Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

NILIMDHANIA KAHABA KUUMBE BIKRA

MTUNZI : SINGANOJR.

Mono no aware.

SEHEMU YA 672.
Maongezi yalimfanya Roma sasa kuelewa kwanini mara baada ya kuingia hapo ndani Eujung alimwangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida, ilionekana yeye na Mzee Park walihakikisha Yezi hafanyi mawasiliano nchini Tanzania.
“Yezi wewe ni mjinga kama kweli nilikuwa sitaki kukuona tena nisingekuja kukutembelea , hivi unajua nimejisikiaje mara baada ya kuniangalia kama vile hunijui”
“Kwahio ulipatwa na huzuni kwasababu tu ya kukukaushia?”
“Hapana , mimi sina tatizo kwa wewe kuwa kauzu na kunikaushia, nisichopenda ni kukasirika kwa ajili yangu , nataka kukuona ukiwa na furaha”Aliongea Roma.
“Bro ni bora hata umekuja , Nadhani ni Mungu aliekuleta huku mapema”
“Kwanini unaongea hivyo?”
“Sitaki kuolewa na Kim Jip mimi, lakini babu analazmisha ndoa ifanyike ndani ya siku mbili zijazo”
“Muone sasa, si dakika zilizopita tu ulikuwa ukijigamba na kumuita mchumba halafu sasa hivi unabadilika tena”Alongea Roma akiweka uso wa utani.
“Wewe,.. mimi pale nilikuwa na hasira na wewe ndio maana “Aliongea na kumfanya Roma kumwelewa.
“Yezi usiwe mjinga ndoa ni jambo muhimu sana na mimi kama mtu wa nje ya familia siwezi kuingilia”
“Kwanini huwezi ,mbona ulizuia ndoa ya Sister Amina , mimi sitaki kuendelea kuishi huku , kwa miezi yote ulioniacha nimekuwa bize kwenye kusoma na kuhudhuria tafrija , haya ni maisha ambayo siyataki , kwani sina mtu wa kuongea nae na hakuna anaejali ni kipi napenda au kipi sipendi…. Umeona mwenyewe Eujung na babu wanavyonidanganya, mimi nataka kurudi Tanzania”
“Amina yule ni tofauti , alikuwa ni mpenzi wangu kabla, hivyo sikutaka aolewe na mtu mwingine ilihali hataki, kuhusu wewe nakuchukulia kama mdogo wangu , babu yako anafanya hivi kwa faida yako , atakuwa ametumia nguvu nyingi kuhakikisha unakuwa mrithi wake na sioni tatizo la Kim Jip”
“Sitaki kusikia , bro si umesema mwenyewe unataka niishi kwa furaha , mimi siwezi kufurahi kwenye maisha yangu kama nitaolewa na Kim Jip”Aliongea na kumfanya Roma kutoa tabasamu la wasiwasi.
Ukweli ni kwamba kuna ishara ambazo Roma alishazijua tokea mwanzo kabisa Yezi ana hisia za kimapenzi kwake lakini hakutaka kabisa kumpa nafasi.
Alitaka Yezi aishi maisha yake kabisa isitoshe siku zote alimchukulia kama mwanamke mwenye uwezo wa kujitegemea.
Roma alikuwa na wanawake wengi na alikuwa na jukumu la kuwahudumia na kuhakikisha wanafuraha hivyo aliona Yezi anapaswa kuwa na mtu ambaye atakuwa mwaminifu kwake angalau anaweza kuwa na amani kuliko kuwa na yeye kimapenzi.
“Yezi mimi nakubaliana na maamuzi ya babu yako , hivyo acha ujeuri wako , naamini baada ya kuwa mtu mzima, baadae utagundua kwanini babu yako alifanya haya maamuzi”Aliongea Roma lakini kauli yake ilionyesha kumkasirisha Yezi.
“Kwanini unanifanyia hivi , Roma nakuchukia sana”Aliongea kwa hasira na kisha alikimbia kuelekea juu.
Roma aliishia kutoa tabasamu la uchungu , ijapokuwa ile hali ya sintofahamu ilikuwa imeisha lakini aliishia kumkasirisha tena lakini hakuwa na chakufanya muda huo.
“Mzee tunawaacha sasa, tutaonana kesho kwenye sherehe”Aliongea Roma mara baada ya kumpa ishara Clark ya kuondoka.
Park Juan alisimama na kisha aliwasindikiza mpaka nje huku Kim Yang na mtoto wake wakisindikiza pia.
“Mr Roma nilifikiria mwanamke alielimika kama Dr Clark asingeweza kupenda mwanaume wa kawaida, nadhani mawazo yangu yalikuwa sahihi, asante kwa kufanya maamuzi”Aliongea Park Juan.
Ilikuwa kauli yenye zaidi ya maana na Roma aliweza kuelewa ukiachana na Mzee huyo kujua uhusiano wa Roma na Clark lakini pia alionekana kujua ni kitu gani ambacho Roma amemuambia Yezi.
“Sir nitakuwa muwazi kwako , ninaweza kuwa mtu wa nje ya familia lakini sitaki kumuona Yezi akiishi maisha ambayo sio ya furaha, hata kama atakuwa ameolewa nitaendelea kumjali na kama nitaona hana furaha sidhani kama nitakuwa na huruma”
Maneno hayo yalionekana kama tishio lakini watu hao waliyachukulia kibusara zaidi.
“Usijali nipo makini na mjukuu wangu”Aliongea na palepale gari ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kuwapeleka hotelini ilisimama mbele yao na kuingia ndani.
Muda tu ambao waliingia katika viunga vya hoteli makundi mawili ya polisi yaliwazunguka.
Makundi hayo yalionyesha kuwa katika hali ya furaha mara baada ya kuwakamata na hio yote ni kutokana na kwamba mchana yote walikuwa wakiwwafatilia.
Hwang Suyeon alitokezea katika kundi hilo la polisi kama kiongozi na kumsogelea Roma.
“Mr Roma mimi ni Superintendant Hwang Suyeon kutoka kituo cha kati Mjini , unashukiwa kwa kuwa sehemu ya kundi la kigaidi na rasmi tunakuweka chini ya ulinzi kama mshukiwa, tafadhari toa ushirikiano wako”
“Ofisa nina uhakika una taarifa zangu za kuingia hapa nchini , una uhakika uchunguzi wako umeufanya ki usahihi?”Aliuliza Roma.
“Tumefanya mawasiliano kutoka Tanzania kujua taarifa zako lakini walizotupatia zinaonekana kuchakachuliwa… ulikuwa mbeba mizigo miaka miwili iliopita halafu wanasema umehitimu chuo cha Harvard , tunazo sababu za kuhisi wewe ni shushu mwenye mafunzo ya hali ya juu na ndio maana umejiweka karibu na watu wakubwa”Alionga na kumfanya Roma kushangaa , hakuamini kama angeitwa Shushu na aliishia kujiambia wameenda mbali.
Kwa upande wa polisi ilileta maana , taarifa ambazo wamepatiwa kuhusu Roma hazikuwa zikijitosheleza kabisa lakini ukweli ndio taarifa ambazo serikali ilikuwa nazo na hata zile ambazo zilikuwa zikijulikana ni za siri hazikuweza kutolewa kirahisi.
“Miss Clark huyu mwanaume ni hatari , kama alivyosema Afande Hwang wasifu wake unatia mashaka hivyo nina uhakika atakuwa na nia nyingine kwa kujenga ukaribu na wewe , tafadhari kaa nae mbali?’Aliongea Zhang Ru ambaye alijitokeza pia huku akimwangalia Roma kwa namna ya wasiwasi.
Upande wa Clark alikuwa akitaka kutoa kicheko lakini alijitahidhi kujizuia na aliishia kumkonyeza Roma , ilionyesha kabisa alikuwa akitaka kuangalia show hio hadi mwisho.
Roma alijikuta akikosa neno , kama Zhang Ru asingekuwa na mahusiano na Afande Jamali angekuwa ashamuadhibu palepale.
“Afande naweza kupiga simu , ninataka kuwatbitishia kwamba mimi sio mhalifu”Aliongea Roma akimwangalia Afande Hwang.
“Bila shaka lakini kumbuka chochote utakacho sema kitatumika zidi yako mbele ya mahakama”Aliongea huku akimpatia simu.
Roma mara baada ya kupokea simu ile palepale alifanya mawasiliano na Omari ili amsaidie kwa kuwasiliana na usalama wa taifa kumtoa katika hali hio ya sintofahamu.
Omari mara baada ya kupokea simu hio na kuelezewa alijikuta akitoa kicheko kikubwa sana kama kawaida yake lakini hata hivyo alimwambia Roma ampe dakika chache ashughulikie hilo swala.
Ni ndani ya dakika kama kumi tu hivi Afande Hwang alipigiwa simu na wakuu wake wakimpa maagizo ya kumwachia Roma.
Alitaka kuuliza zaidi lakini mkuu wake alimwambia maagizo hayo yatekelezwe bila maswali huku akiambiwa anapaswa kumpa heshima Roma kama mgeni wa taifa.
Ukweli ni kwamba Roma alikuwa na Koneksheni nyingi Korea na asingejisumbua hata kumpigia simu Omari ni kwamba tu hakutaka kuwafanya watu wengi wajue yupo hapo , isitoshe Korea na penyewe ana historia kubwa sana.
Ilikuwa zamu ya Afande Hwang kujisikia vibaya wakati akiwapa ishara polisi wenzake kumwachia Roma , Afande Hwang alishia kuonyesha ishara ya heshima mbele ya Roma.
“Mr Roma naomba unisamehe , inaonekana tumefanya makosa”Aliongea na Roma alimpotezea kisha akamsogelea Zhang Ru.
“Sijali kama unanipenda au hunipeni lakini unapaswa kuacha hila zako vinginevyo utajutia hata kama ni mwanafunzi wa Clark”Aliongea Roma kwa sauti nzito kumpa presha ya woga Zhang Ru na alijua amefanya kosa hivyo aliomba msahama palepale
“Roma acha kumuogopesha sasa , alikuwa akifanya yote kwa ajili ya usalama wangu”
“Okey , nitakusikiliza tunaweza kuondoka sasa”Aliongea Roma akimshika mkono Clark kuingia hotelini.
