Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 595

Roma kwa haraka sana kumbukumbu zake ziliweza kurudi siku ambayo alikutana na Kizwe pamoja na Lekcha ndani ya Club B , Lekcha wa kipindi kile alikuwa wa kawaida sana na hakuwa tishio lakini Lekcha ambaye anamuona mbele yake alikuwa ni mwingine kabisa.

Kwa mtu mwingine angepingana na kauli ya Raisi Jeremy kusema Mtu anaefanana na Denisi ndio Joseph Bikindi , ila kwa upande wa Roma ambaye alikuwa na uzoefu wa mambo mengi ya kushangaza ilikuwa rahisi kwake kuweza kuelewa na kuamini.

“Ni wewe … sijategemea kukuona ukiendelea kuishi, nilijua tayari ulishauwawa kwa siri”Aliongea Roma kwa kejeli.

“Kwanini unadhania mwanaume ambaye sikuwa na thamani kama mimi kufa bila sababu ya msingi , siku uliomtuma yule malaya kuja kwangu haukuwahi kudhannia kila kitu unafanya kama nilivyokuwa nikipanga?, Unadhani ni kwa bahati mbaya mtu ambaye alikuwa akiishi kwa kuokota makopo na kuishi chini ya Daraja kuweza kuelea angani kama wewe hivi sasa? , unafikiri hii ni miujiza imeniokea?, wewe huna tofauti na wengine , unatumia wasifu wako kujaribu kudharau viumbe vya hali ya chini ila ukweli ni kwamba nyie watu hampo tofauti na sisi”Aliongea Lekcha.

“Nilidhani ulikuwa ukinichukia ndio maana uliweza kuwa na mipango mingi ya kunichafua , lakini kwa ninachoona hapa unatuchukia wote”

“Hahah… mimi niwachukie ,hamstahili uwekezaji wangu wa kihisia kwa ajili tu ya kuwachukia , kwangu mimi nawaona kama mawindo tu na nitawafanya ninachotaka”

“Unaonekana kujiamini , naona umeweza kumiliki nguvu ya Ant-matter , na kama sikosei naamini umefanikisha hayo yote kupitia Yan Buwen na hili linanifanya kuwa na shuaku ya kutaka kujua umefikia hatua gani, lakini hata hivyo naweza kuona wewe ni wa tofauti”Aliongea Roma huku akitoa kicheko.

“Bado tu unaongea na mimi kwa dharau … hicho ndio kinachonichukiza kuhusu nyie watu, nini kimekufanya kuja hapa na kutaka kuingilia mambo yangu ,au unahisi bado tu unaweza kunishinda?

Unatokea katika familia ambayo inasifika kuwa na nguvu ndani ya Tanzania lakini kwangu mimi naona ni ushenzi tu na utapeli wa famlia yenu ndio maana mnajiona mpo juu , kwangu mimi watu wa aina yenu mnastahili kushushwa kwa kipigo na kuliwa na mimi”Aliongea Joseph Bikindi kwa dharau huku akiwa na uso wa kujiamini.

Wakati Roma akifikiria nini cha kuongea ghafla tu aliweza kuhisi msisimko wa hali ya juu ukiwasogelea na kumfanya kukunja sura , ni msisimko uliokuwa ukitokea upande wa Magharibi.

Ni kufumba na kufumbua tu aliweza kuonekana mwanaume mweusi alievalia mavazi meupe marefu aina ya Robes.

Alikuwa na mwonekano wa kitajiri na kujiamini huku akiwa na sura ambayo imejaa ujeuri , macho yake kwanza aliyaelekezea kwa Raisi Jeremy ambaye alikuwa akizungukwa na mwanga mweupe na kisha akayageuza upande wa Roma aliekuwa juu yake kidogo.

“Master 4 asante kwa kufika mapema”Aliongea Raisi Jeremy huku akonyesha hali ya kupatwa na ahueni, haikueleweka kwanini anaitwa Masetr 4 lakini kwa haraka haraka Roma alitambua inawezekana akawa ndio Master mkuu namba nne katika jamii ya Panas.

Kuhusu uwezo wake Roma aliweza kugundua alikuwa levo ya kuipita dhiki akiwa na uwezo wa kutawala rangi tatu za moto , alionekana kuwa juu zaidi ya Nix na Gesha ila levo yake bado ilikuwa ya chini kuliko Rom ambaye alikuwa na uwezo wa kudhibiti mtoto wa kiroho wa rangi ya bluu pamoja na maji ya kiroho.

“Jeremy wewe mjinga sana , yaani umeshindwa kujilinda mpaka ukafikira hatua ya kutumia hio medali tena wanaokushughulikia ni wanafamilia wako mwenyewe?”Aliongea kwa lugha ya kifaransa.

“Master 4 mambo mengine hayazuiliki na sio kila tunalopanga linatokea , wana nguvu zaidi yangu na mipango yao ilikuwa ya siri tafadhari nisaidie kuwamaliza”Aliongea na Master 4 alimpotezea na kumgeukia Roma.

“Ninakujua wewe kijana kutoka Taifa la Tanzania , una umaarufu mkubwa sana katika ulimwengu wetu kwa kuweza kupita vizuizi vya tamaduni zetu kwa muda mfupi , nashindwa kuona uwezo wako ni katika levo ipi nadhani ni kama sifa zako zinavyojieleza hakika una stahili sifa unazopewa , kwa leo nipo hapa kwa ajili ya kumsaidia ndugu yetu upande wa mama sitaki kujiingiza sana na mambo ya dunia”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa kwani hakuelewa nini maana ya ndugu upande wa mama , akili yake ilifanya kazi kwa haraka sana na kujiuliza inamaana Raisi Jeremy na yeye amezaliwa nusu binadamu nusu jini, alijikuta sasa akielewa kwanini watu kutoka Panasi walitumwa kuja kumlinda , kumbe kuna sababu kubwa na sio maswala ya bahati mbaya.

“Wewe takataka umetokea wapi? , unajiona ni nani mpaka uje kuingilia hapa?”Aliongea Lekcha na bila ya kutaka kusubiri jibu palepale shoti za ant -matter zilimtoka kwenye mkono wake na kumshambulia Master 4 kwa spidi na kumshusha ardhini.

Masetr 4 alijikuta akishangazwa na namna shoti zile zilivyoweza kumtoka Lekcha kwani hakutarajia kama angekuwa na uwezo huo.

“Haha.. kwa udhaifu huo uliokuwa nao bado tu umekuja peke yako na bado unajitamba kutaka kumuokoa Jeremy? ,ila sio mbaya nitakuua nae”Aliongea huku hali ya kujiamini ikiongezeka mara mbili na alizidi kuongeza nguvu ya shoti ya Ant-matter kumshambulia Master 4 kumpeleka mpaka ardhini.

Roma alikuwa na nafasi ya kumzuia Lecka lakini hakutaka kujihusisha kabisa na watu wa jamii hizo zisizoonekana na wakati huo huo alitaka kumuona Lekcha uwezo wake kabla ya kupigana nae.

Upande wa Master 4 alionekana kushindwa kuelewa namna ambavyo aliikuwa akishambuliwa na kujilinda, alijikuta akianza kujutia maamuzi yake , huenda angekuja na watu wengi zaidi kwa ajili ya kupambana lakini alimdharau adui kwa kutarajia atakuwa wa kawaida ndio kilichomfanya kuja peke yake.

Dakika hio hio hakuwa na haja ya kumsaidia kwanza Raisi Jeremy kwani aliona anapoteza nguvu kwa boriti za shoti anazopokea.

Upande wa Raisi Jeremy ile kinga iliokuwa imemzingira ilitoweka palepale , ilionekana dakika therathini za kumlinda zilikuwa zimeisha na kumfanya aanze kuogopa kwani aliweza kushuhudia namna ambavyo Master 4 anavyopokea kichapo.

Muda uleule mwanga ule wa ngao baada ya kupotea Kizwe na Desmond walijikuta wakirejewa na hali zao upya za kujiamini na kutaka kulipiza kisasi.

“Baba umemua kunitelekeza mimi na ukamchagua yule Malaya wa Kitanzania kuwa mrithi wako , usinilaumu kwa kupindua meza muda huu”Aliongea Desmond huku akionyesha hasira kubwa sana zidi ya baba yake na mwili wake ulibadilika na kuwa kama kivuli huku akimsogelea Raisi Jeremy kwa spidi huku aidhamiria kummaliza na pigo moja.

“Kuwa makini!!”

Sauti ilimtoka kizwe na kwa spidi sana aliweza kutokeza mbele ya Desmond akionyesha kumkinga.

“Poof!!”

Ni mlio wa sauti ya kuchoma iliosikika na boriti ya mwanga mweupe kama wa laser ulionekana kumchoma Kizwe katika kifua chake na kutoboa.

Katika umbali mfupi kutoka aliposomama alionekana Master 4 ambaye alikuwa ameinua mkono wake kuelekezea kwa Kizwe na boriti ya mwanga ule mweupe ulionekana kutoka katika kifaa ambacho hakikuwa kikielezeka kiumbo na ilikuwa ni kama dhana ambayo teknolojia yake ni ya hali ya juu sana, hazikuwa kama zile dhana ambazo Roma aliweza kuziona kwa baadhi ya watu wa Hongmeng.

Desmond alijikuta akishangazwa na jambo lile, hakuamini mwanamke ambaye hakuwa akimchukulia tena kama mama yake ameamua kujitoa kafara na kupokea shambulio badala yake.

Kwake ilikuwa ni kama muda ulikuwa ukienda mbele na kurudi kwa wakati mmoja.

Lekcha aliekuwa juu angani hakuonyesha kujali kile kilichokuwa kikiendelea ardhini , Kizwe na mtoto wake aliwaona kama watu ambao hawakuwa na thamani tena baada ya mpango wake kufeli, hivyo hakuwa na haja ya kujali kama wapo hai au ni wafu.

Raisi Jeremy alijikuta akitoa pumzi ya ahuenni , ilikuwa ni bahati kwake Masterr 4 hakuwa amesahau kumlinda , ilikuwa ni kidogo sana tu kuweza kujeruhiwa na Desmond , alijikuta akitoa tabasamu kumwangalia mwanamke huyo aliepiga magoti ardhini akipambana na maumivu.

Upande wa Roma alijikuta akishngazwa na tukio hilo ambalo limekaa kidrama zaidi , hakuweza kutarajia kama Kizwe ambaye hakuwa katika uhalisia wake kuweza kujitoa kafara kwa ajili ya Desmond ambaye pia alikuwa amepitia mabadiliko na kupoteza uhalisi wake.

Ijapokuwa mwili wa Kizwe ulikuwa na uwezo wa juu wa kujiponyesha lakini nishati ambayo imetoka katika Dhana ya Master 4 ilikuwa na kiwango kikubwa cha nishati ambayo haipo kwenye uwiano sawia na mwili wake ili kuweza kupona.

Wakati nguvu ile ya kijini ikitafuta balansi katika mwili wa Kizwe ili aanze kupona eneo ambalo limetoboelwa lilizidi kuongezeka ukubwa na kumfanya damu kuzidi kupotea chini na hakukua na namna ya kuzuia.

Desmond alijikuta akimshikilia Kizwe huku akiwa na macho yaliokuwa mekundu.

“Umefanya nini , kwanini umenikoa , umekua kichaa?”Aliongea kwa sati kubwa ya hasira kama vile ni mwenye hatia na kumfanya Kizwe kuinua mkono wake kwa taabu sana akitaka kumshika Desmond shavu lakini nguvu zake zilizidi kupotea na kuishia njiani .

“Mtoto mjinga … mimi ni mama yako ..”Aliongea Kizwe kwa sauri dhaifu.

Machozi yake alishindwa kuyazuia na yalidondokea katika kifua cha Kizwe na kupita moja kwa moja mpaka chini Ardhini kupitia tundu la jeraha.

“Na … najua ulikuwa ukichukizwa na mimi na unaniona kama malaya hivyo kuniona siwezi kuwa mama yako tena … lakini Des.. mond kwangu wewe siku zote utabakia ,, utabaia ,,,ku..kuwa mtoto waaang..” Kabla hata hajamalizia herufi ya mwisho ya sentensi yake palepale kichwa chake kikalegea na ndio ukawa mwisho kamili wa uhai wake.

“No!!”

Desmond alishindwa kujizuia na kujikuta akitoa ukulele ulichonganyika na maumivu makali , yalikuwa maumivu kama ambayo aliyapata siku alipoambiwa mama yake amefariki na muda huo huo maumivu yale yalijirudia..

Lekcha na shoti zake za Anti -matter alijaribu kila namna ya kuweza kummaliza Master 4 lakini ilikuwa ni kama vile mapigo yake ni dhaifu sana, lakini licha ya hivyo hakutaka kuleta kabisa ujinga kwani alipaswa kuimaliza kazi mapema , hakujali kufariki kwa Kizwe , kwanza katika maisha yake hakuwahi kumpenda na alikuwa amemtumia tu kukamilisha mipango yake ya kupata nguvu na mtu aliekuwa akimpenda kwenye maisha yake ni mwingine kabisa.

Roma palepale aliweza kuzingirwa na nguvu ya Ant – matter ambayo ilikuwa ikimzunguka kama kimbunga na alijitahidi kutengeneza baridi kali ili kujaribu kuipunguza kasi na hakutegemea mbin yake kufanya kazi baada ya kuona mafanikio na kutengeneza annihilation.

Hakutaka kuchelewa zaidi kwani palepale alichukulia hilo kama faida kwake kwani alitoka katika kimbunga kile cha Ant Matter na kwa spidi ya juu alimsogelea Lekcha akinuia kumshambulia.

BOOM!!!

Shambulizi lake lilileta mafanikio kwani baada ya kumsogelea Lekcha alimtandika kisawa sawa ngumi ya kichwa na kuuchangua kichwa chake.

Kichwa chake kilipasuka vipande vipande kama vile kimepigwa na bomu na damu pamoja na nyama nyama pamoja na ubongo vilianza kusambaaa hewani.

Lakini sasa sekunde hio hio tu mwili wa Lekcha ulibadilika na kutoa mn’gao wa aina yake huku zile nyama nyama na damu ziligeuka na kutoa shoti za umeme kama cheche kuelekea kila upande na kwa spidi kubwa sana na ilionekana kama vile ni shambilio , kwani cheche zile ambazo zilikuwa kama mishale midogo zilianza kumpiga Roma kwa spidi ya hali ya juu.

Ijapokuwa ni vjimishale vya Ant- matter vidogo sana lakini ilikuwa na nguvu yake na ikigusanana kitu chochote hutengeneza Annihilation(maangamizi) makubwa.

Roma alijua kama ataruhusu kuguswa na cheche hizo basi angepata pigo kubwa hivyo alijitahidi kukaa mbali na kujilinda kwa wakati mmoja.

Dakika ileile baada ya Lekcha kuona Roma anajikinga ghafla tu mng’ao ule wa ant-matter ulipotea na Lekcha alirudi upya katika umbo la bindamu akiwa na sura ya Denisi.

Roma kwa wakati huo alikosa mbinu ya kummaliza haraka haraka Lekcha kwani alionekana kushambulia kwa tahadhari na aliweza kukiri kimoyo moyo Lekcha alikuwa ni tofauti kabisa na Yan Buwen katika kupambana, alichokifanya ni kujaribu kumshambulia na moto wa rangi nyuepe na wa Bluu kwa wakati mmoja lakini mashambulizi yake yalionekana kukosa nguvu kabisa ya kumdhuru Lekcha.

Licha ya kwamba mapigo yake yalionyesha uwezo wa kumletea maangamizi lakini kwa wakati mmoja ilimfanya Lekcha kuweza kurudi katika hali yake ya kawaida.

Kilichomkasirisha zaidi Roma ni namna ambavyo Lekcha hakuonyesha mpango wa kuachana na mwili wa Denisi na mpaka hapo alijua huenda sio tu kwamba alikuwa amejibadilisha sura kuwa Denisi bali mwili wake ulikuwa umeungana pamoja na wa kwake.

Upande wa Desmond baada ya kutoa kilio cha uchungu mwingi hatimae aliinua sura yake na kumwangalia Raisi Jeremy kwa macho yaliojaa chuki .

Raisi Jeremy hakuwa na kinga tena kwani medali yake haikuwa na uwezo wa kumlinda mara mbili na sasa alikuwa ni mwepesi sana kuweza kushugulikiwa na Desmond.

“Haya yote ni kwasababu yako umemuua mama yangu na nitakuua , nitakucharua charua”Aliongea ka kufoka huku akimsogelea Raisi Jeremy kwa spidi lakini Master 4 ambaye alikuwa mdhaifu aliweza kumkinga Desmond na nguvu ya kijini.

Kutumwa kwake kuja hapo alihitajika kumlinda Raisi Jeremy kwa hali na mali kwani ndio mwakilishi pekee wa mipango yao juu ya uso wa dunia hivyo hakutaka kushindwa kutimiza wajibu wake.

Siraha yake ambayo aliitumia kumuua nayo Kizwe alimshambulia nayo Desmond na ilikuwa ni kwa bahati aliweza kushitukia pigo hilo kwani alifanikiwa kukwepa lakini kwa wakati mmoja akikatwa mkono , jambo ambalo hakuonyesha kuathirika sana kwani mkono wake uliweza kurudi upya ndani ya sekunde tu.

“Desmond umekuwa kichaa? , huyo mwanamke sio mama yako , mama yako alikufa na huyo malaya ametengenezwa na yule mpuuzi mwenzake , alitutelekeza mimi na wewe unawezaje kumuita huyo ni mama yako ilihali hana thamani yoyote ya kuwa sehemu ya familia yangu?”

“Huna aibu baba , eti hana thamani , unafikiria ilikuwa hiari yake kuwa katika hali hio? , kama sio wewe ambaye uliamua kutoka nje ya ndoa na kupata mtoto unadhani haya yote yangetokea , hivi unafikiria kila kitu kilichomtokea ndio alichotoka , amegeuka kutoka kuwa mtu wa heshima na muungwana na kuwa malaya ambaye anachukuliwa na kila mmoja , je haya yote aliomba kumtokea? , ni kwasbabu ya wewe , umemuua mama yangu unapata wapi uthubutu wa kujiita baba yangu?”

Desmond kwa hasira kali alimsogelea Raisi Jeremy kwa spidi kali huku awamu hii akinuia kumuua kwa namna yoyote ile.

Upande mwingine Lekcha alikuwa amemzingira Master 4 na kimbunga chakc cha shoti za Ant-matter na alishindwa kujua namna ya kumlinda tena raisi Jeremy.

“Roma mimi ni baba mkwe wako niokoe”Aliongea Raisi Jeremy kwa nguvu mara baada ya kuona hakuwa na msaada mwingine kwani Master 4 alionekana kuzidiwa.

Ijapokuwa Roma alikuwa akipambana na Lekcha lakini macho yake pia yalikuwa yakimwangalia Raiai Jeremy asidhurike , alijiambia huyo ni baba yake mzazi wa Edna na kwa na namna moja amna nyingine anapaswa kumlinda.

Roma hakutaka hata kuwaza ni kwa na namna gani Edna angemchukia mara baada ya kusikia ameshindwa kumlinda baba yake, hata kama Edna asingefahamu hilo asingepaa ujasiri wa kuweza kumsogelea tena.

Kabla ya Demsond kumfikia Raisi Jeremy palepale alijikuta akifunikwa mwili mzima na moto wa rangi nyeupe na kuanza kuyeyushwa mwili wake kwa spidi.

“Mama… Arggghhh!!”

Alijikuta akishindwa kuhimili maumivu na kwa wakati mmoja akishindwa kuuzima ule moto mwilini mwake, licha ya kuwa na uwezo wa kupona kwa haraka lakini spidi ya mwili wake kuungua ilikuwa ni kubwa mno.

Raisi Jeremy alijikuta akitokwa na jasho jingi mara baada ya kuona namna ambavyo Desmond alikuwa akitoa kilio , kama mzazi alijikuta akiona uchungu kwa swala kama hilo kutokea , lakini kwa upande mwingine aliona hicho ndio anachostahili.

“Mwanaharamu wewe , unastahili kuchomwa moto mpaka kufa , unathubutu vipi kunisaliti mimi baba yako ,nenda kuzimu na huyo mpuuzi unaemwita mama yako”Aliongea kwa hasira na muda uleule aliusogelea mwili wa Kizwe na kuupiga teke.

Desmond alikuwa akiungua na moto wa kijini ambao uliunguza nguo zote na sasa ulikuwa ukiunguzwa mwili na mifupa , alijaribu kutambaa kumsogelea mama yake aliefariki lakini alijikuta akikosa nguvu na kutawaliwa na maumivu na aliishia kulia kama mtoto mdogo.

Ilichukua dakika chache tu mwili wake wote uliyeyuka na vumbi lake likapotea kabisa kwenye hewa.

Roma ambaye aliweza kuona kila kitu alitamani kumyeyusha na baba mzazi pia lakini hakutaka kufanya hivyo kwa ajili ya Edna tu , alikuwa na chuki na Jeremy kwani alimuona mtu ambaye ana siasa nyingi na atakuja tu kumsumbua na mke wake.

“Naona umeweza kuharibu kabisa mipango yangu”Aliongea Lekcha kwa kejeli huku hasira zake zikiwa za viwango , kwa namna ambavyo Roma alikuwa akijiamini ilimfanya kuona anadharaulika.

“Kwa mbinu zako angalau naona kabisa huwezi kuhimili muda mrefu”

“Acha majigambo nitakupa nafasi ya mwisho ya sisi kufanya kazi pamoja?”

“Unataka tufanye kazi gani?”Aliuliza Roma.

“Nifuate mimi na tuubadilishe huu ulimwengu uliojaa ufisadi”

“Unataka mimi na wewe tuubadilishe ulimwengu?”Aliuliza Roma akicheka.

“Upo sahihi , wewe si ndio wanakuita Mfalme Pluto sehemu ya miungu , bila kujali kama kweli wewe ni sehemu ya miungu mimi na wewe tuna nafasi kubwa ya kubadlisha huu ulimwengu?”

“Hahaha.. hakika wewe ni tofauti kabisa na Yan Buwen , angalau yeye alionekana kachizika lakini wewe ni mwendawazimu”

“Wewe ndio mwendawazimu kwenye macho yangu , hustahili kabisa hata kupewa cheo cha U’pluto , huna thamani wala nguvu kwa sifa unazopewa”

“Wewe ni mtu wa aina gani unajiita mungu? , unapaswa kufaidika kutokana na cheo chako lakini nyie miungu mmeamua kuficha vichwa vyenu huku mikia yenu ikionekana , eti hatutapaswi kujihusisha na mambo ya dunia wanafiki wakubwa nyie, bahati mbaya unafiki haupo kwenu tu ni kwa kila mtu na katika kila taifa ,sijutii kwa wewe kumuua baba yangu maana alikuwa mnafiki na yeye lakini najutia kwa wale wote ambao wanajifanyisha ni wa thamani ya juu zaidi na kutuona sisi hatustahili hata kuwasogelea , hebu muangalie mtu ambaye umemlinda sasa hivi unadhani ni mtu wa aina gani , yule ni mnafiki tu ambaye anadanganya taifa huku akiwa na ajenda zake kichwani , ni kiongozi gani ambaye yupo tayari kuua familia kwa maslahi yake , inasitikisha sana .

