Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

We msambaa acha maringo basi.uliahd mwenyewe saa mbili.ishapita wiki vp mgos inatukosea chawa wako arif
Shida yenu mnapenda sana vya dezo, tuliolipia tuliungwa ktk group tumesoma kidogo muendelezo kisha jamaa akatutelekeza kwa group tukawa TUMEPIGWA 😂😂

Ni vyema na wewe umcheki huko whatsapp upigwe ndio uendelee kulalama.

Hakuna vya bure bwashee 😂 😂
 
Shida yenu mnapenda sana vya dezo, tuliolipia tuliungwa ktk group tumesoma kidogo muendelezo kisha jamaa akatutelekeza kwa group tukawa TUMEPIGWA [emoji23][emoji23]

Ni vyema na wewe umcheki huko whatsapp upigwe ndio uendelee kulalama.

Hakuna vya bure bwashee [emoji23] [emoji23]
Naona unapunguza hasira uku bwashee[emoji16][emoji3].mgos anabet sana.
 
SEHEMU YA 587.

Ni muda mchache sana ambao Raisi Senga alikaa ndani ya nyumba hio na kuondoka , huku akiaga kabisa anarejea ikulu ya Dar es salaam.

Upande wa Roma alijikuta akiwaza sana juu ya picha ambazo alikua ameonyeshwa , aliona kitendo kilichofanyika kilikuwa cha kimakusudi kabisa ili kufanya kila mtu amlaumu .

“Mzee nadhani haujanishuku kama mimi ndio nimeenda mpaka Zanzibar kufanya haya si ndio?”

“Ijapokuwa mimi bado ni mzee lakini haimaanishi mimi ni mjinga , lakini licha ya hivyo kukuamini kwangu tu hakutoshi , tukio hili limefanyika usiku ili isitokee namna ya wewe kujitetea kwani muda huo kila mtu alikuwa amelala , hivyo huna ‘Alibi’”Aliongea

“Babu mimi nina uhakika kaka hahusiki katika hili na kwa ninavyoona ni kitu cha kupangwa kabisa hiki”Aliongea Denisi ambae aliweza kutoka mara baada ya baba yake kuondoka.

Roma alijaribu kumwangalia Denisi ili kumuona maneno yake yanaendana na hisia zake , lakini ukweli alimuona Denisi akiwa na uso uliotoulia kabisa na hakuwa na wasiwasi kabisa kwa kile ambacho kinaendelea.

Wakati wakiendelea kujadiliana kiongozi wa walinzi wanaolinda nyumba hio alikuja haraka haraka alipo Afande Kweka huku akionyesha hali ya kuwa na taarifa muhimu.

“Jemadari kuna tatizo”Aliongea yule Afande na kumfanya Afande Kweka kumwangalia kwa macho yasiokuwa na utulivu bila kuongea chochote.

“Nini kinaendelea?”Aliuliza Roma.

“Asubuhi mara baada ya kufanya Patrol tumeweza kugundua nje ya fensi meter hamsini kuna wanajeshi wengi ambao wamezingira wakiwa na siraha za moto , kwa muonekano wa mavazi yao nina uhakika ni kutoka kambi ya jeshi ya mkoa”

“Babu si mkoa huu Brigedia ni Afande Makwera ambaye nilisikia ni mwanafunzi wako?”Aliuliza Denisi

“Hata kama ni mwanafuzni wangu ana mawazo yake mwenyewe , unafikiri atafanya kila kitu ninachomuambia kwasababu mimi ni mwalimu wake?”

“Kwahio mnamaanisha huyu Kamanda Makwera ndio mkuu idara ya kijeshi upande wa hapa Iringa na ndio kawaleta hao wanajeshi?”Aliuliza Roma.

“Upo sahihi , inaonekana kuna baadhi ya watu wamekosa uvumlivu , kuna msemo unao sema linalopangwa kutokea lazima litimie , nadhani ndio kinachokwenda kutokea sasa hivi”Aliongea Afande Kweka.

“Babu inamaana Afande Makwera ameshindwa kuelewa hali ilivyo na sasa hivi anatumika kisiasa , labda unipe nafasi nikajaribu kufanya uchunguzi zaidi huenda hahusiki”Aliongea Denisi.

“Wewe si unafanya kazi jeshini upande wa hapa Iringa , inamaana hakuna kitu umeweza kugndua?”

“Hapana , tokea nianze kazi hapa sijawahi kumuona afande Makwera kwa siku kadhaa , sina uhakika ni nani ambaye alikuwa na mawasiliano nae au kukutana nae”Aliongea Dennisi na palepale Afande Kweka aliomba simu yake na kisha akampigia Raisi Senga na kumuuliza kama anaelewa kinachoendelea na alipewa jibu kwamba ndio amepata taarifa.

“Mpigie simu Makwera na unirudishie jibu , nataka kujua nini kipo kwenye akili yake”Aliongea

“Nafanya hivyo baba”

Upande mwingine katika ikulu ndogo mara baada ya Raisi Senga kupewa taarifa hio aliishia kutoa tabasamu akiwa na Kabwe ofisini na hata simu ya baba yake alivyoona inaita ni kama aliitegemea na aliipokea na baada ya kupewa maagizo alikata na muda huo huo simu yake ilianza kuita tena na alipoangalia jina ni la Afande Tozo.

“Ndio Afande”

“Mheshimiwa Salut, nimekwisha kupata taarifa tayari ya Afande Makwera kuzingira nyumba ya Jemadari”

“Inaonekana wasaliti wa nchi wamekosa uvumilivu na kuchukua hatua , Afande hili linaenda vizuri kwa upande wetu”

“Napaswa kuchukua maamuzi gani mheshimiwa , wasiwasi wangu nitaonekana kama mkuu wa majeshi ambaye sina uwezo wa kuwaongoza vyema waliochini yangu”

“Afande naelewa wasiwasi wako , lakini tunachojaribu kufanya kwa sasa ni kuirudisha nchi katika uimara wake , hili ni swala ambalo tumetarajia na kama hatutachukua nafasi hii nchi yetu itaendelea ikiwa na msingi mbovu wa kiusalama”Aliongea na kisha kilitokea kimya kifupi upande wa pili.

“Afande ndio najiandaa kurudi Dar es salaam kwa ajili ya kukutana na wazee upande wa Zanzibar na kama kila kitu kitaenda sawa nitafanya ziara ya kwenda Zanzibar naomba tuambatane wote kwenda huko”

“Sawa mheshimiwa nadhani kwasasa nihakikishe hiki kinachoendelea kinabakia kuwa siri ili taharuki zisiibuke kwa wananchi”

“Upo sahihi kwasasa hatua zote za kiusalama zimechukuliwa lakini tunapaswa kuwa makini zaidi , nitakuachia ufanyie kazi upande huo”Aliongea Raisi Kigombola na kisha akakata simu na kuvuta pumzi.

“Kuna mstari ambao sipaswi kuuvuka unaotenganisha kati ya jeshi na siasa lakini ili kuirudisha nguvu yangu ya kimadaraka ikulu hili lazima lifanyike”Aliongea na Kabwe aliitikia kwa kutingisha kichwa kumuelewa.

Baada ya kukata simu alijaribu kuipiga namba ya Afande Makwera lakini ilionekana kutopatikana hewani na aliishia kuvuta pumzi na kisha akampigia baba yake simu na kumpa taarifa.

Afande Kweka mara baada ya kupewa taarifa hio alitoa maagizo kwamba hakuna la lazima ambalo linapaswa kufanywa kwa muda huo ila watasubiri kuangalia matokeo , lakini wakati huo huo alichukua walinzi wake wawili na kuwaambia wamfuae kuelekea nje ili kwenda kukutana na Afande Makwera.

Ilikuwa ni ngumu kwa wananchi wa kawaida kujua kile kinachoendelea kutokana na mazingira ya eneo ambalo makazi ya Afande Kweka yalipo , ni upande wa nje kabisa wa mji ambao asimia kubwa eneo lote lilikuwa limezingirwa na misitu na kulikuwa na barabara moja tu ya mchepuo iliokuwa ikitumika kuingilia mjini.

Lakini barabara hio kwa siku hio ilikuwa imefungwa tokea saa kumi usiku na magari ambayo yalipenda kupitia njia hio ya mkato yalilazimika kupita barabara kuu.

Baadhi ya raia ambao waliokuwa karibu pia waliondolewa na wanajeshi hao ili kwamba hata ikitokea majibizano ya risasi basi hakuna ambaye angejali kujeruhi raia wasiokuwa na hatia.

Asilimia kubwa ya walinzi wa Afande Kweka ni wale wanajeshi wastaafu na walikuwa wengi ambao walikuwa wakimpa ulinzi , huenda ulinzi wa eneo la Iringa na kule Dar es salaam eneo hilo ndio ambalo lilikuwa na ulinzi mkubwa.

Sasa nje kabisa ya eneo hilo la Afande Kweka , walionekana wanajeshi kibao waliokuwa katika gwanda za kijeshi huku wakiwa na siraha za moto , walikuwa ni kama vile wanapigana na adui mwenye wanajeshi zaidi ya mia.

Wanajeshi wote wlaiokuwa wamengizwa hapo wakiongozwa na Kapteni Mloso na walikuwa ni wale wa kikosi maalumu.

Ilikuwa kabla hata ya Afande Kweka hajatoka kwenda mbali kukutana na kiongozi wa wanajeshi hao akiwa anafuatiwa na Roma kwa nyuma hatimae waliingia wanajeshi kutoka pande zote na kukutana katikati na kuzingira nyumba hio kwa mita kadhaa kutoka mpango wa kuingiilia na getini na kumfanya Roma kushangazwa na jambo hilo.

“Mambo kweli hayatabiriki , nani ambaye angejua ninakwenda kupitia matatizo ya namna hii , nadhani ninaanza kuzeeka sasa , naamini kabisa huu ni mpango ambao umeandaliwa na mtu ambaye anaifahamu familia yetu vizuri nje ndani, hatukuweza hata kupata taarifa na tunajishutia tu tumezingirwa pande zote”Aliongea Afande Kweka huku akikunja sura na kumfanya Roma kutumia uwezo wake na kujaribu kuangalia kama kuna wanajeshi zaidi ya hao waliokuwa mbele yao.

“Ninaogopa kusema hawa sio wote , kuna wengine zaidi, kuna wandunguaji angalau therathini waliojipanga katika ‘angle’ tofauti , kwasasa ninaweza kusema hakuna mtu ambaye yupo salama aliepo nje ya nyumba”Alongea Roma na Damasi ambaye alikwisha kutoka nje alijikuta akivuta pumzi nyingi na kuzishusha huku akiwa na wasiwasi mkubwa na kutamani angeondoka na mume wake alipompa taarifa anarudi Dar es salaam , lakini kutokana na uwepo wa Denisi na Roma kuishi sehemu moja alihofia kuwaacha pamoja.

“Wewe mtoto mtukutu , umenihakikishia mwenyewe kwa kusema kwamba licha ya chochote kitakachotokea familia yetu haitapatwa najambo lolote baya , vipi kwa hali hii bado unasema tupo salama?”Aliuliza Afande Kweka swali lake likimlenga Roma.

“Nadhani …. Lakini siku zote kuna njia kwa kila tatizo”

Upande wa Denisi alikuwa pembeni na uso wake wa wasiwasi wa maigizo.

Wakati hawajui cha kufanya wakiagaliana na wale wanajeshi , hatimae ulisikika mngurumo wa Helicopter iliokuwa ikikaribia maeneo hayo , ilikuwa ni Helicopter ya kijeshi aina ya American Black Hawk na dakika moja nyingine ziliongezeka mbili ambazo zilikuwa na wanajeshi na ndani ya dakika chache tu wale wanajeshi walitengeneza duara kuruhusu zitue katikati yao.



Baada ya kutua walitoka wanajeshi wanne wote wakiwa na gwanda zilizochafuka vyeo , mmoja wao tu mwenye iuso mweusi sana na ndio ambaye alikuwa ana vyeo vingi akionyesha ndio mkuu huku wale wengine mmoja alikuwa ni Kanali , mwingine Luteni Kanali na wengine wote walikuwa ni Meja.

Kamanda Makwera ndio ambaye alikuwa na cheo kikubwa, kwenye Kombati yake ya kijeshi alikuwa na nyota tatu za dhahabu pamoja na ngao ikimwakilisha yeye ni Brigedia Jenerali.

Baada ya kushuka kwenye Chopa akiwa amezingirwa na wanajeshi wake aliinua uso wake na kumwangalia Afande Kweka na kisha alitoa ishara ya wanajeshi kumpisha njia

“Kamanda, Roma Ramoni hakika ni mkatili kwanini usi..”Mmoja wa wanajeshi aliefika nae alitoa wazo lakini alikatishwa katikati.

“Licha ya ukatili wa Roma, mwalimu wangu ni mtu mpenda haki , hawezi kunidhuru”Aliongea kwa sauti nzito na wale wengine wote walikaa kimya na Afande Makwera alisogea mpaka karibu kabisa na aliposimama Afande Kweka na kisha akaonyesha heshima ya kijeshi kwa Senior wake.

“Mwalimu , mwanafunzi wako nimelazimika kuwa morofi awamu hii kutokana na hali iliyo , natumaini unajua sababu ilionileta hapa na wanajeshi wangu”Aliongea na kumfanya Afande Kweka kutojibu kwanza, ni kama kuna kitu anakiwaza , ukweli alichokuwa akikiwza ni kipindi ambacho anampokea Afande Makwera katika ‘Unit’ yake kama mwanafunzi.

“Nakumbuka nishawahi kukuambia kwamba siraha zetu hazipaswi kunyooshea watu wa ndani bali maadui , nani angejua ungezielekezea kwenye mlango wangu sasa hivi”

“Tutawezaje kulinda maadui zetu kama sisi wenyewe hatuwezi kumaliza matatizo yetu ya ndani, Mr Roma mjukuu wako ana historia mbaya na sio kwa hapa nchini tu mpaka alipotoka lakini baada ya kuingia kwenye taifa letu la amani akaanza kumwaga Damu anavyojisikia yeye, wanajeshi wote kwasasa wapo katika hali ya kupaniki na lazima tumuondoe ili haki itendeke”Aliongea

“Kuniondoa .. hahaha ..”Roma alijikuta akishindwa kuzuia kicheko chake na akaanza kuangalia wanajeshi ambao walikuwa wakimwangalia kwa macho ya hasira.

“Unadhani hawa wote uliokuja nao wanaweza kuniua?”

“Hatujaja hapa kwa ajili ya vita , hivyo unapaswa kukubali kuondoka na sisi na tutakukabidhi kwenye idara zinazohusika na sheria ili kuweza kuhukumiwa kwa makosa yako , hatuwezi kuondoka hapa bila wewe na hili kuisha , huwezi kuchukulia utani jeshi letu tukufu la nchi hii”

Dakika hio hio wakati hali ikizidi kuwa ya moto ziliweza kuingia gari zilizokuwa kwenye spidi ya hatari , wanajeshi hao walitaka kuwazuia wasiingie lakini walionyeshwa vitambulisho na palepale wengine walipiga saluti na kupisha gari kupita.

Ilikuwa ni gari nyesi aina ya Jeep na waliondani yake waliweza kuonekana , mmoja ambaye Roma aliweza kumfahamu haraka haraka alikuwa ni Kanali Tobwe baba yake Magdalena na Mage , kilichomshangaza Afande Makwera ni kwamaba aliweza kushuhudia kombati ya kijeshi ya Afande Tobwe ikiwa imeongezeka cheo kutoka Kanali na kufikia Brigedia Jenerali.

Ieleweka kwamba licha ya Afande Tobwe kuwa na cheo kidogo kuliko Afande Makwera likija swala la mtu wa kwanza kungia jeshini ni Afande Tobwe.

Afande Tobwe yeye aliweza kusota sana jeshini kutokana na kwamba elimu yake ilikuwa ya Diploma tu wakati Afande Makwera yeye aliingia akiwa na Drigii ya ualimu masomo ya Sayansi.

“Tobwe , unafanya nini hapa?”Aliuliza Afande Makwra huku akikunja sura yake.

“Afande , unapewa taarifa ya kuondoka mara moja ndani ya eneo hili kabla haujachelewa”Aliongea Afande Tobwe huku macho yake akiyageuzia kwa Roma.

“Upo kwenye idara maalumu ya maswala ya wanajeshi wanaotumia nguvu za ziada hivyo huna haki ya kuingilia idara yangu ndani ya mkoa niliopewa jukumu la kuulinda , hivyo huna uwezo wa kunipa oda nikaitii”

“Sio kwamba nakupa Oda Afande , ninachofanya sasa hivi mpaka kutoka Dar es salam kuja hapa ni ili kuzuia umwagikaji wa damu ndani ya jeshi letu”Aliongea na kumfanya Afande Makwera kukunja sura.

“Kwahio unasema kwamba hatuwezi kumkamata Roma na kumuweka chini ya ulinzi?”

“Naomba uniwie radhi uongeaji wangu lakini mpaka sasa idara yetu ipo kwenye uchunguzi wa kina juu ya mlolongo wa matukio yanayoendelea , hivyo uchunguzi unaendelea na matokeo yatatoka isitoshe vikosi vyako vya kijeshi bado havina ufanisi mbele ya Mr Roma Ramoni”

“Kama nilivyotarajia , Baba mkwe hakika unanijua vizuri ila Kamanda Makwera yeye ni mjinga , anatumika kisiasa bila hata ya yeyekujielewa”Aliongea Roma kwa sauti akimpa dole gumba baba mkwe wake.

Upande wa Afande Tobwe alikuwa na hasira na Roma lakini hakutaka kuzionyesha waziwazi na njia nzima alikuwa akimlaani mara baada ya kupewa kazi na mkuu wake wa jeshi Afande Maeda kwenda Iringa haraka , alijiambia kila mahali Roma anapopita lazima aache alama ambayo hana wema ndani yake, alikuwa hajamaliza kumlaani kwa kumtoa binti yake na kumpeleka nje ya nchi lakini kaibua mengine.

