Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Binafsi nimesoma riwaya nyingi sana na mm ni mlevi wa kusoma, labda niseme tu kitu Singanojr ni kipaji kikubwa sana, sijazuia maoni ya mtu mwingine juu yake, akiendeleza moto huu kwenye story zingine tano namuona mbali mno, keep it up bro
 
Binafsi nimesoma riwaya nyingi sana na mm ni mlevi wa kusoma, labda niseme tu kitu Singanojr ni kipaji kikubwa sana, sijazuia maoni ya mtu mwingine juu yake, akiendeleza moto huu kwenye story zingine tano namuona mbali mno, keep it up bro
Roma kazid uchaw asee mtu gan anapaa tu
 
Yeye hauzi kwa Jumla bali anauza kwa vipande vipande visivyo kamilifu, ana group huko telegram lenye members 71 Waliolipia 5000 Tsh kujiunga, ila kila mwezi huwatoza 2500 ili awape mwendelezo. ambako kazuia copy & forward.

Ila kwa kuwa telegram sio mali yake hawezi kuzuia watu wasiolipia wasisome story ndani ya hili group, kuna wajanja wanawaunga mabest wao kwa ku add acc kupitia namba ya aliyelipia, so hajui kuwa kuna watu zaidi ya 1k wanasomaga story yake huko telegram pasipo kuilipia 😂😂

Sasa sijui anafaidika nini kwa kuzuia copy & forward, ni heri awe atafute mbinu mpya za kuuza ila wajuba walishamharibia mpango wake wa kuuzia watu wengi zaidi hiyo story, mbaya zaidi hata story yenyewe imekosa mvuto. Insider man kaja juzi juzi tu hapa na keshamzika singanojr kwa story yake ya jinsi biashara ya Uber iliyonikutanisha na mrembo wa ajabu. yenye viewers wasiopungua 2M

Kazi kwake singanojr
Kama hupendi story za singanojr si upige tu kimya ili kuacha wengine wasome wanaomfuatilia?🤔
 
SEHEMU YA 553.
Siku iliofuata Edna akiwa ofisini akiwa bize na majukumu yake aliweza kutolewa katika umakini na mtu aliekuwa akigonga mlango.
“Come in..”
Aliongea huku akirudisha macho yake kwenye chati na baadhi ya namba zilizokuwa kwenye monitor ya Tarakishi yake na hakujisumbua hata kuangalia nani ambaye anaingia.
Mlango wa ofisi ulivyofunguliwa alionekana Recho akiingia huku akiwa na tabasamu usoni.
“Boss! , Amina amefika kuonana na wewe”Aliiongea
“Amina yupi? Nina miadi ya kukutana na mgeni leo?”Aliuliza Edba huku akiwa na mwonekano wa kushangaa kidogo.
“Ni Amina mkurugenzi kutoka Kayanda Group, amesema..”
“Sitaki kuonana nae..”Aliongea Edna kwa sauti ya kikauzu akimkata juu kwa juu Recho.
“Oh!, Sawa .. Boss”Recho alijikuta akishangazwa na bosi wake lakini aliishia kutingisha kichwa kukubali lakini muda huo huo Amina alitokeza nyuma yake.
“Tadaa! Sister Edna ni mimi, kwanini unakataa kukutana na mimi jamani,nimekuletea zawadi”AliongeaAmina kwa kingereza huku akiweka sauti ya ucheshi na hakubakia kwenye mango kwani aliingia moja kwa moja ndani ya ofisi na kumfanya Recho ashindwe kumzuia.
“Wow! Ofisi yako ni kubwa mno na ya kupendeza , lakini haina vitu vingi , unaonaje nikununulie baadhi ya maua ili kuipendezesha?”Aliongea huku akikaa kwenye sofa bila kukaribishwa.
Edna alijikuta aking’ata meno kwani mpaka hapo alishindwa kumfukuza kwani tayari amekwisha ingia , alimwangalia Recho kwa ishara na palepale alielewa na kutoka kisha akafnga mlango.
Aliweka makabrasha yake vizuri kwenye meza na kisha alinyanyuka kutoka kiti cha kazi na kwenda kukaa kwenye sofa , na wakati ambao anataka kumuuliza kwanini yupo hapo alishanga mara baada ya kuona Amina alichobeba.
“Keki hizo?”Aliuliza mara baada ya kunusa harufu yake.
“Sister Edna una pua zinanusa hatari , bado zimefungwa lakini umeweza kufahamu nilichobeba?”
“Imeandikwa hapo juu ya mfuko”Aliongea Edna akinyoosha kidole.
“Ah!, sikuangalia kumbe kuna jina”Aliongea huku akijibaraguza na kumfanya Edna asafishe koo kidogo na kisha akajilazimisha kutoa macho yake kutoka kwenye mfuko huo.
“Haya niambie kwanini upo hapa asubuhi asubuhi?”
“Hehe.. nilitaka kukuona tu”Aliongea Amina huku akisugua mikono yake kwenye mapaja maana alikuwa na wasiwasi.
“Acha kupoteza muda wangu nenda moja kwa moja kwenye pointi”Aliongea kikauzu na kumfanya Amina akakamae mwili na kisha akavuta pumzi na kuzitoa.
“Sister Edna lini unarudi nyumbani? , Rudi bwana naomba usiendelee kuwa na hasira nae”Aliongea na kumfanya Edna amwangalie kwa macho yasio eleweka na kisha akatoa tabasamu hafifuu.
“Unataka kweli nirudi au unanisanifu?”Aliuliza na kumfanya Amina kushangazwa na swali hilo lakini alijibu haraka haraka.
“Ndio nataka urudi , hatujisikii vizuri kwa wewe kugombana na Roma,najikuta najisikia vibaya”
“Kwanini , nadhani ingeweza kuwa jambo zuri kwenu kama tukiachana?”
“Inaweza ikawa vizuri kweli lakini haimaanishi kwamba hiko ndio tunachotaka , Edna natamani wewe na mumeo msiwe na mahusiano mazuri , naamini sio mimi tu ambaye naomba iwe hivyo hata kwa Rose na wengine wanawaeza kutamani hivo , lakini hebu fikiria kwa umakini, wanawake siku zote wamekuwa wakimfuata Roma mwenyewe kipindi alichokuwa nje ya nchi na hakuwakataa , lakini alivyokuja Tanzania licha ya kukutana na Rose na Najma na wakaonyesha kumpenda kweli lakini hakutaka kuanzisha nao mahusiano , kwa mtazamo wangu kipindi hiko siamini kama alikuwa anajali sana kuhusu mahusiano, naamini ameweza kutulia chini baada ya kukutana na mwanamke anaempenda, Edna Roma anachojisikia juu yako ni tofauti na kwetu sisi hivyo hata kama tunampenda na kumuonyesha mapenzi hakuna namna ambayo tunaweza kumuiba kutoka kwako , hivyo usiwe na hasira tena , Mumeo anaweza akawa anaonekana sawa lakini ana mawazo sana sasa hivi”
“Una staili ya kuongea moja kwa moja bila kuzunguka zunguka”Aliongea Edna baada ya kuwa kimya kidogo na kumfanya Amina kucheka na kutoa meno yake meupe nje.
“Najiua sipo smart kama wewe na ndio maana sikutaka kuzunguka zunguka, nimeona ni vizuri kukuambia kile ninachofikiria”
“Yeye ndio kakuambia napenda kula hizo keki?”
“Ndio, alinipa hela jana na aliniambia ni kwa ajili yangu ninunue keki nile , wakati mimi sio mpenzi wa keki kama hizi zenye mchanganyiko wa mchele”
“Una nini wewe kwanini usipende kula hizi keki , hivi unajua zina ntamu kiasi gani?”Aliongea kwa mshangao kutokana na yeye kupenda keki aliamini mwanamke yoyote angezipenda.
“Namaanisha sijawahi kuonja keki za namna hii , nimezoea zile kubwa kubwa”
“Huwa sipendi kuwa na urafiki na watu ambao hawapendi hivyo vikeki”
“Kama ni hivyo nadhani hata mimi nazipenda pia , harufu yake ni nzuri”Aliongea Aina akijitahidi kuwa chawa kadri iwezekanayo ili mradi tu kumfurahisha mke mkubwa.
“Acha hila”Aliongea na kisha alichukua ule mfuko na kutoa keki moja na kutoa ganda la juu na kisha akala kipande na kuanza kutafuna huku akifumba fumba macho kwa kusikilizia utamu.
“Niambie unachotaka , najua una kitu kingine ndio maana umekuja kuniona?”
“Ah! Umejuaje?”
“Kwasababu mtu ambaye angekuja hapa kunibembeleza ni Bi Wema, maana kuruhusu mtu kama wewe kungeniongezea tu hasira , Lazima umejitolea kuja kwa sababu kuna kitu unahitaji”Aliongea na kumfanya Amina kuanza kumuonea huruma Roma kwani moja kwa moja aliona IQ ya mke wake ni kubwa kuliko ya kwake.
“Ni kuhusu kampuni yetu , sijui chochote cha kufanya ndio maana nimekuja kuomba angalau unipe ABC..”
“Kampuni yako inajihusisha na maswala ya vyakula , mahoteli pamoja na nishati nadhani ukitoa upande wa nishati mengine ni biashara ambazo sina uzoefu nazo”
“Lakini sina mtu yoyote wa kumuomba msaada na akili yangu imekwama kabisa”Aliongea kwa kutia huruma.
“Kama ni hivyo kwanini una wasiwasi?”Aliuliza Edna na kumfanya Amina aanze kumwelezea namna ambavyo kampuni yake ipo kwenye ushindani wa kushinda tenda kutoka serikalini ya usambazaji wa gesi kwa teknolojia ya kisasa ya mabomba.
“Wasiwasi wangu ni kwamba kama washindani wetu watafanikisha kupata hio zabuni kutoka serikalini biashara yetu ya kuuza gesi itakufa moja kwa moja , kwani mpaka sasa tunasambaza kwa njia za kawaida za mitungi , ijapokuwa mikoani bado tunaweza kuwa na wateja lakini hapa Dar tuna wateja wetu wakubwa”Aliongea huku Edna akimsikiliza lakini wakati huo huo akiendelea kutafuna keki.
“Kama mnahofia kutoshinda zabuni basi ninaamini kuna mtaalamu ambaye katika kampuni shindani wanamtumia kutokana na teknolojia yake nadhani kama sio hivyo mambo yasingekuwa magumu ukizingatia na uzoefu wenu wa kibiashara , anaeongoza hio Prokekti ndio mtu wa kudili nae , yeye na timu yake nzima”
“Upo sahihi , lakini tupo kwenye hali mbaya kwasasa, kama ulivyosem tokea mwanzo kampuni yetu ilikuwa ikijiandaa na fursa hii , tuliamini itafikia mahali haina haja kwa wakazi wa jiji kuhangaika kununua gesi kwa mitungi zaidi ya kuunganishiwa teknolojia ambayo gesi wanaipata kwa kulipia bili , sasa aliekuwa akiongoza utafiti wa projekti hio aliacha kufanya kazi kwenye kampuni yetu na kisha akaenda nje ya nchi kwa ajili ya kujiendeleza kimasomo na alivyorudi akaajiriwa na washindani wetu , hivyo kapewa kuongoza projekti hio , sikuwa nikifahamu sana kuhusu hilo lakini wafanyakazi wa kampuni ndio waliniambia na inaonekana anafanya kushindana na sisi kwa makusudi kama kulipiza kisasi kwani wakati akiwa ndani ya kampuni hakupewa thamani aliokuwa akiitaka”Aliongea kwa kirefu na kumfanya Edna atingishe kichwa.
“Nitakueezea mbinu kwasababu angalau umeniletea hizi keki, lakini mbinu ninayokwenda kukuelezea itategemeana na bahati yako pamoja na ujasiri”Aliongea na kumfanya Amina kutoa tabasamu.
“Sister Edna kweli unaenda kunisaidia?, ushajua nini chakufanya tayari maana ndio nimekuambia sasa hivi na hujafikiria”
“Sio ngumu sana kama unavyofikiria , kila tatizo linategemeana na mtu , mshindani wako anaonekana ni mtu mwenye majivuno na kujikweza, lakini pia anaonekana kuwa mtu mwenye tamaa na hana mawazo mapana , mtu kama huyo kudili nae ni rahisi sana”
“Unamaanisha huyu mkaka aliepewa kuongoza hio Projekt , kama ni huyo ni kweli kabisa anachukiza mno , lakini kutokana na sifa aliojijengea miaka na miaka anaifanya kampuni yetu kuwa katika upande wa hasara”
“Ngoja nikuulize swali , kama ni hivyo kampuni yao imempatia nini kama ofa ya kufanya nae kazi?”
“Watamchagua kama Mkurugenzi msaidizi na pia watampatia mgao wa asilimia ishirini kutoka katika faida , kama atafanikiwa kupata tenda hio”
“Kama wewe utataka sasa hivi kwenda kumshawishi arudi kwenu , ni kipi unachoweza kumpatia kama ofa?”
“Sister Edna unamaanisha kumpatia kazi tena kwenye kampuni yetu , sidhani kama atakubali kwani anatuchukia sana”
“Unakosea , kila binadamu ana udhaifu hususani kwenye ulimwengu wa biashara , kipaji cha mtu hakiwezi kushinda mbele ya mtu tajiri , kama utapoteza kwa mtu mwenye kipaji inamaanisha huna hela za kutosha ndio maana wafanyabiashara siku zote wanajali sana faida kuliko kitu kingine chochote”Aliongea Edna na kumfanya Amina asielewe anataka kumaanisha nini..
“Kama ni hivyo Sister Edna natakiwa kufanya nini ili kumrudisha katika kampuni yetu?”Aliuliza na kumfanya Edna kumwangalia kwa mwonekano flani hivi ambao hauleweki na kumchanganya Amina.
“Edna usiniambie unataka ni.. ni.. Aaa..”Alianza kusita sita kuongea kwa wasiwasi.





