Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Humi watu [emoji23]hawapendikulipa ila wana force story iletwe mapema
Hili chama la wana kama Faru Dume au Mesina....sio team la kulipia hili team la ku support Hadith yetu iende mbele zaidi. Humu SinganoJr kama Hedes au Messi. Anatakiwa atupia mzigo 3 times kwa week. Akiwa kata itiwa poa haina mbambamba. Mwamba hana maneno sie tunamuamini ataleta zigo tuko pamoja mpaka mwisho wa dahali. Si unaona mtoto Edina anaelekea kibra.
 
Humi watu [emoji23]hawapendikulipa ila wana force story iletwe mapema
weweeeee.. humu NDO kijiwe ambacho mtunzi akitupia akapata likes kumi na comment Saba anafarijika Sanaa kuliko huko kwingine kulikojaa failure kibao hata comment elf kumi hazimfurahishi kama HAPA kwetu.

HAPA mtu unapata credit kubwa sana kuliko huko wassap Facebook na maujinga mengine ikiwemo insta.

Kwa hiyo.

hebu ngoja kwanza kamuite atupie ngalu vipnde vitatu.
 
SEHEMU YA 345.

“Inamaana haukufahamu kama Dr Elvice Daniel ni Afisa usalama mpaka siku ya kifo chake?”Aliuliza Roma hio ni mara baada ya Suzzane kumueleza kwamba Elvice alikuwa ni afisa usalama.

“Ndio nakiri sikumfahamu Elvice kama nilivyokuwa nikidhania , Elvice nilimfahamu kama Daktari wa magonjwa ya uzazi pekee na amesomea Urusi na USA lakini sikudhania wakati huo huo anaweza kuwa afisa usalama”

“Uliwezaje kufahamu hilo?”

“Alinielezea Boss Raheli kila kitu baada ya kifo chake na ndipo nikajua kwanini Elvice alipigwa risasi , ilionyesha aligusa sehemu ambayo hakupaswa kugusa ndio umauti wake ukamkuta”Alijibu Suzzane kwa huzuni.

“Okey nadhani kuna Zaidi ya unachokijua kuhusu Elvice na sio nyaraka tu ambazo umenipatia , lakini kabla ya kuendelea huko nataka unieleze Nyaraka hizi umepatiwa na nani?”

“Nyaraka hizo nilipatiwa na Boss Raheli mwenyewe baada ya mwezi mmoja baada ya kifo cha Elvice , alinipa maagizo nikupatie”Aliongea Suzzane na kumfanya Roma kushangaa , inawezekanaje Raheli kutoa maagizo ya kupatiwa nyaraka ilihali yeye hakuwa akijuana hata na huyo Raheli.

“Suzzane acha kunidanganya , kama unahisi naweza kushughulikia hili swala unapaswa kuwa mkweli maana mpaka kuja hapa ni kwamba nishaamua kulifanyia kazi”

“Ni kweli ninachokuambia, nilichelewa kukupatia kwasababu sikulifahamu jina lako halisi nilifahamu wiki iliopita kupitia Boss Edna”Aliongea Suzzane na kumfanya Roma kujawa na shauku.

“Jina gani?”.

“Hades au Mfalme Pluto, nisubiri kuna kitu nikuonyeshe”Aliongea Suzzane na kunyanyuka huku akimuacha Roma kwenye mshangao na ndani ya dakika tu aliweza kurudi na kumpatia kikadi chenye maandishi (Business card), ambayo juu yake kulikuwa na jina la Hades au Pluto , lakini pia chini yake kulikuwa na nembo ambayo alikuwa akiifahamu , ni nembo ambayo kwenye visiwa vya wafu ilitambulika kama utambulisho wa uraia , nembo hio ilikuwa ikifanana kwa asilimia kubwa na ‘Tatoo’ walizochorwa , Sheikh Assad , Mellisa na Phill.

Roma alijikuta akitabasamu huku akikigeuza kile kikadi kulia na kushoto ni kama alikuwa akikichunguza na hakuongea neno lolote Zaidi ya kukiweka mfukoni.

