SEHEMU YA 353
Naam mashindano ya kizazi nyota yaliweza kuisha Rasmi wa kuweka rekodi kwa kuwa moja ya mashindano ambayo yamefuatiliwa na watu wengi Zaidi , Kampuni ya Vexto Media pia ilipata mapato makubwa sana kupitia mashindano hayo ,jambo ambalo lilifanya hisa za kampuni kupanda Zaidi.
Siku ya pili , yaani siku ya jumatatu Habari kubwa Zaidi ilikuwa ni juu ya Edna kuweka hadharani kuwa ameolewa, mrembo huyu kwa miaka mingi watanzania wengi walifahamu kama alikuwa single , lakini kitendo cha kuweka hadharani kaolewa tena Zaidi ya miezi sita iliopita ilikuwa ni Habari ambayo ilipata hadhira ya watu wengi na kama ujuavyo taifa la Tanzania watu wengi wanapenda Habari zinazohusiana na Maisha ya watu basi ilikuwa hivyo.
Moja ya watu ambao walifurahia kitendo cha Edna kuweka wazi juu ya mahusiano yake ni Blandina.
Ukweli Blandina kuna muda alihisi huenda Edna alikuwa akimficha Roma kama mume kutokana na kwamba Roma hakuwa na hadhi kubwa kwenye jamii ka yeye na ndio maana baada ya Edna kuweka wazi alijjikuta akiwa ni mwenye furaha Zaidi kuliko watu wote na alijiambia hio ni hatua nzuri sana ambayo mwanae amefikia.
Upande mwingine wakati Blandina akiwa mwenye fuaha , upande wa Mage hali haikuwa nzuri hata kidogo , mrembo huyo afisa poilisi ukweli ni kwmaba siku nzima alikuwa ni mwenye fuaraha kutokana na kwamba kwa mahesabu yake siku hio ya Jumapili ndio ilikuwa siku ambayo Roma na Edna mkataba wao wa ndoa ulikuwa ukimalizika , lakini Mage alijikuta akiwa kwenye mshituko mara baada ya Edna kuweka hadharani mahusiano yake na Roma na kuutangazia uma kwamba kwanzia siku hio hayupo mwenyewe bali ameolewa tayari, kwake lilikuwa pigo kwani aliona dalili zote za kukosa ndoa.
Magdalena aliekuwa akijua kinachoendelea alijikuta akimhurumia pacha mwenzake, Magdalenda hata yeye alikuwa akifahamu kupitia Mage kwamba ndoa ya Edna na Roma ilikuwa ni ya mkataba tu ambao unamalizika muda si mrefu.
Usiku wa jumapili mara baada ya Edna kuweka wazi mahusiano yake na Roma aliona kabisa dalili ya wawili hao kutokuachana kabisa , kwani mara nyingi mwanamke akimuweka mwanaume hadharani ilikuwa ikiashriaa kwamba alikuwa tayari kuishi nae milele licha ya changamoto , sasa kwa tafsiri ya haraka haraka alijua naafasi ambayo alikuwa akiitumainia dada yake haiwezi kutokea.
“Mage tunapaswa kuwa na furaha kwa ajili ya Edna , ni rafiki yetu wa utotoni na furaha yake ni furaha yetu , hatuwezi kuwa wanafiki , lakini hata hivyo Roma pia anaonekana kumpenda Edna”Aliongea Magdalena asubuhi mara baada ya kuingia kwenye chumba cha Mage na kumkuta akiwa amelala , jambo ambalo haikuwa kawaida yake.
“Mbona unaweka sisi na sio mimi?”Aliuliza Mage baada ya kumwangalia Magdalena , kilichomfanya kuuliza hivyo ni kutokana na Magdalena kutumia uwingi akijijumlisha tofauti na kutotumia umoja , kwani swala la kumpenda Roma lilikuwa juu yake.
“Aaah…Mage nimeweka neno ‘sisi’ kwasababu furaha yako ni furaha yangu, unafikiri napenda kukuona ukilala hivi , kama kweli unampenda Roma unapaswa kumpenda na kile anachokipenda pia”Aliongea Magdalena na Mage alivuta pumzi na alionekana kufikiria.
