Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 353

Naam mashindano ya kizazi nyota yaliweza kuisha Rasmi wa kuweka rekodi kwa kuwa moja ya mashindano ambayo yamefuatiliwa na watu wengi Zaidi , Kampuni ya Vexto Media pia ilipata mapato makubwa sana kupitia mashindano hayo ,jambo ambalo lilifanya hisa za kampuni kupanda Zaidi.

Siku ya pili , yaani siku ya jumatatu Habari kubwa Zaidi ilikuwa ni juu ya Edna kuweka hadharani kuwa ameolewa, mrembo huyu kwa miaka mingi watanzania wengi walifahamu kama alikuwa single , lakini kitendo cha kuweka hadharani kaolewa tena Zaidi ya miezi sita iliopita ilikuwa ni Habari ambayo ilipata hadhira ya watu wengi na kama ujuavyo taifa la Tanzania watu wengi wanapenda Habari zinazohusiana na Maisha ya watu basi ilikuwa hivyo.

Moja ya watu ambao walifurahia kitendo cha Edna kuweka wazi juu ya mahusiano yake ni Blandina.

Ukweli Blandina kuna muda alihisi huenda Edna alikuwa akimficha Roma kama mume kutokana na kwamba Roma hakuwa na hadhi kubwa kwenye jamii ka yeye na ndio maana baada ya Edna kuweka wazi alijjikuta akiwa ni mwenye furaha Zaidi kuliko watu wote na alijiambia hio ni hatua nzuri sana ambayo mwanae amefikia.

Upande mwingine wakati Blandina akiwa mwenye fuaha , upande wa Mage hali haikuwa nzuri hata kidogo , mrembo huyo afisa poilisi ukweli ni kwmaba siku nzima alikuwa ni mwenye fuaraha kutokana na kwamba kwa mahesabu yake siku hio ya Jumapili ndio ilikuwa siku ambayo Roma na Edna mkataba wao wa ndoa ulikuwa ukimalizika , lakini Mage alijikuta akiwa kwenye mshituko mara baada ya Edna kuweka hadharani mahusiano yake na Roma na kuutangazia uma kwamba kwanzia siku hio hayupo mwenyewe bali ameolewa tayari, kwake lilikuwa pigo kwani aliona dalili zote za kukosa ndoa.

Magdalena aliekuwa akijua kinachoendelea alijikuta akimhurumia pacha mwenzake, Magdalenda hata yeye alikuwa akifahamu kupitia Mage kwamba ndoa ya Edna na Roma ilikuwa ni ya mkataba tu ambao unamalizika muda si mrefu.

Usiku wa jumapili mara baada ya Edna kuweka wazi mahusiano yake na Roma aliona kabisa dalili ya wawili hao kutokuachana kabisa , kwani mara nyingi mwanamke akimuweka mwanaume hadharani ilikuwa ikiashriaa kwamba alikuwa tayari kuishi nae milele licha ya changamoto , sasa kwa tafsiri ya haraka haraka alijua naafasi ambayo alikuwa akiitumainia dada yake haiwezi kutokea.

“Mage tunapaswa kuwa na furaha kwa ajili ya Edna , ni rafiki yetu wa utotoni na furaha yake ni furaha yetu , hatuwezi kuwa wanafiki , lakini hata hivyo Roma pia anaonekana kumpenda Edna”Aliongea Magdalena asubuhi mara baada ya kuingia kwenye chumba cha Mage na kumkuta akiwa amelala , jambo ambalo haikuwa kawaida yake.

“Mbona unaweka sisi na sio mimi?”Aliuliza Mage baada ya kumwangalia Magdalena , kilichomfanya kuuliza hivyo ni kutokana na Magdalena kutumia uwingi akijijumlisha tofauti na kutotumia umoja , kwani swala la kumpenda Roma lilikuwa juu yake.

“Aaah…Mage nimeweka neno ‘sisi’ kwasababu furaha yako ni furaha yangu, unafikiri napenda kukuona ukilala hivi , kama kweli unampenda Roma unapaswa kumpenda na kile anachokipenda pia”Aliongea Magdalena na Mage alivuta pumzi na alionekana kufikiria.

“Najua Magdalena na nilikuwa nikifikiria hilo usiku wote, siku zote nilikuwa nikiwazia kuhusu mkataba wake wa ndoa lakini nikasau kufikiria juu ya hisia zake kwa Edna, najiona mjinga kwa kutegemea makubwa ndio maana niko hivi”.

“Kwahio mpango wako ni kumuacha Roma au ni kuendelea nae”

“Mpango wangu ni kuendelea nae , Roma hawezi kunioa lakini vile vile siwezi kumuacha kwasababu ya neno Ndoa”Aliongea naMagdalena alifikiia kidogo.

“Lakini Mage , Mama yetu anataka wote tuolewe na tuwe na familia, unafikiria atakubali ukimuelezea kuwa mwanaiume unaempenda ni Roma, vipi kuhusu baba?”

“Mage hilo lisikusumbue , mama akubali wala asikubali mimi sijui cha kufanya , nitasikiliza moyo wangu unachoniambia , hata hivyo mimi ni mtu mzima na najua kipi kizuri na kibaya kwangu”

“Jiandae kumpatia mama majibu maana tokea jana aone tukio la Edna kumtambulisha mume wake anataka na sisi tuwe kama Edna na yupo chini sebuleni anakusubiria”Aliongea Magdalena na kisha alitoka kwenye chumba cha Mage.

Mama T ukweli tokea siku ya jana kushuhudia Edna akimtambulisha mume wake Roma Ramoni pasipo ya kuwa na aibu alijikuta akitamani pia Watoto wake mapacha pia kuleta wanaume na kuwatambulisha kwake , Mage alikuwa mkubwa tayari na Magdalena hivyo hivyo alikua mkubwa tayari ila vitendo vyao vya kutoonekana kuwa na wanaume vilikuwa vikimtia mawazo sana.

“Mume wangu nadhani ni muda sahihi wa Mage kumleta mchumba wake tumuone”Aliongea Mama T na kumfanya Afande Tobwe amwangalie.

“Mbona wasiwasi wako ni kwa Mage tu na Magdalena haumzungumzii, yeye hapaswi kuolewa?”

“Mume wangu nimesahau tu kukuambia , ila kuna mwanaume tayari ambaye yupo tayari kumuoa Magdalena na ameonyesha nia thabiti n ahata familia yake inamsapoti”Aliongea Mama T na kumfanya Afande Tobwe kushangaa kidogo.

“Mwanaume gani , mbona sina hio taarifa?”

“Nilisahau kukuambia tu mume wangu , familia yenyewe ni ya Waziri wa Sayansi na Teknolojia, mtoto wao mkubwa Jumbe ndio ameonyesha nia ya kutaka kumuoa Magdalena”Aliongea Mama T na kumfanya Afande Tobwe kushangaa kidogo.

“Jumbe namfahamu vizuri , yupo kikosi kimoja na Magdalena, kumbe ni wapenzi sikuwahi kulifahamu hili , Magdalena ni msiri sana”Aliongea Afande Tobwe na Mama T ametabasamu.

“Kumbe wanafanya kazi kikosi kimoja basi mapenzi yao yanaweza kuwa ya kweli , mimi mama yake Jumbe alivyonielezea nia ya mwanae na kuniambia ni mwanajeshi pia sikuona haja ya kukataa, niliona sawa tu kwa mwanajeshi kuolewa na mwanajeshi mwenzake , lakini pia familia ya Mheshimiwa Hamadi ni moja ya familia bora zenye nguvu na ni mtajiri , itakuwa faida kwetu kama tukiunganisha koo”Aliongea Mama T na kumfanya Afande Tobwe kufikiria kidogo.

“Mama T unapaswa kuongea kwanza na Magdalena mwenyewe, kama wanapendana tutawaruhusu kuona mimi sina kinyongo kabisa , lakini kama Magdalena hampendi basi hatuwezi kulazimisha ,kikubwa ni furaha za Watoto wetu”Aliongea Afande Tobwe.

“Mume wangu huna haja ya kuwa na wasiwasi , Jumbe ni kijana mtanashati naamini Magdalena anampenda”

“Mama mimi simpendi Jumbe”Ilisikika sauti upande wao wa kushoto na kujikuta wote kwa pamoja wakigeuka, aliongea hivyo alikuwa ni Magdalena.

“Magdalena unamaanisha nini humpendi Jumbe , mbona mama yake kaniambia mnapendana na mtoto wake , mpaka akachukua hatua ya kuniambia wanataka kuanza utaratibu wa ndoa?”

“Mama Jumbe ni muongo sijawahi kuwa na mahusiano nae , ni kweli ameniambia mara kadhaa ananipenda na anatamani anioe lakini sijawahi kumkubalia na hatuna mahusiano na sipo tayari kuolewa na Jumbe maana hana vigezo ninavyotaka”Aliongea Magdalana akiwaka uso wake siriasi kabisa na kumfanya Mama T kiumwangalia mume wake.

