Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 223.

Naam ndani ya kampuni ya Edna mambo yalikuwa yakienda kama kawaida na Sasa Edna kidogo alikuwa amepunguza majukumu yake kwa kuyapunguza rasmi kwa CEO msaidizi Marko Ernest Komwe.

Edna alifanya hivyo kwa ajili ya kujikita zadi katika kazi zake nyingine ambazo zilikuwa zinahusiana na kujipanua Zaidi kibiashara huku akiacha maswala ya ndani ya kampuni yakiendeshwa na Ernest , lakini pia alitaka kuendelea kufanyia kazi swala ambalo alilipata kulifahamu kutoka kwa mheshimiwa Senga na hili ni swala ambalo lipo kwenye Flash aliopewa siku za nyuma na raisi , swala ambalo lilikuwa likihusiana na kisasi ambacho alikuwa nacho mama yake , kisasi ambacho hakikuweza kukamilika kutokana na kwamba mama yake alifariki mapema kabla ya jambo hilo kutimia.

Kwahio majukumu ya Edna ni kuhakikisha kisasi hiko kinatimia kwa namna yoyote ile na ili kufanikisha hilo aliamini alikuwa akihitaji muda wa kutosha kwa ajili ya kusuka mipango yake , alikuwa akiamini kuwa ana maadui wengi ambao wanamuangalia kwa kila hatua anayopitia , lakini swala hilo hakuwa tayari kulifanya lipunguze ile ari aliokuwa nayo juu ya utimilifu wa mpango wake.

Asubuhi ya leo mrembo huyu alikuwa ameketi kwenye kiti chake akiwaza hili na lile , ukweli alijiona kwamba siku kadhaa za nyuma kulikuwa na mambo mengi ambayo yamemfanya kutofikiria Maisha yake kwa ujumla na uelekeo ambao anauchukua ,lakini pia sura mpya ya biashara zake ambazo anakwenda kuanzisha.

Katika kichwa cha Edna mawazo yalikuwa mengi kwanza kabisa alikuwa akiwaza juu ya baba yake mzazi wa damu , alikuwa akiliwazia hili swala tokea siku ambayo alipata kujua kuwa Mzee Adebayo sio baba yake wa damu na alikuwa akijitahidi kujisahaulisha , lakini kadri alivykuwa akijitahidi hakuweza kusahau , alikuwa akimfahamu mama yake mzazi nje ndani , licha ya kwamba hawakuishi sana wakiwa Pamoja kutokana na mama yake kuwa bize na maswala ya kampuni lakini vilevile kwa upande wake kuwa bize na masomo mpaka pale mama yake kifo kumkuta Ghafla , lakini kwa machache ambayo alikuwa akifahamu kutoka kwa mama yake , aliamini baba yake huwenda akawa ni mtu ambaye yupo karibu yake kuliko ambavyo anafikiria kwani alimjua mama yake sio mtu wa kuokoteza okoteza wanaume , ni mwanamke ambaye alikuwa na sheria zake.

Mtu aliekuwa akijiita The Protector ni swala ambalo pia alikuwa akilifikiria katika kichwa chake , kuna hisia zilizokuwa zikimwambia kabisa mtu huyo ni baba yake , lakini alijitahidi kupotezea hisia hizo , lakini licha ya hivyo hakushindwa kufikiria juu ya mtu huyo lakini pia juu ya baba yake mzazi.

Edna na Roma sasa ni takribani miezi mitatu Kwenda minne tokea wafunge ndoa yao ya mkataba na ni mambo mengi ambayo yametokea katikati yao, na mengi yalikuwa ya kuogofya sana , lakini licha ya hivyo wazo la kuachana na Roma baada ya miezi sita kuisha aliona ni gumu kutekelezeka , aliamini kama ataendelea na mpango wa kutimiliza kisasi ambacho bado hakujua kinahusiana na nini aliamini katika mchakato huo kutakuwa na maadui wakubwa ambao watajiinua zidi yake , hivyo anahitaji ulinzi na mtu pekee ambaye anapaswa kumlinda kwa hali na mali ni Roma peke yake.

