Mkushi w jani
JF-Expert Member
- Oct 2, 2021
- 1,798
- 1,570
weekend kamokoMkuu ratiba inasemaje?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
weekend kamokoMkuu ratiba inasemaje?
shukhran mkuuweekend kamoko
sawa bhana mkuu si tupobadae mzigo unashuka
twasubiliabadae mzigo unashuka
SawaNILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
BY SINGANOJR
SEASON 16
SEHEMU YA 451.
Roma na Mage waliweza kurudi mpaka Ununio nyumbani kwa Roma na kumkuta Edna bado akiwa eneo la sebuleni akisubiria , alionekana kuwa na wasiwasi mno kutokana na kwamba kama taarifa zingetoka na mshukiwa wa mauaji kuwa ni Seekretari wake basi ingekuwa taarifa mbaya kwa kampuni yake hivyo kupelekea hisa kushuka.
“Vipi Recho kashatoka kituoni?”Aliuliza Roma.
“Bado ila mwanasheria wangu ashaenda kituoni , amesema inawezekana akatoka bila shida yoyote kwani hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa kusema ndio kahusika na kifo cha Dina, Vipi Mage mmeweza kupata nini kwenye kuuchunguza mwili? Maana nina wasiwasi jambo hili lisije kumuathiri Recho na mimi pia ndio maana nataka mpaka asubuhi kila kitu kiwe sawa”
“Hii kesi naamini inakwenda kuwa rahisi kiuchunguzi tu , lakini kwenye kuhitimisha itakuwa changamoto”Aliongea Roma na kumfanya Edna kushangazwa na kauli hio , lakini Roma ilibidi aelezee mwanzo mwisho kwa kile walichoweza kugundua.
Baada ya kumaliza kuongea , Edna alijihisi kichwa chake kitampasuka baada ya kusikia muhusika anaweza kuwa ni Vampire .
“Edna unakumbuka uliniuliza swali kwanini sikuonyesha furaha nilivyokuwa mbele ya Msanii Nessa”
“Ulijibu sijui baba yake ana nini?”
“Ndio ,Nessa baba yake mzazi ni wa jamii hii ya Wanywa damu(Blood Race) lakini si hivyo tu , kama utakuwa na elimu ya kisaikolojia kuweza kugundua watu mapema basi ungeweza kugundua Msanii Dina alikuwa akiongea Kinafiki mbele ya Nessa”
“Unamaanisha nini kuongea Kinafiki?”.
“Aura ya Nessa na Dina zinafanana kwa asilimia sabini , Nessa pia anatokea kwenye kabila la wanywa damu kutokana na baba yake , lakini upande wa Dina pia anatoa Aura inayotolewa na watu wa jamii ya wanywa damu”
“Kwahio unamaanisha na Dina ni Mnywa Damu?”Aliuliza Mage kwa mshangao.
“Hapana ila kuna uwezekano Dina alikuwa kwenye mabadiliko ya kutoka kuwa binadamu wa kawaida na kuwa Vampire”Aliongea Roma
Aura ni kama mionzi au miale ama Vivuli vinavyokaa mwilini mwa kiumbe hai , vinamvyomzunguka mwili wake mzima , unaweza kusema kwa lugha ya kiswahili ule msisimko binadamu anaotoa.
Katika ulimwengu wa roho unaweza kukutana na wachawi wanasema mtu flani harogeki, lakini mtu anaezungumziwa unakuta anaongoza kwa dhambi au hana dalili yoyote ya kumuogopa Mungu , lakini wakati huo huo hana dalili yoyote ya kutegemea nguvu za kichawi kama kinga, sasa kinachomlinda binadamu na wachawi ni msisimko unaofahamika kwa jina la Aura , msisimko ambayo unatofautiana ukubwa baina ya mtu na mtu , kuna mwingine ana Aura ambayo haina nguvu kubwa na ikawa rahisi kurogeka na kuna mwingine ana Aura kali kiasi kwamba haina haja hata ya kufanya chochote kujilinda na nguvu za mapepo mabaya au wachawi.
Sasa basi Aura anayotoa binadamu licha ya kutofautiana kati na mtu na mtu , lakini inafanana kwa asilimia mia moja na inatofautiana vilevile na kiumbe ambacho sio binadamu wa kawaida , kwa mfano Aura inayotoka kwa Jini ni tofauti na Aura itakayotoka kwa Vampire.
Anachomaanisha Roma sasa ni kwamba Dina alikuwa akitoa Aura ambayo inafanana na ya Nessa ambaye ni kutoka Jamii ya Vampire.
Ni ngumu pia sana kwa binadamu wa kawaida kuhisi Aura ya Vampire kutokana na kwamba wana uwezo mkubwa wa kuficha Aura zao wanapokuwa katikati ya kundi la watu nyakati za usiku na ili kuweza kuwatambua ni lazima uwe na nguvu kubwa ya kichawi au kijini(Dark Spirit energy).
“Katika mchakato wa binadamu wa kawaida kuweza kubadilika kwenda kuwa Vampire kuna hatua ambayo inafahamika kwa jina la ‘Initial Embrace’ huu ni mchakato ambao Vampire anafyonza damu ya binadamu wa kawaida ambaye anataka kumbadilisha kwa kiwango kikubwa na baada ya hapo atairudisha tena damu hio baada ya kuchanganyika na ya kwake kwenda kwa binadamu wa kawada na ndipo mchakato wa kubadilika kuwa vampire utaanza mara moja , ni kitendo kinachochukua zaidi ya miezi au mwaka ,unaweza kuita ‘reverse blood transfusion”Aliongea Roma.
Ndio ‘Initial Embrace’ kwa lugha nyepesi ni kama uchukue damu ya Vampire na kisha uchanganye na damu ya binadamu wa kawaida na kisha ujitundikie dripu lenye damu mchanganyiko.
Kitendo hichi kinaitwa Initial Embrace kutokana na kwamba ni mchakato ambao mara nyingi hufanywa kwa maridhiano ambayo huenda sana sana yakawa ni ya kimapenzi , yaani Vampire kujihusisha kimapenzi na binadamu wa kawaida.
“Kutokana na utofauti uliopo kati ya binadamu wa kawaida na Vampire , sasa kuna umakini mkubwa sana unaohitajika katika kuchanganya hizi damu , kwani kama damu ya binadamu wa kawaida ikazidiwa kiwango na damu ya Vampire basi itapelekea moyo kushindwa kusukuma damu na unakufa hapo hapo, hivyo ni jaribio la hatari sana kufanyika”Aliendelea Roma kuongezea
“Kwahio unachomaanisha ni kwamba Dina alitaka kuwa Vampire, na kwanini?”Aliuliza Mage.
“Unatakiwa pia kuelewa kwamba , sifa kubwa ya Vampire hawazeeki haraka licha ya kwamba kuna mwisho wa siku wanapoteza uhai, lakini pia sifa kubwa ni kwamba damu ya Vampire humtengenezea mtu mvuto wa aina yake , hivyo kama ni msanii anaweza kupata mafanikio makubwa sana ndani ya muda mfupi, hivyo kuna uwezekano Dina alihitaji kurefusha maisha yake kwa kutozeeka haraka , lakini wakati huo huo akitaka mvuto, Hata hivyo siku za hivi karibuni Vampire wameweza kugundua teknolojia inayowawezesha kuishi kabisa nyakati za mchana bila shida yoyote, ni teknolojia ya kimiminika maalumu ambacho wanachanganya na damu”Aliongea
“Kwa maelezo yako naamini kabisa sio Nessa aliehusika licha ya yeye pia kuwa wa jamii ya Wanywa damu”
“Upo sahihi Edna na hicho ndio kinanifikirisha hapa , kwanini wakamshambulia Dina na sio mtu mwingine na isitoshe Dina alikuwa karibu kuwa jamii yao, hili linaniambia kuna zaidi ya binadamu Vampire ndani ya Tanzania”
“Kama maelezo yako ni sahihi kwanini Recho alama za vidole zimekutwa kwenye kisu?”Aliuliza Edna.
“Mage kisu kimekutwa sehemu gani?”Aliuliza Roma.
“Juu ya Sink la kunawia mikono”Aliongea.
“Sasa ni kikujibu swali lako Edna ni hivi Vampire wana mbinu yao ya kumfanya binadamu wa kawaida kufanya kitu anachotaka pasipo ya wao wenyewe kufahamu inafahamika kwa jina la Kingereza la ‘Totem of Hypnosis’, hivyo kwa maelezo ya kueleweka hapa inawezekana Recho akili yake ilikuwa ikiongozwa na Vampire na kuna uwezekano baada ya tukio la kumuua Dina ,Recho alibeba kisu na kukipeleka mpaka juu ya Sink na hapo ndipo aliporejewa na akili yake, inawezekana hata kitendo cha Recho kushikwa na haja ndogo ilikuwa ni kazi ya Vampire, pia ninahiai pia aliefanya hivi ni kutaka kuchafua taswira ya kampuni ya Vexto”Aliongea Roma na kumfanya Edna na Mage kuangaliana.
“Sema Roma kama ulikuwa hayo yote kwanini usingefanya chochote muda ule ule , huenda hata Dina asingekufa”
“Babe wewe huelewi na ungekuwa unafautilia hata mitandao ungeweza kugundua kuna watu wengi walijaribu kuuliza maswali mtandaoni namna ya kujibadilisha na kuwa Vampire, watu wengi wanapenda kuwa jamii hio ili waweze kuishi maisha marefu, hata hivyo sijali sana kuishi kwake kwasababu sio kwamba ningemsogelea na kumtongoza kwasababu Babe wewe ndio mwanamke pekee ulieujaza moyo wangu”Aliongea Roma lakini alijikuta akifinywa kwa nguvu na Mage pasipo ya Edna kuona
“Uongo wa Karne huo”Alijibu Edna huku akivuta mdomo , lakini ukweli ni kwamba alijisikia wa pekee kusifiwa mbele ya Mage, lakini wakati huo huo Roma alitumia mkono wake wa kulia kumpeti peti Mage kiaina kumtuliza , ni kama alikuwa akimwambia natania tu hata wewe pia upo moyoni.
