Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Mpk Jumapil bado tu asee, saiz naichungulia Holla Daah huu uraibu sasa inabidi nipambanie asee unitoke
 
SEHEMU YA 202

Kitendo cha Stern kumaliza sentensi yake , upande wa huku kwenye kambi ya jeshi , Prince Sargaras ,Sauroni , Fodesa na wengine walionekana kushangaa mno , kasoro kwa upande wa Roma ambae muda wote alionekana kumjua Stern kama mwenzake katika Sehemu ya Malejend kumi na mbili wa Miungu ya Kigiriki .

Katika historia ya Kigiriki , Apollo anafahamika kwa sifa nyingi , anafahamika kama mungu wa Mziki , mungu wa kucheza , mungu wa jua ,mungu wa kuponya magonjwa na mungu wa mishale, ndio maana hata Depney aliigiza kutumia mshale ili kujifanyisha yeye ni Apollo , lakini vile vile akatumia ‘Sun Gold Totem’ hii ni alama ambayo inamilikiwa na Apollo na ndio iliokuwa ikimtambulisha kama sehemu ya miungu kumi na mbili kama ilivyokuwa kwa Roma na pete yake ya Aides, hivyo hakuna ambaye aliweza kuamini kama Stern kutoka kwa Crommwell family alikuwa ndio Apollo.

“Mbona mnashangaa au mnaona naigiza , yaani Handsome kama mimi mnashindwa kuniamini kama ni Apollo na mtu mwenye sura mbaya kama Roma kuwa Hades”Aliongea Stern kama kawaida yake akiweka utani.

“Hehe..Unajiita Handsome lakini ukaishia kwa dada yako , unatia aibu Apollo”aliongea Roma.

“Bora mimi ninaemkula dada yangu kuliko wewe kukujike unaemuogopa mkeo”Aliongea Apollo na maneno yalimwingia Roma kisawa sawa na kupiga mguu chini kwa hasira na kusababisha mtetemeko.

“Nimewaruhusu mumfuate fuate mke wangu na kula chakula cha bure na hakuna hata siku mliotoa shukrani zenu na sasa naona unanitukana”Aliongea Roma kwa hasira

“Niwe tu mkweli sisi ndio tulikuwa walinzi wa Persephone,tena kama isingekuwa kwa mkeo kuwa na moyo mzuri, mimi na Alice tusingejihangaisha na mipango yako, Kuja Paris nilitaka kumbutua huyu mpuuzi aliekuwa akiigiza kuwa mimi na kunajisi jina langu”Aliongea Stern.

Prince Sargaras mwenyewe alikuwa kwenye mshangao , licha ya kuishi miaka mingi duniani kama Vampire , lakini hakuwahi kudhania Stern ndie Apollo. Ila kwa upande wa Lilith alionekana kuwa na furaha mno kutokana na uso wake.

“Hata kama wewe ni Apollo unadhani unaweza ukanishinda”Aliongea Depney aliekuwa amesimama mita kadhaa kutoka kwa Apollo, akiwa ameshikilia mshale wake ule wa mwanzo.

“Unafikiri na siraha zenu hizo mnaweza kunishinda , let me show you the real divine weapon of Apollo.”Aliongea Stern na palepale aliinua mikonoo yake yote miwili kwa wakati mmoja na kusimama kama Roboti.

“Heliosiiii!!!”

Aliongea Stern kwa nguvu kubwa na palepale macho yake yalibadilika rangi na kuwa kama jua linalocheza cheza na kumfanya kuonekana kama kiumbe cha ajabu kweli na hata Nadia na wanajeshi wengine waliokuwa juu ya Meli walisogea nyuma kwa woga.

Maneno yake yaliambatana na moto ambao ulionekana kushuka kutoka juu kama Kimondo na kufanya eneo lote la baharini kuwa na mwanga kama mchana, ule mwanga ambao ulikuwa kama umeme ulikwenda kutua kwenye kidole cha katikati cha mkono wake wa kushoto na kutengeneza tufe kama vile mpira mfano wa mpira wa kuchezea kikapu na Stern alianza kuzungusha lile tufe kimwangalia Depney kwa macho ya kumkejeli.

Eneo lote lililikuwa na joto sio la kawaida kiasi kwamba Stern ilibidi awatengenezee ngao wengine kama ilibyokuwa kwa Edna huku wanajeshi wakimwachia Nadia na Sten alimpa ishara ya kusogea sehemu ambayo Alice alikuwa amelala chini na palepale alijikuta akiwa ni kama vile amevalishwa PPE za hospital zinazotumika kujikinga na maradhi kama vile Korona.

Depney kabla tu hajarushiwa tufe lililokuwa likizunguka kwenye kidole cha Stern alijikuta akihisi joto ambalo sio la kawaida , ni kama vile alikuwa jangwani na jua kali linamuwakia.

“Hio..ni..”Depney alikosa uvumilivu , ilibidi kuuliza.

“Hii ni siraha inafahamika kwa jina la Helios , huu mpita ni Zaidi ya teknolojia ya Thanatos , ndio maana sisi Miungu hatukuwa na mpango wa teknolojia ya Thanatos na kuwaachia nyie binadamu muigombanie”Aliongea Stern.

“Kwenye historia ya malejend wa kigiriki , nilichokuwa nikifahamu mungu wa jua yupo katika migawanyo mitatu , Hyperion, Helios na Apollo , lakini kwanini Apollo anaweza kuita nguvu zake kwa kutumia neno Helios?”Aliuliza Prince Sargaras aliekuwa kwenye mshitko.

“Hyperion , Helios na Apollo ni mtu mmoja “Aliongea Roma pasipo kumwangalia Prince Sargaras , Roma alitaka kujua ni nini Stern anataka kukifanya kwa Depney.

“Ndio maana hukuwa na wasiwasi na mkeo Edna , kumbe huu ni mpango ambao ulikuwa umeandaa na Apollo tokea mwanzo?”Aliuliza Lilith.

