Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 230.

Nasra alishangaa kumuona rafiki yake muda huo wa usiku , kwani haikuwa kawaida yake kabisa ya Najma kuja kumtembelea usiku, alimkaribisha vizuri ndani kwa kumkumbatia.

“Mbona hujanipigia simu Shosti kama unakuja , huenda usingenikuta”Aliongea Nasra huku akimshika Najma mkono na kumkalisha kwenye sofa.

“Nishazoea kila ninapokuja kukutembelea nakukuta”Aliongea Najma huku akitoa tabasamu hafifu na Nasra alitabasamu na kukaa.

“Juma kaka yako anaendeleaje , mara ya mwisho uliniambia anaumwa?”Aliongea Nasra na kumfanya Najma kunyamaza na kuonyesha wasiwasi kwenye macho yake na hilo kwa Nasra aliliona.

“Hali ya kaka Nasra ni mbaya sana…”Aliongea Najma na kisha akamkumbatia Nasra huku akianza kutoa machozi na kumfanya Nasra kushangaa.

“Kuna nini hebu niambie?”Najma alifuta machozi na kisha akakaa vizuri na kumwangailia Nasra.

“Figo zake zote zimefeli”Aliongea Najma na kumfanya Nasra kupigwa na mshangao na aliishia kumkumbatia Nasra.

“Pole sana rafiki yangu”Aliongea Nasra na kumfanya Najma aanze kulia kwa kwikwi.

“Nasra naogopa mwenzio kumpoteza kaka yangu ..”Aliongea huku akifuta Kamasi.

Tokea mara ya mwisho Najma anaonana na Roma ndani ya mgahawa Mbagara Rangi tatu , siku ambayo Roma alikuwa na Benadetha kwanzia siku hio hawakuwahi kuonana tena na haikueleweka nini kilitokea kwani mara ya mwisho familia ya Najma ikiongozwa na Juma Pamoja na Shangazi yake walikuwa wakizungumzia swala la Ndoa na kijana anaefahaika kwa jina la Hemedi mfanyakazi kutoka Tigo.

“Madaktari wanasemaje mpaka sasa kuhusu afya yake na yupo hospitali gani?”

“Yupo Mloganzila, kuhusu Afya yake ni mbaya wanasema ataishi kwa kufanyiwa ‘Dialysis’ au kubadilishiwa figo(Kidney Transplant)”

Nasra alijikuta akishangaa kwani alikuwa akielewa vyema juu ya ugonjwa wa figo ukifikia hatua ya kufanyiwa Dialysis au Transplant ni kwamba upo hatua ya mwisho.

“Dialysis ni mlolongo wa hatua za kimatibabu ambazo mgonjwa hufanyiwa kutumia mashine maalumu kwa ajili ya kutoa taka mwili , ni tiba mbadala pale ambapo figo zikifikia hatua ya 6 katika kuharibika kwake , sasa tatizo hili likitokea huwa haliponi labda tiba kamili ya kubadilishiwa figo ifanyike ndio mtu anaweza kupona.

Hatua zote hizo za kimatibabu zinagharimu mapesa mengi sana na inaweza kufikia mpaka milioni kumi kwa mwezi kwa kufanyiwa Dialysis tu na kuhusu Kubadilishiwa figo ndio kasheshe Zaidi hapo, kwani lazima apatikane mtu wa kujitolea kutoa figo yake.

Kwahio Najma alikuwa akijua kuwa tatizo la kaka yake lipo nje ya uwezo wa familia yake kimatibabu hivyo aliona kabisa kaka yake anakwenda kufa na ndio maana alikuwa na wasiwasi mno.

Najma alilala kwa Nasra mpaka asubuhi ndio alipoaga kwa ajili ya kurudi hospitalini kuendelea kumuuguza kaka yake, na hata kazi yake ya kule Son And Daughter Orphanage aliomba likizo na Nasra hakuwa na namna ya kumsaidia Najma na aliishia kumuonea huruma rafiki yake , aliona hata kama atamsaidia hela ya matibabu ya Dialysis asingeweza kumudu kwa muda mrefu na hela zingemuishia.

********

Desmond alipata kumsikiliza vizuri Elvice Temba na alijikuta akifurahi kufahamiana nae hasa alipofahamu kuwa Elvice na Roma walikuwa maadui wakubwa na aliamini kwa kumtumia Elvice basi ataweza kumdhibiti Roma kwa urahisi.

“Kwahio unashauri nini , juu ya namna ya kumdhibiti , nimesoma taarifa zake na anaonekana kuwa wa kawaida”Aliongea Desmond na Elivice alitabasamu.

“Hio taarifa uliosoma ni ya uongo”Aliongea

“Unamaanisha nini kuwa ya uongo?”

“Iko hivi Roma sio mtu wa kawaida ni Zaidi ya Shetani na mbaya Zaidi hapa bongo anao wanajeshi wake kutoka The Eagles , hivyo kumdhibiti sio jambo rahisi la kuweza kufanyika, yapo mengi ambayo Roma anaweza kuyafanya ila hata nikikuelezea hutoamini”Aliongea Elvice na kumfanya Desmond kutabasamu ni kama hakumuelewa vizuri.

“Hahaha…Elvice unanichekesha yule jamaa ni wa kawaida sana , huwezi kumlinganisha na mimi kwani utakuwa unanivunjia heshima , hivi unanifahamu mimi ni nani kwanza… ngoja nijitambulishe kwako”

“Naitwa Desmond Jeremy Paul mrithi wa baba yangu raisi Jeremy wa Rwanda”Aliongea kwa kujigamba Desmond na Elvice akatabasamu.

“Nakufahamu ndio maana nikaja kuongea na wewe kama ungekuwa mtu wa kawaida hata nisingejisumbua kuja hapa ndani”Aliongea na kumfanya Desmond kukosa neno la kuongea.

“Sikia Desmond tumejaribu kila mbinu kumdhibiti Roma lakini tumeshindwa na ndio maana nimekuja hapa kwa faida yako na yangu kwani wote tuna adui wa aina moja , mimi nina mpango ila unahitaji pesa kidogo”Aliongea Elvice na kumfanya Desmond kukaa vizuri.

“Mpango gani, nipo tayari kutoa kiasi chochote cha pesa”Elvice alitabasamu.

“Sikia Roma kwa njia ya kawaida ya kupambana nae hatuwezi hivyo jambo pekee la kufanya mpaka sasa nikuhakikisha mke wake anamuacha mwenyewe”

“Unamaanisha Edna?”

“Ndio… , Kama Edna ataamua kumuacha mwenyewe mpango utafanikiwa kirahisi na hilo linawezekana kwa asilimia mia moja”Aliongea Elvice na kumfanya Desmond kutabasamu.

“Tutawezaje kufanya hivyo kama Edna anampenda?”

“Swali zuri hilo , iko hivi mpaka sasa Roma anawanawake kibao nje ya ndoa yake na sina uhakika kama Edna anafahamu hilo sasa sisi tutatumia hao wanawake kuhakikisha Edna anachukua maamuzi ya kuachana na Roma”Desmond hakulifahamu hilo na alishangaa kwa wakati mmoja.

