Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 371

Kwa jinsi Edna alivyoongea , hakuna hata mmoja ambaye alimtilia maanani , ni kama vile kila mtu alikata tamaa, huku wafanyakazi hao wakiangaliana , kwani walishindwa kujua maana ya maneno yake ya start now yanamaanisha nini.

“Boss Edna hakuna haja ya kusita sita Zaidi , tunatakiwa kufanya kitu sio kukata tamaa”Aliongea mmoja wao baada ya Edna kurudisha simu chini.

“Naunga mkono hoja , hatuwezi kuangalia kampuni inafeli , nashauri tuuze baadhi ya thamani za kampuni ili tuweze kupata hela ya kupambana na hali , kwassa hakuna mtu anaenunua hisa zetu hata mmoja, muda si mefu tunatangazwa kufilisika”

“Jamani angalieni kule”Aliongea Nasra kwa kupiga kelele na watu wote waligeukia skrini.

“Nini kinatokea , hisa zetu si zilikuwa chini sana , mbona zimepanda glafla”waliongea wote kwa mshangao , kwani ile Candlestick iliokuwa inakaribia chini kabisa ghafla ilibadilika na kuwa ‘bullish na ilifyatuka kama roketi na kupanda thamani juu , yaani kilikutwa ni kitendo cha kupepesa jicho tu soko la hisa lilikuwa juu angani kileleni.

“Inaonekana kuna mtu ananunua hisa zetu kwa pesa nyingi”Alijibu mmoja , lakini wote walitumbulia skrini macho na kati yao ni Nasra na Dorisi tu waliomgeukia na kumwangalia Edna.

“Yote haya yametokea kwa sababu ya simu yako uliopiga muda huu?”Aliuliza Nasra huku akimwangalia Edna na wote walimgeukia na kumwangalia wakisubiria jibu.

“Ndio nimewaambia Athena wanunue hisa zote kwa uharaka sana”Aliongea Edna

“Lakini boss Edna hata kama utumie mabilioni ya hela kununua hisa zote ,thamani itarudi chini ndani ya muda mfupi tu kutokana na image ya kampuni”Aliongea mmoja wao

Wakati huo Roma ambaye alikuwa amekaa pembeni akiwa ameinamisha kichwa kwenye kiti kwa uchomvu aliwaangalia wafanyakazi hao na kisha aliegamia kwenye kiti chake na kuendeleza kuuchapa usingizi.

Edna aliwaangalia wafanyakazi wake waliokuwa wakitaka majibu na hakuongea chochote Zaidi ya kuchukua bahasha iliokuwa pembeni yake na kisha akaisogeza katikati ya meza kwa kuirusha.

Jambo moja la kukumbuka ni kwamba katika nyaraka ambazo zilivuja mtandaoni moja wapo ilikuwa ni ile ya mnada wa miradi ya Adani , yaani katika taarifa iliovuja ilionyesha ni kiasi gani ambacho Edna aliwakilisha kwa kampuni ya adani kama ofa ya kununua miradi yao.

“Hio ni nyaraka ya kufanikiwa kwa zabuni”Aliongea Edna.

“Zabuni , kushinda kwa zabuni upande upi?”Aliuliza mmoja kwa kuchanganyikiwa , lakini wote walitoa karatasi zilizokuwa kwenye bahasha na kuanza kuzisoma na baadhi yao waliosoma walijikuta wakishangaa.

“Boss Edna unamaanisha tumeshinda zabuni ya mnada wa miradi ya Adani?”Aliuliza kwa mshangao.

“Wewe nae unauliza maswali ya nini , si usome kilichoandika au hujui kusoma?”Alifoka mwingine aliekuwa kwenye kona ambaye hajasoma.

“Siamini kma hii ni ya kweli , mnada si unafanyika mchana?”

“Wewe unae kinachokushinda hapo nini , hujui kutofautisha nyaraka orijino na feki?”Aliongea mmoja wao aliesoma baada ya kuona nyaraka hio ni ya kweli , walikuwa wameshinda.

“Lakini hili limetokeaje , kwanini washindani wetu wakatuachia tukashinda wakati mbinu zotu zote zilikuwa mtandaoni?”Aliongea mmoja wapo na kufanya swali lake liwe la mantiki .ni kweli kwasababu kama wameshinda imekuwaje , kwani sio kampuni ya Vexto tu ambayo iliokuwa ikihusika katika kupata mradi wa Adani, hivyo kuvuja kwa taarifa mtandaoni inamaana ilikuwa ushindi kwao kwani mbinu zote za namna Vexto wangefanya kushinda zilikuwa hadharani , sasa kama ni kushinda walishindaje.

Dorisi , Benadetha na Nasra wote walimwangalia mwanamke Kauzi Edna aliekaa kwenye kiti cha kibosi wakitaka majibu kutoka kwake , je wameshindaje zabuni hio kirahisi hivyo , tena kabla ya mnada wenyewe.

Roma alimwangalia mke wake kwa umakini na alijikuta akiridhishwa na utulivu wake na alijikuta mwenyewe akishindwa kujua anajisikiaje muda huo.

“Benadetha kwanzia sasa nataka utangaze kwenye vyombo vyote vya Habari juu ya kampuni yetu kufanikiwa kuupata mradi wa Adani kutoka kigamboni . ukimaliza kazi hio pamoja na timu yako nenda kwenye ofisi yangu na kafungue sanduku la usalama wa nyaraka kwa kutumia nywira unayoijua sijawahi kuibadilisha”Aliongea na Benadetha aliitikia na kimya kimya kunyanyuka na kuondoka kurudi kwenye idara yake.

******

Upande mwingine huko Bagamoyo Ernest Kamwe alikuwa eneo la sebuleni asubuhi hio akiwa pamoja na Monica , licha ya Monica kuwa na hasira , lakini macho yake yalikuwa katika Tv.

“Monica muangalie boss wako anavyojitahidi kununua hisa za kampuni yake , anafikiri ni lipi jema litatokea kwa kufanya hivyo?”Aliongea huku akitabasamu kifedhuli.

Upande wa Monica alionekana pia kujikatia tamaa, ijapokuwa alikuwa akimwamini Edna , lakini kwa hali iliokuwa ikiendelea aliamini ni Mungu tu anaweza kumsaidia na hali inayoendelea ipo nje ya uwezo wake.

Muda uleule walijikuta wakishangaa huku Ernest akiwa kwenye mshangao Zaidi na hio ni baada ya Habari kutangaza kampuni ya Vexto imefanikiwa kushinda mnada wa ununuzi wa miradi yote mitatu ya kampuni ya Adani ndani ya jiji la Dar.

Ilikuwa ni Habari kubwa sana kwa Ernest , pamoja na kwa kampuni ya Vexto nani angeweza kutarajia kampuni ambayo inadidimia kuweza kufanikiwa kushinda mnada huo.

Miradi ya Adani ndio miradi ambayo ilikuwa ikiangaziwa kwa kipindi kirefu sana ndani ya Tanzania , miradi hii ilikuwa ni ya mahoteli ya kisasa kabisa na sehemu za kupumzikia ndani ya jiji la dar , ambayo kama ikikamilika basi ni kama useme ni kama baadhi ya miradi mikubwa ambayo imetekelezwa nchini UAE ndani ya Dubai.

Ukisikia Tourism recreation business basi ndio ninacho zugumzia , miaka kadhaa nyuma , kipindi cha uongozi wa raisi Kigombola kampuni ya Adani kutoka India ilipewa maeneno matatu ndani ya jiji la Dar kwa ajili ya mageuzi ya maeneo hayo kuwa sehemu za kitalii Zaidi , sehemu zenyewe ilikuwa ni Kigamboni , kisiwani Mbudya pamoja na eneo la Mbweni, sasa baada ya miaka mingi ya kuzorota kwa kampuni ya Adani katika utekelezaji huo hatimae mwaka 2022 wakatangaza kuuza miradi yote pamoja na maeneo yote ambayo walipewa kwa ajili ya miradi hio kwa kampuni yoyote ikayokuwa na uwezo wa kuikamilisha , haikueleweka sababu ni nini kwani kampuni ya Adani haikuweka wazi.

Sasa kutokana na maeneo hayo kuwa sehemu nzuri sana ndani ya jiji la Dar kampuni nyingi zilikuwa zikishindana kupata miradi hio kwa namna yoyote ile , kwani ndio ambayo ingekuwa kama nembo ya Tanzania , yaani nikama useme Marina Bay ilivyokuwa nembo ya utalii wa jiji la Singapore basi ndio miradi hii ya Adani ilivyokuwa inategemewa hivyo , na kampuni ambazo zilikuwa kipaumbele kupata miradi hio ni kampuni ya mwanamama Neema Luwazo.

Sasa jambo ambalo lilifanya kampuni ndani ya Tanzania kuwa macho na mradi huo ni mara baada ya raisi Senga kufanya maboresho kwa kuzuia kampuni za nje ya nchi kuchukua mradi huo na kutangaza kwamba anaruhusu kampuni za ndani pekee kupewa kipaumbele , alifanya hayo kwa ajili ya kuinua uchumi wa Tanzania., kwa kuwafanya wazawa ndio wachukue hatamu ya kulipendezesha jiji, sasa ulikuwa ni mradi wenye thamani ya pesa nyingi sana kutokana na ukubwa wake , ulikuwa na gharama ya dola bilioni nane kama utakamilishwa na ndio mradi mkubwa ambayo unatarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza ndani ya Afrika mashariki yote pengine Afrika , ambao ulikuwa ukiendeshwa na sekta binafsi.

Sasa Vexto kufanikuwa kushinda mradi huo ilikuwa ni Habari njema mno kwa mwanauchumi yoyote yule na kwa ustawi wa kampuni pamoja na taifa.

Monica aliekuwa pembeni , alijikuta tumaini lake likichipuka , hio ndio Habari njema kwa siku zote tatu kutoka kwa kampuni hio .

Lakini sasa lisaa limoja wakati Habari hio haijaisha utamu wake , taarifa nyingine ilitolewa katika vyombo vya Habari kwamba kampuni ya Vexto imeitisha mkutano wa waandishi wa Habari na kuelezea juu ya nyaraka zilizovuja mtandaoni kwamba ni feki.

Sasa Habari hio ilishitua watu wote wnaaofatilia maswala ya uchimi ndani ya Tanzania na dunia kwa ujumla , hakuna aliemini kwamba nyaraka zilizokuwa zimevuja zikionekana kuwa halisi kuwa feki.

Glasi aliokuwa ameshikilia Ernest ilidondoka chini na kupasuka vipande vipande na kushindwa kuongea neno lolote.

Na muda huo huo simu yake ilianza kuita na alivyoiangalia kwa namna ya kutetemeka mikono aliona ni Kizwe ndio anampigia na alijikuta akipokgea kinyonge.

“What is happening you bloody idiot?”Aliuliza kwa kufoka na sauti yake ilikuwa kali mpaka Monica kuweza kusikia

“Madam naomba upunguze jaziba , nina uhakika Edna anafanya maigizo tu , nyaraka nilizovujisha ni zenyewe”

“Ombea maneno yako yawe ya kweli , bado nipo Tanzania usiniache nirudi Rwanda nikiwa sipo kwenye mudi nzuri”Aliongea kwa hasira na kisha akakata simu.

Upande mwingine ndani ya kampuni . Benadetha alifanya kama alivyoagizwa na ndani ya madakika kadhaa tu aliweza kurudi akiwa na furushi la nyaraka alizotoa kwenye kisanduku cha sualama kutoka ofisini kwa Edna.

Kwa muonekano wa Benadetha ni kama kuna jambo zuri kwenye nyaraka alizoshikilia .

“Boss everything you requested is here”Aliongea na kisha akamkabidhi Edna zile nyaraka.

“Vizuri na asante”Aliongea na kisha akaziinua juu akiwa amesimama.

“Here are all the original documents of the allegedly stolen information. Please, take a look.”

“Hizi ni nyaraka halisi ambazo zinahusishwa kuibiwa , mnaweza kuangalia”Aliongea Edna kisha akamsogezea Nasra aliekuwa karibu yake ili kuwapa nafasi wafanyakazi kuangalia.

Kila mmoja alishangazwa na taarifa hio, ni kama hawakumuelewa Edna walijiuliza anamaanisha nini kusema taarrifa hizo ndio halisi zinazohusishwa kuibiwa.

Kila mmoja alipoangalia hizo nyaraka walijikuta wakijawa na mshangao , ni kweli kwamba nyaraka za mtandaoni zilizovuja zilikuwa zikifanana kwakiasi kikubwa na hizo , lakini hizo ambazo zipo zilikuwa zikitofautiana kwa asilimia kadhaa na zilizopo hapo , yaani kwa maneno marahisi kuelezea ni kwamba zilizopo mtandaoni zilibadilishwa baadhi ya mambo.

Sasa wafanyakazi waliweza kuelewa nyaraka hizo kutokana na kwamba wao wenyewe walihusika katika vikao ambavyo vilihusika katika utegenezaji wa nyaraka hizo , kwahio ni rahisi kwa wao kuthibitisha ukweli kwamba za mtandaoni ni feki na hizo ni halisi.

Edna aliwaacha wafanyakazi hao wakijadiliana wao wenyewe kwa muda kama wadakika kumi na kisha aliwaomba utulivu.

“Naomba usikivu wenu kuanzia sasa , mpaka hapo nadhani kila mtu ana uhakika wa nyaraka zilizovuja ni feki, kwanzia sasa namtangaza Nasra Rakimu kuwa CEO msaidizi wa Vexto International”Aliongea Edna na watu wote walitoa macho.

Unaweza ukashangaa hapo kwanini Edna alitoa mapendekezo hayo bila kuwa na kikao cha bodi ya wakurugenzi , ukweli ni kwamba kitendo cha kununua hisa zote kwa pamoja zilimrudishia umiliki wa asilimia tisini wa kampuni , yaani zile hisa ambazo wahisani wengine walizitupa sokoni, yeye alizinunua kwa kusaidiwa na Athena , hivyo maamuzi yake ndio sheria ndani ya kampuni na hakuhitaji kikao cha bodi kufanya Sanctioning ya kumchagua msaidizi wake.

Wakati watu wakishangaa akiwemo Nasra mwenyewe , aliendelea kuongea.

“Nasra majukumu yako kama CEO msaidizi wa kampuni yanaanza mara moja , nakupa kazi mpaka sasa ya Kwenda kuitisha mkutano na waandishi wa Habari na kukanusha nyaraka zilizopo mtandaoni kuwa feki , kazi hio unajua jinsi ya kuifanya”Aliongea na kumnfanya Nasra aliekuwa kwenye mshituko wa mshangao kuitikia.