“Ndio, baada ya kutekwa na kupelekwa msituni mimi Pamoja na mke wangu kuwakuta Stern na Alice wakiwa sehemu ya mateka nilishangaa na kujiuliza kwanini na wao wamekubali kutekwa, lakini niligundua wana mpango wao ndio maana nilijifanyisha kutowajua , lakini baada ya kutoka ndipo walipoenieleza juu ya mpango wao , lakini niliona mpango huo usingefakisha kujua wahusika wote , hivyo niliwapa mbinu mpya ambayo kidogo ilichukua muda , na mpango wangu ulifanikiwa kwa asilimia kubwa kwani tumeweza kugundua uhusika wa Wavatican”Aliongea Roma na haikueleweka ni lini aliongea na Stern , lakini aliacha maswali bado kwa waliokuwa wamemzunguka.

“Mfalme Pluto umeweka nafsi ya uwingi , hivyo kama Stern ni Apollo na Alice ni…?”Aliuliza Sauroni huku wote wakimgeukia kutaka majibu , lakini Roma hakutoa jibu zaidi ya kuwaashiria waendelea kuangalia kinachoendelea.

Kwenye meli sasa Depney ukweli hakuwa na pakukmbilia mpaka muda huo na aliona ni bora kufa akijitetea , alichokifanya ni kuchukua upinde wake na mshale na kisha kuufyatua kwa nguvu kuelekea kwa Apolo lakini palepale Apolo mwili wake ni kama umeongezeka ukubwa mara tatu , huku akiwa na mdomo kama wa Dragoni na alipanua mdomo wake na ule mshale ukaingia mdomoni , ni kama vile ameumeza na palepale akarudi kwenye hali yake ya kawaida akiwa mzima kabisa .

“Sina pakukimbilia hapa , nishaingia cha kike na leo sidhani kama nitachomoka,ila nategemea nguvu ya kichawi ya kitambiko iliopo kwenye huu upinde naamini utanikinga na mota wa jua”Aliwaza Depney huku akimwangalia Apolo.

Na Apollo halutaka kumchelewesha Depney kwani palepale alirusha lile tufe mkononi mwake kuelekea aliposimama Depney na kufanya wanajeshi waliokuwa mita kadhaa kuinama chini kwani wlaiamini lazima na meli ingezama.

Lile tufe lilikuwa ni kama bomu la kurusha na mkono kwani ilimfunika Depney na moto mwingi kiasi kwamba hakuonekana kabisa, lakin baada ya sekunde kama ishirini na tano hivi , moto uliisha , lakini Depney alionekana kuwa hai huku akionekana kukosa nguvu kabisa, lakini pigo lilionesha kutokuwa na athari kubwa kwake..

Apollo aliangalia upinde uliokuwa kwenye mikono ya Depney na kutabasamu.

“Inaonekana huo mshale umejaa nguvu za mizimu ndio maana umeweza kukinga moto wa Helios , lakini haimaanishi kwamba nitakuacha hai”Aliongea Apollo huku akijiandaa kuachia pigo lingine Kwenda kwa Depney, lakini ni kama amechelewa kwani kabla hajarusha.

!Crack, Crack ,Crack!

Ilikuw ani kitendo cha ajabu ambacho kilitokea kwani Depney alianza kugeuka barafu huku akibanduka banduka kuanzia kwenye vidole vya miguu Kwenda juu, huku akirusha rusha chembe chembe za barafu na kusababisha mlio wa mvunjiko kama wa chupa hivi na tukio hilo la kustaajabisha lilidumu kwa dakika moja na Depney aligeuka na kuwa kama sanamu lilotengenezwa kwa barafu ngumu na kudondoka chini na kupasuka vipande vinne huku baadhi ya vipande vikitumbukia baharini na huo ndio ukawa mwisho wa Depney.

“Mpenzi kwanini hii tabia yako ya kutaka kurudia rudia mapigo hupendi kuacha mpaka unanilazimisha kumgandisha na barafu , kila siku nakwambia tumia pigo moja tu mpenzi”Aliongea Alice alienyanyuka alipokuwa amelala na kumsogelea Stern.

“Artemis! dada yangu kipenzi usinilaumu mimi , haya yote ni kutokana na mpuuzi Hades, kama asingeniambia juu ya kuacha kwanza tufahamu ni siri gani Depney anaificha ningeshammaliza muda tu , lakini hapa nimempiga pigo dogo , ili na wewe umalizie”Aliongea Depney akimwita dada yake, Artemis na hapo swali la Sauron lilijibiwa vyema , Alice alikuwa ni sehemu ya miungu kumi na mbili akifahamika kwa jina la Artemis.
 
SEHEMU YA 203

THE HAGUE -NERTHERLAND​

The Hague ni jiji ndani ya taifa la Uholanzi, Serikali yote ya taifa la Uholanzi maamuzi yote hufanyikia ndani ya The Hague,Mji mkuu wa taifa la Uholanzi ni Amsterdam ni kama hapa Tanzania Dodoma na Dar Es salaam, The Hague uaarufu wake unatokana na kuwa na mahakama kuu ya haki ya kimataifa(ICC).

Sasa siku na saa ambayo Roma Ramoni wakiwa ndani ya kambi ya Jeshi ya Le Havre lakini pia Depney akiwa baharini na mateka kwenye meli ya kivita , upande wa Uholanzi kwenye jiji la The Hague kuna mkusanyiko wa kikao Kizito cha siri kilichokuwa kikiendelea, kikao ambacho kilikuwa kikiongozwa na The First Black, ni kikao kilichokuwa kikihusisha mataifa ishirini yenye nguvu duniani , kasoro Urusi peke yake ambayo haikuwa kwenye kikao hiko.

Muundo na mpangilio wa ukumbi ambao mkutano huu ulikuwa ukifanyikia , ulikuwa ni kwa usanifu wa herufi Zero , yaani kulikuwa na meza moja ambayo imechongwa kwa muundo wa herufi Zero huku Viongozi wote wakubwa waliohudhuria ndanii ya kikao hiki wakiwa wamezunguka meza hio huku mbele yao kukiwa na bendera na jina la nchi husika.

Katikati ya hilo eneo kulikuwa na Skrini za Tv, jumla nne zikiwa zimefungwa nakuwapa nafasi viongozi wote kuangalia kile kilichokuwa kikionyeshwa kwenye hizo Skrini.

Naam jambo ambaloo lilikuwa likionekana kwenye hizo Skrini ni tukio la kigaidi lililokuwa likiendelea ndani ya Ufaransa , tukio ambalo liliongozwa na Apollo .

