Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

mnaosema niweke mwendelezo wikiend hii mjitokeze
Wewe sema unataka wafike watu wangapi ili uweke muendelezo[emoji28] au tuambie unataka likes ngapi tuzipige chap maana ukisubiria kila anayesoma story aseme tupo itachukua muda na wengine huwa hawacoment wanasoma then wanasepa.... ila kwa sasa hii ndiyo story inayofuatiliwa zaidi hapa JF
 
SEHEMU YA 118

Mheshimiwa Raisi Kamau alionekana kuwa na wasiwasi mwingi mno na hii ni baada ya kukosekana hewani kwa Dondwe na kumfanya kutofahamu ni nini kinaendelea nchini Tanzania.

Bwana huyu alijilaumu sana kumruhusu Maina kwenda Tanzania pasipo kuchukua tahadhari zozote.

Ukweli ni kwamba baada ya Maina kupanda ndege na baada ya masaa mawili kupita ndipo mheshimiwa alipopewa ujumbe na Deo kuwa inawezekana Madam anaenda kuonana na mke wa tajiri Azizi.

Baada ya mheshimiwa Kamau kupata hii taarifa , alitafuta namna ya kuhakikisha taarifa hio na hapo ndipo alipompigigia mtu wake aliempandikiza ndani ya familia ya Tajiri Azizi na ni kweli alipewa taarifa kwamba Mke wa Tajiri Azizi yaani Jestina alikuwa na ratiba ya kwenda kituo cha kulelea yatima cha Son And Daughter Orphanage, na mpaka hapo ndipo Kamau alipopata kujua jambo ambalo Maina alikuwa akilifanya , alishangaa sana na kuona ni kwanini Maina hakumshirikisha.

“Inanipasa kutulia naamini Blandina anataka tu kuonana na familia yake , na hatoongea Zaidi ya anayoyajua , napaswa kumuamini”Aliwaza Mheshimiwa Kamau huku akichukua maji kwenye glasi na kunywa kidogo ili kujituliza , lakini licha ya kujiambia maneno hayo bado bwana huyu alikosa utulivu kwenye akili yake.

*****

“Mheshimiwa Maina amefanikiwa kuonana na familia yake leo”Aliongea Linda mlinzi wa raisi Jeremy na kumfanya mzee huyu kutabasamu.

“Iliwezekana vipi Kamau akashindwa kumzuia mke wake?”

“Kwa taarifa za watu wetu nchini Tanzania wanasema raisi Kamau alijitahidi kuzuia , ila alishindwa kutokana na Roma kuingilia”Jeremy alitoa macho na kumwangalia Linda ni kama hajasikia vizuri.

“Ilikuwaje Roma akawa ndani ya hiko kituo?”

“Mpaka sasa sijapata taarifa Zaidi Mheshimiwa”.

“Hili swala sikudhania litatokea mapema hivi nadhani ni muda sasa wa kuanzisha mpango wangu niliokuwa nao miaka mingi , lakini bado namuonea huruma Senga”Aliongea Jeremy.

“Lakini Mheshimiwa Naamini Mheshimiwa Kamau hakuna anachokifahamu kuhusu mpango LADO”

“Linda unachoongea ni kweli na mimi nataka kuamini hivyo na nimekuwa nikijitahidi miaka na miaka kuamini hivyo , lakini mienendo ya Kamau haijawahi kunifanya nimwamini , kumbuka Kamau ndio mtu pekee aliekataa kuingia kwenye mpango TASAC licha ya kumlazimisha”

“Naelewa Mheshimiwa lakini bado naona ni swala ambalo linakosa muunganiko , maana swala la kupotea kwa ile ndege ni swala ambalo ni zito mno kwa mtu kama Kamau kulifahamu”Aliongea Linda na kumfanya Mheshimiwa Jeremy awaze kidogo.

“Nadhani swala hili tuangalie DS ya Tanzania watalitolea vipi maamuzi swala la Blandina, Endelea kufuatilia ni sababu gani Roma alikuwepo kwenye kituo cha Son And Daughter Orphanage”

“Sawa Mheshimiwa” Aliongea Linda na kisha akatoka.

DS ni kirefu cha maneno ya ‘Deep State’ au kwa Kiswahili unaweza kusema Serikali ya ndani,DS ni kikundi cha watu ndani ya nchi ambacho kinakuwa na nguvu ya kufanya maamuzi ya kisela katika Nyanja zote , hawa DS ni rahisi kusema wanauwezo wa kuamua ndani ya taifa raisi awe nani kutokana na nguvu yao na mara nyingi wanafanya kazi kwa siri sana.

******

Edna alijikuta akijishangaa kulala muda mrefu mno kuliko isivyokuwa kawaida , saa saba na nusu mrembo huyu alishituka kutoka usingizini na kuanza kukumbuka ni muda gani alilala maana alikuwa na nguvo alizovaa jana yake.

“Ni Roma yule Shetani Sijui alinifanyia nini?”Mrembo huyu alionekana kukumbuka tukio lililotokea , alikumbuka namna ambavyo Roma alimkumbatia kwa nyuma na kwanzia hapo hakuelewa nini kiliendelea.

Edna alijinyanyua kivivu kitandani na kuangalia saa kupitia simu na hapa ndipo aliposhituka , hakuamini ilikuwa ni saa saba mchana , kwani licha ya kwamba alijua amelala muda mrefu , lakini hakujua kuwa siku ilikuwa ikikaribia kuisha , alikumbuka simu yake nyingine iliokuwa kwenye mkoba wake na kuitoa haraka na kuangalia ni nani kapiga na kweli kulikuwa na ‘missed calls’ nane kutoka kwa Monica lakini pia kulikuwa na ujumbe wa maandishi.

“Madam muwekezaji Yan Buwen kutoka China keshafika nchini , Nakupigia hupatikani nimesogeza ratiba ya wewe kuonana nae saa moja za leo jioni”

Ulikuwa ujumbe kutoka kwenye simu ya Edna hakukuwa na jumbe nyingine za muhimu Zaidi na kumfanya mwanamke huyu kuvuta pumzi ya afadhali.

“Miss umeamka?”Ilikuwa ni sauti ya Bi Wema aliekuwa akiandaa chakula mezani na kwa harufu tu ya chakula ilimfanya Edna kuhisi njaa.

“Nimelala sana Bi Wema leo , kwanini hamkuniamsha?”

“Roma alituambia tusikuamshe mpaka utakapo amka mwenyewe na sisi tuliona ni sawa maana ulifanya kazi sana wiki hii pasipo kupumzika”Aliongea Bi Wema na Edna hakubadili muonekano wake , ila alikuwa akiwazia ni nini Roma alimfanya mpaka kulala muda mrefu, alijua Roma sio mtu wa kawaida lakini hakudhania kama anaweza kumfanya pia mtu kulala muda mrefu.