“Najua Magdalena na nilikuwa nikifikiria hilo usiku wote, siku zote nilikuwa nikiwazia kuhusu mkataba wake wa ndoa lakini nikasau kufikiria juu ya hisia zake kwa Edna, najiona mjinga kwa kutegemea makubwa ndio maana niko hivi”.
“Kwahio mpango wako ni kumuacha Roma au ni kuendelea nae”
“Mpango wangu ni kuendelea nae , Roma hawezi kunioa lakini vile vile siwezi kumuacha kwasababu ya neno Ndoa”Aliongea naMagdalena alifikiia kidogo.
“Lakini Mage , Mama yetu anataka wote tuolewe na tuwe na familia, unafikiria atakubali ukimuelezea kuwa mwanaiume unaempenda ni Roma, vipi kuhusu baba?”
“Mage hilo lisikusumbue , mama akubali wala asikubali mimi sijui cha kufanya , nitasikiliza moyo wangu unachoniambia , hata hivyo mimi ni mtu mzima na najua kipi kizuri na kibaya kwangu”
“Jiandae kumpatia mama majibu maana tokea jana aone tukio la Edna kumtambulisha mume wake anataka na sisi tuwe kama Edna na yupo chini sebuleni anakusubiria”Aliongea Magdalena na kisha alitoka kwenye chumba cha Mage.
Mama T ukweli tokea siku ya jana kushuhudia Edna akimtambulisha mume wake Roma Ramoni pasipo ya kuwa na aibu alijikuta akitamani pia Watoto wake mapacha pia kuleta wanaume na kuwatambulisha kwake , Mage alikuwa mkubwa tayari na Magdalena hivyo hivyo alikua mkubwa tayari ila vitendo vyao vya kutoonekana kuwa na wanaume vilikuwa vikimtia mawazo sana.
“Mume wangu nadhani ni muda sahihi wa Mage kumleta mchumba wake tumuone”Aliongea Mama T na kumfanya Afande Tobwe amwangalie.
“Mbona wasiwasi wako ni kwa Mage tu na Magdalena haumzungumzii, yeye hapaswi kuolewa?”
“Mume wangu nimesahau tu kukuambia , ila kuna mwanaume tayari ambaye yupo tayari kumuoa Magdalena na ameonyesha nia thabiti n ahata familia yake inamsapoti”Aliongea Mama T na kumfanya Afande Tobwe kushangaa kidogo.
“Mwanaume gani , mbona sina hio taarifa?”
“Nilisahau kukuambia tu mume wangu , familia yenyewe ni ya Waziri wa Sayansi na Teknolojia, mtoto wao mkubwa Jumbe ndio ameonyesha nia ya kutaka kumuoa Magdalena”Aliongea Mama T na kumfanya Afande Tobwe kushangaa kidogo.
“Jumbe namfahamu vizuri , yupo kikosi kimoja na Magdalena, kumbe ni wapenzi sikuwahi kulifahamu hili , Magdalena ni msiri sana”Aliongea Afande Tobwe na Mama T ametabasamu.
“Kumbe wanafanya kazi kikosi kimoja basi mapenzi yao yanaweza kuwa ya kweli , mimi mama yake Jumbe alivyonielezea nia ya mwanae na kuniambia ni mwanajeshi pia sikuona haja ya kukataa, niliona sawa tu kwa mwanajeshi kuolewa na mwanajeshi mwenzake , lakini pia familia ya Mheshimiwa Hamadi ni moja ya familia bora zenye nguvu na ni mtajiri , itakuwa faida kwetu kama tukiunganisha koo”Aliongea Mama T na kumfanya Afande Tobwe kufikiria kidogo.
“Mama T unapaswa kuongea kwanza na Magdalena mwenyewe, kama wanapendana tutawaruhusu kuona mimi sina kinyongo kabisa , lakini kama Magdalena hampendi basi hatuwezi kulazimisha ,kikubwa ni furaha za Watoto wetu”Aliongea Afande Tobwe.