“F*****ck , So this was all Depney Doing?”Aliongea mwanamke mmoja mwenye umri wa makadirio ya miaka hamsini Kwenda sitini hivi alievalia miwani ,na hii ni mara baada ya Depney kuvua lile Helmet na kufanya viongozi hawa wamuone.

“Miss Eunice calm down it`s done now..”Aliongea First Black mwakilishi wa taifa la Marekani akimsihi Mellisa ambaye alikuwa ni Waziri mkuu wa Ufaransa , aliekuwa ndani ya kikao hiko kuwakilisha taifa lake.

Ni Takribani dakika kama kumi na tano hivi kupita , huku viongozi hawa wakiendelea kuangalia , mara wote kwa Pamoja waliamka kwenye viti vyao na kusimama na kuanza kupiga makofi, kitendo ambacho kilidumu kwa takribani dakika tano na kuketi chini.

“Okey!, Nadhani kila mmoja ameona namna ambavyo Artemis , Apollo na Hades walivyodhibiti magaidi?”Aliongea First Black na viongozi walirudia kupiga makofi na The First Black aliinua mkono juu kuashiria kutulia. Halafu akaendelea.

“Haya yote ni mafanikio ya mipango ambayo imeasisiwa na viongozi wenzetu ambao wametutangulia , kwa kuunda shirika hili la The Zeros Organisation, Shirika ambalo ndio tumaini la usalama wa dunia”Aliongea na wakapiga wote makofi tena kwa heshima ya waasisi wa kundi la The Zeros halafu akaendelea.

“Licha ya mafanikio haya ambayo yametokana na michango ya hali na mali kutoka kila taifa, nikiri kwamba bado tunatatizo moja mpaka sasa”Aliongea na kufanya viongozi wote kutulia kimya na akaendelea.

“I have prepared a Presentation, which will be part of the Agenda of this sixteenth session since the birth of Zeros organization”Aliongea akimaanisha kwamba ameandaa uwasilishaji ambao utakuwa ni sehemu ya Ajenda kwenye kikao hiko cha kumi na sita tokea kuundwa kwa Zeros Organisation.

“Mr First Black, what do you think before your presentation,to tell us who is The Doni and how to control him, that is the question that brought us to this place”

Aliongea Shekhe mmoja kutoka Saudi Arabia ambaye ni mtoto wa Mfalme wa Saudi Arabia lskini pia anacheo cha Waziri mkuu , bwana huyo alimwambia The First Black Kwenda moja kwa moja kwenye jina la The Doni na namna ya kumdhibiti na watu wengi hapa ndani walionekana kukubaliana nae, na First Black kabla ya kuendelea na uwasilishaji wake ambao ungekwenda kuwa Ajenda za kikao, aliona aende moja kwa moja kuelezea jina la The Doni.

“Kuhusu The Doni mpaka sasa hatujaweza kupata jina lake kamili , lakini utafiti wetu pamoja na makisio ambayo tulifikia chini ya uchunguzi wa The Zeros, lakini pia tukio ambalo limetokea siku hii ya leo limetuweka karibu Zaidi na kumtambua The Doni”

“Lay it open Mr First Black”Aliongea Waziri mkuu kutoka Uingereza na First Black kwanza alitabasamu.

“Hatumfahamu The Doni ni nani lakini tunaamini kwa aslimia sabini anapata Msaada kutoka Vatican”Aliongea First Black na kufanya viongozi wote wamwangalie kwa macho ya mshangao na ya kutoelewa.

*******

Ni wachache kati ya wengi waliokuwa wakielewa juu ya miungu watu , hivyo hata wakati Apollo anamuita Alice kwa jina la Artemis walijikuta wakiwa kwenye mshangao mkubwa, Prince Sargaras, Vampire alieishi miaka Zaidi ya mia mbili mwenyewe hakuwa na uelewa juu miungu watu na aliishia kushangaa kama wengine.

Hawakuamini wapenzi ambao walikuwa ndugu kutoka Cromwell Familly walikuwa ni sehemu ya miungu watu kumi na mbili.

Alice na Stern kama kawaida yao , baada ya Depney kugeuka barafu na kudondokea baharini , walikumbatiana na kuanza kupigana mabusu , jambo ambalo lilimkera Roma kwani aliona wanachelewesha muda na mke wake hakuwa amekula muda mrefu.

“Nyie watu hebu acheni huo upuuzi kwanza mtafanya baadae”Aliongea Roma kwa kuamrisha , na Alice aliekuwa akiangaliana nao moja kwa moja alimuachia Apollo na kisha kumwangalia Roma.

“Hades, now that everything has essentially ended, bring the cruise Louis XVI over to us, and sink this warship afterward.”

“Hades Mpaka sasa kwakua kazi ishaisha , leta hio meli ya kifahari ya Luois XVI mpaka tulipo na uzamishe hii meli ya kivita baada ya hapo”Aliongea Alice lakini maneno yake yalikuwa ni kilio kwa wanajeshi ambao walikuwa ni wa Depney , ukweli kutokana na jambo ambalo wamelishuhudia kutoka kwa Depney kugeuzwa barafu , lakini pia nguvu ya Apollo , waliona hawawezi kujitetea kwa namna yoyote ile na ndio maana waliishia kupatwa na wasiwasi , lakini wasiwasi wao ulizidi baada ya Alice kusema Roma apelekee meli na kuzamisha ile ya kivita.

Alice alimwachia Apollo na kisha kuanza kuangalia mazingira ya meli hii huku nywele zake za kizungu zikipeperushwa na upepo, lakini sasa muda uleule hali ilianza kubadilika , kwani wanajeshi walianza kuhisi baridi kali isio kuwa ya kawaida na kitendo kile kilimfanya Apollo awaongezee ngao Edna na wengine ili wasidhurike na baridi lile na ni ndani ya sekunde ishirini tu wanajeshi walibadilika na kuwa kama masanamu yaliotengenezwa na barafu , huku eneo lote la Baharini pia maji kuganda na meli ya kivita kubadilika na kuonekana kama chakavu

Waliokuwa wakiangalia kwa kupitia Skrini kasoro Roma , wote waliishia kuwa kwenye mshangao , hawakuamini Alice alikuwa na uwezo wa kutengeneza mabarafu ya aina hio ndani ya dakika moja , lilikuwa jambo la kushangaza kwao na kuna muda Lilith na baba yake waliona hawa miungu watu walikuwa wakifanya makusudu kwa ajili ya kudhihirisha uwezo wao na aliona kama kweli nia yao ilikuwa hio basi wameshashinda , kwani kwa uwezo huo aliona asingewezakupambana nao hata kidogo.