“Kama walimtumia Recho kuonekana muhusika wa mauaji ya Dina, je ni kwasababu ipi maana sidhani tunaweza kuwa na ugomvi nao mpaka watake kuharibu taswira ya kampuni yangu”
“Hilo tutaweza kufahamu kama tu tutafanikisha kumkamata muuaji”Alijibu Roma
“Roma naamini una mpango wa kuweza kumkamata si ndio?”Aliuliza Mage.
“Ningekuwa na mpango nigekuwa nishamkamata mpaka sasa, Ninaweza kufuatilia harufu yao lakini sijui nianzie wapi , Blood Race wana uwezo wa kuruka kutoka eneo moja kwenda lingine kwa spidi kubwa sana kiasi kwamba hata macho ya binadamu hayawezi kuona , Kumtafuta muuaji ni kama kutafuta shilingi iliorushwa baharini”Aliongea na kumfanya Edna kujikatia tamaa.
“Kama hata wewe huna mbinu yoyote ya kumpata muuaji , basi sidhani kama kutakuwa na uwezekano wa kumkamata na hatuwezi pia kuitisha kikao na waandishi wa habari na kusema kwamba aliemuua Dina ni Vampire nani ataweza kutuamini ni dhahiri lawama zote zitamwangukia Recho”Aliongea Mage.
“Kaaa kwa kutulia , ninaweza kukosa mbinu lakini haimaanishi kwamba nimeshindwa kabisa , Unatakiwa pia kuelewa kwamba Jamii hii ya watu wa Blood Race wana mazuio makuu sita ya kisheria na moja wapo ni inayofahamika kwa jina la Seclusion(Kujitenga), hivyo ni lazima viongozi wake watamtafuta na kumpatia adhabu , swala litakalotupatia wepesi”Aliongea Roma
Roma aliona swala hilo kama jepesi sana kwani haikuwa ikijalisha kwamba muhusika alikuwa akitoka kwenye kundi la Savath au Camarilla , lazima apatiwe adhabu yake ya kifo kwa kuvunja sheria , Roma aliamini mbinu rahisi ni kumshirikisha mtu anaemfahamu kama Vampire kutoka ukoo wa Venture ili swala hilo liweze kushughulikiwa na wao wenyewe.
Kabila la Venture ni moja wapo ya makabila makubwa katika makabila therathini ya Vampire na ndio waliokuwa wakiongoza kundi la Camarilla, hata hivyo ashawahi kusaidia moja wapo ya viongozi wa kundi hilo , ambaye ni Lilith pamojana Prince Sargaras kule Ufaransa.
Roma alitumia simu yake na kutuma ujumbe kwenda kwa Lilith kupitia Email, Roma hakutaka kumpigia kwani alijua kabisa Lilith angeweza kuropoka na siri kugnndulika kwani alishawahi kumnyandua.
Roma alimrudisha Mage kwenda nyumbani kwao na walipokuwa wanakaribia Kawe ndipo Mage alipoweza kupata taarifa kutoka kituo cha Oysterbay alichoshikiliwa Recho kwamba ameruhusiwa kwa kuwekewa dhamana , ilikuwa rahisi kwa Recho kutolewa kwani Mwanasheria alitoa hongo ya pesa.
Roma alimpigia Recho kumwambia kwamba amsubiri aje amsindikize nyumbani , lakini Recho alisisitiza kwamba angechukua usafiri wa Taksi kurudi nyumbani na Roma hakuwa na haja ya kumlazimisha na alimwambia akampuzike na kila kitu kitakuwa sawa.
*****
Recho baada ya kuachwa na mume wake kwa Talaka Mahakamani aliweza kurudi nyumbani na kuendelea kuishi na familia yake ,inasemekana mume wa Recho alikuwa akimnyanyasa sana na hio yote ni kutokana na Recho kutoweza kupata ujauzito tokea alipoolewa kwa miaka mitano mfululizo.
Manyanyaso aliokuwa akiyapata kutoka kwa familia ya wakwe zake pamoja na mume wake yalimchosha na ndio iliompelekea kurudi kuishi na wazazi wake, Recho alikuwa msichana mwenye akili sana ya kimaisha lakini alikuwa akipitia changamoto sana katika mahusiano.
Lakini licha ya madhaifu yote aliokuwa nayo , alikuwa tegemezi kubwa sana kwa familia yake kuanzia wazazi wake ambao hawakuwa na maisha ya juu lakini pia kwa wadogo wake ambao bado walikuwa wakisoma.
Recho alikuwa kama mke wa Hakimi tu , kwani licha ya kwamba aliolewa na mwanaume tajiri lakini aliachwa bila ya kupata hata senti tano zaidi ya kuondoka na nguo tu alizonunua akiwa kwenye ndoa, ilikuwa afadhali sana kwake kwani alikuwa amesoma na kuajiliwa na kampuni kubwa nchini ya Vexto.
Hivyo hata mara baada ya kupandishwa cheo na kuwa Sekretari wa Edina maisha yake yalibadilika kwa kiasi kikubwa , kwanza mshahara alikuwa akipata mara tatu ya mshahara aliokuwa akipata mwanzo na hilo lilimsaidia sana kuitoa familia yake kwenye Kota za Jeshi Lugalo na kuweza kuhamia kwenye nyumba ya kupangisha maeneo ya Ubungo kibada.
Saa tisa kasoro Recho aliweza kushushwa na gari aina ya Nissani nyeusi , ambayo ilikuwa ikitumika kama Taksi.
Nyumba aliokuwa akiishi na wazazi wake ilikuwa mita kadhaa kutoka barabarani , gari haikuwa na uwezo wa kwenda kusimama nje ya nyumba yo kutokana na kwamba chocho ilikuwa nyembaba hivyo ilimlazimu kutembea wa miguu bara baada ya kushushwa, hakuwa na woga kwani eneo hilo halikuwa na vibaka wengi , lakini siku hio alijihisi ni mwenye hofu kutokana na kwamba eneo hilo lilikuwa limetulia mno kuliko isivyo kawaida yake , kwani hakuweza kuona mtu yoyote ambaye alikuwa akikatiza kwenye mtaa wao.
Alipiga hatua kadhaa tu akiwa ameikaribia nyumba yao mara , mbele yake alionekana mtu akija kwa kutembea kwa kasi na moyo wake ulimpiga Paah , kwani haikuwa kawaida kumuona mwanaume wa Kizungu maeneo hayo hasa nyakati za usiku kama huo.
Kilichomshangaza ni kama vile alikuwa kwenye ndoto, Recho alijaribu kurudi nyuma kutaka kukimbia lakini alishindwa kupiga hatua , alijaribu kujilazimisha kupiga hatua kwenda mbele , lakini vile vile alishindwa kupiga hatua , alijikuta akitaka kutoa ukulele lakini vile vile sauti iligoma kumtoka , ilikuwa ni kama jinamizi limemkamata , alijikuta akiishia kutoa machozi huku akimwangalia mwanaume wa kizungu akimkaribia.
Lazima ingeogopesha kwani ni jambo ambalo halikuwa la kawaida kwa eneo ambao limekaa kimasikini kama hilo Mzungu kuonekana, Aliishia kumwangalia yule mzungu akimsogelea mpaka alipokuja kusimama mbele yake.
“Tell me your name”Yule mzungu aliongea kwa lugha ya kingereza
“I am Recho Kabwela”Alijibu Recho huku mapigo ya moyo wake yakienda mbio mno, hunenda angezimia kabisa kama angeweza kusikia simulizi za Vampire kutoka kwa Roma.
“What is your job?”
“The CEO passistant … at Vexto group of companies”Alijibu kwa wasiwasi huku akisema kwamba ni msaidizi wa CEO ndani ya kampuni ya Vexto ,lakini mara baada ya kutoa jibu lile uso wake ulibadilika mwonekano wake na alitoa tabasamu mwanana kabisa kama vile kuna kitu kizuri kimemfurahisha.
Palepale yule mwanaume wa kizungu ghafla tu kucha zake za mikono zilirefuka kwenda mbele na kuwa kama za paka anaetaka kuvamia mtu , lakini vile vile meno yake mawili yalirefuka , huku sura yake ikitengeneza michirizi ya kijani kuanzia kwenye eneo la mdomoni mpaka kwenye macho , lakini sio hivyo tu macho yake kiini chake kilibadilika Rangi na kumfanya kuwa mtu wa kutisha mno.
Alikuwa ni Vampire kabisa na ni dhahiri alikuwa anadhamiria kumnyonya damu Recho.
Jambo la kushangaza ni kwamba licha ya kubadilka mwonekano , lakini Recho aliendelea kumwangalia mtu wa kutisha mbele yake kwa kuweka tabasamu vile vile huku akionyesha hana hata dalili ya kutaka kukimbia.
“Traaa…!!!”
Gauni alilovaa Recho lilichanwa mara moja na kucha za yule Vampire na alianza kupeleka pua zake kunusa katika maeneo ya siri ya Recho na lilionekana kuridhishwa na harufu nzuri ya homoni iliochanganyika na marashi.
SEHEMU YA 452.
Vampire lile lilisogelea nguo nyeupe ya ndani ambayo amevaa Recho na kwa mwembwe zote aliichana mara moja na kumbakisha Recho na Chupi tu , lakini bado iliendelea kushangaza kwani licha ya matendo ya Vampire kufanya hivyo , Recho aliendelea kutabasamu , ni kama kitendo anachofanyiwa kilikuwa kikimfurahisha.
‘BOOM!”
Kitendo cha Vampire kutaka kumchania tena Recho ile Chupi pekee iliobakia kwenye mwili wake , lilipigwa pigo la aina yake na kwenda kugonga kwenye ukuta wa nyumba kwa kishindo kikubwa.
Muda huo huo Roma aliweza kujitokeza mbele ya Recho na kumchapa kibao usoni na palepale Recho aliweza kushituka kama mtu aliekuwa usingizini.
Roma hakumjali Recho kwanza , tageti yake ilikuwa Vampire , haikueleweka alijua vipi Recho angeweza kufuatiliwa na Vampire mpaka kufika eneo hilo na kumuokoa .
