Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 36

RWANDA -KIGALI 2014

Ni ndani ya hoteli kubwa iliokuwa ndani ya jiji hili la Kigali , hoteli iliokuwa ikifahamika kwa jina la The Aquad alionekana mwanamke na mwanaume wakiwa ndani ya chumba kikubwa cha hoteli hii , katika floor ambayo ilikuwa ikihudumia VIP , huku nje ya Floor hii wakiwa walinzi wengi waliokuwa wamevalia suti.

Ndani ya chumba hiki mwanaume alionekana akiwa amepiga magoti chini , huku mwanamke mmmoja mrembo wa mweupe wa kabila la wanawake wa Babati yaani Wairaq akiwa amesimama huku akiwa na machozi mengi usoni , alionekana kulia mfululizo huku akiwa ameshikilia moyo wake.

“Nisamehe sana Raheli, naomba unisamehe mpenzi ,,, sikudhania haya yote yatatokea”

“Jeremy acha kuomba msamaha wako wa kipuuzi mbele yangu , unazidi kuniumiza , kwanini ulinificha muda wote kama Lorraine alikufa , kwanini Jeremy haukuniambia hii.. hiii…kwanini Jeremiiii…..”Mwanamke alionekana kulia kilio ambacho hakikiwa cha kawaida huku akimshutmu Jeremiii.

“Sikuwa na jinsi Rahel , sikutaka upitie maumivu niliopitia mimi”.

“Hata kama Jeremy , Lorraine ni mwanangu nilipaswa kujua haya yote ,hivi unajua ni siku ngapi nilitumia kuchukua maamuzi ya kukukabidhi Lorraine na kubaki na Edna eeh , unajua ni uchungu gani niliopitia kuwa mbali na mwanangu , hayo yote nilifanya kwasababu nakupenda Jeremy .. lakini kwanini ulishindwa kumlinda…..”Kilio kilikuwa ni cha aina yake kwa mwanamama huyu alionekana kumlaumu Jeremy kwa yale ambayo yamemtokea Lorraine , lakini pia anamlalamikia Jremy kwa kutompa taarifa ya kifo cha mwanae ,

“Rahel naomba unisamehe , najua ni maumivu gani unapitia baada ya taarifa hii , najua ulitarajia kumuona Lorraine akiwa na furaha ndani ya mikono yangu , lakini mimi pia kama baba yeke nilikuwa nikimpenda sana Lorraine na nilipanga kumpa Maisha mazuri , lakini haya makafir.. ya Dunia yamenichukulia mwanangu”.

“Unamaanisha nini Jeremy?”Aliuliza mwanamama huyu huku akisimama , hakumuelewa Jeremy baada ya kusema makafir alitaka kujua anamaanisha nini, Na kwa Jeremy alijikuta akijilaumu kwa kuropoka.

“Unamaanisha nini Jeremy ukisema Makafir ndio waliomchukua Lorraine?”

“Sijamaanisna hivyo Lorraine.. ni …”Kabla hajamaliza kuongea alikuwa ashashikwa tai na Raheli , mwanamama huyu alionekana kuzingatia kila neno mtu analoongea na ndio maana aliweza kumsikia vyema Jeremy alipo sema Makafir .

“Rahel namaanisha ,,”

“Usipo nipa maelezo ya kutosha leo Jeremy nakwambia hapa hutoki …”Jeremy alikuwa akimjua sana Rahel akiamua lake jambo lazima litimie , lakini hakutaka kumwambia Rahel juu ya kile anachokijua na anachoendela kukitafutia ukweli wake.

Jeremy aliamini kwa asilimia mia moja Ndege ile haikuanguka , bali kuna mpango wa siri ambao ulikuwa ukiratibiwa na mataifa yenye nguvu duniani , mpango ambao ulihusisha ndege hio kupotea, aliogopa kumwambia Rahel ukweli.

“Jeremy umenificha kwa miaka kumi na sita juu ya kifo cha mtoto wangu .. ukinificha jambo lolote na nikagundua jua sitokuja kukusamehe mpaka naingia kaburini”Aliongea mwanamama huyu huku akionesha hasira zake waziwazi.

Jeremy hakuwa na jinsi aliona Rahel anapaswa kuujua ukweli ule ambaye yeye alikuwa akiufahamu , aliona haina maana ya kumficha.

“Rahel tokea siku ambayo ndege ile ilipotea moyo wangu haukuwa na Amani kabisa , niliona kabisa kuna jambo ambalo halikuwa sawa , sikuwa na amani nilikuwa nikiota kila siku Lorraine yupo hai lakini sehemu aliokuwepo anateseka..”Alitulia kwanza na kufuta machozi na kisha akasimama huku akiwa anaangalia dirisha kama mtu aliekuwa akitafuta kitu.

“Kupotea kwa ndege ya shirika la M ilikuwa ni mpango wa wazungu”Rahel ni kama hakuwa amemsikia vizuri , kwani alinyanyuka na kwenda mpaka mbele ya Mheshimiwa Jeremy na kumwangalia vizuri usoni.

“Nieleze vizuri nielewe Jeremy .. mpango wa Wazungu ,, unanichanganya hebu eleza nielewe”

“Siwezi kukueleza mengi Rahel lakini naamini Lorraine yupo hai .. hakuna ushahidi wowote wa ile ndege kuanguka Rahel , yote ni mipango na mahesanu ya wazungu juu ya mpango ambao mpaka sasa hatuujui , mpango ambao umeratibiwa na mataifa makubwa yenye nguvu.. hii ni siri kubwa Rahel na sitaki kukuambia Zaidi ila naomba uelewe nitahakikisha naujua ukweli wote , nitatumia nguvu zangu zote kuhakikisha naupata ukweli wote na kama Lorraine yupo hai nitamrudisha “.

Taarifa hio ilionekana kuwa nzito sana kwa mwanamama Rahel , alikuwa akimjua Jeremy kwa muda mrefu tokea walivyokutana miaka kadhaa nyuma na kuanzisha mahusiano yao , alikuwa akimjua kuwa hawezi kuongea jambo ambalo hana uhakika nalo , alijikuta nguvu zikimuishia na kurudi kukaa kwenye sofa huku machozi yakiendelea kumbubujika.

Ukweli ni kwamba mwanamama huyu sababu ambayo ilimfanya asigundue kuwa Lorraine amekufa ni kutokana na kwamba Jeremy alitumia Mchezo wa kumuigizia kuwa anamchukia , kipindi chote ambacho Rahel alijaribu kuwasiliana na Jeremy , mheshimiwa huyo alionyesha kumchukia sana Rahel na hakutaka mazungumzo, na hata pale ambapo aliomba kuonana na Lorraine mheshimiwa alimtishia Rahel kukaa mbali na Lorraine la sivyo ataongea ukweli wote na dunia ijue kuwa Edna ni mwanae.

Kwa upande wa Rahel hakuwa tayari kwa watu kujua kuwa Edna sio mtoto wa Adebayo kwani kulikuwa kuna mkataba wa siri ambao alisaini na familia ya Adebayo , mkataba ambao Raheli alisainishwa na mama yake Adebayo.

“Jeremy una uhakika ndege ile haikudondoka na yote uliosema juu ya mpango ya wazungu ni kweli?”Aliuliza kwa sauti ndogo iliokuwa dhaifu na Jeremy alimuonea huruma sana Rahel , alijua ni afadhali kwake maumivu ya kumpoteza Lorraine yamezoeleka kwani tukio lilikuwa ni la muda mrefu tarkribani Zaidi ya miaka kumi na sita , alimsogelea Rahel na kisha akamkumbatia na walianza kuambizana kulia.

Kwa namna ambavyo Jeremy alikuwa akillia usingedhania ni kiongozi mkubwa wa taifa , kiongozi ambaye wananchi wa Rwanda wanamtegemea sana kuwafikisha katika nchi ya Ahadi.

“Ni kweli Rahel nina amini kwa asilimia kubwa Lorraine yupo hai na ninaompango wa kuhakikisha namrudisha”.

Rahel alifuta machozi na kisha alijitoa kwenye mikono ya Jeremy na akaweka sura ya usiriasi .

“Jeremy kama haya unayoyasema ni ya kweli hakikisha unaujua ukweli la sivyo sitokusamehe kwa kumpoteza mwanangu Lorraine”Aliongea mwanamama huyu na akafuta machozi na kuchukua mkoba wake na kutoka ndani ya chumba hiko.

****

Ilikuwa ni muda wa saa sita kamili za mchana alionekana Roma akiingiaa maeneo ya Club B , alikuwa na muda mrefu hajaingia ndani ya hii club , kwani tokea apate mke mara nyingi alikuwa akienda moja kwa moja nyumbani kwa Rose , lakini leo alikuwa amewahi sana kuja haya maeneo na alijua kabisa Rose hakuwa kwake na atakuwa ofisini na mawazo yake yalikuwa sahihi kwani alimkuta mwanada huyo akiwa kazini kama ilivyokuwa kawaida yake na kwa Rose alishangaa ujio wa Roma muda huo wa mchana.

“Hubby karibu” Aliiongea Rose huku akitoka kwenye meza na kuja kukaa kwenye masofa , huku akimwangalia Roma kwa kumsanifu , aliwaza Roma kaja muda huo kwasababu gani.

“Bebi Rose nimekuja leo nina shida”Aliongea Roma mara baada ya kuketi.

“Shida gani mpenzi , ongea tu nipo tayari kukusaidia”

“Unamiliki nyumba ngapi?”

“Bebi kwanini unauliza hivyo nina nyumba nne mbili hapa Dar na nyingine zipo nje kidogo ya Dar , kuna ambayo ipo Kisarawe na Bagamoyo “

“Kwa hapa Dar ukiachana na unayoishi hio nyingine ipo maeneo gani?”

“Ipo Kigamboni Mbutu huko”

“Hio ndio shida yangu , nahitaji nyumba nina marafiki zaku kutoka nje ya nchi ambao wanaingia leo nchini nataka niwahifadhi kwa muda , ila sina nyumba kwa sasa”Aliongea Roma na Rose alitabasamu.

“Hubby chukua ya Kigamboni itakufaa , pia ni sehemu nzuri kwani ipo ufukweni na isitose ni mpya na nilikuwa nikipanga kuipangisha lakini sikupata mtu”Aliongea Rose na Roma alitabasamu na kumkiss Rose.

“Nataka nikaione leo maana marafiki zangu wakifika nchini moja kwa moja nataka niwapeleke na wanaingia leo usiku”Aliongea Roma na Rose hakukataa , kwanza alijisikia fahari kwa Roma kumuomba msaada yeye, msaada ambao Roma ameomba kwake ulikuwa na maana kubwa.

Ni ndani ya dakika chache tu walikuwa washafika Mbutu , hii sehemu ilikuwa nzuri licha ya kwamba haikuwa na nyumba nyingi , lakini mazingira yake yalikuwa safi sana kiasi cha Roma kupapenda na kuona wanajeshi wake kukaa hapo ni chaguzi sahihi.

Waliona jumba hili ambalo lilikuwa kubwa sana kiasi kwamba hata Roma mwenyewe alishangaa , licha ya kwamba alikuwa akijua Rose ni Tajiri kwa kufanya biashara yake ya kuuza madawa ya kulevya , lakini hakujua kama anapesa kiasi hiko cha kumiliki mjengo kama huo. Walikabidhiana nyumba hio na Roma akamrudisha Rose nyumbani.

Saa mbili kamili Roma alikuwa nyumbani kwa ajili ya chakula , sebuleni alimkuta Bi Wema pamoja na Edna kama kawaida na walikuwa washaanza kula, alimsalimia Bi Wema na kisha akamgeukia mke wake na kumwangalia anavyokula kimapozi , Edna alikuwa bize na chakula chake , lakini ile anapeleka kijiko mdomoni alimwangalia Roma na kukuta Roma anamwangalia.

“Mbona unaniangalia hivyo?”

