NILIMDHANIA KAHABA KUUMBE BIKRA
MTUNZI : SINGANOJR.
Mono no aware.
SEHEMU YA 672.
Maongezi yalimfanya Roma sasa kuelewa kwanini mara baada ya kuingia hapo ndani Eujung alimwangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida, ilionekana yeye na Mzee Park walihakikisha Yezi hafanyi mawasiliano nchini Tanzania.
“Yezi wewe ni mjinga kama kweli nilikuwa sitaki kukuona tena nisingekuja kukutembelea , hivi unajua nimejisikiaje mara baada ya kuniangalia kama vile hunijui”
“Kwahio ulipatwa na huzuni kwasababu tu ya kukukaushia?”
“Hapana , mimi sina tatizo kwa wewe kuwa kauzu na kunikaushia, nisichopenda ni kukasirika kwa ajili yangu , nataka kukuona ukiwa na furaha”Aliongea Roma.
“Bro ni bora hata umekuja , Nadhani ni Mungu aliekuleta huku mapema”
“Kwanini unaongea hivyo?”
“Sitaki kuolewa na Kim Jip mimi, lakini babu analazmisha ndoa ifanyike ndani ya siku mbili zijazo”
“Muone sasa, si dakika zilizopita tu ulikuwa ukijigamba na kumuita mchumba halafu sasa hivi unabadilika tena”Alongea Roma akiweka uso wa utani.
“Wewe,.. mimi pale nilikuwa na hasira na wewe ndio maana “Aliongea na kumfanya Roma kumwelewa.
“Yezi usiwe mjinga ndoa ni jambo muhimu sana na mimi kama mtu wa nje ya familia siwezi kuingilia”
“Kwanini huwezi ,mbona ulizuia ndoa ya Sister Amina , mimi sitaki kuendelea kuishi huku , kwa miezi yote ulioniacha nimekuwa bize kwenye kusoma na kuhudhuria tafrija , haya ni maisha ambayo siyataki , kwani sina mtu wa kuongea nae na hakuna anaejali ni kipi napenda au kipi sipendi…. Umeona mwenyewe Eujung na babu wanavyonidanganya, mimi nataka kurudi Tanzania”
“Amina yule ni tofauti , alikuwa ni mpenzi wangu kabla, hivyo sikutaka aolewe na mtu mwingine ilihali hataki, kuhusu wewe nakuchukulia kama mdogo wangu , babu yako anafanya hivi kwa faida yako , atakuwa ametumia nguvu nyingi kuhakikisha unakuwa mrithi wake na sioni tatizo la Kim Jip”
“Sitaki kusikia , bro si umesema mwenyewe unataka niishi kwa furaha , mimi siwezi kufurahi kwenye maisha yangu kama nitaolewa na Kim Jip”Aliongea na kumfanya Roma kutoa tabasamu la wasiwasi.
Ukweli ni kwamba kuna ishara ambazo Roma alishazijua tokea mwanzo kabisa Yezi ana hisia za kimapenzi kwake lakini hakutaka kabisa kumpa nafasi.
Alitaka Yezi aishi maisha yake kabisa isitoshe siku zote alimchukulia kama mwanamke mwenye uwezo wa kujitegemea.
Roma alikuwa na wanawake wengi na alikuwa na jukumu la kuwahudumia na kuhakikisha wanafuraha hivyo aliona Yezi anapaswa kuwa na mtu ambaye atakuwa mwaminifu kwake angalau anaweza kuwa na amani kuliko kuwa na yeye kimapenzi.
“Yezi mimi nakubaliana na maamuzi ya babu yako , hivyo acha ujeuri wako , naamini baada ya kuwa mtu mzima, baadae utagundua kwanini babu yako alifanya haya maamuzi”Aliongea Roma lakini kauli yake ilionyesha kumkasirisha Yezi.
“Kwanini unanifanyia hivi , Roma nakuchukia sana”Aliongea kwa hasira na kisha alikimbia kuelekea juu.
Roma aliishia kutoa tabasamu la uchungu , ijapokuwa ile hali ya sintofahamu ilikuwa imeisha lakini aliishia kumkasirisha tena lakini hakuwa na chakufanya muda huo.
“Mzee tunawaacha sasa, tutaonana kesho kwenye sherehe”Aliongea Roma mara baada ya kumpa ishara Clark ya kuondoka.
Park Juan alisimama na kisha aliwasindikiza mpaka nje huku Kim Yang na mtoto wake wakisindikiza pia.
“Mr Roma nilifikiria mwanamke alielimika kama Dr Clark asingeweza kupenda mwanaume wa kawaida, nadhani mawazo yangu yalikuwa sahihi, asante kwa kufanya maamuzi”Aliongea Park Juan.