“Mume wangu huna haja ya kuwa na wasiwasi , Jumbe ni kijana mtanashati naamini Magdalena anampenda”
“Mama mimi simpendi Jumbe”Ilisikika sauti upande wao wa kushoto na kujikuta wote kwa pamoja wakigeuka, aliongea hivyo alikuwa ni Magdalena.
“Magdalena unamaanisha nini humpendi Jumbe , mbona mama yake kaniambia mnapendana na mtoto wake , mpaka akachukua hatua ya kuniambia wanataka kuanza utaratibu wa ndoa?”
“Mama Jumbe ni muongo sijawahi kuwa na mahusiano nae , ni kweli ameniambia mara kadhaa ananipenda na anatamani anioe lakini sijawahi kumkubalia na hatuna mahusiano na sipo tayari kuolewa na Jumbe maana hana vigezo ninavyotaka”Aliongea Magdalana akiwaka uso wake siriasi kabisa na kumfanya Mama T kiumwangalia mume wake.
“Magdalena hakuna ambaye atakulazimisha kuolewa na mwanaume ambaye humpendi na sio kwako tu hata kwa dada yako Mage , lakini nikushauri kwamba umri wako unasogea na unapaswa uolewe pia hivyo naamini kama humpendi Jumbe kuna mtu unampenda si ndio?”Aliuliza Afande Tobwe.
Afande alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kusoma saikolojia , ukwei ilikuwa ni fani yake kwani kabla hajajiunga na jeshi alisomea maswala ya Saikolojia na anayo shahada moja , hivyo kumuona Magdalena kukasirika mara baada ya kuhusishwa na Jumbe ni kama aliweza kuona mtoto wake pia alikuwa na mwanaume anaempenda.
“Dady ni kweli kuna mwanaume na mpenda , lakini hajui”Alijibu Magdalena kwa aibu na kumfanya Mama T kutoa macho kama amebanwa na mlango.
“Hivi watoto wangu wote mna nini ? Mage ndio huyo anae mtu anampenda lakini anashindwa kumtambulisha kwangu na wewe una mtu unampenda lakini hajui, mbona mnataka kunitia kichaa mimi mama yenu , ni lini mtaolewa na mimi angalau wanawake wenzangu wanichangie pesa za harusi, nimechoka Kwenda kwenye harusi za familia nyingine mimi”
“Mke wangu punguza jaziba Magdalena hapa kakuelezea kuna mwanaume anampenda hio ni hatua nzuri ya kuelekea kwenye harusi unazotaka, halafu wanawake wa Tanzania mnapenda sana harusi kuliko ndoa zenyewe”
“Mume wangu sio hivyo , Mage na Magdalena ni watu wazima sasa na katika masha yao hawajawahi kuonekana na wanaume , hivi unajua wenzao wanawazungumziaje huko nje?”
“Wanawazungumziaje?”
“Sitaki hata kusema wanachozungumza maana kila nikisikia napatwa na hasira, wanasema mapacha wangu ni ‘Lesbian’ ndio maana hawajawahi kuonekana na wanaume”Aliongea na kumfanya Afande Tobwe kuweka uma chini , hakuamini kama Watoto wake ndio wanazungumziwa hivyo huko nje.
Lesbiani ni aina ya wanawake wanaopenda wanawake wenzao kwa lugha nyepesi watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja kwa mfano Athena ni Lesbian.
“Na wewe unaamini Watoto wetu ni Lesbian?”
“Siamini hivyo mume wangu , Mage na Magdalena hawawezi kuwa na tabia za aina hio ,kwanza ni nje na tamaduni za dini yetu, lakini nachoshwa tu na maneno ya watu”
Afande Tobwe alijikuta akimwangalia mke wake na kushindwa kumuelewa , alijiuliza tangu lini mke wake akawa ni mwenye kujali maneno ya watu au kuna jambo ambalo halijui na anafichwa.