Vampire licha ya kupigwa pigo la uhakika la kijini na Roma , lakini liliweza kupona kwa haraka sana na kusimama wima huku likionyesha hali ya kukasirika mno , kwani kucha zake ziliongezeka urefu maradufu huku likiachama midomo yake kwa ukubwa zaidi.
Roma alimwangalia Recho na kuona ashatoka kwenye ‘Hypnosis’ na kutabasamu kidogo.
“Vipi upo sawa”Aliongea Roma huku akigeuza macho kwa lile Vampire ambalo lilionyesha kujiandaa kwa mashambulizi , lakini Recho alijikuta akitoa ukulele baada ya kugundua yupo uchi, lakini alivyoangalia mbele na kuona kiumbe cha kutisha alitimua mbio na kwenda kujificha kwenye kona ya nyumba upande wa kushoto huku mkono mmoja ukiwa umeziba sehemu za siri na mkoba na mkono mmoja akiwa ameweka mdomoni kutotoa ukulele.
“Who is there?”
Vampire lilitoa sauti ya kuuliza nani yupo mbele yake , lakini Roma hakujibu na hapo hapo lile Vampire kwa spidi kubwa lilimsogelea Roma huku kucha zikiwa mbele na lilionekana kumlenga eneo la kwenye macho , Roma hakujisumbua na shambulio lake , tena hata mikono haikuitoa mfukoni kwani wakati lilipomfikia alionekana kunuia jambo na palepale lile Vampire lilirushwa mbali na kurudi tena na kujipigiza kwenye ukuta huku awamu hii ikiwa na mshindo mkubwa mno.
Roma hakulipa nafasi ya kupona na palepale alikimbia kwa spidi ya hali ya juu kama mwanga na kulitwanga teke eneo la kifuani mpaka kupelekea mbavu kuvunjika na palepale lilitema damu kwa namna ya kukohoa huku likishindwa kusimama.
“Ni kwamba tu mimi sio Vampire hivyo siwezi kutumia mbinu ya kuku ‘hypnotize’ ila nitakuhoji kwa namna ya maumivu makali kama tu huwezi kunipatia majibu ninayo yataka, Anza kunniambia majina yako kamili na umetokea kwenye kabila lipi , Mister Vampire”Aliongea Roma huku akiwa ameweka mikono mfukoni.
“Wewe ni.. nani?”Lilijitahidi kunyanyua sura na kumwangalia Roma kwa hofu huku likimuuliza yeye ni nani, lakini Roma aliliongezea teke lingine kwenye kifua palepale alipopiga mwanzo na kulifanya liteme tena damu huku likiugulia maumivu.
“Nauliza maswali hivyo nataka majibu tu , ukishindwa kunijibu nitautoa moyo wako na kuusambaratisha”Aliongea Roma na kumfanya yule mwanaume palepale kumwangalia Roma kwa macho ya hasira lakini hakuwa na chakufanya hivyo aliweza kurejea kwenye mwonekano wa kibinadamu , huku bado akiendelea kuugulia maumivu.
“I am Mourihno”Aliongea
“Jina zuri , niambie wewe ni kizazi cha ngapi na unatokea kabila lipi?”
“Sijui kizazi changu na sina kabila”Alijibu kwa lugha ya Kingereza
“You are peasant , What the terms it is.., Let me think Oh Yeah Caitiff?”
“Wewe ni Peasant , Wanatumia jina gani kuwaita , ngoja nifikiri , Oh ndio Caitif”Aliongea Roma mara baada ya kukumbuka.
“Sipendi kuitwa kwa jina la kundi hilo , lakini upo sahihi”Alijibu Vampire Mourihno kwa sauti ya kugugumia.
“Nishawahi kusikia kuhusu ‘Peasant’ ni wale Vampire ambayo wamefukuzwa kwenye koo au binadamu waliojibadilisha kuwa Vampire bila ya kupata ruhusa kutoka kwa viongozi , Inaonyenyesha maisha yako ni magumu mno kuishi bila sapoti ya ndugu, Vipi umekuja Tanzania kwasababu ulishindwa kuvumilia manyanyaso ndani ya bara la Ulaya?”Aliuliza Roma na kumfanya Mourihno kuogopa.
“Nilikamatwa na kuletwa hapa Tanzania”Aliongea na kumshangaza Roma.
“Nani kakukamata?”
“Unaonekana kuwa binadamu mwenye nguvu kubwa sana hivyo siwezi kushindana na wewe , lakini naomba kufahamu kama utaniachia kuwa hai kabla sijajibu maswali yote ,Sitaki kupoteza nguvu zangu kukujibu maswali yako ilihali ninakwenda kufa”Aliongea na kumfanya Roma kukuna kichwa kwanza
“Unaonekana kuwa Vampire mwenye akili , haya kama utanijibu maswali yangu yote nitakuachia hai”Aliongea Roma na kumpa ishara Vampire Mourihno kusimama.
Na lilionekana tayari limekwisha kupona tayari kutoka kwenye majeraha yake kwa spidi kubwa na ilikuwa likijifanyisha kuwa kwenye maumivu.
“Haya ni jibu maswali yangu , kwaninni ulitaka kumuua Recho Wewe ndio umemuua Msanii Dina na nani amekukamata na kukuleta hapa Tanzania?”Aliongea na Mourihno alionekana kushangaa.
“Nini! mimi nimuue Dina , haiwezekani nilichokuwa nikifanya hapa ni kulipiza kisasi”Aliongea.
“Explain..”
“Jielezee”Aliamrisha Roma.
“Sijui naanzaje kujibu lakini naweza kusema kwamba mtu alienikamata na kunileta hapa Tanzania ni Mchina, Mimi na wenzangu wachache tulijishitukia tupo ndani ya maabara , nadhani walichohitaji kutoka kwetu ni damu , kwani walitoa damu nyingi katika mwili wangu na nikapoteza fahamu na wakadhania labda nimekufa hivyo waliweza kunizika lakini sikuwa mfu hivyo nilitoka kwenye kaburi , kujibu swali lako lingine kama nilivyosema nilikuwa nikilipiza kisasi kwani Dina alikuwa ni mpenzi wangu na nilikuwa nikifanya taratibu za kumbadilisha na kuwa Vampire kama mimi , lakini nimeweza kupata habari leo usiku kwamba ameuliwa na mwanamke afahamikae kwajina la Recho Kabwela hivyo nilikuwa nikitaka kumuua kwa kulipiza kisasi”Aliongea na kumfanya Roma kushangazwa na majibu yake , hapo hapo akili yake ilianza kufanya kazi hususani kwenye neno ‘maabara’
“Inawezekana ni Yan Buwen ndio aliewakamata na kuwaleta Tanzania”Aliwaza Roma .
Ilionekana kuwa mantiki kwake kufanya majaribio ya kisayansi kwa kutumia damu ya Vampire , sababu ya kuchagua Vampire ambao ni Peasanr ni kuamini kwamba hakuna atakaejali kwani kwanza wamekwisha kutelekezwa
Roma alijikuta akiona sasa inawezekana ndio maana hata Clone iliotumwa kumshambuliaAmina siku ile ilikuwa na uwezo wa kujiponyesha , Roma alijiambia kweli Yan Buwen ni mwendawazimu na ni mshindani wa kuchukuliwa siriasi.
“Haukuwa makini angalau ungetumia mbinu ya kumlewesha na kuanza kumhojji kuthibtisha kama yeye ndio amehusika na kifo cha Dina kuliko kuchukua maamuzi ya kumuua , nina kuhakikishia sio yeye bali ni Vampire mwingine”Aliongea na kumfanya Mourihno kushangaa.
“Kweli?”
“Maisha yako yapo mikononni mwangu , kwanini nikuongopee”
“Nakuamini wewe , siku zote watu wenye nguvu kama wewe mnakuwga na kanuni zenu najua mimi ni dhaifu kuliko wewe lakini je unaweza kunisaidia kumtafuta huyo mshenzi nitahakikisha na unyofoa moyo wake mimi mwenyewe , Dina anaweza akawa hakunipenda , lakini alikuwa ni mwanamke wangu”
“Kwanini uliamua kumchagua ,inaonyesha kwamba alitaka kuwa Vampire kwasababu alitaka kutokuzeeka”
“Aliweza kunisaidia kwenye kipindi kigumu cha maisha yangu , Hakuwa akiniogopa hata wakati nilipokuwa nikiifyonza damu yake zaidi ya kuniangalia kwa upole na upendo, haijalishi kama hakunipenda lakini ukarimu wake nilioweza kuhisi kutoka kwake ni kitu ambacho sikuweza kukipata kwa miaka mia moja nilioweza kuishi hapa duniani”Aliongea na kumfanya Roma kutoa pumzi za afadhali , Hata hivyo licha ya kwamba binadamu wengi walikuwa wakiogopa Vampire kama wafu waliofufuka lakini walikuwa na moyo unaodunda na wakipenda wanapenda kweli na wanakuwa wanashukuru kwa ukarimu wanaofanyiwa
“Okey Mourihno nakupa kazi ya kuwatafuta Vampire wengine waliopo ndani ya jiji hili la Dar es salaam kwasababu unaweza kunusa harufu zao kuliko mimi na kama utawapata nitaarifu , naishi sehemu moja inaitwa Ununio”Aliongea Roma na kumfanya Mourihno kutingisha kichwa haraka haraka na kukubali na alipotea.
Roma alimfuata Recho ambaye alikuwa amejikunja kwenye ukuta akiwa ni mwenye kutetemekana, Roma alimwonea huruma kwani alijua alicho kishuhudia ni nje ya uwezo wa binadamu.
“Pole sana Recho, nilijua kuna uwezekano utashambuliwa ndio maana nilikufatilia kwa nyuma ,lakini sikutaka kuchukua hatua kwani nilitaka kwanza kupata ushahidi”Aliongea na kumfanya Recho palepale kuanza kutoa kilio cha kwikw.