Ilikuwa kauli yenye zaidi ya maana na Roma aliweza kuelewa ukiachana na Mzee huyo kujua uhusiano wa Roma na Clark lakini pia alionekana kujua ni kitu gani ambacho Roma amemuambia Yezi.
“Sir nitakuwa muwazi kwako , ninaweza kuwa mtu wa nje ya familia lakini sitaki kumuona Yezi akiishi maisha ambayo sio ya furaha, hata kama atakuwa ameolewa nitaendelea kumjali na kama nitaona hana furaha sidhani kama nitakuwa na huruma”
Maneno hayo yalionekana kama tishio lakini watu hao waliyachukulia kibusara zaidi.
“Usijali nipo makini na mjukuu wangu”Aliongea na palepale gari ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kuwapeleka hotelini ilisimama mbele yao na kuingia ndani.
Muda tu ambao waliingia katika viunga vya hoteli makundi mawili ya polisi yaliwazunguka.
Makundi hayo yalionyesha kuwa katika hali ya furaha mara baada ya kuwakamata na hio yote ni kutokana na kwamba mchana yote walikuwa wakiwwafatilia.
Hwang Suyeon alitokezea katika kundi hilo la polisi kama kiongozi na kumsogelea Roma.
“Mr Roma mimi ni Superintendant Hwang Suyeon kutoka kituo cha kati Mjini , unashukiwa kwa kuwa sehemu ya kundi la kigaidi na rasmi tunakuweka chini ya ulinzi kama mshukiwa, tafadhari toa ushirikiano wako”
“Ofisa nina uhakika una taarifa zangu za kuingia hapa nchini , una uhakika uchunguzi wako umeufanya ki usahihi?”Aliuliza Roma.
“Tumefanya mawasiliano kutoka Tanzania kujua taarifa zako lakini walizotupatia zinaonekana kuchakachuliwa… ulikuwa mbeba mizigo miaka miwili iliopita halafu wanasema umehitimu chuo cha Harvard , tunazo sababu za kuhisi wewe ni shushu mwenye mafunzo ya hali ya juu na ndio maana umejiweka karibu na watu wakubwa”Alionga na kumfanya Roma kushangaa , hakuamini kama angeitwa Shushu na aliishia kujiambia wameenda mbali.
Kwa upande wa polisi ilileta maana , taarifa ambazo wamepatiwa kuhusu Roma hazikuwa zikijitosheleza kabisa lakini ukweli ndio taarifa ambazo serikali ilikuwa nazo na hata zile ambazo zilikuwa zikijulikana ni za siri hazikuweza kutolewa kirahisi.
“Miss Clark huyu mwanaume ni hatari , kama alivyosema Afande Hwang wasifu wake unatia mashaka hivyo nina uhakika atakuwa na nia nyingine kwa kujenga ukaribu na wewe , tafadhari kaa nae mbali?’Aliongea Zhang Ru ambaye alijitokeza pia huku akimwangalia Roma kwa namna ya wasiwasi.
Upande wa Clark alikuwa akitaka kutoa kicheko lakini alijitahidhi kujizuia na aliishia kumkonyeza Roma , ilionyesha kabisa alikuwa akitaka kuangalia show hio hadi mwisho.
Roma alijikuta akikosa neno , kama Zhang Ru asingekuwa na mahusiano na Afande Jamali angekuwa ashamuadhibu palepale.
“Afande naweza kupiga simu , ninataka kuwatbitishia kwamba mimi sio mhalifu”Aliongea Roma akimwangalia Afande Hwang.
“Bila shaka lakini kumbuka chochote utakacho sema kitatumika zidi yako mbele ya mahakama”Aliongea huku akimpatia simu.
Roma mara baada ya kupokea simu ile palepale alifanya mawasiliano na Omari ili amsaidie kwa kuwasiliana na usalama wa taifa kumtoa katika hali hio ya sintofahamu.
Omari mara baada ya kupokea simu hio na kuelezewa alijikuta akitoa kicheko kikubwa sana kama kawaida yake lakini hata hivyo alimwambia Roma ampe dakika chache ashughulikie hilo swala.
Ni ndani ya dakika kama kumi tu hivi Afande Hwang alipigiwa simu na wakuu wake wakimpa maagizo ya kumwachia Roma.
Alitaka kuuliza zaidi lakini mkuu wake alimwambia maagizo hayo yatekelezwe bila maswali huku akiambiwa anapaswa kumpa heshima Roma kama mgeni wa taifa.