“Mke wangu jitahidi sana kuachana na maneno ya watu kwani hayajengi , Magdalena na Mage wote washakuweka wazi wana watu ambao wanawapenda , nadhani ni vyema ukaanza kuwasapoti katika hilo ili hatimae waweze kufunga ndoa”Aliongea AFande Tobwe na kisha alinyanyuka na kuchukua mkoba wake akionekana ndio muda wa kuanza safari umewadia.
“Goodmonring Dady”
“Goodmorngin Daughter , umeamkaje?”Aliongea Afande Tobwe mara baada ya kukutana na Mage ambaye ndio anashuka kunywa chai.
“Niko sawa Dadi”
“Okey Great , mimi naelekea kazini”
“Okey Dady , kazi njema”Aliaga na Afande Tobwe akaondoka.
“Mama mbona unaniangalia sana?”Aliuliza Mage mara baada ya kugundua mama yake alikuwa akimwangalia sana.
“Mage hebu nieleze , dada yako hapa kasema na yeye ana mtu anampenda na hajamuambia , unamfahamu huyo mwanaume?”
“Nini !!, Magdalana ya kweli hayo , mbona hujaniambia?”Aliongea Mage kwa mshangao na Mama T alivyomuona Mage akiwa kwenye mshangao , aliamini huenda na yeye pia hamfahamu huyo mwanaume na alijikuta akivuta pumzi na kuzishusha kwa wakati mmoja.
“Kumbe hata wewe haufahamu?, Yaani nyie Watoto , nimefanikiwa kuwalea na kuwa watu wazima lakini mmefikia hatua nzuri ya umri wengu , lakini mnanifanya kichwa kinaniuma”
“Mama kwanini kichwa kikuume , usiwe hivyo sisi tushakuwa wakubwa na tunajua ni kipi tunataka , unajipa mzigo wa mawazo bure”
“Ndio najua mmekuwa watu wazima na mnajua ni kipi kinawafaa Zaidi na nipo tayari kuwasapoti ndio maana nataka mnieleze , tukianza na wewe Mage ni mwanaue gani ambaye unampenda , niweka wazi ili nijue?”Aliongea Mama Mage huku akiweka sura yenye usiriasi.
“Mama Mwanaume…”Aliongea Mage , lakini Magdalena alimshika Mage mkono akimpa ishara ya kwamba asiongee..
“Haina haja ya kumficha Zaidi , nitamwambia mwanaume ninaempenda na wewe ujiendae kutumbia ni mwanaume gani unaempenda”
“Mama mwanaume ninaempenda unamfahamu sana tu , ni Roma”Aliongea Mage na kumfanya Mama T kufikiria kidogo.
“Roma yupi , namfahamu Roma mmoja tu mume wa Edna , kuna Roma gani mwingine ambaye namfahamu?”
“Mama ni huyo huyo Roma Ramoni ndio mwanaume ambaye nimetokea kumpenda”Aliongea Mage na kumfanya Mama T kuwa kama mtu ambaye hajasikia vizuri.
“Mage huwezi kuwa siriasi , usiniambie unajihusisha kimapenzi na Roma mume wa Edna!!!!”Aliongea Mama T kwa mshangao huku moyo wake ukienda mbio.
“Mama naomba unisamehe…”
“Mage kimyaaa..sitaki kusikia …. Naomba usiendelee kuongea , utaniua wewe mtoto”Aliongea huku akianza kupumua kwa shida na ilibidi Magdalena kumsogelea mama yake na kumzuia asindoke chini na kiti.
Unadhani nini kitaendelea kwa Mage , ni mwanaume gani anampenda Magdalena na hajamwambia?
SEHEMU YA 354.
Edna tokea jana yake kumtambulisha Roma hadharani kama mume wake , ukweli hakuwa na wasiwasi kabisa na ilikuwa kwake ni kama mapenzi yake yaliongezeka Zaidi juu ya Roma na kumchukulia siriasi tofauti na siku kadhaa nyuma , alijiambia kitendo alichofanya jana ni sahihi na hakuna namna ambayo atajutia.
