NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI: SINGANOJR.
Mono no aware.
SEHEMU YA 687.
Magdalena na yeye alikuwa na spidi kubwa katika kusafiri na kwasababu alikuwa katikati ya levo ya nafsi basi isingekuwa tishio kwake kukiuka kanuni za asili za anga.
Roma alitumia uwezo wake wa kijini kumtafuta Magdalena na ndani ya dakika chache tu alimpata na walielekea pamoja.
“Master amesema tutampata katika msitu wa mianzi moja kwa moja, haina haja ya kusumbua wengine”Aliongea Magdalena mara baada ya kufika usawa wa Dhehebu la ngome ya Tang.
Roma alikuwa na shauku kubwa mno, alijiuliza kwanini Master wake Magdalena anataka kukutana nao kwa siri.
Baada ya kufika ndani ya msitu wa mianzi walianza kutembea , haikuwa mara ya kwanza Roma kufika katika eneo hilo na nje kidogo ya msitu huo ndio nyumba ya Master Tang Luyi ilipokuwa na mara baada ya kufika walikuta mlango upo wazi.
Wote waliingia na waliweza kumkutaTang Luyi akiwa amevalia gauni la rangi nyeusi akiwa amekaa mbele ya kioo.
“Master tumefika”Aliongea Magdalena huku akisalimia na kumfanya Tang Luyi kushituka kwani hakuwa amewaona.
Ilikuwa ni ngumu sana kwa Tang Luyi kutowaona kwani alikuwa tayari kwenye levo ya mzunguko kamili , ijapokuwa Roma alikuwa ameficha uwezo wake lakini Magdalena hakuwa ameficha uwezo wake.
Tang Luyi palepale aligeuka na kumwangalia Magdalena kwa mshangao na kisha akageuza macho yake kwa Roma , macho yake yalikuwa na hali ya wasiwasi mno.
“Kumbe mmeshafika?”Aliongea kwa sauti yenye kitetemeshi na kulazimisha tabasamu.
Magdalena kwa kumwangalia tu Master wake alijua kuna kitu ambacho hakikuwa sawa na palepale alimsogelea na kumshika mkono.
“Master kwanini mikono yako ni ya baridi hivi , kuna tatizo gani , kwanini umetuambia mimi na Roma kuja hapa kwa haraka?”
Master Tang Luyi aliishia kumwangalia Magdalena kwa macho yasiokuwa ya kawaida na ilionekana ni kama vile anataka kulia.
“Flamingo , mimi master wako nimekufelisha”Aliongea
“Unamaanisha nini?”
Master Tang Luyi alizungusha shingo yake na kumwangalia Roma kwa wasiwasi na kisha alimwachia Magdalena na kisha alisogea mbele ya Roma na katika hali ya kushitukiza alishuka chini na kupiga magoti , jambo ambalo lilimshangaza Roma
“Master!!!”
“Nini!! .,, Master wake Magdalena, We dada , Shangazi … Mchina…!!”Roma alikuwa akibabaika huku akijaribu kumnyanyua Master wa Magdalena lakini aligoma na muda uleule aliinamisha kichwa chake kwa namna ya kusujudu mbele ya Roma
“Mr Roma tafadhari naomba msaada wako ,muokoe binti yangu, ninakuomba tafadhari …”Aliongea huku akianza kutoa kilio.
“Binti yako!!!?”
Roma alikuwa katika mshangao na kuchanganyikiwa na aliishia kumwangalia Magdalena kama vile anahitaji maelezo kutoka kwake lakini aligundua hata yeye alikuwa kwenye mshangao.
“Master ni lini ukawa na mtoto wa kike ghafla tu , hujawahi kuniambia kuhusu hili?”Aliongea Magdalena aliechuchumaa akijaribu kumwamsha Master wake lakini aligoma na kutaka kuendelea kupiga magoti.
“Magdalena usinisimamishe , haijalishi ni kwa muda gani,napaswa kuwapigia magoti”
“Master haijalishi ni jambo gani naomba utuambie ukiwa umekaa tafadhali”Aliongea Magdalena na palepale alitumia nguvu ya kijini kumwamsha Master wake kwa nguvu.
“Magdalena umeingia levo ya nafsi!?”Aliuliza Master Tang Luyi kwa mshangao.
“Yeah ,,, ndio nipo katikati kufikia mwisho wa levo ya nafsi , zote shukrani ziende kwa mpenzi wangu , amenisaidia sana kama sio yeye nisingefikia hatua hii”
“Oh! sawa sawa … hakika ulichagua mtu sahihi kuwa nae , Master wako nina furaha kwa ajili ya mafanikio yako”
“Master nini kinaendelea , hebu nniambie kwanza”
“Ni stori ndefu sana , napaswa kuanza miaka ishirini iliopita”Alliongea Tang Luyi huku akipumua kwa nguvu.
Miaka mingi iliopita Tang Luyi alikuwa ni msichana mdogo kabisa katika ngome hio ya Tang , baada ya kujifunza mbinu za kichawi za mapigano alijihisi ni kama vile amepanda juu zaidi na kuanza kuletea ujeuri baadhi ya Master kutoka madhehebu mengine na yote hio ni kutokana kwamba alikuwa akijiamini sana lakini pia alihitaji uzoefu.
Siku moja wakati akiwa nje ya ngome alikuja kushuhudia tukio la wizi , mwanzoni alitaka kujaribu kuwa shujaa kwa kuzuia tukio lile na kufukuza wezi lakini alishindwa kwani wale wezi walikuwa wakitumia bunduki na yeye hakuwa na uzoefu na siraha hizo na katika purukushani za wale wezi alijikuta akijeruhiwa na risasi eneo la kiuno.
Dakika hio hio wakati akiwa anaugulia maumivu ya jeraha la risasi alitokea polisi mmoja ambaye ni kama vile ametokea mbinguni na kushuka na palepale aliwashughulikia wale wezi na kuwakamata wote na baada ya hapo alimchukua na kumpeleka hospitalini.
Tang Luyi alishangazwa sana na yule polisi wa kiume kutokana na namna ambavyo alikuwa akipigana , katika kipindi hicho msichana mdogo akiona kijana wa rika lake akipambana vizuri ilikuwa lazima imvutie na yeye hakuwa tofauti na wanawake wengine.
Alijikuta akimtamani sana yule polisi ambaye jina lake alifahamika kama Wang Sheng kwa namna ambavyo alitokea kumjali katika kipindi chote alipokuwa hospitalini.
Wang Sheng na yeye alitokea kuvutiwa na Tang Luyi na katika kipindi cha muda mchache tu walijikuta wote wakiingia kwenye penzi nzito , ijapokuwa Tang Luyi hakudhania kama atakuja kuwa katika mahusiano lakini ndio ikawa hivyo.
Miaka michache ya mahusiano yaliopelekea ndoa walifanikiwa kupata binti yao wa kwanza ambaye walimpatia jina la Wang Shu na kipindi hicho Tang Luyi na mume wake walikuwa wakiishi nje ya ngome ya Tang na mara baada ya kupata binti yao ilimfanya Tang Luyi kuwa na furaha sana na kujiona anamiliki ulimwengu.
Lakini sasa siku moja ikiwa ni siku tatu za kujifungua Tang Luyi aliamka asubuhi na kujikuta yupo peke yake , hakuwepo mtoto wala mume wake na kitu pekee alichoweza kukutana nacho ni ujumbe wa maandishi peke uliosomeka.
“Hatima yetu imefika ukomo , mwanaume anapaswa kwenda na upepo , kwenye droo kuna kidonge cha kijini , kitakusaidia katika nguvu zako za uzazi ulizopoteza kwaheri ya kuonana”
Ulikuwa ni ujumbe wa kuumiza sana ambao aliweza kuusoma Tang Luyi na alijihisi kama vile amefika siku ya kiama, uwepo wa kile kidonge ulimthibitishia mwanaume aliekuwa nae kwenye ndoa hakuwa binadamu wa kawaida bali alikuwa ni jini ambaye amemtumia tu kumzalia na kisha kuchukua mtoto na kupotea.
Baada ya Tang Luyi kupoteza mtoto ndio akarejea ndani ya ngome ya Tang Kuanza maisha mapya ya kimawazo na miaka kadhaa mbele alijifua zaidi na zaidi katika mafunzo mpaka alipokuja kumpokea Magdalena alieletwa hapo kama mwanafunzi katika projekti maalumu ya taifa la Tanzania katika uundaji wa kitengo cha wachawi.
