SEHEMU YA 591.
Ni nje kidogo ya jiji la Kigali katika mlima uliofunikwa na msitu wa miti alionekana Denisi amesimama kando kabisa ya nyumbas ambayo imetengenezwa kwa mabanzi kama banda huku nyuma yake akiwa na wanajeshi wake.
Macho yake yote yalikuwa yakiangalia upande wa jiji la Kigali kwa muonekano ambao ilikuwa ni ngumu kuweza kuusoma kama anafikiria nini.
Muda huo huo alionekana Kizwe alietokea upande wa chini yao akipandisha kuwasogelea.
“Is everything ready?”Aliuliza akimaanisha je kila kitu kipo tayari.
“Jeremy amealikwa kuhudhuria chakula cha usiku na Balozi wa Ujerumani katika hoteli ya Sherati na baada ya hapo moja kwa moja ataenda Area D kwa mapumziko ya Wikiend, tuna muda wa kutosha kujiandaa”Aliongea Kizwe akifafanua ratiba za raisi Jeremy.
“Vizuri sana”Aliongea Denisi akitingisha kichwa.
“Lekcha ni kweli kabisa umebadili maamuzi yako ya kupotezea fursa ya kumuondoa Roma katika urithi wa familia?”
“Mhmh… fursa!?, nimetumia muda mwingi sana kukusanya watu wengi vile lakini mwisho wa siku wamegeuka kutokuwa na thamani , nimefeli kumzuia Roma kurithi uongozi wa familia awamu hi lakini siamini kama kutakuwa na nafasi nyingine ya kufanya hivyo , Roma angekuwa ashaniua leo kama sio Damasi kunikingia kifua , nina uhakika lazima anapanga kuniua kwa siri , hivyo tofauti na kumsubiria na kuniumbua mimi nani napaswa kumalizana na Jeremy kwanza ikiwa bado ni mapema, Roma anaweza kuwa kikwazo ndani ya Tanzania lakini bado tutaweza kupiga hatua kwa rasilimali zilizopo Rwanda”
“Una uhakika unaweza kumshinda Roma kwa kutawala Rwanda , Jeremy alijaribu kuitawala Tanzania kijasusi lakini alishindwa mpaka sasa na njia pekee alioona ni kuungana na familia ya Roma ili uhusiano wake na Tanzania kuimarika kupitia ndoa”
“Kama nilivyosema sio lazima sana kumshinda Roma ili niweze kutimiza malengo yangu , kwasababu kushindana na Roma ana kwa hakuwezi kufanikisha kitu, basi nitamtumia kuendelea kutibua hali ya hewa kama nilivyofanya”Aliongea na kumfanya Kizwe kuridhika na maelezo yake.
“Lekcha , je unaweza kuniahidi kitu?”
“Ongea”
“Najua mpango wako ni kuwadhibiti Gesha na Nix usiku huu lakini kuhusu Jeremy je unaweza kuturuhusu mimi na Desmond kumshughulikia?, kuwa na amani hatuwezi kuharibu mwili wake hivyo haitakuathiri na mipango yako”
“Ilimradi ubongo wake usijekuharibika tu , nina uwezo wa kuutawala mwili wake na kujiponyesha hata kama mtamfanya kuwa kilema , mnaweza kumfanya chochote kupungua hasira zenu , mimi sitojali”Aliongea na kumfanya Kizwe kutabasamu na kisha kumkumbatia.
“Nilijua tu utanikubalia , wewe ni noma”
“Anakwenda kuwa maiti hata hivyo , sitojali kama mtataka kumchezea kwanza”Aliongea Denisi huku akitoa tabasamu lake la kejeli lililochanganika na ukiburi ndani yake.
Ilionekana Lekcha mara baada ya kushindwa vita Tanzania baada ya Roma kumuharibia hatua yake ya pili ni kujaribisha nchini Rwanda, haikueleweka alikuwa na mpango gani kutaka kuitawala Rwanda kwa kumuua Jeremy.
*****
[DI1]
Wakati wa usiku baada ya chakula, Lanlan kama alivyoambiwa na babu yake alienda kulala katika chumba cha wazazi wake.
Lanlan alikuwa amelala katikati huku kulia kwake akiwa ni baba yake na kushoto kwake akiwa ni mama yake.
Edna alikuwa akijishishika shika shingo yake huku akimwanglaia Roma kwa kutabasamu huku akiwa na macho yaliojaa uchokozi ndani yake bila ya Lanlan kuona kama wazazi wake wanaangaliana na kutabasamiana kiuchokozi.
Wakati Lanlan akiwa na furaha ya kulala na wazazi wake upande wa Roma yeye alikuwa akimlaani babu yake kwa kumfanya Lanlan kuja kulala nao maana ameharibu mipango yake yote.
“Daddy mdio unafikiria kuhusu stori ? nataka unihadiithie stori nzuri sana”
“Chubby hebu ongea leo si umekula mapaja yote mawili ya mguu wa kondoo wewe , utakuwa umeshiba sana na unahisi usingizi, unaonaje ukilala?””
“Mimi sina usingizi na sijashiba sana , Daddy sitaki kulala nataka stori”Aliongea na kumfanya Roma kumshangaa kusema hajashiba bado na kujiambia bora hata angemuongezea kidogo chakula chake.
“Lanlan unaonaje mama akianza yeye kukuhadithia stori kwanza?”
“Nishamuambia Stori nyingi tu kipindi chote nilichokuwa nikilala nae , leo wewe ndio zamu yako”
Roma mara baada ya kurushhiwa mpira na mke wake aliona haina haja ya kumuangusha binti yake ilihali alikuwa amejipanga kusikia stori kutoka kwake.
Ukweli kwenye maisha yake hakuwahi kusoma hadithi yoyote wala kusimuliwa, alijiambia kuwa tajiri na nguvu hakukuwa kukitosha tu kwa mtoto wake bali alipaswa pia kuwa msimuliaji mzuri wa stori.
Kwasababu hakuwa na stori ya aina yoyote alioijua aliona kitu pekee ambacho anapaswa kusimulia ni kuhusu maisha yake yaliopitia.
“Lanlan uunaonaje nikikuhadithia namna ambavyo niliweza kupambania maisha yangu katika Wolf Pack huko Alaska?”
“Daddy Alaska ni wapi?”
“Ni sehemu ya mbali sana kutoka hapa, kuna baridi sana na karibia eneo lote limejaa barafu na theluji , upatikanaji wa chakula ni mdogo sana huko”
“Na Wolf pack ndio nini Daddy?”
“Ni mkusanyiko wa Mbwa mwitu zaidi ya mia moja wanaowinda kwa pamoja kwa ajili ya kuweza kuishi”
“Kwahio hao Mbwa mwitu ndio walikuwa wakikuwinda ?”
“Ndio, lakini kulikuwa na watoto wengine waliokuwa katika umri wangu , tulikuwa na miaka kama kumi kwenda kumi na moja”Aliongea Roma na kumfanya Lanlan kutingisha kichwa kwa shauku kukubali kuweza kusikiliza stori hio , lakini kabla ya kuanza aliona kwanza ajaribu kuongea nae kumweleza baadhi ya maneno ambayo hataelewa kwa utoto wake.
“Lanlan unajua ukubwa wa eneo la kuwindia?”
“Ndio Lanlan anajua , ni eneo kubwaaa , kubwa, kubwa sanaa”Alijibu kwa ishara na kumfanya Edna aliekuwa akisikiliza maongezi hayo kushindwa kuzuia kicheko kwa namna ambavyo Lanlan amejibu.
“Edna kuwa siriasi , sisi wazazi wako hapa tunahadithia stori , hivyo kuwa makni katika kusikiliza”Aliongea kwa utani na kumfanya Edna kuendelea kucheka.
“Okey nitasikiliza kwa umakini , hebu anza kuhaditia na mimi nataka kusikia”
Aliongea na kumfanya Roma kuweka mto vizuri ili kukaa vizuri aanze kuhadithia.
****
Ni miaka kadhaa iliopita Kaskazini mwa msitu wa Alaska unaopatkana huko Marekani , anga lilionekana kuwa la bluu huku milima ilionekana kuwa ya rangi nyeupe kutokana na kufunikwa na Theruji.
Ardhi yake ilikuwa kame sana hususani katika kipindi hicho cha baridi kali na hata kwa baadhi ya maeneo yake ya karibu jotoridi ilikuwa likifikia takribani ya nyuzi hasi 10 za jotoridi..