“Bebi unajua hata staili yako ya kula inakufanya uwe mrembo kuliko wanawake wote duniani”Edna alijikuta akimwangalia Bi Wema na kuona aibu kiasi kwamba mwili wake ulipata uwekundu.

“Kaa pakua chakula kula”Aliongea Edna na kumfanya Bi wema aliekuwa pembeni atabasamu kwa kushuhudia aibu za Edna.

Roma alipakua chakula chote kilichokuwa kwenye mabakuli na kujaza kwenye sahani kama mlima Kilimanjaro na kuanza kula , bila habari .

“Roma..!”Aliita Edna huku akimwangalia Roma na sahani yake na Roma alimwangalia Edna bila kuongea.

“Kesho kutwa ndio siku ya kwenda Japan , ujiandae basi nitakupatia baadhi ya karatasi za mkataba uzisome”.

“Mke wangu mimi naenda kama mkalimani kuna haja gani ya kuzisoma?”

“Ndio najua lakini huu mkataba ni muhimu sana kwa kampuni na kukitokea tatizo lolote ninaweza kufirisika moja kwa moja , ni vizuri ukijua nini kinaendelea ili kama ikitokea tatizo iwe rahisi ya wewe kuligundua kuliko kumwachia kila kitu Doris”.

“Sawa nitazipitia mke wangu”.

Baada ya Roma kushiba , aliangalia saa yake na kuona ni muda muafaka wa kuelekea uwanja wa ndege kwa ajili ya kupokea wageni wake , kwani mchana alikuwa ashawasiliana na Sauroni na kumpa taarifa kuwa wataingia Tanzania saa nne usiku.

“Wife ninatoka kidogo”

“Leo naomba usiende”Aliongea Edna na kumfanya Roma ashangae na sio Edna tu hata Bi Wema alishangaa , lakini alitabasamu moyoni .

Ukweli ni kwamba Edna mchana yote alikuwa akifikiria swala la kujaribu kumpa Roma kitumbua na alishinda kwa kutafuta mitandaoni jinsi ya kumuanza mume wake maana alikuwa na aibu sana , alitamani kumuuliza Bi Wema ampe mbinu lakini aliona aibu na msaada pekee aliona ni kuingia mtandaoni na kutafuta namna ya kumuanza Roma.

“kama nitakuwa nampa maramoja moja anaweza kutulia nyumbani”Aliwaza wakati akiendelea kusoma mbinu mtandaoni.

Na alijikuta akipata mpango kabambe wa kumpagawisha Roma huku akiamini kama atafanikiwa katika mpango huo basi anaweza kumtuliza Roma nyumbani.

Na alipanga mpango wenyewe ili ukamilike lazima Roma alale nyumbani na ndio maana baada ya Roma kumwambia anataka kutoka aliona mpango wake hautofanikiwa na alitaka kuukamilisha kabla ya Roma na Dorisi kwenda Japani.

KIONJO .. MWENDELEZO NAUWEKA KABLA YA JOGOO LA ASUBUHI…

Roma hakujua sababu ya Edna kumwambia abaki nyumbani ,lakini kwake yeye alikuwa na jambo muhimu sana la kufanya usiku huo na kwa vyovyote vile asingeweza kukubaliana na mke wake.

“Mke wangu ninatoka ila nitarudi”Aliongea Roma na akanawa mikono na kuchukua ufunguo wa Gari yake na kuondoka.

Edna aliishia kusikilizia tu mngurumo wa gari ukifubaa kwenye masikio yake , Bi wema hata yeye alijisikia vibaya , alitamani Roma abaki nyumbani kama Edna alivyopendekeza lakini hakubaki , aliwaza ni jambo gani la muhimu ambalo Roma anaenda kulifanya nje kuliko kubaki na mke wake , hakujua lakini hakutaka kuwaza Zaidi , kwani Roma alikuwa ni mwanaume na pia hakutaka kuangilia katika mahusiano yake yeye na Edna.

Edna alirudi chumbani kwake , huku akijisikia mnyonge sana lakini pia akiwa na hasira nyingi , katika akili yake alijua kabisa Roma alikuwa akienda kuonana na wanawake wake.

“Mimi sio muhimu kwake , wanawake wake ndio muhimu ..Damn you Roma .. nimejipanga vyote hivyo leo kwa ajili yako halafu unaniona sina thamani… shenz kabisa , nakuambia hivi Roma utanisikia kwenye bomba ,Kwanza nini kilinipata mpaka nikawa na mawazo ya kijinga ya kumpa mwili wangu …Aaah Edna wewe mjinga kweli, Roma sio wa kumpa mwili wako ni Malaya yule mwanaume”Ungemuona Edna anavyoongea na mto usingemdhania ni yule CEO mwenye heshima zake , alikuwa akiongea mweyewe huku akiangalia mto uliokuwa kitandani kwake.

“Ila mimi mjinga sana hadi aibu ..Aaa nisingemwambia abaki nimejidharirisha leo …Edna usie ukarudia tena”Aliendelea kuongea mwenywe na kisha akachukua shuka na kujifunika gubigubi.

Upande wa Roma alifika Uwanja wa ndege kama kawaida muda ulikuwa ni saa tatu hivi kama na nusu , baada ya kusimama nje ya jingo la Terminal 3 akisubiria wageni wake , alikuja mwanaume mmoja wa kizungu alievalia suti bila tai huku akiacha vifungo viwili vya shati lake kuwa wazi na kumfanya nywele za kifuani kuonekana, aligonga gari la Roma mara mbili kwenye kioo cha mbele.

“You are Mister Roma ??”Aliuliza yule mzungu na Roma alitingisha kichwa kukubali kuwa ni yeye , yule mzungu alitoa ufunguo mfukoni na kumpatia na Roma alitabasamu na kisha akauchukua ule ufunguo huku bwana yule wa kizungu akiondoka mbele ya gari la Roma , alionekana kazi ambayo ilikuwa imemleta mahali hapo alikuwa ashaimaliza.

Baada ya dakika kama mbili hivi kupita ,Roma alitoka kwenye gari yake akiwa ameshikilia ile funguo ya gari na kisha alianza kubonyeza bonyeza kitufe cha rimoti iliokuwa imeambatana na ufunguo na gari lilitweak na kuwahsa taa za mbele na Roma alitabasamu na kuisogelea.

Ilikuwa ni gari kubwa kutoka kampuni ya Toyota , iliokuwa na uwezo wa kubeba Zaidi ya watu kumi na tano na ilikuwa imeletwa hapo na Ubalozi kwa ajili ya kuwasafirisha wageni kutoka uwanja wa ndege kwenda kwenye makazi yao.

Roma baada ya kuikagua na kuridhika , alitoka nje na ndani ya dakika chache tu , alishuhudia ndege kubwa kampuni ya KLM ikiiambaambaa kwa kushuka ndani ya uwanja huu wa Dar es salaam, aliendelea kusubiri kwa takribani dakika kumi na tano na hatimae alianza kuona wageni wake wakitoka nje kabisa ya mlango wa ‘Arrivals’.

Wa kwanza kabisa alikuwa ni mwanamke mzungu aina ya Cauccasian aliekuwa amevalia surali ya jeans rangi ya bluu n araba nyeupe huku akiwa amefunga kiunoni shati moja ya draft akiwa amevalia miwani , alionekana mrembo.

Wasichana wengine watatu walitoka huku nyuma yao wakifuatiwa na wanaume sita wote walionekana kuwa katika lika moja la ujana kati ya miaka 25 kwenda 30 , Roma aliwaona wazungu hao na kutabasamu , kwa namna ambavyo walikuwa wamebaba mabegi yao walionekana kama watalii , karibia wote walikuwa wakitafuna bublish.

“Your Majest Pluto”Aliongea yule mwanamke kwa mshangao , huku akionesha heshima ya hali ya juu kwa Roma lakini Roma alimpa ishara na mzungu yule alielewa na wenzake walielewa na kutulia .

“Welcome in Tanzania guys”

“Thank you” waliitikia wote kwa pamoja na Roma alitabasamu na kumrushia kijana mmoja funguo ambaye alikuwa mwembaba.

“You will drive along with me”Aliongea Roma na kuwaonyesha gari iliokuwa upande wao wa kushoto na wote wakatabasamu na kuisogelea na wote wakaingia ndani , lakini wakati Roma ashaanza kulisogeza gari lake kuingia barabara kuu , mara zilikuja gari tatu diffenda na kusimama barabarani na palepale walionekana wanajeshi wakiruka kwa ustadi mkubwa kwenye gari wakiwa na siraha na kisha kulizunguka gari lile walilopanda wazungu , walionekana walikuwa wamejipanga kweli.

Roma alishuhudia kitendo kile akiwa ndani ya gari yake na kujikuta misuli ya uso ikisimama , kwa namna wanajeshi hao walivyokuwa wanaonekana mahali hapo ilionesha kabisa walikuwa na taarifa za kutosha na ndio maana walionekana kujipanga.

Baada ya kuona gari lile limezingirwa Roma alishuka kwenye gari yake na kusogea upande wa wale wanajeshi walipo , lakini kabla hajawafikia gari iliokuwa mbele yake mita kadhaa , gari ambayo ilikuwepo hapo muda mrefu kidogo kwani aliiona , ilifunguliwa na akatoka mzee mmoja hivi mwenye mwili mkubwa wenye afya alievalia miwani pamoja na suti ,Roma hakumjua mzee huyu.

Yule mzee alimsogelea Roma huku wanajeshi watatu wakimzingira upande wa kulia na kushoto na nyuma wakionesha kumlinda ,Roma aliendelea kujiuliza mtu huyu ni nani na kwanini amewazingira wageni wake , kwani swala la wageni wake kuja ndani ya taifa la Tanzania lilikuwa ni siri sana na waliokuwa wakijua ni watu wachache sana ndani ya ubalozi wa Sweden.

“Tunaomba mshuke kwenye gari”Aliongea kwa kingereza moja ya wanajeshi ambae alikuwa na nyota tatu begani na wale wazungu waliangaliana na jamaa mmoja mwenye mwili mkubwa aliwapa ishara wenzake washuke na wakashuka huku wakiwa wamenyoosha mikono juu kuonesha kwamba hawapo kishari.

“Tupo hapa baada ya kupata taarifa ya nyie kuwa wanajeshi mnaokusudia kuingia ndani ya nchi yetu bila ruhusa”Aliongea yule Mwanajeshi alieonekana kuwa kiongozi na wakati huu Roma alikuwa ashafika upande aliosimama mzee ambaye alikuwa amevalia suti na yule mzee alimwangalia Roma na kisha wakasogeleana.

“Habari yako mzee , unaonakana wewe ndio kiongozi mkuu hapa , nini kinaendelea mbona wageni wangu wanazuiwa”.

“Nadhani mpaka sasa ushajua kwanini wanazuiwa Mr Roma Ramoni , Sisi ndio walinzi wa mipaka ya taifa hili na tunajua kinachoendelea nje na ndani ya mipaka yetu na hatupo tayari kuona wanajeshi wanaingia ndani ya taifa hili bila kuwa na kibali maalumu”

“Una Ushahidi gani kama wakujitosheleza kama hawa ni wanajeshi?”Mzee huyu alitabasamu.

“Hawa ni wanajeshi kutoka kundi la The Eagles na taarifa za ujio wao tulizipata kutoka kwa watu wetu ndani ya ubalozi”.Aliongea mzee huyu na Roma alimwangalia na kuwageukia wanajeshi wake waliokuwa katika hali ya wasiwasi.