Kizwe ni mwanamke ambaye alijitaji mapenzi na kusamehewa pale anapoonyesha udhaifu, hata kama imetokea akaguswa na wanaume wengine anatoa wapi hukumu ya kumuua , kama hamtaki si angemtafutia sehemu na kuishi na kuachana nae , kulikuwa na haja yoyote ya kumuua?., haya ni mambo ambayo mimi Joseph Bikindi a.k.a Lekcha nataka kurekebisha , nataka kuondoa uovu wote ndani ya dunia , nataka kubadilisha dunia hii na kufuta kitu kinachoitwa siasa maana ndio chanzo cha ufisadi na uovu , hivyo Pluto unaonaje tukiungana pamoja na kufagia ufisadi wote na kuanza kuwapa watu uhuru kamili , falsafa yetu itakuwa ni kurudisha nguvu kwa wanyonge ili washindane wenyewe na hawa mashetani wasio na huruma , hakuna haja ya dunia hii kuwa na watu wenye nguvu huku hawafanyi chochote na hata wakichukua hatua ni kwa faida zao wenyewe , Mr Roma Ramoni nitaweka yote ulionifanyia nyuma yangu na tuungane pamoja kubadili dunia hii, Hebu tuungane pamoja”

SEHEMU YA 596.

Sauti ya Lekcha ilikuwa kubwa kiasi kwamba ni kama vile anataka dunia yote imsikie.

Usiku huo kulikuwa na upepo mkali na anga halikuwa na dalili yoyote ya wingu kuashiria kama kuna mvua inayoweza kunyesha, ni vivuli tu vya watu ndio vilionekana angani na kwa mtu ambaye alikuwa kilomita moja kwa umbali asingeweza kuona kinachoendelea zaidi ya kusikia sauti na baadhi ya vimulimuli vya hapa na pale.

Lakini kwa sauti yake ilifanya watu wa jiji la Kigali kuwa katika tahadhari kubwa na kutetemeka , ilikuwa ni kama vile Mungu anaongea na binadamu.

Baada ya kimya cha muda mrefu, Roma ambaye alikuwa na mwonekanao usiolezeka alivuta pumzi nyingi na kuzishusha na kisha akainamisha kichwa chake chini na kuanza kucheka.

“Perhaps it is inapropriate for me to say that you are madman, not only you’re a madman but also a coward”Aliongea Roma kwa kingereza akimaasha kwamba huwenda inaweza isiwe sawa kumuita mtu kichaa ila ukweli ni kwamba yeye sio tu kwamba ni kichaa lakini pia ni muoga.

Kauli yake ilimfanya Lekcha kufika kilele cha hasira zake baada ya kusikia jibu hilo na alitamani kumrarua Roma palepale.

“Unaniita mimi muoga? ,, hahaha… nadhani unaota maana muda wenyewe ndio huu umeenda”

Roma hakutaka kujibuzana nae na palepale aliita moto wa njano na kuunganisha na moto wa bluu na nyuepe.

“Tumalize kabisa hili , nimekupa nafasi ya kuishi lakini ukaipotezea , hivyo kila kitu ambacho nilikosea kukifanyia kazi nitakimaliza leo hii mimi mwenyewe”

“Unafikiri barafu na moto ni vitu ambavyo vinaweza kunidhuru? Unachekesha sana”Aliongea huku akiwa na mwonekano wa dharau.

“Hujui lolote kwasababu bado hujawahi kupambana na mimi”Aliongea na hakutaka kuchelewesha, aliuelekeza moto wa kijini kumshambulia Lekcha kwa kasi kubwa.

Halikuwa shambulia la kawaida kwani ilikuwa ni kama vile chembe chembe zote za anga zilikuwa hazitembei huku eneo lote likiwa halina aina yoyote ya upepo na kuufanya ule moto kutoa nguvu kubwa ya kiroho.

Master 4 kuona tukio lile alijikuta akishikwa na mshangao kwani ni kitu ambacho hakuwahi kushuhudia , hakuwahi kuona rangi zote za moto kutolewa kwa wakati mmoja zikiwa zimeunganika , lakini haikuwa hivyo tu kilichomchanganya zaidi ni namna moto ule ulibadilika na kuwa kama vinyoka nyoka , alijua kama yeye ndio anashambuliwa basi ni shambulizi moja tu atakwa tayari amekwisha kufariki.

Alijimbia kwa nguvu ya kiroho ambayo alikuwa akihisi , hana uhakika kama wakubwa zake wote katika miliki ya ulimwengu wao wanaweza kufanikiwa kushinda , alishangaa mara moja na kujiuliza imekuwaje kijana mdogo akawa na uwezo wa aina hio.

Upande wa Roma hakujuwa kwamba alikuwa akimshangaza mtu kwa wakati huo kwani alichokuwa akiwaza ni kumalizana na Lekcha moja kwa moja na kwenda kulala na familia yak.

Ukweli ni kwamba Lekcha alikuwa tofauti sana na Yan Buwen na alikuwa ni kama vile alipenda kuonja kila pigo ambalo alikuwa akipelekewa na Roma , kwani hakukwepa mashambulizo yake na hata ule moto aliacha umshambulie.

Ajabu ni kwamba licha ya Roma kuweza kutumia nguvu kubwa sana ya kutawala moto huo kushambulia lakini mbele ya nishati ya ant-matter ilionekana kutofanya kazi, nguvu ya Lekcha ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba moto ule ulikuwa ni kama vile unanyonywa na kuzimika kila unapogusana nae.

Roma kwa levo aliokuwa akitumia alijua ilikuwa juu zaidi kuliko aliotumia kupambana na Yan Buwen mpaka kumuua na ilimshangaza kwamba wakati huo Lekcha licha ya kumsbambulia alionekana kabisa hana hofu na chochote anachomuandalia na alikuwa na maendeleo ya juu mno.

“Hehe.. naomba unajitahidi sana hata hivyo nitakuchukulia kama jiwe la kujiimarisha zaidi ili niweze kutimiza malengo yangu , naona kabisa mbinu zako zote zimefikia ukomo, ni muda sasa kukuonyesha uwezo wangu halisi”Aliongea Lekcha.

Sekunde hio hio alibadilika kabisa na hakuwa biadamu tena bali nguvu yenyewe ya Ant-matter na alianza kwa kuwa kama mpira wa miguu na akaendelea kutanuka huku shoti zikisambaa kila kona na mpira ule ulizidi kujizungusha na kuanza kuonekana kuwa mkubwa zaidi .

Ni muda uleule wakati Roma akishangaa aliweza kuona shimo likijitengeneza juu yake na liliongezeka ukubwa huku anga likiwa ninazunguka kama vile kimbunga au singularity inayotokea juu kuja chini na ndani ya dakika chache tu sehemu aliosimama ni kama vile yupo kwenye chumba ambacho hakina hewa ndani yake na ilimfanya kushindwa kuita nguvu ya kimaandiko kumlinda kwani alishindwa kuwasiliana na elementi za dunia.

Kilichomshangaza Roma ni ufahamu wake kuanza kumpotea na kujihisi kama vile anaendeshwa kwa rimoti na hakuwa na uwezo wa kusogea kurudi nyuma wale mbele, alisimama kama vile ni sanamu.

“Chochote utakachofanya hakina maana , nishati yangu ya Ant – matter imeongezewa ubora kwa viwango vya juu na kuwa na tabia tofauti na zile ambazo wanasayansi wa kawaida wanajua , yote hayo yamefanikiwa kupitia kifaa maalumu cha kuibadilisha , unafikiri ningekuja kushindana na wewe nikiwa na nguvu kama zile za Yan Buwen … kinachotokea hapo ni matumizi ya magepu yaliopo kati ya anga mbalimbali zilizo sambamba, kwa uwezo wako huo licha ya kuwa na uungu ndani yako huwezi kuitoa roho yako na kutawala mwili mwingine maada itakuwa halali yangu”Sauti ya Lekcha iliweza kusikika lakini Lekcha mwenyewe hakuweza kuonekana na upande wa Roma aliweza kusikia kama vile ni mwangwi.

Roma uso wake ulianza kujikunja kunja kwa namna ya kulazimishwa huku akijaribu kuzuia mwoneknao wake usibadilike lakini mzunguko wa nguvu ya Ant-matter ulikuwa ukifyonza nguvu zake za mbingu na ardhi kila alipokuwa akijaribu kuziita ili kujiondoa kwenye mtego huo , mbaya zaidi ni kiwango kidogo sana ambacho alikuwa na uwezo wa kukiita kutokana na kuingizwa katika eneo ambalo kulikuwa na elemeti za anga hivyo kushindwa kufanya mawasiliano.

Roma alijikuta akipandwa na hasira na kujiambia alimchukulia wa kawaida ndio maana yupo katika hali kama hio , alikuwa bado hajapigana na majini katika ulimwengu usio onekana lakini alikuwa akijiamini kwamba alikuwa na uwezo wa kuwashinda lakini anachofanyiwa na Lekcha kilimpagawisha kwa wakati mmoja na kujiona huenda ni dhaifu.

Roma hakutaka kufanya ujinga ni kweli alikuwa na uungu ndani yake alioweza kurithi kutoka kwa Pluto wa Zamani hivyo kumpa uwezo wa kutawala mwili wowote lakini alihofia kwamba anaweza kuingia katika mwili ambao hauna vigezo na anaweza kuanza upya moja kwa moja kuvuna nishati za mbingu , isitoshe nguvu za kijini hawezi kuhama nazo.

Roma mara baada ya kuona yupo hatarini aliona hana chaguo lingine zaidi ya kuita Chaos Cauldron.

Lakini moyo wake ulikuwa mzito mno kwa kuhofia roho iliokuwa ndani ya Cauldron inaweza kutawala akili yake na asingejua ni kipi ambacho angeweza kufanya baada ya hapo , alihofia hilo kumkumba kwani ingekuwa mwisho wake.

“Roma umeweza kuwashinda watu wengi sana lakini sasa kiko wapi ,,, unakufa kwenye mikono yangu , kabla haujafa ngoja nikupe usharu kama zawadi , udhaifu wako mkubwa unaokufanya usiwe na nguvu ni kwasababu ya wasiwasi wako … huu ulimwengu ni kama msitu na mwenye nguvu ndio anaishi , siku zote binadamu mwenye nguvu atatumia utashi wa mnyama ili kuendelea kuishi , lakini wewe unadhani kutoa kafara matamanio yako ndio utaonekana mjinga , muoga , usie jiamini na dhaifu ,,, hayo yote ndio yanakuua leo hii hustahitili hata kuwa mshindani wangu , wewe ni dhiafu sana”Aliongea Lekcha kwa majigambo na kisulisuli cha nishati ya Ant-matter kikizidi kuongezeka maradufu.

Upande wa Master 4 aliweza kushuhudia mabadiliko hayo lakini hakutaka kujihususha zaidi kwani sio kilichomleta na palepale alibadilika na kuwa kama mwanga wa moto na kupotea eneo hilo akiwa pamoja na Raisi Jeremy.

Lekcha hakutaka kujihusisha zaidi na wao zaidi ya kuweka umakini katika kumuua Roma , alijiambia ni rahisi zaidi kuwatafuta mara baada ya kumalizana na Roma.

Dakika hio hio katika kisulisuli kile cha nishati isio maada ilitokeza miale yenye muundo wa macho rangi nyekundu huku sauti ikibadilika na kuwa kama ngurumo kubwa za radi na kumfanya Lekcha kushituka

“Hiki ni kitu gani?”

Nguvu yote ya Ant Matter ilianza kukosa nguvu , malengo ya Lekcha ilikuwa ni kujibadilisha na kuwa Roma lakini katika hali hio alishangaa mabadiliko makubwa kwani ni kama kuna kitu kilichokuwa kikifyonza nguvu yake kwa hali ya juu sana.

Upande wa Roma hakujali kabisa yupo kwenye hali ya hatari kama hio, kitu pekee ambacho alioona ni sahihi kukifanya ni kutumia cungu chake cha maafa lakini kwa tahadhari kubwa nafsi yake isije kumezwa na mwili wake kutawaliwa.

“Nani unasema hastahili kuwa mshindani wako”Sauti nzito iliweza kusikika.

Nguvu ilikuwa kubwa mno kiasi cha kufanya ule msukosuko wa hewa kupotea palepale na kumfanya Lekcha kurudi katika umbo la kibinadamu, lakini ni kama vile amefanya kosa kwani hapo ndipo aliposhuhudia kilichokuwa chini yake huku ndani yake kukionekana uwepo wa macho ya mnyama.

“Damn it what kind of monster is that….”Lekcha alijikuta akianza kuhofia maisha yake , kwa hali kama hio aliona kabisa ana uwezo mdogo wa kuishi.

Roma hakujali kutoa jibu na alikifanya chungu chake kuzidi kumsogelea Lekcha hatua kwa hatua na kadri kilivyokuwa kikisogea ndio hali ya hatari ilivyozidi kumkumba Lekcha kwani nguvu inavomvuta ilimvamia kwa hali ya juu sana

“Pengine upo sahihi , ulimwengu huu una machukizo mengi , unastahili kuhurumiwa , unastahili kuonyeshewa wema, lakini kwa mtanzao wangu wewe ndio chukizo kubwa zaidi la ulimwengu huu , umesema ni viongozi ambao ndio mafisadi na unataka kupambana zidi ya siasa , kama ni hivyo kwanini ulitaka kujibadilisha na kuwa Jeremy , umesema Kizwe ni mwanamke ambaye alikuwa na maisha magumu kama ni hivyo kwanini ukaaamua kumtumia na kisha ukampotezea , kama kweli ulikuwa ukimpenda kwanini hukumsaidia? , umesema miungu wameficha vichwa huku mikia yao ikionekana lakini kwanini ili tu kutimiza malengo yako unataka kuua watu utakavyo , ni haki gani ambayo unataka kutenda. Upo sahihi mimi Roma sina nguvu na siku zote ni muoga na mwenye wasiwasi mwingi na sina matamanio makubwa na ni mbinafsi na sistahili kabisa hata kuubadilisha huu ulimwengu..”

Wakati anamalizia kuongea alikuwa karibu kabisa na Lekcha na chungu chake kilikuwa kimemsogelea karibu zaidi na ilikuwa ni kama sunami , ni kama anga limekusanywa na kuwekwa sehemu moja na kuchezeshwa.

“Licha ya madhaifu yangu yote hayo sijawahi kujikataa , sijawahi kuficha udhaifu wangu , unafiki wangu na ubinafsi wangu ..mimi ndio mimi Roma ambaye uliweza kukutana nae kwa mara ya kwanza na sijabadilika, kwako wewe Joseph Bikindi mtu muoga sana , umeamua kutotumia sura yako halisi ili tu kutimiza malengo yako huku ukitumia mbinu zako za kusikitisha huku ukijifariji kwa uwezo wako mdogo , unachokionyesha ni inferiority Complex , wewe ni mtu ambaye huna lolote , wewe ni muoga ambaye unaogopa kuuangalia ulimwengu kwa jinsi ulivyo , kwa sifa zako hizo za kiuoga woga unathubutu vipi kupigana na mtu kama mimi”

“Mimi sipo hivyo , unangea upumbavu”Lekcha aliikuwa akijaribu kujitetea .

“Haijalishi kwasababu leo ndio mwisho wa maisha yako”

Roma palepale alizidi kubadilika na alikusanya nguvu zake zote na kukilisha kile chungu na ilimpelekea nguvu yake ya mvutano kuwa kubwa zaidi kama shimo jeusi .

Chungu hicho kilikuwa na uwezo wa kumeza kila kitu hata kama ni Ant Matter , nishati ambayo hufanya kazi kinyume na fizikia , hivyo kwa haraka haraka ni kwamba Lekcha hakuwa na pakukimbilia mbele ya Caulrdon.

Lekcha mpaka hapo alijua akileta mchezo ndio kifo chake , hivyo alitumia kila mbinu aliokuwa nayo kujaribu kukimbia lakini nishati yake ilikuwa ikimezwa kwa spidi kubwa na kumfanya kuzidi kuwa dhaifu.

Ilikuwa ni dakika chache tu wakati Roma akitaka kummaliza kabisa Lekcha kwa kumsukumia kwenye tanuru la kimaafa akili yake iliweza kuvamiwa palepale .

Roma alihisi ni kama ubongo wake umeingiwa na mdudu ambaye alikuwa akitifua tifua kuona sehemu ya kukaa.

Dakika ileile ni kama vile chungu hicho kiliachana na Lekcha na kiumgeukia Roma kuanza kushindana nae , ilikuwa ni mashindano ya nafsi na nafsi na Lekcha baada ya kuona amekuwa huru kutoka katika mvutano palepale aliona hi ndio nafasi pekee ya kukimbia , hakutaka kujiuliza kwanini imetokea hivi na vile lakini utashi wake ulimwambia aokoe maisha yake kwa vyovyote iwezekanavyo.

Alikusanya nguvu ya Ant Matter iliobakia katika mwili wake huku matamanio makubwa ya kujiokoa yakimpa nguvu ambayo ilimuwezesha kukimbia.

Lakini sasa dakika ileile anaweza kujiokoa upande wa Roma aliweza kuitawala akili yake kwa mara nyingine na kudhibiti nafsi ya mnyama iliokuwa kwenye chungu.

“Unaenda wapi?”

Aliongea Roma kwa nguvu akimwangalia Lekcha ambaye anajaribu kukimbia na alichokifanya Romna ni kumsogezea karibu zaidi chungu chake na kumfanya Lekcha kuzidi kuvutwa.

Ghafla tu ulipiga mwanga wa rangi ya Silver kama flash , ilikuwa ni kama mlipuko na uliweza kufanya mwili wa Denisi kujiachia na palepale ukamezwa na Cauldron.

Lekcha alijua kitu pekee ambacho kitamuokoa ni kuishi kama roho yenye umiliki wa nguvu ya Ant matter energy ili kujiuzia kutomezwa na chungu, ndio maana akaamua kuupoteza mwili wa Denisi.

Roma alishindwa kugundua hivyo mapema baada ya mwili wa Denisi kumezwa na chungu chake na baada ya kuelewa kilichotokea aliweza kugundua ni hila za Lekcha kujaribu kutoroka , kilichomezwa ni mwili usiokuwa na roho.

Mbinu aliotumia Lekcha iliweza kumuokoa kwani alitumia sekunde chache tu ambazo Roma alikuwa akizubaa na kupotea mbele yake akiwa ameipatanisha nafsi yake na nguvu ya Ant- matter energy hivyo kubakia katika umbo la mtu aliekuwa kama nishati.

Roma licha ya kugundua amechelewam hakutaka kumuacha aondoke kizembe , ijapokuwa Lekcha alipotea kwa haraka lakini alikuwa bado akipatwa na msisimko wa uelekeo wa nguvu ya Ant – matter na aliitumia hio kumfukuzia.

Roma palepale alirudisha chungu chake na kuanza kumfukuzia Lekcha ambaye alikuwa ni kama mwanga unasafiri angani.

Lekcha aliweza kuelewa hakuwa na spidi ya kutosha ya kumshinda Roma na kujua muda si mrefu anaweza kukamatwa na hapo ndipo wazo la mwisho la kujiokoa lilimjia akilini.

Ilikuwa ni njia pekee ambayo alikuwa ameipanga kwa ajili ya kujiokoa , akiwa katika hali ya hatari na muda kama huo ndio wazo hilo liliweza kumjia akilini na alitoa tabasamu la nia ovu, alijua kwa vovyote vile hakuna namna ambayo Roma anaweza kumdhuru kama atatekeleza wazo lake.

Upande wa Roma hakujua Lekcha anataka kufanya nini kwani ghafla tu alibadilisha uelekeo , lakini licha ya hivyo hakutaka kumuacha , alipanga kummaliza kabisa usiku huo huo.

Zilipita kama dakika herathini za Roma kumfukuzia Lekcha , shukrani kwa spidi ambayo walikuwa wakitumia hawakuweza kuonekana katika maeneo ambayo yalikuwa ni mchana.

Sasa baada ya kufika katika kilele cha mlima ambacho kwa ufahamu wa Roma katika matumizi ya Ramani aliweza kugundua eneo hilo ni ndani ya China , ilikuwa ni rahisi kusema ni mpaka unaoitengeanisha China na Mongolia.

Roma hakuelewa Lekcha anataka kufanya nini ila hisia zake zilimwambia kabisa amefikia mwisho wa kukimbia.

“Emei!!!”

Roma moyo wake ulipiga Kite kwa nguvu mara baada ya kugundua nini Denisi anataka kufanya.

SEHEMU YA 597.

Sio kwasababu tu ya Skendo ndio ilioweza kumfanya Sophia kuachana na maswala ya muziki.

Na sio pia kwasababu ya Skendo ndio akaamua kupotezea hisia zake na kuacha kabisa kumfikiria Roma au kuwa na mpango wa kutokuendelea kumtaka la hasha , mrembo Sophia alikuwa na lake kichwani ambalo alikuwa akipanga , alijiambia alikotoka ni mbali kuliko anakoelekea.

Kuachana na usanii na kurudi Japani ilikuwa ni kisingizio tu lakini katika kichwa chake alikuwa akipanga kujifunza kwa bidii zote namna ya kuvuna nishati za mbingu na Ardhi ili kuwa katika levo ya juu ya kuweza kubeba ujauzito wa Roma akiwa wa kwanza, hakujali Rose na Magdalena walikuwa wamemtangulia lakini alijiambia kutangulia sio kufika na isitoshe kupanda levo hakukutegemeana na muda wa mafunzo bali uwezo wa mtu kuelewa siri alizofichiwa binadamu juu ya ulimwengu.

Sophia aliamini kama ataweza kuwa katika levo za juu za mafunzo ya kijini hata hitaji kuwa na juhudi kubwa za Roma kumtaka.

Maelekezo ya namna ya kuvuna nishti za mbingu na Ardhi huwa mara nyingi yanahitajika maelezo ya mara moja tu ya namna inavyofanyika na baada ya kuelewa kinachofatia ni kazi ya mtu mwenyewe kuweza kufanya Tahajudi na kufikiria ili kupata ufunuo, isitoshe katika kujifunza mbinu za kijini hakuhitaji kuuliza maswali kwani hata kama uulize swali hakuna ambaye anaweza kujibu kutokana na msingi wa kwamba kila moja anapata ufunuo wa kwake mwenyewe juu ya kuweza kuvuna nishati hizo, mwisho wa safari unaweza kuwa mmoja lakini njia zikatofautina hio ndio maana ya uzoefu binafsi unaohitaji kutafuta jibu mwenyewe kwa kila swali.