Katika kufikia sehemu ya mawazo hayo mrembo huyu alijikuta akianza kukumbuka Maisha yake na Roma kuanzia mwanzo mpaka walipofikia , alihesabu meizi walioishi Pamoja , alikumbuka matukio yote kwanzia ya Tanzania mpaka yaliotokea Paris na alijikuta mwili wake ukisisimka.

“Roma kwasasa ashakuwa sehemu ya Maisha yangu , na sijui kama tunaweza kuachana hata baada ya miezi sita ya mkataba wetu kuisha , Mama yake anaonekana pia kunipenda na anaamini mimi ni mume halali wa mtoto wake, nadhani inanipaswa kumkubali sasa Roma kama mume wangu kihalali licha nina wasiwasi na wanawake wake aliokuwa nao, Lakini safari ya mapambano ambayo nimeanzisha inanihitaji kuwa nae kwa kila hatua kwa ajili yakufanikiwa lakini…..”Alijikuta akiishia kuwaza.

“Lakini siwezi kukubali aendelee kuwa na wanawake wengine , ilihali mimi ndio mke wake kihalali , kama nitampokea kama mume kamili jambo la kwanza ni kuhakikisha anaachana na wake zake na kuniangalia mimi tu”Alifikiria Edna , lakini licha ya kuwaza hivyo alionekana kukosa namna ya kulikamilisha jambo hilo.

Upande wa ofisi ya PR , Roma alionekana leo kuhudhuria kazini kama kawaida na alikuwa akicheza gemu kama ilivyokuwa kawaida yake , madhumuni ambayo alikuwa nayo kwa kuja kazini ni kutokana kutaka kuwaaga wafanyakazi wenzake kwasababu muda si mrefu angetakiwa kufanya kazi katika kampuni ambayo imefunguliwa na mke wake.

Wafanyakazi wenzake akiwemo Recho walionekana kuwa bize na kazi kama ilivyokuwa kawaida.

“Kamani leo mnaonaje tukikutana usiku kwa ajili ya kumpongeza Roma kwa kupandishwa cheo na kuwa Director wa kampuni mpya?”Aliongea Benadetha na kumfanya Roma asubirishe gemu lake na kugeuka.

“Naunga mkono hoja”Ilisikika sauti ya Nasra ikiingia ndani ya idara hii na wote wakamwangalia na haikueleweka Nasra alikuwa hapo kufanya nini , lakini alionekana kupendeza , alimwangalia Roma na kutabasamu baada ya kumuona.

“Nani anapinga juu ya hili?”Aliuliza Benadetha na wafanyakazi wote walionekana kukubaliana na jambo hilo na aliebakia Roma kukubaliana na wengine.

“Roma kusanyiko ni kwa ajili yako , kama hukubaliani na sisi tutaghairisha”

“Nakubali gharama zitakuwa juu yangu, chagueni hoteli.”Aliongea Roma na kufanya wote wapige makofi.

“Kilimanjaro hoteli napendekeza”Aliongea Recho haraka haraka na kufanya wote waangaliane kwa pendekezo alilotoa Recho.

“Tina unasemaje , ushawahi kufika Kilimanjaro Hotel?”Aliuliza Recho kwa namna ya kumkeheli Tina.

“Sijawahi kufika .. umefurahi?”Aliongea Tina huku akivuta mdomo lakini Recho alionekana kutojali.

“Roma unasemaje , wewe ndio unakwenda kulipia?”Aliongea Benadetha akimwangalia Roma.

“Limepita kama wote mnataka twende Kilimanjaro Hoteli mimi sina tatizo”Aliongea Roma na kufanya Recho kushangilia.

“Muone wote tunajua hapa unataka ukapige picha tu za kuoshea mtandaoni”Aliongea Tina kwa kumshushua.

“Kama ninaenda kupiga picha wewe inakuuma nini fyuu.. unaongea kama hutopiga hizo picha”Aliongea Recho na kufanya hata Roma acheke kwa utani uliokuwepo kati ya Tina na Recho

……………….