“Roma .. Roma… niambie nilichoshuhudia ni ndoto , nieleze tafadhari”Alionekana kuwa dhaifu mno kulikoRoma alivyotarajia
“Sio ndoto , mtu aliemuua Dina ni Vampire na hata mwanaume huyu wa kizungu uliemwona hapa ni Vampire , Haikuwa akili yako wakati es kushika kisu kilichomuua Dina, Unatakiwa sasa kuelewa zile Muvi unazoangalia na ulicho shuhudia leo ni uhalisia , hata hviyo usijali nipo hapa kwa ajili ya kukupa ulinzi “Aliongea Roma kwa namna ya kubembeleza na kumfanya Recho kumwangalia Roma na kisha akafuta machozi ,ijapokuwa alikuwa kwenye woga lakini kitendo cha Roma kumuokoa na kitu cha kutisha siku hio kilimfanya kumuona kama malaika.
“Roma nataka kujua , uko hivi kwa kila mwanamke?”
“Acha kunitania bwana , ningekuwa hivi nisingekuwa naomba msahama kila mara kwa mke wangu”
“Hapana kila mwanamke kasoro mke wako wanasema wewe ni mwanaume mwenye moyo mzuri wa kujali”Aliongea Recho na kumfanya Roma kufikiria kidogo , lakini alipotezea kwanza hio mada kwani alijua ingekuwa na mwisho mbaya.
“Unaonaje ukivaa suruali yangu , hata hivyo kuna giza na hakuna mtu anaeweza kujua umevaa ya kiume”Aliongea Roma mara baada a kugundua Recho anashindwa kusimama kutokana na kuwa uchi.
Roma alivua suruali haraka haraka na kubakia na boksa , alijua isingekuwa shida kwake kwani angeteleport moja kwa moja mpaka chumbani kwake
Recho alimwangalia Roma alivyokuwa akivua suruali aliokuwa amevaa na kujikuta akianza kutoa kilio kwa mara nyingine na kumfanya Roma kumwangalia kwa kumshangaa.
Recho alikuwa ameathirika kisaikolojia kwa kiasi kikubwa mno , haikueleweka nini kilikuwa kikiendelea kwenye maisha yake , lakini tokea siku alioweza kupeana na mume wake talaka mahakamani , hakuweza kutongozwa tena na mwanaume , alikuwa mzuri mwenye umbo lakini hakuna mwanaume ambaye alimtaka , haikueleweka hata kwa wazazi wake nini kinaendelea , walijaribu kwenda nae kwa mganga kusafisha nyota lakini wapi, alijaribu kwenda kwa Mwamposa kuombewa lakini hakukuwa na mabadiliko.
Kuna muda aliweza hata kujitoa ufahamu na kuvaa nguo fupi kutamanisha wanaume lakini vile vile hakuweza kusogelewa na hata kama mwanaume aweze kumuomba namba leo baada ya hapo hatafutwi tena , maisha yake yaliharibika kwa kiasi kikubwa mno na kama mwanamke kwa hali hio ilimuathiri sana kisaikolojia.
Kitendo cha Roma kuja kwenye kampuni na kuonyesha kuvutiwa na yeye , kilimfanya kujihisi mwenye tumaini jipya , Roma hakuonekana kumkimbia kama ilivyokuwa kwa wanaume wengine, tena kubwa zaidi ni hata pale Roma alipokuwa akimchezea walipokuwa ofisini.
Kilichomtia hofu Recho na kutotaka kumsogelea Roma ni kutokana na kufahamu ni mume wa bosi wake , lakini licha ya hivyo Recho kutokana na kukosa mwanaume wa kumridhisha aliishia kujiridhisha yeye mwenyewe huku akimvutia picha Roma , hayo ndio maisha yake tokea akutane na Roma.
Alijiambia kama mume wake wa zamani alimuwekea uchawi wa kutopendwa tena basi uchawi huo haukuwa ukimuathiri Roma.
Hivyo kitendo cha Roma kuja kumsaidia na hata kuvua nguo mbele yake kumpa avae kilimgusa mno na kuishia kuanza kulia kwa maumivu.
Hayo ndio maisha ya mrembo Recho , licha ya kuwa mzuri na siku zote kuonyesha tabasamu awapo kazini lakini ukweli alikuwa akiteseka ndani kwa ndani na hata wazazi wake walikosa namna ya kumsaidia.
“Mbona sasa unalia ,kama nimekushangaza kwa kuvua suruali yangu na kukufanya ulie basi ninaivaa”Aliongea Roma huku akitaka kuirudisha mwilini lakini Recho alisimama palepale na kumkumbatia Roma.
Hakujali yupo uchi , lakini pia hakujali Roma yupo na boksa tu alichojali muda huo ni kumkumbatia mwanaume aliekuwa mbele yake , ndani ya dakika chache mbele alirudisha kichwa chake na kumwangalia Roma usoni na alisogeza lipsi zake na kuzigusanisha na za Roma.
Haha .. mwamba Hades lazima aisafishe nyota ya mrembo Recho.
*******
Upande mwingine ni muda wa saa sita za usiku nchini Ujerumani katika kanisa la kikatoliki la Magdeburg ambalo limepakana na mto ufahamikao kwa jina la Elbe , sasa ndani ya kanisa hili alionekana mwanaume ambaye amepiga magoti eneo la madhabahuni mbele ya msalaba huku akiwa ameshika Rozari kwenye mikono yake.
Ilikuwa usiku sana hivyo mabenchi yote yalikuwa wazi na ilionekana mwanaume huyu alikuwa akifanya salama ya usiku mnene(Midnight player)
Alikuwa amevalia suti nyeusi na tai nyekundu , alionekana kama kijana ambaye ndio kwanza anaingia kwenye miaka therathini lakini macho yake yalionyesha utu uzima uliopitia mambo mengi , Uso wake wa kizungu ulikua umepauka uliokuwa wa ucheshi lakini kwa wakati mmoja kutisha kwa usiriasi wake.
“Sneijder ya nini kujisumbua kujificha mbele ya Yesu?”Aliongea kwa Lugha ya Kijerumani na ndani ya dakika hizo hizo alionekana mwanaume akijitokeza kwa namna ya kuibukia ambaye amevalia suti na kupiga magoti nyuma ya yule mwanaume.
“Your Royal Highness I’ve received news that might be related to Count Drogba”Aliongea kwa kingereza akimaansha kwamba amepokea taarifa ambazo zinaweza kuwa na uhusiano na mtu anaefahamika kwa jina la Count Drogba.
Yule mwanaume aligeuka na kumwangalia na kuuliza huku sauti yake ikionyesha kuvutiwa na habari hio.
“Oh! Has the kid finally appeared?”Aliuliza akimaanisha kwamba je huyo mtoto hatimae amaweza kujitokeza.
“Hatujaweza kuthibitisha chochote mpaka sasa lakini Camarilla wameweza kupata taarifa kutoka Tanzania kuhusu baadhi ya Vampires kuonekana kudhuru watu ndani ya jiji la Dar es salaam hivyo, Lilith kutoka ukoo wa Venture na Lefayette kutoka ukoo wa Brujah wametumwa Tanzania kwenda kufanya uchunguzi”Aliongea Snejder
“Oh! Hao watoto ndio waliotumwa , inaonekana mtu alieguswa ni mzito”Aliongea huku akitabasamu
“Apparently it was a letter from Pluto who is now in Tanzania but that is as far as our information goes”
“Ni barua iliotoka kwa mfalme Pluto ambaye sasa hivi yupo nchini Tanzania kwa kadri taarifa ilivyotufikia”Aliongea
“Hades !”Aliitaja jina huku akionyesha kushangaa kidogo
“Hakika inavutia sana Huyu si binadamu ambaye ameweza kupata Cheo hicho kutoka kwa Hades wa Zamani ?”
“Ndio , Your Royal Highness , je turuhusu watu kwenda Tanzania kwa ajili ya kumtafuta Count Drogba , nina wasiwasi na kitakachomtokea akikutana na Pluto”
“Don’t bother , He is my son and a pureblood vampire , not even a god would be able to find him so quickly , I’m more interested in Pluto compared to his safety”
“Usijisumbue Ni mtoto wangu na mwenye damu halisi ya Vampire hata miungu haiwezi kuweza kumpata kwa urahisi , navutiwa zaidi na Pluto tofauti na usalama wake”Aliongea huku akionyesha hali ya kuwaza kidogo.
“Kwanini Athena hakumzungumzia Hades kuwa nchini Tanzania , au kahamishia mapenzi yake kwa Hades mpya na anapanga kuzaa nae inawezekana ndio maana anamlinda ,kama ataendelea hivi mipango yetu haiwezi kufanikiwa , anajitengenezea udhaifu”Aliwaza mwenyewe huku akikunja ngumi kwa hasira , alionekana kujua kitu kuhusu Athena.
Sneijder alionyesha woga kwenye macho yake mara baada ya kuona mwanaume anaemwita mfalme kuwa kwenye tafakuri.
“Mtukufu mkuu mfalme , nadhani halitakuwa jambo jema tusipochukua hatua”
“Kwanini?”
“Nilishuhudia kwa macho yangu Ufaransa , Prince Sargaras na Lilith kuonyesha hofu mbele ya Pluto mpya , hatuna uwezo wa kumdhibiti hata kwa uwezo mkubwa uliokuwa nao ewe mtukufu mfalme”
“Hahahaha…. Hahahaha….”Alicheka kicheko kisichokuwa cha furaha.
“Sneijder nashukuru kwa wasiwasi wako lakini ninatambua uwezo wangu”Aliongea na Sneider hakuongea kingine zaidi ya kupotea ndani ya kanisa hilo.
Yule mwanaume aligeukia msalaba wa dhahabu uliokuwa mbele yake na kuuangalia kwa namna ya kejeli.
“God! Hahaha…?”Aliongea huku akicheka kwa dharau na kisha akageuka na kutembea kutoka eneo hilo na ile anapotelea nje kabisa , ule msalaba wa Dhababu ulianza kupitia mabadiliko , ulianza kupukutika kama vumbi kuanzia juu kwenda chini kwa spidi ya hali ya juu na ndani ya dakika chache tu kifusi cha unga unga kilijitengeneza chini ukionyesha kuyeyuka wote kama umeliwa na mchwa.
Naam huyu ndio mwanaume ambaye aliweza kumpokea Athena siku kadhaa zilizopita na wakaitana kaka na dada.
Swali je huyu ni sehemu ya miungu kama ni hivyo je vipi kuhusu uwezo wake.
Vampire Count Drogba ndani ya Tanzania , nini utabiri wako wa kitakachotokea.
