Kijana Jamaa
Member
- Jan 14, 2013
- 21
- 16
Hahaha hatareeee sana, huu ufuatiliaji wa kiwango cha lami🤣🤣🤣umesikika mkuu kesho mapema
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahaha hatareeee sana, huu ufuatiliaji wa kiwango cha lami🤣🤣🤣umesikika mkuu kesho mapema
Hili chama la wana kama Faru Dume au Mesina....sio team la kulipia hili team la ku support Hadith yetu iende mbele zaidi. Humu SinganoJr kama Hedes au Messi. Anatakiwa atupia mzigo 3 times kwa week. Akiwa kata itiwa poa haina mbambamba. Mwamba hana maneno sie tunamuamini ataleta zigo tuko pamoja mpaka mwisho wa dahali. Si unaona mtoto Edina anaelekea kibra.Humi watu [emoji23]hawapendikulipa ila wana force story iletwe mapema
Kesho ndo leo mkuuumesikika mkuu kesho mapema
Ulamaa Singano. usijitafutie dhambi za Bure. Kesho ndio Leo uliyoahidi.....umesikika mkuu kesho mapema
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kwa kujiondolea hii Arosto, nataka nirudie kusoma pale Roma akimla Mage, mwenye kumbukumbu anitajie ni episode ya ngapi jamani?!!
weweeeee.. humu NDO kijiwe ambacho mtunzi akitupia akapata likes kumi na comment Saba anafarijika Sanaa kuliko huko kwingine kulikojaa failure kibao hata comment elf kumi hazimfurahishi kama HAPA kwetu.Humi watu [emoji23]hawapendikulipa ila wana force story iletwe mapema
Si wengine hatutumii tsup.SEHEMU YA 346.
Hakukuwa na muda wa kusimama mlangoni na kuulizana kwani wageni wengine walikuwa wakiingia na shughuli yenyewe ndio kwanza ilikuwa ikianza.
Mhudumu alipewa maagizo ya kumpeleka Roma mpaka eneo la VIP kwani alikuwa ndio Director wa kampuni ya Vexto Media , mwanadada yule aliefahamika kwa Asha alishangaa huku akimpa Roma heshima yake na kumpeleka eneo la VIP.
Roma baada ya kukaa kuna jambo lilimfanya kutamani kucheka , kilichomfurahisha siku hio ni kutokana na kwamba wanawake wake wote walikuwepo , hata Rose ambaye hakumtarajia kabisa kuhudhuria alikuwepo na wote wakiwa wamekaa kwenye mstari mmoja wa eneo la VIP.
Edna alikaa karibu na Roma upande wa kushoto huku michepuko yake ikiwa upande wake wa kulia ,Edna alijikuta akikagua kila mwanamke na kujikuta mwenyewe akimkubali mume wake Roma Ramoni , kwani mtu yoyote angekuja eneo hilo na kuambiwa wanawake wote waliokaa kwenye msururu wa meza moja walikuwa ni wanawake wanaojihusisha na mume wake hakuna ambaye angeamini.
Rose , Dorisi , Nasra, Neema Luwazo, Amina, Mage na Edna wote walikuwa kwenye ukumbi huo wa mashindano na kila mmoja alikuwa akimwangalia Roma kwa wakati wake.
Wanawake wote walikuwa warembo na wakavaa wakapendeza na uzuri wao ulitofautiana vitu vichache sana na kila mmoja alikuwa na kitu cha ziada ambacho mwenzake hana, kwa mfano Rose licha ya kuwa na sura nzuri , lakini pia alibarikiwa mguu wa bia kuliko wenzake wote , ukimwangalia Amina yeye alikuwa na sura flani hivi ya kimaonyesho sana , pamoja na mwili wa kipekee ambao watu wengi wanasema ni ‘Sexy Body’sasa kwa wengine pia ilikuwa hivyo hivyo , kila mmoja alikuwa na kitu cha ziada ambacho mwingine hana.
Edna alijikuta akimwangalia Roma aliekuwa pembeni kwa madakika kadhaa na Roma alijua Edna alikuwa akimwangalia , lakini alijikausha kimya kama sio yeye vile, macho yake yote yalikuwa kwenye steji akiangalia wasanii waliopewa nafasi za kuimba kabla mashindano kuanza.
“Wahenga wanasema jina lina beba tabia”Aliongea Edna kwa sauti ya chini iliosikika kwenye masikioya Roma na kumfanya amwangalie
“Unamaanisha nini mke wangu kipenzi”Alijibu Roma huku akiwa ameweka tabasamu.
“Jana nilikuwa nikisoma Habari za mfalme Pluto na nimegundua aliekupatia hilo jina aliangalia tabia yako kwanza”Aliongea Edna huku akikaza macho mbele na Roma alijikuta akigusa pua yake.
