimemwambia sitohudhuria , sidhani kama atahuzunika kwa jinsi tulivyokubaliana”Aliongea Edna na kumfanya Roma kuelewa , hata hivyo Edna alikuwa karibu sana na maendeleo ya Sophia kuliko ilivyokuwa yeye.

“Hubby! Je utamfundisha na Lanlan kuvuna nishati hapo baadae?”Aliuliza Edna wakati Roma akicheza gemu la kuzungusha boksi la kufananisha rangi.

“Hilo lipo wazi, Lanlan ni binti yetu hatuwezi kumuacha asijifunze na isitoshe Lanlan ana vigezo vikubwa zaidi kuliko hata mimi wakati nikijifunza , mpango wangu ni kumrithisha nguvu ya kimaandiko ya urejesho isio na kikomo , ni mtoto wetu wa kwanza hivyo lazima apate vipaumbele”

“Kama ni hivyo kwanini hujamwelekza chochote?”

“Kwanza kabisa Lanlan bado ni mdogo , hawezi kuelewa baadhi ya mambo kwa umri wake, kitu cha pili siwezi kumpatia vidonge na kisha nikamrithisha andiko anaaweza kugeuka na kuwa mkatili , tatu sina uhakika maadui zangu ambao watajitokeza , kama ujuavyo andiko hili huwindwa na watu wengi hivyo nikimrithisha akiwa na umri mdogo moja kwa moja namfanya kuwa mlengwa , hivyo watu watataka kupata mbinu yangu kupitia kwake na nitamuweka kweye hatari, kwasasa tumuache afurahie utoto wake”

“Malengo yangu ni kumuona akiendelea kuwa na siha njema na kuweza kujilinda yeye mwenyewe , lakini nina wasiwasi anaweza kuja kuwa kama wewe kuanza kupigana nakuwa na utukutu mwingi akishaanza kujifunza , hata kama ataweza kushida kila wakati lakini bado itanifanya kuwa na wasiwasi”Aliongea Roma lakini hakutaka kuongezea neno kwani alijua huo ni waswasi wa kawaida kwa mama kwenda kwa mtoto.

Ilionekana Blandina alikubaliana na Edna, hivyo muda wa mchana warembo wote waliweza kukusanyika katika nyumba ya Roma kusherehekea mafanikio ya Rose, aliekosekana alikuwa ni Neema Luwazo ambaye alikuwa nje ya nchi kikazi pamoja na Mage ambaye alikuwa kazini.

Roma mara baada ya kuona kundi lote hilo la wanawake alijikuta akijisikia vibaya na vizuri kwa wakati mmoja.

Baada ya chakula kama kawaida Blandina alitoa karata na kuwataka wote wakusanyike eneo la sebuleni kwa ajili ya kucheza.

Najma pia alikuwepo na ndio ambaye alitoa sababu kwamba hakuwa akijua kucheza karata na Edna hivyo hivyo alipoambiwa ajiunge kucheza alisema hajui , lakini Nasra alimlazimisha na kumwambia atajifunza.

Roma kwa hali hio hakutaka kuendelea kubakia hapo tena, kwasababu siku hio alikuwa na ratiba ya kuhudhuria tafrija ya Sophia na waigizaji wenzake , basi aliona akatembee na kisha aunge moja kwa moja.

***********

Tafrija ilikuja kumalizika saa nne za usiku na Roma aliagana na Sophia kurudi nyumbani.Sophia alionekana kuzidi kupendeza mno na kila mwanaume ambaye alikuwa akimwangalia alimtamani.

Roma mara baada ya kuingiza gari lake ndani ya geti alishangaa mara baada ya kuona gari la Amina bado lipo , lakini pia taa za sebuleni zikiwaka muda huo.

Baada ya kuingia ndani ndipo alipokuja kushangaa mara baada ya kukuta hali ni kama alivyoiacha , lakini utofauti tu ni kwamba wengine walikuwa washaanza kusinzia kwenye masofa , huku mezani alikuwepo Edna na Amina waliokuwa wakicheza karata wakiwa siriasi.

Blandina mara baada ya Roma kuigia eneo hlo alijikuta akipata ahueni na kumwambia Roma amshawahisi Edna waghairishe wataendelea kesho.

Roma mara baada ya kuambiwa hivyo alitaka kujua kwanza kinachoendelea na hapo ndipo aliposikia kwamba baada ya Edna kufundishwa na kuelewa namna ya kucheza hakutaka kupumzika kabisa na kuchukulia siriasi mchezo huo na mtu ambaye alikuwa akiongoza kushinda ni Amina, hivyo Edna alitaka kulipa pointi zote za Amina,lakini mwishowe kila akicheza anaishia kufungwa na bado hakutaka kukata tamaa.