Ukweli ni kwamba Roma alikuwa na Koneksheni nyingi Korea na asingejisumbua hata kumpigia simu Omari ni kwamba tu hakutaka kuwafanya watu wengi wajue yupo hapo , isitoshe Korea na penyewe ana historia kubwa sana.
Ilikuwa zamu ya Afande Hwang kujisikia vibaya wakati akiwapa ishara polisi wenzake kumwachia Roma , Afande Hwang alishia kuonyesha ishara ya heshima mbele ya Roma.
“Mr Roma naomba unisamehe , inaonekana tumefanya makosa”Aliongea na Roma alimpotezea kisha akamsogelea Zhang Ru.
“Sijali kama unanipenda au hunipeni lakini unapaswa kuacha hila zako vinginevyo utajutia hata kama ni mwanafunzi wa Clark”Aliongea Roma kwa sauti nzito kumpa presha ya woga Zhang Ru na alijua amefanya kosa hivyo aliomba msahama palepale
“Roma acha kumuogopesha sasa , alikuwa akifanya yote kwa ajili ya usalama wangu”
“Okey , nitakusikiliza tunaweza kuondoka sasa”Aliongea Roma akimshika mkono Clark kuingia hotelini.
Baada ya Roma kutokomea ndani kabisa Afande Hwang alimsogelea Zhang Ru.
“Profesa Zhang nadhani tulikuwa tumefanya makosa lakini pia asante pia kwa msaada wako , kwasasa ninapaswa kuangalia maswala ya usalama kwa ajili ya sherehe ya kesho, unapaswa kupumzika kwa ajili ya kesho pia”Aliongea na Zhang Ru aliishia kutingisha kichwa bila ya kuongea chochote na polisi wale waliondoka mmoja mmoja na kumfanya ajisikie upweke.
Upande mwingine Roma na Clark waliweza kufika katika Floor ya juu kabisa ya jengo hilo ambayo inahudumia wageni muhimu wakiwa wameshikana mikono.
Floor hio ilikuwa na vyumba viwili tu vya hadhi ya raisi lakini pia kulikuwa na huduma nyingne kwa ajili ya VIP kama vile Infinity Swimming pool.
Baada ya wapenzi hao kukaribia mlango wao waliweza kugundua kuna mabodigadi wawili waliokuwa wakilinda huku meneja wa floor hio alikuwa akitembea kulia na kushoto akiwa kama vile mtu mwenye wasiwasi.
“Nyie ni wakina nani?”Aliuliza Roma huku akikunja ndita.
“Wewe utakuwa ni Mr Roma kama sikosei na Miss Clark , kutokana na sababu za kidharula kuna marekebisho yamefanyika”
“Marekebisho? , unamaanisha nini ?”Aliuliza Clark aliekuwa katika hali ya mshangao.
“Kutokana na maamuzi yaliofanyika kwa kuchelewa kati ya serikari na idara ya polisi , wageni rasmi wa heshima wa sherehe ya kesho kama vile kiongozi Abbes Yu Lian na Master Zihao watakuwa wanakaa ndani ya hoteli yetu, Vyumba vyote vya hadhi ya juu vimekwisha kuchukuliwa na chumba kimoja cha hadhi ya raisi kimepewa baadhi ya Monk wa kawaida na kilichobbakia ni hiki ambacho imeamuliwa kupewa Abbes Yu Lian na Master Zihao”Aliongea Maneja na kumfanya Roma kukunja ndita ya hasira.
“Sisi ndio wa kwanza kubook hiki chumba na hata kulipia tushalipa na sasa unatuambia umebadilisha chumba chetu bila kututaarifu?”
“Hatukuwa na chaguo , Mr Roma usiwe na wasiwasi tutahakikisha tunakufidia kwa kiasi cha pesa mara mbili ya ulicholipia , tutashukuru sana kama utakuwa muelewa , Abbes Yu Lian anaheshimiwa sana haitokuwa vizuri kama tutamuacha kukaa katika vyumba vya kawaida, polisi na viongozi ndio waliotuambia kufanya huu utaratibu”
“Sitaki kusikia visingizio vyenu vya kipuuzi , nitawaondoa mwenyewe ndani ya hiki chumba kama watakataa kufanya hivyo”
Roma alikuwa tayari hayupo kwenye mudi nzuri kutokana na kudhaniwa ni mhalifu lakini anadharauliwa kwa kutaka kutolewa kwenye chumba ambacho amelipia , hakutaka kukubali kizembe hivyo.
“Mr Roma tafadhari chunga kauli yako , sherehe itafanyika siku ya kesho na ni tukio muhimu ndani ya Korea kwa mwaka huu , Abbes Yu Lian sasa hivi amepunzika akituliza kichwa kwa ajili ya kesho”Aliongea yule bwana huku akionyesha ishara za waziwazi za ubaguzi wa rangi.