Baada ya Roma kutokomea ndani kabisa Afande Hwang alimsogelea Zhang Ru.
“Profesa Zhang nadhani tulikuwa tumefanya makosa lakini pia asante pia kwa msaada wako , kwasasa ninapaswa kuangalia maswala ya usalama kwa ajili ya sherehe ya kesho, unapaswa kupumzika kwa ajili ya kesho pia”Aliongea na Zhang Ru aliishia kutingisha kichwa bila ya kuongea chochote na polisi wale waliondoka mmoja mmoja na kumfanya ajisikie upweke.
Upande mwingine Roma na Clark waliweza kufika katika Floor ya juu kabisa ya jengo hilo ambayo inahudumia wageni muhimu wakiwa wameshikana mikono.
Floor hio ilikuwa na vyumba viwili tu vya hadhi ya raisi lakini pia kulikuwa na huduma nyingne kwa ajili ya VIP kama vile Infinity Swimming pool.
Baada ya wapenzi hao kukaribia mlango wao waliweza kugundua kuna mabodigadi wawili waliokuwa wakilinda huku meneja wa floor hio alikuwa akitembea kulia na kushoto akiwa kama vile mtu mwenye wasiwasi.
“Nyie ni wakina nani?”Aliuliza Roma huku akikunja ndita.
“Wewe utakuwa ni Mr Roma kama sikosei na Miss Clark , kutokana na sababu za kidharula kuna marekebisho yamefanyika”
“Marekebisho? , unamaanisha nini ?”Aliuliza Clark aliekuwa katika hali ya mshangao.
“Kutokana na maamuzi yaliofanyika kwa kuchelewa kati ya serikari na idara ya polisi , wageni rasmi wa heshima wa sherehe ya kesho kama vile kiongozi Abbes Yu Lian na Master Zihao watakuwa wanakaa ndani ya hoteli yetu, Vyumba vyote vya hadhi ya juu vimekwisha kuchukuliwa na chumba kimoja cha hadhi ya raisi kimepewa baadhi ya Monk wa kawaida na kilichobbakia ni hiki ambacho imeamuliwa kupewa Abbes Yu Lian na Master Zihao”Aliongea Maneja na kumfanya Roma kukunja ndita ya hasira.
“Sisi ndio wa kwanza kubook hiki chumba na hata kulipia tushalipa na sasa unatuambia umebadilisha chumba chetu bila kututaarifu?”
“Hatukuwa na chaguo , Mr Roma usiwe na wasiwasi tutahakikisha tunakufidia kwa kiasi cha pesa mara mbili ya ulicholipia , tutashukuru sana kama utakuwa muelewa , Abbes Yu Lian anaheshimiwa sana haitokuwa vizuri kama tutamuacha kukaa katika vyumba vya kawaida, polisi na viongozi ndio waliotuambia kufanya huu utaratibu”
“Sitaki kusikia visingizio vyenu vya kipuuzi , nitawaondoa mwenyewe ndani ya hiki chumba kama watakataa kufanya hivyo”
Roma alikuwa tayari hayupo kwenye mudi nzuri kutokana na kudhaniwa ni mhalifu lakini anadharauliwa kwa kutaka kutolewa kwenye chumba ambacho amelipia , hakutaka kukubali kizembe hivyo.
“Mr Roma tafadhari chunga kauli yako , sherehe itafanyika siku ya kesho na ni tukio muhimu ndani ya Korea kwa mwaka huu , Abbes Yu Lian sasa hivi amepunzika akituliza kichwa kwa ajili ya kesho”Aliongea yule bwana huku akionyesha ishara za waziwazi za ubaguzi wa rangi.
“Naona sasa unaonyesha rangi yako halisi , yaani ninachoona hapa unatafuta tu kisingizio cha kutaka kututoa hapa”
“Kwahio unasemaje sasa , ninachofanya hapa ni kutii maagizo”
“Haha,.. umesema kabisa Monk wa kiume na wa kike wanakaa kwenye chumba kimoja halafu unasema ni watu wa heshima, tunajuaje kama huko ndani hawafanyi dhambi “Aliongea Roma na palepale alimsukuma Meneja pembeni kwa nguvu na kumfanya kujigonga kwenye ukuta kama furushi.
Kitendo kile kiliwafnaya wale mabodigadi kumsogelea Roma kutaka kumdhibiti.
“Ondoka hapa , hii ni Korea sio Afrika”
“Funga domo lako wewe kiherehere”
Baada ya kuongea kauli hio Roma hakutaka kumlembesha na palepale alishika mikono yake na kuizungusha mpaka mabegani kwa staili murua kabisa na kilichosikika ni mpishano wa viungio vya mkono na bega , kutokana na maumivu makali alioweza kusikia palepale alipoteza fahamu.
Mtafaruku huo uliwafanya waliokuwa ndani ya chumba kuweza kutoka .
Mabodigadi wengine waliongezeka huku wakimzingira Roma na Clark na muda huo huo mlango ulifunguliwa na mwanaume mfupi alievalia joho la rangi ya njano huku akiwa ameshikilia Mala.
“Amitabha , nini kinaendelea hapa”Aliongea Master Zihao wakati akimsaidia meneja kusimama.
“Master huyu mwanaume wa kiafrika yupo kifujo fujo , tafadhari amrisha mabodigadi kumuondoa ndani ya hoteli yetu”
Mabodigadi wale walimwangalia Master Zihao kwa ajili ya kupokea maagizo yake.
“Amitabha . Sir hupaswi kuwafanyia wenzio hivi, nahisi kabisa harufu ya chuki inayokuzunguka , inamaana gani kuumiza wenzio ilihali itakuletea madhara wewe mwenyewe?”
Da,kika hio hio sauti ya mwanamke kutoka ndani iliweza kusikika , alikuwa ni Abbess na alifanya watu wote kuinamisha vichwa kasoro Roma na Clark pekee, alikuwa amevalia joho pia na alimwangalia Roma kwa macho ya upole.
“Sir Zihao na mimi tulikuwa tukifanya ibada , hayakuwa malengo yetu kuchukua chumba chenu lakini kila kitu kimetokea haraka sana , viongozi ndio wametaka sisi kukaa hapa kwa ajili ya usalama wetu , Sir ili mradi upo tayari kutuacha tuendelee kukaa hapa tutaliacha hili lipite”
“Abbess Yu Lian hakika wewe ni muungwan sana na mkarimu”Aliongea Meneja.
Muonekano wake ulikuwa wa upole na macho yake ni kama vile amelewa na ilileta aina fali ya msisimko kwa wale waliokuwa wakimwangalia.
Mabodigadi , Meneja na Zihao wote walijikuta wakipata na ahueni mara baada ya kumwangalia Abbes , muonekano wao ulikuwa kama vile wameleweshwa na kitu.
Upande wa Roma alijikuta akizindi kukunja ndita , muonekano wa Abbes ulionekana kabisa haukua wa kawaida na alijihisi ni kama vile kuna mtu anaingilia akili yake.
Roma alimgeukia Clark na kuona yupo kwenye muonekano sawa na wengine wote.
“Wewe mchawi … umetoa wapi ujasiri wa kuwahypnotize”Alifoka Roma kwa nguvu na kufana sauti kugongana ndani ya korido hio.
Clark alijikuta akimwangalia Roma kwa mshangao mara baada ya kusikia enno ‘Hypnotize’ na alijikuta akishangaa na kumwangalia Abbes.
Hypnotize ni kama pumbazo, hali flani hivi ya mtu kuwa kama vile yupo kwenye usingizi mzito na mtu akakuamrisha kufanya jambo lolote na ukafanya bila kujijua , yaani inakuwa kama vile mtu yupo ndotoni na hicho ndio kilichokuwa kikiendelea hapo.
Abbess macho yake yalikuwa katika hali ya ukauzu , alionyesha mshangao katika macho yake lakini hakupoteza ule utulivu wake.
“Sir umekataa kubadilishana chumba na sisi na sitokulazimisha , nitachukulia kama mtu ambaye huwezi kuwa sehemu ya Buddha., So long”
 
SEHEMU YA 673.
“Ndio unataka kukimbia sasa hivi kwasababu nishagundua uchawi wako , unadhani wanaokuamini watachukuliaje kama nitawaambia ufisadi wako wa kiroho kwamba nguvu zako zinategemea uchawi?”Aliongea Roma kwa kutumia lugha ya Kichina
“Sielewi unachomaanisha , tafadhari acha kunisingizia bila ya kuwa na ushahidi”Alijibu na yeye pia kwa kutumia kimandari na palepale aliwapa ishara wale walinzi kumfuata kuelekea kwenye lift,
Walikuwa ni Wakorea na hawakujua kichina hivyo hawakuwa wakielewa Roma alichokuwa akiongea nae ni nini. Walichukulia pengine alikuwa akiongea na Roma maswala ya kidini.
Roma alitaka kuongea tena lakini Clark alimzuia kwa kumshika mkono na kumpa ishara kwa namna ya kutingisha kichwa.
“Yule ndio mwenyekiti wa ushirika wa Kibudhha ndani ya Korea kusini , hatuna ushahidi wa kuthibitisha kama alikuwa akitumia hypnosis, ukiendelea kubishana nae itatuletea tu matatizo , isitoshe tunapaswa kuwa watulivu kama tunataka kuona moyo wa kibudha”Aliongea Clark na Roma aliona ana pointi.
Ijapokuwa aliona yule mwanamke alikuwa na makando kando ambayo hayakai vizuri na dini yake lakini aliona atulie , kurudisha uwezo wake ilikuwa ndio kipaumbele kwa wakati huo kuliko kufichua uovu.
“Yule Mwanamke yupo vizuri katika hypnosis, hata kwa mtu kama wewe ambaye unao uwezo mkubwa kiakiri umeweza kuathirika , kama isingekuwa uwezo wangu mkubwa wa kiroho angeniathiri pia”Aliongea Roma.
