Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 497.
NORTH POLE(NCHA YA KASKAZINI).
Ni katika maabara ambayo ipo ndani ya Manuari katika ncha ya kaskazini ya dunia ,alionekana Lekcha ambaye amevalia koti zito rangi nyeupe ambalo liliziba hadi miguu yake , lilikuwa ni koti maalumu la kimaabara na alikuwa amekaa kwenye kirefu kinachozunguka kwa mtindo wa kuchanua miguu.
Kwa jinsi ambavyo alikuwa akionekana ni ngumu sana kumtambua kama ni yule Lekcha aliekuwa Tanzania akijifanyisha kuwa muokota makopo.
Macho yake yote yalikuwa yapo kwenye skrini kubwa iliokuwa mbele yake huku vidole vyake akivichezesha kwenye batani ambazo zilikuwa ni za kupangusha , Data mbalimbali zilionekana kupanda na kushuka kwenye Skrini na kila alipokuwa akigusa kitufe cha Enter kanuni za kikemia zilizoungana ungana ungana zilionekana zikizunguka.
Taarifa zilizokuwa mbele yake zilikuwa ni za juu sana katika maswala ya kisayansi na tehama , ni taarifa ambazo nyingine zilionekana ni gunduzi ambazo hazijawekwa hadharani bado.
Kwa muonekano wake ni kama vile alikuwa mbele ya muda kwani vitu ambavyo alikuwa akifanya vilikuwa vikipita uwezo wa binadamu wa kawaida kufikiria.
Aliendelea kuchezesha vidole vyake kwenye touch on screen keyboard kwa haraka haraka sana huku akijilamba lamba lipsi zake na baada ya kumaliza alifumba macho na kisha akavuta pumzi nyingi na kuzishusha kisha akagusa batani ya Enter kwa mara nyingine na akafumbua macho yake na alivyoangalia kwenye Skrini macho yake yalichanua huku akionyesha msisimko wa furaha.
“That’s right … That’s right …mmm , yes you don’t say , You may be dead but I must say , you’re fucking genius”Aliongea huku akionyesha mshangao , alikuwa akimaanisha anaweza kusema Yan Buwen amekufa lakini amekubali ana uwezo mkubwa wa akili..
Muda huo mkao wake ulikuwa ni wa kuchanua miguuu na kwa mtu ambaye yupo nyuma yake asingeweza kugundua kuna mtu mwingine ndani ya eneo hilo.
Wakati Lekcha akiwa bize kutumia ubongo wake kuchambua data za kitaarifa alizoacha Yan Buwen upande wa kizwe alikuwa amejichimbia chini ya kiti alichokalia Lekcha akiwa ameshikilia rungu ya Lekcha na kuendelea kuipa joto la mdomo, alionekana alikuwa akimbusti Lekcha.
Sasa baada ya kusikia Lekcha anaongea yeye mwenyewe ndio ilimfanya Kizwe kuamsha kichwa na kumwangalia usoni kutaka kujua nini kimempa msisimko wa furaha.
“What is it!, A break through discovery?”Aliuliza akimaanisha kwamba ameweza kugundua kitu.
“Nishati ya Ant- matter ina matumizi mengi kiasi ambacho sikuweza kudhania”Alimjibu huku akiachia tabasamu lililojaa kebehi ndani yake na hilo ndio jibu pekee ambalo amempatia Kizwe.
Muda huo huo wakati wakiongeleshana, mlango wa kuingilia eneo hilo la maabara ulifunguliwa na alionekana Desmond ambaye amevalia jaketi la rangi nyeusi maarufu kama Black windbreaker huku akiwa na mwokano ambao haukuonyesha kujali kile kilichokuwa kikiendelea hapo ndani.
Alimwangalia mama yake aliepiga magoti katikati ya miguu ya Lekcha na kisha akatoa tabasamu la kejeli na kupotezea kile kinachofanyika.
“Roma is about to leave Tanzania”Aliongea akimaanisha kwamba Roma anakaribia kuondoka Tanzania.
Baada ya Kizwe kusikia sauti ya Desmond alisimama na kisha alichukua gauni lake na kulivaa bila wasiwasi kwani muda wote huo aliokuwa akifanya kazi alikuwa hana nguo yoyote mwilini na wala hakuona shida.
Yan Buwen aliweza kufanikisha kufufua mwili wa Kizwe lakini alionyesha kuna kitu alishindwa kukirudisha upya , Kizwe alipoteza ule utu na hisia zote kama mzazi na hata Desmond licha ya kumfahamu kama mtoto wake lakini alimchukulia kama msela na kwa Desmond hivyo hivyo alimuona mwanamke huyo sio mama yake kabisa kwani mabadiliko hayakuwa tu kimwonekano bali mpaka kitabia.
“Taarifa ilionifikia inaonyesha anatoka Tanzania kwa ndege ya kawaida kwenda Brisbane Australia”Aliongea Desmond mara baada ya Lekcha kumwangalia.
“Anatumia ndege?”Aliuliza hivyo akimaanisha kutokana na uwezo wake asingepaswa kutumia ndege zaidi ya kuteleport.
“Ndio na katika safari yake yupo na Mage Tobwe mtoto wa Kanali wa jeshi la Tanzania lakini pia ameambatana na msichana mwingine anaefahamika kwa jina la Rufi ambaye taarifa zake hazikupatikan”Aliongea .
“My , my he’s quite the gentlemen . As long as he is not coming to the North pole , I say we let him be”Aliongea akimaanisha kwamba kwasababu sio kwamba anakuja ncha ya kaskazini sehemu waliopo basi hawana budi kumuacha.
“Hauna shauku anaenda Australia kufanya nini?”
“Nina uhakika ni jambo ambalo halituhusu”Alijibu na kumfanya Kizwe ambaye ashamaliza kuvaa nguo zake kumgeukia Lekcha.
“Acha kuwa mjinga , kwanini tusitumie nafasi hii akiwa mbali kuwateka wanawake wake na kisha kumtishia nao”Aliongea Kizwe
“Unaongeea upumbavu. kama unaamini kuteka wanawake wake ndio kutaleta majibu ya unachokitafuta basi naweza kusema unajaribu kudharau uwezo wake au unataka kurudia makosa alioyafanya Yan Buwen , hukumbuki alivyoagiza watu wakamuue Queen, licha ya kwamba alikuwa mbali huko Ulaya aliweza kurudi kwa haraka na kuwaokoa”Aliongea.
“Tutaenda sisi wenyewe kuwakamata na sio hao Cyborgs, nina uhakika tunaweza kufanikisha hata kuteka wawili”Aliongea Kizwe na kumfanya Lekcha kutingisha kichwa kwa namna ya kusikitika.
“Mpaka sasa hatujui ni namna gani aliweza kumuua Yan Buwen , tunaweza kufanikisha kwenda Tanzania na kuwateka wanawake wake na kuwaua lakini Roma bado akawa hai ni kitendo hicho cha kujitakia kifo cha mapema”
“Kwahio unamaanisha tusifanye chochote?”
“Ndio maana yake, muda bado sana na hatuwezi kumshambulia, ngoja tujijenge zaidi na zaidi , Yan Buwen alikosea kwa kujiamini kupitiliza na hicho ndio kilimgharimu ,ijapokuwa alipanga namna ya kujirudisha hai lakini bado alikuwa amechelewa na kumfanya Roma aweze kugundua udhaifu wake wote , siraha pekee ambayo kwasasa tunaweza kuitumia kwa faida kwetu ni kwamba Roma bado hajui uwezo wetu halisi na nini tunamwandalia na kama tutaenda sasa hivi ni kama kujidhihirisha kwake na atachukua hatua ya kujihami”Baada ya kumaliza ngonjera zake aligeukia Skrini kwa mara nyingine huku akikagua data zinazoonekana.
“Kabla ya kuona haya maendeleo ya sayansi mawazo yangu yote yalikuwa ni kulipiza kisasi kwa yale alionifanyia mimi na baba yangu , lakini kwa sasa kisasi sio jambo tu ambalo linanifanya niwe hapa bali ni mipango yangu mikubwa zaidi zidi ya dunia, kama tukimuacha akiendelea kuwa hai ni hakika anaweza kunizuia nisifanikishe kileinachokiwazia…..
Kwa sasa tunapaswa kutulia kwanza bila ya kuchukua hatua na muda ambao tutafanya mashambulizi ni ya kummaliza moja kwa moja”Aliongea Lekcha kwa kujiamini alijiambia mwenyewe njia pekee ya kumshinda Roma sio kwenda kichwa kichwa bali ni kwa mahesabu makali sana , hakutaka kufanya makosa ambayo Yan Buwen alifanya na kubwa zaidi baada ya kushuhudia ukuu wa kile alichokuwa akifanya Yan Buwen hata yale mawazo ya kulipiza kisasi yalipotea na tamaa ya kitu kikubwa zaidi ilijijenga na alijiambis Roma kumkata mguu na kumuua na baba yake yaikuwa ni malipo ya kile ambacho ameweza kupata muda huo , hakutaka kuruhusu kisasi kichukue nafasi kwani ndio udhaifu mkubwa wa kushindwa na adui.
“Kuna watu wengi duniani ambao ni maadui zake na wanaandaa mipango ya kummaliza , Yan Buwen na yeye licha ya kuwa na nguvu kubwa lakini alifeli pia ,je unafikiri na sisi tutafanikiwa?”Aliuliza Desmond.
“Yan Buwen is nothing ,in the end he died in my hands , There is no room for failure .Only those who had thought a few steps ahead will receive the final victory”Aliongea huku akisimama kutoka kwenye kiti na alichokuwa akimaanisha ni kwamba Yan Buwen hakuwa kitu kwani mwishowe amekufa kwa mikono yake na kwake hakuna nafasi ya kufeli na watu ambao wapo mbele ya muda siku zote ndio washindi.
“Mpaka sasa nimeweza kuchimba kwa asilimia tisini na tisa kumbukumbu zake zote na kukusanya taarifa zinazohusiana na namna ya kulitumia jiwe la Kimungu na kwanzia sasa nitahakihisha narithi nguvu zake zote na kudhizibiti pamoja na kuboresha zaidi na Roma siku ambayo atakutana na mimi lazima aombe huruma yangu”Aliongea kwa kujigamba , chuki ambayo aliokuwa nayo Kizwe zidi ya Roma kusikia maneno ya Lekcha ilimfanya moyo wake kusuuzika mno.
“Kwahio unamaanisha tutarajie mambo makubwa zaidi?”
“Yap kwasasa tumuache kwanza afurahie maisha kwa kipindi kifupi huku sisi tukiendelea kumfatilia tukiwa gizani, niwahakikishe siku ambayo atakuja kuniona itakuwa ndio mwisho wa maisha yake”
“Natamani sana huo muda ufike”Aliongea Desmond na kisha akageuka kutaka kuondoka.
“Desmond unaondoka kweli?”Aliuliza Kizwe
“Sina cha kufanya hapa napaswa kurudi Rwanda”Aliongea na kumfanya Kizwe kumuonea huruma.
Baada ya mpango wao kufeli Denisi ndio ambaye alimfikisha hapo kwa ajili ya kufanyiwa matibabu ambayo yalichukua wiki moja na kiungo chake cha mwili kupona.
Tatizo la Desmond lilikuwa dogo sana , kama Yan Buwen alifanikisha kumponyesha Lekcha mguu wake mbovu kwa kucheza na DNA zake za mwili sembuse Desmond ambaye tududu yake ndogo iliolala.
Alichokifanya Lekcha mara baada ya Demsond kufikishwa hapo ni kumdunga sindano ya kiowevu cha teknonolojia ya Acceleration Growth ambayo ilivumbuliwa na kampuni ya Maya nchini Canada.
Teknolojia ambayo mara baada ya Yan Buwen kuipata aliongezea ubora zaidi kiasi kwamba ilifanya kazi ya kubadilisha seli za mwili zilizozeeka na kuweka mpya na ndiio maana Kizwe mwonekano wake ukabadilika na kuwa kijana zaidi na hiko ndio ambacho Desmond alifanyiwa zile seli ambazo Roma aliziua katika dushe yake zilibadishwa na kuwekewa mpya ambazo zilikuwa na nguvu zaidi.
Sasa kwasabab tayari alishapona na uanaume wake kurudi hakutaka kuendelea kuishi ndani ya hio Manuari akimwangalia mama yake mzazi akifanyana na Lekcha bila ya aibu.
Lakini hata hivyo hakuwa na majuto tena , alivyoletwa sio anavyoondoka na alijihisi kama mtu ambaye amezaliwa upya na msukumo wake wa kuishi ulikuwa ni ule wa kuona maadui zake wote wakifa mbele ya macho yake.
“Yeye na Denisi itawachukua muda mrefu sana kufanikisha kudhibiti nguvu ya jiwe la Kimungu kwa asilimia kubwa na nimeweza kugundua katika kumbukumbu za Yan Buwen kuna uwezekano wa kutengeneza jiwe lingine lenye robo ya nishati yote ambayo ipo kwenye jiwe halisi”Aliongea na kwa haraka haraka ilifanya kueleweka sasa kwamba Yan Buwen wakati alipokuwa Tanzania aliweza kutoa nguvu nusu yake na kutengeneza jiwe lingine.
Kwahio kwa lugha nyepesi Lekcha alibakiwa na jiwe ambalo lina nguvu nusu na ile ya Awali kabla Roma hajalipoteza.
“Kwahio unamaanisha.”
“Kikubwa kuhusu jiwe hili la kimungu ni nishati yake tu , kwa nje inaonekana kama vile ni jiwe lakini yote hio ni teknolojia ambayo imetumika kutrap(Kunasa) nishati ya ant-matter ndani yake ni teknolojia ambayo kama binadamu wakipata ufunuo basi huenda vichaa wanaweza kuwa wengi na ukawa mwisho wa dunia”Aliongea na kumfanya Kizwe kutabasamu .
“Kizwe wewe kazi yako kubwa ni kuniburudisha wakati nikijijenga ki uwezo na visasi vyako vyote nitalipa mimi”Aliongea
“I thought you were going to call me a bitch”
“Haha…in fact you are my favourite bitch..”Aliongea na palepale alimshika mkono na kumvutia kwake na kuanza kumpapasa na kadri muda ulivyososogea ndio miguno ya kimahaba ilivyozidi kutawala.
*******
Australia – Arnhem Land.
Licha ya kwamba haikuwa mwezi wa sita, mwezi wa baridi kali lakini katika ardhi ya bara mwa Arnhem hali ya hewa ilikuwa tofauti na maeneo mengi ya mwambao wa pwani.
Eneo lote lilikuwa likichukua zaidi ya kilomita za mraba elfu nane ,Arnhem hali yake ya hewa ilikuwa ni ile ya Ki’savanna na kipindi cha kiangazi jua lilikuwa likipiga kweli kweli na eneo kuwa na joto kali mno.
Ndio eneo la kale zaidi la kihistoria katika bara lote la Australia na ndio sehemu ambayo ilikuwa na maeneo mengi ambayo haya kusapoti maisha
Na watu wa asili wa Australia(Aboriginal) licha ya kuyakimbia maeneo mengi lakini kulikuwa na ushahidi mwingi wa kihistoria unaoturudisha nyuma zaidi ya miaka elfu hamsini iliopita.
Licha ya eneo hili kutokuwa na hali ya hewa ya kufanya watu kupendelea kuishi lakini bado watu walikuwepo , maendeleo ya viwanda ambayo yalifanywa na nchi ya Australia katika maeneo ya mijini yalifanya maeneo hayo kuwa ya kitalii zaidi ndani ya nchi na hilo lilifanya watu wale wa asili zaidi kuendelea kuishi katika hayo maeneo na kufurahia faida zinazotokana na wale wanaotembelea.
Ni kama hapa Tanzania ufananishe na makabila kama vile wamasai au Hadzabe ambao bado wanaishi kitamaduni na maeneo yake kufanya kuwa kivutiio basi ni kama ilivyo ndani ya eneo la Arnhem.
Ni eneo ambalo lilifaa kutembelea zaidi kuliko kuishi na mazingira yake hayakuwa ya kuvutia bali yalikuwa yakishangaza zaidi na ni hatarishi vilevile , ukiingia ndani ndani zaidi huko misituni kuna wanyama wengi wakali huishi huko.
Wakati baadhi ya watalii wakiendelea kushangaza macho yao chini , angani ilionekana ndege ndogo ya wastani , ni ndege ambayo ilikuwa chini ya Roma na kabla hajaanza safari yake kutoka Tanzani alikuwa ashatoa taarifa ya ndege hio kusafiri mpaka Brisbane kwani ndio ambayo ilitakiwa kuwachukuwa na kuwapeleka Arnhem Land.

“We’ve now entered the hinterlands, highland grassland , two hundred and seventy meters above sea level , the temperature on the ground is ninety-three Fahrenheit. The Plane now will begin its descend”Alisikika rubani akimaanisha kwamba washaingia upande wa bara, nyanda za juu nyikani, mita mia mbili na sabini kutoka usawa wa bahari , nyuzi joto 330 C(930F) katika ardhi na ndege itaanza kushuka.Baada ya kutoa ripoti hio alisubiria maelekezo kutoka kwa Roma.
Wakati huo kwenye kajichumba ndani ya ndege hio alionekana Mage ambaye miguu yake yote imezunguka kiuno cha Roma na kujifunga nyuma huku upande wa Roma akiwa amesimama akiwa anacheza boringo , kwa jinsi Mage alivyokuwa akionekana ni kama vile dunia ilikuwa ikimuadhibu.
Upande wa Rufi alikuwa peke yake na macho yake yote yalikuwa nje kuangalia mandhari na hakutaka kufuatilia kinachoendelea upande wa pili kwani kilimtia wivu na muwashwasha kama mwanamke.
Hata hivyo alijua nia ya Edna kumfanya Mage aambatane nao kwenye safari hio yote ilikuwa ni kumuweka Roma chini ya uangalizi ili kusitokee kitendo chaochote cha kufanyika matendo ya ki usaliti.
Roma mwenyewe aliondoka Tanzania akiwa hajamalizana na mke wake , alikuwa amemnunia lakini kwasababu safari ilishakaribia hakutaka kupoteza muda sana kumbembeleza kikubwa tu ni kwamba alishapatiwa ruhusa na ndio maana akaja na Mage.
Baada ya taarifa kutoka kwa Rubani ilibidi Roma aghailishe kile alichokuwa akifanya na kisha akatoka huko na kuja kuungana na Rufi.
Wote walikuwa wamevalia mavazi aina ya Camo, ni mavazi flani ya mchanganyiko wa rangi ambayo yanafanana na yale yanayovaliwa na wanajeshi.
Rubani aliwapa taarifa ili wajiandae kujirusha kwenda msituni kwani ndege hio isingekuwa na uwezo wa kutua chini , Mage alikuwa polisi lakini kwenye maisha yake hakuwahi kufikiria kama angekuja kujiusha kutoka kwenye ndge kwani waliofanya mara nyingi kama hivyo ni wanajeshi.
“Hatuwezi kumwambia Rubani aishushe ndege hadi chini”Aliongea kwa wasiwasi kiasi cha kujionea aibu maana alikuwa mwanajeshi halafu anashindwa hata na Rufi ambaye alionekana kutokuwa na wasiwasi.
“Haiwezekani ndege kutua, ardhi haijanyooka na chini kuna miti mirefu njia pekee salama ya kushuka ni kwa kutumia parashuti na nishaandaa kila kitu kwa ajjili ya kujirusha”Aliongea Roma
“Ndio maana Edna akanichagua kuja huku inaonekana hanipendi kabisa”Aliongea kwa kulalama na kumfanya Roma acheke.
“Nilishakuambia huku sio kwa ajili ya utalii bali ni kama kwenye mateso”Aliongea Roma huku akicheka ijapokuwa angepaa tu na kwenda kutua chini lakini kutokana na kumiss sana kuruka kutoka kwenye ndege kijeshi aliona afanye kama binadamu wa kawaida.
“Pilot open the hatch”Aliongea akimaanisha afungeu mlango mara baada ya kuhakikisha wote wapo tayari na palepale mlango wa ndege mkiani ulifunguka na kufanya upepo mwingi kuingia ndani na mabegi yao ndio yaliokuwa ya kwanza kushuka kwenda chini.
Safe trip Your Majesty Pluto”Sauti ya Rubani ilisikika ikimtakia safari njema na palepale Roma alimpa ishara Rufi aanze kuruka na bila ya wasiwasi alisogea na kisha akajirusha chini , hakuwa muoga na alikuwa na mchecheto mno.
Baada ya Rufi kuondoka Roma alimshika kiuno Mage vizuri na kisha alimsukuma mbele na wote wakadondoka kuelekewa chini.





SEHEMU YA 498.
Mage alifumba macho huku akisikilizia upepo na mapigo yake ya moyo kudunda kwa nguvu alikuja kuyafungua mara baada ya kuhisi walikuwa wakielea na upepo umepungua na alipoangalia Parashuti lilikuwa tayari lishajifungua.
“Bado unaogopa?”Aliuliza Roma kwa sauti kubwa kwani upepo ulikuwa mwingi na Mage aliangalia chini pasipo kujibu na kadri walivyokuwa wakishuka chini ndio miti ilivyozidi kuongezeka ukubwa na nyasi nyingi zilizokauka kuonekana vizuri zaidi.
Sekunde chache mbele waliweza kugusa ardhi na kumfanya Mage kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha.
Rufi alikuwa tayari alkwisha kutua umbali kiasi kutoka walipotua wao na alikuwa ameshika kiuno pasipo ya kuwa na habari na parashuti lake lililojibwaga kwenye nyasi.
“Ningejua ningekuja na Miwani ya jua sio kwa kuungua huku macho”Aliongea Rufi maana muda huo jua lilikuwa likipiga sio mchezo iikuwa kipindi cha Vuli lakini kulikuwa na jua kali.
Roma aliokota mabegi yao ambayo ndio yalianza kudondoka chini na kisha kila mmoja akampatia la kwake na begi lake tu ndio kiasi lilikuwa zito kwani alibeba chakula na Rufi na Mage wao walikuwa hawajaweka vitu ndani kwani walitegemea kuhifadhi vitu watakavyopata kwa ajili ya kutengeneza vidonge vya kijini.
Mage alihisi joto kali kwenye mwili wake kiasi kwamba ni kama hali ya hewa ilimkataa na alichokifanya ni kuruhusu nguvu zake za kijini kutawala mwili wake ili kupoza na Roma aligundua hilo.
“Jitahidi usitumie kiwango kikubwa cha nguvu zako zote kujipozesha maana haijulikani tutakaa kwa muda gani kwenye hili eneo kwani ni mpaka tupate tulivyokuja kutafuta”
Ukweli Roma alimkataza kutumia uwezo wake aliopata ili mwili wake upate mazoezi ya ziada katika safari hio ili asije kuwa mnyonge wakati atakapo ingia katika levo ya Mzunguko kamil.i
Baada ya kutoa baadhi ya maelekezo aliwaambiwa wamsubiri na alienda kukusanya parashuti la Rufi na kisha akalitandaza chini sehemu inayonekana vizuri kutoka juu angani na kuchukua mawe na mchanga na kulizuia ili upepo usije kulipeperusha.
“Roma unafanya nini?”Aliuliza Rufi
“Ni alama kwa ajili ya ndege endapo ikiwa ni wakati wakuondoka , lakini pia ni alama ya mwanzo watu na rahisisha mambo ili kama tukifuatwa basi iwe rahisi kuona hii alama”Aliongea Roma na kumfanya Rufi sasa kuelewa na hata Mage pia kuelewa
Hawakuwa na vifaa vyovyote vya mawasiliano kwani safari yenyewe haikuwa na maandalizi makubwa na Roma alijiambia hata kama wangebeba vifaa hivyo visingefanya kazi kwenye eneo hilo kwasababu ya mtandao lakini vilevile chaji isingedumu sana , hivyo simu walikuwa nazo lakini ni kama za kupigia picha.
“Tunaachukua uelekeo upi kutoka hapa?”Aliongea Mage mara baada ya kuangalia ardhi yote iliokuwa ikitanuka kwenda mbali ,sio nyuma wala mbele hakuona mwisho zaidi ya miti na miinuko na sauti ya ndege , eneo hilo lilikuwa kama mbuga kwa mwonekano wake ni kama vile walikuwa katikati ya Serengeti lakini utofauti mkubwa wa eneo hilo ni ule ukavu wake kwani nyasi nyingi zilikaushwa na jua na ilikuwa dhahiri mvua haikunyesha kwa kipindi kirefu.
“Hapa inabidi tuanze kwa kuelekea Kaskazini maeneo ya katikati, asilimia kubwa ya wenyeji wanaishi katika mwambao wa pwani na kama tutakosa huko katikati basi tunaweza kuchukulia kama utalii tu”
“Ah.. unaitaje utalii na jua lote hili , haya ni zaidi ya mateso”Aliongea Mage alikuwa mtoto wa kishua ambaye maisha yake yote alizoea kukaa kwenye kiyoyozi hivyo kukumbana na joto la namna hio ni kama vile yupo jijini Dar, kwake ni zaidi ya mateso.Roma alimshika shavu na kisha akamsukuma mbele atangulie.
Matendo yao yalimfanya Rufi kuona wivu kwani walikuwa wakionyesheana mapenzi waziwazi bila hata ya kujali uwepo wake ,mbaya zaidi Rufi hakuwa amezoeana sana na Mage na mara nyingi waliongea lugha ya kiswahili ambayo hakuwa hata akiifahamu vizuri.
Walianza kutembea huku jua la mchana wa saa tisa likiwachakaza vibaya na kumfanya Mage kuanza kujutia kukubali kuja eneo hilo kwani alihisi kama vile alikuwa kwenye jangwa , kila alipokuwa akitembea kidogo alikunywa maji ili kujipoza .
Rufi na yeye aliishia kufuta jasho na mkono wake tu huku macho yake yote yakiwa ardhini kutafuta mimea ambayo ingekuwa sahihi katika kutengenezea dawa hizo , umakini wake ulimfanya Roma kuvutiwa na aliona huenda alikuwa akijitahidi kufanya yote hayo ili kumsaidia apande levo na mwishowe aje kulipiza kisasi chake na kuwa huru.
Baada ya kutembea kwa umbali wa kama kilomita tatu waliweza kufika juu ya kijimlima na kujitupa kwenye kivuli kwa ajili ya kupumzika na Rufi na Mage walitoa maji na kunywa.
“Roma huna kiu m chukua unywe kidog?”Aliongea Mage.
“Nyie kunyweni tu na msione labda nahofia kuyamaliza mwili wangu ninaweza kuendesha na kumaliza kiu pale inaponitokea”Aliongea Roma kwa lugha ya kingereza ili Rufi asipate shida ya kutafsri.
“Kwa jinsi unavyoongea unafanya sasa nikuone kama sio binadamu”Aliweka maoni yake Rufi huku akitabasamu.
Mage alikuwa mzuri na alijaaliwa umbo lakini upande wa Rufi alikuwa na kasura ka upole sana na mwili kiportable na jinsi jua lilivyompiga na rangi yake ya mchangayiko aliiva kama yai la kisasa na kumfanya kupendeza zaidi.
Baada ya kupumzika kwa dakika kama kumi na tano Roma ndio aliekuwa wa kwanza kusimama.
“Tutembeeni zaidi kwenda mbele kufikia lile bonde naamini kuna mto , tutatafuta eneo la mbali kidogo kupumzika”
“Kwanini tusiende kupumzika karibu kabisa na mto?”
“Tishio kubwa la Arnhem ni uwepo wa Mamba wakubwa maarufu kama Baru , kuna zaidi ya Mamba laki moja wanaoishi mitoni wenye meno marefu na wanaweza kukumeza mzima mzima na usinekane hata ukucha”Aliongea Roma na kuwafanya miili yao kusisimka kwa ubaridi wa uoga na kumfanya Roma kutamani kuwachceka.
“Msiwe na waswasi nitakuwa wa kwanza kufahamu uwepo wa Mamba hata kilomita kadhaa, hatuwezi pia kupumzika karibu na mto kwasababu ya uwepo wa Scorpion na mbu wengi,”
“Australia ndio makazi ya zaidi ya aina ishirini na moja ya Nyoka wenye sumu kali, tokea tunaanza safari nililikuwa nikijitahidi kuwa makini hivyo na nyie pia mnapaswa kuangalia kulia na kushoto”Alitahadharisha Roma
“Roma kwanini unajua mambo mengi kuhusu hili eneo?”Aliuliza Rufi na kumfanya hata Mage mwenyewe ashangae. Na Roma aliishia kutabasamu.
“Nimekulia mazingira hatarishi zaidi ya hili eneo wakati nikiwa nafahamika kwa jina la Thirteen , nishawahi kukaa kwa siku therathini na moja peke yangu katika milima ya Siberrian hivyo ninaweza kusema likija swala la ku’survive’ mimi ni mjuzi na maisha yangu yamenifanya niweze kujifunza Flora na fauna (wanyama na mimea)ya maeneo mengi duniani kwa namna ya kukariri ili kujihami ninapokuwa kwenye maeneo hatarishi lakini pia kufahamu ni mmea upi napaswa kutumia kama chakula na ni mnyama gani napaswa kuwinda na vilevile ni tahadhari gani napaswa kuchukua.
Aliendelea kuwahadithia njia nzima huku wakitembea kulifuata bonde ambalo waliamini uwepo wa mto.
Baada ya kutembea sana hatimae walikaribia karibu zaidi na kweli waliweza kuona mto unaotiririsha maji kiasi.
Muda uleule Rufi macho yake yalichanua mara baada ya kuona kitu ambacho walikuwa wakitafuta na alimpita Roma kwa haraka kusogea mbele lakini Roma palepale kwa spidi alimvuta na kumrudisha nyuma.
Mage mara baada ya kuona kwanini Roma kafanya vile mwili wake ulimsisimka baada ya kuona bonge la Mamba aina ya Baru likiwasogelea.
Asante
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI:ISSAI SINGANO)SINGANOJR)