Wakati Magdalena anafika alikuwa ni msichana mdogo na Tang Luyi alikuwa mkubwa tu , ni sawa na kusema Magdalena alikuwa na umri sawa na wa binti yake aliepotea hivyo licha ya kutofautiana rangi Tang Luyi aliamua kumlea Magdalena kimafunzo.
Stori ya Tang Luyi ni kama ilivyokuwa ya Bi Wema , wote walitumiwa na majini ili kuzaa , tofauti tu ni kwamba Bi Wema ndio ambaye alitia huruma sana kwani hakumjua mwanaume aliempenda alikuwa ni nani haswa na hata mara baada ya kupotea na mtoto wake hakutoa taarifa, yaani alipotea tu na alikuja kujua alikuwa jini mara baada ya kurudi kwa Rufi kwenye maisha yake.
“Lakini Master kwa ninavyojua moja wapo ya koo za kijini zilizopo ndani ya mipaka ya China ni Hongmeng na ukoo wa Xiao , kwanini alijitambulisha kwako kama Wang?”
“Baba aliniambia kwamba majini wengi huchagua maumbo ya sura kutokana na kupenda tamaduni ya jamii husika , kwa mfano **** majini ambayo yatachagua sura za kiarabu na meingine kuwa na sura za watu weusi , wazungu na wachina na wanapotoka katika ulimwengu wao kuja katika ulimwengu wa kawaida hujipa majina kutokana na muonekano wao lakini sio majina yao halisi, koo za kijini sio mbili wala tatu , koo zipo nyingi sana kwa mfano tu miliki ya kijinni ya Panasi inajumuisha koo nyingine ndogo ndogo ambazo zipo chini yao , hivyo hivyo Kekexil , Hongmeng na koo nyingine, hizi chache zinafahamika kutokana na kuwa na nguvu kubwa”
“Ukiachana na hayo , nini kimemtokea binti yako?”Aliuliza Roma.
“Usiku wa jana kuna mtu amerusha mshale karibu na mlango ukiwa umebeba hiki kidani na ujumbe….”Aliongea na kisha palepale alitoa kile kidani na kuonyesha.
“Hiki kidani nilimpatia binti yangu mara tu baada ya kuzaliwa , ni kidani ambacho nilipatiwa mimi wakati nilipozaliwa , hivyo ni rahisi kwa mimi kukifahamu”Aliongea na kisha alimpatia Roma ujumbe ulioandikwa kwa maandishi ya kichina na kwasababu alikuwa akikijua vizuri aliweza kusoma.
“Najua Wang Shu ni binti yako na Wang Sheng , huyu mwanamke mpaka sasa yupo kwenye mikono yangu akiwa na sumu mwilimi mwake , kama unataka binti yako awe salama na kurudi kwako , chukua mbinu ya kijini ya andiko la urejesho usio na kikomo kutoka kwa Roma Ramoni na njoo nayo juu mlima Fale siku ya kesho usiku saa sita , kama utachelewa Wang Shu atakufa”
Magdalena na yeye alikuwa amejifunza kichina hivyo aliweza kusoma ule ujumbe na alijikuta akiziba mdomo kwa mshangao.
“Master kwahio umetuitia kwa ajili ya hili.?”
“Najua hili ni jambo gumu sana kuomba lakini nipo tayari kufanya chochote ,najua pengine mtu huyu ananidanganya lakini bado najikuta nikitaka kuamini”
“Mlima Fale ndio mlima gani mbona sijawahi kuusikia?”Aliuliza Roma.
“Upo Kaskazini mashariki, ni sehemu ya safu za mlima Altai mpakani mwa China na jangwa la Gobi- Mongolia”
“Hivyo kama tusingekuja wewe ungeenda mwenyewe… huyu mtu nadhani ananijua vizuri nje ndani , maana kama anajua mahusiano yangu na Magdalena na wewe na Magdalena ana uhakika kabisa lazima anachokitaka atakipata , nina uhakika serikali ya China inahusika hapa”
“Kwanini tusimuulize Rufi , pengine anaweza kuwa na uelewa juu ya koo nyingine za kijini ambazo zinajiita Wang?”Alishauri Magdalena na Roma palepale aliona ni vizuri kufanya hivyo.
Alitoa simu ake na kumpigia Rufi na ndani ya dakika chache tu ilipokelewa na Roma akamwelezea.
“Honey umejuaje kuna familia ya Wang katika ulimwengu wa kijini , familia hio ni sehemu ya miliki ya ukoo wa kijini wa Xia , kuna majini wengi na binadamu wa kawaida ambao wana mafunzo makubwa ya kijini”
“Rufi ulishawahi kusikia jina la baba na mwana Wang Sheng na Wang Shu?”
“Wang Shu ni msichana wa pekee ndani ya familia ya Wang na baba yake Wang Mian ni jini mkuu kiongozi wa familia ya Wang , kuhusu Wang Shen sijawahi kusikia jina lake”
Roma alikuwa ameweka loudspeaker hivyo Tang Luyi na Magdalena waliweza kusikia na wote wakivuta pumzi mara baada ya kusikia familia hio ya kijini ipo
“Inaonekana majina yake hayakuwa feki lakini hatujui nani ambaye amemteka mtoto wako Wang Shu ..”Aliongea Roma mara baada ya kukata simu.
Roma hakuwa na namna zaidi ya kumsaidia Tang Luyi , alifanya hivyo kwasababu ni Master kwa Magdalena tu na sio vinginevyo.
Upande wa Magdalena hakutaka kumlazimisha Roma kumsaidia kwani masharti yalikuwa magumu sana na alijua kama Roma atatoa mbinu yake ya mafunzo itakuja kuwa hatari lakini Roma alimtoa hofu.
Kulikuwa na tofauti ya kimasaa kutoka Tanzania na China hivyo hawakukaa muda mrefu mpaka muda wa kwenda Mlima Fale kwa ajili ya kuonana na mtekaji.
Roma alikuwa na shauku ya kumuona mtekaji mwenyewe na mara baada ya kusafiri kwa dakika chache tu hatimae waliweza kufika juu ya jangwa la Gobi katika nchi ya Mongolia.
Jangwa hilo Roma alikuwa na historia nalo kwani wakati wa kujifunza mafunzo ya kijini alikuja kujificha huko na Master wake Tang Chi.
Baada ya kufika juu kabisa ya mlima Fale ilikuwa ni kama walivyotarajia kwani Roma kadri alivyokuwa akisogea alikuwa akihisi msuguano wa nguvu za kijini tena za aina mbili , moja ni nguvu ya levo ya mzunguko kamili na nyingine ilikuwa ni nguvu ya zaidi ya mzunguko kamili.
Haikuwa ngumu kumuona mtekaji kwani mlima huo miti yake ilikuwa ni ile mifupi ambayo imeachana achana kutokana na ukame.
Kilichomshangaza Roma mara baada ya kumuona mtekaji ni uvaaji wake , Mtekaji huyo alikuwa amevalia joho la rangi ya njano huku akiwa na nywele ndefu mno akiwa amezisuka kama mkia kwenda nyuma lakini uso wwake alikuwa ameufunika na Mask ya chuma cheusi na kumfanya kutisha kimuonekano.
Nyuma yake kulikuwa na kiroba kilichotengenezwa kwa katani na Roma mara baada ya kupiga jicho alikuja kugundua kuna mtu ndani yake ambaye ndie mwenye nguvu za kijini levo ya mzunguko kamili.
Mtu mwenye mask alikuwa katika levo ya kuyadhibiti maji na Roma aliona kabisa atakuwa hajapita levo ya dhiki bali yupo katika levo ya kuiepuka dhiki.
Ukumbuke levo ya kuipita dhiki ni tofauti na ya kuepuka dhiki , waliopo levo ya kuepuka dhiki ni majini ambayo yanafanya miujiza ya jini ambaye ameipita dhiki , yaani ni sawa na mwanafunzi wa darasa la kwanza kufanya mahesabu ya darasa la nne kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa akili.
“Waoh!! Inaonyesha kweli unampenda binti yako”Sauti ya kiume iliweza kusikika kutoka ndani ya lile Mask la chuma na Roma alijiambia kwanini ana bahati mbaya sana na hawa majini wanaojifunika sura na mavyuma alikumbuka kuna yule mtu mwenye mask ambaye hushirikiana na Athena.
SEHEMU YA 688.
