Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 517.

Park Juan alikuwa ameketi kwenye Sofa ndani ya chumba chake cha kujisomea huku akifuatilia maendeleo ya Yezi katika masomo yake , kwa kumuuliza baadhi ya maswali ambayo alipaswa kujibu.

Licha ya kwamba Park juan hakusoma sana , lakini kutokana na uzoefu wa muda mrefu alikuwa akijua mambo mengi zaidi ya msomi wa kawaida, hivyo alikuwa akijaribu kuuliza baadhi ya maswali muhimu zaidi ambayo yalikuwa yakiendana na maswala ya kibaishara.

Alikuwa akielezea baadhi ya mambo lakini aligundua akili ya Yezi ni kama haipo hapo tofauti na siku nyingine.

“Yezi unafikiria nini? , ni adimu kwangu kuwa na nguvu ya kukuuliza maswali na kukufundisha”

“Babu sitaki kuolewa na yule mwanaume wa kukera”Aliongea Yezi na kumfanya Park Juan kushangaa kidogo lakini aliishia kucheka.

“Bado unafikiria kuhusu hilo ? kwanini niruhusu uolewe nae wakati najua sio mtu mzuri kwako?”

“Kwahio hutokubali niolewe nae si ndio?”

“Bila shaka ..”Aliongea na kisha akamshika mkono.

“Babu yako nakupenda sana hivyo siwezi kukuruhusu uoelewe na mwanaume mtukutu kama yeye , lakini hata hivyo familia ya Gong ndio moja wapo ya koo ambazo zinaushawishi mkubwa , babu yake alikuwa rafiki yangu wa karibu na kama si hivyo nisingeweza kabisa hata kukutana nao , hivyo usiwe na wasiwasi kwani nishasema kuhusu swala hilo tutazungumzia baada ya upasuaji wangu kwenda vizuri”

“Nilijua tu babu huwezi kuniangusha”Aliongea na kumfanya Park Juan kushika mashavu ya Yezi na kuyatingisha huku akitoa tabasamu.

“Walijua mimi ni mzee hivyo naweza kuwa mjinga mpaka kumwalika Dokta Lee eujeong , ni kweli nahitaji daktari bingwa na mwenye ujuzi lakini wamenidharau sana kwa kuona nitaruhusu wanidai fadhila , tutalipa gharama zote za matibabu ili waache kuota ndoto ya kukupata wewe mjukuu wangu”Aliongea.

“Ndio!, Wanataka niolewe na mtoto wao ili waweze kuchukua mali zetu kirahisi , wana nia ovu sana”

“Unaonekana kuwa na akili sana mjukuu wangu na nimefurahi kwamba umeweza kurudi kwenye maisha yangu , usijali kabisa nitahakikisha nakutafutia mtu ambaye ana tabia njema , uwezo na utanashati ili kuwa mume wako’”

“Babu kuhusu mwanaume nitamtafuta mwenye , huu ni ulimwengu wa kisasa kwanini unichagulie mume?”

“Kwanini nisikuchagulie? , au kuna mtu ambaye unampenda , usinidanganye kwani nimeishi miaka mingi kujua kile unachofikiria”Aliuliza na kumfanya Yezi kutingisha kichwa kwa haraka.

“Hapana babu sina mtu ninae mpenda na usifikirie sana kuhusu hilo”

“Yezi mapenzi sio kama mchezo haijalishi kama ni masikini , an asura mbaya au hana akili ili mradi uwe unampenda, kikubwa awe na tabia nzuri lakini pia asiwe na makando kando , lakini pia huwezi kumpenda mwanamme mwenye mke au Casanova”

Casanova ni mwanaume mwenye wake wengi au wapenzi wengi , unaweza kumuita Roma Casanova hivyo babu yake Yezi alimaanisha kwamba asingeruhusu Yezi kuoelewa na Casanova.

“Babu usiongee hivyo siwezi kupenda mwanaume wa hivyo mimi”Alijibu Yezi huku akionyesha aibu.

“Nakuamini mjukuu wangu , baba yako kuondoka nyumbani mpaka kifo kumkuta ni majuto ambayo sitaki yajirudie kwako, hata hivyo naamini mama yako hakuwa mbaya pia, hivyo mtu yoyote ambaye anafaa utakaempenda nitakusapoti”Aliongea na kumfanya Yezi kutabasamu kwa furaha.

******

Gari ambalo lililomteka Najma lilisonga kwa spidi kuelekea katikati ya jiji ambalo lilikuwa na mataa mengi.

Nyuma kabisa ya gari kulikuwa na mwanamke alievalia koti la Leather huku akiwa ameshikilia glasi ambayo alikuwa akizungusha zungusha kuchezesha mvinyo uliokuwa ndani yake.

Alikuwa ni Yoon Yeonhee ambaye alikuwa ndani ya familia ya Park kwa ajili ya chakula cha usiku , haikueleweka alipanga saa ngapi na kukamilisha tukio la kumteka Najma.

Alimwangalia Najma kwa macho ya dharau sana huku akimchunguza kwanzia juu mpaka chini kuona ni kipi cha ziada anacho ambacho yeye hana mpaka akatokea kupendwa na Park Jonhyun.

“Hana uzuri wowote kuliko mimi , lakini pia ni mweusi , nashangaa kwanini Park Jonghyun akapenda mwanamke kama huyu , lazima atakuwa na uchawi wa kiafrika huyu mwanamke lakini bado naona pia kuna kitu kinaendelea kati yake na yule mwafrika mwenzake”Aiongea kwa Dharau..

Yonhee alikuwa na hisia kali sana , alikwa ashajua nini kinaendelea kati ya Najma na Roma kwa kuangalia tu.

Mwanaume aliekuwa amemshikilia Najma alionekana kuongea na simu na kisha akamgeukia Najma.

“Miss , Bar tayari iko tayari”aliongea

“Vizuri sana, mpe taarifa Roma Ramoni na taarifa iwe nzuri”aliongea na kumfanya yule mkorea kutoa tabasamu la maudhi huku akishikilia simu yake vizuri.

Baada ya Yoonhee kuongea hivyo alitoa simu yake tena huku akiendelea kumwangalia Najma kwa macho yasiokuwa na nia njema na kisha akatafuta jina la Park jonghyun kwenye simu yake na kisha akapiga , ilichukua dakika kadhaa mpaka simu kupokelewa.

“Unataka nini ..” mtu upande wa pili aliongea akionyesha kabisa hakupendezwa kupigiwa simu na huyo mwanamke na jambo hilo lilimfanya Yoon Hee kuona wivu.

“Kwahio huwezi kuongea na mimi vizuri licha ya kwamba nimekupigia mimi?”

“Acha porojo na elezea shida yako , nipo na kazi nyingi”

“Haha… unafanya kazi , kazi gani unafanya wakati mnufaika ni binamu yangu Yezi?”

“Twitwii..!!”Simu ilikatwa palepale na kumfanya Yoonhee kupandwa na jazba na kuipigiza simu yake kwenye kioo cha gari.

“Fine…. Si unajifanyisha kunichukia, basi nitahakikisha naharibu maisha ya huyu kapuku wako mweusi, tuone kama uaendelea kunichukia na kumpenda”Aliongea kwa hasira.

******

Upande wa chumba cha wageni katika jumba la familia ya Park katika floor ya pili alionekana Roma ambaye alikuwa akimwangalia mwanamke aliekuwa mbele yake aliekuwa akijifanyisha kuwa bize.

Edna muda huo alikuwa amekaa kiandani huku akiwa ameshikilia tablet ambayo inampa nafasi ya kufanya kazi kwa kutumia software maalumu, alikuwa amevalia tayari nguo za kulalia za kitambaa cha pamba,upande wa Roma yeye alikuwa na buka lake tu pasipo ya kuwa nguo nyigine.

“Mpenzi tumekuja Korea kwa ajili ya mapumziko yetu , unapanga kufanya kazi usiku kucha?”Aliongea Roma lakini Edna hakutoa jibu zaidi ya kuendelea kukodolea macho skrini ya tarakishi yake , ilionyesha kama vile hakuwa amemsikia Roma.

Roma alikosa kabisa uvumilivu na mpaka hapo aliona Edna anamjaribu , hivyo alitoka kitandani na kisha akambeba juu juu kwa kumshitua na kumtupia katikati ya kitanda.

“Ah! Unafanya nini?”Aliongea akijaribu kujitetea lakini Roma hakumjali zaidi ya kupanda huko huko katikati ya kitanda na kisha akashika vidole vya miguu ya Edna na kuanza kuvisugua kwa mkono na kumfanya Edna kuhisi mtekenyo wa ajabu kiasi kwamba alikosa uvumilivu.

“Unastahili hiki ninachokufanyia kwa kushindwa kuwa mtiifu kwa mume , nishasema hapa tupo Honemoon na matendo yetu yanatakiwa kuwa ya ki ‘HaniMuni muni’ halafu wewe unachojali ni kazi , unanifanya nijione nina kasoro kama mume wako”

“Huna aibu wewe mwanaume ..”Aliongea na kumfanya Roma asimjali na kuanza kumtekenya kwa kuchezesha mkono kwenye nyayo zake za miguu.

“Ah.. unanitekenya bwana … acha jamani.. hahaha.. Hubby niachie …haha..mamaa.. sifanyi kazi tena naahidi , hahaha..”Edna alicheka na kuomba kwa wakati mmoja kutokana na namna ambavyo alikuwa akiadhibiwa kwa kutekenywa.

Alijikunja kunja kushindwa kuvumilia na kufanya gauni lake la kulalia kuacha mwili wake wazi mbele ya Rom na hata ile Tablet aliokuwa ameshikilia ilidondoka chini kwenye kapeti.

“Hii ndio adhabu yako kwa kujifanya jeuri”Aliongea Roma na kwa jinsi ambavyo Edna amekaa mtupu mbele yake alijikuta mwanaselele akivimba na hakutaka kuchelewa , alimpandia Edna kwajuu na kisha akafungua kamba ya gauni lake la kulalia na kutupa kule.

Hisia nazo hazikuwa mbali kwani hawakufanya muda mrefu kidogo , hivyo Roma hakutaka kupoteza nafasi hata moja kwa nyakati zote ambazo angekaa Korea.

Mkono wake ulisafiri mpaka ndani ya pichu ya Edna na kisha akaaanza kusugua na kidole kimoja cha kati na kumfanya Edna pumzi kuanza kumuishia kwa msisimko wa ajabu aliokuwa akisikia, ni kama alikuwa akipigwa na shoti kuanzia kwenye kitumbua na umeme kusafiri kwenda mpaka kwenye ubongo na hatimae kwenye macho na kumfanya kuanza kutoa machozi, Roma aliendeleza mapambano mpaka alipoona Edna yupo tayari kumpokea hivyo alivua haraka haraka bukta lake na kutupia kule na kisha akamuweka vizuri.

“Ring!!Ring!”

Ni simu ya chumba karibu na kitanda ndio iliokuwa ikitoa mlio , Park Juan alikuwa ameweka kila chumba simu.

Roma alijikuta akipandwa na hasira na kujiuliza ni nani ambaye alikuwa akimharibia fursa yake muda huo.

Edna kifua chake kilikuwa kikipanda na kushuka na aligeuza uso wake pembeni mara baada ya Roma kuondoka na kwenda kupokea simu.

Baada ya upepo kupuliza kuingia ndani alihisi ubaridi wa hali ya juu katikati ya mapaja yake kutokana na kupandwa na hisia za kiwango vha juu , alijikuta akibana miguu kwa wasiwasi.

Roma alijitahidi kupunguza hasira zake , alikuwa na mpango wa kukata simu hio lakini alijikuta akisikiliza mara baada ya kusikia kitu.

‘Mr Roma Teacher Vivian is with us now and if you don’t want her to be turned into a vegetable you’d beter come here..”Roma aliweza kusikia sauti ya kingereza yenye rafudhi mbovu ikiongea.

Roma alijikuta mikono yake ikimtetemeka wakati alipokuwa akikata simu hio.

Alitoa tabasamu la uchungu mara baada ya kuona Edna kafumba macho yake huku aking’ata lipsi zake kwa wasiwasi, ilionyesha alikuwa akimsubiria Roma , lakini aliona bado alikuwa akichelewa na kumfanya afumbue macho yake na kumwangalia na kushangazwa kuona Roma alikuwa akivaa nguo.

“Wewe., hutaki kufanya tena?”Aliuliza kwa wasiwasi huku akiwa na mshituko na kumfanya Roma kushindwa kutoa jibu.

Edna alijikuta akikaa kitako huku akimwangalia Roma na kulaani ndani kwa ndani huku akijilaumu yeye mwenyewe kwa kutegemea mambo makubwa zaidi.

“Mbona unaonekana kuwa na hasira hivyo , nini tatizo?”Aliuliza na kumfanya Roma asione sababu ya kudanganya.

“Kuna mtu kamteka Najma , hivyo natoka kwenda kuangalia kama ni kweli , unaweza kupumzika kwanza au kunisubiria lakini sina uhakika nitachukua muda gani?”

“Nini! Kuna mtu kamteka najma?”

“Sina uhakika lakini ndio nilivyoambiwa kwenye simu , hivyo ninaenda kuangalia kama ni kweli , usijali hakuna kitu kibaya ambacho kiinaweza kutokea”

“Wasiwasi wangu sio kwako kwani nakuamini lakini kwa Najma ambaye hana namna ya kujjilinda”

“Edna hujakasirika nakuacha mwenyewe?”Aliuliza Roma kwa wasiwasi.

“Unaongea nini wewe ni kweli sipendi uwe na mwanamke mwingine , lakini haimaanishi kwamba nina roho mbaya kiasi cha kupotezea ilihali wapo kwenye haari , Najma anajitahidi kuzuia hisia zake kwa ajili yetu , anafanya yote kwa ajili yetu kwanini niruhusu kuona kuna mtu anajaribu kumchokoza?”Aliongea Edna huku akionyesa wasiwasi hata zile ‘genye’ zilikata.

“Usikasirike ..nilikuwa nikijaribu kuuliza tu?”aliongea Roma huku akiona aibu kutokana na swali lake la kipuuzi , alikuwa akimwona Edna kama mtu mwenye moyo wa baridi likija swala la wanawake wengine ndio maana aliona angekasirika kama angetoka kwenda kumuokoa Najma.

“Acha kuchelewa , nenda haraka”Aliongea na kumfanya Roma asipoteze muda tena na kuondoka hilo eneo kupitia dirishani.

Ijapokuwa kwa nje eneo hilo lilikuwa na ulinzi mkali lakini hakuna mtu ambaye anaweza kudhania kama ametoka , kwani kwake ilikuwa ni swala la kupotea tu.

Roma mara baada ya kutokezea kwenye barabara alipanda Taksi(Cab) na kumpa maagizo dereva kumwendesha kuelekea kwenye Bar aliotajiwa kufika.

Ilimchukua dakika chache tu kuweza kufika kwenye mtaa mmoja wenye barabara nyembaba na gari ile ikasimama na kulia kwake ndio bar ambayo alitajiwa na mtu ambaye alisema amemteka Najma.

Roma alitembea moja kwa moja mpaka kwenye mlango na kusimamishwa na mwanaume alievalia suti ya rangi nyeusi na kwa haraka haraka Roma aligundua hilo eneo usiku huo halikuwa na watu wengi.

“From Tanzania?”Aliongea yule bwana kwa rafudhi mbovu ya kingreza na kumfanya Roma kutingisha kichwa kukubali na palepale walimpisha akaingia

Ilikuwa sio bar bali ni Club kabisa na ilikuwa na eneo kubwa sana ndani na alijiambia mtu ambaye alimteka Najma atakuwa na uwezo wa pesa , baada ya kuingia kulia na kushoto aliona wanaume ambao walisimama huku wakimwangalia.

Kupitia mwanga hafifu Roma aliweza kuona viti ambavyo vilikuwa tupu pamoja na meza ambazo juu yake zilikua na chupa zilizokuwa tupu na glasi huku nyingine zikiwa zimedondoka mpaka chini.

Baada ya kutembea kwenda mbele kwenye Bar aliweza kuona mwanamke wa kikorea ambaye aliweza kumtambua , alikuwa ni Yoon Hee ambaye alikuwa ameshikilia sigara akivuta huku mkononi akiwa na glasi ya mvinyo.

Tokea Roma anaingia hapo mwanamke huyu alikuwa akimwangalia kwa kumchunguza kana kwamba kuna kitu ambacho hakuwa ameridhishwa nacho.

“Miss Yoon yeon Hee nadhani una kinyongo kikubwa na mimi”Aliongea Roma mara baada ya kumfikia na kukaa pembeni yake.

Yoohee alimwangalia Roma kwa tabasamu la dharau kama vile kilichokuwa mbele yake ni kituko

“Bila shaka , sijakuita tu hapa kwa ajili ya kupata kinywaji?”Aliongea na kisha akamnyooshea glasi ya Whiskey kumpatia Roma .

“Mbona unasita au unadhania nimeiweka sumu , wewe ni mgeni wa babu yangu hivyo lazima niwe makini”Aliongea kinafiki na kumfanya Roma kuchukua ile glass yenye kimiiminika cha njano na kisha akashusha yote huku akikunja ndita kutokana na radha yake kuwa chungu.

Baada ya Yoonhee kuona Roma ashainywa alitoa tabasamu la kejeli mno.

“Najua matamanio yako ni kumuona Vivian lakini je unaweza kusikiliza stori yangu kwanza?”Aliuliza na Roma muda huo alishafahamu ni wapi Najma alipo kwa kutumia uwezo wake.

“Ofcourse it’s my pleasure”Aliongea Roma huku akitabasamu na kumfanya Yoonhee kumwangalia kwa kumkagua.

“Mpaka sasa nashangaa kwanini wanawake wanakupenda ilihali hauna mwonekano wa kitanashati kam wanaume wengi wa rangi nyeusi”Aliongea Yoonhee

“Wanaume sio kama wanawake , mwonekano una faida kwa wale wanaokuangalia tu lakini katika mapenzi mambo ni tofauti, wanaangalia kitu kingine kabisa”Aliongea Roma na kumfanya Yoonhee kutingisha kichwa kukubaliana nae.

“Kwasisi wanawake ni tofauti , kama tutaona mwanaume tunaempenda akimpenda mwanamke mwigine itatufanya tujishtukie “

“Mwanamke kama wewe Star na mrembo bado kuna mwanaume anaekukataa?”

“Ndio , na mwanaume huyo ni Park Jonghyun”

“Park Jonghyun!!”Aliongea Roma huku akionyesha mshangao japo alikuwa akitaraji jambo hilo kuwepo.

“Nadhani unashangaa kwanini naweza kuwa mpenzi wa Jonghyun wakati ni binadamu yangu , ngoja nikuambie ukweli, Park jonghyun sio mtoto wa damu wa familia ya Park bali alilelewa na babu yangu na alimfanya akue kwa malezi anayostahili kama mtoto wa kitajiri na kupewa elimu kubwa na baada ya kumaliza babu alimpa nafasi katika kampuni na aliweza kuonyesha uwezo mkubwa sana , kama utaniambia kati ya Yezi na Park Jonghyun nani anastahili kuongoza makampuni ya Starmoon basi nitakwambia Park Jonghyun ni bora zaidi kuliko Yezi.”Aliongea na kumfanya Roma kuendelea kumsikiliza.

“Nilifikiri alinipenda ndio maana akataka tuwe wapenzi licha ya mama yangu hakufurahishwa na jambo hilo lakini mimi niliamua kumpotezea mama na kuendelea na mahusiano yetu , ijapokuwa hatukuwahi kutangaza uhusiano weu hadharani lakini nilikuwa nikitegemea siku zijazo tungwewza kuwa mume na mke , sikujali kusengenywa na watu kwa jambo hilo ili mradi alikuwa akinipenda lakini ,,, Jonghyn alikuwa ni muongo mkubwa , alinipotezea mazima mara baada ya kugundua sikuwa na kidani cha mwezi na mimi sikuwa nikijua ni siri gani iliopo nyuma ya kidani hiko”Aliongea huku akiwa na hasira na hata kukaribia kuvunja glasi ambayo ameshikilia mkononi.

“Kwanini alifikiria unacho hiko kidani , si ni hadhina tu ya familia kuna kingine zaidi?”Aliuliza Roma.

“Kidani cha mwezi na kidani kingine cha kundi la nyota ni kweli ni hadhina ya familia na ambaye ni mrithi wa kuongoza ukoo ndio anajua maana yake halisi ni nini na siri iliopo nyuma yake , lakini Park jonghyun hakuwa akijua kama kuna mtu mwingine alikuwa akijua hilo , kupitia taarifa alizopata mtu anaemiliki kidani hiko ndio mrithi wa mali za familia , alidhania kwamba baba yake Yezi asingekuwa nacho kwani alimsaliti babu na kwenda kuoa mwanamke wa kiafrika hivyo moja kwa moja akamiini mimi ndio nitakuwa nacho , lakini ambacho hakuelewa ni kwamba licha ya babu mtoto wake wa kwanza wa kiume kumsaliti lakini bado alikuwa na mapenzi nae makubwa na kumpatia hadhina hio ya familia ambayo na yeye alikuja kumpatia mwanamke wake wa kiafrika na baada ya hapo mwanamke huyo akampatia Yezi”Aliognea.

“Umeniambia mambo mengi ambayo yananifanya nijawe na shauku ya kutaka kujua maana halisi ya hiko kidani ambacho ni hadhina ya familia yenu na kwanini inahitajika kupitia hiko tu Yezi anatakuwa kuridhi kampuni”

“Nataka pia mimi mwenyewe kufahamu siri yake , lakini sina ninachoelewa vinginvevyo ningekuambia “Aliongea huku akitabasa,u kwa uchungu .

“Mbona huna wasiwasi , hao wote unaowaona ni watu wangu na nikiwapa maagizo tu wanaweza kukudhuru”

“”Kwanini niogope , mke wangu hata hivyo atanishuku kama nitaendelea kubakia hapa kwa muda mrefu”

“Haha… Ni wanaume wote wa Kitanzania waoga kama wewe? Nashindwa kuelewa ni kipi wanawake wamekipenda kwa mwanaume muoga kama wewe , Vivian hampendi Park jonghyun kwasababu yako japo ni jambo zuri kwani linamfanya Park Jonghyun kuteseka , na isingekuwa hivyo ningekuachia uondoke hapa kwa amani”

“Unamaanisha nini?”

“Haujisikii kichwa kuuma wala kizungu zungu ?”

“Sijisikii chochote zaidi ya joto tu”Aliongea Roma

“Joto? Huo ni mwanzo tu ,,, hutopata hata hilo joto tena ,..”Aliongea huku akianza kucheka kwa kejeli.

“Umeniwekea sumu kwenye kinywaji?”Aliuliza Roma na Yoonhee alimjibu kwa kutumia ishara za vidole akimwambia pigia mstari.

Na palepale aliwapa ishara mabodigadi yake kufungua mlango uliokuwa kulia , ni mlango ambao huenda hutumiwa na wafanyakazi wa eneo hilo .

Na baada ya mlango ule kufunguliwa taa ziliwaka na kumfanya Roma sasa kumuona Najma ambaye amezingirwa na wanaume , midomo yake ilikuwa imeingiziwa matambala huku yeye akiwa amefungwa kwenye kiti na alijikuta akimwangalia Roma kwa wasiwasi kama mtu ambaye hakutegemea kama anaweza kufika hapo kwa ajili ya kumuokoa.

Najma alijikuta akikumbuka mara ya mwisho Roma alivyomwokoa kule jijijni Dar es salaam mara baada ya kutekwa na Karim.

“Nilikwambia kweye simu atakuwa salama mpaka utakapofika , lakini sasa umefika na hata sijui ni kipi niwafanye”Aliongea YoonHee.

Roma alisimama kutoka kwenye kiti taratibu na kuanza kuetembea uelekeo wa chumba alipo Najma akimsogelea Yoonhee ambaye alikuwa amesogea upande huo pia akimshika Najma kidevu kwa kejeli.

‘Unataka nini?”Aliuliza Roma na kumfanya Yoonhee kumwangalia .

“Mapigo ya moyo hayakuendi mbio?, Saivi kichwa chako lazima kitakuwa kinaanza kuchanganyikiwa kwa matamanio ya kukutana na mwanamke?”