Ni muda wa saa moja kamili , Roma alionekana kujiandaa tayari kwa ajili ya kuelekea sehemu ambayo alikuwa amekubaliana na wenzake kwa ajili ya Kwenda kuhudhuria kusanyiko kwa ajili ya kupongezwa kwa kupandishwa cheo.

Roma alishuka mpaka chini sebuleni kwa ajili ya kutondoka , Blandina mama yake Roma usiku huo hakuwepo kwani alikuwa ameshinda nyumbani kwa baba yake na alitegemewa kulala huko huko mpaka siku inayofuata.

“Wife natoka”Aliongea Roma huku akimwangalia Edna aliekuwa ameketi kwenye masofa na Yezi na Sophia wakipiga Stori.

“Kama unaenda kwenye kusanyiko na wafanyakazi wa Idara ya PR na mimi naenda”Aliongea Edna na kumfanya Roma kushangaa.

“Wife unauhakika unataka Kwenda?”Aliuliza Roma kwa mshangao.

“Ninaenda nisubiri , labda kama hutaki nikihudhuria”Aliongea Edna huku akianza kupiga hatua kuelekea juu kujiandaa akimuacha Roma akiwa amesimama huku akimshangaa Edna, kusanyiko lilikuwa ni la wafanyakazi wa Idara ya Public Relation, hivyo asingetegemea Edna kuhudhuria kusanyiko kama hilo , lakini swala la pili ni kwamba kama ataenda na Edna inamaanisha uhusiano wao utakuwa wazi kwa wafanyakazi wenzake ndio maana Roma alishangaa.

“Yezi chuo unaanza lini?”aliuliza Roma na kukaa kwenye Sofa akimsubiria Edna.

“ Mwezi wa kumi na moja ndio tunaanza usaili Anko…”

Yezi tokea aje hapo ndani Roma hakuwa amepata nafasi ya kuongea na Yezi kabisa na kumuuliza maswala ya chuo, licha ya kujua mipango hio.

“Umefanya maamuzi mazuri kurudi chuo, inabidi ujitahidi ili baadae uje kufanya kazi , usiwe kama Sophia alieweka vyeti kwenye kabati”Aliongea Roma na kumfanya Sophia amkate Roma jicho na kuendelea kuangalia simu yake.

Ukweli Sophia siku mbili hizi tokea Roma kurudi kutoka Ufaransa alikuwa ametulia sana , hakuwa wa kuongea sana na Roma alishindwa kujua tatizo la Sophia ni nini , ila alishindwa kumuuliza.

Edna alichukua dakika kumi na tano tu kujiandaa na kumfanya Roma afurahi kwani haikuwa mategemeo yake kwa Edna kutumia muda mfupi kwa ajili ya kujiandaa.

“Wife umevaa kawaida sana , lakini ulivyopendeza kama vile umetumia lisaa kujiremba”Aliongea Roma na kumfanya Roma aone aibu na hii ni kutokana Roma alimsifia mbele ya Sophia na Yezi.

Sophia na Yezi waliishia kuangalia Roma na Edna ambao walikuwa wakitomomea nje ya mlango , walionekana ni wenye kutamani Kwenda na wao kwenye bata la usiku.

******

Ni baada ya nusu saa Edna na Roma walionekana wakiikaribia Hoteli ya Kilimanjaro , sehemu ambayo yeye na wafanyakazi wa idara yake ndio walipanga kwa ajili ya Mkusanyiko wa chakula cha usiku.

Hoteli ya Kilimanjaro ni moja ya Hoteli nzuri za nyota tano ambazo zilikuwa zikitoa huduma ya mikusanyiko midogo na mikubwa, Benadetha ndio alipewa kadi ya benki ya Roma kwa ajili ya kuandaa sehemu maalumu kwa ajili ya mkusanyiko wao huo mdogo ambao wameandaa.