“Yaani jamaa licha ya kuwa na mke mrembo kama yule bado anamsaliti.. huyu jamaa kanizidi umalaya hahah…. Mimi muhuni lakini siwezi kumsaliti mwanamke mrembo kama Edna”Aliongea kwa kejeli.

“Jamaa ana nyota ya kifalme anaonekana wa kawaida sana lakini warembo anaotembea nao siamini kama utaweza hata kumpata mmoja wao kati yao ni visu halafu wanajielewa”Aliongea Elvice , licha ya kumsifia Roma lakini moyo wake ulikuwa ukiuma, alitamani fursa zote za Roma ziwe zake.

Ukweli Elvice tokea mara ya mwisho kushindwa kuichukua kampuni ya Edna kwa kuzishusha hisa thamani yeye na Abubakari , hakuwahi kujihusisha moja kwa moja na Edna , aliona kufanya hivyo ni kujitafutia matatizo kwani hata rafiki yake Abubakari kuepusha kukutwa na jambo baya aliamua kukimbilia nje ya nchi pamoja na baba yake.

Lakini ukimya wake sio kama alikuwa hafanyi chochote , ukweli alikuwa akiusuka mpango wake kwa muda mrefu mno na jambo ambalo pia lilimpa nguvu Zaidi ni baada ya kupewa uongozi wa juu wa kundi la madawa ya kulevya la Black Mamba.

Elvice alimfuatilia kimya kimya Roma pasipo yeye mwenyewe kugundua na aliweza kugundua pisi zote ambazo Roma anatembea nazo kuanzia Waziri Neema Luwazo ambaye ni pisi ya mheshimiwa Kigombola, Nasra , Dorisi na Rose wote aliwafahamu kama michepuko ya Roma na alishangazwa na hilo mpaka kujiuliza Roma ana kipi cha kuwachanganya warembo kama hao na kubwa Zaidi ni kwa Neema Luwazo , kwani tokea mwanamke huyo kukutana na Roma hakuwa akiambilika kabisa na alikuwa akisikia tetesi juu ya mgogoro uliokuwepo kati ya Raisi Kigombola na Neema kuwazo , kwani inasemekana mwanamke huyo alimtamkia waziwazi Mheshimiwa mstaafu kuwa hana hisia nae tena.

Sasa haikueleweka ni mpango gani ambao Elvice alikuwa akipanga kwa ajili ya kuufanya ili kumfanya Edna aachane na Roma.

Ngoja tuone kama atafanikiwa…

*****

Blandina haikuwa mara yake ya kwanza kukutana na baba mkwe wake , Camillius Kweka , siku za nyuma baada yakufunga ndoa na Senga alishatambulishwa ukweni , lakini shida kubwa ni kwamba Mzee Kweka hakuwahi kumkubali sana Blandina na hii yote ni kutokana na kwamba Mzee Kweka alimuona Blandina anamfanya mtoto wake kuwa zuzu kutokana na mapenzi , kwani wakati huo Senga hakuwa akiambilika na alichukua mpaka maamuzi ya kujitegemea na kuhamia Songea na kuanza Maisha yake huko pasipo kutaka usaidizi kutoka kwenye familia yake na hili lilimfanya mzee huyu kutompenda kabisa Blandina kwani aliona Senga yupo nje ya mstari wa malenzo ambao ameukusudia kwenye Maisha yake.

Mzee Kweka alimpa Blandina pole za hapa na pale kwa ajili ya kumtuliza , kwa yale ambayo yametokea lakini licha ya hivyo mzee huyu alionekana kutotaka kumuweka wazi Blandina namna ambavyo Roma aliweza kurudi akiwa hai baada ya maika mingi na hata Blandina alipoomba kuwekwa wazi jibu la Mzee Kweka:

“Blandina yote ambayo umeyapitia kwa miaka ishirini iliopita ni kwa ajili ya mtoto wako ,Denisi kama nisingefanya maamuzi magumu miaka ile huenda mpaka sasa tusingekuwa na Denisi(Roma) tena duniani”Aliongea Mzee kweka lakini Blandina aliishia kulia.

“Blandina mtoto wangu , huna haja ya kulia tena , kila kitu kishaisha licha ya kwamba Mzee Mwenzangu hapa alifanya maamuzi yake kwa ajili ya Denisi lakini pia na wewe ulifanya maamuzi yako kuolewa na Kamau Kamau”Aliongea Mzee Atanasi kwa sauti ya chini lakini ya kusikika na wakati huu Jestina na yeye alikuwepo na aliishia kutoa machozi kumuunga mkono dada yake.

“Baba naomba kujua umeniitia nini , unataka kuongea nini na mimi?”Aliuliza Blandina.

“Blandina licha ya kwamba Denisi kwa sasa yupo hai , lakini kwa Senga Denisi bado amekufa”Aliongea Mzee Kweka na kumfanya Blandina kushangaa.

“Unamaanisha nini baba?”

“Unafahamu kila kitu Blandina , mwanangu Senga alikupenda kwa dhati sana na aliomboleza kifo chako kwa muda mrefu na hata maamuzi ya kuoa ni mimi niliemlazimisha , hivyo swala la nyie wote wawili kuwa hai limekuwa jambo kubwa kwake , kwanza anatuona wote hapa tumemsaliti na maamuzi alioyachukua ni kutomtambua Roma kama mtoto wake”

“Lakini hata hivyo hakuna kinachoharibika kitu , kwasasa hatuwezi kumlazimisha kuutambua ukweli kama mpo hai na kuwakubali , lakini hata hivyo hatuwezi kumsubiria mpaka atakapo mkubali Roma kuwa mtoto wake”

“Unamaanisha nini hatuwezi kumsubiria?”

“Blandina licha ya kwamba nia yangu ya kwanza ilikuwa kumtoa sadaka Roma kwa ajili ya kupona ugonjwa wake lakini pia nilikuwa na malengo mengine Zaidi”Aliongea na kisha akamwangalia Mzee Atanasi na kutabasamu.

“Kwasasa sitokueleza ni malengo gani ambayo yapo kwa ajili ya Roma lakini malengo hayo ili yafanikiwe tunataka na wewe utimize wajibu wako”Aliongea na kumfanya hata Jestina kushangaa. Yaani kwanza aliwashangaa hao wazee kwani aliwaona wanaongea upuuzi , mtu ndio kwanza karudi halafu wanaanza kuongea maswala ya wajibu, alikereka.

“Mnataka nifanye nini?, kama ni kwa ajili ya Roma nitafanya chochote”Aliuliza Blandina kwa wasiwasi.

“Tunataka urudi Kenya”Aliongea mzee Atanasi pasipo kumung`unya maneno na kumfanya Blandina ajihisi kama hajasikia vizuri , lakini wazee hao walionekana kumaanisha kile ambacho wameongea.
 
SEHEMU YA 231

“Ndio Blandina tunataka urudi Kenya”Alikazia Mzee Kweka na kumfanya Blandina machozi kumtoka.

“Haitowezekana tena , nishaachana na Kamau”Aliongea Blandina.

“Baba hata mimi sipo tayari kuona Blandina anarudi Kenya , haliwezi kutokea”Aliongea Jestina kwa hasira.