“Kwahio mke wangu unaniambia wanawake wote wenye majina ya Edna ni warembo kama wewe?”
“Mfalme Pluto , unaonaje ukifanya utafiti wewe mwenyewe na kuja na majibu?”Aliongea kiutani huku akiangalia mbele na Roma alijikuta akitabasamu.
“Mke wangu kumbe na wewe unajua kuongea utani”
“Hakuna kigezo cha kumfanya mtu asiwe anaongea matani muda mwingine na isitoshe sijakutania nimeongea jambo la kweli usijitoe ufahamu”Aliongea na kisha akaurudia ukazu wake na kuendelea kuangalia matukio yaliokuwa yakifanyika mbele yake.
“Rose mambo” Alisalimia Nasra aliekuwa amekaa karibu na Rose.
“Poa mambo vipi Nasra”
“Kumbe unanifahamu?”
“Naachaje kutokumfahamu mke mwenzangu”Aliongea Rose huku akitabasamu na kugeuka upande aliokaa Roma na ile anageuka alikutana na macho ya Roma yaliomwangalia kwa tabasamu na kisha akaishia kukonyezwa , kitendo kilichomfanya hata Rose kucheka.
“Mnacheka nini nyie?”Aliingilia Dorisi aliekuwa upande wa kushoto upande wa Rose,hata Dorisi alionekana alikuwa akitafuta nafasi ya kuongea na Rose ila alishindwa kuanza yeye mpaka Nasra alivyo anza.
Wote watatu waliangaliana kwa wakati mmoja na walijikuta wakichekana , walionekana walikuwa wakiongea kwa ishara.
Ukweli mpaka hapo kila mmoja alikuwa akimjua mwenzake alikuwa akitembea na Roma na ndio maana waliishia kuchekana.
Upande wa Edna licha ya macho yake yote kuwa mbele ya jukwaa , lakini alikuwa na jicho la tatu , wakati Rose , Dorisi na Nasra wakiongea kwakucheka alijjikuta akiona wivu na aliona ni kama alikuwa akichekwa yeye kama mke.
Kuna kitu flani kilimfanya kuona wivu ambao mwenyewe alishindwa kuutafsiri na alijisomea tu moyoni mwaka kwamba dawa yao inachemka , alijiambia muda si mrefu atamfanya Roma asiwakumbuke kabisa.
Upande wa Neema Luwazo baada ya Donyi kumuelezea namna alivyokutana na Roma , alijikuta moyo wake ukiwa na amani kwa mara nyingine ,kwani alikuwa akihofia Roma amekwisha kutembea na mtoto wake Donyi.
Neema licha ya kwamba alikuwa akimpenda Roma ila likija swala la wanawake hakuwa akimwamini kabisa , alimuona Roma ni mwanaume ambaye hakuna mwanamke ambaye anaweza kumkimbia , maneno yake aliyaona sahihi kabisa , kwani wanawake waliokuwa wamejipanga msururu mmoja kuanzia kwa Nasra msichana mwenye kujielewa ambaye alikuwa akimfahamu muda mrefu tu tokea aanze kufanya kazi na kampuni ya Vexto , lakini pia upande wa Dorisi pia alikuwa ni msichana anaemfahamu sana tu na alikuwa akimjua kama moja ya wasichana wanaojitambua tena ikampelekea kipindi kutamani kumwajiri lakini Dorisi akakamkatalia huku sababu ikiwa ni kwamba alikuwa akipenda kufanya kazi karibu na Edna ambaye ni rafiki yake , lakini pia Neema Luwazo alimwangalia Edna mwanamke siriasi sana ambaye amemfahamu kwa muda mrefu, msichana ambaye ameshinda vizingiti vyote vya changamoto za kibiashara na kuifanya kampuni ya Vexto kuwa kubwa, msichana ambaye alikuwa akijiheshimu sana na asie na makuu licha ya kupewa uzuri wa kipekee lakini ndio huyo pia ambaye amenasa kwenye mtego wa mwanaume Roma Ramoni , sio kwa hao wenzake tu alijifikiria hata kwa yeye pia, licha ya misimamo yake na namna alivyokuwa makini likija swalala wanaume , lakini pia amenasa kwenye mtego wa Roma , alijiambia hakuna mwanamke ambaye anaweza kumkataa Roma , hivyo aliona licha ya kwamba Donyi mtoto wake hajajihusisha bado kimapenzi na Roma lakini anapaswa kuchukua hatua za kuepusha swala hilo na namna ya kipekee ni kumuweka Domyi wazi juu ya uhusianao wake na Roma.