SEHEMU YA 554.
Edna alijikuta akishangazwa na namna Amina alivyochukulia maneno yake.
“Nini tena?”
“Sister Edna nakubali nimekukosea sana lakini mimi sio mwanamke mhuni , nipo siriasi katika uhusiano wangu nilio nao sasa, kama unaniambia niende kujilengesha kwake siwezi kufanya hivyo kwa namna yoyote ile hata kama utaniona sina akili”Aliongea na kumfanya sasa Edna kuelewa akili ya Amina ilipo na alijikuta akipandwa na hasira.
“Unaongea ujinga gani? , hivi unadhani ukienda kujilengesha kwake utafanikiwa , Aisee wewe ni mjinga kweli””Aliongea na kumfanya Amina kuona aibu kumbe alifikiria vibaya.
“Kama ni hivyo napaswa kufanya nini?”
“Ninachojaribu kukuambia ni kufikiria nini unaweza kumpatia kama ofa”
“Nadhani ni kumuongezea pesa nyingi zaidi kuliko aliopewa , Tenda hio ni ya bilioni arobaini na tano za kitanzania na kama atafanikiwa kuipata nadhani anakwenda kuwa milionea tayari, lakini siwezi kumpatia nafasi kubwa kwenye kampuni yangu zaidi ya alioahidiwa kwenye kampuni nyingine”
“Kama ni hivyo, je umejaribu kuwasiliana nae na kumtajia kiasi kikubwa zaidi kama alichoahidiwa ili kurudi kwenye kampuni yako?”
“Sijajaribu kuwasiliana nae , isingewezekana kwani tumejaribu pia kuwashawishi tushirikiane katika tenda hio lakini wamekataa kutokana na kuamini wanaweza kuipata wenyewe “
“Kama ni hivyo jaribu kuwasiliana nae na umuulize nini anataka apewe na kuweza kurudi kwenye kampuni yenu”
“Si anaweza kuchukulia swali hilo kutajia kitu kikubwa?”
“Wewe nisikilize kwanza..”
“Oh..”
“Baada ya kuwasiliana nae jaribu kuongea nae vizuri bila kujali tabia yake , igiza kama vile unahitaji kweli msaada wake na kama ataomba kitu kikubwa zaidi kwa mfano hisa za kampuni , cheo au gawio, wewe kubali ili mradi tu asiombe nafasi yako kama mkurugenzi mkuu na mwenyekiti wa bodi”
“Lakini si itakuwa..”
“Subiri nimalize sentensi yangu”
“Oh..!”
“Wewe kubali masharti yake licha ya kwamba sio mazuri na mkishakubaliana panga nae miadi ya kukutana kusaini mkataba , tafuta sehemu ambayo ni tulivu na imejitenga ili mradi tu kumlegeza msimamo wake , hakikisha wewe ndio unakutana nae na kuongea nae ana kwa ana , halafu kitu muhimu usisahau kujiremba , ukivutia zaidi litakuwa jambo zuri , sasa ukiwa nae kwenye meza hakikisha unatabasamu muda wote kama vile kuna kitu anakuambia na kinakufurahisha kisha msogezee mkataba na atakapotaka tu kusaini mzuie na mwambie umebadili mawazo na unajutia uamuzi wako”Aliongea Edna na kumfanya Amina kushangaa.
“Sister Edna si juhudi zangu zote zitapotea sasa, naamini atakuwa na hasira zaidi na atatuchukia sana”Aliongea na kumfanya Edna kuangalia pembeni na kutabasamu kwasiri na kisha akamgeukia.
“Ndio, naamini pia haitokuwa rahisi , lakini kumbuka kabla hata hujakutana nae unatafuta mwandishi wa habari wa maswala ya uchumi au hata Paparazi”
“Kwa ajili ya nini?”
“Atakachotakiwa kufanya ni kuficha Kamera katika eneo ambalo mnafanyia mazungumzo na kama ni kuwapiga picha lazima iwe wakati ambao anataka kusaini”Aliongea Edna huku akitoa tabasamu na kumfanya Amina akili yake kufanya kazi palepale na kuelewa Edna anachotaka kumaanisha.
“Nimekuelewa sasa kama nitafanya hivyo kampuni yake haitomuamini tena kwasababu ameonekana kujihusisha na mimi na wataamini amekubali kuungana na sisi kutokana na namna ninavyotoa tabasamu”
“Bingo , kama kampuni wakiona picha hizo , hawatokubali kuendelea nae kwani hawatokubali kutoa nafasi ya kufanya makosa kwa tenda muhimu kama hio , na ikifikia hatua hapo kampuni mara nyingi itamshuku kutokana na kukutana na wewe hata kama hajasaini mkataba , isitoshe walio juu yake hawana udhibiti na kile alichobobea , timu yake pia itaamini amewasaliti na ikifikia wakati huo kuna mawii ambayo yanaweza kutokea , cha kwanza ofa aliopewa inaweza kuondolewa kwake na akabakizwa kwenye kampuni au kampuni ikamfukuza kabisa , kama itatokea haijamfukuza , kwa mtu kama huyo mwenye majigambo na kujikweza kwa vyovyote vile atashindwa kabisa kuvumilia watu kumshuku, hivyo moja kwa moja ataacha kazi kwa hiari yake mwenyewe”
“Sasa hayo yote yakishatokea unachotakiwa kufanya sasa ni kuwasiliana nae kwa mara ya pili na kumpa ofa tofauti na ya mwanzo na atarudi kwenye kampuni yako na ataendelea na projekti , hata kama hatakuwa na furaha lakini bado atafanya kazi na baadhi ya watu katika timu yake wanaweza kumfuata pia, na mpaka hapo utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kushinda zabuni , isitoshe kampuni yako ni kubwa likija swala la uzoefu , Koneksheni na makampuni ya nje lakini pia mnao mzungumko mkubwa wa hela tofauti na mshindani wenu , hivyo mkitumia yote hayo kama sababu basi moja kwa moja mpo katika asilimia kubwa ya kushinda tenda”Aliongea na kumfanya Amina kusimama kwenye sofa kwa mshangao.
“Upo sahihi kabisa , hili litafanya kazi , ah kwanini sikufikiria mbali hivi, nikishampata na akaja kufanya kazi kwetu moja kwa moja… Sister Edna hakika una akili nyingi natamani nikukumbatie…”Kauli yake ilimsaliti kwani tayari ashamkumbatia na kumpiga busu shavuni na kumfanya Edna kutoa macho.
“Hahaha… naenda sasa hivi kuiambia idara ya masoko na uhusiano kutafuta kituo chochote kidogo cha habari kinachojihusisha na maswala ya uchumi na kisha tunawapa rushwa na mambo yatakuwa marahisi”Aliongea na kumfanya Edna kushika eneo alilopigwa busu , hakuzoea kupigwa busu na mwanamke.
“Hapana huwezi kutoa rushwa kwa kituo kizima cha habari bali unaweza kumpa rushwa mwandishi wao tu”
“Kwanini?”
“Ukishafanya hivyo moja kwa moja itakuwa rahisi kampuni yake kuchimba ukweli na wataweza kugundua mchezo wako , hivyo kitu pekee unachoweza kufanya na isigundulike ni kumhonga mmoja wa waandishi wao na atatunza siri , lakini pia tafuta mahali palipo tulia na hakikisha sio ndani ya chumba iwe ni sehemu kama mgahawani eneo la nje ila ambalo halina watu wengi, ikiwa ni ndani ya chumba lazima watajua aliwekewa mtego ila ikiwa nje itakuwa rahisi watu kujiuliza maswali, kumbuka mpango ni kumfanya tu asiaminike haijalishi itakuwa ni kweli au sio kweli ilimradi tu hawapati majibu wanayotataka”Aliongea na kumfanya Amina kumwangalia Edna kwa macho ya mshangao.
“Kwanini unaniangalia hivyo?”
“Hamna najaribu kufikiria kama tungekuwa tukifanya biashara zinazoendana na ukawa mshindani wangu , nadhani ungekuwa ushanunua kampiuni yangu muda mrefu tu”
“Nilijua tu utaniona kama mtu mkatili , hio ni hila nyepesi sana , ni kwasababu udhaifu wake unaonekana wazi hivyo kufanya mambo kuwa marahisi”Aliongea na kumfanya Amina amkumbatie tena.
“Asante sana Sister Edna najua unapenda kunichokoza lakini unanijali”Aliongea lakini Edna hakutaka kumvumilia na alimsukuma kumtoa kwenye mwili wake.
“Usije ukajarabu kunikumbatia tena wala kunibusu sawa”Aliongea na kumfanya Amina kucheka na kukaa chini.
Waliendeea kuongea namna ya kukamilisha mpango huo mpaka muda ambao Amina aliaga na kuondoka.
Edna alijikuta akivuta pumzi na kuzishusha kwa ahueni, ukweli ni kwamba licha ya Amina kuwa umri sawa na yeye lakini alionekana kama mtoto mbele yake , alijiona kama vile anaongea na mdogo wake na alijisikia furaha kumsaidia licha ya kujua ni mchepuko wa bwana yule.
Alianza kujiuliza je ni kweli ashaanza kukubaliana na ukweli juu ya uwepo wa michepuko hio mpaka kufikia kuwajali na kuwasaidia.
Alijikuta akigeukia boksi la keki na kuzingalia kwa mwonekano ambao haukuwa ukitafsirika kwa neno moja.
*****
Ni muda wa jioni saa kumi na mbili, Edna alikuwa akiendesha gari yake aina ya Merecedez S class ya rangi nyekundu huku akiwa ameshusha kioo ili kuruhusu upepo wa baharini kumpuliza.
Alikuwa ndio anarudi kwenye nyumba yake mpya na mwonekano wake ulikuwa ni ule wa usiriasi akiwa sio mwenye kujali watu wanaotembea kwa miguu maeneo ya nje , lakini kwa wakati mmoja moyo wake ulikuwa mzito mno, huenda ingekuwa zamani angekuwa sawa kwani maisha yake alizoea akirudi nyumbani kama hivyo basi angepokelewa kwa shangwe na Lanlan , lakini ilikuwa tofauti kwa nyumba ambayo kwa wakati huo anaiita nyumbani kwake.
Edna aliweza kufika nje ya geti na wakati akiwa anaingiza gari getini alishangaa kuona mbele yake kuna gari nyingine ilioongezeka , gari aina ya Aud A8 , ni gari ambayo hakuweza kuotea mmiliki wake kutokana na kwamba katika gereji yake ya magari kuleUnunio hakukuwa na gari aina hio.
Baada ya kusimamisha gari kwa wasiwasi gari ile ilifunguliwa mlango na akatoka mwanaume ambaye aliweza kumfahamu hata kabla hajamgeukia , alikuwa ni Raisi Jeremy na kwa muonekano wake ni kama alisubiri hapo kwa muda mrefu.
Edna akiwa amekodoa macho Raisi Jeremy aliinua mkono wake wa kulia na kumpungia mkono na kumfanya Edna kwa wasiwasi kusogeza gari yake mpaka katikati ya eneo hilo na kisha akasimamisha pembeni na kutoka nje ya gari huku akiwa na hisia ambazo hakuzielewa.
“Edna ndio unarudi ? Haha… nilimwambia msadizi wangu muda si mrefu ungefika na hatimae ni kweli”Aliongea huku akiweka sura ya uchangamfu kadri awezavyo.
Edna alikuwa kwenye mshangao maana huyo mtu ni raisi wa nchi na anayo majukumu mengi , hivyo alishangaa kumuona kuja mpaka nyumbani kwake.
“Unafanya nini hapa Mheshimiwa?”Aliuliza Edna.
“Nilikuwa na wasiwasi juu yako , hivyo nimekuja kukuangalia na nimeridhika kukuona unaendelea vizuri?”
“Wasiwasi juu yangu kwasababu gani?”
“Hata kama hujaniambia nishasikia kinachoendelea , si umekosana na Roma mpaka kufikia hatua ya kuhama , usinilaumu kwa kuja hapa , ukweli ni kwamba siku zote nakujali sana”
“Mr President sidhani hili la kwangu linakuhusu”
“Linanihusu ndio , wewe ni binti yangu , kwanini niwaangalie tu wakikuchokoza , umefanya maamuzi sahihi kuondoka nyumbani , binti yangu mimi hastahili kutendewa vibaya , nina uhakika wamekukosea , wewe ni mpole na mkarimu huwezi kuwakosea ..”Aliongea na kumfanya Edna kuguswa na maneno yake kidogo lakini hakutaka kuonyesha wazi.
“Inatosha na tuachane na haya maonge , Mheshimiwa nadhani unapaswa kuondoka sasa hivi , hupaswi kuja mahali kama hapa kwa ajili ya mtu kama mim”Aliongea Edna na kumfanya Raisi Jeremy sura yake kujikunja.
“Binti yangu , nipo hapa kwasababu niikuwa na wasiwasi , kwanini usinipe nafasi tukaongea kidogo”Aliongea na kumfanya Edna kujizuia kuendelea kuongea na muda uleule maidizi wake ambaye alikuwa kwenye gari alitoka na hakuwa mwingine bali ni Linda.
“Mheshimiwa utakuwa na mkutano kesho asubuhi nadhani tunapaswa kurudi Rwanda leoleo upate muda wa kujiandaa kwa hotuba”Aliongea Linda.
“Linda huoni nipo hapa naongea na binti yangu ..”Aliongea huku akipandisha sauti kidogo.
“Lakini mheshimiwa..”Linda alijikuta akikosa neno kutokana na mabadiliko ya Raisi Jeremy.
“Mheshimiw anadhani itakuwa jambo zuri kama ukirudi tu”Aliongea Edna na kumfanya Raisi Jeremy kumwangalia kwa dakika kadhaa na kisha akatingisha kichwa.
“Okey nitakuja tena siku nyingine , nitaarifu kama itatokea kuna mtu yoyote anajaribu kukuchokoza nitamshughulikia , si nilikuachia namba yangu ya simu mara ya mwisho , wewe piga tu bila ya kujali muda huo nafanya nini kwani nitapokea simu yako , nitafurahi sana kama utakuwa tayari kunipigia simu”Aliongea na Edna hakuongea lolote zaidi ya kutingisha kichwa nadhani aitaka aondoke tu amuache.
“Kwasasa nadhani napaswa kurudi Rwanda , siku moja unapaswa kuja kunisalimia ukipata muda , nadhani nishakuambia nitakupatia kila kitu changu , sikuwa nikidanganya nipo siriasi”
“Mheshimiwa inatosha”Aliongea Edna huku akianza kutetemeka na alijitahidi kujizuia na Raisi Jeremy hakuongea neno lolote zaidi ya kurudi kwenye gari na kisha kuondoka hapo ndani na dakika mbili tu baada ya gari yake kuingia barabarani magari kadhaa yalionekana yakitokea kila chocho na mangine yalitangulia mbelel na mengine kufuatia nyuma yake , ilionekana ni wasaidizi wake na walikuwa wamejificha ndio maana hata Edna hakuweza kuyaona au aliyaona na akayapuuzia.


















SEHEMU YA 555.
Upande mwingine siku hio hio ikiwa ni majira ya usiku Roma na Rufi walikuwa wakitembea katika mitaa mbali kidogo na eneo wanaloishi, Rufi alitaka kwenda kuona baadhi ya mitaa inayofanyikia biashara wakati wa usiku na ndio maana Roma akatoka nae.
Alifurahi sana kwani aliweza kununua kuku wa kukaanga na njiani na kutafuna.
Kila alipoona kitu kinauzwa njiani na hakijui alimuomba Roma wasimame na amnunulie , alikuwa na furaha mno na huenda hajawahi kuwa katika furaha ya aina hio tokea azaliwe na Roma alifurahi pia kumuona ni mwenye furaha.
Sasa baada ya kutembea umbali mrefu huku wakiongea Roma alijikuta akikunja ndita mara baada ya kugeuka upande wa kulia na kumfanya Rufi kushngaa.
“Hubby nini tatizo?”Aliuliza Rufi huku na yeye akigeuka.
Nyuma yao kulikuwa na vijana wawili wa kizungu ambao wamevalia masweta wote kwa pamoja ya rangi nyeusi yenye kofia , mmoja aikuwa ni msichana na mwingine alikuwa ni mvulana, kwa jinsi ambavyo walikuwa wakionekana ni dhahiri walikuwa wakiwafuatilia Roma na Rufi.
Roma palepale aliwakazia macho na wale wazungu mara baada ya kuona wanaangaliwa walikaza mwendo wakidhamiria kumpita.
“Nyie watu nilijaribu kuwapotezea kwa muda mrefu , hebu jaribuni kuwa na akili muda mwingine , uvumilivu wangu una kikomo , nipo hapa najaribu kumtembeza mpenzi wangu na sitaki kuua usiku huu”Aliongea Roma kwa lugha ya kingereza.
“Wewe shetani nipo hapa kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa ulichomfanyia baba yangu , kama hutaki nikufaatilie tafuta sehemu ya wazi isiokuwa na watu tupigane”Aliongea yule mwanaume kwa lugha ya kingereza akimjibu Roma kwa kumuita shetani.
Roma alikuwa akiwatambua watu hao kwani ashawahi kukutana nao nje ya nchi, walikuwa wakitokea katika kundi la kichawi kutoka Scotland lifahamikalo kwa jina la SIS(Sword in the stone).
Baba yake afahamikae kwa jina la Leswente aliuliwa na Roma na tokea kipindi hiko Prince alikuwa na mipango ya kulipiza kisasi , hakuwa na mpango wa kuacha mawazo yake licha ya kwamba ni moja ya watu walioshuhudia uwezo wa Roma nchini Ufaransa katika mkutano ulioandaliwa na Depney kwa ajili ya teknolojia ya Thanatos.
Msichana aliekuwa nae Prince alifahamika kwa jina la Emma ni mpenzi wake .
“Hubby hao ni wakina nani?, kwanini wanataka kupigana na wewe?”
“Wapotezee tu”Aliongea Roma na kisha alimshika mkono na kuanza kutembea wakiipita shule ya msingi ya Ununio na kwenda mbele.
Wale wazungu wawili hawakuwa na mpango wa kumuacha aondoke , hivyo walimfata kwa nyuma .
Rufi aliekuwa akifurahia muda wake na mpenzi wake Roma Ramoni sasa alijawa na wasiwasi na mudi yote ya furaha ikapotea na hata Roma aliweza kuona wasiwasi wake.
“Rufi nadhani tuishie hapa kwa leo , hivi vitoto haviwezi kuacha kunifuatilia bila kuvipa maumivu”Aliongea Roma na Rufi alikubali na kisha walikunja kulia na kutokea eneo ambalo walikuwa wameegesha gari yao na kuingia kisha kuanza safari ya kurudi na wale wazungu pia ilionekana walifika hapo na gari kwani na wao waliingia kwenye gari iliokuwa pembeni ya gari ya Roma na kuanza kumfuatilia kwa nyuma.
Dakika chache tu tayari Roma alishafika katika maeneo anayoishi na hakuingiza moja kwa moja gari ndani ya uzio wa nymba ya Bi Wema bali aliliegesha pembeni.
“Una ujuzi mzuri wa kuendesha gari , nadhani kweli umedhamiria kupigana na mimi lakini naamini ushaona uwezo wangu kule Ufaransa, s kwasasa nimekuwa na nguvu zaidi ya mwanzo , je bado unaona unaweza kunishinda?”Aliuliza Roma.
“Prince wangu amekuwa na uwezo mkubwa pia , usimdharau”Aliongea yule mwanadada aliefahamika kwa jina la Emma.
“Emma kaa kimya haupo kwenye nafasi ya kuongea , nani kasema mimi ni wako?”Aliongea Prince kwa hasira na kisha akamgeukia Roma.
“I’ve worked hard on improving my soul magic , I am far stronger than my father now , I did all this to get rid of you”Aliongea akimaanisha kwamba amefanya juhudi kujiimarisha katika mbinu yake ya uchawi wa kiroho na kujitapa kwamba ana uwezo mkubwa kuliko baba yake na yote hayo alifanya kwa ajili ya kumdhibiti.
“Nadhani kundi lenu la SIS halijaja hapa Tanzania kwa ajili ya kulipiza kisasi , lakini kwasababu upo hapa ukiwa peke yako nadhani umetoroka, vipi haugopi kupewa adhabu na wakuu wako?”Aliuliza Roma na kumfanya Prince kukasirika zaidi ni kama Roma amegusa penyewe.
“Stop Blabbering take this”
Aliongea na palepale alifungua kiganja cha mikono yake na ulionekana mvuke wenye kung’aa . ulikuwa mwingi kiasi kwamba ni kama vile ni chungu kinachochemka maji.
Kuna utofauti mkubwa kati ya uchawi na nguvu za kijini , wachawi wanachotegemea zaidi ili kushambulia kiroho ni uwezo mkubwa wa akili zao lakini nguvu za kijini zenyewe zinategemea zaidi mkusanyiko wa nishati iliondani ya mwili na sio lazima mtu atumie akili , tofauti nyingine ni kwamba ni rahisi kurithisha uchawi kuliko kurithisha nguvu za kijini hivyo kama nguvu za kijini zingekuwa zinarithishwa basi majini wengi wangekuwa na nguvu kubwa sana za kimababu na Roma asingefikiria kabisa kwenda ujinini.
Na ndio maana wachawi wengi kutoka Ulaya wanazaliwa na vipaji vikubwa ambavyo vinawafanya kuedelea kwa haraka na Prince alikuwa ni mfano hai.
Alichokifanya Prince kutengeneza mvuke ule wa kichawi kubadilisha nishati ya mazingira na kuingizia uchawi wa kurithi kutengeneza shambulizi la kiroho.
Roma aliweza kuhisi mkandamizo wa ajabu kwenye roho yake na kufanya mapigo yake ya moyo kwenda kasi mno na alijua anachokifanya Prince ni kutaka kuikamata akili yake na kumfanya kiachaa lakini kutokana na kuwa na uwezo mkubwa zaidi kuliko wake hakuna athari ambazo zimempata.
Ilibidi kwanza amkinge Rufi kwa kumzingira na kinga ya nguvu za kimaandiko na kisha alimsogelea Prince.
“Ndio njoo,, wewe shetani nitakufanya ujiuwe mwenyewe kwa mikono yako”Aliongea na palepale alianza kuongea maneno ya ajabu ajabu ambayo Roma hakuwa akijua tafsiri ila aliweza kugundua ni lazima alikuwa akijaribu kumroga.
Lakini licha ya hivyo kila alichokuwa akijaribu kuongea hakikuwa kikifanya kazi mbele ya Roma na alijikuta akitokwa na jasho na kuanza kupatwa na hofu.
“Wewe kwanini …”Alijikuta akipagwa na kumfanya Roma amwangalie kwa tabasamu la kifedhuli.
“Ni kheri kwako umekutana na mimi mpya , lakini kama ingekuwa zamani nisingekuacha uendelee kuishi”Aliongea Roma na palepale alimpiga ngumi ya ujazo eneo la tumboni ambayo ilimrudisha mita kadhaa nyuma.
Emma alijikuta akishangazwa na uwezo wa Rom kwani alikuwa ni kama amegusa tu lakini nguvu zake ziilikuwa na madhara makubwa.
“Naona umejitahidi katika kuukuza uchawi wako wa kurithi , hebu nielezee kwanza ni mbingu gani mnatumia , najua wote nyie mpo chini ya jamii ya Merlin magical society , maana lugha uliotumia kuita uchawi wako kama sikosei ni Druid”Aliongea Roma na kumfanya yule mwanadada aliefahamika kwa jina la Emma kushangaa.
“Umejuaje alikuwa akitumia Druid?”
“Hehe… unafikiri niliemuua ni baba yake tu , nimeuwa wachawi wengi wa bara la Ulaya wakiwemo wa kundi lenu la siraha kwenye jiwe”
“Wewe ni shetani … Emma kimbia atakuua na wewe huyu”Aliongea Prnce akijaribu kusimama kwa shida kutokana na maumviu.
“Siwezi kukuacha mwenyewe”Aliongea Emma na kumfanya Roma kucheka.
“Nani kawaambia nitawaua , sina hata hamu ya kuua vitoto kama nyie wakati mimi mwenyewe naitwa baba”Aliongea Roma , lakini muda huo huo gari aina ya Mercedenz Benz G series mbili ziliweza kufika katika hilo eneo kwa spidi kubwa.
Kwa haraka haraka Roma alijua lazima watakuwa wamefuatwa mara baada ya kugundulika hawapo , kwani alijua tu lazima wametoroka.
Baada ya gari zile kusimama alishuka mwanamke wa kizungu mwenye kiini cha macho cha rangi iliofifia akiwa amevalia nguo nyeusi tupu kuanzia juu mpaka chini , kulikuwa na giza lakini aliweza kuonekana vizuri.
“Your Majesty Pluto ,please have mercy on them”Aliongea na kisha akatabasamu na palepale alipotea aliposimama na kufumba na kufumbbua alikuwa mbele ya Roma
“Mfalme Pluto tunaomba uwasamehe Prince ni kijana mdogo na hata miaka kumi na nane hajafikisha , hatokusumbua tena atakapokuja kuelewa hana uwezo wa kushindana na wewe”Aliongea yule mwanamke kwa lugha ya kistaarabu akibembeleza.
“Sina haja ya kuwaua mimi, chukuaneni na mpotee katika hili eneo”Aliongea Roma kwa kuamrisha na yule mwanamke aliwapa ishara Prince na Emma kuingia kwenye gari na kisha wakaondoka.
“Hubby hawa wachawi wanafanya nini Tanzania , inamaana jeshi limewaacha wafanye watakavyo au hawana kitengo cha kupambana na uchawi?”
“Kitengo wanacho lakini naamini wananitega ili mimi niingilie , lakini siwezi kufanya hivyo kwani ni maswala ambayo hayanihusu”Aliongea Roma lakini muda huo huo alitokeza mtu mbele yao na kumfanya Roma kukunja sura , alikuwa akitoa Aura ambayo moja kwa moja ilifanana kwa asilimia kubwa na ninja wa kundi la Yamaguchi.
“Wewe ni nani?”Aiuliza Roma.
“Mr Roma nipo hapa kwa ajili ya kufikisha ujumbe”
“Ujumbe gani? Na wewe ni nani kwanza”
“Nimetumwa hapa na Afande Athumani mimi ni mlinzi wake”Aliongea yule bwana na Roma mara baada ya kusikia jina la Afande Aathumani alikumbuka jina la babu yake Sophia na Edna yaani baba yake Adebayo na alianza kujiuliza kwanini hawa wakuu wa majeshi wanalindwa na watu wa ajabu ajabu , kwani babu yake pia alikuwa hivyo hivyo na hata kwa Marehemu kigombola alikuwa akipewa ulinzi na Yamaguchi.
“Kuna taarifa gan?”
“Mshipi wa Kichawi umefahamika eneo ulipo na nimeambiwa nikufikishe hii taarifa”
“Hio taarifa haina haja ya kuniambie kwani ni swala ambalo halinihusu”Aliongea Roma lakini yule bwana hakuzingatia kauli yake.
“Eneo ni Msasani kwenye moja wapo ya nyumba iliouzwa hivi karibuni”Aliongea yule bwana na palepale moyo wa Roma ulipiga kwa nguvu kwani aliweza kuamini kama ni nyumba iliouzwa hivi karibuni basi mnunuzi alikuwa ni mke wake.
“Unatakiwa kufanya haraka maana taarifa zimetokea leo na wanaweza kuvamia nyumba hio muda si mrefu na Mzee anawasiwasi na hai ya kiusalama ya Edna”Aliongezea na kumfanya Roma amwangalie Rufi.
“Rufi ingia ndani na mwambie Bi Wema sitokuja leo”Aliongea Roma kwa haraka haraka na Rufi alikubali kwa kichwa.
“Mwambie asante kwa kunipatia taarifa”Aliongea Roma na kisha palepale akapotea.
*******
Ilikuwa ni saa mbili tayari, Edna alionekana akitoka bafuni huku akiwa amevalia tayari vazi la katani la kulalia , miguuni alikuwa amevalia visendo vya manyoya vilivyofanana na rangi ya taulo , hakujali hata kuzima TV sebuleni zaidi ya kupunguza sauti.
Muda huo huo simu yake iliingia ujumbe wa meseji na aliisogelea na kisha akaishikilia mkononi na kuufungua na ulionekana ni ujumbe wa meseji uliotoka kwa Blandina mama mkwe wake na alionekana kumwambia Edna kwamba yupo Kenya bado na anaendelea vizuri lakini pia anamuomba msamaha kwa kumshuku hivyo arudi nyumbani kwani Lanlan anahitaji malezi ya baba na mama.
Edna baada ya kusoma ujumbe ule alionekana kuwaza kwa muda na alitabasamu na kisha alipiga simu pale pale na kuweka sikioni na alionekana akiongea na mama mkwe wake kwa muda mfupi na kisha akakata simu.
Mara baada ya simu ile kuikata palepale ilianza kuita tena na alipoangalia ni namba ya Qiang Xi na alipokea na kuweka sikioni.
“Mommy !Lanlan misses you..”Sauti ya Lanlan ilisikika mara tu baada ya kupoktea simuu.
“Mama pia amekumisi sana Lanlan , je unataka kurudi nyumbani?”
“Ndio , Lanlan amekula sana hapa na ameshiba nyama ya bata , sitaki kuendelea kula nyama ya bata , nataka kurudi nyumbani , njoo unichukue”Aliongea na kumfanya Edna kushindwa kuzuia tabasamu na kumwambia anakuja kumchukua.
Waliongea kwa takribani dakika kumi na tano mpaka muda ambao Edna alimuaga Lanlan na kisha akakata simu.
Kutokana na maongezi yake na Lanlan kuwa ya kuhadithiwa namna alivyokula nyama za aina mbalimbali alijikuta njaa ikimshika na alitoka katika chumba chake na kurudi mpaka chini eneo la sebuleni na kisha moja kwa moja alielekea upande wa jikoni , lakini kabla hata hajaingia ndani kengele ya mlango ilisikika na aligeuka kwa wasiwasi na kuusogelea mlango.
Na mara baada ya kusogelea Intercom na kuiwasha ili kuangalia ni nani anagonga kengele , alijikuta mwili wake ukimsisimka kwa ubaridi wa woga mara baada ya kuona sura za watu wa rangi ya kizungu ambazo hakuwa akizifahamu na zilikuwa na mwonekano usiokuwa wa kawaida.
Mwanaume mmoja mwenye nywele nyeupe alisogea karibu na Kamera huku akiweka mwonekano uliojaa jeuri , kilichomuogopesha Edna zaidi ni kwamba watu hao tayari wapo ndani ya nyumba na sio nje ya geti.
“BAM!!”
Mlango wa kuingilia palepale ulipigwa na kitu kizito na ulifyatuka palepale na kufunguka kwa kasi.
Edna alijikuta akijawa na woga na kukimbia kurudi nyuma na muda huo huo wale watu waliingia ndani na kumkuta Edna aliekuwa amejibana kwenye ngazi za kupandishia juu lakini walionyesha kutokumjali ni kama vile hawajamuona.
“Who.. who are you?”Aliuliza Edna lakini hakuna ambaye alijali kujibu swali lake .
“Its around this house , search everywhere Quick”Aliongea akimaanisha kwamba kipo hapo ndani na watafute kila mahali kwa haraka na wote waliitikia na kuanza kutafuta kwa kasi ya ajabu mno isiokuwa ya kawaida na walianza kunyanyua masofa kuyageuza na kuangalia chini , walitafuta kwa njia isio kistaarabu kabisa kwani waiharibu na kurusha rusha vitu na kumfanya Edna azidi kuogopa.
Muda huo huo kicheko kilisikika kutoka nje na watu wengine waliingia huku wakiwa wametangulizwa na mwanaume wa kizungu ambae anasura kidogo yenye utanashati , aliefunga nywele zake nyeusi kwa nyuma , alionekana kama vile ana umri wa miaka ishirini au therathini kutokana na suti yake aliovalia.
“Udinese mbinu yako imetusaidia sana , asante kwa hilo”Aliongea mwanaume ambaye alifika akiwa wa kwanza.
“Una pua kama ya mbwa , Wewe Heinhotz kwanini kwenye ukoo wako wewe ndio upo hapa peke yako? Raphaei yuko wapi?”
“Hakuna haja ya kiongozi wetu kuja mpaka hapa Tanzania , Magic Girdle ni kwa ajili yetu”Aliongea.
ITAENDELEA.
 
