Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Delay technique inavyovuta wateja kule kwenye group pendwa. Sasa Ni mwendo wa kujiunga kwa bk3 naona wateja wanazidi kumiminika, ila wakati huohuo ikiwaumuza wavuta subira huku JF.
 
SEASON 19

SEHEMU YA 541.

Vivuli vya watu wawili , vilisimama kulia na kushoto katika mchanga wa fukwe , Rose alikuwa na hasira lakini upande wa mjumbe wa hongmeng alionekana kuwa katika hali ya dharau.

“Siamiani kama ili kukuchukua kukupeleka Hongmeng napaswa kupigana na binadamu wa aina yako ambaye una uwezo mdogo, nakuruhusu kushambulia kwa kila ulichonacho , usihofu watu wengine hawawezi kuona kinachoendelea zaidi ya ndugu zako”Aliongea.

Blandina , Edna na wengine wote walikuwa wakiona kile kinachoendela mara baada ya kusogea upande huo , hata Edna hakuweza kufahamu ilikuwaje mpaka hali ikafikia katika mapigano.

Raisi Jeremy mwenyewe hakuwahi kuona binadamu mwenye uwezo wa kimaajabu wakipambana na aliona hio ni fursa pekee ya kushuhudia yale ambayo alikuwa ameambiwa na akayaona kuwa hadithi.

Upande wa Rose , hakutaka kuogopa ,ijapokuwa hakuwa na uzoefu wa kimapigano licha ya kipindi chote kujifunza, lakini aliamini atachukulia pambano hilo kama nafasi ya kupata uzoefu.

“Umeongea mwenyewe , siwezi kujizuia tena”Aliongea Rose na palepale alifumba macho na kuruhusu nguvu nyingi kutoka na kuzielekezea juu angani na palepale ilitokea hali kama vile anga linaganda kwa macho ya kawaida.

“Eh.. ni kitu gani unafanya?”Aliuliza yule mchina kwa mshangao. Lakini kabla hata hajaelewa kinachotokea alihisi mlipuko wa nguvu ya kijini ukimsogelea kwa kasi.

Ilikuwa ni kama mvua , alichokifanya Rose ni kuunganisha nguvu zake za kishambulizi na mvuke na kisha akazibadilisha kwenda katika mfumo wa maji na kisha akayaelekezea mahali ambapo amesimama yule mchina.

Ufunuo wake wa kimazingira ambao alifanikiuwa kuupata , ulikuwa ni kutengeneza mvua ya kiroho ambayo huwa kama dhoruba.

Mchina yule licha ya kwamba alikwepa matone yote , lakini bado alihofia kwani kila tone la amvua ambalo lingeweza kumgusa lilibeba madhara makubwa.

Rose hakujali kwamba pigo lake la kwanza amelikwapa, aliendelea kuwa makini kuzidi kugeuza mvuke kuwa maji na kuunganisha na nguvu zake za kijini na kuzidi kutengeneza siraha , hakuhitaji kufumbua macho kuona eneo ambalo adui yake amesimama licha ya muda huo kufumba macho , bali hisia zake zilimwonesha yupo eneo gani na anapaswa kushambulia vipi.

“Palee!!”

Aliongea kwa nguvu na palepale yalitokea matone makubwa ya maji na kumsogelea yule bwana , yalikuwa ni matone ambayo yalitengeneza hadi mwanga flani mweupe , ilikuwa ni kama vile unavyooangalia kimondo kikiungua kwa kasi angani ndio matone yale yalivyosafiri kumshukia adui yake kumshambulia.

Mchina alishindwa hata kuelewa shambulizi namna ambavyo lilifanyika , kwani adui yake alikuwa akitengeneza shambulizi lake mbali na alipo , na alichokifanya mara baada ya shambulizi la kushitukiza ni kujikinga na ngao ya kichawi ili tone hata moja lisimguse na kumletea madhara, ngao yake ilifanikiwa kwani bado uwezo wa Rose ulikuwa mdogo kuliko wake hivyo usingeweza kuivunja licha ya uhatari wa siraha yake ya kiroho.

“Unaonekana kuwa na ujuzi wa hali ya juu , nadhani sitakiwi kukuonea huruma tena”Aliongea na palepale alichomoa upanga wake uliokuwa kwenye ala kiunoni na kuanza kuuzungusha kwa mkono moja kujizingira huku yeye pia akizunguka kwa spidi ya hali ya juu , alikuwa kama mtu ambaye anachukua mazoezi ya kuzungusha upanga.

“Pokea Vifundo visivyo na idadi vya mavunjiko ya uhusianooo..!!”Aliongea kwa nguvu na palepale ule upanga ulitoka kwenye mikono yake na kuendelea kuzunguka kwa kasi na palepale kulianza kuonekana vitu kama herufi(Runes) za michoro mbalimbali zilizokuwa zikimeta meta kwa rangi ya njano na kuuvaa ule upanga .

Rose hakuelewa nini anataka kufanya na pia hakumwelewa alivyosema Vifundo visivyo na idadi vya mavunjiko ya mahusiano.

Ghafla tu yule mchina aliinua vidole vyake na sasa ule upanga ni kama ulijitengeneza kopi zaidi ya mara tano na kuendelea kuzunguka.

“Kama Roho ya Dubu mweupe , shambulia”Aliongea na palepale Rose aliweza kuona yale mapanga yalijitengeneza kuwa mengi yakijipanga kistaili flani hivi chini. Juu, katikati na kushoto na kulia na kuanza kumsogelea kwa kasi kwa nia ya kumchoma. Kama mishale.

Rose kitu pekee alichokifiria ni ni kubadilisha mvuke kwa haraka na kuuganisha na kutengeneza kama kioo mbele yake na yale mapanga baada ya kumfikia kwa umbali wa sentimita sitini yaligusana na ile ngao na kugonga kwa nguvu na kumfanya Rose kurushwa mbali licha ya kwamba alifanikiwa kuyazuia.

“Inapendeza,, hakika inapendeza , ndio kwanza ameingia levo ya Nafsi lakini ameweza kuzuila lile pigo”Aliongea yule bwana mweusi alietangulizana na Raisi Jeremy.

“Dhana ya vifundo fundo ni ya kawaida sana , ipo daraja la kati , sidhani kama ina nguvu ya kutosha”

“Lakini hata hivyo ndio kwanza ameingia kwenye levo ya Nafsi, ni jambo ambalo sio la kawaida”Walianza kubishana wao kwa wao.

“Sister Rose anaonekana kuwa na uwezo mkubwa, inaonekana Roma mbinu yake aliogundua ya kujifunza kanuni za anga ina nguvu mno , nilifikiri Rose asingeweza kuzuia shambulizi hata moja”Aliongea Rufi ambaye alikuwa akifatilia kwa ukaribu.

“Kwanini unaongea hivyo , huyu Roma na yeye yuko wapi?”Aliongea Blandina kwa wasiwasi , kwani muda umepita bila ya Roma kuonekana na isitoshe aliogopa Rose kupatwa na tatizo.

Baada ya hapo hawakuweza kuona tena mashambulizi yanavyofanyika kwani walikuwa wakipambana kwa spidi sana , kilichomsaidia Rose ni wepesi , kwani alikuwa ana mafunzo ya kimapigano.

Hakuwa na uwezo wa kumnpiga yule mchina lakini alihakikisha kila pigo analopigwa nalo ana kinga.

Mjumbe wa Hongmeng alionyesha kukasirishwa mno na kuona aibu kwa wakati mmoja baada ya kushindwa kumdhibiti mtoto wa kike mwenye umri mdogo kama Rose ambaye ndio kwanza ameingia levo ya Nafsi.

“Usije kunilaumu tena , maana umenikasirisha mwenyewe”Aliongea kwa hasira na palepale aliacha kuzungusha upanga wake ambao pia ulionekana kama dhana na haukuwa upanga wa kukata watu kama ilivyozeleka.

“Ngoja nikuonyeshe nini maana ya Hongmeng”Aliongea na palepale alianza kuongea maneno yasioeleweka na muda huo huo Rose aliweza kusikia sauti flani hivi zinazokuja na upepo mkali kama vile sauti zinazosikika zaidi Jangwani wakatai wa upepo mkali unapovuma.

Ile anajaribu kufikiria sauti hizo ni nini ghafla tu aliona kiwingu mbele yake kama moshi wa bomu na palepale alihisi kitu kama mishale ikimsogelea kwa kasi , na alishindwa kuchukua hatua mapema kwani alikuwa kwenye mshangao na alijikuta akikubali kushindwa na kufumba macho yake.

Lakini muda uleule ulisikika mlipuko mkubwa wa upepeo katika eneo hilo kupelekea hata maji ya baharini kutengeneza mawimbi.

Rose mara baada ya kuangaliana aliweza kumuona Roma akiwa mbele yake na ilionekana alifanikisha kumkinga na kile kilichokuwa kikitaka kumshambulia.

Yule mjumbe mara baada ya kumuona Roma mbele yake alijikua akiingiwa na woga usiokuwa na kifani , hakuna mtu wa levo ya chini katoka ujinini ambaye alifannikisha kuzia siraha yake , lakini kwa Roma ilionyesha hakutumia hata ujuzi mkubwa na ndio maana alihofia na kumuona Roma ni wa juu zaidi kuliko yeye.

“Nilivyoona hutokei , nilijua hunitaki tena na ninachukuliwa na hawa watu”Aliongea Rose.

“Nilifika hapa muda mrefu , lakini sikuaka kujitokeza , niliona ni kheri nikikuacha upambane ili upate uzoefu, vipi unaonaje , si umeweza kujifunza vitu vingi?”

“Ndio nimegundua msingi wa kumshinda adui lazima uwe katika levo ya juu kuzidi yeye , haijalishi siraha yako ina nguvu kiasi gani, naamini kama ningekuwa juu yake ningeshinda hili pambano”

Roma aliekuwa amekaa pembeni akiangalia Rose akipambana alijikua akishangaa , kwanni licha ya kwamba alijua Rose alifika levo ya Nafsi lakini bado hakuwa akijua ni aina gani ya ufunuo ambao alipata kama siraha, lakini mara baada ya kuona ni mvua ya kiroho alijikuta akishangaa, ilikuwa siraha kubwa sana tu na aliamini kama Rose atakuja kupanda levo zaidi basi atakuwa na uwezo wa kutengeneza mvua ya kiroho yenye ukubwa.

Roma alijikuta akijawa na shauku ya kutaka kujua ni aina gani ya ufunuo ambao warembo wake wengine wangeweza kupata , alikuwa akisubiria sana.

“Nadhani umekuja muda muafaka , huyo binti kashaingia levo ya nafsi na naamini unafahamu sheria za majini , hapaswi kuendelea kubakia katika ulimwengu wa kawaida”

“Yeye ni binadamu kwanini afuate sheria za majini?”Aliuliza Roma.

“Kwahio unamaanisha kwamba hutaki kutii sheria za majini si ndio?”

“Sijasema sitii sheria za majini, kwani hata kama nitakuwa na uwezo mkubwa lakini naamini kuna watu wengine wenye uwezo mkubwa kama wangu katika miliki zenu”

“Kama unalijua hilo basi nipatie niondoke nae au achague kwenda katika miliki ya PANAS”Aliongea na kumfanya Roma kujawa na shauku ya kutaka kujua zaidi kuhusu jamii ya PANAS , maana siku zote alikuwa akiisikia juu juu tu na hakuwahi kuamini kama ipo kweli.

“Kulingana na sheria za gods treaty mtu yoyote mwenye nguvu za kijini anapaswa kubakia katika mipaka ya China pekee, lakini vilevile sheria inamzuia binadamu wa kawaida kujifunza mbinu za kijini na kana ikatokea akajifunza na kuingia levo ya Nafsi anapaswa kuungana na jamii za kijini”

“Kumbe hayo yote unayajua nadhani huna sababu ya kumzuia kubakia duniani”

“Sijamaliza kuongea , Sheria pia inaturuhusu sisi miungu watu kutoa kibali kwa binadamu kuendelea kuishi nje ya bara la Asia licha ya kwamba yupo levo ya Nafsi”Aliongea Roma na kumfanya yule mjumbe kidogo kuonyesha mshangao.

“Sheria pia inasema katika kifungu kinachofuata , endapo binadamu wa kawaida akapewa kibali cha kuendelea kuishi katika ulimwengu wa kawaida, anapaswa kuishi ndani ya bara la Ulaya pekee na si vinginevyo”Aliongea yule bwana mweusi.

“Upo sahihi , anatakiwa kuishi katika eneo moja ambalo lilichaguliwa , ili kuwa rahisi kuwa chini ya uangalizi na kwa mantiki hio Rose haondoki kwenda popote , bali nitamtoa nje ya bara la Afrika na kwenda kuishi Ulaya”Aliongea Roma na kumfanya hata Rose mwenyewe kushangaa, hakufurahishwa na kauli ya Roma kumpeleka kuishi Ulaya lakini pia hakupenda wazo la kupelekwa katika miliki za kijini

“Una uhakika miungu wenzako watakubai kumpa kibali cha kuendelea kubakia duniani?”

“Hilo ni juu yangu kuwazia”

“Kama ni hivyo tumekubaliana , kama ikifika kesho bado yupo hapa Tanzania , Mjumbe Tao unaweza kumchukua na kuondoka nae na Mr Roma utapaswa kutii sheria”Aliongea yule bwana mweusi asiefahamika jina na Roma alitingisha kichwa kukubali .
 
SEHEMU YA 542.

Yule mjumbe mara baada ya kukubaliana na Roma aliamua kuondoka , huku mpango ukiwa ni kesho kurudi kumwangalia Rose kama bado yupo ili amchukue na kumpeleka katika jamii za kijini kulingana na sheria.

“Hubby unapanga kweli kunipeleka nje ya nchi?”Aliuliza Rose kwa wasiwasi.

“Sina mpango wa kukupeleka nje , nimemtega tu nina mpango nauwazia kichwani”Aliongea Roma na kumfanya Rose kutabasamu baada ya kuona kumbe Roma hakuwa siriasi , hakuwa tayari kwenda kuishi nje ya nchi na kukaa mbali na Roma..

“Kwasasa usiwaze sana kuhusu hili, hebu turudi kuna mtu nikaonane nae”Aliongea Roma na Rose alikubali na wote walirudi na wakati Rose akielekea ndani Roma alimsogelea Raisi jeremy ambaye alikuwa akijiandaa kuondoka.

“Nadhani uliniambia wewe mwenyewe kama huna mpango wa kumtambua Edna kama mtoto wako?”

“Ni kweli nimesema hivyo , lakini siwezi kubadilisha ukweli kwa maneno , Edna damu yake ni damu yangu “

“Acha kuwa mnafiki na sitaki kukuona karibbu na Edna, kwasasa ni mke wangu na huna haki ya kumsogelea kwasababu ulishamtelekeza , kama kweli ulikuwa ukijitambua kama baba usingekwepa majukumu yako”

“Mr Roma najua kwamba una uwezo mkubwa na una nguvu lakini huwezi kunipangia maamuzi juu ya mtoto wangu na isitoshe taifa langu halikuogopi , eti tu kwasababu una nguvu”Aliongea Raisi Jeremy.

“Unaonekana kujiamini kwasababu umezingirwa na hawa watu , lakini nikwambie ukinichokoza naweza kufanya chochote kile juu yako”Aliongea Roma.

“Kijana unaonekana kuwa imara sana na mwenye ujuzi na umebahatika kuwa na uwezo mkubwa wa nguvu za mbingu na ardhi lakini usiwe na kiburi , mke wako anaweza kuwa mke wako , lakini bado haiondoi ukweli kwamba nyumbani kwao ni Rwanda , Ni kweli Jeremy hapa alifanya makosa lakini sisi jamii ya PANAS tunamsapoti kwenye maamuzi yake, kama unajiona kwamba una uwezo hata sisi tunao pia”Aliongea kibabe na kumfanya Roma kuanza kupatwa na hasira, mawazo yake aliona labda angekuwa na urafiki na jamii hio lakini kwa namna ambavyo hali ilivyo aliona kabisa ni tofauti na alivyofikiria.

Alitamani kuita chungu chake palalepale kiwameze na kuwageuza vidonge vya kijini, lakini hakutaka kufanya jambo lolote kwa muda huo ,kwani hakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu jamii hio ya kijini na kubwa zaidi alihofia wanaweza kuwa na mbinu kubwa kuliko yeye kutokana na zile tetesi kwamba mbinu yake ya kimaandiko asili yake ni kutoka katika jamii hio.

Ukweli ni kwamba Roma baada ya kuwaangalia watu hao aliona kabisa walikuwa na mitazamo tofauti kabisa na ile ya watu wa China , hawa kidogo walionekana kustaarabika hata katika mavazi yao na alijiambia huenda anachosikia kuhusu jamii hio ni kweli.

Roma alijikuta aking’ata meno yake kwa hasira na kujituliza , kwa wakati huo aliona kabisa uwezo wake bado ni mdogo kutengeneza maadui wengi wa jamii zisizoonekana hivyo aliamua kuwa mpole

“Nikutahadharishe sijui unachopanga katika akili yako , lakini ni vyema kama nia yako ya kumtambua Edna kama mwanao ni ya dhati la sivyo sitojali ni nguvu gani inayokusapoti , nitahakikisha nakuua”Aliongea Roma na hapo hapo aliingia ndani ya geti la nyuma yake akiwaacha wakiondoka.

“Inatia wasiwasi sana kwa kijana mdogo kama huyu kuwa na uwezo mkubwa wa aina hio , jamii yetu ilikuwa ikimwangalia kwa umakini lakini kwasasa wasiwasi wao juu yake ni mkubwa zaidi “Aliongea yule bwana.

“Mkuu Geni , je hakuna uwezekano wa kuwatumia wakubwa zenu kumdhibiti , nadhani akiendelea kuwa na kiburi hivi mipango yetu haitoenda vizuri kama tulivyopanga”

“Mhmp! , Jeremy hakika wewe ni katili , licha ya yote hupaswi kuongea hivyo kwani bado ni mkwe wako”

“Sina shaka yeye akiendelea kuishi na kuwa mkwe wangu , tatizo ninalohofia ni uwezo wake , unazidi kuwa tishio kwa kila ninachokiwazia na mipango yenu”

“Huna haja ya kuwa na wasiwasi , hawezi kuzuia kile tunachopanga kwani lazima kitokee hata kama tusifanye chochote , tunachofanya sasa hivi ni kujiandaa kwa kuweka mazingira sawa ili pale tu fursa itakapojitokeza isitupite”Aliongea bwana alieitwa Geni.

“Mkuu Geni mpaka sasa siamini yale maneno , kama kweli huu utabiri ukatimia kama ulivyosema nashindwa kutabiri nini kitatokea kwa bara lote la Afrika”

“Kama kila kitu kitaenda sawa ndani ya mipango yetu ,Rwanda itakuwa nchi kubwa ki uchumi na katika maendeleo ya teknolojia, kwa nchi nyingine ambazo hazijaweka msingi mzuri lazima watapitia awamu ya pili ya ukoloni wa jamii zote zenye ngozi nyeupe”

“Hiko ndio kinanichanganya zaidi , ukoloni wa mara ya pili?”

“Huna haja ya kuwaza hilo Jeremy , ukiwa mbele ya muda siku zote utakuwa mshindi , ukoloni wa mara ya pili utakaotokea katika bara la Afrika ni ule uliondelea”Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy kuwa katika kimya kidogo kusharabu maneno yake.

“Roma hakuna kitu kibaya kilichotokea wakati wa mauzngumzo yako na Jeremy?”Aliuliza Blandina aliekuwa akionyesha wasiwasi .

“Niliwapa onyo tu kwa kuwatahadharisha kama wana mpngo wenye nia ovu juu ya Edna sitowaacha salama , kuwa na amani hakuna kibaya kilichotokea”

“Wasiwasi wangu ni kwa mkeo nina miaka nusu karne sasa , lakini nashindwa kujua ni kipi ambacho anafikiria”Aliongea na kumfanya hata Roma kujicheka yeye mwenyewe maana haikuwa kwa mama yake tu ,, hata yeye mwenyewe hakuwa akifahamu Edna kile ambacho anafikiria kabisa na mara nyingi aliishia kuingia kwenye mitengo yake bila hata ya kufikiria.

Roma alipanda mpaka juu kwenye chumba cha mke wake , ili kumwangalia anaendeleaje mara baada ya kongea na baba yake mzazi,

“Ongea taratibu Lanlan kalala , kuna kitu unachotaka?”Aliongea Edna mara baada ya kufungua mlango.

“Wife uko sawa , kuna chochote cha kuumiza alichokuambia??”Aliuliza Roma kwa wasiwasi, hakujua Edna aliongea nini na baba yake na huo ndio ulikuwa wasiwasi wake.

“Hapana , hajaniambia chochote cha kuumiza”

“Lakini kwanini unaonekana kama haupo sawa?Niambie kama huyu Jeremy kaongea chochote ambacho kimekuudhi nimfuate sasa hivi”

“Nimesema hajaongea chochote kibaya na sitaki kulisikia jina lake tena”Aliongea Edna kwa kuonyesha kukasirika na Roma alishangaa mabadiliko yake mara baada ya kutaja jina la baba yake, lakini Edna palepale alijishutikia

“Nisamehe .. sio kwamba nakukasirikia , najua una wasiwasi na mimi lakini sitaki kuongea chochote kinachomuhusu kwasasa”.

Roma aliona kabisa Edna hakuwa sawa , lakini hakutaka kumlazimisha kuongea kama hataki , hivyo alitoka na kurudi kwenye chumba chake kupumzika

Dakika chache mbele mlango wa chumba chake uligongwa na alionekana Blandina ambaye alikuwa amebeba sahani yanye bakuli ambalo lilitoa mvuke wa harufu wenye kupendeza pua.

“Mama umebeba nini?”

“Nimekutengenezea supu ya kuku , angalau upashe utumbo joto”Aliongea na kumfanya Roma kuguswa na kitendo hicho , siku zote Blandina alikosa cha kumfanyia Roma kutokana tayari ameshakuwa mtu mzima na kila kitu alikuwa akijifanyia mwenyewe.

Roma alichukua bakuli na kisha akachota kidogo kwa kutumia kijiko”

“Mama mbona kuna harufu kama ya dawa kwenye hii supu, umeweka kitu gani?”

“Sio kitu kikubwa Roma , kuna kajimzizi tu nimechanganya ni dawa nzuri zaidi kwa afya ya mwili wako”

Roma mara baada ya kujua supu imewekwa kijimzizi hakutaka kuendelea kunywa tena.

“Mama siiaki hii supu tena , nitakula tu chakula”

“Roma haina tatizo kwako , najua una nguvu lakini dawa kama hizi zinasaidia , niliongea na mpemba mmoja wa dawa za miti shamba na aliniambia ni nzuri zaidi kwa mwanaume anaetegemea watoto”Aliongea Bloandina bila aibu na kumfanya Roma kushangazwa na kauli hio ya mama yake.

“Mama wanaume wengine ndio wanaopaswa kuwekewa mizizi mimi sihitaji na nishakuambia siwezi kupata mtoto kwa uwezo wangu huu hata kama nitumie miti shamba ya aina zote”

“Najua lakini Rose si tayari ashapanda panda levo na pia anaendelea kupanda , naamini anaweza kuwa mtu sahihi kukupatia mtoto”Roma alishangazwa na kauli ya mama yake , ndio maana tokea juzi muda wote habari za Rose hazikuwa zikiisha kumbe furaha yote ilikuwa kwenye swala la kupata mjukuu.

“Mama ni kweli amepanda levo , lakini bado hayupo na spidi niliokuwa nayo mimi , tayari yupo kwenye levo ya Nafsi na mimi nakaribia mwisho wa levo ya kuipita dhiki , bado nafasi ya yeye kubeba ujauzito wangu ni ndogo”

“Lakini bado nafasi yake ni kubwa kama utamlinganisha na Edna”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa , hakutegemea mama yake kumlinganisha Edna na Rose.

“Mama kwanini unasema hivyo , swala la mafunzo linategemea vitu vingi , Edna ni kweli bado yupo chini lakini siwezi kumfosi kupanda levo kwa haraka na pia siwezi kumpendelea Rose kwasababu kapanda levo kuliko wengine”

“Najua na sitaki kuwa na upendeleo lakini tabia na matendo ya Edna juu yako mimi sikubaliani nayo kwani hayasaidii kitu, nimekuona ulivyotoka kwenye chumba chake ukiwa umenyongea”

“Kwahio ulisikia kila kitu?”

“Sijasikia chochote , lakini mwonekano wako unaongea kila kitu , Kama angalau anatimiza wajibu wake kama mke nisingekuwa na wasiwasi lakini kwanini mpaka sasa mnalala vyumba tofauti , bado nafasi yake ya kupata ujauzito ni ndogo lakini bado anajitenga na wewe , kila nikifikiria swala hili najikuta nakasirika , unapendwa na wasichana wengi wazuri lakini kwanini kuwa na mke ambaye ana akili za kitoto , ashaolewa sasa na anapaswa kufanya kila kitu kulingana na familia, Roma wewe ndio unaekwenda kuendeleza ukoo wa familia na Edna anapaswa kusaidia katika hilo , sitarajii makubwa kutoka kwake lakini angalau aonyeshe matendo ambayo yanaashiria mapenzi kwako”

“Mama haipo hivyo , uadhani wewe mwenyewe unaifahamu tabia ya Edna , ananijali sana lakini kwasababu ya Lanlan sioni kama ni tatizo sisi kuwa hivi na isitoshe hili linarahisisha pia , kwani nina uwezo wa kutoka muda ninaotaka na kuwafanya wengine wasione kama sitimizi wajibu wangu , kuhusu mtoto sidhani kama kuna haja ya kuharakisha”

“Bado tu unamkingia kifgua hata kwenye swala muhimu kama hili, ni mantiki kwake kupata mtoto kwanza kuliko wengine la sivyo mambo hayawezi kuwa mepesi hapo baadae , unafikiri kama wengine wakifanikiwa kupata mtoto, ni yupi utaanza kumjali, mama wa mtoto au mkeo?, sidhani kama mkeo angekuwa Amina , Rose , Dorisi au Nasra wangekubali kulala tofauti na wewe , angalia sasa mtoto wa kuasili anamfanya kutotimiza majukumu yake”

“Mama ni kosa kusema hivyo , Lanlan anaweza kweli ni wa kuasili , lakini kwangu mimi ni binti yangu kabisa , ni mtoto wetu wa kwanza na hilo haliwezi kubadilisha kitu”.

