SEHEMU YA 132B
BAMAKO-MALI 2005
Ni pembezoni mwa jiji la Bamako kilomita kadhaa kutoka mtaa ufahamikao kwa jina la Nikamaero, sasa ndani ya hili eneo kuna jumba moja kubwa ambalo limejengwa katikati ya eneo ambalo limezungukwa na miti mingi ,jumba hili lilikuwa ni tofauti kidogo na majengo yote ambayo yalikuwa yakipatikana ndani ya mtaa huu wa Nikamaero, ni nyumba ambayo imejengwa kawaida sana lakini kwa mtindo wa kisasa, haikuwa ya ghorofa,kwa watu wa Mali waliokuwa wakiishi karibu na huu mtaa walichukulia nyumba hio kama nyumba ya mtu mwenye pesa ambaye ni mwenyeji wa jiji la Mali , lakini ukweli ni kwamba hio nyumba ilikuwa ni ‘Black Site’ ya CIA
Black Site katika ulimwengu wa kijasusi ni maeneo maalumu ambayo humilikiwa na vitengo vya kijasusi duniani kwa ajili ya kufanyia mateso , unaweza kusema ni maeneo ambayo sio halali au kwa maneno marahisi unaweza kusema gereza ambalo sio halali,yaani unakuta kwa mfano CIA wana operesheni ambayo wanaifanya kwa mfano Tanzania na katika Operesheni hio inahusisha kutesa watu ili kupata taarifa sasa maeneo ambayo yanafanyikia hayo mateso huwa ni maalumu yaliotegenezwa yanayofahamika kwa jina la Black Site.
Ni muda wa asubuhi wa mwaka 2005 zinaonekana gari mbili moja ikiwa ni Benz toleo la Zamani na nyingine ilikuwa ni Toyota Landlover,Gari hizi zilionekana zikiingia ndani ya uzio wa nyumba hii na kwenda kusimama mita kadhaa kutoka mlango wa kuingilia kwenye nyumba hii upande wa kushoto na baada ya hzi Gari kusimama , walishuka mabwana wawili moja akiwa ni mwanaume mzungu mtu mzima wa makadirio ya miaka kama Hamsini hivi alievalia tisheti ya Bluu na Jeans pamo jana na viatu vya Ngozi huku akiwa na miwani ya jua kwenye macho yake na mwingine alikuwa ni mzungu hivyo hivyo ila mwanamke aliekuwa ameavalia Tisheti na suruali ya Silk pamoja na kofia cheperu na yeye akiwa na miwani ya jua , hawa walitoka kwenye gari ya mbele yyani Benz , waliokuwa kwenye gari ya nyuma wote walikuwa ni Wa Afrika waliokuwa wamevalia suti nyeusi na wao walitoka haraka na kuwatangulia wale wazungu wawili na kuwaonyesha ishara ya mkono kama waelekee ndani na wakatingisha vichwa vyao na kuanza kupiga hatua kuingia ndani ya jengo hili,
Kwa ndani hakukua na jambo la kushangaza sana kwani kulikuwa na makochi ya mbao yaliokuwepo eneo la sebuleni pamoja na Tv ya Chogo na baadhi ya chupa za Bia zilizokuwa tupu ,Wale waafrika baada ya kuingia ndani ya hili eneo walikata upande wa kushoto na kufungua chumba kingine na jumla yao wote wanne waliingia ndani ya chumba hiko na baada ya kuingia , jamaa mmoja wa kiafrika mnene , alifungua mlango uliokuwa umetegnenezwa kwenye sakafiu na mbao ngumu huku ukiwa na kufuri kubwa pembeni , baada ya kufungua mlango kwa kuvuta juu , alianza kutumbukia kwa kutumia ngazi kwenda chini.
“Sir ndio hawa hapa”Aliongea yule mwafrika aliefungua mlango baada ya wote kuingia ndani ya eneo hili la chini ya Ardhi ambalo halikuwa kubwa sana , ililikuwa ni saizi ya chumba , lakini kulikuwa kumejengewa vizuri na mawe, ni sehemu iliodhihirisha kweli ni eneo la Mateso na la kufungia wafungwa.
Mbele ya hao mabwana walikuwepo watu wawili wakiwa wamefungwa kwenye viti na Kamba na walionekana walipitia mateso kabla ya hao wazungu kufika hapo ndani , kwani wote walikuwa wamechoka sana na ngozi zo zilikuwa zimevilia damu,wote walikuwa ni wazungu pia mmooja akiwa ni mwanamke na mwingine akiwa ni mwanaume
“Ryani!!”Aliita yule mwanamke kwa sauti kubwa kiasi na kumfanya yule mwanaume wa kizungu alieinamisha kichwa kukinyanyua kivivu.
“Camilah!”Aliita Ryani kwa uchomvu sana , alionekana kumfahamu yule mwanamke wa kizungu ambaye sasa tunamjua kwa jina la Camilah.
“Ooh! Nikajua umenisahau Komredi Ryani , baada ya Zaidi ya miaka kumi na nne ya kupoteana”Aliongea huku akimsogelea na kuchuchumaa na kumwangalia mwanaume aliekuwa mbele yake kwa macho ya kumdadisi.
“Camilah , kwanini mnatufanyia haya?”
“Unajua kila kitu Ryani kwanini upo hapa pamoja na mkeo Epholia , mmefanikiwa kujificha kwa Zaidi ya miaka minne na hatimae tumeweza kuwakamata ,lakini licha ya hivyo bado hatujafanikiwa kwa asilimia zote kwani mmoja wenu hayupo hapa na ndio maana nimetoka Marekani mpaka hapa”Aliongea Camilah na Ryani aliekuwa amechoka pamoja na mke wake alienimanisha kichwa chini muda wote waliangaliana na kutingishiana vichwa kwamba wasiongee.