“Kwahio unanitaka? , sijali kukutana na mwanamke mrembo lakini siwezi kuchafua kiungo changu kwa mwanamke mchafu kama wewe”

“Unasemaje? Unapata wapi ujasiri wakuongea na mimi hivyo wakati hujui hata ni kitu gani nilikuwekea kwenye kinywaji”?

“Yeah , nimekumbuka hujanielezea kuhusu hilo”

“Inaonekana sio wapenzi mpaka sasa kutokana na hali za mahusiano yenu , hivyo nimewawekea kitu ambacho kitawaongezea ujasiri , hakikisha humuonei huruma huyu malaya”Aliongea Yoonhee akimaanisha kwamba ameweka kitu kwenye kinywaji ambacho kitamfanya Roma kuwa na matamanio ya kufanya mapenzi , hivyo alimtaka afanye na Najma mbele yao.

Najma palepale alitolewa kwenye chumba kile na wale wanaume waliojazia miili yao huku akimwangalia Roma kwa macho yaliokuwa yamejaa machozi.

‘Hakika unafurahisha sana, bado dawa ipo?”Aliulizia.

“Unaijua?”Aliulizia Roma.

“Kwanini nisijue, ni dawa ya kuongeza hamu ya mapenzi inayotokana na Red spider(buibui rangi nyekundu),Nilishawahi kuwapatia watu wengi , hivyo nirahisi kwangu kuifahamu”Aliendelea kuongea Roma.

“Lakini kwanini unaone…”

“Kwanini ninaonekana sawa , si ndio unavyotaka kuongea?”

“Haiwezekani , unajaribu kuvumilia athari zake , hakuna mtu ambaye anaweza kuihimili , mishipa ya damu yako itapasukka kama utaendelea kuhimili athari zake”

Roma alichukua kijisturi kidogo kilichokuwa karibu yake na kisha akarusha kwenye kioo cha mlango wa upande wa kushoro karibu nae eneo la steji.

“Clang!!”

Kioo kile kilipasuka palepale vipande vipande na kilio cha mtu kilisikika upande wa mlango wa kioo ambao alipasua , alikuwa ni mwanamke(Strippers) ambaye mkononi ameshikilia Kamera kubwa ya lensi

“Naona mpango wako ulikuwa ni kunichukua vidio nikifanya vitu vya kipuuzi mbele yako si ndio?nadhani hunifahamu hata mimi ni mtaalamu wa hayo mambo”

Yoonhee alishangazwa na jambo hilo nakujiuliza Roma alifamu vipi kuna Stripper(Exotic dancer) alieshikilia kamera kwenye kile chumba , mpango wake ulikuwa rahisi sana , alitaka kwanza awachukue Video ya utupu Roma na Najma kwa ajili ya kuwatishia nayo.

Angeweza kumuumiza Park Jonghyun kutumia picha hizo na kukomesha hisia zake na mawazo ya kuendelea kumtaka Vivian na wakati huo huo angecheza na akili ya Yezi kwa kupitia picha hizo na kumfanya asikubali urithi kwani aliamini Yezi alikuwa akimchukulia Roma kama ndugu yake hivyo asingekubali adhalilike.

Lakini mpaka muda huo aliona mambo hayakuwa yakienda kama ambavyo alikuwa amepanga na kuanza kujiuliza mwanaume aliekuwa mbele yake ni nani.

Mabodigadi wake mpaka hapo walikuwa washaona hatari na walikuwa wakisogelea taratibu kwa ajili ya kumshambulia Roma

Upande wa Roma hakuwa na muda wa kupoteza na Yoonhee zaidi na isitoshe alishamweleza kile ambacho alitaka kusikia kuhusu kidani na mahusiano yake na Park Jonghyun , hivyo alimsogelea Najma.

“Mzuieni na mumkamate”Aliamrisha Yoonhee baada ya kukumbuka alikuwa na watu ambao anaweza kuwaagiza anavyotaka , mabodigadi waliokuwa na miili mikubwa walimkimbilia Roma kwa ajili ya kuanza kupigana nae , lakini Roma hakuona haja hata ya kutumia uwezo wake kwani alitaka kutumia njia za kiinadamu kudili nao

Roma aliinua mkono wake na kabla bodigadi wa kwanza hajamfikia tayari alishaachia ngumi ya ujazo wa kilo hamsini na kumpiga nayo eneo la tumboni na kumfanya arudishwe nyuma kama furushi,kwasababu Bodigadi yule hakutegemea swala hilo alijikuta akikosa kukwepa kungumi yake na kwenda kuvaa meza na kufanya mlio wa kuvunjika kwa meza pamoja na chupa kusikika ndani ya hilo eneo.

Roma hakuishia kwa mmoja tu aliwapiga wote kipigo kitakatifu na kuwalegeza , hakuwa na mpango wa kuwaua kwani alikuwa na sababu tatu , ya kwanza alikuwa bado anawahitaji, ya pili hakutaka kuanza kudidili na maiti na ya tatu na ya mwisho aliona hawakupaswa kufa kwani walikuwa wakifanya kazi kwa maagizo tu ya Yoonhee.

“Miss kimbia , ana nguvu nyingi na hatumuwezi”Bodigadi mmoja ambaye alionekana kuwa kiongozi alimshtuia Yoonhee,Roma mara baada y\ kusikia sauti ya yule mwanaume aliitambua.

“Wewe ndio ulinipigia simu si ndio?”Aliongea Roma huku akicheka na Roma palepale alimuona Yoonhee akitaka kukimbia na alimzuia.

“Unataka kukimbia?”

“Mlindeni Boss”Waliongea wale mabodigadi baada ya kuona Roma anataka kumdhuru bosi wake.
[emoji91][emoji91]
 
SEHEMU YA 521.

Kila mmoja aliona maneno ya Gong Gyechung yanaleta maana , isingewezekana mgonjwa kuweza kuhimili upasuaji wa moyo na baada ya hapo akafanyiwa tena upasuaji wa kubadilishiwa ini.

“Lakini sijasema kwamba tunakwenda kumfanyia upasuaji wa moyo baada ya upasuuaji wa ini”Aliongea Clark

“Lakini haina utofauti pia na haitatui shida yake”Aliongea Dokta Lee.

“Njia pekee ya kufanikisha hili ni kufanya upasuaji wote kwa pamoja”Aliongea akimaanisha kwamba upasuaji wa kubadilisha moyo na wa kubadilisha ini ufanyike kwa wakati mmoja.

“Unasemaje?”

“Una kichaa?’

“Ni daktari kweli huyu?”

Madaktari kutoka timu ya Lee walionyesha kabisa kutoridhshwa na maamuzi ya dokta Clark.

“Dokta Clark naweza kusema unavuka mipaka yako kama daktari , wewe hujui kwamba kufanyiwa upasuaji wa kubadilishiwa moyo na ini kwa wakati mmoja ni kinyume cha sheria na leseni zetu zinaweza kufungiwa”Aliongea Dokta Lee kwa wasiwasi mkubwa.

“Nisingeongea hivyo kama mngeonyesha mna mpango mwingine wa kumsaidia mgonjwa , nitaendelea na msimamo wangu huo kwani ndio njia pekee ya kumuokoa mgonjwa”

‘Hatuwezi kufanya upasuaji mkubwa wa aina mbili kwa wakati mmoja , hakuna mtu ambaye ashawahi kujaribu kufanya hivyo , ni kama unamuua mgonjwa”

“Kwahio kama hakuna mtu ambaye ashawahi kufanya ndio tuseme kwamba haiwezekani?”

“kwahio unasema unkwenda kufanya huo upasuaji?”aliuliza Dokta Lee

“Dokta Vincent anaweza kufanya upasuaji wa kubadilisha ini wakati huo mimi nikifanya upasuaji wa kubadilisha moyo , Wallen yeye atahusika na ganzi , hauwezi kuwa upasuaji mgumu kama tu kila mmoja atatoa ushirikiano”

Vincent na Wallen licha ya kwamba walikuwa wakimkubali Dokta Clark lakini kwa upasuaji wa aina hio waliona ni jambo ambalo haliwezekani.

“Ujinga, huu ni ujinga”Aliongea Dokta Lee kwa hasira huku akisimama na kisha akawageukia familia ya Park.

“Jamani msimuamini na maneno yake , hakuna daktari yoyote duniani ambaye anaweza kuamini jambo hili kuwezekana”

“Kwanini wewe ndio unaonekana kuwa na wasiwasi , ni jukumu la mgonjwa yeye mwenyewe kufanya maamuzi , unaweza kutoa maoni yako kama una njia mbadala ya kumuokoa mgonjwa , lakini kama huna kaa kimya”Aliongea Clark na kumfanya Dokta Lee kushindwa kuongea neno lingine.

Ni kweli kabisa hakuwa na matibabu mbadala ambayo yangeweza kumuokoa Babu yake Yezi.

“Jamani kwasababu Dokta Clark yeye kashatoa wazo la matibabu ya mgonjwa nafikiri ni vyema kama tutamshirikisha mgonjwa mwenyewe kufanya maamuzi , hata kama upasuaji huu unaenda kinyume na sheria lakini kama mgonjwa atakubali basi hakuna tatizo”Aliongea Gong Gyechung na kufanya familia nzima imwangalie , mpaka hapo ni kama alikuwa akijitoa kwenye kusimamia matibabu ya Babu yake Yezi kutokana na kwamba Dokta Lee mwenyewe ashaonyesha kukaa tamaa , hivyo njia pekee ni kumpasia jukumu Dokta Clark.

“Mkurugezi Gong ni…”

“Dokta Lee najua wasiwasi wako , lakini hata mimi nimeona kwamba umejitahidi kadri ya uwezo wako lakini kama Dokta Clark ana njia nzuri ya kumuokoa mgonjwa basi sina budi kumpa nafasi”Aliongea Gong na kumfanya dokta Lee kumeza mate mengi , huku akionyesha kutoridhishiwa na maamuzi ambayo yamefanyika.

Edna walikuwa ni moja wapo ya watu ambao walikuwa na wasiwasi na aliona matumaini ya kupona kwa babu yake Yezi ni madogo.

“Hubby unafikiri anaweza kupona?”Edna alimuuliza Roma.

“Kwa hali aliokuwa anayo ni ngumu , lakini Clark ameonekana kujiamini sana hivyo siwezi kutabiri nini kinakwenda kutokea baada ya upasuaji”

Baada ya kuhitimisha majadiliano wote walitaka kusikia maamuzi ya mgonjwa mwenyewe kama angekubali kufanyiwa upasuaji wa aina mbili kwa wakati mmoja kama Clark alivyopendekeza.

Kwasababu muda ulikuwa umeenda jambo hilo lilighairishwa mpaka siku inayofata na Yezi alishauriwa kurudi nyumbani licha ya kwamba alikuwa akitaka kukaa hapo hospitalini na babu yake.

Mtu pekee ambaye alibakia alikuwa ni Kim Jip ambaye muda wote alikuwa kimya, ijapokuwa ilikuwa ngumu kujua kile alichokuwa akiwaza lakini kwa Roma aliweza kujua bwana huyo alikuwa kwenye hali ya huzuni kutokana na bosi wake kuugua, lakini hata hivyo hakuna ambaye alijaribu kumuongelesha , kwanza inasemekana hakuwa akiongea kabisa na kuna baadhi ya watu wanaamini alikuwa bubu.

Upande mwingine katika wilaya ya Gangnam gari nyeusi aina ya Benz ilisimama kando ya jengo la Apartment na Najma alionekana akishuaka kutoka kwenye gari hio mara baada ya kufunguliwa gari na Park Jonghyun.

“Asante kwa kunileta nyumbani , muda umeenda sana unaweza kurudi nyumbani mapema sasa”Aliongea Najma mara baaada ya Park Jonghyun kumsindikiza mpaka karibu na mlango wa kuingia kwenye jengo hilo.

Park Jonghyun alionyesha kutaka kumkumbatia lakini Najma alipiga hatua moja kurudi nyuma akimkwepa lakini hata hivyo hakuonyesha kukasirika.

“Vivian naomba niwe mkweli , tokea ulivyonikubalia ombi langu nimejikuta kuwa na ari mpya kweli , lini utakuwa mpenzi wangu rasmi?”Aliuliza , ilionekana licha ya kwamba Najma amemkubalia lakini bado hakuwa akipewa nafasi hata ya kugusa mwili wa mpenzi wake ndio maana anauliza ni lini atakuwa mpenzi wake rasmi.

“Nipe muda , bado hatujafahamiana kwa muda mrefu ndio maana”

“Okey nitasubiri , nitafute muda wowote ukinihitaji na nitakuja mara moja”Aliongea Park Jonghyun kwa upole na kumfanya Najma kutingisha kichwa kuonyesha kuelewa.

“Unapaswa kurudi sasa , kuna baridi”Alibembeleza Najma.

“Okey , uwe na usiku mwema Vivian”Aliongea na kisha alirudi kwenye gari na msaidizi wake alilitoa katika eneo hilo.

Najma aliishia kuangalia mtaa huo uliokuwa kimya kutokana na watu kuwa ndani kwenye nyumba na kujikuta akipumua kwa ahueni mara baada ya kuona Jonghyun amekwisha kuondoka.

Wakati akitaka kuingia ndan, aliweza kusikia jina lake likiitwa na kumfanya kugeuka nyuma.

“Najma..!!!”

Baada ya kugeuka alishangazwa mara baada ya kugundua ni Edna ambaye anakuja upande wake kwa namna ya kukimbia akiwa amevalia kofia ya Hat.

“Edna kwanini upo hapa..?”Aliuliza huku akionyesha wasiwsi na kumfanya Edna kuweka tabasamu la urafiki.

“Naweza kuona unapoishi , tunaweza kuongea pia kwani hatujapata nafasi ya kuongea hata kidogo”Aliongea Edna na kumfanya Najma kusita kidogo lakini aliishia kumkaribisha ndani na wote kwa pamoja wkaingia kwenye lift.

Upande mwingine kwenye gari, Park jonghyun alionekana kuegamia kioo cha gari huku msaidizi wake akiwa ndio dereva , alionekana kama mtu ambaye alikuwa kwenye mawazo .

“Boss , mwalimu Vivian ni mwanamke mweusi ambaye anatokea kwenye familia ya kimasikini kwanini unatumia juhuhdi kubwa kutaka kumpata, kwanini usipange mpango wa kumchezea na kisha ukachana nae?”Aliongea Dereva kwa lugha ya kikorea.

“Watu kama nyie mtaendelea kucheza na wanawake wa kwenye mabaa , upo sahihi Vivian anatokea kwenye familia ya kawaida lakini licha ya yote anakata mwanaume tajiri kama mimi , huoni kwama ni wa kipekee kati ya wanawake wote?”Aliongea na kumfanya Msaidizi wake kumeza mate.

“Upo sahihi boss , hata Miss Yoonhee tu analazimisha umpende licha ya umaarufi wake.”

“Mwanamke kama Vivian ndio pekee ambaye anaweza kuziamsha hisia za mwanaume , kwasasa siwezi kumfanyia chochote hivyo nitaenda nae taratibu na kumfanya akolee na baada ya hapo nitamtumia na kumtupa, nadhani hayo ndio mafanikio makubwa kwangu kama mwanaume”Aliongea Park Jonghyun huku akitoa tabasamu la kifedhuli.

“Kama ninavyokujua boss wangu , huwezi kupoteza muda wako kwa mwanamke mweusi , Bosi naomba ukimalizana nae na sisi angalau tujaribu kumuonja kwani nina shauku ya kuonja mwanamke wa kiafrika”Aliongea

“Wewe mpuuzi usie na kitu.. ila usijali siwezi kuwatupa”Aliongea na muda huo huo simu yake ilianza kuita mfululizo na aliitoa na baada ya kuona anaempigia alikunja ndita na kisha akapokea na kuweka sikioni.

“Nini?”Alionekana kuuliza hivyo na kisha akaendelea kusikiliza na baada ya kukata simu alivuta pumzi.

“Siendi nyumbani muda huu , endesha kuelekea hoteli ya Myeondong”Aliongea akimwamrisha msaidizi wake na gari ilikunja kiona palepale na kuchukua upande mwingine.

****

Edna baada ya kuingia ndani ya Apartment ya Najma alionekana kuvutiwa kutokana na ubunifu wa mwonekano wa ndani.

Alivua kofia yake aina ya hat na kisha akaketi kwenye sofa , huku bado macho yake yakikagua mandhari nzuri ya eneo la sebuleni katika hilo eneo.

“Huu ubunifu wa hapa ndani naweza kusema ni wa viwango, kwa utulivu wa hapa nadhani hupati shida kuishi peke yako”Aliongea na Najma aliishia kutabasamu kidogo na kisha alienda hadi upande wa jikoni kuandaa kikombe cha chai ili kumfanya mgeni wake kupasha mwili joto.

“Hii Sehemu imeandaliwa na babu yake Yezi kwani ni karibu na nyumbani kwake , ili kurahisisha kutimiza majikumu yangu ya kumfundisha Yezi”

“Kama ni hivyo angekupa chumba tu ndani ya lile jumba lake”

“Nadhani ni kwasababu ya sheria zao za kifamilia , isitoshe mimi sio kijakazi au mgeni mpaka kuishi nao”aliongea Najma na Edna alitingisha kichwa kukubaliana nae.

Maongezi yao yalidumu kwa sekunde kadhaa tu na kisha kimya kikatawala.

Edna mara baada ya kunywa kidogo chai aliinua uso wake na kumwangalia Najma kwa kumkagua na kisha akauuvaa ujasiri ili kuongea kile ambacho kimefikisha hapo ndani.

“Najma unatoka kimapenzi na Park Jonghyn?”Aliuliza Edna na kumfanya Najma kushangazwa swali la Edna.

“Ni Roma ndio ambaye amekuagizia kuja kunitembelea ili uniulize hilo swali?”Aliongea Najma na kumfanya Edna kuona amekamatika.

“Sio yeye tu ambae alihitaji kuuliza , hata mimi pia”

“Kwanini?”

“Kwasababu wasiwasi wetu ni kwa Park Jonghyun , unaweza kumuona ni mpole kwa nje lakini ana upande mwingine ambao huujui na unaweza kuumia”

“Kuumia?”Aliongea huku akionyesha kusita sita kutamka vizuri.

“Park Jonghyun alimfanya Yoonhee kuwa mpenzi wake baada ya kudhania kwamba ndio anakwenda kuwa mrithi wa mali za familia , lakini alimwacha baada ya kuona hakuwa chaguo la Park Juan””Aliongea Edna.

“Yoo yonhee ni yeye na mimi ni mimi , sina thamani yoyote katika vita yake ya kugombea urithi , hivyo kwanini nifanane na Yoonhee katika hilo”

“Lakini huoni kutokana na hilo tabia yake sio nzuri kuwa nae katika mahusiano?”Aliuliza Edna,

“Edna na mimi nataka nikuambie kuhusu Roma pia , Mbele ya macho yangu Roma kamnyofoa mtu shingo bila ya kuwa na hatia kabisa , hivyo kwa mantiki hio inamfanya kuwa uuuaji na mhalifu mkubwa, je unadhani hio ni tabia nzuri ya wewe kuendelea nae katika mahusiano?””

“Kwanini unajaribu kumlinganisa Park Jonghyun na Roma , yeye hakufanya hivyo kwa kufurahia , alifanya hivyo kukulinda”

“Lakini na Park Jonghyun alimtumia Yoonhee kama chombo ili kunufaika na urithi , unafikiri kitendo hicho kinamfanya kuwa tofauti na Roma”Edna aijikuta akikosa usemi hakuwaza maongezi yao yangefikia katika hatua hio.

“Najua wasiwasi wenu ni kuona huenda ninaweza kuchezewa na kisha kutupwa kama takakata , lakini Edna hivi hujafikiria kwamba kama hatokuwa ni Park Jonghyun kuna mtu mwingine ambaye anaweza kufanya hivyo, naomba nikose aibu kukuambia hili…….

Naweza nikawa kweli nimezaliwa katika familia ya kimasikini , lakini leo hii nipo hapa nikijaribu kuweka ukaribu na mtoto wa tajiri mkubwa ndani ya taifa hilo la Korea , nadhani yote hayo yananifanya kuwa mwanamke ambaye sijazaliwa kwa ajili ya kuwa wa kawaida, wakati nilipokuwa Dar nilishawahi kutekwa na mwanaume na akataka kunibaka na kama sio Roma yangekuwa mengine leo hii.

Nilikushukuru sana kwa kile ambacho ulifanya kwa kaka yangu , kipindi kile kabla sijapokea msaada wako nilikuwa kwenye hali ya mawazo sana kujua ni kipi naweza kufanya, lakini Edna unavyoniambia Park Jonghyun ni mtu mbaya kwangu , je unadhani ninaweza kujihakikishia mwanaume mwingine ambaye atakuja kwenye maisha yangu atakuwa na tabia nzuri , je unafikiri nikirudi leo Tanzania ninaweza kukutana na mwanaume ambaye anaweza kunipenda kweli?”

Najua dunia sio ya watu wabaya siku zote , lakini najaribu kufikiria kama nisipobahatika itakuaje, lakini katika yote nakuonea sana wivu Edna..”Aliongea kwa muda mrefu.

Edna hakutaka kongea lolote na kumuacha Najma kuongea kila anachojisikia ili kupunguza sumu iliokuwa ndani ya moyo wake.

“Edna unaweza kuja hapa bila ya wasiwasi kwa ajili ya kunionya kwasababu unajua kila kitu kipo chini yako , una uhakika kwamba muda wowote utakapopatwa na tatizo Roma atakuja kukusaidia , unaweza kumkasirikia , kumuudhi vile utakavyo na pia kuorodhesha mahitaji yako nayotaka atimize na atahakikisha anafanya vile unavyotaka , hayo ndio mahusiano niliokuwa nikiyaota mimi , nataka kupata mwanaume ambaye ninaweza kumtegemea , mwanaume ambaye atakuwa upande wangu muda wote , lakini mwisho wa siku wewe sio mimi , sina bahati kama uliokuwa nayo wewe”

“Kwahio kwa kuongea hivyo unamaanisha kwamba bado utaendelea na Park Jonghyun?”Aliuliza Edna.

“Kama mpango wake ni wa kunichezea tu mimi naweza kujuaje , sina kitu kikubwa cha kumpa kama faida ya kuwa na mimi , tayari ashachaguliwa kwenda kusimamia kampuni nje ya nchi , hajawahi kunilazimisha kufanya kitu chochote nje ya ridhaa yangu , hivyo kwanini nimkatae?”Aliongea .

Edna mpaka hapo aliona hana neno la kuongezea kwa msimamo aliokua nao Najma , lakini alijua nini Park Jonghyun anaweza kufanya pale ambapo atachokozwa.

Edna alitaka kumwambia Najma kwamba akipatwa na matatizo Roma atakuwepo kwa ajili yake , lakini aliona si itamaanisha kwamba anamuweka Najma kwenye mikono ya Roma.

“Hivyo Edna chochote unachoweza kusema hapa kwangu ni kama kitanzi tu , kadri unavyovuta ndio kinavyozidi kukaza zaidi na mwisho wa siku kinanyonga kabisa”Aliongea kimafumbo akimaanisha kwamba kadri anavyomshauri ndio anavyozidisha kasi.

“Najma unaonekana umekuwa mwanamke mkubwa sasa mwenye misimamo yako”

“Wanaume siku zote ni wenye kujidanganya , Edna kama sio mwanaume flani ambaye upo nae sasa huenda kwa umri huu ningekuwa na mwanaume”

“Inawezekana kabisa na inaweza kuwa tofauti pia kwani kuna muda wa kila kitu, Najma mimi nimekuja tu kukushauri lakini naona mwenzangu unajua kile ambacho unafanya hivyo siwezi kukuamulia maisha ambayo unayataka , kuna wanawake wengi sana huko nje ambao pia wanataka kuwa na mume wangu lakini siwezi kumruhusu kuwaonea huruma wote wakait mimi mwenyewe nakosa uvumilivu , hivyo Najma kama utapawa na shida nipigie tu simju nitakusiaida hata hivyo sisi tulikuwa marafiki”aliongea Edna na kisha akasimama na kutoka nje na kuingia kwenye lift na ndani ya dakika chache tu alikuwa nje ya jengo hilo na akakunja kulia akiachana na njia inayoelekea moja kwa moja barabarani.