“Sidhani kama ni Hypnosis ,, unapaswa kujua Hypnosis ni hali ambayo tunawafanyia wagongwa wetu miili yao kutulia pamoja na akili zao ili kuamsha hisia zao na kuwatengenezea umakini katika kuamsha fikra zao ili kutimiza haja zao. Lakini kwa mbinu ya Abbes Yu Lian haifiti maana halisi ya kitabibu kuhusu hypnosis , mimi nadhani atakuwa na nguvu ya ziada ya kichawi” Alipinga Clark.
Roma aliona maneno yake yalikuwa na maana, isitoshe nguvu za ziada watu wanazo ndani ya dunia hii , kwa mfano wapo wachawi pamoja na watu wanaojifunza mbinu za kijini.
Abbess pengine alimuogopa Roma au alikuwa na aibu ya siri yake kugundulika hivyo hakutaka wengine waweze kujua ndio maana aliondoka kimya kimya.
Usiku Roma alikuwa amelala kitandani akiwa macho na alishindwa kutokuacha kumuwazia Yezi.
Clark alikuwa amelala pembeni yake akiwa amekumbatia kiuno chake kama mtoto anaona woga baba yake atamtoroka ila alipendeza sana kutoana na uzuri wake.
“Ndio unajutia sasa hivi?”Aliuliza Clark alielala kihasara hasara.
“Kujutia na nini?”
“Si umemwambia Yezi aolewe na Kim Jip wewe , au tuseme hukumwambia hivyo?”Roma alishindwa kutoa jibu na kuishia kucheza na nywele za mrembo huyo ambaye macho yake yalikuwa ya bluu na kumfanya kuzidi kupendeza.
“Kwasababu sasa hivi Edna anataka kuachana na wewe sidhani kama kuna mtu atapinga kama utaamua kumrudisha Yezi Tanzania”Aliongea Clark na kumfanya Roma kutoa kicheko cha kivivu.
“Clark hata wewe pia nadhani hilo ni sawa , nimekubali kuachana na Edna nikiamini anaweza kuwa na furaha bila ya mimi , na nimewakubali nyie wote kuwa na mimi ili kuwa na furaha , sijakubali kudate na nyie kwasababu labda nawachukulia kama Tuzo kutokana na kuwamiliki au kujionyesha mimi ni kidume, Yezi anaweza akawa asimpende Kim Jip sasa hivi lakini mara baada ya kuishi nae atakuja kugundua ni mtu sahihi zaidi kwake …”Aliongea Roma kwa kirefu na manneo yake yalionekana kukubalika katika masikio ya Clark lakini mrembo huyo alionekana kutoongea chochote.
“Mbona unaniangalia sana , unashangazwa na mimi?”Aliuliza Roma mara baada ya kuhitiimisha ngonjera zake na uwezo wake wa kifikra ulimpandisha Clark ‘Genye’.
“Babe unaonaje tukifanya?”Aliongea kwa sauti ya chini ya aibu na kumfanya Roma kuhisi shoti mwili mzima lakini hata hivyo Roma hakuwa na mpango wa kufanya nae.
“Hatutofanya mpaka angalau uingie katika levo ya nusu mzunguko”Aliongea Roma na Clark alikuwa akielewa kwani Roma alishamwambia mwanamke bikra ni rahisi kupanda levo kwa haraka kuliko yule amaye sio bikra.
Siku iliofuata sherehe ilifanyika kama ilivyokuwa imepangwa na wao kama wageni wa muhimu wa familia ya Mzee Park , Roma na Clark waliruhusiwa kuingia.
Kutokana na tukio la usiku Zhang Ru alikuwa akijisikia vibaya kila alipokuwa akiangaliana na Roma lakini licha ya hivyo dharau haikuwa imemtoka kwani alimuona Roma kama mtu ambaye ni mwenye majigambo hewa, yaani bado hakuamini kama Roma anastahili kuwa na Clark kimapenzi.
Lakini licha ya hivyo hakutaka sana kuwaza kuhusu hilo kutokana na kwamba alikuwa na kazi ya kuhakiki hotuba yake na baadhi ya viongozi kutokana na utafiti aliofanya.
Siku hio katika eneo lote la Jogyesa kulikuwa kumepambwa mno na yalikuwa ni makelele ya Monk sana sana yalioweza kusikika.
Kama mgeni rasmi na mkuu wa ushirika wa Kibudha , Abbes Yu Lian alikaribishwa kwa heshima kubwa , alikuwa akiheshimika katika dini hio na Monk kutoka sehemu mbalimbali za dunia walikuwa wakitamani kuongea nae.
Kulingana na ratiba , Asubuhi viongozi wa kiserikali wangeongelea kuhusu gunduzi na utafiti ulivyofanyika kuhusu Sarira hio na baada ya hapo maonyesho rasmi yangefanyika.
Mchana moyo huo ungehamishiwa katika ukumbi wa ndani kwa ajili ya kutiwa wakfu ambaye muhusika atakaeongoza tukio hilo ni Abbes na kundi la Monk wakongwe.
Tukio la Wakfu lingedumu mpaka usiku na baada ya hapo wageni wangeruhusiwa kupata chakula katika maeneo maalumu ndani ya eneo hilo hilo yaliotengwa
Kutokana na wageni wengi kuwa ni Monk basi chakula kitakacho andaliwa ni matunda pamoja na mboga mboga na hilo walitangaza kabisa.
Baada ya chakula cha usiku wageni wangeruhusiwa tena kurudi katika temple la Jogyesa kuangalia moyo huo baada ya tukio la kutiwa wakfu kukamilika.
Sasa hapa unachopaswa kuelewa ni kwamba moyo wa kibudha maana yake ni moyo ambayo huwekwa ndani ya lile sanamu la Kibudha.
Lile Sanamu la Kibudha huwa halichongwi tu na kutundikwa bali kuna kifaa cha kiroho huwekwa ndani yake na kulifanya kuwa hai na hicho kifaa ndio hichi ambacho Roma amekijia Korea.
Kwahio mara baada ya moyo huo kuonyeshwa kwa kila mtu ungekaa ndani ya kaburi maalumu(Shrine) na hutolewa mara tu baada ya sanamu lake kukamilika kuchongwa na kutumbukizwa rasmi kufanya sanamu hilo kuwa hai kiroho na baada ya hapo watu ndio wataruhusiwa kuliabudia , ni ngumu sana kuutoa moyo huo kutoka kwenye sanamu kwani namna unavyowekwa moyo huo ni siri sana , hivyo kama ni kuiba labda uibe sanamu lote na kisha ulichangue changue jambo ambalo ni gumu sana kutelezeka bila kukamatwa kwani uzito wa chini sana a Sanamu la Buddha sio chini ya tani moja, kwa mfano Spring Temple Buddha ndani ya China linakadiriwa kuwa na uzito wa tani elfu moja mpaka milioni moja na Sanamu la chini kabisa ki uzito ni Golden Buddha kutoka Thailland ambapo linakadiriwa kuwa na tani tano.
Jambo la kuelewa ni kwamba yale masanamu sio ya kawaida kiroho na kuna nguvu inazindikwa ndani yake ndio maana kuna watu wanayaamini na kuyaabudia na wanajihisi kabisa kupata majibu kama watu wa dini nyingine.
Watu wote waliiangalia familia ya Mzee Park mara baada ya kuingiia eneo la ukumbi mpaka pale walipoketi kwenye siti maalumu walizoandaliwa.
Upande wa mchumba wa Yezi yaani Kim Jip hakuwa akifatishana tena na Park Juan na aliingia tofauti akiwa ameambatana na baba yake.
Wahudhuriaji wengine walikuwa ni familia ya Gong , yaani alikuwepo Gong Gyechung na Gong Woo , kutokana na kupona kwa Park Juan familia hio ilikuwa imetuliza zile tamaa zao za ndoa.
Roma alikuwa akifahamiana na familia hizo zote mbili hivyo alisalimiana nao vizuri tu huku wakiongea , Roma pia aliweza kugundua Gong Woo ambaye mwanzo alipaswa kumuona Yezi alikuwa akimwangalia Yezi kwa macho ya tamaa sana.
Yezi siku hio alikuwa amependeza mno , alikuwa amevalia gauni plain rangi ya pink , alikuwa na uso wa ukauzu mno na mara baada ya kumuona Roma alimwangalia mara moja tu na kisha akampotezea , ilionyesha kabisa bado alikuwa na hasira nae.
Roma hakushangazwa sana na muonekano wa Yezi aliishia kutoa tabasamu tu na kujiambia anastahili kununiwa na kisha akakaa pembeni ya Clark wakisubiria sherehe hio kuanza kutiwa wakfu kwa moyo wa Kibuddha kuanza.
Asubuhi hio kla kitu kilikuwa kikionyeshwa moja kwa moja kupitia runinga na hotuba zake hazikuwa zimemkalia kabisa vizuri Roma.
Alikuwa akiomba muda usogee tu aondoke hapo ndani maana kila kinachoongeleiwa kwake hakikuwa kikimuhusu kabisa, hatimae saa sita kamili iliweza kufika na viongozi wa kiserikali walishuka kutoka kwenye Steji na wanajeshi pamoja na Monk waliingia ndani ya ukumbi huo kwa ajili ya kupokea Sarira.
Muda huo huo Roma alijihisi mwili wake ukipatwa na mabadiliko hususani katika kiini cha nguvu zake za kijini.
Kulikuwa na nguvu tatu ambazo zilikuwa katika mtafaruku nguvu ya nishati ya kimbingu ,nguvu ya nishati ya ardhi na nguvu ya nishati ya maafa.
Licha ya mtafaruku huo kitu ambacho Roma aliweza kuhisia ni kwamba nguvu ya roho ya mnyama ni kama vile imeshuka sana kutokana na hofu.
Ijapokuwa ilikuwa ni ndani ya sekunde chache lakini nguvu zake za kijini zilionyesha ishara ya kumrudia jambo ambalo lilimpa furaha Roma
Clark ambaye alikuwa pembeni yake aliweza kuona mwili wa Roma ukitetemeka na alijikuta akijawa na wasiwasi.
“Hubby nini tatizo?”
“Nguvu ya Chaos imeonyesha kuamka sasa hivi , nafikiri imeweza kunasa nguvu ya Sarira na nguvu yake imeshuka kidogo lakini ikajiponyesha haraka sana , ni kama vile inaogopa kitu flani”Aliongea Roma na kufanya Clark macho yake kuchanua.