“Mama ulifahamina vipi na Anko Roma?”Aliuliza Donyi mara baaada ya kumaliza kumuelezea yeye jinsi ambacho aliweza kukutana na Roma na kumuokoa na majambazi kule baharini.
“Tukiwa tunarudi nyumbani nitakuelezea sawa?”
“Mhmh ! Mama kuna kitu nahisi.. maneno ya baba naanza kuona ukweli wake”Aliognea Donyi.
“Baba yako kakuambia nini?”
“Ameniambia nina baba mwingine wa kambo ila hajaielezea ni nani”Alongea Donyi na kumfanya Neema kumwangalia mwanae kwa muda kidogona kisha alipotezea baada ya msanii wa kwanza kuimba kutokea stejini.
Kutokuonekana kwa Donyi kwa kipindi kirefu ni kutokana na kwamba mrembo huyo alikuwa chuoni nchini Marekani akiendelea na masomo yake na alikuwa nyumbani mwezi huo kwa ajili ya likizo.
Sophia alionekana kukosa mshindani kabisa kwenye mashindano hayo, Uzuri wake , sauti nzuri pamoja na pumzi lakini pia namna ambavyo aliweza kutawala jukwaa vilimbeba sana Sophia na kukonga sana mioyo ya watu wengi.
Alionekana kujiamini kabisa na alikuwa ni msanii halisi, watu walimpigia makofi sana kwanzia mwanzo wa kuimba mpaka anamaliza , majaji hawakuwa na maneno sana na kipaji cha Sophia na aliweza kupita moja kwa moja Kwenda ishirini bora.
Baada ya Sophia kumaliza tu kuimba akijiandaa kutoka jukwaani mara mwanaume Handsdokme alievaa suti akapendeza , alionekana akitokezea jukwaani huku akiwa amebeba ua rangi nyeupe kubwa lenye kupendeza , mwanaume huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Denisi Senga.
Alitembea mpaka kwenye steji karibu na Sophia na kisha akamkabidhi lile ua na kwasababu Sophia alikuwa juu ya jukwaa na kamera zilikuwa zikimmulika alishindwa kabisa kukataa lile ua na kulipokea.
“Hongera sana Sophia”Aliongea Denisi. Na vilio vya shangwe vilirindimwa ukumbi mzima , kila mtu alikuwa akimjua Denisi kama mtoto wa Raisi Senga , hivyo kitendo cha kumzawaida Sophia ua kiliibua misisiimko wa mashabiki.
Denisi aliomba maiki kutoka kwa Amina na akapewa , jambo ambalo lilimfanya Sophia kuwa ni mwenye wasiwasi sana , kwani hakuwa akijua ni kitu gani ambacho Denisi alikuwa akidhamiria kufanya, alikuwa akiogopa Denisi kutangaza hadharani juu ya historia yao ya Maisha ya nyuma.
Upande wa Roma mwenyewe alijikuta akikunja sura na kumwangalia Denisi kwa macho yenye kiulizo , mwenyewe hakuwa akijua kwanini Denisi karuhusiwa kwenye steji , jambo hilo lilimkasirisha na aliona Denisi anafanya mambo ambayo hayana msingi, kabla Denisi hajaanza Roma alitaka kunyanyuka lakini Edna aliekuwa pembeni yake alimzuia kwa mkono.
“Mabibi na mabwana Habari za usiku huu”
“Salamaaa…!!!” watu waliitikia kwa shangwe na kumfanya Denisi kutabasamu alikuwa akijiamini hatari.
“Jamani nimejikukta nimeshindwa kujizuia na kupanda stejini hapa , niseme kabisa mimi ni moja wa mashabiki kindaki ndaki wa Sophia na mpaka sasa Sophia namuona kama mshindi wa mashindano haya”Aliongea Denisi na watu walimuunga mkono kwa shangwe sana na Sophia alijikuta akivuta pumzi ya ahueni.
Baada ya maneno machache ya kumpamba Sophia Denisi aliomnyooshea mkono Sophia kumuomba kumtoa ukumbini hapo na Sophia alijikuta akikosa uamuzi wa moja kwa moja na baada ya dakika moja ya kufikiria aliamua kuupokea mkono wa Denisi na kisha kutoka stejini , jambo ambalo lifurahisha sana watu wengi, lakini kwa upande wa Roma ni kama hakupenda kile kitendo.
Ni siku nyingine habari kubwa mtandaoni ikawa ni tukio la Denisi mtoto wa Raisi kuingia ukumbini na kumtoa mrembo Sophia , kila mmoja aliibuka na dukuduku kwenye kichwa chake , huku wengi wakisema Sophia itakuwa anatoka kimapenzi na mtoto huyo wa Raisi , lakini wengine wakisema kama sio wapenzi ni swala la muda tu mtoto mzuri huyo kuingia kwenye himaya ya Denisi.
