SEHEMU YA 118
Mheshimiwa Raisi Kamau alionekana kuwa na wasiwasi mwingi mno na hii ni baada ya kukosekana hewani kwa Dondwe na kumfanya kutofahamu ni nini kinaendelea nchini Tanzania.
Bwana huyu alijilaumu sana kumruhusu Maina kwenda Tanzania pasipo kuchukua tahadhari zozote.
Ukweli ni kwamba baada ya Maina kupanda ndege na baada ya masaa mawili kupita ndipo mheshimiwa alipopewa ujumbe na Deo kuwa inawezekana Madam anaenda kuonana na mke wa tajiri Azizi.
Baada ya mheshimiwa Kamau kupata hii taarifa , alitafuta namna ya kuhakikisha taarifa hio na hapo ndipo alipompigigia mtu wake aliempandikiza ndani ya familia ya Tajiri Azizi na ni kweli alipewa taarifa kwamba Mke wa Tajiri Azizi yaani Jestina alikuwa na ratiba ya kwenda kituo cha kulelea yatima cha Son And Daughter Orphanage, na mpaka hapo ndipo Kamau alipopata kujua jambo ambalo Maina alikuwa akilifanya , alishangaa sana na kuona ni kwanini Maina hakumshirikisha.
“Inanipasa kutulia naamini Blandina anataka tu kuonana na familia yake , na hatoongea Zaidi ya anayoyajua , napaswa kumuamini”Aliwaza Mheshimiwa Kamau huku akichukua maji kwenye glasi na kunywa kidogo ili kujituliza , lakini licha ya kujiambia maneno hayo bado bwana huyu alikosa utulivu kwenye akili yake.
*****
“Mheshimiwa Maina amefanikiwa kuonana na familia yake leo”Aliongea Linda mlinzi wa raisi Jeremy na kumfanya mzee huyu kutabasamu.
“Iliwezekana vipi Kamau akashindwa kumzuia mke wake?”
“Kwa taarifa za watu wetu nchini Tanzania wanasema raisi Kamau alijitahidi kuzuia , ila alishindwa kutokana na Roma kuingilia”Jeremy alitoa macho na kumwangalia Linda ni kama hajasikia vizuri.
“Ilikuwaje Roma akawa ndani ya hiko kituo?”
“Mpaka sasa sijapata taarifa Zaidi Mheshimiwa”.
“Hili swala sikudhania litatokea mapema hivi nadhani ni muda sasa wa kuanzisha mpango wangu niliokuwa nao miaka mingi , lakini bado namuonea huruma Senga”Aliongea Jeremy.
“Lakini Mheshimiwa Naamini Mheshimiwa Kamau hakuna anachokifahamu kuhusu mpango LADO”
“Linda unachoongea ni kweli na mimi nataka kuamini hivyo na nimekuwa nikijitahidi miaka na miaka kuamini hivyo , lakini mienendo ya Kamau haijawahi kunifanya nimwamini , kumbuka Kamau ndio mtu pekee aliekataa kuingia kwenye mpango TASAC licha ya kumlazimisha”
“Naelewa Mheshimiwa lakini bado naona ni swala ambalo linakosa muunganiko , maana swala la kupotea kwa ile ndege ni swala ambalo ni zito mno kwa mtu kama Kamau kulifahamu”Aliongea Linda na kumfanya Mheshimiwa Jeremy awaze kidogo.
“Nadhani swala hili tuangalie DS ya Tanzania watalitolea vipi maamuzi swala la Blandina, Endelea kufuatilia ni sababu gani Roma alikuwepo kwenye kituo cha Son And Daughter Orphanage”
“Sawa Mheshimiwa” Aliongea Linda na kisha akatoka.
DS ni kirefu cha maneno ya ‘Deep State’ au kwa Kiswahili unaweza kusema Serikali ya ndani,DS ni kikundi cha watu ndani ya nchi ambacho kinakuwa na nguvu ya kufanya maamuzi ya kisela katika Nyanja zote , hawa DS ni rahisi kusema wanauwezo wa kuamua ndani ya taifa raisi awe nani kutokana na nguvu yao na mara nyingi wanafanya kazi kwa siri sana.