Roma mara baada ya kusikia kauli hio alijikuta akijawa na mshangao na kumwangalia Edna namna ambavyo alikuwa siriasi.

“Edna huo mchezo ni wa kubahatisha, hakuna ufundi ,unaweza kucheza mpaka kesho na usipate ushindi”Aliongea Roma na kumfanya Edna kumwangalia na kisha akaangalia watu waliozunguka na kisha akageuza macho kwa Amina.

“Amina nitakupigia simu , lazima nikulipe pointi zako ulizonifunga leo”Aliongea Edna na kisha akasimama.

“Edna huu ni mchezo wa karata tu kwanini unauchukulia kama vile ni ushindani wa kibiashara?”

“Sijauchukulia kama biashara , bali ni kwamba unafurahisha , siku nyingine mkicheza lazima na mimi niwepo”Aliongea na kisha alipandisha juu kumwangalia Lanlan.

Roma alijikuta akipata ahueni na kuwasindikiza, Najma alikuwa akikaa mbezi kwenye apartment hivyo alipanda gari ya Amina na wakaondoka kwani muda ulikuwa umeenda.

Ilipita wiki moja moja , ikiwa ni siku ya jumamosi jioni wakati Roma akitoka nyumbani kwa Najma mbagala, aliweza kupokea simu kutoka nyumbani na aliekuwa akipiga ni mama yake.

“Mama kuna nini?”

“Mheshimiwa raisi Jeremy amefika na yupo na Edna wanaongea”Aliogea Blandina na kumfanya Roma kushagazwa na kauli hio.

“Lakini mbona unaongea kwa wasiwasi sana?”

“Ni kuhusu Rose”

“Rose kafanyaje?”

“Kuna watu wamejitambulisha wanatokea PANAS, wanasema Rose ashafikia levo ya Nafsi na sheria haimruhusu kuendelea kuishi katika ulimwengu wa kawaida , hivyo wanataka kuondoka nae”

“PANAS!!”Roma alijikuta akimaka , kwa mara ya kwanza anasikia watu kutoka PANAS.

“Mama nakuja sasa hivi”

“Wahi maana Rose kakataa na kasema watampata kama wataweza kumshinda baada ya pambano , hivyo wametoka kwenda kupigana”Aliongea na kumfanya Roma kuzidi kuwa na wasiwasi na aliona hawezi kuendesha gari na alimgeukia Najma na kisha akalipaki pembeni na kumpatia ufunguo wa gari na kumwambia anapaswa kuondoka kuwahi nyumbani , lakini nasra alipotaka kumwambia Roma hajui kuendesha gari , Roma ashapotea kwenye macho yake na kumuacha akiwa amekodoa macho.
 
SEHEMU YA 540.

MASAA MACHACHE NYUMA.

Ilikuwa ni siku ya Jumamosi wikiend lakini siku hio Edna aliweza kweda kazini nusu siku.

Wakati akiwa kazini upande wa nyumbani Blandina kutokana na kukosa cha kufanya alimwita Rufi na Rose kuja nyumbani kumchangamsha na waliishia kucheza karata muda mrefu mpaka saa za mchana Lanlan alivyoanza kulalamika njaa ndio waliacha na kwenda kuandaa chakula.

Saa tisa wakati Edna akirudi kazini aliweza kuwakuta wakiwa nyumbani ,Edna licha ya kwamba hakupendezwa na namna mama yake alivyokuwa akiwaita wanawake hao nyumbani , lakini hakuonyesha chuki pale anapowakuta.

Muda wa mchana aliongezeka Mage ambae alikuja kusalimia na Edna alichangamka baada ya kukutana na rafiki yake huyo , ijapokuwa alimsaliti kwa kutoka kimapenzi na mume wake , lakini hakuwa na kinyongo nae.

“Roma yuko wapi?”Aliuliza Edna.

“Ndio unamkumbuka sasa hivi , alitoka asubuhi kasema aaenda nyumbani kwa Najma kuonana na ndugu zake”

Ukweli ni kwamba mara baada ya Najma kumpa taarifa Roma kwamba Juma hakuwa na shida na uhusiano wao na akajitambulishe rasmi kwa shangazi yake hakuona shida na ndio maana siku hio jumamosi aliona akafanye hivyo ili rasmi Najma atambulike kama mchumba wa Rom.

Familia hio kutokaa na karibia ukoo mzima kutokuwa na mtu alietoka kimaisha hakuna ambaye alimkataa Roma ilihali walikuwa wakijua ni mtoto wa Raisi .