“Unamaanisha kwamba roho ya mnyama imeonyesha dalili ya woga?”
“Sijaweza kuhisia kama hio Sarira inanguvu yoyote lakini kupitia roho ya mnyama inaonekana kabisa ni dhana ambayo inaweza kuwa na manufaa , ili mradi tu itaweza kuondoa uwiano na kunioengezea nguvu nitaweza kuishinda”
Roma mara baada a kujituliza aligundua bado ilikuwa mapema sana kuwa na furaha
Muda huo sauti za watu wakiongea maandiko yasiokuwa yakitafsrika zilisikika na walionekana Monk nane wakiingia wakiwa amebeba kiboksi cha pembe nne kilichofunikwa na kitambaa.
Walitembea mpaka katikati ya ukumbi ule na kisha wakakiweka katika eneo maalumu na palepale Abbes Yu Lian alisogea mbele huku akitamka maandiko yasioweza kutafsirika.
Baada ya kuinama palepale alivuta kile kitambaa taratibu sana na palepale kiboksi kile kilidhihirika , kilikuwa ni boksi la kioo ambacho hakipitishi risasi na ndani yake kulikuwa na kifaa cha dhahabu ambacho ilikuwa kikitoa mng’ao uliosababishwa na mwangaza wa jua .
Dhana hio ya kimabaki ya dhababbu iliwapa watu ile hali ya kutaka kupiga magoti mbele yake na kusujudu, wakati huo Roma alihisi kile kifaa kilionekana kuwa na nguvu ya kiroho ndani yake.
Roma alihisi kabisa roho ya mnyama ndani yake ilikuwa ikifurukuta , kuna muda ilionyesha hali ya kukasirika lakini kuna muda ilitulia kimya kuonyesha hali ya woga , ililuwa ikioneysha tabia ambayo sio ya kawaida kabisa.
“Kwahio na wewe kumbe una kitu kinachokutia woga?”Aliwaza Roma na palepale nguvu ile ilianza kufurukuta tena ikionyesha hali ya hasira na kujaribu kuitawala akili ya Roma lakini bahati mbaya ni kwamba Roma nguvu yake ilikuwa kubwa mno hivyo roho hio ilishindwa kuvunja ule uwiano.
“Mr Roma hii safari hakika imekuwa ya thamani kwako , ijapokuwa mimi sio msharika wa Kibuddha lakini nahisi akili yangu kusafishwa kwa kuangalia tu hio Sarira”Alionga Park Juan.
Roma alijikuta akitoa tabasamu ambalo halikusomeka na alijiambia kwenye moyo wake yeye hakuwa hapo kwa ajili ya kungalia tu hio Sarira bali yupo kwa ajili ya kuiba na kuondoka nayo.
Mapema tu ulikuwa ni muda wa Wakfu na Abbess Yu Lian ndio aliekuwa kiongozi wa kundi la Monk Wakongwe na wote kwa pamoja waliingia katika ukumbi wa ndani kabisa katika Temple hilo.
Roma mara baada ya kuona Sarira inaondolewa kwenye macho yake alitaka kupiga hatua kusogea kweenda kuwapokonya lakini Clark alimzuia.
“Hubby hata kama unaitaka , huwezi kuiba kukiwa mchana kweupe”
“Mimi siibi ninataka kuiazima tu , nitairudisha kama haitokuwa na mafunaa kwangu”
“Unaiba ndio , hebu angalia waandishi wa bahari wameshandoka lakini kuna zaidi ya wageni mia moja hapa jumlisha na mabodigadi, polisi pamoja na wanajeshi , kama utaiba mbele yao unafikiri watakuangalia tu wasifanye chochote”
“Kwahio wakiwepo ndio nini , nitaua kila mmoja ambaye atanizuia kukamilisha jambo langu”
“Usifanye hivyo , tutafanikisha kuiiba kwa siri sana , umesahau nilikuambia nina mpango kabla hata ya kuanza safari ya kuja huku”Alionga na kumfanya Roma kuanza kukuna kichwa, hakuna ambaye alikuwa akiwasikia kwani waliongea Kiitaliano.
“Hebu niambie kuhusu huo mpango”
Pale pale Clark alimwinamia Roma na kuanza kumnong’oneza kuhusu mpango wake.
Ilikuwa ni njia rahisi sana , Kabla ya Clark kuanza safari ya kuja Korea alikuwa tayari alishawasiliana na Zhang Ru kumtumia ripoti yenye picha ya moyo huo wa Kibuddha kwa kumwambia kwamba anaangalia tu , lakini ukweli alichosoma katika ripoti hio ni kuangalia muundo wake pamoja na elementi zilizotumika katika utengenezaji wake.
Clark alikuwa na teknolojia ya hali ya juu ya 3D inayohusiana na uchapishaji hivyo kama angetaka kutengeneza kitu feki ingekuwa rahisi sana., hivyo kabla ya kuanza safari alikuwa ashafanya mawasiliano Uingereza kazi hio kufanyika na kifaa feki kusafirishwa kuja Korea.
Hivyo mpango wake ilikuwa ni kusubiri muda wa usiku na kumpatia Roma dhana hio feki na kisha kwenda kuibadili na kuchukua ile orijino na mpango ungefanikiwa asilimia mia.
Hata kama viongozi wangeweza kugundua kwamba moyo wao umeguswa wanasayansi wangeshindwa kutofautisha uhalisi wake kwani uhalisi wa dhana hio ni kwenye nguvu yake na sio umbo lake.
“Hio ni mbinu nzuri , huu moyo utawekwa hapa kwa zaidi ya siku tatu , itakuwa rahisi kuubadilisha”Aliongea Roma na Clark alitoa tabasamu huku akimkonyeza.
Kutokana na Temple hilo kuwa na ulinzi mkali ilikuwa ngumu kwa wahalifu kuingia ndani kabisa ya ukumbi huo , ijapokuwa Roma alikuwa na hamu ya kutaka kuingia kazini lakini alijilazimisha kumsikiliza Clark mpaka wakati ambao Sarira Feki itakapofanikiwa kutengenezwa na kufika Korea.
Lakini hata hivyo Roma alijiambia mpango wake ni kukaa karibu na Temple hilo ili kama kuna chochote ambacho kitatokea iwe rahisi kugundua , aliamini kama kuna mtu ambaye ataiba hio Sarira basi litakuwa ni tatizo kubwa kwake.
“Mr Roma sitohudhuria chakula cha usiku kwani napaswa kumsimamia Yezi katika maandalizi ya mwisho ya harusi yake , tutaondoka wa kwanza”Aliongea Park Juan mara baada ya kumsogelea Roma.
Upande wa Roma hata yeye hakuwa na mpango wa kuhudhuria chakula cha usiku kwani hakutaka kukutana na wageni wengine asiowajua, isitoshe alijiambia nani abaki hapo ale mboga mboga za Kibuddha.
“Yezi anaolewa hivyo mimi kama kaka yake napaswa pia kwenda kuandaa zawadi yake , tutaondoka pamoja”Aliuongea
Yezi mara baada ya kusikia kauli ya Roma muoenakno wake ulizidi kuwa wa kikauzu na alimwangalia Roma kwa chuki kubwa mno.
Roma alishangazwa na jicho kali la Yezi lakini licha ya hivyo alijiambia lazima aandae zawadi hata kama hataki.
Upande wa Park Juan alikuwa katika hali ya furaha kwani mawazo yake yalimwambia kabisa zawadi ambayo Roma ataandaa pengine ni vidonge na kwa haraka sana akiwa na mabodigadi wake aliwapa isara kuelekea upande wa nje ya eneo hilo.
Ukweli ni kwamba alitamani kumwambia Roma kama atatoa zawadi ya kidonge kimoja tu ataridhika, ufanisi wa vidonge vile haukuwa wa kawaida kabisa na katika kipindi hicho chote hata uanaume wake ni kama unarudi ujana sasa hivyo tamaa ya vidonge ilimvaa na alitamani kumwambia Roma kumlipa pesa nyingi kununua lakini hakutaka kuweka nia yake wazi.
Wakati wageni wakianza kutoka katika eneo hilo kwa wale ambao hawakuwa na mpango wa kuhudhuria tafrija ya chakula cha usiku ulitokea mlipuko mkubwa mno karibu na eneo hilo na kufanya wanawake waliokuwa hapo ndani kupiga mayowe,
Roma aligeuka haraka sana na kuangalia uelekeo wa sauti ulikotokea na kitu cha kwanza ambacho aliweza kuona ni moshi mzito pamoja Vumbi mbao ukisambaa juu na kwa haraka sana alijua lazima mlipuko umetokea katika eneo hilo, hakuwa na uhakika sana kutokana na kwamba umetokea umbali mrefu kidogo.
Dakika hio hio milio ya bunduki ilianza kusikika mfululizo upande wa ndani ya Tempo walikotoka na baadhi ya watu walianza kudondoka chini kutokana na kujeruhiwa wengine wakikimbia kwa kupiga mayowe.
“Nini kinatokea , wanajeshi wako wapi , mapolisi wako wapi?”Sauti ya mwanajeshi iliweza kusikika kupitia vipaza kipaza sauti.
“Jenerali Jong habari mbaya , Kikosi namba 27 kmetusaliti”Aliongea mwanajeshi mmoja mara baada ya kumkimbilia yule kiongizi wa kijeshi alieshikilia maiki.
“Nini?”Jenerali Jong macho yalimtoka kwa mshangao.
 
SEHEMU YA 674.
Lakini sasa kabla hata jenerali Jong hajajua ni kipi cha kufanya wanajeshi waliokuwa na hasira kwenye nyuso zao waliweza kuingia katika ukumbi wakiwa wamechafukwa na damu.
Mwanaume mbele yao alikuwa amevaa kombati za kijeshi rangi ya majivu flani hivi , mwanzoni alikuwa na kofia lakini wakati huo alikuwa na kipara tu na palepale aliinua Bunduki yake na kisha akaanza kupiga risasi hewani na kufanya wageni wote waliokuwepo kukimbia kwenda pembeni ya Temple.
“Kaeni kimya , tumezingira eneo lote la Temple , wanajeshi pamoja na polisi wote wamekwisha kufa”Aliongea yule mwanaume huku akiweka tabasamu la uovu.