“Magdalena hakuna ambaye atakulazimisha kuolewa na mwanaume ambaye humpendi na sio kwako tu hata kwa dada yako Mage , lakini nikushauri kwamba umri wako unasogea na unapaswa uolewe pia hivyo naamini kama humpendi Jumbe kuna mtu unampenda si ndio?”Aliuliza Afande Tobwe.

Afande alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kusoma saikolojia , ukwei ilikuwa ni fani yake kwani kabla hajajiunga na jeshi alisomea maswala ya Saikolojia na anayo shahada moja , hivyo kumuona Magdalena kukasirika mara baada ya kuhusishwa na Jumbe ni kama aliweza kuona mtoto wake pia alikuwa na mwanaume anaempenda.

“Dady ni kweli kuna mwanaume na mpenda , lakini hajui”Alijibu Magdalena kwa aibu na kumfanya Mama T kutoa macho kama amebanwa na mlango.

“Hivi watoto wangu wote mna nini ? Mage ndio huyo anae mtu anampenda lakini anashindwa kumtambulisha kwangu na wewe una mtu unampenda lakini hajui, mbona mnataka kunitia kichaa mimi mama yenu , ni lini mtaolewa na mimi angalau wanawake wenzangu wanichangie pesa za harusi, nimechoka Kwenda kwenye harusi za familia nyingine mimi”

“Mke wangu punguza jaziba Magdalena hapa kakuelezea kuna mwanaume anampenda hio ni hatua nzuri ya kuelekea kwenye harusi unazotaka, halafu wanawake wa Tanzania mnapenda sana harusi kuliko ndoa zenyewe”

“Mume wangu sio hivyo , Mage na Magdalena ni watu wazima sasa na katika masha yao hawajawahi kuonekana na wanaume , hivi unajua wenzao wanawazungumziaje huko nje?”

“Wanawazungumziaje?”

“Sitaki hata kusema wanachozungumza maana kila nikisikia napatwa na hasira, wanasema mapacha wangu ni ‘Lesbian’ ndio maana hawajawahi kuonekana na wanaume”Aliongea na kumfanya Afande Tobwe kuweka uma chini , hakuamini kama Watoto wake ndio wanazungumziwa hivyo huko nje.

Lesbiani ni aina ya wanawake wanaopenda wanawake wenzao kwa lugha nyepesi watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja kwa mfano Athena ni Lesbian.

“Na wewe unaamini Watoto wetu ni Lesbian?”

“Siamini hivyo mume wangu , Mage na Magdalena hawawezi kuwa na tabia za aina hio ,kwanza ni nje na tamaduni za dini yetu, lakini nachoshwa tu na maneno ya watu”

Afande Tobwe alijikuta akimwangalia mke wake na kushindwa kumuelewa , alijiuliza tangu lini mke wake akawa ni mwenye kujali maneno ya watu au kuna jambo ambalo halijui na anafichwa.

“Mke wangu jitahidi sana kuachana na maneno ya watu kwani hayajengi , Magdalena na Mage wote washakuweka wazi wana watu ambao wanawapenda , nadhani ni vyema ukaanza kuwasapoti katika hilo ili hatimae waweze kufunga ndoa”Aliongea AFande Tobwe na kisha alinyanyuka na kuchukua mkoba wake akionekana ndio muda wa kuanza safari umewadia.

“Goodmonring Dady”

“Goodmorngin Daughter , umeamkaje?”Aliongea Afande Tobwe mara baada ya kukutana na Mage ambaye ndio anashuka kunywa chai.

“Niko sawa Dadi”

“Okey Great , mimi naelekea kazini”

“Okey Dady , kazi njema”Aliaga na Afande Tobwe akaondoka.

“Mama mbona unaniangalia sana?”Aliuliza Mage mara baada ya kugundua mama yake alikuwa akimwangalia sana.

“Mage hebu nieleze , dada yako hapa kasema na yeye ana mtu anampenda na hajamuambia , unamfahamu huyo mwanaume?”

“Nini !!, Magdalana ya kweli hayo , mbona hujaniambia?”Aliongea Mage kwa mshangao na Mama T alivyomuona Mage akiwa kwenye mshangao , aliamini huenda na yeye pia hamfahamu huyo mwanaume na alijikuta akivuta pumzi na kuzishusha kwa wakati mmoja.

“Kumbe hata wewe haufahamu?, Yaani nyie Watoto , nimefanikiwa kuwalea na kuwa watu wazima lakini mmefikia hatua nzuri ya umri wengu , lakini mnanifanya kichwa kinaniuma”

“Mama kwanini kichwa kikuume , usiwe hivyo sisi tushakuwa wakubwa na tunajua ni kipi tunataka , unajipa mzigo wa mawazo bure”

“Ndio najua mmekuwa watu wazima na mnajua ni kipi kinawafaa Zaidi na nipo tayari kuwasapoti ndio maana nataka mnieleze , tukianza na wewe Mage ni mwanaue gani ambaye unampenda , niweka wazi ili nijue?”Aliongea Mama Mage huku akiweka sura yenye usiriasi.

“Mama Mwanaume…”Aliongea Mage , lakini Magdalena alimshika Mage mkono akimpa ishara ya kwamba asiongee..

“Haina haja ya kumficha Zaidi , nitamwambia mwanaume ninaempenda na wewe ujiendae kutumbia ni mwanaume gani unaempenda”

“Mama mwanaume ninaempenda unamfahamu sana tu , ni Roma”Aliongea Mage na kumfanya Mama T kufikiria kidogo.

“Roma yupi , namfahamu Roma mmoja tu mume wa Edna , kuna Roma gani mwingine ambaye namfahamu?”

“Mama ni huyo huyo Roma Ramoni ndio mwanaume ambaye nimetokea kumpenda”Aliongea Mage na kumfanya Mama T kuwa kama mtu ambaye hajasikia vizuri.

“Mage huwezi kuwa siriasi , usiniambie unajihusisha kimapenzi na Roma mume wa Edna!!!!”Aliongea Mama T kwa mshangao huku moyo wake ukienda mbio.

“Mama naomba unisamehe…”

“Mage kimyaaa..sitaki kusikia …. Naomba usiendelee kuongea , utaniua wewe mtoto”Aliongea huku akianza kupumua kwa shida na ilibidi Magdalena kumsogelea mama yake na kumzuia asindoke chini na kiti.

Unadhani nini kitaendelea kwa Mage , ni mwanaume gani anampenda Magdalena na hajamwambia?

SEHEMU YA 354.

Edna tokea jana yake kumtambulisha Roma hadharani kama mume wake , ukweli hakuwa na wasiwasi kabisa na ilikuwa kwake ni kama mapenzi yake yaliongezeka Zaidi juu ya Roma na kumchukulia siriasi tofauti na siku kadhaa nyuma , alijiambia kitendo alichofanya jana ni sahihi na hakuna namna ambayo atajutia.

Siku ya jana yake wakati wanarudi nyumbani Edna na Roma waliweza kuongea wakiwa kwenye gari juu ya Maisha yao ya baadae, Edna alimwambia Roma ahakikishe kwamba hajutii kwa kile ambacho amekifanya usiku huo.

“Mke wangu sikudhania kama utapata ujasiri wa kunitambulisha hadharani kama vile?”Aliongea Roma mara baada ya wawili hao kuingia kwenye gari.

“Lilikuwa swala la muda tu kuwafanya watu kuelewa , hata hivyo mpaka sasa watu wengi katika kampuni watakuwa wanafahamu uhusiano wetu na hawakuwa na naman ya kupata ukweli , Roma unaonaje kwanzia sasa ukawa siriasis na Maisha yetu , najua una wanawake wengine na sijasema kwamba uwaache , ila ninachotaka unihakikishe kwamba sitojutia maamuzi yangu nilioyafanya ya kukutambulisha kama mume wangu”Aliongea Edna na Roma alijikuta akikuna kichwa .

“Ooh! Edna My love , sidhani kama kuna haja ya kuwa na wasiwasi na Maisha yetu ya baadae , kikubwa ni mapenzi yaliopo katikati yetu , itakuwa ni ngao kwa kila gumu ambalo tutapitia , siwezi kukuahidi kwamba Maisha yetu ya kimapenzi yatakuwa kama ya Hawa na Adamu kwenye bustani ya Edeni , lakini nakuhakikishia kila gumu litakalokuwa mbele ya safari yetu tutalishindwa kwa jina la mapenzi”Aliongea Roma na kumfanya Edna kuona aibu lakini kufurahi kwa wakati mmoja.

“Lakini hakukuwa na haja ya kuchukulia mfano wa Adamu na Hawa , kwani hakuna mifano mingine mizuri zaidi”Aliongea Edna na kumfanya Roma kucheka.

“Hahaha .. Wife niseme kwamba namshukuru sana Hawa kwa kukubali kudanganywa na nyoka, kama sio yeye ningekufahamu vipi mrembo kama wewe, Babe unajua hapa nawaza lile swala la kuhamia..”Aliongea Roma na kumwangalia Edna kwa tabasamu la kifedhuli.