“Suzzane nielezee kingine unachokifahamu kuhusu Kifo cha Raheli , chochote unachokijua”Aliongea Roma na Suzzane alifikiria kidogo.

“Sina taarifa nyingine Zaidi ya hio na nyaraka nyingine ambayo Raheli ameniambia, itapatikana kupitia kwa Edna , lakini mwezi uliopita kuna kitu ambacho nimekigundua”Aliongea Suzzane na kisha alitoa simu yake na Kwenda upande wa ‘Document’ na kisha alibonyeza faili ambalo lipo kwenye mfumo wa PDF na kumuonyesha Roma.

Roma aliangalia faili hilo na alikuwa ni kama mara ya pili kuona taarifa zilizoandikwa ndani yake.

“Hili faili nilishawahi kuliona kwenye meza ya Edna ofisini kwake na limeorodhesha majina ya kampuni na nadhania ni makampuni shindani ya Vexto”Aliongea Roma.

“Unaweza kuwa sahihi lakini kuna kitu hujakiona kuhusu hio orodha , angalia jina la katikati namba nane”Aliongea Suzzane na Roma aliangalia jina hilo na lilisomeka Swiss IN0943.

“Nadhani unajua kwamba Tanzania hakuna kampuni ya Swiss IN, kwa maelezo ya Boss Edna ni kwamba hii orodha alipewa na mama yake na anaamini ni kazi ambayo mama yake amemuachia kuikamilisha na alinipa maagizo ya kufatilia kuhusu hii Swiss IN na mpaka leo hii hatujaweza kufahamu maana ya Swiss IN ni nini kwani hakuna kampuni yenye jina hilo”Aliongea Suzzane.

“Hii sio kampuni”Aliongea Roma na kumfanya Suzzane kushangaa.

“Unaijua?”

“Mhmh Edna anashindwaje kung’amua kitu kidogo kama hiki , hili ni jina la usajili wa ‘Deposit Boxes’ kwa kila taifa . Swiss IN ni Anuani maalumu ya sehemu inapopatikana box husika na namba zilizofuatia mbele ni Box Numbers”Aliongea Roma na Suzzane sasa akili yake ilianza kufunguka na alitabasamu mara moja.

“Ngoja nimueleze Edna”Aliongea Suzzane lakini Roma alimzuia.

“Nitamuelezea mimi mwenyewe kwa sasa usimuambie chochote”Aliongea Roma na Suzzane alitingisha kichwa kukubaliana na Roma.

Kwakua Suzzane hakuwa na kingine ambacho alikuwa akijua Zaidi kuhusu kifo cha Raheli mama yake Edna , basi Roma hakuona haja ya kuendelea kubaki hapo , alipanga kurudi nyumbani kwanza ili kuchukua hatua inayofuata , swala ambalo linahusiana na ‘Deosit Box’, aliamini huenda Raheli kuna kitu ameficha kwenye sanduku hio ndio maana akatumia njia isio ya moja kwa moja kufikisha ujumbe.

Roma wakati akiwa kwenye gari akirudi mjini Dar Es salaam , alikuwa akiangalia kikadi ambacho amepewa na Suzzane , kikadi ambacho kilikuwa na jina lake pamoja na nembo maalumu ya kiraia kutoka visiwa vya wafu.

Kuna hisia zilikuwa zikimwambia Hades wa zamani alikuwa akihusika kwenye maswala mengi ambayo yaliikuwa yakimzunguka ,lakini kadri alivyokuwa akiunganisha matukio ya nyuma na ya wakati huo alikosa jibu moja kwa moja na swali likabakia kwenye kichwa chake kwanini Raheli akawa na hicho Kikadi mpaka akampatia Suzzane kabla ya kifo chake.

Ilikuwa ni jumamosi na usiku wa siku hio kulikuwa na mashindano ya Kizazi nyota hivyo Roma alipanga kuhudhuria na Edna siku hio kushuhudia mashindano hayo kwani ilikuwa ni Weekend na waliona ni vyema kumuunga mkono Sophia ambaye alikuwa akifanya vyema.