Siku ya jana yake wakati wanarudi nyumbani Edna na Roma waliweza kuongea wakiwa kwenye gari juu ya Maisha yao ya baadae, Edna alimwambia Roma ahakikishe kwamba hajutii kwa kile ambacho amekifanya usiku huo.
“Mke wangu sikudhania kama utapata ujasiri wa kunitambulisha hadharani kama vile?”Aliongea Roma mara baada ya wawili hao kuingia kwenye gari.
“Lilikuwa swala la muda tu kuwafanya watu kuelewa , hata hivyo mpaka sasa watu wengi katika kampuni watakuwa wanafahamu uhusiano wetu na hawakuwa na naman ya kupata ukweli , Roma unaonaje kwanzia sasa ukawa siriasis na Maisha yetu , najua una wanawake wengine na sijasema kwamba uwaache , ila ninachotaka unihakikishe kwamba sitojutia maamuzi yangu nilioyafanya ya kukutambulisha kama mume wangu”Aliongea Edna na Roma alijikuta akikuna kichwa .
“Ooh! Edna My love , sidhani kama kuna haja ya kuwa na wasiwasi na Maisha yetu ya baadae , kikubwa ni mapenzi yaliopo katikati yetu , itakuwa ni ngao kwa kila gumu ambalo tutapitia , siwezi kukuahidi kwamba Maisha yetu ya kimapenzi yatakuwa kama ya Hawa na Adamu kwenye bustani ya Edeni , lakini nakuhakikishia kila gumu litakalokuwa mbele ya safari yetu tutalishindwa kwa jina la mapenzi”Aliongea Roma na kumfanya Edna kuona aibu lakini kufurahi kwa wakati mmoja.
“Lakini hakukuwa na haja ya kuchukulia mfano wa Adamu na Hawa , kwani hakuna mifano mingine mizuri zaidi”Aliongea Edna na kumfanya Roma kucheka.
“Hahaha .. Wife niseme kwamba namshukuru sana Hawa kwa kukubali kudanganywa na nyoka, kama sio yeye ningekufahamu vipi mrembo kama wewe, Babe unajua hapa nawaza lile swala la kuhamia..”Aliongea Roma na kumwangalia Edna kwa tabasamu la kifedhuli.
“Mwanaume unaongea pumba wewe ..sitaki kuendelea na haya maongezi maana huwezi kuwa siriasi”Aliongea Edna na kuegamia kiti , ukweli maneno ya Edna yalimfanya hata Dereva aliekuwa akiwaendesha kushindwa kuzuia kucheka kisiri siri.
Sasa ikawa ni siku nyingine ya jumatatu asubuhi,Edna licha ya kwamba alichelewa kulala , lakini alikuwa wa kwanza kuamka na siku hio alimwambia Bi Wema ataandaa chai kabla ya kuelekea kazini ,ijapokuwa Bi Wema alimlazimisha Edna kupumzika kwani ana kazzi kubwa lakini Edna alilazimisha na Bi Wema akamuachia kazi hio Edna huku yeye mwenyewe akiwa anafanya usafi wa nyumba mpaka wanafamilia wote walipoamka.
“Roma unaonaje ukimkaribisha Christen kwenye chakula cha usiku kabla hajarejea Marekani?”aliongea Edna na Roma alimwangalia Mke wake.
“Wife ni wazo zuri , lakini yule mwanamke akija hapa naogopa anaweza kuwaeleza mambo ya uongo kuhusu mimi, hivyo tumuache aondoke tu kazi yake ya kufanya kampuni yetu kuwa maarufu ishaisha”Aliongea Roma na kuwafanya wanafamilia wote kumwangalia kwa mshangao.
“Roma alichopendekeza Mkeo ni jambo zuri , lazima tutoe shukrani kwa alichokifanya Christen kwenye kampuni , amekuwa na mchango mkubwa ndio maana mashindano yalikuwa na mvuto” Roma alijikuta akiacha kula kwanza na kuwaangalia wanawake waliokuwa mbele yake , ukweli nyumba nzima mwanaume alikuwa yeye tu na kadri alivyoangalia nyuso za wanawake wote aliona hana ambaye anamuunga mkono.
