THE JAGGERS
JF-Expert Member
- Apr 3, 2023
- 545
- 410
Kwel mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kasema AlhamisKwahyo mkuu hapo ndio mpaka wiki ijayo?? Ama ?
Vp 2 hours of memoriesHakuna haja yabkuwa worked up , ukiona sijaleta tegemea maswala ya dharula
OhoooooooSEHEMU YA 376
Ernest alimwangalia Kizwe aliejilaza chini akiwa hana fahamu na kisha alimgeukia Roma na kuona yupo siriasi, alimgeukia Monica ambaye amepoteza fahamu na kisha akamrudia kumwangalia Roma.
“Naomba nimtoe hapa Monica kwanza kabla sijafanya kitendo hicho”Aliongea
“Kwanini , Monica hana fahamu huyo na hawezi kujua?”
“Ni kweli lakini siwezi kumvua mwanamke mwingine nguo , wakati yupo mbele yangu nitakuwa nimemkosea heshima yeye na mwanangu , nipe ruhusa yako nimpandishe juu na nitarudi kufanya kazi yako , lakini kama hakuna namna nyingine nitafanya hivyo”Aliongea kwa kuhuzunika na Roma alitabasamu.
“Hongera umepita kwenye jaribio langu”Aliongea na kumfanya Erenst kushangaa kwa furaha.
“Usishangae , umeniambia maneno matupu kwamba huwezi kulipiza kisasi kwa Edna , lakini pia umesema unampenda Monica kwa dhati , sheria yangu ni moja tu najali sana matendo kuliko maneno , hivyo kama ungefanya kitendo cha kumvua nguo yule mwanamke pasipo kumzingatia Monicana mwanao , ningeamini haumpendi”Aliongea Roma
“Kwasasa nimeona kabisa unataka kuwajibika kama baba na mume , hivyo kwasababu mke wangu amesema nisikuue nitakuacha hai , hata hivyo tatizo lilianzia kwa yule mwanamke “Aliongea Roma na kumfanya Ernest kutokwa na machozi ya furaha , hakuamini kama ameokoka kwenye kifo.
“Utaondoka hapa na Monica wako na sitaki urudi ndani ya kampuni tena , fanya taratibu zote uondoke hapa Tanzania na kurudi ulikozaliwa , kama utapata shida yoyote nitumie barua pepe kupitia kampuni yangu na nitakusaidia, mengine kuhusu wewe sijali tena”Aliongea Roma na Ernest alifurahi sana na kumshukuru Roma , alimwamamsha Monica kwa ajili ya kuondoka.
Baada ya Ernest kuondoka ndani ya nyumba hio kwa maelekezo yake , Roma alijikuta akiwaza tena ni maisha gani ambayo Erest anakwenda kuwa nayo yeye na Monica , aliwaza mtoto atakaezaliwa atakuwa na undugu na Edna japo ni kwa mbali .
Roma alijikuta akijishangaaa yeye mwenyewe kuwazia baadhi ya mambo ambayo hayakuwa yakimuhusu kwani zamani hakuwa hivyo na alijiambia ni kweli ana mabadiliko makubwa tokea afikeTanzania.Roma alipotezea na kisha alisogelea mlango.
“Adeline , unaweza kuingia sasa”Aliongea Roma kwa sauti na hapo hapo mlango ulifunguliwa na mwanamke mzungu alievalia tracksuit
“Mfalme Pluto , usiniambie mimi ndio nakwenda kumvua nguo huyu mwanamke?”Aliongea Adeline huku akitabasamu , Adeline alioenakna alikuwa akisikia maongezi yote kwani walikuwa nje ya jumba hilo na ndio waliowadhibiti wale walinzi waliokuwa wakilinda nyumba hio., sasa Kizwe alikuwa akitoa harufu ya mkojo ndio maana akauliza kwa wasiwasi.
Roma alitabasamu kifedhuli na kisha akamwangalia Kizwe kwa kumchunguza kwa ukaribu.
“Anaonekana kuwa mrembo bado na , ngozi yake inaonekana kuwa laini pia licha ya umri mkubwa, naamini bado atauzika kwa haraka ndani ya macasino Halafu kama unashindwa kumvua nguo kwasababu ya mkojo wake naamini hutaki mimi ndio nifanye kazi hio?”Aliongea Roma na kumfanya Adeline kujutia kwanini hakuondoka mapema kama mwenzake Fanny, umbea wake umemsababishia kuingia kwenye mtego wa kumvua mwanamke anaenuka mikojo.