“Hades kwa ninavyofahamu Artemis ni mungu wa Uwindaji , Asili na Mwezi, kwanini ana uwezo wa kugandisha vitu kwa barafu?”Aliuliza Prince Sargaras.

“Hakuna mungu wa barafu kati ya miungu yote kumi na mbili , kama ilivyo usiku kuwa ni wakati wa baridi , ndivyo ilivyo mchana kuwa wakati wa joto, Diana ndio jina halisi la Kirumi la Artemis, na kuhusu kuweza kudhibiti barafu mimi mwenyewe sikuwa na uelewa huo , lakini kwasababu Apollo ni mungu wa jua na kuweza kudhibiti joto inawezekana pia kwa mungu wa mwezi kudhibiti baridi”Alijibu na akaendelea.

“Ukweli ni kwamba haijalishi nani anaweza kudhibiti hiki na kile , lakini kinachojalisha ni makusudio ya nguvu ambazo mtu kuwa nazo , kama una nguvu na unafanya uharibifu basi hazina maana”Aliongea Roma , lakini mazungumzo yao yalionekana kusikika upande wa pili wa meli.

“Ni kweli mwanzoni sikuwa na uwezo wa kudhibiti barafu , lakini ilibidi nijifunze baada ya kupoteza upinde wangu wa mshale wa kiuungu unaofahamika kwa jina la Selene , baada ya kupambana na Athena”Aliongea Alice.

“Bebi usijali sana , sasa hivi pia una uwezo mkubwa , nitahakikisha uniapata siraha yako baada ya kumuua Athena”Aliogea Alice.

“Bebi sidhani kama hilo linawezekana , yule mwanamke ana nguvu isiokuwa ya kawaida, nilipopambana nae mara ya mwisho hakutumia hata siraha yoyote ya kiuungu lakini aliweza kunishinda , hata tuungane Pamoja kupigana nae tutapoteza pambano”Aliongea Alice na kumfanya Roma kushangaa juu ya hilo na kuingia kwenye mawazo.

“Au mtu alienipokonya HollyGraill ni Athena, kama ni yeye kwanini atumbie mbinu za kujificha?”Aliwaza Roma kwenye kichwa chake huku wote wakitoka ndani ya chumba cha mawasiliano kwa ajili ya kuingia kwenye meli ambayo iliwaleta.

Roma na Wenzake walikuja kushangaa mara baada ya kugundua wageni waliokuja nao hapo ndani walikuwa washaondoka na meli ile tayari ya kuachwa wao kisiwani.

“Fodessa mimi ninao uwezo wa kusafiri ndani ya bahari bila ya kutumia meli , ila kwa wenzangu hilo ni jambo ambalo hawawezi, naamini kwa ukubwa wa hii kambi hapakoseni meli nyingine au boti?”Aliuliza Roma baada ya kumgeukia Fodesa,

“Ndio Mfalme Pluto , kuna meli ya mizigo hapa kambini , subirini hapa nitaenda kuileta mwenyewe maana najua kuiendesha”Aliongea Fodesa huku akiwaacha wenzake kwa jili ya kuleta meli.

Baada ya Fodesa kuondoka , Sauroni alimsogelea Roma , akiwa na kiboksi cha teknolojia ya Thanatos mkononi.

“Mfalme Pluto haujanipa maelekzo bado juu ya hii teknolojia”

“Endelea kuishikilia Sauroni , baada ya kufika Paris wakabidhi wanajeshi wa The Eagles waipeleke ndani ya kisiwa cha Wafu na wamkabidhi Ron kwa ajili ya kuihifadhi”

“Mfalme hutembelei kisiwani awamu hii?”

“Haapana Sauroni sitoweza kutembelea kisiwa kwa muda, nipo hapa Paris na mke wanggu na tupo kwa ajili ya biashara , hivyo tutarejea Tanzania mapema tu , lakini pia kuna mambo mengi yanaendelea ndaini ya Tanzania yananihitaji”Aliongea Roma

Roma alikuwa hajakamilisha kazi yake ambayo ilimfanya kuingia Tanzania , bado hakuwa ameweza kukutana na familia yake na hilo ndio jambo ambalo lilikuwa limempeleka Tanzania , hivyo ilikuwa ngumu kwake kurudi ndani ya Visiwa vya wafu kabla ya kukamilisha kuipata familia yake.
 
SEHEMU YA 204

Dakika chache mbele Fodesa aliekuwa akiendesha meli ya mizigo ya jeshi , alifika sehemu waliokuwa wamesimama na kuwaruhusu wote kuingia na kuanza kuchukua uelekeo wa sehemu ambayo walikuwa wakiamini ndio Depney na genge lake walipokuwa wamesimamisha meli ya kivita.

Iliwachukua Zaidi ya lisaa limoja mpaka kufika eneo husika , lakini Fodesa alishindwa kuendelea mbele kwani eneo lote lilikuwa ni barafu kutokana na kitendo cha Alice alichokifanya cha kunganisha maji.

“Mtasubiria hapa , nitaenda mwenyewe na nitarudi muda si mrefu”aliongea Roma huku akinyanyuka na kuacha kundi lote katika mshangao baada ya kupotea mara baada tu ya kumaliza Sentensi yake.

Ni kufumba na kufumbua Roma alikuwa juu ya meli , huku akiwakuta Stern na Alice wakiwa kwenye ulimwengu mwingine wa mahaba , licha ya eneo lote kuwa na baridi kali , lakini kwa Stern na Alice halikuwaathiri,

Roma alimwangalia Edna aliekuwa amelala huku akiwa amefunikwa na ngao ya kiuungu aliotengenezwa , alitumia uwezo wake kumkagua na kuona yupo sawa ni kwamba tu yupo kwenye usingizi , alimwangalia na Nadia ambaye pia alikuwa amefunikwa na kuona yupo sawa , baada ya Roma kuona hali za mateka wote ziko sawa , aliwasogelea Alice na Stern.

“Depney yuko wapi?”Aliuliza Roma.

“Hades kwani kuna ulazima wa kumuhoji nishamuua mimi?” Aliongea Alice.