“Miss Mbona haukuniambia kama Yezi amepatikana?”Aliongea Bi Wema na kumfanya Sophia ajiulize Yezi ni nani.

“Ndio Bi Wema nilisahau , mambo yalikuwa mengi ,Roma ndio kakuambia?”

“Ndio kaniambia leo asubuhi na kampeleka kituoni kuonana na Mama Issa”Edna alishangaa kwasababu hakuwa na hio taarifa.

******

Upande mwingine ndani ya hoteli ya Serena alionekana bwana mmoja hivi wa Kichina aliekuwa amevalia taulo la rangi nyeupe ndani ya hoteli hii akiwa ameshikilia glasi ya wine huku akiwa amevalia miwani yake , kwa kumuangalia tu bwana huyu utafahamu umri wake haukua ukizidi miaka Arobaini.

Wakati bwana huyu akiangalia mandhari ya nje yajiji hili , simu yake ya chumba iliita mfululizo na kumfanya ageuke na kuisogelea na kisha aliipokea.

“Mr Yan Una mgeni eneo la mapokezi anafahamika kwa jina la Scorpion”Aliongea mwanadada wa mapokezi na kumfanya Bwana huyu atabasamu na kisha alijibu kwa Kingereza kama amruhusu aje.

Baada ya kama dakika tano aliingia mlinzi wa kike wa mheshimiwa Kigombola aliekuwa akifahamika kwa jina la Scorpion , alikuwa amevalia mavazi yake ya suti nyeusi akiwa na miwani ya jua , licha ya mwanadada huyu kuwa na sura ngumu lakini leo hii alipendeza.

“Karibu sana Sciorpion , ni muda mrefu hatujawahi kuonana tokea uje Tanzania”Aliongea Yan Buwen huku akitabasamu lakini Scorpion hakutoa aina yoyote ya tabasamu mlinzi huyu alikuwa kauzu hatari.

“Umekuja Tanzania kufanya nini Yan Buwen?”Aliuiza Scorpion kwa sauti ya kibabe.

“Nadhani unajua kwanini nipo hapa Tanzania mpaka muda huu”

“Kama umekuja kwa ajili ya jiwe la Kimungu sahau , washalichukua Yamata”

“Hahaha..Scorpion Baada ya kuja Tanzania naona uwezo wako wa akili umeshuka kwa Zaidi ya asilimia hamsini , Watanzania wamekudumaza kama walivyodumaa”Aliongea Yan Buwen kwa kejeli.

“Unamaanisha nini?”

“Yamata wamepewa jiwe feki , hivi unamchukuliaje Hades wewe, ndio maana nakuambia uwezo wako umedumaa , ulivyokuwa chini yangu haukuwa hivyo Scorpion”Aliongea Yan Buwen na kumfanya Scorpion ashangae.

“Una uhakika ni jiwe feki?”

“Ndio maana nipo hapa Tanzania, The Don anataka hilo jiwe kwa namna yoyote na niimekuita tuonane ili unisaidie kuandaa mpango wa kupata jiwe hilo”.

“Mpango Gani unapanga ili hali unajua hatuna uwezo wa kupambana na Hades”

“Hatuna haja ya kupambana na Hades ,The Doni mwenyewe atapambana nae”Aliongea Yan Buwen kwa tabasamu na alionekana kuwa na shauku kubwa.

“Sasa kama The Don ndio anakwenda kupambana na Hades tunaandaa mpango wa nini?”Aliuliza Scorpion na Yan Buwen alikunywa kidogo kinywaji chake halafu akatabasamu.

“Yapo mambo mengi haufahamu Scorpion na siku sio nyingi utakuja kugundua angalau nusu yake , ujio wangu hapa Tanzania ni kutaka kuhakikisha kama jiwe hilo lipo hapa au Hades kalificha nje ya Tanzania , hio ndio sababu ya mimi kufika hapa Tanzania , lakini pia nadhani mpaka sasa haujafahamu kwanini The Don alikupa maagizo kukaa karibu na mheshimiwa Kigombola?”Scorpion alitngisha kichwa kuonyesha hajui.

“Okey ukikamilisha kazi nitakayokupa siku ya leo, nitakuambia kila kitu”Aliongea na kisha akanyanyuka na kutoa picha na kumpatia Scorpion”

“Nahitaji kusikia kifo cha huyo mtu kabla ya kesho asubuhi”Aliongea Yan buwen na Scorpion aliangalia hio picha na kisha akavuta pumzi.

“Kwahio hili ni dili , nakamilisha kifo cha huyo mtu na utaniambia kwanini The Don kanileta Tanzania”.

“Hahaha…Scorpion , hupaswi kuwa na wasiwasi licha ya kwamba naonekana kama mtu ambaye siaminiki , lakini kuhusu hilo nitakutimizia , Ndani ya dunia hii ni mimi pekee ambaye namfahamu The Don kwa kumuona Hata raisi wa Marekani anamsikia tu … hahahaha”

SEHEMU YA 119.

“Baba , Dada naomba mnisamehe….Hii..Hii”Blandina alikuwa akilia mpaka anatia huruma ,Jestina ambaye alikuwa amekaa upande wa kushoto ndani ya ofisi hii ya Mkuu wa kituo, alimuonea sana huruma dada yake.

Mzee Atanasi licha ya kwamba alikuwa na hasira juu ya mtoto wake huyoo wa kwanza katika familia yake , lakini kwa namna ambavyo Bladnina alivyokuwa akilia na kuonesha hali ya kujutia , alijikuta kama mzazi moyo ukiuma, alijua ni ujasili pekee ambao alikuwa nao Blandina kwa kuishi Zaidi ya miaka ishirini ndani ya sura bandia.

“Dada usilie tena, wote tunahisi maumivu yako uliopitia kwa miaka yote hio,tunafuraha baada ya kuona upo hai”Aliongea na kunyanyuka na kwenda kumkumbatia dada yake.

Mzee Atanasi licha ya uzee wake wa miaka mia moja , lakini mzee huyu akili yake bado ilikuwa ikifanya kazi , muda huu mzee huyu haikueleweka ni nini alichokuwa akiwaza katika akili yake , lakini hisia mchanganyiko zilijionyesha kwenye macho yake.

Baada ya takribani nusu saa kupita za Blandina kueleza nusu ya kile kilichomfanya kutoitaarifu familia yake juu ya yeye kuwa hai, hatimae mzee Atanasi aliona ni wakati wa kutoa maamuzi kama kiongozi mkuu wa familia.