******
Edna alijikuta akijishangaa kulala muda mrefu mno kuliko isivyokuwa kawaida , saa saba na nusu mrembo huyu alishituka kutoka usingizini na kuanza kukumbuka ni muda gani alilala maana alikuwa na nguvo alizovaa jana yake.
“Ni Roma yule Shetani Sijui alinifanyia nini?”Mrembo huyu alionekana kukumbuka tukio lililotokea , alikumbuka namna ambavyo Roma alimkumbatia kwa nyuma na kwanzia hapo hakuelewa nini kiliendelea.
Edna alijinyanyua kivivu kitandani na kuangalia saa kupitia simu na hapa ndipo aliposhituka , hakuamini ilikuwa ni saa saba mchana , kwani licha ya kwamba alijua amelala muda mrefu , lakini hakujua kuwa siku ilikuwa ikikaribia kuisha , alikumbuka simu yake nyingine iliokuwa kwenye mkoba wake na kuitoa haraka na kuangalia ni nani kapiga na kweli kulikuwa na ‘missed calls’ nane kutoka kwa Monica lakini pia kulikuwa na ujumbe wa maandishi.
“Madam muwekezaji Yan Buwen kutoka China keshafika nchini , Nakupigia hupatikani nimesogeza ratiba ya wewe kuonana nae saa moja za leo jioni”
Ulikuwa ujumbe kutoka kwenye simu ya Edna hakukuwa na jumbe nyingine za muhimu Zaidi na kumfanya mwanamke huyu kuvuta pumzi ya afadhali.
“Miss umeamka?”Ilikuwa ni sauti ya Bi Wema aliekuwa akiandaa chakula mezani na kwa harufu tu ya chakula ilimfanya Edna kuhisi njaa.
“Nimelala sana Bi Wema leo , kwanini hamkuniamsha?”
“Roma alituambia tusikuamshe mpaka utakapo amka mwenyewe na sisi tuliona ni sawa maana ulifanya kazi sana wiki hii pasipo kupumzika”Aliongea Bi Wema na Edna hakubadili muonekano wake , ila alikuwa akiwazia ni nini Roma alimfanya mpaka kulala muda mrefu, alijua Roma sio mtu wa kawaida lakini hakudhania kama anaweza kumfanya pia mtu kulala muda mrefu.
“Miss Mbona haukuniambia kama Yezi amepatikana?”Aliongea Bi Wema na kumfanya Sophia ajiulize Yezi ni nani.
“Ndio Bi Wema nilisahau , mambo yalikuwa mengi ,Roma ndio kakuambia?”
“Ndio kaniambia leo asubuhi na kampeleka kituoni kuonana na Mama Issa”Edna alishangaa kwasababu hakuwa na hio taarifa.
******
Upande mwingine ndani ya hoteli ya Serena alionekana bwana mmoja hivi wa Kichina aliekuwa amevalia taulo la rangi nyeupe ndani ya hoteli hii akiwa ameshikilia glasi ya wine huku akiwa amevalia miwani yake , kwa kumuangalia tu bwana huyu utafahamu umri wake haukua ukizidi miaka Arobaini.
Wakati bwana huyu akiangalia mandhari ya nje yajiji hili , simu yake ya chumba iliita mfululizo na kumfanya ageuke na kuisogelea na kisha aliipokea.
“Mr Yan Una mgeni eneo la mapokezi anafahamika kwa jina la Scorpion”Aliongea mwanadada wa mapokezi na kumfanya Bwana huyu atabasamu na kisha alijibu kwa Kingereza kama amruhusu aje.
Baada ya kama dakika tano aliingia mlinzi wa kike wa mheshimiwa Kigombola aliekuwa akifahamika kwa jina la Scorpion , alikuwa amevalia mavazi yake ya suti nyeusi akiwa na miwani ya jua , licha ya mwanadada huyu kuwa na sura ngumu lakini leo hii alipendeza.
“Karibu sana Sciorpion , ni muda mrefu hatujawahi kuonana tokea uje Tanzania”Aliongea Yan Buwen huku akitabasamu lakini Scorpion hakutoa aina yoyote ya tabasamu mlinzi huyu alikuwa kauzu hatari.
“Umekuja Tanzania kufanya nini Yan Buwen?”Aliuiza Scorpion kwa sauti ya kibabe.