Sophia alikuwa akielewa msingi huo na ndio maana hakuona haja ya kuwa na Roma karibu ili aweze kupanda levo bali ni juhudi zake pekee ambazo zingeweza kumpandisha Levo kwa haraka.

Hatua ya kwanza kwa Sophia ni kurudi Japani kwa wazazi wake na baada ya hapo angetafuta eneo tulivu ambalo lingemuwezesha kuvuna nishati ya mbingu na ardhi na sifa za eneo ambalo alikuwa akitaka Japani haikuwa jibu.

Temple ambalo alijifunzia Kung fu , maarufu kwa jina la Emei ndio mahali alipoona panamfaa sana , Emei ni Temple ambalo lilikuwa likipatikana katika mlima wa Emei katika dhehebu la Shushan chini China.

Roma licha ya kwamba hakumtafuta Sophia tokea siku ambayo ameondoka baada ya kutangaza kuachana na mambo ya usanii sio kwamba hakumfatilia.

Kitendo cha kumuona Lekcha ananyoosha moja kwa moja juu ya mlima wa Emei ilimkumbusha kwamba Sophia alikuwa akiishi katika eneo hilo na jambo hilo lilimfanya moyo wake kupiga kite kwani hakutegemea Lekcha angekuwa na uelewa juu ya Sophia kupatikana eneo hilo , kwa jinsi ambavyo walisafiri muda mrefu ilionekana hilo ndio wazo lake Lekcha la muda wote.

Akili yake ilifanya kazi kwa haraka sana na kitu pekee ambacho alihisia ni huenda Lekcha aliweza kufahamu eneo hilo kwa kuweza kutumia kumbukumbu za Denisi maana hata yeye alijifunzia mafunzo yake hapo.

Ndani ya eneo hili Shushan ndio mahali ambapo Sophia alikuwa akifanyia mazoezii yake ya kuvuna nishati ya mbingu na ardhi.

Ilikuwa muda wa asubuhi ndani ya Shushani , eneo hilo lilikuwa limejengwa kwa mtindo wa kizamani zaidi ni rahisi kusema Shushan ilikuwa na mfanano wa kiasi kikubwa na Dhehebu la Tang sehemu ambayo Magdalena alisomea mafunzo yake ya kichawi.

Katati ya eneo hilo kulikuwa na mnara(Tower) ,mrefu kwenda juu ambao ulikuwa umejengwa kwa utofauti mkubwa na minara iliokuwa katika madhehebu mengine, mnara huo ulikuwa na historia ndefu na inasemekana mnara huo ulikuwa ndio wa kwanza kujengwa kabla ya ujenzi wa nyumba na makazi ya kidhehebu na ni zaidi ya miaka mingi iliopita na hakuna historia yoyote ambayo ilieleza ni nani alihusika katika ujenzi, eneo hilo licha ya kuwa chini ya dhehebu la Shushani lakini kuhusu mnara ilikuwa siri ya taifa la China.

Sasa wakati huo ndani ya ukumbi mkubwa ndani ya eneo hilo walionekana wanawake wanne waliokuwa katika mavazi ya vitamba vya hariri vya rangi nyeupe , kati ya wanawake hao ni mmoja tu ndio ambaye alionekana kuwa na utofauti na wengine wote kutokana na rangi yake kuwa na mchanganyiko wa Kiafrika.

Sasa ilikuwa ni dakika chache tu wanawake hao wakati wakiongea kwa furaha ghafla tu kivuli cha mwanga wa Silver kiliweza kuonekana kikiingia hapo ndani na kusogelea wale wanawake kwa spidi kubwa.

Ilikuwa ni dakika ileile wale wanawake walijikuta wakipatwa na mshituko wa ghafla na kukwepa, yule mwingine aliekua na utofauti alijikuta akishikwa shingonni na kitu chenye ubaridi wa aina yake, akiwa kama yeye ndio aliekuwa mzembe wa kuwa kama wenzake lakiini ukweli ni kwamba wale hawakuwa walengwa ndio maana waliweza kuponyoka.

“Ring!!!”

Ulikuwa ni kama mlio wa kengele yule mwanamke alijikuta akifungwa kuanzia miguuni na shingoni kimajaabu na nyuzi za nishati ya Ant- matter.

“Sophia..!!”

Walijikuta wale wanawake wengine wakipiga makelele baada ya kuona kile kinachomtokea mwenzao.

“Wewe ni nani?”Walianza kupiga kelele kwa lugha ya Kimandari na kingereza kwa wakati mmoja.

Sophia akiwa katika hali ya aibu ya kutoweza kujiokoa na chuki alijikuta akishangaa kuona kiumbe kilichokuwa na muonekano wa kibinadamu , ilikuwa sahihi kusema kiumbe kutokana na mwonekano wake kutokuwa wa kawaida lakini palepale kiumbe kile kilibadilika na kuwa katika umbo halisia lakini sura yake bado hakuweza kuitambua.

Sophia alijaribu kuita nguvu ya kijini ili kuweza kujitoa katika vifungo alivyofungwa lakini hakufua dafu na kujikuta kuzidi kujawa na hofu , kilichomshangaza zaidi ni kwamba nguvu ambayo ilikuwa memfunga miguu yake haikuwa ya kawaida kabisa na ilikuwa katika hali ya ubarafu.

Dakika ileile wakati Sophia akifurukuta alijikuta akipigwa na mshituko zaidi mara baada ya Roma kuonekana mbele yake na mpaka hapo akili zake zilimwambia yupo katika hatari.

“Roma..!!”

Ijapokuwa wakati huo mtu aliemfunga kimaajabu alionyesha zaidi ukali wake lakini kwa Sophia alijikuta akipatwa na furaha isiokuwa na kifani , hakuamini angeweza kumuona Roma katika eneo hilo.

“Muachie tafadhari , matendo yako ndio yatarahisisha kifo chako”Aliongea Roma.

Roma mara baada ya kuona kuna nguvu ambayo imeifunga miguu ya Sophia alijua kabisa hapo anapaswa kuwa makini la sivyo ataleta matatizo zaidi.

Roma alijiambia huyo mwendawazimu amefanya chaguo sahihi kabisa kuja kujaribu kumteka Sophia maana alikuwa akimjali sana , ijapokuwa hakuweza kujua ni kwa namna gani mpaka aliamua kufanya chaguzi hio lakini ukweli ni kwamba kwa namna yoyote asingeweza kuona Sophia akipata matatizo.

“Umafikiri najali hilo , kwasababu najua naenda kufa nitamshikilia kama mateka ili nniweze kutoroka, najua una upendo wa juu sana kwa huyu mwanamke”

Roma kabla haa hajaongea Sophia alianza kuongea yeye kwa nguvu.

“Unaongea ujinga, wewe ni nani kwanza ?, mimi sio mwanamke ambaye Bro Roma ana mapenzi nae”

“Hahaha… Sophia kama nitakuwa sijakosea mashabiki zako wanatarajia ujio wako wa mara ya pili katika usanii tena kwa kishindo , wewe tayari ni Celebrity k wanini unajaribu kujishusha , nilishangaa sana kupata taarifa umekuja kujichimbia huku mbali maporini, halafu sijasema neno mapenzi bali nimesemea swala la upendo , inawezekana ni upendo kati ya dada na kaka hehe..”

Sophia mara baada ya kuumbuliwa aijikuta akigeuka kuwa nyanya kwa aibu.

Upande wa Roma hakuwa tayari kumuona Sophia akiwa hatarini na alijitahifi kuvuta pumzi ili kuweza kujituliza.

“Kwahio unadhani kumfanya mateka ndio kutanifanya nishindwe kumuokoa na wewe kukuua?”

“Haha,, kama unachosema ni kweli basi jaribu tuonea nani atakuwa na spidi ya kumuua mwenzake , mimi kumuua huyu mwanamke au wewe kuniua mimi”

Sophia baada ya kusikia maneno hayo aliweza sasa kuelewa nini kinachoendelea , alijua kwamba aliemteka ni adui wa Roma.

“Roma wewe huna haja ya kunijali mimi na kuanza kumsihi aniachie, anaonekana kuwa mhenzi kweli hivyo unapaswa kumuua ,sitojali kama nitadhuli…”Kabla hata hajaendelea kuongea alihisi maumivu makali kwenye shingo yake.

“Unamaanisha nini kwamba nisikujali wewe , kaa kimya maana sijakupa nafasi ya kuongea”Alifoka Roma huuku akimwangalia Sophia kwa macho makali.

Sophia palepale alijikuta akitoa machozi mengi huku akimwangalia Roma lakini upande wa Roma hakutaka kujali machozi yake bali usalama wake kwanza.

Roma palepale alisogea mbele huku akiachia mkandamizo mkali wa hewa wa levo za juu katika kuipita dhiki.

Kitendo cha Lekcha kuhisi mkandamizo ule aliona Roma alikuwa akipingana na onyo lake , Lekcha alikuwa akielewa kwamba kadri Roma anavyochelewa kufanya maamuzi ndio itamuonyesha ni kwa namna gani mateka wake ana thamani.

Lekcha palepale alitoa kamba nyingine kama shoti za Ant-Matter tatu kwa pamoja na kuwakaba shingo wale wanawake wengine waliokuwa wamebakia. Na hali hio ilimfanya Roma kusimama na kuacha kutoa mkandamizo.

“Unaonaje , mipango yangu imefeli kwasababu nilikudharau lakini hii hamaanishi kwamba wengine wanaweza kuhimili mashambulizi yangu , ijapokuwa mimi sio wewe lakini gepu la utofauti wetu kinguvu sio kubwa , hivyo kubali ninachokuambia la sivyo kabla hujanifikia mimi utaokota kwanza maiti ya huyu mrembo”

“Kwahio unanitishia?”

“Utanifanya nini kama unaona na kutishia , najua utahesabu kila kitu kilichotokea nyuma na utaniua kwa namna yoyote ile , hivyo kwanini nisihakikishe nawewe nakupisha kwenye machungu kabla ya kunifikia”Aliongea na kumfanya Roma kupandwa na jazba lakini mpaka hapo hakuwa akijua ni kipi anapaswa kufanya maana asingeweza kukubali kumuona Sophia akigeuka na kuwa maiti.

“Una taka nini?”Aliuliza Roma huku akikunja ngumi yake kwa hasira kiasi cha kufanya kucha zake zitoboe kiganja cha mkono.

‘Tutafanya hivi kwani ni rahisi sana , utaondoka hapa kwenda mbali baada ya kukuwekea nguvu kiasi ya Ant-Matter ambayo itanifanya kujua ni umbali gani umefikia na baada ya hapo nitamuachia Sophia na kukimbia”

‘Kwahio unanifanananisha na kitoto cha darasa la kwanza si ndio ?, kama nitakuacha hapa na kufanya unavyotaka sio tu kwamba utaendelea kumshikiria lakini pia utaenda kujificha na kunifanyia hila kwa mara nyingine, unajuaje huenda ukanigeuka pia na kumuua Sophia”

“Kwahio unataka nini , pointi ya msingi hapa ni wewe kufanya kama ninavyokuambia ,Sophia yupo mikononi mwangu na huna chaguo labda kama unataka kumchukua akiwa maiti “Aliongea na kumfanya Sophia amwangalie Roma na kuzidi kutokwa na machozi na ndani ya dakika kadhaa alijikuta akitoa tabasamu la uchungu , alikuwa ni kama vile kuna wazo limemjia.

“Roma siwezi kukurudisha nyuma na mipango yako”Aliongea

Wakati huo Roma alikuwa akiwaza achukue risk kumuokoa Sophia au afanye kama anavyotaka Lekcha

“Usiwe mjinga Sophia”Aliongea Roma kwa sauti lakini ni kama vile amechelewa kwani palepale Sophia alitema damu nyingi sana huku akiwa ni kama viungo vya ndani mwake vimepasuka.

Roma aliweza kujua Sophia ameweza kufanya jaribio la kujiua kwa kupasua mishipa yake ya damu na nguvu za kijini, hilo liliwezekana kutokana na Sophia alikuwa tayari amekwisha ingia katika levo ya mzunguko kamili.

Kitendo alichokiufanya kilimshangaza Lekcha , hakutegemea swala kama hilo kujitokeza , hakuamini kama Sophia angekuwa na uwezo wa kujiua kwa ajili ushindi wa mwanaume anaempenda

Kitendo chake cha kuchanganywa kidogo na Sophia palepale Roma alitumia nafasi hio vizuri kwani kwa spidi kubwa Roma alikuwa tayari ashamfikia Lekcha mbele yake na kumtwanga ngumi nziro ilioambatana na nguvu za mbingu na ardhi katika eneo la kichwa.

Kitendo cha kutawanyisha eneo la kichwa cha Lekcha hakutaka kusubiri tena kwani palepale alimnyakua Sophia na kupotea nae huku wakati huo huo akiita Caulrodn na kukiacha katika eneo hilohilo.

Roma alikuja kuibukia juu kabisa angani akiwa amemshikilia Sophia ambaye alikuwa amelegea kabisa shingo huku ikiwa haieleweki amepoteza maisha au vipi.

Hasira za Roma ndio ambazo zilimzidia mpaka kuita chungu cha maafa bila kujali matokeo na awamu hio kilikuwa na nguvu kubwa kuliko alivyokitumia mwanzo na kilikuwa na uwezo wa kuvuta kiumbe chochote chenye nguvu ya kiroho mpaka umbali wa kilomita moja.

SEHEMU YA 598A.

Chungu cha maafa kiliuelekezea mdomo wake sehemu ambayo amesimama Lekcha , lakini upande wa Lekcha alikuwa mwepesi sana kufanya maamuzi kwani aligeuka kutoka mwili wa kawaida na kurudi katika umbile la nishati lakini hata hivyo ilikuwa bure.

Lekcha kwa wakati huo alikuwa ametumia kiasi kikubwa sana cha nguvu ya nishati ya Ant- matter na yeye alikuwa tofauti na Roma ambaye nguvu zake hazikutegemea zile ambazo zipo nfdani yake , alikuwa na uwezo wa kuvuna nishati muda wowote na kuzitumia.

Ni muda huo huo mwili wake uliokuwa katika umbile la nguvu ya nishati ya Ant- matter ulianza kutawanyika vipande vipande.

“Hapana siwezi kufa …. Hapana!!”

Lekcha alijikuta akitoa ukulele wa aina yake kwani alishindwa kabisa kuzuia nguvu ya chungu kummeza.

Ilikuwa ni wakati ambao Lekcha aliona kabisa huo ndio mwisho wake, lakini katika hali ambayo hakuwa ameitarajia palepale kulitokea mabadiliko ambayo hayakugegemewa.

Roma mwenyewe hakuweza kutegemea kile ambacho kinakwenda kutokea , ule mnara uliokuwa umejengwa kwa usanifu wa kipekee ulikuwa ukionekana kama vile unacheza cheza , ilikuwa ni kama vile ni tetemeko kubwa la Ardhi ambalo lilikuwa likicheza cheza na ilichukua sekunde hio kulitokea boriti kama tano za mwanga uliokuwa kama Laser rangi ya dhahabuu na kugonga katika wingu ambalo lilikuwa likianza kuzunguka kama vile mvua inataka kunyesha.

Pale juu ya kichwa cha mnara ni kama kulikuwa na kimashine amaalumu kinachofanya kazi na kudhalisha boriti hizo za mwanga.

Cauldron yenyewe palepale iliweza kuzimika na nguvu yake ya mvutano iliisha na ikawa pona ya Lekcha kumezwa.

Roma mwenyewe hakuwa akieleewa ni kitu gani ambacho kinatokea katika hilo eneo na alianza kuzungusha kichwa chake kuangalia kulia na kushoto, hisia ambazo alikuwa akipata zilikuwa tofauti na zile za kupigwana radi baada ya kukiuka kanuni za anga.

Nafsi iliokuwa kwenye Cauldron na yenyewe ilianza kufurukuta kwa namna flani ya kuonyesha woga na jambo hilo lilimshangaza Roma na kujiuliza nini kinatokea

Lekcha ambaye alikuwa dhaifu sana hakuweza hata kukimbia licha ya kuachiwa na chungu na baada ya kuona Roma hakuwa akimwangalia palepale alijaribu kujitengenezea kamba kama vile ni Spider man ili kukimbia lakini ghafla tu ilitokea Flash ya mwanga mkali pamoja na shoti ya aina yake kwenye ule mnara.

Kitendo cha Lekcha kutaka kukimbia tu alijihisi nguvu ya ajabu ikimrudisha nyuma .

“Buzzz!!!!”

Ulisikika mlio wa aina yake wa Radi kutoka katika mawingu yaliokuwa yakizunguka juu na kupiga kwa nguvu ule mnara na kusababisha mpasuko mkubwa wa shoti za umeme.

“What the hell is happening!!!”

Roma alipiga yowe huku akirudi ardhini kwa tahadhari, alijawa na hofu isiokuwa ya kawaida , sekunde moja alidhania huenda n kutoka na kusafiri umbali mrefu sana hivyo akakiuka sheria za anga lakini kilichomshangaza ni kwamba mnara ndio uliokuwa wa kwanza kutoa mwanga wa kimaajabu na ilikuwa ni kama vile ndio uliochokoza radi.

Roma hakutaka kujiuliza mara mbilimbili wakati anahisi hatari alikuwa asharudisha tayari Sophia chini kwa kuhofia angedhurika lakini kwa namna ambavyo mnara huo ulikuwa ukishambuliwa na Radi kwa spidi hakutaka kubakia ttena katika eneo hilo..

Alimnyakua Sophia kwa haraka sana huku akiachana na wazo la kumuua Lekcha tena na kujiokoa yeye mwenyewe na Sophia.

Sophia hakuwa amekufa bado , ijapokuwa damu zimevilia kwa ndani lakini bado alikuwa akipumua kwa mbaali na Roma aliona aondoke ili akamsaidie mbele kwa mbele wakati huo akimwingizia nguvu ya kimaandiko ili kusaidia kupona.

Upande wa wanafunzi wote waliokuwa wakifanya mazooezi katika majumba tofaut tofauti waliweza kukurupuka walipokuwa na kutoka nje kushangaa nini kinaendelea, lakini baada ya kushuhudia mashambulizi kati ya anga na ule mnara walijikuta wakihofia uhai wao.

Dakika hio hio ilikuwa ni kama vile ule mnara unayeyuka katika kilele chake na kuonyesha chuma kikubwa kinachotoa mwanga wa rangi ya gray.ilikuwa rahisi kusema huenda huo mnara ulijengwa kwasababu ya kuzuia radi kutokana na namna ambavyo radi zilivyokuwa zikirindima huku ngurumo kubwa zikisikika pamoja na shoti lakini kwa wakati mmoja mnara ule haukuzima zile boriti zake za rangi ya gold zilizoelekea angani.

Kadri radi iliovyokuwa ikipiga ndio iliwezesha ule mnara kutoa mwanga kama vile ni projector na kuonyesha baadhi ya maumbo ya kimaandishi kama Runes hivi ambazo hazikuwa zikieleweka maana yake.

Roma hakutaka kendelea kushangaa palepale alipaa angani ili kukimbia na wakati huo huo na Lekcha na yeye alitumia nafasi hio kujaribu kutokea lakini ilikuwa ni kitendo cha kasi sana kilichotokea kwani zile boriti za miale ziliancha kumulika juu angani na ziligeuka na kuwa kama minyororo kwani wakati Roma anataka kukimbia alifungwa kiunoni akiwa na Sophia na kuvutwa kwa nguvu kubwa ilikuwa ni kama vile mnara ule ulikuwa ukiendeshwa na mtu na haikuwa kwake tu hata kwa Lekcha ilikuwa hivyo hivyo wote kwa pamoja waliweza kuvutwa kwa nvuvu na mnara ule kuelekea katika eneo ambalo kulikuwa kama vile kuna anga linachemka.

Roma baada ya kuona alikuwa ameshikilia Sophia kwenye mikono yake alikosa uamuzi wa haraka aa aidha amdondoshe chini lakini kiendo cha kutaka kumdondosha chini tu ni kama alishitukiwa na mnara ule kwani palepale na Sophia na yeye alifungwa fungwa na boriti za mwanga na wakaavutwa wote kwa pamoja kwa pamoja

Kilichokuwa kikimtokea Roma ndio kilichokuwa kikimtokea Lekcha , tena kwa Lecha ilikuwa rahisi sana kwani hakuwa na nguvu na alivutwa kwa spidi na kutupiwa katika eneo ambalo anga lake lilikuwa likichemka kama vile ni maji .

Upande wa Roma alijikuta roho ikimuuma kwani kadri alivyokuwa akipambana kwa kuita nguvu za kijini ndio alivyokuwa akizidi kuvutwa na kusogezwa karibu , huku akipatwa na hruuma na kuona anakufa akiwa na Sophia mkononi.

Alijaribbu kuita na chungu chake kiweze kumsaidia lakini hakukuwa na majibu na palepale bila ya kupenda alivutwa kwa kasi sana na kutupiwa katika mchemcho ule wa anga kama ilivyokuwa kwa Lekcha na wakapotea yeye na Sophia.

Ni dakika chache tu baaada ya Roma kupotelea kwenye kiwingu cha mnara ule , palepale ile radi ilipotea na mnara ukaacha kupiga shoti na kukawa kimya kwa mara nyingine

Wale wanafunzi wa pale wenyewe walijikuta wakianza kushangaa na kujaribu kwenda kusimama chini ya mnara kujua Roma na Sophia pamoja na Lekcha wamepotelea wapi lakini hakukuwa na chochote.

Kutokana na eneo hilo kuwa juu mlimani haikuweleweka kama watu wa mbali wameona nini lakini ilibakia kuwa stori ya siku hio kwa wanafunzi na walimu wa dhehebu la Shushani huku habari ikiwa ni kupotea kwa watu juu ya mnara huo ambao kwa mara ya kwanza tokea uwepo hapo hikuwahi kutokea kwa kitu kama hicho.

ITAENDELEA
WATSAPP 0687151346
 
Mgosi singano kwanza pongez kwako kwa uandish ulio na mtiririko murua.ila umekaa muda mrefu sana alafu umetupia mzigo kidgo
 
SEHEMU YA 126

“Chino karibu sana”Aliongea Bi Wema kwa uchangamfu huku akimkaribisha Mzee Chino ambaye alionyesha pia kumfahamu Bi Wema.

“Asante sana Wema , ni muda sasa tokea mara ya mwisho tuonane”

“Ni kweli nadhani ni Zaidi ya miaka mitano sasa”Aliongea Bi Wema huku akiwa na tabasamu , lakini kwa Roma na Edna walikuwa kwenye hali ya mshangao, hawakuelewa kwanini yuke muhudumu wa mgahawa kutoka Upepo Beach Gaeden yupo nyumbani kwao akijitambulisha kama mwanasheria.

“Mr Roma , Miss Edna tunaonanatena , habari za toka jana?”.

“Salama Mzee Chino karibu sana”Alijibu Edna huku akimpatia mkono na Mzee Chino aliekuwa ameshikilia mkoba wake , alikaa chini kwenye masofa hayo.

