Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Nao ndoa huu sasa mkuu!! Tusiuptezee bure!! Maana muda hausubiri mtu! Tuweke mzigo kwa idhini ya Maulana inshallah
 
Vp mliopo kwenye group lake huyu Singanojr anaelewesha.. katuacha na sitofaham.
 
SEHEMU YA 686.

Muda wa jioni nje ya geti la shule ya kimataifa ya JR International kulikuwa na magari mengi ya kifahari ambayo yalikuwa yameegeshwa huku yakiwa na wazazi ambao walikuwa wakisubiria watoto wao.

Hayakuwa magari mengi sana kulingana na idadi ya wanafunzi kwani kulikuwa na watoto ambao walikuwa wakipanda basi la shule , hivyo wale wazazi ambao walikuwa na uwezo wa kuwafuata watoto wao walikuwa wakifika na kusubiria nje ya geti mapema.

Ilikuwa ni shule ya kifahari ya kimataifa ndani ya Afrika mashariki nzima na ilikuwa na sheria kali sana za ki usalama hivyo mara nyingi wazazi wanaowafuata watoto lazima wafike kwenye dawati la mlinzi na kujiandikisha ili kutambulika kabla ya kuruhusiwa kuondoka na mtoto.

Upande wa kulia katika magari mengi ya kifahari yaliokuwa ndani ya eneo hilo lilikuwepo gari la rangi ya pink aina ya Aud ambalo lililikuwa likiendeshwa na Nasra.

Nasra kutokana na kutoenda kazini alikuwa ndio mwenye jukumu la kumfuata Lanlani shuleni na kumrudisha nyumbani.

Alikuwa ndani ya eneo hilo kwa takribani nusu saa nzima na mara baada ya dakika chache tu geti lilifunguliwa na kuruhusu walimu na wanafunzi kutoka na Nasra alitoka nje ya gari ili kumfanya Lanlan amuone.

Wanafunzi wengi walikuwa ni wa rangi mchanganyiko , kulikuwa na wahindi , waarabu na weusi na wote walikuwa na afya nzuri na furaha hivyo kuwafanya kupendeza sana.

Lanlan ndio moja wapo ya watoto waliokuwa wakipendeza sana katika shule hio kutokana na muonekano wake , ijapokuwa alikuwa na rangi ya kawaida ya kiafrika lakini sura yake ilikuwa ni ya kupendeza.

“Lanlan…!!!”

Aliita Nasra mara baada ya kumuona Lanlana akimpungia mkono na kufanya baadhi ya wanaume waliofika shuleni hapo kuchukua watoto wao kumwangalia Nasra kwa macho ya uchu kutokana na urembo wake.

Lanlan mara baada ya kumuona Nasra alimkimbilia na kwenda kumkumbatia huku akiwa ameshikilia Tiara yake ambayo ilionekana kuharibika.

“Lanlan mbona Tiara imeharibika?”

“Maulidi aliikanyaga wakati akikimbizana na wanafunzi wengine”Aliongea Lanlan huku akitia kidogo huruma.

“Ulifanikiwa kuirusha lakini?”

“Ndio Lanan alifannikiwa kuirusha na alishinda wanafunzi wote lakini mara baada ya kuishusha chini ndio Maulid aliikanyaga, nilikasirika sana na kumpiga teka lakini hakuumia”Aliongea na kumfanya Nasra kutamani kucheka na muonekano wake.

“Kama ulifanikiwa kurusha na wanafunzi wengine inatosha , mimi Auntie yako nitakutengenezea nyingine sawa?”Aliongea na Lanlan alitingisha kichwa na Nasra alimshika mkono kumwingiza kwenye gari lakini ghafla Lanlan alisimama.

“Mommy is here”Aliongea Lanlan huku akizungusha macho kushoto na kuia kumtafuta mama yake.

“Mama yako … Edna yupo hapa?”Aliongea Nasra kwa mshangao na yeye kugeuza shingo kulia na kushoto lakini pia alishindwa kumuona

“Lanlan utakuwa umeona mtu ambaye sie, gari ya mama yako haionekani hapa?”Aliongea Nasra huku akikodolea macho gari ya Bentley Continental ilioegeshwa upande wa pili , ukweli gari ile ilikuwa ikivutia na tokea afike hapo alikuwa akiiangalia.

“Ni kweli , Lanlan anaweza kuhisia uwepo wa mama yake popote pale, na alikuwepo hapa muda mfupi tu”Aliongea huku akiwa ameungalia upande wa vibanda vinavyouza matunda ya Apple.

Nasra alijitahidi kuangalia upande alioangalia Lanlan lakini bado hakumuona Edna na aliona pengine ni kutokana na kumisi mama yake ndio maana.

“Lanan twende nyumbani , nimekupikia chakula kitamu…”Aliongea Nasra na kumfanya Lanlan kugeuza uso wake na kisha alitingisha kichwa na kuingia ndani ya gari yake aina ya Aud na kisha aliendesha kuliingiza barabarani.

Pembeni ya kibanda cha kuuza matunda aina ya Apple kulikuwa na duka kubwa la vito vya thamani na Edna aliekuwa amevalia Miwani alikuwa amesimama akiangalia upande wa barabarani.

Alikuwa na huzuni mno na aliangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida kabisa akiiangalia gari ya Nasra ikitokomea.

Ukweli ni kwamba kidogo tu Lanlan amuone na Nasra pia ndio maana alikimbilia kujificha kwenye duka hilo na alishindwa kujua hata Lanlan kwanini anajua uwepo wake mahali popore pale.

Alijikuta akitoa pumzi ya ahueni mara baada ya kuona gari ya Nasra imetokomea na alitembea mpaka upande wa pili na kuingia kwenye gari ya Bentley Continental huku macho ya wafanyabiashara na wapita njia wakimwangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida , ni kama vile wanashangaa mrembo kama huyo anafanya nini katika mtaa huo..

*****

Siku hio hio upande mwingine nchini Rwanda katika makazi ya raisi Jeremy kulikuwa kimya mno na ni ndege tu ambao walikuwa wakisikika katika eneo hilo na makelele ya mvua.

Raisi Jeremy alikuwa amekaa kwenye kiti cha Mahogany akiangalia picha kubwa iliokuwa kwenye fremu katika meza , alikuwa akiiangalia kwa umakini mkubwa mno kama vile kuna kitu ambacho anakitafuta.

Ilikuwa picha ambayo ilipigwa yeye pamoja na Kizwe pamoja na mtoto wao Desmond miaka mingi iliopita , ilikuwa ni picha adimu sana ya kifamilia kipindi hicho alikuwa ni waziri tu wa nchi ya Rwanda na Desmond alikua mdogo na yeye alionekana kuwa kijana zaidi kuliko alivyokuwa kipindi hicho.

Ukiachana na picha hio ya kifamilia ya watu watatu kitu ambacho ameshindwa kukifuta katika kichwa chake ni siku ambayo Kizwe alikufa , muonekano wake siku ile ulikuwa ukijirudia rudia kwenye akili yake mara kwa mara.

Ulikuwa ni ule muonekano baada ya Kizwe kutoka Tanzania kabla ya kufufuliwa na Yan Buwen , kuna muda alijiuliza pengine yalikuwa sio maamuzi sahihi kumuua Kizwe wakati ule.

Alijikuta akiinua kikombe cha chai kilichokuwa kikitoa harufu nzuri na kunywa kidogo.

Nje kulikuwa kunanyesha mvua hivyo kusababisha eneo la ndani kuwa na ubaridi na ilimfanya Raisi Jeremy kutamani kuvaa hata koti licha ya kwamba alikuwa tayari ashawasha AC.

Alikuwa kwenye siasa kwa miaka mingi na katika maisha yake aliamini nguvu na madaraka vingemletea ridhiko la moyo lakini hatimae alikuja kugundua kwamba binadamu hawezi kuwa na kila kitu

Kila kitu huja kwa gharama zake , ukitaka pesa jua kuna kitu lazima ulipie , ukitaka madaraka lazima kuna gharama ambayo lazima ulipie na hicho ndio alikuja kugundua na kuamini kwamba hawezi kuwa na kila kitu kwenye maisha yake.

Alijihisi mpweke mno na alichukia hali aliokuwa nayo muda huo, alikuwa raisi na angeweza kupata mwanamke yoyote wa kumpa kampani lakini ile hali ya kimazoea ya familia ndio ilimfanya kuwa katika hali ya upweke lakini hata hivyo alipaswa kuvumilia kwani ndio yeye mwenyewe ambaye alifanya maamuzi ambayo yalipelekea kuisambaratisha familia yake.

Alipaswa kuvumilia kwa ajli ya nafasi yake kama raisi lakini vile kama mwakiishi miliki ya kijini ya Panas na kupotea kwa Kizwe na Desmond ilikuwa ni kafara ambayo ilihitajika kuimarisha nguvu yake ndani ya taifa hilo.

Ukweli ni kwamba hakujiona kama alikuwa na makosa , kama kuna aliekosea basi ni yule ambaye alichokoza kitu ambacho hakupaswa kuchokoza na watu hao kwake walikuwa ni wajinga.

“Ngoo,,, Ngoo..!!!”

Alishituka kutoka kwwenye hali yake ya kimawazo mara baada ya mlango wa ofisi yake kugongwa na alisimama na kurudisha picha ile mahali pake na kisha kwa sauti nzito alimruhusu anaegonga kuingia kwa lugha ya kifaransa.

Baada ya mlango kufunguliwa alionekana Linda alievalia mavazi ya suti, na uwepo wake hapo kidogo ulifanya raisi Jeremy kuchangamka.

Ijapokuwa Linda alikuwa hajamsamehe kwa yale aliomfanyia lakini bado alikuwa amemuweka karibu zaidi kutokana na muunganiko wake na the Doni.

“Mheshimiwa hizi ni taarifa za Edna kwa siku tatu zote”Aliongea kisha akamkabidhi bahasha ambayo ina nyaraka ndani yake.

Raisi Jeremy alichukua bahasha ile na kisha akatoa nyaraka ile na kuanza kusoma.

Nyaraka hio ilikuwa imeambatanisha taarifa zote ambazo zilikuwa zikihusiana na Edna kwa siku zote tatu , kwa kila alichokuwa anafanya na haikuwa katika maandishi tu lakini pia kulikuwa na picha zimeambatanishwa , picha ambazo zimepigwa kwa Kamera ya teknolojia ya juu mno kiasi ambacho ingekuwa ngumu kwa Edna kujua kama anafuatiliwa kila siku na kupigwa picha.

Raisi Jeremy aliishia kuangalia sura ya mwanamke ambaye alikuwa akionekana na tabasamu lilijipamba kwenye uso wake , ijapokuwa alikuwa amepoteza mtoto lakini alijivunia kwa kuzaa mtoto mwenye muonekano mzuri kama Edna.

Palepale yale mawazo ya familia yake iliokufa aliona ni ya kipuuzi na kujiambia bado hakuwa peke yake , hakuwa mpweke kama alivyokuwa akiwaza yupo Edna katika maisha yake.

Ijapokuwa binti yake alikuwa akiitwa Edna Adebayo tofauti na Edna Jeremy lakini bado alikuwa mtoto wake na aliamini siku moja atamtangaza kwa uma na kila mtu kumtambua kama binti yake na wakati huo kila kitu kingekuwa ‘perfect’.

“Edna alienda shuleni kwa Lanlan?”Aliuliza kwa mshangao kidogo.

“Ndio lakini hakumsogelea Lanlan zaidi ya kumwangalia kwa mbali tu”

“Inaonekana binti yangu sio mkatili kama anavyoonekana”Aliongea Raisi Jeremy huku akitoa kicheko hafifu na kumfanya Linda kutoa tabasamu pia.

“Linda hebu nenda na andaa utaratibbu , nitaelekea Dar es salaam ndani ya siku hizi tatu angalau hata kwa nusu siku tu, iwe ni safari ya siri”

“Sawa mheshimiwa”

*******

Siku ya kwanza ilipita na siku ya pili ikaingia Roma bado alikuwa katika eneo lilelile juu ya bahari.

Alikuwa amegundua mengi kukaa hapo na hakuwa amepoteza muda wake lakini kuna vitu vingi ambavyo hakuwa amevijua.

Wakati alipokuwa akitoka katika ulimwengu wa majini pepo akili yake ilikuwa imejiset kwenye kujiokoa tu lakini sio kwenye kuelewa nguvu ya mapigo tisini na tisa ya radi hivyo mara baada ya kurudiwa na nguvu zake alitaka kuelewa juu ya nguvu yake kikamilifu lakini bado alishindwa kuelewa kabisa

Mafunzo ya mbinu za kijini yalikuwa na changamoto sana na pale unapokumbana na kizuizi hakuna namna ambayo utaweza kupita kwa kutoboa moja kwa moja.

Hivyo Roma hakutaka kuharakisha isitoshe mbinu hizo hazikuwa majaribio ya kisayansi kama tu atakuwa ameelewa nadharia ndio basi, unaweza kuelewa nadharia ya mafunzo hayo lakini mwisho wa siku matokeo yakawa mabaya au yasio sahihi.

Isitoshe mbinu hizo ni za kimaajabu sana na zilihitaji uwezo mkubwa wa kiakiri.

Simu yake ilikuwa imeunganishwa na mawasiliano ya satilaini moja kwa moja hivyo hata kama alikuwa wapi ilikuwa rahisi kumpata kwa namba maalumu na ndio ambacho kilimshitusha katika kile alichokifanya mara baada simu yake kutetema mfukoni.

Baada ya kuitoa nje aligundua aliekuwa akipiga ni Magdalena na alishangaa kwani haikuwa kawaida kwa Magdalena kupiga simu na alipokea palepale.

“Magdalena kuna nini?”Aliuliza Roma swali hilo kwani alishajua hio ni simu ya dharula.

“Unaweza kunisindikiza China kwenye lile dhehebu la ngome ya Tang?”

“Ngome ya Tang tena , hujarudi Tanzania kwa muda mrefu kumsalimia baba yako unafikiria kwenda China?”

“Sio hivyo, Master amenipigia simu anasema kuna kitu muhimu kimetokea na anahitaji kukutana na sisi wote nimejaribu kumuuliza ni kuhusiana na nini lakini hakuwa tayari kuongea , ninaogopa linaweza kuwa tatizo kubwa”

Roma alifikiria kwa muda , usiku huo huo alikuwa na miadi na Maimuna kutokana na mpango wake wa kumuua Mzee Sharif , alijaribu kuangalia saa na kuona anao muda wa kutosha anaweza kwenda China na kurudi.

“Okey fanya safari kuelekea uelekeo wa huko , tutakutana njjiani nitakuwa naenda kwa kukusubiri”Aliongea Roma.

Ilikuwa rahisi kumpata Magdalena kama atatumia uwezo wake wa kijini kumnasa.

*******

UAE- DUBAI 18:00PM.

Ni majira ya jioni ndani ya jiji la kuvutia la kijangwa la Dubai katika hoteli ya kimataifa iliokuwa imesimama kwenye kisiwa cha kutengeneza cha Palm Jumeirah, katika ukumbi maalumu ndani ya hoteli hio kulikuwa na kikao kizito cha siri ambacho kilikuwa kikiendelea.

Kikao hicho kilikuwa kikihusisha baadhi ya wanachama wa umoja wa siri wa kupinga Illuminat duniani yaani Ant-Illuminat.

Katika kikao hicho watu pekee ambaye walikuwa wakijilikana ni mwanamama Mellisa jasusi mstaafu wa kitengo cha Dhoruba nyekundu ambaye aliwahi kusimamia misheni Pro Human iliotekelezwa nchini Bolivia chini ya serikali ya Marekani huku umoja wa Zeros organistaion ukiwa kama kivuli cha umiliki wa mpango wenyewe.

Mwanachama mwingine ambaye alikuwa akifahamika alikuwa ni Shekh Assad pamoja Pastor Cohen au Askofu wa kanisa maarufu la kidunia la kusambaza injili.

Cohen Banos ndio jina lake kamili bwana huyu alikuwa ni mtoto wa Profesa Banosi ambaye alifanikisha kutengeneza virusi kumi na mbili na kuvipatia majina ya miungu kumi na mbili ya kigiriki kutokana na sifa zake.

Uwepo wa watu hao wawili ndani ya eneo hilo ulikuwa ukiwakilisha vyeo vyao vilikuwa vikubwa zaidi.

“Mellissa nini kinaendelea mpaka sasa?”Aliuliza Mwarabu mmoja ambaye alikuwa amevalia kiremba kichwani.

“Nchi mbalimbali kutoka mataifa ya Afrika kupitia viongozi wao wamepokea mikataba inayofanana, tupo kwenye uchunguzi wa kujua kwanini matajiri wengi wananunua ardhi Afrika”Aliongea Mellisa.

“Mellissa nadhani kauli yako haijakaa sawa , ni vizuri kusema wanachama matajiri wa umoja wa Freemason na Illuminat”

“I stand to be corrected Shekh”Aliongea Mellisa huku akitoa tabasamu.

‘Kuna mipango mingi sana inaendelea kuhusu bara la Afrika lakini imekuwa ngumu kujua mipango hii ni kwa ajili ya nini, imekuwa rahisi kuzuia mkataba wa kuongeza idadi ya mashoga nchini Tanzania lakini ni kwa muda tu kabla ya mkataba huu haujawekwa mezani kwa mara nyingine, mawakala wetu wanajitahidi kutoa nguvu kwa kila taifa lakini mafanikio bado yapo chini”Aliongea Shekh Assad.

“Shekh Assad mpango tuliokuwa nao ni kujipanua zaidi na ushawishi wetu kuwa mkubwa zaidi duniani , tumekuwa tukipiga hatua taratibu kutokana na kwamba tunajaribu kwenda kinyume na misingi iliowekwa kwa muda mrefu na kuweka msingi mpya lakini hata hivyo tumepiga hatua lakini kwanini bado kuna kigugumizi kikubwa kutoka Vatican?”

“Pastor sidhani ni swala la kigugumizi , hili ni swala la kimfumo malengo yetu yalikuwa ni kuongeza ushawishi wetu zaidi duniani ili kuwa na nguvu ya kushinandna na Illuminat lakini hili limekuwa gumu kutokana na kujificha kwao ndani ya Freemason, wote tunajua umoja huu haupo Active kwa miaka mingi lakini kikalenda ni swala la muda tu kurudi na kua Active, hivyo kinachoonekana hapa ni kwamba tupo nyuma ya muda”

“Naunga mkono hoja , lakini malengo ya haya yote ilikuwa ni kwababu ya kuona mchoro wa unabii ambao ni sawa na mpango B?”

“Ndio Shekh Khalifa mpango ulikuwa ni mchoro wa unabii lakini je itawezekana kwa Vatican kuuonyesha kwetu kabla ya kuonyesha kwa Illumnati , tunajua chimbuko la umoja huu upo ndani ya Vatican je hakutakuwa na njama?”