Na muda ambao Roma na Edna wapo njiani Recho , Tina Benadetha na wafanyakazi wengine wawili wa kike walikuwa washafika tayari ndani ya hoteli hio na walikuwa washapata eneo maalumu binafsi ndani ya hoteli hii kwa ajili ya mkusanyiko wao.

Na walionekana wakipiga stori za hapa na pale na kufanya eneo lote kusikika sauti zao , Nasra alievalia gauni zuri la kupendeza aliingia ndani ya chumba hiko kikubwa na alionekana ndio kwanza na yeye alikuwa anafika.

“Jamani jamani siku zote nawaambiaga Nasra Mrembo , hebu muangalieni”Aliongea Recho na kufanya wenzake wote wageuze macho na kumwangalia Nasra ambaye aliona aibu kwa namna ambavyo alikuwa akisifiwa.

“Jamani najua na mimi sijaalikwa ila nimehudhuria…”Ilisikika sauti ya kiume kutoka mlangoni na kuwafanya warembo hawa waliopendeza usiku huu kugeuza macho yao na kumwangalia aneongea na kufanya kundi lote kukosa utulivu.

Alikuwa ni Ernest Komwe CEO msaidizi aliekuwa ametangulizana na Dorisi alikuwa amependeza Haswa na suti yake hata kwa Dorisi pia.

“Kuweni na amani hili ni kusanyiko kama tafrija ndogo , hivyo tusiangaliane kwa vyeo vya kazini tuweni huru , nimekuja kuungana na ninyi ili tupate kuzoeana , si eti Nasra?”Aliongea Ernest na kumfanya Nasra kutabasamu na kutingisha kichwa na Ernest alionekana kujiamini kwani alisogea na kwenda kuketi karibu na Benadetha.

Uzuri ni kwamba meza zilikuwa zimeunganishwa Pamoja na viti vilikuwa vingi kiasi kwamba hata watu ishirni wanaweza kutosha ndani ya hilo eneo.

“Hi Guys!”Ilisikika sauti nyingine kutoka mlangoni na kufanya wote wageuke na kuangalia sauti ya mwanamke mrembo aliekuwa akiingia hapo ndani , mrembo mwenyewe hakuwa mwingine bali alikuwa ni Nadia Alfonso na wote baada ya kumuona walitabasamu, Nasra alikuwa amependeza mno n ani kama amefanya makusudi kuchagua mavazi ambayo yatamfanya kupendeza kuliko wengine wote.

Kusanyiko liliandaliwa na idara ya Public Relation kwa ajili ya kumpongeza Roma kwa kupandishwa cheo , lakini wafanyakazi kutoka idara nyingine walihudhuria na haikueleweka taarifa wamezipata vipi.

“Msishangae hata mimi pia ni mmoja ya wafanyakazi wa Vexto hivyo naweza kusema kama ni mhusika kwenye hii tafrija ilioandaliwa kimya kimya”Aliongea Nadia , alionekena kuwa kwenye mudi nzuri mno na ni kama hakuna jambo ambalo limemtokea siku chache nyuma nchini Ufaransa.

“Jamani CEO Edna na yeye yupo njiani kuja kwenye kusanyiko hili”Aliongea Dorisi na kufanya kila mtu kushangaa.

“Dorisi unamaanisha CEO anakuja?”Aliuliza Recho kama mtu ambaye hajasikia vizuri.

“Ndio kanitumia ujumbe yupo njiani”Aliongea Dorisi pasipo kujali na kukaa

IJUMAA ASUBUHI MWENDELEZO

0687151346 nicheki watsapo tuendelee

Ijumaa asubuh mkuu
 
Mkuu Singano jr uliahidi leo asubuhi, be a man of your promises wengine wanatumia simu ambazo hazisupport whatsapp ndiomana wako hapa jukwaani
 
