SEHEMU YA 101
Roma alimwangalia Yezi kwa dakika kadhaa kama mtu aliekuwa akijiuliza maswali na kisha aliweka mfukoni ile cheni iliokuwa na kidani, Roma alitaka ampeleke Yezi sehemu anayoishi kwa kumpa Lift lakini mwanadada huyu alikataa na Roma hakutaka kufosi , alipanga gari na kuduti nyumbani.
“Oooshh…iii, Roma Please fanya taratibu”
“Okey! Wife ila kadri ninavyofanya taratibu ndio muda utaongezeka mpaka kumaliza”Aliongea Roma ambaye alikuwa akipiga kiuno taratibu huku akiwa ameweka kichwa chake kwenye shingo ya Edna.
“Argggh…Roma nimechoka naomba tuache”Aliongea Edna huku akiwa anahema kama mbwa aliekimbia maili nyingi , lakini Roma hakujali aliendelea kumuingia Edna na kutoka.
“Roma .. tuache … nataka nikajisaidie haja ndogo”.
“Hehe.. my Wife kojoa hapahapa”Aliongea Roma na kumfanya Edna akakamae huku akimn`gata Roma kwa nguvu , lakini Roma hakujali maumivu.
“Puuh!!!”Edna aliekuwa amelala kwenye ukingo wa kitanda akiwa amekumbatia mdori ambao ameupatia jina la pili la Roma yaani Ramoni , alijikuta akidondoka chini akiwa usingizini na alionekana alikuwa kwenye ndoto, na kitendo cha kudondoka chini kilimfanya ashituke kutoka usingizini , lakini sasa alijikuta akijishangaa kwa ndoto aliokuwa akiota.
Alichokifanya ni kukimbilia Bafuni na maji ya bomba yalisikika yakitiririka ndani ya chumba hiki na ni Dhahiri mwanadada huyu alikuwa akioga.
Edna aliwasha taa na kusogelea kioo akijiangalia huku akiwa amejifunga taulo, lakini kadri alivyokua akijiangalia na kukumbuka ndoto aliokuwa akiota dakika chache zilizopita , alijionea aibu , hakuelewa ni kwanini kwa mara ya kwanza katika maisha yake kuota ndoto kama hio, ndoto ambayo ilikuwa ikihusisha kufanya mapenzi na Roma.
Swala la kuota ndoto kama hio kwa Edna halikuwa swala dogo kwake na alilichukulia kwa uzito wake. kiasi kwmaba lilimkosesha usingizi , alijikuta akifungua mlango wa kiambaza(Balconi) kwa ajili ya kupigwa na upepo , licha ya kwamba usiku ulikuwa mkubwa na muda huo ilikuwa ni kama saa tano usiku.
Wakati Edna akiwa amesimama mara gari ya mtaalamu Roma ilionekana ikiingia hapo ndani na kuzunguka nyuma sehemu ya maegesho.
“Mh! Yaani ndio anaanza kurudi..!?”Aliongea Edna huku akionesha hali ya kutofurahia Roma kurudi muda huo na katika akili yake aliwaza Roma alikuwa na mwanamke na ndio maana kachelewa , alijikuta ile ndoto aliokuwa akiota ikijirudia rudia kwenye akili yake na kujionea aibu Zaidi na kukimbilia ndani na kujirusha kitandani na kulala.
Ni muda wa asubuhi Roma akiwa ashamaliza kuoga na sasa alikuwa akijikausha kwa taulo , kwa ajili ya kujiandaa kuelekea kazini , simu yake ndogo ilianza kuita mfululizo na kumfanya aisogelee na kuangalia ni nani anampigia , ilikuwa ni namba ngeni ila ya kitanzania.
“Hello!!”
“Bro Roma ni mimi Mhando hapa”Ilisikika suati upande wa pili na kumfanya Roma akumbuke dili aliloingia na Mke wake.
“Yes mhando mambo vipi”
“Safi tu Bro nimekupigia kukupa shukrani zangu,Bro yaani siamini kama nimepata kazi , tena ya kudumu kaka asante sana Mungu akubariki mpaka ushangae”Roma alijikura akitabasamu kwani kwa jinsi ambavyo Mhando alikuwa akiongea kwa furaha ni kama sio yeye, kwnai alikuwa amemzoea Mhando kuwa mpole na mara nyingi alikuwa akiongea kidogo sana , lakini leo hii kutokana na furaha ya kupata kazi alisikika kuwa mchangamfu.
“Ni swala dogo sana hilo Mhando ,kwa vigezo vyako ulipaswa kupata kazi, hivyo nimesaidia kidogo tu”
“Ndio Kaka , lakini kutokana na namna ambavyo nilihangaika kupata kazi lazima nikupe shukrani zangu , I am so Touched bro with your help,nakuombea uzidi kufanikiwa ili utusaidie marafiki zako”Aliongea Mhando na Roma akaitikia kumridhisha.
Baada ya Roma kukata simu , alijikuta akitabasamu lakini pia na kufikiria kwa wakati mmoja , aliona Edna alikuwa ashakamilisha ahadi kwa upande wake na sasa yeye ndio amaetakiwa kutimiza ahadi yake.
