SEHEMU YA 203
THE HAGUE -NERTHERLAND
The Hague ni jiji ndani ya taifa la Uholanzi, Serikali yote ya taifa la Uholanzi maamuzi yote hufanyikia ndani ya The Hague,Mji mkuu wa taifa la Uholanzi ni Amsterdam ni kama hapa Tanzania Dodoma na Dar Es salaam, The Hague uaarufu wake unatokana na kuwa na mahakama kuu ya haki ya kimataifa(ICC).
Sasa siku na saa ambayo Roma Ramoni wakiwa ndani ya kambi ya Jeshi ya Le Havre lakini pia Depney akiwa baharini na mateka kwenye meli ya kivita , upande wa Uholanzi kwenye jiji la The Hague kuna mkusanyiko wa kikao Kizito cha siri kilichokuwa kikiendelea, kikao ambacho kilikuwa kikiongozwa na The First Black, ni kikao kilichokuwa kikihusisha mataifa ishirini yenye nguvu duniani , kasoro Urusi peke yake ambayo haikuwa kwenye kikao hiko.
Muundo na mpangilio wa ukumbi ambao mkutano huu ulikuwa ukifanyikia , ulikuwa ni kwa usanifu wa herufi Zero , yaani kulikuwa na meza moja ambayo imechongwa kwa muundo wa herufi Zero huku Viongozi wote wakubwa waliohudhuria ndanii ya kikao hiki wakiwa wamezunguka meza hio huku mbele yao kukiwa na bendera na jina la nchi husika.
Katikati ya hilo eneo kulikuwa na Skrini za Tv, jumla nne zikiwa zimefungwa nakuwapa nafasi viongozi wote kuangalia kile kilichokuwa kikionyeshwa kwenye hizo Skrini.
Naam jambo ambaloo lilikuwa likionekana kwenye hizo Skrini ni tukio la kigaidi lililokuwa likiendelea ndani ya Ufaransa , tukio ambalo liliongozwa na Apollo .
“F*****ck , So this was all Depney Doing?”Aliongea mwanamke mmoja mwenye umri wa makadirio ya miaka hamsini Kwenda sitini hivi alievalia miwani ,na hii ni mara baada ya Depney kuvua lile Helmet na kufanya viongozi hawa wamuone.
“Miss Eunice calm down it`s done now..”Aliongea First Black mwakilishi wa taifa la Marekani akimsihi Mellisa ambaye alikuwa ni Waziri mkuu wa Ufaransa , aliekuwa ndani ya kikao hiko kuwakilisha taifa lake.
Ni Takribani dakika kama kumi na tano hivi kupita , huku viongozi hawa wakiendelea kuangalia , mara wote kwa Pamoja waliamka kwenye viti vyao na kusimama na kuanza kupiga makofi, kitendo ambacho kilidumu kwa takribani dakika tano na kuketi chini.
“Okey!, Nadhani kila mmoja ameona namna ambavyo Artemis , Apollo na Hades walivyodhibiti magaidi?”Aliongea First Black na viongozi walirudia kupiga makofi na The First Black aliinua mkono juu kuashiria kutulia. Halafu akaendelea.
“Haya yote ni mafanikio ya mipango ambayo imeasisiwa na viongozi wenzetu ambao wametutangulia , kwa kuunda shirika hili la The Zeros Organisation, Shirika ambalo ndio tumaini la usalama wa dunia”Aliongea na wakapiga wote makofi tena kwa heshima ya waasisi wa kundi la The Zeros halafu akaendelea.
“Licha ya mafanikio haya ambayo yametokana na michango ya hali na mali kutoka kila taifa, nikiri kwamba bado tunatatizo moja mpaka sasa”Aliongea na kufanya viongozi wote kutulia kimya na akaendelea.
“I have prepared a Presentation, which will be part of the Agenda of this sixteenth session since the birth of Zeros organization”Aliongea akimaanisha kwamba ameandaa uwasilishaji ambao utakuwa ni sehemu ya Ajenda kwenye kikao hiko cha kumi na sita tokea kuundwa kwa Zeros Organisation.