“Kumbe Chino umeonana na Edna pamoja na Roma ?”

“Yeah nimeshaonana nao jana tu, walikuja kwenye mgahawa wangu”Aliongea Mzee Chino na kumfanya Roma atabasamu.

“Mzee Chino , Unaonekana kuwa na sura nyingi sana,najiuliza baada ya leo utanishangaza kwenye jambo lipi lingine”Aliongea Roma na kumfanya mzee huyu kutabasamu.

“Mr Roma nadhani na mimi pia napaswa kuzungumza hayo maneno”Aliongea.

“Miss Edna nadhani leo ni mara yetu ya pili kuonana, jana ulinifahamu kama mhudumu , lakini leo hii nipo hapa kama mwanasheria wa bibi yako Marium na nadhani mpaka sasa Wema ashakuambia baadhi ya mambo kutokana na kile kinachosambaa mtandaoni , si ndio?”Edna alitingisha kichwa.

“Okey basi nadhani kazi yangu itakuwa rahisi sana kwa siku ya leo”Aliongea huku akifungua mkoba wake uliokuwa pembeni na kutoa bahasha kubwa aina ya Khaki na kutoa karatasi kadhaa na kuziweka mkononi na kisha akarudisha ile bahasha kwenye sofa.

“Hii ni karatasi inayonitambulisha kama mwanasheria Binafsi wa Bibi yako Marium Adebayo”Aliongea na kumpatia Edna ambaye alipitisha macho yake haraka haraka na kuona kweli kulikuwa na sahihi ya mkataba wa kisheria kati ya Bibi yake na Mzee Chino.

“Hii nyingine ni mkataba ambao niliusiimamia miaka ishirini na tano nyuma , mkataba uliofanyika kati ya mama yako ,Adebayo na Bibi yako”Aliongea Mzee Chino na kumfanya Edna auchukue na kisha kuangalia na alijikuta macho yakimtoka mrembo huyu na Roma baada ya kuona Edna kashangaa , alimpokonya na kuangalia ni nini kilichoandikwa kwenye mkataba huo.

Na Roma aliweza kuona kipengele ambacho kilikuwa kikisomeka kwamba , Marium anakiri Edna kutokuwa mtoto halali wa Mzee Adebayo na Pia Raheli anakiri kwa Edna kutokuwa mtoto wa kuzaliwa wa Mzee Adebayo.

Kipengele Cha pili, Edna licha ya kutokuwa mtoto wa damu wa Mzee Adebayo, kupitia mkataba huu unamfanya Edna kuwa mtoto wa pekee wa familia ya Adebayo kutokana na makubaliano kati ya Raheli na Adebayo huku Marium akiwa Shahidi.

Yaani kwa maneno marahisi ni kwamba mkataba huo ulikuwa umesainiwa na watu watatu , Adebayo , Rahel , pamoja na Marium kama shahidi na huo mkataba ulikuwa ukimlinda Edna kama mwanafamilia halali wa kipekee wa familia ya Adebayo , lakini pia mkataba huo ulikuwa ukimzuia Edna kwa hali yoyote ile kutobadilisha jina lake , ama kutomkubali baba yake mzazi kwa namna yoyote ile na kama tu atakubali kuungana na baba yake mzazi basi atakosa haki ya umiliki wa mali zote za familia ya Adebayo.

“Miss Edna , mpaka hapo nadhani ushaelewa kwanini nimekuja siku hiii ya leo, kama utaangalia sehemu ya huo mkataba kuna sehemu haikusainiwa na hio sehemu inakuhusu wewe, na mimi kama mwanasheria wa Marium nitasimamia maamuzi yako ambayo utakwenda kufanya siku hii ya leo”Aliongea Mzee huyu kwa kujiamini na kumwangalia Edna ambaye alikuwa akisoma tena mkataba huo baada ya kuchukua kutoka kwenye mikono ya Roma.

“Kwa Jinsi nilivyoona hapa inaonesha kama nikisaini sitokuwa na haki ya kumtambua baba yangu na nitabakia kuwa mwanafamilia ya Adebayo?”

“Hakika Miss Edna , Kama utasaini hio karatasi , kwanzia siku hii ya leo utakuwa ni mtoto kamili wa familia ya Adebayo na hautakuwa na uwezo wa kubadilisha hapo baadae hata kama baba yako mzazi ajitokeze na kama utataka kuvunja mkataba huu muda wowote basi hautokuwa na haki ya umiliki wa aina yoyote ya mali za kampuni na moja kwa moja mali zote zitakuwa chini ya umiliki wa kituo cha kulelea watoto wa Son And Daughter Orphanage”Aliongea Mzee Chino na kumfanya Edna afikirie kidogo.

“Mzee Chino nadhani tumpe muda wa kufikiria mke wangu kwanza”Aliongea Roma na kumfanya Mzee Chino atingishe kichwa chake na Edna alishukua ile karatasi na kupandisha juu Ghorofani , ni hakika mrembo huyu alikuwa akitaka kufikiria , kwani swala la kusaini huo mkataba ni kwamba lingemzuia yeye kutokuja kumtambua baba yake mzazi katika maisha yake yote na hivyo ni swala ambalo hakutakiwa kukurupuka na pia ilionesha Edna hakupewa kusaini karatasi hio akiwa mdogo na alisubiriwa akiwa mkubw aili afanye maamuzi yake yeye mwenyewe.

Edna baada ya kukaa kwenye kitanda chake , alijikuta akiingia kwenye mawazo ya tokea akiwa mdogo , mrembo huyu alifikiria maisha yake yote alivyokuwa ameishi na bibi yake Marium , Edna katika kuwaza maisha ya Bibi yake Mariuma hakuweza kuona siku yoyote ambayo Marium ashawahi kuonyesha dalili zozote za kumchukia , Marium katika maisha ya Edna alionekana kama mwanamke mwenye upendo wa Dhati kabisa , na Kwa Edna alijitahidi kukumbuka namna yoyote ambayo bibi yake alionyesha kutompenda , lakini alishindwa kupata dosari , bibi yake alikuwa akimpenda kama mjukuu wake halisi na alimpa kila kitu alichokuwa akitaka kwenye maisha yake.

Edna alianza pia kukumbuka maisha ya mama yake na bibi yake yalivyokuwa , lakini mrembo huyu hakuona dosari yoyote kati ya bibi yake na mama yake , licha ya kwamba Mama yake alikuwa akionekana kuwa mpweke sana kwenye maisha yake , lakini siku zote alimuona Bibi yake alikuwa ni mtu wa kumfariji.

Edna aliweza pia kufikiria namna ambavyo aliweza kuishi na baba yake mzee Adebayo na aliona kweli kwa maisha ambayo aliweza kusihi na baba yake , hakuona dalili yoyote ya Mzee Adebayo kumpenda kama mtoto wake , hivyo kukosa kabisa radha ya mapenzi ya baba.

Mrembo huyu pia hakuacha kuwaza kazi aliokuwa ameachiwa na mama yake , juu ya swala la kulipiza kisasi , kisasi ambacho mpaka muda huu hakuwa akikifahamu kinahusiana na nini Zaidi ya kupewa muongozo wa kile cha kufanya , aliwaza na akawaza na akawazua kwa takribani nusu saa kupita na bado hakuwa amefikia kwenye maamuzi.

“Au The Protector ndio baba yangu mzazi?”Aliwaza Edna huku akijikuta akianza kukumbuka kwanzia siku ya kwanza alivyoanza kuwasiliana na mtu ambaye hakuwa akitaka kujitambulisha kwake Zaidi ya kujiita The Ptotector na kumsaidia katika mambo mbali mbali yanayohusiana na kampuni.

“Mr Roma jana nilishindwa kuongea mbele ya mkeo , ila niseme kijana una hatari sana”Aliongea Mzee Chino wakiwa wameketi na Roma sebuleni na muda huu Bi Wema alikuwa yupo jikoni akiandaa kifungua kinywa na Roma licha ya kuwa yupo hapo, lakini pia akili yake ilikuwa ikijiuliza Siphie yuko wapi.

“Mzee Chino kwanini unaongea hivyo?”

“Nadhani ushanielewa mpaka hapo Mr Roma”

“Aah Mzee Chino unamaanisha kuhusu Neema?”

“Ndio Mr Roma , Neema kwangu nikama mtoto wangu kabisa na tokea vifo vya wazazi wake , nimekuwa nikiishi kwa kuangalia kila mtu anaemzunguka kumpa usalama na hata mali ambazo aliachiwa na mama yake, nilisimamia mimi ili kiupata haki yake kisheria , licha ya kuwa na baadhi ya wadogo zake kutoka upande wa baba”Aliongea Mzee Chino na kumshanganza kidogo Roma.

“Point yangu Mr Roma ni kwamba mpaka sasa , Neema anaonekana kukupenda kwa dhati kabisa , jambo ambalo ni mara yake ya kwanza katika maisha yake , najua unaweza kushangaa na kujiuliza kwanini Neema ana mtoto na kisha nikasema ndio anapenda kwa mara ya kwanza , lakini naamini Neema mwenyewe atakuja kukuambia juu ya hilo”Roma alitingisha kichwa kumuelewa mzee Chino kwani wakati huu alionekana kuwa siriasi na sio kama yule aliekuwa muhudumu aliekuwa akipenda kuongea utani.

“Mzee Chino nini kiliwakuta wazazi wa Neema?”

“Kuna ajali ya ndege ilitokea miaka kadhaa iliopita , wakati Neema akiwa mdogo , ilikuwa inahusiana na kupotea kwa ndege ya shirika la M Airline”

“Kupotea kwa ndege?”

“Ndio Mr Roma , kuna ndege ambayo iliopotea miaka kadhaa nyuma ni miaka ya tisini hivi na wazazi wa Neema walikuwa ndani ya ndege hio , ilikuwa ni tukio ambalo lilimumiza sana Neema kwa wakati huo , kwani wazazi wake walikuwa wakienda kumsalimia Neema wakati akiwa yupo nchini China kimasomo”Aliongea Mzee Chino na kumfanya Roma kuelewa, lakini pia kushangaa.

“Mr Roma hakikisha maamuzi ambayo utayafanya kati yako na Neema hayatomuumiza”Aliongea Mzee Chino na wakati huo huo Edna alishuka kutoka juu akiwa ameshikilia ile karatasi na alionekana tayari ashafanya maamuzi.

“Mzee Chino nipo tayari kusaini”Aliongea Edna na kumfanya Roma kushangaa , kwani maamuzi hayo yalikuwa yakimaanisha kwamba Edna anamtelekeza baba yake mahali popote alipo na hatokuja kumtambua.

“Wife unauhakika na maamuzi yako?”Aliuliza Roma huku akimwangalia Edna.

“Ndio nipo na uhakika , kama kweli kuna mtu ambaye alikuwa ni baba yangu mzazi , kwanini mpaka leo nimekuwa mkubwa hivi hakuwahi kujitokea kwangu na kusema mimi ni baba yake na kunifanya niishi kwa kukosa malezi ya baba?”Aliongea Edna kwa msistizo na kumfanya Roma ashindwe hata kuongezea neno, kwanza alitegemea Edna kufanya maamuzi hayo.

Edna alitia sahihi kwenye mkataba huo ambao ulikuwa ni kama wosia kutoka kwa bibi yake Edna pamoja na mama yake.

Baada ya taratibu hizo kuisha, Mzee Chino aliaga na kuondoka licha ya kulazimishwa kusubiria chai , lakini mzee huyu aliwaambia kuwa anapaswa kuwahi kwenda kuhudumia wateja wake wa Mgahawa.

Ni kama simu ya Edna ilikuwa ikimsubiria Mzee Chino aondoke kwani ilianza kuita mfuluizo na kumfanya Edna akili yake sasa irudi na kuanza kukumbuka hali ya kile kinachoendelea ndani ya kampuni , baada ya kuangalia ni nani aliekuwa akipiga, aliona jina ni la Nasra, alipokea haraka haraka na kuweka sikioni.

“Bosi hali ni mbaya , hisa zinazidi kuporomoka mpaka sasa na sijui hata cha kufanya na pesa taslimu kupambana na soko hatuna”Aliongea Nasra kwa wasiwasi na kumfanya Edna awaze kidogo.

“Vipi kuhusu benki ambazo tunashirikiana nazo kibiashara , jaribu kuwasiliana nazo watusaidie kiasi cha pesa ili tuweze kukabiliana na tatizo”

“Bosi nimefanya hayo na ndio maana nimekupigia sasa hivi , hakuna benki ambayo ipo tayari kutukopesha kiasi chochote cha pesa?”

“Nini!!?”

“Ndio Bosi napaswa kufanya nini juu ya hili , nimechanganyikiwa kabisa na Director’s wanapiga simu kila dakika , wanasema kama hautolipatia ufumbuzi swala hili ndani ya muda mfupi ,wataitisha kikao kwa ajili ya kuchagua CEO Mwingine”Aliongea Nasra na kumfanya Edna akunje ngumi ,mrembo huyu tokea hapo ashajua kuna mchezo ambao unachezwa.

“Nitakupigia Nasra”Aliongea Edna na kisha akakata simu

SEHEMU YA 127

Roma alimwangalia Mke wake kwa jinsi alivyokuwa na wasiwasi na alijua kabisa kuna tatizo ambalo linaendelea kwenye kampuni.

“Kuna nini Mke wangu?”Aliongea Roma huku akimwangalia Edna ambaye alijikalisha kivivu kwenye Sofa.

“Inaonekana mtu ambaye amevujisha taarifa , alikuwa na mpango Zaidi ya huo”

“Kwanini , kuna jambo ambalo limetokea kwenye kampuni?”

“Ndio Roma , Benki hawataki kunikopesha licha ya kufanya nao biashara kwa miaka kadhaa”Aliongea Edna huku mrembo huyu kwa mara ya kwanza aliona tatizo lililokuwa mbele yake ni kubwa mno.

Na ni kweli mpaka wakati huo Edna mategemeo yake yote yalikuwa ni kwa upande wa Benki, aliamini hata kama aonyeshe mkataba aliokuwa amesaini muda mchache na Mzee Chino haitosaidia.

Wakati Edna akiwaza chakufanya simu yake ilianza kuita tena mfululizo na baada ya kuangalia jina la mpigaji moyo wake ulipiga kwa nguvu , kwani aliekuwa akipiga alikuwa ni Tikayi., Edna alipokea na kuweka sikioni.

“Miss Edna sisi kama kampuni tumesikitishwa na kinachoendelea kwenye kampuni yako , na kama swala hilo lisipopatiwa ufumbuzi ndani ya msaa kumi na mbili yajayo tutajitoa kwenye mktaba wa kiabishara na kampuni yenu kisheria kabisa kama vipengele vya mkataba vinavyosema”Yaani Tikayi alionesha kuwa na hasira kweli kwani hakutaka hata salamu Zaidi ya kwenda moja kwa moja kwenye dhumuni la kupiga simu.

Edna alijiona kama anachanganyikiwa kwa wakati huo na alijikuta akinyanyka na kukimbilia juu, huku Roma akiwmangalia kwa huzuni , kwa mara ya kwanza alimuona Edna akikosa maamuzi juu ya hali iliokuwa ikiendelea kwenye kampini , lakini pia yule mwanamke ambaye siku zote ambazo alikuwa ni mwenye kujiamini leo hii , alikuwa emekosa kujiamini na karuhusu hisia zimtawale.

Wakati Roma akiangalia kile kilichokuwa kikiendeela kwenye Runinga , mara simu yake ilianza kuita na aliichukua na kuangalia namba na kuona ni ya Ron.

“Leta habari Ron?”

“Mfalme Pluto nishakamilisha kazi na sasa Dokta yupo chini ya vijana wetu wa kazi na wanasubiria utaratibu mwingine,Kama utaniruhusu Mfalme Pluto nimlete chapu na lile Mwewe letu la kivita , nina hamu nalo kweli na nitahakikisha kila atakae nizuia namshushia mayai Viza ya kutosha”

“Nataka wamhoji ni mtu gani ambaye amemuuzia taarifa nyeti ya kihospitali inayomuhusu Jedi Adebayo”Aliongea Roma.

“Mheshimiwa Pluto mpaka hapo nimekuelewa kabisa , tunajua kile kinachoendelea juu ya Malkia na nitakupiga ndani ya muda mfupi na majibu”

“Okey Ron, Mkishafanikisha kupata taarifa kutoka kwake namhitaji Tanzania ndani ya masaa machache yajayo lakini usimlete na ndege ya kivita”Aliongea Roma na kukata simu na muda huu huu , alimuona Edna aliebadilisha nguo akishuka kutoka juu akiwa na mkoba wake.

“Edna kama hawataki kukukopesha utafanya nini? ,au unakwenda kuwapigia magoti wakusaidie kiasi cha pesa unachotaka?”Aliongea Roma na kumfanya Edna asimame.

“Kwenye wakati kama huu nitafanyaje Roma ? ,zaidi ya kwenda kuwabembeleza”

“Usahasema kuna watu wanacheza mchezo na naamini washachukua tahadhari zote kuhakikisha mpango wao unafanikiwa”Aliongea Roma na kisha alimsogegelea Edna ambaye mwenyewe alikuwa akifikiria tu kama Roma , wakati huo alitamani kupata mtu wa kumsaidia kutoka katika hio hali.

Roma alimshika mikono Edna na kumsogeza mpaka kwenye sofa , licha ya Edna kutotegemea kitu kikubwa kwa Roma , lakini wakati huu aijisikia vizuri kuwa na mtu kama Roma ambaye anaweza kumfariji na kuwa upande wake , kwani siku zote mrembo huyu alikuwa mpweke na mtu pekee aliekuwa upande wake alikuwa ni Bi wema.

“Edna licha ya kwamba naonekana kama masikini , lakini katika maisha yangu siwezi kumruhusu mke wangu apigie watu wengine magoti kisa pesa”Aliongea Roma kwa kuwa siriasi na kumfanya Edna amwangalie Roma usoni na kushindwa kujua ni jambo gani Roma anamaanisha , kwani hakuwa njia nyingine Zaidi ya yeye kwenda kupiga magoti na kubembeleza watu wa benki.

Roma baada ya kuona Edna hakuelewa maana ya maneno yake aliingiza mkono wake kwenye mfuko wa suruali na kuibuka na Pete ya ajabu ambayo Edna kwakuangalia tu , alikumbuka tatoo iliokuwa kwenye mgongo wa Roma, ni pete iliokuwa na jina la AIDES, Edna alijikuta akishangazwa na uzuri wa pete hio.

Roma alitabasamu kwa namna ambavyo Edna alikuwa na mshangao na yeye pasipo ya kuongea neno , alichukua mkono wake wa kushoto na kutumbukiza ile pete kwenye kidole cha Edna , na wakati huu Edna mwenyewe alishindwa kuongea chochote kwani alikuwa kwenye mshituko wa namna pete hio ambavyo ilikuwa ikionekana , ilikuwa ikiwaka huku katikati ikiwa na madini ambayo Edna mwenyewe alishndwa kujua ni madini gani.

“Wife si umesema unataka kunijua japo kidogo basi vaa hii pete kwa muda na ukishatatua tatizo ambalo liko mbele yako nitakuambia maana ya hii pete”Aliongea Roma na kumfanya Edna ainue mkono kwa kwa kuangalia , kwa jinsi alivyokuwa ikionekana ni, kama alikuwa amevalishwa pete ya uchumba kwa jinsi alivyokuwa akigeuza geuza mkono wake.

“Inahusiana na nini , kwanini inaonekana ya ajabu?”

“Utauliza baada ya kujua nguvu ya hii pete , kwasasa nenda kashughulikie tatizo linaloendelea kwenye kampuni yako”

“Kivipi Roma unanichanganya ujue , acha utani?”Aliongea Edna kwa sauti kavu kidogo bila kutoa macho yake kwenye hio pete.

“Nenda Swiss Bank , nina uhakika tawi lao lipo hapa Tanzania , si ndio?”

“Ndio lipo , lakini kwnaini niende Swiss Bank?”

“Wife unatakiwa kuniamini mumeo , ninachokuambia nenda Swiss na utapata kiasi cha pesa unachotaka, wewe ukifika omba kuonana na Meneja mkuu wa benki na muoneshe hio pete halafu muambia unahitaji nini?”

Aliongea Roma , lakini wakati huohuo , aliingia Sophia ambaye alionekana kuwa katika haraka na haikueleweka amelala wapi , kwani kwa muonekano wake alionyesha kabisa hakulala hapo nyumbani jana yake usiku.

Sophia mara baada ya kuingia moja kwa moja alienda kumkumbatia Edna , mrembo huyu alionekana alikuwa ashapata habari yakile kinachoendelea mtandaoni.

“Sister pole sana”Aliongea Sophie na kumfanya Edna ajisikie vizuri kuitwa dada.

“Ulilala wapi Sophie?”Aliuliza Roma na kumfanya Sophie amwangalie.

“Nililala kwa rafiki yangu”Aliongea Sophie na Roma alijikuta akishangaa ni rafiki gani huyo wa kulala nae usiku mzima , ila hakutaka kuongezea.

“Sister hii petee….!!”Aliongea Sophia huku akiangalia pete iliokuwa kwenye kidole cha Edna.

“Sophie ninaenda kazini , nitakuelezea nikirudi”Aliongea Edba huku akinyanyuka baada ya kuona muda ulikuwa ukisogea na Sophie aliishia kutoa mshangao kwa kuangalia hio pete kwenye kidole cha Edna na kisha akamgeukia Roma na kumwanagalia na Roma aliishia kutingisha mabega kwa ishara kama hajui kinachoendelea na asimuulize.

Baada ya kama nusu saa ya Edna kuondoka ,Roma alikuwaa kwenye meza akipata kifungua kinywa , huku akila kwa fujo bila wasiwasi wowote na kumfanya Sophie amwangalie kwa jinsi ambavyo Roma alikuwa akila.

“Mr Roma nina wasiwasi na Miss Edna na kinachoendelea kwenye kampuni”Aliongea Bi Wema baada ya kumuona Roma anakula bila wasiwsi huku mke wake akiwa na matatizo na Roma alipunguza spidi kidogo ya kula na kisha akamwangalia Bi Wema.

“Bi Wema wala usiwe na wasiwasi , mpaka sasa hivi tatizo lishaisha”Aliongea Roma na kisha akaendelea kunywa maziwa yaliokuwa kwenye glasi kwa mkupuo mmoja na kushsuha glasi yote chini.

“Wewe umejuaje kama tatizo limeisha?”Aliuliza Sophie huku akioneysha hali ya kukereka na Roma alimwangalia Sophie.

“Una uhakika jana ulikuwa kwa rafiki yako wewe , au unatudanganya tu”

“Kwahio hamini kama nilikuwa kwa rafiki yangu?, halafu kwannini unapenda kubadilisha topic?”

“Siwezi kukuamini”Aliongea Roma na kumfanya Sophie anune na kujisikia vibaya lakini kwa upande wa Bi Wema alijikuta akicheka kwa namna ambavyo Sophie aliweka uso wake, alidhihirisha utoto.