“Nadhani unajua kwanini nipo hapa Tanzania mpaka muda huu”
“Kama umekuja kwa ajili ya jiwe la Kimungu sahau , washalichukua Yamata”
“Hahaha..Scorpion Baada ya kuja Tanzania naona uwezo wako wa akili umeshuka kwa Zaidi ya asilimia hamsini , Watanzania wamekudumaza kama walivyodumaa”Aliongea Yan Buwen kwa kejeli.
“Unamaanisha nini?”
“Yamata wamepewa jiwe feki , hivi unamchukuliaje Hades wewe, ndio maana nakuambia uwezo wako umedumaa , ulivyokuwa chini yangu haukuwa hivyo Scorpion”Aliongea Yan Buwen na kumfanya Scorpion ashangae.
“Una uhakika ni jiwe feki?”
“Ndio maana nipo hapa Tanzania, The Don anataka hilo jiwe kwa namna yoyote na niimekuita tuonane ili unisaidie kuandaa mpango wa kupata jiwe hilo”.
“Mpango Gani unapanga ili hali unajua hatuna uwezo wa kupambana na Hades”
“Hatuna haja ya kupambana na Hades ,The Doni mwenyewe atapambana nae”Aliongea Yan Buwen kwa tabasamu na alionekana kuwa na shauku kubwa.
“Sasa kama The Don ndio anakwenda kupambana na Hades tunaandaa mpango wa nini?”Aliuliza Scorpion na Yan Buwen alikunywa kidogo kinywaji chake halafu akatabasamu.
“Yapo mambo mengi haufahamu Scorpion na siku sio nyingi utakuja kugundua angalau nusu yake , ujio wangu hapa Tanzania ni kutaka kuhakikisha kama jiwe hilo lipo hapa au Hades kalificha nje ya Tanzania , hio ndio sababu ya mimi kufika hapa Tanzania , lakini pia nadhani mpaka sasa haujafahamu kwanini The Don alikupa maagizo kukaa karibu na mheshimiwa Kigombola?”Scorpion alitngisha kichwa kuonyesha hajui.
“Okey ukikamilisha kazi nitakayokupa siku ya leo, nitakuambia kila kitu”Aliongea na kisha akanyanyuka na kutoa picha na kumpatia Scorpion”
“Nahitaji kusikia kifo cha huyo mtu kabla ya kesho asubuhi”Aliongea Yan buwen na Scorpion aliangalia hio picha na kisha akavuta pumzi.
“Kwahio hili ni dili , nakamilisha kifo cha huyo mtu na utaniambia kwanini The Don kanileta Tanzania”.
“Hahaha…Scorpion , hupaswi kuwa na wasiwasi licha ya kwamba naonekana kama mtu ambaye siaminiki , lakini kuhusu hilo nitakutimizia , Ndani ya dunia hii ni mimi pekee ambaye namfahamu The Don kwa kumuona Hata raisi wa Marekani anamsikia tu … hahahaha”
SEHEMU YA 119.
“Baba , Dada naomba mnisamehe….Hii..Hii”Blandina alikuwa akilia mpaka anatia huruma ,Jestina ambaye alikuwa amekaa upande wa kushoto ndani ya ofisi hii ya Mkuu wa kituo, alimuonea sana huruma dada yake.
Mzee Atanasi licha ya kwamba alikuwa na hasira juu ya mtoto wake huyoo wa kwanza katika familia yake , lakini kwa namna ambavyo Bladnina alivyokuwa akilia na kuonesha hali ya kujutia , alijikuta kama mzazi moyo ukiuma, alijua ni ujasili pekee ambao alikuwa nao Blandina kwa kuishi Zaidi ya miaka ishirini ndani ya sura bandia.
“Dada usilie tena, wote tunahisi maumivu yako uliopitia kwa miaka yote hio,tunafuraha baada ya kuona upo hai”Aliongea na kunyanyuka na kwenda kumkumbatia dada yake.
Mzee Atanasi licha ya uzee wake wa miaka mia moja , lakini mzee huyu akili yake bado ilikuwa ikifanya kazi , muda huu mzee huyu haikueleweka ni nini alichokuwa akiwaza katika akili yake , lakini hisia mchanganyiko zilijionyesha kwenye macho yake.