Na kadri baridi katika juu ya usawa wa bahari ilivyozidi kuongezeka ndivyo baadhi ya maeneo pia baridi yake ilizidi kuongezeka na kufikia nyuzi hasi therathini , mbaya zaidi baadhi ya maeneo mengine yalikuwa na mito ambayo ilizidi kufanya eneo kuzidi kuwa na ubaridi wa hali ya juu.
Hili ni eneo ambalo raia wa Marekani wamelibatiza jina la
No man zone yaani eneo ambalo huwezi kuishi au kumkuta binadamu anaishi na hata wale watalii wanaofika hawakuthubutu kukaa kwa muda mrefu katika eneo hilo kutokana na kuhofia kundi la mbwa mwitu na athari za baridi kali.
Mito ya eneo hio ilioganda na kutengeneza barafu yenye upana mkubwa ilirahisisha sana usafiri wa ndani , kwani watu walitumia kama njia kwa kukanyaga juu yake.
Sasa wakati eneo hilo likiwa tulivu huku sauti za kubweka kwa mbwa zikisikika katika kila baadhi ya pande pamoja na upepo uvumao kwa kasi, kando ya mto mkubwa ulioganda aliweza kuonekana kijana mdogo wa kizungu akitembea ambaye amevaa mavazi ya meusi ya Leather marefu pamoja na gloves huku akiwa amejifunika na ngozi yenye manyoya ya mnyama mwili mzima.
Alikuwa na nywele za rangi ya Zambarau iliofifia huku ngozi yake ikiwa na vidoa doa(freackles) vya rangi nyeusi , ijapokuwa kijana huyo alionekana kuwa wa umri mdogo lakini mwonekano wake ulikuwa ni ule wenye ukauzu na uhatari..
Alikuwa akiangalia kulia na kushotio kwake na kugeuka nyuma akiwa kama mtu mwenye wasiwasi huku akipumua kwa nguvu kiasi cha kusababisha pumzi yake kutoka kama mvuke kutokana na baridi kali.
Ili aweze kutoka katika eneo hilo na kufika bandarini alitakiwa kuvuka mito na milima iliokuwa mbele yake.
Kijana yule alitembea huku akiwa na umakini mkubwa kwa kuyapa kazi masikio yake kusikiliza kwa umakini kwa kila kitu kinachomzunguka huku mkononi panga lake likiwa tayari kwa ajili ya kufanya kazi kwa kitu chochote cha hatari kitakachomtokea.
Kwa mazingira hayo ilikuwa ni ajabu sana kumuona kijana kama huyo kuwa peke yake , kwani eneo hilo lenye milima na mabonde lilitisha.
Alikuwa na wasiwasi sana kutokan na kwamba uwepo wa Theruji pamoja na barafu ndani ya eneo hilo hatua za watu hazikuwa zikisikika vizuri hivyo kama kutatokea adui au mnyama kumsbambulia basi ingekuwa ni kwa wepesi sana.
Kijana huyo ni moja wapo ya kundi la watoto ambao wapo katika mafunzo makali ya ku’survive’ katika mbuga za wanyama wakali , ukiachana na hilo eneo hilo lilikuwa ni la kuwindana yaani ‘ ua au uuliwe’ ndio kanuni iliotumika katika eneo hilo , licha ya kwamba walikuwa wamefunzwa pamoja na wenzake lakini ili kuweza kutoka hapo ni kupambania maisha yako kwa kumuua mwenzako atakae tokea mbele yako au yeye akuue, ndio maana umakini wake ulikuwa mkubwa zaidi kwani hakutaka kufa bali alitaka kuua na kuweza kufanikiwa kutoka.
Kulikuwa na mashimo makubwa juu ya mto ulioganda ambayo yametengenezwa kwa kuchimbwa na watu waliokuwa wakijaribu kuvua samaki chini ya barafu.
Kuna baadhi ya mashimo ambayo yenyewe yalikuwa yamechimbwa na mchimbaji ili kuzuia yasijifunge tena alijaza majani makavu kwa juu na baadhi ya miti miti kuziba.
Hayo yote aliweza kuyafahamu kijana huyo mdogo kutokana na kuwa na mafunzo ya hali ya juu kuishi kwenye maeneo hatari kama hayo.
Wakati akitembea kwa umakini aliweza kufikia katika shimo moja juu ya mto likiwa limechimbwa na kuzibwa na majani pamoja na miti miti huku pembeni ya shimo hilo kukiwa na fimbo(Fishing rod) maalumu ya kuvulia samaki iliokuwa imeachwa na kwa haraka haraka kijana yule aliamini kabisa aliekuwa akivua hapo huenda aliondoka kwa haraka haraka mara baada ya kupata kitoeo.
Haikumshangaza sana kwani alijua ndani ya msitu huo kulikuwa na wenzake wengine.
Kuona kifaa hicho cha kuvulia ilimfanya kupata tumaini la kujijpatia chochote kwani alikuwa na njaa sana , hivyo hakutaka kupoteza fursa ya kuvua ilihali vifaa anavyo.
Aliangalia kulia na kushoto na kuona hakuna mtu aliekuwa karibu na eneo lote limetulia na ilimfanya kutabasamu na kujiambia yupo salama hivyo anaweza kuvua samaki kwa utulivu.
Kijana mara baada ya kutoa majani yale na kuingiza ndoano majini alisubiri kwa dakika kadhaa tu na alijikuta tabasamu likipamba uso wake mara baada ya kuhisi uzito kwenye mti na moja kwa moja alielewa kabisa samaki ashanasa kwenye ndoano yake.
Lakini sasa wakati akijaribu kuvuta kamba nje kumtoa samaki alijikuta akigundua kuna kitu hakipo sawa kutokana na uzito wa kamba ile , lakini wakati akipata ufahamu wa kwamba kuna kitu kipo ndani ya shimo hilo katika mto huo alikuwa amechelewa kwani palepale ulitokea mkono kutoka kwenye maji na kumvuta na ile mikono yake inafusa barafu palepale kisu kilipita katika shingo yake kwa haraka sana kabla hata hajajihami.
Kilikuwa ni kitendo cha sekunde kadhaa tu kijana yule wa Kizungu alikuwa tayari ashapatiwa shambulio la kushitukiza akiwa haamini kama alikuwa amejiingiza katia mtego wa adui.
Ilikuwa ni kama vile kile kifaa cha kuvulia hakikuwa kwa ajili ya kuvua samaki bali kilikuwa kimetegwa kumvua yeye.
Dakika ile wakati kijana akipambania uhai na kifo , sura ya kijana mwingine aliekuwa uchi mwenye ngozi nyeusi aliweza kutokezea kwenye lile shimo kama vile ni samaki aina ya Papa, ilionekana alikuwa ametulia chini ya maji kwa ajili tu ya kumtega adui yake kuingia kwenye mtego wake ambao umemleta mafanikio makubwa.
SEHEMU YA 592.
Yule kijana wa ngozi nyeusi hakujali kabisa kwamba alikuwa uchi na alikuwa akitetemeka kwa baridi bali palepale alimsogelea yule kijana mwenzake aliekuwa akikata Roho na kutafuta mshipa wa damu na kuukata kwa meno yake na palepale kuanza kunyonya damu ya moto kama Vampire.
Katika eneo kama hilo hakuna kitu cha thamani kama damu ya moto na haikujalisha ni damu ya binadamu ili mradi tu iwe ya moto.
Yule kijana wa kizungu hakuwa bado amepoteza maisha na aliweza kushuhudia namna mwenzake anavyo mnyonya damu mpaka uhai wake una tamatika.
“Kijana yule mwenye nywele ndefu nyeusi baada ya kuona ametosheka na damu ya moto, kwa haraka sana alimvua yule mwenzake nguo alizovaa na kukata kipande na kuanza kujifuta maji na kisha akavaa zile nyigine na zilionekana kumkaa vizuri kwani maumbo yao yalikuwa yakilingana.
Ukweli ni kwamba kijana wa kizungu wakati akijiona yupo makini na usalama wake , upande wa kijana huyo wa ngozi nyeusi alikuwa ashamuona muda mrefu sana kwa nyuma yake na ndipo kwa haraka sana alipoamua kumtegea mtego wa kumuua.
Alikuwa na njaa sana kiasi kwamba alijua asingemuua kijana huyo mwenzake na kunywa damu yake asingweza kupitisha usiku kwa njaa hivyo hakuwa na maamuzi mengine tofauti na kumla.
Katika mazingira hayo ambayo hakuwa na ufahamu wa adui yake yukoje kimapambano mbinu pekee ambayo aliona ni rahisi ni kumuwekea mtego ambao una nafasi kubwa ya kufanikiwa tofauti na mapigano ya ana kwa ana, hakujali kama mtego wake ulikuwa ni wa kubahatisha lakini hio ndio njia pekee ambayo aliona inamfaa.