Zamani ndio Roma alionekana hohehahe , lakini kipindi hicho hadhi yake ilikuwa ya juu mno na hata wale watu ambao aliofanya nao kazi ya kubeba mzigo na kutokumchangamkia kipindi kile walijilaumu kwa kutofanya hivyo, wakiona kwamba walipishaa na bahati , walijiambia kama wangefahamu huenda Roma angewaunganisha kwenye makampunni makubwa na kufanya kazi.

Najma aliishi Mbagala Chalambe karibia tokea akiwa mdogo , hivyo alifahamika sana na kila mtu, hivyo mara baada ya kurudi eneo lote hilo la uswahilini walifahamu.

Najma ambaye walimfahamu kabla ya kwenda Marekani alikuwa ni tofauti na Najma alierudi, hata wale wanaume ambao zamani walikuwa wakimfukuzia wakati huo walikuwa wakimuogopa na kuona sio saizi yao.

Juma mwenyewe ambaye ni kaka mtu , baada ya kumtia macho dada yake aliona kabisa Najma amebadilika sana na hakuwa mwanamke wa kawaida tena lakini licha ya hivyo alishangazwa na kurudi kwake mapema ilihali mara ya mwisho alimwambia atakaa nje muda mrefu.

Lakinni Juma kama mtu mzima baada ya kumuona dada yake alivyokuwa na furaha , aliamini kuna kitu kinaendelea na hata pale alipohoji na Najma kumwambia kwamba Roma amekuwa rasmi mchumba wake Juma alishangaa.

Hakushangaa kwasababu kwa kipindi hiko hakuwa akimtaka tena Roma kutembea na dada yake , La hasha , kilichomshangaza ni kwamba Roma tayari ana mke na jina la Roma Ramoni liliashiria ni mkristo.

Juma ilibidi kwanza amhoji dada yake , kwani wasiwasi wake ilikuwa ni juu ya mke wa Roma, mwanamke ambaye anamheshimu kwenye maisha yake kwa kumsaidia kupona ugonwa wake wa figo, Juma moyo wake ulikataa dada yake kuendelea na Roma kutokana na sababu ya Edna kuwadai fadhila lakini kwa wakati mmoja aliona Roma ni mtu mzito ndani ya taifa mara baada ya kusikia ni mtoto wa raisi.

Ilibidi Najma achukue jukumu la kumtoa hofu kaka yake na kumweleza kwamba Edna hana shida na yeye kuwa na mahusiano na Roma na juma mara baada ya kusikia hivyo , licha ya kupata ahueni lakini alizidi kuwa na maswali mengi na kumuona huenda Roma sio binadamu wa kawaida, alijiuliza inawezekanaje kuweza kupendwa na mwanamke mrembo na tajiri na bila ya wasiwasi kutoka nje ya ndoa.

Roma mara baada ya kufika katika nyumba ya Najma alishangazwa siku hio kukutana na ndugu wengi , hakuamini kama Najma alikuwa na ndugu wengu kiasi hicho, lakini aliweza kufikia katika hitimisho kwenye kichwa chake.

Wakati Roma sasa akiwa nyumbani kwa Najma upande wa nyumbani aliweza kufika raisi Jeremy , ambaye alikuwa nchini Tanzania kimya kimya akiwa na misheni yake moja tu ya kuongea na Edna.

Raisi Jeremy alifika katika eneo la Ununio kwenye muda wa saa kumi na mbili hivi kwenda saa moja , alikuwa amekuja na gari mbili tu aina ya Range na alitangulizana na watu sita ambao wote walionekana kuwa walinzi wake waliovalia suti.

Rose ambaye alikuwa nyumbani kwa Edna akicheza karata alijikuta mwili wake ukimsisimka kabla hata Raisi Jeremy hajaingia ndani ya hilo eneo, alihisi nguvu za ziada zikiongezeka katika hilo eneo na kufanya vinyweleo vya mwili wake kumsimama.

“Kuna watu wawili wenye sawa na yangu wanakaribia”Aliongea Rose mara baada ya kuacha kucheza karata na kuwafanya watu wote hapo ndani kushangaa.

Nadhani kuna watu wengi pia ambao wapo nje mlango , nitaenda kufungua”Aliongea Rose mara baada ya mlango kugongwa.

Rose alivuta pumzi na kuzishusha na kisha akatoka kwenda kufungua mlango

Rose mara baada ya kufungua tu mlango aliweza kukutana na sura ambayo alikuwa akiifahamu lakini ambayo hakutegemea kuiona katika eneo hilo.Alikuwa ni Jeremy Paul raisi wa taifa la Rwanda na alimfahamu.

“Mheshimiwa…!!?”Aliongea kwa wasiwasi huku akishindwa kujua kwanini raisi huyu wa taifa la jirani kuja mpaka nyumbani kwa Roma na Edna.