“Fanya haraka”Alifoka Roma akimwarisha Adeline mzungu na alichuchumaa kwa kutokupenda huku akijiaminisha mwenyewe kwamba ni mkojo pekee hakuna kinyesi.
Dakika chache mbele Kizwe alivuliwa nguo zote na kumfanya Roma kutabasamu kifedhuli , alijiambia Mheshimiwa Jeremy alikuwa akifaidi , ijapokuwa Kizwe hakuwa mrembo kama mama mkwe wake Raheli , lakini Kizwe alikuwa akivutia mno hata kwenye ukubwa wake
Sasa Kizwe sio kama alijikojolea tu , alitoa na kinyesi pia amacho kilitoa harufu isioelezeka
“Njoo kuna kitu nataka nikuambie namna ya kufanya kazi na huyo mwanamke”Aliongea Roma na Adeline alimsogelea
“Mfalme Pluto nikachukue Kamera?”
“Unafikiria ujinga , unafikiri ninafanyaga michezo hio ya kitoto kumtishia mtu na picha za uchi , wanaofanya hivyo ni wahalifu na watu wasio na maadili , usisahau sisi ni watu gani , inaonekana muda wako wa mafunzo ndani ya The Eagels haujakufunza mambo haya mpaka leo? Tunatakiwa kufanya vitu tofauti na wengine , Wewe ni mwanajeshi usie wa kawaida hivyo unapaswa kufanya mambo ambayo wengine hawawezi kufanya”Aliongea Roma na akaendelea.
“Je sisi ni watu wa chini ? , jibu ni kwamba Hapana , nini kinachotutofautisha na watu wa chini ?, Jibu ni Sanaa , Nini maana ya Sanaa ? jibu ni muundo wa kimaisha tofauti na maisha yenyewe ,hio ndio sehemu ya mafunzo yetu ndani ya The Eagles, kama umefikiria nitampiga picha mke wa raisi na kumtishia nazo umekosea ninachotaka ni kitu kikubwa Zaidi, kitu fikirishi, ambacho kipo kisanaa Zaidi , yaani namaanisha kama Movie flani hivi”Aliongea Roma na kumfanya Adeline mzungu kushangaa na kuchanganyikiwa kwa wakati mmoja maana hajamuelewa Roma.
“Mfalme Pluto , kwahio natakiwa kufanya nini?”Aliuliza Adeline na Roma alimsogelea kwenye sikio na kumnong’oneza na kumfanya mwanadada wa watu kutoa macho.
“Mfalme Pluto kwanini tusimuue tu , adhabu unayotaka kumpatia ni ya kikatili sana”.
“Sio ukatili , nishakuambia itakuwa ni filamu iliotengenezwa kisanaa Zaidi , swali je ni nini maana ya Sanaa kwenye filamu? , Jibu ni kwamba filamu ni muunganiko wa Sanaa na fasihi , Sanaa lazima iguse hisia za hadhira bwana ala”
Baada ya Roma kuongea hivyo Adeline alimkusanya Kizwe aliekuwa mtupu na kumfunga funga na mapazia na kisha akamuweka begani na kutoka nae nje , mita kadhaa tu kutoka getini kulikuwa na gari , alimwingiza ndani na kuondoka nae.
Roma baada ya kuona Adeline kaondoka alipumua kwa madakika kadhaa na kisha palepale akayeyuka.
******
Ni usiku wa saa nne Edna alisharudi muda mrefu tu kutoka kazini na alishakula, hata Lanlan pia alishakula na kumuogesha na kulala , yeye alikuwa nje ya Balconi akiwa amekaa kwenye kiti kilichotengenezwa kwa mianzi huku macho yake yote yakiwa getini na upande wa baharini.
Roma mpaka muda huo haukuwa amerudi na alikuwa ameketi hapo nje kumsubiria, ukweli kwa namna Edna alivyorudi ni nje ya mategemo ya Blandina ,Qiang , Yezi na Bi Wema , Edna alionekana kuchoka Zaidi tofauti na alivyokuwa siku ya jana yake wakati kampuni ikiwa kwenye matatizo , huyu alionekana kuwa na wasiwasi mwingi mno sana usiokuwa wa kawaida.