Ilionekana alikuja hapo akiwa na Roma na alikuwa akimsubiri kwani mara baada ya kusogea mita kadhaa kutoka kwenye jengo hilo aliweza kumuona Roma na kumsogelea na kisha walishikana mikono na kuondoka kwa kutembea..

“Vipi mazungumzo yako yameendaje?”aliuliza Roma.

“Najma amesema anajua kile ambacho anakifanya hivyo hatuna haki ya kumuamulia maisha yake anayoyataka”Aliongea na kumfanya Roma atingishe kichwa kwa huzuni.

“Kama atahitaji msaada naomba umsaidie, labda unaweza pia kuongea na babu yake Yezi kama vipi amsaidie kwa namna nyingine na aweze kurudi Marekani au Tanzania , na isitoshe alikuwa ni rafiki yako sioni kama litakuwa tatizo kama utafanya juu chini urafiki wenu kuendelea”Aliongea Roma na Edna alitingisha kichwa na kumwambia asiwaze kuhusu hilo.

Upande mwingine katika familia ya Gong inayopatikana katika eneo la Gangnam , alionekana Gong Gyevung ambaye amekaa kwenye sofa la leather akiongea na simu , mbele yake alikuwa ameketi Gong Woo mtoto wake pamoja na Dokta Lee Eunjeong.

“Moyo ambao CEO Park anauhitaji tayari umekwisha kupatikana , siku ya upasuaji itakapoamualiwa tutaenda kuuchukua katika hospitaloi ya pili na kwa haraka tutaupeleka katika hospitali yetu kwa ajili ya upasuaji”Aliongea Gong Gyechung mara baada ya kumaliza kuongea na simu.

“Sir naomba unisamehe kwa kuuliza , hivi kwelu unataka kumruhusu yule msichana Clark kufanya upasuaji wa Park Juan? Hii si ingekuwa fursa kwetu kutoa msaada mkubwa kwa familia ya Park??”

“Lakini hata hivyo kufanya upasuaji wa viungo viwili kwa wakati mmoja kwa mtu mzee na dhaifu kama Park Juani unahisia asilimia za mafanikio ni ngapi?”aliuliza Gong Gyechung.

“Ni chini ya asilimia ishirini , lakini ukweli ni kwamba ukiunganisha na makosa ya kibinadamu naweza kusema asilimia ya upasuaji huo kufanikiwa ni chini ya asiliamia moja”

“Nadhani mpaka hapo sasa unapaswa kuelewa , kama tutajihusisha katika huu upasuaji huenda lawama zote zikatuangukia sisi kama upasuaji hautoenda vizuri , hivyo njia rahisi ni kumuacha Clark kufanya upasuaji huo na ukishafeli tutambebesha lawama zote za kumuua Park Juan , hivyo sisi kwa upande wetu tunatakiwa kutoa ushirikiano kuhakikisha kwamba viungo vyote vinavyohiajika vianapatkana na kwa ushirikiano wetu familia yao itaona ni nini tumefanya hivyo hata swala la ndoa kuwa rahisi zaidi kuzungumzika”

“Baba yule Yezi ni mrembo haswa naweza kusema anaweza kushindana na wasichana wengi waliozaliwa hapa hapa Korea, nitafurahi sana kama atakuwa mke wangu’aliongea Gong Woo.

“Acha kuwa mjinga , huruhusiwi kumpenda yule mwanamke , tunachokitaka sisi ni urahisi wa kupata mali zao, mara abaada ya Park Juana kufariki akiwa anafanyiwa upasuaji, baada ya hapo itakuwa juu yako kama utampenda au kumtumia na kuachana nae”

“Baba usijali katika hilo, siwezi kumpenda ila napenda awe sehemu ya wanawake wangu na isitoshe ni bikra nataka niwe mwanaume wake wa kwanza kuitoa”Aliongea huku akitabasamu kifedhuli na kumfanya Gong Gyechung kukunja sura lakini palepale waliangaliana na DoktaLee na kisha wakaangusha kicheko.











SEHEMU YA 522.

Siku iliofuata hali ya Park Juan ilionekana kuimarika na alikuwa kwenye hali nzuri ya kuweza kuongea na kila mtu aliemtembelea.

Asubuhi hio wanafamilia karibia wote walifika hospitali hapo kumjulia hali lakini pia kujua hatima ya matibabu yake kwani kama ni moyo wa kupandikizwa ulishapatikana.

Edna na Roma pia walihudhuria asubuhi hio wakiwa wamemsindikiza Yezi, upande wa wanafamilai wengine walikuwepo wote kasoro YoonHee pekee ambaye haikueleweka mpaka muda huo alikuwa wapi tokea akumbwe na janga la kurekodiwa filamu ya ngono na Roma.

Park Juan alifarijika namna ambavyo Yezi mjukuu wake alivyokuwa na wasiwasi juu ya afya yake , lakini pia kwa wakati mmoja alimuonea huruma kwa namna ambavyo alionyesha kuathirika na hali yake , hivyo kitu pekee ambacho alikifanya ni kumtuliza mjukuu wake kwa kumwambia kwamba atakuwa sawa.

Gong Gyechung alieambatana na Dokta Clark na Dokta Lee walifika hapo kwenye wodi ya VIP aliolazwa wakiwa na fomu maalumu za ridhaa(Consent form) na Gong Gyechung ndio alielezea kwa ufupi kuhusu maamuzi ambayo yamefikiwa ili kutatua tatizo lake la kiafya na Park Juan hakuonyesha kukataa kwani alihitaji kupona kwa wakati huo na isitoshe hakukuwa na njia mbadala ambayo inaweza kumponyesha.

“Mr Park hizi ni fomu tatu za ridhaa ambazo zinahitaji sahihi yako ya kwanza ni kwa ajili ya upasuaji, ya pili ni kwa ajili ya kuongezewa damu na ya tatu ni kwa ajili ya Ganzi , baada ya hapo tutaendelea sasa na taratibu ya upasuaji , moyo wa kupandikiza pamoja na Ini vyote vimeshapaikana chini ya usimamizi wa Mr Gong hapa”Aliongea Profesa Clark.

“Naamini mabadiliko haya ya ghafla ya daktari nadhani upasuaji unakwenda kuwa wa hatari?”AliongeaPArk Juan huku akimwangalia Dokta Lee aliekuwa amesimama upande wa kulia na kumfanya Dokta Lee kuona aibu kiume.

“Nadhani ipo hiyo lakini hata hivyo mimi kuongoza upasuaji wako itakugharimu kiasi kikubwa cha pesa, lakini watu matajiri kama nyie ni kiasi cha kawaida sana”Aliongea na kumfanya Park Juan kutabasamu.

“Paundi milioni ishirini sio kiasi kikubwa sana nitatoa”Alijibu

“Hapana Mr Park naomba nikurekebishe , ukweli ni kwamba ni paundi milioni arobaini”Aliongea bila wasiwasi na kuacha watu wote kuwa katika mshangao.

“Unasemaje?”Aliongea Park Jiyeon kwa mshangao.

“Mwanzoni ilikuwa ni milioni ishirini ya kumpandikiza Ini , lakini sasa hivi upasuaji ambao tunakwenda kumfanyia ni wa kupandikiza moyo pia , hivyo gharama lazima ziongezeke mara mbili yake”

“Wewe ni mwizi na huogopi kuiba na jua lote hili”Aliendelea kulalama Park Jiyeon.

“Unaweza kuongea utakavyo lakini siwezi kwenda kinyume na maneno yangu”

“Wewe…”

Ilibidi Park Juan kuingilia akiwapa ishara kwamba kila mmoja anapaswa kutulia ili yeye aongee.

“Nakubali kulipa , paundi milioni arobaini sio mbaya, kwa kujiamini kwako katika kutaja bei licha ya kwamba unachukua Risk naamini unajua nini unakifanya , lakini kabla ya upasuaji nataka kujua ni miaka mingapi naweza kuishi kama upasuaji utafanikiwa?”

“Kwa kawaida kwa mgonjwa ambaye anapandikizwa moyo ana asilimia themanini na tano kuishi mpaka miaka miwili au zaidi lakini kama utakua chini ya uangalizi mkubwa wa afya yako na kukawa asilimia ndogo ya moyo kukukataa(Heart graft rejection) basi utaweza kuishi mpaka miaka kumi au zaidi, lakini CEO Park kama unataka kuongeza urefu wa maisha yako kwanini usiongee na Mr Roma hapa , anazo mbinu zake za kurefusha maisha , kuokoa maisha yako kunaweza kuwa nje ya uwezo wake lakini kudumisha utendaji mzuri wa mwili wako ndio mahali pake”

“Mr Roma!!!?”Aliongea kwa mshangao huku akimgeukia Roma aliekuwa amekea upande wa kushoto kwake.

“CEO , familia yangu kutoka Tanzania tuna mbinu yetu ya siri ambayo hurithishwa vizazi na vizazi, watu wamezoea kuiita kwa majina mengi, kuna wanaoita Ubatizo wa moto mtakatifu unaodumu kwa siku tatu , wengine pia wanaita , Uumbaji uliotukuka wenye nguvu ya Upako ndani yake, mimi napenda kuita vidonge vya mafuta ya upako, Karne moja iliopita mababu zetu waliweza kupata nafasi ya kwenda kutembelea mbinguni na ndio walikoiba mbinu hio ya kurefusha maisha , upasuaji wako ukimalizika nitakupa ofa ya kukuuzia kidonge kimoja ambacho kitakufanya mwili wako kuwa mgumu kama shoka”Aliongea Roma kwa Kikorea na kufanya watu wote kushangazwa namna ambavyo aliongea kwa muda mrefu bila hata ya kuchapia lakini hata hivyo hakuna ambaye aliamini maneno yake.

“Hubby unamaanisha nini kusema una kitu kama hicho , ni lini tukawa na vidonge vya mafuta ya upako wa kurefusha maisha”Aliuliza Edna baada ya kumfinya Roma aache kuongea pumba.

“Ushasahau na wewe kwamba nina vile vidonge vya kijini vya ubora wa chini , kama nikimpatia ameze kimoja kitamfanya mwili wake kuimarika na anaweza kuishi hata miaka nane mbeleni , ni biashara nzuri yenye faida ya haraka kuliko hata ya kwako ya kuendesha kampuni”Aliongea na kumfanya Edna asiongeze neno.

Baada ya mazungumoz ya mengine ya dakika kama kumi na tano , Park Juana alisaini karatasi za ridhaa na kisha akamkabidhi Dokta Clark.

“Thank you for offering me your trust , I give you my word that your faith will be rewarded , the operation will begin at two in the afternoon”Aliongea akimaanisha kwamba anashukuru kwa kumwamini na imani yake itampa faida , na upasuaji wake utaanza siku hio hio saa nane mchana.

“Much appreciated”Alijibu Park Juan.

Clark hakuwa na haja ya kuandaa upasuaji huo kwa muda mrefu kwanni vuingo vyote vya kupandikiza vilishapatikana.

Upande wa wanafamilia wengine walikuwa na wasiwasi mkubwa kwani waliamini kupona kwa Park Juan ni mwanzo wa kutopata urithi, moja wapo ya watu hao alikuwa ni Park Jonghyun.

“Dr Clark babu yangu ataweza kupona kweli?”Aliuliza Park Jonghyun baada ya kufika kwenye korido ya wodi hizo za hadhi ya juu.

“Sijawahi kufeli “Alijibu Clark na kumfanya Dokta Lee ambaye alikuwa karibu kukunja sura huku akiwa kama mtu ambaye anaamini kabisa upasuaji huo hauwezi kufanikiwa kwa namna yoyote ile kutokana na uzoefu wake katika fani hio ya kitabibu.

Hatimae mchana ukawadia na Profesa Clark na wasaidizi wake walikuwa washajiandaa kwa ajili ya upasuaji, Mgonjwa ambaye ni Park Juan babu yake Yezi alishaingizwa na kuweka tayari katika meza ya upasuaji na tayari alikuwa chini ya nusu kaputi..

Upande wa wanafamilia na watu wengine walikuwa katika eneo maalumu ambalo limetengwa kwa ajili ya uona kile ambacho kinafanyika ndani ya chumba cha upasuaji.

Kabla ya upasuaji kuanza Gong Gyechung aliwapa taarifa kwamba operesheni ya moyo unaotakiwa kupandikizwa mgonjwa katika hospitali ya pili ushaanza kufanyika hivyo ungefika hapo ndani ya lisaa limoja ndani ya muda muafaka, kuhusu ini alisema tayari lipo na upasuaji unaweza kuanza.

Clark mara baada ya kuepwa taarifa hio alitingisha kichwa kuelewa na kisha akawageukia manesi na madaktari wasaidizi wake na kuanza kuwakumbushia majukumu yao kwa mara ya tatu.

“Kama nilivyosema Vincent wewe utadili na upandikizaji wa ini na Walleni utakuwa msimamizi mkuu wa Ganzi na mimi nitakuwa nafuatilia kwa ukaribu maendeleo ya upasuaji , nimeeleweka?”Aliuiza na wote walitingisha vichwa kuelewa.

Baada ya maelezo mafupi hatimae upasuaji ulianza rasmi na Dokta Vincent alitumia kisu vizuri kumkata mgonjwa na kutegneneza nafasi ya kuona ndani.

Upande mwingine wa wale watazamaii , alionekana Yezi akiwa na wasiwasi mno kuliko kila mmoja ambaye yupo katika hilo eneo.

‘Raisi Gong kwanini moyo wa kupandikizwa haujafika bado ,si ungekuwepo hapa kabla ya upasuaji kuanza?”

“Miss Yezi moyo unaopaswa kupandikizwa hautakiwi kukaa nje ya binadamu kwa muda mrefu la sivyo utaweza kupoteza utendaji kazi wake , hivyo kuhakikisha uuendelevu wake lazima ufike ndani ya muda na sio mapema sana”

“Naamini pia haitatokea mpishano wa muda?”aliongea Roma.

“Mr Roma kwa heshima zote , mchakato wa moyo na ini kwa ajili ya upandikizwaji upo chini ya familia yetu ya Gong , hivyo hatuwezi kuruhusu jambo kama hilo litokee kwani litaathiri taswira yetu kama familia , hata kama huheshimu nia yetu ya dhati tunaomba utumie akili ya kawaida tu kufikiria hilo”Aliongea Gong Gyechung na Roma aliishia kutingisha mabega tu akimaanisha kwamba anatarajia maneno yake yawe ya kweli.

Upande wa chumba cha upasuaji Clark alikuwa akifanya upasuaji kwa kasi ya ajabu na kufanya manesi kuwa katika mshangao , hata Dokta Lee mwenyewe hakuwa na spidi kama ya Profesa Clark.

Spidi yake ilimfanya Dokta Vincent kuwa katika presha kubwa ya kumaliza haraka upande wake wa kupandikiza ini.

Ni vitendo vya manesi kupitisha vifaaa vilivyoombwa na wengine kufanya usaidizi katika kukata uzi kila baada ya mshono.

“It’s glued , exceeding the aorta into edge of the heart”(“Umeganda ukipitiliza mpaka kwenye Aota kuingia mpaka kwenye kingo za moyo”)Aliongea Clark huku akionyesha mshangao

“Nini!!”Hata Dokta Lee ambaye alikuwa nje aliweza kuona kitu hicho na kumfanya Yezi kujawa na wasiwasi.

“Dokta Lee nini kimetokea?”Aliuliza Yezi.

“Kuokana na upasuaji uliopita, eneo la moyo wake limefungamana na tishu nyingi hivyo kutengeneza ukovu(Adhesion) kuzunguka eneo lote la nje ya moyo , hivyo itachukua muda mpaka kuondoa mgando huo”Aliongea Dokta Lee.

“Na akishindwa kuondoa Adhesion ndani ya muda mpaka moyo haufika hapa , upandikizaji hauwezi kufanikiwa”Alimalizia dokta mwingine aliekuwa pembeni ya Dokta Lee, walikuwepo wengi wakiangalia wakiwemo wanafunzi..

Upande wa ndani ya chumba cha upasuaji Dokta Clark alikuwa akijitahidi kutuliza watu wake ili kuwa katika hali ya kujiamini kuendelea na kazi.

“Utachukua jukumu la kuondoa Adhesion katike eneo lote kuzunguka moyo fanya haraka lakini kuwa makini”Aliongea dokta Clark akimwambia daktari wa kike ambayr ni msaidizi wake na upasuaji uliendelea.

……………………………

“Upandikizaji wa moyo unatakiwa kufanyika ndani ya masaa manne kamili na sasa yamebakia masaa mawili na dakika therethinni , kama itaendelea hivi hata kama moyo wa kupandikizwa kufika , mchakato wa kuupandikiza hauwezi kukamilika ndani ya muda”Aliongea Dokta Lee upande wa nje na kumfanya Yezi kuzidi kujawa na wasiwasi jumlisha machozi yaliokuwa yakimtoka , kijakazi wake Eunjung alikuwa akijaribu kumtuliza kwa kumpiga piga mgongoni.

“Let me handle the inferior Vena Cava , Probe ponted Scissors..”(Ngoja mimi nishughulike na Vena Cava ya upande wa chini , nipe mkasi Probe pointed Scissor)

Baadhi ya wasaidizi walikuwa wakitokwa na jasho sio kitoto lakini muda huo huo wakiwa katika hali ya kuguswa na namna ambavyo Dokta Clark alikuwa na utulivu wa hali ya juu katika kile anachokifanya

Upande wa Dokta Vincent ambaye yeye alikuwa akidili na Ini alikuwa bize kuhakikisha hachanganywi na changamoto zinzoendelea kujitokeza, aliendelea kufanya kazi kwa juhudi kubwa kukamilisha ndani ya muda .

“Kulingana na upandikizaji wa ini , ateri ya ini tayari imeunganishwa ,nitaendelea na ujenzi wa Gallblader, Twezer line forty…”Aliongea Vincenti na kumfanya Clark kumwangalia mwanafunzi wake na kutingisha kichwa kuonyesha kwamba alikuwa akifurahishwa na uwezo wake.

“Utumbo unazidi kupanuka , ongeza dozi ya kutuliza misuli(muscle relaxant), Dr Clark kama hali itaendelea hivi nafasi yetu ya mafanikio inazidi pia kushuka “Aliongea Dokta Vincent.

“Jipe utulivu, unadhani sijafikiria hilo ,kila kitu kimezingatiwa lakini kama daktari hata kama kuna nafasi ndogo sana ya mafanikio hakikisha unatumia hio hio mpaka itoshe na ifanye kazi”Aliongea na kuwafanya wote kuvuta pumzi na kuongeza umakini.

Upande wa wtazamaji Dokta Lee alianza kumkubali Dokta Clark kwa namna ambavyo alikuwa akijiamini.

Muda huo huo Dean(mganga mkuu) wa hospitali hio alionekana kupokea simu na kusikiliza kwa dakika chache na kisha akaipitisha kwenda kwa mkurugenzi Gong Gyechhung.

“Unafanya ujinga gani wewe mpumbavu ,toka haraka eneo la ajali na uje hapa ndani ya muda”Aliongea Gong Gyechung kwa hasira na kisha akakata simu na kufanya watu wote kumgeukia.

‘Kuna kilichotokea?”Aliuliza yule mganga mkuu kwani mtu aliepiga alitaka kuongea moja kwa moja na mkurugenzi.

“Gari ambalo lilikuwa likisarifisha moyo limekutana na ajali njiani hivyo kusababisha msongamano wa magari mrefu”Aliijibu

“Nini!!! … ni zaidi ya masaa mawili sasa kwanini hakuna ambaye ametoa taarifa?”Aliongea Haoming huku akionyesha kuchanganyikiwa.

“Ulisema mwenyewe hakuna tatizo ambalo linaweza kutokea kwanini sasa hivi?””Aliongea Yezi ambaye alikuwa na hofu kuzidi wote mara baada ya kusikia habari hio.

“Damn it , sijali kama unaniamini au lah , lakini hata mimi sikutarajia kama kunaweza kutokea ajali”Aliongea huku akig’ata meno kwa hasira na kufanya watu wote kuwa katika hali ambayo haielezeki.

“Dr Clark gari ambalo linasafirisha moyo limekwama njiani na barabara yote imefungwa , moyo hauwezi kufika ndani ya muda , narudia moyo hauwezi kufika ndani ya muda , hivyo tafadhari fanya mchakato wa kughairisha upandikizaji wa moyo”Aliongea Dokta Lee kwa kupitia Maiki.

Ndani ya Thieta kila mmoja alishitushwa na taarifa hio na kujikatia tamaa kabisa , hata Clark ambaye alikuwa bize alijikuta akisita kuendelea na kuanza kuangalia kila mmoja ambaye yupo hapo ndani.

“Barabara gani ajali hio imetokea?nitaenda kwa haraka na kuchukua moyo na kuuleta hapa ndani ya muda”Sauti nzito ya Kim jip ilisikika

“Ni upande wa kusini katika daraja la Dongjak , nishatuma tayari watu kufaulisha kupitia barabara nyingine”Aliongea Gong Gyechung,

“Hakuna muda wa kutosha kufanya hivo , waambie wakae sehemu walipo na nitawakuta , nitawafuata kwa kutumia Chopa yangu”Aliongea Kim Jip kwa Amri.

Gong Gyechung mpaka hapo alikuwa katika hali ya wasiwasi kutokana na namna wanafamilia hao walivyokuwa wakimwangalia kwa macho ya lawama namna ambavyo anashughulikia swala hilo.

“Ngoja niende mimi , sidhani kama atafika ndani ya muda , baki na Yezi”aliongea Roma akimwambia Edna kwa kutumia liugha ya kiswahili na Edna hakutaka kumzuia na kumwambia aende haraka na Roma alitoka katika hilo eneo bila ya wengine kufahamu anaenda wapi maana amemuaga Edna tu.

Lakini Yezi alijua Roma ambacho anajaribu kufanya , upande wa chumba cha upasuaji mara baada ya Clark kugeuka na kumuona Roma akiondoka hilo eneo , ujasiri ulirudi na kisha kugeukia wasaidizi wake.

“I need you to handle the superior Vena Cava ,in addition to our prior arrangement , Vincent how is progress?”(“Nataka ushughulikie Vena Cava ya upande wa juu kulingana na mpangilio wetu , Vincent vipi maendeleao?”)

“Kwa sasa naingia hatua ya mwisho mwisho ya kufunganisha utumbo ulioachia..”Aliongea na kumfanya Clark kuridhika.

“Dr Clark unahisi moyo utaweza kufika hapa kwa wakati?”Aliuliza Dokta Wallen.

‘Tusiwe na wasiwasi , tunapaswa kumuamini Roma”Aliongea

“Roma!!”

“Yeah , tupo chini ya masaa mawili mpaka kukamilisha , unapoteza muda,..”Aliogea

Upande mwingine katika eneo la hifadhi ya msitu kusini mwa jiji la Seoul karibu na daraja la Donjak Roma aliweza kutokezea katika upande ambao haukuwa ukipita watu.

Ilikuwa ni mchana hivyo Roma hakutaka kufanya vitendo ambavyo vitaibua taharuki.

Roma yeye alikuwa na haraka zaidi kuliko Kim Jip ambaye anatumia Chopa kufika hapo kwa ajili ya kuchukua moyo

Roma mara baada ya kuchunguza hilo eneo na kutoona kitu ambacho alitarajia alitumia uwezo wake wa kijini kuskani eneo zima hususani katika eneo la juu ambalo kulikuwa na msongamano mkubwa wa magari

Palepale aliweza kugundua tatizo lilikuwa nii moja wapo ya gari aina ya fuso lililokuwa katikati ya daraja likivujisha mafuta na kuanza kuwaka moto huku likiwa limekaa mshazari likizuia magari mengine kutoweza kupita.

Roma kwa haraka haraka alijua mpaka magari hayo kuweza kupita yote basi itachukua masaa mawili , eneo lote lilikuwa na ving’ora vya magari ya polisi ambayo yenyewe yaliongeza msongamano zaidi kwa aneo la mbele.

Ilikuwa ngumu hata kwa Kim Jib kufika hapo na Chopa yake halafu kuweza kufahamu ni gari ipi ambayo imebeba moyo.