“I’m not too convinced with my ability to handle the media so I need you to go in my place. As the company’s representative and vice president, you are more than worthy to stand in my place.”

“Siamini uwezo wangu wa kuongea na vyombo vya Habari hivyo naomba ufanye hivyo kwa niamba yangu kama muwakilishi wangu na CEO msaidizi , una kila thamani ya kusimama badala yangu”Aliongea na kisha kuwageukia wengine.

“Najua wote hapa mnaungua na maswali mengi ni kwa namna gani hili limeweza kutokea , lakini hayo ni maelezo ya muda mwingine , nina wahitaji wote kurudi kwenye idara zenu husika na kuwapa taarifa wafanyakazi wote juu ya hali ya sasa ya kampuni , wakati huo huo mkiendelea na operesheni nyingine , chukueni mapendekezo yote yaliopo kwenye hizi nyaraka na mkafanye kama inavyotakiwa , Benadetha kwa upande wako nataka uwe makini na washirika wetu wa kibiashara , lakini pia matawi yetu yote ya kimataifa , hakikisha unatoa maelezo ya kutosha na kama itahitajika sana unaweza kuwapa faida kidogo ili kuwatuliza”.

Wote kwa pamoja waliitikia kwa msisimko mkubwa huku wakimwangalia Edna kwa kuguswa sana na utawala wake , lakini pia alivyokuwa vyema sana katika kuongoza kampuni.

Hakuna ambaye alikuwa na uhakika ni kwa namna gani kila kitu kimekuwa hivyo , lakini kwa muda huo waliona wakatimize majukumu yao na maelezo hayo yatakua wakati mwingine.

Baada ya wote kwa pamoja kutoka , sasa aliebakia ndani ya ukumbi huo ni Edna na Roma peke yao na Roma alisimamam na kumsogelea Edna.

“Huu mpango ulianza lini?”Aliuliza Roma akiwa na sura iliojaa usiriasi

“Hili sio jambo muhimu kwa sasa Roma , cha kufurahia kwasasa ni kwamba tumeweza kushinda hii hali salama salimini”

“Najua ilikuwa ngumu na hatari , lakini uliwadanganya wafanyakazi wote na wakaingia mtegoni lakini hata mimi pia umenitega na kuniingiza mtegoni vilevile”

“Roma naomba usinifokee , nilichokifanya hapa ni kutimiza majukumu yangu”

“Ooh! Hakika unashangaza sana Miss Edna , unatakiwa kupewa tuzo ya Oscar lakini hebu nielezee huu mpango ulianza lini na ulianza anzaje, ninachotaka hapa ni kukamilisha shauku yangu , that is all my magnificient wife”Aliongea Roma. Akihiraji maelezo yote , juu ya mpango ambao Edna amefanya mpaka akafanikiwa kudanganya kampuni na ulimwengu kama kampuni yake inafilisika.

Ukumbuke ni mara ya pili sasa Roma anaingia kwenye mtego wa Edna , mtego wa kwanza ulikuwa wa Japani na kampuni ya Yamakuza na mtego wa pili ndio huu wa kuonyesha dunia kwamba kampini yake inafilisika.

Simulizi bado , mbichi sana.

Unafikiri Edna alivyokuwa Hongkong kwanini aliumwa kichwa kiasi cha kupoteza fahamu,ule ni mwanzo wa nini.

Vipi kuhusu babu yake Lanlan , Master Chi ,je yuko wapi?. Ni kweli kafa kama alivyojitabiria.

Ni mpango gani Athena anamwandalia Dorisi?”

Unafikiri Raheli aliacha nini kwenye Deposit Box , Hatima ya Kizwe na Ernest ni nini
 
SEHEMU YA 372

Edna alimwangalia Roma kwa jinsi alivyokuwa siriasi na swali lake na alijikuta akiamua kumueleza namna ilivyokuwa.

“Nilianza maandalizi mara baada ya kuja kwa Ernest Komwe ndani ya kampuni yangu kama CEO msaidizi”Aliongea Edna na kumfanya Roma kushangaa.

“Nini kilikufanya ukachukua tahadhari , kwa ninavyofahamu Erest alichaguliwa na Tikayi kutoka kampuni ya Yamakuza kuja ndani ya kampuni kwa ajili ya kukupa msaada katika maswala ya malighafi mpya , nini kilikuamsha?”

“Nilijaribu kufatilia taarifa zinazomuhusu Ernest , kwanini kampuni ya Yamakuza ikamchagua mfanyakazi wangu wa tawi la Kenya kuja kuwa msaidizi wangu ,na niligundua Ernest Komwe kabla ya kuwa mfanyakazi wangu kwenye tawi la Kenya alishawahi kufanya kazi na kampuni ya Yamakuza katika kitengo cha masoko tawi la Hongkong ,sikuweza kupata chochote Zaidi niligundua tu kwamba sio Tikayi tu aliehusika katika kumchagua bali ni jopo lote la wakurugenzi wa kampuni ya Yamakuza”

“Jambo lingine ambalo lilinifanya kuwa na wasiwasi ni kitendo cha Ernest kuwa karibu na Monica muda mwingi wakati huo huo akijipendekeza kwa Benadetha , niliamini kuna jambo anajaribu kulikamilisha, kama ulivyosema mwenyewe ndani ya kampuni yetu kuna wanawake warembo sana na Ernest akamchagua Monica , wasiwasi wangu ulianzia hapo”Aliongea Edna

“Lakini ulijuaje anachopanga ni kuiba nyaraka za siri za kampuni?”

“Sikuwahi kufikiria kuhusu wizi wa nyaraka kama unaweza kuwa tatizo kwa kampuni”

“Sasa kama uliona hilo haliwezi kuwa tatizo kwanini ukategeneza huuu mpango kimya kimya?”Aliuliza Roma.

“Unafikiri kwanini nawalipa Athena zaidi ya bilioni kumi kwa mwaka? , sio kwa ajili ya kunisaidia tu kwenye maswala ya kifedha”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa kidogo.

“Kwahio unamaanisha kwamba uliwahusisha Athena kwanzia mwanzo wa mpango huu?”

“Ndio Roma tulijadiliana , niwe tu mkweli kwako kila muda ninapompa kazi Monica ya kutoa copy nyaraka za siri za kampuni huwa nazichakachua kwanza katika vipengele muhimu, na sio kwake tu , kwa wafanyakazi wote huwa nafanya hivyo, nyaraka zote ninazowapatia watunze huwa nimezichakachua na zile halisi nakaa nazo mwenyewe labda tu kuwe na mmoja wao ambaye atakuwa na akili ya kuzihakiki , kwahio hakuna ambaye anajua uhalisi wa nyaraka hizo Zaidi yangu mwenyewe na kama kuna tenda yoyote kabla haijafikishwa kwa wahusika lazima nyaraka hizo zipite kwangu kwanza na zikiletwa ofisini nitazibadilisha na zile halisi na kumpa muhusika kwa ajili ya kuwakilisha , huo ni utaratibu wangu niliokuwa nao tokea nianze kuichukua kampuni”Aliongea Edna.

Ndio maana muda wote yuko bize kumbe anajipa mzigo mkubwa wa kazi namna hio?Aliwaza Roma , aliona kitendo cha Edna kushughulika na kila nyaraka za kila idara ni jambo kubwa sana kwake ndio maana muda wote anakuwa yupo bize.

“Mpaka hapo nadhani unaelewa sasa kwamba nyaraka alizoiba Ernest Komwe nilizifanyia uchakachuzi wa vipenele muhimu na hivyo kuwa feki”Aliongea Edna na kumfanya Roma kushindwa kujizuia kutabasamu aliona Edna alikuwa kweli akistahili nafasi yake ya kuwa CEO ndani ya kampuni kwani kama asingekuwa makini kama hivyo huenda mpaka muda huo angefilisika kweli.

Lakini pia alimuona Edna kama mwanamke ambaye anajua kuigiza sana , kwani siku zote hizo tatu alijifanya kabisa kuguswa na kile kinachoendelea kwenye kampuni , kumbe yote yalikuwa maigizo tu ya kuwashawishi watu kama kweli kampuni ilikuwa ikifilisika.

Roma alijikuta akijiambia anasafari ndefu ya kumfahamu Edna , kwani kama anaweza kumwigizia namna hio na yeye asifahamu hata kidogo ilikuwa ikimaanisha kwamba hakuwa akimfahamu , na alijiambia siku za usoni atachukua tahadhari ili asiingizwe kwenye mtego tena..

Lisaa limoja mbele hatimae Nasra aliweza kuweka kikao na waandishi wa habari na aliweza kuelezea uhalali wa nyaraka walizonazo na zile ambazo zimevuja na ilieleweka kabisa kwamba nyaraka zilizovuja ni feki , Nasra alikuwa vyema sana kwenye kuongea na waandishi wa habari hivyo alijibu kila swali ambalo liliulizwa kwa ufasaha kabisa.

Wafanyabishara wengi ambao walikuwa wakitarajia anguko la kampuni ya Vexto walijikuta wakiwa kwenye hali isio tamithirika kutokana na mabadiliko hayo ya ghafla , kila mmoja alisema cha kwake kuhusu Edna.

Nasra alimalizia kusema licha ya kwamba nyaraka hizo zilizovuja kuwa feki , lakini watamtafuta yoyote aliehusika na uchafuzi huo wa kampuni na kuomba vyombo vya usalama kutoa msaada katika hilo na kisha akahitimisha.

Kutokana na habari hio , hisa za kampuni zilipanda thamani kwa kasi ya kuungua kwa kifuu cha nazi, na zilipita thamani iliokuwepo wiki kadhaa kabla ya kuvuja kwa taarifa na kilichosababisha hisa hizo kupanda zaidi ni kutokana na kwamba zimebaki siku kadhaa malighafi mpya kuingia sokoni , lakini jambo la pili kampuni hio ilishinda mnada wa uendelezaji wa projetki ya miradi ya Adani , lakini wakati huo huo kukana juu ya nyaraka feki ambazo zinasambaa mtadaoni.

Katika hali hio Edna alionekana kufaidika sana , kwanza kabisa utajiri wake ulizidi kupaa juu Zaidi na kuvuka nafasi kumi kutoka sehemu aliokuwewpo mara baada ya kuvuja kwa nyaraka za siri.

Vyombo vya Habari vya kimataifa ambavyo vilikuwa vikifuatilia swala hilo kwa ukaribu walijikuta wakichambua tukio hilo kiundanni Zaidi huku wakitoa sifa nzuri Kwenda kwa mwanadada Edna , jambo moja ambalo lilimvumisha sana Edna ni juu ya kwamba alikuwa msichana wa umri mdogo sana kuwa na umiliki wa pesa nyingi sana , tena kutoka kwa taifa linaloendelea kama Tanzania , ilikuwa ni ngumu sana kwa kampuni kuweza kuwa kubwa ikiwa ndani ya mataifa madogo na yanayoendelea ndani ya Afrika na wengi wamezoea kuona makampuni makubwa yakitokea ndani ya nchi kama Afrika ya kusini, Nigeria na baadhi ya mabara ya Asia , Ulaya na Ametrika.

Wale mabwana ambao waliuza hisa zao kwa bei ya hasara kwasababu ya mhemko walijikuta wakipumulia mashine, kila mmoja alijilaumu kwa maamuzi yao , huku wengine wakienda mbali kumtukana kabisa Edna , kwani ndio yeye aliewafanya kuuza hiza zao kwa kuwaingiza kwenye mtego wa kuaminisha uma kampuni ilikuwa ikifilisika kumbe sio kweli, vinyongo na chuki zidi ya Edna viliongezeka.

FROM CNN ECONOMIC NEWS: “The young female entrepreneur from Tanzania who had led her company to cruise through seemingly inevitable demise only to achieve new heights had now once again displayed the unthinkable”

KUTOKA CNN TAARIFA ZA UCHUMI: ‘Mjasiriamali mdogo wa kike kutoka Tanzania ambaye ameongoza kampuni yake kupitia changamoto mbili zisizoweza kuepukika ili kufikia mafanikio mapya , sasa tena amedhihirisha jambo lisilowezekana”

Gazeti pia la Times Magazine kutoka Marekani lilimwingiza moja kwa moja Edna katika tatu bora ya washiriki wa mwaka kutoka Afrika walionyesha ukomavu katika biashara.

Lakini wahenga pia wanasema , kwa kila penye hadithi nzuri ya mafanikio ya mshindi hapakosi alieshindwa , basi hiki ndio kilichokuwa kikiendelea upande mwingine nje ya jiji la Dar huko Bagamoyo mkoa wa Pwani kwenye jumba la kifahari..

Ernest Komwe kila chaneli anayobadilisha aliona sifa kedekede akipewa mwanamke Edna kwa ukomavu wake na talanta yake katika maswala ya biashara.

“Hii haiwezekani , nasema hili haliwezekani kutokea”Aliongea huku macho yake yakikosa kabisa kuamini kile ambacho anakiona na alijikuta miguu yake ikikosa nguvu na kupiga magoti kwenye kapeti akiwa kama mtu aliefiwa kwa huzuni.

Monica aliekuwa kwenye sofa alijikuta chozi likimtoka , ijapokuwa mwanzoni alikuwa akishabikia Ernest ashindwe katika mpango wake ovu zidi ya bosi wake Edna , lakini kumuona mwanaume anaempenda kuwa kwenye majonzi ya aina hio alijikuta moyo ukimuuma mno.

“Ernest naomba upunguzwe jazba , kila kitu kinakwenda kuwa sawa , unanitisha mwenzio…”Aliongea na kumfanya Ernest kumgeukia na kumsogelea na kisha akamshika miguu.

“Hapana, Monica usiniambie ulikuwa ukijua hili , Yule mchawi alikuwa akinitumia tokea mwanzo , amenifanya chombo cha kujipatia hela nyingi na sasa ananitupa bila chochote”Aliongea Ernest , hakika alikuwa akitia huruma , kule kujiamini kote kulikuwa kumemwishia na Monica alishindwa kujizuia hakuwa na cha kumwambia Zaidi ya kumuonyeshea machozi.

“Acha kujifanyisha kulia lia , lazima alijua mipango yangu tokea mwanzo kutokana na wewe mwanamke mjinga?”Aliongea huku akianza kumbadilikia Monica na kumchapa kibao ambacho kilimsababishia kudondoka chini.