“Mwanaume unaongea pumba wewe ..sitaki kuendelea na haya maongezi maana huwezi kuwa siriasi”Aliongea Edna na kuegamia kiti , ukweli maneno ya Edna yalimfanya hata Dereva aliekuwa akiwaendesha kushindwa kuzuia kucheka kisiri siri.

Sasa ikawa ni siku nyingine ya jumatatu asubuhi,Edna licha ya kwamba alichelewa kulala , lakini alikuwa wa kwanza kuamka na siku hio alimwambia Bi Wema ataandaa chai kabla ya kuelekea kazini ,ijapokuwa Bi Wema alimlazimisha Edna kupumzika kwani ana kazzi kubwa lakini Edna alilazimisha na Bi Wema akamuachia kazi hio Edna huku yeye mwenyewe akiwa anafanya usafi wa nyumba mpaka wanafamilia wote walipoamka.

“Roma unaonaje ukimkaribisha Christen kwenye chakula cha usiku kabla hajarejea Marekani?”aliongea Edna na Roma alimwangalia Mke wake.

“Wife ni wazo zuri , lakini yule mwanamke akija hapa naogopa anaweza kuwaeleza mambo ya uongo kuhusu mimi, hivyo tumuache aondoke tu kazi yake ya kufanya kampuni yetu kuwa maarufu ishaisha”Aliongea Roma na kuwafanya wanafamilia wote kumwangalia kwa mshangao.

“Roma alichopendekeza Mkeo ni jambo zuri , lazima tutoe shukrani kwa alichokifanya Christen kwenye kampuni , amekuwa na mchango mkubwa ndio maana mashindano yalikuwa na mvuto” Roma alijikuta akiacha kula kwanza na kuwaangalia wanawake waliokuwa mbele yake , ukweli nyumba nzima mwanaume alikuwa yeye tu na kadri alivyoangalia nyuso za wanawake wote aliona hana ambaye anamuunga mkono.

“Okey Okey..Wife nitajitahidi kufanya kama unavyotaka, lakini niwaahidi tu akianza kunisema namfukuza”Aliongea Roma na kuendelea kula.

“Mom Anko anaongea nini?”Aliuliza Lanlan baada ya kushindwa kuwaelewa , kwani hakuwa akielewa Kiswahili kabisa na sio kwake tu hata kwa Qiang.

“Lanlan Roma sio Anko ni baba yako sawa?”Aliongea Edna huku akimfuta midomo na Lanlan alijikuta akimgeukia Roma na kumwangalia kwa kumtathimini na Roma baada ya kusikia Edna anamrekebisha mtoto wake alijikuta akiacha kwanza kula na kumwangalia Lanlan, huku wanafamilia hao wakimwangalia Lanlan pia , waliona ilikuwa makosa mwanzoni kumruhusu Lanlan kumuita Roma anko na Edna kumuita Roma kwani ashazoea.

“Lanlan baba yako ni Roma sawa, kwanzia sasa umuite baba?”Aliongea Blandina na Lanlan aliitikia kwa kichwa na kisha kuendelea na chakula chake na kumfanya hata Edna kushindwa kuelewa Lanlan alikuwa akifikiria nini.

“Chubi unaonaje tukafanya dili?”Aliongea Roma na Lanlan alimwangalia Roma kwa hamasa.

“Lanlani yupo tayari kwa dili”Aliongea na kufanya hata Edna kucheka.

“Ninakupeleka kumuona Simba na Tembo na wewe utaniita baba unaonaje”Aliongea Roma na kumfanya Lanlan kumgeukia mama yake.

“Lanlan tutaenda wote , mimi na baba yako kuangalia Wanyama na nitakunulunia na zawaidi nyingine utakayotaka”

“Hurray!!!, Lanlan anapenda sana kumuona Tembo, Lanlan yupo tayari kumuita anko Roma Baba”Aliongea Lanlan kwa kushangilia na kufanya wanafamilia wote kufurahi , kwani alichangamsha nyumba.

Upande wa Roma alishindwa kuelewa kuna siri gani nyuma ya Lanlan kupenda sana Tembo , kwani akisikia Wanyama yeye atazungumzia Tembo , lakinia alijiona hayupo kwenye nafasi ya kuwaza sana juu ya anachokipenda Lanlan.

Edna baada ya kumaliza kunywa chai safari ya kazini ilianza mara moja na siku zote mrembo huyu alikuwa akiendesha gari mwenyewe na ukiona anaendeshwa jua ni kwenye matukio maalumu , hakupenda sana kuendeshwa.

Kwenye kampuni yake, Habari ya siku hio ilikua ni juu ya Edna na Roma kuwa mume na mke , wafanyakazi wote walionekana kujadili swala hilo , huku wakishindwa kuamini kama kweli mwanaumke kauzu kama chuma mume wake ni Roma Ramoni , mwanaume ambaye anaonekana kutokuwa siriasis na Maisha.

Wafanyakazi wengi walikuwa wakizisikia Habari za Roma Ramoni kucheza gemu tokea aanze kufanya kazi na Vexto , lakini licha ya tabia yake hio aliishia kupandishwa vyeo , jambo hilo liliwafanya kuamini kweli kulikuwa na mahusiano.

Watu ambao walikuwa wamechoka kutokana na kauli ya Edna jana yake ni kitengo cha Mahusiano ya jamii na masoko(PR) kinachoongozwa na mwanadada Benadatha , mrembo Recho, Tina na wenzake walikuwa wakizungumzia swala la Edna kuweka wazi mahusiano yake na Roma.

“Unajua licha ya kwamba nilikuwa nikijua kuna mambo ambayo hayapo sawa kati ya Bosi Edna na Roma lakini sikudhania wanaweza kuwa mke na mume”Aliongea Tina.

“Sio wewe tu hakuna ambaye ameamini kauli ya Edna kabisa , hivi ni nani asiejua ndani ya kampuni Dorisi na Nasra wanatoka kimapenzi na Roma?”

“Wee Kweli?”Aliuliza Benadetha kwa mshangao.

“Wewe nae upo kampuni ipi , kila kitu kipo wazi , lakini nashindwa kuelewa imekuwaje Roma akatoka na wafanyakazi wa kampuni ilihali bosi ni mke wake , hivi nani anamuelewa Roma hapa?”

“Jamani tuache umbea tumekuja kufanya kazi sio kumuelewa Roma”Aliongea Recho baada ya Tina kuongea na kumfanya Benadetha na wenzake kushangaa , inakuwaje leo Recho ndio wa kwanza kusitisha umbea wakati ndio mwenyekiti, ilibidi Tina ampime kwanza Recho joto kuona kama ana dalili ya Malaria kwani alichoongea hakikuwa kikiendana na tabia yake.

Ukweli Recho yeye likuwa kwenye mshituko Zaidi , lakini pia alikuwa ni kama hakupenda , mrembo huyu , ukweli ni kwamba ameachana na mpenzi wake mwezi uliopita na kilichomfanya kuachana na mpenzi wake ambaye ashamtambulisha ukweni ni tabia yake ya kuota usiku na kuanza kutaja jina la Roma.

Recho tokea siku ambayo ashawahi kuchezewa viungo vyake vya siri na Roma akili yake haikutulia kabisa , ni kama tukio hilo lilikuwa likijirudia rudia na alitamani waendelee pale walipoishia na alikuwa akitafuta nafasi ya kumtafuta Roma ,lakini sasa kusikia Habari ya Edna kuwa mume wa Roma , ni kama malengo yake yote yaliingia doa na kujikuta akiwa mwenye huzuni tofauti na wafanyakazi wenzake ambao walikuwa kwenye mshangao.

Yaani wakati wenzake wakishindwa kumuelewa Roma na Edna ,yeye alionekana kumuelewa Roma na Edna na alikuwa akijiweka kwenye nafasi sawa kama ya Edna na aliamini Roma aliweza kumpagawisha Edna ndio maana wakawa mke na mume na alitamani kujua kiundani Zaidi ni jambo lipi likawapagawisha warembo wote watatu wa kampuni yaani Dorisi , Nasra na Edna..

Sasa Recho mapenzi kwa mchumba wake aliekuwa akimpenda sana yalipungua sana kiasi kwamba hakuwa na hamu na mpenzi wake na mara nyingi hata wakiwa wanafanya uzinzi atajikuta anamvutia picha Roma na hivyo kupelekea mpaka kutaja jina lake na hiko kikamfanya kuachwa.

Kila siku ya jumatatu Edna alikuwa akifanya utaratibu wa kupitia kila idara kuangalia baadhi ya projecti mpya ambazo zinafanywa lakini pia kutoa maelekezo , aliweka utaratibu huo kutokana na kupunguza kazi kwa wakuu wa Idara kupanda juu gorofani mara kwa mara kwa ajili tu ya kupata baadhi ya vibali hivyo ilimlazimu kupita kila Floor na kufanya baadhi ya maamuzi na kutoa maagizo mengine.

Sasa siku hio watu walikuwa wakimwangalia kwa macho yasio kuwa ya kwaida na kumfanya hata yeye mwenyewe kukosa kujiamini, lakini hata hivyo kama ilivyokuwa kawaida yake hakupenda sana kuongea na aliweka sura ya ukauzu na kutojali wanachokifikiria wafanyakazi wake.