“Jestina kaa kimya , hili ni swala ambalo linahusu mustakabla wa taifa la Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla wake” aliongea Mzee Atanasi kwa tahadhari.

“Blandina tujaua sasa upo kwenye maumivu makubwa, lakini kwa ajili ya Roma inabidi ukubaliane na sisi”

“Lakini nitawezaje kurudi tena Kenya ilihali Maina ashatangaziwa kufariki, sijaelewa mpaka sasa mnachomaanisha na nipo mwenye kuchanganyikiwa”

“Ndio Blandina upo kwenye kuchanganyikiwa , ni kweli Maina kafariki lakini Blandina Atanasi hajafariki , utarudi Kenya kama Blandina na utatumia jina lako halisi”Aliongea Mzee Kweka na kumfanya Blandina na Jestina kushangaa.

“Hapana sipo tayari kuwa mbali na Roma tena , nitaishi Maisha yangu yote yaliobaki kwa ajili ya kufidia malezi ambavyo sikuyafanya kwa mtoto wangu”Aliongea Blandina na kunyanyuka na kuondoka na Jestina alimkimbilia dada yake kwa ajjili ya Kwenda kumpoza.

“Mzee Mwenzangu hili jambo linaweza kuwa gumu tofauti na tulivyodhania?”Aliongea Afande kweka.

“Kweka licha ya kwamba nina muda mchache sana wa kuishi hapa duniani , lakini natamani kuona ndoto tuliokuwa nayo kwa miaka mingi inatimia natamani angalau kuona hatua za mipango yetu zikifanikiwa kabla sijaaga dunia”

“Ni kweli kabisa , hata mimi natamani swala hili lifanikiwe mapema , lakini hata hivyo hatupaswi kuwaza tena , mipango itaenda kama ilivyopangwa , Urusi wako Pamoja na sisi katika hili na ahadi tuliowekeana na Nyerere lazima tuitimize kwa namna yoyote”Aliongea.

“Unahisi Roma atatuelewa baada ya kumueleza mpango mzima?”Aliuliza Atanasi.

“Atatuelewa lakini halitakuwa jambo rahisi”

Unafikiri hawa vikongwe wanapanga nini?

******

Ni siku nyingine ndani ya hoteli ya Serena wanaonekana watu watatu wakiwa ndani ya chumba kikubwa chenye vitanda vitatu , watu hawa hawakuwa wengine ila ni Nadia Alfonso , Mellisa Luiz , na Zoe Kovac , wote walionekana kukaa kwenye masofa na walikuwa wakijadiliana jambo.

“Nadia najua sikuwa muwazi kwako kwa miaka mingi tokea tulivyokutana mara ya kwanza , lakini mambo yote ambayo niliyafanya juu yako kuhakikisha unakuwa mwanasheria maarufu duniani ni juu ya mpango ambao muda si mrefu tunakwenda kuuanza”Aliongea Mellisa.

“Mellisa unajua nilishangaa miaka ile kusikia mtanzania kusimamia kesi kubwa ya Raisi Kim , niliamini kabisa kuna mkono wa mtu nyuma yake , maana Korea Kusini ilikuwa na wanasheria wabobevu kuzidi hata Nadia”

“Ni kweli kabisa , Korea Kusini ilikuwa na wanasheria wabobevu , lakini kutokana na kesi ilivyokuwa inaenda Nadia alikuwa chaguo sahihi, hata nilipomueleza Kim juu ya kumchukua Nadia kama moja ya wanasheria wa kuongoza kesi yake hakukataa , kwasababu kulikuwa na sababu kubwa ya kufanya hivyo”Aliongea Mellisa.

“Madam najua tokea siku ile sikuweza kukuuliza hili swali , lakini kabla hatujaendelea na mazungumzo yetu naona kuna haja kubwa ya mimi kujua”

“Unaweza kuuliza Nadia , sitokuficha tena kama ninataka mipango yetu kufanikiwa , kwani wote tunapaswa kuaminiana”

“Ilikuwaje mkaweza kumtumia Agent 13 katika mpango ule , mpaka tukapata ushahidi na nikashinda ile kesi?”Aliuliza Nadia.

“Nadia kuna mambo mengi sana yanaendelea katika hii dunia kwa sasa na kama ningekuwa mchungaji au nabii nigekupa jibu moja kwa moja kwamba yale ambayo yametabiliwa yanakwenda kukamilika, ili kujibu swali lako labda nikujibu kwamba, kwanza kabisa yote haya ninayoyafanya sio juu ya kisasi pekee bali kuna Zaidi ya sababu”

“Unaweza ukashangaa lakini huo ndio ukweli kwa sasa , ulieleza kila kitu ambacho uliweza kushuhudia kwa macho yako kule Ufaransa , kuhusu Depney , lakini pia juu ya Apollo na Artemis?”Aliongea na kupozi huku akimwangalia Nadia.

“Ulichokiona na kutueleza ndio uhalisia wa dunia ya sasa inakoelekea?”

“Unamaanisha nini?”Aliuliza Nadia na Mellisa alitabasamu , mpaka hapo aliona hakuna ambacho Nadia ambacho ameelewa.

“Nadia kwakua wewe ni mshirika wangu katika mpango huu , labda nikueleze tu kwamba mpaka sasa dunia imegawanyika mara mbili, kuna upande ambao ni nuru na kuna upande ambao ni giza”Nadia alishangaa lakini Mellisa hakuacha kuongea , aliemeza mate na kuendelea.

“Dunia ya sasa inaelekea kwenye mchakato wa New World Order , nadhani kwa elimu yako unaelewa ninachomaanisha?”Nadia alitingisha kichwa kwamba anaelewa.

“Sasa basi mchakato huo hauwezi kufanikiwa pasipo ya Kiza na Nuru kuungana”

“Lakini Madam hilo haliwezekani , Kiza na Nuru haviwezi kuchangamana”

“Umeongea ki usahihi kabisa lakini jambo hilo linawezekana kwasababu palipo na nuru Kiza hakiwezi kutawala na pasipo kuwa na Nuru Kiza kinatawala”Nadia alijiona hana anachoelewa mpaka hapo kwani aliona Mellisa anaongea kimafumbo sana.,

“Nadia Kiza sio kama Giza ila ni namna ambavyo ninatumia kuwakilisha ujumbe wangu kwako kwa ajili ya kunielewa, wewe hapo unapigania haki katika ulimwengu huu na hio ni kazi yako ambayo umeamua kujitoa kwa hali na mali kuona haki inafuatwa basi wewe kwa maneno mengine ni kwamba U nuru ya ulimwengu huu hivyo moja kwa moja ni kwamba upo upande wa Nuru na mapambano yako ni zidi ya Giza”

“Madam umeongea sana na mengi yote nimeona ni sahihi kabisa , lakini swali langu lipo palepale kwanini Ajent 13 alikuwa sehemu ya mpango wangu au ni kwasababu yeye yupo upande wa Nuru ndio maana?”