Na hata kitendo chake cha kuvua nguo na kuzitupa ndani ya maji ilikuwa ni kuongeza asilimia za mafanikio kwani aliamini kama atakuwa ndani ya maji na mavazi basi uzito wa kuloana kwa nguo utamzuia katika kushambulia ndio maana alikuwa uchi.
Baada ya kijana yule kuchukua mazoezi kidogo ya kupasha mwili joto palepale alikata pande la nyama kutoka katika mwili wa yule mzungu na kula kwa kutosheka ili mradi kuweza kupata nguvu ya kumuwezesha kuipitisha usiku huo kwa kupambana na chochote kitakachokuwa mbele yake.
Baada ya kuona ameridhika , akakata mapande mengine ya nyama na kuyahifadhia katika mfuko wake kwa matumizi ya baadae.
Na kwa maiti iliobaki aliamua kuidumbukiza mtoni , alifanya hivyo ili tu kutofanya washindani wake waliokuwa ndani ya hilo eneo kufaidika na uwindaji wake, isitoshe kadri washindani wanavyoendelea kufa na njaa na kupungua ndio namna pekee ya kumuwezesha kufanikiwa kutoka na kukamilisha mafunzo yake.
Kula nyama ya bindamu katika eneo kama hilo haikumsumbua sana kwani ni kitu ambacho haikuwa mara yake ya kwanza kufanya , baada ya kuthibitisha mwolekeo ambao anatakiwa kuchukua kupitia miale hafifu ya jua alianza kutembea kutoka nje ya mto huo na kupanda juu ya mlima katika msitu..
“Kupitia jua alifahamu muda si mrefu giza litaingia kwani kwa uzoefu wake alijua muda huo ni saa kumi za jioni.
Kama sio kwa hali ya hewa pengine angekaa na kupumzika na kufurahia kuangalia anga lenye kupendeza bila dalili yoyote ya wingu..
Wakati akiendelea kutembea katika miti ghafla mwili wake wote ulimsisimka na haikuwa hivyo tu aliweza kuchukua hatua za haraka sana kuhepa kidogo kuelekea kushoto na ndio ilikuwa pona yake.
Chuma cha rangi ya Silver kiliweza kupita karibu kabisa na koromeo lake na kivuli cha mtu kiliruka kutoka juu ya mti.
“Ambush!”
Aliwaza kwa haraka akijua hilo ni shambulio la kushitukiza na alifanya haraka sana kutoa siraha yake panga ili kumshambulia adui yake.
Matarajio yake yalikuwa tofauti sana na alivyotegemea , kwani adui yake alioneka kuwa vizuri sana katika kushambulia na na kilichosikika ni kelele za kugongana kwa siraha katika eneo hilo.
Jambo moja tu alilolijua kutoka kwa adui yake kwa kumsoma kwa haraka haraka ni nguvu zake , ijapokuwa alikuwa na ujuzi mkubwa wa kushambulia lakini hakuwa na nguvu za kutosha kama yeye , hivyo alichokifanya ni kutumia nguvu kubwa katika kushambulia ili kimchosha adui yake.
Adui yake alikuwa amevaa Mask kiasi cha kumfanya asimuone sura lakini kadri ambavyo alikuwa akipambana nae akili yake ilimtengenezea ufahamu na kujua anapambana na nani.
“Seventeen!!”
Kijana yule aliweza kubweka kwa hali ya juu na kumfanya yule mtu aliemwita kwa jina la Seventeen kusitisha mashambulizi.
“Thirteen , you are lucky”
Sauti ya kike iliweza kusikika ikimwita yule kijana ambaye alionekana kula nyama ya mtu kwa jina la Thirteen huku akimwambia kwamba ana bahati.
“Tumeweza kupambania maisha yetu katika kambi moja ya mafunzo kule Siberia , hakuna haja ya kuwa mkali hivyo isitoshe haitokuwa rahisi kwa wewe kunishinda mimi , tusipoteze nguvu zetu bure kama tukiendelea”
“Don’t try to cheat me , you have two pieces fo human meat in your sack, so you would still survive even if I don’t”
“Acha kudanganya , una mapande mawili ya nyama kwenye mfuko wako , hivyo utaweza kuishi hata kama mimi nitashindwa”
“Kumbe uliniona?”
“Nimekufanyia shambulio la kushitukika kwasababu nilikuona .”Aliongea na kisha palepale Seventeen mwenye saiu tamu ya kike iliojaa usiriasi alimsogelea Thirteen kwa tahadhari.
“Kwasasa sina chochote chakula na nitakosa nguvu muda wowote kadri muda unavyosogea ni kheri kupambana sasa hivi nikiwa na nguvu kuliko kusubiria kifo changu na wewe wewe kula nyama yangu”
“We almost ate each other in siberia and you want to do it again? Aren’t you sick of it ?”Aliongea akimaanisha kwmaba kidogo tu wakulane nyama walivyokuwa Siberia , je hajachoka tu.
“Nitakupa machaguo mawili , nipe chakula nile nishibe au tupambane?”Aliongea huku akiwa siriasi mno na kumfanya Thirteen kutabasamu kifedhuli.
“Kwanini nifanye hivyo unaonekana kabisa unazidi kuchoka na kuwa dhaifu , ninaweza kukuua tu na kula nyama yako , muda huu tofauti na kupamba na mimi angalau ungetafuta hata minyoo chini ya miti na kula, angalau ungweza kuokoa maisha yako”
“Acha ujinga Thirteen , najua sikuwezi kwenye mapambano ya ana kwa ana katika ardhi ilionyooka lakini spidi yangu na wepesi ni kubwa kuliko wewe , unaweza usifanikiwe kunishinda kwenye ardhi kama hii yenye miinuko”Aliongea huku na yeye akitoa tabasamu la kejeli.
“You’re feisty”Aliongea.
Ukweli ni kwamba Thirteen hakuwa akiogopa kupambana nae lakini alijua kabisa kupigana nae hapo hakutokuwa kwepesi hata kidogo kwani aliujua uwezo wa Seventeen ulikuwa ukikaribia na wa kwake na kama ni kumshindana labda ni kutokana na udhaifu wake wa kuwa mwanamke na yeye kuwa mwanaume.
Seventeen hakutaka ubaridi kuendelea kumuathiri mwili wake na kumnyong’onyesha na palepale alimpiga ngumi ya kushitukiza Thirteen , lakini upande wa Thirteen alionekana kuwa mwepesi kwani palepale aliikwepa kwa kupiga sarakasi kurudi nyuma na kujificha na Seventeen hakutaka kumuacha kizembe kwani hapo anapambania maisha yake na walianza kushambuliana kwa kasi kwa kuoteana kutokana na kwamba kulikuwa na miti ambayo walikuwa wakiitumia kama ngao.
Katika hali kama hio Seventeen ndio ambaye alionekana kushambulia zaidi kwa spidi huku Thirteen yeye akijaribu kukinga mapigo yake.
Upande wa Seventeen alijua kabisa kama ataendelea kupambana kwa muda mrefu basi itafikitia muda atakuwa hana nguvu hivyo atampa nafasi Thirteen kumua jambo ambalo hakuwa akitaka litokee kabisa.
Lakini wakati wakiendelea kufukuziana kwa kushuka na kupanda katika eneo hilo ambalo lilikuwa na miinuko na mabonde , ghafla tu walikuja kusimama mara baada ya kusikia ngurumo kubwa za mbwa mwitu.
“A wolf?!?”Alishangaa Seventeen akiuliza.
“No, it’s wolf Pack”Aliongea Thirteen akimaanisha kwamba ni kundi la mbwa mwitu.
Muda huo ngurumo hizo zilianza kusikika kwa kuwasogelea kwa tahadhari sana na kabla hata hawajajiandaa kujua namna gani ya kukabiriana na hali hio, ghafla tu mbwa mwitu hao waliruka kutoka walipojificha na kusimama mbele yao.
Alaska ndio eneo ambalo lilisifika kwa uwepo wa Mbwa mwitu ambao walikuwa wakitembea kimafungu na kutokana na eneo hilo waliokuwepo kuwa la tambrare tofuti na maeneo mengine basi ndio makazi yao.
Seventeen na Thirteen moja kwa moja walijua hapo wapo katika hatari wakiangaliana na macho ya rangi ya njano na nyekundu kutoka kwa mbwa hao.
“Kuna zaidi ya mbwa mwitu hapa zaidi ya therathini , nadhani ni zaidi pia kufikia mia moja , tupo kwenye hatari kubwa”Aliongea Thirteen huku akitoa tabasamu la uchungu.