Edna baada tu ya kufika ofisini, mtu wa kwanza kuingia kwenye ofisi yake ni Richard mwanamitindo ambaye alimwajiri hivi karibuni kwa ajili ya maswala ya kudizaini mavazi yatakyotengenezwa na material mapya.

“Edna Yestarday you were so hot , Marie my wife is calling non stop regarding your marriage and other of our Collegue’s keep asking questions about how and when your relationship progressed so far…..”

“Edna jana ulikuwa ni wa moto sana , Mke wangu Marie anapiga simu bila kuacha kuulizia juu ya ndoa yako na pia wanafunzi wenzetu tuliosoma nao wanauliza maswali mengi kuhusu ni kwa namna gani na wakati gani mahusiano yako yamefikia katika hatua ya ndoa”Aliongea Rich kwa bashasha sana na kumfanya Edna kutabasamu.

“So Rich mmewajibu nini?”

“We didn’t answer anything , I am also in a position of asking questions but rather than getting answers each of us differently , we agreed on something”

“Hatukujibu chochote , hata mimi pia ninapaswa kuuliza maswali lakini licha ya kupata majibu kila mmoja wetu tofauti tuliamua kukubaliana juu ya jambo moja”Aliongea Rich kwa tabasamu na kumfanya Edna kumwangalia kwa shauku.

“Come on Rich .. What!!”

“They are all coming over , here in Tanzania and you are going to answer our questions while everyone is present including your husband”

“Wote wanakuja Tanzania na utakwenda kujibu maswali yetu , wakati kila mmoja akiwepo ,ikiwemo mume wako”Aliongea Richie huku akionyesha mchecheto kweli , lakini kwa Edna ilikuwa mshangao Zaidi.

Alichokuwa akimaanisha Rich ni kwamba wanafunzi wenzake aliosoma nao , wale waliokuwa na ukaribu nae na kumfahamu ndio watakuja Tanzania , ili kupata majibu yao , Edna alijikuta akiwa ni mwenye wasiwasi kwani alikuwa akijua kabisa ni kipi kinakwenda kuulizwa kwani ashawahi kuhudhuria kwenye mkusanyiko wa pamoja na Alumni wenzake na moja ya maswali wanayouliza ni kama vile , kisi lenu la kwanza lilikuwa lini na ulijisikiaje , Date ya kwanza ilikuwa vipi na ilikuwa wai , Kazi ya Roma na mengine mengi msingi ambayo kwake hayana msingi..

“Kwahio Rich mmekubaliana lini?”

“Baada ya Christimass”Aliongea Rich na kumfanya Edna kutabasamu na hakuwa na namna ya kupinga kwani ni wanafunzi wenzake ambaye alitakiwa kuonana nao.

*********

Upande mwingine wakati hayo yakiendelea , siku hio hio Kizwe mke wa raisi wa Rwanda alikua nchini Tanzania.

Ujio wake ulikuwa ni wa kimya kimya na alionekana alikuwa amekuja kwa kazi binafsi sana , muda wa saa nne kamili alikuwa ndani ya hoteli moja maarufu maeneo ya Masaki, upande wa mgahawani akiongea na mwanaume mmoja hivi wa makamo kati ya miaka hamsini , alievalia suti , mweusi na ilikuwa ni takribani kama nusu saa tokea waanze mazungumzo yao.

“Do you have the file?”Aliuliza Kizwe na alimuuliza mwanaume kwamba je faili analo.

“Yes I do and its verified”Aliongea akimaanisha kwamba analo na amelithibitisha.

“I need to verified it too , I don’t trust people , especially Tanzanian”

“Nahitaji kulithibitisha pia , siamini watu , mathalani mtanzania”Aliongea.

“Perhaps with one of your contacts from Diaspora , We can show you the file but how would you confirm it’s realy , we need someone who knows what happened”

“Labda na mtu unaewasiliana nae kutoka Diaspora , tunaweza kukuonesha faili lakini utawezje kuthibitisha ukweli wake , tunahitaji mtu anefahamu kilichotokea”Aliongea yule mwanaume na kumfanya First Lady kufikiria kidogo.

“Actually he is here”Aliongea akimaanisha kwamba mtu mwenyewe yupo hapa na palepale alitoa simu yake na kutuma ujumbe na ndani ya dakika chache tu , alionekana mwanaume mtanashati sana kijana akiwasogelea.

Unafikiri Kizwe anazungumzia faili gani?, linahusiana nini na kisasi chake kwa Edna
 
SEHEMU YA 355

Mwanaume aliewasogelea Kizwe alikuwa ni Ernest Komwe CEO msaidizi wa kampuni ya Vexto Group Limited.

Kizwe alimpa ishara Ernest kukaa chini na yule mwanaume ambaye alikuwa akiongea na Kizwe alimwangalia Ernest kwa namna ya kumchunguza.

“Ndio huyu?”Aliuliza akiwa kama ni mwenye mashaka.

“Ndio ,huyu ni Ernest Komwe , kwasasa anafanya kazi ndani ya kampuni ya Vexto kama CEO msaidizi”Aliongea Kizwe na yule mzee alishangaa kidogo na kisha akarudi kwenye hali yake ya kawaida akificha mshangao wake.

“Anafahamu kilichotokea?”

“Ndio , wakati familia yangu inalazimishwa kuhamia nje ya nchi , nilikuwa ni mdogo wa miaka tisa, ijapokuwa sikujua kinachoendelea , lakini nakumbuka Maisha yetu yalivyokuwa magumu , baada ya miaka kadhaa ndipo nilipokuja kuufahamu ukweli”Aliongea Ernest kwa upole na yule mwanaume alitingisha kichwa na kisha alichukua mkoba uliokuwa pembeni yake na kutoa bahasha na kisha akampatia Ernest Komwe.

“Marium aliniamini , hili faili alipaswa kukabidhiwa Raheli Adebayo, lakini bahati mbaya alikufa kabla halijamfikia, sifahamu mnachopanga , lakini naamini haya ni maamuzi sahihi , natumaini hamtonifanya nikajutia juu ya hili”Aliongea kwa namna ya usiriasi na Ernest alifungua ndani na kuangalia na akamgeukia First Lady na kisha akatingisha kichwa akionyesha ishara kwamba fali ni lenyewe.

“Jambo lingine , sitaki familia yangu kuhusishwa kabisa katika hili, Kizwe nafahamu unajua ninachomaanisha?”

“Be at peace , our arrangement will go as planed”Aliongea First Lady akimaanisha kwamba mpangilio utakwenda kama ulivyopangwa na kumfanya yule mwanaume kusimama na kisha akamwangalia Ernest kwa dakika kadhaa akiwa kama ni mtu mwenye kumtathimini na kisha alitingisha kichwa na kuondoka..

“Madam nini kinafuatia?”

“Umefanikiwa kupata faili?”

“Ndio na Benadetha mpaka sasa hafahamu kama nimelichukua Boss”.

“Good!, Malengo ni wewe kumiliki asilimia arobaini za kampuni na ili kufanikiwa katika hilo tunatakiwa kuzifanya zishuke thamani , kutokana na kufanya vizuri kwa kampuni ya Vexto Media, kwasasa hatuwezi kufanya chochote , tutasubiri kwa muda wa wiki mbili baada ya hapo wasiliana na Matilda atakueleza cha kufanya”

“Sawa Madam”.

“Mr Ernest remember this is your last chance to revive the legacy of your family, Don’t be stupid and let Edna outwits you”

“Mr Ernest kumbuka hii ni nafasi yako ya mwisho ya kufufua urithi wa familia yako, usije kuwa mjinga na ukamfanya Edna akakuzidi akili”.

“Usiwe na wasiwasi Madam , nitahakikisha kila kitu kinaenda kama tulivyopanga”

“Good!, Naamini maneno yako yatakuwa ndio matokeo ninayotarajia , Ernest ukumbuke familia yako ipo mikononi mwangu”Aliongea nakumfanya Ernest kidogo kuwa na huzuni na aliishia kutingisha kichwa , lakini First Lady alionekana kutojali , alichukua mkoba wake na kisha kuondoka eneo hilo na kumuacha Ernest akimwangalia kwa nyuma.

********

Mama T hakutaka kuamini kabisa maneno ya mtoto wake kama ni ya kweli na alijiambia hata kama ni kweli hawezi kumruhusu Mage kuendelea na Roma kabisa labda yeye sio aliemzaa Mage..

Ukweli ni kwamba mwanamama huyu licha ya kwamba alikuwa na furaha ya Roma kuwa mume wa Edna , lakini alishindwa kuelewa kwanini Edna akaolewa na mwanaume aina ya Roma , kwani kwake aliona hakuwa na vigezo vya kutosha na alijiambia kama Raheli mama yake na Edna angekuwepo hai , asingekubali Edna kuolewa nae , sasa jambo hilo lilikuwa hivyo hivyo kwa mtoto wake Mage alikuwa na sababu mbili kubwa ambazo zinamfanya kutokubali Mage kuendelea na Roma , sababu ya kwanza Roma alikuwa tayari mume wa mtu na mwanae hawezi kuwa mchepuko , sababu ya pili ni hakuwa akimuelewa Roma kabisa na alimuona mwanaume wa kawaida sana kuitwa mkwe, kwa maneno marahisi ni kwamba Mama T hakuwa na taarifa za kutosha kuhusu Roma, ijapokuwa aliamini Roma hakuwa mwanaume wa kawaida ndio maana akaweza kumfanya mwanamke makini kama Edna kuweza kufunga nae ndoa.