“Ujinga! , ninaamini ukweli pekee ninao uona , nyie watu ni waoga mbele ya Roma na mkampa ruhusa ya kufanya anachotaka , nilisikia kabisa afande Maeda alimpa ruhusa ya kuua huku yeye akisafisha , hatuwezi kumruhusu mtu kama huyu kuchafua taifa letu lenye amani, hivyo kamanda Tobwe ondoka hapa kwani msimamo wetu hauwezi kuyumbishwa kwasababu tu tumesikia kama ana vinguvu vyake vya kichawi , tutamuonyesha nini maana ya mtu kuitwa mwanajeshi wa ukweli”

“Makwera kwanini unakua mjeuri hivyo na mgumu kuelewa , hebu fikiria kuhusu hili , nani ambaye alikuwa akieneza uzushi? , huu uzushi umeanza kuenezwa na wanasiasa kutoka familia ya Haruni , famili ya Mzee Longoli wana kinyongo na Roma kwasababu tu wanaona yeye ndio alisababisha kifo cha mstaafu Kigombola na Mzee Longoli , hivi unashindwa kufikiria kitu kidogo kama hiki , kwanini unaingiza siasa kwenye jeshi letu?”

“Hayo ni mambo mawili tofauti na usiniambie nini nifanye na kipi nisifanye , kilichotufanya kuchukua maamuzi ya kuja mpaka hapa ni baada ya kifo cha Kamanda alieipenda nchi yake na kuipigania , Kamanda Razaq, isitoshe huyu mtu sio mzuri kwani ameweza hata kumuua binamu yake , bado tu unaendelea kumwamini kwasababu anajihusha na watoto wako kimapenzi”

“Una uhakika gani kama Mr Roma ndio kafanya hayo ilihali uchunguzi haujaisha na unaendelea?”Aliuliza huku akipotezea swali ambalo lilizigusa hisia zake la kuambiwa watoto wake wote wanatoka kimapenzi na Roma.

“Unakosea hakuna haja ya uchunguzi wakati kila kitu kipo wazi”Aliongea na muda uleule ziliingia gari nyeusi mbili na wanajeshi wale hawakuzizuia kabisa kuingia na zilienda kusimama karibu na Afande Makwera na palepale milango ilifunguliwa na wakatokea wanaume waliovalia suti.

Afande Kweka mara baada ya kumuona mmoja wapo alijikuta akikunja sura kwani alikuwa ni ndugu upande wa mume wa mtoto wake wa kike Theresia na wengine wote pia walikuwa ni wana ukoo ambao walionyesha nia zao waziwazi kutotaka Roma akipewa nafasi kama mrithi wa ukoo.

“Nadhani hawakuridhika na maamuzi yangu ya kumpa Roma nafasi yangu katika ukoo wetu”

“Inaonekana kabisa walikuwa wamejificha karibu na hapa”Alimalizia na Roma ni kama vile alikuwa amewaon muda mrefu.

“Senior Afande hawa ni ndugu zako ambao ni kama mashahidi na sio hawa tu wengine wote wameripoti tabia za mjukuu wako na ndio ambao wamenifanya kuchukua haya maamuzi ya kumuondoa hapa nchini”

“Afande Makwera unadanganya wanachofanya hao ni kutokana na kutorishdhwa na maamuzi ya kifamilia”Aliongea Damasi kwa mara ya kwanza akikosa uvumilivu na hofu kwa wakati mmoja na kumfanya Denisi kumwangalia.

“Ndio madam naheshimu mawazo yako , lakini licha ya hawa kuwa sehemu ya familia lakini pia ni raia wa taifa hili ambao sisi kama jeshi tunapaswa kuwalinda”

“Kamanda!, je hakuna njia nyingine ya kutatua hili , inawezekana sana kuna mtu amepanga njama zidi ya kaka yangu”Aliongea Denisi na kumfanya Damasi kumwangalia na kutabasmau huku akitingisha kichwa kukubali swali lake.

“Denisi uwezo wako ulio uonyesha tokea ujiunge na sisi ni wa juu sana na pia nakufahamu , nataka kumsaidia kaka yako lakini tatizo amefanya makosa makubwa sana , siwezi kuangalia pembeni kwa hili”Baada ya kumaliza alimpigia saluti ya mwisho Afande Kweka.

“Afande sina mpango wa kujaribu kuingilia maswala yako ya kifamilia lakini kama utaendelea kumlinda Roma, wanajeshi wangu watamkamata kwa nguvu ndani ya dakika kumi zijazo , Tafadhari naomba ufikirie hili kwa umakini, hayo ndio ambayo yamenileta hapa na sio kuanzisha vita”Baada ya kumaliza kuongea hivyo hakusubiria zaidi kwani alirudi kwa wanajeshi wake lakini alisita na kumgeukia Denisi na kumwangalia kwa dakika kadhaa.

“Una zaidi ya mjukuu mmoja , kumuadhibu ndugu mmoja kwa makosa alioyafanya ili haki kutendeka ni jambo la kishujaa pia”Baada ya kumaliza kauli hio aliendelea na kupiga hatua na kufikia kikosi chake.

“Haya mambo yanazidi kupendeza, kwasasa nipo nimekabwa pande zote nikizungukwa na maadui , interesting”Aliongea Roma huku akikuna kichwa chake huku akicheka kama kilichombele yake ni utani.

“Unapata wapi ujasiri wa kucheka ili hali upo kwenye matatizo?”Aliuliza Afande Tobwe.

“Usiwe na wasiwasi Afande , isitoshe hawa watu wananihitaji mimi , kwasababu ndio mwenye makosa hivyo nitaongea nao na kila kitu kitakuwa sawa ndani ya muda mfupi”Aliongea .

“Roma usifanye vitu kwa papara “aliongea Afande Tobwe huku akimsogelea Roma.

“Baba mkwe , sijasema chochote kwanini una wasiwasi hivyo , isitoshe sidhani kama kuna mtu ambaye anaweza kunizuia hapa hata kama nitaamua kufanya vitu kwa papara.”Aliongea na kumfanya Afande Tobwe kuyameza maneno yake na kumpisha na Roma alizidi kuwasogelea Afande Makwera na watu wake.

Afande Kweka ambaye alikuwa katika hali ya utulivu muda wote aliangalia wanajeshi wake waliokuwa tayari kumrinda kwa kuyatoa maisha yao na kisha akamwaita kiongozi wao.

“Hakikisha hakuna ambaye anafanya chochoe pasipo ya maagizo yangu”

“Ndio Jemadari”Alijibu a kisha akaondoka

Upande wa Denisi alikuwa na wasiwasi ni nini ambacho Roma anapanga kufanya lakini aliamua kutulia.

Roma na Afande Makwera walikaribiaina uso kwa uso bila ya kila mmoja wao kuonyesha hofu ya aina yoyote.

“Ndio umeamua kujisalimisha?”Aliuliza lakini Roma alitingisha kichwa kukataa huku akitoa tabasamu na kumfanya Afande Makwera sura yake kujikunja na kumwangalia kwa macho makali.

“Najua unajjiona una nguvu kubwa na uwezo wa ajabu lakini nikwambie tu hili eneo lote nimeweka wanajeshi wabobezi wa udunguaji kwenye kila mti mrefu , haitojalisha una uwezo gani lakini ukifanya kitu chochote cha kijinga nitatoa maagizo ya wadunguaji kushambulia familia yako , hata kama utatuua lakini hakuna mwanafamilia ambaye ataweza kupona.











SEHEMU YA 588.

Roma alijikuta akitoa tabasamu la kifedhuli , kwenye vitu ambavyo hakuwa akipenda kwenye maisha yake ni kutishiwa usalama wake kwa kutumia watu wake wa karibu..

“Kwahio unanitishia kwa kutumia usalama wa familia yangu?”Aliuliza huku akitoa tabasamu lake la kishetani.

“Maadamu itapunguza majeraha kwa watu wangu na kurahisisha hii misheni , haijalishi kama unaona swala hili kama tishio , unaweza kunichukulia vyovyote kama mhenzi na mtu ambaye napenda vita”Alijibu.

“Nina uhakika kuna watu wangi wanapanga njama zidi yangu , kwasababu ushaamua kutengeneza mpango mkubwa kama huu kwanini usiniambie nani na nani wapo nyuma yako.” Aliongea Roma akiwa bize

“Kama nikikuambia ndio unakwenda kulipiza kisasi , unapanga kuua ndugu zako na raia kwa makosa yako?”

“Hata kama hutaki kuniambia ninachojua ni kwamba Denisi anahusika kwa namna moja ama nyingine”Aliogea Roma na sura yake ilibadilika kidogo na Roma aliongea hivyo makusudi ili kumsoma na licha ya Afande Makwera kujitahidi kurudi katika hali yake ya kawaida lakini Roma hakushindwa kumsoma kwa haraka.

“Sijui unachomaanisha , kwahio unasema kwamba mdogo wako anahusika katika hili , ngoja nikupe ushauri kabisa , usiujaribu moyo wa mwanaume kwa vipimo vya hisia zako”.Aliongea lakini kwa Roma maneno yake yaliingia kulia na kutokea kushoto

“Ukiachana na mzee Kigoda pale , familia ya Aloni , Ndugu wa Mzee Kigombola na familia ya Mzee Longoli na wewe mwenyewe , nina uhakika kuna watu zaidi ambao wapo tayari kuona roho yangu ikuacha mwili”

“Kama ni hivyo inamaanisha kwamba wanaunga mkono mawazo yangu kutokana na makosa yako , hivyo mkono wa sheria lazima ufuate nafasi yake”Aliongea na palepale Roma alipiga hatua moja kurudi nyuma na kisha akaanza kuangalia wanajeshi waliokuwepo hapo kumzunguka huku wakiwa wamemnyooshea siraha kitahadhari.

“Kwenu Maafande Wakubwa kwangu , wakaka na wadada nyie ni wanajeshi ambao mmnafanya kazi kwa bidii”Aliongea kwa nguvu sana na kufanya kila mtu hapo ndani kushangaa ana mpango gani na hata Afande Kweka mwenyewe hakuelewa.

Roma palepale alisogelea baadhi ya wanajeshi na kujaribu kuwapa mkono wa salamu kama kitendo cha kujenga urafiki nao lakini hakuna ambaye alitingishika , walikuwa na ukakamavu na ukomavu wa sura sio kidogo.

“Roma unafanya nini , nimetoa dakika kumi tu na zinakaribia kuisha”Alifoka Afande Makwera akishangawa na kitendo cha Roma.

“Najua kwenu sio rahisi kuwa wanajeshi , kila mtu anafamilia na baadhi yenu bado mpo ‘single’ lakini vilevile kuna ambao mnasubiriwa na wapenzi wenu kwa ajili ya kufunga ndoa , sisi wote ni vijana kutoka sehemu tofauti tofauti hivyo natambua kila maisha ya mmoja hapa ni ya thamani sana na ninaamini wote nyie ni watu wazima ambao kila mtu anao uwezo wa kufanya maamuzi ya kwake mwenyewe , sheria na oda za kijeshi zinaweza kuwa mhimu kufuatwa lakini mnapaswa kuelewa kama mnafanya hayo yote kwa faida ya nchi na sio kufuata maagizo yaliofanywa na mtu mwingine kiubinafsi , nyie wote hapo hamna vinyongo na mimi lakini mmeshikilia siraha kunielekezea mimi kwasababu tu ya huyu Kamanda wenu mwenye kichwa cha Nguruwe , hii ni Tanzania na siraha zenu zinapaswa kulinda mipaka ya nchi hii na sio kuua mwananchi mwenzenu , nawahakikishia mtu akinichokoza lazima nimlipizie na mpaka sasa nimeweza kugundua nani ni adui yangu na nyie wote hamna makosa kwasababu mnatii maagizo hivyo wekeni siraha zenu chini na muondoke , nina wahakikishia baada ya hapa kila mtu atakuwa salama na nyie mtapata heshima ya kumuondoa Kamanda ambaye anatumia madaraka yake vibaya, kama kuna naetaka kubaki abaki lakini nahakikisha kila mtu ataishia kuwa kama wengine wote walioasi jeshi, nitahesabu kuanzia tatu kushuka.’

“Baba anafanya nini? , kama ataamua kushindana nao si hatutokuwa salama?”Aliuliza Damasi aliekuwa katika hali ya wasiwasi.

“Punguza presha, nina uhakika ana mpango wake kichwani”Aliongea Afande Kweka.

Upande wa Denisi aliangalia mazingira yote ya jumba hilo kwa macho yasiokuwa na kielelezo cha jambo fulani na alionekana kuna kitu abacho alikuwa akiwazia.

“Pumbavu zako wewe mtu , unapata wapi uthubutu wa kujaribu kushawishi wanajeshi wangu, unatakiwa kuelwa nikitoa tu maagizo utashambuliwa na kila aina ya siraha niliokuja nayo na nyumba yenu yote itawaka moto na kuharibika kabisa na kila mfugo utakufa hapa ndani”Aliongea lakini upande wa Roma hakuonyesha ishara ya kumjali na pale pale aliinua vidole vyake na kuanza kuhesabu.

“ Tatu”Aliongea kwa nguvu na sauti yake ilikuwa na nguvu kiasi kwamba ilikuwa ikifikika mpaka kwa wale wadunguaji.

“Mbili”

Aliongea tena na kumfanya Afande Makwera kuzidi kumkazia macho huku hasira zikizidi kuongezeka.

Wanajeshi wote waliangaliana na kisha kugeuzia macho yao kwa Roma kwa macho ya tahadhari , lakini upande mwingine wale wanajeshi wa Afande Kweka wote waliogopa kile ambacho kinakwenda kutokea.

Waligopa kwamba Roma anaweza akachukua maamuzi bila ya kujali usalama wao maana wasiwasi wao ulikuwa ni kwa wadunguaji.

“Moja”

Aliongea kwa utulivu kabisa akihesabu kwa mara ya mwisho na kumfanya kamanda Makwera kuwa katika hali ya woga kidogo , lakini aliishia kupoa kwa mara nyingine mara baada ya kuona Roma hachukui maamuzi yoyote na alianza kucheka

“Umemaliza kuhesabu si ndio , nadhani ni muda sasa wa kumaliza huu ujinga , mkamateni”Aliongea akitoa maagizo”

“Ndio Kamanda”

Wanajeshi wake walitii amri na palepale wawili waliojengeka kimwili walisogea mbele kwa kujiamini wakinuia kumkamata Roma kwa kuishikilia mikono yake ili kumtia pingu na kumkalisha chini , lakini kila walipojaribu walishindwa kabisa hata kuusogeza mkono wake.

Wale ndugu wa Roma waliofika na baadhi ya wakilishi kutoka familia ya Mzee Longoli walikimbilia kwenye magari yao , lakini kitendo chao ni kama kilikuwa kikisubiriwa na Roma.

Afande Makwera mara baada ya kuona wanajeshi wake wanasumbukka kumuweka Roma chini palepale alitoa ishara ya wanajeshi kuongezeka ili kutumia nguvu na Roma aliwasubiria wote kwa pamoja na ile wanakaribia kumshika palepalepale walirushwa kwa nguvu kama vile kuna mlipuko wa bomu , licha ya kuvaa ‘bullet Proof’ kwenye vifua vyao na mahelmet z zilichanika chanika na ile wanakwenda kutua chini wote walitema damu na ukawa mwisho wao..

Roma hakujali tena palepale alimsogelea mwanajeshi aliekuwa karibu mara baada ya kuona gari ya wale wana ukoo wake na baadhi ya watu ikitaka kuondoka na aliipiga taili na ikasinyaa, hakuishia hapo kwa spidi kubwa alisogea karibu na kuanza kuwamiminia risasi wote kwa pamoja na ni damu tu ambazo zilikuwa zikiruka na kuchafua vioo na ndani ya dakika chache wote walikufa na baada ya hapo alipiga risasi kwenye boneti la mafuta na kisha akasababisha cheche za moto na ukatokea mlipuko mkubwa wa gari ile.

Afande Makwera alijikuta akishikwa na mshangao kwa kitendo kile , kwani hakuamini kama Roma angeua ndugu zake kikatili vile bila ya kusita sita.

“Wewe kweli ni shetani , unawezaje kuwaua ndugu zako kikatili hivyo ?”

“Haha,,, unamaanisha nini kusema hao ndugu , hawa ni watu ambao wanatamani kuniona nikifa kwanini niwaache hai wakati nishawawahi , wameanzisha vita na katika vita ni kuwahiana na hapa nimerudi kwenye uzamani wangu na sitoacha mtu yoyote hai ambaye ananichokoza”Aliongea kwa mkwara bila ya kujali damu ambazo zishaanza kumchafua.

“Uikichukua hatua ya kushambulia watu wangu nitatoa ishara ya wadunguaji kuachia siraha na kuua familia yako , kama hutaki kumuona mkeo na mtoto wako wakifa mbele yako acha ukichaa wako”Aliongea kwa tahadhari huku akiwa na hali ya woga lakini Roma hakuongea kitu zaidi ya kutoa tabasamu la kejeli na palepale alianza kushambulia baadhi ya wanajeshi waliokuwa wakimsogelea na hakuna risasi yake hata moja iliokosa katika sehemu muhimu za mwili tena akitumia mkono mmoja tu.

Afande Makwera hakutegemea mambo yangefikia pale , alifika hapo na wanajeshi wengi ili kumtishia Afande Kweka kumtoa Roma ili apelekwe mbele ya sheria , lakini matokeo yake ni kwamba ni kama alikuwa akipambana na kichaa kwani kufumba na kufumbua alikuwa tayari ashapoteza watu zaidi ya kumi na tano.

Hakutaka kuzubaa tena palepale alitoa ishara kwa mwanajeshi aliekuwa nyuma yake na mwanajeshi yule aliinua siraha yake juu angani na kuipiga mara mbili na vitu kama fataki za moshi wa njano zilitoka na kupiga hewani.

Roma alijua kabisa hio ni ishara ya kuwaruhusu wale wadunguaji kufanya kazi yao na kweli ndani ya muda mfupi tu bunduki zilianza kukohoa kutoka katika kila pande ya nyumba hio kuelekea upande wa waliposimama familia yake.

Afande Kweka na watu wote walijikuta wakishikwa na kiwewe lakini kwa Afande Tobwe hakuwa na wasiwasi kwani alikuwa akijua uwezo halisi wa Roma kwa kuushuhudia na ni kweli kwani kabla hata ya risasi hazijaifikia nyumba palepale kulitokea ngao kama ukuta wa barafu na kila risasi iliokuwa ikigonga ilidondoka chini

“Ni nini kile?”Aliuliza mmoja ya walinzi kwa wasiwasi.