Hakuna ambaye alikuwa mjinga , wageni wote waliokuwa ndani ya eneo hilo walishajua kabisa nini kimetokea
Hao hawakuwa wanajeshi bali walikuwa ni magaidi ambao walijifanyisha kuwa wanajeshi kwa kuwaua wanajeshi halisi.
Hata Roma mwenyewe alikuwa kwenye mshangao , hakutegemea kama kuna mtu ambaye alikuwa na mpango wa kuiba moyo wa Kibuddha kama yeye tu.
Lakini Roma alisubiri kuona mpaka kila kitu kikiwa wazi kabla ya kuingilia.
“Nyie ni … mnatokea umoja wa North Buyeo?”Aliongea Jenerali Jong kwa mshutuko.
“Jenerali Jong Jun Kamanda mwenye amri ya vikosi vyote , ninakufahamu vyema, nimeua wanajeshi wako wote na hawa unaowaona hapa ni wa kwangu , tii ushauri wangu kaa pembeni kama wengine na utulie na sitokuua”
Kamanda Jong alijikuta akiwa na hasira sana lakini alijizuia kutoonyesha ukinzani kwani mitutu ya bunduki ilikuwa imeelekezewa kwake , alikuwa bado mdogo na hakutaka kufa mapema na kwa wakati mmoja alishukuru kwamba waandishi wa bahari walikuwa washaondoka ndani ya hilo eneo muda mrefu
“Braza Hao , mateka wote hawa hapa kuna wanawake hapa hivyo ni rahisi zaidi “Alionga mwanaume nyuma huku akitoa tabasamu la kifedhuli huku kukiwa na magaidi wengine ambao walikuwa wamewatanguliza wanawake wakiwagizia ndani ya eneo hilo wakiwa wamewanyooshea mitutu ya bunduki.
“Zhang Ru!?”
Clarka lijikuta akiwa kwenye mshutko mara baada ya kumuona Zhang Ru akiwa ni mmoja ya wanawake ambao wameshikiliwa kama mateka wakiingizwa ndani.
Zhang Ru alikuwa kwenye kundi la watafiti ambao waliondoka wa kwanza katika eneo hilo lakini ilishangangaza walikamatwa.
“Kazi nzuri ,,, oh tena naona na Kapteni Hwang mmemuunganisha , niwie radhi Kapteni najua ulikuwa na wasiwasi juu yetu lakini tulikuwa tukikuangalia hatua kwa hatua katika kila mpango wako, kazi nzuri”Aliongea yule kiongozi wa magaidi.
Lilikuwa tusi kwa ambalo sio la moja kwa moja kwa Hwang Suyeon , alikuwa ni mchapakazi mno katika kitengo cha ulinzi na alikuwa amejipanga vilivyo kwa ajili ya tukio hilo lakini bado akashindwa kugundua kuna shushu ndani ya timu yake.
“Mabaradhuli nyie magaidi kutoka North Buyeo , mnadhani mnaweza kukimbia hapa , mapema tu jeshi litazingira hili eneo lote na hamtoweza kutoroka”
“Haukusikia milipuko kutoka mjini?”Aliuliza Bwana Hao kiongozi wa magaidi na kumfanya Kapteni Hwang kushituka.
“Mmetega mabomu ndani ya jiji la Seoul?”
“Upo sahihi tulichagua maeneo flani flani hivi na kutegenesha mabomu kwenye makazi ya watu , kama chochote kitatutokea hapa ndani basi mabomu hayo yatalipuka , nyie watu kama hamtaki maelfu ya raia kufa basi jaribu kuita jeshi eneo hili muone”
“Kwa kuongezea tu sijui hata rimoti nani kaishikilia wala sijui tuna rimoti ngapi..”
Wageni wote walimwangalia katika macho ya mshangao na mshituko kwa wakati mmoja.
Hawakuamini kama magaidi hao wengeweza kwenda mbali kutishia jeshi na maisha ya raia.
“Mpo hapa kwa ajili ya Sarira?”Aliuliza Jenerali Jong.
“Ndio tupo hapa kwa ajili ya Sarira, au unadhani tupo hapa kuchoma ubani na kusali?”Aliongea Hao na palepale aliwageukia watu wake.
“Vijana ingieni ndani na mtoe Sarira nje , kuhusu hao Monk waleteni pia”
Baada ya maagizo hayo wanajeshi wa umoja wa Noth Buyeo walipiga hatua kuingia katika ukumbi wa ndani katika Temple la Jogyesa kwa ajili ya kuchukua Sarira.
Dakika hio hio milindimo ya risasi ilianza kusikika ndani huko na kupelekea hofu kwa raia waliokuwa ni wageni ndani ya eneo hilo.
Dakika chache tu alionekana mwanajeshi gaidi akitoka akiwa amebeba kile kiboksi huku wale wengine wakiwa wamewashikilia wale Monk kwa nguvu.
Abbes na Master Zihao walikuwa moja wapo lakini hawakuonyesha ishara yoyote ya hofu na muonekano wao ulimfanya Clark kukunja ndita.
“Hubby huyu Abbess si anajua kulewesha watu kwa mbinu ya kichawi kwanini hafanyi sasa hivi , au anafanya makusudi?”
“Hata sijui , huyu sister inaonekana kuna kitu anapanga pia ambacho sio kizuri , pengine ni mmoja wapo wa North Buyeo maana umoja huo una konekeshenni kubwa , matajiri wengi pamoja na wanasiasa ndani ya Korea ni wanachama , lakini upande mwigine labda anashindwa kuwaroga wote kwani ni wengi”
“Lakini kwanini huonyeshi wasiwasi , ndio wanachukua Sarira hivyo?”
“Si ndio vizuri sasa , ninachopaswa kufanya ni kuwafatilia na kisha kuiiba na mimi na baada ya hapo nikiulizwa nitawatupia lawama na hakutokuwa na sababu ya kutengeneza feki”Aliongea Roma akitoa tabasamu la kifedhuli na kumfanya Clark kuziba mdomo kwa mshangao na aliishia kutoa tabasamu.
“Aisee kichwa chako kina mipango michafu sana lakini ni sawa kabisa , hawa North Buyeo ndio wale walioniteka mara ya mwisho hivyo unapaswa kuwapa fundisho kwasababu wameshindwa hata kuzingatia usalama wa raia”
Ukumbuke hapa Clark na Roma walikuwa hawajajumuisha kwenye mateka kwani walikuwa tayari washatoka ndani ya Temple hivyo walikuwa wakiangalia kwa nje na North Bueyo hawakuonyesha hata kuwajali ni kama vile wamechagua mateka wa kuondoka nao.
Muda huo huo kiongozi wa magaidi alitoa oda nyingine akiwaamrisha watu wake wawasukumie mateka nje pamoja na wale Monk ili kuondoka eneo hilo.
Upande wa eneo la nje ya Temple hilo kulisikika ving’ora vya magari ya polisi pamoja na wanajeshi kwani walishafika kutoa msaada .
Lakini walishindwa kufanya chochote kutokana na kwamba kulikuwa na mateka lakini pia kuna mabomu yametengwa ambayo bado hawajayapata na moja ndio ambalo limelipuka mnda si mrefu,
Ilikuwa ni tusi kwa kamati ya ulinzi ya taifa na swala hilo lilipigwa pin ili vyombo vya habari visiripoti na ndani ya jiji lote la Seoul kila polisi na wanajeshi walikuwa wametapakaa kila kona.
“Kamanda Jong tutakuacha hai ili ukatoe taarifa kwa watu wako hapo nje ,boti yetu ipo ndani ya mto Han na tutaondoka na hawa mateka pamoja na Sariras na tukifika baharini na kuona tupo nje ya hatarii tutawaachia mateka pamoja na hawa Monk , nitawapa muda wa dakika tano kufanya maamuzi, kama sitopata majibu ndani ya dakika hizo tano basi tegemea milipuko ya mabomu na tutalipua bomu moja moja mpaka mtimize masharti”
Kamanda Jong uso wake ulijawa na hofu kubwa mo pamoja na haisra lakini hakuwa katika nafasi ya kuonyesha ukinzani na aliishia kutingisha kichwa kukubali,
Kamanda Jong palepale aliachiwa na kukimbia kwenda kwenye kikosi cha wanajeshi wenzake nje lakini kabla hata hajafika mbali Hao palepale alitoa bastora aina ya Desert Eagle na kisha akamchapa risasi ya mguu na kumfanya adondoke chini huku damu nyingi zikimtoka.
“Jenerali… unapaswa kutambaa sio kukimbia”Aliongea kuongozi wa magaidi huku akitoa kicheko na wenzake wote wakafatilia
Wanajeshi ambao walifika hapo waliishia kutokwa na jasho tu lakini hawakuweza kumsaidia kamanda Jong kutokana na hofu ya kupeleka hali kuzidi kuwa mbaya.
Kamanda Jong licha ya kuwa na maumivu aliishia kung’ata meno yake na kuanza kutambaa kuelekea upande wa wenzake walipo na alitengeneza michirizi ya damu kila sehemu aliopita.
Wakati huo wanajeshi hao hawakuongea chochote , ukweli ni kwamba kitendo cha umoja wa North Buyeo kuingiza mabomu na siraha kimagendo nyingi hivyo iliwafanya kuwa na hofu kubwa lakini kwa wakati huo swala hilo lilikuwa kama tusi kwa kitengo cha usalama wa taifa.
Ijapokuwa North Buyeo walikuwa washatoka ndani ya temple hilo lakini bado ulinzi uliimarishwa nje ya eneo hilo.
Kila mgeni aliekuwa hapo ndani alikuwa na hofu mno ambayo ilidhihirika kupitia muonekano wao , Park Juan ambaye alikuwa amepitia mengi katika maisha yake alionekana kuwa katika hali ya utulivu huku akiwa makini kulinda familia yake.
Lakini alishangaa kuona Yezi hakuwa kabisa kwenye mshituko wala wasiwasi wowote zaidi ya kushangaa shangaa kama vile kuna mtu ana mtafuta.
“Yezi unamtafuta nani?”Aliuliza Park Juan.