“Mpaka hapo siwezi kufahamu upande ambao yupo na kukujibu swali lako kwa urahisi ni kwamba ajent 13 licha ya kwamba alikusaidia kupata Ushahidi lakini Taifa la Urusi, Saud Arabia na Iran ndio walioweza kufanya makubaliano ya kibiashara na Ajenti 13 kwa ajili ya kukupatia Ushahidi na kama unakumbuka kesi ilikuwa ngumu kutokana na Marekani kuhusika , hivyo ni rahisi kuelewa sasa kwamba ulikuwa ukipambana na Wamarekani”

“Nadia mimi nimemuelewa Mellisa maneno yake , ili kukusaidia ni kwamba sisi mpaka muda huu tunapambana ili swala la New World Order lisifanikiwe , najua linaweza kuwa jambo gumu ,lakini linawezekana”Aliongea Mrembo Zoe.

“Mwanzoni sikuamini kabisa niliposikia juu ya Miungu watu kwa namna yoyote ile na hata mdogo wangu wakati alipokuwa bize juu ya kuzungumzia juu ya miungu hio sikuweza kumuamni kabisa na niliamini ni hadithi za kufikirika, Labda nianze kukueleza ni utofauti gani upo kati ya Hades na miungu mingine na naamini kupitia hapo unaweza kuelewa”Aliongea Zoe na kuchukua mvinyo .

“Kwa maelezo ya Seventeen , New Hades ni binadamu wa kawaida ambaye alibadilishwa na kuwa sehemu ya miungu watu”Nadia alishangaa.

“Unamaanisha nini kusema alibadilishwa?”

“Si ulisema ulimuona Apollo na Artemis? , sasa nitachukulia mfano kutoka kwao”

“Appollo na Artemis wanatumia miili ya binadamu lakini nafsi zao sio za kibinadamu”Aliongea na kumfanya Nadia kuzidi kushangaa Zaidi na Zaidi.

Kwa maelezo ya Zoe alimwambia kuwa inasemekana miaka mingi nyuma kuna viumbe walifika duniani kutoka angani na baada ya viumbe hivyo kufika Duniani mazingira ya dunia hayakuweza kuendana na miili yao hivyo kuwapelekea kuwa katika hati hati ya kufariki na hapo ndipo walipofanya ‘Transmigration’ kwa kuacha Roho za miili yao kuwatoka na kuvaa miili ya kibinadamu.

Akaendelea na kusema kwamba wakati viumbe hao wanakuja duniani walikuwa wamebeba majiwe mviringo(Godstone) na hayo mawe ndio chanzo cha nguvu zao, yaani kama chaji.

“Hayo majiwe yako wapi?”Aliuliza Nadia.

“Haifahamiki yako wapi , lakini inasemekeana yanamilikiwa na binadamu na sehemu ya jiwe hilo lilitua kwenye mikono ya Taifa la Marekani”.

“Na wakalifanyaje?”

“Swali zuri Nadia , Wamarekani baada ya kupata kwanza walilipatia jina la ‘Godstone’ na walianza kulifanyia majaribio na walikuja kugundua uwezo mkubwa uliokuwa kwenye jiwe hasa katika uwezo wake wa kubadilisha DNA za mwili , na kutokana na gunduzi hio mpango wa kutengeneza miungu watu kwa kutumia jiwe hilo ulianza , kwani waliamini linaweza kumpatia mtu nguvu na kukazaliwa kiumbe chenye nguvu na akili kubwa na majaribio yao yote yalifeli kwani binadamu hawakuweza kuendana na mazingira ya mabadiliko ya DNA za Mwili na hapo ndipo njia mpya iliweza kuvumbuliwa?”

“Njia gani Madam?”Aliuliza Nadia kwa wasiwasi mkubwa.

“Virusi! , waliamini kwa kutegeneza virusi ambavvyo vitakuwa na uwezo wa kukomaza miili ya binadamu na kisha ndio wawamulike wale wahanga kwa kutumia miale inayotoka kwenye Godstone na hatimae watapata nguvu kubwa na uwezo mkubwa na hapa ndipo stori ya Mellisa inaingia, hivyo Project Pro Human ilikuwa ni sehemu ya michakato ya kuweza kutumia Godstone kwenye miili ya watu”

“Walifanikiwa?”

“Ndio waliweza kufanikiwa lakini kwa asilimia ndogo sana”Aliongea Zoe.

“Wewe uliweza vipi kufahamu hayo yote?”

“Mwanamke niliekutana nae ndani ya visiwa vya Maldives ndio amenieleza hayo yote na nina uhakika hata Roma anafahamu kila kitu juu ya hii hadithi”Aliongea Zoe.

“Kwahio utofauti wa Roma na miungu mingine ni nini?”Zoe alitabasamu.

“Roma licha ya kwamba anauwezo mkubwa kama miungu mingine , lakini yeye hajarithishwa nafsi, na hili liliwezekana kutokana na mtu aliemrithi”

“Unamaanisha nini kuhusu kumrithi”

“Namaanisha kuna Hades wa kwanza , huyu na yeye alikuwa ni sehemu ya viumbe waliofika hapa duniani na kufanya ‘Transmigration’, lakini utofauti wa Hades na miungu mingine ni kwamba yeye licha ya kuwa na tabia zinazofanana na wenzake , lakini alikuwa akipinga malengo ya wao kufika duniani”

“Malengo gani?”
 
SEHEMU YA 232

“Malengo yao hapa duniani ni kwa ajili ya kuitawala dunia”Aliongea Zoe na kumfanya Nadia kushangaa mno.

“Lakini umesema kwamba wana uwezo mkubwa , kwanini mpaka sasa hawajaweza kufanya hivyo?”

“Niliuliza hivyo hivyo Nadia, na alinijibu kwamba miungu hio mpaka sasa haijaweza kuwa na uwezo wao wa kawaida kwani walipoteza mawe waliokuja nayo duniani ambayo yanawapa nguvu , kwa maneno marahisi ni kwamba miungu hio mpaka sasa ni dhaifu na siku ambapo itaweza kupata ‘Godstone’ zote basi nguvu zao zitarudi upya na watakuwa na uwezo wa kufanya jambo lolote hata kuponya magonjwa, na hapo ndipo ‘New World Order’ itakapoanza , kwasababu watajifanya kuwa wao ndio Mungu, kwani watakuwa na uwezo wa kufanya jambo lolote ambalo Mungu anaweza kulifanya , wataweza kushusha mvua , wataweza kuponya magongwa na kuyasababisha , wtafanya miujiza mingi na kwasababu binadamu tunapenda ushahidi wa kimiujiza basi tutawafuata”Nadia alijikuta akiogopa sana juu ya meneno hayona kwake aliona ni kama jambo ambalo haliwezekani.

“Unaweza ukashangaa ndio maana Kwa kukurahisishia tu ni kwamba hawa viumbe wanabadilisha miili yao kila baada ya miaka kadhaa na wanafanya ‘Transmigration’ tena na hii yote ni kutokana na kwamba miili yetu sisi binadamu ni ‘mortal’ yaani miili yetu inazeeka baada ya muda na kufa”

“Nadia nadhani uliona Cromwell family, Stern na Alice kuwa ndugu wa damu na ukashangaa kwanini hawa ndugu wa damu wa kawa wapenzi , jibu ni kwamba licha ya wao kuwa na damu zinazofanana za kindugu lakini nafsi zao za kibinadamu zishatekwa na wanatawaliwa na nafsi ya Artemis na Apollo”Alimalizia.