Sasa baada ya kumpiga kibao alijikuta akili zake ni kama zinamkaa sawa na kukumbuka Monica alikuwa na kiumbe kilichokuwa tumboni kwake.

“Monica naomba unisamehe sikudhamiria…” Kabla hajamaliza mlango ulifunguliwa na teke na alionekana Kizwe akiingia hapo ndani kwa haraka haraka huku viatu vikikanyaga kwenye tiles na kusababisha makelele , alionekana kuwa na hasira kweli kwani hata tembea yake haikuwa ile ya madaha tena.

“Wewe mjinga kama nitakupa pongezi basi nitakufananisha na ng’ombe , unapata wapi ujasiri wa kuanza kumlilia mwanamke sasa hivi, mjinga kabisa wewe”Aliongea huku akitweta.

“Hahaha.. unachosema ni sahihi , mimi ni mjinga ndio”Aliongea Ernest huku kule kumuogopa Kizwe kumuishia kabisa.

“Unajifanya mjanja , umeharibu mipango yangu yote , nafikiri huu ulimwengu haustahili mtu mjinga kama wewe kundelea kuishi”Aliongea na palepale alitoa bastora kwenye mkoba wake na kumnyooshea Ernest.

Sasa Ernest ni kama akili yake ilimkaa sawa na kuelewa kwamba hali haikuwa nzuri kwa upande wake , kwani bosi wake alikuwa na siraha na alikuwa amemnyooshea.

Upande mwingine kama nusu saa iliopita, ndani ya kampiuni, Edna alionekana ndani ya ofisi yake akiwa na Roma , huku akiwa ameshikilia vijikeki flani hivi vidogo vya mviringo akiwa anakula taratibu taratibu na kushushia na maji , vikeki hivyo alinunuliwa na Roma asubuhi.

Wote kwa pamoja walikuwa wakiangalia habari kwenye Tv kwa namna ambavyo waandishi wa habari walikuwa wakiulizia kuhusu habari za Edna , kwani hakuonekana mubashara katika mkutano na waandishi wa habari , hivyo walikuwa wakiulizia yuko wapi kwani walihitaji kumuona shujaa mwenywe.

Wakati habati hio ikiendelea , Roma aliekuwa amekaa pembeni aliweza kupokea simu kutoka kwa Adeline

“Your Majest Pluto , Madam Kizwe has stopped by the mansion twice it would seem like the condition is pretty much clear now , should we take action?”

“Mfalme Pluto , Madam Kizwe ameonekana akifika ndani ya jumba la ifahari mara mbli na kila kitu kipo wazi mpaka sasa , vipi tunaweza kuchukua hatua?”Aliongea Adeline upande wa pili.

“Msifanye chochote kwa sasa , nadhani ni muda muafaka wa mimi mwenyewe kuingilia swala hilo, nakuja muda si mrefu”Aliongea Roma na baada ya Adeline kuitikia alikata simu na kisha akamgeukia Edna.

“Kuna sehemu naelekea kwa sasa , usinisubiri kama nitachelewa unaweza Kwenda nyumbani peke yako”Aliongea Roma

“Najua unaenda kukutana na Ernest nitaomba uache polisi wamchukue na kama utamkuta Monica usimguse wala kumfanyia vibaya hahusiki katika hili”Aliongea Edna

“Una uhakika hutaki kuongozana na mimi?”

“Nakuamini na umeniahidi kwamba huwezi kuua hivyo sina wasiwasi”Aliongea Edna na kumfanya Roma kutabasamu na kisha akachukua kijikeki kimoja kilichokuwa kwenye boksi na kupeleka mdomoni na kisha kuondoka na kumfanya Edna kuangalia boksi lenye vijikeki vyake na kuhuzunika.

Kwa maelezo ya Bi Wema Edna alikuwa akipenda sana vijikeki hivyo flani ambavyo vinatengenezwa na kufungwa kwenye vikaratasi flani hivi , sasa wakati akiwa mtoto ndio alikuwa akipendelea kula , lakini tabia yake haikuishia hapo tu aliendelea kula hata alipokuwa ukubwani kwasababu alikuwa akivipenda , sasa Roma baada ya asubuhi kuambiwa siri hio na Bi Wema alienda kuvikusanya madukani na kumpelekea huku akiongezea na keki za karanga ambazo pia Edna alikuwa akipenda.

Lakini sasa dakika chache tu kupita baada ya Roma kutoka mlango wa ofisi yake uligongwa na Edna haraka haraka alificha kiboksi chake na kumruhusu mtu huyo kuingia.

“Boss Edna there is parcel here for you”Aliongea mwanadada mmoja alieshikilia bahasha ya khaki , mwanadada huyo alikuwa ni msaidizi wa muda wa Edna akikaimu nafasi ya Monica.

“Naomba uniletee”Aliongea na mwanadada yule alimfikishia kwenye meza yake na kuweka chini na kisha alitoka ofisini na kufunga mlango , na Edna alitoa kiboksi kilichojaa vikeki na kuendelea kula.

Hakujali sana kuhusu bahasha iliomfikia muda huo , kwani ilikuwa kawaida sana kupokea bahasha za khaki za namna hio katika kazi yake hio ya ubosi wa kampuni kubwa ya Vexto hivyo aliachana nayo kwanza.

Baada ya kama dakika kumi kupita kumaliza vijikeki vyake , alijifuta mikono yake na Tissue na kisha alichukua ile bashasha na kufungua ndani kuangalia ni kitu gani kimeletwa ndani yake.

Edna baada tu ya kutoa bahasha ile alikutana na picha kwanza ambayo kwa haraka haraka ilionekana kuwa ya zamani sana , ilikuwa ni ya mwanaume na mwanamke waliovalia mavazi flani maupe na mekundu, picha hio hakuielewa hivyo alihamia kwenye karatasi zilizokuwa ndani yake na alianza kuzisoma moja moja na kadri alivyokuwa akiendelea kuzisoma ndio macho yake yalivyojaa mshangao usiokuwa na kifani , huku mikono yake ikitetemeka.

Upande wa huku Bagamoyo Monica baada ya kuona mwanamke aliengia hapo kuwanyooshea bastora alianza kuogopa mno kiasi cha kutetemeka , hakuhitaji elimu kubwa kuelewa kinachoendelea , alijua mtu huyo ndio aliekuwa akishirikiana na Ernest kuangamiza kampuni ya Vexto pamoja na kumfilisi Edna.

“Madam Kizwe naomba usituue tafadhari”Aliongea Ernest , huku akimzibia Monica kwa mbele.

“Sina sababu ya kukuacha hai Ernest , nilikupa nafasi adhimu kabisa ya kurudisha kilichokuwa cha familia yako , lakini ukaipoteza na ukawa ‘ Stepping stone’ kwa mafanikio Zaidi ya Edna , wewe ni mjinga na mjinga kama wewe huwezi kuendelea kuwa hai”Aliongea huku akionyesha dhamira ya kumuua Ernest na alitoa bastora ile kutoka mfumo wa usalama na kuweka mfumo wa kulipua.

“Naomba usiniue , nina siri kubwa ambayo naifahamu kama utaniacha nikuelezee hio siri hakika wazo lako la kuniua utaliacha mara moja”Aliongea Ernest.

“Hahaha… unasiri gani wewe , unatumia ujanja kuvuta muda , nakuambia hakuna mtu ambaye anaweza kuja hapa ndani na kukuokoa acha kujidanganya”Aliongea Kizwe kwa sura isiokuwa na huruma kweli.

“Nipo serious Madam , naomba uniruhusu ni kuambie siri hio”Aliongea huku akisimama vizuri na Kizwe aliona kuna usiriasi kwenye macho ya Ernest.

“Niambie ni siri gani ambayo unaifahamu?, usijifanye mjanja nataka uniambie hapa hapa ni siri gani ambayo itanifanya nighairishe kukuua”

“Naomba nikunong’oneze”Aliongea Ernest na kumfanya Kizwe kutabasamu.

“Usije ukajifanya kuniwekea mtego maana kwa vyovyote vile hautoniweza, mimi ni mwanajeshi”Aliongea Kizwe.

Ni kweli Kizwe alikuwa ni mwanajeshi na waliweza kukutana na Raisi Jeremy wakati wakiwa kwenye harakazi za kuikomboa Rwanda, kipindi cha miaka hio ya machafuko na ndio mapenzi yao yalipanzia mpaka kufunga ndoa.

Kizwe alimpa ishara Ernest kumsogelea na kumwambia alichokusudia ambacho anakiita siri na Ernest bila hiyana alielezea kila kitu na kumfanya Kizwe kushangaa.

“Hii taarifa ni ya kweli?”

“Ndio hio taarifa ni ya kweli na ikifahamika hadharani itakuwa kashfa kubwa kwa Afande Kweka”Aliongea na kumfanya Kizwe kutabasamu.

“Unataka nini kutoka kwangu baada ya kuniambia hii siri?”

“Nataka nirudi nchini Marekani kuendelea na Maisha yangu mimi na mpenzi wangu, ni mjamzito na siwezi kumuacha Tanzania”Aliongea na kumfanya Kizwe kutabasamu kidharau.

“Hautaki tena kampuni kutoka kwa dada yako Edna?”

“Kwasasa ninachohitaji ni kutulia na kujipanga upya , mwanangu akizaliwa nitarudi kwa mara nyingine kwa ajili ya kupata kilichohaki yangu, Edna ni mtoto wa nje ya familia na hastahili kuendelea kuongoza kampuni”Aliongea na kumfanya Kizwe kufikiria lakini kabla hajajibu chochote mara nyuma yao alitokea mtu, huyu mtu hakuwa mwingine bali ni Roma na kwa inavyoonekana Roma hakutumia usafiri kufika hapo ndani bali alisafiri kichawi.

“Mrs President ni mara ya pili tunaonana sasa”Aliongea Roma na kumfanya Kizwe kugeuka nyuma yake na kumwangalia mwanaume huyo na ni kweli ni mara yao ya pili kuonana , mara ya kwanza ilikuwani nyumbani kwa Tajiri Azizi.
 