SEHEMU YA 556.
Kitendo cha mtu aliefahamika kwa jina la Heinholtz kuonyesha msimamo wake , kundi la wanywa damu kutoka Lasombra na Brujah walianza kungurumiana.
Kucha zao zilianza kurefuka wakionyesha upande wao ambao unatisha pale binadamu wa kawaida anapowaangalia , mara nyingi wakionyesha hivyo jua wapo katika hasira.
Edna kuona kitendo kile alipatwa na kihoro cha aina yake na alichokifanya ni kukaa chini kwenye sakafu na kisha akafumba macho yake asione kile kinachoendelea.
Kwenye maisha yake hakuwahi kuangalia muvi za kutisha , sasa anapata wapi kuangalia vitu vya kimaajabu kama hivyo ambavyo vipo kwenye macho yake kabisa katika uhalisia.
“Mshipi wa kichawi bado haujaonekana lakini bado mshaanza kugombana”Aliongea mwanaume aliefahamika kwa jina la Udinese.
“Acha maigizo Udinese , darubini yetu ya ulozi haiwezi kukosea , kama tusipo upata kwenye hii nyumba basi naamini labda ni chini ya ardhi”Aliongea Heinholtz na palepale kwenye mkono wake kulijitengeneza panga refu la mita moja lenye rangi kama ya damu
“Move! Blood Bursting Slash”
Heinholtz aliongea kwa nguvu na palepale aliinua lile panga lake juu na kisha akalipigiza kwenye sakafu kwa mtindo wa kukata na palepale ulitokea mlipuko ambao haukuwa wa moto bali ni mwanga flani hivi ulichonganika na moshi wenye harufu kama vile matairi ya gari yanapochomwa na mpaka moshi unakuja kupotea palepale eneo la katikati lilijitengeneza shimo kwenda chini.
Edna alijikuta akitoa macho mara baada ya mlipuko huo na alipoangalia kwa umakini katika shimo lile lilichochimbwa kimaajabu alijikuta akihema kwa taabu ya woga mkubwa na mshangao na kuzidi kujibanza kwenye kona.
Baada ya mpasuko ule watu wale vampire wa kizungu waliangalia ndani yake na waliweza kushuhudia kitu kama mkanda flani hivi wanaovalishwa wale washindi wa kimasumbwi au wacheza mieleka, lakini mkanda huo wenyewe ulikuwa na michoro ya kizamani sana ambayo haikuwa ya kueleweka.
“Haha…. nilijua tu upo chini , Marigic Girdle!!!”Aliongea Heinholtz huku akionyesha furaha lakini hakuwa peke yake ambaye alikuwa kwenye mchecheto , Udinese pia alikuwa na mchecheto pia .
“Unacheka nini , huo sio wa kwako”
“Udinese najua wanajeshi wa Brujah ni majasiri lakini sisi tunanguvu zaidi kulinganisha na watu wenu wenye fikra finyu”
“Heinholtz hatutaogopa kupambana na wewe lakini kabla ya hapo kwanini tusiwamalize hao binadamu wa maisha ya thamani ndogo kwanza?”
“We shall see of your underlings are faster or if my peaple are crueller..”Aliongea akimaanisha kwamba wataona kama watu wake wapo na spidi au watu wake yeye ni wakatili zaidi.
Palepale walitoa ishara maalumu ya kichawi ambayo ilifahamika kwa watu wa kundi la mwanywa damu waliokuja nao na muda uleule baada ya watu hao kupata ishara kutoka kwa wakubwa wao ,mita kadhaa kutoka katika nyumba ya Edna yalisikika malalamishi ya maumivu kutoka kwa watu.
“Wametuona, waueni watu wote wa jamii ya wanywa damu haraka , pambaneni” Sauti ya mtu aliekuwa kwenye gari aina ya Noah ilisikikana palepale watu walishuka kwa haraka kutoka katika magari na kuvamia wale wa kabila la wanywa damu.
Ilionekana walikuja wengi lakini baadhi yao ndio waliongiia katika nyumba ya Edna.
Binadamu kutoka katika makundi mbaimbali ya kichawi walianza kupigana na kundi la wanywa damu , wao wenyewe walikuwa wametulia kwenye gari kwani waliamini Mshipi huo ukishapatikana kundi la Sabatt na Camarilla lazima wangeanza kugombana wao kwa wao na wangetumia mwanya huo kuchukua mshipi wa kichawi na kupotea , lakini ilionekana mpango wao sio kama walivyotegemea kwani Udinese wa kundi la Camallira aliungana kwanza na Heinholtz wa kundi la Sabbat kupigana ili kuwamaliza kwanza binadamu hao wachawi.
Uwezo wa mamwinyi(Dukes) pamoja na Makwisi (Marquises) wa kundi la wanywa damu ulikuwa ni mkubwa sana , sasa binadamu hao wangewezeaje kushinda na hapo tu Udinese na Heinholtz hawajaingilia.
Ni ndani ya dakika chache tu binadamu wote wa kawaida wa kichawi waliweza kuangamizwa na watu wa kundi la wanywa damu
“Three Dukes , eight marquises and earls Udineses is Camarila so afraid of Sabbat? Is there a need to bring so much elite over?”
“Mamwinyi watatu , Makwises nane na Udineses nyie wote ni Camarila , je mnatuogopa sana Sabbat mpaka kuleta watu wote hawa wa viwango?”Aliongea Heinholtz.
“Kuwaogopa!? , unaongea upuuzi gani , Heinholtz si wewe pia umewaleta Lashrac na Saka , wanao uwezo mkubwa kuliko mamwinyi wangu watatu”Aliongea Udineses kwa utani na kumfanya Heinholtz kumgeukia Edna aliejikunyata kwenye kona akitetemeka.
“Huyu mwanamke inaonekana anaweza kuwa chakula kizuri..”Aliongea Vampire Heinholtz huku akilamba midomo yake kwa tamaa lakini Udinese palepale alipotea na kuja kuibukia mbele ya Edna.
Edna aijikuta akihisi kitu cha baridi katika shingo yake, alikuwa ni Udinese ambaye tayari amekwisha kushika shingo yake kwa nyuma na kuipindisha kidogo na kuangalia kwa matamanio mshipa wa kijani wa damu unaopita damu kwenda kwenye ubongo.
Edna alijikuta akikosa ujasiri wa kufanya chochote , machozi tu ndio ambayo yalimtoka , ijapokuwa alikuwa kwenye levo ya nusu mzunguko lakini asingeweza kupambana na aina ya watu hao wanaoishi kwa kutegemea damu.
Alijikuta akikosa msaada kabisa na hakujaribu hata kujitetea na aliishia kusubiria shingo yake ikipasuliwa.
Katika wakati kama huo watu wawili ndio waliijaza akili yake , alimuwaza Roma na kujiuliza maswali je itamchukua siku ngapi kuomboleza kifo chake , vipi kuhusu Lanlan je atalia kwa muda gani pale atakaposikia mama yake amepoteza maisha, Je kama ningepunguza ujuaji nisingekuwa nyumbani muda huo nikipata chakula cha usiku na familia yangu?, maswali mbalimbali yalipita katika kichwa chake.
“Ah ..she smells so good , I haven’t smelled blood as sweet as hers , Heinholtz, this woman … I call dibs on her , I’ll enjoy the meal after I kill you”
“Ah ananukia vizuri mno .. sijawahi kuona damu inanukia utamu hivi, Heinholtz , huyu mwanamke nishamuwahi , nitafurahia damu yake baada ya kukuua”Aliongea Udinese na kumfanya Heinholtz kucheka sana.
“Kama ni hivyo basi tutaona kama utakuwa hai muda huo”Baada ya kumaliza kauli yake palepale pepo la rangi ya damu liliamka kama vile ni moto kwenye mikono yake , kutokana na kuwa katika kizazi cha tatu katika koo za wanywa damu alikuwa na uwezo wa kuita pepo mwenye nguvu wa damu ya moto.
Yule pepo wa damu ya moto alikuwa akicheza cheza kama shetani na kufanya eneo kama ni vile vyumba vya joto vya kufanyia masaji kutokana na mvuke wake.
“Saka , Leshrac hebu wadhibitini hao ndugu zetu kutoka Camarilla , nitadili na Prince Udinese..”Aliongea Heinholtz.
“Yes your Highness”
Wachawi waliokuwa ni binadamu wa kawaida walikuwa tayari washauliwa na vita iliobaki ilikuwa ni kati ya makundi mawili ya wanywa damu yaani Camarilla na Sabbat.
Baada ya Heinholtz kutoa maagizo palepale wale mamwinyi walijiandaa kushambulia.
Vita ilianza na kilchoonekana sio watu bali ni vivuli vya watu vinavyotembea kwa kasi sana kuzunguka katika jengo zima nje na ndani huku mbinu mbali mbali za kichawi zikitumika katka kupambana.
“Udinese , hebu chukua hili pepo lenye kiu ya damu ya moto”Aliongea na palepale alipotea aliposimama na alipokuja kuibuka alikuwa mbele ya Udinese na alimpiga ngumi katika uso.
Muda ule Udinese alikuwa tayari ashamtupa Edna pembeni ili asije kushambuliwa na Heinholtz na kufa kabla hajamnyonya damu.
Edna alidondoka vibaya kwa kuzunguka zunguka kwenye tailizi na ilikuwa bahati kwake kwani hakujigonga kichwani lakini wakait mmoja akihisi maumivu makali kama vile kuna mtu kakata mifupa ya mbavu zake , yaani kitendo cha watu hao kumdharau mno kilimfahya kuhisi kudhauraulika sana.
Alijitahidi kusimama huku akimkazia macho Udinese kwa hasira kali .
Udinese hakumjali Edna alichojali muda huo kwanza ni kushinda pambano, palepale alipoletewa shambulizi hakutaka kuendelea kusimama mbele ya adui yake bali alisogea upande wa kushoto kidogo na pigo likapita na aliita nguvu za kichawi na palepale kilionekana kivuli cha mbwa mwitu na kuanza kumng’ata Heinholtz, lakini bwana huyo hakuhofia hata kidogo zaidi ya kuachia shambulio lingine na kumueekezea Udinese.
“Haha.. unadhani unaweza kunikimbia , likija swala la spidi hata Sargaras hawezi kushindana na mimi , kubaliana na majaliwa yako”Aliongea na kumfanya Udinese kuzidi kujawa na wasiwasi kwani kila akisogea upande wowote Heinholzt alikuwa mbele yake na alishajua hawezi kumzidi likija swala la spidi.
“Acha kujiamini sana kama umeshinda, ngoja nikuonyeshe mshenzi wewe”Aliongea Udinese na palepale alitoa chupa kama vile ni zile za spray au manukato na kuanza kumpulizia Heinholtz na kitendo kile kilifanya pepo la Heinholtz kukosa nguvu likionyesha kuathirika.
“Dhana ya Chupa ya Sumu hio , Pumbavu kabisa”Aliongea Heinholtz kwa hasira baada ya kuona nguvu ya pepo lake likimezwa na ule moshi wa sumu ya kichawi.
Kila mwanafamilia katika jumba la kifalme anamiliki dhana maalumu na inasemekana Dhana zote takatifu za kale duniani zipo jumla yake therathini.
Hivyo mojawapo kati ya Dhana hizo ni chupa ya sumu ya kichawi ambayo harufu yake humeza kila aina ya shambuio la kiroho kwa kutumia moshi wake tu.
“Unajaribu kunishinda kwa kutumia pepo la damu , umenidharau sana , nitakufanya uonje utamu halisi wa pepo lako mwenyewe”Aliongea Udinese na palepale aliminya ile chupa kwa wingi na ikaanza kutoa moshi wa rangi nyeusi ambao ulianza kumsogelea Heinholtz kwa spidi.
Heinholtz aijua kabisa akishaguswa na ule moshi moja kwa moja angekosa nguvu na kuwa kama mtu aliepalalaizi hivyo alitumia juhudi zote kuukwepa na palepale alifyatuka na kwenda kutua eneo la juu ya nyumba hio.
“Udinese inaonekana upo siriasi sana na hili pambano , sasa ngoja nikuonyeshe , huwezi kunishinda kizembe hivyo”Aliongea na palepale kwenye mikono yake kulionekana ufunguo wenye umbo la ajabu lakini wa madini ya dhabahu na kumfanya Udinese kushanga.
“Huo si ufunguo wa Shetani , kwanini upo nao?”
“Hahaha… surprise..!!! , Raphael alijua nini kingetokea, alijua tu lazima ungebeba chupa ya sumu ndio maana akanipatia ufunguo wa shetani”
“Pumbavu zake Raphaeli”Aliongea Udinese kwa hasira na Heinholtz hakutaka kuongea chochote bali palepale aliirusha funguo ile kwenye hewa na palepale ilitengeneza kitu kama shimo kwenye anga na ule moshi uliokuwa ukimfuata palepale ulimezwa na shimo lile , likuwa kama vile ni Shimo jeusi.
Katika historia kuna uwepo wa dhana therathini ukiachana na kopo la sumu kuna uwepo ufunguo wa shetani ambao kazi yake kubwa ni kufungua geti la kuzimu.
Kwasababu nguvu zote wanazotumia zinatokana na asili ya ushetani basi palepale geti la kuzimu linapofunguka nguvu zote za giza za kiroho humezwa na kurudi kwenye koloni lake.
Kitendo cha Heinholtz kutoa ufunguo wa shetani na kufungua geti la kuzimu ilimpelekea Udinese kuanza kukosa nguvu.
Edna alikuwa kwenye kiwewe kwani kila alichokuwa akiangalia hakikuwa kikieleweka kwa akili zake za kawaida , alikuwa ni kama yupo ndatoni na alikuwa akiona maluwe luwe.
Heinholtz baada ya kuona Udinese ashaanza kukosa nguvu alimwangalia kwa tabasamu la kejeli na pale pale alimsogelea Edna na kumshika shingo.
“Hey mrembo usiogope , huwezi kuwa na wasiwasi tena wakati nikinyonya damu yako yote”Aliongea na kisha palepale aliruhusu kucha zake kurefuka.
Mkono mmoja uliomshikilia ulimfanya kumchoma kwenye kiuno na akaanza kutokwa na damu licha ya kwamba hakuwa ametumia nguvu kumdhuru.
Edna alijikuta akihisi maumivu makali huku akijaribu kufurukuta kujitoa katika mikono yake lakini hakuweza na ilimfanya kuhisi maumivu zaidi kwani Heinholtz alizidi kukaza mkono wake na kuruhusu kucha kuzama vizuri.
“Nilikuambia huyu binadamu ni kwa ajili yangu usiku huu Udinese, hebu angalia sasa ninavyoenda kumnyonya damu mbele yako na kisha nikuue”Aliongea na palepale alimshika Edna na mkono wa kulia kwenye shingo kwa ajili ya kukata mshipa wake mkubwa wa damu , Edna mpaka hapo alijuwa anakwenda kufa muda ambao kucha hizo zitaingia ndani kwenye ngozi yake ya shingo.
Alijikuta akifumba macho akiwa amekosa kabisa tumaini na kusbiria kifo chake kwani hakuwa na namna ya kujiokoa mpaka hapo.
Wale wengine mara baada ya kumuona anachotaka kufanya , walikaa pembeni na kumwangalia Heinholtz kwa macho ya kutamani kile anachokifanya wawe ndio wao, lakini sasa kabla hata hajazamisha zile kucha zake kwenye shingo ya Edna, ghafla tu kulitokea kivuli ambacho kilipita na mkono wake na kuunyofoa palepale na kumpelekea kumuachia Edna kutokana na maumivu makali.
“Wewe ni nani .. kwanini upo hapa?”Aliuliza huku akivumilia mkono wake ambao ulianza kujiponyesha kurudi katika hali yake ya kawaida.
Vampire kama hao hawakuwa na woga wa kupoteza mkono kutokana na kwamba walikuwa na uwezo mkubwa wa kupona na kuwa kawaida.
Lakini kilichomuogopesha ni kwamba alishambuliwa kwa namna ambavyo hata yeye mwenyewe hakuelewa na alijiuliza mtu huyo aliefika imekuwaje akaweza kuficha Aura yake na asionekane.
Roma palepale aligeuka na kumwangalia Heinholtz aliekuwa kwenye mshangao na maumivu.
Edna mara baada ya kugundua aliefika hapo ni Roma alijikuta akipoteza nguvu zake zote na kujidondokea kwenye sakafu na kumwangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida , ikishindikana kuelezea kile ambacho anajisikia katika moyo wake.
Ijapokuwa alikuwa akihitaji Roma atokee kama muujiza na kumuokoa katika hali aliokuwa nayo kama alivyokuwa akifanya tokea wakutane lakini sasa hivi ameweza kutokea hisia zake zilikuwa katika hali ya kutoeleweka, ni hisia za mshituko , furaha na kutokuamini.
Alishindwa hata kujielewa na ule ujasiri aliokuwa nao muda mchache uliopita ulimpotea na palepale alianza kutoa kilio kama mtoto mdogo.
Roma hakujali machozi yake kabisa na hata hakujihangaisha kumzuia wakati alivyokuwa akidongoka chini.