“Lakini mbona Stern na Alice wananguvu za ajabu kwa nilivyoona?”

“Ndio sijasema hawana nguvu, ila ukweli ni kwamba nguvu wanazo ila ni kidogo sana , robo tatu za nguvu zao zilikuwa zikitawaliwa na miili yao , lakini miili yao ilishindwa kuhimili mazingira ya dunia, hivyo hatua ya kwanza ambayo wataweza kurudisha nguvu zao ni kuhakikisha wanapata Godstone na kwakutumia hizo Godstone wataweza kuifanya miili kuwa Immortal na nguvu zao zitarudi upya na hapo utawala rasmi wa hao viumbe wa kishetani utaanza”

“Wako wangapi waliofika duniani?”

“Paa..Paah …!!”Mrembo Zoe alipiga makofi kwa kufurahishwa na swali la Naidia.

“Mellisa tunae mtu sahihi , swali zuri sana Nadia umeuliza”

“Kwa maelezo ambayo hayajathibitika ni kwamba wapo Zaidi ya maelfu”

“Nini… a!!!”

“Ndio hivyo, lakini licha ya hivyo kati ya hao wote waliokuwa na nguvu Zaidi kuliko wengine ni kumi na mbili pekee na hao wote kumi na mbili ni wa ukoo mmoja yaani familia moja na hadithi zinaonyesha kwamba huenda hao kumi na mbili walitokea katika familia za kifalme huko kwenye dunia yao “

“Kuhusu wengine vipi?”

“Wengine haijafahamika , lakini kuna wanaoamini kwamba wengi wao nafsi zao zimebebwa na raia wengi wa Marekani , Uchina, Korea, Urusi ….. hakuna Ushahidi wowote unao onyesha viumbe hawa kuvaa jamii ya Kiafrika na baadhi ya Sehemu nyingi ndani ya mataifa ya bara la Asia japo wapo”Aliongea na kumfanya Nadia kuvuta pumzi , ukweli siku hio ya leo alijikuta kujua mambo mengi ambayo hakuwahi kuyafahamu hapo kabla.

Sasa mpaka hapo maelezo ya Zoe Pamoja na Mellisa ni kwamba kuna Zaidi ya majiwe ya Kimungu ambayo yapo hapa duniani na yanamilikiwa na binadamu wa kawaida na hawa miungu watu ili kupata nguvu zao upya ni lazima wapate Godstone`s zao.

“Naomba niulize swali la mwisho”

“Nadia kuna mambo mengi sana ambayo sijayaelezea ila kwa sasa hupasiwi kuuliza maswali mengi kwani tutakesha pasipo kuzungumza mpango mwingine , lakini nitakuruhusu kuuliza swali lingine”

“Umesema Hades wa zamani alikuwa na tabia kama za wengine wote , lakini pia ukasema kwamba Roma hajatawaliwa na nafsi ya Hades , sasa kama ni kweli nafsi ya Hades wa zamani iko wapi?”

“Hilo swali halina majibu halisi na hata Seventeen hakuweza kutuelezea , ila inasemekeana Nafsi yake ilikufa kabisa na alijiua yeye mwenyewe , lakini kutoka tetesi kutoka kwa jamii nyingi za siri wanaamini Nafsi ya Hades imerudi ilikotoka”Aliongea Mellisa .

“Kwahio Nadia we are here to fight the Darknes”Aliongea Zoe.

“And what abaout our Allies?”

“You will learn them as far as you prove to be usefull for the plan , as for now the plan is to replicate”

“Unamaanisha nini ku replicate ?”

“Nadia mambo haya mpaka sasa hayajatokea kwasababu tu, watu wa nuru ni wengi kuliko watu wa kiza , ikitokea watu wa kiza wakaongezeka kuliko wa nuru basi ndio utakuwa mwisho , hivyo ili kuhakikisha kiza hakichukui nafasi yake lazima tunaofanana tuwe wengi , huo ndio mpango”Aliongea Mellisa.

“Ni kweli Mungu yupo , yeye mwenye ukuu wa kila kitu?”Aliuliza Nadia lakini Mellisa alitabasamu.

“Nadia nafasi ya kuuliza kwa leo ishaisha , lakini kukupa motisha ni kwamba , yes Mungu yupo na huenda binadamu hatujafaamu namna halisi ya kuuelezea uwepo wake that is why things for now is complicated but all prophecies seems to be true”

Unafikiri wataweza kushindana na unabii , ngoja tuone yajayo.

*********

(UNKOWN PLACE)

SEHEMU ISIOFAHAMIKA NDANI YA DUNIA

Ni sehemu abayo haifahamiki ndani ya dunia kama ipo juu ya Ardhi au chini ya maji , ila ni sehemu ambayo ipo duniani.

Sasa basi ndani ya hii sehemu anaonekana Athena , mwanamke mrembo akiingia ndani ya eneo moja zuri mno lililotegenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu , naweza kusema kwamba eneo hili kama utalitafuta hapa Duniani basi huwezi kupata , juu na chini ndani ya eneo hili kulikuwa kunafanana , yaani nikimaanisha kwamba rangi na muundo uliokuwa upo juu na chini yake vinafanana kwa kila kitu , lakini utofauti wa eneo hili na maeneo mengine ni kwamba tu humu ndani ni kama jengo ambalo linaelea angani , lakini wakati huo huo eneo hili lilionekana kama sehemu ambayo imejengwa juu ya jangwa ni sehemu ambayo uwezi kuelezea kwa maneno yakinifu na yakaeleweka.

Sasa ilishindikikana kuelewa ni wapi ndani ya hili eneo kwasababu namna ambavyo Athena ameweza kuingia ndani ya hili eneo ni kwa namna ya kipekee sana , yaani namna ya kuibukia kama jini.

Sehemu hii ilikuwa na mwanga , lakini chanzo cha mwanga hakikuonekana yaani ni kama uingie ndani ya chumba kuwe na mwanga alafu huoni taa zilipo sasa ndio ndani ya hili eneo.

Mrembo Athena kwenye mikono yake hakuwa peke yake bali alikuwa amembeba mwanamke alievalia mavazi meusi kabisa na kutokana na mwanga ukimwangalia huyu mwanamke anafanana kwa asilimia mia moja na Edna.

Athena alitembea huku akiwa amembeba Mwanamke kwenye mikono yake kama mtoto huku akipita kwenye Korido ambavyo imejengwa kama Tunnel , na alikuja kusimamma mwisho kabisa wa korido hio na mwanga uliokuwa nyuma yake ulipotea na kukawa giza tii, lakini muda uleule mbele yake kukafungunga mlango kwa namna ya ‘pentagon, na eneo la mbele liling`aa kwa mwanga hafifu wa kuvutia rangi ya LED na baada ya kuingia ndani mlango ulijifunga vilevile .

“Naira I am Back”Aliongea Athena huku akiingia ndani ya eneo lililokuwa limejengwa kwa utaalamu mkubwa na vioo vingi na chuma kiasi , huku vifaa vingi vya kilektronic vikibip sauti , lilikuwa ni eneo zuri kwa kweli ambalo halielezeki.

