SEHEMU YA 84
TEXAS-DALLAS
11 YEARS AGO(MIAKA KUMI NA MOJA ILIOPITA)
Ni tarehe ishirini na tatu kuamkia ishirini na nne mwezi wa kumi na mbili ndani ya jimbo la Texasi jijjini Dallas , ndani ya makazi ya watu, sehemu inayofahamika kwa jina la Greenville Avenue muda wa saa sita usiku.
Mwanamama wa umri wa miaka arobaini hivi aliekuwa akifahamika kwa jina la Mary , alionekana akishituka kutoka usingizini , baada ya kulala muda mrefu, mwanamama huyu baada ya kishituka alijikuta akipapasa mkono wake upande wa kushoto pasipo kugeuka kwa nia ya kutafuta mwili wa mime wake Phill, lakini mwanamama huyu baada ya kupapasa juu na chini mkono wake haukuambulia kitu na hii ilimfanya anyanyuke na kukaa kitako na kugeuza macho yake kulia, na hapo alijikuta akitoa shuka taratibu baada ya kumuona mume wake aliekuwa amepitiwa na usingizi katika meza yake ya kusomea huku pembeni ilionekana Printer ambayo na yenyewe ilionekana kuwa imewashwa pamoja na tarakishi.
Bi Mary alionekana kumuonea huruma mume wake kwa kitendo cha kupotelea usingizi akiwa mezani anasoma,mwanamama huuyu ambaye alikuwa amevalia nguo za kulalia alitembea kusogea upande ambao mume wake amelala kwenye meza ,na kabla hajamgusa ili aamke , mara Printer ilianza kutoa mlio wa sauti ya Kuprint karatasi.
Bi Mary alijikuta akighairisha zoezi lake na kisha kuchukua baadhi ya karatasi ambazo zilikuwa zikitemwa na Printer hio, karatasi ya kwanza ndio iliomshangaza mwanamama huyu:
Kwanza kabisa karatasi hio ilikuwa na ‘watermark’ ya neno ‘Confidential’ , ilionekana ilikuwa ni nyaraka ya siri ambayo Mume wake Phill alikuwa akiisubiria kiasi kwamba alijikuta akisinzia kwenye meza.
Bi Mary alijikuta akianza kutetemeka mikono kadiri alivyokuwa akisoma karatasi hio , huku mume wake akiwa bado amelala , mwana mama huyu alielewa kabisa taarifa hio ni nyeti , lakini kutokana na taarifa yenyewe kumshangaza alijikuta akiendelea kusoma, alimaliza katatasi ya kwanza akachukua nyingine akaimaliza , huku kila karatasi anayosoma ikimuacha mdomo wazi , alisoma nukta hadi nukta mwanamama huyu ambaye kazi yake kubwa ni kuuza maua.
Baada ya Bi Mary kumaliza kusoma , alijikuta mwili wake ukikosa nguvu , alichukua karatasi alizokuwa ameshikilia na akazirudisha kwenye mdomo wa Printer na baada ya kumaliza kusoma , alijikuta hata kile ambacho kimemsogeza kwenye meza aliolala mume wake Phill ,alisahau m alijongea na kurudi kwenye kitanda na kisha akajilaza na kujifunika shuka.
“Evidence regarding killing of Professor Banos and M-Airline Plane dissapearencce”
“Detailed Plan to Eliminate the World coming Enemy”
“Project LADO success Rate”
“Twelve Greek God`s to faight against the Wold Coming Enemy”
Hivyo ndio vichwa vya habari ambavyo Bi Mary alikuwa amevisoma na alikuwa akivifikiria akiwa ndani ya Blanketi huku machozi yakiwa yameujaza uso wake, hakuwamini kabisa kwa kile alichokiona.
Kulivyokucha Mary alijitahidi kuwa wa kawaida mbele ya mume wake amaye tayari alikuwa amevaa suti kwa ajili ya kuelekea kazini , ambayo Bi Mary siku zote alikuwa akijua mume wake alikuwa ni Mhandisi ndani ya kampuni ya kutengeneza magreda ya kuchimbia barabara.