SEHEMU YA 557.
Roma alianza kujisambazia nguvu za kijini na kufanya wale watu wote kuanza kuwa na hofu isiokuwa na kifani , ilikuwa ni nguvu kubwa zaidi kuliko nguvu iliokuwa ikisambazwa na geti la mlango wa kuzimu.
Kitendo cha kuwasambazia nguvu za kijini wale watu wote walijikuta wakijawa na woga wa ajabu ambao kwa maisha yao yote hawakuwahi kukutana nao na ilikuwa ni kama wanakiona kifo chao kabla hakijatekelezwa.
Walianza kujiuliza maswai mtu huyu ni nani ambaye amewavamia ghafla na palepale walianza kuunganisha doti na wote kwa pamoja walijikuta wakipatwa na kihoro mara baada ya kuelewa sasa hali ilivyo.
Walikuwa wakisikia habari za miungu watu na kati ya miungu hio mmoja wao aliefahamika kwa jina la Pluto ni mtu mwenye ngozi nyeusi yaani Mwafrika.
“Mama maa ni P…Pluto!!!?”
Udinese ndio aliekuwa wa kwanza kukumbuka na alivyotaja hilo jina ndio kila mmoja alitoa macho.
Jasho lilijitokezea kwenye uso wa Heinholtz huku akiwa mwekundu kutokana na ngozi yake nyeupe , ijapokuwa uwezo wake ulikuwa mkubwa kutokana na kutawaliwa na nguvu ya shetani lakini mtu aliekuwa mbele yake hakuwa na uwezo wa kushindana nae.
“Mfalme Pluto sijui kwanini umeunvunja mkoni wangu lakini ninachojua hakuna chuki kati ya Sabbat na miungu yote , si ndio?”Aliuliza Heinholtz lakini Roma hakumjibu zaidi ya kusimama katika sehemu moja huku koti lake la suti lilikipepesuka na upepo.
Roma baada ya kukagua mazingira alimnyooshea kidole Heinholtz akimuonyesha ishara ya kusogea
“Njoo na ufe”Aliongea Roma kwa sauti ya chini na kumfanya Heinholtz kuwa katika hali ya wasiwasi a kusimama.
“Mfalme Pluto tafadhari usifanye utani wa namna hio , kukuheshimu kwetu haimaanishi kwamba Sabbat ni wepesi , sisi sio wajinga na lazima kuwe na sababu ya wewe kuanza kunishambulia na kama sio hivyo labda na wewe upo hapa kwa ajili ya Mshipi wa kichawi , na kama ni hivyo upo hapo hapo kwenye hilo shimo , tunaweza kukupatia hivyo hakuna haja ya sisi kupambana na wewe”
“Njoo hapa na ufe”Alirudia Roma maneno yake akimwambia Heinholtz na palepale aliachia mkandamizo wa hewa ambao ulizidi kumfanya aogope na hata wale wengine ambao walikuwa wamesimama mbali waliweza kuhisia na hakuna hata mmoja ambaye alikuwa na ujasiri wa kusogea licha ya kwamba waliona jambo hilo kwao ni kama udhalilishaji.
Heinhloltz alijikuta akitetemeka kwa hasira nyingi na akaachana na swala la kuona uoga na kuvaa ujasiri na pale pale alimsogelea Roma kwa ajili ya kumshambulia.
“Umezidi , ngoja nikuonyeshe”Aliongea na palepale spidi yake ilikuwa ya juu mno kiasi kwamba hata kivuli chake hakikuweza kuonekana na alipomkaribia tu aliita nguvu ya kizimu ambayo ilikuwa kama wingu la moshi wa rangi ya majivu.
Roma alikuwa amesimama palepale na hakusogea na hata Heinholtz alivyomvaa hakuonekana kwa upande wa mbele na kuwafanya wale wengine kutoona kinachoendelea lakini kile kiwingu kilivyotoweka walijikuta wakiwa katika kiwewe mara baada ya kumuona Heinholtz akiwa amening’inia hewani ameshikwa na mkono mmoja kwenye shingo.
“Nilikuambia uje hapa ufe na sijakuambia unishambulie kwanini unaleta usumbufu”Aliongea Roma kwa sauti ya kawaida na kumfanya Heinholtz kufurukuta ili ajitoe lakini hakuweza kabisa na alijikuta akipagwa kwani muda huo alikuwa ameruhusu mwili wake kutumiwa na nguvu ya kishetani kwa asilimia mia moja lakini licha ya hivyo hakuwa na uwezo kabisa hata wa kujitetea mbele ya Roma.,
Roma mara baada ya kuona amemshikilia vyema palepale aliita chungu chake cha kijini.
Katika kitu ambacho alikiwaza ni kwamba kama chungu hiko kilikuwa kikitumika kumeza watu wenye nguvu za kijini , itatokea nini kikimeza watu wa jamii ya Vampire.
Udinese na wenzake walijikuta wakitetemeka kwa woga mara baada ya kuona jungu la kichawi mbele yao na kushindwa kuelewa maana yake nini kwani hawakuwahi kuona mtu ambaye anatumia aina hio ya uchawi.
“Hongera kwako , umekuwa mtu wa kwanza kukufanyia majaribio”Aliongea Roma na kisha alinuia maneno na Caulron ya maafa ilikuja chini ya Heinholtz.
Na kilivyomfikia chini ya miguu yake aliweza kuhisi nguvu ya ajabu ikimvuta na kadri alivyojaribu kupiga piga miguu kujiondoa alishindwa kabisa.
“Hapana..!!”
Ile anamaliza kauli yake alimezwa mzima mzima na Caulrdon na akawa haonekani tena kwa nje.
Roma palepale hakujali , aliita moto wa rangi nyeupe na kisha aliutumbukiza kwenye Caudron, huku mpango wake ni kujaribu kutengeneza kidonge cha kijini kwa kutumia mwili wa Vampire.
Wale wanywa damu waliobakia walichoweza kusikia ni upepo tu wa Heinholtz kumezwa na kile chungu na baada ya hapo kikatulia tuli na hata lile geti la kuzimu lilijifunga palepale kutokana na kufa kwa Heinholtz.
Roma aliweza kuhisi nguvu ya kichawi ikitoka kwenye kile chungu mara baada ya Vampite kuyeyuka na aliona huenda ni kwasababu pepo liliouvaa mwili wake limeshindwa kutoroka ndio maana kuna furukuto ndani yake la nguvu za kichawi.
Roma alijikuta akiona hakuna cha maana alichofanya kwani hakuna kitu chochote kilichotokea nje ambacho kingeongeza nguvu ya chungu chake.
Ikumbukwe Dhana ya Caulron ilikuwa na uwezo wa kupanda levo pia kadri Roma anavyopanda levo , lakini pia kama chungu hiko kitameza mtu yoyote mwenye nguvu za kijini moja kwa moja zile nguvu zake zingejigawa kati ,zingine zingebakia kwenye Caudron na zinazobakia zingekuja kwake hivyo angekuwa ameongeza uwezo wake , lakini kwa Vampire hao hakukuwa na aina ya nguvu zozote zilizotoka zaidi ya msisimko wa nguvu za kichawi pekee ambao ulimvaa na kmfanya kaunza kuona vitu visivyo vya kawaida.
Roma alijikuta akipatwa na hisia ambazo zilimpa ufunuo wa aina yake na kugundua huenda hayupo mbali na kuingia katika levo ya kudhibiti elementi za maji , yaani oksijeni na haidrojeni na kutengeneza maji ya kiroho(Ultra purity spiritual water).
Kama angefanikisha hivyo basi moja kwa moja angefanikisha kuwa na siraha ambayo ingekuwa na uwezo wa kumwagia kiumbe chochote na kukiondolea uwezo wake kwa kukisafisha.
Inasemekana katika miliki za kijini Maji ya kiroho yanaogopwa sana kwasababu yanabeba nguvu ambayo ina uwezo wa kusafisha uwezo wa mtu wa nishati za mbingu na ardhi, na sio hivyo tu hata kwa wachawi wa kawaida pia walikuwa wakiogopa sana Maji ya kiroho.
Kwa upande wa Roma hio ilikuwa ni levo ya mwanzo ya kudhibiti elementi za maji kabla ya kufikia levo ya kugandisha au kugeuza mtu kuwa barafu.
Roma akili yake ikiwa inapambana na msisimko wa nguvu za kichawi uliokuwa ukitoka kwenye kile chungu palepale aliita nguvu za kimaandiko na kuzielekezea katika mikono yake, nalifanya hivyo bila hata ya kujielewa ni kama moyo wake ulikuwa ukimwambia cha kufanya na baada ya kukusanya nguvu zake katika kiganja cha mikono palepale aliita na nguvu ya mbingu na ardhi na kisha akauganisha na mvuke wa anga na kulitokea vitu kama mapovu yakielea hewani.
Udinese na wenzake mara baada ya povu lile kutokea walijikuta roho zao zikifurukuta na ilikuwa ni kama kuna kitu kinawavamia rohoni.
“Hahaha… Pure water , Maji ya kiroho”Aliongea Roma akionyesha kufurahi mara baada ya kufanikisha kugundua mbinu ya kutengeneza povu la maji ya kiroho.
“Mfalme Pluto asante sana kwa kuokoa maisha yetu , tutaondoka hapa haraka ili tusikusumbue”Aliongea Udinese baada ya kuona anashindwa kuvumilia msisimko ambao ulikuwa ukipingana na nguvu zao.
“Msisogee , hili halijaisha bado”Aliongea Roma na kumfanya Udinese kutetemeka na kumwangalia.
“Je una maaagizo yoyote kwetu?”Aliongea lakini Roma hakuwajibu na kuangalia Cauldron yake ya maafa.
“Nataka majibu ya maswali yangu , huyu mwanamke ambaye amekaa chini nani ambaye amemgusa?”Aliuliza na kumfanya Udinese kujawa na kihoro kutokana na swali lake na kumfanya Roma kugundua kitu katika macho yake na alianza kupandwa na jazba.
“I… I”Alijikuta akitaka kuongea ila alisita lakini mmoja wa wale watu wa kundi la Sabbat waliingilia.
“Your Majesty Pluto , it’s Udinese he is the first person to hurt this lady , he is culprit”Aliongea akimaanisha kwamba ni Udinese na ndio mtu ambaye ni wa kwanza kumgusa Edna na yeye ndio mshukiwa.
Vampire Lasombra alijitahidi kuongea ili kujiokoa katika hali hio baada ya kushuhudia kifo cha mtoto wa mfalme Heinholtz na mpaka hapo waliona chaguo la pekee ni Roma kumuua Udinese na kuwaacha wao.
“Unaongea ujinga ,Heinholtz ndio ambaye amemuumiza huyu mwanamke , alitaka kumnyonya damu wala sio mimi”Aliongea na wale walimrudishia kwamba yeye ndio aliekuwa wa kwanza na upande wa kundi la Bruja waliwaambia Heinholtz ndio alimuumiza Edna, walianza malumbano ya kurushiana mpira wao kwa wao kila mtu akivutia kwake.
“Acheni kelele , kwanza kabisa haina haja ya nyie kulumbana wenyewe kwa wenyewe”
“Mfalme Pluto sio mimi kweli “Aliongea huku akitingisha kichwa kwa woga.
“Haijalishi ni nani kati yenu , wote nyie mnastahili kifo”Aliongea Roma akiwa kwenye tabasamu .
“Mfalme Pluto huwezi kufanya hivi , si wewe ni mshrika na kundi la Camarilla je haumkumbuki rafiki yako Marquess Lilith"Aliongea Udinese akijaribu kubembeleza.
“Rafiki!! , kama nyie ni marafiki kwanini mmeshindwa kumfahamu mke wangu na kutaka kumnyonya damu , halafu bado mnajinasibu na urafiki”
“Ah…”Udinese alishindwa kuongea neno zaidi ya kupanua mdomo wake kwa wasiwasi baada ya kujua Edna kumbe alikuwa mke wa Pluto.
Wale Vampire waliangaliana na palepale walipeana ishara ya kukimbia , walijiambia kama Heinholtz ameweza kuuliwa wao ni nani hadi waachwe hai.
Lakini bahaii mbaya ni kwamba Roma hakurudisha chungu chake na wakati ambao wanapanga kukimbia palepale lile jungu kama tanuru liliwageuzia mdomo upande wao na kuaanza kuwavuta wote kwa pamoja.
Roma palepale alitengeneza maji mengi ya kiroho na kuyalekeza aliposimama Udinese na ile yanamkaribia , ni kama vile ameguswa na tindikali kwani alianza kubadilika ngozi na ikaanza kuyeyuka.
Dakika mbili tu hakukuwa na mtu yoyote aliebakia katika hilo eneo akiwa hai kwani wote walimezwa na chungu cha maafa hivyo amani ikarudi upya.
Roma baada ya kurudisha chungu chake palepale alimgeukia Edna na kumwangalia na Edna na yeye alimwangalia mume wake kwa macho yasioelezeka.
*******
Ni juu kabisa ya kilele cha mlima kilimanjaro muda huo huo ambao Roma alikuwa akipambana na Vampire..
Sasa basi juu kabisa ya eneo la kilele ambalo limefunikwa na barafu , alionekana mwanamke mmoja mrembo akitembea peku peku akikanyaga barafu bila ya kuathirika na ubaridi.
Mwanamke huyo alikuwa kama vile ni mchoro wa kizamani kutokana na aliivyokuwa akionekana , alikuwa amevaa gauni refu la rangi ya kijani la kitambaa cha hariri , ni gauni ambalo lilikuwa ni kama yale yanayovaliwa na wanawake wa kiarabu maarufu kama Abaya.
Alikuwa mrembo haswa na shepu yake ilionekana waziwazi licha ya kwamba alikuwa amevalia gauni hilo kuu kuu ambalo halikuwa na udarizi wa kibunifu.
Alikuwa na nywele ndefu mno kama vile ni wale wanawake wa Korea kusini wanaoneana katika filamu za kihistoria akiwa amezibana kwa kuchomeka pini ambayo ilmetengenezwa kwa kunakshiwa na Lulu.
Ki ufupi mwanamke huyo ni wa rangi nyeupe mwenye macho yake yenye kiini kama vile ni rangi ya anga.
Baada ya mwanamke yule kusimama kwa muda kidogo , kivuli cha mtu alievalia nguo nyeusi kilionekana na kutua karibu na yule mwanamke .
Alikuwa ni mwanaume ambaye amevalia koti refu la rangi nyeusi, huku nywele zake zikiwa ni nyeupe maarufu kama Blonde hair , alikuwa ni kijana mno na uso wake wa kuvutia.
Mwanaume yule hakuwa mwingine bali ni kiongozi wa kundi la Tzsimisce ambae anafahamika kwa jina la Raphaeli lakini pia akifahamika kwa jina la siri la Hermes.
Hermes mara baada ya kumwangalia mwanamke aliekuwa mbele yake kwa dakika kadhaa alionyesha tabasamu hafifu.
“I like how you’re dresssed today”Aliongea Hermes akimwambia yule mlimbwende kwamba amependa namna ambavyo amevalia, lakini licha ya kutoa sifa hizo , yule mwanamke alimwangalia kwa macho makavu.
“Mpango wetu umeendaje?”Aliuliza kwa kingereza yule mwanamke.
“Mpango umefeli , hata kwa kutumia mbinu ya kilozi ya Athena ya unabii bado tu imeshindikana kutabiri muonekano wa mkanda ule wa kipekee wa hali ya chini lakini bado ni mzuri kuliko wa kwetu”
“Mhmh , nadhani ni bahati tu”Aliongea huku akitoa tabasamu la kejeli na kumfanya Hermes kucheka.
“Vipi lakini kuhusu wewe , je tayari umemkamata yule mtu?”
“That man is extremely cunning , it’s easy to win him over but to get him .. its quite arduous .. but I will get him soon or later”Aliiongea akimaanisha kwamba yule mwanaume ni mjanja sana lakini ni rahisi kumshawishi lakini kumpata ni ngumu , lakini nitampata tu mapema au baadae.
“Kama ni hivyo basi unapaswa kuharakisha , Athena tayari ashapata moyo wa Gaia , ijapokuwa mpango wake una hatua nyingi lakini yeye ndio kaanzisha kwa haraka , kama tutasubiri mpaka akianzisha kila kitu yeye mwenyewe hatutokuwa na nafasi”
“Je unafikiri mpango wake utaendelea vizuri? Ana asilimia therathini tu ya uwezo wake na uwezo wake wa kinabii bado una shida nyingi , vinginevyo asingeingilia kuweka mambo sawa”
“Nina wasiwasi kama mpango wake utafanikiwa, si ataendelea na tabia yake ile ile ya kutaka kutawala akili zetu kwa miaka mingi kama alivyokuwa akifanya katika sayari yetu?”
“Unaogopa nini , kiwango cha uwezo wake kinaweza kuwa kikubwa lakini haitokuwa ngumu kwangu kuimarika, lakini hata hivyo uwezo wangu ni wa tofauti kabisa na wa kwake tokea mwanzo lakini siwezi kuwa na wasiwasi kwasababu mbinu zinazotumika katika miliki za kijini ni nzuri zaidi na pia wana dhana ambazo wamerithi kutoka vizazi vilivyopita ambazo zina uwezo mkubwa , dhana ambazo ni ngumu kushidana nazo, kitu kingine mimi na yeye tunao utofauti, yeye anahitaji moyo wa Gaia kurudisha nguvu zake zote na kutawala upya lakini kwangu mimi hakutakuwa na athari zozote “Aliongea na kumfanya Hermes kutabasamu vibaya.
“Nadhani upo sahihi , kwanini usimfanye yule mtu akatengeneza tena dhana feki kwa mara nyingine ili niendelee kufurahia kamchezo”
“Haina haja, ijapokuwa hawezi kukuua lakini anao uwezo wa kukulazimisha upitie hatua ya kuzaliwa upya kama alivyofanya kwa Hades wa zamani na ukiangalia uwezo wako naamini itakuchukua miaka sita au kumi , nadhani mpaka hapo utakuwa umechelewa sana”Aliongea na kumfanya Hermes kukunja sura na kukosa neno la kuongea.
“Ukiachana na hilo , vipi kuhusu Apollo , Poseidon na wengine ni kipi wameweza kusema?”Aliuliza yule mwanamke.
“Kuhusu wao! Mhmh... , kundi lote hilo linamuogopa Athena na hawana ujasiri wa kumpiga kwa lolote , hatuwezi kuomba msaada kutoka kwao kwani haiwezekani nadhani tujifanyishe hatujui kitu kwa sasa na tuendelee kuangalia nini kinaenda kutokea”
“Basi ni sawa , hata kama Athena ni kama shetani ambaye anastahili kifo lakini bado ni ndugu yetu… mimi sina tatizo na mpango wake wa kufufua moyo wa Gaia lakini kama ndugu zetu roho zao zitaamka siamini kama tutaweza kuwa kama ilivyokuwa kwenye sayari yetu”Aliongea na kumfanya Hermes kutabasamu kisiri siri na palepale alijikuta akitoa macho kama mtu ambaye ana furaha.
Unafikiri mwanamke anaeongea nae Hermes ni nani , kuna mpango gani wanapanga na kwanini anasema mbinu za kijini ni nzuri , je na yeye ni sehemu ya miungu ambaye amechagua kujifunza mbinu za kijini? Kumbuka kati ya miungu ambayo iliweza kutawala roho za binadamu jumla yao ni kumi na mbili ukimuondoa Zeus na Hades wa Zamani ambao haijulikani walipo , kuna Apollo ambaye tushamjua , yupo Artemis , Aphrodite , Poseidon ,Hermes na Athena ambao jumla yao ni saba kama ni hivyo watano wako wapi?
ITAENDELEA.
 