“Inaonekana kama ukuta wa barafu”

Kundi lote la wanajeshi waliofika hapo kushambulia walijikuta wakigeuka kwa macho ya mshangao na kuangalia namna ambavyo risasi zilivyovukuwa zikigonga ule ukuta na kudondoka chini ilikuwa ni zaidi ya mshituko kwao

Upande wa Denis yeye hakuwa hata na mshangao na ni kama alikuwa akiigiza kuonekana kama alikuwa akishangaa.

Roma wala hakutumia hata uwezo wake wa kimaandiko kutengeneza ule ukuta bali ni zile Dhana alizopata mara baada ya kuwaua wale Majini kutoka Hongmeng kule nchini Kenya na kuchukua Dhana zao.

Roma licha ya wingi wa wanajeshi hao , hakuona haja kabisa ya kutumia uwezo wake wote au kuita Dhana yake ya Cauldron kwani licha ya kwamba ilikuwa na msaada katika kushambulia lakini ilikuwa na madhara makubwa katika roho yake na ufahamu wake hivyo aliihifadhi na kujiambia ataitumia siku ambayo ataona anakaribua kuuliwa na adui.

“Hii inawezekanaje , wadunguaji wangu…”

Afande Makwela alijikuta akitetemeka kwa wasiwasi , ijapokuwa alikuwa ni Kamanda ambaye alikuwa na uzoefu mwingi kwa kushiriki katika vita ya kulinda amani katika maeneo mengi ya Afrika lakini kilichokuwa mbele yake kilikuwa kigeni, kwanza alimchukulia Roma kama mchawi tu ndio maana hakumuogopa lakini kwa kile alichokuwa akikiona kilikuwa ni nje ya matarajio yake na alijilaumu kwa kumdharau.

“Mnashangaa nini nyie , mshambulieni”Alitoa Amri kwa wanajeshi wake kwa suati kubwa huku yeye akikimbia kurudi nyuma kwa ajili ya kujikinga akifuatiwa na wale wanajeshi aliofika nao wa vyeo vikubwa.

Lakini licha ya milindimo ya bunduki ikisikika kumlenga Roma , hakuna madhara hata kidogo ambayo yalipmata ni kama vile wanapiga risasi kwenye chuma kigumu.

Mua ule siraha nzito za kivita zilianza kutumika na kurushwa kuelekea katika nyumba ya Roma lakini hakuna hata moja ilioweza kupita kwani kila ilipokutana na ukuta wa kijini ilizimika.

Ndugu wote wa Roma waliokuwepo walijikuta wakiwa katika hali ya mshangao na kumkubali na walijikuta wakianza kumpigia makofi ya kumkubali.

Roma hakujali wanajeshi ambao walikuwa wakimshambulia bali alizidi kusogea mbele kumfuata Kamanda Makwera.

Upande wa Kamanda Makwera licha ya kurudi nyuma kuondoka hilo eneo lakini alijikuta siraha zikisidi kusikika karibu yake na aliishia kugeuka nyuma na kuangalia kinachoendelea na hapo ndipo alipojilkuta akishikwa na ubaridi mara baada ya kuona sura ya Roma ikiwa mbele yake

Roma mara baada ya kumwangalia Kamanda Makwera alijikuta akitoa tabadamu lake la kifedhuli huku akiwa na sura kama ya simba ambaye ameona kitoweo.

Kamanda Makwera aligeuka na kutaka kukimbia lakini hakuelewa hata ni nguvu gani ilioshika mguu yake na kumdondosha chini.

“Kamanda…!!”

Wanajeshi aliokuwa amekuja nao kwenye Chopa walipiga makelele ya kumuita na Kamanda Makwera alijitahidi na akasimama lakini alikuwa amechelewa kwani Roma mtoa roho tayari alikuwa mbele yake na wale wanajeshi wengine washaacha kushambulia kutokana na kugopa kumpiga kamanda wao na waliishia kuangalia kile kinachokwenda kutokea kwa wasiwasi.

Hata hivyo wenyewe walikuwa kwenye kiwewewe kwani ni kama sasa wanaelewa kwanini mwanzo Roma aliwapa onyo na kisha wakalipotezea , kwa lugha nyepesi ni kama walimchukulia kiwepesi na sasa wanaona shughuli yake haikuwa ya kawaida.

Afande Makwera mara baada ya kuona amekamatika sura ilianza kumshuka na mbinu pekee ambayo aliona ingeweza kumuokoa mbele ya mkatili Roma Ramoni ni kumbembeleza asimuue.

“Roma hebu punguza jazba ., mimi ni Kamanda Makwera ,ndio kamanda wa mkoa wote huu wa Iringa , hivi unajua ni watu wangapi wataathirika kama nikifariki , licha ya kwamba sijatokea kwenye familia kubwa lakini ukiniua haikuongezei chochote zaidi ya kukuletea hasara , unaonaje tukikaa chini na kuongea tofauti na kuniua?”Aliongea.

“Ushamaliza kuongea?”Aliuliza Roma.

“Kwahio bado tu unapanga kuniua , hivi utaua kila adui yako anaejitokeza mbele , hivi unajua ni matokeo gani utayapata kwa kufanya hivyo?”

Roma aliona kabisa huyu mzee anaongea ngonjera , mwanzo alitaka kumuua na sasa ameshindwa vita anageuza kibao kuomba kusamehewa, palepale hakutaka kumchelewesha na aliishikilia shingo yake na kumning’niza hewani kwa wepesi kabisa licha ya bwana huyo kuwa na mwili mzito.

“Nitakuambia kitu kabla kujafa , ulikuwa ni ujinga wenu kufikiria kama mnaweza kunishinda lakini ukweli ni kwamba mimi ni tofauti na nyie , sijawahi kuogopa maiti wala kuwa na hatia pale ninapoua mtu , kwangu mimi suluhisho bora zaidi ni kuua kuliko kuwaacha hai maadui zangu , kwani ukisha kufa huwezi kuwa tishio kwangu tena ila nikikuacha hai siku zote utaishi na kinyongo na hatimae kuja kunichokoza tena , hivyo ni heri kabisa kuua kila adui yangu kuliko kumuacha mtu anaeniwinda siku nikionyesha udhaifu…”Kauli yake iliendana na vitendo na ndani ya dakika ileile kutokana na kukaza mkono wake Kamanda Makwera alikosa mpuzi na kupoteza maisha huku mkono wa Roma ukitapakaa damu kutokana na kupasua mshipa mkubwa unaosambaza damu kwenye kichwa.
 
SEHEMU YA 589.

Wanajeshi wote hakuna ambaye aliamini kama Kamanda wao ndio amekufa hivyo ,ilikuwa ni kama vile wapo ndotoni na muda wowote wangeamka na kuona sio kweli.

Kamanda mwenye cheo cha ubrigedia jenerali alikuwa amekufa kiwepesi kwa namna hio .

Matendo ya Roma yaliwaambia kabisa hawakuwa wakiota bali walichokuwa wakiona ni uhalisia mara baada ya kurushiwa mwili wa Kamanda wao uliolegea shingo.

“Baba kamuua Brigedia Makwera haitaleta shida zaidi?”Aliuliza Damasi ambaye alikuwa kwenye taharuki kwa kila ambacho ameshuhudia.

Ni moja wapo ya watu waliokuwa na woga zaidi ya wengine wote na alimuogopa Roma maradufu , ijapokuwa mwanzoni alikua akijua ana uwezo mkubwa na ni mkatili wa hali ya juu lakini kwa matendo ambayo ameyaona kwa macho yake alijihisi kabisa huenda Roma sio mtoto wa Raisi Senga na alisingiziwa mahali.

“Kuna kipi cha kufanya wakati tayari unaona ashakufa”Aliongea Kamanda Mstaafu ,Mzee Kweka huku akionyesa hana wasiwasi wowote , ilikuwa ni kama vile hata yeye angechukua maamuzi yaleyale.

Lakini huo ndio ukweli inawezekana Roma alitengenezwa kisayansi na akawa na ukatili wa hali ya juu na kuua kwake ikawa ni kitu kidogo lakini ukweli ni kwamba Afande Kweka ni moja wapo ya watu wakatili sana sana ambao washawahi kuwepo ndani ya Taifa la Tanzania , watu wengi ambao walimpinga ndani na nje ya jeshi aliwaua kwa siri sana kwa mbinu tofauti tofauti , hivyo anachokifanya Roma ni kama karithi tu na utofauti wake na Roma ni staili zao tu za kuua , yeye alikuwa akiagiza watu wake kutekeleza vifo lakini upande wa Roma alikuwa akiwa hadharani bila hofu yoyote.

Damasi aliekuwa akitaka kutokwa na machozi alitaka kuongea lakini Afande Kweka alonyesha kwamba hakuwa na mpango wowote wa kumsikiliza na palepale aliwapa ishara walinzi wake wamsogelee na kisha akatoa maagizo ambayo waliyafanyia kazi kwa haraka haraka.

Upande wa Denisi lisha ya kuonyesha mwonekano usiokuwa wa kawaida kama wa kukata tamaa lakini yeye hakuona shida kwa watu waliokufa.

“Kamanda wenu ndio huyo amekufa , je bado mnataka kuendelea kumuonyeshea utii muungane nae au utii wenu mtauojesha kwa taifa?”Aliuliza Roma huku akitoa tabasamu lake lilelile la kuogopesha na kuwafanya wale wanajeshi kushikwa na baridi ya woga

“Master Roma , tulilazimishwa kufanya hivi tu , kwanzia leo tupo tayari kukutambua kama Kamanda wetu mpya”Aliongea mmoja ya mwanajeshi mwenye jino la mbele lililokatika.

“Upo sahihi Kamanda Makwera alitumia madaraka yake vibaya kwa faida zake mwenywe , alistahili kufa , nipo tayari kufanya chochote ambacho Master Roma ataniambia”Mwingine aliunga hoja juu kwa juu lakini kauli zao hazikumfurahisha Roma hata kidogo na palepale alichukua bunduki kutoka kwa mwanajeshi aliekuwa karibu yake na ilikua kwa spidi sana wale wanajeshi wote wawili waliokuwa wakimpamba walipasuliwa kichwani palepale na kudondoka chini.

Kila mmoja alimwangalia kwa mshituko mara baada ya tukio hilo na walishindwa kujua anataka kufanya nini.

Roma hakujali mshangao wao kwani alitupa siraha pembeni huku akiwa na uso wa kutokuathirika na kile alichokifanya.

“Bado hamjaelewa tu , nimesema onyesheni utii wenu kwa Taifa sio mimi , au mnanniona mimi ni Makwera wenu kudhania mimi ni mhaini ambaye muda wowote naweza kuanzisha vita?”Aliongea Roma na wale wanajeshi wote waliangaliana huku sura zao zikipauka kwa wasiwasi

Mpaka hapo walijua Roma ni mtu ambaye hatabiriki ndio maana moja kwa moja walikosa ujasiri wa kuongea tena kwa kugopa kusema kimakosa.

“Master Roma tafadhari punguza jazba , tupo tayari kupigana kwa ajili ya taifa letu tutapigana zidi ya wahaini wote wa nchi mpaka mwisho wa maisha yetu “Aliongea mmoja wapo alieonekana kumuelewa Roma na wengine wote walionekana kuelewa na waliongea kwa sauti kwamba wanakwenda kupigana na kuonyesha utii kwa manufaa ya taifa na sio kwa ajili ya mtu mmoja mmoja.na hata wale waliojificha waliweza sasa kutokea misituni na kuungana na wengine.

Ni kama vile dakika hio ilikuwa ikisubiriwa kwani muda uleule waliingia wanajeshi makomandoo kwa spidi zote na kuimarisha ulinzi huku wale waliokuja na Marehemu Afande Makwela wakiponywa siraha zote na kukalishwa chini ya ulinzi.

Dakika hio hio Brigedia Jenerali wa jeshi mkoa waSongea , Afande Murasa aliiweza kufika akiwa na kombati za jeshi.

Na mara baada ya kutoka tu kwenye gari alimsogelea Afande Kweka na kumpigia saluti ya heshima na kugeukia wanajeshi aliokuja nao na kuwapa maelekezo huku yeye akiongozana na Afande Kweka mpaka kwenye ofisi yake ndogo kuanza mazungumzo.

Kila kitu kilitokea kwa kasi sana , ni swala la dakika kama ishirini tokea kuanza kwake na kumalizika .

Afande Tobwe alimwangalia Roma bila kuongea chochote , ijapokuwa walikuwa ni Wakwe lakini alimuogopa.

Kila mwanajeshi aliekuwa njiani alimpishaRoma kwa woga sana na yeye hakujali na muda huo alikuwa amechafuka mwili mzima kwa damu na alitembea kuelekea upande wa nyuma alikomuona Denisi.

“Kaka niseme ujasiri wako umetuokoa , kwa staili hii nadhani kwanzia leo hii kila mtu ndani ya jeshi atatuogopa”Aliongea Denisi mara baada ya kusogelewa na Roma.

“Ndio unavyoona?”Aliongea Roma kwa sauti kali na ghafla tu huyu hapa ashaishika shingo ya Denisi na kuining’iniza hewani.

Kitendo kile kilishangazaza watu sana akiwemo Damasi mwenyewe na hata afande Kweka ambaye alishatoka nje akiambatana na Afande Murasa.

“Master Roma tafadhari punguza hasira?”Walinzi waliongea kwa hofu.

“Ndio, Denisi ni mdogo wako”Wasaidizi na walinzi walijaribu kubembeleza

“Roma tafadhari naomba usimuumize mdogo wako”Sauti ya Damasi iliweza kusikikika kwa nyuma huku akisukuma watu kupita kusogea mbele.

Damasi hakujali tena kule kumuogopa Roma bali alimsogelea na kumshika mkono wake wa kushoto akimbembeleza.

“Roma mwanangu nakuomba , mdogo wako najua amefanya makosa mengi nyuma lakini sasa hivi amebadilika , unatakiwa kumpa na yeye nafasi ya kijirekebisha , huwezi kumshambulia tu bila sababu”Aliongea huku akianza kutoa machozi ya kiutu uzima.

“Roma umesema unaamini Denisi ndio anakufanyia njama lakini huwezi kumshambulia bila ushahidi”Aliingilia Afande Kweka.

Ijapokuwa alikuwa akisita kumuachia Denisi lakini kutokana na mbinu nzuri aliokuwa nayo Denisi kujificha hakuwa na uwezo wa kumuua bila kuwa na ushahidi wa kueleka.

Roma alimwangalia Denisi kwa macho ya kumpa tahadhari na kisha akamsukumia mbali.

Damasi alijikuta akihema kwa ahueni huku akimwangalia Roma kwa macho ya shukrani.

“Brigedia Murasa amenipa taarifa hapa ya kinachoendelea na Afande Tozo yupo Dar es salaam na uchunguzi unakaribia kumalizika na wote waliohusika watakamatwa na kupelekwa mbele ya sheria na hali ya hewa ikitulia watatuutaarifu”Aliongea Afande Kweka.

“Nadhani wanajua kabisa kilichoendelea hapa na wanaangalia tu namna ya kulimaliza hili swala”

“Haijalishi makusudio yao ni nini , walionekana wapo tayari kutumia hela zao kutaka kutuyumbisha lakini sasa yameisha na hili watalimaliza kwa njia zao za kisiasa”

“Vyovyote vile ni sawa tu , hata hivyo sitaki kuuwa viumbe dhaifu tena”Aliongea Roma na kisha aliondoka.

Wakati tukio lote hilo linatokea Edna alikuwa yupo upande wa nyuma.

Muda ambao Roma alifika upande wa nyuma kuingia kwenye Korido ya chumba chao aliweza kumuona Edna ambaye alikua akitembea kurudi nyuma na mbele akionekana kama mtu mwenye kuchanganyikiwa.

Lakini alijikuta akisimama mara baada ya kumuona Roma akiwa kama mwenye hali ya furaha lakini alijikuta akishituka mara baada ya kuona damu katika mwili wake.

Roma aliweza kujua mshangao wa Edna ulikuwa ukihusiana na nini na alijikuta akinusa shati lake lwenye damu na kutoa tabasamu la kifedhuli.

“Mh .. damu zinanuka vibaya hizi , Edna mke wangu usiwe na wasiwasi nitaenda kuoga kwenye chumba kingine”Aliongea Roma huku akitaka kugeuka kuelekea upande mwingine wa vyumba lakini Edna alimkimbilia na kumshika mkono.

“Unaongea kuhusu nini wewe , kwanini ukaoge kwenye chumba kingine , unataka watu wanifikirie vibaya, tumekuwa pamoja kwa muda mrefu hivyo nishazoea , ni damu tu na vinyama nyama kwanini unataka kuyakuza, hebu nifuate huko”Aliongea huku akitangulia kuingia ndani.

Roma moyo wake uliridhika mara baada ya kusikia meneno hayo kutoka kwa mke wake na alishukuru kumuona Lanlan hayupo.

Edna alimwingiza Roma mpaka kwenye bafu lao na baada ya kufika alifungua vifungo vya shati lake pamoja na suruali na kutupia pembeni na baada ya hapo alifungulia bomba la maji ya mvua na kuacha yamwagikie Roma huku yeye akitoka tena na kuchukua sabuni maalumu ya kuogea ya marashi na kurudi nayo akiwa ameshikilia taulo.

Roma alishangazwa na namna Edna ambavyo hakuzingatia mwili wake uliokuwa hauna nguo .

“Mke wangu ni lini umebadilika , nakumbuka mara ya mwisho ulikuwa na aibu hata ya kuingia kwenye chumba changu”Aliongea Roma na kumfanya Edna kushituka kwani akili yake haikuwa ikizingatia mwili wa Roma bali damu zilizokuwa kwenye mwili wake.

“Nini?”

“Ndio maana wahenga wanasema ndoa ni kaburi la mapenzi , nadhani kuanzia sasa inabidi nikuite Mama Lanlan”Aliongea Roma kwa kumtania.

You Suck , nilikuwa nikijaribu kukusaidia kukusafisha na sasa unaanza kunichokoza , nitaenda kulala na Lanlan mimi wewe endelea”

“Edna my Darling , nilikuwa nikitania , usichukulie siriasi , ukiachana na hayo Lanlan yuko wapi?”