Roma mara baada ya kukagua magari yote hatimae aliweza kuona gari dogo ambalo halikuwa ambulance lenye maandishi ubavuni kutoka hospitali ambayo moyo unatokea na palepale alipotea kutoka aliposimama na ile anaibukia ni pembeni ya gari hio karibu na mlango wa dereva na kumfanya aanaendesha kushituka.

“Sir Kuna tatizo lolote ?”

“Nimetokea katika ukoo wa Park , moyo wa kupandikiza uko wapi”Aliuliza Roma.

“Moyo gani tena , kuna mwenzako mwingine kafika hapa na kusema ametokea ukoo wa Park na nimempatia moyo tayari”

“Nini? Una uhakika ametokea katika familia ya Park? Jina lake ni nani?”

“ni bwana mdogo hivi kijana , jina lake ameniambia anaitwa Kim Jip”Aliongea yule dereva na kumfanya Roma kushangaa kwani hakutegemea kama Kim Jip anaweza kufika hapo kabla yake wakati alisema anakwenda na chopa.

“Ameelekea upande upi baada ya kumpatia? Na boksi lililobeba moyo huo linafanana vipi?”

“Ameelekea upande ule wa magharibi , ni ndani ya dakika kama mbili zilizopita na boksi ni rangi nyekundu”Aliongea yule dereva huku akiwa kama aliechaganyikiwa.

Roma mpaka hapo alikuwa tayari na majibu yake ambayo alihitaji na bila kuchelewa alikimbia kuelekea upande wa magharibi.

Roma alijiambia haiwezekani Kim Jip kufika hapo kabla yake , hivyo kwa haraka haraka aliamini mtu ambaye amefika hapo na kuchukua moyo alikuwa na mpango wa kumsingizia kim Jip.

Lakini Roma allijiuliza kwanini Kim Jip ndio ambaye amechaguliwa ili hali alikuwa mtu wa kawaida ambaye hata kuongea kwake ni mara chache sana.

Roma akiwa anasafiri kichawi akiendelea kukagua mazingira aliweza kuona kitu cha rangi nyekundu kilichoshikiliwa na mtu na palepale aliweza kuibukia mbele ya yule mtu .

Alikuwa kama Kim Jip mwenyewe kutokana na mwonekano wake na kama ni mtu mwingine wa kawaida angeweza kudanganyika na kuamini kwa asilimia mia mtu huyo aliekuwa mbele yake ni Kim Jip.

Yule mwanaume alionyesha mshutiko mara baada ya kutokewa na mtu mweusi mbele yake.

“Wewe ni nani?”

“Umeshindwa kunijua mimi , hivyo moja kwa moja inakufanya uwe feki”Aliongea Roma na kumfanya Kim Jip feki kurudi hatua moja nyuma.

“Sijali wewe ni nani , hivyo nipishe”Aliongea lakini Roma hakuwa na matamanio ya kundendeleza maongezi wakati anajua kwamba Clark anasubiria moyo huo kufikishwa ndani ya muda , hivyo alimsogelea kwa spidi yule Kim Jip feki na kwa kutumia mkono mmoja alishika lile boksi la rangi nyekundu.

Mwanaume alikasirishwa na kitendo cha Roma na palepale alitoa kisu mfano wa Daga akidhamiriia kumdunga nacho Roma eneo la tumboni.

Roma alikuwa ashategemea hivyo alimuacha afanye kile anachotaka na yeye kuendelea kung’ang’ania boksi.

Mwanaume yule mara baada ya kisu chake kukutana na ngozi ya Roma ni kama kimegonga kwenye jiwe kwani kilishindwa kupita na kumfanya yule mtu kujawa na mshangao pamoja na mashaka akiamini mtu ambaye yuko mbele yake ni shetani alie katika ngozi ya ubinadamu.

Roma mara baada ya kumpokonya lile boksi alimshikilia shingo na kumning’iniza hewani na kuanza kumkagua ili kujua ni mbinu gani aliotumia kubadilisha sura yake na kuiga ya Kim Jip.

Roma mara baada ya kumchunguza alifahamu staili yake ni kama ya Yamata sect lakini hio yenyewe ilikuwa na utofauti hivyo kwa haraka haraka aligundua inatokea katika makundi ya kininja ya baa la Asia upande wa Kusini Mashariki , mbinu yao haikuwa na muunganiko wowote na makundi ya Kijapani.

“Wewe ni nani?”Aliuliza Roma.

“Naitwa Kim Jip , unapata wapi ujasiri wa kuchokoza familia ya Park?”

“Unashindwa kuelewa upo kwenye hali gani si ndio , ukiendelea na ujinga navunja shingo yako?”Aliongea Roma lakini yule mwanaume alionekana kuwa na mafunzo ya hali ya juu kwani hakuonyesha hofu ya aina yoyote ile na palepale wakati Roma akisubiria jibu ghafla tu yule Kim jip feki alianza kutetema na palepale alitoa povu mdomoni.

Ilionekana tayari amekwisha kujiua na kumfanya Roma kushangazwa na ujasiri wake wa kujiua mwenyewe , mpaka hapo alijua watu waliomtuma sio wa kawaida.

Roma mpaka hapo aliona mtu huyo hana thamani tena huyo hivyo alimtupia pembeni na kuondoka hilo eneo kuanza safari ya kruudi hospitalini.

Hakutaka kumkausha kwani aliamini kama polisi wataweza kugundua miati yake basi wangefanya uchunguzi na ukweli ungejulikana .

Ndani ya hospitali ya Chuo ya Seoul watu wote aliokuwa wakiangalia upasuaji walionekana kuwa katika hali ya wasiwasi mno kutokana na kwamba mpaka muda huo hakukuwa na majibu ya kueleweka juu ya wapi moyo wa kupandikiza ulipo.

“Moyo unafika saa ngapi? , kadri muda unavyozidi kwenda utakosa uwezo wake wa kufanya kazi na kufanya upasuaji usifanikiwe”Aliuliza moja wapo wa madaktari wa hospitali hio.

“Kutokana na kuchelewa kwa kuondoa Adhesion kuzunguka moyo , hawawezi kumaliza ndani ya muda , hivyo sidhani kama wanaweza kufanikiwa hata kama moyo utafika ndani ya muda”Aliongea Dokta Lee na kufanya jopo lote la madaktari na wasiokuwa madaktari kuwa katika hali ya kukata tamaa wakiamini kabisa kwamba upasuaji mpaka hapo umekwisha kufeli.

Upande wa Thieta dokta Vincenti ndio kwanza alikuwa akimalizia kukata uzi wa mwisho wa mshono kukamilisha upandikizaji wa ini.

“The Transplant of the liver has completed , Dr Clark my work end here , I yield good faith on you with the rest of the operation”(Upandikizaji wa ini umekamilika , Dokta Clark kazi yangu inaishia hapa, natoa imani njema kwako na upasuaji uliobakia)

“Good work”Alijibu Dpokta Clark na Daktari msaidizi wa Clark alimwangalia dokta Clark.

‘Hatua ya mwisho tutaanza kuondoa Adhesion upande wa ventrikali ya kushoto , Dr Clark sidhani kama tunaweza kumaliza ndani ya muda”Aliongea na kumfanya Dokta Clark kuangalia kidogo moyo na kisha akaweka vifaa chini.

“Adhesion Complete “Aliongea na kufanya wasaidizi wake kushagnaa akimaanisha kwamba uondoaji wa ukovu umekamilika licha ya kwamba haujakamilika.

“Lakini Dokta Clark hatujamaliza kukata ukovu wa upande wa chini?”

“Yupo sahihi Dokta , huwezi kukata tamaa mapema , si ulisema mwenyewe hakuna kukata tamaa?”Aliongea nesi mkubwa.

Upande wa eneo la watazamaji Dokta Lee alionyesha kuwa katika hasira mara baada ya kuona anachokifanya dokta Clark.

“Clark unafanya nini , kama huwezi kukata ukovu wote ndani ya muda huwezi kumaliza upasuaji”alifoka.

“Nini kinatokea , kwanini Dokta Clark kaacha kuendelea?”Aliuliza Yezi kwa wasiwasi.

“Sijui anafanya nini , lakini kama ukovu wa eneo la Ventrikali ya kushoto usopokatwa hakuna uweezekano wa kuvuta moyo nje na ukatoka”

Wakati ndani ya thieta kila mtu akishindwa kuelewa nini anachotaka kufanya Dokta Clark palepale alianza kuongea.

“Mpaka sasa tunapaswa kusubiri kuona kama anaweza kuleta moyo dani ya muda muafaka”Aliongea na kisha palepale aligeukia saa ya mshale iliokuwa ikisikika ndani ya hiko chumba.

Muda huo kila sekunde ilifanya tumbo la kila mmoja kupatwa na joto kali mno na ilikuwa ni kama ile saa ilikuwa ikibipu ndani ya tumbo la kila mmoja.

Dakika tano zilipita na muda huo huo mlango wa chumba cha thieta ulifunguliwa na nesi ambaye alionekana kuwa katika haraka huku mkononi akiwa maeshikilia boksi la rangi nyekundu.

“Dr Clark the heart , The heart is here”Aliongea akisema moyo uko hapa Dokta clark.

Timu yote ilipatwa na ari mpya mara baada ya kuhakikisha ni moyo kweli wakufanyia upandikizaji na kazi ilianza upya.

Upande wa chumba cha watazamaji Roma aliweza kurudi na kwenda kukaa katika sehemu yake na palepale Clark aliekuwa kwenye chumba cha upasuaji aligeuka na kumwangalia Roma kwa macho yaliokuwa yakiongea kitu na Roma alimpa ishara pia na kisha Clark akarudisha macho kwenye kazi yake na akaendelea.

Upande wa Edna alivyoshuhudia namna ambavyo Roma na Clark wanavyoongea kwa ishara alijikuta moyo wake ukifurukuta.

“Mr Roma umefanikiwa vipi kuweza kurudi kwa haraka mpaka ukamzidi hata Kim Jip ambaye ametumia Chopa?”Aliuliza Gong Gyechung.

“Sidhani kama ni tatizo kwangu kurudi kwa haraka wakati muda ulikuwa unapotea”

“Ah.. ni kweli”Aliongea huku akifuta jasho lililokuwa kwenye uso wake huku akipotezea shauku yake.

Upande wa Park Jonghyun alimwangalia Roma huku akionyesha hali ambayo hajaridhishwa kabisa na matendo yake , lakini hata hivyo hakutaka kuonyesha wazi na watu kumsoma mawazo yake.,

Upande wa Dokta Lee na wenzake hawakuwa hata na habari namna gani Roma amefikisha moyo kwa haraka , mawazo yao yote kama madaktari yalikuwa kwa kile ambacho kinaendelea ndani ya chumba cha upasuaji, walijua hata kama moyo umefika hakuna namna ya upandikizaji kumalizika ndani ya muda ilihali hata moyo ulioharibika bado upo ndani ya kifua cha mgonjwa.

“Clark unafikiria nini…??”Aliuliza Dokta Lee ambaye alikuwa kwenye mhemko wa hali ya juu kwa kile ambacho kinaendelea, maana kidogo tu akiona jambo haelewi lazima ainue maiki na kuongea.

“The Transplant will start now ,Proceed with Piggyback propagation heart transplant”Aliongea .

“Wow!”Madaktari wote waliokuwa wakitazama upasuaji huo walishangazwa na maamuzi yake.

Upande wa Dokta Lee mshipa wa damu ulijitengeneza katika uso wake huku jasho likimtoka

“Oh! Huo ndio mpango wake?”

“What is happening, Piggyback what?”Aliuliza Gong Gyechung akiwa hajaelewa chochote , ijapokuwa maneno ya kingerea ameyasikia lakini hajaelewa maana yake katika maswala ya kitabibu.

“Piggyback unafahamika zaidi kama Parellel heart transplant ni njia ambayo nilisoma kwenye vitabu pekee na sijawahi kuona ikifanyika, ni njia ambayo inatumika kupandikiza mgonjwa na mioyo miwili kwa wakati mmoja , lakini kwa anachotaka kufanya Dokta Clark ni kuacha moyo wa Park Juan wenye shida kuendelea kufanya kazi huku akipandikiza moyo mwingine mpya pembeni yake na kuunganisha na mfumo wa mzunguko wa damu ya mwili, faida yake ni kwamba inamfanya mgonjwa kuwa na mioyo miwili kwa wakati mmoja inayofanya kazi , hivyo inasaidia wakati mpya ukizoea mwili na mwingine unaendelea kutoa sapoti ya kufanya kazi na hata huko mbeleni ukifa kabisa basi mpya utaendeleza kazi ya kusukuma damu”Aliongea Doka Lee na kufanya wale wasiokuwa madaktari kushangazwa na maneno yake.

“Nishawahi kusikia aina hii ya upasuaji kufanyika mara moja tu ndani ya Uk , unataka kumaanisha aliefanikisha ni Dokta Clark?”Aliuliza Dean wa hospitali.

“Lakini hata hivyo ili kuweza kufanikisha hilo lazima moyo wa kwanza auachanishe kwanza na mwili ndio aendelee hivyo mafanikio bado ni madogo”Aliongezea Doka Lee na madaktari wengine wote walikubaliana nae na kutaka kuona ni kipi dokta Clark angeweza kufanya kwa hali hio na muda mchache uliobaki.

Najua mnanidai vipande nitaendelea kuvifidia.
Sawaaa
 
Acheni nae huyo waga anapenda attention sana..
Kulikua na haja gan ya kuwaambia mpaka muda watu wazima sasa?
 
SEHEMU YA 523.

Profesa Clark hakujali sana namna ambavyo watu wa nje ya chumba hicho cha upasuaji walivyokuwa na wasiwasi zaidi ya kuwaambia wasaidizi wake kuwa makini na upasuaji.

Mpaka anakuja kumaliza upasuaji hakuna ambaye aliamini kama amefanikiwa kwa asilimia mia moja kuokoa maisha ya Park Juan..

Dokta Lee ambaye aliangalia mchakato mzima wa upasuaji alihisi ni kama vile anaota kwani mambo ambayo alikuwa akifanya Dokta Clark hakuwahi kuyashuhudia na siku hio ilikuwa mara yake ya kwanza.

Kuna baadhi ya taratibu za kiupasuaji aliishia kuzisoma tu kwenye vitabu na hajawahi kuona zikifanyika kwa vitendo , lakini mbele ya Dokta Clark baadhi ya nadharia ambazo amezisoma katika safari yake ya kuwa daktari ameweza kuona mubashara kabisa zikifanyika.

Madaktari na manesi wasaidizi walimhusudu Dokta Clark pia kwa uwezo wake, ilionekana kwao ni kama vile alikuwa amezingatia kila changamoto ambayo ingeweza kujitokea katika upasuaji huo.

Madaktari wote waliofika kuangalia namna upasuaji unavyofanyika walijikuta wakisimamama na kuanza kupiga makofi.

Yezi alifurahi sana kuona babu yake ameweza kuhimili upasuuaji huo mzito kufanyika , upasuaji wa upandikizaji wa viungo viwili kwa wakati mmoja na mpaka hapo shukrani zake zote zilienda kwa Dokta Clark ambaye amemsaidia babu yake.

Katika watu ambao hawakupenda mafanikio ya upasuaji huo kufanikiwa alikuwa ni Park Jonghyun , lakini kwa kinafiki alitoa shukrani kwa madaktari wote waliohusika katika upasuajji.

Baada ya upasuaji kumalizika wanafamilia wote walikubaliana kutafuta mgahawa kwa ajili ya chakula cha usiku.

Kim Jip ambaye aliondoka kwenda kuchukua moyo aliweza kurudi akiwa ameongozana na baadhi ya mabodigadi wa familia ya Park , pamoja na baadhi ya polisi.

Alikuwa kauzu kama kawaida yake na alikuwa tayari ashapata taarifa ya Roma kurudi hospitalini akiwa amefanikisha kuupata moyo uliohitajika.

“Asante sana Mr Roma”aliongea Kim Jip mara baada ya kumsogelea Roma.

“Umeweza kumpata mtu alieigiza sura yako?”

“Hio ndio sababu ambayo imetufanya tuwe hapa Mr Roma , kwa majina naitwa Jang Yoon kiongozi wa idara ya uchugnzi ya kituo kikuu cha polisi Seoul , kulingana na uchunguzi wetu wa mwanzo dereva ambaye alipewa jukumu la kuendesha gari lililobeba moyo amesema wewe ni mtu pekee wa mwisho ambaye uliweza kukutana na mtuhumiwa , hivyo hili ni swali letu kwako , Mtuhumiwa yuko wapi?”

“Si alishakufa, hamkuweza kupata mwili wake? , alijiua yeye mwenyewe kwa sumu”Alijibu Roma huku akionyesha mshangao kidogo.

“Mr Roma tunataka majibu yako ya kweli , wewe ndio uliechukua moyo kutoka kwake hivyo lazima utakuwa umemuona , tafadhari tuambie yuko wapi mtuhumiwa?”

“Oh! Kwahio mnachojaribu kumaanisha ni kwamba hamjaweza kuona mwili wa mtuhumiwa?”

“Sisi ni polisi , unadhani tunaweza kudanganya juu ya hili , Bwana Kim Jip hapa na yeye atapenda kujua nani ambaye amehusika kuigiza sura yake”Aliongea yule polisi wa Kikorea na kumfanya Roma kujilaumu kwa maamuzi yake alioyafanya, mpaka hapo alijua kabisa waliokuwa nyuma ya Kim Jip feki watakuwa waliwahi eneo la tukio na kisha wakaondoa mwili na kwasababu ya kukosekana kwake kesi ni kama imemwangukia yeye.

“Dereva alithibitisha kama alimuona Kim Jip feki na sisi wakati tukiwa tunamuhoji ndio tulipoweza kusikia taarifa ya moyo umeweza kuufikisha hospitalini , kutokana na mlolongo wa matukio tunapata hisia za wewe kuhusika katika hilo, hivyo basi itakuwa vyema kama utakubali kwa hiari yako kuongozana na sisi mpaka kituo cha polisi ili kutoa maelezo yako rasmi”

“Hamuwezi kumchukua bila ya kuwa na ushahidi , Uncle Roma ndio ambaye ameokoa maisha ya babu yangu”Aliongea Yezi akimkingia Roma kifua.

Edna hakujua kinachoendelea kutokana na kwamba hakuwa akifahamu lugha ya Kikorea na ilibidi aombe kutafsriwa na Roma alimweleza kwa ufupi namna tukio lilivyotokea na kumfanya sasa kuelewa na kuwa na wasiwasi.

Jopo lote mpaka hapo waliweza sasa kujua kama ile ajali iliosababisha moyo kuchelewa haikuwa bahati mbaya bali ulikuwa ni mpango wa watu na hamu yao yote ya kwenda kula ilipotea.

“Mr Roma ni mgeni wa heshima wa ukoo wa Park bila kushahau mchango wake mkubwa aliofanya kwa babu yangu kwa matibabu yake yake ,kapteni Jang nakushauri ufikirie mara mbili unachotaka kufanya”Aliongea Park Jonghyun.

“Bila kuwa na ushahidi wa kueleweka mtu wa mwisho kumuona mtuhudmiwa atageuka kuwa mshukiwa mkubwa wa kile kilichotokea , hivyo naomba ushirikiano wenu kwa jeshi la polisi la jamhuri ya Korea”Aliongea Kapteni Jang.

“Okey hakuna shida , kama unataka kuchukua maelezo yangu basi nitaongozana na wewe , hata mimi pia ninashauku ya kujua mwili umeenda wapi , hivyo nyie endeleeni kwenda kupata chakula na msiwe na wasiwasi”Aliongea Roma na kufanya kundi lote kukubali na Roma aliondoka na polisi.

Upande wa Edna alijua kabisa Roma hakuwa mhusika lakini hakupenda Roma kupelekwa kituo cha polisi.

Roma mara baada ya kuingia kwenye gari la polisi , liliondoshwa na kuelekea upande wa kusini mwa jiji la Seoul na baada umbali kama wa kilomita tatu gari ile ilikunja kulia na ilichukua njia ya pembeni likiachana na barabara kuu na kuingia upande wa viwanda.

“Ofisa Jang inashangaza kituo cha polisi kuwa maeneo haya ya Viwanda?”Aliuliza Roma ambaye muda wote alikuwa ametulia lakini wale mapolisi watatu walipotezea swali lake na gari likaendelea kuserereka

Upande wa Roma aliishia kutabasamu kifedhuli na kisha akakaa kimya kijua mwisho wake ni nini.

Baada ya muda kama dakika tano gari iliingizwa ndani ya eneo lenye ukuta kwa nje, sehemu ambayo ilionekana kuna ujenzi wa kiwanda unaendelea kutokana na uwepo wa magreda ambayo yanaanza kusawazisha ardhi ili kuweka msingi.

“Shuka chini”Aliongea polisi mmoja kwa namna ya kufoka kwa lugha ya kikorea.

“Hatuendi kituo cha polisi?”Aliuliza Roma mara baada ya kukagua mazingira.

“Kituoni kufanya nini?”

“Unamaaisha nini?”

“Kwasababu hapa ndio unakwenda kufia”Alijibu mwanaume aliejitambulisha kwa jina la Jang.

Polisi wawili ambao walikuwa warefu walimsogelea Roma mara moja , kwa haraka haraka.

Roma aliweza kuona miili yao ilikuwa mikakamavu na kuhisia wanaweza kuwa na mafunzo ya kimapigano.

Lakini upande wa Roma hakuwa na hofu kabisa , kwanza kabisa alikubali kuondoka na polisi hao makusudi kwani alishaona nia yao ovu.

Walianza kumshambulia palepale, lakini kila pigo ambalo walijaribu kumpiga nalo Roma aliishia kukwepa na kumfanya yule polisi ambaye alikuwa kama kiongozi kujiunga pia kwenye kushambulia .

Mmoja wapo alileta teke la hewani la kitaekwondo akidhamiria kumpiga Roma shingoni lakini Roma kwa ustadi kabisa aliweza kukamata mguu wake wa kulia yule bwana na kisha akamzungusha hewani na kumtupia kwenye trekta.

Mwingine alijileta kizembe na Roma kwa kutumia mguu wake wa kushoto alimtegua goti pale na akadondoka chini huku akiugulia maumivu.

Jang Yoon alijawa na kiwewe na palepale alitoa bastora yake na kuikoki akitaka kumshambulia Roma kwani mpaka hapo aliona kabisa hakuna namna wanaweza kushinda kwa kupigana nae bila siraha.

Lakini kabla hata hajafyatua kiganja cha mikono yake kilifikiwa na kupindishwa na bastora ikadondoka chini na Roma akaipiga teke kwenda kutua mbali.

“Nyie watu najua mpo katika kundi moja na yule mwigizaji mwenzenu wa sura , si ndio?”Aliuliza Roma na kuwafanya wale mabwana kushindwa kutoa jibu lakini walikuwa wakikiona kifo chao usiku huo kipo karibu , kwani mtu aliekuwa mbele yao hakuwa wa kawaida.

“Nani kawatuma na mnatafuta nini? Nawapa nafasi ya kujibu la sivyo nitawanyonga mmmoja mmoja mpaka mniambie ukweli”Aliongea Roma lakini wale mapolisi walionekana kutotaka kujibu hivyo Roma alimsogelea mmoja ambaye alikuwa amejipigiza kwenye trekta na kumpiga karate ya uti wa mgongo na kilichosikika ni kuvunjika kwa uti wa mgongo na kufariki palepale.

Wale wawili waliobaki walijikuta wakijawa na hofu na kumuona Roma sio mtu wa kawaida kwa namna alivyommaliza mwenzao kikatili mno.

“Kwasabau wote nyie wawili mpaka muda huu hakuna ambaye amejiua kwa sumu hisia zangu zinaniambia nyie hamna mafunzo ya U’ninja, hivyo ni bora kujieleza mapema kabla sijatekeleza vifo vyenu kama mwenzenu”Aliongea na bado walionekana kusita sita na Roma alimsogelea mmoja kwa spidi na kumsukumia kwenye ukuta kwa nguvu akimnyonga shingo.

“Naomba uniache niondoke… sijui chochote tafadhari … sitaki kufa naomba usiniue”aliongea mwanaume yule kwa namna ya kujitetea.

“Nishakwambia nahitaji majibu ..”Aliongea Roma na palepale hakutaka kuendelea nae kwani alimvunja shingo na kumtupa chini.