Sasa wanafamilia hao walijjikuta na wenyewe wakihuzunika na walishindwa pia Kwenda kulala, kwani mwonekano wa Edna ulikuwa ukisikitisha na hakuwa akitaka kuongea , Blandina alijikuta akimlaumu mwanae Roma kwa kutokuwa nyumbani muda wote huo , kwani mke wake alikuwa kwenye huzuni na sio yeye tu aliewaza hivyo , kwa kila mmoja alimlaumu Roma kwa kutokuwepo nyumbani mapema.
Edna alikuwa akitoa machozi huku akiyafuta na mkono, licha ya kwamba familia ya Kayage yote ipo huko nje ya nchi , lakini alijiambia hawezi kuiacha familia hio ikiendelea na Maisha duni waliokuwa nayo.
Alijiambia Maisha yake ya makuzi yalikuwa ni juu ya maumivu ya familia hizo zilizokuwa zikiteseka kwenye taifa geni.
Na mara baada ya mama yake kufariki ni kama mzigo wote wa hatia ulihamia kwake , hicho ndio kilichomhudhunisha Edna na kutokujua ni nini anaweza kukifanya kwa wakati huo.
Wakati akiendelea kuwaza mwenyewe huku upepo ukimpuliza hatimae mlango wa kutokea kwenye balkoni ulifunguliwa na alionekana Roma mbele yake , na alisimama na kumsogelea haraka sana.
“Babe Wife naona unanisubiriia?”Aliongea
“Wanaendeleaje , wako wapi?”Aliuliza Edna kwa wasiwasi huku akifuta machozi
“Unamaanisha nani na nani mke wangu?”
“Namaanisha First Lady alieteka familia ya Ernest na Ernest mwenyewe”Aliongea Edna na Roma alijilamba midomo na kisha kumwangalia mke wake, huku akishindwa kuelewa ni kitu gani anahisi kwenye moyo wake baada ya kuulizwa maswali hayo.
“Kwahio umeshindwa kulala kwasababu ulikuwa ukiwawazia?”Aliongea Roma na kumchanganya Zaidi Edna kwani Roma hajibu swali lake.
“Rom,,, ume.. ume ua mtu tena?” Aliongea Edna huku akiwa na wasiwasi mno mpaka kutamani kuachia kilio na kumfanya Roma kumuonea huruma lakini yeye pia kuumia kwa maswali ya Edna.
“Roma naomba unijibu , acha kukaa kimya unanitia uchizi .. ulinahidi hautouwa mtu , niambie”Aliongea Edna huku akijawa na hofiu , aliamini kama Roma kamuua Ernest pamoja na Kizwe si inaanisha kwamba kaua ukoo mzima.
“Wanafamilia wote wa Ernest wako salama , Ernest na Monica washafanya safari kuelekea Marekani muda ninaongea sasa wapo kwenye ndege , kuhusu Kizwe sijamuua ila nitamuadhibu kwa makosa yake na siwezi kumruhusu kutishia Maisha ya watu wako wa karibu tena”Aliongea Roma kwa sauti kavu na Edna alijikuta akipumua kwa ahueni.
“Asante… Asante sana .. hicho ndio nilichotaka kusikia kutoka kwako”Aliongea Edna huku akirudi nyuma.
“Edna inamaana huniamini ?”Aliuliza na kumfanya Edna kumwangalia Roma taratibu machoni
“Sijui ni kipi unanifikiria au unanionaje lakini tokea tumefunga ndoa siku zote nimeishi kwa kudhania ni jambo gani linaendelea kwenye Maisha yako kwasababu kila ambacho kinakusumbua moyoni haukuwa tayari kukiweka wazi na hii imenifanya kushindwa kukufahamu vizuri, nilijitahidi kwa uwezo wangu kuwa muwazi kwa kila kitu ambacho unauliza licha ya kwamba sikutaka kuonyesha baadhi ya makovu na madoa niliokuwa nayo kwenye Maisha yangu ya nyuma , lakini angalau nimekuonyesha upande mzuri Zaidi kuhusu mimi”
“Edna najijua mwenywe nimekosa aibu kutokana na matendo yangu , na nimefanya mambo mengi ya ajabu , lakini likija swala lako siku zote lazima nikuzingatie , sijawahi kufanya kitu bila kukufikiria wa kwanza , wewe kama mke wangu , nimekuacha kwenye kampuni na Kwenda kushughulikia maadui zako , hivi unafikiri nilijisikiaje baada ya wewe kunipigia simu na kuniambia nisiwaue , unafikiri nilijisikiaje kuonyeshewa dharau na yule mwanamke?”