Jana alitingwa na leo kiasi ila baada ya muda kiasi mzigo utatupiwa tena mwingi kuliko siku zote, muhimu subrah. Wanasema kimya kikuu kina kishindo kikuu ila sio kama ya Nassari ikawa kishindo Cha sponchi inayoteketea
 
watu tuko arosto. ujue ratib et ni alhamis kutokan na kutingwa akasem atatufanyia leo asubh ila pia imeshindikana nna iman kuna jamb linamtatiz allah akufanyie wepes kesho utuwekee mzigo wa maan kufidia
 
kumbe wafuatiliaji ni wengi wanasomaga kimya kimya. Mzee usiweke mzigo mpaka comment zizidi 200 kama itakupendeza
 
SEHEMU YA 224

Sio kwa Recho tu ambaye alishangazwa na ujio wa Boss Edna hapo ndani , ila kwa kila mtu na hii yote ni kwamba tokea Edna apewe kampuni na mama yake hakuwahi kujichanganya na wafanyakazi , ni baadhi ya wafanyakazi tu wajuu ndio ambao Edna alikuwa akiongea nao, na wafanyakazi wengi wa chini walikuwa wakimkubali na kumuogopa pia kutokana na ukauzu wake.

Wakati wafanyakazi hawa wakiendelea kushangaa , waliingia wafanyakazi wengine wa kampuni kutoka Idara ya Finance waliokuwa chini ya Nasra na walisalimia na Kwenda kuketi.

“Jamani msishangae wote hawa hawajaja kwa bahati mbaya , nimewaalika kwa ambao wanataka kuhudhuria kusanyiko hili la chakula cha usiku kwa idara zote , hivyo naweza kusema sio kwa ajili ya idara ya Public Relation tu ambao walipaswa kuhudhuria ila ni kwa idara zote”Aliongea Nasra na kufanya Benadetha alietoa pendekezo hilo aitikie kwa kichwa.

“Umefanya vizuri Nasra , wafanyakazi wengine wangeona tunawatenga”Aliongea Benadetha na kumfanya Nasra kutabasamu kivivu huku Recho na wenzake wakielewa kwanini hata Nadia na CEO msaidizi wamehudhuria.

Roma na Edna walisimamisha gari ndani ya hoteli na kisha akamrushia mfanyakazi wa hoteli anaehusika na kuongoza magari kwa ajili ya kuegesha gari yake aliokuja nayo.

Edna akiongozana na Roma waliingia ndani ya hoteli hii huku baadhi ya watu wakimwangalia Edna aliekuwa amevaa kawaida tu lakini alionekana kuwa mrembo isivyokawaida.

Jumla ya wafanyakazi kumi wa Kampuni ya Vexto ndio waliohudhuria usiku huo huku wanaume wakiwa ni watatu pekee ambao walikuwa wamehuduria yaani Ernest Komwe na wanaume wawili kutoka idara ya fedha iliokuwa chini ya Nasra.

Dakika chache mbele zogo lilitulia kimya baada ya Roma na Edna kuingia ndani ya ukumbi huu na kufanya watu wote macho yawe kwao na Recho ndio aliekuwa wa kwanza kusimama na kumsalimia Edna na kwa jinsi alivyosimama alifanya wenzake watamani kucheka.

“Boss Edna karibu sana , aliongea Benadetha akiwa amesimama Pamoja na wafanyakazi wengine wakimpa heshima yake Edna.

“Haina haja ya kusimama na kunisalimia , nipo hapa kwa ajili ya kuchanganyika na nyie , ondoeni wasiwasi hatupo kazini”Aliongea Edna kwa kutabasamu.

“Hahaha..Boss wetu Edna ashasema amekuja kuchanganyika na sisi kwanini mnaendelea kusimama”Aliongea Roma huku akiwaangalia baadhi ya wafanyakazi waliokuwa wamesimama kasoro Nasra , Dorisi na Nadia ndio walionekana kuwa kawaida.

Wafanyakazi wote ambao hawakuwa wakifahamu mauhusiano ya Edna na Roma walionekana kuwa katika mshangao na walishindwa kuelewa kwanini Roma amekuja Pamoja na Edna, lakini licha ya hivyo hakuna ambaye alikuwa tayari kuamini kama Roma na Edna wana mahusiano.