Roma katika kichwa chake swala linalomuhusu Raheli aliona kwanza aliache kama lilivyo kwa muda mpaka atakapoona ni wakati sahihi wa kumuelezea Edna , alimini taarifa hio inaweza kumletea Edna majonzi sana , hivyo aliona aache kwa muda mpaka angalau mashindano yapite ndio amueleze Edna kuhusu ‘Deposit Box’ iliopo kwenye benki ya Swiss ili wakaangalie kwa pamoja ni kipi kipo ndani ya boksi hio.

Muda wa usiku Roma aliweza kukutana na wafanyakaz wa kampuni ya Vexto yaani Recho , Benadetha na Tina , warembo hao pia walikuja ndani ya maeneo hayo kwa ajili ya kuhudhuria maonyesho ya mashindano hayo.

“Roma hebu tuelezee una mahusiano gani na boss?”Aliongea Recho mara baada ya Edna kutangulia ndani akiwa ameongozana na Nasra pamoja na Dorisi ambao pia walikuwa hapo kwa ajili ya kushuhudia mashindano , Roma peke yake ndio aliebakia nje akiwasabahi wafanyakazi wenzake kutoka idara ya PR.

Sasa baada ya wafanyakazi hao kumuona Roma akiingia ndani ya hilo eneo akiwa kwenye gari moja na Edna walipatwa na maswali na kutaka kujua ni mahusiano gani yapo kati yake na Edna mpaka kupelekea kila kwenye hafla kuja pamoja , kwani ilikuwa ni mara mbili mfululizo Roma anaonekana akiwa na Edna.

“Tina wewe unahisi nina mahusiano gani na Boss?”Aliuliza Roma huku akimwangalia Tina ambaye usiku huo uso wake ulikuwa angavu kwa kujipodoa.

“Mpo tayari niwaambie?, Roma upo tayari nitoboe siri?”Aliongea Tina kwa mbwembe na Recho alimwangalia Tina na kumpa ishara ya kuongea huku akivuta mdomo.

Recho na Tina walikuwa ni marafiki ambao Maisha yao ni kama walikuwa wakichukiana lakini ukweli walikuwa ni marafiki wakubwa na mara nyingi Tina utamkuta akilala nyumbani kwa Recho na Recho mara nyingine pia angelala kwa Tina, sasa Recho alivuta mdomo kwani aliamini Tina hakuwa na ukweli aliokuwa akiujua nan i mbwembwe tu, kwani kama Tina angekuwana umbea wowote ule mtu wa kwanza kufahamu angekuwa yeye.

“Roma tuambie mwenyewe una mahusiano gani na Boss?”Aliuliza Benadetha lakini kabla Roma hajajibu alionekana mrembo Amina akiingia ndani ya eneo hilo akiwa amevalia gauni rangi nyekundu lenye vimeta meta, alikuwa amependeza haswa na alikuwa na mpambe wake nyuma akishikilia gauni hilo lisiburuzike chini.

“Roma hivi uliwezaje kumshawishi mrembo kama huyu kuja kufanya kazi kwenye kampuni ya Vexto Media, tokea tufahamu anafanyakazi kama Secretary wako tulikuwa tukijadili hili swala kwa muda mrefu”Aliongea Recho lakini Roma macho yake yote yalikuwa kwa Amina na ni kama hakuwa akimsikiliza Recho, jambo ambalo lilimkasirisha Recho na kugeuka na kutembea kuelekea ndani kihasira hasira na kumfanya Benadetha na Recho kucheka huku wakimfuata kwa nyuma.

“Babe nadhani usiku wa leo unatafuta nafasi ya kwanza kwa mwanamke mrembo na wa kupendeza kuliko wote”Aliongea Roma mara baada ya kumfikia Amina.