“Mchango wangu nadhani ni kuendelea na mpango B huku tukihakikisha kwamba matukio ya kikalenda yanaendelelea kama ilivyopangwa”Aliongea Pastor Cohen na kufanya jopo kutulia.

“Mellisa kuna maendeleo yoyote kuhusu Edna? , Zimebakia siku chache sana kikalenda kufanya mawasiliano na sisi, unadhani jambo hili litafanikiwa atafanya mawasiliano kweli?”

“Shekh Assad kwanini tusiendelee kuwa na imani , mabadiliko kuhusu Edna ni makubwa na naaini ndani ya siku ya Kalenda atafanya mawasiliano”

“Kuna kitu ambacho nilikuwa nikijiuliza kwa muda mrefu pengine ni kutokana na maradhi yangu , mpango A ni upi na Mpango B ni upi , nimesikia maongezi ya kila pande lakini nadhani mmeniacha nyuma”

“Mufti tuwie radhi hii ni mara yako ya kwanza kuhudhuria kikao kwa muda mrefu kutokana na matatizo ya kiafya , Mpango A ni wa kufuata Kalenda ya uanachama ambayo imeachwa na mwasisi wa umoja na hapa inahusiana na matukio ya kidunia ambayo yanatokea ndani ya Kalenda , mpango B unatokana na matukio ya kikalenda kutotimia kama kaenda inavyoonyesha hivyo ili mwisho kuwa uleule lazima kuwe na tukio mbadala, hatua ya mpango unaofatia ni Malkia Persephone kufanya mawasiliano na umoja wetu tokea mara ya mwisho tulivyomtambua kwa kutuonyesha pete ya muhuri kama kiongozi wetu, hili ni tukio la kikalenda na kama halitofanikiwa inamaana mpango B ni kuhakikisha tunaona mchoro wa kiunabii”

“Kama kweli tunakalenda ambayo inaelezea kila kitu kwanini tunatumia juhudi kubwa ya kusubiria matukio?”

“Mheshimiwa Kalenda ambayo ipo sio inayoonyesha matukio ya moja kwa moja , bali kila pale tukio linapotokea ndio linatokea tukio lingine katika tarehe husika , kalenda yetu haipo kama kalenda za kawaida”Aliongea Mellisa na bwana mmoja alieitwa mheshimiwa alinyamaza.

“Kwahio kama kusipokuwa na mawasiliano kutoka kwa Persephone inamaanisha kwamba inatakiwa kufuata mpango B kama ni hivyo kwanini tusijadili kuhusu mpango B maana kila tukio ambalo linatabiriwa na kalenda kutokea lina asilimia themanini ya uhakika”

“Hio ndio ajenda ya kikao mheshimiwa hivyo naunga mkono hoja yako , lakini dunia ni kubwa na tunapaswa kupiga hatua ‘Collectively’ ili kupunguza matokeo ya kidosari katika kila mpango, ndio maana ma ajenti wetu kila pande ya dunia wanakusanya taarifa na kuzifanyia kazi”.

“Kabla ya kuendelea na ajenda ya mpango B nina swali kwenda kwa Shekh Assad??”Aliongea bwana mmoja ambaye alikuwa amevalia suti alikuwa ni kiongozi mkubwa kutoka bara la Amerika ya kaskazini.

“Ajenda ya kikao cha G7 mwaka huu ilihusisha nini , nadhani mara ya mwisho ulituelezea mmoja ya viongozi ambao ni wanachama wa G7 amekuwa mwanachama wetu?”Aliongea na swali hilo lilionekana kufanya chumba chote kuwa kimya na kumwangalia Shekh Assad ambaye ndio alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA



MTUNZI: SINGANOJR.



Mono no aware.




SEHEMU YA 687.

Magdalena na yeye alikuwa na spidi kubwa katika kusafiri na kwasababu alikuwa katikati ya levo ya nafsi basi isingekuwa tishio kwake kukiuka kanuni za asili za anga.

Roma alitumia uwezo wake wa kijini kumtafuta Magdalena na ndani ya dakika chache tu alimpata na walielekea pamoja.

“Master amesema tutampata katika msitu wa mianzi moja kwa moja, haina haja ya kusumbua wengine”Aliongea Magdalena mara baada ya kufika usawa wa Dhehebu la ngome ya Tang.

Roma alikuwa na shauku kubwa mno, alijiuliza kwanini Master wake Magdalena anataka kukutana nao kwa siri.

Baada ya kufika ndani ya msitu wa mianzi walianza kutembea , haikuwa mara ya kwanza Roma kufika katika eneo hilo na nje kidogo ya msitu huo ndio nyumba ya Master Tang Luyi ilipokuwa na mara baada ya kufika walikuta mlango upo wazi.

Wote waliingia na waliweza kumkutaTang Luyi akiwa amevalia gauni la rangi nyeusi akiwa amekaa mbele ya kioo.

“Master tumefika”Aliongea Magdalena huku akisalimia na kumfanya Tang Luyi kushituka kwani hakuwa amewaona.

Ilikuwa ni ngumu sana kwa Tang Luyi kutowaona kwani alikuwa tayari kwenye levo ya mzunguko kamili , ijapokuwa Roma alikuwa ameficha uwezo wake lakini Magdalena hakuwa ameficha uwezo wake.

Tang Luyi palepale aligeuka na kumwangalia Magdalena kwa mshangao na kisha akageuza macho yake kwa Roma , macho yake yalikuwa na hali ya wasiwasi mno.

“Kumbe mmeshafika?”Aliongea kwa sauti yenye kitetemeshi na kulazimisha tabasamu.

Magdalena kwa kumwangalia tu Master wake alijua kuna kitu ambacho hakikuwa sawa na palepale alimsogelea na kumshika mkono.

“Master kwanini mikono yako ni ya baridi hivi , kuna tatizo gani , kwanini umetuambia mimi na Roma kuja hapa kwa haraka?”

Master Tang Luyi aliishia kumwangalia Magdalena kwa macho yasiokuwa ya kawaida na ilionekana ni kama vile anataka kulia.

“Flamingo , mimi master wako nimekufelisha”Aliongea

“Unamaanisha nini?”

Master Tang Luyi alizungusha shingo yake na kumwangalia Roma kwa wasiwasi na kisha alimwachia Magdalena na kisha alisogea mbele ya Roma na katika hali ya kushitukiza alishuka chini na kupiga magoti , jambo ambalo lilimshangaza Roma

“Master!!!”

“Nini!! .,, Master wake Magdalena, We dada , Shangazi … Mchina…!!”Roma alikuwa akibabaika huku akijaribu kumnyanyua Master wa Magdalena lakini aligoma na muda uleule aliinamisha kichwa chake kwa namna ya kusujudu mbele ya Roma

“Mr Roma tafadhari naomba msaada wako ,muokoe binti yangu, ninakuomba tafadhari …”Aliongea huku akianza kutoa kilio.

“Binti yako!!!?”

Roma alikuwa katika mshangao na kuchanganyikiwa na aliishia kumwangalia Magdalena kama vile anahitaji maelezo kutoka kwake lakini aligundua hata yeye alikuwa kwenye mshangao.

“Master ni lini ukawa na mtoto wa kike ghafla tu , hujawahi kuniambia kuhusu hili?”Aliongea Magdalena aliechuchumaa akijaribu kumwamsha Master wake lakini aligoma na kutaka kuendelea kupiga magoti.

“Magdalena usinisimamishe , haijalishi ni kwa muda gani,napaswa kuwapigia magoti”

“Master haijalishi ni jambo gani naomba utuambie ukiwa umekaa tafadhali”Aliongea Magdalena na palepale alitumia nguvu ya kijini kumwamsha Master wake kwa nguvu.

“Magdalena umeingia levo ya nafsi!?”Aliuliza Master Tang Luyi kwa mshangao.

“Yeah ,,, ndio nipo katikati kufikia mwisho wa levo ya nafsi , zote shukrani ziende kwa mpenzi wangu , amenisaidia sana kama sio yeye nisingefikia hatua hii”

“Oh! sawa sawa … hakika ulichagua mtu sahihi kuwa nae , Master wako nina furaha kwa ajili ya mafanikio yako”

“Master nini kinaendelea , hebu nniambie kwanza”

“Ni stori ndefu sana , napaswa kuanza miaka ishirini iliopita”Alliongea Tang Luyi huku akipumua kwa nguvu.

Miaka mingi iliopita Tang Luyi alikuwa ni msichana mdogo kabisa katika ngome hio ya Tang , baada ya kujifunza mbinu za kichawi za mapigano alijihisi ni kama vile amepanda juu zaidi na kuanza kuletea ujeuri baadhi ya Master kutoka madhehebu mengine na yote hio ni kutokana kwamba alikuwa akijiamini sana lakini pia alihitaji uzoefu.

Siku moja wakati akiwa nje ya ngome alikuja kushuhudia tukio la wizi , mwanzoni alitaka kujaribu kuwa shujaa kwa kuzuia tukio lile na kufukuza wezi lakini alishindwa kwani wale wezi walikuwa wakitumia bunduki na yeye hakuwa na uzoefu na siraha hizo na katika purukushani za wale wezi alijikuta akijeruhiwa na risasi eneo la kiuno.

Dakika hio hio wakati akiwa anaugulia maumivu ya jeraha la risasi alitokea polisi mmoja ambaye ni kama vile ametokea mbinguni na kushuka na palepale aliwashughulikia wale wezi na kuwakamata wote na baada ya hapo alimchukua na kumpeleka hospitalini.

Tang Luyi alishangazwa sana na yule polisi wa kiume kutokana na namna ambavyo alikuwa akipigana , katika kipindi hicho msichana mdogo akiona kijana wa rika lake akipambana vizuri ilikuwa lazima imvutie na yeye hakuwa tofauti na wanawake wengine.

Alijikuta akimtamani sana yule polisi ambaye jina lake alifahamika kama Wang Sheng kwa namna ambavyo alitokea kumjali katika kipindi chote alipokuwa hospitalini.

Wang Sheng na yeye alitokea kuvutiwa na Tang Luyi na katika kipindi cha muda mchache tu walijikuta wote wakiingia kwenye penzi nzito , ijapokuwa Tang Luyi hakudhania kama atakuja kuwa katika mahusiano lakini ndio ikawa hivyo.

Miaka michache ya mahusiano yaliopelekea ndoa walifanikiwa kupata binti yao wa kwanza ambaye walimpatia jina la Wang Shu na kipindi hicho Tang Luyi na mume wake walikuwa wakiishi nje ya ngome ya Tang na mara baada ya kupata binti yao ilimfanya Tang Luyi kuwa na furaha sana na kujiona anamiliki ulimwengu.

Lakini sasa siku moja ikiwa ni siku tatu za kujifungua Tang Luyi aliamka asubuhi na kujikuta yupo peke yake , hakuwepo mtoto wala mume wake na kitu pekee alichoweza kukutana nacho ni ujumbe wa maandishi peke uliosomeka.

“Hatima yetu imefika ukomo , mwanaume anapaswa kwenda na upepo , kwenye droo kuna kidonge cha kijini , kitakusaidia katika nguvu zako za uzazi ulizopoteza kwaheri ya kuonana”

Ulikuwa ni ujumbe wa kuumiza sana ambao aliweza kuusoma Tang Luyi na alijihisi kama vile amefika siku ya kiama, uwepo wa kile kidonge ulimthibitishia mwanaume aliekuwa nae kwenye ndoa hakuwa binadamu wa kawaida bali alikuwa ni jini ambaye amemtumia tu kumzalia na kisha kuchukua mtoto na kupotea.

Baada ya Tang Luyi kupoteza mtoto ndio akarejea ndani ya ngome ya Tang Kuanza maisha mapya ya kimawazo na miaka kadhaa mbele alijifua zaidi na zaidi katika mafunzo mpaka alipokuja kumpokea Magdalena alieletwa hapo kama mwanafunzi katika projekti maalumu ya taifa la Tanzania katika uundaji wa kitengo cha wachawi.

Wakati Magdalena anafika alikuwa ni msichana mdogo na Tang Luyi alikuwa mkubwa tu , ni sawa na kusema Magdalena alikuwa na umri sawa na wa binti yake aliepotea hivyo licha ya kutofautiana rangi Tang Luyi aliamua kumlea Magdalena kimafunzo.

Stori ya Tang Luyi ni kama ilivyokuwa ya Bi Wema , wote walitumiwa na majini ili kuzaa , tofauti tu ni kwamba Bi Wema ndio ambaye alitia huruma sana kwani hakumjua mwanaume aliempenda alikuwa ni nani haswa na hata mara baada ya kupotea na mtoto wake hakutoa taarifa, yaani alipotea tu na alikuja kujua alikuwa jini mara baada ya kurudi kwa Rufi kwenye maisha yake.

“Lakini Master kwa ninavyojua moja wapo ya koo za kijini zilizopo ndani ya mipaka ya China ni Hongmeng na ukoo wa Xiao , kwanini alijitambulisha kwako kama Wang?”

“Baba aliniambia kwamba majini wengi huchagua maumbo ya sura kutokana na kupenda tamaduni ya jamii husika , kwa mfano **** majini ambayo yatachagua sura za kiarabu na meingine kuwa na sura za watu weusi , wazungu na wachina na wanapotoka katika ulimwengu wao kuja katika ulimwengu wa kawaida hujipa majina kutokana na muonekano wao lakini sio majina yao halisi, koo za kijini sio mbili wala tatu , koo zipo nyingi sana kwa mfano tu miliki ya kijinni ya Panasi inajumuisha koo nyingine ndogo ndogo ambazo zipo chini yao , hivyo hivyo Kekexil , Hongmeng na koo nyingine, hizi chache zinafahamika kutokana na kuwa na nguvu kubwa”

“Ukiachana na hayo , nini kimemtokea binti yako?”Aliuliza Roma.

“Usiku wa jana kuna mtu amerusha mshale karibu na mlango ukiwa umebeba hiki kidani na ujumbe….”Aliongea na kisha palepale alitoa kile kidani na kuonyesha.

“Hiki kidani nilimpatia binti yangu mara tu baada ya kuzaliwa , ni kidani ambacho nilipatiwa mimi wakati nilipozaliwa , hivyo ni rahisi kwa mimi kukifahamu”Aliongea na kisha alimpatia Roma ujumbe ulioandikwa kwa maandishi ya kichina na kwasababu alikuwa akikijua vizuri aliweza kusoma.

“Najua Wang Shu ni binti yako na Wang Sheng , huyu mwanamke mpaka sasa yupo kwenye mikono yangu akiwa na sumu mwilimi mwake , kama unataka binti yako awe salama na kurudi kwako , chukua mbinu ya kijini ya andiko la urejesho usio na kikomo kutoka kwa Roma Ramoni na njoo nayo juu mlima Fale siku ya kesho usiku saa sita , kama utachelewa Wang Shu atakufa”

Magdalena na yeye alikuwa amejifunza kichina hivyo aliweza kusoma ule ujumbe na alijikuta akiziba mdomo kwa mshangao.

“Master kwahio umetuitia kwa ajili ya hili.?”

“Najua hili ni jambo gumu sana kuomba lakini nipo tayari kufanya chochote ,najua pengine mtu huyu ananidanganya lakini bado najikuta nikitaka kuamini”

“Mlima Fale ndio mlima gani mbona sijawahi kuusikia?”Aliuliza Roma.

“Upo Kaskazini mashariki, ni sehemu ya safu za mlima Altai mpakani mwa China na jangwa la Gobi- Mongolia”

“Hivyo kama tusingekuja wewe ungeenda mwenyewe… huyu mtu nadhani ananijua vizuri nje ndani , maana kama anajua mahusiano yangu na Magdalena na wewe na Magdalena ana uhakika kabisa lazima anachokitaka atakipata , nina uhakika serikali ya China inahusika hapa”

“Kwanini tusimuulize Rufi , pengine anaweza kuwa na uelewa juu ya koo nyingine za kijini ambazo zinajiita Wang?”Alishauri Magdalena na Roma palepale aliona ni vizuri kufanya hivyo.

Alitoa simu ake na kumpigia Rufi na ndani ya dakika chache tu ilipokelewa na Roma akamwelezea.

“Honey umejuaje kuna familia ya Wang katika ulimwengu wa kijini , familia hio ni sehemu ya miliki ya ukoo wa kijini wa Xia , kuna majini wengi na binadamu wa kawaida ambao wana mafunzo makubwa ya kijini”

“Rufi ulishawahi kusikia jina la baba na mwana Wang Sheng na Wang Shu?”

“Wang Shu ni msichana wa pekee ndani ya familia ya Wang na baba yake Wang Mian ni jini mkuu kiongozi wa familia ya Wang , kuhusu Wang Shen sijawahi kusikia jina lake”

Roma alikuwa ameweka loudspeaker hivyo Tang Luyi na Magdalena waliweza kusikia na wote wakivuta pumzi mara baada ya kusikia familia hio ya kijini ipo

“Inaonekana majina yake hayakuwa feki lakini hatujui nani ambaye amemteka mtoto wako Wang Shu ..”Aliongea Roma mara baada ya kukata simu.

Roma hakuwa na namna zaidi ya kumsaidia Tang Luyi , alifanya hivyo kwasababu ni Master kwa Magdalena tu na sio vinginevyo.

Upande wa Magdalena hakutaka kumlazimisha Roma kumsaidia kwani masharti yalikuwa magumu sana na alijua kama Roma atatoa mbinu yake ya mafunzo itakuja kuwa hatari lakini Roma alimtoa hofu.

Kulikuwa na tofauti ya kimasaa kutoka Tanzania na China hivyo hawakukaa muda mrefu mpaka muda wa kwenda Mlima Fale kwa ajili ya kuonana na mtekaji.

Roma alikuwa na shauku ya kumuona mtekaji mwenyewe na mara baada ya kusafiri kwa dakika chache tu hatimae waliweza kufika juu ya jangwa la Gobi katika nchi ya Mongolia.

Jangwa hilo Roma alikuwa na historia nalo kwani wakati wa kujifunza mafunzo ya kijini alikuja kujificha huko na Master wake Tang Chi.

Baada ya kufika juu kabisa ya mlima Fale ilikuwa ni kama walivyotarajia kwani Roma kadri alivyokuwa akisogea alikuwa akihisi msuguano wa nguvu za kijini tena za aina mbili , moja ni nguvu ya levo ya mzunguko kamili na nyingine ilikuwa ni nguvu ya zaidi ya mzunguko kamili.

Haikuwa ngumu kumuona mtekaji kwani mlima huo miti yake ilikuwa ni ile mifupi ambayo imeachana achana kutokana na ukame.