Hint ya episodes ijayo igeuze hii kauli ya Roma: Okey Mourihno nakupa kazi ya kuwatafuta Vampire wengine waliopo ndani ya jiji hili la Dar es salaam kwasababu unaweza kunusa harufu zao kuliko mimi na kama utawapata nitaarifu , naishi sehemu moja inaitwa Ununio
[emoji91][emoji91][emoji91]SEHEMU YA 453
Ni siku nyingine kabisa , siku iliofuata baada ya usiku wa kashikashi nyingi, Roma siku hio alichelewa sana kuamka kutokana na kuchelewa kulala , muda wa saa mbili za subuhi kwenda na nusu ndipo aliposhikuta kutoka usingizini.
Usiku wa jana alikumbuka namna ambavyo aliweza kuhitimisha usiku yeye na Recho,hakutaka kabisa kufanya chochote na Recho , lakini kitendo cha mwanamke yule kulia mbele yake huku akijiona sio wa thamani kwa kile kilichokuwa kikiendelea kwenye maisha yake , alijikuta akimuonea huruma na kujikuta akifanya nae mapenzi , lakini hata hivyo Recho ilikuwa tofauti, alifanya nae mapenzi kwa kumuonea huruma na hayakuwa mapenzi hivyo aliamini hata kwa Recho pia swala hilo asingelichukulia kubwa sana kwake.
Roma baada ya kujiweka safi mwili wake aliweza kushuka mpaka chini Sebuleni na kulikuwa na utulivu wa hali ya juu , zilikuwa zimepita siku kadhaa pasipo ya kumuona Lanlan na alijihisi kumkumbuka ghafla.
Runinga ilikuwa wazi huku taarifa iliokuwa ikionyesha ni iliokuwa ikihusiana na mauaji ya msanii Dina katika usiku wa Tuzo za Taifa , taarifa ambayo ilikuwa gumzo kiasi cha kuteka hisia za watu wengi waliokuwa wakimfahamu.
“Roma umeamka , kifungua kinywa kipo mezani”Aliongea Blandina mama yake ambaye alionekana kutoka nje , ilionyesha alikuwa akimwagilia maua na Roma alimsalimia huku akimuulizia mke wake.
“Edna keshaenda kazini asubuhi asubuhi , ilionekana alikuwa na dharula aliondoka hata pasipo ya kupata kifungua kinywa”Aliongea .
“Aliondoka saa ngapi?”
“Saa kumi na mbili”
“Itakuwa ni kwasababu ya tukio la Jana”Aliongea Roma akikaa Dining kwa ajili ya kupata kifungua kinywa.
“Nilishitushwa na taaarifa ya kifo cha msanii Dina ,na mkeo alinisimulia asubuhi asubuhi na kusema kuna mtu anahitaji kuonana nae , bila shaka ni kuhusiana na hilo”Aliongea na Roma alitingisha kichwa hata hivyo alijua lazima Edna angefanya hivyo kwani alikuwa akiilinda taswira ya kampuni yake kwa nguvu zote.
“Kuna mwingine ambaye hajapata kifungua kinywa?”Aliuliza Roma.
“Mr Roma jana Sophia alirudi usiku”Alijibu Bi Wema aliekuwa akishuka kutoka juu akiwa amebeba nguo ambazo ilionekana alikuwa akienda kuzifua, Roma alishangazwa kusikia Sophia kurudi jana kwani alijua yupo Nigeria kama Edna alivyomwambia.
Muda huo huo mrembo Sophia alievalia Pajama alishuka kutoka juu huku akifunga nywele zake ndefu kwa nyuma na kumfanya Roma kumwangalia kwa macho ya kumshangaa , Sophia aliondoka kwa siku kadhaa lakini uzuri wake ni kama umeongezeka maradufu na kumfanya Roma kuona huenda ni kutokana kumkumbuka sana ndio maana urembo wake umezidi kuongezeka.
“Bro mbona unaniangalia hivyo?”Aliongea Sophia akimwita Roma, Bro , ijapokuwa alikuwa akijulikana kama mdogo wa Edna hivyo kupaswa kumwita Roma Shemeji lakini alikuwa akimwita Bro na hakutaka kubadilisha.
“Mbona umerudi kimya kimya bila kututaarifu?”
“Kama unajali sana taarifa kwanini unashindwa hata kunitafuta kwa njia ya simu , kila siku Sister Edna ndio mwenye kufanya juhudi ya kunijulia hali”.
“Nadili na mambo mengi ndio maana muda mwingine inatokea siku imeingia na ikaisha bila ya mimi kuelewa”Aliongea Roma na kumfanya Sophia kuvuta mdomo na kukaa kwenye kiti huku akimimina juisi nusu glasi na kumfanya Roma kuendelea kumwangalia kwa maswali mengi.
“Nina Show siku tatu zijazo,lakini pia napaswa kufanya maandalizi ya kuzindua albamu yangu”Aliongea Sophia.
“Wow! Hongera nadhani umetuandalia mambo makubwa kwenye Albamu yako , unaonaje nikasikiliza kabla ya kuitoa”
“Hata usijali nitakupatia usikilize , hata hivyo Menejimenti uliopendekeza kunisimamia ni Superb, imerahisisha mambo mengi”
Ni kweli kabisa menejimenti yote ya Sophia ni Christen ndio alieisimamia kwa kuchagua watu wa kumsapoti Sophia , ijapokuwa Christen ndio aliehusika lakini kama sio uhusiano wa Roma na Christen basi Sophia asingeweza kuweza kupata menejimenti hio , hata wasanii wenzake walikuwa wakimuonea wivu sana kwani kusimamiwa na msanii mkubwa kama Christen halikuwa jambo la kawaida.
“Furaha yangu ni wewe kufanikiwa , kuwa maarufu ni jambo jepesi , lakini kuendelea kubakia maarufu ni kazi kubwa sana inayohitaji nidhamu na uthabiti wa hali ya juu, ndio maana Christen alitaka uzungukwe na watu wenye uzoefu kwenye Mziki ili uweze kutoboa kimataifa”Aliongea Roma na Sophia alitabasamu.
“Sikutaka kuwaambia ninarudi kwasababu imekuwa kero kutokana na umaarufu , mapaparazi wananiwinda kwa kila hatua kiasi kwamba nakosa uhuru, hata hivyo nipo hapa kwa muda mchache sana , menejimenti yangu hawataki nikiishi hapa”Aliongea Roma na kumfanya kufikiria kidogo.
“Nadhani wameongea la maana kwasababu muda wote watahitaji kuwa karibu na wewe , lakini vipi umeamua mahali unapotaka kuishi kwasasa?”
“Yeah , Sister Edna kapendekeza ninaweza kuishi kwenye nyumba ya Kigamboni”Aliongea na Roma hakuwa na pingamizi na hilo.
“Halafu Dina nilitakiwa kufanya nae Show, nilishituka sana kupokea taarifa amefariki ni nini kimetokea?”Aliuliza Sophia.
Ukweli ni kwamba tokea Sophia ashinde mashindano ya Kizazi nyota , watu mbalimbali walikuwa wakitabiri Sophia anakwenda kumfunika Dina katika mziki , kama ujuavyo washabiki wa Tanzania walivyopenda kuwashindanisha wasanii basi ndio ilivyokuwa , Dina hakuwa na mpinzani kwa zaidi ya miaka minne mfululizo , lakini kuchipukia kwa Sophia msanii mwenye sauti na mrembo ndani ya Tanzania lilikuwa swala la muda tu , Dina mwenyewe wakati wa uhai wake alikuwa akihofia sana kuzidiwa kete na kilichomuumiza zaidi ni mahusiano mazuri ya kimziki yaliokuwepo kati ya Sophia na Christen , lakini sio hivyo tu Sophia alikuwa na ‘Backup’ ya kampuni ya Vexto Media akiwa kama balozi.
Roma ilibidi ampe habari ya kile kilichotokea na kumfanya Sophia kushangazwa mno na habari hio kama ilivyokuwa kwa Edna dada yake , kama Sophia angesikia maneno hayo kwa mtu mwingine tofauti na Roma angekataa habari hio , lakini baada ya kuishi na Roma na kugundua sio mtu wa kawaida ilibidi kuamini moja kwa moja, lakini hata hivyo alikuwa kwenye mshangao.
Baada ya kuongea na kupiga stori za hapa na pale za kuchekesha Roma alipandisha chumbani kwake kwa ajili ya kujiandaa kutoka , alipanga kwenda hadi kwenye kampuni ya mke wake ili anunue chochote njiani ampelekee , alijua kabisa Edna muda huo atakuwa hata kunywa chai amesahau kama ilivyo tabia yake.
Wakati anashuka akiwa amevalia koti la suti rangi ya zambarau , suruali ya jeans na tisheti ,upande wa nje geti lilifunguliwa na kuruhusu gari mbili aina ya V8 zote , Blandina aliekuwa eneo la nje alionyesha kushangazwa na ujio wa gari hizo na kujiuliza nani ambaye amekuja kuwatembelea, hata hivyo kwa haraka haraka alishajua ni mtu kutoka serikalini kutokana na Plate number za magari hayo.
Mlango wa dereva ulifunguliwa na msichana alievalia suti mkamavu na kuzunguka upande wa kushoto na kufungua mlango na ndipo alipoonekana Damasi mke wa raisi Senga akitoka, Blandina alishangazwa na ujio wa mke wa Raisi nyumbani kwake bila ya taarifa.
Gari iliokuwepo nyuma pia ilifunguliwa na alitoka Denisi Senga aliekuwa amevalia tisheni ya rangi ya kahawia pamoja na miwani huku akiwa ameshikilia maua mkononi ya rangi nyeupe na pink.
Roma aliekuwa akitoka nje alishangazwa na uwepo wa watu hao nyumbani na kujiuliza wamekuja kufanya nini.
Blandina alisalimiana na first lady wa taifa la Tanzania , aliekuwa amependeza haswa na haiba yake ya upole akionyesha hali ya kijiamini zaidi wakati alipokuwa akiongea.