Dorisi alimwangalia Nasra na kisha akamkonyeza na tukio hilo Roma alilishuhudia na aliamini huenda Dorisi ashamueleza Nasra juu ya mahusiano yake na Edna , kwani Nasra licha ya kuwa kwenye mshangao lakini haukuwa umezidi kama ilivyokuwa kwa wafanyakazi wengine, ila pia alionyesha uso wa wasiwasi mno.

Edna alikaribishwa mpaka upande wa kulia kwenye meza hio kubwa na kuketi ,ukweli hakuwa amezoea kukusanyika na wafanyakazi wake hivyo alikosa utulivu kidogo ,kwa upande wa Roma alienda kukaa karibu na Nasra, huku akimwagalia machoni na kutabasamu na Nasra alimwangalia Roma kwa hasira.

“Kwanini haukuniambia mapema kama Edna ni mke wako?,unajua ni kwa jinsi gani nilivyojisikia baada ya kujua ukweli kupitia Dorisi, naona hata aibu kumwangalia Edna usoni najihisi msaliti”Aliuliza Nasra kwa sauti ya chini wakati Edna akiwa bize kuongea na Dorisi.

“Unahisi aibu ya nini , hata hivyo hujawahi kuniuliza kuhusu mke wangu”Aliongea Roma kwa sauti ya chini.

“Unachukulia rahisi sana baadhi ya mambo Roma ,ningejua mapema nisingekusogelea kabisa , najisikia vibaya kila ninapowaza namna nilivyomwambia juu ya wewe kunisindikiza Kwenda nyumbani kwetu”

Ukwelo ni kwamba muda wa mchana baada ya Nasra kupendekeza swala la kukusanyika usiku kwa ajili ya chakula , Nasra alienda moja kwa moja mpaka ndani ya ofisi ya Dorisi kwa ajili ya kumueleza juu ya jambo hilo.

“Namimi nitahudhuria Nasra”aliongea Dorisi.

“Lakini nafikiria itakuwa vibaya kama tutahusisha idara ya PR pekee”

“Kwahio unashauri nini?”Aliuliza Dorisi.

“Nataka kutangazia baadhi ya idara kupita Grupu za watsapp kwa ambaye atapenda kuhudhuria anakaribishwa”Aliongea Nasra.

“Ni sawa tu kama utafanya hivyo , naona sio mbaya”Aliongea Dorisi.

“Nitawambia na Boss Edna kama atapenda kuhudhuria pia”Aliongea Nasra na kumfanya Dorisi kuwaza kidogo.

“Hivi Nasra unafahamu uhusiano wa Roma na Edna?”Aliuliza Dorisi na kufanya moyo wa Nasra upige kwa nguvu ni kama akili yake ilianza kufikiria baadhi ya mambo , ukweli siku kadhaa nyuma aliweza kufikiria swala la Roma kupandishwa haraka haraka cheo , lakini pia namna ambayo Roma aliweza kusafiri na Edna Kwenda Paris , hili swala lilimpa maswali mengi , lakini licha ya hivyo moyo wake ulishindwa kabisa kukubali kama kuna mahusiano kati ya Roma na Edna, alijipa sababu kadhaa kwenye kichwa chake ambazo zilimuanisha kwa asilimia kubwa kwamba hakuna mahusiano yoyote kati ya Edna na Roma, na sababu kubwa ni kwa namna ambavyo alikuwa akimfahamu Edna , licha ya kwamba hawakuwa marafiki wa karibu kiasi cha kuambiana baadhi mambo binafsi lakini Edna alikuwa akimfahamu vizuri tu misimamo yake hivyo ingekuwa ngumu kwa Roma kuuteka moyo wa Edna.

Lakini hata hivyo siku zote pia Nasra alikuwa akiwaza kuhusu mume wa Edna , alikuwa na taarifa za Edna kufunga ndoa lakini hakuwahi kujiuliza juu ya mwanaume ambaye amefunga nae ndoa, na alitegemea siku yoyote kumfahamu.