Ukweli ni kwamba kabla ya Mzee Atanasi kuja ndani ya kituo hiki kuonana na Blandina , alikuwa ashakaa kikao na ‘National Senior`s’ na kulizungumza hili swala na hii ni kutokana na kwamba swala la Blandina lilikuwa likihusisha nchi ya Tanzania na Kenya moja kwa moja.

National Senior`s ni sawa na kusema DS au Deep State ,Mzee Atanasi alikuwa ndani ya kikundi hiki ambacho kilikuwa na maamuzi makubwa ndani ya Taifa, licha ya kwamba maamuzi yao wanaoyafanya hayakuwa yakifahamika moja kwa moja ndani ya taifa , lakini raisi wa Tanzania pamoja na wasaidizi wake walikuwa wakiyatimiza.

Sasa Mzee Atanasi alikuwa akija hapo kweye kituo akiwa na maamuzi tayari ambayo washayajadili na maamuzi hayo hayakuwa yamejadiliwa na DS wa taifa la Tanzania pekee bali pia yalikuwa yamehusisha na DS wa taifa la Kenya.

Unatakiwa kujua kwamba ni mara chache sana ya wanachama wa DS kumhusisha Raisi katika vikao au viongozi wakubwa wa nchi , DS mara nyingi inakuwa inajitegemea na haiuhusishi viongozi ambao wapo ndani ya mfumo wa moja kwa moja wa uongozi , wao mara nyingi wanapokea miongozo kutoka kwa kikundi hiki tu, kipi wafanye na kipi wasifanye kwa maslahi yao , na hii haipo kwa Tanzania tu ni karibia duniani kote kila nchi ina DS ambayo haihusishi mfumo wa kiuongozi wa moja kwa moja, bali wanakuwa wanajitegemea , ni mara chache sana kumkuta Raisi wa nchi alie madarakani kuwa ndani ya DS , ila Raisi akishastaafu ni rahisi kuingia kwenye DS na hapa ndio maana unaona Mheshimiwa Kamau alikuwa akitaka kuzuia Maina asionanae na Familia yake , lakini wakati huo huo DS wa Kenya walikuwa wanajua kila kitu kuhusu Maina na baada ya kitendo cha Maina kutaka kuonana na familia yake moja kwa moja waliwasiliana na DS ya Taifa la Tanzania kuruhusu Maina kuonana na familia yake lakini wakati huohuo Tahadhari zikichukuliwa na hio yote ni kutokana na heshima na nguvu ya Mzee Atanasi katika uchumi wa Afrika Mashariki kwa ujumla.

“Maina licha ya kwamba sijafurahishwa na maamuzi ya kijinga ambayo umechukua , lakini nimefarijika kukuona kabla ya kuiaga dunia hii”Aliongea Mzee Atanasi na kumfanya Blandina kuzidi kulia na kunyanyuka alipokaa na kumsogelea baba yake na kumshika miguu huku akiwa Analia na Mzee Atanasi alimpiga mpiga mgongoni kumfariji.

“Blandina unatakiwa kurudi nchini Kenya”Aliongea Mzee Atanasi na kumfanya Blandina kumwangalia baba yake kwa wasiwasi , ni kama alikuwa hajamsikia.

“Baba Sitaki kurudi tena nchini Kenya , Nataka niishi na wewe mpaka siku yako itakapofikia , baba naomba usiniambie nirudi nchini Kenya”Aliongea Blandina kwa hali ya wasiwasi, lakini Mzee Atanasi hakupepesa macho.

“Baba ni kweli Blandina anapaswa kuishi na sisi, kwanini arudi Kenya? , sikubaliani na jambo hilo”Aliongea Jestina.

“Jestina utaongozaje familia yangu ukiwa na akili ndogo namna hio , nilishakuambia kila siku usitumie hisia katika kufanya maamuzi , kwanini haupo imara”Aliongea Mzee Atanasi huku sauti yake iliokuwa imenyongea ikidhihirisha msisitizo.

“Baba lakini ….”

“Blandina najua kuna sababu ambayo imekufanya kufanya maamuzi uliofanya ambayo ni Zaidi ya sababu ulizotuambia , lakini kwangu hio sababu haina maana tena , kwasababu ulifanya maamuzi wewe mwenyewe , hivyo unapaswa uwajibike , utarudi nchini Kenya kuendelea na maisha yako , sisi tushafurahi kukuona upo hai hio inatosha, na nitoe msisitizo , swala hili kuanzia sasa litaendelea kuwa siri ya familia”

Aliongea Mzee Atanasi na akampa ishara mlinzi wake kua amsaidie anyanyike kuelekea kwenye gari, mzee huyu alionekana hakutaka jibu lolote kutoka kwa Blandina wala kujua ni mawazo gani mwanae alikuwa akifikiria , yeye aliamini katika maeneno alioongea na hata Blandina hakutaka kupinga , alijua siku zote baba yake neno lake ni sheria na hivyo ndivyo alivyowalea.

“Dada katika ile barua ulituamboia Denisi alikufa kwa ajali ya ile ndege , je ulihakikisha?”Aliuliza Jestina mara baada ya Mzee Atanasi kutoka.

“Nadhani unajua ajali ya Ndege ilivyokuwa Jestina , haikuwa na haja ya mimi kuhakikisha”Aliongea Blandina kwa huzuni.

“Sawa dada , hatupaswi kufikiria sana mambo yaliopita , nimefurahi sana kukuona kwa mara nyingine dada yangu , niliishi kwa maumivu mengi baada ya kupata taarifa ya ile ndege”Aliongea na kukumbatiana kwa mara nyingine huku wakionesha kulia tena,Jestina alikuwa na kitu anacho moyoni lakini hakutaka kuongea kwa wakati huo.

Roma Ramoni alikuwa ashalala muda mrefu sehemu ambayo alikuwa ameketi na hii ni kutokana na kwamba hakuwa na mtu yoyote wakuongea nae , licha Yezi na Mama Issa wapate muda wakuongea na hata wakati Mzee Atanasi anaelekea kwenye gari yake hakumuona.

Jestina na Blandina walitumia muda wa takribani lisaa kuongea na Mama Issa hakutaka kuyaingilia maongzi yao , lakini hata yeye pia alikuwa bize kusikiliza namna ambavyo Yezi aliishi akiwa nje ya Kituo.

Wakati Roma akiwa akiwa anafurahia usingizi wake , simu yake ndogo iliokuwa kwnye mfuko wake wa suruali ilianza kuita na kumfanya apeleke mkono na kuitoa na bila ya kuangalia jina aliweka sikioni.

“Your Majest Habari za saa hizi?”Ilikuwa ni ambayo Roma aliitambua ni ya Diego.

“Salama Diego , kuna mpya gani?”