“Camila! Mwambie Powel anachokitaka kutoka kwetu hatokipata Kamwe. Miaka kumi na nne tulioweza kuishi nje ya Radar zake ni mingi sana na tupo tayari kulinda nyakati zote tulizoishi kwa vifo vyetu”Aliongea Ryan kwa namna ya msisitizo na kumfanya Camilah atabasamu na aliwapa ishara wale waafrika, mmoja amsogezee kiti na baada ya kiti kusogezwa aliketi.
“Ryani ujio wangu wa kufika hapa sio kwa jambo baya kama unavyonifikira n ahata hivyo tushawahi kuwa marafiki , nimekuja kuwaweka huru , hamtakiwi kujificha tena , yaliotokea miaka kumi na nne yalishapita”
“Kama kweli maneno yako ni ya kweli tufungulie tuondoke , kama una maswali yoyote ni tangulie kusema kama siwezi kukujibu”Aliongea Ryani na kumfanya Camilah atabasamu na kisha alimgeukia mzungu mwenzake na kumpa ishara na mzungu yule aliibuka na ‘Digital Camera’ na kumpatia na Camira mara baada ya kupewa ile Camera, aliiwasha na kisha moja kwa moja akaenda upande wa kuhifadhi picha na baada ya kufikiap icha alizokuwa akitaka , alimsogezea Ryan.
“Ryani haukuweza kujificha kama ambayvyo ulikuwa ukifikiria , tulikuwa tukikufuatilia kwa miaka yote tokea ulipokimbilia nchini Tanzania”Aliongea huku akimuonesha picha zake yeye na Epholia pamoja na mtoto wao wakiwa katika pozi la kucheka,Ryani hakuamini macho yake na Camilah wala hakujali mshangao wa Ryani , alichokifanya ni kutabasamu na kisha alifungua picha zingine Zaidi na Zote walionekana wao wakiwa na mtoto wao aliekuwa na makadirio ya miaka nane.
“Nadhani hizi picha unazitambua ,Hapa ni Naira alipokuwa na miezi Tisa , lakini ni mara yenu ya mwisho tokea muweze kumuona kabla hajapotea”Aliongea Camilah na kisha akaendelea kwenda mbele na kutafuta picha nyingine na baada ya kuipata alitabasamu na kisha akamsogezea Naira.
“Nadhani kama wazazi mtakuwa mmemkumbuka sana mtoto wengu tokea kupotea kwake, namimi kwakuwa najali hisia za wazazi kwenda kwa mtoto basi sina budi kuwaonyesha mtoto wenu akiwa na miaka kumi na moja”Aliongea Camira na kumzogezea tena Ryani na bwana huyu mara baada ya kuona picha ya mtoto wake wa kike aliefahamika kwa jina la Naira Machozi yalianza kumtoka , ni kweli alimtambua mtu aliekuwa kwenye picha ni mtoto wao ambaye alipotea alipokuwa na miaka tisa pekee ,Camila hakuishia kumuonyesha Ryani tu alimsogeleza na Epholia mke wa Ryani kumwangalia Naira , aliekuwa amevalia mavazi ya kitabibu akiwa ana tabasamu , alikuwa ni mwanamke mrembo haswa kwenye picha hio na Epholia ule unyonge aliokuwa nao ulimpotea ghafla.
“Where is our Daughter Camila”Aliongea Ryani kwa sauti kubwa awamu hii , lakni kwa Camilah aliishia kutabasamu
“Unaonekana upo tayari kutupa ushirikiano Ryan”Aliongea Camilah na umgeukia yule mzungu wa kiume na wote wakatabasamu.
“Camilah Naira wetu yupo wapi , tumemtafuta kwa Zaidi ya miaka mitano bila mafanikio , kumbe mmemchukua kwetu , Mungu awalaani”
“Hahahaha….,Ryani unaonekana asilimia tisini kuathiriwa na tamaduni za Kitanzania baada ya kuishi kule miaka mingi , nani wa kulaaniwa kati yetu na wewe uliempoteza mtoto wako”Aliongea Camilah na Ryani alimeza fumba la Mate , bwana huyu alikuwa na hasira mno , lakini pia alikuwa akitaka kumuona mtoto wake ambaye walimpoteza kwa Zaidi ya miaka Minne wakiwa nchini Tanzania , haikueleweka ilikuwaje mpaka wakampoteza na pia haikueleweka waliwezaje kufika nchini Tanzania.
“Camillah niambie unataka nini kutoka kwetu , ili tuweze kumpata tena Naira?”Aliuliza Ryani , alionekana yupo tayari kufanya jambo lolote kwa ajili ya kumpata mtoto wake Naira yeye na mke wake.
“Unatakiwa kurudi kazini Ryan na utashirikiana na sisi kutupatia taarifa zote za utoto wa Naira mpaka alipofikisha umri wa miaka Tisa”Ryani alijikuta akifikiriaa kidogo na kisha akamgeukia mke wake ambaye hakuwa na nguvu kabisa ya kuongea na wakatingishiana vichwa kukubaliana huku wote wakitokwa na machzi.
“Camillah tupo tayari”Aliongea Ryan na Camillah akatabasamu.
Hii ilitokea mwaka 2005 huko Mali Bamako , ilikuwaje wakafika nchini Mali na kufngiwa katika chumba cha Ardhi na waliishi vipi na Naira Tanzania?