Roma alimwangalia Denisi na kujikuta akikunja sura ni kama alivyoambiwa , Denisi alionekana kubadilika sana mwili wake na kilichomshangaza sio kwamba Denisi alikuwa na nguvu za kijini lakini alikuwa akitoa ‘Aura’ tofauti ambayo inafanana kwa asilimia kubwa na Clone yake iliotengenezwa na Yan Buwen , moja kwa moja alijua lazima Denisi atakuwa na mahusiano ya moja kwa moja na Yan Buwen , jambo hilo lilimfanya kuvutiwa zaidi na alihisi kabisa huenda hata kifo cha Dina inawezekana Denisi akawa anahusika kwa namna moja ama nyingine.
“My Bro… nimekuja leo tumalize tofauti zetu , pokea salamu yangu”Aliongea Denisi huku akiwa ameweka tabasamu mara baada ya kumfikia Roma ,lakini kwa upande wa Roma aliona kabisa maneno ya Denisi ni ya kinafiki hivyo hakupokea salamu yake zaidi ya kurudi ndani na kumfanya Damasi kuvuta pumzi.
“Sophia hii ni zawadi yako , hatujaonana kwa muda mrefu na nilivyoweza kusikia umerudi nikaona asubuhi hii nije nikuone”Aliongea Denisi huku akimkabidhi Sophia mua alioshikilia mkononi , Sophia hakuwa na hiyana aliyapokea hata hivyo kitendo hicho kilifanyika mbele ya mke wa Raisi, lakini alijiuliza Denisi kafahamu vipi ameweza kurudi kwani ilikuwa nikama siri.
Damasi alitabasamu na kisha alimpa ishara Sophia ya kumsogelea na kisha wakakumbatiana.
“Sophia nataka ujue mimi pia ni shabiki yako , huwa sio mpenzi sana wa mziki ila kupitia wewe nimejikuta nikiufuatilia, nasubiria Albamu yako kwa hamu zote”Aliongea na kumfanya Sophia kucheka kwa aibu huku akishukuru.
“Jamani karibuni mkae , ngoja niwaandalie chochote muweke baraka , ujio wenu ni wa ghafla na hatujajiandaa kabisa”Aliongea Blandina.
“Mama Roma usijali kabisa kuandaa chochote , unaweza kunipa hata juisi ya matunda tu itafaa kabisa kuweka baraka”Aliongea Damasi na Blandina alitabasamu na kwenda kuandaa juisi na ndani ya dakika chache alimaliza na kumuwekea Denisi pamoja na Mama yake ,Blandina ilikuwa mara yake ya kwanza kuitwa Mama Roma , ijapokuwa zamani alizoea kuitwa Mama Denisi lakini kubadili kwa jina kwa Roma kulimfanya kutokuzoea jina la Mama Roma.
“Baba simuoni mkeo Edna , nilitamani kusalimiana nae , lakini naamini atakuwa ashaenda kazini”
“Upo sahihi , nadhani unamjua mke wangu kwa uchapa kazi”Aliongea Roma na kumfanya Damasi kutabasamu.
“Namjua sana Edna , tokea akiwa mdogo anafanana kwa vitu vingi na Ashley”Aliongea na kumfanya Roma kumkumbuka Ashley ni muda mrefu hakuwa amerudi Tanzania wala kuwasiliana nae.
“Ashley ni msichana mzuri naungana na wewe anafanana sana na Edna, hivi yupo wapi kwasasa?”Aliuliza Blandina mara baada ya kusifia kidogo.
“Yupo Uingereza lakini anatarajia kurudi Tanzania hivi karibuni kuendeleza Projekti alioiacha mwalimu wake”Aliongea.
“Bro nipo hapa kwa ajili ya kumaliza tofauti zetu , nimefikiria na kuona wewe ni kaka yangu wa damu licha ya mama tofauti, hivyo haina haja ya sisi kugombana”Aliongea Denisi kuingilia mazungumzo na kufanya watu wote kuwa kimya na kumwangalia Roma.
“Unaongea unafiki”
“Roma mwanangu Denisi ni kweli yupo tayari kupatana na wewe , alivyoniambia anakuja hapa nikaona nije nae , nyie ni ndugu hivyo sipendi mkikoseana , Denisi yupo tayari kuomba radhi kwa pale alipokukosea hivyo naomba umsamehe”Aliongea.
“Nimefurahi kusikia hivyo kutoka kwa Denisi kama kweli yupo tayari kumaliza tofauti zake na Roma”Aliongea Blandina huku akionyesha kufurahi.
“Ni kweli mama , nipo hapa kwa ajili ya kumuomba msamaha Kaka yangu Roma , na kuweka tofauti zetu nyuma, nimepata baraka zote pia kutoka kwa baba”Aliongea lakini maneno yake yalionyesha kumkera Roma kwani aliyaona ni ya kinafiki.
“Denisi ni vyema umetambua hilo na kufika kuomba msamaha , unaweza kuja mara kwa mara naamini Roma atakusamehe”Aliongea Blandina baada ya kuona Roma hayupo tayari kumpokea Denisi.
“Denisi alichoongea Mama Roma ni sahihi , kwanzia sasa jitahidi kuwa karibu na kaka yako na uache kuwa mtukutu”Aliongea Damasi.
“Mama mimi nipo tayari kuweka juhudi kwa ajili ya kuwa na urafiki na kaka yangu”Aliongea.
“Sina haja ya kuwa na ukaribu na wewe , ni vyema ukaheshimu mipaka yako la sivyo nitahakikisha ukiingilia maisha yangu nilichokufanyia mara ya mwisho kitakuwa ni mara mbili yake”Aliongea Roma lakini Denisi aliishia kutabasamu na kumgeukia Sophia.
“Sophia nitahakikisha nafika kwenye Show yako , napanga kukaa kabisa mstari wa mbele , kama utakuwa na shida yoyote nipo tayari kukusaidia”Aliongea
“Maswala ya Sophia ya Show hayakuhusu , hivyo jua biashara zako”Aliongea Roma na Blandina alijaribbu kumtuliza kwa kumshika mkono lakini Roma alitamani kumfukuza Denisi mara moja nyumbani kwake , alishindwa tu kufanya hivyo kutokana na uwepo wa Damasi.
“Kaka nadhani wewe ndio unatakiwa kuniacha mimi na Sophia, nimejuana nae kwa muda mrefu kuliko hata wewe na mpango wangu ni kumuoa kabisa na kumfanya mke wangu labda kama hutaki na mimi nikiwa na mke kama wewe”Aliongea na kumfanya Damasi kumwangalia Sophia kwa shauku.
“Nani kasema utanioa?”.
“Sophia usikasirike , najua sio jambo zuri kwa Denisi kuongea mbele ya watu kama hivi , lakini naamini mtakaa vizuri nakuongea, mimi ukikubali kuolewa na Denisi nakuhakikishia nitakupokea kwa mikono miwili”Aliongea Damasi.
“Sophia ni kweli nimeropoka , naamini tutaongeana kuelewana nitakuwa nakuja mara kwa mara kukutembelea itakuwa pia nafasi kuzoeana na Bro”Aliongea lakini Sophia hakujibu kitu , hata hivyo aliona kama Denisi alikuwa akimtibulia siku yake ambayo ilianza vibaya kwa taarifa ya kifo cha Dina.
“Mama mimi natangulia kwani ninahitajika kuripoti leo makao makuu ya jeshi”Aliongea Denisi na kusimama na Damasi alimpa ruhusa na kisha akaaga na kuondoka, Roma na yeye mara baada ya kuona Denisi katoka , aliwaambia kwamba anaenda kazini.
Denisi mara baada ya kuifikia gari yake aligundua na Roma alikuwa akimfauta kwa nyuma na kutabasamu kifedhuli huku akijiangalia kwenye kioo cha gari na kisha akageuka.
“Brother una lingine unataka kuongea?”
“Acha kunichukulia kama fala, unadhani mimi ninaweza kukuamini kwa kujifanyisha kuwa mpole”
“Roma najua kabisa hunipendi lakini hilo ninaweza kuelewa kulingana na matukio ya nyuma , lakini kwa upande wangu nishaamua kusahau yote na ndio maana nataka tuyamalize , hata hivyo sisi ni ndugu wa damu hivyo haileti picha nzuri kuwa na ugomvi, isitoshe wazazi wetu pia wanatamanni sana tupatane”
“Haina haja ya kuwaingiza wazazi wetu katika hili , ninachotaka kujua kutoka kwako je ni Yan Buwen ndio amekufanya mwili wako kuwa hivyo?”
“Unamaanisha nini ?, sijui unachotaka kusema , Huyu Yan Buwen unaemzungumzia hata sina mazoea nae”Aliongea huku akijifanyisha kuwa kwenye mshangao.
“Acha kujaribu kunidanganya , ili ionekane huna mahusiano na Yan Buwen, najua fika kilichomtokea msanii Dina unahusika , ulimtumia mfanyakazi wa Vexto kwa makusudi kabisa”Aliongea Roma
“Brother unaongea uzushi na siwezi kuhusika , najua kabisa hunipendi lakini huna haki ya kunisingizia”Aliongea lakini Roma palepale alimsogelea kwa spidi Denisi na kumshika shingo na kuiminya kwa nguvu huku akijaribu kumning’iniza hewani.
“Sikia wewe mnafiki , sitaki kwanza uniite kaka na pili nisije kukuona unakanyaga nyumbani kwangu , Kama ukijaribu sitowajibika kwa kile ambacho nitakufanyia”Aliongea Roma huku akiachia msisimko wa ajabu lakini Denisi alikunja midomo kwa dharau.
“Kwahio bro unanitishia ama vipi?”
“Haustahili hata kutishiwa na mtu kama mimi ,ninachokuambia hapa ni kukuelewesha”Aliongea , Denisi licha ya kuminywa kwa nguvu alionekana kuhema kawaida tu.
“Nadhani sasa watu wanapaswa kufahamu mwenye tatizo ni wewe na sio mimi , nimekuja hapa kwa nia njema ya kupatana na wewe , lakini unanishambulia hivi , unaonekana kuwa mbinafsi sana”
“Ndio unavyodhania sio , Je nikikuua sasa hivi utaendelea kuamini sisi ni ndugu?”Aliongea Roma huku akianza kupandwa na Jazba , lakini muda huo huo ndio Damasi na Blandina walitoka nje mara baada ya kuona magari hayangurumi , walidhania kuna uwezekano hali isioyakawaida nje.