“Niiimekupigia kukueleza kwamba tumeweza kunusa uwepo wa Yan Buwen ndani ya Tanzania”Aliongea Diego na kumfanya Roma akae vizuri kwenye kiti.

“Ameingia Lini Tanzania?”

“Ameingia Jana usiku ,Mfalme Pluto”

“Mmegundua ni kwanini yupo Tanzania?”

“Hatujapata kufahamu ni kwanini Yan Buwen yupo Tanzania , lakini tuliweza kufuatilia ratiba yake kwa kudukua tarakishi yake ya mapakato ambayo anatumia,na katika watu ambao wapo kwenye ratiba ya kuonana nao leo ni pamoja na Malkia Persephone”

“Unamaanisha mke wangu ana ‘Appointment na Yan Buwen?”

“Ndio Mfalme pluto na tumefuatilia muda na mahali ambapo wanapaswa kuonana na Malkia , na mwanzo ratiba ilipangwa saa nne za leo asubuhi lakini baadae tukagundua imesogezwa mpaka saa moja ya leo usiku”Aliongea Diego na kumfanya Roma afikirie kidogo , hakujua ni kwanini Edna alikuwa akitaka kuonana na Yan Buwen , licha ya kwamba Roma alikuwa na hisia kuwa linaweza kuwa sawa la kibiashara , lakini kutokana na matukio yaliotokea juu ya The don aliamini huenda kuna jambo la ziada.

“Mtu gani mwingine muhimu yupo kwenye ratiba yake?”

“Yupo Waziri wa Sayansi na Teknolojia ambaye anapanga kuonana nae , lakini pia watu ambao amekutana nao nje ya ratiba yake ni ‘Scorpion’”

“Scorpion!!”

“Ndio Mfalme Pluto ,Mwanzoni hatukuweza kumtambua Scorpion , lakini baada ya kufatilia taarifa zake tumegundua ni ‘Proffessional Killer’ kutoka ‘Assasination Group’ kutoka China linalofahamika kwa jina la Yamaguchi na yupo Tanzania kwa Zaidi ya miaka miwili akihudumu kama mlinzi wa Mheshimiwa Kigombola”

Roma alijikuta akifikiria maneno hayo ya Diego na kujiuliza kwannini Yamaguchi wakamleta Scorpion Tanzania, maana hakuamini kama Muuaji mkubwa anaweza akawa mlinzi pekee wa Kigombola.

“Okey!!Diego nitamsidikiza mke wangu kwa ajili ya kuonana na Yan Buwen na kama kuna swala muhimu ambalo nitaligundua nitawataarifu iili iliweze kuwasaidia katika uchunguzi wenu juu ya The Don”

“Asante sana Mfalme Pluto”.Aliongea Diego na kisha kukata simu huku akiwageukia Mama Issa na Yezi ambao walikuwa bado wakiongea.

“Mfalme Pluto kama angefahamu tumedukua mawasiliano ya Malkia , nadhani asingetuacha salama”Aliongea Bram aliekuwa ameweka Maheadphone yake kichwani huku akimwangalia Diego.

“Ndio,Bram , lakini hatuna namna , ili kumpa ulinzi wa kutosha Malkia lazima tuhakikishe tunajua ratiba za kila mfanyabiashara anaekutaka nae”Aliongea Diego.

Baada ya kama nusu saa hivi ya Roma kuwasiliana na Diego ,hatimae Mke wa Raisi wa kenye alitoka kwenye ofisi ya Mama Issa na alionekana alikuwa tayari kwa ajili ya kurejea nchini Kenya kama baba yake alivyompa maagizo na muda huu na Roma alikuwa amesimama na Mama Issa, na hii ni baada ya Mama Issa kumuomba Yezi alale siku hio ndani ya kituo hiko na arudi kesho yake na Roma alikuwa akijiandaa kuondoka.

“Blandina kwa jinsi alivyokuwa amemkodolea macho Roma ni kama alikuwa akimfananisha,Ukweli ni kwamba licha ya Blandina kuzimishwa na ajenti Dondwe hakuonana na Roma ,kwani ile anazinduka alikuwa ndani ya ofisi ya Mama Issa m hivyo ni rahisi kusema hakuwa amekutana na Roma kabisa.

“Blandina huyu ndio alietusaidia kufanikisha sisi na wewe kuonana.Anaitwa Mr Roma ni mume wa Edna”Aliongea Jestina baada ya kumfikia Roma , lakini muda huu Roma na Blandina walikuwa wameangaliana machoni wakishangaana na Jestina alikuwa akiwaangalia kwa namna ambavyo walikuwa wakiangaliana.

“Ooh! Asante sana Mr Roma ,nimefurahi kufahamu wewe ni mume wa Edna”Aliongea Maina kwa kuweka tabasamu na kumfanya Roma na yeye atabasamu.

“Mr Roma asante sana kwa leo , licha ya kwamba ulinishangaza sana , lakini niseme umekuwa msaada mkubwa kwetu”.

“Mrs Azizi wala huna haja ya kunishukuru namna hio,Nimefanya lile linalotakiwa kufanywa na sio jambo kubwa”Aliongea Roma na kumfanya Mrs Azizi aone Roma anajitahidi tu kuwa ‘Humble’.

“Mama Issa nadhani mimi niondoke kwa muda huu sasa, maana sina nilichobakisha tena hapa”Aliongea Roma.

“Mr Roma asante sana kwa yote ulioyafanya kwa Mwanagu Yezi, hakika umekuwa wa Baraka sana tokea siku uliokuja hapa kituoni ,hakika Edna kajua kutuchagulia mume”Aliongea Mrs Azizi na kumfanya Roma atoe tabasamu la uchungu , yeye pekee ndio aliekuwa akijua yanayoendelea kati yake na Edna, lakini kwa Mama huyu alionekana kabisa kumkubali kama mume wa Edna.

Roma hakutaka kuzikataa shukrani za Mama Issa alizipokea kwa kutabasamu na kisha alimuaga na Yezi pamoja na Mrs Azizi , pamoja na mke wa Raisi wa Kenya na kisha akapiga hatua kuelekea uelekeo wa gari yake ilipo.

“Huenda Denisi angekuwa na umri wa Mr Roma kwa sasa?”Aliongea Blandina aliekuwa akimwangalia Roma mpaka alipoingia kwenye gari yake na Jestina alimsogelea dada yake na kumshika mkono.