******

“Bebi una uhakika hakuna benki ambayo itamkopesha?”

“Matrida mpenzi unanichukuliaje kwa mfano , mimi ndio Musa Omary , Gavana wa benki ya Tanzania na kila benki inanisikiliza kwa maamuzi yangu na ushawishi wangu ni mkubwa , hivyo kaa kwa kutulia mpenzi , hili swala lako nishamaliza na hawezi kupata mkopo wowote, labda aende Swiss Bank lakini na wao hawatomkopesa maana hela zote sio za kwao”

Aliongea Gavana upande wa pili wa simu na asubuhi hii Matrida alikuwa ndani ya ofisi yake kubwa ambayo mwanzoni ilikuwa ikikaliwa na Abubakari Hamadi na mrembo huyu alikuwa akiongea na simu na mtu ambaye alikuwa akiitwa Musa Omary ,Gavana, ndio huyo ni mwanaume ambaye alikuwa ni Danga la Matrida na ndio aliemfanikisha Matrida baada ya kurudi masomoni kiuweza kupata cheo kikubwa ndani ya BOT.

“Lakini Edna anaonekana kuwa na ukaribu na mheshimiwa Senga , unadhani hatoingilia katika hili?”

“Kaa kwa kutulia mpenzi na swala lako hili likiisha baadaye hakikisha tunakutana kufanya yetu ,Raisi Senga licha ya kuwa Raisi , lakini hawezi kunipa maagizo na kutii, kuna nguvu ambayo hawezi kushindana nayo ndani ya Tanzania”Aliongea Mzee huyo kwenye simu na kumfanya Matrida atabasamu.

“Okey Baadae nitakupigia mpenzi”Aliongea na kukata simu na muda huo huo baada ya kukata simu aliingia Isack CEO msaidizi, akiwa na faili mkononi.

“Madam CEO”Aliita Isaack na Matrida alitabasamu na kunyanyuka alipokuwa ameketi na kumsoglea Isack na kubusiana , wawili hawa walionekana kuwa wapenzi kwa mahaba ambayo walikuwa wakifanya.

“Vipi mpango wako , unaenda kama ulivyopanga?”Aliuliza Isack na kumfanya mrembo Matrida kutabasamu na kisha kurudi kwenye kiti chake.

“Nimetokea kuongea na Gavana hapa anasema hakuna benki ambayo itaweza kumkopesha Edna”Aliongea

“Kama ni hivyo basi naamini mpango utafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana ,lakini Matrida unauhakika unataka kumuacha Abubakari kuingiza pesa zake ndani ya Vexto , utanufaika vipi?”

“Hahaha…Isack nina mpango nae , Abubakari ni rahisi kushawishika sana , lakinni jambo la kufurahisha ni kwamba hela ambayo anaingiza ndani ya Vexto sio ya kwake”

“Unamaanisha nini?”

“Baba kaniambia kuwa Abubakari kakopeshwa na Dorisi , nimeshangazwa sana na Dorisi kuwa na uwezo wa kumkopesha Abubakari kiasi chote hiko, ila sitaki kujua Zaidi ni kwa namna gani Dorisi anapesa kiasi hiko , ila nitahakikisha Abubakari ashindwe kurudisha mkopo huo”Aliongea Matrida na kumfanya Isaack ashangae, hata yeye kwani alikuwa akimjua vizuri Dorisi.

“Halafu kuna swala nimekumbuka”

“Umekumbuka nini?”

“Dorisi mpenzi wake ni mfanyakazi mmoja wa Vexto , anaitwa Roma Ramoni kwa taarifa za chini ambazo nipo nazo , ni kwamba Edna na huyo Roma ni mke na mume na wafanyakazi wengi wa Vexto hawalitambui hilo na linafahamika kwa baadhi ya watu tu”

“Huyo Roma ana nini mpaka kuwa na mwanamkke kama Dorisi na Edna kwa wakati mmoja, anapesa kiasi gani?”Aliuliza Matrida kwamshangao.

“Siwezi kufahamu juu ya kiasi ambacho anacho , ila ni jamaa wa kawaida sana , kwani Zaidi ya kujua lugha nyingi , hakuna kitu Spesho kutoka kwake , ila anaonekana pia kuwa moja ya watu wenye uwezo mkubwa ndani ya Vexto kwani ndio aiefanikisha kusainishwa kwa dili lile na Yamakuza na kuifanya kampuni yetu kukosa saini”Aliongea Isack na kumfanya Matrida kushangaa Zaidi na kutaka kumjua hiyo Roma angalau kwa sura.

“Huyu Roma kama ni kweli ana mahusiano na wanawake warembo kama Edna na Dorisi ni kipi cha ziada kikawafanya wanawake wote wawili kumpenda kwa wakati moja nitajaribu kumfuatilia”Aliwaza Matrida lakini wakati huo huo simu yake ilianza kuita tena na kuangalia jina lilisomeka Rambo.

“Rambo nipe taarifa”

“Boss Edna namuona hapa anaingia kwenye jengo la Benki ya Swiss Bank”

“Umesema Swiss Bank?”

“Ndio madam ndani ya jengo la TPA”Aliongea mwanaume huyo upande wa pili na kumfanya Matrida ashangae kwanini Edna ameenda kwenye Bank Ya Swisi , kwani kwa jinsi a mabavyo alikuwa akielewa ni kwamba Benki ya Swiss haikuwa ikitoa aina yoyote ile ya mkopo Zaidi ya kuhifadhi pesa za watu tu na vito vya thamani.

“Jaribu kufatilia kujua ni jambo gani limempeleka hapo”Aliongea Matrida huku akikosa utulivyo kwenye macho yake.

SEHEMU YA 128

Upande mwingine ndani ya Ikulu ya mheshimiwa Senga , muda wa asubuhi wakati mheshimiwa huyu akiwa anaendelea na majukumu yake ya kazi kama kawaida , mara mlango wake ulifunguliwa na Msemaji wa Ikulu Miss Fatum Adinani.

“Mheshimiwa kuna taarifa mbaya imetufikia”Aliongea Fatuma na kumfanya Senga akae vizuri kwenye kiti , bwana huyu alikuwa ashazoea taarifa za kushitusha sana katika uongozi wake na alichukulia kama jambo la kawaida katika kazi yake hii ya uraisi.

“Inahusu nini Fatuma?”

“Profesa Peter Shelukindo pamoja na familia yake yote imeuwawa usiku wa jana muda wa saa tisa usiku baada ya kukatwa mapanga na mtumambaye mpaka sasa hivi hajafahamika”Aliongea Fatuma na kumfanya Mheshimiwa kutoa macho kwa taarifa hio na kuona ni kweli hio taarifa ilikuwa mbaya.

“Ni nani wa kufanya tukio la kinyama kama hilo?”Aliongea Senga huku akiwa na huzuni kwenye macho yake.

“Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi mheshimiwa na nimewasiliana na IGP na ameniambia wanafatilia nani amefanya tukio hilo la kinyama”

“Fatuma hili ni tukio la kutisha sana kutokea kwa mtu muhimu kwa taifa kama Profesa Shelukindo ,nitawasiliana na IGP wafanye uchunguzi wa makini juu ya hilo , hebu toa taarifa ya ya kuomboleza na kusikitishwa na swala hilo”

“Sawa muheshimiwa” Aliongea Fatuma na kisha akatoka na kumuacha Mheshimiwa Senga kwenye mawazo , Raisi huyu alishindwa kujua ni nini kimesababisha kwa watu kwenda kumfanyia unyama huo Profesa Shelukindo , kwani alikuwa ni kama tegemeo la taifa kwa upande wa Sayansi ya kitafiti.

“Nitachimba hili swala mpaka nipate ukweli wote , hata wa kutumia majasusi wangu , hii ni aibu kwa mtu kama Shelukidno kufariki kifo cha kikatili namna hio pamoja na familia yake”Aliwaza Meheshimiwa Senga.

Profesa Shelukindo ni moja ya wasomi wakubwa ndani ya taifa na duniani ambao wamejizolea sifa kubwa sana katika medani za sayansi ya kiutafiti duniani , kiasi kwamba mataifa mengi yalikuwa yakimwangalia kwa ukaribu sana kwa kila kitu alichokuwa akikifanya ndani ya Tanzania.

Elimu yote ya Profesa Shelukindo aliipatia ndani ya chuo cha Harvard Marekani kwanzia ngazi ya Shahada mpaka PhD , akibobea Zaidi katika maswala ya sayansi inayohusiana na maswala ya Energy , na ndio mwafrika wa kwanza kiufundisha masongo kwa ngazi ya PhD ndani ya chuo cha Harvad na katika muda ambao amehudumu katika kufundisha ndani ya Harvard, Profesa Sheliuindo alijizoelea umaarufu baada ya kufanya tafiti mbalimbali zilizokuwa zikihusisha ‘Ant-Matter Energy’ na katika tafiti zake zote kutokana na ushahidi ambao aliweza kuwakilisha na kufanikiwa, ulikubalika na wanasayansi wengi duniani na kusaidia sana kutengeneza ‘formula’ ambayo ilikuwa ikihusisha namna ya kutengeneza aina hio ya Energy na kuitumia.

Moja ya wanasayansi nguli ambao wamepitia kwenye mikono ya Profesa Shelukindo ni Yan Buwen pamoja na Profesa Clark ,na hio ndio inamfanya profesa Shelukindo kufahamika duniani kote jambo ambalo pia lilifanya taifa la Tanzania kutambulika Zaidi kimataifa , mara baada ya Profesa kutangaza kuachana na ufundishaji ndani ya Harvard na kurudi Tanzania , jambo ambalo licha ya kuibua maswali mengi , liliwafanya wanasayansi wengi duniani kutaka kujua ni kwanini Profesa huyo mwenye heshima kubwa ndani ya ulimwengu wa Sayansi kutaka kurudi nchini Tanzania.

Lakini pia kulikuwa na tetesi za chini sana ambazo inasemakana kwamba Profesa amegundua siri kubwa sana juu ya vyanzo vya Energy mbalimbali ndani ya Dunia , siri ambayo ilikuwa ni kubwa sana kwake na Profesa huyo baada ya kugundua kanuni hizo ndio aliona kama hizo kanuni zitawafikia watu ambao wanania mbaya na dunia basi,kunaweza kutokea jambo baya sana ambalo linaweza kupelekea mwisho wa dunia na ndio maana profesa huyo kuharibu tafiti zote ambazo alifanyia kazi na kurudi Tanzania , hizo zilikuwa ni tetesi tu kutoka kwa vyanzo vya chini.

Kifo cha Profesa huyu huenda kikawa gumzo kubwa Zaidi ndani ya dunia , lakini pia kufanya tetesi ambazo zilikuwa zikisambaa , kurudi tena kwa kasi.

******

Ndani ya hoteli ya Serena anaonekana Yan Buwen akiwa amesimama kwenye dirisha akiwa kifua wazi huku mkono mmoja akiwa ameshikilia mvinyo na mkono mwingine akiwa ameshikilia simu mkononi na alionekana kuna mtu aliekuwa akiongea nae.

“Waziri hupaswi kuwa na wasiwasi , licha ya kwamba hata mimi nimeshangazwa na mtu wetu kumaliza familia nzima lakini naamini kuna sababu , hivyo hupaswi kabisa kuwa na wasiwasi juu ya swala hilo , nakuhakikisha hakunajambo baya ambalo linaweza kukufikia wewe na familia yako kama utaamua kukaa kimya”

“Mr Yan mimi mdomo wangu upo kimya na siwezi kuongea chochote , ni kwamba nimesikitishwa na familia nzima kufa kifo cha aina ile”

“Waziri achana na huruma zako za kipuuzi , unapaswa kuwa imara la sivyo jambo baya na wewe linaweza kukufikia , maana unaonesha udhaifu na unaweza kukwamisha mipango yangu ndani ya Tanzania”Aliongea Yan Buwena kwa hasira na kisha akakata simu. Na kisha kuachia tabasamu la kifedhuli.

“Watanzania ni watu waoga waoga sana , ni hatari kufanya nao kazi kwani hawako imara kihisia,ndio maana wengi wao ni masikini”Aliwaza Yan Buwen.

“The Don nishakamilisha kazi ya kwanza ambayo umeniagiza kuifanya ndani ya Tanzania , ni jukumu lako kuhakikisha Napata jiwe la kimungu , ili kuanza kulifanyia kazi, I will Become God Hahahaha.....,Hades baada ya kupata Jiwe la Kimungu hutakuwa na uwezo wa kuogopwa tena maana nitakudhibiti”Aliongea Yan Buwen na kisha akanywa kidogo mvinyo wake , lakini muda huo huo mlango wake ukagongwa .

“Scorpion anaonekana kuwa na mchecheto sana”Aliongea Yan Buwen na kuusogelea mlango na kwenda kufungua na kweli alikuwa ni Scorpion akiwa kwenye sura yake ile ile ngumu ambayo haikuonyesha Furaha wala huzuni na mwonekano wa Scorpion ulimridhisha sana Yan Buwen.

“Kuna haja gani sasa kuja na panga lako Scorpion..hahaha,,, unadhania sitotimiza ahadi yangu”Aliongea Yan Buwen huku akimruhusu Scorpion ambaye baada ya kuingia tu , maajabu upanga ulionekana kwenye mikono yake na alionekana kuuficha kimazingara na upanga bado unaonekana kuwa na damu. Yaani kwa mwonekano wa Scorpion usingedhania kama ni mwanamke alionekana kuwa Zaidi ya neno ukatili.

Roma aliekuwa akiangalia runinga hata yeye pia alijikuta akiwa ni mwenye kushitushwa na taarifa iliokuwa ikionyeshwa kwenye runinga , taarifa iliokuwa ikihusisha kifo cha profesa Shelukindo , Roma alikuwa akimjua vizuri Profesa Shelukindo kwani ni moja ya watu ambao walikuwa wamehusika na elimu ya Profesa Clark.

“Ashley na Profesa Clark watakuwa wapo kwenye maumivu baada ya kifo hiki na nadhani muda si mrefu watakuwa nchini Tanzania”Aliongea Roma huku akiwa sio mwenye kubadilisha mwonekano wake sana , ni kama mtu ambaye hakuwa akijali sana juu ya kifo cha Profesa Shelukindo.

Wakati Roma akiendelea kuangalia taarifa hio , simu yake ilianza kuita na baada ya kuangalia jina lilikuwa ni Diego.

Alipokea na kuweka sikioni kusikiliza kuna taarifa gani nyingine ambayo Deigo anayo.

*****

Edna licha ya kwamba Roma alimwambia kwenda ndani ya benki kubwa sana duniani ya Swisi Bank , lakini mrembo huyu alikuwa ni kama anabahatisha , hakuwa akiamini kabisa maneno ya Roma, aliendesha gari huku muda wote alikuwa akiangalia pete iliokuwa kwenye kidole chake, mrembo huyu alikuwa amevaa pete hio lakini aliogopa kwa kuoana kama inaweza kuibiwa kutokana na uzuri wake , kwa haraka haraka aliamini kabisa hio pete haikuwa ya kawaida sana na katika macho yake ilikuwa ikionekana kuwa na thamani kubwa mno.

Baada ya kuingiza gari lake ndani ya eneo hili la maegesho katika jengo hili refu ndani ya Tanzania , alishuka na kutembea kwa kujiamini na kuingia kwenye Floor ambayo ilikuwa ikionyesha ndio Benki ya Swiss ilipokuwa ikipatikana , baadhi ya wafanyakazi ndani ya jengo hili walimpa heshima yake , kwani walikuwa wakimfahamu na pia licha ya kuona habari iliokuwa ikiendelea mtandaoni.

Dakika kama moja na nusu aliingia ndani ya Floor ya Benki hii na kupokelewa kwa heshima kubwa sana na wafanyakazi , walionekana kumfahamu Edna kama moja ya ‘High Valued Customer’

“Karibu sana Miss Edna , Asante kwa kutembelea tawi letu kwa siku ya leo , nadhani upo hapa kwa ajili ya kuwithdrawal kiasi cha pesa ambacho umetunza kwetu”Aliongea mama mmoja hiivi wa kizungu ambaye alikuwa amevalia ‘uniform’ za nembo ya Benki hio.

“Hapana Madam , leo nipo hapa kwa ajili ya kuonana na Meneja wa Benki”Aliongea Edna na kumfanya mwanamama huyo wa kizungu kishangaa kidogo na kisha akatabasamu.

“Miss Edna naomba kuuliza kama una miadi nae?”

“Sina miadi nae , lakini ni muhimu kwa mimi kuonana nae ?”Aliongea Edna na ukweli ni kwamba huyu mama wa kizungu , alikuwa akimsemesha hivyo Edna kutokana na kwamba alikuwa akijua Edna alikuwa kwenye hali mbaya sana kiuchumi , na pia hata baada ya kumuona aliamini huenda Edna yupo kwa ajili ya kutoa kiasi cha pesa ambacho alikuwa amekihifadhi ndani ya benki hio.

Baada ya mama yule kuona Edna kaweka usiriasi kwenye macho yake , aliacha kuongea na kuingiza namba Fulani kwenye simu ya meza na kisha akaweka sikioni, hatua zilikuwa ni zile zile kama za Dorisi alivyofika ndani ya hii benki wiki kadhaa zilizopita.

“Miss Edna ,Menaja kakubali kuonana na wewe nenda Floor namba ishirini”Aliongea Mama huyu huku akitabasamu.

Ukweli wanawake wote ambao walikuwa wakifanya kazi ndani ya benki hii walikuw awakisikia sana , yaani walijiona kama wapo juu ya kila mfanyakazi ndani ya benki zote ndani ya Tanzania na ndio maana walikuwa wakitembea kwa mwendo wa kumaringo sana na hata Edna aliliona hilo ila hakujali sana.

“Okey Thank you”

“Okey Miss Edna , I wish you Good luck”Aliongea yule mzungu na Edna alitabasamu na kutembea mpaka kufikia lift na kisha akaingia , na kadiri lift ilivyokuwa ikipanda juu , mrembo huyu moyo wake ulikosa utulivu , alikuwa akiogopa kwa Roma kumdanganya na kuumbuka , lakini alipiga moyo Konde baada ya kukumbuka matukio ya ajabu ajabu ya Roma.

Ndani ya dakika kama mbili mlango wa lift ulifunguka na akapokelewa na Katibu Muhtasi mwanamke wa Kiafrika na akamuongoza mpaka ndani ya ofisi ya Meneja ilipo.

“Karibu sana Miss Edna”Aliongea Meneja Harris Pot huku akimuoneysha Edna kuketi kwenye masofa.

“Asante sana Mr Hariss naitwa…”

“No need for Introduction Miss Edna , We know all of our High Valued Customers”aliongea Harrisa na akaketi na yeye

“Enhe Miss Edna nadhani twende moja kwa moja kwenye swala ambalo limekufanya kutaka kuonana na mimi , maana sisi wafanyabiashara kwetu muda ni mali”

“Ni kweli Mr Harris , nimekuja hapa kwa maagizo ya mume wangu na ameniambia ni kuonyeshe hii pete”Aliongea Edna na muda wote alikuwa ameficha mkono uliokuwa na pete na baada ya kuongea hivyo , aliutoa na kumuonyesha Meneja Harriss na meneja huyu baada ya kuangalia ile pete alitoa macho.

“Miss Edna is it Original or Counterfelt one?”Aliuliza akimaanisha kama ni Original au ni feki na, Edna hakutaka kuongea sana , aliichomoa kwenye kidole na kisha akampatia.

“Nadhani una namna ya kujua hio pete ni Guinine or not Mr Harris ?”Aliongea Edna na kumkabidhi.

“Ofcourse yes Miss , Just Few minutes “Aliongea Harris na kunyanyka na kusogelea upande wa pili wa makabati na kufungua mlango wa kabati moja na baada ya kutoa baadhi ya vitu pembeni aliibuka na kifaa kama zile mashine za kupimia presha hospitalini na kwa mbele kikiwa kimeunganishwa na vifaa viwili , kimoja kikiwa kama ni mzani wa dukani lakini mdogo sana ambao haukuwa na uzto mkubwa na kifaa kingine kilikuwa ni kama pen ambayo ina tochi.

Edna alikuwa akimwangalia tu Harris kwa kila anachokifanya na alionekana kuwa na wasiwasi kweli , baada ya Harris kutoka na kile kifaa , alichomeka kifaa kile kwenye umeme na kukiweka mezani pamoja na ile peni na kile kipande kama Mashine za kupimia Presha na baada ya hapo alichukua ile pete na kuweka kwenye mzani.

Harrsi alioneysha kuwa na shauku kweli kwa kila alichokifanya , kwani hata mikono yake ilionekana kukosa utulivu kabisa, baada ya kuweka ile pete kwenye mzani aliangalia kile kimashine ambacho kipo kama Mashine ya Presha na kusoma uzito wa ile pete na macho yalimtoka.

“Precisely…!!,Precisely ..!!!”Aliwaza bwana huyu ba baada ya hapo , alichukua kile kifaa mfano wa pen za Tochi za kidaktari wanazotumia kumulikia wagonjwa na akabonyeza kwa upande wa juu na ile mashine ilitoa mwanga wa ‘laser’ mwekundu sana hivi na baada ya hapo , Harrisi kwa kutetemeka , akalengesha katikati ya neno ‘Aides’ na hapo hapo likatokea jambo la kushakangaza , kwani chumba chote kilibadilika rangi na kuwa na mwanga wa kijani tupu ambao unaumiza macho mno , mwanga uliotolewa na yale maneno ya Aides , Edna alijikuta akishangazwa na tukio hilo mpaka kumpelekea kusimama , lakini pale pale Harrisi , alidondoka chini haraka haraka hku akiweka ile pete kwenye viganja vyake vya mikono kama mtu anaepokea Baraka kutoka kwa Mungu akiwa amepiga magoti , huku ile pete ikiwa kwenye viganja vyake.

“Queen Peresephone”Aliongea Harris kwa kutetemaka huku akiinamisha kichwa chake chini kwa ishara ya heshima mbele ya Malkia .

ITAENDELEA JUMAMOSI JIONI ,ACHA MAONI YAKO HAPO CHINI

NICHEKI WATSAP UIFUATILIE KWA HARAKA , IPO SEHEMU YA 180 NAMBA NI 0687151346

SEHEMU ya 128
Nukta.
 
SEHEMU YA 156

Mwanaume aliekuwa mbele yake hakuwa mwingine bali alikuwa ni Fayezi, mwanaume ambaye siku kadhaa zilizopita aligombana na Roma baada ya kulala na mpenzi wake Amina, alikuwa ni Fayezi mtoto wa Tajiri maarufu kutoka Dubai wamiliki wa Emaar Corporation`s.

Kwa jinsi Edna alivyokuwa akimwangalia Fayezi , Alionekana kumfahamu mtoto huyu wa Tajiri mkubwa kutoka Dubai , lakini pia mrithi wa Emaar Properties.