“Naweza kupendeza sana lakini kwenye uzuri simfikii mkeo Edna”Aliongea Amina kwa sura ye kejeli huku akipita na kumfanya Roma kutabasamu.

Muda ulikuwa umeenda hivyo Amina hakuwa na muda sana wa kuendelea kuongea na alimpita na kuingia mlango tofauti na wageni wengine.

Roma baada ya kuona anaowafahamu wote wameingia ndani na yeye alipiga hatua kuingia ndani ya ukumbi huo.

Mpangilio wa meza ulikuwa ukitokana na uwezo wa mtu kulipia , watu hawakuwa wakiingia bure , kulikuwa na malipo yaliokuwa yakifanyika hivyo kila mtu alikuwa na tiketi , Roma bada ya kuingia ndani alisimamishwa na muhudumu ili aonyeshe tiketi yake.

“Wewe ni mgeni?”Aliuliza Roma mara baada ya kuambiwa aonyeshe tiketi wakati yeye hana, ukweli yule muhudumu hakumfahamu Roma kama Director wa kampuni na sio kwake tu wageni wengi hawakuwa wakimfahamu Roma kwani alikataa kuonekana hadharani na kazi zake zote zilikuwa zikisimamaiwa na Amina pamoja na Daudi, hivyo ni watu wachache sana waliokuwa wakimfahamu kama Mkurugenzi mtendaji wa Vexto Media.

“Mimi sio mgeni kaka ,utaratibu wa kuingia ukumbini ni lazima uwe na tiketi inayooyesha meza unayokaa”Aliongea yule mwanamke.

“Anko Roma!!?”Ilikuwa ni sauti ya kike iliosikika nyuma ya Roma na kumfanya kugeuka.

“Donyi Donyi”Aliongea Roma mara baada ya kumuona mtoto wa kike mrembo ambaye ni siku nyingi kidogo hakuwahi kumuona.

“Rom!!!”Sauti nyingine nyuma ya Donyi ilimwita Roma na alivyogeuza macho alimwona Neema Luwazo alievaa akapendeza na alionekana ameingia hapo akiwa ameongozana na Donyi.

“Mom! Unamfahamu Anko Roma?”Aliongea Donyi kwa mshangao na Neema Luwazo alijikuta akiwa ni mwenye mshangao hata yeye hakudhania mtoto wake alikuwa akifahamiana na Roma , moyo wake ulipiga kwa nguvu na kuomba anachokiwaza kisiwe cha kweli.
 
SEHEMU YA 346.

Hakukuwa na muda wa kusimama mlangoni na kuulizana kwani wageni wengine walikuwa wakiingia na shughuli yenyewe ndio kwanza ilikuwa ikianza.

Mhudumu alipewa maagizo ya kumpeleka Roma mpaka eneo la VIP kwani alikuwa ndio Director wa kampuni ya Vexto Media , mwanadada yule aliefahamika kwa Asha alishangaa huku akimpa Roma heshima yake na kumpeleka eneo la VIP.

Roma baada ya kukaa kuna jambo lilimfanya kutamani kucheka , kilichomfurahisha siku hio ni kutokana na kwamba wanawake wake wote walikuwepo , hata Rose ambaye hakumtarajia kabisa kuhudhuria alikuwepo na wote wakiwa wamekaa kwenye mstari mmoja wa eneo la VIP.

Edna alikaa karibu na Roma upande wa kushoto huku michepuko yake ikiwa upande wake wa kulia ,Edna alijikuta akikagua kila mwanamke na kujikuta mwenyewe akimkubali mume wake Roma Ramoni , kwani mtu yoyote angekuja eneo hilo na kuambiwa wanawake wote waliokaa kwenye msururu wa meza moja walikuwa ni wanawake wanaojihusisha na mume wake hakuna ambaye angeamini.

Rose , Dorisi , Nasra, Neema Luwazo, Amina, Mage na Edna wote walikuwa kwenye ukumbi huo wa mashindano na kila mmoja alikuwa akimwangalia Roma kwa wakati wake.