Haikuchukua muda mrefu sana mtekaji yule alimhakikishia Tang Luyi kama mateka wake ni mtoto wake kwa kumtoa kwenye kile kiroba na kumuonyesha.
Licha ya kwamba Tang Luyi hakuwa akijua muonekano wa mtoto wake kutokana na kutengana nae muda mrefu lakini mara baada ya kumuona tu aliweza kuona kabisa alikuwa akifanana nae vitu vingi na hata Roma alithibitisha hilo.
Wang Shu alikuwa amewekewa sumu , mtekaji alionekana alikuwa amejiandaa vizuri , ilionekana kabisa hakuwa na mpango wa kupigana na Roma na hata upande wa Roma licha ya kujua anaweza kumpiga huyo na kumuua lakini hana uhakika kama ataweza kumuokoa Wang Shu ndani ya muda hivyo hakutaka kubeti.
Baada ya majadiliano ya muda mfupi Roma alitoa andiko la urejesho ambalo alikuwa ameliandika kabla ya kufika hapo na kisha kumpatia mtekaji na baada ya kuhakiki andiko ni lenyewe alitoa tabasamu la ushindi na kisha akapotea huku akisema ndani ya muda flani sumu ambayo Wang Shu ipo ndani ya mwili wake ingetoweka kwani ina muunganiko na nguvu zake za kijini.
Ajabu ni kwamba ilichukua sekunde tu kwa mtekaji kupotea na Roma hakuweza kunasa nguvu zake za kijini kabisa Roma alijiambia hata kama angekuwa na spidi kubwa kwa namna gani hawezi kupotea kwa haraka namna hio na palepale alijiuliza au hilo eneo kuna njia ya kuingia ulimwengu wa kijini.
Magdalena alikuwa ni mwenye wasiwasi mno , kabla ya kuja hapo alijua Roma alikuwa na mpango wa kutotoa mbinu yake ya mafunzo lakini nje ya mategemeo yake Roma alitoa mbinu hio kirahisi tu bila kuchukua hatua nyingine , alidhania labda Roma alikuwa amaendika andiko feki lakini mara baada ya kumuuliza Roma alimwambia aliandika kitu halisi ndio maana ilikuwa rahisi kumfanya mtekaji kumuamini.
Magdalena alimlalamikia Roma kwa kutoa mbinu yake kirahisi lakini Roma alimtoa hofu na kumwambia licha ya kumpatia mbinu hio haiwezi kuwa na msaada kwake.
Baada ya maongezi ya muda mfupi Roma aliondoka kurudi Tanzania huku Magdalena akimsindikiza Master wake na binti yake kurudi ngomeni.
*******
Upande mwingine mkoani Manyara kilomita kadhaa kutoka ziwani kulikuwa na hoteli kubwa ya kisasa iliokuwa ikipatikana ndani ya hili eneo , hoteli hii wamiliki wake walikuwa ni familia ya Mzee Sharif.
Ni hotelia mbayo imejengwa msituni na muundo wake ulikuwa ni wa tofauti kidogo, ukiangalia kwa juu ni kama vichuguu kwani kuna nyumba nyingi ambazo zilikuwa zimejengwa kwa ajili ya wageni.
Ilikuwa ni hoteli ya kitalii ya hadhi ya juu sana ndani ya mkoa huu na ilikuwa imepokea tuzo World Luxury Hotel Award kwa mwaka 2020 na hili iliifanya hoteli hii kutembelewa na watu wakubwa wakiwemo wafanyabiashara, wanamichezo na matajiri.
Lakini sasa tofauti na siku zote hoteli hio usiku huo kulikuwa na hali ya kitofauti kidogo kwani haikupokea mgeni na hata wale waliokuwepo walihamishiwa kwenye hoteli nyingine na asilimia kubwa ya watu waliokuwepo hapo ilikuwa ni walinzi , wanafamilia wa Mzee Sharif na wafuasi wa dini yao.
Dakika ambayo Roma aliweza kufika juu ya hoteli hii alijikuta akitoa tabasamu la kifedhuli kwani chini yake aliweza kuhisi msuguano wa nguvu za kijini za levo ya nafsi lakini pia kulikuwa na msuguano wa nguvu za kijini levo ya kuipita dhiki.
Jambo hili lilimshangaza Roma na alijiambia familia hii sio ya kawaida kabisa na kuna mengi ambayo yamejificha.
Wakati huo ndani ya eneo hilo kulikuwa ni kama kuna tafrija kwani kulikuwa na watu wengi ambao walikuwa wameketi kwenye meza ambayo ilikuwa na vyakula mbalimbali.
Watu hao wengi wao walikuwa ni familia ya mzee Sharif lakini pia kulikuwepo na baadhi ya watu ambao hawakuwa na uhusiano na familia hio lakini walikuwa na vyeo vya Wakuu wa Chemba kulingana na tamaduni za dini ya kidhehebu lao.
Vilikuwa ni vyeo ambavyo hupatiwa viongozi ambao husalisha waumini katika matawi ya imani yao.
Ijulikane kwamba Mzee Sharif alikuwa na dini yake na kusalia miungu yake kabisa na alikuwa pia na wafuasi wake na matawi ambayo wafuasi husalia huongozwa na Wakuu wa Chemba na hao mara nyngi ni binadamu wa kawaida.
Watu wengine waliokuwepo ndani ya enoe hilo ni mwanamke na mwanaume ambao wote walikuwa ni jamii ya kiarabu kabisa akiwemo lakini majini wakiongozwa na Imrah.
“Nina hatia kwa mualiko wetu kwenu Mkuu Nayo na Wami awamu hii, Mimi Jini Imrah ninawasalimu kwa kunywa kikombe hichi kama malipo ya usumbufu”Aliongea na kumfanya yule mzee alieitwa Nayo kutoa kicheko.
“Mkuu Imrah huna haja ya kufanya hivyo , sisi kama majini kutoka familia mbalimbali wote tunaunganishwa na jina moja la ukoo ambalo ni Sharif, tumekuwa watiifu kwa ukoo na ndio maana leo hii tumweza kupata uwezo huu tuliokuwa nao mpaka kualikwa , imekuwa heshima kwangu mimi na mke wangu Wami kutoa mchango wa kwenda kumuua mwizi ambaye ameiba hazina yetu”
“Upo sahihi , Mkuu Imrah umezidisha ukarimu kwetu mimi ba mume wangu…”Aliongea mwanamke mrembo sana aliekuwa amekaa karibu na Nayo huyu mwanamke ndio alieitwa Wami, alikuwa mrembo haswa mweupe mwarabu ambae kimakaridio ana umri wa miaka kama arobaini hivi.
Ijapokuwa walikuwa na uwezo mkubwa wa kijini lakini mbele ya Imrah bado walikuwa chini kicheo kwani familia hio haikutoa cheo kulingana na uwezo.
Ili kumdhibiti Roma kisawasawa hao ndio waliotoka huko walikotoka na kufika hapo na familia nzima akiwemo Mzee Sharif mwenyewe alijua kabisa Roma hachomoki.
“Maimuna kwanini Roma mpaka sasa hivi hajafika , si ulisema umewasiliana nae na akasema yupo njiani?”Aliuliza Mzee Sharif.
Maimuna alimdanganya Roma kwamba babu yake na familia nyingine wangekuwa na kikao cha siri sana ndani ya hoteli yao iliopo Manyara na Roma anapaswa kutumia nafasi hio kupiga bomu wanafamilia hao na kama serikali ingeuliza kuhusu tukio hilo Maimuna yeye angetangaza ni maadui wa kifamilia.
“Babu labda …..”
“Boom!!!!”
Maimuna kabla hata hajamaliza sentensi katika eneo la katikati ya hoteli hio kulikuwa kumejengwa sanamu ya Kifaru ambayo imezingirwa na maji na yote ililipuliwa na kuharibika na kufanya watu wote kupiga yowe.
Dakika ileile kila mmoja akijiuliza nini kimetokea hatimae Roma aliweza kuonekana akiwa amesimama juu ya paa la nyumba ambayo ilikuwa katika hatua za ki ujenzi.
“Romaa…!!!
Mzee Sharif ndio wa kwanza kumtambua Roma na alipiga yowe kwa nguvu huku sura yake ikiwa nyekundu kwa hasira.