SEHEMU YA 499.
Roma alikuwa na uwezo wa kuwabeba wote na kurudi mjini kwa ajili ya kulala na tena asubuhi wakarudi kuendeleza utafutati , lakini kwa maelezo ya Rufi ni kwamba mimea mingi ya ajabu huwa inaonekana katika vipindi tofauti vya siku.
Kwa mfano kuna mimea ambayo ilikuwa ikionekana asubuhi asubuhi wakati jua likiwa linachomoza na kuna ile pia ambayo ilikuwa ikionekana usiku sana wakati wa mbalamwezi na kuna ambayo huonekana wakati wa jua linapozama.
Hivyo ili kuweza kufanikisha kupata aina yote ya mimea hio ya ajabu katika nyika hio ya Arnhem kwanza kabisa walipaswa kuwepo kwa vipindi vyote.
Sasa wakati wanafikia bonde karibu na mto tayari jua ndio linaelekea kuzama upande wa magharibi na ndio maana Rufi aliweza kuona mti ambao alishawahi kuona katika miliki za kijini.
Sasa ule mchecheto wa kukimbilia mbele ulimfanya asiwe makini na Roma ndipo alimposogelea na kumrudisha nyuma kwa haraka.
“Nishakuambia mtembee nyuma yangu muda wote”Aliongea Roma lakini Rufi bado hakuelewa nini ambacho Roma alikuwa akimaanisha lakini muda uleule majani yalianza kucheza cheza na sekunde mbele ndipo waliposikia mngurumo wa mnyama mkubwa akiwasogelea , alikuwa ni Mamba mkubwa mno akiwasogelea kwa kasi ya ajabu licha ya kuwa na mwili mkubwa.
Hali ile ilimfanya Mage kushikwa na ubaridi wa woga kwani ilikuwa mara yake ya kwanza kushuhudia Mamba mkubwa aina ya Baru , Rufi awamu hii alikosa ujasiri na kukimbilia kujificha nyuma ya Mage huku akitetemeka.
Roma aliacha limfikie na ile linataka kumtia meno miguuni aliachia nguvu ya kijini ambayo ilikuwa kama wimbi la upepo na kumbeba mzima mzima yule Mamba na kurudishwa nyuma kwa kasi na kwenda kutua kwenye mti kiasi kwamba ule mkia wake kupinda , lakini licha ya pigo lile bado hakupoteza maisha bali aliamka tena na kuamsha mashambulizi.
“Pumbavu huyu mnyama anaroho ngumu sana ,nilijua pigo moja lakawaida linaweza kumuua”Aliongea Roma huku akimwangalia yule Mamba akimsogelea kwa mara nyingine japo awamu hii hakuwa na kasi zaidi kuliko mwanzo na Roma hakutaka kulipa nafasi tena ya kumpotezea muda ali’chaneli nguvu nyingi zaidi na lilibebwa mzobemzobe na kwenda kujigonga kwenye tawi na lilipodondoka chini lilitingishika kidogo tu na kutulia likiacha meno yake wazi na Roma alitabasamu na kuanza kupiga mluzi kwa furaha.
“Unapata wapi ujasiri wa kupiga mluzi kwenye hali ya hatari kama hii?”Aliongea Mage kwa kulalamika.
“Nilitaka kwanza niwaonyeshe nini maana ya hatari kwenye hili eneo , nishawambia kuna zaidi ya Mamba laki moja hivyo mnapaswa kuwa makini na kila chanzo cha maji mnachokikaribia”
“Rufi kuna kitu uliona kwenye huo mti?”
“Ndio”
“Huu mti kama sijakosea ni aina ya Eucalyptus lakini majani yake yapo tofauti kidogo na pia magamba yake ni ya rangi ya zambarau”Aliongea Roma akiuelezea mti uliokuwa mbele yao”
“Hapana huu ni m’cardinal ni miti ambayo ni adimu sana ndani ya ulimwengu wa kijini na inatengenezea pia vidonge vya kijini vya gredi ya chini”Aliongea mti uliokuwa mbele yao ni miti flani kama ile ambayo hutumika sana kipindi cha Christmasi unaweza kuita Christmas tree.
“Unasema miti pia inaweza kutengeneza dawa , mbona itakuwa ngumu kubeba”
“Hii miti mbona ipo mingi sana Tanzania?”Aliuliza Mage.
“Mage hii miti inaweza ikawa kweli ipo Tanzania lakini haina sifa ya kutengeneza vidonge , kinachoufanya mti huu kuwa na ubora zaidi ya kule kwetu nyumbani ni kwamba huu upo kwenye eneo la kihistoria, hili eneo licha ya kuonekana kama nyika lakini lina historia pana za kimila”Alichokuwa akimaanisha Roma ni kwamba mazingira ya eneo mmea ulipo ndio inaamua uwezo wake , Arnhem ni eneo la kihisitoria ambalo matambiko mengi yalifanyika hivyo kuna kiwango kikubwa cha nguvu za kiroho.
“Rufi kwahio tunachukua majani yake au tunafanyaje?”
“Kwa huu hatuhitaji majani wala mizizi mikubwa bali unachukua manyoya ya mizizi ambayo ni nyuzi nyuzi ambazo hazijaenda chini sana ardhini”Aliongea na kumfanya Roma kuona kila kitu kinasheria zake lakini hata hivyo hakujali zaidi ya kufanya kama alivyoambiwa na kuanza kuchimba na kuchukua vinyuzi nyuzi vya mti huo.
Roma baada ya kupata mafanikio ya mwanzo alijikuta akipata tumaini ya kupata kitu kikubwa zaidi kwani ndio kwanza wamefika.
Siku hio ya kwanza hawakupata shida yoyote ya kusumbuliwa na mnyama na baada ya giza kuingia walitafuta pango ambalo waliona ni salama na kisha wakajaza upepo godoro(air matress) lao na kuupiga usingizi , Roma hakulala kuhakikisha kila mmoja anakuwa salama.
Asubuhi asubuhi kulivyokucha wakati wanataka kujiandaa kuamka kuwahi kutafuta miti inayoota jua Rufi aliweza kuona mmea flani unaotambaa chini na kujifunga funga funga kwa kamba , ni mmea ambao ulikuwa na tabia ya kuchanua usiku maua yake na ikipita asubuhi tu yale maua yananyauka na kudondoka(Dragon knot plant), Roma baada ya kupewa maelekezo hakutaka kujiuliza mara mbilimbili alikusanya kila kitu na kutupia kwenye mkoba .
Siku ya pili ilipita siku ya tatu waliendelea kuzunguka kilomita na kilomita kusaka mimea kwani mpaka kipindi hicho hawakuwa wamepata ile mimea ambayo ingeweza kutengeneza vidonge ya uwezo wa juu lakini licha ya hivyo bado alikuwa na mimea mingi.
Roma kwakuwa alikuwa na Pete ya kufungua anga la Sumeru aliitumia kutupia baadhi ili kupunguza uzito.
Siku ya nne ilipita na yenyewe kwa haraka, Mage na Rufi ni kama sasa washaanza kuzoea kulala vichakani kwani hawakumtegea Roma tena kutafuta mahali salama pakulala
Siku ya tano chakula kilikiwa kishaisha na kilichobaki maji tu, Roma alipendekeza asubuhi awaache hapo na kisha aende mjini kununua mahitaji na kurudi lakini Mage alipendekeza Roma atafute namna ya kuwasiliana na ndege waliokuja nayo kuwafuata ili kurudi mjini maana ashachoka kukaa polini kama ngedere..
Ni muda wa usiku wakati Roma akitaka kuyafumba macho yake ili kupumzisha ubongo mara alihisi msuguano wa hewa ukiongezeka kuzunguka eneo walilokuwepo kiasi cha kufanya mwili wake kusisimka na alisimama haraka kwa tahadhari.
Aliachia utashi wake kutawaliwa na nguvu ya kijini ili kuweza kutambua hatari iliokuwa ikimkaribia na palepale alipotea na kisha akaibukia mita kadhaa mbele.
“Wewe ni nani?”Aliuliza kwa sauti.
Rufi na Mage baada ya kuona Roma kaondoka kwa haraka na wao walitoka kwenye godoro na kusogea upande wake kujua nini kinaendelea.
Muda ule ule alitokea mtu kutoka angani mwenye nywele zake za njano ndefu mno kiasi ambacho sio cha kawaida alikuwa kama mzimu uliofufuka na nguo zake ziilikuwa za kitamaduni zaidi kama zile walizokuwa wakivaa warumi enzi hizo na sura yake haikuonekana kutokana na kuvaa Mask kama kinyago ya chuma(Cloack).
Roma alijikuta akikunja ngumi yake sio kwa hasira bali kwa hofu, hisia zake ni kama zilikuwa zikimwambia mtu ambaye yuko mbele yake ana nguvu kuliko za kwake.
“Who the hell are you?”Aliuliza kwa mara ya pili Roma kwa sauti ambayo ilisambaa kwa kasi kutokana na usiku.
“My identity is not important , the important thing is that you know that you’re no match against me”Aliongea akimaanisha kwamba ubini wake sio muhimu lakini jambo la muhimu ni yeye kuelewa kwamba hana uwezo wa kupambana nae.
Mage na Rufi walijikuta wakishikana kwa woga na kwa muda huo hawakuwa na chakufanya kwani hawakuwa na nguvu yoyote kusema kwamba wangeweza kumsaidia Roma , kitu pekee ambacho walikuwa nacho ni wasiwasi zidi yake.
“Nimeweza kukupata baada ya kukutafuta kwa siku tano mfululizo na nimepoteza muda mwingi sana , hivyo nitakupa chaguzi mbili ili tusipotezeane muda, chaguzi ya kwanza salimisha andiko la urejesho usio na kikomo kwa hiari yako, chaguzi ya pili nimimie mwili wako na kuutawala na kisha nichukue mwenyewe kwa lazima, chaguzi ya pili ni hatari zaidi kwani nitakuvua nguvu zako zote”Aliongea
Roma alikuwa amekasirika sio mchezo , kwenye maisha yake alikuwa akichukia sana uchokozi wa waziwazi na watu wenye kupenda majigambo , ijapokuwa mtu aliekuwa mbele yake alionekana huenda akawa na uwezo mkubwa kuliko wa kwake lakini siku zote hakuwa na hofu ya kupambana ni bora afe kwenye ulingo kuliko kukimbia.
Msuguano wa hewa ambao alisababisha yule mtu haukuwa wa kawaida kabisa na hili lilimfanya Roma kushindwa kujua anakwenda kupambana na mtu gani kwani hakutaka kujidhihirisha kwa kujitambulisha.
Roma alijiambia huenda angekuwa na uwezo wa kudhibiti radi kama alivyofanya mtu ambaye upo kwenye mwili wake angekuwa na uhakika wa kushinda.
Akiwa amekunja sura aliwageukia Rufi na Mage na kuwaangalia namna waliyyokuwa na wasiwasi ,
“Kimbieni kadri ya uwezo wenu wote muondoke hili eneo , sitokuwa na uwezo wa kuwalinda mkibakia hapa”Aliongea Roma na Mage alitaka kuongea neno lakini Rufi mara moja alishamwelewa Roma alichokuwa akimaanisha hivyo alimshika Mage mkono na kumvuta na wakaanza kukimbia kwenda mbele zaidi gizani, hawakujali tena kama kuna wanyama wakali au nyoka ambao wanaweza kuwadhuru.
Kadri walivyozidi kwenda mbali zaidi ilimfanya Roma kupata ahueni alijua kama wangebakia kwenye hilo eneo asingeweza kupambana na wakati huo huo akawa anatoa ulinzi.
Kitu kingine alijua lazima mtu aliekuwa mbele yake ametokea kati ya jamii za kichina za Hongmeng kwasababu alikuwa na uelewa na mbinu yake ya urejesho ya kimaandiko isiokuwa na kikomo , hivyo kwa haraka haraka alijiambia kama akiliamsha akashindwa pambano moja kwa moja angejaribu kutumia kanunzi za anga ili kuwashitua miungu wenzake waje kumsaidia kwani mtu huyo kuja mpaka Australia ilikuwa ni kuvunja vipengele vya kikanuni vilivyopo kwenye The gods treaty.
“Unajaribu kutumia kanuni za anga ili kuwataarifau wenzako?”Aliuliza yule mwanaume kwa lugha ya kingereza huku akionyesha utulivu wa hali ya juu na hilo tu lilimpa hofu Roma.
“Kama unapanga utumie mbinu hizo siwezi kukupa nafasi”Aliongea na palepale alianza kunung’unika kwa lugha isiokuwa ikieleweka na palepale Roma alihisi ubaridi wa hali ya juu mno ukimzunguka pande zote , alijitahidi kutumia akili yake kihisia ili kugundua ni mbinu gani imetumika na alipokuja kuigundua alijikuta akitoa macho.
“Dark Ice soul!!”
Roma alitoa mshangao mara baada ya kugundua mtu alievalia Mask mbele yake alikuwa akitumia mbinu ya Dark ice Soul , alikuwa akiitambua kutokana na kwamba katika maongezi yake na Zenzhei kabla ya kuanza safari kuelekea miliki za kijini, Dark Ice soul ni mbinu ambayo hutumiwa na wazee wa Hongmeng.
“Haha.. naona uko vizuri kwenye kuelewa kwa haraka , ndani ya huu mduara mbinu zako za anga hazifanyi kazi hivyo hakuna yoyote ambaye anaweza kuja kukusaidia”Aliongea kwa cheko la kebehi.
“Wewe ni sehemu ya wazee wa Hongmeng?”.
“Unauliza sana maswali , ninakupa nafasi ya mwisho jisalimishe kwangu na unipatie ninachotaka “
“Njoo uchukue kama una uwezo huo”Aliongea Roma kwa kiburi akimaanisha kwamba hakuwa tayari kujisalimisha.
“Very well , you asked for this”Aliongea akimaanisha kwamba vizuri sana kwa aliloomba.
Yule mwanaume baada ya kusema vile aliinua mikono yake kama vile wale waongoza kwaya kanisani wanavyofanya na aliipopandisha kwenda juu na kushusha chini na kisha alitoa tamko la kijini.
“Mvua nyota barafu , Mazingahombwe …!!!!”
Aliongea na palepale Roma aliona vitu kama vinyota vyota vilivyokuwa kwenye mfumo wa barafu vikiamka kutoka ardhini na kumsogelea kwa kasi.
Rufi na Mage waliokuwa mbali walichokishuhudia ni kama vile wanaona vimulimuli(firefly) wakitoa mwanga mweupe kwa kuamka kimakundi.
Roma mpaka hapo aliona kabisa mtu aliekuwa mbele yake kwanza kabisa hakuwa na hofu na kwa kumsoma kimawazo tu aligundua huenda anadhaau uwezo wake kwa kuona hana lolote la kumfanya hivyo njia ya pekee ambayo aliona ingemuokoa hapo ni kutumia kanuni za anga.
“Unseal , Space barrier!!!”
Aliongea kwa nguvu huku akichezesha vidole na palepale ulitokea mlipuko wa aina yake huku eneo alilosimama anga lake ni kama vile linacheza cheza na vile vinyota vyota vya barafu vilianza kukusanywa sehemu moja katika anga msambo(Pareller space).
Lakini yule mvaa Mask alitoa tabasamu la kejeli akimwangalia Roma alichokuwa akifanya na alishusha tena mikono yake kutoka juu kama anaimbisha kwaya na viliamka vinyota vingine vingi sana na kumvaa Roma na vilianza kutengenza nguvu ya mvutano ya kiasi kikubwa mpaka kumpelekea Roma kuhisi maumivu makali, ilikuwa ni kama vile nguvu zake zinafyonzwa na mwili wake kugeuka barafu.
Kwa staili hio alijua huenda mtu aliekuwa mbele yake alikuwa ashaipita tayari levo ya Dhiki na kufanikisha kuweza kudhibiti elementi za maji na moto katika dunia, ilikuwa levo ambayo Roma hakuwa amefikia licha ya kwamba wote walikuwa kwenye levo moja.
“Umekuwa na akili kutegemea zaidi kanuni za anga kuliko mbinu za kijini , ngoja nikuambie hufikii hata nusu ya uwezo wangu na sio wewe tu hata mtangulizi wako Hades hawezi hata kunisogelea”Aliongea na kumfanya ?Roma apandwe na hasira maradufu na palepale alibadili mbinu na kurudi kwenye mbinu za kijini na kuita moto wa njano na kufanya eneo lote kuwa na mwanga kama vile msitu unaungua huku akidhamiria kuyeyusha hali ya baridi iliokuwa imemzingira maana ilikuwa ikimkosesha pumzi.
Baada ya kuona zoezi la kwanza lilifanikiwa alitumia tena kanuni za anga na kisha akaunganisha na ule moto kuyeyusha vile vinyota ambavyo amekusanya katika anga msambo.
“Space Tremor!!!”
Aliongea kwa nguvu na anga lilianza kutetemeka kama vile ni nguo ilio loana inayotingishwa ili kukausha maji yake na vile vinyota vilirudi chini na palepale akaachia moto mkari ili kuviyeyusha na kilichosikika ni mlipuko mkubwa ambao ulimrudisha nyuma yeye mwenyewe huku akihisi maumivu ya kiwango kikubwa mno ilikuwa ni kama yule mtu alikuwa amemwekea mtego.
“Nishakuambia kanuni zako za anga hapa haziwezi kufanya kazi kwa ufanisi hata wa asilimia hamsini , jifunze kukubali kushindwa”Aliongea lakini Roma alikuwa na kiburi cha kuzaliwa hivyo hakuwa akikubali kama alishindwa na alianza kujikusanya upya lakini yule bwana aliona ni kama anapotezewa muda.
“Nitakupiga pigo moja lakini nitahakikisha hupotezi maisha kutokana na uhitaji wangu wa hilo andiko la urejesho, Ngoja kwanza ni kuonjeshe nguvu ya vipepeo wa kufikirika wa rangi ya pinki”
Roma mara baada ya kusikia anaandaliwa pigo hakutaka hilo litokee na alicho kifanya ni kukusanya uwezo wake wote ili kujitengenezea ngao kwani hakujua hata hao vipepeo wa rangi ya pinki ni nini na yule bwana aliona hilo na kisha akatoa cheko.
“Unachofanya hakitokusaidia?”Aliongea Roma na palepale kitu cha kwanza alihisi kitu kama upepo ulioambatana na harufu nzuri ya marashi yasioelezeka ukimpuliza lakini ghafla mbele yake hakumuona tena yule bwana bali alichoweza kuona mauza uza ya kundi kubwa la vipepeo wakimsogelea kwa kasi.
“Arghiiiiiii…”
Roma alijikuta akitoa kilio cha juu huku akijihisi mwili wake kutawaliwa na nguvu isiokuwa ikielezeka ambayo ni kama inaziba ufasaha wa mtiririko wa nguvu zake za mbingu na ardhi , hata nguvu ya andiko la urejesho ilionekana kufeli kudhibiti nguvu hio ya kichawi iliokuwa ikimtawala , alijihisi kama vile ni mgonjwa wa ugonwa ambao muda si mrefu ungemuua, Alijitahidi kudhibtii uwezo wake wa kufikiria lakini alishindwa na palepale alikosa mhimili na kudondoka chini.
Hata Mage aliekuwa mbali aliweza kuona Roma akishindwa na kudondoka mzima mizma , lilikuwa tukio la mara ya pili Roma akidhibitwa kwa staili ya ajabu , mara ya kwanza ni pale Yan Buwen alipomzimisha Roma na mara ya pili ndio hio ambayo ameweza kiona.
Rufi alimshikilia mkono Mage ili asifanye maamuzi ya kijinga na kumsogelea Roma , lakini alishindwa kuhimili uwezo wa Mage na alijikuta akimwachia huku yeye mwenyewe akikosa nguvu.
“Mage usiende utakufa”Aliongea kwa kingereza lakini Mage hakumsikiliza alitimua mbio kumsogelea Roma bila kujali hatari.
“Wanawake wako wanonekana kweli ni waadilifu , bado tu wanapata ujasiri wa kukufuata ili hali upo kwenye hatua za mwisho”Aliongea mara baada ya kuona Rufi na Mage wanarudi , Rufi alikuwa akimfukuzia Mage kumzuia asimsogelee Roma kwani ingekuwa ni hatari na Mage alikuwa akimkimbilia Romakwa kuona kwamba hawezi kumwangalia akifa bila ya kufanya kitu.
Roma alijitahidi kuamsha kinywa chake amwambie Mage asisogee lakini nguvu zilikuwa zikimwishia , alijitahidi kuita nguvu zake za kijini lakini uwezo huo ni kama hana kwani nguvu ya ajabu iliouvaa mwili wake ni kama vile ilizifunga.
“Mage nenda mbali usisogee…’Alijikakamua kwa mara ya mwisho kumzuia kwa kuongea.
“Acha kupoteza sauti yako , waage kabisa nikumalize nina mambo mengi ya kuhangaika nayo baada ya hapa, nakuahidi nitawaacha hai kwani kuua mwanamke asie na nguvu ni tusi kwangu , kubali kunipa ninachohitaji tumalizane au nichukue kwa nguvu”
Aliongea kwa dharau na palepale alitoka aliposimama na kumsogelea Roma kwa kasi huku akinuia kwenye Roho yake kumzimisha kabisa.
“BAM”
Ni kama vile kioo cha dirisha kinavyogongwa na bunduki au kupasuliwa ndio mlio uliosikika na palepale kilionekana kitu kama mshale ukimkosa kosa yule bwana mwenye Mask na kumfanya asimame kwa kiwewe asimsogelee Roma na ule ukuta wake aliotengeneza kumfanya Roma ashindwe kutumia kanuni za anga ulibomoka.
Lilikuwa ni pigo ambalo sio Roma ambaye amelifanya na alikuwa na mshangao ni nani ambaye amemsaidia lakini mtu mwenyewe hata hivyo hakuonekana , hata kwa yule bwana mwenye Mask alionekana kuwa kwenye mshangao vilevile kama Roma.
“Wewe ni nani , kama una uwezo mkubwa kuzidi wangu jionyeshe’Aliongea yule bwana mwenye Mask.
“Unajua kabisa huna uwezo wa kushindana na mimi na sitaki kukushambulia zaidi, kwanini usiachane na maigizo yako na ukatoweka kabla sijawaita miungu wengine”Sauti yenye mwangi ambayo haikueleweka ilikuwa ya mwanamke au mwanaume ilisikika na kumfanya yule bwana mwenye Mask kutetemeka ni dhahiri alikuwa aking’ata meno yake kwa hasira baada ya pambano lake kuingiliwa, alimwangalia Roma kwa hasira sana.
“Consider yourself Lucky”Aliongea akimaanisha ajichukulie mwenye bahati huku akimwangalia na hakuonekana kutaka kufanya shambulio lingine zaidi ya kupotea katika hilo eneo.
Na Roma ambae alikuwa amelala chini alianza kuhisi msuguano wa hewa ukipotea na hapo hapo alijua kabisa watakuwa washaondoka , yule bwana na mtu mwingine ambae alimpatia msaada kabla hajakutana na kifo chake.
Mage na Rufi baada ya kuona ameondoka walimkimbilia Roma na kumbeba na kumfanya aegamie huku akiwa kama vile ni mlevi aliepewa pombe za kienyeji(gongo) maana alikuwa akifumaba macho na kuyafumbua kama vile ni taa mbovu inayoungua.
“Ongea chochote Roma jamanii , nini kimekutokea?”Alianza kuongea huku akiangua kilio na kumfanya Roma ananyanyue mkono wake kivivu akitaka kumfuta machozi
“Usilie nipo sawa”Aliongea lakini Mage aliekuwa kwenye hofu aliudisha mkono wake chini.
“Uko hivi halafu unasema upo sawa , nini kimekupata unaniogopesha mwenzio”
Ijapokuwa ilikuwa mara ya pili kumuona Roma akidondoka mzima mzima na kuwa kwenye hali mbaya lakini hio ilikuwa ni kama mara ya kwanza kwake na ndio maana alikuwa hofu.
“Nadhani nimepuliziwa harufu ya sumu , sina nguvu yoyote na kichwa ni kizito mno nashindwa hata kuita nguvu zangu… , Daah nilijua kwenye maisha yangu hakuna sumu ambayo inaweza kunidhuru”Aliongea kwa mafadhaiko.na Rufi baada ya kusikia kauli yake alimsogelea ili kumkagua nini kimempata.
“Kuna mbinu yoyote ambayo alitaja wakati wa kukushambulia?”
“Ndio , amesema amesema ananionyesha Vipepeo wa kufikirika”
“Aaah.. Daah”Alimaka Rufi huku akisimama na kuziba mdomo kwa mshangao mkubwa na kumfanya Roma kukunja sura.
“Una ufahamu na hiko kitu?”Aliuliza lakini Rufi alishindwa kujibu kutokana na mshangao.






SEHEMU YA 500
NCHA YA KASKAZINI.
Ijapokuwa ilikuwa ni usiku nchini Australia upande wa Ncha ya kaskazini mwa dunia ilikuwa ni mchana wa saa sita lakini anga lilionekana kama saa kumi za alfajiri na nyota waliweza kuonekana angani kwa wepesi zaidi.
Eneo hilo kama ilivyokuwa Kusini mwa cha ya dunia ni aneo ambalo halikuwa likipata jua la kutosha na ndio maana muda wote kubakia sehemu yenye barafu nyingi na hata mchanga wake ulikuwa ni wa barafu na pale jua linapoonekana ni kama lile la asubuhi asubuhi ambalo linachomoza mara moja na kisha kupotea.
Katika mwinuko mmoja wa barafu(Iceberg) alionekana mtu ambaye alikuwa amesimama huku macho yake yote yakiangalia angani huku gauni lake la rangi nyeusi la malighafi ya halili liliishia kupulizwa na upepo kulia na kushoto kama ilivyokuwa kwa nwele zake.
Licha ya eneo hilo kuwa na ubaridi wa zaidi ya nyuzi joto hasi therathini lakini ngozi yake haikuonekana kuathirika sana na kufanya urembo wake usio tamithilika kuonekana vyema chini ya mwanga wa mbalamwezi
“Mwanamke huyo alionekana kuwa makini kufikiria jambo huku macho yake yote akiangalia angani kwa namna flani hivi kama kuna kitu ambacho alikuwa akiangalia kwa matamanio makubwa.
Muda huo huo nyuma yake alitua kutoka angani mwanaume alievalia Mask , alikuwa ni mwanaume yule yule aliekuwa akipambana na Roma Australia .
“That Hades boy is incompetent. Are you really sure he is the man in your prophecy?”
“Yule Hades mvulana hana uwezo kabisa , una uhakika ndio mwanaume ambaye yupo kwenye unabii wako?”Aliongea kwa sauti nzito akimwangalia yule mwanamke mrembo aliempa mgongo.
Athena hakugeuza sura yake kumwangalia yule mwanaume na aliendelea kuangalia juu angani kama vile mtu ambaye amekumbuka kitu flani ambacho kinamtia huzuni.
“He is not dead?”Sauti yake tamu ilisikika akiuliza kwamba je hajafa.
“Ni katoto kapuuzi sana, nilichokifanya ni kuonyesha theruthi moja tu ya mbinu zangu lakini tayari kashajikatia tamaa , nina uhakika hawezi kuwa tishio kwetu Hongmeng na hata ulipojitokeza kumsaidia alionyesha kupata ahueni kwani ni kama alishajua ndio mwisho wa maisha yake, Kwasasa ameumia lakini kutokana na nguvu ya andiko la Urejesho inawezekana hatokufa lakini sidhani kama atakuwa na uwezo tena”Aliongea huku akionekana kama mtu ambaye anajivunia kile alichomfanyia Roma.
“All is well as long as he is alive”Aliongea akimaanisha kwamba yote ni mema ilimradi tu hajafa na kisha akaendelea kuongea.
“There should be no errors in my prophecy , In the future some things need to be done to tweek the entire situation into reality”
“Hakuna makosa yoyote kwenye unabii wangu , siku za baadae baadhi ya vitu vinatakiwa kufanyika ili kufanya hali yote kuwa uhalisia”
“I’ve heard the king, saying that any failure to your prophecy are your own fault , Why can’t you just admit that you suck at prophecies”
“Nimesikia kutoka kwa mfalme akisema kufeli kwa unabii wako ni makosa yako mwenyewe, kwanini usikubali tu kuwa upo vibaya kwenye maswala ya kinabii”Aliongea
“Wewe mpumbavuu..!!!”Aliongea na palepale vitu vyote vilikuwa vikiwazunguka vilianza kucheza cheza kama vile ni boti iliyoeleela kwenye maji,
Mtikisiko wa ule mlima wa barafu ulianza kubomoka wote na kuwa unga unga wa barafu na yule bwana mwenye Mask baada ya kuona jambo hilo la kuogofya aliruka kurudi nyuma asijefukiwa na mchanga huo lakini palepale Athena alimfuata kwa spidi na kumkanyaga kifuani kwa kumuwekea mguu.
“Nimekosea madam , tafadhari naomba unisamehe”Alijitahidi kuongea kwani nguvu uliokuwa imembana haikuwa ya kawaida na ule ukijogoo wote ulitoweka.
Kwenye maisha yake hakuwahi kushuhudia uwezo halisi wa Athena na alijua fika akileta mchezo anaweza kuyeyushwa mara moja na ndio maana alijishusha mapema.
Kingine ilionekana saikolojia yake ya woga zidi ya Athena ilichukua nafasi yake na ndio maana alishindwa hata kujibu mashambulizi na kutulia kama kuku anaesubiria kuchinjwa , Athena aliemkanyaga alimwangalia kwa kejeli na macho yake ya kiini cha bluu lakini licha ya hivyo urembo wake ulidhihirika zaidi na zaidi.
“Know your place , Your King may not even stand chance against me and yet you are here spewing nonsense ? if this happen again next time I will make sure to turn you into dust”
“Ifahamu nafasi yako , mfalme wako anaweza asipate hata nafasi ya kushindana na mimi lakini bado upo hapa unaongea ujinga , hili likitokea tena nitahakikisha na kugeuza vumbi”Aliongea na kumuondolea mguu.
“Nilikuwa mjinga sana … sirudii tena … sirudii mimi”
Aliongea huku akipiga magoti haraka haraka na kupiga kichwa chake kwenye barafu na Athena aliachana nae na kisha akageuka na kuangalia upande wa pili kama kuna kitu anachokichunguza.
“Simama”Aliongea na bwana yule mwenye maski alisimama haraka kama mwanajeshi.
“Kazi yako kwanzia sasa ni kutafuta na kurekodi alama zote za kiuungu zilizoachwa na makabila yaliotambulika kama miungu ya enzi duniani kote kwa niaba yangu , kazi yako nyingine ni kuhakikisha unafatilia kinachofanyika ndani ya ile maabara nahitaji taarifa za kila siku juu ya maendeleo yao katika matumizi ya jiwe la kimungu na usije ukachukua hatua bila ya maagizo yangu”Aliongea na kumfanya yule mwanaume kutingisha kichwa.
Alichouwa akimaanisha Athena akisema alama za kiuungu ni kama zile ambazo zimeachwa na watu wa Sumeria , miungu ya Misri kama vile Odini na mingine mingi ambayo iliishi kikabila katika maeneo tofauti tofauti duniani kote , sasa haikueleweka kwanini alikuwa akitafuta hizo alama lakini huyi bwana mwenye mask alipewa kazi ya kuzitafuta na kuzirekodi kwa niaba ya Athena.
“Madam bado nimechanganyikiwa kidogo , ukiachana na wewe miungu wengine kama Poseidon na Apollo hawana uwezo wa kupambana na wazee wa Hongmeng pamoja na jamii nyingine zilizojificha , hilo pia sio kwao tu hata kwa Ares na Venus hawawezi hata kusimama kushindana na waliofikia levo ya Nafsi , kwanini umeweka juhudi zako zote kuelewa nguvu ya jiwe la kimungu ili kuwafufua ndugu zako ambao ni wa kawaida?, naamini hata kama waje kufufuka hawawezi kuwa na msaada kwako”Aliuliza na kumfanya Athena kutoa kicheko kikubwa kwa sekunde kadhaa na kisha akamgeukia na kumwangalia kama kituko.
“Unachotaka kumaanisha ni kwamba ukiachana na mimi na Zeus wengine wote hawana thamani si ndio?”Aliuliza na kumfanya yule bwana kutojibu swali lake.
Aliuliza kutokana na uelewa wake, kwani Hongmeng wote walikuwa wakimwogopa Athena tu na kama sio yeye huenda wangeshatoka kwenye miliki zao na kusambaa duniani kote na kuiba hadhina nyingi zenye thamani na hata Roma kwa muda huo angekuwa ashakufa muda na asingekuwepo kule Australia akitafuta malighafi.
“Kama unaamini uwezo wetu tuliokuwa nao ndio wa mwisho kabisa basi nikujibu umekosea , nitakuwa mkweli kwako , kwasasa tulichobakiwa nacho ni namna ya kutumia kanuni za anga pekee na ukiachana namna ambavyo napambana, mimi mwenyewe nimebakiwa na nusu ya uwezo wangu na wengine wote ambao ni dhaifu kuliko mimi na Zeus, uwezo wao ni chini ya asilimia ishirini”Aliongea na kumfanya yule mwanaume kurudi nyuma akionyesha mshangao.
“Unamaanisha?”
“Mbona unaonekana kama huamini?”Aliuliza Athena
“Sio hivyo madam … kama wewe umesema hivyo basi naamini ni kwel”Aliongea kwa hofu na kumfanya Athena kutabasamu.
“Huna haja ya kujilazimisha kuniamini nilichoongea , tokea siku ambayo tulikanyaga ardhi ya dunia nguvu zetu zilikuwa zikipungua kila siku mpaka kufikia hatua ambayo ni kama tunalingana na binadamu wakawaida”Aliongea huku akameza mate na kisha akaendelea.
“This is a humiliatition to us and this is where it hurts most , Not many are willing to bring that up, funnly the friars in Hongmeng had realy thought that we’re only truly capable of this”.
“Hili ni lenye kutudhalilisha na hili ndio linauma zaidi , sio wengi ambao wanapata ujasiri wa kuliongea wazi wazi lakini inachekesha kuona wafia mila(majini) wa Hongmeng wanafikiri uwezo wetu tuliokuwa nao ndio mwisho”Aliongea na kisha akapozi kidogo na kuendelea huku akigeuza uso wake na kuangalia juu angani.
“It won’t be long until I create the thing I desire most , Soon enouph the renaissance of the gods will take place”
“Haitochukua muda mrefu nitaenda kutengeneza kile kitu ninachokitamani sana , hivi punde tu mwamko wa miungu utaanza “Aliongea akiwa na sura yenye usiriasi na ni kama vile kuna watu aliokuwa akiwaongelesha angani kutokana na mwonekano wake.
“Hades kadri unavyopanda levo ndio nafasi ya unabii kutimia inakuwa kubwa , endelea na juhudi hizo hizo”Aliwaza Athena bila ya kueleweka alikuwa akimaanisha nini kusema Hades kadri anavyopanda levo ndio anavyozidi kuufanya unabii utimize lakini huenda ndio maana akamtengeneza yeye mwenyewe.
Sasa unachotakiwa kuelewa nikielezea Athena akitaja miungu anamaanisha watu wote waliotoka katika sayari nyingine na kuja duniani na ndio hao ambao anaelekeza kwamba muda si mrefu wataamka na kuchukua hatamu ya dunia.
Unafikiri atafanikiwa
********.
Huko Arnhem mambo hayakuwa mazuri sana kwa Roma kwani alikuwa bado akihangaika kuita nguvu zake za kijini lakini haziji kabisa , alikuwa ni kama binadamu wa kawaida tu.
Mage ambaye amekaa chini ya shina la mti alimwangalia huku akiwa na wasiwasi mwingi mno na kuomba Roma uwezo wake urudi , alijiambia kama akikosa uwezo wake wangefanya nini maana hawakuwa na kifaa chochote cha mawasiliano na kama wangeamua kutembea kurudi mjini ni zaidi ya kilomita na kilomita.
Rufi na yeye alikuwa kwenye wasiwasi akimwangalia Roma kwahali ya huzuni mno na alikosa kufanya chochote cha kumsaidia.
“Vipi bado imeshindikana?”Aliuliza Mage baada ya Roma kufumbua macho , alikuwa akijaribu kufanya tahajudi kuona angepata uwezo wa kuondoa nguvu ya sumu vipepeo iliokuwa kwenye mwili wake.
“Nimeshindwa kabisa kuita nguvu ya mbingu na ardhi , nahisi kama vile kiini cha uhifadhi wa nguvu zangu kufungwa , njia za mtiriko wa nishati ya mwili zinaonekana kusinyaa na mwili wangu umekuwa mdhaifu mno”Aliongea kwa huzuni.
“Kwahio unamaanisha kwamba umekuwa binadamu wa kawaida?”Aliuliza Rufi na kumfanya Roma amwangalie.
“Hii sumu ya vipepeo wa kufikirika ni kweli haiponi?”
“Mimi sijui , lakini nishawahi kusoma taarifa chache kuhusu maelezo yake na kwa ninavyojua ni sumu ambayo imetengenezwa na wadudu waliokuwepo enzi za kale sana jamii ya vipepeo ambao kwasasa wamepotea duniani , mtumiaji anachokifanya ni kuigeuza sumu hii na kuwa kama moshi wenye harufu ya kuvutia na pale unapovutiwa na harufu hio na kuivuta moja kwa moja inaenda kuleng neva za mwili na mtu aliekusudia uivute akiwa na nguvu kubwa za kijini basi moja kwa moja inaelekea katikati ya mwili sehemu ambayo ndio chanzo cha uwezo wako wote na kufunga moja kwa moja na ndio maana katika miliki za kijini sumu hii inatumika kutolea adhabu majini yanayo asi”
“Sio mbaya sana lakini , najihisi sasa hivi nimekuwa kama binadamu wa kawaida, hizi hisia sijawahi kuwa nazo kwenye maisha yangu”Aliongea huku akicheka.
“Unachekaje kwenye hali kama hio uliokuwa nayo , unachotakiwa kuelewa mpaka sasa upo sawa kwasababu ya mwili wako lakini kwa wengine huenda mpaka sasa wangekuwa wamepooza kabisa mwili”Kauli ya Rufi ilimfanya Mage atamani kulia na kumwonea huruma.
“Rufi kwahio unamaanisha hakuna namna yoyote ya kuiondoa mwili mwangu?”
“Katika nyaraka nilizosoma hakuna sehemu ilionyesha naman ya kuondoa , mpaka sasa naamini uliepambana nae alikuwa akikuogopa sana na ndio maana akaambua kutumia sumu kali kukudhibiti ,inaonekana hakutaka umzidi kwa namna yoyote”Aliongea na Roma aliona kauli ya Rufi ni sahihi , alijiambia kama sio mtu wa ajabu ambaye alitokea na kumsaidia basi hueda angeshakufa.
Aliamini kwa kufanywa binadamu wa kawaida basi muda sio mrefu mtu yule angerudi na kutaka nguvu yake ya andiko mbaya zaidi ni kwamba mtu yule hakuweza kumuona sura na alishindwa kuwa na uhakika kama alikuwa akitokea miliki za hongmeng au lah licha ya kuwa na uwezo ambao alielezewa na Zenzheu.
Hata hivyo Roma hakuwa kwenye nafasi ya kukata tamaa alijiambia lazima kuna namna ya kuondoa sumu hio mwilini na nguvu zake kurudi upya , alijiambia tena kama ni suluhisho linatakiwa kuwa la mapema , kwani alikuwa na maadui wengi.
Alifikiria na kujiambia kama atakosa msaada basi angewauliza hata Christen au Clark kujaribu mbinu za kawaida kumsaidia , hakutaka kukata tamaa ilihali tumaini bado lipo.
Roma aliwaangalia Rufi na Mage waliokuwa kwenye huzuni na Mage na Rufi wenyewe walimwangalia Roma na kushindwa kuongea lolote zaidi ya kukaa kimya katika hali hio ya giza.
“Kwasababu kwasasa hatuwezi kutatua tatizo langu , malengo yetu ya kwanza iwe ni kutoka humu nyikani , ningekuwa bado na uwezo wangu isingekuwa tatizo lakini kwasababu mambo yashabadilika haitokuwa rahisi kwani hatuna vifaa vya mawasiliao kusema tutaweza kuomba msaada lakini pia chakula ndio hiko kishaisha na hatuwezi kukaa chini kusubiria watu waje kututafuta , hapa inabidi safari yetu iwe ni kutembea kwa kulenga uelekeo ambao utatukutanisha na bahari kwa haraka labda tukiwa njiani tunaweza kukutana na mtu ambaye atatusaidia kurudi nyumbani, msiwe na wasiwasi kwani nina uzoefu wa haya maisha hivyo naamini tutatoka salama na mnisamehe kwa kuwaingiza kwenye jambo hili gumu , kwasasa hakuna namna bali safari yetu ya kujikomboa inakwenda kuwa ya mateso makubwa”
“Roma wewe…”Rufi alishindwa hata kuongea , ijapokuwa alifahamu fika alichongea ni kweli lakini kuwaambia wanakwenda kuteseka hakupenda lakini hata hivyo alifarijika kuona Roma hajakata tamaa.
“Kwanini unaniangalia kwa namna hio Mage, ngoja niwaambie kadri nitakavyokuwa naishi siwezi kukata tamaa kabisa, naamini tutaweza kupata suluhisho tu”Aliongea na kumfanya Mage kuguswa na maneno yake , huyo ndio mwanaume ambaye alikuwa akiomba katika maisha yake ajitokeze , mwanaume ambaye hayumbishwi na changamoto.
Kwa mwanamke anaweza kumpenda mwanaume ambaye ni wa kawaida ambaye hata hela hana lakini hawezi kumvumilia mwanaume ambaye hana malengo na muelekeo ambaye ana visirani pale mambo yanapokuwia magumu.
Muda huo wa Mage kujiwazia alijiambia hatokuwa mbaya pia kama atakufa na mpenzi wake akiwa hapo wamekumbatiana na ni muda wake muafaka kuteseka akiwa na mwanaume anaempenda huenda penzi lao likashamiri zaidi na zaidi.
“Mage acha kuniangalia kwa macho yako malegevu , mnaonanye mkarudi kulala kesho haitokuwa rahisi kwani tutatembea bila kupumzika kurudi pwani , naamini inaweza kutuchukua angalau siku tano mpaka kutoboa hivyo lazima tukusanye kila nguvu tuliokuwa nayo”
“Mhmh..!”Waliguna wote kwa kuambizana lakini waliishia kuitikia kwa vichwa vyao na kisha wakarudi eneo lao kwa ajili ya kulala.
Wakati wakiwa wamepotelea usingizini upande wa Roma hakutaka hata kulazimisha usingizi , licha ya kufikiria namna ya kurudisha uwezo wake kwa kuondoa sumu iliopo mwilini , lakini pia aikuwa na hofu kama adui yake akirudi.
Lakini licha ya mawazo mengi , alijiambia hana la kufanya kwa muda huo na ambalo lingetokea mbeleni ya safari basi hana budi kupambana kiume kuyaokoa maisha yake na ya warembo waliolala.
Unaonaje , ngoja lekcha ajue mwamba hana nguvu zozote uone
Tukutane kesho.