Baada ya takribani nusu saa kupita za Blandina kueleza nusu ya kile kilichomfanya kutoitaarifu familia yake juu ya yeye kuwa hai, hatimae mzee Atanasi aliona ni wakati wa kutoa maamuzi kama kiongozi mkuu wa familia.
Ukweli ni kwamba kabla ya Mzee Atanasi kuja ndani ya kituo hiki kuonana na Blandina , alikuwa ashakaa kikao na ‘National Senior`s’ na kulizungumza hili swala na hii ni kutokana na kwamba swala la Blandina lilikuwa likihusisha nchi ya Tanzania na Kenya moja kwa moja.
National Senior`s ni sawa na kusema DS au Deep State ,Mzee Atanasi alikuwa ndani ya kikundi hiki ambacho kilikuwa na maamuzi makubwa ndani ya Taifa, licha ya kwamba maamuzi yao wanaoyafanya hayakuwa yakifahamika moja kwa moja ndani ya taifa , lakini raisi wa Tanzania pamoja na wasaidizi wake walikuwa wakiyatimiza.
Sasa Mzee Atanasi alikuwa akija hapo kweye kituo akiwa na maamuzi tayari ambayo washayajadili na maamuzi hayo hayakuwa yamejadiliwa na DS wa taifa la Tanzania pekee bali pia yalikuwa yamehusisha na DS wa taifa la Kenya.
Unatakiwa kujua kwamba ni mara chache sana ya wanachama wa DS kumhusisha Raisi katika vikao au viongozi wakubwa wa nchi , DS mara nyingi inakuwa inajitegemea na haiuhusishi viongozi ambao wapo ndani ya mfumo wa moja kwa moja wa uongozi , wao mara nyingi wanapokea miongozo kutoka kwa kikundi hiki tu, kipi wafanye na kipi wasifanye kwa maslahi yao , na hii haipo kwa Tanzania tu ni karibia duniani kote kila nchi ina DS ambayo haihusishi mfumo wa kiuongozi wa moja kwa moja, bali wanakuwa wanajitegemea , ni mara chache sana kumkuta Raisi wa nchi alie madarakani kuwa ndani ya DS , ila Raisi akishastaafu ni rahisi kuingia kwenye DS na hapa ndio maana unaona Mheshimiwa Kamau alikuwa akitaka kuzuia Maina asionanae na Familia yake , lakini wakati huo huo DS wa Kenya walikuwa wanajua kila kitu kuhusu Maina na baada ya kitendo cha Maina kutaka kuonana na familia yake moja kwa moja waliwasiliana na DS ya Taifa la Tanzania kuruhusu Maina kuonana na familia yake lakini wakati huohuo Tahadhari zikichukuliwa na hio yote ni kutokana na heshima na nguvu ya Mzee Atanasi katika uchumi wa Afrika Mashariki kwa ujumla.
“Maina licha ya kwamba sijafurahishwa na maamuzi ya kijinga ambayo umechukua , lakini nimefarijika kukuona kabla ya kuiaga dunia hii”Aliongea Mzee Atanasi na kumfanya Blandina kuzidi kulia na kunyanyuka alipokaa na kumsogelea baba yake na kumshika miguu huku akiwa Analia na Mzee Atanasi alimpiga mpiga mgongoni kumfariji.
“Blandina unatakiwa kurudi nchini Kenya”Aliongea Mzee Atanasi na kumfanya Blandina kumwangalia baba yake kwa wasiwasi , ni kama alikuwa hajamsikia.
“Baba Sitaki kurudi tena nchini Kenya , Nataka niishi na wewe mpaka siku yako itakapofikia , baba naomba usiniambie nirudi nchini Kenya”Aliongea Blandina kwa hali ya wasiwasi, lakini Mzee Atanasi hakupepesa macho.
“Baba ni kweli Blandina anapaswa kuishi na sisi, kwanini arudi Kenya? , sikubaliani na jambo hilo”Aliongea Jestina.
“Jestina utaongozaje familia yangu ukiwa na akili ndogo namna hio , nilishakuambia kila siku usitumie hisia katika kufanya maamuzi , kwanini haupo imara”Aliongea Mzee Atanasi huku sauti yake iliokuwa imenyongea ikidhihirisha msisitizo.