“Sawa hata mimi namuona Lanlan kuwa mtoto mzuri na pia nampenda kama mjukuu wangu lakini tatizo ni msichana na hana damu ya ukoo wenu , babu yako na yeye hana muda mwingi wa kuishi duniani , je unataka atangulie mbele za haki bila kuona mjukuu wake wa kiume”Aliongea na kumfanya Roma ashangae , hakuelewa mama yake tangu lini akaanza kumjali mzee kweka.

“Mama nimekuelewa na pia najua wasiwasi wako , kwanzia leo nitahakikisha wanajifunza kwa spidi ili kupanda levo kwa kasi”

“Roma najua unampenda Edna kuliko wengine wote na mimi kama mama yako najitahidi kumkubali , lakini unatakiwa kuelewa wamama wote ni wabinafsi, Edna ni mkwe wangu, lakini wewe ni mtoto wangu wa kiume , siwezi kuona mwanamke mwingine anakuendesha anavyotaka,inaniuma mimi kama mama yako , una uwezo mkubwa na unapendwa na wanawake wengi , kwanini Edna anakuwa udhaifu wako, kuna siri gani ambayo siijui?”

“Mama usiende mbali sana , nitaongea na Edna na tutayaweka sawa”Aliongea Roma akijaribu kumtuliza maana ilionyesha alikuwa na dukuduku la muda mrefu , pengine kujenga ukaribu na michepuko yake alianza kuona walikua na sifa zaidi za kuwa mke kuliko Edna.

Roma mara baada ya mama yake kutoka , aliona ngoja ataongea na Edna ili kujua namna ya kuishi kama mke na mume zaidi na kuacha kuibua maswali.





SEHEMU YA 543.

Kwasababu alikuwa na kazi ya kudili na mjumbe wa Hongmeng, hakutaka kwanza kudili na mambo yake ya nyumbani ya kuongea na Edna , bali kulivyokucha asubuhi moja kwa moja alienda kazini.

Ilimfurahisha kucheza gemu , kuperuzi kwenye mitandao na kuangalia taarifa za habari akiwa kazini , kwake hakuwa akifika kazini bali alifika kupumzika na muda ukiisha atarudi nyumbani.

Siku hio asubuhi wakati anafika ofisini alishangaa kumkuta Kassimu binadamu yake eneo la maegesho ya magari na alivyomuuliza alikuwa akifanya nini hapo alimwambia amekodisha floor ya nne kwani anafungua kampuni ya maswala ya kuchezesha magemu online.

Roma baada ya kusikia taarifa hio hakushangaa sana kwa Kasimu kukodi sehemu ya jengo hilo kwa ajili ya kufanya biashara ya kuchezesha mage,mu , baba yake Tajiri Azizi alikuwa moja wapo ya matajiri wenye pesa nyingi hivyo ilikuwa sawa kwa Kasiimu kuwa na pesa za kumudu kodi.

Roma alijaribbu kumuulizia Kasimu habari za Donyi na aliambiwa anafanya kazi katika kampiuni ya mama yake katika idara ya ubunifu.

Roma alijikuta akimkumbuka Neema luwazo kwani tokea atoke Korea hawakuwa wameonana, Neema luwazo hakuwa na utofauti na Edna tu wote walikuwa wakipenda kujiweka bize na maswala yao ya kibiashara kuliko kitu chochote kile na hiko kilimfanya kushindwa kupanda muda wa kuwa nao karibu, hususani kwa Neema ambaye alimisi mapenzi ya kiutu uzima.

Ni wakati wa usiku wakati wanafamilia wote wakipata chakula,Blandina ndio ambaye alikuwa ametawala maongezi na muda wote alikuwa akizungumza habari zilizotokea mchana mara baada ya kukutana na mama yake Mage.

Siku hio mchana Roma na mama yake waliweza kushiriki kwa pamoja siku ya kuzaliwa ya Mama T ambaye alikuwa akitimiza miaka arobaini , sasa sherehe hio ilimfanya Blandina kujenga sana ukaribu na mama yake Mage kiasi kwamba waliahidiana mengi na upande wa Mama Mage alijitahidi kumpamba Blandina ili kumpigia debe mtoto wake Mage.

Sasa yale yote yaliokuwa yametokea katika sherehe hio Blandina alikuwa akimhadhithia Bi wema na hali ilio ilimfanya Roma kuona si vizuri kuongea mbele ya Edna, hususani namna ambavyo alikuwa akimsifia Mama T kuwa mtu mzuri sana.

Upande wa Edna hakuwa na taarifa juu ya Blandina na Roma kwenda kushiriki sherehe hio , ukweli ni kwamba Roma alipokuwa yupo kazini aliweza kufuatwa na Mage na kumwambia mama yake anataka ashiriki pia katika sherehe yake ya kuzaliwa na kwasababu ilikuwa ni ghafla sana Roma alikosa muda wa kumtaarifu Edna.,

Hali hio ya Blandina kumsifia Mama T ilimfanya Edna kujihisi mnyonge , lakini pia kwa wakati mmoja kumkumbuka mama yake mzazi, alikuwa akimtegemea mama mkwe wake kuwa kama mbadala wa mzazi wake lakini kinachoendelea hapo ndani ni tofauti na matarajio yake.

“Mama usiongee sana unaonaje ukiweka umakini kwenye kula , utamfanya Edna amkumbuke mama yake”Aliongea Roma baada ya kuona mama yake amepitiliza na Blandina alimwangalia Edna na kumiona akionekana mwenye huzuni.

“Edna nisamehe , sikumaanisha kukufanya mwenye huzuni , usiwe na hasira na mimi, sawa?”

“Usiwe na wasiwasi mama , niko sawa sikukasirikii kumsifia Mama T , hata mimi najua ni mtu mzuri”Aliongea Edna ambaye alikuwa akila chakula kama akilazimishwa.

“Kama ni hivyo hakuna tatizo …”Alijibu na kisha akalazimisha tabasamu na kukaa kimya , hali ya hewa ilionekana kubadilika ghafla na kuwa ya baridi kutoka na kwamba hakuna ambaye alikuwa na ujasiri wa kuanzisha maongezi, ambaye hakuwa na wasiwasi na kujali kile kinachoendelea ni Lanlan peke yake kwani hakuwa akiifahamu vizuri lugha ya kiswahili.

Roma aliekuwa akifikiria mbinu ya kurudisha hali ya hewa kuwa ya kawaida alijikuta akikunja sura mara baada ya kuhisi msisimko wa nguvu ya kijini ikikaribia nyumba yake, palepale alijua aliefika hapo alikuwa ni mjumbe kutoka Hongmeng, lakini hata hivyo Roma alikuwa na mpango wake kichwani tokea mchana.

Njia pekee ambayo aliamini ingeweza kumbakisha Rose Tanzania nikutoa hongo , alijuwa watu kutoka Hongmeng huendeshwa na tamaa ya vidonge vya daraja la kwanza vya kijini hivyo kama angempa Hongo Mjumbe huyo basi angepiga kimya kuhusu Rose na kumuacha aendelee kubakia Tanzania.

Roma mara baada ya kutoka nje kuonana nae , alimkuta akiwa amekasirika mno na Roma alitegemea hilo lakini hakujali zaidi ya kuanza mauznumzo nae juu ya uwepo wa vidonge ambavyo vingemsaidia kupanda levo kwa haraka.

Bwana yule mara baada ya kuonyeshwa vidonge hivyo alijikuta akishangaaa na kujiuliza imekuwaje Roma akawa na vidonge hivyo na Roma hakutaka kumpa siri yake , lakini alimhamkikishia kwamba kama angefumbia macho swala la Rose basi angempatia kidonge kimoja cha daraja la juu na viwili vya daraja la kati.

Roma sio kwamba alikuwa akiogopa kupigana nae , alichokuwa akihofia kama atamuua na mjumbe huyo mwingine wa Hongmeng basi angejitengenezea tatizo ambalo angeshindwa kulitatua kwa kipindi hicho ambacho alihitaji kuweka umakini kwenye kufunza warembo wake kupanda levo, lakini na yeye pia kujiimarisha zaidi.

Ijapokuwa mwanzo Balozi huyu wa Hongmeng kujifanyisha mgumu wa kukataa Rushwa lakini mwisho wa siku alikuwa na udhaifu uleule tu ambao binadamu wa kawaida wanao , hivyo Roma alifanikisha kumhonga vidonge na Balozi kumuhakikishia kwamba hakuna mtu kutoka Hongmeng ambaye atajua uwepo wa Rose nchini Tanzania.

Baada ya Roma kukamilisha swala hilo alienda kwa Rose na kumpa taarifa juu ya kumtafutia suluhisho la muda la kuendelea kukaa nchini , ndio lilikuwa suluhisho la muda kwani aliamini siku zijazo lazima Rose atafahamika na huenda sio Rose tu , kwasababu wengine wote walikuwa wakijifunza basi wangefikia katika levo ya nafsi na kuanza kuandamwa.

Roma mara baada ya kumweleza Rose jambo hilo na kuona amefurahi alirudi nyumbani , Blandina na Qiang Xi walikaa kwenye runinga kangalia tamthilia na Edna yeye alikuwa bize kumsaidia Lanlan kukamilisha Homework yake aliopewa shuleni.

Roma alijiunga nao , ijapokuwa Lanlan kwenye mwandiko alikuwa vibaya sana , lakini alikuwa na uelewa wa juu sana hivyo haikumpa shida kwenye kumuelekeza baadhi ya mambo.

Lanlan alikuwa na uwezo mkubwa lakini alikuwa na tabia ya uvivu na hakuwa anapendelea kabisa kufanyia kazi anazopewa shuleni na ni mpaka alazimishwe na hilo ndio jambo pekee ambalo lilimfanya Roma asione ni wakati nzuri wa kumfundisha mbinu za kijini , kwani akili yake bado haikuwa imetulia na alikuwa ni mtoto mwenye mambo mengi na kama angemfudisha asingepata faida zaidi ya kumuweka kwenye hatari.

Roma aliangalia namna Lanlan alivokuwa akiumba herufi, zilikuwa kubwa mno kama vile ni vikatuni na aljikuta akijichekea , hata yeye mwenyewe alikuwa na mwandiko mbaya hivyo hakumshangaa sana Lanlan , lakini kwa Edna alipatwa na wasiwasi na kujiambia sku za baadae Lanlan ataandika sana kwa kuchapa kuliko kuandika kwa mkono.

Roma baada ya kukaa hapo kwa dakika kadhaa , alimpa ishara Edna kumfuata mpaka juu kwenye Lounge ili kuongea na Edna alishangaa na kujiuliza Roma anataka kuongea nini , lakini aliishia kufuata hadi juu na kumwachia Qang Xi kazi ya kuendelea kumsaidia Lanlan kumalizia homework yake.

“Kuna kitu gani unachotaka kuongea?”Aliuliza Edna na Roma aliamua kumwelezea Edna juu ya malalamishi ya mama yake , alijitahidi kuweka maneno yake namna ambavyo hayamkwazi Edna bali kumuelewesha.

“Usimlaumu sana mama , ushakuwa mama tayari lazima utakuwa unajua hisia ambazo wazazi hupitia , mimi sina tatizo na najua wewe ni mwenye hasira za haraka, lakini mama anachotaka ni sisi kuishi kama mume na mke”Aliongea Roma na Edna alionyesha kuelewa na aliishia kung’ata lipsi zake.

“Nimekuelewa, nitamfudisha Lanlan kulala peke , nipe angalau hata wiki moja na baada ya hapo tutaanza kulala chumba kimoja”

“Ni sawa kufanya hivyo lakini usione kama nalazimisha tulale pamoja , na isitoshe nina furaha na huu utaratibu”

“Najua ndio unafuraha , unajua kabisa kulala na mimi itakuwia ngumu kutoka nje usiku kulala na wanawake wako wengine , unafikiri sijui kuhusu hilo , nadhani utaratibu anaotaka hauwezi kukupa furaha ya moja kwa moja, mimi sina tatizo kama unataka rulale pamoja , kwani tayari sisi ni mume na mke”

“Edna nadhani swala analozungumzia mama zaidi sio kuhusu kulala pamoja tu, babe Edna anachomaanisha ni wewe angalau kuwa mpole na mnyenyekevu unapoongea na mimi na kunijali anapokuwa mbele yetu, nadhani ndio namna ya kumfanya kuwa na furaha na atakupenda zaidi”Aliongea na kumfanya Edna kukosa furaha.

“Najua nina madhaifu katika sehemu nyingi kama mke lakini hata kama nije kuwa mpole na mnyenyekevu mbele yako sifanyi kwasababu ya mama , wewe unadhani ni sawa mimi kuigiza kukujali?”

“Hicho sio ninachomaanisha , ninachotaka ni wewe na mama kuwa na mahusiano mazuri , yeye ndio mama yangu wa pekee na wewe ni mke wangu , sio sawa mimi kuwasaidia kuelewana, na kati yenu siwezi kuwalinganisha kwani wote nyie ni muhimu kwangu , Najua mama anakupenda lakini kuna vitu hamvimridhishi hivyo angalau wewe nifanyie unachotaka tukiwa wenyewe lakini mbele yake jaribu kuwa makini”Aliongea na kumfanya Edna kujisikia vibaya ila aliona ana pointi.

“Honey , je nimekuwa mjinga kiasi kwamba imekufanya kuwa na wasiwasi juu ya haya yote kwa ajili yangu..”

“Usichukulie hivyo , isitoshe mimi ndio nakufanya uwe na hasira za mara kwa mara kwani matendo yangu hayaridhishi , wasiwasi wangu ni furaha ya nyumba kupotea na mimi hii ni kazi ngumu sana kwangu kuifanya kuliko kuua , hivyo mke wangu naomba unisaidie katika hili, sawa babe?”Aliongea Roma kwa tabasamu huku akibembeleza.

“Kwanini kila mtu anaona labda na kuchukulia kama sehemu ya kutolea hasira zangu , lakini kila kitu kipo wazi wewe ndio mchokozi..”Aliongea Edna huku akitoa tabasamu na kumfanya Roma kujikuta akipata ahueni.

*****

Siku iliofuata baada ya Roma kufika kazini , alitakiwa kwenda kuhudhuria kikao na idara ya uhusiano na masoko makao makuu ya kampuni ya Vexto.

Baada ya kuendesha gari mpaka katika jengo hilo alishangazwa kuona kuna watu wanaume kwa wanawake waliokuwa wameshikilia mabango nje ya jengo hilo , na kwa macho yake ya haraka alijua ni watu ambao walikuwa wakifanya mgomo.

Hawakuwa watu wengi hivyo haikusababisha barabara kuwa na msongamano na hata wau hawakuwajali , lakini upande wa Roma alipatwa na wasiwasi na palepale alitoa simu na kumpigia Edna.

“What is it Mr Roma Ramoni..”Sauti upande wa pili ya Edna ilisikika na kwa kauli hio alijua tu lazima atakuwa kwenye kikao .

“Nini kimetokea , mbona naona kuna watu wapo chini ya jengo wakiwa na mabango ya shinikizo na wanapiga makelele?”Aliuliza Roma na Edna alikaa kimya kidogo kabla ya kijibu.

“Usiwajali , acha wapige makelele wakavyo wakichoka wataondoka, hata hivyo hali ya hewa kwasasa ni ya mvua sidhani kama watadumu muda mrefu”Aliongea Edna kikauzu na baada ya kumaliza kauli yake alikata simu.

Roma alijikuta akipata mamivu ya kichwa kwani ni jana usiku tu alikuwa akimwambia aonyeshe upole na unyenyekevu wakati wakuongea nae , lakini asubuhi hio matokeo yalikuwa tofauti.

Roma aliamini mtu pekee ambaye anaweza kumpatia majibu ni Daudi, aliamini lazima atakuwa akifahamu kinachoendelea katika makao makuu ya kampuni , hivyo baada ya kurudi katika kampuni yake alimwita ofisini.

“Director didn’t president tell you anything Aren’t you husband and wife?”Aliongea Daudi kwa kingereza akimaanisha je Edna hakumweleza , kwani wao si mume na mke.

“Upuuzi , ningekuuliza kama najua kinachoendelea?”Aliongea Roma huku akiona kidogo aibu kwani Daudi alikuwa na maana , ila asichokijua tu ni kwamba Edna hakuwa akimshirikisha mtu maswala yake ya kibiashara na Roma hakujali maswala ya kushirikishwa pia.









SEHEMU YA 544.

Uapnde wa Daudi alionekana kupatwa na aibu kidogo kuuliza maswali ambayo hayakuwa ya msingi.

“Mkurugenzi hao ni waajiriwa wa kampuni ya maduka ya Beseli(Beseli department store) , wanafanya maandamano baada ya kuona kampuni ya Vexto imenunua kampuni yao kwa njia zisizo halali”

“Beseli Department Store , sijawahi kuisikia?”

“Ndio mkurugenzi , Beseli ni kampuni ya muda mrefu sana iliojikita ndani ya Tanzania, mwanzilishi wake , Mzee Kakolanya pia ni mjasiriamali aliejijengea jina kwa muda mrefu , katika miaka ya hivi karibuni CEO Edna alikuwa akijipanua zaidi na zaidi kibiashara na karibia asilimia hamsini ya Department Store(Maduka makubwa) zote znazopatikana katika eneo la Kibaha zipo chini ya menejimeni ya kampuni ya Vexto, mpango wa kampuni ya Vexto ni kubadilisha mpangilio wa kibiashara katika eneo la Kibaha kwa wa kisasa ili kuvutia zaidi wapangaji katika eneo la Mji wa kisasa , lakini kampuni ya Beseli ambayo inaendesha asilimia sabini ya biashara zake katika wilaya ya kibaha walikuwa wakileta ugumu kuchukuliwa na kampuni ya Vexto , sio tu jina la kampuni yao lakini pia eneo la ardhi katika biashara yao hawapo tayari kuuza , kampuni ya Beseli inalenga wateja wa chini zaidi katika maswala ya fasheni na vyakula lakini staili yao ya kibiashara haiendani na mikakati ya kampuni ya Vexto katika kubadilisha mwonekano wa mji hivyo licha ya viongozi wa kampuni kujaribu kumshawishi Mzee Kakolanya kuuza biashara yake na eneo lote kwa bei kubwa mbali na thamanni ya kampuni yake licha ya kuendesha biashara kwa hasara na kuwa na madeni mengi lakini aligoma”

“Kama ni hivyo kwanini wafanyakazi hawa wanafanya maandamano nje ya jengo la kampuni?”

“Kwanzia wiki iliopita kulizuka taarifa mitandaoni na katika vyombo vya habari juu ya kampuni ya Beseli kuuza bidhaa feki kwa bei ya bidhaa orijino ,Mzee Kakolanya alipandwa na ghadhabu mno kwani taarifa hio ilikuwa na athari kubwa kwa kampuni,

Benki nao walianza kuharakisha Beseli kulipa deni wanalodaiwa au wakubali kuuza hatimiliki kwenda kampuni ya Vexto , hivyo Mzee Kakolanya anaamini Edna ndio ambaye alihonga vyombo vya habari pamoja na watu wa mitandao kuchafua jina la kampuni yake, hivyo wafanyakazi wa muda mrefu wa kampuni hio walishawishiwa na Mzee Kakolanya kufanya maandamano mbele ya kampuni ya Vexto”Aliongea Daudi na sasa Roma aliweza kuelewa tatizo lote , lakini bado ilikuwa ngumu kwake kuamini juu ya swala hilo kama kampuni ya Vexto imehusika.

Lakini Roma bado alikuwa na mashaka , alikuwa akijua staili ya kuendesha biashara kwa Edna na muda mwingine anachukua hatua za kikatili zaidi.

“Daudi , je unaamini kampuni ya Vexto imewahonga watu na vituo vya habari kutoa taarifa ya uzushi?”

“Kama nitakuwa mkweli kwako Mkurugenzi naamini hili ni swala ambalo kampuni ya Vexto inahusika ukiangalia na mpango wa muda mrefu wa kutaka kuinunua kampini hio ya Beseli , ninaweza kusema kilichofanyika ni kuhonga wanahabari ili kuzusha taarifa hizo na wakati huo huo benki iliwalazimisha kulipa deni ambalo lilikuwa kubwa kutokana na malimbikizi , hivyo Beseli mwisho wa siku itabakiwa na chaguzi mbili , aidha wajitutumue kulipa deni ambalo hawana uwezo nalo au wakubali kuuza kampuni yao kwa Vexto”

“Kwahio unachomaanisha ni kwamba mke wangu anawanyanyasa wengine si ndio?”

“Mkurugenzi usinifikirie vibaya , lakini biashara ni vita na siku zote mwanajeshi hawezi kuacha kufanya njia za mikato kupata ushindi , kama ni mpango wa Boss Edna basi nitasapoti maamuzi yake”

“Okey nimekuelewa , unaweza sasa kuondoka”Aliongea Roma na Daudi alitoka kwenye ofisi ya Roma.

********

Katika siku chache zilizofuata Edna alifanikisha kumlazimisha Lanlan kulala katika chumba chake na yeye akahamia katika chumba cha Roma.

Blandina mara baada ya kuona wanalala pamoja , alijikuta sasa akiridhika na tabasamu kwenye uso wake kila alipokuwa akiongea na Edna liliongezeka maradufu.

Blandina alionekana na yeye kuanza kuzeeka vibaya , kwani mara nyingi alikuwa akikaribisha marafiki zake nyumbani na kupiga soga muda mrefu na hata kucheza karata.

Edna kila alipokuwa akirudi kutoka kazini aliweza kukutana na kundi la wanawake wakiwa eneo la sebuleni wakipiga makelele na kugongesheana viganja , kutokana na tabia yake ya kupenda utulivu na maisha ya kujitenga hakufurahishwa na ustaarabu wa mama mkwe wake , lakini aliishia kuvumilia na kuhakikisha kila wanapoongea anajitahidi kuonyesha tabasamu kwa kadri awezavyo.

Muda wa usiku katika chumba chao , Roma hakutaka kupoteza fursa hata siku moja, alikiwasha kila siku na kilichosikika ni milio ya Edna kuomba apumzishwe, lakini Roma hakusikiliza hoja yake na isitoshe mke wake huyo hakuwa na uwezo wa kwenda raundi ya pili..

Hiki kipande kitaendelea …Subiri uone kiakachotokea wataachana tu.







SEHEMU YA 544B

Sheria moja tu ambayo Roma aliwekewa na mke wake ni kwamba hakuna kurudia mara mbili na Roma kwasababu alikuwa akimsikiliza Edna kwa kila anachomwambia alikubali.

Lakini sasa upande wake alihakikisha hio mara moja inakuwa kama ni mara tatu kwa mtu wa kawaida.

Muda huo wa usiku kilikuwa ni kilio kwake , Roma aliekuwa amemlalia kwa juu hakumpa nafasi ya kusogea hata nchi moja, Edna hakujua hata kinachoendelea katia mazingira yanayomzunguka , lakini kwa muda huo ni kama vile yupo juu kileleni mawinguni.mwanaume wake alikuwa na nguvu kiasi kwamba alimfanya kupanda mlima na kushuka mara nyingi iwezakanavyo na kumfanya kila kiungo cha mwili wake kama vile kimepalalaizi.

Ni zaidi ya lisaa limoja na nusu tokea amwingine mkewe , lakini bado alijihisi yupo mbali kabisa kumaliza , alijua hakuwa wa kawaida lakinni alijitahidi kupunguza muda ili isije kutokea mke wake kuchoka haraka kabla ya yeye mwenyewe kumaliza , ukizingatia kulikuwa na mashariti hivyo alitumia akili kwenye kuridhisha mwili wake.

“Huwezi hata kupumzika siku moja ,hiki kitendo unakipenda sana?”Edna alilalamika huku akihema kama mbwa mara baada ya Roma kumwachia.

“Mpenzi , kwanini unaongea kama vile wewe huhusiki isitoshe sijapanda mlima kama ilivyokuwa kwako”

“Hapana usiongee…kwanini huna aibu kuongea mambo hayo”Aliongea Edna huku akiona aibu kama mtoto wa darasa la saba na kumfanya Roma ampige kibao kiwili wili cha chini.

“Mama amesema unatakiwa kuweka juhudi kupata ujauzito wa mtoto wetu wa kwanza ,hapa si ndio nakusaidia?”

“Lakini hata kama sio jambo ninaloweza kuamua na isitoshe kama nni mtoto ninae tayari”

“Wazee wetu wa familia wanataka wajukuu wengi , hivyo unapaswa kuelewa hisia zao”

“Kama nitaendelea kujali kile wanachojisikia , vipi kuhusu mimi?”.

“Unamaanisha nini kuhusu wewe?”Aliuliza Roma alieashangazwa na kauli yake.

“Honey , tutafute muda tuongee na mama kualika watu wengi wa uswahilini kujaa hapa nyumbani , wale mashangazi wana sauti kubwa mno na hawana hata ustaarabu kwenye kuongea, nashangaa kwanini mama ametengenza nao urafiki”

“Mama anajisikia vibaya kukaa mwenyewe muda wote na isitoshe maisha yake karibia yote yalikuwa ni yeye mwenyewe , kwanini tusimuache afanye anachotaka?”