Ndani ya nusu saa , hali yake ya mshituko ilionekana kutengemeaa na alikuwa ameketi kitandanii huku pembeni yake akiwa amekaa Mage.

“Mage mwanangu naomba unisikilize , kuna wanaume wengi ndani ya Tanzania ambao hawajaoa na wanatafuta mwanamke mzuri kama wewe , achana na Roma mume wa mtu , hivi unafikiri Edna akijua unatembea na mume wake itakuwaje , ushawahi kufikiria hilo?”Aliuliza kwa upole huku Mage akishndwa kujibu.

“Lakini mama nifanyaje nishatokea kumpenda tayari ni vigumu kufanya kama unachotaka..”Aliongea Mage na kumfanya Mama T kufumba macho akivuta pumzi kwa nguvu na kuzishusha , alijiambia hakuna faida kuwa kwenye hali ya hasira na anapaswa kuongea na Mage kwa upole ili aweze kumuelewa..

“Mage sijui ni kipi umekipenda kutoka kwa Roma , lakini huwezi kuendelea nae ,unapaswa kunisikiliza mimi mama yako ninachokuambia, wapo wanaume wengi bora Zaidi ya Roma nataka kuanzia sasa macho yako yote uyalekeze kwao na sio mume wa mtu”Aliongea Mama T lakini hata hivyo Mage alionekana kutokumuelewa kabisa mama yake , hakujua kama alikuwa na uwezo wa kumuacha Roma , hakutaka kuongea neno kwani alihofia anaweza kumfanya mama yake kupandwa na presha.

“Mage nadhani ni vyema ukamsikiliza mama”Aliongea Magdalena mara baada ya kuingia kwenye chumba cha Mage.

“Lakini Magdalena siwezi , yule mwanaume nishampenda tayari na sijielewi , sio rahisi na mnavyofikiria”.

“Mage vipi kuhuu Edna, unafikiri atakuchukuliaje akifahamu unatoka kimapenzi na mume wake?”

“Mage unafikiri mimi ndio mwenye makosa tu hapa , Edna pia naamini anahusika katika hili , kama kweli ndoa yao ilikuwa ya mapenzi tokea mwanzo huenda nisingetokea kumpenda mume wake”

“Lakini ulianza nae kabla hata ya kufahamu ndoa yao ni ya mkataba?”Aliongea Magdalena na kumfanya Mage amwangalie.

“Magdalena unafikiri nazungumzia swala la mkataba, nilipokutana na Roma kwa mara ya kwanza alionekana kama mtu ambaye hajaoa, alikuwa yupo yupo tu , tena akiwa na mwanamke usiku wa manane, unafikiri kama kweli alifunga ndoa na Edna ningeweza kukutana nae , huenda wakati ule angekuwa nyumbani na mke wake”Aliongea na kumfanya Magdalena kuvuta pumzi.

“Okey Mage, sio makosa yako kumpenda Roma na nakuunga mkono , ninachotaka kukushauri ni kutokuwa na mategemeo makubwa sana , kwa mfano mambo ya ndoa na mengineyo , kama kweli utataka kuendelea na Roma lazima ujue kwmaba Maisha yako hayatakuwa ya kawaida kama wanawake wengine , lazima uelewe kwamba Roma anampenda Edna na unapaswa kuliheshimu hilo”

“Magdalena nimekusikia, lakini vipi kuhusu wewe?”

“Mimi nini?”

“Kuhusu mwanaume ambaye unampenda na hafahamu”Aliongea Mage na kumfanya Magdalena uso kuanza kubadilika rangi.

“Kuhusu hilo ni mapema kukuambia”

“Magdalena hivi unadhani mimi ni mjinga na kushindwa kujua kama mwanaume unaempenda ni Roma?”

“Nini..!!, Siwezi kumpenda mwanaume Malaya kama Roma mimi?”Aliongea Magdalena na kugeuka na kutoka nje.

“Hahaha...”Mage alijikuta akishindwa kujizuia kucheka kwa jinsi Magdalena alivyoshikuta alivyomhusisha na Roma.

********

Roma alifika kazini kama kawaida na akapokekelwa na mchepuko wake Amina ambaye ni Secretary wake , licha ya kampuni ya Vexto Media kumaliza mashindano ya Kizazi nyota , lakini pia ilikuwa ikihusika na maandalizi ya show ya mrembo YoonHe kutoka Korea Kusini, hivyo pilika za kampuni bado zilikuwa zikiendelea.

Roma alikaa vikao baadhi na wafanyakazi wa kampuni , huku Amina akiwa ndio muongozaji wa kila kilichokuwa kikiendelea kutokana na uzoefu wake, upande wa Roma alishukuru uwepo wa Amina kwani alikuwa akiona nyota nyota tu , hakutaka sana kuumiza kichwa na maswala ya kibiashara, na alikuwa hapo kwa ajili ya mke wake Edna pekee.

Saa saba za mchana wakati akijiandaa Kwenda kupata chakula cha mcnana na mrembo Amina , simu yake ilianza kuita na alivyoangalia namba ilikuwa ni mpya, lakini yenye kodi ya Tanzania , hivyo hakuwa na shida kwenye kuipokea.

“Hello!”

“Habarri za saa hizi Mr Roma ni mimi mama yake na Nasra nishafika nahitaji kuonana na wewe kama una muda”Ilisikika sauti upande wa pili na kumfanya Roma kushangaa kidogo , kwani hakuwa na taarifa ya mama yake Nasra kufika Dar.

“Mama unataka tuonane wapi?”Aliuliza Roma.

“Mimi sio mwenyewe wa jiji la Dar , nataka uje hapa nyumbani”Aliongea

“Okey nitakuja hapo dakika kadhaa zijazo”Aliongea Roma na kisha akakata simu.

“Babe inabidi utangulie kuna mtu napaswa kuonana nae muda huu”Aliongea Roma.

“Ni kuhusiana na Dorisi au Nasra?”

“Ni mama yake na Nasra , yupo mjini na anataka kuonana na mimi mkwe wake”Aliongea Roma na Amina alivuta mdomo.

“Lakini unaelewa Nasra , Dorisi na Rose ni marafiki, Babe naona wivu inapawa na mimi kuanzisha urafiki na Edna la sivyo nitazidiwa”Aliongea Amina na kumfanya Roma kushangaa huku akimwangalia , alijiuliza urafiki unaozungumziwa umeanza lini.

“Babe Amina kama utaweza kumfanya mke wangu na akawa rafiki yako nitakupatia zawadi yoyote utakayotaka”Aliongea Roma.

“Babe uko Siriasi?”Aliongea Amina na Roma aliishia kumpa ishara kwamba yupo siriasi na kutoka kwenye hio ofisi.

Dakika chache tu Roma aliweza kufika Mikocheni kwa Warioba , anapoishi Nasra na alienda moja kwa moja mpaka floor husika na kubonyeza kengele na mlango ukafunguliwa na mama yake Nasra aliejifunga vitenge na kiremba kichwani na kumkaribisha ndani.

SEHEMU YA 356.

Roma kwa kumwangalia tu Mama Nasra ni kama aliona kuna kitu hakipo sawa , ila hakutaka kuuliza maswali kwani yeye ndio ameitwa , alitaka kujua kwanza ni kipi ambacho mama huyo alikuwa akitaka kuzungumza nae.

“Mr Roma naomba unisamehe kwa kukutoa kazini , najua ulikuwa na majukumu”Aliongea Mama Nasra.

“Usijali Mama , sehemu ninayofanyia kazi na hapa sio mbali na huu muda ulikuwa wa chakula cha mchana”Aliongea Roma na Mama Nasra aliitikia kwa kichwa.

“Mr Roma nataka uniweke wazi, una mpango gani na Nasra?”Aliongea Mama Nasra na kumfanya Roma moyo wake Kwenda mbio , hakuelewa kwanini mama huyo alimuuliza swali hilo la ghafla.

“Mama kuna kitu chochote kimetokea?”

“Mr Roma nimeweza kufahamu tayari umeoa na mkeo ni boss wake na Nasra,nadhani pia unaelewa historia ya maisha ya Nasra tokea anafika hapa jijini?”Aliongea na sasa Roma alielewa kwanini mama huyu kamwita kuongea nae nje ya uwepo wa Nasra, swala la mama huyo kujua ukweli aliamini lilikuwa ni swala la muda tu , lakini hakudhania kama lingetokea mapema hivyo.

“Ni kweli mama nimeoa na ni jambo ambalo tulipanga kukuweka wazi baada ya wewe kufika hapa jijini”Aliongea Roma na kumfanya mama Nasra sura yake kujikunja kidogo.