“Naona sasa unaonyesha rangi yako halisi , yaani ninachoona hapa unatafuta tu kisingizio cha kutaka kututoa hapa”
“Kwahio unasemaje sasa , ninachofanya hapa ni kutii maagizo”
“Haha,.. umesema kabisa Monk wa kiume na wa kike wanakaa kwenye chumba kimoja halafu unasema ni watu wa heshima, tunajuaje kama huko ndani hawafanyi dhambi “Aliongea Roma na palepale alimsukuma Meneja pembeni kwa nguvu na kumfanya kujigonga kwenye ukuta kama furushi.
Kitendo kile kiliwafnaya wale mabodigadi kumsogelea Roma kutaka kumdhibiti.
“Ondoka hapa , hii ni Korea sio Afrika”
“Funga domo lako wewe kiherehere”
Baada ya kuongea kauli hio Roma hakutaka kumlembesha na palepale alishika mikono yake na kuizungusha mpaka mabegani kwa staili murua kabisa na kilichosikika ni mpishano wa viungio vya mkono na bega , kutokana na maumivu makali alioweza kusikia palepale alipoteza fahamu.
Mtafaruku huo uliwafanya waliokuwa ndani ya chumba kuweza kutoka .
Mabodigadi wengine waliongezeka huku wakimzingira Roma na Clark na muda huo huo mlango ulifunguliwa na mwanaume mfupi alievalia joho la rangi ya njano huku akiwa ameshikilia Mala.
“Amitabha , nini kinaendelea hapa”Aliongea Master Zihao wakati akimsaidia meneja kusimama.
“Master huyu mwanaume wa kiafrika yupo kifujo fujo , tafadhari amrisha mabodigadi kumuondoa ndani ya hoteli yetu”
Mabodigadi wale walimwangalia Master Zihao kwa ajili ya kupokea maagizo yake.
“Amitabha . Sir hupaswi kuwafanyia wenzio hivi, nahisi kabisa harufu ya chuki inayokuzunguka , inamaana gani kuumiza wenzio ilihali itakuletea madhara wewe mwenyewe?”
Da,kika hio hio sauti ya mwanamke kutoka ndani iliweza kusikika , alikuwa ni Abbess na alifanya watu wote kuinamisha vichwa kasoro Roma na Clark pekee, alikuwa amevalia joho pia na alimwangalia Roma kwa macho ya upole.
“Sir Zihao na mimi tulikuwa tukifanya ibada , hayakuwa malengo yetu kuchukua chumba chenu lakini kila kitu kimetokea haraka sana , viongozi ndio wametaka sisi kukaa hapa kwa ajili ya usalama wetu , Sir ili mradi upo tayari kutuacha tuendelee kukaa hapa tutaliacha hili lipite”
“Abbess Yu Lian hakika wewe ni muungwan sana na mkarimu”Aliongea Meneja.
Muonekano wake ulikuwa wa upole na macho yake ni kama vile amelewa na ilileta aina fali ya msisimko kwa wale waliokuwa wakimwangalia.
Mabodigadi , Meneja na Zihao wote walijikuta wakipata na ahueni mara baada ya kumwangalia Abbes , muonekano wao ulikuwa kama vile wameleweshwa na kitu.
Upande wa Roma alijikuta akizindi kukunja ndita , muonekano wa Abbes ulionekana kabisa haukua wa kawaida na alijihisi ni kama vile kuna mtu anaingilia akili yake.
Roma alimgeukia Clark na kuona yupo kwenye muonekano sawa na wengine wote.
“Wewe mchawi … umetoa wapi ujasiri wa kuwahypnotize”Alifoka Roma kwa nguvu na kufana sauti kugongana ndani ya korido hio.
Clark alijikuta akimwangalia Roma kwa mshangao mara baada ya kusikia enno ‘Hypnotize’ na alijikuta akishangaa na kumwangalia Abbes.
Hypnotize ni kama pumbazo, hali flani hivi ya mtu kuwa kama vile yupo kwenye usingizi mzito na mtu akakuamrisha kufanya jambo lolote na ukafanya bila kujijua , yaani inakuwa kama vile mtu yupo ndotoni na hicho ndio kilichokuwa kikiendelea hapo.
Abbess macho yake yalikuwa katika hali ya ukauzu , alionyesha mshangao katika macho yake lakini hakupoteza ule utulivu wake.
“Sir umekataa kubadilishana chumba na sisi na sitokulazimisha , nitachukulia kama mtu ambaye huwezi kuwa sehemu ya Buddha., So long”