“Okey Okey..Wife nitajitahidi kufanya kama unavyotaka, lakini niwaahidi tu akianza kunisema namfukuza”Aliongea Roma na kuendelea kula.
“Mom Anko anaongea nini?”Aliuliza Lanlan baada ya kushindwa kuwaelewa , kwani hakuwa akielewa Kiswahili kabisa na sio kwake tu hata kwa Qiang.
“Lanlan Roma sio Anko ni baba yako sawa?”Aliongea Edna huku akimfuta midomo na Lanlan alijikuta akimgeukia Roma na kumwangalia kwa kumtathimini na Roma baada ya kusikia Edna anamrekebisha mtoto wake alijikuta akiacha kwanza kula na kumwangalia Lanlan, huku wanafamilia hao wakimwangalia Lanlan pia , waliona ilikuwa makosa mwanzoni kumruhusu Lanlan kumuita Roma anko na Edna kumuita Roma kwani ashazoea.
“Lanlan baba yako ni Roma sawa, kwanzia sasa umuite baba?”Aliongea Blandina na Lanlan aliitikia kwa kichwa na kisha kuendelea na chakula chake na kumfanya hata Edna kushindwa kuelewa Lanlan alikuwa akifikiria nini.
“Chubi unaonaje tukafanya dili?”Aliongea Roma na Lanlan alimwangalia Roma kwa hamasa.
“Lanlani yupo tayari kwa dili”Aliongea na kufanya hata Edna kucheka.
“Ninakupeleka kumuona Simba na Tembo na wewe utaniita baba unaonaje”Aliongea Roma na kumfanya Lanlan kumgeukia mama yake.
“Lanlan tutaenda wote , mimi na baba yako kuangalia Wanyama na nitakunulunia na zawaidi nyingine utakayotaka”
“Hurray!!!, Lanlan anapenda sana kumuona Tembo, Lanlan yupo tayari kumuita anko Roma Baba”Aliongea Lanlan kwa kushangilia na kufanya wanafamilia wote kufurahi , kwani alichangamsha nyumba.
Upande wa Roma alishindwa kuelewa kuna siri gani nyuma ya Lanlan kupenda sana Tembo , kwani akisikia Wanyama yeye atazungumzia Tembo , lakinia alijiona hayupo kwenye nafasi ya kuwaza sana juu ya anachokipenda Lanlan.
Edna baada ya kumaliza kunywa chai safari ya kazini ilianza mara moja na siku zote mrembo huyu alikuwa akiendesha gari mwenyewe na ukiona anaendeshwa jua ni kwenye matukio maalumu , hakupenda sana kuendeshwa.
Kwenye kampuni yake, Habari ya siku hio ilikua ni juu ya Edna na Roma kuwa mume na mke , wafanyakazi wote walionekana kujadili swala hilo , huku wakishindwa kuamini kama kweli mwanaumke kauzu kama chuma mume wake ni Roma Ramoni , mwanaume ambaye anaonekana kutokuwa siriasis na Maisha.
Wafanyakazi wengi walikuwa wakizisikia Habari za Roma Ramoni kucheza gemu tokea aanze kufanya kazi na Vexto , lakini licha ya tabia yake hio aliishia kupandishwa vyeo , jambo hilo liliwafanya kuamini kweli kulikuwa na mahusiano.
Watu ambao walikuwa wamechoka kutokana na kauli ya Edna jana yake ni kitengo cha Mahusiano ya jamii na masoko(PR) kinachoongozwa na mwanadada Benadatha , mrembo Recho, Tina na wenzake walikuwa wakizungumzia swala la Edna kuweka wazi mahusiano yake na Roma.
“Unajua licha ya kwamba nilikuwa nikijua kuna mambo ambayo hayapo sawa kati ya Bosi Edna na Roma lakini sikudhania wanaweza kuwa mke na mume”Aliongea Tina.