Seventeen alichukua hatua moja kurudi nyuma na kisha akamwangalia Thirteen.
“Unaweza kukimbia ?”Aliuliza.
“Unatania nini? Unadhani tunaweza kushindana katika mbio na mbwa mwitu , miguu yao inapanda hata milima kama vile wanateleza kwenye barafu , hapa mbinu pekee ni kupanda juu ya miti la sivyo miguu yetu itang’atwa muda tu ambao tutaamua kukimbia”Aliongea Thriteen lakini Seventeen mwenekano wake haukubadilika.
“We only have one way out of this since we can’t run away , kill the Wolves with me , us working together is our only chance to survive”
“Tuna njjia moja tu kwasababu hatuwezi kukimbia , tushirikiane kuua hawa mbwa mwitu , sisi kufanya kazi kwa pamoja ndio njia pekre hapa ya kuishi”
“Hehehe , mrembo ni muda huu huu tu ulitaka kuniua na sasa hivi unataka tufanye kazi pamoja? , unafikiri ninaweza kukuamini kirahisi hivyo”Aliongea Thriteen huku akiwa na mwoneknao kama vile hakujali kilichokuwa mbele yake , ijapokuwa mbwa mwitu hao walikuwa wengi lakini kwake hakuwa na ule woga wa kutisha.
“Huna chaguo lingine , unatakiwa kujua tofauti iliopo hapa kama wewe sio minga, tuue hawa mbwa mwitu na nitaweza kupata chakula na sitohtarisha maisha yangu tena kupigana na wewe”
Baada ya kuongea vile palepale Thirteen aliingiza mkono wake kwenye mfuko wake na kisha akatoa kitu ambacho kilikuwa na nyama nyana zilizoning’inia na kumpigia mluzi Seventeen na kumrushia.
“This is..”
“Ni jicho lake hilo , Protini zilizopo ndani ya jicho ni nyingi zaidi kuliko nyama , meza hilo kujaza tumbo lako, tutawakaanga hawa mbwa mwitu baada ya kuwaua wote”Aliongea Thirteen akimaanisha kwamba ni jicho la yule mzungu.
Seventeen mara baada ya kuambiwa hivyo hakutaka kusita sita kwani palepale alilipeleka jicho lote mdomoni na kulitafuna mara chache na kumeza na kumfanya Thriteen kumwangalia kwa tabasamu.
“You are Fierce but I like it … let us get to work”Aliongea akimaanisha kwamba yeye ni mkali lakini anapenda hivyo na waingie kazini sasa
Mbwa mwitu walizidi kusisimika mara baada ya kunusa harufu ya damu kutoka mdomoni mwa Seveteen ambaye alikuwa akitafuna jicho la binadamu mwenzake.
Kushambuliwa na kundi la mbwa mwitu ilikuwa ni kama ndoto kwao kwa muda huo ambao miili yao ilikuwa na nguvu za kawaida za kibinadamiu katika kupigana.
Baada ya mbwa mwitu wa kwanza kumrukia Thirteen kwa ajili ya kumshambulia alikwepa kwa kuinama na likapita juu lakini na kwa wepesi zaidi aliinua kisu chake na kulichoma tumboni kwa kuchana.
Kisu chake kwa namna kilivyyoweza kukata nyama na kugusa mifupa ya mbwa mwitu huyo kilifanya sauti za maumivu kutoka kwa mbwa kusikika huku damu nyingi ikimwagikia Thirteen kwenye uso wake, ilikuwa ya moto na yenye kutoa harufu.
Mguno wa maumivu kutoka kwa mbwa mwitu mwenzao mara baada ya kufikia masikio ya wale mbwa wengine iliwainua na kuanza kushambulia wote kwa pamoja.
Kabla hajatoa kisu chake kutoka katika tumbo la mbwa mwitu aliemchoma , alifunikwa na mbwa wengine waliokuwa wakimshambulia katika maeneo mbalimbali ya mwili wake , kwenye tumbo , kichwa, miguuni na mikononi.
Upande wa Seventeen alivuta hewa nyingi na kuitoa na kisha alisogelea wale mbwa mwitu na kuanza kushambulia.
Ili kumuua mbwa mwitu ulitakuwa kulenga katika menno ambayo ni dhaifu kwao na kuyachana kwa haraka sana bila kufikiria na ndio ambacho alikuwa akifanya , alikuwa akiwafyeka kwa spidi kubwa na ustadi huku akipotezea majeraha ya mikwaruzo kutoka kwa kucha na meno ya mbwa mwitu hao.
Ilikuwa ni afadhali aliokuwa amevaa ngozi ya kuzuia baridi hivyo kupunguza majeraha , Seveteen aliendelea na kasi yake huku akilenga zaidi katika macho ya wanyama wale kwa spidi kubwa.
Kitendo cha mbwa wale kushambuliwa kwa kukimbia kulifanya mawe yaliokuwa juu kuwadondokea na kuwafanya kushindwa kubalansi miili yao na iliwafanya kupata wakati mgumu kwenye kushambulia na ndipo walipoamua kushambulia wakiwa wamekaribiana.
Ndani ya madakika mbwa mwitu ishirini tu ndio ambao walibakia huku waliokufa wakiwa ni wengi zaidi.
Seventeen na Thirteen walikuwa wametapakaa damu huku ikiwa ngumu kujua kama ilikuwa ni damu ya mbwa yupi kati yao.
Mbwa wale mara baada ya kuona wenzao wengi wameuliwa walijikuta wakipunguza spidi ya kushambulia na ilifikia hatua sasa walianza kuangaliana kwa macho makali na baada ya akili zao kuwapa ufahamu wanaopambana nao ni hatari kwao waliamua kukimbia na kuwafanya Seventeen na Thirteen kuweza kupatwa na ahueni.
“Hatimae tuna nyama ya kutosha sasa , lakini itakuwa ngumu kuwasha moto na kuwachoma , unaonaje tukiwala hivi hivi?”Aliuliza lakini Seventeen hakutoa jibu na alijaribu kusogelea maiti moja ya mbwa kutaka kuishika lakini Thirteen aliona jeraha katika mkono wa Seventeen na kupeleka mkono kugusa lakini matokeo yake ni kwamba kama sio wepesi wake kisu cha seventeen kingekata shingo yake, aliambulia kukatwa kidole chake tu kutokana na kukwepa shambulizi.
“Unafanya nini?”Aliuliza Thirteen kwa hasira.
“Kwanini umenigusa?”Aliuliza kwa macho makali Seventeen akiwa hana utani na macho yalikuwa yamejaa nia ya kuua tu, alionekana alikasirishwa sana na kitendo cha Thriteen kutaka kumgusa.
“Nilitaka kuangalia jereha lako , kwasababu nguo zako zimechanika angalau unapaswa kujitibu kabla hujapata maambukizi , kwasasa huhisi maumivu kwasababu ya mkono wako upo na Ganzi”Aliongea na kumfanya Seventeen kumwangalia kwa macho ya mshangao huku akichukua hatua moja nyuma kujiweka mbali na Thirteen na kisha aliangalia mkono wake na hapo ndipo alipojua alikuwa ameng’atwa na Mbwa na alikuwa na jeraha kubwa linalotoa damu.
Licha ya jeraha hilo kuwa kubwa lakini kwa Seventeen ilikuwa kawaida na asingweza kulia kama wanawake wa kawaida.
Wakati giza likizidi kuwa kubwa Thirteen hakuonyesha kujali t tena kinachoendelea na alianza kuchuna ngozi ya wale mbwa mwitu na kuanza kula hivyo hivyo nyama mbichi na muda wote Seventeen alikuwa akimwagalia.
“Kwanini umenikumbusha kuhusu jeraha langu?”Aliuliza akiwa siriasi kama vile kilikuwa kitendo ambacho hajapenda.
“Nisingwez kuwaua mbwa wote nikiwa mwenyewe , umenisaidia sana , isitoshe kwasasa nakuona huna nguvu za kutosha kushidana na mimi, hakuna tatizo nikionyesha kukujali , huenda tunaweza kuwa marafiki”
“Sihitaji unijali wala kuwa rafiki yako mimi’Aliongea kwa ukauzu mkubwa na kumfanya Thirteen kutabasmau na kisha kumuonyesha kidole chake alichokata.
“Una hasira za karibu sana, kwani ni vibaya mimi kukujali?”Aliuliza.
SEHEMU YA 593.
Mwanga wa taa ya kitandani ulikuwa ni hafifu sana lakini waliweza kuonekanavizuri , mmoja alikuwa akisimulia na wengine wawili wakisikiliza stori hio yenye kutisha kwa umakini mkubwa kwa zaidi ya lisaa lizima.