ITAENDELEA.
Asante
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA.
MTUNZI: SINGANOJR.

SEHEMU YA 501.

Siku iliofuata kila mmoja alibeba begi lake na safari ikaanza rasmi , kabla ya kuondoka Roma alibeba makaa ya kuni zilizoungua na kuweka kwenye begi lake na kumfanya Mage kushangazwa na jambo hilo.
“Hubby si utachoka sana , kwanini unabeba hayo makaa , tunaweza kutokuwa na chakula lakini kuwasha moto njiani ni rahisi kwani tuna kiberiti”..
Tokea waanze safari alikuwa hajazoea kumwita Roma mpenzi kutokana na Rufi lakini mara baada ya Roma kupoteza uwezo wkae alijikuta akishindwa kujizuia.
“Haya makaa sio kwa ajili ya kuwashia moto , huko tunakoelekea maji hayatokuwa salama na yamejaa minyoo na sumu na pia hatuna uwezo wa kuyachemsha hivyo njia pekee ni kuondoa sumu yake kwa kutumia mkaa nadhani ni bora zaidi kuliko kuugua njiani kwa kuumwa na matumbo”Alielezea Roma huku akitabasamu.
Roma hakuwa tayari kuona wanawake hao wanapatwa na shida yoyote njiani kwani ingekuwa ngumu sana kutoka kwenye msitu huo kwasababu mwili wake ulikuwa na sumu na asingeweza kuwasaidia pale watakapopatwa na ndio maana alikuwa akichukua kila tahadhari.
Mage hakuwa amelifikiria hilo, hivyo mara baada ya kuelewa hakuuliza tena swali hata hivyo alikuwa mgeni kwenye mambo mengi.
Roma ndio ambaye aliongoza njia huku wakichukua uelekeo wa Kaskazini aliamini ndio upande ambao ungekuwa karibu zaidi na bahari kuliko kurudi walikotoka mwanzo, jua lilishaanza kuunguza licha ya kwamba bado ilikuwa ni asubuhi na kadri walivyokuwa wakisonga mbele Roma alikuwa akichoka mno na kuhema kwa nguvu kama ilivyokuwa kwa Mage na Rufi tu.
Kiasi kidogo cha unyevu nvyevu uliokuwa ukidondoshwa na miti ya msitu huo ulimfanya kuelewa kwanini watu hawakupendelea kuishi kwenye hayo maeneo, ilikuwa ni hali ya kisauna mwanzo mwisho.
Mage na Rufi lipsi zao zilianza kupasuka pasuka kutokona na ukosefu wa maji pamoja na njaa lakini kwa wakati huo walikuwa na wasiwasi zaidi juu ya Roma kutokana na sumu iliokuwa ndani ya mwili wake.
Njia yote waliotembea hakukuwa na maji zaidi ya vichaka tu ambavyo vilikuwa vimekauka kutokaa na hali ya ukame na baada ya kutembea mita kadhaa hatimae waliweza kufika kwene eneo ambalo lilikuwa kama bwawa ambalo limeacha tope tu kwa juu na palepale Roma alikata tawi la mti na kufukua lile tope na ndani ya dakika chache tu maji yalianza kuonekana na kuwafanya waangaliane kwa mshangao.
“Mara nyingi ukikuta sehemu yenye mto au bwawa lililoacha tope kwa juu jua chini yake kuna maji ni kama nadharia lakini naona tumekuwa na bahati”Aliongea na kuwafanya wafurahi.
“Ngoja nikusaidie”Aliongea Mage akiruka upande wa pili na akaanza kumsaidia Roma kupanua shimo kwa kutumia mikono yao, Rufi alijikuta akishangazwa na jambo hilo lakini mara moja na yeye aliungana na wakaanza kutengeneza kijidumbwi ili maji yakusanyike sehemu moja.
“Haina haja ya kunisaidia ninaweza kufanya hivi mwenyewe”aliongea Roma mara baada ya kuona wanachafuka.
“Acha kujifanya mgumu na utuache tukusaidie au unajisikia vibaya kwasababu hauna uwezo wako?”
“Ah..! sijamaanisha hivyo”Aliongea huku akimwangalia na aligundua tayari Mage alishajichafua usoni.
“Babe ushajichafua tayari baada ya kujishika pua yako”Aliongea na kumfanya Mage kweli aone amejichagua baana alijifuta na mkono wakushoto akidhania ni msafi.
Roma alijikuta akiguswa na namna wanawake hao wanavyochakarika , ijapokuwa alichokuwa akifanya sio cha kutumia nguvu nyingi lakini ushirikiano wao ulimfanya kuona kweli ana watu sahihi.
Baada ya kutengeneza kidumbwi maji yalianza kutiririka kutoka pande zote na kujaa.
“Yashajaa tayari lakini tunayatoaje hapa na kuyasafisha kwani yana matope?”
“Hio kazi ngoja niifanye mimi wewe angalia tu”Aliongea Roma na kisha akachukua nguo safi kwenye begi na kuiingiza kwenye kile kidumbwi na kisha akakamua kwenye kontena na baada ya hapo alichukua ule mkaa aliobeba na ndani ya dakika chache tu maji yalionekana kuwa masafi kabisa kwa ajili ya kunywa.
Kitendo kile kiliwafanya Rufi na Mage kushangazwa na mbinu zake za kupambania kuishi kwenye hali ngumu kama hio, baada ya kunywa na kutosheka walijaza ya kutosha kwenye makopo yao na kisha safari ikaendelea.
“Kutokana na Roma kukosa uwezo wake alijitahidi kuwa makini sana na vichaka kabla ya kuwaruhusu kupita , lakini bahai nzuti hawakuweza kukutana na hatari yoyote.
Wakati inafika muda kama wa saa tisa Rufi alijikuta nguvu zikimwishia kutokana na njaa na alitembea kinyonge mno akiwa amechoka kutokana na kukosa mazoezi tofauti na Mage na Roma.
Ilibidi wasimame na kumwangalia alivyokuwa akihema kwa shida akiwa ameshikilia magoti na kuinamisha kichwa chini.
“Hubby nina njaa pia na tokea jana hatujala kitu chochote na tumetembea sana”Aliongea Mage na kumfanya hata Rufi kuona aibu maana alijua Mage ameongea hivyo kwa ajili ya kumsaidia.
Kutokana na changamoto walizopitia yale mawazo ya Mage kumuona Rfufi kama Vixen yaliisha kabisa , alijiambia kama alikuwa hivyo huenda siku ya jana asingemfukuzia wakati anajaribu kumsogelea Roma wakati wa hatari.
Roma alijikuta akitingisha kichwa , alikuwa ashasahau kuwa stamina zao sio imara hivyo hawawezi kuvumilia muda mrefu , hivyo kwa muda huo alipaswa kujua namna ya kupoza njaa yao.
Alijaribu kuzungusha macho kwenye msitu huo kuangalia kama anaweza kuona chochote cha kulika lakini hakuona kitu , lakini baada ya kuangalia kwa umakini mbele aliweza kuona mti ambayo ulikuwa una matunda juu yake.
“Nifuateni”Aliongea na kisha wakaanza kutembea kwenda mbele.
Baada ya kuufikia alijaribu kuangalia mizizi yake kwa kufukua kiasi ili kuuchunguza na kisha alioneana kuridhika na kuchuma baadhi ya matuda yaliokuwa juu yake.
“Huu ni mti wa matundwa mwitu , majani yake yana umbo mviringo na mizizi yake imesambaa kwenda chini ardhini ili kutunza maji , kwa sifa hizo matunda yake ni salama, yanaweza yasiwe matamu lakini hatuna namna jitahidi kula kiasi cha kutosha ili angalau muongeze Vitamin C na huko mbele najua tutapata namna ya kupata chakula”Aliongea Roma na kuwafanya wasifikirie mara mbili na kuanza kula huku wakikunja sura kwa uchachu wake.
Roma na yeye hakuwa nyuma alichukua kiasi kwa ajili yake lakini hata hivyo alijua kwa upande wao wasingeweza kudumu kwa muda mrefu pasipo ya kupata chakula chenye calories.
Safari iliendelea kwa muda mrefu kama masaa manne matano hivi na waliweza kufikia mto na kwasababu ilikuwa tayari ni jioni Roma aliwaambia ni muda wa kuweka kambi hapo kupumzika mpaka siku inayofuata , aliwapa kazi ya kutafuta eneo zuri na yeye alienda kutafuta kitu chochote ambacho kingeweza kuwasevu kama chakula cha usiku.
Baada ya Roma kuwaacha, walienda kukusanya kuni zilizokauka kwa ajili ya kuwasha moto .
Roma alitembea kando ya mto kuangalia namna yoyote ya kuweza kupata kitoweo , hakuwa na kifaa chochote cha kumsaidia kuvua lakini pia hakuwa na uhakika kama huo mto ulikuwa na samaki.
Baada ya kuhangaika kwa dakika kumi na tano hatimawe aliweza kuona nyoka wa majini akiambaa ambaa na alisema huyo huyo anafaa na aliingia majini na kisha akamnyaka mkononi na kumbeba juu huku akipinda pinda na alichokifanya ni kutumia meno yake kunyofoa kichwa chake.
Kikawaida nyoka wa baharini hawakuwa na sumu nyungi na katika hali ambayo kama ni binadamu umekosa kabisa chakula unashauriwa kumkamata na kumtumia kama chakula na isitoshe nyoka wa aina hio wana calories nyingi hivyo kiasi kidogo tu kinaweza kukufanya udumu kwa muda mrefu pasipo ya kuhitaji kula tena.
Baada ya kung’ata kichwa chake alikitema chini , hakuwa na namna kwa muda huo zaidi ya kuwa kama watu walioishi zama za kale.
Roma airudi kuelekea kwenye kambi yao hku akiwa ameshikilia nyoka wake lakini wakati akiwa anakaribia alisikia Mage akitoa ukulele upande wa pili na kumfanya kushituka na kuwahi , ilikuwa ni sehemu ambayo wamewasha moto na nyoka mkubwa alionekana akitoa ulimi wake kama matawi akiwasogelea.
“Kaa mbali kabisa , huyu ni Nyoka wa Australia afahamikae kwa jina la Coastal taipan , ndio nyoka namba moja mwenye sumu dunia nzima na akishambulia ni ngumu kumkwepa”Aliongea Roma na kuwafanya wote kwa pamoja kuondoka ndani ya hilo eneo na kukaa mbali.
Roma hakujiuliza mara mbili alitupia nyoka wa majini pembeni na kisha akaokota tawi na kulitengeneza kama fimbo na kuanza kumshambulia kwa kumlenga kichwani..
Lakini muda ambao alikuwa akitaka kumlenga yule nyoka alishituka na kuruka wakwanza kumlenga Roma na alikuwa amechelewa kwani tayari alishang’atwa kwenye mkono.
“F**ck!”
Alilaani , ijapokuwa alikuwa amejipanga kushambuliwa lakini ilimchukiza kushindwa ujanja mpaka na nyoka , kama ingemtokea kabla hajapoteza uwezo wake angekwepa tu kwa kutumia nguvu zake za kijini na hata kanuni za anga.
Hakuwa tu amepoteza uwezo wake lakini pia hata ubongo wake ulifanya kazi taratibu sana na hakuwa na uwezo wa kuanza kufikiria kanuni za anga na akili yake hio na kugeuza kama siraha.
Roma baada ya kuona ashang’atwa hakuona haja tena ya kutumia ule mti hivyo alitupa na kisha akamrukia yule nyoka na kumshika kichwa chake na kumkaba eneo la shingoni kupelekea yule nyoka kuachama na hio ndio nafasi kwa Roma kwani alishika taya lake na kisha akavuta kwa nguvu na kumfanya achanike katikati kama vile ni kitambaa.
“Hubby uko sawa?”Aliuliza Mage baada ya kuona nyoka alishakufa.
“Usijali nipo sawa siwezi kufa”Aliongea Roma huku akishikilia jeraha lake .
“Ijapokuwa nimepoteza nguvu zangu lakini mwili wangu bado una uwezo mkubwa wa kuvumilia sumu ya aina yoyote ile , hivyo nikipumzika kidogo tu nitakuwa sawa”
Aliongea kuwatoa wasiwasi lakini ukweli Coastal taipan kama atamng’ata binadamu wa kawaida ni ngumu sana kupona ,afiti zinasema nyoka mmoja kimahesabu anaua zaidi ya panya elfu ishirini katika uhai wake kwa kutema sumu yake tu.
Licha ya Roma kusema yupo sawa lakini hali yake ilimfanya Mage kushindwa kujizuia, ule upolisi aliokuwa nao ulishaisha muda na hapo alikuwa kama mwanamke tu ambaye anamtegemea mwanaume.
“Kwani kulikuwa na ulazima gani wakumuua si ungemfukuza tu akaenda zake , tayari upo kwenye hii hali lakini bado unatafuta matatizo mengine”Aliongea na kumfanya Roma amwangalie kwa huruma na kisha akachukua nyoka wa majini aliemkamata na kisha akampatia Rufi.
Mage baada ya kuona chakula walichoatafutiwa ni nyoka alijikuta hata kilio kikikata ghafla na kuwa katika bumbuwazi.
Upande wa Rufi hakuona shida , huenda ule uchina kwenye damu yake ulimfanya kutokuwa na wasiwasi na aina hio ya chakula.
“Huyo nyoka mmoja atawatosha nyie tu , sina jinsi na giza ndio linaingia zaidi hivyo nadhani atawaondolea njaa..’Aliongea na kumfanya Rufi kugusuwa na kauli yake maana alikuwa akimaanisha kwamba yeye hana haja ya kula hivyo wao ndio wale, ilimgusa zaidi yeye kutokana na kwamba hakuwa na uhusiano wowote na Roma hivyo hakupaswa kumjali zaidi ya Mage.
“Rufi mchome kwenye moto na kisha kwangua ngozi yake na mpasueni mtoe vitu vyote vya ndani na kisha unazungusha kwenye mti na unachoma tena nyama yake , hakikisha inaiva vizuri kwani nyoka wana minyoo wengi msije kutapika”
Mage alijikuta akichuchumaa chini huku akimwangalia Riufi akifanya kazi hio ,ijapokuwa hata wakati alipokuwa kwenye mafunzo ya kipolisi walifundishwa namna mbalimbali za ku’survive’ wakiwa maeneo kama msituni lakini hakuwahi kufikiria kwamba siku moja angekuwa kwenye hali ya uhalisia.
Roma alipumzika kwa zaidi ya lisaa na aliwasaidia kuhakikisha nyoka ameiva vizuri na kumkata kati na kisha akampatia Rufi na Mage.
Ajabu ni kwamba nyama yake ilipofikia pua za Mage ilionekana kunukia vizuri na njaa aliokuwa nayo alijikuta akianza kula mara baada ya kumuona mwenzake anafurahia.
“Roma kula kidogo tu”Aliongea Mage.
“Hapana kutokana na mwili wangu ulivyo naweza kudumu muda mrefu pasipo ya kula “
“Lakini huwezi kukaa na njaa hivyo, kwasasa huna nguvu yoyote na umeng’atwa na nyoka”
“Mage nimesema kula bwana , ngoja nikajaribu kutafuta chochote kama nitabahatika kupata”Aliongea Roma na kisha alisimama na kuondoka katika hilo eneo.
Ukweli ni kwamba alikuwa na njaa tena sana kutokana na kwamba mwili wake umepoteza nguvu na alichokuwa akitegea ni chakula.
“Inaonekana kashaamua sisi tule yote , tuendelee tu”Aliongea Mage huku akimwangalia Rufi na alitingisha kichwa kukubaliana nae.
Nyama ilikuwa ikinukia vizuri lakini bado haikuwa tamu , lakini licha ya hivyo waliendelea kula kwani hawakuwa na namna nyingine ya kupata chakula.
“Has he always been this good to you guys?”Aliuliza Rufi akimaanisha je Roma muda wote ni mwenye kuwafanyia mazuti muda wote.
“Hata mimi sijajua , muda wote ni mwenye kutulinda lakini hata hivyo huu udhoefu umenipa nafasi ya kumjua zaidi”Aliongea Mage na kumfanya Rufi kutingisha kichwa na hakuongeza swali lingine.
Hakuwa nyoka mdogo hivyo nyama iliwatosheleza kwa zaidi ya asilimia themanini kwani baadhi ya vitu vingine hawakuweza kutafuna kutokana na kuwasha.
Muda huo huo walimuona Roma akirudi kwa kukimbia akiwa kifua wazi, kwa mwonekano wake ilionekana kama kuna kitu ambacho amefanikisha kupata lakini walishangazwa kuona amevua shati.
Baada ya kuwafikia ndipo walipoweza kuona kitu alichobeba kina mchanganyiko wa mchanga , walijikuta wakisimama bila ya kumsogelea.
‘Umebeba nini?”AliulizaMage na Roma alitua lile shati lake chini na hapo hapo waliweza kuona wadudu wakipanda kwa juu na kumuogopesha Mage na Rufi.
“Ah..!!”Walitoa mshangao wao huku wakichungulia ndani na ndipo walipogundua ni wadudu wengi waliokuwa kwenye masega .
“Acheni wasiwaso ni masega ya wadudu aina ya mchwa(termites) hawang’ati na ni wazuri mno”Aliongea Roma.
“Mchwa…!!!”Walishangaa ilikuwa mara ya kwanza kwa Mage kuona aina hio ya mchwa.
“Kwanini umewaleta hapa au unataka kutufanya tupatwe na woga?”Aliuliza Rufi na Roma hakujali alikaa chini na kisha akachukua wadudu hao kwenye mkono na kisha akawapeleka wote mdomoni.
“Ah.. wewe,, wewe!!!” alikuwa akitafuna Roma lakini wao ndio waliokuwa wakihisi kutapika lakini Roma aliishia kutabasamu huku akijilamba lamba alionekana kufurahia utamu wao.”
“Mchwa wana protini mara mbili zaidi ya nyama , najua hamuwezi kuwala hivyo nitakula mimi mwenyewe”
“Kama ndio hivyo ungekula huko huko kabla ya kuja hapa na kubeba mpaka masega yao?”Aliongea Mage huku akishikilia shingo yake.
“Haya masega yametengenezwa na mate na mchanga , kikawaida watu wa asili watayachoma motoni na kufanya moshi wake kuwa na harufu ambayo hufukuza mbu, najua hapo mnavumilia maumivu ya kung’atwa ndio maana nikaja nayo”Aliongea na kuwafanya sasa waelewe , ijapokuwa maelezo yake yaliwagusa lakini hawakuvumilia kumuona akitafuna hao wadudu.
Roma hakujali , ukweli ni kwamba alishawahi kuwatafuna wakati wa utoto wake ili kuishi , alijua angeonekana kama kichaa lakini ili apate nguvu za kuwatoa kwenye msitu huo hana budi kufanya hivyo .
Siku ya pili yake ilipowadia walianza safari tena , walishaanza kumzoea Roma hivyo hawakushangazwa zaidi na tabia yake hata pale alipokamata wanyama wadogo wadogo mfano wa Sungura, Panya wakubwa na Kobe wa Australia wote hao waliwafanya chakula.
Tukio moja ambalo liliwafanya kutaka kupoteza fahamu ni pale alipong’ata kichwa cha spider na kukimeza chote.
Siku ya nne hatimae waliweza kufika kwenye fukwe ya bahari ya Arafura upande wa Kaskazini ni eneo ambalo lilikuwa na kiasi kikubwa cha miti aina ya Pandanus ambayo mingine ilikuwa na matunda na mingine haikuwa na matunda.
Wakati wao wakiwa wamepumzika wakifurahia upepo Roma alitengeneza ndoano kwa kutumia miti na uzi na kisha akatafuta jongoo na kumuweka kama chambo na kurudi tena msituni kwenye mto uliokuwa ukimwaga maji ndani ya bahari na kuanza kuvua samaki, asingeweza kuvua baharini kwani mara nyingi hawapatikani kwenye fukwe hivyo mto waliokuja nao kufuatisha aliona ndio mahali salama pa kuvua na alifanikisha kukamata Kambare wawili wakubwa., Roma hakushangazwa kupata samaki wakubwa kama hao kwenye mto wa maji malaini lakini alijiambia huenda ni kutokana kila mahali wanapatikana.
Baada ya kuwarosti kwenye moto na kula waliamka na kuendelea na safari yao huku awamu hii sasa hawakutembea kwenye vichaka bali kwa kufuatisha fukwe ya bahari.
“Mawazo ya kurudi nyumbani yametufanya kushindwa hata kutafuta tena mimea ya vidonge”Aliongea Rufi
“Sidhani kuna haja ya kujisumbua mpaka sasa nimeshindwa kujua namna ya kurudisha nguvu zangu sembuse kuweza kudhibiti moto wa njano wa kutengenezea hivyo vidonge’
“Usijilazimishe sana najua pia moto wa njano ni ngumu sana kudhibiti zaidi hata ya moto mweupe , kwa umri wako naweza kusema nguvu zako ni kubwa mno na inatosha”Aliongea na Roma aliona Rufi anajaribu kumfariji lakini hakutaka kuongezea neno zaidi ya kutembea mbele.
Kutokana na uwepo wa majabali upande wa Fukwe walirudi ndani msituni kuanza kutembea ili kuzunguka watokezee upande wa pili na baada ya kutembea kwa takribani nusu siku waliweza kutokea eneo la tambarare lenye miti mifupi , muda ulikuwa umeenda na hali ya hewa ilikuwa ya baridi mno.
Muda uleule wakati wakipanga kutokezea tena kwenye fukwe mara kwa mbele yao waliweza kuona wazungu waliovalia kombati za jeshi wakiwasogelea kwa kasi kwa kutumia vyombo vya moto ambavyo huwaruhusu kusafiri hata sehemu ambazo sio za barabara ni kama magari flani hivi yanayotumiwa sana sehemu za jangwani.
Roma baada ya kuangalia ivzuri alijua hata vyombo vya moto wanavyotumia ni vya kijeshi.
Walizidi kuwasogelea kwa kasi na walipowakaribia ndipo Roma alipoweza kuona sura zao vizuri , walikuwa na sura ngumu mno zilizojaa usiriasi huku wakiwa na mashine za bunduki kwenye mikono yao.
“Roma wanatulenga sisi?”Aliuliza Mage kwa hofu lakini Roma alishindwa kujibu kwani hata yeye alikuwa na moyo mzito , asingeogopa kama angekuwa na uwezo wake, lakini muda huo hakujuwa namna ya kujilinda kama watu hao wataamua kushambulia.
Mage alikuwa polisi na alikuwa na mafunzo lakini hakuwa na mafunzo ya kupambana na wanajeshi
“Kaeni kimya , tutajua wanataka nini kwetu”Aliongea Roma huku wakizidi kuwasogelea.
Baada ya wanajeshi wale kuwakaribia na kuwazuguka alitokezea mwanaume aliekuwa na ndevu pande zote kiasi cha kufanya mdogo wake kuonekana kwa shida.
“Black skinned peaple Africa or America?”Aliuliza kwa lugha ya kingereza akisema wati wa ngozi nyeusi je wanatokea Afrika au Amerika
Roma hakuwatambua ni kundi gani wanatokea kutokana na kwamba hakuna taarifa kwenye uniform zao zaidi ya alama ambayo iliashiria walikuwa ni Mercenary , hivyo asingeweza kujitambulisha kwao , aliogopa wasije kuwa maadui zake.
“We’re Tanzanians , our plane crashed so we landed here , what is matter?”Aliongea Roma akidanganya kwamba wao ni watanzania lakini ndege yao ilidondoka na ndio maana wapo hapo.
“Marafiki kutoka Tanzanyia , naamini mmechoka sana mnaonaje mkapumzika hata hivyo sijatarajia kukutana na wanawake warembo kwenye hili eneo , jina langu naitwa Ryan na ni furaha kwangu kuwakaribisha kwenye kambi yetu”Aliongea huku akicheka na kufanya meno yake ya njano kuonekana.
Mage na Rufi waliogopa mno na walijikuta wote wakienda kukaa nyuma ya Roma kwa woga.
“Hubby tunatakiwa kufanya nini?” Aliongea Mage na wale wengine walipiga miluzi kwa furaha wakiwaangalia Rufi na Mage kwa macho ya matamanio.
Roma alijitahidi kurudisha kumbukumbu zake kutafuta jina la kambi ya masenari yenye makazi kwenye ukanda huo na alijikuta sasa akikumbuka, waliokuwa mbele yake ni Grey Marcenaries , alikuwa akijua sana kuhusu taarifa zao ni watu wasiojali utu na ni wenye roho mbaya sana.