“Karudi kulala tena kwenye chumba cha babu yake , inanifanya niwe na wasiwasi maana kila akishiba tu anakimbilia kulala”

“Huna haja ya kuwa na wasiwasi , bado ni mdogo na kuvuna nishati za mbingu ni kuumiza ubongo hivyo ni kawaida, kipindi hicho mimi sikuweza hata kuuruhusu usingizi unichukue ili kuweza kuishi , nilihitajika kuvuna nishati kadri niwezavyo ndani ya muda mfupi kabla ya maadui zangu hawajanipata .. lakini kwa yeye kila kitu anacho na hana haja ya kuhofia usalama wa maisha yake , hivyo naweza kusema amebarikiwa kuliko nilivyokuwa mimi , tena hili jambo linanijia akilini sasa hivi , tokea nije Tanzania nilikuwa nikijiwazia mimi mwenyewe lakini siku hizi kila ninachofanya ni kwa ajili yako na yeye.”Aliongea Roma huku akiendelea kuwa bize na kujisafisha.

Na kukabidhiwa Taulo na mke wake kujifuta maji tayari nguo Edna ashaziandaa na kumsaidia kuvaa naRoma mara baada ya kukaa chini picha ya Denisi ilimjia akilini mwake na kumfanya kuanza kuwa na wasiwasi usioelezeka.

Roma alisita sita kumfanya Denisi chochote kutokana na kujali uwepo wa Damasi tu.

Nitatafuta namna ya kumuua kwa siri”Alijiwazia Roma.

“Unafikiria nini tena?”

“Sio jambo kubwa , nawaza ni kwa namna gani huyu mzee ataweza kulimazliza hili swala”

“Najua sikupaswa kuuliza kilichotokea , lakini nataka kusikia ukweli wote kutoka kwako”

“Nini unataka kujua?”

“Kama bado tupo hatarini?”Aliongea Edna akiwa na wasiwasi.

“Bado nipo na hivyo usiwe na wasiwasi”

“Kama ni hivyo basi niahidi kitu kimoja , kama kitu chochote kitatokea niambie , unanijua mwenyewe mimi sio mwanamke ambaye ni mjinga , nina uwezo wa kuchanganua mambo pia”Aliongea kwa upole na kumanya Roma kumuona mke wake amegeuka na kuwa mke mtiiifu mbele yake na kuonekana kama mtoto.

Roma palepale alinyanyua mkono wake kutaka kushika shavu lake lakini mara baada ya kufikiria kitendo alichokifanya dakika kadhaa zilizopita alijikuta akiishia njiani na kuurudisha , ni kama akili yake ilikuwa ikihofia kumchafua mke wake.

Edna aliona kitendo kile na palepale alichuhukua mkono wake na kuuweka kwenye shavu lake.

“Kwanini hujafanya ulichodhamiria wakati sijakuambia uache , au unaniona mimi mchafu?”

“Hapana mikono yangu ndio nahisi bado inanuka damu na hata kucha zangu sijazisafisha vizuri”

“Nimeongea lolote kuhusu hilo ?”Aliuliza Edna huku macho yakianza kuwa mekundu.

“Mhmh..”Roma alishindwa kuendelea kuongea zaidi ya kuguna na Edna alimsogelea karibu zaidi.

“Hivi unajua kwamba hata mikono yako ichafuke vipi na damu au ni maiti ngapi umweza kushika kwangu ni mikono hii hii ambayo ilinisaidia kipindi nilichokuwa kwenye matatizo , ni mikono hii ambayo ilinikumbaita na kunifanya nilale na ni hiii ambayo ilimshikilia binti yangu .. haitotokea nikaiona ni mikono michafu kwasababu hii ni mikono ya mume wangu , mikono ya mtu ninaempenda”

Roma aliguswa na maneno yake na hakuamini kama ni Edna ambaye anaongea.

“Edna mke wangu nani kakuandikia Script au ni zile roboti za mtandaoni”Alitania Roma.

“Mimi nipo siriasi”Aliongea na kumfanya Roma kumeza utani wake na palepale alisimama na kumbeba juu juu na kumrushia katikati ya kitanda na Edna ashajua nini kinakwenda kutokea.

“Tiusifanye sasa hivi bado ni mapema na sijaoga bado”Alilalamika .

“Mke wangu wewe hujali kama mikono yangu ni michafu kwanini nikuache uoge , isitoshe My darling wife unanukia vizuri muda wote”Aliongea na baada ya pale alijichimbia kwenye kifua cha mkewe na kuanza kazi na ndani ya madakika kadhaatu Edna hakuweza kumpinga tena na kumuacha afanye atakavyo lakini ghafla tu Roma aliacha anachokifanya na kusimama huku akiangalia mlangoni.

Edna alishangaa mara baada ya Roma kuacha lakini alielewa mara baada ya kuona mlango ukifunguliwa.

“Mommy, mommy! Is dady back”(Mama , mama , je baba amerudi)

Lanlan mara baada ya mwili wake wote kuingia ndani alianza kukagua mazingira , mashavu yake yalitingishika mara baada ya kuwaona wazazi wake na alianza kuonyesha hali ya kutoelewa hali inayoendelea.

“Dady ,mommy what kind of game are you playing?”Aliuliza Lanlan akisema ni mchezo gani wanacheza.

Edna alijikuta akibadilika rangi na kuwa mwekundu , alitamani aingie uvunguni , ilikuwa ni afadhari nguo zake bado hazikutolewa mwilini.

“Baba na mama yako tunachukua mazoezi sawa chubby”Aliongea Roma

“Mazoezi!! , Lanlan anataka pia kuchukua mazoez na nyie”

“Lanlan utachukua mazozi kama haya ukishakuwa mkubwa… sasa hivi nenda kacheze na babu yako , usije huku ndani mpaka tutakapotoka”Aliongea Roma lakini Lanlan alionyesha hakufurahishwa na kauli ya baba yake na aliendelea kumwangalia Roma kwa kutia huruma kwani aliona ni kama vile baba yake anamfukuza.

Roma suruali yake ilikuwa ikishituka shituka kama ina uhai na akili yake ni kama anaelekea kuupata uchizi.











SEHEMU YA 590.

Hali aliokuwa nayo Roma ilimfanya Edna kutamani kucheka huku akisahau aibu yake.

“Lanlan kuwa mtoto mzuri na utoke , Lanlan ushawahi kuonja nyama ya Kondoo wa kukaanga?”

“Kondoo ndio wanyama gani baba?”

“Ni wanyama wenye tabia ya kulia, ‘Baa .. baaa’ , ni nyama nzuri sana ikikaangwa, nitahakikisha unaonja kitu kipya kama utaenda kuendelea kucheza na babu yako”

“Daddy you have to keep your promise , I’ll go to play wirh great grandfather”Aliongea akimaanisha kwamba Roma anapaswa kutii ahadi yake na yeye anaenda kucheza na babu yake mkubwa na akakimbilia nje huku akisahau kufunga mlango tena na kumfanya Roma kung’ata meno yake kwa hasira lakini hata hivyo alimuona Lanlan ni mwepesi kudanganyika kila nyama inapotajwa na alishuka kwa hasira na kuubamiza mlango.

“Huyu litoto tundu napaswa kulifundisha , anaachaje mlango wazi kwa mfano” Aliongea na kama chui alimrukia Edna kitandani na namna suruali yake ilivyomtoka kiunoni huenda ni rekodi mpya ya dunia.

Dakika chache mbele chumba chote kilijaa sauti za mguno wa kimahaba kutoka kwa Edna.

*******

Upande mwingine jijini Dar es salaam wakati Roma yeye akijipongeza baada ya kuua ilikuwa ni zamu ya Raisi Senga kukamilisha kile alichopanga.

Hakuamini kila kitu kilienda kama alivyopanga , ijapokuwa namna ambayo Roma ametatua tatzio ilikuwa ndio kama alivyotarajia lakini ukweli ni kwamba aligundua alikuwa na mtoto ni katili mno na kuzidi kumugoopa mara mbilimbili.

Katika jengo la ikulu chumba cha mikutano kulikuwa na kikao kizito ambacho kilikuwa kimeitishwa tokea jana yake na hakikuhusisha wale watu tu ambao walikuwa wamehusika katika mpango wa kumtengenezea Roma matukio.

Raisi wa Visiwani pia alikuwepo katika kikao hicho na baadhi ya wanasiasa wakubwa ambao Raisi Senga alikuwa akijua kabisa utulivu uliokosekana nchini ulianzishwa na wao.

Muda huo mara baada ya kuingia katika chumba hicho na kunagalia sura za kila mtu alietii wito alijikuta akitabasamu ndani kwa ndani na kujiambia yes huo ndio muda wa kukamilisha ndoto yake ya siku nyingi.

Wakati kikao hicho kikiwa kinaendelea ndani ya ikulu, upande wa mitandaonni wananchi walikuwa wamecharuka mara baada ya sauti zinazosemekena kuwa za Waziri wa nishati , Waziri wa ulinzi, Afande Makwera na Mke wa raisi Kigombola kusambaa kwa kasi.

Maudhui yaliokuwa kwenye sauti hio ndio kitu kilichowafanya wananchi kuweza kusikia kila kitu kilichokuwa kikiendelea kwani mipango yote ya Afande Makwera kushawishiwa kumshambulia Afande Kweka na mjukuu wake ziliweza kusikika , ijapokuwa hakukuwa na uthibitisho wa moja kwa moja wa kusema sauti hizo zilikuwa za watu hao lakini zilifanya kila mtu kuwa katika Dilema na kubwa zaidi ni kwamba mtu alieanza kuzisambaza alisifika kuwa kinara kwa kumkosoa Raisi Senga mtandaoni.

Ni dakika chache tu mara baada ya Sauti hizo kusambaa ndipo taarifa ya kifo cha Afande Makwera kilipoweza kutangazwa kwa kuthibitishwa na mkuu wa majeshi wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijinni Dar es salaam , huku sababu halisi kuwekwa wazi , uthibtishwaji wa kifo hicho na namna kilivyotokea haikuhitaji elimu ya kuthibitisha yale maongezi ya sauti yaliokuwa yakisambaa mtandaoni kuwa kweli.

Lakini swali moja tu liliibuka nani ambaye aliwarekodi wenzake kwani vikao hivyo ni vya siri,lakini ilibakia kuwa habari ilioibua mjadala na kumshuku huyu na huyu .

Wakati hayo yanaendelea upande wa Mheshimiwa raisi wa visiwani alikuwa amenywea sana kiasi cha kushindwa hata kumwangalia Raisi Senga usoni , ile hali yake ya kujiamini aliokuwa nayo siku kadhaa zilizopita ilikuwa imemshuka sana na hakuwa yeye tu bali pia kwa baadhi ya wanasiasa wengine.

Hali ya woga ilianza kuwatawala kila mmoja huku wakiwa kama watu ambao wanasubiri hukumu yao kutolewa na Senga, lakini kwa wakati mmoja na wao walikuwa na maswali lukuki imekuwaje mipango yao ikawa inajulikana kwa uwazi namna hio na walianza kuangaliana kwa hasira.

Wakati ambao walikuwa wakijiuliza maswali hayo , upande wa Raisi Senga na yeye alikuwa akijiuliza swali ni nani ambaye yupo nyuma yao , kwani hata kabla ya kufanya kikao hicho alikuwa na mazungumzo ya siri na Raisi wa Visiwani na kujaribu kumhoji lakini mwisho wa siku na yeye hakuwa na jina la mtu ambaye yupo nyuma yao zaidi ya kumjua akiitwa The Don.

Raisi Senga ijapokuwa kila kitu kilienda upande wake , lakini kile ambacho siku zote alikuwa na wasiwasi nacho ni kama kimefufuka upya.

“The Doni amerudi tena?”Ndio kauli aliojiambia.

Raisi Senga ni kwa muda mrefu sana ambao alikuwa akihitaji kumjua The Doni , mtu ambaye alikuwa nyuma ya hayati Raisi mstaafu Kigombola lakini mpaka siku hio hakuwahi kumjua wala kumuotea ni nani , mwanzoni hisia zake zilimwambia ni Roma lakini hakuweza kuthibtisha hilo na kwa yalitokea ni kama yamemthibtishia kabisa kwamba Roma hakuwa The Doni.

Hivyo licha ya kushinda mpango wake lakini bado moyo wake ulikuwa mzito juu ya huyu mtu aliejiita The Doni na kuna hisia pia zilimwambia huenda Denisi ana ukaribu na The Doni kwasababu Yan Buwen alikuwa na ukaribu na The Doni kwa maelezo ya hayati Kigombola, lakini licha ya kuwaza sana hakutaka kusumbua kichwa chake kwanza na kuanza kufikiria namna ya kumaliza swala lililokuwa mbele yake.

Kikao hicho kilijumuisha na Katibu mkuu wa Chana cha Maendeleo na waliweza kujadiliana kwa zaidi ya masaa manne huku mwishoni wakikubaliana vitu vingi.

Lakini matokeo ya kikao hicho yalijumuisha kwa kukamatwa kwa baadhi ya watu ambao sauti zao zilisikika na jeshi la polisi kwa ajili ya uchunguzi huku mheshimiwa Raisi wa Visiwani akipewa nafasi ya mwisho ya kwenda kutuliza wananchi wake ndani ya masaa mawili tu.

Wakati kila kitu kikienda kila alivyopanga hatimae Raisi Wa Visiwani mheshimiwa Huseni Husani alitoa hutuba fupi akiwa ikulu na mbele ya jopo la waandishi wa habari na viongozi wenzake kuwaasa wananchi kuwa na utulivu huku akienda mbali kukanusha Roma kuhusika katika mauaji ya Kamanda Razaq na kusema yote hio ilikuwa ni mipango ya adui kutaka kuigawanya nchi na uchunguzi yakinifu unaendelea kumbaini.

Baada ya hotuba ya Raisi wa Zanzibar , Muongeaji mkuu wa Serikali alitoa Tangazo kwamba siku inayofuata Mheshmiwa Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania atalihutubia taifa kupitia ikulu ya makao makuu ya nchi mkoani Dodoma.

Kutarajiwa kwa hotuba yake hio iliwafanya wananchi wa Tanzania kuwa na shauku ya kutaka kujua kile ambacho Raisi anakwenda kuhutubia.

*********

Kabla hayo yote hayajatokea upande mwingine mwanadada Suzzane ni moja ya watu ambao walikuwa kwenye tafakari nzito sana kuhusu bosi wake Edna kwa kauli yake ya mara mwisho ambayo alimpatia siku moja kabla ya kustaafu kuwa CEO wa kampuni.

“Suzzane kwanzia sasa nataka uachane na uchunguzi wote wa maswala yanayohusiana na mama yangu , najua kila kitu kwa sasa na nawaza namna ya kukabiliana na kilichopo mbele yangu , sitokuambia ni lakini taarifa hii ni siri kwako na asitokee mtu yoyote ukamwambia”

Kauli hio ya Edna ilimchanganya sana mwanadada Suzzane , sababu kubwa ya kumchanganya ni kutokana na namna ambavyo aliitamka , lakini pia kukosa maelezo sahihi ya kile kilichotokea siku kadhaa zilizopita katika hoteli ya Peacock.

Suzzane alikuwa ni tofauti na Edna katika siku ile , alikua kwenye mshangao na maswali mengi kwa kile kitu kilichotokuwa kimetokea , alijiuliza Edna alitoa wapi ile pete na swali hili hakujiuliza yeye mwenyewe bali aliulizwa na wanachama ambao walikuwa ni wa taasisi ambayo ni kama mara ya pili anaisikia jina, jumuia ya siri ya kitaasisi iliojiia Ant- illuminat.

Kitu pekee ambacho kilimfanya Suuzzane kutaka sana kujua kuhusu mama yake Edna ni kutokana na kifo cha mpenzi wake Dr Elvice Daniel , siku zote alitamani kulipa kisasi ka wale waliomuua mpenzi ake kabla hata hawajafunga ndoa lakini mpaka wakati huo hakuwa amepata mwanga namna ya kulipiza kisasi.

Sasa ni masiku tokea mrembo Suzzane akiwa katika mawazo , siku ambayo nchini Tanznia kukiwa na mambo makubwa yanayoendelea , Suzzane yeye alikuwa ndani ya jiji la Doha nchini Qatar.

“Karibu sana Suzzane kwenye umoja wetu wa siri , umefanya maamuzi sahihi sana”Sauti ya mrembo Nadia Alfonso iliweza kusikika ndani ya gari la kifahari refu aina ya Limuosine , gari yenye ufahari wa kila aina ndani yake na kumfanya Suzzane kuwa mara yake ya kwanza kupanda gari aina hio.

“Asante Nadia lakini bado ni mwenye wasiwasi?”Aliongea Suzzane na kumfanya Nadia kutabasamu kidogo.

“Wasiwasi wako ni wa muda , ukishajua nini maaana halisi ya umoja wetu basi hofu yako yote itaisha , kwasasa uvae ujasiri unapokwenda kutamblishwa kwa mara ya kwanza na kupewa nafasi ya awali ya uanachama na kupokea misheni yako ya kwanza ya kujithibitisha”

“Misheni ya kwanza ya kujithibitisha!!!?”Aliuliza Suzzane na kumfanya Malkia wa sheria , mrembo Nadia kutoa abasamu na kuangalia nje.

“Tushafika Suzzane”Aliongea Nadia na kumfanya Suzzane kuangalia mazingira ya nje na kuweza sasa kuelewa kwamba akili yake ilikuwa mbali sana kwnai hakujua hata ni namna gani waliweza kuingia ndani ya ukuta mrefu huku mbele yao kukiwa na jengo kubwa kama hoteli.

*******

Muda wa mchana Roma aliweza kutoka chumbani bila wasiwasi , lakini upande wa Edna alikuwa na aibu kwani ni kama vile kila mtu ndani ya nyumba hio alikuwa akijua kile kilichokuwa kikiendelea na aliishia kuangalia chini huku akitembea kwa mwendo wa kujilaizmisha kwani miguu yake ilikuwa haipo vizuri.

Roma mara baada ya kutokezea kwenye bustani mahali ambapo Afande Kweka hukaa na kuota moto, aliweza kumuona mzee wake akiwa na Lanlan wakiwa katika umakini mkubwa wa kimaongezi.