Roma alishuka mpaka sebuleni na kumkuta Edna akiwa peke yake akijipatia stafutahi ya Asubuhi , akiwa ashajiandaa kuelekea kazini , Roma alimwangalia Mrembo huyu kwa jinsi alivyopendeza, alimuona Edna kama pambo ndani ya nyumba.
“Darling umeamkaje?”
“Safi”Aliitkia Edna huku akiendelea kuwa bize na alichokuwa akifanya , Roma alimwangalia na akatabasamu huku akiwaza ni lini mke wake ataacha ukauzu na kuchangamka mbele yake , kwani kuna muda aliona kama Edna alikuwa akimfanyia makusudi.
“Wife Asante kwa kumsaidia rafiki yangu”
“Hauna haja ya kunishukuru nilichofanya ni kutimiza ahadi na kazi iliobaki ni kwako kufanya kama ulivyoahdi”
“Wife usijali ,mimi ni mwanaume wa kutimiza ahadi na siwezi kwenda kinyume na maneno yangu”Aliongea Roma na Edna akamwangalia kwa dakika kadhaa Roma ni kama alikuwa akimkagua na kutafuta Dosari na Roma pia alishangaa kwanini Edna anamwangalia kwa namna hio.
“Baadae”
Aliongea Edna na kujifuta midomo kupitia kitambaa na akachukua mkoba wake na kuanza kupiga hatua kuelekea nje na kumuacha Roma kumwangalia Mke wake anavyotokomea kwa nje na kumuachia harufu yake nzuri ya Perfume.
Roma baada ya kumaliza kujipatia kifungua kinywa alimuaga Bi Wema na kisha aliingia kwenye gari yake na kuianza safari ya kwenda kazini , huku akiendesha taratibu , lakini pia yeye mwenyewe alikuwa akijishangaa kwani kwa jinsi maisha yake yalivyokuwa yakiendelea ndani ya kampuni , alijiona ni kama hakupaswa kwenda kazini kabisa , kwani hakuwa na mchango wowote.
Roma wakati akiwa kwenye gari simu yake ilianza kuita mfululizo na akaitoa na kupokea baada ya kuona jina la mpigaji.
“Ndio Afande Maeda kuna nini asubuhi yote hi?”
“Mr Roma naomba unisamehe kwa usumbufu ila nimekupigia kuthibitisha jambo”
“Jambo gani?”
“Sisi kama jeshi tulipewa jukumu la kulinda Jiwe la Kimungu na mpaka sasa tupo kwenye sintofahamu baada ya kushindwa kuwakamata Yamata , tupo na kikao hapa na wakuu wa usalama wa Nchi na tunataka kujua kama jiwe ulilotoa ni lenyewe au umewapa feki”
“Afande Maeda nadhani Ajenti Flamingo hakuwaeleza vizuri , mimi nimetoa jiwe lenyewe na sio feki kama mnavyodhania na kama mmeshindwa kuwapata hao Yamata hilo ni swala lenu kulifanyia kazi”Aliongea Roma.
“Okey !Mr Roma tulitaka kupata jibu kutoka kwako na kwakuaa umetuthibitishia kama ni kweli umetoa jiwe hilo kwa Yamata ,basi tunaamini hautoingilia maswala yote ambayo yanahusiana nalo”.
“Kaeni kwa Amani kabisa Afande na wenzio , sitakii kuhusika na jiwe hilo maana linaweza kuleta shida kwa watu wangu wa karibu”Aliongea Roma na kukata simu , lakini wakati huohuo uliingia ujumbe kwenye simu yake na kuangalia.
“Nadhani haujasahau ahadi ya kuonana kwetu , muda ni saa kumi na mbili za jioni Rozana Hoteli”
Ulikuwa ni ujumbe ambao Roma kwa kuangalia tu hio namba alijua inatoka kwa Mage na hakufikiria sana , alizidi kuendesha gari yake na ndani ya madakika kadhaa alikuwa akiingia Posta yalipo makao makuu ya kampuni ya Vexto.
Baada ya kupaki gari yake moja kwa moja alienda mpaka ofisini kwake na kuwakuta wafanyakazi wenzake wakiwa bize , lakini leo hii mazingira ya kampuni yalionesha kuwa sio ya kawaida.
“Recho kuna nini?”Aliuliza Roma mara baada ya kuketi.
“Hivi wewe inakuaje kila kinachoendelea kwenye kampuni haujui , ni mfanyakazi kweli”Aliongea Recho huku akionyesha hali ya kumzodoa Roma , lakini Roma aliishia kutabasamu.
“Niambie bwana acha maneno mengi Recho”
“Kuna mabadiliko katika uongozi,”
“Unamaanisha nini?”
“Leo ni siku ya kutambulishwa CEO msaidizi wa kampuni”Roma alishangaa kidogo , kwanza hakuwahi kujiuliza ni nani msaidizi wa Edna.
“Kumbe hakukuwa na msaidizi?”
“Ndio! Mara nyingi kama Edna akipatwa na dharula Nasra ndio alikuwa akimkaimu”Aliongea Recho na kumfanya Roma aelewe.
“Sasa kwa ajili ya kuja CEO msadizi ndio mmefanya haya mabadiliko ya mpangilio wa ofisi?”
“Huna unachofahamu Roma ,CEO anaekuja anasifika kwa ukali na kutopenda watu wavivu kazini , wafanyakazi wa tawi la Nairobi wanamfahamu kwa ukali wake”Aliongea Recho na kumfanya Roma ashangae kwanza hakuwahi kusikia kuwa Nairobi kuna kampuni iliokuwa ikisimamiwa na mke wake.
“Kwahio na Nairobi kuna kampuni iliochini ya Vexto pia?”Recho alishangaa kwani kwa namna ambavyo Roma alikuwa akiuliza maswali ni kama alikuwa mfanyakazi ambaye alikuwa akianza kufanya kazi ndani ya hio kampuni.
“Naona hauna unachofahamu , ngoja nikuelezee tu , kwa Afrika VExto ina matawi katika nchi nane ,Afrika ya Kusini , Botwana , Kenya Uganga , Rwanda ,Nigeria ,Namibia ,Ghana na Ethiopia”
“Vipi kuhusu nje ya Afrika”Recho alivuta pumzi kidogo.
“Ni Ufaransa peke yake”.
“Alright Mrembo ,ila leo umependeza na yenyewe ni kwa ajili ya CEO Msaidizi?”Aliongea Roma na kugeuza kiti chake kuendelea na kucheza gemu na Recho alimwangalia Roma kwa dakika kadhaa kama vile hajawahi kumuona na kisha aligeukia tarakishi yake na kuendelea na majukumu hakutaka kumjibu Roma na maswali yake ya kihuni.
Muda wa Saa sita hivi , Recho alimfinya Roma baada ya kumuona Edna alieambatana na baadhi ya wafanyakazi wakubwa wa kampuni kuingia hapo ndani ya kitengo cha PR, Edna alikuwa ameongozana na Dorisi , Nasra na wamama wawili ambao walikuwa ni watu wazima , ambao walikuwa ni wafanyakazi wakubwa wa kampuni hii ya Vexto , lakini pia alionekana kijana mmoja hivi anaelingana na Roma , alikuwa ni kijana mtanashati kweli ambaye alifanya warembo wa idara hii kuvutiwa nae.
Recho baada ya kuona anamfinya Roma aamke kutoka kwenye usingizi bila mafanikio alisimama yeye mwenyewe akimuacha Roma.
Benadetha aliekuwa ndio kiongozi wa Idara hii alikuwa akitoa maelezo kwa heshima kwa wakuu wake wa kazi huku akieleza kazi ambazo zinafanyika kwenye idara yao ya PR ,Mwanadada alielezea kwa umakini mkubwa akitumia lugha ya kingereza na bwana ambaye alijitambulisha kwa jina la Michal Ernest Komwe aliridhishwa na maelezo hayo.
Edna , Dorisi na Nasra muda wote macho yao yalikuwa kwenye meza ya Roma na Edna alikasirishwa na tabia ya Roma ila hakutaka kuongea , alijiambia mwisho wa Roma wa kulala kazini ni siku atakayompa kampuni.
“Mr pale ana nini mbona yuko tofauti na wenzake na nikama hayupo kazini”aliuliza bwana Michal.
“Hajisikii vizuri leo , ila ni mchapa kazi mahili ndani ya kampuni na ndie aliefanikisha dili kubwa la Yamakuza”aliongea Benadetha kwa kumtetea Roma na kumfanya Edna amwangalia namna ambavyo Benadetha alikuwa akimtetea , alijisikia vibaya na sio kwake tu hata Dorisi na Nasra hawakupendezwa na namna ambavyo Benadetha aanamkingia kifua Roma.
“Kama hajisikii vizuri kwanini yupo hapa , alipaswa kubaki nyumbani kuliko kushusha morali ya wenzake kufanyakazi kwa kulala ofisini”aliongea Michal.
“Na kama nilianza kujisikia vibaya nikiwa kazini je?”Aliongea Roma na kugeuza kiti chake na kufanya wadada hawa wamwangalie.
“Hilo linaeleweka , kampuni ya Vexto haipo kwa ajili ya kutesa wafanyakazi , ukijisikia vibaya unaaaga na unaondoka, sio ndio Miss Edna”aliuliza Michal huku akimgeukia Edna ambaye haikueleweeka alikuwa na hisia gani kwa wakati huo na alitingisha tu kichwa.
“Okey!Mr Asistant , ila hali yangu imerudi kwenye ukawaida yake baada ya kulala kidogo, sidhani kama itakuwa jambo zuri kama kila mfanyakazi anaejisikia vibaya kuondoka , muda mwingine tunahitaji muda wa dakika chache kupumzika na kurudi sawa”Aliongea Roma na kisha aligeuza kiti chake na kushitua tarakishi yake ambayo ilikuwa imejizima , lakini sasa Michal alijikuta akishangaa Zaidi baada ya kuona gemu la mpira kwenye skrini.
“Michael tushamaliza hapa , tunapaswa kwenda idara nyingine maana muda wa chakula cha mchana unakaribia”Aliongea Dorisi na Edna alikuwa wa kwanza kugeuka na kufanya wadada hawa wa PR washushe pumzi na kumgeukia Roma.
SEHEMU YA 102
Saa kumi na mbili za jioni Roma alitoka ndani ya Kigamboni kuitafuta Sinza eneo ambalo ndio Mage alitaka kwa wao kuonana a , aliendesha gari yake huku akijiuliza kwanini Mage achague maeneo ya mbali hivyo, ila hakutaka kuwaza sana , aliendesha gari yake kwa umakini na kwa spidi na ndani ya kama nusu saa hivi alikuwa akiingia ndani ya hoteli moja maarufu iliokuwa ikifahamika kwa jina la Rozana.
Baada ya kugesha gari yake kabla ya kushuka alitoa simu yake na kumpigia Mage kumuuliza yuko wapi kwani yeye alishafika.
“Ndio naingia na gari sasa hivi”Ilisikika sauti nyororo kwenye masikio ya Roma,.
Nusu dakika baada ya Roma kutoka kwenye gari yake hatimae aliweza kushuhudia gari ya kifahari ya Maserati Ghibli Trofeo ya mwaka 2022, iliokuwa ni ghali ambayo ilifanya watu wote ambao walikuwa kwenye haya maneo kuiangalia kwa macho ya wivu , Roma aliangalia gari hii mpaka pale ilipoisimama.
Roma alijikuta moyo wake ukimwenda spidi baada ya kushuhudia mwanamke mrembo aitoka kwenye gari hii , ni kama haamini kama mtu aliekuwa mbele yake alikuwa ni yule ambaye amemzoea kumuona kwenye mavazi yake ya kazi.
Ndio alikuwa ni mwanadada Mage ambaye leo hii hakuwa kwenye mavazi ya kipolisi , leo alikuwa ni mwanamke mrembo sana kawnye macho ya Roma kiasi kwamba ni kama haamini kama ni mage.
Mage aliikuta akitabasamu baada ya kumuona Roma kuwa katika aina hio ya mshangao.
“Roma..!!”Aliita Mage na kumfanya Roma kutikisha kichwa huku homoni zake za kiume pale aonapo mrembo zikiwa juu.
“Mpaka nimekusahau , Sikudhani yule polisi mbabe leo hii anaweza kuwa mrembo namna hii , Mage umeua leo”Aliongea Roma huku akiweka tabasamu na kumfanya Mage aone aibu na kujisikia utamu.
Mage alimkumbatia Roma , licha ya kwamba Roma hakutaka kabisa kumkumbatia lakini kutokana na watu walikuwa wakiangalia alijikuta akiacha Mage amkubatie kimahaba kabisa ni kama walikuwa wapenzi na hata kwa watu waliokuwa eneo hiilo walijua kabisa hao wawili ni wapenzi , na walimuona Roma kama mwanaume mwenye bahati kwa kung`oa mwanamke mrembo kama huyo na sio urembo tu lakini pia mwenyepesa , kwani kwa gari ambayo Mage amefika nayo ni watu wachache sana ambao wanaweza kuimiliki, lakini pia watu hao hawakumbeza Roma kwani licha ya Roma kuoneakna wa kawaida , lakini alikuwa amekuja na gari nzuri ya kifahari ambayo pia ni moja ya Gari chache sana ambazo zilikuwa zikipatikana ndani ya jiji hili la Dar ,BMW M7.
Mage alitangulia mbele huku Roma akiwa nyuma akimwangalia Mage kwa nyuma , Mage jioni hii alikuwa amevalia kikoti flani hivi aina ya Vest chenye vifungo ambavyo vinafungiwa kwenye ubavu cha rangi ya njano ambacho kwa juu kabisa kilikuwa kimenakishiwa kwa wavu flani hivi , lakini kwa mpangilio wa kupendeza , chini akiwa ametinga surali ya kitambaa yenye marinda mwishoni na kiatu kirefu aina ya Skuna, kwa muonekano wa nguo zake ni Dhahiri kwamba zilikuwa ni ‘Brand’ kutoka nje ya nchi.
Roma hakushangaa na aina haya mavazi ambayo kwake aliona ni ghali sana kwa mtu wa kawaida kuvaa , lakini pia mavazi ambayo yapo kifasheni kwani alikuwa akikumbuka vyema mama yake Mage alikuwa akimilikia bongeala duka la nguo eneo la Posta.
Watu waliokuwa ndani ya ukumbi wa chakula eneo la mgahawa ndani ya hoteli hii ya hadhi ya nyota tatu, walimuonea Roma wivu kwa kuongozana na mrembo kama huyo na hawakuacha kugeuka kuangalia umbo namba nane la Mage, lakini kwa Roma hakujali sana.
Upande mwingine ndani ya eneo la Masaki alionekana mama T ndani ya jumba hili la kifahari akiwa sebuleni akufungua friji na kutoka chupa ya ‘Red Wine’ na kisha akasogea mpaka kwenye masofa na kuweka glasi chini huku akimwangalia Kanali Agustine aliekuwa bize akiangalia Runinga.
“Unaokeana kuwa kwenye mudi nzuri leo mke wangu”aliongea Kanali Tobwe.
“Sana mume wangu”
“Sasa si uniambie hiko ambacho kinakufanya kuwa na furaha tufurahie wote , tumeanza kufichana habari nzuri tangu lini”
“Si naendelea na wewe , mbona unakimbilia mwisho”
“Hehe.. haya niambie mke wangu”
“Ni Mage”
“Kafanya nini Mage”
“Inaonekana Mage kuna mwanaume ambaye amempenda”Aliongea na kumfanya Kanali kushangaa.
“Unasema kweli , Mage kuna mwanaume amempenda?”
“Sina uhakika lakini naamini ni kweli , leo mchana nimepigiwa na Tusi Mage kaenda dukani kwetu kununua mavazi ya kutokea kwa usiku na kwa jinsi Tusi alivyoniambia ni dhahiri kabisa kuna mwanaume ambaye anaenda kuonana nae usiku wa leo, na kwa ninavyomjua mwanangu Mage kwa mavazi ambayo amechagua ni ghahiri mtu anaekwenda kuonana nae ni mwanaume”Aliongea Mama T na kumfanya Kanali atabasamu.
“Unaonaje ukipeleleza tukajua ni mwanume gani Mage katokea kumpenda , unaweza hata kumuuliza”
“Tusiwe na haraka , unajua hii ni mara ya kwanza kwa Mage, hivyo tunaweza kumkatisha tamaa , ngoja tusubiri subiri”Aliongea Mama T na kumfanyab Kanali kutabasamu.
“Utapendelea nini Roma?, unaweza ukaagiza chakula”Aliuliza Mage baada ya kumuona Roma ameshikilia kitabu cha orodha bila kuchagua.
“Hapana Mage , bado ni mapema sana , muda huu kama nitakula njaa itaniuma mapema” Na muda hui huo mhudumu aliwasogelea aktika kuchukua oda yao.
Mage aliagiza juisi kwani hata yeye aliona muda ni mapema sana kuagiza chakula na Roma hakuwa mpenzi wa juisi , yeye aliagiza Wine na kisha akamgeukia Mage ni kama alikuwa akimpa ishara aanze mazungumzo.
“Roma najua unashauku ya kujua ni kwanini leo nimeomba tukutane”
“Ndio na inabidi uniambie sasa”
“Roma ukweli ni kwamba tokea siku ile ya Kusanyiko la wafanya biasahra nimekuwa mtu wa kujiuliza maswali kuhusu wewe , wapi umetokea , ni vitu gani ulikuwa ukifanya huko nyuma na kwanini ulikuwa kama vile , licha ya kwamba ulipigwa Risasi lakini ulionesha hali ya kuwa kawaida, mpaka sasa nimekuwa wa kuwazia hayo maswali”Aliongea Mage kwa sauti ya chini na Roma alimwangalia Mage , lakini pia wakati huo huo mhudumu alileta oda yao na kuwapatia.
“Mage nakumbuka ulisema kwamba unatamani sana tuwe marafiki na mimi pia nikakubali , kama ni kweli unataka urafiki wetu uendelea nadhani itakuwa vyema sana usipo uliza hayo maswali , kwani nikuambie tu siwezi kukujibu na pia nadhani dada yako pia ameshindwa kukupa taarifa zote kuhusu mimi na ndio maana una shauku, hajakuambia kwasaabu huenda taarifa zangu ni nzito kidogo kwa kila mtu kujua”
Jibu hilo lilimfanya Mage kujisikia vibaya , aliona ni kama Roma alikuwa akijiweka mbali na yeye na alijawa na huzuni kwa wakati mmoja na Roma pia aliliona hilo na kushangaa kwanini Mage kabadilika ghafla.
“Mage ni nini tatizo , au hujaridhika na jibu langu?”Aliuliza Roma huku akiangalia saa kwenye simu.
“Roma hebu naomba uwe mkweli na mimi , naataka uniambie kama kukuomba sisi kukutana hapa unajihisi nimekupotezea muda wako?”Roma alishangazwa na aina hii ya swali.
“Kwanini unauliza hivyo Mage?”
“Unaonekana kama mtu ambaye muda wote utaaga na kuondoka , sioni hali ya utulivu kwenye macho yako , lakini pia na kuona kama mtu ambaye unajitahidi kujiweka mbali na mimi”
“Mage sijui ulitaka nikujibu nini , lakini hilo ndio jibu pekee ambalo ninaweza kukupa mpaka sasa , Wewe ni polisi na nadhani mpaka hapo umenielewa ninachojaribu kumaanisha”
“Lakini leo hii sijaja kama polisi Roma , nimekuja kama mwanamke ndio maana nikavaa nikaendeza hii yote ni kwa ajili yako” Roma siku zote alikuwa ni mtu mwenye kutawala maongezi , lakini leo hii mbele ya Mage alikosa jibu.
Wakati Roma kaifikiria jibu la kumpa Mage Mara simu yake ilianza kuita mfululizo na kumfanya aitoe mfukoni na kuangalia ni nani ambaye anampigia kwa wakati huo na alipoangalia jina aliona sio namba ya Tanzania, lakini ni kama alikuwa ashaitambua hio namba kwani ilionekana sio mara ya kwanza namba hio kumpigia.
“Hades habari za muda huu?”
“Balozi!!”
“Ndio Hades ni mimi”
“Ndio nakusikiliza Balozi”
“Hades nakutaarifu Sophie ashafika nchini na nadhani mpaka sasa hajakutaarifu”
“Hapana hajanitaarifu , lakini pia nadhani haina haja ya yeye kunipigia simu kwani hapa Tanzania ana ndugu”
“Hades ndio maana nimekupigia simu , kifupi ni kwamba Sophia bado yupo uwanja wa ndege tokea asubuhi anakusubiri ukampokee, na hata baadhi ya ndugu niliowaagiza kumfuata amewakatalia na anasema pasipo ya wewe kwenda kumpokea haondoki”Aliongea Balozi na Roma alidhania ni kama utani.
“Balozi uko siriasi juu ya hili?”
“Nisingekupigia simu Hades, ninachokuomba ukamtoe mwanangu Sophia uwanja wa ndege”Aliongea balozi na kukata simu.
Roma alijikuta akishangazwa na jambo hilo , ni kama hakuwa akiamini kama kweli Sophia ameshindwa kuondoka uwanja wa ndege kisa yeye hajaenda kumpokea , jambo hili lilimshangaza na kuona nikama majaribu kwake , kwani alikuwa ashaweka wazi msimamo wake kwa balozi kwamba hawezi kumfanya Sophia kuwa mke wake.
“Mage nadhani tutaongea siku nyingine kwa sasa nina dharula”Aliongea Roma huku akinyanyuka ni kama hakutaka kusubiria jibu kutoka kwa Mage.
SEHEMU YA 103
Upande mwingine , ndani ya eneo la Mbezi Beach mkabala na jengo la kanisa la KKKT, ndani ya jumba la kifahari anaonekana mwanadada mrembo Nadia au Goddes of Law akiwa amejiachia sebuleni kwake bila habari , na kwa jinsi ambavyo mwanamke huyu alikuwa amevaa kama ni mwanaume ungekuwa karibu yake ni hakika ungetegeka , kwani kigauni alichokuwa amevalia kilikuwa ni kifupi mno na chepesi na kumfanya mapaja yake yote kuwa wazi.
Muda huu mrembo huyu alikuwa ameshikilia Glassi ambayo ndani yake ilikuwa na kimiminika cha rangi ya Zamabaru iliokolea ikiwa imejaa nusu , na alikuwa akipeleka mdomoni kwa madaha kabisa huku akiangalia runinga iliokuwa ikionyesha ‘live Show’ ya mwanamuziki mkubwa wa kike duniani aliekuwa akifahamika kwa jina la Christine.
Wakati mrembo huyu akiwa ameweka umakini kwenye Runinga , mlango wa eneo la sebulenni ulifunguliwa na akaingia mwanaume mmoja wa Kiafrika mweusi alievalia tisheti ya Levi`s pamoja na jeans na miwani , alikuwa ni kijana alieonekana kuwa mtanashati sana.
“Evansi mpango wangu unaendaje mpaka sasa?”Aliuliza Nadia huku akikaa pozi lile lile pasipo kubadilika na kumtesa kijana huyu ambaye muda wote macho yake yalikuwa yakiufaidi mwili wa mrembo Nadia.
Evansi hakutaka kuongea Zaidi , alitoa simu yake mfukoni na kisha akmpatia Nadia alieipokea na kuangalia.
Kwenye simu hio zilionekana picha Za Mage na Roma wakiwa wamekumbatiana kimahaba , na kwa jinsi walivyokuwa wakionekana kwenye picha ni kama wawili hao walikuwa na mahusiano na haikueleweka ni kwa namna gani walipiga picha hizo kwani ni za muda mchache ambao Roma na Mage walikuwa Rozana ,Nadia aliendelea kuperuzi kwenda kulia kuangalia hizo picha nyingine ambazo zilimuonesha Roma na Mage wakiwa wameketi wakiangaliana uso kwa uso.
“Nataka uendelee kukusanya Zaidi taarifa ambazo , siku tukimtumia Edna lazima awehuke na zimfanye kuzidi kuweka umbali wa kimahusiano na Roma”Aliongea Nadia.
“Sawa bosi”
“Vipi kuhusu Najma?”
“Bado Roma hajakutana na Najma Bado na kwa ninavyoona hawawezi kuonana hivi karibuni”
“Hata wasipoonana tunazo zile picha zingine wakiwa wamekumbatiana najua Edna hafahamu kama Roma na Najma wanafahamiana na hii ni kete nyingine”Aliongea Nadia huku akionyesha hali ya kufurahia , mwanadada huyu alioneysha nia ya kuyavunja mahusiano yaliokuwepo kati ya Roma na Edna.
“Bosi mpaka sasa nashindwa kujua kwanini upo ‘obsessed’ na huyu mwanuame kwani kwangu ni wa kawaida sana”Aliongea Evansi.
“Hupaswi kufikiria sana Evans najua hisia zako juu yangu , lakini mimi nampenda Roma na nnikuwambie ni mtu ambaye hata mtokee Evansi ishirini niwaunganishe pamoja hamuwezi kumfikia Roma , unaweza kwenda”Aliongea Nadia na Evansi hakutaka kubakia hapo , licha ya kwamba maneno ya Nadia yalikuwa yakimuumiza lakini hakutaka kuonyesha hali hio mbele ya Nadia.
****
Roma hakuwa na jinsi kabisa , aliona kama kweli Sophia atakuwa uwanja wa ndege , basi anapaswa kwenda kumtoa, lakini licha ya hivyo alikuwa akiwaza akishamtoa atampeleka wapi.
“Nitajua mbele kwa mbele”Aliongea Roma huku akizidi kukanyaga pedeli kuelekea Gongo La mboto.
Dakika chache mbele alikuwa akiingiza gari sehemu maalumu kwa ajili ya maegesho na baada ya kuzima gari yake alitoka na kutembea kuelekea jengo la Terminal 3.
Roma baada ya kuingia ndani ya hili jengo alianza kuangalia kushoto na kulia kumtafuta Sophie , ni kama bwana huyu hakuwa akiamini maneno ya Balozi , alijongea kuingia ndani Zaidi sehemu ya mapumziko kwa abiria na hapa ndipo alipojikuta akisimama baada ya kumuona mwanadada mrembo aliekuwa ameketi kwenye viti akiwa hana habari kabisa , huku akiwa ameshikilia simu yake.
Katika macho ya Roma Sophia alikuwa ni mrembo sana , tena mrembo ambaye alikuwa akimkaribia Edna lwa asilimia themanini , lakini Roma katika akili yake alijiambia kabisa hawezi kuwa na mahusiano na Sophia kwani mke wake na huyu Sophia ni ndugu hata kama sio wa damu , hivyo aliona ugumu kwenye swala hilo na ndio maana alikataa katakata maneno ya balozi kuhusu kumuoa Sophie.
Roma alijongea taratibu kumsogelea Sophie huku akinwangalia msichana huyu , Sophie kwa muonekano tu alionekana kuwa mdogo , licha ya kwamba muonekano wake ulikuwa umepevuka , lakini sura ya utoto haikujificha kwa Sophia.
“Sophia?”Aliita Roma na kumfanya mwanadada huyu ainue macho na kumwangalia Roma, na walipokutanisha macho yao alijikuta akitoa tabasamu la aibu.
“Hades!!”Aliita Sophia huku akiwa na aibu za kike na kumfanya Roma atabasamu , alijiuliza huyu msichana kwa aibu hizi aliwezaje kukaa hapa ndani kwa Zaidi ya masaa kumi , au balozi kuna kamchezo anamfanyia , ila kwa wakati huo hakutaka kuwaza sana kwakua yupo hapo kwa ajili ya kumchuku Sophia.
Upande mwingine , wakati Roma anaingia hapa ndani ya uwanja wa ndege , mita kadhaa kutoka alipopaki gari yake kulikuwa na gari nyingine ya Forester , ndani ya gari hii alionekana Faridi mlinzi wa karibu wa mstaafu jenerali wa jeshi akibonyeza simu yake na ndani ya sekunde aliweka sikioni.
“Nipe ripoti Faridi?”
“Mr Roma nimemuona ndani ya haya maeneo , inaonekana ndio kafika kumchukua Sophie”
“Vizuri sana, endelea kufatilia ni wapi atampeleka haha.. nina hamu ya kujua Faridi”
“Lakini bosi jambo ambalo tunalifanya naona sio sawa kwani Edna na sophia ni ndugu”
“Faridi unanionaje, kungekuwa na tatizo nisingeruhusu Sophie kumsogelea Hades ,Balozi anajiona mjanja kwa kufanya mambo pasipo kunishirikisha , ila mimi najua kila kitu ,wewe nipe kila hatua wanayofikia”Aliongea Jenerali huku akionesha furaha kwenye simu na Faridi alipumua na kisha akamjibu sawa mkuu wake.
Baada ya kama dakika tano kupita , alimuona Roma na Sophie wakilisogelea gari ambalo Roma amekuja nalo.
“Sophia baba yako amekuambiaje kuhusu maamuzi yangu?”Aliuliza Roma mara baada ya kuweka mabegi kwenye buti ya gari.
“Ameniambie una mke tayari na huna mpango wa kuongeza mke wa pili”
“Sasa kama umelifahamu hilo kwanini upo hapa Tanzania ili hali unajua kuwa siwezi kuwa na mahusiano na wewe?”
“Lakini mimi nataka kuishi na wewe hata kama tusiwe wapenzi , I am full of curiosity abaout you Hades”Roma alijikuta akishangaa lakini pia kuona huyu mtoto anafikiria nini , kwani watawezaje kuishi pamoja bila ya kuwa na mahusiano.
“Utaishije na mimi ikiwa hatuna mahusiano?”
“Sister Edna ni dada yangu licha ya kwamba hanijui ila mimi namjua”
“Sijakuelewa bado”
“Hades unaonaje ukinitambulisha kama mdogo wako , mimi ninachotaka ni kuishi karibu na wewe”Roma alijikuta kichwa kikitaka kumpasuka alikuwa akiwaza hawa wanawake wananini juu yake.
“Sophia nikuambie tu msimamo wangu upo pale pale mimi na wewe hakiwezekani kitu , ila nitakufanya ndugu yangu kwa muda utakaa na Edna na hakikisha unakuwa upande mzuti na yeye akupende na baadaye tutamuambia wewe ni nani na kama atakukubali kama mdogo wako sawa akikataa utaondoka”Aliongea Roma na kumfanya Sophia atabasamu , hakudhania mambo yatakenda namna hiyo.
“Sawa Bro Hades”Alliongea Sophia na kumfanya Roma atamani kucheka , yaani alimuona Sophia kuwa mpole lakini akianza kuongea upole unaisha kabisa.
Roma kazi alioona imebaki kwa wakati huo ni kwenda kumdanganya Edna kwamba Sophia ni ndugu yake.