“Mr Roma tunajua wanajeshi hawa wanauwezo mkubwa wa kimapigano , lakini leo lazima sheria za nchi zifuatwe hatuwezi kuwaachia wakaingia uraiani pasipo kujua ni sababu zipi zimewafanya kuingia hapa nchini , hivyo tutaenda nao pamoja na wewe kambini kwa ajili ya mahojiano”

“Hapana,naondoka na wageni wangu”Aliongea Roma na kumfanya mzee huyu amshangae na kisha akatabasamu

“Hauna uamuzi katika hili”: aliongea na kisha aliwapa ishara wanajeshi wafanye kazi , lakini ile wanataka kuwasogelea wale wanajeshi wa kizungu walishusha mikono chini na wanajeshi wa kitanzania walikuwa fasta sana kwani walikuwa ashakoki siraha zao tayari kwa mashambulizi.



Wanajesh wale wa kuzngu walimwangalia Roma huku wakionesha wanataka Ruhusa kutoka kwake , ila Roma aliwaangalia na kisha akamgeukia huyu mzee huku akiwaza jambo la kufanya , lakini kabla hajaongea ziliingia ndani ya eneo hili gari nyingine mbili moja Range Vx na moja difenda na baada ya gari hizi kusimama alishuka mzee mwingine alievalia gwanda huku mabega yake yakiwa yamechafuka kwa vyeo vingi, wale wanajeshi baada ya kuona mtu huyo ametoka kweye gari na na kumtambua walijikuta wakitoa heshima na kushangaa kwa wakati mmoja kwanini mkuu wao yupo hapo.

Upande wa huyu mzee aliekuwa akiongea na Roma pia alishangazwa na ujio wa mkuu wake , ghafla tu alikakamaa mwili.

“Jambo Afande” lakini Mzee huyu hakuongea chochote Zaidi ya kuinua mkono ya kumwambia alegeze na kumsogelea Roma.

“Mr Roma unaweza kuondoka na wageni wako , mengine tuongee siku ya kesho baada ya kuwasiliana ”Aliongea huyu mzee mwenye manyota mengi na Roma alitingisha kichwa pasipo kusema lolote na kisha akawapa ishara wanajeshi wa kizungu na wote wakaingia kwenye gari na kuondoka eneo hili Roma akiwa ametangulia.
 
SEHEMU YA 38

Ni ndanni ya dakika chache tu Roma alikuwa ashafika Mbutu akiwa na wageni wake , aliingiza gari na kuegesha na kisha akawakaribisha ndani , Wageni hawa walipendezwa sana na nyumba , hio licha kwamba ilikuwa usiku , lakini ilionekana kuwa nyumba nzuri kwao yenye mazingira ya kuvutia.

“Guys here is now your home , all your missions will be operated here , feel free and welcome again in Tanzania”.

“Thank you! ,Your Majest Pluto , it`s has been our dream working with you personally and we ready for any instructions”

Aliongea kijana mmoja kibongea ambaye ndio alionekana kuwa kiongozi katika hili kundi la wazungu na Roma alitabasamu.

Kwanza kabisa aliwanza kuwakagua mmoja mmoja kwa dakika kama nne hivi , akiwazunguka nyuma na mbele na kisha akatabasamu baada ya kuona ya kuridhishwa nao , lakini bado vijana hawa wa kizungu walionesha hali ya wasiwasi , walionekana kukosa kujiamini.

“Okey nimeridhishwa na uwezo wenu, tuingie ndani kwanza”Aliongea Roma kwa kingereza Safi na wakatabasamu na kisha wakamfautisha kwa nyuma na wote wakaingia ndani na kuweka mizigo yao chini kwenye sebule hii kubwa ambayo ilikuwa na furniture za bei kubwa , mabwana hawa waliangaliana na kisha wakatabasamu.

“Kwanza kabisa nataka niwatambue majina yenu mmoja mmoja na kila mmoja kwa uwezo wake cheo ndani ya The Eagles”

Aliongea na wakaanza kuangaliana ni kama kila mmoa alitaka mwenzake aanze huku wakiwa wamesimama na Roma akiwa amekaa huku amekunja nne , alikuwa ni kama bosi hapa ndani kwa muonekano wake na waliokuwa mbele yake walikuwa vijakazi wake.

“My name is Bram Garcia, I am an expert in computer , with various records in hacking issues, in 2016 I managed to hack the communication system of the international space station, also.....”( jina langu Bram Garcia ni mtaalamu katika maswala ya Computer , nikiwa na rekodi mbalimbali katika maswala ya Hacking , mwaka 2016 nilifanikiwa kuhack mfumo wa mawasiliano wa international space station, na pia ..) Roma alimwambia asiendelee kwani asharidhika na kuashiria mwingine aendelee

Baada ya dakika chache Roma aliridhika na utambulisho wa kila mmoja na kusimama na kuwaangalia mmoja mmoja.

“Okey Liutenant Diego utakuwa kiongozi wa kundi hili na utapokea maelekezo yote kutoka kwangu .. kuna mwenye pingamizi?” Wote walipiga Salute.

“Chiara na John mtakuwa na jukumu la kuhakikisha usalama wa mke wangu popote pale anapoenda na iwe kwa siri sana , akiwagundua mnalinda kazi hamna” Walipiga wote saluti.

“Wote nane mliobaki kwanzia leo hii kazi yenu ni kuhakikisha mnajua kila kinachoendelea kwa watu ninaoneda kuwatajia… “alisimama kuongea na akawaangalia wote na wanajeshi hawa walianza kujishuku .Na Diego alijua kwanini Pluto anawaangalia na alimpa ishara Chiara mwanadada ambaye alikuwa ndio aliekuwa amefunga shati kiunoni na Chiara alielewa ishara hio na haraka haraka akatoa notebook na kalamu.

“Nataka muanze kumfatilia mtu anaejiita kwa jina la The Don kwanzia nani anaongea nae , ratiba zake za kila siku na mtandao wake wote wa kibiashara ndani na nje ya nchi , wa pili nataka taarifa za mheshimiwa Senga watu wote ambao anawasiliana nao kwa siri na kila kitu kinachoendelea Ikulu ambacho kina muunganiko na mimi, naomba taarifa hio ipewe kipaumbele na kuchambuliwa vyema , nikija kwenu nitahitaji ripoti tu , kazi ya tatu ambayo nadhani wote mnamfahamu Seventeen nafasi yake ndani ya kikosi na sehemu yake katikamaisha yangu? , nataka mchimbe na mnipatie muunganiko wote uliopo kati ya mke wangu na Seventeen”Walishangaa na Roma akatabasamu.

“Haina haja ya kushangaa maafande , mkishamuona mke wangu mtajua kwnini nawapa hio kazi ,na yangu kwa leo ni hayo tu nasisitiza ulinzi kwa mke wangu lazima upewe kipaumbele naelewa The Eagles tuna teknolojia kubwa , hivyo teknolojia hio nataka itumike katika kumpa ulinzi Edna tumeelewana”

Wote waliitikia kwa kupiga saluti na Roma alinyanyuka na akamwangalia Diego.

“Utawasiliana na Sauron kwa mahitaji yote mtakayohitaji mkiwa hapa nchini , lakini pia mishahara yenu itaongezeka kwa asilimia ishirini kutokana na kazi hii , niwatakie usiku mwema na maukumu mema”Wote walitabasamu kwa shangwe .

Baada ya kusema hayo Roma alitoka na kuwaacha na kugeuza kwenda nyumbani kwake , na muda ulikuwa umeenda kweli , lakini kutoka Mbutu na Sunlight Villa palikuwa ni umbali mdogo sana.

Kama kawaida alikuta walinzi wako macho na kikama walikuwa wanamsubiria kwani ile anafika tu alifunguliwa geti na kuingia ,taa za ndani zilikuwa zimezimwa kuonesha Bi Wema na ,mke wake walikuwa washalala kitambo , na hakujali sana , alijirusha kitandani baada ya kupunguza nguo na kuangalia gypsum.

“Kazi yangu ilionirudisha hapa nchini imeanza na nitaujua ukweli wote kwanini Seventeen na Edna wanafanana na kwanini mimi na Seventeen tukawa peke yetu kwenye kile kisiwa”Alijiongelesha Roma na kisha akalala.

****

Ratiba za asubuhi zilikuwa kama kawaida kwa Roma , alianza kwenda kufanya mazoezi ya kuuweka mwili sawa na baada ya hapo alirudi chumbani kwake baada ya kusalimianan a na Bi Wema ambaye alikuwa bize na usafi pamoja na kuandaa kifungua kinywa.

Baada ya kujiweka sawa kwa ajili ya kuelekea kazini alishuka na ufunguo wake chini kwa ajili ya kifungua kinywa , leo alikuwa amechelewa kidogo kufika mezani kwani Edna alionekana kwenye meza akiwa amenuna , na hakutaka kabisa hata kumwangalia usoni Roma na hata pale Roma alipomsalimia aliishia kutingisa kichwa tu kama salamu na Roma hakujali sana , alikua akijua kwanini Edna amenuna na hakuwa na namna ya kujitetea mbele yake , alichokifanya ni kunywa chai ilioandaliwa.

Wa kwanza kumaliza alikuwa ni Edna alimuanga Bi Wema na mama huyo kumtakia siku njema na kisha kuondoka na ni mgurumo wa gari pekee uliokuwa ukisikika ukifubaa kwenye masikio ya Roma na Bi wema.

Bi wema alimwangalia Roma aliekuwa akimalizia mayai yakukaanga yaliokuwa kwenye sahani , mwanamama huyu alitamani kumuuliza Roma jana kulikuwa na umuhimu gani wa kutoka , kwanini asingebaki nyumbani kama Edna alivyo omba kama Edna , lakini ile anataka kuinua mdomo…

“Bi Wema Asante kwa chai na usiwaze sana kuhusu Edna..”Aliongea Roma na kumfanya mwnamama huyu amuangalie na kujiuliza amejuaje kama alikuwa akiwaza kuhusu Edna , ila Roma hakujali mshangao wa Bi Wema Zaidi ya kufungua mlango… lakini alikumbuka jambo na kusimama.

“Bi Wema kama kuna mtu yoyote akifika hapa wa kizungu naomba umpe nafasi ya kufanya kazi yake , ni maswala ya kiulinzi hivyo haina haja ya kumwambia Edna”.

“Sawa mr Roma kazi njema”Roma alitabasamu na kisha akaondoka na kuchukua gari yake aliodhurumu kule PANZ security Aud Q7 rangi ya Silver , ilikuwa gari nzuri kweli ambayo Roma alikuwa akiendesha , kwa muonekano wa Roma wa sasa usingemdhania kama alikuwa akibeba mizigo siku kadhaa nyuma ndani ya soko la Mbagala , licha ya sasa kuonekana kawaida kimtindo lakinni alikuwa na utofauti mkubwa , uso ulikuwa unang`aa.

Baada ya kufika getini alisimamisha gari na kushusha kioo na kumwangalia Derick aliekuwa ameshikilia gati , licha ya kwamba geti hili lilikuwa likitumia umeme lakini bwana huyu alikuwa akilifungua kwa kulisukuma ili kuonyesha juhudi yake kazini kwa mabosi wake.

Baada ya Derikc kumuona boss wake kasimamamisha gari alimsogelea kwa heshima, huku akipanga ayajenge na Roma kwani tokea siku ambayo alimwita kichaa msafi hawakuwahi kuongea nae tena, kwani muda wote Roma akitoka alikuwa ndani ya gari na hakuwa na ruhusa ya kuingia ndani ya Jumba hilo kwa ajili ya kuongea nae , lakini leo hii bosi wake amesimamisha gari , aliona hio ndio nafasi nzuri.

“Hivi unaitwa nani vile” Aliuliza Roma na ni kweli alikuwa amemsahau jina kwani siku ile alimsikia Edna akimuita ila hakulishika vizuri.

“Naitwa Derick Bosi”.

“Sawa Derick , hebu acha kukakamaa mwili kwa namna hio unaweza ukajamba , kuwa kawaida tu , haina haja ya kuniogopa”

“Sawa bosi” aliongea Derick huku akijiweka sawa kwa kufunga suti yake vizuri .