“Dada huoni kama wanafanana sana, ninavyomuangalia Roma naona sura yake ya utotoni ni sawa kabisa na ya Denisi”

Aliongea Jestina na Maina alitingisha kichwa na kutoa tabasamu la uchungu , ukweli ni kwamba hata yeye alikuwa na mawazo sawa na ya Jestina , lakini asingekubali kuwa Denisi ndio Roma hata kama wanafanana na hii yote ni kutokana na kwamba Denisi alishakufa kwa ndege ambayo ilipotea mpaka leo na hakukuwa na taarifa yoyote ya abiria yoyote kuonekana au kusalia , hivyo hata mtu yoyote ambaye anamuamini sana akija akamwambia Roma ni Denisi asingekubaliana na hilo , kwani alithibitisha kabisa Denisi akiingia kwenye ndege ya M Airline akiwa pamoja Bite.

Roma baada ya kurudi aliandaliwa chakula cha mchana na kula mwenyewe kwani kila mtu hapo ndani alikuwa ashakula, baada ya bwana huyu kumaliza , alipandisha moja kwa moja mpaka ghorofa ya tatu ambako ndio kilipokuwepo chumba cha mke wake , akiwaacha Sophia na Bi Wema ambao walikuwa wakishindia kuangalia Tamthilia.

“Babe nimetudi!!”Aliita Roma baada ya kufungua mlango wa chumba cha kusomea cha Edna na kumuona Mke wake akiwa bize na kazi kama kawaida yake na Edna alimwangalia Roma kwa sekunde na baada ya kutingisha kichwa chake kama ishara ya kuitikia ,akarudisha macho yake kwenye tarakishi.

Ukweli ni kwamba Roma alitaka aende na Edna kukutana na Yan Buwen , lakini hakujua ni namna gani ya kumfanya Edna akubali kwenda nae , kwani kama angemuambia moja kwa moja, Edna angeuliza amefahamu vipi kama anamiadi ya kukutana na Yan Biwen.

Roma aliingia ndani ya chumba hiki kilichokuwa na vitabu vingi na kuanza kuchagua kitabu , alikuwa ni kama akitafuta kitabu cha kusoma , vilikuwa ni vitabu vingi kiasi kwamba ilimfikirisha Roma kama mke wake amekuwa ashamaliza kusoma hivyo vitabu.

Roma alichomoa kitabu kilichokuwa kimeandikwa na Benjamini Graham kilichokuwa na kichwa cha ‘The Intelligence Investor’ na kukichomoa na kurudi kwenye sofa na kuanza kufungua peji harakaharaka bila kusoma na kumfanya Edna amwangalie na mwanadada huyu midomo yake ilicheza kidogo, alionyesha kuchekeshwa na namna ambavyo Roma alikuwa akifungua hiko kitabu kama mtoto ambaye hana mpango wa kusoma , maana sio kama alivyotegemea , yeye alijua Roma anakaa kusoma hiko kitabu , lakini alikuwa akikifungua kwa spidi huku bila kuonyesha nia ya kukisoma.

“Romaa..!!!”Aliita Edna na Roma alimgeukia.

“Yes! Wife”

“Who is Queen Persephone?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma ashangae , alijiuliza ni wapi Edna kasikia hilo jina, na ukweli Edna haikueleweka kwannini ameuliza leo , kwani ni muda kidogo tokea aitwe hilo jina na Chiara.
 
SEHEMU YA 120

“Wife ni wapi umesikia hilo jina?”Aliuliza Roma na kumfanya Edna afikirie kidogo , ukweli ni kwamba licha ya Mrembo huyu alikuwa akijiuliza wale wazungu wana uhusiano gani na Roma, Edna mwenyewe muda mwingine alikuwa akijishangaa ni kwanni licha ya mambo mengi kumtokea yanayohusiana na Roma alikuwa akiyapotezea.

“Ni wale wazungu wako”Aliongea Edna na kumfanya Roma atoe tabasamu la uchungu ,Roma aliona anapaswa kumpa Edna jibu la kueleweka.

“Wife nikitaka nikuelezee maana ya hio ya hilo jina , lazima nikueleze kwanza mimi ni nani na itachukua huenda takribani siku nzima ”Aliongea Roma na kumfanya Edna akose utulivu , huku akishindwa kujielewa, kwanini alikosa utulivu pamoja na wasiwasi.

“Wewe ni Roma ulielelewa Marekani, ulikuja Tanzania kwa ajili ya kutafuta familia yako, ulifanya kazi ya kubeba mizigo mara baada ya kufika Tazania….,unataka kuniambia hayo yote yalikuwa ni uongo?”Aliongea Edna na kumfanya Roma asijue acheke au alie , maana hakuelewa kwanini mke wake ametoa ‘summarry’, lakini kwa Roma pia aliona hio ni fursa kwake kuingiza swala la Yan Buwen.

“Wife najua mpaka sasa ni zaidi ya mwezi mmoja tokea tuanze kuishi pamoja, na ni mambo mengi ambayo yametokea kati yetu na yapo yale yanayohitaji maelezo na ambayo pia hayahitaji maelezo , Unaonaje leo tukitoka jioni na kutafuta sehemu tulivu nikuelezee kidogo ili ujue maana ya ‘Queen Peresephone’”,Aliongea Roma na kumfanya Edna amwangalie Roma kwa sekunde kadhaa na alionekana kufikiria.

“Leo nina ‘Appointment ya kibiashara , labda tupange siku”Aliongea, na Edna ukweli katika moyo wake alikuwa na shauku sana ya kujua Roma ni nani haswa , mrembo huyu ukweli ni kwmaba hakuwa akiamini kabisa eti Roma alikuwa amelelewa Marekani na akarudi Tanzania kwa ajili ya kuitafuta familia yake , aliamini kabisa yote hayo ni uongo na swala ambalo lilimthibitishia Edna ni juu ya Sophia.

Ilikuwa ni siku kadhaa Edna akiwa kazini ndani ya ofisi yake na hii ni baada ya ujio wa Sophia, mlango wake ulifunguliwa na Monica.

“Boss Miss Suzzane anataka kuonana na wewe”Aliongea Monica na Edna alimpa ishara ya kwamba amruhusu.

“Karibu Suzzane”Aliongea Edna mara baada ya Suzzane kufika ndani ya ofisi ya Edna.

“Boss nishapata taarifa za Sophia”Aliongea Suzzane na kupangusa simu yake ya Sumsung S22 na kisha akampatia Edna ambaye alikuwa ana hamu ya kujua ni taarifa gani zinazomuhusu Sophia.

Siku ya jana yake alikuwa amempa kazi Suzzane kufuatilia taarifa za Sophia kwa njia ya simu.

“Ni kama nilivyodhania”Aliwaza Edna huku akiangalia simu hio , hakuonesha kushangaa sana.

“Asante Suzzane”Aliongea Edna na kisha akamrudishia Suzzane simu yake , hio ilikuwa ni siku kadhaa zilizopita baada ya Sophia kufika ndani ya familia yake , sasa siku ya Jumanne akiwa kazini asubuhi pia alipata ugeni.