SEEHEMU YA 502.
Roma mara baada ya kujua ni hatari gani iliokuwa mbele yake alijua kabisa hana la kufanya , ijapokuwa hakujua ilikuwaje mpaka wakawaona lakini kwa wakati huo aliona jambo la pekee ni kufuatisha kwanza kile wanachotaka.
Aliwageukia Rufi na Mage na kisha aliwapa ishara wasiwe na wasiwasi na waongozane nao na kisha akawageukia wale wanajeshi na kuwaambia waongoze njia.
Wote walipandisha kwenye vyombo hivyo vya moto ambavyo muundo wake ni kama yale matrekta ya kulimia yenye matairi mapana.
Safari ilianza huku wakiwa chini ya ulinzi na ndani ya muda mfupi tu walikuja kutokezea kwenye eneo la fukwe na hapo sasa ndio Roma alielewa , mbele yake meli kubwa ya mizigo ilionekana ikiwa imetia nanga.
Upande wote wa fukwe kulikuwa na walinzi ambao walikuwa wakilinda kwa kuzunguka zunguka pande zote..
Ilikuwa ni meli kubwa ya mizigo na pambeni yake kulikuwa na vessels mbili za ulinzi zilizokaa kulia na kushoto na moja kwa moja Roma aliweza kufahamu hili sio eneo lao la kudumu bali huenda kuna biashara haramu zinazofanyika hapo kutokana na uwepo wa mahema mengi kwenye hio fukwe.
Watu waliokuwa tu nje walikuwa kama therathini kwa haraka haraka kuna ambao walikuwa na sura za kiasia na kuna wazungu pia na Roma alijua hao ni smugglers watu wanaoingiza biadhaa kimagendo nchini Australia kupitia baharini.
Wote walitolewa kwenye chombo kile cha usafiri na kufanya kundi lote kuwaangalia huku macho yao ya kimatamanio yakiwaangalia Rufi na Mage na kufanya wazidi kuwa na hofu , mpaka hapo walijua hawana namna ya kuepuka ubakaji hivyo waliona ni vyema kukaa zaidi karibu na Roma.
Wote waliongozwa mbele na kupelekwa mpaka kwenye hema lenye rangi ya zambarau na mwanaume aliejitambulisha kwa jina la Ryan alinyoosha mtutu wake na kuwaonyesha ishara ya kuingia ndani.
Ni eneo ambalo lilikuwa na mahema kama kumi na tano hivi makubwa yaliosimamishwa kwa mita tano nao kuachana na yalikuwa ni makubwa mno.
“Go in our Tanzanyian friends”Aliongea huku akichapia Tanzania na kuita Tanzanyia.
“Mna mpango gani na sisi?”Aliuliza Roma.
“Tusha mtaarifu bosi wetu na utafahamu mara baada ya kufika”Aliongea na kisha akamsukumzia Roma ndani ya hema hilo na wakaongezeka wanajeshi watatu na kulinda nje
“Inaonyesha hawana mpango wa kutuua lakini pia hawajatupa sababu ya sisi kutufungia humu”Aliongea Mage kwa wasiwasi.
“Amesema kiongozi wao atakuja kutuona , nadhani tutajua mpango wao”Aliongea Roma na kisha akaanza kuangalia mazingia ya hema hilo na alijikuta akikunja sura baada ya kuona maboksi mengi ya mbao yaliochongwa vizuri na kuvutia kwa nje , yalionyesha kanisa yalikuwa na vitu vya thamani ndani yake na namna ambavyo yalipangwa ni kama walikuwa wakiogopa yakidondoka na kuharibika.
Roma aliyasogelea na kisha akafungua moja wapo taratibu sana ili walinzi nje wasisikie na ndani yake aliweza kuona kifaa ambacho kimezungushiwa magazeti , alishangaa kutokana na lugha iliotumika kwenye hayo magazeti lugha ilikuwa ya kichina (mandarin) na moja kwa moja alijiambia huenda ni kitu ambacho kinahusiana na nchi hio.
Baada ya kuondoa lile gazeti alikutana na buble wrap iliozungushiwa kwa juu ili kama kifaa hicho kingedondoka chini kisipasuke kwa urahisi , baada ya kumalizia kutoa sasa alijikuta akishangaa baada ya kuona kilichopo ndani ya boksi.
“This is…”Rufi alijikuta akiziba mdomo kwa mshangao na Roma alimtingishia kichwa kukubaliana nae.
“Ni Porcelaini ya rangi nyeupe na bluu ambayo imedariziwa na mchoto wa mawingu na Dragoni , makadirio ya thamani yake nchini China ni zaidi ya dola milioni kumi”Aliongea Roma na kumfanya sasa Mage kuelewa maana aliona ni kama kikombe cha udongo tu na hata hivyo hakuwa na uelewa na tamaduni za China.
“Are they smuggling relics?””Aliuliza Rufi kwa sauti ya kunong’oneza akimaanisha je wanaingiza mabaki ya vitu vya kale vya thamani nchini Australia kwa njia zisizo halali.
“Naamini kuna zaidi ya mabaki , hebu fikiria kwanini wamekuja kutuweka ndani ya hema lenye vitu vya thamani namna hii , jibu ni kwmaba mahema yote huenda yamejaa, ndio maana wametumia meli kubwa ya mizigo , nina uhakika kama serikali ya China wanaelewa hiki kinachoendelea lazima wangewawinda kwani vitu kama hivi ni vya thamani sana kwao”
Wakati Roma akiendelea kuongea aliweza kusikia sauti yenye ucheshi nje ikiongea na ndani ya muda mfupi tu hema lilifunguliwa na akaingia mwanaume mrefu mchina akiwa amevalia T- shirt iliombana vyema mwili wake , alikuwa yupo na mwanaume aliejitambulisha kwa jina la Ryani.
Alianza kumwangalia Mage na kisha akahamia kwa Rufi na halafu akamgeukia Roma sasa.
“Dude I heard from Ryan that you guys were trapped in this place because your plane crashed?”
“Dude nimesikia kutoka kwa Ryani mmekwama mara baada ya ndege yenu kudondoka?”Aliuliza kwa lugha ya kingereza lakini iliojaa rafudhi ya kichina.,
“Wewe ni mchina?”Aliuliza Roma na kumfanya yule bwana kumwangalia kwa namna ya kumchunguza Roma.
“You don’t look like a spy since you don’t recognise me , I’m leader of the Hydralisk Mercenary group , Jin Zhe , They call me Hydra , Havu you heard about me?”
“Unaonekana sio shushu kwasababu haunifahamu , mimi ni kiongozi wakundi la Masenari la Hydralisk nafahamika kwa jina la Jin Zhe lakini wananiita Hydra , ushawahi kusikia kuhusu mimi?”Aliongea huku akimwangalia Roma kama Cobra alieona binadamu wa kumshambulia.
Roma alitingisha kichwa chake akishiria kwamba hajawahi kumsikia na alikuwa akiongea ukweli kwani hajawahi kuwasikia labda huenda hawakuwa maarufu.
“Haijalishi kama hunifahamu lakini naamini nyie sio hao watu wanaonitafuta”Aliongea na kumfanya Roma sasa kidogo kuwa na ahueni, kwasababu hakuwa akiwajua moja kwa moja alijua sio maadui zake hivyo hakuogopa kama atagundulika ni mfalme Pluto.
“Kwahio unamaanisha utatuacha tuondoke?”Aliuliza Mage.
“Go!?, My beutiful you think too highly of us ..”Aliongea huku akitingisha vidole vyake akimaanisha kwamba wamewadhania ndivyo sivyo kwani hawana mpango wa kuwaachia.
Roma alijikuta akikunja ngumi akijiambia mwenyewe mambo yanaweza yasimalizike vizuri.
“Tumekaa hapa kwa muda mrefu na haya maeneo hakuna watu wanaofika hivyo unaweza kusema ni kwa muda mrefu hatujawhai kuona wanawake warembo kama nyie ,itakuwa ujinga kama nitawaachia muondoke bila mabro kunufaika na uzuri wenu”Aliongea na kumfanya Mage na Rufi kukasirika na kuogopa.
“Huna aibu wewe?”Alilaani Rufi
“Nisamehe sana , ijapokuwa hatuna uhasama na nyie lakini siwezi kujali kwasasa , hali ya kimazingira yenyewe ndio hii, ninachomaanisha msiwe na wasiwasi na muwaburudishe mabro wangu vizuri tu na hakuna kibaya kitakachowakuta”
“Sio tu wewe ni mwizi unaeliibia taifa lako mwenyewe, lakini pia ni mchafu wa tabia”Aliongea Rufi
“Nione aibu hahah….. mnaonekana kabisa nyie ni matajiri ndio maana mnatoka nchini kwenu na kudondoka na ndege na hamuwezi kunielewa mtu kama mimi”Aliongea ilionekana kabisa alikuwa na chuki na taifa lake.
“Unaonekana kama mtu mwenye huzuni , inakufanya uonekane kama mtoto”Aliongea Roma.
“Unasemaje wewe , funga domo lako”Aliongea kwa hasira na kumfanya Roma hata asijali na kuendelea kuongea.
“Inaonyesha kabisa nchi yako imekufanyia mabaya lakini lawama zote unaangushia dunia nzima , angalia sasa ulivyo, unaonekana kama mtu ambaye umekufa huku unatembea , nina uhakika kuna kilichokutokea lakini tofauti na kujitafuta ili kujua ulikosea wapi au kulipiza maadui zako kwa kile walichokufanyia lakini upo hapa ukiwa umejificha unaishi bila amani , kwangu wewe ni Loser na mtu mdhaifu sana”Aliongea Roma kwa kujiamini kama kawaida yake na kumfanya Mchina kukasirika zaidi na zaidi.
“Unajifanya mjuaji sana kwa kuongea , lakini ngoja nikushauri wanaume hatuongei sana bali ngumi yetu ndio inazungumza”Aliongea .
“Boss niwapeleke hawa wanawake kwenye hema lako”
“Haina haja, waondoe wanajeshi wanao linda nje”Aliongea na kisha Ryani mzungu alitoka nje na kuwaambia wale walinzi waondoke na kisha akarudi tena ndani.
“Boss huyu mwanaume na yeye tunamfanya nini maana hana faida kwetu?”Aliuliza tena.
“We have brothers who like to go other way right? , he looks young and tender, give him to them !”
“Tuna mabraza ambao wanapenda mlango wa uani si ndio? , huyu bwana anaonekana mdogo lakini pia ni mpole muondoe hapa ukawapatie”Aliongea na kumfanya Ryan kutabasamu huku meno yake ya njano yakiwa nje nje.
“You have to serve our brothers well .. hehe, I’ll send you there myself”
“Unapaswa kuwahudumia mabraza wetu vizuri … hehe nitakupeleka mwenyewe”Aliongea .
Rufi na Mage walijikuta wakijificha nyuma ya Roma , ni kama washasahau kwamba mwenzao hana nguvu yoyote , Mage alikuwa amekunja ngumi alikuwa akijua kupigana kwasababu ashapitia mafunzo lakini aliogopa siraha zao tu
Ryan alianza kumsogelea Roma kwa ajili ya kumnyanyua ili kumpeleka kwa mabraza , lakini ile anamkaribia Roma alinyanyuka kwa staili matata sana na kupiga viungio vya mkino yake.
‘Arrghh,,,”
Alijikuta akitoa ukulele , ijapokuwa Roma hakuwa na nguvu za kijini lakini haikumaanisha alikuwa hajui kupambana kwa njia za kawaida , alikuwa na mafunzo ya hali ya juu ya Kung Fu na alikuwa akijua mbinu zote za kijeshi na isitoshe mwili wake ulikuwa mwepesi kutokana na kwamba alikuwa amemulikwa na mwanga wa jiwe la kimungu na akaja kuwa Agent 13.
Roma kwa haraka sana alinyanyua bunduki ya Ryani na kisha alimfyatua nayo kwa kumlenga kichwa na muda uleule zile purukusani zilifanya wanajeshi wengine wawili kuingia na Roma hakutaka kuwarembesha , bunduki ilikohoa mara mbili mfululizo na kuwapasua wote vichwa na kudondoka chini.
Mchina alijikuta akishangazwa na uwezo wa Roma na alijikuta hana cha kufanya zaidi ya kukimbia nje huku akiita wenzake .
Roma palepale alichuchumaa na kisha akachomia mikebe ya bunduki za wale wawili aliowaua , alikuwa akijua wapo wengi na mikebe mwili haiwezi kutosha kuwamaliza.
“Roma tunapaswa kufanya nini?”Aliuliza Mage.
“Hawawezi kushambulia hili hema bila ya tahadhari kuna vitu vya thamani vya kutosha hapa na kama vitaharibika watapoteza mamilioni ya pesa”Aliongea Roma
“Pumbavu zako , sijategemea ungekuwa na ujuzi wa hali ya juu namna hio lakini siwezi kukuacha hai , ushaua tayari mabraza wetu watatu lazima ulipie’Aliongea Mchina kwa sauti kubwa nje kwa hasira.
“Roma unaonaje tukuchukua bunduki na wote tukashambulia nina uzoefu mkubwa na tunaweza kuwamaliza”Alishauri Mage.
“Hapana tukifanya hivyo ndio watatuua vizuri kwani ni kama tunawachokoza na watatushambulia na ukumbuke wana siraha nzito”
“Kwahio tunafanya nini , tunasubiria hapa ndani watuue?”Aliuliza na kumfanya Roma kushindwa kujibu swali lake kwani hakuwa na wazo, kwenye maisha yake hakuwahi kuwa hivyo , kuwa binadamu wa kawaida ni jambo ambalo hajalizoea
Alichukia hali aliokuwa nayo kwani alishindwa kabisa hata kuwalinda wanawake wake ,kwake ilikuwa kama matusi ambayo ni kama yalikuwa yakimkosesha amani.
Muda huo kwa nje hali ilitulia kabisa , ni kama vile wameondoka lakini Roma hisia zake zilimwambia huenda wanawategea kitu hatari zaidi.
Kabla hajajua ni nini kinaendelea nje , vyuma vilirushwa ndani na baada ya kuangalia kwa umakini aligundua ni mabomu ya machozi .
“Ni mabomu ya machozi fumba macho ”Aliongea, katika maisha yake alikuwa ashapitia changamoto kama hizo na ni kama amekumbushiwa nyuma lakini hata hivyo bado hatari ilikuwa nje nje.
“Hatuna chaguo zaidi ya kutoka nje , Mage chukua hio bunduki na wote hakikisheni mnakuwa nyuma yangu”Aliongea Roma.
Muda huo alijiambia sio wa kusita tena bali ni wa kupambana huku akitegemea Mage kidogo angemsaidia kwani alikuwa mwanajeshi na ukichanganya pia alikuwa kwenye levo ya nusu mzunguko , hivyo alikuwa na uhakika anaweza kudondosha watu kumi.
Alijua walikuwa wakisubiriwa nje hivyo aliona haitokuwa busura kama watatumia mlango wa hema kutoka nje
Wote walikuwa wamefumba macho ili moshi usiwaumize na kuwafanya wawashe na macho.
Roma alitumia hisia zake kujaribu kupata kuona namna wanajeshi hao walivyojipanga na palepale aliachia risasi kupitia upande wa nyuma mwa hema na alidondosha watu wawili bila makosa.
“Kimbieni nje”Aliongea Roma na muda ule alijirusha nje huku akitanguliza mdomo wa bunduki mbele na kufanya hema lichanike kwa wepesi na aliweza kubiringita kama pia huku akirusha risasi ambazo hakuna hata moja iliokosa mtu.
Jambo lile liliwafanya kushangazwa mno na kujiuliza huyu ni komandoo au ni nani kwani haikuwa kawaida, sekunde tano tu alikuwa amedondosha watu watano.
Mage alimtoa Rufi na kumwambia akimbilie baharini zaidi huku yeye akimkinga na siraha, lakini palepale yule mchina alionyesha kuwashitukia tayari.
“Mnajaribu kukimbia sio , Never”Aliongea huku akiwapa vijana wake ishara ya kuzunguka nyuma.
Na Mage alikuwa shapu mno kwani alimdodosha Rufi chini na kisha akauegamiza mgongo wake kwa staili ya kuelekea mbele na akaachia risasi mfululizo ambazo ziliwapata watatu na kudondoka chini , hali ile iliwafanya kusogea upande huo kwa tahadhari.
Muda ule ule kuna wanajeshi wengine wanne waliokuwa kwenye gari waliwasogelea kwa spidi na Roma alielala chini alilenga mara mbili tank la mafuta kwa shabaha kuntu kabisa.
“BOOM!!
Gari ililipuka palepale na wanajeshi wanne walikuwa wafu tayari na kumfanya Jin Zhe kuwa kwenye kiwewe akishangazwa na Roma alivyokuwa vizuti kwenye kuchezesha bunduki.
“Back off and take cover!”
Aliongea kwa sauti akiwamrisha warudi nyuma kwani aliogopa wangeshambuliwa na Roma ambaye alikuwa na shabaha ya hali ya juu kwenye matumizi ya siraha hivyo kuogopa wanajeshi wake kufa wengi.
Ndani ya sekunde tu wote walijificha nyuma ya mahema na kwenye mawe , huku wakiwa wamejaaa sumu ya kuua maradufu.
Upande wa Roma risasi zilikuwa zishamwishia tayari , lakini hata hivyo hakuna ilioharibika na aliwaza mbinu ya pili ya kushambulia.
“Mage unafanya nini acheni kukimbia” Aliongea Roma kwani aliona wangeshambuliwa na pale pale Mage alilala chini kwa haraka
Roma baada ya kuona hawako kwenye hatari alisimama na kisha akamrushia bunduki wanajeshi wawili waliokuwa wakitaka kujitokeza kushambilia na palepale alikimbia nduki kumfuata mwanajeshi mwiengine ambae ashakufa achukue bunduki yake.
Mage aliejificha na Rufi chini ya jiwe alinyanyua sura kidogo kuchungulia , hata yeye siraha yake ilishaisha risashi hivyo alitupilia mbali na wanajeshi waliokufa wapo mbali
“Roma kuwa makini..”
Mage alijikuta akiziba mdomo kwa wasiwasi mara baada ya kushuhudia moja wapo ya mwanajeshi ambaye alilipuka kwenye gari bado hakuwa amekufa na alisimama huku akiwa ameshikilia bomu la kurusha na mkono.
Roma alikosa umakini wa kuangalia nyuma yake hivyo hakumuona na yule mwanajeshi hakutaka kuchelewa palepale alirusha lile bomu uelekeo wa Roma lakini alikuwa fasta mara baada ya kusikia kauli ya Mage na aliruka upande mwingine .
“BOOM!”
Lilipuka lakini Roma hakuwa ameenda mbali hivyo nguvu ya wimbi lake ilimpiga na kumfanya adondoke chini akiugulia maumviu.
“Nice one, very nice”Aliongea Jin Zhe
“Ameishiwa na risasi mfuateni tummalize”Aliongea kwa nguvu.
Roma alikuwa amefunikwa na vumbi la mlipuko wa bomu na alikuwa akijihisi kizungu zungu na viungo vya ndani ni kama vilikuwa vikikamuliwa kwa maumivu aliokuwa akisikia.
Lakini alijiambia hana muda wa kusikilizia maumivu na atumie vumbi lilomfunika kama kinga , alijivingirisha kama pia na kusogelea bunduki iliokuwa kushoto kwake
Mlio wa bunduki ulikuwa umesambaa na wale wanajeshi hawakuangalia pa kulenga ili mradi ni eneo ambalo Roma yupo walirusha huko huko na kwa wingi wa risasi ilikuwa ngumu Roma kukwepa zote.
Roma alijikuta aking’ata meno kwa maumivu mara baada ya kugundua ashapigwa risasi ya tumbo na kwenye kigimbi cha mguu
Ijapokuwa mwili wake bado ulikuwa mkomavu lakini haukuwa na ulinzi tena wa nguvu ya kimaandiko ya urejesho kutokana na sumu iliokuwa kwenye mwili wake , hivyo alijihisi dhaifu mno.
Alijikuta akitema damu nyingi huku akisikilizia maumivu makali kutoka tumboni , alijjitahidi kubingirika upande mwingine lakini bado hakuwa na spidi kama ya mwanzo lakini bahati kulikuwa na jiwe kubwa karibu hivyo alilala chini na kujikinga na risasi.
Mage alishindwa kabisa kuvumilia pale alipokuwepo kwani alishuhudia Roma akipigwa na risasi na akitema damu na alitoka kwenye jiwe na kukimbilia upande wa Roma alipo.
“Mage..!!”Aliita Rufi kwa hofu lakini alikuwa ashachelewa na hata yeye alianza kukimbia kuelekea upande wa Roma.
Roma alijua wanamsogelea ili kumsaidia ,lakini aliona kabisa isingeweza kusaidia palepale aliwapa ishaa wasije upande wake lakini Mage alimpotezea na kukimbia kwa spidi na kwenda kutua alipo na Rufi hivyo hivyo aliweza kufika.
“Roma hapa hatuwezi tena kupambana nao , ni wengi na hatuna siraha njia pekee nitumie uwezo wangu kukubeba kukimbia na wewe kuelekea upande ule”Aliongea Mage na Roma aliona wazo sio baya, alijua ni kweli Mage anao uwezo wa kukimbia nae kwa spidi kutokana na uwezo wake.
Roma kabla hajajibu Mage tayari ashamnyanyua kama mtoto na kuanza kukimbia nae huku Rufi akifuatia.
Kitendo kile kiliwaamsha Jin Zhe na wanajeshi wake na kuanza kuwasogelea bila hofu baada ya kujua Roma hana siraha tena na walikuwa wakiwasogelea huku wakirusha risasi.
Rufi baada ya kuona wanashambuliwa mfululizo alibadilisha upande ili kumpa nafasi Mage akimbie akiwa na Roma na Mage alifanikiwa kufikia chini ya jabali lakini ile wanataka kujificha chini Rufi aliwakimbilia tena lakini alishachelewa kwani palepale alipigwa na risasi ya mgongoni na aliishia kutema damu na kudondoka chini.
“Noo…!!”Roma alijikuta akitoa ukulele bila kuamini na alishindwa tena kujificha zaidi ya kutoka kwenye mikono ya Mage na kumsogelea Rufi.
Jin zhe alionekana kufurahishwa na tukio lile na palepale alitoa bomu la kurusha kwa mkono na kuliotoa pin.
Roma alikuwa ashamfikia Rufi na kumshikilia akiwa amepiga magoti.
“Roma kimbiaaa……!!!””Alijikuta akitoa ukulele Mage mara baada ya kuhushudia bomu likiruswa pale walipo na Roma alijikuta akimwachia Rufi na kuangalia lile bomu na palepale macho yake yalibadilika na kuwa ya rangi ya njano.

0687251346 nicheki watsapp .

ITAENDELEA.
[emoji91][emoji91]
 
SEHEMU YA 503.
Mlipuko wa bomu ulitokea mita chache na waliposimama na hilo ilifanya kuwa bahati yao kwani hawakuuguzwa na moto zaidi ya kurushwa pembenni na presha kubwa ya mlipuko huku vumbi likiwafunika kiasi cha kuwafanya Jin zhe na wanajeshi wake wasione upande wa pili.
Roma maumivu ya majeraha yake aliyasahau kabisa na alichokuwa akiangalia ni Rufi alielala chini akivuja damu na Mage ambaye amesukumwa mbali na mlipuko wa bomu mpaka akapoteza fahamu.
Jin Zhe nia kundi lake walitembea kuwasogelea , mpaka hapo waliamini kwamba washamaliza vita hivyo hakukuwa na haja ya kurusha tena risasi.
“Angalieni kama bado wapo hai?”Alitoa amri
“Yess Boss”
“Niahakikisha nawakata vipande vipande na kisha kuwalisha Papa”Aliongea huku akionyesha hasira kweli kweli , alitamani wasiwe wamekufa ili awape mateso makali.
Wafuasi wake walikuwa na hasira pia ya kiwango cha juu na walisogea mbele ili kuwaangalia maadui zao kama tayari washakufa.
Roma alimwangalia Rufi alielala chini akiugulia maumivu ya kupigwa na risasi na kisha akageuka nyuma na kumwangalia mage alielala chini na alijikuta akijawa na hisia mchanganyikio , hisia za kudharilishwa , hisia za chuki , hasira , kukata tamaa na majonzi, alijihisi ni kama meridian za mwili wake zitapasuka.
Mishipa yake ya damu ilikuwa ikidunda kwa nguvu na kufanya maumivu kuwa makali mno kwani ilikuwa ni kama itampasuka , misuli yake ya mwili pia ilizidi kutanuka na kumfanya kuhisi maumivu makali kwenye miungio ya mifupa.
Sehemu ya kituo katika mwili wake ambayo ndio chanzo cha nguvu zake kiliweza kufunguka kutoka katika kizuizi cha sumu ya vipepeo wa ndoto na mabadiliko hayo yalifanya macho yake kubadilika badilika rangi.
Wale wanajeshi muda ambao walikuwa wakisogea eneo ambalo Roma amesimama walijikuta wakisimama wenyewe mara baada ya kuhisi msisimko mkubwa wa nguvu ya kimauji inayowakaribia na kujikuta kujawa na hofu isiokuwa na kifani na hata eneo lote hali yake ya hewa ilianza kubadilika na mawe madogo yaliaanza kupeperushwa na upepo.
Jin Zhe hatimae aliweza sasa kujua kuna kitu ambacho hakipo sawa , aliinua kicha chake na kuangalia chanzo cha mabadiliko hayo na alijikuta akipagawa mara baada ya kumuona Roma alivyo, kwani macho yake yalikuwa yamegeuka kutoka rangi ya njano na kuwa rangi nyekundu na kuwafanya wazidi kuogopa zaidi na zaidi na kushindwa hata kuchukua maamuzi ya kutumia siraha zao.
Ukweli ni kwamba haikuwa na haja ya Roma kubadilika macho kwani watu waliokuwa mbele yake ni wadhaifu sana , ila wakati huo akili yake alishindwa kuingoza yeye mwenyewe , ule ugonjwa wake ambao siku nyingi ulikuwa ni kama umepotea muda huo ni kama umemrudia upya kutokana na hasira aliokuwa nayo.
Muda uleule wakati wale wanajeshi wakimshangaa Roma alitema mate yaliojaa damu , ndani ya mwili wake ni kama kuna kitu kimepasuka na kumsababishia maumivu mengi, lakini ukweli ni kwamba alikuwa akijaribu kuondoa sumu iliokuwa ipo ndani yake.
Ilimchukua sekunde tu mwili wake wote uliweza kujiponyesha kwa haraka sana na hata risasi zilizokuwa ndani yake hazikuwa na madhara tena na jeraha lake likafunga palepale na sasa alijihisi ni kama nguvu zake zimeongezeka maradufu zaidi.
Kwanini moto?, kwasababu miti , Mawe na radi ni baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kutengeneza moto lakini hata moyo wako unaweza kusababisha moto.
Nishati iliopo kwenye moyo wako unganisha na nishati iliopo kwenye figo zako na kisha malizia na nishati iliopo kwenye kibofu chake ndio trifecta ya kudhibiti moto wa rangi zote.
Ilikuwa ni kama ufunuo katika akili yake , siku zote hakuweza kudhibiti moto wa rangi nyeupe na nyekundu kwasababu hakuwahi kufikiria nguvu zake za kijini zilizojificha katika moyo wake ndio hukamilisha sifa tatu muhimu.
Moto mweupe ulikuwa na nguvu ya kumeza kila kitu , hivyo Roma mara baada ya kupaa ufunuo hu na kujaribu kudhibiti nguvu zake katika moyo , kibofu na figo palepale ile nguvu ilioambatana na vipepeo wa kufikirika iliweza kuisha mara moja na hapo ndipo uwezo wake ukarudi wote tena na zaidi ya kuongezeka.
Lakini licha ya kuwa kwenye mshangao wa kuweza kugundua kitu muhimu sana katika mafunzo yake kwa muda huo hakutaka kwanza kuruhusu mawazo yake yachukue nafasi , bali nafsi yake ilikuwa ikimwambia ua kila mmoja.
Roma palepale aliita nguvu ya kimaandiko na kisha akaunganisha na nguvu ya mbingu na ardhi ambayo ilimpatia ufunuzi wa namna ya kutengeneza moto mweupe na palepale joka la moto liliweza kujitengeneza kwenye mikono yake na hakuwa na muda wa kupoteza tena kwani alilielekeza nini linatakiwa kufanya.
Kilichosikika baada ya hapo ni vilivo na kusaga meno vya wale wanajeshi namna ambavyo walikuwa wakiungua na ndani ya sekunde ishirini tu miili yao iligeuka majivu na muda huo huo akaweza kurejewa na uwezo wake timamu wa kufikiria mara baada ya nguvu ya andiko la urejesho kufunika ugonjwa wake wa ubongo , ugonjwa ambalo aliamini ulipotea kumbe bado ulikuwepo.
Roma palepale alipotea na kuibukia mbele ya Mage ambaye alipoteza fahamu kutokana na mlipuko wa bomu na alijikuta akipata ahueni mara baada ya kuona alikuwa hajaumia sana zaidi ya kupata michubuko tu na palepale alimwingizia nguvu ya kijini na akarejewa na fahamu..
“Roma ume…”Alitaka kuongea lakini Roma alimzuia asiongee na kumuweka chini na kisha akamfuata Rufi kumwangalia maana alijua ndio ambaye alikuwa kwenye hatari kubwa ya kupoteza maisha.
Roma mara baada ya kumkagua alimwona alikuwa amepoteza sana damu kutkana na jeraha la risasi na kumfanya kupauka mno uso na kushindwa hata kupumua vizuri lakini hata hivyo aliamini akimwingizia nguvu ya kijini basi ataweza kumponyesha kwa haraka.
Roma palepale hakutaka kuchelewa aliita nguvu za andiko la urejesho na kuziingiza kwenye mwili wa Rufi ili kuponya majeraha yake pamoja na kumaliza sumu ya risasi lakiini matokeo yake yalimshangaza na kumwacha kuwa na hofu zaidi.
Ijapokuwa kwa nje alionekana akipona , lakini kwa ndani nguvu ya kijini iligoma kumponyesha kabisa ilikuwa ni kama nguvu zake zilikuwa zikikataliwa na nguvu ya aina nyingine na kadri alivyokuwa akijitahidi ilishindikana kabisa.
“Au ni kwasababu kazaliwa na nguvu kubwa ya Yin katika mwili wake?”Alijiuliza Roma kwa mshangao na hapo hapo alijikuta akianza kukusanya doti , ashawahi kumaliza sumu katika mwili wa Rufi na nguvu hio hio lakini aligundua nguvu hio hio ilikuwa ikikataa kumponya viungo vya ndani ya mwili.
“Ir..it’s useless”Rufi alimwangalia Roma kwa taabu huku akijitahidi kuongea akiwa kama mtu aliekata tamaa , alikuwa akimwambia kwamba alichokifanya hakina maana kwani hawezi kupona.
“Huwezi.. huwezi kuniponyesha kwa nguvu zako….”Alijitahidi kuongea lakini kila alipokuwa akijikaza damu zilizidi kumtoka na Roma aliamini huenda kuna mshipa wa damu ambao umepasuka kwa ndani.
Mage baada ya kuona Roma hana anachokifanya alimsogelea kwa haraka kuona kinachoendelea.
“Roma unafanya nini , kama huwezi kumponyesha tatufa namna nyingine ya kumsaidia”Aliongea Mage kwa amri na kumfanya Roma kutoka kwenye mawazo na kuona kweli anapaswa kutafuta mtu mwingine ambaye anaweza kumsaidia
Alijiambia kama kuna mtu atafanikisha kumfanyia upasuaji wa haraka basi kuna uwezekano wa Rufi kupona na hapo hapo jina la Profesa Clark liliibuka kwenye kichwa chake , alijiambia huyo ndio mtu wa pekee ambaye anaweza kumsaidia.
Clark alisomea udaktari kwa sababu ya Roma licha ya kwamba kwa mambo ambayo alikuwa akifanya haikuwa sahihi kumwita dokta lakini alikuwa ameiva sana katika fani hio na alikuwa amezidi madaktari wengi wakubwa duniani.
Clark hakuwa daktari wa kuhudhuria wagonjwa wa kawaida kila siku na kama ataonekana hospitalini badi ni kwa wale wagonjwa ambao wameshindikana au wenye dharula kubwa za kiafya ambazo madaktari wa kawaida hawawezi kupambana nazo.
Roma palepale alisimama na kisha akamgeukia Mage baada ya kuyakusanya mawazo yake na kuyachanganua na kuhitimisha.
“Utanisubiri hapa hapa ninampeleka kwa Clark”Aliongea Roma na Mage hakutaka kubisha wakati huo , hakutaka kuhofia kwamba angebakia mwenyewe katika eneo hilo ila afya ya Rufi ilikuwa kipaumbele.
Roma alijua hawezi kumbeba kwa njia ya kawaida kwani asingeweza kuhimili hivyo alimtengenezea ngaoo ya kijini kama puto na kisha akambeba na kupotea katika eneo hilo la fukwe.
Profesa Clark tokea maswala ya ndoa yake kutoendelea baada ya vifo vya Wolverine , alirejea nyumbani kwao Uingereza kama kawaida na tafiti za madawa nchini Tanzania zilikuwa chini ya wanafunzi wake ambao walikuwa wakiongozwa na Ashley.
Roma akiwa njiani alijua vizuri wapi Clark anafanyia tafiti zake , lakini kwa muda huo atakuwa kwenye jumba lake la kifahari amepumzika kutokana na utofauti wa muda.
Hivyo kwa haraka haraka aliona kumpeleka Rufi moja kwa moja mpaka nyumbani lisingekuwa chaguo bora hivyo aliempeleka Rufi kwenye hospitali ya St Mary’s katika kitengo cha dharula , alitumia dakika tano tu ku’teleport’ kutoka bahari ndogo ya Arafura mpaka London Uingereza.
St Mary’s ilikuwa ni hospitali ambayo inafahamika sana ndani ya London kwa ubora wa huduma zake, Roma alikuwa na mpango kwanza Rufi apatiwe huduma ya dharula na madaktari wa hospitali hio wabobevu na kisha amfuate Clark nyumbani kwake kumleta hapo.
Wakati anatua mbele ya hospitali hio kulikuwa kimya mno kwasababu ni usiku wa kama saa saba kwenda nane hivi.
Wahuhdumu na manesi wa hospitali hio walishangazwa mara baada ya kumuona mwanaume wa kiafrika akiingia akiwa amembeba mwanamke ambaye alikuwa ametapakaa damu., lakini kutokana na taaluma yao hawakushangaa zaidi ya kuchukua maamuzi ya haraka na kumsogelea kwa kumkimbilia huku wakimsogezea kitanda cha hospialini cha mataili na kumfanya Roma amlaze chini taraibu.
“Sir what happened to her?”Aliuliza nsesi akimuuliza Roma nini kimetokea.
“Alipigwa na risasi lakini sasa hivi ameumia viungo vya ndani kutokana na kupigwa na mlipuko wa bomu”Aliongea Roma na kufanya manesi wamwangalie kwa mshituko na walijikuta wakiwa na wasiwasi huku wakiendelea kumsukuma Rufi kuendelea mlango wa chumba cha upasuaji.
“Sir naomba nikuulize wewe ni mtalii au ni raia?”Aliuliza tena nesi mara baada ya Rufi kuingizwa ndani na maswali yake kidogo yalimkasirisha Roma lakini hakutaka kuruhusu hisia zake zimtawale.
“Sisi ni watanzania, kwanini unauliza maswali mengi mtayarisheni kwa ajili ya upasuaji na waiteni madaktari”Aliongea kwa kingereza na kuwafanya wale manesi kumwangalia kwa wasiwasi.
“Grace is doctor Giggs here yet?”Nesi alimuuliza nesi mwenzake akimaanisha je Dokta Giggs hajafika bado.
“Tushampigia simu na amesema anakuja”.
“Sir , tunaomba usubiri nje Dokta Giggs ndio daktari bingwa wa upasuaji ndani ya hospitali hii , atahakikisha anafanya kila liwezekanalo kuokoa hali ya mgonjwa”Aliongea nesi mmoja mzee mzungu ambaye nywele zake zishaanza kubadilika rangi na Roma ilibidi akubali maana kwa muda huo hakuwa na msaada tena hivyo hakutaka kuleta usumbufu.
“Sir kama una wasiwasi sana unaweza kuangalia upasuaji unavyofanyika , zunguka upande wa pili”Aliongea mwanadada ambaye alifahamika kwa jina la Grace.
Lakini kwa muda huo Roma hakuwa na muda wa kuangalia upasuaji huo , alijiambia inawezekana huyo dokta Giggs akawa bingwa lakini imani yake ilikuwa kwa Profesa Clark tu alijiamnbia ndio pekee ambaye anaweza kumuokoa Rufi.
Roma wakati anakaribia kutoka nje , hatimae aliweza kumuona Dokta wa kiume mzungu alievalia Scrub na barakoa akikimbia nduki uelekeao wa chumba cha pasuaji na moja kwa moja Roma alijua atakuwa ndio dokta Giggs mwenyewe, kwani hakuwa peke yake , alikuwa akifuatwa na baadhi ya madaktari wengine ambao Roma alijua watakuwa ni wasaidizi wake.
Dokta yule licha ya kumuona Roma hakujali sana zaidi ya kumpita na Roma alipogueka, alishuhudia akiingia kwenye chumba kile cha upasuaji na Roma alipata ahueni kiduchu ambayo ilimpa ruhusa ya kuondoka katika hilo eneo kumfuata Clark.
Baada ya dakika tatu hatimae Dokta Giggs aliweza kuingia ndani ya chumba cha upasuaji akiwa tayari amevaa Glovuzi na kuruhusu manesi kumvisha gauni maalumu la kufanyia upasuaji.
“What is her condition?”Aliuliza akimaanisha hali yake ikoje huku akimwangalia msichana mwenye kuchanganya rangi akiwa amelazwa kwenye meza ya upasuaji.
“Kuna jeraha la risasi kwenye mgongo wake na pia alipigwa na bomu na kusababisha viungo vya ndani kuharibika , lakini majeraha yake ya nje yanaonekana kutokuwa tatizo, lakini vifaa vimeshindwa kunasa presha ya damu yake”
“What ?! you can’t detect her blood pressure?”Aliuliza kwa mshangao.
“Yes, Doctor Gigg..”Alijibu nesi mmoja mzee akiwa kwenye hali ya wasiwasi.
Upande mwingine, kaskazini mashariki mwa hospitali ni jumba moja la kifahari lililojengwa kwa mtindo wa kasri .
Yalikuwa ndio makazi yake mtoto wa malkia Profesa Clark , ni jumba ambalo limezungukwa na kijani kibichi pande zote na hakuna raia ambaye anaweza kuhoji kwa mtu mmoja kukaa kwenye jumba kubwa kama hilo kutokana na kwamba anatokea kwenye jumba la kifalme.
Licha ya kuwa mtoto aliezaliwa katika koo tajiri sana duniani na yenye nguvu(Roth’schild) lakini maisha yake yalikuwa ya kawaida tofauti sana na watoto wengi wa kitajiri , alikuwa akifanya kazi mchana wote na ifikapo usiku angerudi kwenye jumba lake hilo na kupumzika akiwa peke yake.
Juu ya yote hakuna ambaye alihofia usalama wake , kwani ukiachana na kwamba alikuwa na mafunzo ya kujilinda kwa kupigana lakini pia wengi walikuwa wakimuheshimu kutokana na uwepo wa Hades kwenye maisha yake yeye na mama yake.
Lakini katika siku zote ambazo alihisi kaishi kwa amani bila bughuza siku hio ilikuwa tofuati mara baada ya Roma kutua kwenye nyumba hio upande wa balkoni.
Roma aligonga mlango kwa zaidi ya mara mbili lakini hakukuwa na majibu , hivyo hakutaka kuendelea kugonga tena zaidi ya kuusukuma mlango na kufanya komeo lake la kirembo kuvunjika.
“Who’s there!!?”
Kivuli cha mtu kiliruka kwa ustadi kabisa kutoka kwenye kitanda na mpaka taa inawashwa tayari Clark alionekana kuwa na bastora mkononi ambayo ipo tayari kuachia risasi.
Ijapokuwa alikuwa amelala lakini hisia za kujilinda zilikuwa kubwa mno , hivyo kumfanya kuwa na machale ya haraka,Alijikuta akiwa kwenye mshangao mara baada ya kumuona mwanaume aliesimama mbele yake.
“Roma!!,Why are you here?”Aliuliza mrembo huyo akimaanisha kwanini yupo mahali hapo huku akiweka siraha yake chini na kupumua kwa ahueni
“Clark follow me to St mary’s Hospital! I need you to save someone!”Aiongea akimwambia amfuate mpaka hospitali ya St mary’s kwani kuna mtu wa kumuokoa.
“Kumuokoa mtu?”Alishangaa mwanamke yule alievalia nguo za kulalia lakini kwa mwonekano wa Roma hakutaka kuendelea kuuliza maswali mengi zaidi, alisogelea koti la Burberry kwa haraka na akalivaa n akajiangalia kwenye kioo na kuona yupo sawa.
“Unaweza kunipeleka sasa”Aliongea .
Upande wa hospitalini kwenye chumba cha upasuaji Dokta Giggs alikuwa ameyang’ata meno yake huku akiangalia sura ya Rufi iliopauka akiwa hajitambui.
“Damn it, is she a foreigner?”Aliuliza akimaanisha je sio raia wa nchi hio.
“Mwanaume aliemleta amesema wametokea Tanzania , kwasababu ya haraka hio ndio taarifa iliopo”
“Mambo hayawezi kuwa marahisi hivi , hatuna taarifa zake zote lakini pia ana majeraha ya risasi na yupo kwenye hali hio kwasababu ya kupigwa na bomu”
“Dokta anazidi kupoteza uwezo wake wa kuvuta hewa inabidi tuanze”Aliongea Grace.
“Tumeshindwa hata kunasa presha yake huenda ni kwasababu ya damu kuvuja kwa ndani na hatuwezi kuchukua hatari(risk) wakati sio raia , lakini pia mwanaume aliemleta kakimbia , kama tutamfanyia upasuaji tutalaumiwa kama akipoteza uhai”Aliongea Dokta Giggs na kufanya watu wote kumwangalia kwa mshangao tofauti , lakini hata hivyo walielewa alichokuwa akimaanisha,.
“Hospitali inaweka rekodi ya kila mgonjwa anaeitibiwa hapa na itaharibu taswira kama itafahamika mgonjwa amefia kwenye meza ya upasuaji na isitoshe hatufahamu hata jina la huyu mgonjwa na kwanini ana majeraha ya namna hii , sipo tayari ya kujiingiza kwenye matatizo kama mambo hayatoenda sawa, na nina uhakika kabisa wote wawili hawana hata hela za kulipia gharama za matibabu , kama akifa inabisi sisi wenyewe ndio tulipie gharama zote za matibabu na mnajua kabisa idara yetu haifanyi vizuri kimapato na tutashindwa kujielezea kwa wakurugenzi kwa kupoteza hela za hospitali kwasasabu ya mtanzania ….”Aliongea huku akianza kuvua gloves zake.
“Dokta huwezi kufanya hivi , mgonjwa bado yupo hai na tunapaswa kujitahidi kuyaokoa maisha yake”Aliongea mwanadada aliefahamika kwa jina la Grace, alionekana yeye tu ndio pekee ambaye hakukubaliana na Dokta Giggs na alikuwa na ujasiri wa kusema.
“Grace!!”Nesi aliezeeka aliita kwa namna ya kumtuliza akiwa na hofu kuna ambacho kinaweza kumtokea kwa kubishia maamuzi ya daktari.
Giggs alitoa barakoa yake na kisha akamwangalia Gracke kwa tabasamu lilojaa kejeli.
“You’re the new nurse?”Aliuliza akimaanisha kwamba je yeye ni nesi mpya.
“Dokta Giggs tafadhari usikasirike , Grace ana miaka kumi na nane pekee na yupo ndani ya hii hospitali kwa nusu mwaka pekee , anafanya kazi vizuri lakini bado hana uzoefu wa kutosha”Aliongea nesi aliezeeka.
“Hmph… nina sababu zangu kwa ajili ya kutoendelea na upasuaji wake , ni kupoteza muda wangu tu , kama unataka kuyaokoa maisha yake fanya wewe huo upasuaji na kama huwezi punguza maringo mtoto wa kike , hii ni hospitali na sio kituo cha misaada , Hospitali kama hii inahitai mapato kwa ajili ya kulipa mishahara na kuiendesha pia kihuduma , watu tunaoweza kuwaokoa ni wale wenye uwezo wa kulipia , Kwa umri wako unajua nini maana ya kuendesha hospiali wewe?”
Grace hakuridhika na maneno yake , lakini hakuwa na namna kwasababu hakuwa hata na huo uwezo wa kumsaidia mgonjwa kwani ni nesi wa kawaida.
“Najua wengi wenu mnaweza msikubaliane na mimi lakini lazima tufikirie kimantiki , huyu mgonjwa amepoteza damu nyingi hivyo hawezi kupona , hivyo tusipoteze nguvu zetu na muda kumuokoa , mwambieni yule mtanzania akirudi tumefanya juhudi za kila namna kumsaidia mgonjwa lakini ndio hivyo amefariki”Aliongea na wale wasaidizi wote walitingicha vichwa vyao ,, hata wao wenyewe kwa hali aliokuwa nayo Rufi walijua kabisa kupona kwake ni asilimia kumi tu.