“Okey kuna watu watakuja hapa wazungu , wakiomba kufanya mambo yao hapa waruhusu nni maswala ya kiulinzi sawa”

“Sawa bosi”

Roma alifika kazini akiwa ni wa mwisho kuliko wafanyakazi wote , lakini leo kulikuwa na mabadiliko kidogo , wafanyakazi walionekana kumuangalia sana kiasi cha kuiuliza kuna nini kwanini wenzake wanamwangalia.

“Recho mambo?”

“Poa Vipi Roma”

“Gudi , kuna nini mbona mnaniangalia sana , au nimezidi kuwa handsome”

“Hongera , tumesikia unaenda Japan kesho kikazi , tumeshangazwa na taarifa hio na kila mmoja anashangaa kwanin umechaguliwa , maana tokea ufike haukuwahi kufanya kazi zaidi ya kucheza gemu , na isitoshe hauna uzoefu wa kutosha na Kampuni , lakini wote hapa ndani hatujawahi kupewa hata kazi ya kwenda nje ya mkoa lakini wewe huna hata mwezi umepata nafasi hio , lazima tukuangalie kwa mshangao”

“Sasa mnachoshangaa nini hapo , ushasahu mimi ndio mwanaume peke yangu ndani ya hii idara, hehe ukute CEO mwenyewe kapagawa na uwepo wangu anataka kuniweka karibu , kwahio msiwaze sana pigeni kazi”Recho alibetua midomp na Roma akageukia tarakishi yake , alitoa headohone kwenye droo ya meza na Pad za kuchezea gemu ,haikueleweka ni lini alizinunua, alichomeka na kuanza kucheza gemu la Mpira PES 2021 , huku wafanya kazi wenzake wakizidi kushangaa, maana mtu kazi yake ni kucheza gemu , lakini kapewa kazi ya kwenda Japani kumwakilisha bosi wa kampuni , jambo hilo kwao liliwashangaza na kuona kuna walakini na uongozi wa kamouni.

Licha ya kujua Roma ni mhitimu wa chuo kikuu cha Harvard lakini bado hawakukubali , kwani ndani ya kampuni hio kulikuwa na wasomi wakubwa tu akiwemo Nasra ambaye alisomea masomo yake yote Cambridge Marekani.

Wakati Roma anaendelea kucheza gemu alikuja Miss Airport na kwenda kusimama kwenye meza yake na kumwangalia Roma kwa sekunde namna ananyofurahia gemu , huku baadhi ya wafanya kazi wakishangazwa na uwepo wa Monica hapo ndani , kwani ni mara chache sana kwa Monica kuja kwenye ofisi yao.

Miss Aiport alionekana kutompenda kweli Roma , na alikasirika Zaidi baada ya kuona Roma anacheza gemu wakati wenzake wote wako bize kufanya kazi , alitamani awe na cheo kisha amfukuze. Alimsogelea Roma na kisha akamvua Headphone na kumfanya Roma ageuke.

“Miss Airport!”Alishangaa roma mara baada ya kugundua mtu aliekuwa amesimama nyuma yake ni Monicca.

“Unaitwa na CEO”aliongea Monica na kisha akageuza na kuondoka kwa maringo , huku viatu vyake vikitoa sauti ya ‘kwaa.. kwaaa.. huku sehemu katikati ya mapaja yake ikionekana kutokana na pasua ya sketi nyeusi aliovalia , alionekana kujisikia kweli kwa mnafasi yake alionayo kwenye kampuni.
 
SEHEMU YA 39

Roma alisubirisha gemu lake na kisha akainuka kwenye meza na kujivuta na kuianza safari , huku nyuma akiwaacha Recho ,Tina na warembo wengine wakimwangalia kwa nyuma mpaka pale kisogo chake kilipotokomea nje , walitingisha vichwa vyao na kuendelea na majukumu yao.

Roma baada ya kutoka kwenye lift alitembea kuelekea ofisi ya CEO lakini njiani alikutana na watu wawili , wa kwanza alikuwa ni Dorisi ambaye alikuwa ametangulia kwa mbele mita kadhaa akimuacha Nadia nyuma ,Doris baada ya kukumfikia Roma alimkonyesha na kumpa busu la hewani na kisha akampita , lakini kitendo hiko kilishuhudiwa na Nadia aliekuwa nyuma na hakufurahishwa na jambo lile , alimwangalia Roma kwa hasira na kisha akampita na Roma aligeuka na kumwangalia Nadia na kutabasamu na kuendelea mbele , mpaka kuingia kwenye ofisi ya mke wake.

“Bebi Nishafika”Aliongea Roma mara baada ya kuingia na kumshuhudia mke wake kama kawaida akiwa bize na tarakishi yake , licha ya kwamba Edna alionekana kauzu lakini muonekano wa yeye kuwa bize na kazi ulikuwa ni wa kipekee kabisa na Roma alitaman kuwa na picha ya mke wake akiwa anafanya kazi ilia awe anaikodolea macho.

Edna hakujibu mara moja aliendelea na kazi na Roma alikaa kwenye sofa akimsubiria mke wake amwangalie , baaada ya kuwa bize kwa dakika mbili Edna aliinua macho yake na kumwangalia Roma ambae amepandisha miguu kwenye sofa akiegemea sehemu ya kuwekea mkono na miguu kuning`inia upande mwingine, Roma hakuwa na tofauti na mtoto kwa mambo ambayo alikuwa akifanya , Edna alitingisha kichwa kwa kusikitika na kisha aliangalia pembeni kwenye kitrei flani hivi cha chuma kinachong`aa na kutoa karatasi.Alinyanyuka kwenye kiti chake na kisha akamsogogelea Roma.

“Angalia hizo karatasi , naomba uzisome zote na uelewe , ni sehemu ya vipendelea vya mkataba ambao mtakwenda kusaini huko Japani”.Aliongea Edna huku akiwa Siriasi na Roma aliinua uso wake na kumwangalia Edna.

“Mke wangu , unaonaje kwanza ukinitengenezea kahawa uniletee niwe na kunywa taratibu wakati nikiendelea kusoma hizo karatasi”

“Huo muda sina , katengeneze mwenywe na karatasi hizi utazisoma mpaka uzimalize ndio uondoke”.

“Bila kahawa nakwambia hivi , sizisomi na nalala hapa mpaka muda wa chakula cha mchana na sitaki kahawa iliotengenezwa na Monica nataka uliotengeneza na wewe mke wangu” Aliongea Roma na kisha akarudia staili yake ile ile na kufumba macho , Edna alijikuta akichemka kwa hasira , alimwangalia Roma namna ambavyo amelala , huku akishindwa kuelewa ni kitu gani akifanye. , aliinua karatasi alizoshikilia mkononi na kuziangalia kwa sekunde na kisha akakunja ngumi kwa hasira na kuziweka kwenye meza na kutembea kihasira hasira na kutoka nje ya ofisi yake.

“Boss unahitaji nini?” Aliongea Monica akiwa amekakamaa kwa heshima.

“Unaweza kuendelea na kazi Monicca natengeneza kahawa”Aliongea Edna na kupita kushoto huku akimuacha Monnica ambaye alikuwa kwenye mshangao , maana kwa mara ya kwanza tokea aanze kazi yeye ndio aliekuwa akimtengenezea Edna kahawa , inakuwaje leo , alitingisha kichwa na kisha alikaa chini na kuendelea na kazi.

Roma na yeye baada ya kusikia mlango ukifunguliwa na Edna kutoka nje , aligeuka na kuangalia na kujikuta akitabasamu na kujisemea moyoni kwamba amemuweza leo.

“Nimemuweza na asipoleta kahawa hapa nzuri sizisomi karatasi zake” Alijiwazia na kisha aliendelea kukaa vile vile akisikilizia kaubaridi kakiyoyozi pamoja na harufu nzuri ya ofisi hii ya mke wake.

Dakika tano mbele Edna alirudi akiwa ameshikilia kikombe na kwenda kusimama mbele ya sofa akiwa anamwangalia Roma kwa hasira na Roma aliinua uso wake na kumwangalia Edna na kisha alitabasau na kupokea kikombe.

“Asante mke wangu kipenzi”aliongea Roma huku akitabsamu na kunywa kidogo na kisha akafumba macho akifurahia burudanni ya utamu wa kahawa.

‘kumbe ni mtaalamu kwenye utengenezaji wa kahawa nitakuwanakuja uwe unanitengenezea mumeo mara kwa mara”Edna hakujibu kitu alilirudi kwenye meza yake kuendelea na kazi na Roma alichukua karatasi na kuanza kuzisoma.

Baada ya dakika kumi kupita Edna aliinua shingo yake na kumwangalia Roma na kumuona yupo bize akisoma karatasi hizo kwa umakini mkubwa na alijikuta moyo wake ukipata joto na alishindwa kujizuia na kutabasamu.

Anaonekana mwanaume aliekamilika akiwa siriasi”Aliwaza Edna na kuendelea na kazi.

Baada kama ya dakika arobaini na tano hivi za mara ya kwanza kwa Roma kuwa siriasi tokea aanze kuingia kwenye hii kampuni , simu yake ilipata uhai , na simu hii ilikuwa na kelele maana ilikuwa ni simu ya Tecno batani kitochi aliotoka nayo Mbagala, na kama unavyojua simu hizi kwa makele .

Roma alitoa simu yake mfukoni na kuangalia nani anapiga na namba ilikuwa mpya , alimwangalia mke wake ambaye alijua anajifanya kuwa siriasi na kisha akapokea.

“Mr Roma Ramoni , unaongea na Meja Generali Maeda Mkwizu , tulionana jana Uwanja wa ndege , nimepiga tuonane ofisini kwangu saa sita kamili Lugalo”Ilisikika sauti nzito upande wa pilili.

“Sawa Mr Maeda nitakuwa hapo ndani ya muda”

Baada ya kukata simu , Roma aliangalia muda na kuona ni saa tano na dakika iishirini na saba ,aliangalia karatasi zilizokuwa kwenye meza na kisha akainua macho yake na kumwangalia Edna.

“My Wife utakuja nazo nyumbani hizi karatasi nizimalizie , kuna sehemu naenda”Aliongea Roma na kisha alinyanyuka na kupiga hatua kuelekea nje.

“Romaa.. !, kwanini usizimalizie kabisa”.

“See you at home babe , uje nazo”Aliongea Roma Nakisha akafungua mlango na kutoka , akimuacha Edna alikuwa amekodolea macho mlango.

****

Roma aliendesha Gari yake huku akiwa anasikiliza mziki mdogo mdogo , alitaka atumie muda mwingi mpaka kufika Lugalo , alichukua barabara ya Morogoro na kuendesha mpaka Ubungo na kuchukua barabara ya Mawasiliano ,Sam Nujoma na akaja kutokezea Mwenge na kuingia kwenye barabara ya Bagamoyo , aliendesha kwa utaratibu huku akiendelea kula mziki na pia alifurahishwa na madhani ya jiji.

Dakika chache mbele alikunja kushoto na kusimamaisha gari yake na kisha aliangalia saa na kuona alikuwa na dakika kumi kabla ya muda , alitulia kwa dakika kadhaa na zikiwa zimebaki dakika mbili aliingiza gari yake ndani ya eneo la Brigade baada ya kujitambulisha getini.

Ndani ya ofisi ya uongozi wa juu wa jeshi alionekana Meja General Maeda akiwa kwenye mavazi yake ya Gwanda iliokuwa imechafuka na manyota manyota na mwenge na alama ya x iliokuwa na visu, huku mbele yake akiwa Kanal Augustin Tobwe akiwa ameketi kwa heshima ndani ya ofisi hii

Ilikuwa ni ofisi kubwa iliokuwa na kiyoyozi na harufu nzuri na kufanya eneo hili kuzidi kupendeza , ukiongezea na fanicha za hapa ndani pamoja na kapeti la unyoya lililotandazwa chini , palikuwa panavutia na kuonyesha hadhi ya ofisi ya cheo cha mkuu huyu wa jeshi.