SEHEMU YA 133
Ilikuwa ni baada ya Roma kumwachia mzee Alex , Upande wa nje wa jengo hili la JR alionekana Scorpion ambaye alikuwa amembeba Mzee Alex kama vile amebeba mtoto , huku mzee Alex akiwa amezirai na hakuonesha kuwa na aina yoyote yale ya majeraha kwenye mwili wake.
Baada ya Scorpion kumuingiza mzee Alex kwenye gari aina ya Toyota Corolla alitoweka eneo la tukio huku watu wakiendelea kushangazwa na tukio hilo lililotokea dakika chache nyuma.
Mage aliekuwa ndani ya ofisi alikuwa kwenye mshangao pia kwa namna tukio lilivyokuwa , haikuelewa ilikuwaje, kwani hata yeye wakati alipokimbilia dirisha na kuangalia chini aliona mzee Alex akiwa kwenye mikono ya mwanamke ambaye amevalia suti, wakati mrembo huyu anaendelea kushangaa simu yake ndogo iliokuwa kwenye suruali , ilianza kuita na akaitoa na kisha akapokea.
“Ndio Afande Ajenti flamingo hapa”
“Ajenti Flamingo nini kinaendelea?”
“Afande Hades alimrusha Mzee Alex kwenye Ghorofa”
“Unamaanisha nini Ajenti Flamingo”
“Nilishindwa kumuwahi kumuondoa Mzee Alex kabla ya Hades kufika na alimrushia chini ya ghorofa na bahati nzuri inaonekana kasalimiaka”
“Unamaanisha nini kasalimika wakati karushwa juu ya Ghorofa?”
“Kuna mwanamke ambaye inaonekana alikuwa chini na kamdaka na kuondoka nae”
“Kuna mwanamke kamdaka!! , ni nani huyo mwanamke?”
“Nimeshindwa kumfahamu afande nilikuwa juu kabisa ya ghorofa”Aliongea Magdalena lakini upande wa pili ulionekana kutokuelewa na walihitaji maelezo ya kutosha.
“Okey Ajenti ,Clear the Area na urudi makao makuu , nahitaji taarifa Zaidi”
“Sawa Afande”Alikata somu na Magdalena alimgeukia Matrida ambaye alikuwa bado amezirai chini ya Meza na kumuwekea mkono na aliona bado anapumua , lakini wakati huo huo aliingia Isaack.
“Tafuta msaada mumpeleke hospitali , kapata mshituko”Aliongea Magdalena na kutoka ndani ya ofisi hio , huku akimuacha Isaack kwenye mshangao na kumkimbilia Matrida alielala chini akiwa hajitambui.
Ukweli Roma aliguswa na namna ambavyo Matrida alikuwa akiomba baba yake asimuue na pia Roma aliona sio jambo zuri kumuua Mzee Alex mbele ya mtoto wake, lakini licha ya kuguswa hakutaka kumuaccha Mzee Alex pasipo kumpa onyo ambalo kamwe hawezi kulisahau na ndio maana akamuachia baada ya kuhisi uwepo wa mtu mwenye uwezo mkubwa wa nguvu za kichawi akiwa upande wa chini na kwa hisia zake tu aliamini mtu huyo atakuwa Scorpion kutokana na alivyokuwa akijua aina za mapigano na nguvu ambazo zinamilikuwa na ninja wote wa kundi la Yamaguchi.
Kwahio kumuachia mzee Alex alikuwa na uhakika kwamba Scorpion atafanya jambo kumuokoa Mzee Alex lakini wakati huo huo aliona pia ni jambo jema pia kumpa onyo Mzee Alex kwa kupata uzoefu wa kudondoka kutoka gorofa ya ishirin,na aliamini kwa tukio hil mzee huyu hatokuja kulisahau katika maisha yake.
Roma aliendesha gari yake kuelelekea kazini , huku akijiambia, muda na saa atakapomkamata Abubakari Hamadi ndio itakuwa siku yake ya mwisho wa kuliona jua , Roma hakutaka kuwatumia The Eagles kujua ni uelekeo gani ambao Abubakari yupo na pia alihisi kuenda Afande Maeda kwa kumtumia Ajenti Flamingo watakuwa washachukua tahadhari mapema na ndio maana akaamua kupotezea kwa muda , lakini huku upande mwingine Sababu ya kumuua Abubakari zikiwa nyingi , kwani aliamini kwa taarifa iliosambaa siku hio mtandaoni lazima atakuwa pia na yeye amehusika kwa asilimia mia moja.
Roma alikuwa na mpango wa kwenda kuona hali inavyoendelea kwenye kampuni na pia kuhakiki kama mke wake ameweza kutatua tatizo ambalo lilikuwa linaendelea kwenye kampuni.
Wakati Roma anaegesha gari yake eneo la maegesho ya wafanyakazi wa kampuni alikutana na Nadia ambaye na yeye alionekana ndio alikuwa akiingia kazini, Roma alitabasamu baada ya kumuona Nadia na haikueleweka mara moja alikuwa akiwaza nini kwenye kichwa chake mara baada ya kumuona mrembo huyu na Kwa Nadia hivyo hivyo alitabasamu kwa kumuona Roma eneo hili.
“Hades!!”Aliita Nadia baada ya kumsogelea Nadia.
“Tupo kwenye kampuni niite Roma”Aliongea Roma na kumfanya Nadia atabasamu.
“Napenda uhalisia wako unaotokana na jina la Hades”Aliongea Nadia.