SEHEMU YA 504.
Dokta Giggs alimwangalia kwanza Grace na akamuona anan’gata ng’ata lipsi zake kwa kukosa ujasiri na alitoa tabasamu la kejeli na kisha akageuka na kutoka.
Lakini ile anafungua tu mlango alikumbana na sura za watu wawili , mmoja alikuwa ni mtanzania na mwingine ni mwanamke wa kizungu ambaye hakumgundua mara moja kwa kumwangalia, alikuwa na uzuri ambao ni ethereal na macho yake ya bluu yalikuwa ni ya kustaajabisha.
Kwa uso wake ni kama walikuwa wakiufahamu lakini hawakumkumbuka huenda hawakutaka kuotea, lakini licha ya mwanamke huyo mrembo kuwa katika mavazi ya kihospitali lakini waliamini sio wa hio hospitali.
Daktari aliewafanya kumwangalia kwa mshangao hakuwa mwingine bali ni mtoto wa malkia Catherine afahamikae kwa jina la Clark.
Clark alikuwa akifahamika sana kwa mahospitaloi yote makubwa ambayo yapo ndani ya jiji la London , hivyo mara baada ya kufika hapo ndani alibadilisha haraka mavazi yake na kuvaa Scrubs rangi ya kijani kabla ya kuingia kwenye chumba cha kufanyia upasuaji.
Roma alikuwa ashamwelezea hali ya Rufi wakati wakiwa njiani , hivyo aliingia hapo ndani akielewa kila kitu.
“Giggs are you done with surgery ?”Aliuliza akimuliza dokta Giggs(sio gigi money) kama ndio amekwisha kumaliza kufanya upasuaji.
“Proffessor Clark!!!?”Alijikuta akishituka mara baada ya kusikia sauti yake.
Neno ‘Proffesor Clark’ liliwafanya wafanyakazi wengine wa hospitali hio sasa kuelewa ni kwanini sura ya dokta huyo wa kike alievalia barakoa ilikuwa ikiwajia na kupotea.
Princess Clark kioo cha wanataaluma wengi wa maswala ya kitabibu ndani ya nchi ya Uingereza, hebu subiri , huenda ni dunia nzima.
Giggs alikuwa ni moja ya wanafunzi ambao amefundisha na asingeshindwa kumkumbuka kuokana na kwamba alikuwa vizuri sana kwenye kukariri sura kutokana na akili yake na Giggs alikuwa moja wapo ya wanafunzi wake pendwa.
Na zaidi ya yote Clark alikuwa kama mungu wa kike kwa kila mwanafunzi, alikuwa ni Princess lakini wakati huo akiwa mtafiti namba moja ndani ya jiji lote la London , akiwa vizuri kwenye maswala ya bailojia ya binadamu pamoja na maswala ya siraha za kijeshi.
Alikuwa na vyeo vingi ambavyo hakuna hata mwanasyansi ambaye alikuwa tayari kutaka kulinganishwa nae.
Wote walikuwa kwenye mshngao kwasababu moja , Clark alikuwa ni nadra sana kuonekana hadharani.
Clakr hakufurahishwa na mwonekano wa Giggs kabisa baada ya kumuuliza swali.
“Nipe jibu tafadhari , hali ya mgonjwa ikoje na nini kimetokea wakati wa upasuaji?”
“Uh..teacher … tumefanya kila liwezekanalo lakini moyo wa mgonjwa umeacha kudunda na tayari tulishachelewa kuanza kumfanyia upasuaji kutokana na kupoteza damu nyingi”
“What !!” Roma alihamaki huku akiingiwa na ubaridi usio wa kawaida , ni kama vile amegongwa na nyundo ya utosi , haikuwa kwake tu hata kwa Clark na yeye pia alipatwa na mshangao kwa taarifa hio.
Wale wafanyakazi wengine hakuna alienua mdomo wake kukanusha kauli ya Giggs , waliishia kuinamisha vichwa vyao kwa huzuni, ni kama walikuwa wakiogopa kimwangalia Clark usoni.
“Dokta Clark mgonjwa bado anapumua na hakuna upasuaji uliofanyika , Dokta Giggs alikuwa na wasiwasi kwamba wasingeweza kulipia gharama za matibababu na hakutaka kuchukua risk hivyo akaamua kuacha”Aliongea nesi aliefahamika kwa jina la Grace kwa ujasiri mkubwa na maneno yake ilikuwa ni kama hospitali imepigwa na radi.
Giggs uso wake ulifubaa palepale kwa mshutiko kwani hakutarajia Grace kwenda kinyume na maagizo yake.
“Wewe mwanamke acha kujaribu kukashifu taaluma yangu..”Aliongea akitaka kujitetea lakini Grace alikuwa kama kisiki cha mpingo , moyo wake ulimwambia kumuokoa mgonjwa ndio imani yake na anapapswa kuisimamia.
“Miss Clark I’ve heard about your acomplishments , please save her , she is already at death’s door”
“Bi Clark nimesikia kuhusu mafanikio yako , tafadhari sana muokoe huyu mgonjwa , tayari ashachungulia mlango wa kifo”Grace wa watu mwenye moyo wa kijasiri aliongea na kuwafanya wale wote waliokuwa kimya kama kondoo machinjioni waangaliane wakishindwa kuamini mtoto mdogo kama Grace angekuwa na ujasiri wa namna hio.
Roma palepale alihitaji kwanza kuthibitisha maneno ya Grace , hivyo alitumia mbinu zake za kijini na kisha akam’scan’ Rufi kuona kama bado anapumua na alijiridhisha kwamba yupo hai bado.
Na kwa kupata ufunuo huo kwake ilikuwa sababu tosha ya kumsindikiza Giggs kwanza , alimshikilia shingo palepale na kumnyanyua juu huku akiwa anamkaba.
Giggs ambaye alikuwa kwenye wasiwasi , sasa alijishutikia tu akiwa kwenye kitanzi cha mkono akielea elea huku akipiga miguu huko na kule kama mtu anaekata roho.
“Wewe shetani , wewe ni daktari kweli , leo nakuua mshenzi wewe”aliongea Roma kwa hasira.
“Stop it, this is hospital”
“Acham hapa ni hospitalini”Alifoka Clark
“Hospitalini? Kwahio kama pakiwa hospitalini, ninakwenda kumuua huyu mpuuzi na hakuna wa kunizuia”Aliongea .
“Hii ni hospitalini ukubali au usikubali na mimi kama daktari siwezi kukuangalia ukimuua mtu mbele yangu tena ndani ya hospitali”Aliongea Clark kwa sauti huku akijaribu kumzuia Roma aache kile anachokifanya.
‘Sogea pembeni Clark”
“Sisogei na kama unataka nimuokoe mpenzi wako , acha ukichaa wako”Aliongea na ilikuwa ni kama sasa Roma alielewa alichokuwa akimaanisha na hasira zilishuka palepale na kumrushia kwenye korido nje.
“Roma najua una hasira na kutamani wote wafe na sitojali kama utafanyia nje ya hapa lakini ndani ya hospitali siwezi kuruhusu”Aliongea na kumfanya Roma amwangalie namna Clark alivyosiriasi na aliona alikuwa akichelewa kumukoa Rufi.
“Clark nakuomba tafadhari muda unaenda , nisaidie kumuokoa siwezi kuruhusu mwanamke mwingine akifa chini ya uangalizi wangu’Aliongea na kauli yake ilimfanya Clark kuelewa.
“Nimekuelewa na nnitajitahidi’Aliongea na kisha akazama ndani kabisa na kuvalishwa gauni kwa ajili ya kuanza kumuokoa Rufi.
Roma yeye alitoka zake ili kwenda kuangalia namna upasuaji unavyofanyika upande wa pili huku akimpia Giggs aliekuwa ameshikilia shingo yake akimwangalia Roma kwa wasiwasi.
Wakati Roma akifika mahali ambapo pametengwa maalumu kwa ajili ya wafanyakazi wa hospitalini kuangalia kile kinachoendelea, upande wa ndani katika meza ya upasuaji Clark alikuwa akianza kuwapa maagizo kwa ufasaha kabla ya upasuaji kuanza.
Wataalamu wa ganzi , watalalamu wa mitambo na wasaidizi wote walikuwa wakionekana kuwa bize kusikiliza kila maagizo yanayotolewa na kuyafanyia kazi kwa haraka na baada ya hali kutulia hatimae alianza kazi.
“Scalpel..”Alinyoosha mkono wake kupewa kisu kuanza kuchana lakini mtaalamu wa ganzi alionyesha wasiwasi.
“Dr Clark mgonjwa tayari keshapoteza fahamu na pia amepoteza damu nyingi kama utampasua ..”
“Najua kwamba presha yake itashuka sana hususani kwa damu iliopotea zaidi eneo la tumboni, hivyo kama kila mmoja wenu ataendana na spidi yangu nina uhakika itakuwa rahisi kurahisisha mchakato mzima ,, tupo kitimu hata hivyo , si wote tunakubalina?”Aliuliza na wote walitingicha vichwa.
“So let’s move it , chop-chop”Aliongea na kuwafanya watu wote ndani ya chumba hiko cha upasuaji hali yao kuamka tena na kushawishika kwamba huenda ni vyema kujaribu.
“The patient’s right lower quandrant has seen massive blood loss so to first start off we must first locate the point of injury before we can cut her open ..”
“Mgonjwa upande wa chini wa kulia umeonyesha kupoteza damu nyingi hivyo kabla hatujaanza lazima tutambue ni eneo lipi limeumia kabla ya kupasua”Aliongea Daktari bingwa Clark huku akivuta pumzi nyingi na kuzishusha na kisha akaaanza kazi…………..
“Dokta kapoteza damu nyingi, nakosa ujasiri wa…”Aliongea daktari msaidizi wa kike mara baada ya kuona damu nyingi inayotoka na kumpa ishara ya kuacha hofu.
“Leta spreader na kisha andaa spray ya kusafisha , tutatafuta sehemu iliopata jeraha ..”Aliongea na wakatingisha vichwa kukubali.
Profesa Clark ndani ya muda mchache tu kwa wepesi wa hali ya juu aliweza kufanikisha kuona chanzo cha jeraha ambalo linasababisha damu nyingi kuvuja.
“The patient’s liver is ruptured at three point , S1, S4 and S6”Aliongea akimaanisha ini la mgonjwa limechanika katika sehemu tatu.
“Sehemu tatu?”Walijikuta wakiangaliana kwa mshangao huku wakijikatia tamaa.
“Kama akiendelea hivi hatutoweza kupata muda wa kumaliza kumshona ndani ya muda kwani damu inayovuja katika ini lake itatuletea ukinzani”Aliongea msaidizi..
Upande mwingine nje Roma alikuwa akiona kile ambacho kinaendelea na alikuwa akiomba kila namna Rufi aweze kupona kwani asingeweza kujisamehe kama atapoteza maisha , kwa namna alivyokuwa na wasiwasi hakuwa mfalme Pluto tena yule ambaye kuua ni dakika moja , huyu alikuwa kama binadamu wa kawaida tu ambaye anauguliwa.
“Let us use the patent ductus arteriosus to hold her wound in place !”
“Tutumieni patent ductus arteriosus ili kufanyia kazi majeraha yake”Aliongea Clark mara baada ya kupata wazo.
“Unasemaa..!!”Wote walionyesha kushangaa kama vile hawajamsikia.
“Patent ductus arteriosus”Alirudia.
Timu yote ilikuwa kwenye mshangao kwasababu mbinu hio ya dharula ilihitaji mchakato uchepushaji wa pamoja wa kiumakini wa hali ya juu wa kukata nusu ya mtitirisho wa damu unaoingia kwenye ateri ya ini(hepatic artery) na mshipa wa Cystic(Cystic vein) ili damu isiingie kwenye ini halafu washone majeraha kwa haraka kwa wakati mmoja kwasababu ini limepata majeraha sehemu tatu na kudili na sehemu moja yenyewe ilikuwa ni kazi kubwa na ili mchakato huo ufanikiwe spidi ya hali ya juu sana ya ushonaji inahitajika .
“Tunapoteza muda acheni kushangaa”Aliongea huku akijiamini kile ambacho anakwenda kufanya.
“Hand me the needle kit , thready forty”
“Yes ma’am “
…………….
Kila mmoja alishangazwa na spidi ya profesa Clark , mbinu yake ya kushona kwa haraka iliwaacha mdomo wazi kwani hakutumia nguvu sana, alionekana kuiva kwa kile anachokifanya na ndani ya dakika nne tu alifanikisha kumaliza eneo la kati.
“Blood pressure.!!!”Aliuliza.
“Its out, eighty , sixtty”Aliongea mtaalamu wa ganzi akimaanisha presha ni themanini kwa sitini.
“Nisaidie kushikilia hilo ini , nitaziba sehemu ya tatu”Aliongea na palepale msaidizi aliinua lile ini kujaribu kushikilia lakini walijikuta wakipagawa kwani damu ilifyatuka
“Kwanini kuna damu nyingi inayotoka?”
“Hali sio nzuti , na presha inazidi kuporomoka ,arubaini sasa”Aliongea mtu wa ganzi kwa kupaniki.
“Inabidi kwanza tuipandishe presha na kama jeraha tutaliziba na bado ikaendelea kushuka basi kuna sehemu nyingine imepata jeraha?”
“Kwahio tunatakiwa kufanya nini ?”Aliuliza Grace.
“Allocate the blood funnel, we draw the blood and I will proceed with recycling(Autotranfusion)”Aliongea na kufanya watu wote pia kuchangayikiwa kwani mbinu hio kufanyika kwake ni mara chache na huenda ni mara ya kwanza kufanyika kwenye hio hospitali.
………………..
Ni baada ya masaa kadhaa ya Clark kuonyesha ujuzi wake hatimae aliweza kupata sehemu zote zilizopata majeraha na kuziba kote na damu ilioporuhusiwa kupita tena kwenye ini haikuonekana sehemu inayovuja tena.
“Doctor the patient’s blood presure is now back within normal limit”Sauti ya futaha ilisikika na kufanya kundi lote kupumua kwa ahueni huku wakionyesha furaha zao kupitia macho yao.
Ulikuwa upasuaji uliofanyika ndani ya muda mchache sana na hiko ndio kilichoshangaza na kuona utofauti uliopo kati ya Giggs pamoja na mkufunzi wake.
“Well done everyone “Aliongea kuwapongeza kwa ujasiri waliokuwa nao kumsaidia mpaka akafanikisha na baada ya hapo aligeukia upande wa Roma alipo na kisha akamnyooshea kidole gumba kwamba mambo safi .
Na Roma alijikuta akifurahi na kujiambia Clark hajawahi kumuangusha kila anapopatwa na changamoo kubwa.
“Inaweza kuwa mimi kufeli kwangu mimi kama mkufunzi kwa kuwafundisha maarifa ya kiabibu ila nikashindwa kuwaelesha nini maana ya maadili kama daktari na naamini kupitia tukio la leo mmeweza kujifunza kitu , kama watoa huduma mkumbuke hakuna mgonjwa yoyote ambaye anapaswa kuachwa kufa, mkiwa na mtazamo wenu hupo haitokuwa na utofauti wa kuua mgonjwa mbele ya macho yenu , kama mgonjwa anahitaji huduma na yupo mbele yenu wazo la kwanzo ni kumuokoa na sio kutafuta sababu , kwasababu kazi ya daktari siku zote ni kuokoa maisha kwa mazingira yoyote yale bila kujali aina ya mgonjwa”Aliongea Dokta Clark akijaribu kuwapa shule wale wasaidizi wake.
Mafanikio ya upasuaji huo mgumu uliofanyika usiku huenda ikaacha kumbukumbu kwa wote walioshiriki.
Baada ya kila kitu kumalizika, Clark alimfuata Grace aliekuwa amejikunyata kwenye kona akisinzia kutokana na uchomvu wa kusimama muda mrefu na kisha akamshika mkono.
“Jina lako unaitwa nani?”Aliuliza Clark na kumfanya Grace kushituka kwa haraka huku akiona aibu.
“Naitwa Grace..”
“Grace ni jina zuri mno , ningependa kukushukuru kwa ujasiri ulio uonyesha leo”Aliongea na kumfanya Grace kuinamisha kichwa kwa wasiwasi.
“Hapana daktari , umefanikisha kumuokoa mgonjwa na mimi ni nesi tu..”
“Kama utapenda naomba niwe mwalimu wako kwanzia sasa”Aliongea Clark na kauli yake ilikuwa kama bomu kwa kila mmoa aliemsikia. Grace akiwa mmoja wapo.
Kauli yake iliwafanya kujawa na wivu kwani walielewa nini maana ya kuwa mwalimu chini ya Clark.
Ijapokuwa kimuonekano Grace na Clark wanaweza kuwa katika umri sawa lakini kuwa mwalimu kwa Grace halikuwa tatizo.
Kuwa mwalimu wa Clark haikumaanishaa kwamba kuingia kwenye vipindi vyake akitoa somo chuoni , lakini ilimaanisha kwamba wangeambatana pamoja katika tafiti mbalimbali na kujifunza vitu kwa ukaribu zaidi kama ilivyokuwa kwa Ashley.
“Kama nitakuwa mwanafunzi wako , je nitapata nafasi pia ya kufanya kazi ndani ya hii hospitali?”Aliuliza Grace kwa furaha iliochanganyika na wasiwasi na swali lake lilimshangaza Clark.
“Kwanini unataka kuendelea kubakia hapa?”
“kwasababu nitapamisi hapa na kufanya kazi pamoja na kila mtu na pia napapenda mno , ilikuwa ni kama ndoto yangu kufanya kazi ndani ya hii hospitali”Aliongea kwa sauti ya chini iliojaa aibu na maneno yake yaliwagusa timu nzima na yule nesi aliezeeka alishindwa kuzizuia hisia zake na kutoa machozi ilionekana licha ya kuzeeka alikuwa akimpenda Grace.
“Bila shaka unaweza kufanya kazi hapa na mpaka sasa nadhani tushakubaliana , utakuwa mwanafunzi wangu na siku ambazo upo off utakuja ninakofanyia tafiti au nyumbani kwangu na nitakuwa nakufundisha”
“Really!!?”Grace aliinua kichwa chake kwa msisimko mkubwa wakati akijibu.
“Sure..haha, lakini kama mwanafunzi unatakiwa kuwa tayari na kuwekeza moyo wako wote kwa kile unachojifunza na kama hutofanya vizuri nitakasirika”
“I.. but , I am not smart”Aliongea Grace wa watu akimaanisha kwamba lakini hana akili.
“Kama ungekuwa jiniasi nisingehitaji hata kukufundisha , tabia yako isio ya kichoyo na kumtanguliza mgonjwa kwanza ndio imenifanya nikuone, hata hivyo wewe bado mdogo hivyo kama utaniamini na kufanyia kazi kila ninachokuelekeza nina uhakika utakuwa na kesho inayong’aa”Alimhakikishia Clark.
“Yes doctor Clark I will do my best”Aliongea akimaanisha kwamba atafanya vizuri.
“Umeniita nani?”Aliuliza kwa sauti ya ucheshi.
“Ah..nimesahau namaanisha mwalimu”Aliongea na wote wakacheka na wengine kutabasamu .
Haikuwa tu kwamba Clark alifanya upasuaji wa kushangaza na wa kishujaa lakini pia na bahati ilimwangukia Grace na kupata mwalimu wa viwango.
Waliishia kupompngeza Grace na kumtakia mema katika safari yake ya mafunzo mapya.
Upande mwingine ki asili hakukuwa na haja ya kufikiria sana nini kingempata Giggs kwani kwa tabia alioionyesha ni halali kabisa kupokonywa leseni yake ya udaktari na ndio mwisho wake kutibu na hata hivyo mgonjwa aliemletea dharau ni wa mfalme Pluto ambaye sio kwamba alikuwa na koneksheni bali yeye ndio koneksheni yenyewe hivyo kauli yake moja tu kila kitu kinabadilika.
Hivyo moja kwa moja taarifa zikiwafikia mabosi wa hospitali hio hawatotaka kupewa maagizo mengine zaidi ya kumfukuza.
Baada ya muda mfupi hatimae Rufi alitolewa chumba cha upasuaji na kupelekwa upande wa wagonjwa wa uangalizi wa hali ya juu., Roma mara baada ya kuona angalau hali yake ya ngozi imeimarika alijikuta akivuta pumznni nyingi za ahueni.
“Clark sina maneno halisi ya kuwakilisha shukrani zangu kwako”
“Huna haja ya kunishukuru na kukusaidia nadhani ndio maana nimezaliwa , tokea siku ulipoyaokoa maisha yetu tunaishi kwa kuwa na deni kubwa kwako”
“Unanifanya nione sijaongea kauli sahihi sasa?”Aliongea Roma huku akitoa tabasamu la uchungu.
“Haha.. wakati nilipo ona mgonjwa ambaye natakiwa kumuokoa nilitamani nisiwe daktari ili isiwe jukumu la kuokoa maisha ya mpenzi wako mwingine”
“Hehe.. wewe ndio daktari pekee ninaekujua na kama si vinginevyo nisingemleta huku kwa haraka”
“Muone sasa unajaribu kubadilisha topiki wakati unajua kabisa ninachojaribu kumaanisha”Aliongea na kumfanya Roma kukuna kichwa.
“Anyway… nakushukuru sana na hongera kwa kupata mwanafunzi mwingine ijapokuwa naona maamuzi yako sio sahihi”Alitania.
“Unaongeaje hivyo , Grace ni mkarimu sana na naamini kama nitamfundisha ndani ya miaka ijayo kutokana na tabia yake basi atakuja kuwa daktari mzuri sana , je unakubaliana na mimi?”
“Lakini unafundishaje mwanafunzi ambaye naona kama mnalingana?”Aliongea na kumfanya ang’ae meno kwa hasira.
“Ninarudi kwenda kulala , isitoshe muda umeenda na inakaribia asubuhi , mgonjwa wako anatakiwa alazwe hapa kwa muda ili kupona na siku mbili au zaidi anaweza akaanza kutembea , mhakikishie kwamba mbinu zangu za ushonaji ni za viwango hivyo asihofie kuona kovu”Aliongea na kisha aliwapa ishara ya kwaheri madaktari na wahudumu na kuondoka.
Roma alisimama kwa muda huku akiwa anapumua sasa vizuri na muda huo mawazo ya Mage nchini Australia yalimrudia.
“Kwa mara nyingine tena naomba uangalizi wa mgonjwa wangu , msiwe na wasiwasi nina kiasi cha pesa kingi kuliko ninavyotumia kwahio muangalieni kwa kiwango cha juu kihuduma kwani ninaondoka mara moja”Aliongea Roma.
Rufi aliumia kwa ajili ya kumuokoa yeye na mpaka hapo alijiambia hawezi tena kumpotezea kama Edna anavyotaka na alijiambia akirudi nyumbani atajua namna ya kumalizana na mke wake , lakini kwanzia muda huo na kuendelea Rufi ni mpenzi wake mwingine katika orodha.
Muda huo wahudumu hakuna ambaye alimuona Roma kama mtu wa kawaida , hivyo walimuhakikishia kwamba Rufi angekuwa salama mpaka atakaporejea.
Roma alitoka hapo hospitalini na kisha aliteleport kurudi Australia , muda ulikuwa umeenda na alipokuwa akiingia kwenye anga la Australia muda nao ulikuwa ukikaribia jioni.
Roma alitokeza nyuma ya Mage aliepiga magoi kuelekea baharini akionyesha kama mtu asie na tumaini na kwa haraka haraka Roma alitambua Mage ana Sali , lakini wakati huo huo akilia kama mtoto alietelekezwa.
Roma alijiambia siku zote mwanamke ni mwanamke tu hata kama ni polisi.
“Babe Mage usiniambie umeshaanza kuwa mchungaji?” Aliuliza Roma na kauli yake ilimshitua Mage na kugeuka haraka huku akisimama.
“Hali ya Rufi inaendeleaje ?”Ndio swali la kwanza ambalo alitaka kusikia kutoka kwa Roma.
“Yupo salama kwasasa na Clark amefanikisha kumuokoa kwa kumfanyia upasuaji, atakaa hospitalini kwa siku kadhaa mpaka atakapokuwa sawa”Aliongea Roma na kumfanya Mage kutoa machozi ya furaha.
“Asante Mungu , Asante sana Mungu , asingepona ningeshindwa kujisamehe maisha yangu yote…”Aliongea na kumfanya Roma amvute kwake na kumkumbatia.
Ndio
 
SEHEMU YA 509.

Siku tatu zilipita haraka haraka tokea arudi kutoka Australia, katika siku hizo tatu Roma alikuwa karibu sana na Amina ambaye baba yake amerejea nchini akiwa mgonjwa bado lakini alikuwa mwenye nafuu.

Amina alionekana kuwa mwenye huzuni na kumlaumu baba yake kwa kutokumwambia hali halisi ya ugonjwa wake.

Mzee Kanani alikuwa amegundulika kuwa na saratani ya kongosho ambayo ipo hatua ya pili , ugonjwa ambao ulikuwa ni changamoo sana kwenye uponaji, sasa ilionekeana tokea afahamike kuwa na ugonjwa huo aliamua kukaa kimya na kutokumwambia mwanae Amina na baada ya kuona hana maisha marefu kutokana na kukosa matibabu nje ya nchi ndio akaamua kumwambia ukweli ili ajiandae kisaikolojia kabisa na kumwangaa kama mrithi wa mali zake.

Licha ya kwamba baba yake kuna mambo aliomfanyia ambayo hajaridhika nayo , lakini kwake ndio mzazi pekee ambaye alibaki nae duniani ndio maana alihuzunishwa mno, ilikuwa afadhali kwake uwepo wa Roma kidogo umemfanya kuweza kusharabu kwa haraka taarifa hio.

Roma baada ya wiki moja kupita alifanya maamuzi ya kurejea tena Uingereza kwa ajili ya kumchukua Yezi na kumpeleka visiwa vya wafu kuthibitisha Cauldron alioipata kule kwenye fukwe ya Arafura.