“Unataka kusema nini Dorisi?”Aliuliza Nasra kwa wasiwasi.

“Nauliza kama unafahamu Roma na Edna ni mume na mke”Aliongea na kumfanya Nasra kushikwa na mshangao.

“Unasema kweli?”

“Ndio..”Aliongea Dorisi huku akitabasamu kwa jinsi Nasra alivyokuwa kwenye mshangao na alicheka kabisa baada ya Nasra kuroka nje pasipo ya kuongea tena.

Nasra baada tu ya kutoka kwenye ofisi ya Dorisi alikimbilia Bafuni na kufungulia maji ya bomba na kuweka uso wake kwenye Sink la maji kama mtu ambaye alikuwa akijikosesha pumzi, na alijifunika na maji kwa dakika moja mpaka kuinua kichwa chake huku akihema kwa nguvu.

“Damn you Roma…kwnini hukuniambia mapema”Alijiongelesha Nasra huku akitamani hata Ardhi ipasuke.

“Sijui Edna anafahamu uhusiano niliokuwa nao na Roma?”Alijiuliza Nasra huku akiegamia ukuta kwa wasiwasi , alijihisi moyo wake kumuuma mno.

“Edna kwanini hukuniambia mapema kuhusu Roma kuwa mumeo , unajua ni makosa gani nimefanya kutembea na mumeo …,Nitamwangalia vipi Rahel mama yako mimi, haya yote ni makosa yangu sipaswi kujilaumu tena juu ya jambo hili , napaswa kumuomba Edna msamaha na nitakaa mbali na mume wake”Aliongea Nasra akiwa bafuni peke yake kama chizi , mrembo huyu alionekana amechanganyikiwa , kuna sehemu katika moyo wake ilikuwa ikimlaumu Roma kwa kutokumwambia , lakini pia kuna sehemu ambayo alikuwa akimlaumu Edna kwa kutokumtambulisha Roma kwake ,lakini pia kuna sehemu ambayo alikuwa akijilaumu yeye mwenyewe kwa kutoweza kuunganisha hata nukta kwa kile kilichokuwa kikiendelea ndani ya kampuni , alijiambia kama angekuwa ni mtu wa kusoma alama basi asingeshindwa kufahamu mahusiano ya Roma na Edna , alikumbuka baadhi ya mambo kadhaa tokea Roma afike ndani ya kampuni.

“Hapana ninaenda kumuomba Edna msamaha sasa hivi…. Edna ni mkimya sana huenda siku zote anajua uhusiao wangu na Roma na ameamua kukaa kimya ila anaumia moyoni”Aliwaza Nasra na kujinawisha uso kwa mara nyingine na kujifuta na kitambaa na kisha akajiweka sawa na kutoka Kwenda ofisini kwa Edna.

“Boss..!!!”Aliita Nasra kwa sauri ya Kinyonge huku akiingia ndani ya ofisi ya Edna , alimwangalia bosi wake alivyokuwa bize na kazi na kujiuliza Edna ni mwanamke wa aina gani kwa kuweza kukaa na siri moyoni mwake kiasi kwamba anashindwa hata kumueleza kuhusu Roma.

“Vipi Nasra , mbona unaonekana kuwa na wasiwasi, sio kawaida yako”Aliongea Edna aliekuwa bize na tarakishi yake, lakini Edna alijikuta akishangaa Zaidi baada ya Nasra kupiga Magoti mbele yake.

“Edna naomba unisamehe… sikufahamu kuhusu Roma na wewe ..”Nasra alishindwa kuendelea na alijikuta akitokwa na machozi palepale na kuanza kulia kwa kwikwi na mpaka hapo Edna alikuwa ashafahamu Nasra alichokuwa akimaanisha, hakujua Nasra amefahamu vipi kuhusu uhusiano wake na Roma.

“Nasra kwahio unakiri mahusiano yako na Roma au unataka msamaha?”Aliuliza Edna huku akimwangalia Nasra aliekuwa na machozi mengi.