Jang Yoon mara baada ya kushuhudia wenzake wote wakiwa wamepoteza maisha kirahisi aliangalia namna ya kukimbia na baada ya kupata upendo alitoka nduki , lakini Roma hakutaka kumpa nafasi na hakutumia uwezo wake wa kijini bali aliokota jiwe na kulivurumisha upande wake na kumpiga nalo mgongonni karibu na kiuno na kudondoka chini palepale huku akigulia maumivu na akamsogelea.

“Nitaongea , nitaongea tafadhari usiniue”Aliongea Jang Yoon huku kila akijaribu kusimama alikuwa akidondoka chini kwa mauamivu.




“Kwanini ulikuwa ukileta ugumu , pengine nisingechafua mikono yangu kwa kuuwa wenzako”Aliongea Roma kwa tabasamu lake la kuogopesha na kumfanya Jang Yoon kuanza kuinua mdomo wake kwa wasiwasi.

“Nime.. nimetokea katika umoja wa siri wa North Buyeo, yalikuwa ni maagizo tuliopewa kutoka kwa viongozi kukuleta hapa na kukuua kwani umeingilia mipango ya jamii yetu “Aliongea na kumfanya Roma kushangaa

“North Buyeo, unaongea ukweli?”

“Ndio , sisi ni Double agent ambao tumepandikizwa katika kituo cha polisi kufanya kazi kwa manufaa ya taasisi”

“Kwa maelezo yako unamaanisha mpo wengi zaidi , huenda kila nyanja ndani ya taifa, si ndiio? Kama ni hivyo wewe nafasi yako katika jamii hio ni ipi?”

“Nafasi yangu ni ya chini lakini sio chini kabisa”

“Nani mwingine anajua kuhusu hii taasisi ambaye yupo ndani ya kituo cha polisi?”

“Sina uhakika lakini mkuu wa kituo cha polisi ni mwanachama pia ambaye yupo ngazi ya kati”

Roma alishangazwa na ufunuo huo, mwanzoni alidhania labda ni kundi tu la maninja ndani ya Korea lakini mpaka hapo alijua kabisa sio kundi bali ni taasisi na kama ni hivyo mizizi yake ndani ya Korea itakuwa mikubwa mno.

Roma hakuwa na matamanio sana na taasisi hio kwasababu haipo nchini kwake na pia sheria hazikumruhusu kuingilia mambo ya binadamu wa kawaida , lakini kilichomfanya kutaka kuingilia ni kwasababu ya Yezi , kama moyo wa upandikizaji umechelewesha na taasisi hio moja kwa moja alijua kabisa hata Yezi pia anaweza kuwa katika hatari akiendelea kuishi Korea.

“Mr Roma ,, je naweza kuondoka?”

“Ndio unaweza kuondoka lakini nitakusindikiza”

“Hapana hapana , nitaenda mwenyewe”Aliongea huku akijikongoja kusimama na kuanza kusogea kuelekea getini , lakini Roma hakuwa na nia ya kumuacha aende hivyo alimsogelea na kummaliza palepale baada ya kumpiga ngumi ya utosini na kwasababu ngumi yake haikuwa ya kawaida kichwa chake kilichanguka paleplae na kumfanya nguo aliovaa kurukiwa na matone ya damu.

“Nilikwambia nitakusindikiza kuna haja gani ya kukimbia, haya umekufa sasa wasalimie kuzimu”Aliongea mwenyewe na kisha palepale akaita nguvu za kijini na kukausha miili yote kimazingara na sehemu ikawa safi bila ya kuacha ushahidi wowote kama kuna watu waliokufa katika hilo eneo,.

Baada ya kumalizana na maiti zao alifungua gari la polisi na kulichunguza na hakuona cha maana na palepale aliita moto wa kijini na gari lile lilipuka kama limetegeshewa bomu , lakini ulipukaji wake haukutoa sauti yoyote kutoka eneo hilo.

Baada ya kumalizana na tatizo hilo dogo alitoa simu yake na kumpigia Edna ,tokea wafike hapo Korea walisajili laini za mitandao ya nchi hio ili kurahisisha mawasiliano.

“Wife kazi imeisha , mpo wapi sasa hivi?”Aliongea Roma kwa kiswahili na Edna alishangazwa na maneno yake na kumwambia sehemu waliopo.

Roma mara baada ya kukata simu alitafuta namba ya simu ya Makedoni na kupiga palepale, aliamini swala kubwa kama hilo la jamii ya siri hawezi kulifanyia kazi yeye mwenyewe bila ya kuhusisha mtaalamu wa maswala ya ujasusi.

“Master Pluto nilikuwa nikipanga kwenda kuoga , unataka nikusaidie nini?”Aliuliza Sauroni upande wa pili mara baada ya simu kupokelewa.

“Nataka kujua kati ya watu wetu ambao wapo Korea kusini , mahsusi walipo ndani ya jiji la Seoul , naweza kuwapataje?”aliuliza Roma.

“Tuna wanajeshi wa kundi la Guerilla lakini wapo Korea ya Kaskazini,kuhusu Seoul sidhani kama kuna uwezekano wa watu wetu kuingia huko bila ya kushitukiwa kwani mipaka yao ina ulinzi wa viwango vya juu sana”Aliongea Makedon na kumfanya Roma kuona ni kweli Korea kaskazini ni mbali kuwaleta watu wake ndani ya Korea kusini.

“Pumbavu , kwanini hakuna watu wowote ambao mmewaweka Korea kusini?”

“Master Pluto nadhani unaelewa kwamba kuna mgogoro kati ya Korea kusini na Korea kaskazini , kama tutaweka watu wetu ndani ya Korea kusini hakuna faida yoyote kwani hakuna misheni ya kufanya , upande wa Korea kaskazini imekuwa rahisi kwani tunafanya na biashara ya siraha katika ukanda huo”Aliongea Roma na hakutaka hata kusikiliza zaidi ya kumpatia maelekezo ya kufatilia maswala ya North Buyeo halafu amtumie kwenye Email yake na kisha akatoweka katika eneo hilo.

Baada ya dakika chache aliweza kutokea katika mgahawa uliojengwa kitamaduni ambao familia ya Gong na ya Park walikuwa wakipata chakula cha usiku na baada ya kuona amerudi walimkaribisha kwa ukaribu na kumuonyesha sehemu kukaa chini kwani hakukuwa na viti.

Upande wa Park Jonghyun mara baada ya kumuona Roma alionyesha mshangao ulioambatana na mshituko na kumfanya Roma amwangalie na kisha kumuonyesha tabasamu la kejeli na kisha akaketi chini , ni kama alikuwa akimwambia kwamba anajua kile ambacho anafanya sirini.




“Mr Rom , unaonyesha haupo vizuri nadhani ni uchomvu wa wiki hii yote , lakini niseme asante sana kwa kumsaidia babu yangu kwani kama sio wewe hatujui nini kingetokea”

“Naamini maneno yako ni ya dhati bwana Jonghyun”aliongea Roma na kukaa katikati ya Edna na Clark,

Clark alikuwa ashabadili mavazi yake na yupo hapo kuungana na kila mmoja kusherehekea mafanikio yake ya kukamilisha upasuaji.

Chakula kiliendelea huku Roma akiwa bize kuongea na Clark ambaye muda wote alikuwa akimshukuru kwa kumsaidia kuokoa taswira yake kama daktari kwa kufanikisha kufikisha moyo ndani ya muda.

Upande wa Edna chakula hata hakikuwa kizuri kabisa kwake kutokana na namna ambavyo Clark anaongea kwa kujibebisha mbele ya mume wake na wivu ulimjaa mno.

Clark usiku huo huo alichukuwa nafasi ya kutoa taarifa anarudi Uingereza siku inayofuatia na jambo hilo lilimfanya Edna kupatwa na ahueni maana aliona kama akiendelea kubakia nchini hapo angeharibu furaha yake.

Baada ya chakula kila mmoja alirejea nyumbani na upande wa Roma na mke wake walirudi katika jumba la Park Juan.

Roma mara baada ya kuingia chumbani haraka alimwambia Edna ampatie Laptop kwanni kuna kitu anataka kufanya na Edna ambae alijinunisha njia nzima alimpatia bila ya kuongea neno.

Roma alielewa kinachomsumbua Edna ni wivu kutokana na namna alivyokuwa akiongea na Clark kwa kutaniana na kujibebisha.

Roma mara baada ya kuchukua laptop hio alifungua haraka haraka na kisha akaunganisha na mtandao kisha akafungua baadhi ya taarifa ambazo zimetumwa na Makedoni kwa njia ya barua pepe yake,alianza ku’scroll’ kwa kusoma kila kitu kwa umakini na alishangazwa mara baada ya kuona mawazo yake yalikuwa sahihi, North Buyeo halikuwa kundi la kawaida la sirii ndani ya Korea kusini.











SEHEMI YA 524.

Msingi wa jamii ya siri inayojiita North Buyeo ulianza zamani sana tokea kipindi cha utawala Goguryeo , wakati ambao Buyeo ilikuwa ipo upande wa Kaskazini mwa bara hilo la Asia.

Katika historia mara baada ya utawala wa Goguryeo kusimikwa rasmi, utawala wa kifalme wa Buyeo ulikufa na kubakia kama kundi la waumini tu ambao walikuwa na matamanio ya kurudisha nchi yao.

Sasa taarifa ambayo Roma alikuwa akisoma ni kwamba North Buyeo ni jamii ya watu ambao walikuwa wakibeba maono ya mababu na kutokana na mipango yao ndani ya taifa la Korea kusini na korea kaskazini walianza kujipenyeza katika nyanja zote za kitaifa.

Roma mara baada ya kusoma taarifa yote aliona ni mgumu sana kumaliza watu wote wanaohusika katika Buyeo licha ya kwamba ni tishio kwa usalama wa Yezi.

Muda huo wakati akiendeea kuwaza , Edna alikuwa ndio anatoka bafuni na kufanya eneo lote la chumba kuwa na harufu nzuri ya Shower gel huku akijifuta maji na taulo na Roma alimwangalia na kuishia kumeza mate kwani urembo wa Edna kwake ni kama unaongezeka kila saa anayomwangalia.

Edna baada ya kuona Roma yupo bize na tarakishi alisogea kuangalia ni kitu gani anasoma na alishangazwa na taarifa hio na kutaka Roma amwelezee kwanini anasoma hio taarifa.

“Norht Buyeo mbona ni kama mambo ya kihistoria kwannii unasoma?”Aliuliza

“Babe Edna , umejuaje ni mambo ya kihistoria?”

“Nakumbuka nishawahi kusoma kitabu kimoja ambacho kimeelezea hio historia , nadhamni unaelewa hobi yangu ya kusoma vitabu ”Aliongea na kumfanya Roma kweli aone inawezekana hata hivyo Edna kama CEO alikuwa akipenda sana kusoma ili kupanua ufahamu wake hususani katika maswala ya kibiashara.

Roma ilibidi mwelezee namna tukio lilivvyotokea masaa kadhaa yaliopita na hisia zake juu ya jamii hio kutishia usalama wa Yezi, Edna alishagaa na kuwa na wasiwasi kwa wakati mmoja.

“Ni malengo gani wanayo hio jamii? Ni kheri kama watakuwa adui yako lakini kama wanataka kumdhhuru Park Juan basi haitakuwa salama kwa Yezi kuendelea kuishi hapa”

“Ndio maana kabla hatujarudi Tanzania napaswa kujua kila kitu kinachoendelea kuhusu hii jamii na kitu ambacho nina uhakika nacho ni kwamba Park Jonghyun ni mwanachama pia”Aliongea Roma na Edna alikubaliana nae kwani hakuwa tayari kuona Yezi anapatwa na shida ili hali kwake alikuwa akimchukulia kama mdogo wake.

“Wife una akili nyingi sana , nilidhania huna uelewa wowote kuhusu maswala ya kiihistoria ya nchi za huku, umenizidi hata mimi ambaye leo hii ndio kwanza najua maswala ya Buyeo kuwa katika historia ya kikorea”

“Lakini ni dhahiri simfikii Clark , ana akili nyingi na ana kipaji kikubwa mno?”Aliongea Edna huku akionyesha kabisa bado alikuwa na kisirani..

“Edna mke wangu , kwanini mpaka sasa una wivu, Clark na mimi hakuna kinachoendelea zaidi ya kwamba alikuwa kama mdogo wangu ambaye nilimuona akikuwa mpaka kufikia utu uzima ndio maana anakua huru akiwa mbele yangu”

“Ulimuona?, kama ni hivyo wakati huo wewe ulikuwa na miaka mingapi na yeye alikuwa na mingapi?”

“Yeye alikuwa na miaka kama nane au tisa hivi na mimi nilikuwa na miaka kumi na nne kwenda kumi na tano”

“Kama ni hivyo kwanzia sasa nataka nikuwekeee mipaka , kumuona akikua haimaanishi kwamba ndio umfanye awe mpenzi wako wa utotoni”Aliongea kikauzu na kisha alichukua rimoti na kuwasha Tv.

Na Roma alishindwa kujielezea zaidi maana Edna maneno yake ni kama hayaamini kabisa kila anapomuambia hakuna mahusiano.

Hofu ya Edna ilikuwa ni kwamba Clark ukiachana na kwamba alikuwa mrembo karibia kumfikia yeye , lakini pia alikuwa na akili nyingi na huenda ana msaada mkubwa kwa Roma kuliko yeye mwenyewe hivyo hofu yake ni kupinduliwa .

Wanawake wengine hakuwa na hofu nao kutokana na kwamba walikuwa wa kawaida sana na siku zote wapo chini yake na anaweza kuwamudu lakini kwa Clark ilikuwa tofauti.

Mtu mwingine ambaye alikuwa akiogopa Roma kuanzisha nae mahusiano ni Sophia.

Sophia anaweza asiwe na kitu kikubwa kama yeye , lakini likija swala la uzuri walikuwa wakikaribiana sana na yeye na Edna alikuwa amenuia kwenye moyo wake hatokaa aone mahusiano kati ya Roma na Sophia yanatokea.

Muda huo huo wakati Roma na yeye akijiandaa kwenda kuoga , walisikia mtu akigonga mlangoni na kumfanya Edna amwangalie Roma kwani haikuwa kawaida kwa kugongewa muda huo.

Roma alisogelea mlango na kufungua na aliweza kukutana na mwanaume ambaye amevalia mavazi ya suti yenye nembo maalumu kumtambulisha ni mfanyakazi wa hapo ndani.

“Mr Roma ,Mrs Edna kila kitu kipo sawa?”Aliuliza kwa lugha Kikorea.

“Wewe ni nani?”Aliuliza Roma na kumfanya yule bwana kushangaa.

“Mimi ni mlinzi katika hii nyumba na dakika chache zilizopita niliweza kusikia purukushani ikitokea upande huu ndio maana nimewagongea kuona kama mpo sawa”Aliongea

“Kama ni hivo kwanini umeshikilia kisu mkononi na kukificha au upo hapa kwa ajili ya kutuua?”Aliuliza Roma na ku,fanya yule bwana kushangazwa na jambo hilo , kwani hakujua Roma ameonaje kisu aina ya daga alichoshikilia kwani aliificha vyema kwa kukibana na ukuta.

Lakini hata hivyo hakuwa na muda wa kupoteza baada ya kuona mpango wake ushagundulika hivyo alitoa mkono kwa haraka na kuipeleka ile Daga usawa wa kifua cha Roma , lakini Roma kutokana na wepesi wake aliwahi kushikilia mkono wake ulioshikilia kisu na kuupindisha na kumfanya yule bwana kutoa ukulele na kukidondosha chini.

Edna ambaye macho yake yalikuwa kwenye runinga alishangazwa na purukushani hizo na kusimama kwa wasiwasi

“Wewe ni nani? North Buyeo wamekutuma?”aliuliza Roma.

Yule mwanaume alionekana kuchezesha meno yake palepale mara baada ya kuona amekamatika , lakini Roma alitegemea hilo hivyo alimuwahi kwa kumpiga shingoni na kumfanya palepale kupoteza fahamu.

Dakika hio hio Roma aliweza kusikia purukushani zingine zikisikika kutoka juu na mpaka hapo alijua wapo wengi zaidi.

“Edna kuwa makini , ngoja nikamwagalie Yezi inaonekana wapo wengi”Aliongea Roma na kwa haraka alitoka hapo akihofia Yezi anaweza kuwa katika hatari.

Muda uleule aliweza kutokea mbele ya chumba cha Yezi sehemu ambayo ndio aliweza kusikia sauti.

Muda huo Roma aliweza kushuhudia kijakazi wa kike akipigana na kijakazi mwingine wa nyumba hio, alikuwa ni kijakazi afahamikae kwa jina la Eujung msaidizi wake Yezi.

Eujung alionekana kuwa vizuri kwenye mapigano na Roma palepale aliweza kugundua huenda alikuwa na mafunzo ya juu ya Taekweond kwani hata mpinzani wake hakuwa haba lakini alikuwa akionyesha kumdhibiti vizuri.

Eujung hakuwa mzembe baada ya kukwepa mapigo mawili , alipiga sarakasi mzunguzo ambayo ilimpiga yule adui mtama na akadondoka chini na kabla hajamka , Eujeong tayari amekwisha kupiga teke lingine la shingo na kumlegeza kabisa na kumuweka chini ya ulinzi.

Roma alishangazwa na jambo hilo kwani hakutegemea kuona msichana wa kikorea aliekuwa mpole na kijakazi wa familia hio alikuwa na uwezo mkubwa kama huo , aliona huenda yote hio ni mipango ya Park juan babu yake Yezi kuhakikisha mjukuu wake anakuwa chini ya ulinzi mkali.

Eunjung alikosa umakini na adui yake na ghafla tu yule Ninja aliamka kwa mara nyingine na kutaka kumchoma na kisu tumboni na Roma palepele kwa haraka sana alimkaribia kijini na kumzuia kwa kumpiga utosini na palepale alilegea na kudondoka chini na ukawa mwisho wa uhai wake.

“Asante sana Mr Roma kwa msaada wako”Aliongea Eunjung na muda uleule Yezi aliekuwa akitetemeka aliweza kufungua mlango.

“Oh asante umekuja , naogopa mimi”Aliongea Yezi kwa hofu kubwa.

“Upo na Eujung hapa kwanini unapatwa na hofu wakati yupo vizuri kwenye kukulinda?”

“Sikujua hata kama anajua kupigana , babu nilimwambia sitaki mabodigadi na akinniahidi hatoniwekea , lakini inaonekana alinidanganya”

“Usikarisike Miss , Master kafanya yote kwa ajili yako”

“Sio kama nakasirika, asante kwa kuweza kuyaokoa maisha yangu”Aliongea na Eunjung alitingisha kichwa kukubali shukrani yake.

“Kama hapa kumefanyika mashambulizi vipi kuhusu hospitalini?”Aliuliza Eunjung kwa wasiwasi.

Eunjung kuongea hivyo hata Roma aliona uwezekano wa kushambuliwa kwa wakati mmoja hapo nyumbani na hospitalini ni mkubwa , lakini hata hivyo asingeweza kuondoka na kuelekea huko kwani bado usalama wa Yezi na Edna ulikuwa juu yake.

Edna alikuwa katika levo ya mwanzoni katika nusu mzunguko hivyo aliona hata kama anaweza kuweza kujilinda lakini hana uzoefu na kama atakutana na adui ambaye ana siraha kama bastora basi moja kwa moja angemdhuru.

Muda huo huo Edna alitoka na kuja mahali walipo huku akiwa ameshikilia simu ya Roma.

“Hubby simu yako inaita?”Aliongea na Roma alimsogelea na kuichukua na kisha akpokea palepale.

“Mr Roma nimeshangazwa sana kuona mpaka sasa bado upo hai?”Sauti ilisikika kwa lugha ya kikotea.

“Wewe ni nani au ndio nyie North Buyeo?”

“Mhh.. umetisha sana Mr Roma , mbali kabisa na matarajio yangu”

“Unataka nini kutoka kwangu?”

“Labda hujagundua kitu bado lakini kabla hamjarudi hapo nyumbani tayari mpango ulikuwa ushaandaliwa na hospitalini pia kwa wakati mmoja , kwa ajili yako Roma tutahakikisha unaendelea kuburudika kile tulichokupangia”Aliongea mwanaume huyo kwa sauti yake ya besi huku akicheka kicheko cha dharau.

“Nadhani mpango wako ni kulipua hii nyumba si ndio?”

“Upo sahihi , nyumba yote tushatega mabomu ya ukubwa wa C4 yanayotosha kutengeneza wingu kubwa la mlipuko na kuharibu jumba lote”

“Pumbavu zenu nyie wakorea naona mnaona mambo yanaweza kufanikiwa kirahisi hivyo , mnafikiri mnaigiza muvi sio? Hamchoshwi na huo upuuzi wenu?””

“Kama kitu hakivunjiki kuna haja gani ya kukirekebisha, Mr Roma kama hutaki kuona hio nyumba ikilipuka na mkeo pamoja na mdogo wenu Yezi kuangamia basi hakikisha unafanya kama tunavyokuelekeza”ilisikika sauti.

Roma hakuwa na wasiwasi hata hivyo na vitisho vyao kwani alikuwa na uhakika wa kuwakoa Edna na Yezi kwa wakati , lakini bado jambo moja ambalo lilimpa mashaka ni upande wa hospitalini lazima na penyewe kuna mtego ambao umetegwa.

“Mnataka nifanye nini?”

“Ni rahisi sana unachotakiwa kufanya ni kutoka mpaka nje na utaona gari aina ya BMW sedani nyeusi , ingia kwenye hio gari na endesha mpaka hoteli ya Myeondong kuna watu watakupokea hapo”Aliongea mwanaume huyo upande wa pili na Roma alikubali.

“Nini kinaendelea, ni watu kutoka North Buyeo?”aliuliza Edna na kumfanya Roma kucheka na kisha alimsogelea sikioni na kumnong’oneza.

“Utafanya kazi?”Aliuliza Edna huku akikunja ndita.

“Hio itategemeana na wewe CEO Edna , una uwezo mkubwa wa kuigiza hata wa kunidanganya mimi kwanini tusifanikiwe”Aliongea Roma ilionyesha kuna mpango ambao walikuwa wakipanga na Edna ni sehemu ya kuukamilisha.

“Kuwa makini sasa , tutaendelea kufuata mpango wako”Aliongea Edna na kumfanya Roma amshike Edna mashavu kama mtoto na kisha alitoka hilo eneo na kuanza kushuka kwa ngazi kuelekea chini.

“Anaenda wapi?”aliuliza Yezi.

“Tumepewa maagizo kutoka kwa watu waliotuma wauaji hapa na wanataka Roma afuate maagizo yao la sivyo hii nyumba na jengo la hispitali alilolazwa babu yako litalipuka kwani kumetegewa mabomu”

“Kwanini wanataka kufanya kitu kama hicho?”Alilalamika Yezi na muda huo huo mabodigadi waliingia ndani ya nyumba hio na kuizingira huku wakimpa ulinzi Yezi.

Kwasababu walikuwa aneo la juu katika Lounge waliweza kumuona Roma akitokea nje ya geti na kuingia kwenye gari ambayo imegeegeshwa na baada ya kuiwasha kwa kutoa mwanga wa taa palepale ulitokea mlipuko wa aina yake.

“BOOM!!”

“Mama..!! ulikuwa ni mtego”Aliongea Eujung kwa kikorea huku akishindwa kuzuia mshituko wake mara baada ya kuona gari lililipukaRoma akiwa ndani na kuishia kushika mdomo

“Uncle Roma…!!Yezi alijikuta akitoa ukulele akiwa kama mtu ambaye haamini macho yake.

Muda huo huo magari yaliokuwa yapo karibu na hayo maeneo yalianza kulia alarm baada ya mlipuko huo kutokea,

Haikuchukua muda mrefu mara baada ya mlipuko gari nyingine nyeusi kampuni ya Honda ilifika katika hilo eneo na walitoka wanaume waliovalia suti na kuanza kuchunguza gari hio inayowaka moto.

Edna na yeye aliekuwa ameona tukio hilo aliishia kutoa machozi huku akiwa amesimama kama sanamu.
[emoji91][emoji91][emoji91]
 
SEHEMU YA 525.