“Bro.. namaanisha Mr Roma kapotea”Aliongea kwa kugwaya.
Park Juan alishangaa , na familia yake pamoja na familia ya Kim wote walimwangalia Clark aliekuwa peke yake , dakika chache zilizopita alikuwa amesimama na Roma sehemu moja lakini cha ajabu haonekani.
“Msiniulize chochote maana sijui ni wapi ameelekea pia?”Aliongea Clark mara baada ya kuona familia hio inataka majibu kutoka kwake.
Roma aliondoka ndani ya eneo hilo mara baada ya kuona kiboksi cha Sarira kikitokomea upande wa kushoto.
Ilikuwa rahisi kwa Roma kuondoka ndani ya eeo hilo kwani alizunguka sehemu ambayo haionekani na mara baada ya kufikia ukuta aliruka na kutokomea nje.
Upande wa baadhi ya watu wa North Buyeo walishangaa kuona kivuli cha mtu kikiruka ukuta lakini walishindwa kumnasa kutokana na wepesi wake na baadhi yao waliamini pengine wameona vibaya.
Roma alikuwa akitumia mbinu za kininja alizofundishwa tokea akiwa mdogo na alikuwa na spidi ya ajabu mno na hakuna ambaye anaweza kumnasa kama anawafatilia.
Dakika chache tu Roma aliweza kufika katika moja wapo ya jengo la kitamaduni pembeni na eneo la Jogyesa na aliweza kuwaangalia watu wa North Bueyeo upande wa chni yake, alichagua eneo hilo ili kuona kila kinachoendelea.
Boksi ambalo lilikuwa na moyo wakibudhha ndani yae alikuwa amelishikilia Hao ambaye alikuwa akiwaangalia wanajeshi kwa macho ya kiuchokozi wakimpisha bila ya kumgusa akisogelea wakuu wa jeshi waliofika hapo.
Wanajeshi walikuwa wamesimama kando ya barabara na alionekana kiongozi wao kila muda alikuwa akiwasiliana na wakuu wake na kwa muonekano wake tu ni kama vile upande wa pili alikuwa akipewa maelekezo ya kutofanya jambo lolote la kuhatarisha usalama wa raia.
“Dakika tatu zimepita na bado sijapata majibu kutoka kwa wakubwa wenu , Kapteni Hwang Wakubwa wako ni wakatili sana , kwanini usiungane na sisi tu”Aliongea Hao akimtania Afande Hwang Suyeon aliesimama akiwa ameshikilia pamoja na Abbes Yu Lian.
“Acha kuota , kama utalipua mabomu dunia haitokuacha salama , vikosiv vya kupambana na ugaidi dunia nzima vitawaandama na mtamalizwa”Aliongea lakini kauli yake ilionyesha kumchokoza Gaidi Hao na palepale alimlamba kibao na kuzidi kufanya sura ya mwanamke huyo kuwa nyekundu.
“Acha kuongea ujinga , tayari tushalipua bomu moja unadhani tunashindwa kuachilia mengine yaliobaki, viongozi wenu wanachojali ni manufaa yao tu na mengine yote ni vitu vya juu juu vya kuongezea radha starehe zao , wewe tayari upo na miaka arobaini lakini mpaka sasa bado unaamini uongo wa wanasiasa?”
“Amitabbha sir , Huo moyo wa Kibudha ua nguvu ya kipepo ya uzimaji, huogopi kukasirisha miungu ya Kibuddha na vitendo vyako viovu?”aliongea Abbess Yu Lian.
“Kaa kimya wewe Monk Mzee , ninachoamini ni bunduki yangu tu sio miungu yenu ya kipuuzi”Aliongea na palepale alimlamba kibao Abbess Yu Lian na kufanya Monk wengine kupiga kelele ya ‘Amitabha’ bila kuongea neno lingine.
“Zimepita dakika nne na nusu mpaka sasa , nadhani nyie watu bado mnajiuliza ni eneo lipi mlipuko utatokea ngoja niwaonyeshe”Aliongea huku akiangalia saa na palepale alitoa tabasamu akionyesha ishra muda wowote atatoa agizo la bomu kuachiliwa.
“Subiri..”Alipiga kelele Kamanda akimzuia.
“Tumekubali masharti yako yote lakini hauruhusiwi kudhuru hao mateka na uhakikishe usalama wa watu ndani ya Temple”
“Acha kuongea ujinga , kama kweli umekubali masharti basi sogeza magari karibu”Alibweka Hao.
Wanajeshi wale walijitahidi kuzuia hasira zao na dakika hio hio gari za kijeshi zilisogezwa karibu na walizichunguza kama hazina vifaa vya hatari na baada ya kuhakiki walipanda.
Kwasabau walikuwa wakiondoka na mateka basi waliwaingiza katia magari matatu kwa wakati mmoja.
Dakika chache mbele wanajeshi waliishia kuangalia magari hayo ya magaidi yakiondoka ndani ya eneo hilo taratibu kwa mbwembwe zote , ilikuwa ngumu kunasa mabomu yote ndani ya Seoul ndani ya muda mfupi ndio maana hawakuwa na namna ya kuwaruhusu.
Roma aliekuwa akiangalia kwa mbali kinachoendelea baada ya kuona magari yaliobeba magaidi yameondoka alianza kufatilia kwa nyuma , ijapokuwa walikuwa wakiendesha kwa spidi kubwa lakini kwake ilikuwa rahisi kuwafatilia kwa kukimbia tu.
Safari ya magaidi wa North Buyeo ni kuelekea katika mto wa Han , wanajeshi wote waliishia kuwaangalia kupitia darubini zao kwa huzuni kubwa , hawakutaka kuwafailia nyuma nyuma ili kuwapa sifa.
Bot mbili zilikuwa zikiwasubiri katika mto huo , ijapokuwa kulikuwa na helicopter ambazo zilikuwa zikiwsindikiza kwa juu lakini hawakuthubutu kushambulia.
Hao akiwa ndio kiongozi wa kundi alitoka katika magari na kisha kuingia ndani ya Yatcht na moyo wake na ndani ya dakika chache tu ziliondolewa ndani ya eneo hilo kuitafuta bahari.
Roma aliishia kung’ata meno yake kwa hasira wakati akiwaangalia wakiondoka na boti , hata kama angeleta fujo ndani ya eneo hilo na kuchukua Sarira ingekuwa ngumu kuondoka nayo kwani wanajeshi walikuwa wakiangalia hivyo njia pekee ambayo aliona itawezesha mpango wake ni kuendelea kuwafuatisha mpaka baharini.
“Nitawafuata mpaka baharani , hata kama jeshi likiwazimisha nintakachofanya ni kuchukua moyo wa Kibuddha , kama wataniletea ukinzani hawa magaidi wa North Buyeo basi sitokuwa na huruma nao , nitawaua kulipiza kisasi cha Clark”Aliwaza Roma katika akili yake
Roma aliishia kuangalia boti hizo zikichanja mbuga kwa spidi na aliishia kutoa pumzi na kushukuru kwa wakati mmoja kuwa na mwili ambao sio wa kibinadamu la sivyo ingekuwa ngumu sana kuupata huo Moyo.
Roma alitembea mpaka eneo ambalo aliona kabisa hakuna anaemwangalia na kisha alivua nguo zake zote na kubakiwa na boksa tu na palepale alizificha kwa kutumia pete yake ya kijini na baada ya kumaliza zoezi hilo alijitupa kama kambale kwenye maji na kupotea .
Muda huo macho yake yalikuwa yamewaka taa za rangi ya njano na alikuwa akiogelea kama vile ni mashine , ijapokuwa spidi yake haikuwa kubwa kama alivyokuwa akikimbia akiwa ardhini lakini ilitosha kufatilia boti hizo kupitia sauti yake.
Wakati huo jeshi la Korea kusini halikutulia , lilikuwa bize kutafuta mabomu yote yaliotegwa ndani ya Seoul na walihitaji kuhakikisha mabomu yote yamepatikana ndio kutolewa maagizo mengine ya kushambulia magaidi.
Jeshi hilo lilikuwa likijali taswira yake tu na kwao mateka na moyo wa Kibudhha sio vitu vya kujali sana katika wakati kama huo,
Baada ya masaa manne mbele boti zile hatimae ziliweza kuingia katika maji ya bahari ya kimataifa , ilikuwa tayari ni usiku wa mwezi angavu.
Boti zile baada ya kutembea kwa umbali kidogo hatimae ziliweza kufikia katika meli kubwa ya kirusi ya kijeshi(Russian 956 destroyer).
Baada ya kuingia katika meli hio alionekana bwana mmoja mzungu ambaye amevalia kofia ya ki New Zelaand na alisalimiana kwa kushikana mkono na bwana Hao na wakaanza kuongea kwa kingereza.
“Chief Hao, Congratulations , I’m sure the patriach will reward you handsomely”
“Chifu Zhao hongera , naamini mkuu wetu atakuzawadia”
“Thank you General Mason , we must have troubled you with the sudden request”Alijibu Hao kwa namna ya upole akimwambia kwamba nadhani watakuwa wamemsumbua kutokana na ombi lao.
“Kama sio kwa mkuu , nisingekuwa na haya mafanikio , hakika uwezo wako ni mkubwa zaidi kuliko Chifu aliepita bwana Gao Ge, naamini uwezo wako utazidi kuwa mkubwa zaidi”
“Haha… Jenerali Masoni tafadhari acha kunitaia , yule alikuwa mjinga tu ,, ila sio mbaya kwasasa nitapeleka huu mzigo katika chumba cha kiongozi wetu”Aliongea
Mason aliangalia kifaa hicho , ijapokuwa hakujua imekuwaje mpaka wakaenda mbali hivyo ili tu kupata hicho kifaa lakini hakutaka kuwaza sana zaidi ya kumuonyesha uelekeo Hao.
“Wafungieni hawa wanawake katika ghala namba nne na hao monk katika ghala namba saba mpaka tutakapopata maagizo mengine kutoka kwa wakubwa”Alitoa maagizo Mason kwa kingereza
 
SEHEMU YA 675.
Mason alikuwa ndio kamanda wa meli hio na alikuwa akiaminiwa sana , mara baada ya kutoa maagizo palepale wale mateka walitenganishwa na kisha wakapelekewa kuelekea maghala tofauti tofauti huku wengine wakitoa ulinzi.