Aliwaaga wanafamilia wake kwamba siku hio angerudi na Yezi hivyo kuwa siku rasmi ya kuungana nae kwa chakula cha usiku na mama yake alifurahi kusikia hivyo.

Aliweza kufika ndani ya hospitali ya St Mary’s katika wodi aliolazwa yezi baada ya kufanya malipo ya matibabu akiamini muda huo atakuwa peke yake, lakini mara baada ya kuingia ndani alishangaa kumkuta Clark akiwa anapiga stori na Yezi.

“Ona sasa aliefika hapa kwa ajili ya kumchukua mpenzi wake , lakini anakosa muda wa kunitembelea na kunipa salamu tu”Aliongea Clark kwa namna ya kulalalma na kauli yake ya neno ‘mpenzi’ ilimfanya Rufi kuona aibu kwani haikuwa ya kweli licha ya kwamba alikuwa akimpenda kweli Roma.

“Naonaga sio jambo zuri kukusumbua na mambo yangu mengi muda wote ndio maana”

“Na mimi nashukuru sana kwa kutonisaidia kuniondolea upweke niliokuwa nao, yaani mtu anaweza afikirie huwa unaniepuka, kama usingenikuta hapa sidhanni kama ungepata nafasi hata ya kunitembelea”Aliongea lakini Roma aliona ni muda sahihi wa kubadilisha topiki , hata hivyo ni kweli asingeenda kumtembelea siku hio , mpango wake ulikuwa ni kumchukua Rufi na kurudi nae tu na kuonana kwao ndani ya hio hospiali ni bahati.

“Haya niambieni kwanza mnaongea nini, daktari na mgonjwa? Maana ni kama mmeshakuwa marafiki sasa”

“Tulikuwa utkiongelea kuhusu maswala vikokotoo na mambo mengine kama hayo ya kimahesabu , inaonyesha dokta Clark anapendelea sana topiki hizo ndio maana , sio tu kwamba ni daktari lakini pia yuko vizuri kwenye maarifa yanayohusiana na vikokotoo ambavyo husaidia katika maswala ya ki udukuzi”

“Upo sahihi , Clark ni jiniasi , maswala ya kidaktari yanaweza kuwa ndio taaluma yake kubwa lakini kila sehemu ameweka miguu”

“Kwanini kama unajisifia wewe mwenyewe na sio mimi?”Aliuliza Clark.

“Hehe.. upo sahihi ni kwamba najivunia kuwa na koneksheni na mtu mzito kama wewe”Aliongea na kumfanya clark kucheka kidogo.

“Nimekuja kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya Rufi , nimemfanyia upasuaji mimi mwenyewe hivyo inamfanya kuwa mgonjwa wangu , mpaka sasa niseme afya yake imeimarika kabisa na ndani ya siku mbili zijazo anakwenda kuwa sawa kabisa , naamini yote haya yamewezekana kutokana na mbinu zako”Aliongea na Roma alitingisha kchwa.

“Upo saihihi , ili mradi anakuwa sawa haijalishi namna ambavyo anapona, lakini mbona unaonekana kama unajiandaa kusafiri?”

“Upo sahihi nasafiri kwenda Marekani, nimepigiwa simu na moja wapo ya wanafunzi wangu juu ya upasuaji wenye changamoto , hivyo akaniomba nihudhhurie nikamsaidie kumwona mgonjwa na nitoe mawazo yangu”

“Nina uhakika hawakuiti tu bure bure , itakuwa wanakulipa pesa nyingi ndio maana upo tayari kusafiri umbali mrefu hivyo?”

“Kwanza kabisa napenda changamoto zinazohusiana na taaluma yangu ili kupata uzoefu zaidi , pili wananilipa ndio ,tena kiwango kizuri ambacho kinanifanya kupata hela ya kuwekeza kwenye tafiti ninazoendeleza , hivyo unaweza kusema ni shinda ni shinde.”Aliongea na kisha palepale alionekana hakutaka kukaa zaidi kwani aliaga na kuondoka.

“Roma kwanini hujamchukua Clark kama mpenzi wako , mimi mwenywe kama mwanamke nimeona anavutia zaidi

, ana akili nyingi , anajiamini , lakini pia uwepo wake tu ni burudani tosha bila kusahau urembo wake, kwanini umejizuia kwake?”Aliuliza Rufi mara baada ya Clark kutoka.

“Ndio , najua pia mimi ni mdhaifu sana mbele ya wanawake warembo lakini kwa Clark ni tofauti , nimekutana na Clark miaka kumi iliopita na alikuwa ni mtoto kabisa hivyo unaweza kusema nilimwangalia wakati akiwa anakua , hivyo haraka haraka unaweza kusema alikuwa mdogo wangu ,kwangu mimi nataka apate mtu sahihi zaidi wa kuwa nae,.. halafu huu sio muda wa kuanza kujadiliana kwani nataka kurudi nyumbani mapema , amka hapo nimekuja kukuchukua ili ukachunguze Caulron kama ni yenyewe na baada ya hapo nikupeleke nyumbani kwani mama yangu na wengine wanasubiria ujio wako ili waweze kutoa shukrani zao kwa kuyaokoa maisha yangu”

“Tulia kidogo basi , nataka kuwaaga manesi wote walionihudumia , nadhani unamfahamu mwanafunzi wa Profesor Clark afahamikae kwa jina la Grace? Alikuwa akinijali sana tokea ulivoondoka hivyo siwezi kuondoka bila kumuaga”

“Nilijua jambo kama hili ushalifanya mapema kabla sijaja hapa”

“Mhmh… unalalamika nini sasa wakati ulikuwa kimya wkati Clark akiwa hapa, mimi bado ni mgonjwa unatakiwa kulifahamu hilo”

“Nisingeweza kulalamika mbele ya dakari wako , lakini ratiba zako ndio zinanifanya nilalaamike ilihali tayari nishakupatia taarifa ninakuja kuchukua leo”

“Kwahio ilikuwa sawa kwako kupoteza muda kwa kuanza kuongea na Clark hapa kupoteza muda , lakini mimi nikitaka kwenda kuaga unaona napoteza muda , wanaume mnasikitisha sana”Aliongea huku akijiweka kwa kuvaa nguo ambazo aliletewa na Clark.

“Basi fanya haraka, isitoshe Clark ni rafiki yangu , na sio kama nilikua nakulalamikia , ila nipo hivyo kwa vipenzi wangu wote, Babe Rufi usikasirike”Aliongea Roma akilegezza sauti na kumfanya Rufi ngozi yake kuwa nyekundu kutokana na kauli ya kuitwa Babe.

“Eww..!! eti Babe Rufi.. huoni aibu?”Aliongea na kisha akandoka ndani ya chumba hiko haraka haraka, alijisikia vizuri sana kuona ameunganishwa akatika kundi la wapenzi na kujawa na mategemeo zaidi ya kile kinachomsubiria katika maisha ya mbeleni.

Katika maisha yake yote hakuna siku ambayo ilitokea akajihisi utamu ndani ya moyo wake kama hivyo.

Baada ya dakika chache za kuawaaga manesi na kuwashukuru kwa huduma za kikarimu

walizomwonyeshea , hatimae walichukuana na Roma na kisha kuondoka kwani Roma alikuwa ashafanya tayari malipo yote yaliohitajika.

Ndani ya dakika chache tu waliweza kutua visiwa vya wafu katika ngome ya Roma, hakushangazwa na namna walivyosafiri kutokana na kwamba alishazoea sana wakati akiwa katika miliki za kijini , kilichomshangaza ni mazingira ya visiwa hivyo na Roma ilibidi kwanza amuelezee kwa ufupi mara baada ya kuingia ndani , lakini Yezi licha ya kupagawa na maelezo hayo hakushangaa sana , kwani hata yeye mwenyewe ametokewa kwenye mazingira ambayo yapo kiajabu ajabu kiasi cha kumfanya mtu yoyote asiamini akimwelezea.

Baada ya nusu saa kuongea hatimae waliwenda moja kwa moja mpaka vyumba vya chini ya ardhi , sehemu ambako Roma alihifadhi mimea waliokusanya kule Australia pamoja na Cauldorn.

“Ulikuwa unaongelea hiki Cauldron?”Aliuliza Rufi mara baada ya kuona kifaa ambacho sufuria sio sufuria wala chungu sio chungu kutokana na namna kilivyotengenezwa.

“Unaonaje , nguvu yake isiokuwa ya kawaida inayotoka , ninaweza kuinasa kwa urahisi sana , naamini kama utaipanga katika Dhana za kijini basi hii inaweza kuwa daraja la kati au la juu”aliongea Roma na kumfanya Rufi kuchuchumaa na kuanza kukikagua.

“Hiki ni Cauldron ndio , lakini mwonekano wake sijawahi kuuona wala kuusikia katika miliki za kijini lakini pia hata mchoro wake haueleweki , kama nitakifananisha labda kinafanana na Taotie , lakini hata hivyo Taotie katika nyaraka inaonyesha tofauti sana na hiki , kama sio

Taotie basi sijui dhana hii ya kijini ilitokea kwenye miliki ambazo hazihusiani na China”

“Jaribu kwanza kuchunguza madini yake , huenda ikawa rahisi kutambua?”Alishauri Roma na kumfanya Rufi aanze kupangusa kutu na kusogelea kwa ukaribu zaidi na alijikuta akitoa mshangao.

“This is ethereal hyacinth gold”Aliongea Rufi kwa mshangao akimaanisha kwamba chungu hiko kimetengenezwa kwa madini ya dhahabu aina ya hyacinth.

Hyacinth ni aina ya dhahabu ambayo rangi yake ni kama imetoka kuwa njano na kuwa shaba , ni dhababu ambayo imechanganyika na madini mengine ili kuifanya iwe na ugumu wa kiwango cha juu.

“Hyacinth Gold, mbona unaonekana kama vile ni madini ambayo ni adimu , wakati kama kumbukumbu zangu ziko sawa Urusi wanayo aina hio ya dhahabu?”Aliongea Roma.

“Hapo si ndio mwisho wa ufahamu wako, sasa kuhusu aina hii ya madini , yanaitwa ethereal hyacinth gold kwasababu maalumu (ethereal ni sawa na kitu adimu kisichokuwa cha kawaida).

“Katika ngano za miliki ya kijini inasemekana wanyama wakubwa wa enzi hizo wanapokufa maiti zao pamoja na mifupa hugeuka kuwa madini haya baada ya miaka elfu kumi , ni ngano ambazo zipo kwa muda mrefu na zimesambaa mpaka katika baadhi ya mila katika ulimwengu wa kawaida,, sasa kuhusu aina hii ya dhahabu mara nyingi ni adimu sana kuiona , na dhahabu zote za rangi ya shaba unazoona nni kutokana na mchanganyiko wa madini mengine , kwenye maisha yangu nimeshuhudia kisahani kimoja tu tena ujinini kilichotengenezwa na madini haya katika hali safi na asilia , sasa hebu jiulize wewe una Chungu kikubwa kama hichi kilichotengenezwa kwa madini hayo adimu , unafikiri miliki yoyote ya kijini ikifahamu watakuacha salama?, lazima mtaingia kwenye vita”

“Kwahhio unachomaanisha ni kwamba kutengeneza vidonge kwenye hiki chungu , vitakuwa vya viwango si ndio?”

“Upo sahihi , lakini sijawahi kusikia Cauldron ambayo imetengenezwa kwa dhahabu hii adimu lakini naamini kabisa ni nguvu sana kuyeyuka na moto wa rangi nyeupe(pure fire)

Moto mweupe unaozungumziwa ni tofauti sana na ule wa gesi wa nyumbani kwani ule una mchanganyiko kidogo na rangi ya bluu , moto mweupe ni mweupe kabisa ambao ni msafri usiokuwa na moshi hata kidogo na mara nyingi moto huu ni ngumu sana kutenganishwa , ijapokuwa moto wa bluu unaweza kuwa na joto kali mpaka kufikia nyuzi 1600 lakini unakosa sifa ya ‘pure’ hivyo katika miliki za kijini wanaamini moto mweupe ndio ungamanisho na nafsi zao na ndio ambao upo kiroho zaidi.

“Kama maneno yako ni sahihi na kina uwezo wa kuhimili moto mweupe je kimetengenezwaje?”Aliuliza Roma.

“Kwanza kabisa hii ndio mara yangu ya kwanza kuona Cauldron ya namna hii ila nina uhakika sio kwamba hakiwezi kuyeyuka kama tutaweka kisayansi zadi, lakini ukija kiroho ni ngumu sana kukiyeyusha kwani kina maungamano ya nafsi kali za enzi na enzi tena za wanyama wakubwa ambao ni hatari”Roma alionekana kuelewa kiduchu lakini kwasababu alimuona Rufi kukosa maelezo sahihi ya kuelezea jungu hilo aliona asiulize zaidi kwani muda unapotea.

“Unaonaje ukanisaidia kupangilia mimea ambayo tuliipata kimakundi , nataka kesho nirudi kujaribu kutengeneza vidonge nione kama naweza fanikisha, nyumbani watakuwa wanasubiri ujio wako hivyo lazima tuondoke mapema”

“Kwahio ulikuwa ukimaanisha kwamba leo hii ndio napaswa kujumuika na familia yako katika chakula?”Aliuliza na Roma alitingisha kichwa. “Kwanini tusivute vute siku , bado najihisi sipo tayari kwenda kuonana nao”Aliongea na kumfanya Roma kufikiria kwa muda.

“Kama ni hivyo basi , hakuna shida, nitawapigia simu ili kuwaeleza nadhani wataelewa”

Rufi alikuwa akihofia kwani mpaka muda huo alijua kabisa hataenda nyumbani kwa Roma kama Rufi wa mwanzo ,bali mahusiano yake na Roma yamepiga hatua hivyo bado alikosa ujasiri hasa mbele ya Edna.

Baada ya kukubaliana Roma ilibidi kwanza afanye mawasiliano nchini Tanzania kuwaeleza kwamba hatoweza kurudi kwa muda wa siku mbili kwani kuna kazi anaifanya na kwasababu hakuwa akiomba ruhusa baada ya kujielezea hakuhitaji ruhusa kutoka kwa mke wake, kwani baada ya Edna kuitikia kwa neno ‘okay’ bila nyama nyama alikata simu.

Rufi alimwaga mimea yoe waliotafuta katika nyika ya Arnhem na kuanza kuipanga kutokana na aina ya vidonge ambavyo wanatarajjia kutengeneza na ndani ya masaa mawili walikuwa wametenganisha mimea katika makundi matatu , yaani mimea ambayo ingetegneneza vidonge vya daraja la kwanza , la pili na la tatu.

Daraja lwa kwanza vilikuwa ni vile ambavyo mara nyingi mtu anapotumia humuingizia nguvu ya ajabu ambayo hufanya akili yake kuwa tulivu mno kama vile mtu ambaye ametumia madawa ya kulevya kwa kusudi la kuona picha flani la kufikirisha , vilikuwa vinasaidia sana mtu kukusanya nishati ya mazingira.

Kundi la pili ni vya kumsaidia mtu kumbusti uwezo wake ili kuweza kupata ufunuo wa mbingu na matumizi ya elementi za dunia kwa kupitia tahajudi na kundi la tatu sasa hivi ndio ambavyo Roma alipaswa kutumia yeye , ni vidonge ambavo vinasaidia mtu kuvuka levo kwa haraka.

Baada ya makusanyo hayo ya mimea , hatua iliofuata kwanza ni Roma kuanza kujua namna ya kutumia

Cauldron hiyo ya madini ya dhahabu rangi ya shaba.

Katika utengenezaji wa vidonge katika miliki za kijini ni kubadilisha mmea katika mfumo wa majani kwenda kiroho zaidi , hivyo Roma angepaswa kwanza kudhibiti Cauldron kwa kubalansi joto la moto mweupe na kisha mimea hile ndio aitupie kwenye jungu hilo.

Haikuwa chungu cha kawaida na ndio maana hata mbinu zake za utengenezaji wake wa vidonge haukuwa wa kawaida, kwani Roma alipaswa kudhibiti joto lake na kutupia ile mimea na baada ya hapo vidonge vingejitengeneza vyenyewe na kubakia chini kama chembechembe ambazo angekusanya na kufanya ziwe kidonge.

Sasa Roma alikikalisha chimi kile chungu na baada ya hapo Rufi akasogea pembeni na yeye akakaa chini kama vile anafanya Tahajudi na hatua ya kwanza alikusanya nguvu za kimaandiko na kuzituma kwenye kile chungu ili kuunganisha akili yake na kile chungu cha kichawi.

Baada ya hapo angeruhusu nguvu zake za kijini katika kiwango chote cha juu cha levo ya kuipita dhiki na kisha angeanza kudhibiti sasa moto kwa kubalansi nguvu ya kijini iliokuwa kwenye kibofu , moyo na figo.

Sasa Roma baada ya kufuata hatua zote hizo na kuanza kufanya kazi ghafla tu kilianza kutoa moto ndani yake kwa kuanza na wa rangi ya njano na bluu na baada ya Roma kuweza kusafisha na kubakiza moto wa mweupe kile chungu kilielekea hewani kwa namna ya ajabu mno huku kikianza kufoka kwa sauti zizizokuwa za kawaida , lakini muda huohuo Roma alihisi ni kama mwili wake unaingiliwa na nguvu ya ajabu mno ambayo palepale iliteka akili yake na akawa hajitambui tena, ni kama vile yupo ndotoni kwenye ulimwengu usiokuwa wa kawaida huku yeye mwenyewe akiwa kama mnyama anaefanana kama vile ni Dragon , ambalo linatema moto wa rangi nyeupe.

Roma alijitahidi kudhibiti akili yake kwa kuurudisha ufahamu wake , lakini kadri alivyokuwa akijitahidi alishindwa kabisa na katika ndoto aliona ndio kwanza yeye akiwa katika umbo la mnyama wa kutisha akikasirika zaidi na zaidi na kupaa angani huku akikausha kila kiumbe anachoona chini yake.
Amen
 
SEHEMU YA 510.

Hakikuwa chungu cha kawaida kabisa na huenda Roma asingekuwa na uwezo mkubwa wa nguvu ya kimaandiko basi akili yake ingekamatwa kabisa na akageuuka kuwa binadamu mwenye nafsi ya mnyama.

Kwa haraka haraka kama ingetokea mtu ambaye mafunzo yake ya kijini yalikuwa kwenye levo ya Nafsi huenda ufahamu wake ngetekwa kabisa , lakini Roma kwasababu nguvu yake ilikuwa kubwa kuliko Jungu hilo basi aliweza kufanikisha kurudi kwenye hali yake ya kawaida baada ya baada ya nafsi yake kushinda.

Roma mara baada ya kushinda pambano la nafsi palepale kile chungu kiilipotea kwenye hewa na ndio wakati ambao alifumbua macho.

“Rufii…!!”Roma alimwita Rufi baada ya kumkosa mbele yake huku akihofia huenda kitu kibaya kimempata kutokana na yeye mwenyewe fahamu zake kutekwa kwa muda , lakini mara baada ya kugeka nyuma alimwona Rufi ambaye alikuwa amejificha kwenye kona akiwa amepauka kwa woga.

“Ooh ..Asante Mungu uko sawa”Aliongea Roma huku akivuta pumzi na kuzishusha kwa ahueni.

“Umeona nini na chungu kiko wapi?”Aliuliza kwa shauku na Rufi alijikuta akimeza mate mengi na kujirudisha katika hali ya kawaida kwani alionekana kuwa katika hali ya mshangao na mshituko.

“That… cauldron ..i’m afraid isn’t an ethereal hyacinth gold”Aliongea akimaanisha kwamba jungu hilo la kijini sio kama alivyofikiria kuwa ni la madini ya dhahabu yanayokaribia rangi ya shaba.

“Unamaanisha nini?’Aliuliza Roma akiwa kwenye mshangao wa kuchanganyikiwa.

“Baada ya chungu kukutana na pure fire ndio kilijidhihirisha na kunifanya nitambue sio kama nilivyofikiria , nahisi ni zaidi ya chungu cha dhahabu , kama fikra zangu zinaweza kuwa sahihi basi kinaweza kuendana na immortal item aina ya dhana ambazo ni adimu sana katika miliki ya kijini.”Aliongea na kumshangaza Roima.

Immortal item?”Aliuliza Roma huku hisia zake zikimwambia huenda ikawa Dhana ya kijini ya thamanni kubwa.

“Umejuaje ni immortal item?”.

“Mwenyewe sifahamu lakini ninachoelewa ni kwamba Dhana ya aina ya immortal zina upekee wake , maarifa ya kijini yanaeleza kwamba ni dhana ambazo zimeunganishwa na nafsi au roho za wanyama wakubwa ambao walitokea enzi kubwa za kale na kwasababu hio kama utataka kukiyeyusha, lazima kwanza uvunje nguvu yake ya kiroho ilioshikiria nafsi za mnyama huyo na kadri mnyama anavyokuwa nkubwa zaidi ndio nguvu yake huwa kubwa zaidi”

Immortal item ni dhana za kijini za kale sana ambazo inasemekana maisha yake ni marefu, ni vifaa ambavyo vinadumu pasipo ya kupotea au kuharibika kwa muda mrefu sana , sasa vifaa hivi vimetengenezwa na madini lakini madini ambayo yameungamanishwa na roho za wanyama(Beast) wakubwa waliowahi kutokea duniani mfano wa mnyama kama Dragoni.

Maelezo ya Rufi yalikuwa yakiendana kabisa na kile Roma ambacho alikishuhudia kwenye ndoto , aliona mnyama mkubwa ambaye alishindwa kumtambua , mnyama ambaye alitaka kuivaa roho yake na kuutawala mwili wake.

“Kuna jambo lingine pia , Dhana kama hizo huwa zinatabia ya kuchagua nani anaweza kumiliki hivyo sio watu wote ambao wanauwezo wa kuvimiliki na kuviendesha na pale kinapopata mmiliki basi kitakuwa kama mtumwa kwako na kufanyia kazi maagizo yote kadri ambavyo mmiliki atakavyoendelea kuishi”

“Inaonekana nimebahatisha kitu cha thamani kweli?”Aliongea Roma huku akitabasamu.

“Ndio umebahatisha, aina hio ya Cauldron naweza kusema huwezi kuikuta kabisa katika miliki za kijini na cauldron ambazo unaweza kukuta haziwezi kuwa na nguvu kama ilionyesha hapa , jambo moja la kuzingatia ambalo linaweza kuwa la faida kwako ni kwamba hii dhana ikishakuchagua basi moja kwa moja inaungana na roho yako , hivyo kadri unavyopanda levo na yenyewe inapanda levo vilevile na kuwa kali zaidi na kama fikra zangu zipo sahihi kupotea kwake ni uhakika wa kwamba kishaungana na nafsi yako na muda wowote unaweza kukiita na kikafanyia kazi maagizo yako”Aliongea Rufi na kumfanya Roma kujawa na msisimko zaidi.

Cauldron haikuwa dhana ya kawaida kabisa, licha ya kwamba mwanzoni Roma alitafuta kwa ajili ya kutengenezea vidonge lakini kazi yake haikuwa kutengenezea vidonge tu , ni Jungu ambalo linatumika kumeza nafsi dhaifu.

Hivyo kwa lugha nyepesi ni siraha ya hatari sana kwa majini ambao wapo kwenye levo ilio chini ya Roma au waliopo kwenye levo sawa na yeye ambao hawana kinga , kama watakutana na mdomo wa Jungu hilo basi ni hakika watamezwa.

Sifa yake nyingine ni kwamba mdomo wake upo kama shimo jeusi(black hole) , yaani shimo ambalo linavuta kila kitu kilichopo karibu yake na kumeza palepale , ilikuwa ni makosa kufananisha chungu hicho na vyungu vya kawaida kwani chenyewe ni roho ya mnyama hatari ambaye yupo katika mfumo wa Chungu, hivyo Roma mara baada ya kukiingizia moto mweupe ni kama amefanya kukiwasha(activate) na kubadilika kutoka kuwa chungu na kuwa Jungu sasa la ajabu.

“Naamini nikikutana tena na yule bwana mwenye maski lazima atanitambua , nitamfanya roho yake kumezwa na chungu changu”Aliongea Roma huku aking’ata meno kwa hasira , alionekana kama mtu ambaye alitamani wakati akiwa anapambana na mtu yule awe na hiko chungu.

Roma palepale alijaribisha kukiita kwa kunuia tu na kikatokezea tena hewani kikifuka moto wa rangi nyeupe(pure fire), Rufi aliishia kushangazwa na jambo lile licha ya kwamba ni mara ya pili kuona , lakini bado hakuwa amezoea kabisa.

“Babe Rufi nikipatie jina gani hiki chungu changu?”Aliuliza Roma.

“Unaweza kukipatia jina lolote unalotaka , hata hivyo sio kwamba kina ufahamu kwani roho iliofungamana nacho ni ya mnyama”

“Unaonaje nikikiita , Jungu akili, bingwa na kiboko ya majini?”Aliuliza Roma huku akicheka kifedhuli.

“Acha kuongea pumba na tuanze kazi ya kujaribu kutengeneza vidonge”Aliongea Rufi huku akikaa chini kiwasiwasi maana Jungu hilo kwa namna linavyotoa msisimko na sauti kama ya mnyama ilimuogopesha.

Kwa mara ya kwanza Roma alifanikisha kutengeneza vidonge tena havikuwa vidonge vya kawaida , bali vilikuwa ni vidonge vyenye ubora wa hali ya ju, kiasi kwamba aliona haitofaaa kuviita vidonge vya Poya , hivyo akaamua kuvipatia jina ambalo aliona linafaa katika kichwa chake , ili kuendana na ubora wake.

Alitumia mimea yote walioweza kukusanya ndani ya bara la Australia mpaka ikaisha , lakini licha ya hivyo Roma bado hakuridhika kabisa na alijiambia ni kheri akaenda tena kutafuta mimea mingine ili kuendeleza kazi.

Alikuwa na mpango kumalizana kabisa na utengenezaji wa vidonge kabla ya safari yake ya kuelekea Korea haijaanza rasmi.

Roma alishauriana na Rufi kwenda kutafuta tena mimea katika maeneo mengine ambayo hawajaenda na Rufi kwasababu alikuwa akitaka kuwa karibu zaidi na Roma alikubali mara moja na safari yao ikaanza , na mpango wa kwanza ilikuwa ni kwenda msitu wa Amazoni , wakiwa na uhakika ndani ya msitu huo wangefanikisha kupata kile wanachokitafuta.

Roma hakuwa na wasiwasi tena kuhusu kushambuliwa kutokana na kwamba kujiamini kwake kuliongezeka mara dufu mara baada ya kupata Chungu cha ajabu ambacho kilikuwa na nguvu ya kumsaidia kupambana na maadui zake.

Kutokana na msitu kuwa mkubwa mno na kutopatikana kwa haraka mimea waliokuwa wakihitaji iliwachukua siku zaidi ya nne ndani ya msitu huo.

Roma hakuwa na wasiwasi , kwani alishampigia simu mama yake kwamba anaelekea Amazoni hivyo angechelewa kurudi nyumbani.

*********

Ni alhamisi mchana nchini Tanzania katika makao makuu ya kampunni ya Vexto kulikuwa na kikao cha watendaji wa juu wa makampuni ya Vexto , kikao ambacho kilikuwa kikiongozwa na Edna mwenyewe.

Ndani ya ukumbi huo wa mikutano kulikuwa na kimya cha muda mrefu huku wanaume na wanawake waliovalia suti wakimwangalia CEO ambaye alikuwa ameshikilia karatasi na kuzisoma, ilikuwa ni kama kuna maamuzi ambayo wanasubiria kuyasikia kutoka kwake.

Kila mmoja alimwangalia Edna kwa mawazo tofauti , hususani namna mwanadada huyu mwenye umri mdogo jinsi ambavyo amefanikisha kuipaisha kampuni ya Vexto.

Kwa wale wamama ambao tayari wana watoto wa kike wenye umri wa Edna walitamani angalau watoto kufikia nusu ya uwezo wa Edna.

Nasra na Dorisi pia walikuwa ni moja wapo ya wafanyakazi waliohudhuria katika kikao hiko kama viongozi wa juu wa kampuni na walikuwa wamekaa upande wa kulia na kushoto karibu na alipo Edna na wote walikuwa wakimwangalia kutoa mawazo yake mara baada ya presentation(uwasilishaji iliotolewa na mkuu wa idara ya Quality Assurance.

“CEO is there anything you are dissatisfied about?”Nasra aliamua kuvunja ukimya mara baada ya kumuona Edna hatoi mawazo yake ilihali kila mmoja alikuwa akimsubiria yeye.

Ukweli ni kwamba katika wiki yote hivyo Nasra alimuona kabisa Edna hakuwa yule ambaye amemzoea , alionekana kama mwanamke ambaye alikuwa na mawazo.

“Nothing much , I am aware that the profit of this project are viable , but it involves venturing ino uncharted territory…..”

“Naelewa kwamba faida ya mradi huu inawezekana lakini ni swala la kujitosa katika eneo ambalo halitambuliki….., kwasasa umakini wetu tumeulekezea kwenye mradi wa Adani na pia katika maswala ya fasheni , huu mradi unahusisha uwekezaji mkubwa kwanzia matayarisho yake mpaka kukamilika, hivyo kwa maoni yangu nadhani tuendelee kuangalia kwanza namna hali ilivyo kuliko kuingia moja kwa moja , haya ni mawazo yangu tu hivyo nitaacha kila mmoja atoe mchangao wake ili kufikia makubalino…”Aliongea na kisha akapumua kidogo.

“I hereby annaounce to those who are in favour of our collaboration with the Hanson enterprise and BMW group for this project please raise your hands”

“Natakangaza kwa wale ambao wanaunga mkono ushirikiano na kampuni ya Hanson na BMW GROUP kwenye hii projekti wanyooshe mikono”

Hakuna ambaye alinyoosha mkono kwani tayari Edna ashatoa mawazo yake , hivyo hawakutaka kumpinga wazi licha ya kwamba ushirikiano wa kibiashaa na kampuni ya BMW ukanda wa Afrika mashariki ungekuwa na faida kubwa na sio hivyo tu ungeipaisha Vexto zaidi kibiashara , lakini licha ya hivyo hawakutaka kupiga kula ya ndio walikuwa washaelewa kwanini Edna alianguliza kutoa mawazo yake na kisha akaanzisha upigaji kura , katika siku za nyuma Edna sio mtu wa kukosa maamuzi, kama mradi ungekuwa na faida kwake basi angeukubali moja kwa moja ama kukataa na hakuna wa kupinga mawazo yake , lakini siku hio ilikuwa tofauti.

Nasra alijikuta akiangaliana na Dorisi na kutafsiri kitu kuhusu Edna na walijua huenda Edna maamuzi yake yameathiriwa na maswala yake binafsi.

Walikuwa wakifahamu Hanson na Edna walikuwa na ukaribu ambao ulianzia chuoni lakini hawakuwa wakifahamu kama Roma alikuwa akielewana vibaya na Mzungu Hanson.

Upande wa Edna ni kweli dili lilikuwa nono, lakini aliamini kama angekubaliana nalo basi asingeweza kuzuia ukaribu kati yake na Hanson, hivyo ili kuepusha mgogoro na mume wake , aliona bora apotezee tu dili hilo.

Baada ya Edna kuona hakuna ambaye alikuwa akipingana na mawazo yake , hatimae alihitimisha kikao na kila mmoja akaondoka, hivyo rasmi ikawa imejulikana kwamba ombi la biashara kati ya kampuni ya Vexto na kampuni ya BMW limekufa rasmi.

“Edna nimeona ulivyokuwa kwenye kikao na hisia zangu zimeniambia sio maswala ya kibiashara yaliokufanya ufanya maamuzi ya aina hii?”Aliongea Nasra bala baada ya kumfuata Edna ofisini kwake.

Edna baada ya kuulizwa hivyo alijua kabisa hana sababu ya msingi , hivyo hakuwa na haja ya kumficha Nasra.

“Nadhani unajua kwanini nimefanya maamuzi haya”Aliongea kwa sauti ya chini na kumfanya Nasra kucheka.

“Naona umemkumbuka sana mumeo , lakini sio kwamba ni mara yake ya kwanza kusafiri , sikudhania kwamba mahusiano yako yanaweza yakaingilia utendaji wako wa kazi.. , sio kwa Edna ninaemfahamu mimi, kipinid cha nyuma licha ya kwamba ulikuwa kwenye majonzi ya kufiwa na mama mzazi , lakini bado uliweza kuongoza kampuni vizuri na kuipitisha katika kipindi cha mpito , lakini sasa hivi ni Roma ambaye amesafiri na Rufi peke yao imekufanya uathirike namna hii kweli!”Aliongea Nasra na kumfanya Edna kukosa jibu.

Ulikuwa ukweli mtupu kitendo cha Roma kuwa nje ya nchi akiwa na Rufi lilimfanya kukosa utulivu wa akili mno , alihisi wivu wa kiwango cha juu kiasi cha kumfanya utendaji wake wa kazi kupungua.

Yule Edna ambaye muda wote alikuwa akijali biashara ru alikuwa ni kama amepotea kwenye macho ya Nasra , dili la kibiashara ambalo liliwekwa mezani na Hanson hakuna mtu yoyote ambaye ni mpenda faida akalikataa , kwa Edna hata yeye alijiambia kama mtu ambaye anakwenda kufanya kazi asingekuwa Hanson basi angelikubali na biashara ikaendelea.

“Inaonekana mwanamke mfanyabishara makini tuliekuwa tukimfahamu kwasasa amekuwa mke kweli anaefikiria nyumba yake muda wote”

“Nasra naomba uache”Aliongea Edna ambaye hakutegemea Nasra kuongea hivyo kuhusiana na namna mpya ya maisha yake.