SEHEMU YA 373.
“Ooh! Jamani , sikutegemea kama utaifahamu hii sehemu mapema mno kuliko nilivyotarajia”Aliongea Kizwe huku akimwangalia Roma kwa sura iliojaa kejeli.
Ernest mara baada ya kumuona Roma , lakini pia kuona kwamba Kizwe hana mpango wa kumuua tena , alikimbilia na Kwenda kujikusanya kwenye kona ndani ya eneo hilo la sebuleni akimwacha ‘First Lady’ kuendelea na Roma.
Roma alijisogeza mpaka katikati, huku akimwangalia Ernest aliejikusanya kwenye kona na alitabasamu kifedhuli
“Unajificha , unafikiri kwa ulioyafanya utaachwa salama , nimemuahidi Edna sitokuua , lakini nitapenda wewe mwenyewe kujipeleka polisi na kukiri makosa yako”
“Sihitaji huruma za yule mwanamke , ni mchawi kama mama yake tu , kama unaniua fanya hivyo ila siwezi kuishi kwa huruma za adui yangu”Aliongea Ernest.
“Haha.. unaona ulivyomnafiki , nilikusikia kabisa ukimuomba huyu mwanamke asikuue, ana utofauti gani na adui yako, Una radhi kufa kuliko kukubari huruma za Edna?”Aliongea Roma akiuliza na Kizwe alimwangalia Roma na kucheka.
“Nadhani hata wewe haufahamu kilichotokea miaka kadhaa iliopita , je unafahamu ni kitendo gani mama mkwe wako Raheli alifanya?”
“Unamaanisha nini?”Aliuliza Roma kwa mshangao.
Katika faili ambalo Roma aliweza kulipokea kutoka kwa The Eagles lilielezea kwamba Edna na Ernest ni kitu na binadamu yake , Ernest na familia yake wanaishi nje ya nchi.
Miaka kadhaa nyuma Afande generali wa jeshi , Bwama Kingu ambaye ndio baba yake Afande Kweka alikuwa akiwapa sapoti famiia ya Kayage ambayo kipindi hicho ilikuwa na makazi yake huko Manyara, kwa maana nyepesi ni kwamba Afande Kingu na Afande Kayage walikuwa ni marafiki sana ambao walikuwa wakisaidiana kwenye mambo mengi.
Kwahio basi Ernest jina lake halisi sio Ernest bali ni Swalehe Karim Kayage , hivyo hivyo Raheli ambaye ni mama yake na Edna anafahamika kwa jina kamili la Raheli Elibariki Kayage , kwa maana hio Karimu baba yake na Ernest ni ndugu na Elibariki baba yake na Raheli , huyu Elibariki na Karimu baba yao ni Afande Kayage.
Kwahio ni rahisi kusema kwamba urafiki uliokuwepo kati ya jenerali wa jeshi Afande Kingu na Kanali Kayage unaifanya familia hio kuwa na urafiki ulioanzia zamani.
Hio ni taarifa tu iliotolewa na The Eagles Kwenda kwa Roma , taarifa ambayo inamfanya Ernest na Edna kuwa na udungu kwa upande wa Mama.
Kizwe mara baada ya kuona Roma hakuwa na uelewa wowote wa kile kilichotokea kwa familia ya Ernest alikaa kimapozi huku akicheza na bastora yake na kukunja nne kwenye sofa.
“Kwa sababu hauna uelewa wowote kuhusu kilichotokea miaka iliopita basi nadhani napaswa angalau kukuelezea”
“Hivi unajua ni nani alieanzisha kampuni ya Vexto?”Aliuliza Kizwe akimwangalia Roma.
“Unamaanisha kwamba sio Bibi yake na Edna?”Aliuliza Roma kwa mshangao.
“Hapana”Alijibu Kizwe na palepale ni kama Ernest na yeye alipata nguvu kwani alisimama.
“Kampuni ya Vexto ni ya kwetu , ilianzishwa na familia yetu ya Kayage”Aliongea Ernest na kumfanya Roma kushangaa Zaidi.
Kilichomfanya Roma kushangaa ni kwamba alichojua kutoka kwa maelezo ya Bi Wema ni kwamba kampuni ya Vexto ilianzishwa na Mariaum bibi yake Edna na kutokana na kwamba Adebayo alikuwa hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba basi Raheli alichukuliwa kama mke wakati akiwa mjamzito kwa ajili ya kumsitiri Adebayo na siri ya ugonjwa wake huku wakiandikishiana mkataba wa mtoto atakaezaliwa kuwa mtoto wa Adebayo na ndio atakuwa mrithi wa kampuni ya Vexto , ambaye sasa ni Edna, Sasa kama kampuni haikuanzishwa na Marium inamaana kwamba Bi Wema taarifa yake haikuwa sahihi.
“Hakuna mtu yoyote anaweza kuzungumzia mambo yaliopita , hususani kama mambo hayo hataki yafahamike”Aliongea Kizwe .
*******
Familia ya Kayage , ni moja ya familia zilizokuwa za kawaida sana zisizokuwa na jina kubwa ndani ya jamii katika mkoa wa Arusha wilaya ya Manyara(kabla ya Manyara kuwa mkoa 2002) mpaka baada ya kumalizika kwa vita ya Kagera 1979 , ndio familia hio ilivyojipatia jina kubwa na hio ni mara baada ya Mzee Kayage kushiriki katika vita ya Kagera na kuweza kukutana na wanajeshi wenye vyeo vikubwa ,akiwemo Afande Kingu ambaye alikuwa akiongoza Kikosi maalumu kama mwanajeshi mwenye cheo cha lieutenant Genaral enzi hizo.
Taarifa haikuwekwa wazi sana , lakini inasemekana kwamba Kayage alimuokoa Afande Kingu katika shambulio la risasi ambayo halikutemgemewa kutoka kwa mateka wa vita hivyo waliokuwa chini ya Iddi Amini kwa kumkinga na kuruhusu risasi kumpiga kwenye bega la mkono wa kushoto.
Sasa kitendo Afande Kayage alichokifanya kwa ajili ya kumlinda Afande Kingu kilikuwa cha kishujaa sana kilichosifiwa na wanajeshi wengi , lakini kubwa Zaidi Kayage aliweza kufanya jambo kubwa kwa Afande Kingu na kuanzia hapo ndipo alipotambulika na kumfanya Afande kingu kuwa karibu na familia ya Mzee Kayage.
Miaka michache baadae , yaani baada ya matokeo ya vita , uchumi wa Tanzania uliyumba sana kutokana na madhara yaliosababishwa na vita na hapo ndipo raisi Nyerere alipoanza ubinafsishaji wa baadhi ya viwanda vilivyokuwa chini ya serikali , kipindi hicho ilikuwa ni miaka ya themanini, katika watu ambao walipata koneksheni ya kuingizwa kwenye biashara ni familia hio ya Kayage , kwani kwa msaada wa Afande Kingu waliweza kupata moja ya kiwanda kilichokuwa kipo Iringa , ilikuwa ni kama fadhila aliofanya Afande Kingu Kwenda kwa familia ya Kayage.
Sasa kwanzia hapo uchumi wa familia ya Kayage uliinuka kwa kiasi kikubwa sana kiasi kwamba walianzisha biashara ndani ya jiji la Dar es salaam na baada ya biashara kukua kwa kiasi kikubwa waliweza kusajili kampuni kwa jina la Vexto.
Moja ya wafanyakazi walioajiriwa ndani ya kampuni hio katika miaka ya tisini ni Marium, .moja ya sababu ya Marium kupata nafasi katika kampuni ya Vexto ni kutokana na elimu yake alioweza kuipata nje ya nchi.
Baada ya kifo cha Afande Kingu mtoto wake Camilius Kweka Kingu aliweza kuchukua hatamu ya kuendeleza urithi wake ndani ya familia na inasemekana kuanzia hapo ndipo shida ilipoanzia hususani miaka miwili mbele ya kifo cha Afande Kayage, sasa taarifa hazikuwekwa wazi ila ilisemekana mtoto wa Mzee Kayage yaani Koplo Karimu Kayage ambaye alikuwa mwanajeshi kama baba yake aliasi jeshi la Tanzania kwa kushirikiana na maadui kutoka nchi ya Congo na hivyo ndio ikawa anguko la familia ya Kayage, kwanza serikali ilitaifisha baadhi ya mali za familia hio huku upande wa Karimu akikimbilia nchini Congo ambako ilisemekana tayari alikuwa na mtoto wa kiume, baadae ilifahamika alikimbilia Marekani na Maisha mapya yalianzia huko na hata kuzaliwa kwa mjukuu wake Ernest ilikuwa ni huko huko Marekani.
Upande wa mtoto wa pili wa Mzee Kayage yaani Elibariki walikuwa ni aina ya Watoto ambao walikuwa na uwezo mdogo sana kiakili hivyo hata mali za familia alishindwa kuzipigania kabisa na mtu pekee aliekuwa akitegemewa kipindi chote uendesha mali alikuwa ni huyu Karim ambaye ilisemekana aliasi jeshi la Tanzania kwa kushirikiana na waasi wa taifa la Congo.
Kipindi hicho hayo yote yanatokea ni miaka ya tisini na kampuni ya Vexto kwa kiasi flani ilikuwa ikifanya vizuri sana kwa msaada wa Marium na alikuwa ndio kiongozi mkuu wa kampuni kutokana na elimu yake, hivyo baada ya kusambaratika kwa familia ya Kayage na yeye hakuzubaa alichukua mwanya huo kujimilikisha baadhi ya mali za familia kwa msaada wa familia ya Afande Kweka na ya Afande Athumani.
Mariuam alijiingiza kwenye mapenzi na Afande Athumbani kipindi cha nyuma kidogo kwa maslahi yake ya kumiliki mali za Kayage , lakini pia kufuta historia iliokuwa nyuma ya mali hizo.
Elibariki kwa upande wake kipindi hicho tayari alikuwa ashaoa mwanamke wa kabila la wairaq kutoka huko Babati na alikuwa na mtoto wa kike tayari afahamikae kwa jina la Raheli , inasemekana baada ya Raheli kuzaliwa mama yake alimtelekeza kwa baba yake Elibariki , hivyo malezi yakahamia kwa Elibariki peke yake kumlea Raheli
Maisha ya Raheli unaambiwa yalikuwa magumu sana kutokana na aina ya baba yake , kwani inasemekana Elibariki alikuwa mlevi kupindukia mara baada ya kuachwa na mwanamke wake , lakini licha ya hivyo Raheli uwezo wake wa akili ulikuwa mkubwa sana na aliweza kusoma hivyo hivyo kwa taabu mpaka kufikia kidato cha nne na hapo ndipo alipoweza kupata ufadhili kutoka serikalini na Kwenda kusomea nje ya nchi na hio ni mara baada ya kufanya vizuri katika masomo, lakini kipindi hicho baba yake alikuwa ashamzika tayari kwani alipoteza Maisha kwa kuwekewa sumu kwenye pombe na wadeni wake.
Na ni huko masomoni Afrika ya kusini ndiko alikoweza kukutana na Kizwe na kuunda urafiki , lakini pia kupitia Kizwe akaweza kumfahamu Jeremy na mapenzi yao kuanzia.
Upande wa Marium alikuwa akijua uwepo wa Raheli kwa maana kwamba alikuwa akimfatilia kwa ukaribu sana Elibariki ambaye alibakia Tanzania na hata baada ya Elibariki alivyofariki wakati Raheli akiwa anamaliza kidato cha nne akili yake ikamgeukia Raheli.
Na ukweli ni kwmaba ni Marium aliekuwa akisimamia elimu ya Raheli kwa siri sana pasipo kwa Raheli mwenyewe kufahamu , yaani hata ufadhili wa masomo ya Raheli ulisimamiwa na Marium mwenyewe na ni Marium huyo huyo alieweza kujua wa kwanza mahusiano yaliokuwepo kati ya Raisi Jeremy na Raheli.
Kwahio kitendo cha Raheli kurudi Tanzania na kupata kazi kwenye kampuni ya Vexto mpaka kufanywa kuwa CEO ulikuwa ni mpango wa Marium, alitengeneza mpango wa kupiga ndege wawili kwa jiwe moja , yaani alimfanya Raheli kuolewa na mtoto wake Adebayo licha ya kuwa na mimba kwa ajili ya kumsitiri lakini wakati huo huo aliamini kumfanya Raheli CEO ni kuzuia historia ya miaka iliopita isimuwinde.
Kwahio kwa maneno marahisi wakati Raheli akiona ameweza kuwa CEO wa kampuni ya Vexto kwa juhhudi zake lakini pia kuweza kuolewa na Adebayo , ukweli ni kwamba kampuni aliokuwa akiiendesha ilikuwa ni mali ya familia yao.
Sasa haikueleweka mara moja ni mchezo gani Marium alicheza mpaka kuweza kumiliki mali za kampuni ya Vexto licha ya serikali kutaifisha baadhi , lakini jamb la uhakika ni kwmaba alipata msaada kutoka kwa Afande Kweka na Familia ya Afande Athumani.
Sasa inasemekana mara baada ya miaka kadhaa kupita , yaani miaka ya elfu mbili familia ya Karim Kayage kutoka Marekani iliweza kuwasiliana na Raheli , yaani mama yake na Edna na kujaribu kuelezea kile kilicotokea na kuhitaji msaada kwani huko Marekani walikuwa wakiishi Maisha duni sana, lakini Raheli aliwapa jibu moja tu kwamba hafahamu kama ana ndugu wa aina yoyote , akaenda mbali kwamba ndugu yake alikuwa ni baba yake tu na alishakufa na kumzika peke yake hivyo wasimsumbue.
Yaani kwa maneno marahisi Raheli aliwafungia vioo kabisa ndugu zake kutoka huko Marekani na kufunika kila kilichotokea , licha ya kujua kwamba mali alizokuwa akisimamia zilikuwa za familia yake kihalali lakini aliamini ni kwa juhudi za Marium ndio maana mali hizo zipo mpaka wakati huo, kwani ni makosa ya baba yake mkubwa ndio yaliofanya familia kusambaratika, hivyo Raheli hakumchukia Marium lakini wakati huo huo hakutaka kuwatambua ndugu zake, yaani hakutaka kuifahamu familia ya baba mkubwa wake iliokuwa nchini Marekani mafichoni.
Karimu ambaye alitakiwa kuwa babu yake na Edna na Ernest kwa upande wa Mama alishakufa hivyo familia ilikuwa ikisimamiwa na baba yake Ernest anaefahamika kwa jina la Roger.
Kwahio kitendo cha Raheli kutelekeza ndugu zake huko ughaibuni kilijenga chuki sana kwa Maisha ya Ernest baada ya kuhadithiwa na baba yake na kuanzia siku hio alikuwa akiamini kwamba kampuni ya Vexto ni mali yao , hivyo alikuwa na haki ya kuimiliki na kuishi Maisha mazuri kuliko anayoyaishi hapo Marekani ndani ya jimbo la Philadephia.
******
Kizwe hakuishia kwenye historia ya familia ya Kayage tu , bali aliendelea kuhadithia namna ambavyo aliweza kukutana na Raheli nchini South Afrika na wakaja kuwa marafiki wakubwa , lakini pia akaendelea namna ambavyo Raheli alimsaliti na mume wake Jeremy kwa kuanzisha nae mahusiano mpaka kumzalia mtoto.
Kizwe alionekana kuwa na chuki kubwa sana zidi ya Raheli na ilionekana yeye na Ernest walikuwa wakishirikiana kwa lengo moja , kulipiza kisasi kwa Raheli kwa yale aliowafanyia , kwa upande wa Ernest alikuwa akitaka kulipiza kisasi kwa kitendo chake cha kuitelekeza familia yake lakini kwa upande wa Raheli alikuwa na chuki kwa Raheli kwasababu ya kutembea na mume wake.
Roma alishangazwa na maelezo yaliotolewa na Kizwe na kuona kwamba kumbe yote hayo yalisababishwa na Raheli mwenyewe kuanzia kumsaliti rafiki yake , lakini pia kuitelekeza familia yake iliokuwa uhamishoni huko Marekani.
Lakini pia sasa anapata kujua kwamba Marium sio mwanzilishi wa Vexto , bali ni familia ya Kayage ndio ilioanzisha kampuni hio , lakini kutokana na makosa alioyafanya Karimu kwa kusaliti serikali , ndio kilipelekea anguko la familia ya Kayage na hatimae mali zao kuangukia kwenye mikono ya mwanadada Marium.
Kwa maana kwamba Roma historia zote alizokuwa akizifahamu kuhusu Marium alizoelewa na Bi Wema pamoja na Mzee Chino hazikuwa na ukweli wowote , lakini sio kwake tu , pia kwa Edna ambaye siku zote alikuwa akijua mwanzilishi wa kampuni ya Vexto ni bibi yake hakuwa akijua kwamba kampuni hio ilianzishwa na ndugu zake kwa upande wa mama.
Roma alijiambia katika Maisha huwa kuna mengi sana ambayo yanajificha ndani yake , huenda pia kuna Zaidi ya stori inayohusiana na Marium mpaka kupelekea Karimu kukimbilia nje ya nchi kwa kuhusishwa kuisaliti serikali.
Unajua bwana usione makampuni makubwa duniani yamesimama na yanaongoza kwa mipesa mingi , lakini ukifatilia nyuma utakuja kugundua kwamba kuna makando kando mengi ambayo yamefanyika , lakini hayaweki wazi , waanzilishi hao ukiwauliza siri za mafanikio yao watakuambia tulianza na kuuza vitumbua au nyanya na hatukukata tamaa mpaka tukafanikiwa , lakini kumbe kuna mengi sana nyuma ya mafanikio hayo.
Katika Maisha unachotakiwa kuelewa ni kwamba kama kuna kitu unakiona jua kuna kile ambacho hukioni na huu ndio msingi wa dunia tokea kuanza kwake , kama Mungu mwenyewe alidhamiria tuone kila kitu basi angetuwekea macho kisogoni kwamba ukiwa unatembea Kwenda mbele uwe unaona yalionyuma yako , lakini bahati mbaya tuna macho ya mbele tu , hivyo hatuoni ya nyuma hivyo tafsiri ni kwamba kama kuna unachokiona jua kuna kile ambacho hukioni.
Sasa je yale ambayo hatuyaoni yalifichwa kwa makusudi gani kwetu na je wale wanaoyafahamu kwa kiasi kidogo je wamefaidikaje.
 
SEHEMU YA 374

“Nadhani mpaka sasa unaona kwamba kampuni ilikua yetu kutoka mwanzo ni Raheli tu ndio aliisaliti familia yetu , na kuacha jina la babu yangu Karimu kuendelea kuchafuka mpaka leo hii”Aliongea Ernest kwa hisia.