Kwasababu North Buyeo walikuwa washamaliza kazi yao hawakuhitajjka tena hivyo wengine walitumia muda huo kupumzka na wengine kuanza kucheza michezo mbalimbali wenyewe kwa wenyewe.
Dakika hio hio wakati wengine wakila bata hakuna ambaye aliweza kuona mwanachama mmoja wapo wa North Bueyeo ambaye amevalia sare za jeshi la Korea kusini na Kofia akitembea kitahadhari kuelekea ghala namba nne.
“Hey , unafanya nini , hili ghala ni kwa ajili ya mateka kama unatafuta sehemu wenzako walipo ni upande ule”Aliongea mwanajeshi ambaye alikuwa akilinda.
Mwanaume yule alishikilia kofia yake akiwa kama anaiweka vizuri na aliweza kuonekana na sura ya kiume wa kawaida wa Kikorea.
Dakika ileile ni kama yule mwanajeshi aligundua yule mwanaume hakuwa akielewa lugha ya Kikorea lakini kabla hata hajaulizia mara ya pili yule mwanaume aliruka kiustadi na kumpiga yule mlinzi kwa kigoti cha mguu na kumpeleka chini na dakika ileile alikuwa tayair ashapeleka mikono yake kwenye kichwa chake na kumvunja shingo palepale , ni tukio ambalo limetokea ndani ya sekunde tano tu.
Shambulizi lile lilikuwa la kitaalamu mno na halikuleta makelele ya aina yoyote na mara baada ya yule mwanaume kugundua hakuna ambaye alikua akimwangalia palepale akiwa amevalia Gloves nyeusi alifungua mlango wa ghala na kuingia ndani.
Katika ghala hilo ukichana na mateka wengine alikuwepo Zhang Ru pamoja na Kapetni Hwang ambao walikuwa wamejikalisha kwenye kona pamoja na walishituka mara baada ya kuona mtu huyo akifungua mlango na nyuma yake kukiwa na mwanajeshi aliepoteza kumbukumbu.
Yule mwanaume mara baada ya kuingia ndani ya eneo hilo palepale alivua Gloves zake na vidole vya rangi nyeusi viliweza kuonekana na hakuishia kutoa gloves tu kwani alitoa na ile kofia na kisha akaanza kujibabua katika eneo lake la sura na mpaka anakuja kumaliza kuondoa sura bandia aligeuka na kuwa mtu mwingine kabisa.
Zhang Ru mara baada ya kumwangalia kwa umakini alijikuta akipigwa na mshituko.
“Jamalii…!!!”Aliita akiwa kama vile haamini mtu anemuona ni Jamali
Jamali aliishia kutoa tabasamu hafifu na kisha alisogea na kumsimamisha Zhang Ru kwa kumshika mkono huku akiwa na uhakika hajapatwa na shida yoyote.
“Msiongee chochote , hakuna wanajeshi wengi wanaolinda nje , ninaweza kuwatoa hapa wote, kuna Chelezo nimeitegesha nje na inaweza kubeba zaidi ya watu ishirini , tunapaswa kuondoka ndani ya hili eneo kukiwa na giza”Aliongea Jamali, haikueleweka alifika vipi Korea kwani mara ya mwisho Roma wakati anawasiliana nae alikuwa Tanzania.
Zhang Ru alijikuta akitokwa na machozi mengi , hakuwahi kutegemea kama Jamali anaweza kuja mpaka huku kwa ajili ya kumuokoa , Tanzania ilikuwa mbali sana na alidhani ni kama anaota.
Zhang Ru kwenye maisha yake alitokea kumpenda huyo mwanaume sana lakini alimchukia mno mara baada ya mtoto wao kufariki na kuanzia hapo hakuwahi kuonana na Jamali tena na alichukia watu wa ngozi nyeusi , lakini kitendo cha kumuona Jamali hapo kilimfanya moyo wake kumsamehe , hakushangazwa na uwezo wa Jamali kuja hapo kwa sura bandia kutokana na kwamba alishajua tokea muda mrefu ni jasusi wa hatari sana wa Kitanzania ambaye alikuwa ni Undercover kilichomliza ni kwamba hakuamini kama Jamali bado alikuwa akimpenda kiasi cha kuhatarisha maisha yake.
Zhang Ru tokea aachane na Jamali alishaingia kwenye mapenzi na wanaume wengi sana tofauti tofauti lakini wote hakudumu nao na hio yote ni kutokana na kwamba kitu ambacho alikuwa akikipata kwa Jamali alikikosa kwao na mpaka wakati huo alikuwa Single na alikuwa akimuwazia Jamali lakini hakupata ujasiri wa kumtafuta.
Mateka wote waliokuwa wamefungiwa licha ya kuwa katika hali ya wasiwasi kutokana na kuokolewa na mtu mwenye ngozi nyeusi , waliishia kufuata nyuma nyuma huku Afande Jamali akiangalia usalama eneo la nje.
Lakini sasa mara baada ya Kapteni Hwang kumfikia yule mwanajeshi ambaye ameuliwa na Jamali palepale alichukua siraha yake na kuikoki na kumfanya Jamali kugeuka.
“Unafanya nini?”Aliuliza Jamali akiwa katika hali ya mshangao na alikunja ndita.
“Mimi ni polisi na ninajua namna ya kutumia bunduki , hivyo ninaweza kupigana”
Afande Jamali licha ya giza alitumia simu na kumulika upande wa bega la Kapteni Hwang na kusoma Isignia na alitingisha kichwa kumwelewa.
“Tunapaswa kuondoka haraka , hakuna mlinzi yoyore anaefanya doria kwasasa”Aliongea Afande Jamali huku akikunja kurudi upande wa nyuma wa meli hio.
“Paa.. , Paah!!!”
Risasi mbili ziliweza kusikika kutoka nyuma na palepale Afande Jamali alijikuta akidondoka chini huku damu nyingi zikimtoka eneo la mkono wake wa kulia na kwenye paja la mguu.
“Hwanga Suyeon , unafanya nini?”Aliongea Zhang Ru kwa nguvu mara baada ya kugundua ni Afande Hwang ndio aliempiga Jamali.
“Una akili ya haraka kufanya maamuzi ya wepesi , sina uhakika ila naamini wewe ni ajent hatari sana , nilitegemea ungetokea upande wa China lakini umekuja wewe , kwa bahati nzuri au mbaya tulikuwa na wasiwasi mtu angezamia kwenye meli yetu na kuokoa mateka”Aliongea Hwang Suyeon kwa lugha ya kingereza na kufanya mateka wote kumwangalia kwa mshituko na hofu.
“Wewe .. ni mmoja wapo wa kundi la North Buyeo ..?”Aliuliza Jamali aliekuwa akigulia maumivu na alijitahidi kusimama lakini alishindwa.
“Umeshachelewa , unafikiri imewezekana vipi kuua wanajeshi na polisi wengi vile ndani ya muda mfupi , bila ya kuwa na mpango wa kueleweka nilioandaa , hili swala lisingefanikiwa bila ya uwepo wa majeruhi”
Zhang Ru alimkimbilia Jamali pale alipokuwa amekaa na aliishia kutoa machozi.
“Jamali naomba unisamehe , bora nisingekupigia simu , haya ni makosa yangu”Aliongea kwa kichina kwani Jamali pia alikuwa akikijua vizuri kutokana na kufundishwa na Zhang Ru wakati alipokuwa wapenzi.
“Xiao Ru ,, usiongee hivyo , sikulaumu kwa chochote”
“Hahaha…. Zhang Ru nilidhani una ubaguzi wa Rangi ndio maana ukamshuku yule Mtanzania kutokana na rangi yake lakini kumbe una mpenzi wa rangi hio hio , aisee mapenzi ni tafsiri pana sana”Aliongea na palepale aligeuza siraha yake na kumnyooshea Jamali kwa mara nyingine akiwa na sura ya kikauzu.
“Ongea kama umekuja na watu wengine ndani ya hii meli?”Aliuliza kwa hasira na Jamali alimwangalia mwanamke huyo kwa hasira tu.
“Nini kinakufanya uone ninaweza kuongea ukweli?”
“Hakuna shida , nitakupeleka kwa kiongozi wetu , yeye ndio atakufanya uongee”Aliongea na muda huo huo wanajeshi walifika ndani ya eneo hilo na Kamanda Hwang aliwapa amri ya kufungia mateka na kuongeza walinzi wanaolinda maghala huku akimchukua Zhang Ru na Afande Jamali kwenda kuonana na viongozi.
Muda huo Hao alikuwa kwenye eneo la kifahari ndani ya meli hio, alikuwa amesimama huku kichwa chake akiwa amekiinamisha chini na mbele yake kwenye sofa la leather alikuwa amekaa Abbes Yu Lian ambaye alikuwa ameshikilia lile boksi la kioo akiangalia kitu kilichoppo ndani yake na kuishia kutoa tabasamu.
“Kazi nzuri Hao , maigizo yako yalikuwa kamilifu , nilikuwa na wasiwasi ungeshindwa kunipiga kibao pale lakini hukuniangusha”Aliongea ijapokuwa alikuwa na muonekano wa kipole lakini sauti yake ni ya kikauzu sana tofauti na mwanzo.
“Yote yamefanikuwa kutokana na muongozo wako , juhudi zangu si kitu ukifananisha na za kwako Master , ninapaswa kuadhibiwa kwa kukupiga kibao wewe kiongozi wetu”Aliongea na kumfanya Abbes kutingisha kichwa kutokana na sifa za Hao.
“Tutaacha kila kitu mikononi mwa Hwang Suyeon , ngoja awe shujaa kwa kuwarudisha mateka Korea kusini , kupitia hilo atapandishwa cheo na atakuwa na manufaa kwetu hapo baadae , nimeshawaroga wale Monk wengine , hivyo waleteni na wale mateka baadae niwaroge pia na baada ya hapo watarudi na Hwang Suyeon na mpango wetu utakuwa umekamilika kwa aslimia mia”
Aliongea na Hao alitingisha kichwa kukubali huku akitoa tabasamu la kishetani lakini wakati alipotaka kuongea neno palepale mlango ulifunguliwa na Jenerali Mason.