Yezi ndio aliekuwa wa kwanza kukurupuka kutoka juu na kukimbia kuelekea nje na walinzi walichelewa kumzuia lakini wakafannikiwa kumkamara akiwa tayari yupo getini na kumzingira.

Ziliongezeka gari nyingne tatu nyeusi aina ya Range na wakatoka wanaume ambao wamevalia suti huku mkononi wakiwa wameshikilia siraha na wakasogelea upande ambao wapo walinzi wa familia ya Park.

Edna na Eunjung na wao waliweza kufika katika eneo hilo na mpaka hapo waliweza kuona hatari inayotaka kutokea kwani maadui walikuwa washaingia ndani ya ukuta tayari.

Walikuwa ni kama kundi la Mafia Gang kutokana na wingi wao na namna walivyovalia na usiriasi uliokuwa kwenye macho yao.

Kiongozi wao,bwana mmoja mwembamba mwenye nywele nyeupe alievalia koti la Leather palepale aliwapa ishara ya kushambulia na ilikuwa ni kama wanaendeshwa kwani waliwasogelea walinzi na kuanza kushambulia kwa spidi , walipiga mateke virungu na wengine walikuwa wameshikilia visu.

Mpala dakika tano zinapita walibakia walinzi wanne tu ambao hawakuwa wamepata majeraha.

“Nyie ni wakina nani?”Aliuliza Eujung akimwangalia mwanaume ambaye nywele zake aliziweka dawa na kuwa za rangi nyeupe.

“Huna haja ya kufahamu sisi ni nani , nyoosheni mikono juu na mwangalie ukuta , tupo hapa kumchukua Yezi pekee”Aliongea na kumfanya Yezi kuwaangalia huku akiwa na machozi mengi yaliosababishwa na majonzi ya kuona Roma kalipukiwa na bomu.

“Huwezi kumchukua ikiwa nipo hai, wekeni umakini wenu wote kwa ulinzi wa Yezi na msiruhusu wamchukue”Aliongea Eujung kijasiri akiwapa maelekezo wale walinzi waliobaki lakini hawakufanya kama alivyoongea zaidi ya kuangaliana kwa sekunde kadhaa na kisha wakanyoosha mikono juu kujisalimisha na wakashikilia ukuta.

“Nyie wapuuzi , kwahio hivi ndio mnavyomlipa Mzee kwa mema yote aliowafanyia?”Aliongea Eujung kwa hasira huku aking’ata meno, mpaka hapo aliona hakuwa na msaada tena na watu waliokuwa mbele yake ni wengi kuweza kupambana nao wote.

Upande wa Yezi licha ya kwamba sasa walinzi wake washamgeuka na kujisalimisha yeye alisimama vilevile bila hofu akiwa kama sanamu, alikuwa kama mtu ambaye amepoteza tumaini la kuendelea kuishi.

Kitendo kile kilimfanya Edna ambaye alikuwa pembeni yake kushangazwa na kujiuliza je yote hayo ni kwasababu ya kushuhudia Roma akilipuka ndani ya gari, je Roma ni mtu muhimu kwake mpaka kuwa katika hali hio.

“Wewe mwanamke ni kichefu chefu , sheria yetu ni kutotaka kuumiza watu wengi zaidi lakini kwasababu unataka kutuzuia umeyataka mwenyewe , mshambulienni kwa risasi tuondoke hapa”aliongea na palepale wanaume wawili ambao walikuwa na bastora walisogea mbele na kuanza kuzirusha kuelekea sehemu aliposimama Eujung.

Eujung hakutaka kufa kizembe , alipiga sarakasi ya haraka kabla hawajavuta triga na aliweza kuwawahi wawili waliokaribu yake na kuwapiga mateke ya kifuani na kudondoka chini.

Kitendo kile kiliwafanya wale wengine kurudi nyuma na kujiunga kwa kumlenga kwa risasi , milio ya bunduki haikuwa mikubwa kutokana na siraha zao kufungwa viwambo vya kuzuia sauti.,

Sasa walichokuja kugundua ni kwamba hakuna risasi yoyote ambayo imeweza kumpata Eujung na yule bwana mwenye nywele nyeupe alishangazwa na jambo hilo lakini sio yeye tu ambaye alikuwa akishangaa hata Eujung hakuamini kama ni kwa uwezo wake ndio amefanikisha kuzikwepa risasi zote na isitokee hata moja kumpata, lakini hakutaka kuupa mshangao wake nafasi , watu waliokuwa mbele yake walikuwa wakijiamini kutokana na kwamba walikuwa na siraha za moto , lakini kwasababu siraha zao hakuna hata moja iliomdhuru aliona kabisa anaweza kuwamudu kuwadhibiti kwani walikuwa dhaifu kwenye mapigano ya bila siraha.

Yule kiongozi hakutaka kuamini kama msichana kijakazi ndio ambaye anawamaliza watu wake , ilikuwa ni ngumu kuamini na alianza kuingiwa na hofu na kuanza kulisogelea geti ili atoke , lakini palepale alijikuta akisimama huku akiingiwa na ubaridi wa uti wa mgongo.

“Nimerudi”Aliongea Roma na palepale alimbutua yule mwanaume kiongozi teke ambalo lilimpeleka chini , lakini licha ya kupigwa bado alikuwa akimwangalia Roma kama mzimu uliofufuka.

“Mzimu..!!!”Alipiga kelele huku akisogea kurudi nyuma.

Upande wa Yezi mara baada ya kumuona Roma alishindwa kujiuzuia na palepale alimkimbilia na kumkumbuatia na hakuishia hapo tu alimpiga mabusu ya shavuni akijisahau Edna yuko mbele yake.

Roma kitendo kile kilimfanya amwangalie Edna kwa wasiwasi , maana matendo ya Yezi ni kama vile ni ya kimapenzi.

“Wife amefanya mwenyewe, kwa kunishitukiza”Roma alijishuku.

Edna yeye alikuwa akijua Roma hajafa na wasiwasi aliokuwa akiuonyesha ni kuweka maigizo tu na hicho ndio ambacho aliambiwa na Roma afanye mara baada ya kunong’onezwa, hivyo kumuona Roma amerudi akiwa hajapata madhara alipata ahueni lakini kitendo cha Yezi kumbusu mume wake aliingiwa na hisia za kuchanganyikiwa.

“Sister Sijamaanisna vibaya , ni kwamba nimeshindwa kuzuia furaha yangu”Aliongea Yezi kwa aibu huku akijitoa kwa Roma na kusogea pembeni.

“Haina haja ya kuwa na aibu unaweza kumbusu utakavyo kwanza ananuka”

“Hey wife unanisemaje vibaya ilihali tunalala wote kitanda kimoja”

“Unanuka moshi ndio , unaonaje kwanza ukamalizana na hao watu maana mpaka sasa hatujui kama hospitalini kwenyewe kupo salama”

“Sidhani kama kuna chochote ambacho kimetokea hospitalini na siamini kama ni kweli wametega mabomu kwani kufanya hivyo sio kazi nyepesi ukilinganisha na ulinzi wa hospitali yenyewe na isitoshe wapo hapa kumchukua Yezi hivyo inamaanisha kwsamba babu yake bado yupo hai”Aliongea Roma

“Kwahio tunafanya nini baada ya hapa?”

“Kilichobaki ni mimi kutafuta bosi wao aliewaagiza kuondoa mzizi kabisa, wakati anatupigia si alisemaa niende Myeondong hoteli naamini hio ndio sehemu nzuri ya kuanzia”aliongea Roma na Edna alielelewa.

“Eujung utafanya maamuzi namna ya kuwafanyia hawa waliobaki hapa ndani, usiwaue kwani wanaweza kusaidia katika uchunguzi”Aliongea Roma na Eujung alitingisha kichwa kukubali.

“Asante sana Mr Roma kwa mara nyingine”Alishukuru Eujung alikuwa akijua kabisa kuna kitu ambacho Roma alifanya wakati akivurumishiwa risasi na Roma alitabasamu na kisha akamuaga Edna na kuondoka katika hilo eneo.

Dakika chache mbele Roma alikuja kutua katika hoteli ya Myeondong , ni hoteli ambayo haikuwa mbali kwani ilikuwa pia ndani ya wilaya ya Gangnam hivyo haikumsumbua Roma kuipata.,

Roma mara baada ya kutua nje ya bustani ya hoteli hii katika eneo la bwawa la kuogelea alianza kuchunguza jengo lote na kuamini kabisa kazi itakuwa ngumu kujua watu wote ambao ni wanachama wa North Buyeo kwasababu hoteli ilikuwa kubwa na ilikuwa na wageni wengine .

Jambo moja tu aliamini linaweza kurahisisha kazi yake ni kuingia kwenye Casino ndani ya hoteli hio.

Ndani ya hoteli hio upande wa vyumba vya chini kabisa ya ardhi ndio Casino kubwa ya kisasa ililikuwepo na ajabu ni kwamba licha ya giza kubwa nje lakini eneo hilo lilikuwa limechangamka sana na watu walikuwa bize wakicheza kamari.

Sera za kikorea zinaruhusu Kamari kuchezwa katika eneo la makasino tu na sio nje ya hapo kwani ni uvunjaji wa sheria huenda ndio maana kulikuwa na watu wengi sana.

Ulimwengu ambao pesa ni mfalme hakuna ambaye anasinsinzia katika hilo eneo na kwao ni kama ndio kwanza kumekucha , kila meza kulikuwa na watu wenye usiriasi wa uso huku macho yao yote yakiwa kwa wanawake warembo ambao ndio dealers(wachezesha kamari).

Ni eneo ambalo lilikuwa na mwanga hafifu , eneo la kisasa ambalo mziki wake ulisikika vizuri katika eneo zima na kutosababisha makelele zaidi ya kutoa burudani , wanawake waliovalia vinguo vifupi walipita huku na huko kufanya huduma, kuna waliokuwa wakitoa huduma ya vinywaji lakini kuna wale ambao walikuwa wakitoa huduma ya miili yao ilimradi kufurahisha wateja , kiasi kwamba hata kama mtu akipoteza kibunda katika kubahatisha asiwe mnyonge sana.

Upande wa kulia katikati ndio sehemu ambay kuna chuba maalumu ambacho kukaa kiongozi wa Kasino ambaye muda wote huangalia kila meza kwa kutumia Kamera zilizofungwa.

Ilikuwa ni kawaida sana kwa viongozi wa Kasino kujua kila mteja wao alieibuka mshindi na yule ambaye aliepoteza hivyo walijua kabisa kila mteja anaeingia na ambaye anatoka na yote hayo yalifanikishwa na teknolojia ya Camera za kisasa.

Sasa katika chumba hicho ambacho kilikuwa na ulinzi mkubwa na ambacho wateja wakawaida hawakupaswa kuingia , alikuwa ameketi bwana mmoja wa makamo kwenye masofa ya kisasa ya Leather akiwa ameshikilia glasi yenye kinywaji cha rangi ya dhahabu ndani yake .

Hakuwa peke yake bali kulikuwepo na wanaume wengine ambao walikuwa pembeni yake wanaofanana kimuonekano na macho yao yote walikuwa wameyaelekeza kwenye meza wakiwa wanacheza karata mchezo maarufu wa Poker.

Kila mmoja ambaye alikuwa ndani ya hiko chumba alikuwa ni mwenye kuashiria kumiliki ukwasi mkubwa , kwani kila kitu chao kilionekana cha thamani kubwa.

“Mr Go kuna simu yako hapa?”Waiter alimletea karibu bwana huyu wa makamo na kumkabidhi simu ambayo inaita.

“Nani anaingilia burudani yangu ya mchezo”Aliongea kwa Kikorea huku akionyesha amechukizwa na simu hio.

“Ni Park Jonghyun”Baada ya kijibiwa hivyo alighairisha kile ambacho anakifanya na kisha akachukua ile simu.

“Huyu mpuuzi mpaka sasa bado ananiamini”Aliongea kabla ya kupokea ile simu huku akitoa tabasamu ambalo liliashiria kutokujali na kujali kwa wakati mmoja.

“Msema sana , bwana Park mambo yanaendaje?”

“Unaniuliza mimi tena , Go Chak uliniambia kabisa mpango wako hakuna ambaye anaweza kuukwepa , vijana wako ni kipi wamefanya?”Sauti ya kufoka na kulalamika kwa wakati mmoja ilisikika upande wa pili na kumfanya bwana aliefahamika kwa jina la Go Chak kukaa vizuri kwenye Sofa.

“Unaongea nini? Vijana wangu ni kipi kimewakuta?”

“Wewe mpumbavu m unashindwaje kuelewa hali uliokuwa nayo , ngoja nikuambie watu wako wote wameweza kudhibitiwa na mpaka sasa umeshindwa kuweza kupata taarifa kutokana na kwamba hakuna aliesalia

Go Chak wewe mpuuzi , narudia watu wako wameweza kudhibitiwa na kijakazi wa familia na sasa wamepelekwa kituo cha polisi na muda sio mrefu naamini watataja makao makuu yako wapi , yaani sio tu umeshindwa kumpata Yezi lakini umeshindwa pia kumdhibiti yule nzi Roma Ramoni, unaniweka katika hatari”Aliongea Park Jonghyun alionekana mpaka muda huo amechafukwa sana.

“Inawezekana vipi?, nimetuma wanajeshi wastaafu wa kitengo cha operesheni maalumu kumaliza kazi , unataka kuniambia watu wote hao wamedhibitiwa?”

“Unauliza majibu sio maswali, nilikuambia usimpuuzie na Kim Jip haya umeshindwa hata kumuua yule mzee na sasa unaniambia hujui kinachoendelea , tokea uwe Chief wa Nothr Buyeo Kikanda huna chochote ambacho umefanya kikatimia , kwanzia sasa mimi na wewe hatukuwahi kuwa na ukaribu wowote”Aliongea na Park jonghyun alipigiza simu ukutani na ikajikata yenyewe

Go Chak na yeye mara baada ya kupewa taarifa hio alijikuta akibeba glasi iliokuwa kwenye meza na kuitupia kwenye ukuta

“Ondokeni hapa mbele yangu”Aliongea kwa kufoka na wale wanaume ambao alikuwa nao walisimama wote na kuondoka kwani walijua kabisa Go Chak akikasirika ni mtu mwingine kabisa.

“Wafanye kila mmoja kuondoka hapa ndani ya Casino , sio mahali salama tena na baada ya kila mmoja kuondoka kusanya nyaraka zote na zifiche , hakikisha huachi ushahidi wa aina yoyote”Aliongea Go Chak akimpa maelekezo Meneja.

“Lakini Mr Go hakuna muda wa kutosha kufanya hivyo”

“Unafikiri ufanisi wa polisi ni kiasi gani ?, kama nitawapa muda wa kufika hapa ni lisaa limoja kamili , hata hivyo tuna watu wetu ndani ya polisi hivyo tunaweza kuwaamini kuwachelewesha kufika hapa , ili mradi watu wetu wakubwa serikalini hakuna ushahidi unao wafunga tunaweza kuepuka lawama zote , fanya kama nilivyokuambia”

“Yes sir”

Dakika chache tu baadhi ya watu waliokuwa wakichezesha kamari palepale waligeuka na kuwa kama wanajeshi na kuanza kuwaondoa watu kutoka nje ya eneo hilo na wale ambao walikuwa wakilalamika kupewa Chip zao waliishia kupigwa mateke na ngumi na kukimbia.

Upande wa Go Chak katika ofisi yake alifungua boksi lake la usalama la kuhifadhia vitu na kisha akasukuma maburungutu yote ya hela kutoka nje na kisha akayakweka kwenye begi na hakuishia hapo tu alitoa na baadhi ya vito vya thamani na kuvikusanya pia.

Chini ya ulinzi wa vijana wake alitoka alianza safari ya kutoka Casino hio kuelekea nje na muda huo karibia watu wote walikuwa washatoka.

Walinzi waliotangulia mbele ya Go Chak kabla hawajatokea kwenye mlango walirudishwa ndani kwa kurushwa na kutua chini kama vile ni kiroba cha mchele.

Go Chak palepale aliinua kichwa chake kuangalia mbele na hapo ndipo alipojikuta akipatwa na ubaridi mara baada ya kumuona Roma.

“Roma Ramoni”Aliongea kwa mshituko.

“Hahaha…. Kuliita jina langu kumenirahisishia kukufahamu wewe ndio kiongozi”Aliongea Roma kwa Kikorea na kumfanya Go Chak kung’ata meno yake kwa hasira na palepale aliwapa ishara vijana wake walioshikilia siraha za moto kumshambulia Roma.

“BANG! BANG…!!”.

Milio ya risasi ililirindima eneo lote na kufanya lifuke moshi, hisia zao ziliwaambia kabisa mtu aliekuwa mbele yao ni hatari hivyo hakupaswa kupigwa na risasi moja ndio maana walishambulia kwa pamoja mfululizo.

Lakini sasa ile wanamaliza risasi zao na kusimamisha mashambulizi walishangaa mbele yao hakuna mtu, Go Chak kabla hata hajaelewa Roma yuko wapi alishangaa akivutwa kwa nyuma na kushikwa shingo na Roma na kuanzwa kukabwa.

“Niambie nani kaagiza mshambulie familia ya Park?”Aliuliza Roma lakini Go Chak aliishia kufurukuta huku akionyesha kabisa hayupo tayari kuongea chochote.

“Nitajie kiongozi wako?”Aliuliza Roma kwa mara ya pili.

Wale walinzi walishidnwa kufanya chochote kutokana na kwamba wenyewe walikuwa kwenye mshituko wakijiuliza imekuwaje mtu waliekuwa wakimshambulia mbele yao ghafla tu yupo nyuma yao.

Roma hakuwa na muda wa kuchelewesha na haraka haraka aliona angechelewa kumhoji Go Chak kwani hakuonyesha nia ya kuongea chochote na hakutaka kukutwa hapo na polisi hivyo alimvunja shingo palepale.

“Kamuua bosi wetu , tumshambulie”Aliongea mmoja wapo wa wale mabodigadi na kuanza kumshambulia Roma , lakini ilimchukua dakika tano tu kuwavunja wote shingo, kwasababu walikuwa wengi hakutaka kuwaacha hapo na kukutwa na polisi hivyo aliwayeyusha na kuwageuza majivu na mtu pekee ambaye hakutaka kumgusa ili kubakia kama ushahidi ni Go Chak.

Roma mara baada ya kukamilisha kazi yake alichukua mkoba alioshikilia Go Chak pamoja na wa meneja na kuangalia ndani na alijikuta akikutana na nyaraka mbalimbali kwenye mkoba wa meneja na alizotoa na kuanza kuzisoma , lakini kati ya nyaraka zote moja wapo ni nyaraka iliosainiwa na Park Jonghyun

Ni nyaraka ambao ilikuwa kama mkataba ambao umesainiwa na Park Jonghyun kwa niaba ya familia yote ambao ulikuwa ukiwapa haki ya uendeshaji wa baadhi ya mali za familia hio , ilikuwa ni rahisi kusema Park jonghyun ameuza sehemu ya mali za kampuni bila ya familia kufahamu.

Roma baada ya kupata ushahidi huo alitabasamu , hivyo alichukua begi lenye nyaraka huku akichana na lile lenye pesa, alijiambia kazi yake mpaka hapo imeisha na ushahidi aliokuwa akitafuta ameupata , hivyo moja kwa moja alipanga kwenda kumuonyesha babu yake Yezi ili kuchukua hatua zaidi juu ya Park Jonghyun.

Roma mara baada ya kusikia purukushani za watu kuingia katika hilo eneo palepale alipotea.

********

Upande mwingine katika makazi ya Park Jonghyun , bwana huyo alishindwa kabisa kukaa chini kwani alikuwa akizunguka huku na huko, kila saa akijifuta jasho , alionyesha kuwa na wasiwasi mno na ilikuwa ni kama kuna taarifa mbaya ambayo anaomba isimfikie.

Muda huo huo msaidzi wake aliingia katika hilo eneo huku akiwa ameshikilia simu.

“Boss tumeweza kupata taarifa kutoka hoteli ya Myeondong, inasemekana polisi baada ya kufika hakukuwa na ushahidi wowote zaidi ya kuonyesha kulikwa na mapigano makali ya kurushiana risasi na Go Chak amekutwa amefariki”Aliongea msaidiizi.

“Nini , amefariki?Wengine wote wako wapi , hususani meneja wake?”Aliuliza kwa kufoka.

“Huneda wakawa wamekufa Sir , kwani magari yapo parking na hawajaonekana kama walitoka”

“Sijali kama wamekufa , lakini vipi kuhusu nyaraka ya siri ya makubaliano yangu na North Buyeo , je wamezipata na zenyewe?”

‘”Mtu wetu ndani ya polisi amesema hakuna nyaraka za aina hio zimepatikana zaidi ya mkoba pekee ambao una pesa, kwa maana hio ni afadhali kwetu kwani uwezekano wa Go Chak kuzificha kabla ya kufa ni mkubwa”

“Sidhani kama inawezekana , hakuna namna Go Chak akaziweza sehemu nyingine tofauti na ndani ya Casino, vipi kuhusu kamera za ulinzi?”

“Hilo ndio tatizo bosi , Kamera za ulinzi zimeonyesha mtu alieingia ndani ya Casino ndani ya muda ni Roma Ramoni”Aliongea msaidizi na kumfanyaPark Jonghyun kupeleka mikono yake kichwani huku akitoa macho.

“Hahaha.. Roma! oh Roma Ramoni !!, ni yeye tena, si alikuwa nyumbani kwanini akawa ndani ya hio hoteli?”

“Ni ngumu kujua kwasasa bosi na tumechelewa , Bosi kama Roma ndio ambaye amezichukua nyaraka na akampelekea Mzee , itakuwa ndio..”

“Itakuwa ndio mwisho wetu , si ndio?”Aliuliza na kumfanya msaidizi wake kutingisha kichwa kwa huzuni kuonyesha kwamba mpaka hapo hawatakuwa na haki tena ya kusogelea kampuni ya Starmoon.

Tena itakuwa ni bahati kwao kama watafanikiwa kutoroka kabla ya kujikuta gerezni na sio hivyo tu hata kama wanaweza kupelekwa gerezani hakuna uhakika kama wanaweza kuendelea kuishi kwani North Buyeo wasingeweza kuwaacha hai na kutoa siri zao.







SEHEMU YA 526.

Baada ya Park Jonghyun kutafakari kidogo , alionekana kupata wazo na kisha akamgeukia msaidizi wake.

“Nenda kwenye ofisi yangu haraka sana , na fungua safebox kwa kutumia nywira za mwaka niliozaliwa na kuunganisha na mwaka wa kampuni ilipoanzishwa na kuna kiasi cha pesa ambacho kinaweza kukutosha wewe na wengine”Aliongea

“Bosi unamaanisha unataka ku..”

“Huu ndio mwisho wetu, mipango yetu yote mmoja baada ya mwingine imefeli , ninachoweza kusema yule mzee ana bahati sana kwa Roma kuweza kuwahi kuja Korea mapema …,Kwa muda mrefu umekuwa ukinifuaa na kutii maagizo yangu , nitakupa kile ambacho unastahili , lakini kwa namna ambavyo utaishi wewe na wengine hilo litakuwa juu yenu”

“Boss kwanini tusiende hadi hospitalini n kuomba msamaha , wewe ni mjukuu wake sidhani kama anaweza kukutupa kabisa bila ya msamaha”

“Unafikiri anaweza kunifanya nini mimi ambaye sina uhusiano wowote wa damu na familia yake? , kwenye macho yake Yezi peke yake ndio ambaye anaweza kuendeleza legacy ya familia , kama nitaenda sasa hivi itakuwa kama misheni ya kujitoa muhanga”

“Kama ni hivyo bosi kwanini usiungane na sisi , namfahamu mtu mmoja ambaye anaingiza vitu nchini kimagendo, anaweza kutusaidia kutorokea nje ya nchi, tunaweza kutafuta kisiwa chochote na kujificha huko , huenda siku moja tukarudi kwenye utukufu wetu”

“Unajidanganya , hivi unajua kwanini yule mzee amewezaje kutawala bara la Asia lote , haha,, biashara za magendo huko kote kuna mizizi yake na nitakamatika kirahisi , kwasasa jiokoe wewe mwenyewe na mimi nitajisaidia mwenyewe, hivyo nenda kabla mambo hayajanikuta kuna kitu kimoja lazima nikifanye”Aliongea na palepale alichukua funguo za gari.