“Who is this?”Aliuliza Naira alievalia Miwani kubwa na nguo za bluu tupu kwanzia juu hadi chini , alikuwa ni mwanamke mrembo sana na kwa kumwangalia umbo lake ni kama Nasra, tofauti pekee ni kwamba yeye alikuwa mzungu.

“Huyu ni Seventeen , Mpenzi wa Hades”Aliongea Athena huku akimpita Naira aliesimama na alikunja kushoto na kufikia mlango wa kioo na ulijufungua wenyewe na akaingia ndani , sehemu ambayo ipo na makabati mengi majeneza lakiini ya kioo tupu jumla yake manne , yaliopangwa kwa ustadi mkubwa kwakuachana kwa mita moja moja , huku eneo hilo linatoa mwanga flani hivi ambao umeambatana na mvuke kama vile maji yanachemka na haikueleweka mvuke huo unatoka wapi.

“Nishaua nafsi yake na kuiharibu kabisa , hivyo kwasasa huyu sio binadamu bali ni Shell”Aliongea.

“Unataka kutumia mwili wake?”Aliuliza Naira na Athena mrembo alitabasamu.

“Yes , ana mwili mzuri sana na ni mrembo kupindukia na napenda mwili wa mwanamke mrembo kama nitataka kuitawala dunia, nitamtumia lakini sio sasa , huu mwili niliokuwa nao unanitosha , she will be in Cryosleep mpaka nitakapo muhitaji”Aliongea huku akiingiza mwili wa Seventeen kwenye jeneza la kisasa.

“Boss lakini kwanini nahisi kama kuna jambo halipo sawa na sauti yako , there is no Confidence the way you sound”Aliongea Naira na Athena alifikiria kidogo huku akinuna.

“It`s nothing Naira , twende ukanipe ripoti”Aliongea na kisha wakatoka na kwa jinsi eneo hili lilivyokuwa tulivu ilionyesha kabisa wapo watu wawili pekee.

Walirudi katikati ya lile na kisha wakachukua upande wa kulia na walisimama mbele ya mlango ambao ulijifungua kwa namna flani hivi ya kushangaza kama vile uliyeyuka hewani , yaani unachotakiwa kuelewa ndani ya hili eneo vifaa vyote havijatengenezwa kwa mundo wa pembe nne , ni duara na Pentagon peke yake..

Baada ya kuingia ndani ya chumba kingine, hatimae ilionekana maabara kubwa ya kisasa , lakini jambo la kushangaza ni kwamba hakukuwa na ina yoyote ya kemikali bali kulikuwa na meza kubwa upande wa kulia , juu ya meza hii kulikuwa na vifaa flani hivi kama vile jiko la mkaa lakini la bati ambalo ni duara kamili , juu yake kulikuwa na sinia flani linalong`aa kama kijiko ila juu ya sinia limefunikwa na bakuli muundo wa chupa kubwa ,ila yenye rangi ya kioo , ukiangalia kwa mbali utadhania ni balbu za taa , kwani machupa yale yalikuwa yakitoa mng`ao flani hivi na ilionyesha nani yake kuna kitu ambacho kilikuwa kikisababisha mwanga kutoka , jumla yake machupa yapo kumi pekee.

“Naweza kuona maendeleo ni mazuri Naira , you worked hard for this, When we find the last one , we will finalize the Mission and Stage four will follow”Aliongea na kisha akafunua bakuli moja na palepale mwanga ukapotea kwenye lile bakuli na ndani yake kulionekna jiwe la Kimungu, ‘Godstone”

“Boss kwahio likipatikana jiwe la mwisho misheni itakuwa tayari?”

“Ndio Naira kila kitu kitakuwa tayari “

“Lakini kwa maelezo ulisema mawe haya yanatakiwa kuwa kumi mbili na hapa yapo kumi na moja pekee”

“Uko sahihi hapa kuna mawili hayapo, moja lipo kwenye misheni nyingine na la mwisho sijalipata bado, Naira wewe ni rafiki yangu na nimekupenda kwakua umeamua kunitii ,hata nilivyoamua kuwaua wazazi wako Pamoja na wa rafiki yako Dorisi hukuweka kinyongo na mimi , ndio maana nakujibu kila unapouliza swali”Aliongea na kurudisha lile bakuli juu yake na likaungana na mengine kuwaka rangi kwa namna ya kupumua.

“Nilikubali kuwa mshirika wako, licha ya kuwaua Ryan na Epholia wazazi wangu kwasababu una ndoto za kuubadilisha ulimwengu na kuwa sehemu salama Zaidi , wamekufa kwa ajili ya sababu kubwa hivyo naamini vifo vyao havitopotea bure”Aliongea Naira na Athena alitabasamu na kisha wote wakatoka.

“Una akili kubwa sana you are far different”Aliongea

“Thank you The Doni”Aliongea Naira huku akicheka cheka.

“I hate those Stupid human being when they address me with that horrible name, it`s no swag at all”



“Ni kwasababu hukuwapatia jina zuri kwa ajili ya kukuita”aliongea Naira na Athena akatabasamu.

“Naira naona kila kitu unachofikiria kwenye moyo wako, nitakutumia kwa sasa na baada ya thamani yako kwangu kuisha nitakuua , umepata bahati ya kufanya kazi na mimi kwasababu ulikuwa wa tofauti”Aliwaza Athena kwenye moyo wake.

Sasa hapa haikueleweka Athena alikuwa na mpango gani , lakini pia haikueleweka , Mchina yaani babu yake Lanlan waliishia wapi kwani jana yake walikuwa wakifukuziana na sasa tunamuona



Seventeen akiwa ashakufa tayari na mwili wake upo kwenye Cryosleep.

Transmigration ni kitendo cha nafsi(Saoul) kuhama kutoka katika mwili mmoja Kwenda kwa mwingine.

Cryosleep ni pale binadamu anapohifadhiwa kwenye mashine kama friji ili asiweze kuoza ama kuzeeka hata kama alale miaka mingapi.

Hapa inaonekana Seventeen alikuwa akikiona kifo chake ndio maana akavunja uhusiano na mtoto wake , je atakuwa anafahamu uwepo wa Edna ndio maana akafanya vile, noja tuone.

Usichanganyikiwe kila kitu nimekipangilia vizuri yaani…..
 
SEHEHMU YA 233

Ni siku mbili zilikuwa zimepita Edna aliendelea kumchunia Roma kama kawaida yake na hakukuwa na maongezi mengi kati yao zaidi ya Edna kumtingishia Roma kichwa kila wanapoamka asubuhi kama salama , Edna alikuwa ameongeza ukauzu kwa asilimia mia na kumfanya hata Bi Wema na wanafamilia wengine wasielewe kinachoendelea baina yao.

“Kuna jambo naliona haliko sawa Bi Wema na naomba nikuulize kwasababu wewe umeishi na Roma na Edna kwa muda mrefu kidogo”Aliongea Mama yake Roma , yaani Blandina muda wa usiku.