Imrah , Nayo , na Wami wote walijikuta wakiingiwa na mshangao kwani kwa haraka haraka waliweza kugundua alichotumia Roma kulipua ni nguvu za kijini, sasa walijiuliza kwanini hawaoni uwezo wake wa kijini kiasi cha kushindwa hata kuhisia kama amefika.
Kutokana na taarifa walizokuwa nazo ni kwamba Roma alikuwa na mwili wenye nguvu tu ya kuhimili mapigo ya kijini na hakuwa na uwezo mwingine .
“Inaonekana mna hamu kubwa ya kuniona nikiwa maiti , yaani mmewahi wenyewe na kujikusanya sehemu moja mkinisubiria”Aliongea Roma.
“Wewe mtoto acha kuonyesha kiburi mbele ya Mkuu Wami na Nayo , leo walinzi wetu wa familia watakukamata , huwezi kutumia mikombora yako tena hapa , jisalimishe mapema na rudisha hazina yetu”Aliongea Imrah kwa kujigamba.
Roma aliishia kutoa tabasamu la kejeli na kisha palepale alitumia nguvu za kijini na kutoa lile jiwe lao la hazina kwenye hifadhi pete yake.
“Yaani ndio mmenikumbusha hapa , mnaichukuliaje hii kokoto kuwa hazina, mtu yoyote ambaye ataniambia maana yake basi nitamuacha aendelee kuishi leo hii”
Roma tokea ajifunze mbinu za kijini hilo jiwe ndio kitu pekee ambacho hakuwa akikielewa kabisa tokea akipate , hata baada ya kurudiwa na nguvu zake za kijini alishindwa kuweza kutambua kabisa kitu hicho kwani hakikuwa na nguvu za kijini , lilikuwa jiwe kama jiwe lakini familia hio ilikuwa ikilichukulia kama hazina.
Lakini sasa kuona familia hio ilikuwa ikifanya juhudi kutaka kuirudisha ilionekana ni kitu chenye thamani lakini ilimsumbua akili kutoelewa uthamni wake unatokana na nini.
“Acha kujigamba , maongezi yako na Maimuna tumeyarekodi na ulikiri kwa mdomo wako wazi umeiba hazina yetu , ni ushahidi tosha kwetu wa kukuchukulia hatua , kama leo hii usiporudisha hazina yetu hatutojali wewe ni mtoto wa nani ndani ya taifa hili tutakupoteza”
“Nina mashaka hata wewe na ujini wako hujui hiki kitu ni nini , lakini kama hamtaki kuongea basi nadhani nitawafanyia majaribio kwa mbinu yangu mpya ya kimaajabu niliogundua ndani ya siku hizi mbili”
“Mkuu Imrah acha kujibishana nae mpandieni hewani mumkamate na chukueni hazina yetu na kisha tafuta vidonge vyake vyote na mbinu yake ya mafunzo na muda ukiwadia ukoo wetu utakumbukwa kwa mafanikio yetu”
Jini Imrah alitingisha kichwa palepale , alijua kabisa wapo na majini wenye nguvu ndani hapo na alipaswa kuhusika pia katika kushambulia ili aonekane na yeye alikuwa shujaa.
“Wewe mvulana , ni kosa baya sana umefanya kuchokoza ukoo wetu”
Mwanamke mrembo Wami aliongea na alikuwa ndio wa kwanza kumsogelea Roma huku akiwa ameshikilia upanga ukatao kuwili ambao ulikuwa ukiwaka waka.
“Chukua pigo langu la mwezi mwandamo mwanaharamu wee”
Aliongea kwa nguvu na palepale nguvu ya kijini ilimtawala na kufumba na kufumbua alifutika alipokuwa amesimama na ile anakuja kuonekana alikuwa mbele ya Roma huku ile siraha yake ikitoa mng’ao ikiwa imejikunja kama vile ni mwezi unaoandama huku ikiwa imetawaliwa na nguvu kubwa ya kijini ambayo iliambatana na ubaridi mkali sana.
Roma mbinu hio aliona kabisa ni ya kitoto kwake , na aliinua mkono wake kidogo tu na kuachilia nguvu ya kijini na palepale ile nguvu iliomtoka jini Wami ilioputana na ya Roma ilisambararishwa.
Nguvu zile mara baada ya kukutana ni kama vile zilikataana kwani zilisambaa na kwenda kupiga kwenye nyumba iliokuwa imeezekwa kama kichuguu na palepale paa lake likaharibika huku mawe mengi yakiruka na kwenda kuwashambulia walinzi waliokuwa wakilinda ndani ya eneo hilo na kuwajeruhi.
Jini Wami alipatwa na mshangao wa tukio lile na palepale pasipo kumsogelea karibu Roma aliendelea kufyeka ule upanga hewani huku ukitoa nguvu ya kijini ambayo ilibadilika na kuwa mithili ya mng;ao wa mwezi mwandamo na kumlenga Roma.
Hio ndio mbinu ya mwezi mchomoko aliokuwa akimaanisha , yaani nguvu yake ilikuwa kwenye ule upanga ukatao kuwili na kila anapofyeka hewani ulituma shambulizi la kimwezi mchomoko na kumshambulia Roma.
Lakini sasa Roma ni kama alikuwa akifanya makusudi kwani aliacha mapigo yale kumfikia na kumshambulia lakini hayakuonyesha athari yoyote ile.
Wami alishangazwa na jambo lile kwani shambulizi lake ni kama lilikuwa likisambaratika kila linapomfikia Roma.
“Ni mwili wa aina gani wa kishetani uliokuwa nao , yaani huumii hata kidogo?”Aliongea Nayo kwa nguvu mara baada ya kuona hakuna shambulizi ambalo linamuathiri Roma .
Upande wa Jini Imrah alikuwa na wasiwasi Roma anatoroka hivyo na yeye alifuatia kushambulia.
“Nguvu ya Jani la Mtendee..!!!!”
Aliongea kwa nguvu kilugha na palepale mbele ya kiganja cha mkono wake ulitoa mwanga kama vile ni jani la mtende na nguvu za kijini zilianza kuchomoza huku zikiwa katika staili kama vile ni majani na kuanza kupelekea upepo mkali.
“Duara la Moto!!!”
Aliongea Jini Nayo na yeye na palepale kulitokea maduara ya moto kama mishale kutoka juu na kumvaa Roma kutoka kichwani na kuanza kumzingira.
Roma hakujali sana kuhusu mashambulizi hayo na palepale aliinua kiganja chake cha mikono na kuachilia nguvu ya kijini ambayo ilivaana na zile boriti za nguvu za kijini zilizokuwa zimemzingira.
Wakati Imrah akimtengenezea mtafaruku Roma upande wa jini Nayo na Wami walikuwa wakimshanbulia kwa kasi
Watu waliokuwa chini walikuwa wakiangalia mapigano hayo bila ya kuelewa kinachoendelea lakini walikuwa wakiwaangalia majini wao wakipambana tu na walikuwa na matumaini ya kushinda.
“Mimi kama mkuu wa ukoo katika ulimwengu na kiongozi wa imani ya utajiri, Roma Ramoni leo ni siku yake ya hukumu”Aliongea Mzee Sharif kwa chuki kubwa na palepale wafuasi wa imani ya utajiri pamoja na ndugu walipiga makofi ya shangwe.
Upande wa Maimuna macho yake yalikuwa yamechanua na alikuwa na umakni mkubwa katika kufatilia pambano na hakuonyesha furaha wala huzuni.
Lakini sasa dakika hio hio Roma ambaye alikuwa akishambuliwa na mapigo ya nguvu za kijini hakuwa akihisi chochote ni kama vile kuna vitu vinamtekenya tu kutokana na uwezo wake wa kijini kuwa mkubwa zaidi , sasa ile nguvu ya mbingu na ardhi iliokuwa ikimzingira iliongezeka kadri ambavyo alikuwa akishambuliwa
Hoteli hio ilikuwa imejengwa kitamaduni zaidi hivyo hata kuezekwa kwake ni kwa nyasi na mapaa yake yote yalikuwa yameharibika huku baadhi ya nyumba zikiwa zishaanza kubomoka kutokana na upepo mwingi na nguvu ya kijini iliokuwa ikisambaa.
Dakika ileile boriti nyingine ya nguvu ya kijjini ambayo ilimsogelea kama Mshale ilimkaribia na Roma alijiambia kuendelea kuwasoma wanavyopigana ni kupoteza muda hivyo ni zamu yake kushambulia.