Wanawake wote walikuwa warembo na wakavaa wakapendeza na uzuri wao ulitofautiana vitu vichache sana na kila mmoja alikuwa na kitu cha ziada ambacho mwenzake hana, kwa mfano Rose licha ya kuwa na sura nzuri , lakini pia alibarikiwa mguu wa bia kuliko wenzake wote , ukimwangalia Amina yeye alikuwa na sura flani hivi ya kimaonyesho sana , pamoja na mwili wa kipekee ambao watu wengi wanasema ni ‘Sexy Body’sasa kwa wengine pia ilikuwa hivyo hivyo , kila mmoja alikuwa na kitu cha ziada ambacho mwingine hana.

Edna alijikuta akimwangalia Roma aliekuwa pembeni kwa madakika kadhaa na Roma alijua Edna alikuwa akimwangalia , lakini alijikausha kimya kama sio yeye vile, macho yake yote yalikuwa kwenye steji akiangalia wasanii waliopewa nafasi za kuimba kabla mashindano kuanza.

“Wahenga wanasema jina lina beba tabia”Aliongea Edna kwa sauti ya chini iliosikika kwenye masikioya Roma na kumfanya amwangalie

“Unamaanisha nini mke wangu kipenzi”Alijibu Roma huku akiwa ameweka tabasamu.

“Jana nilikuwa nikisoma Habari za mfalme Pluto na nimegundua aliekupatia hilo jina aliangalia tabia yako kwanza”Aliongea Edna huku akikaza macho mbele na Roma alijikuta akigusa pua yake.

“Kwahio mke wangu unaniambia wanawake wote wenye majina ya Edna ni warembo kama wewe?”

“Mfalme Pluto , unaonaje ukifanya utafiti wewe mwenyewe na kuja na majibu?”Aliongea kiutani huku akiangalia mbele na Roma alijikuta akitabasamu.

“Mke wangu kumbe na wewe unajua kuongea utani”

“Hakuna kigezo cha kumfanya mtu asiwe anaongea matani muda mwingine na isitoshe sijakutania nimeongea jambo la kweli usijitoe ufahamu”Aliongea na kisha akaurudia ukazu wake na kuendelea kuangalia matukio yaliokuwa yakifanyika mbele yake.

“Rose mambo” Alisalimia Nasra aliekuwa amekaa karibu na Rose.

“Poa mambo vipi Nasra”

“Kumbe unanifahamu?”

“Naachaje kutokumfahamu mke mwenzangu”Aliongea Rose huku akitabasamu na kugeuka upande aliokaa Roma na ile anageuka alikutana na macho ya Roma yaliomwangalia kwa tabasamu na kisha akaishia kukonyezwa , kitendo kilichomfanya hata Rose kucheka.

“Mnacheka nini nyie?”Aliingilia Dorisi aliekuwa upande wa kushoto upande wa Rose,hata Dorisi alionekana alikuwa akitafuta nafasi ya kuongea na Rose ila alishindwa kuanza yeye mpaka Nasra alivyo anza.

Wote watatu waliangaliana kwa wakati mmoja na walijikuta wakichekana , walionekana walikuwa wakiongea kwa ishara.

Ukweli mpaka hapo kila mmoja alikuwa akimjua mwenzake alikuwa akitembea na Roma na ndio maana waliishia kuchekana.

Upande wa Edna licha ya macho yake yote kuwa mbele ya jukwaa , lakini alikuwa na jicho la tatu , wakati Rose , Dorisi na Nasra wakiongea kwakucheka alijjikuta akiona wivu na aliona ni kama alikuwa akichekwa yeye kama mke.

Kuna kitu flani kilimfanya kuona wivu ambao mwenyewe alishindwa kuutafsiri na alijisomea tu moyoni mwaka kwamba dawa yao inachemka , alijiambia muda si mrefu atamfanya Roma asiwakumbuke kabisa.

Upande wa Neema Luwazo baada ya Donyi kumuelezea namna alivyokutana na Roma , alijikuta moyo wake ukiwa na amani kwa mara nyingine ,kwani alikuwa akihofia Roma amekwisha kutembea na mtoto wake Donyi.