“Nyie watu mnaongea nini mpaka kuwa na umakini hivyo?”Aliuliza Roma kwa kiswahili

“Daddy , babu alikuwa ananihadithia stori namna alivyoweza kuwashinda watu wabaya”Aliongea .

“Babu yako huyo anajua kujisifia tu kama utaendelea kumsikiliza”

“Ukorofi huo”Aliongea huku akimpotezea na kujivuta mwili na muda uleule kijakazi aliweza kuwasogelea.

“Master mtu wa hoteli ametupigia simu na kuuliza kama kuna kingine zaidi tunatakakuagiza”

“Waambie waandae tulichowaagiza kama kuna cha kuongezea wanaona inafaa basi wafanye hivyo”Aliongea na yule mfanyakazi wa kiume aliitikia na kuondoka.

“Mnazungumzia nini mambo ya hoteli hoteli?”

“”Unapata wapi ujasiri wa kuniuliza wakati ni wewe mwenyewe ulioemwambia binti yako utampa nyama ya mnyama anaelia ‘Baa.. baa ‘wa kukaanga, mimi hao kondoo nawatolewa wapi muda huu , nimeamua kupitia hoteli maarufu hapa Iringa wanaopika nyama ya Kondoo watuandalie”

“Asiee wewe mzee upo makini , wakati naongea hata sikuwa siriasi , angalau umefanya mambo kua mepesi hehe..”Aliongea Roma na kumfanya Afande Kweka kutoa tabasamu la kifedhuli ambalo linafanana kabisa na la Roma licha ya uzee wake.

“Lanlan leo usiku ukalale na wazazi wako na umwambie baba yako akuhadithie stori , anazo stori za kimapigano nzuri zaidi kuliko za kwangu”Aliongea na kumfanya Lanlan kumgeukia baba yake kwa shauku aone anasema nini.

Roma alijikuta midomo yake ikicheza alijua tu huyo babu yake anamfanyia makusudi, alikuwa akimzuia kutofanya mazoezi na mke wake.

Edna hakuwa mbali na aliweza kusikia kila kitu lakini hata hivyo alikuwa na shauku na yeye ya kusikia stori ambayo Roma atamwambia Lanlan.

“Kijana najua una Stamina nzuri lakini ni kheri kujizuia muda mwingine..”Aliongea huku akipotezea muonekano wake

*****

Upande mwingine nje ya chumba cha Damasi alionekan Denisi ambaye ni kama vile alikuwa akijishauri lakini dakika ileile aligonga mlango na ukafunguliwa na mama yake ambaye alishangaa kumuona Denisi.

“Vipi Denisi uliesema unaenda kumsaidia baba yako baadih ya majukumu kwanini upo hapa?”

“Kila kitu kinaonekana kumalizika hivyo hakuna kingine ambacho ninaweza kufanya”

“Kama ni hivyo , mbona unaonekana kama una kitu unataka kuongea na mimi?”

“Ndio mama , lakini sio kitu kikubwa sana, nilitaka kuona unaendeleaje , lazima utakuwa kwenye mshituko mkubwa kwa kilichomtokea Binamu Aloni na tukio la leo pia”Aliongea na kumfanya Damasi kutabasamu kwa mbali na kisha akamshika mtoto wake mkono.

“Denisi najua unanijali sana kama mama yako ila nipo sawa , ninajisikia vizuri kwa kupumzika kwa muda mrefu kidogo , kaka yako ndio ambaye anannigopesha , ni mtu mwepesi sana na hasira zake”Aliongea na kumfanya Denisi kumwangalia Damasi kwa macho ya huruma.

“Mama , kwanzia sasa jitahidi kujali afya yako , usiwe na wasiwasi sana na siku zote kumbuka afya yako ni muhimu”Aliongea na kumfanya Madam Damasi kuwa na mshangao kidogo na kumwangalia Denisi kwa wasiwasi.

“Kwanini unaongea maneno hayo ghafla tu , ni kama vile hayapo sawa”

“Mama ni kwasababu binadamu tunabadilika muda mwingine hata kama hatutaki kubadilika , siku zote tunalazimika kufanya maamuzi na kubadili maisha yetu kwa sababu ya watu na matukio “

“Unazidi kunitia wasiwasi na maneno yako Densi kuna kitu chochote kinakusumbua , niambie mimi mama yako na kama sitoweza kukusadia nitakuombea kwa baba yako akusaidie yeye”

“Hapana sina tatizo , nimefurahi kwamba upo sawa , ninatoka sasa kwenda kambini kwani kuna mambo nataka kudili nayo na naweza nisirudi kwa muda”

“Sawa nenda mwanangu huna haja ya kuwa na wasiwasi na mimi”Aliongea Damasi bila ya kufikiria mara mbili mbili na baada ya Denisi kutembea mita kadhaa aligeuka na kumwangalia mama yake aliekuwa akimwangalia.

“Kwaheri ya kuonana mama”Aliongea ndani ya nafsi yake na Damasi ambaye hakujua nini kipo kichwani mwa Denisi aliinua mkono wake kwa tabasamu na kumpiugnia mkono wa kwaheri bila kujua hio ndio kwaheri ya moja kwa moja kuiona sura ya mwanae wa kiume katika uhalisia.

Na mara baada ya kuingia kwenye gari lake palepale macho yake yalibadilika rangi na kiini cha macho kupotea na kuwa kama vile ni sananmu la rangi ya Silver.

ITAENDELEA.
 
SEHEMU YA 591.

Ni nje kidogo ya jiji la Kigali katika mlima uliofunikwa na msitu wa miti alionekana Denisi amesimama kando kabisa ya nyumbas ambayo imetengenezwa kwa mabanzi kama banda huku nyuma yake akiwa na wanajeshi wake.

Macho yake yote yalikuwa yakiangalia upande wa jiji la Kigali kwa muonekano ambao ilikuwa ni ngumu kuweza kuusoma kama anafikiria nini.

Muda huo huo alionekana Kizwe alietokea upande wa chini yao akipandisha kuwasogelea.

“Is everything ready?”Aliuliza akimaanisha je kila kitu kipo tayari.

“Jeremy amealikwa kuhudhuria chakula cha usiku na Balozi wa Ujerumani katika hoteli ya Sherati na baada ya hapo moja kwa moja ataenda Area D kwa mapumziko ya Wikiend, tuna muda wa kutosha kujiandaa”Aliongea Kizwe akifafanua ratiba za raisi Jeremy.

“Vizuri sana”Aliongea Denisi akitingisha kichwa.

“Lekcha ni kweli kabisa umebadili maamuzi yako ya kupotezea fursa ya kumuondoa Roma katika urithi wa familia?”

“Mhmh… fursa!?, nimetumia muda mwingi sana kukusanya watu wengi vile lakini mwisho wa siku wamegeuka kutokuwa na thamani , nimefeli kumzuia Roma kurithi uongozi wa familia awamu hi lakini siamini kama kutakuwa na nafasi nyingine ya kufanya hivyo , Roma angekuwa ashaniua leo kama sio Damasi kunikingia kifua , nina uhakika lazima anapanga kuniua kwa siri , hivyo tofauti na kumsubiria na kuniumbua mimi nani napaswa kumalizana na Jeremy kwanza ikiwa bado ni mapema, Roma anaweza kuwa kikwazo ndani ya Tanzania lakini bado tutaweza kupiga hatua kwa rasilimali zilizopo Rwanda”

“Una uhakika unaweza kumshinda Roma kwa kutawala Rwanda , Jeremy alijaribu kuitawala Tanzania kijasusi lakini alishindwa mpaka sasa na njia pekee alioona ni kuungana na familia ya Roma ili uhusiano wake na Tanzania kuimarika kupitia ndoa”

“Kama nilivyosema sio lazima sana kumshinda Roma ili niweze kutimiza malengo yangu , kwasababu kushindana na Roma ana kwa hakuwezi kufanikisha kitu, basi nitamtumia kuendelea kutibua hali ya hewa kama nilivyofanya”Aliongea na kumfanya Kizwe kuridhika na maelezo yake.

“Lekcha , je unaweza kuniahidi kitu?”

“Ongea”

“Najua mpango wako ni kuwadhibiti Gesha na Nix usiku huu lakini kuhusu Jeremy je unaweza kuturuhusu mimi na Desmond kumshughulikia?, kuwa na amani hatuwezi kuharibu mwili wake hivyo haitakuathiri na mipango yako”

“Ilimradi ubongo wake usijekuharibika tu , nina uwezo wa kuutawala mwili wake na kujiponyesha hata kama mtamfanya kuwa kilema , mnaweza kumfanya chochote kupungua hasira zenu , mimi sitojali”Aliongea na kumfanya Kizwe kutabasamu na kisha kumkumbatia.

“Nilijua tu utanikubalia , wewe ni noma”

“Anakwenda kuwa maiti hata hivyo , sitojali kama mtataka kumchezea kwanza”Aliongea Denisi huku akitoa tabasamu lake la kejeli lililochanganika na ukiburi ndani yake.

Ilionekana Lekcha mara baada ya kushindwa vita Tanzania baada ya Roma kumuharibia hatua yake ya pili ni kujaribisha nchini Rwanda, haikueleweka alikuwa na mpango gani kutaka kuitawala Rwanda kwa kumuua Jeremy.

*****[DI1]

Wakati wa usiku baada ya chakula, Lanlan kama alivyoambiwa na babu yake alienda kulala katika chumba cha wazazi wake.

Lanlan alikuwa amelala katikati huku kulia kwake akiwa ni baba yake na kushoto kwake akiwa ni mama yake.

Edna alikuwa akijishishika shika shingo yake huku akimwanglaia Roma kwa kutabasamu huku akiwa na macho yaliojaa uchokozi ndani yake bila ya Lanlan kuona kama wazazi wake wanaangaliana na kutabasamiana kiuchokozi.

Wakati Lanlan akiwa na furaha ya kulala na wazazi wake upande wa Roma yeye alikuwa akimlaani babu yake kwa kumfanya Lanlan kuja kulala nao maana ameharibu mipango yake yote.

“Daddy mdio unafikiria kuhusu stori ? nataka unihadiithie stori nzuri sana”

“Chubby hebu ongea leo si umekula mapaja yote mawili ya mguu wa kondoo wewe , utakuwa umeshiba sana na unahisi usingizi, unaonaje ukilala?””

“Mimi sina usingizi na sijashiba sana , Daddy sitaki kulala nataka stori”Aliongea na kumfanya Roma kumshangaa kusema hajashiba bado na kujiambia bora hata angemuongezea kidogo chakula chake.

“Lanlan unaonaje mama akianza yeye kukuhadithia stori kwanza?”

“Nishamuambia Stori nyingi tu kipindi chote nilichokuwa nikilala nae , leo wewe ndio zamu yako”

Roma mara baada ya kurushhiwa mpira na mke wake aliona haina haja ya kumuangusha binti yake ilihali alikuwa amejipanga kusikia stori kutoka kwake.

Ukweli kwenye maisha yake hakuwahi kusoma hadithi yoyote wala kusimuliwa, alijiambia kuwa tajiri na nguvu hakukuwa kukitosha tu kwa mtoto wake bali alipaswa pia kuwa msimuliaji mzuri wa stori.

Kwasababu hakuwa na stori ya aina yoyote alioijua aliona kitu pekee ambacho anapaswa kusimulia ni kuhusu maisha yake yaliopitia.

“Lanlan uunaonaje nikikuhadithia namna ambavyo niliweza kupambania maisha yangu katika Wolf Pack huko Alaska?”

“Daddy Alaska ni wapi?”

“Ni sehemu ya mbali sana kutoka hapa, kuna baridi sana na karibia eneo lote limejaa barafu na theluji , upatikanaji wa chakula ni mdogo sana huko”

“Na Wolf pack ndio nini Daddy?”

“Ni mkusanyiko wa Mbwa mwitu zaidi ya mia moja wanaowinda kwa pamoja kwa ajili ya kuweza kuishi”

“Kwahio hao Mbwa mwitu ndio walikuwa wakikuwinda ?”

“Ndio, lakini kulikuwa na watoto wengine waliokuwa katika umri wangu , tulikuwa na miaka kama kumi kwenda kumi na moja”Aliongea Roma na kumfanya Lanlan kutingisha kichwa kwa shauku kukubali kuweza kusikiliza stori hio , lakini kabla ya kuanza aliona kwanza ajaribu kuongea nae kumweleza baadhi ya maneno ambayo hataelewa kwa utoto wake.

“Lanlan unajua ukubwa wa eneo la kuwindia?”

“Ndio Lanlan anajua , ni eneo kubwaaa , kubwa, kubwa sanaa”Alijibu kwa ishara na kumfanya Edna aliekuwa akisikiliza maongezi hayo kushindwa kuzuia kicheko kwa namna ambavyo Lanlan amejibu.

“Edna kuwa siriasi , sisi wazazi wako hapa tunahadithia stori , hivyo kuwa makni katika kusikiliza”Aliongea kwa utani na kumfanya Edna kuendelea kucheka.

“Okey nitasikiliza kwa umakini , hebu anza kuhaditia na mimi nataka kusikia”

Aliongea na kumfanya Roma kuweka mto vizuri ili kukaa vizuri aanze kuhadithia.



****

Ni miaka kadhaa iliopita Kaskazini mwa msitu wa Alaska unaopatkana huko Marekani , anga lilionekana kuwa la bluu huku milima ilionekana kuwa ya rangi nyeupe kutokana na kufunikwa na Theruji.

Ardhi yake ilikuwa kame sana hususani katika kipindi hicho cha baridi kali na hata kwa baadhi ya maeneo yake ya karibu jotoridi ilikuwa likifikia takribani ya nyuzi hasi 10 za jotoridi..

Na kadri baridi katika juu ya usawa wa bahari ilivyozidi kuongezeka ndivyo baadhi ya maeneo pia baridi yake ilizidi kuongezeka na kufikia nyuzi hasi therathini , mbaya zaidi baadhi ya maeneo mengine yalikuwa na mito ambayo ilizidi kufanya eneo kuzidi kuwa na ubaridi wa hali ya juu.

Hili ni eneo ambalo raia wa Marekani wamelibatiza jina la No man zone yaani eneo ambalo huwezi kuishi au kumkuta binadamu anaishi na hata wale watalii wanaofika hawakuthubutu kukaa kwa muda mrefu katika eneo hilo kutokana na kuhofia kundi la mbwa mwitu na athari za baridi kali.

Mito ya eneo hio ilioganda na kutengeneza barafu yenye upana mkubwa ilirahisisha sana usafiri wa ndani , kwani watu walitumia kama njia kwa kukanyaga juu yake.

Sasa wakati eneo hilo likiwa tulivu huku sauti za kubweka kwa mbwa zikisikika katika kila baadhi ya pande pamoja na upepo uvumao kwa kasi, kando ya mto mkubwa ulioganda aliweza kuonekana kijana mdogo wa kizungu akitembea ambaye amevaa mavazi ya meusi ya Leather marefu pamoja na gloves huku akiwa amejifunika na ngozi yenye manyoya ya mnyama mwili mzima.

Alikuwa na nywele za rangi ya Zambarau iliofifia huku ngozi yake ikiwa na vidoa doa(freackles) vya rangi nyeusi , ijapokuwa kijana huyo alionekana kuwa wa umri mdogo lakini mwonekano wake ulikuwa ni ule wenye ukauzu na uhatari..

Alikuwa akiangalia kulia na kushotio kwake na kugeuka nyuma akiwa kama mtu mwenye wasiwasi huku akipumua kwa nguvu kiasi cha kusababisha pumzi yake kutoka kama mvuke kutokana na baridi kali.

Ili aweze kutoka katika eneo hilo na kufika bandarini alitakiwa kuvuka mito na milima iliokuwa mbele yake.

Kijana yule alitembea huku akiwa na umakini mkubwa kwa kuyapa kazi masikio yake kusikiliza kwa umakini kwa kila kitu kinachomzunguka huku mkononi panga lake likiwa tayari kwa ajili ya kufanya kazi kwa kitu chochote cha hatari kitakachomtokea.

Kwa mazingira hayo ilikuwa ni ajabu sana kumuona kijana kama huyo kuwa peke yake , kwani eneo hilo lenye milima na mabonde lilitisha.

Alikuwa na wasiwasi sana kutokan na kwamba uwepo wa Theruji pamoja na barafu ndani ya eneo hilo hatua za watu hazikuwa zikisikika vizuri hivyo kama kutatokea adui au mnyama kumsbambulia basi ingekuwa ni kwa wepesi sana.

Kijana huyo ni moja wapo ya kundi la watoto ambao wapo katika mafunzo makali ya ku’survive’ katika mbuga za wanyama wakali , ukiachana na hilo eneo hilo lilikuwa ni la kuwindana yaani ‘ ua au uuliwe’ ndio kanuni iliotumika katika eneo hilo , licha ya kwamba walikuwa wamefunzwa pamoja na wenzake lakini ili kuweza kutoka hapo ni kupambania maisha yako kwa kumuua mwenzako atakae tokea mbele yako au yeye akuue, ndio maana umakini wake ulikuwa mkubwa zaidi kwani hakutaka kufa bali alitaka kuua na kuweza kufanikiwa kutoka.

Kulikuwa na mashimo makubwa juu ya mto ulioganda ambayo yametengenezwa kwa kuchimbwa na watu waliokuwa wakijaribu kuvua samaki chini ya barafu.

Kuna baadhi ya mashimo ambayo yenyewe yalikuwa yamechimbwa na mchimbaji ili kuzuia yasijifunge tena alijaza majani makavu kwa juu na baadhi ya miti miti kuziba.

Hayo yote aliweza kuyafahamu kijana huyo mdogo kutokana na kuwa na mafunzo ya hali ya juu kuishi kwenye maeneo hatari kama hayo.

Wakati akitembea kwa umakini aliweza kufikia katika shimo moja juu ya mto likiwa limechimbwa na kuzibwa na majani pamoja na miti miti huku pembeni ya shimo hilo kukiwa na fimbo(Fishing rod) maalumu ya kuvulia samaki iliokuwa imeachwa na kwa haraka haraka kijana yule aliamini kabisa aliekuwa akivua hapo huenda aliondoka kwa haraka haraka mara baada ya kupata kitoeo.

Haikumshangaza sana kwani alijua ndani ya msitu huo kulikuwa na wenzake wengine.