Baada ya dakika chache tu aliingia mwanajeshi cheo cha luteni kwa nyota zake mbili na kutoa saluti kwa wakuu wake .

“Mr Roma amefika”

“Okey! Mruhusu aingie”.

Roma aliingia ndani hapa kama kawaida yake ,sura kutokuwa na wasiwasi na kujiamini ndio ilikuwa imemvaa , alikuwa ni Roma yule yule ambaye hakuw akibadilisha na mazingira, watu walokuwa ndani ya hii ofisi wote alikuwa akiwajua , wa kwanza aliekuwa amekaa upande wa kulia , alikuwa ni mzee aliekutana nae jana na kumpiga biti la kutaka kuondoka nae kwenda kambini pamoja na wageni kwa mahojiano na aliekuwa kwenye meza alikuwa ni Meja jenerali mwenyewe Maeda Mkwizu.

“Karibu Mr Roma , naitwa kanali Augustin Tobwe”Aliongea mzee wa jana aliempiga biti na Roma alitabasamu na kupokea mkono wake.

“Unaitwa Tobo au Tobwe”Mzee yule aling`ata meno kwa hasira na kisha akatabasamu .

“Naitwa Augustin Tobwe sio Tobo tafadhari”

“Sawa Afande Tobo nishalinakiri jina lako hivyo ili iwe rahisi kukumbuka”Aliongea Roma na kumfanya Afande Maeda atabasamu na kuona Roma alikuwa akilipiza kisasi cha jana na hakutaka kutia neno na mzee alietwa Tobo alikuwa ni mwenye bisara hakutaka kuonesha hasira zake waziwazi.

“Karibu sana mr Roma , nadhani sina haja ya kujitambulisha kwani nishafanya hivyo kwenye simu”Roma alitingisha kichwa na wote wakaketi kwenye masofa yaliopo hapo ndani.

“Mr Roma nadhani niende moja kwa moja kwenye jambo ambalo limefanya tuonane , na kabla ya kuendelea naomba tusahau ya jana”.

“Meja nishasahau yote mimi na Afande Tobo hatuna shida kabisa , yaliotokea na ni sehemu ya majukumu yake ya kikazi”

Aliongea Roma huku akitabasamu , lakini bado alikuwa akishangazwa na namna Meja alivyokuwa akiongea hakuwa akifanannia na cheo chake , kwani aliongea kama mwanasiasa.

“Mheshimiwa Afande twende sasa moja kwa moja kwenye maongezi , tusiwe kama wanasiasa , nimeondoka bila ruhusa ya mke wangu nataka nirudi nikampet peti” Aliongea Roma na Meja jenerali alitabasamu na kisha aligundua alikuwa anaongea na mtu wa aina gani , kwani alionekana kujiamini mno.

Baada ya Roma kuongea hivyo Afande Maeda alimpa ishara Kanali na akaibua fomu iliokuwa pembeni yake na kisha akatoa karatasi na kumkabidhi Roma ambaye alizichukua na kuanza kuzipitia.

“Hio ni katatasi ya kikosi chetu maalumu kinachoendelea na mafumbo ndani ya kambi ya Mirambo”

“ Mr Meja ndio ni kikosi , lakini sijaelewa kwanini umenipa majina yao?”alitabasamu.

“Mr Roma miezi miwili iliopita tuliomba msaada wa wakufunzi kutoka jeshi la Urusi kwa ajili ya kuwafundisha wanajeshi wetu mbinu maalumu za kivita kupitia ofisi ya CDF lakini ombi letu lilikataliwa kwa pendekezo”

“Unamaanisha nini kwa Pendekezo”

“Uongozi wa Jeshi la urusi walipendekeza tukuombe wewe usaidie katika kufundisha wanajeshi wetu baada ya kutupitishia taarifa ya ujuzi wako wa kimapigano , lakini pia uongozi wako wa juu ndani ya Kikosi cha The Eagles na nadhani dunia nzima inajua umahili wa kikosi cha The Eagles , hivyo hata sisi tulishangaa baada ya kusikia kuwa wewe ni sehemu ya wanajeshi kikosi hiko”Alitulia na kisha akamwangalia Roma , ila Roma hakuonesha mshangao , wala hakuonyesha mabadiliko yoyote.

“Lakini swala hili hatukuombi ulifanye bure , sisi kama jeshi tumekaa tukaridhia wanajeshi wako kuendelea kukaa hapa nchini lakini wewe utatusaidia kuwafundisha vijana wetu mbinu mpya ambazo sisi jeshi la Tanzania hatuna , ikiwemo baadhi ya siri mnazotumia ndani ya jeshi la The Eagles”Aliongea Afande Maeda na kumwangalia Roma.

“Kwa hio Afande milikuwa mnasubiri mpate Collateral ili uandae haya mazungumzo na mimi?”

“Ndio hivyo Mr Ramon licha sisi ya kuwa wanajeshi ila tunaelewa kanununi za kuwa katika nafasi nzuri katika mazungumzo”

Roma alifkiria kwa dakika kadhaa na kuona jambo hilo sio baya , kama ni kuwafundisha tu anaweza kawapa kazi hio wanajeshi wake , na asiende yeye lakini pia alikuwa akihitaji sana wanajeshi wake kuwa ndani ya taifa la Tanzania kwa kazi yake iliomleta.

“Sawa meja , lakini kabla ya kukubaliana na ombi lenu nina masharti makuu mawili , kwanza kabisa nataka nijue , ilikuwaje mpaka afande Tobo hapa kupata taarifa zangu na kuintercept wanajeshi wangu , kwani kwa maelezo yako na kwa tukio lile inaonekana kabisa hakukuwa na muunganiko wa taarifa kati yenu”

“Ni kweli Mr Roma , kilichotokea ni Misunderstanding kati yetu , Project ya kikosi kinachoendelea na mafunzo huko Mirambo haikuwa imemfikia kanali hapa na niseme tu kuwa kanali ni moja ya wanajeshi wenye weledi mkubwa ndani ya jeshi letu na ndio maana licha ya kukosa taarifa kamili kutoka kwetu aliweza kunusa harufu ya wanajeshi wanaozamia ndani ya Tanzania”.Roma alikubali maelezo

“Sharti langu la pili ni hili Afande Meja jenerali , nataka unihakikishie jambo lolote kutonikuta nikiwa hapa Tanzania , ikiwa nitafanya maauzi ya kuua mtu , hapa naomba usinielewe vibaya ila ni kwamba kuna watu ni wachokozi sana ndani ya taifa hili na mimi sipendi mtu anaenichokoza , hivyo afande ikitokea nimeua you have to clean up the mess for me”Aliongea Roma na Mzee huyu alitoa macho , kwani aliona sharti hilo kuwa kubwa na Roma aliona kusitasita kwa Meja.

“Meja ombi langu ni hilo , kama haliwezekani sinabudi pia kukataa ombi lako na kuhusu wanajeshi wangu nitatafuta namna ya kuwabakisha Tanzania maana hilo lipo ndani ya uwezo wangu”Aliongea Roma na Afande Maeda alifikiria ombi hilo kwa dakika kadhaa.

“Okey Deal Mr Ramoni , utafundisha jeshi letu mafunzo ya hali ya juu na mbinu zote zinazomilikuwa na jeshi la The Eagles na mimi nitahakikisha na ‘Clean up the Mess’ lakini licha ya hivyo Mr Roma nataka kukuambia kuwa hii nchi inaendeshwa kwa sheria , hivyo hatutakuwa tayari kuona unavunja sharia kwa namna ambavyo unapenda”Roma alitabasamu na kisha alipeana mkono na Meja Generali Maeda.

“Kanali hapa atakuwa na wewe bega kwa bega katika zoezi hilo , na tunatarajia mafunzo hayo yaanze mwenzi ujao yaani baada ya wiki tatu kuisha kutoka leo”

“Hakuna shida Meja”Aliongea Roma na kisha wakaagana huku akisindikizwa mpaka nje eneo la kuegesha Magali , jambo ambalo kwa wanajeshi walikuwepo eneo hili kushangaa.

Wakati wanapeana mikono mara iliingia pikipiki na kwenda kusimama mita kadhaa umbali walipokuwa wamesimama Roma.

Na dereva wa pikipiki alitoa helmeti na hapo ndipo Roma alipomshuhudia Mage mwanadada mrembo ambaye kila siku wanapokutana ni kwa shari., alijiuliza mrembo huyu kaja hapa ndani kufanya nini maana kwa kumbukummbu zake alikuwa anaelewa kuwa Mage alikuwa ni polisi na hapa ndani hapakuwa pakimuhusu.


NITARUDI BAADA YA SEASON 3 KUISHA KWENYE GRUPU UNTILL THEN SEE YOU GUYS.. ACHA MAONI HAPO CHINNI

CHANGIA KIASI KWANZIA 2000 KAMA UMEIPENDA NIKUTUMIE INBOX AU NIKUUNGE GRUPU KILA SIKU NADHUSHA DOZI VIPANDE VITATU KWENYE GRUPU WATSAPP , LIPIA NAMBA HIZI 0623367345 HALOPESA AU 0657195492 TIGOPESA AU 0687151346 AIRTEL JINA ISSAI SINGANO , UKILIPA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA 0687151346
 
SEASON 2
SEHEMU YA 31

Ilikuwa ni Jumapili tulivu , kwa wale wakristo waliokuwa wakienda kanisani walikuwa wakienda na kwa wale ambao walikuwa ni wa dini nyingine walikuwa na pilipilika za mambo mengine za Maisha yao.

Roma kama kawaida yake aliamka asubuhi asubuhi na kwenda kufanya mazoezi ya hapa na pale ili kuweka mwili wake katika hali nzuri , kwa upande wa Bi wema alikuwa bize na kuandaa kifungua kinywa kwa siku hio na kwa upande wa Edna alikuwa bize na kusoma kama ilivyokuwa kawaida yake , aliamini matatizo yake yote yanaweza kutatuliwa na kusoma na ndio maana aliamini katika kusoma sana.

Alijitahidi kusoma kwa muda , lakini akili yake haikuwa ni yenye kutulia , alionekana kuna jambo lilikuwa likimuumiza kichwa kwani alikosa utulivu , baada ya kuona haelewi kile alichokuwa anakisoma alisogelea tarakishi yake ya mapakato na kuingia kwenye mtandao maarifu wa Google na kuanza kutafuta taarifa zinazohusiana na macho ya mtu kubadilika Rangi , lakini kila majibu yaliokuwa yamekuja yalionekana kutokumridhisha kabisa na kukosa jibu alilokuwa analitaka.

“Au nimuulize mimi mwenywe kwanini macho yake yanabadilika Rangi?” Aliwaza mrembo huyu huku akiwa amevalia kigauni chake kilichoufanya mwili wake mnene kiasi kupendeza.

“Ila naamini siku moja ataniambia mwenyewe kwanini yuko vile , sitakiwi kumuuliza”Alijijibu mwanamke huyu huku akiona hayupo kwenye nafasi ya kumuuliza mume wake Roma kwanini macho yake yanabadilika rangi anapokuwa na hasira kali.

Saa mbili kamili za asubuhi Edna alishuka chini kwa ajili ya kupata kifungua kinywa baada ya kuitwa na Bi Wema , Roma alikuwa tayari yupo mezani , na alikuwa anamsubiria mke wake waanze , baada ya Edna kuketi wanafamilia hawa watatu ndani ya jumba hili kubwa la kifahari walianza kupata kifungua kinywa chao ambacho kwa familia za Maisha ya chini wangedhania moja kwa moja aina hio ya chukula ni kwa ajili ya sherehe.

“Miss unaonaje ukienda na Mr Roma leo kituoni?”Aliongea Bi Wema na kupendekeza .