Baada ya kuchunguza watu waliokuwa pembeni yake kulia na kushoto sasa ndio aliweza kugundua uwepo wa watu wawili ambao walikuwa na nguvu za kijini katika levo ya Nafs.

Wale mabwana walimwangalia Rose kwa mshangao kwani hawakutarajia kuona mtu mwenye nguvu za kijini katika levo yaNafsi kuwa mwanamke mrembo wa umri mdogo ambaye anaishi katika dunia ya kawaida.

“Binti je nimemkuta CEO Edna?”Aliuliza raisi Jeremy mara baada ya kuona Rose anashangaa.

“Ndio , yupo karibuni”Alijibu Rose kwa kushituka na kisha alifungua mlango wote na sasa kufanya waliokuwa ndani kuweza kuona mgeni ambaye amefika.

Edna ndio ambaye alikuwa kwenye mshituko zaidi mara baada ya kuona sura ya Raisi Jeremy.

Upande wa Blandina alishangaa pia lakini kuwa na wasiwasi kwa wakati mmoja.

“Mheshimiwa Jeremy!! Karibu sana”Aliongea Blandina na kumsogelea raisi Jeremy na kumsalimia kwa kumpa mkono.

“Blandina na wewe upo , ni miaka mingi sana tokea tuwahi kukutanam, tafadhari naomba unichulie kama mgeni wa kawaida , nimefika hapa kwani nataka kuonana na Edna”Aliongea.

Bi Wema yeye tu ndio alikuwa na uelewa kuwa Edna baba yake mzazi ni raisi Jeremy ila wengine wote hawakuwa wakiuja ukweli.

Raisi Jeremy aliamrisha walinzi wake wengine kukaa nje na walioingia nao ni wanaume wawili weusi waliokuwa nyuma yake , ambao walikuwa wakisambaza nguvu za kijini.

Warembo wote hapo ndani walijikuta wakikosa utulivu , Raisi Jeremy licha ya nchi yake kuwa ndogo lakini mara nyingi alisifika sana kwa uongozi wake uliotukuta na kwa wanawake hao ni mtu ambaye ni waheshima sana , mtu pekee ambaye angepata ujasiri wa kumpotezea ni Roma pekee na sio wao.

“Jamani haina haja ya kuwa na wasiwasi, mnaweza wote kukaa , nipo hapa kumuona Edna”Aliongea Raisi Jeremy na kuenda kumsogelea karibu Edna.

“Edna nimekuja leo kwako kwa moyo mkunjufu , je tunaweza kuongea?”Alimuuliza Edna ambaye alionyesha kabisa hakuwa amependezwa na ujio wake , tokea siku aone kila dalili ya Jeremy kutokumkubali kama mtoto wake hakuwa na hamu nae tena.

“Sina chochote cha kuongea”Alijibu Edna mara baada ya kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha, alionekana kutumia ujasiri mkubwa kuongea hio kauli.

“Mimi nina cha kuongea”Aliongea kwa sauti yenye upole ndani yake na kuwashangaza Mage na Rose.

“Tunaweza kuongea pale”Aliongea Edna akionyesha eneo la chumba cha mbele ya Dining na yeye alianza kuelekea upande huo na Raisi Jeremy alifuatisha.

“Mama nini kinaendelea?, Edna ana uhusiano wowote na Raisi Jeremy?”Aliuliza Mage kwa sauti ya chini na kumfanya Blandina kuwaleza kwa ufupi.

“Nini! Edna ni mtoto wa raisi Jeremy?”Aliuliza Rose kwa mshangao.

“Ni kama ndoto , sijawahi hata kuwaza”Aliongea Mage.

“Haina haja ya kushangaa , isitoshe mshakuwa familia hivyo mnapaswa kujua lakini niwatahadharishe msiropoke hilo mbele ya Edna maana hapendi”Aliongea na kuwafanya wote kutingisha kichwa chao kukubali.

“Mheshimiwa tafadhari ongea kwa haraka, muda umeenda sana”Aliongea Edna kama kawaida yake akiwa katika sura ya ukauzu.