“I didn’t expect Boss Edna to personally attend the event, have my warmest welcome”Aliongea Fayezi kwa Kingereza kwa kuweka tabasamu huku macho yake hayakuwa yakitoka kwa Roma , alikuwa akijiuliza ni uhusiano gani Roma alikuwa nayo na Boss Mrembo Edna.

“Huyu ni Fayez Moja ya Wahisani wakubwa wa maandalizi ya hili tukio n ani moja ya familia Rafiki na Mheshimiwa Kigombola”Aliongea Edna akimwambia Roma , lakini kwa upande wa Roma alikuwa akimfahamu Fayezi Vizuri, lakini hakujua kuwa familia ya Tajiri mkubwa kutoka Uarabuni ni Rafiki wa karibu na Familia ya Mheshimiwa Kigombola.

“Fayezi Asante kwa ukaribisho , huyu ni mume wangu anaitwa Roma Ramoni”aliongea Edna kwa kujiamini na kumfanya Fayezi kutoa macho,unajua licha ya kwamba alikuwa akimfahamu Roma kama mwanaume ambaye alikuwa na kisasi nae moyoni kwa kitendo cha kulala na mwanamke wake aliekuwa akimpenda hakuweza kudhania kuwa Roma atakuwa mume wa mwanamke mrembo kama Edna , hapo hapo kichwa chake kilijaa maswali mengi , aliamini kama Roma alikuwa kweli ni mume wa Edna basi hakuwa wa kawaida tokea siku ya kwanza wanaonana na ndio maana hata Amina akajirahisisha kwake, kwani baada ya siku ile kutoka pale , alijaribu kufuatilia taarifa za Roma Ramoni lakini hakuwa na taarifa nyingi ambazo amepatiwa Zaidi ya kujua kuwa Roma alikuwa ni mfanyakazi wa kampuni ya Vexto , lakini pia msomi kutoka chou cha Harvard, ambaye kabala ya kuanza kazi ndani ya kampuni ya Vexto alikuwa akibeba mizigo.

Roma alijikuta akijisikia furaha kwa namna Edna alivyomtambulisha kikawaida sana pasipo kuwa na kusitasita.

“Mr Fayezi naona umepatwa na mshangao kwa kuwa na mwanamke mrembo kama huyu dunia nzima”Aliongea Roma kwa namna ya kiuchokozi na kumfanya Fayezi amwangalie kwa sekunde kadhaa na kisha kutabasamu , wote walikuwa wakiigiza mbele ya Edna , Fayezi hakutaka kuonyesha kuwa anamfahamu Roma mbele ya Edna, kwani tukio la Amina na Roma hakutaka kabisa kulifanya lifahamike, Fayezi baada ya kuachana na Edna na Roma alimpa ishara mlinzi wake wa karibu amsogelee.

“Hakikisha unamchimba huyo mwanaume nje ndani, sihitaji taarifa nyepesi”Aliongea kwa kingereza.

“Sawa Boss”Aliitika Mlinzi huku Fayezi akirudisha macho yake kwa Roma aliekuwa akiongea na baadhi ya watu.

Moja ya watu maarufu waliokuwa hapo ndani ni pamoja na Mheshimiwa Kigombola , raisi mstaafu wa Tanzania , lakini pia kulikuwa na wasanii wakubwa tu waliokuwa wamehudhuria ,wafanyabiashara wakubwa , pamoja na wanasiasa, lakini mtu ambaye hakusahauliwa kualikwa alikuwa ni Yan Buwen.

Wanaume wengi walimwangalia Edna kwa matamanio lakini pia na wivu na chuki kwa Roma aliekuwa amemshikilia Edna , kuna baadhi waliokuwa wakimfahamu mahusiano ya Edna na Roma , hawakuyazoea kabisa, wengi walijiambia Edna ni mwanamke aliekuwa amechanganyikiwa na mapenzi na ndio maana akafia kwa mwanaume kama Roma, mwanaume asiekuwa na mwonekano wa kumiliki mrembo kama Edna.

Wageni walikuwa wengi hivyo ilikuwa ngumu kwa Edna na Roma kupitia kusalimia watu wengi , walichokifanya nikuchukua vinywaji vyao na kusogelea sehemu ambayo wamepangiwa kukaa.

Sasa wakari Roma amekaa pamoja na mke wake wakiwa wameshikilia Glass zao za Wine , mara walisogelewa na warembo wawili mapacha na hawa wanawake hawakuwa wengine bali alikuwa ni Mage na Magdalena, na wote kwa pamoja walichukua viti baada ya kusalimiana na Edna kwa bashasha, ukweli Roma hakupenda sana ujjio wa watu hao wawili kwenye meza yao, alionekana kutokuwa huru kiasi flani.

“Roma adui yako naona macho hayatoki kwako”Aliongea Mage kwa kuvunja ukimya na kumfanya hata Edna ashangae maneno ya Mage.

“Mage unamaanisha nini , Roma ana adui humu ndani?”Aliuliza Edna kwa mshangao na Mage alitabasamu baada ya kuona Edna hakuelewa,Mage alimwangalia Roma na kisha akatabasamu.

Naona hujamwambia mkeo kuhusu Fayezi , leo nalipiza kisasi change hapa hapa”Aliwaza Mage

Ukweli licha ya Edna kujua kitendo cha Edna kulala na Amina mpaka kutuma mwanasheria kumtoa siku kadhaa nyuma , hakuwa akijua kama Roma alikutana na Fayez.

“Namzungumzia Fayez Edna nadhani unakumbuka lile tukio la Mrembo Amina”Aliongea Mage na kumfanya Roma aone Mage anamfanyia makusudi na ‘anachomoa Betri’ mbele ya mke wake.

Baada ya Mage kuongea hayo maneno , Edna alijikuta akikumbuka hilo tukio na kujikuta akianza kupandwa na hasira ila hakutaka kuzidhihirisha hapo.

“Wife hayo mambo yashapita , usimsikilize sana Mage , nitakuelezea tukio zima lilivyokuwa kama utapenda”Aliongea Roma kwa namna ya kujitetea baada ya kuona mabadiliko ya Edna.

“Huna haja yakunielezea , hayo ni matatizo yako , hata hivyo siwezi kukuzuia”Aliongea Edna akipotezea , lakini alijihisi kuumia hasa mbele ya marafiki zake wa utotoni.

Kama mwanamke alijisikia vibaya , maana kitendo cha Roma kulala na mchumba wa mtu mwingine , mpaka kupelekwa polisi , ilikuwa aibu kwa yeye kama mke wake na aliona kama marafiki zake walikuwa wakimcheka moyoni, licha ya kwamba mahusiano yao hayakuwa na uzito mkubwa , lakini bado watu walikuwa wakimfahamu kama mke wa Roma.

“Wife hupaswi kukasirika , najua matendo yangu yanaweza kukuumiza , lakini kukasirika kutakufanya uzeeke haraka”.

“Huna haja ya kujali uzee wangu…”Aliongea Edna kwa hasira na kunyanyuka kwenye hio meza na kumfanya hata Mage alielezea tukio zima ajione kakosea , hakutegemea mabadiliko ya aina hio ya Edna , Walinyanyuka wote kwa pamoja na kumsogelea Edna alieenda kusimama upande wa nyuma.

Ghafla tu Roma akajikuta kwenye meza yupo mwenyewe, unajua Roma muda mwingine alikuwa akifanya kile anachotaka kutokana na aina ya ndoa ambayo amefunga na Edna , lakini kwa jinsi hali inavyoonekana ni kwamba Edna alikuwa akianza kumpenda na hilo ndio aliogopa Zaidi, kwani kama hisia za Edna zikiwa za dhati zidi yake alijiuliza nini kitatokea kwa michepuko yake, na kwa jinsi moyo wake ulivyo alijiona kabisa hakuwa tayari kuacha mwanamke wake hata mmoja, alijikuta akinywa vilevi vilivyokuwa kwenye meza karibia vyote kwa dakika.

Lakini sasa wakati akiangalia kulia na kushoto , mara alisogelewa na wanaume wawili wa makamo waliokuwa wamevalia suti wote mmoja akiwa ni Shombe na mwingine alikuwa ni Mwarabu kabisa.

“Mr Roma naitwa Khatibu Omaar , nimepewa utambulisho wako kutoka kwa Ndugu yangu Fayez , na amenieleza kama wewe ndio mwanaume ulietembea na mpenzi wake”aliongea yule mwarabu ambaye amejitambulisha kwa jila la Khatib na Roma aliwaangalia hawa wanaume waliokuwa mbele yake , na kwa jinsi alivyowaona ni kama walikuwa hapo kivurugu.

“Mr Roma tunajua Maisha yako , ulikuwa ni mbeba mizigo kwenye Soko la Mbagala Rangi Tatu,hivyo acha kuonyesha dharau maana usione hapa watu wamejaa ukaona hatuwezi kukufanya lolote”aliongea yule Shombe na alionekana kuwa mswahili kutokana na namna ambavyo alikuwa akizungumza.

“Kwahio mnafikiri mnaweza kumfanya nini?:Ilikuwa ni sauti ya kike iliowafanya mabwana hawa kugeuka na hata Roma aligeuka na kumuona mwanamke mrembo aliekuwa hajaonana nae siku nyingi kidogo , alikuwa ni Neema Luwazo.

SEE YOU WIKIEND

NICHEKI WATSAPP 0687151346 NIKUPE UTARATIBU WA MWENDELEZO
SEHEMU YA 156.
Ni tamu sana.
NUKTA.
 
SEHEMU YA 538.

Ijapokuwa mwanzoni alisema hatomtambua Edna hadharani kama mtoto wake , lakini likija swala linalomuhusu mara nyingi huwa siriasi sana , hivyo mara baada ya Linda kumwmabia kwamba kuna kitu kinachoendelea katika jumuia ya siri ya Ant- illuminat kinachohusiana na Edna mapigo yake ya moyo yaliongezeka kasi.

“Edna anaetarajiwa kuwa kiongozi wa kundi la Ant – illuminat”Aliongea Linda na kumfanya raisi Jeremy kuwa kama mtu ambaye hajasikia vizuri.

“Linda unataka kumaanisha nini ?”

“Ni kama nilivyosema mheshimiwa , Edna ndio kiongozi mtarajiwa wa kundi la Ant- illuminat na mpaka sasa umoja upo katika hatua ya pili kuthibitisha hilo”Aliongea Linda na kumfanya Raisi Jeremy kuegamia kiti chake kwa muda kama mtu ambaye anajaribu kusharabu maneno ambayo amaeambiwa.

“Mheshimiwa nadhani upo kwenye mshutuko na taarifa hii , lakini ninachojaribu kukuambia ni kitu kilichotokea , Edna amepitia hatua ya kwanza kuthibitika kama kiongozi”

“Kama kauli yako ni sahihi, Linda unamaanisha nini swala la kuthibitisha , Edna hana uhusiano wowote na kundi la Ant- illuminat na sio mwanachama kwanini itokee tu awe kiongozi?”

“Hata hilo ni swali ambalo wengi walijiuliza na mpaka sasa hakuna jibu kamili”

“Unamaanisha nini hakuna jibu kamili?”Aliuliza na kumfanya Linda kufikiria na kisha akaamua kumwelezea kwa ufupi kile kilichotokea Tanzania mwezi uliopita Edna kutoa pete ambayo inamtambulisha kama kiongozi , mpaka anakuja kumaliza Raisi Jeremy alikuwa kwenye mshangao mno na hakuamini maneno ya Linda.

“Linda hiki ulichosema ni kweli?”

“Ni kweli mheshimiwa , lakini licha ya hivyo mpaka sasa Edna bado hajatambulika kama kiongozi , kilichofanyika ni hatua ya kwanza tu ya kuona kama kweli ni yeye”.Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy kuwaza, kama kweli kulikuwa na pete je pete hio Edna kaitoa wapi? Au Roma ndio kampatia , alijiuliza maswali ya aina hio.

“Okey tuseme maneno yako ni sahihi, vipi kuhusu hatua ya pili?”

“Mheshimiwa kuhusu hilo sijui chochote, lakini ninachofahamu upo mchoro wa unabii ambao ndio utathibitisha hilo”

“Mchoro wa unabii!!?”

Kila neno ambalo amesikia kutoka kwa Linda lilikuwa la kushangaza ambalo halikuaminika kabisa kwake.

“Mheshimiwa nilichojaribu kukuambia ni siri ya jumuia, nimejitoa muhanga kuvunja sheria kutokana na deni kubwa ambalo unanidai, hivo sina kingine cha kuelezea ila hiko ndio kinachoendelea na kinachomuhusu Edna”Aliongea na Raisi Jremy hakutoa jibu lolote zaidi ya kuonekana kuwaza kwa takribanni dakika mbili a kisha akamwangalia Linda.

“Jana nimepewa taarifa ya siri ambayo inahusiana na mpango TASAC na nilichosikia ni kwamba jamii hii ya Ant- illuminat ipo chini ya ushawishi wa ukamilishwaji wa mpango TASAC na mimi ndio kiongozi ambaye nilipatia jukumu la kuusimamia katika bara la Afrika”

“Najua hilo mheshimiwa wewe kuwa kiongozi wa mpango huo , lakini sina taarifa za mpango huu kuwa chini ya ushawishi wa umoja wetu”

“Ninachotaka kusema Linda kamnitaendelea kuendelea kuwa kiongozi basi nitahitaji majibu ninayoyataka”Aliongea Jeremy na kumfanya Linda kushangaa.

“Mheshimiwa unamaanisha?”

“Linda nadhani unakumbuka makubaliano yangu na raisi wa Urusi yalikuwaje?”

“Ndio nakumbuka mheshimiwa”

“Nilikubali kuongoza mpango huu kutokana na kwamba nilihitaji majibu , kwa upande wangu nimefanya kazi kubwa lakini kwa upande wao hawajatimiza ahadi yao mpaka sasa , ni kweli kwamba nilipata baadhi ya taarifa lakini hawakutimiza kitu nilichokuwa nikitaka , kitu kinachohusiana na mtoto wangu Lorraine, kama kweli mpango TASAC upo chini ya ushawishi wa umoja huu basi nahitaji majibu zaidi”

“Lakini mheshimiwa ulishasema serikali ya Urusi imeacha kabisa kufatilia swala linahosiana na mpango LADO, unafikiri wanaweza kuwa na majibu unayoyataka?”

“Upo sahihi Linda kwasasa wanaweza wasinipe majibu kwasababu Rwanda ni nchi ndogo , ila kwa kushirikiana na PANAS nitapata majibu ya maswali yangu yote na isitoshe ushasema kuna mchoro wa unabii”

“Ndio mheshimiwa nimesema hilo lakini ni swala ambalo halijathibitishwa”

“Na siwezi kusubiri lisibitishwe ndio nichukue hatua , kwasasa Desmond hayupo nchini na haonekani mahali alipo na inabidi nianze harakati za kumrudisha Edna nchini Rwanda kwa namna yoyote ile na hatua ya kwanza lazima nimwambie kila kitu kuhusu pacha wake nadhani ana maswali juu ya hilo”Aliongea.

“Mheshimiwa kila kitu?, huoni kama mume wake kamficha kwasababu maalumu”

“Unafikiri kuna sababu gani ya kumficha mpaka sasa , Roma alipaswa amuambie kabla hata hawajaenda kufanya sherehe lakini akamficha , kama ameshindwa kumwambia yeye nitamwambia mimi kama mzazi”

**********

“Mkurugenzi , timu ambayo inasimamia filamu imetuma ripoti kwamba wanamalizia kipengele cha mwisho hapa nchini Tanzania kukamilisha muvi yote , hivyo mpango wao ni kuandaa sherehe ya kuwapongeza waigizaji na watu wote waliohusika?”Aliongea Daudi.

“Unamaanisha Muvi anayoongoza director Fabby Lassay?”

“Ndio mkurugenzi”.

Roma alijikuta kidogo akiwaza tokea muvi ianze ni kama hajahusika hata kidogo kufatilia maendeleo ya Sophia na isitoshe ni mara yake ya kwanza kuigiza filamu.

“Sindhani kama ni tatizo kampuni yetu inaweza kusaidia kuandaa kila kitu nadhani ndio maana wakakupatia taarifa”Aliongea Roma na Daudi alikubali.

“Sijamuona Wendy tokea asubuhi?”

“Ndio mkurugenzi Wendy yupo likizo ya uzazi?”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa lakini aliishia kutingisha kichwa.

Roma alijiuliza kama asingekuwa wa tofauti huenda muda huo angekuwa na watoto wengi tu , lakini vilevile aliona huenda maisha yake yasingekuwa ya aina hio, baada ya kupata wazo la watoto hapo hapo alimkumbuka Rose ambaye hakuw akijua maendeleo yake , kwani katika wanawake wake wote aliekuwa akipanda levo kwa spidi alikuwa ni Rose.

Siku chache mbele , ikiwa ndio inaelekea mwishoni mwa mwezi wa sita Roma alitumia muda mwingi kufika kazini kama kawaida, ijapokuwa hakuwa na majukumu makubwa lakini aliweza kufanya baadhi ya vikao na kushiriki baadhi ya matukio ya kampuni na hakuboreka kwani aliona ratiba hizo ni kama kiungo tu kwenye maisha yake ya kiburudani, hakutaka kujichosha sana , kwani alichukulia kama vile yupo likizo ya maisha,

Aliona kazi kubwa alishafanya tokea alipokuwa mdogo na siku ambayo aliamua kujitoa katika maisha yake aliokuwa akifanya na kurejea Tanzania ilikuwa ni kama mapumziko au kustaafu , lakini licha ya hivyo historia ilikuwa ikimfuata kila mahali , hivyo hakutaka kushidana na kile kinachotokea mbele yake , kukiwa na tatizo aliona atashughulika nalo na akipata muda wa mapumziko anautumia vizuri.

Upande wa Tanya aliweza kukamilisha kazi ambayo aliagizwa na siku chache tu kifo cha Mzee Longoli kilitangazwa katika vyombo vya habari , huku chanzo cha kifo chake kikiwa ni mzee huyo kujipiga mwenyewe risasi , lakini ukweli ni kwamba Tanya aliweza kumchoma Mzee huyo na dawa maalumu ambayo ilimsababishia maumivu makali sana , maumivu ambayo alishindwa kuyavumilia na kuishia kukatisha uhai wake.

Staili hio ya kimauaji ilikuwa ikifanyika sana katika ulimwengu wa kihalifu lakini tatizo ni kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kutoa dawa hio na asigundulike.

Baada ya kifo cha Mzee Longoli moja kwa moja aliehusishwa kufanya jambo hilo ni ukoo wa Kweka , kwani kwa muda mrefu Raisi Senga na familia yake hawakuwa na mahusiano mazuri kutokana na mzee huyo kumsapoti sana marehemu raisi Kigombola, hivyo kifo chake kilitafsiriwa kama ukoo huo unajaribu kumaliza maadui zake na kuendeleza kujikita zaidi katika siasa ndani ya Tanzania.

Ilionekana kama babu yake Roma alikuwa akitarajia maamuzi ambayo angefanya kwani mara baada ya taarifa ya kifo cha Mzee Longoli kazi kubwa ilifanyika kutuliza familia nzima hususani mtoto wake mkubwa ambaye ni raisi.

Mheshimiwa Raisi Hassani Longoli kutoka Zanzibar alijua ni kipi kinaendelea lakini kwa wakati huo hakuwa na nguvu ya kisiaza zaidi kama ilivyo kuwa mwanzo wakati Raisi Kigombola akiwa hai, hivyo akafunika kombe mwanaharamu apite.

Jambo moja ambalo lilimshangaza Roma ni namna ambavyo Raisi Senga alihusika kwa kiasi kikubwa kuzima swala hilo na haikumshangaza yeye tu hata babu yake Afande Kweka aliliona hilo na moja kwa moja alichukulia kama ishara nzuri ya familia kurudi na kuwa kitu kimoja.

Tanya mara baada ya kazi hio , Roma hakuta aendeleee kubaki Tanzania , kwani alimleta kutokana na hofu ya Yan Buwen , hivyo alimpa likizo ya kurudi Japani ili kuendelea kusimamia maendeleo ya kundi la Yamata.

Roma alitumia muda mwingi kusimamia warembo wake kujifunza mbinu za kijini na wakati huo huo akiendelea kutengeneza vidonge na alijikuta akifarijika mara baada ya kuona karibia wote walikuwa na maendeleo makubwa zaidi.

Mtu ambaye alikuwa ndio anaanza ni Najma lakini alibahatika yeye kuanza na vidonge hivyo hakutumia nguvu nyingi kama ilivyokuwa kwa wenzake ambao walianza bila viodonge , lakini licha ya hivyo Roma aliamini atapanda levo taratibu.

Ilikuwa bado ni giza licha ya kwamba saa kumi na mbili asubuhi ilikuwa imetimia , pengine ni kutokana na dalili ya mvua ya siku hio.

Katika kitanda kikubwa cha tano kwa sita alionekana Amina ambaye alikuwa amelalia kifua cha Roma kama kifaranga cha kuku , mabega yake ya rangi nyeupe yalionekana wazi lakini muda huo alikuwa kwenye usingizi mzito na hio yote ni kutokana na kazi nzito ambayo imefanyika usiku kucha.

Roma tokea arudi Korea utaratibu wake ulikuwa ni uleule , kwasababu Lanlan alikazania kulala na mama yake, basi asingeendelea kulala peke yake na kukumbatia mto , hiyo ilimpa nafasi ya kwenda kutembelea wanawake zake usiku.

Mara nyingi Roma kila muda wa chai ukikaribia basi atakuwa chumbani kwake ndani ya muda akiwa ashajiandaa tayari ili kuonyesha kwamba alikuwa amelala ndani ya nyumba , lakini ukweli alikuwa akijua kabisa wanafamilia hao walikuwa wakijua kile kinachoendelea , lakini licha ya hivyo hakuna ambaye alikuwa na ujasiri wa kuongea neno lolote kuuliza.

Wakati Roma akiwa amefumba macho ghafla tu alishtuka kutoka usingizini na kufumbua macho na kitendo cha kutingishika kilimwamsha Amina.

Honey , unafanya nini , bado nina usingizi”Alilalamika mrembo Amina.

“Nimeweza hata kupata msisimko kwa hapa , Rose kafanikiwa kupata ufunuo na kukamilisha kuingia katika levo ya Nafsi”Aliongea Roma huku akionyesha furaha.

SEHEMU YA 539.

Kwa kipindi chote ambacho Roma alikuwa nje ya nchi Rose ndio ambaye pekee alionyesha jitihada kubwa za kujifunza mbinu hizo za kichawi , alikuwa ni mara chache sana kuonekana mtaani , kila alipoamka alikuwa akijifungia chumbani kwake na muda mwingine angetafuta mlima wowote na kutulia huko akiendelea kujifunza kuvuna nishati za mbingu na ardhi.

Roma tokea arudi alishindwa kumpata , kwani hakuwepo hata nyumbani na alijua atakuwa sehemu akiendelea kujifunza , hivyo hakutaka kumsumbua kumtafuta na kuacha yeye mwenyewe kuweza kufanikisha bila ya kumuingilia.