Roma alikuwa ashasimulia kiasi cha kubadili pozi lile ambalo alikuwa ameweka katika kuegamia mto na sasa alikuwa amekaa huku akiwa amekunja miguu yake , alikuwa ni kama vile yupo kwenye uhalisia wa maisha yake yaliopita na hata kusahau kabisa kama muda huo alikuwa akimsimulia Lanlan.
Hakuweza hata kuelewa kama Lanlan alikuwa ashapotelea usingizini muda mrefu katika mto akijizungusha zungusha na kutafuna kama vile kuna kitu ambacho kimewekwa katitka mdomo wake.
Sio kwamba alikuwa hapendi stori yake , ukweli ni kwamba kulikuwa na vitu vingi sana kwake kama mtoto kuvifikiria ndio maana aliweza kupotelea usingizi kwa haraka.
“Lanlan unajua nilitaka kumwambia nini , nilitaka kumwambia Seventeen aache maigizo , alionekana kabisa alikuwa mpweke na pia alikuwa na aibu , lakini hakuna ambae alikuwa akitujali kwa hali ambayo tunapitia , nilikuwa na Master wangu ambaye alinifundisha Kung fu alikuwa akinijali sana na aliniambia maneno machache ya kuweza kuongea ili kunasa moyo wa mtu , ukweli ni kwamba sikuwa hata siriasi kivile lakini alichonijibu kilinifanya kujisikia vibaya na baada ya usiku ule kila mtu aliondoka kivyake”Aliongea Roma kana kwamba Lanlan bado alikuwa akimsikiliza hakujua kama alikuwa ashalala.
“Lanlan hivi unajua ni jibu gani aliniambia mara baada ya kumuuliza kama ilikuwa vibaya kwa mimi kumjali?”Aliongea Roma na ndio muda ambao aligeuza macho yake kumwangalia Lanlan na aligundua Lanlan hakuwa akimsikiliza na amekwisha kulala na kumfanya kidogo kujisikia vibaya kwani alikuwa akijaribu kuelelzea hitoria ya maisha yake licha ya kwamba Lanlan alikuwamoto.
“Tafuta wasichana wengine wa kuwajali kwani hawawezi kukufanyia kama mimi kwa kukukata kidole na kisu changu”Sauti pembeni ya Roma iliweza kujibu , Sentensi hio kwenye maisha yake haikuwahi kufutika katika akili yake kwa miaka mingi , lakini katika hali na mazingiraambayo hajayategemea anaisikia kwamara nyingin.
Sauti hio ilikuwa ikifanana kwa kila kitu na aliosikia kipindi kile , haikuwa sauti tu lakini pia hisia zilizoambatana na sauti hio ni vilevile.
Roma alijikuta akipanua macho yake na kumwangalia mwanamke ambaye alikuwa amelala pembeni yaLanla , alikuwa na uhakika kabisa aliongoea hivyo ni Edna.
Ni kweli aliejibu swali la Roma ni Edna na kwa muda huo ni kama mtu ambaye alikuwa kwenye mawazo makubwa ya maisha yake yaliopita na muonekano wake ulimuonyesha kama vile ni mtu ambaye amepitia magumu mengi.
Yaani alichokuwa akihadithia Roma kwa upande wa Edna ni kama vile stori hio ilikuwa ikimuhusu yeye kabisa.
“Edna ume,, umejuaje alinijibu hivyo?”
Aliongea Roma huku akiwa kama vile sio mwenye kuamini kile alichosikia kimeweza kutoka katika mdomo wa Edna.
Edna sasa alielewa ameongea kitu ambacho hakuelewa ameongea nini na alimwangalia Roma kwa mwonenao usiokuwa wa kawaida.
“Hubby kwanini unanniangalia hivyo kwa kushanga?”Aliuliza Edna huku akiwa kama vile haelewi kinachoendelea na kumfanya Roma kumeza mate mengi kujiutiliza..
“Nakuuliza umejuaje alijibu hivyo?”
“Mwenyewe sijui chochote , umeuliza swali na mimi jibu likanijia kwenye akili yangu bila kujielewa , kwani nimejibu kama alivyojibu yeye?”aliuliza Edna mwenyewe akiwa kama amechanganyikiwa.
Upande wa Roma alijiambia huenda alikuwa akiwaza sana ndio maana, kwani mwonekano wa Edna ulikuwani ule wa kutolewa kitu, alijiambia huenda kwasababu Edna na Seventeen walikuwa mapacha kuna uwezekano wa wao kuwa na mawazo yanayofanana.
Ijapokuwa alijihisi kuna kitu hakipo sawa kuhusu Edna na namna alivyomjibu lakini hakutaka kuuliza zaidi
“Naona unafurahia mwenyewe kumsimulia binti yako jinsi ulivyoweza kukutana na Ex wako?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma kujisikia vibaya kidogo pamoja na aibu.
“Babe wife sikudhamilia hivyo , nitakuwa mwangalifu siku nyingine”Aliongea Roma.
*******
Hoteli ya Sherati ndani ya jiji la Kigali ilikuwa nje kidogo na jiji hilo , ni rahisi kusema ni hoteli ambayo imejengwa katika eneo ambalo limejitenga na mji ili kupata eneo kubwa na mandhari ya msitu.
Hoteli hio hupendelewa sana na viongozi wa kisiasa na baadhi ya mtajiri kufanyia sherehe hapo na mikutano , hio yote ni kutokaa na kwamba ilidizainiwa kwa mtindo wa kiusalama sana na ilikuwa na kumbi kubwa za kukirimu sherehe kubwa za watu mbalimbali mashuhuri.
Raisi Jeremy hakuwa mtu wa kupenda sana kutoka ikulu na kwenda kuhudhuria sherehe za kimwaliko mbali na ikulu yake kwani kulikuwa na umbali mrefu ukijumlisha na msururu wa magari yake basi huleta shida ya kiusafiri katikati ya jiji na kusababisha msongamanio wa takribani dakika ishirini.
Lakini hata hivyo kutokana na mtu aliemwalika katika hafla fupi alikuwa ni balozi wa Ujerumani na rafiki yake sana hakuwa na namna ya kukataa kuelekea huko ndio maana taarifa zake za kufika kuhudhuria zilikuwa zikijulikana ndani ya hoteli hio na protokali za kiulinzi zilikuwa zishaanza kuchukuliwa kabla hata ya muda wa kuanza safari ya kutoka Ikulu.
Kama raisi chakula chake kilikuwa kikiandaliwa tofauti sana na kwa umakini mkubwa na ndio maana hata wapishi maalumu wa raisi walikuwa washaagizwa ndani ya hoteli hio kuandaa pamoja na kuonja , ijapokuwa chakula kilikuwa kilekile ambacho kinaandaliwa katika hafla hio lakini cha kwake kidogo kilikuwa na utofauti kimaandalizi .
Kwa kiongozi mkubwa wa nchi ilimaanisha kutokuwa huru na baadhi ya vitu ndio maana alikula kila kilichoandaliwa kwa utaratibu maalumu.
Saa mbili kamili za usiku alikuwa tayari ashafika katika hafla hio na hata hatua za mwanzo za hafla hio zilikuwa zimekwisha kufanyika na sasa watu mbalimbali waliohudhuria walikuwa wakipata chakula cha usiku.
“Mheshimiwa karibu sana kufurahia chakula chako”Aliongea mhudumu mara baada ya chakula chake kuhakikishwa.
Raisi Jeremy alikuwa amekaa kwenye meza ambayo ilikuwa Imezungukwa na watu wachache huku ikiwa na vyakula mbalimbali.
Wakati kama huo alijikuta akikumbuka maisha yake ya nyuma , wakati kama huo angetakiwa kuwepo hapo na mke wake huenda hata mtoto wake na hakuna mtu ambaye angeweza kumwangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida.
Tokea familia yake kuanza kusambaratika kulikuwa na maneno mengi ya chini chini ya yaliokuwa yakiongelewa kuhusu yeye , ijapokuwa hakupenda lakini ilikuwa ni ngumu kuwazuia watu kuongea kile wanachojisikia.
Hata hivyo ni yeye ambaye alikuwa amemuua mke wake mwenyewe na katika hali hio imemfanya hata mtoto wake wa kiume ambaye alikuwa akitarajia kuwa mrithi wake kumchukia na kutengeneza uadui.
Mawazo kuhusu familia yake na maisha yake yalivyokuwa miaka kadhaa nyuma yalipita katika akili yake kwa muda mfupi sana na kupotezea.