“Kama unapenda uhalisia wangu wa jina hilo , basi unaishi kizamani kwani jina hilo nishaliacha kwa sasa”
“Sio kweli”
“Kwa vigezo gani Nadia”
“Roma ni jina lako la kawaida , utambulisho ambao unataka watu wakuone mtu wa kawaida lakini kwa ninavyokuangalia hauwezi kuwa wa kawaida hata kidogo na mwisho wa siku utaishia kutumia utambulisho wako wa Hades”Roma alitabasamu kidogo.
“Unaonekana unajua kile kinachoendelea kwenye kampuni Nadia Alfonso”Aliongea Roma na kumfanya Nadia atabasamu.
“Usisahau kwamba licha ya wewe kunisaidia kupata ushahidi Nchini Korea Kusini na kuua maadui 34 waliotaka kumfunga Kim , akili yangu ndio iliotumika kwa asilimia mia kuufanya ushahidi uwe na nguvu mbele ya ‘Court’ na Kim kupata haki yake”
“Sikatai hilo Nadia, ila swali langu kwanini ukaja kufanya kazi ndani ya kampuni ya mke wangu,maana kutokana na ukubwa wako ni jambo pia la kufikirisha uwepo wako ndani ya Vexto?”Aliuliza Roma bila ya kupepesa macho na kumfanya Nadia akose utulivu.
“Hades nadhani ushajua sababu kwanini nipo ndani ya kampuni ya mkeo, yote ni kutaka kuwa karibu yako”
Aliongea Nadia bila aibu huku akimsogelea Roma, lakini kwa upande wa Roma alishindwa kujua acheke au alie, maana hakuwaelewa hawa wanawake kwa wakati mmoja.
“Unauhakika upo kwa ajili yangu?”Aliongea Roma na kumfanya Nadia asitishe kile alichokuwa akitaka kufanya.
“Unahisi kwanini nipo hapa?”
“Nadia nakuona kama mwanamke mwenye wivu na ndio maana nina wasiwasi na ukaribu wako kwa mke wangu , natumaini hautanifanya nikasirike mbeleni”Aliongea Roma na kisha akapiga hatua kuelekea upande wa kuingilia ndani ya jengo hili na kumfanya Nadia aliesimama ajiulize kwanini Roma kamuambia yale maneno , mwanadada huyu alianza kujishuku na kujihisi huenda mipango yake imegundulika.
“Hapana huenda ni hisia zake tu , hawezi kugundua kuwa nina mpango wa kuwafanya waachane , muda wote nimekuwa makini kwa kila hatua ninayopiga”Aliongea Nadia huku akiogopa maneno ya Roma kwa wakati mmoja , mrembo huyu licha ya kwamba alikuwa akimpenda Roma lakini alikuwa akijua upande wa pili wa Roma , kwani aliweza kuwacharanga mapanga Zaidi ya wanasiasa 34 wa Korea kusini pasipo huruma kwa ajili tu ya kupata ushahidi juu ya kesi iliokuwa ikimwandama Raisi Kim.
Roma alienda moja kwa moja mpaka ilipokuwa ofisi yake ya PR , alitaka kujua ni nini kinaendelea, kwani tokea atoke asubuhi hakupata kufatilia , baada ya kuingia ndani ya ofisi hii aliona wafanyakazi wenzake wakiwa kwenye hali ya kawaida na kwa jinsi alivyowaona tu , alijua lazima kila kitu kipo sawa na hali ya kampuni imerudi katika ukawaida wake.
Lakini licha ya kuaangalia wafanyakazi wenzake kwa macho ya kuwadadisi na wao walikuwa wakimwangalia Roma kwa macho ya mshangao ni kama walikuwa wakijiuliza huyu mwanaume alikuwa wapi muda wote huo wao wakiwa na presha juu ya jambo ambalo limetokea juu ya kampuni na Roma hakujali macho ya mshangao ya warembo hao Zaidi ya kutabasamu na kumpungia mkono kila mmoja.
“Boss ndio unafika kazini kwa raha zako”Aliongea Recho kuvunja ukimya wa mshangao wa wenzake.
“Recho acha maneno yako nilikuwa mgonjwa”Aliongea Roma huku akitabasamu.
“Nani wa kukuamini , hata hivyo huna mchango wowote ,na tulishakusahau”
“Kwahio mrembo unamaanisha haujanimisi na hautaki kuniona?”
“Nani!! mimi , kwanini nikukumbuke mwanaume suruali kama wewe , labda Nasra asie na pakwenda”Aliongea Recho na kumfanya Roma amkumbuke Nasra ni muda mrefu kidogo hakuwa amemuona mrembo Nasra.
“Nasra anaingiaje tena??”
“Unajifanya hujui , Mtoto wa watu kila saa anakuja kuchungulia kama umefika kazini , leo kaja kama mara tatu”Aliongea Recho na kumfanya Roma kushangaa , lakini pia hata yeye kujiona mkosaji , ni kweli alikuwa kwenye mahusiano na Nasra lakini hakukumbuka hata kumpigia simu , Roma alifikiria kidogo na kisha akanyanyuka na kumfanya Recho abetue midomo na kusonya , alijua Roma anaenda ofisini kwa Nasra .
Lakini sasa wakati Roma anaingia kwenye lift simu yake ilianza kuita mfululizo na kumfanya aitoe na kuangalia nani anaempigia na aligundua ni Sophia aliekuwa akipiga , alipokea na kuweka sikioni.