“Edna sikufahamu …. Naona aibu mimi hata ya kukuomba msamaha”

“Kwahio unamaanisha kama ungefahamu mapema usingekuwa na mahusiano na Roma?’Aliuliza Edna kwa sauti kavu , mrembo huyu alikuwa akifikiria swala la Roma na michepuko yake masaa kadhaa yaliopita ila hakujua moja ya mchepuko utakuja kumpigia magoti muda huo.

Nasra licha ya kuulizwa swali hilo na Edna, ila alishindwa kabisa kulijibu , alijiuliza yeye mwenyewee kama angefahamu Edna na Roma wana mahusiano ya Ndoa je angeweza kuzishinda hisia zake juu ya Roma.

“Nasra ngoja nikuambia kitu , unashindwa kujibu hili swali kwasababu haupo na Roma kwenye mahusiano kwasababu ya kutofahamu ukweli juu ya mahusiano yangu na yeye , ila kwasababu ulifanya chaguo la kuwa nae”

“Edna…”

“Kwani kabla ya yote hukufahamu kama Roma ameoa?”Aliuliza Edna tena na Nasra swali hilo lilimkamata vilivyo , ni kweli kabla ya kujihusisha na Roma alikuwa akifahamu kabisa Roma ana mke.

“Umeona sasa..”Aliongea Edna huku akitoa tabasamu la hasira.

“Nasra kama uliamua kuwa kwenye mahusiano na Roma ilihali unajua kabisa ameoa basi haina haja ya kupiga magoti na kuomba msamaha, sina neno la kuongea juu ya hili kabisa , japo s sijui sababu halisi ya kuoana na yule mwanaume lakini kwangu mimi sijui namna ya kumzuia kutokuwa na wanawake wengine”

“Edna nao..”

“Nasra kaendelee na majukumu yako haina haja ya kuomba msamaha…”Aliongea Edna kwa ukauzu na kisha akageukia tarakishi yake na kuendelea na alichokuwa akikifanya na kwa Nasra hakuona haja ya kuendelea kupiga magoti , maneno yote alioongea Edna yalionekana kuwa ya ukweli kabisa.

“Ni kweli Edna yupo sahihi sipaswi kuomba msamaha kwa jambo hili , mimi ndio niliofanya maamuzi ya kutembea na Roma wakati nikijua fika alikuwa mume wa mtu , haijalishi huyo mwannamke ni Edna au mwanamke mwingine ni vilevile tu , kama nilikuwa naheshimu ndoa yake nisingetembea nae”Aliwaza Nasra kwenye kichwa chake huku akipiga hatua..

“Nasra ukweli nilipogundua mahusiano yako na Roma sikuweza kuwa na furaha na sidhani ingekuwa kwangu tu , kwa mwanamke yoyote asingependa kuona mwanaume wake kutembea na kila mwanamke lakini siwezi kukufokea wala kukulaumu juu ya hili … naamini Roma kakubali kuwa na wewe katika mahusiano kutokana na vitu ambavyo hapati kutoka kwangu hivyo sio kosa lako na sitaki swala hili liingiliane na maswala ya kazi , nenda kaendelee na majukumu yako ya kazi”Aliongea Edna na Nasra alijisikia kuumia moyoni , lakini alishindwa kuongea lolote na kutoka nje ya ofisi hio.

Sasa haikueleweka Edna alifahamu vipi juu ya kusanyiko ambalo limeandaliwa na idara ya PR , lakini alionekana kuwa na mpango wa kuhudhuria tokea mchana.

Kwa upande wa Nasra maneno ya Edna yalikuwa yakijirudia tudia kwenye akili yake , lakini alishindwa kujua cha kufanya kwa wakati huo , kuna moyo ulikuwa ukimwambia kuwa aachane na Roma lakini pia kuna upande ambao ulikuwa ukimwambia aendelee na Roma na alishindwa kuchukua maamuzi kwa muda huo na kuliweka swala hilo kiporo mpaka muda ambao wanafika ndani ya hoteli ya Kilimanjaro kwa ajili ya kusanyiko.
 
Back
Top Bottom