Wakati mheshimiwa Jeremy akiwa katika hafla hio akila na kuongea na baadhi ya watu waliokuwa kwenye meza yeke , upande wa walinzi wake kutoka miliki ya kijini hawakucheza mbali , walikuwa mita kadhaa kutoka alipokuwepo na walikuwa wakihakikisha hakuna kitu chochote kibaya ambacho kinaweza kumpata raisi huyo na kupelekea mipango yao hapa duniani kuvurugika ndio maana walikuwa tayari kumpa ulinzi kwa namna yoyote ile.
Raisi Jeremy alikuwa akijua sana kuhusu maswala ya kuvuna nishati za mbingu na faida zake katika kurefursha maisha , na kwa nafasi yake hio ya uongozi huenda angependa kuishi miaka mingi zaidi kuongoza lakini kwa sababu ambayo hakuwa akiilewa hakupenda kabisa kujifunza na hata kuulizia kuhusu namna nishati hizo zinavyovunwa.
Mheshimiwa Jeremy aliweza kudumu katika hoteli hio kwa masaa zaidi ya matatu na kisha muda wake hapo ulifikia tamati na kurejea kwenye gari kurudi katika makazi yake.
Siku hio ilikuwa ni ijumaa na inaingia Wikiend na kama kawaida kila inapofika Wikiend hakupenda kukaa katika ikulu kubwa na alipendalea kuishi katika nyumba yake ya mapumziko, hivyo safari ya kutoka hoteli hio ni moja kwa moja mpaka State Area D .
Safari nzima haikuwa na tishio lolote la usalama na aliweza kufika vizuri ndani ya jumba hilo maarufu ndani ya jiji la Kigali na ulinzi ulikuwa tayari ushaimarishwa muda mrefu.
Mara baada ya kurudi katika hilo mapumziko la raisi hakutaka kufanya kitu kingine zaidi ya kujipumzisha kwani muda ulikuwa umeenda sana.
Sasa akiwa chumbanni kwake akijiandaa kulala aliweza kugongewa mlago na kumfanya kidogo kukunja sura kwani haikuwa kawaida kwa wakati kama huo kusumbuliwana wafanyakazi wak.
‘Nani!!?”
Aliuliza kwa nguvu lakini ajabu ni kwamba hakuna sauti ambayo ilisikika kutoka nje kwa zaidi ya dakika kama mbili hivi na kuzidi kumshangaza lakini mara baada ya kukatashauri kwenda kufunguaajue nani anagonga mlango ulifunguliwa kwa nguvu.
Alijikuta akishangaa mara baada ya kuona mtu aliekuwa akiingia ndani alikuwa ni Mtoto wake wa kiume Desmond akiwa ametangulizana na mwanamke mrembo.
Alijikuta akihisi kuna kitu kinachoendelea kwani hata walinzi hawakumzuia kuingia na mbaya zaidi mwanamke huyo hakuwa akimjua na ilikuwa sio kawaida kwa Demsond kuingia chumbani kwake na mwanamke kama hivyo.
“Desmond unafanya nini ?”Aliuliza Raisi Jeremy kwa hofu huku akimwangalia yule mwanamke , alihisi mwanamke huyo alikuwa akimjua licha ya kwamba hakukumbuka ni wapi alimuona.
“Desmond huyo ni nani na walinzi wako wapi?”Aliuliza .
“Kuwa na amani , wamekufa vifo vya amani sana”Aliongea yule mwanamke kwa kujiamini.
“Wewe ni nani ?”Aliuliza Jeremy na dakika chache tu kuna kitu kilimjia , alikumbuka maelezo ya Linda wakati uchunguzi wa kumtafuta Joseph Bikindi ukifanyika katia chuo cha Rwanda baada ya kupotea kwake.
“Hubby tulioana kwa miaka mingi sana , usiniambie hunikumbuki mke wako”Aliongea Kizwe na kumfanya Raisi Jeremy kupatwa na mshutko huku macho yakimtoka.
“Ni… ni wewe!!”
“Hahaha… ushanifahamu sasa , Jeremy najua ulikuwa ukinitafuta sana lakini umeshindwa kudhania kama siku nitajileta mwenyewe”Aliongea Kizwe kwa dharau.
“Mama hebu acha maneno mengi , si unaona anataka kujikojolea”Aloiongea Desmond.
“Mwanaharamu wewe , unapata wapi uthubutu wa kupanga njama na huyo malaya”Aliongea Jeremy huku sasa akielewa kile kitendawaili cha kupotea kwa Demsond na kuonekana kwa ghafla hatimae kimeteguka na anajua sasa alikuwa akifanya kazi na mwanamke anaejinasibu kuwa mama yake , ijapokuwa mwanzoni hisia zake zilikuwa zikimwambia hivyo lakini bado alikuwa na mashaka.
Alianza kujilaumu na kusema ni kheri kama angezichukulia hatua hisia zake na kuhakikisha ana mdhitbiti.
Ukweli ni kwamba aliamini angekuwa salama bila ya kumdhibiti Desmond kutokana na uwepo wa Nix na Gesha lakini kwa muda huo alishindwa hata kujua nini kimetokea mpaka jumba lake hilo lenye ulinzi imara kuvamiwa kirahisi tena muda mfupi tu mara baada ya kurudi.
“Mmewafanya nini Nix na Gesha , hapana, haiwezekani, nyie wawili hamna uwezo wa kuwashinda”Aliiongea huku akizidi kurudi nyuma kusogelea kabati la nguo.
“Hatuna uwezo wa kushidana nao ndio lakini haimaniishi kwamba hakuna mtu wa kuwashinda , Jeremy wewe ni mtu wa mahesabu sana na nakusifia kwa hilo lakini siku zote utabakia kuwa binadamu tu ambae umezaliwa na madhaifu “
Raisi Jeremy alijikuta akimeza mate mengi huku mwili wake akishindwa kuuzuia kutetemeka kwa kuangalia chuki iliokuwepo katika macho ya mwanamke aliekuwa mbele yake.
Wakati akiwa anaomba Nix na Geisha kutokezea , kulitokea kishindo kizito katika paa na kufanya nyumba yote kutetema na ile anasikia kishindo kingine kutoka eneo la nje ya chumba chake , hatimae aliweza kumuona Nix na Gesha wakidondoka chini wakionekana kuna kitu kimewapiga ..
Muda huo huo wakati eneo hilo likitawaliwa na vumbi la kutosha aliweza kuonekana Denisi aliekuwa ameshikilia kitu cha kung’aa kama kitenesi mkononi.
“Denisi!!!”Alijikuta akiongea kwa mshangao mara baada ya kumuona Denisi.
“Mheshimiwa Raisi , umekosea mimi sio Denisi”Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy akili yake kufanya kazi kwa haraka.
“Kama wewe sio Denisi … Lekcha,, I mean Joseph”Aliongea huku sasa akianza kuelewa kinachomtokea usiku huo na kuweza kufahamu kwanini Denisi alihusika katika taarifa za kuchafua amani ndani ya taifa la Tanzania , kumbe hakuwa Denisi bali ni Joseph Bikindi
“Wewe mtumwa wa fikra , nilikusamehe kipindi kile nikakuacha hai , lakin leo hii umerudi na unataka kunidhuru?”
“Mhehimiwa Raisi unapaswa kunishukuru sijajibadilisha na kuwa wewe, nimekuwa na hruuma sana kwako lakini ndugu zako wapo hapa kwa ajili ya kulipa kisasi”
“Mwanaharamu!!”Aliongea kwa sauti kubwa.
Muda huo huo Nix na Gesha walijitahidi kuamka baada ya kupigwa pigo takatifu lakushitukiza , sasa walianza kuita Dhana zao za kijini kwa ajili ya kupambana.
“Nyiwe watu bado tu mpo hai na hamjakata tamaa?”Aliongea Lekcha huku akiwangalia kwa tabasamu la kejeli.
Nyumba ya Area D ilikuw imejengwa kama hoteli , ilikuwa ni jengo ambalo halipo katika mfumo wa gorofa , ilikuwa imejengwa na madirisha makubwa kama mlango ya vioo ili kuweza kumpa nafasi mtu kuona mandhari yote ya nje.
“Mwanga wa Dhahabu wa kiroho”
Aliongea kwa nguvu Nix na sauti yake ile ilisikika vizuri katika masikio ya Lekcha na palepale alipotea na kilichosikika ni mpasuko wa vioo vya dirisha nyuma ya Raisi Jeremy na kutokea nje kabisa.