“Bi Wema kituo gani?”Aliuliza Roma

“Kuna kituo cha kulelea yatima kipo Mkoa wa pwani Bagamoyo Kiwangwa, Ni kituo ambacho kampuni inakifadhili na imekuwa utamaduni kila jumapili Miss Edna kwenda huko kuwatembelea Watoto hao na kuwapelekea baadhi ya mahitaji muhimu”Roma alishangaa.

Edna alimwangalia Roma , hakuwa akipinga swala hilo la kwenda nae , kwanza kabisa mrembo huyu alipanga kujiweka kidogo karibu na Roma ili kuweza kujua ni kwanini macho yake yanabadilika Rangi , aliamini kama watakuwa marafiki Roma anaweza kumfungukia.

“Bi Wema kama mke wangu anapenda kuongozana na mimi nipo tayari , isitoshe leo sina pakwenda na sijazoea kukaa ndani”Aliongea Roma.

“Roma itakuwa vizuri kama tutaenda wote , unisaidie kwenye kubeba mizigo ya kwenda nayo”Aliongea Edna na Roma aliitikia kwa kichwa.

Baada ya nusu saa Roma alikuwa ashajiandaa kwa ajili ya kuianza safari ya kuelekea Bagamoyo , alikuwa sebuleni akimsubiria Edna ambaye kama ilivyokuwa tabia ya wanawake kujiandaa muda mrefu Edna alichukua lisaa mpaka kuonekana akiwa anashuka.

Roma siku zote alikuwa akijivunia hata kuitwa mume wa Edna , kwani mwanamke huyu hata avae nini , alikuwa akipendeza sana na kuvutia,Edna alikuwa amevaa leo Suruali ya jeans rangi ya Bluu iliomfanya umbo lake kuonekana vyema, na kishati flani kitambaa mtelezo mikono mirefu , na akakikunJa hadi kwenye kiwiko cha mikono , chini akiwa amevalia viatu vyeupe kama Raba Rangi ya pink.

Edna alimpa Roma ufunguo na Roma alitangulia mpaka sehemu ya kuegeshea magari na kubonyeza Rimoti na Pickup aina ya Cadillac Escalade EX ili Tweak na kuwasha taa ,Roma alitabasamu na ufahari wa hii gari , aliitoa na kuleta mpaka katikati na Edna aliingia.

Bi Wema aliekuwa juu ya Gorofa alikuwa akitabasamu kwa furaha baada ya kuona Edna na Roma wakitoka , alijiambia ni mwenye akili sana kushauri waende pamoja.

“Kuanzia sasa misheni yangu ni kuhakikisha wanafanya mambo kwa pamoja , hii itawaongezea kuwa karibu” Aliwaza Bi Wema huku akijiona jasusi mbobezi likija swala la mapenzi.

Safari ya wanandoa hawa iliishia Mliman City , Watu waliokuwa ndani ya eneo hili waliwaangalia kwa macho ya tofauti kabisa huku kila mtu akiwa na mawazo yake ,Edna alikuwa amevalia miwani ambayo ilimfanya apendeze lakini yeye hakuvaa kwa ajili ya kupendeza , alikuwa amevaa kwa ajili ya kufanya watu wasimtambue.

Roma alievalia jeans lake Rangi nyeusi na koti la Ugolo alijongea upande upande na mke wake , huku akijisikia fahari namna ambavyo wanaume wa eneo hili walivyokuwa wanamwangalia kwa macho ya wivu.

Walinunua mahitaji mengi ndani maduka ya vyakula , baadhi ya nguo , taulo za kike na makolo koloo mengi sana ambayo yalikwa ni sehemu ya mahitaji ya Watoto , walichukua na baadhi ya zawadi kwa Watoto hao ikiwemo biskuti pipi na vitu vingine.

Baada ya kumaliza kufanya manunuzi , Roma kusaidiana na baadhi wafanya kazi walipakia huku Edna akiwa bize kulipia.

Wakati Roma akiwa bize kupandisha vitu , mara alisikia sauti iliokuwa ikimuita nyuma yake , sauti ya kike ambayo alikuwa akifahamu vyema, alikuwa ni mrembo Doris ambaye alikuwa akiegesha gari yake , akiwa yupo peke yake aliependeza kama kawaida.

“Doris !”Aliongea Roma kwa kushangaa baada ya kumuona mrembo huyu mbele yake.. wakati Doris anamwangalia Roma kwa mshangao mara alikuja Edna na kwenda kusimama karibu na Roma.

“Edna!”Macho yalimtoka Doris , hakuelewa ni kwanini wawili hao wako pamoja .

“Vipi Doris umekuja kufanya Shopping?”Aliuliza Edna wa kwanza baada ya kuona Dorisi yupo kwenye mshangao pasipo kuongea neno.

“Ndio Edna , lakini kwanini upo na Roma?”

“Nisamehe Dorisi rafiki yangu , nadhani unakumbuka nilikuambia nina mume?”

“Usiniambie Edna huyu ndio mumeo na siku zote huniambii?”.

“Ndio Dorisi huyu ni mke wangu,Tunaelekea Bagamoyo na muda unaenda tutaongea Zaidi”Aliongea Roma akikata mazungumzo hayo , hakutaka waendeleee kusimama ndani ya eneo hilo la maegeisho ya magari

“Nitakupigia simu Doris , tutaongea”Aliongea Edna na Roma alimshika bega Edna na kumsukumizia ndani na kufunga mlango na kisha akazunguka upande wa dereva na kuingia ndani na kuliwasha huku wakimwangalia Doris aliekuwa amesimama akiangalia gari yao ikitokomea.

“F**ck you Roma , siku zote unanichora tu kumbe mkeo ni Edna , halafu kwanini Edna hajaniambia”Alijiongelesha mwenyewe na kusahau kuwa baadhi ya watu walikuwa wakimshangaa , alifuta machozi kwa mkono ambayo yalikuwa yashaanza kujitengeneza ndani ya mboni za macho yake na kufungua mlango wa gari na kuingia na kisha akatoa gari ndani ya eneo hilo , alionekana kughairi , alichokuwa amefata hapo.

“Doris atakuwa amekasirika”Alianzisha maongezi Edna wakati wakipita Lugalo.

“Kwanini unasema hivyo?”

“Doris ni Rafiki yangu wa muda mrefu na niseme ni Zaidi ya Rafiki yangu , tumekuwa pamoja kwa muda mrefu kidogo , nilimwambia nimeolewa na kumuhaidi nitakutambulisha kwake lakini sikufanya hivyo na leo ametuona pamoja , kama marafiki atakasirika na kujisikia vibaya”.

“Mke wangu usiwe ni mwenye wasiwasi , Doris ni Rafiki yako na wewe ulikuwa pia na sababu za kutonitambulisha kwake mapema , hivyo atakuelewa , isitoshe hatuna muda mrefu tokea tumesajili ndoa yetu”.Edna aliitikia kwa kichwa.

“Kila jumapili unakujaga huku kutembelea kituo?”Aliuliza Roma kwa makusudi a ya kubadilisha stori.

“Ndio , imekuwa utamaduni , kila jumapili lazima nitembelee , napenda Watoto na najisikia faraja ninapokuwa nao karibu”.

“Mke wangu nilijua wewe ni kauzu kila sekta , kumbe una upande wako mwingine ambao sikuwa nikiufahamu”.

“Mimi sio kauzu ila napenda kuwa siriasi kwenye maeneo yanayonitaka kuwa hivyo , sipo kama wewe kila eneo haupo siriasi”.

“Kwa hio mke wangu wewe unataka niwe vipi?”Edna hakujibu aliendelea kukaza macho barabarani na Roma hakutaka kuongea Zaidi.

Ni masaa machache tu walikuwa washafika ndani ya kituo hiki , kilikuwa ni kituo kikubwa sana, kilikuwa na majengo makubwa kama chuo , jambo ambalo lilimshangaza Roma.

“Mke wangu hiki kituo ni kikubwa ni shirika gani limejenga hiki kituo?”

“Sio shirika ni mke wa raisi wa Kenya ndio amejenga hapa Tanzania”Roma alishangaa ,yaani mke wa raisi atoke Kenya kwao ambako kuna Watoto wengi waliozagaa mtaani aje ajenge Tanzania , alishangazwa na jambo hilo.

“Kwanini ajenge Tanzania sio Kwao Kenya?”

“Hata Kenya kajenga vituo vingi tu na sio Kenya wala Tanzania ,Uganda , Rwanda na Kongo kajenga vituo vinavyofanana hivi hivi, ni mwanamke ambaye ana moyo mzuri sana na anasifika sana ndani ya Afrika kwa kuisadia jamii.

Roma alitingisha kichwa baada ya kupewa jibu hilo na mke wake , aliona huyo mwanamama anapaswa kupewa tuzo kwa msaada mkubwa ambao anaufanya kwa jamii zenye uhitaji.

Kitendo cha kumaliza kuegesha Gari Tu ni kama Watoto waliokuwa ndani ya hili eneo walikuwa wakimsubiria Edna kwani kundi lote lilimkimbilia na kumzingira huku wakionyesha furaha yake na Edna na yeye hakuwa nyuma , alionekana kufurahi kweli uwepo wa Watoto na kwa mara ya kwanza Roma anamshuhudia Edna akiwa na furaha sana.

“Sikujua mke wangu kumbe mzuri hivi akicheka , halafu anaonekana kuwa na moyo mzuri sana , kanaigiza tu kuwa siriasi”Aliwaza Roma huku Watoto hao wakiwa hawana habari nae.

“Edna karibu” Aliongea mwanamama mmoja hivi mnene mwili wa kibonge mwenye umri si chini ya hamsini hivi alikuwa wa maji ya kunde.

“Asante Mama Issa ”Alijibu Edna aliekuwa akiwaangalia Watoto hawa , lakini kwa upande wa yule mama alimwangalia Roma na hapa ndipo Edna aliekuwa amemshau Roma akainuka.

“Mama Issa Watoto wamenifanya nisahau kukutambulisha , huyu ni mume wangu anaitwa Roma Ramoni” Mama huyu macho yalimtoka kwa mshangao huku Roma akiwa ni mwenye kutabasamu , alijiuliza huyu mwanaume ana nini mpaka kupata nafasi katika maisha ya Edna.

“Sikujua.. kumbe umepata mume Edna .. jamanii.. karibu baba mimi naitwa Tabea Singano ni mkuu wa hiki kituo”Aliongea mama huyu huku akionyesha furaha yake waziwazi , alionekana pia ni mtu ambaye alitamani siku moja Edna kumtambulisha mume wake kwake.

“Nashukuru sana kukufahamu Mama”.

“Karibu sana , unabahati sana kumpata Edna katika Maisha yako , umchunge sana”Aliongea mwanamama huyu huku Edna hata hakuwa akiwasikia , kwani alikuwa bize na Watoto aliokuwa akiwabeba mmoja mmoja juu.

Walishusha mizigo kwa kusaidiana na wafanya kazi wa hapa ndani , na Roma pia alisaidia katika kazi hio na baada ya zoezi hilo dogo kuisha Edna na Roma walichukua zawaidi walizokuwa wamekuja nazo na kuanza kuzigawa kwa Watoto hao .

Roma alimkubali sana aliejenga hiki kituo kutokana na wingi wa Watoto hao , kilikuwa mpaka na shule kubwa ya msingi mpaka sekondari , ni kituo ambacho kilionesha kujitosheleza sana kwa kila kitu.

Mama Issa alimchukua Roma na kuanza kumtembeza ndani ya kituo hichi , kwa kumuonesha baadhi ya huduma ambazo wanatoa kwa Watoto hawa ya kimalezi , mama huyu alionekana kuwa mkarimu sana.

“Edna ni msichana wa kipekee sana ,nimemuona akikua kwanzia alivyokuwa mdogo”Roma alishanga

“Mlikuwa maishi majirani?”.aliuliza Roma na mwanamama huyu alitabasamu.