Blandina alishindwa kuelewa kinachoendelea kabisa kati ya Roma na Edna ,kwani kwa jinsi walivyokuwa wakiishi ni kama hawakuwa mume na mke na ndio maana alitaka kujua japo kidogo , alishangazwa na kitendo cha Edna na Roma kulala vyumba tofauti ilihali walikuwa wameoana lakini pia alishangaa wawili hao walikuwa wakichuniana , hasa kwa upande wa Edna ,jambo ambalo hakuwa amelizoea kabisa kwa mke kumchunia mume wake.

“Unataka kujua nini Blandina?”Aliongea Bi Wema na muda huu walikuwa wakijiandaa kulala.

“Najua sina muda mrefu sana ndani ya hii familia na bado ukaribu wangu na Roma unaonekana kuwa mdogo , jambo ambalo nalifanyia kazi mpaka sasa , lakini jambo moja linalonisumbua ni namna Edna na Roma wanvyoishi , sioni kama ni mke na mume kwa tamaduni zetu za kiafrika”Aliongea.

Bi Wema alinyamaza kidogo , ukweli ni kwmaba mwanamke huyu kabla ya Blandina hajaja hapo ndani kwenye familia, alikuwa ashaongea tayari na Edna na walikubaliana swala la wao kuoana kimkataba libakie siri na Blandina asifahamu , hivyo swali aliloulizwa hapo ndani na Blandina lilimkosesha jibu la moja kwa moja.

“Ni kweli kwa kila ulichoona ni sahihi kabisa na nilitegemea utauliza”Alivuta pumzi.

“Nakiri kwamba makuzi ya Edna yalikuwa ya tofauti sana na ya wanawake wengine , Edna alilelewa kwa malengo ya kuongoza kampuni pekee, na wazazi wake waliacha jambo muhimu la kumjenga Edna kama mwanamke, na haya unayo yaona hapa ndani ni moja ya athari zake , Edna anampenda sana Mr Roma sana tu na kwa Mr Roma pia anampenda sana Edna na haya yote nimeyashuhudia mwenyewe tokea waanze kuishi Pamoja”Blandina alijikuta akivuta pumzi kwa maneno hayo machache , alielewa nini ambacho Bi Wema alikuwa akimaanisha..

“Bi Wema lakini hili la Edna kumchunua mume wake linanitia ukakasi kidogo na mbaya Zaidi ni wawili kuishi vyumba tofauti kwa staili hii mtoto atapatikana vip, kuna ugomvi uliotokea mpaka wakaamua kuishi vyumba tofauti?”Bi Wema alitabasamu.

“Edna na Roma hawajawahi kulala chumba kimoja”Aliongea Bi Wema na kumfanya Blandina kushangaa.

“Kwahio Bi Wema unamaanisha hawajawahi…”Bi Wema alitabasamu kwani alielewa kabisa anachomaanisha Blandina.

“Kuhusu kufanya mapenzi washafanya na Miss Edna usichana wake ulitolewa na Mr Roma”Aliongea Bi Wema na kumfanya Blandina kushangaa , alishindwa kuamini maneno ya Bi Wema kabisa.

Ukweli kwa mtu yoyote asingeamini kama Edna alikuwa Bikra miezi kadhaa nyuma kwa namna ambavyo alikuwa mrembo , ilikuwa ngumu sana kwa urembo wake kushinda vishawishi vyote vya wanaume..

“Najua unafikiria sana juu ya hilo , ila hilo ndio ukweli , Edna hajawahi kuwa na mwanaume mwingine kwenye Maisha yake na Roma ni wa kwanza na ndio maana nasema Edna anampenda sana Mr Roma , mengine unayo yaona ni namna ya Edna alivyolelewa”Aliongea na Blandina alijikuta akishindwa kuzuia alijikuta akitabasamu ndani kwa ndani, aliona kama maneno ya Bi Wema yana ukweli wake basi Edna ni Mke bora sana.

“Bi Wema asante kwa kuniambia haya yote, nilikuwa nikishangaa sana namna Maisha yao yanavyoenda , lakini kwasababu nipo hapa nitahakikisha namlea Edna kama mwanangu na nitamuelekeza yote ambayo hakuwa akiyafahamu kama mwanamke katika utoto wake, lakini hata hivyo naamini kuna jambo ambalo linaendelea kati yao”Bi Wema alitabasamu.

“Ni kweli na naanimi ni wivu tu wa Miss Edna , namjua sana kama kuna jambo linamsumbua moyoni baada ya kuliweka wazi yeye anakuwa kimya , ni yale yale yanayoendelea , lakini siwezi kumlaumu Mr Roma juu ya hilo”

“Unamaanisha nini kuhusu Wivu , usiniambie Roma anatoka nje ya ndoa!!?”Aliongea Blandina kwa kuhamaki na Bi Wema ukweli hakutaka kuonekana mwanamke mbea , hivyo alishindwa kuelezea vizuri.

“Blandina nadhani kadiri unavyoishi na sisi utaelewa kila kitu kinachoendelea sina haja ya kukuelezea kila kitu , Roma ni mwanao hivyo jitahidi kuwa nae karibu”Aliongea Bi Wema na kupanda kitandani.

******

Upande wa Roma yeye hakujali sana mikausho ya Edna, ni kweli alikuwa amefanya kosa kule hotelini la kumuacha peke yake na kupotea na Nadia , lakini kwenye moyo wake alikuwa akijua ukweli kwamba hakuwa amefanya chochote na Nadia , hivyo hakuwa na haja ya kujielezea ilihali Edna hataki kusikia melezo yake , hivyo aliona ajue mambo yake kwa muda huo.

Ni asubuhi ya siku ya Ijumaa Roma kama kawaida alitimiza ratiba zake kama zilivyokuwa zikimtaka kufanya na baada ya hapo alipata kifungua kinywa na wanafamilia wote na kisha akatoka na gari lake huku kichwani kwake akipanga Kwenda kambi ya jeshi ya Mirambo kwa ajili ya kuangalia mafunzo yanavyoendelea.

Saa nne kamili ndio muda ambao aliweza kuingia ndani ya kambi ya Mirambo, ukweli Roma jambo moja ambalo lilikuwa limemsukuma kuja ndani ya kambi hio ni juu ya Magreth mtoto wa Kanali Tobwe , alikuwa akikumbuka maneno ya kanali sana na hata jana yake Kanali alimpigia juu ya swala ambalo hawakumaliza kuongea , hivyo Roma leo hii alikuwa hapo ndani kwa mambo mawili katika kichwa chake , la kwanza ni kuangalia maendeleo na la pili ni kuonana na mrembo Mage.

Baada ya kufika tu alipokelewa na Diego Pamoja na Adeline , huku Mollin akikosekana ndani ya eneo hilo , ila hakuuliza sana , baada ya kupokelewa na wanajeshi wake , alisalimiana pia na mkuu wa kambi kwa bashasha na baada ya hapo alitaka kusikia maendeleo kutoka kwa Diego na Diego alimweleza kila kitu.

“Mfalme Pluto mwanzoni niliwadhatau , ila naona uwezo wao wa kujifunza ni mkubwa sana”Aliongea Deigo huku akitabasamu.