Neema licha ya kwamba alikuwa akimpenda Roma ila likija swala la wanawake hakuwa akimwamini kabisa , alimuona Roma ni mwanaume ambaye hakuna mwanamke ambaye anaweza kumkimbia , maneno yake aliyaona sahihi kabisa , kwani wanawake waliokuwa wamejipanga msururu mmoja kuanzia kwa Nasra msichana mwenye kujielewa ambaye alikuwa akimfahamu muda mrefu tu tokea aanze kufanya kazi na kampuni ya Vexto , lakini pia upande wa Dorisi pia alikuwa ni msichana anaemfahamu sana tu na alikuwa akimjua kama moja ya wasichana wanaojitambua tena ikampelekea kipindi kutamani kumwajiri lakini Dorisi akakamkatalia huku sababu ikiwa ni kwamba alikuwa akipenda kufanya kazi karibu na Edna ambaye ni rafiki yake , lakini pia Neema Luwazo alimwangalia Edna mwanamke siriasi sana ambaye amemfahamu kwa muda mrefu, msichana ambaye ameshinda vizingiti vyote vya changamoto za kibiashara na kuifanya kampuni ya Vexto kuwa kubwa, msichana ambaye alikuwa akijiheshimu sana na asie na makuu licha ya kupewa uzuri wa kipekee lakini ndio huyo pia ambaye amenasa kwenye mtego wa mwanaume Roma Ramoni , sio kwa hao wenzake tu alijifikiria hata kwa yeye pia, licha ya misimamo yake na namna alivyokuwa makini likija swalala wanaume , lakini pia amenasa kwenye mtego wa Roma , alijiambia hakuna mwanamke ambaye anaweza kumkataa Roma , hivyo aliona licha ya kwamba Donyi mtoto wake hajajihusisha bado kimapenzi na Roma lakini anapaswa kuchukua hatua za kuepusha swala hilo na namna ya kipekee ni kumuweka Domyi wazi juu ya uhusianao wake na Roma.

“Mama ulifahamina vipi na Anko Roma?”Aliuliza Donyi mara baaada ya kumaliza kumuelezea yeye jinsi ambacho aliweza kukutana na Roma na kumuokoa na majambazi kule baharini.

“Tukiwa tunarudi nyumbani nitakuelezea sawa?”

“Mhmh ! Mama kuna kitu nahisi.. maneno ya baba naanza kuona ukweli wake”Aliognea Donyi.

“Baba yako kakuambia nini?”

“Ameniambia nina baba mwingine wa kambo ila hajaielezea ni nani”Alongea Donyi na kumfanya Neema kumwangalia mwanae kwa muda kidogona kisha alipotezea baada ya msanii wa kwanza kuimba kutokea stejini.

Kutokuonekana kwa Donyi kwa kipindi kirefu ni kutokana na kwamba mrembo huyo alikuwa chuoni nchini Marekani akiendelea na masomo yake na alikuwa nyumbani mwezi huo kwa ajili ya likizo.

Sophia alionekana kukosa mshindani kabisa kwenye mashindano hayo, Uzuri wake , sauti nzuri pamoja na pumzi lakini pia namna ambavyo aliweza kutawala jukwaa vilimbeba sana Sophia na kukonga sana mioyo ya watu wengi.

Alionekana kujiamini kabisa na alikuwa ni msanii halisi, watu walimpigia makofi sana kwanzia mwanzo wa kuimba mpaka anamaliza , majaji hawakuwa na maneno sana na kipaji cha Sophia na aliweza kupita moja kwa moja Kwenda ishirini bora.

Baada ya Sophia kumaliza tu kuimba akijiandaa kutoka jukwaani mara mwanaume Handsdokme alievaa suti akapendeza , alionekana akitokezea jukwaani huku akiwa amebeba ua rangi nyeupe kubwa lenye kupendeza , mwanaume huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Denisi Senga.