“Edna ifikie hatua nikirudi kama hivi swali la kwanza unalopaswa kuuliza sio wako wapi au wanaendeleaje , nilichotaka kusikia kwako ni kama niko sawa?, sijapatwa na shida yoyote, najua unaniona kama mtu ambaye siwezi kudhurika na chochote lakini mimi pia ni binadamu na nakufa pia kama wengine, mimi sio roboti kwamba sina hisia baada ya kudharauliwa na mwanamke kama yule , ndio ninaweza kudharauliwa na mtu yoyote yule na nikavumilia kwa ajili yako , lakini angalau ujari kile ninachojisikia pia”Aliongea Mfalme Pluto akilalamika mbele ya mke wake , kwa alivyoonekana a ni kama hakuwa Hades au mfalme Pluto anaesifika kwa roho ya kikatili likija swala la kudili na maadui zake.
Kilichomkasirisha Roma ni kitendo cha Edna kutojali hali yake na kukimbilia kuuliza maswali yanayohusu familia yake , hivyo alitafsiri kwamba Edna anajali ndugu zake Zaidi kuliko yeye.
Edna kwa mara ya kwanza alimuona Roma akilalamika kwa muda mrefu hivyo tokea kule Ufaransa , alijikuta machozi yakimtoka , hakujua kama kuuliza swali lile lingemfanya mume wake kuumia , maneno ya Roma pia yalimuumiza kisawa sawa na kila alipojaribu kuongea alishindwa kabisa na kuishia kutoa machozi pekee.
“Okey! Potezea tu maneno yangu,inabidi uamke hapo na ukalae sasa , muda umeenda na kesho una kazi za kufanya , naona hata kubadilisha mavazi umesahau”Aliongea Roma na kisha kugeuka akimwacha Edna anatoa machozi
“Roma.. subiri, unaenda wapi?”
“Sijisikii kulala , ngoja nikapunge upepo , huenda pia nikapata bia mbili tatu za baridi kunituliza kwa sasa, usijali hakuna cha kunisibu huko nje”Aliongea Roma na hakusubiri neno lingine na kisha kuondoka na ndani ya madakika kadhaa aliweza kushuhudia BMW X7 ikitokomea nje ya geti.
Lakini sasa huku nyuma aliacha kilio kwani Edna alieshindwa kumzuia Roma kuondoka alijikuta akikaa chini na kuanza kulia kama mtoto, alilia kama vile hakuna kesho , lakini wakati akiwa kwenye kilio mlango ulifunguliwa na Lanlan alieonekana kufikicha macho na Kwenda kumkumbatia mama yake aliekuwa akilia , haikueleweka nini kilisababisha kuamka muda huo , kwani alikuwa kwenye chumba cha Qiang Xi.
*****
Roma baada dakika kama tatu hivi ya kutoka na gari yake alijikuta akija kusimamisha upande wa kulia kwake ndani ya eneo maarufu la Element, sehemu hio ilikuwa imechangamka sana na ndio maana ilimvutia Roma kwani aliamini sehemu yenye watu wengi inakuwa na mambo mengi , hivyo aliweza kujongea baada ya kuegesha gari lake na kujitafutia nafasi ya kukaa.
Na aliweza kupata meza iliokuwa upande wa nje kabisa karibu na barabara na kukaa chini na ndani ya madakika kadhaa tu alisogelewa na muhudumu akihitaji kuchukua oda yake na Roma aliagiza Windhoek chupa mbili.