“Kuna mgeni wako”Aliongea Sophie moja kwa moja mara baada ya Roma kupokea na Roma alijikuta akitabasamu kwani alihisi ukisirani kutoka kwa Sophie
“Sophia ni nani huyo mgeni?”
“Simfahamu , ila ni bora ukarudi mapema kabla ya Sister Edna hajarudi”Aliongea Sophia na kisha akakata simu na kumfanya Roma afikirie kidogo na aliona ngoja aghairishe kwenda kuonana na Nasra na arudi nyumbani , alitaka kujua ni mgeni gani huyo ambaye anamfahamu yeye mpaka kwenda nyumbani kwake.
SEHEMU YA 134
Ni ndani ya ofisi ya ikulu ya taifa la Kenya anaonekana mheshimiwa Kamau Kamau akiwa ndani ya ofisi akiendelea na majukumu yake , huku mbele yake akiwa amesimama katibu muhtasi wake , Mheshimiwa huyu alioneskana kuna karatasi ambazo alikuwa akisaini kwani alipitia kila ukurasa na kisha kutia saini yake , kitendo ambacho kilidumu kwa takribani dakika kama kumi hivi mpaka kumaliza na kisha akamkabidhi katibu muhtasi wake hilo faili na akaondoka, lakini wakati huo huo wakati Katibu Muhtasi akitoka aliingiia Deo akiwa na faili mkononi.
“Mheshimiwa nimepata taarifa zote zinazomuhusu Roma”Aliongea Deo kwa heshima na kisha akamsogezea mheshimiwa faili na mzee huyu aliangalia faili hilo kwa madakika kadhaa kwa kulisoma na kisha akaweka chini , huku akionyesha hali ya mshangao kidogo.
“Hii Taarifa ni ya kweli Deo?”
“Ndio mheshimiwa , nido nilvyoweza kupata kwenye Data Base ya Taifa ,licha ya kuonyesha kusomea ndani ya chuo cha Harvard lakini hakuna taarifa nyingine”Aliongea Deo.
“Vipi kuhusu familia yake?”
“Mheshimiwa nadhani haujaangalia vizuri faili nimeambatanisha mwisho”Aliongea Deo kwa heshima na Mheshimiwa Kamau alichukua tena faili na kufungua ukurasa wa mwisho.
“Huyu Roma….!!”
“Ndio mheshimiwa anaonekana kulelewa ndani ya familia ya Tajiri Robert Eglon kutoka Michigani”Aliongea Deo na Mheshimiwa Kamau alirudisha chini lile faili na kuvuta pumzi kidogo.
“Unaweza kwenda kuendelea na majukumu yako Deo”Aliongea Mheshimiwa Kamau na Deo aliinama kwa heshima na kisha akageuka na kutoka ndani ya ofisi ya mheshimiwa Kamau.
“Kama ni kweli aliwezaje kuwadhibiti walinzi wote kwa wakati mmoja, maelezo ya walinzi hayaendani kabisa na wasifu huu”Aliwaza mheshimiwa kidogo na kisha akachukua simu yake kati ya nne zilzokuwa mezani aina ya Sumsung na kisha akapiga.
“Ndio Mheshimiwa Kamau Kamau”Ilisikika sauti nzito kutoka upande wa pili.
“Nataka ufatilie jina la Roma Ramoni , amelelewa ndani ya familia ya tajiri Roert Eblon Marekani , nahitaji utafutaji uwe wa haraka “Aliongea kwa Lugha ya kingengeza na kisha akakata simu.
******
Upande mwingine ndani ya Rwanda siku hii hii ya Ijumaa muda wa saa tisa mchana , alionekana Tajiri Mohamed Azizi akiingia ndani ya ofisi ya ikulu ya mheshimiwa Jeremy , baada ya tajiri huyu kuingia huku leo hii akiwa amepigilia suti yake ya rangi ya majivu , walisalimiana na mheshimiwa Jeremy kwa bashasha sana na kisha wote wakaketi.
“Niambie Jeremy , nimeshangazwa na wito wako , kuna jipya gani umegundua?”Aliuliza Tajiri Mohamedi Azizi huku akimwangalia Rafiki yake Jeremy.
“Azizi najua ulikuwa nchini Hispania na huna taarifa zote ya kile kinachoendelea nchini Tanzania?”
“Ni kweli kabisa Jeremy Project ya kibiashara ilionipeleka Madrid imechukua muda wangu mwingi , lakini namshukuru Mwenyezi kwa kuniwezesha,Vipi unaonekana kuwa na jambo ambalo unataka kuniambia Jeremy liweke wazi , ili nikirejea Tanzania nisiwe na maswali mengi”
“Blandina karudi Tanzania na kaonana na Mzee Atanasi”Aliongea Jeremy na kumfanya Tajiri kushangaa.
“Sina kabisa hio taarifa,Jeremy na sijui kwanini Jestina hajaniambia?”
“Nadhani yatakuwa ni maelekezo ya Baba yake , ila ndio hivyo washaonana na wanajua sasa hivi Maina ndio Blandina”
“Nini kiliendelea?”Aliongea Azizi huku akionyesha kidogo mkunjo wa sura , alikuwa na hasira kwanini swala kubwa hivyo la kifamilia hakuwa na taarifa nalo , kwani kila siku alikuwa akiwasiliana na mke wake.
“Inaonekana kabla ya Mzee Atanasi kwenda kuonana na Blandina washaongea na DS ya Tanzania na Kenya na walishafikia kwenye maamuzi”Aliongea Raisi Jeremy na kumfanya Azizi kuvuta pumzi.