“Unamaanisha nini kuchafuka kwa jina la babu yako?”Aliuliza Roma na Kizwwe aliachia cheko.

“Nilichokuelezea ni nusu tu ya ukweli juu ya kile kilichotokea , ukweli ni kwamba kila kitu ilikuwa ni mipango ya Marium, kuasi jeshi kwa Karimu haikuwa kweli , bali ni mpango uliosukwa na Marium kwa kushirikiana na mpenzi wake Athumani”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa Zaidi.

Kwa maelezo ya Kizwe ni kwamba ni kweli kwamba Karimu alikuwa akisafiri mara kwa mara Kwenda nchini Congo , lakini safari zak hazikuwa zikihusiana na kazi yake ya uanajeshi , bali kilichokuwa kinampeleka Kongo ni mwanamke alietookea kumpenda, lakini asichokijua kipindi hicho Karimu ni kwamba serikali ya Tanzania ilikuwa ikuhusishwa na serikali ya Congo kupitisha siraha za waasi kinyemela Kwenda Congo, sasa Habari hizo hazikuwahi kuweka hadharani lakini serikali ya Tanzania yenyewe haikuwa ikujua kinachoendelea juu ya tuhuma hizo , lakini jambo moja ni kwamba ni kweli kuna siraha zilikuwa zikisafirishwa Kwenda Congo kupitia Tanzania na mhusika mkuu hakuwekwa hadhariani ila inasemekana ni moja ya familia iliokuwa na nguvu sana kipindi hicho na aliekuwa akihusika ni moja ya watu wa karibu sana na raisi, sasa wakati uchunguzi unafanyika ili serikali ya Tanzania kujitoa katika tuhuma hizo ndipo walipombebesha lawama zote Karim.

Mwanzoni safari za Karimu Kwenda Congo hazikuwa zikifahamika na serikali kutokana na kwamba alikuwa akienda kwa siri , lakini Marium alikuwa akijua safari hizo za Congo na yeye ndie aliemtumia Afande Athumani kuhakikisha tuhuma za kesi ya siraha anabebeshwa yeye , yaani kwa maneno marahisi ni kwamba nchini Congo Karim alitengenezewa watu wa kukutana nao na watu hao walikuwa wakijihusisha sana na machafuko yaliokuwa yakiendelea ndani ya taifa hilo , sasa kitendo cha Karimu kukutana na watu hao ulikuwa ni Ushahidi tosha wa kumkamatisha kama muhusika , lakini ukweli hakuwa muhusika na aliekuwa akifanya biashara hio baadhi ya watu kutoka serikalini walikuwa wakimlinda na watu wachache pekee ndio waliokuwa wakijua jambo hilo akiwemo Marium.

Sasa Marum malengo yake ilikuwa ni kampuni , hivyo alichonga tu mchongo na muhusika ambaye alikuwa kweli akisafirisha siraha ili kumsaidia kuipata kampuni ya Vexto kihalali na kwakuwa Marium alikuwa akijua ukweli basi alizibwa mdomo kwa kutimiziwa haja yake, kipindi hicho tayari alikuwa na mtoto Adebayo.

Sasa kilichotokea ni kwamba Afande Athumbani ni kweli alikuwa akimpenda Marium na walikuwa wapenzi , lakini familia yake ilimfosi kumuoa mwanamke mwingine na kwakua pendekezo alilopewa lilikuwa lina maslahi ya familia basi Athumani aliachana na Marium, kitendo ambacho Marium alikitafsiri kama vile alitelekezwa.

Sasa wakati wa mipango yote hio inaendelea Marium alikuwa tayari ashamzaa Adebayo na upande wa Athumani alikuwa ashaoa tayari na ana familia kabisa na mtoto, hivyo msaada aliokuwa akiupata kutoka kwa Mzee Athumani ni kama ulikuwa wa kumfidia tu Marium.

Sasa Marium alijua kuchanga karata zake vizuri , kwanza kabisa alikataa kuolewa kama mke wa pili na Athumani huku akiendelea pia kumfanya Athumani kuwa mwenye hatia , hivyo kuendelea kumsaidia katika mipango yake.

“Kwahio unachomaanisha ni kwamba Karimu hakuwa akihusika na kesi aliopewa?”

“Babu hakuwa akihusika kabisa, yote alisingiziwa na watu wa serikali”Aliongea Ernest kwa hisia.

“Raheli alikuwa akijua kwamba babu yake alikuwa amesingiziwa?”

“Unafikiri kwanini famili yote tunamchukia , ni kwasababu aliamua kuungana na maadui na kuisaliti familia , yule mwanamke ni shetani”Aliijibu.

“Okey tuseme yote mlioyaelezea hapa ni kweli , nataka kujua imekuwaje nyie wawili mkafahamiana mpaka kuja kuanza kulipiza kisasi chenu kwa Edna?”AliongeaRoma na kumfanya Kizwe kutabasamu kidharau.

“Mr Roma nadhani ushasahau mimi ni mke wa raisi, nina rasilimali nyingi za kuujua ukweli wote , kitendo cha Raheli kunisaliti na kutembea na mume wangu ndio kilichonifanya kufuatilia Maisha yake ya nyuma na bahati tu kwa kutumia konesheni zangu ndio nilivyoweza kujua siri hio , ambayo ilinipeleka mpaka Philadephia Marekani”

Haikueleweka Kizwe aliweza kufahamu vipi siri iliokuwa nyuma ya kesi ya Karimu kuhusishwana kupitisha siraha Kwenda Congo , lakini baada ya kujua historia nzima aliazimia kuitafuta familia ya Karimu ndani ya taifa la Marekani , na kwakua alikuwa na rasilimali nyingi kutoka kwa taifa la Rwanda akiwa kama First Lady basi ilikuwa rahisi kwake kuweza kugundua familia hio ilikuwa ikiishi jimbo la Philadephia.

Kizwe wakati anafika sehemu wanayoishi ndugu zake na Edna, Maisha kwakweli yalikuwa magumu sana kwao na Watoto wote waliokuwa ndani ya familia hio walikuwa wakifanya vibaya sana kimasomo na hata Ernest ambaye ndio aliekuwa mkubwa alimkuta akiwa gerezani kwa kosa la kujihusisha na madawa ya kulevya na ndio Kizwe aliehusika kumtoa Ernest Gerezani.

Wakati Ernest anatolewa gerezani hakuwa akijua chochote kuhusu kampuni ya Vexto na Kizzwe alimuelezea kidogo na kumwambia kwamba ukweli wote ataujua kutoka kwa baba yake Mzee Roger.

Ernest alivyoenda kwa baba yake kutaka kuujua ukweli , mzee huyyo licha ya kwamba hakutaka kumwambia ilibidi amuweke wazi tu juu ya ukweli wote.

Sasa baada ya Ernest kufahamu kwamba asili yao ni kutoka Tanzania na familia yao ilikuwa na kampuni kubwa ya Vexto alijikuta akipandwa na hasira sana mpaka kwa baba yake , kwani alikuwa akiishi Maisha magumu mno kumbe walikuwa na pesa kibao.

Kwanzia hapo ndipo Ernest alipoomba msaada kwa Kizwe na Kizwe hicho ndio alichotaka , alitaka kumtumia Ernest kulipiza kisasi kwa Raheli, hivyo alichokifanya kwanza ni kumsaidia Ernest kimasomo kwanza akiwa hapo hapo Marekani na kumpa majina mapya kabisa akiachana na jina la Swalehe.

Baada ya Ernest kuweza kuhitimu chuo Kizwe alimfanyia mpango ndani ya kampuni ya Yamakuza tawi la Hongkong na jambo hilo liliwezekana kutoka na mahusiano yake aliokuwa nayo na mheshimiwa Kigombola.

Ukweli maelezo ya Kizwe hayakuwa ukweli wote kwani kuna baadhi alificha hasa yaliokuwa yakihusiana na Raheli na yeye , kwa mfano swala la kufa kwa Raheli hakutaka kulielezea kabisa , ila upande wa Roma hakutaka pia kuuliza , alijua tu kuna namna ambayo ataweza kuujua ukweli wote.

“Nilichotaka ni familia kuuna wenyewe kwa wenyewe huo ndio mtego wangu , lakini naona umefeli kwa sasa”Aliongea Kizwe kwa kuhitimisha na kisha alichukua mkoba wake na kuondoka lakini ile anafikia mlangoni , Roma alimsogelea.

“Sijakuambia uondoke, kwasababu hatujamalizana”Aliongea Roma.

“Kama hutaki niondoke unafikiria utanifanya nini , Roma labda huelewi ila mimi ni Kizwe Jeremy Paul ,First lady wa taifa la Rwanda , huwezi kunifanya chochote”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu kifedhuli , alionekana ashazoea kukutana na watu wa aina ya kizwe , hivyo hakuwa akitishika kabisa.

“Napanga kukuua ndio na hakuna namna ya kuepuka adhabu ya kifo , lakini nashidwa kujua ni kifo cha aina gani kinaweza kukufaa kwa kumchokoza mke wangu, mimi sijali yalitokea ninachojali ni kuguswa kwa watu wangu wa karibu tu basi hilo ndio kosa lako na adhabu yake ni kifo”Aliongea Roma akiwa siriasi.

Lakini kizwe hakumjali alitoa bastora yake na kumyooshe Roma.

“Huna uwezo wa kunizua kutoka hapa ndani , la sivyo nitakufumua ubongo wako”Aliongea Kizwe lakini Roma alitabasamu kifedhuli na kilikuwa kitendo cha kufumba na kufumbua Kizwe hakuwa tena na bastora na ilikuwa kwenye mikono ya Roma.

Ernest na Monica wote walijikuta wakishangazwa na kitendo hicho , hawakuelewa Roma aliwezaje kukifanya , kwani spidi aliotumia haikuwa ya kawaida kabisa.

Licha ya Kizwe kupokonywa bastora , upande wa Kizwe hakuwa na woga kabisa na hakujiuliza ni kwa namna gani Roma aliweza kumpokonya siraha yake kwa haraka hivyo.

“Hahaha.. Roma nishakuambia huwezi kunifanya chochote , nadhani umtafute mkeo kwanza kabla ya kufanya maamuzi ya kuruhusu risasi”Aliongea Kizwe lakini palepale simu ya Roma mfukon ilianza kuita mfulululizo na Baada ya Roma kuitoa aligundua aliekuwa akipiga ni Edna mke wake, alipokea haraka haraka na kuweka sikioni akiwa na wasiwasi.

“Edna nini kimetokea?”

“Roma naomba usimuue…”Aliongea Edna.

“Unamaanisha nini , nani nisimuue? harafu kwanini unalia?”

“Kaniletea nyaraka zote ofisini kwangu zina Ushahidi .. kwa sasa naomba usimfanye chochote”Aliongea Edna na ni kweli sauti yake ilionyesha kabisa alikuwa kwenye majonzi.

Kizwe alimwangalia Roma na kujikuta akibetua mdomo kwa dharau , ni kama alikuwa akijua Roma alikuwa akiambiwa nini na Edna.
 
SEHEMU YA 375.

Roma kwa mara ya kwanza alimsikia Edna akiwa kwenye hali ya kuomba sana na kwa vyovyote aliona huenda Kizwe kapata udhaifu wa kumshika Edna ndio maana alikuwa akiongea kwa sauti ya kubembeleza.

“Okey nielezee kwanza ni nini kinaendelea..”Aliongea Roma.

“Familia ya Kayage iliopo huko Marekani Firstlady ameiteka , mjomba na famiia yote ipo kwenye himaya yake , sitaki kitu chochote kiwakute kwani mimi na mama tuna deni kubwa kwa ajili yao”Aliongea Edna kwenye simu na kumfanya sasa Roma kuelewa, lakini wakati huo huo alijisikia vibaya sana kwenye moyo wake , kwani hakuwahi kumsikia Edna akiwa kwenye hali kama hio hata siku moja

“Nadhani mkeo tayari ashakuambia usiniguse , unatakiwa ufikirie vizuri ni maamuzi gani ya busara unatakiwa kufanya , nasikia familia yako inataka kukufanya kiongozi wa familia hivyo angalau unatakiwa kuonyesha ukomavu wako katika kuamua mambo”Aliongea Kizwe na kisha bila kumjali Roma aliokota mkoba wake na kisha alianza safari ya kutoka kwenye jumba hilo

“Unajali sana kuhusu Maisha yao?, Namaanisha hao ndugu zako”Aliuliza Roma akimuongelesha Edna ambaye hakuwa amekata simu bado , huku akimwangalia Kizwe aliekuwa akitokomea nje.

“Siwezi kuwatoa kafara tena , wamepitia magumu kwa sababu yetu”

“Okey nimekuelewa”Aliongea Roma na kukata simu.

Sasa upande mwingine ndani ya kampuni Edna alionekana kukaa kwenye sofa huku akiwa kwenye mawazo , kwenye mikono yake alikuwa ameshikilia picha mbili , na katika picha hizo ni picha moja ambayo ilikuwa ikimuonyesha mama yake pamoja na babu yake Elibariki, wakati huo mama yake Raheli alionekana kuwa mtoto mdogo, picha nyingine ya pili ilikuwa ikimuonyesha babu yake Elibariki pamoja na Babu yake Karimu wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye pozi la kucheka.

Kwa maana kwamba picha hio ilikuwa ikithibitisha ukweli kwamba babu yake Elibariki na Karimu walikuwa ni ndugu kwani hata nyuma ya picha hio kulikuwa na maandishi ilionyesha watu hao walikuwa ndugu.

“Mama nimechoka , kwanini haya yote yanatokea baada ya kuniacha mwenyewe…”Aliongea Edna huku machozi yakimtoka , ukweli mrembo huyo Maisha yake yote aliishi kwa kujua kama hakuwahi kuwa na ndugu upande wa mama, sasa baada ya siku hio kujua kama alikuwa na ndugu tena waliohai ni taarifa ya kushitusha kwake.

Kizwe alikuwa amekusanya Ushahidi wote, yaani namna ambavyo Raheli aliwakataa ndugu zake mara baada ya kufanya mawasiliano , jambo moja tu ambalo halikuwa kwenye bahasha alioletewa ni ule uthibtiisho kwamba familia yao ilifanyiwa hujuma miaka iliopita na Marium, mpaka kupoteza haki ya uraia na mali zao ndani ya taifa walilozaliwa.