Upande wa msadizi wake , alianza kusita sita lakini palepale alijipa ujasiri na kisha akakimbilai kwenye ngazi ili kuelekea juu kwenye ofisi ya Park jonghyun , lakini kabla hata hajapiga hatua nne kupanda , mlio wa risasi ulisikika palepale na yule msadizi alidondoka chini huku damu zikisambaa na alianza kufurukuta huku macho yake yakionyesha kama vile ni mtu ambaye anakufa kifo ambacho hakutarajia.

Park Jonghyun alieshikilia risasi alimwangalia namna msaidizi wake anavokufa na kisha alitoa tabasamu la kejeli.

“Sikutarajia utakuwa mtiifu namna hii , kama nazama na nyie mnapaswa kuzama “Aliongea huku akionyesha kutojutia kwa kile ambacho amefanya.

*******

Roma kwa haraka haraka alikadiria mpaka muda huo Park Juan atakuwa ameamka na ndio maana hakutaka kwanza kurudi kwa mke wake mpaka kuonana nae.

Roma alitaka kukamilisha kila kitu mapema kabla ya kurudi Tanzania na isitoshe siku zilikuwa zinaenda kwa kasi na nyumbani walimuacha Lanlan ambaye hakupaswa kuendelea kukaa bila ya kuwa na ukaribu wa mama yake na hata kwa Edna mwenyewe alishaona kabisa ashamkumbuka mtoto wake na alikubali kuendelea kubakia hapo nchini kwasababbu ya swala la Yezi tu na kama si vinginevyo heunda angekuwa Tanzania tayari.

Roma akiwa na mkoba wake aliweza kuruhusiwa kuingia katika wodi aliolazwa Park Juan na ilikuwa ni kama alivyotarajia kwani Park Juan aikuwa ashatoka kwenye usingizi wa Ganzi na muda huo hata dripu zishaondolewa na aliwekewa tu nasal prongs ambazo zilimsaidia kupata hawa safi.

Kim Jip kwa namna ambavyo alionekana ni kama vile dakika moja hakuwa akipigana kwa kudhibiti watu ambao walitaka kumdhuru bosi wake.

Mara baada ya Roma kufika hakuongea neno zaidi ya kumtingishia kichwa tu kumuonyesha ishara ya kumkaribisha.

Roma mara baada ya kusalimiana na Park Juan ambaye alionekana kuwa dhaifu mno hata kwenye kuongea, aliamua kutoa kidonge cha kijini kwenye kijimkebe alichokuwa nacho na kisha akamuwekea Park Juan Mdomoni na kisha akakimeza.

Roma aliona kisingeweza kumponyesha kwa haraka hivyo palepale alishika mkono wake na kuanza kumuingizia nguvu ya urejesho na Park Juan alijikuta akitoa macho kwani ni kama alihisi mwili wake ulikuwa ikiingiwa na chaji kwa haraka sana na hata mishono yote ilijifunga na maumivu yalianza kupotea.

Athari chanya za kidonge jumlisha nguvu ya urejesho vilimfanya Park Juan kurejewa na nguvu kabisa kama mtu ambaye amepona kabisa na alishangazwa sana na jambo hilo na haikuwa kwake tu hata kwa Kim Jip alionyesha kushngaaa licha ya kwamba hakuonyesha sana kwenye macho yake kama alikuwa kwenye mshangao.

“Mr Roma wewe ni nani haswa?”Aliuliza Park Juan mara baada ya kutoa mpira wa kupumulia lakini Roma aliishia kutabasamu huku akionyesha hayupo tayari kujielezea zaidi na kuweka siri zake zote hadharani.

“CEO Park kama nilivyokueleza hizi ni mbinu nilizorithishwa , kama unataka kuishi zaidi ya miaka mia ni juu yako kama upo tayari kulipia kwa hilo maana sio bure”

“Nipo tayari , una vidonge vingi zaidi kama hiki ulichonipatia?, kama vipo vingi nitanunua vyote”Aliongea huku akionyesha kuwa na tamaa.

Roma alishangazwa na kauli yake , ijapokuwa ilikuwa kweli kidonge alichompatia kilikuwa cha daraja la chini lakini asingemuuzia vyote .

“Hivi vidonge ni hadhina ya familia yangu , ninavyo vitatu pekee ambavyo vimebakia, unaweza kuwa tajiri dunia nzima lakini huwezi pata kirahisi hivi vidonge , nimeamua kukusaidia kwasababu wewe ni babu yake Yezi”

“Mr Roma nina uhitaji sana na hivyo vidonge angalau vinipe miaka miachache ya kuishi , mjukuu wangu Yezi kuna mambo mengi ambayo hayajui kuhusu kuongoza kampuni na isitoshe maadui hawawezi kumuacha salama. Unaonaje kuhusu hili, taja bei yoyote ambavyo ungependa kuuza na mimi nitanunua”Aliongea na kumfanya Roma kufikiria.

“Unaonaje kuhusu hili CEO Park , nitakuuzia kidonge kimoja kwa dolla milioni kumi(bilioni ishirini na tatu za kitanzania)?”.

“Kidonge jimoja tu?, kama vipi nipatie vyote kabisa , najua ni kitu cha thamani kubwa , unaonaje kama nitakuongezea milioni ishirini zaidi unipatie vyote?”Aliongea na kumfanya Roma kushikwa na tamaa ya pesa ya haraka namna hio , alijiambia kwa staili hii bora amwambie Sauroni aachane na biashara zake za kutengeneza na kuuza siraha na waanze kutengeneza vidonge na kusambaza dunia nzima.

Lakini mawazo hayo aliona hayawezi kukamilika kutokana na kwamba vidonge hivyo haviwezi kutengenezwa vingi kukidhi mahitaji.

Roma hakutaka kukataa ofa hio ya hela hivyo alitoa vile vilivyobakia na kisha akampatia Park Juan na bwana huyo alifurahi mno kuona Roma amekubali . siku zote ndoto ya tajiri ni kuishi muda mrefu ili kufurahia pesa zake lakini kwasababu hakuna binadamu ambaye anao uwezo wa kurefusha maisha ni jambo ambalo hubakia kama ndoto.

Hivyo kwa mtu kama Park Juan asingeshindwa kutoa kiasi hicho cha pesa ambacho hakifikii hata asilimia moja ya utajiri wake kwa ajili ya kidonge cha kurefusha maisha.

Alimpa ishara kim Jip kumpa cheque(cheki) na akasaini kwa kuandika kiasi cha pesa tajwa alichopaswa kulipa na kisha akampatia Roma , hivyo mpaka muda huo Roma akawa na milioni therathini za kimarekani sawa na zaidi ya bilioni sitini za kitanzania.

Roma mara baada ya kuona sasa mzee huyo hali yake ya afya imekuwa sawa alichukua mkoba aliokuja nao na kisha akatoa nyaraka ambazo Park Juan alipaswa kuziona.

“Hizi nyraka ni halisi na nimezithibitisha lakini naamini unapaswa kuziangalia wewe mwenyewe , siwezi kuongea chochote kwani mimi sio mwanafamilia”Aliongea Roma na akamkabidhi na baada ya Park Juan kupitisha macho sura yake ilikunjamana.

“Nilijua tu huyu mkorofi kuna mambo anafanya , lakini sikuwahi kuwaza kama anaweza kushirikiana na North Buyeo?”

“Unajua kuhusu hawa North Buyeo?”Aliuliza Roma.

“Kwanini nisiwajue , ukweli ni kwamba nimekuwa kwenye mashindano makali na wanachama wote ambao wapo chini ya huu umoja wa siri kwa zaidi ya miaka miwili sasa , lakini licha ya hivyo kutokana na ushawishi wangu hawakuweza kunifanya chochote , lakini bahari mbaya kutokana na afya yangu kudhorota sikuwa na mtu mwingine wa kumuamini zaidi ya park Jonghyun.”

“Unaweza usiwe na ufahamu wa hili Mr Roma , lakini North Buyeo malengo yao makuu ni kuunganisha Korea kusini na Korea kaskazini kuwa nchi moja, huu mwaka kwa hapa Korea ni wa uchaguzi na upande ambao nasapoti ni ambao una ukinzani mkubwa na serikali ya Korea kaskazini ,siku hizi teknolojoia imekuwa kubwa sana, hivyo ukifanya kosa kidogo tu linaweza kupelekea mamia ya watu kuwa hatarini, hawa North Bueyo hapa nchini wanachotaka ni kuchafua nchi na kuiingiza kwenye vita ya pili”Aliongea na kufanya Roma kushangaa na kuona kumbe mambo yote hayo yana muunganiko wa kisiasa ndani yake.

“Kwangu usalama wa Yezi ndio kitu ninachojali , hivyo nakuomba kwa haraka kushughulikia hili na kulimaliza mara moja ukishakuwa tayari”Aliongea na kumfanya Park Juan kutingisha kichwa na kisha palepale alimpa ishara Kim Jip kumpatia nguo zake abadili .

“Kim Jip weka gari tayari , waambie na wengine kwenda nyumbani kwa huyo mwanaharamu na wamlete kwangu”Aliongea

“Aye”

*********

Upande mwingine katika makazi anayo ishi Najma , gari nyeusi aina ya Bernz ilisimama kando ya jengo hilo na kwa haraka haraka aliekuwa akiendesha alitoka nje ya gari na kisha akatoa simu yake na kutafuta namba na kuipiga.

“Vivian , ninajisikia vibaya muda huu , kama hutojali naomba nije tuongee kwa dakika kadhaa”

“Muda umeenda ,najiandaa kulala”Aliongea Najma upande wa pili na kumfanya Park Jonghyun kukunja sura.

“Nipo tayari nje ya Apartment yako , nahitaji kweli kuongea na wewe leo leo , ninaondoka kwenda Ulaya wiki ijayo , hivyo hii inaweza kuwa mara ya mwisho tunaonana”Aliongea kwa kubembeleza na kumfanya Najma aliekuwa ndani akijisomea kufikiria kidogo na kutokana na sauti ya Park Jonghyun ilivyokuwa kinyonge alimuonea huruma hivyo akampa ruhusa ya kupandisha juu.

Dakika chache mbele Park Jonghyn aliweza kufika nje na kugonga mlango na Najma ambaye alivalia gauni la pinki la maua maua na visendo manyoya alifungua mlango na kumkaribisha ndani.

Park Jonghyun mara baada ya kuingia alimchunguza mrembo huyo wa kiafrika kwa macho ya uchu , ijapokuwa yeye alikuwa Mkorea na wanawake wa Kkorea hawakujaaliwa shepu lakini kwa Najma alipenda sana shepu yake.

“Mr Park je kuna kitu kinachokusumbbua , unaonekana kutokuwa vizuri?”aliongea Najma mara baada ya kumkaribisha mwanaume huyo kwenye sofa na kisha kwenda upande wa jiko kuandaa kikombe cha kawahawa ili kumchangamsha.

Upande wa Park Jonghyun alikuwa amekula bata sana na wanawake wa aina tofauti alipokuwa nje ya nchi na ndani ya nchi , lakini kwake ilikuwa mara ya kwanza kukutana na mwanamke ambaye alikuwa mpole na asie na mambo mengi kama Najma , hisia zake zilikuwa zikimwambia kabisa Najma alikuwa bikra na hio ilimuongezea shauku ya kutaka kuona kama mawazo yake yapo sahihi.

“Vivian vipi kama nisingeanza kukufukuzia , je ungeweza kunipenda wewe mwenyewe licha ya sisi kuwa wa rangi tofauti?””Aliuliza Park Jonghyun na kumfanya Najma kushitushwa na swali lake lakini aliishia kutingisha kichwa kukataa.

“Kwaini iwe hivyo… au ni kwasbabu sitamaniki ? hivi nachukiza sana?”Aliuliza huku akionyesha huzuni ya kukataliwa na mrembo kama Najma.

“Ukweli ni kwamba sio kama nakuchukia au huvutii, kama ni mwanamke yoyote wa rangi yetu angefurahi kupendwa na mwanaume kama wewe , lakini kwangu mimi ni vugumu kufanya hivyo kutokana na kwamba moyo wangu ushampenda mtu mwingine na ndio huyo ambaye ananifanya nishindwe kabisa kumpenda mtu mwingine , nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kupotezea mapenzi yangu kwake lakini nimeshindwa , huenda mtu yoyote anaweza kuniona kama mtu dhaifu lakini ndio hivyo nimeshindwa kumsahau kabisa”Park Jonghyun alijikuta akikunja ngumi na kung’ata meno kwa wakati mmoja.

“Je mtu huyo ni Roma Ramoni?”Aliuliza na Najma alitigisha kichwa kukubalia.

“Nafasi yake katika moyo wangu haiwezi kuzibwa na mtu yoyote”Aliongea na kumfanya Park Jonghyun kusimama na kuanza kucheka kicheko cha uchungu, ni kama lile jibu ambalo hakuwa ametegemea hatimae limewekwa hadharani.

“Roma Ramoni,,, muda wote ni Roma Ramoni , kila kitu ni Roma , nimemkosea nini mimi huyu Roma Ramoni ,mpaka kuharibu maisha yangu”Alianza kuongea kama kichaa na mpaka hapo Najma alijua kabisa amefanya kosa kumtaja.

“Mr Park kwanini .. upo..”

“Kaa Kimya”Aliongea kwa kufoka na palepale alitoka aliposimama na kumsogelea Najma na kisha akambana kwenye kabati la jiko.
[emoji91][emoji91]
 
SEHEMU YA 527.

Najma mpaka hapo alijua alifanya kosa kubwa sana kumruhusu Park Jonghyun kuingia ndani kwake na sio hivyo tu pia kumtaja Roma kama mwanaume anaempenda , lakini alifanya hivyo kwasababu ya kwamba hakuwa akija kama Park Jopnhyun na Roma wana ugomvi.

Kutokana na namna ambavyo ameshikiliwa alishindwa kabisa kujitoa katika mikono ya Park Jonghyun na alishia kuangalia pembeni akikwepa pumzi yake ya moto.

“Biashara zangu zimeharibika , hivyo hivyo maisha yangu yameharibika na kila kitu changu kimechukuliwa kwasababu ya yule mwanaharamu , hebu angalia nilivyo sasa , nimeachwa sina kitu na mwanamke ambaye kwa mara ya kwanza nimetokea kumpenda na yeye amechukuliwa kutoka kwangu na Roma Ramoni , kila saa ni Roma Ramoni kwanini , hebu niambie ana kitu gani cha ziada mnachokipenda?”Aliongea kwa hasira.

Machozi pekee ndio ambayo yalikuwa yakimtoka Najma hakuweza kuongea kuwakilisha kile ambacho anajisikia moyoni.

“Kwanni huongei?, Oh.. itakuwa naogopesha , itakuwa nakutisha si ndio ,, hahaha , sikupanga kuwa hivi , kama ungesema hata uongo huenda ningekuachia , lakini hata wewe mtu wa mwisho ambaye niliweka matumaini yangu unakuwa mkatili kwangu?”Aliongea na hasira zake zilianza kugeuka machozi , alionekana kabis ahakuwa hana tumaini tena.

“Mr Park tafadhari naomba usifanye hivi ,, nini kimetokea? Roma kakufanya nini?”

“Uthithubutu kutaja jina lake mbele yangu”Aliongea huku akionyesha kabisa muda huo ni kama akili haikuwa yake kabisa.

“Kwasababu Roma ameharibu kila kitu changu , nitakurudishia kila kitu , na wewe nakuharibia kama kulipiza”

“Mr Park .. unataka kufanya nini?”Najma ambaye sura yake ni ya kipole ilijawa na majonzi aliuliza kwa kujipa ujasiri , huku hofu ikiwa juu.

“Unafikiri mimi mjinga , inaonyesha kabisa Roma anakujali hivyo nitafanya mapenzi na wewe na kitakachotokea hapa kitamuumiza sana maisha yake yote”

Najma baada ya kusikia hivyo alizidi kuogopa , alizidi kukusanya nguvu zake zote ili kuweza kujitoa katika mikono ya Park Jonghyun lakini alikuwa ameshikiliwa vizuri sana kiasi kwamba hakuwa na namna ya kujiokoa.

Jasho lilianza kumtoka palepale , alishindwa hata kupiga kelele , Park Jonghyun aliongea kwa vitendo pia kwanni palepale alimchania gauni Najma na kumuacha na nguo za ndani pamoja na Bra tu.

Shepu yake ilionona ilikuwa wazi katika macho ya Park Jonghyun , jambo ambalo liliamsha mashetani yake zaidi ya kimatamanio .

“Naomba usinifanyie hivi… hapapna,, arhg tafadhari naomba uache ugh…”Hata kama alitoa kilio ilikuwa ngumu kusikika kwani nyumba hizo zimejengwa kwa mtindo wa soundproff.

Kilio chake kilimfanya Park Jongyun kuwa kama chizi na kuachia kicheko ambacho kilisambaa chumba kizima na kufanya hata sauti yake ya kilio isisikike.

****

Roma aliondoka hospitalini hapo akiwa ndani ya gari ya Park Juan akijiweka kuwa huru kwenye gari hilo mpaka kuanza kupiga miayo ya usingizi.

Upande wa Park Juan alikuwa na nguvu mpya , alikuwa ni kama amezaliwa upya hivyo hata usingizi hakuwa nao zaidi ya furaha ya kwamba anakwenda kuishi maisha marefu tofauti na alivyowaza siku kadhaa zilizopita, alijichukulia kama mzee mwenye bahati sana katika maisha yake.

Upande wa Kim Jip alionekana kuongea na simu kwa dakika kadhaa na kisha akageuka nyuma na kumwangalia bosi wake kumpatia taarifa.

“Sir Tumepotkea taarifa Park Jonghyun amemuua msaidizi wake na mlinzi wake na sasa yupo mafichoni , lakini kwa taarifa zinazoonyesha hajatoka nje ya Gangnam”Aliongea Kim Jip.

“Lazima atakuwa amejua hawezi kutoka bila ya kukamatika , endeleeni kumuwinda mpaka mumpate , nahitaji kujua kila kitu alichofanya bila ya mimi kujua”Aliongea Park Juan na Kim Jip alitingisha kichwa kukubali.

Upande wa Roma mara baada masikio yake kusikia maneno ya Kim Jip alikunja ndita , lakini kwa wakati mmoja kushangazwa na kitendo cha Park Jonghyun kumuua msaidizi wake mwenyewe pamoja na mlinzi wake.

Alijiuliza kama kweli alikuwa ana mpango wa kutoroka kwanini kaamua kumaliza watu wake wa karibu , ilihali huenda wangemsaidia kutoroka , au inamaanisha kwamba hakuwa na mpango wa kutoroka, Roma alijiuliza hayo maswali na palepale alamu ilipiga kwenya ubongo wake.

“Simamisha gari?”Aliongea Roma kwa kushituka na kumfanya dereva kushangazwa na kauli yake ya kibabe lakini alisogeza gari pembeni na kulisimamisha

“Mr Roma kuna tatizo?”Aliuliza Park Juan lakini Roma hakuwa na muda wa kujibu zaidi ya kufungua mlango haraka haraka na kutoka na alienda hadi nyuma ya bustani ambapo watu wa barabarani hawamuoni na kisha akapotea.

Roma alishajua kabisa kutokana na kitendo ambacho amefanya Park Jonghyun basi lazima agefanya zaidi ya hilo hivyo moja kwa moja alioa mtu ambae anaweza kuwa katika hatari ni Najma.

Ilikuwa bahati kwamba alikuwa akijua eneo ambalo anaishi Najma mpaka chumba chake baada ya kumsindikiza Edna kukutana nae na hilo ndio ambalo lilimsaidia kutopata tabu.

Roma mara tu ya kuibukia nje ya jengo la analoishi Najma alitumia uwezo wake wa kijini kuanza kuangalia mazingira ya jengo huku roho yake ikinuia kumtafuta Najma ili kuona kama yupo sawa.

Na palepale alipotea na ile anakuja kuibukia alikuwa juu kabisa ya balkoni ya apartment anayoishia Najma .

Park jonghyun alikuwa ashafanikisha kumlaza chini kwenye sakafu Najma na sasa alikuwa akimpiga mabusu kuanzia kwenye shingo kushuka chini huku akiwa ameshikilia mikono vizuri pamoja na kumbana kiwiliwili cha chini na miguu yake.

Baada ya kulizika na hatua ya kwanza alihamia chini na kisha akavuta Tight nyeupe aliokuwa amevaa na kuichana kabisa na kumfanya sasa kuwa mtupu .

“Hahaha..Vivian you are mine now”Aliongea kwa kingereza huku akizidi kupandishwa na mumkari mara baada ya kuona tunda ambalo halikuwa na dalili ya kumegwa kabisa.

Upande wa Roma aliweza kusikia maneno ya Park Jonghyun na yaliyamfanya kuwa katika hasira ya kiwango cha juu mno na Park Jonghyun aliweza kumuona kutokana na Roma kuingia kwa kufosi mlango.

“Hatimae umekuja wakati ambao sikukutegemea , nilikuwa nikijiandaa kuonja utamu hapa , lakini naona umekuja kuniharibia tena”Aliongea Park Jonghyun mara baada ya kumuona Roma.

Roma hakuwa na haja ya kuwa mpole tena kwa Park Jonghyun , alimsogelea kwa kasi na kisha akamwinua juu juu na kumshikilia shingo yake.

“Kumbuka haya macho , kama ikitokea ukawa mzimu na kurudi kwangu nitakuua tena zaidi ya mara elfu moja”Aliongea Roma na palepale akiwa ameng’ata meno yake kwa hasira alikaza kiganya chake cha mikono na kufanya mshipa mkubwa wa damu kupasuka palepale lakini hakuachia mpaka alipohakikisha Park Jonghyun alipopoteza maisha na alimtupia chini huku damu nyingi zikimtoka kama bomba la maji.

Roma bado ni kama hakuwa ameridhika na kifo chake , hivyo aliweka na mguu kwenye kifua chake na kisha akakanyaga kwa nguvu na kufanya mguu wake kutengeneza unyao kwenye kifua na kiasi flani hali yake ya utulivu ilirudi kawaida na kisha akamsogelea Najma ambaye amelala chini akiwa hana nguo.

Ijapokuwa Park Jonghyun hakufanikiwa kumbaka kutokana na yeye kufika ndani ya muda , lakini bado alikuwa na wasiwasi na hali yake.

Najma tokea aonane na Roma nchini hapo ni kama maisha yake yalibabadilika na hata ile furaha na hali ya kujiamini ilimpotea kabisa na kubakia kama Najma ambaye alikuwa wa miaka kadhaa iliopita.

“Najma…!!”Roma alijaribu kumuita mara baada ya kumkalisha na kumuegamiza kwenye mikono yake , lakini licha ya kwamba Najma alionekana kuwa na fahamu lakini hakuna kitu ambacho alijibu.

“Kila kitu kipo sawa Najma , nimekuja..”Aliogea Roma na kisha akavua jaketi lake na kumvalisha na baada ya kuona amejisitiri alimsimamisha lakini Najma alionekana kama kukosa nguvu na alianza kuzungusha kichwa taratibu huku akiwa na mwonekano usioelezeka.

Alimwangalia Roma kwa muda na palepale alianza kuongea maneno yasioeleweka kwa sekunde na ghafla tu palepale alipoteza fahamu kwenye mikono ya Roma.

“Najma”

Roma alijua huenda baada ya kumuokoa angesimama na kisha kumkumbatia na kuanza kulia , lakini ajabu ilikuwa tofauti na mategemeo yake , hakutegemea kama angepoteza fahamu muda huo huo.

Roma palepale alijikuta akipeleka mkono wake na kushika kiganya chake cha mikono na kumuingizia nguvu ya urejesho isio na kikomo ili kujaribu kuangalia kama kuna tatizo lolote ndani ya mwili wake , lakini alikuja kugundua Najma hakupata majeraha yoyote ya ndani.

“Inawezekanaje akapoteza fahamu..?”Aliwaza Roma na palepale aliona hilo ni swala ambalo hawezi kurekebisha kwa kutumia uwezo wake , Roma palepale alimlaza kwenye sofa na kutafuta gauni kwenye kabati na kisha akamvalisha na kumbeba na akapotea nae na alikuja kutokezea hospitalini na kupokelewa na manesi.