“Jeremy nadhani hii sio jambo pekee ambalo umeniitia?”Aliongea Jeremy.
“Ni kweli Azizi nadhani mpaka sasa unafahamu fika kwamba Taifa la Kenya ndio pekee ambalo halikubaliani na mpango TASAC na mheshimiwa kutoka Urusi amekuwa wakunilazimisha niharakishe sana hilo swala”
“Ndio naelewa kabisa, lakini naona ni kama wanakupa presha bure kwani mpaka sasa hakuna jambo kubwa ambalo wamelifanya kwa upande wao”
“Ni kweli , lakini mwezi uliopita walinitumia ushahidi ambao umenifanya nione, ukweli unakaribia kutoka”Aliongea na kumfanya Azizi kushangaa.
“Unamaanisha nini?”Aliuliza na Mheshimiwa Jeremy aliinuka na kuvuta bahasha kwenye meza yake na kisha akatoa picha pili na kumpatia Tajiri Azizi na alianza kuziangalia.
“Hizi ni…”
“Hio picha ya kwanza ya mtoto imepigwa mwaka 1998 m nadhani unaona kabisa hapo chini kuna tarehe na hio ya pili vile vile imepigwa mwaka 2007”
“Unamaaisha hawa watu wote ni mtu mmoja na kwanini kama naona sura ya Hades?”.
“Ndio hio sura ni ya Roma Ramoni ambaye sisi na watu wachache wanamfahamu kama Hades na hizo picha zimetumwa na shirika la kijasusi la Urusi(FSB) kwa maelekezo kutoka Kremlin”Aliongea mheshimiwa Jeremy na kumfanya Tajiri Azizi kushangaa.
“Jeremy unamaanisha….”
“Ndio huu ni ushahidi pekee ambao unathibitisha kupotea kwa ndege ya shirika la M Arline ni tukio la kupangwa”Aliongea na kumfanya Tajiri Azizi aone pointi hio ina mashiko ndani yake.
“Sasa nini kinafuatia baada ya huu ushahidi?”
“Ndio maana nimekuita tuonane , nataka hizi picha ukaonane na Mzee Kweka”Aliongea na kumfanya tajiri Azizi kushangaa.
“Jeremy unamaanisha unataka kumpatia hizi picha baba yake Mheshimiwa Senga! ,kwanini?”Aliuliza tajiri na kumfanya Mheshimiwa Jeremy akunje nne kwanza.
“Ni Rahisi sana Azizi , Senga kwa sasa hawezi kuhimili ukweli wote , ila kwa Mzee Kweka ni rahisi kuhimili lakini pia hili swala nataka niliingize kwenye DS ya Tanzania”Aliongea Mheshimiwa Jeremy na kumfanya Tajiri Azizi kuvuta pumzi.
“Lakini mpaka sasa sijaelewa malengo ni nini , maana sidhani DS wataguswa sana na swala hili”Jeremy alitabasamu.
“Azizi kuna mambo ambayo bado sijakuambia , unajua licha ya kwamba wewe ni rafiki yangu lakini pia nina ukomo wa kukuambia mambo ya kiserikali”
“Ndio naelewa Jeremy na sijawahi kulalamika juu ya hilo , mbona unajihami”Huku akitabasamu.
“Niambie Azizi kwa mfano DS ya Tanzania wakipatiwa faili halisi , nazungumzia lile lenyewe linalohusiana na Roma unafikiri watachukua uamuzi gani?” Tajiri Aziiz alionekana kuwaza.
“Sikia Azizi usifikirie sana , hebu mchukulie Hades kiiashara utaelewa pointi yangu”
“Hahaha,,, DS watataka kumfanya Hades mtu wao”
“Hio ndio point yangu Azizi, lakini kabla ya kuwapa faili lote linalomuhusu Roma , nataka kwanza wapate kumjua Roma ni nani, kazaliwa wapi na baba yake halisi ni nani , hii itawapa nguvu kuingia kwenye mpango ninaotaka mimi, ni kama nawaongezea Motisha, na nikwambie tu mpaka sasa hivi Jeshi la Tanzania limeonyesha nia ya kumtaka Hades kuwafundisha wanajeshi mbinu zake za kivita zinazomilikuwa na kundi la The Eagles”Aliongea na kumfanya Azizi ashangae kidogo kwani hakuwa na uelewa wa hilo jambo.
“Vipi kuhusu Blandina , nadhani inapaswa ajue kama mtoto wake bado yupo hai”
“Hilo analifanyia kazi Linda , tunachotaka kwa sasa hivi ni kuhakikisha kwamba Roma aliesafiri kwa shirika la Ndege la M Airline ndio Denis, tukiwa na mashuhuda ya watu wengi ni Rahisi kuweka ukweli wazi pasipo ya Marekani kupinga na wataweka wazi nyaraka zinazohusiana na mpango LADO wenyewe”
“Ni kweli kabisa , Lakini Jeremy ushatambua sasa Roma ndio Denisi na walipanda ndege moja na Lorraine kwanini usingeanza kufatilia kwanza habari za Lorraine na kujua kama yupo hai au hayupo hai”
“Ninatamani sana kujua Azizi , lakini kutokana na kwamaba huu ni mpango mkubwa siruhusiwi kuingiza hisia katika kufanya maamuzi , nitafanya kila jambo kwa hatua na uhakika , japo mpaka sasa hivi najikuta kuwa ni mwenye hisia mbaya juu ya Lorraine”Tajiri Azizi alionekana kumuelewa sana rafiki yake, baada ya maongezi yalidumu takribani lisaa limoja kuisha Azizi aliaga huku akimwambia Jeremy anawahi msiba wa kitafia wa mwanasayansi nguli duniani aliekufa kicho cha kutatanisha
SEHEMU YA 135
Roma aliendesha gari yake kuelekea nyumbani , bwana huyu alikuwa na hamu ya kutaka kujua ni mgeni gani ambaye amekuja moja kwa moja nyumbani kwake , kwani Roma alikuwa sio mtu wa kufahamika sana na hivyo kuwa na mzunguko wa watu wachache sana , lakini pia ni watu wachache sana ambao wanafahamu sehemu ambayo alikuwa akiishi.