Bi Mary aliwaangalia watoto wake watatu kwa namna ya kuwaonea huruma , na kisha akamgeukia mume wake Phill ambaye alionekana kutabasamu muda wote.
“Mary Yo seem to be off today , what the matter , Tomorrow is Christmas , why you are not happy like everyone else, Come on tell me”
“No Phill , I am fine ,Why?”
“Its nothing Mary if you are fine , then it`s okay , I will be off to work now”Aliongea bwana huyu na kisha alimsogelea mke wake na kumbusu shavuni na kisha akahamia kwa watoto wake wote ambao mmoja wa kike alikuwa na miaka kumi na mbili mwingine kumi na mmoja mine.
Baada ya dakika kadhaa za Phili kutoweka kwenye macho ya Mary , alikimbilia chumbani kwake na kuanza kutafuta zile karatasi sehemu ambazo alikuwa akiamini atazipata , lakini hakuweza kuzipata.
“Atakuwa ameenda nazo”Alijiongelesha huku akijilaumu kwanini hakupiga picha
“Pastor Edwardo , I have something very important to discuss with you”Aliongea akimaanisha kwamba anajambo la kuongea na mchungaji aliemtaja kwa jina la Edwardo na hii ni baada ya kusalimiana.
“Unaonaje mara baada ya mkesha wa leo , litakuwa jambo zuri , maana mchana wa leo ratiba zimebanana”Ilisikika sauti upande wa pili na Mary akakubaliana na Pastor.
“Sijui kama ninachofanya ni sahihi , lakini naamini ni vyema nikiongea na kiongozi wa dini , Phill sio wa kunidanganya mimi kwa Zaidi ya miaka ishirini tokea tuone, he is undercover agent with Zeros Organisation all this time?, Damn you Phill”Alijiongelesha mwanamama huyu huku akianza kutoa machozi ,alionekana taarifa ya jana usiku aliosoma ilikuwa ni kubwa kwake na yenye kumuumiza.
Usiku wa saa sita hivi kwenda saa saba za usiku ndipo tukio la kutisha lilipotokea na mkurdish Afshar alivyofanya yake ya kuwarushia risasi waumini wa kanisa la
The Forgivven.
Upande wa Pastor na Mary walikufa wakiwa ndani ya chumba ambacho kilikuwa kinatumiaka kama ofisi ya mchungaji ndani ya kanisa hili la
The Forgiveen.
Watoto watatu wote wa bwana Phill mzungu walikufa ndani ya tukio hilo wakiwa pamoja na mama yao.
Nini kilitokea , ni siri gani iliop juu ya mpango LADO , Nyaraka ya siri aliosoma Mary inamaanisha nini juu ya Adui wa ulimwengu anaekiuja, kwanini The God`s ndio inatakiw akupambana na Adui utaelewa kadiri tunavyosonga.
*****
Ni jumamosi muda wa saa moja kamili Mrembo Rose mmiliki wa kundi la Tembo alionekana kuwa ni mwenye wasiwasi sana , huku akiwa ndani ya gari iliokuwa ikielekea Kisarawe.
Mwanadada huyu , jambo ambalo lilimfanya kuwa na wasiwasi ni kutokupatikana kwa Roma hewani, kwani alijaribu kwa Zaidi ya mara kumi kwa muda tofauti , lakini bado hakuweza kumpata hewani.
Ile hali ya kujiamini aliokuwa nayo Rose , ilikuwa imepotea , alikuwa akijiamini kwa ajili ya mpango wake kutokana na kwamba alikuwa na uhakika wa Roma kuwepo , lakini sasa mtu ambaye alimuahidi kwa ajili ya kwenda nae Kisarawe kwenye sherehe iliokuwa ikihusisha maadui zake ndani ya biashara ya madawa ya kulevya hakuwa akipatikana.
“Hubby Come on!,Where are you?” Mwanamke huyu alikuwa akipiga piga simu yake mapajani huku akiwa ni mwenye kujiuliza Roma yuko wapi , alikuwa akipata hisia ambazo ni kama za mwanamke ambaye alikuwa ametelekezwa.
“Boss uko sawa?”Aliuliza Zonga ambaye muda huu alikuwa akiendesha gari.