Palepale alimsogelea Nayo kwa spidi na kumshika mkono na akaruhusu nguvu za kijini kumtoka na kuanza kumvaa na palepale nguvu ile ya kijini ilianza kubadilika na kuwa maji.
Jini Nayo macho yake yalisinyaa na kabla hajajua cha kufanaya alikuwa ashachelewa kwani alijua tayari kuna kitu ambacho hakipo sawa kuhusu Roma
“Asilimia tisini ya mshambulizi yako hayakunilenga , hivyo ni kama vile umepoteza nguvu zako tu , unao uwezo mkubwa lakini ukweli ni kwamba mashambulizi yako ni ya kijinga jinga”Aliongea Roma na palepale kulitokea kitu kama povu la sabuni na kumfunika Jini Nayo .
“Hii.. ni..”
Wami na Imrah walijikuta wakipagawa kwani Nayo alikuwa amekamatika kirahisi mno na Jini Nayo aliishia kuita jina la mke wake tu kama ishara ya kumpa tahadhari na palepale alipoteza maisha huku roho yake ikioshwa na maji ya kiroho.
Maji ya kiroho ilikuwa ni kama vile ni tindikiali na inapogusana na jini ambalo lina uwezo mkubwa wa kijini linapotumia kwa jini mwenye uwezo mdogo ni kama vile ni mionzi ya nyuklia na maji yake hayaumizi mwili bali yanaumiza roho au nafsi.
Jini Nayo alikufa palepale na kuwa kama maiti ya kawaida tu huku macho yake yaliobadilika rangi yakichomoza nje.
“Hili linawezekana vipi ,,, au tuseme upo katika hatua ya kudhibiti maji ya kiroho ,,, subiri hata kama iwe hivyo hatujawahi kusikia binadamu yoyote ambaye ana uwezo wa kudhibiti maji ya kiroho”Aliongea Wami , hakuwa katika hali ya kumuomboleza mume wake lakini alikuwa katika hofu ya uwezo wa Roma.
Mpaka hatua hio alishajua kuendelea kupambana na Roma ni kujitafutia kifo tu.
Roma hakua na haja haya ya kumuelimisha na palepale kama kivuri alimsogelea na moto uliokuwa kama radi , rangi ya Zambarau ulitokeza katika mikono yake.
Siku ya jana yake wakati Roma akifanya tahajudi ili kugundua ni nguvu ipi aliweza kuipata baada ya mapigo ya radi tisini na tisa na alikuja kugundua kwamba radi ya Zambarau huundwa na mchanganyiko wa elementi za maji pamoja na msuguano wa Plasma hivyo alijaribu kudhibiti Free electrons ambazo zipo hewani na kisha kuzisuguanisha na elementi za maji.
Jini Wami kabla hata hajajiuliza imekuwaje Roma kutoa shoti za rangi ya zambarau kama radi lakini alikuwa amechelewa kwani Roma alimsogelea kwa kasi na kumchapa ngumi ya tumbo ambayo iliungana na zile shoti na nguvu ya kijini.
Mlio uliosikika ni kama vile puto linapopasuka na mkono wa Roma ulipita huku cheche za moto zikijitokeza na kuanza kuyeyusha mwili wa jini Wami kwa kasi sana.
SEHEMU YA 689.
Roma aliridhishwa na nguvu mpya ambayo amejipatia , ijapokuwa mshindani wake alikuwa dhaifu kumdhibiti kwa pigo moja tu lakini hata hivyo alichukulia kama mafanikio kwani ni kitu ambacho kimefanikiwa.
Roma ni kama alivyofikiria siku ya jana , majini wote ambao hawajapita dhiki lakini wana uwezo wa kudhibiti elementi za maji hawawezi kuhimili shambulizi moja la siraha yake mpya aliogundua.
Roma hakuona haja ya kutumia chungu kuwamaliza kutokana na wote walikuwa dhaifu sana hivo aliona kitu pekee ni kuwamaliza na nguvu ya kijini tu ya radi ya zambarau.
Familia yote ya Sharif ilikuwa katika bumbuwazi , dakika chache zilizopita walikuwa na uhakika wa kushinda lakini nini kimetokea , yaani wamepoteza namna hio.
Mzee Sharif na mtoto wake na wengine wote walikuwa wakipatwa na jasho ambalo sio la kawaida , upande mwingine Maimuna alikuwa kwenye mshituko na alionyesha hali ambayo haikueleweka katika macho yake.
Sekunde chache tu Wami alikuwa ameharibiwa mwili wake huku Jini Nayo mwili wake ukishuka kutoka juu huku ukiwa umetengeneza michirizi kama mizizi ya mti.
Aliebakia alikuwa ni jini Imrah pekee na alikuwa akitetemeka kama vile tayari alishajua huo ndio mwisho wake.
“Imetokea tokea je hivi jamani…”Aliongea kwa huzuni na muda uleule akijiandaa kukimbia lakini Roma ni kama alitegemea nini angefanya kwani palepale nguvu zake za kijini ziligeuka kama kamba ndefu na kumzingira jini Imrah
Alikuwa kwenye levo ya nafsi tu hivyo spidi yake ilikuwa ndogo ndio maana Roma alimuwahi na asingeweza kujitoa kwenye kamba alizofungwa nazo.
“Hii ni kama heshima kwako kufa na moto wa bluu”Aliongea Roma kwa sauti kavu na dakika ileile jini Imrah aliyeyuka kama karatasi inayoungua.
Roma alifanya mashambulizi matatu tu na yote yalimaliza majini yote matatu kwa wakati mmoja na kama sio uharibifu uliotokea chini yake hakuna mtu ambaye angejua kama kuna mapigano ya majini na binadamu yalitokea hapo.
Walinzi na wafuasi wa familia ya Mzee Sharif walijikuta wakiwa katika hatari , mbele ya nguvu kamili walikuwa ni kama kuku tu.
“Roma fikiria mara mbilimbili , huu sio mwisho wa uwezo wetu , kama utatudhuru basi subiria ghadhabu ya wakuu wetu , ninaapia kufanya mazungumzo ya amani na wewe na kuacha hili lipite”Aliongea Mzee Sharif na kumfanya Roma kutoa kicheko.
“Naona sasa unataka tufanye maongezi, nilijua ungepiga magoti kuomba au kujiua mwenyewe kuniepushia dhambi “
“Unathubutu vipi kunidhalilisha , mimi siwezi kupiga magoti mbele ya wafuasi wangu”Aliongea kwa hasira lakini dakika ileile mara baada ya Roma kukanyaga ardhi Maimuna alikimbia mbele na kupiga magoti mbele ya Roma.
“Master , Hongera kwa ushindi wako na kisasi”Aliongea Maimuna na kufanya watu wote kumwangalia kwa mshangao.
“Maimuna!!”
“Mai..!!”
“Unathubutu vipi kutusaliti?”
Sauti mbalimbali zilimwita Maimuna kwa kufoka na mshangao lakini Maimuna hakujali laana wala matusi yao, alimwangalia Roma kwa macho yaliojawa na heshima na matamanio.
“Unafuraha kweli ya mimi kushinda au ndio unafiki ?”Aliuliza Roma
“Bila shaka Master , tafadhari nisamehe mimi kwa kutokuwa na uwezo wa kupigana pembeni yako lakini nilikuwa na wasiwasi juu yako muda wote , ninayo furaha kuona hujadhulika”
“Masikini usie na aibu wewe , wewe ni laana ya ukoo wetu , msaliti mkubwa wewe”Aliongea Mzee Sharif kwa hasira.
“Haha… hivi ulifikiria nitawasaidia ili tu kumsaiti Master wangu wakati mlichukulia maisha yangu hayana thamani , nilijiapiza lazima niharibu hii familia hivyo acha kunilaumu”Aliongea Maimuna akimwangalia babu yake kwa kejeli.
“Nitakuua Maimuna”Aliongea baba yake kwa hasira.
Maimuna alikuwa kwenye levo ya mzunguko kamili hivyo hakumhofia baba yake tena ambaye alikuwa kwenye levo ya nusu mzunguko.
“Master , Mzee Sharif amelinda hili eneo kwa umakini mkubwa na kunipelekea kusindwa kutega mabomu hivyo naomba umuue kunisaidia kulipa kisasi”Aliongea Maimuna na kumfanya Roma kutoa tabasamu la kejeli.