Sasa alikuwa na uwezo wa kuweza kupata hisia za uwepo wa mtu anaetumia nguvu za kijini hata kwa mbali kwasababu Tanzania ni nchi tulivu na ina nguvu kidogo sana za kiroho tofauti na nchi nyingine.

“Kweli , lakini umejuaje?”

“Tanzania inatembelewa na majini ndio , lakini hakuna jini lolote ambalo linajifunza kuvuna nishati za mbingu na ardhi na sio hivyo tu kwa binadamu pia , ukiachana na mtu ambaye najua yupo kwenye levo ya Nafsi , sidhani kama kuna mwingine ambaye anaweza kuwa katika levo hio akawa hapa Tanzania ,sasa kumeongezeka mtu mwingine ambaye yupo tayari kwenye levo ya Nafsi ambaye ashapata ufunuo wa siraha , unadhani atakuwa nani kama si Rose?”Aliongea Roma na palepale alitoka kitandani na kuvaa mavazi yake na kuondoka akimuaga kwamba anaenda kumtafuta Rose

Dakika chache mbele Roma aliweza kufuata upande ambao anapata msisimko na alikuja kutokezea kwenye kilele cha mlima wa msitu wa Pugu.

Kwa mazingira namna yalivyotulia , hakika ilionyesha Rose alikuwa ameamua haswa kutaka kujifunza mbinu hizo , maana ni ngumu sana kumkuta mtu ndani ya msitu huo bila ya kuwa na wasiwasi na baridi yote hio ya asubuhi , lakini licha ya hivyo Rose mwili wake haukua ukipata baridi kwani tayari alikuwa na nguvu za kijini zinazozunguka kwenye mwili wake , hivyo kuwa rahisi kuvumilia baridi kali.

Roma alimkuta Rose akiwa amesimama kwenye kilele hicho akionekana kushangaa mazingira , alikuwa amevalia sweta la rangi ya bluu na suruali ya jeans.

Katika macho ya Roma alimuona kama mrembo huyo amezaliwa upya , urembo wake uliongezeka maradufu mno na kwa mwanaume yoyote ambaye angemuona huenda angetokea kumpenda sana kwani alikuwa akisambaza Aura ya mvuto usiokuwa wa kawaida, hakika nguvu za kijini zilikuwa zinafaida.

Rose mara baada ya kuhisi mtu nyuma yake aligeuka na alijikuta akishangaa huku akimwangalia Roma , alijikuta akijawa na tabasamu kwani ni zaidi ya mwezi hawakuwa wameonana.

“Vipi unaonaje , kama vile umeingia kwenye ulimwengu mpya kabisa si ndio?”Aliuliza Roma

“Hapana”

“Kama sio hivyo unajisikiaje?”

“Ni ulimwengu huu huu, lakini kila kitu kinaonekana kuwa tofauti na zamani”Aliongea na kumfanya Roma kutingisha kichwa.

“Kila mtu ni tofauti hususani kwenye swala la utashi na hisia za kimazingira , hata kama kuwe kuna mfanano lakini ufunuo wa kiuelewa utakuwa tofauti , hivyo siwezi kuelewa ni kipi umefunuliwa mpaka kukamilisha levo ya nafsi na hivyo hivyo siwezi kujua wengine watapata ufunuo gani wa kimazingira”

Baada ya kuingia levo ya Nafsi moja kwa moja Rose ni kama amezaliwa upya kimwonekano , ijapokuwa alikuwa akionekana kwa nje ni yuleyule na ngozi yake ileile , lakini alikuwa akizingirwa na nguvu isiokuwa ya kawaida ambayo ilikuwa ikimlinda

Muda huo huo alihisi mkono waRoma ukipita ukipita juu ya uso wake na palepale wimbi la nguvu ya mbingu na ardhi liliweza kutikisa miti na kuinua upepo mkali.

“Ijapokuwa ni mwaka na nusu sasa tokea mara ya kwanza tulivyokutana lakini ni mara yangu ya kwanza kuhisi kuwa na ukaribu zaidi na wewe , ijapokuwa uwezo wangu bado ni wa chini lakini nimeanza kuelewa mawazo yako pamoja na hisia zako , kila kitu sasa ni uhalisia wenye kueleweka katika akili yangu , ninajihisi kuwa mwenye furaha sana”Aliongea Rose.

“Nadhani ni vizuri ukiachana na maswala ya furaha kwa sasa , ushaingia katika levo ya Nafsi lakini bado unapaswa kuendelea zaidi na zaidi , nimekuja na vidonge vya daraja la kati , unaweza sasa kutumia kwasababu ushapata ufunuo wako “Aliongea na kisha palepale alicheza na kauni za anga na palepale lilionekaa vijichupa vya platiki ambavyo huhifadhia vidonge kwenye mikono yake.

“Kuna vidonge vitano hapa vya mawingu na kimoja cha anga la bluu , unaweza kumeza kidongea cha mawingu ili kukusaidia kuweza kukusanya mvuke na kuugeuza mai na baada ya hapo kufanya maji kuwa siraha ya kiroho ya msisimko na baada ya hapo utatumia sasa kidonge cha anga la bluu na kitakusaidia sasa kuelewa zaidi mpangilio wa mbingu , kwa maelezo ya Rufi kidonge cha anga la bluu ni adimu sana katika miliki za kijini , kama sio bahati na uwezo wangu basi ingekuwa ni ngumu kwa binadamu wa kawaida kama wewe kuweza kupata kidonge cha aina hii”

Aliongea Roma na kisha akampatia Rose kijichupa ambacho kilikuwa na vidonge vya mawiangu na kimoja cha anga la bluu.alikwa anapenda sana kuendelea kuvuna nishati ya mbingu na ardhi hivyo hakutaka kukosa nafasi ya kupata kidonge.

Roma mara baada ya kumwangalia Rose aliekuwa na mwoneonako wa furaha na moyo wake ulipata joto la furaha pia.

“Nimekupa vidonge vya thamani kubwa , ni muda wako na wewe angalau kunipa hata zawadi”Aliongea Roma na Rose palepale alimkumbatia Roma na kuzungusha mikono shingoni na kumbusu

“Hubby kwahio mpaka sasa siwezi kuzeeka haraka ?”Aliuliza Rose na Roma alitingisha kichwa kukubali.

“Kwasasa huwezi kuzeeka haraka , lakini licha ya hivyo hupaswi kupumzika jitahidi angalau ufikie mwisho kabisa mwa levo ya Nafsi huenda ukafanikiwa kuingia katika levo ya Dhiki na kuipita kabisa lakini yote hayo yatatokea baaada ya kukusanya nguvu nyingi”

“Kwahio kama nitafika katika levo ya kupita dhiki nitakuwa na uwezo wa kuingia katika steji ya kudhibiti moto wa aina tatu , kubadilisha mvuke kuwa barafu na kudhibiti Radi si ndio?”Aliuliza Rose.

“Sijajua lakini naamini ni zaidi ya hivyo, mbinu yangu niliowapatia ni ya kipekee sana, sidhani kama ni kweli imeweza kutokea katika miliki ya kijini ya PANAS kama wengi walivyosema lakini kwa staili nilivyoirahisisha ni zaidi ya mbinu zote zinazotumiwa na majini”

PANAS ni jamii ya kijini pia kama ilivyo kwa Hongmeng , lakini inasemekana utofauti wa PANAS na Hongmeng ni kwamba miliki hio ipo nje ya bara la Asia na hata Hongmeng ambao walijaribu kusafiri kwenda PANAS ilibidi kwanza wasafiri kuja Afrika, ni jamii ambayo haina muunganiko wowote kabisa na jamii kibinadamu kwa miaka na miaka , lakini hivi karibuni jamii hio inaanza kuonyesha matamanio yao na binadamu wa kawaida.,

Rose sasa alikua sio wa kawaida, alikuwa binadamu ambaye amefanikiwa kupata ufunuo wa nguvu za kijini na hisia alizokuwa akipata akiangalia mazingira ni tofauti kabisa na binadamu wa kawaida na alijikuta hata kundi lake la Tembo kuona ni kitu ambacho hakina maisha marefu kabla ya serikali kuingilia.

Rose sasa alikuwa akipaa tu angani kama Roma na zoezi lake la kwanza kufanikiwa kupaa ni kurudi nyumbani kwa kumfuata Roma nyuma na alijikuta kufumba na kufumbua wapo maeneo ya Ununio na alijikuta mapigo ya moyo yakidunda kasi mno akiwa kama haamini , kwani kila kitu kinaonekana kuwa kipya kwake.

Baada ya kutembea wakipita nje ya nyumba ya Nasra waliweza kukukutana na mama yake Nasra ambaye alikuwa akitoka kwenda kukimbia kuchukua mazoezi.

Tokea mama yake Nasra kufika jijini alikuwa amebadilika mno , kwanza alinenepa na pia mwonekano wake ni wa kitajiri zaidi , hakuwa tofauti sana na Blandina au Bi Wema.

Licha ya kumuona Roma na Rose wakiwa pamoja asubuhi hio hakushangaa sana kwani alikuwa akijua bwana huyo alikuwa na zaidi ya wanawake wengine nje na hata ile hatia aliokuwanayo juu ya Nasra kutoka na mume wa rafiki yake kupungua.

Roma mara baada ya kufika katika nyumba ya Rose waliweza kumkuta Dorisi akitokea jikoni , ilionekana ndio alikuwa akiandaa kifungua kinywa.

Dorisi uwezo wake wa kuvuna nishati za mbingu na Ardhi ulimtegemea zaidi Roma katika kufanya nae mapenzi, baada ya kusikia mwenzake kapasua , alijikuta akiona wivu na kuamini mtu ambaye ataweza kupata mtto wa Roma mapema basi ni Rose na sio yeye.

Roma hakujali sana mawazo ya Dorisi zaidi ya kumwambia ahimize kufungua kinywa kwani leo atapatia hapo hapo kabla ya kurudi nyumbani.

Roma mara baada ya kusema hivyo alimpigia simu mama yake na kumweleza kwamba asihesabiwe kwenye kifugua kinywa , lakini pia alimweleza juu ya mafanikio ya Rose na mara baada ya Blandina kusikia taarifa hio alijikuta akifurahi mno.

Alikuwa na wasiwasi kutokana na Roma kutokuwa wa kawaida hivyo kumpelekea kutokupata mtoto , lakini mara baada ya kusikia kuhusu Rose kupanda levo alijikuta akifurahi mno hakujali ni mwanamke gani wa kwanza kumzalia Roma mtoto , yeye shida yake ni mjukuu tu , alikuwa na mjukuu Lanlan lakini bado hakuridhika kwani bado alijua Lanlan ni wa kulelewa.

“Roma nadhani tusherehekee mafanikio ya Rose”

“Mama unataka tusherehekee vipi??”

“Leo si wikiend na hakuna mambo mengi ya kufanya , kwanini tusiwaalike wengine wakifika nyumbani na kupika chakula na kufurahi?”Aliongea Blandina na kumfanya Roma kuona sio jambo zuri kidogo kutokana na Edna lakini aliependekeza ni mama yake na ni kweli Rose kapata mafanikio makubwa na anapaswa kupongezwa.

“Kama ni hivyo basi tumshirikishe Edna kwanza na baada ya hapo nitawaambia”Aliongea Roma na kisha walikubaliana na kukata simu.

“Mbona unacheka Dorisi?”Aliuliza Roma mara baada ya kuwaambia pendekezo la mama yake.

“Najua mama anamtumia Rose kama kisingizio tu , ukweli ni kwamba ulivyokuwa Korea mara nyingi tulishinda nyumbai kwako tukicheza karata, nadhani anataka tukusanyike tuendelee na mchezo”

“Kucheza karata?”Roma alishangaa kwani ilikuwa ni habari mpya lakini wakati huo huo moyo wake ukiwa na wasiwasi , kwanni kama kitu kama hiko kikiendelea basi Edna lazima hatopendezwa na jambo hilo na kupelekea migogoro.

Roma mara baada ya kumaliza kifungua kinywa alipokea simu kutoka kwa Daudi akimkumbushia swala la tafrija ndogo inayohusiana na waigizaji wote walioshiriki katika filamu hivyo kumweleza eneo ambalo tafrija hio ingefanyika, baada ya kukata simu aliona itakuwa vizuri kumpigia simu Sophia kwa kufanikisha swala hilo.

Baada ya kukaa muda mfupi aliondoka na kurudi nyumbani na aliweza kumkuta Edna akicheza na Lanlan eneo la sebuleni na alimweleza juu ya Sophia na watu wa kampuni ya Penguin kuandaa tafrija lakini Edna alionyesha kujua kila kitu.

“Unaweza kwenda , mimi nitashiriki siku ya uzinduzi wa filamu “

“Lakini Sophia anaweza kuwa na huzuni kama hutoenda”

“Nishampigia tayari Sophia na kumpongeza na nimemwambia sitohudhuria , sidhani kama atahuzunika kwa jinsi tulivyokubaliana”Aliongea Edna na kumfanya Roma kuelewa , hata hivyo Edna alikuwa karibu sana na maendeleo ya Sophia kuliko ilivyokuwa yeye.

“Hubby! Je utamfundisha na Lanlan kuvuna nishati hapo baadae?”Aliuliza Edna wakati Roma akicheza gemu la kuzungusha boksi la kufananisha rangi.

“Hilo lipo wazi, Lanlan ni binti yetu hatuwezi kumuacha asijifunze na isitoshe Lanlan ana vigezo vikubwa zaidi kuliko hata mimi wakati nikijifunza , mpango wangu ni kumrithisha nguvu ya kimaandiko ya urejesho isio na kikomo , ni mtoto wetu wa kwanza hivyo lazima apate vipaumbele”

“Kama ni hivyo kwanini hujamwelekza chochote?”

“Kwanza kabisa Lanlan bado ni mdogo , hawezi kuelewa baadhi ya mambo kwa umri wake, kitu cha pili siwezi kumpatia vidonge na kisha nikamrithisha andiko anaaweza kugeuka na kuwa mkatili , tatu sina uhakika maadui zangu ambao watajitokeza , kama ujuavyo andiko hili huwindwa na watu wengi hivyo nikimrithisha akiwa na umri mdogo moja kwa moja namfanya kuwa mlengwa , hivyo watu watataka kupata mbinu yangu kupitia kwake na nitamuweka kweye hatari, kwasasa tumuache afurahie utoto wake”

“Malengo yangu ni kumuona akiendelea kuwa na siha njema na kuweza kujilinda yeye mwenyewe , lakini nina wasiwasi anaweza kuja kuwa kama wewe kuanza kupigana nakuwa na utukutu mwingi akishaanza kujifunza , hata kama ataweza kushida kila wakati lakini bado itanifanya kuwa na wasiwasi”Aliongea Roma lakini hakutaka kuongezea neno kwani alijua huo ni waswasi wa kawaida kwa mama kwenda kwa mtoto.

Ilionekana Blandina alikubaliana na Edna, hivyo muda wa mchana warembo wote waliweza kukusanyika katika nyumba ya Roma kusherehekea mafanikio ya Rose, aliekosekana alikuwa ni Neema Luwazo ambaye alikuwa nje ya nchi kikazi pamoja na Mage ambaye alikuwa kazini.

Roma mara baada ya kuona kundi lote hilo la wanawake alijikuta akijisikia vibaya na vizuri kwa wakati mmoja.

Baada ya chakula kama kawaida Blandina alitoa karata na kuwataka wote wakusanyike eneo la sebuleni kwa ajili ya kucheza.

Najma pia alikuwepo na ndio ambaye alitoa sababu kwamba hakuwa akijua kucheza karata na Edna hivyo hivyo alipoambiwa ajiunge kucheza alisema hajui , lakini Nasra alimlazimisha na kumwambia atajifunza.

Roma kwa hali hio hakutaka kuendelea kubakia hapo tena, kwasababu siku hio alikuwa na ratiba ya kuhudhuria tafrija ya Sophia na waigizaji wenzake , basi aliona akatembee na kisha aunge moja kwa moja.

***********

Tafrija ilikuja kumalizika saa nne za usiku na Roma aliagana na Sophia kurudi nyumbani.Sophia alionekana kuzidi kupendeza mno na kila mwanaume ambaye alikuwa akimwangalia alimtamani.

Roma mara baada ya kuingiza gari lake ndani ya geti alishangaa mara baada ya kuona gari la Amina bado lipo , lakini pia taa za sebuleni zikiwaka muda huo.

Baada ya kuingia ndani ndipo alipokuja kushangaa mara baada ya kukuta hali ni kama alivyoiacha , lakini utofauti tu ni kwamba wengine walikuwa washaanza kusinzia kwenye masofa , huku mezani alikuwepo Edna na Amina waliokuwa wakicheza karata wakiwa siriasi.

Blandina mara baada ya Roma kuigia eneo hlo alijikuta akipata ahueni na kumwambia Roma amshawahisi Edna waghairishe wataendelea kesho.

Roma mara baada ya kuambiwa hivyo alitaka kujua kwanza kinachoendelea na hapo ndipo aliposikia kwamba baada ya Edna kufundishwa na kuelewa namna ya kucheza hakutaka kupumzika kabisa na kuchukulia siriasi mchezo huo na mtu ambaye alikuwa akiongoza kushinda ni Amina, hivyo Edna alitaka kulipa pointi zote za Amina,lakini mwishowe kila akicheza anaishia kufungwa na bado hakutaka kukata tamaa.

Roma mara baada ya kusikia kauli hio alijikuta akijawa na mshangao na kumwangalia Edna namna ambavyo alikuwa siriasi.

“Edna huo mchezo ni wa kubahatisha, hakuna ufundi ,unaweza kucheza mpaka kesho na usipate ushindi”Aliongea Roma na kumfanya Edna kumwangalia na kisha akaangalia watu waliozunguka na kisha akageuza macho kwa Amina.

“Amina nitakupigia simu , lazima nikulipe pointi zako ulizonifunga leo”Aliongea Edna na kisha akasimama.

“Edna huu ni mchezo wa karata tu kwanini unauchukulia kama vile ni ushindani wa kibiashara?”

“Sijauchukulia kama biashara , bali ni kwamba unafurahisha , siku nyingine mkicheza lazima na mimi niwepo”Aliongea na kisha alipandisha juu kumwangalia Lanlan.

Roma alijikuta akipata ahueni na kuwasindikiza, Najma alikuwa akikaa mbezi kwenye apartment hivyo alipanda gari ya Amina na wakaondoka kwani muda ulikuwa umeenda.

Ilipita wiki moja moja , ikiwa ni siku ya jumamosi jioni wakati Roma akitoka nyumbani kwa Najma mbagala, aliweza kupokea simu kutoka nyumbani na aliekuwa akipiga ni mama yake.

“Mama kuna nini?”

“Mheshimiwa raisi Jeremy amefika na yupo na Edna wanaongea”Aliogea Blandina na kumfanya Roma kushagazwa na kauli hio.

“Lakini mbona unaongea kwa wasiwasi sana?”

“Ni kuhusu Rose”

“Rose kafanyaje?”

“Kuna watu wamejitambulisha wanatokea PANAS, wanasema Rose ashafikia levo ya Nafsi na sheria haimruhusu kuendelea kuishi katika ulimwengu wa kawaida , hivyo wanataka kuondoka nae”

“PANAS!!”Roma alijikuta akimaka , kwa mara ya kwanza anasikia watu kutoka PANAS.

“Mama nakuja sasa hivi”

“Wahi maana Rose kakataa na kasema watampata kama wataweza kumshinda baada ya pambano , hivyo wametoka kwenda kupigana”Aliongea na kumfanya Roma kuzidi kuwa na wasiwasi na aliona hawezi kuendesha gari na alimgeukia Najma na kisha akalipaki pembeni na kumpatia ufunguo wa gari na kumwambia anapaswa kuondoka kuwahi nyumbani , lakini nasra alipotaka kumwambia Roma hajui kuendesha gari , Roma ashapotea kwenye macho yake na kumuacha akiwa amekodoa macho.
[emoji3059][emoji3059][emoji373]
 
SEHEMU YA 540.

MASAA MACHACHE NYUMA.

Ilikuwa ni siku ya Jumamosi wikiend lakini siku hio Edna aliweza kweda kazini nusu siku.

Wakati akiwa kazini upande wa nyumbani Blandina kutokana na kukosa cha kufanya alimwita Rufi na Rose kuja nyumbani kumchangamsha na waliishia kucheza karata muda mrefu mpaka saa za mchana Lanlan alivyoanza kulalamika njaa ndio waliacha na kwenda kuandaa chakula.

Saa tisa wakati Edna akirudi kazini aliweza kuwakuta wakiwa nyumbani ,Edna licha ya kwamba hakupendezwa na namna mama yake alivyokuwa akiwaita wanawake hao nyumbani , lakini hakuonyesha chuki pale anapowakuta.

Muda wa mchana aliongezeka Mage ambae alikuja kusalimia na Edna alichangamka baada ya kukutana na rafiki yake huyo , ijapokuwa alimsaliti kwa kutoka kimapenzi na mume wake , lakini hakuwa na kinyongo nae.

“Roma yuko wapi?”Aliuliza Edna.

“Ndio unamkumbuka sasa hivi , alitoka asubuhi kasema aaenda nyumbani kwa Najma kuonana na ndugu zake”

Ukweli ni kwamba mara baada ya Najma kumpa taarifa Roma kwamba Juma hakuwa na shida na uhusiano wao na akajitambulishe rasmi kwa shangazi yake hakuona shida na ndio maana siku hio jumamosi aliona akafanye hivyo ili rasmi Najma atambulike kama mchumba wa Rom.

Familia hio kutokaa na karibia ukoo mzima kutokuwa na mtu alietoka kimaisha hakuna ambaye alimkataa Roma ilihali walikuwa wakijua ni mtoto wa Raisi .

Zamani ndio Roma alionekana hohehahe , lakini kipindi hicho hadhi yake ilikuwa ya juu mno na hata wale watu ambao aliofanya nao kazi ya kubeba mzigo na kutokumchangamkia kipindi kile walijilaumu kwa kutofanya hivyo, wakiona kwamba walipishaa na bahati , walijiambia kama wangefahamu huenda Roma angewaunganisha kwenye makampunni makubwa na kufanya kazi.

Najma aliishi Mbagala Chalambe karibia tokea akiwa mdogo , hivyo alifahamika sana na kila mtu, hivyo mara baada ya kurudi eneo lote hilo la uswahilini walifahamu.

Najma ambaye walimfahamu kabla ya kwenda Marekani alikuwa ni tofauti na Najma alierudi, hata wale wanaume ambao zamani walikuwa wakimfukuzia wakati huo walikuwa wakimuogopa na kuona sio saizi yao.

Juma mwenyewe ambaye ni kaka mtu , baada ya kumtia macho dada yake aliona kabisa Najma amebadilika sana na hakuwa mwanamke wa kawaida tena lakini licha ya hivyo alishangazwa na kurudi kwake mapema ilihali mara ya mwisho alimwambia atakaa nje muda mrefu.