“Hapana , wakati wa utoto wake alikuwa akija na bibi yake hapa mara kwa mara kucheza na Watoto na naweza kusema Muda wake wa utoto mwingi alicheza na Watoto ambao walikuwa kwenye hiki kituo”Aliongea mama huyu na kumfanya Roma ashangae , na wakati huu walikuwa wakiingia ndani ya mejengo ya ofisi hizi za kituo hiki kilichokuwa kinafahamika kwa jina la Son and Daughter Orphanage(SDO)..

Roma baada ya kuingia ndani ya hii ofisi kubwa ya mama Issa alijikuta akishangaa picha iliokuwa juu ya ukuta ,ilikuwa ni picha ya mwanamama mmoja maji ya kunde aliekuwa kwenye pozi la kutabasamu, kichwa chake kilianza kuuma na kupiga kama Radi na picha picha za matukio zikianza kupita .. macho yake yalianza kubadilika palepale na kuwa ya kijani.

SEHEMU YA 32

Roma alishindwa kuvumilia , alikuwa akishindana na hali iliokuwa ikiendelea kwenye mwili wake , alifumba macho yake haraka sana , ili Mama Issa asimuone akibadilika na kisha akageuka, Uzuri ni kwamba mwanamama huyu alikuwa amempa mgongo Roma na hakuwa akijua kilichokuwa kikiendelea kwenye kichwa chake.

Roma alikimbilia nje , lakini ile anatoka kwenye ofisi alijikuta akikumbana na Edna ambaye aliona hali yake ya macho Alitaka kumwepa lakini Edna hakufanya hivyo , alimshika mkono.

“Roma Calm Down”Aliongea Edna na Roma ni kama ameshituka kwani macho yake yaligeuka na kurudi katika hali yake ya kawaida na kumwangalia Edna.

“Am Sorry Edna”.

“Sorry ya nini?”

“Sijui …”Kabla Roma hajaibu walishitushwa na sauti ya Bi Tabea.

“Nilishangaa umeenda wapi kumbe umemfata mkeo”Aliongea Bi Tabea na Edna alitabasamu.

“Edna niseme tu hongera sana kwa kupata mume , Roma anaonekana kuwa kijana mzuri naamini mama yako na bibi yako watakuwa na furaha na wanaweza kupumzika kwa amani maana wewe..”

“Mama Issa Maana nini…”aliongea huku akicheka.

“Umekuwa mgumu sana , nakumbuka yule nani yule .. ee Elvice alikuwa akitoka jeshini lazima aje hapa kulalamika..”Mama huyu alijikuta akiishia njiani kuongea na kujiona ameropoka ila kwa Roma alikuwa amesikia kila kitu na akajiuliza kuna historia gani kati ya Elvice na Edna ambayo hakuwa akiijua , ila hakutaka kuuliza.

Saa moja kamili za jioni ndio muda ambao wawili hawa walitoka ndani ya kituo hiki kurudi nyumbani , Edna alionekana kuchoka kweli kutokana na kucheza na Watoto , kwa upande wa Roma yeye hakuwa amechoka , kwanza hakucheza kabisa na Watoto kwani sio mtu wakupenda sana kama ilivyokuwa kwa Edna.

Alimwangalia mke wake aliekuwa amesinzia pembeni na kujikuta moyo wake ukiwa wa moto , alitamani Maisha yake yawe kama hivyo kila siku ,awe anapendana na mke wake , watembee hapa na pale kurefresh mind, alitamani kufurahi na kuendeleza Maisha ya ukawaida , lakini Roma Maisha ya aina hio yalikuwa kwake ni ndoto.

“Hapana lazima nifanye juu chini nina kamilisha yote yalionileta Tanzania , nikishachimba swala hili kwa undani na kujua kwanini nilikuwa kwenye kile kisiwa cha mateso mimi na Seventeen na kuifahamu familia yangu nadhani nitatulia na mke wangu, Edna licha ya kwamba hatujaoana kimapenzi , lakini sidhani kama itakuja siku nitakuacha hata pale mkataba utakapoisha”Roma aliwaza mawazo hayo mchanganyiko huku akizidi kukanyaga pedeli kuelekea jijini Dar es salaam.

Wakati akiendelea kuendesha gari alikumbuka kauli ya Bi Issa kumuuliza hali ya kimaendeleao ya Nasra , alijiuliza kwanini mwanamama yule kauliza juu ya maendeleo ya Nasra ila alikosa majibu kwa wakati mmoja , alijiambia kuwa atafahamu kadri atakavyokuwa karibu na Nasra.

****

Doris alijikuta ni mwenye hasira sana , baada ya kujua kuwa Edna na Roma ni mume na mke , alikasirika sana , lakini na kuumizwa kwa wakati mmoja.

Alianza kukumbuka tukio ambalo Roma alimuomba hela ya nauli wakati akiwa anarudi nyumbani na kumpatia , alikumbuka usiku wao waliotumia na kufanya mapenzi na mwanadada huyu alizidi kutokwa na machozi ,alihisi moyo wake ulikuwa ukimuuma sana kiasi cha kwamba mwenyewe alishindwa kuelewa kwamba moyo wake ulikuwa ukimuuma kutokana na kwamba Edna na Roma walimficha na kumuona mjinga siku zote , au ni kwasababu alijua kuwa Roma mke wake ni Edna mwanamke mrembo na kilichokuwa kikimliza ni wivu wa kimapenzi.

Alisimama kukodolea maji ya baharini muda huu wa jioni huku machozi yakiwa yanamtoka , lakini kila alipokuwa akiangalia baadhi ya wapenzi waliokwa ndani ya fukwe hii ya Coco walivyokuwa wakifurahi na kuonyesheana mapenzi , aliijikuta akizidi kutoa machozi.

“Ninaonekana kutokuwa na bahati katika Maisha yangu , Edna nifanye nini mimi nahisi kumpenda sana mumeo , najiona kabisa siwezi kumuacha hata kidogo , kwanini iwe wewe rafiki yangu”Aliwaza mwanadada huyu na kuwazua huku akionekana ni mwenye kukosa jibu , alionekana alikuwa akishindana na hisia zake.

Doris licha ya kwamba alikuwa sio mwenye kuonyesha waziwazi mapenzi yake kwa Roma alikuwa ashampenda tokea siku ya kwanza wanaonana ,Roma alivyomuomba kiasi cha pesa , tokea siku ile alikuwa alikuwa ni mwenye kumkumbuka Roma , hakujua ni kwanini alikuwa akimkiumbuka mwanaume huyo , lakini picha yake haikuwa ni yenye kutoka kwenye kichwa chake.

Siku ambayo anamuona Roma kwa mara nyingine ndani ya kampuni yake , akija kufanya usaili , alijiambia kabisa ni Mungu ndie aliekuwa amewakutanisha kwa mara nyingine na hivyo hapaswi kuzarau kile Mungu alichompatia na ndio maana siku ile ile aliona atumie nafasi ile kumtambulisha Roma kwa mwanaume mzee aliekuwa akimsumbua , mwanaume aliekuwa akimfahamu kama Mr Kijembe .

Hakujali kabisa katika moyo wake kwamba Roma ameoa , alichokuwa akiamini ni Kwamba Roma alikuwa amepangiwa kuwa nae katika Maisha yao yote na mke aliemua ni makosa ambayo Roma alikuwa amefanya , hayo ndio yalikuwa mawazo ya mwanadada huyu mrembo , aliamini mke wa Roma sio mtu sahihi kwa Roma na yeye ndio alikuwa sahihi , kwani matukio yao ya kukutana ni kama Mungu aliwakutanisha.

Hata pale alipopata taarifa ya Roma kulala na mwanamke Neema Luwazo Mwanamke ambaye alikuwa akimjua sana tu, kwa kuwa na mahusiano na Raisi mstaafu , alijiambia kuwa ni mihemko tu ya Roma ya kukosa mtu sahihi wa kumtuliza na kama atampata basi Roma angetulia kwake na kuachana na mambo ya wanawake , kwani angempa kile kitu ambacho anakitafuta nje , kitu ambacho aliamini ni kwamba alikuwa akikikosa kwa mke wake.

Siku ya Jumapili ndio siku ambayo alipanga kutimiza jambo lake la kuanza kuweka ukaribu na Roma , aliamini anapaswa kufanikisha swala la yeye kuwa karibu kabla ya kwenda safari ya kikazi Japani , alitaka katika safari hio waitumie kama sehemu yao ya matembezi kama wapenzi , na ili kukamilisha swala hilo anachotakiwa kufanya ni kuhakikisha Roma anakuwa karibu yake anamzoea na hatimae kumpenda.

Baada ya kuwaza hayo , hatua ya kwanza aliofikiria ni kwenda kutafuta zawadi yoyote ambayo aliamini itamfurahisha Roma na eneo pekee alipoona panafaa kupata zawadi hio kwa siko hio ya jumapili ni Mlimani City.

Nwanadada huyu alijiandaa , alichukua kadi yake ya benki aina ya ‘Black Card’ kadi ambayo ilikuwa ikimruhusu kutoa kiasi chochote kile cha pesa na kuiweka katika mkoba wake , na kisha akachukua ufunguo wa gari yake na kutoka ndani ya jumba hili la kifahari alilokuwa akiishi mwenywe na wafanya kazi.,Jumba ambalo alikuwa amenunuliwa kama zawaidi na baba yake .

Lakini baada ya kufanya safari yake na kufika Mlimani anajikuta akishuhudia kitu ambacho moyo wake haukutarajia kukiona , alimuona mwanamke ambaye aliamini sio sahihi kwa Roma akiwa ni Edna , Rafiki yake kipenzi , bosi wake kazini, moyo wake ulipigwa na ganzi.

“Doris!!”Ilikuwa ni sauti ya mwanaume iliosikika nyuma yake na kumfanya mwanadada huyu ageuke ni nani anamuita , lakini ile anageika alikutana na uso wa Abu.

“Abu vipi , kwanini uko hapa ?”Aliuliza Doris kwa namna ya kushangaa.

“Nimekuja kupunga upepo kama wengine Doris , wewe vipi , kwanini uko hapa?”.

“Namini nipo kwa ajili ya kupunga upepo “Abu alijikuta akitabasamu .

“Doris najua unaonekana kuwa katika hali ya mawazo , lakini nimekuwa nikisubiria sana jibu lako”

Doris alishangaa na kuanza kuvuta pumzi kwa nguvu na kumgeukia Abuu….

Ni jibu gani ??

SEHEMU YA 33

2010 -KIGALI STATE HOUSE

Ni mwaka 2010 muda wa saa tano za Asubuhi mheshimiwa Jeremy alionekana ndani ya ofisi yake akifanya kazi kama kawaida, katika kuwatumikia wananchi wa Rwanda, lakini siku hii kwa mheshimiwa huyu hali yake ilionekana kuwa sio ya kawaida , kwani alionekana kuwa ni mwenye wasiwasi sana kuliko siku zote hali ambayo ilimfanya kukosa utulivu , kila saa alionekana kuangalia saa ya ukutani kama mtu ambae alikuwa na jambo ambalo alikuwa akilisubiria.Ilivyofika saa sita na nusu aliingia Linda mlinzi wa karibu wa Mheshimiwa Jeremy.

“Mheshimiwa Ashafika”Aliongea Linda na kumfanya mheshimiwa Jeremy avute pumzi .

“Mruhusu aingie”Aliongea mheshimiwa na kisha akatoka kwenye meza yake na kwenda kwenye masofa na hapo hapo mlango ulifunguliwa na aliingia mwanaume mmoja wa kizungu alievalia shati la Blue bahari na suruali ya kadeti , muonekano wa huyu jamaa ni kama vile hakuwa akiingia kuonana na mheshimiwa , kwani alivaa kikawaida sana kama muhuni flani hivi.

“Welcome Mr Viladkov”Aliongea mheshimiwa kwa kingereza.