“Edna binti yangu , najua unanichukia na nashikwa hata na aibu kuongea hili…, lakini leo niliwaza mara kibao na nimejipa ujasiri mwingi kuja kukuona , nipo leo hapa kwa ajili ya kukuomba msamaha wewe na mama yako”

“Msamaha! Tafadhari mheshimiwa huna haja ya kuniomba msamaha kwani mimi ni raia wa kawaida tu ambaye ni mfanyabiashara, hatna uhusiano wowote mpaka kuombana msamaha”

“Edna nakubali kwamba tamaa ilinipofusha na kunifanya nitende dhambi kuchafua taswira yangu , lakini Edna wewe ni msichana mwenye akili sana kama alivyokuwa mama yako , kama mwanaume mwenye jina katika jamii na madaraka ilinipasa kuzingatia vitu vingi na kutimiza wajibu wangu , siku zangu zote za kuishi hazikuwahi kuwa rahisi kwangu , Edna inawezekana nilisita kuchukua hatua ya kujitokeza kwako ana kwa ana na kukutambua kama mtoto wangu lakini unajua wewe mwenyewe namna ambavyo nilikuwa nikikulinda , nilivyokuwa nikikusaidia , sio kwamba najaribu kuchukua sifa kwa nilioyafanya lakini nashukuru kwamba nilikuona ukikua ”

“Umeongea sana mheshimiwa , lakini nikutoe hofu mimi sikuchukii na isitoshe nina furaha hata pasipo ya uwepo wako kwenye maisha yangu , kwani sasa nina familia na najua nifanye nini ili kuwa na furaha, hivyo kama unapenda niendelea kuwa na furaha , tafadhari naomba usinitafute tena”Aliongea Edna kikauzu

“Edna kwanini kauli yako inaonyesha kunikataa , unatakiwa kujua mimi ni baba yako , najua nina mapungufu mengi , najua nimemumiza sana mama yako , lakini bado Edna wewe ndio uliebakia kwenye maisha yangu , Edna watoto wangu wawili walipotea mbele ya macho yangu na watatu haonekani alipo , wewe ndio pekee ambaye naweza kujivunia”Aliongea na kumfanya Edna asimwelewe , kilichomuumiza Edna sio kuhusu yeye , ila ni kuhusu mama yake mzazi , kipindi chote ambacho alikuwa akipitia magumu mpaka akaja kuwekewa sumu hakuna mtu ambaye alimpa msaada na alipigana vita vya peke yake na hilo ndio jambo ambalo lilimfanya kuwa na hasira na raisi Jeremy, aliamini kama angalau angemjali japo kidogo tu huenda mama yake angekuwa hai mpaka muda huo.

“Edna nimetoka Rwanda mpaka hapa licha ya majukumu mengi , yote ni nia yangu ya kutaka kukurudisha katika ukoo wangu , nataka uwe mrithi wa familia”Aliongea na kumfanya Edna kushituka kwani hakutarajia kama angetaja maswala ya urithi.

“Siwezi kuwa mrihi wako , kwasababu mimi ni Edna Adebayo na ukoo wako haunihusu , mimi ni Mtanzania”

“Hapana Edna wewe ni binti yangu , wewe sio mtanzania , wewe ni Mrwanda na jina lako ni Edna Jeremy Paul Murekezi , Edna nitambue mimi kama baba yako na kuitambua Rwanda kama nchi ya baba yako na ukoo wako”Aliongea na kufosi na kumfanya Edna kuanza kutokwa na machozi, hakuamini Raisi Jeremy angefika hapo na jioni hio na kuanza kumfosi kumkubali kama baba.

“Sitaki kuendelea na haya maongezi , nimechoka hivyo tafadharai naomba uondoke”Aliongea Edna na kumfanya Raisi Jeremy kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha.

“Okey, mimi baba yako sitoendelea kukulazimisha kwa leo , nitakuja kukutembelea siku nyingine”Aliongea na kisha alimwangalia Edna kwa dakika na kisha kutoa tabasamu.

“Nadhani nimekuja muda mbaya , Lanlan atakuwa amelala muda huu si ndio , usishangae nina taarifa zote wewe na Roma mmeamua kuasili mtoto ,hivyo moja kwa moja anakuwa mjukuu wangu wa kwanza , siku nyingine nikija nitamletea Zawadi”Aliongea na kisha akasimama.

Edna alimwangalia kwa dakika kadhaa na kisha alifumba macho na kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha.

“Je nilizaliwa na pacha wangu?”Aliongea Edna na kumfanya Raisi Jeremy ambaye alikuwa akitaka kupiga hatua kutoka eneo hilo kusimama ghafla na kumwangalia Edna kwa mshangao na kisha akaupotezea palepale.

“Pacha wako! , unamaanisha nini?”Aliongea akionyesha kutoelewa kitu , lakini Edna hakuwa mtoto mdogo aliweza kusoma mabadiliko ya raisi Jeremy kabla hata kuupotezea.

“Basi, nadhani sikupaswa kuuliza”Aliongea Edna na akatangulia.

Wakati Edna anaongea na Raisi Jeremy , wale watu weusi wawili ambao walikuwa na nguvu za kijini walimwangalia Rose kwa maswali mengi.