“Hawa watu kwangu ni kama kunguni tu hivi na kuua mmoja mmoja ni kupoteza muda hivyo nitawaua kwa shambulizi moja “Aliongea Roma na palepale nguvu ya kijini ilitoka kama moto uliokuwa katika umbo la vinyoka nyoka na kuanza kuwashambulia kwa kasi.
Moto wa njano wa kijini licha ya kwamba haukua mkali lakini ulikuwa na athari kubwa kwa mtu ambaye hana nguvu za kijini. Au ambao wapo katika levo ya mzunguko kamili.
Vilikuwa ni vilio vya kusaga meno ambavyo vilisikika ndani ya hilo eneo ni kama vile tayari wapo jehanamu na wanapokea adhabu yao ya kumuasi Mungu na kusalia miungu.
Roma alijikuta akihema kwa nguvu na kujifikiria ameua watu zaidi ya mia moja usiku huo lakini licha ya hivyo hakujihisi kabisa hatia.
Dakika chache tu ilibakia majivu na hakuna kilichoonekana hapo ndani hata mfupa haukubakia na mtu pekee ambaye alibakia ni Maimuna peke yake.
Wakati Roma anaruhusu moto Maimuna alikuwa amezingirwa na nguvu za kijini hivyo ule moto haukumgusa ,Roma alifanya hivyo kwasababu hakuwa na muda wa kudhibiti vinyoka vya moto kwani vilishambulia kila kiumbe chenye nguvu ya kiroho ndani yake.
Roma mara baada ya kuona kila kitu kimeisha palepale alimchukua Maimuna na kupotea nae na kufumba na kufumbua alikuwa juu ya kilele cha Maweni Mlima kilimanajro huku akiwa amemshikilia Maimuna.
“Kwahio bado utaendelea kuongea ujinga?”Aliongea Roma mara baada a kumtua chini Maimuna.
“Master bado sijakuelewa”
“Unanionga mjinga?, Majini wawili walikuwepo na hukuniambia , ulitaka kuona nani atashinda si ndio? , naamini ulipanga kuona upande wowote kushinda , kama ningeshindwa ungepata sifa na kama wangeshindwa ungerithi kila kitu, haikujalisha matokeo uliamini kila upande utakaoshinda ungefaidika”
“Hapana Master , Sikuweza kukujulisha ndani ya muda kwasababu walikuwa wakiniangalia sana kwa ukaribu”
“Oh ,,, haya niambie ni kwa namna gani walijua kama nina vidonge , si nilikuambia iwe ni siri , unataka kuniambia walifahamu wakati ulipokuwa ukivuna nishati za mbingu au imetokea kwa bahanti mbaya?”
“Ndio , ndio , sikuwa makini Master walinikamata wakati nameza baaada ya kushangazwa na kupanda levo kwa haraka”
“Kwa hio unamaanisha haya ni makisio yangu tu , kwasababu sina ushahidi siwezi kusema umennisaliti si ndio?”
“Ndio Master , tokea siku ambayo nilitoka kwenye ile boti sikuwahi kuwaza nitakusaliti m mimi nilikuwa mtu wako mwaminifu”
“Hujui mambo mawili kuhusu mimi wewe ,, kwanza ninaweza kuua mtu yoyote hata kama sina ushihidi ili mradi namshuku tu pili siamini kuhusu uaminifu unaongea hapa ambao umeuharibu wewe mwenyewe tena umeenda mbali hata kuweka kisasi na familia yako”Aliongea Roma huku akimwangalia Maimuna kwa macho makali.
“Master tafadhari naomba usiniue nitakupa kila kitu”Aliongea Maimuna huku jasho likimtoka na dakika hio hio alichana chana gauni lake ambalo alikuwa amevaa na kubakia uchi.
“Master naomba unifanye niwe wako , nipo safi kabisa , Master nina uhakika utaweza kuhisia ukunjufu wangu wa moyo”
Ili tu kupata nafasi ya kusihi Maimuna alitupilia mbali utu wake na alipiga magoti chini akiwa hana nguo huku akimuonyesha Roma sehemu zake za uzazi zilivyo na hakuishia hapo tu alimsogelea na Roma karibu na kuanza kujisuguanisha nae.
Maimuna alikuwa mtundu mno , ijapokuwa ni kweli Roma aliona alikuwa hajaguswa lakini alijua kutokana na namna anavyo jua kujiigizia mbele yake basi hata kunako sita kwa sita atakuwa na utundu wa hali ya juu, kutokana na mwanga wa mwezi aliweza kuona kila kitu na jamaa mdogo alishindwa kuvumilia na kuanza kufurukuta.
Lakini Roma hata hvyo hakutaka kumgusa , isitoshe Maimuna licha ya uarabu wake hakuwa akimfikia Amina kwa uzuri, hapo tu hujalinganisha na warembo wengine kama Najma,Nasra na Rose.
Uhuni wa Maimuna ulisukumwa na tamaa zake na kama angalau angelinda utu wake hata katika hatua kama hio basi Roma kidogo angerudisha moyo nyuma lakini maigizo yake yalimfanya kumpuuza zaidi na zaidi.
“Hata kama unionyeshe kila kitu sikutamani unadhani nitakutamani mwanamke kama wewe ?”Aliongea Roma na maneno yale yalimchoma mno Maimuna na alijikuta akitoa machozi.
Ijapokuwa katika eneo hilo kulikuwa na upepo na baridi kali lakini kutokana na uwezo wake wa kijini alikuwa sawa hata katika kupumua lakini mara baada ya kuambiwa maneno hayo na Roma alijihisi kukosa pumzi ghafla.
“Unalia nini ,naona nimegusa penyewe , ndio unaonyesha kukasirika sasa hivi?”Aliongea Roma kwa kejeli na Maimuna palepale alipotezea uchungu wake wa moyo na kujigeuza katika hali ya kutia huruma.
“Siwezi kukukasirikia , tafadhari Master naomba uniamini , sijaguswa na mwanaume yoyote yule , nilichofanya ni kutaka tu kuwa na wewe”
“Huna maana tena , lakini nadhani ni vizuri maana sitopoteza tena juhudi zangu juu yako’
Maimuna hakuelewa Roma anachomaanisha lakini dakika ileile alikumbana na nguvu ya kijini ambayo ilimfanya kupoteza fahamu palepale Roma alimbeba na kupotea nae.
*******
Upande wa anga la jiji la Dar es salaam kulikuwa tayari giza lishaingia na kufanya taa nyingi kuwaka na kupelekea jiji hilo kupendeza.
Upande wa Ununio sauti pekee ambazo zilikuwa zikisikika ni za mawimbi ya bahari pamoja na baadhi ya sauti za magari na pikipiki ambazo zilipita mara moja moja kutokana na utulivu wa mtaa huo.
Dakika chache mbele gari aina ya Audi A8 toleo la mwisho rangi nyeusi ilisimama mbele ya geti la nyumba ya Edna.
Dakika hio hio mlango wa abiria uliweza kufunguliwa na mwanaume alievalia suti na kumruhusu mwanaume alievalia jacket na kofia ya hat pamoja na miwani kushuka.
Alikuwa ni Raisi Jeremy na kwa staili ya uvaaji wake ilionekana ni dhahiri kabisa hakutaka mtu yoyote kumfahamu.
Baada ya kusogelea geti palepale aliminya kengele maalumu nje ya geti hilo na ndani ya dakika chache tu sauti ilisikika kutoka ndani na ilikuwa ni ya Bi wema.
Upande wa ndani Bi Wema alikuwa bize kuangalia tamthilia na mara baada ya kusikia kengele hio aliangalia kwenye kifaa maalumu cha kuweza kutambua nani anabonyeza kengele na palepale mara baada ya kuangalia kwa umakini alishtuka na kisha akakimbilia nje.
“Mheshimiwa!!?”
Aliongea Bi Wema kwa wasiwasi mara baada ya kufungua geti , alikuwa akimjua Raisi wa Rwanda kwani sio mara ya kwanza kumuona na alikuwa akijua ni baba yake Edna na alikosa ile hali ya kujiamini kwani alikuwa mtu mzito.
“Hello Bi Wema … naomba radhi kwa kuwavamia usiku huu lakini sikuwa na muda mchana , Edna yupo ndani?”Aliuliza Raisi Jeremy kwa tabasamu.
Upande wa Bi Wema alijikuta akijisikia vizuri kwa Raisi Jeremy kumuongelesha kwa upole .
“Edna ndio… “
“Bi Wema huyo mgeni ni nani?”Sauti ya Edna kutoka ndani iliweza kusikika.