“Sawa nitaacha , najua una mawazo yako mengine lakini kwasasa unaonaje tukienda mpaka chini nje upande wa pili angalau kupata keki , najua huna mpango wa kusubiria chakula cha usiku moja kwa moja kama mimi”Aliongea na kumfanya Edna akubali , alikuwa akipenda sana kula keki hivyo mara baada ya kutajiwa na Nasra hamu ilimvaa hapo hapo na aliona inafaa kuongozana kwani wangenunua keki moja na kushirikiana kula.

“Nisubiri niweke vizuri vitu vyangu halafu tuondoke”

*********

Upande mwingine , nyumbani kwa Roma alionekana Blandina mama yake Roma akiwa ameketi kwenye masofa huku mkononi akiwa ameshikilia kalenda ya familia, baada ya kuangalia tarehe aligundua siku ya kesho ilikuwa ni sikukuu ya Eid kama mwezi ungeandama , lakini pia siku hio hio ya kesho katika kalenda ya kifamilia ilionyesha ni siku ya kumbukumbu ya tarehe kifo cha bibi yake Edna.

Tokea Marium bibi yake Edna kufariki ulianzishwa utaratibu wa kifamilia wa wa kuzuru kaburi lake na hata wanafamilia walikuwa wakifanya kazi nusu siku au kutokwenda kabisa kazini..

Baada ya Blandina kuona tarehe hio alifikiria jambo na kisha akamgeukia Bi Wema ambaye alikuwa akimfundisha Qiang Xi kuongea kiswahili.

“Wema nadhani kesho itakuwa jambo zuri kama nitamsindikiza Edna kwenda kutembelea kaburi la mama yake , lakini pia sio mbaya kama tutaungana na waislamu kusheherekea sikukuu ya Eid , hivyo naona ni vizuri kama nitaenda sokoni kabisa kwa ajili ya kununua mahitaji, najua Roma anaweza asirudi leo usiku kama ilivyopangwa lakini kesho lazima atarudi , hivyo ni vizuri kujiandaa mapema”Aliongea na kumfanya Bi Wema kufurahishwa na namna ambavyo Blandina alikuwa makini kwenye mambo madogo ya kifamilia, alikuwa ashasahau kama siku ya kesho ndio ambayo Edna alipaswa kutembelea kaburi la Bibi yake pamoja na mama yake.

“Nadhani sio mbaya kama tutamkumbusha Edna kwa njia ya simu”

“Anaweza kuwa bize muda huu , haina haja ya kumsumba kwa kumpigia kuna mzigo wangu nitaufuata posta hivyo nitampitia ofisini kwake ili angalau nione na mazingira anayofanyia kazi”Aliongea Blandina na kumfanya Bi Wema kutabasamu na kuona ni wazo zuri.

************

Edna na Nasra waliweza kufika ndani ya mgahawa uliokuwa upande wa pili wa jengo hilo la kampuni na kisha wakachukua keki moja na juisi ya matunda na kwenda kukaa upande wa dirishani kabisa upande wa barabara.

Nasra alionekana na yeye kupenda keki zenye sukari kama Edna tu na wakati akiwa kipande cha pili Edna alikuwa cha kwanza

“Hakika malkia uko ligi tofauti na sisi masuria, hata kwenye ulaji wa keki?”Aliongea Nasra akimtania Edna kutokana na kula keki kipole sana lakini kauli yake ilimfanya Edna kushangaa kwani ni kama hakuitegemea

“Nasra huoni kuongea hivyo si vizuri?”

“Kwanini sio vizuri?”

“Unajua kwa muda mrefu nilikuwa najiuliza maswali , kwa mfano kwa mwanamke kama Rose kutokana na namna alivyolelewa ni sawa tu kuwa na mwanaume bila ya kutegemea kuolewa na asione shida , lakini kwa wewe. Mage Dorisi na wengine mngechagua maisha mengine mazuri zaidi , kuliko kuwa katika mahusiano yasio na malengo, najua naweza kuonekana labda ni mkatili lakini angalau napaswa kuwa mkweli , siamini kama kuna kitu kikubwa ambacho mnaweza kukipata kwenye mahusiano haya mnayo endelea nayo”Aliongea Edna na kumfanya Nasra furaha yake kupotea na alishika glasi yake na kunywa kidogo juisi kwa kutumia mrija.

“Edna ni kwamba unanionea huruma au unaniona kama mwanamke niliepotea?”

“Sijamaanisha hivyo , siku zote nimekuwa mwenye kuamini maamuzi yako na tumefahamiana kwa muda mrefu sana, na nilichokuuliza ni swali nililokuwa nalo kwa muda mrefu sana”

“Kwa swali hili naaweza kusema ndani ya moyo wako unatuchukia na kumchukia Roma pia , si ndio?”

“Vipi kuhusu wewe , nadhani lazima ufikirie hivyo kwani mwanaume unaempenda ndio huyo huyo ambaye amenioa mimi , haijatokea siku ukanichukia kwa sababu hio?”Aliuliza Edna.

“Nadhani sasa nimepata majibu kwanini wiki hii yote ulionekana kukosa utulivu , wasiwasi wako upo kwa Rufi ,unaogopa Roma anaweza kuleta mwanamke mwingine kama mpenzi wake.

“Hapana sio kwamba nina hofu , anaweza akafanya kile anacho taka na sio kwamba nina uwezo wa kzmzuia”

“Unadanganya , unaonyesha kabisa umechukia”Alikandamiza zaidi Nasra

“Hata kama nimechukia unahisi nitafanyaje , vipi kuhusu wewe huna hofu kwa yeye kuongeza wanawake wengine zaidi , au ni kwasababu sio mume wako , unafikiri hayo ni mapenzi kuona sawa tu akiongeza michepuko kadri anavyojisikia?”Aliongea Edna huku sauti yake ikionekana kama ya kulalamika , ni kama alikuwa akimlaumu Nasra kuwa na mahusiano na Roma na wanawake wengine.

“Edna umebadilika sana , sijawahi kudhania unaweza kutia huruma kiasi hiki”Aliongea Nasra huku akionyesha kama hasira zinaanza kujitengeneza.

“Nataka unipe jibu la swali langu?”

“Unajua nini , nilikuwa nikikuonea wivu sana wewe ni mrembo kuliko mimi na hata kipindi ambacho mume wako alikuwa na wanawake wengi nje hukuonyesha ishara yoyote ya kuathirika kwasababu uliamini kila kitu kipo chini ya kiganja cha mikono yako , unajua nini kipindi chote hiko kwangu wewe ulikuwa kama mwanga, namaanisha kila saa nilipofikiria namna ulivyo ilinifanya niyachukie maisha yangu , nilijua siku zote nitakuwa wa pili na sio kwangu tu hata kwa Rose na wengine wote hakuna ambaye anaweza kukutoa katika nafasi yako”

“Edna hivi unadhani naendelea kubakia kwenye hii kampuni kwasababu nina deni la kulipa kwa yale ambayo mama yako alinifanyia? Hapana , naijua thamani yangu na huenda mpaka sasa ningeshaondoka kwenye kampuni na kwenda kwenye kampni nyingine kufanya kazi au kuanzisha ya kwangu , nimekaa ndani ya kampuni ya Vexto kwasababbu yako sio mtu mwingine , ulinihakikishia kwamba Vexto ndio sehemu ambayo natakiwa kuwepo , hata kama inaleta kashkashi na uhusiano wangu na Roma lakini licha ya yote niliona hapa ndio sehemu ambayo napaswa kubakia ili kukupa sapoti”Ijapokuwa alikuwa akiongea kwa sauti ndogo lakini alionyesha kuongea kwa hisia na usiriasi wa hali ya juu.

“Edna ambaye namwangalia kwasasa naona kama ni mgeni mbele ya macho yangu ,Edna ambaye anaogopesha kwa ukauzu wake , mwenye kujiamini na mwenye maamuzi naona kama hayupo tena , ninachokiona kwasasa ni Edna ambaye muda wote anajishtukia na mke ambaye anajichukia yeye mwenyewe”Aliongea na kisha akasimama na kuchukua pochi yake.

“Edna nimekuja kugundua jinsi ulivyokuwa mjinga , hauna taarifa zote za wapi unaelekea na bado hujajua maana halisi ya maisha, hujaishi wala hujakaa kuyafurahia maisha kwasababu bado huelewi maana ya maisha nini , acha kulaumu kwa kutoridhika kwako , kujishtukia kwako sio kosa letu wala sio kosa la Roma bali ni wewe mwenyewe.

Mahusiano sio kama kitabu kwamba ukisoma utaelewa , bali unatakiwa kuruhusu hisia zako ili kuyahisi yalivyo.

Kwa upande wangu kuwa na mwanaume ambaye ananipenda na kuwa tayari kukutana na mimi muda wowote inanitosha kabisa , mwanaume ambaye yupo tayari kuingia katika hatari kwa ajili kutafuta madawa ambayo yatanisaidia kuendelea kuwa kijana milele hio ni tosha kabisa na siwezi kuomba kitu kingine na kitu pekee ambacho naweza kumlipa ni uaminifu wangu kwake, nitamfanya atambue kwamba ninafuraha sana kuwa nae katika mahusiano.

Edna nisikilize kuna kipindi katika maisha yangu nilijali sana cheo cha mume na mke lakini kwasasa najua ni nini kinanifanya niwe na furaha na hilo ndio swala linalonifanya nijihisi kuridhika.

Kama unahitaji mwanaume ambaye muda wote atakidhi haja zako na kuendeleza hadhi yako basi naweza kusema itafikia kipindi Roma atakuja kutambua wewe kuwa mke wake yalikuwa makosa”Baada ya mchepuko kumaliza ngonjera zake alisimama na kisha akaondoka ndani ya eneo hilo.

Edna hata keki ambayo siku zote alikuwa akiipenda aliona haikuwa nzuri tena, juisi ya Strawberry hakuitamani tena , hamu yake ya kula ilikuwa imeyeyuka kabisa na sasa kilichobaki ni woga , hasira pamoja na wasiwasi wa kutokuwa salama kama mwanamke.

Muda huo huo wakati akiwa amezama kwenye mawazo ya kutafakari maneno ya Nasra, alihisi kivuli cha mtu kusimama mbele yake.
[emoji91][emoji91]
 
SEHEMU YA 512.

Blandina mara baada ya kusikia gari likitoka na wao walitoka haraka akiwa yeye na Bi Wema.

“Roma unafanya nini?, nini kimetokea?”Aliuliza Blandina mara baada ya kumuona Roma akiwa anazunguka zunguka kama kichaa.

“Mama rudi tu ndani?”Aliongea huku kidogo akionyesha amekasirika ila alijitahidi kutoonyesha mbele ya mama yake.

“Nimefanya nini mimi … nisingeingilia?”Aliongea huku akiona kabisa amekosea kile ambacho amefanya na kuona kheri kama angekaa kimya.

“Sio kosa lako kwani haya yote yanatokea kwasababu yangu , hivyo usijilaumu”Aliongea Roma

“Mr Roma nadhani itakuwa vizuri kama ukimfatilia mkeo , kwani muda huu ni hatari akiwa peke yake huko nje”Aliongea Bi Wema ambaye alikuwa na wasiwasi mno.

Roma hata yeye aliona alichoongea Bi Wema ni sahihi , hakupaswa kumwacha Edna akawa peke yake katika mazingira hatarishi ukizingatia alikuwa na maadui wengi na hapo hapo hakutaka kusubiri muda mrefu kwani alirudi ndani na kuchukua ufungo wa gari na kisha akaondoka.

Upande Wa Edna mara baada ya kutoka hapo , hakuwa hata akijua ni wapi aelekee , kwani akili yake haikuwa sawa kabisa.

Alijikuta akiendesha gari umbali mrefu na kuja kuliingiza katika moja ya mgahawa ulioungana na Bar uliopo ndani ya eneo la Tegeta.

Edna aliingia kwenye mgahawa huo huku akikodolewa macho na baadhi ya wanaume waliokuwepo hapo ndani , lakini kwa upande wake yeye hakujali kabisa.

Baada ya kutafuta sehemu ambayo aliona inafaa , aliketi chini na muda uleule na mhudmu hakucheza mbali , kwani alimsogelea Edna akihitaji kuchukua oda yake.

Upande wa Roma alimuona Edna akiingia ndani ya mgahawa huo ambao una bar ndani yake, hakutaka kumzuia Edna kwa muda huo kwani alijua ana hasira na kwa upande wake hakuna chochote ambacho anaweza kufanya , hivyo baada ya kumuona Edna amechagua meza na kukaa na yeye alitafuta meza ya pembeni na kukaa huku akihakikisha Edna hamuoni,

Ijapokuwa hakupendezwa na macho ya wanaume wakola namna ambavyo wanamwangalia mke wake kwa macho ya matamanio lakini alijtahidi kujizuia.

Baada ya muda mchache tu Edna kutoa oda , mhudumu alifika na chupa ya mvinyo ambao una kiwango cha juu cha kilevi na Roma licha ya kwamba alikuwa mbali lakini aliweza kuona jina la mvinyo ule na aliamini Edna kaagiza aina hio ya mvinyo ili kulewa kidogo kupunguza mawazo.

Dakika kumi na tano zilipita , hatimae dakika kumi na tano nyingine zilipita na Edna aifanikisha kumaliza chupa mbili ya mvinyo na kilichomshangaza Roma ni kwamba Edna hakuwa akilewa haraka kama alivyotarajia , alikuwa akimsubiri alewe ili iwe rahisi kumbeba na kumrudisha nyumbani.

Ukweli Roma sio kwamba alihisi kuna kitu kimetokea kati yake na Hanson , lakini kilichomchanganya ni pale Edna alipodanganya kwamba hakukutana na Hanson siku hio wakati ushahidi ulionyesha kabisa walikutana.

Baada ya kama dakika arobaini na tano hatimae kilevi kilimkolea Edna na sasa kuanza kupendeza na kuwafanya wanaume waliokuwa ndani ya eneo hilo wakiburudika waone sasa ni wakati mzuri wa kumsogelea mrembo huyo ili kujaribu kurusha ndoano zao.

Kilichowafanya wasimsogelee mapema ni kutokana na ile hali ya kukosa ujasiri wa kumsogelea kutokana namna alivyoingia , isitoshe ndani ya hilo eneo kuna wale ambao walikuwa wakimfahamu na ambao pia hawakuwa wakimfahamu.

Katika watu ambao hawakuwa wakimfahamu ni mfanyabiashara mmoja wa madini kutoka nje ya nchi , ambaye alikuwa kwenye meza moja na wapambe wake.

Mwanaume yule mwenye kitambi mara baada ya kuona hakuna mwanaume hapo ndani mwenye ujasiri wa kumsogelea mrembo alieingia hapo ndani, alifanya maamuzi ya kusogea wewe ili kuonyesha umwamba wake.

Hata hivyo historia yake na wanawake ilikuwa nzuri sana , hakuwahi kukataliwa na mwanamke mrembo wa aina yoyote, hivyo aliamini kwa mrembo Edna mambo yangekuwa marahisi pia, alikuwa akijiamini kutokana na kwamba alikuwa na hela za kuhonga.

“Mrembo unaonyesha kuwa mpweke leo , je naweza kuungana na wewe?”Mwanaume mwenye kitambi aliongea huku akilegeza sauti kidogo na kumfanya Edna ainue kichwa chake kivivu na kumwangalia.

“Kwenda zako”Aliongea, licha ya kwamba alishaanza kulewa lakini akili yake ilikuwa ikifanya kazi vizuri tu, lakini kwa yule mwanaume wala hakukata tamaa, alishazoea kukutana na changamoto za aina hio kwa warembo mwanzo mwanzo.

“Maisha yana changamoto nyingi, Biashara kutoenda vizuri, mahusiano kuvunjika, na mambo mengi ya kukatisha tamaa ,nina shauku ya kujua upande wako wewe kipi kinakusumbua bibie”.Aliongea lakini Edna kwasababu hakuwa kwenye mudi ya kumjjibu , alijikuta palepale akiona huo ni muda wa kuondoka m hivyo alisimama lakini baada ya kusimama alijihisi kichwa kuwa kizito mno na kushindwa kabisa hata kupiga hatua kwenda mbele na kuanza kulega lega.

“Kuwa makini , ngoja nikusaidie?”Aliongea yule mwanaume akitaka kumshika Edna lakini palepale alijikuta akivutwa na nguvu ya ajabu kwenye shingo na kumfanya adondoke chini na baada ya kugeuka nyuma ndio alikutana na Sura ya mwanaume ambaye hakuwa akimfahamu.

“Kaa mbali, unaetaka kumshika ni mwanamke wangu”Aliongea Roma kibabe na kufanya watu wote macho kuwa upande wao, kwani hawakutgemea tukio lile.

Edna mara baada ya kusikia sauti ya Roma aliinua kichwa chake na kumwangalia na kisha akatoa tabasamu ambalo halikueleweka ni la furaha au la huzuni.

“Nani mwanamke wako , wewe kaka tunafahamiana?”Aliongea huku akijitahidi kutaka kupiga hatua lakini bado alishindwa kufanya hivyo kwani kichwa kilikuwa kinazunguka zunguka.

“Bro kisingizio chako kinachekesha , unajifanyisha kufahamika mbele ya huyu mrembo , ngoja nikwambie katika eneo kama hili fursa ni kuwahi, kama ni mwanamke wako kweli ondoka nae bila kumlazimisha”Aliongea mwanaume mwenye kitambi lakini Roma aliona ampotezee kwani hata yeye alionekana kwanza ashaanza kulewa.

“Kama unashindwa kuhimili kilevi hivi kwanini unalewa , nimekufuata turudi nyumbani t”ongea Roma akimshika Edna.

“Niachie bwana , wewe ni nani kwanza?”Aliongea Edna huku akijitoa kwa Roma na kitendo kile cha Roma kumlazimisha Edna mwanaume mwenye kitambi aliona hio ni nafasi nzuri ya kujichukulia pointi.

“Mwachie bwana , mtu hata hakufahamu wewe unalazimisha?”Aliongea na kumfanya Roma amwangalie asijue hata amfanye nini kuingilia mambo yake , huenda ingekuwa zamani tayari ashamuadhibu lakini kwa kipindi hiko alipenda sana kufikiria kabla ya kutenda.

“Mimi ni mume wake na kama utaendelea kulazimisha mambo ya kijinga nitakuchukulia hatua”

“Mume wake haha.. , unaongea upuuzi gani?”Roma alianza kupandwa na jazba, alielewa hakuna ambaye angemuamini kwa muda huo kwani ukweli siku zote huja mwisho.

Hivyo alimshika yule mwanaume tai na kisha akamsukumia mbele yake na kutua kama zigo,licha ya Roma kutumia nguvu kidogo lakini yule mwanaume mwenye kitambi alirushwa mbali sana na kwenda kuvaa viti ndani ya hilo eneo na kuzua taharki.

Roma hakutaka kuendelea kubaki ndani ya hilo eneo , kwani alimbeba Edna palepale na kuondoka nae.

“You asshole! Damn you Roma ,,nimekuambia niache kabla sijakupasua pasua”Edna alianza kufurukuta huku akiongea kilevi mara aweke kingereza mara kiswahili lakini haikumpa sababu Roma ya kumwacha na hata hakujali pia macho ya watu waliokuwa wakimwangalia.

Roma alikuwa ameegesha gari lake upande wa pili hivyo alichukua muda kulifikia na ile anataka kumwigiza ndani kwenye gari, alianza kumwona akijinyoga.

‘Edna una tatizo gani?”

“Mkojo!”Aliongea na kumfanya Roma kushangazwa na kauli hio na alielewa ni sawa kuongea hivyo kwani alikunywa kiasi kikubwa cha kilevi.

“Tupo mjini hapa na hakuna choo cha kulipia karibu, vumilia tufike nyumbani”

“Mimi siwezi kujizuia tena , umenibana”Aliongea na palepale alikimbia kivivu upande wa pili wa nyuma ya duka na kumfanya Roma amsogelee huko huko.

“Edna huwezi jisaidia hapa , watu wanakuangalia”Aliongea lakini Edna akili yake imetawaliwa na pombe hivyo hakutaka kujali , Roma baada ya kuona hivyo alimshika na kumpeleka sehemu salama zaidi nyuma ya ukuta wa kiwanda na kumwonyesha sehemu nzuri huku yeye akilinda kwa mbele watu wapita njia wasione na alichoweza kusikia ni mlio wa ‘chwaaa..’ na kumfanya kushindwa kujizuia na kuanza kucheka.

Hakuwahi kufikiria kwenye maisha yake angemzibia mwanamke kama hivyo ili ajisaidie tena mwanamke huyo akiwa Edna mke wake , ilikuwa ni picha ya kudmu kwenye akili yake.

Edna baada ya kumaliza alijikuta akianza kutoa kilio kama mtoto huku akiwa ameshikilia ukuta na kumfanya Roma kumwangalia kwa huzuni.

“Edna ni..”

“Hebu angalia hali niliokuwa nayo , nimesingiziwa na mama , mume wangu ananishuku na wote mnanidharau, nimefanya kosa gani mpaka nikafikia hapa, nipo uje usiku huu nikiogopa hata kurudi nyumbani na kuishia kulewa mpaka kujisaidia mtaani….

Tokea tuanze kuishi pamoja nilijihisi kama mwanamke kichaa ambaye hajui nini maana ya kuwa mke , nilijiona mpumbavu nisiekuwa na thamani katika maisha yako , lakini upande mwingine kila siku nakuwa ni mwenye wasiwasi juu yako . najihisi kama vile maisha yangu siku hizi yanaendeshwa na watu wengine.

Huenda hata alichoongea Nasra ni sahihi , mimi sio Edna tena na hata sijifahamu mimi mwenyewe ni nani .. Roma siwezi kuendelea kuishi hivi kama mjinga , mimi ndio Edna……, na kama hali hii ya kukosa utulivu wa moyo itaendelea nitafikia hatua siwezi kuendelea tena”Aliongea na kumfanya Roma ashindwe kabisa kuongea lolote na hata kumsogelea alishindwa, aliishia kumuonea huruma kwani alijua anayopiia yeye ndio msababishaji.

“Hubby…!!”Aliita Edna mara baada ya muda kupita bila ya Roma kuongea lolote.

“Nipo hapa”Aliongea Roma na Edna alifuta machozi na kupiga hatuua moja mbele na kumsogelea Roma.

“Nakuambia sasa kilichotokea , ni kweli nilikutana na Hanson , lakini yeye ndio alienifuata na alikuwa akijaribu kunibembeleza kwa ajili ya ombi lake la ubia wa kibiashara , alikuwa akiomba sana kiasi cha kufikia hatua ya kunishika mkono …, najua una wasiwasi kwasababu tulifahamuna chuoni na ashawahi kunitongoza lakini hayo yote yalikuwa ni ya zamani na sio sasa.

Wewe ndio mwanaume wangu wa kwanza kukupenda kwa moyo wangu wote , najua siwezi kukumiliki mwenyewe lakini nilijiambia naweza kuvumilia wanawake wako wengine , wewe ndio ambaye ulibadilisha mtazamo wangu na kunifanya nianze kufikiria maisha tofauti na biashara, nakupenda sana mpaka nahisi uchizi…

Najua naweza kuonekana mchoyo kwa kutaka uwe wangu peke yangu lakini naamini hayo ni makosa yangu ambayo yalipita na nimeamua kupotezea mawazo yote ambayo yananifanya nisiwe na furaha, lakini kwanini kama kweli unanipenda unashindwa hata kuniamini?”Aliongea huku akianza kulega lega na kutaka kudondoka lakini Roma alimuwahi na kumshikiria.

‘Nakuamini saa ni makosa yangu..I am sorry…”Aliongea Roma lakini palepale Edna aliishia kujilaza kwenye kifua na kuonekana kama mtu ambae yupo kwenye usingizi mzito na kumfanya Roma avute pumzi na kumbeba tena kulisogelea gari lake.

Ni baada ya dakika kama ishirini hatimae Roma aliweza kurudi nyumbani na kupokelewa na Bi Wema pamoja na Blandina ambao bado walikuwa wapo macho wakiwa wanawasubiri.

“Roma kwanini yupo hivyo jamani, yaani mtu kakosea anakimbilia kulewa”Aliongea Blandina mara baada ya kumuona Edna akiwa amelewa.

“Mama hebu acha kumsema , kashachoka na mambo ya kusingiziwa na hana sehemu yoyote ya kutolea hasira ndio maana kakimbia kulewa , unaonaje asubuhi ukamwomba msamaha yaishe , najua sio vizuri kufanya hivyo lakini pia umekosea”Aliongea Roma na kumfanya Blandina kushangaa.

“Siwezi kufanya hivyo,kwani hata mimi nishawahi kuwa katika rika lake najua sisi wanawake ni wapi tunakosea na isitoshe nia yangu haikuwa mbaya , kama asingekutana na yule mwaname sidhani yote haya yangekuwa yametokea , naweza nikawa nimekosea kweli lakini nikimwomba msahama ni kujishushia heshima kama mama yako”

“Mama , tupo karne ya ishirini na moja sasa na sio tatizo mzazi kuomba msamaha pale anapomkosea mtoto”

“Sawa nitajirahidi kumuomba msamaha lakini nitafanya hivyo sio kwa ajili yake bali kwa ajili yako , mimi sio mzee kihivyo kushindwa kuelewa wapi nimekosea”Aliongea Blandina huku akionyesha hapendezwi na namna Roma anavyomkingia kifua mke wake , alikuwa ni kama anataka Roma ndio awe upande wake , lakini kwa Roma mke wake ndio kila kitu kwani ndio mtu anaekwenda kuishi nae maisha yake yote.

“Blandina ni sawa na wew alichoongea , kama mzazi huwezi kushinda kila mazungumzo, najua unahisi upo sahihi juu ya hili lakini kwa ajili ya familia ni kheri ukaamua kujishusha tu ili amani irudi”Alishauri Bi Wema na kumfanya Blandina akubalikwa kichwa.

“Huenda ndio maana tamthilia za siku hizi lazima ziwe na mama mkwe kigeugeu , kama sijaelimika huenda ningekuwa kama watu wa kwenye tamthilia kwa kumtaka mwanangu kuwa upande wangu tofuati na upande wa mke wake”aliongea Blandina na kumfanya Bi Wema kucheka.

Roma mara baada ya kumwingiza Edna kwenye chumba chake , aligundua Lanlan hakuwepo hapo ndani na alijua huenda kalala na Qiang xi.

Baada ya kumuweka kitandani alipunguza nguo alizovaa na kisha akamfunika ili alale , Edna muda huo alionekana hakuwa akijua kabisa kinachoendelea zaidi ya kutafuna tafuna na alipowekwa kwenye kitanda ni kama ambeambiwa ndio alale.

Roma hakuondoka baada ya kumuweka Edna kitandani , alionekana kuongea maneno mengi kwa hisia sana kwa zaidi ya dakika kama tano na kisha alimwinamia Edna na kumbusu usoni na kisha akazima taa na kuondoka.

Ilikuwa ni siku nyingine Roma akiwa usingizini , mlango uligongwa kwa nguvu mno kiasi kwamba Roma ilimshangaza kwani hakuwahi kugongewa kwa nguvu kiasi hicho na isitoshe mlango ulikuwa wazi, ilikuwa ni kama anegona ana hasira.

Muda uleule mlango ulifunguliwa na baada ya kuangalia aliekuwa akigonga aligundua alikuwa ni Lanlan.

“Lanlan mlango upo wazi kwanini unagonga kwa nguvu?”

“Mama ameniambia nigonge mlango kabla ya kuingia”

“Kwahio hajakufundisha kugonga taratibu?”

“Hapana?”Alijibu na kumfanya Roma kumwangalia kwa kumchunguza.

“Bad Dady, Bibi kasema uamke, kwani hatuwezi kupata kifungua kinywa mpaka uwepo na Lanlan ananjaa sana”Aliongea Lanlan na kisha kwa hasira alisogelea shuka ambalo Roma amejifunika na kulivuta kwa nguvu na kumfanya Roma abakie kifua wazi na mpaka hapo alijuwa kwanini Lanlan alikuwa akigonga kwa nguvu.

“Lanlan nipe shuka langu?”Aliongea Roma huku akijaribu kujifunika na mto.

“Bad Daddy unakifua kidogo kuliko cha mama”Aliongea Lanlan kwa kingereza na kisha alikimbia kutoka nje na Roma alicheka na kisha akavuta tena shuka kulala kidogo , lakini muda ule ule na mlango ulifunguliwa na Edna ambaye alionekana kushikilia nguo mkononi zilizokunjwa.

Alimwangalia Roma alielala kwenye kitanda na kisha alienda moja kwa moja mpaka kwenye makabati na kuanza kupanga nguo katika sehemu husika , zilionekana kuwa nguo za Roma ambazo zimetoka kusafishwa na kukaushwa na mashine.

“Wife bado umekasirika?”

“Ndio bado nimekasirika , lakini licha ya yote bado wewe ni mume wangu”Aliongea kwa sauti ndogo na kumfanya Roma kushangazwa na kuguswa na kauli yake na palepale alitoka kama mshale kitandani na kumsogelea kisha akampakua na kwenda kumlaza kitandani.

“Nilijua tu mke wangu ushanisamehe tokea jana ile ile”Aliongea Roma huku akionyesha furaha na Edna alimwangalia na kuanza kuona aibu kwani kuna kitu kizito kilichokuwa kikimgusa upande wa chini mapajani.

Ukweli ni kwamba Edna wala hakuwa amelewa kiasi cha kutojitambua , wakati Roma anamrudisha nyumbani alikuwa akisikia kila kitu lakini alijifanyisha kuwa katika hali ya ulevi wa kupindukia.

Uwezo wake wa kijini ambao alianza kujifunza ulikuwa umemsaidia sana kuweza kuhimili kiasi kikubwa cha pombe , hivyo hata wakati Roma anamlanza kitandani na kuanza kuongea ngonjera zake za kimapenzi aliweza kumsikia na maneno yake yalimgusa mno na ndio maana hata alivyoamka alikuwa na mudi nzuri.

Baada ya kama nusu saa waliweza kushuka sebuleni wakiwa pamoja kwa ajili ya kifungua kinywa , Blandina licha ya kwamba Edna alionekana kuwa katika mudi nzuri na kuonyesha kupatana na Roma lakini bado kwenye moyo wake alikuwa na kiwingu , lakini alijitahidi kutoonyesha tofauti yoyote.

Bi Wema baada ya kuona kuna ukimya mkubwa kwenye meza ilibidi awwashe Tv ili kuchangamsha hali.

Wakati wakiendelea kupata kifungua kinywa Roma alikuwa ndio wa kwanza kuangalia moja wapo ya taarifa ya habari iliokuwa ikitolewa na mojawapo ya chaneli maarufu nchini.

Ilikuwa ni habari inayohusiana na kifo cha Hanson , habari hio haikumshangaza Roma tu lakini hata Blandina ambaye aliweza kumjua siku ya jana Hanson , sura yake iliokuwa ikionyeshwa kweny runinga ilimfanya aifahamu palepale, upande wa Edna hakushitushwa kabisa na habari hio na aliishia kutoa tabasamu la kebehi ni kama mtu alietangazwa kufariki alikuwa adui yake.

Kwa maelezo ya taarifa hio inasemekana kwamba Hanson alikutwa hotelini akiwa amekufa huku uchunguzi ukionyesha kwamba amekunywa sumu, taarifa za awali zilionyesha huenda kilichomuua mtoto wa tajiri huyo kutoka Norway ni msongo wa mawazo ambao umesababishwa na kile kilichosemwa ni kushindwa kufikia makubaliano na kampuni ya Vexto.

Katika maelezo ya waandishi wa habari wanasema Hanson alifika nchini akiwakilisha kampni ya Hanson enterprises na BMW ukanda wa Afrika na alipaswa kuingia kwenye makubaliano ya kibiashara na kampuni ya Vexto , makubaliambayo hayakufanikiwa.

Sasa taarifa ya pili yake ndio ilimshngaza sana Roma na kumfanya amwangalie Edna kwa mshangao na sio yeye tu hata Blandina pia alimwangalia Edna huku wote wakionekana kuhitaji maelezo.











SEHEMU YA 513.

Ilikuwa ngumu sana kwa mwanamke mfanyabiashara kama Edna kuacha mkataba wa kibiashara mnono na kampunni kubwa duniani ya BMW , Edna mshindani wake mkuu kibiashara ilikuwa ni kampuni ya Maple Group ambao walikuwa na mkataba wakibiashara na kampuni ya Toyota, hivyo Edna ili kuwa katika levo sawa na kampuni ya Maple upande wa biashara za magari alihitaji kampuni ya BMW.

Siku chache zilizopita kipindi Edna aliporudi kutoka Mediterranian aliweza kupokea proposal’s mbili za kibiashara kutoka kwa kampuni ya Hanson enterprises yenye makao yake makuu jijini Oslo Norway , pendekezo la kwanza liliwakilishwa kwake na Hanson kupitia kampuni yao Hanson Enteprises na pendekezo la pili lilitumwa kwake kwa kupitia barua pepe na mkurugenzi msaidizi wa kampuni ya Hanson afahamikae kwa jina la Asam Scott Hanson.

Mapendekezo yote mawili yalikuwa yakifanana , kilichotofautiana ni kwamba wawasilishaji walikuwa ni watu wawili tofauti , yaani kulikuwa na Hanson halafu kuna mwingine aliejitambulisha kama mkuruguezi msaidizi wa kampuni ya Hanson enterprises afahamike kwa jina la Asam Hanson.

Ikumbukwe Hanson Enterprises yenye makao yake makuu nchini Norway ndio walikuwa wanatakiwa kuwa kama daraja la biashara kati ya BMW na kampuni ya Vexto ili kukuza soko la magari yao katika soko la Afrika mashariki na kati kwa ujumla., haikueleweka sababu kwanini BWM waliichagua moja kwa moja kampuni ya Vexto iliopo nchini Tanzania lakini masharti ambayo kampuni ya Hanson ilipewa ni kuhakikisha kampuni ya Vexto inahusishwa katika ubia kwa lazima.