Alitembea mpaka kwenye steji karibu na Sophia na kisha akamkabidhi lile ua na kwasababu Sophia alikuwa juu ya jukwaa na kamera zilikuwa zikimmulika alishindwa kabisa kukataa lile ua na kulipokea.

“Hongera sana Sophia”Aliongea Denisi. Na vilio vya shangwe vilirindimwa ukumbi mzima , kila mtu alikuwa akimjua Denisi kama mtoto wa Raisi Senga , hivyo kitendo cha kumzawaida Sophia ua kiliibua misisiimko wa mashabiki.

Denisi aliomba maiki kutoka kwa Amina na akapewa , jambo ambalo lilimfanya Sophia kuwa ni mwenye wasiwasi sana , kwani hakuwa akijua ni kitu gani ambacho Denisi alikuwa akidhamiria kufanya, alikuwa akiogopa Denisi kutangaza hadharani juu ya historia yao ya Maisha ya nyuma.

Upande wa Roma mwenyewe alijikuta akikunja sura na kumwangalia Denisi kwa macho yenye kiulizo , mwenyewe hakuwa akijua kwanini Denisi karuhusiwa kwenye steji , jambo hilo lilimkasirisha na aliona Denisi anafanya mambo ambayo hayana msingi, kabla Denisi hajaanza Roma alitaka kunyanyuka lakini Edna aliekuwa pembeni yake alimzuia kwa mkono.

“Mabibi na mabwana Habari za usiku huu”

“Salamaaa…!!!” watu waliitikia kwa shangwe na kumfanya Denisi kutabasamu alikuwa akijiamini hatari.

“Jamani nimejikukta nimeshindwa kujizuia na kupanda stejini hapa , niseme kabisa mimi ni moja wa mashabiki kindaki ndaki wa Sophia na mpaka sasa Sophia namuona kama mshindi wa mashindano haya”Aliongea Denisi na watu walimuunga mkono kwa shangwe sana na Sophia alijikuta akivuta pumzi ya ahueni.

Baada ya maneno machache ya kumpamba Sophia Denisi aliomnyooshea mkono Sophia kumuomba kumtoa ukumbini hapo na Sophia alijikuta akikosa uamuzi wa moja kwa moja na baada ya dakika moja ya kufikiria aliamua kuupokea mkono wa Denisi na kisha kutoka stejini , jambo ambalo lifurahisha sana watu wengi, lakini kwa upande wa Roma ni kama hakupenda kile kitendo.

Ni siku nyingine habari kubwa mtandaoni ikawa ni tukio la Denisi mtoto wa Raisi kuingia ukumbini na kumtoa mrembo Sophia , kila mmoja aliibuka na dukuduku kwenye kichwa chake , huku wengi wakisema Sophia itakuwa anatoka kimapenzi na mtoto huyo wa Raisi , lakini wengine wakisema kama sio wapenzi ni swala la muda tu mtoto mzuri huyo kuingia kwenye himaya ya Denisi.

Sophia alikuwa maarufu sana ndani ya muda mfupi na siku hio ya jumapili alionekana ku’trend’ sana mtandaoni.

Upande wa Roma ambaye hakuwa sana na habari na mitandao alijikuta akiingia mtandaoni kuangalia kile kinachoendelea , kwani sasa hivi alikuwa na siku ambayo amepewa zawadi na mke wake Edna na alikuta picha nyingi za Sophia zikiwa zimesambaa mtandaoni , wengi wakimsifia kwa kipaji na wengine wakiongelea swala la Sophia na Denisi.

Upande wa nyumbani kwa Abubakari , walionekana vijana sita wakiwa kwenye furaha sana, vijana wenyewe walikuwa ni Abubakari Hamadi , Denisi , Desmond ,Elvice Temba , Sali pamoja na kijana mwingine mnene hivi, Wote kwa pamoja walikuwa wakimpoongeza Denisi kwa kitendo chake alichoweza kufanya siku ya jana yake na kupelekea siku hio ya jumapili picha zake kusambaa mtandaoni.