Roma baada ya kufunguliwa geti na Derick aliingiza gari yake na kwenda kuegesha sehemu maalumu huku akiangalia ongezeko la magari , lakini hakukuwa na gari yoyote iliokuwa imeongezeka na kujiuliza huyo mgeni kaja bila usafiri nini.
Alishuka na kupiga hatua kuelekea ndani na ile anaingia ndani alijikuta akisikia vicheko vilivyokuwa vikitoka sebuleni.
Upande wa eneo la Sebuleni walionekana watu watatu wote wakiwa ni wanawake lakini mtu alieongezeka leo hii hakuwa wa kawaida kutokana na urembo wake , lakini pia pamoja na rangi yake , huyu hakuwa mwingine bali alikuw ani Profesa Clark Stephanie mtoto wa Malkia wa Wales , mwanamke mrembo na maarufu sana ndani ya bala la ulaya na duniani kote kutokana na uzuri wake , lakini pia mafanikio yake ya kielimu aliofikia katika umri mdogo.
“Profesa Clark ndio aliekuwa wa kwanza kumuona Roma akiingia kutokana na sehemu aliokuwa amekaa kuwa rahisi kuona mlangoni na ile anamuona tu Roma alinyanyuka na kumkimbilia na kwenda kumkumbatia na kuwafanya Sophie na Bi Wema kushangaa.
“Karibu Nyumbani”Aliongea Profesa Clark kwa lugha ya Kiswahili na kumfanya Roma atamani kucheka na rafudhi ya Profesa Clark, alijiuliza huyu mrembo wa kizungu amejifunzia wapi kuzunguma Kiswahili.
“Clark umewezaje kugundua mahali ninapoishi?”
“Ushasahau mimi ni nani Roma?”Aliongea Clark na kuona kweli kauliza swali la kijinga maana ktuokana na uwezo wa Profesa Clark ni jambo rahisi sana kujua taarifa za mtu.
Sophie aliekuwa akimwangalia Roma na Profesa Clark wanavyoongea , alijikuka akiwa ni mwenye wivu sana, ukweli kama mwanamke kuna kitu ambacho alikiona kwenye macho ya Profesa Clark , mwanadada huyu aliona mapenzi ya waziwazi ya Profesa Clark kwenda kwa Roma.
“Pole kwa kumpoteza Senior na mwalimu wako Clark”Aliongea Roma kwa Kingereza na kumfanya Clark ageuke na kuelekea upande wa masofa na Roma alifatia huku akimsalimia na Bi Wema.
“Roma sisi tutaenda kuandaa chakula , unaweza ukaongea na mgeni wako”Aliongea Bi Wema huku akimpa ishara Sophia anyanyuke na Sophia alijikuta akimwangalia Roma halafu akajinunisha na kunyanyuka.
“Tanzania ni nzuri sana Roma , nadhani najua ni kwasababu gani umechagua kurudi kwenye nchi yako”
“Tanzania inaonekana kuwa nzuri, ila mimi tokea nifike ndani ya hili taifa najua baadhi ya sehemu tu , hivyo siwezi kuzungumza sana juu ya kuisifia”Aliongea Roma na kumfanya Clark atabasamu , huku akimwangalia Roma kama daktari anaemchunguza Mgonjwa na alionekana kuridhika.
“Kifo cha Profesa umekipokeaje Clark?”
“Nimekipokea kwa mshangao , lakini naweza kusema ni kama nilitegemea”
“Kwanini uansema ni kama umetegemea?”
“Unajua Roma Profesa alikuwa akiandamwa sana na watu wengi kutokana na gunduzi aliokuwa nayo,wakiwemo marajiri, wanasiasa na wanasayansi”
“Kuna tetesi nilizosikiaga kipindi juu ya mambo ya Ant-Matter Energy , unataka kuniambia ni kweli zile tetesi?”
“Ni kweli kabisa na hilo aliniambia Profesa mwenyewe baada ya kunikabidhi baadhi ya Formula nijaribu kuzifanyia kazi na niseme ukweli baada ya mwezi mmoja wa utafiti wangu nimeona kununi zake kihesabu zinafiti kwa asilimia kubwa sana , licha ya kwamba utekelezaji wake kwa hapa Duniani ni mdogo mno”Aliongea Profesa huku akionyesha hali ya huzuni.
“Unamaanisha nini ni mdogo?”
“Moja ya hitaji kubwa kwa kanuni zake kufanya kazi ni Madini yenye haiba ambayo kwa hapa Duniani hayapatikani na kwa maelezo ya Profesa, Marekani ndio taifa pekee ambalo wanamiliki jiwe la madini hayo”
“Unamaanisha madini yanayotoka kwenye GodStone?”Aliongea Roma na kumfanya Clark ashangae , alijiuliza inakuwaje Roma akajua hio habari.
“Unaonekana kufahamu uwepo wa madini hayo Roma?” Aliongea na kumfanya Roma atabasamu.