“Baba lakini ….”
“Blandina najua kuna sababu ambayo imekufanya kufanya maamuzi uliofanya ambayo ni Zaidi ya sababu ulizotuambia , lakini kwangu hio sababu haina maana tena , kwasababu ulifanya maamuzi wewe mwenyewe , hivyo unapaswa uwajibike , utarudi nchini Kenya kuendelea na maisha yako , sisi tushafurahi kukuona upo hai hio inatosha, na nitoe msisitizo , swala hili kuanzia sasa litaendelea kuwa siri ya familia”
Aliongea Mzee Atanasi na akampa ishara mlinzi wake kua amsaidie anyanyike kuelekea kwenye gari, mzee huyu alionekana hakutaka jibu lolote kutoka kwa Blandina wala kujua ni mawazo gani mwanae alikuwa akifikiria , yeye aliamini katika maeneno alioongea na hata Blandina hakutaka kupinga , alijua siku zote baba yake neno lake ni sheria na hivyo ndivyo alivyowalea.
“Dada katika ile barua ulituamboia Denisi alikufa kwa ajali ya ile ndege , je ulihakikisha?”Aliuliza Jestina mara baada ya Mzee Atanasi kutoka.
“Nadhani unajua ajali ya Ndege ilivyokuwa Jestina , haikuwa na haja ya mimi kuhakikisha”Aliongea Blandina kwa huzuni.
“Sawa dada , hatupaswi kufikiria sana mambo yaliopita , nimefurahi sana kukuona kwa mara nyingine dada yangu , niliishi kwa maumivu mengi baada ya kupata taarifa ya ile ndege”Aliongea na kukumbatiana kwa mara nyingine huku wakionesha kulia tena,Jestina alikuwa na kitu anacho moyoni lakini hakutaka kuongea kwa wakati huo.
Roma Ramoni alikuwa ashalala muda mrefu sehemu ambayo alikuwa ameketi na hii ni kutokana na kwamba hakuwa na mtu yoyote wakuongea nae , licha Yezi na Mama Issa wapate muda wakuongea na hata wakati Mzee Atanasi anaelekea kwenye gari yake hakumuona.
Jestina na Blandina walitumia muda wa takribani lisaa kuongea na Mama Issa hakutaka kuyaingilia maongzi yao , lakini hata yeye pia alikuwa bize kusikiliza namna ambavyo Yezi aliishi akiwa nje ya Kituo.
Wakati Roma akiwa akiwa anafurahia usingizi wake , simu yake ndogo iliokuwa kwnye mfuko wake wa suruali ilianza kuita na kumfanya apeleke mkono na kuitoa na bila ya kuangalia jina aliweka sikioni.
“Your Majest Habari za saa hizi?”Ilikuwa ni ambayo Roma aliitambua ni ya Diego.
“Salama Diego , kuna mpya gani?”
“Niiimekupigia kukueleza kwamba tumeweza kunusa uwepo wa Yan Buwen ndani ya Tanzania”Aliongea Diego na kumfanya Roma akae vizuri kwenye kiti.
“Ameingia Lini Tanzania?”
“Ameingia Jana usiku ,Mfalme Pluto”
“Mmegundua ni kwanini yupo Tanzania?”
“Hatujapata kufahamu ni kwanini Yan Buwen yupo Tanzania , lakini tuliweza kufuatilia ratiba yake kwa kudukua tarakishi yake ya mapakato ambayo anatumia,na katika watu ambao wapo kwenye ratiba ya kuonana nao leo ni pamoja na Malkia Persephone”
“Unamaanisha mke wangu ana ‘Appointment na Yan Buwen?”
“Ndio Mfalme pluto na tumefuatilia muda na mahali ambapo wanapaswa kuonana na Malkia , na mwanzo ratiba ilipangwa saa nne za leo asubuhi lakini baadae tukagundua imesogezwa mpaka saa moja ya leo usiku”Aliongea Diego na kumfanya Roma afikirie kidogo , hakujua ni kwanini Edna alikuwa akitaka kuonana na Yan Buwen , licha ya kwamba Roma alikuwa na hisia kuwa linaweza kuwa sawa la kibiashara , lakini kutokana na matukio yaliotokea juu ya The don aliamini huenda kuna jambo la ziada.