Muhudumu yule wa kike alitabasamu na kisha akaitikia kwa heshima kuleta alichoagizwa , Elementi pia kuna tabia moja ya wahudumu kuangalia namna mteja wao anavyofika , unajua hilo ni eneo maarufu ambalo lipo ndani ya mtaa wa wenye nazo , hivyo wanakuchora kuanzia mavazi , simu na namna ulivyoingia, sasa kama umekuja kwa mguu watajua tu hasa hasa madanga wanaofika hapo kuweka mitego , lakini kwa Roma aliweza kufika na gari kali alioichukuaga kipindi alipoenda kudai hela za mkopo za kapuni kule kwa Azizi Ally Temeke.
Roma baada ya kuletewa kinywaji chake alijikuta akivutiwa na meza iliokuwa na mwanaume na mwanamke kwenye kona.
Kitu kimoja unachotakiwa pia kujua kuhusu Roma ni kwamba alikuwa na uwezo wa kusikia mtu hata akiwa kwa umbali mrefu kama wamita mia moja kwa kutumia uwezo wake wa kijini.
Sasa kwa upande wa mwanamke aliekuwa upande wake wa kushoto kutoka sehemu aliokaa na mwanaume , ni kama vile aliweza kumtambua lakini hakuwa na uhakika na ilibidi atumie uwezo wake kumjua ni nani , na alijikuta akishangaa mara baada ya kugundua ni Benadetha.
Roma alijiuliza mwanamke huyo anafanya nini hapo muda huo , lakini hakutaka kuwa na papara , kwasababu Benadetha hakuwa peke yake,Hivyo alitumia uwezo wake kusiki kinachongelewa.
“Benadetha wewe ni mjinga sana , nilikuita hapa sio kuzungumzia mapenzi yetu ya utotoni”Aliongea mwanaume aliekuwa amekaa nae.
“Kama hujaniitia kwa ajili hio Yakobo , umeniitia nini?, hivi unajua ni miaka mingapi nimekusubiria tokea ulivyosema unaelekea nje ya nchi kimasomo , uliniambia siku utakayo rudi tu tutaanza mapenzi yetu na hatimae kunioa , ukaniambia nijitunze kwa ajili yako na wewe utajitunza kwa ajili yangu , unachoongea sikuelewi Yakobo ni nje ya ahadi zako”
“Benadetha kwanza naomba unisamehe , ila nisikudanganye sasa hivi nishapata mwanamke wa hadhi yangu , kipindi naelekea nje ya nchi, nilikuwa na utoto mwingi sana na nikajikuta naongea maneno yasiokuwa na maana , Benadetha hata wewe mwenyewe ulikuwa ukifahamu kipindi kile akili yangu haikuwa sawa , kwanini uliamua kuamini maneno yangu”Aliongea Yakobo na kumfanya Roma kutabasamu kifedhuli.
“Yakobo huwezi kunifanyia hivi , nakupenda Yakobo hivi unadhani maisha yangu yalikuwa rahisi bila ya uwepo wako hapa Tanzania , kwanini unanikataa siku yako ya kwanza kurudi Tanzania? Unafahamu ni wanawake wangapi nimewakataa kwa ajili yako?”
“Sijakukataa Benadetha ila nimekuita hapa kwa ajili ya kuweka jambo langu wazi , ili usije ukavuruga mapenzi yangu na mwanamke ninaempenda ndio maana nikataka tuyaweke sawa, mimi sina kinyongo na ninakiri kwa kuwa mpumbavu kipindi kile na kuongea maneno ya ajabu kwako , Benadetha usinifanye mjinga kuamini huna mwanaume tokea nilivyoondoka miaka mitano iliopita, hayo mapenzi yalishapitwaga na wakati , ila hayo sio niliokuja nayo leo ninachokuambia ni kwamba wewe ni mrembo sana , ila sikuhitaji kwani nina mpenzi tayari”
Sasa muda ule Roma akiendelea kuangalia kile kinachoendelea , alijikuta akimuona mwanamke akifika hapo ndani ya bar akiwa amevalia kihasara hasara kiasi kwamba alifanya wanaume waliokuwepo kumwangalia kwa uchu, mwanamke yule ni kama alikuwa akijua pa Kwenda kwani aliwasogelea mwanaume anaeitwa Yakobo na Benadetha na alimvyomfikia Yakobo alimbusu shavuni.
Sasa Roma alikuwa akiona yote pamoja na kusikia yote na mpaka hapo aliona Benadetha alikuwa akilazimisha mapenzi , lakini jambo hilo lilimshangaza, kwani kwa maneno ya Benadetha siku chache zilizopita alimwambia kwamba hana mwanaume.