“Kama nni hivyo angalau atafute watu wastaarabu kwa mfano maa yake Nasra hana shida , lakini wale wengine siwajui hata wanatokea wapi “

“Kama ni hivyo kwanini kama vile unataka miimi ndio niongee nae , kwanini usimfate na kumwambia kistaarabu wewe mwenyewe , isitoshe sisi ni wanafamilia na mama amestaarabika”

“Ninaogopa nitamfanya awe na hasira na mimi , siku za hivi karibuni amekuwa akinijali , lakini kama hutaki kunisaidia sahau kama nimeomba”Roma kuona mke wake anaomba kwa sauti ya kubembeleza alishindwa kumkatalia , ijapokuwa aliona sio jambo zuri yeye kuingilia , lakini anapaswa kufanya.

Siku iliofuata katika meza , wanafamilia wakiwa wanajipatia kifungua kinywa Roma aliona aweke wazi dukuduku la Edna mbele ya mama yake apate kulisikia.

“Mama , je unaweza kunisaidia kitu?”Aliongea Roma baada ya kufikiria gia ya kuanza nayo.

“Kitu gani unataka nikusaidie , unafikiria nini wewe toto korofi”Aliongea Blandina kwa furaha.

“Sio jambo kubwa , ni kwamba umekuwa ukialika watu kuja nyumbani kupiga soga na hata kucheza karata , nadhani sio jambo zuri kwa Lanlan, unaonaje ukiacha kuwaita?”Aliongea Roma.

Blandina ambaye alikuwa akibandua maganda ya yai la kuchemsha ailiweka chini ya sahani na tabasamu ambalo lipo kwenye uso wake lilipotea palepale .

“Roma mwanangu , je inakufanya ujisikie vibaya mimi mama yako kualika hao wanawake kuja hapa nyumbani?”

“Sijamaanisha hivyo, Mama yake Nasra yupo pia , siwwezi kusema ni jambo la aibu kwangu”Alijitetea na kummfanya Blandina kutoa tabasamu hafifu na kisha kugeuza macho yake kwa Edna .

“Najua likija swala la kustaarabika tabia na mengineyo wale wamama hawakufikii kwani hawajasoma kama ilivyo kwakko , hawajui hata taratibu za familia zenye kipato cha juu , labda kwa macho yen nyie watoto wa siku hizi , ni watu wa kupotezewa, lakini katika maisha yangu ndani ya miaka kadhaa iliopita nilijifunza mambo mengi wakati nazunguka katika nchi nyingi za Afrika kufuatilia maendeleo ya vito vya Yatima nilivyovianzisha katika kuomba taisi udhamini wa michango , nishawahi kukutana na aina ya wato wa aina zote , wakati nilipokuwa mdogo hata mimi vilevile niliona wamama kama hao wamekosa ustaarabu kwa namna ambavyo wanaongea kama wanafoka , namna wanavyokunywa vinywaji kama vile ni wanaume na kweli haipendezi kwa mwanamke”Alipozi kidogo na kisha akamwangalia Edna.

“Edna naamini hata wewe pia unawaona kama hawajastaariabika na tabia ao hazivumiliki si ndio?”

Edna ambaye alikwa akipeleka kikombe cha maziwa mdomoni alijikuta akiishia njiani na akikosa ujasiri wa kutoa jibu kwa kutingisha kichwa au kuitikia , lakini kwa Blandina ni kama alijuwa Edna asingemjibu.

“Katika vitu ambavyo nimejifunza , kamautalinganisha wanawake wenzangu ambao wameolewa katika familia za kitajiri na pengine kukulia katika familia hizo na hawa wa mtaani , wale wa kitajiri licha ya kwamba wamestaarabika na pia ni wasomi lakini wengi wao hawana moyo wa kusaidia ni kama sio binadamu na hili limenifanya niwachoke mno, wakati nikikaa na kubadilishana mawazo na wanawake wa kitajiri mara nyingi lazima nifikirie kile ambacho naongea …ninachotaka kumaanisha ni kwamba licha ya kwamba wamebarikiw vitu vingi ambavyo katika macho ya wengi ni vya kutamani lakini wengi wao ni wanafiki na maisha yao mengi ni ya kushindana na wivu , lakini ninapokuwa na hawa wa uswahilini wengi wao sio wanafiki na hawatangulizi hela na usomi wao kwenye kusaidiana mambo ya kijamii, mimi kwangu ni watu wazuri zaidi licha ya kwmaba nyie mnawaona kamasio wastaarabu , najisikia huru zaidi kuongea nao”Aliongea Blandina huku macho yake yote yakimwangalia Edna.

Katika meza yote ni kama aliekuwa akiongeleshwa ni Edna na sio mwingine na Edna mwenyeewe hakujuwa kwanini mama yake alikuwa akimwangalia yeye katika kuongea, lakini palepale alikisia kwamba huenda mama mkwe wake kashajua kwamba yeye alimtumia Roma kungea nae .

Upande wa Roma hakuwa ameelewa mamabo na isitoshe hata yeye hakujichanganya sana na watu wa kawaida katika makuzi yake na mahusianyo yake na jamii ni kitu ambacho hakukiweka akilini , lakini maneno alioongea mama yake yalimgusa.

“Hata mimi naunga mkono hoja , ijapokuwa kweli ni wa maisha ya chini na hawajastaaranbika wala kuwa na elimu ya juu lakini inaleta amani wakati wakuongea nao , mara nyingi nikifika sokoni wananichagamkia mno , wanawake wenye pesa na utajiri wengi wamejaa maringo”Aliongezea Bi Wema ambaye kila siku anawahi hapo kufanya usafi na kupata kifungua kinywa.

“Mama sio kwamba niliwadharau hao mashangazi ni kwamba nyumba inakuwa na makelele sana , kama itawezekana unaonaje mkatafta mahali pazuri kwa ajili ya maongezi”

“Roma najua hayo sio maneno yako , bali Edna ndio kakuambia unje uongee na mimi , si ndio?”

“Mama kwanini..”Roma alijikuta akikosa usemina kujiuliza mama yake amejuaje kuhusu hilo.

“Usishangae , ulivyorudi Tanzania uliweza kufanya kazi ya kubeba mizigo na kuishi maeneo ya uswahilini na familia za kawaida , kwanini uchukie wanawake wachache waliokuja nyumbani kunitembelea na kuongea kwa sauti , kama sio mke wako je ungelalamika?”

Ilileta mantiki , Roma ni kweli aliishi mazingira ya kawaida sana wakati alivyorudi Tanzania lakini hakuona tatizo kabisa na alifurahia maisha na kupta uzoefu mpya , alikula chakula hata kwenye migahawa ambayo usafci wake ulikuwa wa kubabaisha, sasa anakerwa vipi na wamama wanaopiga makelele na kucheka nyumbani kama sio Edna.

Edna mpaka hapo alionekana kabisa amekamatika., aliona mama yake alikuwa na pounti ya msingi kwa kile alichoongea.

“Edna kumtumia mumeo kama siraha ya kumshambulia mama mkwe wako sio jambo zuri”

“Mama .. sikumaanisha hiyyo.. “Edna alishindw akabisa kujitetea

“Edna je unaniona kama vile mtu ambaye naweza kufoka au kukasirika bila sababu , au mimi mama mkwe wako sijastaarabika , kuna haja gani ya kumtumia mume kuongea na mimi , unaweza kuniambia nyumba ina maekele sana na inamuathiri Lanlan, Au unaniogopa?”

“Hapana”

“Sisi ni wanafamilia , na unaweza kuongea chochote na mimi ambacho hakikuridhishi , kama niliweza kuruhusu wewe kuasili mtoto kwanini unaniona kama mtu ambaye naweza kukasirika bila sababu?”Aliongea kwa kufoka na kumfanya Edna machozi kuanza kujitengeneza kwenye macho yake na Roma aliona hilo.

“Mama acha sasa kumfokea na naahidi siwezi kuwa mjumbe wa Edna tena , anakuheshimu ndio maana alipatwa na wasiwasi kuongea na wewemoja kwa moja”

“Sawa nimeacha na nitakusikiliza ewe , isitoshe mkeo ndio mtu muhimu zaidi kwenye moyo wako”Aliongea Blandina na kisha akakaa kimya na kuchukua yai lake na kuendelea kulibabua maganda.

Roma alikosa usemi , alijikuta akimwangalia Edna na kisha akamgeungia na Bi Wema na kukosa cha kufanya , alitamani kuongea maneno machache ili kuweka hali hio sawa lakini alikosa ni neno gani la kuongea , lakini Bi Wema alimwangalia na kumuonyeshea tabasamu bila ya kuongea chochote.

Upande wa Lanlan hakujali malumbano hayo ya asubuhi kati ya bibi yake na mama yake , yeye kwanza hakuwa akisikiliza na isitoshe kiswahili kilimpiga chenga.

Baada ya kumaliza maziwa yote aliowekewa na mama yake kwenye kikombe , aligusha tumbo lake na kuona sasa limeshiba.

“Nanny !Lanlan want to go to the school”Aliongea akimwambiaQiang Xi kwamba anataka sasa kwenda shule.

Qiang xi alikuwa ashajiandaa , hivyo alichukua kijibegi cha rangi ya pingi chenye maua maua cha Lanlan na kumshika mkono naLanlan aliaga kwa furaha kwa kila mmoj.

“Tumekuwa kichekesho asubuhi asubuhi mbele ya mtoto”Aliongea Blandina mara baada ya kumwangalia Lkanlan akitokomea nje.

“Mama naahidi sitofanya hivyo tena , nisamehe nimekosea”Aliongea Edna

“Ulichokusudia ni sahihi , mama yako sikufikiria mara mbilimbili nilitii hisia zangu bila kuzingatia mnajisikiaje kama wanafamilia , lakini haikuwa sahihi kumfanya Roma ndio aongee na mimi kwaniaba yako , hivyo siku nyingine uniambie wewe mwenyewe sawa?”Aliongea na Edna alitingisha kichwa kukubali.

Muda huo huo gari lilisikika likisimama getini na kupiga honi , kwasababu nyumba ilikuwa kimya waliweza kusikia /

“Kuna kitu Lanlan kasahau?”Aliuliza Bi Wema maana Edna alikuwa ashambadilishia Lanlan utaratibu wa kwenda shule kwa kutumia gari ya shule na Qiang Xi ndio alikuwa na jukumu la kumpeleka na gari na kumrudisha.

“Ni gari nyingine , nadhani kuna tuna mgeni”Aliongea Roma na muda huo huo kengele ya ndani iligonga.

“Mh ni nani anakuja nyumbani asubuhi asubhi yote hii?”Aliongea Bi Wema kwa mshangao huku akinyanyuka kutokta nje kujua mgeni ni nani.
 
SEHEMU YA 545.

Bi Wema alienda mpaka getini na kufungua mlango na aliweza kukuta watu wawili wamesimama , wote wanaume , mmoja akiwa amevalia suti na mwingine akiwa amevalia mavazi ya kawaida , mwanaume alikuwa mzee miaka kama sabini hivi kupanda na mwngine alikuwa ni wa umri kama wa Roma

“Karibuni”Aliongea Bi Wema na palepale yule mwanaume mzee aligeuka, maana alikuwa akichunguza mazingira ya hilo eneo

“Kwa jina naitwa Kakolanya Masauni , ni CEO wa kampuni ya Beseli , je hii ni nyumba ya Edna Bosi wa kampuni ya Vexto?”Aliuliza yule mzee.

“Oh , kumbe ni wewe mmilikki wa maduka ya Beseli nishawahi kusikia jina lako mara nyingi , kipindi naanza kufika jiji la Dar sehemu niliokuwa naishi kulikuwa na duka lako , karibu sana hapa ndio nyumbani kwa Edna”Aliongea Bi Wema na Mzee Kakolanya , mzee flani hivi mwenye uchebe alimwangalia Bi Wema kwa dakika na kisha akaingia ndani ya geti.

“Karibuni ndani kabisa , Miss Edna yupo bado hajaenda kazini, mmekuwa na bahati leo kachelewa kutoka”

“Hapa hapa panatosha , hatuna hadhi ya kuingia ndani kabisa kwani tunahofia tusije pachafua , unaonaje ukimwita na akatoka ili tuongee nae?”Aliongea yule mzee na kwa kauli yake alionekana kabisa ana kinyongo , lakini Bi Wema hakuwa kwenye nafasi ya kuhoji.

“Edna mgeni aliefika ni Mzee Kakolanya , wapo hapa kwa ajili yako na wamekataa kuingia ndani na wanakuomba utoke”Aliongea Bi Wema na kumfanya Edna kushangaa.

“Waambie waondoke, sina sababu ya kuongea nao”Aliongea Edna kikauzu kama kawaida yake, lakini Blandina alionekana kulifahamu jina la Mzee Kakolanya.

“Ni Mr Kakolanya ,mmiliki wa maduka ya Beseli?”

“Mama unamfahamu?”Aliuliza Roma na kumfanya Blandina palepale kuweka mavazi yake sawa na kukunja sura baada ya kumwangalia Edna na jibu lake.

“Edna kwanini unaongea hivyo kwa wageni , namjua ndio na ni rafiki yetu wa muda mrefu mimi na Mama Issa , alikuwa akinijua kwa jina langu kabisa licha ya kutumia sura bandia”Aliongea Blandina na kumfanya Roma kushangaa.

Baada ya Blandina kutoka nje Mzee Kakolanya alijikuta akitoa macho kwa mshangao mara baada ya kumuona Blandina.

“Blandina , unafanya nini hapa?”Aliongea Mzee Kakonya huku akibadilika mwoneknao na kuweka wa kirafiki na Blandina alitabasamu na kumsogelea na kisha akampa mkono wa salamu

“Naishi hapa , ni kwa mtoto wangu na mke mwana”Aliongea huku akiweka sauti ya utani kidogo , lakini Mzee Kakolanya alikuwa ni mwenye mshangao,

Roma na Edna na wao waliweza kutoka nje , upande wa Roma alikuwa na hisia mbaya kwamba kuna kitu kingekwenda kutokea kutokana na taarifa aliopewa na Daudi mara baada ya kuona wafanyakazi wa kampuni ya Beseli kuandamana.

Upande wa Edna yeye hakuwa na furaha kwenye uso wake na aliishia kung’ata lipsi zake kwa wasiwasi , alikuwa akijua lazima angekutana nao lakini bado alikosa ujasiri kwani aliogopa mambo yangefikiaa pabaya.

Mzee Kakolanya mtu ambaye ameambatana nae alikuwa ni mtoto wake , mwenye rangi mchanganyiko hivi kama msomali , ilionekana amechanganya damu kwani Mzee Kakolanya alikuwa ni mweusi.

Upande wa Mzee Kakolanya alionekana kuanza kutetemeka mikono mara baada ya kumuona Edna na Roma wakitoka pamoja.

“Blandina , unachomaanisha ni kwamba Edna bosi wa kampuni ya Vexto ni mke wa mtoto wako?”

“Ndio Mr Kakolanya , je kuna sintofahamu kati yako na Edna?”

“Mh! ,Sintofahamu…!?”Aliongea huku akitoa tabasamu la kejeli, alionekana kuwa na hasira kweli na palepale alianza kukohoa mfululizo , ilionekana na hali yake ya afya haikuwa nzuri zaidi na mtoto wake alimshikilia asije akadondoka.

“Baba punguza hasira , nishakwambia tusije hapa kwa hali yako hii ya kiafya…”Aliongea mtoto wake akitaka kumshika mkono lakini baba yake alimzuia.

“Niko sawa , Madam Blandina , sikujua kama bosi wa kamupuni ya Vexto ni mke wa mtoto wako , lakini kwasababu nimefahamu leo nadhani maongezi yatakuwa rahisi kidogo”

“Mzee Kakolanya nakuheshimu kwasababu wewe ni mtu mzima na mtu ulienitangulia katika biashara , naomba mambo ya kazi tukayaongelee ofisini, sitaki maswala haya kuingiliana na mambo ya familia yangu”Aliongea Edna.

“Wewe binti hivi bado unaniona kama mtu mzima kwako? Ni kweli kabisa mimi nina umri mkubwa wa wewe kuwa mjukuu wangu , lakini je haya unayoafanya ndio heshima kwa watu waliokupita umri, umefanya mambo ya kifedhuli kwa siri halafu unataka niondoke hapa na kuja ofisini kwako , nilishatuma watu kibao kuja katika kampuni yako kuonana na wewe lakini waliishia kufukuzwa mara tu baada ya kufika eneo la mapokezi na nifanya maamuzi ya kuja mwenyewe nikaambiwa upo kwenye kikao siku nzima , kama nisingekuja hapa muda huu je ningeweza kukuona?”Blandina alijikuta akikosa ujasiri baada ya kumuona mtu mzima kukasirika.

“Edna nini kimetokea kwani, kwanini umemfanya mtu kama bosi Kakolanya kwa na hasira namna hii?”

“Mama ni maswala ambayo yanahusiana na kampuni na hapa ninapozungumza nishatuma mtu kutatua swala hili , hivo naomba uniamini na usiwe na wasiwasi”

“Najua ndio ni maswala ya kampuni lakini linahusiana na Boss Kakolanya , siwezi kukaa pembeni na kuangalia tu”

“Mama nadhani anachoongea Edna ni sahihi , kwanini tusimwache amalize yeye mwenyewe pasipo kuingilia?”

“Ingekuwa mtu mwingine ningekubali , lakini Boss Kakolanya licha ya kuwa na umri mkubwa lakini alikuwa rafiki yangu na alinishauri mambo mengi na ndio mtu wa kwanza ambaye alishiriki kwenye ujenzi wa kituo cha watoto Yatima kule Bagamoyo , yeye ndio alietoa pesa lakini sio hivyo tu alitusaidia kupata wafanyakazi ambao hatukuwalipa kiasi kikubwa cha pesa, tokea kumalizika kwa ujenzi hakuacha kuchangia licha ya kipindi flani maduka yake kupitia changamoto, unadhani imekuwaje akajijengea jina katika jamii?, ni kutokana na moyo wake wa kutoa na kusaidia , maisha yake yote faida aliopata alisaidia watu wenye uhitaji, Mzee Kakolanya ndio tafsiri sahihi ya mjasiriamali , ni mtu mpole sana lakini angalia yupo hapa asubuhi asubuhi kwenye nymba yetu akiwa amekasirika akisema Edna amemchezea mchezo mchafu bila yeye kujua siwezi kukaa nje ya hili”

Roma mara baada ya kusikia kauli ya mama yake alijikuta akishangaa , mwanaume huyo licha ya kwamba ni kweli amevalia suti lakini ni zile za mtumba kabisa na hakuonyesha dalili ya kuwa na pesa nyingi , mwonekano wake tu uliashilia kwamba alikuwa akiishi maisha ya kawaida

Wanasema ni sawa kwa binadamu kufanya wema angalau mara moja kwa siku au kwa mwezi hata kwa mwaka , lakini kufanya wema kwa maisha yake yote ni jambo ambalo sio la kawaida na aliona huenda ni mtu wa dini sana.

Mtu wa aina hio ilikuwa sahihi kwa mtu kama Blandina kumheshimu sana na kumsaidia pale anapohitaji msaada

“Blandina usiongee kama vile mimi ni mtu mwema sana , ni binadamu pia ninae kosea pia, ambayo nilifanya sio kutaka kuonekana mwema , ni jamboa mbalo nilipaswa kufanya kwasabu nisingezikwa na hela zangu. Leo nipo hapa kwa ajili ya kupata haki yangu, nataka CEO Edna kuomba msamaha na kufidia kwa kile alichofanya na kurudisha heshima yangu alioichafua”

“Edna nini kimetokea , niambie mama yako sasa hivi?”

“Mama kwasasa sina cha kusema”

“Wewe .. mtoto , ni tabia gani hio , wakubwa wanakuuliza na hilo ndio jibu lako?”

“Mama punguza jazba Edna atakuwa na sababu zake”Aliongea Roma akimtetea.

“Sababu!? , siwezi kuamini kama anasababu”Aliongea Blandina hakutaka kumwamini Edna , alimgeukia yule mtoto wa Mzee Kakolanya.

“Hashim wewe tuambie nini kimetokea”Aliongea Blandina , alionekana kumfahamu mtoto wa Mzee Kakolanya jina lake.

Hashim alimwangalia Edna kwa wasiwasi na kisha akamwangalia baba yake ambaye alimpa ishara ya kuelezea kilichotokea.

“Madam ipo hivi , kampuni ya Vexto ilitaka kununnua kampuni yetu lakini baba alikataa kuiuza , wiki iliopita kituo kimoja cha habari kikubwa nchini kilitoa taarifa kupitia akaunti zake za mtandao wa kijamii zikizungumzia bidhaa feki ambazo zinauzwa katika maduka yetu ya vyakula , na ushahidi ulionekana ni kweli bidhaa hizo kuwa feki na zimetoka kwetu, haikuishia hapo tu , kwenye mitandao ya kijamii kupitia wahamasishaji pia uvumi ulisambaa tena juu ya bidhaa hizo feki zina madhara kwa watumiaji , ni kwa kipindi kirefu mpaka sasa kampuni yetu ilikuwa ikiuza bidhaa za bei rahisi kwa wananchi wa hali za chini lakini zilikuwa za ubora wa hali ya juu na hicho ndio kinafanya maduka yetu mengi kuwa maarufu , taarifa hizo ambazo zinarudiwa mara kwa mara kwenye mitandao zimefanya wateja kutukimbia na sisi kukosa mzunguko wa pesa na benki mara baada ya kuona taarifa hio wanalazimisha tulipe malimbikizi yote ya madeni au tuuze kampuni, na pesa ya kulipa mara moja hatuna hivyo hakuna njia nyepesi kwetu”Aliongea Hashim.

“Kama una ushahidi naomba ukanishitaki na kama ushahidi huna na ni hisia tu naombeni muondoke”Aliongea Edna kikauzu kabisa , hakuwa akiyumbishwa wala nini na sura yake ilikuwa ni ile yenye macho ya kutisha ambayo siku zote inamwogopesha Roma licha ya ubabe wake.

“Ushahidi , Hahaha…. Mtu yoyote mwenye akili hana haja ya kuwa na ushahidi kwani ataweza kutabiri nani ambaye anasambaza uzushi kwenye vyombo vya habari na kulipa wahamasishaji wa mitandao kutuchafua , Mwaka uliopita uliweza kuinunua kampuni ya Mr Titu kwa njia zako hizi hizi na mwaka huu unataka kurudia kwangu , kama kweli unalenga kampuni yangu ndogo hapa nchini sasa nipo hapa, ongea na mimi bila ya kusita sita , niweke wazi , kwanini unakuwa mkatili?”

“Mr Kakolanya tafadhari punguza jazba , naomba niulizie kwanza huenda hili ni swala ambalo halihusiani kabisa na Edna”

“Blandina najua wewe ni mtu mzuri sana, lakini imekuwaje ukaja kuwa na mkwe muovu aina hii , hivi ushawahi kusikia jina lake la utani, anafahamika kama ‘Tandabui’ kwa wafanyabiashara wote wadogo wadogo , kila mwaka ananunua kampuni licha ya kujali ukubwa wake wala udogo wake”

Blandina alikuwa akitetemeka mikono na alijikuta akimsogelea Edna na kumkodolea macho

“Edna mtoto wangu niambie mama yako ukweli , nahitaji kujua kama ni wewe ulietoa maagizo ya chochote kilichotokea katika kampuni ya Beseli”

“Mama unafanya nini , kwnaini unamuuliza kwa kumkodolea macho hivyo , huoni inaumiza hisia zake?”

“Kwanini nisifanye hivi, kuna lolote ambalo limejjificha hapa, mtu anapaswa kuwa mkweli kwa kile anachoongea au alichokifanya , kama kweli hahusiki aseme hahusiki na sihitaji ushahidi wowote , nahitaji kumsikia mkwe wangu akiniambia kwamba hahusiki”

“Mama wewe unaonaje , je unafikiri nahusika katika hili kwa jinsi unavyonifahamu?”Aliongea Edna lakini Blandina alishindwa kutoa jibu kwani hakutegemea kuulizwa na yeye swali wakati ameuliza.

“Mke wangu… mpatie jibu analotaka usimuulize maswali?”

“Vipi kuhusu wewe , je unadhani nimehusika katika hili?”Aliuliza Edna huku akianza kukosa uvumilivu na kuanza kutoa machozi baada ya kumuonaRoma anashindwa kutoa jibu.

Ukweli Roma hakutaka kujibu kama anaamuamini au hamwamini , akikumbuka tukio la Hanson lilivyotokea aliamini ni mbinu zile zile za Edna.

Edna alifumba macho kwa dakika kadhaa huku akionyesha kama mtu aliejikatia tamaa na kisha akamwangalia Mzee Kakolanya na mtoto wake.

“Hakuna ushahidi wowote kama nimehusika na sijui ni jibu nini maana naona siaminiki , Mzee Kakolanya sina kingine cha kukuambia , nitakusubiri ofisini ufike usaini karatasi za makubaliano ya kampuni yako kununuliwa na kampuni yangu”Baada ya maneno hayo kutamkwa Roma na Blandina walijikuta wakikosa kabisa tumaini juu yake.

















SEHEMU YA 546.

Edna muonekano wake pamoja na sauti yake vilionyesha kutofanana na mwonekano wake , hakujali hata kujitetea yeye mwenyewe kutokana na kile kinachoongelewa , ijapokuwa hakukubali moja kwa moja kama anahusika majibu yake yalionyesha kila kitu.