“Sir ana tatizo gani?”Aliuliza nesi wa kikorea huku akijua hajaeleweka kutokana na lugha.

“Alipatwa na mshituko na kupoteza fahamu , nimejaribu kumuamsha lakini meshindikana”Aliongea Roma kwa lugha ya kikorea na alipokelewa haraka na madaktari wa kitengo cha dharula na baada ya kufanyiwa vipimo vya awali walishauri afanyiwe CT scan.

Roma baada ya kuona Najma kashaingizwa kufanyiwa vipimo alitoa simu yake na kukuta kulikuwa na missed call kama tatu kutoka kwa Edna, na moja kwa moja alidhania kabisa mke wake atakuwa kwenye wasiwasi na palepale simu ilianza kuita upya na alipokea.

“Honey uko wapi , kwanini babu yake Yezi ndio amerudi wewe huonekani?”

“Najma amepoteza fahamu na nipo hospitalini saivi , usiwe na wasiwasi hakuna kibaya kinachoweza kunikuta”

“Usiniambie Najma ameba..”

“Hapana ,ilikuwa afadhali nilifika ndani ya muda”Aliongea Roma huku akitoa tabasamu la uchungu , aliona kama angechelewa hata dakika moja tu basi huenda Najma angenajisiwa na angejilaumu maisha yake yote maana yeye mwenyewe ndio ambaye alikuwa na makosa kwa kumuacha Park jonghyun akiendelea kuishi licha ya kufahamu uovu wake.

“Kama ni hivyo nitamwambia babu yake Yezi ili kusafisha hali , nitajiandaa kukufauta sasa hivi”Aliongea Edna na Roma alitaka kumzuia lakini aliona asifanye hivyo kwani Edna angefikiria mambo mengine .

Haikupita hata nusu saa Edna aliweza kufika hospitalini akiwa amevalia sweta kubwa la manyoya na kujifunga na scarf kwenye shingo kuzuia baridi, alikuwa ameshikilia kijimfuko.

“Njmenunua kahawa njiani, kunywa kidogo kupasha mwili joto”aliongea

Wakorea ni watu wa kahawa na mara nyingi huwa zinauzwa mpaka madukani tena zikiwa za moto kabisa.

Roma alijikuta akifurahishwa na harufu nzuri ya kahawa na baada ya kunywa kidogo iliweza kurudisha mudi yake.

“Ilikuwa siku ngumu kwako leo , rudi mapema ukapumzike”

“Mpaka nione hali ya Najma ikoje, nitakuwa popote ulipo”Aliongea Edna.

“Bado una wasiwasi nikiwa karibu na wanawake wengine?”Aliongea Roma huku akicheka kivivu.

“Nina wasiwasi na hali ya Najma , ni rafiki yangu licha ya yote yaliotokea , hivyo nitakaa hapa mpaka nione kinachoendelea”Aliongea na muda huo huo daktari aliwasogelea akiwa ameshikilia faili kwenye mikono yake.

“Wewe ndio Mr Roma , naitwa Zeng Guozhong mChief daktari wa hospitali , raisi Park alinipigia simu, nisameheni kwa kuchelewa kufika, ndio nimetoka nyumbani , tutafanya kila linawezekana kuhakikisha hali ya mgonjywa inatengemaa , kwasasa naomba mnifuate kwenda kwenye ofisi yangu”Aliongea na kumfanya Roma asitarajie kama Park Juan angechukua hatua ya kumpigia Chief daktari mkuu.

Kwa muda huo alijua kabisa angepaswa kushughulikia maswala ya Park Jonghyun pamoja na North Buyeo hivyo alijuwa yupo bize , lakini lichia ya hivyo aliweza kumuita daktari ambaye ashatoka hospitalini kurudi.

Ndio maana alikuwa mfanyabiashara mkubwa ndani ya bara la Asia kutokana na ushapu wake na uwezo wa kufanya maamuzi kwa haraka

“Dokta Zheng hali ya mgonjwa wetu ipo je , yupo kwenye hatari?”Aliuliza Roma mara baada ya kukaribishwa ndani ya ofisi.

“Hayupo kwenye hatari , lakini hali yake sio rahisi”Aliongea huku akilazimisha tabasamu.

“Nini tatizo?”

“Mr Roma je mgonjwa alifanyiwa kitendo cha ukatili , nesi amesema alikutwa na baadhi ya alama kwenye mwili wake”Aliuliza na Roma alitingisha kichwa.

“Kuna mtu alikuwa na nia yakumfanyia hivyo lakini niliweza kuzuia kabla haijatokea”

“Haishangazi , je aliweza kugonga kichwa chake kwa namna yoyote wakati wa tukio hilo?”Aliuliza na kumfanya Roma kushangaa lakini aliishia kukumbuka tukio zima namna ambavyo alilikuta.

“Nilimkuta akiwa amekandamizwa kwenye sakafu lakini sijui namna ambavyo aliweza kulazwa chini , inawekzekana akawa amejigonga ndio , hata mwonekano wake alioniangalia nao ni kama vile hanijui”Aliongea Roma kwa kikorea na Edna aliekuwa pembeni aliomba kutafsiriwa na alijikuta akishikwa na huzuni mara abaada ya kusikia kinachoendelea ,

“Mr Roma kwa heshima zote naomba niseme hali ya tatizo la mgonjwa linaweza kuwa nje ya matibabu ya kawaida ambayo sisi madaktari tunaweza kufanya?”

“Unamaanisha nini?”

“Miss Najma amegonga kichwa chake vibaya na kupata majeraha kwenye Cerebral Cortex , ingazwa jeraha sio kubwa sana lakini baadhi ya neva zake zimeharibika l wakati huo huo ufahamu wake umepitia mshituko mkubwa , hivyo utambuzi wake wa fahamu , na kujieleweza vyote havipo sawa,, kwasasa tumempa dawa ya usingizi mara baada ya kuamka.

Kabla ya kuchomwa sindano ya usingizi alikuwa akitetemeka sana huku akitaja neno ‘hapana’kwa nguvu na tulishindwa kuwasiliana nae , hivyo kwa uzoefu wangu naweza kusema amepatwa na ugonjwa wa akili kama PTSD (Post-traumatic stress disorder) au Phobia(Woga maalumu).

Roma alijikuta hata akisahau kumtafsiria Edna kutokana na taarifa hio mbaya na Edna aliona wasiwasi wa Roma na kumwambia amtafisirie na Roma alifanya hivyo kinyonge na kumfanya Edna Chozi kumtoka, hakuamini kama Najma anaweza kuchanganyikiwa kwa tukio la kutaka kubakwa.

“Kwanini iwe hivi?”

“Kwa kawaida ukatili peke yake hauwezi kumfanya mgonjwa kuwa katika hali kama hio , nina makisio Miss Najma alikuwa na msongo mkubwa wa mawazo , hali ambayo ni kama imempelekea kujikatia tamaa na inawezeana alikuwa kwenye uvumilivu wa hali ya juu sana, hivyo mara baada ya kuwa katika hali ya kubakwa alijikatia tamaa na kuruhusu utu wake wa ndani kumpotea na kujizima kabisa”Aliongea daktar Zheng na baada ya kuona Roma bado alikuwa katika hali ya mawazo aliendelea kuuliza swali.

“Mr Roma je mgonjwa alikuwa na matatizo hayo bainishi?”















SEHEMU YA 528.

Roma alijikuta kwanza akinywa kidogo kahawa ambayo ishaanza kupoa iliokuwa kwenye mkono yake , mwanzo ilikuwa tamu lakini wakati huo aliiona ni chungu.

Roma alijua kabisa kuhusu kumkataa Najma kusingemsababishia matatizo makubwa mpaka kujikatia tamaa ya kuishi.

“Dokta je tunamsaidieje sasa , atakuwa hivyo maisha yake yote?”

“Hatuwezi kusema kwa uhakika , labda mgonjwa anaweza kupona yeye mwenyewe lakini kuna uwezekano hali yake kuzidi kuwa mbaya”

Edna mara baada ya kusikia tafsiri alijikuta akikumbuka mazungumzo yake na Najma katika Apartment yake, maneno ya Najma baada ya kujirudi katika kichwa chake , alihihisi ni mwenye hatia na kujiona ni yeye pekee ambaye alikuwa kwenye nafasi ya kumsaidia lakini hakufanya hivyo na kumuacha afanye atakavyo.

Edna hata yeye mwenyewe alianza kujishangaa , kwanini moyo wake ulikuwa ukiuma , kwanini anajisikia huzuni kiasi cha kukosa raha kabisa.

Roma alimuona namna Edna alivyobadilika na aliamua kumshikilia mkono ili kumtuliza na alivyoinua macho yake aliona tayari Dokta Zheng alikwisha kuondoka bila kuelewa ameondoka hapo muda gani.

“Usifikirie sana , hili halijatokea kwasababu yako , sio wewe uliemuagiza Park Jonghyun , sio jambo zuri kujibebesha lawama kwa kitu ambacho hujafanya”

“Najihisi kuwa mwanamke mkatili…”Aliongea Edna huku machozi yakianza kumtoka , kilichomuuma Edna zaidi ni kuona kwamba yeye ni kama alinunua hisia za Najma , kule Tanzania yeye ndio ambaye alimshauri Najma kuondoka kwenye maisha ya Roma na kwenda kuishi Marekani kwa sababu ya kimasomo akiamini kwamba Najma angeweza kumsahau Roma kwa haraka,lakini mambo yaligeuka ndivyo sivyo Najma alionekana kupenda kweli na mapenzi yake kushindwa kumpotea mara moja, hivyo kuwa nchini Marekani ni kama hisia zake zilinunuliwa kwa pesa taslimu na ndio kilichompelekea kujitoa katika ufadhili na kuja kukimbilia mpaka Korea ambako ndio anakuja kupatwa na tatizo ambalo linampelekea uchizi.

“Kama wewe utakuwa mwanamke mkatili basi mimi nitakuwa mwanaume mkatili zaidi kuwahi kuishi katika uso wa dunia, hujafanya kosa lolote , kuna baadhi ya vitu sisi kama binadamu vipo nje ya uwezo wetu , niamini mimi Najma hajawahi kukuchukia”

“Kweli?”

“Ndio”Aliongea Roma na kumfuta machozi kwa kutumia kiganja cha mkono wake

“Twende tukamuangalie Najma anaendeleaje”Aliongea na kumfanya kusita sita lakini alitingisha kichwa kiukubali na akasimama.

Ilikuwa ni usiku bado , hivyo hospitali ilikuwa na ukimya wa hali ya juu sana, walitembea kwenye korido na hatimae kuweza kufika katika wodi ambayo amelazwa Najma , huku akiwa mkononi ametundikiwa dripu.

“Najma ataamka lini?”Aliuliza Edna.

“Sijui , ameishi mwenyewe kwa muda mrefu , hana rafiki wala familia , kama tungekuwa Tanzania angalau kaka yake angekuwa karibu yake na kumsaidia”

“Kama ni hivyo basi tusiondoke , tukae hapa hapa mpaka atakapo amka”Aliongea Edna na Roma alikuwa na mawazo sawa , alikuwa akiwaza kama hali yake ikiendelea hivyo huenda wamtoe hapo na kumpeleka nchi nyingine au kurudi nae Tanzania kabisa kama asingeweza kupona.

Masaa nayo yalipita kwa haraka na hata hivyo muda ulikuwa umeenda hivyo Edna alijikuta akisinzia kwenye bega la Roma huku Roma yeye akiwa macho muda wote , hakuwa na shida kukaa macho muda mrefu kutokana na uwezo wake.

Kulivokucha mtu wa kwanza kuwapigia simu alikuwa ni Park Juan akiulizia hali ya afya ya Najma na kuuliza kama kuna kitu chochote cha kusaidia , lakini kwa hali yake aliokuwa nayo Roma aliona kwamba mzee huyo asingeweza kufanya chochote kama yeye mwenyewe tu ameshindwa.

Saa moja kamili hatimae Najma aliweza kufumbua macho yake , lakini licha ya hivyo mwonekano wake ulikuwa kama wa mtu ambaye hana uelewa wowote kama yupo wapi.

“Najma umeamka , unajisikiaje?”Aliongea Edna lakini Najma aliishia kumwangalia bila ya kutoa jibu , ilikuwa ni kama vile hamjui.

“Kiu…”

“Una kiu , ngoja nikupe maji”Aliongea Edna na kisha akachukua maji ambayo yalipashwa moto kidogo kupunguza ubaridi na kisha akamsaidia kumnywesha.

“Najma vipi hali yako bado unajisikia vibaya?”

“Wewe ni nani?”Aliuliza Najma huku akionyesha kumshangaa Edna.

Edna baada kuulizwa swali hilo alijikuta kikombe kikimponyoka bila ya kujielewa na kudondoka chini huku akiwa ameshikwa na bumbuwazi akiwa kama mtu asieamini.

Upande wa Roma kidogo aliona ni ahueni baada ya kuona hali yake haikuwa mbaya kama alivyotegemea lakini mara baada ya kumuuliza Edna yeye ni nani kauli yake ilishitua moyo wake.

“Najma hautujui sisi?”Aliuliza Roma na kumfanya sasa Najma kuona kumbe kuna mtu mwingine ndani ya hiko chumba.

“Ah…Ondoka , Ondoka ..”alianza kufurukuta kwenye kitanda kama vile mtu ambae ameona kitu cha kutisha mara baada ya kumwangalia Roma.

Roma ilibidi amuwahi na kumshikilia mikono na miguu ili aisje akadondoka chini , lakini hakuacha kupiga makelele.

“Niache …Argg.. Niache mimi ,. Ondoka zako”

“Najma hebu tulia , mimi ni Roma , Roma Ramoni”

“Najma hutujui sisi , usilie”Aliongea Edna akiwa amemshikilai mkonno mwingine kwa namna ya kubembeleza , lakini bado Najma alianza kurusha rusha miguu.

“Roma inabidi uondoke , Inaonekana Najma anakuogopa”Aliongea Edna na kumkumbatia Najma akimshikilia kwa nguvu.

Roma alielewa na kumwangalia Najma kwa wasiwasi na kisha akatoka ndani ya hio wodi. Na ilionekana kuwa kweli , kwani Roma mara baada ya kutoka alitulia na kuishia kumkumbatia Edna na kuanza kuporomosha kilio kama mtoto mdogo.

Muda huo huo na manesi waliweza kufika kwa kukimbia kumsaidia Edna na walikuwa wakiongea kikorea tu jambo ambalo lilimfanya Edna asielewe , hivyo mwanamama mmoja alimshika Edna mkono na kumtoa nje,

“Sir, hali ya mgonjwa kwasasa haijatulia , je daktari hajawaambia msimsogelee kwani angefanyiwa uchunguzi tena , kwanzia sasa kaeni mbali na mgonjwa”Aliongea yule nesi huku akionyesha kuchukizwa kiaina lakini Roma alielewa nesi huyo alikuwa akijali zaidi kuhusu hali ya mgonjwa.

“Nesi kwanini mgonjwa ananiogopa mimi ilihali mke wangu yeye hamuogpi”

“Kutokana na kilichomtokea kusababishwa na wanaume hivyo woga wake anaelekezea kwenu , hivyo kumfanya kuzidi kuwa katika hali hatarishi”Aliongea yule nesi na kumfanya Roma kuhisi maumivu kwenye moyo wake.

Edna alishindwa kuvumilia kumwangalia Najma ambaye alikuwa akihudumiwa na manesi, kadri alivyokuwa akimwangalia alizidi kujibebesha lawama kwa kuona yeye ndio mhusika mkuu wa yote hayo , hata hivyo Najma alikuwa hana kosa , kama kuonana na Roma yeye ndio wa kwanza na hata kumpenda yeye ndio wa kwanza , lakini licha yote yeye ndio akawa mhanga mkubwa wa mapenzi,Roma alikosa hata nguvu za kumfariji Edna tena.

Nusu saa mbele daktari wa wagonjwa wa akili aliweza kufika hapo kwa ajili ya kumchunguza Najma , lakini ilishindikana kwni Najma alikuwa akileta vurugu na mwishowe daktari wa kike aliitwa.

Yezi na Park Juan pia waliweza kufika hapo lakini Najma hakuweza kuwatambua kabisa na Najma alimuogopa hata Park juan licha ya uzee wake.

Yezi kumuona mwalimu wake kuwa katika hali mbaya kama hio alijikuta akishindwa kujizuia na kutoa machozi.

“Vipi tuwataarifau familia yake , nadhani litakuwa jambo zuri kumpa taarifa kaka yake”

“Hapana , nyumbani inaonekana wanajua kabisa Najma anaendelea vizuri , unafikiri tukiwaambia yupo kwenye hali kama hii tutaeleza sababu iliosababisha ni nini”

“Tutafanyeje sasa yupo katika hali hii na kama ikiendelea kubakia hivyo?”

“Kwasababu hawa madaktari wamekusoa suluhu ya tiba yake , naamini Clark anaweza kusaidia katika hili”Aliongea Roma na ikawa imepita hio , Roma aliamini Clark asingekosa suluhisho.

Taarifa zilionyesha Clark tayari alikwisha kupanda ndege , hivyo Roma alikadiria muda ambao Clark angekuwa ashafika na kisha aende akamrudishe tena Korea.

Siku iliofatia mara baada ya hali ya Najma kuendelea vilevile na madaktari wa hospitali hio kubwa kukosa suluhu hakutaka kuendelea kumwangalia Najma akiwa kaenye hali yake hio , hivyo moja kwa moja alienda Uingereza.

Clark alishangazwa na uwezo wa Roma kusafiri anavyotaka ndani ya sekunde tu na alijikuta akianza kupatwa na tamaa na yeye kuutaka kujifunza mbinu za kijini , akijiambia kwamba angeweza kusafiri kwa muda mfupi sana kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Roma alimweleza Clark njiani juu ya tatizo la Najma hivyo mara baada ya kufika Korea kwasababu daktari mkuu wa hapo alikuwa akimfahamu alipewa ushiriano wa kutosha.

Na kwa upande wa Najma hata baada ya kuonana na Dokta Clark alionyesha pia kutokumfahamu.

Clark alitumia zaidi ya masaa mawii kuwa na mgonjwa kuongea nae na kumchunguza tatizo lake na kisha aliweza kutoka kumpatia majibu Roma.

“Hali yake kwasasa ni ngumu sana kuielewa ,ameamua kufunga baadhi ya kumbukumbu zake na kupatwa na tatizo la woga maalumu kwenda kwa wanaume , kama hali yake isiposhughulikiwa haraka basi moja kwa moja hali yake itakuwa mbaya zaidi”

“Kwahio tunamsaidiaje, madaktari wote wa hapa Korea wameshindwa kuwa na njia”

“Sio kama wameshindwa kuwa na njia , ila ni kwamba hawana uhakika njia ipi inaweza kumfaa , kikawaida kuna matibabu ya aina nyingi kwa mgonjwa kama huyu , kuna tiba ya hypnotherapy , tiba ya utambuzi, tiba ya ulazimishaji , tiba ya kimazingira na nyingine nyingi… ila nitajaribu na tiba ya hypnotherapy , kama nitaweza kugundua ni tatizo ganni linasababisha woga wake basi itakuwa rahisi kuamua matibabu mengine”Aliongea kwa kingereza.

“Ni hatari hio tiba?”Aliuliza Edna.

“Kama itafikia hatua mgonjwa ataonyesha kuwa katika hatari basi tutaghailisha , isitoshe nina uzoefu wa kutosha hivyo usiwe na wasiwasi’Aliongea Clark huku akitabasamu kumtoa Edna wasiwasi.

Baada ya hapo Najma alihamishiwa na kupelekwa katika chumba maalumu cha ukimya na kufayiwa taratibu za mwazo ili kuanza matibabu mengine.

Edna kwanini usirudi kwanza katika makazi ya Park, nadhani itakuwa sawa nikiendelea kubakia hapa , mwambie Yezi asiwe na wasiwasi lazima kutakuwa na njia ya kmsaidia”Aliongea Roma na Edna aliona afanye hivyo kwanza alikuwa akijihisi uchomvu wa aina yake.

“Honey , kama Najma asipopona , utafanya nini?”Aliuliza kabla ya kuondoka.

“Nahusika moja kwa moja kwa hali ambayo amepata , hivyo kama matibabu yatashindikana sina jinsi nitamrudisha Tanzania na kumweleza kaka yake kilichotokea , kama atanichukia sio mbaya , lakini nitaendelea kumhudumia”Aliongea na kumfanya Edna kutoa tabasamu la kulazimisha.

“Muda mwingine inaonekana sahihi kufanya hivyo lakini matokeo yake mzigo unaniegamia mimi”Aliongea Edna na Roma alijua Edna anachojaribu kumaanisha , lakini kwa muda huo hakuwa na cha kuongea zaidi ya kumwambia akapumzike.

Baada ya saa moja kupita Clark alirudi kwa Roma tena kumweleza hali inavoendelea.

“Umefanikiwa?”

“Imeshindikana kabisa , tumejaribu kumwambiea aingie ndani kabisa ya mawazo yake ili kukumbuka matukio yote , lakini alionekana kuwa katika taharuki ya hali ya juu na presha yake kupanda hivyo tukakatisha asije akapatwa na Stroke”

“Clark najua hili sio rahisi kufanya , lakini nakuomba sana umsaidie apone , yupo kwenye miaka ishirini tu na ameteseka sana , itakuwaje akaendelea kuwa hivyo bila ya kukamilisha ndoto zake”Aliongea Roma kwa wasiwasi huku akibembeleza kwa dhati kabisa.

“Kwanini upo na wasiwasi hivyo , lakini mimi hata hunionei huruma hata mara moja”Aliongea na kumfanya Roma kushangazwa na kauli yake kidogo.

“Wewe ni wa tofauti , sisi ni marafiki wazuri sana”

“Marafiki wazuri ,,, yaani baada ya miaka yote hio , na yote nilioyafanya bado to sisi ni marafiki wazuri”Alilalamika huku aking’ata lipsi zake.

“Roma kwanini unanikatili namna hio?”Aliendelea kuongea.

“Clark naomba tuache hii topiki , ni muda mrefu sana sijapata uchomvu na wasiwasi wa namna hii , naomba kwanza tafadhari unisaidie kumrudisha Najma kwenya hali yake ya kawaida”

“The only person in this world who can let the murderous His Majesty Pluto beg is probably me”Aliongea Clark akimaanisha kwamba mtu pakee ambaye anaweza kumfanya Mfalme Pluto muuaji kuomba basi ni yeye.

“Sioni tatizo kukuomba hata hivyo”Aliongea na kumfanya Clakr kutingisha kichwa kumsikitikia .

“Ukweli ni kwamba nishapata wazo la kutatua shida yake”

“Ni wazo gani hilo?”

“Vipi kwanza mkeo hayupo hapa si ndio?”

“Tatizo nini akiwepo , wazo hilo linamuhusu , nimemuambia aende akapumzike”Aliongea Roma na kumfanya Clark kutabasamu kidogo.

“Kumbuka nilichokuambiwa mwanzo , kwamba tunaweza kumtibu kwa njia ya hali ya kimazingira pamoja na tiba lazimishi(compulsive therapy)”

“Ndio nakumbuka , lakini inafanyika vipi?”Aliuliza Roma na Clark alimwonyesha Roma ishara ya kumsogelea karibu amnong’oneze.

“Ah.. ndio maana ukauliza kwanza kama Edna yupo hapa , kumbe tiba yenyewe ni hio”Aliongea Roma huku akionyesha mshangao.

“Hio ndio njia yenyewe ambayo inaweza kumsaidia , najua unaweza kuona haifai hivyo sikulazimishi kwani anaweza akapona mwenyewe siku yoyote , lakini kwa hali yake aliokuwa nayo naamini atazidi kudhorota kadri ziku zitakavyosogea , na isitoshe kama ataendelea kuogopa wanaume basi maisha yake yatakuwa magumu sana”Aliongea na kumfanya Roma kuelewa , lakini njia yenyewe ilikuwa na changamoto kwani ilibidi yeye ndio afanye kumponyesha Najma.

Unafikiri ni tiba gani hio ambayo Edna hatakiwi kuwepo?”

ITAENDELEA
Xxxxx
 
Back
Top Bottom