Roma hakutaka kuingilia kwanza alitaka pia kumjua mwanamke aliefika hapo ndani ni nani mpaka Kwenda kumbusu bwana Yakobo ,alichokifanya ni kuangalia watu wengine waliokuwa karibu ambao angehisia kwamba wanamzungumzia yule mwanamke na katika makundi yote aliweza kuona waliokuwa wakimwangalia yule mwanamke na kisha wakawa wanacheka, Roma alirekebisha sikio lake la umbea ili kusikiliza maongezi ya baadh ya kundi hilo..
“Yule jamaa ni fala , usikute pale kawagonganisha wanawake”Aliongea mmoja kwenye kundi.
“Unamjua yule manzi aliefika?”
“Nani asiemjua yule mwanamke ndani ya viunga hivi , yule demu anaitwa Kareni ni mtoto wa Waziri wa Sayani na Teknolojia, inasemekana anapenda ngono balaa kuliko mapenzi”aliongea mwingine na kumfanya Roma kushangaa mwenyewe inakuwaje mwanamke kupenda ngoni kuliko mapenzi.
“Unamaanisha nini Davie?”
“Sikia yule demu hana mapenzi ya dhati , unaweza kuona anakuganda sana ukadhania anakupenda sio hivyo , nasikia anachokitafuta Zaidi ni mwanaume anaemridhisha kitandani tu, na ukiwa mchovu mchovu anakutema ila ukiwa vizuri atakuganda balaa na utakula Maisha , naamini hata yule boya kanasa kwenye mtego wa yule demu na sio muda tu atotoswa , Kareni hatembei na mwanaume Zaidi ya mara tatu , Maisha yake ni kuwabadilisha badilisha tu”Aliongea na kumfanya sasa Roma kuelewa.
“Sina namna inabidi nimsaidie Benadetha kwenye hili swala “Aliwaza Roma kwenye akili yake na kisha kusimama na kuanza kuelekea upande wa ile Meza. Muda huo Benadetha alikuwa ashaanza kutoa machozi kwani Yakobo ilionekana alipanga kumdhalilisha.
Upande mwingine nyuma yake Roma kulikuwa na bwana ambaye hajamtilia maanani , yaani wakati Roma anafika hapo ndani , kuna bwana alikuwa akimwangalia sana.
Mtu huyo hakuwa mwingine bali alikuwa ni Omari , tuliemuona siku kadhaa ndani ya uwanja wa ndege akipokelewa na Matilda pamoja na Queen.
“Hahaha… Hades usiku wangu umekuwa mzuri sana , siamini kama nimekupatia hapa kirahisi”Alijiongelesha yule mwanaume.
“Kaka Mambo!”Omari alisalimiwa na mrembo mmoja alievalia kimini na kumfanya kumwangalia.
“Poa mambo?”
“Salama kaka, naweza kujumuika na wewe , nikupe kampani nimekuona muda wote ukiwa peke yako, si ajabu mpenzi wako atakuwa na mwanaume mwingine muda huu”Aliongea huku akiweka mapozi na kumfanya Omari kutabasamu.
“Kukaa hapa sio shida dada yangu , lakini kukupa ofa ya bia Hapana , nikuweke wazi tu sina hela ,nimekuja na buku jero tu ya bia ya safari na ndio hii inaisha niondoke zangu, kuhusu usafiri nimetumia kirikuu kufika hapa maana hakitumii mafuta mengi ,ila kama utajihudumia sawa , unaweza kukaa”Aliongea Omari huku akigeuza macho upande wa Roma, ni kweli kabisa Omari alifika hayo maeneo kwa kutumia usafiri wa kirikuu na wakat anakuja hakuwa akijali kabisa macho ya watu , alijua mambo yake na mbaya Zaidi ni kwamba alipaki katikati ya V8 mbili.
“Hahaha…”Alijikuta akicheka cheko na haikueleweka alikuwa akifurahia jambo gani kwani macho yake yalikuwa upande wa aliko Roma na kumfanya yule mwanamke aliekuja kujishobokesha kuvuta mdomo na kutafuta mawindo sehemu nyingine.
ITAENDELEA ALHAMISI NICHEKI WATSAPP 0687151346
Hupokei simu