SEHEMU YA 556.
Damu zililikuwa zikitoka kwenye majeraha yake na alikuwa na michubuko kutokana na kudondoshwa chini, jambo ambalo lilimfanya iwe ngumu kusogea.
Ijapokuwa Roma alikuwa ashageuka na kumwangalia lakini hakufanya chochote zaidi ya kumwangalia tu.
“Huwezi kuendelea kuishi hapa tena”Aliongea Roma mara baada ya kimya kifupi.
“Mmh..!”
Jumba lote lililokuwa likionekana kuwa zuri kwa nje lilishaharibiwa na hata kama angetafuta mafundi kurekebisha ingechukua muda.
“Usisogee ngoja nikusaidie kupona”Aliongea Roma na kisha akamnyooshea mkono ili kumsaidia kusimama lakini Roma mikono yake ilikuwa ikimtetemeka na kumfanya Edna amwangalie usoni na kugundua hakuwa na hasira bali alionekana kuwa na wasiwasi.
“Nini tatizo?Kwanini mkono wako unatetemeka?”Aliuliza Edna huku akimwangalia Roma kwa wasiwasi lakini upande wa Roma aliangalia pembenni huku akificha macho yake ambayo yashaanza kuwa mekundu kama mtu anaetaka kutoa machozi.
Lakini kitendo kile Edna aliweza kukiona na alipatwa na mshutuko halafu akaingiwa na wasiwasi zaidi.
“Bado tupo kwenye hatari , nini kinaendelea?”Aliuliza Edna.
“Hatari gani? Kidogo tu ungekufa”Aliongea Roma huku sauti yake ikiwa tofauti na ile iliozoleka , sauti kama ya mtu ambaye amekosa ujasiri na kumfanya Edna kushangaa na hapo hapo kujua kilichomjaa Roma ni hisia za woga.
Alikuwa akijaribu kuficha lakini alikuwa na woga ambao umemvaa na Edna alfikia hatua ya kujiuliza ni hofu gani aliokuwa nayo mpaka akawa hivyo kwani ni mara yake ya kwanza kuwa hivyo.
“Je unajua ungekuwa maiti iliokauka kama ningechelewa kidogo tu , kwanini haya yanatokea , kwanini inaonekana kama nashindwa kukulinda wakati bado nipo hai?”
“Je mimi sina maana tena , nilishashuhudia kifo chake yule mwanamke akiwa na mtoto wangu tumboni miaka mitatu iliopita , sina ujasiri kama nitaweza kuvumilia kama ikitokea mara nyingine , Edna nakuomba usije ukafa mbele yangu hata kama ni mwisho wetu naomba nife mimi kwanza tafadhari”
“Na…”Alitaka kuongea neno lakini Roma alimkatisha.
“Usiongee chochote ..”Baada ya kuongea vile mkononi mwake ilionekana ile bangiri .
“Najua unanioona kama vile mimi ni mbinfasi m, niawezaje kukuambia haya ikiwa mimi ndio mwenye makosa , sio kwamba nakulazimisha kunisamehe na pia sina ujasiri wa kusema siwezi kukasirisha tena lakini tafadhari vaa hii bangiri ili angalau niweze kujisikia vizuri , ni kwa ajili ya usalama wako”
Edna alimwangalia kwa upole na aliishia kuchukua bila ukinzani ile bangiri katika mikono yake na kisha akaivaa.
Muda huo huo waliweza kusikia magari yakiingia hapo ndani kwa kufuatana , wale wachawi kutoka Scotland wa kundi la siraha kwenye jiwe inaonekana wamekuja kwa kuchelewa.
Tukio zima lilitokea kwa takribani dakika ishirini na Roma yeye aliwahi kufika kutokana na kwamba ameteleport lakini kwa watu hao walifanya kuendesha magari yao ndio maana iliwachukua muda kufika.
Mwanamke wa kizungu aliefahamika kwa jina la Lola alitoka nje ya gari na alijikuta akipigwa na butwaa mara baada ya kuona miili ya watu waliokufa ikiwa imesambaa.
Muda huo Roma aliweza kutoa ule Mshipi wa Kichawi na kuushikiria mkononi na Lola na watu wake walijikutua wakiungaa mara baada ya kuuona lakini kilichowashangaza zaidi ni kukuta alieushikilia ni Roma.
“Damn it we came too late This divil has killed everyone”Aliongea Prince akimaanisha kwama wamekuja kwa kuchelewa na Shetani Roma ameua kila mtu.
“Funga domo lako Prince , hujakoma tu”Alifoka yule mwanamke aliewafuata ambaye jina lake ni Lola.
“ Hali ni mbaya , kwanini hakuna maiti yoyote ya kundi la wanywa damu hapa?”Aliuliza mmoja wao kwa lugha ya kingereza.
Roma hakujali mshangao wao zaidi ya kuchunguza mshipi ule wa kichawi uliokuwa kwenye mikono yake huku pembeni yake akiwepo Edna.
“Sijui nani ameuweka hapa kwenye hii nyumba , lakini hii Dhana ni feki”Aliongea na wale wachawi wa kuzngu hakuna ambaye aliongea lolote wala kusogea kutokana na kuogopa uwezo wake.
Roma aliwaangalia kwa macho ya dharau na kisha aliutupa ule mkanda hewani na palepale aliita moto wa kijini wa rangi ya njano na aliiunguza , lakini kutokana na ule mkanda kuwa na nguvu ya ziada ya kichawi ulivyokutana na nguvu ya Roma ulilipuka kama bomu na palepale ukageuka na kuwa majivu.
Wale wachawi wa Siraha kwenye Jiwe walijikuta wakipatwa na mshutko kwani hawakugetemea kitendo hicho.
“Okey , Sijui nani kaanzisha huu uzushi lakini nyie wote safari yenu ya kuja Tanzania haikuwa ya maana , Rada za jeshi kitengo cha wachawi zimewashawanasa , nadhani mnapaswa kurudi nchini kwenu Scotland , nani anaweza kujua, huenda kuna chochote kinachoweza kutokea nyumbani kwenu na ukawa huu ni mtego”
Mwanamke wa kizungu aliefahamika kwa jina la Lola alitingisha kichwa kumuelewa Roma na kisha akainamisha kichwa chake mbele yake kwa ishara ya heshima.
“Mfalme Pluto asante kwa kututaarifu tuondoka Tanzania mapema iwezekanavyo”Baada ya kuongea hivyo Lola aliwapa ishara wachawi wenzake na waliingia kwenye gari na kuondoka katika eneo hilo.
Tunafanya nini kuhusu hizi maiti , au tuwapigie simu polisi?”Aliuliza Edna mara baada ya kuponyeshwa majeraha yake.
“Usiwe na wasiwasi , Jeshi kitengo cha wachawi watadili na hili , turudi nyumbani”Aliongea Roma.
Ndio polisi wa kawaida wasingeweza kudili na hali ya namna hio kutokana na kwamba hawakuwa na kitengo chochote cha kudili na uchawi pamoja na nguvu za ziada , hivyo maswala yote ya giza ndani ya taifa yalishughulikuwa na wanajeshi maalumu ambao walienda nchini China kufundishwa kupambana na uchawi na ndio kikaja kuwepo kwa mara ya kwanza katika jeshi la Tanzania.
Kwa mfano nchini Scotland jeshi lao lilikuwa likishirikiana kwa karibu zaidi na SIS(Sword in the Stone) kupambana na nguvu za ziada ambazo zinahatarisha usalama wa nchi.
Roma hakujali mavazi ya Edna ya kulalia , alimbeba juu juu kama mtoto na kisha akapotea nae kurudi nyumbani.
Roma mara baada ya kufika nyumbani akiwa na Edna aliweza kumpigia simu Bi Wema na kumtaarifu kwamba Edna amerudi na taarifa hio ilimfurashisha Bi Wema na kuahidi kufika kesho kuendelea na majukumu yake .
Upande wa Rufi mara baada ya kusikia Edna karudi alijikuta akipatwa na huzuni kwani angekosa muda wa kukaa na mama yake.
Bi Wema aliichukulia siriasi kazi yake na isitoshe mshahara wake ulikuwa ukiingia kwa mwezi hivyo alipaswa kuzingatia wajibu wake na ndio maana Rufi alikuwa na huzuni kwani mama yake hushinda huko na hurudi kila ifikapo jioni.
Edna yeye mara baada ya kufikishwa nyumbani moja kwa moja aliingia mpaka ndani ya chumba cha Roma na kuoga , ijapokuwa walikuwa wamekosana lakini baada ya tukio Edna moyo wake ulishasahau kila kitu na sasa alitaka angalau kuanza upya ndio maana alimsubiria chumbani walale wote.
Sasa Edna alikaa zaidi ya nusu saa kumsubiri Roma aingie chumbani walale lakini hakuingia na ilimfanya Edna kuwa na wasiwasi na kutoka kwenda kumwangalia na alishangazwa mara baada ya kumkuta akiwa ameketi kwenye Sofa bila ya kufanya chochote akiwa kama mtu mwenye mawazo.
Aliweza kumuona mwanaume huyo kuwa katika hali ya usiriasi mno , hali ambayo hakuwa ameizoea na kumfanya kuwa na wasiwasi kwenye moyo wake.
“Huna usingizi?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma kugeuza shingo yake kumwangalia.
“Tangulia kulala kwanza , kuna kitu nafikiria hivyo nahitaji utulivu kidogo”Aliongea Roma kwa sauti kavu.
“Bado una hasira na mimi?Najua nina hasira za haraka..”Aliongea kwa sauti ya chini kama vile ni mwenye kujutia kitendo cha kuondoka hapo nyumbani mpaka kuingia kwenye matatizo na kumfanya Roma kukumbuka yalitokea kwenye maisha yake ya nyuma.
“Usiwaze sana , ni swala ambao halihusiani na wewe, ni mimi mwenyewe”Aliongea Roma na kumfanya Edna kutingisha kichwa licha ya kutoridhishwa na jibu lake na akarudi juu kulala na ndani ya dakika chache alipitiwa na usingizi.
Siku iliofuata Bi Wema saa kumi na mbili alishafika kwa ajili ya kuandaa kifungua kinywa na kufanya usafi na wakati akiwa bize ndio aliweza kumupona Edna akishuka kuja chini.
“Edna hatimae umerudi, nimeona taarifa ya habari leo asubuhi inayohusiana na nyumba ulionunua kushika moto na kuteketea , bora hata ulitoka mapema kabla ya janga hilo halijakukuta , siku nyingine usiwe mwepesi wa kuondoka baada ya kutokea migogoro sawa”Aliongea Bi Wema na Edna alijikuta akishangaa mara baada ya kusikia jumba lake lote kushika moto lakini ndio muda ambao alikumbuka kuhusu Roma kumwambia jeshi kitengo cha wachawi lingefuta aina yote ya ushahidi.
Hakujali zaidi kwamba amepoteza mabilionni ya pesa kununua nyumba hio wala kuomba fidia , alijiambia angetumia kiwanja hicho kujenga nyumba nyingine kwani ni eneo ambalo ni zuri zaidi.
Baada ya kusalimiana na Bi Wema alijikuta akianza kuangaza kichwa chake kulia na kushoto kumtafuta Roma , maana wakati alivyoamka aligundua hakupandisha kuja kulala.
“Bi Wema hujamuona Roma?”
“Sijamuona , nikajua bado amelala”
Alijibu Bi Wema na kumfanya Roma kushindwa kuzuia hisia zake kujisikia vibaya kidogo ijapokuwa Roma alimwambia hajakasirika kwa chochote lakini moyo wake ulikuwa mzito kuamini maneno yake na aliona bado Roma alikuwa amekasirika.
Kikawaida Roma asingetoka asubuhi bila ya kuaga na muda kama huo wanegejiandaa pamoja kwa ajili ya kupata kifungua kinywa.
“Kwanini usimpigie simu na kumuuliza , huenda kuna jambo baya limetokea?”Alishauri Bi Wema na Edna aliinua simu yake na kutafuta namba yake kwa ajili ya kumpigia lakini alisita.
“Tusahau tu , pengine yupo bize sasa hivi , siwezi kumuongoza na kumzuia kufanya baadhi ya vitu muda wote”Aliongea huku akilazmisha tabasamu.
“Upo sahihi , huna haja ya kuwazia yupo wapi na kujisikia vibaya , isitoshe ndio kwanza mmepatana”
“Mmmh.. sawa Bi Wema, kesho nitaenda kumchukua Lanlan, naomba chakula kisiwe na mafuta sana, nimeambiwa anakula tu nyama huko aliko na sitaki aendelee hivyo kwani atakuwa bonge”
“Sawa hata mimi nimemkumbuka sana , Kaa kwanza upate kifungua kinywa kabla ya kwenda kazini”Aliongea na Edna aliketi na wakati anataka kupeleka kikombe mdomoni alijikuta akisita na kuanza kuandamwa na mawazo ya kujiuliza wapi alipo Roma , kwani hakuzoea kukaa mezani kama hivyo akiwa peke yake.
******
Upande mwingine nchini Rwanda alionekana Raisi Jeremy akiwa ameketi katika makazi yake ya mapumziko maarufu kama State Area D.
Raisi Jeremy alikuwa ameketi eneo la nje pembeni ya bwawa la kuvulia samaki huku pembeni yake kulikwa na mabwana wawili ambao walijitambulisha walikuwa wakitokea katika jamii ya kijini ya Panas.
Raisi Jeremy tokea anuse harufu ya hatari kutoka kwa aliekuwa mke wake Kizwe aliongeza ulinzi unaomzunguka.
Haikueleweka moja kwa moja alikuwa na uhusiano gani na jamii hio ya Panas lakini mwanaume aliefahamika kwa jina la Geni pamoja na Nix wote walikuwa ni walinzi wake, watu ambao walikuwa na uwezo wa kijini katika levo ya Nafsi.
Ijapokuwa Linda alikuwa na uwezo mkubwa wa kumlinda lakini hakumuamini sana kama alivyokuwa akiamini watu kutoka jamii ya Panas.
Kwanza hakueleweka raisi huyu ilikuwaje mpaka akawa na mahusiano ya karibu na jamii hio ambayo ilikuwa ikiogopwa sana katika ulimwngu wa wavuna nishati ya mbingu na ardhi.
“Huku duniani kuna hali mbaya sana ya kutuwezesha kuvuna nishati za mbingu na Ardhi, kuna vitu vingi vya kutamanisha ambavyo ni vya kupita na asilimia kubwa vinaharibu nguvu ya moyo”Aliongea jini kutoka Panasi aliefahamika kwa jina la Geni.
“Mkuu Geni kuvuna nishati ya mbingu na ardhi tafsiri yake kimafanikio ni kuweza kuendana na mazingira , haina haja ya kukazana sana”
“Haha.. ni kweli , ndio maana umekuwa raisi , upo sahihi kabisa”
“Haijalishi kama tutaendelea kuvuna nishati za mbingu hapa lakini Jeremy vipi kuhusu binti yako na yule mtoto wa familia ya Kweka , kama wataachana utakosa ushawishi mkubwa na taifa la Tanzania na mipango yetu kufeli”Aliongea bwana aliefahamika kwa jina la Nix.
“Msiwe na wasiwasi kabisa naendelea kuwafatilia kwa siri , ukweli ni kwamba Roma na binti yangu wameoana kwa zaidi ya mwaka sasa, lakini kwa hali ninayoona hawezi kumuacha Edna kwani matendo yake yanaeleza kila kitu , ugomvi wao wa hivi karibuni umenipa faida ya kuonana nae , lazima atajisikia vizuri nilienda kumuona”
“Kama ni hivyo basi ni vyema kusikia , yule mtoto sio mwepesi kabisa na hatujui ni mbinu gani ameweza kutumia katika mafunzo yake ya kijini , inashangaza kuona hata wanawake wake wameweza kufikia katika levo zile, kama utafanikisha kumfanya binti yako kukutambua kama baba moja kwa moja taifa la Tanzania litakuwa la wakwe zako , nadhani ikifikia hatua hio ujitahidi kujenga ukaribu na yule kijana kwani itatusaidia zaidi katika ukamilishaji wa mpango wetu hapa duniani”Aliongea Geisha na Raisi Jeremy alitingisha kichwa kuelewa.
********
Siku ilienda haraka haraka kwa mrembo Edna , huenda ni kutokana na hamu yake ya kurudi nyumbani mapema.
Edna mara baada ya kutoka kwenye lift moja kw amoja alipita eneo la mapokezi huku baadhi ya wafanyakazi wakimpa heshima yake kila alipopishana nao na Edna aliwarudishia kukubali salamu yake na kisha aliwapita akiwa na uso wa nusu kujali nusu kutojali..
Kipindi cha nyuma Edna angepanda Lift ambayo ingempeleka moja kwa moja mpaka eneo la maegesho ya magari lakini siku za hivi karibuni alikuwa akipitia eneo la mapokezi na kisha ndio aelekee kwenye maegesho ya magari.
Utaratibu huo ulitokana na uwezo wake wa akili kuimarika zaidi, kipindi cha nyuma hakupenda hata kukutana na wafanyakazi njiani lakini kipindi hicho mara baada ya kujua nini maana ya familia alipenda kupitia eneo la mapokezi ili angalau kusalimiana na wafanyakazi hata kwa kupungiana mikono tu.
Edna mwenyewe alikubali kabisa ile tabia yake ya kujitenga tenga mbali na watu ilikuwa ishaanza kubadilika mara baada ya kuoana na Roma.
Angalau kwa kipindi hicho wafanyakazi hawakuzidi kumuogopa na walipata ujasiri wa kumsalimia , lakini zamani hakuna ambaye alitamani kabisa hata kwenda ofisini kwake kutokana na kuhofia ukauzu wake.
Licha ya hivyo Edna hakujua tabia yake mpya ni nzuri au mbaya kama bosi wa kampuni lakini angalau kuona wafanyakazi wakimsalimia kwa tabasamu na matamanio kulimfanya kujihisi hisia za aina mbili , hisia za kufurahi na kutoridhika kwa wakati mmoja.
Uwezo wake uliomfikisha kuwa na pesa nyingi , umaarufu na kuwa msomi ilikuwa ni msingi mkubwa sana kwake kama mwanamke , alijihisi kujiamini na kujiona ni mwanamke ambaye amejitosheleza , wanawake wengine walitegmeea sana wanaume wao kuwasapoti kimaisha lakini yeye alijitegemea katika kila kitu.
Moja ya hisia kubwa ambayo ilimfanya kujisikia vizuri na kujiona kama mwanamke mwenye mafanikio ni pale alipoona wafanyakazi wengi walikuwa wakiendesha maisha yao kwa furaha kupitia kipato wanachopata kwa kufanya kazi katika kampuni yake, kutokana na kuajili watu wengi ilimpa nguvu hata pale anapopatwa na changamoto binafsi kuendelea kufanya kazi bila kuathirika.
Baada ya kuingia kwenye gari yake aliitoa katika jengo hilo na moja kwa moja aliingia katika barabara kuu na kukanyaga pedeli ya kuongezea spidi na kuzidi kuendesha kuingia katikati zaidi ya jiji, lakini licha ya kuwa makini na barabara akili yake ilikuwa ikimuwazia Roma tu , akiwa na shauku ya kujua kama tayari amekwisha kurudi nyumbani.
Siku nzima ya leo alitamani sana angalau kumpigia simu na kumuuliza ni wapi alipo , lakini alihofia kufanya hivyo kwa kudhania kwamba simu yake inaweza isipokelewe au isipatikane.
Kitendo cha kuwa na wasiwasi , hofu pamoja na huzuni vilimfanya kutoweza kuzuia hisia za mawazo yake, hisia alizokuwa nazo wiki iliopita wakati akiiishi mwenyewe baada ya kutoka nyumbani hakuwa nazo , pengine huenda aliamini Roma atakuja tu kwake na kumbembeleza ndio maana hakuwa na hofu .
Lakini wakati huo ambao Roma aliondoka bila kumuaga alihofia huenda mwanaume huyo amemkatia tamaa ndio maana akaondoka.
Alihisi maisha yake yamebadilika kwa viwango vkubwa sana , kwa mfano miaka kadhaa iliopita kitu ambacho alikuwa akifikiria muda wote akirudi ni namna ya kupandisha mauzo katika kampuni yake,yaani muda wote ilikuwa ni kampuni na hakudhania kama maisha yake yangeweza kubadilika na muda huo kuwazia familia.
Hakuweza hata kufahamu ameweza vipi kufika nyumbani , lakini alijishtukia ameendesha umbali mrefu mpaka kufika nje ya geti
Kwa namna ambavyo alikuwa mzuri ukijumlisha na mafanikio yake pengine huenda kama angeolewa na mwanaume wa kawaida angemnyenyekea sana , lakini mrembo Edna bahati mbaya mwanaume ambaye moyo wake umependa ndio huyo mwenye wanawake kibao na tena haonyeshi kujali kabisa.
Kwa mtu wa nje huenda angeuliza mwanamke mrembo kama Edna kampendea nini mwanaume kicheche kama Roma. Lakini mwisho wa siku mwenye kujiuliza maswali angekosa majibu sahihi na pengine angeweza kupata maswali zaidi kama angekutana na Rose , Rufi , Amina , Najma , Mage ,Dorisi na wengineo.
Edna mara baada ya kuingia ndani moja kwa moja alichungulia chumbani kwa Roma na kukagua mazingira haraka haraka na hakuona dalili ya mtu na alijikuta huzuni ikimwandama , alienda na chumbani kwake kuangalia lakini hakukuwa na dalili na mwisho kabisa aliamua kushuka mpaka chini akiwa bado hajabadilisha mavazi aliotoka nayo kazini.
Baada ya kufika sebuleni alikuwa kama vile ni mgeni amefika sasa anatafuta wenyeji..
Bi Wema aliekuwa akishuka kutoka juu alishangazwa na mwonekano wa Edna na kujiuliza ni kitu gani anatafuta.
“Miss , umerudi saaa ngapi , kwanini unaonekana kama kuna kitu unatafuta?”Aliuliza Bi Wema kwa upole na Edna mara baada ya kumwangalia Bi Wema kwa dakika kadhaa alijikuta akikosa ujasiri na machozi yalianza kumtoka palepale na kuanza kulia kwa kwikwi huku akiwa ameegemeza kchwa chake katika kifua cha Bi Wema.
“Edna mwanangu una tatizo gani , kuna mtu yoyote kakuchokoza,nini kimekupata , kwanini unalia?”Aliuliza Bi Wema ambaye alikuwa kwenye mshituko na wasiwasi.
“Bi Wema, Roma hanitaki tena ..”Aliongea huku akifuta machozi na kumfanya Bi Wema kukosa neno la kusema kwani aliishia kushangaa ,
“Bado ana hasira na mimi , nadhani ananiona nina kiburi na simsikilizi hivyo kaamua kunipotezea ..”Aliongea huku akiendelea kulia kwa kwikwi
“Miss hakuna jambo kama hilo”Aijaribu kufariji Bi Wema.
“Lipo Bi Wema, angalia sasa tokea asubuhi haonekani , anaoneana hataki kuoniona tena ,, na ameenda kujificha..”
“Unamaanisha nini haonekani , si ndio amerudi sasa hivi tu”Aliongea Bi Wema huku akiwa ni mwenye mshangao na kauli yake ilimfanya Edna kuacha kulia na kumwangalia Bi Wema kama vile amemsikia vibaya.
“Amerudi!!”
“Ndio , na huo mfuko umejaa nguo zake chafu na sijui hata ametokea wapi maana zimejaa matope , ni kama vile alilala porini”Aliongea Bi Wema na kisha alifungua ule mfuko mweusi wa plastic na kumuonyesha Edna.
Baada ya kuangalia na kuona kweli ni nguo za Roma zilizochafuka alijikuta palepale kuanza kushikwa na aibu mbele ya Bi Wema.
“Mr atakuwa anaoga sasa hivi , usiwe na wasiwasi”Aliongea Bi Wema huku akimgusa mabega yake.
Edna alijikuta akiangalia sakafu bila kuinua uso wake , alitamani ardhi itengeneze shimo na atumbukie kutokana na aibu aliokuwa nayo mbele ya Bi Wema , alianza kujilaumu kwanini hakuthibitisha kwanza.
Likija swala la mahusiano akili ya mwanamke haifanyi kazi kisawa sawa na Edna aliweza kuamini siku hio , mwanzoni alikuwa akipinga lakini mara baada ya kuwa katika hali hio aliamini moja kwa moja na kile kilichokuwa kikisemwa.
“Basi Bi Wema… nadhani napaswa kwenda juu”Aliongea Edna kiaibu na hakutaka kusubiri jibu kutoka kwa Bi Wema kwani aliona aibu kumwangalia usoni na palepale alikimbia nduki kupandisha ngazi na kumfanya Bi Wema awe na wasiwasi kwani aliogopa anaweza kuteleza na kudondoka.