“Mtu gani mwingine muhimu yupo kwenye ratiba yake?”
“Yupo Waziri wa Sayansi na Teknolojia ambaye anapanga kuonana nae , lakini pia watu ambao amekutana nao nje ya ratiba yake ni ‘Scorpion’”
“Scorpion!!”
“Ndio Mfalme Pluto ,Mwanzoni hatukuweza kumtambua Scorpion , lakini baada ya kufatilia taarifa zake tumegundua ni ‘Proffessional Killer’ kutoka ‘Assasination Group’ kutoka China linalofahamika kwa jina la Yamaguchi na yupo Tanzania kwa Zaidi ya miaka miwili akihudumu kama mlinzi wa Mheshimiwa Kigombola”
Roma alijikuta akifikiria maneno hayo ya Diego na kujiuliza kwannini Yamaguchi wakamleta Scorpion Tanzania, maana hakuamini kama Muuaji mkubwa anaweza akawa mlinzi pekee wa Kigombola.
“Okey!!Diego nitamsidikiza mke wangu kwa ajili ya kuonana na Yan Buwen na kama kuna swala muhimu ambalo nitaligundua nitawataarifu iili iliweze kuwasaidia katika uchunguzi wenu juu ya The Don”
“Asante sana Mfalme Pluto”.Aliongea Diego na kisha kukata simu huku akiwageukia Mama Issa na Yezi ambao walikuwa bado wakiongea.
“Mfalme Pluto kama angefahamu tumedukua mawasiliano ya Malkia , nadhani asingetuacha salama”Aliongea Bram aliekuwa ameweka Maheadphone yake kichwani huku akimwangalia Diego.
“Ndio,Bram , lakini hatuna namna , ili kumpa ulinzi wa kutosha Malkia lazima tuhakikishe tunajua ratiba za kila mfanyabiashara anaekutaka nae”Aliongea Diego.
Baada ya kama nusu saa hivi ya Roma kuwasiliana na Diego ,hatimae Mke wa Raisi wa kenye alitoka kwenye ofisi ya Mama Issa na alionekana alikuwa tayari kwa ajili ya kurejea nchini Kenya kama baba yake alivyompa maagizo na muda huu na Roma alikuwa amesimama na Mama Issa, na hii ni baada ya Mama Issa kumuomba Yezi alale siku hio ndani ya kituo hiko na arudi kesho yake na Roma alikuwa akijiandaa kuondoka.
“Blandina kwa jinsi alivyokuwa amemkodolea macho Roma ni kama alikuwa akimfananisha,Ukweli ni kwamba licha ya Blandina kuzimishwa na ajenti Dondwe hakuonana na Roma ,kwani ile anazinduka alikuwa ndani ya ofisi ya Mama Issa m hivyo ni rahisi kusema hakuwa amekutana na Roma kabisa.
“Blandina huyu ndio alietusaidia kufanikisha sisi na wewe kuonana.Anaitwa Mr Roma ni mume wa Edna”Aliongea Jestina baada ya kumfikia Roma , lakini muda huu Roma na Blandina walikuwa wameangaliana machoni wakishangaana na Jestina alikuwa akiwaangalia kwa namna ambavyo walikuwa wakiangaliana.
“Ooh! Asante sana Mr Roma ,nimefurahi kufahamu wewe ni mume wa Edna”Aliongea Maina kwa kuweka tabasamu na kumfanya Roma na yeye atabasamu.
“Mr Roma asante sana kwa leo , licha ya kwamba ulinishangaza sana , lakini niseme umekuwa msaada mkubwa kwetu”.
“Mrs Azizi wala huna haja ya kunishukuru namna hio,Nimefanya lile linalotakiwa kufanywa na sio jambo kubwa”Aliongea Roma na kumfanya Mrs Azizi aone Roma anajitahidi tu kuwa ‘Humble’.
“Mama Issa nadhani mimi niondoke kwa muda huu sasa, maana sina nilichobakisha tena hapa”Aliongea Roma.