“Uwezo wako wa kuvuna nishati ni wa juu sana , kwa umri huo mdogo tayari ushafika katika levo ya Nafsi , je unatokea katika jamii yoyote ya kijini, au ni binadamu uliejifunza bila usimamizi na sasa una tangatanga?”

“Una uhakika gani kama nina umri mdogo , kwa levo yangu hata kama niishi miaka mingi muonekano wangu utaendelea kuwa hivi hivi”

“Haha..nani kakuambia tunaangalia mwonekano kujua umri wa mtu anaejifunza tamaduni za kijini , tunachoangalia ni vitu vingi , jinsi unavyotembea , unavyoongea na tabia yako kwa ujumla , kwa namna navyoongea na kutembea unaonekana ndio kwanza umeingia levo ya Nafsi”

“Hata kama ni kweli , kwanini mnaniuliza maswali?”

“Hutokei katika familia maalumu ndani ya taifa hili si ndio?”

“Kwahio kama sitokei katika familia maalumu , unataka kusema nini?”

“Hehe.. unaonekana kuwa mkali , kama hutokei katika koo maalumu , unapaswa kuaga familia yako na marafiki , kwani huwezi kuendelea kuishi katika ulimwengu wa kawaida kwani nisheria”

“Unamaanisha nini?”Aliuliza Rose kwa wasiwasi.

“Nadhani hajaelewa ninachozungumza na ulijifunza tamaduni zetu bila ya kupewa taarifa , iko hivi kuna sheria kali ambazo zimewekwa zinazowazuia binadamu wa kawaida kujifunza mbinu za kijini na ikitokea binadamu akajifunza na kufikia levo ya Nafsi anapaswa kuacha ulimwengu wa kawaida na kwenda kuishi katika miliki za kijini , sasa kuna chaguzi mbili , unaweza kuongozana na sisi kurudi katika miliki ya kijini ya PANAS au uende China”Aliongea yule mwanaume mweusi, blandina alijikuta hata akishindwa kuelewa kile kinachongelewa.

“PANAS ndio jamii gani?”Aliuliza Blandina ambaye alielewa nusu ya kauli yake?”

“Ni jamii ya kijini , mahali tunapotokea sisi , huyu binti ashafika katika levo ya Nafsi na sheria hazimruhusu kuendelea kubakia katika ulimwengu wa kawaida , hivyo lazima aungane na sisi kwa hiari yake kwenda katika miliki za kijini la sivyo tutamlazimisha”Aliongea na kumfanya Blandina kujawa na hofu juu ya Rose.

“Lakini sheria hio ipo kwa watu wa China , Afrika na mabara mengine nje ya Asia haiwahusu”Aliongea Rufi.

“Kwa umri wako unajua nini maswala ya sheria , hakuna kanuni iliosema hivyo kwa ajili ya Wachina , The gods treaty ni mkataba wa dunia wenye vipengele vya kudumisha amani na uwiano, moja ya kipengele chake ni kuzuia binadamu wa kawaida kujifunza mbinu za kijini na wale wanaojifunza bila ya kuelewa sheria na wakafikia levo ya Nafsi lazima watoke katika ulimwengu wa kawaida, hio yote ni kuepusha madhara kwa binadamu wa kawaida”

“Unamaanisha binadamu wa kawaida kujifunza mbinu za kijini ni kosa?”

“Kanuni inazuia lakini haijasema ni kosa , kutokana na kwamba kujifunza mbinu za kijini ni swala linaolendana na utashi wa hali ya juu wa akili na halitokei kwa bahati mbaya, hivyo pale binadamu anapofanikisha hilo inamaana uwezo wake ni mkubwa na amejaaliwa talanta, lakini haiwezekani kila ambaye anaweza kuwa na nguvu kubwa tofauti na binadamu wa kawaida kuendelea kuishi hapa duniani, nadhani wote mnaweza kujua madhara yake si ndio?”Aliongea yule bwana na Blandina alielewa mantiki yake , lakini Rose hakuwa kwenye kundi la watu anaolenga.

“Hakuna wa kunilazimisha kwenda katika miliki za kijini?”