Lakinni Juma kama mtu mzima baada ya kumuona dada yake alivyokuwa na furaha , aliamini kuna kitu kinaendelea na hata pale alipohoji na Najma kumwambia kwamba Roma amekuwa rasmi mchumba wake Juma alishangaa.

Hakushangaa kwasababu kwa kipindi hiko hakuwa akimtaka tena Roma kutembea na dada yake , La hasha , kilichomshangaza ni kwamba Roma tayari ana mke na jina la Roma Ramoni liliashiria ni mkristo.

Juma ilibidi kwanza amhoji dada yake , kwani wasiwasi wake ilikuwa ni juu ya mke wa Roma, mwanamke ambaye anamheshimu kwenye maisha yake kwa kumsaidia kupona ugonwa wake wa figo, Juma moyo wake ulikataa dada yake kuendelea na Roma kutokana na sababu ya Edna kuwadai fadhila lakini kwa wakati mmoja aliona Roma ni mtu mzito ndani ya taifa mara baada ya kusikia ni mtoto wa raisi.

Ilibidi Najma achukue jukumu la kumtoa hofu kaka yake na kumweleza kwamba Edna hana shida na yeye kuwa na mahusiano na Roma na juma mara baada ya kusikia hivyo , licha ya kupata ahueni lakini alizidi kuwa na maswali mengi na kumuona huenda Roma sio binadamu wa kawaida, alijiuliza inawezekanaje kuweza kupendwa na mwanamke mrembo na tajiri na bila ya wasiwasi kutoka nje ya ndoa.

Roma mara baada ya kufika katika nyumba ya Najma alishangazwa siku hio kukutana na ndugu wengi , hakuamini kama Najma alikuwa na ndugu wengu kiasi hicho, lakini aliweza kufikia katika hitimisho kwenye kichwa chake.

Wakati Roma sasa akiwa nyumbani kwa Najma upande wa nyumbani aliweza kufika raisi Jeremy , ambaye alikuwa nchini Tanzania kimya kimya akiwa na misheni yake moja tu ya kuongea na Edna.

Raisi Jeremy alifika katika eneo la Ununio kwenye muda wa saa kumi na mbili hivi kwenda saa moja , alikuwa amekuja na gari mbili tu aina ya Range na alitangulizana na watu sita ambao wote walionekana kuwa walinzi wake waliovalia suti.

Rose ambaye alikuwa nyumbani kwa Edna akicheza karata alijikuta mwili wake ukimsisimka kabla hata Raisi Jeremy hajaingia ndani ya hilo eneo, alihisi nguvu za ziada zikiongezeka katika hilo eneo na kufanya vinyweleo vya mwili wake kumsimama.

“Kuna watu wawili wenye sawa na yangu wanakaribia”Aliongea Rose mara baada ya kuacha kucheza karata na kuwafanya watu wote hapo ndani kushangaa.

Nadhani kuna watu wengi pia ambao wapo nje mlango , nitaenda kufungua”Aliongea Rose mara baada ya mlango kugongwa.

Rose alivuta pumzi na kuzishusha na kisha akatoka kwenda kufungua mlango

Rose mara baada ya kufungua tu mlango aliweza kukutana na sura ambayo alikuwa akiifahamu lakini ambayo hakutegemea kuiona katika eneo hilo.Alikuwa ni Jeremy Paul raisi wa taifa la Rwanda na alimfahamu.

“Mheshimiwa…!!?”Aliongea kwa wasiwasi huku akishindwa kujua kwanini raisi huyu wa taifa la jirani kuja mpaka nyumbani kwa Roma na Edna.

Baada ya kuchunguza watu waliokuwa pembeni yake kulia na kushoto sasa ndio aliweza kugundua uwepo wa watu wawili ambao walikuwa na nguvu za kijini katika levo ya Nafs.

Wale mabwana walimwangalia Rose kwa mshangao kwani hawakutarajia kuona mtu mwenye nguvu za kijini katika levo yaNafsi kuwa mwanamke mrembo wa umri mdogo ambaye anaishi katika dunia ya kawaida.

“Binti je nimemkuta CEO Edna?”Aliuliza raisi Jeremy mara baada ya kuona Rose anashangaa.

“Ndio , yupo karibuni”Alijibu Rose kwa kushituka na kisha alifungua mlango wote na sasa kufanya waliokuwa ndani kuweza kuona mgeni ambaye amefika.

Edna ndio ambaye alikuwa kwenye mshituko zaidi mara baada ya kuona sura ya Raisi Jeremy.

Upande wa Blandina alishangaa pia lakini kuwa na wasiwasi kwa wakati mmoja.

“Mheshimiwa Jeremy!! Karibu sana”Aliongea Blandina na kumsogelea raisi Jeremy na kumsalimia kwa kumpa mkono.

“Blandina na wewe upo , ni miaka mingi sana tokea tuwahi kukutanam, tafadhari naomba unichulie kama mgeni wa kawaida , nimefika hapa kwani nataka kuonana na Edna”Aliongea.

Bi Wema yeye tu ndio alikuwa na uelewa kuwa Edna baba yake mzazi ni raisi Jeremy ila wengine wote hawakuwa wakiuja ukweli.

Raisi Jeremy aliamrisha walinzi wake wengine kukaa nje na walioingia nao ni wanaume wawili weusi waliokuwa nyuma yake , ambao walikuwa wakisambaza nguvu za kijini.

Warembo wote hapo ndani walijikuta wakikosa utulivu , Raisi Jeremy licha ya nchi yake kuwa ndogo lakini mara nyingi alisifika sana kwa uongozi wake uliotukuta na kwa wanawake hao ni mtu ambaye ni waheshima sana , mtu pekee ambaye angepata ujasiri wa kumpotezea ni Roma pekee na sio wao.

“Jamani haina haja ya kuwa na wasiwasi, mnaweza wote kukaa , nipo hapa kumuona Edna”Aliongea Raisi Jeremy na kuenda kumsogelea karibu Edna.

“Edna nimekuja leo kwako kwa moyo mkunjufu , je tunaweza kuongea?”Alimuuliza Edna ambaye alionyesha kabisa hakuwa amependezwa na ujio wake , tokea siku aone kila dalili ya Jeremy kutokumkubali kama mtoto wake hakuwa na hamu nae tena.

“Sina chochote cha kuongea”Alijibu Edna mara baada ya kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha, alionekana kutumia ujasiri mkubwa kuongea hio kauli.

“Mimi nina cha kuongea”Aliongea kwa sauti yenye upole ndani yake na kuwashangaza Mage na Rose.

“Tunaweza kuongea pale”Aliongea Edna akionyesha eneo la chumba cha mbele ya Dining na yeye alianza kuelekea upande huo na Raisi Jeremy alifuatisha.

“Mama nini kinaendelea?, Edna ana uhusiano wowote na Raisi Jeremy?”Aliuliza Mage kwa sauti ya chini na kumfanya Blandina kuwaleza kwa ufupi.

“Nini! Edna ni mtoto wa raisi Jeremy?”Aliuliza Rose kwa mshangao.

“Ni kama ndoto , sijawahi hata kuwaza”Aliongea Mage.

“Haina haja ya kushangaa , isitoshe mshakuwa familia hivyo mnapaswa kujua lakini niwatahadharishe msiropoke hilo mbele ya Edna maana hapendi”Aliongea na kuwafanya wote kutingisha kichwa chao kukubali.

“Mheshimiwa tafadhari ongea kwa haraka, muda umeenda sana”Aliongea Edna kama kawaida yake akiwa katika sura ya ukauzu.

“Edna binti yangu , najua unanichukia na nashikwa hata na aibu kuongea hili…, lakini leo niliwaza mara kibao na nimejipa ujasiri mwingi kuja kukuona , nipo leo hapa kwa ajili ya kukuomba msamaha wewe na mama yako”

“Msamaha! Tafadhari mheshimiwa huna haja ya kuniomba msamaha kwani mimi ni raia wa kawaida tu ambaye ni mfanyabiashara, hatna uhusiano wowote mpaka kuombana msamaha”

“Edna nakubali kwamba tamaa ilinipofusha na kunifanya nitende dhambi kuchafua taswira yangu , lakini Edna wewe ni msichana mwenye akili sana kama alivyokuwa mama yako , kama mwanaume mwenye jina katika jamii na madaraka ilinipasa kuzingatia vitu vingi na kutimiza wajibu wangu , siku zangu zote za kuishi hazikuwahi kuwa rahisi kwangu , Edna inawezekana nilisita kuchukua hatua ya kujitokeza kwako ana kwa ana na kukutambua kama mtoto wangu lakini unajua wewe mwenyewe namna ambavyo nilikuwa nikikulinda , nilivyokuwa nikikusaidia , sio kwamba najaribu kuchukua sifa kwa nilioyafanya lakini nashukuru kwamba nilikuona ukikua ”

“Umeongea sana mheshimiwa , lakini nikutoe hofu mimi sikuchukii na isitoshe nina furaha hata pasipo ya uwepo wako kwenye maisha yangu , kwani sasa nina familia na najua nifanye nini ili kuwa na furaha, hivyo kama unapenda niendelea kuwa na furaha , tafadhari naomba usinitafute tena”Aliongea Edna kikauzu

“Edna kwanini kauli yako inaonyesha kunikataa , unatakiwa kujua mimi ni baba yako , najua nina mapungufu mengi , najua nimemumiza sana mama yako , lakini bado Edna wewe ndio uliebakia kwenye maisha yangu , Edna watoto wangu wawili walipotea mbele ya macho yangu na watatu haonekani alipo , wewe ndio pekee ambaye naweza kujivunia”Aliongea na kumfanya Edna asimwelewe , kilichomuumiza Edna sio kuhusu yeye , ila ni kuhusu mama yake mzazi , kipindi chote ambacho alikuwa akipitia magumu mpaka akaja kuwekewa sumu hakuna mtu ambaye alimpa msaada na alipigana vita vya peke yake na hilo ndio jambo ambalo lilimfanya kuwa na hasira na raisi Jeremy, aliamini kama angalau angemjali japo kidogo tu huenda mama yake angekuwa hai mpaka muda huo.

“Edna nimetoka Rwanda mpaka hapa licha ya majukumu mengi , yote ni nia yangu ya kutaka kukurudisha katika ukoo wangu , nataka uwe mrithi wa familia”Aliongea na kumfanya Edna kushituka kwani hakutarajia kama angetaja maswala ya urithi.

“Siwezi kuwa mrihi wako , kwasababu mimi ni Edna Adebayo na ukoo wako haunihusu , mimi ni Mtanzania”

“Hapana Edna wewe ni binti yangu , wewe sio mtanzania , wewe ni Mrwanda na jina lako ni Edna Jeremy Paul Murekezi , Edna nitambue mimi kama baba yako na kuitambua Rwanda kama nchi ya baba yako na ukoo wako”Aliongea na kufosi na kumfanya Edna kuanza kutokwa na machozi, hakuamini Raisi Jeremy angefika hapo na jioni hio na kuanza kumfosi kumkubali kama baba.

“Sitaki kuendelea na haya maongezi , nimechoka hivyo tafadharai naomba uondoke”Aliongea Edna na kumfanya Raisi Jeremy kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha.

“Okey, mimi baba yako sitoendelea kukulazimisha kwa leo , nitakuja kukutembelea siku nyingine”Aliongea na kisha alimwangalia Edna kwa dakika na kisha kutoa tabasamu.

“Nadhani nimekuja muda mbaya , Lanlan atakuwa amelala muda huu si ndio , usishangae nina taarifa zote wewe na Roma mmeamua kuasili mtoto ,hivyo moja kwa moja anakuwa mjukuu wangu wa kwanza , siku nyingine nikija nitamletea Zawadi”Aliongea na kisha akasimama.

Edna alimwangalia kwa dakika kadhaa na kisha alifumba macho na kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha.

“Je nilizaliwa na pacha wangu?”Aliongea Edna na kumfanya Raisi Jeremy ambaye alikuwa akitaka kupiga hatua kutoka eneo hilo kusimama ghafla na kumwangalia Edna kwa mshangao na kisha akaupotezea palepale.

“Pacha wako! , unamaanisha nini?”Aliongea akionyesha kutoelewa kitu , lakini Edna hakuwa mtoto mdogo aliweza kusoma mabadiliko ya raisi Jeremy kabla hata kuupotezea.

“Basi, nadhani sikupaswa kuuliza”Aliongea Edna na akatangulia.

Wakati Edna anaongea na Raisi Jeremy , wale watu weusi wawili ambao walikuwa na nguvu za kijini walimwangalia Rose kwa maswali mengi.

“Uwezo wako wa kuvuna nishati ni wa juu sana , kwa umri huo mdogo tayari ushafika katika levo ya Nafsi , je unatokea katika jamii yoyote ya kijini, au ni binadamu uliejifunza bila usimamizi na sasa una tangatanga?”

“Una uhakika gani kama nina umri mdogo , kwa levo yangu hata kama niishi miaka mingi muonekano wangu utaendelea kuwa hivi hivi”

“Haha..nani kakuambia tunaangalia mwonekano kujua umri wa mtu anaejifunza tamaduni za kijini , tunachoangalia ni vitu vingi , jinsi unavyotembea , unavyoongea na tabia yako kwa ujumla , kwa namna navyoongea na kutembea unaonekana ndio kwanza umeingia levo ya Nafsi”

“Hata kama ni kweli , kwanini mnaniuliza maswali?”

“Hutokei katika familia maalumu ndani ya taifa hili si ndio?”

“Kwahio kama sitokei katika familia maalumu , unataka kusema nini?”

“Hehe.. unaonekana kuwa mkali , kama hutokei katika koo maalumu , unapaswa kuaga familia yako na marafiki , kwani huwezi kuendelea kuishi katika ulimwengu wa kawaida kwani nisheria”

“Unamaanisha nini?”Aliuliza Rose kwa wasiwasi.

“Nadhani hajaelewa ninachozungumza na ulijifunza tamaduni zetu bila ya kupewa taarifa , iko hivi kuna sheria kali ambazo zimewekwa zinazowazuia binadamu wa kawaida kujifunza mbinu za kijini na ikitokea binadamu akajifunza na kufikia levo ya Nafsi anapaswa kuacha ulimwengu wa kawaida na kwenda kuishi katika miliki za kijini , sasa kuna chaguzi mbili , unaweza kuongozana na sisi kurudi katika miliki ya kijini ya PANAS au uende China”Aliongea yule mwanaume mweusi, blandina alijikuta hata akishindwa kuelewa kile kinachongelewa.

“PANAS ndio jamii gani?”Aliuliza Blandina ambaye alielewa nusu ya kauli yake?”

“Ni jamii ya kijini , mahali tunapotokea sisi , huyu binti ashafika katika levo ya Nafsi na sheria hazimruhusu kuendelea kubakia katika ulimwengu wa kawaida , hivyo lazima aungane na sisi kwa hiari yake kwenda katika miliki za kijini la sivyo tutamlazimisha”Aliongea na kumfanya Blandina kujawa na hofu juu ya Rose.

“Lakini sheria hio ipo kwa watu wa China , Afrika na mabara mengine nje ya Asia haiwahusu”Aliongea Rufi.

“Kwa umri wako unajua nini maswala ya sheria , hakuna kanuni iliosema hivyo kwa ajili ya Wachina , The gods treaty ni mkataba wa dunia wenye vipengele vya kudumisha amani na uwiano, moja ya kipengele chake ni kuzuia binadamu wa kawaida kujifunza mbinu za kijini na wale wanaojifunza bila ya kuelewa sheria na wakafikia levo ya Nafsi lazima watoke katika ulimwengu wa kawaida, hio yote ni kuepusha madhara kwa binadamu wa kawaida”

“Unamaanisha binadamu wa kawaida kujifunza mbinu za kijini ni kosa?”

“Kanuni inazuia lakini haijasema ni kosa , kutokana na kwamba kujifunza mbinu za kijini ni swala linaolendana na utashi wa hali ya juu wa akili na halitokei kwa bahati mbaya, hivyo pale binadamu anapofanikisha hilo inamaana uwezo wake ni mkubwa na amejaaliwa talanta, lakini haiwezekani kila ambaye anaweza kuwa na nguvu kubwa tofauti na binadamu wa kawaida kuendelea kuishi hapa duniani, nadhani wote mnaweza kujua madhara yake si ndio?”Aliongea yule bwana na Blandina alielewa mantiki yake , lakini Rose hakuwa kwenye kundi la watu anaolenga.

“Hakuna wa kunilazimisha kwenda katika miliki za kijini?”

“Hehe.. binti hakuna anaekulazimisha, bali sheria inakutaka , inakupasa kufanya hivyo , ni sheria ambayo watangulizi wenu wa kuilinda dunia na majanga walisaini, hivyo kama hutaki kwenda kwa hiari utaenda kwa lazima”

“Ni mpaka mtakapofanikiwa sasa kunipeleka kwa lazima”

“Hehe … unaongea sana , lakini siwezi kupoteza muda kuongea na wewe , hata hivyo nadhani muhusika ashakuja , kama kweli unajiamini jiandae kupambana”Aliongea na kuwafanya wote wasielewe anachomaanisha , lakini Rose hapo hapo alihisi mkandamizo wa hewa , huku msisimko ukizidi kumvaa , ilionyesha kuna kiumbe kingine kiliongezeka katika hilo eneo”

Muda huo huo Blandina alijua kuna hatari inayoweza kutokea na alikimbilia jikoni kumpigia simu Roma na ile anarudi alimkuta tayari Jeremy ashamaliza maongezi yake na Edna.

“Blandina naomba ni kusihi uendelee kumjali Edna kwasababu tayari ashakuwa mkwe wako , nitarudi siku nyingine kumtembelea”

“Nitafanya hivyo na isitoshe amekubalika katika familia tayari”

“Ninafuraha kwamba Afande Camillius Kweka amemkubali na kumpenda kama mkwe , lakini ni huzuni Edna hataki kunitambua kama baba yake, lakini kwasasa sitoharakisha mambo nitakuwa na subira”

“Sidhani kuna haja ya kuwa na wasiwasi , Edna ni mtu mzima sasa na anajali sana familia , naamini siku moja atakukubali , ili mradi uwe na nia ya dhati”

“Nia yangu ni ya dhati kabisa”Aliongea na kumfanya Blandina kutabasamu na kukosa neno la kuongea.

“Blandina najua mengi yametokea , lakini nina furaha kuona unaendelea vizuri”Aliongea na Blandina alijua ni kipi Jeremy anamaanisha.

Raisi Jeremy hakua mwongeaji sana , kwasababu alifika hapo kwa ajili ya Edna hivyo aliaga.

Muda uleule wakati raisi Jeremy na watu wake wanatoka nje, wakiwa wanasindikizwa na Rose na Blandina, ghafla tu alijitokeza mwanaume alievalia mavazi ya kitamaduni ya kichina , alikuwa mchina kabisa na kumtanya sasa Rose kuelewa huyo ndio mtu ambaye alikuwa ameongezeka hapo ndani , alikuwa kwenye levo yaka ya kwake ya Nafsi.

Wale mabwana mara baada ya kumuona waliangaliana na kisha walipeana ishara.

“Jini Tao , naona unajiamini kwa kuzururula dunia nzima na kuingia mpaka kwenye mipaka ambayo hupaswi kupita”Aliongea yule bwana mweusi aliekuwa akiongea na Rose.

“Mhmp.. nadhani maneno yako yamekaa kinafiki , sipo hapa katika ulimwengu wa kawaida kama adui , bali nipo hapa kama mjumbe lakini pia sheria inaniruhusu kutafuta binadamu wote wanaojifunza tamaduni zetu kuwarudisha ujinini wanapoingia levo ya Nafsi”Aliongea huku akimwangalia Rose.

“Jini Tao hakika wewe ni mwenyewe kujiamini sana, lakini unapaswa kutoa heshima kwetu jamii ya PANAS kwa namna mababu zetu walivyosaidia jamii yenu na kuwawekea msingi”

“Hahaha… haina haja ya malumbano ya kudai heshima , inashangaza pia nyie kuonekana katika ulimwengu wa kawaida , ilihali ni zaidi ya karne na karne kujificha na kutopenda kujihusisha na maswala ya ulimwengu wa kawaida”

“Miaka imebadilika na dunia inatuhitaji , hatuwezi kuendelea kuona viumbe kutoka sayari nyingine wakiendeleza unafiki wao wa kulinda dunia ilihali mipango yao ni kuiangamiza”Alijibu na kumfanya yule mchina kucheka.

“Nipo hapa nikitafuta wajumbe kutoka Hongmeng waliopotelea duniani na nimetokea kunasa uwepo wako binti”Aliongea akimwangalia Rose.

“Unamaanisha nini kunasa uwepo wangu”

“Nadhani watu wa PANAS wamekuambia , upo tayari levo ya Nafsi na hupaswi kuendelea kuishi katika dunia ya kawaida, tuongozane kuelekea Hongmeng , umekuwa binadamu mwenye bahati kupata ufunuo katika umri mdogo , ukiwa ndani ya Hongmeng utafanikiwa kupanda levo zaidi”

“Siwezi kwenda popote”Aliijibu Rose.

“Binti unaweza kuchagua mahali pa kwenda, unaweza ukaja kwenye miliki yetu yaPANAS na hutojutia maamuzi yako”

“Nishasema siendi popote na kama utanilazimisha , pigana na mimi kwanza ukishinda nipeleke”Aliongea Rose kwa kiburi na kumfanya yule mchina kucheka sana.

“Umetaka mwenyewe binti , nitakupa unachotaka”Aliongea yule mchina huku akimwangalia Rose kwa kejeli , aliamini hakuna namna ambayo anaweza kuzidiwa na mtu ambaye ndio kwanza anaingia levo ya Nafsi.

“Nadhani bwana Tao mkafanyie pambano lenu baharini ili msije kuharibu makazi ya watu , ningependa kuona namna ambavyo jamii ya Hongmeng mlivyo imarika kimbinu”Aliongea yule bwana mwingine ambaye alikuwa kimya muda wote na kisha akaangaliana na mwenzake na wakacheka.

Ijapokuwa kila mtu alikuwa na wasiwasi juu ya usalama wa Rose, lakini hawakuwa na namna ya kumzuia Rose kutopambana.

END OF SEASON 18
NICHEKI WATSAPP KUPATA MWENDELEZO NAMBA 0687151346
[emoji2923][emoji2923][emoji2923][emoji373]
 
[emoji2923][emoji2923][emoji2923][emoji373]
Kumekucha.kila mtu akifanya hiv itakuwa hapatosh utascrol mpaka charge inakata ila wakulungwa tunasoma dhen tunavunga Kumpa mwandish muda wa kuleta jiwe jingine
 
Kumekucha.kila mtu akifanya hiv itakuwa hapatosh utascrol mpaka charge inakata ila wakulungwa tunasoma dhen tunavunga Kumpa mwandish muda wa kuleta jiwe jingine
Wa ignore mkuu hutaona post zao wala notification zao
 
Back
Top Bottom