Kuona kifaa hicho cha kuvulia ilimfanya kupata tumaini la kujijpatia chochote kwani alikuwa na njaa sana , hivyo hakutaka kupoteza fursa ya kuvua ilihali vifaa anavyo.

Aliangalia kulia na kushoto na kuona hakuna mtu aliekuwa karibu na eneo lote limetulia na ilimfanya kutabasamu na kujiambia yupo salama hivyo anaweza kuvua samaki kwa utulivu.

Kijana mara baada ya kutoa majani yale na kuingiza ndoano majini alisubiri kwa dakika kadhaa tu na alijikuta tabasamu likipamba uso wake mara baada ya kuhisi uzito kwenye mti na moja kwa moja alielewa kabisa samaki ashanasa kwenye ndoano yake.

Lakini sasa wakati akijaribu kuvuta kamba nje kumtoa samaki alijikuta akigundua kuna kitu hakipo sawa kutokana na uzito wa kamba ile , lakini wakati akipata ufahamu wa kwamba kuna kitu kipo ndani ya shimo hilo katika mto huo alikuwa amechelewa kwani palepale ulitokea mkono kutoka kwenye maji na kumvuta na ile mikono yake inafusa barafu palepale kisu kilipita katika shingo yake kwa haraka sana kabla hata hajajihami.

Kilikuwa ni kitendo cha sekunde kadhaa tu kijana yule wa Kizungu alikuwa tayari ashapatiwa shambulio la kushitukiza akiwa haamini kama alikuwa amejiingiza katia mtego wa adui.

Ilikuwa ni kama vile kile kifaa cha kuvulia hakikuwa kwa ajili ya kuvua samaki bali kilikuwa kimetegwa kumvua yeye.

Dakika ile wakati kijana akipambania uhai na kifo , sura ya kijana mwingine aliekuwa uchi mwenye ngozi nyeusi aliweza kutokezea kwenye lile shimo kama vile ni samaki aina ya Papa, ilionekana alikuwa ametulia chini ya maji kwa ajili tu ya kumtega adui yake kuingia kwenye mtego wake ambao umemleta mafanikio makubwa.















SEHEMU YA 592.

Yule kijana wa ngozi nyeusi hakujali kabisa kwamba alikuwa uchi na alikuwa akitetemeka kwa baridi bali palepale alimsogelea yule kijana mwenzake aliekuwa akikata Roho na kutafuta mshipa wa damu na kuukata kwa meno yake na palepale kuanza kunyonya damu ya moto kama Vampire.

Katika eneo kama hilo hakuna kitu cha thamani kama damu ya moto na haikujalisha ni damu ya binadamu ili mradi tu iwe ya moto.

Yule kijana wa kizungu hakuwa bado amepoteza maisha na aliweza kushuhudia namna mwenzake anavyo mnyonya damu mpaka uhai wake una tamatika.

“Kijana yule mwenye nywele ndefu nyeusi baada ya kuona ametosheka na damu ya moto, kwa haraka sana alimvua yule mwenzake nguo alizovaa na kukata kipande na kuanza kujifuta maji na kisha akavaa zile nyigine na zilionekana kumkaa vizuri kwani maumbo yao yalikuwa yakilingana.

Ukweli ni kwamba kijana wa kizungu wakati akijiona yupo makini na usalama wake , upande wa kijana huyo wa ngozi nyeusi alikuwa ashamuona muda mrefu sana kwa nyuma yake na ndipo kwa haraka sana alipoamua kumtegea mtego wa kumuua.

Alikuwa na njaa sana kiasi kwamba alijua asingemuua kijana huyo mwenzake na kunywa damu yake asingweza kupitisha usiku kwa njaa hivyo hakuwa na maamuzi mengine tofauti na kumla.

Katika mazingira hayo ambayo hakuwa na ufahamu wa adui yake yukoje kimapambano mbinu pekee ambayo aliona ni rahisi ni kumuwekea mtego ambao una nafasi kubwa ya kufanikiwa tofauti na mapigano ya ana kwa ana, hakujali kama mtego wake ulikuwa ni wa kubahatisha lakini hio ndio njia pekee ambayo aliona inamfaa.

Na hata kitendo chake cha kuvua nguo na kuzitupa ndani ya maji ilikuwa ni kuongeza asilimia za mafanikio kwani aliamini kama atakuwa ndani ya maji na mavazi basi uzito wa kuloana kwa nguo utamzuia katika kushambulia ndio maana alikuwa uchi.

Baada ya kijana yule kuchukua mazoezi kidogo ya kupasha mwili joto palepale alikata pande la nyama kutoka katika mwili wa yule mzungu na kula kwa kutosheka ili mradi kuweza kupata nguvu ya kumuwezesha kuipitisha usiku huo kwa kupambana na chochote kitakachokuwa mbele yake.

Baada ya kuona ameridhika , akakata mapande mengine ya nyama na kuyahifadhia katika mfuko wake kwa matumizi ya baadae.

Na kwa maiti iliobaki aliamua kuidumbukiza mtoni , alifanya hivyo ili tu kutofanya washindani wake waliokuwa ndani ya hilo eneo kufaidika na uwindaji wake, isitoshe kadri washindani wanavyoendelea kufa na njaa na kupungua ndio namna pekee ya kumuwezesha kufanikiwa kutoka na kukamilisha mafunzo yake.

Kula nyama ya bindamu katika eneo kama hilo haikumsumbua sana kwani ni kitu ambacho haikuwa mara yake ya kwanza kufanya , baada ya kuthibitisha mwolekeo ambao anatakiwa kuchukua kupitia miale hafifu ya jua alianza kutembea kutoka nje ya mto huo na kupanda juu ya mlima katika msitu..

“Kupitia jua alifahamu muda si mrefu giza litaingia kwani kwa uzoefu wake alijua muda huo ni saa kumi za jioni.

Kama sio kwa hali ya hewa pengine angekaa na kupumzika na kufurahia kuangalia anga lenye kupendeza bila dalili yoyote ya wingu..

Wakati akiendelea kutembea katika miti ghafla mwili wake wote ulimsisimka na haikuwa hivyo tu aliweza kuchukua hatua za haraka sana kuhepa kidogo kuelekea kushoto na ndio ilikuwa pona yake.

Chuma cha rangi ya Silver kiliweza kupita karibu kabisa na koromeo lake na kivuli cha mtu kiliruka kutoka juu ya mti.

“Ambush!”

Aliwaza kwa haraka akijua hilo ni shambulio la kushitukiza na alifanya haraka sana kutoa siraha yake panga ili kumshambulia adui yake.

Matarajio yake yalikuwa tofauti sana na alivyotegemea , kwani adui yake alioneka kuwa vizuri sana katika kushambulia na na kilichosikika ni kelele za kugongana kwa siraha katika eneo hilo.

Jambo moja tu alilolijua kutoka kwa adui yake kwa kumsoma kwa haraka haraka ni nguvu zake , ijapokuwa alikuwa na ujuzi mkubwa wa kushambulia lakini hakuwa na nguvu za kutosha kama yeye , hivyo alichokifanya ni kutumia nguvu kubwa katika kushambulia ili kimchosha adui yake.

Adui yake alikuwa amevaa Mask kiasi cha kumfanya asimuone sura lakini kadri ambavyo alikuwa akipambana nae akili yake ilimtengenezea ufahamu na kujua anapambana na nani.

“Seventeen!!”

Kijana yule aliweza kubweka kwa hali ya juu na kumfanya yule mtu aliemwita kwa jina la Seventeen kusitisha mashambulizi.

“Thirteen , you are lucky”

Sauti ya kike iliweza kusikika ikimwita yule kijana ambaye alionekana kula nyama ya mtu kwa jina la Thirteen huku akimwambia kwamba ana bahati.

“Tumeweza kupambania maisha yetu katika kambi moja ya mafunzo kule Siberia , hakuna haja ya kuwa mkali hivyo isitoshe haitokuwa rahisi kwa wewe kunishinda mimi , tusipoteze nguvu zetu bure kama tukiendelea”

“Don’t try to cheat me , you have two pieces fo human meat in your sack, so you would still survive even if I don’t”

“Acha kudanganya , una mapande mawili ya nyama kwenye mfuko wako , hivyo utaweza kuishi hata kama mimi nitashindwa”

“Kumbe uliniona?”

“Nimekufanyia shambulio la kushitukika kwasababu nilikuona .”Aliongea na kisha palepale Seventeen mwenye saiu tamu ya kike iliojaa usiriasi alimsogelea Thirteen kwa tahadhari.

“Kwasasa sina chochote chakula na nitakosa nguvu muda wowote kadri muda unavyosogea ni kheri kupambana sasa hivi nikiwa na nguvu kuliko kusubiria kifo changu na wewe wewe kula nyama yangu”

“We almost ate each other in siberia and you want to do it again? Aren’t you sick of it ?”Aliongea akimaanisha kwmaba kidogo tu wakulane nyama walivyokuwa Siberia , je hajachoka tu.

“Nitakupa machaguo mawili , nipe chakula nile nishibe au tupambane?”Aliongea huku akiwa siriasi mno na kumfanya Thirteen kutabasamu kifedhuli.

“Kwanini nifanye hivyo unaonekana kabisa unazidi kuchoka na kuwa dhaifu , ninaweza kukuua tu na kula nyama yako , muda huu tofauti na kupamba na mimi angalau ungetafuta hata minyoo chini ya miti na kula, angalau ungweza kuokoa maisha yako”

“Acha ujinga Thirteen , najua sikuwezi kwenye mapambano ya ana kwa ana katika ardhi ilionyooka lakini spidi yangu na wepesi ni kubwa kuliko wewe , unaweza usifanikiwe kunishinda kwenye ardhi kama hii yenye miinuko”Aliongea huku na yeye akitoa tabasamu la kejeli.

“You’re feisty”Aliongea.

Ukweli ni kwamba Thirteen hakuwa akiogopa kupambana nae lakini alijua kabisa kupigana nae hapo hakutokuwa kwepesi hata kidogo kwani aliujua uwezo wa Seventeen ulikuwa ukikaribia na wa kwake na kama ni kumshindana labda ni kutokana na udhaifu wake wa kuwa mwanamke na yeye kuwa mwanaume.

Seventeen hakutaka ubaridi kuendelea kumuathiri mwili wake na kumnyong’onyesha na palepale alimpiga ngumi ya kushitukiza Thirteen , lakini upande wa Thirteen alionekana kuwa mwepesi kwani palepale aliikwepa kwa kupiga sarakasi kurudi nyuma na kujificha na Seventeen hakutaka kumuacha kizembe kwani hapo anapambania maisha yake na walianza kushambuliana kwa kasi kwa kuoteana kutokana na kwamba kulikuwa na miti ambayo walikuwa wakiitumia kama ngao.

Katika hali kama hio Seventeen ndio ambaye alionekana kushambulia zaidi kwa spidi huku Thirteen yeye akijaribu kukinga mapigo yake.

Upande wa Seventeen alijua kabisa kama ataendelea kupambana kwa muda mrefu basi itafikitia muda atakuwa hana nguvu hivyo atampa nafasi Thirteen kumua jambo ambalo hakuwa akitaka litokee kabisa.

Lakini wakati wakiendelea kufukuziana kwa kushuka na kupanda katika eneo hilo ambalo lilikuwa na miinuko na mabonde , ghafla tu walikuja kusimama mara baada ya kusikia ngurumo kubwa za mbwa mwitu.

“A wolf?!?”Alishangaa Seventeen akiuliza.

“No, it’s wolf Pack”Aliongea Thirteen akimaanisha kwamba ni kundi la mbwa mwitu.

Muda huo ngurumo hizo zilianza kusikika kwa kuwasogelea kwa tahadhari sana na kabla hata hawajajiandaa kujua namna gani ya kukabiriana na hali hio, ghafla tu mbwa mwitu hao waliruka kutoka walipojificha na kusimama mbele yao.

Alaska ndio eneo ambalo lilisifika kwa uwepo wa Mbwa mwitu ambao walikuwa wakitembea kimafungu na kutokana na eneo hilo waliokuwepo kuwa la tambrare tofuti na maeneo mengine basi ndio makazi yao.

Seventeen na Thirteen moja kwa moja walijua hapo wapo katika hatari wakiangaliana na macho ya rangi ya njano na nyekundu kutoka kwa mbwa hao.

“Kuna zaidi ya mbwa mwitu hapa zaidi ya therathini , nadhani ni zaidi pia kufikia mia moja , tupo kwenye hatari kubwa”Aliongea Thirteen huku akitoa tabasamu la uchungu.

Seventeen alichukua hatua moja kurudi nyuma na kisha akamwangalia Thirteen.

“Unaweza kukimbia ?”Aliuliza.

“Unatania nini? Unadhani tunaweza kushindana katika mbio na mbwa mwitu , miguu yao inapanda hata milima kama vile wanateleza kwenye barafu , hapa mbinu pekee ni kupanda juu ya miti la sivyo miguu yetu itang’atwa muda tu ambao tutaamua kukimbia”Aliongea Thriteen lakini Seventeen mwenekano wake haukubadilika.

“We only have one way out of this since we can’t run away , kill the Wolves with me , us working together is our only chance to survive”

“Tuna njjia moja tu kwasababu hatuwezi kukimbia , tushirikiane kuua hawa mbwa mwitu , sisi kufanya kazi kwa pamoja ndio njia pekre hapa ya kuishi”

“Hehehe , mrembo ni muda huu huu tu ulitaka kuniua na sasa hivi unataka tufanye kazi pamoja? , unafikiri ninaweza kukuamini kirahisi hivyo”Aliongea Thriteen huku akiwa na mwoneknao kama vile hakujali kilichokuwa mbele yake , ijapokuwa mbwa mwitu hao walikuwa wengi lakini kwake hakuwa na ule woga wa kutisha.

“Huna chaguo lingine , unatakiwa kujua tofauti iliopo hapa kama wewe sio minga, tuue hawa mbwa mwitu na nitaweza kupata chakula na sitohtarisha maisha yangu tena kupigana na wewe”

Baada ya kuongea vile palepale Thirteen aliingiza mkono wake kwenye mfuko wake na kisha akatoa kitu ambacho kilikuwa na nyama nyana zilizoning’inia na kumpigia mluzi Seventeen na kumrushia.

“This is..”

“Ni jicho lake hilo , Protini zilizopo ndani ya jicho ni nyingi zaidi kuliko nyama , meza hilo kujaza tumbo lako, tutawakaanga hawa mbwa mwitu baada ya kuwaua wote”Aliongea Thirteen akimaanisha kwamba ni jicho la yule mzungu.

Seventeen mara baada ya kuambiwa hivyo hakutaka kusita sita kwani palepale alilipeleka jicho lote mdomoni na kulitafuna mara chache na kumeza na kumfanya Thriteen kumwangalia kwa tabasamu.

“You are Fierce but I like it … let us get to work”Aliongea akimaanisha kwamba yeye ni mkali lakini anapenda hivyo na waingie kazini sasa

Mbwa mwitu walizidi kusisimika mara baada ya kunusa harufu ya damu kutoka mdomoni mwa Seveteen ambaye alikuwa akitafuna jicho la binadamu mwenzake.

Kushambuliwa na kundi la mbwa mwitu ilikuwa ni kama ndoto kwao kwa muda huo ambao miili yao ilikuwa na nguvu za kawaida za kibinadamiu katika kupigana.

Baada ya mbwa mwitu wa kwanza kumrukia Thirteen kwa ajili ya kumshambulia alikwepa kwa kuinama na likapita juu lakini na kwa wepesi zaidi aliinua kisu chake na kulichoma tumboni kwa kuchana.

Kisu chake kwa namna kilivyyoweza kukata nyama na kugusa mifupa ya mbwa mwitu huyo kilifanya sauti za maumivu kutoka kwa mbwa kusikika huku damu nyingi ikimwagikia Thirteen kwenye uso wake, ilikuwa ya moto na yenye kutoa harufu.

Mguno wa maumivu kutoka kwa mbwa mwitu mwenzao mara baada ya kufikia masikio ya wale mbwa wengine iliwainua na kuanza kushambulia wote kwa pamoja.

Kabla hajatoa kisu chake kutoka katika tumbo la mbwa mwitu aliemchoma , alifunikwa na mbwa wengine waliokuwa wakimshambulia katika maeneo mbalimbali ya mwili wake , kwenye tumbo , kichwa, miguuni na mikononi.

Upande wa Seventeen alivuta hewa nyingi na kuitoa na kisha alisogelea wale mbwa mwitu na kuanza kushambulia.

Ili kumuua mbwa mwitu ulitakuwa kulenga katika menno ambayo ni dhaifu kwao na kuyachana kwa haraka sana bila kufikiria na ndio ambacho alikuwa akifanya , alikuwa akiwafyeka kwa spidi kubwa na ustadi huku akipotezea majeraha ya mikwaruzo kutoka kwa kucha na meno ya mbwa mwitu hao.

Ilikuwa ni afadhali aliokuwa amevaa ngozi ya kuzuia baridi hivyo kupunguza majeraha , Seveteen aliendelea na kasi yake huku akilenga zaidi katika macho ya wanyama wale kwa spidi kubwa.

Kitendo cha mbwa wale kushambuliwa kwa kukimbia kulifanya mawe yaliokuwa juu kuwadondokea na kuwafanya kushindwa kubalansi miili yao na iliwafanya kupata wakati mgumu kwenye kushambulia na ndipo walipoamua kushambulia wakiwa wamekaribiana.

Ndani ya madakika mbwa mwitu ishirini tu ndio ambao walibakia huku waliokufa wakiwa ni wengi zaidi.

Seventeen na Thirteen walikuwa wametapakaa damu huku ikiwa ngumu kujua kama ilikuwa ni damu ya mbwa yupi kati yao.

Mbwa wale mara baada ya kuona wenzao wengi wameuliwa walijikuta wakipunguza spidi ya kushambulia na ilifikia hatua sasa walianza kuangaliana kwa macho makali na baada ya akili zao kuwapa ufahamu wanaopambana nao ni hatari kwao waliamua kukimbia na kuwafanya Seventeen na Thirteen kuweza kupatwa na ahueni.