“Mr Roma nimekuitia hapa ili niweke msimamo wangu wazi kama mzazi , najua kwamba wewe sio mtu mbaya kwa Nasra na una nia nzuri kwake ndio maana ukaambatana nae nakuja mpaka kijijini kwetu , lakini mimi kama mzazi naamini hili linaloendelea sio sawa , Mr Roma nataka uachane na Nasra”Aliongea Mama Nasra huku akionyesha kutumia nguvu sana kutamka maneno hayo , kwani alionyesha hali ya kukoa utulivu , lakini hata hivyo maneno yake yalijaa hisia za kile ambacho amekiamua moyoni mwake.

“Mama najua swala la mimi kuoa limekuwa jambo kubwa kwako , lakini bado tunaweza kuongea , najua naweza kutoeleweka na kuonekana kama mbinafsi ,lakini Nasra ni mwanamke muhimu kwangu na nampa thamani yake kama mwanamke wangu yoyote yule na nipo tayari kufanya chochote kwa ajili yake”Aliongea Roma kwa namna ya kujitetea na kumfanya Mama Nasra kifua chake kupanda na kushuka.

“Kwahio Mr Roma unamaanisha kwamba unataka kumuoa Nasra kama mke wa pili au unataka kumfanya kama mchepuko tu?”

“Mama kuhusu kumuoa Nasra na kumpa cheo cha mke naomba niwe tu wazi, hilo ni swala ambalo lipo nje ya uwezo wangu kwani nishaoa tayari,, lakini ninachoweza kukuhakikishia , nitajitahidi kumpa vile vyote vilivyopo ndani ya uwezo wangu ambavyo anastahili kama mwanamke , atakachokosa ni cheo cha kuitwa mke tu, hiko ndio kitu cha pekee ambacho siwezi kumpatia”

“Mr Roma kama huwezi kumuoa hivyo naomba uachane nae , siwezi kuruhusu mahusiano yenu kuendelea ukizingatia fadhila ambazo Nasra amefaniyiwa na familia ya mke wako , Hapana , Mr Roma naomba usifanye swala hili kuwa gumu kwa Nasra kufanya maamuzi sahihi kwake , naomba uachane nae kiamani, Nasra atapata mwanaume ambaye atakuwa tayari kufunga nae ndoa na hatimae kuwa na familia na kuwa kama wanawake wengine wenye furaha”Aliongea Mama Nasra , ijapokuwa sauti yake ilikuwa ya chini , lakini hata hivyo alionyesha kuwa siriasi kwa kile alichokuwa akiongea.

“Sidhani Nasra ndio anachotaka na siwezi kumuacha kwa maamuzi yangu ilihali nampenda pia , kama shida ipo kwa mke wangu nitayaweka sawa lakini sio kuachana na Nasra labda yeye mwenyewe anitamkie kama hawezi kuendelea na mimi”Aliongea Roma na kumfanya Mama Nasra kukosa usemi aliona jambo linakuwa gumu kuliko alivyokuwa akidhania.

“Mr Roma naomba uniahidi kitu kimoja ,kama itatokea Nasra akakuacha yeye mwenyewe naomba usije ukamsumbua tena , naomba umuache aende kwa amani, niahidi katika hilo”Aliongea Mama Nasra na kumfanya Roma kufikiria kidogo na aliishia kutingisha kichwa kama anakubali, aliona anachokifanya Mama Nasra ni kitu ambacho mzazi yoyote angefanya kwa mtoto wake , lakini hata hivyo kuna kitu alihisi ni kama hakipo sawa , ijapokuwa hakuwa ameishi Tanzania kwa muda mrefu , lakini alikuwa akijua Maisha ya wamama wengi wa vijijini hususani wale ambao wapo katika Imani za kislamu kama ilivyokuwa kwa Mama Nasra, yeye alijiambia kutoka mwanzoni Mama Nasra asingeweka ngumu kwa Nasra kuendelea na yeye kutokana na historia ya Maisha ya Nasra jinsi ambavyo wazazi wake akiwemo mama yake kutaka kumuozesha kwa Mzee Shabani ambaye alikuwa tayari na mke kwa taratibu za kidini.

“Siwezi kumuacha Nasra kufa kwa kuendelea na Roma, Hapana lazima waachane”Aliongea Mama Nasra kwa sauti huku akitoa machozi na muda huo Roma alikuwa ashaondoka tayari, sasa haikueleweka kwanini aikuwa akimaanisha Nasra atakufa kwa kuendelea na mahusiano na Roma.

Upande wa Nasra alienda kazini, lakini hakua sawa kabisa kimawazo, ukweli aliweza kumtuliza mama yake kwa kumwambia kwamba ataachana na Roma , lakini ampe muda wa kufikiria , lakini licha ya kumueleza mama yake hivyo ukweli hakuw a na sababu yoyote amayo ingemfanya kuachana na Roma.

Saa moja kamili za jioni Roma aliweza kufika nyumbani , siku hio ilibdi kughairisha Kwenda nyumbani kwa Rose licha ya mrembo huyo kumuita , Roma alikuwa tayari ashampigia Christen kufika nyumbani kwake kujumuika chakula cha usiku , hivyo alihofia kwamba kama atachelewa kufika nyumbani Christne anaweza kuongea vitu ambavyo havina ulazima na kumfanya Edna kukasirika.

Baada ya kutoka kwenye gari aliweza kuona gari nyingine ambayo ilikuwa ikiashria kwamba jnyumbani kwake kuna mgeni , Roma alitembea taratibu na kuingia ndani huku akikaribishwa na harufu nzuri ya maandalizi ya chakula , sebuleni aliweza kumshuhudia Christen akiwa na mwanaume mwingine mzungu aliempa kisogo wakiwa wamekaa kwenye Sofa moja , huku upande wa kulia akiwa amekaa Blandina.

“Roma umerudi?”Aliongea Blandina kwa tabasamu na Roma alisogea na kuangalia wageni wake na alijikuta akishituka baada ya kumuona mtu ambaye hakuwa amemtegemea na alijiuliza kwanini Christne akamleta mwanaume huyu ndani ya familia yake, lakini kutokana na uwepo wa mama yake alijituliza.

“Roma huna haja ya kuniangalia kwa macho mabaya , Mr Mendelev kaniomba na yeye kuhudhuria chakula cha usiku”Aliongea Christen huku akimwangalia mwanaume aliekaa kwenye sofa huku akitoa tabasamu.

Mwanaume aliekuwa mbele yao hakuwa mwingine bali alikuwa ni Ares, ambaye sasa hivi amejibadilisha jina na kujiita Mendelev , jina lenye asili ya Urusi, Roma mwenyewe alishangazwa na utambulisho wa jina hilo kutokaka Christen.

“Roma ongea na wageni wako , ngoja nikasaidie kuandaa chakula cha usiku”Aliongea Blandina na Roma alitingisha kichwa.

“Christen kwanini umeleta huyu mtu nyumbani kwangu , unafahamu fika ni mtu wa shari na anaweza kudhuru familia yangu”Aliongea Roma na Christen alimwangalia na kutabasamu.

“Toka lini Hades ukamuogopa Ares , mara ya mwisho nilisikia mlipigana na wewe ndio ulieshinda, hata hivyo nadhani unajua tabia yake , nisingekuja nae hapa angefika tu kwa namna yoyote”Aliongea.

“Aphrodite unachongea ni kinyume chake , ukweli ni kwamba tulitoka Droo”Aliongea Ares na kumfanya Roma kumwangalia mzungu huyo kwa macho ambayo hayakuwa na furaha.

“Anachoongea ni sahihi , Ares ulitoa Droo na mimi , hivyo mada hii iishe na unieleze kwanini upo hapa nyumbani kwangu kisha uondoke”Aliongea Roma na Ares alikaa kimya kidogo.

“Hades kwa namna unavyonyesha hali ya kutonipenda, inanipa furaha sana na kuona uko mbali sana na mimi kwenye vitu vingi”

“Ares acha kuongea upuuzi , nenda moja kwa moja kwenye jambo ambalo limekuleta Tanzania na urudi ulikotoka ,sitaki uwe karibu na familia yangu”Aliongea Roma huku akiwa siriasi na Christen aliekaa pembeni hakutaka kuingilia.

“Okey , hakuna haja ya kukasirka Hades , kilichonileta hapa Tanzania ni kutaka maelezo yanayohusiana na God’stone”Aliongea Ares na kumfanya Romakutabasamu kifedhuli.

“Kumbe bado tu haujakata tamaa na kutafuta Jiwe la Kimungu?”

“Hades kwako jiwe la kimungu linaweza lisiwe na thamani lakini kwangu mimi ni kitu chenye thamani kubwa, kwasababu licha ya kwamba unacheo sawa na sisi cha uungu lakini bado utabakia kuwa binadamu tu”

“Ares sidhani umekuja kunichamba , cheo cha uungu sikupata kwa kupewa bali nilikipata kwa nguvu zangu , mimi ni binadamu kweli na najivunia vilevile, hivyo huwezi kuindoa thamani yangu kwa maneno yako , kama swala lako linausiana na hilo jiwe basi tambua kwamba lishachukuliwa na halipo chini ya umiliki wangu tena”Aliongea Roma na Ares alimwangalia Christen.