“Mr First Black, what do you think before your presentation,to tell us who is The Doni and how to control him, that is the question that brought us to this place”
Aliongea Shekhe mmoja kutoka Saudi Arabia ambaye ni mtoto wa Mfalme wa Saudi Arabia lskini pia anacheo cha Waziri mkuu , bwana huyo alimwambia The First Black Kwenda moja kwa moja kwenye jina la The Doni na namna ya kumdhibiti na watu wengi hapa ndani walionekana kukubaliana nae, na First Black kabla ya kuendelea na uwasilishaji wake ambao ungekwenda kuwa Ajenda za kikao, aliona aende moja kwa moja kuelezea jina la The Doni.
“Kuhusu The Doni mpaka sasa hatujaweza kupata jina lake kamili , lakini utafiti wetu pamoja na makisio ambayo tulifikia chini ya uchunguzi wa The Zeros, lakini pia tukio ambalo limetokea siku hii ya leo limetuweka karibu Zaidi na kumtambua The Doni”
“Lay it open Mr First Black”Aliongea Waziri mkuu kutoka Uingereza na First Black kwanza alitabasamu.
“Hatumfahamu The Doni ni nani lakini tunaamini kwa aslimia sabini anapata Msaada kutoka Vatican”Aliongea First Black na kufanya viongozi wote wamwangalie kwa macho ya mshangao na ya kutoelewa.
*******
Ni wachache kati ya wengi waliokuwa wakielewa juu ya miungu watu , hivyo hata wakati Apollo anamuita Alice kwa jina la Artemis walijikuta wakiwa kwenye mshangao mkubwa, Prince Sargaras, Vampire alieishi miaka Zaidi ya mia mbili mwenyewe hakuwa na uelewa juu miungu watu na aliishia kushangaa kama wengine.
Hawakuamini wapenzi ambao walikuwa ndugu kutoka Cromwell Familly walikuwa ni sehemu ya miungu watu kumi na mbili.
Alice na Stern kama kawaida yao , baada ya Depney kugeuka barafu na kudondokea baharini , walikumbatiana na kuanza kupigana mabusu , jambo ambalo lilimkera Roma kwani aliona wanachelewesha muda na mke wake hakuwa amekula muda mrefu.
“Nyie watu hebu acheni huo upuuzi kwanza mtafanya baadae”Aliongea Roma kwa kuamrisha , na Alice aliekuwa akiangaliana nao moja kwa moja alimuachia Apollo na kisha kumwangalia Roma.
“Hades, now that everything has essentially ended, bring the cruise Louis XVI over to us, and sink this warship afterward.”
“Hades Mpaka sasa kwakua kazi ishaisha , leta hio meli ya kifahari ya Luois XVI mpaka tulipo na uzamishe hii meli ya kivita baada ya hapo”Aliongea Alice lakini maneno yake yalikuwa ni kilio kwa wanajeshi ambao walikuwa ni wa Depney , ukweli kutokana na jambo ambalo wamelishuhudia kutoka kwa Depney kugeuzwa barafu , lakini pia nguvu ya Apollo , waliona hawawezi kujitetea kwa namna yoyote ile na ndio maana waliishia kupatwa na wasiwasi , lakini wasiwasi wao ulizidi baada ya Alice kusema Roma apelekee meli na kuzamisha ile ya kivita.
Alice alimwachia Apollo na kisha kuanza kuangalia mazingira ya meli hii huku nywele zake za kizungu zikipeperushwa na upepo, lakini sasa muda uleule hali ilianza kubadilika , kwani wanajeshi walianza kuhisi baridi kali isio kuwa ya kawaida na kitendo kile kilimfanya Apollo awaongezee ngao Edna na wengine ili wasidhurike na baridi lile na ni ndani ya sekunde ishirini tu wanajeshi walibadilika na kuwa kama masanamu yaliotengenezwa na barafu , huku eneo lote la Baharini pia maji kuganda na meli ya kivita kubadilika na kuonekana kama chakavu
Waliokuwa wakiangalia kwa kupitia Skrini kasoro Roma , wote waliishia kuwa kwenye mshangao , hawakuamini Alice alikuwa na uwezo wa kutengeneza mabarafu ya aina hio ndani ya dakika moja , lilikuwa jambo la kushangaza kwao na kuna muda Lilith na baba yake waliona hawa miungu watu walikuwa wakifanya makusudu kwa ajili ya kudhihirisha uwezo wao na aliona kama kweli nia yao ilikuwa hio basi wameshashinda , kwani kwa uwezo huo aliona asingewezakupambana nao hata kidogo.