Nix na Gesha hawakutaka kuchelewa walifuata huko huko na Lekcha ile anakuja kutua kwenye bustani aishambuliwa na Dhana ambayo ilikuwa ikitoa mng’ao wa mwanga rangi ya Dhahabu , ilikuwa ni kama vile mwanga wa Laser ambao ulitoboa katika kifua chake eneo la moyo ni shambulizi ambalo lilitokea kwa Nix na muda huo huo na Gesha hakutaka kuchelewesha kwani palepale alituma upanga ukatao kuwili wa kimaajabu na kabla hata Lekcha hakufanya chochote kwani shingo yake ilichanwa na panga lile huku eneo la kifuani likutengeneza tundu.
Pigo la Nix na mwenzake lilionekana kufanikiwa na waliamini asingweza kupona kwa namna walivomwadhibu lakini sekunde hio hio walijikuta wakipagawa mara baada ya Denisi kupona kwa haraka sana huku kila damu iliokuwa imetoka ikiwa kama vile imeganda hewani kuanza kumrudia kwa kasi sana.
“Inaonekana kabisa nguvu zenu za kijini hazitoshi nimejifunza sana kuhusu namna mnavyoshambulia , lakini niwaambie tu hakuna kitu cha kawaida ambacho kinaweza kunidhuru”Aliongea Lekca kwa kejeli huku akiokota lile panga na kuliyeyusha palepale na Ant- materr.
Gesha na Nix walijikuta wakipagawa kwa kitendo kile. Kwani hakuna ambaye alitegemea siraha ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa muunganiko wa moto wa rangi nyeupe na nguvu za ziada za kijini imeweza kuyeyushwa kirahisi namna hio..
Baada ya Lekcha kumaliza kuyeyusha ile siraha aliwageuka Kizwe na Desmond waliokuwa wakimwangalia kutoka ndani.
“Fanyeni haraka kama mnataka kufanya maongezi na Raisi Jeremy , nitajibadilisha kuwa yeye nikishamalizana na hawa”Aliongea Lekcha kwa sauti na palepale Lekcha alibadirika na kuwa kama sanamu la chuma cha kung’aa kama bati na kupaa juu angani kuwasogelea Nix pamoja na Gesha ambao walionekana kumsubiria na ile anawakaribia alitengeneza shoti za umeme wa rangi ya kung’aa kama radi na kuwashambulia lakini Nix na Gesha walijaribu kukwepa nyuzi nyuzi zile za shoti zilizokuwa zikiwasogeea na kukimbialjuu zaidi angani.
Nix na Gesha walijua kabisa hawana uwezo wa kushindana na adui yake kwani alionekana kuwa na nguvu zaidi nje ya matarajio yao , kitu pekee ambacho waliona wanaweza kufanya ni kujikinga na mashambulizi yake , kwani hawakuelewa mbinu ya kuweza kumshambulia ilihali hakuonekana kama binadamu.
Mara baada ya ngao waliojitengeneza kugusana na nyuzi zile za shoti walijihisi nguvu zao ni kama vile zinafyonzwa na waliweza kupata ufahamu adui yao anatumia nishati isiokuwa na aada ndio maana wananynywa.
Nix na mwenzake mara baada ya kuona hatari hio palepale waliweza kupaa kwenda juu zaidi angani na kisha akaachia msisimko mkubwa wa nguvu za kijini pasipo kueleweka wanafanya nini.
Lekcha hakujua ni kitu gani wanajaribu kufanya , ila hakujali sana katika kichwa chake alitaka kushinda tu na aliona adui yake hakuwa na mbinu za kumzidi.
Lekcha palepale alianza kutumia kumbukumbu za Yan buwen alizoziunganisha na ubongo wake kwa kutumia Biochip , alichukua zile muhimu tu kwa ajili ya kujua namna ya kupambana na nguvu kubwa ya Ant-matter energy.
Pale pale aliweza kuona kitu ambacho Yan Buwen alikosea wakati akiwa ana pambana , alijiambia hapaswi kuficha jiwe la kimungu ndani ya mwili wake bali anapaswa kulitumia katika mashambulizi na yeye kujibadilisha kuwa nguvu yenyewe.
Upande wa Kizwe hakutaka kupoteza muda kwani alijua kusambaa kwa kiasi kikubwa cha nguvu ya kijini kunaweza kumshitua Roma licha ya umbali mrefu uliokuwepo kati ya Iringa na Rwanda..
“Jeremy utanisamehe sana , nipo hapa kwa ajili ya kukurudishia maumivu ulionisababishia”Aliongea Kizwe na hakutaka kuchelewa kwani palepale alimsogelea Raisi Jeremy kwa spidi huku akidhamiria kumpiga na kigoti eneo la tumboni lakini wakati anamkaribia tu kulitokea mwanga mkali kama wa radi na kumzingira Raisi Jeremy na palepale Kizwe alipigwa na wimbi la upepo usiokuwa kawaida na kwenda kutua kwenye ukuta, akiwa haamini kilichomtokea na huenda angekuwa binadamu wa kawaida ingekuwa ndio mwisho wake .
SEHEM YA 594.
Kizwe alijikuta akiwa kwenye mshangao bila ya kuelewa nini kimekukumba kwa ghafla namna ile na hakuwa yeye tu hata kwa Desmond mwenyewe hakutegemea hilo kutokea.
“Nini kimetokea..?”Alijikuta akiuliza huku akimwangalia Jeremy na hata Lekcha ambaye alikuwa kwa nje aliweza kushuhudia kitu hicho na alishindwa kuelewa nini kinaendelea.
“Mnaonaje , nadhani hamjafikiria kuhusu hiki kutokea , Kizwe wewe ni mjinga sana unajiona unanifahamu sana kwasababu n tulishawahi kulala kitanda kimoja si ndio? , Mimi Jeremy sio wa kawaida kama unavyofikiria na kuona kwamba unaweza kuniua kiwepesi, nimezaliwa kwa mchanganiko wa jamii mbili tofauti”Aliongea kwa jeuri huku akiwa ndani ya duara la mwanga mweupe unaomzingira kama ngao na palepale alitoa cheni yenye kidani kikubwa sana cha duara na kumfanya Demsond ajue nini kinamlinda baba yake..
“Pumbavu kabisa analindwa na dhana ya kijini”Aliongea Demsond kwa mshangao , aliweza kujua kwa haraka kwani ilikuwa ni kama mara ya pili wanakumbwa na kitu cha kushitukiza kama hicho , mara ya kwanza iliweza kutokea kwa Edna wakati walipokuwa wanataka kumshambulia.
Ukweli haikuwa mara ya kwanza kwa Desmond kuona hiko kidani baba yake akiwa amekivaa na katika maisha yake hakujua kina maana gani , lakini kwa kile kilichokuwa kimetokea hapo ndio anaelewa kwamba hakikuwa kitu cha kawaida kabisa ndio maana baba yake hakuwahi kumuona akikivua kabisa tokea aweze kujielewa kama mtoto.
Ni kidani flani cha madini ya Dhahabu ambacho kilikuwa na mchoro wa mnyama ambaye hakuwa akieleweka alikuwa ni mnyama wa aina gani.
“Hii sio dhana tu kama mnavojua, pia hutumika kama king’ora kuwajulisha watu wa ukoo wa mama yangu katika miliki za kijini na kuwaka kwake ni kutokana na kuhisia nipo hatarini hivyo lazima kitakuwa kimetoa taarifa tayari kwamba nipo kwenye hatari na muda wowote wanajeshi wa miliki ya kijini ya Panas watafika , je bado mnataka kuendelea kubakia”
Nix na mwenzake walimwangalia Jeremy na walijikuwa wenyewe wakishangazwa na jambo hilo kwani hawakuwahi kusikia , hawakujua kama Jeremy alikuwa na Dhana kwenye mwili wake ameivaa na sasa baada ya kuiona kwa macho yao ya kijini waliweza kuifahamu.
“Jeremy hio ni Golden Toad Amulet?Hahaha.,, kazi nzuri sana Jeremy, hio dhana katika jamii yetu inatumika kama kifaa cha kumlinda mkuu wa ukoo na inatumika kwa dakika therathini tu kila baada ya miezi mitatu, kwa umbali uliopo kati ya Panas na hapa nina uhakika wenzetu wenye uwezo zaidi watafika ndani ya dakika kumi na tano, ni kheri kama mtaondoka kama hamtaki kuuliwa”Aliongea Nix
Desmond na mama yake walijaribu tena kumsogelea Jeremy kwa ajili ya kumshambulia , lakini waliambulia patupu kwani kuna nguvu kubwa ambayo ilikuwa ikiwasukuma kuwarudisha nyuma kabla hata ya kuufikia ule mwanga unaomzunguka Jeremy.