Kilichomshangaza Roma mara baada ya kumuona mtekaji ni uvaaji wake , Mtekaji huyo alikuwa amevalia joho la rangi ya njano huku akiwa na nywele ndefu mno akiwa amezisuka kama mkia kwenda nyuma lakini uso wwake alikuwa ameufunika na Mask ya chuma cheusi na kumfanya kutisha kimuonekano.

Nyuma yake kulikuwa na kiroba kilichotengenezwa kwa katani na Roma mara baada ya kupiga jicho alikuja kugundua kuna mtu ndani yake ambaye ndie mwenye nguvu za kijini levo ya mzunguko kamili.

Mtu mwenye mask alikuwa katika levo ya kuyadhibiti maji na Roma aliona kabisa atakuwa hajapita levo ya dhiki bali yupo katika levo ya kuiepuka dhiki.

Ukumbuke levo ya kuipita dhiki ni tofauti na ya kuepuka dhiki , waliopo levo ya kuepuka dhiki ni majini ambayo yanafanya miujiza ya jini ambaye ameipita dhiki , yaani ni sawa na mwanafunzi wa darasa la kwanza kufanya mahesabu ya darasa la nne kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa akili.

“Waoh!! Inaonyesha kweli unampenda binti yako”Sauti ya kiume iliweza kusikika kutoka ndani ya lile Mask la chuma na Roma alijiambia kwanini ana bahati mbaya sana na hawa majini wanaojifunika sura na mavyuma alikumbuka kuna yule mtu mwenye mask ambaye hushirikiana na Athena.













SEHEMU YA 688.

Haikuchukua muda mrefu sana mtekaji yule alimhakikishia Tang Luyi kama mateka wake ni mtoto wake kwa kumtoa kwenye kile kiroba na kumuonyesha.

Licha ya kwamba Tang Luyi hakuwa akijua muonekano wa mtoto wake kutokana na kutengana nae muda mrefu lakini mara baada ya kumuona tu aliweza kuona kabisa alikuwa akifanana nae vitu vingi na hata Roma alithibitisha hilo.

Wang Shu alikuwa amewekewa sumu , mtekaji alionekana alikuwa amejiandaa vizuri , ilionekana kabisa hakuwa na mpango wa kupigana na Roma na hata upande wa Roma licha ya kujua anaweza kumpiga huyo na kumuua lakini hana uhakika kama ataweza kumuokoa Wang Shu ndani ya muda hivyo hakutaka kubeti.

Baada ya majadiliano ya muda mfupi Roma alitoa andiko la urejesho ambalo alikuwa ameliandika kabla ya kufika hapo na kisha kumpatia mtekaji na baada ya kuhakiki andiko ni lenyewe alitoa tabasamu la ushindi na kisha akapotea huku akisema ndani ya muda flani sumu ambayo Wang Shu ipo ndani ya mwili wake ingetoweka kwani ina muunganiko na nguvu zake za kijini.

Ajabu ni kwamba ilichukua sekunde tu kwa mtekaji kupotea na Roma hakuweza kunasa nguvu zake za kijini kabisa Roma alijiambia hata kama angekuwa na spidi kubwa kwa namna gani hawezi kupotea kwa haraka namna hio na palepale alijiuliza au hilo eneo kuna njia ya kuingia ulimwengu wa kijini.

Magdalena alikuwa ni mwenye wasiwasi mno , kabla ya kuja hapo alijua Roma alikuwa na mpango wa kutotoa mbinu yake ya mafunzo lakini nje ya mategemeo yake Roma alitoa mbinu hio kirahisi tu bila kuchukua hatua nyingine , alidhania labda Roma alikuwa amaendika andiko feki lakini mara baada ya kumuuliza Roma alimwambia aliandika kitu halisi ndio maana ilikuwa rahisi kumfanya mtekaji kumuamini.

Magdalena alimlalamikia Roma kwa kutoa mbinu yake kirahisi lakini Roma alimtoa hofu na kumwambia licha ya kumpatia mbinu hio haiwezi kuwa na msaada kwake.

Baada ya maongezi ya muda mfupi Roma aliondoka kurudi Tanzania huku Magdalena akimsindikiza Master wake na binti yake kurudi ngomeni.

*******

Upande mwingine mkoani Manyara kilomita kadhaa kutoka ziwani kulikuwa na hoteli kubwa ya kisasa iliokuwa ikipatikana ndani ya hili eneo , hoteli hii wamiliki wake walikuwa ni familia ya Mzee Sharif.

Ni hotelia mbayo imejengwa msituni na muundo wake ulikuwa ni wa tofauti kidogo, ukiangalia kwa juu ni kama vichuguu kwani kuna nyumba nyingi ambazo zilikuwa zimejengwa kwa ajili ya wageni.

Ilikuwa ni hoteli ya kitalii ya hadhi ya juu sana ndani ya mkoa huu na ilikuwa imepokea tuzo World Luxury Hotel Award kwa mwaka 2020 na hili iliifanya hoteli hii kutembelewa na watu wakubwa wakiwemo wafanyabiashara, wanamichezo na matajiri.

Lakini sasa tofauti na siku zote hoteli hio usiku huo kulikuwa na hali ya kitofauti kidogo kwani haikupokea mgeni na hata wale waliokuwepo walihamishiwa kwenye hoteli nyingine na asilimia kubwa ya watu waliokuwepo hapo ilikuwa ni walinzi , wanafamilia wa Mzee Sharif na wafuasi wa dini yao.

Dakika ambayo Roma aliweza kufika juu ya hoteli hii alijikuta akitoa tabasamu la kifedhuli kwani chini yake aliweza kuhisi msuguano wa nguvu za kijini za levo ya nafsi lakini pia kulikuwa na msuguano wa nguvu za kijini levo ya kuipita dhiki.

Jambo hili lilimshangaza Roma na alijiambia familia hii sio ya kawaida kabisa na kuna mengi ambayo yamejificha.

Wakati huo ndani ya eneo hilo kulikuwa ni kama kuna tafrija kwani kulikuwa na watu wengi ambao walikuwa wameketi kwenye meza ambayo ilikuwa na vyakula mbalimbali.

Watu hao wengi wao walikuwa ni familia ya mzee Sharif lakini pia kulikuwepo na baadhi ya watu ambao hawakuwa na uhusiano na familia hio lakini walikuwa na vyeo vya Wakuu wa Chemba kulingana na tamaduni za dini ya kidhehebu lao.

Vilikuwa ni vyeo ambavyo hupatiwa viongozi ambao husalisha waumini katika matawi ya imani yao.

Ijulikane kwamba Mzee Sharif alikuwa na dini yake na kusalia miungu yake kabisa na alikuwa pia na wafuasi wake na matawi ambayo wafuasi husalia huongozwa na Wakuu wa Chemba na hao mara nyngi ni binadamu wa kawaida.

Watu wengine waliokuwepo ndani ya enoe hilo ni mwanamke na mwanaume ambao wote walikuwa ni jamii ya kiarabu kabisa akiwemo lakini majini wakiongozwa na Imrah.

“Nina hatia kwa mualiko wetu kwenu Mkuu Nayo na Wami awamu hii, Mimi Jini Imrah ninawasalimu kwa kunywa kikombe hichi kama malipo ya usumbufu”Aliongea na kumfanya yule mzee alieitwa Nayo kutoa kicheko.

“Mkuu Imrah huna haja ya kufanya hivyo , sisi kama majini kutoka familia mbalimbali wote tunaunganishwa na jina moja la ukoo ambalo ni Sharif, tumekuwa watiifu kwa ukoo na ndio maana leo hii tumweza kupata uwezo huu tuliokuwa nao mpaka kualikwa , imekuwa heshima kwangu mimi na mke wangu Wami kutoa mchango wa kwenda kumuua mwizi ambaye ameiba hazina yetu”

“Upo sahihi , Mkuu Imrah umezidisha ukarimu kwetu mimi ba mume wangu…”Aliongea mwanamke mrembo sana aliekuwa amekaa karibu na Nayo huyu mwanamke ndio alieitwa Wami, alikuwa mrembo haswa mweupe mwarabu ambae kimakaridio ana umri wa miaka kama arobaini hivi.

Ijapokuwa walikuwa na uwezo mkubwa wa kijini lakini mbele ya Imrah bado walikuwa chini kicheo kwani familia hio haikutoa cheo kulingana na uwezo.

Ili kumdhibiti Roma kisawasawa hao ndio waliotoka huko walikotoka na kufika hapo na familia nzima akiwemo Mzee Sharif mwenyewe alijua kabisa Roma hachomoki.

“Maimuna kwanini Roma mpaka sasa hivi hajafika , si ulisema umewasiliana nae na akasema yupo njiani?”Aliuliza Mzee Sharif.

Maimuna alimdanganya Roma kwamba babu yake na familia nyingine wangekuwa na kikao cha siri sana ndani ya hoteli yao iliopo Manyara na Roma anapaswa kutumia nafasi hio kupiga bomu wanafamilia hao na kama serikali ingeuliza kuhusu tukio hilo Maimuna yeye angetangaza ni maadui wa kifamilia.

“Babu labda …..”

“Boom!!!!”

Maimuna kabla hata hajamaliza sentensi katika eneo la katikati ya hoteli hio kulikuwa kumejengwa sanamu ya Kifaru ambayo imezingirwa na maji na yote ililipuliwa na kuharibika na kufanya watu wote kupiga yowe.

Dakika ileile kila mmoja akijiuliza nini kimetokea hatimae Roma aliweza kuonekana akiwa amesimama juu ya paa la nyumba ambayo ilikuwa katika hatua za ki ujenzi.

“Romaa…!!!

Mzee Sharif ndio wa kwanza kumtambua Roma na alipiga yowe kwa nguvu huku sura yake ikiwa nyekundu kwa hasira.

Imrah , Nayo , na Wami wote walijikuta wakiingiwa na mshangao kwani kwa haraka haraka waliweza kugundua alichotumia Roma kulipua ni nguvu za kijini, sasa walijiuliza kwanini hawaoni uwezo wake wa kijini kiasi cha kushindwa hata kuhisia kama amefika.

Kutokana na taarifa walizokuwa nazo ni kwamba Roma alikuwa na mwili wenye nguvu tu ya kuhimili mapigo ya kijini na hakuwa na uwezo mwingine .

“Inaonekana mna hamu kubwa ya kuniona nikiwa maiti , yaani mmewahi wenyewe na kujikusanya sehemu moja mkinisubiria”Aliongea Roma.

“Wewe mtoto acha kuonyesha kiburi mbele ya Mkuu Wami na Nayo , leo walinzi wetu wa familia watakukamata , huwezi kutumia mikombora yako tena hapa , jisalimishe mapema na rudisha hazina yetu”Aliongea Imrah kwa kujigamba.

Roma aliishia kutoa tabasamu la kejeli na kisha palepale alitumia nguvu za kijini na kutoa lile jiwe lao la hazina kwenye hifadhi pete yake.

“Yaani ndio mmenikumbusha hapa , mnaichukuliaje hii kokoto kuwa hazina, mtu yoyote ambaye ataniambia maana yake basi nitamuacha aendelee kuishi leo hii”

Roma tokea ajifunze mbinu za kijini hilo jiwe ndio kitu pekee ambacho hakuwa akikielewa kabisa tokea akipate , hata baada ya kurudiwa na nguvu zake za kijini alishindwa kuweza kutambua kabisa kitu hicho kwani hakikuwa na nguvu za kijini , lilikuwa jiwe kama jiwe lakini familia hio ilikuwa ikilichukulia kama hazina.

Lakini sasa kuona familia hio ilikuwa ikifanya juhudi kutaka kuirudisha ilionekana ni kitu chenye thamani lakini ilimsumbua akili kutoelewa uthamni wake unatokana na nini.

“Acha kujigamba , maongezi yako na Maimuna tumeyarekodi na ulikiri kwa mdomo wako wazi umeiba hazina yetu , ni ushahidi tosha kwetu wa kukuchukulia hatua , kama leo hii usiporudisha hazina yetu hatutojali wewe ni mtoto wa nani ndani ya taifa hili tutakupoteza”

“Nina mashaka hata wewe na ujini wako hujui hiki kitu ni nini , lakini kama hamtaki kuongea basi nadhani nitawafanyia majaribio kwa mbinu yangu mpya ya kimaajabu niliogundua ndani ya siku hizi mbili”

“Mkuu Imrah acha kujibishana nae mpandieni hewani mumkamate na chukueni hazina yetu na kisha tafuta vidonge vyake vyote na mbinu yake ya mafunzo na muda ukiwadia ukoo wetu utakumbukwa kwa mafanikio yetu”

Jini Imrah alitingisha kichwa palepale , alijua kabisa wapo na majini wenye nguvu ndani hapo na alipaswa kuhusika pia katika kushambulia ili aonekane na yeye alikuwa shujaa.

“Wewe mvulana , ni kosa baya sana umefanya kuchokoza ukoo wetu”

Mwanamke mrembo Wami aliongea na alikuwa ndio wa kwanza kumsogelea Roma huku akiwa ameshikilia upanga ukatao kuwili ambao ulikuwa ukiwaka waka.

“Chukua pigo langu la mwezi mwandamo mwanaharamu wee”

Aliongea kwa nguvu na palepale nguvu ya kijini ilimtawala na kufumba na kufumbua alifutika alipokuwa amesimama na ile anakuja kuonekana alikuwa mbele ya Roma huku ile siraha yake ikitoa mng’ao ikiwa imejikunja kama vile ni mwezi unaoandama huku ikiwa imetawaliwa na nguvu kubwa ya kijini ambayo iliambatana na ubaridi mkali sana.

Roma mbinu hio aliona kabisa ni ya kitoto kwake , na aliinua mkono wake kidogo tu na kuachilia nguvu ya kijini na palepale ile nguvu iliomtoka jini Wami ilioputana na ya Roma ilisambararishwa.

Nguvu zile mara baada ya kukutana ni kama vile zilikataana kwani zilisambaa na kwenda kupiga kwenye nyumba iliokuwa imeezekwa kama kichuguu na palepale paa lake likaharibika huku mawe mengi yakiruka na kwenda kuwashambulia walinzi waliokuwa wakilinda ndani ya eneo hilo na kuwajeruhi.

Jini Wami alipatwa na mshangao wa tukio lile na palepale pasipo kumsogelea karibu Roma aliendelea kufyeka ule upanga hewani huku ukitoa nguvu ya kijini ambayo ilibadilika na kuwa mithili ya mng;ao wa mwezi mwandamo na kumlenga Roma.

Hio ndio mbinu ya mwezi mchomoko aliokuwa akimaanisha , yaani nguvu yake ilikuwa kwenye ule upanga ukatao kuwili na kila anapofyeka hewani ulituma shambulizi la kimwezi mchomoko na kumshambulia Roma.

Lakini sasa Roma ni kama alikuwa akifanya makusudi kwani aliacha mapigo yale kumfikia na kumshambulia lakini hayakuonyesha athari yoyote ile.

Wami alishangazwa na jambo lile kwani shambulizi lake ni kama lilikuwa likisambaratika kila linapomfikia Roma.

“Ni mwili wa aina gani wa kishetani uliokuwa nao , yaani huumii hata kidogo?”Aliongea Nayo kwa nguvu mara baada ya kuona hakuna shambulizi ambalo linamuathiri Roma .

Upande wa Jini Imrah alikuwa na wasiwasi Roma anatoroka hivyo na yeye alifuatia kushambulia.

“Nguvu ya Jani la Mtendee..!!!!”

Aliongea kwa nguvu kilugha na palepale mbele ya kiganja cha mkono wake ulitoa mwanga kama vile ni jani la mtende na nguvu za kijini zilianza kuchomoza huku zikiwa katika staili kama vile ni majani na kuanza kupelekea upepo mkali.

“Duara la Moto!!!”

Aliongea Jini Nayo na yeye na palepale kulitokea maduara ya moto kama mishale kutoka juu na kumvaa Roma kutoka kichwani na kuanza kumzingira.

Roma hakujali sana kuhusu mashambulizi hayo na palepale aliinua kiganja chake cha mikono na kuachilia nguvu ya kijini ambayo ilivaana na zile boriti za nguvu za kijini zilizokuwa zimemzingira.

Wakati Imrah akimtengenezea mtafaruku Roma upande wa jini Nayo na Wami walikuwa wakimshanbulia kwa kasi

Watu waliokuwa chini walikuwa wakiangalia mapigano hayo bila ya kuelewa kinachoendelea lakini walikuwa wakiwaangalia majini wao wakipambana tu na walikuwa na matumaini ya kushinda.

“Mimi kama mkuu wa ukoo katika ulimwengu na kiongozi wa imani ya utajiri, Roma Ramoni leo ni siku yake ya hukumu”Aliongea Mzee Sharif kwa chuki kubwa na palepale wafuasi wa imani ya utajiri pamoja na ndugu walipiga makofi ya shangwe.

Upande wa Maimuna macho yake yalikuwa yamechanua na alikuwa na umakni mkubwa katika kufatilia pambano na hakuonyesha furaha wala huzuni.

Lakini sasa dakika hio hio Roma ambaye alikuwa akishambuliwa na mapigo ya nguvu za kijini hakuwa akihisi chochote ni kama vile kuna vitu vinamtekenya tu kutokana na uwezo wake wa kijini kuwa mkubwa zaidi , sasa ile nguvu ya mbingu na ardhi iliokuwa ikimzingira iliongezeka kadri ambavyo alikuwa akishambuliwa

Hoteli hio ilikuwa imejengwa kitamaduni zaidi hivyo hata kuezekwa kwake ni kwa nyasi na mapaa yake yote yalikuwa yameharibika huku baadhi ya nyumba zikiwa zishaanza kubomoka kutokana na upepo mwingi na nguvu ya kijini iliokuwa ikisambaa.

Dakika ileile boriti nyingine ya nguvu ya kijjini ambayo ilimsogelea kama Mshale ilimkaribia na Roma alijiambia kuendelea kuwasoma wanavyopigana ni kupoteza muda hivyo ni zamu yake kushambulia.

Palepale alimsogelea Nayo kwa spidi na kumshika mkono na akaruhusu nguvu za kijini kumtoka na kuanza kumvaa na palepale nguvu ile ya kijini ilianza kubadilika na kuwa maji.

Jini Nayo macho yake yalisinyaa na kabla hajajua cha kufanaya alikuwa ashachelewa kwani alijua tayari kuna kitu ambacho hakipo sawa kuhusu Roma

“Asilimia tisini ya mshambulizi yako hayakunilenga , hivyo ni kama vile umepoteza nguvu zako tu , unao uwezo mkubwa lakini ukweli ni kwamba mashambulizi yako ni ya kijinga jinga”Aliongea Roma na palepale kulitokea kitu kama povu la sabuni na kumfunika Jini Nayo .

“Hii.. ni..”

Wami na Imrah walijikuta wakipagawa kwani Nayo alikuwa amekamatika kirahisi mno na Jini Nayo aliishia kuita jina la mke wake tu kama ishara ya kumpa tahadhari na palepale alipoteza maisha huku roho yake ikioshwa na maji ya kiroho.