“Sio wewe tu hakuna ambaye ameamini kauli ya Edna kabisa , hivi ni nani asiejua ndani ya kampuni Dorisi na Nasra wanatoka kimapenzi na Roma?”
“Wee Kweli?”Aliuliza Benadetha kwa mshangao.
“Wewe nae upo kampuni ipi , kila kitu kipo wazi , lakini nashindwa kuelewa imekuwaje Roma akatoka na wafanyakazi wa kampuni ilihali bosi ni mke wake , hivi nani anamuelewa Roma hapa?”
“Jamani tuache umbea tumekuja kufanya kazi sio kumuelewa Roma”Aliongea Recho baada ya Tina kuongea na kumfanya Benadetha na wenzake kushangaa , inakuwaje leo Recho ndio wa kwanza kusitisha umbea wakati ndio mwenyekiti, ilibidi Tina ampime kwanza Recho joto kuona kama ana dalili ya Malaria kwani alichoongea hakikuwa kikiendana na tabia yake.
Ukweli Recho yeye likuwa kwenye mshituko Zaidi , lakini pia alikuwa ni kama hakupenda , mrembo huyu , ukweli ni kwamba ameachana na mpenzi wake mwezi uliopita na kilichomfanya kuachana na mpenzi wake ambaye ashamtambulisha ukweni ni tabia yake ya kuota usiku na kuanza kutaja jina la Roma.
Recho tokea siku ambayo ashawahi kuchezewa viungo vyake vya siri na Roma akili yake haikutulia kabisa , ni kama tukio hilo lilikuwa likijirudia rudia na alitamani waendelee pale walipoishia na alikuwa akitafuta nafasi ya kumtafuta Roma ,lakini sasa kusikia Habari ya Edna kuwa mume wa Roma , ni kama malengo yake yote yaliingia doa na kujikuta akiwa mwenye huzuni tofauti na wafanyakazi wenzake ambao walikuwa kwenye mshangao.
Yaani wakati wenzake wakishindwa kumuelewa Roma na Edna ,yeye alionekana kumuelewa Roma na Edna na alikuwa akijiweka kwenye nafasi sawa kama ya Edna na aliamini Roma aliweza kumpagawisha Edna ndio maana wakawa mke na mume na alitamani kujua kiundani Zaidi ni jambo lipi likawapagawisha warembo wote watatu wa kampuni yaani Dorisi , Nasra na Edna..
Sasa Recho mapenzi kwa mchumba wake aliekuwa akimpenda sana yalipungua sana kiasi kwamba hakuwa na hamu na mpenzi wake na mara nyingi hata wakiwa wanafanya uzinzi atajikuta anamvutia picha Roma na hivyo kupelekea mpaka kutaja jina lake na hiko kikamfanya kuachwa.
Kila siku ya jumatatu Edna alikuwa akifanya utaratibu wa kupitia kila idara kuangalia baadhi ya projecti mpya ambazo zinafanywa lakini pia kutoa maelekezo , aliweka utaratibu huo kutokana na kupunguza kazi kwa wakuu wa Idara kupanda juu gorofani mara kwa mara kwa ajili tu ya kupata baadhi ya vibali hivyo ilimlazimu kupita kila Floor na kufanya baadhi ya maamuzi na kutoa maagizo mengine.
Sasa siku hio watu walikuwa wakimwangalia kwa macho yasio kuwa ya kwaida na kumfanya hata yeye mwenyewe kukosa kujiamini, lakini hata hivyo kama ilivyokuwa kawaida yake hakupenda sana kuongea na aliweka sura ya ukauzu na kutojali wanachokifikiria wafanyakazi wake.
Edna baada tu ya kufika ofisini, mtu wa kwanza kuingia kwenye ofisi yake ni Richard mwanamitindo ambaye alimwajiri hivi karibuni kwa ajili ya maswala ya kudizaini mavazi yatakyotengenezwa na material mapya.
“Edna Yestarday you were so hot , Marie my wife is calling non stop regarding your marriage and other of our Collegue’s keep asking questions about how and when your relationship progressed so far…..”