“Roma unafanya nini , mwachie mdogo wako jamani”Aliongea Blandina huku Damasi akiziba mdomo na mkono , hakuamini hali ingefikia hapo , hata mlizi aliekuwa amekuja nae alishindwa kufanya lolote na kuishia kuangalia tu.
Roma alikuwa na uwezo wa kuliamsha varangati hapo ndani kwa kumpasua pasua Denisi , lakini hakutaka kufanya hivyo ,alihofia Denisi kuwa na uwezo kama wa Clone na kurudi hai baada ya kumuua , hivyo inaweza kumuathiri mama yake.
“Roma naomba umuachie Denisi , amekuja kwa nia nzuri mpate kuyamaliza usifanye hivyo”Aliongea Damasi na kumfanya Denisi kutabasamu huku akimwangalia Roma usoni ni kama aliamini Roma asingeweza kumfanya chochote mbele ya wazazi.
“Naona umekuja na mama yako kumtumia kama Kinga si ndio?”Denisi hakujibu zaidi ya kuwageukia mama yake na mama yake Rom.
“Mama zangu Roma hajaniumiza inaonekana tu amekuwa na hasira na mimi hivyo msiwe na wasiwasi”Aliongea Denisi mara baada ya kuachiwa na Roma ambaye alikuwa akitetemeka kwa hasira , kwenye maisha yake alikuwa akichukia mno watu wanafiki na adhabu yake ilikuwa kifo , lakini kitendo cha kushindwa kumuua Denisi aliona kabisa ni kama haki haikutendeka.
“Roma najua una hasira na Denisi , lakini huwezi kumshambulia kama yupo tayari kuyamaliza , tumeharibu ratiba kwa ajili ya kuja hapa , hii yote nni kuonyesha kwamba tunafanya juhudi kwa ajili ya familia”Aliongea Damasi.
“Roma mwanangu ni kweli anachoongea mama yako , unapaswa sasa kuacha yaliopita yapite , Denisi anaweza asiwe mwanangu wa kumzaa lakini nyie wote ni wa baba mmoja hivyo kupatana kwenu kutanifanya niwe na amani”Aliongea Blandina lakini Roma akili yake ilikuwa inazuguka mno , alitegemea na mama yake angemsapoti yeye na sio kukaa upande wa Denisi, alichukia kuona kila mtu ameweza kununua maneno ya kinafiki ya Denisi.
Roma hakutaka kubakia hata sekunde hapo ndani zaidi ya kusogelea gari yake na kuliwasha kisha akaondoka kwa kasi , namna ambavyo Roma aliondoka ilimfanya Blandina kuwa katika wasiwasi na moyo wake kuuma , ijapokuwa alipaswa kuwa upande wa Roma ,lakini aliamini kama ndugu hao wasipopatana basi mwisho wa siku ingepelekea matokeo mabaya hata ya mmoja wao kupoteza maisha.
Dakika chache mbele Roma aliweza kupitia fastfood na kununua vyakula vyepesi ambavyo aliamini vingemfaa Edna , hakusahau pia kununua portion mbili kwa ajili ya Dorisi na Nasra.
Dakika chache mbele aliweza kufika ndani ya ofisi ya Nasra na kumpatia msaidizi wake , lakini hivyo hivyo alimpatia msaidizi wa Dorisi , kwani wote hakuwakuta baada ya kupewa taarifa kwamba wapo kwenye usaili.
Aliweza kukutana na Recho ambaye alikuwa akiendelea na majukumu yake na alivyomuona Roma alitabasamu , Recho asubuhi hio alikuwa amevalia gauni la rangi ya pinki la maua maua lenye kufungwa mkanda mkubwa kiononi.
“Kifungua kinywa kwa ajili ya bosi?”Aliuliza Recho na Roma alitingisha kichwa.
“Niliona habari asubuhi, Vipi unajisikia vizuri kwasasa?”
“Ndio nipo sawa , asante kwa msaada wako , unaweza kuingia tu ofisini nipo na kazi nyingi hapa”Aliongea na Roma na kuzama kwenye ofosi ya mke wake huku akimuacha Recho akiwa na tabasamu.
Roma alivyoingia ndani aliweza kumuona Edna akiwa amekazia macho skrini ya tarakishi huku akitype kwa haraka ,akionekana kuandika kitu na alipomuona Roma akiingia aliacha kuandika huku akiangalia mfuko aliokuja nao Roma.
“Kaa kidogo basi , kuna kitu nimalizie haraka halafu nitakula”Aliongea kwa sauti ya kirafiki na kumfanya Roma kushangaa kidogo.
“Inaonyesha uliamka vizuri , kuna kipindi nikikuletea chakula lazima uanze kuniwekea ngumu”Aliongea na kumfanya Edna kumwangalia na kisha akatabasamu.
“Uneonekana haupo kwenye mudi nzuri , Nikitaka uanze kunibembeleza kwa hali uliokuwa nayo ni utomvu wa nidhamu kwa mume wangu”.
“Umejuaje sipo kwenye mudi nzuri?”
“Umeingia kimya kimya leo ofisini kwangu bila kuanza kunisalimia na uneonyesha hali ya kuwa mpole kuliko siku zote, tabia yako haiendani na mwonekano wako wa leo,”
“Inaonekana unanifahamu mno mke wangu”
“Ni sehemu ya ujuzi lakini pia uzoefu ,tumeishi muda mrefu pamoja unafikiri nitashindwa kutofahamu ni wakati gani ukiwa na kitu kunakusumbua”
“Umepatia, Unafiki wa Denisi leo umeniharibia mudi kabisa nilitamani kummaliza mbele ya mama yake”Aliongea na kumfanya Edna macho kuongezeka ukubwa na kutoka nyuma ya meza na kuja kwenye masofa.
“Unaonaje ukinielezea wakati nikiendelea kula ulichoniletea”Aliongea huku akiangalia mfukoni.
“Sipendi hata kuelezea kwani inaboa na unaweza pia kupoteza mudi yako na kusikitika tu”
“Haiwezi kunisikitisha , unaweza kunihudumia kama nitafilisika lakini siwezi kuikokoa familia iliogawanyika, Denisi , Ashley ni ndugu kwangu pia kwasababu nimeolewa na wewe na siku zote nitapenda kuona amani baina yenu”Aliongea
“Edna mke wangu , leo unaongea kama sio wewe vile”
“Vipi na wewe, siamini ni mwenye kukasirishwa na vitu vidogo vidogo kama hivyo”Aliongea na kumfanya Roma kushindwa kujibu na kuishia kumwangalia Edna na kisha kuegamia sofa huku akionyesha kuwaza.
Kutokana na unafiki wa Denisi familia inaweza kuona yeye ndio mwenye matatizo na hataki kuyajenga na hicho ndio kilichomtoa mudi kwani hata mama yake mzazi alionyesha kuamini unafiki wa Denisi na kuwa upande wake, muda mwingine aliona kuwa mjinga kunasaidia baadhi ya sehemu , kama angekuwa mjinga angekubaliana na maneno ya Denisi na kila mmoja angeona amefanya jambo zuri , lakini kujua kila kitu nyuma ya tabasamu la mtu , yeye ndio alionyesha kwamba hayupo tayari kuyajenga.
“Sijui nini Denisi alichoongea wala watu walivyochukulia maneno yake , lakni unachotakiwa kujua , wote sisi kama wanafamilia tunakuamini zaidi ya mtu mwingine yoyote yule na maamuzi yako yanasababu nyuma yake”Aliongea Edna na Roma alionekana kubakia vile vile bila kuongea neno na Edna alisimama na kumwambia amfuate.
Walifuatishana na kuingia upande wa ngazi na kwenda kutokea juu kabisa ya jengo hilo na kufanya kuona sehemu zote za jiji la Dar na mandhari yake , huku upepo ukiwapuliza , Edna alitembea na kwenda kusimama kwenye fensi akiangalia upande wa daraja la Tanzanite na Roma alisimama pembeni yake.
“Roma”
“Naam”
“Recho alinihadithia namna ulivyomuokoa na anaonekana kuwa sawa leo , inaonekana jana ulifanya kazi kubwa ya kumuweka sawa licha ya tukio lenyewe kuwa la kutisha”Aliongea
“Hio kauli kidogo haijakaa sawa kwasababu inatoka kwako , lakini nadhani nimesaidia”Aliongea na Edna alifungua mfuko na kutoa vyakula vyake , ila hakuwa na pakukaa na Roma aliona hilo na kuvua koti la suti na kulitandika chini na kumwambia akae.
Edna alishangazwa na kitendo kile lakini aliishia kutabasamu na kisha wakaketi wote kwa pamoja , huku akila taratibu na kunywa na juisi.
“Niambie nini kimetokea nyumbani”Aliongea na Roma alimwelezea kwa ufupi.
“Kwahio kilichokuhuzunisha ni Mama kuamini maneno ya Denisi?”
“Sio hivyo niliamini nikimuua , hakuna ambaye angeweza kusimama upande wangu na kuonekana nimefanya maamuzi yasio sahihi ndio maana nilihuzunika kwamba kwanini mimi tu ndio ninaeona upande mwingine wa watu?”
“Inawezekana mama pia hakumuamini lakini kwasababu alikuwepo Damasi mke wa raisi aliamua kukaa upande wa Denisi, nakumbuka wakati nikiwa mtoto nilishawahi kupigana na mwanafunzi mwenzangu kiasi kilichopelekea mama kuitwa shuleni, ijapokuwa mwenye kosa ni mwananfuzi mwenzangu kwa kunichokoza lakini mama badala ya kunitetea mimi kama mtoto wake aliamua kusimama upande wa yule mwenzangu na kunifanya nionekane ndio nilikuwa mkosaji niliishia kulia na kuona nimeonewa lakini baada ya siku ile nilijua mama alikuwa na maana kubwa ya kufanya vile, Mama anakupenda sana na anakuamini na chochote anachofikiria ni kwa ajili ya ustawi wako,anaonekana kujutia kwa muda wote ambao hakuwa karibu yako”Aliongea Ednana kumfanya Roma kutabasamu.