Sophia alikuwa maarufu sana ndani ya muda mfupi na siku hio ya jumapili alionekana ku’trend’ sana mtandaoni.
Upande wa Roma ambaye hakuwa sana na habari na mitandao alijikuta akiingia mtandaoni kuangalia kile kinachoendelea , kwani sasa hivi alikuwa na siku ambayo amepewa zawadi na mke wake Edna na alikuta picha nyingi za Sophia zikiwa zimesambaa mtandaoni , wengi wakimsifia kwa kipaji na wengine wakiongelea swala la Sophia na Denisi.
Upande wa nyumbani kwa Abubakari , walionekana vijana sita wakiwa kwenye furaha sana, vijana wenyewe walikuwa ni Abubakari Hamadi , Denisi , Desmond ,Elvice Temba , Sali pamoja na kijana mwingine mnene hivi, Wote kwa pamoja walikuwa wakimpoongeza Denisi kwa kitendo chake alichoweza kufanya siku ya jana yake na kupelekea siku hio ya jumapili picha zake kusambaa mtandaoni.
Haikueleweka vijana hawa waliwezaje kukutana pamoja na kuunda urafiki , lakini walionekana kuendana vyema kitabia kwa asilimia nyingi.
“Denisi hupaswi kuzembea Zaidi sasa , unatakiwa kuchukua hatua inayofuata ya kujiweka karibu na mrembo Sophia”Aliongea Abubakari , huku akiwa ameshikilia kikombe aina ya Solo Cup kilichojaa bia ndani yake, ni kama walikuwa wakisherehekea licha ya kwamba muda huo ilikuwa ni asubuhi ya saa nne.
“Kwanzia leo hii nitakuwa namtembelea mara kwa mara kambini kwao na nitatumia nafasi hio kuuteka moyo wake”Aliongea Denisi na kuungwa mkono na kila mmoja.
“Hapa anaefuatia ni Desmond na Edna”Aliongea Elvice na wote kwa pamoja wakamgeukia Desmond ambaye alionekan usiku mzima aliutumia kulewa.
“Muda si mrefu Edna anakuwa wangu , kuna mpango upo jikoni, unajua Edna kinachompa kiburi ni ile kampuni, nikishaichukua atakuja kwangu tu”Aliongea Desmond na wenzake wote walimgeukia na kumsikiliza, huku Denisi akionyesha kuwa ndio mwenye shauku Zaidi.
“Desmond utaweza vipi kumpokonya Roma mke wake , kuna jambo sijaweka wazi , nafikir wote mnafahamu yule choko ni ndugu yangu wa damu?”Aliuliza Denisi na wenzake wote walionekana kushangaa kwani taarifa hio ilionekana kuwa mpya kabisa.
“Acha utani Denisi , Roma ni ndugu yako?”Aliuliza Abubakari kwa shauku.
“Ndio , ni mtoto wa kwanza kwa baba na Blandina mtoto wa Mzeee Atanasi”Aliongea Denisi kivivu huku akijibwaga kwenye sofa kwani muda wote alikuwa amesimama.
“Unasema Mzee Atanasi , familia alioa Tajiri Mohemedi!!?”Aliuliza Abubakari kwa mshangao sana huku pia hofu ikimjaa tofauti na Desmod.
“Inaonekana hata hamjamfahamu vizuri adui yenu”Aliongea Denisi huku akitabasamu kikejeli..
“Atanasi ndio nani?”Aliuliza Desmind na Abubakari alimuelezea kwa ufupi na Desmond alijikuta na yeye akijawa na hofu.
“Kwa maana hio unamaanisha Roma na Tajiri Azizi ni ndugu?”
“Ndio kwa upande wa mama Roma ana undugu wa karibu na Tajiri Atanasi na kwa upande wa Baba ndio ana undugu na familia ya Denisi hapa”Aliongea Elvice huku akikaa kwenye masofa kwa wasiwasi.
“Sikilizeni, acheni woga mnafikiri yule choko kuwa na undugu na familia hizi kubwa hapa Dar ndio nini labda , Desmond wewe ni mtoto pia wa Raisi wa Rwanda lakini pia upo na mimi ninaekusapoti na kuna Elvice hapa na bwana Abubakari ambao wote tunakusapoti lakini pia kuna Sali hapa kutoka kwa familia ya raisi Mstaafu Kigombola , huna haja ya kumhofia mtu kama Roma”Aliongea Denisi.
“Sikieni muda si mrefu Roma anakufa”Aliongea Denisi na kuwafanya wenzake wote kujawa na shauku.
“Kivipi Denisi?”Aliuliza Elvice kwa shauku.
ITAENDELEA-0687151346 NICHEKI WATSAPP
Haya Sawahaitokawia