“Mr Roma asante sana kwa yote ulioyafanya kwa Mwanagu Yezi, hakika umekuwa wa Baraka sana tokea siku uliokuja hapa kituoni ,hakika Edna kajua kutuchagulia mume”Aliongea Mrs Azizi na kumfanya Roma atoe tabasamu la uchungu , yeye pekee ndio aliekuwa akijua yanayoendelea kati yake na Edna, lakini kwa Mama huyu alionekana kabisa kumkubali kama mume wa Edna.
Roma hakutaka kuzikataa shukrani za Mama Issa alizipokea kwa kutabasamu na kisha alimuaga na Yezi pamoja na Mrs Azizi , pamoja na mke wa Raisi wa Kenya na kisha akapiga hatua kuelekea uelekeo wa gari yake ilipo.
“Huenda Denisi angekuwa na umri wa Mr Roma kwa sasa?”Aliongea Blandina aliekuwa akimwangalia Roma mpaka alipoingia kwenye gari yake na Jestina alimsogelea dada yake na kumshika mkono.
“Dada huoni kama wanafanana sana, ninavyomuangalia Roma naona sura yake ya utotoni ni sawa kabisa na ya Denisi”
Aliongea Jestina na Maina alitingisha kichwa na kutoa tabasamu la uchungu , ukweli ni kwamba hata yeye alikuwa na mawazo sawa na ya Jestina , lakini asingekubali kuwa Denisi ndio Roma hata kama wanafanana na hii yote ni kutokana na kwamba Denisi alishakufa kwa ndege ambayo ilipotea mpaka leo na hakukuwa na taarifa yoyote ya abiria yoyote kuonekana au kusalia , hivyo hata mtu yoyote ambaye anamuamini sana akija akamwambia Roma ni Denisi asingekubaliana na hilo , kwani alithibitisha kabisa Denisi akiingia kwenye ndege ya M Airline akiwa pamoja Bite.
Roma baada ya kurudi aliandaliwa chakula cha mchana na kula mwenyewe kwani kila mtu hapo ndani alikuwa ashakula, baada ya bwana huyu kumaliza , alipandisha moja kwa moja mpaka ghorofa ya tatu ambako ndio kilipokuwepo chumba cha mke wake , akiwaacha Sophia na Bi Wema ambao walikuwa wakishindia kuangalia Tamthilia.
“Babe nimetudi!!”Aliita Roma baada ya kufungua mlango wa chumba cha kusomea cha Edna na kumuona Mke wake akiwa bize na kazi kama kawaida yake na Edna alimwangalia Roma kwa sekunde na baada ya kutingisha kichwa chake kama ishara ya kuitikia ,akarudisha macho yake kwenye tarakishi.
Ukweli ni kwamba Roma alitaka aende na Edna kukutana na Yan Buwen , lakini hakujua ni namna gani ya kumfanya Edna akubali kwenda nae , kwani kama angemuambia moja kwa moja, Edna angeuliza amefahamu vipi kama anamiadi ya kukutana na Yan Biwen.
Roma aliingia ndani ya chumba hiki kilichokuwa na vitabu vingi na kuanza kuchagua kitabu , alikuwa ni kama akitafuta kitabu cha kusoma , vilikuwa ni vitabu vingi kiasi kwamba ilimfikirisha Roma kama mke wake amekuwa ashamaliza kusoma hivyo vitabu.
Roma alichomoa kitabu kilichokuwa kimeandikwa na Benjamini Graham kilichokuwa na kichwa cha ‘The Intelligence Investor’ na kukichomoa na kurudi kwenye sofa na kuanza kufungua peji harakaharaka bila kusoma na kumfanya Edna amwangalie na mwanadada huyu midomo yake ilicheza kidogo, alionyesha kuchekeshwa na namna ambavyo Roma alikuwa akifungua hiko kitabu kama mtoto ambaye hana mpango wa kusoma , maana sio kama alivyotegemea , yeye alijua Roma anakaa kusoma hiko kitabu , lakini alikuwa akikifungua kwa spidi huku bila kuonyesha nia ya kukisoma.
“Romaa..!!!”Aliita Edna na Roma alimgeukia.
“Yes! Wife”
“Who is Queen Persephone?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma ashangae , alijiuliza ni wapi Edna kasikia hilo jina, na ukweli Edna haikueleweka kwannini ameuliza leo , kwani ni muda kidogo tokea aitwe hilo jina na Chiara.