“Hatimae tuna nyama ya kutosha sasa , lakini itakuwa ngumu kuwasha moto na kuwachoma , unaonaje tukiwala hivi hivi?”Aliuliza lakini Seventeen hakutoa jibu na alijaribu kusogelea maiti moja ya mbwa kutaka kuishika lakini Thirteen aliona jeraha katika mkono wa Seventeen na kupeleka mkono kugusa lakini matokeo yake ni kwamba kama sio wepesi wake kisu cha seventeen kingekata shingo yake, aliambulia kukatwa kidole chake tu kutokana na kukwepa shambulizi.

“Unafanya nini?”Aliuliza Thirteen kwa hasira.

“Kwanini umenigusa?”Aliuliza kwa macho makali Seventeen akiwa hana utani na macho yalikuwa yamejaa nia ya kuua tu, alionekana alikasirishwa sana na kitendo cha Thriteen kutaka kumgusa.

“Nilitaka kuangalia jereha lako , kwasababu nguo zako zimechanika angalau unapaswa kujitibu kabla hujapata maambukizi , kwasasa huhisi maumivu kwasababu ya mkono wako upo na Ganzi”Aliongea na kumfanya Seventeen kumwangalia kwa macho ya mshangao huku akichukua hatua moja nyuma kujiweka mbali na Thirteen na kisha aliangalia mkono wake na hapo ndipo alipojua alikuwa ameng’atwa na Mbwa na alikuwa na jeraha kubwa linalotoa damu.

Licha ya jeraha hilo kuwa kubwa lakini kwa Seventeen ilikuwa kawaida na asingweza kulia kama wanawake wa kawaida.

Wakati giza likizidi kuwa kubwa Thirteen hakuonyesha kujali t tena kinachoendelea na alianza kuchuna ngozi ya wale mbwa mwitu na kuanza kula hivyo hivyo nyama mbichi na muda wote Seventeen alikuwa akimwagalia.

“Kwanini umenikumbusha kuhusu jeraha langu?”Aliuliza akiwa siriasi kama vile kilikuwa kitendo ambacho hajapenda.

“Nisingwez kuwaua mbwa wote nikiwa mwenyewe , umenisaidia sana , isitoshe kwasasa nakuona huna nguvu za kutosha kushidana na mimi, hakuna tatizo nikionyesha kukujali , huenda tunaweza kuwa marafiki”

“Sihitaji unijali wala kuwa rafiki yako mimi’Aliongea kwa ukauzu mkubwa na kumfanya Thirteen kutabasmau na kisha kumuonyesha kidole chake alichokata.

“Una hasira za karibu sana, kwani ni vibaya mimi kukujali?”Aliuliza.











SEHEMU YA 593.

Mwanga wa taa ya kitandani ulikuwa ni hafifu sana lakini waliweza kuonekanavizuri , mmoja alikuwa akisimulia na wengine wawili wakisikiliza stori hio yenye kutisha kwa umakini mkubwa kwa zaidi ya lisaa lizima.

Roma alikuwa ashasimulia kiasi cha kubadili pozi lile ambalo alikuwa ameweka katika kuegamia mto na sasa alikuwa amekaa huku akiwa amekunja miguu yake , alikuwa ni kama vile yupo kwenye uhalisia wa maisha yake yaliopita na hata kusahau kabisa kama muda huo alikuwa akimsimulia Lanlan.

Hakuweza hata kuelewa kama Lanlan alikuwa ashapotelea usingizini muda mrefu katika mto akijizungusha zungusha na kutafuna kama vile kuna kitu ambacho kimewekwa katitka mdomo wake.

Sio kwamba alikuwa hapendi stori yake , ukweli ni kwamba kulikuwa na vitu vingi sana kwake kama mtoto kuvifikiria ndio maana aliweza kupotelea usingizi kwa haraka.

“Lanlan unajua nilitaka kumwambia nini , nilitaka kumwambia Seventeen aache maigizo , alionekana kabisa alikuwa mpweke na pia alikuwa na aibu , lakini hakuna ambae alikuwa akitujali kwa hali ambayo tunapitia , nilikuwa na Master wangu ambaye alinifundisha Kung fu alikuwa akinijali sana na aliniambia maneno machache ya kuweza kuongea ili kunasa moyo wa mtu , ukweli ni kwamba sikuwa hata siriasi kivile lakini alichonijibu kilinifanya kujisikia vibaya na baada ya usiku ule kila mtu aliondoka kivyake”Aliongea Roma kana kwamba Lanlan bado alikuwa akimsikiliza hakujua kama alikuwa ashalala.

“Lanlan hivi unajua ni jibu gani aliniambia mara baada ya kumuuliza kama ilikuwa vibaya kwa mimi kumjali?”Aliongea Roma na ndio muda ambao aligeuza macho yake kumwangalia Lanlan na aligundua Lanlan hakuwa akimsikiliza na amekwisha kulala na kumfanya kidogo kujisikia vibaya kwani alikuwa akijaribu kuelelzea hitoria ya maisha yake licha ya kwamba Lanlan alikuwamoto.

“Tafuta wasichana wengine wa kuwajali kwani hawawezi kukufanyia kama mimi kwa kukukata kidole na kisu changu”Sauti pembeni ya Roma iliweza kujibu , Sentensi hio kwenye maisha yake haikuwahi kufutika katika akili yake kwa miaka mingi , lakini katika hali na mazingiraambayo hajayategemea anaisikia kwamara nyingin.

Sauti hio ilikuwa ikifanana kwa kila kitu na aliosikia kipindi kile , haikuwa sauti tu lakini pia hisia zilizoambatana na sauti hio ni vilevile.

Roma alijikuta akipanua macho yake na kumwangalia mwanamke ambaye alikuwa amelala pembeni yaLanla , alikuwa na uhakika kabisa aliongoea hivyo ni Edna.

Ni kweli aliejibu swali la Roma ni Edna na kwa muda huo ni kama mtu ambaye alikuwa kwenye mawazo makubwa ya maisha yake yaliopita na muonekano wake ulimuonyesha kama vile ni mtu ambaye amepitia magumu mengi.

Yaani alichokuwa akihadithia Roma kwa upande wa Edna ni kama vile stori hio ilikuwa ikimuhusu yeye kabisa.

“Edna ume,, umejuaje alinijibu hivyo?”

Aliongea Roma huku akiwa kama vile sio mwenye kuamini kile alichosikia kimeweza kutoka katika mdomo wa Edna.

Edna sasa alielewa ameongea kitu ambacho hakuelewa ameongea nini na alimwangalia Roma kwa mwonenao usiokuwa wa kawaida.

“Hubby kwanini unanniangalia hivyo kwa kushanga?”Aliuliza Edna huku akiwa kama vile haelewi kinachoendelea na kumfanya Roma kumeza mate mengi kujiutiliza..

“Nakuuliza umejuaje alijibu hivyo?”

“Mwenyewe sijui chochote , umeuliza swali na mimi jibu likanijia kwenye akili yangu bila kujielewa , kwani nimejibu kama alivyojibu yeye?”aliuliza Edna mwenyewe akiwa kama amechanganyikiwa.

Upande wa Roma alijiambia huenda alikuwa akiwaza sana ndio maana, kwani mwonekano wa Edna ulikuwani ule wa kutolewa kitu, alijiambia huenda kwasababu Edna na Seventeen walikuwa mapacha kuna uwezekano wa wao kuwa na mawazo yanayofanana.

Ijapokuwa alijihisi kuna kitu hakipo sawa kuhusu Edna na namna alivyomjibu lakini hakutaka kuuliza zaidi

“Naona unafurahia mwenyewe kumsimulia binti yako jinsi ulivyoweza kukutana na Ex wako?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma kujisikia vibaya kidogo pamoja na aibu.

“Babe wife sikudhamilia hivyo , nitakuwa mwangalifu siku nyingine”Aliongea Roma.

*******

Hoteli ya Sherati ndani ya jiji la Kigali ilikuwa nje kidogo na jiji hilo , ni rahisi kusema ni hoteli ambayo imejengwa katika eneo ambalo limejitenga na mji ili kupata eneo kubwa na mandhari ya msitu.

Hoteli hio hupendelewa sana na viongozi wa kisiasa na baadhi ya mtajiri kufanyia sherehe hapo na mikutano , hio yote ni kutokaa na kwamba ilidizainiwa kwa mtindo wa kiusalama sana na ilikuwa na kumbi kubwa za kukirimu sherehe kubwa za watu mbalimbali mashuhuri.

Raisi Jeremy hakuwa mtu wa kupenda sana kutoka ikulu na kwenda kuhudhuria sherehe za kimwaliko mbali na ikulu yake kwani kulikuwa na umbali mrefu ukijumlisha na msururu wa magari yake basi huleta shida ya kiusafiri katikati ya jiji na kusababisha msongamanio wa takribani dakika ishirini.

Lakini hata hivyo kutokana na mtu aliemwalika katika hafla fupi alikuwa ni balozi wa Ujerumani na rafiki yake sana hakuwa na namna ya kukataa kuelekea huko ndio maana taarifa zake za kufika kuhudhuria zilikuwa zikijulikana ndani ya hoteli hio na protokali za kiulinzi zilikuwa zishaanza kuchukuliwa kabla hata ya muda wa kuanza safari ya kutoka Ikulu.

Kama raisi chakula chake kilikuwa kikiandaliwa tofauti sana na kwa umakini mkubwa na ndio maana hata wapishi maalumu wa raisi walikuwa washaagizwa ndani ya hoteli hio kuandaa pamoja na kuonja , ijapokuwa chakula kilikuwa kilekile ambacho kinaandaliwa katika hafla hio lakini cha kwake kidogo kilikuwa na utofauti kimaandalizi .

Kwa kiongozi mkubwa wa nchi ilimaanisha kutokuwa huru na baadhi ya vitu ndio maana alikula kila kilichoandaliwa kwa utaratibu maalumu.

Saa mbili kamili za usiku alikuwa tayari ashafika katika hafla hio na hata hatua za mwanzo za hafla hio zilikuwa zimekwisha kufanyika na sasa watu mbalimbali waliohudhuria walikuwa wakipata chakula cha usiku.

“Mheshimiwa karibu sana kufurahia chakula chako”Aliongea mhudumu mara baada ya chakula chake kuhakikishwa.

Raisi Jeremy alikuwa amekaa kwenye meza ambayo ilikuwa Imezungukwa na watu wachache huku ikiwa na vyakula mbalimbali.

Wakati kama huo alijikuta akikumbuka maisha yake ya nyuma , wakati kama huo angetakiwa kuwepo hapo na mke wake huenda hata mtoto wake na hakuna mtu ambaye angeweza kumwangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida.

Tokea familia yake kuanza kusambaratika kulikuwa na maneno mengi ya chini chini ya yaliokuwa yakiongelewa kuhusu yeye , ijapokuwa hakupenda lakini ilikuwa ni ngumu kuwazuia watu kuongea kile wanachojisikia.

Hata hivyo ni yeye ambaye alikuwa amemuua mke wake mwenyewe na katika hali hio imemfanya hata mtoto wake wa kiume ambaye alikuwa akitarajia kuwa mrithi wake kumchukia na kutengeneza uadui.

Mawazo kuhusu familia yake na maisha yake yalivyokuwa miaka kadhaa nyuma yalipita katika akili yake kwa muda mfupi sana na kupotezea.

Wakati mheshimiwa Jeremy akiwa katika hafla hio akila na kuongea na baadhi ya watu waliokuwa kwenye meza yeke , upande wa walinzi wake kutoka miliki ya kijini hawakucheza mbali , walikuwa mita kadhaa kutoka alipokuwepo na walikuwa wakihakikisha hakuna kitu chochote kibaya ambacho kinaweza kumpata raisi huyo na kupelekea mipango yao hapa duniani kuvurugika ndio maana walikuwa tayari kumpa ulinzi kwa namna yoyote ile.

Raisi Jeremy alikuwa akijua sana kuhusu maswala ya kuvuna nishati za mbingu na faida zake katika kurefursha maisha , na kwa nafasi yake hio ya uongozi huenda angependa kuishi miaka mingi zaidi kuongoza lakini kwa sababu ambayo hakuwa akiilewa hakupenda kabisa kujifunza na hata kuulizia kuhusu namna nishati hizo zinavyovunwa.

Mheshimiwa Jeremy aliweza kudumu katika hoteli hio kwa masaa zaidi ya matatu na kisha muda wake hapo ulifikia tamati na kurejea kwenye gari kurudi katika makazi yake.

Siku hio ilikuwa ni ijumaa na inaingia Wikiend na kama kawaida kila inapofika Wikiend hakupenda kukaa katika ikulu kubwa na alipendalea kuishi katika nyumba yake ya mapumziko, hivyo safari ya kutoka hoteli hio ni moja kwa moja mpaka State Area D .

Safari nzima haikuwa na tishio lolote la usalama na aliweza kufika vizuri ndani ya jumba hilo maarufu ndani ya jiji la Kigali na ulinzi ulikuwa tayari ushaimarishwa muda mrefu.

Mara baada ya kurudi katika hilo mapumziko la raisi hakutaka kufanya kitu kingine zaidi ya kujipumzisha kwani muda ulikuwa umeenda sana.

Sasa akiwa chumbanni kwake akijiandaa kulala aliweza kugongewa mlago na kumfanya kidogo kukunja sura kwani haikuwa kawaida kwa wakati kama huo kusumbuliwana wafanyakazi wak.

‘Nani!!?”

Aliuliza kwa nguvu lakini ajabu ni kwamba hakuna sauti ambayo ilisikika kutoka nje kwa zaidi ya dakika kama mbili hivi na kuzidi kumshangaza lakini mara baada ya kukatashauri kwenda kufunguaajue nani anagonga mlango ulifunguliwa kwa nguvu.

Alijikuta akishangaa mara baada ya kuona mtu aliekuwa akiingia ndani alikuwa ni Mtoto wake wa kiume Desmond akiwa ametangulizana na mwanamke mrembo.

Alijikuta akihisi kuna kitu kinachoendelea kwani hata walinzi hawakumzuia kuingia na mbaya zaidi mwanamke huyo hakuwa akimjua na ilikuwa sio kawaida kwa Demsond kuingia chumbani kwake na mwanamke kama hivyo.

“Desmond unafanya nini ?”Aliuliza Raisi Jeremy kwa hofu huku akimwangalia yule mwanamke , alihisi mwanamke huyo alikuwa akimjua licha ya kwamba hakukumbuka ni wapi alimuona.

“Desmond huyo ni nani na walinzi wako wapi?”Aliuliza .

“Kuwa na amani , wamekufa vifo vya amani sana”Aliongea yule mwanamke kwa kujiamini.

“Wewe ni nani ?”Aliuliza Jeremy na dakika chache tu kuna kitu kilimjia , alikumbuka maelezo ya Linda wakati uchunguzi wa kumtafuta Joseph Bikindi ukifanyika katia chuo cha Rwanda baada ya kupotea kwake.

“Hubby tulioana kwa miaka mingi sana , usiniambie hunikumbuki mke wako”Aliongea Kizwe na kumfanya Raisi Jeremy kupatwa na mshutko huku macho yakimtoka.

“Ni… ni wewe!!”

“Hahaha… ushanifahamu sasa , Jeremy najua ulikuwa ukinitafuta sana lakini umeshindwa kudhania kama siku nitajileta mwenyewe”Aliongea Kizwe kwa dharau.

“Mama hebu acha maneno mengi , si unaona anataka kujikojolea”Aloiongea Desmond.

“Mwanaharamu wewe , unapata wapi uthubutu wa kupanga njama na huyo malaya”Aliongea Jeremy huku sasa akielewa kile kitendawaili cha kupotea kwa Demsond na kuonekana kwa ghafla hatimae kimeteguka na anajua sasa alikuwa akifanya kazi na mwanamke anaejinasibu kuwa mama yake , ijapokuwa mwanzoni hisia zake zilikuwa zikimwambia hivyo lakini bado alikuwa na mashaka.

Alianza kujilaumu na kusema ni kheri kama angezichukulia hatua hisia zake na kuhakikisha ana mdhitbiti.

Ukweli ni kwamba aliamini angekuwa salama bila ya kumdhibiti Desmond kutokana na uwepo wa Nix na Gesha lakini kwa muda huo alishindwa hata kujua nini kimetokea mpaka jumba lake hilo lenye ulinzi imara kuvamiwa kirahisi tena muda mfupi tu mara baada ya kurudi.

“Mmewafanya nini Nix na Gesha , hapana, haiwezekani, nyie wawili hamna uwezo wa kuwashinda”Aliiongea huku akizidi kurudi nyuma kusogelea kabati la nguo.

“Hatuna uwezo wa kushidana nao ndio lakini haimaniishi kwamba hakuna mtu wa kuwashinda , Jeremy wewe ni mtu wa mahesabu sana na nakusifia kwa hilo lakini siku zote utabakia kuwa binadamu tu ambae umezaliwa na madhaifu “

Raisi Jeremy alijikuta akimeza mate mengi huku mwili wake akishindwa kuuzuia kutetemeka kwa kuangalia chuki iliokuwepo katika macho ya mwanamke aliekuwa mbele yake.

Wakati akiwa anaomba Nix na Geisha kutokezea , kulitokea kishindo kizito katika paa na kufanya nyumba yote kutetema na ile anasikia kishindo kingine kutoka eneo la nje ya chumba chake , hatimae aliweza kumuona Nix na Gesha wakidondoka chini wakionekana kuna kitu kimewapiga ..

Muda huo huo wakati eneo hilo likitawaliwa na vumbi la kutosha aliweza kuonekana Denisi aliekuwa ameshikilia kitu cha kung’aa kama kitenesi mkononi.

“Denisi!!!”Alijikuta akiongea kwa mshangao mara baada ya kumuona Denisi.

“Mheshimiwa Raisi , umekosea mimi sio Denisi”Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy akili yake kufanya kazi kwa haraka.

“Kama wewe sio Denisi … Lekcha,, I mean Joseph”Aliongea huku sasa akianza kuelewa kinachomtokea usiku huo na kuweza kufahamu kwanini Denisi alihusika katika taarifa za kuchafua amani ndani ya taifa la Tanzania , kumbe hakuwa Denisi bali ni Joseph Bikindi

“Wewe mtumwa wa fikra , nilikusamehe kipindi kile nikakuacha hai , lakin leo hii umerudi na unataka kunidhuru?”