Upande wa Kizwe baada ya kutoka kabisa kwenye mlango akitaka kuufunga , alijikuta akivutwa ndani na nguvu isiokuwa ya kawaida , yaaani ilikuwa ni kama alikuwa akipeperushwa na upepo na alishindwa kushindana na nguvu inayomvuta na alijikuta akitua kwenye miguu ya Roma huku akitoa ukulele, kwa mara yake ya kwanza ndio anapata kukumbwa na kitu cha ajabu cha aina hio.

“Roma unafanya nini , unataka familia ya ndugu wa mkeo kufa?”Aliuliza Kizwe huku akiwa kwenye woga wa hali ya juu , mpaka hapo aliamini Roma sio mtu wa kawaida , kwani kwa jinsi alivyoweza kurudishwa ndani ilikuwa ni nguvu isiokuwa ya kawaida kabisa.

Roma hakujali swali lake , bali alimwangalia Kizwe ambaye yupo chini kwenye miguu yake na kisha akamlamba kibao kilichomlaza chini na kumfanya akili yake kuwehuka kwa sekunde kwani alikuwa akisikia mivumo isokuwa ya kawaida kwenye akili yake.

Roma baada ya kuona kibao kimemuingia vyema Kizwe alimgeukia Ernest ambae alikuwa anatetemeka kwa woga huku Monica yeye akiwa ashapoteza fahamu , walishuhudia wote Kizwe kurudi ndani pasipo ya kupenda kwa kusukumwa na nguvu isio onekana , kwanini wasiogope, mpaka hapo waliona Roma sio mtu wa kawaida licha ya kuonekana kawaida, kwa Ernest ilikuwa sawa ila kwa Monica alipoteza fahamu kwa mshituko.

“Familia yako bado ipo Marekani huko Philadephia?”Aliuliza Roma huku akielekeza swali hilo kwa Ernest.

“Not Anymore “Alijibu kwa woga huku akimwangalia Roma aliekuwa siriasi , hakuwa yule aliekuwa akimzoea kumuona ndani ya kampuni , ila huyu alikuwa siriasi kweli , sasa alijibu kwa kusema kwamba familia yao haipo tena ndani ya Philadephia.

“Wako wapi kama hawapo Philadephia?”

“Walihamia Baltimore , Meryland miaka miwili iliopita”Alijibu Ernest. Huku akikwepesha macho yake na ya Roma kutokana na namna alivyokuwa akiogopesha , ijapokuwa Roma hakuwa amebadilika macho wala nini , lakini alikuwa akidhalisha hisia ambazo ni kama mtu anapokutana na mchawi au jini usiku, wazungu wanaita ‘ killing Aura’.

Roma baada ya kupewa jibu hilo alitoa simu yake alioirudisha mfukoni bila kumjali Kizwe na Ernest ambao walionekana kuchanganyikiwa.

Roma alionekana mtu aliekuwa akimpigia alikuwa ni Sauron na simu ilipiga na kupokelewa.

“Your Majest Pluto this is Sudden , Do you have any order?”Aliongea Sauroni upande wa pili na sauti yake ilionekana kuwa ya heshima.akimaanisha kwamba Roma amepiga simu jambo ambalo sio la kawaida kwa muda huo hivyo aliuliza kama kuna maagizo.

“Who is closest Agent to Baltimore , Maryland that can be dispatched ?”

“Ni ajenti gani aliekaribu na Baltimore Meryland ambaye anaweza kupewa kazi ya haraka?”

“For that area , the tactictal team on land is made up of retired American soldier’s from the Delta force and the Navy SEALs, together they form the elite ‘DSEAL’ mercenaries for hire , they are estimated to be around ahundred or so in numbers , Baltimore is also a port city, so if needed we can use the secret transport route spanning countries like Canada and Norway , Codenamed Maple #039,on such short notice we can still deploy at least three ship destroyers and more than ten Apache attack helicopters “

“Kwa eneo hilo kuna timu ya kimbinu ya ardhini inayojumuisha wanajeshi wastaafu kutoka Marekani , kikosi cha Delta Force na Navy SEALs , umoja wao unajumusiha wapiganaji bora wa kulipwa wanaoitwa DSEAL, wapo kama mia na Zaidi hivi ,lakini pia Baltimore ni mji wa bandari hivyo tunaweza kutumia njia za usafirishaji za siri kutoka nchi kama Canada na Norway inayoitwa jina la Codi Maple#039, kwa uharaka sana tunaweza kutumia meli tatu za uharibifu na Zaidi ya helikopta kumi za shambulizi aina ya Apache” Roma alijikuta akishangaa.

“DSEAL are ours too?, When were they added to our payroll?”

“Kikosi cha DSEAL pia ni cha kwetu , tulianza kuwalipa lini?”

“Kwanzia mwaka jana , mfalme Pluto ulitupa maelekezo tusikuhusise kwenye mambo madogo madogo ndio maana sikupata nafasi ya kukuelezea”Aliongea Sauroni na kumfanya Roma mwenyewe kushindwa kuelewa ni lini alimwambia kwamba asihusishwe kwenye mambo madogo.

“Vyovyote vile , kuna familia…”Alitaka kuongea na akasita na kumgeukia Ernest.

“Marekani mnatambulika kwa jina gani kama familia?”

“Roger’s family”Aliongea.

“Sauroni kuna familia ya Roger’s , nataka mkusanye taarifa zinazowahusu , wanaishi Baltimore, inawezekana wakawa wametekwa au wamezungukwa nataka swala hili ulishughulikie mapema iwezekanavyo pasipo ya mwanafamilia yoyote kuathirika , tuma timu yako, unaweza kuilipa utakavyo lakini nakupa nusu saa tu ukamilishe , siwezi kuvumilia Zaidi ya hapo”Aliongea Roma akitoa oda Kwenda kwa Sauroni

“Copy that”Alijibu Sauroni bila hata ya swali na kisha Roma akakata simu. Na kisha akamgeukia Kizwe.

Kizwe na Ernest walikuwa wanaelewa kingereza vizuri , hivyo aliweza kusikia kila neno lililozungumzwa na waliweza kujua Roma anaagiza watu kuokoa familia hio.

“Mrs President kwenye makosa yako yote ulioyafanya ni kudhania vitu viwili..”Aliongea Roma na kisha aliinua mkono na alionyesha vidole viwili na akaendelea.

“Kosa lako la kwanza ni kujihatarisha Maisha yako mwenyewe kwa kuingilia Maisha ya familia nyingine .. najua una walinzi wanaokulinda kwa siri hapa Tanzania lakini unachopaswa kuelewa hakuna ambaye aliniona nikiingia hapa ndani , hivyo hawajui pia kinachoendelea, Kosa lako la pili ni kujihusisha na familia iliopo nje ya nchi ya Tanzania , labda nikueleze tu unawezza kuwa na koneksheni ndani ya Rwanda na hapa Tanzania lakini kwa upande wangu ukishavuka mipaka tu wa bara la Afrika , haunizidi kwa chochote Zaidi ya kwamba nakuona kama takataka , nina koneksheni kila taifa na konesheni zangu sio za kubembeleza bali ni kutoa maagizo tu”Aliongea Roma na kumfanya Kizwe kuanza kuona woga na kupaniki.

Alichoongea Roma ni sahihi , kama Kizwe hatakuwa na uwezo wa kutoa taarifa nje kwamba yupo hatarini , basi hakuna mlinzi wake yoyote ambaye anaweza kuingia ndani ya jumba hilo , hata wakiingia watamfanya nini Roma, lakini kosa lingine ni kwamba kama Kizwe alitaka kushinda angehakikisha familia ya Kayage yote anaipeleka Rwanda lakini sio kuiteka ikiwa nchini Marekani , kwani huko ndio Roma amewekeza Zaidi.

“Hahaha.. usiogope sana , ninakuhakikisha kwamba nina uwezo wa kushambulia hata ikulu ya Marekani muda huu kwa kutoa oda tun a hakuna wa kupinga hata kama misheni ni ya kujitoa muhanga”Aliongea Roma na kuzidi kumfanya Kizwe kutetemeka.

Sasa alichokuwa akifanya Roma nikuachia nguvu ya kijini kutawala eneo lote , hii ni mbinu ambayo majini pia wanafanya sana wanapokutana na adui , unaambiwa jini linaweza kumuua mtu kwa kumsabazia tu aina flani ya baridi la woga na mtu huyo kupoteza Maisha bila ya kuguswa na hiki ndio kitu ambacho alikuwa akikifanya , lakini kwasababu Roma hakuwa akidhamiria kuwaua basi aliachia kidogo lakini sasa hiko kidogo chenyewe kilimfanya Kizwe kushindwa hata kupumua vizuri licha ya kwamba hajaguswa.

Ernest aliemshikilia mpenzi wake ambaye hana fahamu nyuma ya Roma aliweza kuona majimaji yakitambaa kwenye tailizi kutokea sehemu aliokaa Kizwe , kwa maana kwamba alikuwa ashaanza kuachia haja ndogo

********

USA , MERYLAND -BALTIMORE.

Ndani ya taifa la Marekani upande wa jimbo la Meryland -Baltimore ilikuwa ni asubuhi , ambapo jua lilishachomoza muda mrefu , katika barabara iliokuwa ikiingia ndani ya makazi ya watu inaonekana gari aina ya ChevyRovlet, haya ni aina flani ya magari muundo wa Hiace lakini yanakuwa kama nyumba inayotembea.

Sasa ndani ya gari hio kulionekana watu watatu yaani Dereva aliekuwa akiendesha na mwanamke wa kizungu mwenye nywele nyeupe mdogo wa miaka kama ishirini na mwanaume mwenye Ngozi nyeusi alieshikiria simu ya upepo, wote wakiwa wameketi kwenye viti aina ya sofa, mwanamke akiwa na tarakishi mpakato kwenye mapaja yake akibonyeza bonyeza , huku akiwa amefunga kifaa flani hivi vya mawasiliano kilichokuwa kikizunguka kichwa chake kutoka sikioni na kuja kutokezea mdomoni na gari hio ilikuwa kisonga mdogo mdogo sana.

“D37 your target ‘ numbers are 235 and 214 on the third floor , D48 your target are number 387 and 552 on the fifth floor . Radio in once you assumed your positions”

“D37 walengwa wako , namba 235 na 214 gorofa ya tatu , D48 walengwa wako ,, namba 387 na 552 gorofa ya tano , taarifa haraka ukiwa kwenye nafasi”Aliongea yule mwanaume kwa kingereza safi na ndani ya dakika majibu yalirudishwa.

“D37 in position”

“D48 in position”

“Roger ,Landon , can you confirm any enemy activity?”Aliuliza yule mwanaume alievalia jaketi la rangi nyeusi lenye michoro isioelezeka akimuuliza yule mwanamke mzungu .

“Captain, D55 apprehended an enemy on the street and D21 proceeded to disguise themselves as them. The plan is going without a hitch. There are five hostiles in total and the remaining four will be taken care of soon.”

“Kapteni D55 amemkamata adui barabarani , D21 anaendelea kujifanysiha kama mwenzao , mpango unaenda vyema bila tatizo , jumla ya maadui ni watano , wanne walibakia watashughulikiwa mapema tu”

“Strike team, get ready to lock in on the remaining hostiles. I want a clean take out, I repeat, I want a clean take out . D55 and D21, you two are in charge of cleanup. Engage in twenty seconds.”

“Kikosi cha mapigo , jipangeni kuwamaliza wahalifu waliobaki , Nataka kazi ifanyike kwa usafi , narudia kazi ifanyike kwa usafi , D55 na D21 nyie ndio mtasafisha , Anza kazi baada ya sekunde ishirini”Aliongea yule jamaa mweusi na upande wa pili alijibiwa kwa pamoja na kisha akavuta Redbull iliokuwa pembeni yake na kunywa kidogo na kisha akamgeukia yule mzungu.

“Plan an escape route now and make sure to cut all the lines to the police or any other authorities.”

“Andaa njia ya kutokea , hakikisha unafuta Ushahidi wote unaotuunganisha na polisi pamoja na mamlaka nyingine”Aliongea

“Roger that, Captain. This mission is way below our paygrade. The hostiles were not even able to take on a single one of our agents, what a piece of cake”

“Roger That Kapteni , Hii misheni ni ndogo sana kimalipo , Maadui wenyewe wameshindwa hata kumdhuru ajenti wetu hata mmoja, kama kipande cha keki tu”

“Kaa kimya , tunapaswa kuchukilia misheni zote kwa uzito , hii ni mara yetu ya kwanza kufanya kazi ya yule kijana mdogo mwenye kiburi , ni bora tufanye haraka haraka na kwa umakini kwani tukikosea kidogo tu anaweza kutuua yule”Aliongea na yule kapteni na yule mdada alitingisha kichwa na kutulia kimya.

Ndani ya sekunde chache tu ilisikika milio ya bunduki ndani ya hilo eneo tulivu sana la makazi ya watu ,jambo ambalo sio la kawaida.

******

Ndani ya nusu saa tu Roma aliweza kupatiwa taarifa na Sauroni kwamba mateka wote wapo salama salimini na anasubiri maagizo mengine , Roma aliangalia saa yake na kupiga mahesabu na kugundua mchakato mzima wa kuwaokoa watu hao umechukua dakika kumi na tano tu na kujiambia kweli wanajeshi wa staafu wa jeshi la Marekani wapo makini na kazi zao.

“Watu uliowatuma kuwazingira familia ya Ernest washakufa , una neno gani la mwisho la kujitetea?”Aliuliza Roma akimwangalia Kizwe.

“Unabahati kwasababu niliajili wapumbavu kufanya kazi yangu , sina lolote la kusema amua unachotaka”Aliongea Kizwe huku akimwangalia Roma kama nyoka inayojitayarisha kutema sumu.

“Kwasababu umesema hivyo basi sina sababu ya kukuua , ila kwa mtazamo wangu , mwanamke kama wewe kama nitakuacha urudi mtaani utarudi tu na kunisababishia matatizo”

“Acha kujibaraguza , fanya kuniua kama ulivyodhamiria”Aliongea kwa hasira Kizwe , alionekana hakuwa na tumaini lingine.

“Nikikuua vilevile naweza kujiingiza kwenye matatizo Zaidi , kwani wewe ni mke wa raisi , mimi sio mjinga”

“Nilijua tu utakosa ujasiri wa kuniua , nimekutana na watu waovu kwenye Maisha yangu wa aina tofauti tofauti , lakini kwa upande wako niliweza kukusoma, huna uwezo wa kuniua wewe”Aliongea na Roma akatabasamu kifedhuli.