“Hehe.. binti hakuna anaekulazimisha, bali sheria inakutaka , inakupasa kufanya hivyo , ni sheria ambayo watangulizi wenu wa kuilinda dunia na majanga walisaini, hivyo kama hutaki kwenda kwa hiari utaenda kwa lazima”

“Ni mpaka mtakapofanikiwa sasa kunipeleka kwa lazima”

“Hehe … unaongea sana , lakini siwezi kupoteza muda kuongea na wewe , hata hivyo nadhani muhusika ashakuja , kama kweli unajiamini jiandae kupambana”Aliongea na kuwafanya wote wasielewe anachomaanisha , lakini Rose hapo hapo alihisi mkandamizo wa hewa , huku msisimko ukizidi kumvaa , ilionyesha kuna kiumbe kingine kiliongezeka katika hilo eneo”

Muda huo huo Blandina alijua kuna hatari inayoweza kutokea na alikimbilia jikoni kumpigia simu Roma na ile anarudi alimkuta tayari Jeremy ashamaliza maongezi yake na Edna.

“Blandina naomba ni kusihi uendelee kumjali Edna kwasababu tayari ashakuwa mkwe wako , nitarudi siku nyingine kumtembelea”

“Nitafanya hivyo na isitoshe amekubalika katika familia tayari”

“Ninafuraha kwamba Afande Camillius Kweka amemkubali na kumpenda kama mkwe , lakini ni huzuni Edna hataki kunitambua kama baba yake, lakini kwasasa sitoharakisha mambo nitakuwa na subira”

“Sidhani kuna haja ya kuwa na wasiwasi , Edna ni mtu mzima sasa na anajali sana familia , naamini siku moja atakukubali , ili mradi uwe na nia ya dhati”

“Nia yangu ni ya dhati kabisa”Aliongea na kumfanya Blandina kutabasamu na kukosa neno la kuongea.

“Blandina najua mengi yametokea , lakini nina furaha kuona unaendelea vizuri”Aliongea na Blandina alijua ni kipi Jeremy anamaanisha.

Raisi Jeremy hakua mwongeaji sana , kwasababu alifika hapo kwa ajili ya Edna hivyo aliaga.

Muda uleule wakati raisi Jeremy na watu wake wanatoka nje, wakiwa wanasindikizwa na Rose na Blandina, ghafla tu alijitokeza mwanaume alievalia mavazi ya kitamaduni ya kichina , alikuwa mchina kabisa na kumtanya sasa Rose kuelewa huyo ndio mtu ambaye alikuwa ameongezeka hapo ndani , alikuwa kwenye levo yaka ya kwake ya Nafsi.

Wale mabwana mara baada ya kumuona waliangaliana na kisha walipeana ishara.

“Jini Tao , naona unajiamini kwa kuzururula dunia nzima na kuingia mpaka kwenye mipaka ambayo hupaswi kupita”Aliongea yule bwana mweusi aliekuwa akiongea na Rose.

“Mhmp.. nadhani maneno yako yamekaa kinafiki , sipo hapa katika ulimwengu wa kawaida kama adui , bali nipo hapa kama mjumbe lakini pia sheria inaniruhusu kutafuta binadamu wote wanaojifunza tamaduni zetu kuwarudisha ujinini wanapoingia levo ya Nafsi”Aliongea huku akimwangalia Rose.

“Jini Tao hakika wewe ni mwenyewe kujiamini sana, lakini unapaswa kutoa heshima kwetu jamii ya PANAS kwa namna mababu zetu walivyosaidia jamii yenu na kuwawekea msingi”

“Hahaha… haina haja ya malumbano ya kudai heshima , inashangaza pia nyie kuonekana katika ulimwengu wa kawaida , ilihali ni zaidi ya karne na karne kujificha na kutopenda kujihusisha na maswala ya ulimwengu wa kawaida”

“Miaka imebadilika na dunia inatuhitaji , hatuwezi kuendelea kuona viumbe kutoka sayari nyingine wakiendeleza unafiki wao wa kulinda dunia ilihali mipango yao ni kuiangamiza”Alijibu na kumfanya yule mchina kucheka.

“Nipo hapa nikitafuta wajumbe kutoka Hongmeng waliopotelea duniani na nimetokea kunasa uwepo wako binti”Aliongea akimwangalia Rose.

“Unamaanisha nini kunasa uwepo wangu”

“Nadhani watu wa PANAS wamekuambia , upo tayari levo ya Nafsi na hupaswi kuendelea kuishi katika dunia ya kawaida, tuongozane kuelekea Hongmeng , umekuwa binadamu mwenye bahati kupata ufunuo katika umri mdogo , ukiwa ndani ya Hongmeng utafanikiwa kupanda levo zaidi”

“Siwezi kwenda popote”Aliijibu Rose.

“Binti unaweza kuchagua mahali pa kwenda, unaweza ukaja kwenye miliki yetu yaPANAS na hutojutia maamuzi yako”

“Nishasema siendi popote na kama utanilazimisha , pigana na mimi kwanza ukishinda nipeleke”Aliongea Rose kwa kiburi na kumfanya yule mchina kucheka sana.