Edna mara baada ya kupata mapendekezo mawili ya kibiashara kwa wakati mmoja ilimfanya kuingiwa na wasiwasi kidogo na wasiwasi wake ndio uliompelekea kuwapa kazi Athena kumfatilia Asam Hanson ni nani na kwanini na yeye akamtumia ombili la kibiashara wakati kuna mwakilishi tayari amekwisha kutumwa.

Hanson ilikuwa ni kampuni kubwa hivyo taarifa hazikuwa ngumu kupatikana , Athena waliweza kugundua Asam ni kaka yake Hanson(Half brother), na ilionyesha Hanson ndio alipewa kazi ya kusimamia mkataba wa kibishara na kampuni ya Vexto nchini Tanzania kupimwa uwezo wake lakini kaka yake alionyesha kumzunguka mdogo wake na kuanza mchakato wa kukamilisha dili yeye mwenyewe na kampuni ya Vexto.

Edna mara baada ya kupata taarifa aliona inaleta mantiki kwani Asam katika mkataba wake aliweka kiasi kikubwa cha faida ambacho kampuni ya Vexti ugeweza kupata kama tu itasaini mkataba wa ubia na yeye , ilikuwa ni kama Asam alikuwa akijua ni kiasi gani ambacho Hanson angeweka katika mkataba , hivyo alichokifanya ni kuoneza namba tu na kumpiku Hanson.

Lakini vilevile Edna alishindwa kuelewa kwanini kampuni kubwa ya Hanson ikang’ang’ania kampni yake nchini Tanzania kutaka kufanya nae kibiashara lakini hakutaka kuuliza swali kama hilo kwani ni kama angeishusha thamani ya kampuni yake hivyo alijiambia tu anapaswa kuwa makini.

Mwanzoni Edna alitaka kusaini mkataba ulioletwa na Hanson kwake na kuachana na wa kaka yake kutokana na kwamba walisoma pamoja,lakini ugomvi wa Hanson na Roma lakini pia yeye mwenyewe kuwa na wasiwasi na nia halisi ya Hanson ndio iliomsukuma kuchagua kusaini mkataba wa kibiashara uliotumwa na Asam na isitoshe hakuona ni hasara kufanya hivyo kwani mkataba wa Asam ulioonyesha kuwa na faida kubwa kuliko iliowekwa katika mkataba wa Hanson.

Hivyo wakati siku ya jana kikao kinaendelea ndani ya kampuni ya Vexto, upande wa Nairobi alikuwep Benadetha ambaye alienda kumwakilisha Edna katika maongezi ya kibiashara na Asam, ambaye aligoma kufika nchini Tanzania kutokana na sababu hakutaka kuzitaja, Edna alielewa ndio maana akamwagiza Benadetha kwenda kusimamia.

Hivyo polisi wanaamini kifo cha Hanson ni kwasababu ya msongo wa mawazo baada ya kugundua kwamba mkataba ambao alipaswa kuufanikisha yeye Kaka yake Asam tayari ashaufanikisha na rasmi kampuni ya Vexto ikawa na ubia wa kibiashara na kampuni ya BMW na yeye kukosa sifa kutokana na kwamba kazi hio ilikuwa kama majaribio kwake.

Sasa haikueleweka kulikuwa na sababu nyingine ipi ambayo moja kw moja ilipelekea Hanson kujiua kwa kutumia sumu , kwani kusema alikufa kwasababu ya mkataba ni jambo lenye ukakasi kidogo na hili huenda ndio linaelezea ni kwanini Hanson alikuwa akimbembeleza sana Edna kumkubalia kusaini nae ubia huo wa biashara.

Hivyo hata Nasra ambaye ni CEO msaidizi hakuwa akifahamu mpango wa Edna ni upi na alijua kabisa Edna alikuwa ameacha dili hilo nono kwasababu ya Roma , lakini ukweli Edna hakuwa na mpango wa kuachana na dili hilo kwani alikuwa ni mfanyabiashara na siku zote mfanyabiasha haachi fursa impite kirahisi bila sababu ya msingi na Edna amelelewa katika misingi ya kibiashara.

“Mwanzoni nilitaka kabisa kuachana na Projekti hio na kumfanya Hanson kwenda kutafuta kampuni nyingine , lakini alinikasirisha ndio maana nikaamua kumkomesha , lakini sikudhania kama anaweza kuchukua maauzi ya kujua yeye mwenyewe”Aliongea Edna baada kuelezea kile kilichotokea.

Mpaka Edna anamaliza kuelezea mlolongo mzima wa tukio la siku ya jana ndipo sasa Blandina anaelewa ni kweli alikosea kwa kumfikiria vibaya.

“Jana baada ya kikao kuisha sikutaka Hanson anikute ofisini na kuanza kunibembeleza ndio maana nikatoka bila hata ya kumwambia Recho ni wpai naenda , lakini nilishangaa aliweza kujua mahali nilipo kwa urahisi na akili yangu iliniambia moja kwa moja ndani ya kampuni kuna watu aliowapandikiza kufatilia nyendo zangu”Aliongea Edna na kumfanya Roma kuelewa , lakini kwa wakati mmoja aliona kabisa uhai wa Hanson ulikuwa mikononi mwa Edna na muda na saa aliokubali kusaini mkataba na kaka yake alikuwa ndio anammaliza, lakini kwakuwa yeye pia hakuwa mtu wa huruma sana hakuona shida ukatili wa Edna.

“Kama ungesema siku ya jana juu ya mpango wako , mama asingekushuku”Aliongea Roma.

“Ni kweli ungeniambia kila kitu ningekuelewa na nisingekufikiria vibaya , kwanini ukaamua kuficha kila kitu?”

“Haikuwa mpango wangu kumsaliti Hanson na kuamua kuchagua pendekezo aliloleta kaka yake na kama habari hii isingetokea kwenye vyombo vya habari nisingeenda nayo kaburini”Aliongea Edna.

Upande wa Roma hakutaka kushangaa zaidi kwani haikuwa mara ya kwanza kwa Edna kufanya hivyo tokea akutane nae, alikuwa ni mtu wakucheza na akili za watu sana.

Ilikuwa siku ya sikukuu na siku pia ya kumbukumbu ya kifo cha bibi yake Edna hivyo hakuna ambaye alienda kazini siku hio, hata Roma alibakia nyumbani na muda wa mchana ndio alimfuata Rufi ili kuja kujuamuika na familia yake kama makubaliano yalivyokuwa.

Rufi haikuwa mara yake ya kwanza kufika nyumbani kwa Roma , lakini likuwa ni mara yake ya kwanza kukutana na Blandina mama yake Roma.

Baada ya Roma kumfikisha nyumbani alipokelewa kwa ukarimu mkubwa na hata Edna ambaye alikuwa na wasiwasi na Rufi kuingia katika mahusiano na Roma alimchangamkia ili ajisikie yupo nyumbani

Ilikuwa rahisi zaidi kwa Rufi kuzoena na Lanlan , huenda ni kutokana na wote kuongea lugha moja, hivyo baada ya kufika hapo ndani walianza kucheza m pamoja jambo ambalo lilimfurahisha Roma kwani alimuona Lanlan akiwa kwenye furaha ya kiwango cha juu.

Baada ya chakula kuiva wote walijumuika mezani na kuanza kupata chakula cha pamoja na Rufi alipendezwa sana na namna maisha yalivyokuwa hapo ndani , ilikuwa mara yake ya kwanza kushuhudia familia inaishi kwa upendo namna hio, huenda ni kwasababu hakuwahi kuwa na familia ambayo inamjali na kumpenda.

******

Ni baada ya chakula wakati wanafamilia hao wakiwa wameketi eneo la sebuleni , Blandina alitumia nafasi hio kumuuliza maswali kuhusu Rufi ili kumfahamu zaidi , maana kitendo chake cha kujtolea kumsaidia Roma ilimfanya amuone wa kipekee, lakini kilichomshangaza Blandina ni mara baada ya kuona Rufi amechanganya rangi yaani akiwa mchanganyiko wa mafrika na mchina.

Bi Wema alikuwa amekaa sebuleni na yeye macho yake yote yalikuwa kwenye runginga kwani hakuwa akielewa lugha ya kingereza vizuri hivyo hakuelewa kile kilichokuwa kikiongelewa.

Upande wa Blandina alishangazwa na stori ya maisha ya Rufi kwanzia alipokuwa mdogo mpaka kufikia umri huo , historia yake ilionyesha kuwa ya maumivu na aijikuta akimwonea huruma na kumpa pole kwa yale aliopiitia .

“Umesema mama mzazi wako ametokea Afrika mashariki?”Aliuliza Blandina na Riufi alitingisha kichwa kukubali.

“Ingeleta faraja kama ungeweza kukutana na mama yako mara baada ya kutoka kwenye hayo mateso, una njia yoyote ambayo inaweza kusaidia kuweza kumpata mama yako mzazi, niikimanisha picha au mahali alipoishi?”

“Kuhusu mama sina taarifa zozote kuhusu yeye, lakini mlezi wangu aliniambia njia pekee ya mama yangu mzazi kunitambua ni alama niliozaliwa nayo”Aliongea Rufi na kumfanya hata Edna kushangazwa na kauli hio.

“Alama gani?”aliuliza Blandina kwa shauku na palepale Rufi alivua blazia yake upande mmoja na kuacha bega lake la kushoto kuwa wazi na hapo ndipo walipoweza kuona alama ambavo Rufi anazungumzia.

Ilikuwa ni kama tatoo ya rangi nyeusi katika bega la Rufi , alikuwa ni mweupe mwili mzima lakini hio sehemu ya bega ilikuwa nyeusi mno huku ikiwa imekaa kama michirizi ya ngozi nyeusi.

Bi Wema baada ya kuona tukio lile na kumwangalia Rufi , alijikuta macho yakimtoka na kusimama kiwasiwasi na kusogea karibu zaidi na alipokaa , kiendo kile kilimfanya Edna na Roma kumwangalia Bi Wema kwa shauku.

Kitendo cha Rufi kuzaliwa na mama mwafrika na baba mchina ni stori ambayo ilikuwa ikifanana kwa kiasi kikubwa na ya Bi Eema na ndio maana walitaka kumpa nafasi ya kuweza kumwangalia Rufi kama hana uhusiano wowote na yeye.

‘Hii Alama..!!!!’Bi Wema alijikuta akimwangalia Rufi kwa namba isioelezeka na kuanza kutetemeka.

“Wema unaifaham hii alama?”Aliuliza Blandina baada ya kumuona Bi Wema akiwa amebung’aa.

“Mtoto wangu nakumbuka kabisa alikuwa na alama ya kuzaliwa kama hii eneo hili hili”Aliongea na kuwafanya wote kuanza kujawa na msisimko.

Upande wa Rufi hakuelewa alichoongea Bi wema na alishangazwa na mshituko wake na aliishia kumwangalia Roma ili amtafsirie kile ambacho kinaendelea na ilibidi afanye hivyo na Rufi alishangazwa.

“Bi Wema si una picha ya baba mtoto wako?”Aliuliza Edna na palepale Bi Wema alikumbuka jambo hilo na kutoka nduki kupandisha juu kwa ajili ya kuleta picha hio na ndani ya sekunde chache tu alirudi akiwa na picha moja iliochakaa kutokana na kuishi muda mrefu , lakini sura ya mtu aliekuwa kwenye picha ilikuwa ikionekana vyema.

“Rufi umeweza kumtambua mtu wa kwenye hio picha?”Aliuliza Edna na Rufi aliishia kutingisha kichwa huku machozi yakianza kujitengeneza kwenye mboni za macho yake.

“Huyu ni baba yangu”

Aliongea na Bi wema aliweza kusikikia ile kauli na kumfanya amwangalie Rufi akiwa kama haamini, haikuwa kwake tu hata kwa Blandina na wengine wote walishangazwa kuona Rufi ameweza kumpata mama yake kiahisi sana.

Ilikuwa ni jambo ambalo lilileta msisimko wa mshangao , lakini pia na furaha ndani yake , nani angeweza kugundua kwamba Rufi mama yake alikuwa ni Bi Wema , hata Roma mwenyewe alishangaa.

Bi Wema alijikuta akianza kutoa kilio mara baada ya kugundua Rufi alikuwa ni mtoto wake , mateso alioshi nayo muda mrefu pasipo ya kumuona mtoto wae yalimuumiza sana na muda huo furaha yake ilikuwa ya juu sana kiasi kwamba alijihisi ni kama yupo ndotoni na muda wowote angeamka lakini kila kitu kilikuwa halisia , aliekuwa mbele yake ni mtoto wake ambaye alimsurubiria kwa muda mrefu sana kukutana nae.

Baada ya kama nusu saa kupita ndio muda ambao sasa kila mmoja alitulia na ilibidi Bi Wema achukuea nafasi ya kumwelezea Rufi kuhusu stori ya maisha yake na baba yake namna walivyokutana mpaka wakatokea kupata mtoto na namna ambavyo aliishia mara baada ya kumpoteza mtoto wake.

Stori yake ilimhuzunisha sana Rufi na kumuona baba yake alikuwa moja ya watu wakatili sana kuwahi kutokea.

Alimtenganisha na mama yake lakini baada ya kumpeleka katika miliki za kijini na kwenyewe hakuonyesha kumjali na kumchukulia kama kifaa cha majaribio.

Upande wa Bi Wema alishangazwa kusikia kwamba mwanaume wa kichina ambaye alitokea kumpenda hakuwa mtu wa kawaida , bali ni kutoka katika jamii za kijini.

Blandina alijikuta akimwangalia Roma na kumuona kama amefanya jambo la maana kumkutanisha Rufi na mama yake , mpaka hapo waliamini Bi Wema sasa angeishi kwa furaha na sio mwenye mawazo tena na kuendelea kuwa mwanamke mwenye upweke.

“Nadhani naweza kufa sasa kwa amani”Aliongea Bi Wema kwa furaha.

“Mama usiongee hivyo”Aliongea Rufi kana kwamba alielewa kauli ya mama yake na kumfanya Bi Wema kuanza kutoa kilio tena cha furaha kuitwa mama.

Edna na yeye alimpongeza Bi Wema kwa kumpata mtoto wake na pia akampongeza Rufi kwa kumpata mama yake , huenda yale maisha ya upweke ambayo Rufi aliishi nayo yanakwenda kuisha.

Rufi alifurahi sana na kuona kama asingemsogelea Roma siku ile kule marekani huenda asingeweza kumuona mama yake na maisha yake kuchukua sura mpya..

Baada ya maongezi yaliodumu muda mrefu kuisha Roma alimchukua Rufi na Bi Wema kuwasikikiza kwenda Kerege kwenye nyumba ya Bi Wema ili akamuonyeshe namna ambavyo aliishi kwa kukadiria umri wake kwa kununua viatu kila inapofikia siku yake ya kuzaliwa.

Nama ikawa ndio namna ambavyo Bi Wema aliweza kukutana na mtoto wake wa kike aliempoteza kwa zaidi ya miaka ishirini, Bi Wema alijiambia kwa siku ambazo ataishi atahakikisha anafidia kila kitu ambacho Rufi alikosa katika makuzi yake.

“Mr Roma sijui namna gani nikushukuru , umekuja kwenye hii familia na ukamsaidia miss Edna na sasa umenisaidia na mimi kuweza kukutana na mtoto wangu”Aliongea Bi Wema mara baada ya kufika ndani ya jumba lake eneo la kerege.

“Hehe.. Bi Wema huna haja ya kuwa hivyo kwani muda si mrefu unakwendada kuwa mama mkwe wangu , ijapokuwa sisi ni familia lakini uwepo wa Rufi utatufanya kuwa ndugu zaidi”Aliongea Roma bila aibu na kumfanya Bi Wema kumwangalia Rufi na kutabasamu.

Edna alipendekeza Rufi kuishi nyumba moja , lakini kutokana na uhusiano uliokuwepo baina yake na Roma Bi Wema aligoma.

Ilikuwa ni sahihi Edna kumjali Rufi mpaka hatua hio kwani alikuwa ni mtoto wa Bi wema na yeye Bi Wema alikuwa kama mzazi kwake , lakini isingeleta picha nzuri na Edna mwisho wa siku asingejisikia vizuri.

Hivyo Bi Wema na yeye akawa na mipango ya aina mbili , wa kwanza ni aidha Rufi akaishi Kerege kwenye nyumba ya mama yake au Bi Wema anunnue nyumba nyingine karibu na mtaa huo ili iwe rahisi kuhudumia familia zote mbili na mpango uliokubalika na Bi Wema kununua nyumba eneo hilo hilo la karibu..

Ijapokuwa Edna alitaka kunnua yeye kwa hela zake lakini Bi Wema aligoma na kutaka kununua na hela zake kabisa na jambo hilo lilimshangaza Blandina mama yake Roma , kwani ilionyesha Bi Wema alikuwa na mapesa mengi na hata Qiang Xi aliekuwa kama mfanyakazi tu alishangazwa.

“Wema kumbe na wewe ni tajiri usiependa makuu na hatuambiani?”Aliongea Blandina kiutani na kumfanya Bi Wema kucheka.

“Bi Wema mshahara wake ni mkubwa kuliko hata wa kwangu?”

“Haiwezekani?”Aliongea Qiang xi na kumfanya Edna aelezee namna ambavyo Bi Wema analipwa.

Kwa maelezo ya Edna Bi Wema alikuwa akilipwa kwa mwaka sio kwa mwezi na hela zake hazikuingia moja kwa moja kwenye akaunti yake ili asikatwe kodi bali zilikuwa zikiingia kwenye hadhina ya kampuni, ilikuwa ni rahisi kusema kila mshahara wake wote alikuwa akiwekeza katika kampuni ya Vexto.

“Kimahesabu Bi Wema hela zake mpaka sasa naweza kusema sio chini ya bilioni therathini za kitanzania”Aliongea Edna na kufawafanya watu wote kushangazwa na taarifa hio, Bilioni ishirini sio hela ndogo kwa mtu anaefanya kazi za ndani, lakini ilieleweka , Edna hakuwa na mzazi wa kumlea hivyo wazazi wake walihakikisha Bi Wema analipwa pesa nyingi ili kumhudumia Edna vizuri.

********

Baada ya siku mbili kupita Bi Wema aliweza kupata nyumba ya bilioni moja na nusu eneo la ununnio na kuinunua na rasmi ikawa anaishi yeye na mtoto wake Rufi na Edna ndio alisimamia utaratibu wa Rufi kuthibtishwa kuwa raia wa Tanzania kwa kuzaliwa

Bi Wema sasa hakulala tena nyumbani kwa Roma bali alifika nyumbani hapo kwa ajili ya majukumu ya kazi na kila jioni angerudi nyumbani kwa mtoto wake Rufi na kulala pamoja.

Hata ule uzee ambao ulikuwa ukianza kumnnyemelea ulianza kumpotea na sasa alionekana kuwa na furaha.

***************

Siku nazo hazikuganda kabisa na zilienda kwa kasi , katika kipindi chote hicho Roma aliendelea kuwafuatilia wanawake wake kwa ukaribu kabisa juu ya kuangalia mafunzo yao kila giza linapoingia na kitendo cha Lanlan kugangania kulala na mama yake aliona ni jambo zuri mno kwani lilimpunguzia migogoro.

Na kutumia vile vidonge ambacho alitengeneza , hakika mafanikio yalikuwa makubwa mno na hata Neema ambaye uwezo wake ulikuwa wa taratibu sana aliweza kufika kwa haraka katika levo ya nusu mzunguko.

Mage na Rose ndio ambao waliweza kupanda levo kwa haraka mno na kuingia mwishoni mwa levo ya mzunguko kamili na Roma alikuwa akihesabu tu siku mpaka wakatapo ingia katika levo ya Nafsi, yalikuwa ni mafanikio ambayo yalimfurahisha sana.

Upande wa Edna licha ya kwamba alikuwa ndio kwanza anaanza kuingia levo ya nusu mzunguko lakini bado mwili wake haukuwa na mabadiliko makubwa sana , kilichomsaidia sana ni kwamba mafunzo hayo yalimpunguzia uchomvu na alikuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa urahisi zaidi bila ya kuchoka na kichwa chake kuwa chepesi katika kufanya maamuzi.

Baada ya wiki moja kubakia kabla ya safari ya kuelekea Korea kusini haijaanza Roma alienda kwanza kazini kuangalia kinachoendelea na alifurahi kuona Tanya alikuwa akijitahidi kufanya kazi kubwa, lakini hata hivyo aliona kumwachia Tanya majukumu makubwa kama hayo ni kumchosha , hivyo alijiambia atakaporudi Korea atatafuta mtu wa kukaimu nafasi yake kwani yeye alikuwa na mambo mengi.

Upande wa Sophia rasmi sasa mkataba wake wa kuigiza filamu ulisainiwa na kampuni ya Vexto Media na taratibu za kushoot zilikuwa zikiendelea kwa usimamizi wa kampuni ya Penguin Production na ni zaidi ya mwezi tokea aelekee nchini Afrika ya kusini kwa maandalizi.

Mashabiki zake wengi walikuwa wakitarajia sana kuona namna ambavyo Movie hio itakuwa , kwani walikuwa wakimpenda sana Sophia sio kwa sauti yake tu lakini pia kwa namna ambavyo alijaliwa uzuri.
[emoji91][emoji91]
 
SEHEMU YA 514.

Tarehe mbili ya mwezi wa sita ndio safari ya kwenda Korea ilianza rasmi, Edna ilikuwa mara yake ya kwanza kwenda Korea tofauti na Roma ambaye alishawahi kufika mara kadhaa, hivyo kwake alikuwa kama mwenyeweji.

Edna alikuwa na shauku ya kuona jiji la Seoul kwani ndio mahali ambapo tamthilia nyingi za kikorea zilikuwa zikiigiziwa na isitoshe kwa kipindi hiko alikuwa mpenzi kweli wa filamu hizo.

Upande wa Roma sio kwamba alikuwa na shauku kubwa ya kwenda Korea , kwake taifa kama hilo alilichukulia kama dogo kwenda na isitoshe hakuwa na koneksheni sana Korea tofauti na mataifa ya Amerika na Ulaya , lakini kwasababu alikuwa akienda kwa ajili ya Yezi hakujali sana kukaa muda mrefu kwenye ndege japo swala hilo kwake hakulipenda kwani alijiambia alikuwa na uwezo wa kupaa tu na kuibukia moja kwa moja Korea kuliko kupoteza muda , lakini kwasababu ya Edna aliona afuatishe hatua za kawaida za kibinadamu.

Jini la Seoul lilikuwa na joto la wastani , hakukuwa na baridi sana wala joto sana kwa mwezi huo, ki ufupi hali yake ya hewa ni ile ya kuzoeleka kwa wepesi.

Muda wa jioni ndio ambao waliweza kutua na ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Incheon.

Park Jonghyun ndio mtu ambaye alipewa jukumu la kuwapokea kiwanjani hapo na baada ya kuwaona wageni wake alijjikuta akifaurahi huku akipeana nao mikono ya salamu kwa ukarimu wa hali ya juu akiwakaribisha Korea.

“Yezi amewakumbuka sana , alitaka hata kuja hapa kuwapokea lakini yupo na ratiba ya masomo na mwalimu wake Vivian hivyo kashindwa kufika”Aliongea Park Jonghyun.

“Teacher Vivian ? is she a westerner?”aliuliza Edna akimaanisha je huyo mwalimu Vivian ni mzungu , kwani ni ngumu kwa Korea kukutana majina ya aina hio .

“She is not a westerner but a Tanzanian woman who is fluent in english and Korean my grandfather’s proffesor from states recommended his best student”Aliongea akimaanisha kwamba sio mmagharibu bali ni mwanamke wa kitanzania ambaye anajua kuongea lugha ya kikorea na kingereza na moja wapo ya Profesa kutoka Marekani ambaye ni rafiki yake na Park Juan ndio alimpendekeza Vivian kumfundisha Yezi.

“Kwanini mnabana sana na masomo wakati ana muda wa kutosha wa kwenda chuoni?”Aliuliza Roma kwa kikorea na Edna hakutaka kuingilia maongezi yao tena zaidi ya kugeukia dirisha kuangalia mandhari ya jiji hilo la kuvutia.

Seoul ulikuwa mji mkubwa wenye miundombin ya kuvutia , ilimfikirisha Edna na kujiambia jiji hilo lingekuwa Tanzania angejivunia sana.

Baada ya madakika kadhaa ya kuwa barabaranni hatimae waliweza kufika kwenye jumba la kifahari la Park Juan ambalo lilikuwa ndani ya wilaya maarufu ufahamikao kama Gangnam.

Lilikuwa jumba kubwa mno ambalo lilimfanya Edna kuona kweli Yezi amekuwa mtoto wa kishua sio kwa mandhari nzuri kama hio.

Kwa haraka haraka Roma aligundua kuna zaidi ya watu waliokuwa wakiwasubiria hapo ndani , kwani nje kulikuwa n magari mengi ya kifahari yaliokuwa yameegeshwa.

Kwanzia mlangongi mpaka ndani kulikuwa na wahudumu waliokuwa wamejipanga mstari wakiwainamishia vichwa kwa heshima , jambo ambalo lilimmfanya Edna kushanganzwa na utamaduni huo , lakini mara baada ya kukumbuka kwenye filamu za kikorea maisha yapo hivyo alituliza mshangao wake.

Baada ya kuingia ndani kabisa ya eneo la sebuleni waliweza kukutana na watu wengi wa rangi nyeupe wakiwa wamesimama kwa ishara ya kuwakaribisha ni mtu mmoja pekee ambaye alikuwa amekaa huku akiwa ameshikilia fimbo ya kutembelea.

Alikuwa ni Park Juan na Roma na Edna waliweza kumtambua kwani alikuwa maarufu na isitoshe picha zake washawahi kuziona mara kibao.

Upande wa Roma mara baada ya kuwakagua watu wote waliokuwa hapo ndani mtu pekee aliemvutia ni bwana wa makamo ambaye alikuwa amekaa nyuma ya Sofa ambalo amekalia Park Juan , uso wake kwa namna ambavyo ulikuwa ukionekana ni kama mtu ambaye hakujali chochote ambacho kinaendelea hapo ndani na macho yake yote yalikuwa kwenye mkono wake wa kulia ambao alikuwa ameshikilia gololi atu akizichezesha kwa kuzisuguanisha.

Roma kwa haraka haraka aliweza kugundua mtu yule alikuwa ni hatari sana , licha ya kwamba hakuwa na nguvu za kijini kama yeye na hisia zake zilimwambia lazima atakuwa ni Bodigadi wa babu yake yezi yaani Park Juan.

Upande wa kulia alikuwa amesimama Park Jiyeon na Haoming na kwa ufupi aliokuwa nao Haoming alimfanya kuonekana mdogo mbele ya Park Jieyeon.

Msichana mwingine mrembo ambaye aliwashangaza Roma na Edna simwingine bali ni msanii Yoon Hee .

Kwa namna alivyojipamba ilimfanya kupendeza zaidi na kutokana na weupe wake lipsi zake nyekundu zilionekana vizuri zaidi , alikuwa amevalia kitop cha rangi nyeusi cha mkato wa V huku shingoni akiwa amejifunga scarf.

“Karibuni sana , naona mmeshangazwa kuniona hapa?”aliongea Yoon Hee kwa kingereza huku akimwangalia Roma kwa kebehi.

“YoonHee kuwa mtaratibu?”Alifoka Park Juan.

“Yes grandfather”Alijibu.

“Mr Roma na Miss Edna nice to meet you , mimi ni shangazi yake na Yezi nafahamika kwa jina la Park Jiyeon na huyu ni mume wangu anaitwa Haoming , Yoonhee ni mtoto wetu wa kike , asanteni kwa kumkarimu vizuri alipokuwa Tanzania”aliongea Park jiyeon huku akionyesha tabasamu.

Roma na Edna sasa waliweza kufahamu kumbe YoonHee na Yezi ni wajukuu wa Park juan.

Utofauti wao tu ni kwamba Yezi yeye alikuwa ni mtoto wa mtoto wa kwanza wa Park Juan na Yoonhe alikuwa ni mtoto wa Park Jieyeon , hivyo mwenye uzito zaidi katika familia alikuwa ni Yezi kwa tamadunni za Korea,

Roma alikumbuka kitu kipindi cha nyuma nchini Tanzania Yoonhee aliweza kugombana na Park Jonghyun na walionekana kama walikuwa wapenzi na palepale alijiuliza je hawakuwa ndugu?

Baada ya utambulisho mfupi Park Juani aliwaonyeshea ishara ya kuketi na ni muda huo huo ambao waliweza kusikia sauti wanayoifahamu ikiwaita.

“Bro Roma , Sister Edna”Alikuwa ni Yezi ambaye alitokea huku akikimbia kushuka ngazi kwa shangwe.

Walikuwa hawajamuona kwa kipindi kirefu na waliweza kumuona ameongezeka na kuwa mzuri zaidi , nywele zake zilionekana kuwa nyeusi zaidi tofauti na alivyokuwa Tanzania , ijapokuwa waligundua alikuwa amekonda kidogo lakini ilimfanya kupendeza zaidi na zaidi.

Roma alijiambia Rufi alikuwa akianza kuwa kama mkorea halisi sasa na kwa uzuri wake hakuhitaji kufanya hata upasuaji wa sura ili kuonekana mrembo kama ilivyotabia za wanawake wengi wa Korea.

“Kuwa makini usije ukadondoka”Aliongea Park Juan kwa sauti akimtahadharisha mjukuu wake na aliweza kuonyesha wasiwasi namna ambavyo Yezi anashuka kiasi kwamba Edna na Roma waligundua kuna mapenzi makubwa sana kati ya Yezi na babu yake.

Upande wa Yoonhee alijikuta akibetua mdomo kwa kejeli ni kama alimuona Yezi ni kituko , alionyesha waziwazi hakuwa akimpenda , lakini Yezi hata hakulitambua hilo kwani macho yake yote yalikuwa kwa Roma na Edna na alianza kumkumbatia Roma na kisha akahamia kwa Edna.

“Jamani siamini kama mmefika , nilitaka nije niwapokee lakini mwalimu wangu amenizuia , nimejikutaka hata nikipoteza mudi kwasababu hio”

“Ulikuwa ukosoma hadi muda huu?”aliuliza Edna na Yezi alijibu kwa kingereza ili kumfanya na babu yake asikie.

“Mwalimu Vivian ni mkali sana na babu hataki hata kunisaidia?”Aliongea na kumfanya Park Juan kucheka.

“Naweza kuruhusu ufanye kila unachotaka , lakini siwezi kukuona unacheza likija swala la masomo yako , maelfu ya watu wanaweza kupoteza ajira zao kama hutakuwa na elimu ya kutosha ya kuongoza kampuni”Aliongea Park Juan na kuwafanya watu waliokuwa hapo ndani kuona wivu ndani kwa ndani huku wakiweka tabasamu bandia katika nyuso zao.

Muda huo huo mwanamke mwingine mrembo alionekana akishuka kutoka juu kwa madaha kabisa , alikuwa amevalia gauni ambalo limeishia magotini pamoja na koti kwa juu alionekana kuwa mrembo mno na rangi yake ya kiafrika.

“Teacher Vivian you’ve worked hard , stay back and have dinner with us”Aliongea Park Jonghyun ambaye alikuwa akimwangalia Vivian kwa macho ya matamanio kweli.

“Najma…!!”Roma ndio aliekuwa wa kwanza kumtambua Najma, jina la Vivian lilikuwa jipya kwake na ukijumlisha na mavazi yake ya kisasa ndio kilichomfanya kutomfahamu kwa haraka na sio kwake tu hata kwa Edna vilevile na aliweza kumtambua mara baada ya kumsikia Roma anaita hilo jina.

Najma hata yeye alishangazwa na uwepo wa Roma na Edna hapo ndani na mshtuko wake uliwafanya kila mmoja kushangaa na kuamini lazima wanafahamiana.

Edna alijikuta maswali kibao yakiianza kupita kwenye kichwa chake , tokea siku ambayo aliweza kupata taarifa kutoka kwa Suzzane juu ya Najma kukatisha ufadhili wake wa masomo , sasa alishangaa Najma ambaye alikuwa akiitwa Vivian yupo nchini Korea lakini hakutaka kuumiza kichwa sana aliamini ana muda mzuri wa kuongea na Najma.

“Kwahio wewe ndio mwalimu Vivian?”Aliongea Edna huku akijitahidi kutabasamu , Najma alikuwa ni rafiki yake wa kwanza kukutana nae katika kituo cha kulelea watoto cha Son and daughter orphanage.

Roma alijikuta kumbukumbu zake zikimpeleka nyuma sana kipindi ambacho ndio kwa mara ya kwanza anafika nchini Tanzania , namna alivyoweza kukutana na Najma na kumpokea kwa ukarimu na kumpatia chumba katika nyumba yao na kupanga , alikumbuka vitu vingi namna mrembo huyo alivyotokea kumpenda na yeye kumpotezea.

Ijapokuwa Najma yule na huyu walikuwa mtu mmoja lakini Najma mpya alikuwa wa tofauti sana , huyu alionekana kama mwanamke aliekomaa kiakili mno na kuzidi kustaarabika.

Najma wa kipindi kile alikuwa akivaa Hijab lakini huyu alikuwa kichwa wazi huku nywele zake zikiwa ndefu zilizowekwa dawa ya kupendeza na ilikuwa ni kama ameachana na maswala ya dini.

“Mr Roma and Mrs Edna its been a long time”Aliongea kwa kingereza cheye rafudhi safi na kauli yake iliwashangaza mno Park jonghyun na wengine.
[emoji91][emoji91][emoji91][emoji373]
 
Back
Top Bottom