SEHEMU YA 557.
Bi Wema mara baada ya kusikia mlango ukifungwa kwa juu alijikuta akivuta pumzi na kuzishusha na akachukua mfuko wake na kutembea mpaka chumba maalumu cha kufulia na kuziingiza kwenye mashine ya kufulia.
Baada ya kumaliza na kazi hio ndogo alitoka kimya kimya kurudi sebuleni na kusogelea shelfu maalumu ya kuwekea picha.
Bi Wema aliinua picha iliokuwa kwenye fremu , ilikuwa ni picha ambayo Edna aikuwa mdogo akiwa amebebwa na Bibi yake , pembeni alikuwepo Mama yake Edna aitwae Raheli , Bi Wema pamoja na Mzee Adebayo ambaye yeye pekee alionekana ni mwenye kununa kutokana na kukosa furaha.
“Madam kabla hujaondoka katika huu ulimwengu uliniambia niendelee kumlea Edna mpaka atakapokuwa mkubwa , niliamini akishaolewa atakuwa tayari mkubwa na mwenye kujitegemea lakini mpaka sasa bado namuona ni kama mtoto .. bado ni mwenye kulia lia kama alivyokuwa mdogo..”Aliongea Bi Wema huku akiweka tabasamu ambalo lilishiria huzuni.
Upande mwingine ndani ya chumba chake Edna alikuwa akitembea kutoka dirishani hadi mlangoni na kisha anarudi tena dirishani , muonekano wake ulikuwa ni kama wa msichana ambaye hajavunja ungo ambaye yupo katika hali ya aibu.
Kutokana na kioja alichofanya hakupata ujasiri hata wa kurudi tena sebuleni na kuonana na Bi Wema tena , yeye mwenyewe hakumbuki ni lini aliweza kulia kitoto namna hio bila sababu ya msngi.
Edna alijikuta akiwa na aibu na alitamani arudishe muda nyuma na iwe ni wakati ambao ndio anatoka kwenye gari na kuingia ndani , lakini uwezo huo hakuwa nao ziadi ya kuzidi kuficha sura yake na mikono.“Haya yote yananitokea kwasababu ya huyu mpuuzi Roma”Alijikuta aking’ata meno yake kwa hasira huku akimlaani Roma lakini muda huo huo mlango wa chumba chake uligongwa.
Edna alijua lazima atakuwa ni Bi Wema hivyo alivuta pumzi nyigi na kujituliza na kujiambia Edna tulia na hili litapita na kisha akasogelea mlango na kwenda kuufungua.
Lakini mara baada ya kufngua mlango alikutana na uso wa Roma , ambaye amekwisha kumaliza kuoga na muda huo alikuwa amevalia tisheti.
Edna alijikuta akianza kumkagua mwanaume huyo kwanzia kichwani mpaka miguunni na kumfanya Roma acheke namna ambavyo anakaguliwa.
“My Dear Edna , kwanini uko hivyo , mbona kama ulikuwa ukilia , kwanini macho yako ni mekundu hivyo?”
“Sikuwa nikilia , niliingiwa na mchanga machoni wakati nikitoka kwenye gari”Alitafuta sababu yoyote ya kudanganya lakini tukio alilolifanya bado lilimfanya kukosa kujiamini.
“Kuna kitu unataka?”Alijitutumua na kuuliza huku akiwa na hisia mchanganyiko.
“Ndio kuna kitu nataka , nimemuambia Bi Wema akimaliza arudi tu nyumbani maana ninakutoa Dinner , kwasababu Lanlan anarudi kesho nadhani sio mbaya kutumia muda huu peke yetu”
Edna alijikuta akishangaa , alikumbuka kabisa alionekana kwenye mawazo jana usiku , kwanin ameweza kurejea katika hali yake ya kawaida ghafla tu na sasa anataka kwenda nae kupata chakula cha usiku.
Ijapokuwa sio jambo la kushangaza mume na mke kutoka kwa ajili ya chakula cha usiku lakini ‘timing’ haikukaa vizuri.
“Kuna chochote unataka kuongea?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma kubadilika na kutabasamu kidogo.
“Sina.. usifikirie sana ..”
“Tatizo mwonekano wako unaonyesha kama kuna kitu unanificha”Alongea akionyesha kutoridhika.
“Tutaongea tukiwa njiani , hatuwezi kuendelea kusimama hapa , muda unaenda”
Ukweli ni kwamba Edna alikuwa akikumbuka siku ile ambayo Roma alimpeleka katika lile jengo la hoteli na kutaka waachane, kutokana na kile kilichotokea jana yake alijuwa tu kuna jambo ambalo Roma anataka kumwambia , huenda mwanaume huyo ameshafanya maamuzi ya kuachana nae na anataka kwenda kuongea nae katika sehemu tulivu ili waachane kistaarabu.
Kitendo chake cha kukosa kujiamini na kujishutikia kilimfanya kujishangaa hata yeye mwenyewe lakini Roma alijitahidi kuonekana wa kawaida.
“Darling , usifikirie sana nishafanya booking , tondoke”Aliongea Roma huku akionyesha wasiwasi kwani ni kama Edna anataka kukataa.
Edna aliamua kuvuta pumzi na kuzishusha na kujiambia atakubaliana na kila maamuzi yake na isitoshe ndoa hailazimishwi, yaani alikuwa ashasahau kama siku zilizopita yeye ndio alietaka kuvunja ndoa tena kwa jeuri kabisa.
Lakini haikushangaza kwani ni mwanamke, na ni tabia ya kawaida kwa mwanamke likija swala la hisia kuwa mbinafsi.
“Sawa , lakini je ni mbali , napaswa kuvaa vizuri zaidi?”Aliuliza Edna kinyonge.
“Sio mbali tutafika mapema tu , tayari unaonekana mrembo na inatosha”Aliongea Roma akiwa ni mwenye tabasamu na kumfanya Edna aone huenda anavyowaza ni tofauti.
Baada ya Edna kujiweka sawa kidogo waliweza kutoka pamoja na baada ya kufika eneo la nje Edna alitaka kuelekea kwenye maegesho ya magari lakini Roma alimvuta kwake.
“Hatutotumia gari , kwasababbu hatuwezi fika kwa gari”
“Kwanini?”Aliuliza akiwa katika mshangao.
“Kwasababu tunaenda nje ya nchi kwa ajili ya chakula cha usiku”Aliongea huku akimkonyeza na Edna alieshangaa kabla hata hajatoa neno alijikuta akibebwa juu juu kama mtoto.
“Hey! , unafanya nini , wapi tunaenda?”Aliongea huku akishikilia vizuri shingo yake akiogopa kudondoka.
“Utajua tukishafika nishikilie vizuri , nitapunguza spidi lakini bado nitakuwa na haraka ukidondoka angani halitakuwa jambo zuri”Baada ya kumaliza kuongea maneno yale palepale walipotea kijini.
Ilikua mara yake ya kwanza kusafiri umbali mrefu kwa njia ya kijini , aliweza kuona nyota na mwezi kwa urahisi kabisa , ijapokuwa upepo upepo ulikuwa mkali lakini kwasababu ya kujikinga na ngao ya kichawi hawakuathirika..
Baada ya kugeuza macho yake na kuangalia chini alijikuta akishikwa na mshangao , kwani ni kama vile yupo katika sayari nyingine kabisa kutokana na mataa yaliokuwa yakionekana chini yake , na kadri alivyokuwa akishuka chini ndio ambavyo alivutiwa na mandhari.
“Hapa ni wapi??”Aliuliza Edna , hisia zake zilimwambia kabisa hapo ni wapi lakini kutoana na mshangao wake hakutaka kuamini.
“Hapa ni Dubai”Aliongea Roma na kumfanya Edna kukosa neno , ni kweli sehemu ilikuwa ni Dubai kutokana na kwamba haikuwa mara yake ya kwanza kufika , lakini hakuamini kama wametumia dakika chache kutoka Tanzania kuja Dubai tena kwa ajili ya chakula cha usiku.
“Tupo hapa kwa ajili ya chakula lakini nina surprise nyingine”Aliongea Roma.
Muda huo licha ya kwamba jiji la Dubai lilikuwa limechangamka kutokana na kuwa jiji la kibiashara , lakini eneo ambalo walikuwepo halikuwa na watu wengi kwani ni eneo ambalo limejitenga na mjini.
Mbele yao kulikuwa na jumba kubwa ambalo limejengwa kwa mtindo wa tamaduni za kiarabu, lilikuwa ni jumba la kifahari ambalo limezungukwa na bustani nzuri sana na Edna licha ya kwamba ametembelea mahoteli mengi ya kisasa na kuishi , lakini jumba binafsi kama hilo la kitajiri hakuwahi kutembelea , sio kama hakuwa na uwezo huo lakini kutokana na miasha yake kutojihusisha na kupenda ‘bata’ , huenda ndio maana sehemu nzuri kama hio ilikuwa ni ya kipekee kwake.
“Unajaribu kufanya nini?”Aliuliza Edna lakini Roma hakumjibu zaidi ya kumshikilia mkono na kusogelea jumba ambalo liko mbele yao , jumba ambalo limezingirwa na miti midogo midogo ya kupendeza.
Baada ya kukaribia na kupokelewa na miti maalumu ya maua Roma alisimama na kumfanya Edna kushangaa na kumuuliza kama ndio washafika lakini Roma alimpa jibu tofauti.
“Miss Edna please close your eyes and wait for me to count untill three then open them , alright?”Aliongea Roma kwa lugha ya kingereza akiwambia kwamba afumbe macho yake na amruhusu kuhesabu mpaka tatu ndio ayafumbue.
Edna alikuwa ni mwenye maswali mengi , lakini alishia kuyafumba ili kujua nini kinakwenda kutokea.
“Moja .. mbili..tatu”Baada ya kusema tatu alifumbua macho yake na kuangalia lakini alijikuta akiwa katika hali ya mshangao mara baada ya kuona kitu kilicho mbele yake na kuishia kuziba mdomo, ukiachana na namna ambavyo sehemu hio imepambwa na miti midogo midogo iliofungwa taa za rangi na kupendeza , lakini neno One year down , a lifetime to Go, Celebrating our marriage -HAPPY ONE YEAR MARRIAGE ANNIVERSALLY lilimfanya kumbukumbu zake kurudi nyuma.
Alijkuta palepale akikumbuka siku hio ndio siku ambayo alifunga nae ndoa ya Bomani na Roma.
Alishangaa maana hakuwa akikumbuka chochote kabisa siku hio. Alijiuliza inamaana kupotea kwake siku nzima alikuja kuandaa kitu kama hicho?
Edna moyo wake uliliainika kwa kitendo hicho , alimdhania vibaya Roma kama anaenda kumuacha kumbe alikuwa akiandaa surprise kwa ajili yake.
TUTAENDELEA KITAMBO KIDOGO.
 