“Edna jana ulikuwa ni wa moto sana , Mke wangu Marie anapiga simu bila kuacha kuulizia juu ya ndoa yako na pia wanafunzi wenzetu tuliosoma nao wanauliza maswali mengi kuhusu ni kwa namna gani na wakati gani mahusiano yako yamefikia katika hatua ya ndoa”Aliongea Rich kwa bashasha sana na kumfanya Edna kutabasamu.
“So Rich mmewajibu nini?”
“We didn’t answer anything , I am also in a position of asking questions but rather than getting answers each of us differently , we agreed on something”
“Hatukujibu chochote , hata mimi pia ninapaswa kuuliza maswali lakini licha ya kupata majibu kila mmoja wetu tofauti tuliamua kukubaliana juu ya jambo moja”Aliongea Rich kwa tabasamu na kumfanya Edna kumwangalia kwa shauku.
“Come on Rich .. What!!”
“They are all coming over , here in Tanzania and you are going to answer our questions while everyone is present including your husband”
“Wote wanakuja Tanzania na utakwenda kujibu maswali yetu , wakati kila mmoja akiwepo ,ikiwemo mume wako”Aliongea Richie huku akionyesha mchecheto kweli , lakini kwa Edna ilikuwa mshangao Zaidi.
Alichokuwa akimaanisha Rich ni kwamba wanafunzi wenzake aliosoma nao , wale waliokuwa na ukaribu nae na kumfahamu ndio watakuja Tanzania , ili kupata majibu yao , Edna alijikuta akiwa ni mwenye wasiwasi kwani alikuwa akijua kabisa ni kipi kinakwenda kuulizwa kwani ashawahi kuhudhuria kwenye mkusanyiko wa pamoja na Alumni wenzake na moja ya maswali wanayouliza ni kama vile , kisi lenu la kwanza lilikuwa lini na ulijisikiaje , Date ya kwanza ilikuwa vipi na ilikuwa wai , Kazi ya Roma na mengine mengi msingi ambayo kwake hayana msingi..
“Kwahio Rich mmekubaliana lini?”
“Baada ya Christimass”Aliongea Rich na kumfanya Edna kutabasamu na hakuwa na namna ya kupinga kwani ni wanafunzi wenzake ambaye alitakiwa kuonana nao.
*********
Upande mwingine wakati hayo yakiendelea , siku hio hio Kizwe mke wa raisi wa Rwanda alikua nchini Tanzania.
Ujio wake ulikuwa ni wa kimya kimya na alionekana alikuwa amekuja kwa kazi binafsi sana , muda wa saa nne kamili alikuwa ndani ya hoteli moja maarufu maeneo ya Masaki, upande wa mgahawani akiongea na mwanaume mmoja hivi wa makamo kati ya miaka hamsini , alievalia suti , mweusi na ilikuwa ni takribani kama nusu saa tokea waanze mazungumzo yao.
“Do you have the file?”Aliuliza Kizwe na alimuuliza mwanaume kwamba je faili analo.
“Yes I do and its verified”Aliongea akimaanisha kwamba analo na amelithibitisha.
“I need to verified it too , I don’t trust people , especially Tanzanian”
“Nahitaji kulithibitisha pia , siamini watu , mathalani mtanzania”Aliongea.
“Perhaps with one of your contacts from Diaspora , We can show you the file but how would you confirm it’s realy , we need someone who knows what happened”
“Labda na mtu unaewasiliana nae kutoka Diaspora , tunaweza kukuonesha faili lakini utawezje kuthibitisha ukweli wake , tunahitaji mtu anefahamu kilichotokea”Aliongea yule mwanaume na kumfanya First Lady kufikiria kidogo.
“Actually he is here”Aliongea akimaanisha kwamba mtu mwenyewe yupo hapa na palepale alitoa simu yake na kutuma ujumbe na ndani ya dakika chache tu , alionekana mwanaume mtanashati sana kijana akiwasogelea.
Unafikiri Kizwe anazungumzia faili gani?, linahusiana nini na kisasi chake kwa Edna