Maji ya kiroho ilikuwa ni kama vile ni tindikiali na inapogusana na jini ambalo lina uwezo mkubwa wa kijini linapotumia kwa jini mwenye uwezo mdogo ni kama vile ni mionzi ya nyuklia na maji yake hayaumizi mwili bali yanaumiza roho au nafsi.

Jini Nayo alikufa palepale na kuwa kama maiti ya kawaida tu huku macho yake yaliobadilika rangi yakichomoza nje.

“Hili linawezekana vipi ,,, au tuseme upo katika hatua ya kudhibiti maji ya kiroho ,,, subiri hata kama iwe hivyo hatujawahi kusikia binadamu yoyote ambaye ana uwezo wa kudhibiti maji ya kiroho”Aliongea Wami , hakuwa katika hali ya kumuomboleza mume wake lakini alikuwa katika hofu ya uwezo wa Roma.

Mpaka hatua hio alishajua kuendelea kupambana na Roma ni kujitafutia kifo tu.

Roma hakua na haja haya ya kumuelimisha na palepale kama kivuri alimsogelea na moto uliokuwa kama radi , rangi ya Zambarau ulitokeza katika mikono yake.

Siku ya jana yake wakati Roma akifanya tahajudi ili kugundua ni nguvu ipi aliweza kuipata baada ya mapigo ya radi tisini na tisa na alikuja kugundua kwamba radi ya Zambarau huundwa na mchanganyiko wa elementi za maji pamoja na msuguano wa Plasma hivyo alijaribu kudhibiti Free electrons ambazo zipo hewani na kisha kuzisuguanisha na elementi za maji.

Jini Wami kabla hata hajajiuliza imekuwaje Roma kutoa shoti za rangi ya zambarau kama radi lakini alikuwa amechelewa kwani Roma alimsogelea kwa kasi na kumchapa ngumi ya tumbo ambayo iliungana na zile shoti na nguvu ya kijini.

Mlio uliosikika ni kama vile puto linapopasuka na mkono wa Roma ulipita huku cheche za moto zikijitokeza na kuanza kuyeyusha mwili wa jini Wami kwa kasi sana.













SEHEMU YA 689.

Roma aliridhishwa na nguvu mpya ambayo amejipatia , ijapokuwa mshindani wake alikuwa dhaifu kumdhibiti kwa pigo moja tu lakini hata hivyo alichukulia kama mafanikio kwani ni kitu ambacho kimefanikiwa.

Roma ni kama alivyofikiria siku ya jana , majini wote ambao hawajapita dhiki lakini wana uwezo wa kudhibiti elementi za maji hawawezi kuhimili shambulizi moja la siraha yake mpya aliogundua.

Roma hakuona haja ya kutumia chungu kuwamaliza kutokana na wote walikuwa dhaifu sana hivo aliona kitu pekee ni kuwamaliza na nguvu ya kijini tu ya radi ya zambarau.

Familia yote ya Sharif ilikuwa katika bumbuwazi , dakika chache zilizopita walikuwa na uhakika wa kushinda lakini nini kimetokea , yaani wamepoteza namna hio.

Mzee Sharif na mtoto wake na wengine wote walikuwa wakipatwa na jasho ambalo sio la kawaida , upande mwingine Maimuna alikuwa kwenye mshituko na alionyesha hali ambayo haikueleweka katika macho yake.

Sekunde chache tu Wami alikuwa ameharibiwa mwili wake huku Jini Nayo mwili wake ukishuka kutoka juu huku ukiwa umetengeneza michirizi kama mizizi ya mti.

Aliebakia alikuwa ni jini Imrah pekee na alikuwa akitetemeka kama vile tayari alishajua huo ndio mwisho wake.

“Imetokea tokea je hivi jamani…”Aliongea kwa huzuni na muda uleule akijiandaa kukimbia lakini Roma ni kama alitegemea nini angefanya kwani palepale nguvu zake za kijini ziligeuka kama kamba ndefu na kumzingira jini Imrah

Alikuwa kwenye levo ya nafsi tu hivyo spidi yake ilikuwa ndogo ndio maana Roma alimuwahi na asingeweza kujitoa kwenye kamba alizofungwa nazo.

“Hii ni kama heshima kwako kufa na moto wa bluu”Aliongea Roma kwa sauti kavu na dakika ileile jini Imrah aliyeyuka kama karatasi inayoungua.

Roma alifanya mashambulizi matatu tu na yote yalimaliza majini yote matatu kwa wakati mmoja na kama sio uharibifu uliotokea chini yake hakuna mtu ambaye angejua kama kuna mapigano ya majini na binadamu yalitokea hapo.

Walinzi na wafuasi wa familia ya Mzee Sharif walijikuta wakiwa katika hatari , mbele ya nguvu kamili walikuwa ni kama kuku tu.

“Roma fikiria mara mbilimbili , huu sio mwisho wa uwezo wetu , kama utatudhuru basi subiria ghadhabu ya wakuu wetu , ninaapia kufanya mazungumzo ya amani na wewe na kuacha hili lipite”Aliongea Mzee Sharif na kumfanya Roma kutoa kicheko.

“Naona sasa unataka tufanye maongezi, nilijua ungepiga magoti kuomba au kujiua mwenyewe kuniepushia dhambi “

“Unathubutu vipi kunidhalilisha , mimi siwezi kupiga magoti mbele ya wafuasi wangu”Aliongea kwa hasira lakini dakika ileile mara baada ya Roma kukanyaga ardhi Maimuna alikimbia mbele na kupiga magoti mbele ya Roma.

“Master , Hongera kwa ushindi wako na kisasi”Aliongea Maimuna na kufanya watu wote kumwangalia kwa mshangao.

“Maimuna!!”

“Mai..!!”

“Unathubutu vipi kutusaliti?”

Sauti mbalimbali zilimwita Maimuna kwa kufoka na mshangao lakini Maimuna hakujali laana wala matusi yao, alimwangalia Roma kwa macho yaliojawa na heshima na matamanio.

“Unafuraha kweli ya mimi kushinda au ndio unafiki ?”Aliuliza Roma

“Bila shaka Master , tafadhari nisamehe mimi kwa kutokuwa na uwezo wa kupigana pembeni yako lakini nilikuwa na wasiwasi juu yako muda wote , ninayo furaha kuona hujadhulika”

“Masikini usie na aibu wewe , wewe ni laana ya ukoo wetu , msaliti mkubwa wewe”Aliongea Mzee Sharif kwa hasira.

“Haha… hivi ulifikiria nitawasaidia ili tu kumsaiti Master wangu wakati mlichukulia maisha yangu hayana thamani , nilijiapiza lazima niharibu hii familia hivyo acha kunilaumu”Aliongea Maimuna akimwangalia babu yake kwa kejeli.

“Nitakuua Maimuna”Aliongea baba yake kwa hasira.

Maimuna alikuwa kwenye levo ya mzunguko kamili hivyo hakumhofia baba yake tena ambaye alikuwa kwenye levo ya nusu mzunguko.

“Master , Mzee Sharif amelinda hili eneo kwa umakini mkubwa na kunipelekea kusindwa kutega mabomu hivyo naomba umuue kunisaidia kulipa kisasi”Aliongea Maimuna na kumfanya Roma kutoa tabasamu la kejeli.

“Hawa watu kwangu ni kama kunguni tu hivi na kuua mmoja mmoja ni kupoteza muda hivyo nitawaua kwa shambulizi moja “Aliongea Roma na palepale nguvu ya kijini ilitoka kama moto uliokuwa katika umbo la vinyoka nyoka na kuanza kuwashambulia kwa kasi.

Moto wa njano wa kijini licha ya kwamba haukua mkali lakini ulikuwa na athari kubwa kwa mtu ambaye hana nguvu za kijini. Au ambao wapo katika levo ya mzunguko kamili.

Vilikuwa ni vilio vya kusaga meno ambavyo vilisikika ndani ya hilo eneo ni kama vile tayari wapo jehanamu na wanapokea adhabu yao ya kumuasi Mungu na kusalia miungu.

Roma alijikuta akihema kwa nguvu na kujifikiria ameua watu zaidi ya mia moja usiku huo lakini licha ya hivyo hakujihisi kabisa hatia.

Dakika chache tu ilibakia majivu na hakuna kilichoonekana hapo ndani hata mfupa haukubakia na mtu pekee ambaye alibakia ni Maimuna peke yake.

Wakati Roma anaruhusu moto Maimuna alikuwa amezingirwa na nguvu za kijini hivyo ule moto haukumgusa ,Roma alifanya hivyo kwasababu hakuwa na muda wa kudhibiti vinyoka vya moto kwani vilishambulia kila kiumbe chenye nguvu ya kiroho ndani yake.

Roma mara baada ya kuona kila kitu kimeisha palepale alimchukua Maimuna na kupotea nae na kufumba na kufumbua alikuwa juu ya kilele cha Maweni Mlima kilimanajro huku akiwa amemshikilia Maimuna.

“Kwahio bado utaendelea kuongea ujinga?”Aliongea Roma mara baada a kumtua chini Maimuna.

“Master bado sijakuelewa”

“Unanionga mjinga?, Majini wawili walikuwepo na hukuniambia , ulitaka kuona nani atashinda si ndio? , naamini ulipanga kuona upande wowote kushinda , kama ningeshindwa ungepata sifa na kama wangeshindwa ungerithi kila kitu, haikujalisha matokeo uliamini kila upande utakaoshinda ungefaidika”

“Hapana Master , Sikuweza kukujulisha ndani ya muda kwasababu walikuwa wakiniangalia sana kwa ukaribu”

“Oh ,,, haya niambie ni kwa namna gani walijua kama nina vidonge , si nilikuambia iwe ni siri , unataka kuniambia walifahamu wakati ulipokuwa ukivuna nishati za mbingu au imetokea kwa bahanti mbaya?”

“Ndio , ndio , sikuwa makini Master walinikamata wakati nameza baaada ya kushangazwa na kupanda levo kwa haraka”

“Kwa hio unamaanisha haya ni makisio yangu tu , kwasababu sina ushahidi siwezi kusema umennisaliti si ndio?”

“Ndio Master , tokea siku ambayo nilitoka kwenye ile boti sikuwahi kuwaza nitakusaliti m mimi nilikuwa mtu wako mwaminifu”

“Hujui mambo mawili kuhusu mimi wewe ,, kwanza ninaweza kuua mtu yoyote hata kama sina ushihidi ili mradi namshuku tu pili siamini kuhusu uaminifu unaongea hapa ambao umeuharibu wewe mwenyewe tena umeenda mbali hata kuweka kisasi na familia yako”Aliongea Roma huku akimwangalia Maimuna kwa macho makali.

“Master tafadhari naomba usiniue nitakupa kila kitu”Aliongea Maimuna huku jasho likimtoka na dakika hio hio alichana chana gauni lake ambalo alikuwa amevaa na kubakia uchi.

“Master naomba unifanye niwe wako , nipo safi kabisa , Master nina uhakika utaweza kuhisia ukunjufu wangu wa moyo”

Ili tu kupata nafasi ya kusihi Maimuna alitupilia mbali utu wake na alipiga magoti chini akiwa hana nguo huku akimuonyesha Roma sehemu zake za uzazi zilivyo na hakuishia hapo tu alimsogelea na Roma karibu na kuanza kujisuguanisha nae.

Maimuna alikuwa mtundu mno , ijapokuwa ni kweli Roma aliona alikuwa hajaguswa lakini alijua kutokana na namna anavyo jua kujiigizia mbele yake basi hata kunako sita kwa sita atakuwa na utundu wa hali ya juu, kutokana na mwanga wa mwezi aliweza kuona kila kitu na jamaa mdogo alishindwa kuvumilia na kuanza kufurukuta.

Lakini Roma hata hvyo hakutaka kumgusa , isitoshe Maimuna licha ya uarabu wake hakuwa akimfikia Amina kwa uzuri, hapo tu hujalinganisha na warembo wengine kama Najma,Nasra na Rose.

Uhuni wa Maimuna ulisukumwa na tamaa zake na kama angalau angelinda utu wake hata katika hatua kama hio basi Roma kidogo angerudisha moyo nyuma lakini maigizo yake yalimfanya kumpuuza zaidi na zaidi.

“Hata kama unionyeshe kila kitu sikutamani unadhani nitakutamani mwanamke kama wewe ?”Aliongea Roma na maneno yale yalimchoma mno Maimuna na alijikuta akitoa machozi.

Ijapokuwa katika eneo hilo kulikuwa na upepo na baridi kali lakini kutokana na uwezo wake wa kijini alikuwa sawa hata katika kupumua lakini mara baada ya kuambiwa maneno hayo na Roma alijihisi kukosa pumzi ghafla.

“Unalia nini ,naona nimegusa penyewe , ndio unaonyesha kukasirika sasa hivi?”Aliongea Roma kwa kejeli na Maimuna palepale alipotezea uchungu wake wa moyo na kujigeuza katika hali ya kutia huruma.

“Siwezi kukukasirikia , tafadhari Master naomba uniamini , sijaguswa na mwanaume yoyote yule , nilichofanya ni kutaka tu kuwa na wewe”

“Huna maana tena , lakini nadhani ni vizuri maana sitopoteza tena juhudi zangu juu yako’

Maimuna hakuelewa Roma anachomaanisha lakini dakika ileile alikumbana na nguvu ya kijini ambayo ilimfanya kupoteza fahamu palepale Roma alimbeba na kupotea nae.

*******

Upande wa anga la jiji la Dar es salaam kulikuwa tayari giza lishaingia na kufanya taa nyingi kuwaka na kupelekea jiji hilo kupendeza.

Upande wa Ununio sauti pekee ambazo zilikuwa zikisikika ni za mawimbi ya bahari pamoja na baadhi ya sauti za magari na pikipiki ambazo zilipita mara moja moja kutokana na utulivu wa mtaa huo.

Dakika chache mbele gari aina ya Audi A8 toleo la mwisho rangi nyeusi ilisimama mbele ya geti la nyumba ya Edna.

Dakika hio hio mlango wa abiria uliweza kufunguliwa na mwanaume alievalia suti na kumruhusu mwanaume alievalia jacket na kofia ya hat pamoja na miwani kushuka.

Alikuwa ni Raisi Jeremy na kwa staili ya uvaaji wake ilionekana ni dhahiri kabisa hakutaka mtu yoyote kumfahamu.

Baada ya kusogelea geti palepale aliminya kengele maalumu nje ya geti hilo na ndani ya dakika chache tu sauti ilisikika kutoka ndani na ilikuwa ni ya Bi wema.

Upande wa ndani Bi Wema alikuwa bize kuangalia tamthilia na mara baada ya kusikia kengele hio aliangalia kwenye kifaa maalumu cha kuweza kutambua nani anabonyeza kengele na palepale mara baada ya kuangalia kwa umakini alishtuka na kisha akakimbilia nje.

“Mheshimiwa!!?”

Aliongea Bi Wema kwa wasiwasi mara baada ya kufungua geti , alikuwa akimjua Raisi wa Rwanda kwani sio mara ya kwanza kumuona na alikuwa akijua ni baba yake Edna na alikosa ile hali ya kujiamini kwani alikuwa mtu mzito.

“Hello Bi Wema … naomba radhi kwa kuwavamia usiku huu lakini sikuwa na muda mchana , Edna yupo ndani?”Aliuliza Raisi Jeremy kwa tabasamu.

Upande wa Bi Wema alijikuta akijisikia vizuri kwa Raisi Jeremy kumuongelesha kwa upole .

“Edna ndio… “

“Bi Wema huyo mgeni ni nani?”Sauti ya Edna kutoka ndani iliweza kusikika.









































SEHEMU YA 690.

Bi Wema alikuwa ametoka nje kabisa ya geti , Edna mara baada ya kusikia kengele alitoka kujua ni mgeni gani kafika muda huo lakini mara baada ya kuangalia hakumuona Bi Wema na alijikuta akitembea kuelekea getini.

Raisi Jeremy mara baada ya kusikia sauti ya Edna alijikuta mapigo yake ya moyo yakienda kasi na alishindwa kujizuia na kupiga jicho ndani na palepale aliweza kumuona Edna ambaye alikuwa amevalia gauni na visendo manyoya akitembea kuja getini.

Dakika ambayo Edna alimuona Raisi Jeremy alisimama palepale na kushindwa kusogea mbele kama vile amegandishwa.

“Edna nimefurahi nimekukuta hujalala naamini hutojali kwa ujio wangu huu wa ghafla”Aliongea Raisi Jeremy huku akitoa tabasamu.

“Una sababu gani ya kuja usiku huu nyumbani kwetu mheshimiwa?”Aliongea Edna.

“Nilitaka kuja mapema lakini nilikuwa bize sana na vikao na vilisha muda umeenda lakini nilihitaji kukuona kabla sijarudi Rwanda kesho”

“Sawa umekwisha kuniona tayari mheshimiwa naomba uondoke”Aliongea Edna kikauzu hakujali kama Jeremy alikuwa baba yake au raisi , nadhani alimzingatia kama baba yake mzazi kuliko raisi kutokana na alivyokuwa na hasira.

“Edna najua pengine hutaki kuniona lakini ninataka tuongee tafadhari naomba leo unipe kampani ya kupata chakula cha usiku pamoja , sijapata dinner bado na nina njaa”Aliongea na Jeremy mara baada ya kuona hapewi jibu aliongezea.

“Please , my daughter”

Edna muda huo alishageuka na aliishia kung’ata lips zake na kauli ya kuitwa mwanangu ilimlainisha.

Kwasababu mheshimiwa ameomba sana aliona itakuwa ukatili kumkatalia, baada ya kuvuta pumzi nyingi aligeuka.

“Bi Wema nitachelewa kurudi , unaweza kwenda kulala mapema kama umechoka”Aliongea Edna na kumfanya Raisi Jeremy kutoa tabasamu.

Edna hakuwa na haja ya kubadilisha isitoshe alikuwa amevalia mavazi ya kawaida na hata visendo vyake havikuwa na shida hivyo aliingia kwenye gari la baba yake mzazi na kisha liliondoshwa.

“Edna unaijua hoteli ya White Sand , ile ni hoteli yetu, mara nyingi napenda kwenda kulala pale ninapokuja Dar kwa safari za siri”Aliongea Raisi Jeremy mara baada ya kumwangalia Edna akiwa amekodolea nje kupitia kioo akikwepesha macho na Jeremy.