“Kumuhoji ni lazima, nadhani unajua fika Depney aliweza kushambulia kambi za jeshi za NATO amabazo zinalindwa na ulinzi mkubwa sana , jambo ambalo kwa kundi la kigaidi la kawaida wasingeweza kufanya”Aliongea Roma na pointi yak eina mashiko kitendo cha Depney kujifanyisha Apollo na kuweza kushambulia kambi za jeshi la NATO na lile la EU halikuwa jambo dogo kwani kambi hizo hulindwa na teknolojia kubwa.

Na ukumbuke pia tulimuona Depney akigandishwa kwa barafu na sanamu lake la barafu kudondoka chini na baadhi ya vipande kudondokea baharini.

Alice alitabasamu na kisha akamwachia Stern na kusogea mpaka alipokuwa amesimama Depney mwanzo na kisha alitumia mkono wa kulia na kupanua kiganja na kulenga eneo sehemu ileile na alianza kuongea lugha ambayo haikuwa ikieleweka ,kwa sauti ya chini sana,

Nadia ambaye alikuwa amesimama hakuwa akielewa kinachoendelea , lakini hakuweza kusikia sauti kutokana na kuwa ndani ya mfuko ambao haukumuwezesha kusikia sauti za nje , wakati akiendelesa kushangaa, alijikuta mwili wake ukilegea na kudondoka , lakini kabla hajatua chini Roma alikuwa ameshamfikia kimazingara na kumshikilia na kisha akamuweka chini.

“I only killed his Physical Body not his soul”Aliongea Alice akimaansiha kwamba amemuua Depney mwili wake wa nje tu na sio roho yake au nafsi.

“Umefanya vizuri Alice , sikutaka watu wengine wafahamu tunachokwenda kuongea na Depney”Aliongea Roma na palepae kulitokea ‘Hologram’ yenye muonekano wa Depney , kama alivyokuwa dakika chache nyuma kabla ya kugandishwa na Alice , lilikuwa ni tukio la ajabu kweli kuonekana kutokana na kwamba hakuwa Depney kimwli bali alikuwa ni Depney kiroho.

Na ilionekana Alice alifanya vile kwa ajili ya kuwaaminisha Fodesa na wenzake kwamba Depney ashakufa kabisa.

“Hades unazo dakika kumi na tano tu kumuhoji , siwezi kuzuia Roho yake duniani kwa Zaidi ya dakika hizo”Aliongea Alice baada ya kurudisha Roho ya Depney iliokuwa kwa mfumo wa Hologram.

Hologram kisanyansi ni picha iliotengenezwa kwa kutumia vyanzo vya mwanga wa pande tatu(Dimension) ambazo zimeingiliana, nimetumia neno Hologram kukupa picha halisi ya kile ambacho amekifanya Alice kumuwezesha Roma kuongea na Roho ya Depney,Sasa hapo ni jambo lingine la kushangaza kwa Alice kuweza kuzuia Roho ya mtu aliekufa kwa dakika kadhaa kabla ya kuiruhusu kuchukua safari nyingine.

Maneno ya mtu anaekata roho siku zote yamejaa ukweli , hivi ndivyo Roma alitegemea kwani Depney alikuwa tayari ni mfu hivyo asingeweza kuongea neno lolote la uongo kwa wakati huo na haikuhitajika nguvu nyingine ya ziada ya kumfanya Depney kuongea ukweli.

“Depney tuambie ukweli wewe ni nani haswa, kwanini unauwezo mkubwa sana kiasi cha wewe peke yako kuweza kulipua kambi za NATO , Huwezi kuwa mjinga kwa kufanya kitendo cha kujiigiza kuwa Apollo,Kwanini mwili wako ulikuwa na nguvu za ziada?”Aliuliza Roma na Depney ambaye alionekana kama vile picha ya kwenye Televisheni yenye chenga kutokana na mtandao mbovu alimwanngalia Roma kwa sekunde.

“Nishakufa tayari , hivyo sinabudi kukuambia ukweli”Aliongea Depney kwa Kingereza na kisha akaendelea.

“Nimepata uwezo wangu mkubwa kwa kupitia Divine Light”Alionea Depney na kumfanya Roma kushangaa mno.

“Divine Light?, You were shone on by the divine light?”

“Devine Light , Ulipingwa na Mwanga wa kiuungu?”Aliuliza Roma.

“Ndio Hades , mbona unaongea kama huniamini?”

“Endelea kuongea..”

“Over thirty years ago, I was captured along with other youths of the same age to an underground research base in Madagascar to be used as test subjects. I’m am sure you are well aware of the organization and their experiments,”

“Miaka therathini iliopita , nilikamatwa Pamoja na vijana wenzangu wa umri sawa na kupelekwa ndani ya kambi ya Ardhini kisiwani Madagascar ili kutumika kama sehemu ya majaribio , nadhani unatambua taasisi hio Pamoja na majaribio yao?”Aliongea Depney na kumfanya Roma kushangaa Zaidi.

“Zeros Organisation!!?!”Aliuliza Roma kwa wasiwasi. ,Alikuwa akijua hio taasisi ya siri ya Zeros kwani hata yeye alipitia humo na ashafanyiwa pia hayo majaribio kwenye mwili wake.

Mawazo ya Roma yalimrudisha nyuma siku ambayo aliweza kuharibu kambi hio ya Zeros iliokuwa ndani ya visiwa vya Madagascar , alikuwa akikumbuka majaribio yaliokuwa yakifanyika ndani ya kambi hio, yalikuwa yakiendeshwa kwa kutumia Godstone, yaani mwanga uliozalishwa na Godstone ndio ambao unafahamika kwa jina la Divine Light, hivyo Roma baada ya kufaulu kupita kwenye majaribio hayo jambo ambalo liliwezekana kufanikiwa baada ya kupitia mateso kwenye kisiwa ambacho hakuwa akikifahamu , kisiwa kilichopewa jina la LADO.

Yaani kwa maneno marahisi ni kwamba Roma aliweza kupata uwezo wake aliokuwa nao kwa kupigwa na mwanga ambao unatoka kwenye jiwe la kimungu na jambo hilo liliwezekana kwake baada ya kupitia operesheni ya kwanza iliopewa jina la LADO(Life and Death Operation)

“Ukweli ni kwamba mimi ni jaribio la kisayansi lililofeli , sijui nini kilichotokea kwa hao wanasayansi vichaa ,ila nilijikuta siku kadhaa mbele baada ya majaribio , nikiwa katikati ya maiti za vijana wenzangu tukiwa tumetupwa na mpaka leo hii sikuelewa nini kilichotokea mpaka wanasayansi wakashindwa kufahamu kama sikuwa nimekufa”Aliongea Depney ambaye alikuwa kwenye mfumo wa roho.