“Ndio ulivyoweza kunisoma hivyo, Vipi na wewe Ernest unataka kuendelea kuishi?”Aliuliza Roma huku akimwangalia Ernest ambaye alikuwa na uhakika kwamba siku hio ndio mwisho wa uhai wake. Lakini baada ya kuulizwa swali na Roma ni kama chembe ya tumaini la uhai liliibuka.

“Nahitaji kuishi tafadhari , naomba usiniue?”Aliongea Ernest , alijiambia hana namna lazima atafute uhai ili kuweza kushuhudia mtoto wake atakapozaliwa na muda huo huo alitoka alipokuwa amekaa na kupiga magoti mbele ya Roma na kisha akamwangalia mpenzi wake Monica kwa uchungu , alionekana alikuwa akimpenda kweli.

Roma mwenyewe aliweza kushangazwa na namna ambavyo Ernest alikuwa akimpenda Monica , mwanzoni aliona Ernest alikuwa akimtumia tu mwanadada huyo kwenye mipango yake.

“Sikudhania kama utamleta hapa Monica ,inaonyesha unampenda kweli?”Aliuliza Roma.

“Mwanzoni sikuwa nikimpenda , nilikuwa nikimtumia tu kwenye malengo yangu , lakini kadri nilivyokuwa nae nilianza kumpenda , ndio mwanamke wangu wa kwanza ambaye hakuwa akihitaji chochote kutoka kwangu Zaidi ya kunijali kwa juhudi zake zote, ametokea kunielewa ninachotaka kama mwanaume kuliko wanawake wote niliokutana nao”aliongea Ernest na Kizwe aliekuwa pembeni alitabasamu kifedhuli.

“How Pathetic Spouting anything that could keep you alive , Do you realy think your sob story would be enough to keep you alive? He might be afraid to kill me but he is definitely not afraid to kill you”

“Inasikitishaje kuongea chochote ambacho kitakufanya uishi , unafikiri stori yako ya majonzi itatosha kukuweka hai , anaogopa kuniua mimi lakini nina uhakika haogopi kukua wewe”Aliongea Kizwe. Lakini Roma aliekuwa pembani yake aliinua mguu wake wa kushoto na kumpita teke Kizwe ambalo lilimfanya kupeperuka na Kwenda kuvamia chungu cha kuhifadhia maua na kupasuka na alipoteza fahamu hapo hapo.

“Kama nikikuacha hai utanihakikishiaje hutafanya ujinga kumdhuru Edna tena?”

“Hapana naapia kwa Maisha yangu yote sitokuwa na kinyongo cha kisasi tena kwa Edna”

“Una uhakika?”

“Napanga kumchukua huyu mwanamke na Kwenda kumtambulisha kwa wazazi wangu huko Marekani, baada ya mtoto kuzaliwa nitatafta kibarua halali na kuendeleza Maisha yangu , sitaki mtoto wangu kupitia changamoto nilizopitia mimi , Maisha ya kimasikini nilioishi mpaka kupelekea kuwekwa gerezani”Aliongea kwa kutia huruma lakini Roma jambo hilo lilimshangaza kwani hakujua kama Monica ni mjamzito.

“Mtoto.., Monica ana mimba?”

“Ndio mwenyewe kaniambia siku mbili zilizopita, Mr Roma naomba uniache hai , kama ni jela nitaenda ila nataka mtoto wangu atakapozaliwa awe na baba”Aliongea , sasa usichokijua hapo Monica alizimia dakika kadhaa zilizopita mara baada ya Kizwe kurudishwa na nguvu ya ajabu.

“Okey . nitakuachia lakini unapaswa kufanya jambo moja , ambalo litanihakikishia ukweli wako”

“Nitafanya chochote”Aliongea.

“Nataka umvue nguo zote yule mwanamke”Aliongea Roma akimnyooshea kidole Kizwe aliezimia.

“Unatania…”

“Niko siriasis”Aliongea Roma.
 
SEHEMU YA 376

Ernest alimwangalia Kizwe aliejilaza chini akiwa hana fahamu na kisha alimgeukia Roma na kuona yupo siriasi, alimgeukia Monica ambaye amepoteza fahamu na kisha akamrudia kumwangalia Roma.

“Naomba nimtoe hapa Monica kwanza kabla sijafanya kitendo hicho”Aliongea

“Kwanini , Monica hana fahamu huyo na hawezi kujua?”

“Ni kweli lakini siwezi kumvua mwanamke mwingine nguo , wakati yupo mbele yangu nitakuwa nimemkosea heshima yeye na mwanangu , nipe ruhusa yako nimpandishe juu na nitarudi kufanya kazi yako , lakini kama hakuna namna nyingine nitafanya hivyo”Aliongea kwa kuhuzunika na Roma alitabasamu.

“Hongera umepita kwenye jaribio langu”Aliongea na kumfanya Erenst kushangaa kwa furaha.

“Usishangae , umeniambia maneno matupu kwamba huwezi kulipiza kisasi kwa Edna , lakini pia umesema unampenda Monica kwa dhati , sheria yangu ni moja tu najali sana matendo kuliko maneno , hivyo kama ungefanya kitendo cha kumvua nguo yule mwanamke pasipo kumzingatia Monicana mwanao , ningeamini haumpendi”Aliongea Roma

“Kwasasa nimeona kabisa unataka kuwajibika kama baba na mume , hivyo kwasababu mke wangu amesema nisikuue nitakuacha hai , hata hivyo tatizo lilianzia kwa yule mwanamke “Aliongea Roma na kumfanya Ernest kutokwa na machozi ya furaha , hakuamini kama ameokoka kwenye kifo.

“Utaondoka hapa na Monica wako na sitaki urudi ndani ya kampuni tena , fanya taratibu zote uondoke hapa Tanzania na kurudi ulikozaliwa , kama utapata shida yoyote nitumie barua pepe kupitia kampuni yangu na nitakusaidia, mengine kuhusu wewe sijali tena”Aliongea Roma na Ernest alifurahi sana na kumshukuru Roma , alimwamamsha Monica kwa ajili ya kuondoka.

Baada ya Ernest kuondoka ndani ya nyumba hio kwa maelekezo yake , Roma alijikuta akiwaza tena ni maisha gani ambayo Erest anakwenda kuwa nayo yeye na Monica , aliwaza mtoto atakaezaliwa atakuwa na undugu na Edna japo ni kwa mbali .

Roma alijikuta akijishangaaa yeye mwenyewe kuwazia baadhi ya mambo ambayo hayakuwa yakimuhusu kwani zamani hakuwa hivyo na alijiambia ni kweli ana mabadiliko makubwa tokea afikeTanzania.Roma alipotezea na kisha alisogelea mlango.

“Adeline , unaweza kuingia sasa”Aliongea Roma kwa sauti na hapo hapo mlango ulifunguliwa na mwanamke mzungu alievalia tracksuit

“Mfalme Pluto , usiniambie mimi ndio nakwenda kumvua nguo huyu mwanamke?”Aliongea Adeline huku akitabasamu , Adeline alioenakna alikuwa akisikia maongezi yote kwani walikuwa nje ya jumba hilo na ndio waliowadhibiti wale walinzi waliokuwa wakilinda nyumba hio., sasa Kizwe alikuwa akitoa harufu ya mkojo ndio maana akauliza kwa wasiwasi.

Roma alitabasamu kifedhuli na kisha akamwangalia Kizwe kwa kumchunguza kwa ukaribu.

“Anaonekana kuwa mrembo bado na , ngozi yake inaonekana kuwa laini pia licha ya umri mkubwa, naamini bado atauzika kwa haraka ndani ya macasino Halafu kama unashindwa kumvua nguo kwasababu ya mkojo wake naamini hutaki mimi ndio nifanye kazi hio?”Aliongea Roma na kumfanya Adeline kujutia kwanini hakuondoka mapema kama mwenzake Fanny, umbea wake umemsababishia kuingia kwenye mtego wa kumvua mwanamke anaenuka mikojo.

“Fanya haraka”Alifoka Roma akimwarisha Adeline mzungu na alichuchumaa kwa kutokupenda huku akijiaminisha mwenyewe kwamba ni mkojo pekee hakuna kinyesi.

Dakika chache mbele Kizwe alivuliwa nguo zote na kumfanya Roma kutabasamu kifedhuli , alijiambia Mheshimiwa Jeremy alikuwa akifaidi , ijapokuwa Kizwe hakuwa mrembo kama mama mkwe wake Raheli , lakini Kizwe alikuwa akivutia mno hata kwenye ukubwa wake

Sasa Kizwe sio kama alijikojolea tu , alitoa na kinyesi pia amacho kilitoa harufu isioelezeka

“Njoo kuna kitu nataka nikuambie namna ya kufanya kazi na huyo mwanamke”Aliongea Roma na Adeline alimsogelea

“Mfalme Pluto nikachukue Kamera?”

“Unafikiria ujinga , unafikiri ninafanyaga michezo hio ya kitoto kumtishia mtu na picha za uchi , wanaofanya hivyo ni wahalifu na watu wasio na maadili , usisahau sisi ni watu gani , inaonekana muda wako wa mafunzo ndani ya The Eagels haujakufunza mambo haya mpaka leo? Tunatakiwa kufanya vitu tofauti na wengine , Wewe ni mwanajeshi usie wa kawaida hivyo unapaswa kufanya mambo ambayo wengine hawawezi kufanya”Aliongea Roma na akaendelea.

“Je sisi ni watu wa chini ? , jibu ni kwamba Hapana , nini kinachotutofautisha na watu wa chini ?, Jibu ni Sanaa , Nini maana ya Sanaa ? jibu ni muundo wa kimaisha tofauti na maisha yenyewe ,hio ndio sehemu ya mafunzo yetu ndani ya The Eagles, kama umefikiria nitampiga picha mke wa raisi na kumtishia nazo umekosea ninachotaka ni kitu kikubwa Zaidi, kitu fikirishi, ambacho kipo kisanaa Zaidi , yaani namaanisha kama Movie flani hivi”Aliongea Roma na kumfanya Adeline mzungu kushangaa na kuchanganyikiwa kwa wakati mmoja maana hajamuelewa Roma.

“Mfalme Pluto , kwahio natakiwa kufanya nini?”Aliuliza Adeline na Roma alimsogelea kwenye sikio na kumnong’oneza na kumfanya mwanadada wa watu kutoa macho.

“Mfalme Pluto kwanini tusimuue tu , adhabu unayotaka kumpatia ni ya kikatili sana”.

“Sio ukatili , nishakuambia itakuwa ni filamu iliotengenezwa kisanaa Zaidi , swali je ni nini maana ya Sanaa kwenye filamu? , Jibu ni kwamba filamu ni muunganiko wa Sanaa na fasihi , Sanaa lazima iguse hisia za hadhira bwana ala”

Baada ya Roma kuongea hivyo Adeline alimkusanya Kizwe aliekuwa mtupu na kumfunga funga na mapazia na kisha akamuweka begani na kutoka nae nje , mita kadhaa tu kutoka getini kulikuwa na gari , alimwingiza ndani na kuondoka nae.

Roma baada ya kuona Adeline kaondoka alipumua kwa madakika kadhaa na kisha palepale akayeyuka.

******

Ni usiku wa saa nne Edna alisharudi muda mrefu tu kutoka kazini na alishakula, hata Lanlan pia alishakula na kumuogesha na kulala , yeye alikuwa nje ya Balconi akiwa amekaa kwenye kiti kilichotengenezwa kwa mianzi huku macho yake yote yakiwa getini na upande wa baharini.

Roma mpaka muda huo haukuwa amerudi na alikuwa ameketi hapo nje kumsubiria, ukweli kwa namna Edna alivyorudi ni nje ya mategemo ya Blandina ,Qiang , Yezi na Bi Wema , Edna alionekana kuchoka Zaidi tofauti na alivyokuwa siku ya jana yake wakati kampuni ikiwa kwenye matatizo , huyu alionekana kuwa na wasiwasi mwingi mno sana usiokuwa wa kawaida.

Sasa wanafamilia hao walijjikuta na wenyewe wakihuzunika na walishindwa pia Kwenda kulala, kwani mwonekano wa Edna ulikuwa ukisikitisha na hakuwa akitaka kuongea , Blandina alijikuta akimlaumu mwanae Roma kwa kutokuwa nyumbani muda wote huo , kwani mke wake alikuwa kwenye huzuni na sio yeye tu aliewaza hivyo , kwa kila mmoja alimlaumu Roma kwa kutokuwepo nyumbani mapema.

Edna alikuwa akitoa machozi huku akiyafuta na mkono, licha ya kwamba familia ya Kayage yote ipo huko nje ya nchi , lakini alijiambia hawezi kuiacha familia hio ikiendelea na Maisha duni waliokuwa nayo.

Alijiambia Maisha yake ya makuzi yalikuwa ni juu ya maumivu ya familia hizo zilizokuwa zikiteseka kwenye taifa geni.

Na mara baada ya mama yake kufariki ni kama mzigo wote wa hatia ulihamia kwake , hicho ndio kilichomhudhunisha Edna na kutokujua ni nini anaweza kukifanya kwa wakati huo.

Wakati akiendelea kuwaza mwenyewe huku upepo ukimpuliza hatimae mlango wa kutokea kwenye balkoni ulifunguliwa na alionekana Roma mbele yake , na alisimama na kumsogelea haraka sana.

“Babe Wife naona unanisubiriia?”Aliongea

“Wanaendeleaje , wako wapi?”Aliuliza Edna kwa wasiwasi huku akifuta machozi

“Unamaanisha nani na nani mke wangu?”

“Namaanisha First Lady alieteka familia ya Ernest na Ernest mwenyewe”Aliongea Edna na Roma alijilamba midomo na kisha kumwangalia mke wake, huku akishindwa kuelewa ni kitu gani anahisi kwenye moyo wake baada ya kuulizwa maswali hayo.

“Kwahio umeshindwa kulala kwasababu ulikuwa ukiwawazia?”Aliongea Roma na kumchanganya Zaidi Edna kwani Roma hajibu swali lake.

“Rom,,, ume.. ume ua mtu tena?” Aliongea Edna huku akiwa na wasiwasi mno mpaka kutamani kuachia kilio na kumfanya Roma kumuonea huruma lakini yeye pia kuumia kwa maswali ya Edna.

“Roma naomba unijibu , acha kukaa kimya unanitia uchizi .. ulinahidi hautouwa mtu , niambie”Aliongea Edna huku akijawa na hofiu , aliamini kama Roma kamuua Ernest pamoja na Kizwe si inaanisha kwamba kaua ukoo mzima.