“Kwa kauli yako ni sawa na kukubali ulichokifanya si ndio , ni kizazi gani hiki , kipindi cha nyuma ijapokuwa bosi wa kampuni ya Vexto alikuwa mwanamke lakini tabia yake ilikuwa ni ya kuigwa kwa wanawake wengi wa umri wake , alipanua msingi wa kampuni yeye mwenyewe na kila mtu ndani ya jiji hili alimkubali sana , nani angeweza kujua mrithi wake ni kama Simba mwenye njaa , kurarua na kuwinda kila kinachomvutia , unajua hata kitu kinachoitwa maadili ya kibiashara wewe?, umevuna hela za kutosha , unaishi kwenye jumba hili kubwa na una magari kibao ya kifahari lakini bado uanataka familia za kawaida kuteseka , huogopi hata laana zinatakzo kurudia?”

“CEO Kakolanya nakuheshimu sana kama mtu mzima , lakini sitaki kuona unamwingiza bibi yangu katika hili”

“Huna haki ya kunizuia na nitaongea , Blandina kuna athari nyingi zitatokea kwa maelfu ya wafanyakazi wangu , katika maisha yangu yote ya kibiashara hakuna siku tuliowahi kuuzia watu bidhaa feki , kuna zile ambazo tunatengeneza wenyewe na zile ambazo zinaingiza kutoka kwa kampuni nyingine lakini tulihakikisha ni zenyewe kwa vipimo sahihi ambavyo tulitumia miaka na miaka , Vexto bidhaa zao nyingi ninazozijua ni mavazi ambayo wanatengeneza na ni ya bei ghali sana kwa jamii za chini kumudu, kama kampuni ikinunuliwa kwangu mimi sio tatizo lakini kwa familia na wafanyakazi wangu waliofanya kazi miaka na miaka wanaenda kuteseka kwani wengi wao maisha yao yanategemea kile ambacho kinatoka katika kampuni yangu”Aliongea kwa huzuni na kumfanya Blandina kujawa na huruma.

“Edna kwanini kuwa mkatili hivi, kwanini usiache kampuni ya Beseli ikiendelea kuwa chini yao?”

“Thamani ya kampuni yao ni bilioni kumi na tatu, mimi nilienda kwao nikapendekeza kuinunua kwa bilioni kumi na tano, kiasi cha pesa ambacho ni kikubwa sana kulingana na thamani yao sokoni , kutokana na namna ya uendeshaji wa biashara wa mzee Kakolanya na falsafa yake ya kizamani , Idara ya Audit walifanya makadirio na majibu yaliotoka ni kwamba Beseli haiwezi kufikisha miaka miwili ijayo kabla ya kufilisika kwa kukosa mtaji kutokana na malimbikizo mengi ya madeni na biashara kujiendesha kihasara, mpaka ikifikia kipindi hicho hao wafanyakazi ambao anawatetea watajikuta wanaondoka mikono mitupu licha ya kufanya kazi muda mrefu , je sio sahihi kwasasa kuuza biashara na kupokea pesa ambao itakusaidia kuwapa wafanyakazi wako fidia na kutafuta uelekeo mwingine wa kimaisha?”

“Unajua nini wewe , ni zaidi ya miaka arobaini sasa tokea nilivyoanza kuendesha biashara , Beseli ni maisha yangu na roho yangu , unafikiri hela zinaweza kutatua shida zote , unadhani pesa zinaweza kubadilisha hisia za wanfanyakazi wangu waliofanya kazi na mimi kwa zaidi ya miongo kadhaa ? Unaweza kuwa tajiri na kuendelea kutukanyaga sisi wazee na kuendelea kupaa juu kitajiri lakini sikiliza Edna , hata kama Beseli ikafilisika kesho siwezi kukubali kampini yangu ikawa chini yako , siwezi kuuza roho yangu kwa shetani kama wewe”Aliongea na kumfanya Edna kutoa macho na kutoa tabasamu la kejeli.

“Vizuri sana , kwasababu umesema mwenyewe na upo tayari kushindana na mimi mwenye hela , ngoja tuone sasa , kama bilioni kumi na tano niliokutajia haitoshi naongeza mpaka Bilioni 20, tuone kama thamani ya roho yako inazidi thamani ya hio pesa”

“Nyamaza!!”

Ilikuwa ni kauli kutoka kwa Blandina na haikuwa kauli pekee yake , aliinua mkono kutaka kumchapa Edna kibao kwasababu alikuwa karibu yake , lakini mkono uliishia hewani akisita kufanya hivyo

Upande wa Roma mwenyewe hakuamini maneno alioyaskia yalikuwa yakitoka kwa Edba mke wake , yalikuwa ya kikatili mno na dharau juu kwa Mzee Kakolanya.

Katika sura ya huzuni na huruma , Blandina aliishia kutingisha kichwa chake kwa huzuni na machozi hayakuwa mbali pia.

“Kwanini unakuwa mkatili hivi , kwanini unaongea maneno ya kikatili hivi?”Edna hakujali hali ilivyo na muonekano wake ulikuwa ni kama kila kitu kinachoendelea hakimuhusu na hata Blandina alivyoinua mkono kutaka kumpiga kibao hakuhofia kabisa.

“Kipindi nilichokuona ukicheza na wale watoto m nilijiambia ijapokuwa ulionekana kuwa na ukauzu kwa nje lakini moyo wako ulikuwa ni wa moto na wewe ni mtu mzuri na mwenye ukarimu, lakini leo , umeyasambaratisha matumaini yangu yote niliokuwa nayo juu yako , Edna hivi unajua kwamba matendo yako sasa hivi ni kama kisu kinachochoma moyo wangu?”Aliongea na kujikuta akitetemeka mikono na palepale alimgeukia Mzee Kakolanya na kumwangalia kwa huzun.

“Naomba msahama kwako Mzee Kakolanya , sikutegemea mambo yanaweza kuwa hivi , msimamo wako ni sahihi , huwezi kuwatelekeza wafanyakazi wako wengi hivyo , usijali kabisa siwezi kumruhusu akaichukua kampuni yako”Baada ya kuongea hivyo alimgeukia Edna.

“Edna acha kuwa na tamaa na uache mara moja la sivo kwanzia leo mimi sio mama mkwe wako , sihitaji mkwe mwenye roho mbaya na ya kikatili kama wewe”

“Mama unachoongea sio sahihi na unaruhusu hasira kukutawala , mambo hajafika mbali hivyo?”Aliongea Roma

“Una matatizo gani wewe? , kwanini mpaka sasa unamkingia kifua licha ya kujua matendo yake , kama kweli anakuchukulia kama mume na mimi kama mama mkwe kwake unafikiri angekuwa na tabia hii”Edna baada ya kusikia maneno ya mama mwe alitoa kicheko cha karaha huku akimwangalia Mzee kakolanya na kisha akaongea kama vile anajiongelesha mwenyewe.

“Kama kampuni yako nisipoinunua mmi sidhani kama kuna mtu anaeweza kuinunua , upatikanaji wa kampuni yako lazima ukamilike hata kama unanipinga na siwezi kubadili msimamo wangu… na kama hutokubali basi naamini haikupangwa ,, isitoshe kiasi cha pesa nilichokutajia ni kama upendeleo na hakuna mfanyabiashara anaeweza kufanya hivyo ukilinganisha na madeni ya kampuni yako”

Baada ya kuongea hivyo alimwangalia Roma muonekano wake na kabla hajageuka kwenda ndani alitumia lugha ya kingereza.

“Mr Kakolanya , you may leave now , I welcome you to Vexto to sign the contract anytime”Akimaanisha kwamba anamkaribisha kwenye kampuni kusaini karatasi za mkataba muda wowote

Mzee Kakolanya alikuwa na hasira mno kiasi kwamba alianza kupumua kwa shida na kujikalia chini akionekana kama vile anakwenda kupoteza fahamu.

Blandina aliachana na maswala ya kuwa na hasira na Edna na kisha akamsogelea Mzee Kakolaya kwa ajili ya kumsaidia.

“Kwasasa achana na maswala ya kampunoi , mchukue baba yako na umpeleke hospitali , hali yake ikiendelea hivi inaweza kuwa mbaya zaidi”Aliongea Blandina akimpa maelekezo Hashim ambaye alitingisha kichwa haraka haraka na kumsaidia baba yake kusimama na kumtoa nje ya geti na baada ya kushuhudia gari aina ya IST waliokuja nayo ikitokomea , aliridi ndani na kumkuta Roma ambaye alikuwa amesimama kama gogo

“Roma acha ndoto za mchana, najua unashindwa kuamini kilichotokea sasa hivi lakini natamani kisiwe kweli , kwasasa jikaze na utafute suluhisho”

Roma alivuta pumzi nyingi na kuzishusha na kisha aligeuka na kurudi ndani.

Baada ya kufika ndani aliweza kumuona Bi Wema ambaye anazunguka huku na huko bila cha kufanya akionekana kuwa mwenye wasiwasi.

“Bi Wema Edna yuko wapi?”

“Kapandisha juu , sijui hata ni kipi anapanga kufanya , Mr Roma sijawahi kumuona Edna akionyesha upande huo kwa muda mrefu sana , imekuwaje mpaka mambo yakafikia hivi, muda si mrefu mambo yalikuwa na amani kabla ya kifungua kinywa lakini hil…”

“Usiwe na wasiwasi Bi Wema , nadhani ni kwasababu Edna hakuwa kwenye mudi nzuri ndio maana , tutaongea na hili litaisha”Aliongea lakini licha ya hivyo Bi Wema aliona hilo swala haliwezi kuwa rahisi maana alikuwa akimjua Edna , siku alioona muonekano huo mambo hayakuwa marahisi hata kidogo.

Baada ya muda mfupi Edna alishuka kutoka juu , lakini alikuwa akiburuza mabegi mawili makubwa huku begani akiwa na mkoba mkubwa wa rangi nyekundu lakini pia na makaratasi mkonini.

Muda huo Roma aliekuwa akifikiria kwanini mke wake aliongea vile alishitushwa na mwonekano wa Edna , na alijikuta akikosa uvumilivu.

“Edna , unajarinu kufanya ujinga gani?”

“Acha kunifokea , wewe ni nani kwangu mpaka unifokee”Aliongea kwa sauti ya makasiriko na kisha aliweka vitu vyake chini mbele yao wakiwa wanashangaa na kisha alichukua zile karatasi kwa mikono yote miwili .

Roma mara baada ya kuzipiga jicho palepale moyo wake ulimshituka.

“MARRIAGE CONTRACT’(MKATABA WA NDOA)

Edna hakujali mshituko wa Roma , alimuonyesha mama yake Roma ambaye dakika chache zilizopita alimkataa kwa kusema hawezi kukubali kuwa na mkwe mwenye Roho mbaya.

“Mlikuwa kwenye ndoa ya mkataba?”Aliuliza Blandina huku akiwa kwenye mshituko usio na kifani.

Upande wa Bi Wema alishangaa , lakini kilichomshangaza sio mkataba huo lakini maana ilionyuma ya Edna kuonyesha mkataba huo ambao kwa siku nyingi aliufanya siri hata kwa Blandina.

“Edna upo siriasi kweli wewe!?”Aliongea Roma huku kifua kikimpanda na kumshuka kwa hasira kali.

Mwanzoni alijua huenda ni kisirani tu na baada ya muda angetulia na hata yeye mwenyewe kufikia namna ya kumbembeleza lakini hakutegemea kama angefanya kitu cha kuumiza cha namna hio.

Kilichopo kwenye mkataba sio jambo kubwa licha ya kwamba lilikuwa ni la siri baina yao , lakini pia mkataba huo hauna maana kutokana na historia yao ya maisha tokea waishi pamoja , lakini tokea mwanzo waliweza kuwa na mahusiano kutokana na mkataba huo, hivyo sio wa kupuuzwa na alishangaa mpaka muda huo Edna hakuuchana kwani ulishaisha muda wake

Hivyo Maana halisi ya matendo ya Edna ndio ambacho kilimfanya Roma kuwa katika hasira kali sana na wasiwasi

“Ulikuwa unakosea sana , sijawahi kuwa siriasi na wewe..”Aliongea Edna huku akianza kulia na kufuta machozi kwa mkono na kisha akaendelea kuongea huku akitawaliwa na kilio cha kwikwi.

“Kipindi kile nilikuambia usome vipengele lakini uliniambia kwamba unajua kilichopo ndani ya mkataba , hivyo sasa hivi nataka nikuonyeshe vipengele vilivyopo , katika moja wapo ya kipengele kinasema ninaweza kuivunja hii ndoa muda wowote ninaotaka”Aliongea na kumfanya Roma kutoa cheko licha ya kwamba alikuwa na hasira.

“Kwahio unamaanisha kwamba unahitaji talaka?”

“Ndio , nishachoka mambo haya , sihitaji mwanaume ambaye haniamini , mwanaume ambaye anagawa hisia zake kila mahali anapojisikia , nitakuachia hii nyumba kama inavyoonyesha katika huu mkataba kama malipo ya kuuvunja , Na kwasasa ninaondoka mimi na wewe basi”

“Edna kwa jambo dogo kama hili unakimbilia kufanya mamuzi ya aina hii , umekuwa kichaa?”

“Nimekuambia usinifokee , siku zote mimi ni kigeugeu na mtu mbaya sana na zaidi ya yote pia mimi ni mwanamke kichaa , hivyo hata kama ukichaa wangu umezidi haikuhusu , hustahili hisia zangu”

Kuona wawili hao wakilumbana kutokana na hio karatasi , Blandina alikuwa na hasira kiasi kwamba pumzi zilianza kumuishia na miguu yake kukosa nguvu , kama sio Bi Wema huenda angedondoka

“Blandina punguza hasira , jamani nini hiki kinaendelea hapa..”Blandina hakuwa akijua namna ya kutuliza hio hali

“Nyie hebu nielezeni , hayo makaratasi maana yake nini, hivi nyie ndoa kwenu ni kichekesho si ndio ?”Aliuliza Blandina huku akianza kutoa machozi , hakuamini siku zote alikuwa akidanganywa kumbe ndoa ilikuwa feki.

“Nini kingine sasa, mnafikiri naweza kumpa mwanaume maisha yangu yote ambaye nimefahamiana nae kwa kosa la usiku mmoja?”

“Bado unapata ujasiri wa kunijibu vibaya , ukoo wa Roma unaweza kuwa na mkwe wa aina yoyote, awe masikini au tajiri lakini haihitaji mkwe ambaye ni tapeli , Vizuri sana , kwasababu unataka kuondoka basi unaweza kuondoka utakavyo lakini ulichovaa ukiache hapa hapa”Aliongea akinyooshea ile bangiri ya familia aliopewa na Afande Kweka.

“As you wish..(Kamaunavyotaka)”

Aliongea na kisha aliivua ile bangiri na kuikweka kwenye sofa na kisha alimwangalia mama mkwe wake kwa uonekano ambao hauelezeki na kisha akampita Roma na kutoka akiburuza mabegi yake kihasira hasira.

“Roma naomba umzuie .. tafadhari”Aliongea Bi Wema,

“Siwezi , kama mpango wake ni kuumiza moyo wangu siwezi kujilazimisha kwake pia , aondoke kama anataka kuondoka , ninaweza kupata kwa urahisi mwanamke ninaetaka muda wowote , kwanini ni mnyenyekee”

“Jamani jamani ..”Aliongea Bi Wema huku chozi la kiutu uzima likimtoka na alitoka nje kumkimbilia Edna na kabla hajaingiza mabegi kwenye garii alimzuia kwa mbele.

“Edna binti yangu , punguza hasira hapa ni nyumbani kwako unaenda wapi?”Aliongea na kumfanya Edna kufuta machozi

“Bi Wema huna haja ya kunizuia , ninaweza kukosa kila kitu katika maisha yangu lakini nimejaariwa pesa , nina weza kununua nyumba yoyote na kuishi mahali popote pale”

“Lakini huwezi kufanya hivyo , hebu fikiria imepita mwaka sasa na nusu , hata kama ndoa ilianzia na mkataba lakini tayari nyie ni mke na mume huwezi kuvunja mahusiano kirahisi hivi na kudai talaka”

“Lakini hata kama nikiendelea kubaki hapa nitawafanya kuwakosesha amani na kunishuku mara kwa mara, siwezi kuendelea”

“Vipi kuhusu mimi , nimekuona ukikua tokea ukiwa mdogo , unafikiri ninaweza kukuona ukiondoka hivi , vipi kuhusu Lanlan , akirudi asipo muona mama yake atafanya nini ndio kwanza amepata mzazi hivi majuzi tu kwanini unataka kumtelekeza tena?”Baada ya kusikia neno Lanlan kidogo alibadilika.

“Nitamfuata muda si mrefu nikipata pakuishi , akirudi mwambie tu mama amesafiri kwenda mbali kwa ajili ya kazi , Bi Wema niko vibaya sasa hivi , siwezi hata kujizuia mimi mwenyewe nitawezaje kumlea mtoto kwa hali hii … usijali tena mimi sio mtoto tena ninaweza kujihudimia mwenyewe, wewe unatakiwa kubaki ili kuendelea kuwa karibu na Rufi , maisha yake yalikuwa magumu hivyo siwezi kuondoka na wewe”

Bi Wema hakuwa na uwezo wa kumzuia tena , alichokifanya ni kumsihi amtajie sehemu atakayoishi baada ya kupata eneo na Edna hakuona haja ya kumkatalia, alimhakikishia angemwambia na kisha akaingiza vitu vyake kwenye gari na kuliwasha na kisha akaondoka.

Upande wa ndani Roma alijikuta akijikalia kwenye ngazi na bila ya kuelelewa na kisha akasimama na kwenda kukaa kwenye sofa karibu na mama yake na kumshika bega baada ya kumuona alikuwa akilia.

“Mama … I am sorry”

“Wewe mtoto bado unakuwa tu mjinga , huna haja ya kuniomba msamaha mimi , najua ulikubali kusaini hizo karatasi kwasababu ulimuonea huruma”Aliongea lakini Roma alitoa tabasamu la uchungu. Kama kawaida siku zote wamama lazima wafikirie mazuri ya watoto wao , maana ukweli alikuwa amefanya mambo mabaya sana kwa Edna lakini mpaka wakati huo anambebesha kila kitu Edna, lawama zote kadri iwezekanavyo.

Lakini kwa muda huu hakutaka tena kubaki upande wa Edna tena , ukatili na ukauzu wa Edna uliufanya moyo wake kuwa wa baridi muda huo na hata kufikia hatua ya kujiuliza kama bado alikuwa akiendelea kumpenda kama mke.

Jana tu walikuwa wakizungushana kitandani lakini asubihi hii ya leo mambo yamebadilika , aliona kabisa Edna ni mkatili sana zaidi hata anavyojiona yeye mwenyewe, angalau yeye hawezi kumfanyia mwanamke ukatili wa namna hio kama alivyomfanyia yeye.

“Mwanangu usiwe na hasira wala huzuni tena , kwasababu hakuridhishwa na yote uliomfanyia basi unapaswa kujijali wewe mweenyewe , wewe ndio mtoto mkubwa na tegemezi katika ukoo wa baba yako , una akili na umejaaliwa vitu vingi , naamini utapata mwanamke mzuri zaidi wa kuwa mkeo , kwa ushauri wangu nadhani Nasra au Amina mmojawapo anafaa kuwa mkeo , kama utakuwa tayari nitampigia babu yako simu na kumweleza kila kitu hata hivyo ni kitendo tu cha kubadiisha mkwe feki na kuweka halisi”

“Mama kila kitu ndio kimetokea muda huu huu kwanini unafikira mbali , Edna ameongea tu kwa mdomo lakini bado sisi ni mume na mke kisheria , hata hivyo hili swala la kampuni ya Beseli anaweza akawa hahusiki kabisa”

“Yaani licha ya kukuumiza , unamuongelea mazuri ?”

“Sio kwamba namsaidia wala kumuongelea mazuri , nina hasira tu na namna anavyochukulia mambo kirahisi kwa kutumia hisia m sitaki kuendelea na hii sintofahamu hata mimi”

“Yaani ashukuru tu kwamba nafahamiana na mama yake vizuri , lakini nisingeweza kumvumilia mpaka sasa , ni mtu gani hapendi kufokewa na kurekebishwa , najua amezaliwa akakuta kila kitu , laiti angejua mimi nilivyonyanyaswa nilivyoolewa na baba yako angekuwa na uvumilivu, maana hanifikii hata kidogo ,Jamani mwanamke gani hana heshima kwa wakubwa na hawezi hata kumjali mume wake”

“Mama acha kuongea sasa , ngoja kwanza nitokea mra moja”

“Unatoka kwenda wapi?”

“Nataka nimtafute Nasra kwanza ,anaweza kuniambia chochote kuhusu kampuni ya Beseli”

“Acha kudanganya Roma , unaenda kumtafuta na kuanza kumuomba msamaha si ndio?”Aliongea na kumfanya Roma kuona aibu kidogo.

“Haitokuja kutokea nikamuomba Edna tena msamaha, siwezi kujishusha kihivyo nina hadhi yangu pia”Aliongea.

Unadhani Edna kahusika na kilimchotokea Mzee Kakolanya , vipi watarudiana au Roma ataoa mke mwingine usikose
 
SEHEMU YA 547.

Roma mara baaada ya kumfariji kidogo mama yake alitoka na kwenda nyumbani kwa Nasra.

Baada tu ya kuingia ndani alimkuta Nasra ashajiandaa kwenda kazini na alishangazwa na namna Roma alivyoingia, kwani alionekana kuwa katiika haraka sana.

“Honey, mbona una haraka hivvo?”Aliuliza Nasra.

“Mama yupo wapi?”

“Mama yupo juu chumbani kwake”Alijibu Nasra na kumfanya Roma avute pumzi na kumwangalia Nasra kwa dakika..

“Unaonekana una wasiwasi , nini tatizo?”Aliuliza kwa mara ya pili mara baada ya kuona haongei kitu.

“Je umesikia kuhusu kampuni ya Beseli?”Aliuliza Roma moja kwa moja hakuona haja ya kuzunguka zunguka.

“Ndio , wafanyakazi wao walikuwa wakifanya maandamano nje ya kampuni yetu, Vipi kuna tatizo?”

“Nasra najua hujawahi kunidanganya na huwezi kunidanganya , hebu niambie ukweli , kuna mtu ambaye alikuwa akisambaza taarifa za uzushi kuhusu kampuni hio , je ni kampuni yetu ya Vexto?”Aliuliza Roma akiwa siriasi, lakini swali lake lilimshangaza.

Nasra alizunguka kuangalia nyuma akionekana kuwaza na kisha akamgeukia Roma.

“Honey , je unauliza kama Edna ndio kahusika si ndio?”

“Nadhani unaweza kusema hivyo…..”Aliongea huku akionyesha kukosa kujiamini moja kwa moja.

“Kama ni hivyo kwanini unauliza , Edna si yupo nyumbani kwanini usimuulize yeye?”

Roma baada ya kupigwa swali hilo hakuona haja kabisa ya kuficha ukweli wote , alielezea kila kitu ambacho kimetokea asubuhi hio namna ambavyo Mzee Kakolanya alivyofika nyumbani na wakaishia kwenye kutoelewana na Edna kuondoka.

Nasra alijikuta akiziba mdomo kwa mshangao na hakuishia hapo tu alianza kulia kwa kwikwi huku akianza kumpiga piga Roma na mkoba wake kifuani na Roma hakusogea hata inch na yeye alikuwa kwenye mshangao na alihitaji majibu pia.

“Umejiingiza kwenye matatizo makubwa , kwanini mlifanya hivyo , Edna mwenyewe anatia huruma tayari , lakini wewe na Mama yako mlishindwa vipi kumuamini na kusimama upande wake?”

“Nasra hebu acha kuwa hivyo , niambie nini kimetokea , kwanini unaona mimi ndio mkosaji?”

“Nilijua tu kuna kitu kinakwenda kutokea , lakini sikuwahi kuwaza mambo yanakwenda kuwa mabaya kiasi hiki”Aliongea kwa hasira.

“Nasra niambie bwana , unanifanya napatwa na wasiwasi zaidi…Niambie kama Edna ana husika au hahusiki?”Nasra alijikuta akivuta pumzi nyingi kabla ya kujibu.

“Edna hahusiki ndio , Mzee Kakolanya na bibi yake Edna walikuwa ni watu wenye uhusiano wa kibiashara na kwa ninavyojua Bibi yake Edna alishawishiwa na Mzee Kakolanya kutoa michango ya ufadhili kwenye kile kituo cha kulelea watoto kule Kiwanga wakati kinaanza, uhusiano huo mpaka leo hii Edna anauheshimu na ndio maana hata yeye anaendeleza kile alichoanzisha bibi yake ,ndio maana kila mwaka anatenga bajeti kubwa ya kusaidia wale watoto. Edna ana mheshimu sana Mzee Kakolanya unafikiri anaweza kumfanyia kitu cha namna hio, ni kweli kwamba kampuni yetu ilishatangaza nia ya kutaka kuinunua kampuni ya Beseli lakini je Edna anaweza kucheza mchezo wa kitoto namna hio ili tu kuipata , si kila mtu atamnyooshea vidole?”Aliuliza Najma na kumfanya Roma kweli ajilaumu kwanini hakufikiria hilo.

Edna siku zote alikuwa ni mwenye kutumia mipango madhuibuti sana anapotaka kitu na hawezi kufanya mchezo ambao atashitukiwa , katika mipango yote ambayo alifanya hata Roma yeye mwenyewe hakuwahi kugundua , sasa anawezaje kupanga mtego wa wazi namna hio.

“Kama ni hivyo nani anahusika?”Aliuliza na kumfanya Nasra kufuta machozi na kuvuta pumzi na kuzishusha.

“Baada ya taarifa hizo mbaya kusambaa mtandaoni na katika vyombo vya habari Edna alinipatia kazi ya kufanya uchunguzi na tuliweza kuhonga pia ili tu kujua ukweli..”

“Nani kahusika?”

“Hakuna mtu mwingine ambaye amefanya zaidi ya mtu mliekutana nae asubuhi hii , ni Hashimu mtoto wa kipekee wa Mzee Kakolanya”

“Hashimu mtoto wake?”Roma alijikuta akishangaa.