Haikueleweka vijana hawa waliwezaje kukutana pamoja na kuunda urafiki , lakini walionekana kuendana vyema kitabia kwa asilimia nyingi.

“Denisi hupaswi kuzembea Zaidi sasa , unatakiwa kuchukua hatua inayofuata ya kujiweka karibu na mrembo Sophia”Aliongea Abubakari , huku akiwa ameshikilia kikombe aina ya Solo Cup kilichojaa bia ndani yake, ni kama walikuwa wakisherehekea licha ya kwamba muda huo ilikuwa ni asubuhi ya saa nne.

“Kwanzia leo hii nitakuwa namtembelea mara kwa mara kambini kwao na nitatumia nafasi hio kuuteka moyo wake”Aliongea Denisi na kuungwa mkono na kila mmoja.

“Hapa anaefuatia ni Desmond na Edna”Aliongea Elvice na wote kwa pamoja wakamgeukia Desmond ambaye alionekan usiku mzima aliutumia kulewa.

“Muda si mrefu Edna anakuwa wangu , kuna mpango upo jikoni, unajua Edna kinachompa kiburi ni ile kampuni, nikishaichukua atakuja kwangu tu”Aliongea Desmond na wenzake wote walimgeukia na kumsikiliza, huku Denisi akionyesha kuwa ndio mwenye shauku Zaidi.

“Desmond utaweza vipi kumpokonya Roma mke wake , kuna jambo sijaweka wazi , nafikir wote mnafahamu yule choko ni ndugu yangu wa damu?”Aliuliza Denisi na wenzake wote walionekana kushangaa kwani taarifa hio ilionekana kuwa mpya kabisa.

“Acha utani Denisi , Roma ni ndugu yako?”Aliuliza Abubakari kwa shauku.

“Ndio , ni mtoto wa kwanza kwa baba na Blandina mtoto wa Mzeee Atanasi”Aliongea Denisi kivivu huku akijibwaga kwenye sofa kwani muda wote alikuwa amesimama.

“Unasema Mzee Atanasi , familia alioa Tajiri Mohemedi!!?”Aliuliza Abubakari kwa mshangao sana huku pia hofu ikimjaa tofauti na Desmod.

“Inaonekana hata hamjamfahamu vizuri adui yenu”Aliongea Denisi huku akitabasamu kikejeli..

“Atanasi ndio nani?”Aliuliza Desmind na Abubakari alimuelezea kwa ufupi na Desmond alijikuta na yeye akijawa na hofu.

“Kwa maana hio unamaanisha Roma na Tajiri Azizi ni ndugu?”

“Ndio kwa upande wa mama Roma ana undugu wa karibu na Tajiri Atanasi na kwa upande wa Baba ndio ana undugu na familia ya Denisi hapa”Aliongea Elvice huku akikaa kwenye masofa kwa wasiwasi.

“Sikilizeni, acheni woga mnafikiri yule choko kuwa na undugu na familia hizi kubwa hapa Dar ndio nini labda , Desmond wewe ni mtoto pia wa Raisi wa Rwanda lakini pia upo na mimi ninaekusapoti na kuna Elvice hapa na bwana Abubakari ambao wote tunakusapoti lakini pia kuna Sali hapa kutoka kwa familia ya raisi Mstaafu Kigombola , huna haja ya kumhofia mtu kama Roma”Aliongea Denisi.

“Sikieni muda si mrefu Roma anakufa”Aliongea Denisi na kuwafanya wenzake wote kujawa na shauku.

“Kivipi Denisi?”Aliuliza Elvice kwa shauku.

ITAENDELEA-0687151346 NICHEKI WATSAPP
 
Si wengine hatutumii tsup.
Stry ni nzuri kweli lkn inachelewa sana aiseh
 
Kuna nyuzi wadau walikuwa wanatupia vitabu soft copy siionj kabisa kwangu au imefutwa nn? Naomba link yake wakuu
 
Back
Top Bottom