SEHEMU YA 558.
Kama ni chakula cha usiku , kilikuwa chakula cha usiku kweli kutokana na eneo ambavyo lilipambwa na kupendeza na ilimgusa mno Edna.
Upande wa Roma alionekana kufanya hivyo kumuonyesha Edna namna gani anaheshimu ndoa yake na mrembo huyo licha ya kwamba ilianzia katika mkataba.
Kitendo cha Edna siku nzima kuhofia pengine Roma hamtaki tena kutokana na kilichotokea usiku , ilimfanya kuguswa mno mara baada ya kugundua kumbe yeye alichokiwaza ilikuwa tofauti kabisa.
Inasemekeana wanawake wanapenda sana surprise na kwa mwonekano wa Edna alionekana ameguswa mno , kwanza ameguswa na namna ambavyo eneo limepambwa , lakini pili aligusswa na namna ambavyo Roma aliamua kuonyesha namna ambavyo yupo siriasi na yeye.
Wanasema ‘Surprise’ humfanya mwanamke kujihisi kuwa wa kipekee na kumuonyeshea kwamba muda wote unamfikiria.
Roma mara baada ya kuona mke wake yuko katika hali ya kukumbwa na mshituko wa kisaikolojia palepale alimvutia kwake na kumkumbatia.
“Hey Babe hata kama umeguswa na ‘surprise’ yangu haina haja ya kutoa machozi , nimefanya haya yote ili uwe na furaha”Aliongea Roma.
“Wewe ni mtu mbaya sana”Alilalamika huku akianza kumpiga piga kwenye kifua chake mara nyingi , lakini vingumi vyake vilikuwa vile vilaini.
“Unajua ni kwa kiasi gani nilikuwa na wasiwasi wewe kuondoka bila ya kuaga na kutokuwepo kwako nyumbani asubuhi , nilifikiiri hukutaka kuongea na mimi tena , nili,, nilifikiri umeshanitelekeza tayari na hunipendi, unajua ni kwa namna gani nimeogopa?”Aliongea na kumfanya Roma kushangazwa na kauli yake na palepale akamshika mikono.
“Sikufikiria hivyo , nilikuwa nikitafuta namna ya kukufanya uwe na furaha , najua ndoa yetu ilianza kwa mkataba na hakukuwa na hisia zozote zilizohusika , lakini unapaswa kuelewa siku ile sikufanya maamuzi kwa kukurupuka , Edna nataka utambue ni kwa kiasi gani nakuheshimu na kukupenda kama mke wangu, siku zote utakuwa kipaumbele kwenye maisha yangu..”
“Usiongee tena nitalia..”
“Lakini ushalia tayari “
“Wewe ndio umenifanya nilie”
“Lakini sijakulazimisha ulie si ndio , Tangu lini ukawa na adabu hivi?”
“Mkorofi sana wewe”
“Hehe.. kheri ya mwaka mmoja wa ndoa mke wangu”Aliongea Roma huku akimkumbatia.
“Usinikumbatie, bado nina hasira na wewe na nakuchukia kwa kunichanganya”
“Lakini nilitaka kukumbatia na kukufanya uwe na furaha kwasababu nakupenda”
“Roma nakuchukia”
“Edna nakupenda”.
Sauti ya kimapenzi kati ya mwaname na mwanamke ilisikika ndani ya eneo zima , lilikuwa ni eneo tulivu mno ambalo haikuweleweka kama kulikuwa na mtu mwingine.
Baada ya kubishana kwa muda na kukumbatiana hatimae Edna aliishia kucheka kwa furaha na sasa kuingia ndani katika jumba hilo kwa ajili ya chakula cha usiku maarufu kama Candlelight dinner.
***********
Siku iliofuata iliwakuta kwenye kitanda cha sita kwa sita katika jumba hilo la kifahari.
Mazingira ya jumba hilo yalizidi kuvutia mara baada ya jua la asubuhi kuangaza , ni kama vile miti iliozunguka jumba hilo ilipandwa kuakisi namna nzuri ya mwanga unavyomulika madirisha na kuingia ndani.
Alijihisi uchomvu mno licha ya kwamba alilala fofofo , hio yote ni kutokana na kile kilichotokea usiku mzima.
Kutokana na juhudi alizoonyesha mwanaume wake hakuwa na nguvu ya kumkatalia kufanya ule mchezo ndio maana wakajikuta wakifanya muda mrefu na hata muda ambao alipotelea usingizini hakuelewa.
Sasa muda ambao Edna alimaliza kupambana na mwanga wa jua akitaka kujiondoa katika mwili wa Roma uliomkubatia alijikuta akiguna, alikuwa kama alivyozaliwa na namna ambavyo manyonyo yake yalivyokandamiza kifua cha mwanaume huyo ilimfanya kuona aibu na kuchukia kidogo kwa wakati mmoja.
Lakini hata hivyo wakati alivyotaka kurudisha kiuno nyuma alijikuta akitoa mguno mkubwa zaidi kuliko wa mwanzo .
Ni kwasababu Gobole la uhai la mwanaume huyo bado lilikuwa limemwingia katika sehemu zake za uzazi, Edna hakuelewa ilikuwa ni Roma ambaye hakumaliza usiku hivyo kumsababishia Gobole hilo kutuna au alimfanyia hivyo asubuhi asubuhi.
Alitaka kujiondoa kwake lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na kushikiliwa lakini kwa wakati mmoja kuona aibu za kike.
Wakati akiendelelea kuwaza cha kufanya huku akimwangalia Roma , aliweza kuona Lips za mwanaume huyo zikicheza.
“Wewe,, kumbe upo macho..halafu unajifanyisha kulala”Aliongea huku akimsukuma Roma kifuani kwa nguvu.
“Hahaha..”Roma alijikuta akitoa cheko mara baada ya mchezo wake kugundulika.
“Wewe…acha kucheka mtoe huyo shetani wako nje”Aliongea akitaka kujichomoa lakini alikuwa ameshikiliwa vizuri sana.
“Kwanini nimtoe , My Dear Edna ni vizuri kama tutafanya mazoezi ya asubuhi asubuhi , ukiendelea kujipinda pinda utaimeza yote , sikujua kumbe una hamu ya kula kiasi hicho”
“Wewe ndio mwenye hamu kubwa ya kula , umeilazimisha hapo , siwezi kuendelea hivi”
“Kweli?’ mbona kama unaipenda iwe yote angalia namna ulivyo mwekundu sasa”
“Wewe.. Ah.. hapana”Edna alitaka kujitoa lakini aliwekwa vizuri na kabla hajashitukia ilikuwa tayari kimiani
“Babe , jana ulilala mapema kabla hata ya kuniruhusu nishushe japo risasi moja , nimevumilia kwa kutokukuamsha , tusifanye chochote asubuhi hii mpaka nikushushie mzigo wote , ukikataa sitokuwa na uwezo wa kuvumilia”Baada ya kuongea hivyo alimpelekea mdomo mke wake na kilichoendelea hapo ni miguno iliodumu muda mrefu.
******
Naam ilipita wiki moja tokea Roma na Edna kupata chakula cha usiku katika jiji la Dubai kusherehekea mwaka wao mmoja wa ndoa.
Katika wiki hio Magdalena aliweza kufika katika levo ya Nafsi akiwa sawa na Rose.
Kutokana na kwamba sheria zilikuwa zikimzuia Magdalena kubakia katika ulimwengu wa kawaida mara baada ya kufikia levo hio ilibidi Roma apendekeze Rose na Magdalena kwenda kuishi visiwa vya wafu kwa muda huku wakiendelea kujifunza zaidi kuvuna nishati za mbingu na ardhi kwani asingeweza kuhonga tena kama Magdalena atashitukiwa.
Mwanzoni Rose alikataa kwenda visiwa vya wafu kwa kuogopa kwamba angekuwa mpweke , lakini mara baada ya kuona hata Magdalena anapaswa kwenda huko hakuona tatizo tena ns isitoshe alikuwa na shauku ya kuona nchi ya Roma.
Upande wa Magdalena licha ya kwamba hakuwa na mahusiano na Roma lakini alijisikia vizuri kwamba ni yeye pia ni sehemu ya watu Roma anaowajali.
Magdalena licha ya kwamba alilazimishwa mara kibao kuoana na mwanaume aliefahamika kwa jina la Jumbe aliweka ngumu zaidi huku sababu yake kubwa ikiwa ni kisingizio cha mafunzo ya mbinu za kijini.
Wakati Magdalena alivyoenda nchini China akiwa na Roma aliambiwa na Master wake kwamba kama anataka kupanda levo kwa haraka katika mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na Ardhi basi ahakikishe hafanyi mapenzi na anabakia kuwa bikra kwani ingemsaidia sana.
Hivyo Mage alitumia mbinu hio kuepuka ndoa na hata swala la kwenda nje ya nchi kwa muda kuepuka kupelekwa katika miliki za kijini kulingana na sheria kwake alichukulia hio kama fursa ya kukimbia usumbufu wa Jumbe.
Afande Tobwe mara baada ya kuambiwa sheria iliopo juu ya binadamu anaejifunza mbinu za kijini aliefikia katika Levo ya Nafsi alishangaa na hakuwa tayari kuona Magdalena anaenda katika miliki za kijini kuishi , hivyo yeye na mke wake walikubali Roma amchukue na ampeleke katika miliki yake.
Mama T kitendo cha Magdalena kutaka kwenda nje ya nchi , tena katika miliki ya Roma alipatwa na wasiwasi kwa kuona mapenzi ya Magdalena kwa Roma yangeongezeka maradufu na kusababisha watoto wake wote mapacha kuwa michepuko wa mwanaume mmoja , lakini licha ya wasiwasi wake huo hakutaka pia kumuona Magdalena akienda miliki za kijini kulingana na sheria, hivyo kishingo upande alikubali huku akimsisitiza Mwanae huyo kuachana na mawazo juu ya mpenzi wa pacha mwenzake , lakini kwa Magdalena maneno ya mama yake yaliingia sikio la kulia na kutokea la kushoto , alijiambia ‘what if’ yeye na pacha wake wakitoka kimapenzi na mwanaume mmoja kwanza yeye na pacha wake walishakaa chini na kuyaongea na kukubaliana kufuata mioyo yao , ilikuwa ujinga lakini mapenzi yalikoleza ujinga wao na hawakujali huko mbeleni watu wangewachukuliaje.
Ni siku moja kabla ya Roma kumpeleka Rose na Magdalena katika visiwa vya wafu, usiku wa siku hio Sophia aliweza kurudi kutoka Japani , alikokuwa ameenda kwa ajili ya kusalimia familia yake.
Kurudi kwa Sophia usiku huo kumlimfanya Lanlan kufurahi kwani alimtaka Shangazi yake huyo amfundishe namna ya kuimba.
Lanlan siku iliokuwa ikifuatiwa walikuwa na maonyesho maalumu shuleni kwao ambayo yalihusisha na kuimba na hata Edna na Roma walipaswa kushiriki kama wazazi.
Hivyo wanafunzi wote walipewa kazi ya kuchukua mazoezi nyumbani namna ya kuimba ili siku inaofuata kufanya vizuri mbele ya wazazi.
Sasa Lanlan mara baada ya kugndua mama yake Edna hakuwa akijua kuimba ndio maana alimkimbilia Sophia amsaidie yeye katika kufanya mazoezi hayo.
Sophia kama shangazi alivyoombwa na Lanlan alikubali kumsaidia kwa furaha zote, kwanza kabisa alimpenda Lanlan kutokana na akili yake na siku hio Lanlan aliishia kulala chumbani kwa Sophia mpaka asubuhi.
Siku iliofuata kwasababu Sophia hakuwa na chakufanya nyumbani Edna alimuomba waende pamoja shuleni kwa Lanlan kwa ajili ya kuangalia maonyesho yao na Sophia hakubisha lakini ilimbidi kwanza kutafuta kofia na miwani kuvaa ili asitambulike kutokana kipindi hicho umaarufu wake ulizidi kuwa mkubwa kutokana na kuigiza muvi ambayo kwa mara ya kwanza ilikuwa ikitarajiwa kuonekana katika mtandao wa Netflix.
Baada ya kufika chuleni hapo,waliweza kupokelekewa na kuonyeshwa mahali maalumu pa kukaa.
Braeburn ilikuwa shule kubwa na watoto hawakufundishwa kusoma tu , lakini pia walipewa nafasi ya kushiriki katika michezo mbalimbali , lakini pia kuwajengea hali ya kujiamini na zaidi sana kuwasaidia kutambua vipaji vyao, ndio maana waliwapatia nafasi ya kufanya matukio ya aina nyingi , yawe ni ya kuimba ya kucheza mpira , kuchora , kuvutana kamba na kuruka.
Kwenye maonyesho ya kuimba Edna alimuacha Lanlan afanye atakavyo , lakini akamuonya kwenye maonyesho ya kutumia nguvu asitumie uwezo wake afanye kawaida tu na Lanlan alionekana kuelewa.
Edna alifurahi sana kuona kwamba mtoto wake alikuwa akichangamana na marafiki zake vizuri tokea mara ya mwisho kutokea kwa tukio la Lanlan kumnyofoa mtoto mwenzie nywele, watoto ni wepesi kusahau na hiko ndio kilichotokea na ilimfurahisha zaidi.
Asubuhi michezo ilioanza kwa watoto ilikuwa ni kuruka kamba , kuvuta kamba kitimu , pamoja na kushuti maputo angani kwa siraha maalumu za kitoto.
Katika maonyesho yote hayo Lanlan alifanikiwa kuibuka kidedea , alishusha karibia maputo yote kwenye kushuti na wakati wa kuvutana kamba alisaidia sana timu yake kushinda na lilipokuja tukio la kuruka Kamba alionyesha ubingw wa kuruka pasipo ya kuchoka haraka.
Roma aliona mambo aliofanya Lanlan ni kawaida lakini kwa Edna alikuwa akijivunia mno kuona mwanae ndio kawa kivutio kikubwa.
Baadhi ya wazazi walimuuliza Edna na Roma siri ya mafanikio yao ni nini mpaka mtoto wao kuwa na nguvu hizo na Roma alichukua nafasi hio kujigamba na kuawaambia siri kubwa ni msosi.
Wakati wa mchana mara baada ya mapumziko ulikuwa ni wakati wa wazazi kupata chakula kilichoandaliwa hapo shuleni.
Shule kubwa kama hio haikuona tatizo kufanya matukio ya namna hio na kuonekana kwenye vipindi vya watoto kwenye runinga ili kuzidi kujiongezea umaarufu, lilikuwa tukio ambalo lipo kimkakati zaidi wa kimatangazo.
Baada ya chakula cha mchana, uliwadia muda sasa wa watoto kuonyesha vipaji vya kucheza mziki pamoja na kuimba.
Zamu ya Lanlan na wenzake ilipowadia Edna alishindwa kujizuia na kusimama ili kuosgea mbele kumrekodi lakini Roma alimwambia ataenda yeye.
“Hapana nitaenda mimi , ili kuleta maana zaidi”Aliongea Edna akikataa na kumfanya Roma ashindwe kuongea chochote huku akishindwa kuelewa kuna maana gani tofati akimrekodi yeye.
“Sister Edna anaonekana amekolea kwenye malezi”Aliongea Sophia aliekuwa pembeni huku akiwa anacheka.
Edna ijapokuwa alikuwa bize katika kazi lakini pia alionekana likija swala la malezi alikuwa vizuri zaidi na Roma aliona Edna ni mama mzuri kuliko mke.
Sasa kuna muda ambao Sophia alijisahau na kutoa kofia yake aina ya Hat pamoja na miwani na kumfanya sura yake kuonekana muda huo, kitendo kile kilimfanya Paparazi aliekuwa mita kadhaa kutoka walipokuwa wamekaa yeye na Roma apige picha kwa kutumia Kamera yake ya Lens kubwa bila ya uelewa wa sophia wao.
Baada ya kundi la Lanlan kumaliza kuimba na Roma kumgeukia Sophia , aligundua ashajisahau na kuacha sura yake kuonekana na palepele alimsaidia kumvalisha kofia na akampa ishara na kumwambia avae miwani vizuri ili asionekane sura yake kwa watu kutokana na umaarufu wake.
Na Sophia mwenyewe alishangaa kujisahau kwake , huenda ni kutokana na kufarahishwa na kile ambacho watoto walikuwa wakifanya , kwani ukiachana na kuimba lakini walifanya vizri sana kwenye kucheza na kilichomfurahisha zaidi wimbo wake ndio waliokuwa wakitumia watoto hao kucheza.
Baada ya matukio yote kumalizika wote kwa pamoja waliingia kwenye gari na kuanza safari ya nyumbani.
Lanlan alikuwa amechoka mno na mara baada ya kuingia tu kwenye gari alipotelea usingizini kwenye mikono ya Edna , huku akichezesha midmo yake kana kwamba kuna kitu ambacho anakula.
Edna na Sophia walikuwa wamekaa siti ya nyuma , Sophia yeye alikuwa bize kungalia vidio zote zilichochukuliwa kwa simu na Edna kwa kuzirudia rudia , na alijikuta zikimfurahisha na aliendelea kuzingalia huku akiwa amepunguza sauti ili asimsumbue Lanlan aliekuwa usingizini.
Roma aliekuwa akiendesha baada ya kuangalia Kamera ya nyuma na kuona namna ambavyo Sophia na Edna walivyotabasamu pamoja na mtoto wake kuwa katika pozi la usingizi alijikuta moyo wake ukipatwa na joto ambalo halikuwa la kawaida kabisa, hakuamini maisha yake yamefikia steji hio na alijiambia kweli safari ya binadamu ni yenye mambo mengi ambayo sio yenye kufahamika zaidi ya muda pekee kuamua.
Aina ya maisha hayo miaka kadhaa yalikuwa kama ndoto tu na hata wakati aliporudi Tanzania ilikuwa ni kwa ajili ya kutafuta familia yake na angalau kutibu tatizo lake , lakini mambo yalitokea mfululizo kiasi kwamba yamemfikisha katika hatua hio , aliweza kujisikia hali ya kuridhika na furaha kwa wakati mmoja na alijiambia kama hakuna mtu ambaye angeweza kumsmbua kwa wakati huo basi maisha yatakuwa mazuri sana kwake .
Siku iliofuata alfajiri Roma aliwachukua Rose pamoja na Magdalena kuwapelekea katika makazi yake ya visiwa vya wafu.
Kabla ya kuanza safari alikuwa tayari ashamtaarifu Ron ili kuandaa mazingira na mahitaji kwa ajili ya wanawake wawili.
Na aliweza kurejeshwa taarifa kwamba tayari amekwisha kutafuta wafanyakazi wa ndani ambao wangewasaidia katika mahitaji yao ya kila siku.
Hawakubeba nguo nyingi kuelekea huko , ni mabegi tu ya mgongoni ndio ambayo walitumia na hio yote ilikuwa ni kupunguza uzito.
Ilikuwa mara ya kwanza Roma kupaa angani akiwa amefuatana na warembo wake , hakika alijisikia kama mtu ambae amefanikkisha jambo kubwa sana katika maisha yake.
Iliwachukua dakika ishirini tu kutoka Tanzania mpaka visiwa vya wafu , kwasababu Rose na Magdalena hawakuwa mwishoni mwa levo ya Nafsi Roma hakuhofa wao kukumbwa na adha ya kupigwa na radi kutokana na kukiuka kanuni za anga.






SEHEMJU YA 559.
Muda ambao waliweza kufika ilikuwa ni usiku kama saa tisa hivi, lakini licha ya hivyo kutokana na uwezo wao wa kichawi haikuwazuia kushangazwa na mazingira.
“Nyie watu mpo hapa ndani ya muda muafaka kipupwe ni cha wastani na mvua sio nyingi lakini sio kukavu wala ubaridi vilevile , mpo hapa kufurahi”Aliongea Roma kwa tabasamu mara tu baada ya kufika
Rose na Magdalena walikuwa na mshangao wa kuvutiwa na namna mazingira yalivyokuwa yakionekana , mwanzoni walikuwa wakisita sita kuja lakini mara baada ya kujionea wenyewe kwa macho yao waliona ni kama wamepiga ndege wawili na jiwe moja , wangeweza kuwa mbali na watu jamii ya majini na vilevile wangetumia muda huo kama wa mapumziko.
Kwa namna ambavyo waliweza kutua katika fukwe ya bahari , huenda mtu ambaye angeweza kuwashuhudia moja kwa moja angejisemea hao ni Majini halisi.
Roma aliwaongoza warembo hao kuelekea katika makazi yake maana haikuwa mbali na sehemu waliotua.
“Honey , umesema kila kitu hapa ni cha kwako ?”Aliuliza Rose ambaye alikuwa akichezea gamba la konokono wa baharini.
“Unaweza kusema hivyo , lakini watu wa hapa niliwakuta hivyo siwezi kusema nawamiliki lakini jeshi lote lipo chini yangu, hili eneo ni Grey Zone hivyo hakuna taifa ambalo linawea kusogea wala kulinasa katika ramani”
“Je miungu wote wana maeneo yao au ni kwa wewe tu?”Aliuliza Magdalena na kumfanya Roma kufikiria kidogo.
“Hata mimi mwenyewe sina uhakika , dunia sio kubwa kihivyo lakini sio ndogo vilevile , miungu yote iliopo hapa duniani wana miaka mingi sana hivyo wanajua kila kona ya dunia , kama wangetaka kuwa na eneo kama hili nadhani ni rahisi sana kwao labda tu kama hawakuwa tayair lakni niliwahi kusikia Christen ana eneo lake nchini Canada na Poseidon yeye ana eneo lake katika visiwa vya Hawaii Marekani , sijui kuhusu wengine , kila mmoja vipaumbele vyake ni tofauti hivyo kuna uwezekano wasipendelee kuwa na maeneo binafsi.”
“Kama ipo hivyo nadhani majini ndio yanatia huruma , maisha yao yote ni kujificha katika ulimwengu wa kufikirika”
“Huenda ni kwasababu ya uwepo wa Athena na isitoshe kuvuna nishati za mbingu na ardhi sio jambo jepesi , sio wote ambao wana uwezo wa kupanda levo zaidi kupita nafsi ili kuweza kushindana nao”
Roma alifikiria katika moyo wake kama miungu kipindi hiki walikuwa na asilimia therathini ya uwezo wao je kipindi wakati wanafika ilikuwaje.
Alijiambia huenda Majini yalikuwa yakiogopa kitu ambacho hawakijui ndio maanda waliishia kujifiacha katika ulimwngu wa kufikirika , huku kisingizio chao kikubwa ni kutotaka kuingilia maswala ya dunia ya kawaida.
Bila kuelewa wakati wakiendelea kuongea hatimae waliweza kufika chini ya ngome kubwa.
Rose na Magdalena wote walimwangalia Roma kwa mshangao kutokana na jengo hilo lilivyokuwa kubwa , ilikuwa ni kama ngome za wafalme wa Ulaya wa enzi hizo.
Roma aliwashika wanawake hao wte wawili mikono na kisha aliruka nao wote kwa pamoja walikwenda kutua juu ya mlima katika mlango wa kuingilia katika jengo hilo .
Nje kabisa alionekana Ron ambaye alikuwa akisubiria, alikuwa amevalia suti ya rangi nyeusi na tai nyekundu , hakuwa peke yake, aliambatana na baadhi ya watu waliokuwa wakiishi katika visiwa vya wafu ambao wote kwa pamoja walikuwa wamepanga mstari kumsubiria Roma.
“Your Majesty Pluto , two beutifull ladies welcome home”Aliongea Ron kwa lugha ya kingereza na huku akiinamisha kichwa chake kwa heshima na wale wanaume na wanawake alioambatana nao pia waliinamisha vichwa kwa heshima.
Roma alimsogelea Ron na kisha alimpiga piga beganni na kisha akamalizia kusalimiana na kila moja aliekuwepo hapo , wote walikuwa wakimjua Roma hivyo salamu zilikuwa ni zile za kuulizana maendeleo yao.
Wanaume hao na wanawake walikuwa ni maninja na wanajeshi wastaafu wa kikosi cha New Zero na Sea Eagles.
Uhusiano wao ulikuwa upo zaidi katika damu walizomwanga wakati walipokuwa wakipambana pembeni ya Roma, ni uhusiano ambao haukuwa na meneno mengi ya kuuelezea kwani ulijitambulisha.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Rose na Magdalena kuona upande wa pili wa kivuli cha Roma kwa ukaribu zaidi , wanaume waliokuwa mbele yao licha ya kwamba walionekana kuwa wakarimu kwao lakini bado walitoa aura ambayo ilionyesha wamemwaga damu nyingi na kuwafanya washindwe kujua nini cha kusema zaidi ya kutoa tu mikono na kutabasamu.
Baada ya kuingia ndani kila mmoja alitafuta siti yake ya kuketi katika meza kubwa ya chakula na muda huo huo Vijakazi wa kizungu waliovalia sare maalumu waliweza kuandaa chakula.
Ron na wengine hawakuwa na wasiwasi sana na wanawake hao wawili ambao hwakuwa wakiwafahamu na waliweza kuongea nao kawaida jambo ambalo lilimfanya Rose na Magdalena kupata utulivu.
“Enyi wanawake wawili , nimewaleta wapishi wawili wakubwa mmoja ametokea Ufaransa na mwingine kutokea Tanzania kwa ajili ya kuwaandalia chakula, mnaweza kuwaagiza chochote mnachotaka”
“Asante sana Mr Ron, umewaza vizuri”Aliongea Magdalena.
“Msijali hapa hatuna watu wengi , hivyo tunakaribisha wageni kuungana na sisi , isitoshe nyie wote ni Wapenzi wa mfalme Pluto hivyo moja kwa moja mtapewa heshima yenu”Aliongea na kumfanya Magdalena kuona aibu kwani hakuwa kwenye hatua ya kuitwa mpenzi wa Roma , upande wa Rose yeye hakuona tatizo , lakini ndio hivyo kutokana na waembo hao kuambatana na Roma kwenye macho ya watu wa visiwa hivyo wangewachukuliwa kama michepuko yake.
Baada ya Ron na wezake kunywa nusu chupa ya mvinyo sauti zao sasa zilianza kupoteza ustaarabu na kuwa za juu na hali ile ilifanya eneo kuchamganka
Mwanaume aliekuwa na nywele nyingi kuzunguka mdomo wake aliefahamika kwa jina la Collejon , ni bwana mmoja ambaye ashawahi kuwa kiongozi wa kikosi cha The Eagles katika Ukanda wa Kaskazini mwa Ulaya, ashawahi pia kuishi kwa miaka mitano nchini Kenya na muda huo alikuwa tayari kwenye umri miaka sabini hivi.
Muda huo alikuwa ameshilikia Goblet(kikombe) rangi ya madini ya fedha(Silver) na baada ya kunywa kidogo alimwangalia Roma na kisha akaongea.
“Mfalme Pluto wiki ijayo ni ‘Caesar Conference’ kwanini usikae kwa muda na kuchukua familia yako kwenda kuwaangalia vijana?”Aliongea bwana aliefahamika kwa jina la Callejon.
“Caesar Conference? Ni kweli imepita miaka miine tayari ni wapi linafanyika mwaka huu?”Aliuliza Roma.
“Sio mbalisana ni upande wa pili nyumbani kwao Ron”Alijibu mwanaume mwngine mwembamba.
“Linafanyikia Visiwa vya Cicilly , naona Ron utakuwa bize , usije kuruhusu watu kusogelea hadhina yako?”Aliongea Roma kwa kutania.
“Sijahusika na maswala ya kifamilia kwa muda , nadhani niwaache tu wafanye wakavyo”Alijibu Ron
Rose hakuwa akielewa lugha waliokuwa wakiongea na alimwangalia Magdalena.
“Wanaongea kuhusu nini?”
“Wanaongea kwa lugha ya kiitaliano na kirusi, mimi najua kingereza, kifaransa na kispanishi”Aliongea Magdalena na Ron aliona warembo hao hawakuwa wakielewa chochotehivyo aliamua kuwatafsiria.
“Tunazungumzia kuhusu Caesar Conferenece”
“Ndio nini?”Aliuliza Rose.
“Baraza la Kaisari ni baraza linahusisha makudi ya kimasenari dunia nzima ambayo yanajiamini kuwa na uwezo wa kushindana , sababu ambayo imefanya baraza hili kuitwa Baraza la Kaisari ni kwasababu mwanzoni kabisa lilianzishwa katika kusherehekea mashujaa wa kirumi waliopambana chini ya utawala wa Kaisari, katika miaka ya hivi karibuni pia baraza hili linafahamika kwa jina la Mkusanyiko wa Masenali, imani yetu ni kwamba kama tunahitaji kupata tenda zaidi kutupatia hela itatupasa kuwa katika sehemu ya juu katika mashindano haya ,Baraza la Kaisari lilikuwa ni endelevu tokea enzi za zama zile na lilikuja kusitishwa wakati wa vita ya pili ya dunia kwasababu masenari wa kupindi hicho walikuwa na utajiri mkubwa lakini mara baada ya vita ya pili ya dunia lilianza kufanyika kila baada ya miaka miinne , ni tukio kubwa sana la siri na ukiachana na wateja wetu wakubwa duniani wanaoishiriki lakini pia baadhi ya mataifa makubwa hutuma wawakilishi ili kuangalia ni Masenari wapi wenye uwezo ambao wanaweza kuwachukua , hivyo kila kundi kubwa la Masenari lazima wajiunge la sivyo wataonekena wadhaifu”
Baraza la kaisari ni kusanyiko la siri ambalo hufanyika kila mara baada ya miaka minne ambalo huhusisha wanajeshi wa kukodi wa makundi maalumu binafsi ambao kwa lugha ya kingereza ndio huitwa Marcenary , mfano wa kundi la Marcenari ni Wagner Group na Sea Eagles na mengineyo.
Rose ambaye alikuwa ni wa ulimwengu wa kiza na Magdalena ambaye ni mwanajeshi wa kitengo maalumu cha taifa, wote kwa pamoja walivutiwa na kusanyiko hilo.
Walijiambia mapigano ya Masenari duniani kote? , huenda ni kitu kizuti kushuhudia kikifanyika.
‘Mr Ron nani ambaye alishinda katika baraza hilo miaka minne iliopita?”Aliuliza Rose kwa kingereza.
“Should be Sea Eagles right , aren’t they the strongest mercenary corps along with Red Storm?”Alijibu Magdalena akisema lazima watakuwa ni The Eagles , kwani wao ndio kundi la Masenari ambalo lina nguvu duniani pamoja na kundi la Dhoruba nyekundu.
Ron mara baada ya Magdalena kuongea hivyo alitingisha kichwa kuashiria kwamba sio kweli kwamba Sea Eagles na Red Storm ndio ambao walishinda kwenye baraza hilo la Kaisari.
NB: Red Sand Storm inamaanisha kundi la masenari la Dhoruba nyekundu, hili lipo chini ya Zeros organisation na Zeros organisation kiongozi wao mkuu ambaye ni kivuli ni Athena , ambaye siku zote huwakilishwa sana sana na taifa la Marekani tutaona mbele.