“Madam kuna mgeni wako eneo la mapokezi , anafahamika kwa jina la Mrs Ramadhani, mke wa Balozi , anasema anataka kuongea na wewe”Ilikuwa ni taarifa iliotoka kwa Monica na kumfanya Edna ashangae kidogo , lakini aliishia kumwambia Monica awaambie watu wa mapokezi wamruhusu.

“Edna…!!!”Aliingia mama mmoja hivi Shombeshombe aliekuwa mnene mfupi huku akiliita jina la Edna kwa rafudhi yake ilioathiriwa na lugha ya kiarabu.

“Madam Rukaiyah!!,Karibu sana”Aliongea Edna akimkaribisha mwanamama huyu huku akimwita mke wa Balozi Ramadhani Rukaiyah , na kwa jinsi mwanamama huyu alivyokuwa akiongea na Edna ungefahamu tu kwamba sio mara yao ya kwanza kuonana.

“Edna nimekuja leo kazini kwako tuonane maana sikutaka Sophia afahamu nipo Tanzania”Aliongea Rukaiyah huku akiweka tabasamu usoni kwake,alionekana mchshi mno.

“Niambie Madam”

“Edna nilikuwa safarini nyumbani kwetu huko Abu dhabi kwa muda ,nilivyofika nyumbani sikumkuta Sophia na nikamuuliza baba Sophia kuhusu alipo mwanangu , ndio kaniambia yupo Tanzania anaishi kwako, niliuliza sababu ya Sophie ghafla tu kutaka kuja kuishi na wewe ukizingatia na namna familia zetu zilivyo , ndio balozi kaniambia eti Sophia anataka kuwa karibu na wewe , nilishangaa mwenzio , lakini kuna jambo ambalo lilinishangaza Zaidi”Aliongea Mama huyu na kumfanya Edna atake kujua Zaidi.

“Nini kilikushangaza Zaidi?”

“Kumbe mumeo ndio alimuokoa mwanangu wakati alivyotekwa,sikufahamu kama ushapata mume”Edna alishangaa.

“Nani alimteka Sophie!?”

“Edna kwani mumeo hajakuambia , unaonekana huna unachojua kabisa”Aliuliza mama huyu akishangaa Zaidi.

“Ndio sifahamu juu ya hilo?”Alijibu Edna kwa aibu na Mama Sophie alitabasamu.

“Sophie alitekwa pamoja na mtoto wa waziri mkuu wa Japani na watu wa Korea Kaskazini , nakuambia siku nilizimia hio nilivyopewa hio habari na nilipanga kabisa kuachana na Ramadhani kama Sophie asingerudi….,Edna najua familia zetu hazina ukaribu , lakini naomba Sophie akae nyumbani kwako , naogopa yasije yakamkuta tena, Yaani nakuambia Mwenzio sipendi kabisa kuishi Japani lakini Ramadhani hanielewei na sijui anafadika nini na ubalozi wake , mimi kwangu naona ni upuuzi tu na hauna faida ukilinganisha na biashara zetu”Aliongea mwanamama huyu mfululizo,lakini Edna hakuwa na taarifa za Roma kumuokoa mtoto wa waziri mkuu wa Japani na Sophia, hio ilikuwa ni siku ya jumatano mchana,

Edna hakutaa kumuuliza sana Roma kuhusu kumdanganya juu ya Sophia, Edna alijua Roma lazima atakuwa ameombwa na Balozi Ramadhani kwani mwanadada huyu alikuwa akikumbuka siku ya Kusanyiko ,Balozi Ramadhani alimuomba Roma kuongea nae na aliunganisha matukio na kuona huenda lilikuwa ni swala la Sophia , lakini pia mwanadada huyu aliweza kuona huenda pia sababu ya Roma kutomuambia juu ya Sophia ni kutokana na kutoelewana kwa familia ya Adebayo pamoja na Athumani.Hivyo Edna alimuona Sophie kama mdogo wake na Edna hakutaka kumwambie Roma , alijiambia kwasababu na yeye amemdanganya inapaswa alipize kisasi kwa kutomuambia yaani ,jino kwa jino’.

Roma alitabasamu baada ya kuona Edna kaingia kwenye topic ambayo alikuwa akiitaka , topic ya ‘Appointment’.

“Wife kama una appointment , basi tutapanga kwenda siku nyingine , lakini unaonaje leo nikikusindiza?”Aliongea Roma na kumfanya Edna afikirie na kuona hakuna ubaya kama atamsindikiza , kwanza miadi hio ilikuwa ni usiku na aliona na uwepo wa Roma atajiskia kuwa salama Zaidi, kabla ya Edna kumjibu Roma simu yake iliita na jina lilisomeka Monica.

“Kuna nini Monica?”

“Madam Mr Yan kabadilisha sehemu ambayo mnapaswa kuonana , anasema makutano yatafanyikia ndani ya Grape Hotel, anasema pia anayo miadi na mtu mwingine ndani ya hio hoteli ndio maana”Aliongea Monica

“Okey! Hakuna shida Monica “

“Boss !Unaonaje nikikusindikiza?”

“Nitaenda na mume wangu Monica , unaweza kwenda nyumbani ukapumzike , tutaonana kesho”Roma alisikia mazungumzo ya Edna na Miss Airport na kuona mpango wake umefanikiwa kwa asilimia mia moja na kilichobaki ni kwenda kuonana na huyu mtu anaeitwa Yan Buwen , alitaka kufahamu ni kwanini Yan Buwem alikuwa akimiliki Kadi ya kibenki inayotoa hela kutoka kwa akaunti ya Hegemeoni ,akaunti ambayo ilikuwa ikipokea miamala kutoka pande zote za dunia , lakini akaunti ambayo alikuwa akiamini mmiliki wake ni The Don,Licha ya kwamba Roma alikuwa na wasiwasi juu ya Dorisi pia , lakini aliamini jibu linaweza kupatikana kwa urahisi kupitia Yan Buwen.

Ni muda wa saa kumi na mbili kama na dakika aribaini na tano hivi , ndio muda ambao Roma alishuka kwenye gari aina ya Roll Royce akiwa ameambatana na Edna.

Edna leo hii alikuwa amevalia kiprofesheno kabisa ,kwani alikuwa amevalia Suti ya rangi ya Zambatau pamoja na viatu vya skuna , alikuwa amependeza na alionekana kujiamini kama kawaida yake , Roma kwa upande wake hakukuwa na jipya sana , alikuwa amevaa koti la suti na jeansi pamoja na miwani ya jua.