“Asante sana mheshimiwa”Aliongea na kisha alitoa karamu nyeusi flani hivi pana kidogo lakini ya kawaida , kama zile za rangi na kisha alianza kuifungua kama mtu ambae anatoa ule mrija wa wino, na akatoa kifaa Fulani hivi kama kile kichwa cha kuchomekea kwenye Earphone lakini hiki kwa juu mwisho kina kitu kama kigoroli.

“Hili ndio faili mheshimiwa”Aliongea na kisha alimpatia Jeremy kile kidude na mheshimiwa alishangaa m inakuwaje kadude kama hako kawe ndio faili ambalo alikuwa akilisubiria kwa hamu.

‘”Usishangae mheshimiwa Hata Urusi sasa imeendelea kwenye teknolojia , na hio ni mbinu yetu mpya kuficha taarifa wakati wa kuzisafirisha” ’Mheshimiwa Jeremy hapa alishangaa na akachukua Tablet iliokuwa kwenye meza yake na kuchomeka kale kadude na baada ya tablet ile kusoma kama Earphone ilisoma kama memori , alishangaa na Viladkov akatabasamu.

“Ni taarifa nyeti sana hio , na serikali ya Urusi imelipa kiasi kikubwa kuinunua kwa mtu aliekuwa akiuza”Aliongea bwana huyu na mheshimiwa Jeremy aliifungua na ajabu ni kwamba alikutana na picha.

“Mbona ni picha sio kama faili nilivyokuwa nikitegemea?”

“Angalia kwanza hizo picha mheshimiwa kwa umakini na uniambie umegundua nini?”

Alianza kuangalia hizo picha kwa kuzizoom na katika picha hizo kulionekana meli kubwa ya mizigo ikiwa inashusha mavyuma , lakini baada ya mheshimiwa kuangalia kwa ukaribu Zaidi aligundua ni bawa la Ndege.

“Linaonekana kama bawa la Ndege”

“Angalia na hio nyingine” Aliangalia na pia yenyewe ilionekana kama baadhi ya vipandevvipande vya mabaki ya ndege.

“Hio meli inamilikiwa na kampuni Neptune , kampuni ambayo ni sehemu ya kampuni kubwa ya kuzalisha ndege ya kimarekani inayofahamika kwa jina la Ngebo Aeronautical”Mheshimiwa alionekana kushangaa , lakini pia alizidi kuongeza umakini.

“Hizo picha zilipigwa Tarehe saba March 1998”Aliongea na mheshimiwa huyu alishangaa sana.

“Unataka kumaanisha kwamba ni siku moja kabla ya ndege ya Malaysia kupotea?”

“Ndio kutoka sehemu ambayo meli hio ilipo na sehemu ambavyo ndege ya shirika M ilipotea ni umbali wa kilomita ishirini tu , kwa maana hio hayo ni mahesabu ambayo yamepigwa kabisa na hio meli ilitupa mabaki hayo unayoyaona kwenye hizo picha eneo hilo”Mheshimiwa Raisi alijikuta akitetemeka maana anacho ambiwa hapo ni taarifa nzito sana , tena nzito kweli kweli.

“Mheshimiwa hii ni siri ninayokupatia ambayo ni siri kubwa ndani ya taifa la Urusi na ni kama Asset kwetu , hivyo taarifa hii inapaswa kuwa siri , mheshimiwa Raisi Viladmn karuhusu upatiwe taarifa hio ili kwa ajili ya kushawishi mataifa ya Afrika kuingia kwenye Mpango TASAC”Mheshimiwa alishangaa Zaidi.

:Mheshimiwa chomoa hio flash na uichomeke tena” aliongea Viladkov na mheshimiwa alichomoa na kuichomeka tena na ikasoma tena kama memori , aligusa ten ana zile picha zikawa zimefutika ils sasa kulionekana faili lililokuwa kwa mfumo wa ‘Xml’ , mheshimiwa alilifungua na kuanza kusoma na hapa ndipo aliposhangaa.

“Hio ni barua ya wito iliotumwa kwa mashirika ya kijasusi makubwa yote duniani na katika hio barua inaonesha kulikuwa na makubaliano ambayo yalikuwa yanatakiwa kufanyika juu ya mpango ambao ulipewa jina la LADO ambapo sisi tulishindwa kung`amua kirefu cha neno hilo , na shirika letu pekee ndiio halikutuma muwakilishi kwenda kuhudhuria kikao hiko ambacho kilifanyikia nchini Italy”Mheshimiwa jasho lilimtoka maana kadiri anavyoambiwa ndio anavyoona siri hii kuzidi kuwa nzito na kuhofia Maisha yake.

“Kwa hio unamaanisha kwamba LADO na kupotea kwa ndege ya shirika la M ni swala ambalo lina muunganiko na limeratibiwa kwa makubaliano ya mashirika makubwa ya kijasusi duniani?” Aliuliza na jamaa alitingisha kichwa kukubaliana nae.

“Kwanini mmeamua kunipa hii taarifa?”

“Mpango TASAC ni mpango ambao unahusisha serikali ya Urusi kurudisha umoja wa Kisoviet , lakini hili ili liweze kufanikiwa , tunahitaji sapoti kutoka Afrika , tunahitaji udhaifu kutoka kwa mataifa makubwa ambao utatusaidia pale itakapobidi serikali yetu kuingia vitani , mataifa haya hayatoi msaada , lakini nyie wa mataifa ya Afrika mnapaswa kutuunga mkono kwa kukaa kimya.”

“Na ili swala hili lifanikiwe unapaswa kuhakikisha asiliamia sabini ya mataifa ya Afrika yanakuwa kwenye huu mpango TASAC na mheshimiwa Raisi wa Urusi amekuchagua wewe kutokana na uzoefu wako katika uongozi, ukifanikisha mpango huu basi serikali ya Urusi itafanya juu chini kubaini ni nini kipo ndani ya operesheni iliopewa jina la LADO”.

“Natakiwa kukubali swala hili hapa hapa?”

“Hapana mheshimiwa , swala hili lina umuhimu sana kwa nchi yetu na mheshimiwa Raisi atakupigia simu na mimi nipo hapa kwa ajili ya kukueleza haya , kwani tunajua kuwa wewe ni mmoja ya wahanga wa AJali ya ndege na unataka kulipiza kisasi , lakini kutokana na ukubwa wa tukio lenyewe na udogo wa taifa lako, hautoweza kupata hio nafasi ya kuujua ukweli”Aliongea bwana huyu na heshimiwa Jeremy alikubali kuwa kiongozi wa juu wa mpango TASAC.

****

“Sauron habari za muda huu?”

“Salama kabisa mfalme Pluto, habari za Tanzania?”

“Hapa ni kwema kabisa Sauron , nimekupigia kupata ripori ya yale tilioongea jana”

“Mfalme Pluto , nimeshayakamilisha yote na nimepanga vijana kumi wenye uwezo wa hali ya juu kwa ajili ya kuja nchini Tanzania, lakini kuna jambo moja nimeona nitoe pendekezo”

“Edelea kuongea Sauron nakusikiliza”

“Nimeona makomandoo hawa wakiingia nchini kama watalii hawatapata kibali cha muda mrefu cha kukaa hapo Tanzania , hivyo nimejaribu kuwasiliana na balozi ya Sweeden nchini Tanzania na kuwaomba watufanyie mpango wa kuwaingiza wanajeshi wetu kama wafanya kazi wao”Roma Alitabasamu.

“Sauron wewe unakili sana , hili sikulifikiria , ni kweli watapaswa kukaa nchini muda mrefu kidogo kwani pia nataka wamlinde mke wangu”Sauron alishangaa.

“Mfalme Pluto usiniambie umepata mke?”

“Ndio Sauron , sio muda mrefu sana nimefanikiwa kupata mke”

“Hongera sana mfalme Pluto , ila kwa hatua hio sidhani kama utarudi huku kisiwani”

“Yanayotokea kesho hatuyajui Sauonoi hivyo siwezi kuongea lolote juu ya hili”.

“Ni kweli Mheshimiwa Pluto , ila nitatamani kumuona malkia wetu”Roma alitabasamu

“Utamuona Sauron nitakuja nae siku moja , Sauron kuna jipya lolote kutoka The Zeros?”

“Mfalme Pluto vijana bado wanaendelea kufuatilia na naamini muda si mrefu watatupatia taarifa “

“Sawa Sauron , nadhani tutawasiliana baada ya vijana kufika Tanzania”Baada ya hapo waliagana na Roma akakata simu .

Muda huu Roma anawasiliana na Sauron ilikuwa ni saa moja kwenda saa mbili hivi , hivyo baada ya kumaliza tu aliitwa na Bi wema kwa ajili ya chakula cha usiku.

Baada ya kufika tu chini na Edna alikuwa akishuka alievalia kigauni kilichokuwa kikipeperuka kiasi kwamba kilimfanya Roma aliekuwa chini ya ngazi aone mapaja ya malaini ya Edna na alijikuta hisia za mapenzi zikimuandama.

“Kukaa na mwanamke kama Edna halafu hupati kitumbua chake ni swala ambalo nina uhakika madaktari wataniambia ni sumu kwa Afya yangu , nikimaliza hapa nduki kwa Rose nikapunguze kichupa”Aliwaza Roma huku akivuta kiti na kuketi.

Edna na yeye alijikuta akitabasamu baada ya kumuona Roma leo hajatoka kabakia nyumbani , kwani mara nyingi hakuwa akipenda sana Roma a tabia yake ya kutoka na kurudi asubuhi yeye kama mke aliona sio vizuri.

Wanafamilia hawa walikula wakashiba na baada ya hapo Edna aliungana na Bi wema kusafisha vyombo , lakini wakati Edna akiwa bize na vyombo upande wa jikoni Roma alimchungulia kwenye mlango.

“Bebi ndio natoka hivyo , hapa hadi kesho”Aliongea Roma na Edna ambaye alikuwa ameweka mikono yake kwenye Sink alijikuta akikunja ngumi kwenye maji na kung`ata meno , kwani kila ambacho kilikuwa kikimfurahisha dakika chache nyuma kimegeuka ndivyo sivyo,Edna aliishia kutingisha kichwa na Roma hakujali aliondoka.

“Yaani huyu mwanaume hatulii nyumbani”Aliongea Edna kwasauti pasipo kujua nyuma yake kasimama jasusi mbobezi wa mapenzi Bi Wema.

“Miss ulifikiri sasa atafanyaje , mmeoana lakini hamlali chumba kimoja , yule ni mwanaume na wanaume tendo la nndoa ni kama hitaji lao la msingi hawezi kukaa na mtoto mrembo kama wewe halafu akuangalie kama picha ya ukutani”Edna alifikiria kidogo.

“Bi Wema nitafanyaje , bado sina hisia nae na wewe unaelewa tumeoana kimkataba”.

“Naelewa ndio , lakini miss angalau jaribu kuufungua moyo kwa Roma , huenda ukampenda na mkawa Mume na mke kimapenzi sio kimkataba”Edna alitingisha kichwa kuelewa

Baada ya kufika chumbani kwake alionekana kuwaza maneno ya Bi Wema na kuona kidogo yana maana.

“Au nijaribu kumpa?”Aliwaza Edna akimaanisha ajaribu kumpa Roma kitumbua.
Unafikiri nini mwisho wa yote ....??
WIKIEND NJEMA TUONANE JUMATATU

CHANGIA KAZI HII KWA KULIPIA KUANZIA 2000 KUENDELEA NIKUUNGANISHE NA GRUPU UIFATILIE KWA VIPANDE VITATU KILA SIKU TUPO SEASON 2 KWENYE GRUPU

GRUPU NI KWA AJILI YA SIMULIZI HAKUNA KUCHAT

LIPIA NAMBA 0687151346 AIRTEL AU 0623367345 HALOPESA AU 0657195492 TIGOPESA JINA ISSAI SINGANO UKILIPA TUMA MESEJI YA MUAMALA NAMBA 0687151346 WATSAPP


View attachment 2336156
Unyama mwingi bro

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom