Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

“You Can Never get a second chance to make a First
impression, Being in A good side with Queen Persephone
is good way to build my Carear,This is my only
Chance” Maneno ya Harris Meneja wa Bank ga Swiss[emoji3][emoji3]
 
“You Can Never get a second chance to make a First
impression, Being in A good side with Queen Persephone
is good way to build my Carear,This is my only
Chance” Maneno ya Harris Meneja wa Bank ga Swiss[emoji3][emoji3]
Mkuu unajua sana ninasoma sana Riwaya zako. Kuna ile ya kina Masumbuko/Peter/Rania/Najma/Nasma nayo ni [emoji108]
 
“You Can Never get a second chance to make a First
impression, Being in A good side with Queen Persephone
is good way to build my Carear,This is my only
Chance” Maneno ya Harris Meneja wa Bank ga Swiss[emoji3][emoji3]

Mkuu muendelezo plz
 
SEHEMU YA 129

Edna alishangaa kwa kitendo cha Meneja wa Benki ya Swiss kupiga magoti huku akionyesha hali ya kumuogopa , kwake ilikuwa ni mshangao kwani kwanza bado mshangao wa kwanza kuhusu pete kutoa mwanga wa ajabu haukuwa umeisha , lakini na Harris anaendelea kumshangaza Zaidi.

“Meneja Harriss! Naomba unyanyuke tuongee”Aliongea Edna huku akiwa na wasiwasi kweli , hakujua ni nini kilichotokea, alijiuliza kwanini hawa wazungu walikuwa wakimuita Malkia Persephone , ilikuw ani mara yake ya pili kukutana na mzungu na kumuitra kwa jina hilo hilo na ndio maana mrembo huyu alikuwa akishangaa , lakini hata pale alipomuuliza Roma juu ya maana ya jina hilo hakuwa amemuambia , mrembo huyu alishindwa kuelewa na alikuwa akihitaji maelezo , lakini sio kwa wakati huo , jambo ambalo lilikuwa ni kipaumbele kwake kwa wakati huo ilikuwa ni kwenda kuokoa hali mbaya ya kampuni yake juu ya hisa kushuka Thamani.

“Harris alitii maneno ya Edna na kisha akanyanyuka na Edna ambaye bado alikuwa kwenye mshangao akarudi na kuketi kwenye sofa.

“Malkia Persephone naomba unisamehe kwa kutokukutambua mapema , ni makosa yangu nastahili Adhabu”Aliongea Harris huku akiwe ameweka mikono miwili mbele kama mtoto aliekosa na anasubiria adhabu kutoka kwa wazazi wake , Edna licha ya kwamba alikuwa kwenye mshangao , ila alitamani kucheka hakuelewa kwanini huyu mzungu ambayye dakika chache nyuma alionyesha kujiamini sasa hivi anaonekana kunywea , alijiuliza ni siri gani ipo nyuma ya hio pete na pia hakuacha kujiuliza Roma ni nani haswa mpaka kufikia hatua ya meneja mkubwa wa benki ya Swiss kuwa katika hali kama hio..

“Mr Harris Kama unavyojua , kampuni yangu kwasasa , ipo kwenye hali mbaya na ndio maana nipo hapa kwa maagizo ya mume wangu , nataka kujua kama ninaweza kupata kiasi cha pesa?”Aliongea Edna mara baada ya kuchukua ile pete na kuingiza kwenye kidole chake, huku Harrisi akiendelea kuangalia ile pete kama mtu ambaye bado hakuwa akiamini kama ile pete ilikuwa ni ya Edna.

“Queen Persee…..”

“Mr Harris naomba unite Miss Edna , na uwe kawaida kama mwanzo ili tuzungumze tuelewane , nina haraka kidogo”Aliongea Edna na kumfanya Mr Harris kujiamini na kukaa chini.

“Miss Edna mpaka sasa benki ippo tayari kukupatia kiasi chochote cha pesa hata Dola bilioni tisini , ninachotakiwa ni kupiga simu tu makao makuu na hela hio itaingizwa moja kwa moja kwenye akaunti yako”Aliongea Harris pasipo utani na kumfanya Edna kutoa macho.

“Dollar Bilioni Tisini??”Alishangaa Edna maana hela hizo ukizibadilisha kibongo bongo zinaweza kukosa jina zuri la kuzitamka na ni zaidi ya mara kumi ya utajiri wake.

“Ndio Miss Edna, nitajie tu kiasi chochote unachohitaji na ndani ya dakika moja kitaingia kwenye akaunti yako”Aliongea Harris lakini Edna bado alikuwa kwenye mshangao , lakini pia wakati huo huo hakutaka kuufanya mshangao wake kumchelewesha kutatua lile tatizo ambalo lilikuwa ni kipaumbele kwa muda huo , aliamini kwakua Roma ndie aliempa pete hio atampatia maelezo ya kutosha.

“Okey Mr Harris nitahitaji bilioni mbili za kimatekani”Aliongea Edna kwa kingereza Safi na Harris akatabasamu na kunyanyuka na Edna alimpatia kadi ambayo ilikuwa na namba za akaunti ya benki.

“Miss Edna tafadhari naomba usubiri kwa dakika moja nipige simu makao makuu kwa ajili ya kiasi hiko kutumwa Tanzania”Aliongea Harriss kwa heshima na Edna alitingisha kichwa kukubaliana nae.

Huyu mwanaume siku zote anajifanyisha masikini kumbe anapesa haata kunizidi bado sijui kuna jambo lipi lingine ambalo atanishangaza tena?”Aliwaza Edna huku akimwangalia Meneja Harris akiongea na simu.

“Yes! I`ts not Three billion , just Two billion , make it hurry”Aliongea Harris akionekana kutoa maelekezo kwa mtu wa makao makuu huko Uswisi na alikuwa akimuelekeza kwamba asitume bilioni tatu bali atume mbili tu.

Ndani ya sekunde chache tu kiutani utani , Hela iliingia kwenye akaunti ya Benki ya Vexto na Hata Edna aliweza kupokea ujumbe wa meseji na aliishia kuzuia mshangao wake ndani kwa ndani, Na Edna baada ya kuona jambo hilo limefanikiwa alinyanyuka kwa ajili ya kuondoka.

“Miss Edna nitakusindikiza mpaka nje”Aliongea Harris.

“Hapana Mr Harris , ninashukuru mpaka hapa”. Aliongea Edna ila kwa Harrisi hakuridhishwa na maneno ya Edna kabisa , alijiambia katika nafsi yake huo ni muda mzuri wa kuwa ‘Chawa’ Wa Edna hata kwa kumlamba miguu , ndio alikuwa akijua mtu aliekuwa mbele yake ni Queem Persephone.

Queen Persephone ni jina linalotoka katika ugiriki ya kale , yaani mke wake Hades hapo kale alikuwa ni malkia anaefahamika kwa jina la Queen Persephone mtoto wa Zeus kaka yake Hades na Demeter , ukisoma historia za Miungu ya Ugiriki ya kale utaelewa , sasa katika uhalisia wa Dunia ya leo haikueleweka kwanini Harrsi alikuwa akionyesha heshima kubwa kwa Persephone kwani hizo zilikuwa Historia za mambo ya kale , ila kadri utakavyosoma hii simulizi utaelewa baadae.

“You Can Never get a second chance to make a First impression, Being in A good side with Queen Persephone is good way to build my Carear,This is my only Chance”Aliwaza Harrison na muda huu alikuwa akimuongoza Edna kuelekea kwenye lift kazi ambayo hata Katibu muhtasi wake alitaka kuifanya yeye lakini alimpa ishara ya kumuambia atulize mshono.

Dakika chache walikuwa ndani ya eneo la Maegesho ya gari na Edna aliagana na Harris na kisha akaingia kwenye gari yake huku Harrisi akiinamisha kichwa chini kama heshima ya ishara jambo ambalo moja ya wafanyakazi wamapokezi walilishuhudia na kushangaa sana.

Hali ya kampuni ya Vexto haikuwa ya kawaida hata kidogo ,kuanzia asubuhi wafanyakazi wa kampuni hii walikuwa na wasiwasi mno kwa kile kilichokuwa kikiendelea kwa kampuni yao , wale ambalo walikuwa ni walolole walikuwa washaanza kufanya maombo haraka haraka na kwa wamama walichukua hata hatua ya kuwasiliana na Mwamposa kuweka kampuni yao kwenye mikono ya Mungu ili tatizo linaloendelea lipite, hakuna mfanyakazi ambaye alipenda kuwa kwenye orodha ya wafanyakazi ambao watapunguzwa kutokana na uchumi mbaya wa kampuni , wengi waliogopa mno kutokana na kwamba walikuwa wakitegemea kuendesha maisha yao , kupitia kampuni hio.

Recho, Benadetha walikuwa bize kujibu maswali mbalimbali ya wateja wao , kuhusiana na kile kinachoendelea kwenye kampuni , pia baadhi ya watu ambao walikuw awakimkubali Edna walipiga simu kuulizia hali ya CEO na moja ya watu ambao hawakuwa nyuma katika kupiga simu ni Kibonge ambaye alikuja kufanya usaili kwa mara ya kwanza akiwa na Roma na kutopata nafasi, bwana huyu alimfanya Recho aliekuwa amepokea simu yake kucheka , licha ya hali mbaya ya kampuni.

“Recho mbona unacheka , wakati unaona kampuni inakwenda mlama?”Aliuliza Tina mfanyakazi na Recho alimwangalia na kisha akaguna kidogo.

“Kuna mtu kapiga simu hapa , nilidhanii ni moja ya wateja wetu wanaopiga simu kila siku , ila huyu sio mteja ila kajitambulisha kama anamkubali sana CEO na amesikitishwa na kinachoendelea mitandaoni maana hakina ukweli wowote”Aliongea Recho na kumfanya na Tina atabasamu.

“Ila naamini CEO atalitafutia ufumbuzi hili swala muda si mrefu”Aliongea Tina.

“Hata mimi naamini hivyo , Edna ana akili sana na siku zote amekuwa ni wa kuingoza kampuni hii kwa weledi wa juu kabisa na kufanya kupata umaarufu kimataifa, tunapaswa kufanya kazi kwa bidii kutimiza majukumu yetu”Aliongea Benadetha akiwaambia wafanyakazi wenzake na wote waliitikia na kuendelea na kazi na kati ya wafanyakazi hawa wa PR ni Roma pekee ndio ambaye hakuwa ameonekana na aliwafanya pia hawa wafanyakazi wajiulize inakuwaje Roma anafanyakazi kama vile kampuni ni ya baba yake.

Nasra na Dorisi wote walikuwa kwenye kuchanganyikiwa na hali ilivyokuwa inaendelea tokea asubuhi, kati ya watu waliokuwa kwenye wasiwasi mkubwa sana ni Nasra , huyu alikuwa na wasiwasi sana na kampuni hii na hii yote ni kutokana na ahadi aliokuwa ameweka kati yake na mama yake Edna juu ya kulinda kampuni ya Vexto kwa namna yoyote ile, na kuwa bega kwa bega na Edna.

Mrembo huyu tokea aongee na Edna , ilikuw imepita Zaidi ya lisaa limoja na hakuwa akijua ni kipi Bosi wake alikuwa akifanya kushugulikia tatizo lililokuwa likiendelea ndani ya kampuni, lakini sasa wakati akiwa kwenye wasiwasi mkubwa , mara meseji ya simu anayotumia kufanyia shughuli za kampuni , iliingiza ujumbe wa kuingia kwa muamala wa kiasi cha Dollar Bilioni mbili na kumfanya Nasra atoe macho

“Dollar Bilioni mbili? Bosi kazipataje?”Ndio swali la Nasra lililoibuka kwenye kichwa chake , lakini akiwa anashangaa muda huo huo simu ilianza kuita na baada ya kuona jina ni Bosi wake Edna alipokea haraka haraka na kuweka sikioni.

“Nasra nadhani ushaona kiasi cha pesa ambacho kimeingia kwenye akaunti ,nimepata mkopo wa kiasi hiko na nadhani unajua nini cha kufanya?”

“Bosii…”

“Najua unamaswali , ila shughulika na tatizo kwanza Nasra”Aliongea Edna na kisha akakata simu na kumfanya Nasra atabasamu , alikuwa akiwaza imekuwaje Edna akaweza kupata kiasi hiko cha pesa kwa wakati mfupi namna hio , hakuwa ametegemea kabisa na alione anayo mengi ya kujifunza Zaidi kutoka kwa Edna.

Upande wa Mzee Chino baada ya kutoka nyumbani kwa Edna alienda moja kwa moja mpaka ndani ya hoteli ya Maple Grupu iliokuwa ikimilikiwa na Neema Luwazo iliokuwa imepakana na Mgahawa wake.

Baada ya mzee huyu kufika ndanin ya hoteli hii , alionekana kama mtu ambaye alikuwa ameandaa mkutano na waandishi wa habati , kwani walikuwpo baadhi yao wakiwa wanaingia ndani ya jengo hilo.

“Boss tayari kila kitu”Aliongea kijana mmoja hivi ambaye alikuwa na meno yake ya Kichaga mrefu mweusi mwembaba alievalia suti.

“Shukrani Niko”aliongea Mzee huyu na kisha aliingia kwenye lift na ndani ya dakika chache alitokea kwenye ukumbi mkubwa uliokuwa ndani ya hoteli hii ,ukiwa na waandishi wa habari waliokuwa wakimsubiria.

Mzee huyu aliangalia waandishi hawa na kisha akavuta pumzi na kusogelea maiki zilizokuwa zimepangwa kwenye meza yake na kisha akaketi .

“Ni muda wa kukamilisha kazi yangu Marium , baada ya hapa Edna atakuwa ndio mmiliki halali wa mali zako na mimi kazi yangu itakuwa imeisha”Aliongea Mzee huyu alionekana alikuwa amewaita waandishi wa habari kwa ajili yakuongea kuhusu mkataba uliosainiwa na watu wa tatu ,yaani wazazi wake wa Edna yaani bibi yake , mama yake na baba yake.







SEHEMU YA 130

Edna baada ya kutoka ndani ya benki ya Swiss moja kwa moja alinyoosha mpaka ndani ya Paradise Hotel iliokuwa ikipatikana kando ya ufukwe wa Coco ni moja ya hoteli ya nyota tano pia maarufu ambayo alikuwa akiimiliki .

Baada ya kuegesha gari yake sehemu maalumu , alishuka na kuingia moja kwa moja eneo la mapokezi na baada ya wafanyakazi hawa kumuona tu , walikosa utulivu huku wakiinama kwa heshima.

“Naomba ufunguo wa chumba changu?”Aliongea Edna mara baada ya kufika eneo la mapokezi na vijana wanne waliokuwa hapa eneo la mapokezi waliinama kwa heshma na mwanadada mmoja mrembo wa kiarabu alitoa kadi ya mlango na kumpatia Edna.

“Boss! Kuna kitu chochote utahitaji kuhudumiwa?”Aliuliza kwa heshima yule mwanamke.

“Nitaagiza kwa simu Tesha”Aliongea Edna na mwanadada aliefahamika kwa jina la Tesha aliitikia kwa heshima na Edna akapiga mwendo kuelekea kwenye lift na ndani ya dakika chache tu alikuwa chumba cha juu kabisa cha hoteli hii yenye urefu wa Ghorofa ishirini na tano, chumba kilichokuwa kikiangaliana na Bahari , kilikuwa chumba aina ya ‘Presidential Suite Room’, upande wa kulia wa chumba hiki kulikuwa na picha kubwa ya mama yake Raheli iliokuwa imetundikwa ukutani lakini pia upande wa kushoto kukiwa na picha ya bibi yake , upande wa nyuma pia kulikuwa na picha ya yeye akiwa amepakatwa na bibi yake lakini pia nyingine akiwa amepakatwa na mama yake , Edna aliangalia picha hizo huku akiwa amesimama na kadri alivyokuwa akiziangalia machozi yalizidi kumtoka na ndani ya dakika kadhaa mrembo huyu alijikuta akikaa sakafuni na kuanza kulia kwa kwikwi.

Ukweli taarifa ya Edna kutokua mzazi wa damu wa Mzee Adebayo ilionekana kumuumiza na kuwa kubwa kwake na alionekana muda wote alikuwa akijizuia , lakini kwa jinsi muda huu ailvyokuwa akilia ni kama alikuwa mtoto , alikuwa akilia huku akiwa amejishikilia kifua chake , siri nzito ya familia alioifahamu siku hii ya leo , ilimfanya mrembo huyu kuumia sana kwa wakati mmoja , haikueleweka pia kwanini chumba hiki alikuwa ameweka picha hizo na sio kule nyumbani anapokaa.

“Mamaa…hihii… hiii… ,Pole sana mama yangu ,,hiii hiii”Mrembo huyu alionekana kumuomboleza mama yake kwa mara nyingine , inaoneasha pia maisha ambayo Raheli aliyaishi kipindi akiwa katika uhai wake yalikuwa yakuumiza sana na ndio maana alikuwa akiomboleza mrembo huyu.

******

“Your Majesty Pluto habari ya kifo cha Profesa Shelukindo umeipata?”Aliuliza Deigo mara baada ya Roma kupokea simu.

“Ndio Deigo ndio nimeipokea muda sio mrefu , kuna jambo gani mmenasa kweye rada zenu?”

“Mfalme ,tumegundua aliehusika na kifo cha Profesa Shelukindo ni Scorpion mlinzi wa mheshmiwa Kigombola, baada ya kumfatilia kwa kila hatua tokea alipotoka kuonana na Yan Buwen”

“Kwahio Diego unataka kumaanisha kuwa Yan Buwen anahusika na kifo cha Profesa Shelukindo?”

“Ndio mfalme “Roma alijikuta akiwaza kidogo , kama ni kweli huyu Profesa, Yan Buwen alikuwa amehusika ni kwa sababu ipi , licha ya kwamba Roma alikuwa akitambua nguvu ya Profesa Shelukindo likija swala la Sayansi inyohusiana na Energy , lakini kwa kitendo cha Yan Buwen kumuagiza Scorpion kumua Profesa shelukindo , ni swala la kufikirisha kidogo.

“Diego mnafikiri kuna dhamira gani ya Yan Buwen kumuua Profesa kama ni kweli kafanya hivyo?”

“Mpaka sasa hatujajua mheshimiwa Pluto , kwa namna ambavyo tumeendelea kufatilia kwa kila mtu ambaye amekutana na Profea mmoja wapo ni Waziri wa Sayansi na Teknolojia na tumejaribu kunasa mawasiliano yake ambayo anafanya na tumegundua ni dakika kadhaa chache nyuma ametoka kuwasiliana na Yan Buwen , licha ya kutokujua ni kipi wamezungumza.”Aliongea Diego.

“Okey!Kwa sasa hilo inabidi muendelee kulifatilia na mjue ni kwanini Yan Buwen kamuua Pofesa Shelukindo na mkipata majibu ya aina yoyote mtanijuza”

“Sawa Mfalme”Aliongea na Roma akakata simu.

“Inaonekana wapo Tanzania kwa ajili ya Godstone , ngoja Clark akifika Tanzania nitamuuliza kama Profesa kagundua teknolojia ya namna ya kutumia madini yanayopatikana kwenye Godstone

Aliwaza Roma kwenye kichwa chake, huku akibadilisha baadhi ya chaneli kuangalia kama kuna kitu cha maana , lakini hakuweza kuona cha maana Zaidi lakini ile anataka kuzima ndipo alipoweza kiuona taarifa ya Mzee Chino akiongea na waandishi wa habari , alisikiliza mpaka mwisho na aliyoongea Mzee Chino yalikuwa ni yale yale ambayo yalikuwa kwenye mkataba ambao Edna alisaini asubuhi .

Roma bado alikuwa na mchecheto wa kusikia taarifa kutoka kwa Ron , alitaka kufahamu ni mtu gani ambaye kavujisha taarifa za ripoti ya kimatibabu za baba yake na Edna, katika kichwa chake alipanga kama mtu huyo bado yupo ndani ya Tanzania ni lazima amuuwe maana aliona ni uchokozi wa waziwazi kabisa kumgusa mke wake.

Na ni kweli ndani ya muda mfupi tu simu yake iliita tena na alipokea haraka haraka na kuweka sikioni baada ya kuona jina la mpiganji alikuwa ni Ron.

“Niambie Ron”

“Mfalme yule Dokta kaongea ukweli wote na kasema taarifa alimuuzia Alex Mathayo”

“Alex Mathayo?”

“Ndio mfalme Pluto na tumejaribu kufatilia jina la huyo Alex na anaonekana kuwa mfanyabiashara mkubwa ndani ya Tanzania , ni mwanzilishi wa kampuni ya JR , kampuni ambayo kwa taarifa tulizonazo kwasasa mwenyekiti wake wa Bodi ni CEO Edna , malkia wetu”Aliongea Ron na kumfanya Roma aone kumbe yale yote yaliokuwa kwenye mtandao yalikuwa ni kulipiza kisasi kwa Edna kutokana na kumpokonya mzee huyo kampuni.

“Ron Asante sana kwa taarifa , kwasasa nitaendelea kwa kazi iliobaki, na kuhusu huyo Dokta haina haja ya kupoteza pesa kumleta mpaka Tanzania , nataka mumpe maumivu makali ya kiwango cha Daraja A kwa muda wa masaa Arobaini na nane na kisha mpigeni Risasi na wapelekee familia yake maiti wakazike”

“Hakuna shida Mfalme Pluto. Yaani hata usijali , nilikuwa nikiongea na Sergei hapa anasema amemisi sana kuona damu ya binadamu , nadhani ombi lake limejibiwa”

“Shukrani Rona , Punguza kupenda Malaya Wewe mzee”

“Haha…Sawa Mfalme Pluto naendelea kuufanyia kazi ushauri wako”Aliongea Ron na Roma akacheka na kisha kukata , Roma alionekana kuwa na mazoea sana na vijana wake.

Roma baada tu ya kukata simu , alimpigia Diego na kumwambia ajaribu kufatilia ni sehemu gani Mzee Alex anapatikana , alipanga akishajua akamuue maana yeye hakuona mke wake alikuwa na makosa kwa yeye kupoteza kampuni yake kwa Edna , yeye alimuona Mzee Alex kama mtu mchokozi akishirkiana na mtoto wake Abubakari na ndio maana , aliamini watu hawa wakiendelea kuvuta Pumzi ndani ya jiji la Dar , basi hawataacha kumsumbua mke wakena dawa ya matatizo ya aina hio kwake aliyatibu kwa kuwaondoa watu wa aina hio Duniani.

“Mfalme Mzee Alex anaonekana ndani ya jengo la Kampuni yake ndani ya Posta”Aliongea Diego na Roma alitabasamu kifedhuli .

“Okey Diego!Wasisitize vijana waendelee kumpa ulinzi mke wangu”Aliongea Roma na kisha akakata simu na alivaa nguo zingine na kuchukua ufunguo na kutoka , huku akipanga moja kwa moja kwenda ndani ya jengo la kampuni ya JR kuua.
 
SEHEMU YA 131

Abubakari na Elvice tukio la kwanza kuwafanya wachanganyikiwe likuwa ni juu ya taarifa ya Mzee Chino kuitisha waandishi wa habari na kutolea ufafanuzi kile kilichokuwa kikiendelea kwenye mtandao.

“Kwa taarifa hii naamini ni moja ya hatua nzuri ambayo Edna amechukua”Aliongea Elvice huku akikodolea Skrini ya soko la hisa , ukweli licha yataarifa hio kutolewa lakini soko halikuonyesha mabadiliko makubwa.

“Mtueleze ni nini kinafatia kwa sasa”Aliongea Abubakari huku akiwaangalia vijana wataalamu wabobezi wa hisa wakiendelea na kazi yao.

“licha ya taarifa ya ufafanuzi uliotolewa, thamani za hisa haziwezi kupanda kwa kiasi kikubwa Zaidi ya kutengeneza ‘Small Retracement’?”Aliongea mtaalamu wa soko namba moja.

“Mr Abubakari nadhani mpaka sasa unaelewa kuwa ndani ya kampuni ya VEXTO kuna financial Problem?”

“Kwahio unamaanisha kutokana na uhafifu wa Hela Taslimu ndani ya kampuni thamani ya hisa haziwezi kuwashawishi watu kununua na kupanda?”

“Wengi watanunua , lakini hio itatokana na ni kipi wanaona kwenye soko na kama unavyojua sio wafanyabiashara wote wanaonunua hisa hutumia taarifa za kimsingi(Fundamental news) kununua hisa , kuna wengine ambao pia hutumia Uchambuzi wa kimbinu(Technical Analysis),na tunachotakiwa hapa ni kuwafanyia mchezo”Aliongea mtaalamu wa soko namba moja.

“Mchezo gani?”

“Tutatengeneza ‘False Buy’ kwakununua kiasi kidogo cha hisa na baada ya dakika kumi na tano tunauza hisa zote sokoni na hapa tutakuwa tumewafanya watu wanaotumia ‘Technical Analysis’ kuingia kwenye mtego na kuuza na wao na hapa ni lazima soko litaendelea kushuka , labda tu kama Vexto watafanikiwa kupata kiasi kikubwa cha pesa na kushindana na ‘Momentum ya soko’”Aliongea kijana mtaalamu namba tatu na hawa vijana wote walionekana kuwa na hamu sana kwa kile kinachoendelea.

Upande wa pili baada ya kiasi cha pesa kuingia kwenye akaunti ya kampuni , swala lile Nasra hakuliweka wazi kwa muda na alichokifanya ni kuwasiliana na kundi la Athena kwanza ili kuwapa maelekezo.

Ukweli Nasra alikuwa akijua kuna kundi hili la Athena kupitia kwa Edna , lakini siku zote hakuwahi kujua kama kundi hilo lipo hapa nchini , lakini pia hakujua kama kundi hilo lilikuwa likipatikana nchi gani , yeye alikuwa akijua tu kwamba kundi hilo ni wataalamu wabobezi wa kampuni maswala ya Hisa na ndio maana mara nyingi alikuwa akiwasiliana nao , pale ambapo akiachiwa majukumu ya kikampuni na Edna

“Nasra unatakiwa kwanza kutulia tuangalie upepo wa soko kwanza unavyoendelea ndio tuanze mchakato wa kupandisha thamani za hisa”Aliongea Amiri kwenye simu.

“Okey!Mkiwa tayri mtaniambia ili niidhinishe pesa kuingia kwenye mzunguko”

“Hakuna shida Nasra”Aliongea Amiri upande wa pili wa simu na kisha simu hio ikakatwa na Nasra aliegamia kwenye kiti chake na kutoa pumzi.

“Msaidizi wa Edna arudi tu kwa namna hii nashangaa Edna anawezaje kufanya maamuzi yote ya kampuni peke yake?”Aliwaza Nasra huku akijipumzisha kwa muda na alichokuwa akimaanisha ni kwamba Asistant CEO wa Edna arudi , kwani alikuwa yupo nje ya nchi kikazi na hakuwa ameanza majukumu yake ya kazi rasmi na alikuwa ametambulishwa tu kwenye kampuni na Edna siku chache nyuma.

“Amiri unafikiri mpango wako utafanikiwa?”aliuliza Mzungu Adrin aliekuwa amevalia Bukta yake na visendo vya manyoya huku akila zake popcorn huku akiangalia Soko la hisa la Vexto.

Na muda huu walikuwa ndani ya jengo lao la kifahari ambalo walikuwa wakifanyia kazi , kwa namna ambavyo mabwana hawa walivyokuwa wakiishi , masha yao yalionekana ya kifahari sana , kwani kwanza jengo hili lilikuwa refu na kila mfanyakazi hapo ndani alikuwa na Apartment yake ya vymba vitatu na jiko , sebule na choo , yaani maisha yao ni kama walikuwa tu huko uzunguni na huenda hata kama wangekuwa huko uzunguni wasingeweza kuishi maisha mazuri kama wanavyoishi hapo ndani , kwani kwanza Edna alikuwa akiwalipa vizuri , lakini pia mazingira ya kufanyia kazi yalikuwa mazuri na pia licha ya kazi yao kuwa ya kukaa kwenye tarakishi muda mrefu , lakini hawakuchoka sana , kwani wlaikuwa wakipeana zamu na pia walipata muda wa kula bata siku za wikiend .

“Kwasababu waliovujisha ile taarifa ni watu ambao hawana nia nzuri kwa Vexro ni lazima watakuja na kamchezo kao na ninataka nikaone hapa , ili tukiwafanyia shambulizi wasije kuelewa hata nini kimetokea”Aliongea Amiri na mrembo moja hivi wa kiarabu aliekuwa amevcalia hijabu yake akiendelea na majukumu yake alimwangalia na kutabasamu , alionekana alikuwa akimsoma sana huyu Amiri kwa mpango wake na Adrin hakutaka kuongezea neno Zaidi ya kuondoka ndani ya chumba hiko na haikuelewekana alikuwa akienda wapi.

“Guys! Kesho Wikiend tumalize kazi hapa kitaalamu kabisa na wanaokwenda Zanzibar , waende wale wa Mbudya pia waende”Aliongea Amiri na alipigiwa makofi na kila mmoja , ukweli Amiri alikuwa kiongozi mzuri sana na sikuzote alikuwa akijitahidi kumuonyesha bosi wake Edna juhudi na uwezo wake wa akili katika kuchanganua mambo hasa likija swala linalohusiana na uchumi , bwana huyu alikuwa na mpango hata wa kumtongoza Edna na hata kuna siku kabla ya Edna kumtambulisaha Roma kwao , alikuwa ashaanza kuchukua hatua taratibu , lakini kwa wakati huu jamaa alionekana kukata tamaa baada ya Edna kufanya makusudi ya kumtambulisha Roma kwao.

“Amiri , unafikiri ni nani ambaye katoa pesa yote ile kuingia kwenye kampuni?”Aliuliza jamaa mmoja wa ki Nigeria na huyu leo hii alionekana kuwa mgeni kwani ile siku ambayo Roma alifika hapo ndani huyo jamaa hakuwepo.

“Ogobe mimi siwezi kufahamu hilo pia hatuwezi kujua , lazima tuifahamu mipaka yetu , sisi ni wafanyakazi tu hapa ndani na hatupaswi kufatilia sana”Aliongea Amiri na Ogobe akakubali kwa kichwa na kuendelea na kile alichokuwa akifanya.

Upande mwingine Abubakari na Elvice walikuwa wakifanya kama walivyoshauriwa na wataalamu wao wa masoko ya hisa ambao hata haikueleweka wataalamu hao walikuwa wamewatolea wapi , Waliingiza kiasi cha pesa kwenye soko na kweli wakalifanya soko kupanda thamani kidogo na baada ya kuona mpango wao umefanikiwa , wakauza tena na ni kweli kwa maelezo ya wale vijana walionekana kuwa sahihi , kwani baada ya wao kuuza kulionekana baadhi ya wanunuzi wadogo wa hisa wakifuata na wao mkumbo na wakaunza mfululizo na kulifanya soko kuendelea kuporomoka na kumfanya Abubakari kutabasamu.

“Boss kwa hapa soko lilipofikia nashauri tununue hisa kwa kiasi chote cha pesa kabla hazijapanda thamani?”Aliongea mtaalamu namba moja na kumfanya Abuu aangaliane na Elvice.

“Acheni zishuke shuke ndio tununue , hela tuliokuwa nayo haiwezi kununua hisa zote asilimia arobaini”

“Mr Abubakari hapa sio swala la kununua asilimia Arobaini bali nazungumzia swala la kupata faida kama tukinunua zikiwa bei ya chini hivi”

“Kijana sisi ndio tumekuleta hapa na kukulipa , usijifanye unataka tukusikilize kwa kila ambacho unatuambia , sisi ndio mabosi wako elewa nafasi yako na fanya tunachokuambia”Aliongea Elvice Temba baada ya kuona kijana huyo anatoa sana ushauri kama vile pesa ni zake na mtaalamu namba moja hakutaka kuleta ubishi , alichokifanya ni kutulia na kuona mwisho wake , lakini alichokua anaamini yeye kama mtaalamu wa soko la hisa, ni kwama hisa zitapanda thamani na hazitoendelea kushuka.

“Okey!Bosi basi nitauza asilimia zote za hisa tulizonunua sokoni”

“Hivi tumenunua asilimia ngapi?”

“Ishirini bosi”

“Uza zote na zikishuka thamani kidogo fanyeni mpango wa kununua”Aliongea Abubakari kwa kujiamini na mtaalamu namb moja alitabasamu chini chini na kufanya kama alivyoambiwa na ile anamaliza kugonga kitufe cha ‘Enter’ kuruhusu hisa zote kuzitupa sokoni hapo hapo , Soko lilifyatuka kama Roketi na kupanda mara moja thamani na kupitiliza zaiid ya Thamani iliokuwa jana yake kabla ya taarifa kusambaa, sio Abubakari , sio Elvice , wote walishangaa kwa kile walichokuwa wakikiona.

“Imekuwaje hivi?”Aliuliza Elvice kwa mshangao na hata Abuu akisogea karibu akishindwa ni kipi ambacho kinaendelea.

“Nilikuwambia bosi tununue Hisa zote za hii kampuni kabla hazijapanda, na kama ungekubali kwa kiasi cha bilioni ulichokuwa nacho ungepata Zaidi blioni nyingine kama faida kama ungenisikiliza na sasa huna cha kufanya tena ,kwa thamani hio ya hisa hata kama ununue huwezi kupata faida Zaidi ya hasara au usubilie soko lishuke tena thamani ndio ununue na hilo linaweza lisitokee leo wala kesho”Aliongea Mtalamu namba moja na kisha alichukua simu yake ya I phone 14 na kunyanyuka.

“Sihitaji hata malipo , siwezi kufanya kazi na mabosi ambao hamko Flexible na chuki zenu zinawafanya msifanye maamuzi sahihi”Aliongea Mtalamu namba moja na kisha aliondoka na wala Elvice na Abubakari hawakumjali sana na hio ni kutokana na kwamba mabwana hawa walikuwa hawaamini kama hisa za kampuni ya Edna zimepada thamani kwa namna hio.

Upande wa nje ya nyumba baada ya Mtaalamu namba moja kutoka nje kabisa alipiga simu.

“Amiri leo sifanyi kazi nyingine mpaka jumatatu nawaza kwenda Zanzibar tu kukinukisha na Warembo ”aliongea yule Mtaalamu namba moja na huku akitabasamu.

“Good Job Issa kwa kazi nzuri ,unaweza kurudi mjengoni au kuendelea kula bata”Iisikika sauti ya Amiri upande wa pili, ndio ni Amiri kiongozi mkuu wa Athena na haikueleweka walimwingizaje Issa ndani ya vijana wa Abu kwa ajili ya kuwafanyia utaalamu wa kimasoko.

****

Matrida alijikuta akitoa mshangao kiasi cha kunyanyuka na kumfanya Mzee Alex aliekuwa amekaa kwenye sofa kumshangaa na kujiuliza ni kitu gani kimemfanya Matrida kushangaa namna hio kiasi cha kumpelekea kuziba mdomo.

“Kuna nini Matrida?”Aliuliza Mzee Alex alieingia hapo ndani dakika mbili zilizopita na alikuwa amefika ndani ya kampuni hio kufatilia kwa ukaribu kile kilichokuwa kikiendelea kwenye kampuni ya Edna.

“Baba Angalia mwenyewe”Aliongea Matrida huku akigeuza Skrini ya tarakishi yake ili kumfanya baba yake aone na mzee Alex na yeye alishangaa kuona Hisa za kampuni ya Edna kuwa juu angani kileleni kithamani.

“Huyu mtoto nishawahi kusema huenda akawa Freemason, haiwezekani hii , hisa zikapanda ghafla tu”Aliongea Mzee Alex huku akivuta pumzi , kuna muda alitamani hata Edna angekuwa ndio mtoto wake , maana kwa mambo ambayo alikuwa akiyafanya yalikuwa ni Zaidi ya mwanaume.

Wakati Matrida akiendelea kushangaa , Mara muda huo huo , aliingia Magdalena huku akihema kama mtu ambaye amekimbizwa maili nyingi Mzee Alex aliweza kumtambua Magdalena haraka sana , kwani alikuwa akimkumbuka kama moja ya watoto wa Afande kanali Tobwe na alikuwa akifahamu fika mapacha hao moja alikuwa ni mwanajeshi na pia mwingine alikuwa ni polisi , lakini mzee uyu licha ya kuwafahamu , lakini haikuwahi tokea siku hata moja kujua kuwatofautisha kwani wote walikuwa wakifanana sana na kwa upande wa Matrida alikuwa akimfahamu Magdalena na Mage lakini hakuwa sana na mazoea nao.

“Mzee Alex huu sio muda wa kunishangaa , ila mpapaswa kukimbia”Aliongea Magdalena kwa sauti ya usiriasi.

“Ajenti Flamingo Acha kuwashauri upuuzi , nani kasema wanaweza kukimbia”Aliongea Roma ambaye alifungua mlango na kumfanya Mzee Alex kuogopa mno na hata yeye mwenyewe hakujua ni kwanini





SEHEMU YA 132

Unajua nini baada ya taarifa inayomuhusu Edna kuanza kusambaa mtandaoni , Ajenti Flamingo alipigiwa simu na afande Maeda kuwa makini na Hades , kwani kwa namna ambavyo anaona hio taarifa , aliamini ni Dhahiri Hades angeua mtu na ndio maana Magdalena asubuhi yote alikuwa amejibanza mita kadhaa kutoka lilipokuwepo geti la nyumba ya Edna na hata wakati ambao ,Mzee Chino anaingia alimuona lakini pia wakati wa kutoka kwake pia alimuona na alijiuliza Mzee huyo alikuwa ameingia hapo ndani kwa ajili ya kufanya nini , lakini pia aliweza kumuona Edna akitoka akiwa peke yake na wala hakujisumbua sana na Edna , yeye tageti yake ilikuwa ni Roma laikuwa akitaka kujua kila kitu ambacho Roma atakuwa anafanya kwa siku hio , ili kama akifanya jambo la ajabu amzuie kwani alikuwa akiamini kabisa kuwa Roma hakuwa mtu wa kujali matokeo likija swala la kuua na hio ni moja ya tabia ambazo aliweza kuzisikia alipokuwa kwenya mafunzo ya kichawi nchini China.

Sasa baada ya kusubiri kwa masaa kadhaa hatimae aliweza kuona gari ya Roma ikitoka mpaka ilipochukua ueleweko wa Daraja la kigamboni , alianza kufartilia gari yake kwa nyuma , lakini kitu ambacho hakuweza kukijua Magdalena ni kwamba Roma alikuwa ashamuona tokea anatoka na gari yake na aliishia kutabasamu tu na kujiambia katika nafsi yake , leo hata jeshi lote litake kumzuia kile alichokipanga kwenye moyo kwake ni lazima akitimize kwa namna yoyote ile.

Na aliendesha gari pasipo yakua na wasiwasi wowote hata pale Magdalena alipompita na pikipiki yake , wala hakujali na kuendelea kuendesha taratibu.

“Mr Roma umekuja kufanya nini hapa?”Aliuliza mzee Alex kwa kujikakamua kwani alikuwa na woga ambao ulikuwa umemjaa kweli, licha ya kwamba hakuwa ameshuhudia uwezo wote wa Roma Zaidi ya kuhadithiwa , lakini pia kuona baadhi ya matukio kama lile lililotokea kwenye kusanyiko , lakini bado alianza kuamini maneno ya Abubakari juu ya uwezo wa Roma na ndio maana mzee huyu alikuwa kwenye kiwewe.

“Sidhani kama unapaswa kuuliza wewe mzee ilihali unajua kabisa kosa lako , nipo hapa kwa ajili ya kukuua”Aliongea Roma pasipo kumjali matrida na Magdaleana waliokuwa wakimwangalia , kwa Matrida ndio sasa alikuwa anafahamu mtu aliekuwa mbele yake alikuwa ni Roma ambaye alimsikia kutoka kwa Isaack baada ya baba yake kutamka jina la Roma.

“Roma naomba upunguze hasira , usije ukawaua tafadhari”aliongea Magdalena kwa kuomba huku akiwa na wasiwasi mno.

“Wewe ni nani wa kunizuia kile ambacho nataka kufanya ,mimi Roma Ramoni hakuna mtu wa kunizuia kutoa adhabu kwa mtu yoyote ambaye amenikosea hata awe raisi wa nchi ya Marekani”Aliongea Roma na kumpiga kikumbo Magdalena na kwa spidi ya hali ya juu Mzee Alex alifikiwa na kushikwa shingo yake na kunining`izwa hewani na kufanya hali hapa ibadilike na Matrida kutoa macho ya woga kwa kitendo cha Roma alichokifanya huku akimuona baba yake akitapatapa akikosa pumzi.

“Watu wa aina yenu huwa hamsikii hata kama nikitoa msamhaha , hivyo ili kujipunguzia matatizo na usumbufu bora niwaue tu”Aliongea Roma na kumzidi kumkaba mzee wa watu kiasi kwamba hata Bukta alilokuwa amevaa lilikuwa likionekana huku mkojo ukitiririka kwenye surali yake.

“Naomba usimuue baba yangu tafadhari”

“Niushafanya maamuzi , hakuna wakunizuia”Aliongea Roma na kisha akafungua Dirisha na kumpitisha mzee Alex bila ya kujali udogo wa Dirisha.

Magdaena alishindwa kukosa kuvumilia kwa kitendo hiko na kumsogelea Roma na kumshika shati asifanye anachotaka kufanya , lakini Roma licha ya kuvutwa hakusogea hata kwa kutikisika , yaani Magdaleana na nguvu zake zote za mazoezi hakuweza hata kuzitumia mbele ya Roma , alijua mtu aliekuwa mbele yake ni Hades na kwake ni kama nzi tu.

“Fyuuu…..”Ulikuwa ni kajiupepo tu kalikosikika baada ya Roma kumuachia mzee Alex Dirishani kwenye Ghorofa namba ishirini juu kabisa kuelekea chini ,

Matrida baada ya kuona Roma akirudisha mikono yake ndani pasipo kuwa na mzee Alex alizima palepale, huku Magdalena akikimbilia dirishani kuangalia mwili wa Mzee Alex.

Roma hakujali sana Matrida aliepoteza fahamu , yeye alichokifanya ni kutoka bila ya kuongea neno lolote, kwani kwanza kazi iliokuwa imemleta hapo ndani , alikuwa ashaimaliza na hapo alikuwa akiwaza kwenda kumtafuta Abubakari na Elvice , alijiambia pasipo kusafisha jiji hao watu watamsumbua tu na kumpansiha hasira.

******
 
SEHEMU YA 132B

BAMAKO-MALI 2005

Ni pembezoni mwa jiji la Bamako kilomita kadhaa kutoka mtaa ufahamikao kwa jina la Nikamaero, sasa ndani ya hili eneo kuna jumba moja kubwa ambalo limejengwa katikati ya eneo ambalo limezungukwa na miti mingi ,jumba hili lilikuwa ni tofauti kidogo na majengo yote ambayo yalikuwa yakipatikana ndani ya mtaa huu wa Nikamaero, ni nyumba ambayo imejengwa kawaida sana lakini kwa mtindo wa kisasa, haikuwa ya ghorofa,kwa watu wa Mali waliokuwa wakiishi karibu na huu mtaa walichukulia nyumba hio kama nyumba ya mtu mwenye pesa ambaye ni mwenyeji wa jiji la Mali , lakini ukweli ni kwamba hio nyumba ilikuwa ni ‘Black Site’ ya CIA

Black Site katika ulimwengu wa kijasusi ni maeneo maalumu ambayo humilikiwa na vitengo vya kijasusi duniani kwa ajili ya kufanyia mateso , unaweza kusema ni maeneo ambayo sio halali au kwa maneno marahisi unaweza kusema gereza ambalo sio halali,yaani unakuta kwa mfano CIA wana operesheni ambayo wanaifanya kwa mfano Tanzania na katika Operesheni hio inahusisha kutesa watu ili kupata taarifa sasa maeneo ambayo yanafanyikia hayo mateso huwa ni maalumu yaliotegenezwa yanayofahamika kwa jina la Black Site.

Ni muda wa asubuhi wa mwaka 2005 zinaonekana gari mbili moja ikiwa ni Benz toleo la Zamani na nyingine ilikuwa ni Toyota Landlover,Gari hizi zilionekana zikiingia ndani ya uzio wa nyumba hii na kwenda kusimama mita kadhaa kutoka mlango wa kuingilia kwenye nyumba hii upande wa kushoto na baada ya hzi Gari kusimama , walishuka mabwana wawili moja akiwa ni mwanaume mzungu mtu mzima wa makadirio ya miaka kama Hamsini hivi alievalia tisheti ya Bluu na Jeans pamo jana na viatu vya Ngozi huku akiwa na miwani ya jua kwenye macho yake na mwingine alikuwa ni mzungu hivyo hivyo ila mwanamke aliekuwa ameavalia Tisheti na suruali ya Silk pamoja na kofia cheperu na yeye akiwa na miwani ya jua , hawa walitoka kwenye gari ya mbele yyani Benz , waliokuwa kwenye gari ya nyuma wote walikuwa ni Wa Afrika waliokuwa wamevalia suti nyeusi na wao walitoka haraka na kuwatangulia wale wazungu wawili na kuwaonyesha ishara ya mkono kama waelekee ndani na wakatingisha vichwa vyao na kuanza kupiga hatua kuingia ndani ya jengo hili,

Kwa ndani hakukua na jambo la kushangaza sana kwani kulikuwa na makochi ya mbao yaliokuwepo eneo la sebuleni pamoja na Tv ya Chogo na baadhi ya chupa za Bia zilizokuwa tupu ,Wale waafrika baada ya kuingia ndani ya hili eneo walikata upande wa kushoto na kufungua chumba kingine na jumla yao wote wanne waliingia ndani ya chumba hiko na baada ya kuingia , jamaa mmoja wa kiafrika mnene , alifungua mlango uliokuwa umetegnenezwa kwenye sakafiu na mbao ngumu huku ukiwa na kufuri kubwa pembeni , baada ya kufungua mlango kwa kuvuta juu , alianza kutumbukia kwa kutumia ngazi kwenda chini.

“Sir ndio hawa hapa”Aliongea yule mwafrika aliefungua mlango baada ya wote kuingia ndani ya eneo hili la chini ya Ardhi ambalo halikuwa kubwa sana , ililikuwa ni saizi ya chumba , lakini kulikuwa kumejengewa vizuri na mawe, ni sehemu iliodhihirisha kweli ni eneo la Mateso na la kufungia wafungwa.

Mbele ya hao mabwana walikuwepo watu wawili wakiwa wamefungwa kwenye viti na Kamba na walionekana walipitia mateso kabla ya hao wazungu kufika hapo ndani , kwani wote walikuwa wamechoka sana na ngozi zo zilikuwa zimevilia damu,wote walikuwa ni wazungu pia mmooja akiwa ni mwanamke na mwingine akiwa ni mwanaume

“Ryani!!”Aliita yule mwanamke kwa sauti kubwa kiasi na kumfanya yule mwanaume wa kizungu alieinamisha kichwa kukinyanyua kivivu.

“Camilah!”Aliita Ryani kwa uchomvu sana , alionekana kumfahamu yule mwanamke wa kizungu ambaye sasa tunamjua kwa jina la Camilah.

“Ooh! Nikajua umenisahau Komredi Ryani , baada ya Zaidi ya miaka kumi na nne ya kupoteana”Aliongea huku akimsogelea na kuchuchumaa na kumwangalia mwanaume aliekuwa mbele yake kwa macho ya kumdadisi.

“Camilah , kwanini mnatufanyia haya?”

“Unajua kila kitu Ryani kwanini upo hapa pamoja na mkeo Epholia , mmefanikiwa kujificha kwa Zaidi ya miaka minne na hatimae tumeweza kuwakamata ,lakini licha ya hivyo bado hatujafanikiwa kwa asilimia zote kwani mmoja wenu hayupo hapa na ndio maana nimetoka Marekani mpaka hapa”Aliongea Camilah na Ryani aliekuwa amechoka pamoja na mke wake alienimanisha kichwa chini muda wote waliangaliana na kutingishiana vichwa kwamba wasiongee.

“Camila! Mwambie Powel anachokitaka kutoka kwetu hatokipata Kamwe. Miaka kumi na nne tulioweza kuishi nje ya Radar zake ni mingi sana na tupo tayari kulinda nyakati zote tulizoishi kwa vifo vyetu”Aliongea Ryan kwa namna ya msisitizo na kumfanya Camilah atabasamu na aliwapa ishara wale waafrika, mmoja amsogezee kiti na baada ya kiti kusogezwa aliketi.

“Ryani ujio wangu wa kufika hapa sio kwa jambo baya kama unavyonifikira n ahata hivyo tushawahi kuwa marafiki , nimekuja kuwaweka huru , hamtakiwi kujificha tena , yaliotokea miaka kumi na nne yalishapita”

“Kama kweli maneno yako ni ya kweli tufungulie tuondoke , kama una maswali yoyote ni tangulie kusema kama siwezi kukujibu”Aliongea Ryani na kumfanya Camilah atabasamu na kisha alimgeukia mzungu mwenzake na kumpa ishara na mzungu yule aliibuka na ‘Digital Camera’ na kumpatia na Camira mara baada ya kupewa ile Camera, aliiwasha na kisha moja kwa moja akaenda upande wa kuhifadhi picha na baada ya kufikiap icha alizokuwa akitaka , alimsogezea Ryan.

“Ryani haukuweza kujificha kama ambayvyo ulikuwa ukifikiria , tulikuwa tukikufuatilia kwa miaka yote tokea ulipokimbilia nchini Tanzania”Aliongea huku akimuonesha picha zake yeye na Epholia pamoja na mtoto wao wakiwa katika pozi la kucheka,Ryani hakuamini macho yake na Camilah wala hakujali mshangao wa Ryani , alichokifanya ni kutabasamu na kisha alifungua picha zingine Zaidi na Zote walionekana wao wakiwa na mtoto wao aliekuwa na makadirio ya miaka nane.

“Nadhani hizi picha unazitambua ,Hapa ni Naira alipokuwa na miezi Tisa , lakini ni mara yenu ya mwisho tokea muweze kumuona kabla hajapotea”Aliongea Camilah na kisha akaendelea kwenda mbele na kutafuta picha nyingine na baada ya kuipata alitabasamu na kisha akamsogezea Naira.

“Nadhani kama wazazi mtakuwa mmemkumbuka sana mtoto wengu tokea kupotea kwake, namimi kwakuwa najali hisia za wazazi kwenda kwa mtoto basi sina budi kuwaonyesha mtoto wenu akiwa na miaka kumi na moja”Aliongea Camira na kumzogezea tena Ryani na bwana huyu mara baada ya kuona picha ya mtoto wake wa kike aliefahamika kwa jina la Naira Machozi yalianza kumtoka , ni kweli alimtambua mtu aliekuwa kwenye picha ni mtoto wao ambaye alipotea alipokuwa na miaka tisa pekee ,Camila hakuishia kumuonyesha Ryani tu alimsogeleza na Epholia mke wa Ryani kumwangalia Naira , aliekuwa amevalia mavazi ya kitabibu akiwa ana tabasamu , alikuwa ni mwanamke mrembo haswa kwenye picha hio na Epholia ule unyonge aliokuwa nao ulimpotea ghafla.

“Where is our Daughter Camila”Aliongea Ryani kwa sauti kubwa awamu hii , lakni kwa Camilah aliishia kutabasamu

“Unaonekana upo tayari kutupa ushirikiano Ryan”Aliongea Camilah na umgeukia yule mzungu wa kiume na wote wakatabasamu.

“Camilah Naira wetu yupo wapi , tumemtafuta kwa Zaidi ya miaka mitano bila mafanikio , kumbe mmemchukua kwetu , Mungu awalaani”

“Hahahaha….,Ryani unaonekana asilimia tisini kuathiriwa na tamaduni za Kitanzania baada ya kuishi kule miaka mingi , nani wa kulaaniwa kati yetu na wewe uliempoteza mtoto wako”Aliongea Camilah na Ryani alimeza fumba la Mate , bwana huyu alikuwa na hasira mno , lakini pia alikuwa akitaka kumuona mtoto wake ambaye walimpoteza kwa Zaidi ya miaka Minne wakiwa nchini Tanzania , haikueleweka ilikuwaje mpaka wakampoteza na pia haikueleweka waliwezaje kufika nchini Tanzania.

“Camillah niambie unataka nini kutoka kwetu , ili tuweze kumpata tena Naira?”Aliuliza Ryani , alionekana yupo tayari kufanya jambo lolote kwa ajili ya kumpata mtoto wake Naira yeye na mke wake.

“Unatakiwa kurudi kazini Ryan na utashirikiana na sisi kutupatia taarifa zote za utoto wa Naira mpaka alipofikisha umri wa miaka Tisa”Ryani alijikuta akifikiriaa kidogo na kisha akamgeukia mke wake ambaye hakuwa na nguvu kabisa ya kuongea na wakatingishiana vichwa kukubaliana huku wote wakitokwa na machzi.

“Camillah tupo tayari”Aliongea Ryan na Camillah akatabasamu.

Hii ilitokea mwaka 2005 huko Mali Bamako , ilikuwaje wakafika nchini Mali na kufngiwa katika chumba cha Ardhi na waliishi vipi na Naira Tanzania?



SEHEMU YA 133

Ilikuwa ni baada ya Roma kumwachia mzee Alex , Upande wa nje wa jengo hili la JR alionekana Scorpion ambaye alikuwa amembeba Mzee Alex kama vile amebeba mtoto , huku mzee Alex akiwa amezirai na hakuonesha kuwa na aina yoyote yale ya majeraha kwenye mwili wake.

Baada ya Scorpion kumuingiza mzee Alex kwenye gari aina ya Toyota Corolla alitoweka eneo la tukio huku watu wakiendelea kushangazwa na tukio hilo lililotokea dakika chache nyuma.

Mage aliekuwa ndani ya ofisi alikuwa kwenye mshangao pia kwa namna tukio lilivyokuwa , haikuelewa ilikuwaje, kwani hata yeye wakati alipokimbilia dirisha na kuangalia chini aliona mzee Alex akiwa kwenye mikono ya mwanamke ambaye amevalia suti, wakati mrembo huyu anaendelea kushangaa simu yake ndogo iliokuwa kwenye suruali , ilianza kuita na akaitoa na kisha akapokea.

“Ndio Afande Ajenti flamingo hapa”

“Ajenti Flamingo nini kinaendelea?”

“Afande Hades alimrusha Mzee Alex kwenye Ghorofa”

“Unamaanisha nini Ajenti Flamingo”

“Nilishindwa kumuwahi kumuondoa Mzee Alex kabla ya Hades kufika na alimrushia chini ya ghorofa na bahati nzuri inaonekana kasalimiaka”

“Unamaanisha nini kasalimika wakati karushwa juu ya Ghorofa?”

“Kuna mwanamke ambaye inaonekana alikuwa chini na kamdaka na kuondoka nae”

“Kuna mwanamke kamdaka!! , ni nani huyo mwanamke?”

“Nimeshindwa kumfahamu afande nilikuwa juu kabisa ya ghorofa”Aliongea Magdalena lakini upande wa pili ulionekana kutokuelewa na walihitaji maelezo ya kutosha.

“Okey Ajenti ,Clear the Area na urudi makao makuu , nahitaji taarifa Zaidi”

“Sawa Afande”Alikata somu na Magdalena alimgeukia Matrida ambaye alikuwa bado amezirai chini ya Meza na kumuwekea mkono na aliona bado anapumua , lakini wakati huo huo aliingia Isaack.

“Tafuta msaada mumpeleke hospitali , kapata mshituko”Aliongea Magdalena na kutoka ndani ya ofisi hio , huku akimuacha Isaack kwenye mshangao na kumkimbilia Matrida alielala chini akiwa hajitambui.

Ukweli Roma aliguswa na namna ambavyo Matrida alikuwa akiomba baba yake asimuue na pia Roma aliona sio jambo zuri kumuua Mzee Alex mbele ya mtoto wake, lakini licha ya kuguswa hakutaka kumuaccha Mzee Alex pasipo kumpa onyo ambalo kamwe hawezi kulisahau na ndio maana akamuachia baada ya kuhisi uwepo wa mtu mwenye uwezo mkubwa wa nguvu za kichawi akiwa upande wa chini na kwa hisia zake tu aliamini mtu huyo atakuwa Scorpion kutokana na alivyokuwa akijua aina za mapigano na nguvu ambazo zinamilikuwa na ninja wote wa kundi la Yamaguchi.

Kwahio kumuachia mzee Alex alikuwa na uhakika kwamba Scorpion atafanya jambo kumuokoa Mzee Alex lakini wakati huo huo aliona pia ni jambo jema pia kumpa onyo Mzee Alex kwa kupata uzoefu wa kudondoka kutoka gorofa ya ishirin,na aliamini kwa tukio hil mzee huyu hatokuja kulisahau katika maisha yake.

Roma aliendesha gari yake kuelelekea kazini , huku akijiambia, muda na saa atakapomkamata Abubakari Hamadi ndio itakuwa siku yake ya mwisho wa kuliona jua , Roma hakutaka kuwatumia The Eagles kujua ni uelekeo gani ambao Abubakari yupo na pia alihisi kuenda Afande Maeda kwa kumtumia Ajenti Flamingo watakuwa washachukua tahadhari mapema na ndio maana akaamua kupotezea kwa muda , lakini huku upande mwingine Sababu ya kumuua Abubakari zikiwa nyingi , kwani aliamini kwa taarifa iliosambaa siku hio mtandaoni lazima atakuwa pia na yeye amehusika kwa asilimia mia moja.

Roma alikuwa na mpango wa kwenda kuona hali inavyoendelea kwenye kampuni na pia kuhakiki kama mke wake ameweza kutatua tatizo ambalo lilikuwa linaendelea kwenye kampuni.

Wakati Roma anaegesha gari yake eneo la maegesho ya wafanyakazi wa kampuni alikutana na Nadia ambaye na yeye alionekana ndio alikuwa akiingia kazini, Roma alitabasamu baada ya kumuona Nadia na haikueleweka mara moja alikuwa akiwaza nini kwenye kichwa chake mara baada ya kumuona mrembo huyu na Kwa Nadia hivyo hivyo alitabasamu kwa kumuona Roma eneo hili.

“Hades!!”Aliita Nadia baada ya kumsogelea Nadia.

“Tupo kwenye kampuni niite Roma”Aliongea Roma na kumfanya Nadia atabasamu.

“Napenda uhalisia wako unaotokana na jina la Hades”Aliongea Nadia.

“Kama unapenda uhalisia wangu wa jina hilo , basi unaishi kizamani kwani jina hilo nishaliacha kwa sasa”

“Sio kweli”

“Kwa vigezo gani Nadia”

“Roma ni jina lako la kawaida , utambulisho ambao unataka watu wakuone mtu wa kawaida lakini kwa ninavyokuangalia hauwezi kuwa wa kawaida hata kidogo na mwisho wa siku utaishia kutumia utambulisho wako wa Hades”Roma alitabasamu kidogo.

“Unaonekana unajua kile kinachoendelea kwenye kampuni Nadia Alfonso”Aliongea Roma na kumfanya Nadia atabasamu.

“Usisahau kwamba licha ya wewe kunisaidia kupata ushahidi Nchini Korea Kusini na kuua maadui 34 waliotaka kumfunga Kim , akili yangu ndio iliotumika kwa asilimia mia kuufanya ushahidi uwe na nguvu mbele ya ‘Court’ na Kim kupata haki yake”

“Sikatai hilo Nadia, ila swali langu kwanini ukaja kufanya kazi ndani ya kampuni ya mke wangu,maana kutokana na ukubwa wako ni jambo pia la kufikirisha uwepo wako ndani ya Vexto?”Aliuliza Roma bila ya kupepesa macho na kumfanya Nadia akose utulivu.

“Hades nadhani ushajua sababu kwanini nipo ndani ya kampuni ya mkeo, yote ni kutaka kuwa karibu yako”

Aliongea Nadia bila aibu huku akimsogelea Roma, lakini kwa upande wa Roma alishindwa kujua acheke au alie, maana hakuwaelewa hawa wanawake kwa wakati mmoja.

“Unauhakika upo kwa ajili yangu?”Aliongea Roma na kumfanya Nadia asitishe kile alichokuwa akitaka kufanya.

“Unahisi kwanini nipo hapa?”

“Nadia nakuona kama mwanamke mwenye wivu na ndio maana nina wasiwasi na ukaribu wako kwa mke wangu , natumaini hautanifanya nikasirike mbeleni”Aliongea Roma na kisha akapiga hatua kuelekea upande wa kuingilia ndani ya jengo hili na kumfanya Nadia aliesimama ajiulize kwanini Roma kamuambia yale maneno , mwanadada huyu alianza kujishuku na kujihisi huenda mipango yake imegundulika.

“Hapana huenda ni hisia zake tu , hawezi kugundua kuwa nina mpango wa kuwafanya waachane , muda wote nimekuwa makini kwa kila hatua ninayopiga”Aliongea Nadia huku akiogopa maneno ya Roma kwa wakati mmoja , mrembo huyu licha ya kwamba alikuwa akimpenda Roma lakini alikuwa akijua upande wa pili wa Roma , kwani aliweza kuwacharanga mapanga Zaidi ya wanasiasa 34 wa Korea kusini pasipo huruma kwa ajili tu ya kupata ushahidi juu ya kesi iliokuwa ikimwandama Raisi Kim.

Roma alienda moja kwa moja mpaka ilipokuwa ofisi yake ya PR , alitaka kujua ni nini kinaendelea, kwani tokea atoke asubuhi hakupata kufatilia , baada ya kuingia ndani ya ofisi hii aliona wafanyakazi wenzake wakiwa kwenye hali ya kawaida na kwa jinsi alivyowaona tu , alijua lazima kila kitu kipo sawa na hali ya kampuni imerudi katika ukawaida wake.

Lakini licha ya kuaangalia wafanyakazi wenzake kwa macho ya kuwadadisi na wao walikuwa wakimwangalia Roma kwa macho ya mshangao ni kama walikuwa wakijiuliza huyu mwanaume alikuwa wapi muda wote huo wao wakiwa na presha juu ya jambo ambalo limetokea juu ya kampuni na Roma hakujali macho ya mshangao ya warembo hao Zaidi ya kutabasamu na kumpungia mkono kila mmoja.

“Boss ndio unafika kazini kwa raha zako”Aliongea Recho kuvunja ukimya wa mshangao wa wenzake.

“Recho acha maneno yako nilikuwa mgonjwa”Aliongea Roma huku akitabasamu.

“Nani wa kukuamini , hata hivyo huna mchango wowote ,na tulishakusahau”

“Kwahio mrembo unamaanisha haujanimisi na hautaki kuniona?”

“Nani!! mimi , kwanini nikukumbuke mwanaume suruali kama wewe , labda Nasra asie na pakwenda”Aliongea Recho na kumfanya Roma amkumbuke Nasra ni muda mrefu kidogo hakuwa amemuona mrembo Nasra.

“Nasra anaingiaje tena??”

“Unajifanya hujui , Mtoto wa watu kila saa anakuja kuchungulia kama umefika kazini , leo kaja kama mara tatu”Aliongea Recho na kumfanya Roma kushangaa , lakini pia hata yeye kujiona mkosaji , ni kweli alikuwa kwenye mahusiano na Nasra lakini hakukumbuka hata kumpigia simu , Roma alifikiria kidogo na kisha akanyanyuka na kumfanya Recho abetue midomo na kusonya , alijua Roma anaenda ofisini kwa Nasra .

Lakini sasa wakati Roma anaingia kwenye lift simu yake ilianza kuita mfululizo na kumfanya aitoe na kuangalia nani anaempigia na aligundua ni Sophia aliekuwa akipiga , alipokea na kuweka sikioni.

“Kuna mgeni wako”Aliongea Sophie moja kwa moja mara baada ya Roma kupokea na Roma alijikuta akitabasamu kwani alihisi ukisirani kutoka kwa Sophie

“Sophia ni nani huyo mgeni?”

“Simfahamu , ila ni bora ukarudi mapema kabla ya Sister Edna hajarudi”Aliongea Sophia na kisha akakata simu na kumfanya Roma afikirie kidogo na aliona ngoja aghairishe kwenda kuonana na Nasra na arudi nyumbani , alitaka kujua ni mgeni gani huyo ambaye anamfahamu yeye mpaka kwenda nyumbani kwake.



SEHEMU YA 134

Ni ndani ya ofisi ya ikulu ya taifa la Kenya anaonekana mheshimiwa Kamau Kamau akiwa ndani ya ofisi akiendelea na majukumu yake , huku mbele yake akiwa amesimama katibu muhtasi wake , Mheshimiwa huyu alioneskana kuna karatasi ambazo alikuwa akisaini kwani alipitia kila ukurasa na kisha kutia saini yake , kitendo ambacho kilidumu kwa takribani dakika kama kumi hivi mpaka kumaliza na kisha akamkabidhi katibu muhtasi wake hilo faili na akaondoka, lakini wakati huo huo wakati Katibu Muhtasi akitoka aliingiia Deo akiwa na faili mkononi.

“Mheshimiwa nimepata taarifa zote zinazomuhusu Roma”Aliongea Deo kwa heshima na kisha akamsogezea mheshimiwa faili na mzee huyu aliangalia faili hilo kwa madakika kadhaa kwa kulisoma na kisha akaweka chini , huku akionyesha hali ya mshangao kidogo.

“Hii Taarifa ni ya kweli Deo?”

“Ndio mheshimiwa , nido nilvyoweza kupata kwenye Data Base ya Taifa ,licha ya kuonyesha kusomea ndani ya chuo cha Harvard lakini hakuna taarifa nyingine”Aliongea Deo.

“Vipi kuhusu familia yake?”

“Mheshimiwa nadhani haujaangalia vizuri faili nimeambatanisha mwisho”Aliongea Deo kwa heshima na Mheshimiwa Kamau alichukua tena faili na kufungua ukurasa wa mwisho.

“Huyu Roma….!!”

“Ndio mheshimiwa anaonekana kulelewa ndani ya familia ya Tajiri Robert Eglon kutoka Michigani”Aliongea Deo na Mheshimiwa Kamau alirudisha chini lile faili na kuvuta pumzi kidogo.

“Unaweza kwenda kuendelea na majukumu yako Deo”Aliongea Mheshimiwa Kamau na Deo aliinama kwa heshima na kisha akageuka na kutoka ndani ya ofisi ya mheshimiwa Kamau.

“Kama ni kweli aliwezaje kuwadhibiti walinzi wote kwa wakati mmoja, maelezo ya walinzi hayaendani kabisa na wasifu huu”Aliwaza mheshimiwa kidogo na kisha akachukua simu yake kati ya nne zilzokuwa mezani aina ya Sumsung na kisha akapiga.

“Ndio Mheshimiwa Kamau Kamau”Ilisikika sauti nzito kutoka upande wa pili.

“Nataka ufatilie jina la Roma Ramoni , amelelewa ndani ya familia ya tajiri Roert Eblon Marekani , nahitaji utafutaji uwe wa haraka “Aliongea kwa Lugha ya kingengeza na kisha akakata simu.

******

Upande mwingine ndani ya Rwanda siku hii hii ya Ijumaa muda wa saa tisa mchana , alionekana Tajiri Mohamed Azizi akiingia ndani ya ofisi ya ikulu ya mheshimiwa Jeremy , baada ya tajiri huyu kuingia huku leo hii akiwa amepigilia suti yake ya rangi ya majivu , walisalimiana na mheshimiwa Jeremy kwa bashasha sana na kisha wote wakaketi.

“Niambie Jeremy , nimeshangazwa na wito wako , kuna jipya gani umegundua?”Aliuliza Tajiri Mohamedi Azizi huku akimwangalia Rafiki yake Jeremy.

“Azizi najua ulikuwa nchini Hispania na huna taarifa zote ya kile kinachoendelea nchini Tanzania?”

“Ni kweli kabisa Jeremy Project ya kibiashara ilionipeleka Madrid imechukua muda wangu mwingi , lakini namshukuru Mwenyezi kwa kuniwezesha,Vipi unaonekana kuwa na jambo ambalo unataka kuniambia Jeremy liweke wazi , ili nikirejea Tanzania nisiwe na maswali mengi”

“Blandina karudi Tanzania na kaonana na Mzee Atanasi”Aliongea Jeremy na kumfanya Tajiri kushangaa.

“Sina kabisa hio taarifa,Jeremy na sijui kwanini Jestina hajaniambia?”

“Nadhani yatakuwa ni maelekezo ya Baba yake , ila ndio hivyo washaonana na wanajua sasa hivi Maina ndio Blandina”

“Nini kiliendelea?”Aliongea Azizi huku akionyesha kidogo mkunjo wa sura , alikuwa na hasira kwanini swala kubwa hivyo la kifamilia hakuwa na taarifa nalo , kwani kila siku alikuwa akiwasiliana na mke wake.

“Inaonekana kabla ya Mzee Atanasi kwenda kuonana na Blandina washaongea na DS ya Tanzania na Kenya na walishafikia kwenye maamuzi”Aliongea Raisi Jeremy na kumfanya Azizi kuvuta pumzi.

“Jeremy nadhani hii sio jambo pekee ambalo umeniitia?”Aliongea Jeremy.

“Ni kweli Azizi nadhani mpaka sasa unafahamu fika kwamba Taifa la Kenya ndio pekee ambalo halikubaliani na mpango TASAC na mheshimiwa kutoka Urusi amekuwa wakunilazimisha niharakishe sana hilo swala”

“Ndio naelewa kabisa, lakini naona ni kama wanakupa presha bure kwani mpaka sasa hakuna jambo kubwa ambalo wamelifanya kwa upande wao”

“Ni kweli , lakini mwezi uliopita walinitumia ushahidi ambao umenifanya nione, ukweli unakaribia kutoka”Aliongea na kumfanya Azizi kushangaa.

“Unamaanisha nini?”Aliuliza na Mheshimiwa Jeremy aliinuka na kuvuta bahasha kwenye meza yake na kisha akatoa picha pili na kumpatia Tajiri Azizi na alianza kuziangalia.

“Hizi ni…”

“Hio picha ya kwanza ya mtoto imepigwa mwaka 1998 m nadhani unaona kabisa hapo chini kuna tarehe na hio ya pili vile vile imepigwa mwaka 2007”

“Unamaaisha hawa watu wote ni mtu mmoja na kwanini kama naona sura ya Hades?”.

“Ndio hio sura ni ya Roma Ramoni ambaye sisi na watu wachache wanamfahamu kama Hades na hizo picha zimetumwa na shirika la kijasusi la Urusi(FSB) kwa maelekezo kutoka Kremlin”Aliongea mheshimiwa Jeremy na kumfanya Tajiri Azizi kushangaa.

“Jeremy unamaanisha….”

“Ndio huu ni ushahidi pekee ambao unathibitisha kupotea kwa ndege ya shirika la M Arline ni tukio la kupangwa”Aliongea na kumfanya Tajiri Azizi aone pointi hio ina mashiko ndani yake.

“Sasa nini kinafuatia baada ya huu ushahidi?”

“Ndio maana nimekuita tuonane , nataka hizi picha ukaonane na Mzee Kweka”Aliongea na kumfanya tajiri Azizi kushangaa.

“Jeremy unamaanisha unataka kumpatia hizi picha baba yake Mheshimiwa Senga! ,kwanini?”Aliuliza tajiri na kumfanya Mheshimiwa Jeremy akunje nne kwanza.

“Ni Rahisi sana Azizi , Senga kwa sasa hawezi kuhimili ukweli wote , ila kwa Mzee Kweka ni rahisi kuhimili lakini pia hili swala nataka niliingize kwenye DS ya Tanzania”Aliongea Mheshimiwa Jeremy na kumfanya Tajiri Azizi kuvuta pumzi.

“Lakini mpaka sasa sijaelewa malengo ni nini , maana sidhani DS wataguswa sana na swala hili”Jeremy alitabasamu.

“Azizi kuna mambo ambayo bado sijakuambia , unajua licha ya kwamba wewe ni rafiki yangu lakini pia nina ukomo wa kukuambia mambo ya kiserikali”

“Ndio naelewa Jeremy na sijawahi kulalamika juu ya hilo , mbona unajihami”Huku akitabasamu.

“Niambie Azizi kwa mfano DS ya Tanzania wakipatiwa faili halisi , nazungumzia lile lenyewe linalohusiana na Roma unafikiri watachukua uamuzi gani?” Tajiri Aziiz alionekana kuwaza.

“Sikia Azizi usifikirie sana , hebu mchukulie Hades kiiashara utaelewa pointi yangu”

“Hahaha,,, DS watataka kumfanya Hades mtu wao”

“Hio ndio point yangu Azizi, lakini kabla ya kuwapa faili lote linalomuhusu Roma , nataka kwanza wapate kumjua Roma ni nani, kazaliwa wapi na baba yake halisi ni nani , hii itawapa nguvu kuingia kwenye mpango ninaotaka mimi, ni kama nawaongezea Motisha, na nikwambie tu mpaka sasa hivi Jeshi la Tanzania limeonyesha nia ya kumtaka Hades kuwafundisha wanajeshi mbinu zake za kivita zinazomilikuwa na kundi la The Eagles”Aliongea na kumfanya Azizi ashangae kidogo kwani hakuwa na uelewa wa hilo jambo.

“Vipi kuhusu Blandina , nadhani inapaswa ajue kama mtoto wake bado yupo hai”

“Hilo analifanyia kazi Linda , tunachotaka kwa sasa hivi ni kuhakikisha kwamba Roma aliesafiri kwa shirika la Ndege la M Airline ndio Denis, tukiwa na mashuhuda ya watu wengi ni Rahisi kuweka ukweli wazi pasipo ya Marekani kupinga na wataweka wazi nyaraka zinazohusiana na mpango LADO wenyewe”

“Ni kweli kabisa , Lakini Jeremy ushatambua sasa Roma ndio Denisi na walipanda ndege moja na Lorraine kwanini usingeanza kufatilia kwanza habari za Lorraine na kujua kama yupo hai au hayupo hai”

“Ninatamani sana kujua Azizi , lakini kutokana na kwamaba huu ni mpango mkubwa siruhusiwi kuingiza hisia katika kufanya maamuzi , nitafanya kila jambo kwa hatua na uhakika , japo mpaka sasa hivi najikuta kuwa ni mwenye hisia mbaya juu ya Lorraine”Tajiri Azizi alionekana kumuelewa sana rafiki yake, baada ya maongezi yalidumu takribani lisaa limoja kuisha Azizi aliaga huku akimwambia Jeremy anawahi msiba wa kitafia wa mwanasayansi nguli duniani aliekufa kicho cha kutatanisha







SEHEMU YA 135

Roma aliendesha gari yake kuelekea nyumbani , bwana huyu alikuwa na hamu ya kutaka kujua ni mgeni gani ambaye amekuja moja kwa moja nyumbani kwake , kwani Roma alikuwa sio mtu wa kufahamika sana na hivyo kuwa na mzunguko wa watu wachache sana , lakini pia ni watu wachache sana ambao wanafahamu sehemu ambayo alikuwa akiishi.

Roma baada ya kufunguliwa geti na Derick aliingiza gari yake na kwenda kuegesha sehemu maalumu huku akiangalia ongezeko la magari , lakini hakukuwa na gari yoyote iliokuwa imeongezeka na kujiuliza huyo mgeni kaja bila usafiri nini.

Alishuka na kupiga hatua kuelekea ndani na ile anaingia ndani alijikuta akisikia vicheko vilivyokuwa vikitoka sebuleni.

Upande wa eneo la Sebuleni walionekana watu watatu wote wakiwa ni wanawake lakini mtu alieongezeka leo hii hakuwa wa kawaida kutokana na urembo wake , lakini pia pamoja na rangi yake , huyu hakuwa mwingine bali alikuw ani Profesa Clark Stephanie mtoto wa Malkia wa Wales , mwanamke mrembo na maarufu sana ndani ya bala la ulaya na duniani kote kutokana na uzuri wake , lakini pia mafanikio yake ya kielimu aliofikia katika umri mdogo.

“Profesa Clark ndio aliekuwa wa kwanza kumuona Roma akiingia kutokana na sehemu aliokuwa amekaa kuwa rahisi kuona mlangoni na ile anamuona tu Roma alinyanyuka na kumkimbilia na kwenda kumkumbatia na kuwafanya Sophie na Bi Wema kushangaa.

“Karibu Nyumbani”Aliongea Profesa Clark kwa lugha ya Kiswahili na kumfanya Roma atamani kucheka na rafudhi ya Profesa Clark, alijiuliza huyu mrembo wa kizungu amejifunzia wapi kuzunguma Kiswahili.

“Clark umewezaje kugundua mahali ninapoishi?”

“Ushasahau mimi ni nani Roma?”Aliongea Clark na kuona kweli kauliza swali la kijinga maana ktuokana na uwezo wa Profesa Clark ni jambo rahisi sana kujua taarifa za mtu.

Sophie aliekuwa akimwangalia Roma na Profesa Clark wanavyoongea , alijikuka akiwa ni mwenye wivu sana, ukweli kama mwanamke kuna kitu ambacho alikiona kwenye macho ya Profesa Clark , mwanadada huyu aliona mapenzi ya waziwazi ya Profesa Clark kwenda kwa Roma.

“Pole kwa kumpoteza Senior na mwalimu wako Clark”Aliongea Roma kwa Kingereza na kumfanya Clark ageuke na kuelekea upande wa masofa na Roma alifatia huku akimsalimia na Bi Wema.

“Roma sisi tutaenda kuandaa chakula , unaweza ukaongea na mgeni wako”Aliongea Bi Wema huku akimpa ishara Sophia anyanyuke na Sophia alijikuta akimwangalia Roma halafu akajinunisha na kunyanyuka.

“Tanzania ni nzuri sana Roma , nadhani najua ni kwasababu gani umechagua kurudi kwenye nchi yako”

“Tanzania inaonekana kuwa nzuri, ila mimi tokea nifike ndani ya hili taifa najua baadhi ya sehemu tu , hivyo siwezi kuzungumza sana juu ya kuisifia”Aliongea Roma na kumfanya Clark atabasamu , huku akimwangalia Roma kama daktari anaemchunguza Mgonjwa na alionekana kuridhika.

“Kifo cha Profesa umekipokeaje Clark?”

“Nimekipokea kwa mshangao , lakini naweza kusema ni kama nilitegemea”

“Kwanini uansema ni kama umetegemea?”

“Unajua Roma Profesa alikuwa akiandamwa sana na watu wengi kutokana na gunduzi aliokuwa nayo,wakiwemo marajiri, wanasiasa na wanasayansi”

“Kuna tetesi nilizosikiaga kipindi juu ya mambo ya Ant-Matter Energy , unataka kuniambia ni kweli zile tetesi?”

“Ni kweli kabisa na hilo aliniambia Profesa mwenyewe baada ya kunikabidhi baadhi ya Formula nijaribu kuzifanyia kazi na niseme ukweli baada ya mwezi mmoja wa utafiti wangu nimeona kununi zake kihesabu zinafiti kwa asilimia kubwa sana , licha ya kwamba utekelezaji wake kwa hapa Duniani ni mdogo mno”Aliongea Profesa huku akionyesha hali ya huzuni.

“Unamaanisha nini ni mdogo?”

“Moja ya hitaji kubwa kwa kanuni zake kufanya kazi ni Madini yenye haiba ambayo kwa hapa Duniani hayapatikani na kwa maelezo ya Profesa, Marekani ndio taifa pekee ambalo wanamiliki jiwe la madini hayo”

“Unamaanisha madini yanayotoka kwenye GodStone?”Aliongea Roma na kumfanya Clark ashangae , alijiuliza inakuwaje Roma akajua hio habari.

“Unaonekana kufahamu uwepo wa madini hayo Roma?” Aliongea na kumfanya Roma atabasamu.

“Yeah! Nimesikia baadhi ya habari juu ya jiwe la Godstone, lakini Clark ukiachana na maswala ya Godstone unamfahamu vipi Yan Buwen?”Roma aliona achomekee swali la Yan buwen kwa muda huo , kwani kutokana na kwamba Yan Buwen alikuwa moja ya wanafunzi ambao wapo chini ya Profesa Clark , basi ni lazima agekuwa anamjua Zaidi kuliko watu wengine , haswa likija swala linalohusiana na taaruma yake,Clark alionekana kushangaa , lakini pia kusikitika kwa wakati mmoja.

“Yan Buwen naweza kusema kati ya wanafunzi wangu ambao nimefundisha yeye ndio wa kipekee sana, uwezo wake wa kuchanganua mambo ulikuwa mkubwa mno na alielewa kila nilichokuwa namfundisha na Zaidi”Aliongea Profesa Clark kwa huzuni na Roma aligundua hilo.

“Lakini mbona unaongea kama hujivunii kuwa na mwanafuzni kama Yan Buwen , kuna shida iliotokea kati yenu?”

“Yeah!,Baada ya Yan Buwen kumaliza masomo yake ya ngazi ya juu hakutaka tena kunitambua kama mwalimu wake na hakunisikiliza kwa lolote , yaani upole wake na unyenyekevu ulikuwa ni kipindi akihitaji nimsimamie katika PhD yake , lakini baada ya kuhitimu alidiriki kuniambie yeye ana akili Zaidi kuliko mimi , ili niumiza”Aliongea Profesa na kufanya Roma kweli aone kama ni hivyo Yan Buwen anao uwezo asilimia zote za kumuua Profesa Shelukindo.

“Roma umemfahamu vipi Yan Buwen?”

“Yupo hapa Tanzania na ninao vijana wangu wa kijeshi walikuwa wakimfatilia kwa kila hatua ili kubaini ni jambo gani ambalo limemleta Tanzania , lakini kutokana na watu aliokutana nao tunakisia kwa asilimia kubwa ndio kahusika na mauaji ya Profesa Shelukindo “Aliongea na kumfanya Clark kushangaa mno.

“Clark unahisi ni kwanini Yan Buwen kamuua Profesa?”Aliuliza Roma huku akimwangalia Clark ambaye bado alikuwa kwenye mashangao.

“May Be ni kwasababu ya kanuni ya Ant- Matter Energy”

“Kwanini unahisi hivyo?”

“Nakumbuka mara ya mwisho nilivyowasiliana na Profesa Shelukindo ,nilimgusia kuhusu Yan Buwen na alichonijibu sikukitilia maanani nilidhani hisia za Profesa zilikuwa ni kama zangu tu”

“Alikujibu nini?”

“Alisema kwenye moja ya makosa aliofanya basi ni kuwa mwanafunzi wa Yan Buwen”Aliongea Clark na kumfanya Roma achakate kwanza hayo maneno kwenye akili yake ili kuyapatia maana.

“Lakini Clark Profesa si aliacha kujihusisha na maswala ya kiutafiti baada ya kurudi Tanzania?”Swali lilimfanya Clark akili yake sasa kufanya kazi.

“Hapana ,Mara ya mwisho wakati nawasiliana na Profesa Shelukindo kwa njia ya Vidio alikuwa kwenye maabara”

“Maabara!! Unamaanisha alikuwa anaendelea na utafiti wake?”Aliuliza Roma na Clark alitingisha kichwa kukubali na mpaka hapo Roma aliona kabisa basi huenda Yan Buwen yupo Tanzania kwa ajili ya kukusanya Tafiti za Profesa Shelukindo na kama ni hivyo basi huenda mpaka sasa Yan Buwen huenda amepata kile alichokuwa akikihitaji lakini licha ya hivyo aliamini bado yuko mbali na mafanikio kwani kama ni kweli yupo kwa ajili nya kanuni ya kutengeneza Ant-Matter Energy hawezi kufanikiwa mpaka awe na Godstone.

“Clark uliweza kufahamu sehemu ambayo alikuwa akifanyia utafiti wake?”

“No Hakuniambia na pia sikumuuliza”Alijiu na kumfanya Roma afikirie kidogo na kuona hili ni swala ambalo linatakiwa kufanywa na wanajeshi wake na alifanya mawasiliano muda huo huo na kuwapa kazi hio The Eagles kufuatilia.

Chakula cha mchana kiliwekwa mezani na Bi wema alimkaribisha Clark na Roma Mezani , Clark alionekana kuzoeana na Bi wema huku akitumia Kiswahili chake cha kuunga uunga na haikueleweka alijifunza lini na hata Roma alishangazwa na hilo, baada ya chakula kuisha Roma na Clark walitoka nje na kukaa sehemu ya Bustani na kuendelea na Stori zao za kukumbushia baadhi ya mambo waliokuwa wamefanya na kwa jinsi wawili hawa walivyoonekana ni Dhahiri kabisa walifahamiana tokea wakiwa watoto , kwani walikuwa na Stori nyingi ambazo zote zilihusisha kipindi wakiwa watoto.

Saa kumi na mbili za jioni hivi wakati Roma wakiwa bado wapo nje , mara simu ya Roma ilitoa mlio na haraka haraka aliitoa na kuangalia ni nani aliekuwa akimpigia na aliona jina ni la Chiara na aliweka sikioni haraka haaka maana Chiara hakuwa mtu wa kupiga labda kama kuna tatizo ambalo limemtokea mke wake.

“Your Majesty……”
 
SEHEMU YA 136

“Niambie kuna nini Chiara”Aliliuliza Roma kwa sauti ya Amri.

“Mfalme Madam amepoteza fahamu anachukuliwa kwenda hospitalini sasa hivi na gari ya wagongwa, tupo nyuma tunafuatilia”Aliongea Chiara na kumfanya Roma kushangaa na kusimama kwa wakati mmoja na kumfanya hata Clark ambaye amemzoea Roma, hakuwahi kumuona kwenye wasiwasi namna hio.

“Nakuja sasa hivi endelea kufuatilia ni hospitali gani anapelekwa”Aliongea Roma , hakukata kuuliza maswali mengi kwa wakaati huo , aliamini atapata majibu yote akiwa hospitalini.

“Roma kuna nini?”

“Clark mke wangu anaonekana kupatwa na tatizo la kiafya na kwasasa anapelekwa hospitalini , napaswa kwenda kujua shida ni nini”Aliongea Roma na kuingia ndani kwa ajili ya kumpa taarifa Bi Wema na Baada ya kumwambia bibi huyo na yeye alishikwa na huzuni.

“Bi Wema mtabaki hapa nitawapa taarifa kile kinachoendelea”Aliongea Roma

“Ninaenda”Aliongea Sophia na Roma alimwangalia kwa dakika na kisha akampa ishara amfuate na ile anatoka nje pia Clark aliwafuatisha nyuma.

“Nitaenda pia”

“Clark unapaswa kupumzika…”

“I am Doctor”Aliongea Clark na kusogelea upande wa kushoto wa gari na kuingia , Sophia akakaa mbele na Roma , Clark nyuma na gari ikatolewa kwa spidi , Roma alikuwa na wasiwasi ni nini kimemkuta mke wake , ila alijiambia atajua akishafika hospitalini.

*****

Chiara ambao walikuwa na jukumu la kuhakikisha Edna anakuwa salama walikuwa nyuma kwa nyuma kumfuatilia Edna tokea anatoka ndani ya Benki ya Swiss mpaka anaingia ndani ya hoteli Paradise na baada ya kuona Edna kachukua kadi eneo la mapokezi na wao wakaingia ndani ya hoteli hii na kuchukua chumba mkabala na chumba ambacho alikuwa ameingia Edna , wao kuhusu pesa haikuwa tatizo kwanni Gharama zote za ulinzi kwa Edna zilikuwa zikilipwa na Hades kupitia kundi la The Eagles , hivyo kuchukua chumba cha ‘Presidential Suite’ haikuwa tatizo kwao lakini pia walikuwa na Baraka zote kutoka kwa Diego.

Baada tu ya kuchcukua chumba hiko ambacho milango yao ilikuwa ikiangalia kulia na kushoto walitega kamera ndogo sana sehemu ya kuwekea Kadi na madhumuni yao wlaitaka kuangalia kila anaeingia na anaetoka ndani ya chumba cha Edna ili kuhakikisha anakuwa salama.

Sasa mabwana hawa walikaa kwa Zaidi ya masaa saba tokea Edna aingine ndani ya chumba hiko na hakukuonekana mtu anaeingia wala kutoka , lakini katika kishikwambi chao cha kampuni ya Microsoft Surface Book waliokuwa nayo hapo ndani ilionyesha Edna bado alikuwa ndani , hivyo hawakuwa na wasiwasi kabisa,lakini pia jambo ambalo liliwafanya kuzidi kujihakikisha kuwa Edna ana ulinzi ni kwamba na Bram alikuwa akiangalia upande wa pili wa jengo hili yaani upande wa Dirishani kama kuna aina yoyote hatarishi kwa Edna kwa njia ya satilaiti ya Crogo, kwa namna ambavyo Edna alikuwa akilindwa ni kama Kiongizi mkubwa wa kitaifa ni hivyo tu hakuwa akijua kama alikuwa akipewa ulinzi wa aina hio.

Sasa baada ya mabwana hawa kuona muda umeenda sana pasipo ya Edna kutoka , walishangazwa na jambo hilo na kuna muda walihisi huenda labda Edna kuna mtu yupo nae ndani ya chumba hiko , lakini walipotezea wazo hilo , kilichowafanya hawa mabwana wachukue hatua ni kutokana na kutoonekana kwa muhudumu yoyote kufika ndani ya chumba hiko kwa ajili ya chakula na huduma nyingine. Na waliona wachukua hatua kuhakikisha kama Edna yupo salama na John alishuka mpaka chini mapokezi.

“Samahani”

“Yes bila samahani mteja wetu wa thamani”Aliongea mwanadada mwingine ambae alikuwa eneo la mapokezi na sio wale ambao walikuwepo asubuhi kwani ilionekana wale Shift yao iliisha.

“Nahitaji kuonana na Miss Edna Adebayo kutoka Vexto Group”Aliongea John na kumfanya yule mwanadada ambaye alikuwa na bango la jina lake kwenye sare yake kwa jina la Winnie , baada ya John kuomba ,Winne aliinamia tarakishi yake na kuangaliana na wahudumu wenzake wanaume , ni kama kuna kosa ambalo walikuwa wamelifanya na walikuwa wakishangaa.

“Kwanini Tesha hajatuambia kama Madam yupo hapa , na mimi nilijisahau sijapitia majina ya wageni wote wa VIP”

“Sio kosa lako Winie ,Madam amekuwa anakuja mara chache sana ndani ya hii hoteli ndio maana”Aliongea Muhudumu mwingine kumfariji mwenzake na wakati wote walikuwa wakiongea kwa Kiswahili na Chiara aliweza kusikia mazungumzo yao maana hata yeye alikuwa akielewa Kiswahili japo sio sana.

“Samahanni una miadi nae?”Aliuliza Winie baada ya kujituliza , lakini waswasi haukuondoka kwenye macho yake, kwenye siku zote ambazo aliona alifanya makosa ndio hio ya leo, kwani hakuwa amechunguza VIP Guest wote waliokuwa ndani ya hio hoteli kwa majina yao.

“Sina miadi nae , lakini unaweza kupiga simu na kumtajia jina la Business Partner atakuelewa”Aliongea John na Winie alitafakari kidogo na kuchukua simu na kupiga , lakini mwanamke huyu wa kitanzania licha ya kupiga simu haikupokelewa na hapo John aliona kuna shida.

“Mr Hapokei simu”

“Nadhani itakuwa vyema kama utaenda kuanga……”Kabla John hajamaliza kuongea , aliingia mwanamme mmoja mwenye kitambi alievalia suti ya Kaunda ya rangi ya Zambarau na Baada ya wahudumu hawa kumuona walikaa sawa kumsalimia , huyu alikuwa ni meneja wa Hoteli.

“Winie Tesha kanipigia simu ,Madam amefika tokea asubuhi?””.

“Ndio Meneja , lakini kuna tatizo hapokei simu”Aliongea.

“Floor Meneja yuko wapi mpaka akashindwa kuelewa swala kama hilo?”Aliongea kwa sauti ya kufoka lakini wale wahudumu walionesha hali ya kuangaliana na kutoelewa na Meneja huyu aliona Uzembe.

“Nipe Kadi ya dharula”Aliongea na kisha akapewa haraka haraka na akatoka hapo eneo la mapokezi na kukimbilia kwenye lift. Na John alifuatia huku akimtumia ujumbe Chiara.

Ndani ya dakika chache tu Meneja huyu wa kiume alikuwa mbele ya mlango na kuanza kugonga kwa sekunde kama sitini hivi , lakini hakukuwa na majibu na ndipo alipofanya maamuzi ya kutaka kufungua lakini wakati huo huo , alipigwa kikumbo na Chiara…

“Stay Back”Aliongea Chiara kwa Amri na akachukua ile kadi na kufungua na muda huu huu walikuja na wahudumu waliokuwa wakihudumia floor hio , wakiwa kwenye kimuhemuhe.

Chiara baada ya kuingia alijikuta akipigwa na mshangao , kwani alimkuta Edna akiwa amelala chini kwenye Zuria huku akionekana hajitambui.

“Nini kimemtokea?”aliuliza John.

“Ni mzima anaoenekana kudhirai”Aliongea Chiara huku akimbeba Edna.

“Call ambulance now “Aliamrisha Chiara na Meneja ni kama aligutuka kwenye mshangao , kwani ni kama alikuwa amekufa ganzi , hakuelewa ni nini kinaendelea hususani kwa upande wa hao wazungu.

Dakika chache mbele Edna alikuwa akitolewa ndani ya jengo hili la hoteli Paradise akiwa ndani ya gari ya dharula ya Ambulance iliokuwa ikimilikiwa na hoteli hio na hapo ndipo alipompigia Hades kumtaarifu kinachoendelea.

“Chiara unafikiri Mfalme Pluto hatokasirishwa na kuchelewa kwetu kugundua kama Malkia alikuwa na shida?”.

“Usiwe na wasiwasi John , jukumu letu ilikuwa ni kumlinda Malkia pasipo watu kugundua na yeye pia kujua kama tunamlinda hivyo ilikuwa ngumu kujua nini kinaendelea ndani”Aliongea Chiara huku wakifuatilia gari iliompandisha Edna kwa nyuma.

Roma ,Profesa Clark na Sophie waliingia haraka haraka ndani ya hospitali ya Aghakhani na hii ni mara baada ya Roma kufahamishwa kuwa yupo ndani ya hio hospitali.

Roma ndio aliekuwa wa kwanza kumuona Chiara pamoja na John, Profesa Clark licha ya kutowatambua hao wazungu lakini hisia zake zilimwambia kuwa hao ni moja ya wanajeshi wa Roma.

Watu waliokuwa eneo hili la VIP walikuwa wakimwangalia sana Profesa Clark , walionekana wengi walikuwa wakimfahamu na kujiuliza inakuwaje profesa kam huyu kuwa ndani ya hospitali hii ya Aghakhani Ghafla tu , kwani alikuwa ni mtu mwenye hadhi ya juu , ukiachana na Elimu yake , lakini pia Profesa Clark alikuwa ni mtoto wa Malkia Catherine wa Wales.

“Nini kimetokea kwa mke wangu Chiara?”Aliuliza Roma na Chiara aliekuwa kwenye wasiwasi alikakamaa na kujibu kwa heshima na kumfanya Sophia ashangae.

“Tumemkuta akiwa amezirai ndani ya hoteli ya Paradise Sir”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa , aliwaza Edna alikuwa akifanya nini hotelini , ila hakutaka kuhoji sana.

Baada ya kama dakika kumi hivi tokea Edna kuingizwa ndani ya chumba cha matibabu , ghorofa ya juu kabisa ya jengo hili la hospitali ,Floor iliokuwa ikitibu wagonjwa wa hadhi ya juu , Madaktari bingwa wawili walitoka na Roma aliwaosgelea.

“Poleni sana kwa kusubiri muda mrefu , Naitwa Dokta Shukuru Omary “

“Dokta Shukuru niambie hali ya mke wangu ikoje?”Aliongea Roma na kumfanya dokta huyu aonyeshe mshangao kidogo , ni kama hakujua mwanaume aliekuwa mbele yake ndio mume wa mwanamke mrembo Tajiri, alionyesha kuguswa na chaguzi ya Edna , kwani mwanaume aliekuwa mbele yake hakuwa hata na sura ya kuwa mume wa Edna , lakini pia Dokta huyu alikuwa akimwangaliaProfesa Clark muda wote na ni kama alikuwa akimfananisha.

“Tumemfanyia vipimo vya aina mbalimbali kulingana na tatizo na kugundua hana tatizo kubwa , hali yake ya kupoteza fahamu imesababishwa na Uchomvu , pamoja na mshituko kutokana na presha yake kuwa juu , ila kwa sasa yupo salama kabisa na muda wowote atarejewa na fahamu, na atahitajika kupumzishwa kwa muda wa siku saba hapa hospitalini”Aliongea Dokta Shukuru na kumfanya Roma kupata afadhali.

Mita kadhaa tokea chumba alichokuwa ameingizwa Edna yaani mlango wa pili , alionekana Matrida na yeye akiwa kwenye kitanda , huku akionekana kurejewa na fahamu , pembeni yake alikuwa yupo mdogo wake Queen na Isaack

Matrida ndio kwanza fahamu zilikuwa zimemrejea hivyo hakuonekana kuwa sawa , ni kama alikuwa akijitahidi kukumbuka vizuri nini kilitokea dakika kadhaa nyuma na akili yake ilifanya kazi kwa dakika kadhaa na hatimae kuanza kukumbuka tukio la baba yake kurushwa nje ya Ghorofa kupitia Dirishani.

“Noo…!!! Dadii”Alianza kulia Matrida mara baada ya kukumbuka tukio na kuwafanya Queen na Isaack kumsogelea.

“Sister Calm Down”

“No Queen .. baba karushwa chini Ghorofa , baba yatu kafariki Queen.. Aaa,…. Hiiii”Alianza kulia kwa kwikwi na kuwafanya Queen na Isaack waangaliane na kuonekana kutoelewa kile kilichotokea.

Ndio Isaack hakua akijua nini kimemtokea kabisa Matrida , kwani wakati Mzee Alex anaingia ndani ya jengo la kampuni yao , hakuwepo na wakati anarudi ndipo alipoweza kukutana na Roma njiani na kugundua huenda kuna tatizo na ndio maana akakimbilia kwenda kuingia ndani ya Ofisi ya CEO na ndipo alipoweza kumkuta Magdalena na Matrida aliekuwa hajitambui na mpaka kumleta hapo hospitalini hakuwa akijua ni nini kilitokea na alikuwa akihitajiu maelezo , lakini alikuwa pia akihisi kuenda Roma alikuwa akihusika.

“Matrida hebu tuambie ni nini kilichotokea , hatukuelewi”Aliongea Isaack akimtaka Matrida kunyamaza lakini Matrida aliendelea kulia mfululimzo huku akijitoa Dripu iliokuwa imechomekwa kwenye mkono wake wa kushoto na kunyanyuka na kumsogelea mdogo wake na kumkumbatia huku wakiendelea kulia.

Queen ambaye licha ya kusikia maneno ya Dada yake kuhusu baba yake kurushwa Ghorofani , hakuelewa kabisa na aliishia kuungana na dada yake kutoa kilio na kumfanya Isaack ashindwe hata kujua ni namna gani anaweza akawanyamazisha , kwani alikuwa ni kama anachanganyikiwa.

Wakati wakiendelea kulia , mara mlango wao ulifunguliwa na mwanaume mzee alievalia suti na kumfanya Isaack ageuke.











SEHEMU YA 137

Mheahimiwa Senga aliekuwa ndani ya ofisi yake alionekana kuchanganuyikiwa kutokana na simu mbalimbali zilizokuwa zikiingia kwa siku nzima ya siku hio kutoka kwa viongozi wakubwa duniani waliokuwa wakipiga na yote hio ilikuwa ni juu ya kifo cha Profesa Shelukindo.

Viongozi wengi walikuwa wakitaka kujua sababu iliopelekea mpaka Profesa Shelukindo kuuwawa kikatili ndani ya taifa linalosifika kwa Amani kama Tanzania, lakini licha ya simu hizo Raisi Senga alionekana kushindwa kutoa maelezo ya kueleweka Zaidi ya kuwapa jibu moja tu kama uchunguzi unafanyika hivyo wawe wapole.

Na muda huu ilikuwa ni Saa kumi kamili za jioni na alionekana kuchoka kweli , kwani kazi siku hio zilionekana nyingi ambazo zilikuwa zikimuhitaji yeye mwenyewe kuzifanyia kazi kwani wasaidizi wake wasingeweza kuzifanya , kwani nyingi zilikuwa ni kuongea na viongzi wakubwa wa kimataifa.

Wakati Raisi huyu wa wananchi wa Tanzania akiendelea na majukumu yake , huku akipanga muda huo atoke ofisini kwa ajili ya kwenda kupumzika , ofisi yake ilifunguliwa na akaingia katibu Muhtasi wake.

“Mheshimiwa kuna faili limefika muda huu , linaonekana kuwa la muhimu”

“Okey nipatie”Aliongea Mheshimiwa na Katibu alimsogelea mheshimiwa na kumkabidhi Bahasha kubwa ya Khakhi , ndio ilionekana kuwa nyaraka muhimu kwani ilikuwa na neno ‘Confidential’ Juu yake.

Baada ya mheshimiwa tu kupokea lile faili na kumruhusu katibu kuondoka , simu yake muda huo huo iliita na haikuwa simu ya ofisi ila ilikuwa ni simu ya mawasiliano yake binafsi nje ya ofisi na baada ya kuangalia jina la mpigaji , alikuwa ni Raisi Jeremy.

“Niambie Senior”

“Senga nadhani faili limekufikia?”Aliongea Raisi Jeremy upande wa pili wa simu na kumfanya Raisi Senga kushangaa.

“Ndio limeletwa sasa hivi na kwa linavyoonekana halionyeshi kutoka kwenye ofisi yakow ala kuja kwenye ofisi yangu”

“Ndio Senga , ni kwasababu taarifa hio ni muhismu sana na ya siri ndio maana sikutaka watu wafahamu linakuja kwako , ni taarifa inayomuhusu Roma Ramoni”Aliongea Senga na kumfanya Mheshimiwa Senga aibane simu na Bega na kuanza kuchana ile bahasha kwa haraka haraka ili kujua ni taarifa gani iliokuwa kwenye karatasi , baada ya kukata simu tu karatasi iliokuwa na jumla ya peji tano ilikuwa kwenye mikono yake.

Alianza kusoma taratibu huku kila sekunde mikono yake ilianza kutetemeka na mshangao pia ukionekana kwenye macho yake na zilipita sekunde kama kumi hivi Mheshimiwa alirekebisha Miwani yake , kwani alihisi nikama hakuwa akiona vizuri.

*******

MASAA MACHACHE NYUMA.

“Yan Buwen nishakamilisha kazi ni wakati wako wa kutimiza ahadi”Aliongea Scorpion baada ya kukaribishwa ndani na Yan Buwen.

“Scorpion kwanza hongera kwa kumaliza kazi , na niseme umeifanya vizuri sana nje ya mategemeo yangu , sikudhania utaimaliza familia nzima”

“Sikuwa na jinsi , walikuwa wakijifanya kuonyesha mapenzi kwa baba yao kwa kumkumbatia kumbatia ndio maana nikaamua kuwamaliza wote na pia waliona sura yangu”Aliongea Scorpion huku akiketi kwenye sofa , lakini Yan Buwen aliishia kutabasamu tu , bwana huyu hakujali kwa kile ambacho Scorpion amekifanya , yeye kwa wakarti huo alikuwa akijali malengo yake kufanikiwa na ndio maana hakuwa na hata hatia ya vifo cya watu wasio na hatia.

Yan Buwen kwanza alijimiminia Whiskey kwenye Glass yake na kisha akachukua glass nyingine na kumimina na kumpatia Scorpion lakini Scorpion aliikataaa na Yan Buwen aliishia kutabasamu na kisha akanywa kidogo na kukunja nne na kufanya Boksa yake iliokuwa imezibwa na taulo kuonekana ila kwa Scorpion licha ya kuwa mwanamke hakujali sana.

“Scorpion nadhani unafahamu kama wewe ni muuaji na siku zote wauaji ni ngumu sana kuwakuta wakifanya kazi ya Ubodigadi..”

“Ndio maana nataka kujua kwanini nimepewa kazi hii , kazi ambazo nilipaswa kufanya mimi ni kama hii ya leo na natamani kurudi kwenye kazi kama hizi”Aliongea na kumfanya Yan Buwena kutabasamu kidogo na kisha akakaa vizuri.

“Ushawahi kuwasiliana na wenzako mara baada ya kutoka kambini?”

“Hapana , sijawahi kuwasiliana na hata mmoja na sitaki hata kuwa na namna ya kuwasiliana nao”

“Hahaha,,, Sio kama hutaki kuwasiliana nao Scorpion mafunzo yenu mlifundiushwa kujitegemea , lakini pia mmeelekezwa kuwasiliana ni kosa kisheria”Aliongea Yan Buwen na kumfanya Scorpion kutingisha kichwa kwamba anakubali kwamba Moja ya sheria yao kama Maninja wa kundi la Yamaguchi ni kutokuwa na aina yoyote ya mawasiliano na kutotambuana labda kwa ruhusa maalumu.

“Ngoja nikuambie siri moja tu kwa leo ambayo utatambua kwanini upo Tanzania kama Bodigadi”

“Nataka kujua kila kitu Yan Buwen ndio ahadi ulioniwekea”

“Ninachokuambia kama una uwezo wa kufikiria basi utaweza kufungua kodi na kujua kila kitu na nakuambia siri hii kutokana na kwamba kati ya Ninja wote ambao wametoka kwenye kundi la Yamaguchi , wewe umakuwa ni wa kipekee sana lakini pia nimependezwa na uwezo wako , hususani upande wa ukatili hahahaha…”Aliongea lakini Scorpion hakubadilika , alionekana kama roboti lisilokuwa na hisia.

“Dunia hii ina nchi jumla 195, kati ya nchi hizo ni mbili pkee ambazo hazipo kwenye umoja wa mataifa lakini haimaanishi kama hizo nchi hazina nguvu , vile vile katika kila nchi licha ya kuongozwa na raisi , mfalme au Malkia , kila nchi ina angalau watu wenye nguvu wasiopungua 100 iwe ni kwenye maswala ya kiuchumi , Kisiasa au Kijeshi”

“Unataka kumaanisha nini Yan Buwen?”

“Ninachomaanisha ni kwamba kama kila nchi ina watu wenye nguvu wasiopungua 100 basi tarajia kila nchi kuwa na Ninja wa Yamaguchi wasiopungua Mia moja , kwa mananeo marahisi ni kwamba na wewe ni sehemu ya Ninja 100 mliopo ndani ya taifa la Tanzania pekee tukichukulia kama mfano” Scorpion alijikuta akishangaa mno.

“Hahahaha….. Hahahahaha……Unaokana kuelewa pointi yangu sasa mpaka hapo”

“Unamaanisha kuwa mafunzo yetu yote hayakuwa ni kwa ajili ya kuua bali kulinda watu wenye nguvu duniani?”

“Hhahaha…. Scorpion unaonekana kutonielewa vizuri bado , labda nikuulize, je unafahamu maana ya ‘Sleeper Agent’?”

“Ni rahisi kusema Sleeper ajenti ni wakala ambao amewekwa sehemu kwa misheni fulani ambayo haitakiwi kuanza mpaka atakapopewa ruhusa”Aliongea Scorpion na Yan Buwen akatabasamu.

“Mpaka hapo sasa unatakiwa uelewe wewe unafanana kwakiasi kikubwa na Sleeper ajenti , The Don amekuweka karibu na Kigombola kwa kazi moja tu ya kumlinda asije akauliwa na mtu yoyote yule nje ya The Don mwenyewe , hivyo ni rahisi kusema licha ya kwamba unamlinda Kigombola lakini itafikia siku unaweza pewa misheni ya kummaliza hahahaha.....”Aliongea Yan Buen nakunyanyuka na kulisogelea Dirisha na kutoa pazia , alionekana kufurahi mno.

Scorpion mpaka hapo alikuwa ameelewa kwamba ndani ya taifa hakuwa peke yake , kwani kwa maelezo ya Yan Buwen ni kwamba wapo Zaidi ya mia moja sasa swali likaibuka kama ni kweli wenzake mbona hakuwahi kuwaona wala kukutana nao hata kwa bahati mbaya.

“Who is The Don?”

“Hahaha… Scorpion ahadi yangu nishatimiza , subiri siku nikihtaji msaada nitaweka ofa nyingine ya kukupatia taarifa Zaidi”

“Naomba unijibu swali moja na kama utalifanya kuwa deni nipo tayari kudaiwa , niambie kama The Don ni binadamu au sio binadamu?”