“Wanafamilia wote wa Ernest wako salama , Ernest na Monica washafanya safari kuelekea Marekani muda ninaongea sasa wapo kwenye ndege , kuhusu Kizwe sijamuua ila nitamuadhibu kwa makosa yake na siwezi kumruhusu kutishia Maisha ya watu wako wa karibu tena”Aliongea Roma kwa sauti kavu na Edna alijikuta akipumua kwa ahueni.

“Asante… Asante sana .. hicho ndio nilichotaka kusikia kutoka kwako”Aliongea Edna huku akirudi nyuma.

“Edna inamaana huniamini ?”Aliuliza na kumfanya Edna kumwangalia Roma taratibu machoni

“Sijui ni kipi unanifikiria au unanionaje lakini tokea tumefunga ndoa siku zote nimeishi kwa kudhania ni jambo gani linaendelea kwenye Maisha yako kwasababu kila ambacho kinakusumbua moyoni haukuwa tayari kukiweka wazi na hii imenifanya kushindwa kukufahamu vizuri, nilijitahidi kwa uwezo wangu kuwa muwazi kwa kila kitu ambacho unauliza licha ya kwamba sikutaka kuonyesha baadhi ya makovu na madoa niliokuwa nayo kwenye Maisha yangu ya nyuma , lakini angalau nimekuonyesha upande mzuri Zaidi kuhusu mimi”

“Edna najijua mwenywe nimekosa aibu kutokana na matendo yangu , na nimefanya mambo mengi ya ajabu , lakini likija swala lako siku zote lazima nikuzingatie , sijawahi kufanya kitu bila kukufikiria wa kwanza , wewe kama mke wangu , nimekuacha kwenye kampuni na Kwenda kushughulikia maadui zako , hivi unafikiri nilijisikiaje baada ya wewe kunipigia simu na kuniambia nisiwaue , unafikiri nilijisikiaje kuonyeshewa dharau na yule mwanamke?”

“Edna ifikie hatua nikirudi kama hivi swali la kwanza unalopaswa kuuliza sio wako wapi au wanaendeleaje , nilichotaka kusikia kwako ni kama niko sawa?, sijapatwa na shida yoyote, najua unaniona kama mtu ambaye siwezi kudhurika na chochote lakini mimi pia ni binadamu na nakufa pia kama wengine, mimi sio roboti kwamba sina hisia baada ya kudharauliwa na mwanamke kama yule , ndio ninaweza kudharauliwa na mtu yoyote yule na nikavumilia kwa ajili yako , lakini angalau ujari kile ninachojisikia pia”Aliongea Mfalme Pluto akilalamika mbele ya mke wake , kwa alivyoonekana a ni kama hakuwa Hades au mfalme Pluto anaesifika kwa roho ya kikatili likija swala la kudili na maadui zake.

Kilichomkasirisha Roma ni kitendo cha Edna kutojali hali yake na kukimbilia kuuliza maswali yanayohusu familia yake , hivyo alitafsiri kwamba Edna anajali ndugu zake Zaidi kuliko yeye.

Edna kwa mara ya kwanza alimuona Roma akilalamika kwa muda mrefu hivyo tokea kule Ufaransa , alijikuta machozi yakimtoka , hakujua kama kuuliza swali lile lingemfanya mume wake kuumia , maneno ya Roma pia yalimuumiza kisawa sawa na kila alipojaribu kuongea alishindwa kabisa na kuishia kutoa machozi pekee.

“Okey! Potezea tu maneno yangu,inabidi uamke hapo na ukalae sasa , muda umeenda na kesho una kazi za kufanya , naona hata kubadilisha mavazi umesahau”Aliongea Roma na kisha kugeuka akimwacha Edna anatoa machozi

“Roma.. subiri, unaenda wapi?”

“Sijisikii kulala , ngoja nikapunge upepo , huenda pia nikapata bia mbili tatu za baridi kunituliza kwa sasa, usijali hakuna cha kunisibu huko nje”Aliongea Roma na hakusubiri neno lingine na kisha kuondoka na ndani ya madakika kadhaa aliweza kushuhudia BMW X7 ikitokomea nje ya geti.

Lakini sasa huku nyuma aliacha kilio kwani Edna alieshindwa kumzuia Roma kuondoka alijikuta akikaa chini na kuanza kulia kama mtoto, alilia kama vile hakuna kesho , lakini wakati akiwa kwenye kilio mlango ulifunguliwa na Lanlan alieonekana kufikicha macho na Kwenda kumkumbatia mama yake aliekuwa akilia , haikueleweka nini kilisababisha kuamka muda huo , kwani alikuwa kwenye chumba cha Qiang Xi.

*****

Roma baada dakika kama tatu hivi ya kutoka na gari yake alijikuta akija kusimamisha upande wa kulia kwake ndani ya eneo maarufu la Element, sehemu hio ilikuwa imechangamka sana na ndio maana ilimvutia Roma kwani aliamini sehemu yenye watu wengi inakuwa na mambo mengi , hivyo aliweza kujongea baada ya kuegesha gari lake na kujitafutia nafasi ya kukaa.

Na aliweza kupata meza iliokuwa upande wa nje kabisa karibu na barabara na kukaa chini na ndani ya madakika kadhaa tu alisogelewa na muhudumu akihitaji kuchukua oda yake na Roma aliagiza Windhoek chupa mbili.

Muhudumu yule wa kike alitabasamu na kisha akaitikia kwa heshima kuleta alichoagizwa , Elementi pia kuna tabia moja ya wahudumu kuangalia namna mteja wao anavyofika , unajua hilo ni eneo maarufu ambalo lipo ndani ya mtaa wa wenye nazo , hivyo wanakuchora kuanzia mavazi , simu na namna ulivyoingia, sasa kama umekuja kwa mguu watajua tu hasa hasa madanga wanaofika hapo kuweka mitego , lakini kwa Roma aliweza kufika na gari kali alioichukuaga kipindi alipoenda kudai hela za mkopo za kapuni kule kwa Azizi Ally Temeke.

Roma baada ya kuletewa kinywaji chake alijikuta akivutiwa na meza iliokuwa na mwanaume na mwanamke kwenye kona.

Kitu kimoja unachotakiwa pia kujua kuhusu Roma ni kwamba alikuwa na uwezo wa kusikia mtu hata akiwa kwa umbali mrefu kama wamita mia moja kwa kutumia uwezo wake wa kijini.

Sasa kwa upande wa mwanamke aliekuwa upande wake wa kushoto kutoka sehemu aliokaa na mwanaume , ni kama vile aliweza kumtambua lakini hakuwa na uhakika na ilibidi atumie uwezo wake kumjua ni nani , na alijikuta akishangaa mara baada ya kugundua ni Benadetha.

Roma alijiuliza mwanamke huyo anafanya nini hapo muda huo , lakini hakutaka kuwa na papara , kwasababu Benadetha hakuwa peke yake,Hivyo alitumia uwezo wake kusiki kinachongelewa.

“Benadetha wewe ni mjinga sana , nilikuita hapa sio kuzungumzia mapenzi yetu ya utotoni”Aliongea mwanaume aliekuwa amekaa nae.

“Kama hujaniitia kwa ajili hio Yakobo , umeniitia nini?, hivi unajua ni miaka mingapi nimekusubiria tokea ulivyosema unaelekea nje ya nchi kimasomo , uliniambia siku utakayo rudi tu tutaanza mapenzi yetu na hatimae kunioa , ukaniambia nijitunze kwa ajili yako na wewe utajitunza kwa ajili yangu , unachoongea sikuelewi Yakobo ni nje ya ahadi zako”

“Benadetha kwanza naomba unisamehe , ila nisikudanganye sasa hivi nishapata mwanamke wa hadhi yangu , kipindi naelekea nje ya nchi, nilikuwa na utoto mwingi sana na nikajikuta naongea maneno yasiokuwa na maana , Benadetha hata wewe mwenyewe ulikuwa ukifahamu kipindi kile akili yangu haikuwa sawa , kwanini uliamua kuamini maneno yangu”Aliongea Yakobo na kumfanya Roma kutabasamu kifedhuli.

“Yakobo huwezi kunifanyia hivi , nakupenda Yakobo hivi unadhani maisha yangu yalikuwa rahisi bila ya uwepo wako hapa Tanzania , kwanini unanikataa siku yako ya kwanza kurudi Tanzania? Unafahamu ni wanawake wangapi nimewakataa kwa ajili yako?”

“Sijakukataa Benadetha ila nimekuita hapa kwa ajili ya kuweka jambo langu wazi , ili usije ukavuruga mapenzi yangu na mwanamke ninaempenda ndio maana nikataka tuyaweke sawa, mimi sina kinyongo na ninakiri kwa kuwa mpumbavu kipindi kile na kuongea maneno ya ajabu kwako , Benadetha usinifanye mjinga kuamini huna mwanaume tokea nilivyoondoka miaka mitano iliopita, hayo mapenzi yalishapitwaga na wakati , ila hayo sio niliokuja nayo leo ninachokuambia ni kwamba wewe ni mrembo sana , ila sikuhitaji kwani nina mpenzi tayari”

Sasa muda ule Roma akiendelea kuangalia kile kinachoendelea , alijikuta akimuona mwanamke akifika hapo ndani ya bar akiwa amevalia kihasara hasara kiasi kwamba alifanya wanaume waliokuwepo kumwangalia kwa uchu, mwanamke yule ni kama alikuwa akijua pa Kwenda kwani aliwasogelea mwanaume anaeitwa Yakobo na Benadetha na alimvyomfikia Yakobo alimbusu shavuni.

Sasa Roma alikuwa akiona yote pamoja na kusikia yote na mpaka hapo aliona Benadetha alikuwa akilazimisha mapenzi , lakini jambo hilo lilimshangaza, kwani kwa maneno ya Benadetha siku chache zilizopita alimwambia kwamba hana mwanaume.

Roma hakutaka kuingilia kwanza alitaka pia kumjua mwanamke aliefika hapo ndani ni nani mpaka Kwenda kumbusu bwana Yakobo ,alichokifanya ni kuangalia watu wengine waliokuwa karibu ambao angehisia kwamba wanamzungumzia yule mwanamke na katika makundi yote aliweza kuona waliokuwa wakimwangalia yule mwanamke na kisha wakawa wanacheka, Roma alirekebisha sikio lake la umbea ili kusikiliza maongezi ya baadh ya kundi hilo..

“Yule jamaa ni fala , usikute pale kawagonganisha wanawake”Aliongea mmoja kwenye kundi.

“Unamjua yule manzi aliefika?”

“Nani asiemjua yule mwanamke ndani ya viunga hivi , yule demu anaitwa Kareni ni mtoto wa Waziri wa Sayani na Teknolojia, inasemekana anapenda ngono balaa kuliko mapenzi”aliongea mwingine na kumfanya Roma kushangaa mwenyewe inakuwaje mwanamke kupenda ngoni kuliko mapenzi.

“Unamaanisha nini Davie?”

“Sikia yule demu hana mapenzi ya dhati , unaweza kuona anakuganda sana ukadhania anakupenda sio hivyo , nasikia anachokitafuta Zaidi ni mwanaume anaemridhisha kitandani tu, na ukiwa mchovu mchovu anakutema ila ukiwa vizuri atakuganda balaa na utakula Maisha , naamini hata yule boya kanasa kwenye mtego wa yule demu na sio muda tu atotoswa , Kareni hatembei na mwanaume Zaidi ya mara tatu , Maisha yake ni kuwabadilisha badilisha tu”Aliongea na kumfanya sasa Roma kuelewa.

“Sina namna inabidi nimsaidie Benadetha kwenye hili swala “Aliwaza Roma kwenye akili yake na kisha kusimama na kuanza kuelekea upande wa ile Meza. Muda huo Benadetha alikuwa ashaanza kutoa machozi kwani Yakobo ilionekana alipanga kumdhalilisha.

Upande mwingine nyuma yake Roma kulikuwa na bwana ambaye hajamtilia maanani , yaani wakati Roma anafika hapo ndani , kuna bwana alikuwa akimwangalia sana.

Mtu huyo hakuwa mwingine bali alikuwa ni Omari , tuliemuona siku kadhaa ndani ya uwanja wa ndege akipokelewa na Matilda pamoja na Queen.

“Hahaha… Hades usiku wangu umekuwa mzuri sana , siamini kama nimekupatia hapa kirahisi”Alijiongelesha yule mwanaume.

“Kaka Mambo!”Omari alisalimiwa na mrembo mmoja alievalia kimini na kumfanya kumwangalia.

“Poa mambo?”

“Salama kaka, naweza kujumuika na wewe , nikupe kampani nimekuona muda wote ukiwa peke yako, si ajabu mpenzi wako atakuwa na mwanaume mwingine muda huu”Aliongea huku akiweka mapozi na kumfanya Omari kutabasamu.

“Kukaa hapa sio shida dada yangu , lakini kukupa ofa ya bia Hapana , nikuweke wazi tu sina hela ,nimekuja na buku jero tu ya bia ya safari na ndio hii inaisha niondoke zangu, kuhusu usafiri nimetumia kirikuu kufika hapa maana hakitumii mafuta mengi ,ila kama utajihudumia sawa , unaweza kukaa”Aliongea Omari huku akigeuza macho upande wa Roma, ni kweli kabisa Omari alifika hayo maeneo kwa kutumia usafiri wa kirikuu na wakat anakuja hakuwa akijali kabisa macho ya watu , alijua mambo yake na mbaya Zaidi ni kwamba alipaki katikati ya V8 mbili.

“Hahaha…”Alijikuta akicheka cheko na haikueleweka alikuwa akifurahia jambo gani kwani macho yake yalikuwa upande wa aliko Roma na kumfanya yule mwanamke aliekuja kujishobokesha kuvuta mdomo na kutafuta mawindo sehemu nyingine.

ITAENDELEA ALHAMISI NICHEKI WATSAPP 0687151346
 
SEMA JAMAA UMEKUA MZINGUAJI HATA KAMA UNATUPA BURE LAKINI HIZI MAMBO ZA KUTOA AHADI ALAFU HUTOKEI UNATUFEDHEHESHA KINOMA
Hakuna haja yabkuwa worked up , ukiona sijaleta tegemea maswala ya dharula
 
Daaah!!! Uyu roma wa sasa namwona ka mwanaume wa DAR,,nmemmic roma wa chinjachinja aiseee
 
Ohooooooo
 
Back
Top Bottom