“Mhehimiwa Raisi unapaswa kunishukuru sijajibadilisha na kuwa wewe, nimekuwa na hruuma sana kwako lakini ndugu zako wapo hapa kwa ajili ya kulipa kisasi”

“Mwanaharamu!!”Aliongea kwa sauti kubwa.

Muda huo huo Nix na Gesha walijitahidi kuamka baada ya kupigwa pigo takatifu lakushitukiza , sasa walianza kuita Dhana zao za kijini kwa ajili ya kupambana.

“Nyiwe watu bado tu mpo hai na hamjakata tamaa?”Aliongea Lekcha huku akiwangalia kwa tabasamu la kejeli.

Nyumba ya Area D ilikuw imejengwa kama hoteli , ilikuwa ni jengo ambalo halipo katika mfumo wa gorofa , ilikuwa imejengwa na madirisha makubwa kama mlango ya vioo ili kuweza kumpa nafasi mtu kuona mandhari yote ya nje.

“Mwanga wa Dhahabu wa kiroho”

Aliongea kwa nguvu Nix na sauti yake ile ilisikika vizuri katika masikio ya Lekcha na palepale alipotea na kilichosikika ni mpasuko wa vioo vya dirisha nyuma ya Raisi Jeremy na kutokea nje kabisa.

Nix na Gesha hawakutaka kuchelewa walifuata huko huko na Lekcha ile anakuja kutua kwenye bustani aishambuliwa na Dhana ambayo ilikuwa ikitoa mng’ao wa mwanga rangi ya Dhahabu , ilikuwa ni kama vile mwanga wa Laser ambao ulitoboa katika kifua chake eneo la moyo ni shambulizi ambalo lilitokea kwa Nix na muda huo huo na Gesha hakutaka kuchelewesha kwani palepale alituma upanga ukatao kuwili wa kimaajabu na kabla hata Lekcha hakufanya chochote kwani shingo yake ilichanwa na panga lile huku eneo la kifuani likutengeneza tundu.

Pigo la Nix na mwenzake lilionekana kufanikiwa na waliamini asingweza kupona kwa namna walivomwadhibu lakini sekunde hio hio walijikuta wakipagawa mara baada ya Denisi kupona kwa haraka sana huku kila damu iliokuwa imetoka ikiwa kama vile imeganda hewani kuanza kumrudia kwa kasi sana.

“Inaonekana kabisa nguvu zenu za kijini hazitoshi nimejifunza sana kuhusu namna mnavyoshambulia , lakini niwaambie tu hakuna kitu cha kawaida ambacho kinaweza kunidhuru”Aliongea Lekca kwa kejeli huku akiokota lile panga na kuliyeyusha palepale na Ant- materr.

Gesha na Nix walijikuta wakipagawa kwa kitendo kile. Kwani hakuna ambaye alitegemea siraha ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa muunganiko wa moto wa rangi nyeupe na nguvu za ziada za kijini imeweza kuyeyushwa kirahisi namna hio..

Baada ya Lekcha kumaliza kuyeyusha ile siraha aliwageuka Kizwe na Desmond waliokuwa wakimwangalia kutoka ndani.

“Fanyeni haraka kama mnataka kufanya maongezi na Raisi Jeremy , nitajibadilisha kuwa yeye nikishamalizana na hawa”Aliongea Lekcha kwa sauti na palepale Lekcha alibadirika na kuwa kama sanamu la chuma cha kung’aa kama bati na kupaa juu angani kuwasogelea Nix pamoja na Gesha ambao walionekana kumsubiria na ile anawakaribia alitengeneza shoti za umeme wa rangi ya kung’aa kama radi na kuwashambulia lakini Nix na Gesha walijaribu kukwepa nyuzi nyuzi zile za shoti zilizokuwa zikiwasogeea na kukimbialjuu zaidi angani.

Nix na Gesha walijua kabisa hawana uwezo wa kushindana na adui yake kwani alionekana kuwa na nguvu zaidi nje ya matarajio yao , kitu pekee ambacho waliona wanaweza kufanya ni kujikinga na mashambulizi yake , kwani hawakuelewa mbinu ya kuweza kumshambulia ilihali hakuonekana kama binadamu.

Mara baada ya ngao waliojitengeneza kugusana na nyuzi zile za shoti walijihisi nguvu zao ni kama vile zinafyonzwa na waliweza kupata ufahamu adui yao anatumia nishati isiokuwa na aada ndio maana wananynywa.

Nix na mwenzake mara baada ya kuona hatari hio palepale waliweza kupaa kwenda juu zaidi angani na kisha akaachia msisimko mkubwa wa nguvu za kijini pasipo kueleweka wanafanya nini.

Lekcha hakujua ni kitu gani wanajaribu kufanya , ila hakujali sana katika kichwa chake alitaka kushinda tu na aliona adui yake hakuwa na mbinu za kumzidi.

Lekcha palepale alianza kutumia kumbukumbu za Yan buwen alizoziunganisha na ubongo wake kwa kutumia Biochip , alichukua zile muhimu tu kwa ajili ya kujua namna ya kupambana na nguvu kubwa ya Ant-matter energy.

Pale pale aliweza kuona kitu ambacho Yan Buwen alikosea wakati akiwa ana pambana , alijiambia hapaswi kuficha jiwe la kimungu ndani ya mwili wake bali anapaswa kulitumia katika mashambulizi na yeye kujibadilisha kuwa nguvu yenyewe.

Upande wa Kizwe hakutaka kupoteza muda kwani alijua kusambaa kwa kiasi kikubwa cha nguvu ya kijini kunaweza kumshitua Roma licha ya umbali mrefu uliokuwepo kati ya Iringa na Rwanda..

“Jeremy utanisamehe sana , nipo hapa kwa ajili ya kukurudishia maumivu ulionisababishia”Aliongea Kizwe na hakutaka kuchelewa kwani palepale alimsogelea Raisi Jeremy kwa spidi huku akidhamiria kumpiga na kigoti eneo la tumboni lakini wakati anamkaribia tu kulitokea mwanga mkali kama wa radi na kumzingira Raisi Jeremy na palepale Kizwe alipigwa na wimbi la upepo usiokuwa kawaida na kwenda kutua kwenye ukuta, akiwa haamini kilichomtokea na huenda angekuwa binadamu wa kawaida ingekuwa ndio mwisho wake .









SEHEM YA 594.

Kizwe alijikuta akiwa kwenye mshangao bila ya kuelewa nini kimekukumba kwa ghafla namna ile na hakuwa yeye tu hata kwa Desmond mwenyewe hakutegemea hilo kutokea.

“Nini kimetokea..?”Alijikuta akiuliza huku akimwangalia Jeremy na hata Lekcha ambaye alikuwa kwa nje aliweza kushuhudia kitu hicho na alishindwa kuelewa nini kinaendelea.

“Mnaonaje , nadhani hamjafikiria kuhusu hiki kutokea , Kizwe wewe ni mjinga sana unajiona unanifahamu sana kwasababu n tulishawahi kulala kitanda kimoja si ndio? , Mimi Jeremy sio wa kawaida kama unavyofikiria na kuona kwamba unaweza kuniua kiwepesi, nimezaliwa kwa mchanganiko wa jamii mbili tofauti”Aliongea kwa jeuri huku akiwa ndani ya duara la mwanga mweupe unaomzingira kama ngao na palepale alitoa cheni yenye kidani kikubwa sana cha duara na kumfanya Demsond ajue nini kinamlinda baba yake..

“Pumbavu kabisa analindwa na dhana ya kijini”Aliongea Demsond kwa mshangao , aliweza kujua kwa haraka kwani ilikuwa ni kama mara ya pili wanakumbwa na kitu cha kushitukiza kama hicho , mara ya kwanza iliweza kutokea kwa Edna wakati walipokuwa wanataka kumshambulia.

Ukweli haikuwa mara ya kwanza kwa Desmond kuona hiko kidani baba yake akiwa amekivaa na katika maisha yake hakujua kina maana gani , lakini kwa kile kilichokuwa kimetokea hapo ndio anaelewa kwamba hakikuwa kitu cha kawaida kabisa ndio maana baba yake hakuwahi kumuona akikivua kabisa tokea aweze kujielewa kama mtoto.

Ni kidani flani cha madini ya Dhahabu ambacho kilikuwa na mchoro wa mnyama ambaye hakuwa akieleweka alikuwa ni mnyama wa aina gani.

“Hii sio dhana tu kama mnavojua, pia hutumika kama king’ora kuwajulisha watu wa ukoo wa mama yangu katika miliki za kijini na kuwaka kwake ni kutokana na kuhisia nipo hatarini hivyo lazima kitakuwa kimetoa taarifa tayari kwamba nipo kwenye hatari na muda wowote wanajeshi wa miliki ya kijini ya Panas watafika , je bado mnataka kuendelea kubakia”

Nix na mwenzake walimwangalia Jeremy na walijikuwa wenyewe wakishangazwa na jambo hilo kwani hawakuwahi kusikia , hawakujua kama Jeremy alikuwa na Dhana kwenye mwili wake ameivaa na sasa baada ya kuiona kwa macho yao ya kijini waliweza kuifahamu.

“Jeremy hio ni Golden Toad Amulet?Hahaha.,, kazi nzuri sana Jeremy, hio dhana katika jamii yetu inatumika kama kifaa cha kumlinda mkuu wa ukoo na inatumika kwa dakika therathini tu kila baada ya miezi mitatu, kwa umbali uliopo kati ya Panas na hapa nina uhakika wenzetu wenye uwezo zaidi watafika ndani ya dakika kumi na tano, ni kheri kama mtaondoka kama hamtaki kuuliwa”Aliongea Nix

Desmond na mama yake walijaribu tena kumsogelea Jeremy kwa ajili ya kumshambulia , lakini waliambulia patupu kwani kuna nguvu kubwa ambayo ilikuwa ikiwasukuma kuwarudisha nyuma kabla hata ya kuufikia ule mwanga unaomzunguka Jeremy.

Ilikiuwa ni kama kilichowatokea kule Tanzania wakati wakimshambulia Edna na walijikua wakiwa katika hali ya kutoamini kitu kama hicho kingetokea pia kwa Raisi Jeremy , wote kwa pamoa waling’ata meno yao kwa hasira sana kwa kuona mpango wao unakwenda kufeli.

Upande wa Lekcha mwenywewe alijikuta akipandwa na jazba sana kwani hawakuwa wametegemea kama Jeremy anaweza kuwa na siri nziro ambayo ameificha kwa muda mrefu , kauli yake ya kusema watu wa ukoo wa mama yake ilimchanganya sana.

Ukweli hata wao wenyewe walikuwa kwenye maswali mengi kwani hawakuwa wakijua ni kwanini Wale majini kutoka Panasi walikuwa wakimlinda Jeremy.

Kizwe licha ya kumfahamu Jeremy hakuwahi kujua kuhusu siri zake zinazohusiana na wazazi wake na mara zote alisema walikufa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe na yeye kukimbilia nje, hakuwahi hata kuwaza kama Jeremy angekuwa na uhusinao na jamii za kijini.

Lakini hata hivyo mpango wao walipaswa kuumaliza siku hio hio kwani hawana muda mwingine wa kufanya baadae.

Mango wao wa kwanza ulikuwa ni kumuondoa Roma katika kurithi ukoo nchini Tanzania , lakini ukashindwa kufanikiwa , kama watashindwa kumpata na Jeremy inabidi waanze kufikira namna nyingine ya kuandaa mipango yao upya jambo ambalo lingewachukua muda kufanikisha lakini kwa wakati mmoja kuwapa nafasi wapinzani wao kujiimarisha zaidi na pia Roma kuanza kuwatafuta.

“Nitatumia njia nyingine nyepesi , nitajibadilisha kuwa wewe kwanza na baada ya hapo nitaharibu hio dhana kwenye shingo yako”Aliongea Lekcha na kuanza kuwashambulia haraka haraka Nix na Geisha bila kuwabembeleza ten.

Upande wa Gesha na Nix waliweza kuzidiwa nguvu zao na kuwa dhaifu na dani ya dakika kama mbili tu ilikuwa ni kama wamerudi levo ya nusu mzunguko na ndio muda ambao Lekcha hakutaka kupoteza muda kabisa.

Ghafla tu Nix na Gesha walijikuwa wakifunikwa na mwanga mkali kama wa shoti ambao ulisababisha uwepo wao kutoweza kuonekana tena wala kutorok.

Upande wa Iringa ilikuwa ni wakati ambao Roma alikuwa akimuweka Lanlan vizuri ili na yeye kulala , lakini alijikuta palepale akikaa kitako ghafla.

Edna alionekana kushangazwa na kitendo kile kwani Roma alionekana kama mtu ambaye amekumbwa na hofu,

“Nini tatizo , au bado ni mapema kwa wewe kulala?”

“Hapana nahisi uwiano usio sahihi wa nguvu za mbingu na Ardhi , nahisi kuna majini yanapambana”Aliongea na kumfanya Edna kumwangalia kwa wasiwasi.

“Kivipi , ningeweza kuhisia pia , je ni mbali na hapa?”

“Inaonekana kuwa ni umbali mrefu sana na hapa ndio maana huwezi kuhisia , nitaenda kuangalia , napata hisia kabisa zinatoka katika mtu levo ya Nafsi”Aliongea naEdna aliishia kutingisha kichwa kwani alijua kabisa asingeweza kumzuia hata hivyo.

Roma kwa haraka sana alivaa nguo zake za kawaida na kuondoka hapo ndani na ile anatoka nje ya mlango tu na kuufunga alikuwa tayari ashapotea na alikuja kusimama juu zaidi angani katika eneo hilo na kufumba macho akitafuta uelekeo wa nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi inatokea wapi maana msisimko wake ulikuwa wa chini sana na kama asingekuwa kwenye levo ya Kuipita dhiki asingeweza kuinasa.

Baada ya kupata uelekeo palepale alipotea na ile anakuja kuibukia kwa mara nyingine alikuwa kwenye mpaka wa Rwanda na Tanzania na aliweza kuhisi nishati ya Ant – matter.

Palepale hakutaka kujiuliza mara mbilimbili kwani shauku yake ilizidi kuongezeka na dakika chache tu alikuwa karibu kabisa na sasa macho yake ya kijini yaliweza kuona alichokuwa akitarajia.

Aliweza kuona mtu nje ya jengo ambaye alikuwa amezungukwa na mwanga wa rangi nyeupe ya kung’aa huku pembeni yake likionekana jengo ambalo limeharibika paa lake.

Baada ya kuchunguza kwa umakini aliweza kungudua aliekuwa amezungukwa na mng’ao huo ni Raisi Jeremy akionekana kuwa katika hali ya hofu.

“Ant – matter energy!!!!, kwanini inatokea hapa?”Aliongea Roma kwa mshangao .,

Ndio alipaswa kushangaa kutokana na mtu ambaye alikuwa akimiliki nguvu hio alikuwa ni Yan Buwen pekee ambaye aliamini kabisa amekwisha kumuua.

Roma alijikuta sasa akielewa kinachoendelea mara baada ya kuweza kumuona Desmond na Kizwe ambao walikuwa wamesimama pembeni.

Roma alijiambia licha ya kwamba hakuwa na ukaribu mkubwa na Jeremy asingemuona akifa mbele yake kwani ni baba mzazi wa mke wake.

Roma palepale aliita kitenesi cha moto mweupe na kisha alikirusha upande ambao kulikuwa na mkusanyiko wa mwanga uliokuwa ukitoa shoti ya nguvu ya Ant Matter.

Dakika ileile ambayo kitenesi kile cha moto mweupe kilipotoka katika mkono wake kilibadilika na kuwa kama mshale mrefu ulioonekana katika mstari mnyoofu.

Lakini sasa shambulio lake ile linafikia ile sehemu ambayo kulikuwa na mkusanyiko wa nguvu ya Ant Matter halikuweza kushambulia kwani mkusanyiko ule ulisogea pembeni kwa spidi.

Kitendo kile cha shambulio lile kuonekana kupishwa ule mwanga ulianza kupungua na palepale alionekana Denisi ambaye alikuwa akija upande wake.

Raisi Jeremy alijikuta akipatwa na ahueni mara baada ya kuona kumuona Roma kwani alidhania siku zake ndio zimefika mwisho hivyo na alishukuru pia kwa kuwa na Dhana ambayo alipewa na mama yake inayomlinda siku hio.

“Nilijua tu wewe sio Denisi , ijapokuwa sijui ni mbinu gani umeitumia kuficha uwezo wako na kwa namna ipi umeweza kumiliki nguvu ya Ant-mater , najua kabisa Denisi hana akili ya kupanga mipango yote”Aliongea Roma mara baada ya kumuona mtu mwenye sura ya Denisi mbele yake,

“Hahah .,.. mipango yangu imefeli kutokana Jeremy kutokana na Dhana kumiliki Dhana ya ajabu , ila sio mbaya nitaacha maigizo kwasababu ushaniona”Aliongea Lekcha huku akionyesha kufurahishwa na Roma kujitokeza.

“Ulitakiwa kujua hilo kabla ya kupanga mipango yako , unadhani unaweza kushinda kirahisi kama kuna wenzako ambao waliweza kushindwa mwanzo”

“Nidio unavyowaza .. kitu pekee ambacho naweza kujilaumu nacho ni bahati kutokuwa upande wangu kwa kukosa uwezo mkubwa kama wa kwako la sivyo kama mpango wanguungefanikiwa , ningeweza kutawala taifa lote la Tanzania”

“Je nichukulie maneno yako kama sifa”

“Hapana , ninachomaanisha ni kwamba una bahati sana mpango wangu kufeli”

“Kama ni hivyo je unaweza kuniambia wewe ni nani?”

“Hahaha.. mimi nni nani tena ,, ushaniona tayari , mimi ni Denisi”Aliongea Lekcha kwa kucheka

“Roma usimsikilze huyo , sio Denisi ni Joseph Bikindi maarufu kama Lekcha , ndio yeye pekee ambaye anweza kushirikiana na Kizwe, najua namna anavyoongea , ndio yeye”Aliongea Raisi Jeremy ambaye aliikuwa akisikia maongezi yao

Roma alijikuwa akishangaa mno , hakutegemea Denisi ni Lekcha , mwanaume ambaye alimsaidia Kizwe nchini Tanzania na alijikuta akikumbuka taarifa ya uchunguzi wa The Eagles na kujikuta akiona sasa mambo yamefikia pale anapopataka.
 
Back
Top Bottom