“Edna nikuulize kitu?”
“Niulize tu sisi ni mume na mke na hatuna haja ya kufichana?”
“Lakini swali langu linaweza kukuhuzunisha?”
“Uliza kama litanihuzunisha au kunikasirisha nitakupiga hapa hapa kumaliza hasira zangu”
“Nilikuwa nawaza kama baba yako atakukataa kama mtoto wake , je utampotezea moja kwa moja?”Aliongea na kumfanya Edna mwili wake kuwa baridi na kushindwa kujibu .
“Edna ni sawa tu hata usipo nijibu m ninachotaka kujua ni hatua gani utachukua , maana unaonekana kuweka familia mbele sana kwenye mambo mengi”
“Sijui kwanini umeuliza hivyo lakini siwezi kumpotezea , unaweza kuniona labda ni kichaa na asiwasiliane na mimi , lakini siwezi kumpotezea kwani ndio baba aliesababisha ujio wangu duniani, Hivyo naamini kama atanikataa itaniumiza lakini nitafanyaje ataendelea kuishi kwenye moyo wangu nikimtambua kama mzazi wangu, natamani sana kuongea na baba na nimekuwa wakati mwingine mwenye wivu kwako kwani una mama na babu wote wanakupenda , lakini mimi sina ndugu yoyote zaidi ya Bi Wema”
“Akikukataa na ukinipa ruhusa ni muue nitafanya hivyo”Aliongea Roma huku akiweka utani na kupitisha mkono kumshika Edna bega lake la kulia.
“Najaribu kuwa na mawazo chanya kwamba atakuja kunitafuta siku moja na kujitambulisha kwangu lakini kama atanikataa na asiponitafuta nitaendelea kuishi”
“Hakika utaendelea kuishi, wewe ni mke wangu na ninaweza kuwa ndugu yako zaidi ya baba asiekuhitaji”Aliongea na kumfanya Edna amwangalie usoni kwa mahaba.
“Nina hisi usingizi nataka nilale kidogo”Aliongea.
“Unajichosha sana kwa kufanya kazi muda mrefu”
“Nimekula ndio maana na hisi usingizi , ngoja nipumzike baadae nitaenda kumchukua Lanlan ili wiki ijayo tukamwandikishe shule aanze kuzoea mazingira na wenzake”Aliongea na Roma alitingisha kichwa na kisha akampa ishara ya kulala kwenye mapaja ya miguu yake na dakika tano zilikuwa nyingi Edna alipotelea usingizini kwa amani kabisa.
Dakika nyingine therathini kupita mwanaume na mwanamke wa kizungu walitua juu ya jengo hilo huku wote wakiwa wamevalia suti za rangi nyeusi.
“Well , Well , What a lovely scene we have here , We might have dropped in on the wrong time”
“Vizuri , vizuri , Ni tukio gani zuri la kupendeza tunalo hapa , Inawezekana tumefika ndani ya muda mbaya”Aliongea mmoja wapo.
Ni mwanamke huyu wa kizungu mwenye nywele nyeupe , alin’gaa na kuonekana mrembo , hakuna ambaye angeweza kuamini kwamba alikuwa na zaidi ya miaka mia moja na ni Vampire.
Alikuwa ni Lilith ambaye ametangulizana na mwanaume mwingine ambaye kwa haraka haraka na Roma alitambua ni Vampire pia , Mwanaume yule alimwangalia Roma kwa macho yenye chuki ndani yake.
Roma hakujali sana namna mwanaume huyo anavyomwangalia , Edna alikuwa amelala kwenye mapaja yake na alishamwahidi atakaa hapo mpaka usingizi utakapoisha , hivyo hakuhitaji kabisa usumbufu.
Roma alitumia mbinu ya kijini ya Kimaandiko na kisha alimzingira Edna ili makelele yasimfikie .
“Asanteni kwa kuja kwa haraka , lakini kama mnavyoona nipo bize kwa muda huu kwanini msitafute hoteli kwanza mpumzike”
“That is very sweet of you , your Majesty Pluto alright then , but let me introduce to you..”
“Usijali Lilith ninaweza kujitambulisha , kwa majina naitwa Lefayette Marquess kutoka ukoo wa Brujah , mimi ni mchumba wa Lilith”Aliongea kwa rafudhi yake ya kiitaliano na kumfanya Roma kushangazwa na aina ya utambulisho huo.
“Lefayette , Rudi Itally kama utaendelea kuwa hivyo”Aliongea Lilith kwa kufoka ni kama hakupenda namna Lefayette alivyomalizia na neno mchumba.
“Lilith nimekuwa mpenzi wako kwa zaidi ya karne hata wazazi wetu wanatambua mahusiano yetu , kwanini siwezi kujitambulisha mbele ya watu kama mchumba wako?”
“Nilishakwambia muda wote nilikuwa nikitania sisi kuwa wapenzi na sitaki kabisa uje kunioa”Walianza kugombana wao kwa wao mbele ya Roma.
“Nyie wapenzi mnaopendana kama manataska kugombana nadhani itafaa mkiondoka hapa , mtamuamsha mke wangu”
“Hapana mfalme Pluto , usimsikilize Lefayette kwa maneno yake ya kipuuzi , sina mahusiano nae”
“Sawa lakini sitaki kujua kama mna mahusiano”
“Mfalme Pluto , Lilith alianza kunitenga na kuona sifai mara baada ya kukutana na wewe umempa nini cha kumchanganya mchumba wangu?”
“Kaa kimya Lefayette , nimekuruhusu unifuate kwasababu yalikuwa maagizo kutoka Camarilla lakini ukumbuke maagizo yalikuwa na masharti ya kutonikasirisha”
“Sijakukasirisha ninachotaka kujua kwa huyu binadamu ni kipi amekupatia mpaka usinipende tena?”Aliongea na kumfanya Roma kuwaza , alichokuwa akikumbuka hakuwahi kumsogelea Lilith na ni yeye aliejilengesha kwake na kama mwanaume alishindwa kukwepa mtego wake.
“Sijui ni kipi viongozi wetu wanacho ogopa kutoka kwako , lakini nakutahadharisha kaa mbali na mpenzi wangu la sivyo nikishamaliza kufanya uchunguzi wa tukio lililotokea na kuwakamata wahusika nitahakikisha naivunja shingo yako, Endelea kumbembeleza mkeo alale”Aliongea Lefayette kwa kingereza na kisha akapotea kwenye jengo hilo.
“Mfalme Pluto usimjali sana na maneno yake , ana majigambo makubwa kuliko hata saizi ya kichwa chake”
“Nitaamua nafanya maamuzi gani zidi yake ,ila kwasasa unaweza kuongozana nae na nitakuja kuwapa msaada mke wangu akiamka, kama utahitaji msaada wa dharula unaweza kuwasiliana na mimi”
“Ni swala rahisi sana kwetu kuwapata kama watakuwepo ndani ya jiji la Dar kwani tumekuja na kifaa maalumu cha kuwa nasa”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa hakuwa akijua kuna kifaa cha kuweza kutambua Vampire.
“Okey , kama utakutana na bwana anaefahamika kwa jina la Mourihno mwache huru , wengine ukiwapata nitaarifu kwani nataka kuwaona pia , usiwaue kwani ninataka kuwahoji”Aliongea na Lilith alikubaliana na Roma na kisha na yeye alipotea palepale.
Upande mwingine ndani ya maeneo ya Kigamboni ndani ya jumba ambalo lipo pembezoni mwa bahari alionekana mwanaume ambaye amekaa kwenye Sofa la Leather huku akiangalia upande wa nje wa baharini akiwa ameshikilia glasi yenye kimiminika cha rangi nyekundu.
Alikuwa ni mzungu ambaye ngozi yake kidogo ilikuwa na vidoa vidoa vya rangi nyeusi shingoni ambalo ni dhahiri huenda ni kutokana na mazingira ya joto ya jiji.
“Je unafahamu ni damu ipi ndani ya dunia hii ni tamu na tamu sana?, Kwanza kabisa ni damu inayoka kwenye mwili wa mtu aliejengeka kimazoezi , Pili damu inayotoka kwa mwanamke bikra na mwisho kabisa ya damu tamu zaidi ni kutoka kwa kitoto kichanga ambacho kimetoka kuzaliwa”Aliongea.
“Vipi umetoka mawindoni tena?” Ilisikika sauti nyuma yake na yule mzungu alilamba lipsi zake .
“Kwanini niende mawindoni wakati natafutwa na jiji lote na isitoshe sina uwezo wa kupambana na kaka yako”
“He is not my brother”Aliongea Denisi ambaye sasa alionekana vyema kwa mwanga wa jua.
“Yule sio kaka yangu , bali ni mjinga mmoja ambaye ana uwezo kuliko wajinga wengine”Aliongea na kumfanya yule mzungu macho yake kuongezeka kidogo.
“Inaonekana umeweza kumdanganya, nilitegemea ukirudi hapa utakuwa nusu mfu”
“Hahaha… hio ilikuwa zamani na sio sasa hivi , yule kwangu ni kama mdoli tu wa kucheza nao”Alijibu Denisi
“Kwanini unajiamini hivyo , mnaweza kuwa ndugu lakini anaweza kukuua”
“Hawezi “
“Kwanini?”
“Kwasababu maisha yake yalikuwa ni ya upweke ,akiniua ataonekana kama kichaa na wanaompenda watamkimbia na kutokumuamini”
“Ubinadamu si ndio?”
“Ndio, kila binadamu anazo hisia pale anapozungukwa na watu wanaompenda na huo ndio udhaifu wake Roma , so if he cares about his family , friends and lovers he ll never be a true god , He is defeitable”
Ni dhahiri kwamba Denisi alikuwa na ushirikano na Vampire ambalo limemuua msanii Dina na hata kutoa sabababu kwamba anaenda kuripoti jeshini ulikuwa uongo na alikuwa akija hapo kwa ajili ya kukutana na Vampire.
Sasa haikueleweka wote hao ni washirika wa Yan Buwen au Lah , lakini kwa maelezo ya Mourihno ni kwamba alikamatwa na wenzake na kuletwa Dar kwa ajili ya Yan Buwen kuhitaji damu zao.