“Ares nadhani uashaamini maneno yangu sasa?”Aliongea Christen.

“Aphrodite wewe na Hades wa Zamani sijui mlikuwa mkifikiria nini mpaka mkamuamini binadamu na kumpatia kitu cha thamani”

“Ares kwanini unamhofia sana Athena kumiliki Jiwe la Kimungu , unapaswa kuwa mwenye furaha kwani ni ndugu yako”.

“Hades huelewi unachokizungumzia, siwezi kumuamini Athena mtu ambaye mpaka sasa sijui anavaa sura ya nani?”Aliongea Ares na kumfanya Roma kumwangalia Christen.

“Christen hata wewe umeshindwa kujua Athena anaishi kwa sura ya nani?”

“Hades hilo nadhani tushazungumza muda mrefu tu , kutokumfahamu Athena sura yake ndio kunatufanya kuwa kwenye wasiwasi na kile anachokipanga”Aliongea Christen.

“Hades hakuna namna yoyote ukaweza kumtambua Athena uhalisia wake? ,wewe ndio ulieweza kukutana nae , mpaka akachukua jiwe la kimungu kwenye mikono yako?”

“Ningekuwa najua sura yake ningekuwa nishamwambia Christen tayari”Aliongea na kumfanya Ares kuonyesha kukata tamaa kabisa , alikija Tanzania kwa minajiri ya kupata taarifa yoyote ambayo inaweza kumsaidia kumjua Athena anatumia sura ya nani.

“Hades umefanya kosa kubwa sana kupoteza jiwe la Kimungu tena kwa mtu kama Athena, kwa upande wangu sina cha kupoteza , chochote anachofanya Athena huko alipo naomba afanikiwe kwani naamini nitakuwa mnufaika wa kwanza”.

“Kwangu haijalishi nani anamiliki jiwe hilo, ila haitotokea siku hata moja nikakaa chini wakati mnafanya mambo ambayo yanadhuru watu wangu wa karibu aidha kwa njia ya moja kwa moja au isiokuwa ya moja kwa moja, hata awe nani nitahakikisha namzuia kwa namna yoyote ile”

“Hahaha.. Hades kama kawaida yako ya kujaa upepo, nikueleze tu, licha ya kwamba unaonekana kuwa na uwezo mkubwa kuliko sisi , lakini ni kwa muda tu, siku ambayo nguvu zetu zitakapoweza kuturejea nitakuwa wa kwanza kukuua Hades”Aliongea Ares na baada ya kumaliza kauli yake palepale alipotea.
 
SEHEMU YA 357

Jumatatu ndio ilikuwa siku ambayo Roma na Edna walianza kulala pamoja huku Lanlan akihamia chumbani kwa mlezi wake Qiang, Edna kwenye siku ya kwanza alionekana kuwa na wasiwasi mno na Roma alilitambua hilo na aliona ni wajibu wake kumtoa wasiwasi mke wake.

“Wife huna haja ya kuwa na wasiwasi”

“Nani kasema nina wasiwasi?”Alijibu Edna huku akijibaraguza , alikuwa na aibu kweli ya kufanya baadhi ya vitu vingi ambavyo amevizoea kabla ya kulala.

Wakati huo Edna alikuwa amekaa kwenye sofa akiwa ameshikilia kitabu na Roma alikuwa amekaa kwenye kitanda akiwa hana wasiwasi , kwa jinsi Edna ambavyo hakuwa akielewa kile alichokuwa akisoma ni dhahiri kabisa alikuwa akisubiria Roma apitiwe na usingizi ndio na yeye apande kitandani.

Upande wa Roma alijua Edna alikuwa akizuga tu kusoma kitabu, kwani kwanza haikuwa kawaida ya Edna kuingia chumba cha kulala akiwa ameshikilia kitabu , mara nyingi kama utamuona anasoma kitabu basi ni kwenye chumba chake cha kujisomea na akiingia kwenye chumba chake cha kulalia huwa kazi ni kulala tu.

“Babe wife kwahio unaniambia kwamba hauna wasiwasi Eh?”Aliuliza Roma huku akitoka kitandani na kumsogelea Edna pale alipokaa.

“Sina wasiwasi mimi , kwani sikulala tu au kuna lingine”

“Una uhakika unasoma hiko kitabu?”

“Una nini Roma , si unaona nimeshika kitabu”

“Lakini umekigeuza juu chini”Aliongea Roma huku akiangalia kitabu alichoshikilia Edna , ni kweli alikuwa amekigeuza juu chini . Edna alijikuta akimwangalia Roma na kuona aibu baada ya kuumbuka ila Roma hakumcheka Zaidi ya kumshika mkono na kumpeleka kitandani , huku Edna akiwa amejawa na wasiwasi kwenye macho yake, Edna alionekana kama mtoto wa darasa la saba likija swala la mahusiano , hakuwa akijiamini kabisa.

Roma alijua mke wake Edna alikuwa mgeni sana kwenye maswala ya mapenzi , hivyo lilikuwa ni jukumu lake kumuondolea hofu.

“Huna haja ya kuwa na wasiwasi , hatuwezi kufanya chochote kama haupo tayari , hata hivyo napenda nilale karibu yako mke wangu”Aliongea Roma akimwangalia Edna usoni wakati wakiwa wamekaa kitandani na Edna alijikuta aking’ata lipsi zake na kuitikia kwa kichwa.

Roma alipanda kabisa kitandani na kisha akampa ishara Edna kumsogelea na Edna hakubisha , alipanda kitandani na kumsogelea Roma na alijishtukia akikumbatiwa na kulazwa kifuani kwa Roma.

Mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda mno kiasi kwamba hata Roma alijua hofu ambayo alikuwa nayo Edna , ukweli Edna licha ya kwamba alishatolewa usichana wake lakini bado alikuwa ni kama hakuwahi kufanya mapenzi , huenda sababu ni kwamba siku ambayo Roma anamtoa usichana wake alikuwa usingizini hivyo hakuelewa chochote.

“Ndio tunalala hivi?”

“Ndio babe , hivi ndio namna nzuri ya kupata usingizi mapema”Aliongea Roma na Edna alishindwa kutia neno na kutulia kimya akisubiria kifuatacho hakuamini kama anaweza kupona usiku huo , Roma alisogeza mkono na kuzima taa ya kitandani.

Dakika chache tu Edna alipotelea usingizini juu ya kifua cha Roma, jambo ambalo lilimfurahisha Roma , kwani Edna akilala anakuwa kama Lanlan tu, wote wanakuwa na tabia ya kulala fofo.

Roma jambo moja ambalo lilikuwa likisumbua akili yake ni swala la Nasra na mama yake , Roma hakuweza kabisa kuongea na Nasra kwa takribani wiki nzima yote.

Ukweli ni kwamba mara baada ya Edna kuona Nasra hakuwa vizuri kimawazo alimpa likizo ya mwezi mmoja , sasa kitendo cha Nasra kukosekana kwenye kampuni kilimfanya Roma kutoshindwa kumpata na hata alivyopiga simu haikuwa ikipatikana hewani na Roma alishindwa pia Kwenda nyumbani kwao..

Kuna muda Roma aliwaza huenda Nasra amemua kufuatisha kile ambacho mama yake alikuwa akimwambia ndio maana hakuwa akipatikana hewani.

*******

Ni siku ya jumatano Roma aliweza kukutana na Mage muda wa saa kumi kamili za jioni mara baada ya kutoka kazini,Mage ndio aliempigia Roma akihitaji kuonana nae kwa ajili ya kuongea na Roma kwakua ndio muda wa kutoka kazini walikubaliana kukutana maeneo ya karibu karibu na nyumbani na waliweza kuchagua mgahawa wa Mama Afrika uliokuwa maeneo ya Masaki.

Roma baada ya kufika aliweza kuelezwa na Mage namna ambavyo mama yake alikuwa akikomalia mapenzi yao yasiendelee na Rom alijikuta akishangazwa na jambo hilo kwani hakuwa amelitegemea pia kutokea kwa Mage , kwani mpaka muda huo hakuw amemaliza swala la Nasra na mama yake na hilo pia linajitokeza.

“Roma unaonaje ukafika nyumbani na kuongea na mama , huenda wewe akakuelewa, ijapokuwa hautonioa lakini ni angalau ukaja kuyaweka sawa na familia yangu na wakakujua kama mwanaume wangu”Aliongea Mage na kumfanya Roma kukuna kichwa.

“Lakini si wananifahamu tayari na umeniambia mama yako anakugomea kuendelea na mimi?”

“Ndio , lakini angalau ukiwaweka wazi nia yako kwangu wanaweza kukubali tukaendelea na mahusiano yetu ,siwezi kuishi na kuwa single kwa Maisha yangu yote” Aliongea Mage na kumfanya Roma kufikiria kidogo na kuona Mage kweli anaongea jambo la maana , ni kweli kwamba asingeweza kumuoa Mage , lakini Kwenda nyumbani kwao na kuyaweka sawa ni wajibu wake , kwani alikuwa akijulikana tayari amekwisha oa.