SEHEMU YA 560.
Magdalena na Rose waliangaliana mara baada ya kuona Ron akipingana na kauli zao , kwani wao wote waliamini kundi la Masenari ambalo lingeshinda katika pambano hilo ni The Eagles kutokana na sifa zake zilizotukuka.
“Ukweli ni kwamba licha ya The Eagles kuwa kundi namba moija la kimasenari au la pili ambalo ni bora lakini halijawahi kushinda zidi ya Masenari wanaoshindana katika Baraza la Kaisari”Aliongea Ron na kuwafanya Rose na Magdalena kujawa na shauku ya kutaka kujua ni kundi gani la Masenati ambalo limeshinda katika mashindano hayo kama sio The Eagles wala Dhoruba nyekundu.
“Mr Ron kwanini usituambie , unatuacha hewani , tuambie kuhusu hilo kundi ni lipi?”Aliuliza Rose kwa shauku kubwa na Roma mara baada ya kuona namna Rose alivyo ilibidi aingilie yeye mwenyewe.
“Ni kundi ambalo linatoka katika ukoo unaoitwa PS , lilikuwa kundi namba moja duniani kabla sijaja kumiliki The Eagles”Aliongea Roma.
“PS! , Inamaanisha nini?”
“Inamaanisha Cyclops , wametengenezwa na Mungu kama ilivyo kwa Titans , wanasifika kwa ujuzi wa kutengneeza siraha”Alijibu Ron. Na kisha akaendelea kuelezea.
“Ijapokuwa ukoo huo ni wa kushangaza sana na hakuna ambaye anajua makao makuu yao yako wapi lakini ni binadamu wa kawaida na sio Cyclops halisi , lakini hata hivyo kila mwanajeshi wao ana nguvu kubwa pamoja na miili mikubwa , ni wakatili mno na kuna muda baadhi ya watu wanashuku chanzo cha damu yao halisi kinatokana na nini , lakini mwisho wa siku haikushangaza sana kwani kuna makundi mengine ya siri kama vile Panther na Shaman ambayo wanachama wake wote wamezaliwa na uwezo wa ajabu ukijumlisha pia na kundi la wachawi kutoka Scotland la SIS ambao uwezo wao ni wa kurithi, hawa Ps kuna tajiri mmoja alitaka kuwakodi lakini aliishia kuuliwa yeye mwenyewe na pesa yake ikachukuliwa , licha ya kuwa na sifa mbaya lakini bado kila mashindano yanapofanyika wanaruhusiwa kushindana katika Baraza la kaisari , lakini hata hivyo hawafahamiki sana kwani sio wenye kujiweka wazi hivyo ni watu wachache sana wanaowafahamu”
“Aisee , inaonekana wanaogofya sana”Aliongea Rose na kisha akamgeukia Roma aliekuwa kimya akiwa bize na chakula.
“Hubby vipi kuhusu wewe , mwaka jana hukujiunga kwenye mashindano hayo , je wana nguvu kuliko wewe?”
“Unafikiria sana , siruhusiwi kuingia katika mashindano hayo na isitoshe siwezi kukodi Masenari na pia mimi nina uungu ndani yangu hivyo sheria zinanizuia kuhusika katia maswala ya kimataifa , wanaoshiriki katika mashindano hayo kwa upande wangu ni wanajeshi wabobevu wa The Eagles lakini hata hivyo Ps wanauwezo wa ajabu hivyo ni halali kwamba hawakuhaki kushika namba moja”
“Bahati nzuri ni kwamba katika Baraza hili hairuhusiwi kuua kwa makusudi “Aliongea Callejon huku akicheka.
“Mfalme Pluto unaonaje tukienda pamoja kuangalia mechi angalau hata moja jumatatu ijayo ,, nimesikia washiriki kutoka kikosi cha The Ealges wa mwaka huu wana ujuzi wa hali ya juu . kuna uwezekano wakawaangusha Ps awamu hii”Aliongea Callejon.
Roma hakuwa na tamaa ya kwenda kuangalia , kitu ambacho ameweza kukishuhudia miaka minne iliopita ni kwamba hao wanachama wa kundi la ps kama angewafananisha na majini basi wangekuwa katika levo ya mzunguko kamili kutokana na namna ambavyo walikuwa na miiili iliojengeka na nguvu za ajabu.
Hivyo alijua kabisa hata kama wanajeshi wake kuwa na uwezo mkubwa lakini hawawezi kuwashinda Ps.
Rose na Magdalena alikuwa wakimwangalia kwa namna ya kumtaka akubali kushiriki ili na wao waende wakaone kitu hiko kinavyofanyika katika ulimwngu wa underworld,.
Ndio Baraza la Kaisari halikuwa likisimamiwa na sheria za ulimwngu wa halali bali shetia zake zilikuwa ni zile zilizokuwa zikitumika katika ulimwngu wa wahalifu maarufu kama Undeworld.
“Mbona mnanniangalia hivyo , mnataka kwenda kuona?”Aliuliza Roma na wote kwa pamoja walitingisha vichwa vyao.
“Tunaweza kwenda , lakini siwezi kukaa hapa kwa wiki nzima , nyie mnaweza kubakia hapa kwanza na nitarudi wiki ijayo kuwasindikiza”Aliongea Roma , hakutaka kubakia hapo kwani angemfanya Edna kuwa na wivu.
Roma mara baada ya kuongea hivyo Magdalena na Rose walijawa na shauku kubwa na kuisubiria siku ifike kwa hamu zote.
Kwa mtu yoyote ambaye akisikia wanajeshi wakipigana ndani ya ulingo lazima awe na shauku ya kutaka kuhudhuria kwani tamaduni hizo ni kama zimeshsahaulika kwani zilifanyika katika miaka mingi iliopita.
Lakini ajabu ni kwamba bado tamaduni hizo zilikuwa zikifanyika ila kwa siri sana na hata wale watu wakubwa wanaoenda kushiriki kuangalia mapambanno hayo ni wale ambao wanapokea mialiko maalumu na wenye uhusiano wa moja kwa moja na ulinwengu wa kihalifu.
Unaweza ukashangaa na kuona labda Baraza hilo halikuwa na faida , lakini ukweli ni kwamba faida yake ni kubwa sana , ukisikia biashara ni matanganzo basi baraza hilo ni kama sehemu ya matanganzo kwani wanajeshi hao wa kukodi wangeonyesha ustadi wao wote ili kuweza kupata tenda.
Baada ya chakula Roma aliwatembeza Rose na Magdaleana katika vyumba vyote vilivyokuwa ndani ya ngome hio , baada ya kuona vyumba ni vingi na vyote vikiwa ni vya kulala ukijumlisha na tabia yake waliweza kupata kujua nia yake kama ilivyokuwa kwa Edna mara ya kwanza kufika hapo.
Roma aliwaonyesha baadhi ya vitu vyake vya thamani alivyokusanya na baadhi ya vifaa vya mazoezi na kisha akampa Ron baadhi ya maelekezo na kisha akaaga na kuondoka.
Ilikuwa ni mchana kabisa wakati ambao anafika Dar, alikuwa ametumia zaidi ya masaa matatu kwenda na kurudi.
Baada ya kufika nymbani , nyumba ilikuwa nyeupe kwani Sophia alikuwa ashasafiri kuelekea Dodoma ambako ndio makazi rasmi ya babu yake Afande Athuman.
Roma alifanya maamuzi ya haraka kuelekea ofisni na alitumia muda mchache sana kuendesha gari mpaka kufika kutokana na muda huo hakukuwa na foleni kubwa.
Baada ya kufika katika Floor ya kampuni yake ya habari alijikuta akishangaa kidogo kwani hali ya hewa kidogo ilionekana haikuwa sawa kama alivyozoea , ni kama vile kuna kitu kinaendelea.
Roma mara baada ya kuingia ofisni kwake aliweza kumuona Daudi aliekuwa akitembea huku na huko akiwa kama mtu ambaye amechangayikiwa na baada ya kumuona Roma alionekana kupata ahueni.
“Mkurugenzi hatimae umefika “
“Nini kinaendelea , kwanini kila mtu anaonekana kama kuna jambo baya ambalo limetokea?”
“Nilijua tu hutakuwa na taarifa , nimempigia simu Boss Edna muda si mrefu na ameniambia nikupe taarifa uende makao makuu kwa ajili ya kikao, nilikuwa nikikusubiri hapa”Aliongea
“Edna ananiita kwenye kikao?”Aliuliza Roma huku akikunja sura kwani ilikuwa ni mara chache sana Edna kumwita ofisini kwake kwa ajili ya kikao kwasababu hakupenda namna watu wanavyowaangalia kutokana na uhusiano wao.
Daudi palepale alimvuta Roma mpaka kwenye meza yake na kumwonyesha Monitor ya tarakishi kabla ya kumuonyesha magazeti na baadhi ya habari zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
“Angalia Mkurugezi hili jambo mpaka sasa linaelekea kuwa nje ya uwezo wetu”
Roma alijikuta sura yake ikikunjamana mara baada ya kuona kitu kinachozungumziwa .
“Sophia Achafua hali ya hewa , Wahi kwenye App Fasta”
“Mrembo na Malkia wa Mziki Sophia ni mchepuko wa kiongozi mkubwa wa kampuni anayomdhamini”
“Sophia Star wa kimataifa aonekana katika shule ya watoto ya Braeburn , Inawezekana akawa na mtoto kwa muda mrefu”
“CEO wa kampuni ya Vexto kudhalilishiwa, Msanii aliepo chini ya kampuni yake anatoka kimapenzi na mume wake”
“Mrembo wa kupindukia hatimae kila kitu kipowazi juu ya mtu anaetoka nae kimapenzi , aonekana kwenye picha za kimahaba na mwanaume”.
“Siri ya mafanikio ya Mrembo Sophia yafichuka , inasemekana anatoka kimapenzi na bosi wa kampuni ilioendesha mashindano ya Kizazi nyota”
Vilikuwa ni vichwa vya habari katika magazeti na baadhi ya chaneli za mitandaoni za habari , zikimzungumzia Sophia huku mwanadada kutoka Marekani , Mtanzania mbea wa taifa akilivalia sana swala hilo njuga.
Katika baadhi ya picha zilizoambatanishwa katika habari hizo ni wakati ambao Roma alimvalisha Sophia kofia baada ya kujisahau na kuivua wakati wakimpigia makofi Lanlan mara baada ya kumaliza kucheza na kuimba na kundi la watoto wenzake.
Zilikuwa ni picha shawishi kuamini watu ambao wapo kwenye hizo picha kuwa katika mahusiano , kwani Roma alikuwa kwenye tabasamu na Sophia vilevile alikuwa kwenye tabasamu.
Huenda Paparazi aliechukua picha hizo alifanya makusudi kwani kabla ya tukio la Sophia kujisahau na kutoa miwani na kofia yake , Edna alikuwa ndio kwanza ameondoka kwenda mbele kwa ajili ya kumpiga Lanlan picha.
Roma mikono yake ilianza kumtetemeka mno kwa hasira na kidogo tu avunje meza.
“Uzushi , Uzushi, nani ambaye amevujisha huu uzushi mitandaoni , je wanakitafuta kifo?”Aliongea kwa hasira.
Ilikuwa bora kama wangemuhusisha yeye mwenyewe , lakini kitendo cha kumuingiza Edna katika jambo hilo kilimuuzi sana na kumfanya Sophia aonekane kama malaya.
Hakuwahi kudhania kama kuna mtu ambaye anaweza kuwachukua picha kwa muda mfupi sana ambao Edna aliwaacha na alijilaumu kwa kufanya kosa la namna hio kwa kutokuwa makini.
“Director hata mimi nakuamini”
“Daah , nitawaua hao wapuuzi ambao hawatuamini”
“Director punguza jazba , hatuwezi kutatua hili tatizo kwa namna hio ,nilituma mtu kuulizia ni Paparazi gani aliwezesha kuchukua hizio picha na kuzisambaza mtandani lakini hatukupata maelezo ya kutosha , lakini taarifa ya watu walioanza kuisambaza ni kwamba zilipigwa na watu kutumia simu kwa siri na kisha wakaziuza kwa mwanadada mmoja anaefahamika kwa jina la Kimambi na kuzisambaza, tuna uhusiano wa karibu na baadhi ya vituo vikubwa vya habari hivyo hawajaripoti mpaka sasa hivi na wanaosambaza ni baadhi ya chaneli za mitandaoni na baadhi ya Blog, kwasasa kinachopaswa kufanyika ni kuanglaia namna gani tunaweza kulisafisha jina la Sophia pamoja na Boss Edna”
“Okey nitaenda makao makuu kwasasa kwa ajili ya kikao , fanya chochote kinachowezekana ili tuweze kudhibiti hio hali , pia jaribu kuchimba ili kujua chanzo cha picha hizo ni kutoka kwa nani , ninataka niwafahamishe hao wajinga kwamba wamechokoza mtu ambaye hawakupaswa kuchokoza”Aliongea Roma kibabe.
Dakika chache tu Roma aliweza kufika katika ofisi ya Ednam, alimkuta akiongea na simu,
“Mh..Sawa , asante sana mama .. nipo sawa”Aliongea Edna na kisha akakata simu na kumwangalia Roma.
“Umemuomba mama msaada?”Aliuliza Roma mara baada ya kusikia Edna anataja jina la Mama.
“Ndio sina koneksheni kubwa na viongozi , mama ana njia zake ndio maana nikaona nijaribu kumuomba msaada”Aliongea Edna na Roma hakuona ni jambo baya , ilikuwa sahihi kumuomba msaada mama yake kwani alikuwa na koneksheni zake licha ya kwamba sio mke wa raisi wa Kenya tena, lakini kupitia familia yake nchini Tanzania ilikuwa rahisi kuomba msaada.
Asichokijua Roma ni kwamba mama yake alikuwa na mahusiano mazuri tu na baba yake mzazi ambaye ni raisi wa Tanzania na ashaanza ya kumfanya Raisi Senga kumtambua Roma kama mwanae na maendeleo yaliridhisha.
“Edna sijategemea hili kutokea , ni kosa langu sikuwa makini , sikuweza kuhisia kuna mtu ambaye anatupiga picha”Aliongea Roma
“Hatuna haja ya kulaumiana nani anakosa , kwasasa tunapaswa kutafuta namna ya kumsaidia Sophia kwani anasingiziwa kitu ambacho hajafanya, bado ni mdogo na hajui mambo mengi , sijui kama anaweza kuvumilia”Aliongea Edna huku akianza kutokwa na machozi
“Nilikuwa na wasiwasi ulimwengu wa kistaa utakuwa mgumu kwake na nilianzisha kampuni kwa ajili ya kumlinda lakini licha ya hivyo bado tu hili limeweza kutokea , haya yote ni kwasababu ya miimi kumuomba twende nae kule shuleni”
“Usiongee hivyo , ulikuwa na nia nzuri tu ya kutomfanya kujisikia vibaya akibaki mwenyewe nyumbani na isitoshe Sophia anafurahia kazi yake hivyo usijipe lawama , Je umewasiliana na walimu wa shulenni kwa Lanlan , maana waandishi wa habari lazima watawatafuta na kuwahoji”
“Nimempa kazi hio Benadetha kushughulika nayo , yupo vizuri sana kwenye maswala ya kijamii kama haya , tatizo kubwa ni kwmaba kuna vituo vingi vya habari mitandaoni ambavyo vinavumisha sana hili swala na inakuwa ngumu kudili nao mmoja mmoja , kama hili litaendelea tunafanyaje?”
Aliuliza lakini Roma alikosa jibu kwani hakuwahi kushughulika na maswala ya aina hio.
Muda huo huo wakati wakifikiria cha kufanya sauti ya Recho ilisikika ikijaribu kumzuia mtu kuingia ofisini kwa Edna na palepale mlango ulifunguliwa na kumfanya Roma kukunja sura.
Aliengia hapo ndani alikuwa ni Balozi Ramadhani baba yake Sophia na ilimshangaza Roma kumuona Mzee huyo kuwepo nchini.
Balozi alionekana kuwa katika kukasirika mno, huenda habari ya uvumi unaosambaa mtandaoni umemkasirisha sana kama mzazi.
“Edna nipo hapa kuhitaji majibu tu , nini kinachoendelea?”aliongea kibabe pasipo hata kujali kusalimia.
“Balozi najua mimi ndio niliemruhusu Sophia kufanya kazi za kisanii ambazo zimemfanya kuwa maarufu, kosa hili nusu limesababishwa na mimi hivyo nitafanya juu chini kusafisha jina lake”Aliongea Edna.
“Niambieni mnapanga vipi kusafisha jina lake , huu uzushi unasambaa kwa haraka sana lakini sioni hatua yoyote mnayofanya , kila mmoja anamuongelea vibaya , nyie ndio mmemfanya mwanangu kuwa maarufu hivyo mlipaswa kuchukua tahadhari mapema …..” Roma na Edna ilikuwa mara yao ya kwanza kumuona Balozi amekasirika hivyo , huenda ni kwasababu ya kumpenda sana binti yake maana alifoka na kuanza kumsingizia Edna kuwa yeye ndio kafanya mchezo huo kwa kuogopa Sophia kumpokonya mume , ilibidi Roma achukue hatua ya kumtuliza.
Muda huo huo wakati wakiendelea kuzozana kati ya Balozi , Edna na Roma aliongezeka mtu mwingine katika ofisi hio , alikuwa ni mlinzi wa Afande Athumanni afahamikae kwa jina la Faridi na ilimshangaza Roma kumuona hapo.
“Balozi nadhani hili swala sio la kumlaumu Mr Roma na Edna , tunapaswa kuelekea Dodoma , unapaswa kuwa karibu na binti yako”Aliongea Farid.
Balozi alionekana kuheshimu pendekezo ambalo limetolewa na mlinzi wa mzee Athumani na alituliza jazba yake na kuwahimiza Roma na Edna kutafuta ufumbuzi mapema.
Kwa jinsi alivyokuwa amebadilika utadhani sio yule ambaye alikuwa akimlazimisha Roma kumuoa binti yake kwa lazima, alionyesha hali ya kukasirika na hata ule woga wa kumuogopa Roma hakuwa nao tena.
“Farid ,Asante kwa msaada wako wa siku ile nilifanikiwa kumuokoa Edna kwasababu yako”Aliongea Roma akimshukuru mlinzi wa mzee Athumani.
“Msaada wangu!? , unamaanisha nini?”Aliuliza yule mlinzi kwa mshangao akionyesha hajui Roma anachomaanisha.
“Ni kuhusiana na mshipi wa kichawi , ulikuja nyumbani na kunipatia taarifa nikamsaidie Edna”Aliongea Roma na kumfanya yule bwana kushangaa na kukunja sura kwa wakati mmoja.
“Umenifananisha nilikuwa Japan kwa muda mrefu sana na tumerudi hivi majuzi , nadhani unapaswa kuelewa sasa hivi nimekuwa Bodigadi wa Balozi, nahusika vipi na mshipi wa kichawi?”Aliuliza na kumfanya Roma kushangaa na kujiuliza kama sio yeye yule aliekuja kumpa taarifa alikuwa nani.
Roma hapo hapo baada ya kumchunguza Farid aligundua alikutana na wat wawili tofauti , yule aliekutana nae alikuwa akitoa Aura inayofanana na maninja wa kundi la Yamaguchi lakini Faridi huyu alikuwa na mafunzo ya Kung Fu tu na hakuwa amebadilika kwani hata kipindi alipokutana nae mara ya kwanza alikuwa hivyo hivyo.
Roma alijikuta akijipiga kichwa kwa kutoweza kutilia mashaka jambo hilo , lakini swali liliibuka kama sio Faridi yule ni nani, alin’gata meno kwa hasira kwa kuona kuna mtu alimchezea hata kama alimsaidia.
ITAENDELEA
 
Binafsi nimesoma riwaya nyingi sana na mm ni mlevi wa kusoma, labda niseme tu kitu Singanojr ni kipaji kikubwa sana, sijazuia maoni ya mtu mwingine juu yake, akiendeleza moto huu kwenye story zingine tano namuona mbali mno, keep it up bro
huyu jamaa mimi nilishamvulia kofia story ni ya kutengeneza lakini kuna mambo yapo kweli kabisa unakuta yaliwahi kutokea hata nawaza singano amejuaje aliwaza nini kabla ya kutunga story nabaki nimeshangaa tu aisee.
 
Singano kile kizungu kule kwenye group hebu tutafsilie jamaa yangu,tuma na yakiswahili
 
Back
Top Bottom