Stori ya Depney ilikuwa hivi , wakati alivyokuwa mdogo alikamatwa na kupelekwa ndani ya visiwa vya Madagascar kwa ajili ya kutumika kama sehemu ya majaribio kama ilivyokuwa kwa Roma chini ya taasiisi ya Zero , lakini utofauti ni kwamba Depney ndie aliekuwa wa kwanza kufanyiwa majaribio kipindi hicho, hivyo wanasayansi hawakuwa na mafanikio makubwa Zaidi ya kila waliekuwa wakimjaribu kummulika na mwanga wa Divine Light uliotoka kwenye jiwe la kimungu , watu wote waliishia kufa na Kwenda kuwatupa sehemu maalumu, lakini wasichokuwa wakijua ni kwamba Depney hakuwa amekufa kama walivyokuwa wamedhania

Depney kutokana na sehemu alipokuwa amemwagwa kama maiti, kutokana na kuwa mbali na kambi hio ya Zeros alishindwa kurudi kambini.

Licha ya kwamba majaribio hayo ya kisayansi hayakuwa yamekamilika kwa asilimia mia moja lakini Depney alijihisi mwili wake kutokuwa kawaida kama ilivyokuwa mwanzo na alijihisi kuwa na uwezo usio kuwa kawaida.

Na kwanzia siku alivyoweza kuruid Ufaransa Maisha yake yaliendelea na alijiunga na jeshi , lakini katika mawazo yake alikuwa na mpango wa kulipiza kisasi kwa kile alichofanyiwa , yaani kuilipua kambi ya Zeros, lakini sasa baada ya miaka kupita na kupandishwa cheo na kuwa kiongozi mkuu wa kitendo cha usalama wa taifa ndio alipoweza kugundua kuwa kambi ya Zeros iliokuwa ndani ya kisiwa cha Madagascar ishalipuliwa

Lakini licha ya hivyo hakutaka kuishia hapo , alikuwa na mwili uliokuwa na nguvu kuliko mtu yoyote wa kawaida , hivyo tamaa ya kutawala watu wasiokuwa na uwezo kama wake ilimvaa na hapo ndipo alipoanza kufanya maajabu kama vile kulipua kambi za jeshi za NATO , EU na kufanya utekaji hii yote ni kutaka kutawala kutokana na kujihisi kuwa kama sehemu ya miungu watu , hata pale alipoweza kunusa uwezo wa teknolojia ya Thanatos iliokuwa ikimilikiwa na serikali ya Ufaransa, alipata mchecheto na kuanza kupanga mpango wake wa kuipata teknolojia hio kwa mpango maalumu ambao kutokana na uwepo wa Apollo , Artemiss na Hades ilishindikana.

Kwahio mpaka hapo nadhani unaelewa sasa kwanini Godstone ilikuwa ikiwindwa na watu wengi , ni kutokana na nguvu iliokuwa ikitoka kwenye jiwe hilo inaweza kumfanya mtu kuwa god’s.

“Okey Depney asante ka maelezo yako ,tusalimie huko uendako”

“Naomba msiniue”

“Haha,, ushakufa tayari , licha ya kwamba tumeweza kuzuia roho yaku kwa madakika kadhaa , haimaanishi kama tunao uwezo wa kukurudishia mwili wako , huo uwezo upo nje ya uwezo wetu”Aliongea Roma na palepale Alice alinyoosha mkono wake na roho ya Depney ilipotea.

Lakini sasa wakati Roma akiwa ameangalia upande wa baharini , mara alihisi kitu ambacho sio kawaida nyuma yake na ile anageuka alimwona Edna akiwa amesimama.
 
SEHEMU YA 205

TANZANIA

Ni siku nzima mheshimiwa Senga hakuonekana kabisa ndani ya ofisi yake , tokea jana yake kupewa taarifa kubwa sana kutoka kwa baba yake ,taarifa iliokuwa ikihusiana na Blandina Pamoja na mtoto wake Denisi ambao alikuwa akiamini kwa Zaidi ya miaka ishirini walikuwa wamekufa na ajali ya ndege.

Mheshimiwa alikuwa kwenye maumivu makali mno , hakuamini rafiki yake alieshibana na kupambana nae katika kutafuta Maisha alikuwa ndio aliemfanyia hayo mpaka kumficha mwanamke aliekuwa akimpenda kwa moyo wake wote.

Mheshimiwa Senga hakuwa kwenye hali nzuri hata kidogo , alikuwa kwenye majonzi na majuto , kama sio ujasiri wake na uwezo wa kuhimili maumivu mpaka wakati huo huenda angekuwa ashafanya jambo baya sana.

Sasa ni muda wa saa kumi za jioni , mheshimiwa Senga alikuwa ndani ya chumba chake cha kulala akiwa amepumzika huku mawazo yakiendelea kumuandama.

Mheshimiwa Senga baada ya kulala kitandani kwa muda akiwa peke yake , alitoa shuka aililokuwa amejifunika na kisha akashuka chini na kusogelea simu yake iliokuwa mezani na baada ya simu kuwa kwenye mikono yake , alitafuta jina na kisha akapiga na kuweka sikioni.

“Ndio mheshimiwa”Ilisikika sauti upande wa pili.

“Kabwe fanya maandalizi , kesho asubuhi nitakwenda Kenya”Aliongea mheshimiwa.

“Sawa mheshimiwa”Ilisikika sauti kutoka upande wa pili na hapo hapo mheshimiwa Senga alikata simu na kuirudisha sehemu husika na ile anageuka kuruid kitandani , mlango wa chumba hiki kikubwa ulifunguliwa na mke wake Damasi aliebeba juisi mkononi.

“Senga naomba unywe hii juisi na ikiisha nieleze bila ya kunificha jambo lolote , kwanini upo hivi”Aliongea Damasi First Lady wa Tanzania huku akimwangalia mume wake alieonekana kuwa katika hali ya unyonge.