“Tafadhari mheshimiwa usinijumuishe, mimi ni Edna Adebayo na itabakiwa kuwa hivyo”

“Edna najua ni ngumu kwa wewe kunikubali mimi kama baba yako kutokana na kukukosea mara nyingi , vilevile najua ni ngumu kwa wewe kurudi kwenye ukoo wetu lakini unapaswa kujua kwasasa sijali sana watu wananionaje , nmekuja kugundua uhusiano ambao hufungamanishwa na damu hauwezi kuvunjika , watu wengi ndani ya nchi hii washajua tayari wewe ni binti yangu na hata ndani ya Rwanda na haijalishi wanasema nini lakini ninajivunia kuwa baba yako , najua nimekuumzia mara nyingi na matendo yangu pengine na maneno yangu pia lakini najutia na kuomba msamaha kiasi cha kunifanya usiku kukosa usingizi na kupandwa na ndoto za mara kwa mara , kila siku kunapokucha moyo wangu huuma sana kujua kwamba sipo huru kuwasiliana na wewe , najihisi sina thamani , mara ya mwisho wakati familia ya mumeo ilipokuwa kwenye matatizo nilitaka kuja kukuchukua na kukurudisha Rwanda lakini nilikuwa na wasiwasi kwamba ungekataa na nikaishia kuweka matumaini kwa Roma kwamba atalimaliza tatizo lakini nilikuwa na asiwasi mno kiasi kwamba nilishindwa kupumua vizuri..”

Kwa jinsi ambavyo alikuwa akiongea ni kama vile alikuwa akijiongelesha yeye mwenewe.

Edna hakutoa jibu na macho yake yalikuwa yamekodolea mataa ya jiji la Dar.

Raisi Jeremy alieleza ngonjera zake kwa zaidi ya dakika ishirini zote na ndani ya dakika hizo gari iliweza kufika ndani ya hoteli ya White Sand iliokuwa ikipatikana Africana.

Hoteli hio siku hio ilikuwa ikipokea wageni maalumu wale muhimu na taratibu ilikuwa hivyo kila wakati ambapo Raisi Jeremy anapofika, haikupokea wageni wa kawaida ambao walikuwa wakifika kwa ajili ya chakula cha usiku.

Baada ya kupokewa moja kwa moja alienda mpaka kwenye ukumbi binafsi na palepal e Raisi Jeremy aliagiza wahudumu kuleta chakula ambacho alikuwa ameagiza kiandaliwe kwa ajili ya binti yake.

Kama kawaida hakusahau vikijikeki ambavyo Edna alikuwa akipendelea na awamu hio vikeki hivyo vilikuwa vitamu mno kutokana na kwamba ulifanyika uwekezaji mkubwa wa kuvitengeneza, baba yake Recho ndio ambaye alikuwa akiendesha biashara hio mara baada ya Edna kumpatia mkopo Recho wa kufungua biashara.

“Unaonaje , leo tunaanza na hivi vikeki pamoja na baada ya hapo tutahamia kwenye vyakula vyote unavyopenda , utashangaa na kujiuliza kwanini najua ni kipi unapenda na kipi hupendi?”Aliongea huku akicheka lakini Edna alikuwa kimya tu.

“Edna nilikuwa nakuangalia tokea ukiwa mdogo, nakumbuka ni kipi unapenda na kipi hupendi”Aliongea bila ya kujali muonekano wa Edna wa kikauzu.

Dakika hio aliagiza aletewe mvinyo ambao alikuwa ameandaa mwenyewe na huku chakula kikiandaliwa kwa wingi na kufanya eneo hilo kujaa harufu nzuri ya kutia njaa.

Moja wapo ya vyakula ambavyo viliandaliwa vya kuongeza radha vya thamani kubwa ni Italian white truffles, French Foie gras, Middle East Cavier na mengineyo.

Kati ya hivyo ghali zaidi ni White Truffle na ilikuwa ngumu sana kupata hata kama unahela kwasababu kikawaida huharibika ndani ya siku kumi tu baada ya kuvunwa na pia kwa mwaka huvunwa mara moja tu, kutokana na uadimu wake basi thamani yake ilikuwa kubwa mno.

Sasa Edna alikuwa akipenda sana White Truffle kuliko alivyokuwa akipenda hata hivyo vjijiketi na ndio chakula ghali sana alichokuwa akinunua mara nyingi akisafiri nje ya nchi .

Lakini alijikuta akishangaa Raisi Jeremy aliwezaje kujua hayo yote.

“Nimeagiza watu wangu kusafirisha kwa kutumia ndege , hebu kata uonje kidogo”Aliongea kwa muonekano wa kubembeleza.

Na Edna alishindwa kujizuia na kuona shambulizi hilo limemwingia na hakugoma na kuchukua kisu na uma na kukata kidogo.

Edna mate yalimjaa na alikata na kupeleka mdomoni wakati huo raisi Jeremy akiwa bize kumwangalia na Edna ile anameza alijikuta akiona aibu mara baada ya kugundua macho ya Jeremy na aliishia kutoa tabasamu.

“Hatimae umetabasamu haha… nadhani sijafeli kama baba yako mzazi , ninao uwezo wa kumfanya binti yangu kutabasamu , ni hatua kubwa”Aliongea kwa kujigamba na kauli hio iilimfanya Edna kulainika.

Edna wakati huo na yeye alikuwa akifikiria na kujiuliza yaani kutabasamu kwake tu kumemfanya kuwa na furaha hivyo , pengine anapitia magumu ndio maana , Edna alijaribu kuvaa viatu vya Jeremy na kuona ana maisha ya upweke sana na pengine maisha yake yote alikuwa akiumia kuwa mbali na yeye.

Mawazo hayo yalimfanya kumuonea huruma baba yake na alianza kula kile chakula kwa kutokujilazimisha.

“Edna kula utosheke , mimi napendelea kula kabla ya kuungwa”Aliongea na kisha alikata pande na kumuwekewa Edna kwenye sahani.

“Inatosha siwezi kula sana ,,, na wewe unapaswa kula , si umesema hujakula bado”Aliongea Edna na kumfanya Raisi Jeremy kujisikia vizuri na alitoa kicheko cha furaha.

“Okey kwasababu umesema nile na mimi nakula”Aliongea huku akila kwa amani.

“Edna kama unapenda sana White Truffle nitakuwa nakuagizia”

“Hapana , kula mara moja moja kama hivi inatosha”Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy kukumbuka kitu.

“Ndio ndio , tena nilikuwa nishasahau kwamba binti yangu ni mwanamke tajiri Afrika nzima , kwako kutumia kiasi kidogo cha pesa kuagiza halitokuwa jambo gumu, nilisahau kabisa pengine ni kwasababu tu niliwaza kukupatia kitu kizuri unachopenda”

“Najua”

Muda huo hali ilikuwa ya kuchangamka na Raisi Jeremy aliongea kama vile kiredio chenye betri mpya.

“Edna wakati ulipokuwa shuleni nakumbuka somo la Kiswahili lilikuwa likikupiga chenga sana , wakati wa mtihani wako wa sekondari nilihofia kabisa ndio somo ambalo litakuangisha kimaksi hivyo niliongea na mtu na akakubadilishia maksi , kama nisingefanya vile wastani wako ungeshuuka kwa maksi ishirini… Athumani yule bwana badala ya kufanya mambo ya kuelekewa yeye kazi yake ni kutuma watu kukulinda tu, mimi ndio nilikuwa hatua mbele zaidi kufanya maamuzi, lakini hata hivyo ulikuwa ni kipanga kwenye masomo mengine ndio hivyo tamaa ziliniingia na kutaka kuona ukipata masomo yote A…..”

Jeremy aliongea kila matukio ambayo yalimtokea Edna shulenni , alionekana alikuwa akimfatilia Edna mwanzo mwisho lakini uongeaji wake ni kama ulikuwa ukienda nje ya mipaka na Edna aliweka uma na kisu chini.

“Mheshimiwa , si umesema unataka kuongea na mimi , nishamaliza chakula hivyo nenda moja kwa moja kwenye topiki”Aliongea Edna na kumfanya Jeremy kufunga mdomo huku akishangaa kidogo.

“Edna bado unanichukia kwasababu niliagiza watu kuwashughulikia wewe na Lanlan?”

Aliongea na Edna ambaye ndio mara ya kwanza anasikia Jeremy akikiri alijikuta akikunja ngumi chini ya meza , hakuamini angekiri bila wasiwasi.

“Edna kuna mambo mengi yanaendelea kwenye maisha yangu , kama nitasema nililazimishwa je utaweza kunniamini?, Edna unaweza usijue hili lakini mama yangu mzazi , yaani bibi yako anatokea ulimwengu usio onekana , nafasi yangu ndani ya ukoo wa mama ni ndogo na nilipewa jukumu ili kupandisha hadhi yangu napaswa kuhakikisha kutoa mchango ambao ni kuhakikisha napata mbinu ya mafunzo ya Roma , lakini Roma ni mgumu sana kudili nae ndio maana niliagiza watu lakini sikutaka kwenda mbali hivyo, uendelevu wa uongozi wangu pale Rwanda unategemeana na hizi jamii ambazo hazionekani ni rahisi kuniondoa madarakani kama ningekataaa waziwazi”

“Kwahio unachojaribu kusema ni kwamba madaraka kwako ni muhimu sana , yaani mpaka kupelekea kumteka mtoto na kuanza kumpiga?”

“Edna najua nilikosea na najisikia aibu kukiri hili, lakini Edna hebu fikiria , kama nitakuwa na nguvu kutoka ulimwengu usio onekana lakini pia kuweza kutawala taifa la Rwanda bila hofu itanisaidia kufanya mambo mengi kwa raia , lakini kama mtu atachukua nafasi yangu mipango yote ambayo nimepanga kwa ajili ya Rwanda haitoendelea, kupata mbinu ya Roma ya mafunzo ya kijini ilikuwa njia tu ya kuwafurahisha , najutia lakini ni swala la mara moja tu haliwezi kutokea tena”

“Kwahio umeniambia hayo yote na unataka nikushukuru?”

“Hapana ,, ninacho..”Jamaa alikosa usemi na palepale aliinua glasi ya mvinyo uliojaa na kisha alikunywa wote akaongeza na kidogo na kunywa.

“Mheshimiwa kama ushamaliza mimi naondoka”

Edna hakuwa na mpango wa kutaka kurudishwa, alipanga kupanda hata Taksi au hata kutembea maana tayari alikuwa kwenye levo ya mzunguko kamili.

Lakini muda uleule Jeremy alisimama kilevi na kisha akamsogelea Edna kama vile anataka kupigia magoti

“Mheshiiwa unataka kufanya ni..”Edna alijikuta akishangazwa na matendo yake.

“Edna hapana usiniite mheshimiwa , niite baba , Edna mwanangu niite baba”Aliongea kama vile kalewa.

Edna alikuwa ashasimama na alipiga hatua moja kurudi nyuma na alikuwa na wasiwasi kama kweli Raisi Jeremy alikuwa amelewa.

“Mheshimiwa hebu jitahadhari na matendo yako”

“Edna hivi unadhani nimelewa , hapa sijalewa kabisa nipo fiti”Aliongea huku akianza kulegea legea kama mlevi.

“Edna binti yangu nipo mpweke sana, naumia na kujutia kwa kila kitu, Mama yako ,Kizwe na Desmond wote walikufa mapema kwasababu yangu , mimi ndio mwenye makosa , tamaa zangu ndio zimepelekea vifo vyao , nimefanya mambo mengi ya kijinga….”

Edna aliishia kumwangalia hku akiwa kama haamini masikio yake na macho yake.

Raisi Jeremy aliinamisha kichwa chache chini kama kuna kitu anaangalia na kuanza kukitingisha.

“Edna naogopa kurudi Rwanda , naogopa kukaa ndani ya lile jengo la ikulu peke yangu , niko mwenyewe pale na kila anaenizunguka simwamini , najutia kweli , najua nilikosea lakini adhabu ninayopitia haivumiliki…”Aliongea huku akifikicha macho kama vile analia.

Alitia huruma, kama ni maigizo alikuwa amefaulu kwa kiasi kikubwa kwani alimfanya Edna kutokwa na machozi ya huruma.

Dakika ileile alimsogelea Edna na kumshika mikono yake kwa namna ya kubembeleza.

“Edna nisikilize , naomba usitalakiane na Roma , najua unahasira kwasababu ya Sophia na Lanlan lakini usitalakiane nae , utajutia huko mbeleni”

Dakika ambaye aliongea kauli hio Edna alibadilika na kutaka amwachie mkono wake lakini alikuwa akiogopa atadondoka na kuumia.

“Niachie mheshimiwa ,,,, hayo ni mambo yangu binafsi”

“Mambo yako ni yangu , mimi ni baba yako”

“Edna mmeoana ndani ya miaka mwili tu na unataka kuachana nae,inamaana mlioana kwa ajili ya kuachana , ndoa sio mchezo wa kitoto , kuishi peke yako ni rahisi lakini mambo ni tofauti kama mtakuwa pamoja , najua anakupenda sana hivyo nisikilize , haijalishi ni mara ngapi amekukosea lakini anao uwezo wa kukulinda , anakupenda sana na nitapata ahueni kama atakuwa upande wako, huelewi tu bado , Edna mimi kama mzazi wako nakuambia talaka ni kitu kibaya sana sijui kuhusu wengine lakini wewe ni binti yangu , mtoto wa kipenzi changu Raheli , njivunia sana na wewe ndio mtu pekee uliebakia ninaekujali , kama utatalakiana nae siwezi kumwangalia mama yako tena na bibi yako … Edna tafadhari kwa ajili yangu naomba usiachane na Roma, niambie muda huu unakwenda kurudiana nae”Aliongea kwa kulazimisha na kumfanya Edna kuanza kupandwa na jazba.

I
 
NILIMSHANIA KAHABA KUMBE BIKRA



MRUNZI: SINGANOJR



Mono no Aware.



SEOSON 24.



SEHEMU YA 691.


TULIKOTOKA NA TUNAKOELEKEA.

Hades wa Zamani ndio mwasisi wa jamii ya siri ya An- Illuminat, jamii ambayo jukumu lake kubwa ni kwenda kinyume na jamii ambayo ishawahi kuwepo ya Illuminat ambayo hufanya kazi chini ya kivuli cha Freemason.

Yaani katika uhalisia Illuminat inaonekana kutokuwa ‘active’ lakini nyuma ya pazia umoja huu hupo ‘Active’ na unafanya kazi kivulini kwa kuwatanguliza Freemason kama mti wao wa kivuli.

Hivyo ni sawa na kusema kwamba Illuminat ipo ndani ya Freemason na wanafanya kazi kivulini kwa kujiongezea nguvu mpaka wakati ambao watakuwa na uwezo wa kutoka kivulini.

Illumnat ni jamii ya siri ambayo ina nguvu kubwa sana ya ki ushawishi katika kila nyanja , uchumi , elimu , dini , siasa na mengine mengi.

Ikumbukwe kwamba malengo ya Illuminat ni tofauti kabisa na malengo na mtazamo wa freemason.

Wakati wa kuanzishwa kwa Fremason miaka 1700 kuendelea msimamo wao mkubwa ilikuwa ni kuimarisha upendo wa kindugu baina ya wanachama , kusaidiana na kuelezana ukweli kati yao juu ya yale yote yanayoendelea katika dunia.

Ni sawa na kusema kwamba ukishakuwa mwanachama moja kwa moja unafungamanishwa kindugu na wanachama wengine na hapa ndio utaweza kupata faida za kuwa mwanachama , kwa mfano kama ni mfanyabiashara na unataka kupanda zaidi kibiashara kinachofanyika wale wafanyabiashara wakubwa watakusaidia kupanda kibiashara zaidi , hivyo hivyo katika kila Career, yaani kwa lugha nyepesi ni kwamba wanachama hao wanabebana wao kwa wao kwa kutengenezeana ‘koneksheni’.

Upande wa Illuminat wenyewe malengo yao yalikuwa tofauti na Freemason , kwanza kabisa lengo lao kuu la msingi ni Enlightment(Kuelimika), yaani ni jamii ya watu walioelimika lakini pia jamii ya watu ambao wapo huru kufanya chochote kile bila kufungwa na sheria za kiimani na vilevile kuhubiri usawa na haki katika jamii.

Sasa katika kuelimika ndio uendelezaji wa sayansi na teknolojia na ndio yalikuwa malengo yao makuu.

Baada ya jamii hizi mbili kuungana, yaani Illumnat mara baada ya kuzimwa na kanisa moja kwa moja walimezwa na umoja wa Freemason na baada ya kumezwa ndio sasa Freemason ikawa na malengo mengine , kumbuka mwanzo ilikuwa ni jamii ya kusaidiana kindugu lakini baadae sasa wakaja kuwa na malengo ya kuendeleza kile ambacho kilikuwa ni malengo ya Illuminat..

Athena mara baada ya kutoka usingizini kwa muda mrefu sana malengo yake ya kwanza ilikuwa ni kufufua ndugu zake , yaani wale ambao roho zao zilimezwa na binadamu mara baada ya kujaribu kuteka nafsi zao.

Wakati Athena akifikiria kuamsha ndugu zake upande wa Hades wa Zamani yeye aliona ni hatari kama Athena atafanikiwa , akiamini kwamba malengo ya Athena ni sawa na kufufua utamaduni ambao ulipelekea sayari yao kukumbwa na janga ambalo liliwafanya kutoroka na kuja duniani.

Ni kweli kwamba kwenye sayari yao kulikuwa na teknolojia kubwa kuliko hapa duniani lakini Hades aliamini maendeleo ya taratibu ya uelewa wa binadamu katika sayansi ni salama zaidi kuliko maendeleo ya haraka utambuzi.

Sasa katika kipindi kirefu yaani tokea vita ya majini na viumbe hao kutokea asilimia kubwa ya miungu yote iliamini kwamba Zeus alikufa na Athena kupotea kiasi cha waliobaki kukubali kutia saini ya the gods treaty.

Hades wa Zamani pia aliamini Athena yupo kwenye usingizi mzito na itamchukua miaka mingi mpaka kuamka tena na jambo hili lilimfanya kuishi bila mipango yoyote lakini siku ambayo alikuja kugundua kurudi kwa Athena, mipango yake ilikuwa amekwisha kupiga hatua kubwa sana.

Hades hakuwa amejipanga kwa wakati huo hivyo kitu pekee ambacho alifanya ili kukwamisha mipango ya Athena ni kurudisha mashambulizi ya kuzorotesha mipango yake.

Athena kwa wakati huo alikuwa ashajijengea ushawishi mkubwa sana kwa kupitia jamii za siri karibia dunia nzima na ‘underwold’ yote, hili liliwezekana kutokana na kipaji chake kisiasa na nguvu ya ajabu.

Katika sayari yao familia yao ilikuwa ni ya kisiasa zaidi na yenye nguvu huku Hades wa Zamani yeye akiwa ni mwanasayansi zaidi.