“Kiongozi , Afande Hwang amekamata shushu aliezamia kwenye meli yetu”
“Nilijua tu , hebu mruhusu aingie”
Muda uleue Hwang Suyeon alimwingiza Afande Jamali pamoja na Zhang Ru , Afande Jamali yeye alisukumiwa na kudondoka chini kwenye sakafu wakati huo Zhang Ru alikuwa akilia kutokana na majeraha ya Jamali.
Upande wa Abbess na Hao wote walikuwa katika mshangao mara baada ya kugundua shushu aliekuwa akiongelewa ni Mwafrika
Zhang Ru alipigwa na mshangao mara baada ya kumuona Abbes Yu Lian akiwa katika utulivu kwani mwanzoni alijua yeye ni mateka.
“Wewe pia ni,,, “
“Upo sahihi , mimi ndio kiongozi wa North Buyeo .. imekuwa bahati mbaya kwama mmefanikisha kufumbua fumbo lakini hamuwezi kutoka hapa mkiwa hai , ila imenishangaza kuona mtu mweusi ndio kaja kuokoa mateka , hawa watu weusi nimekuwa na bahati mbaya nao sana tokea kuanza kwa misheni”Aliongea Abbess huku akiwaza siku ya jana yake alikwaruzana na Roma Ramoni mwafrika mwingine.
“Kiongozi mwenyewe nimeshangaa pia , anaonyesha kabisa ni Ajent mwenye mafunzo makali lakini tumeshindwa kujua ametokea China au nchi gani lakini nina uhakika anahusika na maswala ya kiserikali , wasiwasi wetu ni kwamba amekuja na wenzake hivyo nimeshindwa kumuua ili uweze kutumia uwezo wako kumuhoji”Aliongea Hwang Suyeon.
“Ana uhusiano gani na huyu Mchina?”
“Wanaonekana kuwa wapenzi”Aliongea Hwang Suyeon na kumfanya Abbess kukunja sura.
“Kazi nzuri”Aliongea na ksiha akamgeukia Afande Jamali aliekuwa ameshikilia jeraha lake la mguu ambalo linatoa damu.
“Kama hutaki mpenzi wako afe mbele yako usilete ukinzani au vinginevyo watambaka kwanza kabla ya kumtupia baharini”
“Wewe ni mchawi tu..”
Zhang Ru alikuwa katika mshangao mkubwa , mwanzoni alimchukulia Jamali kama afisa usalama wa kawaida wa Tanzania lakini kwa kinachoendelea hapo inaonekana alikuwa ni zaidi ya vile anavyomfikiria kwani ukiachana na namna alivyojitokeza ndani ya meli hio lakini uwezo wake wa kuvumilia maumivu ulikuwa mkubwa mno.
Hata hivyo hakutaka kuwaza sana kwani Jamali alikuwa mtu wa siri sana na ndio maana walikuja kutengana licha ya kupendana sana baada ya mtoto wao kufariki.
Inasemekana siku ambayo mtoto wa Jamali anafariki alikuwa hapatikani hewani , mtoto wao alizaliwa akiwa na ugonjwa wa damu, Jamali alitafutwa kwa kila namna kwa ajili ya kumchangia mtoto wake damu kutokana na kundi lake la damu kuwa adimu lakini hakupatikana hewani na mpaka anakuja kutokea alikuwa amekwisha kufariki na hio ndio Zhang Ru alijenga chuki kubwa zidi ya Jamali na kuamini yeye ndio alimuua.
Upande wa Jamali tokea tukio hilo litokee maisha yake aliishi kwa majuto sana na alijiona kama mtu mwenye deni kubwa sana kwa Zhang Ru na marehemu mtoto wake , Zhang Ru ndio mwanamke ambaye alimpenda bila kumbagua rangi yake , Wachina walisifika kwa ubaguzi wa rangi hasa wanawake likija swala la kudate na wanaume weusi lakin Zhang Ru alikuwa ni wa tofauti , swala ambalo lilipelekea mpaka kutengwa na familia yake lakini alisimamia penzi lake kwa Jamali.
“Niambie wewe ni nani na unatokea wapi na je umekuja hapa na wenzako?”Aliuliza Abbess huku sauti yake ikiwika kama vile ametawalia na pepo.
“Kwa jina naitwa Jamali Mloko , ni naibu mkuu wa kituo cha polisi kutoka Tanzania mkoa wa Dar es salaam, lakini pia nafanya kazi kama Jasusi wa kujitegemea, …mke.. mpenzi wangu Zhang Ru alimchokoza mwanaume hatari sana duniani na nilipatwa na wasiwasi juu ya usalama wake hivyo nikafanya safari ya Dharula kuja nchini Korea Kusini kwa ajili ya kumtafuta , kwasababu sikutaka kujitokeza mbele yake niliamua kumfatilia kwa siri nikitumia sura bandia mpaka nilipomuona akiwa katika sehemu ya mateka wenu, hivyo niliua mwanajeshi wenu mmoja na kisha nikachukua mavazi yake na kuwa sehemu ya kikosi na kuja mpaka hapa , nilikuwa nikisubiri muda muafaka kuwatorosha mateka wote hapa kwa kutumia boti ya uokozi , nimekuja mwenyewe na hakuna mtu mwingine aliembatana na mimi”
Afande Jamali aliongea kila kitu , ijapokuwa ujasiri wake uliwashangaza watu wote lakini aliishia kupatwa na ahueni , mwanzoni walihofia pengine ni jasusi kutoka China maana walikuwa na taarifa taifa la China lilikuwa likifunza majasusi kutoka Afrika na kuwaingiza katika misheni ambazo hawataki kutambuliwa.
Hii ipo kabisa imekuwa mbinu ya China kutengeneza Majasusi nje ya rangi yao ili kuwezesha misheni zao kuwa rahisi katika mataifa ya nje, mara nyingi majasusi hawa hupokea mafunzo chini ya usimamizi wa serikali na baada ya hapo hupewa misheni maalumu.
Kwa mfano Mwaka 2018 alikamatwa Jasusi wa China mwenye asili ya Kiafrika nchini Kenya akiwa na nyaraka muhimu za Kenya akizisambaza kwenda China , Jasusi huyu kwa taarifa ya kiserikali ni kwamba alikuwa ni Jasusi wa serikali ya Kenya pamoja na Serikali ya China wanawaita Double Agent , haikuwa hivyo tu mwaka 2020 CIA walikamata jasusi mwafrika wa China pia swala hilo hilo lilitokea Marekani na ndio chanzo kabisa cha kampuni ya simu ya Huwawei kupigwa marufuku.
Ijapokuwa hawakumuamini Jamali moja kwa moja kama hana muunganiko na serikali ya China lakini maelezo yake yalionekana kuwa ya kweli kwani Abbes alionekana kutumia uchawi kumtawala.
“Huyo mtu hatari duniani ambae umemtaja ndio nani?”Aliuliza Abbess
“Ni…”
“Ni mimi hapa”
Sauti nzito ya mwanaume iliweza kusikika kutoka eneo la nje na kufanya kila mtu ambaye alikuwa ndani ya chumba hicho kushikwa na hofu.
Abbess alijikuta akiacha kumfanyia uchawi Jamali na palepale Jamali baada ya akili yake kurudi katika hali ya kawaida aliangalia pembeni na kukutanisha macho yake na Zhang Ru aliekuwa akimwangalia kwa mahaba mazito sana.
Ukweli mpaka hapo Zhang Ru alishajua Jamali kaja kwa ajili ya kumsaidia mara baada ya ile simu na alishajua ni nini alimaanisha baada ya kusema mtu wa hatari , alishajua aliekuwa akimzungumzia ni Roma lakini bado alishindwa kuamini.
Mason , Hao na Hwang Suyeon walinyanyua siraha zao na kuzielekezea mlangoni.
“Wewe ni nani?”Aliuliza Abbes kikauzu lakini wakati mmoja akipatwa na hisia kama vile alikuwa akichezewa akili na Jamali.
Dakika ileile Mlango ule ulipigwa teke na kufunguka na mbele yao aliweza kuonekana Roma alievalia boksa tu akiwa ametapakaa magugu maji kiasi cha kufanya eneo lake la mbele mtutu wake kujichora.
Nyuma yake kulikuwa na maiti zimetapakaa , wengine wakiwa na shingo ambazo zimepinda na wengine waliobakia walikuwa na matundu ya risasi kwenye vifua vyao.
Muda huo Roma alikuwa amemshikilia Samaki aliekuwa akicheza cheza kwa mkono wake wa kushoto na palepale alimng’ata na kuanza kumtafuna.
Roma alijikuta akimwangalia Jamali aliekuwa chini akimwangalia kwa macho ya furaha baada ya kuona mkombozi wake amefika na Roma alimrudishia kicheko.
“Hehe… unafurahi nini wakati umeniita mtu hatari duniani na utajuta , lakini angalau sijachelewa , ila unaonekana una uwezo wa aina yake , sijadhania kama utakuja kuzamia kwenye hii meli , umefika lini Korea ..Oh,,, nadhani utakuwa unampenda sana huyo mwanamke mpaka ukaamua kujitoa muhanga”Aliongea Roma.
Ukweli ni kwamba Jamali alikuwa akijiuliza kwanini Roma hajatokea bado ,ujasiri wa kuzamia kwenye hio meli ni kutokana na kwamba Alimuona pia Roma katika sherehe kule kwenye madhehebu ya Kibuddha na alijua lazima angechukua hatua na hisia zake zilionekenaka ni kweli.
Yaanni kwa lugha nyepesi ni kama aliyabetia maisha yake kwa Roma.
Unadhani nini kitaendelea baada ya hapo mpango wa Athena unaendeleaje tuendelee kula mtori nyama zipo chin
 
Shukrani sana mwamba Hades mwenyewe singanojr ikikupendeza utatupia mwendelezo tena. Kuna sisi ambao hatuna hiyo hela ya kununua hivyo tutasubiri huruma zako
 
Kwa.wasiomjua roma na edna na clark👇
941083d9da624c318d9f304f4f5a44eb.jpg
roma kushoto edna kulia clark yuko chini ya roma
 
Back
Top Bottom