SEHEMU YA 690.
Bi Wema alikuwa ametoka nje kabisa ya geti , Edna mara baada ya kusikia kengele alitoka kujua ni mgeni gani kafika muda huo lakini mara baada ya kuangalia hakumuona Bi Wema na alijikuta akitembea kuelekea getini.
Raisi Jeremy mara baada ya kusikia sauti ya Edna alijikuta mapigo yake ya moyo yakienda kasi na alishindwa kujizuia na kupiga jicho ndani na palepale aliweza kumuona Edna ambaye alikuwa amevalia gauni na visendo manyoya akitembea kuja getini.
Dakika ambayo Edna alimuona Raisi Jeremy alisimama palepale na kushindwa kusogea mbele kama vile amegandishwa.
“Edna nimefurahi nimekukuta hujalala naamini hutojali kwa ujio wangu huu wa ghafla”Aliongea Raisi Jeremy huku akitoa tabasamu.
“Una sababu gani ya kuja usiku huu nyumbani kwetu mheshimiwa?”Aliongea Edna.
“Nilitaka kuja mapema lakini nilikuwa bize sana na vikao na vilisha muda umeenda lakini nilihitaji kukuona kabla sijarudi Rwanda kesho”
“Sawa umekwisha kuniona tayari mheshimiwa naomba uondoke”Aliongea Edna kikauzu hakujali kama Jeremy alikuwa baba yake au raisi , nadhani alimzingatia kama baba yake mzazi kuliko raisi kutokana na alivyokuwa na hasira.
“Edna najua pengine hutaki kuniona lakini ninataka tuongee tafadhari naomba leo unipe kampani ya kupata chakula cha usiku pamoja , sijapata dinner bado na nina njaa”Aliongea na Jeremy mara baada ya kuona hapewi jibu aliongezea.
“Please , my daughter”
Edna muda huo alishageuka na aliishia kung’ata lips zake na kauli ya kuitwa mwanangu ilimlainisha.
Kwasababu mheshimiwa ameomba sana aliona itakuwa ukatili kumkatalia, baada ya kuvuta pumzi nyingi aligeuka.
“Bi Wema nitachelewa kurudi , unaweza kwenda kulala mapema kama umechoka”Aliongea Edna na kumfanya Raisi Jeremy kutoa tabasamu.
Edna hakuwa na haja ya kubadilisha isitoshe alikuwa amevalia mavazi ya kawaida na hata visendo vyake havikuwa na shida hivyo aliingia kwenye gari la baba yake mzazi na kisha liliondoshwa.
“Edna unaijua hoteli ya White Sand , ile ni hoteli yetu, mara nyingi napenda kwenda kulala pale ninapokuja Dar kwa safari za siri”Aliongea Raisi Jeremy mara baada ya kumwangalia Edna akiwa amekodolea nje kupitia kioo akikwepesha macho na Jeremy.
“Tafadhari mheshimiwa usinijumuishe, mimi ni Edna Adebayo na itabakiwa kuwa hivyo”
“Edna najua ni ngumu kwa wewe kunikubali mimi kama baba yako kutokana na kukukosea mara nyingi , vilevile najua ni ngumu kwa wewe kurudi kwenye ukoo wetu lakini unapaswa kujua kwasasa sijali sana watu wananionaje , nmekuja kugundua uhusiano ambao hufungamanishwa na damu hauwezi kuvunjika , watu wengi ndani ya nchi hii washajua tayari wewe ni binti yangu na hata ndani ya Rwanda na haijalishi wanasema nini lakini ninajivunia kuwa baba yako , najua nimekuumzia mara nyingi na matendo yangu pengine na maneno yangu pia lakini najutia na kuomba msamaha kiasi cha kunifanya usiku kukosa usingizi na kupandwa na ndoto za mara kwa mara , kila siku kunapokucha moyo wangu huuma sana kujua kwamba sipo huru kuwasiliana na wewe , najihisi sina thamani , mara ya mwisho wakati familia ya mumeo ilipokuwa kwenye matatizo nilitaka kuja kukuchukua na kukurudisha Rwanda lakini nilikuwa na wasiwasi kwamba ungekataa na nikaishia kuweka matumaini kwa Roma kwamba atalimaliza tatizo lakini nilikuwa na asiwasi mno kiasi kwamba nilishindwa kupumua vizuri..”
Kwa jinsi ambavyo alikuwa akiongea ni kama vile alikuwa akijiongelesha yeye mwenewe.
Edna hakutoa jibu na macho yake yalikuwa yamekodolea mataa ya jiji la Dar.
Raisi Jeremy alieleza ngonjera zake kwa zaidi ya dakika ishirini zote na ndani ya dakika hizo gari iliweza kufika ndani ya hoteli ya White Sand iliokuwa ikipatikana Africana.
Hoteli hio siku hio ilikuwa ikipokea wageni maalumu wale muhimu na taratibu ilikuwa hivyo kila wakati ambapo Raisi Jeremy anapofika, haikupokea wageni wa kawaida ambao walikuwa wakifika kwa ajili ya chakula cha usiku.
Baada ya kupokewa moja kwa moja alienda mpaka kwenye ukumbi binafsi na palepal e Raisi Jeremy aliagiza wahudumu kuleta chakula ambacho alikuwa ameagiza kiandaliwe kwa ajili ya binti yake.
Kama kawaida hakusahau vikijikeki ambavyo Edna alikuwa akipendelea na awamu hio vikeki hivyo vilikuwa vitamu mno kutokana na kwamba ulifanyika uwekezaji mkubwa wa kuvitengeneza, baba yake Recho ndio ambaye alikuwa akiendesha biashara hio mara baada ya Edna kumpatia mkopo Recho wa kufungua biashara.
“Unaonaje , leo tunaanza na hivi vikeki pamoja na baada ya hapo tutahamia kwenye vyakula vyote unavyopenda , utashangaa na kujiuliza kwanini najua ni kipi unapenda na kipi hupendi?”Aliongea huku akicheka lakini Edna alikuwa kimya tu.
“Edna nilikuwa nakuangalia tokea ukiwa mdogo, nakumbuka ni kipi unapenda na kipi hupendi”Aliongea bila ya kujali muonekano wa Edna wa kikauzu.
Dakika hio aliagiza aletewe mvinyo ambao alikuwa ameandaa mwenyewe na huku chakula kikiandaliwa kwa wingi na kufanya eneo hilo kujaa harufu nzuri ya kutia njaa.
Moja wapo ya vyakula ambavyo viliandaliwa vya kuongeza radha vya thamani kubwa ni Italian white truffles, French Foie gras, Middle East Cavier na mengineyo.
Kati ya hivyo ghali zaidi ni White Truffle na ilikuwa ngumu sana kupata hata kama unahela kwasababu kikawaida huharibika ndani ya siku kumi tu baada ya kuvunwa na pia kwa mwaka huvunwa mara moja tu, kutokana na uadimu wake basi thamani yake ilikuwa kubwa mno.
Sasa Edna alikuwa akipenda sana White Truffle kuliko alivyokuwa akipenda hata hivyo vjijiketi na ndio chakula ghali sana alichokuwa akinunua mara nyingi akisafiri nje ya nchi .
Lakini alijikuta akishangaa Raisi Jeremy aliwezaje kujua hayo yote.
“Nimeagiza watu wangu kusafirisha kwa kutumia ndege , hebu kata uonje kidogo”Aliongea kwa muonekano wa kubembeleza.
Na Edna alishindwa kujizuia na kuona shambulizi hilo limemwingia na hakugoma na kuchukua kisu na uma na kukata kidogo.
Edna mate yalimjaa na alikata na kupeleka mdomoni wakati huo raisi Jeremy akiwa bize kumwangalia na Edna ile anameza alijikuta akiona aibu mara baada ya kugundua macho ya Jeremy na aliishia kutoa tabasamu.
“Hatimae umetabasamu haha… nadhani sijafeli kama baba yako mzazi , ninao uwezo wa kumfanya binti yangu kutabasamu , ni hatua kubwa”Aliongea kwa kujigamba na kauli hio iilimfanya Edna kulainika.
Edna wakati huo na yeye alikuwa akifikiria na kujiuliza yaani kutabasamu kwake tu kumemfanya kuwa na furaha hivyo , pengine anapitia magumu ndio maana , Edna alijaribu kuvaa viatu vya Jeremy na kuona ana maisha ya upweke sana na pengine maisha yake yote alikuwa akiumia kuwa mbali na yeye.