“Umetaka mwenyewe binti , nitakupa unachotaka”Aliongea yule mchina huku akimwangalia Rose kwa kejeli , aliamini hakuna namna ambayo anaweza kuzidiwa na mtu ambaye ndio kwanza anaingia levo ya Nafsi.

“Nadhani bwana Tao mkafanyie pambano lenu baharini ili msije kuharibu makazi ya watu , ningependa kuona namna ambavyo jamii ya Hongmeng mlivyo imarika kimbinu”Aliongea yule bwana mwingine ambaye alikuwa kimya muda wote na kisha akaangaliana na mwenzake na wakacheka.

Ijapokuwa kila mtu alikuwa na wasiwasi juu ya usalama wa Rose, lakini hawakuwa na namna ya kumzuia Rose kutopambana.



END OF SEASON 18
NICHEKI WATSAPP KUPATA MWENDELEZO NAMBA 0687151346
 
 
The psychological situation where someone feels inferior over others' accomplishments and instead of complimenting their success, raises doubts about their success is called devaluation.

Devaluation is a defense mechanism that people use to protect themselves from feeling inadequate or threatened by others. It is a way of coping with negative emotions such as envy, jealousy, and insecurity.

Mfano katika jamii utakutana na baadhi ya watu akimuona jirani kafanikiwa tofauti na kumpongeza ataanza kutoa dukuduku lake atasema utajiri wa aina yake ule ni wa majini , sijui freemason.
Hii tabia ikikukithiri inageuka na kuwa ugonjwa wa akili na athari zake utaona wengi uliokuwa nao levo sawa wanakupiga gepu kimafanikio.


Na mwisho wa siku unajikuta unaenda kwa waganga kumroga bahati mbaya unakuta unaemroga harogeki aloo[emoji1787][emoji1787]

NB hio tabia wanayo sana wanawake ndio maana nilikuuliza jinsia yako huko juu
Huu ni ushauri tu kutoka kwa Dr Singanojr uchukue au uache hapa hapa
 
Mtu ukimjua akupiih shida
Wapiga porojo wapo
Ndo wachawii wa maendleo
Mtu ndani ya 24hrs kufatilia
Mambo ya watu na kukosoa
Alf yy akun Cha maan alicho
Fanya kweny jamiii iliyo mznguka
singanojr bro ukionaah hvy
Kazii yako ameielewa hila
Ndoiv anashindwa kufungah tu.
 
Hakuna shida, elimu inatafutwa kwa njia zote, maadamu anatuletea vitu ambavyo sisi hatujui wacha tusome.

Kwa hiyo hoja zako hazina mashiko iwe anatunga au anacopy.

Asante sana mdau.
 
Hakuna shida, elimu inatafutwa kwa njia zote, maadamu anatuletea vitu ambavyo sisi hatujui wacha tusome.

Kwa hiyo hoja zako hazina mashiko iwe anatunga au anacopy.

Asante sana mdau.
One of the best replies ever [emoji120][emoji110][emoji123]
 
Lakini Cha ajabu kaka singanojr ...jamaa kila siku yupo hapa hapa jukwaan akikusubir ushushe vitu [emoji16][emoji16]
Movie si anaijua, basi akaingalie
 
Singano hongera.nimeanza mwez huu kusoma sikuianza mapema
Hongera kwa kutafiti,ni mara ya kwanza kusoma angalau fiction yenye vitu ambavyo vipo kidunia kama story za dan brown. Umesema unajua kuvuna nguvu za mbingu na ardh sijui sasa labda wewe ni muumin wa budha
Nakusahihisha kwenye maneno haya:
Sio dhana ni Zana.( kitu au kifaa)
Sio hadhina ni Hazina. Vingine hongera maana inaonesha umetumia muda wako kutafiti na kutaja maeneo kiuhakika. Nipe namba niingie kwenye grupu nisisubir huku kama yule dogo anayelia kila siku anamsubiri zainabu
 
Dg tulia hujui chochote we soma ukimaliza ulale mtoto mdg unaongea shombo kama za wazanzibari
 
Singano mpaka alambwe lambwe ndo alete mwendelezo.... [[emoji35]
 
Singano pole na majukumu,nakubali sana kazi zako,hii simulizi Kuna kipindi ilikuwa nikiikosa nakosa amani kabisa,nafikiri Mimi ni mmojawapo wa mwanzo kununua,lakini kwangu naona inaanza kukosa ule mvuto wa mwanzo,hata nikiikosa mwezi naona kawaida tu,nafikiri steringi roma anapoteza mvuto,ngono zimezidi kuliko action!
 
Asante mkuu kwa marekebisho
 
Mimi ndo niko hapa![emoji23]
 
Nimefika hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…