Hivyo Hades aliona njia pekee ya kukwamisha mipango ya Athena ni kufanya kinyume chake , kwa mfano Hades alijua ushawishi wa Athena kwenye jumuia za siri kama Freemason ambayo ndani yake wapo Illuminat hivyo aliona kitu pekee ambacho kitakwamisha mipango yake ni kuunda jumuia nyingine ya siri ambayo ingeenda kinyume na jamii hizo ambayo ndio aliipatia jina la Ant- Illumant.

Hades hakuishia hapo alihakikisha alikuwa na taarifa ya kila mpango wa Athena kupitia mashushu wake aliopandikiza katika jumuia hizo.

Hades wa Zamani alijua ili Athena kufanikiwa katika mipango yake hatua ya kwanza lazima apate rasilimali zote ambazo walifika nazo hapa duniani ikiwemo Moyo wa Gaia na nishati ya ‘Ant-Matter’ ambayo ziehifadhiwa katika teknolojia iliopewa jina la the gods stone.

Hades aliamini kutokana na ushawishi wa Athena ingekuwa rahisi kwake kupata rasilimali hizo , ijapokuwa zilipotea miaka mingi sana lakini bado hakuna binadamu ambaye alifanikiwa kutumia teknolojia yake hivyo ilimaanisha ni kwamba hazikupotea bali zipo katika mikono ya watu.

Ukiachana na Athena kuwa mwenye nguvu kubwa ya kimapigano kuliko wote lakini pia alikuwa na kipaji kikubwa cha unabii na hapa ndio sehemu ambayo nguvu ya Athena ilipokuwepo.

Hades aliamini asingeweza kumzuia Athena katika mipango yake yeye kama yeye bali binadamu ndio ambao wana uwezo wa kumzuia Athena katika mipango yake wenyewe na kulinda sayari yao, hivyo kitu pekee ambacho aliona anaweza kufanya ni kuwawezesha binadamu wenyewe kuwa na uwezo huo na hapo ndipo alipoanza kutengeneza taasisi ambazo zilienda kinyume na zile za Athena yaani ni kama vile aliunda vyama pinzani ndio ambacho alifanya Hades wa Zamani.

Baada ya miaka mingi kupita hatimae Athena alifanikuwa kutumia jiwe la Kimungu kwa binadamu.

Mpango wake ulikuwa ni kutengeneza binadamu mwenye akili zaidi ambaye ataweza kumsaidia katika mipango yake na ili kuweza kumtengeneza binadamu huyo sharti ilikuwa lazima atengeneze binadamu ambaye ana muundo mpya wa DNA(vinasaba) za mwili na teknolojiia pekee ambayo ilipaswa kutumika kutengenezea DNA hizo ni mionzi ya jiwe la Kimungu ambayo Profesa Banosi aliibadilisha jina na kuita Divine Light yaani mwanga wa kiuungu.

Sasa katika mipango yake ndio ilipokuja kuzaliwa mpango LADO na katika kipindi hicho tayari alikuwa amekwisha kuunda umoja ambao husimamia maswala yote ya kisayansi na umoja huu uliitwa jina la Zeros organisation.

Chini ya Zeros mpango LADO ulipangwa kutekelezeka huku Athena akiwa na zaidi ya malengo ya mpango huo, kwanza kabisa katika unabii wake aliamini mpango LADO ndio ufunguo wa kupata moyo wa Gaia na ndani ya mpango huo huo angeweza kutengeneza kizazi kipya cha binadamu mwenye uwezo tofauti na hapa ndio ambapo alikuja kutokea Roma na Seventeen.

Athena hakuwa mwanasayansi na hakuwa na uelewa na sayansi , Hades Wa Zamani yeye alikuwa ni mwanasayansi kati ya miungu yote.

Athena alijaribu kumshawishi Hades kumsaidia katika mpango wake wa kufufua ndugu zao lakini Hades alikataa na hapo ndipo Athena alipomuambia Hades kwamba atafanikiwa mwenyewe bila ya msaada wake.

Kitendo cha Hades wa Zamani kukataa kumsaidia katika mpango wake kilimkasirisha sana Athena lakini licha ya hivyo aliamini ili kufanikiwa katika mipango yake lazima atumie akili ya Hades wa Zamani kwa namna yoyote ile.

Athena tokea mwanzo alishajua kwamba Hades wa Zamani yupo katika harakati za kumzuia asifanikiwe na hata kwenda kumuomba kumuunga mkono katika mipango yake ilikuwa ni kutaka tu kuhakiki nia yake.

Licha ya binadamu kufanya kazi kubwa katika utekelezaji wa mpango LADO Athena alikuwa na wasiwasi wa mpango huo kufeli na njia pekee ambayo aliamini ingeweza kufanikiwa ni kuhakikisha Hades wa Zamani anahusika katika mpango LADO.

Hivyo taratibu zote za mpango LADO kupitia Zeros zilivujishwa kwenda kwa Hades kwa kutumia shushu wake ndani ya umoja.

Hades wa Zamani mara baada ya kusoma taarifa yote ya mpango LADO aliona kuna mapungufu makubwa ya Mpango huo lakini licha ya mapungufu hayo alikubari sana juhudi za wanasayansi hao kwani walikuwa wamepatia kwa zaidi ya asilimia sabini.

Kilichomfanya Hades wa zamani kujua mpango LADO ulikuwa na hitilafu ni kwamba na yeye alikuwa na malengo ya kumtengeneza mrithi wake kwa muda mrefu ambaye angekwenda kushindana na Athena na alitaka mrithi wake afanyiwe ‘racial enginearing’ , yaani awe na asili nusu ya ubinadamu na pia awe na asili nusu ya uungu ili afanane na yeye kwa asilimia nusu , alifanya hivi kwa kuamini kwamba hata kama Athena akija kufanikiwa basi mrithi wake hatoweza kutawaliwa kimawazo na Athena.

Sasa kitendo cha kuvujishiwa nyaraka ya siri ya mpango LADO licha ya kwamba aliona ni mtego ambao Athena amemuwekea kutumia akili yake lakini aliamini ni fursa kubwa kuhakikisha mpango wake unakamilika kupitia mpango wa Athena, yaani kwamba yeye atengeneze mrithi wake kupitia mpango LADO.

Aliona hilo litawezekana kwa urahisi zaidi kutokana na kwamba kama angefanya mwenywe angekosa sapoti kutoka kwa serikali nyingi kutokana na kwmaba Athena ndio alikuwa mwenye ushawishi mkubwa kuliko yeye.

Hiyyo Hades alitumia akili yake kuziba zile asilimia therathini za hitilafu ya mpango LADO.

Zeros walitaka kufanya majaribio kwa binadamu kwa kuwaambukiza na kirusi kilichoundwa kwa teknolojia ya ‘Nanovirus’ ili pale binadamu ambaye atapona katika mpango kwa kujitengenezea kinga mfumo wa DNA utabadilika na kuwa na uwezo wa kustahimili mwanga wa jiwe la Kimungu.

Kumbuka hawa virusi walitengenezwa na Profesa Banosi mara baada ya kufanya majaribio ya muda mrefu ya matumizi ya jiwe la kimungu na kushindikana na ndipo alipoomba ruhusa ya kwenda kujichimbia msituni ili kukamilisha nadharia yake.

Maamuzi ya mpango LADO yalitokana na mafanikio ya asilimia kumi na moja ya misheni Pro Human.

Misheni Pro Human ilikuwa ni sehemu ya majaribio ya maandalizi ya mpango LADO lakini misheni hio haikudhalisha majibu ambayo yalihitajika kwani Naira hakuwa na mfumo wa DNA za mwili ambazo zingehimili mwanga wa jiwe la kimungu.

Sasa alichokifanya Hades ni kuhakikisha katika watu ambao wamechaguliwa kuhusishwa katika mpango LADO anaingiza wa kwake ambao hawapo katika mpango huo , ambao aliamini kabisa wangeweza kuhimili kirusi hicho na kisha kuingia katika hatua ya pili ya kumulikwa na jiwe la Kimungu.

Haikueleweka aliwezaje kujua kuhusu binadamu hao lakini binadamu ambao aliweza kuwachagua ni Denis Senga Kweka pamoja na mtoto wa Raheli ambaye hakuwa bado amezaliwa.

Kwa maelezo ya Hades mwenyewe ni kwamba Denisi na pacha wake Edna yaani Lorraine walikuwa ni ‘complete mutant’, yaani binadamu ambao wana mfumo tofauti wa vinasaba vya damu tofauti na binadamu wengine(Waliosoma simulizi ya 2hours of memories wataelewa hapa)

Mpango wake wa kuwaingiza binadamu hao ndani ya mpango LADO ulifanikiwa kwa asilimia moja mara baada ya kumhusisha Pastor Cohen ambaye baba yake Profesa Banosi alikufa wakati wa utekelezaji wa Misheni Pro Human na pia kumuhusisha mwanajeshi kutoka Tanzania Afande Cammiulius Kweka ambaye ni babu wa Denisi.

Upande wa Athena kumuhusisha Hades wa Zamani katika mpango LADO ulifanikuwa kwa asilimia mia moja na hakujali kama Hades alikuwa na ajenda ya siri , aliamini kwa namna yoyote ajenda ambayo alikuwa nayo Hades ataweza kuifuta baada ya mafanikio.

Wakati wa utekelezwaji wa mpango LADO Hades wa Zamani alikuwa tayari ashaunda umoja wa Ant- Illuminat na malengo yake ya mwanzo katika kuunda huu umoja ni kuhakikisha kwamba inakuwa ni jamii ambayo pia ina ushawishi duniani kama ilivyo kwa Freemason na jumuia nyingine.

Baada ya mafanikio ya Mpango LADO Hades alitengeneza kitu alichokiita Kalenda ya unabii kwa kutumia teknolojia maalumu, haikueleweka alitengeneza vipi lakini Kalenda hii ndio ilikuwa msingi wa uendeshwaji wa Ant- Illuminat mpaka leo hii.

Malengo ya kutengeneza kelenda hio ilikuwa ni kuhakikisha kwamba hata kama ikitokea hayupo tena duniani basi umoja huo unajiendesha bila kuathirika.

Sasa Hades hakuishia katika utekelezwaji wa mpango LADO tu bali aliendelea na ufuatiliaji wa mpango LADO.

Wakati mpango huo ulipokuwa katika hatua ya pili ya kuimarisha utimamu wa mwili pamoja na kumulikwa kwa Somo na mwanga wa jiwe la kimungu na kuachiwa kwa Somo kujitegemea huku tabia zake zikifatiliwa ndipo wakati ambao aliingia yeye katika hatua ya pili , yaani wakati wa Zeros wanakamilisha hatua ya pili yeye ndio aliingia katika hatua ya pili , hatua ya kwanza ilikuwa ni kumwingiza binadamu ambaye atafanikisha mpango LADO na hatua ya pili ni kuhakikisha Somo anajifunza mbinu za kijini , mbinu tofauti kabisa na kanuni za anga.

Na katika hatua hio ndio alipokuja kupata historia ya majini waliokimbilia kutoka ulimwengu wa kijini kuja katika ulimwengu wa kawaida , katika stori ya majini hao alikuja kugundua waliacha mtoto ambaye walimrithisha mbinu za mafunzo ya kijini ya kipekee mno.

Sasa mara baada ya utafiti ndipo alipokuja kumpata huyu mtoto alieachwa duniani ambaye alikuwa ni jini na huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Zhenzhei ninja wa kundi la Yamaguchi Gumi.

Ilikuwa rahisi sana kwa Hades wa Zamani kumshawishi Zenzhei kumfundisha Denisi mafunzo ya kijini , lakini wakati huo huo aliona pia ni hatari kwa Zenzhei kuhusika katika kumfunza Denis au Ajent 13 mafunzo ya kijini kutokana na kwamba alishakuwa ninja tayari wa kundi la Yamaguchi ambalo linamilikiwa na The Doni.

Hivyo baada ya kuongea na jini Zenzhei ndipo alipokuja kupata taarifa ambayo ilimtosha kabisa katika mpango wake na hapo ndipo jina la Master Tang Chi lilipokuja kufahamika kwa Hades.

Ilikuwa rahisi kumshawishi Master Tang Chi kumfanya Master kwa ajent 13 kutokana na kwamba alipewa koneksheni na Zenzhei.

Kilichomfanya Hades wa Zamani kuona Tang Chi ni mwalimu sahihi kwa Roma ni kwamba yeye alikuwa binadamu wa kawaida ambaye alikuwa akijifunza mbinu za kijini.

Sasa Ajent 13 ambaye ni Roma sasa kukutana na Master Tang Chi halikuwa jambo la bahati mbaya bali ni mchoro uliochorwa muda mrefu..

Kitendo cha Ajent 13 kufunzwa mbinu za kijini ziliwauzi sana Zeros organisation na kwa kutumia kikosi chao cha Dhoruba nyekundu walimdaka Tang Chi na kisha kumpa mateso makali mpaka kufikia kumuua na mara baada ya kuona amekufa ndio walimtupa msituni na hapo ndio wakati ambao Tang Chi aliingia katika levo ya kifo na uhai na kuzaliwa upya huku akiwa amekamilisha misheni yake.

Tang Chi alimrithisha Roma tu mbinu ya andiko la urejesho na Roma mafunzo yote alifanya mwenyewe bila ya maelekezo kutoka kwa Tang Chi hivyo Master Tang Chi sio master wa moja kwa moja wa Roma.

Baada ya hatua ya pili kufanikiwa Hades aliingia katika hatua ya tatu na kipindi ambacho anawazia hatua ya tatu.

Thirteen alikuwa huru kabisa na wakati huo alikuwa ashajua kwamba watu ambao wamemtengeneza yeye na Seventeen ashawaua wote na hio ni mara baada ya kulipua kituo cha utafiti huko Madagascer.

Lakini ukweli ni kwamba ule ulikuwa ni mpango wa Zeros organisation kumfanya ajent 13 na ajent 17 kuamini kwamba wapo huru ili kuhakikisha mpango wao hauathiriki kutokana na somo kugundua kwamba anachunguzwa.

Wakati wa hatua hio kwa zeros upande wa Hades wa Zamani aliingia katika hatua ya tatu na hii ilikuwa ni kutengeneza mpango ambao utamfanya Ajent 13 na Ajent 17 kukutana nae na kuwa na ukaribu.

Mchoro aliotengeneza ni kumfanya Ajent 13 kuwa na matamanio ya kumiliki visiwa vya wafu ambavyo vilikuwa chini yake.

Kumbuka wakati wote huo Roma au Ajent 13 hapa hajui kama Hades ndio alihusika kwa asilimia mia moja kwenye kumuingiza kwenye mpango LADO na hajawahi kukutana nae.

Ajent 13 na 17 walitamani visiwa vya wafu kama ilivyokuwa mpango wa Hades.

Sababu ambazo zilimfanya Ajent 13 kutamani visiwa vya wafu ni kutokana kipindi hicho alikuwa akimiliki kundi la kininja ambalo lilifahamika kwa jina la New Zero.

Yaani Roma mara baada ya kuharibu kambi ya Madagascar ya Zeros aliamua atengeneze kundi ambalo alilipa jina la New Zero yaani Zero mpya.

Hili lilikuwa kundi la kininja tisho mno na kipindi hicho Ajent 13 ambaye ndio Roma wa sasa alikuwa ameua watu wengi na alikuwa akisakwa na serikali nyingi na maadui , hivyo sehemu ya kimbilio pekee ambapo aliona anaweza kuweka makao makuu ya kundi lake ni visiwa vya wafu, kilichomvutia ni kwamba Visiwa vya wafu havikuwa na serikali rasmi bali kulikuwa na jeshi la Sea Eagles ambalo lilikuwa likilinda kisiwa hicho huku raia wakiishi kwa amani licha ya kuwa na historia pana ya uhalifu.

Hades wa zamani mara baada ya kuona Ajent 13 kaashaanza kutamani eneo lake alitengeneza mpango mwingine na huu ulikuwa ni mpango wa kumkutanisha Ajent 13 na binti mfalme Catherine(Princess Catherine) mama yake Clark.

Ilikuwa ni kwa kipindi kirefu Rothchild hawakupenda Catherine kuwa mtawala anaefautia mrithi wa kiti cha ufalme kwani alikuwa akitofautiana nao kimtazamo na familia hio ndio ambayo ilikuwa yenye nguvu ndani ya Uingereza na Ulaya yote.

Sasa ili kuhakikisha kwamba Catherine hapewi cheo cha umalkia suruhisho pekee ni kumuua yeye na binti yake Clark kwani kama Catherine angekufa ambaye angekuwa mtu halali kukalia kiti cha ufalme angekuwa ni Clark hivyo waliona ni kuua mama na mwana kuondoa mzizi.

Catherine alijua hila hio mapema sana na ndio alipokimbilia Italy katika jiji la Milan.

Sasa alichokuwa akifanya Catherine alikuwa akifuatisha mchoro wa Hades wa Zamani.

Katika ulimwengu wa wahalifu wakati huo yaani Underwold kulikuwa na maagizo ya kumkamata na kumuua Catherine na mtoto wake na atakaefanikisha hilo angejipatia pesa nyingi sana kutoka kwa familia ya Rothchild.

Sasa uelewe ulimwengu wa uhalifu ndio kunapatikana makundi ya kimanja hatari sana ikiwemo kundi la New Zero hivyo ilikuwa rahisi kwa Ajent 13 kuwa na taarifa za kutafutwa kwa Catherine.

Wakati huo Ajent 13 akiwa Italy na demu wake ajent 17 wakila maisha alipokea oda ya haraka ya kumuua mchungaji flani wa kanisa la Milan, haikueleweka ilitokea nini na hapo ndio Ajent 13 alipokutana na Catherine aliekuwa katika hatihati ya kubakwa na kumuokoa.

Catherine alifanikiwa kumshawishi Ajent 13 kumsaidia kupata haki yake ya kurithi kiti cha ufalme na kufyeka maadui zake na kama kawaida Ajent 13 alikubali kwani ukiachana na pesa, aliamini angefaidika na urembo wa Catherine licha ya kumzidi umri maana kipindi hicho alikuwa akipenda warembo balaa licha ya kuwa na mwanamke anaempenda ambaye ni Ajent 17 yaani Seventeen.

Sasa mara baada ya kufanikisha kumsaidia Catherine palepale aliambiwa na malkia aombe zawadi anayotaka na hapa sasa Hades wa Zamani alikuwa amembetia huyu Somo katika kufanya maamuzi sahihi.

Wakati huo Hades alikuwa kwenye mtafaruku wa muda mrefu na serikali ya Uingereza kutokana na kusema visiwa vya Wafu vilikuwa ni vya kwao kwani ndio sehemu ambayo yalikuwa ni magereza yao ya wafungwa watukutu, upande wa Hades yeye aligoma kutoa visiwa hivyo kwa Uingereza na aliungana na wakazi wa hapo na kusema ni vya kwao mara baada ya serikali ya Uingereza kuwatelekeza wakati wa vita.