“Nilikuambia mimi Diego kwamba uanajeshi hautokani na muonekano wa nje , bali nia ya mtu ya kutaka kujifunza Pamoja na uvumilivu”Aliongea Roma huku wakitembea kuelekea upande wa vyumba vya mazoezi ndani ya kambii hii.

Kambi ya Mirambo ni moja ya kambi ambazo zimeendelea sana na jeshi liliwekeza sana kwenye kambi hio kwenye vifaa vya kujifunzia na hili liliwezesha wanafunzi kuwa bize Zaidi katika kujiufunza kwa urahisi.

Baada ya Roma kupitia baadhi ya wanajeshi waliokuwa chini ya mafunzo wakichukua mazoezi kimakundi , alitabasamu na kuona kweli Diego alikuwa amefanya kazi kubwa na alistahili pongezi Pamoja na Adeline na Mollin.

Macho yote ya Roma yaliikuwa yakimtafuta Mage , kwani yeye hakuonekana katika baadhi ya sehemu za mazoezi alizopita.

“Diego mwanafuzi Mage yuko wapi?”

“Mfalme unamaanisha mwanafunzi namba ishirni na moja?”

“Ndio huyo huyo “Aliongea Roma na Diego alitabasamu na kuangaliana na Adeline.

“Mfalme Pluto , kwenye wanafunzi ambao nimefundisha yeye ndio ambaye anajuhudi kubwa sana kuliko wote , sijui ni kipi kinamsukuma ndani yake lakini amekuwa sio wa kupunzika na muda wote anachukua mazoezi , tulijaribu kumuasa kupunguza kasi lakini haelewi”Aliongea Adeline.

“Kwasasa yupo wapi?”

“Atakuwa kwenye ukumbi wa mafunzo ya Judo”Aliongea Diego na Roma aliomba kuonyeshwa uelekeo wa ukumbi huo.

Roma aliweza kuingia ndani ya ukumbi ambao ulikuwa ni kwa ajili ya mafunzo maalumu ya Judo na aliweza kumshuhudia Mage akipambana na mwanajeshi ambaye siku ya kwanza alimvimbia kwa kutaka kupigana nae.

Roma aliacha kwanza mapambano kati ya hao wawili yaishe kwanza kabla ya kingilia.

Roma alijikuta akisadiki maneno ya Adeline , Mage alionekana kweli kubadilika na uwezo wake kuongezeka maradufu , hakuwa Mage alekutana nae miezi kadhaa nyuma , ila Mage huyu alionekana kuiva kwa siku kadhaa tu tokea kuanza kwake kwa mafunzo.

Baada ya dakika tano za kusubiri hatimae afande Mage alimshinda Afande Baga na kumfanya Roma kutabasamu na kisha kuanza kupiga makofi na kuwafanya Mage na Afande Baga kugeuka na kumwangalia Roma , kwani hawakuwa wamemuona wakati akiingia.

“Afande Baga , nilijuwa uko vizuri kimapigano kumbe hata Mage alieanza mafunzo juzi anakuzidi?”Aliongea Roma huku akitabasamu na Baga alijikuta akinuna baada ya kugundua aliekuwa mbele yake ni Roma , alionekana kutompenda Roma.

“Komredi Mage tuondoke tukapumzike kwa ajili ya baadae”Aliongea Baga pasipo kumzingatia Roma na Mage na yeye alitingisha kichwa kukubaliana na Baga na kuanza kupita hatua kutoka nje na Mage alionekana kutotaka kabisa kuongea na Roma.

“Nimekuja hapa kwa ajili ya kuongea na wewe halafu unaniacha hapa ndani?”Aliongea Roma akiwa siriasi na Mage alimwangalia Roma kwa hasira .

“Afande Roma , Komredi Mage kwasasa amechoka na sidhani kama kuna jambo lolote unaweza ukaongea nae kwani wote sisi ni wanafunzi na hakuna sheria inayomzuia kukataa ombi lako”Aliongea Baga huku akiwa amekunja sura , ila Roma hakumjali sana Baga , alikuwa ashamuona kama mwanaume ambaye anammendeea Mage , hivyo maneno yote hayo aliyatafsiri kama wivu.

“Okey! Kama afande Mage hataki kuongea na mimi na amechoka basi mnaweza kuendelea na safari yenu”Aliongea Roma akiachia mkono wa Mage na Baga alivuta pumzi ya ahueni na afadhari.

Roma hakuona haja ya kulazimisha kuongea na Mage hivyo alimuacha aendelee na safari yake , huku yeye akitembea ndani ya eneo hili la mazoezi akilikagua.

“Komredi tangulia nakuja”Aliongea Mage baada ya kutoka nje akiwa ametangulizana na Baga.

“Komredi Mage , haina haja ya kujilazimisha kuongea na yule mtu , huna haja ya kuogopa , tuondoke”Aliongea Baga huku kuna kitu ambacho kilikuwa kikimtekenya moyoni , alikuwa akihisi wivu na hakuwa tayari kuona Roma na Mage wanajenga ukaribu na ndio maaana alitaka kuweka ukuta.

“Ni muhimu kwangu kuongea nae, tutakutana baadae”Aliongea Mage na hata kabla ya kusubiri jibu kutoka kwa Baga aligeuka na kukimbilia ndani alikotoka.

“F***ck”Alitukana kimya kimya Afande Baga huku akimwangalia namna mpododo wa Mage unavyotingisiha akimbilia ndani alikomuacha Roma.

Roma aliekuwa upande wa mbele wa jengo hili akiwa ameupa mgongo mlango , alijikuta akitabasamu baada ya kuhisi uwepo wa mtu nyuma yake.

“Romaa..!!!!”Aliita Mage huku akiwa amesimama kita kadhaa na kumfanya Roma ageuke na kumwangalia mrembo huyu anaejifanya mjuaji hata kwenye mambo ambayo hana uwezo nayo , mambo kama vile hisia za mwili wake

Roma alimpa ishara Mage ya kumsogelea huku akitanua mikono kama ishara ya kutaka kumbatio kutoka kwake na Mage alisimama vilevile kama sanamu huko akikosa maamuzi , ni kama alikuwa akishindana na mwili wake na zilipita dakika chache tu , Mage alimkimbilia Roma na kwenda kudua kifuani huku akianza kulia kwa kwikwi , lakini Roma hakutaka Mage aendelee kulia kwani alimshika Mabegani na kumsogezea mdomo na Mage alijikuta akifumba macho kusubiri kinachoendela.
 
SEHEHMU YA 233


Roma alimpa ishara Mage ya kumsogelea huku akitanua mikono kama ishara ya kutaka kumbatio kutoka kwake na Mage alisimama vilevile kama sanamu huko akikosa maamuzi , ni kama alikuwa akishindana na mwili wake na zilipita dakika chache tu , Mage alimkimbilia Roma na kwenda kudua kifuani huku akianza kulia kwa kwikwi , lakini Roma hakutaka Mage aendelee kulia kwani alimshika Mabegani na kumsogezea mdomo na Mage alijikuta akifumba macho kusubiri kinachoendela.
Mr. Roma, kitombi boy.
Hapa lazima Mage agongwe tu, no way.
 
Back
Top Bottom