Mawazo hayo yalimfanya kumuonea huruma baba yake na alianza kula kile chakula kwa kutokujilazimisha.
“Edna kula utosheke , mimi napendelea kula kabla ya kuungwa”Aliongea na kisha alikata pande na kumuwekewa Edna kwenye sahani.
“Inatosha siwezi kula sana ,,, na wewe unapaswa kula , si umesema hujakula bado”Aliongea Edna na kumfanya Raisi Jeremy kujisikia vizuri na alitoa kicheko cha furaha.
“Okey kwasababu umesema nile na mimi nakula”Aliongea huku akila kwa amani.
“Edna kama unapenda sana White Truffle nitakuwa nakuagizia”
“Hapana , kula mara moja moja kama hivi inatosha”Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy kukumbuka kitu.
“Ndio ndio , tena nilikuwa nishasahau kwamba binti yangu ni mwanamke tajiri Afrika nzima , kwako kutumia kiasi kidogo cha pesa kuagiza halitokuwa jambo gumu, nilisahau kabisa pengine ni kwasababu tu niliwaza kukupatia kitu kizuri unachopenda”
“Najua”
Muda huo hali ilikuwa ya kuchangamka na Raisi Jeremy aliongea kama vile kiredio chenye betri mpya.
“Edna wakati ulipokuwa shuleni nakumbuka somo la Kiswahili lilikuwa likikupiga chenga sana , wakati wa mtihani wako wa sekondari nilihofia kabisa ndio somo ambalo litakuangisha kimaksi hivyo niliongea na mtu na akakubadilishia maksi , kama nisingefanya vile wastani wako ungeshuuka kwa maksi ishirini… Athumani yule bwana badala ya kufanya mambo ya kuelekewa yeye kazi yake ni kutuma watu kukulinda tu, mimi ndio nilikuwa hatua mbele zaidi kufanya maamuzi, lakini hata hivyo ulikuwa ni kipanga kwenye masomo mengine ndio hivyo tamaa ziliniingia na kutaka kuona ukipata masomo yote A…..”
Jeremy aliongea kila matukio ambayo yalimtokea Edna shulenni , alionekana alikuwa akimfatilia Edna mwanzo mwisho lakini uongeaji wake ni kama ulikuwa ukienda nje ya mipaka na Edna aliweka uma na kisu chini.
“Mheshimiwa , si umesema unataka kuongea na mimi , nishamaliza chakula hivyo nenda moja kwa moja kwenye topiki”Aliongea Edna na kumfanya Jeremy kufunga mdomo huku akishangaa kidogo.
“Edna bado unanichukia kwasababu niliagiza watu kuwashughulikia wewe na Lanlan?”
Aliongea na Edna ambaye ndio mara ya kwanza anasikia Jeremy akikiri alijikuta akikunja ngumi chini ya meza , hakuamini angekiri bila wasiwasi.
“Edna kuna mambo mengi yanaendelea kwenye maisha yangu , kama nitasema nililazimishwa je utaweza kunniamini?, Edna unaweza usijue hili lakini mama yangu mzazi , yaani bibi yako anatokea ulimwengu usio onekana , nafasi yangu ndani ya ukoo wa mama ni ndogo na nilipewa jukumu ili kupandisha hadhi yangu napaswa kuhakikisha kutoa mchango ambao ni kuhakikisha napata mbinu ya mafunzo ya Roma , lakini Roma ni mgumu sana kudili nae ndio maana niliagiza watu lakini sikutaka kwenda mbali hivyo, uendelevu wa uongozi wangu pale Rwanda unategemeana na hizi jamii ambazo hazionekani ni rahisi kuniondoa madarakani kama ningekataaa waziwazi”
“Kwahio unachojaribu kusema ni kwamba madaraka kwako ni muhimu sana , yaani mpaka kupelekea kumteka mtoto na kuanza kumpiga?”
“Edna najua nilikosea na najisikia aibu kukiri hili, lakini Edna hebu fikiria , kama nitakuwa na nguvu kutoka ulimwengu usio onekana lakini pia kuweza kutawala taifa la Rwanda bila hofu itanisaidia kufanya mambo mengi kwa raia , lakini kama mtu atachukua nafasi yangu mipango yote ambayo nimepanga kwa ajili ya Rwanda haitoendelea, kupata mbinu ya Roma ya mafunzo ya kijini ilikuwa njia tu ya kuwafurahisha , najutia lakini ni swala la mara moja tu haliwezi kutokea tena”
“Kwahio umeniambia hayo yote na unataka nikushukuru?”
“Hapana ,, ninacho..”Jamaa alikosa usemi na palepale aliinua glasi ya mvinyo uliojaa na kisha alikunywa wote akaongeza na kidogo na kunywa.
“Mheshimiwa kama ushamaliza mimi naondoka”
Edna hakuwa na mpango wa kutaka kurudishwa, alipanga kupanda hata Taksi au hata kutembea maana tayari alikuwa kwenye levo ya mzunguko kamili.
Lakini muda uleule Jeremy alisimama kilevi na kisha akamsogelea Edna kama vile anataka kupigia magoti
“Mheshiiwa unataka kufanya ni..”Edna alijikuta akishangazwa na matendo yake.
“Edna hapana usiniite mheshimiwa , niite baba , Edna mwanangu niite baba”Aliongea kama vile kalewa.
Edna alikuwa ashasimama na alipiga hatua moja kurudi nyuma na alikuwa na wasiwasi kama kweli Raisi Jeremy alikuwa amelewa.
“Mheshimiwa hebu jitahadhari na matendo yako”
“Edna hivi unadhani nimelewa , hapa sijalewa kabisa nipo fiti”Aliongea huku akianza kulegea legea kama mlevi.
“Edna binti yangu nipo mpweke sana, naumia na kujutia kwa kila kitu, Mama yako ,Kizwe na Desmond wote walikufa mapema kwasababu yangu , mimi ndio mwenye makosa , tamaa zangu ndio zimepelekea vifo vyao , nimefanya mambo mengi ya kijinga….”
Edna aliishia kumwangalia hku akiwa kama haamini masikio yake na macho yake.
Raisi Jeremy aliinamisha kichwa chache chini kama kuna kitu anaangalia na kuanza kukitingisha.
“Edna naogopa kurudi Rwanda , naogopa kukaa ndani ya lile jengo la ikulu peke yangu , niko mwenyewe pale na kila anaenizunguka simwamini , najutia kweli , najua nilikosea lakini adhabu ninayopitia haivumiliki…”Aliongea huku akifikicha macho kama vile analia.
Alitia huruma, kama ni maigizo alikuwa amefaulu kwa kiasi kikubwa kwani alimfanya Edna kutokwa na machozi ya huruma.
Dakika ileile alimsogelea Edna na kumshika mikono yake kwa namna ya kubembeleza.
“Edna nisikilize , naomba usitalakiane na Roma , najua unahasira kwasababu ya Sophia na Lanlan lakini usitalakiane nae , utajutia huko mbeleni”
Dakika ambaye aliongea kauli hio Edna alibadilika na kutaka amwachie mkono wake lakini alikuwa akiogopa atadondoka na kuumia.
“Niachie mheshimiwa ,,,, hayo ni mambo yangu binafsi”
“Mambo yako ni yangu , mimi ni baba yako”
“Edna mmeoana ndani ya miaka mwili tu na unataka kuachana nae,inamaana mlioana kwa ajili ya kuachana , ndoa sio mchezo wa kitoto , kuishi peke yako ni rahisi lakini mambo ni tofauti kama mtakuwa pamoja , najua anakupenda sana hivyo nisikilize , haijalishi ni mara ngapi amekukosea lakini anao uwezo wa kukulinda , anakupenda sana na nitapata ahueni kama atakuwa upande wako, huelewi tu bado , Edna mimi kama mzazi wako nakuambia talaka ni kitu kibaya sana sijui kuhusu wengine lakini wewe ni binti yangu , mtoto wa kipenzi changu Raheli , njivunia sana na wewe ndio mtu pekee uliebakia ninaekujali , kama utatalakiana nae siwezi kumwangalia mama yako tena na bibi yako … Edna tafadhari kwa ajili yangu naomba usiachane na Roma, niambie muda huu unakwenda kurudiana nae”Aliongea kwa kulazimisha na kumfanya Edna kuanza kupandwa na jazba.
I