Kitendo hicho kilifanya kuwe na vita kati ya serikali ya Uingereza na watu wanaoishi katika visiwa hivyo huku kamanda aliekuwa akiongoza mapambano hayo alikuwa ni Hades wa Zamani mwenyewe.

Uingereza walishindwa kupambana nae kutokana na siraha zake kuwa na teknolojia ya juu mno lakini licha ya kushindwa hawakutulia kushambulia.

Ukumbuke hapa Hades wa zamani hakutumia uwezo wake kutokana na kwamba alikuwa kwenye kifungo cha the gods treaty hivyo alipambana na Uingereza kibinadamu.

Sasa mara baada ya Ajent 13 kuambiwa achague zawadi palepale alimwambia malkia kwamba ampatie hati ya umiliki wa Visiwa vyote vya wafu, Catherine alishangaa kwani licha ya kwamba serikali ya Uingereza ilikuwa na hati ya umiliki wa visiwa hivyo lakini havikuwa vya kwao moja kwa moja lakini mwisho wa siku alikubali na kumpatia.

Ajent mara baada ya kupata hati ndio alikomesha rasmi vita iliokuwepo kati ya visiwa hivyo na Uingereza na kutokana na mchango wake ndipo aliporuhusiwa kuwa sehemu ya raia wa huko na ndio alipokutana na Hades wa Zamani kwa mara ya kwanza na kujenga ukaribu.

Ukaribu ambao ulikuwa mkubwa mno ambao ulipelekea Hades kutangaza Ajent 13 na Ajent 17 wangekuwa warithi wa utawala wake na jeshi lake lote la Sea Eagles au The Eagles.

Rasmi mchoro wake ukawa umekamilika rasmi na hapo ndipo alipomrithisha Roma uungu wake yaani ule uasili wake yaani alimfanya sasa Ajent 13 kuwa nusu binadamu na nusu kiumbe kutoka sayari nyingine na hapo ndipo jina la Ajent 13 lilipokufa na akafahamika rasmi kama Hades a.k. a mfalme Pluto.

Sasa licha ya haya yote kuendelea upande wa Zeros walikuwa wakifatilia kwa ukaribu zaidi hawakutaka kwa namna yoyote Hades mpya kujua kama wanamfatilia na yupo ndani ya mipango yao hivyo walikuwa makini san na ndio hao hao ambao walimtengnezea Hades changamoto mpya , kwa mfano kifo feki cha Seventeen walihusika , Roma kupambana na watu kutoka mataifa mengi walihusika wao, yote hio ilikuwa ni kumkomaza.

Mfano chukulia wakati Roma alivyokuwa akipambana na yule Monk kule Japan , lakini vilevile kupambana na Ares yote ilikuwa ni michoro ya Zeros organisation na mapambano yale yalikuwa yakirushwa mubashara na kikosi cha Dhoruba nyekundu.

Mchoro wa Hades wa Zamani sasa ulikuwa ukifanana na mchoro wa Athena wote kwa asilimia mia moja , yaani Hades wa Zamani alikuwa akifanya vitu amavyo vipo ndani ya mpango wa Athena kitu pekee ambacho walitofautiana ni pale alimpomfanya Roma kujifunza mbinu za kijini tofauti na kanuni za anga..Athena na ndio maana mara baada ya kifo cha Hades alichukua mwili wa Hades wa Zamani na kwenda kuuhifadhi bila kueleweka alikuwa na mpango gani.

Upande wa Hades wa Zamani yeye pia alikuwa akijua kila anachokifanya kipo ndani ya mpango wa Athena na ndio maana alitumia akili ya ziada kuhakikisha mpango wake unakuja kufanikiwa hapo baadae hata kama amekufa.

Hades aliamini kwamba kuna uwezekano wa mrithi wake kutoweza kumshinda Athena kama ataweza kuufufua moyo wa Gaia na kurudiwa na nguvu zake asilimia mia moja.

Hivyo hatua ya kwanza hakutaka kumhusisha mrithi wake na umoja wa Ant- Illumnat hata kidogo , wakati huo huo akamuhusisha Seventeen kwa siri sana na mipango ya Ant-Illuminat na hapa ndio unajua sasa kwanini mara baada ya Zoe Kovac alimhadithia Roma kwamba alikutana na Seventeen visiwa vya Maldives.

Mara ya mwisho wakati Hades anamkabidhi Seventeen Kalenda ya unabii kwenda kuiwakilisha kwa umoja Ant-Illuminat alimwambia ni ngumu sana kumshinda Athena, lakini ni binadamu wenywe ambao wanao uwezo wa kushinda pale watakapoamua huku akimpa mfano wa jaribio lao ambalo walitaka kulifanya na kutawala dunia kupitia kumeza roho za binadamu lakini tukio hilo likafeli.

Hades wa Zamani ili kuhakikisha mipango yake inafanikiwa kwanza kabisa hakuwa na haja ya Roma kumshinda Athena kimapambano bali Roma kumtengenezea njia mtu mwingine kumshinda Athena bila mapambano lakini licha ya hivyo alimpa Athena asilimia hamsini ya kufanikiwa na wakati huo huo aliwapa binadamu asilimia hamsini ya kuweza kulinda sayari yao na kufanikiwa.

Sasa swali je nani atashinda , je Athena atafanikiwa katika mipango yake yote au binadamu watashinda hakuna jibu sahihi kwani kila mmoja ana nafasi ya kushinda.

Lakini swali kubwa je kama Roma hakutengenezwa kumshinda Athena bali kumtengenezea mtu mwingine kushinda huyo mtu ni nani.





SEHEMU YA 692.

Edna alikuwa akitoa machozi , haikueleweka alikuwa akitoa machozi kwasababu ya mwanaume aliekuwa mbele yake au mwanaume yule aliekuwa hajui hata yupo upande gani wakati huo.

Edna aliishia kusimama tu huku akishindwa kuongea neno lolote na baada ya kutulia alijitoa katika mikono ya baba yake.

“Mambo ya talaka ni kati yangu na Roma , Mheshimiwa kama unanitakia mema tafadhari naomba usiingilie kwenye mambo yangu binafsi , nina wasiwasi kila kitu ulichoongea hapa baadae kitageuka na kuwa uongo na wakati huo ukifikia sidhani kama tutakuja kuongea tena”

“Edna una…”

“Basi inatosha sitaki kusikia tena ukiongea wala kukusikiliza , tuhitimishe maongezi yetu hapa mimi naondoka”Aliongea Edna na kisha alimpita Raisi Jeremy na mara baada ya kufika kwenye mlango alitulia na kugeuka nyuma.

“Unaonekana umelewa , upumzike mapema”Baada ya kuongea kauli hio palepale alifungua mlango na kutoka.

Walinzi na wasaidizi wa raisi Jeremy mara baada ya kumuona ametoka walimsogelea na kumuuliza kama kuna chochote anachotaka.

Walikuwa wamefanya kazi chini ya Raisi Jeremy kwa muda mrefu hivyo walikuwa wakijua Edna ni mtoto wa mheshimiwa na walikuwa wakielewa kabisa Raisi Jeremy anajaribu kufufua uhusiano na binti yake.

Edna hakutaka kuongea nao na kwa muonekano wa kikauzu alioweka iliwafanya wale wasaidizi na walinzi kutouliza chochote zaidi na kumpisha apite lakini dakika hio hio Raisi Jeremy alitoa maagizo ye Edna kurudishwa nyumbani na usafiri lakini kitendo cha wasaidizi kutoka nje kumtafuta Edna hakuonekana tena , ilikuwa ni kama amepotea maana hata kama alikuwa na haraka vipi asingeweza kuondoka ndani ya eneo hilo ndani ya muda mfupi namna hio.

Msaidizi wa Raisi Jeremy mara baada ya kurudi kwenye chumba alichomuacha mheshimiwa alimkuta akijaribu kukaa kwenye meza kivivu kama mlevi.

“Mheshimiwa upo sawa?”

“Nipo sawa , nadhani unajua uwezo wangu wa kihimili kilevi”Aliongea mheshimiwa na palepale alisimama taratibu kwa ajili ya kuondoka.

“Edna ameshaondoka?”

“Ndio , tulitaka kumpeleka nyumbani kama ulivyoagiza lakini mara baada ya kumtafuta nje ya maegesho ya magari hakuonekana tena , ni kama amepotea”Aliongea na kumfanya mheshimiwa kucheka kivivu.

“Nadhani zile taarifa ni za kweli za Roma kumfundisha mafunzo ya kijini”

“Mheshimiwa nadhani kwasababu amekubali kuonana na wewe , nadhani haitakuwa nguvu kurudisha mahusiano yako na yeye , mimi naona labda tu ni kwasababu ya kutozoea”Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy kumwangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida na aliishia kutoa kicheko hafifu kama vile anajicheka na palepale aliinua chupa ya mvinyo na kisha akajaza kwenye glasi kwa mara nyingine na kisha kunywa yote.

“Edna binti yangu , haijalishi utajitahidi vipi kunikwepa na kujifanya hunipendi kama baba yako lakini uzoefu wa kuficha hisia zako huna na siku zote una moyo mwepesi kama alivyokuwa mama yako Rahel… haha yaani unasema nimelewa na nilale mapema , nalewaje kirahisi hivyo , lakini niseme tu kuna raha ya kuwa na binti ambaye anaonyesha kukujali”Alijiongelesha mwenyewe .

Upande mwingine dakika hio hio kilionekana kivuli cha mtu kikitua kutoka angani juu ya balkoni ya Mansion iliokuwa ndani ya eneo la Ununio.

Upepo wa baharini wa usiku uliyapangusa mashavu yake kwa kasi na kumfanya Edna kugeuza macho yake na kuangalia angani na mwanga wa mwezi uliakisi macho yake ambayo yalionyesha kujawa na hisia mchanganyiko

Edna hakujua ni kwa namna gani na kivipi ameweza kuwa na uwezo wa kupaa kwa wepesi zaidi namna hi o, hakuna ambaye alishawahi kumfundisha kufanya kitu kama hicho na hajawahi pia kujifunza lakini akili yake ilimwambia tu kwamba anao huo uwezo na alijikuta akifanya kitu nje ya mategemeo yake , ilikuwa ni kama vile ni kitu ambacho amezaliwa nacho na sasa hakujua kama kilikuwa kipo mwilini mwake na ndio amegundua.

Ukumbuke kwamba alikuwa kwenye levo ya nusu mzunguko na haikumruhusu kupaa kwani ni mpaka kufikia levo ya Nafsi.

Lakini kwa wakati huo akili yake haikuweka makini katika uwezo wake huo mpya , wakati akiendelea kuangalia nyota na mwezi alisikika akiongea kwa sauti nyororo kwa upole.

“Hubby moyo wangu umekuwa mdhaifu tena mbele ya baba , najua kila alichoongea ni uongo lakini nashindwa kujizuia kumwamini , nini napaswa kufanya? , upo wapi mume wangu..”Aliongea Edna huku akiwa na hali ya kumkumbuka Roma na kutamani kumuona mbele yake na kumpa majibu ya hisia zake mchanganyiko.

Edna udhaifu wake ulikuwa ni kwenye ndugu zake na Jeremy alitumia udhaifu huo kwa manufaa.

******

TOKYO – JAPAN 03:15AM

Moja ya vitu ambavyo vinalifanya jiji la Tokyo kupendeza na kuonekana kama vile upo mbele ya muda ni kutokana na wingi wa maghorofa yalioenda hewani na kuzingirwa na mwanga wa Neon.

Tokyo ndio jiji namba moja ambalo lipo kiteknolojia zaidi duniani na jiji ambalo linapendeza sana nyakati za usiku.

Ilikuwa ni saa tisa za usiku nchini Japani katika jiji hilo wakati Roma alivyofika na kutua juu ya jengo refu zaidi katika jiji hilo lilofahamika kama Azabudai hills Tower.

Ni kipindi cha majira ya baridi ndani ya jiji la Tokyo ambapo kikawaida hudumu kuanzia mwezi wa kumi na mbili mpaka mwezi wa tatu na juu ya jengo ambalo amesimama Roma pengine ndio sehemu yenye baridi zaidi ndani ya jiji hilo.

Moja ya sababu ambazo zinafanya majiji mengi kama Tokyo kuwa na majengo mengi kwenda juu ni kutokana na watu wengi kuishi mjini, katika jiji kama Tokyo ni ngumu kupata ardhi na kujenga nyumba yako mwenyewe , kinachofanyika kampuni au serikali inajenga majengo ya maghorofa kama hayo na kisha ndio inauza nyumba hizo au kupangaisha kwa mfumo wa Apartment.

Sasa asilimia kubwa ya familia za kipato cha kati ndani ya jiji hilo wanaishi juu kabisa ya majengo hayo huku familia nyingine tajiri zikiw ana makazi binafsi pembezoni mwa jiji.

Roma alidumu juu ya ghorofa kwa dakika chache tu na kisha akamchukua tena Maimuna na kupotea nae na ile anakwenda kuibukia alikuwa ndani ya jengo lingine.

Kitendo cha kuingia kwenye floor tu ya kwanza kutoka juu palepale vivuli kutoka sehemu mbalimbali za msituni walitokeza na kuwazingira..

“Sio mbaya , naona tayari mpo mwishoni mwa levo ya nusu mzunguko , Tannya inaonekana anafanya kazi nzuri kuliko Noriko Okawa”Aliongea Roma kwa kijapani.

“Wewe ni nani?”Aliuliza mmoja wa Maninja ambao walikuwa wamemzingira Roma ambaye alionekana ndio kiongozi na Roma alitoa tabasamu na kisha akamtua chini Maimuna.

“Tannya jitokeze”Aliongea Roma , ijapokuwa aliongea kwa sauti ya chini lakini alitumia nguvu ya kijini ili kusafirisha sauti ndani ya jengo lote..

Dakika hio hio Tannya alijitokeza juu ya Balkoni akiwa na mavazi meusi ya kulalia na ilionekana kutokana na haraka alishindwa hata kujifunga vizuri eneo la kifuani kwani manyonyo yalikuwa wazi.

Dakika ileile alipiga magoti mbele ya Roma na kuongea kwa sauti iliojaa heshima na mshangao.

“I am sorry for my tardness Master”Aliongea Tannya kwa lugha ya kingereza akimaanisha anaomba radhi kwa kuchelewa.

“Ni sawa , nimekuja kwa kushitukiza hata hivyo , sio mbaya sio mbaya naona tayari ushaingia levo ya Mzunguko kamili , ni muda muafaka kunisaidia jambo”Aliongea Roma kwa kijapani awamu hio huku akiwa na tabasamu.

Wale maninja waliokuwa wamemzingira Roma mara baada ya kusikia mkuu wao wa Yamata anamwita Roma Master palepale akili zao ziliwaambia huyo ni mfalme Pluto.

Walikuwa wakijua baada ya kifo cha Noriko Okawa mmiliki alikuwa ni Roma huku Tannya akiwa kiongozi wa kundi hilo tu , na hapo hapo jasho lilianza kuwatoka wakiogopa Roma anaweza kuwaadhibu.

Roma mara baada ya kuhisi woga wao alitoa kicheko hata hivyo alisifika kwa ukatili hivyo ilileta maana kwa watu hao kumuogopa .

“Mnaweza kuondoka , siwezi kuwaadhibu kwa kuwajibika kwenu kuimalisha ulinzi kwa bosi wenu”Aliongea Roma na mara baada ya kusikia kauli hio kama wachawi walipotea palepale.

Dakika hio hio Tannya sasa aliweza kuona sura ya Maimuna, alikuwa akimfahamu na alishangaa kumuona akiwa na Roma.

“Master kwanini huyu mwanamke umekuja nae?”aliuliza na Roma hakutoa jibu kwani hakuwa na haraka yakuelezea na alitembea uelekeo wa swimming pool.

Hali ya hewa ya ubaridi ilimfanya kuvutiwa na maji hayo ambayo yalikuwa yakitoa mvuke wa joto kama chemchem na kwa upande wa Roma ni muda mrefu hajaingia kwenye swimming pool.

Tannya mara baada ya kuona Roma anataka kuingia kwenye bwawa la kuogelea palepale alisogea kwa haraka ili kumsaidia kuvua mavazi..

Ijapokuwa kwenye maisha yake hakuwahi kumpenda Noriko Okawa lakini alikuwa amejifunza kumhudumia hivyo ujuzi ule aliutumia mbele ya master wake Mfalme Pluto.

Baada ya nguo zote kutolewa mwilini Roma alibakia na boksa tu ambayo alikuwa akiipenda kutokana na kununuliwa na mke wake Edna.

Na Tannya hakutaka kumvua kabla ya kuomba ruhusa yake kuitoa na Roma alitingisha kichwa kukubali kwa tabasamu na kumfanya Tannya kuwa mwekundu kama yai la kisasa.

Tannya palepale alisogea kwa mbele na kisha alipiga magoti na kumvua Roma boksa yake mpaka chini na kumfanya kuona mtalimbo ukicheza cheza , ijapokuwa haukua umesimama wima lakini bado ulimfanya kupatwa na joto la mwili.

Ijapokuwa Tannya alipoteza usichana wake kwa Noriko Okawa kwa kuwekwa vidole lakini hakuwahi kupata uzoefu wa kuonja utamu halisi wa mb** , alijitahidi kujilengesha kwa Roma lakini alikataliwa kila wakati na aliamini alfajiri hio itakuwa ni wakati sahihi lakini kwa namna moja ama nyingine alihofia na kuona kwamba pengine angeshindwa kuhimili ukubwa wake.

Kutokana na maumivu ambayo alipita tokea akiwa mdogo hakutaka kujihusisha katika mapenzi na mwanaume yoyote tofauti na Roma.

Upande wa Roma hakujali sana muonekano wa Tannya , kwake kuvua nguo mbele ya mwanamke kama hivyo ilikuwa kawaida sana , wakati alipokuwa Ulaya aliishi maisha ya hatari sana hivyo kuwa na tabia ambayo wazungu wanasema ni open-minded.

Roma mara ya kuingia kwenye maji hayo alijkuta akipatwa na raha ya ajabu na kumgeukia Tannya.

“Tannya hakika unainjoi sana hii sehemu inavutia”Aliongea Roma huku akigeuzia uso wake upande wa jiji na kumfanya Tannya aliekuwa nyuma yake kuingiza mkono kisirisiri katika gauni lake na kujipapasa na msisimko alioupata ulimfanya kuimba wimbo wa ‘Amelowa’.

Wakati wa kukurupuka kuja eneo hilo hakuwa na muda hata wa kuvaa nguo ya ndani hivyo kwa haraka sana alishusha gauni lake kwa hofu ya kuonekana uchi mbele ya Roma.

“Master nimehamia katika jengo hili kutokana na kupewa hongo tu”Aliongea Tannya huku akibana miguu kwani alihisi ni kama upepo unamwingia.