“Yeah! Nimesikia baadhi ya habari juu ya jiwe la Godstone, lakini Clark ukiachana na maswala ya Godstone unamfahamu vipi Yan Buwen?”Roma aliona achomekee swali la Yan buwen kwa muda huo , kwani kutokana na kwamba Yan Buwen alikuwa moja ya wanafunzi ambao wapo chini ya Profesa Clark , basi ni lazima agekuwa anamjua Zaidi kuliko watu wengine , haswa likija swala linalohusiana na taaruma yake,Clark alionekana kushangaa , lakini pia kusikitika kwa wakati mmoja.
“Yan Buwen naweza kusema kati ya wanafunzi wangu ambao nimefundisha yeye ndio wa kipekee sana, uwezo wake wa kuchanganua mambo ulikuwa mkubwa mno na alielewa kila nilichokuwa namfundisha na Zaidi”Aliongea Profesa Clark kwa huzuni na Roma aligundua hilo.
“Lakini mbona unaongea kama hujivunii kuwa na mwanafuzni kama Yan Buwen , kuna shida iliotokea kati yenu?”
“Yeah!,Baada ya Yan Buwen kumaliza masomo yake ya ngazi ya juu hakutaka tena kunitambua kama mwalimu wake na hakunisikiliza kwa lolote , yaani upole wake na unyenyekevu ulikuwa ni kipindi akihitaji nimsimamie katika PhD yake , lakini baada ya kuhitimu alidiriki kuniambie yeye ana akili Zaidi kuliko mimi , ili niumiza”Aliongea Profesa na kufanya Roma kweli aone kama ni hivyo Yan Buwen anao uwezo asilimia zote za kumuua Profesa Shelukindo.
“Roma umemfahamu vipi Yan Buwen?”
“Yupo hapa Tanzania na ninao vijana wangu wa kijeshi walikuwa wakimfatilia kwa kila hatua ili kubaini ni jambo gani ambalo limemleta Tanzania , lakini kutokana na watu aliokutana nao tunakisia kwa asilimia kubwa ndio kahusika na mauaji ya Profesa Shelukindo “Aliongea na kumfanya Clark kushangaa mno.
“Clark unahisi ni kwanini Yan Buwen kamuua Profesa?”Aliuliza Roma huku akimwangalia Clark ambaye bado alikuwa kwenye mashangao.
“May Be ni kwasababu ya kanuni ya Ant- Matter Energy”
“Kwanini unahisi hivyo?”
“Nakumbuka mara ya mwisho nilivyowasiliana na Profesa Shelukindo ,nilimgusia kuhusu Yan Buwen na alichonijibu sikukitilia maanani nilidhani hisia za Profesa zilikuwa ni kama zangu tu”
“Alikujibu nini?”
“Alisema kwenye moja ya makosa aliofanya basi ni kuwa mwanafunzi wa Yan Buwen”Aliongea Clark na kumfanya Roma achakate kwanza hayo maneno kwenye akili yake ili kuyapatia maana.
“Lakini Clark Profesa si aliacha kujihusisha na maswala ya kiutafiti baada ya kurudi Tanzania?”Swali lilimfanya Clark akili yake sasa kufanya kazi.
“Hapana ,Mara ya mwisho wakati nawasiliana na Profesa Shelukindo kwa njia ya Vidio alikuwa kwenye maabara”
“Maabara!! Unamaanisha alikuwa anaendelea na utafiti wake?”Aliuliza Roma na Clark alitingisha kichwa kukubali na mpaka hapo Roma aliona kabisa basi huenda Yan Buwen yupo Tanzania kwa ajili ya kukusanya Tafiti za Profesa Shelukindo na kama ni hivyo basi huenda mpaka sasa Yan Buwen huenda amepata kile alichokuwa akikihitaji lakini licha ya hivyo aliamini bado yuko mbali na mafanikio kwani kama ni kweli yupo kwa ajili nya kanuni ya kutengeneza Ant-Matter Energy hawezi kufanikiwa mpaka awe na Godstone.
“Clark uliweza kufahamu sehemu ambayo alikuwa akifanyia utafiti wake?”
“No Hakuniambia na pia sikumuuliza”Alijiu na kumfanya Roma afikirie kidogo na kuona hili ni swala ambalo linatakiwa kufanywa na wanajeshi wake na alifanya mawasiliano muda huo huo na kuwapa kazi hio The Eagles kufuatilia.
Chakula cha mchana kiliwekwa mezani na Bi wema alimkaribisha Clark na Roma Mezani , Clark alionekana kuzoeana na Bi wema huku akitumia Kiswahili chake cha kuunga uunga na haikueleweka alijifunza lini na hata Roma alishangazwa na hilo, baada ya chakula kuisha Roma na Clark walitoka nje na kukaa sehemu ya Bustani na kuendelea na Stori zao za kukumbushia baadhi ya mambo waliokuwa wamefanya na kwa jinsi wawili hawa walivyoonekana ni Dhahiri kabisa walifahamiana tokea wakiwa watoto , kwani walikuwa na Stori nyingi ambazo zote zilihusisha kipindi wakiwa watoto.
Saa kumi na mbili za jioni hivi wakati Roma wakiwa bado wapo nje , mara simu ya Roma ilitoa mlio na haraka haraka aliitoa na kuangalia ni nani aliekuwa akimpigia na aliona jina ni la Chiara na aliweka sikioni haraka haaka maana Chiara hakuwa mtu wa kupiga labda kama kuna tatizo ambalo limemtokea mke wake.
“Your Majesty……”