“Hahahaha…..hahahaha…..Good! ,Swali zuri Scorpion ila siku ya leo sitoweza kukujibu , subiria siku nikiwa na kazi maalamu jibu langu litakuwa kama malipo kwako, unaweza kwenda na kwanzia sasa hakikisha hatufahamiani , kesho ninakuja kuonana na Mheshimiwa Kigombola kwa misheni yangu ya pili ilionifikisha nchini Tanzania”

Ilikuwa ni siku ya kesho yake , siku ambayo taarifa ya Edna ilikuwa ikisambaa mtandaoni. Ndani ya Village G katika ofisi ya mheshimiwa Kigombola alionekana Yan Buwen pamoja na Mheshimiwa wakiwa wameketi kwenye masofa wakiongea , lakini wakati huo huo aliingia Erick msaidizi wa karibu wa mheshimiwa Kigombola.

“Kuna nini Erick?”

“Mheshimiwa kuna taarifa inayosambaa mitandaoni inayomuhusu Edna , niliona unapaswa kuiona kwani waliohusika kuisambaza ni Mzee Alex na Abubakari”Aliongea Erick na mheshimiwa alifikiria kidogo.

“Erick fuatilia kila kinachoendelea na utanipatia taarifa”Aliongea Mheshimiwa na Erick alitoka , mheshimiwa Kigombola alionekana kuwa na jambo muhimu sana alilokuwa akiongea na Yan Buwen.

“Tunaweza kuondelea Mr yan”Aliongea kwa Kingereza.

“Mheshimiwa kabla ya kuweka wazi nia na madhumuni yalionifanya kufika ndani ya Tanzania nataka unitambue kama nipo hapa kwa Baraka zote kutoka kwa Afande Yang Gongming kutoka China”Aliongea Yan Buwen na kumfanya Kigombola ashangae kidogo , lakini Yan Buwen hakutaka kuongea maneno tu , alitoa flash disk na kisha akampatia mheshimiwa.

“Kuna faili ambalo lina nyaraka mbili , ya utambulisho wangu kutoka kwa jenerali . na nyaraka ya pili ni zawadi kwako juu ya taarifa inayohusiana na Roma Ramoni”

Aliongea Yan Buwen na kumfanya mheshimiwa kuangalia Flash hio ya kampuni ya ‘SanDisk kama mtu ambaye hakuwa akiamini , alionyesha hali ya shauku kwenye macho yake.

Na haraka haraka alivuta tarakishi mapakato iliokuwa kwenye meza ya kampuni ya Apple na kuchomeka hio flash,Mheshimiwa Kigombola hakuwa na hata hamu ya kujua utamulisho wa Yan Buwen yeye kitu kikubwa alichokuwa akitaka ni juu ya taarifa inayohusiana na Roma pekee, Yan Buwen alitabasamu kwa namna ambavyo mheshimiwa alikuwa na haraka ya kuangalia hilo faili.

“Mr Yan faili hili lina nywira?”Aliongea na kumfanya Yan Buen atabasamu.

“Ndio najua Mhehimiwa na ndio maana nakuomba usome faili la kwanza na la pili yake utalifungua mara baada ya sisi kufanya mazungumzo na kama mazungumzo yetu yakienda sawa , basi moja kwa moja nitakuambia nywira za hilo faili.









SEHEMU YA 138

Wote hawakuwa wakimtambua mwanaume ambaye alikuwa ameingia ndani ya chumba hiko cha Wodi ya daraja la Kwanza ndani ya hospitali hii kubwa ya Aghakhani.Matrida na Queen ambao walikuwa kwenye majonzi walimwangalia huyo mwanaume na kuonyesha kusubiria utambulisho wake.

Alikuwa ni mwanaume kijana lika la umri wa miaka therahini na tano hivi maji ya kunde alievalia suti.

“Habari yenu jamani, naitwa Felix Ndimbo”Alisalimia yule kijana lakini bado alionekana kutoleweka mbele ya Matrida na Isaack , na aliishia kutabasamu.

“Kama nilivyosema naitwa Felix ndimbo ni msaidizi wa karibu wa Mzee Kweka , nipo hapa kuwapa taarifa sehemu ambayo baba yenu anapatiwa matibabu”Aliongea Felix na kumfanya Matrida amtoe Queen kidogo ni kama hakuwa ameelewa.

“Unasema baba anatibiwa!Anatibiwa wapi , yupo hai?”

“Nipo hapa kwa ajili ya kuwapatia taarifa hii ili msije mkawa na wasiwasi ,Abubakari Hamadi ataendelea kuwa karibu na Mzee Alex mpaka hali yake itakapotengemaa”Aliongea yule bwana na kumfanya Matrida aone kama huyu bwana anamfariji.

“Falix sijui Ndimbo ,, hebu naomba uwe mkweli , baba alirushwa kutoka juu Ghorofani ni majeraha kiasi gani kapata?”

“Miss Matrida nadhani haukuona vizuri kilichotokea “

“Unamaanisha nini?”

“Sipo kwenye nafasi ya kueleza kila kitu kwa sasa , jukumu langu hapa lishaisha kama unataka kuhakikisha baba yako ni mzima wasiliana na Abubakari Hamadi kabla hajatoka nje ya Nchi , lakini nikusisitizie tu kaa mbali na Roma Ramoni kwanni kilichotokea leo kinaweza kujirudia na kuleta madhara makubwa kwa familia nzima”Aliongea kidogo na kisha akapiga hatua kuelekea mangoni na akageuka.

“Matrida kaa mbali na watu wote wanaohusiana moja kwa moja na Roma Ramoni”

Aliongea Felix na bwana huyu alionekana kumaliza kwani hakusubiri swali lolotea kutoka kwa wanafamilia hao , alitoka kwenye chumba hiko , lakini Queen alieshika simu ndio alianza kumtafuta Abubakari ,Mrembo huyu ukweli hakuwa akielewa kilichokuwa kikiendelea kabisa licha ya dada yake kusema baba yake amerushwa kutoka juu Ghorofani , alijiuliza kama jambo hilo ni la kweli nani kawa na ujasili wa aina hio wa kufanya hivyo , lakini pia alijiuliza huyo Roma Ramoni ni nani na sio kwake tu hata Isaack pia alikuwa akishangaa..

“Abu naomba kuongea na baba”Aliongea Queen lakini muda ule ule Mateida aliipakua ile simu kutoka kwa Matrida.

“Abubakari nini kinaendelea, baba yangu ni Mzima?”

“Ndio licha ya kwamba yupo kwenye mshituko , kutokana na tukio lililomtokea ila kwa maelezo ya daktari atakuwa sawa na muda si mrefu nitasafiri nae kwenda nje ya Nchi”

“Nje ya Nchi !!..umesema ni mzima na ana mshituko wa kawaida , kwaninni nje ya nchi?”

“Matrida kwanza hebu niambie ni nini kimemtokea Mzee, mbona unaongea kwa wasiwasi sana?”Aliuliza Abubakari upande wa pili na Matrida alijikuta akianza kuvutia tukio lilivyotokea masaa kadhaa yaliopita na akaelezea.

“Sasa kama alirushwa juu ya Ghorofa mbona anaonekana kuwa katika hali ya kawaida?”Aliuliza Abubakari lakini kwa Matrida aliona ni kama Abubakari alikuwa akimchanganya tu.

“Abubakari usije ukaondoka nje ya nchi kabla sijamuona baba yangu”Aliongea Matrida lakini hakusikia jibu lolote kutoka upande wa pili kwani simu ilikuwa imeshakatwa.

“F**ck”Alitukana Matrida , alionekana uwa ni mwenye hasira.

Queen sasa ni kama alikuwa ashapata picha ya kile kilichokuwa kimetokea lakini hata yeye alijikuta akijiuliza kama ni kweli baba yake alirushwa kutoka kwenye ofisi ya Dada yake mpaka chini kasalimikaje mpaka kuwa mzima , aliona huenda na dada yake ana matatizo na kushindwa kumuamini ,na haikuwa kwa Queen tu hata kwa Isack pia ambaye alikuwa akisikiliza maongezi yote hapo ndani hakuamini maelezo ya Matrida ya kwamba Eti Mzee Alex karushwa kutoka juu ya Ghorofa na kaishia kupata mshituko tu kama Abubakari alicyoongea.

Upande wa eneo la megesho ya ,alionekana yule mwanaume aliejitambulisha kwa jina la Felix akipiga simu.

“Ushawaambia!?”

“Ndio bosi , walikuwa kwenye majonzi na nilivyowaeleza wakawa na wasiwasi”

“Kazi nzuri Felix , kama hawatalichukulia swala lililotokea kama fundisho hatutaweza kuilinda hio familia tena licha ya kwamba wamekuwa na msaada mkubwa kwetu, unaweza kurudi kuendelea na majukum yako mengine”

“Sawa Bosi”Aliongea Felix na kisha akaingia kwenye gari yake aina ya Harrier na kutoweka ndani ya eneo hilo.

Ni baada ya lisaa kupita ,hatimae Edna alirejewa na fahamu na kujikuta akiwa ndani ya chumba ambacho baada ya kupepesa pepesa macho aligundua hapo ni hospitalini.

Mwanamke huyu alifikiria ni nini kilitokea mpaka kufika hapo ndani pasipo kujitambua , na katika harakati zake za kurudisha kumbukumbu nyuma alikumbuka alikuwa ndani ya hoteli ya Paradise kwenye chumba maalumu ambacho kilikuwa kama urithi kutoka kwa mama yake , kwani Raheli enzi za uhai wake ndio mahali alipokuewa akipendelea sana kwenda akiwa na maswala ya kufikiria na kutokana na tabia hio ya mama yake na Edna akarithi tabia hio na siku zote akiwa na jambo ambalo linamsumbua kichwa ni lazima angeenda ndani ya chumba cha hoteli ya Paradise.

Wakati Edna akifikira mlango ulifunguliwa na waliingia watu watatu wawili akiwa anawatambua , mmoja akiwa amemtambua kama Roma na mwingine akiwa amemtambua kama Sophie , lakini kwa mwanamke mwingine mrembo wa kizungu hakuwa amemtambua na alijiuliza huyo mwanamke ni nani.

“Dada..!”alikimbia Sophie na kwenda kumkumbatia Edna.

Roma aliwaangalia wawili hao na alijikuta akipatwa na hisia mchanganyio , ukweli hakuelewa kama Sophie alikuwa akiigiza mbele ya Edna au matendo aliokuwa akiyaonyesha yalikuwa ndio anachojisikia moyoni , hakuelewa kabisa lakini alijisikia vizuri kuona wawili hao wakiendanana.

Roma muda wote alikuwa ameweka mikono yake nyuma huku akimwangalia Edna na kwa upande wa Edna na yeye alikuwa akijiuliza mwanamke ambaye yupo na Roma ni nani kwani ni kama alikuwa akimfahamu hivi.

“Wife zawadi yako hii ya kukutakia kupona haraka”Aliongea Roma na kumkabidhi Edna maua ya kununua na kumfanya Edna ashindwe kukataa hayo maua na kuyapokea baada ya kusaidiwa kunyanyuka na Sophie ,na Edna alitabasamu.

“Asante!”Aliitikia Edna huku akiona aibu, kwanza kabisa jambo ambalo linamfanya kuona aibu ni kuzirai mpaka kuletwa hospitalini na kwa jinsi alivyowaona hao ndugu zake aliona washajua kuwa asubuhi alikuwa akijifanyisha kuwa imara mbele yao , lakini pia Edna hakutarajia kama Roma atamletea maua , alijikuta tu akijisikia vizuri kama mwanamke.

Ukweli ni kwamba Profesa Clark ndio aliemlazimisha Roma kumnunulia Edna zawadi baada ya kuona mtu wa maua anayapitisha huku akiuza na mwanzoni Roma alishangaa , lakini alivyopewa maelezo na Clark aliona ni jambo lenye mantiki na kununua, Roma alikuwa ashazoea wazungu ndio waliokuwa wakipelekewa maua wakati wakiwa wagonjwa na waafrika hawakuwa sana na aina hio ya utamaduni, lakini kwa jinsi alivyomuona Edna akitabasamu baada ya kupokea maua hayo , aliona kweli mbinu imefanya kazi.

“Edna pole sana”Aliongea Clark na kumfanya Edna amwangalie .

“Asante”Alijibu huku akimwangalia Roma ni kama alikuwa akisubiri amwambie huyo mwanamke ni nani na Roma aligundua hilo.

“My wife huyu ni Profesa Clark Stephanie ni rafiki yangu kutoka Uingereza”Aliongea Roma na kumfanya Edna kushangaa.

“You mean Prince…!!”Aliongea Edna lakini alikatishwa na Clark alimsogelea Edna na kumshika mkono Edna.

“Edna nimefurahi kwa kumkumbalia huyu mwanaume na kuwa mumeo , maana kwa muonekano wake niliamini akija Tanzania asingepata mwanamke kabisa na angeishia kuwa single”Aliongea Clark na kumfanya Roma asijue atabasamu au anune kwa matani ya Clark.

“Ndio uelewe kama nyota yangu ni kubwa”Aliongea Roma huku akitabasamu na kumkonyeza Edna aliekuwa akimwangalia , Edna alikuwa akijiuliza inakuwaje Roma akawa na urafiki na mwanamke mrembo kama huyu mwenye hadhi kubwa duniani na wakaendelea kuitana marafiki , alihisi ni kama alikuwa akidanganywa lakini wakati huo huo , alijikuta akikumbuka kuhusu nguvu ya ile pete na kuinua tena macho yake na kumwangalia Roma na Roma alimtingishia mabega kumuonyesha hajui, yaani ni kama Roma alikuwa akijua ni jambo gani Edna alikuwa akiwaza kwa wakati huo,

Roma simu yake iliokuwa kwenye mfuko wake ilianza kuita mfululizo kwa sauti mbaya ya juu na kuwafanya warembo hawa kumgeukia kwa mlio aliouweka na Roma aliwaangalia na kutabasamu , alijua ni kwanini walikuwa wakimwamngalia , kwani simu yake hio ndogo aina ya Tecno ilikuwa na mlio wa juu sana na mbaya kiasi kwamba ikiita ni kama inakoroma.

Roma baada ya kuangalia jina aliona ni namba kutoka nje ya nchi , lakini namba ambayo ni kama alikuwa akiikumbuka. Vizuri.

“Sauron!!”Aliwaza baada ya kuweka silent na kisha akawaangalia hao wanawake na kuwaonyesha ishara kama anakwenda kuongea na simu , Roma hakujua ni kwanini Sauroni alikuwa amempiga baada ya muda mrefu kidogo lakini pia mar azote alikuwa yeye ndio wa kumtafuta kwanza , aliwaza huenda akawa na taarifa za The Zeros Organisation.

“Ooh!!! Sorry!!”Aliongea Roma baada ya kugongana na Queen ambaye alikuwa akitoka kwenye chumba kilichokuwa mkabala na cha mke wake wakati akitafuta sehemu nzuri ya kusimama kwa ajili ya kuongea na simu na walijikuta wakiangaliana.

ITAENDELEA JUMANNE

Sleeper`s Agent is a spy who is placed in a target country or organization not to undertake an immediate mission but to act as a potential asset if activated.

Yan Buwen anasema ndani ya mataifa kuna Zaidi ya Ninja 100 , swali je aliemuokoa Mzee Alex kwenye lile jengo ni Scorpion kama Roma alivyodhania au yeye alikosea kutokana na kutojua kuwa kuna Zaidi ya ninja 100 ndani ya Tanzania.
NICHEKI WATSAPP NIKUPTE UTARATIBBU WA KUPATA MWENDELEZO TUPO SEHEMU YA 182 0687151346
 
singanojr unajua Mkuu Sema nini baadhi ya simulizi zako huwa hazifikii mwisho kabisa kama UMOJA namba 97, Waraka wa mwisho wa raisi, Kitabu cha majina yote na ile Masaa mawili ya Kumbukumbu unatukatili sana Mkuu au mpaka tulipie?
 
Back
Top Bottom