“Wife Naona leo umenifanya niwe bodigadi wako sio mume”Aliongea Roma aliekuwa amevalishwa miwani na Edna na alionekana kama jambazi.

Ukweli Edna hakutaka kumtambulisha Roma kama mume wake, walikuwa wamepatana, Roma atakuwa ni mlinzi na msaidizi wake wa karibu na ,Edna aliona angeonekana labda hakuwa akijiamini kama angemtambulisha Roma kama mume wake mbele ye Mgeni wake.

“Ndio uwe kama Bodigadi , kumbuka Bodigadi haongei ongei , ole wako upanua mdomo wako , kila nitakachoongea unatingisha kichwa na kusema Sawa Boss”Aliongea Edna wakati wakiwa kwenye Lift na kumfanya Roma afurahishwe na ubabe wa mke wake.

“Sawa Boss”Alijibu Roma na kumfanya Edna atabasamu na hata yeye alishangaa kwanini alishindwa kujizuia kutabasamu, labda ni namna Roma alivyoitikia

END OF SEASON 04
 
SEHEMU YA 121

Grape hoteli ni moja ya hoteli maarufu sana ndani ya jiji la Dar ambayo wafanyabiashara wengi hupenda kufikia hapo kwa ajili ya mazunguzo ya kibiashara , moja ya sababu kubwa ambayo inaifanya hoteli hii kupendwa sana , ni kutokana na wateja wanavyopewa ‘high privacy’ kwa kile ambacho wanafanya pasipo kuingiliwa kwa namna yoyote ile na inasemekana moja ya mmiliki wa hoteli hii ni kigogo kutoka serikalini.

Wafanyabiashara wengi wa ulimwengu usionekana wanaita hoteli hii kama makao makuu ya ‘Underwold’ hii ikimaanisha kwamba yapo mambo mengi ambayo sio halali ambayo yanafanyika ndani ya hii hoteli na hakuna chombo chochote cha usalama ambacho kinaweza kuingia hapo ndani na kufanya ukaguzi wa aina yoyote ile.

Floor namba kumi na tisa ndio walikuja kutokea Edna na Roma na hii ni kutokana na maelekezo ya Yan Buwen, Floor hii ilikuwa ni kwa ajili ya VVIP , haikuwa na chumba chochote kwa ajili ya kulala bali kulikuwa na ukumbi mkubwa wa mikutano lakini pia ofisi ndogo mbalimbali zinazojitegemea.

“Madam Karibu sana”Aliongea General Manager wa Floor hii na Edna aliitikia kwa kichwa na ni kama walikuwa wakisubiriwa , GM aliwaongoza mpaka kwenye mlango uliokuwa na maandishi ya VIP ROOM NO 7.

Roma alikuwa akikagua eneo lolote kuhakikisha hakuna jambo ambalo linaweza kuleta shida kwa mke wake.

Edna na Roma baada ya kuingia ndani waliweza kumshuhudia mwanaume ambaye alikuwa amekaa kwenye masofa , alikuwa ni mwanaume ambaye amevalia suti na rangi nyeusi shati jeupe na tai nyekundu,Edna na Roma hawakumtambua mara moja bwana huyu katika wote wawili hawakuwahi kuonana na Yan Buwen.

“Karibu sana Miss Edna ,Naitwa Yan Buwenau unaweza kuniita Profesa Yan”Aliongea Yan Buwen kwa kuweka tabasamu.

“Ni jambo la furaha kukutana na wewe Mr Yan ana kwa ana, huyu ni ‘personal Asistatnt wangu anafahamika kwa jina la Roma Ramoni”Edna alimtambulisha Roma na Yan Buwen alimwangalia Roma na alionyesha hali ya kutofurahishwa na ujio wake na Roma aliligundua hilo , ila hakutaka kujali sana, Yan Buwen alimuonyesha Edna sehemu ya kukaa kwa mkono huyu akiweka tabasamu lake.

Kikao cha Yan Buwen na Edma kilidumu kwa Zaidi ya dakika kama kumi na tano hivi , Roma baada ya kuona Yan Buwen anazungumzia maswala ya uwekezaji , hakutaka kuingilia sana maongezi hayo, lakini pia Roma hakuona jambo lolote ambalo sio la kawaida kwa Yan Buwen.

Edna aliagana na Yan Buwen na kisha wakaingia kwenye lifr na kushuka mpaka chini na hatimae kufika eneo la maegesho ya magari , Roma alimfungulia mlango Edna na akaingia na akafuatia yeye upande wa Dereva.

“Mbona unaendesha gari uelekeo ambao sio wa nyumbani?”Aliuliza Edna baada ya kuona Roma baada ya kuelekea Kigamboni yeye alikuwa akielekea njia ya kwenda Mwenge.

“Wife mapema sana leo , tutatumia huu muda kula chakula cha usiku sehemu nzuri tulivu”Aliongea Roma na kumfanya Edna amwangalie na kisha sijui mrembo huyu alifikiria nini , ila hakutaka kusema maneno mengi , alitulia kwenye siti yake na kusubiri kuona ni wapi Roma anampeleka.

“Nilisahau kukuuliza kuhusu Yezi , vipi alionana na mama Issa?”

“Ndio ameonana nae na amefurahi , kalala hukohuko”Alijibu Roma na kumfanya Edna atingishwe kichwa.

Baada ya Roma kuendesha gari kama nusu saa hatimae alikuwa akiingiza gari ndani ya Upepo Beach Garden, sehemu ambayo siku zilizopita Roma alikuja na Neema Luwazo ndani ya hilo eneo na haikueleweka kwanini Roma akachagua hilo eneo.

Edna alionyesha kupendezwa na mazingira yaliokuwa hapa ndani , ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufika na ilikuwa ikishangaza kwani matajiri wengi ndani ya Taifa la Tanzani washafika ndani ya hili eneo , lakini Edna peke yake ndio ambaye hakuwahi kufika , licha ya kwamba mrembo huyu alikuwa na pesa nyingi.

“Umepajuaje hapa Roma?”Aliuliza Edna huku akishangaa kulia na kushoto na akiangalia baadhi pia ya watu waliokuwa hapa nani wakiwa na wenza wao.

“Alinileta Neema”Alijibu Roma huku akimshika mkono Edna na kumfanya mrembo huyu aangalie namna ambavyo ameshikwa mkono na alishindwa kuutoa.

Waliongozana mpaka sehemu ambayo Roma na Neema walikaa wiki chache zilizopita,Roma alimsogezea Edna kiti na akakaa na yeye pia akakaa na wakawa wanaangaliana.

“Kijana!!!”Aliita Mzee chino na kumfanya Roma ageuke na kutabasamu baada ya kumuona huyu mzee kwa mara ya pili.