Ukweli tokea asubuhi Mama Ashley alikuwa akimsisitiza mume wake kumueleza nini kinaendelea , kwani alikuwa amebadilika mno tokea alipotoka na Kwenda kuonana na baba yake , Mama huyu alielewa kabisa kuna jambo ambalo limetokea nyumbanni kwa baba yake ambalo ni kubwa ndio maana likabadilisha hali aliokuwa nayo mume wake , lakini licha ya kumsihi Senga kumwambia juu ya jambo hilo , lakini mume wake hakuwa tayari kuongea na hakupenda pia kumlazimisha , lakini mwanamama huyu aliumia sana kwani alikuwa akimpenda mno mume wake kiasi kwamba yupo tayari kufanya lolote kwa ajili ya Senga baba wa Watoto wake.

Senga kabla hajamjibu mke wake aligeuka na Kwenda kukaa kweye sofa lililokuwa ndani ya hiko chumba chao wanacholala na kisha akamwangalia Damasi mke wake.

Na Damasi baada ya kuona Senga kakaa kwenye sofa ,ilimbidi kuweka kwanza juisi kando na kusogea kwenye sofa lingine na yeye kuketi , huku akimwangalia mume wake ambaye alionekana kuwa katika maumu.

“Senga maumivu yako ni maumivu yangu , naomba uniambie ni kipi kimekusibu mume wangu”Aliongea Damasi na Senga alimuonea huruma mke wake , kwani aliona wasiwasi aliokuwa nao.

“Damasi Blandina na Denisi wapo hai”Aliongea Senga na kumfanya Damasi aonekane kama hakuwa amesikia vizuri , alikuwa akijua historia ya Maisha ya nyuma ya Blandina na mtoto wake Denisi , historia ambayo ilikuwa na hitimisho la kifo kwa wawili hao , lakini sasa hivi kuambiwa kuwa watu hao walikuwa hai ni swala ambalo lilimshangaza mno.

**********

Edna alionekana kushituka baada ya Roma kumaliza kuongea na Roho ya Depney, Ngao ambayo ilikuwa imemfunika haikuwa imetoka mwilini , ilimzunguka baada ya kusimama.

Roma alimwangalia Edna ambaye alionekana kama mtu ambaye amepoteza kumbukumbu kabisa na kutokumbuka chochote , kwani licha ya Edna kuwa katika mazingira ambayo hayakuwa ya kawaida , lakini alionekana kutokuwa kwenye mshangao Zaidi ya kumkodolea macho Roma kama mtu aliekuwa akishangaa.

Roma alimsogelea Edna mpaka alipokuwa amesimama na kisha akachukua mkono wake, lakini ajabu ni kwamba Edna hakuleta upinzani wa aina yoyote ile Zaidi ya kumwangalia Roma ambaye alikuwa amemshikilia.

“Kuna kitu hakipo sawa kwa Edna”Aliwaza Roma , kwani alikuwa akimjua sana Edna vizuri na kwa jinsi ambavyo Roma alikuwa amemshhika Edna ,ingekuwa Edna yupo sawa angekuwa ashatoa mkono wake kwake , lakini hapa Edna alikuwa akimshangaa Roma pasipo kufanya chochote na alionekana kama mtoto.

Roma alitumia mkono wake wa kulia na kisha alimshika Edna mashavuni na kuingiza nguvu isio ya kawaida kwenye mwili wa Edna kwa ajil ya kumuacha na joto baada ya kutoa ngao iliokuwa imewekwa na Stern, lakini licha ya Roma kuweka mikono yake kwenye mashavu ya Edna , alionekana kutoleta shida kabisa , Edna aliendelea kumshangaa Roma kama vile hakuwa akimfahamu.

“Edna..!!!”Aliita Roma lakini Edna hakuonekana kuitikia Zaidi ya kuendelea kuangalia tu.

“Stern mke wangu anatatizo gani?”aliuliza Roma.

“Hehe…Mfalme Pluto sisi kazi yetu ilikuwa ni kumlinda tu mkeo , lakini kuwa katika hali hio hatufahamu”aliongea Stern na kumfanya Roma aone huenda Edna yupo kwenye mshituko.

Basi Alice na Stern ilibidi wasaidiane kuwabeba Harry Pamoja na mama yake , huku upande wa Roma alimbeba Nadia ambaye alikuwa usingizini bado pamoja na Edna na kuwarudisha kwenye meli ya mizigo.

Na Fodesa alifurahi sana kuunganishwa na familia yake kwa mara nyingine na safari ya kuanza kurudi Le havre bandarini ilianza mara moja , safari iliotumia lisaa tu walikuwa washafika.

Roma baada ya kufika bandarini alimtoa Edna na kumuongoza mpaka kwenye gari alilokuwa amebaki mita kadhaa kutoka ilipo bandari na kisha akamwingiza huku Nadia na Pamoja na Harry walichukuliwa na kupelekwa hospitalini na wanajeshi waliokuwa wapo bandarini wanasubiri.

“Wife pumzika kwanza hapa nitarudi ndani ya muda mfupi”Aliongea Roma na Edna hakumjibu Zaidi ya kuendelea kumwangalia kwa kumshangaa , lakini Roma hakujali , kwani alifunga mlango na kisha akarudi bandarini alikowaacha wengine , ilionekana alikuwa na mambo mengine ya kufanya.

Bandarini pale kulikuwa na wanajeshi wengi ambao walikuwa wametunwa na serikali ya Ufaransa baada ya taarifa kutolewa kwenye mamlaka na wale walioweza kurudi , hivyo ulinzi ulikuwa ni wa aina yake.

Fodesa alikuwa akihojiwa na mkuu wa majeshi ya Ufaransa na aliweza kueleza kila kitu kilichotokea kwa kudanganya baadhi ya mambo , kwa mfano Fodesa hakuweza kusema kama Alice , Roma na Stern walikuwa ni Miungu watu , hilo alikaa nalo moyoni na hio ni baada ya kupewa maagizo hayo na Roma.

Swala la miungu watu lilikuwa ni swala la siri sana ndani ya dunia , hivyo watu wachache sana walikuwa wakilifahamu , na kama dunia itajua uwepo wao , huenda ikaleta shida na ndio maana Zeros walikuwa wakihakikisha swala hilo linabakia siri.