“Niko sawa Zonga”
“Bosi usiwe na wasiwasi , mpango wetu lazima ufanikiwe , vijana tuliowapandikiza ndani ya kundi la Fupa Faru ni mzuri sana na Situ hawezi kuchomoka”Aliongea Zonga huku akiwa ni mwenye kujiamini , lakini licha ya hivyo kwa Rose bado hakuwa akijiamini.
Masaa kadhaa nyuma alikuwa akijiamini pale alipokuwa akikumbuka kuwa Roma ataongozana nae kwenye sherehe hio, lakini sasa kule kujiamini kulikuwa kumepungua kwa asilimia sitini.
Ndani ya dakika Arobaini na tano tu , walikuwa wakiingia ndani ya eneo la Ngekewa , ambapo ndipo linapatikana jumba lake la kifahari ambalo kwa sasa lilikuwa chini ya baba yake Situ mmiliki wa kundi la Fupa Faru.
Zonga alimfungulia mlango bosi wake mara baada ya kufika getini muda huu wa usiku wa saa mbili , na walinzi wa kundi la Fupa Faru , waliwapapasa kuhakikisha kama hawana siraha na baada ya hapo waliruhusiwa kuingia ndani.
Sherehe ilionekana kufanyikia eneo la nje ya nyumba kwenye bustani , ndani ya jumba hili ambalo kwa muonekano wake utadhani ni kasri , lilikuwa ni jumba kubwa ambalo ungeambiwa aliekuwa mmiliki ni Rose ungeshangaa.
Rose aliangalia watu waliokuwepo hapa ndani , alikagua mazingira yote na alijikuta akiridhika mara baada ya kuona baadhi ya vijana wake wakiwa ni walinzi nay eye mwenyewe alishangaa , kwani vijana wake pekee ndio walionekana kuwa walinzi licha ya mpango wao, alikuwa akiamini watakuwa walinzi mchanganyiko na wa kundi la Fupa Faru.
Unajua Situ alikuwa na vijana wengi sana , ambao walikuwa kwenye kundi lake la biashara na hakuwa akiwajua wote hivyo hii ilikuwa rahisi kwa rose kuingiza kikosi chake kwa siri kwa kuua baadhi ya vijana wa kundi la Fupa Faru.
Rose alikuwa amependeza sana usiku huu , alionekana kuwa kama malkia na hapa ndani licha ya kwamba walikuwa wapo wanawake warembo , lakini kwa Rose hakuna ambaye alikuwa akimfikia , ukiachana na uzuri wa Rose pia vazi alilokuwa amevaa usiku huu , lilikuwa sio la kawaida na baadhi ya wanawake walimwangalia na kujiuliza ni mwanamitindo gani ameweza kumtengenezea gauni hilo Rose , kwani lilikuwa na uzuri usio wa kawaida , lakini pia lilionekana kuwa na gharama kubwa.
Rose alijikuta akijisikia faraja baada ya kuona watu walivyhokuwa wakimwangalia kwa namna ya kumhusudu , wanaume kwa wanawake.
Zonga nae hakuwa nyuma, alikuwa amependeza na suti yake nyeusi , huku akijirembesha na kijiua kilichokuwa kwenye mfuko wa koti cha rangi nyekundu.
“Mungu nisaidie jaribio hili lifanikiwe , sijui ni nini kimemkuta Roma , najua ananipenda na chochote kinachoendelea naomba Mungu amlinde”Aliongea mwanadada huyu na haikueleweka alikuwa akiomba Mungu gani amlinde Roma kwani ni siku nyingi sana alikuwa ashaachana na mambo ya dini.
Wakati akiwa amesimama huku akisogea upande wa walipo wageni , mara alisogelewa na muhudumu wa kiume alievalia suruali nyeusi pamoja na shati jupe na kikofia.
“Mrembo umependeza sana leo , unaonaje ukitumia kinywaji ambacho nimekiandaa kwa ajili yako Usiku huu”Aliongea kwa sauti ya chini kidogo na kumfanya Rose atoe macho.
“Romaa…!”Rose hakuamini mtu aliekuwa mbele yake ni Mwanaume anaempenda m Roma, alitamani amrudikie.