“Sahihi , mwanzoni baada ya kujua ukweli nilishindwa kujua sababu nini mpaka akaamua kufanya hivyo , lakini mara baada ya kumwambia Edna alinielezea sababu”

“Sababbu gani?”

“Alisema kwasasa jiji la Dar es salaam na maeneo ya karibu maendeleo yake yanakuwa kwa kasi , na ukuajji wake huenda sambamba na namna biashara nyingi na makampuni kubadilika na kutoa huduma kisasa zaidi , lakini kampuni ya Beseli wanafanya biashara bila kuzingaia nyakati na kwa staili hio miaka michache ijayo watafunga biashara kutokana na kutohimili ushindani wa soko , ni kampuni tu ya Vexto ambayo iliweka nia ya kununua Beseli na kuiboresha baadhi yitu ndani ya mfumo wao wa kibiashara , sasa Mzee Kakolanya aligoma kuuza kampuni, hivyo moja kwa moja ni kwamba kampuni yake muda wowote itafilisika. Anaichukulia kampuni yake kama maisha yake na roho yake lakini kwa mtoto wake Hashim ni tofauti , alijua kabisa baba yake hawezi kuuza kampuni kwa namna yoyote ile licha ya kwamba inajiendesha kihasara hivyo hakutaka kuona biashara inakufa ilihali kuna kampuni ambayo inataka kutoa zaidi ya bilioni 15 kuinunua , thamani ambayo ni kubwa zaidi kuliko uhalisia wa biashara yao, hivyo akatengeneza mbinu ya kumfosi baba yake kuuza hata kama hataki…”

“Kwahio unamaanisha kwamba kwasababu Hashim anataka kurithi mali za baba yake kabla hazijafilisika , hivyo akawasiliana na waandishi wa habari kwa siri na kuweka biadhaa feki dukani, huku akiamini hakuna mtu ambaye anaweza kumshitukia kwasababu ni mwanafamilia , si ndio?”

“Ni kweli , tena hata kama Mzee Kakolanya mwenyewe angefanya utafiti kidogo kujua chanzo cha tatizo angefahamu Edna hahusiki , hivyo hata kwasasa ni sisi pekee ndani ya kampuni tunaujua ukweli na sasa na wewe ndio nakuambia”

“Babe Nasra haya ulioniambia ni kweli?”

“Kwahio huniamini hata mimi , ni lini mimi Nasra nikakudanganya?”

“Hapana sio hivyo, inanishangaza kama Edna alikuwa akijua ukweli muhusika ni Hashim kwanini hakuelezea na kujitetea , kama angeongea na akakuita wewe ukawa kama shahidi , mimi na mama tusingefikia hatua ya kumshuku na yote haya yasingetokea”

“Ndio maana nikakuambia namuonea Edna huruma..”

“Unamaanisha nini?”

“Wewe haukuona mwenyewe hali ya kiafya ya Mzee Kakolanya sio nzuri, miaka ya hivi karibuni afya yake haikuwa nzuri kabisa , huenda ni kutokana na uzee na alishauriwa kujizuia na maswala ambayo yanaweza kupandisha presha yake na kumpelekea kupata kiharusi”Roma alitingisha kichwa kukubali kwani ni kweli hali ya kiafya ya Mzee Kakolanya haikuwa nzuri na hata walivyoondoka Hashim alimpeleka hospitalini.

“Hii ndio sababu ambayo inanifanya namkubali Edna, nilitaka kutoa tangazo rasmi kuhabarisha watu kwamba kampuni ya Vexto haihusiki na mhusika ni Hashim aliehonga waandishi wa habari na wahamasishaji wa mitandao , lakini Edna alinizuia kufanya hivyo kwa kuniambia Mzee Kakolanya afya yake sio nzuri na kwa jinsi ambavyo anampenda mtoto wake na kujisifia mbele za watu kwa kumtangaza kama mrithi habari hio kama ingemfikia moja kwa moja ingempelekea hata kupatwa na mshituko wa moyo na hata kama asipatwe na tatizo moja kwa moja angejiona kama baba aliefelisha wafanyakazi wake wanaomuamini… kama wewe ni mzazi ungejisikiaje pale mtoto wako akienda kinyume na kile unachoamini , moja kwa moja ungeumia sana hivyo ingepelekea presha kupanda sana na hata kupoteza maisha kwa mshituko”

Roma mara baada ya kusikia maelezo hayo alijikuta moyo wake ukiuma na kujikatia tamaa kabisa.

“Hakutaka kujitetea yeye mwenyewe kwa kumtaja muhusika kwasababu alihofia afya ya mzee Kakolanya?”Alijikuta akibwabwaba.

Roma alijiambia inawezekanaje huyu mwanamke akafanya kitu kama hiki kwa mtu ambaye hana hata undugu nae na kufanya yeye mwenyewe kuonekana ndio mtu mbaya.

Roma alijikuta kichwa chake kikitaka kumpasuka , alikumbuka muda ambao mke wake akimwangalia kwa macho ya kumkatia tamaa na muonekano ule ulimfanya kujihisi pumzi kumuishia.

“Haikuwa rahisi kwa Edna pia , kuvuja kwa habari ile kulichafua sana taswira ya kampuni na hata wafanyakazi kuanza kumsema vibaya , lakini licha ya yote hayo aliniambia nisiongee kitu kwa kuhofia namna ambavyo mzee Kakolanya angelichukulia swala hilo”Aligongea msumari Nasra na kumfanya Roma kutoa kicheko huku akijidharau yeye mwenyewe.

“Kama ni hivyo kwanini asingeniambia hata kwa siri kwamba hahusiki na isitoshe alikuwa akiongea kijeuri sana na kauli zake hakuna ambaye angemwamini kama hahusiki”

“Ni kwasababu ya hasira , inaonyesha sio mara ya kwanza kutokumuamini ndio maana, kwa yale ambayo unaendelea kufanya na yeye kuendelea kukuvumilia kwanini ulishindwa kumuamini , hata kama ni mimi ningekuwa kama Edna tu , Roma wewe ndio mtu wa pekee ambaye hukupaswa kumtilia shaka mkeo”

“Kwanini unanifanya mimi ndio nionekane kama nina makosa , kama asingefanya mambo mengi bila mimi kujua kwa wafanyabiashara wenzake mambo yasingekuwa magumu kwangu na isitoshe hili lililotokea ni kama vile ana uwezo wa kulifanya , siku zote anaamini mambo ya hisia na mapenzi yasiingiliane na biashara zake , ninaweza vipi kujua kuhusu hili, nilimuuliza kwa kumpigia simu lakini hakunitolea maelezo na kunikatia simu , mimi ninakosa gani?”Roma alijikuta akimgeukia Nasra na kuanza kumfokea yeye.

“Wewe..!”Nasra alimnyooshea kidole mara baada ya kuona anafokewa.

“Hivyo ndio ilivyo”Sauti kutoka juu ilisikika ,ilikuwa ni ya mama yake na Nasra

“Umekuja asubuhi asubuhi , kwanini usiongee vizuri tofauti ya kufoka , haraka za nini?”Aliongea na kumfanya Roma kuona aibu maana siku zote mama yake Nasra hakuwa akimpenda sana .

“Mama ni kwasababu ya wasiwasi?”

“Nimesikia kila kitu , najua mimi sio msomi na sijastaarabika kama wanawake wengine , lakini ninachoamini mkiwa familia hakuna fundo ambalo mtashindwa kufungua , baba yangu enzi zake alipenda kuniambia, Shida humalizwa na aliezisababisha , isitoshe katika sintofahamu zote zinazotokea katika mahusiano , mwanaume ndio anaepaswa kuwa mkirimu , jaribu kupiga hatua moja nyuma utagundua wewe ndio mkosaji na Edna hana makosa,hebu jaribu kujishusha japo kidogo”Aliongea Mama yake Nasra maneno ya busara.

“Ni kweli anachoongea , Mpenzi hebu kwa haraka mtafute Edna , atakuwa analia akiwa mwenyewe sasa hivi”Aliongea Nasra.

“Wewe ndio wa kuniambia hivyo , nikajua ungefurahi kama tungepeana talaka”Aliongea Roma na kumfanya Nasra kumfinya.

“Unaongea nini , siwezi siwezi kabisa kuyachukulia matatizo yako na Edna kuwa faida kwangu”Aliongea kwa msisitizo.

“Nilikuwa natania , sijui hata namna ya kwenda kuongea nae kwasasa , siku zote nimekuwa mwenye kuomba msamaha , siwezi kujishushia thamani yangu yote kwasasa”

“Kama ni hivyo nadhani usubirie angalau siku hata chache zipite , subiri Edna akipunguza hasira zake ndio umuombe msamaha yaishe”Roma alifikiria kidogo na kuona Nasra anapointi na muda huo huo aliona akamwambie na mama yake mzazi kilichokuwa kikiendelea.

“Nasra kwa siku hizi chache nilizomfahamu, nadhani haiwezi kuwa rahisi kutulia na kurudi nyumbani”

“Ndio mama hata mimi najua , lakini kwanini unasema hivyo , una wazo lolote?”

“Acha kuwa mjinga wewe mtoto , ninachokuambia ni kuwa karibu na Blandina ujenge ukaribu nae ,unaweza kumsaidia kufanya kazi za ndani au kuongea nae chochote tu cha kumfurahisha lakini usionyeshe ishara ya kujipendekeza”

“Mama najua unachotaka kumaanisha lakni unanifanya niwe mtu mbaya sasa , wewe ni sasa hivi tu ulikuwa ukimshauri Roma kwenda kumtafuta mke wake wayamalize , kwanini unani…”

“Oh , Nasra mtoto wangu , unadhani ni kipi ningepeaswa kumwambia, si nitaonekana mnafiki , kumuacha aende akamtafute mke wake ni kumfanya aone kwamba na sisi tunajali lakini Roma na Eda mpango wao ni kupeana talaka, kwa maoni yangu unafaa sana kumrithi Edna nafasi yake”

“Mama kwanini unasema hivyo , sijawahi kuwaza kumuondoa Edna katika nafasi yake , na isitoshe kwanini nimsaliti katika kipindi hiki ambacho ana hasira , nishamsaliti mwanzo na siwezi kurudia , na isitoshe wewe mwenyewe umenifundisha kuwa na shukrani”

“Nasra huelewi kitu wewe , kama ilivyo kwa Blandina kutopenda mtoto wake kuteseka na mimi pia siwezi kuona ukiteseka , unafikiri napenda wewe kuendelea kuwa mchepuko maisha yako yote, hata kama anaweza akakujali kwa kila kitu na kukupatia kila kitu lakini bado ni huzuni kwani huwezi kutambulika kama mke wake bali mchepuko tu , lakini kwasababu ulichukua hatua ya kwanza ya kukubali kuwa mchepuko , kwanini usipige nyingine mbele kwa kujifanyisha mjinga , sio swala kubwa hata hivyo”Aliongea na Nasra alijikuta akinuna.

“Mama sitaki kusikiliza maneno yako tena , kama utaendelea hivi nitakasirika , Hata hivyo naenda kazini maana nimechelewa”Aliongea na kisha alichukua mkoba na funguo ya gari na akaondoka.

“Mtoto mjinga kama nini , hata kama mama yako nitaonekana mbaya lakini nakushauri hivyo kwa faida yako”Alijiongelesha yeye mwenyewe.

********

Roma mara baada ya kufika nyumbani alikaa chini na kumweleza mama yake kila kitu.

Blandina mara baada ya kusikia ukweli , mwonekano wake ulibadilika na kuwa ni wenye kujutia na kujilaumu lakini kwa wakati mmoja akiwa na hali ya kutoridhika pamojana hasira na kujikuta akijichokea kabisa.

“Sikutegemea mambo yanaweza kuwa hivi , nimemkosea Edna , Roma naomba unisamehe mama yako”Aliongea huku akimshika mikono Roma.

“Kuna kipi cha kuomba msamaha mama , mimi pia nina makosa , ninachoweza kusema ni kwamba mpaka sasa sijawahi kumwelewa Edna kama nilivyofikiria, Mama usjilaumu sana nishafikiria ninachokwenda kukifanya, ni kumuomba Edna tu msamaha baada ya siku chache na naamini kila kitu kitarudi kama mwanzo”

“Lakini nyie wawili si ndoa yenu ilikuwa ya mkataba na sasa ulishaisha?, Kwa maneno yake inanifanya nipatwe na wasiwasi , itakuwaje kama akikataa kuendelea na maswala ya ndoa , maana haki hio anayo , kama mkataba wenu ni wa miezi sita na umeisha inamaana yupo huru na anaweza kukataa kurudiana na wewe”

“Hawezi kufanya mambo kwa kujiamulia tu kirahisi , kwani yeye mwenyewe ndio aliekubali tuoane mara ya pili baada ya mkataba kuisha , nashindwa hata kujua kwanini bado anayo yale makaratasi, lakini hata hivyo Edna siwezi kumpa talaka labda sio mimi”Aliongea akiwa siriasi na kumfanya Blandina kushitushwa kidogo na msimamo wake.

“Kwahio unachomaanisha , Edna ndio atakuwa mke wako milele na hakuna mwingine anaeweza kuwa mkeo?”

“Mama nimepitia mengi katika maisha yangu na mpaka sasa najua ni yupi kwenye maisha yangu siwezi kumuacha , na isitoshe ndoa yetu inafahamika kwa watu wengi , hatuwezi kupeana tu talaka , itaathiri taswira yake pia”Aliongea na kumfanya Blandina kutingisha kichwa chake bila ya kuongea neno .

Roma baada ya kuona nyumba ipo kimya na hana cha kufanya alifanya maamuzi ya kwenda ofisini kwake.

Baada ya Blandina kufikiria kwa muda , akiwa nje ya bustani alirudi ndani na kuchukua simu yake na palepale alitafuta namba ya Afande Kweka.

Afande Kweka licha ya mpango wake wa kuishi Iringa moja kwa moja , lakini kutokana na baridi kali alirudi kwanza katika nyumba yake ya Dar es salaam.

Tokea Zenzhei kuondoka maisha yake yalikuwa ya upweke na aliishia kuota jua na kutengeneza bustani kuzunguka numba yake na muda huo wakati akinyweshea maua , mfanyakazi alitoka akiwa ameshikilia simu yake na kumwambia inaita na alipoangalia anaepiga ni Blandina alishangaa kidogo kiutu uzima na kisha akapokea na kuweka sikioni.

Baada ya salamu Blandina alienda moja kwa moja kwenye swala ambalo limemfanya kumpigia mzee huyo.

“Baba.. nadhani unapaswa kujua kinachoendelea huku nyumbann..”

“Niambie ni nini , unaonekana kuwa na wasiwasi”Aliongea na palepale alionekana Afande Kweka akisikiliza kwa muda na kisha akavuta pumzi na kuzishusha.

“Nimekuelewa , lakini ni swala ambalo hupaswi kuwa na wasiwasi na isitoshe sio kwamba limesambaa ,sisi pekee ndio tunafahamu kuhusu hilo, mkataba huo mpaka sasa hauna kazi kwani ulishaisha , kinachofanya kazi kwasasa ni vyeti vyao vya ndoa na harusi waliofanya , Edna ana hasira kwa sasa ndio maana kaamua kuondoka , kwangu sioni tatizo”Aliongea

“Lakini baba , kinachoniuma ni namna Edna anavyomchukulia mume wake”Alilalamika Blandina kwenye simu.

“Kwani Roma mwenyewe anasemaje?”

“Amesema anaenda kuomba msamaha , nashindwa hata kumuelewa,kwenye vitu vingine ni jasiri lakini likija swala la mke wake anakuwa muoga, tayari anao wengine lakini kwanini mawazo yake yote yapo kwa mwanamke mmoja tu”

“Hahaha…ni jambo zuri, hilo linatuonyesha kwamba ana kanuni zake mwenyewe kama mwanaume, maisha yake yote amekulia nje ya nchi na damu yake imejaa dhambi na uzoefu wa wanawake nadhani anajua nini anachokifanya, kwasasa wewe usiingilie mahusiano yao na kaa mbali , unatakiwa kuelewa wewe huwezi kuishi nae milele , majukumu yako kama mzazi yanahamia asmi kwa mke wake”Aliongea na kumfanya Blandina upande wa pili kunyamaza na kuishia kuitikia, kwani alichoongea mzee huyo ni jambo sahihi.

Blandina na Afande kweka mara baada ya kufanya sherehe ya kimila Songea uhusiano wao uliimarika mno , kwani mzee huyo alitumia nafasi kumuomba msamaha kwa yale yaliotokea miaka ya nyuma na ndio ambaye alimwambia akae karibu na Roma na Edna ili kumpa kila taarifa ya kinachoendelea.

Alionekana kuendelea kuongea nae na muda ambao anamaliza kuongea na simu ndio muda geti la nyumba yake lilifunguliwa na gari aina ya Range Rover sport nyeusi kuingia na kwenda kuegesha katika maegesho ya muda mfupi.

Muda huo huo mwanaume wa kizungu wa makamo alievalia suti , alitoka katika gari hio na kuzunguka upande wa dereva na kisha akafungua mlango na alionekana mzee wa kizungu mwenye kichwa chenye uwalalaza akitoka , huku mkononi akiwa anatumia mkongojo.Alikuwa si mwingine bali ni Paster Cohen.

Muda mchache tu Afande Kweka aliekuwa upande wa pili alisogelewa tena na kijakazi na kumwambia kuna mgeni na Afande Kwaka hakuuliza mgeni huyo ni nani zaidi ya kutoa tabasamu hafifu la kizee na kumwambia anakuja na amkaribishe mgeni ndani kwa kumkirimu..









SEHEMU YA 648.

Roma aliweza kurudi kazini muda wa jioni saa kumi , wakati akiwa ofisini alitamani kwenda kumtafuta Edna lakini aliona asifanye hivyo kwani angefanya mambo yawe mabaya zaidi.

Baada ya kuingia ndani aliweza kukutana na Bi Wema ambaye alionekana alikuwa akitoka huku mkononi akiwa ameshikilia mabegi.

“Bi wema unasafiri kwenda wapi?”

“Siendi popote , haya ni mabegi ya Edna, kuna baadhi ya vitu vyake hakuchukua hivyo nampelekea”

“Ni sehemu gani kahamia?”Aliuliza Roma kwa shauku na kumfanya Bi Wema kutabasamu.

“Usijali Mr, Kabahatisha nyumba eneo la Msasani ni pazuri na kuna ulinzi wa kutosha”Aliongea na Roma alitingisha kichwa kuelewa, ijapokuwa kwa wakati mmoja alishangaa maana kwa muda mchache aliokaa Tanzania alipata kujua ilikuwa ngumu kupata nyumba kwa haraka kwa eneo kama Msasani , lakini aliamini huenda hela ndio imefanya kazi.

Bi Wema alimpatia anuani ya nyumba hio bila kinyongo na kisha akaondoka , upande wa Roma hakuona haja ya kwenda siku hio hio , alipanga wikiend ndio ataenda kujaribu kuongea nae.

Alitembea kivivu na kjibwaga kwenye sofa na kisha akawasha runinga na na ni kama TV ilikuwa ikimsubiria kwani taarifa iliokuwa ikitangazwa ni Kampuni ya Vexto kununua kampuni ya Beseli kwa kiasi kikibwa cha pesa.

Ilionekana licha ya kwamba Edna alikuwa na mawazo , lakini alikuwa na uwezo wa kuendesha kampuni bila shida yoyote.

Muda huo huo aliweza kusikia mngurumo wa gari ukiingia ndani na ilichukua kama dakika tano tu Qiang Xi alieongozana na Lanlan walifika , Lanlan mkononi akiwa ameshikilia Sosejiu(Sausage) huku mlezi wake akiwa amembebea begi.

Kwa jinsi midomo yake ilivyokuwa na mafuta alionyesha njia nzima alikuwa anakula.

Edna mara alitoa pesa nyingi sana na kumkabidhi Qiang Xi kwa ajili ya matumizi ya Lanlan akiwa shuleni.

Roma mara baada ya kumuona Lanan alijikuta moyo wake ukipata joto na angalau wasiwasi aliokuuwa nao ukapungua, ni kama vile Lanlan alimpa tumaini kwamba Edna hawezi kwenda mbali kwani tayari wana mtoto.

“Chubi njoo umpe baba yako kumbatio haraka”Aliongea Roma kwa kingereza lakini Lanan kama kawaida hakupenda kuitwa Chubi lakini alimrukia baba yake na kumkumbatia na Roma alishika mashavu yake yaliojaa nyama kwa siha nzuri.

“Daddy , mama yuko wapi?”Aliuliza na kumfanya Roma kushituka kwa swali hilo.

“Mama yako kaenda sehemu ya mbali na hatorudi hivi karibuni”Aliongea Roma na kumfanya Qiang kuvuta pumzi na kuzishusha , alikuwa ashaambiwa na Bi Wema kilichotokea kabla ya kurudi.

“Je mama kaondoka kwasababu ya utundu wangu?”

“Muangaliena ujinga wake , wewe ni mtoto mtiifu sana kwa mama yako na hawezi kukutelekeza sawa?”Aliongea huku akitabasamu.

“Lakini mama mara ya mwisho alisema hivyo hivyo , anaenda sehemu ya mbali na hakurudi kwa muda mrefu , sasa hivi nimempata sitaki kumpoteza tena”Aliongea Lanlan , ilionekana alikuwa akimzunguzia mama yake kabla ya Edna.

Kauli yake ilimfanya moyo wa Roma kuongeza spidi ya kusukuma damu na kuona huzuni kwa mtoto mdogo kama huyu asiejua chochote zaidi ya kula kuwa na matumaini hayo.

“Hapana mama hawezi kukuacha tena , naahidi atarudi ndani ya muda mfupi tu , tupinge”Aliongea Roma na Lanlan alinyoosha kidole chake cha mwisho na kupitisha kwenye kidole cha baba yake kwa furaha.

Wanasema hali za kimawazo ya mtoto hubadilika kwa haraka zaidi , licha ya mwanzo kuonyesha wasiwasi lakini baada ya kuahidiwa mama anarudi tayari furaha imerudi na kuendeea kutafuna Soseji yake.

Muda huo huo na Blandina alishuka kutoka juu na alijikuta akipata ahueni mara baada ya kuona baba na mwana wanaendana vizuri.

“Lanlan kuwa mtoto mzuri , njoo unikumbatie bibi yako”Aliongea Blandina na Lanlan hakuleta ubishi alimsogelea Blandina na kumkumbatia.

Baada ya muda Blandina alianzisha maongezi na Roma na alimwambia kwamba anaondoka kuelekea nchini Kenya na baada ya hapo angeenda Afrika ya kusini na kukaa kwa muda kufuatiia baadhi ya biashara zake”

Roma alishangazwa na taarifa huo na kujaribu kumtoa hofu mama yake kwamba asijilaumu kwa kile kilichotokea kwani yeye ndio mwenye makosa , lakini Blandina alimwambia safari hio alishapanga muda mrefu na anapaswa kwenda kwani ni muda mrefu tokea atoke kwenye nchi ya Kenya bila ya kuweka baadhi ya vitu sawa.

Roma mara baada ya kuona mama yake anasisitiza hakutaka kumzuia na Blandina aliongea na mtoto wake mambo mengi na mwishowe kabisa akampatia ile Bangiri na kumwambia ampatie Edna na kumuombea msamaha kwa kile kilichotokea , huku akimuachia Roma maneno ya kumwambia Edna watakapokutana.

Siku hio hio Roma alipigiwa simu na Afande Kweka na kumwambia anaagiza mtu kuja kumchukua mjukuu wake Lanlan kwa muda mpaka mambo yake yatakapokaa sawa, hakushangazwa na taarifa hio kwasababu mama yake alishampasha habari kwamba aliongea na babu yake.

Roma na yeye hakukataa , alimruhusu Lanlan kundoka pamoja na iang Xi, aliona ni kheri akae na Afande Kweka kwanza mpaka atakapoweka mambo yake sawa.

Siku nzima Roma alibakia nyumbani na hata siku ya pili yake mara baada ya mama yake kuondoka alienda kazini na kama kawaida baada ya kumaliza kucheza gemu alirudi nyumbani kulala.

Hata hamu ya kutembelea warembo wake hakuwa nayo tena , hivyo aliishia kukaa nyumbani peke yake maana hata Bi Wema alimruhusu kukaa tu nyumbani na Rufi na asisumbuke kuja kumsaidia kupika.

Ulikuwa uzoefu wa aina yake , kipindi mahusiano yake na Edna yakiwa imara alikuwa akipenda kutembelea michepuko yake kwa kasi kama zote , lakini muda hui ambao ameondoka alikosa kabisa hamu nao.

Siku tatu zlipita bila ya kuonana na Edna , alikuwa amemkumbuka mno na kutamani kumuona.

Kwasababu alipanga wikiend ndio aende anapoishi kuonana nae na siku hio ilikuwa Jumamosi basi kulivyokucha tu hakutaka kufanya chochote , hata kifungua kinywa hakufikiria zaidi ya kudamka kwenda anapoishi Edna.

Alikuwa amekadiria muda kutoka eneo hilo kwa gari mpaka Msasani ingemchukua dakika kadhaa , alipiga na mahesabu ya muda ambao Edna huamka na kuanza taratibu zingine na kuona saa nzuiri ya kufika ni saa mbili kamili.

Roma mara baada ya kuendesha gari kwa nusu saa hatimae aliweza kufika katika anuani husika na aliweza kuegesha gari kwenye geti na kisha akabonyeza kengele ya geti na mlango uliweza kufunguliwa na mlizi wa moja wapo ya kampuni ya ulinzi maarufu ndani ya jiji la Dar Es salaam.

Jumba ambalo amenunu ilikuwa kubwa mno , lilikuwa na ukukubwa wa mita 400 za mraba na ghorofa moja kwenda juu na hata Roma mwenyewe mara baada ya kufika nje ya jumba hilo alishangaa na kujiuliza ni mtu gani aliekuwa akiishi hapo ndani na kuja kumuuzia Edna kwani nyumba ilikuwa mpya na madhari yake ni nzuri mno, ila hakutaka kushangaa Edna alikuwa ni mtu mwenye pesa na ilikuwa ni hivyo tu nyumba ya Oysterbay ilikuwa imepangishwa na kigogo wa serikali huenda angerudi kuishi hapo.

Edna asubuhi hio alikuwa bado na mavazi yake ya kulalia , kwa jinsi macho yale yaivyoonekana , ilionyesha hakupata usingizi wa kutosha .

Baada ya kusikia Kengele kutoka getini alisogea mpaka kwenye mlango na kuangalia Skrini maalumu, alimwangalia Roma kwa muonekano usiolezeka huku akionyesha kama vile hakuwa akimfahamu.

Baada ya kusimama kwa muda kidogo alitoa maagizo kwenda kwa walinzi asiruhusiwe kuingia kwani hamjui na baada ya hapo alitembea kuzifuata ngazi na kupandisha juu.

Roma huku nje mara baada ya kuambiwa na walinzi haruhusiwi kuingia kwani mwenye nyumba hamfahamu alikunja ndita na alifikiria kidogo kisha akondoka mbele ya geti na kuanza kuangaia jengo hilo kwa nje akiwa upande wa nyuma, baada ya kuangalia kulia na kushoto hakukuwa na mtu palepale alipotea alipokuwa amesimama na alikija kuibukia kwenye balkoni.

Baada ya kuifikia Balkoni kabla hata hajafungua mlango kuingia ndani , Edna alitokea mbele yake huku akiwa na ukauzu usiokuwa wa kawaida , ilikuwa ni kama alitarajia Roma kuingia kwa kutumia Balkoni.

“Mpenzi umetoka hapa kuniiona?, kwanini umevaa nguo hizo za kulalia , kuna upepo mwingi unaweza kusababishia maumivu ya kifua “Aliongea Roma kiunafiki maana alijua kwa mafunzo ya mbingu na Ardhi ambayo Edna amejifunza hawezi kuathiriwa na baridi wala upepo..

“Naomba uondoke , sitaki kukuona”

“Hey, hebu nisikilize kwanza , siku mbili zimepita nadhani hasira zimepungua sasa”Aliongea Roma.

“Hasira!, kwanini niwe na hasira , hakuna maana kuwa na hasira kwa sababu ya baadhi ya watu”

Kwa namna ambavyo alimuona alijua kabisa ni ngumu kumlegeza hivyo aliishia kutoa ile bangiri na kisha akamsogelea.

“Sijali kama bado una hasira na mimi , lakini nipo hapa kukuambia mama kaondoka kaelekea Kenya na hajasema ni lini atarudi au huenda asirudi kabisa kuishi na sisi , Lanlan na yeye yupo kwa babu yake , kabla ya kuondoka aliniambia nikueeze haya maneno kwasababu ameshindwa kuja yeye mwenyewe kuomba msamaha, amesema unapaswa kuvaa hii bangiri lakini kama hutaki haitochukuliwa na mtu mwingine kwani ni ya kwako na itabakia kuwa hivyo”Aliongea Roma lakini maneno yake hayakufanya kazi.

Roma alimsogelea kwa haraka na kumvalisha , lakini Edna ambaye alikuwa akitokwa na machozi mara baada ya kuiona kwenye mikono yake aliivua haraka na kumrudishia.

“Ichukue tu maana siitaki , hio ni kwa ajili ya mkwe wa familia yenu , ndoa yetu ilikuwa ni ya mkataba na mkataba umeisha hivyo mimi sio mkeo tena , sihitaji kuwa mke feki”

“Edna hebu acha hizo , sisi sio watoto wadogo , sisi ni watu wazima na pia ni wazazi vilevile , nakuomba acha kuwa mgumu , kwanini unakuwa na kiburi hivyo , sisi tumeshafunga ndoa na nilikuwa nikikufikiria kwa siku zote tatu tokea uondoke , kwanini unashindwa hata kufikiria mara mbilimbili , nakubali kwamba nilikuelewa vibaya na nimekosea lakini hukuniambia ulichofanya ndio maana na ni sawa mimi tu kukutuhumu , kama ungeniambia ungedhani ningekushuku , hebu jaribu basi kuwa ‘fair’, Unasema ndoa sijui ya mkataba sijui nini …Fu*ck that shit , nimetumia mabilioni ya hela kwa ajili ya ndoa yetu , unafikiria hela zangu nimezipata kimazingaombwe?”

“Kwahio unachosema niwe mtiifu kwako , kwasababu ulitumia hela nyingi kwa ajili ya ndoa si ndio , Unataka nifirisike ili kukulipa gharama zote?”

“Najaribu kukuelezea .. na sijamaanisha unilipe , ninachotaka kusema ungeniambia kila kitu kinachoendelea nisingekushuku tokea mwanzo”

“Usiongee kama vile hili ni mara ya kwanza kutokea , nyie watu mlikuwa na mashaka na mimi tokea mara ya mwisho wakati wa tukio la Hanson , kama kweli ulikuwa unaniamini usingekubali watu wa nje kunituhumu na kunichokoza , kwanini niishi na mtu ambaye haridhishwi na mimi , nadhani itakuwa vizuri zaidi ukitafuta mwanamke mwingine unaemuamini”Aliongea kwa sauti na kumfanya Roma kuzidi kujaa hasira.

“Edna kwanini unataka kushindana na mimi? , nilikuvumilia kwa mengi kwasababu nakupenda lakini usione kwamba nakuogopa”

“Eti unanipenda, hahaha…”Aiongea na kisha akaanza kucheka na kisha akamgeukia na kumwangalia kwa macho makali.

“Ulisema unanipenda lakini je ushawahi kufikiria kuhusu hisia zangu wakani nilipokuwa na wewe , je ushawahi kujua kwamba kuna baadhi ya vitu vitanisababishia taabu tu kwenye maisha yangu , kwangu mimi wewe ni moja ya vitu hivyo”Aliongea lakini Roma hakutaka kukubali maneno yake kirahisi na isitoshe na hasira zilikuwa juu.

“Kwangu mimi Katika dunia hii hakuna vitu au watu ambao wanaweza kunifanya niwe na furaha na wewe ni mmoja wapo”Aliongea Roma.



ITAENDELEA.
 
SEHEMU YA 549.

Edna alijikuta akimeza maneno yake aliotaka kuongea kutokana na namna Roma alivyomwangalia.

Maneno yale aliongea Roma ni kama yaligeuka na kuwa jiwe ambalo limetua moja kwa moja kugonga katika moyo wake uliokuwa kama barafu.

Alimwangalia machoni kwa muda mrefu kabla ya kuvuta pumzi na kuzitoa na kisha akalamba lipsi za midmo yake na kuongea.

“Wewe ni mbinafsi sana”

“Nakubali mimi ni mninafsi , ndio maana sitokubali sisi kutalakiana . siwezi kukuruhusu ukaondoka kwenye maisha yangu ,siwezi kupiga magoti pia na kukuomba tena wala sitoomba msamaha , unayo kila haki yakubakia hapa lakini wewe ni wangu na hilo haliwezi kubadilika”

“Unaongea mambo ambayo hayana sababu ya msingi”Aliongea huku akishikilia kwa nguvu nguo yake ya kulalia.

“Nataka uone uhalisia ulivyo , wewe unadhani mama amekukera sana kwa kualika wale wanawake nyumbani , unafikiria sisi wote tulikuwa tukikuchokoza kwa kukushuku , mbona unakuwa mwenye kutukandamiza , unaweza kuwa na kisirani chako kwangu utakavyo na naweza kuvumilia lakini hasira zako za haraka zilifanya kila mtu kukosa furaha , je unadhani wewe ndio unaepaswa kufanya tu hivyo , kwanini unataka kushindana na mimi? , mimi ni mume wako na uyle ni mama mkwe wako na sisi ni wanafamilia , kwanini unataka kutuletea tabu”

“Wewe… nilijua tu hujawahi kunionea huruma”

“Naongea ukweli”

“Inaniuma kwasababu kila kitu ulichoongea ni ukweli”Baada ya kumaliza kauli hio aliingia ndani na kufunga mlango wa balkoni na Roma aliishia kumwangalia lakini hakuwa na sababu ya kumsogelea tena kuingia ndani , aliamua zake kupotea na kurudi nje.

Alijikuta akisimama nje kwa muda akivuta upepo mkali unaotoka baharini na baada ya dakika tano aliingia kwenye gari , lakini ile anataka tkuliwasha simu yake ilianza kuita na aliekuwa akimpigia ni Neema Luwazo.

“Kipenzi changu , uko wapi?”Sauti ya kichokozi ya kumnyanyua nyoka pangoni ilisikika kwenye ngoma zake za masikio.

“Sauti yako inaonyesha kama unajua kinachoendelea”

“Wewe hujui wafanyabiashara mtaji wetu ni taarifa na isitoshe ni swala linalokuhusu , nasikia umekosana na mkeo na amehama kabisa nyumbani?”

“Umesikia wapi , Nasra ndio kakuambia?”

“Ah..,! Nasra sio mtu wa kuongea ongea umbea nadhani hata wengine hajawaambia , nilienda nyumbani kwenu nikakuta hakuna mtu ndio nilipofanya maamzui ya kumpigia Bi Wema na akaniambia kinachondelea , kwanini unajaribu kutuficha , haujui mtu kama mimi ambaye siku zote nina ajenda za siri nilikuwa nikisubiria hii siku itimie kwa hamu zote , namchukulia Edna kama mshindani wangu hata hivyo”Aliongea huku akicheka na kumfanya na Roma pia kucheka kutokana na utani wake.

“Inakupasa usubiri muda mrefu, kwani kisheria haturuhusiwi kupeana talaka angalau tuwe tumeishi pamoja miaka miwili”

“Haha.. Naamini atarudi tu ndani ya siku chache zijazo , nadhani sina haja ya kuendela na mpango wangu , unaonaje ukinisindikiza twende Shopping, hutujaonana muda mrefu”

“Si kwasababu muda wote unasema upo bize wewe , uko wapi nije sasa hivi kukuchukua”

“Nipo nyumbani kwangu , Donyi kaondoka leo asubuhi kulekea Los Angels na mchumba wake Kasimu nipo mpweke mno”

Baada ya kuambiwa hivyo moja kwa moja aliendesha gari kurudi uelekeo wa nyumbani kwa ajili ya kumfuata Neema.

Ndani ya madakika kadhaa Roma aliweza kufika na kusimamisha gari nje ya geti na Neema Luwazo alikuwa ashatoka nje na kumpokea kwa kumbatio , alionekana ashajiandaa tyaari kwa ajili ya kuondoka, aikuwa amevalia blauzi na suruali ya jeans ambayo ilimpendeza na kuchora umbo lake namba nane.

“Unaangalia nini , ingia kwenye gari tuondoke”Aliongea kwani Roma alikua akiangalia mtetemno kwa nyuma huku akiwa ameweka tabasamu a kifedhuli , aliishia kucheka na kungia ndani ya gari.

“Mh! Jamani mbona hili gari linanuka sigara”Aliuliza lakini Roma hakujibu zaidi ya kuguna na kumfanya Neema kumwangalia.

“Kwahio mawazo yamekuwa mengi , sijawahi kukuona ukivuta sigara , nilidhani mwanaume wangu ni wa kipekee lakini inaonekana kumbe hauko imara kudhibiti mawazo yako”Aliongea huku akivuta mdomo na kumfanya Roma kucheka.

“Okey kwanzia leo nitaacha, Wapi unataka kwenda?”

“Mimani City , tunaweza pia kula huko huko chakula cha mchana , unaonaje?”Aliuliza na Roma hakubisha kwanza hata hivyo asingerudi nyumbani na kukaa peke yake wikiend yote hio , hivyo aliona huenda ingekuwa afadhali.

Baada ya kufika Mlimani walianza kupita kwenye kila duka kwasababu Neema hakuwa na kitu kichwani anachotaka kununua hivyo alijaribisha kila kitu kilichomfurahisha , lakini mwisho wake hakuridhika na wakaishia kwenda kwenye Brand maarufu za Balenciarga , Dr Martens, Luis Vuiton na lancome.

Roma aliishia kumsindikiza maana wafanyakazi walikuwa wakimsaidia kushika kila ambacho anachagua , lakini Roma kwenye upande wa nguo hakuona kwanini Neema anachagua aina hizo za nguo kwani hazikuwa zikimvutia.

“Hey , kama unataka kununua nguo nadhani ulizopita kule nyuma ndio zinakufaa zaidi , hizi nguo nadhani ni kwa ajili ya maonyesho ya fasheni, hakuna maana kuziangalia”Aliongea Roma.

“Wewe mwanaume huelewi kama nisipovaa nguo ambazo ni za brand kubwa nikienda kwenye vikao wataniona kituko , sisi wanawake siku hizi tunajali sana kile ambacho tunavaa kuendana na wakati”

“Kuna haja gani ya kujali watu wanasemanini , kwani hakuna anaeweza kuipima thamani yako kupitia mavazi”.

“Hehe ndio dunia inavyoenda , kama sio hivyo unadhani makampuni kama haya yangekuwa maarufu , kampuni ya mkeo ukiachana na upande wa kampuni zake ndogo ndogo za ujenzi na mambo ya mafuta lakini pia upande wa fasheni umemuinua sana kiuchumi”

“Inaonekaa hufatilii sana kile ambacho kinaendelea kwenye kampuni , hivi majuzi tu aliweza kuingia ubia wa kibiashara na kampuni zenye majina makubwa makubwa kuomba haki ya kusambaza bidhaa zinazotokana na malighafi mpya , kampuni alizoingia nazo mkataba ni kama Prada , Hermes na Burberry , faida alizopata kwenye ubia na kampini hizo ni mara mbili yake anayopata kwenye kampuni zake za ujenzi ukiachana na mafuta pamoja na viwanda vya utengenezaji wa bidhaa za ndani”

“Ana kipaji cha kufanya biashara , lakini nadhani anapaswa kujifunza namna ya kuwa mke bora”Aliongea lakini Neema alicheka.

“Mbona unacheka?”

“Ni hivyo uliposema ana kipaji cha biashara lakini kwa mtazamo wangu naamini ni kinyume chake , ameweza kufanikisha yote hayo kutokana na ukweli kwamba baba yake ni mtu mzito na ana ushawishi mkubwa kwa Raisi Senga na nchi zote za Afrika ya mashariki na kati

“Unamaanisha nini?”

“Wafanyabiashara kama sisi siku zote tunapaswa kufanya vitu kwa wakati sahihi , sehemu sahihi na watu sahihi , kuwa na watu sahihi sio kitu kigumu kwasababu unachotakiwa ni kuwa na ushawishi tu na maipo mazuri , kuhusu sehemu sahihi inategemeana na bahati yako katika biashara , kama sio kampuni ya Vexto kuchagua maeneo sahihi katika kufanya biashara basi siamini ingeweza kuwa na mafanikio makubwa kwa nchi kama hii ya kwetu ambayo ndio kwanza inaendelea , kitu kigumu katika biashara ni kufanya vitu kwa wakati sahihi kwasababu kikawaida inategemnea sana na sera za nchi , kadri utakavyofanya vitu ndani ya sera za serikali basi huna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu fursa za kibiashara , kama sera haiendani na biashara yako hata uwe na mtaji mkubwa kiasi gani huwezi kufanikiwa na ndio maana wawekezaji wanapoenda kuwekeza kufanya biashara katika mataifa ya nje wanachoangalia ni Sera”

“Kwahio unachomaanisha ni kwamba Raisi Jeremy alikuwa akimsaidia Edna katika maswala ya sera ndio maana kampuni yake inafanya vizuri?”

“Ndio maana nakushauri kuwa makini na Raisi Jeremy , ijapokuwa hakuwahi kumtambua Edna waziwazi kama mtoto wake, lakini amesaidia sana kampuni ya Vexto kufikia pale ilipo, huenda kama atakuja kumwambia Edna mambo ambayo amefanya Edna moja kwa moja ataguswa”Aliongea Neema na kumfanya Roma kukumbuka kuna siku Edna ashawahi kumwambia kuhusu mtu anaefahamika kwa jina la the Protector ni kama maneno ya Neema yamemkumbusha kuhusu hilo jina kwani alikuwa amesahau kwa muda mrefu.

“Kwanini unaniambia haya ghafla tu, unadhani kwanini Jeremy anaushawishi mkubwa ndani ya Afrika mashariki na kati?”

“Kuna kitu sikukuambia kwasababu nilikuwa bize na kazi , lakini katika moja ya vitu ambavyo niliweza kugundua katika baadhi ya nyaraka alizoacha mstaafu Kigombola ni juu ya raisi Jeremy na siri zake”

“Siri zake!”

“Ukweli kama ningeona taarifa hizo miaka ya nyuma kabla ya kukutana na wewe nisingezielewa wala kuamini , lakini kwa kipindi ambacho tumekutana na nikajua mengi ambayo hayaonekani katika huu ulimwengu ndio maana nimefanikiwa kuelewa kile alichoandika”

“Umegundua nini?”

“Kwa maelezo ya Kigombola ni kwmaba Raisi Jeremy ana nguvu kubwa nyuma yake ambayo inamlinda na inahusiana na viumbe wasioonekana(majini) , katika nyaraka nilizoweza kupata kusoma jamii hio inafahamjka kwa jina la Panas kama sikosei”Roma alishangaa maneno ya Neema.

“Amejuaje kuhusu hii jamii kuwa nyuma ya Jeremy , mwenyewe nilianza kufikiria hili swala mara baada ya kuona watu wawili kutoka Panas ambao tayari wapo katika levo ya Nafsi wakimsindikiza kama mabodigadi”

“Nini!!, kwahio nilichosoma ni kweli jamii hio ipo, kama ndio hivyo inamaanisha kwamba wametoka katika maficho yao sasa wanataka kuingilia amswala ya kawaida ya dunia?”Aliongea Neema Luwazo kwa mshangao.

“Siwezi kujua, lakini uwepo wao hapa nchini ulinipa maswali mengi ambayo sijayapatia majibu bado na kama uliosema ni kweli basi naanza kupata picha lakini pia shauku yangu kuzidi kuongezeka , je hakuna kitu kingine ambacho uliweza kupata katika maelezo uliosoma?”

“Maelezo niliosoma ni hayo pekee na ndio nguvu kubwa ya Raisi Jeremy nchini Rwanda , ilionekana Kigombola bado hakuwa na majibu ya kutosha na hata alichokiandika hakikuwa na ushahidi , lakini baada ya wewe kusema wameonekana hapa Tanzania sasa naamini maneno yake”Roma alifikiria kidogo na kuona huenda kuna sababu ambayo watu wa Panas wakaamua kuja upande wa duniani , lakini kama ni hivyo kwanini Aphrodite na wenzake hawakumweleza kuhusu hii jamii maana kama na wao walikuwa wakitumia nguvu za kuvuna nishati za mbingu na Ardhi basi wangewalaetea mtafaruku wakati walipokuja duniani.

“Kama ni hivyo je unadhani swala hili linaweza kumuhusu Edna?”

“Lazima liwe linamuhusu , nadhani mpaka sasa huna taarifa, ukweli ni kwamba mpaka sasa mtoto wa pekee wa Raisi Jeremy hafahamiki alipo , ijapokuwa taarifa hio ni ya siri lakini hawezi kuificha kwa watu kama sisi ambao tunahusiano wa moja kwa moja na serikali, kama hisia zangu zitakuwa sahihi basi naamini anataka kumfanya Edna kuwa mrithi wake”Aliongea na kumfanya sasa Roma kuelewa kitu.

“Nadhani ndio maana alionekana kuwa na haraka ya kumtaka Edna kumtambua kama baba”

“Unamaanisha alishaanza kuongea na Edna?”

“Siku ambayo niliwaona hao watu kutoka Panas ndio wakati ambao alifika nyumbani kwetu kwa ajili ya kuongea nae , lakini inaonyesha Edna hakuwa tayari kukubali”

“Wasiwasi wangu ni kwamba ataishia kukubali na kama hilo litatokea mkeo anaweza akakuingiza kwenye mtego , mpaka sasa naamini Hongmeng ni maadui zako na hata jamii hio ya Panas sidhani kama wanakuchukulia kama rafiki au adui, Jeremy ndio mtu pekee ambaye atafanya kila kitu kwa faida yake na mawazo yake yote ni kuona Rwanda inakuwa kimaendeleo kwa kunyonya rasimali za nchi zinazomzunguka kupitia njia za kijasusi”Roma alijikuta akianza kuwa na wasiwasi, alijua msimamo wa Edna ulivyo likija swala la familia.

“Lakini sidhani Edna anaweza kuwa mwepesi namna hio”Aliongea Roma.

“Hata mimi natumaini asiwe mwepesi wa kukubali kila kitu”

“Okey, nimekuja kurelex sio kuongea mazungumzo haya , hebu tuendelee na kilichotuleta”Aliongea Roma na kisha waliendelea kufanya shoping.

Ni muda wa saa saba wakati wakiwa kwenye mgahawa wakipata chakula cha mchana Roma aliweza kupata msisimko wa kuongezeka kwa mtu mwenye nguvu za kijini na kujikuta kugeuza shingo yake kuangalia upande wa kulia na palepale aliweza kumuona Omari Tozo akiingia eneo hilo.

Omari alikuwa amevalia mavazi ya suti na kwa mwonekano wake ni kama vile amekuja hapo ndani kwa ajili ya kuonana na mtu , baana ya kukagua baadhi ya watu palepale aligeukia upande wa aliposimama Roma na kisha akatabasamu na kupiga hatua kumsogelea.

Tokea siku ambayo waliweza kuhudhuria harusi yake hawakuwahi kuonana tena.

“Madam Neema nadhani hutonilaumu kwa kuingilia muda huu mzuri kwenu wa chakula cha mchana nikimchukua kwa dakika huyu kiumbe , si ndio?”Aliongea Omari huku akiweka tabasamu.

Kwa muonekano wa Omari alivyo alijua tu kuna kitu anahitaji kuongea nae.

“Nadhani ndoa tamu , naona una mabadiliko makubwa ya kiafya”Aliongea Neema kwa utani na kumfanya Omari kutoa cheko kama kawaida yake.

“Nadekezwa mwenzenu , nashindwaje kunenepa sasa”Aliongea na kisha wakasogea meza ya pembeni kwa ajili ya kuongea,.

“Kwa muonekano wako nadhani hatujakutana hapa kwa bahati mbaya si ndio?”

“Upo sahihi , nipo hapa kwa niaba ya serikali chini ya TSS kukuuliza maswali kadhaa ya kiusalama”

“Maswala ya kiusalama , tangu lini serikali ikaniuliza maswala ya kiusalama wakati mimi ni rais mwema?”Aliuliza Roma kwa mshangao.











SEHEMU YA 550.

Roma alijua sio rahisi kwa Omari kumtafuta na kutaka kuongea nae maswala ya kiusalama , lazima kutakuwa na kitu ambacho kinaendelea ambacho yeye hakifahamu , imepita wiki kama tatu tokea The Eagles kuondoka Tanzania na kurudi visiwa vya Mediterranian hivyo hakuwa na chanzo sahihi cha taarifa.

Aliwaondoa kwasababu ya kwamba tishio la kiusalama lilishaisha kutokana na kumuua Yan Buwen na washirika wake akiwemo Mzee Longoli.

“Kwa muonekano wako naamini huna taarifa ya makundi ya watu waliongia Tanzania hivi majuzi?”

“Ndio sina taarifa nadhani mnafahamu The Eagles project yao hapa Tanzania imesitishwa na kurudi, kwasasa nipo mwenyewe tu hapa Dar es salaam”

“Ndio maana hujaweza kupata taarifa”

“Kuna nini kinachoendelea?”

“Intellijensia ya usalama wa taifa imeweza kubaini kikosi cha giza cha Siraha Kwenye Jiwe(SIS) kutoka Scotland ,Bunge la Kiza likijumuisha wanachama wao wa kundi la Camarilla na Sabbat wapo hapa nchini , kuna pia baadhi ya makundi madogo ya watu wanaotumia nguvu za giza pia wamefika”Aliongea Omari na kumfanya Roma kushangaa.

“Wamekuja hapa Tanzania , kwasabau gani , kama ni jiwe la Kimungu nadhani wanajua halipo chini ya umiliki wangu?”

“Nadhani hawajaja kwa ajili yako na isitoshe sidhani kama wana uwezo wakupigana na wewe”

“Kama sio hivyo kwanini wamefika?”

“Intellijensia tulioweza kuvujishiwa kutoka nje ya nchi ni kwamba wapo hapa kwa ajili ya siraha ya kichawi ifahamikayo kwa jina la Magical Girdle”Aliongea Omari na kumfanya Roma kushangaa kwani neno la Magical Girdle ashawahi kusikia.

“Unamaanisha siraha iliopo kwenye hadithi za miungu ya kigiriki ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Aphrodite?”

Katika hadithi za miungu ya kigiriki na kiroma , mungu wa urembo aliefahamika kwa jina la Venus kwa kirumi au Aphrodite kwa kigiriki alikuwa na siraha ya mvuto ya mshipi wa kichawi wa dhahabu ambao uliwafanya miungu mingine kuvutiwa nae sana kimapenzi.

Inasemekana alitumia siraha hio kuwapumbaza miungu na kutawala akili zao kihisia , alifikia hatua ya kushindana na Athena pamoja na Hera katika kujiongezea mvuto kwa kutumia siraha hio na alifanya miungu yote kumchagua yeye kama mrembo zaidi.

Lakini hata hivyo ni hadithi tu , kitu ambacho kilitungwa na binadamu wakiwa wamedhibiitwa kiakili ili kufanya binadamu wengine kuwaabudu viumbe hao waliovamia dunia na kuona Binadamu ni kiumbe dhaifu.

Sasa Roma hakuwahi kusikia kutoka kwa Christen kama kweli alishawahi kuwa na siraha hio ya kichawi ifahamikayo kwa jina a magical Girdle lakini kama ilivyokuwa kwa Hades wa zamani kutokumuambia kuhusu siraha yake ya Helmeti of Invisibility(Helmet la kutokuonekana) wakati alivyomuachia urithi basi aliona huenda ni sawa kwa Christen pia.

Siraha za aina hio hata hivyo hazikuwa na maana sana kwa viumbe hawa wa sayari nyingine ambao wameishi hapa duniani kwa muda mrefu , kutokana na kwamba wanakosa miili yao halisi.

Na Roma aliona kama Christen kweli alikuwa na huo mshipi kwa alivyokuwa akimtamani huenda angeshaidhibiti akili yake na kumfanya alale nae au kufanya zaidi ya hivyo na hana uhakika kama angeweza pia kutawala akili ya Zeus na wengine.

“Kama ni hivyo unamaanisha wanatafuta huo mshipi hapa Dar es salaam ,unamaanisha mshipi huo umeonaka hapa Tanzania?”

“Hata sisi hatuna uhakika pia , na tumeshindwa kuweza kujua taarifa kamili”

“Kama ni hivyo wamejuaje kama Mshipi huu wa kichawi upo hapa Tanzania?”

“Kuna mtu ambaye ametumia Mshipi huo wa kichawi kuwadhibiti wanajeshi wa kitengo maalumu na aliweza kuonekana kwenye Rekodi ya Vidio , hio Vidio ndio ambayo imesambazwa kwa Kundi la SIS , Bunge la Kiza na baadhi ya makundi madogo madogo, Eneo ambalo limeonekana kwenye Vidio hio ni katika kambi yetu ya kijeshi ya Ruvu”

“Kama unayo hio vidio unaweza kunionyesha?”Aliuliza Roma huku akianza kuwa siriasi na Omari alionekana alishajiandaa kabla ya kufika hapo na alitoa simu yake na kuchezesha kicha akamkabidhi Roma.

“Kwenye Vidio hio ilionyesha kivuli cha mtu mwenye ngozi nyeusi yaani muafrika akijaribu kutawala akili za wanajeshi waliokuwa katika Demo ya mazoezi ya siraha na kwa kutumia Mshipi wa Dhahabu palepale wale wanajeshi waligeukana wao wenyewe na kupigana risasi.

“Ni Vidio fupi sana , tukio hili mpaka sasa ni siri ya serikali na limetokea wiki iliopita , baada ya uchunguzi wa kina kufanyika na kivuli cha mtu kinachoonekana kwenye hio Vidio kutotambulika Serikali ilipanga kikao kuzima swala hili ili kubakia siri , lakini ajabu ni kwamba hio Vidio ilisambaa nje ya nchi kwa makundi hayo ya watumiaji wa nguvu za giza”

“Inasemekena pia mtu ambaye anatumia hio Dhana ametangaza kwamba ameipata kwabahati mbaya na anashindwa kufahamu namna ya kuitumia hivyo anapanga kuiachia kwa watu wengine wenye uwezo na ameificha ndani ya jiji la Dar es salaam na mtu ambaye atabahatika kuipata ndio atakuwa mmiliki”Roma alijikuta akiwaza kidogo kusharabu maneno hayo.

“Nadhani sio sawa ,kama kweli hio dhana ni yenyewe sidhani Aphrodite angeshindwa kuinasa kihisia, lakini mpaka sasa hakuna hatua aliochukua na isitoshe siraha hio haiwezi kutumiwa na mtu yoyote kwani inahitajika kuwa na nguvu ya kiuungu ndani yake, Kwahio hamjatambua kabisa hiko kivuli cha mtu ni nani na nia yake ya kufanya hivyo?”

“Bado hatujaweza kufahamu , ni swala ambalo ucunguzi wake unaendelea kwani mpaka sasa linaumiza vichwa vya wakuu wa majeshi , maana tukio la kupigana risasi wanajeshi kwa wanajeshi ni la kuogofya sana kwa usalama wa nchi”Aliongea na kumfanya Roma aanze kufikiri.

Kuna kipindi wakati alipokuwa Ufaransa watu walikusanyika kwa ajili tu ya kutaka kuipata siraha ya Thanatos , lakini sio hivyo tu hapa Dar es salaam ni kama tukio hilo linajirudia , kwani mara ya kwanza Dhana ya Holly Grail ilionekana Tanzania na makunndi ya nguvu za giza na za Nuru walifika na kuanza kupigana kuipata.

Roma mara baada ya kuwaza aliishia kucheka , alijua hata kama inaweza kuwa halisi , hakuna uwezekano kwamba wanaweza kuitumia kupumbaza watu kwani ni siraha inayomjua mmiliki.

“Lakini kwanini hili swala naona kama ni mtego , nadhani nyie watu msijisumbue , ngoja wafanye wanachoweza kufanya na sisi tuone”Aishauri Roma,

“Bro unapaswa kutusaidia katika hili , hawa watu kama itatokea wakahatarisha usalama wa nchi vikosi vyetu vya idara ya uchawi sidhani kama wanaweza kufanikisha kuwadhibiti na isitoshe wewe pi ni mtoto wa raisi na familia yenu imeweka mizizi katika usaama wa taifa”

“Ohoo!, siwezi hata kumdhibiti mke wangu mwenyewe, halafu nijihusishe katika haya mambo . kwanini niingilie?”Aliongea Roma akijaribu kukataa.

“Kama huwezi kuingilia tunalo ombi moja kwa sasa , wewe unafahamiana na miungu wenzako mathalani Aphrodite mungu wa urembo, kama kutakuwa na uwezekano wa kujitokeza na kutusaidia , maana kama watu hao wataanzisha vurugu mambo yanaweza kuwa nje ya uwezo wetu”Roma alifikiria kidogo.

“Okey nitampigia simu baadae”

“Mpigie sasa hivi Bro wakuu wanasubiri majibu muda huu”Aliongea kwa msisitizo na kumfanya Roma kukosa neno la kuongea na palepale aliamua kutoa simu yake na kutafuta namba ya Christen na kupiga na iliita kwa muda mrefu kidogo lakini Roma hakukata tamaa kwani alijua muda huo Los Angeles itakuwa ni usiku kukikaribia kupambazuka.

“Hades , are you calling to ask me about Magical Girdle too?”Aliuliza akimaanisha kwamba je anampigia kwa ajili ya kuulizia mshipi wa kichawi pia.

“Ndio”Alijibu Roma.

“Mshipi wangu wa thamani kubwa haujaibiwa , ninao siku zote hivyo naomba usiulizie tafadhari , Mshipi ambao umeonekana kwenye vidio unafanana sana na wa kwangu lakini ni feki , kuna wachawi wengi wa kiroho dunia hii, kwa mfano kundi la kichawi la Siraha kwenye Jiwe wanaweza kutengeneza udanganyifu , hivyo kwanini iwe dhana yangu ya Mshipi wa dhahabu”Aliongea kwa namna ya kujitetea na kukereka kwa wakati mmoja na kumfanyaRoma kukunja sura.

“Kwanini sasa unaonekana kuwa na hasira , miimi nimepiga simu kwa niaba ya jeshi la Tanzania kitengo cha wachawi kwani hawana uwezo wa kukuuliza moja kwa moja na isitoshe nilijua usingeshindwa kunasa kihisia pale mtu anapotumia dhana yako”

“Tatizo mnanisumbua , muda si mrefu Poseidon ,Hermes na Artemis wamenipigia na kuniamsha kwenye usingizi , naomba usijihusishe , waache watafute kama wanavyoamani lakini kama utagundua muhusika wa kuzusha uongo huo ni nani niambie nitahakikisha namchuna ngozi akiwa hai”

“Sawa lakini kwa nilivyosikia kundi la Sabbat pia lipo hapa nchini , nadhani chuki zako uzielekezee kwa Raphael kwani ndio kiongozi wa kundi hilo ambae ameagiza watu wake kuja hapa nchini na wakafatia kundi la Camarilla”

Raphaeli ndio kiongozi wa kunti la Tzimisce ambaye anatumia mwili wa Vampire , ni kiumbe kutoka sayari nyingine ambaye alifanya watu duniani wamuabudu kwa kumuita Hermes mchunga kondoo.

“Hermes ni mtu wa ajabu na sipendi kuongea nae, nadhani amefanya hivyo kutokana na kuficha uhusika wake, mpaka sasa hakuna Vampire anaemfahamu kwa jina la Hermes, Hades nitakuw amkweli kwako kila dhana ambayo tulikuja nayo imeunganishwa na roho zetu kuna zile zilizopotea na tulizobakiwa nazo , ndio maana hata Artemis aliweza kuhisia uwepo wa Selene nchini Korea kusini licha ya kwamba alikuwa umbali wa takribani nusu ya dunia, mpaka sasa dhana pekee ambayo imepotea na na imeshindikana kufahamika imepotelea wapi ni Helmeti la kutokuonekana ambalo ni siraha yako , kama hujui, Helmet hilo ni kama taji na nitofauti sana na dhana tulizokuja nazo kwani teknolojia yake ilikuwa ni ya hali ya juu sana na Hades wa dhamani kwasababu alikuwa ni mwanasayansi ndio anajua siri yake”

“Ndio maana Hades wa zamanni sikuwahi kumuona nalo , kumbe ni dhana ambayo haionekani”

“Nadhani umeelewa sasa narudi zangu kulala , kama utakuwa na muda naomba uniangalizie nani kaanzisha huo uvumi , niambie na nitakuja kumuua mwenyewe , anadhani kujificha Tanzania siwezi kumpata na kumuua”

“Kuhusu hilo usijali nitakusaidia ,lakini na mimi utanisaidia kujibu maswali yangu yote ya kile kilichotokea Korea kusini bila kunificha kitu”Aliongea Roma na kauli yake ilimfanya Christen kuwa kimya.

“Nilishakujibu tokea muda mrefu hukuzingatia ndio maana , mimi nalala”Aliongea na kisha akakata simu na kumfanya Roma kukuna kichwa chake na kujiambia atajua tu ukweli wote kuliko mambo nusu nusu wanayomwambia.

Roma ilibidi amwelezee Omari juu ya alichoweza kupata na wote walijikuta wakiwa na ahueni na aliwathibitisha hakuna mgogoro unaoweza kutokea baina ya wageni hao kama tu Mshipi huo hautakuwa halisi.

“Asante sana Bro , nadhani napaswa kuondoka sasa nikuache na shemeji, tutakutaarifu tukimpata muhusika”

“Haina haja ya kunifahamisha , hilo ni swala ambalo halinihusu”Aliongea na Omari aliaga na kuondoka.

Neema hakumuuuliza sana maswali Roma juu ya kile ambacho alikuwa akiongea na Denisi , kwani mara baada ya kurudi kwenye meza walikula chakula kama wapenzi huku wakishushia na mvinyo.

Wikiend nzima Roma alimalizia kwa Neema Luwazo na walipika na kupakua na alimsaidia pia kwenye kuvuna nishati za mbingu na ardhi.

Siku ya jumatatu mara baada ya kuamka mawazo ya Edna yalianza kukisumbua kichwa chake na wakati alipokuwa akipata kifungua kinywa kilichoandaliwa na Neema alimkumbuka na alijiambia kutokana na anavyo mjua Edna muda huo atakuwa hajapata chochote , hivyo alimwambia Neema amwandalie vitu vya kuondoka navyo kwani anampelekea mke wake, aliongea bila ya kupindisha kauli.

Neema baada ya kuambiwa hivyo alimuonea wivu Edna lakini aliishia kuandaa kwani alijua yeye ni mchepuko tu na ili aendeee kufurahia penzi na kijana huyo mdogo basi ni kuhakikisha anamfurahisha na kumsapoti kwa kila kitu na isitoshe anapata faida kubwa ya kuvuna nishati kitu kitakachompeekea kuwa mrembo muda mrefu.

Roma asubuhi hio mara baada ya kufika nje ya ofisi ya Edna aliweza kukutana na Recho ambaye alikuwa akitoka katika ofisi ya Edna na kwa haraka haraka alijua huenda alikuwa akisafisha na kuweka mazingira sawa lakini aligundua sio hivyo mara baada ya kuona amebeba mabakuli na juisi kwenye mfuko wa plastiki.

Hakuwa amemuona Recho kwa muda mrefu kidogo ni kama zaidi ya miezi mwili , lakini alionekan hakuwa amebadilika sana zaidi ya kwamba kipindi hiko alionekana ni mwanamke mwenye kujiamini sana kuliko alivyokuwa mwanzo na ni kama urembo wake umeongezeka zaidi.

“Ni wewe .,… nikajua Boss ndio amefika”Aliongea huku kidogo akionyesha hofu.

Tokea kitendo kilichotokea miezi kadhaa iliopita ilifanya wao kujihisi vibaya kila pale wanapokutana .

“Edna yuko wapi , bado hajafika kazini?”Aliuliza Roma na kumfanya Recho kushangaa kidogo.

“Kuna chochote kilichotokea kati yako na Boss? Kwanini amehamia Msasani?”

“Nadhani haina haja ya kuongelea hilo kwasasa”Aliongea Roma maana hakutaka kutanganza matatizo ya ndoa yake hadharani.

“Ulichobeba ni kifungua kinywa kwa ajili ya Edna?”Aliulizia Roma kupotezea mada.

“Ndio , amenipigia simu nimwandalie ..”Aliongea Sekretari Recho huku macho yake yote akiwa ameyaelekeza chini , alikuwa na aibu za kike kwani alishindwa kumwangalia Roma usoni.

Ukweli ni kwamba Recho licha ya kwamba alikuwa na maisha mazuri na kule kukataliwa na wanaume kuisha , lakini akili yake haikufuta tukio la kufanya mapenzi na Roma , ni tukio ambalo muda mwingine hujirudia hata wakati anapofanya mapenzi na mpenzi wake mpya na kadri siku zinavyozidi kuendelea ndio ambavyo tukio lilizidi kutawala akili yake lakini hakupata ujasiri wa kumsogelea Roma tena kwani ni mke wa bosi wake na aliogopa ikija kugundulika , kwani maisha yake wakati huo na familia yake yalikuwa mazurri kutokana na mshahara mnono pamoja na posho anazopata kutoka kwa Edna.

Muda huo ambao hawakuwa wakijua ni topiki gani waendelee nayo kuongea wakimsubiria Bosi hatimae Edna alitokea kwenye lift na kuingia eneo hilo na alijikuta akipatwa na ubaridi mara baada ya kumuona Roma mbele yake.

Jicho moja tu kwa Recho ni kama aliona lazima kuna kitu kilichotokea kati ya Roma na sekretari wake na hapo hapo alizidi kuongeza ukauzu wake.

“Boss karibu kazini , nimekuandalia ulichoniagiza”Aliongea Recho kwa mtindo wa heshima kwa bosi huku akiwa na afadhali.

Edna alimpita Roma kama hamjui na kisha alimsogelea Recho na kuchukua mfuko alioshikilia mkononi na kisha akatingisha kichwa kama ishara ya kushukuru na kupiga hatua kuingia ofisini kuingia kwake , lakini kabla hajafikia mlango Roma alianzisha maongezi.

“Edna na mimi nimekuletea kifungua kinywa mke wangu, niliju tu muda huu utakuwa hujapata chochote”Aliongea huku akimwonyeshea mfuko alioshikilia na Edna alijikuta akitoa kicheko hafifu cha kukera.

“Una uhakika umeleta kwa ajili yangu?”











SEHEMU YS 551.

Upande mwingine nyumbani kwa Afande Kweka mara baada ya Lanlan kufika nyumbani hapo akiwa ametangulizana na Qiang , aliweza kupokelewa kwa furaha na wazee wawili ngozi tofauti ,mmoja akiwa ni Mzee Kweka mwenyewe na mwingine alikuwa ni Pastor Cohen.

Pastor Cohen mara baada ya kumuona Lanan alimwangalia Afande Kweka kwa tabasamu kubwa na kutingisha kichwa kuonyesha ishara ya kukubali jambo.

Ukiachana na maswala mengi ambayo Afande Kweka na Pastor Cohen waliweza kuzungumza lakini kubwa zaidi ni swala la Lanlan kuwa mtoto wa Seventeen pacha wa Edna ambaye aichanganywa na Roma kwenye mpango LADO.

Pastor Cohen na Afande Kweka ndio watu ambao walioratibu mchakato wa kumuingiza Roma na Seventeen katika mpango LADO na moja wapo ya matokeo hayo ni uwepo wa Lanlan duniani.

“Komredi nikiri hapa hakuna ubishi , lakini nashindwa kuelewa inakuaje Roma kushindwa kumfahamu binti yake mwenyewe”

“Komredi hilo ni swali gumu kwangu , najua nilihusika kuwaingiza kwenye mpango LADO lakini uendelevu wake sikuhusika”

“Sio wewe tu ambaye hukuhusika , wote hatukuhusika, mpango LADO kumbuka ulikuwa chini ya Zeros organisation na sisi tulichokifanya ni kufuata maagizo ya kuchomeka watu ambao hawakuwa katika mpango ili kutengeneza mafanikio”Aliongea na Afande Kweka alionekan kutopinga.

“Nadhani imekuwa ngumu kutokumfahamu mtoto wake kutokana na kilichomtokea Seventeen”

“Nakuunga mkono , lakini bado kuna kitu nashindwa bado kuelewa , kama wewe umeweza kumfahamu mjukuu wako kwanini yeye baba ameshindwa hilo”

“Ukiniuliza hilo nitasema ni uzoefu lakini nikikujibu kwa niaba yake nitasema licha ya mengi ambayo yametokea lakini bado mtoto wake ameweza kurudi nyumbani kumfuata , damu ni nzito kuliko maji”

“Ningetamani kujua kila kilichotokea , nadhani mzee mwenzangu una shauku ya kujua pia nini kilitokea baada ya kupotea kwa ile ndege , kwani mpaka sasa ni mpango wa siri ambao ni watu wachache sana duniani wanaoufahamu”

“Ninatamani sana , lakini kwa uzee huu nadhani naweza kuangulie mbele za haki bila kujua kile kilichotokea”Aliongea na kumfanya Pastor Cohen kutingisha kichwa.

“Wewe ni mimi Komredi hatuna haja ya kuwa na huzuni ilimradi tulichokifanya kinakwenda kuisaidia dunia , kwasasa nadhani shauku yangu imetimia sasa , nimemwona kitukuu chako, nadhani ni muda wa mimi kuondoka , lakini kabla ya yote nataka kukueezea kile kinachoendelea ndani ya umoja”

“Nakusikiliza Komredi”

“Kwasasa ndani ya kundi , kuna ‘interval’ kubwa ya tarehe katika kalenda kwa kile ambacho wanachana wanapaswa kufanya”

“Unamaanisha nini Komredi?”

“Ukiachana na taratibu za kawaida ambazo zinaendelezwa kufanywa na wanachama kwa sasa kinachosubiriwa ni siku ya kwanza ya mvua ya theluji kwa bara la Afrika”Aliongea na kumfanya Afande Kweka kushangaa.

“Mvua ya kwanza ya Theluji katika bara la Afrika , unamaanisha Tanzania Mvua ya Theluji itawezekana kunyesha?”

“Hakika , ndio ishara kubwa inayosubiriwa “

“Ishara hii inamaanisha nini?”

“Katika umoja wetu ishara hii inamaanisha ule wakati uliosubiriwa umetimia ni kama unabii umetimia , kwa upande wa Illuminat na Allien kwao ni ishara ya utawala wao duniani kuanza”

“Nini kitatokea baada ya hapo?”

“Kwasasa hakuna majibu sahihi ,mpaka itakapojulikana ni kipi kingine kinapaswa kufanyika kulingana na Kalenda , lakini mpaka sasa tunaweza kufanya makisio, nadhani unajua nini kinasababisha Theluji?”

“Najua ni Baridi?”

“Sahihi kabisa, makisio ni kwamba kuna uwezekano joto la dunia kushuka katika viwango vya chini sana kiasi cha kupelekea bara la Afrika kuweza kupitia vipindi vya majira ya mvua ya Theluji”Aliongea na kumfanya Afande Kweka kushika kidevu , ijapokuwa hakuonyesha mshangao wake waziwazi lakini ilikuwa dhahiri taarifa hio ilikuwa ya kumshangaza.

*****

Roma alijikuta akishangazwa na swali la mke wake kwani hakuwa amemulewa kabisa , alimbebea yeye kifungua kinywa lakini tena anatilia mashana nia yake ya kumletea.

“Edna unamaanisha nini?”

“Nadhani Recho hajapata kifungua kinywa bado , usipoteze hela zako kwa mtu kama mimi , nitajifanya sijaona chochote”Aliongea na Roma palepale aliweza kuelewa anachomaanisha na kushindwa kuzuia hasira zake .

“Edna hata kama unataka kuonyesha hasira zako hupaswi kwenda mbali hivyo , ndio nimefika sasa hivi na kukutana na Recho hapa , hata kama unadhani sina jema lakini huwezi kuongea hivyo kwa kumsingizia msaidizi wako”

“Nimeonyesha wapi hasira? , au umeelewa vipi kauli yangu , kwanini unajishtukia kama huna hatia?”Aliongea na kumfanya Roma kuwa katika mtego wa maneno.

Alikuwa na hasira na kauli ya Edna lakini alishindwa kukataa wala kukubali , kwani ni kweli kuna dhambi ambayo alishawahi kufanya na Recho.Aliona kama angekataa asingeweza kuituliza roho yake yenye dhamira ya kuhukumu.

“Madam , tafadhari naomba usituelewe vibava Mr Roma amenikuta hapa na amekuletea kifungua kinywa , hakuna chochote kinachoendelea baina yetu naomba usifikirie hivyo tafadhari”Aliongea kwa uwoga huku akiangalia chini.

Roma baada ya kumuona namna ambavyo Recho anajitetea ilimfanya amuonee huruma , kwani alikuwa kwenye hali ya taharuki mno , alikuwa kama mtu ambaye amekamatika katika jambo na sasa anahofia kibarua chake kuota nyasi.

“Recho wewe unaweza kutumia hiki kifungua , kama mtu hataki haina haja ya kumlazimisha ilihali wahitaji wapo”Aliongea Roma na kuweka kwenye miguu ya Recho ule mfuko na kisha aliondoka hilo eneo na kuzisogelea lift.

Recho mara baada ya kuona ameachiwa msala alitamani kupiga magoti , lakini palepale aliushika ule mfuko kwenye sakafu na kisha akamnyoshea Edna aupokee.

“Madam naomba usimfikirie vibaya , Mr Roma kakuletea hiki kifungua kinywa kwa ajili yangu naomba ukichukue..”

Edna aliangalia ule mfuko aliopewa na Recho ulivyotuna na kisha alimsogelea Recho na kuuweka chini.

“Unaweza kuchukua na hiki pia , sina hamu ya kula chochote leo”Baada ya kusema hivyo aliingia ofisini kwake.

Recho aliona siku hio imeanza vibaya sana kwake , alijikuta akiangalia ile mifuko yote miwili , alioleta Roma na alioleta yeye mwenyewe na kujikuta akikosa cha kufanya kwani aliishia kusimama katika sehemu moja bila ya kusogea.

**********

Upande mwingine katika ofisi ya Raisi Senga asubuhi hio , Raisi wa nchi ya Tanzania akiwa ofisini kwake akiendelea na majuku yake , aliweza kufika Kabwe nje ya ofisini huku ameshikilia faili mkononi na baada ya kuruhusiwa kuingia ndani moja kwa moja alimsalimia Mheshimiwa.

“Vipi kuna jipya , kuna chochote ambacho mmefanikiwa kupata?”Aliuliza Raisi Senga kwa shauku.

“Mheshimiwa mpaka sasa hatujapata mwanga wowote wa kumpata Denisi , lakini vijana wamejjitahidi kutafuta taarifa ambazo kwa kiasi flani zinatupa tafsiri ya kile kinachoendelea”Aliongea Kabwe.

“Nipe taarifa”

“Kuna baadhi ya watu hapa nchini tuliweza kuwahoji , mmoja wapo ni Abubakari Hamadi mtoto wa Mzee Alex mmiliki wa kampuni ya JR na mwingine ni Elvis Temba mtoto wa Mkuu wa mkoa wa Dodoma”

“Na mlichogundua ni kitu gani?”

“Nadhani Denisi alikuwa na mpango anaoendeleza yeye na Yan Buween kwa siri hapa nchini kwani kwa maelezo tuliokusanya ni kwamba aliwaambia marafiki zake wote kwamba kuna kitu ambacho wanapanga kumfanyia Roma”

“Lakini Yan Buwen si ameshakufa?”

“Hili ni tukio ambalo limetokea miezi takribani mitano nyuma Mheshimiwa kabla hata ya mheshimiwa Kigombola na Yan Buwen kufariki”

“Kama usemayo ni sahihi basi hayapingani na taarifa tulioweza kupata ya Denisi kuwa na uwezo wa ajabu si ndio?”

“Ndio Mheshimiwa”

“Kama ni hivyo kapotelea wapi?, mwezi wa pii na nusu huu haonekani nyumbani na mbaya zaidi kakomba hela zangu zote zilizokuwa chini ya jina lake katika visiwa vya Shelishei , kapeleka wapi pesa zote hizo?”

“Mheshimiwa nadhani swala hili linahusiana na kinachoendelea nchini Rwanda kwani kati ya marafiki wa karibu wa Denisi ni Desmond mtoto wa Raisi Jeremy”

“Nimejaribbu kumuhoji Jeremy lakini anakuwa mgumu wa kufunguka , lakini chanzo kinaanzia katika kifo cha mke wake, sijui nini ananificha kwasasa inanipa wasiwasi kuhusu Denisi mahali alipo kama yupo salama”

“Mheshimiwa kwanini usifanye kama ambavyo Madam anapendekeza , nadhani Mr Roma atakuwa na majibu sahihi zaidi”Alipendekeza Kabwe na kumfanya Raisi Senga kusimama akitoka kwenye kiti chake.

Ukweli ni kwamba Raisi Jeremy familia yake haikuwa na amanni hata kidogo na yote hayo ni juu ya swala la kupotea kwa Denisi , lakini vile vile kuwa na uwezo wa ajabu ambao alikuwa na uhakika ni uwezo ambao amepewa na Yan Buwen.

Mama yake Denisi yaani Damasi alikuwa na mawazo sana na muda wote ni mwenye kumbebesha Lawama mume wake kwa kutokuwa makini na mtoto mpaka kufikia katika hatua ya kupotea.

Ilikuwa ni miezi miwlii imepita sasa , tokea Denisi alivyopotea ghafla mara baada ya kuweza kukwapua kiasi kikubwa cha pesa cha baba yake alichokificha katika visiwa vya Shelisheli.

Hofu ya Damasi ni kwamba alijua fika kuna uwezekano kuna jambo baya ambalo Denisi analiandaa na hilo linaweza kumuweka katika hatari ya kuuliwa na Roma kwani kwa muda mrefu alishaweza kufahamu kinyongo cha Denisi kwenda kwa kaka yake , hivyo hofu yake ilikuwa ni kubwa mno huku akimlazimisha mume wake kuchukua hatua za haraka kuweza kunusuru hali hio kabla kubwa zaidi halijatokea.

Kilichomshangaza zaidi Senga ni kwamba tukio ambalo linamtokea yeye mwenyewe ni kama linalomtokea rafiki yake Jeremy raisi wa Rwanda, kwani wote watoto wao wa kiume ambao wanaamini kuwa warithi wao hawaonekani walipo na kila dalili inaonyesha hawawezi kuwa sawa tena.

Ilikuwa ni afadhali kwa Raisi Senga kwani alikuwa na Ashley ambaye ni mkubwa na angemrithisha kila kitu chake , lakini bado sheria za ukoo wako zinampa nafasi kubwa mtoto wa kiume.

“Kabwe nadhani kwasasa sina jinsi , ni muda sahihi wa kumkubali Den.. namaanisha Roma kama mtoto wangu”Aliongea Raisi Senga na kumfanya Kabwe kidogo kutoa macho ya mshangao.

“Mheshimiwa unataka nifanye nini?”

“Blandina aliniomba nimsaidie yule msichana Najma nafasi serikalini kama hatua ya kwanza ya kujenga uhusiano wangu na Roma nadhani kwanza nitekeleze hilo”

“Ndio mheshimiwa nitakuletea faili lake”

“Haina haja, fanya utaratibu wa kuangalia nafasi gani itaweza kumfaa katika Wizara ya elimu”

“Sawa mheshimiwa”

“Kingine nitaenda nyumbani kuonana na mzee jioni ya leo na nitapata chakula cha usiku huko huko”

“Sawa mheshimiwa nitaandaa itifaki?”Aliongea na kisha akampa ruhusa ya kuondoka na kumfanya Raisi Senga kuonekana kuwa katika mawazo.

“Huenda uamuzi wangu ukawa sahihi , nikirudisha ukaribu na Roma na kuzuia hatari yoyote kumtokea Denisi nitaweza kupata faida nyingine , naweza kuushinda udhaifu walionitengenezea Freemason na naweza kurudi kwenye mstali kama kiongozi wa taifa hili”Aliwaza mheshimiwa Senga lakini muda ule ule katibu Muhtasi aligonga mlango na kumshtua katika mawazo na aimruhusu kuingia.







SEHEMU YA 552.

Ilikuwa ni saa moja za jioni , haikueleweka Roma alishinda wapi lakini muda huo alionekana ndio kwanza anarudi kuelekea Ununio nyumbani, alikuwa na haraka kwani alikuwa na miadi na Rufi siku hio kwenda kula chakula cha usiku nyumbani kwa Bi Wema , kwani tokea Bi Wema anunue nyumba ambayo anaishi na Rufi mtoto wake wa kike hakuwahi kufika.

Sasa wakati akiwa Tegeta aliweza kupokea ujumbe wa meseji ambao ulimfanya atabasamu kifedhuli ulikuwa ni ujumbe unaotoka kwa namba ambayo hajaisajili kwenye simu yake lakini kutokana na kilichotokea dakika chache zilizopita alijua nani katuma ujumbe huo na alishangaa kwa kuona kwamba mtu huyo hakuwa amekata tamaa , kwani ilikuwa ni kama mwezi mmoja umepita huenda na zaidi tokea akutane nae.

Dakika chache nyuma wakati akiwa anatokea Mbagala akiwa anapita uwanja wa taifa aliweza kugundua kuna gari inamfuatilia nyuma na licha ya kugundua hilo hakutaka kwanza kumchezea mchezo mtu aliekuwa akimfuatilia , kwani aliendesha gari kusonga mbele bila wasiwasi lakini alipokuja kupita katika daraja la Kijazi interchange Ubungo ndio alipanga namna ya kumpotezea mtu ambaye alikuwa akimfatilia nyuma nyuma.

Mtu aliekuwa anemfuatilia alikuwa ashamtambua na ilionekana pia hata mtu huyo ashajua kama ashajulikana kutokana na kwamba alikuwa akisambaza nguvu za kijini na kwa kufahamu uwezo wa Roma alijuwa atakuwa amehisi uwepo wake, lakini haikumkatisha tamaa kutimiza dhamira yake.

Roma mara baada ya kuingia katika barabara ya Sam Nujoma sehemu pekee ambaye aliamini anaweza kumpoteza mtu anaemfatilia ni eneo la Mwenge Mataa na kweli aliweza kufanikisha hilo kwani alihakikisha alikuwa mbele kabisa anagalau mbele ya magari mawili kutoka kwa mtu anaemfatilia na hio alilifanikisha na wakati tu ambao anakaribia Mwenge taa za kijani zilimruhusu kupita lakini kitendo cha kupita tu taa za rangi nyekundu ziliwaka na kuzuia magari yaliokuwa nyuma yake kupita.

Ilikuwa ni tukio la kushangaza kwani ilionekana kwa wale wanaoendesha magari kama taa hizo zilikosea kimahesabu katika kupitisha magari kwani taa iliwaka kwa sekunde sita tu na kuzima na kisha ikawaka nyekundu.

Mtu aliekuwa akimfatilia Roma katika gari aina ya Toyota Camry alitoa tusi kwa lugha ya kichina huku akigonga usukani kwa hasira na kujiapiza.

Sasa Roma alipokuwa katika eneo la Mbuyuni akikaribia Tegeta aliweza kupokea ujumbe kutoka kwa namba ambayo hakuwahi kuisevu lakini alikuwa akiikumbuka ilikuwa ikimtumia meseji za ajabu ajabu.

Roma licha ya kwamba aliweza kumpoteza mtu huyo lakini wasiwasi wake ni kwa Rufi kwani aliamini kama mtu huyo ataendeea kumfuatiia na kujua anapoishi na kuja mara kwa mara basi nafasi ya kumuona Rufi ingekuwa kubwa.

Ndio alikuwa ni msichana wa kichina afahamikae kwa jina la Xiao Xiao ambaye kwa maelezo ya Rufi alikuwa anatokea katika familia ya wakwe zake katika ulimwengu wa jamii za watu wasionekana za kichina.

Roma alipotezea kwanza swala hilo na kuwa na umakini katika kuendesha gari kwani muda umeenda, ndani ya dakika chache tu aliwea kufika nyumbani kwake na laishangaa kumkuta mtu akiwa amesimama nje ya geti na alipoangalia kwa umakini alikuwa ni Rufi na ilionyesha alishindwa kuingia ndani kwani alikuwa amefunga geti kabisa wakati wa kutoka.

“Rufi kwanini umenisubiri hapa, ungekaa nyumbani kwenu tu ningekukuta”Aliongea Roma mara baada ya kusimamisha gari.

“Ni sawa tu , nilikuwa nikipata hewa safi ya bahari”

“Msichana mjinga , huwezi kuvuna nishati za mbingu na ardhi na mishipa yako ya damu ni myembaba kwasasbu ya kiwango kikubwa cha nishati ya Yin, unatakiwa ujali afya yako upepo kama huu unakuumiza”

“Kweli?”

“Ndio”

“Nilipatwa na wasiwasi maana sikukuona siku zaidi ya tatu zote , nilikuwa na shauku kubwa ulivyosema utakuja kuungana na sisi kwa ajili ya chakula cha usiku, niishindwa kuvumilia ndani ndio maana nikaja kukusubiri hapa”Aliongea na kumfanya Roma kuguswa na matedo yake na kumwambia aingie kwenye gari waelekee nyumbani kwao , kwani ilikuwa ni upande wa pili.

Baada ya kufika na kuingiza gari ndani Roma alishuka na kumfugulia Rufi mlango na kisha alimshika mkono na kumfanya mrembo huyo kutoa tabasamu na kuona aibu kwa wakati mmoja.

Bi Wema alikuwa amenunua nyumba nzuri , ijapokuwa haikuwa kubwa kama ya kwao , lakini ilitosha familia ya watu saba na mazingira yake yalikuwa mazuri pia kufanya watu wanaoishi hapo kuonekana wa kipato cha juu , lakini ajabu kwake ni kwamba hakuwahi kuingia ndani , licha ya kwamba alipafahamu.

Baada ya kuingia ndani aliweza kuona ubunifu wa mapambo ya ndani haukuwa na utofauti na nyumbani kwake , kitu kidogo kiichotofatiana ni kwamba nyumba hio haikuwa na mapambo mengi eneo la sebuleni , ubunifu wake ulikuwa ni ule wanaoitwa Simple enterior design.

Bi Wema alitoka akiwa ameshikilia mabakuli akionekana alikuwa jikoni akiandaa chakula.

“Sir ushafika , karibu sana ndio naandaa chakula na kuna vitu vichache naendelea navyo muda si mrefu chakula kitakuwa tayari , karibu uketi”Aliongea Bi Wema kwa ukarimu.

Ukwei Bi Wema hapo alikuwa akimchukulia Roma kama Mkwe wake sio kwa Edna bali kwa mtoto wake wa kike Rufi.

“Halafu nimesahau kwenye gari nimenunu samaki , ngoja nikawalete”Aliongea Roma akitaka kutoka lakini Bi Wema alimzuia na kumpa kazi hio Rufi aifanye na Roma alitingisha kichwa kukubali na kumwachia Rufi ufunguo.

Muda wa saa mbili wakati Roma aipojikaribisha Mezani kwa ajili ya kushambulia chakula mlango wa kuingiia ulifunguliwa na kumfanya Roma ageuke na kumwangalia mgeni aliefika.

“Aisee, kunanukia vizuri jamani , naona nimechelewa , Bi Wema , Rufi nimekuja tena”Ilikuwa ni sauti ya Amina na kiswahili chake kisichonyooka na alijikuta akishangaa baada ya kumuona Roma pia yupo kwenye meza.

“Mpenzi kwanini uko hapa , na wewe umekuja kwa ajili ya chakula cha usiku?”Aliuliza kwa kingereza.

“Kwannini inaonekana kama vile unakuja mara kwa mara?”Aliuliza Roma huku akiwa ameupamba uso wake na tabasamu kwa furaha ya kumuona huyo mrembo na alishangazwa siku hio kumuona Amina akiwa amevalia Shungi kichwanni na kumfanya kupendeza zaidi.

“Anasema hajisikii kula peke yake , lakini pia anapenda mapishi ya Mama , amekuwa bize kwenye siku hizi chache hatujaonana kwa muda”Aliongea Rufi.

Amina kutokana na baba yake kusafiri kwenda nje ya nchi kimatibabu kwa mara nyingine alijikuta akiishi peke yake , kutokana na kwamba hakuwa na uzoefu na maswala ya biashara za baba yake ilimchukua muda mrefu kukaa kazini na kukamilisha majukumu yake.

“Mr unaweza ukawa hujui , ukweli ni kwamba Amina na Rufi ni marafikii wakubwa na kipidi ulipokuwa nnje ya nchi walikuwa wakitoka mara nyingi pamoja kufanya shopping na aimfundisha pia namna ya kujiremba”Aliongea Bi Wema.

“Yeah mimi sio kama nakula bure nafanya juhudi pia”Aliongea Amina na kisha aliweka chini mifuko aliokuja nayo na kusogea mezani.

Roma aligundua hakuwa makini na hawa wanawake, hakuwa na uelewa kwamba Rufi na Amina wamekuwa marafiki kama iivyokuwa kwa Dorisi na Rose kuwa marafiki, lakini ilileta maana , ukiachana na kwamba wote hawakuwa wakielewa vizuri kiswahili lakini pia walikuwa na tabia zinazoendana.

Muda wote wa chakula Amina alikuwa akipiga stori na Rufi ambazo hazikuwa na miguu wala kichwa na Roma hakutaka kuingilia zaidi ya kuweka umakini wake kwenye kula.

“Halafu sikukuona wiki nzima , ulikuwa umeenda wapi?”Aliuiza Rufi na kumfanya Amina kushika shingo yake kuizungusha kuonyesha ishara ya kuchoka.

“Nimekuja kugundua kuongoza kampuni sio mchezo , tokea nirithi nafasi ya baba yaani mambo ndani ya kampuni ni mengi , wakurugenzi wa bodi kazi yao ni kunilalamikia hili halipo sawa lile halipo sawa khaa”

“Nini kimetokea kwani?”

“Washindani wetu wa kibiashara wanahati hati ya kupata tenda ya kufunga mitambo ya gesi kwenye baadhi ya hoteli na majumbani hio ni mara baada ya kupata uwekezaji mkubwa kutoka nje ya nchi , nadhani unajua tunajihusisha zaidi katika uwekezaji wa nishati , sasa kama zabuni hio tukikosa hisa za kampuni zitaporomoka maana washindani wetu wanasapoti kubwa serikalini”Aliongea huku akitia huruma.

“Lakini kampuni yenu si ilifanya Merge na baadhi ya biashara zilizokuwa chini ya Tajiri Khalifa Tanzania , bado kuna kampuni inayoweza kuwaletea ushindani?”

“Hakika ipo , mambo kwasasa yanabadilika sana tena kwa haraka sana , ni rahisi kujenga kampuni yenye msingi mzuri wa kibiashara kadri utakavyokuwa na rasilimali watu wenye talanta kubwa ya ubunifu lakini pia wenye ushawishi wa juu , Washindani wetu inapokea sapoti kubwa kutoka serikaini hivyo kazi lazima ifanyike kwa umakini katika kudili nao , najihisi muda mwingine kuzimia nikiwa ofisini”

“Hubby tafadhari msaidie Amina anatia huruma , wewe si una hela nyingi kwanini usinunue hio kampuni?”Aliongea Rufi.

“Ujinga , kwanini nifanye hivyo wakati hawajafanya hila yoyote , wameonyesha ushindani wa haki na kama nitaingilia kwasababu tu mimi tajiri itanifanya nionekane muhun na sina maadilii, hata kama nikifanikiwa kununua vipi kuhusu makampuni mengine lazima na yenyewe niyanunue ili kumuondolea ushindani, haina haja ya kuwa na wasiwasi , Amina hata kama kampuni yako ikifilisika nitakuwa na pesa za kuwatunza wote”

“Okey nimeelewa , lakini sipendi kuona akipoteza kampuni ambayo ndio kwanza amepewa kuongoza”

“Nilishawahi kujiambia kuongoza kampuni sio jambo gumu sana lakini tokea nilivyopewa majukumu yote na baba , niligundua ni kazi ngumu mno , kuna baadhi ya vitu najikuta kwenye Dilemma hata kuvitolea maamuzi , nimejikuta nikimkubali Dada Edna , Ameweza kuwa CEO wa kampuni katika umri mdogo lakini anazidi kung’ara tu”Aliongea kwa kulalamika , lakini mara baada ya kmtaja Edna moyo wa Roma ulishituka tena na hata hamu ya chakula ikapungua palepale.

“Sir sijawahi kukuuliza , Je ulienda kumtafuta Edna nakuongea nae kwenye siku hizi mbli , amekubali kurudi nyumbani?”Aliuliza Bi Wema mara baada ya kusikia jina la Edna, kwa wakati huo Bi Wema alikuwa akijua kingeereza licha ya kwamba alikuwa na ugumu kwenye kuongea lakini aliweza kusikia baadhi ya maneno na alijifunza kwa ajili ya Rufi.

Amina na Rufi walimwangalia Roma wakitaka kusikia jibu kutoka kwake kuhusu Edna, lakini swali hilo lilimfanya Roma kuvuta pumzi na kuzishusha.

“Bi Wema nafikiri Edna hatorudi nyumbani hivi karibuni?”

“Kwanini unaongea hivyo , nini kimetokea?”Aliliza Bi Wema kwa wasiwasi na Roma hakuona haja ya kuwaficha na aliwaeleza mambo alioyafanya katika siku zote alizoenda kuongea na Edna na kuchomolewa.

“Bi Wema nashindwa kujua ni namna gani naweza kumaliza tatizo , nilimpelekea kifungua kinywa kwasababu nilikuwa nikimuwazia lakini badala ya kunipoktea alinishuku na Recho ambaye nilimkuta ofisini akiwa yeye hajafika kazini, kwanini akaanza kupandisha jazba na kutaka ugomvi?”Aliongea kwa kulalamika na kumfanya Rufi na Amina kiumwangalia kwa huzuni na walishindwa kuongea chochote.

“Mr Najua umekasirika namna ambavyo Edna anakufanyia lakini naamini anajua unafanya hayo yote kumbembeleza , lakini muda mwingine wanawake wanapofikiria kitu hawazingatii kipi ni sahihi na kipi sio sahihi wala kujali nani anatakiwa kuwajibika “

“Kwahio anataka nini sasa?”

“Mtazamo wako”

“Mtazamo wangu?”

“Ndio wanawake wanajali sana mtazamo wa mwanaume kwao , inaweza ikaonekena labda napindisha lakini hata kama amefanya makosa kukufanyia hivyo , mtazamo wako ndio tatizo , kwa mfano ulienda anapoishi kuomba msamaha lakini hukumtaarifu kwamba unaenda na ulienda kama vile atakusikiliza na kukusamehe hapohapo, nadhani hicho kimemfanya ajisikie vibaya zaidi , Edna anatabia ngumu sana kuzoeleka lakini ni mtu mkarimu na mwenye moyo mzuri, angekusamehe kama ungeongea nae vizuri , kuhusu kifungua kinywa cha leo nadhani usingemjibu wala kuonyesha kukasirika , alikuwa anajaribu kutafuta sababu tu ya kukukasirikia , sidhani kama alifikiria kweli kuna kitu kinaendelea kati yako na Recho”Aliongea Bi Wema na Roma aliona ni sahihi , alikuwa akijiamini sana mambo yangekuwa marahisi kwake kusamehewa , ijapokuwa aliomba msamaha kwa dhati lakini hakuonyesha uhatari wa kuona kwamba hatosamehewa alionyesha mwonekano ambao ni kama vile ni haki yake Edna kumsamehe na hapo ndio alipoona amekosea..

“Bi Wema upo sahihi , lakini bado naweza kusema mpaka sasa hatua ambayo tumefikia sidhani mambo yatakuwa marahisi na sioni sababu yake ni hasira zake juu yangu kumshuku au kuna mengine , sina mpango wa kumtafuta kwa sasa”Aliongea Roma.

“Unaonaje mimi nikienda na kuongea nae?”Amina aliongea na kumfanya Roma kucheka.

“Amina humuogopi Edna ?”

“Namuogopa ndio lakini sidhani kama atakataa kuonana na mimi , kwasababu siku zote ananichukulia mimi ni mwepesi kwake .. ninaweza kwenda na kumuuliza baadhi ya mbinu za kibiashara pia”Aliongea na kumfanya Roma kufikiria.

Ijapokuwa aliona sio wazo zuri kwani lingemkasirisha zaidi Edna , ila aliona ni kheri Amina na yeye kwenda kujaribu maana yeye amekwama.
ITAENDELEA - MAWASILIANO 0687151346
Watsapp tunaelekea mwishoni mwishoni mwa hii simulizi... tunaelekea sehemu ya 700 wiki hii nicheki kama unahitaji mwendelezo
 
Ufafanuzi
Katika hii simulizi nimetumia neno Dhana tofauti na Zana kwa makusudi ya kuongezea maana ya kiimani ya maajabu( Belief's or Sense of mystery) ....
Zana ni kifaa lakini neno Dhana ni zaidi ya kifaa....Hivyo sijakosea kusema neno Dhana tofauti na Zana...

Kama upo makini utagundua nimetumia herufi kubwa kwa kila neno Dhana.

Mwishoni nitaweka reference ya vitabu baadhi.
Mengine ni makosa ya kiuandishi na yanafanyiwa kazi wakati kitabu kitakapotoka...
 
Kuna kigongo kipya kitaingizwa Jf kwa mara ya kwanza kabisa.
Wale wapenzi wa vitu vya kijasusi vilivyoshiba msikose hii kitu ..(MABADUNI WA SERIKALI).
Kigongo kina sura sita tu, na bado sura mbili kikamilike.


Ningepost lakini naijua arosto ya wadau humu wanaweza kukuombea dua mbaya hivyo naiheshimu sana hadhira.
Wakosoaji wasikose, narudia tena, wasikose. Maana wanaleta ukamilifu ambao nautaka...
SOON TO BE THERE.
 
Kuna kigongo kipya kitaingizwa Jf kwa mara ya kwanza kabisa.
Wale wapenzi wa vitu vya kijasusi vilivyoshiba msikose hii kitu ..(MABADUNI WA SERIKALI).
Kigongo kina sura sita tu, na bado sura mbili kikamilike.


Ningepost lakini naijua arosto ya wadau humu wanaweza kukuombea dua mbaya hivyo naiheshimu sana hadhira.
Wakosoaji wasikose, narudia tena, wasikose. Maana wanaleta ukamilifu ambao nautaka...
SOON TO BE THERE.

Seem like unatafuta attention, siku zote kizuri kinajiuza kibaya kinajitembeza. Ukishaanza kusaka attention hivi bila shaka story mbaya, afu unakuja kwenye nyuzi za wanaume wenzako kutafuta antention
 
Seem like unatafuta attention, siku zote kizuri kinajiuza kibaya kinajitembeza. Ukishaanza kusaka attention hivi bila shaka story mbaya, afu unakuja kwenye nyuzi za wanaume wenzako kutafuta antention
Usipende kushambulia kila mtu
Hasa inaniuma unanishambulia na unatumia ID yetu
 
Usipende kushambulia kila mtu
Hasa inaniuma unanishambulia na unatumia ID yetu

Nimekwambia Ukweli wewe kama una uzi ushushe sio kusaka attention, mwenzako Singano hakusaka attention kama wewe hata Insider kule hakusaka attention ila fans wanasoma wenyewe.
 
Usipende kushambulia kila mtu
Hasa inaniuma unanishambulia na unatumia ID yetu
Seem like unatafuta attention, siku zote kizuri kinajiuza kibaya kinajitembeza. Ukishaanza kusaka attention hivi bila shaka story mbaya, afu unakuja kwenye nyuzi za wanaume wenzako kutafuta antention
Pia nikukumbushe tu,
Nigga Pac sina issue personal na wew
Natangaza tu Sanaa yangu, pia kama nakukera nisamehe but yote kwa yote subiri Nikianzisha uzi nitakutag wew kwanza ili uwatag na wenzio sina bifu mkuu Pia umenionesha kuwa ujumbe umekufikia Ahsante.
 
Nimekwambia Ukweli wewe kama una uzi ushushe sio kusaka attention, mwenzako Singano hakusaka attention kama wewe hata Insider kule hakusaka attention ila fans wanasoma wenyewe.
Attention ni muhimu sana Nigga Pac
Hata Pepsi na Coca wanalipia matangazo daily na tunawafaham zaidi ya miaka 20 sokoni.
Huwezi kunizuia, Najua nachokifanya maana mimi ni mtu wa branding pia.
Riwaya ni property yangu so I have to go for all on it.( Market)
 
Pia nikukumbushe tu,
Nigga Pac sina issue personal na wew
Natangaza tu Sanaa yangu, pia kama nakukera nisamehe but yote kwa yote subiri Nikianzisha uzi nitakutag wew kwanza ili uwatag na wenzio sina bifu mkuu Pia umenionesha kuwa ujumbe umekufikia Ahsante.
Mim nadhan ilete story tuione.tujue ipo kama roma ramom au chenga. Mwenzako kafanya research ya nguvu.
Hebu na wewe ilete yako tuione
 
Mim nadhan ilete story tuione.tujue ipo kama roma ramom au chenga. Mwenzako kafanya research ya nguvu.
Hebu na wewe ilete yako tuione
Ya Roma Ramoni ni magical, na inaruhusiwa mtunzi kuchagua aina ya Riwaya iwe Fictional au ya kawaida inayoakisi maisha ya watu wa kawaida.
Mimi siandiki magical natembea na visa vya maisha ya kawida tu
Ingia youtube search "SOKORO" ili upate taste ya uandishi wangu kisha uje uniambie kama inafaa nianzishe uzi au lah!!!
 
Tusiandike mate wakati wino upoo!
Ya Roma Ramoni ni magical, na inaruhusiwa mtunzi kuchagua aina ya Riwaya iwe Fictional au ya kawaida inayoakisi maisha ya watu wa kawaida.
Mimi siandiki magical natembea na visa vya maisha ya kawida tu
Ingia youtube search "SOKORO" ili upate taste ya uandishi wangu kisha uje uniambie kama inafaa nianzishe uzi au lah!!!
 
Back
Top Bottom