Stern na Alice waliendelea na magizo yao na kufanya wanajeshi wengi wasiwazingatie na kuwaona kama watu waliokuwa wamerukwa na akili , walikuwa wakijua stori zote za familia ya Cromwell kuwa na hao ndugu ambao ni wapenzi , jambo ambalo kwao waliona ni kama chukizo kwa Mungu aliowaumba.

Sifa zote za kuangamizwa kwa Apollo zilienda kwa Roma , na hio ni kutokana na maelezo aliotoa Fodesa baada ya kujohiwa juu ya kile kilichotokea ,na serikali ilielewa maelezo hayo mafupi na kuahidi kujadili swala hilo kwenye vikao, na baada ya maelezo hayo ilibidi baadhi ya makundi ya kijasusi yaanze kuondoka , kwani muda wote walikuwa ndani ya hilo eneo kutaka kujua muafaka wa kile kilichokuwa kikiendelea kambini baada ya wao kukimbia.

“Mr Roma , unaonaje tukiongozana mpaka nyumbani kwangu , ukaone jumba la kifahari lililojengwa maiaka Zaidi ya elfu moja iliopita?”aliuliza Prince Sargaras.

“Sina mpango wa kuona jumba la miaka elfu moja mimi , unapaswa kurudi kuuguza jeraha lako lililosababishwa na siraha ya Gabriel Lance of Longinus”aliongea Roma.

“Ni kweli kabisa mfalme shukrani ziende kwako kwa kutusaidia , hakika siku moja tutalipa wema uliotutendea”Aliongea Prince Sargaras , lakini Roma aliishia kutabasamu huku akijiambia hana mpango wa kupokea shukrani kutoka kwa Vampires ,baada ya Pince Sargaras Pamoja na Lilith kumuaga Roma na kuondoka,Sauroni alimsogelea Roma kwa ajili ya kuagana nae huku mkononi akiwa ameshikilia Teknolojia ya siraha ya Thanatos.

“Mfalme Pluto kwanini teknolojia hii usikae nayo”aliuliza Sauroni , ni kama hakuwa akiamini amini kama Roma alikuwa amemruhusu kuondoka na hio teknolojia, kwani licha ya kuwa mshirika wa Roma , lakini aliamini Teknolojia hio inaweza kuwa salama Zaidi akikaa nayo mwenyewe.

“Sauroni hii kampatie Ron aitunze kwa muda mpaka siku nitakaporudi visiwa vya wafu na tutanngalia namna ya kuitumia kwa wanajeshi wetu”Aliongea Roma.

Ukweli Fodesa hakujali tena kuhusu Thanatos , aliona haina haja ya serikali yake kukaa nayo , hivyo aliacha the Eagles waendelee kubaki nayo na isitoshe pia Apollo na kundi lake walikuwa washadhibitiwa hivyo taifa kwa wakati huo lina amani.

“Okey sawa Mfalme Pluto , sisi nadhani ni muda wa kuondoka hapa , nikutakie safari njema na mafanikio mema wewe na malkia , watu wa Kisiwa cha wafu wanasubiria siku utakayompeleka Queen Persephone”

“Sauroni usiniambie mshatangazia raia tayari nimeoa”

“Mfalme Pluto naomba unisamehe juu ya hilo , lakini tokea ulivvyoondoka hatukuweza kuishi kwa amani kwani raia wanakuulizia kila siku , na tuliishia kuwaambia umeoa, lakini hatukutoa taarifa nyingine Zaidi”Aliongea Sauron.

“Okey! Sauron nitamleta malkia wenu siku za usoni baada ya hali kutulia”

“Sawa mfalme Pluto” Aliongea Sauroni aliekuwa kwenye tabasamu na kisha akawapa ishara wanajeshi wake na kuanza kuondoka ndani ya bandari.

Lakini sasa kabla ya Sauroni alieshikilia kiboksi kuingia kwenye gari , mita kadhaa kutoka aliposimama Roma , mara kulitokea mkandamizo wa hewa wa aina yake ambao umeambatana na upepo mkali na palepale kiboksi kilichokuwa kipo kwenye mikono ya Sauroni kilionekana kuwa hewani kikielewa huku kikiwa wazi.

Mpaka Roma akili yake inafanya kazi vizuri , alikuwa amechelewa kwani eneo lote lilitulia kama vile hakijatokea kitu na kiboksi kile kilitua chini ardhini na Roma alisogea mpaka aliposimama Sauroni na kukifungua ndani yake na hapo ndipo alipopigwa na mshangao kwani hakuweza kuona kitabu kilichokuwa ndani yake Zaidi ya boksi tupu na kuona tayari teknolojia imeibiwa.

“Sh******t!!!!! anatumia nguvu isio ya kawaida kabisa , sikutarajia kama anaweza kutokea muda kama huu”Aliongea Roma kwa sauti ya chini lakini iliosikika vyema kwa Sauroni.

“Mfalme….!”Aliongea Sauroni kwa kushangaa , kwani hakuelewa imekuwaje Roma akawa na kiboksi cha teknolojia ya Thanatos , kwani alikuwa ameshika kiboksi hiko yeye.

“Sauroni huwezi kuelewa nini kimetokea , ila mpaka sasa Thanatos haipo kwenye mikono yetu”Aliongea Roma huku akivuta pumzi ya ahueni.

“Huyu mtu sio kawaida , uwezo wa kusimamisha muda sio wa kawaida hata kidogo”Alifikiria Roma na ilionekana Sauroni hakuelewa kilivhotokea kutokana na muda kusimamishwa kwa dakika kadhaa na ukumbuke muda ukisimamishwa kwa mtu wa kawaida huwezi kujua , utaona ni kawaida tu

Haya Sasa mbabe wa Roma kajitokeza, unadhani atakuwa nani.

ITAENDELEA 0687151346 watsapp nicheki kama unahitaji mwendelezo
 
Huyo ni Edna og mkuu , Edna alitekwa pamoja na stern , alice , mke wa Fodesa na Harry mtoto wa Alice
Kuhusu uwepo wa Nadia hilo eneo itajua episodes inayokuja Goodman akichezeshwa Bungee jumping [emoji3][emoji3]
kuhus nadia nakumbuk aliwah kupokea sim akifokewa kua kapew kz aifanye kuhus roma ila bado hajaikamilisha na boss wake alikasirik sana, nadhan bos mwenyew alikua ni apollo fek
 
Back
Top Bottom