“Mage siwezi Kwenda nyumbani kwenu leo wala kesho ila kuna maswala yanayohusiana na Edna yanaendelea kwasasa , yakishaisha nitakuja kujitambulisha rasmi, na nitahakikisha mama yako anakubali tuendelee na mahusiano yetu”Aliongea Roma na kumfanya Mage kutabasamu kwa furaha.

“Vipi leo unawahi kurudi?”Aliuliza Mage na swali lake ni kama Roma alijua lilikuwa likimaanisha nini , lakini kabla hata hajajibu simu yake ilianza kuita mfululizo na alipoitoa na kuangalia jina la mpigaji , alikuta ni mama yake.

“Roma kuna mambo yanaendelea hapa nyumbani , unaweza kurudi sasa hivi”Aliongea Blandina

“Mama nini kimetokea?”Aliuliza Roma huku akikunja sura.

“Kuna mwanaunme wa kikorea kafika hapa nyumbani kwa ajili ya Yezi na amesema ni ndugu yake, lakini Yezi hataki kumuelewa na amejifungia chumbani kwake analia tumeshindw akujua cha kufanya”Aliongea Blandina na kumfanya Roma kushangaa kidogo.

“Okey !, nakuja sasa hivi , siko mbali na nyumbani”Aliongea Roma na kisha akakata simu na ilibidi amuage Mage huku akimwahidi atamtafuta siku kadhaa zijazo , kisha aliingia kwenye gari na kuendesha kuelekea nyumbani, na ilimchukua dakika kama kumi tu hivi kufika.

Roma baada tu ya kulikaribia geti aliweza kushuhudia magari matatu aina ya Mercedenz Benz S600 rangi nyeusi yote yakiwa yameegeshwa pembeni ya geti la nyumba yao na ile anasogelea geti kwa ajili ya kuingia ndani alizuiwa na wanaume wawili waliovalia mavazi meusi, wote wakiwa ni wa Kikorea.

“Sir Please Prove your identity”Mmoja wao aliongea na kumfanya Roma kugundua kuwa watu hao walikuwa ni mabodigadi.

“I am owner of this house , can’t I go back to my own place?”Aliuliza Roma akimaanisha kwamba yeye ni mwenye nyumba na je hapaswi kuingia nyumbani kwake.

Wale mabodigadi mara baada ya kusikia hivyo walishangaa kidogo lakini muda huo huo waliweza kusikia sauti kutoka ndani ikiwaamrisha wapishe hio gari iingie na sauti hio iliongea kwa lugha ya kikorea na Roma kwakua alikuwa pia akiifahamu hio lugha aliweza kujua kinachoongelewa na wale mabodigadi walipisha njia na Roma aliweza kuingiza gari yake ndani.

Roma baada ya kutoka kwenye gari aliweza sasa kushuhudia mwanaume mmoja alievalia suti ya bei ghali, alievalia miwani ambayo ilikuwa ni ya madini ya dhahabu tupu , mwenye nywele nyingi zilizofunika kichwa chake kiasi cha kuziba masikio , makadirio ya umri kati ya miaka therathini hivi Kwenda mbele na hakuwa peke yake pembeni alionekana pia kijana wa makamo ambaye amevalia pia suti ya rangi ya bluu , ambaye kwa haraka haraka alionekana kuwa msadizi wa bwana alievalia miwani.

“You Must Be Mr Roma, I am glad to meet you , I am Park Jonghyun, Yezi Cousin Brother , I had waited forever to see her”

“Lazima utakuwa ni bwana Roma , nimefurahi kukutana na wewe , naitwa Park Jonghyun Binamu yake na Yezi , nimesubiri kwa muda mrefu kukutana nae”Aliongea hivyo kwa lugha ya kingereza huku wote wakiingia ndani ya eneo la sebuleni, muda huu Edna alionekana bado hajarudi kutoka kazini.

“Kwahio bwana Park unaamanisha kwamba Yezi anaeishi hapa ni mdogo wako?”

“Ndio Mr Roma,tulikuwa tukimtafuta kwa miaka miwili mfululizo na siku chache zilizopita baada ya kupata taarifa ya kupatikana kwake hapa Tanzania ndio maana nikafanya safari licha ya kutokuwa na uthibitisho, lakini naamini kuja hapa sijafanya makosa , nina uhakika Yezi ni Binamu yangu”Aliongea na kumfanya Roma kumwangalia mama yake , ukweli wote walikuwa wakielewa historia ya Yezi alivyoweza kuokotwa nje ya kituo cha kulelea Yatima Kiwangwa , lakini swala la mwanaume kusema ni ndugu wa Yezi kidogo liliwapa ukakasi licha ya kwamba lilionekana kuwa na ukweli ndani yake kwani Yezi alikuwa na asili ya kikorea.

Katika maelezo ya Park Jonhyun ni kwamba Yezi baba yake alikuwa akifahamika kwa jina la Park Joonchen, mtoto wa kwanza kutoka ukoo wa Park huko Korea.

Park Joonchen miaka mingi iliopita aliweza kuanzisha mahusiano na mwanamke wa kitanzania afahamikae kwa jina la Leah na mahusiano yao yalikuwa makubwa mpaka ikafikia hatua ya Park Joonchen kumpeleka Leah Korea kwa ajili ya kumtambulisha kwenye familai yake na hatimae kumuoa ,lakini mara baada ya kumtambulisha hakuna mwanafamilia ambaye alimkubali Leah kabisa kutokana na rangi yake ya kiafrika, lakini licha ya familia hio kumkataa Leah upande wa mchumba wake Park JoonChen hakumtelekeza Zaidi ya kwamba mapenzi yalizidi nguvu na wote kwa pamoja walikimbilia kusiko julikana kuendeleza mapemzi yao, kipindi ambacho Leah anatambulishwa alikuwa tayari mjamziro na familia hio ilikuwa ikilifahamu swala hilo lakini hata hivyo bado hawakutaka kukubali Ngozi nyeusi kwenye ukoo wao.

Sasa haikueleweka ilitokea lini lakini Park Joonchen ndani ya mwaka huo huo alipotoroka alikutwa na umauti akiwa nchini Kenya Nairobi , kifo chake ambacho ripoti ilielezea kwamba alipigwa risasi na polisi wa Kenya mara baada ya kuhisiwa ni jambazi.

Baada ya mwili wa Prk Joonchen kusafirishwa na kurudishwa korea kwa ajili ya mazishi upande wa Leah haikufahamika alikuwa wapi kwa muda huo na familia hio haikujisumbua tena kumtafuta na walimchukia na kumuona kama alikuwa chanzo cha kifo cha mtoto wao na ndio maana wakampotezea.

Sasa familia hio ilianza kumtafuta Yezi miaka miwili iliopita baada ya babu yake Yezi kuanza kuugua ugonjwa wa saratani , ndipo alipoanza kutamani kukutana na mjukuu wake kabla ya kuaga dunia.

Katika familia ya Park mtoto wa kiume wakati huo alikuwa ni Park Joonchen tu pamoja na dada zake , hivyo alikuwa ni kama mrithi , hivyo baada ya kifo chake familia ikakosa mrithi wa moja kwa moja ambaye ana damu halisi ya Park Joonchen.

“I am impressed Tanzania is such huge country but still your family managed to track Yezi?”

“Nimeguswa , Tanzania ni taifa kubwa kwa eneo lakini bado familia yako imeweza kumtafuta Yezi na kumpata?”

“Yeah , I wonder if Mr Roma has heard of Starmoon Group before , its business empire built by our Park clan?”

“Ndio! ,Nauliza kama M Roma ushawahi kusikia kuhusu Starmoon Group ni biashara kubwa ilioanzishwa na ukoo wa Park”

“ If its StarMoon Group , You are Director Park Jonghyun?”Iliikika sauti ya Edna nyuma yao na kumfanya yule mwanaume kugeuka na kumwangalia.

ITAENDELEA ; 0687151346 NDIO NAMBA YANGU YA WATSAPP , KWA WALE WANAOTAKA MWENDELEZO NICHEKI NIKUPE UTARATIBU.
 
Twajua muda sio rafikiyo lakini punguza hii adhabu ya subira mkuu!!!! Ni kusema na kutenda.
Mkuu huku kuhanikiza kwako nimekukubali!
Wewe kama sio wa Heru juu, basi itakuwa Kanyanyamahela ps au Kakonko kabisa kule ndanindini sawa na burundi kwakina JARUDO...
 
Atadinywa tu huyo Roma anamlembesha
Sasa hiyo sehemu ilete kwanza alafu utaendelea na zingine hata kama iko mbele....alafu schedule yetu ni j4 ,Alhamis na jumamosi... Hades SinganoJr.
 
simulizi za hivi utakuta anadinywa na jamaa jingine na sio roma[emoji1787]
 
Back
Top Bottom