“Licha sipendi kuongea uongo ila kwa sasa sina jinsi , Ngoja Sophia akaishi na sisi atakapozeana na Edna nitamueleza ukweli wote”Aliwaza Roma na kukanyaga pedeli, na aliendesha kwa muda mfupi tu Sophia alikuwa ashalala muda mrefu na alionekana kuchoka mno na Roma alimuonea huruma Sophia.
“Sophia mimi ni kaka yako kuanzaia sasa sawa , na utamuheshimu Edna kama wifi yako na umetokea Marekani ,Michigani”Aliongea baada ya kumuamsha
“Bro kwanini nitokee Marekani sio hapa Tanzania?”
“Kwasababu Tanzania sina familia na Edna anafahamu hilo”
“Kwahio Bro Roma ndugu zako wapo Marekani?”
“Ndio ila ni familia niliolelewa , usiulize maswali mengi”
“Sasa kuhusu Kiswahili je?”Aliuliza na ni kama Roma alikuwa anakumbuka sasa kumbe Sophie alikuwa akizungumza Kiswahili na hii ingeleta maswali kwa Edna na muda wote wakati wakiongea walikuwa wamesimama nje ya geti Kigamboni na Geti lilikuwa limefunguliwa muda mrefu tu.
“Bro si umesema umelelewa Marekani?”Aliuliza Sophie mara baada ya kumuona Roma anafikiria sana na Roma aliitikia kwa kichwa.
“Na vipi ulimwambia Siter kuhusu familia iliokulelea?”Hapo Roma ni kama alikumbuka ni kweli hakumwambia Edna ni familia gani iliokuwa ikimlea huko Marekani.
“Sijamwambia , umepata wazo gani?”
“Okey Hades! Unaonekana hata huna akili za kutunga uongo ,Script yetu itakuwa rahisi, Mimi Sophia niliishi Tanzania kabla ya kwenda kuishi nchini Marekani “
“Ndio ushamaliza hivyo?”
“Ndio Bro hapo utamalizia au hujaelewa mpaka hapo?”Roma alijikuta akitoa tabasamu la uchungu kwani kwa namna ambavyo Sophie alikuwa akiongea ni kama walikuwa wamefahamiana miaka kadhaa nyuma.
“Elezea nikuelewe sasa mpango unakaa vipi , nikwambie tu mke wangu ana akili sana na hadanganyiki kizembe kwahio ni bora uongo wako ukanyooka na ukafanana na ukweli”Sophie alijikuta akijisikia Vibaya kwa namna ambavyo Roma anamsifia mke wake.
“Hapo ni rahisi tu unanitambulisha kama mtoto wa Baba mdogo kwa upande wa familia iliokulelea huko Marekani na niliishi na familia yangu Hapa Tanzania kabla ya kuhamia nchini Marekanni”Roma hapo alijikuta akimuelewa Sophia.
“Sikia huu uongo utadumu kwa muda mchache tu , misheni yako ni kuhakikisha Edna anakupenda kama mdogo wake na tutamuambia ukweli sawa , ukishindwa nitamuambia ukweli na akikufukuza au akitufukuza nitakuwa sina msaada tena,Misheni yako ni ya miezi miwili tu”
“Bro hilo hata usiwaze mimi ni rahisi kupendeka”Aliongea Sophie na kumfanya Roma asiongee kitu na kuingiza gari ndani.
“Hades nitakufanya unanipenda kwa namna yoyote ile na utanianza mwenyewe”Aliwaza Sophie aliekuwa akitabasamu wakiingia ndani ya jumba hili.
“Nipe ripoti Faridi?”Ilisikika upande wa pili wa simu Faridi akiwa amesimamisha gari mita kadhaa kutoka iliponyuma ya Roma.
“Kamleta nyumbani kwake”
“Hahahaha…,Asante kwa kazi nzuri Faridi unaweza kurudi sasa , sisi tutakuwa ni wenye kuangalia nini kitaendelea Kama Edna akikubali kupokonywa mume ni shauri yake , akiweza kumfanya Sophie kama Mdogo wake hilo pia ni juu yake”Faridi aliitikia huku akishindwa kuelewa ni mpango gani Mzee Athumani anauandaa , maana alishindwa kung`amua kwa wakati mmoja.
Edna leo hii alikuwa ameketi sebuleni akiangalia Runinga huku Bi Wema akiwa bize kuandaa chakula na leo hii haikuwa kawaida , kwani walikuwa wamechelewa kidogo kupika ,kwani muda huo ilikuwa ya pata saa mbili na nusu za usiku na ratiba za kumaliza kula zilikuwa ni saa mbili.
Wakati Edna akiwa ameweka umakini kwenye taarifa ya habari mara mlango ulisukumwa na Roma na kumuona mume wake wa mkataba akiwa na mabegi, alishangaa kwanini Rmma karudi usiku na mabegi , lakini wakati akiwa amemkodolea macho Roma aliekuwa kwenye tabasamu , mara alitokea mwanamke mrembo sana aliekuwa nyuma ya Roma na kufanya moyo wake upige kwa nguvu , huku akishindwa kujielewa ni hali gani inaendelea kwenye moyo wake , kwani kwa jinsi msichana aelikuwa nyuma alivyokuwa mrembo alijihisi kuzidiwa uzuri.
“Roma nini kinaendelea?”Aliuliza Edna kwa wasiwasi .