“Hades kwa ninavyofahamu Artemis ni mungu wa Uwindaji , Asili na Mwezi, kwanini ana uwezo wa kugandisha vitu kwa barafu?”Aliuliza Prince Sargaras.
“Hakuna mungu wa barafu kati ya miungu yote kumi na mbili , kama ilivyo usiku kuwa ni wakati wa baridi , ndivyo ilivyo mchana kuwa wakati wa joto, Diana ndio jina halisi la Kirumi la Artemis, na kuhusu kuweza kudhibiti barafu mimi mwenyewe sikuwa na uelewa huo , lakini kwasababu Apollo ni mungu wa jua na kuweza kudhibiti joto inawezekana pia kwa mungu wa mwezi kudhibiti baridi”Alijibu na akaendelea.
“Ukweli ni kwamba haijalishi nani anaweza kudhibiti hiki na kile , lakini kinachojalisha ni makusudio ya nguvu ambazo mtu kuwa nazo , kama una nguvu na unafanya uharibifu basi hazina maana”Aliongea Roma , lakini mazungumzo yao yalionekana kusikika upande wa pili wa meli.
“Ni kweli mwanzoni sikuwa na uwezo wa kudhibiti barafu , lakini ilibidi nijifunze baada ya kupoteza upinde wangu wa mshale wa kiuungu unaofahamika kwa jina la Selene , baada ya kupambana na Athena”Aliongea Alice.
“Bebi usijali sana , sasa hivi pia una uwezo mkubwa , nitahakikisha uniapata siraha yako baada ya kumuua Athena”Aliogea Alice.
“Bebi sidhani kama hilo linawezekana , yule mwanamke ana nguvu isiokuwa ya kawaida, nilipopambana nae mara ya mwisho hakutumia hata siraha yoyote ya kiuungu lakini aliweza kunishinda , hata tuungane Pamoja kupigana nae tutapoteza pambano”Aliongea Alice na kumfanya Roma kushangaa juu ya hilo na kuingia kwenye mawazo.
“Au mtu alienipokonya HollyGraill ni Athena, kama ni yeye kwanini atumbie mbinu za kujificha?”Aliwaza Roma kwenye kichwa chake huku wote wakitoka ndani ya chumba cha mawasiliano kwa ajili ya kuingia kwenye meli ambayo iliwaleta.
Roma na Wenzake walikuja kushangaa mara baada ya kugundua wageni waliokuja nao hapo ndani walikuwa washaondoka na meli ile tayari ya kuachwa wao kisiwani.
“Fodessa mimi ninao uwezo wa kusafiri ndani ya bahari bila ya kutumia meli , ila kwa wenzangu hilo ni jambo ambalo hawawezi, naamini kwa ukubwa wa hii kambi hapakoseni meli nyingine au boti?”Aliuliza Roma baada ya kumgeukia Fodesa,
“Ndio Mfalme Pluto , kuna meli ya mizigo hapa kambini , subirini hapa nitaenda kuileta mwenyewe maana najua kuiendesha”Aliongea Fodesa huku akiwaacha wenzake kwa jili ya kuleta meli.
Baada ya Fodesa kuondoka , Sauroni alimsogelea Roma , akiwa na kiboksi cha teknolojia ya Thanatos mkononi.
“Mfalme Pluto haujanipa maelekzo bado juu ya hii teknolojia”
“Endelea kuishikilia Sauroni , baada ya kufika Paris wakabidhi wanajeshi wa The Eagles waipeleke ndani ya kisiwa cha Wafu na wamkabidhi Ron kwa ajili ya kuihifadhi”
“Mfalme hutembelei kisiwani awamu hii?”
“Haapana Sauroni sitoweza kutembelea kisiwa kwa muda, nipo hapa Paris na mke wanggu na tupo kwa ajili ya biashara , hivyo tutarejea Tanzania mapema tu , lakini pia kuna mambo mengi yanaendelea ndaini ya Tanzania yananihitaji”Aliongea Roma
Roma alikuwa hajakamilisha kazi yake ambayo ilimfanya kuingia Tanzania , bado hakuwa ameweza kukutana na familia yake na hilo ndio jambo ambalo lilikuwa limempeleka Tanzania , hivyo ilikuwa ngumu kwake kurudi ndani ya Visiwa vya wafu kabla ya kukamilisha kuipata familia yake.