Ilikiuwa ni kama kilichowatokea kule Tanzania wakati wakimshambulia Edna na walijikua wakiwa katika hali ya kutoamini kitu kama hicho kingetokea pia kwa Raisi Jeremy , wote kwa pamoa waling’ata meno yao kwa hasira sana kwa kuona mpango wao unakwenda kufeli.
Upande wa Lekcha mwenywewe alijikuta akipandwa na jazba sana kwani hawakuwa wametegemea kama Jeremy anaweza kuwa na siri nziro ambayo ameificha kwa muda mrefu , kauli yake ya kusema watu wa ukoo wa mama yake ilimchanganya sana.
Ukweli hata wao wenyewe walikuwa kwenye maswali mengi kwani hawakuwa wakijua ni kwanini Wale majini kutoka Panasi walikuwa wakimlinda Jeremy.
Kizwe licha ya kumfahamu Jeremy hakuwahi kujua kuhusu siri zake zinazohusiana na wazazi wake na mara zote alisema walikufa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe na yeye kukimbilia nje, hakuwahi hata kuwaza kama Jeremy angekuwa na uhusinao na jamii za kijini.
Lakini hata hivyo mpango wao walipaswa kuumaliza siku hio hio kwani hawana muda mwingine wa kufanya baadae.
Mango wao wa kwanza ulikuwa ni kumuondoa Roma katika kurithi ukoo nchini Tanzania , lakini ukashindwa kufanikiwa , kama watashindwa kumpata na Jeremy inabidi waanze kufikira namna nyingine ya kuandaa mipango yao upya jambo ambalo lingewachukua muda kufanikisha lakini kwa wakati mmoja kuwapa nafasi wapinzani wao kujiimarisha zaidi na pia Roma kuanza kuwatafuta.
“Nitatumia njia nyingine nyepesi , nitajibadilisha kuwa wewe kwanza na baada ya hapo nitaharibu hio dhana kwenye shingo yako”Aliongea Lekcha na kuanza kuwashambulia haraka haraka Nix na Geisha bila kuwabembeleza ten.
Upande wa Gesha na Nix waliweza kuzidiwa nguvu zao na kuwa dhaifu na dani ya dakika kama mbili tu ilikuwa ni kama wamerudi levo ya nusu mzunguko na ndio muda ambao Lekcha hakutaka kupoteza muda kabisa.
Ghafla tu Nix na Gesha walijikuwa wakifunikwa na mwanga mkali kama wa shoti ambao ulisababisha uwepo wao kutoweza kuonekana tena wala kutorok.
Upande wa Iringa ilikuwa ni wakati ambao Roma alikuwa akimuweka Lanlan vizuri ili na yeye kulala , lakini alijikuta palepale akikaa kitako ghafla.
Edna alionekana kushangazwa na kitendo kile kwani Roma alionekana kama mtu ambaye amekumbwa na hofu,
“Nini tatizo , au bado ni mapema kwa wewe kulala?”
“Hapana nahisi uwiano usio sahihi wa nguvu za mbingu na Ardhi , nahisi kuna majini yanapambana”Aliongea na kumfanya Edna kumwangalia kwa wasiwasi.
“Kivipi , ningeweza kuhisia pia , je ni mbali na hapa?”
“Inaonekana kuwa ni umbali mrefu sana na hapa ndio maana huwezi kuhisia , nitaenda kuangalia , napata hisia kabisa zinatoka katika mtu levo ya Nafsi”Aliongea naEdna aliishia kutingisha kichwa kwani alijua kabisa asingeweza kumzuia hata hivyo.
Roma kwa haraka sana alivaa nguo zake za kawaida na kuondoka hapo ndani na ile anatoka nje ya mlango tu na kuufunga alikuwa tayari ashapotea na alikuja kusimama juu zaidi angani katika eneo hilo na kufumba macho akitafuta uelekeo wa nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi inatokea wapi maana msisimko wake ulikuwa wa chini sana na kama asingekuwa kwenye levo ya Kuipita dhiki asingeweza kuinasa.
Baada ya kupata uelekeo palepale alipotea na ile anakuja kuibukia kwa mara nyingine alikuwa kwenye mpaka wa Rwanda na Tanzania na aliweza kuhisi nishati ya Ant – matter.
Palepale hakutaka kujiuliza mara mbilimbili kwani shauku yake ilizidi kuongezeka na dakika chache tu alikuwa karibu kabisa na sasa macho yake ya kijini yaliweza kuona alichokuwa akitarajia.
Aliweza kuona mtu nje ya jengo ambaye alikuwa amezungukwa na mwanga wa rangi nyeupe ya kung’aa huku pembeni yake likionekana jengo ambalo limeharibika paa lake.
Baada ya kuchunguza kwa umakini aliweza kungudua aliekuwa amezungukwa na mng’ao huo ni Raisi Jeremy akionekana kuwa katika hali ya hofu.
“Ant – matter energy!!!!, kwanini inatokea hapa?”Aliongea Roma kwa mshangao .,
Ndio alipaswa kushangaa kutokana na mtu ambaye alikuwa akimiliki nguvu hio alikuwa ni Yan Buwen pekee ambaye aliamini kabisa amekwisha kumuua.
Roma alijikuta sasa akielewa kinachoendelea mara baada ya kuweza kumuona Desmond na Kizwe ambao walikuwa wamesimama pembeni.
Roma alijiambia licha ya kwamba hakuwa na ukaribu mkubwa na Jeremy asingemuona akifa mbele yake kwani ni baba mzazi wa mke wake.
Roma palepale aliita kitenesi cha moto mweupe na kisha alikirusha upande ambao kulikuwa na mkusanyiko wa mwanga uliokuwa ukitoa shoti ya nguvu ya Ant Matter.
Dakika ileile ambayo kitenesi kile cha moto mweupe kilipotoka katika mkono wake kilibadilika na kuwa kama mshale mrefu ulioonekana katika mstari mnyoofu.
Lakini sasa shambulio lake ile linafikia ile sehemu ambayo kulikuwa na mkusanyiko wa nguvu ya Ant Matter halikuweza kushambulia kwani mkusanyiko ule ulisogea pembeni kwa spidi.
Kitendo kile cha shambulio lile kuonekana kupishwa ule mwanga ulianza kupungua na palepale alionekana Denisi ambaye alikuwa akija upande wake.
Raisi Jeremy alijikuta akipatwa na ahueni mara baada ya kuona kumuona Roma kwani alidhania siku zake ndio zimefika mwisho hivyo na alishukuru pia kwa kuwa na Dhana ambayo alipewa na mama yake inayomlinda siku hio.
“Nilijua tu wewe sio Denisi , ijapokuwa sijui ni mbinu gani umeitumia kuficha uwezo wako na kwa namna ipi umeweza kumiliki nguvu ya Ant-mater , najua kabisa Denisi hana akili ya kupanga mipango yote”Aliongea Roma mara baada ya kumuona mtu mwenye sura ya Denisi mbele yake,
“Hahah .,.. mipango yangu imefeli kutokana Jeremy kutokana na Dhana kumiliki Dhana ya ajabu , ila sio mbaya nitaacha maigizo kwasababu ushaniona”Aliongea Lekcha huku akionyesha kufurahishwa na Roma kujitokeza.
“Ulitakiwa kujua hilo kabla ya kupanga mipango yako , unadhani unaweza kushinda kirahisi kama kuna wenzako ambao waliweza kushindwa mwanzo”
“Nidio unavyowaza .. kitu pekee ambacho naweza kujilaumu nacho ni bahati kutokuwa upande wangu kwa kukosa uwezo mkubwa kama wa kwako la sivyo kama mpango wanguungefanikiwa , ningeweza kutawala taifa lote la Tanzania”
“Je nichukulie maneno yako kama sifa”
“Hapana , ninachomaanisha ni kwamba una bahati sana mpango wangu kufeli”
“Kama ni hivyo je unaweza kuniambia wewe ni nani?”
“Hahaha.. mimi nni nani tena ,, ushaniona tayari , mimi ni Denisi”Aliongea Lekcha kwa kucheka
“Roma usimsikilze huyo , sio Denisi ni Joseph Bikindi maarufu kama Lekcha , ndio yeye pekee ambaye anweza kushirikiana na Kizwe, najua namna anavyoongea , ndio yeye”Aliongea Raisi Jeremy ambaye aliikuwa akisikia maongezi yao
Roma alijikuwa akishangaa mno , hakutegemea Denisi ni Lekcha , mwanaume ambaye alimsaidia Kizwe nchini Tanzania na alijikuta akikumbuka taarifa ya uchunguzi wa The Eagles na kujikuta akiona sasa mambo yamefikia pale anapopataka.