Upande wa Roma licha ya kumpa mgongo alikuwa anajua ni nini Tannya anachofanya muda huo nyuma yake.

“Hebu njoo na unimpe kampani”Aliongea na kumfanya Tannya kurembua ki’aibu huku mapigo ya moyo wake yakidunda kwa kasi sana kama mtoto wa kike ambaye ndio anatongozwa na mwanaume anaempenda.

Dakika ileile kwa kusita sita aliachia kamba za gauni lake kutoka mabegani na kulifanya lidondoke lenyewe mpaka chini na kisha kwa wasiwasi kwa namna ya kunyata alitembea na kuingia ndani ya Swimming pool.

Licha ya kuingia kwake aliishia kukaa pembeni yake ki’adabu bila kugusana na Roma.

Kutokana na mwezi na taa za ndani ya maji ilimfanya Roma kuona vyote ndani ya maji na hakukwepesha macho ni kama alikuwa akimchunguza.

Roma alishangaa kutokana na usafi wa Tannya katika eneo la Ikulu kwani hapakuwa na majani kabisa.

“Tannya huna haja ya kuwa na wasiwasi , mimi sio mtu wa kukurupuka kama mvulana alieanza balehe , ninaweza kukuangalia kama hivi lakini nitaishia kukutamani tu bila kukufanya chochote”

“Master Kama utapenda nipo tayari muda wowote”

“Haha.. nina wanawake wengi na wewe umefanya mambo mengi kwa ajili yangu na najua hilo , kama upo tayari kuachana na uninja na kutaka kuanza maisha mapya ya amani tafuta mtu anaefaa kurithi cheo chako ndani ya Yamata na uolewe , nitakupa sapoti ya kujitosheleza”

“Hapana , mimi nakuamini wewe tu Master”Aliongea Tannya akiwa siriasi na kumfanya Roma kumuona kama mtoto.

Roma mara baada ya kumaliza mshangao wake aliacha kumshawishi zaidi , imani yake ilikuwa ni ya upande mmoja tu , kutokana na kuishi kama ninja , ijapokuwa alionekana kama mwanamke mjinga lakini bado alikuwa akivutia.

“Nadhani unajiuliza kwanini nimemleta yule mwanamke kutoka Tanzania… hiki ndio ambacho kimetokea…”Aliongea Roma na kuanza kumhadithia tukio zima.

Likija kwenye swala kama hilo Tannya ile aibu ilipotea na kuonekana kuwa siriasi.

“Master unataka nifanye nini?”

“Ile familia mpaka sasa imepata hasara kubwa na wana wafuasi wengi sana nazungumzia kuhusu imani yao ya kikafara , kwasababu nimeua viongizi wote wa juu basi muda wowote kutaibuka mgogoro wa kugombania mali kati ya wanachama na uongozi, bila familia ya Sharif basi kutatokea shida kubwa ambayo inaweza kuathiri jamii , lakini pia itamkasirisha Master namba moja, ijapokuwa bado sijamjua ki undani sitaki watu wasio na hatia kuathirika hivyo nina hitaji mtu ambaye anaweza kuwa kiongozi wa ile familia kwa muda … nahitaji mtu ambaye atanipatia taarifa ya familia nzima chimbuko lake na kile wanachosalia ni nini , amebakia Maimuna hai kama mrithi lakini ni mjanja sana na hana maadili ya kuheshimu maagizo yangu hivyo sitaki yeye awe kiongozi”

“Kwahio Master unataka nitumie mbinu zetu za kichawi kuwa na muonekano wa Maimuna na kuingia ndani ya familia hio ya Sharif na kuwa kiongozi?”

“Unaa akili sana , unao uwezo wa kuigiza kuwa mtu mwingine na kufanikiwa, hivyo naamini utafanya vizuri na kama itatokea majini yao yatatoka huko yalipo na kukukamata basi nitakusaidia , ukweli ni kwamba natamani yajitokeze ni yakamate ili niweze kujua yanatokea wapi”

“Itakuwa ngumu sana kwani inaonekana ni familia ambayo ina muunganiko mkubwa , itanipasa kuchukua taarifa nyingi kutoka kwa Maimuna hususani majina ya kila mtu na kuyakariri na hili napaswa kulifanya mimi mwenyewe ili ufanisi uwepo”

“Huna muda mrefu sana , hakikisha hili linafanikiwa kabla ya kesho mchana , sitaki wagundue kupotea kwa Maimuna mapema , baada ya kupata taarifa chukua watu wako Elekea Tanzania , kuhusu namna ya kupita mpakani nitahakikisha kitengo cha wachawi hakiwafanyi chochote, nina koneksheni na kamanda wao nchini Tanzania, unaweza kumchukua na kuondoka nae pia na kumficha ili kumuuliza baadhi ya taarifa na ili kukurahisia kazi nitamuondolea nguvu zote za kijini”

“Naona kabisa bado ni bikra , naamini kama nitamtumia kama kahaba ndani ya club zetu za Yamata atauza sana , isitoshe wanawake wa aina yake wanatafutwa sana hapa Japan”

“Hio sasa itakuwa juu yako kuamua , ila ombi langu nataka kesho saa tatu nikuone ukiwa unafanana na Maimuna”

“Ndio Master”

Roma muda huo huo alimfuata Maimuna ambaye bado alikuwa hana fahamu na kisha alimuondolea nguvu zake zote za kijini na kuwa binadamu wakawaida na kisha Tannya alimchukua na kuondoka nae kumfanyia mazingara.

Dakika ambayo Maimuna alishituka kutoka usingizini alijikuta akiwa ndani ya chumba ambacho kina mwanga haififu na aligundua hakuwa na nguvu zozote za kijini na mbele yake yupo Tannya na kundi la wanaume waliokuwa uchi wakiwa wamesimama mbele yake na mitalimbo yao kuonyesha nia ya kumtamani.

“Nipo wapi hapa , Roma yupo wapi , Master yuko wapi?”Aliuliza maswali mfululizo.

“Nisikilize kwa umakini kwa sasa wewe si chochote , kama unataka kuishi jibu maswali yangu yote , kama nitaona ishara ya kusita sita kwenye macho yako , usijali nitakuondolea usichana wako lakini hata hivyo nadhani unaona hawa wanaume waliopo mbele yako, watahakikisha wanapita njia zote. Hivyo unapaswa kunisikiliza na kunijibu”Aliongea Tannya na kumfanya Maimuna kuhisi pumzi haimtoki na ndani ya sekunde chache alipoteza tena fahamu na kumfanya Tannya kumwangalia kwa kejeli na aliona udhaifu wa Maimuna ni kutokana na kupoteza uwezo wake wa kijini.

Aliachwa apoteze fahamu ndani ya dakika tano na palepale alimwagiwa maji ya baridi na kushituka.









SEHEMU YA 693.

NORTH POLE(NCHA YA KASKAZINI)

Kama kawaida ndani ya eneo la ncha ya kaskazini haikueleweka ni mchana au ni jioni na ardhi yote ilikuwa imefunikwa na barafu kutokana na ufinyu wa upatikanaji wa jua.

Athena alionekana akiwa amevalia gauni la rangi nyeusi huku akiwa ameelea juu ya anga kama vile alikuwa amesimama juu ya ncha ya mnara mrefu mno , macho yake yote yalikuwa yakiangalia mazingira ya chini yake kana kwamba kuna kitu cha kuvutia macho.

Nyuma yake alikuwa amesimama mtu mwingine ,huyu alikuwa ni yule yule mwanaume ambaye huvalia joho la rangi nyeusi na Mask ya chuma , alikuwa amesimama huku macho yake yakiangalia kifaa alichoshikilia Athena mkononi mwake.

Kifaa hicho kilikuwa na umbo kama wa yai la kuku na kilikuwa kikitoa mmg’ao hafifu wa rangi ya njano , ukisogea kwa ukaribbu zaidi lazima ungegundua ulikuwa ni moyo wa Gaia.

Lakini kama utafananisha na mwanzo awamu hio ulionekana kuwa mkubwa mno.

“Its almost time”Aliongea Athena ndani ya nafsi yake akimaanisha kwamba muda hatimae umewadia , haikueleweka sasa umewadia kufanya nini.

Dakika ileile aliachia ule moyo wa Gaia na kuufanya udondoke kushuka chini huku ukitoa mng’ao wa rangi ya njano na mara baada ya kukutana na ardhi ya barafu ulichimba na kisha ukatoboa na ndani ya dakika chache tu uliweza kutumbukia chini ya majji ya bahari mpaka ulipofika chini kabisa ya uvungu wa bahari na kuanza kushuka kwenye mlima wa ardhi kama vile tairi inayodondoka kwenye mlima.

Baada ya kufika kwenye bonde chini ya maji nq kuchimba kwenda chini ardhini hatimae uliweza kufika kwenye ardhi yenye rutuba ya madini ya ajabu chini ya maji hayo na hatimae ulitulia..

Dakika ileile ni kama sumaku iliowekwa sehemu yenye misumali kwani nyuzi nyuzi za nishati zilianza kujikusanya kutoka kwenye madini kuusogelea ule moyo.

Kadri kitendo kile kilivyokuwa kikifanyika kwa kasi kubwa ule moyo ulianza kufutuka na kusinyaa kama vile ni pulizo linalopulizwa na kutolewa hewa kwa wakati mmoja , ilikuwa ni kama vile ni moyo wa binadamu , yaani jinsi moyo wako unavyofanya kazi ndio kilichokuwa kikifanyika ndani ya eneo hilo.

!Dum Dam ,, Dam dumb’” ndio sauti yake huku nishati kama mionzi ikizidi kuzingira ule moyo.

Wakati moyo huo unatolewa kwenye jiwe la kimungu ambalo limezungukwa na ubaridi wa Selene ulikuwa ni kama mwanga mwanga ndani yake lakini wakati huo Athena alikuwa amefanikiwa kuufufua na kuutengenezea ngozi kwa juu na kitendo cha kuutupia majini ni kuupa nafasi ya kufanya kazi.

Sasa moyo kazi yake ni kusukuma damu lakini moyo huyo haikueleweka ulikuwa ukisukuma nini kwani ulidunda kama moyo wa kawaida.

Dakika hio hio wote wakiwa wamekodolea macho chini ya bahari wakiona vizuri kinachoendelea , bwana mwenye Mask alionekana kushindwa kuvumilia kutokana na shauku yake.

“Is that it , why isn’t anything happening yet?”Aliuliza akimaanisha je ndio hivyo na kwanini hakuna kinachotokea.

Athena aliongea na sauti yake ilisikika kama mwangi au kama Maika kutoka mbinguni.

“Wewe sio sehemu ya miungu , hivyo huwezi kupata hisia zinazotolewa , kufufuka kwa moyo wa Gaia ni jambo ambalo hakuna mtu wa kuweza kuzuia”Aliongea huku akionyesha muonekano usio na tabasamu lakini wenye kuridhika na kisha akaendelea.

“This world would eventually belong to us gods , its time for the ten -thousand year long grudge to be resolved”

“Huu ulimwengu hatimae unakwenda kuwa wetu sisi miungu , ni wakati wa kinyongo cha miaka elfu kumi kumalizwa”

Kitendo cha moyo wa Gaia kuanza kudunda kama moyo wa binadamu miungu wote kumi na mbili kupitia uungu wao waliweza kuhisia ndio maana Athena akasema yeye sio miungu ndio maana hawezi kuhisi.

Ndani ya Hollywood, Christen ambaye alikuwa akikamilisha kufanyiwa Make up kwa ajili ya kushoot filamu alijikuta akiruka mbele ya kioo kwa mshituko wa aina yake.

“Has she lost her mind!!?”

Aliongea akisema je Athena amepatwa na ukichaa huku akianza kutetemeka ,ilikuwa ni aina ya hisia juu ya jambo flani la kutisha ambalo unaogopa kutokea litokee hatimae ndio limetokea.

Upande mwingine jijini London Uingereza ilikuwa ni usiku na wenza waliokuwa ndani ya jumba la kifahari wakitoa miguno ya kimahaba walijikuta wakishutuka na kuacha kile wanachofanya.

Stern alikuwa amelala chini na demu wake Alice alikuwa amemkalia kwenye kiuno ,staili ambayo wajuvi wanaita xxxx, Stern aliishia kumwangalia Alice msisimko wake wa kimahaba ukipotea kwenye macho yake na yeye pia.

“It has begun…”Walijikuta wakitamka neno moja kwa wakati mmoja wakimaanisha hatimae umeanza.

Katika hoteli ya kifahari ndani ya jiji la Dubai katika chumba cha hadhi ya raisi alionekana Ares akiwa anafuta futa bunduki yake kama vile ina vumbi na ghafla tu alisimama kutoka kwenye sofa.

Palepale tabasamu kichaa liliuvaa uso wake na alijikuta akitoa cheko kama kichaa.

“My powers… My powers are returning”

“Nguvu zangu ,,, nguvu zangu jamani zinarudiii”Aliongea kwa furaha.

Upande mwingine ulisikika mziki wa classical opera ukisikika ndani ya chumba katika ngome iliokuwa ikipatikana ndani ya nchi ya Italy .

Raphaeli ambaye alikuwa amevalia suti ya bei ghali alikuwa amemkumbatia mwanamke wa Kilatini, mwanamke yule alikuwa amelala kivivu akiwa ameleweshwa na hakujua wakati huo Raphaeli alikuwa akimnyonya damu na kumtoboa kwa kutumia kucha zake ambazo zimekwisha kurefuka huku macho yake yakiwa mekundu kama yamejaa damu.

Lakini sasa ghafla tu alishituka na macho yake yalisinyaa palepale huku akirudiwa na hali ya ubinadamu lakini mikono yake ilikaza na bila kujielewa alijikuta akimchana chana yule mwanamke na kumsambaratisha na damu nyingi kuruka chini na palepale hakujali kama amekwisha kumuua kwani alimtupia chini kwenye sakafu.

“Haha… haha , Athena , you are really incredible ..its done so soon”

Ijapokuwa alikuwa akitetemeka haikueleweka kicheko chake ni cha huzuni au furaha ila alionekana kutokuamini kama Athena amekamilisha ndani ya muda mfupi hivyo..

****

Asubuhi ilimkuta Roma akiwa ndani ya jiji la Tokyo na alikuwa amekaa kwenye kiti tokea afike ndani ya nyumba hio anayoishi Tannya tokea dakika ambayo aliweza kuhisi uungu wake aliorithishwa na Hades wa zamani umeongezeka kidogo.

Mpaka wakati huo Roma hakuwa akielewa kisawasawa kuhusu uungu , kilikuwa ni kitu kama chip ndani ya akili yake ambacho kilikuwa ni cha maajabu sana lakini sio kifaa.

Kwa lugha nyepesi unaweza kusema ni alama ya ishara ya nguvu ya kiroho ndani yake na hii ndio inawatambulisha upekee wao.

Kwa mfano hapa duniani inasemekeana kwamba fingerprint(Alama za vidole) na kiini cha macho havifanani na binadamu yoyote yule basi ndio hivyo hivyo kwa miungu hao au viumbe kutoka sayari nyingine , kwao upekee wao sio kupitia vidole au macho bali alama ya nguvu ya kiroho ndani yao ambayo huita kama uungu ndio huwatofautisha, yaani Hades ana alama ya kiuungu ya aina yake ambayo haiwezi kufanana na ya Aphrodite au Poseidon.

Sasa Roma alikuwa akihisi kabisa nguvu yake ya kiuungu ndani yake ilikuwa ikiongezeka, ni kitu ambacho kimetokea bila ishara yoyote kana kwamba kuna nguvu ya nishati ambayo inachochewa ndani ya mwili wake bila ruhusa na kuimarisha ufahamu wake wa kifikra.

Roma alihisi kabisa kama kitu hichi kitaendelea basi atakuwa na uwezo wa kuelewa kanuni za anga bila hata ya kujifunza, lakini swali likaja imetokea tokea vipi , ni kwa yeye tu au hata pia kwa miungu mingine

Roma aliingia kwenye tafakari nzito ambayo ilikuja kutolewa na sauti ya Tannya.

“Master!!”

Roma aligeuza shingo yake na kumwangalia Tannya na palepale alipotezea kwanza alichokuwa akiwaza na kujiambia angemtafuta Christen baadae ili kumuuliza.

“Maimuna!!! , not bad appearance-wise and bearing-wise , you are realy Maimuna now , did the interrogation go well?”Aliuliza Roma.

Tannya alikuwa amebadilika kwa asilimia mia moja na kuwa Maimuna na usingemtoa dosari yoyote kama sio yeye, alikuwa amevalia mavazi yaleyale ya mara ya mwisho ambayo Maimuna alivaa na kilichomfurahisha Roma ni kwamba Tannya alikuwa katika levo ya mzunguko kamili na hivyo hivyo kwa Maimuna.

“Aliogopa kubakwa na wanaume hivyo alionyesha ushirikiano wa hali ya juu”

“Anaonekana sio mjinga , nadhani anajua ukiburi usingemletea faida yoyote , bado ana thamani kwetu hivyo hakikisha watu wako hawamdhuru , unaweza kukaa nae karibu pia ili kuendelea kumuuliza vitu ambavyo huelewi”Aliongea Roma.

“Sawa Master”

“Nadhani ni muda sasa wa sisi kuondoka, mimi nitakupeleka na kukusimika kama kiongozi”Aliongea Roma na palepale kupitia Dhana ya Jani la Upofu sura yake ilibadilika kabisa na akawa na muonekano kama wa Jini Imrah

Na kumfanya Tannya kuwa na mshangao usio wa kawaida , Roma aliamini wafuasi wa familia ya Mzee Sharif lazima wakubali Tannya kuwa kiongozi kama tu jini Imrah atamkubali.

Roma hakuwa na haja ya kumwelezea Tannya imekuwaje muonekano wake kubadilika bali palepale alimchukua Tannya kwa kumkumbatia na kisha akapotea nae kurudi Tanzania.

Roma alihitaji kumalizana na swala la familia ya Mzee Sharif na baada ya haada ya hapo asafiri kwenda Marekani kumtafuta Christen ili kujibu maswali yake.

ITAENDELEA , UNAWEZA SASA KUIMALIZIA KWA NJIA YA WATSAPP 0687151346
 
Boss sis tunakusubiri uku nafikiri tumalize sasa kama ulivyotupa ahadi..
 
Huyu mtu mbona anakuwa kama Tanesco? Yaan anaona tunapata raha sana tukiipata kwa muda sahihi?
 
Huyu mtu mbona anakuwa kama Tanesco? Yaan anaona tunapata raha sana tukiipata kwa muda sahihi?
Naona hii isidingo imegoma kuisha, ahadi ya kuisha mwezi wa tatu ilikuwa ni fix tu kutoka kwa Singano Jr.
 
Back
Top Bottom