“Mzee Chino nimetokea kupenda hili eneo”Aliongea Roma na Mzee Chino alitabasamu huku akimwangalia Edna ni kama alikuwa akimfananisha.

“Mzee Chino naona unamshangaa sana mke wangu,Edna huyu ni mzee Chino ndio anaemiliki hili eneo licha ya kwamba anaonekana kama masikini”Aliongea Roma akimtambulisha Edna.

“Haha..una maneno sana kijana , ila nikupe pongezi una mke mzuri sana,Karibu Sana Miss Edna”

“Asante”Alijibu Edna akiwa na tabasamu na Eda hakuacha kugeuka geuka kuangalia hayo mazingira.

“Mzee Chino tuletee Carribean Lobster Soup”

Aliongea Roma na kumfanya Edna ashangae , kwani licha ya kwamba alikuwa akikifahamu hiko chakula , lakini hakuwahi kukionja.

“Hakuna Shida Mr Roma , ila mkeo ni kama namfananisha na mfanyabishara mmoja mkubwa Tanzania”

“Unamfananisha na nani mzee Chino?, mimi nakuona kama haujamfananisha ila ushamfahamu”

“Haha… kijana unaonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kumsoma mtu ,Miss Edna nakukaribisha sana kwenye mgahawa wangu , imekuwa heshima kwangu leo kutembelewa na mfanyabiashara mkubwa ndani ya taifa hili”Aliongea Mzee Chino huku akionyesha heshima kwa Edna ,Mzee huyu alionekana kumfahamu vyema , lakini pia alifurahia leo kumuona Edna akiwa amefika ndani ya mgahawa wake.

“Asante Mzee Chino”Aliongea Edna kwa sauti yake myororo na kutabasamu.

“Mr Roma!,Wewe ni hatari”Aliongea Mzee Chino kwa utani huku akiondoka na kumfanya Roma atoe tabasamu la uchungu, alijua alichokuwa anachomaanisha Mzee Chino ila alipanga kupotezea.

“Wife ushawahi kunywa Carribean Lobster Soup ?”Aliuliza Roma baada ya Mzee Chino kuleta mabakuli mawili na kuyaweka mbele ya Edna , ambaye alikuwa akishangaa , hakuwahi kula aina hio ya chakula.

“Nishawahi kula ‘Seafood’ kama vile Sushi, lakini sijawahi kunywa hii supu ya Lobster”Aliongea Edna huku akishika kijiko na kuzungusha zungusha kama mtu ambaye hakuwa na mpango wa kula na Roma alimwangalia anachokifanya Edna na kutabasamu.

Lobster kishwahili chake ni samaki aina ya Kamba ndio samaki ambaye anauzwa kwa bei kubwa sana ndani ya mahoteli , kilo moja ya Lobster inafikia Zaidi ya Elfu sabini za kitanzania.

“Kumbe tamu hivi?”Aliongea Edna kwa mshangao mara baada ya kuonja na kumfanya Roma atabasamu, alishindwa kuelewa kwanini mke wake hakuwahi kuonja chakula cha aina hio , wakati matajiri wengi hupendelea sana.

“Nichakula kitamu, lakini pia kina virutubisho vingi sana kwa ajili ya afya ya mwili , siku moja moja unapaswa kula cyakula vya aina hii”Aliongea Roma na kumfanya Edna amwangalie na kutingisha kichwa kukubaliana nae na kuendelea kula.

Ndani ya nusu saa mbele Roma na Edna walikuwa wakitembea upande wa fukwe hii Edna akiwa mbele na Roma akiwa nyuma,, Roma alijikuta akipendezwa na namna mke wake alivyokuwa akionekana ndani ya eneo hili , hususani kwa jinsi ambavyo alikuwa ameshikilia viatu vyake na kutembea.

Walitembea kwa umbali kama wa mita mia hivi na Edna akasimama huku akiangalia upande wa baharini , na sehemu waliosimama ni ile ile ambayo Roma na Neema luwazo walisimama, na Roma alijikuta akijiwazia na kumkumbuka Neema Luwazo alivyomkimbia siku ile , lakini pia namna ambavyo alimkumbatia na kuanza kubusiana,Kwa mawazo hayo ni kama Roma alipata ‘idea’ na alimsogelea Edna ambaye nywele zake zilikuwa zikipeperushwa na upepo na kisha akamkumbatia kwa nyma na kupitisha mikono kwa mbele, Edna alipata mshituko na kutaka kujitoa kwenye mikono ya Roma , ila Roma alimshikilia kwa nguvu , hakutaka kumpa nafasi hio hata kidogo

“Edna my Wife , I love you so much”Aliongea Roma na kumfanya Edna moyo wake upige kwa nguvu huku akiisikilizia pumzi ya Roma iliokuwa ikimpuliza shingoni, kwa wakati huu mrembo huyu alishindwa hata ajibu nini Zaidi ya kukodolea macho bahari ilikuwa ni mara yake ya kwanza kukumbatiwa namna hio , lakini pia kuambiwa maneno hayo, hakuwa hata akijielewa kwa wakati huo na alishindwa pia kuelewa kwanini Roma ghafla tu akamwambia hayo maneno na alishindwa pia kuelewa ni hatua gani aichukue kwa wakati huo.

Roma aliemkumbatia Edna kwa nyuma alijikuta akitabasamu huku akifurahia marashi yanayotoka kwa mke wake,Ilikuwa ni picha ya kupendeza kwa namna ambavyo walikuwa wakionekana, na walisimama wakiwa wamekumbatiana kwa dakika kama mbili hivi mpaka pale Edna alipogeuza uso wake na kumwangalia Roma usoni na kadri walivyokuwa wakiangaliana ni kama kuna nguvu flani iliokuwa ikiwafanya wasogeleane.

“Moja , Mbili , Tatu..”Roma alianza kuhesabu kwenye akili yake na haikueleweka kwanini alikuwa akihesabu , lakini kabla hajatamka Nne , tayari Lipsi za Edna na Zake zilikuwa zishagusana.

Edna ambaye ilikuwa mara yake ya kwanza kufanya hivyo alijikuta automatic akitoa ulimi wake na Roma na yeye akaupokea na kilichoendelea hapo ,ilikuwa ni kunyonyana midomo , huku mrembo Edna akiwa amefumba macho na upande wa Roma hakuwa amefumba, Edna aliekuwa ameshikilia viatu vyake alijikuta akividondosha pasipo kuelewa vimedondoka muda Gani na Roma aliekuwa amepitisha mikono kwenye kiono cha Edna alizidi kumbana Edna kuelekea kwake
ITAENDELEA , KWA MWENDELEZO NICHEKI WATSAPP 0687151346
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…